most OT books

This commit is contained in:
Larry Versaw 2018-09-27 16:59:39 -06:00
parent e7f7505949
commit 02ff68ea09
35 changed files with 42397 additions and 12 deletions

2908
01-GEN.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2908 @@
\id GEN
\ide UTF-8
\h Mwanzo
\toc1 Mwanzo
\toc2 Mwanzo
\toc3 gen
\mt Mwanzo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.
\v 2 Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji.
\s5
\v 3 Mungu akasema, "na kuwe nuru," na kulikuwa na nuru.
\v 4 Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza.
\v 5 Mungu akaiita nuru " mchana" na giza akaliita "usiku." Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.
\s5
\v 6 Mungu akasema, " na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji."
\v 7 Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo.
\v 8 Mungu akaita anga "mbingu." Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili.
\s5
\v 9 Mungu akasema, "maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane." Ikawa hivyo.
\v 10 Mungu aliita ardhi kavu "nchi," na maji yaliyo kusanyika akayaita "bahari." Akaona kuwa ni vyema.
\s5
\v 11 Mungu akasema, nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake." Ikawa hivyo.
\v 12 Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
\v 13 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu.
\s5
\v 14 Mungu akasema, "kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.
\v 15 Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi." Ikawa hivyo.
\s5
\v 16 Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.
\v 17 Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi,
\v 18 kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.
\v 19 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne.
\s5
\v 20 Mungu akasema, "maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu."
\v 21 Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.
\s5
\v 22 Mungu akavibariki, akisema, "zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi."
\v 23 Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano.
\s5
\v 24 Mungu akasema, " nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake." Ikawa hivyo.
\v 25 Mungu akafanya wanyama wa nchi kwa aina yake, wanyama wa kufugwa kwa aina yake, na kila kitambaaho juu ya ardhi kwa aina yake. Akaona kuwani vyema.
\s5
\v 26 Mung akasema, "na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi."
\v 27 Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake. Katika mfano wake alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba.
\s5
\v 28 Mungu akawabariki na akawaambia, "zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,"
\v 29 Mungu akasema, "tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu.
\s5
\v 30 Kwa kila mnyama wa nchi, kwa kila ndege wa angani, na kila kitambaacho juu ya nchi, na kila kiumbe ambacho kina pumzi ya uhai ni metoa kila mmea kwa ajili ya chakula." ikawa hivyo.
\v 31 Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha mbingu na nchi zilimalizika, na viumbe hai vyote vilivyo jaza mbingu na nchi.
\v 2 Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.
\v 3 Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.
\s5
\v 4 Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa, katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba nchi na mbingu.
\v 5 Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi.
\v 6 Lakini ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi na kuutia maji uso wote wa ardhi.
\s5
\v 7 Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai.
\v 8 Yahwe Mungu aliotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, na pale akamuweka mtu ambaye alimuumba.
\s5
\v 9 Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
\v 10 Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani. Na kutoka pale ukagawanyika na kuwa mito minne.
\s5
\v 11 Jina la ule wa kwanza ni Pishoni. Huu ni ule ambao unatiririka kupitia nchi yote ya Havila, ambapo kuna dhahabu.
\v 12 Dhahabu ya inchi ile ni nzuri. pia kuna bedola na jiwe shohamu.
\s5
\v 13 Jina la mto wa pili ni Gihoni. Huu unatiririka kupitia nchi yote ya kushi.
\v 14 Jina la mto wa tatu ni Hidekeli, ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.
\s5
\v 15 Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.
\v 16 Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, "kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru.
\v 17 Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika."
\s5
\v 18 Kisha Yahwe Mungu akasema, "siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa."
\v 19 Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake.
\v 20 Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye.
\s5
\v 21 Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu.
\v 22 Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu.
\v 23 Mwanaume akasema, "kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume.
\s5
\v 24 Kwa hiyo mwanaume atawaacha baba yake na mama yake, ataungamanika na mke wake, na watakuwa mwili mmoja.
\v 25 Wote wawili walikuwa uchi, mwanaume na mke wake, lakini hawakuona aibu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, "Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?"
\v 2 Mwanamke akamwambia nyoka, "Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani,
\v 3 lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, 'msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.'"
\s5
\v 4 Nyoka akamwambia mwanamke, "hakika hamtakufa.
\v 5 Kwasababu Mungu anajua kwamba siku mkila macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya."
\v 6 Na mwanamke alipoona kuwa mti ni mzuri kwa chakula, na kuwa unapendeza macho, na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu, alichukua sehemu ya tunda na akala. Na sehemu yake pia akampatia mumewe aliyekuwa naye, naye akala.
\s5
\v 7 Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe.
\v 8 Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu.
\s5
\v 9 Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, " uko wapi?"
\v 10 Mwanaume akasema, "nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha."
\v 11 Mungu akasema, "Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?"
\s5
\v 12 Mwanaume akasema, " Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala."
\v 13 Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, " Nini hiki ulichofanya?" mwanamke akasema, "nyoka alinidanganya, na nikala."
\s5
\v 14 Yahwe Mungu akamwambia nyoka, " kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako.
\v 15 Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake."
\s5
\v 16 Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala."
\s5
\v 17 Kwa Adam akasema, "kwa sababu umesikiliza sauti ya mke wako, na umekula kutoka katika mti, ambao nilikuagiza, nikisema, " usile matunda yake', ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kupitia kazi yenye maumivu utakula matunda ya ardhi kwa siku zote za maisha yako.
\v 18 Ardhi itazaa miiba na mbigili kwa ajili yako, na utakula mimea ya shambani.
\v 19 Kwa jasho la uso wako utakula mkate, mpaka utakapo irudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa. kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi."
\s5
\v 20 Mwanaume akaita mke wake jina Hawa kwa sababu alikuwa mama wa wote wenye uhai.
\v 21 Yahwe Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi kwa ajili ya Adam na mke wake na akawavalisha.
\s5
\v 22 Yahwe Mungu akasema, " sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele."
\v 23 Kwa hiyo Yahwe Mungu akamuondoa kutoka kwenye bustani ya Edeni, kwenda kulima ardhi ambayo kwahiyo alikuwa ametwaliwa.
\v 24 Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, " nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe."
\v 2 Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo.
\s5
\v 3 Ikawa kwamba baada ya muda Kaini alileta sehemu ya mazao ya ardhi kama sadaka kwa Yahwe.
\v 4 Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake,
\v 5 lakini Kaini pamoja na sadaka yake Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana.
\s5
\v 6 Yahwe akamwambia Kaini, " kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana?
\v 7 Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde.
\s5
\v 8 Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. (Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, " twende mashambani." Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua).
\v 9 Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, "Ndugu yako Habili yuko wapi?" Akasema, "sijui. Je mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?"
\s5
\v 10 Yahwe akasema, "umefanya nini? damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini.
\v 11 Na sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhi ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako kutoka mikononi mwako.
\v 12 Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani."
\s5
\v 13 Kaini akamwambia Yahwe, "Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili.
\v 14 Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua."
\v 15 Yahwe akamwambia, "ikiwa mtuyeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba." Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu awayeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie.
\s5
\v 16 Kwa hiyo Kaini akatoka mbele ya uwepo wa Yahwe na akaishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.
\v 17 Kaini akamjua mke wake na akapata mimba. Akamzaa Henoko. Akajenga mji na akauita kwa jina la mwanae Henoko.
\s5
\v 18 Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki.
\v 19 Lameki akajitwalia wake wawili: jinala mmoja alikuwa Ada, na jina la yule mwingine alikuwa Sila.
\s5
\v 20 Ada akamzaa Yabali. Huyu ndiye alikuwa baba yao na wale walioishi hemani ambao wanafuga wanyama.
\v 21 Ndugu yake aliitwa Yubali. Huyu alikuwa baba yao na wale wapigao kinubi na filimbi.
\v 22 Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama.
\s5
\v 23 Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua.
\v 24 Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba."
\s5
\v 25 Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, " Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa."
\v 26 Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
\v 2 Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.
\s5
\v 3 Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.
\v 4 Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.
\v 5 Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.
\s5
\v 6 Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
\v 7 Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.
\v 8 Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.
\s5
\v 9 Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
\v 10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 11 Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.
\s5
\v 12 Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
\v 13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 14 Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.
\s5
\v 15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.
\v 16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 17 Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
\s5
\v 18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.
\v 19 Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake.
\v 20 Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.
\s5
\v 21 Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.
\v 22 Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 23 Henoko aliishi miaka 365.
\v 24 Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
\s5
\v 25 Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.
\v 26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
\v 27 Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
\s5
\v 28 Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
\v 29 Akamuita jina lake Nuhu, akisema, "Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani."
\s5
\v 30 Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake.
\v 31 Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.
\s5
\v 32 Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao,
\v 2 wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia. waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua.
\v 3 Yahwe akaema, " roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120."
\s5
\v 4 Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
\s5
\v 5 Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima inaelekea tu katika uovu.
\v 6 Yahwe akajuta kuwa amemuumba mwanadamu juu ya nchi, na ikamuhuzunisha moyo wake.
\s5
\v 7 Kwa hiyo Yahwe akasema, "Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba."
\v 8 Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe.
\s5
\v 9 Kulikuwa na matukio kumuhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu.
\v 10 Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti.
\s5
\v 11 Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia.
\v 12 Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi.
\s5
\v 13 Mungu akamwambia Nuhu, "Nimeona kuwa sasa niwakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa inchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi.
\v 14 Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje.
\v 15 Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini.
\s5
\v 16 Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu.
\v 17 Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa.
\s5
\v 18 Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao.
\v 19 Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume.
\s5
\v 20 Katika ndege kwa jinsi yake, na wanyama wakubwa kwa jinsi yake, kila kitambaacho ardhini kwa jinsi yake, viwili viwili vya kila aina vitakuja kwako ili viwe salama.
\v 21 Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao."
\v 22 Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Yahwe akamwambia Nuhu, "Njoo, wewe na nyumba yako wote, katika safina, kwa kuwa nimeona kuwa wewe ni mwenye haki mbele yangu katika kizazi hiki.
\v 2 Kwa kila mnyama aliye safi utakuja nao saba wa kiume na saba wa kike. Na kwa wanyama wasio safi, lete wawili wawili, wakiume na wakike.
\v 3 Pia na kwa ndege wa angani, lete saba wa kiume na saba wa kike, ili kuhifadhi kizazi chao juu ya uso wa nchi yote.
\s5
\v 4 Kwa kuwa ndani ya siku saba nitasababisha mvua kunyesha juu ya nchi muda wa siku arobaini mchana na usiku. Nitaharibu kila kiumbe hai nilichokiumba juu ya uso wa ardhi."
\v 5 Nuhu alifanya yote ambayo Yahwe alimuagiza.
\s5
\v 6 Nuhu alikuwa na umri wa miaka mia sita wakati gharika ilipokuja juu ya nchi.
\v 7 Nuhu, watoto wake wa kiume, mke wake, na wake za watoto wake waliingia katika safina pamoja kwa sababu ya maji ya gharika.
\s5
\v 8 Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi,
\v 9 wawili wawili mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu.
\v 10 Ikawa kwamba baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya nchi.
\s5
\v 11 Katika mwaka wa mia sita wa maisha yake Nuhu, katika mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi, katika siku iyo hiyo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka, na madirisha ya mbinguni yakafunguka.
\v 12 Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.
\s5
\v 13 Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina.
\v 14 Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa.
\s5
\v 15 Viwili viwili katika kila chenye mwili ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai kilikuja kwa Nuhu na kuingia katika safina.
\v 16 Wanyama walioingia ndani walikuwa wakiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango.
\s5
\v 17 Kisha gharika ikaja juu ya nchi kwa siku arobaini, na maji yakaongezeka na kuinua safina juu ya nchi.
\v 18 Maji yakafunika kabisa nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.
\s5
\v 19 Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi kiasi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya anga ikafunikwa.
\v 20 Maji yakaongezeka dhiraa kumi na tano juu ya vilele vya milima.
\s5
\v 21 Vitu vyote vyenye uhai ambavyo vilitembea juu ya nchi vilikufa: ndege, mifugo, wanyama wa mwituni, viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi, pamoja na watu.
\v 22 Viumbe hai vyote ambavyo vilikaa juu ya ardhi, vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua, vilikufa.
\s5
\v 23 Hivyo kila kilichokuwa hai ambacho kilikuwa juu ya uso wa mchi kilifutwa, kuanzia watu mpaka wanyama wakubwa, mpaka vitambaavyo, na mpaka ndege wa angani. Vyote viliangamizwa kutoka kwenye nchi. Nuhu tu pamoja na wale waliokuwa naye kwenye safina ndio walisalia.
\v 24 Maji haya kuzama chini ya nchi kwa muda wa siku miamoja na hamsini.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini.
\v 2 Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha.
\v 3 Maji ya gharika yakaanza kuzama kidogo kidogo katika nchi. na mwisho wa siku miamoja na hamsini maji yakawa yamezama chini.
\s5
\v 4 safina ikatulia katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, juu ya milima ya Ararati.
\v 5 Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
\s5
\v 6 Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza.
\v 7 Akatuma kunguru na akaruka hadi maji yalipo kauka katika nchi.
\s5
\v 8 Kisha akatuma njiwa kuona kama maji yamezama chini kutoka kwenye uso wa nchi,
\v 9 lakini njiwa hakuona sehemu ya kutua unyayo wake, na akarudi kwake ndani ya safina, kwa kuwa maji yalikuwa bado yamefunika nchi yote. Akanyoosha mkono wake, akamchukua na kumuweka ndani ya safina pamoja naye.
\s5
\v 10 Akasubiri siku saba zingine akatuma tena njiwa kutoka kwenye safina.
\v 11 Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi.
\v 12 Akasubiri siku saba zingine na akamtuma njiwa tena. Njiwa hakurudi kwake tena.
\s5
\v 13 Ikawa kwamba katika mwaka wa mia sita na moja, katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, akatazama nje, na akaona kwamba, Tazama, uso wa nchi ulikuwa umekauka.
\v 14 Katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa imekauka.
\s5
\v 15 Mungu akamwambia Nuhu,
\v 16 "Toka nje ya safina, wewe, mke wako, wanao wa kiume, na wake wa wanao pamoja nawe.
\v 17 Wachukuwe utoke nje pamoja nao kila kiumbe hai chenye mwili ambacho kiko nawe - ndege, wanyama wa kufugwa, na kila kitambaacho ambacho hutambaa juu ya nchi - ili kwamba viweze kukua na kuwa na idadi kubwa zaidi ya viumbe hai katika nchi yote, kwa kuzaliana na kuongezeka juu ya nchi."
\s5
\v 18 Kwa hiyo Nuhu akatoka nje pamoja na watoto wake wa kiume, mke wake, na wake wa wa wanawe pamoja naye.
\v 19 Kila kiumbe hai, kila kitambaacho, na kila ndege, na kila kiendacho juu ya nchi, kwa kabila zao, wakaiacha safina.
\s5
\v 20 Nuhu akajenga madhabahu kwa Yahwe. Akachukua baadhi ya wanyama walio safi na baadhi ya ndege walio safi, na kutoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.
\v 21 Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, " Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kilakitu chenye uhai, kama nilivyo fanya.
\v 22 Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma."
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha Mungu akambariki Nuhu na wanawe, na kuwaambia, "Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi.
\v 2 Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai juu ya nchi, juu ya kila ndege wa angani, juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi, na juu ya samaki wote wa baharini. Vimetolewa katika mikono yenu.
\s5
\v 3 Kila kitu kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula kwa ajili yenu. Kama nilivyo wapa mimea, sasa nawapa kila kitu.
\v 4 Lakini msile nyama pamoja na uhai wake - yaani damu yake - ndani yake.
\s5
\v 5 Lakini kwa ajili ya damu yenu, uhai uliomo katika damu yenu nitataka malipo. Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka. Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo.
\v 6 Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa, kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu.
\v 7 Na hivyo nanyi zaeni na kuongezeka, sambaeni katika inchi yote na muongezeke juu yake."
\s5
\v 8 Kisha Mungu akazungumza na Nuhu na wanae pamoja naye, akisema,
\v 9 "Kwa ajili yangu, sikiliza! Ninakwenda kulithibitisha agano langu pamoja nawe na uzao wenu baada yenu,
\v 10 na kwa kila kiumbe hai kilicho pamoja nawe, pamoja na ndege, mnyama wa kufugwa, na kila kiumbe cha nchi pamoja nawe, kuanzia kwa wote waliotoka kwenye safina, mpaka kwa kila kiumbe hai juu ya nchi.
\s5
\v 11 Kwa sababu hii ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi, kwamba hapatatokea kuangamizwa kwa mwenye mwili kwa njia ya maji ya gharika. Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi."
\v 12 Mungu akasema, " na hii ndiyo ishara ya agano ambalo ninafanya kati yangu na ninyi pamoja na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote vya baadaye:
\v 13 Nimeweka upinde wangu wa mvua katika wingu, na itakuwa ndiyo ishara ya agano kati yangu na nchi.
\s5
\v 14 Hata itakuwa nitakapoleta wingu juu ya nchi na upinde wa mvua ukaonekana katika wingu,
\v 15 ndipo nitakumbuka agano langu, ambalo ni kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai cha wote mwenye mwili. Maji hayatafanyika tena gharika kuharibu wote wenye mwili.
\s5
\v 16 Upinde wa mvua utakuwa katika mawingu na nitauona, ili kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na kila kiumbe hai cha wote wenye mwili ambacho kiko juu ya nchi."
\v 17 Kisha Mungu akamwambia Nuhu, " Hii ni ishara ya agano ambalo nimelithibitisha kati yangu na wenye mwili wote ambao wako juu ya nchi."
\s5
\v 18 Wana wa Nuhu ambao walitoka katika safina walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi. Na Hamu akamzaa kanaani.
\v 19 Watatu hawa walikuwa ndio wana wa Nuhu, na kutokea kwa hawa nchi yote ikajaa watu.
\s5
\v 20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, na akapanda mizabibu.
\v 21 Akanywa sehemu ya divai na akalewa. Akawa amelala hemeani uchi.
\s5
\v 22 Kisha Hamu, baba yake na Kanaani, akaona uchi wa baba yake na akawaambia ndugu zake wawili waliokuwa nje.
\v 23 Kwa hiyo Shemu na Yafethi wakachukua kanzu wakaitanda juu ya mabega yao, na wakatembea kinyumenyume na wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zikiwa zimegeuka nyuma upande mwingine, kwa hiyo hawakuona uchi wa baba yao.
\s5
\v 24 Nuhu alipozinduka kutoka katika ulevi wake, alijua ni jambo gani mtoto wake mdogo amemfanyia.
\v 25 Hivyo akasema, "Alaaniwe Kanaani. Na awe mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake."
\s5
\v 26 Akasema pia, Yahwe, Mungu wa Shemu, abarikiwe, Kanaani na awe mtumwa wake.
\v 27 Mungu na apanuwe mipaka ya Yafethi, na afanye makazi yake katika hema za Shemu. Kanaani na awe mtumwa wake."
\s5
\v 28 Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka miatatu na hamsini.
\v 29 Siku zote za Nuhu zilikuwa ni miaka mia tisa na hamsini, na kisha alikufa.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika.
\s5
\v 2 Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi.
\v 3 Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama.
\v 4 Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu.
\v 5 Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao.
\s5
\v 6 Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani.
\v 7 Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
\s5
\v 8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi.
\v 9 Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, "Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe."
\v 10 Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari.
\s5
\v 11 Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala,
\v 12 na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa.
\v 13 Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi,
\v 14 Wapathrusi na Wakasluhi ( ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori.
\s5
\v 15 Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
\v 16 pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi,
\v 17 Mhivi, Mwarki, Msini,
\v 18 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa.
\s5
\v 19 Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha.
\v 20 Hawa walikuwa wana wa Ham, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao.
\s5
\v 21 Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi.
\v 22 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu.
\v 23 Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
\s5
\v 24 Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber.
\v 25 Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani.
\s5
\v 26 Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
\v 27 Hadoram, Uzali, Dikla,
\v 28 Obali, Abimaeli, Sheba,
\v 29 Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
\s5
\v 30 Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki.
\v 31 Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao.
\s5
\v 32 Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Sasa nchi yote ilikuwa inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja.
\v 2 Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale.
\s5
\v 3 Wakasemezana, "Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu." Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa.
\v 4 Wakasema, "njoni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote."
\s5
\v 5 Kwa hiyo Yahwe akashuka kuona mji na mnara ambao wazao wa Ibrahimu walikuwa wamejenga.
\v 6 Yahwe akasema, "Tazama, watu hawa ni taifa moja na lugha moja, na wameanza kufanya hivi! Hivikaribuni halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya.
\v 7 Njoni, tushuke na tuvuruge lugha yao pale, ili kwamba wasielewane."
\s5
\v 8 Kwa hiyo Yahwe akawatawanya kutoka pale kwenda pande zote za uso wa nchi na wakaacha kujenga mji.
\v 9 Kwa hiyo, jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga lugha ya nchi yote na tangu pale Yahwe akawatawanya ng'ambo juu ya uso wa nchi yote.
\s5
\v 10 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu. Shemu alikuwa na umri wa miaka mia moja, na akamzaa Alfaksadi miaka miwili baada ya gharika.
\v 11 Shemu akaishi miaka miatano baada ya kumzaa Alfaksadi. Pia akazaa wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 12 Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka thelathini na mitano akamzaa Shela.
\v 13 Alfaksadi aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Shela. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 14 Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.
\v 15 Shela aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Eberi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 16 Wakati Eberi alipokuwa ameishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.
\v 17 Eberi aliishi miaka 430 baada ya kumzaa Pelegi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 18 Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Reu.
\v 19 Pelegi aliishi miaka 209 baada ya kumza a Reu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 20 Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka thelathini na miwili, alimzaa Serugi.
\v 21 Reu aliishi miaka207 baada ya kumzaa Seregu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 22 Wakati Seregu alipokuwa ameishi miaka thelathini, akamzaa Nahori.
\v 23 Seregu aliishi miaka mia mbili baada ya kumzaa Nahori. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\s5
\v 24 Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera.
\v 25 Nahori aliishi mika 119 baada ya kumzaa Tera. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.
\v 26 Baada ya Tera kuishi miaka sabini, akamzaa Abram, Nahori, na Haran.
\s5
\v 27 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera. Tera alimzaa Abram, Nahori, na Harani, na Harani akamzaa Lutu.
\v 28 Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo.
\s5
\v 29 Abram na Nahori wakajitwalia wake. Mke wa Abram aliitwa Sarai na mke wa Nahori aliitwa Milka, binti wa Harani, aliyekuwa baba wa Milka na Iska.
\v 30 Sasa Sarai alikuwa Tasa; hakuwa na mtoto.
\s5
\v 31 Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale.
\v 32 Tera akaishi miaka 205 kisha akafa hapao Harani.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kisha Yahwe akamwambia Abram, "Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako, na kwa jamaa za baba yako, uende katika nchi nitakayo kuonesha.
\v 2 Nitakufanya uwe taifa kubwa, na nitakubariki na kulifanya jinalako kuwa kubwa, na utafanyika baraka.
\v 3 Nitawabariki wakubarikio, lakini asiye kuheshimu nita mlaani. Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa.
\s5
\v 4 Kwa hiyo Abram akaondoka kama vile Yahwe alivyo mwambia kufanya, na Lutu akaenda pamoja naye. Abram alikuwa na miaka sabini na mitano wakati alipotoka Harani.
\v 5 Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani.
\s5
\v 6 Abram akapitia katikati ya nchi hadi Shekemu, hadi mwaloni wa More. Wakati huo wakanaani waliishi katika nchi hiyo.
\v 7 Yahwe akamtokea Abram, na kusema, "Nitawapa uzao wako nchi hii." Kwa hiyo Abram akamjengea madhabahu, Yahwe ambaye alimtokea.
\s5
\v 8 Kutoka pale akaenda kwenye nchi ya mlima mashariki mwa Betheli, ambapo alipiga hema yake, magaribi kukiwa na Betheli na mashariki kukiwa na mji wa Ai. Akajenga madhabahu ya Yahwe pale na kuliitia jina la Yahwe.
\v 9 Kisha Abram akaendelea kusafiri, akielekea upande wa Negebu.
\s5
\v 10 Kulikuwa na njaa katika nchi, kwa hiyo Abram akaenda kukaa Misri, kwa kuwa njaa ilikua kali katika nchi.
\v 11 Wakati alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, "tazama, najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri.
\v 12 Wamisri watakapokuona watasema, huyu ni mke wake, na wataniua mimi, lakini watakuacha wewe hai.
\v 13 Hivyo wewe sema kuwa ni dada yangu, ili kwamba niwe salama kwa sababu yako, na kumba maisha yangu yatasalimika kwa sababu yako."
\s5
\v 14 Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana.
\v 15 Wakuu wa Farao wakamuona, na kumsifia kwa Farao, na huyu mwanamke akachukuliwa kupelekwa nyumbani mwa Farao.
\v 16 Farao akamtendea kwa wema Abram kwa ajili yake, na akampatia kondoo, maksai, punda waume watumishi wa kiume, watumishi wa kike, punda wake, na ngamia.
\s5
\v 17 Kisha Yahwe akampiga Farao na nyumba yake kwa mapigo makuu kwa sababau ya Sarai, mke wa Abram.
\v 18 Farao akamwita Abram na kusema, "Nini hiki ambacho umenifanyia? Kwa nini hukuniambia kuwa alikuwa mke wako?
\v 19 Kwa nini ulisema, 'ni dada yangu; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako."
\v 20 Kisha Farao akatoa amri kwa watu wake kuhusiana naye, na wakamuondoa, yeye pamoja na mke wake na vyote alivyokuwa navyo.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kwa hiyo Abram akaondoka akatoka Misri na akaenda Negebu, Yeye, mke wake, na vyote alivyokuwa navyo. Lutu pia akaenda pamoja naye.
\v 2 Na sasa Abram alikuwa tajiri wa mifugo, fedha na dhahabu.
\s5
\v 3 Aliendelea na safari yake kutoka Negebu hadi Betheli, mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo, kati ya Betheli na mji wa Ai.
\v 4 Akaenda mahali ambapo madhabahu ilikuwa imejengwa mwanzoni. Hapa akaliitia jina la Yahwe.
\s5
\v 5 aliyekuwa anasafiri na Abram, alikuwa pia na ngo'mbe, makundi ya mifugo, na mahema.
\v 6 Nchi haikuwatosha wote kukaa pamoja karibu kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana, kiasi kwamba hawakuweza kukaa pamoja.
\v 7 Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo.
\s5
\v 8 Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, "Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia.
\v 9 Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge na mi. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia. au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto."
\s5
\v 10 Kwa hiyo Lutu akatazama, na akaona kuwa nchi yote tambarare ya Yorodani ilikuwa na maji kila mahali hadi Zoari, kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri. Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora.
\v 11 Kwa hiyo Lutu akajichagulia yeye mwenyewe nchi tambarare ya Yorodani na akasafiri mashariki, na ndugu hawa wakatengana wao kwa wao.
\s5
\v 12 Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma.
\v 13 Na sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu na wenye dhambi nyingi dhidi ya Yahwe.
\s5
\v 14 Yahwe akamwambia Abram baada ya Lutu kuondoka kwake, "Angalia kuanzia mahali ulipo simama hadi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi.
\v 15 Nchi yote hii uionayo, nitakupatia wewe pamoja na uzao wako milele.
\s5
\v 16 Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama mavumbi ya nchi, kiasi kwamba kama kuna mtu anaweza kuhesabu mavumbi ya nchi, ndipo na uzao wako pia utahesabika.
\v 17 Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia."
\v 18 Kwa hiyo Abram akachukua hema yake, akaja na kukaa katika mwaloni wa Mamre, ambao uko Hebroni, na pale akajenga Madhabahu ya Yahwe.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Ikiwa katika siku za Amrafeli, mfalme wa shinari, Arioko, mfalme wa Elasari, Kedorlaoma, mfalme wa Elam na Tidali, mfalme wa Goimu,
\v 2 walifanya vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha, mfalme wa Gomora, Shinabu, mfalme wa Adma, Shemeberi, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela(pia ikiitwa Soari).
\s5
\v 3 Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja katika bonde la Sidim (pia likiitwa bahari ya chumvi).
\v 4 Kwa miaka kumi na mbili walimtumikia Kedorlaoma, lakini katika mwaka wa kumi na tatu waliasi.
\v 5 Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu,
\v 6 na Wahori katika mlima wao wa Seiri, mpaka El Parani iliyo karibu na jangwa.
\s5
\v 7 Kisha wakarudi wakaja En Misifati (Pia ikiitwa Kadeshi), na kuishinda nchi yote ya Waamaleki, na pia Waamori ambao waliishi Hasasoni Tamari.
\v 8 Kisha mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari) walikwenda na kuandaa vita
\v 9 dhidi ya Kadorlaoma, mfalme wa Elam, Tidali mfalme wa Goim, Amrafeli, mfalme wa Shinari, Arioki, mfalme wa Elasari; wafme wanne dhidi ya wale watano.
\s5
\v 10 Na sasa bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, na wafalme wa Sodoma na Gomora walipokimbia, wakaanguka pale. Wale waliosalia wakakimbilia milimani.
\v 11 Kwa hiyo adui akachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, na wakaenda zao,
\v 12 walipoondoka, wakamchukua pia Lutu, mtoto wa ndugu yake na Abram ambaye aliishi Sodoma, pamoja na mali zake zote.
\s5
\v 13 Mmoja ambaye alitoroka alikuja na kumwambia Abram mwebrania. Alikuwa anaishi katika mialoni ya Mamre, mwamori ambaye alikuwa ni ndugu wa Eshkoli na Aneri ambao walikuwa washirika wa Abram.
\v 14 Abram aliposikia kuwa maadui wamemteka ndugu yake, akawaongoza wanaume waliofunzwa na kuzaliwa nyumbani mwake 318 na akawaongoza hadi Dani.
\s5
\v 15 Akawagawanya watu wake dhidi yao usiku na kuwavamia, na kuwafukuza mpaka Hoba, ambayo iko kaskazini mwa Dameski.
\v 16 Kisha akarudisha mali zote, pia akamrudisha ndugu yake Lutu na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.
\s5
\v 17 Baada ya Abram kurudi kutoka kumpiga Kadorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja nae, mfalme wa Sodoma akatoka kuonana nae katika bonde la Shawe (pia iliitwa bonde la mfalme).
\v 18 Melkizedeki, mfalme wa Salem, akaleta mkate na divai. Alikuwa ni kuhani wa Mungu aliye juu sana.
\s5
\v 19 Alimbariki akisema, "Abarikiwea Abram na Mungu aliye juu sana, muumba wa mbingu na nchi.
\v 20 Abarikiwe Mungu aliye juu sana, ambaye amekupatia adui zako katika mikono yako." Kisha Abram akampatia sehemu ya kumi ya kila kitu.
\s5
\v 21 Mfalme wa Sodama akamwambia Abram, "Nipatie watu, na ujichukulie wewe mwenyewe mali."
\v 22 Abram akamwambia mfalme wa Sodoma, "Nimeinua juu mkono wangu kwa Yahwe, Mungu aliye juu sana, muumbaji wa mbingu na nchi,
\v 23 kwamba sitachukua uzi wala gidamu ya kiatu, au kitu chochote ambacho ni chako, 'ili kwamba usiseme, nimemfanya Abram kuwa tajiri.'
\v 24 Sitachukua chochote isipokuwa kile ambacho vijana wamekula na sehemu za watu waliokwenda nami. Aneri, Eskoli, na Mamre na wachukue sehemu zao."
\s5
\c 15
\p
\v 1 Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, "Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana."
\v 2 Abram akasema, "Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?"
\v 3 Abram akasema, "Kwakuwa hujanipatia uzao, tazama, mwangalizi wa nyumba yangu ndiye mrithi wangu."
\s5
\v 4 Kisha, tazama, neno la Yahwe likaja kwake, kusema, "Mtu huyu hatakuwa mrithi wako; isipokuwa atakaye toka katika mwili wako ndiye atakuwa mrithi wako."
\v 5 Kisha akamtoa nje, na akasema, Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu." Kisha akamwambia, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.
\s5
\v 6 Akamwamini Yahwe, na akamuhesabia jambo hili kuwa mwenye haki.
\v 7 Akamwambia, Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi."
\v 8 Akasema, "Bwana Yahwe, nitajua je kuwa nitairithi?"
\s5
\v 9 Kisha akamwambia, "Nipatie ndama wa umri wa miaka mitatu, mbuzi mke wa umri wa miaka mitatu, na kondoo mume wa umri wa miaka mitatu, na njiwa na mwana njiwa."
\v 10 Akamletea hivi vyote, akavipasua katika sehemu mbili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuawapasua.
\v 11 Wakati ndege walipokuja juu ya mizoga, Abram akawafukuza.
\s5
\v 12 Kisha wakati jua lilipokuwa likizama, Abram akalala usingizi mzito na tazama, hofu ya giza kuu ikamfunika.
\v 13 Kisha Yahwe akamwambia Abram, "Ujuwe kwa hakika kwamba uzao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo si ya kwao, na watatumikishwa na kuteswa kwa miaka mia nne.
\s5
\v 14 Nitahukumu taifa ambalo watalitumikia, na baadye watatoka wakiwa na mali nyingi.
\v 15 Lakini utakwenda kwa baba zako kwa amani, na utazikwa katika uzee mwema.
\v 16 Katika kizazi cha nne watakuja tena hapa, kwa sababu uovu wa Waamori haujafikia mwisho wake."
\s5
\v 17 Jua lilipokuwa limezama na kuwa giza, tazama, chungu cha moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande.
\v 18 Siku hiyo Yahwe akafanya agano na Abram, akisema, "Ninatoa nchi hii kwa uzao wako, kutoka mto wa Misri hadi kwenye mto mkuu, Frati -
\v 19 Mkeni, Mkenizi, na Mkadmoni,
\v 20 Mhiti, Mperizi, Mrefai,
\v 21 Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri.
\v 2 Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, "Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye." Abram akasikiliza sauti ya Sarai.
\v 3 Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake.
\v 4 Kwa hiyo akawa na mahusiano na Hajiri, na akabeba mimba. Na alipoona kuwa amebeba mimba, akamdharau bibi yake.
\s5
\v 5 Kisha Sarai akamwambia Abram, "Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe."
\v 6 Lakini Abram akamwambia Sarai, "Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake." Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.
\s5
\v 7 Malaika wa Yahwe akamkuta karibu na chemichemi ya maji katika jangwa, chemichemi iliyo katika njia kuelekea Shuri.
\v 8 Akasema, Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?" Na akasema, ninamtoroka bibi yangu Sarai."
\s5
\v 9 Malaika wa Yahwe akamwambia, " Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake."
\v 10 Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, "Nitazidisha uzao wako maradufu, kiasi kwamba watakuwa wengi wasioweza kuhesabika."
\s5
\v 11 Malaika wa Yahwe pia akamwambia, " Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwasabab Yahwe amesikia mateso yako.
\v 12 Atakuwa punda mwitu wa mtu. Atakuwa adui dhidi ya kila mtu, na kila mtu atakuwa adui yake, na ataishi kando na ndugu zake wote."
\s5
\v 13 Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, "Wewe ni Mungu unionaye mimi," kwa kuwa alisema, "je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?"
\v 14 Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
\s5
\v 15 Hajiri akamzalia Abram mwana wa kiume, na Abram akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa jina, Ishmaeli.
\v 16 Abram alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hajiri alipomzaa Ishmaeli kwa Abram.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, "Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu.
\v 2 Kisha nitalithibitisha agano langu kati yangu mimi na wewe, na nitakuzidisha sana.
\s5
\v 3 Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema,
\v 4 "Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi.
\v 5 Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi.
\v 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako.
\s5
\v 7 Nitaimarisha agao langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele, nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako.
\v 8 Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao."
\s5
\v 9 Kisha Mungu akamwambia Abraham, "nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao.
\v 10 Hili ndilo agano langu, ambalo utalishika, kati yangu na wewe na wazao wako baada yako: Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe.
\v 11 Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele, na hii itakuwa ishara ya agano kati yangu mimi na ninyi.
\s5
\v 12 Kila mwanaume wa kwenu aliye na umri wa siku nane lazima atahiriwe, katika vizazi ya watu wenu. Hii ni pamoja na yule azaliwaye katika nyumba yako na yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni yeyote ambaye si mmoja wa wazao wako.
\v 13 Mtu ambaye amezaliwa katika nyumba yako na yule aliye nunuliwa kwa fedha yako lazima atahiriwe. Hivyo agano langu litakuwa katika mwili wenu kuwa agano la milele.
\v 14 Mwanaume yeyote asiye tahiriwa katika mwili govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake. Amevunja agano langu."
\s5
\v 15 Mungu akamwambia Abraham, "kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara.
\v 16 Nitambariki, na nitakupatia mtoto wa kiume kwake. Nitambariki, na atakuwa mama wa mataifa. Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye.
\s5
\v 17 Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?"
\v 18 Abraham akamwambia Mungu, "Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!"
\s5
\v 19 Mungu akasema, Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake.
\v 20 Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na mbili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu.
\v 21 Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani."
\s5
\v 22 Alipo kuwa amemaliza kuzungumza naye, Mungu akaondoka kwa Abraham.
\v 23 Kisha Abraham akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote ambao walizaliwa katika nyumba yake, na wote ambao walinunuliwa kwa fedha yake, kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham, walitahiriwa mwili wa magovi ya ngozi ya mbele katika siku iyo hiyo, kama Mungu alivyo kuwa amesema.
\s5
\v 24 Abraham alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.
\v 25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.
\v 26 Siku ile ile ambayo wote wawili Abraham na Ishmael mwanawe walipotahiriwa, ndipo
\v 27 wanaume wote wa nyumba yake walitahiriwa pia, hawa ni pamoja na wale waliozaliwa katika nyumba ile na wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Yahwe alimtokea Abraham katika Mialoni ya Mamre, alipokua ameketi mlangoni pa hema wakati wa jua.
\v 2 Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama mbele yake. Alipo waona, alikimbia kupitia mlango wa hema kuwalaki na kuinama chini hadi ardhini.
\s5
\v 3 Akasema, "Bwana, kama nimepata upendelea machoni pako, nakuomba usinipite na kuniacha mtumishi wako.
\v 4 Naomba maji kidogo yaletwe, mnawe miguu yenu, na mjipumzishe chini ya mti.
\v 5 Nami acha nilete chakula kidogo, ili kwamba mjiburudishe wenyewe. Ndipo baadae mwaweza kwenda zenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu." Nao wakasema, "Fanya kama ulivyo sema."
\s5
\v 6 Kisha Abraham akaenda upesi hemani kwa Sara, na akasema, "Harakisha, chukua vipimo vitatu vya unga safi, uukande, na fanya mkate."
\v 7 Kisha Abraham akakimbia kundini, akachukua ndama wa ng'ombe aliye laini na mzuri, na akampatia mtumishi na kwa haraka akamwandaa.
\v 8 Akatwaa siagi na maziwa na ndama aliye kwisha andaliwa, na akaweka chakula mbele yao, naye akasimama karibu nao chini ya mti wakati wanakula.
\s5
\v 9 Wakamwambia, "Mke wako Sara yuko wapi?" akajibu. "pale hemani."
\v 10 akasema, "Hakika nitarejea kwako majira ya machipuko, na tazama Sara mkeo atakuwa na mtoto wa kiume." Sara alikuwa akisikiliza mlangoni pa hema iliyokuwa nyuma yake.
\s5
\v 11 Abraham na Sara walikuwa wazee, umri wao ulikuwa umeendelea sana, na Sara alikuwa amepita umri ambao mwanamke anaweza kuzaa watoto.
\v 12 Kwa hiyo Sara akajicheka mwenyewe, akijisemesha mwenyewe, "baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je ni tapata furaha hii?"
\s5
\v 13 Yahwe akamwambia Abraham, "Kwa nini Sara amecheka na kusema, Je ni kweli nitazaa mtoto, nikiwa mzee'?
\v 14 Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani Sara atakuwa na mtoto wa kiume."
\v 15 Kisha Sara akakataa na kusema, "sikucheka," kwa kuwa aliogopa. Yahwe akasema, "hapana ulicheka."
\s5
\v 16 Kisha wale wanaume walisimama kuondoka na wakatazama chini kuelekea Sodoma. Abraham akafuatana nao kuona njia yao.
\v 17 Lakini Yahwe akasema, Je ni mfiche Abraham kile ninacho kusudia kufanya,
\v 18 Ikiwa kwa hakika Abraham atakuwa mkuu na taifa lenye nguvu, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
\v 19 Kwa kuwa nimemchagua ili awaelekeze wanawe na nyumba yake baada yake waishike njia ya Yahwe, watende utakatifu na haki, ili kwamba Yahwe ampatie Abraham yale aliyo yasema kwake."
\s5
\v 20 Kisha Yahwe akasema, "Kwa sababu kilio cha Sodoma na Gomora ni kikuu, na kwa kuwa dhambi yao ni kubwa,
\v 21 sasa nitashuka pale na kuona kilio kilicho nifikia dhidi yake, ikiwa kweli wamefanya au hawakufanya, nitajua."
\s5
\v 22 Kwa hiyo wale wanaume wakageuka toka pale, na kuelekea Sodoma, lakini Abraham akabaki amesimama mbele ya Yahwe.
\v 23 Kisha Abraham alikaribia na kusema, "Je utawafutilia mbali watakatifu pamoja na waovu?
\s5
\v 24 Huenda wakawepo wenye haki hamsini katika mji. Je utawakatilia mbali na usiuache mji kwa ajili ya hao watakatifu hamsini walioko hapo?
\v 25 Hasha usifanye hivyo, kuwauwa watakatifu pamoja na waovu, ili kwamba watakatifu watendewe sawa na waovu. Hasha! Je muhukumu wa ulimwengu wote hatatenda haki?"
\v 26 Yahwe akasema, "Katika Sodoma nikipata watakatifu hamsini kwenye mji, nita uacha mji wote kwa ajili ya hao."
\s5
\v 27 Abraham akajibu na kusema, "Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu, hata kama mimi ni mavumbi na majivu!
\v 28 Itakuwaje ikiwa kuna watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini? Je utaangamiza mji wote kwa upungufu wa hao watano?" Akasema, "Sitaangamiza, ikiwa nitapata watu arobaini na watano pale."
\s5
\v 29 Akaongea naye tena, na kusema, "Itakuwaje ikiwa arobaini watapatikana pale?" Akajibu, "Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini."
\v 30 Akasema, Tafadhali usikasirike, Bwana, nikiongea. Pengine thelathini watapatikana pale." Akajibu, 'Sitafanya, ikiwa nitapata thelathini pale."
\v 31 Akasema, Tazama, Nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale." Akajibu, "Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini."
\s5
\v 32 Akasema, "Tafadhali usikasirike, Bwana, na nitasema jambo hili kwa mara ya mwisho. Huenda kumi wakaonekana kule." Na akasema, sitaangamiza kwa ajili ya hao kumi."
\v 33 Yahwe akaendelea na njia yake mara tu baada ya kumaliza kuongea na Abraham, na Abraham akarudi nyumbani.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Malaika wawili wakaja Sodoma jioni, wakati ambao Lutu alikuwa amekaa langoni mwa Sodoma. Lutu akawaona, akainuka kuwalaki, na akainama uso wake chini ardhini.
\v 2 Akasema, Tafadhari Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke." Nao wakasema, "Hapana, usiku tutalala mjini."
\v 3 Lakini akawasihi sana, mwishowe wakaondoka pamoja nae, na wakaingia katika nyumba yake. Akaandaa chakula na kuoka mkate usiotiwa chachu, wakala.
\s5
\v 4 Lakini kabla hawaja lala, wanaume wa mji, wa Sodoma, vijana kwa wazee wakaizunguka nyumba, wanaume wote kutoka kila kona ya mji.
\v 5 Wakamwita Lutu, na kumwambia, "Wale wanaume walioingia kwako usiku wakowapi? watoe hapa nje waje kwetu, ili tuweze kulala nao."
\s5
\v 6 Lutu akatoka nje na akafunga mlango.
\v 7 Akasema, "Nawasihi, ndugu zangu, msitende uovu.
\v 8 Tazama, nina mabinti wawili ambao hawajawahi kulala na mwanaume yeyote. Nawaomba tafadhari niwalete kwenu, na muwafanyie lolote muonalo kuwa jema machoni penu. Msitende lolote kwa wanaume hawa, kwa kuwa wamekuja chini ya kivuli cha dari yangu."
\s5
\v 9 Wakasema, "Ondoka hapa!" Wakasema pia, huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni, na sasa amekuwa mwamuzi! Sasa tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao." Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango.
\s5
\v 10 Lakini wale wanaume wakamkamata Lutu na kumweka ndani na wakafunga mlango.
\v 11 Kisha wale wageni wa Lutu wakawapiga kwa upofu wale wanaume waliokuwa nje ya nyumba, vijana na wazee kwa pamoja, kiasi kwamba wakachoka wakati wakiutafuta mlango.
\s5
\v 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je una mtu mwingine yeyote hapa? wakwe zako, wanao na mabinti zako, na yeyote mwingine katika huu mji, ukawatoe hapa.
\v 13 Kwa kuwa tunakaribia kuiangamiza sehemu hii, kwa sababu mashitaka dhidi yake mbele ya Yahwe yamezidi kiasi kwamba ametutuma kuuangamiza."
\s5
\v 14 Lutu akatoka na akazungumza na wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake, akawambia, "Ondokeni upesi mahali hapa, kwa kuwa Yahwe anakaribia kuuangamiza mji." Lakini kwa wakwe zake alionekana kuwa anawatania.
\v 15 Alfajiri, malaika wakamsihi Lutu, wakisema, ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili ambao wako hapa, ili kwamba usipotelee katika adhabu ya mji huu."
\s5
\v 16 Lakini akakawia-kawia. Kwa hiyo watu wale wakamshika mkono wake, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa sababu Yahwe alimhurumia. Wakawatoa nje, na kuwaweka nje ya mji.
\v 17 Wakisha kuwatoa nje mmoja wa wale watu akasema, "jiponye nafsi yako! usitazame nyuma, au usikae mahali popote kwenye hili bonde. Toroka uende milimani ili kwamba usije ukatoweshwa mbali."
\s5
\v 18 Lutu akawambia, "Hapana, tafadhali bwana zangu!
\v 19 Mtumishi wenu amepata kibali machoni pako, na umenionesha wema ulio mkuu kwa kuokoa maisha yangu, lakini sitaweza kutorokea milimani, kwa sababu mabaya yataniwahi na nitakufa.
\v 20 Tazama, ule mji pale uko karibu nijisalimishe pale, na ni mdogo. Tafadhari niacheni nikimbilie pale ( Je Siyo mdogo ule?), na maisha yangu yataokolewa."
\s5
\v 21 Akamwambia, "Sawa, nimekubali ombi hili pia, kwamba sitaangamiza mji ambaoumeutaja.
\v 22 Harakisha! toroka uende pale, kwa kuwa sitafanya chochote mpaka ufike pale." kwa hiyo mji ule ukaitwa Soari.
\s5
\v 23 Jua lilikuwa limekwisha chomoza juu ya nchi wakati Lutu alipofika Soari.
\v 24 Kisha Yahwe akanyesha juu ya Sodoma na Gomora kiberiti na moto toka kwa Yahwe mbinguni.
\v 25 Akaharibu miji ile, na bonde lote, na vyote vilivyomo katika miji, na mimea iliyo chipua juu ya ardhi.
\s5
\v 26 Lakini mke wa Lutu aliye kuwa nyuma yake, akatazama nyuma, na akawa nguzo ya chumvi.
\v 27 Abraham akaamuka asubuhi na mapema akaenda mahali alipokuwa amesimama mbele ya Yahwe.
\v 28 Akatazama chini kuelekea Sodoma na Gomora na kuelekea katika nchi yote bondeni. Akaona na tazama, moshi ulikuwauki ukienda juu kutoka chini kama moshi wa tanuru.
\s5
\v 29 Wakati Mungu alipoharibu miji ya bondeni, Mungu akamkumbuka Abraham. Akamtoa Lutu kutoka katika maangamizi alipoangamiza miji ambayo katika hiyo Lutu aliishi.
\s5
\v 30 Lakini Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima akiwa pamoja na binti zake wawili, kwa sababu aliogopa kuishi Soari. Kwa hiyo akaishi pangoni, yeye na binti zake wawili.
\s5
\v 31 Yule wa kwanza akamwambia yule mdogo, "Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanaume mahali popote wa kulala na sisi kulingana na desturi ya dunia yote.
\v 32 Njoo na tumnyweshe baba yetu mvinyo na tulale naye ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu."
\v 33 Kwa hiyo wakamnywesha baba yako mvinyo usiku ule. Kisha yule wa kwanza akaingia na akalala na baba yake; Baba yake hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka.
\s5
\v 34 Siku iliyo fuata yule wa kwanza akamwambia mdogowake, "Sikiliza, usiku wa jana nililala na baba yangu. Na tumnyweshe mvinyo usiku wa leo pia, na uingie ukalale naye. Ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu."
\v 35 Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule pia, na yule mdogo akaenda na akalala naye. Baba yake hakujua ni wakati gani alilala, wala wakati alipoamka.
\s5
\v 36 Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.
\v 37 Wa kwanza akazaa mwana wa kiume, na akamwita jina lake Moabu. Akawa ndiye baba wa wamoabu hata leo.
\v 38 Nayule mdogo naye akazaa mwana wa kiume, na akamwita Benami. Huyu ndiye baba wa watu wa Waamoni hata leo.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Abraham akasafiri kutoka pale hadi nchi ya Negebu, na akakaa kati ya Kadeshi na Shuri. Akawa mgeni akiishi Gerari.
\v 2 Abraham akasema kususu mkewe Sara, "ni dada yangu." Kwa hiyo Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wake kumchukua Sara.
\v 3 Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, "Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu."
\s5
\v 4 Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, "Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki?
\v 5 Je si yeye mwenyewe aliye niambia, 'Sara ni dada yangu?' Hata Sara mwenyewe alisema, 'ni kaka yangu.' Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia."
\s5
\v 6 Kisha Mungu akasema naye katika ndoto, "Kweli, ninajua pia kwamba umefanya hili katika uadilifu wa moyo wako, na pia nilikuzuia usitende dhambi dhidi yangu mimi. Ndiyo maana sikuruhusu umshike.
\v 7 Kwa hiyo, mrudishe huyo mke wa mtu, kwa kuwa ni nabii. Atakuombea, na utaishi. Lakini usipo mrudisha, ujuwe kwamba wewe pamoja na wote walio wa kwako mtakufa hakika.
\s5
\v 8 Abimeleki akaamka asubuhi na mapema akawaita watumishi wake wote waje kwake. Akawasimulia mambo haya yote, na watu wale wakaogopa sana.
\v 9 Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, "Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa."
\s5
\v 10 Abimeleki akamwambia Abraham, "Nini kilikushawishi wewe kutenda jambo hili?"
\v 11 Abraham akasema, "Ni kwasababu nilifikiri hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.'
\v 12 Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu.
\s5
\v 13 Wakati Mungu aliponiondoa katika nyumba ya baba yangu na kusafiri kutoka mahali kwenda mahali pengine, nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unioneshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, "Ni kaka yangu."'''
\v 14 Ndipo Abimeleki akatwaa kondoo, maksai, watumwa wa kiume na wa kike akampatia Abraham. Basi Abimeleki akamrudisha Sara, mke wa Abraham.
\s5
\v 15 Abimeleki akasema, Tazama, Nchi yangu i mbele yako. Kaa mahali utakapopendezewa."
\v 16 Na kwa Sara akasema, Tazama, nimempatia kaka yako vipande elfu vya fedha. Navyo ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe, na mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki."
\s5
\v 17 Kisha Abraham akaomba kwa Mungu, Na Mungu akamponya Abimeleki, mkewe, na watumwa wake wa kike kiasi kwamba wakaweza kupata watoto.
\v 18 Kwa kuwa Yahwe alikuwa amewafanya wanawake wote wa nyumaba ya Abimeleki kuwa tasa kabisa, kwa sababu ya Sara, mke wa Abraham.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yahwe akamsikiliza Sara kwa umakini kama alivyo kuwa amemwambia, Yahwe akamfanyia Sara kama alivyo kuwa amemwahidi.
\v 2 Sara akachukua mimba na akamzalia Abraham mtoto wa kiume katika uzee wake, katika muda ule ule ambao Mungu alikuwa amemwambia.
\v 3 Abraham akamwita jina mwanawe, ambaye alizaliwa kwake, na Sara, Isaka.
\v 4 Abraham akamtahiri mwanawe Isaka alipofikisha siku nane, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza.
\s5
\v 5 Abraham alikuwa na umri wa miaka mia moja wakati mwanawe Isaka anazaliwa kwake.
\v 6 Sara akasema, "Mungu amenifanya nicheke; kila mtu atakaye sikia atacheka pamoja na nami."
\v 7 Pia akasema, "Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto, na sasa kweli nimemzalia mtoto wakiume katika uzee wake!"
\s5
\v 8 Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya, na Abraham akafanya sherehe kubwa katika siku ambayo Isaka aliachishwa.
\v 9 Sara akamwona mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alikuwa amezaliwa kwa Abraham, akidhihaki.
\s5
\v 10 Kwa hiyo akamwambia Abraham, "Mfukuze huyu mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake: kwa kuwa mtoto huyu wa mwanamke mtumwa hawezi kuwa mrithi pamoja na mwanangu Isaka."
\v 11 Jambo hili likamuhuzunisha sana Abraham kwa sababu ya mwanawe.
\s5
\v 12 Lakini Mungu akamwambia Abraham, "Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako. Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili, kwa sababu itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa.
\v 13 Nitamfanya pia mtoto wa mjakazi kuwa taifa, kwa sababu ni uzao wako."
\s5
\v 14 Abraham akaamka asubuhi na mapema, akachukua mkate na kiriba cha maji, akampatia Hajiri, akiweka juu ya bega lake. Akamtoa kijana akampatia Hajiri na akawaondoa. Hajiri akaondoka akapotea katika jangwa la Beerisheba.
\v 15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba akamtelekeza kijana katika moja ya vichaka.
\v 16 Kisha akaondoka, na akakaa umbali kidogo na yule kijana, umbali kama wa kutupa mshale, kwa vile alisema, "Na nisitazame kifo cha mtoto." Alipokuwa amekaa kumkabili, akapaza sauti yake akalia.
\s5
\v 17 Mungu akasikia kilio cha kijana, na malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, "Nini kinakusumbua? Usiogope, kwa kuwa Mungu amesikia kilio cha kijana mahali alipo.
\v 18 Inuka msimamishe mtoto, na umtie moyo; kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa."
\s5
\v 19 Kisha Mungu akayafunua macho ya Hajiri, natazama akaona kisima cha maji. Akaenda akajaza kiriba maji, na akampatia kijana akanywa.
\v 20 Mungu akawa pamoja na kijana, na akakua. Akaishi jangwani akawa mwindaji.
\v 21 Akaishi katka jangwa la Parani, na mama yake akampatia mke kutoka Misri.
\s5
\v 22 Ikawa kwamba katika wakati ule Abimeleki na Fikoli kamanda wa jeshi lake akamwambia Abraham, akisema, "Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo.
\v 23 Sasa niapie kwa Mungu kwamba hutanifanyia baya, wala mwanangu, wala uzao wangu. Onesha kwangu na kwa nchi ambayo umekuwa ukikaa agano lile lile la uaminifu ambalo nimekuonesha wewe."
\v 24 Abraham akasema, "Nina apa."
\s5
\v 25 Abraham pia akamlalamikia Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya.
\v 26 Abimeleki akasema, "Sijui ni nani amefanya jambo hili. Hukuniambia mapema; na sijalisikia ila leo hii."
\v 27 Kwa hiyo Abraham akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki, na wawili hawa wakafanya agano.
\s5
\v 28 Kisha Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba pekeyao.
\v 29 Abimeleki akamwambia Abraham, "Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga pekeyao?"
\v 30 Akajibu, "Hawa wanakondoo wa kike saba utawapokea kutoka mkonono mwangu, ili kwamba uwe ushahidi kwangu, kuwa nichimba kisima hiki."
\s5
\v 31 Kwa hiyo akaita mahali pale Beerisheba, kwa sababu mahali pale wote wawili wali apa kiapo.
\v 32 Walifanya agano hapo Bersheba, kisha Abimeleki na Fikoli, amiri wa jeshi, wakarudi katika nchi ya Wafilisti.
\s5
\v 33 Abraham akapanda mti wa mkwaju katika Beerisheba. Na pale akamwabudu Yahwe, Mungu wa milele.
\v 34 Abraham akasalia kuwa mgeni katika nchi ya Wafilisti kwa siku nyingi.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, "Abraham!" Abraham akasema, "Mimi hapa."
\v 2 Kisha Mungu akasema, "Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia."
\v 3 Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia.
\s5
\v 4 Siku ya tatu Abraham akatazama juu na akaona mahali pakiwa mbali.
\v 5 Abraham akawambia vijana wake, "kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu."
\v 6 Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja.
\s5
\v 7 Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, "Baba yangu," naye akasema, " Ndiyo mwanangu." Akasema, "Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?"
\v 8 Abraham akasema, "Mungu mwenyewe atatupatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mwanangu." Kwa hiyo wakaendelea, wote wawili pamoja.
\s5
\v 9 Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
\v 10 Abraham akanyoosha mkono wake akachukua kisu ili kumuua mwanawe.
\s5
\v 11 Ndipo malaika wa Yahwe akamwita kutoka mbinguni na kusema, "Abraham, Abraham!" naye akasema, "Mimi hapa."
\v 12 Akasema, "usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru, kwa kuwa sasa najua unamcha Mungu, kwa kuona kuwa hukumzuilia mwanao, mwanao wa pekee, kwa ajili yangu."
\s5
\v 13 Abraham akatazama juu na tazama, nyuma yake kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani. Abraham akaenda akamchukua kondoo na akamtoa kama sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
\v 14 Kwa hiyo Abraham akapaita mahali pale, Yahwe atatoa," na panaitwa hivyo hata leo. "Juu ya mlima wa Yahwe itatolewa."
\s5
\v 15 Malaika wa Yahwe akamwita Abraham kwa mara ya pili kutoka mbinguni
\v 16 na kusema - Hiki ni kiapo cha Yahwe, "Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa kwamba kwa kuwa umefanya jambo hili, na hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
\v 17 hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao.
\s5
\v 18 Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa, kwa sababu umetii sauti yangu."
\v 19 Kwa hiyo Abraham akarejea kwa vijana wake, na wakaondoka wakaenda pamoja Beerisheba, hivyo akakaa Beerisheba.
\s5
\v 20 Ikawa kwamba baada ya mambo haya ambayo Abraham aliambiwa, "Milka amemzalia pia watoto, ndugu yako Nahori."
\v 21 Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu,
\v 22 Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu, na Bethueli.
\s5
\v 23 Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham.
\v 24 Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Sara akaishi mika mia moja na ishirini na saba. Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara.
\v 2 Sara akafa katika Kiriathi Arba, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abraham akaomboleza na kumlilia Sara.
\s5
\v 3 Kisha Abraham akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa, akanena na watoto wa kiume wa Hethi, akisema,
\v 4 "Mimi ni mgeni kati yenu. Tafadhari nipatieni mahali pa kuzikia miongoni mwenu, ili kwamba niweze kuzika wafu wangu."
\s5
\v 5 Wana wa Hethi wakamjibu Abraham, wakasema,
\v 6 "Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako."
\s5
\v 7 Abraham akainuka na kusujudu chini kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi.
\v 8 Akawaambia, akisema, "ikiwa mmekubali mimi kuzika wafu wangu, ndipo nisikilizeni, msihini Efroni mwana wa Sohari kwa ajili yangu.
\v 9 Mwambieni aniuzie pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake. Kwa bei kamili aniuzie waziwazi mbele ya watu kama miliki ya kuzikia."
\s5
\v 10 Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi, hivyo Efroni Mhiti akamjibu Abraham alipowasikia wana wa Hethi, wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake, akasema,
\v 11 "Hapana, bwana wangu, nisikilize. Ninakupatia shamba na pango ambalo limo ndani yake. Ninakupatia mbele ya wana wa watu wangu. Ninakupatia uzike wafu wako."
\s5
\v 12 Kisha Abraham akasujudu chini mbele ya watu wa nchi ile.
\v 13 Akamwambia Efroni watu wa nchi ile wakisikiliza, akasema, ikiwa uko radhi, tafadhari nisikilize. Nitalipia shamba. Chukua fedha kwangu, na nitazika wafu wangu pale."
\s5
\v 14 Efroni akamjibu Abraham, akisema,
\v 15 "Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako."
\v 16 Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.
\s5
\v 17 Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa
\v 18 kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake.
\s5
\v 19 Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani.
\v 20 Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Basi Abraham alikuwa mzee sana na Yahwe akawa amembariki katika mambo yote.
\v 2 Abraham akamwambia mtumwa wake, ambaye alikuwa mkubwa kuliko wote wa nyumbani mwake na mkuu wa vyote alivyo kuwa navyo."Weka mkono wako chini ya paja langu
\v 3 na nitakufanya uape kwa Yahwe, Mungu wa Mbingu na nchi, kwamba hutampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, miongoni mwao wale nikaao kati yao.
\v 4 Lakini utakwenda kwenye nchi yangu, na kwa ndugu zangu, na kumtafutia mwanangu Isaka mke."
\s5
\v 5 Yule mtumwa wake akamwambia, "Itakuwaje ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kufuatana nami hadi katika nchi hii? Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka?"
\v 6 Abraham akamwambia, "Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu kule!
\v 7 Yahwe, Mungu wa mbingu, ambaye alinitoa mimi kutoka katika nyumba ya baba yangu na kutoka katika nchi ya ndugu zangu, na ambaye aliniahidia kwa kiapo maalumu akisema, 'Nitawapa uzao wako nchi hii,' atatuma malaika wake mbele yako, na utapata mke kwa ajili ya mwanangu kutoka huko.
\s5
\v 8 Lakini ikiwa mwanamke hatakuwa tayari, ndipo utakuwa huru katika hiki kiapo changu. Cha muhimu tu ni kwamba usije ukamrudisha mwanangu huko."
\v 9 Kwa hiyo mtumwa akaweka mkono wake jini ya paja la Abraham bwana wake, na akaapa kuhusiana na jambo hili.
\s5
\v 10 Mtumwa akachukua ngamia kumi wa bwana wake na akaondoka. Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake. Akaondoka na kwenda katika mkoa wa Aramu Naharaimu, mji wa Nahori.
\v 11 Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji. Ilikuwa jioni wakati ambao wanawake huenda kuchota maji.
\s5
\v 12 Kisha akasema, "Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, anijalie kufanikiwa leo na aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abraham.
\v 13 Tazama, nimesimama hapa karibu na chemchemi ya maji na binti za watu wa mji wanakuja kuteka maji.
\v 14 Na itokee hivi kwamba. Nikimwambia msichana, tafadhari tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,' na akiniambia, 'Kunywa, na kwamba nitawanywesha ngamia wako pia,' huyo ndiye awe ambaye umemchagulia mtumwa wako Isaka. Kwa njia hii nitajua kuwa umeonesha agano la uaminifu kwa bwana wangu."
\s5
\v 15 Ikawa kwamba hata kabla hajamaliza kuzungumza, tazama, Rebeka akaja akiwa na mtungi wake wa maji begani mwake. Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abraham.
\v 16 Msichana huyu alikuwa mzuri na alikuwa bikira. Hapana mwanaume aliye kuwa amekwisha lala naye. Akashuka kisimani na kuujaza mtungi wake, na kupanda juu.
\s5
\v 17 Kisha mtumwa yule akakimbia kumlaki yule msichana, na kusema, "Tafadhari nipatie maji kidogo ya kunywa kutoka katika mtungi wako."
\v 18 Akasema, "kunywa tafadhari bwana wangu," na kwa haraka akatua mtungi wake juu ya mkono wake, na akampatia maji ya kunywa.
\s5
\v 19 Alipokuwa amemaliza kumpatia maji, akasema, "Nitachota maji kwa ajili ya ngamia wako pia, mpaka watakapomaliza kunywa."
\v 20 Hivyo akaharakisha akamwaga maji yaliyokuwa mtungini kwenye chombo cha kunywshea mifugo, kisha akakimbia tena kisimani kuchota maji, na kuwanywesha ngamia wake wote.
\s5
\v 21 Yule mtu akamtazama msichana akiwa kimya kuona kama Yahwe amefanikisha njia yake au la.
\v 22 Ngamia walipomaliza kunywa maji, yule mtu akaleta pete ya pua ya dhahabu yenye uzito wa nusu shekeli, na bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa shekeli kumi,
\v 23 akamuuliza, "wewe ni binti wa nani? Niambie tafadhali, Je kuna nafasi nyumbani mwa baba yako kwa ajili yetu kupumzika usiku?"
\s5
\v 24 Akamwambia, "Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, ambaye alimzaa kwa Nahori."
\v 25 Akasema pia, "Tunayo malisho tele na chakula, na iko nafasi kwa ajili yako kulala usiku."
\s5
\v 26 Kisha yume mtu akainama chini na kumwabudu Yahwe.
\v 27 Akasema, "Abarikiwe Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, ambaye hakuacha agano lake la uaminifu na kweli yake mbele ya bwana wangu. Kwa vile Yahwe ameniongoza moja kwa moja kwenye nyumba ya ndugu zake bwana wangu."
\s5
\v 28 Kisha yule msichana akakimbia na kwenda kuwaeleza watu wa nyumba ya mama yake juu ya mambo yote haya.
\v 29 Na sasa Rebeka alikuwa na kaka yake, jina lake aliitwa Labani. Labani akakimbia kwa yule mtu aliye kuwa nje barabarani karibu na kisima.
\v 30 Akisha kuona hereni ya puani pamoja na zile bangili kwenye mikono ya dada yake, na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, "Hivi ndivyo yule mtu alicho niambia," alikwenda kwa yule mtu, na, Tazama, alikuwa amesimama karibu na ngamia pale kisimani.
\s5
\v 31 Labani akasema, "Njoo, wewe uliye barikiwa na Yahwe. Kwa nini umesimama nje? nimekwisha andaa nyumba, pamoja na mahali kwa ajili ya ngamia."
\v 32 Kwa hiyo yule mtu akaingia ndani ya nyumba na akashusha mizigo kutoka kwa wale ngamia. Ngamia wakapatiwa malisho na chakula, na maji yakatolewa kuosha miguu yake pamoja na miguu ya wale watu aliokuwa pamoja nao.
\s5
\v 33 Wakaandaa chakula mbele yake ale, lakini akasema, "Sitakula mpaka niseme kile ninacho paswa kusema." Kwa hiyo Labani akmwambia, "Sema."
\v 34 Akasema, "Mimi ni mtumwa wa Abraham.
\v 35 Yahwe amembariki sana bwana wangu na amekuwa mtu mkuu. Amempatia mifugo na makundi ya wanyama, fedha, dhahabu, watumwa wa kiume na watumwa wa kike, pamoja na ngamia na punda.
\s5
\v 36 Sara, mke wa bwana wangu, alimzalia mwana bwana wangu alipokuwa mzee, na amempatia mwanawe kila kitu anachomiliki.
\v 37 Bwana wangu aliniapisha, akisema, "Usije ukampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, ambao kwao nimefanya makazi.
\v 38 Badala yake, lazima uende kwa familia ya baba yangu, na kwa ndugu zangu, na kupata mke kwa ajili ya mwanangu.'
\s5
\v 39 Nikamwambia bwana wangu, pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami.'
\v 40 Lakini akaniambia, Yahwe, ambaye ninakwenda mbele yake, atatuma malaika wake pamoja nawe na atakufanikisha njia yako, kwamba utapata mke kwa ajili ya mwangu kutoka miongoni mwa ndugu zangu na kutoka katika ukoo wa baba yangu.
\v 41 Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu.
\s5
\v 42 Hivyo nimefika leo kisimani, na nikasema, 'O Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, tafadhari, ikiwa kweli umekusudia kuifanya safari yangu kuwa yenye kufanikiwa -
\v 43 tazama niko hapa nimesimama karibu na kisima cha maji - na iwe kwamba binti ajaye kuchota maji, nitakaye mwambia, "Tafadhari unipatie maji kidoka kutoka kwenye mtungi wako ninywe," mwanamke atakaye niabia,
\v 44 "Kunywa, na nitakuchotea pia maji kwa ajili ya ngamia wako" - na awe ndiye ambaye wewe Yahwe, umemchagulia mtoto wa bwana wangu."
\s5
\v 45 Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, Tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, 'Tafadhari nipatie maji ninywe.'
\v 46 Ndipo kwa haraka alipoushusha mtungi wake begani mwake na akasema, 'Kunywa, na pia nitawapatia maji ngamia wak.' Kwa hiyo nikanywa, na akawanywesha ngamia pia.
\s5
\v 47 Nikamuuliza na kusema, 'Wewe ni binti wa nani?' Akasema, 'Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.' Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake.
\v 48 Kisha nikainama chini nikamwabudu Yahwe, na kumbariki Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, ambaye ameniongoza katika njia sahihi kumpata binti wa ndugu za bwana wangu kwa ajili ya mwanawe.
\s5
\v 49 Kwa hiyo, ikiwa mko tayari kumfanyia rehema na kweli, niambieni. Lakini kama sivyo, niambieni, ili kwamba niweze kwenda upande wa kulia, au kushoto."
\s5
\v 50 Ndipo Labani na Bethueli wakajibu na kusema, "Jambo hili limetoka kwa Yahwe; hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri.
\v 51 Tazama, Rebeka yu mbele yako. Mchukue na uende, ili awe mke wa mtoto wa bwana wako, kama Yahwe alivyosema."
\s5
\v 52 Mtumwa wa Abraham aliposikia maneno yao, akainama mwenyewe chini ardhini kwa Yahwe.
\v 53 Mtumwa akaleta vipande vya fedha na vipande vya dhahabu, na nguo, akampatia Rebeka. Akampatia pia kaka yake na mama yake zawadi zenye thamani.
\s5
\v 54 Kisha yeye na watu aliokuwa nao wakala na kunywa. wakakaa pale mpaka usiku, na walipoamka asubuhi, akasema, Niruhusuni niende kwa bwana wangu."
\v 55 Kaka yake na mama yake wakasema, mwache binti abaki nasi kwa siku chache zingine, angalau siku kumi. baada ya hapo anaweza kwenda."
\s5
\v 56 Lakini akawambia, msinizuie, kwa kuwa Yahwe amefanikisha njia yangu. Niruhusuni niende kwa bwana wangu."
\v 57 Wakasema, "Tutamwita binti na kumuuliza."
\v 58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, "Je utakwenda na mtu huyu?" Akajibu, "Nitakwenda."
\s5
\v 59 Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka, pamoja na watumishi wake wa kike, kwenda njiani pamoja na mtumishi wa Abraham na watu wake.
\v 60 Wakambarikia Rebeka, na wakamwambia, "Ndugu yetu, na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu, uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia."
\s5
\v 61 Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake kwa hesabu ya ngamia, na wakamfuata yule mtu. Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao.
\v 62 Nyakati hizo Isaka alikuwa anakaa katika Negebu, na alikuwa tu amerejea kutoka Beerlahairoi.
\s5
\v 63 Isaka akaenda kutafakari shambani jioni. Alipotazama akaona, natazama, kulikuwa na ngamia wakija!
\v 64 Rebeka akatazama na alipomwona Isaka, akaruka kutoka kwenye ngamia.
\v 65 Akamwambia mtumwa, "mtu huyo ni nani anaye tembea shambani akija kutupokea?" Mtumwa akasema, "Ni bwana wangu." Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.
\s5
\v 66 Mtumwa akamwambia Isaka mambo yote ambayo amefanya.
\v 67 Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Abraham akaoa mke mwingine; jina lake aliitwa Ketura.
\v 2 Akamzalia Zimrani, Jokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua.
\v 3 Jokshani akamzaa Sheba na Dedani. Wana wa Dedani walikuwa ni Waashuru, Waletushi, na Waleumi.
\v 4 Wana wa Midiani walikuwa ni Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Hawa wote walikuwa ni wana wa Ketura.
\s5
\v 5 Abraham akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo.
\v 6 Ingawaje, wakati alipokua angali akiishi, aliwapatia zawadi wana wa masuria wake na kuwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka, mwanae.
\s5
\v 7 Hizi ndizo zilikuwa siku za miaka ya uhai wake Abraham alizoishi, miaka 175.
\v 8 Abraham akapumua pumzi ya mwisho na akafa katika uzee mwema, mzee aliye shiba siku, na akakusanywa kwa watu wake.
\s5
\v 9 Isaka na Ishmaili, wanae wakamzika katika pango la Makipela, katika shamba la Efron mwana wa Soari Mhiti, pango lililokuwa karibu na Mamre.
\v 10 Shamba hili Abraham alilinunua kwa watoto wa Hethi. Abraham akazikwa pale pamoja na Sara mkewe.
\v 11 Baada ya kifo cha Abraham, Mungu akambariki Isaka mwanae, na Isaka akaishi karibu na Beerlalahairoi.
\s5
\v 12 Na sasa hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, mwana wa Abraham, ambaye Hajiri Mmisri mtumishi wake Sara, alizaa kwa Abraham.
\s5
\v 13 Haya ndiyo yalikuwa majina ya wana wa Ishimaeli, kuanzia mzaliwa wa kwanza: Nebayothi - mzaliwa wa kwanza wa Ishimaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,
\v 14 Mishma, Duma, Masa,
\v 15 Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi, na Kedema.
\v 16 Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao.
\s5
\v 17 Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137: akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa pamoja na watu wake.
\v 18 Walioshi toka Havila mpaka Shuri, ambayo iko karibu na Misri, kuelekea Ashuru. Waliishi kwa uadui kati yao.
\s5
\v 19 Haya ndiyo yalikuwa matukio kumuhusu Isaka, mwana wa Abraham: Abraham alimzaa Isaka.
\v 20 Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa ethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami.
\s5
\v 21 Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba.
\v 22 Watoto hawa walipokuwa tumboni mwake wakasumbuka, naye akasema, "Kwa nini jambo hili linatokea kwangu mimi?" Akaenda kumuuliza Yahwe kuhusu jambo hili.
\s5
\v 23 Yahwe akamwambia, "Mataifa mawili yako katika tumbo lako, na mataifa haya mawili yatatengana ndani yako. Taifa moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine, na yule mkubwa atamtumikia mdogo.
\s5
\v 24 Ulipo wadia wakati wa kujifungua, tazama, kulikuwa na mapacha ndani ya tumbo lake.
\v 25 Wakwanza akatoka akiwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.
\v 26 Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto.
\s5
\v 27 Vijana hawa wakakua, Hesau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema.
\v 28 Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo.
\s5
\v 29 Yakobo akapika mchuzi. Esau akaja kutoka nyikani, akiwa dhaifu kutokana na njaa.
\v 30 Esau akamwambia Yakobo, "Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhari, nimechoka!" Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu.
\s5
\v 31 Yakobo akasema, "Kwanza uniuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza."
\v 32 Esau akasema, "Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?"
\v 33 Yakobo akasema, "Kwanza uape kwangu mimi," kwa hiyo Esau akaapa kiapo na kwa njia hii akawa ameuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo.
\v 34 Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Basi njaa ikatokea katika nchi, mbali na njaa ya kwanza iliyotokea siku za Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisiti huko Gerari.
\s5
\v 2 Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, "Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia.
\v 3 Kaa katika nchi hii hii niliyokuambia, nami nitakuwa pamoja nawe na kukubariki; kwani kwako wewe na uzao wako, nitawapa nchi hii yote, nami nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.
\s5
\v 4 Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote. Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.
\v 5 Nitalifanya hili kwa sababu Ibrahimu aliitii sauti yangu na kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu."
\s5
\v 6 Hivyo Isaka akakaa Gerari.
\v 7 Watu wa eneo hilo walipomwuliza juu ya mke wake, alisema, "Yeye ni dada yangu." Aliogopa kusema, "Yeye ni mke wangu," kwa kuwa alidhani, "Watu wa nchi hii wataniua ili wamchukue Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa uso."
\v 8 Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, Ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake.
\s5
\v 9 Abimeleki akamwita Isaka kwake na kusema, "Tazama, kwa hakika yeye ni mke wako. Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?" Isaka akamwambia, "Kwa sababu nilidhani mtu mmoja aweza kuniua ili amchukue."
\v 10 Abimeleki akamwambia, "Ni jambo gani hili ulilotufanyia? Mmojawapo wa watu angeweza bila shaka kulala na mke wako, nawe ungeweza kuleta hatia juu yetu."
\v 11 Hivyo Abimeleki akawaonya watu wote na kusema, "Mtu yeyote atakayemgusa mtu huyu au mke wake atauwawa."
\s5
\v 12 Isaka akapanda mazao katika nchi hiyo na kuvuna mwaka huo vipimo mia, kwa kuwa Yahwe alimbariki.
\v 13 Mtu huyo akawa tajiri, naye akaongezeka zaidi hata akawa mkuu sana.
\v 14 Alikuwa na kondoo na ngombe na familia kubwa. Wafilisiti wakamwonea wivu.
\s5
\v 15 Basi visima vyote watumishi wa baba yake walikuwawamevichimba katika siku za Ibrahimu baba yake, Wafilisiti wakavikatalia kwa kwa kuvijaza kifusi.
\v 16 Abimeleki akamwambia Isaka, "Ondoka kati yetu, kwa kuwa wewe una nguvu kuliko sisi."
\v 17 Hivyo Isaka akaondoka pale na kukaa katika bonde la Gerari, na kuishi pale.
\s5
\v 18 Kwa mara nyingine tena Isaka akachimba visima vya maji, vilivyokuwa vimechimbwa siku za Ibrahimu baba yake. Wafilisiti walikuwa wamevizuia baada ya kufa kwake Ibrahimu. Isaka akaviita visima kwa majina aliyokuwa ameviita baba yake.
\s5
\v 19 Watumishi wa Isaka walipochimba katika bonde, wakaona kisima cha maji yaliyokuwakuwa yakibubujika.
\v 20 Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka, na kusema, "Haya ni maji yetu."Hivyo Isaka akakiita kisima hicho "Eseki," kwa sababu waligombana naye.
\s5
\v 21 Wakachimba kisima kingine, wakakigombania hicho nacho, hivyo akakiita "Sitina."
\v 22 Akatoka hapo na akachimba kisima kingine, lakini hicho hawakukigombania. Hivyo akakiita Rehobothi, na akasema, "Sasa Yahwe ametufanyia nafasi, na tutafanikiwa katika nchi."
\s5
\v 23 Kisha Isaka akaenda Beersheba.
\v 24 Yahwe akamtokea usiku huohuo na akasema, "Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi nipo pamoja nawe na nitakubariki na kuvidisha vizazi vyako, kwa ajili ya mtumishi wangu Ibrahimu."
\v 25 Isaka akajenga madhabahu pale na akaliita jina la Yahwe. Akapiga hema yake pale, na watumishi wake wakachimba kisima.
\s5
\v 26 Kisha Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi, rafiki yake, na Fikoli, jemedari wa jeshi.
\v 27 Isaka akawambia, "Kwa nini mmekuja kwangu, kwani mlinichukia na kunifukuza kwenu.
\s5
\v 28 Nao wakasema, "Tumeona yakini kwamba Yahwe amekuwa nawe. Hivyo tukaamua kwamba kuwe na kiapo kati yetu, ndiyo, kati yetu nawe. Hivyo na tufanye agano nawe,
\v 29 kwamba hautatudhuru, kama ambavyo sisi hatukukudhuru, na kama sisi tulivyokutendea vema wewe na tumekuacha uondoke kwa amani. Kwa kweli, Yahwe amekubariki."
\s5
\v 30 Hivyo Isaka akawaandalia sherehe, na wakala na kunywa.
\v 31 Wakaamuka mapema asubuhi na wakaapiana kiapo. Kisha Isaka akawaruhusu kuondoka, nao wakamwacha katika amani.
\s5
\v 32 Siku hiyohiyo watumishi wake wakaja na kumwambia juu ya kisima walichokuwa wamekichimba. Wakasema, "Tumeona maji."
\v 33 Akakiita kile kisima Shiba, hivyo jina la mji ule ni Beersheba hata leo.
\s5
\v 34 Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akajitwalia mke, Yudithi binti Beeri Mhiti, na Basemathi binti Eloni Mhiti.
\v 35 Wakamhuzunisha Isaka na Rebeka.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Isaka alipozeeka na macho yake kuwa mazito kiasi cha kutokuona, alimwita Esau, mwanawe mkubwa, na akamwambia, "Mwanangu. Yeye akasema, "Mimi hapa."
\v 2 Akamwambia, "Tazama, mimi nimezeeka. Sijui siku ya kufa kwangu.
\s5
\v 3 Kwahiyo chukua silaha zako, podo lako na upinde wako, na uende uwandani ukaniwindie mnyama.
\v 4 Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo, uniletee ili nikile na kukubariki kabla sijafa.
\s5
\v 5 Basi Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe. Esau akaenda uwandani kuwinda mawindo na kuja nayo.
\v 6 Rebeka akaongea na Yakobo mwanawe na kumwambia, "Tazama, nimemsikia baba yako akiongea na Esau ndugu yako. Akasema,
\v 7 'Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu.'
\s5
\v 8 Kwa hiyo sasa, mwanangu, usikilize sauti yangu kama ninavyokuagiza,
\v 9 Nenda kundini, na uniletee wanambuzi wawili; nami nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo.
\v 10 Utakipeleka kwa baba yako, ili kwamba akile, na kukubariki kabla hajafa."
\s5
\v 11 Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, "Tazama, Ndugu yangu Esau ni mtu mwenye manyoya, na mimi ni mtu laini.
\v 12 Pengine baba yangu atanigusa, nami nitaonekana kama mdanganyifu kwake. Nami nitajiletea laana badala ya baraka."
\s5
\v 13 Mama yake akamwambia, "Mwanangu, acha laana yoyote iwe juu yangu. Wewe sikiliza sauti yangu, nenda, uniletee."
\v 14 Hivyo Yakobo alikwenda na kuchukua wanambuzi na kuwaleta kwa mama yake, na mama yake akaandaa chakula kitamu, kama alichokipenda baba yake.
\s5
\v 15 Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau, mwanawe mkubwa, alizokuwa nazo nyumbani mwake, na akamvika Yakobo, mwanawe mdogo.
\v 16 Akamvalisha ngozi ya mwanambuzi katika mikono yake na katika sehemu laini za shingo yake.
\v 17 Akaweka katika mikono ya Yakobo kile chakula kitamu na mkate aliokuwa ameuandaa.
\s5
\v 18 Yakobo akaenda kwa baba yake na kumwambia, "Babangu." Yeye akasema, "Mimi hapa; U nani wewe, mwanangu?"
\v 19 Yakobo akamwambia baba yake, "Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza; nimefanya kama ulivyoniagiza. Basi kaa na ule sehemu ya mawindo yangu, ili unibariki."
\s5
\v 20 Isaka akamwambia mwanawe, "Imekuwaje umepata kwa haraka hivyo, mwanangu?" Akasema, "Ni kwa sababu Yahwe Mungu wako ameniletea."
\v 21 Isaka akamwambia Yakobo, "Njoo karibu nami, ili nikuguse, mwanangu, ili nijue kama kweli wewe ni mwanangu Esau au hapana."
\s5
\v 22 Yakobo akamkaribia Isaka baba yake; na Isaka akamgusa na kusema, "Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mkikono ya Esau."
\v 23 Isaka hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na manyoya, kama mikono ya Esau ndugu yake, hivyo Isaka akambariki."
\s5
\v 24 Akasema, "Wewe kweli ni mwanangu Esau?" Naye akasema, "Ni mimi."
\v 25 Isaka akasema, "Kilete chakula kwangu, na nile mawindo yako, ili nikubariki." Yakobo akakileta chakula kwake. Isaka akala, na Yakobo akamletea mvinyo, akanywa.
\s5
\v 26 Kisha Isaka baba yake akamwambia, "Sogea karibu nami na unibusu, mwanangu."
\v 27 Yakobo akasogea na kumbusu, naye akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki. Akasema, "Tazama, harufu ya mwanangu ni kama harufu ya shamba alilolibariki Yahwe.
\s5
\v 28 Mungu akupe sehemu ya umande wa mbinguni, sehemu ya unono wa nchi, na wingi wa nafaka na mvinyo mpya.
\s5
\v 29 Watu na wakutumikie na mataifa yainame chini yako. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wainame chini yako. Kila anayekulaani na alaaniwe; na kila anayekubariki abarikiwe."
\s5
\v 30 Mara Isaka alipomaliza kumbariki Yakobo, na Yakobo ndo ametoka mbele ya Isaka baba yake, Esau ndugu yake akaja kutoka kuwinda.
\v 31 Yeye pia akaandaa chakula kitamu na kukileta kwa baba yake. Akamwambia baba yake, "Baba, inuka na ule baadhi ya mawindo ya mwanao, ili uweze kunibariki."
\s5
\v 32 Isaka baba yake akamwambia, "U nani wewe? Akasema, "Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza."
\v 33 Isaka akatetemeka sana na kusema, "Alikuwa nani aliyewinda mawindo nakuniletea? Nilikula chote kabla haujaja, nami nimembariki. Atabarikiwa, kwa kweli."
\s5
\v 34 Esau aliposikia maneno ya baba yake, akalia kwa kilio kikubwa na cha uchungu sana, na akamwambia baba yake, "Unibariki nami, mimi pia, babangu."
\v 35 Isaka akasema, "Ndugu yako alikuja hapa kwa hila na amechukua baraka yako."
\s5
\v 36 Esau akasema, "Je hakuitwa Yakobo kwa haki? Kwa maana amenidanganya mara mbili hizi. Alichukua haki ya uzaliwa wangu wa kwanza, na tazama, sasa amechukua baraka yangu." Na akasema, "Je haukuniachia baraka?
\v 37 Isaka akajibu na kumwambia Esau, "Tazama, nimemfanya kuwa bwana wako, na nimempa ndugu zake kuwa watumishi wake. Na nimempa nafaka na divai. Je nikufanyie nini mwanangu?
\s5
\v 38 Esau akamwambia babaye, "Je hauna hata baraka moja kwa ajili yangu, babangu? Nibariki nami, hata mimi pia, babangu." Esau akalia kwa sauti.
\s5
\v 39 Isaka baba yake akajibu na kumwambia, "Tazama, mahali unapoishi patakuwa mbali na utajiri wa nchi, mbali na umande juu angani.
\v 40 Kwa upanga wako utaishi, nawe utamtumikia ndugu yako. lakini utakapoasi, utaiondoa nira yake shingoni mwako."
\s5
\v 41 Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka ambayo baba yake alimpa. Esau akajisemea moyoni, "Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia; baada ya hapo nitamwua Yakobo ndugu yangu."
\v 42 Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa. Hivyo akatuma na kumwita Yakobo mwanawe mdogo na kumwambia, "Tazama, Esau ndugu yako anajifariji juu yako kwa kupanga kukuuwa.
\s5
\v 43 Kwa hiyo sasa, mwanangu, unisikie na kukimbilia kwa Labani, ndugu yangu, huko Harani.
\v 44 Ukae naye kitambo, mpaka hasira ya ndugu yako itakapopungua,
\v 45 hata hasira ya ndugu yako itakapokuondokea, na kusahau ulivyomtenda. Kisha nitatuma na kukurudisha kutoka pale. Kwa nini niwapoteze ninyi nyote katika siku moja?
\s5
\v 46 Rebeka akamwambia Isaka, "Nimechoka na maisha kwa sababu ya hawa binti za Hethi. Ikiwa Yakobo atachukua mmojawapo wa binti wa Hethi kuwa mkewe, kama wanawake hawa, baadhi ya binti za nchi, maisha yatakuwa na maana gani kwangu?"
\s5
\c 28
\p
\v 1 Isaka akamwita Yakobo, akambariki, na kumwagiza, "Usichukuwe mwanamke katika wanawake wa Kikanaani.
\v 2 Inuka, nenda Padani Aramu, katika nyumba ya Bethueli baba wa mama yako, na uchukue mwanamke pale, mmojawapo wa binti za Labani, kaka wa mama yako.
\s5
\v 3 Mungu Mwenyezi na akubariki, akupe uzao na akuzidishe, hata uwe wingi wa watu.
\v 4 Na akupe baraka ya Ibrahimu, wewe, na uzao wako baada yako, kwamba uweze kumilki nchi ambapo umekuwa ukiishi, ambayo Mungu alimpa Ibrahimu."
\s5
\v 5 Hivyo Isaka akamwondoa Yakobo. Yakobo akaenda Padani Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, kaka wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
\s5
\v 6 Basi Esau alipoona kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padani Aramu, kuchukua mke kutoka pale. Lakini pia akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki na kumwagiza, akisema, "Usichukue mke katika wanawake wa Kanaani."
\v 7 Esau pia akaona kwamba Yakobo alikuwa amemtii baba yake na mama yake, na alikuwa amekwenda Padani Aramu.
\s5
\v 8 Esau akaona kwamba wanawake wa Kanaani hawakumpendeza Isaka baba yake.
\v 9 Hivyo akaenda kwa Ishmaeli, na kuchukua, mbali na wake aliokuwa nao, Mahalathi binti Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, dada wa Nebayothi, kuwa mke wake.
\s5
\v 10 Yakobo akatoka Beersheba na akaelekea Harani.
\v 11 Akaja mahali fulani na akakaa pale usiku kucha, kwa kuwa jua lilikuwa limekuchwa. Akachukua mojawapo ya mawe katika eneo hilo, akaliweka chini ya kichwa chake, na akalala usingizi katika eneo hilo.
\s5
\v 12 Akaota na kuona ngazi imewekwa juu ya nchi. Ncha yake ilifika hata mbinguni na malaika wa Mungu walikuwa wakishuka na kupanda juu yake.
\v 13 Tazama, Yahwe amesimama juu yake na kusema, "Mimi ni Yahwe, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi uliyolala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.
\s5
\v 14 Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya ardhi, na utaenea mbali kuelekea magharibi, mashariki, kaskazini, na kusini. Kupitia kwako na kupitia uzao wako familia zote za dunia zitabarikiwa.
\v 15 Tazama, mimi nipo nawe, na nitakulinda kila uendako, Nitakurudisha katika nchi hii tena; kwani sitakuacha. Nitafanya kila nililokuahidi."
\s5
\v 16 Yakobo akaamka katika usingizi, na akasema, "Hakika Yahwe yupo mahali hapa, sikujua hili."
\v 17 Akaogopa na kusema, "Eneo hili linatisha kama nini! Hili sio kingine zaidi ya nyumba ya Mungu. Hili ni lango la mbinguni."
\s5
\v 18 Yakobo akaamka mapema asubuhi na akachukua jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake. Akaliweka kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.
\v 19 Akapaita pale Betheli, lakini jina la kawaida la mji lilikuwa Luzu.
\s5
\v 20 Yakobo akatoa nadhiri, kusema, "Ikiwa Mungu atakuwa nami na atanilinda katika njia nipitayo, na atanipa mkate wa kula, na mavazi ya kuvaa,
\v 21 hata nikarudi salama katika nyumba ya baba yangu, ndipo Yahwe atakapokuwa Mungu wangu.
\v 22 Kisha jiwe hili nililoliweka kama nguzo litakuwa jiwe takatifu. Kutoka katika kila utakachonipa, kwa hakika nitakupa tena sehemu ya kumi."
