sw_ulb_rev/06-JOS.usfm

1330 lines
102 KiB
Plaintext
Raw Normal View History

2018-09-27 22:59:39 +00:00
\id JOS
\ide UTF-8
\h Yoshua
\toc1 Yoshua
\toc2 Yoshua
\toc3 jos
\mt Yoshua
\s5
\c 1
\p
\v 1 Sasa ilitokea baada ya kufa kwa Musa, mtumishi wa Yahweh, Yahweh alimwambia Yoshua, mwana wa Nuni, msaidizi mkuu wa Musa, kusema,
\v 2 "Musa, mtumishi wangu amekufa. Sasa basi inuka, vuka mto huu wa Yordani, wewe na watu hawa wote, kuingia katika nchi ambayo ninawapa - watu waisraeli.
\v 3 Nimewapa ninyi kila sehemu ambapo nyayo za miguu yenu itakanyaga. Nimewapa ninyi, kama nilivyomwahidi Musa.
\s5
\v 4 kuanzia jangwani na Lebanoni, hadi mto mkubwa wa Frati, nchi yote ya Wahiti, na hata Bahari kuu, ambako jua huzama, itakuwa nchi yenu.
\v 5 Hakuna mtu awaye yote atakayeweza kusimama kinyume chako siku zote za maisha yako. Nitakuwa pamoja nawe kama nilivyokuwa na Musa. Sitakupungukia wala kukuacha.
\s5
\v 6 Uwe hodari na jasiri. Wewe utawafanya watu hawa wairithi nchi ambayo niliwaahidi baba zao kuwa ningewapa.
\v 7 Uwe hodari na jasiri sana. uwe makini kutii sheria zote ambazo Musa mtumishi wangu alikuagiza. Usikengeuke upande wa kulia au wa kushoto, ili uweze kufanikiwa kila mahali utakapoenda.
\s5
\v 8 Siku zote uuongee juu ya kitabu hiki cha sheria. Utakitafakari mchana na usiku ili kwamba uweze kutii yote yaliyoandikwa humo. Kisha utastawi na kufanikiwa.
\v 9 Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hadori na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko.
\s5
\v 10 Kisha Yoshua akawaagiza viongozi wa watu,
\v 11 "Nendeni katika kambi na waagizeni watu, 'andaeni chakula kwa ajili yenu. Baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani na kuingia ndani na kuimiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi ili kuimiliki.""
\s5
\v 12 Yoshua akawaambia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase,
\v 13 "Kumbukeni maneno ambayo Musa, mtumishi wa Yahweh, aliwaaagiza aliposema, 'Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi pumziko, naye awapeni ninyi nchi hii.'
\s5
\v 14 Wake zenu, na watoto wenu na mifugo yenu itakaa katika nchi ambayo Musa aliwapa ninyi ng'ambo ya Yordani. Lakini watu wenu wa vita wataenda pamoja na ndugu zao na kuwasaidia.
\v 15 Mpaka hapo Yahweh atakapowapa ndugu zenu pumziko kama alivyowapa ninyi. Na wao pia watamiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi. Kisha mtarudi katika nchi yenu na kuimiliki, nchi ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa ninyi ng'ambo ya Yordani, mahali pa mapambazuko ya jua."
\s5
\v 16 Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, " Mambo yote uliyotuagiza tutayafanya, na kila mahali utakapotutuma tutaenda.
\v 17 Tutakutii kama tulivyomtii Musa. Yahweh Mungu wako na awe pamoja nawe tu kama aliyokuwa pamoja na Musa.
\v 18 Yeyote anayeasi maagizo yako na kutotii maneno yako atauawa. Uwe hodari na jasiri tu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni aliwatuma watu wawili kwa siri kama wapelelezi kutoka Shitimu. Akisema, "Nendeni mkaiangalie nchi, hasa Yeriko." Walienda na wakafika katika nyumba ya kahaba ambaye jina lake ni Rahabu, na wakalala hapo.
\v 2 Mfalme wa Yeriko aliambiwa, "Tazama watu wa Israeli wamekuja kuipeleleza nchi."
\v 3 Mfalme akatuma neno kwa Rahabu kusema, " Watoe watu waliokuja kwako ambao wameingia nyumbani mwako, kwa kuwa wamekuja kuipeleleza nchi yote."
\s5
\v 4 Lakini mwanamke alikuwa amekwisha kuwachukua wale watu wawili na kuwaficha. Na akasema, "Ndiyo, watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka.
\v 5 Ilipokuwa jioni wakati wa kufungwa kwa lango la mji, waliondoka. Sijui mahali walikoelekea. Mnaweza kuwakamata kama mtawafuata upesi.
\s5
\v 6 Lakini yeye aliwapandisha juu darini na kuwaficha kwa mabua ya kitani ambayo alikuwa ameyalaza darini.
\v 7 Hivyo, watu waliwafuatilia njiani iliyoeleka katika vivuko vya Yordani. Na milango ilifungwa mara tu baada ya wale watu waliofuata kutoka nje.
\s5
\v 8 Wale wanaume walikuwa hajalala usiku, wakati alipowaendea kule darini.
\v 9 Akawaambia, " Ninajua kwamba Yahweh amewapa ninyi nchi na kwamba hofu juu yenu imetuingia. Watu wote wanaoishi katika nchi watayeyuka mbele yenu.
\s5
\v 10 Tumesikia jinsi ambavyo Yahweh alivyokausha maji ya Bahari ya Mianzi kwa ajili yenu wakati mkitoka Misri. Na tumesikia mlichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori walioko upande mwingine wa Yordani - Sihoni na Ogu - ambao mmewaangamiza kabisa.
\v 11 Mara tu tuliposikia, mioyo yetu iliyeyuka na hapakuwa na ujasiri wowote uliosalia kwa mtu yeyote - kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ni Mungu aliye juu mbinguni na chini duniani.
\s5
\v 12 Sasa basi, tafadhali mniapie kwa Yahweh kwamba kama nilivyokuwa mwema kweu, nanyi pia mtaitendea mema nyumba ya baba yangu. Nipeni ishara ya uhakika
\v 13 kwamba mtanihifadhi maisha ya baba, mama, kaka, dada zangu na famiie zao, na kwamba mtatuokoa kutoka katika kifo.
\s5
\v 14 Wanaume wakamjibu, "maisha yetu kwa ajili ya yenu, hata kifo! Kama hamtasema habari zetu, na Yahweh akisha kutupa nchi hii, tutakuwa wenye huruma na waaminifu kwenu."
\s5
\v 15 hivyo aliwashusha chini kwa kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Nyumba ambayo alikuwa anaishi ilijengwa katika ukuta wa mji.
\v 16 Akawaambia, "Nendeni milimani la sivyo watu waliowafuata watawaona. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watu waliowafuata watakaporudi. Kisha nendeni zenu."
\v 17 Wanaume wakamwambia, "Hatutakuwa tumefungwa na ahadi ulizotufanya tuape mbele zako, kama hautalifanya hili.
\s5
\v 18 Tutakapokuja katika nchi, ni lazima uifunge kamba hii nyekundu katika dirisha ulilotushushia chini, na utawakusanya katika nyumba baba yako, mama yako, kaka zako na wote wa nyumba ya baba yako.
\v 19 Na yeyote aendaye mtaani nje ya milango ya nyumba yako,, damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao na hatutakuwa na hatia yoyote. Lakini kama mkono utanyoshwa juu ya mtu yeyote aliye pamoja nawe katika nyumba, damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu.
\s5
\v 20 Na ikiwa utaongea juu ya suala letu, tutakuwa huru dhidi ya kiapo ulichotuapisha.
\v 21 Rahabu akawajibu, " Yote mliyosema nayatimie." Akawatoa mbali na wakaondoka. Kisha akaifunga kamba nyekundu katika dirisha.
\s5
\v 22 Wakaondoka na kwenda juu milimani na walikaa huko kwa siku tatu hadi pale wale waliowafuatilia waliporudi. Wale waliowafuata walitafuta njiani pote bila kuwaona.
\s5
\v 23 Wale watu wawili walirudi na kuvuka mto na wakafika kwa Yoshua mwana wa Nuni, na walimwambia kila kitu kilichotokea kwao.
\v 24 Nao wakasema kwa Joshua, "kwa kweli Yahweh ametupa nchi hii. Wenyeji wote wa nchi wanayeyuka kwasababu yetu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Yoshua aliamka asubuhi na mapema, nao walisafiri kutoka Shitimu. Walifika Yordani, yeye na watu wote wa Israeli, na wakapiga kambi hapo kabla hawajavuka ng'ambo.
\s5
\v 2 Baada ya siku tatu, maafisa walienda katika kambi, wakawaagiza watu,
\v 3 "Mtakapoona sanduku la agano la Yahweh Mungu wenu, na makuhani kutoka miongoni mwa Walawi wamelibeba, ni lazima muondoke sehemu hii na kulifuata.
\v 4 Lazima kuwe na umbali wa dhiraa elfu moja kati yenu na sanduku. Msilisogelee karibu, ili muweze kuiona njia ya kupitia, kwakuwa hamjawahi kupita njia hii kabla.
\s5
\v 5 Yoshua akawaambia watu, "Jitakaseni ninyi wenyewe keso, kwa kuwa Yahweh atafanya maajabu miongoni mwenu."
\v 6 Kisha Yoshua akawaambia makuhani, "Chukueni sanduku la agano, na kulipitisha mbele za watu." Hivyo, wakalichukua sanduku la agano na wakaenda mbele za watu.
\s5
\v 7 Yahweh akamwambia Yoshua, "Siku hii nitakufanya kuwa mtu mkubwa katika macho ya Waisraeli wote. Watajua kuwa kama nilivyokuwa na Musa ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe.
\v 8 Utawaamuru makuhani ambao hulibeba sanduku la agano, 'Mtakapofika katika ukingo wa maji ya Yordani, ni lazima msimame katika Mto Yordani.'"
\s5
\v 9 Kisha Yoshu akawaambia watu wa Israeli, "Njooni hapa na msikilize maneno ya Yahweh Mungu wenu.
\v 10 Kwa hili mtajua kwamba Mungu aliye hai yuko miongoni mwenu na kwamba atawaondosha mbele yenu Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagrigashi, Waamori na Wayebusi.
\v 11 Tazama! Sanduku la agano la Bwana wa nchi yote litavuka mbele yenu katika Yordani.
\s5
\v 12 Sasa chagueni wanaume kumi na wawili kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja katika kila kabila.
\v 13 Wakati nyayo za miguu ya makuhani walichukualo sanduku la Yahweh, Bwana wa nchi yote, zitakapogusa maji ya Yordani, maji ya Yordani yatatindika, na hata maji yatiririkayo kutoka juu yatakoma kutiririka nayo yatasimama kama chuguu.
\s5
\v 14 Hivyo wakati watu walipotoka ili kuvuka Yordani, makuhani waliobeba sanduku la agano waende mbele ya watu.
\v 15 Mara tu wale walichukuao sanduku wakiisha kufika Yordani, na miguu ya watu wale waliobeba sanduku itakapotiwa katika ukingo wa maji (maana sasa Yordani hujaa hadi katika kingo zake zote katika kipindi chote cha mavuno),
\v 16 maji yote yaliyotiririka kutoka juu yalisimama katika chuguu kimoja. Maji yakakoma kutiririka kutoka katika umbali mrefu. Maji yaliacha kutiririka kutoka Adam, mji ulio karibu na Zarethani, hadi bahari ya Negevu, Bahari ya Chumvi. Na watu walivuka ng'ambo karibu na Yeriko.
\s5
\v 17 Makuhani waliolibeba sanduku la agano la Yahweh walisimama katika nchi kavu katikati ya Yordani mpaka watu wote wa Israeli walipokwisha kuvuka katika nchi kavu.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Watu wote walipokwisha kuvuka Yordani, Yahweh akamwambia Yoshua,
\v 2 "Chagueni wenyewe watu waume kumi na wawili, mmoja katika kila kabila.
\v 3 Wape agizo hilo: 'Chukueni mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani mahali wanaposimama makuhani katika nchi kavu, na wayalete na kuyaweka chini katika sehemu ambapo mtalala usiku wa leo.
\s5
\v 4 Kisha Yoshua akawaita wanaume kumi na wawili ambao aliwachagua kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja kutoka kila kabila.
\v 5 Yoshua akawaambia, "Nendeni mbele za sanduku la Yahweh Mungu wenu katikati ya Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe moja mabegani mwake, kulingana na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli.
\s5
\v 6 Hii itakuwa ni ishara miongoni mwenu kwa ajili yenu wakati watoto wenu watakapowauliza katika siku zijazo, 'Nini maana ya mawe haya kwenu?'
\v 7 Ndipo mtakapowaambia, 'Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh. Lililpopitishwa katika Yordani, maji ya Yordani yalisimamishwa. Hivyo, mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.'"
\s5
\v 8 Watu waisraeli walifanya kama Yoshua alivyowaagiza, na walichukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani, kama Yahweh alivyomwambia Yoshua, walipangwa sawa sawa na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli. Waliyachukua mawe mpaka mahali walipolala na wakayaweka chini huko.
\v 9 Kisha Yoshua akayapanga mawe kumi na mbili katikati ya Yordani, katika sehemu ambapo ilisimama miguu ya makuhani waliolichukua sanduku la agano. Na kumbukumbu hiyo ipo hadi leo.
\s5
\v 10 Makuhani waliolichukua sanduku walisimama katikati ya Yordani mpaka pale kila kitu ambacho Yahweh alimwamuru Yoshua kuwaambia watu kilipokamilika, sawa sawa na yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua. Watu walifanya haraka na wakavuka.
\v 11 Wakati watu wote walipokwisha kuvuka, sanduku la Yahweh pamoja na makuhani walivuka mbele za watu.
\s5
\v 12 Kabila la Rubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase walipita kama jeshi mbele ya watu wa Israeli, kama ambavyo Musa alivyowaambia.
\v 13 Yapata watu watu elfu arobaini walioandaliwa kwa vita walipita mbele za Yahweh, kwa ajili ya vita katika uwanda wa Yeriko.
\v 14 Katika siku hiyo Yahweh alimfanya Yoshua kuwa mkuu katika macho ya watu wote wa Israeli. Walimheshimu - kama walivyomheshimu Musa - siku zake zote.
\s5
\v 15 Kisha Yahweh akamwambia Yoshua,
\v 16 "Waamuru makuhani wanaolibeba sanduku la ushuhuda watoke katika Yordani."
\s5
\v 17 Hivyo Yoshua akawaamuru makuhani, '' pandeni mtoke Yordani."