\s5
\c 29
\p
\v 1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika katika nchi ya watu wa mashariki.
\v 2 Hata alipotazama, akaona kisima kondeni, na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake. Kwani kutoka katika hicho wangeyanywesha makundi, na jiwe juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa.
\v 3 Wakati makundi yote yangekusanyika pale, wachungaji wangevingirisha jiwe kutoka katika mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo, na kisha kurudisha jiwe juu ya mdomo wa kisima, mahali pake.
\s5
\v 4 Yakobo akawambia, "Ndugu zangu, ninyi mnatokea wapi?" nao wakasema, "Tunatoka Harani."
\v 5 Akawambia, "Mnamfahamu Labani mwana wa Nahori?" Wakasema, "Tunamfahamu."
\v 6 Akawambia, "Je hajambo?" Wakasema, "Hajambo, na, tazama pale, Raheli binti yake anakuja na kondoo."
\s5
\v 7 Yakobo akasema, "Tazama, ni mchana. Siyo wakati wa kukusanya kondoo pamoja. Mnapaswa kuwanywesha kondoo na kisha mkaenda na kuwaacha wachunge."
\v 8 Wakamwambia, "Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja. Ndipo wanaume watakapovingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na ndipo tutakapowanywesha kondoo."
\s5
\v 9 Wakati bado Yakobo anaongea nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa babaye, kwani alikuwa akiwachunga.
\v 10 Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake.
\s5
\v 11 Yakobo akambusu Raheli na akalia kwa sauti.
\v 12 Yakobo akamwambia Raheli kwamba alikuwa ni ndugu wa baba yake, na kwamba alikuwa mwana wa Rebeka. Kisha yeye akakimbia kumwambia baba yake.
\s5
\v 13 Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo mwana wa dada yake, akaenda kukutana naye, akamkumbatia, akambusu, na kumleta nyumbani kwake. Yakobo akamwambia Labani mambo haya yote.
\v 14 Labani akamwambia, "Kwa hakika wewe ni mfupa wangu na nyama yangu." Kisha Yakobo akakaa naye kama mwezi mmoja.
\s5
\v 15 Kisha Labani akamwambia Yakobo, "Je unitumikie bure kwa kuwa wewe ni ndugu yangu? Niambie, ujira wako utakuwaje?
\v 16 Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli.
\v 17 Macho ya Lea yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo na mwonekano.
\v 18 Yakobo alimpenda Raheli, hivyo akasema, "Nitakutumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, binti yako mdogo."
\s5
\v 19 Labani akasema, Itakuwa vema kukupa wewe, kuliko kumpa mtu mwingine. Kaa nami."
\v 20 Hivyo Yakobo akamtumikia kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli; nayo ilionekana kwake kama siku chache tu, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake.
\s5
\v 21 Kisha Yakobo akamwambia Labani, "Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia - ili kwamba nimwoe!
\v 22 Hivyo Labani akawaalika watu wa mahali hapo na kuandaa sherehe.
\s5
\v 23 Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye.
\v 24 Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa kuwa mjakazi wa Lea.
\v 25 Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, "Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa?
\s5
\v 26 Labani akamwambia, "Siyo utamaduni wetu kumtoa bindi mdogo kabla ya mzaliwa wa kwanza.
\v 27 Timiza juma la bibi arusi, na tutakupa yule mwingine pia kwa mbadala wa kunitumikia miaka mingine saba."
\s5
\v 28 Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.
\v 29 Lakini pia Labani akampa Raheli binti yake Bilha, kuwa mjakazi wake.
\v 30 Hivyo Yakobo akalala na Raheli, pia, lakini akampenda Raheli zaidi ya Lea. Hivyo Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka saba mingine.
\s5
\v 31 Yahwe akaona kwamba Lea hakupendwa, hivyo akalifungua tumbo lake, lakini Raheli hakuwa na mtoto.
\v 32 Lea akashika mimba na kuzaa mwana, naye akamwita Rubeni. Kwani alisema, "Kwa sababu Yahwe ameliangalia teso langu; bila shaka mme wangu sasa atanipenda."
\s5
\v 33 Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, "Kwa sababu Yahwe amesikia kwamba sipendwi, kwa hiyo amenipa mwana mwingine," na akamwita Simoni.
\v 34 Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, "Wakati huu mme wangu ataungana nami, kwa kuwa nimemzalia wana watatu." Kwa hiyo akaitwa Lawi.
\s5
\v 35 Akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, "Wakati huu nitamsifu Yahwe." Kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; kisha akaacha kuzaa watoto.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto, Raheli akamwonea wivu dada yake. Akamwambia Yakobo, "Nipe watoto, sivyo nitakufa."
\v 2 Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, "Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?
\s5
\v 3 Akasema, "Tazama, kuna mjakazi wangu Bilha. Lala naye, hivyo aweze kuzaa watoto magotini pangu, nami nitapata watoto kwake.
\v 4 Hivyo akampa Bilha mjakazi kama mke wake, na Yakobo akalala naye.
\s5
\v 5 Bilha akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana.
\v 6 Kisha Raheli akasema, "Mungu ameamua kwa faida yangu. Ameyasikiliza maombi yangu na kunipa mwana." Kwa sababu hiyo akamwita jina lake Dani
\s5
\v 7 Bilha, mjakazi wa Raheli, akashika mimba tena na kumzalia Yakobo mwana wa pili.
\v 8 Raheli akasema, "Kwa mashindano yenye nguvu nimeshindana na dada yangu na kushinda." Akamwita jina lake Naftali.
\s5
\v 9 Lea alipoona kwamba ameacha kuzaa, akamchukua Zilpa, mjakazi wake, na kumpa Yakobo kama mke wake.
\v 10 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.
\v 11 Lea akasema, "Hii ni bahati njema!" Hivyo akamwita jina lake Gadi.
\s5
\v 12 Kisha Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.
\v 13 Lea akasema, "Nina furaha! Kwa maana mabinti wataniita furaha." Hivyo akamwita jina lake Asheri.
\s5
\v 14 Siku za mavuno ya ngano Rubeni akaenda shambani na kuona tunguja. Akazileta kwa mama yake. Kisha Raheli akamwambia Lea, "Nipe baadhi ya tunguja za mwanao."
\v 15 Lea akamwambia, "Je ni jambo dogo kwako, kumchukua mme wangu? Je na sasa unataka kuchukua tunguja za mwanangu pia? Raheli akasema, "Kisha atalala nawe leo usiku, kwa kubadilishana na tunguja za mwanao.
\s5
\v 16 Jioni Yakobo akaja kutoka uwandani. Lea akaenda kumlaki na kusema, "Leo usiku utalala nami, kwani nimekuajiri kwa tunguja za mwanangu." Hivyo Yakobo akalala na Lea usiku huo.
\v 17 Mungu akamsikia Lea, na akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana wa tano.
\v 18 Lea akasema, "Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nilimpa mme wangu mjakazi wangu." Akamwita jina lake Isakari.
\s5
\v 19 Lea akashika mimba tena na kuzaa mwana wa tano kwa Yakobo.
\v 20 Lea akasema, "Mungu amenipa zawadi njema. Sasa mme wangu ataniheshimu, kwa sababu nimemzalia wana sita." Akamwita jina lake Zabuloni.
\v 21 Baadaye akazaa binti na kumwita jina lake Dina.
\s5
\v 22 Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza. Akampa kushika mimba.
\v 23 Akashika mimba na kuzaa mwana. Akasema, "Mungu ameiondoa aibu yangu."
\v 24 Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Yahwe ameniongeza mwana mwingine."
\s5
\v 25 Baada ya Raheli kumzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, "Niache niande, ili kwamba niende nyumbani kwetu na katika nchi yangu.
\v 26 Nipe wake zangu na watoto wangu niliokutumikia kwa ajili yao, na uniache niondoke, kwani unafahamu nilivyokutumikia.
\s5
\v 27 Labani akamwambia, "Ikiwa nimepata kibali machoni pako, subiri, kwa sababu nimejifunza kwa kutumia uaguzi kwamba Yahwe amenibariki kwa ajili yako."
\v 28 Kisha akasema, "Taja ujira wako, nami nitalipa."
\s5
\v 29 Yakobo akamwambia, "Unajua nilivyokutumikia, na jinsi ambavyo mifugo wako wamekuwa nami.
\v 30 Kwani walikuwa wachache kabla sijaja, na wameongezeka kwa wingi. Popote nilipokutumikia Mungu amekubariki. Je ni lini mimi nitaandaa kwa ajili ya nyumba yangu pia?"
\s5
\v 31 Hivyo Labani akasema, "Je nikulipe nini? Yakobo akasema, 'Usinipe chochote. Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu, nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza.
\v 32 Niache nipite kati ya kundi lako lote leo, kwa kuondoa kila kondoo mwenye milia na mabaka, na kila kondoo mweusi kati yao, na kati ya wenye mabaka na milia katika mbuzi. Hawa watakuwa ujira wangu.
\s5
\v 33 Uadilifu wangu utashuhudia kwa ajili yangu hapo baadaye, utakapokuja kuangalia ujira wangu. Kila ambaye hana milia na hana madoa miongoni mwa mbuzi, na mweusi kati ya kondoo, ikiwa wataonekana kwangu, watahesabiwa kuwa wameibwa."
\v 34 Labani akasema, "Nakubali. Na iwe kama yalivyo maneno yako."
\s5
\v 35 Siku hiyo Labani akaondoa mabeberu yaliyokuwa na milia na madoa, na majike ya mbuzi yaliyokuwa na milia na madoa, kila aliyekuwa mweupe, na weusi wote katika mbuzi, akawakabidhi katika mikono ya wanaye.
\v 36 Pia Labani akaweka safari ya siku tatu kati yake na Yakobo. Hivyo Yakobo akabaki kuchunga wale kondoo wa Labani waliosalia.
\s5
\v 37 Yakobo akachukua matawi mabichi yaliyokatwa ya mipopla, mlozi na mwaramoni mbichi akatoa maganda ili michilizi myeupe ionekane, na akaifanya sehemu nyeupe ya ndani ya mti iliyokuwa ndani ya fito ionekane.
\v 38 Kisha akaziweka fito alizokuwa amezibambua mbele ya makundi ya kondoo, mbele ya mabirika yakunyweshea walipokuja kunywa maji. Wakashika mimba walipokuja kunywa maji.
\s5
\v 39 Wanyama wakapandana mbele ya fito; nao wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa.
\v 40 Yakobo akawatenga hawa wanakondoo, lakini akawafanya waliosalia kuelekea wanyama wenye milia na kondoo weusi wote katika kundi la Labani. Kisha akayatenga makundi yake mwenyewe pekee na hakuwaweka pamoja na wale wa Labani.
\s5
\v 41 Pindi kondoo wenye nguvu katika kundi walipopandana, Yakobo alilaza fito katika mabirika ya maji mbele ya macho ya kundi, ili kwamba washike mimba kati ya fito.
\v 42 Lakini wakati waliodhaifu walipokuja, hakuweka fito mbele yao. Hivyo wanyama dhaifu wakawa wa Labani, na wenye nguvu wakawa wa Yakobo.
\s5
\v 43 Mtu huyo akastawi sana. Akawa na kundi kubwa la kondoo, wajakazi na wajoli, ngamia na punda.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, "Yakobo amechukuwa yote yaliyokuwa ya baba yetu, na ni kutoka katika mali ya baba yetu amepata utajiri wake."
\v 2 Yakobo akaona mwonekano katika uso wa Labani. Akaona kwamba nia yake imebadilika.
\v 3 Kisha Yahwe akamwambia Yakobo, "Rudi katika nchi ya baba zako na ya ndugu zako, nami nitakuwa nawe."
\s5
\v 4 Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwandani katika kundi lake la kondoo
\v 5 naye akawambia, "Naona nia ya baba yenu kwangu imebadilika, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa nami.
\v 6 Nanyi mnajua kwamba ni kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu.
\s5
\v 7 Baba yenu amenidanganya na amebadilisha ujira wangu mara kumi, lakini Mungu hakumruhusu kunidhuru.
\v 8 Ikiwa alisema, 'Wanyama wenye mabaka watakuwa ujira wako,' ndipo kondoo wote walipozaa watoto wenye mabaka. Na aliposema, wenye milia watakuwa ujira wako,' ndipo kundi lote lilipozaa watoto wenye milia.
\v 9 Kwa njia hii Mungu amemnyang'anya mifugo baba yenu na kunipa mimi.
\s5
\v 10 Wakati fulani wa majira ya kupandana, niliona katika ndoto mabeberu yaliyowapanda kundi. Mabeberu yalikuwa ya milia, mabaka na madoa.
\v 11 Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, 'Yakobo.' Nikasema, 'Mimi hapa.'
\s5
\v 12 Akasema, 'Inua macho yako uone mabeberu wanaolipanda kundi. Wana milia, madoa na na mabaka, kwani nimeona kila jambo Labani analokutendea.
\v 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, mahali ulipoitia nguzo mafuta, mahali uliponitolea nadhiri. Basi sasa inuka na uondoke katika nchi hii na kurudi katika nchi uliyozaliwa.
\s5
\v 14 Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, "Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu?
\v 15 Je hatutendei kama wageni? Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu.
\v 16 Mali zote ambazo sasa Mungu amemnyang'anya baba yetu ni zetu na watoto wetu. Sasa basi, lolote Mungu alilokuambia, fanya.
\s5
\v 17 Kisha Yakobo akainuka na kuwapandisha wanawe na wakeze kwenye ngamia.
\v 18 Akawaongoza mifugo wake wote mbele yake, pamoja na mali zake zote, wakiwemo wanyama aliowapata huko Padani Aramu. Kisha akaenda kuelekea kwa Isaka baba yake katika nchi ya Kanaani.
\s5
\v 19 Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake, Raheli akaiba miungu ya nyumba ya baba yake.
\v 20 Yakobo pia akamdanganya Labani Mwarami, kwa kutomtaarifu kwamba anaondoka.
\v 21 Hivyo akaondoka na vyote alivyokuwa navyo na kwa haraka akavuka mto, na akaenda kuelekea nchi ya vilima ya Gileadi.
\s5
\v 22 Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia.
\v 23 Hivyo akawachukua ndugu zake pamoja naye na kumfuatia kwa safari ya siku saba. Akampata katika nchi ya vilima ya Gileadi.
\s5
\v 24 Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku na kumwambia, "Ujiadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya."
\v 25 Labani akampata Yakobo. Basi Yakobo alikuwa amepiga hema yake katika nchi ya vilima. Labani pia akapiga kambi pamoja na ndugu zake katika nchi ya kilima ya Gileadi.
\s5
\v 26 Labani akamwambia Yakobo, "Umefanya nini, kwamba umewachukua binti zangu kama mateka wa vita?
\v 27 Kwa nini umekimbia kwa siri na kunihadaa kwa kutokuniambia? Ningekuruhusu uondoke kwa sherehe na kwa nyimbo, kwa matari na vinubi.
\v 28 Haukuniacha niwabusu wajukuu wangu na binti zangu kwa kuwaaga. Basi umefanya upumbavu.
\s5
\v 29 Iko katika uwezo wangu kukudhuru, lakini Mungu wa baba yako alisema nami usiku wa leo na kuniambia, 'Jiadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari.'
\v 30 Na sasa, umeondoka kwa sababu umeitamani sana nyumba ya baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?
\s5
\v 31 Yakobo akajibu na kumwambia Labani, "Ni kwa sababu niliogopa na kudhani kuwa ungeninyang'anya binti zako kwa nguvu ndiyo maana nikaondoka kwa siri.
\v 32 Yeyote aliyeiiba miungu yako hataendelea kuishi. Mbele ya ndugu zetu, onesha chochote kilichochako nilichonacho na uchukue." Kwa maana Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameviiba.
\s5
\v 33 Labani akaingia katika hema ya Yakobo, katika hema ya Lea, na katika hema za wale wajakazi wawili, lakini hakuviona. Akatoka katika hema ya Lea na kuingia katika hema ya Raheli.
\s5
\v 34 Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona.
\v 35 Akamwambia baba yake, "Usikasirike, bwana wangu, kwamba siwezi kusimama mbele yako, kwani nipo katika kipindi changu." Hivyo akatafuta lakini hakuiona miungu ya nyumbani mwake.
\s5
\v 36 Yakobo akakasirika na kuojiana na Labani. Akamwambia, "Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali?
\v 37 Kwa maana umechunguza mali zangu zote. Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako? Viweke hapa mbele ya ndugu zetu, ili waamue kati yetu wawili.
\s5
\v 38 Kwa miaka ishirini nimekuwa nawe. Kondoo wako na mbuzi wako hawakutoa mimba, wala sikula dume lolote la kondoo katika wanyama wako.
\v 39 Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea. Badala yake, nilichukua upotevu huo, kwamba wameibwa mchana au usiku.
\v 40 Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku; na sikupata usingizi.
\s5
\v 41 Miaka hii ishirini nimekuwa katika nyumba yako. Nilikufanyia kazi miaka kumi na nne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita kwa ajili ya wanyama wako. Umebadili ujira wangu mara kumi.
\v 42 Isipokuwa Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu, yule Isaka anayemwofu, amekuwa nami, bila shaka sasa ungenipeleka mikono mitupu. Mungu ameliona teso langu na jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii, na hivyo akakukemea usiku wa leo.
\s5
\v 43 Labani akajibu na kumwambia Yakobo, "Mabinti hawa ni mabinti zangu, wajukuu ni wajukuu wangu, na wanyama ni wanyama wangu. Yote uyaonayo ni yangu. Lakini nitafanya nini leo kwa hawa binti zangu, au kwa watoto wao waliowazaa?
\v 44 Hivyo sasa, na tufanye agano, wewe nami, na liwe shahidi kati yangu nawe."
\s5
\v 45 Hivyo Yakobo akachukua jiwe na kuliweka kama nguzo.
\v 46 Yakobo akawambia ndugu zake, "Kusanyeni mawe." Hivyo wakachukua mawe na kufanya rundo. Kisha wakala pale kati ya lile rundo.
\v 47 Labani aliliita Yega Saha Dutha, lakini Yakobo akaiita Galeedi
\s5
\v 48 Labani akasema, "Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo." Kwa hiyo jina lake likaitwa Galedi.
\v 49 Inaitwa pia Mispa, kwa sababu Labani alisema, "Yahwe na atuangalie mimi nawe, tunapokuwa hatuonani.
\v 50 Ikiwa utawatesa binti zangu, au ikiwa utachukua wanawake wengine mbali na binti zangu, japokuwa hakuna mwingine yupo nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati yangu nawe."
\s5
\v 51 Labani akamwambia Yakobo, Tazama rundo hili, na tazama nguzo, nililoliweka kati yako nami.
\v 52 Rundo hili ni shahidi, na nguzo ni shahidi, kwamba sitapita rundo hili kuja kwako, na kwamba wewe hautapita rundo hili kuja kwangu, kwa madhara.
\v 53 Mungu wa Ibrahimu, na mungu wa Nahori, miungu ya baba zao, waamue kati yetu."Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.
\s5
\v 54 Yakobo akatoa sadaka juu ya mlima na akawaita ndugu zake kula chakula. Walikula na kukaa usiku kucha juu ya mlima.
\v 55 Labani akaamka asubuhi na mapema, akawabusu wajuu zake na binti zake na kuwabariki. Kisha Labani akaondoka na kurudi kwake.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Yakobo pia akaendelea na safari yake, na malaika wa Mungu wakakutana naye.
\v 2 Yakobo alipowaona, akasema, "Hii ni kambi ya Mungu," hivyo akapaita mahali pale Mahanaimu.
\s5
\v 3 Yakobo akatuma wajumbe mbele yake waende kwa Esau ndugu yake katika nchi ya Seiri, katika eneo la Edomu.
\v 4 Aliwaagiza, kusema, "Hivi ndivyo mtakavyosema kwa bwana wangu Esau: Hivi ndivyo mtumishi wako Yakobo asemavyo: 'Nimekuwa nikikaa na Labani, naye amekawilisha kurudi kwangu hata sasa.
\v 5 Nina ng'ombe, punda, na kondoo, wajori na wajakazi. Nimetuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili kwamba nipate kibali mbele zako."
\s5
\v 6 Wajumbe wakarudi kwa Yakobo na kusema, "Tulikwenda kwa Esau ndugu yako. Anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye."
\v 7 Ndipo Yakobo alipoogopa sana na kutaabika. Hivyo akagawanya watu aliokuwa nao katika kambi mbili, na kondoo pia, mbuzi na ngamia.
\v 8 Akasema, "Ikiwa Esau ataishambulia kambi moja, ndipo kambi nyingine itakaposalimika."
\s5
\v 9 Yakobo akasema, "Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe, uliyeniambia, 'Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha,'
\v 10 Mimi sistahili matendo yako yote ya agano la uaminifu na ustahilifu wote uliomfanyia mtumishi wako. Kwa maana nilikuwa na fimbo tu nilipovuka mto huu wa Yordani, na sasa nimekuwa matuo mawili.
\s5
\v 11 Tafadhari niokoe kutoka katika mikono ya ndugu yangu, mikono ya Esau, kwa maana namwogopa, kwamba atakuja na kunishambulia mimi na wamama na watoto.
\v 12 Lakini ulisema, 'hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari, ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake."
\s5
\v 13 Yakobo akakaa pale usiku huo. Akachukua baadhi ya alivyokuwa navyo kama zawadi kwa Esau, ndugu yake:
\v 14 mbuzi majike mia mbili na mabeberu ishirini, kondoo majike mia mbili na madume ya kondoo ishirini,
\v 15 ngamia wakamwao thelathini na wana wao, ng'ombe madume arobaini na madume kumi ya ng'ombe, punda wa kike ishirini na madume yake ishirini.
\v 16 Akawaweka katika mikono ya watumishi wake, kila kundi peke yake. Akawambia watumishi, "Tangulieni mbele yangu na mwache nafasi kati ya makundi ya wanyama."
\s5
\v 17 Akamwagiza mtumishi wa kwanza, akisema, "Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, akasema, 'Ninyi ni wa nani? Mnakwenda wapi? Na wanyama hawa mbele yenu ni wa nani?
\v 18 Ndipo umwambie, 'Ni wa mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi wanaopelekwa kwa bwana wangu Esau. Na tazama, yeye pia anakuja nyuma yetu."
\s5
\v 19 Yakobo akatoa maelekezo kwa kundi la pili pia, la tatu, na watu wote walioyafuata makundi ya wanyama. Akasema, mseme vilevile kwa Esau mtakapokutana naye.
\v 20 Mnapaswa pia kusema, 'mtumwa wako Yakobo pia anakuja nyuma yetu." Kwani alifikiri, "nitamtuliza Esau kwa zawadi nilizozituma mbele yangu. Kisha baadaye, nitakapomwona, bila shaka atanipokea."
\v 21 Hivyo zawadi zikatangulia mbele yake. Yeye mwenyewe akakaa kambini usiku huo
\s5
\v 22 Yakobo akaamka wakati wa usiku, na akawachukua wakeze, wajakazi wake na wanaye kumi na wawili. Akawawavusha kijito cha Yaboki.
\v 23 Kwa njia hii akawapeleka kupitia chemichemi pamoja na mali yake yote.
\s5
\v 24 Yakobo akaachwa peke yake, na mtu akashindana naya mpaka alfajiri.
\v 25 Mtu yule alipoona kwamba hawezi kumshinda, akalipiga paja lake. Paja la Yakobo likatenguka alipokuwa akishindana naye.
\v 26 Yule mtu akasema, "Niache niende, kwani kunakucha." Yakobo akasema, sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki."
\s5
\v 27 Yule mtu akamwuliza, "Jina lako ni nani?" Yakobo akasema, "Yakobo." Yule mtu akasema,
\v 28 "Jina lako halitakuwa Yakobo tena, ila Israeli. Kwa kuwa umeshindana na Mungu na wanadamu na umeshinda."
\s5
\v 29 Yakobo akamwambia, "Tafadhari niambie jina lako." Akasema, "Kwa nini kuniuliza jina langu?" Kisha akambariki pale.
\v 30 Yakobo akapaita mahali pale Penieli kwani alisema, "Nimemwona Mungu uso kwa uso, na maisha yangu yamesalimika."
\s5
\v 31 Jua likatoka wakati Yakobo anaipita Penieli. Alikuwa akichechemea kwa sababu ya paja lake.
\v 32 Ndiyo maana wana wa Israeli hawali kano ya paja iliyopo katika nyonga ya paja, kwa sababu yule mtu aliziumiza hizo kano alipotegua paja la Yakobo.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Yakobo akainua macho yake na, tazama, Esau alikuwa anakuja, na alikuwa na watu mia nne pamoja naye. Yakobo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli, na wale wajakazi wawili.
\v 2 Kisha akawaweka wajakazi na wanao mbele, wakifuatiwa na Lea na watoto wake, Raheli na Yusufu wakafuata mwisho wa wote.
\v 3 Yeye mwenyewe akatangulia mbele yao. Akasujudu mara saba kuelekea ardhi, hata alipomkaribia ndugu yake.
\s5
\v 4 Esau akakimbia kumlaki, akamkumbatia, akakumbatia shingo yake na kumbusu. Kisha wakalia.
\v 5 Esau alipoinua macho, aliona wanawake na watoto. Akauliza, "Hawa watu pamoja nawe ni kinanani?" Yakobo akasema, Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema."
\s5
\v 6 Kisha wajakazi wakakaribia pamoja na watoto wao, nao wakasujudia.
\v 7 Akafuata Lea pia na watoto wake wakaja na kusujudia. Mwisho Yusufu na Raheli wakaja na kusujudia.
\v 8 Esau akasema, Unamaanisha nini kwa makundi haya yote niliyokutana nayo?" Yakobo akasema, "Kutafuta kibali mbele za bwana wangu.
\s5
\v 9 Esau akasema, "Ninayo ya kutosha, ndugu yangu. Tunza uliyonayo kwa ajili yako mwenyewe."
\v 10 Yakobo akasema, "Hapana, tafadhari, ikiwa nimeona kibali mbele zako, basi upokee zawadi yangu kutoka mkononi mwangu, na ni kama kuona uso wa Mungu, na umenipokea.
\v 11 Tafadhari pokea zawadi yangu uliyoletewa, kwa sababu Mungu amenitendea kwa neema, na kwa sababu ninavyo vya kutosha." Hivyo Yakobo akamsihi, na Esau akamkubali.
\s5
\v 12 Kisha Esau akasema, "Haya na tuondoke. Nitakutangulia."
\v 13 Yakobo akamwambia, "Bwana wangu anajua kwamba watoto ni wadogo, na kwamba kondoo na ng'ombe wananyonyesha ndama wao. Ikiwa watapelekwa kwa haraka hata siku moja, wanyama wote watakufa.
\v 14 Tafadhari bwana wangu na amtangulie mtumishi wake. Nitasafiri polopole, kwa kadili ya mifugo iliyo mbele yangu, na kadili ya watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri."
\s5
\v 15 Esau akasema, haya nikuachie baadhi ya watu wangu waliopamoja nami." Yakobo akasema, "Kwa nini kufanya hivyo? Bwana wangu amekuwa mkalimu kwangu kiasi cha kutosha."
\v 16 Hivyo Esau akaanza kurudi Seiri.
\v 17 Yakobo akasafiri kuelekea Sukothi, akajijengea nyumba, na akafanya mazizi kwa ajili ya mifugo wake. Hivyo jina la eneo linaitwa Sukothi.
\s5
\v 18 Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu, akafika salama katika mji wa Shekemu, uliyo katika nchi ya Kanaani. Akapiga kambi karibu na mji.
\v 19 Kisha akanunu sehemu ya ardhi alipokuwa ameweka hema yake kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia vya fedha.
\v 20 Akajenga madhabahu pale na kuiita El Elohe Israeli.
\s5
\c 34
\p
\v 1 Basi Dina, Binti wa Lea aliyemzalia Yakobo, akaenda kuwaona wasichana wa nchi.
\v 2 Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mwana mfalme wa nchi, akamwona na akamkamata kwa nguvu na kulala naye.
\v 3 Akavutiwa na Dina, binti Yakobo. Akampenda msichana na kuongea naye kwa upole.
\s5
\v 4 Shekemu akamwambia Hamori baba yeke, kusema, "Nipe msichana huyu kuwa mke wangu."
\v 5 Basi Yakobo akasikia kwamba alikuwa amemchafua Dina binti yake. Wanawe walikuwa pamoja na wanyama uwandani, hivyo Yakaobo akawangoja hata walipokuja.
\s5
\v 6 Hamori baba wa Shekemu akaenda kuongea na Yakobo.
\v 7 Wana wa Yakobo waliposikia neno hili wakaja kutoka uwandani. Watu hawa walichukizwa sana. Walikasirika sana kwa sababu alikuwa amemwaibisha Israeli kwa kumlazimisha binti wa Yakobo, kwa maana jambo kama hilo halikupasa kutendeka.
\s5
\v 8 Hamori akaongea nao, akisema, "Shekemu mwanangu anampenda binti yenu. Tafadhari mpeni kuwa mke wake.
\v 9 Mwoane nasi, tupeni binti zenu, na mjichukulie binti zetu kwa ajili yenu wenyewe.
\v 10 Mtaishi nasi, na nchi itakuwa wazi kwa ajili yenu kufanya biashara humo, na kupata mali."
\s5
\v 11 Shekemu akamwambia baba yake na ndugu zake, "Na nione kibari machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa.
\v 12 Niambieni kiasi kikubwa chochote cha mahari na zawadi kama mtakavyo, nami nitatoa chochote msemacho, lakini mnipe msichana kuwa mke wangu."
\v 13 Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila, kwa sababu Shekemu alikuwa amemnajisi Dina dada yao.
\s5
\v 14 Wakawambia, "Hatuwezi kufanya jambo hili, kumpa dada yetu mtu yeyote ambaye hajatailiwa; kwani hiyo ni aibu kwetu.
\v 15 Kwa sharti hili peke yake tutakubaliana nanyi: iwapo mtatailiwa kama sisi, ikiwa kila mtu mme miongoni mwenu atatailiwa.
\v 16 Ndipo tutakapowapa binti zetu, nasi tutachukua binti zenu kwetu sisi wenyewe, na tutaishi nanyi na kuwa wamoja.
\v 17 Lakini kama hamtusikilizi na kutailiwa, ndipo tutakapomchukua dada yetu na kuondoka.
\s5
\v 18 Maneno yao yakawafurahisha Hamori na Shekemu mwanaye.
\v 19 Kijana hakukawia kufanya walichokisema, kwa maana alipendezwa na binti Yakobo, na kwa sababu alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika nyumba ya babaye.
\s5
\v 20 Hamori na Shekemu mwanaye wakaenda katika lango la mji wao na kuongea na watu wa mji, kusema,
\v 21 "Watu hawa wanaamani nasi, hivyo na waishi katika nchi na kufanya biashara humo kwa maana, kweli, nchi ni kubwa ya kuwatosha. Haya na tuwachukue binti zao kuwa wake, nasi tuwape binti zetu.
\s5
\v 22 Kwa shariti hili pekee watu hawa wanakubali kuishi nasi na kuwa wamoja: ikiwa kila mwanamme miongoni mwetu atatailiwa, kama wao.
\v 23 Je wanyama wao na vitu vyao - wanyama wao wote kuwa wetu? Haya na tukubaliane nao, nao wataishi kati yetu."
\s5
\v 24 Watu wote wa mji wakamsikiliza Hamori na Shekemu, mwanaye. Kila mwanamme akatailiwa.
\v 25 Katika siku ya tatu, walipokuwa katika maumivu bado, wawili wa wana wa Yakobo (Simoni na Lawi, kaka zake Dina), wakachukua kila mmoja upanga wake na kuushambulia mji ambao ulikuwa na uhakika wa ulinzi wake, nao wakauwa wanamme wote.
\v 26 Wakamwua Hamori na Shekemu kwa makali ya upanga. Wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka.
\s5
\v 27 Wale wana wengine wa Yakobo wakaja kwa maiti na kuuteka nyara mji, kwa sababu watu wale walikuwa wamemnajisi dada yao.
\v 28 Wakachukua makundi yao ya kondoo, mbuzi, punda, na kila kitu ndani ya mji na viunga vyake
\v 29 utajiri wote. Watoto na wake zao wote, wakawachukua. Hata wakachukua kila kitu kilichokua katika nyumba.
\s5
\v 30 Yakobo akawambia Simoni na Lawi, "Mmeleta shida juu yangu, kunifanya ninuke kwa wenyeji wa nchi, Wakanaani na Waperizi. Mimi nina watu wachache. Ikiwa watajikusanya pamoja kinyume changu na kunishambulia."
\v 31 Lakini Simoni na Lawi wakasema, "Je Shekemu alipaswa kumtendea dada yetu kama kahaba?"
\s5
\c 35
\p
\v 1 Mungu akamwambia Yakobo, "Inuka, panda kwenda Betheli, na ukae pale. Unijengee madhabahu pale, niliyekutokea pale ulipomkimbia Esau kaka yako."
\v 2 Kisha Yakobo akawambia nyumba yake na wote aliokuwa nao, "Wekeni mbali miungu yote ya kigeni iliyo kati yenu, jitakaseni wenyewe, na kubadili mavazi yenu.
\v 3 Kisha tuondoke na kwenda Betheli. Nitajenga pale madhabahu kwa Mungu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, naye amekuwa pamoja nami kila nilikokwenda.
\s5
\v 4 Hivyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni iliyokuwa mikononi mwao, na heleni zilizokuwa katika masikio yao. Yakobo akazifukia chini ya mwaloni uliokuwa karibu na Shekemu.
\v 5 Kwa kadili walivyo safiri, Mungu akaifanya miji yote iliyokuwa karibu nao kuhofu, hivyo watu hao hawakuwafuatia wana wa Yakobo.
\s5
\v 6 Hivyo Yakobo akafika Luzu(ndiyo Betheli), ulioko katika nchi ya Kanaani, yeye na watu wote aliokuwa nao.
\v 7 Alijenge madhabahu na kuliita eneo hilo El Betheli, kwa sababu Mungu alikuwa amejifunua kwake, alipokuwa akimkimbia ndugu yake.
\v 8 Debora, mlezi wa Rebeka, akafa. Akazikwa chini kutoka Betheli chini ya mwaloni, hivyo ikaitwa Aloni Bakuthi.
\s5
\v 9 Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu, Mungu akamtokea tena na kumbariki.
\v 10 Mungu akamwambia, "Jina lako ni Yakobo, lakini jina lako halitakuwa Yakobo tena. Jina lako litakuwa Israeli." Hivyo Mungu akamwita jina lake Israeli.
\s5
\v 11 Mungu akamwambia, "Mimi ni Mungu Mwenyezi, Uwe mwenye kuzaa na kuongezeka. Taifa na wingi wa mataifa watakujia, na wafalme watatoka miongoni mwa uzao wako.
\v 12 Nchi ambayo nilimpa Ibrahimu na Isaka, nitakupa wewe. Nami nitaupa pia uzao wako baada yako nchi hii."
\v 13 Mungu akapanda kutoka mahali alipoongea naye.
\s5
\v 14 Yakobo akaweka nguzo katika eneo ambalo Mungu alikuwa ameongea naye, nguzo ya jiwe. Akamimina juu yake sadaka ya kinywaji na akamimina mafuta juu yake.
\v 15 Yakobo akaiita sehemu Mungu aliyoongea naye, Betheli
\s5
\v 16 Wakaendelea na safari kutoka Betheli. Walipokuwa kitambo kabla ya kufika Efrathi, Raheli akashikwa na uchungu.
\v 17 Akawa na utungu mzito. Alipokuwa katika utungu mzito zaidi, mkunga akamwambia, "Usiogope, kwani sasa utapata mtoto mwingine wa kiume."
\v 18 Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini.
\v 19 Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).
\v 20 Yakobo akaweka nguzo katika kaburi lake. Ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo.
\s5
\v 21 Israeli akaendelea na safari na akaweka hema yake kuvuka mnara wa walinzi wa kondoo.
\v 22 Yakobo alipokuwa akiishi katika nchi hiyo, Rubeni akalala na Bilha suria wa baba yake, na Israeli akasikia kuhusu hilo. Basi Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili.
\s5
\v 23 Wanawe kwa Lea walikuwa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zabuloni.
\v 24 Wanawe kwa Raheli walikuwa Yusufu na Benjamini.
\v 25 Wanawe kwa Bilha, mjakazi wa Raheli walikuwa Dani na Naftali.
\s5
\v 26 Wana wa Zilpa, mjakazi wa Lea, walikuwa Gadi na Asheri. Hawa wote walikuwa wana wa Yakobo waliozaliwa kwake huko Padani Aramu.
\v 27 Yakobo akaja kwa Isaka, baba yake, huko Mamre katika Kiriathi Arba (jina sawa na Hebroni), alipoishi Ibrahimu na Isaka.
\s5
\v 28 Isaka akaishi miaka mia moja na themanini.
\v 29 Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa kwa wahenga wake, na mtu mzee amejaa siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.
\s5
\c 36
\p
\v 1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edom).
\v 2 Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na
\v 3 Basemathi, binti Ishmaeli, dada wa Nebayothi.
\s5
\v 4 Ada akamzaa Elifazi kwa Esau, na Basemathi akamzaa Reueli.
\v 5 Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu, na Kora. Hawa walikuwa wana wa Esau waliozaliwa kwake katika nchi ya Kananaani.
\s5
\v 6 Esau akawachukua wakeze, wanawe, binti zake, na watu wote wa nyumba yake, mifugo wake - wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyokuwa amekusanya katika nchi ya Kanaani, na akaenda katika nchi iliyoko mbali kutoka kwa Yakobo nduguye.
\v 7 Alifanya hivi kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana kwa wao kuishi pamoja. Nchi waliyokuwa wamekaa isingeweza kuwafaa kwa mifugo yao.
\v 8 Hivyo Esau, aliyejulikana pia kama Edomu, akakaa katika nchi ya kilima Seiri.
\s5
\v 9 Hivi ndivyo vizazi vya Esau, babu wa Waedomu katika nchi ya mlima Seiri.
\v 10 Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau.
\v 11 Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi.
\v 12 Timna, suria wa Elifazi, mwana wa Esau, akamzaa Amaleki. Hawa walikuwa wajukuu wa Ada, mkewe Esau.
\s5
\v 13 Hawa walikuwa wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama, na Miza. Hawa walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
\v 14 Hawa walikuwa wana wa Oholibama, mkewe Esau, aliyekuwa binti Ana na mjukuu wa Zibeoni. Alimzalia Esau Yeushi, Yalamu, na Kora.
\s5
\v 15 Hizi zilikuwa koo kati ya vizazi vya Esau: uzao wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau: Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora,
\v 16 Gatamu, na Amaleki. Hivi vilikuwa vizazi vya koo kutoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Ada.
\s5
\v 17 Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli, mwana wa Esau: Nahathi, Zera, Shama, Miza. Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.
\v 18 Hizi zilikuwa koo za Oholibama, mkewe Esau: Yeushi, Yalamu, Kora. Hizi ni koo zilizotoka kwa Oholibama mkewe Esau, binti Ana.
\v 19 Hawa walikuwa wana wa Esau na koo zao.
\s5
\v 20 Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, wenyeji wa nchi hiyo: Lotani, Shobali, Zibeoni, Ana,
\v 21 Dishoni, Ezeri, na Dishani. Hizi zilikuwa koo the Wahori, wenyeji wa Seiri katika nchi ya Edomu.
\v 22 Wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemani, na Timna alikuwa dada wa Lotani.
\s5
\v 23 Hawa walikuwa wana wa Shobali: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu.
\v 24 Hawa walikuwa wana wa Zibeoni: Aia na Ana. Huyu ndiye Ana aliyeona chemichemi za moto nyikani, alipokuwa akichunga punda wa Zibeoni babaye.
\s5
\v 25 Hawa walikuwa watoto wa Ana: Dishoni na Oholibama, binti Ana.
\v 26 Hawa walikuwa wana wa Dishoni: Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
\v 27 Hawa walikuwa wana wa Ezeri: Bilhani, Zaavani, na Akani.
\v 28 Hawa walikuwa wana wa Dishani: Uzi na Arani.
\s5
\v 29 Hizi zilikuwa koo za Wahori: Lotani, Shobali, Zibeoni, na Ana,
\v 30 Dishoni, Ezeri, Dishani: hizi zilikuwa koo za Wahori, kulingana na ukoo ulivyoorodheshwa katika nchi ya Seiri.
\s5
\v 31 Hawa walikuwa wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kumilika juu ya Waisraeli:
\v 32 Bela mwana wa Beori, alitawala huko Edomu, na jina la mji wake lilikuwa Dinhaba.
\v 33 Bela alipofariki, kisha Yobabu mwana wa Zera kutoka Bozra, akatawala mahali pake.
\s5
\v 34 Yobabu alipofariki, Hushamu aliyekuwa wa nchi ya Watemani, akatawala mahali pake.
\v 35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi aliyewashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu, akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Avithi.
\v 36 Hadadi alipofariki, kisha Samla wa Masreka akatawala mahali pake.
\s5
\v 37 Samla alipofariki, kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake.
\v 38 Shauli alipofariki, kisha Baali Hanani mwana wa Akbori akatawala mahali pake.
\v 39 Baali Hanani mwana wa Akbori, alipokufa, kisha Hadari akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Pau. Jina la mkewe lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, mjukuu wa Me Zahabu.
\s5
\v 40 Haya ndiyo yalikuwa majina ya wakuu wa koo kutoka uzao wa Esau, kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao: Timna, Alva, Yethethi,
\v 41 Oholibama, Ela, Pinoni,
\v 42 Kenazi, Temani, Mbza,
\v 43 Magdieli, na Iramu. Hawa walikuwa wakuu wa ukoo wa Edomu, kwa kufuata makao yao katika nchi waliyomiliki. Nao ni Esau, baba wa Waedomu.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Yakobo akaishi katika nchi aliyokaa babaye, katika nchi ya Kanaani.
\v 2 Haya ndiyo matukio yaliyomhusu Yakobo. Yusufu, aliyekuwa kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akilichunga kundi pamoja na ndugu zake. Alikuwa pamoja na wana wa Bilha na pamoja na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akaleta taarifa yao mbaya kwa baba yao.
\s5
\v 3 Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote kwa sababu alikuwa mwana wa uzee wake. Akamshonea vazi zuri.
\v 4 Ndugu zake wakaona kwamba baba yao alimpenda sana kuliko ndugu zake wote. Wakamchukia na hawakuongea naye vema.
\s5
\v 5 Yusufu akaota ndoto, na akawambia ndugu zake. Wakamchukia zaidi.
\v 6 Aliwambia, "Tafadhari sikilizeni ndoto hii niliyoiota.
\s5
\v 7 Tazama, tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani na tazama, mganda wangu ukainuka na kusimama wima, na tazama, miganda yenu ikasogea na kuuinamia mganda wangu"
\v 8 Ndugu zake wakamwambia, "Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu? Hata wakamchukia zaidi kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake.
\s5
\v 9 Akaota ndoto nyingine na kuwasimulia ndugu zake. Alisema, "Tazama, nimeota ndoto nyingine: Jua na mwezi na nyota kumi na moja ziliniinamia."
\v 10 Akamwambia baba yake vile vile alivyowambia ndugu zake, na baba yake akamkemea. Akamwambia, Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako na mimi na ndugu zako kweli tutakuja kukuinamia mpaka chini?"
\v 11 Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliwema jambo hilo moyoni.
\s5
\v 12 Ndugu zake wakaenda kulichunga kundi la baba yao huko Shekemu.
\v 13 Israeli akamwambia Yusufu, 'Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Njoo, nami nitakutuma kwao." Yusufu akamwambia, "nipo tayari."
\v 14 Akamwambia, "Basi nenda, uwaone ndugu zako na kundi wanaendeleaje, na uniletee neno." Hivyo Yakobo akamtuma kutoka katika bonde la Hebroni, na Yusufu akaenda Shekemu.
\s5
\v 15 Mtu mmoja akamwona Yusufu. Tazama, Yusufu alikuwa akizunguka kondeni. Yule mtu akamwuliza, "Unatafuta nini?"
\v 16 Yusufu akamwambia, "Nawatafuta ndugu zangu. Tafadhari, niambie, wananalichunga wapi kundi."
\v 17 Yule mtu akasema, "Waliondoka mahali hapa, kwa maana niliwasikia wakisema, 'Haya twende Dothani." Yusufu akawafuata ndugu zake na kuwaona huko Dothani.
\s5
\v 18 Wakamwona kutokea mbali, na kabla hajawakaribia, wakapanga njama ya kumwua.
\v 19 Ndugu zake wakaambiana wao kwa wao, "Tazama, mwotaji anakaribia.
\v 20 Njoni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, 'Mnyama mkali amemrarua.' Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje."
\s5
\v 21 Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, "Tusiuondoe uhai wake."
\v 22 Rubeni aliwambia, "Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake" - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake.
\s5
\v 23 Ikawa Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua vazi lake zuri.
\v 24 Wakamchukua na kumtupa shimoni. Shimo lilikuwa tupu bila maji.
\s5
\v 25 Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri.
\v 26 Yuda akawambia ndugu zake, "Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake?
\s5
\v 27 Haya, na tumwuze kwa Waishmaeli na wala tusiweke mikono yetu juu yake. Kwani yeye ni ndugu yetu, nyama yetu." Ndugu zake wakamsikiliza.
\v 28 Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
\s5
\v 29 Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni. Akararua mavazi yake.
\v 30 Akarudi kwa ndugu zake na kusema, "Kijana yuko wapi? Na mimi, je niende wapi?"
\s5
\v 31 Wakachinja mbuzi na kisha wakalichukua vazi la Yusufu na kulichovya katika damu.
\v 32 Kisha wakalipeleka kwa baba yao na kusema, "Tumeiona hii. Tafadhari angalia kwamba ni vazi la mwanao au hapana."
\v 33 "Yakobo akaitambua na kusema, "Ni nguo ya mwanangu. Mnyama wa mwitu amemrarua. Bila shaka Yusufu ameraruliwa katika vipande.
\s5
\v 34 Yakobo akararua mavazi yake na kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake. Akaomboleza kwa ajili ya mwanawe siku nyingi.
\v 35 Wanawe na binti zake wote wakainuka na kumfariji, lakini alikataa kufarijiwa. Akasema, "Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea mwanangu." Babaye akamlilia.
\v 36 Wamidiani wakamwuza huko Misri kwa Potifa, afisa wa Farao, kepteni wa walinzi.
\s5
\c 38
\p
\v 1 Ikawa wakati ule Yuda akawaacha ndugu zake na kukaa na Mwadulami fulani, jina lake Hira.
\v 2 Pale akakutana na binti Mkanaani jina lake Shua. Akamwoa na kulala naye.
\s5
\v 3 Akawa mjamzito na kuzaa mwana. Akaitwa Eri.
\v 4 Akawa mjamzito tena na kuzaa mwana tena. Akamwita jina lake Onani.
\v 5 Akazaa mwana mwingine akamwita jina lake Shela. Alikuwa huko Kezibu alipomzaa.
\s5
\v 6 Yuda akaona mke kwa ajili ya Eri, mzaliwa wake wa kwanza. Jina lake Tamari.
\v 7 Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele za Yahwe. Yahwe akamwua.
\s5
\v 8 Yuda akamwambia Onani, "Lala na mke wa nduguyo. Fanya wajibu wa shemeji kwake, na umwinulie nduguyo mwana."
\v 9 Onani alijua kwamba mtoto asingekuwa wake. Pindi alipolala na mke wa kaka yake, alimwaga mbegu juu ya ardhi ili kwamba asimpatie nduguye mtoto.
\v 10 Alilolifanya lilikuwa ovu mbele za Yahwe. Yahwe akamwua pia.
\s5
\v 11 Kisha Yuda akamwambia Tamari, mkwewe, "Ukakae mjane katika nyumb aya baba yako hadi Shela, mwanangu, atakapokuwa." Kwani aliogopa, "Asije akafa pia, kama nduguze." Tamari akaondoka na kuishi katika nyumba ya babaye.
\s5
\v 12 Baada ya muda mrefu, binti Shua, mkewe Yuda, alikufa. Yuda akafarijika na kwenda kwa wakatao kondoo wake manyoya huko Timna, yeye na rafiki yake, Hira Mwadulami.
\v 13 Tamari akaambiwa, "Tazama, mkweo anakwenda Timna kukata kondoo wake manyoya."
\v 14 Akavua mavazi yake ya ujane na akajifunika kwa ushungi. Akakaa katika lango la Enaimu, lililoko kando ya njia iendayo Timna. Kwa maana aliona kwamba Shela amekua lakini akupewe kuwa mke wake.
\s5
\v 15 Yuda alipomwona alidhani ni kahaba kwa maana alikuwa amefunika uso wake.
\v 16 Akamwendea kando ya njia na kusema, "Njoo, tafadhari uniruhusu kulala nawe" - kwani hakujua kwamba alikuwa ni mkwewe - naye akasema, "Utanipa nini ili ulale nami?
\s5
\v 17 Akasema, "Nitakuletea mwana mbuzu wa kundi." Akasema, "Je utanipa rehani hata utakapo leta?"
\v 18 Akasema, "Nikupe rehani gani?" Naye akasema, "Mhuri wako na mshipi, na fimbo iliyo mkononi mwako." Akampa na kulala naye. Akawa mjamzito.
\s5
\v 19 Akaamka na kuondoka. Akavua ushungi wake na kuvaa vazi la ujane wake.
\v 20 Yuda akatuma mwana mbuzi kutoka kundini kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami ili aichukue rehani kutoka katika mkono wa mwanamke, lakini hakumwona.
\s5
\v 21 Kisha Mwadulami akauliza watu wa sehemu hiyo,"Yupo wapi kahaba aliyekuwa Enaimu kando ya njia?" Wakasema, hapajawai tokea kahaba hapa."
\v 22 Akarudi kwa Yuda na kusema, "Sikumwona. Pia watu wa eneo hilo wamesema, 'Hajawai kuwapo kahaba hapa."
\v 23 Yuda akasema, "Mwache akae na vitu, tusije tukaaibika. Hakika, nimemletea mwanambuzi, lakini hukumwona."
\s5
\v 24 Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, "Tamari mkweo amefanya ukahaba, na kwa hakika, yeye ni mjamzito." Yuda akasema, "Mleteni hapa ili achomwe."
\v 25 Alipoletwa nje, alipeleka ujumbe kwa mkwewe, "Mimi ni mjamzito kwa mtu mwenye vitu hivi." Akasema, "Tambua tafadhari, mhuri huu na mshipi na fimbo ni vya nani."
\v 26 Yuda akavitambua na kusema, "Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwani sikumpa Shela, mwanangu awe mme wake." Hakulala naye tena.
\s5
\v 27 Muda wake wa kujifungua ukafika, tazama, mapacha walikuwa tumboni mwake.
\v 28 Ikawa alipokuwa akijifungua mmoja akatoa mkono nje, na mkunga akachukua kitambaa cha rangi ya zambarau na kukifunga katika mkono wake na kusema, "Huyu ametoka wa kwanza."
\s5
\v 29 Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka kwanza. Mkunga akasema, "Umetokaje" Na akaitwa Peresi.
\v 30 Kisha ndugu yake akatoka, akiwa na utepe wa zambarau juu ya mkono wake, naye akaitwa Zera.
\s5
\c 39
\p
\v 1 Yusufu akaletwa Misri. Potifa, aliyekuwa afisa wa Farao mkuu wa walinzi na Mmisri, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli, waliokuwa wamempeleka pale.
\v 2 Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na akawa mtu aliyefanikiwa. Aliishi katika nyumba ya Mmisri bwana wake.
\s5
\v 3 Bwana wake akaona kwamba Yahwe alikuwa pamoja naye na kwamba Yahwe alifanikisha kila kitu alichokifanya.
\v 4 Yusufu akapata kibali mbele zake. Akamtumikia Potifa. Potifa akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake, na kila alichokimiliki, akakiweka chini ya uangalizi wake.
\s5
\v 5 Ikawa alipomfanya msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki, Yahwe akaibariki nyumba ya Mmisri kwa sababu ya Yusufu. Baraka za Yahwe zilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa nyumbani na shambani.
\v 6 Potifa akaweka kila alichokuwa nacho chini ya uangalizi wa Yusufu. Hakuwa na haja ya kufikiri juu ya lolote isipokuwa chakula alichokula tu. Basi Yusufu alikuwa kijana mzuri na wa kuvutia.
\s5
\v 7 Ikawa baada ya hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu. Akamwambia, "Lala nami."
\v 8 Lakini yeye alikataa na kumwambia mke wa bwana wake, "Tazama, bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani, na ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu.
\v 9 Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi. Hajanidhuiria chochote isipokuwa wewe, kwa sababu wewe ni mkewe. Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?
\s5
\v 10 Akamwambia Yusufu siku baada ya siku, lakini yeye akakataa kulala naye wala kuwa naye.
\v 11 Ikawa siku moja aliingia ndani kufanya kazi yake. Hakuna mtu yeyote wa nyumbani aliyekuwepo pale ndani.
\v 12 Akashika nguo zake na kusema, "Lala nami." Akaacha nguo zake mikononi mwake, akakimbia, na kutoka nje.
\s5
\v 13 Ikawa, alipoona kwamba ameziacha nguo zake mikononi mwake na kwamba amekimbia nje,
\v 14 akawaita watu wa nyumbani mwake na kuwambia, "Tazama, Potifa ameleta Mwebrania huyu kutudhihaki. Aliingia kulala nami, na nikapiga kelele.
\v 15 Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha na nguo yake, akakimbia, na kutoka nje."
\s5
\v 16 Akaweka nguo zake karibu naye hata bwana yake alipokuja nyumbani.
\v 17 Akamwambia maelelezo haya, "Yule mtumishi Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kunidhihaki.
\v 18 Ikawa nilipopiga kelele, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje."
\s5
\v 19 Ikawa, bwana wake aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe, "Hivi ndivyo mtumishi wako alivyonitenda," alikasirika sana.
\v 20 Bwana wa Yusufu akamchukua na kumweka gerezani, mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme. Akawa pale kifungoni.
\s5
\v 21 Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na kumwonyesha uaminifu wa agano. Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza.
\v 22 Mlinzi wa gereza akawaweka mikononi mwa Yusufu wafungwa wote waliokuwa gerezani. Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu.
\v 23 Mlinzi wa gereza hakuwa na wasiwasi juu ya chochote kilichokuwa mkononi mwake, kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye. Yahwe akafanikisha kila alichokifanya.
\s5
\c 40
\p
\v 1 Ikawa baada ya mambo haya, mnyweshaji wa mfalme wa Misri na mwokaji wa mfalime walimkosa bwana wao, mfalme wa Misri.
\v 2 Farao akawakasirikia hawa maafsa wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji.
\v 3 Akawaweka katika lindo katika nyumba ya kapteni wa walinzi, katika gereza lile Yusufu alimofungwa.
\s5
\v 4 Kapteni wa walinzi akamweka Yusufu kuwa mtumishi wao. Walikaa kifungoni kwa muda fulani.
\v 5 Wote wakaota ndoto - mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliokuwa wamefungwa gerezani - kila mmoja akaota ndoto usiku huo huo, na kila ndoto ilikuwa na tafsiri yake.
\s5
\v 6 Yusufu akaja kwao asubuhi na kuwaona. Tazama, walikuwa na uzuni.
\v 7 Akawauliza maafsa wa Farao waliokuwa pamoja naye kifungoni katika nyumba ya bwana wake, kusema, "Kwa nini leo mnaoneka wenye uzuni?"
\v 8 Wakamwambia, Sisi wote tumeota ndoto na hakuna wakuitafsiri." Yusufu akawambia, "Je tafsiri haitoki kwa Mungu? Niambieni, tafadhari."
\s5
\v 9 Mkuu wa wanyweshaji akamwambia Yusufu ndoto yake. Akamwambia, "Katika ndoto yangu, tazama, kulikuwa na mzabibu mbele yangu.
\v 10 Na kulikuwa na matawi matatu katika mzabibu huo. Ulipochipua, ukachanua maua na kuzaa vichala vya zabibu.
\v 11 Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu. Nikachukua zabibu na kuzikamua katika kikombe cha Farao, na kukiweka kikombe katika mkono wa Farao."
\s5
\v 12 Yusufu akamwambia, "Tafsiri yake ni hii. Yale matawi matatu ni siku tatu.
\v 13 Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako na kukurudisha katika nafasi yako. Utakiweka kikombe cha Farao katika mkono wake, kama ulivyokuwa ulipokuwa mnyweshaji wake.
\s5
\v 14 Lakini unikumbuke ukifanikiwa, na unionesha wema. Unitaje kwa Farao na kuniondoa hapa gerezani.
\v 15 Maana hakika nilitekwa kutoka katika nchi ya Waebrania. Na hapa sijafanya chochote kinachonipasa niwekwe gerezani."
\s5
\v 16 Mkuu wa waokaji alipoona kwamba tafsiri ilikuwa ya kuvutia, akamwambia Yusufu, "Mimi pia niliota ndoto, na tazama, vikapu vitatu vya mikate vilikuwa juu ya kichwa changu.
\v 17 Katika kikapu cha juu kulikuwa na kila aina za bidhaa ya kuokwa kwa Farao, lakini ndege wakavila ndani ya kikapu juu ya kichwa changu."
\s5
\v 18 Yusufu akajibu na kusema, "Tafsiri ni hii. Vikapu vitatu ni siku tatu.
\v 19 Ndani ya siku tatu Fareao atakiinua kichwa chako kutoka kwako na atakutundika juu ya mtu. Ndege watakula mwili wako."
\s5
\v 20 Ikawa siku ya tatu ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Farao. Akafanya sherehe kwa watumishi wake wote. "Akakiinua juu" kichwa cha mkuu wa wanyweshaji na kichwa cha mkuu wa waokaji, kati ya watumishi wake.
\v 21 Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika majukumu yake, na akakiweka tena kikombe katika mkono wa Farao.
\v 22 Lakini akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyokuwa amewatafsiria.
\v 23 Hata hivyo mkuu wa wanyweshaji hakukumbuka kumsaidia Yusufu. Badala yake, alimsahau.
\s5
\c 41
\p
\v 1 Ikawa mwishoni mwa miaka miwili mizima Farao akaota ndoto.
\v 2 Tazama, alikuwa amesimama kando ya Nile. Tazama, ng'ombe saba wakatoka katika mto Nile, wakupendeza na wanene, na wakajilisha katika nyasi.
\v 3 Tazama, ng'ombe wengine saba wakatoka katika Nile baada yao, wasiopendeza na wamekondeana. Wakasimama ukingoni mwa mto kando ya wale ng'ombe wengine.
\s5
\v 4 Kisha wale ng'ombe wasiopendeza na waliokonda wakawala wale waliokuwa wanapendeza na walionenepa.
\v 5 Kisha Farao akaamka. Kisha akalala na kuota mara ya pili. Tazama, masuke saba ya nafaka yalichipua katika mche mmoja, mema na mazuri.
\v 6 Tazama, masuke saba, membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.
\s5
\v 7 Masuke membamba yakayameza yale masuke saba mema yote. Farao akaamka, na, tazama, ilikuwa ni ndoto tu.
\v 8 Ikawa wakati wa asubuhi roho yake ikafadhaika. Akatuma na kuwaita waganga na wenye hekima wote wa Misri. Farao akawasimlia ndoto zake, lakini hakuna aliyeweza kumtafsiria Farao.
\s5
\v 9 Kisha mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao, "Leo ninayafikiri makosa yangu.
\v 10 Farao aliwakasirikia watumishi wake, na kutuweka kifungoni katika nyumba ya kapteni wa walinzi, mkuu wa waokaji na mimi.
\v 11 Tuliota ndoto usiku huo mmoja, yeye na mimi. Kila mmoja aliota kwa kadili ya tafsiri yake.
\s5
\v 12 Pamoja nasi kulikuwa na kijana Mwebrania, mtumishi wa kapteni wa walinzi. Tulimwambia na akatutafsiria ndoto zetu. Alitutafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.
\v 13 Ikawa kama alivyotutafsiria, ndivyo ilivyokuwa. Farao alinirudisha katika nafasi yangu, lakini akamtundika yule mwingine."
\s5
\v 14 Ndipo Farao alipotuma na kumwita Yusufu. Kwa haraka wakamtoa gerezani. Akajinyoa mwenyewe, akabadili mavazi yake, na akaingia kwa Farao.
\v 15 Farao akamwambia Yusufu, "Nimeoda ndoto, lakini hakuna wa kuitafsiri. Lakini nimesikia kuhusu wewe, kwamba unaposikia ndoto unaweza kuitafsiri."
\v 16 Yusufu akamjibu Farao, kusema, "Siyo katika mimi. Mungu atamjibu Farao kwa uhakika."
\s5
\v 17 Farao akamwambia Yusufu, "Katika ndoto yangu, tazama, nilisimama katika ukingo wa Nile.
\v 18 Tazama, ng'ombe saba wakatoka ndani ya Nile, wanene na wakuvutia, nao wakajilisha katika nyasi.
\s5
\v 19 Tazama, ng'ombe wengine saba wakapanda baada yao, dhaifu, wabaya, na wembaba. Sijawao kuona wabaya kama hao katika nchi yote ya Misri.
\v 20 Wale ng'ombe wembamba na wabaya wakawala wale ng'ombe saba na wanene.
\v 21 Walipokuwa wamemaliza kuwala wote, haikujulikana kama walikuwa wamewala, kwani walibaki wabaya kama mwanzo. Kisha nikaamka.
\s5
\v 22 Niliona katika ndoto yangu, na tazama, masuke saba yakatoka katika bua moja, jema na limejaa.
\v 23 Tazama, masuke saba zaidi, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.
\v 24 Yale masuke membamba yakayameza masuke saba mema. Niliwaambia waganga ndoto hizi, lakini hakuna aliyeweza kunielezea."
\s5
\v 25 Yusufu akamwambia Farao, "Ndoto za Farao ni moja. Mungu amemwambia Farao kuhusu jambo analokwenda kulifanya.
\v 26 Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba, na masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.
\s5
\v 27 Na wale ng'ombe saba wembamba na wabaya waliokuja baadaye ni miaka saba, na pia masuke saba membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki itakuwa miaka saba ya njaa.
\v 28 Hilo ni jambo nililomwambia Farao. Mungu amemfunulia Farao jambo analokwenda kulifanya.
\v 29 Tazama, miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri.
\s5
\v 30 Na miaka saba ya njaa itakuja baada yake, na utele wote katika nchi ya Misri utasahaulika, na njaa itaiaribu nchi.
\v 31 Utele hautakumbukwa katika nchi kwa sababu ya njaa itakayofuata, kwa kuwa itakuwa kali sana.
\v 32 Kwamb ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu, na Mungu atalitimiza hivi karibuni.
\s5
\v 33 Basi Farao atafute mtu mwenye maharifa na busara, na kumweka juu ya nchi ya Misri.
\v 34 Farao na afanye hivi: achague wasimamizi juu ya nchi. Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri katika miaka saba ya shibe.
\s5
\v 35 Na wakusanye chakula chote cha hii miaka myema ijayo na kuitunza nafaka chini ya mamlaka ya Farao, kwa chakula kutumika katika miji. Wakiifadhi.
\v 36 Chakula kitakuwa matumizi ya nchi kwa miaka saba ya njaa itakayokuwa katika nchi ya Misri. Kwa njia hii nchi haitaaribiwa na njaa."
\s5
\v 37 Ushauri huu ukawa mwema machoni pa Farao na machoni pa watumishi wake wote.
\v 38 Farao akawambia watumishi wake, "Je tunaweza kumpata mtu kama huyu, ambaye ndani yake kuna Roho wa Mungu?"
\s5
\v 39 Hivyo Farao akamwambia Yusufu, "Kwa vile Mungu amekuonesha yote haya, hakuna mtu mwenye ufahamu na busara kama wewe.
\v 40 Utakuwa juu ya nyumba yangu, watu wangu watatawaliwa kwa kadili ya neno lako. Katika kiti cha enzi peke yake mimi nitakuwa mkuu kuliko wewe."
\v 41 Farao akamwambia Yusufu, "Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri."
\s5
\v 42 Farao akavua pete yake ya mhuri kutoka katika mkono wake na kuiweka katika mkono wa Yusufu. Akamvika kwa mavazi ya kitani safi, na kuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
\v 43 Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho. Watu wakapiga kelele mbele yake, "Pigeni magoti." Farao akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
\s5
\v 44 Farao akamwambia Yusufu, "Mimi ni Farao, mbali na wewe, hakuna mtu atakayeinua mkono wake au mguu wake katika nchi ya Misri."
\v 45 Farao akamwita Yusufu jina la Zafenathi Panea." Akampa Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, kuwa mke wake. Yusufu akaenda juu ya nchi yote ya Misri.
\s5
\v 46 Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya Farao, na kwenda katika nchi yote ya Misri.
\v 47 Katika miaka saba ya shibe nchi ilipozaa kwa wingi.
\s5
\v 48 Akakusanya chakula chote cha miaka saba iliyokuwako katika nchi ya Misri na kukiweka chakula katika miji. Akaweka katika kila mji chakula cha mashamba yaliyokizunguka.
\v 49 Yusufu akahifadhi nafaka kama mchanga wa bahari, kingi kiasi kwamba akaacha kuhesabu, kwa sababu kilikuwa hakihesabiki.
\s5
\v 50 Kabla miaka ya njaa kuingia Yusufu akapata wana wawili, ambao Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa On, alimzalia.
\v 51 Yusufu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, kwani alisema, "Mungu amenisahaurisha shida zangu zote na nyumba yote ya baba yangu."
\v 52 Akamwita mwanawe wa pili Efraimu, kwani alisema, Mungu amenipa uzao katika nchi ya mateso yangu."
\s5
\v 53 Miaka saba ya shibe iliyokuwa katika nchi ya Misri ikafika mwisho.
\v 54 Miaka saba ya njaa ikaanza, kama alivyokuwa amesema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi zote, lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula.
\s5
\v 55 Nchi yote ya Misri ilipokuwa na njaa, watu wakapiga kelele kwa Farao kwa ajili ya chakula. Farao akawambia Wamisri wote, "Nendeni kwa Yusufu na mfanye atakavyosema."
\v 56 Njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi. Yusufu akafungua ghala zote na kuuza chakula kwa Wamisri. Njaa ilikuwa kali sana katika nchi ya Misri.
\v 57 Dunia yote ikaja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yusufu, kwani njaa ilikuwa kali katika dunia yote.
\s5
\c 42
\p
\v 1 Basi Yakobo akafahamu kwamba kuna nafaka huko Misri. Akawambia wanawe, "Kwa nini mnatazamana?
\v 2 Akasema, "Tazama, nimesikia kwamba kuna nafaka huko Misri. Shukeni huko mkatununulie chakula ili tuishi wala tusife."
\v 3 Ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri kununua chakula.
\v 4 Lakini Benjamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumtuma na ndugu zake, kwani alihofu kwamba madhara yaweza kumpata.
\s5
\v 5 Wana wa Israeli wakaja kununua miongoni mwao waliokuja, kwani njaa ilikuwapo katika nchi ya Kanaani.
\v 6 Basi Yusufu alikuwa mtawala juu ya nchi. Ndiye aliyekuwa akiwauzia watu wote wa nchi. Ndugu zake Yusufu wakaja na kumwinamia na nyuso zao hata chini.
\s5
\v 7 Yusufu akawaona ndugu zake na kuwatambua, lakini alijibadili kwao na kuongea nao kwa ukali. Akawambia, "Mmetoka wapi?" Wakasema, "Kutoka nchi ya Kanaani ili kununua chakula."
\v 8 Yusufu akawatambua ndugu zake, lakini wao hawakumtambua.
\s5
\v 9 Yusufu akazikumbuka ndoto aliyoziota kuhusu wao. Akawambia, "Ninyi ni wapelelezi. Mmekuja kuona sehemu za nchi zisizolindwa."
\v 10 Wakamwambia, "Hapana, bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula.
\v 11 Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Ni watu wa kweli. Watumishi wako siyo wapelelezi."
\s5
\v 12 Akawambia, "Hapana, mmekuja kuangalia sehemu za nchi zisizolindwa."
\v 13 Wakasema, "Sisi watumishi wako tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja katika nchi ya Kanaani. Tazama, mdogo yupo na baba yetu, na mwingine hayupo hai tena."
\s5
\v 14 Yusufu akawambia, "Ndivyo nilivyowambia; ninyi ni wapelelezi.
\v 15 Mtajaribiwa kwa njia hii. Kama aishivyo Farao, hamtaondoka hapa, mdogo wenu asipokuja hapa.
\v 16 Mtumeni mmoja wenu amlete mdogo wenu. Mtabaki gerezani, hata maneno yenu yatakapothibitishwa, kwamba kuna ukweli ndani yenu."
\v 17 Akawaweka kifungoni kwa siku tatu.
\s5
\v 18 Katika siku ya tatu Yusufu akaongea nao, "Fanyeni hivi nanyi mtaishi, kwani ninamcha Mungu.
\v 19 Kama ninyi ni watu wa kweli, mmoja wenu atazuiliwa hapa gerezani, lakini ninyi nendeni, chukueni nafaka kwa ajili ya nyumba zenu.
\v 20 Mleteni mdogo wenu kwangu ili kwamba maneno yenu yathibitishwe nanyi hamtakufa." Wakafanya hivyo.
\s5
\v 21 Wakasemezana wao kwa wao, "Kwa kweli tuna hatia juu ya ndugu yetu kwani tuliona tabu ya nafsi yake alipotusihi nasi hatukusikia. Kwa hiyo taabu hii imeturudia."
\v 22 Rubeni akawajibu, "Je sikuwambia, 'Msitende dhambi juu ya kijana,' lakini hamkusikia? Basi, tazama, damu yake inatakiwa juu yetu."
\s5
\v 23 Lakini hawakuja kwamba Yusufu anawaelewa, kwani kulikuwa na mkalimani kati yao.
\v 24 Akatoka kwao na kulia. Akarudi kwao na kuongea nao. Akamchukua Simoni miongoni mwao na kumfunga mbele ya macho yao.
\v 25 Kisha Yusufu akaagiza watumishi kujaza mifuko yao kwa nafaka, na kurudisha pesa ya kila mmoja katika gunia lake, nakuwapa mahitaji kwa safari. Wakatendewa hivyo.
\s5
\v 26 Hawa ndugu wakapandisha chakula chao juu ya punda zao na kuondoka pale.
\v 27 Mmoja wao alipofungua gunia lake ili kumlisha punda wao katika sehemu waliyokuwa, akaona pesa yake. Tazama, ilikuwa mdomoni mwa gunia lake.
\v 28 Akawambia ndugu zake, "Pesa yangu imerudishwa. Tazama, imo katika gunia langu."Mioyo yao ikazimia na wakageukiana kila mmoja huku wakitetemeka. Wakasema, "Ni nini hiki alichotutendea Mungu?"
\s5
\v 29 Wakaenda kwa Yakobo, baba yao katika nchi ya Kanaani na kumwambia yote yaliyowapata.
\v 30 Wakasema, "Yule mtu, bwana wa nchi, aliongea nasi kwa ukali na kutudhania kuwa wapelelezi katika nchi.
\v 31 Tukamwambia, 'Tu watu wa kweli sisi. Sisi siyo wapelelezi.
\v 32 Tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayupo hai tena, na mdogo yupo na baba yetu katika nchi ya Kanaani."
\s5
\v 33 Yule mtu, bwana wa nchi, akatwambia, 'Kwa hili nitajua kwamba ni watu wa kweli ninyi. Mwacheni mmojawapo wa ndugu zenu, chukueni chakula kwa ajili ya njaa katika nyumba zenu, na mwondoke.
\v 34 Mleteni mdogo wenu kwangu. Ndipo nitakapojua kwamba ninyi si wapelelezi, lakini ni watu wa kweli. Kisha nitamwachilia ndugu yenu, na mtafanya biashara katika nchi."
\s5
\v 35 Ikawa walipoyafungua magunia yao, na tazama, kila mfuko wa fedha wa mmojawao ulikuwa katika gunia lake. Wakati wao na baba yao walipoona mifuko yao ya fedha, wakaogopa.
\v 36 Yakobo baba yao akawambia, "Mmeniharibia watoto wao. Yusufu hayupo hai tena, Simoni ameondoka, nanyi mmpeleke Benjamini naye. Mambo haya yote ni kunyume changu."
\s5
\v 37 Rubeni akamwambia baba yake, kusema, "Unaweza kuwaua wanangu wawili nisipomrudisha Benjamini kwako. Mweke mikononi mwangu, nami nitamrudisha tena kwako."
\v 38 Yakobo akasema, "Mwanangu atashuka pamoja nanyi. Kwani ndugu yake amekufa na yeye peke yake amebaki. Ikiwa madhara yatampata katika njia mnayoiendea, ndipo mtakapozishusha mvi zangu kaburini kwa huzuni."
\s5
\c 43
\p
\v 1 Njaa ilikuwa kali katika nchi.
\v 2 Ikawa walipokuwa wametumia chakula chote walichokitoa Misri, baba yao akawambia, "Nendeni tena; mtununulie chakula."
\s5
\v 3 Yuda akamwambia, "Yule mtu alituonya kwa ukali, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi.'
\v 4 Ikiwa utamtuma ndugu yetu pamoja nasi, tutashuka na kuwanunulia chakula.
\v 5 Lakini usipompeleka, hatutashuka. Kwa maana yule mtu alitwambia, 'Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi."
\s5
\v 6 Israeli akawambia, "Kwa nini mlinitendea mimi vibaya hivyo kwa kumwambia mtu huyo kwamba mnaye ndugu mwingine?"
\v 7 Wakasema, "Yule mtu alituuliza habari zetu na familia yetu kwa kina. Akasema, 'Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?'Tukamjibu kulingana na maswali haya. Tungejuaje kwamba angetwambia, 'Mleteni ndugu yenu?"
\s5
\v 8 Yuda akamwambia Israeli baba yake, "Mtume kijana pamoja nami. Tutainuka na kwenda ili kwamba tuishi tusife, wote sisi, wewe, na hata watoto wetu.
\v 9 Mimi nitakuwa mdhamini wake. Utaniwajibisha mimi. Kama nisipomleta na kumweka mbele yako, basi nibebe lawama daima.
\v 10 Kwani kama tusingekawia, bila shaka hata sasa tungekuwa tumekwisha rudi mara ya pili."
\s5
\v 11 Israeli baba yao akawambia, "Kama ni hivyo, basi fanyeni hivi. Chukueni baadhi ya mazao mazuri ya nchi katika mifuko yenu. Mchukulieni yule mtu zawadi: baadhi ya malhamu, asali, viungo na manemane, jozi na lozi.
\v 12 Chukueni pesa mara mbili mikononi mwenu. Pesa iliyorudishwa katika magunia yenu, muichukue tena katika mikono yenu. Pengine walikosea.
\s5
\v 13 Mchukueni ndugu yenu pia. Inukeni na mwende tena kwa mtu yule.
\v 14 Mungu Mwenyezi na awape kuona rehema mbele ya huyo mtu, hivyo kwamba awafungulie ndugu yenu mwingine na Benjamini. Kama nikipotelewa na watoto, nimepotelewa."
\v 15 Watu wale wakachukua zawadi hii, na katika mikono yao wakachukua mara mbili ya kiasi cha pesa, pamoja na Benjamini. Wakaamka na kushuka Misri na kusimama mbele ya Yusufu.
\s5
\v 16 Yusufu alipomwona Benjamini akiwa nao, akamwambia mtunzaji wa nyumba yake, "Walete watu hao ndani ya nyumba, chinja mnyama na umwandae, kwani watu hawa watakula chakula cha mchana pamoja nami."
\v 17 Mtunzaji wa nyumba akafanya kama Yusufu alivyosema. Akawaleta wale watu nyumbani kwa Yusufu.
\s5
\v 18 Wale ndugu wakaogopa kwa vile walivyoletwa katika nyumba ya Yusufu. Wakasema, "Ni kwa sababu ya pesa iliyorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tulipoletwa ndani, kwamba atafute nafasi kinyume chetu. Kwamba aweze kutukamata na kutuchukua kama watumwa, na kuchukua punda wetu." Wakamsogelea mtunzaji wa nyumba ya Yusufu,
\v 19 nao wakaongea naye mlangoni mwa nyumba,
\v 20 wakisema, "Bwana wangu, tulikuja mara ya kwanza kununua chakula.
\s5
\v 21 Ikawa, tulipofika katika eneo la kupumzikia, tukafungua magunia yetu, na, tazama, pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili. Tumeileta katika mikono yetu.
\v 22 Tumekuja na pesa nyingine pia mikonon mwetu ili kununua chakula. Hatujui aliyeziweka pesa katika magunia yetu."
\v 23 Mtunzaji wa nyumba akasema, "Amani iwe kwenu, msiogope. Mungu wenu na Mungu wa baba yenu ndiye aliyeweka pesa katika magunia yenu. Nilipokea pesa yenu." Kisha mtunzaji wa nyumba akamleta Simoni kwao.
\s5
\v 24 Msimamizi wa nyumba akawapeleka watu hao katika nyumba ya Yusufu. Akawapa maji, nao wakaosha miguu yao. Akawalisha punda wao.
\v 25 Wakaandaa zawadi kwa ajili ya Yusufu aliyekuwa akija mchana, kwani walikuwa wamesikia kwamba watakula pale.
\s5
\v 26 Yusufu alipokuja nyumbani, wakaleta nyumbani zawadi iliyokuwa mikononi mwao, nao wakainama mbele yake hata chini.
\v 27 Akawauliza juu ya hali zao na kusema,"Je baba yenu hajambo, yule mzee mliyemnena? Je bado yu hai?"
\s5
\v 28 Wakasema, "Mtumishi wako baba yetu hajambo. Na bado yu hai" Wakajinyenyekeza na kuinama chini.
\v 29 Alipoinua macho yake akamwona Benjamini ndugu yake, mwana wa mamaye, naye akasema, "Je huyu ndiye mdogo wenu mliyemsema?" Na kisha akasema, "Mungu na awe mwenye neema kwako, mwanangu."
\s5
\v 30 Yusufu akaharakisha kutoka chumbani, kwani aliguswa sana kuhusu nduguye. Akatafuta mahali pa kulia. Akaingia chumbani mwake na kulia umo.
\v 31 Akaosha uso wake na kutoka nje. Akajizuia mwenyewe, akasema, "karibuni chakula."
\s5
\v 32 Watumishi wakamhudumia Yusufu peke yake na wale ndugu peke yao. Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao kwa sababu Wamisri hawakuweza kula mkate na Waebrania, kwani hilo ni chukizo kwa Wamisri.
\v 33 Wale ndugu wakakaa mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa kulingana na haki yake ya uzaliwa, na mdogo kulingana na ujana wake. Wale watu wakashangaa wote.
\v 34 Yusufu akapeleka sehemu kwao kutoka katika chakula kilichokuwa mbele yake. Lakini sehemu ya Benjamini ilikuwa mara tano zaidi ya kila ndugu zake. Wakanywa na wakamfurahia.
\s5
\c 44
\p
\v 1 Yusufu akamwamru msimamizi wa nyumba yake, akisema, "Jaza magunia ya watu hawa kwa chakula, kiasi wawezacho kubeba, na uweke pesa ya kila mtu katika mdomo wa gunia lake.
\v 2 Uweke kikombe changu, cha fedha, katika mdomo wa gunia la mdogo, na pesa yake ya chakula pia." Msimamizi akafanya kama Yusufu alivyosema.
\s5
\v 3 Kukapambazuka asubuhi, na wale watu wakaruhusiwa kuondoka, wao na punda zao.
\v 4 Walipokuwa wametoka mjini lakini hawajafika mbali, Yusufu akamwambia msimamizi wa nyumba yake, "Inuka, uwafuatie wale watu, na utakapowapata, wambie, 'Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema?
\v 5 Je hiki siyo kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi? Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya."
\s5
\v 6 Msimamizi wa nyumba akawapata na kuwambia maneno haya.
\v 7 Wakasema, "Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama haya? Na iwe mbali na watumishi wako kwamba wanaweza kufanya jambo hili.
\s5
\v 8 Tazama, pesa tulizozikuta katika midomo ya magunia yetu, tulizileta kwako kutoka katika nchi ya Kanaani. Ni kwa jinsi gani basi tunaweza kuiba katika nyumba ya bwana wako fedha au dhahabu?
\v 9 Yeyote kitakayeonekana kwake miongoni mwa watumishi wako, atakufa, nasi sote tutakuwa watumwa wa bwana wangu."
\v 10 Msimamizi akasema, "Basi na iwe kwa kadili ya maneno yenu. Yeye ambaye kikombe kitaonekana kwake atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine mtakuwa bila hatia."
\s5
\v 11 Kisha kila mtu akaharakisha na kulishusha gunia lake chini. na kila mtu akalifungua gunia lake.
\v 12 Msimamizi akatafuta. akaanza na mkubwa wa wote na kumaliza kwa mdogo wa wote, na kikombe kikaonekana katika gunia la Benjamini.
\v 13 Wakararua mavazi yao. Kila mtu akapakia juu ya punda wake nao wakarudi mjini.
\s5
\v 14 Yuda na ndugu zake wakaja katika nyumba ya Yusufu. Bado alikuwepo pale, nao wakainama mbele zake hata chini.
\v 15 Yusufu akawambia, "Je ni nini hili mlilolifanya? Je hamjui kwamba mtu kama mimi anafanya uaguzi.
\s5
\v 16 Yuda akasema, "Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu? Tuseme nini? au ni jinsi gani twaweza kujithibitisha wenyewe? Mungu ameona uovu wa watumishi wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, wote sisi na yule ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake."
\v 17 Yusufu akasema, "Na iwe mbali nami kwamba naweza kufanya hivyo. Mtu ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake, huyu ndiye atakuwa mtumwa wangu, lakini ninyi wengine, nendeni kwa amani kwa baba yenu."
\s5
\v 18 Ndipo Yuda alipomkaribia na kusema, "Bwana wangu, tafadhari mwache mtumishi wako aseme neno katika masikio ya bwana wangu, na usiziache hasira zako kuwaka dhidi ya mtumishi wako, kwani wewe ni kama Farao.
\v 19 Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, kusema, Je mnaye baba au ndugu?'
\s5
\v 20 Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Tunaye baba, ni mzee, na mwana wa uzee wake, ni mdogo. Na ndugu yake alishakufa, na yeye peke yake ndiye amebaki kwa mama yake, na baba yake anampenda.'
\v 21 Nawe ukawambia matumishi wako, 'Mleteni ili nimwone.'
\v 22 Nasi tukamwambia bwana wangu, 'Kijana hawezi kumwacha babaye. Kwani akimwacha babaye baba yake angekufa.'
\s5
\v 23 Na ukawambia watumishi wako, 'Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.'
\v 24 Na ikawa tulipokwenda kwa mtumishi wako baba yangu, tulimwambia maneno ya bwana wangu.
\v 25 Na baba yetu akasema, Nendeni tena, mkatununulie chakula.'
\v 26 Nasi tukasema, "Hatuwezi kushuka. Ikiwa mdogo wetu atakuwa nasi, ndipo tutakaposhuka, kwani hatuwezi kuuona uso wa mtu yule mdogo wetu asipokuwa pamoja nasi.'
\s5
\v 27 Mtumishi wako baba yetu akatwambia, 'Mnajua kwamba mke wangu alinizalia wana wawili.
\v 28 Na mmoja akatoka kwangu nami nikasema, "Bila shaka ameraruliwa vipande, na tangu hapo sijamwona."
\v 29 Nanyi mkimchukua huyu naye kutoka kwangu mabaya yanaweza kumpata, mtashusha mvi zangu kwa kaburini kwa huzuni.
\s5
\v 30 Kwa hiyo, basi, nitapokuja kwa mtumishi wako baba yangu, na kijana hayupo nasi, kwa kuwa uhai wake umefungamanishwa katika uhai wa kijana,
\v 31 itakuwa, atakapoona kwamba kijana hayupo nasi atakufa. Na watumishi wako watazishusha mvi za mtumishi wako baba yetu kaburini kwa masikitiko.
\v 32 Kwani mtumishi wako alikuwa mdhamini wa kijana kwa baba yangu na alisema, 'Ikiwa sitamleta kwako, ndipo nitakapokuwa mwenye hatia kwa baba yangu daima."
\s5
\v 33 Kwa hiyo sasa, tafadhari mwache mtumishi wake akae kama mtumwa kwa bwana wangu badala ya kijana, na umwache kijana aende na ndugu zake.
\v 34 Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami? Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu."
\s5
\c 45
\p
\v 1 Ndipo Yusufu hakuweza kujizuia mwenyewe mbele ya watumishi waliosimama kando yake. Akasema kwa sauti, "Kila mtu aondoke." Hivyo hakuna mtumishi aliyesimama kando yake wakati Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake.
\v 2 Akalia kwa sauti, Wamisri wakasikia, na nyumba ya Farao wakasikia kuhusu hilo.
\v 3 Yusufu akawambia ndugu zake, "Mimi ni Yusufu. Je baba yangu ni mzima bado? Ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walitishwa na uwepo wake.
\s5
\v 4 Kisha Yusufu akawambia ndugu zake, "Nikaribieni, tafadhari." Nao wakasogea. Akawambia, "Mimi ni Yusufu ndugu yenu, mliyemwuza Misri.
\v 5 Lakini sasa msihuzunike au kukasirika miongoni mwenu kwamba mliniuza huku, kwani Mungu alinituma mbele yenu ili kutunza uhai.
\v 6 Maana ni miaka miwili njaa imekuwa katika nchi, na bado kuna miaka mitano ambayo hakutakuwa na kulima wala kuvuna.
\s5
\v 7 Mungu alinituma mbele yenu kuwahifadhi kama masalia duniani, na kuwaweka hai kwa ukombozi mkuu.
\v 8 Hivyo si ninyi mlionipeleka huku bali ni Mungu, na amenifanya baba kwa Farao, bwana wa nyumba yake yote, na mtawala wa nchi yote ya Misri.
\s5
\v 9 Fanyeni haraka mwende kwa baba yangu na mmwambie, 'Hivi ndivyo asemavyo Yusufu mwanao, "Mungu amenifanya bwana kwa Wamisri wote. Shuka kwangu, usikawie.
\v 10 Utaishi katika nchi ya Gosheni, nawe utakuwa karibu nami, wewe na watoto wako na watoto wa watoto wako, na kondoo wako na mbuzi wako, na yote uliyonayo.
\v 11 Nami nitakuhudumia pale, kwa maana bado kuna miaka mitano ya njaa, hivyo usije ukaingia katika uhitaji, wewe, nyumba yako, na yote uliyonayo."
\s5
\v 12 Tazama, macho yenu yanaona, na macho ya Benjamini ndugu yangu, kwamba ni kinywa changu kinachoongea nanyi.
\v 13 Mtamwambia baba yangu juu ya heshima yangu yote huku Misri na yote mliyoyaona. Mtaharakisha na kumleta baba yangu huku."
\s5
\v 14 Akaikumbatia shingo ya Benjamini ndugu yake na kulia, na Benjamini akalia shongoni mwake.
\v 15 Akawabusu ndugu zake wote na kulia kwa ajili yao. Baada ya hayo ndugu zake wakaongea naye.
\s5
\v 16 Habari ya jambo hili ikasemwa katika nyumba ya Farao: "Ndugu zake Yusufu wamekuja." Ikampendeza sana Farao na watumishi wake.
\v 17 Farao akamwambia Yusufu, "Wambie ndugu zako, 'Fanyeni hivi: Wapakieni wanyama wenu na mwende katika nchi ya Kanaani.
\v 18 Mchukueni baba yenu na nyumba zenu mnijie. Nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.'
\s5
\v 19 Basi mmeamriwa, 'Fanyeni hivi, chukueni mikokoteni kutoka Misri kwa ajili ya watoto wenu na kwa ajili ya wake zenu. Mchukueni baba yenu na kuja.
\v 20 Msijari kuhusu mali zenu, kwani mema yote ya nchi ya Misri ni yenu."
\s5
\v 21 Wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yusufu akawapa mikokoteni, kwa kadili ya agizo la Farao, na akawapa mahitaji ya safari.
\v 22 Akawapa wote mavazi ya kubadilisha, lakini akampa Benjamini vipande mia tatu vya fedha na mavazi matano ya kubadilisha.
\v 23 Akampelekea baba yake: punda kumi waliobeba mema ya Misri, punda majike kumi wamebeba nafaka, mikate, na mahitaji mengine kwa baba yake kwa ajili ya safari.
\s5
\v 24 Hivyo akawaruhusu ndugu zake nao wakaondoka. Akawambia, "Angalieni msijemkagombana njiani."
\v 25 Wakapanda kutoka Misri na kuja katika nchi ya Kanaani, kwa Yakobo baba yao.
\v 26 Wakamwambia "Yusufu bado yu hai, na ndiye mtawala juu ya nchi yote ya Misri." Na moyo wake ulishikwa na ushangao, kwani hakuwaamini.
\s5
\v 27 Wakamwambia maneno yote ya Yusufu aliyokuwa amewambia. Yakobo alipoona mikokoteni Yusufu aliyokuwa amepeleka kuwabeba, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.
\v 28 Israeli akasema, "Inatosha. Yusufu mwanangu yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa."
\s5
\c 46
\p
\v 1 Israeli akasafiri na yote aliyokuwa nayo na akaja Beersheba. Pale akatoa sadaka kwa Mungu wa Isaka baba yake.
\v 2 Mungu akamwambia Israeli katika ndoto usiku, akisema, "Yakobo, Yakobo."
\v 3 Akasema, "Mimi hapa." Akasema, "Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana nitakufanya taifa kubwa huko.
\v 4 Nitakwenda pamoja nawe huko Misri, Nami nitakupandisha huku tena bila shaka. Na Yusufu akayafunika macho yako kwa mikono wake."
\s5
\v 5 Yakobo akainuka kutoka Beersheba. Wana wa Israeli wakamsafirisha Yakobo baba yao, watoto wao, na wake wao, katika mikokotene ambayo Farao alikuwa ameipeleka kuwachukua.
\v 6 Wakachukua mifugo yao na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani. Wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.
\v 7 Akaja Misri pamoja na wanawe na wana wa wanawe, binti zake na wana wa binti zake, na uzao wake wote.
\s5
\v 8 Haya ni majina ya watoto wa Israeli waliokuja Misri, Yakobo na wanawe: Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo;
\v 9 wana wa Rubeni Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi;
\v 10 wana wa Simoni, Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli, wana wa mwanamke Mkanaani;
\v 11 wana wa Lawi Gershoni, Kohathi, na Merari.
\s5
\v 12 Wana wa Yuda: Eri, Shela, Peresi, na Zera, (Lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani). Na wana wa Peresi walikuwa Hezroni na Hamuli.
\v 13 Wana wa Isakari walikuwa Tola, Puva, Lobu, na Shimroni;
\v 14 Wana wa Zabuloni walikuwa Seredi, Eloni, na Yahleeli
\v 15 Hawa walikuwa wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padani Aramu, pamoja na na Dina binti yake. Wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.
\s5
\v 16 Wana wa Gadi walikuwa Zifioni, Hagi, Shuni, Ezboni, Eri, Arodi, na Areli.
\v 17 Wana wa Asheri walikuwa Imna, Ishva, Ishvi, na Beria; na Sera alikuwa dada yao. Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malkieli.