\v 18 Wakati makuhani wenye kulibeba sanduku la agano la Yahweh walitoka katikati ya Yordani, na nyayo za miguu yao ilikuwa imeinuliwa katika nchi kavu, kisha maji ya Yordani yalirudi katika sehemu zake na kujaa hadi katika kingo zake kama ilivyokuwa siku nne zilizopita.
\s5
\v 19 Katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, watu walikwea kutoka Yordani. Wakakaa huko Gilgali, mashariki mwa Yeriko.
\v 20 Mawe kumi na mawili ambayo yalichukuliwa katika Yordani, Yoshuua aliyasimamisha hapo Gilgali.
\v 21 Aliwaambia watu wa Israeli, " wakati watoto wenu watakapowauliza baba zao katika wakai ujao, 'Mawe haya ni ya nini?'
\s5
\v 22 Waambieni watoto wenu, 'Hapa ndipo Waisraeli walivuka Yordani katika nchi kavu.
\v 23 Yahweh Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mpaka hapo Yahweh Mungu wako aliyoyafanya katika bahari ya mianzi, ambayo aliikausha kwa ajili yetu ili tupite juu yakes,
\v 24 ili kwamba watu wote wa nchi wajue kwamba mkono wa Yahweh ni nguvu, na kwamba mtamweshimu Yahweh Mungu wenu milele.''
\s5
\c 5
\p
\v 1 Mara tu waliposikia wafalme wa Waamori walio upande wa magharibi wa Yordani, na wafalme wote wa Wakanaani waliokuwa katika pwani ya Ziwa kuu, waliposikia ya kwamba Yahweh alikuwa ameyakausha maji ya Yordani mpaka pale waisraeli wote walipomaliza kuvuka, mioyo yao ikayeyuka, na hapakuwa na moyo wowote ndani yao kwa sababu ya watu wa Israeli.
\s5
\v 2 Kwa wakati huo Yahweh alimwambia Yoshua, "Tengenezeni visu vya mawe na mara moja mwatahiri wanaume wote wa Israeli."
\v 3 Kisha Yoshua alijifanyia visu vya mawe na akawatahiri wanaume wote wa Gibea Haaraloti.
\s5
\v 4 Na hii ndo sababu ya Yoshua kuwatahiri; wanaume wote waliotoka Misri, pamoja na wanaume wa vita walikuwa wamekwisha kufa njiani katika nyikani, baada ya kukwea kutoka Misri.
\v 5 Ingawa wanaume wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, bado hapakuwa na kijana yeyote aliyekuwa ametahiriwa kati ya vijana wote waliozaliwa nyikani katika njia ya kutoka Misri.
\s5
\v 6 Kwasababu watu wa Israeli walitembea nyikani miaka arobaini, mpaka watu wa vita, yaani wanaume wote waliotoka Misri walikufa, kwasababu hawakuitii sauti ya Yahweh. Yahweh aliwaapia kwamba hawataruhusu kuiona nchi ambayo aliwaapia mababa zao kwamba angetupatia sisi, nchi inayotiririka maziwa na asali.
\v 7 Na badala yao, Yahweh aliwainua watoto wao kuchukua nafasi zao ambao Yoshua aliwatahiri, kwasababu walikuwa bado hajatahiriwa njiani.
\s5
\v 8 Walipokwisha kutahiriwa wote, walibaki mahali walipokuwa katika kambi mpaka walipopona.
\v 9 Na Yahweh akasema na Yoshua, "Siku hii nimeiondoa kwenu aibu ya Misri." Hivyo, mahali pale paliitwa Gilgali hadi leo.
\s5
\v 10 Watu wa Israeli walipiga kambi hapo Gilgali. Waliitunza Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika uwanda wa Yeriko.
\v 11 Na siku iliyofuata baada ya Pasaka, walikula sehemu ya mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka iliyokaangwa katika siku hiyo iyo.
\s5
\v 12 Mana zilikoma siku ile walipokula mazao ya nchi. Hapakuwa tena na mana kwa watu wa Israeli, bali walikula mazao ya nchi ya Kanaani mwaka huo.
\s5
\v 13 Wakati Yoshua alipokaribia Yeriko, aliinua macho na kuangalia, na tazama, mtu alikuwa amesimama mbele yake, alikuwa amechomoa upanga wake na ulikuwa mkononi mwake. Yoshua alimwendea na kumwambia, "Je uko kwa ajili yetu au kwa ajli ya maadui zetu?"
\s5
\v 14 Akajibu, la hasha. Maana mimi ni amiri wa jeshi la Yahweh. Sasa nimekuja. Kisha Yoshua akainamisha uso wake juu ya nchi akaabudu na akamwambia, "Bwana wangu anasema nini kwa mtumwa wake?"
\v 15 Amiri wa jeshi la Yahweh akamwambia Musa, "Vua viatu vyako miguuni mwako, kwasababu sehemu uliyosimama ni takatifu." Na Yoshua akafanya hivyo.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Basi, milango yote ya Yeriko ilikuwa imefungwa kwasababu ya jeshi la Israeli. Hapakuwa na mtu wa kutoka nje au kuingia ndani.
\v 2 Yahweh akamwambia Yoshua, "Tazama, nimeweka Yeriko katika mkono wako, mfalme wake pamoja na wanajeshi wake waliofunzwa.
\s5
\v 3 Ni lazima kutembea kwa kuuzunguka mji, wanaume wote wa vita wauzunguke mji mara moja. Ni lazima mfanye hivi kwa siku sita.
\v 4 Makuhani saba lazima wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele za sanduku. Na katika siku ya saba, ni lazima mtembee kwa kuuzunguka mji mara saba, na makuhani lazima wapulize tarumbeta.
\s5
\v 5 Kisha watapuliza pembe za kondoo waume kwa nguvu kuu, na mtakaposikia sauti za tarumbeta watu wote na wapige kelele kwa mshindo mkuu, na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale. Wanajeshi ni lazime washambulie, kila mmoja eende mbele moja kwa moja.
\s5
\v 6 Ndipo Yoshua mwana wa Nuni, aliwaita makuhani na kuwaambia, "Lichukueni sanduku la agano, na waacheni makuhani saba wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Yahweh."
\v 7 Yoshua aliwaambia watu, "Nendeni na mkatembee kuuzunguka mji, na watu wa vita wataenda mbele ya sanduku la Yahweh."
\s5
\v 8 Makuhani saba walibeba tarumbeta saba za pembe za kondoo mbele ya Yahweh kama Yoshua alivyowaambia watu. Na walivyokuwa akiendelea mbele, walipuliza tarumbeta.
\v 9 Sanduku la Yahweh liliwafuata kwa nyuma yao. Watu wa vita walitembea mbele ya makuhani, na walipuliza tarumbeta zao, lakini walinzi wa nyuma walilifuata sanduku kwa nyuma, na makuhani waliendelea kupuliza tarumbeta zao.
\s5
\v 10 Lakini Yoshua aliwaagiza watu, akisema, "Msipige kelele. Sauti yoyote isitoke vinywani mwenu mpaka siku nitakayowaambia kupiga kelele. Ndipo hapo mtakapopiga kelele."
\v 11 Hivyo, alisababisha sanduku la Yahweh kuuzunguka mji mara moja kwa siku hiyo. Kisha wakaingia katika kambi yao, wakakaa usiku ule katika kambi.
\s5
\v 12 Basi Yoshua aliamka asubuhi na mapema, na makuhani wakalichukua sanduku la Yahweh.
\v 13 Makuhani saba waliobeba tarumbeta saba za pembe za kondoo waume walikuwa mbele ya sanduku la Yahweh, wakitembea kwa ushupavu, huku wakipuliza tarumbeta. Wanajeshi wenye silaha walikuwa wakitembea mbele yao, lakini walinzi wa nyuma walitembea nyuma ya sanduku la Yahweh, huku tarumbeta ziliendelea kupigwa.
\v 14 Walitembea kuuzunguka mji mara moja katika siku ya pili na kisha wakarudi kambini. Walifanya hivi kwa siku sita.
\s5
\v 15 Ilikuwa ni katika siku ya saba ambayo waliamka mapema katika mapambazuko, na walitembea kuuzunguka mji kwa namna ile kama ilivyokuwa kawaida yao, katika siku hii walifanya mara saba.
\v 16 Ilikuwa ni katika siku ya saba ambapo makuhani walipiga tarumbeta, na ya kwamba Yoshua aliwaagiza watu, "Pigeni kelele! Kwa kuwa Yahweh amewapa ninyi mji.
\s5
\v 17 Mji pamoja na vitu vyote ndani yake vitatengwa kwa Yahweh kwa ajili ya uharibifu. Ni Rahabu yule kahaba pekee ataishi - yeye pamoja wote waliokuwa pamoja naye katika nyumba - kwasababu aliwaficha watu tuliowatuma.
\v 18 Lakini kwenu, iweni waangalifu juu ya kuchukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu, ili baada ya kuvitia alama kwa ajili ya kuharibiwa, msichukue hata kimoja wapo. Na kama mtafanya hivi, mtaifanya kambi ya Waisraeli iharibiwe na mtaleta matatizo katika kambi.
\v 19 Fedha zote, dhahabu na vitu vilivyotengenezwa kwa shaba na chuma vilitengwa kwa ajli ya Yahweh."
\s5
\v 20 Hivyo, watu wakapiga kelele, na wakatoa sauti kwa kupuliza tarumbeta. Ilikuwa watu waliposikia sauti za tarumbeta, walipiga kelele kwa sauti kuu, na ukuta ulianguka chini kabisa na kwamba watu waliungia mji, kila mmoja alisonga mbele moja kwa moja. Na waliuteka mji.
\v 21 Waliteketeza kabisa kila kitu kilichokuwa katika mji kwa makali ya upanga - wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa, ng'ombe, kondoo na punda.
\s5
\v 22 Kisha Yoshua akawaambia wale watu wawili walioipeleleza nchi, "Nendeni katika nyumba ya kahaba, mtoeni mwanamke na wote walio pamoja naye, kama mlivyomwapia."
\s5
\v 23 Basi, vijana wale walioipeleleza nchi waliingia ndani na kumtoa Rahabu nje. Walimtoa nje baba yake, mama, kaka, na ndugu wote waliokuwa pamoja naye. waliwaleta katika sehemu ya nje ya kambi ya Waisraeli.
\v 24 Na ndipo waliuteketeza mji na kila kitu ndani yake. Isipokuwa fedha, dhahabu na vyombo vya fedha na chuma viliwekwa kwa hazina ya nyumba ya Yahweh.
\s5
\v 25 Bali Yoshua alimruhusu Rahabu kahaba, nyumba ya baba yake, na wote waliokuwa pamoja naye waishi. Mpaka leo hivi anaishi Israeli kwasababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko.
\s5
\v 26 Kisha katika kipindi hicho, Yoshua aliwaamuru kwa kiapo na kusema, "Alaaniwe machoni pa Yahweh mtu yule anayeujenga mji huu, Yeriko. Ataujenga msingi kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza, na kwa gharama ya mzaliwa wake wa pili atapachika milango yake."
\v 27 Basi Yahweh alikuwa pamoja na Yoshua, na umaarufu wake ulienea katika nchi yote.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Lakini watu wa Israeli hawakutenda katika uaminifu kuhusiana na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu. Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, kutoka katika kabila la Yuda, alivitwaa baadhi ya vitu hivyo vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya uharibifu, na hasira ya Yahweh iliwaka juu yawatu wa Israeli.
\s5
\v 2 Yoshua alituma watu kutoka Yeriko kwenda Ai, mji uliokuwa karibu na Bethi Aveni, mashariki mwa Betheli. Aliwaambia, "Nendeni na mkaipeleleza nchi." Wale watu walikwea na kuipeleleza Ai.
\v 3 Waliporudi kwa Yoshua, walimwambia, "Usitume watu wote kwenda Ai. Tuma tu watu elfu mbili au elfu tatu waende kuiteka Ai. Usiwafanye watu wateseke katika vita, kwani ni watu wachache."
\s5
\v 4 Hivyo ni watu wapatao elfu tatu tu kutoka katika jeshi ndio walioenda, lakini watu hawa waliwakimbia watu wa Ai.
\v 5 Watu wa Ai waliwaua watu wapatao thelathini na sita, waliwafuata katika lango la mji hadi katika machimbo ya mawe, na waliwauwa walipokuwa wakishuka katika kilima. Na mioyo ya watu ilijawa hofu na ujasiri wao ukawatoka.
\s5
\v 6 Basi Yoshua alizirarua nguo zake. Yeye pamoja na wazewe wa Israeli waliweka mavumbi juu ya vichwa vyao na wakainamisha vichwa vyao hadi katika nchi mbele ya sanduku la Yahweh, na walibaki pale mpaka jioni.
\v 7 Kisha Yoshua akasema, "Oo, Yahweh Bwana, kwanini umewavusha watu hawa ng'ambo ya Yordani? Kutuweka katika mikono ya Waamori ili kutuangamiza? ikiwa kama tulifanya maamuzi tofauti na tungekaa katika upande mwingine wa Yordani!
\s5
\v 8 Bwana, niseme nini, baada ya Israeli kuwatega migongo maadui zao?
\v 9 Kwa kuwa Wakaanani na wenyeji wote wa nchi watakaposikia, watatuzunguka na kuwafanya watu wa nchi kulisahau jina letu. Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
\s5
\v 10 Yahweh akamwambia Yoshua, "Inuka! kwanini umelala kifudifudi?
\v 11 Israeli imetenda dhambi. Wamevunja agano langu nililowaagiza. Wameiba baadhi ya vitu vilivyokuwa vimetengwa. Wameiba na kisha pia wakaficha dhambi yao kwa kuweka vitu vile walivyochukua miongoni mwa mali zao wenyewe.
\v 12 Na matokeo yake ni kwamba watu wa Israeli hawataweza kusimama mbele za maadui zao. Walitega migongo yao kwa maadui zao kwasababu wao wenyewe wametengwa kwa ajili ya uharibifu. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka pale mtakapoteketeza vitu vile vilivyotakiwa kuharibiwa, lakini sasa bado viko miongoni mwenu.
\s5
\v 13 Inuka! Waweke watu wakfu kwangu, na uwaambie, 'Jiwekeeni wakfu ninyi wenyewe kesho. Kwa kuwa, Yahweh, Mungu wa Israeli asema hivi, "Kuna vitu vilitengwa ili kuteketezwa ambavyo bado viko miongoni mwenu, Israeli. Hamtaweza kusimama mbele ya maadui zenu mpaka pale mtakapoviondoa miongoni mwenu vitu vyote ambavyo vilitengwa kwa ajili ya kuteketezwa."