\v 18 Hawa walikuwa wana wa Zilpa, ambaye Labani alikuwa amempa Lea binti yake. Wana aliomzalia Yakobo wote walikuwa kumi na sita.
\s5
\v 19 Wana wa Raheli mkewe Yakobo walikuwa Yusufu na Benjamini.
\v 20 Huko Misri Manase na Efraimu walizaliwa kwa Yusufu na Asenathi, binti Potifera kuhani wa Oni.
\v 21 Wana wa Benjamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu, na Ardi.
\v 22 Hawa walikuwa wana wa Raheli waliozaliwa kwa Yakobo - jumla yao kumi na wanne.
\s5
\v 23 Mwana wa Dani alikuwa Hushimu.
\v 24 Wana wa Naftali walikuwa Yahzeeli, Guni, Yezeri, na Shilemi.
\v 25 Hawa walikuwa wana Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alimpa Raheli binti yake - wote walikuwa saba.
\s5
\v 26 Wate waliokwenda na Yakobo, waliokuwa uzao wake, bila kuhesabu wake wa wana wa Yakobo walikuwa sitini na sita.
\v 27 Pamoja na wana wawili wa Yusufu waliozaliwa kwake huko Misri, watu wa familia yake waliokwenda Misri walikuwa sabini jumla yao.
\s5
\v 28 Yakobo akamtuma Yuda kuwatangulia mbele kwa Yusufu kuonesha njia mbele yake kwenda Gosheni, nao wakaja katika eneo la Gosheni.
\v 29 Yusufu akaandaa kibandawazi chake na akaenda kumlaki baba yake huko Gosheni. Akamwona, akaikumbatia shingo yake, na akalia shingoni mwake kwa kitambo.
\v 30 Israeli akamwambia Yusufu, "Basi na nife sasa, kwa kuwa nimeuona uso wako, kwamba bado uko hai."
\s5
\v 31 Yusufu akawambia ndungu zake na nyumba ya baba yake, "Nitakwenda na kumwambia Farao, kusema, 'Ndugu zangu na nyumba ya baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia.
\v 32 Watu hawa ni wafugaji, kwani wamekuwa watunza wanyama. Wamekuja na makundi yao ya kondoo, na mbuzi, na vyote walivyonavyo.'
\s5
\v 33 Itakuwa, Farao atakapowaita na kuwauliza, 'Kazi yenu ni ipi?'
\v 34 mwambieni, 'Watumishi wako wamekuwa watunza wanyama tangu ujana wetu mpaka sasa, sisi, na baba zetu.' Fanyeni hivyo ili mweze kuishi katika nchi ya Gosheni, kwani kila mfugaji ni chukizo kwa Wamisri."
\s5
\c 47
\p
\v 1 Kisha Yusufu akaingia kwa Farao na kumwambia, "Baba yangu na ndugu zangu, kondoo wao, mbuzi wao, na yote waliyonayo, wamefika kutoka katika nchi ya Kanaani. Tazama, wapo katika nchi ya Gosheni."
\v 2 Akawachukua watano katika ndugu zake na kuwatambulisha kwa Farao.
\s5
\v 3 Farao akawambia ndugu zake, "Kazi yenu ni nini?" Wakamwambia Farao, "Watumishi wako ni wafugaji, kama mababu zetu."
\v 4 Kisha wakamwambia Farao, "Tumekuja kukaa kwa muda katika nchi. Hakuna malisho kwa ajili ya makundi ya watumishi wako, kwa maana njaa ni kali sana katika nchi ya Kanaani. Hivyo, tafadhari waache watumishi wako wakae katika nchi ya Gosheni."
\s5
\v 5 Kisha Farao akamwambia Yusufu, kusema, "Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako.
\v 6 Nchi ya Misri iko mbele yako. Mkalishe baba yako na ndugu zako katika eneo zuri, nchi ya Gosheni. Ikiwa unafahamu watu wenye uwezo miongoni mwao, uwaweke kuwatunza wanyama wangu."
\s5
\v 7 Kisha Yusufu akamwingiza Yakobo baba yake na kumweka mbele ya Farao. Yakobo akambariki Farao.
\v 8 Farao akamwambia Yakobo, "Umeishi kwa muda gani?"
\v 9 Yakobo akamwambia Farao, "Miaka ya safari zangu ni mia moja na thelathini. Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi na ya maumivu. Siyo kama miaka ya baba zangu."
\v 10 Kisha Yakobo akambariki Farao na kuondoka mbele zake.
\s5
\v 11 Kisha Yusufu akamweka baba yake na ndugu zake. Akawapa eneo katika nchi ya Misri, sehemu nzuri sana ya nchi, katika eneo la Ramesesi, kama Farao alivyokuwa ameagiza.
\v 12 Yusufu akamhudumia baba yake kwa chakula, ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake, kulingana na hesabu ya wahitaji wao.
\s5
\v 13 Basi hakukuwa na chakula katika nchi yote; kwani njaa ilikuwa kali sana. Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani ikaharibika kwa sababu ya njaa.
\v 14 Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake chakula. Kisha Yusufu akaleta ile pesa katika kasri la Farao.
\s5
\v 15 Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, "Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?"
\v 16 Yusufu akasema, "Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu."
\v 17 Hivyo wakaleta wanyama wao kwa Yusufu. Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo, mbuzi na kwa punda. Akawalisha kwa mkate kwa kubadilisha na wanyama wao mwaka ule.
\s5
\v 18 Mwaka ule ulipokwisha, wakaja kwake mwaka uliofuata na kumwambia, "Hatutaficha kwa bwana wangu kwamba pesa yetu yote imekwisha, na wanyama ni wa bwana wangu. Hakuna kilichobaki mbele za bwana wangu, isipokuwa miili yetu na nchi yetu.
\v 19 Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu.
\s5
\v 20 Hivyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Kwani kila Mmisri akauza shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana. Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao.
\v 21 Na watu, akawafanya kuwa watumwa kutoka mpaka mmoja wa Misri hata mkapa mwingine.
\v 22 Ilikuwa ni nchi ya makuhani pekee ambayo Yusufu hakuinunua, kwa maana makuhani walikuwa wakipewa posho. Walikula katika sehemu aliyowapa Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
\s5
\v 23 Kisha Yusufu akawambia watu, "Tazama, nimewanunua ninyi na nchi yenu leo kwa ajili ya Farao. Basi mbegu hii hapa kwa ajili yenu, nanyi mtapanda katika nchi.
\v 24 Wakati wa mavuno, mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu, kwa mbegu za shamba na kwa chakula cha nyumba zenu na watoto wenu."
\s5
\v 25 Wakasema, "Umeokoa maisha yetu. Na tupate kibali machoni pako. Tutakuwa watumishi wa Farao."
\v 26 Hivyo Yusufu akaifanya kuwa sheria inayofanya kazi hata leo katika nchi ya Misri, kwamba moja ya tano ni ya Farao. Eneo la makuhani peke yake ndo halikufanywa kuwa la Farao.
\s5
\v 27 Hivyo Israeli akaishi katika nchi ya Misri, katika eneo la Gosheni. Watu wake wakapata umiliki pale. Walikuwa wenye kuzaa na kuongezeka sana.
\v 28 Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, kwa hiyo miaka ya maisha ya Yakobo ilikuwa miaka mia moja arobaini na saba.
\s5
\v 29 Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia, alimwita Yusufu mwanaye na kumwambia, "Ikiwa nimepata kibali mbele zako, weka mkono wako chini ya paja langu, na unitendee kwa uaminifu na kweli. Tafadhari usinizike Misri.
\v 30 Nitakapolala na baba zangu, utanitoa Misri na kunizika katika eneo la kuzikia la baba zangu." Yusufu akasema, "Nitafanya kama ulivyosema."
\v 31 Israeli akasema, "Niapie," na Yusufu akamwapia. Kisha Israeli akainama chini mbele ya kitanda chake.
\s5
\c 48
\p
\v 1 Ikawa baada ya mambo haya, mmojawapo akamwambia Yusufu, "Tazama, baba yako ni mgonjwa." Hivyo akaondoka pamoja na wanawe wawili, Manase na Efrahimu.
\v 2 Yakobo alipoambiwa, "Tazama, mwanao Yusufu amekuja kukuona," Israeli akakusanya nguvu na kukaa juu ya kitanda.
\s5
\v 3 Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani. Akanibariki na
\v 4 kuniambia, 'Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele.'
\s5
\v 5 Na sasa wanao wawili, waliozaliwa kwako katika nchi ya Misri kabla sijaja Misri, ni wangu. Efrahimu na Manase watakuwa wangu, kama walivyo Rubeni na Simioni.
\v 6 Watoto utakaowapata baada ya hapo ni wako; watahesabiwa katika majina ya ndugu zao katika urithi wao.
\v 7 Lakini kwangu mimi, nilipokuja kutoka Padani, kwa uzuni yangu Raheli alikufa njiani katika nchi ya Kanaani, wakati kungalipo kitambo kwenda Efrathi. Nilimzika pale katika njia iendayo Efrathi" (ndio, Bethlehemu).
\s5
\v 8 Israeli alipowaona wana wa Yusufu, akasema, "Ni nani hawa?"
\v 9 Yusufu akamwambia baba yake, "Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa:" Israeli akasema, "Walete kwangu, kwamba niwabariki."
\v 10 Basi macho ya Israeli yalikuwa yanashindwa kwa ajili ya umri wake, hivyo hakuweza kuona. Hivyo Yusufu akawasogeza karibu yake, na akawabusu na kuwakumbatia.
\s5
\v 11 Israeli akamwambia Yusufu, "Sikutazamia kuuona uso wako tena, Lakini Mungu ameniruhusu kuwaona hata wanao."
\v 12 Yusufu akawaondoa kati ya magoti ya Israeli, na kisha akainama na uso wake juu ya nchi.
\v 13 Yusufu akawachukua wote wawili, Efrahimu katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli, na akawasogeza kwake.
\s5
\v 14 Israeli akainua mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kichwa cha Efrahimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto juu ya kichwa cha Manase. Akaipishanisha mikono yake, kwani Manase ndiye alikuwa mzaliwa wa kwanza.
\v 15 Israeli akambariki Yusufu, akisema, Mungu ambaye mbele zake baba zangu Ibrahimu na Isaka walitembea, Mungu aliyenilinda hata leo,
\v 16 malaika walionilinda na madhara yote, awabariki vijana hawa. Jina langu na litajwe kwao, na majina ya baba zangu Ibrahimu na Isaka. Na wawe makutano ya watu juu ya nchi."
\s5
\v 17 Yusufu alipoona baba yake ameweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Efrahimu, haikumpendeza. Akauchukuwa mkono wa baba yake auweke katika kichwa cha Manase.
\v 18 Yusufu akamwambia baba yake, "Sivyo babangu; kwani huyu ndiye mzaliwa wa kwanza. Uweke mkono wako juu ya kichwa chake."
\s5
\v 19 Baba yake akakataa na kusema, "Ninafahamu, mwanangu, nafahamu. Yeye naye atakuwa watu, naye pia atakuwa mkuu. Lakini mdogo wake atakuwa mkuu kuliko yeye, na uzao wake utakuwa wingi wa mataifa."
\v 20 Israeli akawabariki siku hiyo kwa maneno haya, "Watu wa Israeli watatamka baraka kwa majina yenu wakisema, Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase'. "Kwa njia hii, Israeli akamweka Efrahimu mbele ya Manase.
\s5
\v 21 Israeli akamwambia Yusufu, "Tazama, ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu.
\v 22 Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu."
\s5
\c 49
\p
\v 1 Kisha Yakobo akawaita wana wake, na kusema: "Jikusanyeni pamoja, ili niwaambie yatakayowapata nyakati zijazo.
\v 2 Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.
\s5
\v 3 Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu, aliyesalia katika heshima na nguvu.
\v 4 Asiyezuilika kama maji yarukayo, hautakuwa na umaharufu, kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulikipanda kwa kuvizia.
\s5
\v 5 Simoni na Lawi ni ndugu. Panga zao ni silaha za vurugu.
\v 6 Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe.
\s5
\v 7 Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili. Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli.
\s5
\v 8 Yuda, ndugu zako watakusifu. Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watainama mbele zako
\s5
\v 9 Yuda ni mwana simba. Mwanangu, umetoka katika mawindo yako. Alisimama chini, alijikunyata kama simba, kama simba jike. Je nana atakayejaribu kumwamsha?
\s5
\v 10 Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake, hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii.
\s5
\v 11 Kumfunga punda wake kwenye mzabibu, na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri, amefua mavazi yake katika divai, na kanzu yake katika damu ya vichala vya mzabibu.
\v 12 Macho yake yatakuwa mausi kama mvinyo, na meno yake meupe kama maziwa.
\s5
\v 13 Zabuloni atakaa katika fukwe ya bahari. Atakuwa bandari kwa ajili ya meli, na mpaka wake utakuwa hata Sidoni.
\s5
\v 14 Isakari ni punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya kondoo.
\v 15 Anaona mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza. Atainamisha bega lake kwa mzigo na kuwa mtumishi wake.
\s5
\v 16 Dani atawaamua watu wake kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
\v 17 Dani atakuwa nyoka kando ya njia, nyoka mwenye sumu aumaye visigino vya farasi katika njia, hivyo aongozaye farasi huanguka nyuma.
\v 18 Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.
\s5
\v 19 Gadi - wapanda farasi watamshambulia, lakini yeye atawapiga katika visigino vyao.
\v 20 Vyakula vya Asheri vitakuwa vingi, naye ataandaa vyakula vya kifalme.
\v 21 Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri.
\s5
\v 22 Yusufu ni tawi lizaalo, tawi lizaalo karibu na kijito, ambaye matawi yake yako juu wa ukuta.
\v 23 Mpiga mishale atamshambulia na kumrushia na kumsumbua.
\s5
\v 24 Lakini upinde wake utakuwa imara, na mikono yake itakuwa hodari kwa sababu ya mikono ya Mwenyenguvu wa Yakobo, kwa ajili ya jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli.
\s5
\v 25 Mungu wa baba yako atakusaidia na Mungu Mwenye enzi atakubariki kwa baraka mbinguni juu, baraka za vilindi vilivyo chini, na baraka za maziwa na tumbo.
\s5
\v 26 Baraka za baba yako ni kuu kuliko baraka za milima ya zamani au vitu vilivyotamaniwa vya milima ya kale. Na viwe katika kichwa cha Yusufu, hata juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake.
\s5
\v 27 Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa. Wakati wa asubuhi atalarua mawindo, na jioni atagawa mateka."
\s5
\v 28 Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli. Hiki ndicho baba yao alichowambia alipowabariki. Aliwabariki kila mmoja kwa baraka iliyomstahili.
\v 29 Kisha akawaelekeza na kuwaambia, "Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti,
\v 30 katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia.
\s5
\v 31 Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea.
\v 32 Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi."
\v 33 Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake
\s5
\c 50
\p
\v 1 Yusufu akahuzunika sana hata akauangukia uso wa baba yake, akamlilia, na kumbusu.
\v 2 Yusufu akawaagiza watumishi wake matabibu kumtia dawa babaye. Hivyo matabibu wakampaka dawa Israeli.
\v 3 Wakatimiza siku arobain, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini
\s5
\v 4 Siku za maombolezo zilipotimia, Yusufu akaongea na watumishi wa baraza la kifalme wa Farao kusema, "Ikiwa nimepata kibali machoni penu, tafadharini ongeeni na Farao, kusema,
\v 5 'Baba yangu aliniapisha, kusema, "Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika." Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi."
\v 6 Farao akajibu, "Nenda na umzika baba yako, kama alivyokuwapisha."
\s5
\v 7 Yusufu akaenda kumzika baba yake. Maofisa wa Farao wote wakaenda pamoja naye - washauri wa nyumba yake, maofisa waandamizi wote wa nchi ya Misri,
\v 8 pamoja na nyumba yote ya Yusufu na ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake. Lakini watoto wao, kondoo wao na makundi ya mbuzi wao yaliachwa katika nchi ya Gosheni.
\v 9 Vibandawazi na wapanda farasi pia walikwenda pamoja naye. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu.
\s5
\v 10 Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale.
\v 11 Wenyeji wa nchi, Wakanaani, walipoona maombolezo katika sakafu ya Atadi, wakasema, "Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri." Ndiyo maana eneo hilo likaitwa Abeli Mizraimu, lililoko mbele ya Yordani.
\s5
\v 12 Hivyo wanawe wakamfanyia Yakobo kama alivyokuwa amewaagiza.
\v 13 Wana wake wakampeleka katika nchi ya Kanaani na wakamzika katika pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre. Ibrahimi alikuwa amelinunua pango pamoja na shamba kwa ajili ya eneo la kuzikia. Alikuwa amelinunua kutoka kwa Efroni Mhiti.
\v 14 Baada ya kuwa amemzika babaye, Yusufu akarudi Misri, yeye, pamoja na ndugu zake, na wote waliokuwa wamemsindikiza ili kumzika babaye.
\s5
\v 15 Nduguze Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, "Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia na akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda?"
\v 16 Hivyo wakamwagiza Yusufu, kusema, "Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema,
\v 17 'Mwambieni hivi Yusufu, "Tafadhari samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda." Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako." Yusufu akalia walipomwambia.
\s5
\v 18 Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, "Tazama, sisi ni watumishi wako."
\v 19 Lakini Yusufu akawajibu, "Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu?
\v 20 Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo.
\v 21 Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo." Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole.
\s5
\v 22 Yusufu akakaa Misri, pamoja na familia ya baba yake. Akaishi miaka mia moja na kumi.
\v 23 Yusufu akawaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu. Pia aliwaona wana wa Makiri mwana wa Manase, waliowekwa katika magoti ya Yusufu.
\s5
\v 24 Yusufu akawambia ndugu zake, "Ninakaribia kufa; lakini kwa hakika Mungu atawajilia na kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nch aliyoapa kumpa Ibrahimu, kwa Isaka na kwa Yakobo."
\v 25 Kisha Yusufu akawaapisha watu wa Israeli kwa kiapo. Akasema, "Bila shaka Mungu atawajilia. Wakati huo mtachukuwa mifupa yangu kutoka hapa."
\v 26 Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.

2240
02-EXO.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2240 @@
\id EXO
\ide UTF-8
\h Kutoka
\toc1 Kutoka
\toc2 Kutoka
\toc3 exo
\mt Kutoka
\s5
\c 1
\p
\v 1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli waliokuja Misri pamoja na Yakobo kila moja na familia yake:
\v 2 Rubeni, Simioni, Lawi, na Yuda,
\v 3 Isakari, Zebuluni, na Benjamini,
\v 4 Dani, Naftali, Gadi, na Asheri.
\v 5 Jumla ya watu wa ukoo wa Yakobo walikuwa sabini. Yusufu alikuwa Misri tayari.
\s5
\v 6 Ndipo Yusufu, pamoja na kaka zake wote, na kizazi chote wakafa.
\v 7 Waisraeli walifanikiwa sana, wakaongezeka sana idadi yao, na wakawa na nguvu maana nchi ilijazwa na wao.
\s5
\v 8 Wakati huu sasa mfalme mpya asiyemjua Yusufu aliinuka katika Misri.
\v 9 Akawaambia watu wake, "Tazama, hawa Waisraeli ni wengi na wenye nguvu kuliko sisi.
\v 10 Njooni na tukae nao kwa akili, ama sivyo wataendelea kuongezeka na kama vita ikiibuka, wataungana na adui zetu, watapigana nasi, na kisha wataondoka."
\s5
\v 11 Hivyo wakawekea walinzi ambao waliwatesa kwa kuwatumikisha kazi ngumu. Waisraeli walijenga maghala ya miji kwa ajili ya Farao: Pishoni na Ramsei.
\v 12 Lakini kadiri Wamisri walivyowatesa, ndivyo Waisraeli waliendelea kuongezeka na kusambaa. Hivyo Wamisri wakaanza kuwaogopa Waisraeli.
\s5
\v 13 Wamisri waliwafanya Waisraeli wafanye kazi kwa nguvu nyingi.
\v 14 Waliyafanya maisha yao kuwa machungu kwa kuwafanyisha kazi ngumu kwa vinu na matofali na kwa kila aina ya kazi za shambani. Kazi zao zote zilikuwa ngumu.
\s5
\v 15 Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kiebrania; mmoja wao aliitwa jina lake Shifra, na mwingine aliitwa Puha.
\v 16 Akasema, "Wakati mnapowasaidia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, chunguzeni wanapozaa. Ikiwa ni mtoto wa kiume, basi muueni; bali ikiwa ni mtoto wa kike, basi mwacheni aishi."
\v 17 Lakini wale Wakunga walimwogopa Mungu na hawakufanya kama mfalme wa Misri alivyowaagiza; badala yake waliwaacha watoto wa kiume waishi.
\s5
\v 18 Mfalme wa Misri akawaita Wakunga na kuwaambia, "Kwanini mmefanya haya, na kuwaacha watoto wa kiume wakaishi?"
\v 19 Wale Wakunga wakamjibu Farao, "Hawa wanawake wa Kiebrania siyo kama wanawake wa Kimisri. Hawa wana nguvu na jasiri sana maana wao humaliza kuzaa kabla hata mkunga hajafika."
\s5
\v 20 Mungu aliwalinda hawa Wakunga. Watu waliongezeka kwa idadi na kuwa na nguvu sana.
\v 21 Kwa sababu wale Wakunga walimwogopa Mungu, aliwapa familia.
\v 22 Farao akawaagiza watu wote, "Lazima mmutupe kila mtoto wa kiume anayezaliwa katika mto, lakini kila mtoto wa kike wamwache aishi."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Sasa mwanamme wa kabila la Lawi alimuoa mwanamke Mlawi.
\v 2 Yule mwanamke akapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Alipoona ya kuwa alikuwa mtoto mwenye afaya, alimficha kwa miezi mitatu.
\s5
\v 3 Lakini alipokuwa hawezi kuendelea kumficha tena, alichukua kikapu cha manyasi akakipaka sifa na lami. Akamtia mtoto ndani yake na kukiweka juu ya maji katika majani kando ya mto.
\v 4 Dada yake akasimama kwa mbali ili ajue yatakayompata.
\s5
\v 5 Binti Farao akashuka kuoga mtoni wakati vijakazi wake wakitembea kando ya mto. Naye akaona kile kikapu katika majani na akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.
\v 6 Alipokifungua, aliomwona mtoto. Tazama, mtoto alikuwa analia. Alimhurumia na kusema, "Bila shaka huyu ni mmoja wapo wa watoto wa Waebrania."
\s5
\v 7 Basi dada wa yule mtoto akamwambia binti Farao, "Je naweza kwenda kukutafutia mwanamke wa Kiebrania aje akulele mtoto kwa ajili yako?"
\v 8 Binti Farao akamwambia, "Nenda." Hivyo yule binti akaenda na kumwita mama yake yule mtoto.
\s5
\v 9 Binti Farao akamwambia mama yake yule mtoto, "Mchukue mtoto huyu ukaninyonyeshee, nami nitakupa posho." Hivyo yule mwanamke akamchukua mtoto na kumnyonyesha.
\v 10 Mtoto alipokuwa mkubwa, akamleta kwa binti Farao, na akawa mtoto wake. Akamwita jina lake Musa akisema, "Kwa sababu nilimtoa katika maji."
\s5
\v 11 Musa alipokuwa mtu mzima, alienda kwa watu wake na kuona kazi ngumu walizokuwa wanafanya. Alimuona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmoja wa watu wa jamii yake.
\v 12 Aliangalia huku na kule, na alipoona ya kuwa hakuna mtu, alimuua yule mmisri na kuuficha mwili wake katika mchanga.
\s5
\v 13 Alienda tena siku iliyofuata, na tazama, Waebrania wawili walikuwa wanapigana. Alimwambia yule aliyekuwa na makosa, "Kwa nini unampigia mwenzako?"
\v 14 Lakini yule mtu alisema, "Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi juu yetu? Unataka kuniua na mimi kama ulivyomuua yule mmisri?" Ndipo Musa akaogopa na kusema, "Hakika niliyoyafanya yamejulikana."
\s5
\v 15 Farao aliposikia habari hizi, alijaribu kumuua Musa. Lakini Musa alikimbia na kwenda kuishi katika nchi ya Wamidiani. Kule alikaa chini kando ya mto.
\v 16 Wakati huo kuhani wa Midiani alikuwa na mabinti saba. Walikuja mtoni kuchota maji na kujaza vyombo vyao ili wawanyweshe mifuko ya baba yao.
\v 17 Wachungaji walikuja na kutaka kuwafukuza, lakini Musa alienda kuwasaidia. Kisha akawanywesha mifugo wao.
\s5
\v 18 Wale mabinti walipoenda kwa Reueli baba yao, aliwauliza, "Kwa nini mmerudi nyumbani mapema hivi leo?"
\v 19 Wakamwambia, "Mmisri mmoja alituokoa dhidi ya wachungaji. Pia alichota maji na kuwanywesha mifugo wetu."
\v 20 Kisha akawauliza binti zake, "Yu wapi sasa? Kwa nini mlimwacha? Mwiteni ili apate kula chakula pamoja nasi."
\s5
\v 21 Musa akakubali kukaa na yule mtu ambaye pia alimpa binti yake Zipora ili amuoe.
\v 22 Alizaa mtoto wa kiume, na Musa akamwita jina lake Geshomu; akisema; "Nimekuwa mkazi katika nchi ya ugeni."
\s5
\v 23 Muda mrefu baadaye, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli walilalamika kwa sababu ya kazi za utumwa. Walilia kutafuta msaada, na maombi yao yakamfikia Mungu kwa sababu ya mateso yao.
\v 24 Mungu aliposikia malalamiko yao, Mungu alikumbuka agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.
\v 25 Mungu aliwaona Waisraeli na akaielewa hali yao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Wakati huu Musa aliendelea kuchunga mifugo ya Yethro baba mkwe wake, kuhani wa Midiani. Musa aliliongoza kundi la mifugo kuelekea upande wa mbali wa jangwa mpaka kufika Horebu, mlima wa Mungu.
\v 2 Akiwa pale malaika wa Yahwe akamtokea kama mwali wa moto katika kichaka. Musa aliangalia, na tazama, kichaka kiliwaka moto lakini hakikuteketea.
\v 3 Musa akasema, "Nitageuka ili nione kitaku hiki cha ajabu, kwa nini kichaka hakiteketei."
\s5
\v 4 Yahwe alipoona ya kuwa amegeuka upande ili aone, Mungu alimwita kutoka katika kile kichaka na kusema, "Musa, Musa." Musa akasema, "Mimi hapa."
\v 5 Mungu akasema, "Usinikaribie! Vua viatu katika miguu yako, kwa kuwa mahali uliposimama ni mahali palipowekwa wakfu kwa ajili yangu."
\v 6 Aliongeza kusema, "Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo." Kisha Musa akaufunika uso wake, kwa kuwa aliogopa kumwangalia Mungu.
\s5
\v 7 Yahwe akasema, "Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri. Nimesikia kelele zao kwa sababu ya mabwana wao, kwa kuwa nayajua mateso yao.
\v 8 Nimekuja chini kuwaokoa dhidi ya mamlaka ya Wamisri na kuwatoa katika nchi ile na kuwaleta katika nchi nzuri, pana, nchi ijaayo maziwa na asali; kwenye ukanda wa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
\s5
\v 9 Sasa kilio cha watu wa Israeli kimenifikia mimi. Zaidi sana, Mimi nimeyaona mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
\v 10 Sasa basi, nitakutuma wewe kwa Farao ili upate kuwatoa watu wangu, wana wa Israeli, kutoka katika nchi ya Misri."
\s5
\v 11 Lakini Musa akamwambia Mungu, "Mimi ni nani hata niende kwa Farao na kuwatoa Waisraeli kutoka Misri?"
\v 12 Mungu akamjibu, "Hakika nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako ya kuwa nimekutuma. Utakapokuwa umewatoa watu kutoka Misri, mtaniabubu mimi katika mlima huu."
\s5
\v 13 Musa akamwambia Mungu, "Nikienda kwa Waisraeli na kuwaambia, 'Mungu wa baba zenu amenituma mimi kwenu,' na kisha wakiniambia, 'jina lake nani?' nitawaambia nini?"
\v 14 Mungu akamwambia Musa, "MIMI NIPO AMBAYE NIPO." Mungu akasema, "Ni lazima uwaambie Waisraeli, "MIMI NIPO amenituma kwenu."
\v 15 Pia Mungu akamwambia Musa, "Lazima uwaambie Waisraeli, 'Yahwe, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma mimi kwenu. Hili ndio jina langu milele, na hivi ndivyo nitakavyokumbukwa na vizazi vyote.'
\s5
\v 16 Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja. Waambie, 'Yahwe, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, wa Isaka na Yakobo, amenitokea mimi na kusema, "Hakika nimewatazama na nimeona yale mliyotendewa huko Misri.
\v 17 Nimeahidi kuwatoa ninyi katika mateso ya Misri na kuwaleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Wamwori, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi. Nchi ijaayo maziwa na asali."
\v 18 Watakusikiliza. Wewe pamoja na wazee wa Israeeli itawapasa kwenda kwa mfalme wa Misri, na imewapasa kumwambia, 'Yahwe, Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Hivyo tuache sisi twende safari ya siku tatu katika jangwa ili tupate kutoa sadaka kwa Yahwe Mungu wetu.'
\s5
\v 19 Lakini nafahamu ya kuwa mfalme wa Misri hatawaacha ninyi mwende, isipokuwa kwa kulazimishwa.
\v 20 Nitainua mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa miujiza yote nitakayoifanya kati yao. Baada ya hayo, atawaacha mwende.
\v 21 Nitawapa watu hawa kufadhiliwa kutoka kwa Wamisri ili muondokapo msiende mikono mitupu.
\v 22 Kila mwanamke ataomba kwa jirani yake Mmisri na kwa kila mwanamke akaaye kwenye nyumba ya jirani yake, vyombo vya fedha na vya dhahabu na nguo. Nanyi mtawavika watoto wenu wa kiume na binti zenu. Kwa njia hii mtawateka nyara Wamisri."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Musa akajibu, "Lakini itakuwaje wasiponiamini mimi au wasiponisikiliza na kusema, 'Yahwe hajakutokea wewe?"
\v 2 Yahwe akamwambia, "Hicho ni nini mkononi mwako?" Musa aksema, "Ni fimbo."
\v 3 Yahwe akasema, "Itupe chini." Musa akaitupa chini ile fimbo, nayo ikageuka na kuwa nyoka. Musa akarudi nyumba.
\s5
\v 4 Yahwe akamwambia Musa, "Mchukue kwa kumshikia mkia wake." Hivyo alimchukua yule nyoka. Mara ikaggeuka na kuwa fimbo mkononi mwake tena.
\v 5 "Hii ni ili wapate kuamini ya kuwa Yahwe, Mungu wa baba zao, Mungu wa wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amekutokea wewe."
\s5
\v 6 Yahwe pia alimwambia, "Sasaingiza mkono wako ndani ya vazi lako." Hivyo Musa akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake. Na alipoutoa nje, tazama, mkono wake ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.
\v 7 Yahwe akasema, "Ingiza mkono wako ndani ya vazi lako tena." Hivyo akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake, na alipoutoa nje aliona ukiwa mzima tena kama ulivyo mwili wake wote.
\s5
\v 8 Yahwe akasema, "Kama hawatakuamini wewe - kama hawatazingatia ishara yanggu ya kwanza ya nguvu zangu au kuziamini, basi wataamini ishara ya pili.
\v 9 Na ikiwa hawataamini hata ishara hizi zote mbili za nguvu zangu, au wasipokusikiliza wewe, basi chota maji kutoka katika mto na uyamwage katika nchi kavu. Maji utakayoyamwaga yatakuwa damu katika nchi kavu."
\s5
\v 10 Ndipo Musa akamwambia Yahwe, "Bwana, mimi ni mzuri wa kuongea, si hapo kwanza au hata baada ya kuwa umeongea na mtumishi wako. Mimi ni mdhaifu wa kuongea na nina kigugumizi."
\v 11 Yahwe akamwambia, "Ni nani anayeumba mdomo wa mwanadamu? Ni nani amfanyaye mwanadamu kuwa bubu au aone au kipofu? Je si mimi Yahwe?
\v 12 Sasa nenda, nami nitauongoza mdomo wako na nitakufundisha cha kusema."
\v 13 Lakini Musa akasema, "Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine, yeyote unayependa kumtuma."
\s5
\v 14 Kisha Yahwe akamkasirikia Musa. Akasema, "Vipi kuhusu Aroni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha.
\v 15 Wewe utaongea naye na utaweka maneno ya kusema kinywani mwake. Nami nitakiongoza kinywa chako na kinywa chake pia, nami nitaonesha ninyi nyote yawapasayo kutenda.
\v 16 Yeye ataongea na watu kwa niaba yako. Yeye atakuwa msemaji wako, na wewe utakuwa kama Mungu kwake.
\v 17 Utachukua hii fimbo pamoja nawe mkononi mwako. Kwa fimbo hii utafanya ishara."
\s5
\v 18 Hivyo Musa alirudi kwa Yethro - baba mkwe wake na kumwambia, "Niruhusu nipate kurudi kwa ndugu zangu walioko Misri ili niweze kuona kama bado wako hai." Yethro akwambia Musa, "Nenda kwa amani."
\v 19 Yahwe akamwambia Musa kule Midiani, "Nenda, rudi Misri, kwa kuwa watu wote waliotaka kukuua wameshakufa."
\v 20 Musa akamchukua mke wake na watoto wake wa kiume na kuwapandisha kwenye punda. Akarudi mpaka nchi ya Misri, naye alichukua fimbo ya Mungu pamoja naye mkononi mwake.
\s5
\v 21 Yahwe akamwambia Musa, "Utakaporudi Misri, jitahidi kufanya ishara zote nilizokupa kufanya mbele ya Farao. Lakini nitaufanya moyo wake kuwa mgumu, naye hawatawaacha watu waende.
\v 22 Lazima umwambie Farao, 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Israeli ni mtoto wangu, mzaliwa wa kwanza wangu,
\v 23 nami nakuamuru, "Mwache mwanangu aende ili apate kuniabudu mimi." Lakini kwa kuwa umekataa kumwachia, hakika nitamuua mtoto wako wa kiume, mzaliwa wa kwanza wako."'
\s5
\v 24 Sasa wakiwa njiani, wakati wa usiku walipopumzika, Yahwe alikutana na Musa na kutaka kumuua.
\v 25 Kisha Zipora akachukua kisu kikali na kukata govi la mtoto wake wa kiume na kuligusisha miguuni pake. Kisha akasema, "Hakika wewe ni bwana harusi wangu kwa njia ya damu."
\v 26 Hivyo Yahwe akamwachia. Akasema, "Wewe ni bwana harusi wa damu" kwa sababu ya kutahiriwa.
\s5
\v 27 Yahwe akamwambia Aroni, "Nenda nyikani ukutane na Musa." Aroni akaenda na kukutana naye katika mlima wa Mungu, na kumbusu.
\v 28 Musa akwambia Aroni maneno yote ya Yahwe ambayo alimtuma kusema na kwa habari za ishara zote za nguvu za Yahwe ambazo alimwagiza kutenda.
\s5
\v 29 Kisha Musa na Aroni wakaenda na kuwakusanya wazee wote wa Israeli.
\v 30 Aroni akawaambia maneno yote ambayo Yahwe alimwambia Musa. Pia alionesha ishara na miujiza ya nguvu za Yahwe mbele ya watu.
\v 31 Watu waliamini. Waliposikia ya kuwa Yahwe aliwaona Waisraeli na ya kwamba aliyaona mateso yao, waliinamisha vichwa vyao na kumwabudu.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Baada ya mambo haya kutokea, Musa na Aruni walienda kwa Farao na kumwambia, ""Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli anasema: 'Waache watu wangu waende, ili wapate kunifanyia karamu jangwani.'"
\v 2 Farao akasema, "Yahwe ni nani? Kwa nini mimi nisikiliz sauti yake na kuwaacha Israeli waende? Mimi simjui Yahwe; na la zaidi, sitawaacha Israeli waende."
\s5
\v 3 Wakasema, "Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Tuache twende safari jangwani kwa siku tatu ili tutoe sadaka kwa Yahwe Mungu wetu ili asituadhibu kwa mapigo au kwa upanga."
\v 4 Lakini mfalme wa Misri aliwaambia, "Musa na Aruni, kwa nini mnawatoa watu kazini mwao? Nendeni kazini kwenu."
\v 5 Pia alisema, "Sasa kuna Waebrania wengi nchini mwetu, na ninyi mnawafanya waache kazi zao."
\s5
\v 6 Siku ile ile, Farao alitoa amri kwa wasimamizi na wanyapara wa wale watu. Akasema,
\v 7 "Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, "Tofauti ni ilivyokuwa awali, msiwapatie tena watu majani ya kutengenezea tofali. Waacheni wao waende kujitafutia majani wenyewe.
\v 8 Ingawa wanapaswa kuleta hesabu sawa ya matofali watakayotengeneza kama ilivyokuwa awali. Msipokee pungufu, kwasababu wao ni wavivu. Ndiyo maana wanapiga kelele na kusema, 'turuhusu tuende tukamtolee sadaka Mungu wetu.'
\v 9 Waongezeeni kazi wanaume ili wasipate tena muda wa kusikiliza maneno ya upotoshaji."
\s5
\v 10 Kwa hiyo viongozi wa watu na waangalizi wao waliwajulisha watu. Walisema, "Hivi ndivyo farao amesema: 'Sitawapeni tena malighafi.
\v 11 Nyinyi wenyewe mtaenda kutafuta majani popote mtakapopata, lakini kazi zenu hazitapunguzwa.
\s5
\v 12 Basi watu hao wakatawanyika katika nchi yote ya Misri ili wapate kukusanya matakataka badala ya majani.
\v 13 Wasimamizi wao wakawahimiza na kusema, "Malizeni kazi zenu, sawa na wakati ule majani yalipokuwapo."
\v 14 Wanyapara wa Farao wakawapiga wasimamizi wa Waisraeli, watu walewale ambao waliwaweka kuwa wasimamizi wa watumishi. Wale Wanyapara wakakazana kuwauliza, "Kwanini hamjatimiza idadi ya matofali inayotakiwa kwenu, siku ya jana na hata leo kama ambavyo mlifanya siku za nyuma?"
\s5
\v 15 Basi Wanyapara wa wana wa Israeli wakamwendea Farao na kumlilia. Walisema, "Kwanini unawatendea watumishi wako hivi?
\v 16 Sisi watumishi wako hatupewi majani tena, lakini bado wanatuambia sisi, "Tengenezeni tofali!' Sisi watumwa wako tunapigwa sasa, lakini kosa hilo ni la watu wako."
\v 17 Lakini Farao akasema, "Ninyi ni wavivu! Wavivu ninyi! Ninyi mwasema, 'Turuhusu twende kumtolea Yahwe sadaka.'
\v 18 Sasa rudini kazini. Hamtapewa majani tena, lakini mnapaswa kutengeneza idadi ile ile ya matofali."
\s5
\v 19 Wanyapara wa wana wa Israeli wakagundua ya kuwa walikuwa kwenye shida kubwa mara walipoambiwa, "Hamtapunguza kamwe idadi ya matofali mnayotengeneza kila siku."
\v 20 Wakakutana na Musa na Haruni, waliokuwa wamesimama nje ya Ikulu wakati wanatoka kwa Farao.
\v 21 Wakawaambia Musa na Haruni, "Yahwe awatazame ninyi na kuwaadhibu, kwa sababu mmetufanya sisi kuonekana wabaya mbele ya Farao na watumishi wake. Mmetia upanga mikononi mwao ili watuue."
\s5
\v 22 Musa akarudi kwa BWANA na kumwambia, "Bwana, kwanini umewatenda mabaya watu hawa? Kwanini kunituma mimi kwanza?
\v 23 Tangu nilipokuja kwa Farao kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa, wala hujawaokoa watu wako hata kidogo."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kisha Yahweh akasema na Musa, "Sasa utaona nitakacho fanya kwa Farao. Utaona hili, kwa kuwa ata waacha waenda kwa mkono wangu hodari. Kwasababu ya mkono wangu hodari, ata waondoa nje ya nchi."
\s5
\v 2 Mungu akasema na Musa na kumwambia, "Mimi ni Yahweh.
\v 3 Nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama Mungu mwenye nguvu; lakini kwa jina langu, Yahweh, sikujuliikana kwao.
\v 4 Pia niliimarisha agano langu na wao, ilikuwapatia nchi ya Kanani, nchi walioishi kama sio raia, nchi walio tanga tanga.
\v 5 Zaidi ya yote, nimesikia kilio cha Waisraeli ambao wa Misri wame wa chukua watumwa, na nimekumbuka agano langu.
\s5
\v 6 Kisha basi, sema kwa Waisraeli, 'Mimi ni Yahweh. Nitawatoa kwenye utumwa chini ya wa Misri, na kuwaweka huru na nguvu zao. Nitawaokoa kwa kudhihirisha nguvu zangu, na kwa matendo ya ajabu ya hukumu.
\v 7 Nitawaleta kwangu kama watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu. Mtajua kuwa mimi ndiye Yahweh Mungu wenu, aliye watoa kwenye utumwa chini ya wa Misri.
\s5
\v 8 Nitawaleta kwenye nchi niliyo muahidi kumpa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Nitawapa kama mali yenu. Mimi ni Yahweh."'
\v 9 Musa alipo waambia haya Waisraeli, hawakumsiliza kwasababu ya mateso magumu ya utumwa wao.
\s5
\v 10 Hivyo Yahweh akazungumza na Musa na kumwambia,
\v 11 "Nenda umwambie Farao, mfalme wa Misri, awaache watu wa Israeli waondoke kwenye nchi yake."
\v 12 Musa akamwambia Yahweh, "Kama Waisraeli hawajanisikiliza mimi, kwa nini Farao anisikillize mimi, tangu mimi sio mzuri wakuzungumza?"
\v 13 Yahweh akasema na Musa na Aruni. Akawapa amri ya Waisraeli na Farao, mfalme wa Misri, awatoe Waisraeli kutoka nchi ya Misri.
\s5
\v 14 Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao: wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Rubeni.
\v 15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli - mwana wa mwanamke wa Kanani. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Simeoni.
\s5
\v 16 Hapa yameorodheshwa majina ya wana wa Lawi, pamoja na uzo wao. Walikuwa ni Gerishoni, Kohathi, na Merari. Lawi aliishi mpaka alipo kuwa na miaka 137.
\v 17 Wana wa Gerishoni walikuwa Libni na Shimei.
\v 18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. Kohathi aliishi hadi miaka 133.
\v 19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hawa walikuja kuwa mababu wa ukoo wa Walawi, pamoja na uzao wao.
\s5
\v 20 Amramu alimuoa Yokebedi, dada yake baba yake. Alimzalia Aruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137 na akafa.
\v 21 Wana wa Izhari walikuwa Kora, Nefegi, na Zikri.
\v 22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elizafani na Sithri.
\s5
\v 23 Aruni alimuoa Elisheba, binti wa Aminadabu, dada wa Nashoni. Alimzaa Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.
\v 24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasa. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Wakora.
\v 25 Eleazari, mwana wa Aruni, alimuoa mmoja wa mabinti Wa Putieli. Alimzalia Fineazi. Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao miongoni mwa Walawi, pamoja na uzao wao.
\s5
\v 26 Hawa wanaume wawili walikuwa Musa na Aruni ambao Yahweh alisema, "Waleteni Waisraeli kutoka nchi ya Misri, kwa makundi ya wanaume wapiganaji."
\v 27 Aruni na Musa wakazungumza na Farao, mfalme wa Misri, awaruhusu Waisraeli watoke Misri. Hawa walikuwa Musa na Aruni wale wale.
\s5
\v 28 Pale Yahweh alipo zungumza na Musa katika nchi ya Misri,
\v 29 alimwambia, "Mimi ni Yahweh. Sema kwa Farao, mfalme wa MIsri, kila kitu nitacho kwambia."
\v 30 Lakini Musa alimwambia Yahweh, "Mimi sio mzuri wa kuongea, hivyo kwanini Farao anisikilize mimi?"
\s5
\c 7
\p
\v 1 Yahweh akasema na Musa, "Ona, nimekufanya kama mungu kwa Farao. Aruni kaka yako atakuwa nabii wako.
\v 2 Utasema kila kitu nitacho kuamuru kusema. Aruni kaka yako ata sema na Farao iliawaachie watu wa Israeli watoke kwenye nchi yake.
\s5
\v 3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao mgumu, na nitaonyesha ishara nyingi za nguvu zangu, maajabu mengi, katika nchi ya Misri.
\v 4 Lakini Farao hata kusikiliza, kwahiyo nitaueka mkono wangu juu ya Misri na kutoa makundi yangu ya wanaume wapiganaji, watu wangu, wazao wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa matendo makubwa ya hukumu.
\v 5 Wamisri watajua kuwa mimi ni Yahweh nitapo nyoosha mkono wangu kwa Misri na kuwatoa Waisraeli kutoka miongoni mwao."
\s5
\v 6 Musa na Aruni wakafanya hivyo; walifanya kama Yahweh alivyo waamuru.
\v 7 Musa alikuwa na miaka themanini, na Aruni miaka themanini na tatu walipo ongea na Farao.
\s5
\v 8 Yahweh akamwambia Musa na Aruni,
\v 9 "Wakati Farao atakapo waambia, 'Fanya muujiza,' utamwambia Aruni, 'Chukuwa gongo lako na ulirushe chini mbele ya Farao, ililigeuke nyoka."'
\v 10 Kisha Musa na Aruni wakaenda kwa Farao, na wakafanya kama Yahweh alivyo waamuru. Aruni akarusha chini gongo lake mbele ya Farao na watumishi wake, na likageuka nyoka.
\s5
\v 11 Kisha naye Farao akawaita wazee wenye hekima na wachawi. Wakafanya jambo hilo hilo kwa uchawi wao.
\v 12 Kila mtu akarusha chini gongo lake, na magongo yakawa nyoka. Lakini gongo la Aruni lilimeza nyoka zao.
\v 13 Moyo wa Farao ulikuwa mgumu, na akusikiliza, kama Yahweh alivyo tabiri.
\s5
\v 14 Yahweh akasema na Musa, "Moyo wa Farao ni mgumu, na anakataa kuacha watu waende.
\v 15 Nenda kwa Farao asubui anapoenda kwenye maji. Simama kwenye chanzo cha mto kukutana naye, na uchukuwe mkononi mwako gongo ambalo liligeuka nyoka.
\s5
\v 16 Mwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, amenituma kwako, "Acha watu wangu waende, iliwaniabudu nyikani. Mpaka sasa haujanisikiliza."
\v 17 Yahweh anasema hili: "Kwa hili utajua kuwa mimi ni Yahweh. Ninaenda kupiga maji ya mto wa Misri kwa gongo langu lililo mikono mwangu, na mto utageuzwa kuwa damu.
\v 18 Samaki walio kwenye mto watakufa, na mto utanuka. Wa Misri Hawataweza kunywa maji yalio kwenye mto."'''
\s5
\v 19 Kisha Yahweh akasema na Musa, "Mwambie Aruni, 'Chukuwa gongo lako na unyooshe mkono kwenye maji ya Misri, na juu ya mito yake, mifereji, visima, na madimbwi yote, ili maji yao ya damu. Fanya hivi ilikuwe na damu nchi nzima ya Misri, hadi kwenye vyombo vyote vya mbao na mawe."'
\s5
\v 20 Musa na Aruni walifanya kama Yahweh alivyo waamuru. Aruni alinyanyua gongo na kupiga maji ya mto, machoni pa Farao na watumishi wake. Maji yote kwenye mto yaligeuga damu.
\v 21 Samaki kwenye mto wakafa, na mto ukaanza kunuka. Wamisri hawakuweza kunywa maji kwenye mto, na damu ilikuwa kila mahali katika nchii ya Misri.
\v 22 Lakini wachawi walifanya vivyo hivyo na uchawi wao. Kwaiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, na akakataa kuwasikiliza Musa na Aruni, kama Yahweh alivyo sema itatokea.
\s5
\v 23 Kisha Farao akarudi na kwenda nyumbani kwake. Wala hakutilia maanani hili.
\v 24 Wamisri wote walichimba pembeni ya mto kwa ajili ya maji ya kunywa, lakini hawakuweza kunywa maji ya mto.
\v 25 Siku saba zilipita baada ya Yahweh kushambulia mto.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Kisha Yahweh akazungumza na Musa, "Nenda kwa Farao na umwambie, 'Yahweh anasema hivi: Acha watu wangu waende hili wakaniabudu.
\v 2 Ukikataa kuwaruhusu waende, nitaidhuru nchi yako yote kwa vyura.
\v 3 Mito itajawa na vyura. Watatoka na kuingia nyumbani kwako, chumbani kwako, na kitandani kwako. Wataenda nyumbani mwa watumishi wako. Wataenda kwa watu wako, kwenye majiko yako, na vyombo vya kukandia mkate.
\v 4 Vyura watakushambulia wewe, watu wako, na watumishi wako wote.""'
\s5
\v 5 Yahweh akamwambia Musa, "Mwambie Aruni, 'Nyoosha mkono wako na gongo lako kwenye mito, mifereji, na kwenye mabwawa, na uwatoe vyura juu ya nchi ya Misri."'
\v 6 Aruni akanyoosha mkono juu ya maji ya Misri, na vyura wakatoka na kujaza nchi ya Misri.
\v 7 Lakini wachawi walifanya vivyo hivyo na uchawi wao: waliwatoa vyura juu ya nchi ya Misri.
\s5
\v 8 Kisha Farao akawaita Musa na Aruni na kuwaambia, "Muombeni Yahweh iliawaondoe vyura kwangu na kwa watu wangu. Kisha nitawaacha watu waende, iliwamtolee dhabihu."
\v 9 Musa akamwambia Farao, "Unaweza chukuwa fursa ya kuniambia lini nikuombee wewe, watumishi wako, na watu wako, ili vyura waondolewe kwako na nyumbani kwako na wabaki tu kwenye mito."
\s5
\v 10 Farao akasema, "Kesho." Musa akasema, "Acha iwe kama ulivyo sema, ili kwamba ujue hakuna Mungu mwengine kama Yahweh, Mungu wetu.
\v 11 Vyura wataondoka kutoka kwako, nyumbani mwako, kwa watumishi wako, na kwa watu wako. Watabaki tu kwenye mito."
\v 12 Musa na Aruni wakaondoka kwa Farao. Kisha Musa akamlilia Yahweh kuhusu hao vyura alio waleta kwa Farao.
\s5
\v 13 Yahweh akafanya kama Musa alivyo omba: Vyura wakafa kwenye nyumba, nyuani, na mashambani.
\v 14 Watu wakawakusanya kwa mafungu, na nchi ikanuka.
\v 15 Lakini Farao alipoona kuna afadhali, aliufanya moyo wake kuwa mgumu na hakumsikiliza Musa na Aruni, kama Yahweh alivyo sema.
\s5
\v 16 Yahweh akamwambia Musa, "Mwambie Aruni, 'Nyoosha gongo lako na upige udongo chini, iliuwe chawa kati nchi yote ya Misri."'
\v 17 Wakanya hivyo: Aruni akanyoosha mkono wake na gongo lake. Akaupiga udongo wa ardhi. Chawa wakaja juu ya watu na wanyama. Udongo wote kwenye ardhi ukawa chawa katika nchi ya Misri.
\s5
\v 18 Wachawi walijaribu kufanya chawa kwa uganga wao lakini hawakuweza. Palikuwa na chawa kwa watu na kwa wanyama.
\v 19 Kisha wachawi wakamwambia Farao, "Hichi ni kidole cha Mungu." Lakini moyo wa Farao ulikuwa Mgumu, hivyo akakataa kuwasikiliza. Ilikuwa kama Yahweh alivyo sema Farao atafanya.
\s5
\v 20 Yahweh akamwambia Musa, "Inuka asubui mapema na usimame mbele ya Farao anapoenda mtoni. Umwambie, 'Yahweh anasema hivi: "Acha watu wangu waende wakaniabudu mimi.
\v 21 Lakini usipo acha watu wangu waende nitatuma kundi la nzi kwako, watumishi wako, na watu wako, na kwenye nyumba zenu. Nyumba za wa Misri zitajawa na makundi ya nzi, na ata ardhi wanayo simama itajawa na nzi.
\s5
\v 22 Lakini katika siku hiyo nitaitendea nchi ya Gosheni tofauti, nchi ambayo watu wangu wanaishi, ilikwamba kusiwe na makundi ya nzi huko. Hili litatokea ili kwamba mjue mimi ni Yahweh katika hii nchi.
\v 23 Nitaweka utofauti kati ya watu wangu na watu wako. Hii ishara ya nguvu zangu itatokea kesho""'
\v 24 Yahweh akafanya hivyo, na kundi kubwa la nzi likaja nyumbani mwa Farao na nyumbani mwa watumishi wake. Katika nchi yote ya Misri, nchi iliharibiwa na makundi ya nzi.
\s5
\v 25 Farao akawaita Musa na Aruni na kuwaambia, "Nendeni, mtolee Mungu wenu dhabihu kwenye nchi yetu."
\v 26 Musa akasema, "Sio vyema sisi kufanya hivyo, kwa kuwa dhabihu tunazo mtolea Yahweh Mungu wetu zinachukiza kwa Wamisri. Kama tutatoa dhabihu mbele ya macho yao zilizo chukizo kwa Wamisri, hawata tupiga mawe?
\v 27 Hapana, ni safari ya siku tatu kwenda nyikani ambayo lazima tuende, ili kiutoa dhabihu kwa Yahweh Mungu wetu, kama anavyo tuamuru."
\s5
\v 28 Farao akasema, "Nitakuruhusu kwenda kumtolea dhabihu Yahweh Mungu wenu nyikani. Ila usiende mbali sana. Niombee."
\v 29 Musa akasema, "Wakati tu nitakapoenda kutoka kwako, nitamuomba Yahweh ili makundi ya nzi yatoke kwako, wewe Farao, na watumishi wako na watu kesho. Lakini usifanye udhalimu tena kwa kutowaacha watu wetu waende kumtolea dhabihu Yahweh."
\s5
\v 30 Musa akaenda nje kutoka kwa Farao na kumuomba Yahweh.
\v 31 Yahweh akafanya kama Musa alivyo muomba: alitoa makundi ya nzi kutoka kwa Farao, watumishi wake, na watu wake. Hakuna ata mmoja aliye baki.
\v 32 Lakini Farao aliufanya moyo wake mgumu tena, na hakuwaacha watu waende.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha Yahweh akamwambia Musa, Nenda kwa Farao na umwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: "Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi."
\v 2 Lakini ukikataa kuwaruhusu waende, kama utaendelea kuwa bakiza nyuma,
\v 3 basi mkono wa Yahweh utakuwa kinyume dhidi ya mifugo yako shambani na kwa farasi, punda, ngamia, ng'ombe na kondoo, naitasababisha ugonjwa mbaya sana.
\v 4 Yahweh ata tendea tofauti mifugo ya Israeli na mifugo Misri: Haukuna mnyama wa Waisraeli ataye kufa.
\s5
\v 5 Yahweh ametenga muda; amesema, "Ni kesho ambapo nitafanya ilitukio katika nchi.""'
\v 6 Yahweh akafanya hivi siku iliyofuata: mifugo yote ya Misri ikafa. Lakini hamna mnyama wa Waisraeli aliye kufa, hamna mnyama ata mmoja.
\v 7 Farao akafanya utafiti, na tazama, hakuna mnyama ata mmoja aliye kufa. Lakini moyo wake ulikuwa mjeuri, hivyo hakuwaacha watu waende.
\s5
\v 8 Kisha Yahweh akawambia Musa na Aruni, "Chukuwa majivu na uyajaze mkononi kutoka kwenye tanuru. Wewe, Musa, lazima uyarushe juu wakati Farao akitazama.
\v 9 Yatakuwa vumbi safi nchi nzima ya Misri. Yatasababisha majipu na mafua kulipuka kwa watu na wanyama katika nchi yote ya Msri."
\v 10 Hivyo Musa na Aruni wakachukuwa majivu kutoka kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. KIsha Musa akarusha majivu juu. Majivu yakasababisha majipu na mafua kutokea kwa watu na wanyama.
\s5
\v 11 Waganga hawakuweza kumzuia Musa kwasababu ya majipu, kwasababu majipu yalikuwa kwao na kwa Wamisri wote.
\v 12 Yahweh akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, Farao hakuwasikiliza Musa na Aruni. Hili ndilo Yahweh alilo mwambia Musa Farao atalo fanya.
\s5
\v 13 Kisha Yahweh akamwambia Musa, Amka asubui mapema, simama mbele ya Farao, na umwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.
\v 14 Kwa muda huu nitatuma mapigo kwako wewe, kwa watumishi wako na watu wako. Nitafanya hivi ili ujue hakuna kama mimi kwenye dunia yote.
\s5
\v 15 Mpaka sasa ningeweza kuunyosha mkono wangu na kukushambulia wewe na watu wako kwa ugonjwa, na ungeondelewa kwenye nchi.
\v 16 Lakini ni kwa sababu hii nimekuruhusu uishi: ili kukuonyesha nguvu zangu, ili kwamba jina langu litangazwe dunia nzima.
\v 17 Bado unajiinua dhidi ya watu wangu kwa kuwaacha wasiende.
\s5
\v 18 Sikiliza! Kesho muda kama huu nita leta mvua ya mawe ya barafu kubwa, kama ambayo haijawai kuonekana Misri toka ilipo anza hadi sasa.
\v 19 Kisha sasa, tuma wanaume na ukusanye mifugo yako na vitu vyote ulivyo navyo mashambani sehemu salama. Kila mtu na mnyama aliyeko shambani na hajaletwa nyumbani - mawe ya barufu yatawashukia, na watakufa.""'
\s5
\v 20 Kisha hao wa watumishi wa Farao walio amini ujumbe wa Yahweh waka harakisha kuleta watumwa na mifugo yao ndani ya nyumba zao.
\v 21 Lakini hao ambao hawa kuchukuwa ujumbe wa Yahweh maanani waliacha watumwa wao na mifugo shambani.
\s5
\v 22 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Nyoosha mkono wako kuelekea mbingu ili kuwe na mawe ya barafu katika nchi yote ya Misri, kwa watu, kwa wanyama, na kwenye mimea yote shambani na nchi nzima ya Misri."
\v 23 Musa akanyoosha mkono na gongo lake kuelekea mbiguni, na Yahweh akatuma mngurumo, mawe ya barafu, na radi kwenye nchi. Pia alinyesha mvua kwenye nchi ya Misri.
\v 24 Hivyo kulikuwa na radi iliyo changanyika na mawe ya barafu, ilikuwa hatari sana, kuliko yeyote iliyowai kutokea kwenye nchi ya Misri tangu liwe taifa.
\s5
\v 25 Katika nchi yote ya Misri, barafu ya mawe ilipiga kila kitu kwenye shamba, watu na wanyama. Ilipiga kila mmea shambani na kuvunja kila mti.
\v 26 Isipo kuwa tu nchi ya Gosheni, walipo ishi Waisraeli, hapakuwa na mawe ya barafu.
\s5
\v 27 Kisha Farao akatuma wanaume wakawaite Musa na Aruni. Akawaambia, "Nimetenda dhambi wakati huu. Yahweh ni mwenye haki, na mimi na watu wangu ni waovu.
\v 28 Muombe Yahweh, kwasababu radi na barafu ya mawe imezidi. Nitawaacha muende, na hamtabaki tena hapa."
\s5
\v 29 Musa akamwambia, "Nitakapo ondoka tu kwenye mji, nitaitanua mikono yangu kwa Yahweh. Mngurumo utaacha, na hakutakuwa na barafu ya mawe tena. Kwa ili utajua kuwa nchi ni ya Yahweh.
\v 30 Lakini kwa wewe na watu wako, najua bado hamu mheshimu Yahweh Mungu."
\s5
\v 31 Sasa kitani na shayiri ziliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa katika kukomaa, na kitani ilikuwa imestawi.
\v 32 Lakini ngano na kusemethu hazikupigwa mana zinachelewa kukua.
\v 33 Musa alipo muacha Farao na mji, alitanua mikono yake kwa Yahweh; mngurumo na barafu ya mawe ikasimama, na mvua haikunyesha tena.
\s5
\v 34 Farao alipoona mvua, barafu ya mawe, na mngurumo umekatika, akatenda dhambi na kufanya moyo wake kuwa mgumu, pamoja na watumishi wake.
\v 35 Moyo wa Farao ulikuwa mgumu, hakuacha watu wa Israeli waende. Hivi ndivyo Yahweh alimwambia Musa Farao atafanya.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa, "Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake mgumu na moyo wa watumishi wake. Nimefanya hivi kuonyesha hizi ishara za nguvu zangu miongoni mwao.
\v 2 Pia nimefanya hivi ili muwaambie watoto wenu na wajukuu wenu vitu nilivyo fanya, jinsi nilivyo itendea Misri kwa ukali, na jinsi nilivyo onyesha aina tofauti za ishara za nguvu zangu miongoni mwao. Kwa hili mtajua kuwa mimi ni Yahweh."
\s5
\v 3 Hivyo Musa na Aruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, "Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: 'Kwa muda gani utaendelea kukataa kujinyenyekesha mbele zangu? Acha watu wangu waenda ili wakaniabudu.
\v 4 Lakini ukikataa kuwaruhusu watu wangu kwenda, sikiliza, kesho nitaleta nzige kwenye nchi yako.
\s5
\v 5 Watafunika ardhi ya juu ili kwamba mtu asiweze kuona udongo. Watakula mabaki yote yalio salia kwenye mvua ya barafu ya mawe. Pia watakula kila mti unaokua shambani.
\v 6 Watajaza nyumba zenu, zote za watumishi wenu, na zote za Wamisri wote - jambo ambalo baba zenu wala mababu zenu hawakuwai kuona, jambo ambalo halikuwai shuhudiwa toka walipo kuwa duniani hadi leo."' Kisha Musa akaondoka na kutoka kwa Farao.
\s5
\v 7 Watumishi wa Farao wakamwambia, "Mpaka lini huyu mwanaume ata kuwa msumbufu kwetu? Acha Waisraeli waende wakamuabudu Yahweh Mungu wao. Bado haujatambua kuwa Misri imeharibiwa?"
\v 8 Musa na Aruni wakaletwa tena kwa Farao, ambaye aliwaambia, "Nendeni amkamuabudu Yahweh Mungu wenu. Lakini watu gani wataenda?"
\s5
\v 9 Musa akasema, "Tutaondoka na wadogo wetu na wakubwa wetu, pamoja na wana wetu na mabinti zetu. Tutaondoka na ng'ombe na kondoo zetu, maana lazima tufanye siku kuu ya Yahweh."
\v 10 Farao akawaambia, "Yahweh kwa kweli awe nanyi, kama nitawaacha muende na wadogo zenu waende. Angalia, una uovu kwenye nia.
\v 11 Hapana! Nenda, wanaume tu miongoni mwenu, na mmuabudu Yahweh, kwa kuwa hilo ndilo mnalo litaka." Kisha Musa na Aruni wakaondolewa uweponi mwa Farao.
\s5
\v 12 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Nyoosha mkono wako kwenye nchi ya Misri palipo na nzige, ili washambulie nchi ya Misri na kula kila mmea, kila kitu barua ya mawe iliyo acha."
\v 13 Musa akanyoosha na gongo lake juu ya nchi ya Misri, na Yahweh akaleta upepo wa mashariki juu ya nchi mchana wote na usiku mzima. Palipo kuwa asubui, upepo wa mashariki ulileta nzige.
\s5
\v 14 Nzige wakaenda nchi yote ya Misri na kuharibu sehemu zote. Hapajawai kuwa na kundi kama hilo la nzige juu ya nchi, hakuna kama tena kama hilo litawai kutokea.
\v 15 Walifunika ardhi yote ya juu ikawa giza. Walikula kila mmea na kila tunda la miti ambayo barafu ya mawe ilibakiza. Kila eneo la nchi ya Misri, hakuna mmea wa kijani ulibaki, wala mti au mmea wa shambani.
\s5
\v 16 Kisha Farao akawaita Musa na Aruni na kuwaambia, "Nimefanya dhambi dhidi ya Yahweh na dhidi yako.
\v 17 Kisha sasa, nisamehe dhambi yangu wakati huu, na uombe kwa Yahweh Mungu wako aondoe hichi kifo kwangu."
\v 18 Musa akaondoka kwa Farao na kumuomba Yahweh.
\s5
\v 19 Yahweh akaleta upepo mkali wa magharibi ulio wachukuwa wale nzige na kuwapeleka Bahari ya Shamu; hakuna nzige ata mmoja aliye baki eneo la Misri.
\v 20 Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao mgumu, na Farao hakuacha Waisraeli waende.
\s5
\v 21 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Nyoosha mkono wako kuelekea mbingu, ili kuwe na giza nchi yote ya Misri, giza linalo weza kuhisiwa."
\v 22 Musa akanyoosha mkono wake kuelekea mbingu, na kulikuwa na giza nene nchi yote ya Misri kwa siku tatu.
\v 23 Hakuna aliye muona mwingine; hakuna aliye toka nyumbani mwake kwa siku tatu. Walakini, Waisraeli wote walikuwa na taa katika sehemu walizo ishi.
\s5
\v 24 Farao alimuita Musa na kusema, "Nenda umuabudu Yahweh. Ata familia zenu za weza kwenda nanyie, lakini ng'ombe zenu na kondoo zenu zitabaki."
\v 25 Lakini Musa akasema, "Lazima utupe wanyama kwa ajili ya dhabihu na sadaka za kuteketeza ili tuwatoe dhabihu kwa Yahweh Mungu wetu.
\v 26 Mifugo yetu lazima iende na sisi; ata mmoja hawezi kubaki, lazima tuwapeleke wakamuabudu Yahweh Mungu wetu. Kwa kuwa hatujui tutakacho muabudu nacho Yahweh mpaka tufike pale.
\s5
\v 27 Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao mgumu, na hakuwaacha waende.
\v 28 Farao alimwambia Musa, "Toka kwangu! Kuwa muangalifu na jambo moja, kwamba usinione tena, kwa kuwa siku utakapo uona uso wangu, utakufa."
\v 29 Musa akasema, "Wewe mwenyewe umesema. Sitauona uso wako tena."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Bado kuna pigo moja nitalo lileta kwa Farao na Misri. Baada ya hilo, atakuacha uondoke hapa. Atakapo kuachia uende, ata kuondoa kabisa.
\v 2 Waelekeze watu kwamba kila mwanaume na mwanamke amuulizie jirani yake vitu vya fedha na vitu vya dhahabu."
\v 3 Sasa Yahweh aliwafanya Wamisri kuwa na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Aidha, Musa alikuwa wakuvutia sana machoni pa watumishi wa Farao na watu wa Misri.
\s5
\v 4 Musa akasema, "Yahweh asema hivi: 'Wakati wa usiku wa manane nitaenda Misri yote.
\v 5 Wazaliwa wa kwanza wote wa nchi ya Misri watakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, anaye keti kiti chake cha enzi, mpaka mzaliwa wa kwanza wa misichana mtumwa anaye saga mbegu, na kwa wazaliwa wa kwanza wa mifugo.
\s5
\v 6 Kisha kutakuwa na kilio kikubwa nchi yote ya Misri, kama ambacho hakijawai wala hakitatokea tena.
\v 7 Lakini ata mbwa hata bweka kwa watu wa Israeli, dhidi ya mtu au mnyama. Kwa hili utajuwa kuwa nina watendea Wamisri na Waisraeli tofauti.'
\v 8 Watumishi wote hawa wako, Farao, watakuja chini yangu na kunisujudu mimi. Watasema, 'Nenda, wewe na watu wote wanao kufuata!' Baada ya hapo nitaondoka." Kisha akaondoka mbele ya Farao kwa hasira kubwa.
\s5
\v 9 Yahweh akamwambia Musa, Farao hatakusikiliza. Hii ni ili nifanye mambo ya ajabu katika nchi ya Misri."
\v 10 Musa na Aruni wakafanya mambo haya ya kushangaza mbele za Farao. Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao mgumu, na Farao hakuwaacha watu wa Israeli kuondoka katika nchi yake.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Yahweh akasema na Musa na Aruni katika nchi ya Misri. Alisema,
\v 2 "Kwako wewe, mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi, mwezi wa kwanza wa mwaka kwako.
\s5
\v 3 Liambie kusanyiko la Israeli, 'Siku ya kumi mwezi huu kila mtu lazima achukuwe mwana kondoo au mbuzi mdogo wa kwake, kila familia ifanye hivi, mwana kondoo kwa kila nyumba.
\v 4 Kama hiyo nyumba ni ndogo sana kwa mwana kondoo, mwanaume na jirani yake wachukuwe mwana kondoo au nyama ya mbuzi mdogo ambayo itatosha watu. Lazima iwe yatosha kwa kila mtu kula, kwaiyo lazima wachukuwe nyama ya kutosha kulisha wote.
\s5
\v 5 Mwana kondoo wako au mbuzi wako mdogo lazima asiwe na upungufu, dume mwenye mwaka mmoja. Unaweza kuchukuwa mmoja wa kondoo au mbuzi.
\v 6 Lazima umtunze mpaka siku ya kumi na nne ya huo mwezi. Kisha kusanyiko lote la Israeli lazima liwaue hawa wanyama jioni.
\v 7 Lazima uchukuwe baadhi ya damu na uweke kwenye sehemu mbili za mihimili ya milango na juu ya fremu za milango ambapo utalia hizo nyama.
\v 8 Lazima ule hizo nyama usiku, baada ya kuchoma kwenye moto. Kula na mkate ulio andaliwa kwa hamira, pamoja na mimea michungu.
\s5
\v 9 Usiile mbichi au imechemshwa kwenye maji. Badala yake, choma kwenye moto na kichwa chake, miguu na sehemu za ndani.
\v 10 Usiache ata kidogo kubaki mpaka asubui. Lazima uchome chochote kilicho baki asubui.
\v 11 Hivi ndivyo wa paswa kula: ukiwa umefunga mkanda wako, umevaa viatu vyako, na gongo lako mkononi mwako. Lazima ule kwa haraka. Ni Pasaka ya Yahweh.
\s5
\v 12 Yahweh anasema hili: Nitaenda katika nchi ya Misri usiku na kushambulia wazaliwa wote wa kwanza wa wanadamu na wanyama katika nchi ya Misri. Nitaleta pigo kwa miungu yote ya Misri. Mimi ni Yahweh.
\v 13 Damu itakuwa ishara kwenye nyumba zenu ya kuja kwangu. Nitakapo ona damu, nitapita nitakapo shambulia nchi ya Misri. Ili pigo halitawajia na kuwaharibu.
\v 14 Hii siku itakuwa kumbukumbu kwenu, ambayo lazima muadhimishe kama sherehe ya Yahweh. Itakuwa sheria kwenu pia, kwenye vizazi vyote vya watu wenu, ambayo mwapaswa kuadhimisha leo.
\s5
\v 15 Utakula mkate bila hamira wakati wa siku saba. Siku ya kwanza utaondoa hamira kwenye nyumba zenu. Yeyote atakaye kula mkate uliyotiwa chachu kwanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, huyo mtu lazima akatwe kutoka Israeli.
\v 16 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko lililo tengwa kwa ajili yangu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko kama hilo. Hakuna kazi itakayo fanywa hizi siku, zaidi ya kupika kila mmoja ale. Hiyo ndio kazi pekee itakayo fanywa na wewe.
\s5
\v 17 Lazima uadhimishe hii Sherehe ya Mkate Usiotiwa Chachu kwasababu ni siku hii ambayo nitawaleta watu wako, makundi yaliyo na silaha, kwa makundi yaliyo na silaha, kutoka nchi ya Misri. Lazima uadhimishe hii siku kwa vizazi vyote vya watu wako. Hii itakuwa sheria kwako.
\v 18 Lazima ule mkate usiotiwa chachu kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa mwaka, mpaka jioni ya siku ya ishirini na moja ya mwezi.
\s5
\v 19 Wakati wa hizi siku, nyumbani mwenu kusipatikane na hamira. Yeyote atakaye kula mkate ulio andaliwa na hamira lazima akatwe kutoka jamii ya Israeli, huyo mtu awe ni mgeni au mtu aliye zaliwa nchini mwenu.
\v 20 Hautakula chochote kilicho andaliwa na hamira. Popote utapo ishi, lazima ule mkate usio na hamira."'
\s5
\v 21 Kisha Musa akawaita viongozi wote wa Israeli na kuwaambia, "Nendeni na mchague mwana kondoo au mbuzi watakao tosha kulisha familia zenu na muue mwana kondoo wa pasaka.
\v 22 Kisha chukua jani la hisopu na uchovye kwenye damu itakayo kuwa kwenye beseni. Paka damu iliyo kwenye beseni juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimili miwili ya mlango. Hakuna ata mmoja atakaye toka nje ya mlango wake mpaka asubui.
\s5
\v 23 Kwa kuwa Yahweh atapita kushambulia Wamisri. Atakapo ona damu juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimili miwili ya mlango, atapita mlango wako na ata ruhusu mharibifu kuja nyumbani kwenu kuwashambulia.
\s5
\v 24 Lazima uadhimishe hili tukio. Hili litakuwa daima sheria kwako na kwa uzao wenu.
\v 25 Utakapo ingia nchi Yahweh atakayo kupa, kama alivyo ahidi kufanya, lazima uadhimishe hili tendo la ibada.
\s5
\v 26 Watoto wako watakapo kuuliza, 'Hili tendo la ibada lina maana gani?'
\v 27 kisha lazima useme, 'Ni sadaka ya Pasaka ya Yahweh, kwasababu Yahweh kapita nyumba za Waisraeli Misri alipo washambulia Wamisri. Aliweka nyumba zetu huru."' Kisha watu wakamsujudia Yahweh.
\v 28 Waisraeli wakaenda na kufanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Aruni.
\s5
\v 29 Ikawa usiku wa manane kuwa Yahweh akawashambulia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, aliye keti kiti chake cha enzi, mzaliwa wa kwanza wa mtu aliye gerezani na wazaliwa wote wa kwanza wa mifugo.
\v 30 Farao akaamka usiku - yeye, watumishi wake, na Wamisri. Palikuwa na kelele za maombolezo Misri, kwa kuwa hakukuwa na nyumba ambayo hamna mtu hakufa.
\s5
\v 31 Farao akamuita Musa na Aruni usiku na kusema, "Inuka, tokeni miongoni mwa watu wangu, nyie pamoja na Waisraeli. Nenda, mmuabudu Yahweh, kama mlivyo sema mnataka kufanya.
\v 32 Chukuweni ng'ombe zenu na kondoo zenu, kama mlivyo sema, na muende, na pia mnibariki."
\v 33 Wamisri walikuwa na haraka ya kuwa ondoa nchini, kwa kuwa walisema, "Sisi ni watu tuliokufa."
\s5
\v 34 Watu wakachukuwa ngano yao pasipo kuongeza hamira yeyote. Bakuli zao zakukandia ngano zilifungiwa kwenye nguo zao na kwenye mabega yao.
\v 35 Watu Waisraeli walifanya kama Musa alivyo waambia. Waliwaomba Wamisri vitu vya fedha, vitu vya dhahabu, na nguo.
\v 36 Yahweh aliwafanya Wamisri na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Hivyo Wamisri waliwapa chochote walicho waomba. Katika hili, Waisraeli waliwachukulia vingi Wamisri.
\s5
\v 37 Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesi kwenda Sakothi. Walikuwa na idadi ya wanaume 600, 000 kwa miguu, kuongezea kwa wanawake na watoto.
\v 38 Mchanganyiko wa kundi la wasio Waisraeli pia walienda nao, pamoja na ng'ombe na kondoo, idadi kumbwa ya mifugo.
\v 39 Walioka mikate na unga wa ngano wenye hamira walio utoa Misri. Ulikuwa hauna hamira kwasababu waliondolewa Misri na hawakuweza chelewa kuandaa chakula.
\v 40 Waisraeli waliishi Misri kwa miaka 430.
\s5
\v 41 Baada ya miaka 430, siku hiyo hiyo, majeshi yote ya Yahweh yalio jiami waliondoka kutoka nchi ya Misri.
\v 42 Huu ulikuwa usiku wakuwa macho, ili Yahweh awatoe kutoka nchi ya Misri. Huu ulikuwa usiku wa Yahweh wa kuadhimishwa na Waisraeli wote na watu wa vizazi vyao vyote.
\s5
\v 43 Yahweh akamwambia Musa na Aruni, "Hii ni sheria ya Pasaka: hakuna mgeni anaye ruhusiwa kuila.
\v 44 Walakini, kila mtumwa wa Misraeli, aliye nunuliwa kwa pesa, anaeza kula baada ya kutahiriwa.
\s5
\v 45 Wageni na watumishi waajiriwa hawapaswi kula chakula chochote.
\v 46 Chakula chapaswa kuliwa ndani ya nyumba moja. Hauruhusiwi kubeba nyama yeyote nje ya nyumba, na hauruhusiwi kuvunja mfumba wowote.
\s5
\v 47 Jamii zote za Israeli za paswa kuadhimisha sherehe.
\v 48 Kama mgeni anaishi na wewe na anataka kuadhimisha Pasaka kwa Yahweh, ndugu zake wote wa kiume wapaswa kutahiriwa. Kisha anaeza kuja na kuadhimisha. Atakuwa kama watu walio zaliwa kwenye nchi. Walakini, hakuna mtu asiye tahiriwa anaruhusiwa kula chakula chochote.
\s5
\v 49 Sheria hii hii itahusika kwa mzaliwa wa asili na mgeni anayeishi miongoni mwenu."
\v 50 Waisraeli wote walifanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Aruni.
\v 51 Ikaja kuwa siku hiyo Yahweh akawaleta Israeli kutoka nchi ya Misri kwa makundi yalio jiami.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
\v 2 "Nitengee wazaliwa wote wa kwanza, kila mzaliwa wa kwanza wa Waisraeli, watu na wanyama. Mzaliwa wa kwanza ni wangu."
\s5
\v 3 Musa akawambia watu, "Hii kumbukeni hii siku, siku mliyo toka Misri, kutoka nyumba ya utumwa, kwa mkono hodari wa Yahweh amewatoa kutoka hii sehemu. Hakuna mkate wa hamira waruhusiwa kuliwa.
\v 4 Mnatoka Misri hii siku, mwezi wa Abibu.
\v 5 Yahweh atakapo waleta nchi ya Wakanani, Wahiti, Waamori, Wahivi, na Wayebusi, nchi aliyo waapia mababu zenu kuwapa, nchi inayo tiririka kwa maziwa na asali - kisha wapaswa kuadhimisha hili tendo la ibada kila mwezi.
\s5
\v 6 Kwa siku saba utakula mkate bila hamira; siku ya saba kutakuwa na maakuli ya kumuadhimisha Yahweh.
\v 7 Mkate usio na hamira wapaswa kuliwa kwa siku saba zote; hakuna mkate ulio na hamira wapaswa kuliwa miongoni mwenu. Hakuna hamira yapaswa kuonekana kwenye mipaka yenu.
\s5
\v 8 Hiyo siku utasema kwa watoto wako, 'Hii ni kwasababu ya kile Yahweh alichofanya kwangu nilipo taka Misri.'
\v 9 Hii itakuwa kumbukumbu mkononi mwako, na kumbukumbu kwenye paji la uso wako. Hii ni ili sheria ya Yahweh iwe kinywani mwako, maana kwa mkono hodari Yahweh amewatoa kutoka Misri.
\v 10 Kisha basi wapaswa kushika hii sheria kwa wakati uliyo kusudiwa kutoka mwaka hadi mwaka.
\s5
\v 11 Yahweh atakapo waleta kwenye nchi ya Wakanani, kama alivyo apa kwenu na kwa mababu zenu kufanya, na atakapo wapa nchi ninyi,
\v 12 lazima umtengee mzaliwa wa kwanza mtoto na uzao wa kwanza wa wanyama wenu. Wakiume watakuwa wa Yahweh.
\v 13 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda lazima umnunue tena na mwana kondoo. Kama hautamnunua tena, lazima uivunje shingo yake. Lakini kila mzaliwa wa kwanza wakiume miongoni mwenu - lazima umnunue tena.
\s5
\v 14 Mwanae atakapo kuuliza baadae, 'Hii ina maana gani?' kisha utamwambia, 'Ni kwa mkono hodari Yahweh katutoa Misri, kutoka nyumba ya utumwa.
\v 15 Farao alipo kataa kwa ujeuri kutuachia twende, Yahweh aliwaua wazaliwa wa kwanza wa nchi ya Misri, wazaliwa wa kwanza wa watu na wa wanyama. Ndio sababu ninatoa dhabihu kwa Yahweh kwa kila mzaliwa wa kwanza wa kila mnyama, na pia sababu nina nunua wazaliwa wa kwanza wa wanangu tena.'
\v 16 Hii itakuwa kumbukumbu mikononi mwako na kumbukumbu kwenye paji lako la uso, kwa kuwa ni kwa mkono hodari Yahweh alitutoa kutoka Misri."
\s5
\v 17 Farao alipo waachia watu waende, Mungu akuwaongoza kwa njia ya Wafilisti, japo hiyo njia ilikuwa karibu. Kwa kuwa Mungu alisema, "Labda watu watabadili nia zao watakapo ona vita na watarudi Misri."
\v 18 Hivyo Mungu akawaongoza watu kuzunguka nyikani kupita Bahari ya Shamu. Waisraeli waliondoka kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiami kwa pambano.
\s5
\v 19 Musa akachukuwa mifupa ya Yusufu pamoja naye, kwa kuwa Yusufu aliwaapisha Waisraeli na kusema, "Mungu atawaokoa, na muibebe mifupa yangu na nyie."
\v 20 Waisraeli walisafiri kutoka Sakothi na kuweka kambi Ethamu pembezoni mwa nyikani.
\v 21 Yahweh alitangulia mbele yao mchana kama nguzo ya wingu kuwaongoza njiani. Usiku alienda kama nguzo ya moto kuwapa mwanga. Kwa namna hii waliweza kusafiri mchana na usiku.
\v 22 Yahweh hakuchukuwa kutoka kwa watu nguzo ya wingu mchana wala nguzo ya moto usiku.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
\v 2 "Waambie Waisraeli wageuke na kueka kambi mbele ya Pi Hahirothi, katikati ya Migdoli na bahari, mbele ya Baali Zefoni. Wapaswa kueka kambi pembenni ya Pi Hahirothi.
\v 3 Farao atasema kuhusu Waisraeli, 'Wanaangaika kwenye nchi. Nyikani imewafunika.'
\s5
\v 4 Nitaufanya moyo wa Farao mgumu, na yeye ata wakimbiza. Nitapata utukufu kwasababu ya Farao na jeshi lake lote. Wamisri watajua mimi ni Yahweh." Kisha Waisraeli wakaeka kambi kama walivyo elekezwa.
\v 5 Mfalme wa Misri alipo ambiwa Waisraeli wametoroka, nia ya Farao na watumishi wake ikageuka dhidi ya watu. Wakasema, "Tumefanya nini kwa kuwaacha Waisraeli waende huru na wasitutumikie?"
\s5
\v 6 Kisha Farao akachukuwa magari yake ya farasi na jeshi lake.
\v 7 Alichukuwa magari ya farasi mia sita imara na magari yote ya farasi ya Misri, pamoja na maafisa wa hayo magari.
\v 8 Yahweh akafanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, na mfalme akawafukuzia Waisraeli. Sasa Waisraeli waliondoka kwa shangwe.
\v 9 Lakini Wamisri wali wafukuzia, pamoja na farasi na magari ya farasi, wapanda farasi, na jeshi lake. Walikuta Waisraeli wameeka kambi pembezoni mwa bahari kati ya Pi Hahirothi na Baali Zefoni.
\s5
\v 10 Farao alipo karibia, Waisraeli walitaza juu na kushangaa. Wamisri walikuwa wakija kwao, na waliogopa. Waisraeli walimlilia Yahweh.
\v 11 Walimwambia Musa, "Ni kwasababu hakukuwa na makaburi Misri, hadi umetuleta tufe huku nyikani? Kwanini umetutendea hivi, kwa kututoa Misri?
\v 12 Hili si ndilo tulilo kwambia Misri? Tulikwambia, 'Utuache, ili tuwafanyie Wamisri kazi.' Ingekuwa bora kwetu sisi kuwafanyia kazi kuliko kufa nyikani."
\s5
\v 13 Musa akawaambia watu, "Msiogope. Simameni imara na muone wokovu Yahweh atakao uleta kwenu leo. Kwa maana hamtawaona tena Wamisri mnao waona leo.
\v 14 Yahweh ata wapigania, na ninyi mtasima imara."
\s5
\v 15 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Kwanini wewe, Musa, unaendelea kuniita mimi? Waambie Waisraeli waendelee mbele.
\v 16 Nyanyua gongo lako juu, nyoosha mkono wako kuelekea baharini na uigawanye sehemu mbili, ili watu wa Israeli wapite baharini kwenye nchi kavu.
\v 17 Jitahadharishe kuwa nitafanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu ili wawafuate. Nitapata utukufu kwasababu ya Farao na jeshi lake lote, magari yake ya farasi, na wapanda farasi.
\v 18 Kisha Wamisri watajua kuwa mimi ni Yahweh nitakapo pata utukufu kwasababu ya Farao, magari yake ya farasi, na wapanda farasi wake."
\s5
\v 19 Malaika wa Mungu, aliyeenda mbele ya Waisraeli, aliama na kwenda nyuma yao. Nguzo ya wingu ili sogea mbele yao na kwenda kusimama nyumba yao.
\v 20 Wingu lilikuja katikati ya kambi ya Misri na kambi ya Israeli. Lilikuwa wingu jeusi kwa Wamisri, lakini liliangaza usiku kwa ajili ya Waisraeli, hivyo upande mmoja haukuweza kuja karibu ya mwingine usiku wote.
\s5
\v 21 Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari. Yahweh akasogeza bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku huo wote na kufanya bahari nchi kavu. Kwa namna hii maji yaligawanyika.
\v 22 Waisraeli walienda katikati ya bahari kwa nchi kavu. Maji yaliunda ukuta mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto.
\s5
\v 23 Wamisri waka wafukuzia. Wali wafuata hadi katikati ya bahari - farasi wote wa Farao, magari ya farasi, na wapanda farasi.
\v 24 Lakini masaa ya mapema ya asubui, Yahweh alitazama chini jeshi la Wamisri kupitia nguzo ya moto na wingu. Alisababisha hofu miongoni mwa Wamisri.
\v 25 Magari yao ya farasi yalikuwa yana kwama matairi, na wapanda farasi waliendesha kwa ugumu. Hivyo Wamisri walisema, "Acha tuwakimbie Waisraeli, kwa kuwa Yahweh anawapigania dhidi yetu."
\s5
\v 26 Yahweh akamwambia Musa, "Nyoosha mkono kuelekea bahari ili maji yawarudie Wamisri, magari yao ya farasi, na wapanda farasi wao."
\v 27 Hivyo Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari, na ikarudi kwenye hali yake ya kawaida palipo pambazuka. Wamisri walikimbilia ndani ya bahari, na Yahweh akawaingiza Wamisri katikati ndani yake.
\v 28 Maji yakarudi na kufunika magari ya farasi ya Farao, wapanda farasi, na jeshi lake lote lililo fuata magari ya farasi kwenye bahari. Hakuna aliyepona.
\s5
\v 29 Walakini, Waisraeli walitembea kwenye nchi kavu katikati ya bahari. Maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kulia na mkono wa kushoto.
\v 30 Hivyo Yahweh akaokoa Israeli hiyo siku kutoka mkono wa Wamisri, na Israeli ikaona maiti za Wamisri ufukweni.
\v 31 Israeli ilipoona nguvu kubwa Yahweh aliyo itumia dhidi ya Wamisri, watu walimsifu Yahweh, na kumwamini Yahweh na mtumishi wake Musa.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Kisha Musa na watu wa Israeli wakaimba hii nyimbo kwa Yahweh. Waliimba, "Nitaimba kwa Yahweh, kwa kuwa ameshinda kwa utukufu; farasi na dereva wake amewatupa kwenye bahari.
\s5
\v 2 Yahweh ni uweza wangu na nyimbo yangu, na amekuwa wokovu wangu. Huyu ni Mungu wangu, na nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nitamtukuza.
\v 3 Yahweh ni shujaa; Yahweh ni jina lake.
\s5
\v 4 Ametupa magari ya farasi ya Farao na jeshi lake kwenye bahari. Maafisa wa Farao hodari walizama kwenye Bahari ya Shamu.
\v 5 Kina kiliwafunika; walienda kwenye kina kama jiwe.
\s5
\v 6 Mkono wako wakulia, Yahweh, una nguvu ya utukufu; mkono wako, Yahweh, umewavunja adui.
\v 7 Kwa utukufu mkubwa umewapindua walio inuka dhidi yako. Umetuma gadhabu; imewateketeza kama karatasi.
\v 8 Kwa pumzi ya pua yako maji yalijaa; maji yanayo tembea yalisimama wima na kujaa juu; maji yalikuwa manene ndani ya kilindi cha bahari.
\s5
\v 9 Adui alisema, 'Nitakimbiza, nitapita, nitagawa nitakacho chukuwa; tamanio langu litatimizwa kwao; nitavuta upanga wangu; mkono wangu utawaharibu wao.'
\v 10 Lakini ulipuliza kwa upepo wako, na bahari ikawafunika wao; walizama kama chuma nzito kwenye maji mengi.
\v 11 Ni nani kama wewe, Yahweh, miongoni mwa miungu? Nani kama wewe, mtakatifu wa utukufu, katika sifa umetukuzwa, anaye fanya miujiza?
\s5
\v 12 Ulinyoosha mkono wako wa kulia, na dunia ikawameza.
\v 13 Katika uaminifu wa agano lako umewaongoza watu ulio waokoa. Katika uweza wako umewaongoza katika sehemu takatifu unayo ishi.
\s5
\v 14 Watu watasikia, na watatetemeka; hofu itawakumba wakazi wa Filistia.
\v 15 Kisha wazee wa Edomu wataogopa; wanajeshi wa Moabu watetemeka; wakazi wote wa Kanani watayayuka.
\s5
\v 16 Mshituko na hofu vitawaangukia. Kwasababu ya nguvu ya mkono wako, watakuwa kimya kama jiwe hadi watu wako watakapo pita, Yahweh - hadi watu ulio waokoa watakapo pita.
\s5
\v 17 Utawaleta na kuwapanda kwenye mlima wa urithi wako, sehemu, Yahweh, ulio jenga ya kuishi, sehemu takatifu, Bwana wetu, mikono yako iliyo jenga.
\v 18 Yahweh ata tawala milele na milele."
\s5
\v 19 Kwa kuwa farasi wa Farao walienda na magari ya farasi na wapanda farasi kwenye bahari. Yahweh alileta maji ya bahari juu yao. Lakini Waisraeli walienda juu ya nchi kavu katikati ya bahari.
\v 20 Miriamu nabii wa kike, dada wa Aruni, akanyanyua tari, na wanawake wote wakatoka na matari, wakicheza nae.
\v 21 Miriamu akawaimbia: "Muimbieni Yahweh, kwa kuwa ameshinda kwa utukufu. Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
\s5
\v 22 Kisha Musa akaongoza Israeli mbele kupita Bahari ya Shamu. Walienda nyikani ya Shuri. Walisafiri kwa siku tatu nyikani pasipo kuona maji yeyote.