\s5
\v 14 Asubuhi, mtajisogeza wenyewe kwa makabila. Kabila lile ambalo Yahweh atalichagua litasogea karibu kwa koo zake. Ukoo ule ambao Yahweh atauchagua lazima usogee karibu kwa nyumba. Nyumba ambayo Yahweh ataichagua lazima isogee karibu kwa mtu mmoja mmoja.
\v 15 Itakuwa hivi mtu yule atakayechaguliwa na aliye navyo vitu hivyo vilivyotengwa kwa ajili ya kuharibiwa, atachomwa moto, yeye na kila kitu alichonacho, kwasababu amelivunja agano la Yahweh na kwasababu amefanya jambo la aibu katika Israeli.'"
\s5
\v 16 Basi, Yoshua aliamka asubuhi na mapema na aliwaleta Israeli karibu, kabila kwa kabila, na kabila la Yuda lilichaguliwa.
\v 17 Yoshua akazisogeza koo za Yuda karibu, na ukoo wa Zera ulichaguliwa. Akausogeza karibu ukoo wa Zera mtu kwa mtu, na Zabdi alichaguliwa.
\v 18 Akaisogeza karibu nyumba ya Zabdi mtu kwa mtu, na Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, kutoka kabila la Yuda, alichaguliwa.
\s5
\v 19 Kisha Yoshua akamwambia Akani, "Mwanangu, niambie ukweli mbele za Yahweh, Mungu wa Israel, na ufanye ukiri wako kwake. Tafadhali niambie kile ulichofanya. Usinifiche."
\v 20 Akani akamjibu Yoshua, " Kwa kweli nimetenda dhambi mbele Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 21 Nilichofanya ni hiki: Nilipoona miongoni mwa nyara mkoti mzuri kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kipande cha dhahabu chenye uzito wa shekeli hamsini, nilivitamani na nikavichukua. Vimefichwa chini ardhini katikati ya hema langu, na fedha iko chini yake."
\s5
\v 22 Yoshua akatuma wajumbe waliokimbia mpaka kwenye hema mahali palipokuwa na vile vitu. Walipoangalia, waliviona vimefichwa katika hema lake, na fedha chini yake.
\v 23 Walivichukua vitu hivyo kutoka katikati ya hema na kuvileta kwa Yoshua na watu wote wa Israeli. Walivimwaga mbele za Yahweh.
\s5
\v 24 Kisha Yoshua na Waisraeli wote pamoja naye, walimchukua Akani mwana wa Zera, na fedha, na koti, na kipande cha dhahabu, wana na binti zake, ng'ombe zake, punda zake, kondoo zake, hema lake, na kila kitu alichokuwa nacho, na wakavileta hata bonde la Akori.
\s5
\v 25 Kisha Yoshua akasema, "Kwanini umetusumbua? Leo Yahweh atakutesa na wewe." Waisraeli wote wakampiga kwa mawe. Na wakawachoma wote kwa moto, na wakawapiga mawe.
\v 26 Kisha wakaweka juu yake kichuguu kikubwa cha mawe ambayo yapo hata leo. Yahweh akaachilia mbali hasira yake. Hivyo basi, jina la mahali hapo likawa Akori hata leo.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Yoshua, "Usiogope; usivunjike moyo. Chukua pamoja nawe watu wa vita. Pandeni kwenda Ai. Tazama nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai, watu wake, mji wake na nchi yake.
\v 2 Mtafanya hivyo pia huko Ai na mfalme wake kama mlivyofanya kwa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mtachukua nyara na mifugo kwa ajili yenu. Pangeni mashambulizi ya uviziaji nyuma ya mji."
\s5
\v 3 Basi Yoshua aliinuka na akawachukua kwenda Ai watu wote wa vita. Kisha Yoshua akachagua watu elfu thelathini - wenye nguvu na ujasiri - na aliwatuma waende wakati wa usiku.
\v 4 Aliwaamuru, "Tazama, mtalala katika hali ya mashambulizi ya uviziaji dhidi ya mji, kwa nyuma yake. Usiende mbali sana na mji, lakini ninyi nyote muwe tayari.
\s5
\v 5 Mimi pamoja na watu wote walio pamoja nami tutaukaribia mji. Na wakati watakapokuja kutushambulia sisi, tutawakimbia kama tulivyofanya hapo mwanzo.
\v 6 Watatoka nje watukimbize mpaka hapo tutakapokuwa tumewavuta mbali sana na mji, watasema, "Wanatukimbia kama walivyofanya mara ya mwisho.' Hivyo tutawakimbia na kwenda mbali.
\v 7 Kisha mtapanda kutoka sehemu mliyojificha, na mtauteka mji. Yahweh Mungu wenu atawapa mkononi mwenu.
\s5
\v 8 Tazama nimewaamuru, mtakapouteka mji, mtauchoma moto. Mtayafanya haya wakati mtakapotii agizo lililotolewa katika neno la Yahweh."
\v 9 Yoshua akawatuma, na wakaenda sehemu ya uviziajia, na wakajificha kati ya Betheli na Ai sehemu ya magharibi ya Ai. Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku ule.
\s5
\v 10 Yoshua aliamka asubuhi na mapema na akawaandaa tayari wanajeshi wake, Yoshua na wazee wa Israeli walishambuliwa watu wa Ai.
\v 11 Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda na kuukaribia mji. Walisogea karibu na mji na wakapiga kambi sehemu ya kasikazini mwa Ai. Kulikuwa na bonde kati yao na Ai.
\v 12 Alichukua watu wapatao elfu tano hivi na akawaweka katika hali ya kuvizia katika upande wa magharibi mwa mji kati ya Betheli na Ai.
\s5
\v 13 Waliwapanga wanajeshi wote, jeshi kuu katika upande wa kasikazini mwa mji, na walinzi wa nyuma upande wa magharibi mwa mji. Yoshua alilala bondeni usiku ule.
\v 14 Na ilikuwa alipoona hilo mfalme wa Ai, yeye pamoja na jeshi lake, waliamka asubuhi na mapema na walitoka kwa haraka kwenda kuwashambulia Israeli katika eneo linalokabili bonde la Mto Yordani. Hakujua kuwa kulikuwa na shambulizi la kuvizia lilikuwa linasubiria kushambulia kutokea kwa nyuma ya mji.
\s5
\v 15 Yoshua na Waisraeli wote walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu, na wakakimbia kuelekea nyikani.
\v 16 Watu wote waliokuwa kwenye mji waliitwa kwa pamoja waende mbele yao, na walienda mbele ya Yoshua na kwa jinsi hiyo walivutwa mbali na mji.
\v 17 Hapakuwa na mtu mme aliyesalia Ai na Betheli ambaye alikuwa hajaenda nje kuwafuatilia waisraeli. Na walipokuwa wanawafuatilia Waisraeli, Wakatoka na waliuacha mji wazi.
\s5
\v 18 Yahweh akamwambia Yoshua, "Nyosha mkuki huo ulio mkononi mwako kuelekea Ai, kwa kuwa nitaitia Ai mikononi mwako." Yoshua akaunyosha mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea mji.
\v 19 Wanajeshi waliojificha katika hali ya kuvizia walitoka upesi katika eneo lao mara tu alipounyosha mkono wake. Walikimbia mbio na kuuingia mji na kuuteka. Na kwa haraka wakauchoma moto mji.
\s5
\v 20 Watu wa Ai waligeuka na kuangalia nyuma. Waliona moshi kutoka katika mji ukipanda kwenda angani, na hawakuweza kutoroka kwa njia hii au ile. Kwa kuwa wanajeshi wa Israelei waliokuwa wamekimbia katika nyika, sasa walirudi kuwakabili wale waliokuwa wanawafuatilia.
\v 21 Na wakati Yoshua na Israeli wote walipoona kuwa wale watu wa kuvizia wameuteka mji kwa ule moshi uliokuwa ukipanda, waligeuka nyuma na kuwaua watu wa Ai.
\s5
\v 22 Na wanajeshi wengine wa Israeli, wale waliokuwa wameingia ndani ya mji, walitoka nje ili kuwashambulia. Hivyo, watu wa Ai walikamatwa katikati ya majeshi ya Israeli, baadhi katika upande huu na wengine katika upande ule.
\v 23 Lakini walimhifadhi mfalme wa Ai, ambaye walimteka akiwa hai, na kisha wakamleta kwa Yoshua.
\s5
\v 24 Ilikuwa baada ya Israeli walipokuwa wamemaliza kuuwaua wenyeji wote wa Ai katika uwanda kariibu na nyika mahali walipowafuata, na baada ya wao wote, hata yule wa mwisho, walipokuwa wamekwisha kulala kwa ncha ya upanga, Waisraeli wote walirudi Ai. Waliuteka mji kwa ncha ya upanga.
\v 25 Wale wote walikufa siku hiyo walikuwa watu elfu kumi na mbili elfu, wanaume na wanawake, wote ni watu wa Ai.
\v 26 Yoshua hakuukunja mkono wake ambao alikuwa ameunyosha huku akishikilia mkuki wake, mpaka pale alipowateketeza kabisa watu wote wa Ai.
\s5
\v 27 Waisraeli walichukua tu wanyama na nyara kutoka katika mji kwa ajili yao wenyewe, kama Yahweh alivyokuwa amemwagiza Yoshua.
\v 28 Yoshua aliichoma Ai na kuigeuza kuwa kichuguu cha mapango. Ni mahali palipoachwa ukiwa hata leo.
\s5
\v 29 Alimtundika mfalme wa Ai juu ya mti mpaka jioni. Na jua lilipokuwa linaenda kuzama, Yoshua aliwaagiza na wakautoa mwili wa mfalme wakaushusha chini ya mti na kuutupa mbele ya malango ya mji. Huko wakaweka kichuguu kikubwa cha mawe juu yake. Kichuguu hicho kimebaki huko hata leo.
\s5
\v 30 Kisha Yoshua akajenga madhabahu kwa Yahweh, Mungu wa Israeli katika Mlima wa Ebali,
\v 31 kama vile Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza watu wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa: "Madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna mtu yeyote aliyetumia zana ya chuma." Na allimtolea Yahweh sadaka ya kuteketezwa juu yake na wakatoa sadaka ya amani.
\v 32 Na huko aliandika juu ya mawe nakala ya sheria za Musa mbele ya watu wa Israeli.
\s5
\v 33 Waisraeli wote, wazee wao, maafisa, na waamuzi wao walisimama katika sehemu mbili za sanduku mbele ya makuhani na Walawi ambao hulibeba sanduku la Agano la Yahweh - wageni pamoja na wazalia, nusu yao walisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu walisimama mbele ya Mlima Ebali. Waliwabariki watu wa Israeli kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza hapo mwanzo.
\s5
\v 34 Baada ya hayo, Yoshua alisoma maneno yote ya sheria, baraka na laana, kama zilivyoandikwa katika kitabu cha sheria.
\v 35 Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa mbele ya kusanyiko la Waisraeli lilojumuisha wanawake, watoto wadogo na wageni walioishi miongoni mwao.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha wafalme wote walioishi ng'ambo ya mto Yordani katika nchi ya milima, na katika nchi za chini katika pwani za Bahari Kuu mbele ya Lebanoni - Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi -
\v 2 hawa waliungana pamoja chini ya amri moja kuinua vita dhidi ya Yoshua na Israeli.
\s5
\v 3 Waliposikia wenyeji wa Gibeoni juu ya mambo aliyoyafanya Yoshua katika Yeriko na Ai,
\v 4 walipanga mpango wa udanganyifu. Walienda kama wajumbe. Walichukua magunia yaliyochakaa na kuyaweka juu ya punda. Walichukua pia viriba vilivyochakaa na kuchanika chanika na vilivyozibwa zibwa.
\v 5 Walivaa miguuni mwao viatu vilivyozeeka na kutoboka toboka, na walivaa nguo kuukuu, zilichanika chanika. Na mikate yote katika chombo ilikuwa mikavu na yenye uvundo.
\s5
\v 6 Kisha wakamwendea Yoshua katika kambi huko Giligali na wakamwambia yeye pamoja wa watu wa Israeli wakisema, "
\v 7 Tumesafiri kutoka nchi ya mbali, basi fanyeni agano nasi." Watu wa Israeli wakawaamba Wahivi, "Huenda mnaishi karibu nasi. Twawezeje kufanya agano nanyi?"
\v 8 Wakamwambia Yoshua, "Sisi ni watumishi wako."Yoshua akawauliza, "Ninyi ni akina nani? Mnatokea wapi?
\s5
\v 9 Wakamwambia, "Watumishi wako wamekuja hapa kutokea nchi ya mbali, kwasababu ya jina la Yahweh Mungu wako. Tumesikia habari kumhusu na kuhusu kila kitu alichokifanya Misri -
\v 10 na kila kitu alichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori katika upande mwingine wa Yordani - kwa mfalme Sihoni wa Heshiboni, na kwa Ogu wa Bashani aliyekuwa katika Ashitarothi.
\s5
\v 11 Wazee wetu na wenyeji wote wa nchi yetu walituambia," Chukueni chakula mikononi mwenu kwa ajili ya safari. Nendeni mkakutane nao, na kisha muwambie, "Sisi ni watumishi wenu. Fanyeni agano pamoja nasi."
\v 12 Huu ni mkate wetu, ulikuwa wa moto tulipouchukua kutoka katika nyumba zetu katika siku ile tulipotoka kuja kwenu. Lakini sasa, tazama, imekuwa kavu na yenye ukungu.
\v 13 Viriba hivi vilikuwa vipya tulipovijaza, na tazama, sasa vinavuja. Nguo zetu na viatu vyetu vimechakaa na kuwa vikuukuu kwasababu ya safari ndefu."
\s5
\v 14 kwahiyo, Waisraeli wakatwaa sehemu ya vyakula vyao, lakini walifanya hivyo bila ya kumwuliza Yahweh ili awaongoze.
\v 15 Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia.
\s5
\v 16 Siku tatu baada ya Waisraeli kufanya agano pamoja nao, waligundua kuwa walikuwa ni majirani zao na ya kwamba waliishi karibu nao.
\v 17 Kisha watu wa Israeli walisafiri na kufika katika miji yao katika siku ya tatu. Miji yao ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi, na Kiriathi Yearimu.
\s5
\v 18 Watu wa Israeli wahakushambulia kwasababu viongozi wao walikuwa wamewaapia mbele za Yahweh, Mungu wa Israeli. Waisraeli wote walikuwa wananung'unika kinyume na viongozi wao.
\v 19 Lakini viongozi wote waliawaambia watu wote wa Israeli, "Tumeapa kwa Yahweh, Mungu wa Israeli kwa ajili yao, na sasa hatuwezi kuwadhuru.