\v 23 Kisha wakaja Mara, lakini hawakunywa maji ya huko kwasababu yalikuwa machungu. Hivyo wakaita hiyo sehemu Mara.
\s5
\v 24 Hivyo watu wakamlalamikia Musa na kusema, "Nini tunaweza kunywa?"
\v 25 Musa akamlilia Yahweh, na kumonyesha mti. Musa akautupa kwenye maji, na maji yakawa matamu kunywa. Ndio pale Yahweh alipowapa sheria kali, na ndio pale alipo wajaribu.
\v 26 Alisema, "Kama utasikiliza sauti ya Yahweh Mungu wako kwa umakini, na kufanya yalio sahihi machoni pake, na kama utatega sikio kwa amri zake na kutii sheria zake zote - sitawaekea ninyi magonjwa yale niliyo waekea Wamisri, kwa kuwa mimi ni Yahweh ninaye kuponya."
\s5
\v 27 Kisha watu wakaja Elimu, palipo kuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mtende. Walieka kambi hapo pembeni ya maji.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Watu wakaendelea na safari kutoka Elimu, na jamii yote ya Waisraeli ikaja nyikani mwa Sinu, iliyopo katikati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili walipo toka Misri.
\v 2 Jamii yote ya Waisraeli wali walalamikia Musa na Aruni nyikani.
\v 3 Waisraeli waliwaambia, "Kama tu tungekufa kwa mkono wa Yahweh nchi ya Misri tulipo kuwa tumeketi kwenye vyombo vya nyama na tulikuwa tunakula mkate kwa tele. Maana umetuleta nyikani uuwe jamii zetu zote kwa njaa."
\s5
\v 4 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Nitakunyeshea mvua ya mkate. Watu wataenda na kukusanya kiasi cha siku kila siku ili niwajaribu kama wataendelea kushika sheria yangu au hapana.
\v 5 Itakuja kuwa siku ya sita, kwamba watakusanya mara mbili zaidi ya wanavyo kusanyaga, na watapika wanacholeta."
\s5
\v 6 Kisha Musa na Aruni wakawaambia watu wote wa Israeli, "Jioni mtajua kuwa ni Yahweh aliye waleta kutoka nchi ya Misri.
\v 7 Asubui utaona utukufu wa Yahweh, kwa maana anasikia mna mlalamikia. Sisi ni nani hadi mtulalamikie?"
\v 8 Musa pia akasema, "Utajua hili pale Yahweh atakapo kupa nyama jioni na mkate asubui kwa tele - kwa kuwa amesikia malalamishi mnayo tamka dhidi yake. Nani ni Aruni na mimi? Malalamishi yenu sio dhidi yetu; ni dhidi ya Yahweh."
\s5
\v 9 Musa akamwambia Aruni, "Sema kwa jamii yote ya watu wa Israeli, 'Njoo karibu ya Yahweh, kwa kuwa amesikia malalamishi yenu.'"
\v 10 Ikawa, Aruni alipo sema na jamii yote ya watu wa Israeli, wakaangalia kuelekea nyikani, na, tazama, utukufu wa Yahweh ukatokea kwenye wingu.
\v 11 Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
\v 12 "Nimesikia malalamishi ya watu wa Israeli. Sema nao na useme, 'Jioni utakula nyama, na asubui utashiba mkate. Kisha utajua mimi ni Yahweh Mungu wako.'"
\s5
\v 13 Ikaja kuwa kwamba jioni kware wakaja juu na kufunika kambi. Asubui umande ulitanda kambini.
\v 14 Umande ulipo kwisha, pale juu ya ardhi ya nyikani kulikuwa na kama barafu iliyo ganda kwenye ardhi.
\v 15 Watu wa Israeli walipo ona, walisema mmoja kwa mwenzake, "Hii ni nini?" Hawakujua ilikuwa ni nini. Musa akawaambia, "Ni mkate Yahweh aliyo wapa mle.
\s5
\v 16 Hii ni amri Yahweh aliyotoa: 'Lazima ukusanye, kila mmoja wenu, kiasi unacho itaji kula, lita mbili kwa kila mtu. Hivi ndivyo utakavyo kusanya: Kusanya cha kutosha kula cha kila mtu anaye ishi hemani mwako.'"
\v 17 Watu wa Israeli wakafanya hivyo. Baadhi wakakusanya zaidi, baadhi wakakusanya kidogo.
\v 18 Walipo pima kwa kipimo cha lita, hao walio kusanya zaidi hawakuwa na kilicho salia, na hao walio kusanya kidogo hawakuwa na pungufu. Kila mmoja alikusanya cha kutosha kukidhi maitaji yake.
\s5
\v 19 Kisha Musa akawaambia, "Hakuna ata mmoja kubakiza hadi asubui."
\v 20 Walakini, hawakumsikiliza Musa. Baadhi yao waliacha baadhi hadi asubui, lakini ilizalisha wadudu na kuwa batili. Kisha Musa akawa na hasira juu yao.
\v 21 Walikusanya asubui kwa asubui. Kila mtu alikusanya cha kutosha kula kwa hiyo siku. Jua lilipo kuwa kali, ili yayuka.
\s5
\v 22 siku ya sita walikusanya mkate mara mbili zaidi, lita mbili kwa kila mtu. Viongozi wote wa jamii walikuja na kumwambia hili kwa Musa.
\v 23 Aliwaambia, "Hili ndilo Yahweh alililo lisema: 'Kesho ni mapumziko ya kujiliwaza, sabato takatifu kwa utukufu wa Yahweh. Oka kile unataka kuoka, na chemsha kile unataka kuchemsha. Vyote vitakavyo baki, jihifadhie hadi asubui."'
\s5
\v 24 Hivyo wakaeka pembeni hadi asubui, kama Musa alivyo elekeza. Haikuharibika, wala haikuwa na mdudu yeyote.
\v 25 Musa alisema, "Kula hicho cha kula leo, kwa kuwa leo ni siku iliyo tengwa ya kumtukuza Yahweh. Leo hamtaikuta mashambani.
\s5
\v 26 Mtaikusanya ndani ya siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato. Siku ya Sabato hakuta kuwa na manna."
\v 27 Ilikuja kuwa siku ya saba ambapo baadhi ya watu walienda kukusanya manna, lakini hawakukuta
\s5
\v 28 Kisha Yahweh akamwambia Musa, Kwa muda gani utaendelea kukataa kushika amri zangu na sheria zangu?
\v 29 Tazama, Yahweh amekupa Sabato. Hivyo siku ya sita anakupa mkate wa siku mbili. Kila mmoja wenu lazima akae kwenye sehemu yake; hakuna hata mmoja wa kutoka sehemu yake siku ya saba."
\v 30 Hivyo watu watapumzika siku ya saba.
\s5
\v 31 Watu wa Israeli walikiita chakula kile "manna." Ilikuwa ni nyeupe kama mbegu ya mgiligani, na ladha yake kama maandazi yaliyo pikwa na asali.
\v 32 Musa akasema, "Hili ndilo Yahweh alilo amuru: 'Acha lita mbili ya manna ihifadhiwe kwa ajili vizazi vya watu wako ili kwamba uzao wako uone mkate niliyo kulisha nyikani, baada ya kukutoa kutoka nchi ya Misri.
\s5
\v 33 Musa akamwambia Aruni, "Chukuwa jagi na uweke lita mbili za manna ndani yake. Hifadhi kwa Yahweh i dumu vizazi vyote vya watu."
\v 34 Kama Yahweh alivyo muamuru Musa, Aruni akahifadhi pembeni mwa mawe yaliyo kuwa na amri za agano.
\v 35 Watu wa Israeli walikula manna miaka arobaini mpaka walipo kuja nchi yenye watu. Walikula mpaka walipo fika kwenye mipaka ya nchi ya Kanani.
\v 36 Lita mbili ni makumi ya efa.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Jamii yote ya Israeli ili safiri kutoka nyikani ya Sinu, wakifuata maelekezo ya Yahweh. Walieka kambi Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.
\v 2 Hivyo watu wakamlaumu Musa kwa hali yao na kusema, "Tupe maji ya kunywa." Musa akasema, "Kwanini mnagombana na mimi? Kwanini mnajaribu Yahweh?"
\v 3 Watu walikuwa na kiu sana, na waka mlalamikia Musa. Wakasema, "Kwanini umetutoa Misri? Ili utuue sisi na watoto wetu na mifugo yetu kwa kiu?"
\s5
\v 4 Kisha Musa akamlilia Yahweh, "Nini ni fanya kwa hawa watu? Wako tayari ata kunipiga mawe."
\v 5 Yahweh akamwambia Musa, "Nenda mbele yao, na uchukuwe baadhi ya wazee wa Israeli. Chukuwa gongo ulilo piga nalo mto, na uende.
\v 6 Nitasimama mbele yako pale kwenye mwamba wa Horebu, na utaupiga mwamba. Maji yatatoka ya watu kunywa." Kisha Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.
\v 7 Aliita ile sehemu Massa na Meriba kwasababu ya malalamishi ya Waisraeli, na kwasababu walimjaribu Bwana kwa kusema, "Je Yahweh yupo miongoni mwetu au hapana?"
\s5
\v 8 Kisha jeshi la watu wa Ameleki wakaja na kushambulia Israeli huko Refidimu.
\v 9 Hivyo Musa akamwambia Yoshua, "Chagau wanaume kadha na uende nje. Pigana na Ameleki. Kesho nitasimama juu ya kilima na gongo la Mungu mkononi mwangu."
\v 10 Hivyo Yoshua akapigana na Ameleki kama Musa alivyo elekeza, wakati Musa, Aruni, na Huri walienda juu ya kilima.
\s5
\v 11 Wakati Musa alipo kuwa ameshikilia mikono yake juu, Israeli ilikuwa yashinda; alipo acha mikono yake ipumzike, Ameleki alianza kushinda.
\v 12 Mikono ya Musa alipo kuwa mizito, Aruni na Huri walichukuwa jiwe na kuweka chini yake alikalie. Muda huo huo, Aruni na Huri walinyanyua mikono yake juu, mtu mmoja upande mmoja, na mtu mmoja upande mwingine. Hivyo mikono ya Musa ilishikiliwa tuli mpaka jua lilipo zama.
\v 13 Hivyo Yoshua akawashinda watu wa Ameleki kwa upanga.
\s5
\v 14 Yahweh akamwambia Musa, "Andika haya kwenye kitabu na umsomee Yoshua, kwasababu nitaondoa kumbukumbu ya Ameleki kutoka chini ya mbingu."
\v 15 Kisha Musa akajenga madhabahu na kuiita "Yahweh ni bendera yangu."
\v 16 Alisema, "Kwa kuwa mkono ulinyanyuliwa juu kuelekea kiti cha enzi cha Yahweh - kwamba Yahweh ata fanya vita na Ameleki vizazi na vizazi."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wake Musa, alisikia yote Mungu aliyo fanya kwa Musa na kwa Israeli watu wake. Alisikia Yahweh ametoa Israeli kutoka Misri.
\v 2 Yethro, baba mkwe wake Musa, akamchukuwa Zipora, mke wa Musa, baada ya kumpeleka nyumbani,
\v 3 na wana wake wawili; jina mmoja lilikuwa Gershomu, kwa kuwa Musa alisema, "Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni."
\v 4 Jina la mwingine lilikuwa Eliezeri, kwa kuwa Musa alisema, "Mungu wa babu yangu alikuwa msaada wangu. Aliniokoa na mkono wa Farao."
\s5
\v 5 Yethro, baba mkwe wake Musa, alikuja na watoto wake Musa na mke wake Musa nyikani alipo eka kambi katika mlima wa Mungu.
\v 6 Alimwambia Musa, "Mimi, baba mkwe wako Yethro, nina kuja kwako na mke wako na wanao wawili."
\s5
\v 7 Musa alitoka kwenda kukutana na baba mkwe wake, akamwinamia, na kumbusu. Wakajuliana hali na wakaingia ndani ya hema.
\v 8 Musa akamwambia baba mkwe wake yale yote Yahweh aliyo ya fanya kwa Farao na Wamisri kwa ajili ya Waisraeli, magumu yote yaliyo watoke njianim na jinsi Yahweh alivyo waokoa.
\s5
\v 9 Yethro akafurahia yale mema yote Yahweh aliyo watendea Israeli, kwa hilo amewaokoa na mkono wa Wamisri.
\v 10 Yethro akasema, "Yahweh atukuzwe, kwa kuwa amekuokoa na mkono wa Wamisri na mkono wa Faraom na kuwatoa watu kwenye mkono wa Wamisri.
\v 11 Sasa najua Yahweh ni mkuu kuliko miungu yote, kwasababu Wamisri walipo watenda Waisraeli kwa kiburi, Mungu aliwaokoa watu wake."
\s5
\v 12 Yethro, baba mkwe wake Musa, akaleta sadaka ya kuteketeza na dhabihu kwa Mungu. Aruni na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula mbele za Yahweh na baba mkwe wake Musa.
\s5
\v 13 Siku iliyofuata Musa aliketi kuwa hukumu watu. Watu walisimama kumzunguka Musa kwanzia asubui hadi jioni.
\v 14 Baba mkwe wake Musa alipo ona yale yote aliyo yafanya kwa watu, alisema, "Ni nini unachofanya na watu? Kwanini unaketi peke yako na watu wote wamesimama kukuzunguka asubui hadi jioni?"
\s5
\v 15 Musa akamwambia baba mkwe wake, "Watu wanakuja kuniuliza muongozo wa Mungu.
\v 16 Wanapo kuwa na malumbano, wanakuja kwangu. Ninaamua kati ya mtu mmoja na mwingine, na nina wafundisha maagizo na sheria."
\s5
\v 17 Baba mkwe wake Musa alimwambia, "Unachofanya sicho kizuri sana.
\v 18 Hakika utajichosha, wewe na watu waliyopo na wewe. Huu mzigo ni mzito sana kwako. Hauwezi kufanya peke yako.
\v 19 Nisikilize. Nitakupa ushauri, na Mungu ata kuwa na wewe, kwasababu wewe nimwakilishi wa watu kwa Mungu, na una leta malumbano yao kwake.
\v 20 Lazima uwafundishe maagizo yake na sheria. Lazima uwafundishe njia yakutembea na kazi ya kufanya.
\s5
\v 21 Mbali zaidi, lazima uchague wanaume wenye uwezo kutoka watu wote, wanaume wanao muheshimu Mungu, wanaume wa kweli wanao chukuia mapato ya ufisadi. Lazima uwaeke juu ya watu, kuwa viongozi wa maelfu, mamia, hamsini, na makumi.
\v 22 Watawa hukumu watu na kesi za kawaida, lakini kesi ngumu wataleta kwako. Kwa kesi ndogo, wanaweza kuhukumu wenyewe. Kwa hivyo itakuwa rahisi kwako, na watabeba mzigo na wewe.
\v 23 Ukifanya hivi, na kama Mungu akikuamuru kufanya al kadhalika, basi utaweza kuvumilia, na watu wote watarudi nyumbani wameridhika."
\s5
\v 24 Hivyo Musa akasikiliza maneno ya baba mkwe wake na akafanya yale yote aliyo yasema.
\v 25 Musa alichagua wanaume wenye uwezo kutoka Israeli na kuwa fanya vichwa juu ya watu, viongozi wahusika wa maelfu, mamia, hamsini, na makumi.
\v 26 Waliwa hukumu watu katika hali za kawaida. Kesi ngumu walimletea Musa, lakini wao wenyewe wali hukumu kesi ndogo.
\v 27 Kisha Musa akamwacha baba mkwe wake kuondoka, na Yethro akarudi kwenye nchi yake.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Katika mwezi wa tatu baada ya watu wa Israeli kutoka Misri, siku hiyo, walikwenda nyikani ya Sinai.
\v 2 Walipo ondoka Refidimu na kuja nyikani ya Sinai, walieka kambi mbele ya mlima.
\s5
\v 3 Musa akaenda juu kwa Mungu. Yahweh alimuita kutoka mlimani na kusema, "Lazima uiambie nyumba ya Yakobo, watu wa Israeli:
\v 4 Uliona nilicho fanya kwa Wamisri, jinsi nilivyo kubeba kwa mabawa ya tai na kukuleta kwangu.
\v 5 Kisha sasa, ukinisikiliza kwa utii sauti yangu na kushika agano langu, kisha utakuwa mali yangu ya pekee miongoni mwa watu wote, kwa kuwa dunia yote ni yangu.
\v 6 Utakuwa ufalme wa kikuhani na taifa takatifu langu. Haya ni maneno wapaswa kuwaambia Waisraeli.
\s5
\v 7 Hivyo Musa akaja na kuwaita wazee wa watu. Aliweke mbele yao maneno yote haya Yahweh aliyo muamuru.
\v 8 Watu wote walijibu pamoja na kusema, "Tutafanya yote Yahweh aliyo tuambia." Kisha musa akaja kutoa taarifa ya maneno watu kwa Yahweh.
\v 9 Yahweh akamwambia Musa, "Nitakuja kwako kwa wingu nene ili watu wasikie ninapo sema na wewe na wakuamini milele." Kisha Musa kamwambia Yahweh maneno ya Yahweh.
\s5
\v 10 Yahweh akamwambia Musa, "Nenda kwa watu. Leo na kesho lazima uwatenge, na kuwafanya waoshe mavazi yao.
\v 11 Kuwa tayari kwa siku ya tatu, kwa kuwa siku ya tatu Yahweh atashuka chini ya Mlima Sayuni.
\s5
\v 12 Lazima uweke mipaka kote kuzunguka mlima kwa ajili ya watu. Uwaambie, 'Kuweni waangalifu msiende juu ya mlima au kushika mipaka yake. Yeyote atakaye shika mlima ata uawa.'
\v 13 Hakuna mkono wa mtu yeyote kumshika mtu huyu. Badala yake, lazima apigwe mawe au kuchomwa mshale. Iwe ni mtu au mnyama, lazima auawe. Tarumbeta itakapo pigwa muda mrefu, wanaweza kuja chini ya mguu wa mlima."
\s5
\v 14 Kisha Musa akashuka mlimani kwenda kwa watu. Aliwatenga watu kwa ajili ya Yahweh na wakaosha mavazi yao.
\v 15 Aliwaambia watu, "Kuweni tayari siku ya tatu; msiwakaribie wake zenu."
\s5
\v 16 Siku ya tatu, ilipo fika asubui, kulikuwa na ngurumo na radi na wingu nene kwenye mlima, na sauti kubwa ya tarumbeta. Watu wote kambini waliogopa.
\v 17 Musa akaleta watu kutoka kambini kukutana na Mungu, na wakasimama miguuni mwa mlima.
\v 18 Mlima Sina ulijwa kabisa na moshi kwasababu Yahweh alishuka na moto na moshi. Moshi ulipanda juu kama moshi wa tanuru, na mlima wote ulitikisika kwa vurugu.
\s5
\v 19 Sauti ya tarumbeta ilipo ongezeka na zaidi, Musa akazungumza, na Mungu kamjibu kwa sauti.
\v 20 Yahweh akashuka chini ya Mlima Sinai, juu ya mlima, na akamuita Musa kuja juu. Kisha Musa akapanda juu.
\v 21 Yahweh akamwabia Musa, "Shuka chini na uwaonye watu wasipite kuniangalia, au wengi wao wataangamia.
\v 22 Acha pia mukuhani wanao kuja karibu yangu wakitenge - wajiandae kwa ujio - ili nisiwashambulie."
\s5
\v 23 Musa akamwabia Yahweh, "Watu hawawezi kuja juu ya mlima, kwa kuwa umetuamuru: 'Eka mipaka kuzunguka mlima na utenge kwa ajili ya Yahweh.'"
\v 24 Yahweh akamwambia, Nenda, shuka chini ya mlima, na umelete Aruni na wewe, lakini usiache makuhani na watu kupita vizuizi na kuja kwangu, au nitawashambulia."
\v 25 Hivyo Musa akaenda chini kwa watu na kusema nao.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Mungu alisema maneno yote haya:
\v 2 Ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa katika ardhi Misri, nje ya nyumba ya utumwa.
\v 3 Msiwe na miungu mingine ila mimi tu.
\s5
\v 4 Msijitengenezee sanamu za kuchonga kufananisha na kitu chochote kilichopo juu ya mbingu, chini ya ardhi, au ndani ya maji.
\v 5 Msipinde na kuabudu sanamu, mimi Yahweh Mungu wenu, ni Mungu mwenye wivu. Nitaadhibu uovu wa mabubu kwa kuleta adhabu juu ya kizazi, cha tatu hadi kizazi cha nne kwa wale wanao nichukia.
\v 6 Ila nitaweka agano la uaminifu kwa maelfu watakao nipenda na kushika amri zangu.
\s5
\v 7 Usilitaje bure jina la Yahweh Mungu wako, sitkuwa na hatia kwa yeyote atakaye taja jina langu bure.
\s5
\v 8 Ikumbuke siku ya Sabato, na kunitengea.
\v 9 lazima ufanye kazi zako zote kwa siku sita.
\v 10 Ila siku ya saba ni Sabato kwaajili ya Yahweh Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, au mwana wako, au binti yako, au mtumishi wako wakiume, au mtumishi wako mwanamke, au ng'ombe zako, au mgeni aliye ndani ya malango yako.
\v 11 Kwa siku sita Yahweh aliumba mbingu na nchi, bahari, na vitu vyote vilivyomo, na siku ya saba alipumzika. Kwa hiyo Yahweh aliibariki siku ya Sabato na kuitenga.
\s5
\v 12 Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.
\v 13 Usiue.
\v 14 Usifanye uasherati (usizini).
\s5
\v 15 Usiibe kwa mtu yoyote.
\v 16 Usishuhudie uongo dhidi ya jirani yako.
\v 17 Usitaman nyumba ya jirani yako; usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wakiume, mtumishi wake mwanamke, ng'ombe wake, punda wake, au chochote cha jirani yako.
\s5
\v 18 Watu wote waliona radi na umeme, na kusikia sauti ya mbiu, na mlima ukitoa moshi. Watu walipoona hivo, walitetemeka na kusimama mbali.
\v 19 Wakamwambia Musa, ongea na sisi, na tutakusikiliza; lakini usiruhusu Mungu kuongea nasi, ama tutakufa.
\v 20 Musa akawaambia watu, "msiogope, Mungu alikuja kuwajaribu ili heshima yake iwe ndani yenu, kwa hiyo msitende dhambi."
\v 21 hivyo watu walisimama mbali, na Musa alikaribia giza nene Mungu alipokuwa.
\s5
\v 22 Yahweh alimwambia Musa, "Ni lazima uwaambie hili Waisraeli: 'Wewe mwenyewe umeona niliongea na wewe kutoka mbinguni.
\v 23 Misjitengenezee miungu mingine pamoja nami, miungu ya fedha au miungu ya dhahabu.
\s5
\v 24 Tengenezeni madhabahu ya udongo kwa ajili yangu, na lazima mtoe sadaka ya kuteketeza, sadaka ya ushirika, kondoo, na ng'ombe. kila sehemu ntakapotaka jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki.
\v 25 Kama mtatengeneza madhabahu ya mawe, msijenge na mawe yaiyokatika, na kama mtatumia vyombo vyenu juu yake, mtaweka unajisi.
\v 26 msije juu ya madhabahu yangu kwa hatua zenu; hii ni ili msioneshe sehemu zenu za siri."
\s5
\c 21
\p
\v 1 Sasa hizi ni amri utakazoweka kabla yao:
\s5
\v 2 'kama mtanunua mtumishi wa kiebrania, atatumikia kwa miaka sita, na mwaka wa saba ataachiwa huru bila kilipwa chochote.
\v 3 Kama alikuja mwenyewe, ataenda huru kwa ridhaa yake;
\v 4 kama bwana wake atampa mke na kumzalia mwana na binti, mke pamoja na watoto wake watabaki mali ya bwana wake, na ataenda zake huru.
\s5
\v 5 Lakini kama mtumishi atasema waziwazi, "Nampenda bwana wangu, mke wangu, na watoto; sitaenda nje,"
\v 6 "kisha bwana wake atapaswa kumleta kwa Mungu. Bwana wake atapaswa kumleta katika mlango au katika muhimili wa mlango, na bwana wake atatoboa sikio lake na sindano. Kisha mtumishi wake atamtumikia kwa maisha yake yote.
\s5
\v 7 Kama mwanaume ata muuza binti wake kama mtumishi wa kike, ata weza kwenda huru kama watumishi wa kiume wanavyo enda.
\v 8 Kama hamridhishi bwana wake, aliye mtenga kwa ajili yake, kisha lazima amnunue tena. Hana ruhusa ya kumuuza kwa watu wengine wa kigeni. Hana ruhusa hiyo, sababu amemtendea kwa hila.
\s5
\v 9 Ikiwa bwana wake atamposa awe mke wa mwanae, atamtendea kama desturi zipasavyo sawa na binti zake.
\v 10 Ikiwa atajitwalia mke mwingine, asimpunguzie huyo chakula chake, nguo na haki zake za unyumba.
\v 11 Lakini asipofanyiwa mambo haya matatu, basi anaweza kwenda bure pasipo kutolewa mali.
\s5
\v 12 Mtu awaye yote ampigaye mtu hata akafa, inampasa mtu huyo auawe pia.
\v 13 Lakini kama hakumvizia, ila kwa bahati mbaya, basi nitamfanyia mahali pa kukimbilia.
\v 14 Lakini mtu akimwendea mwenzake kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata kama ni madhabahuni pangu, ili auawe.
\s5
\v 15 Yeyote atakaye mpiga baba au mama yake lazima auawe.
\v 16 Yeyote atakaye mteka mtu na kumuuza, au mtu amekutwa kama mali yake, huyo mtekaji lazima auawe.
\v 17 Yeyote atakaye mlaani baba au mama yake lazima auawe.
\s5
\v 18 Kama wanaume watapigana na mmoja akimpiga mwengine kwa jiwe au ngumi, na huyo mtu asife, lakini alazwe kitandani;
\v 19 kisha akapona na anaweza kutembea kwa gongo lake, yeye aliye mpiga lazima alipe muda aliye mpotezea; na lazima alipe matibabu yake yote. Lakini huyo mtu hana hatia ya mauaji.
\s5
\v 20 Kama mwanaume akimpiga mtumishi wake wa kiume au wa kike kwa gongo, na kama mtumishi huyo akifa kwa madhara ya pigo, kisha huyo mtu lazima ahadhibiwe.
\v 21 Walakini, mtumishi huyo akiishi siku moja au mbili, bwana aruhusiwi kuadhibiwa, kwa kuwa atateseka kupoteza mtumishi huyo.
\s5
\v 22 Kama wanaume wakipigana pamoja na wakamuumiza wanamke mwenye mimba na kuiharibu, lakini hakuna majeraha mengine kwake, kisha huyo mwanaume mwenye hatia lazima alipe kama mme wa mwanamke anavyo taka kwake, na kulipa kama hakimu anavyo kusudia.
\v 23 Lakini kama kuna majeraha makubwa, lazima utoe uhai kwa uhai, jicho kwa jicho,
\v 24 jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,
\v 25 kuchoma kwa kuchoma, jeraha kwa jeraha, au mkwaruzo kwa mkwaruzo.
\s5
\v 26 Kama mwanaume akipiga jicho la mtumishi wake kiume au mtumishi wake wa kike na kuliharibu, kisha lazima amuache mtumishi aende pasipo fidia ya jicho.
\v 27 Kama akitoa jino la mtumishi wake wa kiume au mtumishi wake wa kike, lazima amuache mtumishi kwenda huru kama fidia ya jino.
\s5
\v 28 Kama ng'ombe akimpiga mwanaume au mwanamke akafa, ng'ombe lazima apigwe mawe, na nyama yake hairuhusiwi kuliwa; lakini mmiliki wa ng'ombe lazima awe huru kwa hatia.
\v 29 Lakini kama ng'ombe alikuwa na tabia ya kupiga hapo awali, na mmiliki wake alionywa lakini hakumzuia, na ng'ombe ameua mwanaume au mwanamke, huyo ng'ombe lazima apigwe mawe, na mmiliki wake lazima auawe pia.
\v 30 Kama malipo ya uhai yanaitajika, lazima alipe chochote anachotakiwa kulipa.
\s5
\v 31 Kama ng'ombe amempiga mwana wa mwanaume au binti wake, mmiliki wa ng'ombe anapaswa kufanya kama masharti yanavyo mlazimu.
\v 32 Kama ng'ombe akimpiga mtumishi wa kiume au wakike, mmiliki wa ngombe lazima alipe shekeli thelathini za fedha, na ng'ombe lazima apigwe mawe.
\s5
\v 33 Kama mwanaume akifungua shimo, au kama mwanume akichimba shimo na asifunike, na ng'ombe au punda akaanguka ndani,
\v 34 mmiliki wa shimo lazima alipe madhara. Lazima atoe hela kwa mmiliki wa mnyama aliye kufa, na mnyama aliye kufa atakuwa wake.
\s5
\v 35 Kama ng'ombe wa mwanaume akimuumiza ng'ombe wa mwanume mwengine hadi kufa, kisha lazima wamuuze ng'ombe aliye hai na kugawana gharama, na pia lazima wagawane ng'ombe aliye kufa.
\v 36 Lakini kama ilijulikana kama ng'ombe alikuwa na tabia ya kupiga hapo awali, na mmiliki wake hakumfunga ndani, hakika lazima alipe ng'ombe kwa ng'ombe, na mnyama aliye kufa atakuwa wake.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kama mwanaume akiiba ng'ombe aua kondoo na kumuua au kumuuza, kisha lazima alipe ng'ombe watano au ng'ombe mmoja, na kondoo wanne kwa mmoja.
\v 2 Kama mwizi akikutwa anavunja ndani, na kama akipigwa na kufa, hakutakuwa na hatia ya mauaji hayatakuwa juu ya mtu yeyote.
\v 3 Lakini kama jua limechomoza kabla ya yeye kuvunja ndani, hatia ya mauaji itakuwa juu ya aliyemuua. Mwizi lazima afanya alipe alichoiba. Kama hana chochote, kisha lazima auzwe kwa uwizi wake.
\v 4 Kama mnyama amekutwa hai eneo lake, kama ni ng'ombe, punda, au kondoo, lazima alipe mara mbili.
\s5
\v 5 Kama mwanaume akiwapeleka malishoni mifugo yake au shamba la mizabibu na akawaachia wanyama wake, na kawa wanakula shambani mwa mwanaume mwengine, lazima afanye malipo bora kutoka shambani mwake na shamba lake la mizabibu.
\s5
\v 6 Kama moto ukitokea na kusambaa kwenye miba hadi mbegu, au mimea, au shamba kuteketezwa, yeye aliye anzisha moto lazima afanye malipo.
\s5
\v 7 Kama mwanaume akitoa pesa au mali kwa jirani yake amtunzie, na kama itaibiwa nyumbani mwa huyo mwanaume, kama mwizi akipatikana, huyo mwizi lazima alipe mara mbili.
\v 8 Lakini kama mwizi asipo patikana, kisha mmiliki wa nyumba ata kuja mbele za waamuzi kuona kama ameeka mkono wake kwenye mali za jirani yake.
\v 9 Kwa kila lumbano kuhusu jambo, kama ni ng'ombe, punda, kondoo, nguo, au chochote kilichopotea mtu anacho sema, "Hichi ni changu," malalamiko ya pande zote lazima zije kwa waamuzi. Mwanaume ambaye waamuzi wanamkuta na hatia ata lipa mara mbili kwa jirani yake.
\s5
\v 10 Kama mwanaume akimpa jirani yake punda, ng'ombe, kondoo, au mnyama yeyote kumuhifadhia, na kama akifa au kuumia au akibebwa pasipo mtu kumuona,
\v 11 kiapo kwa Yahweh lazima wafanye wote wawili, kama ndio au hapana mtu ameeka mkono wake kwenye mali ya jirani yake. Mmiliki lazima akubali hili, na mwengine hatafanya malipo.
\v 12 Lakini kama iliibwa kwake, mwengine lazima afanye malipo kwa mmiliki kwa ajili yake.
\v 13 Kama mnyama alikatwa vipande, acha mwanaume mwengine alete huyo mnyama kama ushahidi. Hatalipa kwa ajili ya vile vipande.
\s5
\v 14 Kama mwanaume akiazima mnyama kutoka kwa jirani yake na mnyama akajeruhia au akafa pasipo mmiliki kuwa naye, mwanaume mwengine lazima afanya malipo.
\v 15 Lakini kama mmiliki alikuwa nae, mwanaume mwengine haitaji kulipa; kama mnyama aliazimwa, atalipwa kwa gharama ya kuazima.
\s5
\v 16 Kama mwanaume akimtongoza bikra ambaye hana mchumba, na kama akilala naye, lazima amfanye kuwa mke wake kwa kulipa gharama za bibi arusi zinazo stahili.
\v 17 Kama baba yake akikataa kabisa kumpatia, lazima alipe hela inayo lingana na gharama za bibi arusi bikra.
\s5
\v 18 Hautamwacha mchawi kuishi.
\v 19 Yeyote atakaye lala na mnyama lazima auawe.
\s5
\v 20 Yeyote atakaye toa dhabihu kwa mungu mwengine isipo kuwa Yahweh lazima auawe.
\v 21 Hauta mkosea mgeni au kumnyanyasa, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
\s5
\v 22 Hauruhusiwi kumtendea vibaya mjane au mtoto asiye kuwa na baba.
\v 23 Ukiwadhuru ata kidogo, na kama wakiniita mimi, hakika nitasikia sauti yao.
\v 24 Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba.
\s5
\v 25 Ukiazima hela kwa watu wangu walio maskini, haupaswi kuwa kama anaye kopesha hela kwake au kutoza faida.
\v 26 Ukichukuwa vazi la jirani yako kwa deni, lazima umrudishie kabla jua kuzama,
\v 27 kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma.
\s5
\v 28 Usinikufuru mimi, Mungu, wala kumtukana mtawala wa watu wako.
\s5
\v 29 Husizuie sadaka kutoka kwenye mavuno yako au kwenye hifadhi ya mvinyo wako. Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.
\v 30 Lazima ufanye hivyo hivyo kwa ng'ombe na kondoo wako. Kwa siku saba lazima wabaki na mama zao, lakini siku ya nane lazima unipe mimi.
\v 31 Mtakuwa watu walio tengwa kwa ajili yangu. Hivyo hamtakula nyama iliyo uliwa na wanyama porini. Badala yake, uwatupie mbwa.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Haupaswi kutoa taarifa ya uongo kuhusu yeyote. usijiunge na mwanaume muovu kuwa shahidi wa uongo.
\v 2 Haupaswi kufuata umati kufanya uovu, wala kutoa ushahidi ukiwa na umati ili kupotosha haki.
\v 3 Haupaswi kumpendelea mwanaume maskini kwenye kesi yake.
\s5
\v 4 Ukikutana na ng'ombe wa adui wako au punda wake amepotea, lazima umrudishie.
\v 5 Ukiona punda wa yule anaye kuchukia ameanguka chini na mzigo wake, hauta muacha huyo mtu. Lazima umsaidie na punda wake
\s5
\v 6 Haupaswi kupotosha haki kama yapaswa kwenda kwa watu maskini katika kesi ya mwanaume maskini.
\v 7 Usijiunge na wengine kufanya shutuma za uongo, na usiue asiye na hatia wala mwenye haki, kwa kuwa sitamuacha muovu.
\v 8 Husiwai chukuwa rushwa, kwa kuwa rushwa inawapofusha wanaoona, na kupotosha maneno ya wakweli.
\v 9 Haupaswi kumnyanyasa mgeni, kwa kuwa wewe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri.
\s5
\v 10 Kwa miaka sita utapanda mbegu kwenye nchi yako na kukusanya mazao yake.
\v 11 Lakini katika mwezi wa saba utaacha hakujalimwa, ili kwamba maskini miongoni mwenu wale. Wanacho acha, wanyama wa porini watakula. Utafanya hivyo na mashamba yenu ya mizabibu na ya mizaituni.
\s5
\v 12 Wakati wa siku sita utafanya kazi, lakini siku ta saba utapumzika. Fanya hivi ili ng'ombe na punda wako wapumzike, na ili wana wa watumwa wako wa kike na wageni wapumzike na kupata hauweni.
\v 13 Kuwa makini kwa kila kitu nilicho kwambia. Husitaje majina ya miungu mingine, wala kuruhusu majina yao kusikika kutoka mdomoni mwako.
\s5
\v 14 Lazima usafiri kusherehekea mara tatu kwa ajili yangu kila mwaka.
\v 15 Lazima uadhimishe sherehe ya Mkate usiotiwa Chachu. Kama nilivyo kuamuru, utakula mkate usiotiwa chachu kwa siku saba. Wakati huo, utajitokeza kwangu mwezi wa Abibu, uliowekwa kwa ajili ya kusudi hili. Ni kwa mwezi huu uliyo toka Misri. Lakini usijitokeze kwangu mikono mitupu.
\s5
\v 16 Lazima uadhimishe Sherehe ya Mavuno, matunda ya kwanza ya kazi yako ulipo panda mbegu shambani. Pia lazima uadhimishe Sherehe ya Ukusanyaji wa mwisho wa mwaka, unapo kusanya mazao yako kutoka shambani.
\v 17 Wanaume wote wako lazima wajitokeze kwa Bwana Yahweh mara tatu kila mwaka.
\s5
\v 18 Haupaswi kutoa damu iliyo tolewa dhabihu kwangu na mkate uliyotiwa hamira. Mafuta kutoka kwa dhabihu za sherehe zangu hayapaswi kubaki usiku wote mpaka asubui.
\v 19 Lazima ulete matunda ya kwanza bora kutoka shambani mwako ndani ya nyumba yangu, nyumba ya Yahweh Mungu wako. Haupaswi kumchemsha mbuzi mtoto akiwa bado ananyonya.
\s5
\v 20 Ninaenda kumleta malaika mbele yako kukuongoza njiani, na kukuleta sehemu niliyo iandaa.
\v 21 Kuwa makini naye na kumtii.
\v 22 Husimkasirishe, kwa kuwa hatasamehe makosa yako. Jina langu liko kwake. Kama hakika ukimtii sauti yake na kufanya kila ninacho kwambia, kisha nitakuwa adui kwa adui zako na mpinzani kwa wapinzani wako.
\s5
\v 23 Malaika mwangu ataenda mbele zako na kukuleta kwa Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanani, Wahivi, na Wayebusi. Nitawaharibu.
\v 24 Haupaswi kuinamia miungu yao, kuabudu, au kufanya wanavyo fanya. Badala yake, lazima uwapindue kabisa na kuvunja nguzo zao za mawe vipande vipande.
\v 25 Lazima umuabudu Yahweh Mungu wako, na atabariki mkate wako na maji. Nitaondoa magonjwa miongoni mwenu.
\s5
\v 26 Hakuna mwanamke atakaye kuwa tasa au mimba kuharibika katika nchi yako. Nitawapa maisha marefu.
\v 27 Nitatuma hofu yangu kwao ambao mnaenda. Nitaua wote mnao kutana nao. Nitafanya maadui zenu wawaogope kwa kugeuza migongo yao kwenu.
\v 28 Nitatuma mavu kwenu watakao fukuza Wahivi, Wakanani, na Wahiti mbele zenu.
\v 29 Sitawaondoa kwenu kwa mwaka mmoja, au nchi itakuwa imetelekezwa, na wanyama wa porini watakuwa wengi kwenu.
\s5
\v 30 Badala yake, nitawafukuza kidogo kidogo kutoka kwenu mpaka utakapo kuwa umestawi na kurithi nchi.
\v 31 Nitatengeneza mipaka yako kutoka Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kutoka nyikani hadi Mto Frati. Nitakupa ushindi juu ya wakazi wote wa nchi. Utawaondoa kutoka kwako mwenyewe.
\v 32 Haupaswi kufanya agano na wao au na miungu yao.
\v 33 Hawapaswi kuishi nchini mwako, au watakufanya ufanya dhambi dhidi yangu. Ukiabudu miungu yao, hakika watakuwa mtego kwako.'"
\s5
\c 24
\p
\v 1 Kisha Yahweh akamwabia Musa, "Njoo juu kwangu -wewe, Aruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli, na kuniabudu kwa mbali.
\v 2 Musa peke yake anaweza kuja karibu yangu. Wengine hawapaswi kuja karibu, wala watu kuja juu na yeye."
\s5
\v 3 Musa akaenda juu na kuwaambia watu maneno yote ya Yahweh na amri zake. Watu wote wakajibu kwa sauti moja na kusema, "Tutafanya maneno yote Yahweh aliyo tuamuru."
\v 4 Kisha Musa akaandika chini maneno yote ya Yahweh. Asubui mapema, Musa akajenga madhabahu chini ya mguu wa mlima na kupanga nguzo kumi na mbili za mawe, ili mawe yawakilishe makabila kumi na mbili ya Israeli.
\s5
\v 5 Aliwatuma vijana Wakiisraeli kutoa sadaka ya kuteketeza na kutoa dhabihu za ng'ombe za sadaka ya ushirika kwa Yahweh.
\v 6 Musa allichukuwa nusu ya damu na kuweka kwenye mabeseni; alinyunyuzia nusu ingine kwenye madhabahu.
\s5
\v 7 Alichukuwa kitabu cha agano na kuwasomea kwa nguvu watu. Walisema, "Tutafanya yote Yahweh aliyo sema. Tutakuwa watiifu."
\v 8 Kisha Musa akachukuwa damu na kunyunyiza kwa watu. Alisema, "Hii ni damu ya agano Yahweh alilo lifanya nanyi kwa kuwapa hii ahadi kwa maneno yote haya."
\s5
\v 9 Kisha Musa, Aruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli wakaenda juu ya mlima.
\v 10 Walimuona Mungu wa Israeli.
\v 11 Chini ya miguu yake kulikuwa na sakafu iliyo jengwa kwa jiwe la yakuti samawi, safi kama mbingu yenyewe. Mungu hakugusa na mkono kwa hasira viongozi Waisraeli. Walimuona Mungu, na wakanywa na kula.
\s5
\v 12 Yahweh akamwambia Musa, "Njoo juu kwangu mlimani na ubaki pale. Nitakupa saani za mawe na sheria na amri nilizo ziandika, ili uwafundishe."
\v 13 Hivyo Musa akaenda na msaidizi wake Yoshua na kwenda juu mlima wa Mungu.
\s5
\v 14 Musa akawaambia wazee, "Baki hapa na mtusubiri hadi tutakapo warudia. Aruni na Huri wapo nanyi. Kama kuna mtu mwenye malalamiko, acha awaende."
\v 15 Hivyo Musa akaenda juu ya mlima, na wingu likafunika.
\s5
\v 16 Utukufu wa Yahweh ukabaki juu ya Mlima wa Sinai, na wingu likafunika kwa siku sita. Siku ya saba alimuita Musa kutoka ndani ya wingu.
\v 17 Utukufu wa Yahweh ulikuwa kama moto ulao juu ya mlima kwenye macho ya Waisraeli.
\v 18 Musa akaingia kwenye wingu na kwenda juu ya mlima. Alikuwa mlimani siku arobaini na usiku arobaini.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa,
\v 2 “Waambie Waisraeli wanitolee sadaka kila mtu nawe utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu. Lazima upokee hizi sadaka kwa ajili yangu.
\s5
\v 3 Hizi ndio sadaka utakazopokea kwao; dhahabu, fedha na shaba,
\v 4 buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na manyoya ya mbuzi;
\v 5 na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, miti ya mjohoro,
\v 6 mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;
\v 7 mawe ya shohamu na mawe mengine ya kutiwa kwa ile naivera na kwa kile kifuko cha kifuani.
\s5
\v 8 Waache wanifanyie patakatifu ili nipate kukaa kati yao.
\v 9 Lazima ufanye sawa na haya yote nikuoneshayo mfano wa maskani, na vifaa vyake, ndivyo utakavyovifanya.
\s5
\v 10 Wana paswa wafanye sanduku la mti wa mjohoro. Urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu; na upana wake moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
\v 11 Lazima ulifunike nadni kwa dhahabu safi, na utie na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
\s5
\v 12 Nawe uta yayusha katika viduara vinne vya dhahabu, na kuviweka katika miguu yake minne; viduara viwili upande mmoja, na viduara viwili upande wake wa pili.
\v 13 Nawe lazima ufanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu.
\v 14 Nawe lazima uweka hiyo miti katika vile viduara vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.
\s5
\v 15 Hiyo miti itakaa katika vile viduara vya sanduku; haitaondolewa.
\v 16 Kisha weka ndani ya sanduku hizo amri nitakazokupa.
\v 17 Nawe lazima utengeneze kifuniko cha dhahabu safi. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu.
\v 18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu katika hiyo miisho miwili ya kiti cha rehema.
\s5
\v 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja wa kiti cha rehema, na kerubi la pili mwisho wa pili. Lazima hao makerubi wawe kitu kimoja na kiti cha rehema.
\v 20 Na hao makerubi watainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao. Nyuso zao makerubi zitaelekeana na zitaelekea kiti cha rehema.
\v 21 Lazima uweke kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha uwe hizo amri nitakazokupa ndani ya sanduku.
\s5
\v 22 Nami nitaonana nawe hapo katika sanduku. Nitazungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema. Itakuwa katikati ya hao makerubi mawili waliyo juu ya sanduku la ushuhuda nitakapo zungumza na wewe katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
\s5
\v 23 Nawe fanya meza ya mti wa mshiti. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
\v 24 Uifunike dhahabu safi na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote.
\s5
\v 25 Lazima ufanyie fremu ya kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, ukingo wa dhahabu wa kuuzunguka fremu pande zote.
\v 26 Uifanyie viduara vinne vya dhahabu na kuvitia vile viduara katika pembe zake nne, katika miguu yake minne ilipo kuwa.
\v 27 Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza.
\s5
\v 28 Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.
\v 29 Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia. Vifanye vyote vya dhahabu safi.
\v 30 Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.
\s5
\v 31 Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho.
\v 32 Nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake - matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili.
\s5
\v 33 Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara.
\v 34 Katika hicho kinara, lazima kuwe na vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake.
\s5
\v 35 Lazima kuwe na tovu chini ya matawi - mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara.
\v 36 Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho, kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.
\s5
\v 37 Lazima nawe uzifanye hivyo vinara saba na taa zake saba, nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.
\v 38 Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.
\v 39 Tumia talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.
\v 40 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Lazima ufanye hiyo maskani iwe na mapazia kumi ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi. Kazi ya fundi stadi.
\v 2 Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne. Mapazia yote yatakuwa ya kipimo kimoja.
\v 3 Mapazia matano yataungwa pamoja, na mapazia matano mengine yataungwa pamoja.
\s5
\v 4 Lazima ufanye tanzi za rangi ya samawati upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake. Vivyo hivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili.
\v 5 Fanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upande wa mwisho wa ile pazia iliyo katika kuungana kwa pili.
\v 6 Fanya hivi ili hizo tanzi zielekeana. Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganisha hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo na hiyo maskani itakuwa ni moja.
\s5
\v 7 Lazima ufanye mapazia ya nywele za mbuzi yawe hema juu ya maskani. Lazima ufanye mapazia kumi na moja.
\v 8 Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne. Hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja.
\v 9 Lazima utaunganisha mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalikunja hapo upande wa mbele wa ile hema.
\s5
\v 10 Ufanye tanzi hamsini upande wa mwisho wa pazia lile lililo la mwisho katika hayo yaliyounganywa pamoja, na tanzi hamsini upande wa mwisho wa lile pazia lililo nje katika hayo ya pili yaliyounganywa pamoja.
\v 11 Kisha ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja.
\s5
\v 12 Kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani.
\v 13 Lazima kuwe na dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili - ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika.
\v 14 Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.
\s5
\v 15 Nawe lazima ufanye hizo fremu za maskani za mti wa mjohoro.
\v 16 Kila fremu utakuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wake kila ubao utakuwa dhiraa moja na nusu.
\v 17 Kila fremu itakuwa na ndimi mbili, zenye kuunganishwa huu na huu. Ndivyo utakavyozifanya mbao zote za maskani.
\v 18 Kisha ufanye zile mbao za maskani, mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini.
\s5
\v 19 Lazima nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile fremu ishirini. Vitako viwili chini ya fremu moja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya fremu nyingine kupokea zile ndimi zake mbili.
\v 20 Kwa upande wa pili wa maskani, upande wa kaskazini, mbao ishirini
\v 21 na vitako vyake vya fedha arubaini. Lazima kuwe na vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya fremu nyingine.
\s5
\v 22 Ufanye fremu sita kwa ajili ya upande wa nyuma wa maskani kuelekea magharibi.
\v 23 Tena ufanye fremu mbili kwa ajili ya hizo pembe za maskani zilizo upande wa nyuma.
\v 24 Hizi fremu zitakuwa zimetengana upande wa chini, lakini zimeshinkana kwa juu ya duara moja.
\v 25 Fremu zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha. Vitako kumi na sita, vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili.
\s5
\v 26 Lazima ufanye mataruma ya mti wa mshita- mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani,
\v 27 na mataruma matano kwa ajili ya fremu za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya fremu za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi.
\v 28 Na hilo taruma la katikati lililo katikati ya zile fremu, litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu.
\s5
\v 29 lazima uzifunuke hizo fremu kwa dhahabu. Nawe lazima ufanye maduara yake ya za dhahabu, kuwa kama vishikizo, na hayo mataruma utayafunika dhahabu.
\v 30 Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani.
\s5
\v 31 Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi.
\v 32 Kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne.
\v 33 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda. Lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.
\s5
\v 34 Nawe lazima utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. Na ile meza utaiweka nje ya pazia.
\v 35 Lazima uweke kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini. Lile meza utaiweka upande wa kaskazini.
\s5
\v 36 Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa hema, cha nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji wa taraza.
\v 37 Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu. Nawe utasubu vitako vya shaba vitano kwa ajili yake.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita, urefu wake utakuwa ni dhiraa tano na upana wake dhiraa tano. Hiyo madhabahu itakuwa mraba na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.
\v 2 Nawe fanya pembe nne kama mfano wa pembe za ng'ombe. Hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu, nawe utayafunika kwa shaba.
\s5
\v 3 Lazima vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake. Vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.
\v 4 Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba. Kisha utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu.
\s5
\v 5 Nawe lazima uweke huo wavu chini ya kizingo kiizungukacho madhabahu upande wa chini.
\v 6 Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba.
\s5
\v 7 Na hiyo miti itatiwa katika viduara, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua.
\v 8 Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake kama ulivyooneshwa mlimani.
\s5
\v 9 Nawe ufanye ua wa maskani. Upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja.
\v 10 Na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
\s5
\v 11 Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba, kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.
\v 12 Na upande wa magharibi, upana wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi, na vitako vyake kumi.
\v 13 Na upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini.
\s5
\v 14 Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa dhiraa kumi na tano upana wake. Lazima nguzo zake zitakuwa tatu na vitako vyake vitatu.
\v 15 Upande wa pili ni vivyo hivyo chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu, na vitako vyake vitatu.
\v 16 Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.
\s5
\v 17 Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba.
\v 18 Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba.
\v 19 Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.
\s5
\v 20 awe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.
\v 21 Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Umuite Aruni kaka yako na wana wake - Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari - miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
\v 2 Nawe utamfanyia Aruni ndugu yako mavazi matakatifu, kwa utukufu na kwa uzuri.
\v 3 Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Aruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani.
\s5
\v 4 Na mavazi watakayoyafanya ni kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo, na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Aruni nduguye, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
\v 5 Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu.
\s5
\v 6 Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawi, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi.
\v 7 Lazima itakuwa na vipande viwili vya mabegani, vilivyoungana kwenye ncha zake mbili; ili ipate kuunganywa.
\v 8 Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.
\v 9 Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu, ya rangi ya chani-kiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;
\s5
\v 10 Majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao.
\v 11 Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
\v 12 Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli. Naye Aruni atayachukua majina yao mbele za Yahweh juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho.
\s5
\v 13 Nawe fanya vijalizo viwili vya dhahabu
\v 14 na mikufu miwili ya dhahabu safi; utaifanya iwe mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa; nawe uitie ile mikufu ya kazi ya kusokotwa katika vile vijalizo.
\s5
\v 15 Nawe lazima utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera. Fanya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.
\v 16 Kitakuwa mraba, tena cha kukunjwa; urefu wake utakuwa shibiri moja, na upana wake shibiri moja.
\s5
\v 17 Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza.
\v 18 Na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi.
\v 19 Na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto.
\v 20 Na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi. Vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.
\s5
\v 21 Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao. Mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili.
\v 22 Nawe lazima utie katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa, ya dhahabu safi.
\v 23 Nawe utie maduara mawili ya dhahabu katika kile kifuko cha kifuani, na kuzitia hizo pete mbili katika ncha mbili za kifuko cha kifuani.
\v 24 Nawe utie hiyo mikufu miwili ya dhahabu iliyosokotwa katika zile pete mbili zilizo katika ncha za kifuko cha kifuani.
\s5
\v 25 Na ncha zile nyingine za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa utazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera upande wa mbele.
\v 26 Nawe utafanya viduara vili vya dhahabu, uzitie katika hizo ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake.
\s5
\v 27 Nawe lazima ufanye viduara vili vya dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
\v 28 Nao watakikaza kile kileso kwa vile viduara vyake kwenye viduara za naivera kwa ukanda wa rangi ya samawi, ili kwamba kikae pale juu ya ule mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, ili kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera.
\s5
\v 29 Na Aruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake kwa kufanya maamuzi, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele yaYahweh daima.
\v 30 Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Aruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Yahweh na Aruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Yahweh daima.
\s5
\v 31 Nawe fanya hiyo joho ya naivera ya rangi ya samawi yote.
\v 32 Nayo itakuwa na tundu katikati yake kwa kupitisha kichwa; itakuwa na utepe wa kazi ya kusokotwa kuzunguka hilo tundu lake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, ili lisipasuke.
\s5
\v 33 Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote.
\v 34 Kengele ya dhahabu na komamanga, kengele ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote.
\v 35 Nayo itakuwa juu ya Aruni akitumika; na sauti ya hizo kengele itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Yahweh na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
\s5
\v 36 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, "Mtakatifu kwa Yahweh."
\v 37 Nawe ulitie hilo bamba katika ukanda wa rangi ya samawi, nalo litakuwa katika kile kilemba; litakuwa upande wa mbele wa kile kilemba.
\v 38 Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Aruni, na Aruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za Yahweh.
\s5
\v 39 Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wa kazi ya mwenye kutia taraza.
\s5
\v 40 Kisha utafany kanzu kwa ajili ya wana wa Aruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.
\v 41 Nawe mvike huyo nduguye Aruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.
\s5
\v 42 Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani.
\v 43 Aruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Sasa Hivi ndivyo wapaswa kufanya kuwatenga ili wanitumikie kama makuhani. Chukuwa mtoto wa ng'ombe dume na kondoo bila lawama,
\v 2 mkate bila hamira, na keki bila hamira iliyo changanywa na mafuta. Pia chukuwa maandazi bila hamira yalio pakwa mafuta. Fanya maandazi kwa unga mzuri wa ngano.
\s5
\v 3 Lazima uweke kwenye ndoo moja, leta kwenye ndoo, na kuleta pamoja na ng'ombe dume na wana kondoo wawili.
\v 4 Lazima nawe umlete Aruni na wana wake wawili katika lango la kuingilia hema la kukutania. Lazima uwasafishe Aruni na wana wake kwenye maji.
\s5
\v 5 Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho ya naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
\v 6 Nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba.
\v 7 Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta.
\s5
\v 8 Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu.
\v 9 Nawe uwakaze mishipi, Aruni na wanawe, na kuwavika kofia. Nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele. Nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.
\s5
\v 10 Kisha utamleta huyo ngombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ngombe.
\v 11 Kisha utamchinja huyo ngombe mbele ya Yahweh pa hema ya kukutania. BWANA,
\s5
\v 12 Kisha twaa baadhi ya damu ya ngombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.
\v 13 Kisha chukuwa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.
\v 14 Lakini nyama yake huyo ngombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marago; ni sadaka kwa ajili ya dhambi.
\s5
\v 15 Pia mtwae kondoo mume mmoja; na Aruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo mume.
\v 16 Kisha utamchinja huyo kondoo mume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kando-kando.
\v 17 Kisha utamkata-kata kondoo vipande vyake, na kuyaosha matumbo yake na miguu yake, na kuiweka pamoja na vipande vyake na kichwa chake,
\v 18 nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yaYahweh; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa Yahweh kwa njia ya moto.
\s5
\v 19 Kisha mtwae huyo kondoo mwingine; na Aruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo.
\v 20 Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Aruni la upande wa kuume, na katika ncha za masikio ya kuume ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kuume, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kando-kando.
\s5
\v 21 Kisha twaa katika hiyo damu iliyo juu ya madhabahu, na katika hayo mafuta ya kutiwa, na kumnyunyizia Aruni, juu ya mavazi yake, na wanawe, na mavazi yao pia, pamoja naye; naye atatakaswa, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye.
\s5
\v 22 Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu.
\v 23 Utwae na mkate mmoja wa unga, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na kaki moja katika kile kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichowekwa mbele ya Yahweh.
\s5
\v 24 Nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Aruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisa-tikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
\v 25 Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, viwe harufu nzuri mbele yangu; ni sadaka iliyotengenezwa kwangu kwa njia ya moto.
\s5
\v 26 Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahwe nacho kitakuwa ni sehemu yako.
\v 27 Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Aruni na wanawe.
\v 28 Navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 29 Na hayo mavazi matakatifu ya Aruni yatakuwa ya wanawe baada yake, wayavae watakapotiwa mafuta, na watakapowekwa kwa kazi takatifu.
\v 30 Huyo mwanawe atakayekuwa kuhani badala yake atayavaa muda wa siku saba, hapo atakapoingia ndani ya hiyo hema ya kukutania, ili atumike ndani ya mahali patakatifu.
\s5
\v 31 Nawe twaa huyo kondoo mume aliyekuwa wa kuwekwa kwa kazi takatifu, na kuitokosa nyama yake katika mahali patakatifu.
\v 32 Na Aruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania.
\v 33 Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu.
\v 34 Na kwamba kitu cho chote cha ile nyama, iliyo kwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au cho chote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu
\s5
\v 35 Ni hivyo utakavyowatendea Aruni na wanawe kama nilivyo kuagiza. Utawaweka kwa kazi takatifu siku saba.
\v 36 Kila siku utamtoa ngombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa.
\v 37 Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.
\s5
\v 38 Lazima utoe kwenye madhabahu wana-kondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku
\v 39 daima. Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni
\s5
\v 40 Pamoja na mwana-kondoo mmoja utatoa vibaba vitatu vya unga mzuri uliochanganyika na mafuta yenye kupondwa, kiasi cha kibaba na robo kibaba; na divai kiasi cha kibaba na robo kibaba, iwe sadaka ya kinywaji.
\s5
\v 41 Na huyo mwana-kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni. Nawe utamfanyia vivyo kama ile sadaka ya unga ya asubuhi, na kama ile sadaka yake ya kinywaji. Hii itatoa harufu nzuri, ni dhabihu ya kusongezwa kwangu kwa njia ya moto.
\v 42 Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya Yahweh, hapo nitakapokutana nanyi, ili niseme na wewe hapo.
\s5
\v 43 Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo; na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu wangu. Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu.
\v 44 Pia Aruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
\s5
\v 45 Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao.
\v 46 Nao watanijua kuwa mimi ndimi Yahweh, Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao. Ni mimi Yahweh, Mungu wao.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Nawe fanya madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita.
\v 2 Urefu wake utakuwa dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; itakuwa mraba; na kwenda juu kwake dhiraa mbili; pembe zake zitakuwa za kitu kimoja nayo.
\s5
\v 3 Nawe utaifunikiza dhahabu safi juu yake - na mbavu zake kando kando, na pembe zake. Nawe utaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka.
\v 4 Kisha utaifanyia pete mbili za dhahabu, chini ya ukingo wake katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili utazifanya; nazo zitakuwa mahali pa kuitia miti ya kuichukulia madhabahu.
\s5
\v 5 Na ile miti utaifanya kwa mti wa mshita, na kuifunikiza dhahabu safi.
\v 6 Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe.
\s5
\v 7 Na Aruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi. Atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza,
\v 8 na Aruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Yahweh katika vizazi vyenu vyote.
\v 9 Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinywaji.
\s5
\v 10 Naye Aruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka. Kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote. Ni takatifu sana kwa Yahweh."
\s5
\v 11 BWANA akanena na Musa,
\v 12 "Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu.
\v 13 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini). Nusu shekeli kwa sadaka ya Yahweh.
\v 14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka kwangu.
\s5
\v 15 Watu watakapo leta hii sadaka kwangu kufanya upatananisho, matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua katika hiyo nusu shekeli.
\v 16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania. Ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele yangu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
\s5
\v 17 Yahweh akamwambia Musa,
\v 18 "Fanya na birika la shaba, na tako lake la shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji.
\s5
\v 19 Na Aruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo.
\v 20 Hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania au waendepo karibu na madhabahu kunitumikia kwa kuchoma sadaka, watajiosha majini, ili wasife.
\v 21 Basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.
\s5
\v 22 Kisha Yahweh akasema na Musa,
\v 23 "Jitwalie manukato yaliyo bora, manemane mbichi shekeli mia tano, na mdalasini wenye harufu nzuri 250, na kane shekeli 250
\v 24 na kida shekeli mia tano, kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu, na mafuta ya zeituni kiasi cha vibaba vitano.
\v 25 Nawe utayafanya mafuta ya kutiwa matakatifu, marhamu iliyochanganywa kwa kazi ya ustadi ya mtengezaji manukato; yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa.
\s5
\v 26 Nawe utaipaka hema ya kukutania kwa mafuta hayo, na hilo sanduku la ushuhuda,
\v 27 na hiyo meza, na vyombo vyake vyote, na kinara cha taa, na vyombo vyake,
\v 28 na madhabahu ya kufukizia uvumba, na madhabahu ya kuteketezea sadaka, pamoja na vyombo vyake vyote, na birika, na tako lake.
\s5
\v 29 Nawe utavitakasa vitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusacho vyombo vile kitakuwa kitakatifu.
\v 30 Nawe utawatia mafuta Aruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
\v 31 Nawe utanena na wana wa Israeli na kuwaambia, Haya yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa kwa ajili yangu mimi katika vizazi vyenu vyote.
\s5
\v 32 Hayatamiminwa katika kiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine mfano wa haya kama yalivyoungwa kwa viungo vyake; ni matakatifu, na kwenu ninyi yatakuwa matakatifu.
\v 33 Mtu awaye yote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu awaye yote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.'"
\s5
\v 34 Yahweh akamwambia Musa, "Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja.
\v 35 Nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu.
\v 36 Nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.
\s5
\v 37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili yangu.
\v 38 Mtu ye yote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Yahweh akasema na Musa,
\v 2 "Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda
\s5
\v 3 Nami nimemjaza Bezaleli na roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
\v 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,
\v 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.
\s5
\v 6 Tena, nimemchagua, awe pamoja naye Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani. Nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza. Hii ni,
\v 7 hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;
\v 8 na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote,
\v 9 na madhabahu ya kufukizia uvumba; na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake.
\s5
\v 10 Pia mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.
\v 11 Pia mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.
\s5
\v 12 akasema na Musa,
\v 13 "Waambie wana wa Israeli, 'Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.
\v 14 Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
\v 15 Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa.
\s5
\v 16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato. Kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.
\v 17 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Yahweh alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.
\s5
\v 18 Hapo Mungu alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa mkono wake.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Aruni, wakamwambia, "Njoo, katufanyizie sanamu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata."
\v 2 Hivyo Aruni akawaambia, "Zitoeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee."
\s5
\v 3 Watu wote wakavua pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, na wakamletea Aruni.
\v 4 Akapoke mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha. Nao wakasema, "Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri."
\s5
\v 5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Aruni akatangaza akasema,
\v 6 "Kesho itakuwa sikukuu kwa Yahweh." Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.
\s5
\v 7 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Shuka upesi, kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao.
\v 8 Wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu. Wakasema, 'Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.
\s5
\v 9 Kisha Yahweh akamwambia Musa, "Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu.
\v 10 Basi sasa usinizuie. Ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize. Nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu."
\v 11 Musa akamsihi sana Yahweh Mungu wake, na kusema,"Yahweh, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
\s5
\v 12 Kwa nini Wamisri kusema, 'Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi?' Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.
\v 13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, 'Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.'"
\v 14 Na Yahweh akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.
\s5
\v 15 Kisha Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake. Mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa.
\v 16 Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao.
\s5
\v 17 Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, "Kuna kelele ya vita kambini.
\v 18 "Lakini Musa akasema, "Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi."
\s5
\v 19 Hata alipoyakaribia kambini akaiona ile ndama, na watu wakicheza. Hasira ya Musa ikawaka. Akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
\v 20 Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji. Akawanywesha wana wa Israeli.
\s5
\v 21 Musa akamwambia Aruni, "Watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao?
\v 22 Aruni akasema, "Hasira yako isiwake, bwana wangu. Wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya.
\v 23 Maana waliniambia, 'Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu. Kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.'
\v 24 Nikawaambia, 'Mtu ye yote aliye na dhahabu na aivue; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu."
\s5
\v 25 Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi (maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao)
\v 26 Ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, "Mtu awaye yote aliye upande wa Yahweh na aje kwangu." Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia.
\v 27 Akawaambia, Yahweh, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.'"
\s5
\v 28 Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.
\v 29 Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa Yahweh leo, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili Yahweh awape baraka leo."
\s5
\v 30 Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, "Mmetenda dhambi kuu. Sasa nitakwenda juu kwa Yahweh. Labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu."
\v 31 Musa akarejea kwa Yahweh akasema," Oh! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.
\v 32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika."
\s5
\v 33 Yahweh akamwambia Musa, "Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.
\v 34 Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake. Tazama, malaika wangu atakutangulia. Lakini pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao."
\v 35 Kisha Yahweh akawapiga hao watu, kwa walivyoifanya ile ndama, ambayo Aruni aliifanya.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Yahweh anasema na Musa, "Nenda kutoka hapa, wewe na watu ulio watoa kutoka nchi ya Misri. Nenda kwenye nchi nilio fanya nadhiri na Ibrahimu, Isaka, Yakobo, nilipo sema, 'Nitakupa wewe na uzao wako'.'
\v 2 Nitatuma malaika mbele yako, na kuwaondoa Wakanani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
\v 3 Nenda kwenye hiyo nchi, inayo tiririka kwa maziwa na asali, lakini sitaenda nawe, kwasababu ninyi ni watu wajehuri. Ninaweza kuwaharibu njiani."
\s5
\v 4 Watu walipo sikia haya maneno ya kushtua, walilia, na hakuna aliye vaa mikufu.
\v 5 Yahweh alisema kwa Musa, "Waambie Waisraeli, 'Ninyi ni watu wakorofi. Kama ningeenda miongoni mwenu ata kwa muda kidogo, nigewaharibu ninyi. Hivyo sasa, toa mikufu yenu ili niamue nini cha kufanya kwenu."'
\v 6 Hivyo Waisraeli hawaku vaa mikufu kutoka Mlima Horebu na kwendelea.
\s5
\v 7 Musa akachukua hema na kukita nje ya kambi, umbali kidogo na kambini. Aliita hema ya kukutania. Kila mtu alliye muuliza Yahweh kitu chochote alienda kwenye hema ya kukutania, nje ya kambi.
\v 8 Kisha Musa alipo enda kwenye hema, watu wote walisima kando ya hema yao na kumuangalia Musa hadi alipo ingia ndani.
\v 9 Wakati wowote Musa alipo ingia hemani, nguzo ya wingu ilishuka chini na kusimama nje ya lango la hema, na Yahweh alizungumza na Musa.
\s5
\v 10 Wakati wowote watu walipo ona nguzo ya wingu imesimama langoni mwa hema, waliamka na kuabudu, kila langoni mwa hema yake.
\v 11 Yahweh alizungumza na Musa uso kwa uso, kama mtu anapo zungumza na rafiki yake. Kisha Musa alirudi kambini, lakini mtumishi wake Yoshua mwana wa Nuni, kijana, alibaki hemani.
\s5
\v 12 Musa alisema na Yahweh, "Ona, umekuwa ukisema na mimi, 'Chukuwa watu hawa safarini,' lakini hauja niambia nani utamtuma na mimi. Umesema, 'Nina kujua kwa jina, na umepata upendeleo kwangu.'
\v 13 Kama nimepata upendeleo machoni pako, nionyeshe njia zako ili nikujue na kuendelea kupata upendeleo machoni pako. Kumbuka ili taifa ni watu wako."
\s5
\v 14 Yahweh akajibu, "Uwepo wangu utaenda nawe, na nitakupa pumziko."
\v 15 Musa akasema, "Kama uwepo wako hautaenda nasi, usitutoe hapa.
\v 16 Au je, itajulikanaje niimepata upendeleo machoni pako, mimi na watu wako? Haitakuwa kuwa tu kama ukienda nasi mimi na watu wako tutakuwa na utofauti na watu wengine wote waliopo katika uso wa dunia?"
\s5
\v 17 Yahweh akamwambia Musa, "Nitafanya pia hichi kitu ulicho niomba, kwa kuwa umepata upendeleo machoni mwangu, na nina kujua kwa jina lako."
\v 18 Musa akasema, Tafadhali nionyeshe utukufu wako."
\s5
\v 19 Yahweh akasema, "Nitafanya wema wangu wote ujulikani kwako, na nitatangaza jina langu 'Yahweh' kwako. Nitakuwa na neema kwake nitakae kuwa na neema, na nitaonyesha rehema kwake nitakaye onyesha rehema."
\v 20 Lakini Yahweh akasema, "Hauta ona uso wangu, kwa kuwa hakuna aonaye uso wangu na kuiishi."
\s5
\v 21 Yahweh akasema, "Ona, hapa kuna sehemu yangu; utasimama kwenye huu mwamba.
\v 22 Wakati utukufu wangu unapita, nitakuweka kwenye shimo kubwa la mwamba na kukufunika kwa mkono wangu mpaka nitakapo pita.
\v 23 Kisha nitaondoa mkono wangu, na utaona mgongo wangu, ila uso wangu hautaonekana."
\s5
\c 34
\p
\v 1 Yahweh akamwabia Musa, "Kata mbao mbili za mawe kama zile za awali. Nitaandika kwenye hizi mbao za mawe maneno yaliyo kuwa kwenye mbao za mawe za mwanzo, mbao za mawe ulizo zivunja.
\v 2 Kuwa tayari asubui na uje Mlima Sinai, na uje mbele zangu juu ya mlima.
\s5
\v 3 Hakuna atakaye kuja nawe. Usiruhusu mtu yeyote aonekana popote kwenye mlima. Hakuna kundi la mifugo wanao ruhusiwa ata kula mbele ya mlima."
\v 4 Hivyo Musa akakata mbao mbili za mawe kama za mwanzo, na akaamka asubui mapema na kwenda juu ya Mlima Sinai, kama Yahweh alivyo muelekeza. Musa alibeba mbao za mawe mikononi mwake.
\s5
\v 5 Yahweh akaja chini katika wingu na akasima mbele za Musa, na akatamka jina "Yahweh."
\v 6 Yahweh akapita kwake na kukiri, "Yahweh, Yahweh, Mungu ni wa rehema na wa neema, sio mwepesi wa hasira, na anadumu katika uwaminifu wa agano na uadilifu,
\v 7 ukishika uaminifu wa agano kwa vizazi maelfu, ukisamehe maasi, makosa, na dhambi. Lakini hamsafishi mwenye hatia. Ataleta adhabu ya dhambi za baba kwa watoto wao na watoto wa watoto wao, kwa kizazi cha tatu na hadi cha nne."
\s5
\v 8 Musa haraka akainamisha kichwa chake kwenye ardhi na kuabudu.
\v 9 Kisha akasema, "Kama sasa nimepata upendeleo machoni pako, Bwana wangu, tafadhali nenda pamoja nasi, kwa kuwa hawa watu ni wa korofi. Samehe maasi yetu na dhambi zetu, na utuchukuwe kama urithi wako."
\s5
\v 10 Yahweh akasema, "Ona, ninakaribu kufanya agano. Mbele za watu wako, nitafanya maajabu ambayo hayajawai kufanywa duniani kote wala kwenye taifa lote. Watu wote miongoni mwako wataona matendo yangu, kwa kuwa ni kitu cha hofu ninacho fanya kwako.
\v 11 Tii amri zangu leo. Ninawaondoa mbele yako Waamori, Wakanani, Wahivi, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
\s5
\v 12 Kuwa mwanglifu usifanye agano na wakazi wa nchi unayo kwenda, au wata kuwa mtego kwako.
\v 13 Badala yake, lazima uvunje madhabahu zao, ponda nguzo zao za mawe, na kukata nguzo zao za Ashera.
\v 14 Kwa kuwa wewe haupaswi kumuabudu mungu mwingine, maana Yahweh, ambaye jina lake ni Uwivu, ni Mungu wa uwivu.
\s5
\v 15 Hivyo kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi, kwa kuwa wanajifanyia ukahaba kwa miungu yao, na wanatoa dhabihu kwa miungu yao. Kisha mmoja wao ata kukaribisha na wewe utakula baadhi ya dhabihu zake,
\v 16 na kisha utachukuwa baadhi ya mabinti zake kwa wanao, na mabinti wake watafanya ukahaba kwa miungu yao, na watafanya wanao kufanya ukahaba kwa miungu yao.
\v 17 Usifanye Miungu ya chuma ya kuyayusha.
\s5
\v 18 Laziam ushike Sherehe ya Mkate Usiotiwachachu. Kama nilivyo kuamuru, lazima ule mkate usio na hamira kwa siku saba kwa muda uliotengwa wa mwezi wa Abibu, maana nikatika mwezi wa Abibu ulitoka Misri.
\s5
\v 19 Wazaliwa wote ni mwangu, ata mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo, yote ya ng'ombe na kondoo.
\v 20 Lazima umnunue tena mzaliwa kwanza wa punda kwa kondoo, lakini usipo mnunua tena, kisha uivunje shingo yake. Lazima ununue tena wazaliwa wa kwanza wote wa wanao. Hakuna ata mmoja atakye kuja kwangu mikono mitupu.
\s5
\v 21 Utafanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba utapumzika. Ata wakati wakilimo na wa mavuno, lazima upumzike.
\v 22 Lazima uadhimishe Sherehe ya Majuma kwa mazao ya kwanza ya mavuno ya ngano, na lazima uadhimishe Sherehe ya Makusanyo mwisho wa mwaka.
\s5
\v 23 Mara tatu kwa mwaka wanaume wenu wote watajitokeza kwa Bwana Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 24 Kwa kuwa nitaondoa mataifa mbele yenu na kutanua mipika. Hakuna atakaye tamani kuwa na ardhi yenu kama yao utakapo toka mbele za Yahweh mara tatu kwa mwaka.
\s5
\v 25 Hautatoa damu ya dhabihu yangu na hamira yeyote, wala nyama yeyote kutoka dhabihu za Sherehe ya Pasaka kubaki hadi asubui.
\v 26 Lazima ulete matunda ya kwanza yalio bora kutoka nyumbani kwako. Usimchemshe mbuzi mtoto katika maziwa ya mama yake."
\s5
\v 27 Yahweh akamwabia Musa, "Andika chini haya maneno, kwa kuwa nimejiahidi haya maneno niliyo yasema, na nimefanya agano kwako na Israeli."
\v 28 Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi.
\s5
\v 29 Musa alipo shuka chini ya Mlima Sinai na mbao mbili za agano za ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa ngozi ya kuwa uso wake ulikuwa wa'ngaa akizungumza na Mungu.
\v 30 Wakati Aruni na Waisraeli walipo muona Musa, ngozi ya uso wake ulikuwa wa ng'aa, na waliogopa kuja karibu yake.
\v 31 Lakini Musa aliwaita, na Aruni na viongozi wa jamii wakaja kwake. Kisha Musa akasema nao.
\s5
\v 32 Baada ya haya, watu wote wa Israeli wakaja kwa Musa, na akawambia amri zote Yahweh alizo mpa katika Mlima Sinai.
\v 33 Musa alipo maliza kuzungumza nao, alifunika uso wake kwa kitambaa.
\s5
\v 34 Wakati Musa alipoenda mbele za Yahweh kusema naye, aliondoa kitambaa, hadi alipo toka. Alipo toka, aliwaambia Waisraeli alicho amriwa kusema.
\v 35 Waisraeli walipo muona Musa ana'ngaa uso, alirudisha kitambaa tena usoni mpaka alipokuwa anaenda kuongea na Yahweh.
\s5
\c 35
\p
\v 1 Musa akawakusanya jamii yote ya Waisraeli na kuwaambia, "Haya ndio mambo Yahweh aliyo waamuru mfanye.
\v 2 Kwa siku sita kazi ya weza fanywa, lakini kwako, siku ya saba lazima iwe siku takatifu, siku ya Sabato ya mapumziko, takatifu kwa Yahweh. Yeyote atakaye fanya kazi hiyo siku lazima auawe.
\v 3 Haupaswi kuwasha moto kwenye nyumba zenu siku ya Sabato."
\s5
\v 4 Musa akasema na jamii yote ya Waisraeli, kwa kusema, "Hichi ndicho kitu Yahweh alicho amuru.
\v 5 Chukuwa sadaka kwa ajili ya Yahweh, wote wenye moyo mkunjufu. Leta sadaka kwa Yahweh - dhahabu, fedha, shaba,
\v 6 buluu, zambarau, sufu nyekundu na kitambaa kizuri; nywele za mbuzi;
\v 7 ngozi za kondoo zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo; na mbao za mshita;
\v 8 mafuta ya taa kwa pahali patakatifu, viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa,
\v 9 kwa uvumba mzuri na vito vya shohamu na vito vya kutiwa kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani.
\s5
\v 10 Kila mwanaume mwenye ustadi kati yenu aje na afanye kila kitu ambacho Yahweh aliyaamuru --
\v 11 hema la kuabudia, na kifuniko chake, na vifungo vyake, na mbao zake, nguzo, na sakafu;
\v 12 pia sanduku na nguzo zake, kiti cha rehema, na pazia la kusitiri.
\s5
\v 13 Walileta meza na miguu yake, vyombo vyake vyote, na mkate wa wonyesho;
\v 14 kinara cha taa, vyombo vyake, taa, na mafuta ya zile taa;
\v 15 ile madhabahu ya uvumba na nguzo zake, mafuta ya upako na uvumba ulitiwa maukato; kishikizo cha mwingilio wa hema ya kuabudia;
\v 16 madhabahu ya sadaka ya kuteketeza na kitunzi cha shaba na nguzo na vyombo; na ile beseni kubwa na sakafu yake.
\s5
\v 17 Walileta vishikizo kwa ajili ya nyuani na nguzo zake na sakafu yake, na pazia kwa ajili mwingilio wa nyauni;
\v 18 na ile misumari ya hema la kuabudia na nyuani, pamoja na kamba zake.
\v 19 Walileta mavazi yaliyofumwa kutumikia sehemu takatifu, mavazi takatifu ya Aruni kuhani na wanae, kwa wao kutumika kama makuhani."
\s5
\v 20 Kisha makabila yote ya Israeli yakaondoka na kwenda kutoka uweponi mwa Musa.
\v 21 Kila mtu moyo wake ulimchochea na aliye andaliwa na roho yake alikuja na kuleta sadaka kwa Yahweh kwa matengenezo ya hema ya kuabudia, kwa vitu vyote kwajili ya huduma ndani yake, na kwa vazi takatifu.
\v 22 Walikuja, wote wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa utayari. Walileta madini, hereni, pete, na vitu vya thamani, vitu vyote tofauti vyenye madini ya dhahabu. Waliwasilisha sadaka za dhahabu kama sadaka ya kupunga kwa Yahweh.
\s5
\v 23 Kila mmoja alikuwa na sufu ya buluu, dhambarau, au nyekundu, nguo nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo zilizobadili kuwa nyekundu, na ngozi ya pomboo walivileta.
\v 24 kila mmoja alitengeneza sadaka ya fedha au shaba walizileta kama sadaka kwa Yahweh, na kila mmoja aliyekuwa na mti wa mshita kwa matumizi ya kazi aliuleta.
\s5
\v 25 kila mwanamke mwenye ustadi walisokota sufu kwa mikono yao na walileta sufu walizosokota za buluu, dhambarau, au sufu nyekundu, au nguo nzuri.
\v 26 Wanawake wote wenye mioyo iliyochochewa na walio na ustadi walisokota singa za mbuzi.
\s5
\v 27 Viongozi walileta mawe ya shohamu na mawe mengine kwaajili ya kuwekwa kwenye hiyo naivera na hicho kifuko cha kifuani;
\v 28 walileta viungo na mafuta kwaajili ya taa, kwa mafuta ya upako, na kwa uvumba wa manukato.
\v 29 Waisraeli walileta sadaka ya hiyari kwa Yahweh; kila mwanaume na mwanamke ambao mioyo yao ilikuwa tayari walileta vifaa kwaajili kazi zote ambazo Yahweh aliamuru kupitia Musa zifanyike.
\s5
\v 30 Musa alisema kwa waisraeli, "Tazama, Yahweh ameita kwa jina juu ya Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huri, kutoka kabila la Yuda.
\v 31 Aliijaza Bezaleli kwa Roho yake, kumpa hekima, uwelewa, na maarifa, kwa aina zote za ujenzi,
\v 32 kufanya sanaa ya ubunifu na kufanya kazi za dhahabu, shaba, na shaba;
\v 33 pia kukata na kupanga mawe na mbao iliochongwa- kufanya kazi za aina zote kwa ubunifu na ujenzi.
\s5
\v 34 Aliiweka kufundisha ndani ya moyo wake, yeye pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, kutoka kabila la Dani.
\v 35 Aliwajaza kwa ustadi wa kufanya kazi za aina zote, kufanya kazi ya kama kuchora mawe, kama mwerevu, kama mtia taraza katika nyuzi za rangu ya buluu, dhambarau, na nyekundu na nguo nzuri, na kama washonaji. Walikuwa wachonga mawe wa kazi zote, na walikuwa wabunifu wa sanaa.
\s5
\c 36
\p
\v 1 Hivyo Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Yahweh aliye mpa ustadi na uwezo kujua jinsi ya kufanya kazi katika ujenzi wa sehemu takatifu wafanye kazi kadiri ya yote Yahweh aliyo amuru."
\s5
\v 2 Musa akamuita Bezaleli, Oholiabu, na kila mtu mwenye ujuzi ambaye Yahweh kampa ujuzi, na ambaye moyoni mwake ulichochewa kuja na kufanya kazi.
\v 3 Walipokea kutoka kwa Musa sadaka zote ambazo Waisraeli walizo leta kwa ujenzi ya sehemu takatifu. Watu walikuwa bado wanaleta sadaka za hiari kila asubui kwa Musa.
\v 4 Hivyo watu wote walikuwa na ujuzi walikuwa wakifanya kazi sehemu takatifu walikuja kutoka kwenye kazi walikuwa wakifanya.
\s5
\v 5 Wachonga mawe walimwabia Musa, "Watu wanaleta zaidi sana ya yanayo itajika kufanya kazi Yahweh aliyo tuamuru."
\v 6 Hivyo Musa akaamuru mtu yeyote asilete tena kwa ujenzi wa sehemu takatifu. Kisha watu wakaacha kuleta hivi vitu.
\v 7 Walikuwa na zaidi ya vitu vya ujenzi.
\s5
\v 8 Hivyo wachonga mawe miongoni mwao wakajenga lile hema la kuabudia kwa mapazia kumi yaliyo jengwa kitamba kizuri na buluu, zambarau, na sufu nyekundu kwa aina ya kerubi. Hii ni kazi ya Bezaleli, mjenzi mwenye ujuzi sana.
\v 9 Urefu wa kila pazia ulikuwa mikono ishirini na nane, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa vyote hivyo vilikuwa na kipimo kimoja.
\v 10 Bezaleli akaunganisha vitambaa vitano pamoja, na vile vitambaa vingine vitano akaviunganisha pamoja.
\s5
\v 11 Kisha akafanya vitanzi vya uzi wa bluu kwenye upindo wa kitambaa kilicho mahali pa kuungania. Akafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pale pengine pa kuungania.
\v 12 Akafanya vitanzi hamsini kwenye kitambaa kimoja, akafanya vitanzi hamsini kwenye mwisho wa kitambaa kilichokuwa mahali pale pengine pa kuungania, vitanzi hivyo vikiwa vinaelekeana.
\v 13 Mwishowe akafanya kulabu hamsini za dhahabu na kuviunganisha vitambaa hivyo pamoja kwa kulabu hizo, hivi kwamba hiyo ikawa maskani moja.
\s5
\v 14 Bezaleli akafanya vitambaa vya mahema vya manyoya ya mbuzi kwa ajili ya hema lililo juu ya maskani. Vitambaa kumi na moja ndivyo alivyofanyiza.
\v 15 Urefu wa kila kitambaa ulikuwa mikono thelathini, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa hivyo kumi na moja vilikuwa na kipimo kimoja.
\v 16 Kisha akaunganisha vitambaa vitano pamoja na vile vitambaa vingine sita pamoja.
\v 17 Kisha akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pa kuungania, naye akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kile kitambaa kingine kilichoungana nacho.
\s5
\v 18 Bezaleli akafanya kulabu hamsini za shaba kwa ajili ya kuliunganisha hilo hema pamoja liwe kipande kimoja.
\v 19 Naye akafanya kifuniko cha hema kutokana na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko kutokana na ngozi za sili, upande wa juu.
\s5
\v 20 Bezaleli akafanya viunzi vya mbao vya hema ya kukutani kutokana na mbao za mshita.
\v 21 Urefu wa kiunzi ulikuwa mikono kumi, nao upana wa kila kiunzi ulikuwa mkono mmoja na nusu.
\v 22 Kila kiunzi kilikuwa na ndimi mbili zilizounganishwa. Hivyo ndivyo alivyofanya viunzi vyote vya maskani.
\v 23 Basi akafanya viunzi vya maskani, viunzi ishirini kwa ajili ya upande kuelekea kusini.
\s5
\v 24 Bezaleli akafanya vikalio arobaini vya fedha viwe chini ya vile viunzi ishirini, vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja pamoja na ndimi zake mbili na vikalio vingine viwili chini ya kiunzi kingine pamoja na ndimi zake mbili.
\v 25 Na kwa ajili ya ule upande mwingine wa maskani, upande wa kaskazini, akafanya viunzi ishirini
\v 26 na vikalio vyake arobaini vya fedha. Vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio viwili chini ya kiunzi kingine
\s5
\v 27 Na kwa ajili ya zile pande za nyuma za maskani kuelekea magharibi akafanya viunzi sita.
\v 28 Naye akafanya viunzi viwili vya pembeni ya maskani kwenye pande zake mbili za nyuma
\s5
\v 29 Hizi zilikuwa pacha upande wa chini, lakini juu ya kila moja kwenye pete ya kwanza. Hivyo ndivyo alivyoifanya yote miwili, ile miimo ya pembeni.
\v 30 Basi vikajumlika kuwa viunzi vinane na vikalio vyake kumi na sita vya fedha, vikalio viwili kando ya vikalio viwili chini ya kila kiunzi.
\s5
\v 31 Bezaleli akafanya miti ya mshita, mitano kwa ajili ya viunzi vya upande mmoja wa maskani,
\v 32 na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya upande ule mwingine wa maskani na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya maskani kwa ajili ya zile pande mbili za nyuma za magharibi.
\v 33 Kisha akafanya mti wa katikati upitie katikati ya vile viunzi toka mwisho mmoja mpaka ule mwingine.
\v 34 Naye akavifunika vile viunzi kwa dhahabu, akafanyiza pete zake za dhahabu ziwe vitegemezo kwa ajili ya ile miti, akaifunika ile miti kwa dhahabu.
\s5
\v 35 Bezaleli akafanya pazia, la uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa cha rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kalitia makerubi kwa kazi ya mjenzi.
\v 36 Kisha akalifanyia nguzo nne za mshita na kuzifunika kwa dhahabu, vibanio vyake vikiwa vya dhahabu, na kutengeneza vikalio vinne vya fedha kwa ajili yake.
\s5
\v 37 Naye akafanya kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema kutokana na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kazi ya mfumaji.
\v 38 Pia akafanya na nguzo zake tano na vibanio vyake. Naye akavifunika vilele vyake na viungo vyake kwa dhahabu, lakini vile vikalio vyake vitano vilikuwa vya shaba.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Bezaleli akafanya Sanduku la mbao za mshita. Mikono miwili na nusu urefu wake, na mkono mmoja na nusu upana wake, na mkono mmoja na nusu kimo chake.
\v 2 Kisha akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje na kulifanyia ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
\v 3 Kisha akalitengenezea pete nne za dhahabu, za juu ya miguu yake minne, pete mbili upande wake mmoja na pete mbili upande wake mwingine
\s5
\v 4 Kisha akafanya miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.
\v 5 Halafu akaitia miti hiyo kwenye zile pete zilizo pande za Sanduku ili kulibeba Sanduku.
\v 6 Naye akafanya kifuniko cha dhahabu safi. Mikono miwili na nusu urefu wake, na mkono mmoja na nusu upana wake.
\s5
\v 7 Bezaleli akafanya makerubi wawili wa dhahabu. Kwa kazi ya kufua akawafanya kwenye miisho yote miwili ya kifuniko.
\v 8 Kerubi mmoja kwenye mwisho ule, na yule kerubi mwingine kwenye mwisho huu. Aliwafanya makerubi juu ya kifuniko kwenye miisho yote miwili.
\v 9 Nao wakawa makerubi wanaonyoosha mabawa yao mawili kuelekea juu, wakisitiri kifuniko kwa mabawa yao, nazo nyuso zao zilikuwa zikielekeana. Nyuso za makerubi hao zilielekea kifuniko hicho.
\s5
\v 10 Bezaleli akafanya meza ya mbao za mshita. Mikono miwili urefu wake, na mkono mmoja upana wake, na mkono mmoja na nusu kimo chake.
\v 11 Halafu akaifunika kwa dhahabu safi na kufanya ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.
\v 12 Kisha akafanya mzingo wa upana wa kiganja kuizunguka na kufanya ukingo wa dhahabu kwa ajili ya mzingo wake kuizunguka pande zote.
\v 13 Tena, akatengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili yake na kuziweka pete hizo kwenye zile pembe nne zilizokuwa kwa ajili ya ile miguu minne.
\s5
\v 14 Pete hizo zilikuwa karibu na ule mzingo, ili kutegemeza ile miti ya kuibeba meza hiyo.
\v 15 Halafu akafanya ile miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu ili kuibeba ile meza.
\v 16 Baada ya hilo akafanya kutokana na dhahabu safi vile vyombo vilivyo juu ya meza, sahani zake na vikombe vyake na mabakuli yake na mitungi yake iliyotumiwa kumimina matoleo ya kinywaji.
\s5
\v 17 Kisha akafanya kinara cha taa cha dhahabu safi. Kwa kazi ya kufua akakifanya kinara cha taa. Pande zake na matawi yake, vikombe vyake, mafundo yake na maua yake vikatokea kwake.