\s5
\v 20 Hiki ndicho tutakachowafanyia: Tutawaacha waishi ili tuepuke ghadhabu ambayo yaweza kuja juu yetu kwasababu ya kiapo tulichowaapia."
\v 21 Viongozi wakawaambia watu, "Waacheni waishi." Hivyo Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote, kama vile viongozi walivyosema juu yao.
\s5
\v 22 Yoshua aliwaita na kuwaambia, " Kwanini mlitudanya wakati mliposema, "Tuko mbali sana nanyi' wakati mnaishi hapa hapa miongoni mwetu?
\v 23 Na kwasababu hii, mmelaaniwa na baadhi yenu mtakuwa watumwa siku zote, wenye kukata kuni na kuchota maji kwa ajli ya nyumba ya Mungu wangu."
\s5
\v 24 Walimjibu Yoshua na kusema, "Ni kwasababu watumishi wako waliambiwa kwamba Yahweh Mungu wenu alimwagiza Musa mtumishi wake kuwapa ninyi nchi yote, na kuwateteza wenyeji wote wa nchi mbele yenu - hivyo tuliogopa kwasababu yenu kwa ajili ya maisha yetu. Ndio maana tulifanya jambo hili.
\v 25 Tazama sasa, mnatumiliki chini ya utawala wenu. Chochote kilichochema na haki kwenu kutufanyia, fanyeni."
\s5
\v 26 Basi Yoshua aliwafanyia hivi: aliwaondoa katika mamlaka ya watu wa Israeli, na Waisraeli hawakuwaua.
\v 27 Siku hiyo Yoshua aliwafanya Wagibeoni kuwa wakata kuni na wachotaji wa maji kwa jamii, na kwa madhabahu ya Yahweh hadi leo katika sehemu ambayo Yahweh huichagua.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Ikawa Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alisikia kuwa Yoshua ameiteka Ai na ameiteketeza kabisa, kama alivyokwisha kufaya huko Yeriko na mfalme wake. Na alisikia jinsi ambavyo watu wa Gibeoni walivyofanya amani na watu wa Israeli na walikuwa wanaishi miongoni mwao.
\v 2 Watu wa Yerusalemu waliogopa sana kwasababu Gibeoni ulikuwa mji mkubwa, kama mmoja wa miji ya kifalme. Ilikuwa kubwa kuliko Ai, na watu wake wote walikuwa ni mashujaa wenye nguvu.
\s5
\v 3 Hivyo Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alituma ujumbe kwa Hohamu, mfalme wa Hebroni, na kwa Piramu, mfalme wa Yarimuthi, na kwaYafia, mfalme wa Lakishi, na kwa Debiri, mfalme wa Eguloni:
\v 4 "Njooni kwangu na mnisaidie. Tuishambulie Gibeoni kwasababu wamefanya amani na Yoshua pamoja na watu wa Israeli.
\s5
\v 5 Wafalme watano wa Waamori; mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarimuthi, mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Eguloni walikwea, wao pamoja na majeshi yao yote. Walipanga sehemu yao kinyume na Wagibeoni na waliwashambulia.
\s5
\v 6 Watu wa Gibeoni walituma ujumbe kwa Yoshua na kwa jeshi huko Giligali. Walisema, " Upesi! Msiuondoa mkono wenu kutoka kwa watumishi wenu. Kwaeni mje haraka na mtuokoe. Mtusaide, maana wafalme wote wa Waamori wanaoishi katika nchi ya milima wamekusanyika kwa pamoja ili watushambulie.
\v 7 "Yoshua alipanda kutoka Giligali, yeye na watu wote wa vita pamoja naye, na watu wote wapiganaji.
\s5
\v 8 Yahweh akamwambia Yoshua, "Usiwaogope. Nimewatiwa wote katika mkono wako. Hakuna hata mmoja wao atakayeweza kuzuia mashambulizi yako."
\s5
\v 9 Baada ya kutembea usiku kucha kutoka Giligali, ghafla Yoshua aliwafikilia.
\v 10 Na Yahweh alichanganya maadui mbele za Israeli - ambao waliwaua mauaji makubwa mno huko Gibeoni, na wale waliowafuata njiani iendayo Bethi Horoni, nao waliuwaua katika njia iendayo Azeka na Makeda.
\s5
\v 11 Na walipokuwa wakikimbia mbio kutoka kwa Waisraeli, chini ya mlima kutoka Bethi Horoni, Yahweh alitupa mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao wote katika njia iendayo Azeka, nao wakafa. Watu waliouawa kwa mawe walikuwa ni wengi zaidi kuliko wale waliouawa kwa upanga wa watu wa Israeli.
\s5
\v 12 Kisha Yoshua akamwambia Yahweh katika siku ambayo Yahweh aliwapa watu wa Israeli ushindi dhidi ya Waamori. Hiki ndicho Yoshua alichosema kwa Yahweh mbele ya Israeli. " Jua lisimame katika Gibeoni, na mwezi, usimame katika bonde la Aijaloni."
\s5
\v 13 Jua lilisimama, na mwezi ukaacha kwenda mpaka taifa lilipolipiza kisasi dhidi ya maadui zao. Je hili halikuandikwa katika Kitabu cha Yashari? Jua lilikaa katikati ya anga; halilkuzama kwa siku nzima hivi.
\v 14 Haijawahi kutokea siku nyingine kama hiyo kabla au baada yake, wakati Yahweh alipotii sauti ya mtu. Kwa kuwa Yahweh alikuwa akifanya vita badala ya Israeli.
\s5
\v 15 Yoshua na Israeli yote pamoja naye walirudi kambini huko Giligali.
\v 16 Basi wale wafalme watano walikuwa wametoroka na kujificha wao wenyewe katika pango huko Makeda.
\v 17 Taarifa zilimfikia Yoshua kusema, "Wafalme watano wamepatikana wamejificha katika pango huko Makeda!"
\s5
\v 18 Yoshua akasema, "Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.
\v 19 Msibaki na kukaa nyie wenyewe. Bali wafuatilieni maadui zenu na kuwashumbulia kutokea kwa nyuma. Msiwaruhusu kuingia katika miji yao, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu amewatia katika mkono wenu."
\s5
\v 20 Yoshua na wana Waisraeli walikuwa wamemaliza kuwaua kwa mauaji makubwa sana, mpaka pale walipokuwa wameteketezwa kabisa; watu wachache tu walipona waliotoroka walifika miji ya ngome.
\v 21 Kisha jeshi lote lilirudi kwa Yoshua likiwa na amani katika kambi huko Makeda. Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.
\s5
\v 22 Kisha Yoshua akasema, "Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano."
\v 23 Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.
\s5
\v 24 Na walipowaleta wafalme kwa Yoshua, alimwita kila mtu wa Israeli, na aliwaambia maakida wa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani pamoja naye " Kanyageni miguu yenu juu ya shingo zao." Basi walikuja na kukanyaga miguu yao juu ya shingo zao.
\v 25 Kisha akawaambia, 'Msiogope wala kufadhaika. uwe na moyo mkuu na jasiri. Na hiki ndicho Mungu atakachokifanya kwa maadui wenu wote ambao mtapigana nao'.
\s5
\v 26 Kisha Yoshua akawashambulia na kuwaua wafalme. Aliwatundika wote watano juu ya miti. Waliwatundika juu ya miti hata jioni.
\v 27 Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.
\s5
\v 28 Na kwa namna hii, katika siku hiyo Yoshua aliuteka mji wa Makeda na aliwaua watu wote huko kwa upanga, pamoja na mfalme wake. Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia. Alichomfanyia mfalme wa Makeda ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
\s5
\v 29 Yoshua na Israeli wote waliipita Makeda na kufika Libna. Na huko waliingia katika vita dhidi ya Libna.
\v 30 Yahweh pia aliitia katika mkono wa Israeli pamoja na mfalme wake. Yoshua alishambulia kila kiumbe hai ndani yake kwa upanga. Hakuacha hai hata mtu mmoja. Alichomfanyia mfalme ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
\s5
\v 31 Baadaye Yoshua na Israeli wote pamoja naye walipanda kutoka Libna na kwenda Lakishi. Alipiga kambi karibu yake na wakafanya vita dhidi yake.
\v 32 Yahweh aliitia Lakishi katika mkono wa Israeli. Yoshua aliiteka katika siku ya pili. Alishambulia kwa upanga kilia kiumbe hai kilichokuwa ndani yake, kama vile aliyokuwa amefanya huko Libna.
\s5
\v 33 Kisha Horamu, mfalme wa Gezeri alikwea ili kuisaida Lakishi. Yoshua alimshambulia yeye na jeshi lake mpaka pale ambapo hapakuwa na mtu hata mmoja aliyesalia.
\s5
\v 34 Baada ya hapo, Yoshua na Israeli wote walitoka Lakishi na kwenda Egloni. Walipiga kambi karibu yake na kisha wakafanya vita dhidi yake,
\v 35 na siku hiyo hiyo wakaiteka. Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake kama vile Yoshua alivyofanya huko Lakishi.
\s5
\v 36 Kisha Joshua na Israeli wote wakatoka Egloni na kwenda Hebroni. Wakainua vita dhidi yake.
\v 37 Waliuteka mji na kuwaua kwa upanga watu wote ndani yake pamoja na mfalme wake, kujumuisha na vijiji vyote vilivyoizunguka. Waliteketeza kabisa kila kiumbe hai ndani yake, hawakuacha hata mtu mmoja aliyesalia, ni sawa sawa na vile Yoshua alivyoitenda Egloni. Aliiteketeza kabisa, na kila kiumbe hai ndani yake.
\s5
\v 38 Baada ya hapo, Yoshua alirudi pamoja na jeshi lote la Israeli pamoja naye, wakasafiri kwenda Debiri na kufanya vita dhidi yake.
\v 39 Aliuteka mji na mfalme wake, pamoja na vijiji vyake vya jirani. Waliwaua wote kwa upanga na waliteketeza kila kiumbe hai ndani yake. Joshua hakuacha hata mmoja hai, kama alivyokuwa amefanya kwa Hebroni na mfalme wake, na kama alivyokuwa amefanya kwa Libna na mfalme wake.
\s5
\v 40 Yoshua aliishinda nchi yote, nchi ya milima, Negevu, nchi, nchi ya tambarare na nchi ya miteremko. Hakuna hata mfalme moja aliyebaki hai kati ya wafalme wake wote. Kwa kweli aliteketeza kila kiumbe hai, kama ambavyo Yahweh, Mungu wa Israeli alivyomwaagiza.
\v 41 Yoshua aliwaua kwa upanga kutoka Kadeshi Barnea hadi Gaza, na nchi yote ya Gosheni hata Gibeoni.
\s5
\v 42 Yoshua aliwateka wafalme wote hawa na nchi zao kwa wakati mmoja, kwasababu Yahweh, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli.
\v 43 Baada ya hayo Yoshua na Waisraeli wote pamoja naye, walirudi katika kambi huko Gilgali.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi ikawa aliposikia haya, Yabini, mfalme wa Hazori, alituma ujumbe kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu.
\v 2 Alituma pia ujumbe kwa wafalme walikuwa katika mlima wa kaskazini mwa nchi, katika bonde la Mto Yordani kusini mwa Kinerethi, katika nchi za tambarare, na katika nchi za milima ya Dori kuelekea magharibi.
\v 3 Pia, alituma ujumbe kwa Wakanaani walioko mashariki na magharibi, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wayebusi katika nchi za milima, na Wahivi karibu na Mlima Hermoni katika nchi ya Mizipa.
\s5
\v 4 Maadui zao wote walitoka pamoja nao, wanajeshi wengi sana, hesabu yao ilikuwa kama mchanga wa pwani. Walikuwa na farasi wengi sana na magari.
\v 5 Wafalme wote hawa walikutana katika muda waliokuwa wameupanga, na walipiga kambi katika maji ya Meromu ili kupigana vita na Israeli.
\s5
\v 6 Yahweh akamwambia Yoshua, "Usiogope mbele zao, kwa kuwa muda kama huu kesho ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu. Utaivunja vunja miguu ya farasi zao, na utayachoma moto magari yao."
\v 7 Yoshua na watu wote wa vita walitoka na mara wakafika katika maji ya Meromu, na wakawashambulia maadui.
\s5
\v 8 Yahweh akawatia maadui katika mkono wa Israeli, na waliwapiga kwa upanga na wakawafuata mpaka Sidoni, Misrefothi - Maimu, na katika bonde la Mizipa upande wa mashariki. Waliwaua wote hakuna hata mmoja aliyeachwa hai.
\v 9 Yoshua aliwatendea kama vile Yahweh alivyomwambia. Alivunja miguu ya farasi na magari aliyachoma moto.
\s5
\v 10 Kwa wakati huo, Yoshua alirudi na akauteka mji wa Hazori. Alimwua mfalme wake kwa upanga (Hazori ulikuwa ni kichwa cha falme hizi zote).
\v 11 Waliwapiga kwa upanga kila kiumbe chenye uhai kilichokuwa huko, na alivitenga ili viteketezwe, hivyo hapakuwa na kiumbe hai kilichoachwa hai. Na kisha aliuchoma moto Hazori.
\s5
\v 12 Yoshua aliiteka miji yote ya wafalme hawa. Aliwateka pia wafalme wake wote na akawapiga wote kwa upanga. Aliwateketeza kabisa kwa upanga, kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyoagiza.
\v 13 Waisraeli hawakuchoma moto mji wowote miongoni mwa miji iliyojengwa juu ya vilima vya vifuasi vya udongo, isipokuwa Hazori, ndio mji pekee ambao Yoshua aliuchoma kwa moto.
\s5
\v 14 Jeshi la Israeli lilichukua nyara kutoka katika miji pamoja na mifugo kwa ajili yao wenyewe. Waliua kila mtu kwa upanga hadi pale walipokufa wote. Hakuna kiumbe hai kilichoachwa hai.
\v 15 Kama vile Yahweh alivyomwagiza mtumishi wake Musa, na kwa namna hiyo hiyo, Musa alivyomwagiza Yoshua. Na katika mambo yote ambayo Yahweh alimwamuru Musa kuyafanya, Yoshua hakuacha kufanya hata jambo moja.
\s5
\v 16 Yoshua alitwaa nchi hiyo yote, nchi ya milima, Negevu yote, nchi yote ya Gosheni, nchi ya vilima vidogo, bonde la Mto Yordani, nchi ya milima ya Israeli, na nchi tambarare.
\v 17 Kutoka Mlima Halaki karibu na Edomu, kuelekea kasikazini hadi Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni chini ya Mlima Hermoni, aliwateka wafalme wake wote na kuwaua.
\s5
\v 18 Yoshua alipigana vita na wafalme wote kwa muda mrefu.