\v 18 Na matawi sita yalikuwa yakitoka kwenye pande zake, matawi matatu ya kinara cha taa kutoka kwenye upande wake mmoja na matawi mengine matatu ya kinara cha taa kutoka kwenye ule upande wake mwingine.
\v 19 Vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi vilikuwa kwenye kikundi kimoja cha matawi, vifundo na maua yakifuatana; na vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi vilikuwa kwenye kile kikundi kingine cha matawi, vifundo na maua yakifuatana. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa yale matawi sita yaliyokuwa yakitoka katika kile kinara cha taa.
\s5
\v 20 Na kwenye kile kinara cha taa kulikuwa na vikombe vinne vyenye umbo la maua ya mlozi, vifundo vyake na maua yake yakifuatana.
\v 21 Na kile kifundo chini ya matawi mawili kilitoka kwake, na kifundo kilicho chini ya yale matawi mengine mawili kilitoka kwake, na kifundo kingine kilicho chini ya matawi mengine mawili zaidi kilitoka kwake, kwa ajili ya matawi sita yanayotoka katika kinara.
\v 22 Vifundo vyake na matawi yake vilitoka kwake, vyote vilikuwa kitu kimoja cha kazi ya kufua, cha dhahabu safi.
\s5
\v 23 Kisha akafanya taa zake saba na mikasi ya tambi zake na vyetezo vyake kutokana na dhahabu safi.
\v 24 Alikifanya kwa talanta ya dhahabu safi, hicho pamoja na vyombo vyake vyote.
\s5
\v 25 Sasa akafanya madhabahu ya uvumba+ kutokana na mbao za mshita. + Mkono mmoja urefu wake na mkono mmoja upana wake, ikiwa mraba, na mikono miwili kimo chake. Pembe zake zilitoka kwake.
\v 26 Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, upande wake wa juu na pande zake za kando kuizunguka na pembe zake, naye akafanya ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.
\s5
\v 27 Naye akaifanyia pete mbili za dhahabu chini ya ukingo wake kwenye pande zake mbili, kwenye pande zake mbili zinazoelekeana, za kutegemeza ile miti ya kuibeba.
\v 28 Kisha akafanya ile miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.
\v 29 Tena akafanya yale mafuta yanayotumiwa kutia mafuta na ule uvumba safi uliotiwa manukato, + kazi ya mtengenezaji wa marhamu.
\s5
\c 38
\p
\v 1 Naye akafanya madhabahu ya toleo la kuteketezwa kwa mbao za mshita. Mikono mitano urefu wake, na mikono mitano upana wake, ilikuwa mraba, na mikono mitatu kimo chake.
\v 2 Halafu akafanya pembe zake kwenye zile ncha zake nne. Pembe zake zilitoka kwake. Kisha akaifunika kwa shaba.
\v 3 Baada ya hilo akavifanya vyombo vyote vya madhabahu, yale makopo na zile sepetu na yale mabakuli, zile nyuma na vile vyetezo. Vyombo vyake vyote alivifanya kwa shaba.
\s5
\v 4 Tena akaifanyia madhabahu kiunzi cha fito, mtandao wa shaba, chini ya ukingo wake, chini kuelekea katikati yake.
\v 5 Halafu akatengeneza pete nne kwenye ile miisho minne karibu na kile kiunzi cha shaba, ili kuitegemeza ile miti.
\s5
\v 6 Bezaleli akafanya miti ya mshita na kuifunika kwa shaba.
\v 7 Kisha akaitia ile miti kwenye zile pete zilizo pande za madhabahu ili kuibeba. Akaifanya kuwa sanduku la mbao lenye uwazi.
\s5
\v 8 Kisha akafanya beseni ya shaba na kinara chake cha shaba. Kwa kutumia vioo vya watumishi wanawake ambao walifanya utumishi uliopangwa kwenye mwingilio wa hema la mkutano.
\s5
\v 9 Naye akafanya ule ua. Upande unaokabili Negebu, kuelekea kusini, mapazia ya ua yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa, kwa mikono mia moja.
\v 10 Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha
\s5
\v 11 Pia, kwa ajili ya upande wa kaskazini kulikuwa na mikono mia. Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha.
\v 12 Lakini kwa ajili ya upande wa magharibi mapazia yalikuwa mikono hamsini. Nguzo zake zilikuwa kumi na vikalio vyake kumi. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha.
\s5
\v 13 Na kwa ajili ya upande wa mashariki kulikuwa na mikono hamsini.
\v 14 Mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano kwa upande mmoja. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu.
\v 15 Na kwa ajili ya upande ule mwingine, huu na ule, wa lango la ua, mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu.
\v 16 Mapazia yote ya ua kuzunguka pande zote yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa.
\s5
\v 17 Navyo vikalio vya nguzo vilikuwa vya shaba. Vibanio vya vikalio na viungo vyake vilikuwa vya fedha navyo vilifunikwa kwa shaba sehemu ya juu, na kulikuwa na viungo vya shaba kwa ajili ya nguzo zote za ua.
\v 18 Nacho kisitiri cha lango la ua kilikuwa na mikono ishirini urefu. Cha uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, na urefu wake ulikuwa mikono ishirini, nacho kimo kotekote kilikuwa mikono mitano sawasawa na mapazia ya ua.
\v 19 Na nguzo zake nne na vikalio vyake vinne vilikuwa vya shaba. Misumari yake ilikuwa ya fedha na utando wa vichwa vyake na viungo vyake ulikuwa wa fedha.
\v 20 Na misumari yote ya hema kwa ajili ya maskani na kwa ajili ya ua kuzunguka pande zote ilikuwa ya shaba
\s5
\v 21 Hivi ndivyo vitu vilivyohesabiwa vya maskani, maskani ya Ushuhuda, vilivyohesabiwa kwa amri ya Musa, kuwa utumishi wa Walawi chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa Aruni kuhani.
\v 22 Naye Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huru wa kabila la Yuda alifanya yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.
\v 23 Na pamoja naye alikuwa Oholiabu mwana wa Ahisamaki wa kabila la Dani, fundi na mtarizi na mfumaji wa uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora.
\s5
\v 24 Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya kazi katika kazi yote ya mahali patakatifu ikawa jumla ya dhahabu ya toleo la kutikisa, + talanta ishirini na tisa na shekeli 730 kulingana na shekeli+ ya mahali patakatifu.
\v 25 Nayo fedha ya wale walioandikishwa kati ya kusanyiko ilikuwa talanta mia moja na shekeli 1, 775 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,
\v 26 ile nusu shekeli kwa ajili ya mtu mmoja ilikuwa nusu shekeli kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,. Kwa kila mtu aliyekuwa akipita kuingia upande wa wale waliokuwa wameandikishwa kuanzia miaka ishirini na zaidi, jumla ya watu 603, 550.
\s5
\v 27 Na talanta mia moja za fedha zilitumiwa kutengeneza vikalio vya mahali patakatifu na vikalio vya lile pazia. Vikalio mia moja vilitoshana na talanta mia moja, talanta moja kwa kikalio kimoja.
\v 28 Na kutokana na zile shekeli 1, 775 alifanyiza vibanio vya nguzo na kuvifunika sehemu yake ya juu na kuviunganisha pamoja.
\v 29 Nayo shaba ya toleo la kutikisa ilikuwa talanta sabini na shekeli 2, 400.
\s5
\v 30 Naye akaitumia kufanya vile vikalio vya mwingilio wa hema la mkutano na ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, na vyombo vyote vya madhabahu,
\v 31 na vile vikalio vya ua kuzunguka pande zote, na vile vikalio vya lango la ua, na misumari yote ya maskani na misumari+ yote ya ua kuzunguka pande zote.
\s5
\c 39
\p
\v 1 Na kutokana na ule uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Basi wakafanya yale mavazi matakatifu yaliyokuwa kwa ajili ya Aruni, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 2 Basi akaifanya ile naivera ya dhahabu, uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.
\v 3 Kisha wakafua mabamba ya dhahabu yawe mabamba membamba, naye akakata nyuzi za kufuma pamoja na ule uzi wa bluu na ile sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kile kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kile kitani bora, kama kazi ya mjenzi.
\s5
\v 4 Wakaifanyia vipande vya begani vilivyounganishwa. Iliunganishwa kwenye miisho yake miwili.
\v 5 Nao mshipi, uliokuwa juu yake ili kuifunga, ulikuwa wa kitambaa kilekile kulingana na ufundi wake, wa dhahabu, uzi wa bluu, na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 6 Kisha wakafanya mawe ya shohamu yaliyopangwa kwenye mapambo ya dhahabu, yaliyochongwa kwa michoro ya muhuri kulingana na majina ya wana wa Israeli.
\v 7 Bezaleli akayaweka kwenye vile vipande vya begani vya naivera yawe mawe ya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli, kama vile Yehova alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 8 Kisha akafanya kile kifuko cha kifuani kwa ufundi wa mjenzi, kama ule ufundi wa naivera, kutokana na dhahabu, uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.
\v 9 Kilikuwa mraba kilipokunjwa. Walikifanya kile kifuko cha kifuani, kinapokunjwa, shubiri moja urefu wake na shubiri moja upana wake.
\s5
\v 10 Kisha wakakijaza kwa mistari minne ya mawe. Mstari wa zabarijadi, topazi na zumaridi ulikuwa mstari wa kwanza.
\v 11 Nao mstari wa pili ulikuwa feruzi, yakuti na yaspi.
\v 12 Nao mstari wa tatu ulikuwa jiwe la leshemi, akiki na amethisti.
\v 13 Nao mstari wa nne ulikuwa krisolito na shohamu na yashefi. Yaliwekwa katika mapambo ya dhahabu katika mahali pake.
\s5
\v 14 Na mawe hayo yalikuwa kulingana na majina ya wana wa Israeli. Yalikuwa kumi na mawili kulingana na majina yao, kwa michongo ya muhuri, kila moja kulingana na jina lake kwa ajili ya yale makabila kumi na mawili.
\v 15 Nao wakafanya juu ya kile kifuko cha kifuani minyororo yenye mashada, msokoto wa kamba, wa dhahabu safi.
\v 16 Kisha wakafanya mapambo mawili ya dhahabu na pete mbili za dhahabu na kuziweka hizo pete mbili kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani.
\s5
\v 17 Baada ya hilo wakapitisha zile kamba mbili za dhahabu kwenye zile pete mbili zilizo kwenye miisho ya kile kifuko cha kifuani.
\v 18 Nao wakapitisha ile miisho miwili ya zile kamba mbili kwenye yale mapambo mawili. Halafu wakaiweka juu ya vile vipande vya begani vya naivera, mbele yake.
\s5
\v 19 Kisha wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani kwenye upindo wake ulio upande unaoelekea ile efodi upande wa ndani.
\v 20 Halafu wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka juu ya vile vipande viwili vya begani vya efodi upande wake wa chini, sehemu yake ya mbele, karibu na mahali pake pa kuungania, juu ya ule mshipi wa naivera.
\s5
\v 21 Mwishowe wakakifunga kile kifuko cha kifuani kwa pete zake kwenye zile pete za efodi kwa uzi wa bluu, ili kipate kuwa juu ya mshipi wa efodi na kile kifuko cha kifuani kisiondoke juu ya efodi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 22 Bezaleli akafanya lile koti la naivera, lote la uzi wa zambarau, kazi ya mshonaji.
\v 23 Na sehemu wazi ya hilo koti ilikuwa katikati yake, kama sehemu wazi ya vazi la chuma. Sehemu hiyo iliyo wazi ilikuwa na ukingo kuizunguka pande zote ili isiraruke.
\v 24 Halafu wakafanya kwenye upindo wa hilo koti makomamanga ya uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, vilivyosokotwa pamoja.
\s5
\v 25 Wakafanya kengele za dhahabu safi na kuziweka kengele hizo katikati ya makomamanga kwenye upindo wa lile koti kuzunguka pande zote, katikati ya makomamanga;
\v 26 kengele na komamanga, kengele na komamanga kwenye upindo wa hilo koti kuzunguka pande zote, kwa ajili ya kuhudumu, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 27 Kisha wakafanya zile kamba za kitani bora, kwa ajili ya Haruni na wanawe.
\v 28 Na kile kilemba cha kitani bora na yale mavalio ya kichwani ya mapambo ya kitani bora na zile suruali za kitani bora kilichosokotwa,
\v 29 na ule ukumbuu wa kitani bora kilichosokotwa na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, kazi ya mfumaji, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 30 Mwishowe wakafanya lile bamba linalongaa, ishara takatifu ya wakfu, kutokana na dhahabu safi na kuandika juu yake maandishi kwa mchongo wa muhuri: “Utakatifu kwa Yahweh. ”
\v 31 Kisha wakalitia uzi wa bluu ili waliweke juu ya kile kilemba upande wa juu. Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 32 Basi kazi ya ile maskani ya hema la mkutano ikafikia mwisho wake. Kwa maana wana wa Israeli waliendelea kufanya kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.
\v 33 Nao wakaileta maskani kwa Musa, lile hema pamoja na vyombo vyake vyote, kulabu zake, viunzi vyake vya mbao, miti yake na nguzo zake na vikalio vyake,
\v 34 na kifuniko chake cha ngozi za kondoo-dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko chake cha ngozi za sili na pazia la kisitiri,
\v 35 na sanduku la ushuhuda na miti yake na kifuniko.
\s5
\v 36 Wakaleta meza, vyombo vyake vyote, na ule mkate wa wonyesho,
\v 37 kile kinara cha taa cha dhahabu safi, taa zake, ule mstari wa taa, na vyombo vyake vyote na yale mafuta ya kuangazia taa,
\v 38 na madhabahu ya dhahabu na yale mafuta yanayotumiwa kutia mafuta na ule uvumba uliotiwa manukato na kile kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema,
\v 39 ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, miti yake na vyombo vyake vyote, ile beseni na kinara chake,
\s5
\v 40 Wakaleta mapazia ya ua, nguzo zake na vikalio vyake na kile kisitiri+ kwa ajili ya lango la ua, kamba zake za hema na misumari yake ya hema na vyombo vyote kwa ajili ya utumishi wa maskani, kwa ajili ya hema ya kukutania.
\v 41 Wakaleta yale mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika patakatifu, yale mavazi matakatifu kwa ajili ya Aruni kuhani na mavazi ya wanawe ya kutumikia wakiwa makuhani.
\s5
\v 42 Kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa, hivyo ndivyo wana wa Israeli walivyoufanya utumishi wote.
\v 43 Naye Musa akaiona ile kazi yote, na, tazama, walikuwa wameifanya kama vile Yahweh alivyokuwa ameamuru. Hivyo ndivyo walivyokuwa wamefanya. Basi Musa akawabariki.
\s5
\c 40
\p
\v 1 Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
\v 2 "Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka lazima wewe uandae hema la kukutania.
\s5
\v 3 Utaweka sanduku la ushuhuda ndani yake, na utaziba sanduku kwa pazia.
\v 4 Utaleta ndani meza na kuandaa kwa mpangilio vitu vyake. Kisha utaleta kinara cha taa na kuandaa taa.
\s5
\v 5 Nawe utaweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na utaweka pazia katika mwingilio wa hema la kukutania.
\v 6 Utaweka madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa mbele ya mwingilio wa hema ya kukutania.
\v 7 Utaweka ile saani kubwa katikati ya hema la kukutania na madhabahu na utaweka maji ndani yake.
\s5
\v 8 Uandae nyuani inayoizunguka, na utundike pazia katika mwingilio wa nyuani.
\v 9 Lazima uchukuwe mafuta ya upako na upake hema la kukutania na kila kitu kilichopo ndani yake. Lazima uitenge na samani zake kwangu; kisha itakuwa takatifu.
\v 10 Lazima upake mafuta madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake. Lazima utenge madhabhu kwa ajili yangu na itakuwa takatifu kwangu.
\v 11 Upake mafuta beseni la shaba na sakafu yake na uitenge kwa ajili yangu.
\s5
\v 12 Umlete Aruni na wanae kwa mwingilio wa hema la kukutania na uwaoshe wote kwa maji.
\v 13 Utamfunika Aruni kwa mavazi yaliyo tengwa kwa ajili yangu, mpake mafuta na umtenge ili anitumikie kama kuhani.
\s5
\v 14 Utawaleta wana wake na kuwafunika kwa nguo nzito.
\v 15 Utawapaka mafuta kama ulivyo mpaka baba yao ili wanitumikie kama makuhani. Upako wao utawafanya makuhani wa kudumu vizazi vyote vya watu wao."
\v 16 Hivi ndivyo Musa alivyo sema; alifuata yote Yahweh aliyo muamuru. Alifanya vitu vyote hivi.
\s5
\v 17 Hivyo hema la kukutania liliandaliwa siku ya kwanza ya mwezi wa mwaka wa pili.
\v 18 Musa alianda hema la kukutania, akaeka sakafu zake sehemu yake, akaanda fremu zake, akashikisha chuma zake, na akaanda minara na nguzo zake.
\v 19 Alitandaza mfuniko juu ya hema la kukutania na kuweka hema juu yake, kama Yahweh alivyo muamuru.
\v 20 Alichukuwa amri za agano na kuweka kwenye sanduku. Pia aliweka nguzo kwenye sanduku na kuweka mfuniko wa kiti cha rehema.
\s5
\v 21 Aliichukuwa sanduku na kuweka ndani ya hema la kukutania. Aliandaa pazia ili lizibe sanduku la ushuhuda, kama Yahweh alivyo muamuru.
\v 22 Alieka meza kwenye hema la kukutania, kwa upande wa kaskazini mwa hema la kukutania, nje ya pazia.
\v 23 Alieka mkate kwa mpangilio katika meza ya Yahweh, kama Yahweh alivyo amuru.
\s5
\v 24 Alieka kinara cha taa kwenye hema la kukutania, upande wa pili wa meza, kusini mwa hema la kukutani.
\v 25 Aliwasha taa mbele za Yahweh, kama Yahweh alivyo muamuru.
\s5
\v 26 Aliweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba ndani ya hema la kukutania mbele ya pazia.
\v 27 Alichoma uvumba wa manukato hapo, kama Yahweh alivyo muamuru.
\s5
\v 28 Alitundika pazia katika hema ya kukutania.
\v 29 Aliweka madhabahu ya sadaka ya kuteketeza katika hema ya kukutania. Aliitolea sadaka ya kuteketeza na sadaka ya unga, kama Yahweh alivyo muamuru.
\v 30 Aliweka beseni katikati ya hema ya kukutunia na madhabahu, na maji ya kuoshea.
\s5
\v 31 Musa, Aruni, na wanae waliosha mikono yao na miguu kwenye beseni
\v 32 muda wowote walipoenda kwenye hema ya kukutania na muda wowote walipoenda kwenye madhabahu. Walijisafisha, kama Yahweh alivyo muamuru Musa.
\v 33 Musa alianda nyuani nyuma ya hema ya kukutania na madhabahu. Alianda pazia katika mwingilio wa nyuani. Katika hili, Musa alimaliza kazi.
\s5
\v 34 Kisha wingu likafunika hema ya kukutania, na utukufu wa Yahweh ukafunika hema ya kukutania.
\v 35 Musa hakuweza kuingia hema ya kukutania kwasababu wingu lilikuwa juu yake, na kwasababu utukufu wa Yahweh ulijaza hema ya kukutania.
\s5
\v 36 Muda wowote wingu lilipo chukuliwa juu kutoka hema ya kukutania, watu wa Israeli waliendelea na safari yao.
\v 37 Lakini kama wingu haliku nyanyuka juu kutoka hema ya kukutania, kisha basi watu hawaku safiri. Walibaki hadi siku lilipo nyanyuliwa juu.
\v 38 Kwa kuwa wingu la Yahweh lilikuwa juu ya hema ya kukutania mchana, na moto wake ulikuwa juu yake usiku, wazi kwa watu wote wa Israeli kipindi chote cha safari yao.

1664
03-LEV.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1664 @@
\id LEV
\ide UTF-8
\h Mambo ya Walawi
\toc1 Mambo ya Walawi
\toc2 Mambo ya Walawi
\toc3 lev
\mt Mambo ya Walawi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mungu alimwita Musa na alisema naye kutoka kweye hema la kukutania, akasema,
\v 2 "Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mwanaume yeyote miongoni mwenu akileta sadaka kwa Bwana, aleta kama matoleo katika wanyama wako, iwapo mifugo au katika kundi."
\s5
\v 3 Kama matoleo yake ni ya sadaka ya kutekezwa kutoka katika kundi, atatoa dume asiyekuwa na kasoro. Atamtoa katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania, ili iwe imekubaliwa mbele za Bwana.
\v 4 Ataweka mikono yake kichwani pa sadaka ya kuteketezwa, na ndipo itakuwa imekubaliwa badala yake kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe.
\s5
\v 5 Ndipo atapaswa kuchinja ng'ombe mbele ya Bwana. Watoto wa Aroni, makuhani wataleta damu na kuinyunyizia katika madhabahu iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema la kukutania.
\v 6 Ndipo ataichuna sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande.
\s5
\v 7 Kisha wana wa Haruni kuhani wataweka moto katika madhabahu na kuweka kuni ili kuchochea moto.
\v 8 Wana wa Haruni, makuhani wataweka vipande, kichwa na mafuta, watazipanga juu ya kuni zilizoko juu ya moto ulio madhabahuni.
\v 9 Lakini matumbo yake na miguu lazima ataiosha kwa maji. Kisha kuhani atateketeza kila kitu kilicho juu ya madhabahu kama sadaka ya kuteketeza. Italeta harufu nzuri sana kwangu; itakuwa sadaka iliyotolewa kwa moto kwa ajili yangu.
\s5
\v 10 Kama sadaka kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza kutoka kundi, kondoo au mbuzi, lazima atoe dume asiye na kasoro.
\v 11 Lazima atamchinja juu ya madhabahu iliyo katika upande wa kaskazini mbele ya Bwana. Wana wa Haruni makuhani, watanyunyiza damu kila upande wa madhabahu.
\s5
\v 12 Kisha ataikata katika vipande, pamoja na kichwa na mafuta yake, kuhani atavipanga juu ya kuni zilizo katika moto ulio madhabahuni,
\v 13 lakini matumbo yake na miguu yake lazima ioshwe kwa maji. Kisha kuhani atatoa yote na kuiteketeza juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa, italeta harufu nzuri kwa ajili ya Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
\s5
\v 14 Kama sadaka yake kwa Bwana itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa ni ndege, ndipo ataleta kama sadaka yake aidha ni huwa au kinda la njiwa.
\v 15 Kuhani ataileta madhabahuni, atamnyonga kichwa chake, na kuiteketeza juu ya madhabahu. Kisha damu yake itachuruzishwa juu ya pande za madhabahu.
\s5
\v 16 Kisha atakiondoa kibofu chake pamoja na uchafu wake, na kukiweka upande wa mashariki mwa madhabahu, katika sehemu ya majivu.
\v 17 Kisha atapasua mabawa yake, lakini hatagawanya katika vipande viwili. Kisha Kuhani atamtekeza katika madhabahu, juu ya kuni amabazo ziko juu ya moto. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa, na italeta harufu nzuri sana kwa Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Yeyote akitoa sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake lazima iwe unga safi, na atamwaga mafuta juu yake na kuweka ubani juu yake.
\v 2 Atachukua sadaka kwa wana wa Haruni, makuhani na pale kuhani atachukua konzi moja ya unga safi pamoja na mafuta na ubani. Kisha kuhani atateketeza hiyo sadaka juu ya madhabahu kuwa shukrani kwa uzuri wa Bwana. Italeta harufu nzuri sana kwa Bwana, itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
\v 3 Unga wowote uliobaki utakuwa ni wa Haruni na watoto wake. Ni takatifu sana kwa Bwana iliyotolewa sadaka kwa Bwana kwa moto.
\s5
\v 4 Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate lainiya unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta.
\v 5 Kama matoleo yako ya nafaka yameokwa na kikaango cha chuma ni lazima iwe unga safi bila chachu uliochanganywa na mafuta.
\s5
\v 6 Utagawanya katika vipande na kumwaga mafuta juu yake. Hii ni sadaka ya nafaka.
\v 7 Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa katika kikaango, ni lazima iwe imetengenezwa kwa unga safi na mafuta.
\s5
\v 8 Utaleta matoleo ya nafaka yaliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana, italeta kwa kuhani, ambaye ataleta mbele ya madhabahu.
\v 9 Ndipo kuhani atachukua baadhi ya sadaka ya nafaka ya shukrani ya Bwana, ataitekeza katika madhabahu. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, italeta harufu nzuri kwa Bwana.
\v 10 Itakayobaki sadaka ya nafaka itakuwa ya Haruni na wanawe. Itakuwa takatifu kamili ya Bwana kutoka matoleo kwa Bwana yatolewayo kwa moto.
\s5
\v 11 Sadaka ya nafaka itolewayo kwa Bwana isiwe na chachu, hautatekeza chachu wala asali kama matoleo yatakayotekezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana.
\v 12 Utayatoa kwa Bwana kama mazao ya kwanza, lakini hayatatumika kama matoleo ya harufu nzuri ya moto juu ya madhabahu.
\v 13 Utaweka chumvi katika kila matoleo yako ya nafaka. Usipungukie chumvi ya agano la Bwana katika matoleo yako ya unga. Matoleo yako yote hayatapungukiwa na chumvi.
\s5
\v 14 Kama ukitoa matoleo ya nafaka ya mazao ya kwanza kwa Bwana, utatoa nafaka mbichi yaliyookwa kwa moto, na yaliyopondwa.
\v 15 Lazima utaweka mafuta na ubani juu yake. Haya ni matoleo ya nafaka.
\v 16 Kuhani atatoa sehemu ya nafaka iliyopondwa na mafuta na ubani, kama sadaka ya shukrani itolewayo kwa uzuri wa Bwana. Hii ni sadaka ya Bwana inayotolewa kwa moto.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kama mtu atoa dhabihu ambayo ni matoleo ya amani ya mnyama kutoka katika kundi, dume au jike, lazima atatoa mnyama asiyena kasoro mbele ya Bwana.
\v 2 Ataweka mikono yake juu ya sadaka yake na atamchinja mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Kisha wana wa Haruni makuhani watanyunyizia damu yake katika pande za madhabahu.
\s5
\v 3 Mtu akitoa dhabihu ya amani itolewayo kwa moto kwa ajili ya Bwana. Mafuta yanayofunika au yanayoungana na hizo sehemu za ndani,
\v 4 figo mbili na mafuta yaliyofunika kiunoni na yanayozunguka ini, pamoja na figo atayatoa pamoja.
\v 5 Wana wa Haruni watayachoma hayo katika madhabahu pamoja na sadaka ya kutekezwa, juu ya kuni zilizo kwenye moto. Zitaleta harufu nzuri mbele ya Bwana; itakuwa sadaka ya itolewayo kwake kwa moto.
\s5
\v 6 Kama dhabihu ya amani ya mtu itolewayo kwa Bwana ni kutoka katika mifugo ni mbuzi au kondoo ni dume au jike, atatoa dhabihu isiyo na kasoro.
\v 7 Kama atatoa mwanakondoo kwa ajili ya dhabihu yake, atamtoa mbele za Bwana.
\v 8 Ataweka mkono wake juu ya ya kichwa cha dhabihu yake na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande za madhabahu.
\s5
\v 9 Mtu akitoa sadaka ya dhabihu ya amani kama sadaka ya kusogezwa kwa moto kwa Bwana. Mafuta, mafuta ya mkia yatakatwa hapo karibu na mfupa wa kiuno, na mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yaliyo katika matumbo,
\v 10 na figo zote mbili na mafuta yanayofunika yaliyo karibu na kiuno kitambi kilicho karibu na ini na figo ataziondoa zote.
\v 11 Na kuhani atayatekeza yote kwa moto katika madhabahu kama sadaka ya chakula isogezwayo kwa moto kwa Bwana.
\s5
\v 12 Kama matoleo ya mtu ni mbuzi, ndipo ataitoa mbele ya Bwana.
\v 13 Ataweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande zote za madhabahu.
\v 14 Mtu akitoa dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto. Ataondoa mafuta yanayozunguka matumbo, na mafuta yote yanayozunguka matumbo.
\s5
\v 15 Ataondoa pia figo mbili na mafuta yanayozunguka, ambayo yanazunguka kiuno na kitambi cha maini pamoja na figo.
\v 16 Kuhani atateketeza yote juu ya madhabahu kama matoleo ya chakula yatolewayo kwa moto, ni sadaka ya kuleta harufu nzuri sana. Mafuta yote ni ya Bwana.
\v 17 Itakuwa ni amri ya kudumu kwa kizazi cha watu katika maeneo yote mtakapotengeneza makazi, kwamba hamtakula mafuta au damu."'
\s5
\c 4
\p
\v 1 Bwana alisema na Musa na kumwambi,
\v 2 "Waambie wana wa Israeli 'mtu yeyote akifanya dhambi bila kukusudia, kufanya chochote ambacho Bwana ameagiza kutofanya, na kama akifanya chochote kilichozuiliwa, yafuatayo lazima yatatendeka.
\v 3 Kama ni kuhani mkuu aliyetenda dhambi na kuleta hatia kwa watu, atatoa dume asiyekuwa na kasoro kwa Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda kama sadaka ya dhambi.
\s5
\v 4 Ataleta dume mbele ya mlango wa hema ya kukutania mbele ya Bwana, ataweka mikono juu ya dume, na atamchinja huyo dume mbele za Bwana.
\v 5 Kuhani aliyewekewa mafuta atachukua damu ya dume na kuileta mbele ya hema ya kukutania.
\s5
\v 6 Kuhani atazamisha kidole chake katika damu na kuinyunyiza mara saba mbele za Bwana, mbele ya pazia la mahali pa takatifu.
\v 7 Na kuhani ataweka kiasi cha damu ya huyo dume juu ya pembe za madhabahu ya kuvukizia uvumba mbele za Bwana, katika hema ya kukutania na ataimwaga yote iliyobaki chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mahali pa kuinglia katika hema ya kukutania.
\s5
\v 8 Atakata mafuta yote ya dume wa sadaka ya dhambi, mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo katika matumbo,
\v 9 figo mbili na mafuta yaliyopo pamoja nazo, yaliyo karibu na kiuno na kitambi cha maini pamoja na hizo figo.
\v 10 Ataondoa zote vile vile kama yanavyoondolewa katika dume wa sadaka ya dhabihu ya amani. Kuhani atatekeza sehemu hizo katika madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.
\s5
\v 11 Ngozi ya dume na mabaki yoyote ya nyama, pamoja na kichwa chake, miguu yake, matumbo yake na mavi yake,
\v 12 mabaki yote ya dume atayachukua nje ya mji mahali palipo safi, mahali wanapomwaga majivu; watateketeza sehemu zote juu ya kuni. Watateketeza sehemu zote mahali wanapomwaga majivu.
\s5
\v 13 Kama mkutano wote wa wana wa Israeli wakitenda dhambi bila kukusudia, na mkutano hawatakumbuka kwamba wametenda dhambi, na kufanya vile Bwana aliagiza wasifanye na wakajisikia hatia.
\v 14 Na dhambi waliyofanya ikajulikana, mkutano watatoa ng'ombe dume mchanga kuwa sadaka ya dhambi watamleta mbele ya hema ya kukutania.
\v 15 Wazee wa mkutano wataweka mikono yao juu ya kichwa cha ng'ombe mbele za Bwana, na ng'ombe atachinjwa mbele za Bwana.
\s5
\v 16 Kuhani aliyetiwa mafuta ataleta damu ya ng'ombe katika hema ya kukutania,
\v 17 kuhani atachovya kidole chake katika damu na kuinyunyizia mara saba mbele za Bwana mbele ya pazia.
\s5
\v 18 Ataweka kiasi cha damu katika pembe za madhabahu mbele za Bwana iliyo katika hema ya kukutania na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania.
\v 19 Atakata mafuta yote na kuyatekeza katika madhabahu.
\s5
\v 20 Hivyo ndivyo atakavyomfanya huyo ng'ombe, kama alivyomfanya ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia vivyo hivyo huyu ng'ombe, kuhani atawafanyia upatanisho watu nao watasamehewa.
\v 21 Atamchukua huyo ng'ombe nje ya mji na kumteketeza kama alivyomteketeza ng, ombe wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano.
\s5
\v 22 Mtawala akitenda dhambi bila kukusudia kufanya moja ya yale Bwana Mungu wake ameagiza kutotenda, na anajisikia hatia
\v 23 na kama dhambi yake aliyotenda anaifahamu, ataleta dhabihu yake mbuzi mme asiye na kasoro.
\s5
\v 24 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi na kumchinja mahali ambapo huchinja sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
\v 25 Kuhani atachukua damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuiweka juu ya pembe za madhabahu kwa dhabihu ya kuteketezwa, na atamwaga damu chini ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa.
\s5
\v 26 Atateketeza mafuta yote katika madhabahu, kama vile mafuta ya dhabihu ya sadaka ya amani, Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mtawala kulingana na dhambi yake, na mtawala atakuwa amesamehewa.
\s5
\v 27 Kama yeyote wa watu wa kawaida akitenda dhambi bila kukusudia, kufanya vitu ambavyo Bwana ameagiza kutokufanywa na kama ana hatia,
\v 28 ndipo dhambi yake aliyoitenda ikajulikana kwake, ndipo ataleta mbuzi mke asiyekuwa na kasoro awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zake alizotenda.
\s5
\v 29 Ataweka mikono yake juu ya sadaka ya dhambi na kuchinja sadaka ya dhambi mahali pa sadaka ya kuteketezwa.
\v 30 Kuhani atachukua kiasi cha damu kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa. Damu yote iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu.
\s5
\v 31 Atayaondoa mafuta yote, kama alivyoondoa mafuta katika dhabihu ya amani. Kuhani ataiteketeza katika madhabahu ili kuwa harufu nzuri kwa Bwana. Kuhani atafanya upatanisho kwa mtu, na atasamehewa.
\s5
\v 32 Kama mtu ataleta mwanakondoo kama dhabihu yake kwa sadaka ya dhambi, ataleta jike asiye na kasoro.
\v 33 Ataweka mikono kichwani mwa sadaka ya dhambi na atamchinja kuwa sadaka ya dhambi mahali wanapochinjwa sadaka ya kuteketezwa.
\s5
\v 34 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu.
\v 35 Ataondoa mafuta yote, kama akatavyo mafuta ya mwanakondoo dhabihu ya sadaka ya amani na kuhani ataiteketeza juu ya madhabahu juu ya sadaka ya Bwana itolewayo kwa moto. Kuhani ataleta upatanisho kwa dhambi aliyoifanya, naye atasamehewa.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kama mtu atatenda dhambi kwa sababu hakusema ukweli wakati alipotakiwa kutoa ushahidi fulani kuhusu kile alichotakiwa, ameona au kufahamu habari zake, yeye anastahili adhabu.
\v 2 Au mtu akigusa kitu chochote ambacho Mungu amekitaja kuwa ni najisi hata kama ni mzoga wa wanyama wa porini au ni mzoga wa wanyama wa kufugwa au wataambaao hata kama mtu huyo hakukusudia kumgusa, yeye ni najisi na mwenye hatia.
\s5
\v 3 Au amegusa kitu chochote kilicho kichafu, kwa vyovyote kama hakujua, ndipo atakuwa na hatia akijua vile.
\v 4 Au kama yeyote akiapa bila kufikiri kwa midomo yake kufanya ubaya, au kufanya vyema kwa vyovyote vile mtu ameapa kwa haraka atakapotambua atakuwa na hatia kwa vitu hivyo.
\s5
\v 5 Mtu yeyote akiwa na hatia kwa vitu hivi, lazima akiri kwa yoyote dhambi aliyotenda.
\v 6 Ndipo atakapoleta sadaka yake ya hatia mbele za Bwana kwa dhambi aliyokwisha tenda. Ataleta kondoo jike au mbuzi kutoka katika kundi lake kuwa matoleo ya dhambi, kuhani atafanya upatanisho kuhusu dhambi yake.
\s5
\v 7 Kama hataweza kununua mwana kondoo ataleta kama sadaka ya hatia, hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana, mmoja kwa sadaka ya dhambi na mwingine ni sadaka ya kutekeketezwa.
\v 8 Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.
\v 9 Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.
\s5
\v 10 Ndipo ataoa ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoelekezwa, na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi alizokwisha kufanya, na huyo mtu atakuwa amesamehewa.
\s5
\v 11 Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.
\s5
\v 12 Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
\v 13 Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.'"
\s5
\v 14 Bwana akamwambia Musa, akasema,
\v 15 "Kama mtu akikiuka amri na kufanya dhambi kinyume na mambo matakatifu ya Bwana, lakini akifanya bila kukusudia ataleta sadaka ya hatia kwa Bwana. Sadaka hii itakuwa ni kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi; thamani yake halisi kifedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kama sadaka ya hatia.
\v 16 Lazima atalipa kwa Bwana kwa kile alichokosa kulingana na kitakatifu, na ataongezea moja ya tano na kumpa kuhani. Ndipo kuhani ataweka upatanisho kwa ajili yake pamoja na kondoo wa sadaka ya hatia, na mtu atakuwa amesamehewa.
\s5
\v 17 Kama mtu akitenda dhambi kwa kufanya kile ambacho Bwana aliagiza kisifanyike, hata kama hakujuwa, atakuwa na hatia na ataibeba hatia yake.
\v 18 Lazima ataleta kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi, anayestahili thamani ya fedha, kama sadaka ya hatia kwa kuhani. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kulingana na dhambi aliyotenda, ambayo hakujua atakuwa amesamehewa.
\v 19 Ni sadaka ya hatia, na amekuwa na hatia mbele za Bwana."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Bwana alisema na Musa kumwabia,
\v 2 "Kama mtu akifanya dhambi na kuvunja amri kinyume na Bwana, kama kujihusisha na uongo dhidi ya jirani yake kuhusu kitu fulani cha kutokuwa mwaminifu, au kama akidanganya au kuiba au amemdhurumu jirani.
\v 3 Au akiokota kitu fulani ambacho jirani yake amepoteza na kusema uongo kuhusu hicho, na kuapa kwa uongo au kwa mambo kama haya ambayo watu wanaweza kutenda dhambi.
\v 4 Ndipo itakuwa hivi, kama ametenda dhambi na hatia, kwamba lazima akirudishe kwa vyovyote alichoiba au kudanganya au amedhurumu au kitu kilichopotea naye kukiokota.
\s5
\v 5 Au kama amedanganya kwa jambo lolote, lazima atakirudisha kamilina kuongezea sehemu ya tano kwa kumlipa anayedai, kwa siku ile anayopatikana na hatia.
\v 6 Ataleta sadka ya hatia kwa Bwana: kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi lake kulingana na thamani yake, kama sadaka ya hatia kwa kuhani.
\v 7 Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele ya Bwana, atakuwa amesamehewa kulingana na chochote kilicho mfanya kuwa na hatia."
\s5
\v 8 Ndipo Bwana alisema na Musa kumwambia,
\v 9 "Mwagize Haruni na wanawe, kusema, 'hii ni sheria ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa lazima iwe juu ya makaa ya madhabahu usiku wote hata asubuhi, na moto wa madhabahu utaendelea kuwaka.
\s5
\v 10 Kuhani atavaa nguo zake za kitani na atavaa nguo za kitani ndani yake. Atatoa majivu yaliyobaki baada ya moto kutekeza sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu, na ataweka majivu pembeni mwa madhabahu.
\v 11 Atavua mavazi haya na kuvaa mavazi mengine ili kuchukua majivu nje ya kambi na kupeleka mahali palipo safi.
\s5
\v 12 Moto katika madhabahu utaendelea kuwaka. Usizimike, na kuhani ataongeza kuni kila asubuhi. Atapanga juu yake sadaka ya kuteketezwa kama inavyotakiwa, na atateketeza juu yake mafuta ya sadaka ya amani.
\v 13 Moto lazima utaendelea kuwaka katika madhabahu, kamwe usizimike.
\s5
\v 14 Hii ni sheria ya sadaka ya nafaka. Wana wa Haruni watatoa mbele ya Bwana katika madhabahu.
\v 15 Kuhani atachukua konzi ya unga laini wa sadaka ya nafaka na mafuta na ubani ambao uko juu ya sadaka ya nafaka, atateketeza juu ya madhabahu kuleta harufu nzuri ya shukrani ya kumpendeza Bwana.
\s5
\v 16 Haruni na wanae watakula sadaka inayobaki, italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu. Watakula katika ua ya hema ya kukutania.
\v 17 Haitaokwa pamoja na chachu. Nimewapa kama sehemu ya sadaka yangu itolewayo kwa moto, ni takatifu sana, kama sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
\v 18 Kwa nyakati zote zijazo kupitia watu wa kizazi chako, mwanaume yeyote mzaliwa kutoka kwa Haruni aweza kula ni sehemu yake, ichukuliwayo katika sadaka ya Bwana kwa moto. Yeyote anayeigusa atakuwa mtakatifu."
\s5
\v 19 Bwana aliongea tena na Musa kumwambia,
\v 20 "Hii ni sadaka ya Haruni na wanawe ambayo watatoa kwa Bwana katika siku ambayo kila mwana atawekwa wakfu: sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kama kawaida sadaka ya nafaka nusu yake asubuhi na nusu yake jioni.
\s5
\v 21 Itatengenezwa na mafuta katika kikaango, utaileta ikiwa imeandaliwa imeokwa katika vipande utatoa sadaka ya nafaka ili kuleta harufu nzuri kwa Bwana.
\v 22 Mwana wa Kuhani Mkuu atakayekuwa Kuhani Mkuu mpya kutoka miongoni mwa wanawe ataitoa. Kama amri ya milele, yote itateketezwa kwa Bwana.
\v 23 Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itatekezwa yote. Haitaliwa kamwe."
\s5
\v 24 Bwana alisema tena Musa, kumwambia,
\v 25 "Sema na Haruni na watoto wake kwamba, 'Hii ni sheria ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi lazima kuchinjwa mahali pa sadaka ya kuteketezwa itachinjwa mbeleya Bwana. Ni takatifu sana.
\v 26 Kuhani atakayeitoa kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila. Italiwa mahali patakatifu katika ua wa hema ya kukutania.
\s5
\v 27 Yeyote atakayeigusa nyama yake atakuwa ni mtakatifu na kama damu itadondokea mavazi yatafuliwa mahali palipodondokewa, mahali patakatifu.
\v 28 Lakini chungu kikipikiwa kitavunjwa, kama imepikiwa katika chombo cha shaba, lazima kitasuguliwa na kusafishwa kwa maji.
\s5
\v 29 Mwanaume yeyote miongoni mwa makuhani anaweza kula nyama hiyo kwa sababu ni takatifu sana.
\v 30 Na hakuna sadaka ya dhambi italiwa ambayo damu yake imeletwa katika hema ya kukutania kufanya upatanisho katika mahali patakatifu. Ni lazima iteketezwe.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Hii ndiyo sheria ya sadaka ya hatia. Kwa sababu hiyo ni sadaka takatifu sana.
\v 2 Ni lazima waichinje sadaka ya hatia mahali panapostali kuchinjwa, na ni lazima watainyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.
\v 3 Mafuta yote yaliyomo ndani yake yataondolewa: mafuta ya mkiani, mafuta yaliyo sehamu za ndani,
\v 4 zile figo mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake, yaliyo karibu na kiuno, na yanayofunika ini—nyama hii yote lazima iondolewe pamoja na hizo figo.
\s5
\v 5 Kuhani ataviteketeza vipande hivi juu ya madhabahu viwe dhabihu iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia
\v 6 Kila mwanaume miongoni mwa familia ya kuhani anaweza kula sehemu ya sadaka hii. Lakini ni lazima iliwe ndani ya mahali patakatifu kwa sababu ni takatifu sana.
\s5
\v 7 Nayo sadaka ya dhambi ni kama ilivyo sadaka ya hatia. Ni sheria ileile hutumika kwa zote mbili. Zote ni mali ya kuhani azitumiaye kufanya upatanisho.
\v 8 Kuhani atoaye sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuchuku ngozi ya sadaka hiyo kwa ajili yake mwenyewe.
\s5
\v 9 Kila sadaka ya nafaka inayookwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.
\v 10 Kila sadaka ya nafaka, ama iwe unga mkavu au uliochanganywa na mafuta ya zeitu itakuwa ya ukoo wa Aroni kwa usawa.
\s5
\v 11 Hii ndiyo sheria ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo watu watazitoa kwa Yahweh.
\v 12 Iwapo mtu yeyote anaitoa ili kuonyesha shukrani kwa Yahweh, basi ataitoa pamoja na dhabih uya mikate iliyotengenezwa bila hamira, bali kwa mafuta ya zeituni yaliyochanganywa na unga lakini bila hamira, na maandazi yaliyotengenezwa bila hamira, bali yaliyopakwa mafuta juu yake, na mikate miembamba iliyofanywa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta.
\s5
\v 13 Kwa kusudi la kutoa shukrani, pia anapaswa kutoa pamoja na sadaka yake ya amani, vipande vya mikate iliyotiwa hamira.
\v 14 Ni lazima atatoa moja kila aina ya sadaka hizi kama sadaka iliyoletwa kwa Yahweh. Nayo itakuwa ya makuhani wanaonyunyizia damu ya sadaka ya amani kwenye madhabahu.
\s5
\v 15 Mtu anayeleta sadaka ya amani kwa kusudi la kutoa shukrani ni lazima ataila nyama ya sadaka yake siku ya kutoa dhabihu. Hatakiwi kusaza chochote kilicho cha sadaka hiyo hata asubuhi ya pili.
\v 16 Lakini iwapo dhabihu ya matoleo yake kusudi lake ni nadhiri, au kwa kusudi la sadaka ya hiari, nyama yake italiwa siku iyo hiyo aitoapo dhabihu yake, lakini chochote kinachosalia cha sadaka hiyo kinaweza kuliwa siku inayofuata.
\s5
\v 17 Hata hivyo, nyama yoyote ya dhabihu inayobaki siku ya tatu ni lazima ichomwe moto.
\v 18 Iwapo kipande chochote cha nyama hiyo ya dhabihu kinachobaki kinaliwa katika siku ya tatu, hakitakubalika, wala hakitatolewa kwa aliyeitoa. Kitakuwa ni kitu cha kuchukiza, na mtu akilaye atabeba hatia ya dhambi mwenyewe yake.
\s5
\v 19 Nyama yoyote inayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa. Ni lazima ichomwe moto. Na kwa ajili ya nyama inayobaki, yeyote aliye safi anaweza kuila.
\v 20 Hata hivyo, mtu najisi anayekula nyama kutoka kwenye dhabihu ya matoleo ya amani ambayo ni ya Yahweh yapasa mtu huyu akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
\s5
\v 21 Iwapo mtu yeyote anagusa kitu chochote kilichonajisi—iwe ni unajisi wa binadamu, au wa mnyama aliyenajisi, au wa kitu fulani kilichonajisi na chenye kuchukiza, na kisha akala baadhi ya nyama ya dhabihu ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Yahweh, lazima mtu huyo akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.
\s5
\v 22 Kisha Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 23 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.
\v 24 Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
\s5
\v 25 Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
\v 26 Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
\v 27 Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'"
\s5
\v 28 Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
\v 29 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
\v 30 Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
\s5
\v 31 Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Aroni na uzao wake.
\v 32 Ni lazima utatoa paja la kulia kwa kuhani kama sadaka iliyotokana na dhabihu ya sadaka yako ya amani.
\s5
\v 33 Yule kuhani, mmoja wa wazao wa Aroni, atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani—ni lazima atapata paja la kulia kama mgao wake wa sadaka.
\v 34 Kwa kuwa nimetwaa kidari, na paja la sadaka ya kutikiswa kutoka kwa watu wa Israeli uwe mchango wao, na amepewa Aroni kuhani na wanawe kuwa mgao wao wa kawaida.
\s5
\v 35 Huu ndiyo mgao wa Aroni na uzao wake utokanao na matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, siku ile Musa alipowaweka wakfu ili kumtumikia Yahweh katika kazi ya kuhani.
\v 36 Huu ndio mgao ambao Yahweh aliamru waweze kupewa kutoka kwa watu wa Israeli, katika siku hiyo aliyowatia mafuta ya upako wawe makuhani. Nao utakuwa mgao wao wa kila siku katika vizazi vyote.
\s5
\v 37 Hii ndiyo sheria ya sadaka ya kuteketezwa, ya sadaka ya nafaka, ya sadaka ya dhambi, ya sadaka ya hatia, ya sadaka ya kuweka wakfu, na ya dhabihu, ya sadaka za amani,
\v 38 ni sheria ambazo Yahweh alizitoa kwa Musa kwenye Mlima Sinai siku aliyowaamru watu wa Israeli kutoa dhabihu zao kwa Yahweh katika jangwa la Sinai.'"
\s5
\c 8
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 2 "Walete Aroni na wanawe pamoja naye, mavazi na mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili, na kikapu cha mkate usio na hamira.
\v 3 Ita kusanyiko lote kwenye ingilio la hema la kukutania."
\s5
\v 4 Kwa hiyo Musa akafanya kama Yahweh alivyomwamru, nalo kusanyiko lilikuja pamoja mbele ya ingilio la hema la kukutania. Kisha Musa akaliambia kusanyiko,
\v 5 "Hivi ndivyo alivyotuamru Yahweh tutende."
\s5
\v 6 Musa akamleta Aroni na wanawe na kuwaosha kwa maji.
\v 7 Akamvika Aroni kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini na kumfunga ukumbuu kiunoni mwake, akamvika joho la nje lenye mikono mirefu na kumvika kile kizibao chenye vipande viwili tumboni na mgongoni na kukifunga kuzunguka kiunoni mwake kwa mshipi uliosokotwa kwa ustadi na kukikaza mwilini mwake.
\s5
\v 8 Kisha Musa akaweka kifuko kifuani mwa Aroni, na ndani ya kifuko hicho akaweka Urimu na Thumimu.
\v 9 Na kisha akamfunga kiremba kichwani, na juu ya kiremba kwa mbele, akaweka bamba la dhahabu; liwe taji takatifu, kama Yahweh alivyomwamru yeye.
\s5
\v 10 Musa akayatwaa hayo mafuta ya upako, akalipaka lile hema la kukutania na kila kitu kilichokuwamo ndani yake na kuvitenga kwa ajili ya Yahweh.
\v 11 Akayanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kisha akaipaka mafuta hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na sinia la kunawia na kitako chake ili kuvitenga wa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 12 Akamimina sehemu ya mafuta ya upako juu ya kichwa cha Aroni na kisha akampaka mafuta ili kumtenga.
\v 13 Musa akawaleta wana wa Aroni na kuwavika kila mmoja kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini. Kila mmoja wao akamfunga kwa ukumbuu kiunoni mwake na kuwafunga vitambaa vya kitani kichwani pao, kama vile Yahweh alivyokuwa amemru Musa.
\s5
\v 14 Musa akamleta huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha fahali ambaye wamemelete kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
\v 15 Musa akamchinja, na kisha akachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuiweka juu ya mpembe za madhabahu, akaitakasa hiyo madhabahu, na kuitenga kwa Mungu, ambapo kwa kufanya hivyo, aliisababisha madhabahu kuwa sehemu ya kufaa kwa kufanyia upatanisho.
\s5
\v 16 Akachukua mafuta yote yaliyokuwa sehemu za ndani, kile kiwambo cha ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake, Musa akaichoma hiyo nyama yote juu ya madhabahu.
\v 17 Lakini yule fahali, ngozi yake, nyama yake na kinyesi chake, akavichoma nje ya kambi, kama vile Yehweh alivyokuwa amemwamru yeye.
\s5
\v 18 Musa akamleta yule konndoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo kondoo.
\v 19 Musa akamchinja kondoo na kuinyunyizia damu yake kila upande wa madhabahu.
\s5
\v 20 Naye akamkatakata kondoo vipande vipande na akakiteketeza kichwa chake pamoja na vile vipande na mafuta.
\v 21 Akaziosha kwa maji zile sehemu za ndani pamoja na miguu na akamteketeza kandoo mzima juu ya madhabahu. Ilikuwa ni dhabihu ya kuteketezwa na ilitoa harufu ya kupendeza, sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
\s5
\v 22 Kisha Musa akamleta yule kondoo dume mwingine, kondoo wa kuwekwa wakfu, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo.
\v 23 Aroni akamchinja, naye Musa akachukua sehemu ya damu na kuiweka kwenye ncha ya sikio la Aroni la kulia, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye kidole kikumbwa cha mguu wake wa kulia.
\v 24 Akawaleta wana wa Aroni, naye akaweka sehemu ya damu ya kondoo yule kwenye ncha ya sikio lao la kulia, kwenye dole gumba lao cha mkono wa kulia na kwenye kidole chao kikubwa cha mguu wa kulia. Kisha Musa akainyunyiza damu ya huyo kila upande wa madhabahu
\s5
\v 25 Naye akayatwaa yale mafuta, mafuta ya mkiani, mafuta liyolikuwa sehemu za ndani, na mafuta yafunikayo ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.
\v 26 Akachukua mkate mmoja kutoka kwenye kikapu cha mikate isiyo na hamira ambayoo ilikuwa mbele za Yahweh, akatwaa mkate moja usio na hamira, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na mkate mwemba wa kaki na akaiweka juu ya mafuta na juu ya paja la kulia la kondoo.
\v 27 Akaiweka yote mikoni mwa Aroni na katika mikono ya wanawe na kuitikisa mbele za Yahweh kuwa sadaka ya kutikiswa
\s5
\v 28 Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto.
\v 29 Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahweh. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru yeye.
\s5
\v 30 Musa akatwaa sehemu ya mafuta ya upako na damu iliyokuwa juu ya madhabahu; naye akayanyunyiza haya juu ya nguo za Aroni, juu ya nguo zake mwenyewe na juu ya nguo za wana wa Aruni waliokua pamoja naye. Kwa njia hii alimtenga Aroni na nguo zake, na wanawe na nguo zao kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 31 Kwa hiyo Musa akawambia Aruni na wanawe, "Ipikeni nyama mbele ya ingilio la hema la kukutania, na hapo mtaila pamoja na mkate ulio kwenye kikapu cha kuwekwa wakfu, kama ilivyoamriwa, kusema, 'Aroni na wanawe wataila.'
\v 32 Masalio yoyote ya nyama na mikate utayateketeza kwa moto.
\v 33 Na hamtatoka kwenye ingilio la hema la kukutania kwa muda wa siku saba, hata zitakapotimia siku za kuwekwa mikono kwenu. Kwa kuwa kwa muda wa siku saba, Yahweh atawaweka wakfu.
\s5
\v 34 Kilichotendeka siku hii— Yahweh ndiye amekiamru kitendekeke ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
\v 35 Mtakaa kwenye ingilio la hema la kukutania mchana na usiku siku saba, nanyi ishikeni amri ya Yahweh ili msije mkafa, kwa sababu hivi ndivyo ilivyoamriwa.
\v 36 Kwa hiyo Aroni na wanawe wakafanya mambo yote ambayo Yahweh alikuwa amewaamru kwa kinywa cha Musa.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Katika siku ya nane, Musa akawaita Aroni na wanawe pamoja na wazee wa Israeli.
\v 2 Akamwambia Aroni, "Twaa ndama dume kutoka kundini kwa ajili ya sadaka ya dhambi zako, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, na uwatoe mbele za Yahweh.
\s5
\v 3 Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Twaeni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi na ndama na mwana-kondoo, hawa wawili wawe na umri wa mwaka mmoja na bila dosari, ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;
\v 4 pia twaeni fahali na kondoo dume kwa sadaka za amani ili kuwatoa mbele za Yahweh, na sadaka za nafaka iliyochanganywa na mafuta, kwa sababu leo Yahweh atajidhihirisha kwenu.
\v 5 Kwa hiyo wakaleta kwenye hema la kukutania vyote ambavyo Musa aliagiza, nalo kusanyiko lote la Israeli likakaribia na kusimama mbele za Yahweh.
\s5
\v 6 Kisha Musa akasema, "Hivi ndivyo Yahweh amewaamru nyinyi mfanye, ili kwamba utukufu wake uweze kuonekana kwenu.
\v 7 "Musa akamwambia Aroni, "Njoo karibu na Madhabahu na uteo sadaka yako ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu ili kufanya upatanisho kwa ajili yao kama vile ambavyo Yahweh amekwishaamru."
\s5
\v 8 Kwa hiyo Aroni akaikaribia madhabahu na akamchinja yule ndama kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ambayo ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe.
\v 9 Nao wana wa Aroni wakamletea hiyo damu, naye akakichofya kidole chake kwenye damu na kuiweka kwenye pembe za madhabahu, kisha akaimwaga damu chini ya kitako cha madhabahu.
\s5
\v 10 Hata hivyo, aliyateketeza hayo mafuta, figo, na mafuta yanafunika ini juu ya madhabahu kuwa sadaka ya dhambi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
\v 11 Na akaiteketeza hiyo nyama pamoja na ngozi nje ya kambi
\s5
\v 12 Aroni akaichinja sadaka ya kuteketezwa, nao wanawe wakampa hiyo damu, ambayo aliinyunza pande zote za madhabahu.
\v 13 Kisha wakampa ile sadaka ya kuteketezwa, kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.
\v 14 Akaziosha sehemu za ndani pamoja na miguu na kuziteketeza juu ya dhabihu ya kuteketezwa juu ya Madhabahu.
\s5
\v 15 Aroni akaleta dhabihu ya watu— mbuzi, kisha akamtoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi yao naye akamchinja, akaitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi, kama alivyofanya kwa yule mbuzi wa kwanza.
\v 16 Akaileta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama Yahweh alivyokuwa ameamru.
\v 17 Akaileta sadaka ya nafaka; akakijaza kiganja chake nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa.
\s5
\v 18 Pia akamchinja fahali na yule kondoo dume, dhabihu kwa ajili ya sadaka ya amani, ambayo ilikuwa kwa ajili ya watu. Nao wana wa Aronni wakampa damu, ambayo aliinyunyiza kila upande wa mdhabahu.
\v 19 Hata hivyo, waliyakata mafuta ya fahali na ya yule kondoo dume, mafuta ya kwenye mkia, mafuta yafunikayo sehemu za ndani, figo, na yale mafuta yaliyofunika mapafu.
\s5
\v 20 Wakazichukua hizi sehemu zilizokatwa wakaziweka juu ya vidari, na kisha Aroni akateketeza mafuta juu ya madhabahu.
\v 21 Naye Aroni akavitikisa vidari na paja la kulia kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh, kama vile Musa alivyokuwa ameamru,
\s5
\v 22 Kisha Aroni akainua juu mikono yake mbele ya watu na kuwabariki, kisha akashuka chini kutoka mahali alipokuwa akitoa hiyo sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani.
\v 23 Musa na Aroni wakaingia ndani ya hema la kukutania, kisha wakatoka nje tena na kuwabariki watu, na utukufu wa Yahweh ukaonekana kwa watu wote.
\v 24 Moto ukashuka kutoka kwa Yahweh na ukairamba sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wlipoona jambo hili, wakapiga kelele na kulala chini.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua kila mtu kifukizo chake, akaweka moto ndani yake, na kisha uvumba. Kisha wakatoa moto usiokuabalika mbele za Yahweh, moto ambao hakuwaamru wao kuutoa.
\v 2 Kwa hiyo moto ukashuka chini mbele za Yahweh na kuwala, nao wakafa mbele za Yahweh.
\s5
\v 3 Kisha Musa akamwambia Aroni, Hivi ndiyo Yahweh alivyokuwa akizunguzia aliposema, 'Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.'" Naye Aroni hakusema neno lolote.
\v 4 Musa akamwita Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mjomba wa Aroni, naye akamwambia, "njoo huku na uwatowe ndugu zako nje ya kambi watoke mbele ya hema."
\s5
\v 5 Hivyo wakakaribia na kuwachukua wangali wamevaa kanzu zao za kikuhani, nao wakawapeleka nje ya kambi, kama Musa alivyokuwa ameelekeza. Kisha Musa akamwambia Aroni na wanawe wengine wawili, Eliezari na Ithamari, "
\v 6 Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu, ili kwamba msije mkafa, na kwamba Yahweh asilikasirikie kusanyiko zima. Lakini waacheni jamaa zenu, nyumba yote ya Israeli waweze kufanya ibada za maombolezo kwa ajili ya hao ambao Yahweh amewaangamiza kwa moto.
\v 7 Msiende nje kutoka kwenye ingilio la hema la kukutania, ama sivyo mtakufa, kwa kuwa mafuta ya Yahweh ya upako yako juu yenu." Kwa hiyo wakatenda sawasawa na maelekezo ya Musa.
\s5
\v 8 Mungu akazungumza na Aroni, akisema,
\v 9 "Msinywe mvinyo wala kinywaji kikali, wewe, au wanao wanaobaki pamoja nawe, ili kwamba mtakapoingia kwenye hema ya kukutania msije mkafa. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu,
\v 10 ili kupaambanua kati ya mambo matakatifu na mambo ya kawaida, na kati ya najisi na safi,
\v 11 ili kwamba mweze kuwafundisha watu wa Israeli amri zote ambazo Yahweh ameziamru kwa kinywa cha Musa.
\s5
\v 12 Musa akazungumza na Aroni na wanawe wawili waliosalia; Eliazari naIthamari, Twaeni sadaka ya nafaka inayobaki kutokana na sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto, nanyi ileni kando ya madhabahu bila hamiara, kwa kuwa ni takatifu sana.
\v 13 lazima mtaila mahali patatifu kwa sababu huo ni mgao wako wewe na mgao wa wanao wa matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, kwa kuwa hivi ndivyo limeamriwa niwaambie.
\s5
\v 14 Kile kidari kitikiswacho na lile paja ambalo hutolewa kwa Yahweh, yapasa mzile mahali palipo safi panapokubalika kwa Mungu. Wewe mwenyewe, wanao na binti zako waliopamoja nawe mtakula sehemu hizo, kwa kuwa zimetolewa kuwa mgao wako na mgao wa wanao kutokana na dhabihu ya sadaka ya ushirika wa watu wa Israeli.
\v 15 Lile paja lililotolewa na kidari kilichotikiswa, ni lazima ziletwe pamoja na sadaka ya mafuta iliyofanywa kwa moto, ili kutikiswa mbele za Yahweh. Nazo zitakuwa zako wewe na wanao kuwa mgao wenu daima, kama Yahweh alivyoamru.
\s5
\v 16 Kisha Musa akauliza kuhusu yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye akagundua kwamba alikuwa ametekezwa kwa moto. Kwa hiyo akawakasirikia Eliazari na Ithamari, wana wa Aroni waliosalia; akawaambia,
\v 17 "Kwa nini hamjaila sadaka ya dhambi katika eneo la hema, kwa kuwa ni takatifu sana, na kwa kuwa Yahweh amishaitoa kwenu ili kuchukua uovu wa kusanyiko, ili kufanya upatanisho kwa aijli yao mbele zake?
\v 18 Tazama, damu yake haikuletwa ndani ya hema, kwa hiyo iliwapasa kwa hakika kuwa mekwisha ila kwenye eneo la hema, kama nilivyoagiza?
\s5
\v 19 Kisha Aroni akamjibu Musa, " Tazama, leo walitoa sadaka yao ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa mbele za Yahweh, na jambo hili vilevile limetendeka kwangu leo. Ikiwa nimeshakula sadaka ya dhambi leo, Je! Isingekuwa imeshapendeza mbele za Yahweh?"
\v 20 Naye Musa aliposikia hivyo, akaridhika.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa na Aroni, akasema,
\v 2 "Sungumzeni na watu wa Israeli muwaambie, 'Hivi ndivyo viumbe vyenye uhai ambavyo mwaweza kula miongoni mwa wanyama walioko juu ya nchi.
\s5
\v 3 Mnaweza kula mnyama yeyote aliye na kwato zenye kugawanyika na ambaye pia hucheua.
\v 4 Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.
\s5
\v 5 Pimbi pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyo pia ni najisi kwenu.
\v 6 Na sungura pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyu naye ni najisi kwenu.
\v 7 Na nguruwe pia: ingawaje yeye anazo kwato zilizogawanyika lakini hacheui, kwa hiyo yeye ni najisi kwenu.
\v 8 Msile aina yoyote ya nyama yao, wala msiiguse mizoga yao. Hao ni najisi kwenu.
\s5
\v 9 Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala ni wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni.
\v 10 Lakini viumbe wote hai wasio na mapezi na magamba waliomo baharini au mitoni, pamoja na wale waendao majini na viumbe hai waliomo majini —watakuwa chukizo kwenu.
\s5
\v 11 Kwa kuwa watakuwa chukizo, msile nyama yao, pia mizoga yao sharti itakuwa chukizo.
\v 12 Chochote kisichokuwa na mapezi au magamba kilichomo majini ni lazima kiwe chukizo kwenu.
\s5
\v 13 Nao ndege mtakaowachukia na msiopaswa kuwala ni hawa wafuatao: tai, furukombe, kipungu,
\v 14 mwewe mwekundu, aina yoyote ya kipanga,
\v 15 kila aina ya kunguru,
\v 16 kiruka-njia, kipasuasanda, Shakwe, na aina yoyote ya mwewe.
\s5
\v 17 Ni lazima pia bundi mdogo na bundi mkubwa muwaone kuwa chukizo, mnandi,
\v 18 bundi mweupe na mwari,
\v 19 korongo na ina zote za koikoi, huduhudi na popo pia.
\s5
\v 20 Wadudu wote wenye mabawa wanatembea kwa miguu minne kwenu ni machukizo.
\v 21 Lakini manaweza kula wadudu wenye mabawa wanaotembea kwa miguu minne ya kurukia ardhini yenye vifundo.
\v 22 Na manaweza kula kula aina zote za nzige, senene, parare, au panzi.
\v 23 Lakini wadudu wote warukao wenye miguu minne ni chulkizo kwenu.
\s5
\v 24 Nanyi mtakuwa najisi hata jioni kutokana na wanyama hawa endapo mtagusa mizogo yao.
\v 25 Na yeyote atakayeokota mojawapo wa mizoga yao ni lazima atazifua ngua zake naye atakuwa najisi hata jioni.
\s5
\v 26 Mnyama yeyote ambaye anazo kwato ziliachana ambazo hazikugawanyika kabisa au hacheui huyo ni najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa najisi.
\v 27 Mnyama yeyote anayetembea kwa vitanga vyake miongoni mwa wanyama waendao kwa miguu yote minne ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mzoga kama huo atakuwa najisi hata jioni.
\v 28 Na yeyote aokotaye mzoga kama huo ni zazima atazifua nguo zake na kuwa najisi hata jioni. Wanyama hawa watakuwa najisi kwenu.
\s5
\v 29 Kuhusiana na wanyama wataambaao juu ya ardhi, hawa ndiyo walio najisi kwenu: kicheche, panya, aina zote za mijusi mikubwa, guruguru,
\v 30 kenge, mijusi ya ukutani, goromoe, na kinyonga.
\s5
\v 31 Wanyama hawa wote ambao hutambaa, hawa ndiyo watakuwa najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa njisi hata jioni.
\v 32 Na iwapo mmoja wao anakufa na kuanguka juu ya chombo, chombo hicho kitakuwa najisi, ama kiwe kimetengenezwa kwa mbao, nguo, ngozi, au gunia. Kiwe chombo cha namna gani na kiwe kwa matumizi gani, ni lazima kitalowekwa katika maji nacho kitakuwa najisi hata jio. Kisha kitakuwa safi.
\v 33 Kwa hiyo kila chungu ambacho mnyama najisi atakiangukia juu yake au ndani yake, chochote kilichomo kwenye chungu hicho kitakuwa najisi, na ni lazima mtakivunja chungu hicho.
\s5
\v 34 Vyakula vyote ambavyo ni safi na kilichuhusiwa kuliwa, lakini kikaingiwa na maji kutoka kwenye chungu najisi kilichoanguka, nacho kitakuwa najisi.
\v 35 Na kitu chochote kinachoweza kunywewa kutoka kwenye chungu kama hicho kitakuwa najisi. Kila kitu kitakachoangukiwa juu yake na kipande cha mzoga wa mnyama najisi nacho kitakuwa najisi, ama liwe ni jiko au vyungu vya kupikia. Ni najisi na ni lazima kiwe najisi kwenu.
\s5
\v 36 Chemchemi au kisima cha maji ya kunywa yanapokusanyika patabaki kuwa safi iwapo kiumbe najisi kama hicho kitaangukia humo. Lakini ikiwa yeyote anaugusa mzoga wa mnyama aliye najisi uliomo ndani ya maji, yeye atakuwa najisi.
\v 37 Iwapo sehehemu yoyote ya mzoga wa mnyama aliyenajisi inaangukia juu ya mbegu zozote zilizo kwa ajili ya kupanda. Mbegu hizo zitakuwa bado zingali safi.
\v 38 Lakini kama maji yanawekwa juu ya mbegu, na kama sehemu ya mzoga unaangukia juu yake, nazo zitakuwa najisi kwenu.
\s5
\v 39 Iwapo mnyama yeyote awezaye kuliwa anakufa, naye yeyote amgusaye atakuwa najisi hata jioni.
\v 40 Na yeyote alaye chochote cha mzoga huo atalazimika kufua nguo zake naye atakuwa anjisi hata jioni. Na yeyote aokotaye mzoga kama huo atafua nguo zake na kuwa najisi hata jioni.
\s5
\v 41 Kila mnyama atambaaye juu ya ardhi atakuwa chukizo; hatakuwa wa kuliwa.
\v 42 Chochote kitambaacho kwa kujivuta juu ya tumbo lake, na chochote kitembeacho kwa miguu yake yote minne, au chochote kilicho na miguu mingi—wanyama wote ambao hutambaa juu ya nchi, hawa msiwale, kwa sababu watakuwa machukizo.
\s5
\v 43 Msijinajisi wenyewe kwa kiumbe chochote nnajisi kitaambacho; msijinasi wenyewe kwavyo, ili kwamba msije mkachafuliwa navyo.
\v 44 Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu. Nanyi lazima muwe watakatifu, kwa hiyo na iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu. Haiwapasi kujichafua kwa aina yoyote ya kiendacho juu ya nchi.
\v 45 Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh, aliyewaleta ninyi kutoka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo lazima muwe watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.
\s5
\v 46 Hii ndiyo sheria kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho majini, na ya kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi,
\v 47 kwa jili ya kilie kinachopaswa kutofautishwa kati ya kilicho najisi na kilicho safi, na kati ya vitu vilivyokufa na vilivyo hai ambavyo vyaweza kuliwa na vitu vyenye uihai visivyoweza kuliwa."
\s5
\c 12
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa,
\v 2 "zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, 'endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wasiku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi.
\v 3 Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa.
\s5
\v 4 Kisha utakaso wa mama wa kutokwa damu yake utaendelea kwa muda wa siku tatu. Haimpasi kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kukaribia eneo la hema mpaka zitakapomalizika siku za kutakaswa kwake.
\v 5 Lakini kama atajifungua mtoto wa kike, naye atakuwa najisi kwa mud wa majuma mawili, kama alivyo wakati wa kipindi chake. Kisha utakaso wa mama utaendelea kwa siku sitini sita.
\s5
\v 6 Siku za kutakaswa kwake zitakapoisha, kwa ajili ya mwana au binti, atalazimika kuleta kwa kuhani mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au huwa kuwa sadaka ya dhambi, mbele ya ingilio la hema la kukutania,
\s5
\v 7 Kisha atawatoa mbele za Yahweh na kufanya sadaka ya upatanisho kwa ajili yake, naye atatakaswa kutokana kutiririka kwa damu yake. Hii ndiyo sheria kuhusu mwanamke aifunguaye ama mtoto wa kiume au wa kike.
\v 8 Na kama hana uwezo wa kutoa mwana-kondoo, naye ataleta makinda mawili ya njiwa ua hua, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kuwa sadaka ya dhambi, naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake; naye atakuwa safi."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa na Aroni, akasema,
\v 2 Mtu yeyote anayeonekana na uvimbe au pele au doa ling'aalo juu ya ngozi ya mwili wake, na likawa limeambukizwa ugonjwa wa ngozi mwilini mwake, ni lazima aletwe kwa Aroni kuhani mkuu au kwa mmoja wa wanawe makuhani.
\s5
\v 3 Naye kuhanai atachunguza ugonjwa huo kwenye ngozi ya mwili wake. Iwapo malaika zilizopo eneo lenye ugonjwa zimegeuka kuwa nyeupe, na iwapo ugonjwa umejitokeza juu ya ngozi, huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Baada cha kuhani kumchunguza, atamtangaza kuwa ni najisi.
\v 4 Iwapo lile doa ling'aalo katika ngozi yake ni jeupe, na kuonekana kwake halikwenda chini zaidi ya ngozi, na iwapo malaika za eneo lenye ugonjwa hazijabadilika kuwa nyeupe, naye kuhani atamtenga mgonjwa kwa siku saba.
\s5
\v 5 Katika siku ya saba, huyo kuhani itambidi kumchunguza tena ili kuona kama katika maamzi yake huo ugonjwa siyo mbaya, na kama haujaenea kwenye ngozi. Iwapo haujaenea, basi, kuhani atamtenga kwa siku saba zaidi.
\v 6 Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa ubepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.
\s5
\v 7 Lakini endapo ule upele utakuwa umishasambaa kwenye ngozi baada ya kuwa amejionyesha kwa kuhani kwa ajili kusafishwa kwake, itambidi kujionyesha tena kwa kuhani.
\v 8 Naye kuhani atamchunguza ilikuona kama huo upele umsambaa zaidi ndani ya ngozi. Na endapo utakuwa umesambaa, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\s5
\v 9 Iwapo ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza umo kwa mtu fulani, naye mtu huyo yapasa aletwe kwa kuhan.
\v 10 Kuhani atamchunguza ili kuona kama kunauvimbe mweupe katika ngozi yake, endapo malaika zitakuwa zimebadilika kuwa nyeupe, au kumekuwa na nyama mbichi kwenye uvimbe.
\v 11 Kama ipo, basi, huo ni ugonjwa sugu wa ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Hatamtenga kwa kuwa yeye tayari ni najisi.
\s5
\v 12 Iwapo huo ugonjwa unajitokeza na kupanuka zaidi kwenye ngozi, na kuifunika ngozi ya mtu kwa ugonjwa tangu kichwani pake hata miguuni, maadamu anajitokeza kwa kuhani,
\v 13 naye kuhani atamchunguza ili kuona kama huo ugonjwa umeshaenea mwili wake wote. Ikiwa imetokeo hivyo, kuhani atamtangaza mtu huyo aliye na ugonjwa kuwa ni safi. Ikiwa amebadilika kuwa mweupe, huyo ni safi.
\v 14 Lakini ikiwa nyama mbichi imeonekana juu yake, atakuwa najisi.
\s5
\v 15 Kuhani ataiangalia hiyo nyama mbichi na kumtanga kuwa najisi kwa sababu hiyo nyama mbichi ni najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\v 16 Lakini endapo hiyo nyama mbichi inageuka kuwa nyeupe tena, naye huyo mtu hana budi kwenda kwa kuhani.
\v 17 Kuhani atamchunguza ili kuona kama hiyo nyama imebadilika kuwa nyeupe. Kama imekuwa hivyo naye kuhani atatangaza kwamba mtu huyo kuwa ni safi.
\s5
\v 18 Mtu anapokuwa na jipu juu yangozi yake na limishapona,
\v 19 na mahali pa jipu pamekuwa na uvimbe au doa lenye kung'aa, wekundu unaochanganyikana na weupe, yapasa kuonyeshwa kwa kuhani.
\v 20 Naye kuhani atalichunguza ili kuona kama linaonekana limekwenda chini ya ngozi, na kama hizo malaika zimebadilika kuwa nyeupe, kama ni hivyo, kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza, endapo utakuwa umezalishwa mahali lilipokuwa jipu hilo.
\s5
\v 21 Lakini endapo kuhani atakuwa amelichunguza na haoni malaika nyeupe ndani yake, na kwamba iliko chini ya ngozi bali limefifia, kisha kuhani atamtenga kwa siku saba.
\v 22 Kama linaenea kwa kupanuka kwenye ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\v 23 Lakini kama hilo doa lenye kung'ara linabaki mahali pake na halijasambaa, basi hilo ni kovu la jipu, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
\s5
\v 24 Ngozi inapoungua na nyama mbichi ya inamekuwa na wekundu uliochanganyika na weupe au doa jeupe,
\v 25 kisha kuhani ataichunguza kuona kama malaika zilizoko kwenye doa hilo zimebadilika na kuwa nyeupe, na kama limeonekana kwenda chini zaidi ya ngozi, kama limekuwa hivyo, basi huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Umejitokeza kwenye jeraha la moto, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
\s5
\v 26 Lakini endapo kuahani analichunguza na naona kwamba hakuna malaika nyeupe kwenye doa, na kwamba halikuenda chini ya ngozi bali linafifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.
\v 27 Kisha yapasa kuahani kumchunguza tena katika siku ya saba. Iwapo litakuwa limesambaa kwa upana kwenye ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugojwa wa kuambukiza.
\v 28 Iwapo hilo doa lisalia mahali pake na halitakuwa limesambaa kwenye ngozi bali limefifia, ni uvimbe tu kutokana na kuungua moto, naye kuhani atamtangaza kuwa safi, kwa kuwa siyo zaidi ya jeraha la kuungua.
\s5
\v 29 Iwapo mwanaume au mwanamke ana ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni pake,
\v 30 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo kwa ajili ya ugonjwa wa kuambukiza ili kuona kama unakwenda ndani zaidi ya ngozi, na kama kuna nywele za manjano, nyembamba ndani yake. endapo zinaonekana, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni mwasho, ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni.
\s5
\v 31 Iwapo kuhani anachunguza ugonjwa wa mwasho na anagundu kuwa hauko chini ya ngozi, na kama hakuna nywele nyeusi ndani yake, kisha kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
\s5
\v 32 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena huo ugonjwa ili kuona kama umesambaa, Endapo hakuna malaika za manjano, na iwapo ugonjwa uko usawa ngozi tu,
\v 33 basi, yapasa mtu huyo kunyolewa., lakini sehemu yenye ugonjwa haitanyolewa, naye kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.
\s5
\v 34 Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena ugonjwa ili kuona kama umacha kusambaa ndani ya ngozi. Iwapo unaonekana kuwa hukwenda chini zaidi ya ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa safi. Mtu huyo yapasa kufua nguo zake, na kisha atakuwa safi.
\s5
\v 35 Lakini ikiwa ugonjwa wa mwasho umeenea kwa sehemu kubwa kwenye ngozi baada ya kuhani kutangaza kuwa alikuwa safi,
\v 36 naye kuhani itabidi amchunguze tena. Iwapo ugonjwa utakuwa umesambaa katika ngozi, kuhani hahitajiki kutafuta nywele za manjano. Mtu huyo ni najisi.
\v 37 Lakini iwapo katika mtazamo wa kuhani inaonekana kuwa huo ugonjwa wa mwasho umekoma kusambaa, basi huo ugonjwa umekwisha pona. Yeye ni safi, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
\s5
\v 38 Iwapo mwanume au mwanamke ana madoa juu ya ngozi,
\v 39 kisha kuhani atamchunguza mtu huyo ili kuona kama hayo madoa ni meupe kwa kufiifia, ambalo ni kovu tu lililojitokeza kwenye ngozi. Yeye yu safi.
\s5
\v 40 Iwapo nywele za mtu zimenyonyoka kichwani, yeye ni kipara lakini yu safi.
\v 41 Na iwapo nywele zake zimenyonyoka upande wa mbele wa kichwa chake, na iwapo paji lake la uso lina kipara, yeye yu safi.
\s5
\v 42 Lakini endapo kuna kidonda chenye wekundu uliochanganyika na weupe, juu ya kipara chake au paji lake la uso, huo ni ugonjwa wa kuambukiza uliojitokeza.
\v 43 Naye kuhani atamchunguza ili kuona iwapo uvimbe wa eneo linaugua juu ya upara wake au paji lake la uso lina wekundu uliochanganyika na weupe, kama kuonekana kwa ugonjwa wa kuambukiza kwenye ngozi.
\v 44 Ikionekana hivyo, basi huyo ana ugonjwa wa kuambukiza naye ni najisi. Hakika kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya ugonjwa wake kichwani pake.
\s5
\v 45 Mtu aliye na ugojwa wa kuambukiza atavaa nguo zilizochanika, ni lazima nywele zake ziachwe wazi, na yampasa kufunika uso wake mpaka puani na kupiga kelele, 'Najisi, najisi.'
\v 46 Naye atakuwa najisi siku zote za ugonjwa wake wa kuambukiza. Kwa sababu anao ugonjwa unaosambaa, yapasa kuishi peke yake nje ya kambi.
\s5
\v 47 Kuna wakati fulani vazi la mtu hupata ukungu juu yake. Laweza kuwa vazi, ama la sufu au kitani,
\v 48 au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi.
\v 49 Iwapo sehemu iliyochafuliwa ina rangi ya kijani au nyekundu katika vazi, ngozi, kifaa kilichosukwa au kufumwa, basi huo ni ukungu uanasambaa, ni lazima uonyeshwe kwa kuhani.
\s5
\v 50 Yapasa kuhani akichunguze hicho kifaa kwa ajili ya ukungu; ni lazima akitenge kitu chochote kilicho na ukungu kwa siku saba.
\v 51 Naye atauchunguza tena huo ukungu katika siku ya saba. Endapo utakuwa umesambaa katika kifaa hicho, basi ni wazi kwamba huo ni ukungu wenye kuangamiza, na hicho kifaa ni najisi.
\v 52 Na mwenye kukimiliki atalazimika kukichoma na kukiteketeza kabisa hicho kifaa kilichoonekana na ukungu ndani yake, haijalishi kiwe ni kifaa cha aina gani, kwani huo ukungu unaweza kusababisha ugonjwa.
\s5
\v 53 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa na kuona kwamba ukungu haujaenea kwenye vazi au chombo kilichosukwa au kusokotwa kutokana na sufu, kitani au ngozi,
\v 54 basi atawaagiza wakisafishe hicho kifaa kilichopatikana na ukungu, naye yampasa kukitenga kwa siku saba zaidi.
\v 55 Kisha kuhani atakichunguza tena hicho kifaa chenye ukungu baada ya kuwa kimesafinshwa. Kama ukungu haukubadilika rangi yake, hata kama haukusambaa, kifaa hicho ni najisi. Yapasa kichomwe, haijalishi ni wapi ukungu huo utakuwa umekichafua.
\s5
\v 56 Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa, na kama ukungu umefifia baada ya kuwa umeoshwa, basi atakirarua kile kipande kilichochaufuliwa kutoka kwenye vazi au kutoka kwenye ngozi, au kutoka kwenye chombo kilichosukwa au kusokotwa.
\v 57 Ikiwa ukungu unazidi kuonekana katika vazi, ama katika chombo kilichosukwa au kufumwa, au katika kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi, basi, ukungu utakuwa unasambaa. Kifaa chochote kilicho na ukungu ni lazima kichomwe.
\v 58 Vazi au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi—iwapo unakisafisha kifaa nao ukungu ukawa umetoka, nacho kifaa lazima kisafishwe mara ya pili, kisha kitakuwa safi.
\s5
\v 59 Hii ndiyo sheria ihusuyo ukungu katika vazi la sufu au kitani, au kwenye kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au kitu chochote kilichotengenewa kwa ngozi, ili kwamba mweze kuvitangaza kuwa safi au najisi.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Yahwe alizungumza na Musa, akisema,
\v 2 "Hii itakuwa sheria kwaajili ya mtu aliyekufa kwenye siku ya utakaso. Lazima aletwe kwa kuhani.
\s5
\v 3 Kuhani atakwenda nje ya kambi kumchunguza mtu kuona kama madhara ya ugonjwa wa ngozi yameponywa.
\v 4 Ndipo kuhani ataamuru kwamba mtu mwenye kutakaswa lazima achukue ndege safi wawili, waliohai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.
\v 5 Kuhani atamwamuru kuua moja ya hao ndege juu ya maji safi yaliyo kwenye chungu cha udongo.
\s5
\v 6 Ndipo kuhani atamchukua ndege aliyehai na mti wa mwerezi, na kitani nyekundu na hisopo, na vyote hivi, pamoja na ndege aliyehai atavichovya kwenye damu ya ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi.
\v 7 Ndipo kuhani atanyunyiza maji haya mara saba juu ya mtu anayetakaswa katika ugonjwa, na ndipo kuhani atamtangaza kuwa msafi. Ndipo kuhani atamwachia ndege aliyehai katika eneo wazi.
\s5
\v 8 Mtu aliyetakaswa atafua nguo zake, atanyoa nywele zake zote, ataoga kwa maji, na ndipo atakuwa safi. Baada ya hayo lazima aje kwenye kambi, lakini ataishi nje ya hema lake kwa siku saba.
\v 9 Katika siku ya saba lazima anyoe nywele za kichwa chake, na lazima pia anyoe ndevu zake na nyusi. Lazima anyoe nywele zake zote, na lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji; ndipo atakuwa safi.
\s5
\v 10 Katika siku ya nane lazima achukue dume wa wana kondoo wawili wasio na lawama, mwana kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na lawama, na tatu ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa mafuta kama sadaka ya nafaka, na kipimo kimoja cha mafuta.
\v 11 Kuhani ambaye amemtakasa mtu atamsimamisha mtu ambaye aliyemtakasa, pamoja na vile vitu, mbele ya Yahwe mahali pa kuingilia kwenye hema ya mkutano.
\s5
\v 12 Kuhani atachukua mmoja wa wanakondoo dume na kumtoa kama sadaka ya hatia, pamoja na kipimo cha mafuta; atavitikisa kwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Yahwe.
\v 13 Lazima aue mwana kondoo dume mahali ambapo wanapochinjia sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, katika eneo la hema, sababu sadaka ya dhambi ni ya kuhani, kama afanyavyo sadaka ya hatia, kwasababu ni takatifu zaidi.
\s5
\v 14 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu yule wa kutakaswa, katika dole gumba la kulia, katika dole la mguu wa kulia.
\v 15 Ndipo kuhani atachukua mafuta kutoka chombo na kuyamimina katika kiganja cha mkono wake wa kushoto, na kuzamisha kidole chake katika mafuta hayo yaliyo kwenye mkono wa kushoto,
\v 16 na kunyunyiza baadhi ya mafuta kwa kidole mara saba mbele za Yahwe.
\s5
\v 17 kuhani ataweka mafuta yaliyobaki kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu wa kutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wa kulia, na katika dole kubwa la mguu wa kulia. Lazima aweke mafuta haya juu ya damu kutoka kwenye sadaka ya hatia.
\v 18 Kama kwa mafuta yaliyosalia kwamba katika mkono wa kuhani, atayaweka juu ya kichwa cha mtu ambaye atakaswaye, na kuhani atafanya utakaso kwaajili yake mbele za Yahwe.
\s5
\v 19 Ndipo kuhani atatoa sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwaajili yake atakaswaye kwa sababu ya kutokuwa safi kwake, na badaye ataua sadaka ya kuchomwa.
\v 20 Ndipo kuhani atatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya mtu huyo, na ndipo atakuwa safi.
\s5
\v 21 Kwa namna hiyo, kama mtu ni masikini na hawezi kumudu matoleo haya, ndipo anaweza kuchukua kondoo mmoja dume kama sadaka ya hatia ya kutikiswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe, na moja ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, na chombo cha mafuta,
\v 22 pamoja na njiwa wawili au kinda mbili za njiwa, ambao anaweza kupata; ndege mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na mwingine sadaka ya kuteketezwa.
\v 23 Katika siku ya nane lazima awalete kwa kuhani kwaajili ya utakaso, pakuigilia katika hema ya mkutano, mbele ya Yahwe.
\s5
\v 24 Kuhani atachukua mwana kondoo kwaajili ya sadaka, na atachukua pamoja na kiasi cha mafuta ya mzeituni, na ataviinua juu kama anaviwasilisha kwa Yahwe.
\v 25 Atamuua mwana kondoo kwaajili ya sadaka ya hatia, na atachukua baadhi ya ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka juu ya ncha ya sikio la kulia la yule wakutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye dole kubwa la mguu, wa kulia.
\s5
\v 26 Ndipo kuhani atamimina baadhi ya mafuta katika kiganja cha mkono wake wa kushoto,
\v 27 na atanyunyiza kwa kidole chake cha kulia baadhi ya mafuta ambayo yako kwenye mkono wa kushoto mara saba mbele za Yahwe.
\s5
\v 28 Ndipo kuhani ataweka kiasi cha mafuta ambayo yako kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la yule mtu wa kutakaswa, katika dole gumba lake la mkono wa kulia, na dole kubwa la mguu wa kulia, maeneo yale yale ambayo kaweka damu ya sadaka ya hatia.
\v 29 Ataweka mafuta yaliyobaki yaliyo mkononi mwake juu ya yule wakutakaswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe.
\s5
\v 30 Lazima atoe sadaka ya njiwa au makinda ya njiwa, yale ambayo mtu ameweza kupata -
\v 31 moja kama ya sadaka ya dhambi na nyingine kama sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya yule ambaye atatakaswa mbele za Yahwe.
\v 32 Hii ni sheria kwaajili ya mtu kwake kuna athari za ugonjwa wa ngozi, ambaye hawezi kumudu kiwango cha sadaka kwaajili ya utakaso wake."
\s5
\v 33 Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
\v 34 "Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,
\v 35 ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme 'Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.' "
\s5
\v 36 Ndipo kuhani ataamuru kwamba watoe vitu vyote ndani kabla hajaenda ndani kuona uthibitisho wa ukungu, kiasi kwamba hakuna ndani ya nyumba kitakachofanywa najisi. Badaye kuhani lazima aende ndani kuona humo ndani.
\v 37 Yeye lazima achunguze ukungu kuona kama umo katika kuta za nyumba, na kuona ikiwa kunaonekana ukijani au wekundu katika bonde za mwonekano wa kuta.
\v 38 Kama nyumba inao ukungu, ndipo kuhani atatoka nje ya nyuma na kufunga mlango wa nyumba kwa siku saba.
\s5
\v 39 Ndipo kuhani atarudi tena katika siku ya saba na kuichunguza kuona kama ukungu umeenea katika kuta za nyumba.
\v 40 Kama hivyo, ndipo kuhani ataamuru kwamba wayaondoe mawe ambayo ukungu umepatikana na yatupwe katika sehemu najisi nje ya mji.
\s5
\v 41 Yeye atataka kuta zote za ndani ya nyumba zikwanguliwe, na lazima achukue vitu vilivyochafuliwa na hivyo vilivyokwanguliwa nje ya mji na kuvitupa kwenye eneo lisilosafi.
\v 42 Lazima wayachukue mawe mengine na kuyaweka katika sehemu ya mawe yaliyoondolewa, na lazima watumie udongo mpya kupigia lipu nyumba.
\s5
\v 43 Kama ukungu unakuja tena na unaingia katika nyumba ambayo mawe yameondolewa na kuta zimekwanguliwa na kupigwa lipu upya,
\v 44 ndipo kuhani lazima aje aingie ndani na kuchunguza nyumba kuona kama ukungu umeenea ndani ya nyumba. Kama hivyo, huo ni ukungu mbaya, na nyumba ni najisi.
\s5
\v 45 Nyumba hiyo lazima iangushwe chini. Hayo mawe, mbao, na lipu yote ndani ya nyumba lazima vibebwe kupelekwa nje ya mji kwenye sehemu najisi.