\v 19 Hakuna hata mji mmoja uliofanya amani na jeshi la Israeli isipokuwa Wahivi walioishi Gibeoni. Israeli ilitwaa miji yote iliyosalia katika vita.
\v 20 Kwa kuwa alikuwa ni Yahweh ambaye alikuwa ameifanya kuwa migumu mioyo yao ili wapande na kufanya vita dhidi ya Israeli, ili kwamba aweze kuwaangamiza kabisa, na kutowaonesha huruma, kama alivyomwaagiza Musa.
\s5
\v 21 Kisha Yoshua akaja kwa wakati ule na aliiangamiza Anakimu. Aliyafanya haya katika nchi ya milima, huko Hebroni, Debiri, Anabu, na katika nchi yote ya Yuda, na katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua aliwaangamiza kabisa pamoja na miji yao.
\v 22 Hakuna hata mmoja wa watu wa Anakimu aliyeachwa katika nchi ya Israeli, isipokuwa huko Gaza, Gathi na Ashidodi.
\s5
\v 23 Hivyo Yoshua aliiteka nchi yote, kama vile Yahweh alivyomwambia Musa. Yoshua aliwapa Israeli kama urithi, kila kabila lilipewa sehemu yake. Kisha nchi ikapumzika bila vita.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao watu wa Israeli walishindwa. Waisraeli walichukua miliki ya nchi katika upande wa mashariki mwa Yordani sehemu ambako jua huchomoza, kutoka bonde la Mto Arnoni hadi Mlima Hermoni, na nchi yote ya Araba kuelekea kusini.
\v 2 Sihoni, mfalme wa Waamori, aliishi katika Heshiboni. Alitawala kutoka Aroeri, ambayo iko juu ya bonde la Arnoni kutoka katikati ya bonde, na nusu ya Geleadi kushuka mpaka Mto Yaboki katika mpaka wa Waamori.
\s5
\v 3 Sihoni pia alitawala juu ya Araba mpaka Bahari ya Kinerethi, kwenda mashariki, kuelekea Bahari ya Araba (Bahari ya Chumvi) upande wa mashariki, hadi huko Bethi Yeshimothi na upande wa kusini, kuelekea chini ya miteremko wa Mlima Pisiga.
\v 4 Ogu, mfalme wa Bashani, mmoja kati ya mabaki ya Rephaimu, aliyeishi huko Shatarothi na Edrei.
\v 5 Alitawala juu ya Mlima Hermoni, Saleka, na Bahani yote, hadi mpaka wa watu wa Geshuri na Wamakathi, na nusu ya Gleadi, hadi kufika mpaka wa Sihohi, mfalme wa Heshboni.
\s5
\v 6 Musa mtumishi wa Yahweh, na watu wa Israeli walikuwa wamewashinda, na Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa nchi kama mali ya Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.
\s5
\v 7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambayo Yoshua na watu wa Israeli waliwashinda katika upande wa magharibi mwa mto Yordani, kutoka Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni hadi Mlima Halaki karibu na Edom. Yoshua aliyapa nchi makabila ya Israeli ili yaimiliki.
\v 8 Aliwapa nchi ya milima, tambarare, Araba, sehemu za milima, nyika na Negevu, nchi ya Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
\s5
\v 9 Wafalme hawa walikuwa ni mfalme wa Yeriko, mfalme wa Ai iliyo karibu na Betheli,
\v 10 mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Enaimu,
\v 11 mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi,
\v 12 mfalme wa Egloni, mfalme wa Gezeri,
\s5
\v 13 mfalme wa Debiri, mfalme wa Gederi,
\v 14 mfalme wa Horima, mfalme wa Aradi,
\v 15 mfalme wa Libna, mfalme wa Adula,
\v 16 mfalme wa Makeda, mfalme wa Betheli,
\s5
\v 17 mfalme wa Tapua, mfalme wa Heferi,
\v 18 mfalme wa Afeki, mfalme wa Lasharoni,
\v 19 mfalme wa Madoni, mfalme wa Hazori,
\v 20 mfalme wa Shimroni - Meroni, mfalme wa Akshafu.
\s5
\v 21 mfalme wa Taanaki, mfalme wa Megido,
\v 22 mfalme wa Kedeshi, mfalme wa Jokineamu katika Karmeli,
\v 23 mfalme wa Dori katika Nafutali Dori, mfalme Goyimu katika Giligali, na
\v 24 mfalme Tiriza. Hesabu ya wafalme ilikuwa ni thelathini na moja kwa ujumla wake.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Sasa Yoshua alikuwa mzee wakati Yahweh alipomwambia, "Umekuwa mzee, lakini bado kuna nchi kubwa ya kuteka.
\s5
\v 2 Nchi iliyosalia ndio hii: mikoa yote ya Wafilisti, na mikoa ile ya Wageshuri,
\v 3 (tangu Shihori, iliyoko mashariki mwa Misri, na upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Ekroni, inayofikiriwa kuwa ni mali ya Wakanaani; wafalme watano wa Wafilisti, wale wafalme wa Gaza, Ashidodi, Ashikeloni, Gathi na Ekroni - miliki ya Waavi.
\s5
\v 4 Katika upande wa kusini, kulisalia nchi yote ya Wakanaani, na Meara ambayo ni miliki ya Wasidoni, hadi Afeki, hata mpaka wa Waamori;
\v 5 nchi ya Wagebali, Lebanoni kuelekea upande wa mapambazuko ya jua, kutoka Baali- Gadi chini ya Mlima Hermoni mpaka Lebo Hamathi.
\s5
\v 6 Pia, wenyeji wote wa nchi ya milima kutoka Lebanoni hadi Misrefothi - Maimu, pamoja na watu wa Sidoni. Nitawafukuza mbele ya jeshi la Israeli. Uwe na uhakika wa kuwapa Waisraeli nchi kama urithi, kama nilivyokuagiza.
\v 7 Igawanye nchi hii kama urithi kwa makabila tisa na kwa nusu ya kabila la Manase.
\s5
\v 8 Pamoja na nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi wamekwisha kupokea urithi wao ambao Musa aliwapa katika upande wa mashariki wa Yordani,
\v 9 kutoka Aroeri, iliyo katika ukingo wa bonde la mto Arnoni (kujumuisha na mji ambao uko katikati ya bonde), kwa nyanda zote za Medeba hadi Diboni;
\s5
\v 10 miji yote ya Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala katika Heshiboni, hata mpaka wa Waamori,
\v 11 Gileadi na mkoa wa Wageshuri na Maakathi, mlima wote wa Hermoni, Bashani yote mpaka Saleka;
\v 12 ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyetawala katika Ashitarothi na Edrei - hawa ni wale waliosalia katika Refaimu - ambao Musa aliwapiga na kuwafukuzia mbali.
\s5
\v 13 Lakini watu wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri wala Wamakathi. Badala yake, Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo.
\s5
\v 14 Kabila la Lawi pekee halikupewa urithi na Musa. Urithi wao ni sadaka za Yahweh, Mungu wa Israeli, zilizotolewa kwa moto, kama Mungu alivyomwagiza Musa.
\s5
\v 15 Musa aliwapa urithi kabila la Rubeni, ukoo kwa ukoo.
\v 16 Miliki yao ilikuwa kutoka Aroeri, juu ya ukingo wa bonde la Mto Arnoni, na mji ulio katikati ya bonde, na nyanda zote za Medeba.
\s5
\v 17 Wareubeni walipata pia Heshiboni, na miji yake yote zilizo katika uwanda, Diboni, na Bamathi Baali, na Bethi Baalimeoni,
\v 18 na Yahazi, na Kedemothi, na Mefaathi,
\v 19 na Kiriathaimu, na Sibuma, na Zerethishahari juu ya kilima cha bonde.
\s5
\v 20 Wareubeni walipata pia Bethi Peori, miteremko ya Pisiga, Bethi Yeshimothi,
\v 21 miji yote ya uwanda, na ufalme wote wa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa ametawala katika Heshiboni, ambaye Musa alikuwa amemshinda pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Zuri, Huri na Reba, wana wa mfalme wa Sihoni, ambao walikuwa wameishi katika nchi.
\s5
\v 22 Pia, watu wa Israeli walimwua kwa upanga Baalam mwana wa Beori, ambaye alifanya mambo ya uaguzi, miongoni mwa wale waliowaua.
\v 23 Mpaka wa kabila la Rubeni ni Mto Yordani; huu ndio mpaka wao. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Rubeni, uliotolewa kwa kila ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.
\s5
\v 24 Hiki ndicho Musa alilipa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:
\v 25 Himaya yao ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Waamoni, hadi Aroeri, iliyo mashariki mwa Raba,
\v 26 kutoka Heshiboni hadi Ramathi - Mizipe na Betonimu, kutoka Mahanaimu mpaka himaya ya Debiri.
\s5
\v 27 Katika bonde, Musa aliwapa Bethi -Haramu, Bethi - Nimra, Sukothi, na Zafoni, ufalme uliobakia wa Sihoni mfalme wa Heshiboni, pamoja na Yordani kama mpaka, katika sehemu za chini za mwisho wa Bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki ng'ambo ya Yordani.
\v 28 Huu ni urithi wa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.
\s5
\v 29 Musa aliwapa urithi nusu ya kabila la Manase. Urithi uligawiwa kwa nusu ya kabila la watu wa Manase kutokana na kabila zao.
\v 30 Miliki yao ilikuwa kutoka Mahanaimu, Bashani yote, ufalme wote wa mfalme Ogu wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;
\v 31 nusu ya Gileadi, na Ashitarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Miji hii iligawanywa kwa ukoo wa Makiri mwana wa Manase -nusu ya watu wa Makiri, walipewa kwa kila familia zao.
\s5
\v 32 Huu ndio urithi ambao Musa aliowagawia katika nyanda za Moabu, ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko.
\v 33 Musa hakulipa urithi kabila la Lawi. kwa kuwa Yahweh, Mungu wa israeli, ni urithi wao, kama vile alivyowaambia.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Maeneo haya ya nchi ambayo watu wa Israeli waliyapokea kama urithi wao katika nchi ya Kanaani. Urith huu uligawanywa kwao na Eliazeri kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya mababu wa familia zao kati ya watu wa Israeli.
\s5
\v 2 Urithi wao ulichaguliwa kwa kupiga kura kwa makabila tisa na nusu, kama vile Yahweh alivyoagiza kwa mkono wa Musa.
\v 3 Kwa kuwa Musa alikuwa amewapa urithi makabila mawili na nusu ng'ambo ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi wowote.
\v 4 Kabila la Yusufu kwa uhalisia yalikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Na hakuna sehemu yoyote ya urithi waliyopewa Walawi katika nchi, lakini walipewa miji ya kuishi ndani yake pamoja na sehemu ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya riziki zao.
\v 5 Watu wa Israeli walifanya hivyo kama vile Yahweh alivyomwagiza Musa, basi waliiganywa nchi.
\s5
\v 6 Kisha kabila la Yuda lilikuja kwa Yoshua huko Giligali. Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, akamwambia,"Unajua kile Yahweh alichomwambia Musa mtu wa Mungu juu yako na mimi huko Barnea.
\v 7 Nilikuwa na umri wa miaka arobani wakati Musa mtumishi wa Yahweh aliponituma kutoka Kadeshi Barnea kuipeleleza nchi. Nilimletea taarifa tena kama nilivyotakiwa kufanya katika moyo wangu.
\s5
\v 8 Lakini ndugu zangu walioenda pamoja nami waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa woga. Lakini mimi nilimfuata Yahweh kabisa.
\v 9 Musa aliapa katika siku hiyo akisema, "Hakika nchi ambayo miguu yako imetembea juu yake itakuwa urithi wako na kwa watoto wako milele, kwasababu umemfuata kabisa Yahweh Mungu wangu.
\s5
\v 10 Tazama! sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano.
\v 11 Bado hata siku hii ya leo nina nguvu kama nilivyokuwa katika siku ile ambayo Musa alinituma. Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile, kwa ajili ya vita na kwa kwenda na kwa kuja.
\s5
\v 12 Sasa basi, nipe nchi hii ya milima, ambayo Yahweh aliniahidi katika siku hiyo. Kwa kuwa ulisikia katika siku hiyo kuwa Wanakimu walikuwa huko katika miji yenye ngome. Itakuwa kwamba Yahweh atakuwa pamoja nami na ya kwamba nitawafukuzia mbali, kama vile Yahweh alivyosema."
\s5
\v 13 Kisha Yoshua alimbariki Kalebu mwana wa Yefune na alimpa Hebroni kama urithi wake.
\v 14 Hivyo Hebroni ikawa urithi wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi hata leo, kwasababu alimfuata kabisa Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 15 Basi, jina la Hebroni hapo mwanzo lilikuwa ni Kiriathi Arba ( Arba ambaye alikuwa ni mtu mkuu miongoni mwa Wanakim). Kisha nchi ikawa na raha bila vita.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.
\v 2 Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.
\s5
\v 3 Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.
\v 4 Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.
\s5
\v 5 Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.
\v 6 Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata JIwe la Bohani mwana wa Rubeni.
\s5
\v 7 Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za Eni Shemeshi na kufika Eni Rogeli.
\v 8 kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi ( ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kasikazini.
\s5
\v 9 Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala ( ambao ndio Kiriathi Yearimu).
\v 10 Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.
\s5
\v 11 Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kasikazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambasamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.
\v 12 Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.
\s5
\v 13 Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
\v 14 Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.
\v 15 Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
\s5
\v 16 Kalebu akasema, "Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.
\v 17 Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake na Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.
\s5
\v 18 Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, "Unataka nini?"
\s5
\v 19 Akisa akamjibu, "Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negevu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji." Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.
\s5
\v 20 Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na koo zao.
\s5
\v 21 Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,
\v 22 Kina, Dimona, Adada,
\v 23 Kadeshi, Hazor, Ithinani,
\v 24 Zifu, Telemu, Bealothi.
\s5
\v 25 Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),
\v 26 Amamu, shema, Molada,
\v 27 Hazari Gada, Heshimoni, Bethi Peleti,
\v 28 Hazari Shuali, Beerisheba, Biziothia.
\s5
\v 29 Baala, Limu, Ezemu,
\v 30 Eltoladi, Kesili, Horma,
\v 31 Ziklagi, Madimana, Sansana,
\v 32 Lebaothi, Shilihimu, Aini, na Rimoni. Miji hii ilikuwa ishirini na tisa kwa ujumla, kujumlisha na vijiji vyake.
\s5
\v 33 Katika nchi iliyo chini ya mlima upande wa magharibi, kulikuwa na miji ya Eshtaoli, Zora, Ashina,
\v 34 Zanaoa, Eni Ganimu, Tapua, Enamu,
\v 35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
\v 36 Shaaraimu, Adithaimu, na Gedera ( ambayo ndio Gederothaimu). Hesabu ya miji hii ilikuwa ni kumi na nne, pamoja na vijiji vyao.
\s5
\v 37 Zena, Hadasha, Migidagadi,
\v 38 Dileani, Mizipa, Yokitheeli,
\v 39 Lakishi, Bozikathi, Egloni.
\s5
\v 40 Kaboni, Lahmamu, Kitilishi,
\v 41 Gederothi, Bethi Dagoni, Naama, Makeda. Hesabu ya miji hii ilikuwa kumi na sita, kujumlisha na vijiji vyao.
\s5
\v 42 Libna, Etheri, Ashani,
\v 43 Ifuta, Ashina, Nezibu,
\v 44 Keila, Akizibu, na Maresha. Hii ilikuwa ni miji tisa, kujumlisha na vijiji vyao.
\s5
\v 45 Ekroni, pamoja na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka;
\v 46 kutoka Ekroni kuelekea Bahari Kuu, makazi yote ambayo yalikuwa karibu na Ashidodi, pamoja na vijiji vyake.
\v 47 Ashidodi, na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; Gaza na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; hata kufika kijito cha Misri, na kuelekea Bahari Kuu pamoja na ukanda wake wa pwani.
\s5
\v 48 Katika nchi ya milima, kuna miji ya Shamiri, Yatiri, Soko,
\v 49 Dana, Kiriathi Sana (ambayo ndio Debiri),
\v 50 Anabu, Eshitemo, Animu,
\v 51 Gosheni, Holoni, na Gilo. Hii ilikuwa ni miji kumi na moja, kujumuisha na vijiji vyake.
\s5
\v 52 Arabu, Duma, Ehani,
\v 53 Yanimu, Bethi Tapua, Afeka,
\v 54 Humta, Kiriathi Arba (ambayo ndio Hebroni), na Ziori. Hii ilikuwa miji tisa, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
\v 56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
\v 57 Kaini, Gibea, na Timna. Hii ilikuwa ni miji kumi, kujumuisha na vijiji vyake.
\s5
\v 58 Halhuli, Bethi Zuri, Gedori,
\v 59 Maarathi, Bethi Anothi, na Elitekoni. Hii ilikuwa miji sita, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 60 Kiriathi Baali (ambayo ndio Kiriathi Yearimu), na Raba. Hii ilikuwa ni miji miwili, pamoja na vijiji vyake.
\v 61 Katika nyika, kulikuwa na miji ya Bethi Araba, Midini, Sekaka,
\v 62 Nibushani, mji wa chumvi, na Eni Gedi. Hii ilikuwa miji, pamoja na vijiji vyao.
\s5
\v 63 Lakini kwa Wayebusi, wenyeji wa Yerusalemu, kabila la Yuda halikuweza kuwafukuza, na hivyo, Wayebusi wanaishi pamoja na kabila la Yuda hadi leo hii.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Nchi waliyopewa kabila la Yusufu ilianzia katika Yordani huko Yeriko, mashariki mwa chemichemi za Yeriko, kupitia nyikani, kupanda kutoka Yeriko kupitia nchi ya milima ya Betheli.
\v 2 Kisha uliendelea kutoka Betheli hadi Luzi na kupita hata Atarothi, iliyo miliki ya Waarkiti.
\s5
\v 3 Kisha ilishuka chini upande wa magharibi kuelekea himaya ya Wayafuleti, hadi kufika miliki ya Loweri Bethi Horoni, na kisha iliendelea hadi Gezeri; na ilikomea katika bahari.
\v 4 Ilikuwa ni kwa njia hii makabila ya Yusufu, yaani Manase na Efraimu yalipata urithi wao.
\s5
\v 5 Eneo la kabila la Efraimu ambalo lilikuwa limegawanya kwa koo zao lilikuwa kama ifuatavyo: mpaka wa urithi wao katika upande wa mashariki ulikuwa Atarothi Ada uliopanda kuelekea Bethi Horoni ya juu,
\v 6 na kutoka pale uliendelea hadi katika bahari. Kutoka Mikimethathi katika upande wa Kasikazini ulipinda upande wa mashariki kuelkea Taanathi Shilo na kupita ng'ambo yake katika upande wa mashariki kukabili Yanoa.
\v 7 Kisha ulishuka kutoka Yanoa hadi Atarothi na hata Naara, na kisha ukafika Yeriko, na kuishia katika Yordani.
\s5
\v 8 Kutoka Tapua, mpaka uliendelea katika upande wa magharibi hata kijito cha Kana na ulikomea katika bahari. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Efraimu, uliogawanywa katika koo zao,
\v 9 pamoja na miji yao iliyochaguliwa kwa ajili ya kabila la Efraimu iliyokuwa ndani ya urithi wa kabila la Manase - miji yote pamoja na vijiji vyao.
\s5
\v 10 Lakini hawakuwafukuza Wakanaani walioishi katika Gezeri, hivyo basi Wakanaani wanaishi ndani ya Efraimu hadi leo, lakini watu hawa walifanywa kuwa watumwa.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Na huu ndio mgao wa nchi kwa ajili ya kabila la Manase (aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Yusufu), ambayo ilikuwa kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, ambaye alikuwa ni baba wa Gilieadi. Watoto wa Makiri walipewa nchi ya Gileadi na Bashani, kwasababu Makiri alikuwa ni mtu wa vita.
\v 2 Nchi iliyobaki iligawiwa kwa kabila la Manase, walipewa kwa koo zao, ambazo ni Abi Ezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi, na Shemida. Hawa walikuwa ni watoto wa kiume wa Manase mwana wa Yusufu, waliwakilishwa na koo zao.
\s5
\v 3 Basi Zelofehadi mwana wa Heferi mwana wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase hakuwa na watoto wa kiume, bali alikuwa na watoto wa kike tu. Na majina ya binti zake yalikuwa Mahila, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.
\v 4 Walimwendea Eliazeri kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi na wakasema, "Yahweh alimwagiza Musa atupatie urithi wetu pamoja na kaka zetu." Hivyo, kwa kuzingatia agizo la Yahweh, aliwapa wanawake hao urithi miongoni mwa ndugu za baba yao.
\s5
\v 5 Manase alipewa sehemu kumi za nchi katika Gileadi na Bashani, ambayo iko upande mwingine wa Yordani,
\v 6 kwasababu ya binti za Manase walipokea urithi pamona na watoto wake wa kiume. Nchi ya Gileadi iligawanywa kwa kabila la Manase lililosalia.
\s5
\v 7 Eneo la Manase lilianzia Asheri hadi Mikimethathi, ambayo iko mashariki mwa Shekemu. Kisha mpaka ulienda upande wa kusini kwa wale walioishi karibu na chemichemi ya Tapua.
\v 8 ( Nchi ya Tapua ilikuwa ni miliki ya Manase, lakini mji wa Tapua katika mpaka wa Manase ilikuwa ni mali ya kabila la Efraimu.)
\s5
\v 9 Kisha mpaka ulishuka kuelekea kijito cha Kana. Miji hii kusini mwa kijito miongoni mwa miji ya Manase ilikuwa ni mali ya Efraimu. Mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa kijito, na ulikomea katika
\v 10 bahari. Na nchi iliyokuwa upande wa kusini ilikuwa ni ya Efraimu, na nchi iliyo upande wa Kasikazini ilikuwa ni ya Manase; bahari ilikuwa ndoi mpaka. Kwa upande wa kaskazini ulifika hata Asheri, na upande wa mashariki, Isakari.
\s5
\v 11 Pia katika Isakari na katika Asheri, Manase alimiliki Bethi Shani na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, wenyeji wa Dori na vijiji vyake, wenyeji wa Endori na vijiji vyake, wenyeji wa Taanaki na vijiji vyake, na wenyeji wa Megido na vijiji vyake (na mji wa tatu ni Nafethi).
\v 12 Lakini kabila la Manase halikuweza kuimiliki miji hiyo, kwa kuwa Wakanaani waliendelea kuishi katika nchi hii.
\s5
\v 13 Hata wakati watu wa Israeli walipopata nguvu zaidi, hawakuwafukuzia mbali kabisa Wakanaani, bali waliwafanya kuwa watumwa.
\s5
\v 14 Kisha wazawa wa Yusufu wakamwambia Yoshua, wakisema, " Kwanini umetupa mgao mmoja wa nchi na sehemu moja kwa ajili ya urithi, kwa kuwa tuko wengi, na kwa muda wote Yahweh umetubaliriki?
\v 15 Yoshua akawaambia, "Kama ninyi ni watu wengi katika hesabu, pandeni ninyi wenyewe katika msitu na kuisafisha nchi kwa ajili yenu wenyewe katika nchi ya Waperizi na ya Refaimu. Fanyeni hivi kwa kuwa nchi ya milima ya Efraimu ni ndogo kwenu."
\s5
\v 16 Wazawa wa Yusufu wakasema, "Nchi ya milima haitutoshi. Lakini Wakanaani wote wanaoishi katika bonde wana magari ya chuma, wote walio katikaBethi Shani na vijiji vyake, na wale walio katika bonde la Yezreeli."
\v 17 Kisha Yoshua akawaambi nyumba ya Yusufu, ambao ni Efraimu na Manase, " Ninyi ni watu mlio wengi katika hesabu, na mna nguvu kubwa. Hamtakiwi kuwa na sehemu moja ya nchi mliogawiwa.
\v 18 Nchi ya milima itakuwa yenu pia. Ingawa ni msitu, mtaufyeka na kuimiliki hata mipaka yake ya mbali. Mtawafukuzia mbali Wakanaani, ingawa wanayo magari ya chuma na ingawa pia wanazo nguvu."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Kisha kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika pamoja hapo Shilo. Walilijenga hema la kukutania hapo na waliishinda nchi mbele yao.
\v 2 Kulikuwa na makabila saba miongoni mwa watu wa Israeli ambayo yalikuwa bado hayajapewa urithi wao.
\s5
\v 3 Yoshua aliwaambia watu wa Israeli, "Je mtaacha mpaka lini katika kuingia nchi ambayo Yahweh, Mungu wa baba zenu, amewapeni ninyi?
\v 4 Chagueni ninyi wenyewe watu watatu kutoka katika kila kabila, na nitawatuma. Wataenda na kuipeleleza nchi juu na chini. Wataandika maelezo pamoja na maelekezo kuhusu urithi wao, na kisha watarudi kwangu.
\s5
\v 5 Wataigawanya nchi katika sehemu saba. Yuda itasalia katika eneo lao upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu itaendelea katika himaya yao katika upande wa kaskazini.
\v 6 Mtaigawanya nchi katika sehemu saba na kisha mtaniletea maelezo hayo hapa kwangu. Nami nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh Mungu wetu.
\s5
\v 7 Walawi hana sehemu miongoni mwenu, kwa kuwa ukuhani wa Yahweh ni urithi wao. Makabila ya Gadi, Rubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapokea urithi wao ng'ambo ya Yordani. Huu ni urithi ambao Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa wao.
\s5
\v 8 Hivyo, watu waliinuka na wakaenda. Yoshua akawaamuru wale walioenda kuandika maelezo ya nchi, akisema, "Pandeni juu na mshuke chini katika nchi na andikeni maelezo kuhusu nchi na kisha mrejee kwangu. Nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh huko Shilo.
\v 9 Watu walienda na walitembea juu na chini katika nchi na wakaandika maelezo kuihusu nchi hiyo juu ya gombo kwa miji yake katika sehemu saba, kwa kutaja miji, kila mmoja katika sehemu moja. Kisha wakarudi kwa Yoshua katika kambi huko Shilo.
\s5
\v 10 Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za Yahweh. Na hapo Yoshua akaigawa nchi kwa watu wa Israeli, kila kabila lilipewa sehemu ya nchi.
\s5
\v 11 Katika kabila la Benyamini, ugawanaji wa nchi ulifanyika kwa kupewa kwa koo zao. Eneo la nchi waliyopewa lilikuwa kati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu.
\v 12 Katika upande wa kusini, mpaka wao ulianzia katika Yordani. Mpaka ulipanda hata sehemu ya juu kaskazini mwa Yeriko, na kisha ukapita katikati ya nchi ya milima upande wa magharibi. Huko ukafika hadi nyika ya Bethi Aveni.
\s5
\v 13 Kutoka hapo mpaka ulipita upande wa kusini katika mwelekeo wa Luzi (sehemu ile ile inayoitwa Betheli). Kisha mpaka ukashuka chini hata Atarothi Adda, karibu na mlima uliolekea kusini mwa Bethi Horoni.
\v 14 Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali ( ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.
\s5
\v 15 Katika upande wa kusini, mpaka ulianzia nje tu ya Kiriathi Yearimu. Mpaka uliendelea kutoka Efroni hata chemichemi ya maji ya Neftoa.
\v 16 Kisha mpaka ulishuka chini hadi mpaka wa mlima ambao ulikuwa mkabala ya bonde la Beni Hinomu, ambalo lililokuwa katika upande wa kaskazini mwishoni mwa bonde la Refaimu. Kisha ulishuka chini kuelekea bonde la Hinomu, sehemu ya kusini mwa mteremko wa Wayebusi, na uliendelea kushuka chini hadi Eni Rogeli.
\s5
\v 17 Ulizunguka upande wa kaskazini, kuelekea mwelekeo wa Eni Shemeshi, na kutoka hapa ulienda hadi Gelilothi, ambao ulikuwa mkabala na mwinuko wa Adumimu. Kisha ulishuka chini kuelekea Jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.
\v 18 Ulipita kuelekea upande wa kaskazini wa bega la Bethi Araba na chini kuelekea Araba.
\s5
\v 19 Mpaka ulipita hadi upande wa bega la kaskazini la Bethi Hogla. Mpaka ulikome katika ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, katika upande wa kusini mwishoni mwa Yordani. Huu ulikuwa ni mpaka wa upande wa kusini.
\v 20 Yordani ulikuwa mpaka wake katika upande wa mashariki. Na huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini, na walipewa kwa kila ukoo wao, mpaka baada ya mpaka, kwa kuizunguka nchi yote.
\s5
\v 21 Kwa hiyo sasa miji ya kabila la Benyamini kufuatana na koo zao ilikuwa ni Yeriko,
\v 22 Bethi Hogla, Emeki Kezizi, Bethi Araba, Zemaraimu, Betheli,
\v 23 Avimu, Para, Ofra,
\v 24 Kefari Amoni, Ofini, na Geba. Ilikuwa ni miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 25 Kulikuwa pia na miji ya Gibeoni, Rama, Beerothi,
\v 26 Mizpe, Kefira, Moza,
\v 27 Rekemu, Iripeeli, Tarala,
\v 28 Zela, Haelefu, Yebusi (ambao ndio Yerusalemu), Gibea, na Kiriathi. Kulikuwa na miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Huu ulikuwa ni urithi wa Benyamini kufuatana na koo zao.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni na waligawiwa kwa kila ukoo wao. Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.