\v 46 Kwa nyongeza, yeyote anaenda ndani ya nyumba wakati imefungwa atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 47 Na yeyote aliyelala ndani ya nyumba lazima afue nguo zake, na yeyote aliyekula ndani ya nyumba lazima afue nguo zake.
\s5
\v 48 Kama kuhani akaingia hiyo kuichunguza kuona ikiwa ukungu umeenea katika nyumba baada ya nyumba kupigwa lipu, ndipo, kama ukungu umetoweka, ataitangaza nyumba hiyo kuwa ni safi.
\s5
\v 49 Ndipo kuhani lazima achukue ndege wawili kuitakasa nyumba, na mti wa mwelezi, na sufu nyekundu, na hisopo.
\v 50 Atamuua ndege mmojawapo katika maji masafi kwenye dumu la udongo.
\v 51 Atachukua mti wa mwerezi, hisopo, sufu nyekundu na ndege aliyehai, na kuvichovya kwenye damu ya ndege aliyekufa, kwenye maji safi, na kunyunyizia nyumba mara saba.
\s5
\v 52 Ataitakasa nyumba kwa damu ya ndege na maji safi, pamoja na ndege aliyehai, mti wa mwerezi, hisopo, na sufu nyekundu. Lakini atamwachia ndege aliyehai aende nje ya mji mashambani.
\v 53 Kwa njia hii lazima afanye upatanisho kwaajili ya nyumba, na itakuwa safi.
\s5
\v 54 Hii ni sheria kwa aina zote za athari ya ugonjwa wa ngozi na vitu vyote vinavyosababisha ugonjwa kama huo, na kwaajili ya kuwashwa,
\v 55 na kwa ukungu kwenye mavazi na nyumba,
\v 56 kwaajili ya uvimbe, kwaajili ya vipele, madoa,
\v 57 kutambua wakati wowote tatizo hili ni najisi au lini limetakaswa. Hii ni sheria kwaajili ya athari za ugonjwa wa ukungu.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
\v 2 "Waambie watu wa Israeli, na sema kwao, 'Wakati mtu yeyote kisonono kimemwathiri mwili wake unatoa ugiligili, anakuwa najisi.
\v 3 Unajisi wake unatokana na athari ya kisonono. Iwe mwili wake unatoa ugiligili au umekoma, huo ni unajisi."
\s5
\v 4 Kitanda chochote anachokilalia kitakuwa najisi, na kila kitu ambacho anakaa juu yake kitakuwa najisi.
\v 5 Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na awe amenajisika mpaka jioni.
\s5
\v 6 Yeyote anayekaa katika kitu chochote ambacho mtu ambaye ameathiriwa na kisonono alikaa, mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 7 Na yeyote anayegusa mwili wa ambaye ameathirika na kisonono lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na awe najisi hadi jioni.
\s5
\v 8 Kama mtu ambaye anaona majimaji kama hayo kwa mtu fulani ambaye ametakasika, ndipo mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na atakuwa najisi hata jioni.
\v 9 Tandiko lolote ambalo ambaye anamajimaji ya kisonono atalikalia litakuwa najisi.
\s5
\v 10 Yeyote anayegusa kitu chochote kilichokuwa chini ya mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni, na yeyote anayebeba vitu hivyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji; atanajisika mpaka jioni.
\v 11 Ambaye anamajimaji kama hayo akimgusa kabla kwanza ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 12 Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.
\s5
\v 13 Wakati mwenye kisonono anapotakaswa katika kisonono chake, ndipo lazima ahesabu kwaajili yake siku saba kwaajili ya kutakasika kwake; ndipo afue nguo na aoshe mwili wake kwenye maji yatiririkayo. Ndipo atakuwa safi.
\v 14 Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.
\v 15 Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe kwaajili ya kisonono chake.
\s5
\v 16 Kama mtu yeyote ametokwa na shahawa, ndipo lazima aoge mwili wake wote katika maji; atanajisika mpaka jioni.
\v 17 Kila vazi au ngozi ambayo juu yake kuna shahawa lazama paoshwe kwa maji; itakuwa najisi mpaka jioni.
\v 18 Na kama mwanamke na mwanaume watalala pamoja na kunakutokwa kwa shahawa kwenda kwa mwanamke, lazima wote wawili waoge katika maji; watakuwa najisi mpaka jioni.
\s5
\v 19 Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 20 Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
\s5
\v 21 Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 22 Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
\v 23 Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
\s5
\v 24 Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.
\s5
\v 25 Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.
\v 26 Kila kitanda anachokilalia wakati wote wa kutokwa damu itakuwa kwake sawa tu kama kitanda anacholalia wakati wa hedhi, na kila kitu ambacho anakalia kitakuwa najisi, kama tu unajisi wa hedhi yake.
\v 27 Na yeyote anayegusa kitu kati ya vitu hivyo atakuwa najisi; lazima yeye afue nguo zake na aoge mwenyewe kwenye maji, na atakuwa amenajisika mpaka jioni.
\s5
\v 28 Lakini kama mwanamke ametakasika katika kutokwa na damu, ndipo atahesabu kwaajili yake siku saba, baada ya hizo atakuwa safi.
\v 29 Katika siku ya nane atachukua kwake njiwa wawili au kinda wawili wa njiwa na atawaleta kwa kuhani pakuingilia hema ya mkutano.
\v 30 Huyo kuhani atatoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa, na atafanya upatanisho kwaajili ya huyo mbele ya Yahwe kwaajili unajisi wa mwanamke atokwaye damu.
\s5
\v 31 Hivi ndivyo lazima uwatenge watu wa Israeli katika unajisi wao, hivyo hawatakufa tokana na unajisi wao, kwa kuchafua hema langu, ambapo naishi kati yao.
\s5
\v 32 Huu ndio utaratibu kwa kila ambaye anakisonono, kwaajili kila mwanaume ambaye shahawa yake inatoka na inamfanya kuwa najisi,
\v 33 kwaajili ya mwanamke ambaye yuko katika kipindi cha hedhi, kwaajili ya yeyote aliye na kisonono, awe mwanaume au mwanamke, na kwaajili ya yeyote anayelala na mwanamke najisi.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Yahwe alizungumza na Musa - hii ni baada vifo vya wana wawili wa Haruni, walipomkaribia Yahwe na ndipo wakafa.
\v 2 Yahwe alimwambia Musa, "Ongea na Haruni kaka yako na umwambie hapana kuja tu wakati wowote katika patakatifu pa patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kifuniko cha upatanisho kilicho juu ya sanduku. Akifanya hivyo, anakufa, kwasababu naonekana katika wingu juu ya kifuniko cha upatanisho.
\s5
\v 3 Hivi ndivyo jinsi Haruni lazima aje katika patakatifu pa patakatifu. Yeye lazima aingie pamoja na ndama kama sadaka ya dhambi, na kondoo dume kama sadaka ya dhambi.
\v 4 Ni lazima avae kanzu ya kitatani, na lazima avae ndani yake nguo ya kitani, na lazima avae mshipi wa kitani na kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu. Lazima aoge mwili wake katika maji na avae mavazi haya.
\v 5 Lazima achukue kwenye umati wa watu wa Israeli mbuzi wawili waume kama sadaka ya dhambi na kondoo dume moja ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa.
\s5
\v 6 Ndipo Haruni lazima alete ng'ombe kama sadaka ya dhambi, ambayo itakuwa kwaajili yake mwenyewe, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na familia yake.
\v 7 Ndipo lazima achukue mbuzi wawili na kuwaweka mbele ya Yahwe katika mlango wa kuingilia kwenye hema ya mkutano.
\s5
\v 8 Ndipo Haruni lazima apige kura kwaajili ya mbuzi hao wawili, kura moja kwaajili ya Yahwe, na kura nyingine kwaajili ya msingiziwa.
\v 9 Ndipo Haruni lazima awasilishe mbuzi ambaye kura imeangukia kwa Yahwe, na kumtoa mbuzi huyo kama sadaka ya dhambi.
\v 10 Lakini mbuzi ambaye kura ya usingiziwa imemwangukia lazima aletwe kwa Yahwe akiwa hai, kufanya upatanisho kwa kumwachia aende porini kama, mbuzimsingiziwa.
\s5
\v 11 Pia Haruni lazima alete ng'ombe kwaajili ya sadaka ya dhambi, ambayo itakuwa kwaajili yake mwenyewe, lazima afanye upatanisho kwaajili yake mwenyewe na familia yake, hivyo lazima yeye amuue huyo ng'ombe kama sadaka ya dhambi kwaajili yake mwenyewe.
\s5
\v 12 Haruni lazima achukue chetezo iliyojaa mkaa wa moto kutoka kwenye madhabahu mbele ya Yahwe, na mikono imejaa ubani mzuri, na kuleta vitu hivi ndani ya pazia.
\v 13 Hapo lazima aweke ubani juu ya moto mbele za Yahwe ili kwamba wingu kutoka kwenye ubani liweze kufunika kifuniko cha agano la imani ya upatanisho. Yeye afanye hivyo ili kwamba asife.
\s5
\v 14 Ndipo lazima achukue kiasi cha damu ya ng'ombe na kuinyunyiza kwa kidole chake mbele ya kifuniko cha upatanisho. Lazima anyunyize kiasi cha damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kifuniko cha upatanisho.
\s5
\v 15 Ndipo lazima aue mbuzi kwaajili ya sadaka ya dhambi ambayo ni kwaajili ya watu na kuileta damu yake ndani kwenye pazi. Hapo lazima aifanyie damu kama alivyofanya kwenye damu ya fahali: lazima ainyunyize juu ya kifuniko cha upatanisho na mbele ya kifunuko cha upatanisho.
\v 16 Yeye lazima afanye upatanisho kwaajili ya mahali patakatifu kwa sababu ya matendo ya unajisi ya watu wa Israeli, na kwa sababu ya uasi na dhambi zao zote. Yeye pia lazima afanye haya kwaajili ya hema ya mkutano, ambapo Yahwe anaishi kati yao, katika uwepo wa matendo yao ya unajisi.
\s5
\v 17 Hakuna mtu anayetakiwa kuwepo katika hema ya mkutano wakati Haruni anaingia kufanya upatanisho katika mahali patakatifu pa patakatifu, na mpaka atoke nje na amemaliza kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na kwaajili ya familia yake, na kwaajili umati wa Israeli.
\v 18 Yeye lazima aende nje kwenye madhabahu hapo mbele za Yahwe na kufanya upatanisho kwaajili ya hiyo, na lazima achukue kiasi cha damu ya mbuzi na kuiweka juu ya pembe za madhabahu yote kuzunguka.
\v 19 Anatakiwa anyunyize kiasi cha damu juu yake kwa kidole chake mara saba kuitakasa na kuitenga maalumu kwa Yahwe, mbali kutoka matendo ya unajisi wa watu wa Israeli.
\s5
\v 20 Atakapo maliza kupatanisha kwaajili ya mahali patakatifu sana, hema la mkutano, na madhabahu, lazima amlete mbuzi aliyehai.
\v 21 Haruni lazima aweke mikono yake yote juu ya kichwa cha mbuzi huyu aliyehai na akiri juu yake maovu yote ya watu wa Israeli, uasi wao wote, dhambi zao zote. Ndipo lazima aweke dhambi hizo juu ya kichwa cha mbuzi na amwachie katika uangalizi wa mtu aliyetari kumwongoza mbuzi huyo porini.
\v 22 Mbuzi lazima abebe juu yake mwenyewe uovu wote kwenda mahali pakiwa. Kule msituni, huyo mtu amwache mbuzi aende huru.
\s5
\v 23 Ndipo Haruni anapaswa kwenda tena humo kwenye hema ya mkutano na kuvua mavazi ya kitani ambayo amayavaa kabla hajaenda mahali patakatifu sana, na anatakiwa kuyaacha mavazi hayo pale.
\v 24 Anapaswa aoshe mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na avae nguo zake za kawaida; pia lazima atoke nje kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa kwaajili ya wale watu, na kwa njia hii anafanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe na kwaajili ya watu.
\s5
\v 25 Lazima yeye achome mafuta ya sadaka ya dhambi juu ya madhabahu.
\v 26 Huyu mtu anayemwacha mbuzi msingiziwa aende huru anafua nguo zake na kuosha mwili wake katika maji; baada ya hayo, anaweza kurudi tena kambini.
\s5
\v 27 Yule fahali kwaajili ya sadaka ya dhambi na mbuzi kwaajili ya sadaka za dhambi, ambaye damu yake ililetwa kufanya upatanisho katika mahali patakatifu, lazima ipelekwe nje ya kambi. kule lazima wachome, ngozi zao, nyama yao na kinyesi chao.
\v 28 Huyu anayechoma sehemu hizo lazima afue nguo zake na aoge mwili wake katika maji; baada ya hapo, anaweza kurudi tena kwenye kambi.
\s5
\v 29 Hii itakuwa sharti kwaajili yenu kwamba katika mwezi wa saba, kwenye siku ya kumi ya mwezi, mtanyenyekea wenyewe na msifanye kazi, iwe mwenyeji wa kuzaliwa au mgeni anayeishi kati yenu.
\v 30 Hii ni kwasababu katika siku hii ya upatanisho utafanywa kwaajili yenu, kuwatakasa ninyi kutoka dhambi zenu zote ili mwe safi mbele za Yahwe.
\v 31 Hii ni maalumu kwa Sabato ya kupumzika kwaajili yenu, na lazima mnyenyekee wenyewe na msifanye kazi. Hili litakuwa sharti kati yenu.
\s5
\v 32 Kuhani mkuu, ambaye atapakwa mafuta na kuwekwa wakfu kuwa kuhani mkuu katika nafasi ya baba yake, lazima afanye upatanisho huu na kuvaa mavazi ya kitani, hayo ni mavazi matakatifu.
\v 33 Lazima afanye upatanisho kwaajili ya mahali patakatifu sana; lazima afanye upatanisho kwaajili ya hema ya mkutano na madhabahu, na lazima afanye upatanisho kwaajili ya makuhani na kwaajili ya kusanyiko la watu.
\s5
\v 34 Hii daima itakuwa sharti kwaajili yako, kufanya upatanisho kwaajili ya watu wa Israeli kwasababu ya dhambi zao zote, mara moja kwa kila mwaka." Na ilikuwa ikifanika kama Yahwe alivyomwamuru Musa.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa,
\v 2 "Zungumza na Aroni na wanawe, na watu wote wa Israeli. Waambie mambo ambayo ameamru Yahweh:
\v 3 Mtu yeyote wa Isreli anayeua fahali au mwana—kondoo au mbuzi kambini, au amuuaye nje ya kambi, ili kumtoa dhabihu—
\v 4 kama hamleti katika ingilio la hema la kukutania ili kumtoa dhabihu kwa Yahweh mbele za hema lake la kukutania, mtu huyo ana hatia ya damu iliyomwagika. Amemwaga damu, na mtu huyo ni sharti akatiliwe mabali kutoka miongoni mwa watu wake.
\s5
\v 5 Kusudi la amri hii ni kwamba watu wa Israeli wataleta dhabihu zao kwa Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania, watazileta kwa kuhani ziweze kutolewa kuwa matoleo ya shukrani kwa Yahweh, badala ya kutoa dhabihu hadharani katika shamba.
\v 6 Kuhani atainyunyiza damu juu ya madhabahu ya Yahweh kwenye ingilio la hema la kukutania; atayachoma mafuta yake ili kutoa harufu ya kupendeza mbele za Yahweh.
\s5
\v 7 Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.
\s5
\v 8 Ni lazima uwaambie, 'Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atoweye dhabihu
\v 9 na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'
\s5
\v 10 Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
\v 11 Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake. Nimeitoa damu yake kwenu kufanya upatanisho juu ya madhabahu kwa ajili ya uhai wenu, kwa sababu ni damu ndiyo ifanyayo upatanisho, kwa kuwa ni damu ipatanishayo kwa ajili ya uhai
\s5
\v 12 Kwa hiyo Niliwaambia Watu wa Israeli kwamba hayupo miongoni mwenu impasaye kula damu, wala yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu atakaye kula damu.
\v 13 Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mafumbi.
\s5
\v 14 Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyeote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.
\s5
\v 15 Mtu yeyote alaye mnyama aliyekufa au ambaye amelaruliwa na wanyama pori, ama yule mtu ni mwenyeji wa kuzaliwa au ni mgeni aishiye miongoni mwenu, ni lazima atazifua nguo zake na kujiosha katika maji, naye atakuwa najisi hata jioni. Kisha atakuwa safi.
\v 16 Lakini kama hazifui nguo zake au kuosha mwili wake, ni lazima aichukue hatia yake".
\s5
\c 18
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, "Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 3 Msitende mambo ambayo watu wa Misri huyatenda, mahali mlikokuwa mkiishi awali. Na ni lazima msitende mambo yale wanayoyatenda watu wa Kanaani, nchi ambayo ninawapeleka nyinyi. Msifuate desturi zao.
\s5
\v 4 Sheria zangu ndizo mtakazozitenda, na amri zangu ndizo mtakazozishika, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 5 Kwa hiyo ni lazima mzitunze hukumu zangu na sheria zangu. Ikiwa mtu amezitii, ataishi kwa sababu ya hizo. Mimi Ndimi Yahweh.
\s5
\v 6 Pasiwepo kwenu atakayelala na yeyote aliye na uhusiano wa karibu naye. Mimi ndimi Yahweh.
\v 7 Usimfedheheshe baba yako kwa kulala na mama yako. Yeye ni mama yako! Haikupasi kumfedhehesha yeye.
\v 8 Usilale na yeyote wa wake za baba yako; Usimfedheheshe namna hiyo baba yako.
\s5
\v 9 Usilale na yeyote aliye mmoja miongoni mwa dada zako, ama ni binti ya baba yako au ni binti ya mama yako, ama aliyelelewa nyumbani mwenu au mbali nawe. Usilale na dada zako.
\v 10 Usilale na binti ya mwanao, au binti ya binti yako. Hiyo ingekuwa aibu yako mwenyewe.
\v 11 Usilale na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa kwa baba yako, yeye ni dada yako, na usilale naye.
\s5
\v 12 Usilale na dada ya baba yako. Yeye ni ndugu wa karibu kwa baba yako.
\v 13 Usilale na dada ya mama yako. Yeye ni ndugu wa mama yako.
\v 14 Usimfedheheshe ndug wa baba yako kwa kulala na mke wake. Usimkaribie kwa kusudi hilo; yeye ni shangazi yako.
\s5
\v 15 Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.
\v 16 Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.
\s5
\v 17 Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.
\v 18 Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.
\s5
\v 19 Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.
\v 20 Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jilani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.
\s5
\v 21 Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 22 Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.
\v 23 Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama ye yote. Huo ungekuwa upotovu.
\s5
\v 24 Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.
\v 25 Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake
\s5
\v 26 Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagiza yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.
\v 27 Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.
\v 28 Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.
\s5
\v 29 Yeyote anayefanya mambo haya ya kuchukiza, watu wafanyao mambo hayo ya kuchukiza lazima watakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu wao.
\v 30 Kw a hiyo inawapasa kuzishika amri zangu na sitende mojawapo ya desturi hizi zenyekuchukiza ambazo zilitendwa hapo kabla yenu, ili msijinajisi wenyewe kwa hizo. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akisema.
\v 2 Zungumza na kusanyiko lote la watu wa Israeli na uwaambie, 'Ni lazima muwe watakatifu, kwa kuwa mimi Yahweh Mungu wenu ni mtakatifu.
\v 3 Kila mtu amstahi mama yake na baba yake. Na ni lazima muzishike Sabato zangu. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 4 Msizigeukie sanamu zisizo na thamani, wala kujitengenezea wenyewe miungu kutokana na chuma. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 5 Unapotoa dhabihu za sadaka ya ushirika kwa Yahweh, utatoa ili kupata kibali.
\v 6 Ni sharti iliwe siku hiyo hiyo uliyoitoa, au siku inayofuata.
\v 7 Kama kinabaki kitu cho chote hata siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. Kama kitaliwa katika siku ya tatu kitakuwa najisi. Hakitakubalika,
\v 8 lakini kila akilaye ni lazima atachukua hatia yake kwa sababu amekivunjia heshima kilicho kitakatifu kwa Yahweh. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
\s5
\v 9 Unapovuna mavuno ya ardhi yako, usivune hata pembezo mwa shamba lako kabisa, wala hutakusanya mabaki ya mavuno yako yote.
\v 10 Usikusanye kila zabibu kutoka katika mizabibu yako, wala usiziokote dhabibu zilizoanguka chini katika shamba la mizabibu. Ni lazima uziache kwa ajili ya masikini na kwa ajili ya wageni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
\s5
\v 11 Usiibe. Usiseme uongo. Msidanganyane.
\v 12 Usiape kwa jina langu kwa uongo na kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh
\s5
\v 13 Usimgandamize jirani yako wala kumwibia. Usishikilie malipo ya kibarua usiku kucha hata asubuhi.
\v 14 Usimlaani kiziwi au kuweka kikwazo mbele ya kipofu. Badala yake, yakupasa umwogope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 15 Usisababishe hukumu ikawa ya uongo. Usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni masikini na usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni mtu muhimu. Badala yake, amua juu ya jirani yako kwa haki.
\v 16 Usiende huku na huko ukisema habari za uchochezi miongoni mwa watu wako, bali tafuta kuyalinda maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 17 Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Mkemee jirani yako kwa heshima ili kwamba usishiriki katika dhambi kwa sababu yake.
\v 18 Usijilipize kisasi au kuwa na chuki yoyote dhidi ya mtu yeyote wa watu wako, lakini badala yake mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 19 Shika amri zangu. Usiwazalishe wanyama wako kwa kutumia wanyama wa aina nyingine tofauti. Usichanganye aina mbili tofauti za mbegu unapopanda shamba lako. Usivae vazi lililofumwa kwa kutumia nyuzi za rangi mbili tofauti zilizochanganywa pamoja.
\s5
\v 20 Yeyote anayelala na msichana mtumwa aliyeposwa na mume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa au hajaachwa huru, lazima waadhibiwe. Hawatauawa kwa sababu yule msichana hakuwa huru.
\v 21 Ni lazima mtu huyo alete sadaka yake ya hatia kwenye ingilio la hema la kukutania—kondoo dume iwe sadaka ya hatia.
\v 22 Kisha kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kandoo dume mbele za Yahweh kutokana na dhambi aliyoitenda. Nayo dhambi iliyotendwa itasamehewa.
\s5
\v 23 Mtakapoingia katika nchi na kupanda aina zote za miti kwa chakula, kisha mtayahesabu matunda yatakayozaliwa kuwa yamekatazwa kuliwa. Tunda litakatazwa kwako kwa miaka mitatu. Halitaliwa.
\v 24 Lakini katika mwaka wa nne matunda yote yatakuwa matakatiifu, matoleo ya sifa kwa Yahweh.
\v 25 Katika mwaka wa tano unaweza kula tunda, ambalo umelisubiri ili kwamba mti uweze kuzaa zaidi. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
\s5
\v 26 Usile nyama yoyote amabayo damu ingalimo ndani yake. Usiulize kwa roho juu ya wakati ujao,
\v 27 Usitafute kuwadhibiti wengine kwa njia ya nguvu za kichawi. Msifuate tabia za kipagani kama vile kunyoa denge au kunyoa pembe za ndevu zeu.
\v 28 Usiukate mwili wako kwa ajili ya wafu au kuchanja chale juu ya mwili wako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 29 Usimwaibishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo taifa litaangukia kwenye ukahaba na nchi itajawa na uovu.
\v 30 Utazitunza Sabato zangu na kupaheshimu mahali patakatifu pa hema langu la kukutania. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 31 Msiwageukie wale wanaoongea na wafu au roho wachafu. msiwatafute, la sivyo watawanajisi ninyi, Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 32 Ni lazima usimame mbele za mtu mwenye mvi na uheshimu uwepo wa mzee. Yakupasa umwegope Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 33 Mgeni anapoishi miongoni mwenu katika nchi yanu, usimtendee lolote lililobaya.
\v 34 Mgeni anayeishi pamoja nanyi ni lazima awe kama mwenyeji Mwisraeli mzaliwa anayeishi kwenu, na sharti umpende kama unavyojipenda wewe mwenyewe, ni kwa sababu wewe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
\s5
\v 35 Unapopima urefu, uzito, au wingi usitumie vipimo vya udanganyifu.
\v 36 Tumia mizani iliyo halali, mawe ya kupimia uzito yaliyo halali, efa halali, hini iliyo halali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya utumwa ya Misri.
\v 37 Utayatii maagizo yangu na sheria zangu zote na kuzitenda. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, akasema,
\v 2 "Waambie watu wa Waisraeli, 'mtu yeyote miongoni mwa watu Israeli, au Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwa Waisraeli atakayemtoa mtoto wake yeyote kwa Moleki, hakika atauawa. Ni lazima watu wa nchi wamponde kwa mawe.
\s5
\v 3 Pia nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake kwa sababu amemtoa mtoto wake kwa Moleki, ili kupatia unajisi mahali pangu patakatifu na kulinajisi jina langu takatifu.
\v 4 Na kama watu wa nchi watayafumba macho yao kwa mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa Moleki, kama hawatamwua mtu huyo, ndipo Mimi mwenyewe nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na ukoo wake,
\v 5 Nami nitamkatilia mbali pamoja na yeyote anayejifanya kahaba ili kufanya umalaya na Moleki.
\s5
\v 6 Mtu yule anayewageukia wanaozungumza na wafu, au na wale wanaozungumza na roho ili kufanya ukahaba nao, Nitakaza uso wangu dhidi ya mtu huyo; Nami nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
\v 7 Kwa hiyo jitakaseni wenyewe na muwe watakatifu, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 8 Mtazitunza amari zangu na kuzifuta. Mimi ndimi Yahweh anayewatenga ninyi muwe watakatifu.
\v 9 Yeyote amlaaniye baba yake au mama yake hakika mtu huyo atauawa. Amemlaani baba yake au mama yake, kwa hiyo ana hatia na anastahili kufa.
\s5
\v 10 Mwanaume yeyote afanyaye uzinzi na mke wa mwanaume mwingine, yaani, yeyote anayezini na mke wa jirani yake—yule mwanaume mzinzi na mwanamke mzinzi ni lazima wote wawili wauawe.
\v 11 Mwanaume yeyote anayelala na mke wa baba yake ili kukutana naye kimwili amemfedhehesha baba yake mwenye. Wote wawili; mwana huyo na mke huyo wa baba yake kwa hakika watauawa. wanahatia na wanastahili kufa.
\v 12 Kama mwanaume atalala na mke wa mwanawe, wote wawili; mwanaume huyo na mke huyo wa mwanawe hakika watauawa. Wametenda upotovu. Wana hatia na wanastahili kufa.
\s5
\v 13 Kama mwanaume analala na mwanaume mwingine kama alalavyo na mwanamke, wote wawili watakuwa wamefanya jambo lililo ovu. Hakika watauawa. Wana hatia na wanastahili kufa.
\v 14 Ikiwa mwanaume atamwoa mwanamke na pia akamwoa mama wa mwanamke huyo, huu ni uovu. Ni lazima wachomwe kwa moto, wote wawili, mwanaume huyo na manamke huyo, ili kwamba hapatakuwepo na uovu miongoni mwenu.
\s5
\v 15 Ikiwa mwanaume analala na mnyama, hakika atauawa, ni lazima mumuue na mnyama huyo pia.
\v 16 Ikiwa mwanamke anamkaribia mnyama ili kulala naye, ni lazima mmuuwe mwanamke huyo pamoja na mnyama. Kwa hakika ni lazima wauawe. wana hatia na wanastahili kufa.
\s5
\v 17 Ikiwa mwanaume analala na dada yake, ama ni binti ya baba yake au binti ya mama yake—ikiwa wamelala pamoja, hilo ni jambo la aibu. Ni lazima wakatiliwe mbali watoke machoni pa watu wao, kwa sababu amelala na dada yake. Ni lazima aibebe hatia yake.
\v 18 Kama mwanaume analala na mwanamke katika kipindi cha hedhi yake, na amekutana naye kimwili, atakuwa amefunua mtiririko wa damu yake, chanzo cha damu yake. Ni lizima wote wawili wakatiliwe mbali kutoka mingoni mwa watu wao.
\s5
\v 19 Usilale na dada ya mama yako, au dada ya baba yako, kwa sababu ungeweza kumwaibisha jamaa yako wa karibu. Ni lazima utabeba hatia yako mwenyewe.
\v 20 Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao.
\v 21 Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote amabayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao.
\s5
\v 22 Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi.
\v 23 Msienende katika desturi za mataifa ambayo nitayafukuza mbele yenu, ni kwa sababu wamefanya mambo haya yote, nami mimewachukia wao.
\s5
\v 24 Nami nikawaambia ninyi, "Mtaimiliki nchi yao, nitaitoa kwenu ili muimiliki, nchi itiririkayo amaziwa na asali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine.
\v 25 Ni lazima pia mtofautishe kati ya wanya najisi na wale walio safi, na kati ya ndege walio najisi na walio safi. Msijichafue wenyewe kwa wanyama au ndege au kiumbe kitambaacho juu ya nchi kilicho najisi, ambacho nimekitenga kuwa najisi.
\s5
\v 26 Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi, Yahweh, ni mtakakatifu, nami nimewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine, kwa kuwa nyinyi ni wangu.
\s5
\v 27 Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa, "Zungumza na makuhani, wana wa Aroni, nawe waambie, 'hakuna hata mmoja miongoni mwenu atakayejitia unajisi kwa wale wanaokufa miongoni mwa watu wake,
\v 2 isipokuwa yule aliye ndugu wa karibu—mama yake, baba yake, mwanawe, bintiye, nduguye,
\v 3 au dada yake bikira anayemtegemea, kwa kuwa hana mume—kwake huyo anaweza kujitia unajisi.
\s5
\v 4 Lakini hatajitia unajisi na kujichafu kwa ajili ya jamaa wengine.
\v 5 Makuhanai hawatanyoa vichwa vyo wala kunyoa pembeni mwa ndevu zao, wala hawatachanja chale miili yao.
\v 6 Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala hawataliaibisha jina la Mungu wao, kwa sababu makuhani hutoa sadaka ya Yahweh ya chakula, mkate wa Mungu wao. Kwa hiyo makuhani lazima wawe watakatifu.
\s5
\v 7 Hawataoa mwanamke aliye kahaba na aliyetiwa unajisi, na hawataoa mwanamke aliyetalikiwa kutoka kwa mume wake kwa sababu wametengwa kwa ajili ya Mungu wao.
\v 8 Utamtenga kwa sababu yeye ndiye anayetoa mkate kwa Mungu wako. Ni lazima awe mtakatifu, kwa sababu—Mimi, Yahweh, ndimi niwatakasaye nyinyi—pia Mimi mwenyewe ni mtakatifu.
\v 9 Binti yeyote wa kuhani anayejitia unajisi kwa kujifanya kahaba anajifedhehesha mwenyewe. Ni lazima ateketezwe kwa moto.
\s5
\v 10 Mtu ambaye ni kuhani mkuu miongoni mwa nduguze, ambaye mafuta ya upako yamekwisha kumiminwa kichwani pake, na ambaye amekwisha kuwekwa wakfu ili kuvaa mavazi maalum ya kuhani mkuu, kamwe hataziacha wazi nywele zake wala hatazirarua nguo zake.
\v 11 Hataingia kamwe mahali popote ambapo kuna maiti na kujitia unajisi, hata kama ni maiti ya baba yake au ya mama yake.
\v 12 Kuhani mkuu hataondoka eneo takatifu la hema la kukutania au kupatia unajisi patakatifu pa Mungu wake, kwa sababu amewekwa wakfu kuwa kuhani mkuu kwa kutiwa mafuta ya upako ya Mungu wake. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 13 Kuhani mkuu nilazima aoe bikira kuwa mke wake.
\v 14 Hataoa mjene, mwanamke mtalaka au mwanamke aliye kahaba. Anaweza kuoa mwanamke bikira kutoka kwa watu wake,
\v 15 kwa hiyo asiwatia unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. kwa kuwa Mimi Yahweh, ndimi ninayemfanya yeye mtakatifu."
\s5
\v 16 Yahweh akamwambia Musa, akasema,
\v 17 Zungumza na Aroni na umwambie, 'mtu yeyote wa ukoo wako katika vizazi vyako vyote mwenye kasoro mwilini mwake, asisogee kutoa chakula kwa Mungu wake.
\s5
\v 18 Mtu yeyote mwenye kasoro mwilini mwake asimkaribie Yahweh,
\v 19 mtu kama vile: kipofu au mtu asiyeweza kutembea, mtu aliyeharibiwa uso au kupungukiwa na viungo mwilini, mtu aliye na mguu au mkono wenye ulemavu,
\v 20 mtu mwenye kibiongo mgongoni mwake au aliye na kimo kidogo au wembamba usio wa kawaida, au mtu mwenye kasoro machoni mwake, au mwenye ugonjwa, kidonda, upele, au yule ambaye korodani zake zimeharibiwa.
\v 21 Hakutakuwa na mtu miongoni mwa ukoo wa Aroni kuhani mkuu mwenye kasoro mwilini atakayekaribia kutoa matoleo yatakayoteketezwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh. Mtu kama huyo mwenye kasoro mwilini hatakaribia ili kutoa mkate wa Mungu wake.
\s5
\v 22 Anaweza kula chakula cha Mungu wake, ama iwe baadhi ya vile vilivyo vitakatifu sana au vile vitakatifu.
\v 23 Hata hivyo, hataingia ndani ya pazia wala kuisogelea madhabahu, kwa sababu ana kasoro mwilini mwake, ili kwamba asipanajisi mahali patakatifu pangu, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh anayewafanya watakatifu."
\v 24 Kwa hiyo Musa akamwambia maneno haya Aroni, wanawe, na watu wote wa Israeli.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa, kusema,
\v 2 "Ongea na Aroni na wanawe, waambie wajiepushe na vitu vitakatifu vya watu wa Israeli wanavyovitenga kwangu. Wasilinajisi jina langu. Mimi ndimi Yahweh.
\v 3 Waambie, 'Ikiwa mmoja wa wazao wenu katika vizazi vyenu vyote anakaribia vitu vitakatiifu vile ambavyo watu wa Israeli wamevitenga kwa Yahweh, wakati akiwa najisi, sharti mtu huyo akatiliwe mbali atoke mbele zangu. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 4 Hatakuwapo yeyote wa uzao wa Aroni aliye na ungonjwa wa ngozi wa kuambukiza, au maambukizi yatirirkayo kutoka mwilini mwake, atakayekula sehemu yoyote ya dhabihu inatolewayo kwa Yahweh mpaka atakapotakasika. Yeyote agusaye kitu chochote kilichonajisi kwa njia ya kugusa maiti, au kwa kumgusa mtu yeyote aliyetokwa na shahawa,
\v 5 au yeyote agusaye mnyama atakayemtia unajisi, au mtu yeyote atakayemfanya najisi, kwa hiyo unajisi wowote unaweza kuwa—
\v 6 kuhani yeyote agusaye kitu chochote kisichosafi atakuwa najisi hata jioni. Hatakula chochote cha vitu vitakatifu, isipokuwa ameuosha mwili wake katika maji.
\s5
\v 7 Jua linapotua, ndipo atakuwa safi. Baada ya machweo anaweza kula kutoka katika vitu vitakatifu, kwasababu hivyo ni vyakuala vyake.
\v 8 Asile mzoga wowote uliookotwa au mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori, ambaye kwake atajitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh.
\v 9 Ni lazima makuhani wafuate maagizo yangu, ama sivyo watakuwa na hatia ya dhambi na wangeweza kufa kwa kunitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh ninayewafanya wao watakatifu.
\s5
\v 10 Hakuna mtu kutoka nje ya familia ya kuahani, wakiwemo wageni wa kuhani au watumwa wake wa kuajiliwa, atakayeweza kula kitu chochote kilicho kitakatifu.
\v 11 Lakini kama huyo kuhani amenunua mtumwa kwa fedha yake mwenyewe, mtumwa huyo anaweza kula kutoka katika vitu vilivyotengwa kwa Yahweh. Na watu wa familia ya kuhani na watumwa waliozaliwa nyumbani mwake, pia wanaweza kula pamoja naye kutoka katika vitu hivyo.
\s5
\v 12 Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, hataweza kula chochote cha mchango wa matoleo matakatifu.
\v 13 Lakini ikiwa huyo binti wa kuhani ni mjane au ametalikiwa, na ikiwa hana mtoto, na anarudi kuishi knyumbani kwa baba yake kama alivyokuwa wakati wa ujana wake, anaweza kula kutoka katika chakula cha baba yake. Lakini hakuna yeyote asiye wa familia ya kikuhani anatakayeruhusiwa kula kutoka katika chakula cha kuhani.
\s5
\v 14 Kama mtu anakula chakula kitakatifu bila ya kukijua, naye atamlipa kuahani kwa ajili ya hicho; itampasa kuongeza moja ya tano juu yake na kukirejesha kwa kuhani.
\v 15 Haiwapasi watu wa Israeli kutoheshimu vitu vitakatifu ambavyo vimeinuliwa juu na kuletwa kwa Yahweh,
\v 16 kisha wakajisababishia wenyewe kuchukua dhambi amabyo ingewafanya kuwa na hatia ya kula chakula kitakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Yahweh awafanyaye wao watakatifu."
\s5
\v 17 Yahweh akazungumza na Musa, akasema,
\v 18 "Sema na Aroni na wanawe, na kwa watu wa Israeli wote. Waambie, Mwisraeli yeyote, au Mgeni anayeishi katika Israeli, waletapo dhabihu—iwe ni kutimiza kiapo, au iwe ni sadaka ya hiari, au wanaleta kwa Yahweh sadaka ya kuteketezwa kwa moto,
\v 19 ikiwa wanataka ikubalike, ni lazima watowe mnyama dume asiye na dosari, kutoka kwenye kundi la ng'ombe, kondoo au mbuzi
\s5
\v 20 Lakini hamtatoa chochote kilicho na dosari. Sitakipokea kwa niaba yenu.
\v 21 Yeyote atoae dhabihu ya sadaka ya ushirika kutoka katika kundi la ng'ombe au la kondoo kwa Yahweh ili kutimiza kiapo, au kama sadaka ya hiari, ili ikubalike, ni lazima isiwe na kilema. Ni lazima pasiweko na kasoro katika mnyama.
\s5
\v 22 Msitoe kabisa wanyama waliovipofu, waliojeruhiwa, wala walio na kilema, wenye upele, vidonda vitokavyo usaha, wala wenye vigaga. Msiwatoe hawa kuwa dhabihu ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa Yahweh juu ya madhabahu.
\v 23 Unaweza kumleta makisai au mwana-kondoo mlemavu au aliyedumaa kuwa sadaka ya hiari, lakini sadaka kama hiyo kwa ajili kutimiza kiapo, haitapokelewa.
\s5
\v 24 Usitoe kwa Yahweh mnyama yeyote aliyetiwa jeraha, kupondwa, au kukatwa korodani zake.
\v 25 Usifanye haya katika nchi yako. Usilete mkate wa Mungu wako kutoka mkononi mwa mgeni. Hao wanyama wenye vilema na dosari ndani yao, hawatapokelewa kabisa kwa ajili yako.
\s5
\v 26 Yahweh akamwambia Musa na akasema,
\v 27 "Wakati ndama, mwana—kondo au mwana—mbuzi azaliwapo, sharti abaki na mama yake kwa muda wa siku saba. Ndipo kuanzia siku ya nane na kuendelea, anaweza kupokelewa kuwa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh.
\s5
\v 28 Usimchinje ng'ombe jike pamoja na ndama wake au mbuzi jike pamoja na kitoto chake kwa siku moja.
\v 29 Utoapo sadaka ya shukrani kwa Yahweh utaitoa kwa njia iliyokubalika.
\v 30 Ni lazima iliwe siku iyo hiyo inayotolewa. Hutakiwi kubakiza chochote hata asubuhi. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 31 Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Yahweh.
\v 32 Msiliabishe jina langu takatifu. Ni lazima nitambuliwe kuwa ni mtakatifu na watu wa Israeli. Mimi ndimi Yahweh niwafanyaye ninyi watakatifu,
\v 33 ambaye amewaleta kutoka katika nchi ya Misri ili niwe Mungu wenu: Mimi ndimi Yahweh."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa:
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli, na uwaambie, 'Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo ni lazima mzitangaze kuwa makusanyiko matakatifu, ni sikukuu zangu za mara kwa mara.
\s5
\v 3 Mnaweza kufanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika kabisa. Usifanye kazi kwa sababu ni Sabato kwa ajili ya Yahweh mahali pote mnaposhi.
\s5
\v 4 Hizi ndizo sikukuu za Yahweh zilizoamriwa, Makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilioamriwa:
\v 5 Katika mwenzi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi kwenye mwanga hafifu wa machweo ya jua, ni Pasaka ya Yahweh.
\v 6 Siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu ya mikate isiotiwa hamira kwa ajili ya Yahweh. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiotiwa hamira.
\s5
\v 7 Siku ya kwanza ni lazima mjitenge kwa pamoja, hamtafanya kazi ya kawaida.
\v 8 Kwa siku saba mtamletea Yahweh matoleo ya chakula. Siku ya saba ni ya kusanyiko takatifu lililotengwa kwa ajili ya Yahweh, nanyi katika siku hiyo hamtafanya kazi yoyote ya kawaida."
\s5
\v 9 Yahweh akamwambia Musa, akisema,
\v 10 "Sema na watu wa Israeli uwaambie, 'mtakapika kwenye nchi nitakayowapa nyinyi, na mtakapovuna mazao yake, nanyi yawapasa kumletea kuhani fungu la masuke ya nafaka ya matunda yake ya kwanza.
\v 11 Naye ataliinua hilo fungu la masuke ya nafaka mbele za Yahweh na kulileta kwake, kwa kuwa litakubalika kwa niaba yenu. Nalo litaletwa siku baada ya Sabato ili kwamba kuhani ataliinua na kulileta kwangu.
\s5
\v 12 Siku ile mtakapoliinua lile fungu la masuke ya nafaka na kulileta kwangu, itawabidi kutoa mwana—kondoo dume wa mwaka mmoja na asiye na dosari awe sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh.
\v 13 Matoleo ya nafaka yatakuwa sehemu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, uwe matoleo yaliyofanywa kwa moto kwa Yahweh, ili kutoa harufu nzuri ya kupendeza, pamoja na hiyo kutakuwa na matoleo ya kinywaji ya divai, moja ya nne ya hini.
\v 14 Hamtakula mkate, wala nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya hata siku ile mliyoleta matoleo haya kwa Mungu wenu. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu, popote pale mnapoishi.
\s5
\v 15 Tangu siku iliyofuata baada ya Sabato—hiyo ilikuwa siku mlipolileta lie fungu la nafaka la matoleo ya kutikiswa—hesabuni majuma saba kamili.
\v 16 Mtahesabu siku hamsini, ambazo zingekuwa siku baada ya Sabato ya saba. Kisha mtaleta matoleo ya nafaka mpya kwa Yahweh.
\s5
\v 17 Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahweh.
\v 18 Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahweh, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahweh.
\s5
\v 19 Ni lazima mtowe mbuzi dume mmoja kwa ajili ya matoleo ya dhambi, na wana—kondoo dume wawili wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu, wawe matoleo ya ushirika.
\v 20 Ni lazima kuhani azitikise pamoja na mkate wa malimbuko ya kwanza mbele za Yahweh na kuzileta kwake kuwa matoleo pamoja na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka takatifu kwa Yahweh kwa ajili ya kuhani.
\v 21 Mtatoa tangazo siku iyo hiyo. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
\s5
\v 22 Mtakapovuna mazao ya nchi yenu, Msivune kabisa kabisa pembeni mwa mashamba yenu, wala msivune mazazo ya mavuno yenu. Inawapasa kuyaacha kwa ajili ya masikini na mgeni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu."
\s5
\v 23 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 24 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, "Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza itakuwa siku ya pumzika makini kwa ajili yenu, kumbukumbu pamoja na kupigwa kwa tarumbeta na kusanyiko takatifu,
\v 25 Hamtafanya kazi ya kawaida, na ni lazima mtoe dhabihu inayofanywa kwa moto kwa Yahweh."
\s5
\v 26 Kisha Yahweh akamwambia Musa, akisema,
\v 27 "Sasa, siku ya kumi ya mwezi huu wa saba, ni Siku ya Upatanisho. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na ni lazima mjinyenyekeze na kuleta kwa Yahweh matoleo kwa moto.
\s5
\v 28 Hamtafanya kazi katika siku hiyo kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Yahweh Mungu wenu.
\v 29 Yeyote asiyejinyenyekeza siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.
\s5
\v 30 Yeye afanyaye kazi yoyote katika siku hiyo, Mimi, Yahweh, nitamwangamiza atoke miongoni mwa watu wake.
\v 31 Msifanye kazi ya aina yoyote katika siku hiyo. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
\v 32 Siku hii itakuwa Sabato ya pumziko lenye utlivu, na ni lzima siku ya tisa ya mwezi mjinyenyekeze katika majira ya jioni. Tangu jioni hata jioni mtaishika Sabato yenu."
\s5
\v 33 Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
\v 34 "Zungumza na watu ISraeli, uwaambie 'Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba kutakuwa na Sikukuu ya vibanda kwa Yahweh. nayo itadumu siku saba.
\s5
\v 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi ya kawaida.
\v 36 Kwa muda wa siku saba mtatoa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu, nanyi mtato dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Hili ni kusanyiko lenye utulivu, nanyi msifanye kazi yoyote ya kawaida.
\s5
\v 37 Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo mnapaswa kuzitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu ya kutoa dhabihu kwa moto kwa Yahweh, matoleo ya kuteketezwa na matoleo ya nafaka, dhabihu na matoleo ya vinywaji, kila moja kwa siku yake.
\v 38 Sikukuu hizi zitakuwa nyongeza kwa Sabato za Yahweh na zawadi zenu, viapo vyenu vyote, na sadaka zenu zote za hiari mzitoazo kwa Yahweh.
\s5
\v 39 Kuhusu Sikukuu ya vibanda, siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmeyakusanya ndani matunda ya nchi, ni lazima muitunze sikukuu hii ya Yehweh kwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza itakuwa ya pumziko lenye utulivu, na siku ya nane pia itakuwa ya pumziko lenye utulivu.
\s5
\v 40 Siku ya kwanza mtachuma tunda lililobora kutoka kwenye miti, mtakata makuti ya mtende, na matawi ya miti minene yenye majani mengi, na majani ya mierebi kutoka chemchemi za maji, nanyi mtashangilia mbele za Yahweh Mungu wenu kwa siku saba.
\v 41 Kwa muda wa siku saba kila mwaka, mtaisherehekea sikukuu hii kwa Yahweh. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali potepote mtakapoishi. Mtaisherehekea sikukuu hii katika mwezi wa saba.
\s5
\v 42 Mtaishi kwenye vibanda vidogovidogo kwa siku saba. Waisraeli wenyeji wa kuzaliwa wote itawapasa kuishi katika vibanda vidogovidogo kwa siku saba,
\v 43 ili kwamba wazao wenu, kizazi baada ya kizazi, waweze kujifunza nilivyowafanya wana wa Israeli kuishi kwenye vibanda kama hivi nilipowaongoza kutoka katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.'"
\v 44 Katika njia hii Musa akazitangaza kwa watu wa ISraeli sikukuu zilizoamria kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Musa, akisema,
\v 2 "Waamru watu wa Israeli wakuletee mafuta halisi yaliyokamliwa kutokana na mizeituni ili yatumike kwenye taa, ili kwamba taa ziweze kuwaka daima na kuleta mwanga.
\s5
\v 3 Nje ya pazia lililoko mbele ya sanduku la maamzi ndani ya hema la kukutania, Aroni ataiwasha daima taa mbele za Yahweh, tangu asubuhi hata jioni. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu.
\v 4 Kuhani mkuu atazifanya taa ziwake daima mbele za Yahweh, taa hizo zilizo kwenye kinara cha dhahabu safi.
\s5
\v 5 Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate.
\v 6 Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahweh katika safu mbili, mikate sita katika kila safu,
\s5
\v 7 Mtaweka uvumba safi kando ya kila safu ya mikata kuwa sadaka ya kuwakilisha. Uvumba huo utachomwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh.
\v 8 Kila siku ya Sabato kuhani mkuu sharti aipange kwa utaratibu hiyo mikate mbele za Yahweh kwa niaba ya watu wa Israeli, iwe ishara ya agano la milele.
\v 9 Sadaka hii itakuwa kwa ajili ya Aroni na wanawe, na ni lazima waile mahali palipo patakatifu, kwa kuwa ni sehemu ya matoleo kwa Yahweh yaliyofanywa kwa moto."
\s5
\v 10 Sasa ilitokea kwamba mwana wa mwanamke Mwisraeli, ambaye baba yake alikuwa Mmisri, alikwenda miongoni mwa watu wa Israeli. Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akagombana na mwanume Mwisraeli kambini.
\v 11 Mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru jina la Yahweh na kumlaani Mungu, kwa hiyo watu wakamleta kwa Musa. Jina la mama yake aliitwa Shelomithi, binti wa Dibri, kutoka kabila la Dani.
\v 12 Wakamweka kizuizini mpaka Yahweh mwenyewe atakapotangaza mapenzi yake kwao.
\s5
\v 13 Kisha Yahweh akamwambia Musa,
\v 14 "Mchukue nje ya kambi huyo aliyemlaani Mungu. Wale wote waliomskia wataweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kusanyiko lote watamponda kwa mawe.
\s5
\v 15 Ni lazima uwaeleze watu wa Israeli na kusema, 'Yeyote anayemlaani Mungu wake imempasa kubeba hatia yake mwenyewe.
\v 16 Yeye anayelikufuru jina la Yahweh kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahweh, ni lazima auawe.
\s5
\v 17 Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auewa.
\v 18 Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.
\s5
\v 19 Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:
\v 20 Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.
\v 21 Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.
\s5
\v 22 Ni lazima mwe na sheria moja kwa wote, mgeni na Mwisraeli mwenyeji mzaliwa, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wanu."
\v 23 Kwa hiyo Musa akazungumza na watu wa Israeli, nao watu wakamleta mwanaume huyo nje ya kambi, yule ambaye alikuwa amemlaani Yahweh. Wakampiga kwa mawe. Watu waisraeli wakaitekeleza amri ya Yahweh aliyoitoa kupitia Musa.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa kwenye Mlima wa Sinai, akisema,
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, "Mtakapoingia katika nchi ambayo ninawapa, kisha hiyo nchi lazima ifanywe iwe ya kuishika Sabato kwa ajili ya Yahweh.
\s5
\v 3 Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake.
\v 4 Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahweh. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake.
\s5
\v 5 Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
\v 6 Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.
\v 7 Na wnyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.
\s5
\v 8 Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
\v 9 Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.
\s5
\v 10 Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.
\s5
\v 11 Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.
\v 12 Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.
\s5
\v 13 Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.
\v 14 Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.
\s5
\v 15 Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.
\v 16 Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.
\v 17 Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 18 Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagiza, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.
\v 19 Nayo nchi itawapa mavuno yake, nanyi mtakula matunda yenu na mtaishi humo salama.
\s5
\v 20 Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu."
\v 21 Nitaiamru baraaka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.
\v 22 Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita
\s5
\v 23 Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.
\v 24 Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.
\v 25 Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.
\s5
\v 26 Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,
\v 27 kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuerejea kwenye miliki yake mwenyewe.
\v 28 Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.
\s5
\v 29 Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.
\v 30 Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
\s5
\v 31 Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
\v 32 Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.
\s5
\v 33 Iwapo mmoja wa makuhani haikombowi nyumba iliyozwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji ilimo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.
\v 34 Lakini yale mashamba yanayozunguka miji yao hayataweza kuuzwa kwa sababu hiyo ni mali ya kudumu ya Makuhani.
\s5
\v 35 Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.
\v 36 Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.
\v 37 Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
\v 38 Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.
\s5
\v 39 Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.
\v 40 Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.
\v 41 Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
\s5
\v 42 Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.
\v 43 Usitawale juu yao kwa ukatili, bali yakupasa kumheshimu Mungu wako.
\v 44 Kwa upande wa watumwa wako wakiume na watumwa wako wa kike, unaowezao kuwapata kutok kwa mataifa yanayokuzunguka, waweza kununua watumwa kutoka kwao.
\s5
\v 45 Unaweza pia kununua watumwa kutoka kwa wageni wanaoishi miongoni mwenu, yaani, kutoka familia zao waliopamoja nawe, wale wtoto waliozaliwa katika nchi yako. Wanaweza kuwa mali yako.
\v 46 Unaweza kuzalisha watumwa hao kama urithi kwa watoto wako baada yako, ili kuwamiliki kama mali. Kutoka kwao waweza kununua watumwa daima, lakini hamtawezi kutawala kwa ukali juu ya ndugu zenu walio miogoni mwa watu wa Israeli.
\s5
\v 47 Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,
\v 48 baada ya Mwisraeli mwenzako kuwa amenunuliwa. Anaweza kurejeshwa kwa maliopo. Iwapo anaweza kurejeshwa. Mtu fulani katika familia yake anaweza kumkomboa.
\s5
\v 49 Anaweza kuwa mjomba wake, au mjomba wa mwanawe, anayemkomboa yeye, au yeyote aliye ndugu yake wa karibu kutoka kwa ukoo wake. Au, iwapo ni mwenye mafanikio, anaweza kujikomboa mwenyewe.
\v 50 Ni lazima apatane na mtu aliyemnunua, itawapasa kuhesabu miaka tangu mwaka aliojiuza kwa mnunuzi wake mpaka mwaka wa Yubile. Ile thamani ya ukombozi wake ihesabiwe kulingana na kiwango cha mshahara anaolipwa mtumishi aliyeajiriwa, kwa idadi ya miaka ambayo angeweza kuendelea kufanya kazi kwa yule aliyemnunua.
\s5
\v 51 Endapo kutakuwa kungali na miaka mingi iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atalazimika kulipa fungu kubwa la fedha kwa ajili ya ukombozi ambao ni uwino wa idadi ya miaka hiyo.
\v 52 Iwapo kuna miaka michache tu iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atapatana na aliyemnunua ili kuipitia idadi ya miaka iliyobaki mpaka Yubile, naye atalazimika kulipia ukombozi wake kulingana na idadi ya miaka.
\s5
\v 53 Naye atatendewa kama mtu aliyeajiriwa mwaka kwa mwaka. Utahakikisha kwamba hatendewi kwa ukali.
\v 54 Iwapo hakukombolewa katika njia hizi, basi atatumika mpaka mwaka wa Yubile, yeye pamoja na watoto wake.
\v 55 Kwangu mimi watu wa Israeli ni watumishi. Wao ni watumishi wangu ambao Niliwatoa katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Msijitengenezee sanamu, wala msisimamishe kinyago cha kuchonga au nguzo ya jiwe ya kuabudia, na msisimamisha sura ya jiwe la kuchonga katika nchi yenu mtayoiinamia, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
\v 2 Ni lazima muitunze Sabato Yangu na kupaheshimu patakatifu pangu. Mimi ndimi Yahweh.
\s5
\v 3 Iwapo mtatembea katika sheria zangu na kuzishika amri zangu na kuzitii,
\v 4 Nami nitawapa ninyi mvua katika majira yake; nayo nchi itatoa mazao yake, na miti ya shambani itatoa matunda yake.
\s5
\v 5 Upuraji wenu utaendelea hata wakati wa mavuno ya zabibu, na mavuno ya zabibu yataendelea mpaka majira ya kupada mbegu. Nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi salama mahali mtakapofanya mji wenu katika nchi.
\v 6 Nitawapa amani; mtalala bila ya kitu chochote kuwatia hofu. Nitawaondolea mbali wanyama waliohatari katika nchi, na upanga hautapita katika nchi yenu.
\s5
\v 7 Mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele yenu kwa upanga.
\v 8 Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi; adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
\s5
\v 9 Nitawatazama kwa upendeleo na kuwafanya nyinyi mzae na kuwazidisha nyinyi.
\v 10 Mtakula chakula kilichotunzwa ghalani kwa muda mrefu. Mtayaondoa mazao yaliyohifadhiwa ghalani kwa sababu mtahitaji ghala kwa ajili ya mavuno mapya.
\s5
\v 11 Nitaliweka hema langu katikati yenu, nami stachukizwa nanyi.
\v 12 Nitatembea miongoni mwenu nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
\v 13 Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewaleta nyinyi kutoka nchi ya Misri, ili kwamba msingeendelea kuwa watumwa wao. Nimevunja makomeo ya nira yenu na nikawafanya mtembee kwa kunyooka.
\s5
\v 14 Lakini ikiwa hamtanisikiliza mimi,
\v 15 na kutozitii amri hizi, na ikiwa mtayakataa maagizo yangu, na kuzichukia sana sheria zangu, kiasi kwamba hamtaweza kuzitii amri zangu zote, lakini mkalivunja agano langu—
\s5
\v 16 —kama mtafanya mambo haya, Nami nitafanya hili kwenu: Nitasababisha hofu juu yenu, maradhi na homa kali itakayoangamiza macho na kuondoa uhai wenu. Mtapanda mbegu zenu kwa hasara, kwa sababu adui zenu watakula mazao yake.
\v 17 Nitakaza uso wangu dhidi yenu, na mtashindwa na adui zenu. Watu wanaowachukia watatawala juu yenu, na mtakimbia hata kama hakutakuwa na yeyote anayewafukuza.
\s5
\v 18 Iwapo hamtasikiliza maagizo yangu, Nami niwataadhibu vikali mara saba kwa dhambi zenu.
\v 19 Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.
\v 20 Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.
\s5
\v 21 Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.
\v 22 Nitatuma wanyama mapori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya mwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.
\s5
\v 23 Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,
\v 24 ndipo nami pia nitaenenda kinyume chenu, na Mimi mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa sababu ya dhambi zenu.
\s5
\v 25 Nitaleta upanga juu yenu utakaowaadhibu kwa kisasi kwa sababu ya kulivunja agano. Nanyi mtajikusanya kwenye miji yenu, Nami nitatuma humo maafa miongoni mwenu, na mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu.
\v 26 Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
\s5
\v 27 Endapo hamtanisikiliza pamoja na mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,
\v 28 kisha nami nitakwenda kinyume nanyi katika hasira, Nami nitawaadhibu hata mara saba kulingana na wingi wa dhambi zenu.
\s5
\v 29 Ndipo mtakapokula nyama ya wana wenu; mtakula nyama ya binti zenu.
\v 30 Nitapaangamiza mahali penu pa juu, kuziangusha chini madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzitupa maiti zenu juu ya maiti ya sanamu zenu, na Mimi mwenyewe nitawadharau nyinyi.
\s5
\v 31 Nitaigeuza miji yennu kuwa magofu na kupaharibu patakatifu penu. Nami sitapendezwa na harufu nzuri ya matoleo yenu.
\v 32 Nami nitaiharibu nchi. Adui zenu watakaokuwa wakiishi humo watashtushwa na uharibifu huo.
\v 33 Nami nitawatawanya nyinyi katika mataifa, na nitaufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itatelekezwa, na miji yenu itakuwa magofu.
\s5
\v 34 Nayo nchi itazifurahia Sabato zake kwa kuwa itakuwa imetelekezwa na ninyi mkiwa katika nchi za daui zenu. Katika nyakati hizo, nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.
\v 35 Maadamu itakuwa imetelekezwa, itakuwa na pumziko, ambalo litakuwa ni pumziko iliyolikosa pamoja na Sabato zenu mlipokuwa mkiishi ndani yake.
\v 36 Na kwa wale watakoachwa humo kwenye nchi za adui zenu, Nitatuma hofu ndani ya mioyo yenu kiasi kwamba hata kama ni maelfu ya majani tu yatakapopeperushwa katika upepo yatawaogofyeni. Nanyi mtaanguka hata kama hakutakuwa na awafukuzaye.
\s5
\v 37 Mtajikwaa kila mmoja juu ya mwenzake kama vile mlikuwa mkiukimbia upanga, hata kama hakutakuwa na awafukuzaye nyinyi. Hamtakuwa na nguvu ya kusimama mbele ya daui zenu.
\v 38 Nanyi mtaangamia miongoni mwa mataifa, nayo nchi ya adui zenu yenyewe itawamezani.
\v 39 Wale watakosalia miongoni mwenu watapotelea katika dhambi zao, huko kwenye nchi za adui zenu, na kwa sababu ya dhambi zao, na kwa sababu ya dhambi za baba zao watapotelea mbali pia.
\s5
\v 40 Lakini kama watakiri dhambi zao na dhambi ya baba zao, na usaliti wao ambao kwao hawakuwa waaminifu kwangu, pia na mwenendo wao dhidi yangu—
\v 41 ambao ulinisababisha kuwa kinyume nao, na kuwaleta katika nchi ya adui zao—iwapo mioyo yao isiyotahiriwa itanynyekezwa,
\v 42 na iwapo wataikubali adhabu kwa ajili ya dhambi zao, nami nitalikumbuka agano langu na Yakobo, agano langu na Isaka, agano langu na Abrahamu; Pia, nitaikumbuka nchi.
\s5
\v 43 Nchi itakayotelekezwa na wao, hivyo itapendezwa na Sabato zake inapobaki imetelekezwa na wao. Itawapasa kulipa hatia kwa dhambi zao kwa sababu ni wao wenyewe ndiyo walioyakataa maagizo yangu na kuzichukia sheria zangu.
\s5
\v 44 Lakini pamoja na haya yote, watapokuwa katika nchi ya adui zao, Mimi stawakataa wao, wala sitawachukia ili kuwaangamiza kabisa na kulifutilia mbali agano langu nilililoagana nao, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wao.
\v 45 Bali kwa ajili yao, nitalikumbuka agano langu na baba zao, niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri machoni pa mataifa, ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Yahweh."
\s5
\v 46 Hizi ndizo amri, hukumu, na sheria ambazo Yahweh alifanya baina yake na watu wa Israeli kwenye Mlima Sinai kwa kupitia Musa.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
\v 2 "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Iwapo mtu yeyote anatoa kiapo maalum cha kuwa mnathiri kwa Yahweh, tumieni tathmini zifuatazo:
\s5
\v 3 Viwango vyenu vya thamani kwa mwanaume aliye na umri kati ya miaka ishirini na miaka sitini yaweza kuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na vipimo vya shekeli ya mahali pa patakatifu.
\v 4 Kwa mwanamke wa umri uleule viwango vyenu vya thamani yapasa viwe shekeli thelathini vya fedha.
\s5
\v 5 Tangu wenye umri wa miaka mitano mpaka wa miaka ishirini viwango vyenu vya thamani kwa mwananume vitakuwa shekeli ishirini za fedha, na kwa mwanamke ni shekeli kumi za fedha,
\v 6 Kwa wenye umri wa tangu mwezi mmoja mpaka miaka mitano viwango vyenu vya thamani kwa mawanaume vitakuwa shekeli tano za fedha na kwa mwanamke shekeli tatu za fedha.
\s5
\v 7 Tangu wenye umri wa miaka sitini na zaidi kwa mwanaume viwango vyenu vya thamani vitakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke ni shekeli kumi.
\v 8 Lakini kama mtu atoaye kiapo cha mnadhiri hawezi kulipa kiwango hicho cha thamani, kisha huyo mtu anayetolewa lazima atapelekwa kwa kuhani, naye kuhani atamthamanisha huyo atolewaye kwa kiasi anachoweza kutoa yule anayetoa kiapo cha mnadhiri.
\s5
\v 9 Iwapo mtu anataka kutoa sadaka ya mnyama kwa Yahweh, na iwapo Yahweh ataikubali, kisha huyo mnyama atatengwa kwake.
\v 10 Mtu huyo hataruhusiwa kumtoa madhabahuni au kumbadilisha huyo mnyama, mzuri kwa mbaya au mbaya kwa mzuri. endapo atatoa mnyama badala ya mwingine, kisha wanyama hao wawili; yule anayetolewa na yule anayebadilishwa wanakuwa watakatifu.
\s5
\v 11 Hata hivyo, iwapo kile mtu amishaapa kumtolea Yahweh kwa uhalisia siyo kisafi, kwa hiyo, Yahweh hatakikubali, naye huyo mtu atalazimika kumleta huyo mnyama kwa kuhani.
\v 12 Kuhani atamthamanisha, kwa thamani ya soko la mnyama. Thamani yoyote kuhani atakayoiweka juu ya mnyama, hiyo ndiyo itakuwa thamani yake.
\v 13 Na kama mmiliki anapenda kumkomboa, kisha tano ya thamani yake itaongezwa kwenye gharama yake ya ukombozi.
\s5
\v 14 Mtu aitengapo nyumba yake iwe zawadi takatifu kwa Yahweh, kisha kuhani ataweka thamani yake ama iwe ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote itakayowekwa na kuhani juu yake, ndiyo itakuwa thamani yake.
\v 15 Lakini kama mmiliki wake anayeitenga nyumba yake anapenda kuikomboa, atalazimika kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake kwenye gharama ya ukombozi wake, nayo nyumba itakuwa yake.
\s5
\v 16 Iwapo mtu anatenga sehemu ya ardhi yake mwenye, kisha tathmini yake itakuwa katika uwiano kwa kiwango cha kiasi cha mbegu inayotakiwa kuipanda katika ardhi hiyo—homeri moja ya mbegu za shairi ambayo itathamanishwa kwa shekeli hamsini za fedha.
\s5
\v 17 Na kama analitenga shamba lake katika mwaka wa Yubile, tathmini yake ya awali itabaki kuwa ileile.
\v 18 Lakini endapo atalitenga shamba hilo baada ya mwaka wa Yubile, kisha kuhani atalazimika kukokotoa thamani yake kwa idadi ya miaka inayobaki mpaka mwaka wa Yubile, na thamani yake lazima ishushwe.
\s5
\v 19 Iwapo mtu anayelitenga shamba lake anapenda kuliko, mboa, naye atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani, nalo shamba litakuwa lake tena.
\v 20 Iwapo halikomboi shamba, au iwapo amishaliuza shamba kwa mtu mwingine, haliwezi kukombolewa tena.
\v 21 Badala yake, shamba hilo litakapoachwa huru katika mwaka wa Yubile, litakuwa zawadi takatifu kwa Yahweh, kama lilivyo shamba lililotolewa kabisa kwa Yahweh. Nalo litakuwa mali ya kuhani.
\s5
\v 22 Iwapo mtu anatenga shamba alilolinunua, lakini hilo shamba siyo sehemu ya ardhi ya familia yake,
\v 23 kuhani atafanya tathmini yake mpaka mwaka wa Yubile, na mtu huyo lazima atalipa thamani yake katika siku hiyo hiyo kuwa zawadi takatifu kwa Yahweh.
\s5
\v 24 Katika mwaka wa Yubile, shamba litarejeshwa kwa mtu yule ambaye lilikuwa limenunuliwa, kwa mmiliki wa ardhi.
\v 25 Tathmani yote lazima ifanywe kwa uzani wa shekeli ya mahali pa patakatifu. Gera ishirini kwa shekeli moja.
\s5
\v 26 Asiwepo mtu atakayetenga mzaliwa wa kwanza miongoni mwa wanyama, kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza wa wanyama tayari ni mali ya Yahweh; iwe ni maksai au kondoo, ni wa Yahweh.
\v 27 Na kama ni mnyama aliye najisi, kisha mmiliki wake anaweza kumnunua tena sawasawa na thamani yake, na sehemu ya tano lazima itaongezwa kwenye thamani hiyo. Na kama mnyama hakombolewi, naye atauzwa kwa thamani iliyowekwa.
\s5
\v 28 Hakutakuwa na kitu amabacho mtu anakitoa kwa Yahweh, kutoka katika vyote alivyonavyo, iwe ni mwanadamu au mnyama, au ardhi ya familia yake, ambacho chaweza kuuzwa au kukombolewa. Kila kitu kitolewacho ni kitakatifu sana kwa Yahweh.
\v 29 Hakuna fidia inayoweza kulipwa kwa ajili ya mtu aliyetolewa ili kuangamizwa. Mtu huyo sharti auawe
\s5
\v 30 Zaka yote iliyo ya ardhini, iwe nafaka ichipukayo juu ya ardhi au tunda kutoka kwenye miti, ni mali ya Yahweh. Ni takatifu kwa Yahweh.
\v 31 Iwapo mtu anakomboa chochote cha zaka yake, atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani yake.
\s5
\v 32 Na kwa kila mnyama wa kumi wa kundi la ng'ombe au la kondoo, yeyote anayepita chini ya fimbo ya mchungaji, atatengwa kwa ajili ya Yahweh.
\v 33 Mchungaji hatatafuta wanyma waliobora au wabaya kabisa, na haruhusiwi kubadili mnyama mmoja kwa mnyama mwingine. Iwapo anambadilisha kwa namna yoyote ile, kisha wote wawili yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa watakuwa watakatifu. Mnyama huyo atolewaye hawezi kukombolewa.'"
\s5
\v 34 Hizi ndizo amri ambazo Yahweh alimpa Musa kwenye mlima Sinai kwa ajili ya watu wa Israeli.

2447
04-NUM.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2447 @@
\id NUM
\ide UTF-8
\h Hesabu
\toc1 Hesabu
\toc2 Hesabu
\toc3 num
\mt Hesabu
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mungu alimwambia Musa katika hema ya kukutania walipokuwa katika jangwa la Sinai. Hii ilitokea katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili miaka miwili baadaya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Mungu alisema,
\v 2 'fanya sensa ya wanaume wote wa Israel kutoka kila ukoo, katika familia za baba zao. Wahesabu kwa majina, wahesabu kila mume, kila mwanamume
\v 3 kuanzia umri a miaka ishirini na zaidi. Uwahesabu wote wanaoweza kupigana kama askari wa Israel. Wewe na Haruni mtaandika idadi ya wanaume katika makundi ya majeshi yao.
\s5
\v 4 Kila mwanamume kwa kila kabila, kichwa cha ukoo, lazima atumike na wewe kama kiongozi wa kabila.
\v 5 Haya ndiyo majina ya viongozi ambao watapigana pamoja na wewe: Kutoka kabila la Reubeni, Elizuri mwana wa Shedeuri;
\v 6 kutoka kabila la Simeoni, Shelumiel mwana wa Zurishadai
\s5
\v 7 Kutoka kabila la Yuda, Nashoni mwana wa Aminadabu;
\v 8 Ktoka kabila la Isakari, Nethaneli mwana wa Zuari;
\v 9 kutoka kabila Zebuluni, Eliabu mwana wa Heloni
\s5
\v 10 kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yusufu, Elishama mwana wa Ammihudi; kutoka kabila la Manase, Gamaliel mwan wa Pedazuri;
\v 11 kutoka kabila la Benjamini mwana wa Ysufu, Abidani mwan wa Gidion;
\s5
\v 12 Kutoka kabila la Dan, Ahizeri mwana wa Amishadai;
\v 13 kutoka kabila Asheri, Pagieli mwana wa Okirani;
\v 14 kutoka kabila la Gadi, Eliasafu mwana wa Deuli;
\v 15 na kutoka kabila la Naftali, Ahira mwana wa Enani."
\s5
\v 16 Hawa ndio wanaume waliochaguliwa kutoka kwa watu. Waliongoza kabila za mababu zao. Walikuwa viongozi wa koo katika Israel.
\s5
\v 17 Musa na Haruni wakawachukua wale wanaume, waliokuwa wameandikwa kwa majina,
\v 18 na pamoja na wanaume hao waliwakusanya wanume wote katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Kisha kila mwanume wa miaka ishirini na zaidi alitambua babu zake. Alitakiwa kutaja koo na famila kutoka katika ukoo.
\v 19 Kisha Musa akaandika hesabu yao huko katika nyika ya Sinai, Kama Mungu alivyokuwa amemwamuru kufanya.
\s5
\v 20 Kutoka uzao wa Reubeni, mtoto wa kwanza wa Israel, yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka hesabu ya ukoo na familia.
\v 21 Waliwahesabu wanaume 46, 000 kutoka ukoo wa Reubeni.
\s5
\v 22 Kutoka uzao wa Simeoni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi au wenye uwezo wa kwenda vitani, kutokana na hesabu ya ukoo na familia.
\v 23 Walihesabu wanaume 59, 300 kutoka kabila la Simeoni.
\s5
\v 24 Kutoka uzao wa Gadi yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 25 Walihesabu wanaume 45, 650 kutoka kabila la Gadi.
\s5
\v 26 Kutoka uzao wa Yuda yalihesabiwa majina yote ya wanaume wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 27 walihesabiwa wanume 74, 000 kutoka kabila la Yuda.
\s5
\v 28 Kutoka uzao wa Isakari yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 29 Walihesabiwa wanaume 54, 000 kutoka kabila la Isakari.
\s5
\v 30 Kutoka uzao wa Zabuloni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 31 Walihesabiwa wanume 57, 400 kutoka kabila la Zabuloni.
\s5
\v 32 Kutoka uzao wa Efraimu mwana wa Yusufu yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 33 Walihesabiwa wanaume 40, 500 kutoka kabila la Efraimu.
\s5
\v 34 Kutoka uzao wa Manase mwana wa Yusufu yaliheabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia.
\v 35 Walihesabiwa wanaume 32, 000 kutoka kabila la Manase.
\s5
\v 36 Kutoka uzao wa Benjamini yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 37 Walihesabiwa wanaume 35, 000 kutoka kabila la Benjamini.
\s5
\v 38 Kutoka uzao wa Dani yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, Kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 39 Walihesabiwa wanaume 62, 000 kutoka kabila la Dani.
\s5
\v 40 Kutoka uzao wa Asheri yalihesabiwa majina yote ya kila mwanume mwenye umri wa miaka ishirini au zadi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia.
\v 41 Walihesabiwa wanaume 41, 500 kutoka ukoo wa Asheri.
\s5
\v 42 Kutoka ukoo wa Naftali yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
\v 43 Walihesabiwa wanaume 53, 400 kutoka kabila la Naftari
\s5
\v 44 Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote hawa, pamoja na wale wanaume kumi na wawili waliokuwa wakiongoza yale makabila kumi na mawili ya Israeli.
\v 45 Kwa hiyo wanaume wote wa Israeli wenye umri wa miak ishirini au zaidi, wote wenye uwezo wa kwenda vitani, walihesabiwa kutoka kwenye familia zao.
\v 46 Walihesabu wanaume 603, 550.
\s5
\v 47 Lakini wanaume toka uzao wa Lawi hawakuhesabiwa,
\v 48 Kwa sababu BWANA alimwambia Musa,
\v 49 "usiwahesabu wale wa kabila la Lawi wala kuwajumuisha kwenye jumla ya watu wa Israeli.
\s5
\v 50 Badala yake, waagize Walawi kuliangalia hema la amri za agano, na kuangalia mapambo ya hema na vyote vilivyomo. Walawi watalazimika kulibeba hema na lazima wayabebe mapambo ya hema. Lazima waliangalie hema na kuyatengeneza mazingira yake. Wataiangalia masikani na kuzitengeneza kambi zinazolizunguka.
\s5
\v 51 Kila hema litakapotakiwa kuhamishiwa eneo jingine, Walawi ndio watakaolipeleka pale. Na kila hema litakapotakiwa kusimamishwa, Walawi ndio watakao lisimamisha. Na mgeni yeyote atakayelisogelea hema lazima auawe.
\v 52 Wakati watu wa Israeli watakaposimamisha hema zao, kila mwanaume lazima awe karibu na bango la jeshi lake.
\s5
\v 53 Hata hivyo Walawi lazima waweke hema zao kuizunguka hiyo masikani ya amri za agano ili kwamba hasira yangu isije ikawaka juu ya wana wa Israeli. Walawi lazima wailinde hiyo masikani ya amri za agano."
\v 54 Wana wa Israeli walifanya yote haya. Walifanya yote ambayo BWANA aliagiza kupitia Musa.
\s5
\c 2
\p
\v 1 BWANA akasema na Musa na Haruni tena. Akamwambia,
\v 2 Kila mtu atapanga kulingana na mahali pake, pamoja na mabango ya baba zao. Watapanga kuzunguka hema ya kukutania kila upande.
\s5
\v 3 Wale watakaopanga mashariki mwa hema ya kukutania, mahali ambapo juu huonekana wakati wa jua kuchomoza, ni makambi ya Yuda nao watakuwa katika kundi lao. Nashoni mwana wa Aminadabu ni kiongozi wa watu wa Yuda.
\v 4 Idadi ya watu wa Yuda ni 74, 600.
\s5
\v 5 Kabila la Isakari litapanga mbele ya Yuda. Nethaneli mwana wa Zuari ataliongoza jeshi la Isakari.
\v 6 Idadi ya kikosi chake ni wanaume 54, 000.
\s5
\v 7 Kabila la Zabuloni litapanga mbele ya Isakari. Eliabu mwana wa Heloni ndiye atakayeliongoza jeshi la Zabuloni.
\v 8 Idadi ya kikosi chake ni 57, 400.
\s5
\v 9 Idadi yote ya kambi y a Yuda ni 186, 400. Watakuwa wa kwanza kuondoka.
\s5
\v 10 Upande wa kusini kutakuwa na kambi ya Reubeni katika kundi lao. Kiongozi wa kundi la Reubeni ni Elizuri mwana wa Shedeuri.
\v 11 Idadi ya kikosi chake ni 46, 500.
\s5
\v 12 Simeoni atapanga mbele ya Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Zurishadai.
\v 13 Waliohesabiwa kwenye kikosi chake ni 59, 300.
\s5
\v 14 Kabila la Gadi litafuatia. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deuli.
\v 15 Idadi ya kikosi chake ni 45, 650.
\s5
\v 16 Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Reubeni, kulingana na kikosi chake, ni 151, 450. Watakuwa wa pili kuondoka.
\s5
\v 17 Kifuatacho, ni hema la kukutania kuondoka kambini pamoja na Walawi likiwa katikati ya kambi zote. Lazima waondoke hapo kambini kwa mpangilio huo kama walivyoingia kwenye kambi. Kila mwanamume lazima awe mahali pake kwa kufuata bango lake.
\s5
\v 18 Migawanyiko ya kambi y Efraimu kufuata mahali pake. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.
\v 19 Hesabu ya kikosi hiki ni 40, 500.
\s5
\v 20 Baada ya hao lilifuata kabila la Manase. Kiongozi wa Manase ni Gamaliel mwana wa Pedazuri.
\v 21 Hesabu ya kikosi hiki ni 32, 200.
\s5
\v 22 Kabila litakalofuata ni la Benjamini. Kiongozi wa Benjamini n Abidani mwana wa Gidioni.
\v 23 Hesabu ya kikosi hiki ni 35, 000
\s5
\v 24 Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu ni 108, 100. Watakuwa wa tatu kuondoka.
\s5
\v 25 Upande wa kaskazini kutakuwa na kambi ya kikosi cha Dani. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
\v 26 Hesabu ya kikosi hiki ni 62, 700.
\s5
\v 27 Watu wa kabila ya Asheri watapanga mbele ya Dani. Kiongozi wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okirani.
\v 28 Hesabu ya Kikosi hiki ni 41, 500.
\s5
\v 29 Kabila la Naftali ndilo litakalofuatia. Kiongozi wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.
\v 30 Hesabu ya kikosi hiki ni 53, 400.
\s5
\v 31 Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Dani ni 157, 600. Hawa watakuwa wa mwisho kuondoka kambini, wakifuata bango lao.
\s5
\v 32 Hawa ndio Waisraeli, waliohesabiwa kufuata familia zao. Wote waliohesabiwa kwenye kambi zao, kwa kufuata vikosi vyao ni 603, 550.
\v 33 Lakini Musa na Haruni hawakujumuisha Walawi kwenye Hesabu ya Waisrael. Ilikuwa kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Musa.
\s5
\v 34 Watu wa Israel walifanya yote ambayo BWANA alimwagiza Musa. Walipanga kwa kufuata mabango yao. Walisafiri kutoka kambini kwa kufuata jamaa zao, kwa mpangilio wa familia za koo zao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa hii ndiyo historia ya uzao wa Haruni na Musa wakati BWANA aliposema na Musa kwenye mlima Sinai.
\v 2 Majina ya watoto wa Haruni walikuwa Nadabu ambaye ndiyo mtoto wa kwanza, na Abihu, na Eliezeri, na Ithamari.
\s5
\v 3 Haya ndiyo majina ya wana wa Haruni, makuhani waliokuwa wamepakwa mafuta na kuwekwa wakfu kutumika kama makuhani.
\v 4 Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya BWANA walipomtolea moto usiokubalika walipokuwa katika nyika ya Sinai. Nadabu na Abihu hawakuwa na watoto, kwa hiyo Eliazari na Ithamari walitumika kama makuhani pamoja na baba yao.
\s5
\v 5 BWANA alinena na Musa, akamwambia,
\v 6 "Walete kabila ya Lawi na uwaweke kwa Haruni kuhani ili wamsaidie
\s5
\v 7 Nao lazima wafanye majukumu badala ya Haruni na jumuiya yote mbele ya hema ya kukutania. Lazima watumike hemani.
\v 8 Watayatunza mapambo ya hema ya kukutania, na watawatumikia makabila ya Israel kwa huduma ya hemani.
\s5
\v 9 Uwaweke Walawi kwa Haruni na watoto wake. Nimewatoa kikamilifu ili wamsaidie kuwatumikia watu wa Israel.
\v 10 Umchague Haruni na watoto wake kuwa makuhani, lakini mgeni yeyote atakayekaribia lazima auawe."
\s5
\v 11 BWANA alinena na Musa. akamwambia,
\v 12 "Tazama, nimewachagua Walawi katika watu wa Israel. Nimefanya hivyo badala ya kuchukua mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wana wa Israel. Hawa Walawi ni wangu.
\v 13 Na hata wazaliwa wa kwanza ni mali yangu. Katika siku ambyo niliwavamia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, Niliwatenga wazaliwa wa kwanza wa Israeli kwa ajili yangu, watu na wanyama pia. Ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA."
\s5
\v 14 BWANA alinena na Musa katika nyika ya Sinai. Akasema,
\v 15 "Wahesabu uzao wa Lawi katika kila familia, katika nyumba za koo zao. Hesabu kila mume kuanzia mwezi mmoja au zaidi."
\v 16 Musa aliwahesabu, kufuata maelekezo ya BWANA, kama alivyoamriwa kufanya.
\s5
\v 17 Majina ya watoto waLawi yalikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
\v 18 Ukoo uliotokana na watoto wa Gerishoni walikuwa ni Libni na Shimei.
\v 19 Ukoo uliotokana na watoto Kohathi walikuwa ni Amramu na, Izihari, Hebroni, na Uzieli.
\v 20 Ukoo uliotokana na watoto wa Merari walikuwa ni Mahili na Mushi. Hizi ndizo koo za Walawi, zilizoorodheshwa ukoo kwa ukoo.
\s5
\v 21 Koo za Walibini na Washimei zilitokana na Wagerishoni. Hizi ndizo koo za Wagerishoni.
\v 22 Wanaume wote wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa na kufikia idadi ya 7, 500.
\v 23 Koo za Wagerishoni watapanga upande wa magharibi wa hema.
\s5
\v 24 Eliasafu mwana wa Laeli ataongoza koo za uzao wa Wagerishoni.
\v 25 Familia ya Gerishoni watalilinda hema la kukutania pamoja na hiyo masikani. Watalilinda hema, kifuniko chake, na lile pazia la lango la hema ya kukutania.
\v 26 Wataulinda ua, lile pazia la kwenye lango--ua unaozunguka mahali patakatifu na madhabahu. Watazilinda kamba za hema ya kukutania na vyote vilivyomo.
\s5
\v 27 Koo zifuatazo zinatokana na Kohathi: ukoo wa Waamrami, ukoo wa Waizihari ukoo wa Wahebroni, na ukoo wa Wauzieli. Koo hizi zinatokana na Wakohathi.
\v 28 Wanaume 8, 600 wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa ili kulinda vitu vya BWANA.
\v 29 Familia ya uzao wa Kohathi watapanga upande wa kusini wa Hema.
\s5
\v 30 Elizafani mwana wa Uzieli ndiye atakayeongoza ukoo wa Wakohathi.
\v 31 Watalilinda sanduku, meza, vikalishio vya taa, madhabahu, vitu vitakatifu ambvyo hutumika katika huduma yao, pazia, na kazi zote zinazoambatana na hema.
\v 32 Eliazari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza wanaume wanaowaongoza Walawi. Atawasimamia wanaume wanaongoza eneo takatifu.
\s5
\v 33 Koo mbili zimetoka kwa Merari: Ukoo wa Mahili na ukoo wa Mushi. Koo hizi zimetokana na Merari,
\v 34 Wanaume 6, 200 wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi walihesabiwa.
\v 35 Zurieli mwana wa Abihaili ataongoza ukoo wa Merari. Hawa watapanga upande wa kaskazini mwa hema.
\s5
\v 36 Uzao wa Merari utatunza mbao za hema, mataruma, nguzo, makalishio, viifaa vya ujenzi na vitu vyote vinavyohusika,
\v 37 na nguzo za ua zinazozunguka hema, makalishio, vigingi na kamba zake.
\s5
\v 38 Musa na Haruni na watoto wake watapanga upande wa mashariki wa masikani, mbele ya hema ya kukutania kuelekea mawio ya jua. Wao wataajibika na majukumu ya mahali patakatifu na majukumu ya wana wa Israeli. Mgeni atakayekaribia mahali patakatifu auawe.
\v 39 Musa na Haruni wakawahesabu wanaume wote wa ukoo wa Walawi walikuwa na umri wa mwezi mmoja na zaidi, kama vile BWANA alivyokuwa ameagiza.. Walihesabu wanaume ishirini na mbili elfu.
\s5
\v 40 BWANA alisema na Musa, "Wahesabu wanaume wote ambo ni wazaliwa wa kwanza wa Israeli ambao wana umri wa mwezi mmoja na zaidi. Orodhesha majina yao.
\v 41 Unitwalie walawi kwa ajili yangu badala ya wazaliwa wa kwanza wa Israeli, Mimi ndimi BWANA. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa uzao wa Israeli,"
\s5
\v 42 Musa akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli kama BWANA alivyomwagiza kufanya.
\v 43 Aliwahesabu wazaliwa wote wa kwanza kwa mjina, wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi. Alihesabu wanaume 22, 273.
\s5
\v 44 Tena BWANA alinena na Musa. Akasema,
\v 45 "Watwae Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa wana wa Israeli. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wanyama wa Waisreli wengine. Walawi ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.
\s5
\v 46 Unikusanyie shekeli tano za wokovu kwa kila hao 273 za hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli za hao wanaozidi idadi ya Walawi.
\v 47 Utazitumia hizo shekeli tano kwa kipimo cha mahali patakatifu. Shekeli moja ni sawa na gera ishirini.
\v 48 Utawalipa hizo shekeli za wokovu kwa Haruni na wanawe."
\v 49 Kwa hiyo Musa akakusanya shakeli za wokovu kutoka kwa wale waliozidi idadi ya wale waliookolewa na Walawi.
\v 50 Musa akakusanya zile fedha kutoka kwa hao wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli. Alikusanya jumla ya shekeli 1, 365, zenye kipimo sawa na mahali patakatifu. Musa akamlipa Haruni na wanawe hizo shekeli za wokovu.
\v 51 Musa akafanya kila kitu alichoagizwa na neno la BWANA kama BWANA alivyomwagiza.
\s5
\c 4
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa na Haruni. Akasema,
\v 2 Fanya sensa ya uzao waume wa Kohathi kutoka kwa Walawi, kwa kufuata jamaa na na familia za koo.
\v 3 Uwahesabu wanaume ambao wana umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Hawa wataungana na kundi linalotumika kutoa huduma kwenye hema ya kukutania.
\v 4 Uzao wa Kohathi watalinda vile vitu vitakatifu zaidi vilivyohifadhiwa kwa ajili yangu katika hema ya kukutania.
\s5
\v 5 Wakati kambi inapojiandaa kusonga mbele, Haruni na wanawe lazima waende hemani, kulishusha pazia linalotenganisha mahali patakatifu na kulifunika sanduku la ushuhuda kwa pazia hilo. Watalifunika hilo sanduku kwa ngozi za pomboo.
\v 6 Watatandika juu yake nguo za rangi ya samawi. Watachomeka hiyo miti ya kubebea.
\s5
\v 7 Watatandika nguo ya rangi ya samawi kwenye meza ya mikate ya wonyesho. Juu yake wataweka sahani, vijiko, mabakuli na vikombe vya kumiminia. Mikate itakuwepo daima mezani.
\v 8 Wataifunika na nguo ya rangi nyekundu na ngozi za pomboo. na kuweka miti ya kubebea.
\s5
\v 9 Watachukua nguo ya rangi ya samawi na kukifunika kinara, pamoja na taa zake, na koleo zake, na sahani zake na vikombe vyake vya kuwekea mafuta ya taa.
\v 10 Wataweka kinara na vifaa vyake vikiwa vimefunikwa na ngozi ya pomboo, na wataweka kwenye miti ya kukibebea.
\v 11 Watafunika na nguo ya samawi katika madhabau ya dhahabu. Wataifunika na ngozi za pomboo, na kuweka ile miti ya kubebea.
\s5
\v 12 Watavichukua vyombo vyote vya kazi takatifu na kuvizonga kwenye hiyo nguo ya rangi ya samawi. Watavifunika na ngozi za pomboo na kuviweka hivyo vyombo kwenye miti ya kubebea.
\v 13 Watayaondoa majivu kwenye madhabahu na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake.
\v 14 Watavieka kwenye miti ya kubebea vyombo vyote wanavyovitumia kwa kazi ya madhabahuni. Vyombo hivi ni vyetezo, majembe, mabakuli na vitu vingine vya madhabahuni. Wataifuniks madhabahu na ngozi za pomboo na kuweka ile miti ya kubebea.
\s5
\v 15 Wakati Haruni na wanawe walipokuwa wamekamilisha kupafunika mahali patakatifu na vyombo vyote, na kambi itakapoanza kuendelea mbele, ndipo wana wa Kohathi watakapokuja kubeba vitu vya mahali patakatifu. Kama watagusa vyombo vitakatifu, lazima watakufa. Hii ni kazi ya wana wa uzao wa Kohathi, kubeba mapambo ya hema ya kukutania.
\v 16 Eliazari mwana wa Haruni kuhani atalinda na kusimamia mafuta ya taa, ubani mzuri, sadaka za mara kwa mara na mafuta ya upako. Atasimamia ulinzi wa hema lote na vyote vilivyomo, mahali patakatifu na vyombo vyake."
\s5
\v 17 BWANA akanena na Musa na Haruni. Akasema,
\v 18 Usiruhusu kabila la Wakohathi kuondolewa kati ya Walawi.
\v 19 Walinde waishi ili wasije wakafa, kwa kufanya hivi. Wanapokuwa wanasogelea
\v 20 wasije wakaingia ndani ili kuona eneo takatifu hata kwa kitambo, vinginevyo watakufa. Bali Haruni na wanawe wanaweza kuingia, ndipo Haruni na Wanawe watakapowapangia Wakohathi kazi maalumu ya kufanya, kwa kila mmoj."
\s5
\v 21 BWANA akanena na Musa tena, Akasema, "Fanya sensa kwa wana Gerishoni pia, kwa kufuata familia za mababu zao, koo zao.
\v 22 Uwahesabu wale wenye umri wa mika thelathini hadi miaka hamsini.
\v 23 Uwahesabu wote ili waje kuungana na wale wanaotumika katika hema ya kukutania.
\s5
\v 24 Hii ndiyo itakuwa kazi ya koo za Gerishoni, wanapotumikia na wanachobeba.
\v 25 Watabeba pazia la masikani, hema la kukutania, na vifunikio vyake, vifuniko vya ngozi ya pomboo ambvyo viko juu yake, na pazia kwenye lango la hema ya kukutania.
\v 26 Watabeba pazia la ua, pazia la kwenye mlango wa ua, ambao uko karibu na maskani karibu na madhabahu, kamba zake na vifaa vyote vya utumishi wake. Chochote kinachotakiwa kufanywa kutokana na vitu hivi, wao ndio watakaofanya.
\s5
\v 27 Haruni na wanawe ndio watakaongoza utumishi wa uzao wa Wagerishoni, kwa vitu vyote vile vya kusafirisha, na katika utumishi wao wote. Lazima uwagawie majukumu yao yote.
\v 28 Huu ndio utumishi wa koo za uzao wa wana wa Wagerishoni katka hema ya kukutania. Ithamari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza katika utumishi.
\s5
\v 29 Utawahesabu uzao wa Merari kwa koo zao, na uwapange katika familia za mabau zao,
\v 30 kuanzia wenye umri wa miaka thelatini hadi miaka hamsini. Umuhesabu kila atakayeungana na kundi lenye utumishi katika hema ya kukutania.
\s5
\v 31 Huu ndio wajibu na kazi yao katika utumishi wao kwenye hema ya kukutania. Watazilinda mbao za maskani, mataluma yake, nguzo na makalishio yake,
\v 32 pamoja na nguzo za ua zinazozunguka masikani, makalishio yake, vigingi na kamba zake, na vifaa vinginevya ujenzi. Waorodheshe kwa majina na majukumu yao.
\s5
\v 33 Huu ndio utumishi wa koo za uzao wa Merari, ambao wanatakiwa kufanya katika hema ya kukutania, chini ya uongozi wa Ithmari mwana wa Haruni kuhani."
\s5
\v 34 Musa na Haruni na viongozi wa watu waliwahesabu wana wa uzao wa Wakohathi kwa kufuata koo za familia za mababu zao.
\v 35 Waliwahesabu wale wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Walimhesabu kila mmoja aliyepaswa kuungana na kundi linalotoa huduma ya utumishi kwenye hema ya kukutania.
\v 36 Waliwahesabu wanaume 2, 750 kwa kufuata koo zao.
\s5
\v 37 Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote kutoka koo na familia za Wakohathi ambao hutumika kwenye hema ya kukutania. Walifanya hivi kwa kumtii BWANA aliyewaagiza kupitia kwa Musa.
\s5
\v 38 Uzao wa Gerishoni walihesabiwa kufuata koo na familia za mababu zao,
\v 39 kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini, kwa kila mmoja aliyetakiwa kuungana na watu wanaotoa huduma kwenye hema ya kukutania.
\v 40 Wanaume wote waliohesabiwa kufuata koo na familia za mababu zao walikuwa 2, 630.
\s5
\v 41 Musa na Haruni walizihesabu koo za uzao wa Gerishoni ambao watatumika kwenye hema ya kukutania. Walifanya hivi ili kutii ambacho BWANA aliwaamuru kufanya kuptia kwa Musa.
\s5
\v 42 Uzao wa Merari walihesabiwa kwa koo kupitia familia za mababu zao,
\v 43 kuanzia wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini, kila anayepaswa kuungana na watu wanaotumika kwenye hema ya kukutania.
\v 44 Wanaume wote waliohesabiwa kupitia koo za familia za mababu zao walikuwa 3. 200.
\s5
\v 45 Musa na Haruni waliwahesabu wanaume hawa, uzao wa Merari. Kw kufanya hivi walitii amri ya BWANA aliyowaaagiza kufanya kupitia kwa Musa.
\s5
\v 46 Kwa hiyo Musa na Haruni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kw kufuata koo na familia za mababu zao
\v 47 kuanzia wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. walimhesabu kila aliyepaswa kufanya kazi kwenye masikani, na kila aliyepaswa kubeba na kulinda vitu vya kwenye hema ya kukutania.
\v 48 Waliwahesabu wanaume 8, 580.
\s5
\v 49 Kwa agizo la BWANA, Musa alimhesabu kila mwanamume na kutunza kumbukumbu ya kazi ambayo kila mmoja anaweza kufanya. Kwa hivyo, walitii kile ambacho BWANA alikuwa amewaagiza kufanya kupitia kwa Musa.
\s5
\c 5
\p
\v 1 BWANA alinena na Musa. Akasema,
\v 2 "Waamuru wana wa Israel wawatoe watu wote wenye magonjwa ya ngozi yanayoambukiza, na kila mwenye mwenye vidonda vinavyotoa harufu, na ambaye amenajisika kwa kugusa maiti.
\v 3 Awe mme au mke, umtoa kambini. Ili wasije wakaitia unajisi kambi, kwa sababu Mimi huishi ndani yake,"
\v 4 Watu wa Israeli walifanya hivyo. Waliwatoa kambini, Kama BWANA alivyomwagiza Musa. Watu wa Israeli walimtii BWANA.
\s5
\v 5 Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,
\v 6 "Nena na wana wa Israeli. mtu mume na mtu mke akifanya dhambi yeyote ambayo watu hufanyiana wao kwa wao, na mtu huyo akamwasi BWANA, mtu huyo atakuwa na hatia.
\v 7 Ndipo huyo mtu ataungama hiyo dhambi aliyoifanya. Mtu huyo atarudisha malipo ya hatia yake na kuongeza kwenye malipo hayo sehemu ya tano zaidi. Atamlipa huyo aliyemtendea makosa
\s5
\v 8 Lakini kama huyo mtu huyu aliyetendewa kosa hana ndugu wa kupokea hayo malipo, basi atalipa hayo malipo ya hatia kwangu kupitia kuhani pamoja na kondoo dume kwa ajili ya sadaka yake mwenyewe.
\v 9 Kila sadaka ya wana wa Israeli, vitu ambavyo vimetengwa na vikaletwa kwa kuhani na watu wa Israeli, vitakuwa vyake.
\v 10 Sadaka ya kila mtu itakuwa ya kuhani; kama mtu yeyote atatoa kitu chochote kwa kuhani, kitakuwa chake."
\s5
\v 11 Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,
\v 12 "Nena na wana wa Israel. Uwaambie, 'kama mke wa mtu ataasi na kufanya dhambi dhidi ya mume wake.
\s5
\v 13 Halafu mtu mwingine akalala naye. Kwa sababu, hiyo atakuwa amenajisika. Na hata kama mume wake hakuona na hajui, hata kama hakuna mtu aliyemkamta akiwa katika tendo na hakuna mtu wa kushuhudia dhidi yake; hata hivyo ile roho ya wivu itaendele kumjulisha yule mume kuwa mke wake amenajisika.
\v 14 Ingawa, roho ya wivu inaweza kumdanganya yule mwanamume wakati mke wake hajanajisika.
\s5
\v 15 Kwa mazingira hayo, yule mwanamume anapaswa kumpeleka mke wake kwa kuhani. Yule mwanamume anapaswa kutoa sadaka ya divai kwa ajili yake. Atapaswa kuleta sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri. Asitie mafuta juu yake wala asitie ubani juu yake maana ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho wa uovu.
\s5
\v 16 Ndipo kuhani atasogeza karibu na kumweka mbele ya BWANA.
\v 17 Kuhani atachukua kikombe cha maji matakatifu na atachukua mavumbi ya kwenye masikani. Ataweka yale mavumbi kwenye maji.
\s5
\v 18 Kisha kuhani atamweka huyo mwanamke mbele za BWANA na atazifungua nywele kichwani kwa huyo mwanamke. Atamwekea mikononi mwake hiyo sadaka ya unga kwa ajili ya ukumbusho, ambayo ni sadaka ya unga kwa ajili ya wivu.
\v 19 Kuhani atashikilia mikononi mwake maji machungu yanayoweza kuleta laana. Kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya kiapo na kumwambia. 'Kama haujafanya uzinzi na mwanaume mwingine, na kama hajakengeuka na kufanya uovu, basi utakuwa huru na maji haya yanayoweza kuleta laana.
\s5
\v 20 Lakini kama wewe, mwanamke uliye chini ya mume wako, umekengeuka, na kama umenajisika, na kama mwanamume mwingina amelala nawe,
\v 21 ndipo, (kuhani atamtaka huyo mwanamke aape kiapo kinachoweza kuleta laana kwake, na kwamba ataendelea kumwambia yule mwanamke) 'BWANA atakufanya wewe kuwa laana itakayooneshwa kuwa hivyo kwa watu wako. Hii itatokea pale BWANA atakapoyafanya mapaja yako kuoza na tumbo lako kuvimba.
\v 22 Haya maji ambayo huleta laana yataingia tumboni mwako na kulifanya tumbo lako kuvimba na mapaja yako kuoza,' mwanamke alitakiwa kujibu, 'Ndiyo, hayo yanipate kama mimi ni mwenye hatia.'
\s5
\v 23 Naye kuhani ataziandika laana hizi kwenye kitabu, na kisha kuzifuta laana zilizoandikwa kwa maji ya uchungu.
\s5
\v 24 Naye kuhani atamwelekeza yule mwanamke kunywa yale maji machungu yaletayo laana. Yale maji yaletayo laana yataingia na kuwa machungu.
\v 25 Kuhani ataitwaa ile sadaka ya unga ya wivu mikononi mwa yule mwanamke. Atailekeza ile sadaka ya unga mbele ya BWANA na kuileta madhabahuni.
\v 26 Kuhani atachukua konzi ya sadaka ya unga mkononi mwake kama sadaka ya kuwakilisha, na kuiteketeza madhabahuni. Ndipo atakapompatia mwanamke yale maji machungu ili ayanywe.
\s5
\v 27 Wakati wa kumpa yale maji ili anywe, kama amenajisika kwa sababu alifanya uovu dhidi ya mume wake, ndipo yale maji yaletayo laana yatamwingia na kuwa machungu. Tumbo lake litavimba na paja lake litaoza. Yule mwanamke atalaaniwa kati ya watu wake.
\v 28 Lakini kama yule mwanake hajanajisika na kama ni msafi, basi atakuwa huru. Tena ataweza kubeba uja uzito.
\s5
\v 29 Hii ndiyo sheria ya wivu. Ni sheria ya mwanamke anayekengeuka kwa mumewe na kunajisika.
\v 30 Ni sheria ya mwanamume mwenye roho ya wivu kwa mkewe. Atamleta mwanamke mbele ya BWANA, na kuhani atamfanyia huyo mwanamke kila kitu ambacho sheria ya wivu inamtaka kufanya.
\s5
\v 31 Yule mwanamume atakuwa hana hatia kwa kumleta mke wake kwa kuhani. Na yule mwanmke atauchukua uovu wake."
\s5
\c 6
\p
\v 1 BWANA alinena na Musa. Akamwabia,
\v 2 'Nena na wana wa Israeli, uwaambie, 'Kama mume au mke ataweka nadhiri kwa BWANA kwa kiapo maalumu cha mnadhiri, ndipo atajiepusha na divai na vileo. hatakunywa siki itokanayo na divai.
\v 3 Asinywe kileo kitokanacho na siki au kilevi. Asinywe maji ya divai yeyote au kula zabibu mbichi wala zilizokauka.
\v 4 Katika siku zote ambazo amejitenga kwa ajili yangu, asile chochote kinachotokana na zabibu, wala kitu chochote kitokanacho na makokwa hadi maganda.
\s5
\v 5 Wakati wote wa nadhiri yake, wembe usiipite kichwani mwake mpaka siku zake za nadhiri kwa BWANA zitimilike. Lazima ajitenge kwa BWANA. Ataziacha nywele zake zikue kichwani mwake.
\s5
\v 6 Wakati wote wa kujidhiri kwake kwa BWANA, asiikaribie maiti.
\v 7 Asijinajisi kwa namna yeyote hata kama atakufa baba yake, mama, dada, au ndugu yake. Hii ni kwa sababu amejitenga kwa ajili ya Mungu, kama ambavyo kila mmoja anavyoweza kumuona kwa uerfu wa nywele zake.
\v 8 Wakati wote wa kujidhiri kwake atakuwa mtakatifu, alijitunza kwa ajili ya BWANA.
\s5
\v 9 Ikitokea mtu amekufa ghafla pembeni yake na kukitia unajisi kichwa chake kitakatifu, ndipo atakaponyoa kichwa chake katika siku ya kujitakasa --Siku ya saba atanyoa kichwa chake.
\s5
\v 10 Siku ya nane atamletea kuhani njiwa wawili au makinda mawili ya njiwa kwenye lango la hema ya kukutania.
\v 11 Naye kuhani atamtoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa. Hawa watafanyika sadaka ya upatanisho kwake kwa sababu atakuwa ametenda dhambi ya kuwa karibu na mfu. Atatakasika kichwa chake siku hiyo.
\s5
\v 12 Atajitenga kwa BWANA tena katika siku hizo za utakaso. Ataleta kondoo mume mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Zile siku zake kabla ya kunajisika hazitahesabiwa, kwa sababu kujiweka wakfu kwake kulinajisika.
\s5
\v 13 Hii ndiyo sheria ya mnadhiri wakati wa muda wa kujidhiri unapokuwa umetimia. Ataletwa kwenye mlango wa hema ya kukutania.
\v 14 Ataleta sadaka yake kwa BWANA. Atatoa mwanakondoo mume wa mwaka mmoja asiye na hila kama sadaka ya kuteketezwa. Ataleta kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na hila kama sadaka ya dhambi. Ataleta kondoo mume asiye na hila kama sadaka ya amani.
\v 15 Ataleta kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila amira, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, mikate ya kaki isiyo na amira iliyopakwa mafuta, pamoja na sadaka za unga na sadaka za vinywaji.
\s5
\v 16 Kuhani atawaleta mbele za BWANA. Atazitoa hizo sadaka zake za dhambi na kuteketezwa.
\v 17 Na kikapu cha mikate isiyowekwa amira, atamtoa yule kondoo mume kama sadaka ya amani kwa BWANA. Pia kuhani atatoa hiyo sadaka ya unga na sadaka ya vinywaji.
\s5
\v 18 Mnadhiri atanyoa nywele zake kama ishara ya kujitenga kwa ajili ya Mungu kwenye mlango wa hema ya kukutania. Atazitoa nywele zake kichwani kwake na kuzichoma kwa moto ulio chini ya sadaka ya amani.
\s5
\v 19 Kuhani atachukua bega la kondoo mume lililotokoswa, na mkate usiotiwa amira toka kikapuni, na mkate mmoja wa kaki usiotiwa amira. Atauweka kwenye mikono ya Mnadhiri baada ya kuwa amenyoa nywele kwa ishara ya kujidhiri.
\v 20 Kisha kuhani atavitikisa kuwa sadaka kwa BWANA, sehemu takatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa na paja lililotolewa kwa kwa kuhani. Baadaye, Mnadhiri anaweza kunywa divai.
\s5
\v 21 Hii ndiyo sheri ya Mnadhiri anayeapia sadaka yake kwa BWANA kwa ajili ya kujidhiri kwake. Chochote atakachotoa, lazima afanye kama alivyoapa, kuilinda ahadi yake kama ilivyoaniswa katika sheria ya Mnadhiri.
\s5
\v 22 Tena BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 23 "nena na Harunu na wanawe. Uwaambie, 'mtawabariki wana wa Israeli kwa njia hii. Mtawaambia,
\v 24 BWANA na awabariki na kuwatunza.
\s5
\v 25 BWANA na awaangazie nuru ya uso wake na awe mwenye neema kwenu.
\v 26 BWANA na awatazame kwa neema na awape amani.'"
\v 27 Ni kwa jinsi hii kwamba wanaweza kuwapa jina langu wana wa Israeli."
\s5
\c 7
\p
\v 1 Siku ambayo Musa alikamilsha masikani, alitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA, pamoja na mapambo yake. Aliifanyia hivyo madhabahu na vyombo vyake. Aliitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA.
\v 2 Siku hiyo, viongozi wa Israeli na wale vichwa vya familia za mababu walitoa sadaka. Hawa wanaume walikuwa viongozi wa makabila. Walisaidia kuhesabu watu kwenye ile sensa.
\v 3 Walileta sadaka zao kwa BWANA. Walileta magari sita yaliyofunikwa na mafahari kumi na mbili. Walileta gari moja kwa kila viongozi wawili, kila kiongozi alileta fahari moja. Walileta vitu hivi mbele ya masikani.
\s5
\v 4 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 5 "Uzipokee hizo sadaka kutoka kwao na uzitumie kwa matumizi ya kazi ya hema ya kukutania. Uwape hizo sadaka Walawi, kwa kila mmoja kadri ya uhitaji wa kazi yake."
\s5
\v 6 Musa akayatwaa yale magari na mafahari. na kuwapatia Walawi.
\v 7 Aliwapa magari mawili na mafahari wanne wale wa uzao wa Gerishoni, kwa sababu ndivyo kazi yao ilivyohitaji.
\v 8 Aliwapatia uzao wa Merari magari manne na mafahari nane, chini ya uangalizi wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Alifanya hivi kwa sababu ya uhitaji wa kazi yao.
\s5
\v 9 Lakini wale wa uzao wa Kohathi hakuwapa chochote kwa sababu wao waliangalia vitu vtakatifu amabvyo vilipaswa vibebwe mabagani mwao, siyo kwa magari.
\s5
\v 10 Viongozi walitoa bidhaa zo zingine kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu katika siku ile ambayo Musa aliitia mafuta madhabahu. Viongozi walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu hiyo.
\v 11 BWANA akasema na Musa, "kila kiongozi atatoa sadaka kwa siku yake kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu."
\s5
\v 12 Katika siku ya kwanza, Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda, alitoa sadaka yake.
\v 13 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja ya fedha ambayo uzito wake ni shekeli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 14 Pia alimpa unga wa dhahabu kiasi cha bakuli moja chenye uzani wa shekeli kumi kilichojaa ubani
\s5
\v 15 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
\v 16 Alitoa beberu kama kama sadaka ya hatia.
\v 17 Alitoa makisai mbili, kondoo waume watano, beberu watano na wanakondoo dume watano wenye umri wa mwaka mmoja mmoja, kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
\s5
\v 18 Siku ya pili, Nethanel mwana wa Zuari, kiongozi wa Isakari, alitoa sadaka yake.
\v 19 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha ya uzito wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa sheli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Viyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga.
\s5
\v 20 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, iliyojaa ubani.
\v 21 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo mmoja dume.
\v 22 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 23 Alitoa makisai wawili, Kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hiii likuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Zuari.
\s5
\v 24 Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa uzao wa Zabuloni alitoa sadaka yake.
\v 25 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. vyombo vyote hivi vilikuwa vimeja unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 26 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 27 Alitoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja.
\v 28 Alitoa beberu mmoja kama sadaka ya dhambi.
\v 29 Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja. kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana Heloni.
\s5
\v 30 Siku ya nne, Elizuri mwana wa shedeuri, kiongozi wa uzao wa Reubeni, alitoa sadaka yake.
\v 31 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 32 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichoo jaa ubani.
\s5
\v 33 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, mwanakondoo dume mmoja mchanga wa mwaka mmoja.
\v 34 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 35 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Elizuri mwana wa Shedeuri.
\s5
\v 36 Siku ya tano, Shelumieli mwana wa Zurishadai, kiongozi wa uzao wa Simeoni, alitoa sadaka yake.
\v 37 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekali 130 na bakuli mojala fedha lenye uzani wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 38 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, uliojaa ubani.
\s5
\v 39 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, dume la kondoo, na dume la mwanakondoo la mwaka mmoja.
\v 40 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 41 Alitao maksai wawili, dume wawili wa kondoo, beberu watano, na dume watano wa wanakondoo wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka y amani. Hiindiyo iliyokuwa sadka ya Shelumei mwana wa Zurishadai.
\s5
\v 42 Siku ya sita, Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa uzao wa Gadi, alitoa sadaka yake.
\v 43 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga.
\v 44 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 45 Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari changa, kondoo dume mmoja, na dume la mwanakondoo mmoja wa mwaka mmoja.
\v 46 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 47 Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.
\s5
\v 48 Siku ya saba, Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa uzao wa Efraimu, alitoa sadaka yake.
\v 49 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 50 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu, kilichojaa ubani
\s5
\v 51 Alitoa sadaka ya kuteketezwa, fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
\v 52 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 53 Alitoa maksai wawili, kondo dume watano, beberu watano, na na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sdaka ya Elishama mwana wa Amidu.
\s5
\v 54 Siku y a nane, Gamaliel mwana wa Pedazuri, kiongozi wa uzao wa Manase, alitoa sadaka yake.
\v 55 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 56 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 57 Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
\v 58 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 59 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Gamaliel mwana wa Pedazuri.
\s5
\v 60 Siku ya tisa, Abidani mwana wa Gidioni, kiongozi wa uzao wa Benjamini, alitoa sadaka yake.
\v 61 Sadaka yake ilikuwa sahani moja yafedha yenye uzani wa sheli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 62 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 63 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
\v 64 Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 65 Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gidioni.
\s5
\v 66 Siku ya kumi, Ahizeri mwana wa Amishadai kiongozi wa Dani alitoa sadaka yake.
\v 67 Alitoa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 68 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 69 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
\v 70 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 71 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja, kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahizeri mwana wa Amishadai.
\s5
\v 72 Siku ya kumi na moja. Pagieli mwana wa Okrani kiongozi wa uzao wa Asheri alaitoa sadaka yake.
\v 73 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabani, kwa kipimo cha shekeli ya mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 74 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 75 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga. dume la kondoo moja, dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
\v 76 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 77 Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
\s5
\v 78 Siku ya kumi na mbili., Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa uzao wa Naftali, alitoa sadaka yake.
\v 79 Sadaka yake ailikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba ulichanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
\v 80 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
\s5
\v 81 Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na mwanakondoo dume moja wa mwaka mmoja.
\v 82 Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 83 Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahra mwana wa Enani.
\s5
\v 84 Viongozi wa Israeli waliviweka wakfu hivi vitu vyote siku ambayo Musa alimimina mafuta kwenye madhabahu. Waliziweka wakfu zile sahani kumi na mbili za fedha, Bakuli kumi na mbili za fedha, na vijiko kumi na vili vya dhahabu.
\v 85 Zile sahani za fedha kila moja ilikuwa na uzani wa shaekeli 130 na kila bakuli ye fedha ilikuwa na uzani wa shekeli sabini. Vyombo vyote vya fedh vilikuwa na ujumla ya uzani wa shekeli 2, 400, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu.
\v 86 Vile vijiko vya dhahabu vilivyokuwa vimejaa ubani, vilikuwa na uzani wa shekeli kumi kila kimoja. Vijiko vyote vya dhahabu vilikuwa na uzani wa shekeli 120.
\s5
\v 87 Waliwatenga wanyama wote kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, fahari kumi na wawili, kondoo dume kumi na wawili, na wanakondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja mmoja. Walitoa sadaka yao ya unga. Walitoa beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi.
\v 88 Kutokana na ng'ombe zao, walitoa fahari ishirini na nne, kondoo dume sitini beberu sitini, na wanakondoo dume sitini wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa kwa ajiliya kuiweka wafu ile madhabahu baada ya kumiminiwa mafuta.
\s5
\v 89 Musa alipoingia kwenye hema ya kukutania kusema na BWANA, ndipo alipoisikia sauti yake ikisema naye. BWANA alinena naye kutoka juu ya kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, kutoka katikati ya makerubi. Alinena naye.
\s5
\c 8
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 2 "Sema na Haruni umwambie, 'zile taa saba lazima zimulike mbele ya kinara utakapoziwasha,"
\s5
\v 3 Haruni alifanya haya. Aliziwasha zile taa juu ya kinara ili ziangaze mbele yake kama BWANA alivyomwagiza Musa.
\v 4 Kinara kilitengenezwa kwa njia hii kama BWANA alivyomwelekeza Musa muundo wake. Kiitakaiwa kutengenezwa kwa dhahabu kuanzia kwenye kitako chake hadi juu, ndivyo kilivyotakiwa kutengenezwa kwa dhahabu kwa maua hadi juu.
\s5
\v 5 Tena, BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 6 '"Uwatwae Walawi kati ya wana wa Israeli na uwatakase."
\s5
\v 7 Uwafanyie hivi ili kuwatakasa: Uwanyunyizie maji ya utakaso juu yao. Hakikisha wamenyoa miili yao yote, wafue nguo zao, na kwa njia hii wajitakase wenyewe.
\v 8 Kisha wachukue fahari mchanga na sadaka ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta. Halafu wachukue fahari mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
\s5
\v 9 Uwalete Walawi mbele ya hema ya kukutania, na uwakusanye jamii yote ya wana wa Israeli.
\v 10 Uwalete Walawi mbele yangu, BWANA. Wana wa Israeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.
\v 11 Haruni atawatoa Walawi mbele yangu, kuwa sadaka ya kutikiswa. Atafanya hivi ili kwamba Walawi wanitumikie.
\s5
\v 12 Walawi wataweka mikono yao juu ya hao fahari. Mtatoa fahari mmoja kuwa sadaka ya dhambi na fahari mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa kwangu, ili kuwa upatanisho kwa Walawi.
\v 13 Walete Walawi mbele ya Haruni na mbele ya wana wake, uwainue kuwa sadaka ya kutikiswa kwa ajili yangu.
\s5
\v 14 Kwa njia hii utawatenganisha Walawi toka wana wa Israeli. Walawi watakuwa wangu.
\v 15 Baadaye Walawi wataingia ndani ya hema ya kukutania. Utawatakasa. utawatoa kuwa sadaka ya kutikiswa
\s5
\v 16 Fanya hivi kwa sababu wao ni wangu wote kutoka kwa wana wa Israeli. Watachukua nafasi ya kila mzaliwa wa kwanza afunguaye tumbo, mzaliwa wa kwanza wa uzao wa Israeli. Nimewachukua Walawi kwa ajili yangu.
\v 17 Wazaliwa wa kwanza wote kutoka kwa wana wa Israeli ni wangu, watu wote pamoja na wanyama pia. Siku ile nilipowachukua wazaliwa wa kwanza katika nchi ya Misri, Niliwatenga kwa ajili yangu
\s5
\v 18 Nimewachukua Walawi kutoka kwa wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza.
\v 19 Nimewatoa Walawi kuwa zawadi kwa Haruni na wana wake. Nimewachukua toka wana wa Isreali ili kuwatumikia wana wa Israeli katika hema ya kukutania. Nimewatoa ili kuwa upatanisho kwa watu ili kwamba wasipatwe na mapigo wakati wanapokaribia kwenye eneo takatifu.
\s5
\v 20 Musa, Haruni na jamii ya Waisraeli wote waliwafanyia Walawi hivi. Walifanya kila kitu ambacho BWANA alikuwa amemwamuru Musa kuhusu Walawi. Wana wa Israeli wakafanya haya pamoja nao.
\v 21 Walawi wakajitakasa wenyewe na kufua mavazi yao, Na Haruni akawatoa kama sadaka ya kutikiswa kwa BWANA na akafanya upatanisho kwao ili kuwatakasa.
\s5
\v 22 Baada ya hayo, Walawi waliingia ndani kufanya utumishi wao katika hema ya kukutania mbele ya Haruni na mbele ya wanawe. Kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Musa juu ya Walawi. Waliwahudumia Walawi wote kwa jinsi hii.
\s5
\v 23 BWANA akanena na Musa tena, Akasema,
\v 24 "Haya yote ni kwa ajili ya Walawi ambao wana umri wa miaka ishirini na mitano na zaidi. Wataungana na wale wanaohudumia hekaluni.
\s5
\v 25 Wataacha kutoa huduma hii watakapokuwa na umri wa miaka hamsini. Katika umri huu hawatakiwi kuendelea na huduma tena.
\v 26 Wanaweza kuwasaidia ndugu zao wanaoendelea kufanya kazi ndani ya hema ya kukutania, lakini hawatakiwai kufanya kazi tena. Utawaelekeza Walawi kuyafahamu haya yote."
\s5
\c 9
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa katika katika jangwa la Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka katika nci ya Misri. Akasema,
\v 2 "Wana wa Israeli wataikumbuka Pasaka katika wakati wake kila mwaka.
\v 3 Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, muda wa jioni, utaikumbuka Pasaka kila mwaka kwa muda uliopanggwa. Lazima uikumbuke, fuata taratibu zake zote na utii sheria zake zote zinazohusiana na tukio hilo.
\s5
\v 4 Kwa hiyo, Musa akawaambia wana wa Isareli kuwa wataishika sikukuu ya Pasaka.
\v 5 Kwa hiyo wakaishika sikuu ya Pasaka katika mwezi wa kwanza, wakati wa jioni wa siku ya kumi na nne ya mwezi katika jangwa la Sinai. Wana wa Israeli walitii kila kitu ambacho BWANA alimwamuru Musa kukifanya.
\s5
\v 6 Kulikuwa na watu fulani walionajisika kwa sababu ya maiti ya mtu. Hawakuweza kuishika Pasaka siku hiyo. Kwa hiyo walikwenda kwa Musa na Haruni siku hiyohiyo.
\v 7 Wakamwambia Musa, "Sisi tumenajisika kwa sababu ya maiti ya mtu. Kwa nini basi unatutaka tuendelee kutoa sadaka kwa BWANA kwa wakati wa mwaka uliopangwa kwa wana wa Israeli?"
\v 8 Naye Musa akawaambia, "Subirini nimsikilize BWANA ataniambia nini juu Yenu."
\s5
\v 9 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 10 "Nena na wana wa Israeli, uwaambie, 'kama mmoja wenu au mwana wa uzao wenu amenajisika kwa sababu ya maiti, au ana safari ndefu, bado anaweza kuishika Pasaka ya BWANA.
\s5
\v 11 Wataishika Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili wakati wa jioni. Wataila kwa mikate isyotiwa chahcu na mboga chungu.
\v 12 Wasiiache mpaka jioni, au kuvunja mifupa yake. Watafuata taratibu zote za Pasaka.
\s5
\v 13 Lakini mtu yeyote asiye najisi na hayuko safarini, na akashindwa kuishika Pasaka, huyo mtu lazima aondolewe kati ya watu wake kwa sababu hakutoa sadaka ambayo BWANA huitaka kwa wakati wa mwaka uliopangwa. Huyo mtu lazima aibebe dhambi yake.
\v 14 Kama mtu mgeni anayeishi kati yenu na akaishika, Pasaka kwa heshima ya BWANA, ataishika na kufanya amri zote, na kutii taratibu zake. Utakuwa na sheria hizohizo kwa wageni na kwa wote waliaozaliwa katika nchi.
\s5
\v 15 Na siku hiyo ambayo masikani iliposimamishwa, wingu lilifunika masikani, ile hema ya amari ya agano. Ilipokuwa jioni wingu lilkuwa juu ya masikani. Lilionekana kama moto mpaka asubuhi.
\v 16 Liliendelea hivyohivyo. Lile wingu lilifunika masikani na kuonekana kama moto wakati wa usiku.
\v 17 Na kila wingu lilipochukuliwa kutoka kwenye hema, wana wa Isareli waliendelea na safari yao. Na kila wingu liliposimama, watu waliweka kambi.
\s5
\v 18 Wana wa Israrli walisafiri kwa amri ya BWANA, na kwa amri yake waliweka kambi. Wakati wingu liliposimama juu ya masikani, nao walikaa kwenye kambi zao.
\v 19 Na wingu lilipobaki kwenye masikani kwa siku nyingi, wana wa Israeli walitakiwa kutii maelekezo ya BWANA na kusitisha safari yao.
\s5
\v 20 Wakati mwingine wingu lilibaki kwa siku chache tu kwenye masikani. Kwa mazingira kama hayo walilazimika kutii amri ya BWANA - waliweka kambi na kisha kuendelea na safari tena kwa amri yake.
\v 21 Wakati mwingine wingu lilikuwepo kambini kuanzia jioni mpaka asubuhi. Na wingu liliponyanyuliwa asubuhi, walisafiri. Kama liliendelea kwa mchana wote na kwa usiku wote, ni pale tu wingu liliponyanyuliwa ndipo walipoendelea na safari.
\s5
\v 22 Hata kama wingu lilibaki kwenye masikini kwa siku mbili, kwa mwezi mmoja, au kwa mwaka mmoja, ili mradi tu limebaki pale, wana wa Israeli walibaki kwenye kambi zao na kusitisha safari. Lakini pale wingu liliponyanyuliwa, walianza safari yao.
\v 23 Walifanya kambi kwa amri ya BWANA, na walisafiri kwa amri yake. Walitii amri ya BWANA iliyotolewa kupitia kwa Musa
\s5
\c 10
\p
\v 1 BWANA alinena na Musa, akasema,
\v 2 "tengenza tarumbeta mbili za fedha. Uzitengeneze kwa kufua hizo fedha. Utazitumia hizo tarumbeta kwa kuwaita watu waje pamoja na kwa kuwaita watu wote wakati wa kuondoka kwenye kambi zao.
\s5
\v 3 Makuhani watapiga tarumbeta kwa ajili ya kuwaita watu wote mbele yako kwenye lango la hema ya kukutania.
\v 4 Kama makuhani watapiga tarumbeta moja tu, basi viongozi, vichwa koo za Israeli ndipo watakapokutana kwako.
\v 5 Utakapopiga tarumbeta ya sauti kuu, ile kambi ya upande wa mashariki itaanza kusafiri.
\s5
\v 6 Nawe utakapopiga tarumeta kwa sauti kuu mara ya pili, ile kambi ya upande wa kusini wataanza kusafiri. Watapiga tarumbeta kwa sauti kuu ili kuanza safari yao.
\v 7 Watu wote watakapokutana pamoja, piga hizo tarumbeta lakini si kwa sauti kuu.
\v 8 Wana wa Haruni, makuhani, watapiga hizo tarumbeta. Huu ndio utakaokuwa utaratibu wa watu wako kwa vizazi vyote.
\s5
\v 9 Nanyi mtakapoenda vitani katika ardhi yenu dhidi ya maadui wenu wanaowakandamiza, ndipo mtakapotoa ishara ya sauti ya tarumbeta. Mimi, BWANA Mungu wako nitawaita kuwakumbuka na kuwaokoa kutoka kwa maadui wenu.
\s5
\v 10 Pia, wakati wa kusherehekea, sikukuu zenu za kawaida na katika miandamo ya miezi, mtapiga tarumbeta zenu kwa heshima ya sadaka zenu za kuteketezwa na kwa sadaka zenu za amani. Huu utakuwa ukumbusho wenu kwangu, Mungu wenu. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu."
\s5
\v 11 Katika siku ya ishrini, mwezi wa pili, mwaka wa pili, Lile wingu liliinuliwa toka masikani ya amri za maagano.
\v 12 Wana wa Israeli wakaendelea na safari yao toka jangwa la Sinai. Lile wingu likasimama kwenye jangwa la Parani.
\v 13 Walifanya safari yao ya kwanza, kufuatia amri ya BWANA iliyotolewa kupitia kwa Musa.
\s5
\v 14 Kambi ya mahali pa uzao wa Yuda iliondoka ya kanza, wakiondoa majeshi yao binafsi. Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyeongoza jeshi la Yuda.
\v 15 Nethaneli mwana wa Zuari aliongoza jeshi la kabila la uzao wa Isakari.
\v 16 Eliabu mwana wa Heloni aliongoza jeshi la kabila la Zabuloni.
\s5
\v 17 Uzao wa Gerishoni na Merari, ambao walitunza masikani, na kuanza kusafiri.
\v 18 Baadaye Walifuata jeshi la mahali pa kambi ya Reubeni walianza safari yao. Elizuri mwana wa Shedeuri alliongoza jeshi la Reubebni.
\v 19 Shelumieli mwana wa Zurishadai aliliongoza jeshi la kabila la uzao wa Simeoni.
\v 20 Eliasafu mwana Deuli aliliongoza jeshi la kabila la uzao wa Gadi.
\s5
\v 21 Kabila la Kohathi nalo lilianza safari. Wao walibebba vyombo vya mahali patakatifu. Wengine waliisimamisha masikani kabla ya Wakohathi kufika kambi inayofuata.
\v 22 Majeshi ya kabila la uzao wa Efraimu ndio waliofuata. Elishama mwana wa Amihudi ndiye aliyeongoza jeshi la Efraimu.
\v 23 Gamalieli mwana wa Pedazuri aliongoza jeshi la uzao wa Manase.
\v 24 Abidani mwana wa Gidioni aliongoza jeshi la uzao wa kabila la Benjamini.
\s5
\v 25 Lile jeshi lililoweka kambi mahali pa bango la uzao wa Dani lilikuwa la mwisho kuondoka. Ahizeri mwana wa Amishadai ndiye aliyeongoza jeshi la Dani.
\v 26 Pagieli mwana wa Okirani aliongoza jeshi la wana wa uzao wa Asheri.
\v 27 Ahira mwana wa Enani aliongoza jeshi la uzao wa kabila ya Naftali.
\v 28 Hivi ndivyo majeshi ya wana wa Israeli yalivyosafiri.
\s5
\v 29 Musa alinena na Hobibu mwana wa Reueli wa Kabila la Midiani. Reueli alikuwa baba mke wa Musa. Musa akanena na Hobibu akasema, "Tunasafiri kuelekea mahali ambapo BWANA ametuahidi. BWANA alisema kuwa, "Nitawapeni ninyi hilo eneo, 'Njoni pamoja nasi na tutawatendea mema. BWANA ameahidi kuwafanyia mema Waisraeli."
\v 30 Lakini Hobibu akmwambia Musa, "Sitaambatana nanyi."
\s5
\v 31 Naye Musa akamjibu, "Tafadhali msituache. Mnajua jinsi ilivyo kuweka kambi jangwani. Tunaomba mtujali.
\v 32 Kama mtaambatana nasi tutawatendea mema sawa na jinsi BWANA anavyotutendea."
\s5
\v 33 Walisafiri kutoka mlima wa BWANA kwa siku tatu. Sanduku la agano la BWANA liliwatangulia kwa siku tatu ili kupata mahali pa kupumzika.
\v 34 Wingu la BWANA lilikuwa juu yao muda wote wa mchana walipokuwa safarini.
\s5
\v 35 Kila hilo sanduku liliposafiri kwenda mbele, Musa alisema, "Inuka BWANA, Uwatawanye maadui wako. Uwafanye wale wanaokuchukia kukukimbia."
\v 36 Na kila lile sanduku liliposimama, Musa alisema, "BWANA uwarudie, hawa Waisraeli makumi elfu."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Sasa watu wakanung'unika juu ya matatizo yao wakati BWANA alipokuwa akiwasikiliza. BWANA akawasikia watu naye akakasirika. Moto kutoka kwa BWANA ukashuka na ukawaka kati yao na kuteketeza baadhi ya kambi kwenye pembe zake.
\v 2 Ndipo watu wakamwita Musa kwa nguvu, Naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukazimika.
\v 3 Mahali pale paliitwa Tabera, kwa sababu moto wa BWANA uliwaka kati yao.
\s5
\v 4 Baadhi ya wageni wakaanza kuweka kambi zao pamoja na wana wa wa Israeli. Walitaka kula chakula kizuri. Kisha wana wa Israeli walipoanza kulia wakisema, "Ni nani atakayetupatia nyama za kula?
\v 5 Tunakumbuka samaki tulizokula bure kule Misri, yale matango, na matikiti maji, na mboga na vitunguu na vitunguu saumu.
\v 6 Na sasa hatuna hamu ya kula, kwa sababu tunaona mana tu.
\s5
\v 7 Mana ilifanana na punje ya mtama. ilionekana kama bedola.
\v 8 watu wakazunguka kisha wakakusanyika. Wakaisaga, wakaitwanga kwa vinu, wakaitokosa nyunguni, na kuitengeneza mikate. radha yake ilikuwa kama mafuta mapya ya mizeituni.
\s5
\v 9 Na umande ulipoanguka kambini usiku ule, na mana ilianguka pia.
\v 10 Musa akawasikia watu wakilia katika familia zao, na kila mtu alikuwa kwenye lango la hema yake. BWANA alikasirika sana, na mbele ya macho ya Musa malalamiko yao yalikuwa mabaya.
\s5
\v 11 Musa akasema na BWANA, "Kwa nini umemtendea mtumishi wako vibaya namna hiyo? kwa nini hujapendezwa na mimi? unanifanya kubeba mizigo ya hawa watu.
\v 12 Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia, "wabebe kwa ukaribu vifuani mwako kama baba abebavyo mtoto wake? Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ambayo uliwaahidi mababu zao kuwapa?
\s5
\v 13 Naweza kupata wapi nyama za kuwapa watu wote hawa? Wanalia mbele zangu na wanasema, 'tupe nyama tule.'
\v 14 Mimi peke yangu siwezi kuwabeba watu wote hawa. Ni wengi sana kwangu.
\v 15 Kwa vile unanitendea hivi, basi uniue, na kama wewe ni mpole kwangu, basi niondolee mzigo huu."
\s5
\v 16 BWANA akamwambia Musa, "Niletee wazee sabini miongoni mwa Waisraeli. Hakikisha ni wazee na viongozi wa watu. Uwalete kwenye hema ya kukutania wasimame pamoja na wewe.
\v 17 Nami nitashuka niseme nawe mahali pale. Nitatoa sehemu ya roho iliyo ndani yako na kuwapatia wao. Nao watabeba mzigo wa watu pamoja nawe. na hautaubeba peke yako.
\s5
\v 18 Waambie watu, 'Jitakaseni ninyi wenyewe, kwa kuwa kesho mtakuala nyama, kwa kuwa mmelia na BWANA amesikia, "Mlipokuwa mkisema kuwa nani atakayetupa nyama tule? Kule Misri tulikula chakula kizuri!" Kwa hiyo BWANA atawapeni nyama, nanyi mtakula nyama.
\v 19 Hamtakula nyama kwa siku moja tu, au siku mbili, au siku tano, au siku kumi, au siku ishirini,
\v 20 Lakini mtakula nyama kwa mwezi mmoja mpaka zitakapowatokea puani. Mpaka zitawakinai kwa sababu mmemkataa BWANA ambaye yuko kati yenu. Mmelia mbele yake. mmesema, "Kwa nini tulitoka Misri?""
\s5
\v 21 Kisha Musa akasema, "Mimi nina watu 600, 000, na wewe umesema, "Nitawapa nyama mle kwa mwezi mmoja,'
\v 22 Je, tutayachinja haya makundi ya ng'ombe na kondoo ili kuwatosheleza?"
\v 23 BWANA akasema na Musa, "Je mkono wangu ni mfupi? Sasa utaona kama maneno yangu ni ya kweli ama sivyo.
\s5
\v 24 Musa alitoka nje kwenda kuwaambia watu maneno ya BWANA. Aliwakusanya wazee sabini wa watu na kuwaweka kuizunguka hema.
\v 25 BWANA akashuka chini katika wingu akaongea na Musa. BWANA akachukua sehemu ya roho iliyokuwa kwa Musa na kuiweka kwa wale wazee sabini. Roho alipowashukia, wakaanza kutoa unabii, lakini ilitokea kwenye tukio hilo tu na haikujirudia tena.
\s5
\v 26 Watu wawili waitwao Elidadi na Medadi walibaki kambini. Lakini Roho aliwashukia pia. Majina yao yalikuwa yameandikwa kwenye orodha lakini walikuwa hawajaenda hemani. Hata hivyo nao walitoa unabii wakiwa kambini.
\v 27 Kijana mmoja huko kambini alikimbia akaenda kumwambia Musa, "Elidadi na Medadi wanatoa unabii kambini."
\s5
\v 28 Joshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa, ambaye ni miongoni mwa wale aliowachagua akamwambia Musa, "Bwana wangu Musa, wazuie."
\v 29 Musa akamwambia, "una wivu kwa niaba yangu? Natamani kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kwamba angeweka Roho yake juu yao wote!"
\v 30 Kisha Musa na wale wazee wakarudi kambini.
\s5
\v 31 Kisha upepo ukavuma kutoka kwa BWANA ukaja na kware kutokea baharini. Wakaanguka karibu na kambi, kiasi cha umbali wa safari ya siku moja upande huu na umbali wa siku moja upande mwingine. Wale kware wakaizunguka kambi kiasi cha mita moja toka uso wa dunia.
\v 32 Watu wakawakusanya hao kware kwa bidii mchana huo wote na usiku huo wote, na mchana wote uliofuatia. Hakuna aliyekusanya pungufu ya mita mbili za uajazo. Wakawaanika kweye ardhi yote hapo kambini.
\s5
\v 33 Wakati ile nyama ikiwa bado iko kwenye meno yao, wakiwa bado wanatafuna, BWANA akawakasirikia. Akwapiga watu wale kwa gonjwa kubwa sana.
\v 34 Mahali pale paliitwa Kibroti Hataava, kwa sababu pale walizika watu waliotamani nyama.
\v 35 Kutoka Kibroti Hataava watu wakasafiri hadi Hazeroti, ambapo walipumzika.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kisha Miriamu na Haruni wakasema kinyume na Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi ambaye alikuwa amemwoa.
\v 2 Walisema. " Hivi BWANA amesema na Musa tu? Ni kweli hajawahi kusema nasi pia? Sasa BWANA akasikia kile walichokuwa wanaongea. Sasa
\v 3 Musa alikuwa mtu mpole sana, mpole kuliko mtu yeyote duniani.
\s5
\v 4 Wakati huo, BWANA akanena na Musa, Haruni na Miriamu: "tokeni nje ninyi watatu kwenye hema ya kukutania." kwa hiyo wale watatu wakatokanje.
\v 5 Kisha BWANA akashuka katika nguzo ya wingu. Akasimama kwenye lango la hema na akamwita Haruni na Miriamu. wote wakaja mbele.
\s5
\v 6 BWANA akasema, "Sasa sikilizeni maneo yangu, Nabii wangu anapokuwa nanyi, Mimi nitajifunua kwake kwa maono na kusema naye katika ndoto.
\v 7 Lakini si hivyo kwa mtumishi wangu Musa. Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.
\v 8 Mimi huongea na Musa moja kwa moja, si kwa maono wala mafumbo. Yeye huniona umbo langu. Kwa hiyo, kwa nini hamuogoopi kumnenea kinyume, mtumishi wangu Musa?"
\s5
\v 9 Hasira ya BWANA ikawawakia, kisha akawaacha.
\v 10 Lile wingu likainuka juu ya hema, Miriamu akapata ukoma ghafla - akawa mweupe kama theluji. Naye Haruni alipogeuka kumwona Miriamu, akamwona amepata ukoma.
\s5
\v 11 Haruni akamwambia Musa, "Bwana wangu, usituadhibu kwa uovu wetu huu. Tumenena katka upumbuvu, na tumetenda dhambi.
\v 12 Tafadhali nakuomba usimwache akawa kama mtoto mchanga aliyekufa ambaye nusu ya nyama yake imeoza tangu kuzaliwa"
\s5
\v 13 Kwa hiyo Musa akamwomba BWANA, akasema, "Mungu ninakusihi umponye tafadhali."
\v 14 BWANA akamwambia Musa, " kama baba yake angemtemea usoni angepata aibu kwa muda wa siku saba. Umfungie nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Kisha umrejeshe ndani tena."
\v 15 Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba. Watu hawakusafiri mpaka aliporudi kambini.
\s5
\v 16 Kisha watu wakasafiri kutoka Hazeroti na kuweka kambi kwenye jangwa la Parani.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, "tuma watu waende kuipeleleza nchi ya Kanani, ambayo nimewapa wana wa Israeli.
\v 2 Tuma mwanamume mmoja kutoka kila jamaa ya kabila. Kila mwanamume awe kiongozi katika kabila lake."
\s5
\v 3 Musa akawatuma kutoka jangwa la Parani, ili watii amri ya BWANA. Watu wote hao walikuwa viongozi wa watu wa Israeli.
\v 4 Majina yao yalikuwa haya yafuatayo: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
\s5
\v 5 Kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
\v 6 Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
\v 7 Kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu,
\v 8 Kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
\s5
\v 9 Kutoka kabila la Benjamini, Paliti mwana wa Rafu;
\v 10 kutoka kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi;
\v 11 kutoka kabila la Yusufu (hiyo inamaanisha kutoka kabila la Manase), Gadi mwana wa Susi;
\v 12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemalili;
\s5
\v 13 kutoka kabila Asheri, Setu mwana wa Mikaili;
\v 14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofisi;
\v 15 kutoka kabila la Gadi, Geuli mwana wa Machi.
\v 16 Haya ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuipelelza ile nchi. Musa akamwita Hoshea mwana wa Nuni kwa jina la Joshua.
\s5
\v 17 Musa akawatuma kwenda kuipeleleza ile nchi ya Kanani. Naye akawaambia, " Mkaanzie Negebu hadi mahali pa milima.
\v 18 Kaipelelezeni nchi kujua ni nchi ya namna gani. Wachunguzeni watu wake, kama ni watu wenye nguvu au dhaifu, kama ni wachache au ni wengi.
\v 19 Chunguzeni nchi hiyo wanayoishi ni nchi ya namna gani. Ni nzuri au mbaya? Miji yao ikoje? Je iko kama kambi au ni miji yenye ngome?
\v 20 Chunguzeni ni nchi ya namna gani, kama ni njema kwa mazao au la kama kuna miti au hapana. Mwe hodari mkalete sampuli za mazao ya nchi," Sasa ni muda wa msimu wa malimbuko ya mizabibu.
\s5
\v 21 Kwa hiyo wale wanaume wakaenda kuipeleleza ile nchi kutoka jangwa la Sini mpaka Rehobi, karibu na Lebo Hamati.
\v 22 Walienda kutoka Negebu nao wakafika Hebroni. Ahimani, Sheshai, na Talmai, Uzao wa Anaki nao walikuweko, Sasa Hebroni ilikuwa imejengwa miaka saba iliyokuwa imepita kabla ya Zoani wa Misri.
\s5
\v 23 Nao walipofika katika bonde la Eshikoli, walikata matawi ya mizabibu lenye kishada cha zabibu. Na makundi mawili ya wapelelezi wakakibeba kwenye mti. Pia wakaleta makomamanga na mtini.
\v 24 Mahali pale paliitwa Eshikoli, kwa sababu ya kishada cha mizabibu ambacho wana wa Israeli walikata kule.
\s5
\v 25 Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
\v 26 Wakaja kwa Musa, Haruni na kwa watu wote wa Israeli katka jangwa la Parani, kule Kadeshi. Wakaleta taarifa kwao na kwa Waisraeli wote, na kuwaonyesha matunda ya nchi ile.
\s5
\v 27 Wakamwambia Musa, "Tulifika katika ile nchi uliyotutuma. Kwa hakika ni nchi ya kutiririka maziwa na asali. Na baadhi ya matunda yake ni haya hapa.
\v 28 Hata hivyo, watu wanaoishi huko ni wenye nguvu. Miji yao ni mikubwa tena ina maboma. Pia tuliwaona wana wa Anaki huko.
\v 29 Waamaleki wanaishi Negebu. Wahiti, Wayebusi, na Waamori nao wanaishi katika milima ya hiyo nchi. Wakanaani wanaishi kando ya bahari na mto Yorodani."
\s5
\v 30 Kisha Kalebu akawatuliza watu waliokuwa mbele ya Musa, akasema, "Twendeni tukaiteke nyara hiyo nchi, kwa kuwa tuna uhakika wa kuikamata."
\v 31 Lakini wale watu waliokuwa wameenda naye walisema, "Hatutaweza kuwashinda hao watu kwa kuwa wao ni hodari kuliko sisi."
\s5
\v 32 Kwa hiyo wakasambaza taarifa za kukatisha tamaa kwa Wana wa Israeli juu ya nchi ile waliyoipeleleza. Walisema, "Ile nchi tuliyoiona ni nchi inayowala watu wake. Watu wote tuliowaona ni watu warefu.
\v 33 Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao nii uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilingsnisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia."
\s5
\c 14
\p
\v 1 Usiku huo watu wote walilia kwa sauti.
\v 2 Watu wote wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haruni. Watu wote wakawaambia, "Ni bora kama tungelifia katika nchi ya Misri, au katika hili!
\v 3 Kwa nini BWANA alituleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa watumwa wao. Je, si bora kwetu kurudi Misri?"
\s5
\v 4 Wakasemezana wao kwa wao, "Na tuchague kiongozi mwingine, turudi Misri."
\v 5 Ndipo Musa na Haruni wakalala kifudifudi mbele ya kundi lote la wana wa Israeli.
\s5
\v 6 Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa waemtumwa kwenda kuipeleleza nchi wakachana mavazi yao.
\v 7 Wakawaambia watu wote wa Israeli. Walisema, "Ile nchi tuliyopita katikati yake ni nchi nzuri sana.
\v 8 Kama BWANA amependezwa nasi, basi atatuingiza katika nchi hii na kutupatia. Ile nchi inatiririka maziwa na asali.
\s5
\v 9 Lakini msimwasi BWANA, na msiwahofie hao wakazi wa nchi hiyo. Tutawateketeza kwa urahisi kama kula chakula. Ulinzi wao utaondolewa kutoka kwao, kwa sababu BWANA yuko pamoja nasi. Msiwahofie."
\v 10 Lakini watu wote walitishia kuwapiga kwa mawe mpaka wafe. Kisha utukufuwa BWANA ukaonekana kwenye hema ya kukutania kwa watu wote wa Israeli.
\s5
\v 11 BWANA akamwambi Musa, "watu hawa watanidharau hadi lini? Wataendelea kutoniamini mpaka lini? Nijapokuwa nimefanya ishara kwa nguvu zangu kati yao?
\v 12 Nitawapiga kwa mapigo, na kuwaondolea urithi, na kufanya taifa kubwa kutoka kwenye ukoo wako ambalo litakuwa kubwa na lenye nguvu kuliko wao.
\s5
\v 13 Musa akamwambia BWANA, "Kama utafanya hivi, Na Wamisiri wakisikia habari hizi, na kwa sababu uliwaokoa kutoka kwao kwa nguvu zako.
\v 14 Basi watawaambia wakazi wa nchi hii. Wamesikia ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa, kwa sababu uso wako waonekana. Wingu lako husimama juu ya watu wetu. Wewe huwatangulia katika nguzo ya wingu wakati wa mchana na katika nguzo ya moto wakati wa usiku.
\s5
\v 15 Sasa kama utawaua hawa watu kama mtu mmoja, basi mataifa ambao wamesikia sifa zako watasema,
\v 16 "Kwa Sababu BWANA hana uwezo wa kuwapeleka watu hawa katika nchi ambayo aliwaapia kuwapa, ndiyo maana amewaua katika jangwa hili.'
\s5
\v 17 Sasa, nakusihi, utumie uweza wako. Kwa kuwa umesema kuwa,
\v 18 'BWANA si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa uaminifu katika agano. Yeye husamehe uovu na uasi. Kwa vyovyote vile atafutilia hatia atakapoleta hukumu ya dhambi za mababu juu ya wazao wao, kwa kizazi cha tatu na cha nne.'
\v 19 Ninakusihi uwasameha watu hawa dhambi zao kwa sababu ya ukuu wa uaminifu wa agano lako, kama vile ambavyo umekuwa ukiwasamehe watu hawa tokea wakati wakiwa Misri mpaka sasa."
\s5
\v 20 BWANA akasema, Nimewasamehe kwa kama ulivyoomba,
\v 21 bali kama Niishivyo, na kama vile dunia yote itakavyojazwa na utukufu wangu,
\v 22 watu wote walioona utukufu wangu na ishara za nguvu zangu nilizotenda kule Misri na kule jangwani - Lakini bado wamenijaribu mara kumi sasa na hawakuisikiliza sauti yangu.
\s5
\v 23 Kwa hiyo nasema kwamba hakika hawataiona nchi ile ambayo niliwaahdi kuwapa mababu zao. Hakuna hata mmoja wao ambao wamenidharau watakaoiona,
\v 24 isipokuwa mtumishi wangu Kalebu, kwa sababu alikuwa na roho nyingine. Yeye amenifuata kwa ukamilifu; Yeye nitampeleka katika nchi hiyo ambayo alienda kuipeleleza. Wazao wake wataimilki.
\v 25 (Sasa Waamaleki na Wakanani waliishi katika bonde.) Kesho mtageuka na kwenda katika jangwa kwa njia ya bahari ya Shamu."
\s5
\v 26 BWANA akanena na Musa na Haruni, akasema,
\v 27 "Nitaivumilia jamii ya watu hawa waovu ambao wananinung'unikia mpaka lini? Nimeyasikia malalamiko ya wana wa Israeli dhidi yangu.
\s5
\v 28 Waambie, 'Kama niishivyo,' asema BWANA, 'kama vile mlivyosema katika masikio yake, nitawafanyia jambo hili:
\v 29 Maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili, Ninyi nyote mliolalamika dhidi yangu, ninyi mliohesabiwa kwenye ile sensa, idadi yote ya watu kuanzia umri wa mika ishirini na kuendelea.
\v 30 Kwa hakika hamtaingia kwenye ile nchi ambayo niliahidi kuwapa kuwa makazi yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.
\s5
\v 31 Bali watoto wenu ambao mlisema kuwa watakuwa watumwa, wao ndio nitakaowapeleka katika nchi hiyo. Wao wataifurahia nchi ambayo nInyi mmeikataa!
\v 32 Lakini ninyi, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili.
\v 33 Watoto wenu watakuwa wachungaji katika jangwa hili kwa muda wa miaka arobaini. Lazima watabeba madhara ya matendo yenu ya kutokuamini mpaka mwisho wa maiti ya mwisho jangwani.
\s5
\v 34 Kama vile ilivyo hesabu ya siku ambayo mliipeleleza nchi--siku arobaini, vivyo hivyo mtabeba madhara ya dhambi zenu kwa muda wa miaka arobaini--mwaka mmoja kwa kila siku moja, na mtajua kuwa ni sawa na kuwa adui yangu.
\v 35 Mimi BWANA nimesema. Hakika nitafanya hivi kwa kizazi hiki chote kiovu ambacho kimekusanyika kinyume na Mimi. Wao watakatwa kabisa, na watafia hapa.'"
\s5
\v 36 Kwa hiyo wale wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuingalia ile nchi wote walikufa kwa tauni mbele ya BWANA.
\v 37 Hawa ni wale ambao waliorudi na kutoa taarifa mbaya juu ya nchi. Hii iliwafanya watu wote wamlalamikie Musa.
\v 38 Kati ya watu wale waliokuwa wameenda kuiangalia nchi ile, ni Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune tu ndio waliobaki hai.
\s5
\v 39 Musa alipowataarifu mambo haya watu wote wa Israeli waliomboleza sana.
\v 40 Waliamka asubuhi na mapema wakaenda juu ya mlima na kisha wakasema, "Tazama, tuko hapa, na tutaenda mahali pale ambapo BWANA ametuahidi, kwa kuwa tumetenda dhambi."
\s5
\v 41 Lakini Musa akasema, "Kwa nini sasa mnapinga amri ya BWANA? hamtafanikiwa.
\v 42 Msiende, kwa sababu BWANA hayuko pamoja nanyi kuwalinda dhidi ya maadui zenu.
\v 43 Waamaleki na Wakanaani wako kule, na mtakufa kwa upanga kwa sababu mliumtegea mgongo BWANA na hamkumfuata. Kwa hiyo hatakuwa pamoja nanyi.
\s5
\v 44 Lakini walithubutu kukwea mlimani; lakini si Musa wala Sanduku la agano la BWANA walioondoka kambini.
\v 45 Kisha Waamaleki walikuja chini, pia wale Wakanaani walioshi kwenye hiyo milima. Wakawavamia Waisreli wakawapiga na kuwaangusha mpaka Horima.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Kisha BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 2 "Sema na wana wa Israeli uwaambie, 'Mtakapoingia katka nchi ambayo mtaishi, ambayo BWANA atawapa,
\v 3 mtatakiwa kuandaa sadaka kwa moto kwa BWANA, sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kukamilisha kiapo au sadaka ya hiari, au sadaka katika sikukuu zenu, ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA ya ng'ombe au ya kondoo.
\s5
\v 4 Utamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya sadaka ya unga mwembamba uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta.
\v 5 Na tena mtatoa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa sadaka ya divai robo ya hini ya sadaka ya vinywaji kwa kila mwanakondoo.
\s5
\v 6 Kama unatoa sadaka ya kondoo dume, utaandaa sadaka ya unga ya sehemu za kumi mbili za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na sehemu ya tatu ya hini ya divai.
\v 7 Kwa sadaka ya kinywaji, mtatoa sehemu ya tatu ya hini ya divai ambayo itatoa harufu nzuri kwa BWANA.
\s5
\v 8 Utakapoandaa fahari kwa ajiliy a sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kutimiza kiapo, au sadaka ya amani kwa BWANA,
\v 9 Ndipo utakapotoa sadaka ya fahari pamoja na sadaka ya unga ya sehemu za kumi tatu za unga mwembamba uliochanganywa na nusu ya hini ya mafuta.
\v 10 Mtatoa sadaka ya kinywaji nusu ya hini ya divai, sadaka iloyotengenezwa kwa moto ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA.
\s5
\v 11 Itafanyika hivi kwa kila fahari, kwa kila kondoo dume, na kila mwanakondoo dume au mbuzi mchanga.
\v 12 Kila sdaka utakayoindaa na kuitoa itafanyika kama ilivyoanishwa hapa.
\v 13 Wazawa wote wa Israeli watafanya mambo haya kwa utaratibu huu, yeyote atakayeleta sadaka iliyotengenezwa kwa moto, ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA.
\s5
\v 14 Na kama kuna mgeni anayeishi kati yenu, au yeyote atakayeishi na watu wa vizazi vyenu vyote, lazima atengeneze sadaka iliytoengenezwa kwa moto, ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Atafanya kama mnavyofanya.
\v 15 Kutakuwa na sheria hiyo hiyo kwa watu wote na kwa mgeni anayeishi kati yenu, sheria ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Ninyi mlivyo, ndivyo atakavyokuwa mgeni aliyeishi kati yenu. Atafanya kama mnavyofanya mbele ya BWANA.
\v 16 Sheria na amri hiyohiyo ndiyo itakayotumika kwa mgeni anayeishi kati yenu."
\s5
\v 17 Tena BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 18 "Nena wana wa Israeli uwaambie, 'mtakapofika katika nchi ninayowapeleka,
\v 19 mtakapokula chakula kinachozalishwa katika nchi hiyo, mtatoa sadaka ya kunipendeza mimi.
\s5
\v 20 Kutoka kwenye mikate yenu ya kwanza mtatoa mkate wa kuinuliwa kama sadaka iliyoinuliwa kutoka mahali pa kupuria nafaka. Mtaiinua kwa jinsi hii.
\v 21 Watu wa uzao wako wote wtanitolea sadaka ya kuinuliwa kutoka kwenye unga wenu wa kwanza.
\s5
\v 22 Wakati mwingine mtafanya dhambi pasipo kukusudia, Kama hamtatii amri zote hizi ambazo nimemwambia Musa
\v 23 -kila kitu ambacho nimewaamuru kupitia Musa kuanzia siku ambayo nilianza kuwaamuru na kuendelea kwa watu wote wa uzao wako.
\v 24 Kwa swala la dhambi isiyokusudiwa ambayo watu wote hawaijui, basi watu wote watatoa fahari mchanga sadaka ya kuteketezwa ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Pamoja na haya yote, lazima itengenezwe sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji, kama ilivyoagaizwa katika amri, na beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\s5
\v 25 Kuhani atafanya sadaka upatanisho kwa watu wote wa Israeli. Watasemehewa kwa sababu dhambi haikukusudiwa. Wametoa sadaka yao, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili yangu. Wameleta sadaka yao kwangu iliyotengenezwa kwa moto. Wameleta sadaka yao ya uovu mbele yangu kwa ajili ya kosa lao.
\v 26 Ndipo watu wote wa Israeli watasamehewa, pia wageni wote wanaoishi kati yao, kwa sababu watu wote walitenda dhambi pasipo kukusudia.
\s5
\v 27 Kama mtu atatenda dhambi bila kukusudia, atatoa mbuzi jike wa umri wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
\v 28 Naye kuhani atafanya upatanisho kwa BWANA kwa ajili ya mtu yule aliyefanya dhambi pasipo kukusudia. Yule mtu atasamehewa baada ya upatanisho kufanyika.
\v 29 Mtakuwa na sheria hiyohiyo kwa mtu yeyote anayefanya dhambi hiyo pasipo kukusudia, sheria hiyohiyo hata kwa mzawa wa Isreli na kwa wageni wanaoishi kati yao.
\s5
\v 30 Lakini mtu afanyaye chochote kwa KUkusudia, awe mzawa au mgeni, ananikufuru mimi. Huyo mtu ataondolewa kati ya watu wake.
\v 31 Kwa sababu atakuwa amedharau neno langu na amevunja neno amri yangu, mtu huyo ataondolewa kabisa. Dhambi yake itakuwa juu yake.'"
\s5
\v 32 Wakati wana wa Israeli walipokuwa katika jangwa, wakamuona mwanamume akikusanya kuni sikiu ya Sabato.
\v 33 Wale waliomwona wakamleta kwa Musa, Haruni na kwa watu wote.
\v 34 Wakamweka kifungoni kwa sababu ilikuwa haijaamuliwa atakachotendewa.
\s5
\v 35 Kisha BWANA akanena na Musa, "Yule mwanamume lazima auawe. Watu wote lazima wampige kwa mawe nje ya kambi."
\v 36 Kwa hiyo watu wote wakamtoa nje ya kambi nao wakampiga kwa mawe mpaka akafa kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 37 BWANA akanena na Musa tena, akasema,
\v 38 "Waambie wana wa Israeli na uwaamuru wajifanyie vishada wavining'inize katika mapindo ya mavazi yao, wavining'ineze katika ncha zote kwa nyuzi za rangi ya samawi. Watu wote watafanya hivi kwa watu wote wa kizazi chote.
\v 39 Huu utakuwa ukumbusho maalumu kwenu, kila mtakapovitazama, mtakumbuka amri zangu, na kuzishika ili kwamba msije mkatangatanga katika mioyo na macho yenu na kuwa waasherati wa hayo.
\s5
\v 40 Fanyeni hivi ili kwamba mweze kukumbuka na kutii amri zangu zote, na ili kwamba mpate kuwa watakatifu, waliotunzwa kwa ajili yangu, Mungu wenu.
\v 41 Mimi ndimi BWANA Mungu wenu niliyekutoa toka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu."
\s5
\c 16
\p
\v 1 Sasa Kora mwana wa Izihari mwana wa Kohathi mwana wa Lawi, pamoja na Dathani na Abiramu mwana wa Eliabu, na Oni mwana wa Peleti, wa uzao wa Reubeni, waliwakusanya wanaume kadhaa.
\v 2 Wakamwinukia Musa, pamoja na wanaume fulani kutoka wana wa Israeli, viongozi wa watu wapatao mia mbili na hamsini waliokuwa wakifahamika katika ile jamii.
\v 3 Walikusanyika pamoja kumpinga Musa na Haruni. Wakawaambia, "Ninyi sasa mnatumia mamlaka zaidi ya uwezo wenu! Watu wote wamejitenga, kila mmoja wao, na BWANA yuko pamoja nao. Kwa nini mnajiinua sana juu ya watu wengine wa BWANA?"
\s5
\v 4 Musa alipoyasikia hayo, akalala kifudifudi.
\v 5 Akamwambia Kora na wote aliokuwa nao, "Asubuhi BWANA atafanya ijulikane ni nani walio wake na nani aliyetengwa kwa ajili yake. Atamleta huyo mtu karibu na yeye. Yule anayemchagua atamleta karibu naye.
\s5
\v 6 Fanya hivi, wewe Kora na kundi lako.
\v 7 Kesho mchukue vyetezo na muweke moto na ubani ndani yake mbele ya BWANA. Yule ambaye BWANA amemchagua, atamtenga kwa BWANA. Sasa imetosha ninyi watu wa uzao wa Lawi,"
\s5
\v 8 Tena Musa akamwambia Kora, "Sasa unisililize, ninyi watu wa uzao wa Lawi:
\v 9 Je ni jambo dogo kwenu kwamba Mngu wa mbinguni amewatenga ninyi kutoka watu wa Israeli, ili awalete ninyi karibu na yeye, ili mfanye kazi katika masikani ya BWANA na kusimama mbele ya watu ili muwatumikie?
\v 10 Amewasogeza karibu, na ndugu zako, wa uzao wa Lawi pamoja nanyi, na sasa mnataka na ukuhani pia!
\v 11 Hiyo ndiyo sababu wewe na kundi lako mmekusanyika pamoja kinyume na BWANA. Kwa nini mnalalamika juu ya Haruni, ambaye anamtii BWANA?"
\s5
\v 12 Kisha Musa akamwita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, lakini wakasema, "hatutakuja.
\v 13 Kwani jambo dogo kwamba umetuleta mpaka kwenye nchi inayotiririka maziwa na asali, ili kutuua katika jangwa hili? Sasa unataka kujifanya kuwa mtawala wetu!
\v 14 Na kwa nyongeza, haujatuingiza kwenye nchi ya kutiririka maziwa na asali, au kutupa urithi wa mashamba na mashamba ya mizabibu. Sasa unataka kutupofusha na ahadi hewa? Hatutakuja kwako."
\s5
\v 15 Musa alikasirika sana na akamwambia BWANA, "Usisipokee sadaka zao. Sijachukua punda mmoja kutoka kwao, na sijamdhuru hata mmoja wao."
\v 16 Kisha Musa akamwambia Kora, "Kesho wewe na kundi lako mtaenda mbele za BWANA-wewe na wao na Haruni.
\v 17 Kila mmoja wenu atatwaa chetezo na kuweka ubani ndani yake. Ndipo kila mtu atamletea BWANA chetezo chake, vyetezo mia mbili na hamsini. Wewe na Haruni, pia, kila mmoja ataleta chetezo chake.
\s5
\v 18 Kwa hiyo kila mtu alitwaa chetezo chake, akaweka moto ndani yake, akaweka na ubani ndani yake, na kusimama mbele ya lango la hema ya kukutania pamoja na Musa na Haruni.
\v 19 Kora naye akawakusanya watu wote waliokuwa kinyume na Musa na Haruni hapo kwenye lango la hema ya kukutania, na kisha utukufu wa BWANA ukaonekana kwa watu wote.
\s5
\v 20 Ndipo BWANA aliposema na Musa na Haruni:
\v 21 "Tokeni ninyi kutoka hawa watu ili nipate kuwaangamiza haraka."
\v 22 Musa na Haruni wakalala kifudifudi na kusema, "Mungu, Mungu wa wote wenye mwili, kama mtu akitenda dhambi, ni lazima uwe na hasira na watu wote?"
\s5
\v 23 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 24 "Sema na watu wote, uwaaambie, 'Tokeni kwenye hema ya Kora, Dathani, na Abiramu.'"
\s5
\v 25 Kisha Musa akaamuka akaenda kwa Dathani na Kwa Abiramu; viongozi wa Israeli wakamfuata.
\v 26 Akaongea na watu wote akasema, "Sasa jitengeni na hema ya hawa watu waovu na msiguse kitu chochote kilicho chao, vinginevyo mtaangamizwa na dhambi zao."
\v 27 Kwa hiyo watu wote toka pande zote za hema ya Kora, Dathani na Abiramu wakaondoka. Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama kwenye lango la hema zao, wakiwa na wake wao, wana, na watoto wao.
\s5
\v 28 Kisha Musa akasema, "Kwa hili sasa mtatambua kuwa BWANA amenituma kufanya kazi hizi zote, kwa kuwa sijazifanya kwa uwezo wangu.
\v 29 Kama hawa watu watakufa kifo cha kawaida ambacho humpata kila mmoja, basi BWANA hakunituma.
\v 30 Lakini kama BWANA aumbaye malango ya ardhi ambayo huwameza kama mdomo mkubwa, pamoja na familia zao, na kama wataingia ndani ya shimo wakiwa hai, ndipo mtakapojua kuwa wamemdharau BWANA,"
\s5
\v 31 Mara ghafla Musa alipomaliza kusema maneno haya, aridhi ya pale walipokuwa ikafunguka.
\v 32 Dunia ikafungua makanwa yake na kuwameza, familia zao na watu wote wa Kora, pamoja na mali zao zote.
\s5
\v 33 Wao na kila mmoja kwenye familia zao wakaingia ndani shimoni wakiwa hai. Dunia ikwafunika, na kwa njia hii wakapotea kutoka miongoni mwa ile jamii.
\v 34 Nao Israeli yote waliokuwa karibu nao wakakimbia kwa sababu ya vilio vyao. Walisema kwa mshangao, "Nchi isije kutumeza na sisi!"
\v 35 Kisha moto ukashuka toka kwa BWANA na kuwaangamiza wale wanaume 250 waliokuwa wametoa ubani.
\s5
\v 36 Tena BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 37 "Mwambie Eliazari mwana wa Haruni yule kuhani achukue vile vyetezo kutoka ule moto, kwa kuwa vile vyetezo vimetengwa ka ajili yangu. Na aumwage ule moto mbali.
\v 38 Vitwae vile vyetezo vya wale waliopoteza maisha yao kwa sababu ya dhambi zao. Na vifanyike kuwa mbao za kufuliwa ili viwe vifuniko vya madhabahu. Kwa kuwa wale watu walivitoa kwangu, kwa hiyo ni vitakatifu. Vitakuwa ishara ya uwepo wangu kwa wana wa Israeli."
\s5
\v 39 Naye Eleazari yule kuhani akavichukue vile vyetezo vya shaba ambavyo vilikuwa vimetumiwa na wale watu walioungua, na vikafuliwa kuwa vifuniko vya madhbahu,
\v 40 ili kuwa ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili kwamba asije akatokea mtu toka nje ya uzao wa Haruni akaja kutoa ubani kwa BWANA, ili wasije kuwa kama Kora na kundi lake-- kama vile BWANA alivyoamuru kupitia kinywa cha Musa.
\s5
\v 41 Lakini siku iliyofuata asubuhi watu wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haruni. Nao walisema, "Umeua watu wa BWANA."
\v 42 Kisha ikatokea, wakati watu walipokuwa wamekusanyika kinyume na Musa na Haruni, wakatazama kuielekea hema ya kukutania, na tazama lile wingu lilikuwa likiifunika. Utukufu wa BWANA ukaonekana,
\v 43 Musa na Haruni wakaja mbele ya hema ya kukutania.
\s5
\v 44 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 45 "Toka kati ya watu hawa ili niwaangamize haraka." Musa na Haruni wakalala chini kifudifudi.
\v 46 Musa akamwambia Haruni, uchukue chetezo, na utie ndani moto kutoka madhabahuni, tia na uvumba ndani yake, upeleke haraka kwa watu, na ukafanye upatanisho kwao, kwa sababu hasira hii inatoka kwa BWANA. Tauni imeanza."
\s5
\v 47 Kwa hiyo Haruni akafanya kama alivyoelekezwa na Musa. Akakimbia kati ya watu. na Tauni ilikuwa imeanza kuenea kati ya watu, kwa hiyo akaweka ndani yake uvumba na akafanya upatanisho wa watu.
\v 48 Haruni akasimama kati kati ya zile maiti na watu hai; na kwa njia hii ile tauni ikazuiwa.
\s5
\v 49 Idadi ya wale waliokuwa wamekufa kwa tauni walikuwa14, 000, nje na wale waliokufa kutokana na swala la Kora.
\v 50 Haruni akarudi kwa Musa kwenye lango la hema ya kukutania, na ile tauni ikakoma.
\s5
\c 17
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 2 "Waambie wana wa Israeli wakuletee fimbo za kutembelea moja kwa kila jamaa, fimbo kumi na mbili. Uandika jina la kila mmoja kwenye hizo fimbo.
\s5
\v 3 Utaandika jina la Haruni kwenye jina la Lawi. Kutakuwa na fimbo moja kwa kila kiongozi kutoka kwenye kabila la mababu zake.
\v 4 Utaziweka hizo fimbo kwenye hema ya kukutania mbele ya amri za agano, ambapo Mimi hukutana na wewe. Itakuwa hivi,
\v 5 fimbo ya mtu yule ninayemchagua itachipua. Nitazuia watu wa Israeli walalamikao, ambao wanaongea kinyume na wewe."
\s5
\v 6 Kwa hiyo Musa akawaambia wana wa Israeli. Viongozi wote wa kabila wakampatia fimbo, fimbo moja kutoka kwa kila kiongozi, aliyechaguliwa kutoka kwenye kila kabila ya babu zao, jumla yake fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Haruni ilikuwa miongoni mwa fimbo hizo.
\v 7 Ndipo Musa alipoziweka zile fimbo mbele ya BWANA katika hema ya amri ya agano.
\s5
\v 8 Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye hema ya amri ya agano, na tazama, fimbo ya Haruni kwa ajili ya Kabila la Lawi ilikuwa imetoa machipukizi. Machipukizi yalikuwa hadi kuchanua maua na kuzaa malozi mabivu!
\v 9 Musa akazitoa fimbo zote kutoka kwa BWANA kwa watu wote wa Israeli, na kila mtu akachukua fimbo yake.
\s5
\v 10 BWANA akamwambua Musa, "Iweke fimbo ya Haruni mbele ya amri za agano. Iweke iwe ishara ya hatia mbele ya watu waliopinga ili ukomeshe malalamiko dhidi yangu, vinginevyo watakufa."
\v 11 Musa akafanya kama BWANA alivyoagiza.
\s5
\v 12 Wana wa Israeli wakanena na Musa wakisema, "tutakufa hapa! Wote tutaangamia!
\v 13 Kila mmoja anayekuja hapa, anayekaribia masikani ya BWANA, atakufa. Je, ni lazima wote tuangamie?"
\s5
\c 18
\p
\v 1 BWANA akamwambia Haruni, "Wewe, wana wako, na uzao wa baba yako watawajibika kwa dhambi zote zilizotendwa mahali patakatifu. Lakini wewe na wana wako pekee mtawajibika kwa uovu uliofanywa na yeyote mahali patakatifu.
\v 2 Na ndugu zako nao wa kabila ya Lawi, kabila la ukoo wako, utawaleta pamoja na wewe ili kwamba waweze kuungana na wewe ili wakusaidie wakati wewe na wanao mnapokuwa mnatumikia mbele ya hema ya amri ya agano.
\s5
\v 3 Watakutumikia wewe na hema yote. Hata hivyo, wasisogee karibu na chochote ndani ya mahali patakatifu au kitu chochote kilichounganishwa na madhabahu, vinginevyo wewe na wao mtakufa.
\v 4 Wataungana na wewe na kuitunza hema ya kukutania, kwa kazi zote zinazohusiana na hema. Mtu mgeni asikusogelee.
\v 5 Wewe utaajibika kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya madhabahu ili kwamba hasira yangu isiwajilie watu wa Israeli tena.
\s5
\v 6 Tazama, Mmi mwenyewe nimewachagua ndugu zako wa kabila ya Walawi kutoka mioingoni mwa uzao wa Israeli. Wao ni zawadi kwako. walitolewa kwangu ili waifanye kazi inayohusiana na hema ya kukutania.
\v 7 Lakini ni wewe pekee yako na wanao ndio mnaoruhusiwa kufanya kazi ya ukuhani kuhusiana na kila kitu kilichounganishwa na madhabahu na kitu chochote ndani ya lile pazia. Wewe mwenyewe lazima ukamilishe majukumu hayo. Mimi ninakupa ukuhani kama zawadi. Mgeni yeyote anayekaribia atauawa."
\s5
\v 8 Kisha BWANA akamwambia Haruni, "Tazama, Nimekupa majukumu ya kusimamia sadaka za kuinuliwa kwangu, na sadaka zengine takatifu ambazo wana wa Israeli wanatoa kwangu. Nimekupa sadaka hizi wewe na wana wako kuwa haki yako milele.
\v 9 Hivi ni vitu vitakatifu sana, amabavyo visiteketezwe kwa moto: kutoka kwenye sadaka zao-kila sadaka ya unga, kila sadaka ya dhambi, na kila sadaka ya hatia- ni vitu vitakatifu sana kwa ajili yako na wana wako.
\s5
\v 10 Sadaka hizi ni takatifu sana; kila mume lazima aile, kwa kuwa ni vitakatifu kwako.
\v 11 Hizi ni sadaka ambazo zitakuwa zako: Sadaka zao, sadaka zote za kuinuliwa za wana wa Israeli. Nimekupa wewe, wana wako na binti zako kuwa gawio lako la milele. Kila mmoja ambaye ni msafi katika familia yako anaweza kula sadaka zozote katika hizi.
\s5
\v 12 Mafuta yote mazuri, ile divai nzuri yote mpya na unga, malimbuko ambyo watu hutoa kwangu- vitu hivi vyote nimekupa wewe.
\v 13 Mavuno ya kwanza yaliyoiva yaliyo katika ardhi yao ambayo wanaleta kwangu, yatakuwa yako. Kila mtu aliye msafi kwenye famila yako anaweza kula vitu hivi.
\s5
\v 14 Kila kitu kilichotolewa wakfu katika Israeli kitakuwa chako.
\v 15 Kila kitu kinachofungua tumbo, kila limbuko ambalo watu hutoa kwa BWANA, vyote vya watu na wanyama, vitakuwa vyako. Hata hivyo, watu lazima wawakomboe wazaliwa wa kwanza wa kiume, na watawakomboa wazaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi.
\v 16 Wale ambao wanahitaji kukombolewa na watu watakombolewa wakiwa na umri wa mwezi mmoja. Ndipo watu watawakomboa kwa bei ya shekeli tano, kwa kiwango cha shekeli za mahali patakatifu, ambacho ni sawa na gera ishirini.
\s5
\v 17 Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwana wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi-msiwakomboe hawa wanyama, wametengwa kwa ajili yangu. Utanyunyizia damu yake madhabahuni na kuteketeza mafuta yao kama sadaka ya moto, ambayo ni harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
\v 18 Nyama yao itakuwa yako. Kama kidali cha kuinuliwa na paja la kulia, nyama yao itakuwa yako.
\s5
\v 19 Sadaka yote takatifu ambayo watu wa Israeli wanaitoa kwa BWANA, nimekupa wewe, na wana wako na binti zako walio pamoja nawe. Kama gawio la kudumu. Hili ni agano la milele la chumvi, agano linalofunga milele, mbele za BWANA kwako wewe na uzao wako walio pamoja na wewe."
\v 20 BWANA akasema na Haruni. "hautakuwa na urithi katika ardhi ya watu, wala hautakuwa na gawio miongoni mwa watu. Mimi ndimi gawiio lenu na urithi wenu miongoni mwa watu wa Israeli.
\s5
\v 21 Tazama, Nimewapatia uzao wa Lawi, zaka zote za Israeli kuwa urithi wao kwa sababu ya huduma wanayotoa katika hema ya kukutania.
\v 22 Kuanzi a sasa, watu wa Israeli wasisogee karibu na hema ya kukutania, vinginevyo wataajibika kwa dhambi hii na kufa.
\s5
\v 23 Walawi wafanya kazi inayohusiana na hema ya kukutania. Wataajibika kwa dhambi inyohusiana na hema. Hii itakuwa sheri ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Na miongoni mwa watu wa Israeli hawa hawatakuwa na urithi.
\v 24 Kwa kuwa zaka za wana wa Israeli, wanazotoa kama mchango kwangu -ndivyo hivyo ambavyo nimewapa Walawi kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu ya kuwaambia, Kuwa hawatakuwa na urithi kati ya watu wa Israeli.
\s5
\v 25 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 26 "Inakupasa ukaseme na Walawi uwaambie, 'Mnapopokea zaka toka kwa watu ambayo BWANA amewapa kutoka kwao kuwa urithi, ndipo na nyie mtakapotoa sehemu ya kumi ya zaka hizo.
\v 27 Zaka yenu itahesabika kama moja ya mapato ya sakafu ya kupuria nafaka ya mazao yenu au mazao ya vinu vya kukamulia zabibu.
\s5
\v 28 Kwa hiyo na ninyi lazima mtoe mchango wenu kwa BWANA kutokana na zaka mnazopata kutoka kwa watu wa Israeli. Kutokana na hizo mtatoa matoleo yenu kwa Haruni yule kuhani.
\v 29 Kwa kila sadaka mnayopata, mtatoa matoleo yenu kwa BWANA. Mtafanya hivi kutokana na vitu vizuri na vitakatifu sana ambavyo mmepewa.
\s5
\v 30 Kwa hiyo utawaambia, 'Mnapotoa hayo matoleo mazuri, ndipo itahesabika kwa Walawi kuwa ni mazao yao kutoka kwenye sakafu za kupuria na vinu vyao vya kukamulia.
\v 31 Ndipo matakapokula nafaka zote zinazobaki mahali popote, ninyi na famailia zenu kwa sababu ndiyo malipo yenu ya kazi y a kwenye hema ya kukutania.
\v 32 Hamtakuwa na hatia yeyote kwa kuvila na kuvinywa, kama mtatoa kwa BWANA matoleo yenu mazuri mliyopokea. Lakini msizinajisi sadaka takatifu za wana wa Israeli, vinginevyo mtakufa.,"
\s5
\c 19
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa na Haruni, Akasema,
\v 2 "Hii ni amri, ni sheria ninayokuamuru: Waambie wana waIsraeli wakuletee ng'ombe mke mwekundu asiyekuwa na kipaku wala waa, ambaye hajawahi kubeba nira.
\s5
\v 3 Mpatie Eliazari kuhani huyo ng'ombe jike. Naye atamtoa nje ya kambi, na mtu mmoja amchinje mbele yake.
\v 4 Kisha Eliazari kuhani atachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuinyunyiza mara saba akielekea sehemu ya mbele ya ile hema ya kukutania.
\v 5 Na kuhani mwingine atamchoma huyo ng'ombe mbele ya macho yake. Ataichoma ngozi yake, nyama yake, na damu yake pamoja na mavi yake,
\v 6 Yule kuhani atachukua mti wa mwerezi, na hisopo na sufu na kivitupa katikati ya huyo ng'ombe anayechomwa.
\s5
\v 7 Kisha atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Ndipo atakuja kambini, ambapo atabaki najisi mpaka jioni ya siku hiyo.
\v 8 Yule aliyemchoma huyo ng'ombe mke atafua nguo zake kwa maji na kuoga majini. Naye atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile.
\s5
\v 9 Baadaye mtu aliyesafi atayakusanya hayo majivu ya ng'ombe huyo na kuyaweka nje ya kambi kwenye eneo safi. Majivu haya yatatunzwa kwa ajili ya jamii ya watu wa Israeli. Watayachanganya majivu na maji kwa ajili ya utakaso wa dhambi, kwa kuwa majivu yalitokana na sadaka ya dhambi.
\v 10 Yule aliyeyakusanya majivu ya ng'ombe huyo lazima afue mavazi yake. Atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile. Hii itakuwa sheria ya kudumu kwa watu wa Israeli na kwa wageni wanaoishi nao.
\s5
\v 11 Yeyote atakayegusa maiti ya mtu atakuwa najisi kwa siku saba.
\v 12 Mtu wa jinsi hiyo atajitakasa mwenyewe siku ya tatu na siku ya saba. Ndipo atakapokuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu, basi hatakuwa safi siku ya saba.
\v 13 Yeyote atakayegusa mtu aliyekufa, maiti ya mtu aliyekufa na hajajitakasa - mtu huyu anainajisi masikani ya BWANA. Mtu huyo ataondolewa kuwa miongoni mwa Waisraeli kwa sababu maji ya farakano hayakunyunyiziwa kwake. Atabaki najisi; na unajisi wake utabaki kwake.
\s5
\v 14 Hii ndiyo sheri ya mtu anayefia hemani. Kila mtu aingiaye hemani na kila mtu ambaye tayari yumo hemani atakuwa najisi kwa siku saba.
\v 15 Kila chombo ambacho hakina kifuniko kinanajisika.
\v 16 Vivyo hivyo, kwa mtu aliye nje ya hema ambaye atamgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga wowote, au mfupa wa mtu, au kaburi--mtu huyo atakuwa najisi kwa siku saba.
\s5
\v 17 Fanyeni hivi kwa mtu najisi: twaeni majivu ya sadaka ya dhaambi ya kuteketezwa na myacahanganye kwenye chombo chenye maji ya mto.
\v 18 Ndipo mtu aliye safi atachukua hisopo, na kutia katika hayo maji, na kunyunyizia juu ya hema, na katika vyombo vyote vilivyo hemani, na kwa watu waliokuwepo, na kwa yule aliyegusa ule mfupa, mtu aliyeuawa, maiti, au kaburi.
\v 19 Katika siku ya tatu na siku ya saba, yule mtu aliye msafi atamnyunyizia yule mtu asiyekuwa safi. Katika siku ya saba mtu najisi atajitakasa mwenyewe. Atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Jioni yake atakuwa safi.
\s5
\v 20 Lakini yule atakayebaki najisi, anayekataa kujitakasa mwenyewe -- huyo mtu ataondolewa kutoka kwenye jamii, kwa sababu amepanajisi patakatifu pa BWANA. Hajanyunyiziwa maji ya utakaso; atabaki najisi.
\v 21 Hii itakuwa sheria ya kudumu kuhusiana na hali ya hivi. Yule mtu anayenyunyizia maji ya farakano atafua mavazi yake. Yule atakayeyagusa maji ya farakano atakuwa najisi mpaka jioni.
\v 22 Chochote kile ambacho kitaguswa na mtu najisi kitakuwa najisi. na mtu atakayekigusa naye atakuwa najisi mpaka jioni.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Kwa hiyo wana wa Israeli, na jamii yote ya watu, wakaenda katika jangwa la Sini katika mwezi wa kwanza; wakaa Kadeshi. Hapo ndipo Miriamu alipofia na kuzikwa.
\s5
\v 2 Huko hapakuwa na maji kwa ajili ya watu, kwa hiyo wakakusanyika kinyume na Musa na Haruni huko.
\v 3 Watu wakamlalamikia Musa. Wakasema, "Ilikuwa ni bora kama tungelikufa wakati Waisraeli wenzetu walipokufa mbele za BWANA.
\s5
\v 4 Kwa nini umewaleta watu wa BWANA kufia katika jangwa hili, sisi na wanyama wetu?
\v 5 Kwa nini ulitutoa Misri na kutuleta katika eneo hili baya? Hapa hakuna nafaka, wala mitini, wala mizabibu, wala makomamanga. Na hakuna maji ya kunywa."
\s5
\v 6 Basi Musa na Haruni wakatoweka mbele ya mkutano huo. Wakaenda kwenye hema ya kukutania wakalala kifudifudi. Ndipo pale utukufu wa Busara wa BWANA ukaonekana kwao.
\s5
\v 7 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 8 "Chukua fimbo yako na uwakusanye watu, wewe na Haruni ndugu yako. Uumbie huu mwamba mbele ya macho yao, na uumuru utoe maji. Nawe utawapa maji kutoka kwenye huu mwamba, nawe utawapa maji ya kunywa hao watu na wanyama wao."
\v 9 Musa akachukua hiyo fimbo mbele ya BWANA, kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
\s5
\v 10 Kisha Musa na Haruni wakawakusanya watu pamoja mbele ya ule mwamba. Ndipo Musa akawaambia, "Sasa sikilizeni, enyi wapinzani. Lazima tuwape maji kutoka kwenye huu mwamba?"