\s5
\v 2 Urithi waliokuwa nao ni Beerisheba, Sheba, Molada,
\v 3 Hazari Shuali, Bala, Ezemu,
\v 4 Elitoladi, Bethuli na Horma.
\s5
\v 5 Simoni alikuwa pia na Ziklagi, Bethi Markabothi, Hazari Susa,
\v 6 Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile
\v 7 Simoni alimiliki Aini, Rimon, Etheri, na Ashani. Hii ilikuwa ni miji minne pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 8 Miji hii pamoja na vijiji vilivyoizunguka hata kufika Baalathi Beeri (ambao ndio Rama katika Negevu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simoni, waliopewa kwa koo zao.
\v 9 Urithi wa kabila la Simoni ulikuwa sehemu ya himaya ya kabila la Yuda. Hii ni kwasababu nchi waliyopewa kabila la Yuda ilikuwa ni kubwa kwao, na hivyo kabila la Simoni lilipokea urithi wao kutoka katika sehemu yao ya katikati.
\s5
\v 10 Upigaji wa kura ya tatu uliangukia kwa kabila la Zabuloni, na walipewa kwa koo zao. Mpaka wa urithi wao ulianzia huko Saridi.
\v 11 Mpaka wao ulipanda upande wa magharibi kuelekea Marala na ukaigusa Dabeshethi, na kisha ukasonga kuelekea kijito kilichokuwa mkabala na Yokineamu.
\s5
\v 12 Kutoka Saridi mpaka ulizunguka upande wa mashariki kuelekea mashariki na ulienda hadi mpaka wa Kislothi Tabori. Kutoka hapo uliendelea hadi Daberathi na kisha ulipanda hata Yafia.
\v 13 Kutoka hapo ulipita katika upande wa mashariki mwa Gathi Heferi, na kisha ukafika Ethikazini, baadaye ulienda hadi Rimoni na kisha ukageuka kuelekea Nea.
\s5
\v 14 Mpaka ulizunguka kueleka kaskazini ukafika Hanathoni na ulikomea katika bonde la Ifta Eli.
\v 15 Mkoa huu ulijumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala, na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
\v 16 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni, waliopewa kwa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 17 Upigaji kura wa nne uliangukia kwa Isakari, na waligawiwa kufuatana na koo zao.
\v 18 Eneo lao lilijumuisha Jezreelli, Kesuloothi, Shunemu,
\v 19 Hafaraimu, Shioni, na Anaharathi.
\s5
\v 20 Pia ilijumuisha miji ya Rabithi, Kishioni, Ebezi,
\v 21 Remethi, Enganimu, Enihada, na Bethipazezi.
\v 22 Mpaka wao ulifika Tabor, Shahazuma, na Bethi Shemeshi, na ukakomea katika Yordani. Ilikuwa ni miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 23 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari, na walipewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 24 Upigaji wa kura ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri, na walipewa kwa koo zao.
\v 25 Eneo lao lilijumuisha miji ya Helikathi, Hali, Beteni, Akashafu,
\v 26 Alameleki, Amadi, na Mshali. Mpaka wa magharibi ulitanuka hadi Karmeli na Shihori Libnathi.
\s5
\v 27 Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la ifutaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.
\v 28 Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.
\s5
\v 29 Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,
\v 30 Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 31 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 32 Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.
\v 33 Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.
\v 34 Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.
\s5
\v 35 Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinnerethi,
\v 36 Adama, Rama, Hazori,
\v 37 Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.
\s5
\v 38 Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
\v 39 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.
\s5
\v 40 Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.
\v 41 Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,
\v 42 Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.
\s5
\v 43 Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,
\v 44 Eliteke, Gibethoni, Baalathi,
\v 45 Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,
\v 46 Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.
\s5
\v 47 Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.
\v 48 Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 49 Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.
\v 50 Kwa amri ya Yahweh walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.
\s5
\v 51 Na huu ndio urithi ambao Eliazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli, waligawa kwa kupiga kura huko Shilo, mbele za Yahweh katika mlango wa hema la kukutania. Na hivyo wakamaliza kuigawa nchi.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Baada ya hayo, Yahweh akamwambia Yoshua,
\v 2 "Waambia watu wa Israeli, na kusema, 'Chagueni miji ya makimbilio ambayo niliwaambia kupitia kwa Musa.
\v 3 Fanyeni hivi ili mtu akiua mtu bila kukusudia aweze kwenda huko. Miji hii itakuwa ni sehemu ya kukimbilia kutoka kwa mtu yeyote yule anayetaka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu aliyeuliwa.
\s5
\v 4 Atakimbilia kwa mji mmoja miongoni mwa miji hiyo na atasimama mlangoni mwa lango la mji, na ataeleza kesi yake kwa wazee wa mji ule. Kisha watamwingiza ndani ya mji na watampatia sehemu yake ya kuishi miongoni mwao.
\s5
\v 5 Na kama mtu akija akataka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu yule ambaye aliuliwa, ndipo watu wa mji hawatatakiwa kumtoa kwa wenye mamlaka mtu huyo aliyeua. Hawaruhusiwi kufanya hivyo kwasababu alimwua jirani bila kukusudia na hakuwa na chuki naye hapo awali.
\v 6 Ni lazima akae katika mji ule mpaka pale atakapokuwa amesimama mbele ya kusanyiko kwa ajili ya kuhukumiwa, hadi pale atakapokufa mtu yule anayetumika katika nafasi ya kuhani mkuu katka siku hizo. Na kisha mtu yule aliyeua bila kukusudia aweza kurudi nyumbani kwake, katika mji ule ulikotoka.
\s5
\v 7 Kwahiyo, Waisraeli wakaichaguia Kedeshi iliyoko Galilaya katika nchi ya milima ya Nafutali, Shekemu katika nchi ya milima ya Efraimu, na Kiriathi Arba (ambayo ndio Herbroni) katika nchi ya milima ya Yuda.
\v 8 Katika ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri huko nyikani katika nyanda za kabila la Rubeni; na Ramothi Gileadi kutoka kabila la Gadi; na Golani katika Bashani, kutoka katika kabila la Manase.
\s5
\v 9 Hii ni miji iliyochaguliwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwao, ili kwamba mtu yeyote amwuaye mtu bila kukusudia aweza kukimbilia huko kwa ajili ya kupata usalama. Mtu huyu hatakufa kwa mkono wa mtu yule anayetake kulipiza kisasi cha damu iliyomwagwa, mpaka hapo kwanza mtuhumiwa atakaposimama mbele ya kusanyiko la watu.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha wakuu wa koo za Walawi walimwendea Eliazari kuhani, na kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli.
\v 2 Waliwaambia, "Yahweh aliwaagizeni ninyi kwa mkono wa Musa kwamba mtupatieni miji ya kuishi yenye maeneo kwa ajili ya kuchungia ya mifugo." waliyasema haya huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
\s5
\v 3 Hivyo, kwa agizo la Yahweh, watu wa Israeli waliwapa Walawi kutoka katika urithi wa wao miji ifuatayo pamoja na maeneo yao ya kuchungia.
\s5
\v 4 Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini.
\v 5 Koo zilizobaki za Wakohathi walipokea kwa kupiga kura kwa miji kumi kutoka katika kabila za Efraimu, Dani, na kutoka kwa nusu ya kabila la Manase.
\s5
\v 6 Na watu wazawa wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kwa kupigiwa kura kutoka kwa koo za kabila la Isakari, Asheri, Nafutali, na nusu ya kabila la Manase katika Bashani.
\v 7 Watu waliokuwa wazawa wa Merari walipokea miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Rubeni, Gadi na Zabuloni.
\s5
\v 8 Basi, watu wa Israeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yao ya kuchungia, kwa kupiga kura, kama vile Yahweh alivyokuwa ameagiza kwa mkono wa Musa.
\v 9 Kutoka kwa makabila la Yuda na Simoni, waliwapa nchi katika miji ifuatayo iliyoorodheshwa kwa majina.
\v 10 Miji hii walipewa wazawa wa Haruni, ambao walikuwa miongoni mwa koo za Wakohathi, ambao walitoka katika kabila la Lawi. Kwa kuwa upigaji wa kura ya kwanza uliwaangukiwa wao.
\s5
\v 11 Waisraeli waliwapatia Kiriathi Arba ( Arba alikuwa ni baba wa Anaki), eneo hilo liliitwa pia Hebroni, katika nchi ya milima ya Yuda, pamoja na maeneo ya kulishia mifugo yaliyouzunguka mji.
\v 12 Lakini mashamba ya mji na vijiji vyake vilikuwa tayari ameshapewa Kalebu mwana Yefune, kama mali yake.
\s5
\v 13 Na kwa wana wa Haruni kuhani, waliwapa Hebroni pamoja na eneo lake la kulishia mifugo ambao ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia na Libna pamoja na maeneo ya kulishia mifugo.
\v 14 Na Yatiri pamoaja na maeno yake ya kuchungia, na Eshitemoa pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 15 Lakini pia waliwapa Holoni pamoja na maeneo yake ya malisho, Debiri pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 16 Aini pampoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. Ilikuwa ni miji kumi na tisa ambayo walipewa kutoka katika makabila haya mawilil.
\s5
\v 17 Kutoka katika kabilala Benyamini walipewa Gibea pamoja na maeneo yake ya malisho, na Geba pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 18 na Anathothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na amoni pamoja na vitongoji vyake vinne.
\v 19 Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.
\s5
\v 20 Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.
\v 21 Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 22 na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.
\s5
\v 23 Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na
\v 24 Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.
\s5
\v 25 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 26 Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.
\s5
\v 27 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.
\s5
\v 28 Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 29 Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Engnimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 30 Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali pamoja na maeneo yake ya malisho, Abdoni pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 31 Helikathi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Rehobu pamoja na maeneo yake ya malisho.
\s5
\v 32 Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi katika Galilaya pamoja na maeneo yake ya malisho, ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia; na Hamothidori pamoja na maeneo yake ya malisho, na Kartani pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 33 Kulikuwa na miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumuisha na maeneo yake ya malisho, kwa ajili ya koo za Gershoni.
\s5
\v 34 Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu pamoa na maeneo yake ya marisho, Karta pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 35 Dimna pamoja na maeneo yake ya malisho, na Nahalali pamoja na maeneo yake ya malisho- ilikuwa ni miji minne kwa ujumla.
\s5
\v 36 Kwa mbari za Merari walipewa miji minne kutoka katika kabila la Rubeni: Bezeri pamoja na maeneo yake ya malisho, Yahazi pamoja na maene yake ya malisho,
\v 37 na Kedemothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 38 Kutoka katika kabila la Gadi walipewa miji ya Ramothi katika Gileadi pamoja na sehemu zake za malisho - huu ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu mwenzake bila kukusudia - na Mahanaimu pamoja na sehemu zake za malisho.
\s5
\v 39 Koo za Merari zilipewa pia Heshiboni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Yazeri pamoja na malisho yake.
\v 40 Hii ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake. Hii yote ilikuwa ni miji ya koo kadhaa za Merari, ambao walitoka katika kabila la Lawi, miji kumi na miwili walipewa wao kwa kupiga kura.
\s5
\v 41 Miji waliyopewa Walawi kutoka katikati ya nchi iliyomilikiwa na watu wa Israeli ilikuwa miji arobaini na nane, kujumuisha na sehemu za malisho yao.
\v 42 Miji hii kila mmoja ulikuwa na maeneo yake ya malisho kwa kuuzunguka mji. Miji hii yote ilikuwa hivyo.
\s5
\v 43 Basi Yahweh aliwapa Israeli nchi yote ambayo aliwaapia baba zao kuwa atawapa. Waisraeli waliimiliki nchi na wakakaa humo.
\v 44 Kisha Yahweh akawapa pumziko kwa kila upande, kama tu alivyowaahidia baba zao. Hakuna hata adui mmoja atakayeweza kuwashinda. Yawhew aliwatia maadui wao wote mikononi mwao.
\v 45 Hakuna hata kitu kimoja miongoni kwa ahadi nzuri ambazo Yahweh alizisema kwa nyumba ya Israeli ambazo hazikutimia. Ahadi zote zilitimia.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kwa wakati huo, Yoshua aliwaita Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase.
\v 2 Aliwaambia, "Mmefanya kila kitu ambacho Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi. Mmeitii sauti yangu katika yote niliyowaagiza.
\v 3 Bado hamjawaacha ndugu zenu hawa kwa siku zote hizi, mpaka siku hii ya leo. Na mmetimiza wajibu unaotakiwa na amri za Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 4 Sasa Yahweh Mungu wenu amewapa pumziko ndugu zenu, kama alivyowaahidi. Hivyo basi, rudini na mwende katika hema zenu katika nchi mnayoimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapeni katika upande mwingine wa Yordani.
\v 5 Lakini zingatieni kuzishika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi, kumpenda Yahweh Mungu wenu, kutembea katika njia zake, kuzitunza amri zake, na kuambatana naye na kumwabudu yeye kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.
\v 6 Basi Yoshua akawabariki na kisha akawaacha waende zao, nao wakarudi katika hema zao.
\s5
\v 7 Na kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa urithi katika Bashani, lakini kwa nusu ya kabila hilo, Yoshua aliwapa urithi karibu na ndugu zao katika nchi magharibi mwa Yordani. Yoshua aliwaaga waende katika hema zao; aliwabarikia,
\v 8 na kisha akawaambia, "Rudini katika hema zenu mkiwa na pesa nyingi, na mkiwa na mifugo mingi, pamoja na na fedha, na dhahabu, na shaba na chuma, na nguo nyingi. Gawaneni na ndugu zenu nyara mlizochukua kutoka kwa maadui zenu.
\s5
\v 9 Hivyo, wazawa wa Rubeni, wazawa wa Gadi na nusu ya kabila la Manase walirudi nyumbani, waliwaacha watu wa Isaeli hapo Shilo, ambayo imo ndani ya nchi ya Kanaani. Waliondoka wakaenda katika mkoa wa Gileadi, katika nchi yao, ambayo wao wenyewe waliimiliki, katika utiifu wa amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.
\s5
\v 10 Nao walipofika hapo Yordani iliyo katika nchi ya Kanaani, Warubeni na Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu karibu na Yordani, madhabahu kubwa na iliyotokeza na mashuhuri.
\v 11 Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseam, "Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli."