\v 11 Ndipo Musa akanyosha mkono wake na kuupiga ule mwamba mara mbili kwa fimbo yake, na maji mengi yakatoka. Wale watu wakanywa pamoja na wanyama wao.
\s5
\v 12 Kisha BWANA akamwambia Musa na Haruni, "Kwa kuwa hamkuniheshimu mimi na kuniamini mbele ya watu wa Israeli, hamtawaingiza hawa watu katika nchi niliyowaahidi.
\v 13 Mahali hapa paliitwa maji ya Meriba kwa sababu wana wa Israeli walitofautiana na BWANA pale, na akajionyesha kwao kuwa mtakatifu.
\s5
\v 14 Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwa mfalme wa Edom: Ndugu yako Israeli anasema hivi: "Wewe unajua magumu yote ambayo yametupata.
\v 15 Na unajua kuwa babu zetu walienda Misri na waliishi Misri kwa muda mrefu. Wamisri walitutendea vibaya pamoja na babu zetu.
\v 16 Tulipomlilia BWANA, akatusikia na kututumia malaika ambaye alitutoa toka Misri. Tazama, sasa tuko Kadeshi, mji unaopakana na nchi yako.
\s5
\v 17 Tunakuomba uturuhusu kupita katika nchi yako. Hatutapita mashambani wala kwenye mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita kwenye njia kuu ya mfalme. Hatutageuka upande wa kulia wala upande wa kushoto mpaka tutakapopita mpaka wako."
\s5
\v 18 Lakini mfalme wa Edomu akamjibu, "Msipite hapa. Kama mtafanya hivyo, Nitakuja na upanga kukuvamia."
\v 19 Ndipo wana wa Israeli wakamwambia,"tutapitia njia kuu. Kama sisi au wanyama wetu watakunywa maji yako, basi tutalipa. Tunaomba uturuhusu tupite tukitembea kwa miguu yetu, bila kufanya jambo lolote lile."
\s5
\v 20 Lakini mfalme wa Edomu akajibu, "Usipite hapa." Kwa hiyo nfalme wa Edomu akawa kinyume cha Israeli kwa mkono wenye nguvu pamoja na jeshi kubwa sana.
\v 21 Mfame wa Edomu akawazuia wana wa Israeli kupita kwenye mipaka yake. Kwa sababu ya hili, Israeli akageuka kuiacha nchi ya Edomu.
\s5
\v 22 Kwa hiyo watu wakasafiri kutoka Kadeshi. Wana wa Israeli, watu wote, wakafika Mlima Hori.
\v 23 BWANA akanena na Musa na Haruni hapo kwenye Mlima Hori, kwenye mpaka wa Edomu. Akasema,
\v 24 "Sasa ni wakati wa Haruni kukusanyika na watu wake, hataingia katika nchi ile niliyowaahidi wana wa Israeli. Hii ni kwa sababu ninyi wawili hamkuitii sauti yangu pale kwenye maji ya Meriba.
\s5
\v 25 Mchukue Haruni na Eliazari mwanaye, na uwalete juu ya Mlima Hori.
\v 26 Umvulishi HarunI yale mavazi ya kikuhani na umvalishe Eliazari mwanaye. Haruni atakufa na kulazwa pamoja na watu wake."
\s5
\v 27 Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru. Wakaenda juu y a Mlima Hori na watu wote wakiona.
\v 28 Musa akamvulisha Haruni yale mavazi ya kikuhani na kumvalisha Mwanaye Eliazari. Haruni akafa pale juu ya Mlima Hori. Kisha Musa na Eliazari wakashuka.
\v 29 Watu walipoona kuwa Haruni amekufa, taifa lote wakamlilia Haruni kwa siku arobaini.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Aradi mfalme wa Wakanaani, aliyekuwa akiishi Negebu, aliposikia kuwa Israeli alikuwa akisafiri kwa kupitia barabara kuelekea Atharimu, akapigana dhidi ya Israeli na kujitwalia baadhi ya mateka.
\v 2 Israeli akaapa mbele ya BWANA akasema, "Kama utatupa ushindi dhidi ya hawa watu, ndipo tutakapoingamiza kabisa miji yao,"
\v 3 BWANA akaisikia sautiya Israeli na kuwapa ushindi dhidi ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. Mahali pale paliitwa Horima.
\s5
\v 4 Wakasafiri kutoka Mlima Hori kwa barabara kuelekea bahari ya shamu wakiizunguka nchi ya Edomu. Watu walikufa moyo kwa njia hiyo.
\v 5 Watu wakamnung'unikia Mungu na Musa: "Kwa nini umetutoa Misiri ili tufa katika jangwa hili? Hapa hakuna mikate, wala maji, na chakula hiki dhaifu kimetukinai."
\s5
\v 6 Basi Mungu akatuma nyoka wa sumu kati yao. Wale nyoka wakawauma wale watu; watu wengi walikufa.
\v 7 Watu wakaenda kwa Musa wakamwambia, "Tumetenda dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu na wewe. Mwombe Mungu atuondolee hawa nyoka." Kwa hiyo Musa akawaombea watu.
\s5
\v 8 BWANA akamwambia Musa, "Tengeneza nyoka na umweke kwenye nguzo. Na itakuwa kila anayeumwa, akimwangalia huyo nyoka atapona,"
\v 9 Kwa hiyo Musa akatengeneza nyoka wa shaba naye akamweka juu ya nguzo. Na kila mtu alipoumwa na nyoka na kumwangalia huyo nyoka alipona.
\s5
\v 10 Kisha watu wa Israeli wakasafiri na kisha kuweka kambi Obothi.
\v 11 Kisha wakasafiri kutoka pale na kuweka kambi Iye Abarimu katika jangwa linalokabili Moabu kuelekea upande wa mashariki.
\s5
\v 12 Kutoka pale wakasafiri na kuweka kambi katika bonde la Zeredi.
\v 13 Kutoka pale walisafiri na kuweka kambi kwenye upande mwingine wa mto Amoni, ambao ukubwa wake unaanzia kwenye mpaka wa Waamori. Mto wa Amoni ndio unaootengeneza mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
\s5
\v 14 Ndiyo maana imeandikwa katika gombo la Kitabu cha BWANA, "Wahebu katika Sufa, na bonde la Amoni,
\v 15 mtelemko wa bonde linaloelekea katika mji wa Ari na kuelekea kwenye mpaka wa Moabu,"
\s5
\v 16 Kutoka pale wakasafiri mpaka Beeri, hapo ndipo palipo na kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, "Wakusanye watu kwa ajili yangu ili uwape maji,"
\s5
\v 17 Ndipo Israeli waipoimba wimbo huu: "enyi visima, yajazeni maji. Imbeni juu ya kisima hiki.
\v 18 Kisima ambacho viongozi wetu walichimba, kisima ambacho wenye hekima walichimba kwa fimbo ya kifalme na kwa fimbo ya kutembelea." Kisha kutoka jangwani walitembea mpaka Matanaha.
\s5
\v 19 Kutoka Matanaha walisafiri mpaka Nathalieli, na kutoka Nathalieli mpaka Bamothi,
\v 20 na kutoka Bamothi hadi kwenye bonde la Moabu. Hapo ndipo kilele cha Mlima Piska kinapoonekana jangwani.
\s5
\v 21 Kisha Israeli akatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamori akisema,
\v 22 Tunaomba tupite katika nchi yako. hatutapita katika shamba au kwenye shamba la mizabibu. Hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita katika njia kuu ya mfalme mpaka tutakapopita mpaka wako."
\v 23 Lakini mfalme Sihoni hakumruhusu Israeli kupita kwenye mpaka wao. Badala yake, Sihoni akakusanya jeshi lake lote na kumvamia Isreli huko jangwani. Akaja kwa Jahazi, ambapo alipigana dhidi ya Israeli.
\s5
\v 24 Israeli akalivamia jeshi la Sihoni na nchi ya upanga na kuchukua nchi yao kutoka Amon mpaka mto Jabboki, hadi kufikia nchi ya watu wa Amoni. Sasa mpaka wa watu wa Amoni ulikuwa umefungwa.
\v 25 Israeli akachukua miji yote ya Waamori na akaishi ndani yake, pamoja na Heshiboni na vijiji vyake wote.
\v 26 Heshiboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alipigana dhidi ya mfalme wa kwanza wa Moabu. Sihoni alikuwa ameteka ardhi yake yote toka mipaka yake mpaka mto wa Amoni.
\s5
\v 27 Hiyo ndiyo sababu wala ambao huongea kwa Mitahali husema, "Njoni Heshboni. Mji wa Sihoni ujengwe na kuimarishwa tena.
\v 28 Moto uliwaka toka Heshiboni, moto kutoka mji wa Sihoni ambao uliiteketeza Ari ya Moabu, na wenyeji wa miji ya juu ya Amoni.
\s5
\v 29 Ole wako, Moabu! umepotea, enyi watu wa Chemoshi. Amewafanya watu wake kuwa wakimbizi na binti zake kuwa wafungwa wa Sihoni mfalme wa Waamori.
\v 30 Lakini tumempiga Sihoni. Tumeiangsmiza Heshibon mpaka Diboni. Tumewaharibu wote mpaka Nofa, ambayo inafika mpaka Madeba."
\s5
\v 31 Kwa hiyo Israeli akaanza kuishi katika nchi ya Waamori,
\v 32 Kisha Musa akatuma watu kwenda kuingalia Yaziri. Waliviteka vijiji vyake na kuwafukuza Waamori waliokuwa wakiishi humo.
\s5
\v 33 Kisha wakageuka na kuelekea njia inayoelekea Bashani. Ogu mfalme wa Bashani akatofautiana nao, yeye na Jeshi lake lote, ili apigane nao kule Ederei.
\v 34 Kisha BWANA akasema na Musa, "Msimwogope, kwa sababu nimewapeni ushindi dhidi yake, Jeshi lake lote na nchi yake. Mfanyeni kama mlivyomfanya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akiishi Heshiboni."
\v 35 Kwa hiyo wakamuua, na wanawe, na jeshi lake lote, mpaka wote wakaishi na hakubaki hata mmoja aliyebaki hai. Kisha wakaichukua nchi yake.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Watu wa Israeli wakasafiri mpaka wakaweka kambi kwenye uwanda wa Moabu karibu na Yeriko, kwenye upande mwingine wa mto Yorodani kutoka mji ule.
\s5
\v 2 Balaki mwana wa Zippori aliona yote ambayo Israeli aliwafanyia Waamori. Moabu aliogopa sana hao watu kwa sababu walikuwa wengi sana,
\v 3 na Moabu alIwahofia wana wa Israeli.
\v 4 Mfalme wa Moabu akawaambia wazee wa Midiani, "Huu umati utakula kila kitu tulicho nacho na maksai hula nyasi za kondeni." Sasa Balaki mwana wa Zippori alikuwa mfalme wa Moabu.
\s5
\v 5 Akatuma wajumbe kwenda kwa Balamu mwana wa Beori, kule Petho ambayo iko karibu na mto Frati, katika nchi ya taifa lake na watu wake. Akamwita na kumwambia, "Tazama, Kuna taifa ambalo wamekuja hapa tokea Misiri. Wanafunika uso wa dunia na sasa wananifuatia mimi.
\v 6 Tafadhali naomba uje unilaanie hili taifa, kwa sababu wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwavamia na kuwafukuza watoke katika nchi yangu. Najua kuwa yeyote unayembariki hubarikiwa na yeyote unayemlaani atalaaniwa."
\s5
\v 7 Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki.
\v 8 Balaamu akawaambia, "Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA." Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo.
\s5
\v 9 Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, "Ni akina nani hawa waliokuja kwako?"
\v 10 Balaamu akamjibu Mungu, "Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema,
\v 11 'Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwa kuwashinda na kuwafukuza.'"
\s5
\v 12 Mungu akamjiu Balaam, "Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa."
\v 13 Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki,. "Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi."
\v 14 Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, "Balaamu amekataa kuambatana nasi."
\s5
\v 15 Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.
\v 16 Wakaja kwa Balaamu na kumwambia, "Balaki mwana wa Zippori anasema hivi, 'Tafadhali hebu kitu chochote kisikuzuie kuja kwangu,
\v 17 kwa sababu nitakulipa malipo mazuri sana na kukupa heshima kubwa, nami nitakufanyia chochote utakachoniambia. Tafadhali sana uje unilaanie hawa watu.'"
\s5
\v 18 Balaamu akawajibu watu wa Balaki akawaambia, "Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitaweza kufanya dhidi ya maneno ya BWANA, Mungu wangu na kufanya pungufu au zaidi ya kile anachoniambia.
\v 19 Sasa basi, tafadhali subirini hapa usiku wa leo pia, ili kwamba nipate kujifunza kitu zaidi ambacho BWANA ananiambia."
\v 20 BWANA akaja kwa Balaamu usiku ule na kumwambia, "kwa kuwa hawa watu wamekuja kukuita, inuka uende nao. Lakini utafanya tu kile nitakachokuambia kufanya."
\s5
\v 21 Balaamu akainuka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na viongozi wa Moabu.
\v 22 Lakini kwa sababu alienda, hasira za Mungu zikawaka. Malaika wa BWANA akasimama barabarani kama adui wa Balaamu, aliyekuwa akimpanda yule punda. Watumishi wawili wa Balaamu walikuwa pamoja naye.
\v 23 Yule punda alimwona yule malaika wa BWANA akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Yule punda akageuka na kwenda shambani. Balaamu akampiga yule punda ili arudi barabarani.
\s5
\v 24 Sasa malaika wa BWANA akasimama kwenye njia nyembamba katikati ya mashamba ya mizabibu, na kushoto kwake kulikuwa na ukuta.
\v 25 Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda.
\s5
\v 26 Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.
\v 27 Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.
\s5
\v 28 Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, "Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?"
\v 29 Balaamu akamjibu yule punda, "Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua."
\v 30 Yule punda akamwambia Balaamu, "Je, mimi si punda wako ambaye umenipanda maishani mwako mwote mpaka hivi sasa? Je, nimewahi kuwa na tabia ya kukufanyia hivi hapo awali?" Balaamu akasema "hapana."
\s5
\v 31 Basi BWANA akafungua macho ya Balaamu, na akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Balaamu akainamisha kichwa chake chini.
\v 32 Yule malaika wa BWANA akamwambia, "Kwa nini umempiga punda wako mara tatu? Tazama, Nimekuja kama adui yako kwa sababu matendo yako kwangu yamekuwa maovu.
\v 33 Yule punda aliniona na akageuka kutoka kwangu mara tatu. Kama asingekuwa amegeuka kutoka kwangu, hakika ningekuwa nimekua na yeye kumwacha hai.
\s5
\v 34 Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, nimetenda dhambi. Sikujua kuwa ulisimama kinyume na mimi barabarani. Kwa hiyo sasa, kama haikupendezi, Nitageuka."
\v 35 Lakini yule malaika wa BWANA akamwambia Balaamu, "endelea na wale watu. Lakini utasema maneno nitakayokwambia tu."Kwa hiyo Balaamu akaendelea na wale vioingozi wa Balaki.
\s5
\v 36 Balaki aliposikia kuwa Balaamu alikuwa amekuja, alienda kukutana naye kule mjini Moabu pale Amoni, ambao uko mpakani.
\v 37 Balaki akamwambia Balaamu, "Je, mimi sikutuma watu kukuita? Basi kwa nini hukuja kwangu? Je, mimi sina uwezo wa kukufanya uheshimike?"
\s5
\v 38 Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, "Tazama, mimi nimekuja kwako. Je mimi sina mamlaka ya kusema chochote? Mimi ninaweza kusema maneno ambayo Mungu ameweka kinywani mwangu."
\v 39 Balaamu akaenda na Balaki, na Wakafika Kiriathi Huzothi.
\v 40 Kisha Balaki akatoa sadaka ya maksai na kondoo na kumpatia Balaamu baadhi ya hiyo nyama na wale viongozi waliokuwa pamoja naye.
\s5
\v 41 Kesho yake asubuhi, Balaki akampeleka Balaamu mpaka juu mahali pa Baali. Kule juu Balaamu aliweza kuona sehemu tu ya kambi za Waisraeli.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Balaamu akamwabia Balaki, "Jenga madhabahu saba kwa ajili yangu na uandae mafahari saba na kondoo dume saba."
\v 2 Kwa hiyo Balaki akafanya kama Balaamu alivyoomba. Kisha Balaki na Balaamu wakatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume mmoja kwa kila madhabahu.
\v 3 Ndipo Balaamu alipomwamiba Balaki, "Simama kwenye sadaka yako ya kuteketezwa na mimi nitaenda. Labda BWANA atakuja kukutana na mimi. Chochote atakachoniambia nitakuambia." Kwa hiyo akaenda juu ya mlima usiokuwa na miti.
\s5
\v 4 Wakati bado akiwa juu ya mlima. Mungu akakutana naye, na Balaamu akamwambia, "Nimejenga madhabahu saba, na nimetoa sadaka ya fahari na kondoo dume kwa kila madhabahu."
\v 5 BWANA akaweka ujumbe kwenye kinywa cha Baalamu akasema, "Rudi kwa Balaki ukamwambie."
\v 6 Kwa hiyo Balaamu akarudi kwa Balaki aliyekuwa amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na viongozi wote wa Moabu walikuwa pamoja naye.
\s5
\v 7 Ndipo Balaamu alipoanza kunena unabii wake akisema, "Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka katika milima ya mashariki, 'Njoo, nilaanie Yakobo kwa ajili yangu,' alisema, 'Njoo umtie unajisi Israeli,'
\v 8 Nawezaje kuwalaani wale ambao Mungu hajawalaani? Nawezaje kuwapinga wale ambao Mungu hawapingi?
\s5
\v 9 Kwa kuwa kutoka juu ya miamba Ninamwona; kutoka kwenye milima ninamtazama. Kuna watu wanaoishi pekee yao na hawajioni wenyewe kama ni taifa la kawaida.
\s5
\v 10 Nani awezaye kuyahesabu mavumbi ya Yakobo au kuhesabu hata robo ya Israeli? Naomba nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wa maisha yangu uwe kama wake!"
\s5
\v 11 Balaki akamwambia Balaamu, "Umenifanyia nini? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini ona, umewabariki,"
\v 12 Balaamu akajibu akasema, "Kwa nini nisiwe mwangalifu kusema kile ambacho BWANA anaweka kinywani mwangu?"
\s5
\v 13 Basi Balaki akamwambia, "Hebu uje nami kwenye eneo jingine ili uwaone. Utakaowaona ni wale wa karibu tu, huwezi kuwaona wote. Huko sasa unaweza kunilaania hawa watu."
\v 14 Kwa hiyo akampeleka Balaamu kwenye shamba la Zofimu, lililo juu ya Mlima Pisiga, na kule akajenga madhabau zingine saba. Akatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume kwa kila madhabahu.
\v 15 Kisha Balaamu akamwambia Balaki, "Simama hapa karibu na sadaka zako, wakati mimi naenda kukutana na BWANA kule."
\s5
\v 16 Kwa hiyo BWANA akakutana na Balaamu na kumwekea ujumbe kinywani mwake. Alimwambia, "Rudi kwa Balaki ukamwambie huu ujumbe toka kwangu."
\v 17 Balaamu akamrudia, na tazama, alikuwa amesimama karibu na sadaka zake za kuteketezwa, na vionigozi wa Moabu walikuwa pamoja naye. Balaki akamwuliza, "BWANA amekwambiaje?"
\v 18 Balaamu akaanza kutoa unabii. Akasema, "Inuka, Balaki na usikilize. Nisikilize mimi wewe mwana wa Zippori.
\s5
\v 19 Mungu siyo mtu, kwamba umdanganye, au mwanadamu awezaye kubadili mawazo. Je, alishawahi kuahidi kitu pasipo kukitekeleza? Je, alishawahi kusema kuwa atafanya kitu bila kufanya kama alivyosema?
\v 20 Tazama, Mimi nimeamriwa kuwabariki. Mungu ametoa baraka, nami siwezi kuibadilisha.
\s5
\v 21 Hajawahi kuona magumu katika Yakobo au tabu katika Israeli. BWANA Mungu wao yuko pamoja nao, na kelele za wafalme wao ziko pamoja nao.
\v 22 Mungu aliwatoa Misri kwa nguvu kama za nyati.
\s5
\v 23 Hakuna uganga utakaofanikiwa dhidi ya Yakobo, na hakuna uchawi utakaomwumiza Israeli. Badala yake, itasemwa juu ya Yakobo na Israeli, 'Tazama kile ambacho Mungu amefanya!'
\s5
\v 24 Tazama, watu wanainuka kama simba jike, kama vile simba ainukavyo na kuvamia. Halali chini mpaka ale windo lake na kunywa damu ya windo lake,"
\s5
\v 25 Kisha Balaki akamwambia Balaamu, "Kamwe usiwalaani wala kuwabariki."
\v 26 Lakini Balaamu akamjibu Balaki, "Sijakuambia kuwa nitasema yote ambayo BWANA ananiambia kusema?
\v 27 Balaki akamwambia Balaamu, "Njoo sasa, Nami nitakupeleka mahali pengine. Labda kule itampendeza Mungu kunilaania hawa hawa watu."
\s5
\v 28 Kwa hiyo Balaki akampeleka Balaamu juu ya Mlima Peori, ambao unalitazama chini lile jangwa,
\v 29 Balaamu akamwambia Balaki, "Nijengee madhabahu saba hapa na uniandalie mafahari saba na kondoo duume saba.
\v 30 "Kwa hiyo Balaki akafanya kama alivyoambiwa; akatoa sadaka ya fahari na kondoo mume kwenye kila madhabahu.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Balaamu alipooa kuwa ilimpendeza BWANA kubariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, kwa kutumia uganga, badala yake akatazama jangwani.
\s5
\v 2 Akayainua macho yake na kumwona Isreli akiwa kwenye kambi, kila mmoja kwa kabila yake, na Roho wa Mungu akamjia.
\v 3 Akapokea huu unabii na kusema, "Balaamu mwana wa Beori anataka kusema, yeye ambaye macho yake yemefunuliwa sana.
\s5
\v 4 Huongea na kusikia maneno ya Mungu. Huona maono toka kwa Mwenyezi, ambaye mbele zake humwinamia na macho yake yakiwa yamefumbuliwa.
\v 5 Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli!
\s5
\v 6 Wamesambaa kama bonde, kama bustani zilizo pembezoni mwa mto, Kama miti ya mishubiri iliyopandwa na BWANA, ni kama mfano wa mielezi pembezoni mwa maji.
\s5
\v 7 Maji yanatiririka katika ndoo zao, na mbegu zao zimemwagiwa maji vizuri. Mfalme wao atakuwa juu ya Agagi, na ufalme wao utaheshimiwa.
\s5
\v 8 Mungu anamtoa Misri, na nguvu kama za nyati. Atawameza mataifa wanaopigana nao. Ataivunja mifupa yao katika vipande vipande. atawapiga kwa mishale yake.
\s5
\v 9 Ananyatia kama simba mume, na kamaa simba jike. Ni nani atakayejaribu kumsumbua? Kila mmoja anayembariki na abarikiwe; na kila mmoja anayemlaani na alaaniwe."
\s5
\v 10 Hasira za Balaki zikawaka dhidi ya Balaamu naye akaipiga mikono yake kwa pamoja. Balaki akamwambia Balaamu, "Nilkuita ili uwalaani maadui zangu, Lakini tazama, umewabariki mara tatu.
\v 11 Kwa hiyo ondoka uende nyumbani uniache sasa hivi. Nilisema ningekupa zawadi kubwa sana, lakini BWANA amekuzuilia kupata zawadi."
\s5
\v 12 Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, "Niliwaambia wale wajumbe ulionitumia,
\v 13 'Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitafanya zaidi ya maneno ya BWANA kwa lolote zuri au baya, au kwa chochote ambacho ningetaka kufanya. Ninaweza kusema kile tu ambacho BWANA ananiambia kusema,' Je, sikuwaambia haya?
\v 14 Kwa hiyo sasa, tazama, nitarudi kwa watu wangu. Lakini kwanza nikuonye kile ambacho hawa watu watawafanyia watu wako katika siku zijazo."
\s5
\v 15 Balaamu alianza unabii huu. Akisema, "Balaamu mwana wa Beori anasema, Mtu yule aliyefumbuliwa macho yake.
\v 16 Huu ni unabii wa mtu alisikiaye neno la Mungu, aliye na maarifa toka kwake Yeye aliye juu, aliye na maono kutoka kwa Mwenyezi, Yeye ambaye humpigia magoti macho yakiwa yamefumbuliwa.
\s5
\v 17 Ninamwona, lakini hayuko hapa sasa. Ninamtazama, lakini siyo karibu. Nyota itatokea katika Yakobo, na fimbp ya enzi itatokea katika Israeli. Naye atawapigapiga viongozi wa Moabu na kuwaharibu wa uzao wa Sethi
\s5
\v 18 Ndipo Edomu atakapokuwa miliki ya Israeli, na Seiri pia itakuwa milki yao, maadui wa Israeli, ambao Israeli atawashinda kwa nguvu zake.
\v 19 Kutoka kwa Yakobo atatoka mfalme ambaye utawala wake naye atawaangamiza waliosalia katika mji."
\s5
\v 20 Kisha Balaamu akamtazama Amaleki na akaanza kutoa unabii wake. Alisema, "Amaleki alikuwa mkuu katika mataifa, lakini mwisho wake utakuwa uharibifu."
\s5
\v 21 Kisha Balaamu akawatazama Wakeni na akaanza kutoa unabii wake. Akasema, "Mahali unapoishi pana usalama, na viiota vyake viko kwenye miamba.
\v 22 Lakini pamoja na hayo, Kaini ataharibiwa na Ashuru atakapowachukua mateka."
\s5
\v 23 Kisha Balaamu akanza unabii wake wa mwisho. Akasema, "Ole wake atakayesalia Mungu atakapoyafanya haya?
\v 24 Merikebu zitakuja toka pwani ya Kittimu; Zitaivamia Ashuru na kuiharibu Eberi, lakini wao pia wataishia kwenye uharibifu."
\v 25 Kisha Balaamu akainuka na kuondoka. Akarudi nyumbani kwake, na Balaki naye akaondoka.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Israeli akakaa Shitimu, na wanaume wakaanza kufanya ukahaba na wanawake wa Moabu,
\v 2 kwa kuwa Wamoabu waliwakaribishsa kutoa sadaka kwa miungu yao. Kwa hiyo watu wakala na kuisujudia miungu ya Moabu.
\v 3 Watu wa Israeli wakaungana kumwabudu Baali wa Peori, na hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Israeli.
\s5
\v 4 BWANA akamwambia Musa, "Waue viongozi wote wa watu na uwanyonge mbele yangu ili waonekane wakati wa mchana, ili kwamba hasira yangu kali iondoke kwa Israeli."
\v 5 Kwa hiyo Musa akawaambia viongozi wa Israeli, "Kila mmoja wenu lazima awanyonge watu wake ambao wameshiriki kumwabudu Baali wa Peori."
\s5
\v 6 Kisha mtu mmoja wa Israeli akaleta mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa familia yake. Hili lilitokea mbele ya macho ya Musa na watu wa Israeli, wakati walipokuwa wakilia mbele ya lango la hema ya kukutania.
\v 7 Finehasi mwana wa Eliazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona hivyo, akainuka kutoka jamii ya watu akachukua mkuki mkononi mwake.
\s5
\v 8 Akamfuata yule mwanaume Muisraeli hemani na kuwachoma kwa mkuki wote wawili kwenye miili yao, wote yule Muisraeli na yule mwanamke. Kwa hiyo ile tauni ambayo Mungu alikuwa ameituma kwa watu wa Israeli ikakoma.
\v 9 Idadi ya wale waliokufa kwa tauni walikuwa elfu ishirini na nne.
\s5
\v 10 BWANA akanena na Musa, akasema,
\v 11 "Finehasi mwana wa Eliazari mwana wa Haruni, kuhani amaigeuza hasira yangu isiwe kwa wana wa Israeli kwa sababu alikuwa na wivu kati yao juu ya wivu wangu. Kwa hiyo sijawaangamiza watu wa Israeli kwa hasira yangu.
\s5
\v 12 Kwa hiyo waambie, 'BWANA anasema, "Tazama, Ninampa Finehasi agano la amani.
\v 13 Kwake na kwa wana wake baada yake, litakuwa agano la kudumu la ukuhani kwa sababu alikuwa na wivu juu yangu, Mungu wake. Amewapatanisha wana wa Israeli.
\s5
\v 14 Sasa yule Muisraeli aliyeuwawa pamoja na Yule mwanamke Mmidiani alikuwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa familia ya uzao wa Simeoni.
\v 15 Jina la yule Mmidiani aliyeuwawa lilikuwa Cozibi binti wa Zuri, ambaye alikuwa mkuu wa familia wa kabila huko Midiani.
\s5
\v 16 Kwa hiyo BWANA akanena na Musa na kusema,
\v 17 "Watendee Wamidiani kama maadui na uwaangamize, kwa kuwa waliwatendea kama maadui
\v 18 kwa kuwadanganya. Waliwaongoza katika uovu kwa swala la Peori na kwa swala la dada yao Cozibi, binti wa kiongozi wa Wamidiani, ambaye aliuawa siku ile ya tauni kwa swala la Peori."
\s5
\c 26
\p
\v 1 Ilitokea baada ya tauni ambayo BWANA alimwambia Musa na Eliazari mwana wa Haruni kuhani, Alisema,
\v 2 Wahesabu watu wote wa Israeli, kuanzia miaka ishirini na zaidi, kwa jamaa ya familia zao wote ambao wanaweza kwenda kwenye vita kwa ajili ya Israeli."
\s5
\v 3 Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakawaambia katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko na kusema,
\v 4 Wahesabuni watu, kuanzi umri wa miaka ishirini na zaidi kama BWANA alivyomwamuru Musa na watu wa Israeli walitoka katika nchi ya Misri."
\s5
\v 5 Reubeni ndiye aliyekuwa wa kwanza, Kutoka kwa mwana wake Hanoki ulitokea ukoo wa Wahanoki. Kutoka kwa Palu ulitokea ukoo wa Wapalu.
\v 6 Kutoka Hezroni. ulitokea ukoo wa Wahezroni. Kutoka kwa Kami ulitokea ukoo wa Wakami.
\v 7 Hizi ndizo zilikuwa koo za uzao wa Reubeni, ambzo idadi yao ilikuwa wanaume 43, 730.
\s5
\v 8 Eliabu alikuwa mwana wa Palu.
\v 9 Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.
\s5
\v 10 Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, amboa wlikuwa ishara ya onyo.
\v 11 Lakini uzao wa Kora haukufa.
\s5
\v 12 Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,
\v 13 kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
\v 14 Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22, 200.
\s5
\v 15 Koo za uzao wa Gadi zilikuwa hizi: Kwa Zefoni, Ukoo wa Wazefoni, kwa Hagi, ukoo wa Wahagi, kwa Shuni, ukoo wa Washuni,
\v 16 kwa Ozini, ukoo wa Waozini, kwa Eri, ukoo wa Waeri,
\v 17 kwa Arodi, ukoo wa Waarodi, kwa Areli, ukoo wa Waareli.
\v 18 Hizi ndizo koo za uzao wa Gadi, idadi yao walikuwa wanaume 40, 500.
\s5
\v 19 Wana wa Yuda walikwa Er na Onani, lakini hawa walifia katika nchi ya Kanaani.
\v 20 Koo zingine za uzao wa Yuda zilikuwa hizi: Kwa Shela, ukoo wa Washela, kwa Perezi, ukoo wa Waperezi, na kwa Zera, ukoo wa Wazera.
\v 21 Uzao wa Perezi walikuwa hawa: Kwa Hezroni, ukoo wa Wahezroni, kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
\v 22 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda, idadi yao ilikuwa wanaume 76, 500.
\s5
\v 23 Koo za uzao wa Isakari zilikuwa hizi: Kwa Tola, ukoo wa Watola, kwa Puva, ukoo wa Wapuva,
\v 24 kwa Jashubu, ukoo wa Wajashubu, kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
\v 25 Hizi ndizo zilikuwa koo za Isakari, Idadi yao ilikuwa wanaume 64, 300.
\s5
\v 26 Koo za uzao wa Zabuloni zilikuwa hizi: Kwa Seredi, ukoo wa Waseredi, kwa Eloni, ukoo wa Waeloni, kwa Jahaleeli, ukoo wa Wajahaleeli.
\v 27 Hizi ndizo zilikuwa koo za Zabuloni, idadi y ao ilikuwa wanaume 60, 500.
\s5
\v 28 Koo za uzao wa Ysufu zilikuwa Manase na Efraimu.
\v 29 Huu ndio uliokuwa uzao wa Manase: Kwa Machiri, ukoo wa Wamachiri (Machiri ndiye aliyekuwa baba wa Giliedi), kwa Giliedi, ukoo wa Wagiliedi.
\s5
\v 30 Wazo wa Giliedi walikuwa hawa wfuatao: Kwa Lezeri, ukoo wa Walezeri, kwa Helweki, ukoo wa Waheleki, kwa Asrieli,
\v 31 ukoo wa Asrieli wa Waasrieli, kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu,
\v 32 kwa Shemida, ukoo wa Washemida, kwa Hefa, ukoo wa Wahefa.
\s5
\v 33 Zelofehadi mwana wa Hefa hakuwa na watoto wa kiume bali alikuwa na mabinti. Majina ya binti zake yalikuwa Mahilahi, Noha, Hoglaha, Milika, na Tiriza.
\v 34 Hizi ndizo koo za Manase, idadi yao ilikuwa wanaume 52, 700.
\s5
\v 35 Koo za wana wa uzao wa Efraimu zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuthelaha, ukoo wa Washutheleha, kwa Becheri, ukoo wa Wabecheri, kwa Tahana, ukoo wa Watahana.
\v 36 Uzao wa Shuthelaha walikuwa, kwa Erani, ukoo wa Waerani.
\v 37 Hizi ndizo koo za uzao wa Efraimu, idadi yao ilikuwa wanaume 32, 500. Huu ndio uzao wa Yusufu, uliohesabiwa toka kila koo zao.
\s5
\v 38 Koo za uzao wa Benjamini zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Bela ukoo wa Wabela, kwa Ashibeli, ukoo wa Washibeli, kwa Ahiramu, ukoo wa Wahiramu,
\v 39 kwa Shefufamu, ukoo wa Washefumamu, kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
\v 40 Wana wa Bela walikuwa ni Ardi na Naamani. Kutoka kwa Ardi ulijitokeza ukoo wa Waardi, na kutoka kwa Naamani ukajaitokeza ukoo wa Wanaamani.
\v 41 Hizi ndizo koo za uzao wa Benjamini. Idadai yao ilikuwa wanaume 45, 600.
\s5
\v 42 Kooo za uzao wa Dani zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo koo za uzao wa Dani.
\v 43 Idadi ya koo zote za Washuhamu ilikuwa wanaume 64, 400.
\s5
\v 44 Koo za uzao wa Asheri zilikuwa zifuatazo: Kwa Imna, ukoo wa Waimna, kwa Ishvi, ukoo wa Waishivi, kwa Beria, ukoo wa Waberia.
\v 45 Uzao wa Beria walikuwa hawa: Kwa Heberi, ukoo wa Waheberi, kwa Malikieli, ukoo wa Wamalikieli.
\v 46 Jina la binti wa Asheri lilikuwa Sera.
\v 47 Hizi ndizo koo za uzao wa Asheri, idadi yao ilikuwa wanaume 53, 400.
\s5
\v 48 Koo za uzao wa Naftali zilikuwa zifuatazo: Kwa Jahazeeli, ukoo wa Wajahazeel, kwa Guni, ukoo wa Waguni,
\v 49 kwa Jezeri, ukoo wa Wajezeri, kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.
\v 50 Hizi ndizo zilizokuwa koo za uzao wa Naftali, idadi yao walikuwa wanaume 45, 000.
\s5
\v 51 Hii ndiyo iliyokuwa jumla kuu ya wanaume wa Israeli: 601, 730.
\s5
\v 52 BWANA akanena na Musa akamwambia,
\v 53 Ile ardhi itagawanywa kati ya wanaume hawa kama urithi wao kwa kufuata idadi ya majina yao.
\s5
\v 54 Kwa zile koo kubwa utawagawia urithi mkubwa, na kwa koo ndogo ndogo utawagawia urithi kidogo. Kwa kila familia utawapa urithi kufuata idadi ya wanaume waliohesabiwa.
\v 55 Lakini ardhi itagawiwa kwa kupigiwa kura. Watairithi nchi kama itakavyogawiwa kwa kufuata koo za mababu.
\v 56 Urithi huu utagiwiwa kufuata koo kubwa na ndogo, watagawiwa kwa kufuata kura zitakavyokuwa.
\s5
\v 57 Koo za Walawi, zilizohesabiwa kwa kufuata ukoo kwa ukoo, walikuwa hivi: Kwa Gerishoni, ukoo wa Wagerishoni, kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi, kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
\v 58 Koo za walawi zilikuwa hzi: ukoo wa Walibni, Ukoo wa Wahebroni, ukoo wa Wamahali, ukoo wa Wamushi, na ukoo wa Wakora. Kohathi alikuwa wa uzao wa Amramu.
\v 59 Jina la mke wa Amramu lilikuwa Jokibed, wa ukoo wa Lawi, aliyekuwa amezaliwa kwa Walawi kule Misri. Alimzalia Amramu watoto wao, ambao walikuwa ni Haruni, Musa, na Miriamu dada yao.
\s5
\v 60 Kwa Haruni alizaliwa Nadabu na Abihu, Eliazari na Ithamari.
\v 61 Nadabu na Abihu walikufa walipotoa sadaka kwa BWANA sadaka ya moto isiyokubalika.
\v 62 Waume walioheabaiwa miionigoni mwao walikuwa elfu ishirini na tatu, hawa nia wale wa umri wa mwezi mmoja na zaidi. Lakini hawakuhesabiwa kati ya wazawa wa Israeli kwa sababu hawakupewa urithi miongoni mwa wana wa Israeli.
\s5
\v 63 Hawa nadio wale walihesabiwa na Musa na Eliazari kuhani. Waliwahesabu watu wa Israeli katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko.
\v 64 Lakini miongoni mwa hawa hapakuwa na mwanamume aliyehasabiwa na Musa na Haruni kuhani wakati wana wa uzao wa Israeli walipohesabiwa katika jangwa la Sinai.
\s5
\v 65 Kwa BWANA alikuwa amesema kuwa kwa hakika watu hao wote wangefia jangwani. Hapakuwa na mtu aliyebaki miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Kisah wakaja kwa Musa binti wa Zelofehadi mwana wa Hefa mwana wa Gilied mwana wa Machiri mwana wa Manase, wa ukoo wa Manase mwana wa Yusufu. Hawa ndio waliokuwa binti zake: Mahala, Noha, Hogla, Milika, na Tiriza.
\s5
\v 2 Walisimama mbele ya Musa, Eliazari kuhani, kwa. viongozi, na mbele ya watu wote langoni mwa hema ya kukutania. Walisema,
\v 3 "Baba yetu alifia jangwani. Hakuwa mmoja wa wale waliompinga BWANA katika lile kundi la Kora. Alikufa kwa dhambi zake, na hakuwa na watoto wa kiume.
\s5
\v 4 Kwa nini jina la baba yetu liondolewe mioingoni mwa ukoo wa jamaa zake kwa sababu ya kukosa wana? Tupeni ardhi miongoni mwa ndugu wa baba zetu."
\v 5 Kwa hiyo Musa alileta shauri hilo mbele za BWANA.
\s5
\v 6 BWANA akanena na Musa akamwambia, " Binti wa
\v 7 Zelofehadi wanasema kitu sahihi. Lazima uwaptie ardhi kama urithi miongoni mwa ndugu wa baba zao, na uhakikishe kuwa urithi wa baba zao wanapata.
\v 8 Utawaambia wana wa Israeli na kusema, 'Kama mtu anakufa na hana mtoto wa kiume, basi utaufanya urithi wake wapewe binti zake.
\s5
\v 9 Kama hana binti, basi urithi wake atapewa kaka zake.
\v 10 Kama hana kaka zake basi huo urithi watapewa ndugu wa baba yake.
\v 11 Kama baba yake hana ndugu, basi huo urithi atapewa ndugu yake wa karibu katika ukoo, na utauchukua kuwa wake. Hii itakuwa sheria iliyoanzishwa kwa amri kwa ajili ya watu wa Israeli kama BWANA akivyoniamuru."
\s5
\v 12 BWANA alimwamia Musa, "Nenda juu ya mlima Abaraimu na uitazama nchi ambyo nimewapa wana wa Israeli.
\v 13 Baada ya kuwa umeiona, pia lazima ufe, kama Haruni kaka yako.
\v 14 Hii itatokea kwa sababu ulipinga amri yangu katika jangwa la Sini. Pale ambapo maji yalitoka kwenye mwamba, katika hasira yako ulishindwa kuniheshimu mimi kama mtakatifu mbele ya macho ya watu wote." Haya ni yale maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.
\s5
\v 15 Ndipo Musa akamwambia BWANA akisema,
\v 16 "Wewe, BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, uchague mtu awe juu ya watu,
\v 17 mtu ambaye atatoka na kuingia kuja kwao na kuwatoa kisha kuwarudisha, ili kwamba watu wako wasije kuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji."
\s5
\v 18 BWANA akanena na Musa, "Mchukue Joshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yangu hukaa, na umwekee mikono yako juu yake.
\v 19 Umweke mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya watu wote, na umwamuru kuwaongoza mbele ya macho yao.
\s5
\v 20 Utaweka baadhi ya mamlaka yako kwake, ili kwamba watu wote wa Isareli wamtii.
\v 21 Ataenda mbele ya Eliazari kuhani ili kutafuta mapenzi yangu kwake kwa ajili ya maamuzi ya kura. Yeye ndiyo atakayetoa amri ili watu kutoka na kuingia, yeye pamoja na watu wa Israeli, ambao ni watu wote."
\s5
\v 22 Kwa hiyo Musa akafanya kama alivyoagizwa na BWANA. Alimchukua Joshua na kumweka mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya jamii yote.
\v 23 Akaweka mikono yake juuy ake na kumwamuru aongoze, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
\s5
\c 28
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa akamwambia,
\v 2 "Waamuru wana wa Isrseli uwaambie, 'Mtanitolea sadaka kwa wakati uliopangwa, chakula cha sadaka yangu kilichotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa ajili yangu.
\s5
\v 3 Pia uwaambie, 'Hii ni sadaka iliyotengenezwa kwa moto ambayo mtaitoa kwa BWANA- mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiyekuwa na waa, wawili kila siku kuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.
\v 4 Mwanakodoo mmoja atatolewa sadaka asubuhi, na mwingine atatolewa sadaka jioni.
\v 5 Mtatoa sadaka ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta yaliyokamuliwa.
\s5
\v 6 Hii ni sadaka ya ya kuteketezwa ya kila siku iliyoamriwa mlima Sinai ili kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili ya BWANA.
\v 7 Pamoja na robo ya hini ya sadaka ya kinywaji kwa mmoja wa hao wanakondoo. Utaimimina mahali patakatifu hiyo sadaka ya kinywaji kwa BWANA.
\v 8 Yule mwanakondoo mwingine utamtoa sadaka jioni pamoja na sadaka ya unga kama kama yule wa asubuhi alivyotolewa. Pia utatoa tena sadaka ya kinywaji pamoja naye, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA.
\s5
\v 9 Katika siku ya Sabato utatoa wanakondoo dume wawili, wa umri wa mwaka mmoja kila mmoja wasiokuwa na dosari, na sehemu ya kumi mbili ya efa ya unga mwembamba kwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka ya kinywaji.
\v 10 Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa kila siku ya Sabato, kama nyongeza ya ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya kinywaji.
\s5
\v 11 Kila mwanzo wa mwezi, mtatoa sadaka za kuteketezwa kwa BWANA. Utatoa sadaka ya fahari wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na wanakondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari.
\v 12 Pia mtatoa sehemu ya kumi tatu ya efa unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari, na sehemu za kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa yule kondoo mume mmoja.
\v 13 Pia mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwanakondoo. Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa, ya kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajilI ya BWANA.
\s5
\v 14 Sadaka ya kinywaji ya watu itakuwa nusu ya hini ya divai ya yule fahari, sehemu ya tatu ya hini ya kondoo dume, na robo ya hini ya mwanakondoo. Hii ndiyo itakuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi kwa miezi yote ya mwaka.
\v 15 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA. Hii itakuwa nyongeza kwa ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya viinywaji.
\s5
\v 16 Katika siku kumi na nne, ya mwezi wa kwanza itakuwa Pasaka ya BWANA.
\v 17 Katika sku ya kumi na tano ya mwezi huu kutakuwa na sikukuu. Mtakuka mikate isiyo na chachu kwa siku saba.
\v 18 Katika siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA. Katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku
\s5
\v 19 Hata hivyo, mtatoa sadaka iliyotengenezwa kwa moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari wawili, kondoo dume mmoja, na kondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wakamilifu.
\v 20 Pamoja na yule fahari, mtatoa sadaka sehemu za tatu efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, pamoja na yule kondoo mume sehemu za pili za kumi.
\v 21 Kwa kila wale wanakondoo saba, mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta,
\v 22 na beberu mmoja kuwa sdaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
\s5
\v 23 Mtotoa hivi vitu kama sadaka ya nyongeza katika ile sadaka ya kila siku inayotakiwa kila asubuhi.
\v 24 Kama ilivyofafanuliwa hapa, mtatoa sadaka hizi kila siku, kwa zile siku saba za Pasaka, kile chakula cha sadaka kilichotengenezwa kwa moto kuwa harufu nzuri kwa BWANA. Hiki kitatolewa kuwa sadaka ya nyongeza ya ile sadaka ya kuteketezwa na pamoja na ile sadaka ya vinywaji.
\v 25 Siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu ili kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye zile kazi zenu zakila siku.
\s5
\v 26 Pia katika siku ya malimbuko, mtakapokuwa mnatoa sadaka ya unga mpya katika sikukuu zenu za Majuma, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku.
\v 27 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari wawili wachanga, kondoo mume mmoja, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja.
\v 28 Pamoja na hiyo mtatoa sadaka ya unga: unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari na sehemu kumi mbili za yule kondoo mume.
\s5
\v 29 Toeni sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila wale wanakondoo saba,
\v 30 na beberu mmoja ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
\v 31 Mtakapotoa hao wanyama wasio na dosari, pamoja na sadaka zake za vinywaji, hii itakuwa sadaka ya nyongeza katika zile sadaka za kila siku na pamoja na zile sadaka za unga.'"
\s5
\c 29
\p
\v 1 Katika siku ya kwanza, ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Katika siku hiyo hamtafanya kazi zenu za kila siku. Itakuwa siku ya kupiga matarumbeta.
\s5
\v 2 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ya kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja na wanakondoo dume saba wa mwaka mmoja, kila mmoja mkamilifu.
\s5
\v 3 Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya huyo fahari, sehemu mbili za kumi kwa ajili ya huyo kondoo mume,
\v 4 na sehemu ya kumi ya kila hao wanakondoo waume saba.
\v 5 Na mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
\s5
\v 6 Toeni hizo sadaka katika mwezi wa saba kama nyongeza ya sadaka mtakazotoa kila mwanzo wa kila mwezi: pamoja na sadaka maalumu za kuteketezwa na sadaka za unga. Hizi zitakuwa nyongeza za sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji. Utakapokuwa ukiendelea na sadaka hizi, utakuwa ukitii kile kilichoamriwa kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa BWANA.
\s5
\v 7 Siku ya kumi ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Mtajinyeneyekeza na hamtafanya kazi.
\v 8 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja mchanga ili kutoa harufu nzuri, kondoo mmoja mume, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.
\s5
\v 9 Pamoja na sadaka hizo utatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya fahari, sehemu mbili za kumi za kondoo dume mmoja,
\v 10 na sehemu ya kumi ya efa moja kwa kila mwanakondoo wale saba.
\v 11 Mtatatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya upatanisho. Hii itakuwa sadaka ya nyongeza ya upatanisho, ya sadaka ya kila siku ya kuteketezwa, pamoja na sadaka za unga, na sadaka zake za vinywaji.
\s5
\v 12 Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu lakumwabudu BWANA. Siku hiyo hamtafanya kazi za kila siku, na mtazitunza hizo sikukuu kwa muda wa siku saba kwa ajili ya BWANA.
\v 13 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ilikutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa mafahari wachanga kumi na tatu, kondoo waume wawili, na wanakondoo waume kumi na nne wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.
\s5
\v 14 Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembaba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa kila fahari katika hao kumi na tatu, sehemu mbili za kumi kwa kila hao kondoo dume wawili,
\v 15 na sehemu ya kumi ya efa ya hao wanakondoo kumi na nne.
\v 16 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa, sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka za vinywaji.
\s5
\v 17 Siku ya pili ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi na mbili, kondoo dume wawili na wanakondoo dume kumi na mbili wa umri wa mwaka mmoja, wote wakamilifu.
\v 18 Pamoja nao mtatoa sadaka ya unga, na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na kwa ajili ya wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilvyoamriwa.
\v 19 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kila siku, sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
\s5
\v 20 Siku ya tatu ya kusanyiko, mtatoa sadaka mafahari kumi na moja, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.
\v 21 Pamoja na hizo sadaka mtatoa sadaka ya unga na sdaka ya vinywaji kwa wale mafahari, kwa wale kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, utoe sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
\v 22 Mtatoa sadaka beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya zile sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
\s5
\v 23 Siku ya nne ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
\v 24 Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sdaka za vinywaji kwa wale mafahari, na kwa wale kondoo dume na kwa wale wanakodoo, mtatoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
\v 25 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji
\s5
\v 26 Siku ya tano ya kusanyiko, mtatoa mafahari tisa, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
\v 27 Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na wale wanakondoo, mkitoa sdaka nyingi kama ilivyoamriwa.
\v 28 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka za vinywaji.
\s5
\v 29 Siku ya sita ya kusanyiko, mtatoa mafahari wanane, kondoo dume wawili, na wanakondoo kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
\v 30 Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga nasadaka za vinywaji kwa wale mafahari, kondoo wa dume na wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
\v 31 Mtatoa beberu kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku za kuteketezwa, sadaka zadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
\s5
\v 32 Siku ya saba ya kusanyiko, mtatoa mafahari saba, kondoo dume saba, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
\v 33 Pamoja nao mtataengeneza sadaka ya unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, na kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
\v 34 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya vinywaji.
\s5
\v 35 Siku ya nane mtakuwa na kusanyiko lingine makini. Hamtafanya kazi zenu za kila siku.
\v 36 Mtafanya sadaka za kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja, kondoo mmoja dume, na wanakondoo saba dume wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.
\s5
\v 37 Mtatoa sadaka zake za unga na sadaka zake za vinywaji kwa ajili ya yule fahari, kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkifanya sadaka nyingi kadri ilivyoamriwa.
\v 38 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
\s5
\v 39 Hivi ndivyo utakavyotoa sadaka kwa BWANA katika sikukuu zenu za kila mwaka. Hivi vitakuwa nyongeza ya viapo vyenu na sadaka zenu za hiari. Mtavitoa hivi kama sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za unga, sadaka za vinywaji, na sadaka za amani."
\v 40 Musa aliwaambia wana wa Israeli kila kitu ambacho BWANA alikuwa amemwamuru kusema.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Musa aliwambia viongizi wote wa makabila ya watu wa Israeli. "Hiki ndicho ambacho BWANA ameamuru.
\v 2 Mtu yeyote atakayefanya nadhiri kwa BWANA, au kuapa kwa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asivunje neno lake. Atafanya sawa na ahadi yake imtokayo kinywani mwake.
\s5
\v 3 Na kama binti anaishi katika nyumba ya baba yake kwa atafanya nadhiri kwa BWANA na kuifunga nafsi yake kwa kiapo,
\v 4 na kama baba yake atasikia hiyo nadhirina ahadi ambayo ametumia kuifunga nafsi yake, naye asiseme kitu kumzuia, ndipo nadhiri zake zitakuwa na nguvu. Kila ahadi ambayo ameitumia kuifunga nafsi yake itabaki kuwa na nguvu.
\s5
\v 5 Lakini kama baba yake atasikia nadhairi yake na ahadi zake, na kama hatasema chochote kwake, ndipo nadhiri zake zote na ahadi alizofanya zitakapokuwa na nguvu.
\s5
\v 6 Hata hivyo, kama baba yake atasikia nadhri zake zote alizofanya na ahadi zake makini ambazo ametumia kufunga nafsi yake, na kama atazitengua ndani ya siku hiyo, ndipo hizo nadhiri hazitakuwa na nguvu. BWANA atamsamehe kwa kuwa baba yake amemzuia.
\v 7 Kama ataolewa angali katika hivyo viapo, au kama atafanya ahadi za bila kufikiri ambazo atajifunga nazo, hivyo vifungo vitakuwa na nguvu.
\s5
\v 8 Lakini kama mume wake atamzuia siku hiyo hiyo ambayo atamskia akiapa, basi atabatailisha hicho kiapo alichokifanya, maneno yake ya midomo yaka ya bila kufikiri ambayo kwayo amefunga nafsi yake. BWANA atamfungua.
\s5
\v 9 Lakini kwa mjane au kwa mwanamke aliyetalikiwa, kila kitu amabacho atakisema kufunga nafsi yake lazima kitabaki na nguvu kinyume na yeye.
\v 10 Na kama mwanamke atafanya kiapo katika nyumba ya mume wake au akijifunga mwenyewe kwa kufanaya kiapo,
\v 11 na mume wake akakisikia hicho kiapo na hakusema chochote kwake na hakumpinga, basi viapo vyake vitasimama na vifungo alivyovifanaya vitabaki na nguvu.
\s5
\v 12 Lakini kama mume wake atamzuilia katika siku hiyo ambayo atavisikia, basi chochote ambacho kitatoka katika kinywa chake kuhusu viapo vyake au ahadi zake havitabaki kuwa na nguvu. Mume wake atkuwa amevibatilisha. BWANA atamfungua.
\s5
\v 13 Kila kiapo ambacho mwanamke anakifanya ambacho kinamfunga ili kujikana kianaweza kuthibitika au kubatilishwa na mume wake.
\v 14 Lakini kama hatasema chochote kwake siku baada ya siku, basi atathibitisha nadhiri zake na ahadi zake zinazomfunga ambazo amefanya. Atakuwa amezithibitisha kwa sababu hakusema chochote wakati alipozisikia.
\s5
\v 15 Na kama mume wake atajariibu kubatilisha kiapo cha mke wake baada ya kuzisikia kwa muda mrefu, basi ataajibika kwa dhambi zake."
\v 16 Hizi ndizo amri ambazo Mungu alimwamuru Musa kuzitangaza - amri ambazo ziko kati ya mume na mke wake na kati ya baba na binti yake wakati akiwa katika ujana wake katika familia ya baba yake.
\s5
\c 31
\p
\v 1 BWANA alinena na Musa na kumwambia,
\v 2 "Uwalipizie kisasi Wamidiani kwa kile walichowafanya Waisraeli. Baada ya kufanya hivyo utakufa na kukusanyika na watu wako."
\s5
\v 3 Kwa hiyo Musa akawaambia watu. Akasema, "andaeni baadhi ya majeshi yenu kwa ajili ya vita ili kwamba wakawapige Wamidiani na kubeba kiapo cha BWANA.
\v 4 Kwa kila kabila la Israeli watatuma askari elfu moja kwa ajili ya vita."
\v 5 Kwa hiyo kati ya wanaume maelfu elfu wa Israeli, wanaume elfu moja walitolewa kwa ajili ya vita, jumla ya wanaume elfu kumi na mbili.
\s5
\v 6 Kisha Musa akawatuma kwenda vitani, elfu moja toka kila kabila pamoja na Finehasi mwana wa Eliazari kuhanai, wakiwa na vitu kutoka mahali patakatifu wakiwa na matarumbeta kwa ajili ya ishara za sauti.
\v 7 Wakapigana na Midiani, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Wakamwua kila mwanaume.
\v 8 Wakawaua wafalme wa Midiani pamoja na wengine waliowaua ni: Evi, Rekimu, Zuri, Huri, na Reba, hawa walaikuwa ndio waflme watano wa Midiani. pia walimwua Balaamu mwana wa Beori, kwa upanga.
\s5
\v 9 Jeshi la Israeli likawachukua mateka wanawake wa Midiani, watoto wao, mifugo yao yote, kondoo wao na bidhaa zao zote. walivichukua hivi kama mateka.
\v 10 Waliichoma moto miji yao yote walimoishi na kambi zao zote.
\s5
\v 11 Walichukua vitu vyote na wafungwa, watu na wanyama.
\v 12 Wakawaleta mateka, nyara, na wakakamata vitu wakavileta kwa Musa, na Eliazari kuhani, na kwa jamii ya watu wa Israeli. Wakavileta hivi vitu kambini katika uwanda wa Moabu, kule Yorodani karibu na Yeriko.
\s5
\v 13 Musa, Eliazari kuhani, pamoja na viongozi wa watu wakaenda kukutana nao nje ya kambi.
\v 14 Lakini Musa alikuwa na hasira dhidi ya viongozi wa jeshi, Wale majemedari wa maelfu na maakida wa mamia, waliotoka kupigana.
\v 15 Musa akawaambia, "Je, mmeawaacha wanawake wote kuishi?
\s5
\v 16 Tazama, wanawake hawa ndio waliosababisha watu wa Israeli, kwa kupitia ushauri wa Balaamu, kufanya dhambi dhidi ya BWANA huko Peori, wakati ile tauni iliposambaa kwa watu wa Mungu.
\v 17 Sasa basi, ueni kila mwanaume kuanzia wadogo, na ueni kila mwanamke aliyelala na mwanamume.
\s5
\v 18 Lakini chukueni wale mabinti wadogo ambao hawajalala na mwanamume.
\v 19 Mtaweka kambi nje na kambi za Israeli kwa muda wa siku saba. Ninyi wote ambao mmeua watu au ambao mmegusa maiti yeyote mtajitakasa wenyewe katika siku ya tatu na katika siku ya saba - ninyi na mateka wenu.
\v 20 Na mtayatakasa mavazi yenu yote, na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi za wanyama, na manyoya ya mbuzi, na kila kitu kilichotengenezwa kwa mbao."
\s5
\v 21 Eliazarai kuahani akawaambia wale wanajeshi waliokuwa wameenda vitani, "Hii ni amri ya sheria ambayo BWANA alimpa Musa:
\v 22 Zile dhahabu, fedha, vyuma, bati, risasi,
\v 23 na kila kitu knaweza kuhhimili moto, mtakiweka katka moto, navyo vitakuwa safi. Nakisha mtavitakasa vitu hivyo na maji ya farakano. Na vitu vyote ambavyo haviwezi kupita katika moto, mtavitakasa kwa maji hayo.
\v 24 Na mtazifua nguao zenu katika siku ya saba, ndipo mtakapokuwa safi. Baada ya hapo mnaweza kurudi kwenye kambi za Israeli."
\s5
\v 25 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
\v 26 "Vihesabu vitu vyote vilivyochukuliwa nyara, wote watu na wanyama. Wewe, Eliazari kuhani, na viongozi wa watu kufuata koo
\v 27 watavigawa hivi vitu katika mkundi mawili. Mvigawe kwa wanajeshi walioenda kupigana na kwa watu wote.
\s5
\v 28 Kisha toza kodi ambayo itatolewa kwangu kutoka kwa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani. Hii kodi itakuwa moja kati ya mia tano, katika watu, ng'ombe, punda, kondoo, au mbuzi.
\v 29 Uichukue hii kodi kutoka katika nusu yao na umpe Eliazari kuhani kwa ajili ya sadaka itakayotolewa kwangu.
\s5
\v 30 Pia kutoka katika nusu ya watu wa Israeli, utachukua moja kati ya hamsini -kutoka vitu, ng'ombe, punda, na mbuzi. Uvitoe hivi kwa Walawi wanaotumika katika masikani yangu."
\v 31 Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.
\s5
\v 32 Sasa zile nyara zilizokuwa zimebaki ambazo wanajeshi walikuwa wameteka zilikuwa kondoo 675, 000,
\v 33 maksai elfu sabini na mbili,
\v 34 punda elfu sitini na moja,
\v 35 na wanawake elfu thelathini na mbili ambao walikuwa hawajalala na mwanamume yeyote.
\s5
\v 36 Ile hesabu ya nusu iliyokuwa imetunzwa kwa ajili ya wanajeshi ilikuwa kondoo 337, 000. Ile sehemu ya
\v 37 BWANA ya kondoo ilikuwa kondoo 675.
\v 38 Maksai walikuwa elfu thelathini na sita ambayo kodi ya BWANA ilikuwa sabini na mbili.
\s5
\v 39 Punda walikuwa 30, 500 ambao sehemu ya BWANA ilikuwa sitini na moja.
\v 40 Watu walikuwa wanawake elfu kumi na sita ambao kodi ya BWANA ilikuwa thelathini na mbili.
\v 41 Musa aliichukua ile kodi ambayo ilitakiwa kuwekwa sadaka kwa BWANA. Akampatia Eliazari kuhani, kama BWANA alivyomwamuru Musa.
\s5
\v 42 Ile nusu ya watu wa Israeli ambayo Musa alikuwa ameichukua toka kwa wanawjeshi waliokuwa wameenda vitani -
\v 43 ile nusu y a watu ilikuwa kondoo 337, 500,
\v 44 maksai elfu thelathini na sita,
\v 45 punda 30, 500,
\v 46 na wanawake elfu kumi na sita.
\s5
\v 47 Kutoka kwenye nusu ya watu wa Israeli, Musa alichukua moja katika hamsini, wote watu na wanyama. Aliwapa Walawi ambao huitumikia masikani ya BWANA, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
\s5
\v 48 Kisha wale maakida wa jeshi, makamanda wa elfu na makapteni wa mamia, wakaja kwa Musa.
\v 49 Wakamwambia, "watumishi wako wamewahesabu wanajeshi ambao wako chini yetu, hakuna hata mmoja wao aliyekosa.
\s5
\v 50 Tumemletea BWANA sadaka, ambayo kila mmoja amepata, vitu vya dhahabu, metali, timbi, pete za mhuri, vipini na vikuku, ili kujifanyia upatanisho kwa BWANA."
\v 51 Musa na Eliazari kuhani akapokea kutoka kwao dhahabu na vitu vyote vilivyotengenezwa kwa ufundi.
\s5
\v 52 Vitu vyote vya sadaka ya dhahabu ambavyo walimpa BWANA- sadaka toka kwa makamanda wa maelfu na kutoka kwa makepteni wa mamia - vilikuwa na uzito wa shekeli 16, 750.
\v 53 Kila mwanajeshi alikuwa ameteka nyara ya kila mtu kwa ajili yake.
\v 54 Musa na Eliazari kuhani wakazichukuazile dhahabu toka kwa makamanda wa maelfu na makepteni wa mamia. Wakavipeleka kwenye hema ya kukutania kama ukumbusho wa watu wa Israeli kwa BWANA.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Sasa wana wa uzao wa Reubeni na wa Gadi walikuwa na idadi kubwa ya wanyama. Waliiona ardhi ya Jazeri na Gileadi, kuwa ni ardhi nzuri kwa mifugo.
\v 2 Kwa hiyo wana wa Gadi na wa Reubeni wakaja kumwambia Musa, na Eliazari kuhani, na viongozi wa watu. Wakasema,
\v 3 "Hii ndiyo orodha ya maeneo ambayo tumeyatembelea: Diboni, Jazeri, Nimraha, Heshibonni, Ellealehi, Sebamu, Nebo, na Beoni.
\s5
\v 4 Haya ni maeneo ambayo BWANA aliyachukua mbele ya watu wa Israeli, na maeneo mazuri kwa ajili ya mifugo. Sisi watumishi wako tuna mifugo mingi sana.
\v 5 Wakasema kuwa, "Kama tutapata kibali mbele ya macho yako, tunaomba ardhi hii tupewe, sisi watumishi wako, kuwa urithi. Usituvushe ng'ambo ya Yorodani."
\s5
\v 6 Musa akawajibu wale wana wa auzao wa Gadi na Reubeni, "Je, mngependa ndugu zenu waende vitani wakati ninyi mkikaa hapa?
\v 7 Kwa nini kuwafish moyo watu wa Israeli wasivuke kwenda kwenye nchi ambayo BWANA amewapa?
\s5
\v 8 Baba zenu walifanya hivyo nilipowatuma kutoka Kadeshi Banea kwenda kuipeleleza ile nchi.
\v 9 Walienda mpaka kwenye bonde la Eskoli. Waliiona ile ardhi kisha wakawafisha moyo watu wa Israeli kwa hiyo wakagoma kuingia kwenye nchi ambayo BWANA alikuwa amewapa.
\s5
\v 10 Siku hiyo hasira ya BWANA iliwaka. Akaapa akisema,
\v 11 'Kwa hakika hakuna mtu aliyetoka Misri, kuanzia wa umri wa miaka ishirini na zaidi ambao wataiona nchi ambao niliwaapia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwa sababu hawakunifuata mimi kwa ukamilifu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni.
\v 12 Ni Kalebu na Joshua tu ndio walionifuata kwa ukamilifu.'
\s5
\v 13 Kwa hiyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israei. Akawafanya wazunguke zunguke jangwani kwa miaka arobaini mpaka kile kizazi kilichofanya maovu mbele za macho yake kilipoteketea.
\v 14 Tazama, mmetokea katika nafasi za baba zenu, kama watu wengine wenye dhambi zaidi, ili kuongeza hasira ya BWANA kwa Israeli.
\v 15 Kama hamtamfuata, ataiacha Israeli jangwani na mtakuwa mmewateketeza watu hawa wote.
\s5
\v 16 Kwa hiyo wakaja karibu na Musa wakamwambia, "Turuhusu tujenga hapa uzio kwa ajili ya ng'ombe zetu na miji hapa kwa ajili ya familia zetu.
\v 17 Hata hivyo, sisi wenyewe tutajipanga kijeshi kwenda na jeshi la Israeli mpaka tumewaongoza kupata maeneo yao. Lakini familia zetu zitakuwa kwenye miji ya maboma kwa ssbabu ya watu wengine ambao bado wanaishi katika nchi hii.
\s5
\v 18 Hatutarudi kwenye familia zetu mpaka kila mmoja watu wa Israeli apate urithi wake.
\v 19 Sisi hatutachukua urithi wa ardhi pamoja nao kule ng'ambo ya Yorodani, kwa sababu urithi wetu uko hapa upande wa mashariki mwa Yorodani."
\s5
\v 20 Kwa hiyo Musa akawajibu, "Kama mtafanya mnachokisema, kama mtajipanga wenyewe mbele za BWANA kwenda vitani,
\v 21 basi kila mmoja wa wanajeshi wenu lazima avuke Yorodani mbele za BWANA, mpaka atakapowafukuza maadui zake kutoka mbele zake
\v 22 na nchi itawaliwe na Israeli mbele zake. Kisha mtaweza kurudi. Hamtakuwa na hatia mbele za BWANA na mbele ya Israeli. Hii nchi itakuwa miliki yenu mbele za BWANA.
\s5
\v 23 Bali kama hamtafnya hivyo, tazama, mtakuwa mmefanya dhambi mbele ya BWANA. Mwe na hakika kuwa dhambi yenu itaonekana
\v 24 wazi. Jengeni miji kwa ajili ya familia zenu na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; kisha fanyeni kile mlichokisema."
\v 25 Wale wana wa Gadi na Reubeni wakamwambia Musa, wakisema, "Watumishi wako wtafanya kama vile wewe, bwana wetu, unavyotuamuru.
\s5
\v 26 Watoto wetu, wake zetu, makundi yetu, na wanyama wetu wote watakaa huko kwenye miji ya Gileadi.
\v 27 Hata hivyo, sisi watumishi wako, tutavuka kwenda ng'ambo mbele za BWANA kupigana, kila mtu ambaye yuko tayari kwa vita, kama vile wewe, bwana wetu, unavyosema."
\s5
\v 28 Kwa hiyo Musa akawapa maelekezo yayowahusu kwa Eliazari kuhani, kwa Joshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa koo kufuata jamaa zao katika makabila ya wana wa Israeli.
\v 29 Musa akawaambia, "Kama uzao wa Reubeni na Gadi watavuka ng'ambo ya Yorodani pamoja nanyi, kila mwanamume anayetakiwa kuwa vitani mbele za BWANA, na kama nchi mtaitawala mbele zenu, ndipo mtakapowapa eneo la Gileadi kuwa miliki yao.
\v 30 Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa na silaha zao, basi mtawapa urithi wao katika nchi ya Kanaani."
\s5
\v 31 Kwas hiyo wana wa uzao wa Gadi na wa Reubeni wakamjibu wakisema, Kama vile BWANA alivyosema nasi, sisi watumwa wako, hiki ndicho tutakachokifanya.
\v 32 Tutavuka tukiwa na silaha zetu mbele za BWANA kuingia katika nchi ya Kanaani, lakini urithi wetu utabaki utabaki upande huu wa Yorodani."
\s5
\v 33 Kwa hiyo uzao wa Gadi na Reubeni, na pia nusu ya kabila la Manase mwana wa Yusufu, Musa akawapa ufalme wa Sihoni, mfalme wa Waamori, na wa Ogi, mafalme wa Bashani, Aliwapa hiyo nchi, na kuwagawia miji yake yote pamoja na mipaka yake, miji yote ya nchi inayowazunguka.
\s5
\v 34 Wale wa uzao wa Gadi wakaijenga Diboni,
\v 35 Atarothi, Aroeri, Atrothi, Jazeri, Jogbehaha, Bethi Nimraha,
\v 36 na Bethi Harani kuwa miji iliyo na maboma na mazizi ya kondoo wao.
\s5
\v 37 Wale wa uzao wa Reubeni wakaijenga Heshiboni. Elealehi, Kiriathaimu,
\v 38 Nebo, Baali Meoni - baadaye waliyabadili majina yao, na Sibimaha.
\v 39 Wale wa uzao wa Machiri mwana wa Manase walienda Gileadi na kuutwaa kutoka kwa Waamori waliokuwa wakiishi humo.
\s5
\v 40 Kisha Musa akaitoa Gileadi kwa Machiri mwana wa Manase, na watu wake wakaishi humo.
\v 41 Jairi mwana wa Manase alienda kuiteka miji yake na kuiita Havothi Jairi.
\v 42 Nobaha alienda kuitieka Kenathi na vijiji vyake, na akauita kwa jina lake Nobaha.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Hizi ndizo safari za wana wa Israeli hapo walipotoka katika nchi ya Misri pamoja na makundi yao ya kijeshi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.
\v 2 Musa aliandika maeneo yote tangu walipoondoka mpaka walipofika, kama alivyoamuriwa na BWANA. Hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa kwa kila walipotoka.
\s5
\v 3 Mwezi wa kwanza walisafiri kutoka Ramesi, waliondoka siku ya kumi na tano. Asubuhi siku iliyofuata baada ya Pasaka, Wana wa Israeli waliondoka wazi wazi, mbele ya machoya Wamisri wote.
\v 4 Hii ilitokea wakati Wamisiri walipokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza, ambao BWANA alikuwa amewaua miongoni mwao, kwa kuwa pia alikuwa ameiadhibu miungu yao.
\s5
\v 5 Wana wa Israeli walisafiri kutoka Ramesi na kuweka kambi
\v 6 Sukothi. Walisafiri toka Sukothi na kuweka kambi Ethamu, mwisho wa nyika.
\v 7 Wakasafiri kutoka Ethamu wakarudi mpaka Pi-Hahirothi, ambayo inaikabili Baali Zephoni, ambapo waliweka kambi kuikabili Migidoli
\s5
\v 8 Kisha wakasafiri toka mkabala wa Pi-Hairothi na kupita katikati ya bahari kuelekea nyikani. Wakasafiri safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu na kuweka kambi Mara.
\v 9 Wakasafiri kutoka Mara kufika Elimu. Pale Elimu kulikuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mitende. hapo ndipo walipoweka kambi.
\v 10 Walisafiri kutoka Elimu na kuweka kambi karibu na Bahari ya Shamu.
\s5
\v 11 Walisafiri kutoka Bahari ya Shamu na kuweka kambi katika nyika ya Sini.
\v 12 Walisafiri kutoka nyika ya Sini na kuweka kambi Dofka.
\v 13 Wakasafiri kutoka Dofka na kuweka kambi Alushi.
\v 14 Wakasafiri kutoka Alushi na kuweka kambi Refidimu, ambapo watu walikosa maji ya kunywa.
\s5
\v 15 Walisafiri kutoka Refidimu na kuweka kambi kwenye nyika ya Sinai.
\v 16 Walisafiri kutoka nyika ya Sinai na kuweka kambi Kibrothi Hataava.
\v 17 Walisafiri kutoka Kibrothi Hataava na kuweka kambi Hazerothi.
\v 18 Walisafiri kutoka Hazerothi na kuweka kambi Rithima.
\s5
\v 19 Walisafiri kutoka Rithima na kuweka kambi Rimoni Perezi.
\v 20 Walisafiri kutoka Rimoni Perezi na kuweka kambi Libna.
\v 21 Walisafiri kutoka Libna na kuweka kambi Risa.
\v 22 Walisafiri kutoka Risa na kuweka kambi Kehelatha.
\s5
\v 23 Walisafiri kutoka Kehelatha na kuweka kambi kwenye Mlima Sheferi.
\v 24 Walisafiri kutoka Mlima Sheferi na kuweka kambi Harada.
\v 25 Walisafiri kutoka Harada na kuweka kambi Makelothi.
\v 26 Walisafiri kutoka Makelothi na kuweka kambi Tahathi.
\s5
\v 27 Walisafiri kutoka Ttahalathi na kuweka kambi Tera.
\v 28 Walisafiri kutokaTera na kuweka kambi Mithika.
\v 29 Walisafiri kutoka Mithika na kuweka kambi Hashimona.
\v 30 Walisafiri kutoka Hashimona na kuweka kambi Moserothi.
\s5
\v 31 Walisafiri kutoka Moserothi na kuweka kambi Bene Jaakani.
\v 32 Walisafiri kutoka Bene Jaakani na kuweka kambi Hori Hagidigadi.
\v 33 Walisafiri kutoka Hori Hagidigadi na kuweka kambi Jotibatha.
\v 34 Walisafiri kutoka Jotibatha na kuweka kambi Abrona.
\s5
\v 35 Walisafiri kutoka Abrona na kuweka kambi Ezioni Geberi.
\v 36 Walisafiri toka Ezioini Geberi na kuweka kambi katika nyika ya Sini kule Kadeshi.
\v 37 Walisafiri kutoka Kadeshi na kuweka kambi Mlima Hori, Pembezoni mwa nchi ya Edomu.
\s5
\v 38 Hapo ndipo Haruni kuhani alipoenda kwenye Mlima Hori kwa amri ya BWANA na kufa kule mwaka wa arobaini bada ya Wisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano.
\v 39 Haruni alikuwa na umri wa mika 123 alipokufa pale juu ya Mlima Hori.
\s5
\v 40 Wakanaani, mfalme wa Aradi, ambao waliishi kusini mwa nyika katika nchi ya Kanaani, walisikia juu ya ujio wa wana wa Israeli.
\s5
\v 41 Walisafiri kutika Mlima Hori n a kuweka kambi Zalimona.
\v 42 Walisafiri kutoka Zalimona na kuweka kambi Punoni.
\v 43 Walisafiri kutoka Punoni na kuweka kambi Obothi.
\s5
\v 44 Walisafiri kutoka Obothi na kuweka kambi Abarimu, katika mpaka wa Moabu.
\v 45 Walisafiri kutoka Abarimu na kuweka kambi Diboni Gadi.
\v 46 Walisafiri kutoka Diboni Gadi na kuweka kambi Alimoni Diblathaimu.
\s5
\v 47 Walisafiri kutoka Alimoni Diblathaimu na kuweka kambi kwenye milima ya Abarimu mkabala na Nebo.
\v 48 Walisafiri kutoka mlima wa Abarimuna kuweka kambi kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.
\v 49 Waliweka kambi karibu na Yorodani, kutoka Bethi Jeshimothi mpaka Abeli Shitimu katika nyanda za Moabu.
\s5
\v 50 Hapo BWANA alinenana Musa katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,
\v 51 "Nena na wana wa Israeli uwaambie. 'Mtakapovuka mto Yorodani kuingia Kanaani,
\v 52 ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zote za kuchongwa. Mtaziharibu sanamu zao za kusubu na kuharibu mahali pao pote palipoinuka.
\s5
\v 53 Mtachukua hiyo ardhi iwe mali yenu na muishi ndani yake, kwa sababu nimewapeni hiyo nchi iwe mali yenu.
\v 54 Mtairithi hiyo nchi kwa kupiga kura, kwa kufuata kila ukoo. Kwa zile koo kubwa kubwa mtawapa sehemu kubwa ya ardhi, na kwa zile koo ndogo ndogo mtawapa sehemu ndogo ya ardhi. Kura itakapoanguka kwenye kila ukoo, hiyo ardhi itakuwa mali yake. Mtairithi ardhi kufuata ukoo wa kabilla la jamaa zenu.
\s5
\v 55 Lakini kama hamtawafukuza wenyeji wa nchi hiyo watoke mbele yenu, ndipo wale watu mtakaowaruhusu wakae nanyi watakapokuwa kama sindano machoni mwenu na miiba katika mbavu zenu. Watayafanya maisha yenu yawe magumu katika nchi mnayoishi.
\v 56 Ndipo itakapotokea kuwa kile ambacho Mimi ninakusudia kufanya kwa wale watu, Nitawafanyia pia ninyi'"
\s5
\c 34
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa akasema,
\v 2 "Waamuru watu wa Israeli na uwaambie, 'Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, nchi ambayo itakuwa mali yenu, nchi ya Kanaani na mipaka yake, mpaka wenu wa kusini utaendelea kutoka nyika ya Sini hadi mpaka wa Edomu.
\v 3 Mwisho wa mpaka wa kusini utakuwa mwisho wa bahari ya chumvi kuelekea mashariki.
\s5
\v 4 Mpaka wenu utageukia kusini kutoka mlima kuelekea Akrabimu na kupitia nyika ya Sini. na kutokea huko utaelelkea kusini mwa Kadeshi Barinea na kuelekea Hazari Adari mpaka Azimoni.
\v 5 Kutoka huko, mpaka utageuka kutoka Azimoni kuelekea kijito cha Misri na kukifuata mpaka baharini.
\s5
\v 6 Mpaka wa Magharibi utakuwa pwani ya bahari kuu. Huu ndio utakuwa mpaka wenuwa Magharibi.
\s5
\v 7 Mpaka wenu wa kaskazini utaanzia kwenye bahari kuu hadi Mlima Hori,
\v 8 kisha kutoka Mlima Hori hadi Lebo Hamathi, kisha Zedadi.
\v 9 Mpaka utaendelea hadi Zifroni na kuishia Hazari Enani. Huu ndio utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
\s5
\v 10 Kisha mtaweka alama za mpaka wenu wa mashariki ambao utaanzia Hazari Enani kuelekea kusini Shefamu.
\v 11 Kisha mpaka wa kusini utaendelea kutoka Shefamu hadi Ribla, upande wa masharikia mwa Aini. Mpaka utaedelea upande huo wa mashariki hadi upande wa mashariki wa bahari ya Kinerethi.
\v 12 Kisha mpaka utaendelea kuelekea kusini hadi mto Yorodani na hadi bahari ya chumvi. Hii ndiyo itakuwa nchi yenu, kwa kuifuata mipaka yake yote inayozunguka.'"
\s5
\v 13 Kisha Musa akawaamuru watu wa Israeli akasema, "Hii ndiyo nchi ambayo mtaipokes kwa kura, ambayo BWANA ameamuru kuwapa wale makabila tisa na nusu.
\v 14 Kabila ya uzao wa Reubeni, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na uzao wa kabila la Gadi, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na nusu ya Manase wamepata ardhi yao.
\v 15 Wale makabila mawili na nusu wameshapata mgawo wao ng'ambo ya mto Yorodani upande wa mashariki, kuelekea kule linakotokea jua."
\s5
\v 16 BWANA akanena na Musa akasema,
\v 17 "Haya ndiyo majinaya watu watakaoigawa ardhi kwa ajili ya urithi wao: Eliazari kuhani na Joshua mwana wa Nuni.
\v 18 Mtachagua kiongozi mmoja toka kila kabila ili kuigawa ardhi kwa koo zao.
\s5
\v 19 Haya ndiyo majina ya wanaume: Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
\v 20 Kutoka kwenye kabila la uzao wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
\s5
\v 21 Kutoka kabila la Benjamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
\v 22 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Dani, Buki mwana wa Jogili.
\v 23 Kiongozi kutoka uzao wa Yusufu, kwenye kabila la Manase, Hannieli mwana wa Efodi.
\s5
\v 24 Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Efraimu, Kemueli mwana wa Shiftani.
\v 25 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Zabuloni, Elizafani mwana wa Parinaki.
\v 26 Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Isakari, Palitieli mwana wa Azzani.
\s5
\v 27 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi.
\v 28 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi."
\v 29 BWANA aliwaamuru wanaume hawa kuigawa nchi ya Kanaani na kuwapa kila kabla sehemu yao.
\s5
\c 35
\p
\v 1 BWANA akanena na Musa kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,
\v 2 "Waamuru watu wa Israeli kutoa sehemu ya urithi wa ardhi yao kwa Walawi. Watawapa miji ya kuishi ndani yake na eneo la malisho kuzunguka miji hiyo.
\s5
\v 3 Walawi watakuwa na miji hiyo ya kuishi. Eneo la malisho litakuwa kwa ajili ya ng'ombe zao, kondoo zao, na wanyama wao wote.
\v 4 Hayo malisho yatakayozunguka miji hiyo ambayo mtawapa Walawi yataanzia kwenye maboma kwa ukubwa wa "mita 457" kila upande.
\s5
\v 5 Utapima dhiraa elfu mbili kutoka nje ya mji kuelekea mashariki, na dhiraa elfu mbili kuelekea kusini, na dhiraa elfu mbili kuelekea upande wa magharibi, na dhiraa elfu mbilii kuelekea upandewa kaskazini. Haya yatakuwa maeneo ya malisho yao. Miji itakuwa katikati.
\s5
\v 6 Katika hiyo miji sita mtakayowapatia Walawi itatumika kama miji ya ukimbizi. Mtatoa maeneo haya ili kama mtu ameua mtu apate mahali pa kukimbilia. Pia mtatoa miji mingine arobaini na mbli.
\v 7 Jumla ya miji ambyo mtawapa Walawi itakuwa arobaini na nane. Mtawapa hiyo miji pamoja na maeneo yao ya malisho.
\s5
\v 8 Zile kabila kubwa za watu wa Israeli, kabila ambalo lina ardhi zaidi, watatoa ardhi zaidi. Makabila madogo madogo watatoa miji michache. Kila kabila lazima watoe kwa ajili ya Walawi kwa kufuata mgawo waliopata."
\s5
\v 9 Kisha BWANA akanena na Musa akamwambia,
\v 10 "Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mtakapovuka Yorodani kuingia Kanaani,
\v 11 Kisha mchague miji itakayotumika kama miji ya ukimbizi kwa, ajili yenu, mahali ambapo mtu aliyeua mtu pasipo kukusudia anaweza kukimbilia.
\s5
\v 12 Hii miji itakuwa kwenu miji ya ukimbizi kwa mtu anayetaka kulipa kisasi. ili kwamba mtuhumiwa asije akauawa bila kwanza kusikilizwa na jamii.
\v 13 Mtachagua miji sita kuwa miji ya ukimbizi.
\s5
\v 14 Mtatoa miji mitatu kule ng'ambo ya Yorodani na miji mitatu huko Kanaani. Itakuwa miji ya ukimbizi.
\v 15 Kwa ajili ya watu wa Israeli, wageni, kwa, yeyote anayeishi kati yenu, hii miji sita itatumika kama miji ya ukimbizi kwa mtu yeyote atakayeua mtu bila kukusudia anaweza kukimbila.
\s5
\v 16 Lakini kama mtuhumiwa amempiga mtu na chombo cha chuma, na huyo mtu akafa, basi kwa hakika yule mtuhumiwa ni muuaji. Kwa hiyo anatakiwa kuuawa.
\v 17 Kama yule mtuhumiwa amempiga mtu kwa jiwe mkonono mwake ambalo linaweza kumwua mtu, na kama yule mtu atakufa, basi hakika huyo mtuhumiwa ni mwuaji. Kwa hakika anatakiwa kuuawa.
\v 18 Kama mtuhumiwa amempiga mtu kwa silaha ya mti ambayo inaweza kuua mtu na kama huyo mtu atakufa, basi kwa hakika huyo mtuhumiwa ni mwuaji. kwa hakika huyo anataikwa kuuawa.
\s5
\v 19 Mwenye kulipa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji. atkapokutana naye, anaweza kumwua.
\v 20 Lakini kama yule mtuhumiwa atamshinda mtu yeyote yule anayemchukia au kama atamtupia kitu, wakati akimvizia, kiasi kwamba huyo mtu akafa,
\v 21 au kama atampiga ngumi kwa chuki na mtu huyo akafa, ndipo yule mtuhumiwa aliyempiga hakika atauawa. Yeye ni mwuaji. Yule mlipa kisasi cha damu anaweza kumwua muuaji pale atakapokutana naye.
\s5
\v 22 Lakini kama mtuhumiwa atampiga mtu ghafla bila kuwa na chuki hapo awali, au kama atamtupia kitu ambacho kitampiga mtu bila kumvizia
\v 23 au kama atatupa jiwe amabalo linaweza kumwua mtu bila kumwona, basi huyo mtu hakua adui yake, hakukusudia kumwumiza huyo mtu. Basi hiki ndicho kitachofanywa kama mtu huyo atakufa.
\s5
\v 24 Kwa tatizo la jinsi hiyo, Watu wataamua kati ya mlipa kisasi na mtuhumiwa kwa kufuata taratibu zifuatazo.
\v 25 Watu watamwokoa mtuhumiwa kutoka kwenye nguvu za mlipa kisasi cha damu. Watu watamrudisha mtuhumiwa katika mji wa ukimbizi ambao hapo awali alikimbilia. Ataishi pale mpaka yule kuhani anayetumikia atakapokufa, ambaye alipakwa mafuta matakatifu.
\s5
\v 26 Lakini kama yule mtuhumiwa muda fulani ataenda nje ya mipaka ya mji a ukimbizi ambao alikimbilia,
\v 27 na kama yule mlipa kisasi cha damu atamwona nje ya mipaka ya mji wake wa ukimbizi, kama atamwua huyo mtuhumiwa, mlipa kisasi cha damu hatakuwa na hatia ya mauaji hayo.
\v 28 Hii ni kwa sababu yule mtuhumiwa alitakiwa kubaki katika mji wake wa ukimbizi mpaka kuhani mkuu atakapokufa. Baada ya kifo cha kuhani mkuu, yule mtuhumiwa atarejea kwenye nchi yake ambako kuna mali yake.
\s5
\v 29 Hizi amri zitakuwa maagizo kwenu kwa kizazi chote mahali kote mnakoishi.
\v 30 Yeyote amwuaye mtu, mwuaji atauawa, kama neno la ushahidi litakavyotolewa. Lakini ushahidi wa mtu mmoja unaweza usitoshe kusababisha mtu kuuawa.
\s5
\v 31 Pia, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji ambaye ana hatia ya mauti. Kwa hakika lazima auawe.
\v 32 Na msipokee fidia ya mtu aliyekimbilia kwenye miji ya ukimbizi. Msimruhusu kwa namna yeyote kurudi kwenye mali zake mpaka pale kuhani mkuu atakapokufa.
\s5
\v 33 Msiiharibu nchi mnayokaa kwa namna hii, kwa kuwa damu ya mwuaji huharibu nchi. Hakuna sadaka ya upatanisho inayoweza kufanywa kwa nchi pale damu inapomwagika juu yake, isipokuwa kwa damu ya mtu aliyeimwaga.
\v 34 Kwa hiyo msiinajisi nchi mnayoishi kwa sababu Mimi ninaishi ndani yake. Mimi BWANA huishi kati ya watu wa Israeli."'
\s5
\c 36
\p
\v 1 Kisha wale viongozi wa nyumba za mababa wa ukoo wa Gileadi mwana wa Machiri (ambaye alikuwa mwana wa Manase), ambao walikuwa wa ukoo wa uzao wa Yusufu, walikuja wakasema mbele za Musa na mbele za vionigozi wa familia za mababa wa watu wa Israeli.
\v 2 Wakasema, "BWANA alikuamuru, wewe bwana wetu, kutupa mgawo wa ardhi kwa kura kwa wana wa Israeli. Uliamuriwa na BWANA kutoa mgawo wa Zerofehadi kaka yetu kwa binti zake.
\s5
\v 3 Lakini hawa binti wameolewa na wanaume toka kabila zingine za wana wa Israeli, basi mgawo wao wa ardhi utaondolewa kutoka kwenye mgawo wa mababa zao. Utaongezwa kwenye mgawo wa makabila ambayo wao wanaungana nao. Kwa sababu hiyo, Utaondolewa kwenye mgawo uliopangwa kwenye urithi wetu.
\v 4 Kwa sababu hiyo, wakati wa mwaka wa yubilee ya wana wa Israeli utakapofika, mgawo wao utaunganishwa na kabila ile waliyoungana nao. Kwa sababu hii mgawo wao utaondolewa kwenye mgawo wa mababa zetu."
\s5
\v 5 Basi Musa akawapa amri wana wa Israeli, kwa neno la BWANA. Akasema, "Kile wanachosema watu wa kabila la Yusufu kiko sahihi.
\v 6 Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, 'Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.'
\s5
\v 7 Hakuna mgawo wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgawo wa kabila ya baba y ake.
\s5
\v 8 Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababa zake.
\v 9 Hakuna mgawo utakaobadilika kutoka kabila nyingine kwenda kabila nyingine. Kila mtu wa kabila za watu wa Israeli atalinda urithi wake."
\s5
\v 10 Kwa hiyo wale binti wa Zelofehadi walifanya kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Mahila, Tiriza, Hogila, Milika, na Noha, binti za
\v 11 Zelofehadi, waliolewa na wana wa uzao wa Manase.
\v 12 Waliolewa katika koo za uzao wa Manase mwana wa Yusufu. Kwa sababu hii, urithi wao ulibaki kwenye kabila la ukoo ambalo baba yao alikuwa anatoka.
\s5
\v 13 Hizi ndizo amri na maagizo ambayo BWANAaliyatoa kupitia Musa kwa wana wa Israeli katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.

1329
06-JOS.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1329 @@
\id JOS
\ide UTF-8
\h Yoshua
\toc1 Yoshua
\toc2 Yoshua
\toc3 jos
\mt Yoshua
\s5
\c 1
\p
\v 1 Sasa ilitokea baada ya kufa kwa Musa, mtumishi wa Yahweh, Yahweh alimwambia Yoshua, mwana wa Nuni, msaidizi mkuu wa Musa, kusema,
\v 2 "Musa, mtumishi wangu amekufa. Sasa basi inuka, vuka mto huu wa Yordani