\s5
\v 12 Wakati watu wa Israeli waliposikia hivyo, kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande kupigana vita nao.
\s5
\v 13 Kisha watu wa Israeli walituma wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi. Walimtuma pia Finehasi mwana wa Eliezari, kuhani,
\v 14 na viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka katika familia za mababa wa Israeli, na kila mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa ukoo miongoni mwa watu wa Israeli.
\s5
\v 15 Walienda kwa watu wa Rubeni, Gadi, na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakawaambia:
\v 16 "Kusanyiko lote la Yahweh linasema kuwa, ' Ni jambo gani hili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa Israeli, kwa kugeuka badala ya kumfuata Yahweh siku hii na kujijengea wenyewe madhabahu katika uasi kinyume na Yahweh katika siku hii?
\s5
\v 17 Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha? Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo. Kwa ajili ya dhambi ile lilikuja pigo kwa kusanyiko lote la Yahweh.
\v 18 Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh? Kama mtaasi kinyume na Yahweh leo, kesho atakuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.
\s5
\v 19 Na kama nchi ambayo mnaimiliki imetiwa unajisi, basi mwaweza kuvuka katika nchi ambayo Sanduku la Yahweh lasimama na mjichukulie kwa ajili yenu umiliki miongoni mwetu. Hamtakiwi kuasi kinyume na Yahweh tu, wala kuasi kinyume chetu kwa kujenga madhabahu kwa ajili yenu wenyewe badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wa wetu.
\v 20 Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli? Mtu yule hakuangamia peke yake kwa uovu wake.
\s5
\v 21 Kisha makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakawajibu wazee wa koo za Israeli:
\v 22 "Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijue yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo
\v 23 kwa ajili ya kujenga madhabahu ili tugeuka na kuacha kumfuata Yahweh. Kama tumejenga madhabahu hii ili kutoa juu yake sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, au sadaka ya amani, basi Yahweh na atuadhibu.
\s5
\v 24 La hasha, tulifanya hivyo kwa sababu ya hofu kwamba katika siku zijazo watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu, ' Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?
\s5
\v 25 Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote naYahweh.' Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh.
\s5
\v 26 Basi tukasema, 'Hebu na tujenge sasa madhabahu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa wala si kwa sadaka yoyote ile,
\v 27 ila iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi, na kati ya kizazi chetu baada yetu, kwamba tutafanya ibada ya Yahweh mbele yake, pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa na dhabihu zetu na sadaka zetu za amani, ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, "Hamna sehemu katika Yahweh."'
\s5
\v 28 Hivyo tukasema, 'kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, " Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi."
\v 29 Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh, na kuacha kumfuata yeye kwa kujenga madhabahu kwa ajili sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya nafaka, au kwa dhabihu, badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu ambayo iko mbele ya hema la kukutania.'"
\s5
\v 30 Finehasi kuhani na viongozi wa watu, ambao ni wakuu wa koo za Waisraeli ambao walikuwa pamoja naye, waliposikia maneno amabayo watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, kwamba yalikuwa ni mazuri machoni pao.
\v 31 Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani aliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na Manase, "Leo tumejua kwambaYahweh yuko miongoni mwetu, kwa kuwa hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye. Sasa, mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh."
\s5
\v 32 Kisha Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani, na viongozi walirudi kutoka kwa Warubeni na Wagadi, kutoka katika nchi ya Gileadi, na kurudi katika nchi ya Kanaani, kwa watu wa Israeli, na waliwaletea taarifa.
\v 33 Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu wa Israeli. Watu wa Israeli walimbarikia Mungu na hawakuendelea kusema tena juu ya kuinua vita dhidi ya Warubeni na Wagadi, ili kuiharibu nchi ambayo walikuwa wanaishi.
\s5
\v 34 Warubeni na Wagadi waliita ile madhabahu "Ushahidi," kwa kuwa walisema, "Ni ushahidi miongoni mwetu kuwa Yahweh ni Mungu."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Na baada ya siku nyingi, kipindi ambacho Yahweh alikuwa ameipa Israeli pumziko kutoka maadui zao waliowazunguka,
\v 2 Joshua alikuwa mzee sana. Yoshua aliwaita Waisraeli wote, na wazee wao, na viongozi, na waamuzi, na kwa maafisa, na kisha akawaambia, "Mimi nimezeeka sana.
\v 3 Mmeshaona kila kitu ambacho Yahweh Mungu wenu ameshafanya kwa mataifa haya yote kwa ajili yenu, kwa kuwa ni Yahweh Mungu wenu ambaye amewapigania ninyi.
\s5
\v 4 Tazama! Nimeshawakabidhi kwenu mataifa yaliyosalia ili kuyateka kwa ajili ya kupata urithi ya makabila yenu, sambasamba na mataifa yote ambayo tayari nimeshayaangamiza, tangu Yordani hadi Bahari kuu katika upande wa magharibi.
\v 5 Yahweh Mungu wenu atayaondoa. Atayafukuzia mbali kutoka kwenu. Ataiteka nchi yao, nanyi mtaimiliki nchi yao, kama vile Yahweh Mungu wenu alivyowaahidi ninyi.
\s5
\v 6 Hivyo, iweni jasiri, ili kwamba mtunze na kuyafanya yale yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa, msikengeuke upande wa kulia wala upande wa kushoto,
\v 7 basi msichanganyikane na mataifa haya ambayo yamesalia miongoni mwenu, wala msiyataje majina ya miungu yao, wala msiape kwayo, wala msiiabudu, wala msiipigie magoti.
\v 8 Badala yake, mnatakiwa kumshika sana Yahweh Mungu wenu kama vile mlivyofanya siku hii ya leo.
\s5
\v 9 Kwa kuwa Yahweh ameyafukuzia mbali mbele yenu mataifa makubwa yenye nguvu. Hakuna hata mmoja aliyeweza kusimama mbele yenu hata siku hii ya leo.
\v 10 Mtu yeyote mmoja wa kwenu atawafanya watu elfu wakimbie mbali, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ndiye anayepigania ninyi, kama vile alivyowaahidi.
\v 11 Zingatieni kwa uangalifu ili mmpende Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 12 Lakini kama mkiegeuka na kushikamana na watu walioalia wa mataifa haya waliobaki miongoni mwenu, au kuoana nao, au kama mkishirikiana pamoja nao, na wao pamoja nanyi,
\v 13 jueni kwa hakika kwamba Yahweh Mungu wenu hatayafukuzia mbali mataifa haya yatoke kati yenu. Badala yake, watakuwa kitanzi na mtego kwenu, viboko migongoni mwenu na miiba machoni mwenu, mpaka pale mtakapoangamia katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
\s5
\v 14 Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote, na mnajua kwa moyo na roho zenu zote kwamba hakuna hata neno moja ambalo halijatimia kati ya mambo yote mazuri ambayo Yahweh Mungu wenu aliyaahidi juu yenu. Vitu hivi vyote vimetokea kwa ajili yenu. Hakuna hata moja lililoshindikana.
\v 15 Lakini kama kila neno ambalo Yahweh Mungu wenu alilowaahidi limekwisha kutimia, hivyo Yahweh atawaletea juu yenu mabaya yote mpaka pale atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
\s5
\v 16 Atafanya hivi kama mtalivunja agano la Yahweh Mungu wenu, ambalo aliwaagizeni kulitunza. Kama mtaenda na kuiabudu miungu mingine na kuiinamia, ndipo hasira ya Yahweh itawaka kinyume nanyi, na ninyi mtaangamia upesi katika nchi nzuri ambayo amekwisha kuwapeni ninyi."
\s5
\c 24
\p
\v 1 Kisha Yoshua aliyakusanya pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu na aliwaita wazee wa Israeli, viongozi, waamuzi na maafisa wao, nao wakajihudhurisha mbele za Mungu.
\v 2 Yoshua akawaambia watu wote, "Hiki ndicho Yahweh, Mungu wa Israeli anachokisema, 'Mababu zenu kwa miaka mingi iliyopita waliishi ng'ambo ya mto Frati - Tera, baba wa Ibrahimu na baba wa Nahori - nao waliabudu miungu mingine.
\s5
\v 3 Lakini nilimchukua baba yenu kutoka ng'ambo ya Frati na nikamwongoza mpaka katika nchi ya Kanaani, na nilimpa watoto wengi kupitia kwa Isaka mwanaye.
\v 4 Na Isaka nikampa Yakobo na Esau. Nilimpa Esau nchi ya milima ya Seiri ili aimiliki, lakini Yakobo na watoto wake walishuka kwenda Misri.
\s5
\v 5 Nilimtuma Musa na Haruni, na niliwapiga Wamisri kwa mapigo. Baada ya hapo, niliwatoa ninyi.
\v 6 Niliwatoa baba zenu nje ya nchi ya Misri, nanyi mkafika hata katika bahari. Wamisri waliwafuata kwa magari na wapanda farasi hata katika bahari ya matete.
\s5
\v 7 Na baba zenu walipomwita Yahweh, aliweka giza kati yenu na Wamisri. Aliileta bahari ije juu yao na kuwafunika. Mliona yale niliyoyakifanya huko Misri. Kisha mliishi jangwaani kwa muda mrefu.
\s5
\v 8 Niliwaleta katika nchi wa Waamori, ambao waliishi katika upande mwingine mwa Yordani. Walipigana nanyi, nami niliwatia katika mkono wenu. Mliimiliki nchi yao, nami niliwaangamiza mbele yenu.
\s5
\v 9 Kisha Balaki mwana wa Zipori, mfalme wa Moabu, aliinuka na kuishambulia Israeli. Alimwita na kumtuma Baalamu mwana wa Beori, ili kuwalaani ninyi.
\v 10 Lakini sikumsikiliza Balaamu. Kwa hakika, aliwabarikia ninyi. Basi, niliwaokoa na mkono wake.
\s5
\v 11 Mlivuka Yordani na mkafika Yeriko. Viongozi wa Yeriko waliinuka wapigane nanyi, pamoja na Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi. Niliwapa ninyi ushindi dhidi yao na niliwaweka chini ya mamlaka yenu.
\v 12 Nilituma manyingu mbele yenu, ambayo yaliwafukuzia mbali na wafalme wawili wa Waamori watoke mbele yenu. Haikutokea kwa sababu ya upanga wenu wala kwa upinde wenu.
\s5
\v 13 Niliwapeni ninyi nchi ambayo hamkuifanyia kazi na miji ambayo hamkuijenga, na sasa mnaishi ndani yake. Mnakula matunda ya mizabibu na na mashamba ya mizeituni ambayo hamkuyapanda'.
\s5
\v 14 Basi sasa mcheni Yahweh na kumwabudu yeye kwa uadilifu na uaminifu wote; jitengeni na miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati na katika Misri, na mkamwabudu Yahweh.
\v 15 Na kama inaonekana kuwa ni vibaya machoni penu kumwabudu Yahweh, chagueni ninyi katika siku hii ya leo ni nani mtakayemtumikia, kama ni miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao ninyi mnakaa ndani ya nchi yao. Lakini kwangu mimi na nyumba yangu, tutumwabudu Yahweh."
\s5
\v 16 Watu walijibu na kusema, "Hatutaweza kumwacha Yahweh na kuitumikia miungu mingine,
\v 17 kwa kuwa ni Yahweh Mungu wetu ambaye alitutoa sisi na baba zetu kutoka katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, na ambaye alifanya hizo ishara kubwa mbele yetu, na ambaye alituhifadhi sisi katika njia zote ambazo sisi tuliziendea, na miongoni mwa mataifa yote ambayo tulipita kati kati yake,
\v 18 Na Yahweh aliwaondoa mbele yetu watu wote, na Waamori walioishi katika nchi hii. Hivyo, tutamwabudu Yahweh pia, kwa kuwa ni Mungu wetu"
\s5
\v 19 Lakini Yoshua akawaambia watu, "Hamwezi kumtumikia Yahweh, kwa kuwa ni Mungu mtakatifu; ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa na dhambi zenu.
\v 20 Kama mtamwacha Yahweh na kuabudu miungu ya kigeni, basi atageuka na kuwaharibu. Atawaangamizeni baada ya kuwa amewatendea mema."
\s5
\v 21 Lakini watu walimwambia Yoshua, "Hapana, tutamwabudu Yahweh."
\v 22 Kisha Yoshua akawaambia watu, "Ninyi ni mashahidi dhidi yenu wenyewe kuwa mmemchagua Yahweh ninyi wenyewe, ili mmwabudu yeye." Watu walijibu, "Sisi ni mashahidi."
\v 23 "Sasa wekeni mbali miungu ya kigeni iliyoko kwenu, na geuzeni moyo wenu umwelekee Yahweh, Mungu wa Israeli."
\s5
\v 24 Watu wakamwambia Yoshua, "Tutamwabudu Yahweh Mungu wetu. Tutaisikiliza sauti yake.
\v 25 Yoshua alifanya agano na watu siku hiyo. Aliziweka maagizo na sheria huko Shekemu.
\v 26 Yoshua aliyaandika maneno haya katika kitabu cha sheria za Mungu. Alichukua jiwe kubwa na kulisimamisha hapo chini ya mti wa mwaloni uliokuwa karibu na mahali pa takatifu pa Yahweh.
\s5
\v 27 Yoshua akawaambia watu, "Tazama, jiwe hili litakuwa ushuhuda dhidi yenu. Limeyasikia maneno yote ambayo Yahweh alitwambia. Hivyo, litakuwa ni shahidi dhidi yenu, hamtakiwi kumkana Mungu wenu."
\v 28 Basi Yoshua aliwaacha watu waende zao, kila mmoja alienda kwenye urithi wake.
\s5
\v 29 Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Yahweh, alikufa akiwa na miaka 110.
\v 30 Walimzika katika mpaka wa urithi wake mwenyewe huko Timnathi Sera, ambayo iko kwenye nchi ya milima ya Efraimu, upande wa Mlima Gaashi.
\s5
\v 31 Israeli ilimwabudu Yahweh siku zote za maisha ya Yoshua, na siku zote za wazee ambao walidumu pamoja na Yoshua, wale ambao waliona kila kitu ambacho Yahweh alikuwa ameifanyia Israeli.
\s5
\v 32 Mifupa ya Yusufu ambayo watu wa Israeli waliileta kutoka Misri, waliizika huko shekemu, katika sehemu ya nchi ambayo Yakobo alikuwa ameinunua kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu. Aliinunua kwa vipande mia moja vya fedha, na ulikuwa urithi kwa wazawa wa Yusufu.
\v 33 Eliazeri mwana wa Haruni alikufa pia. Walimzika huko Gibea, katika mji wa ambao alikuwa amepewa Finehasi mwanaye, na ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu.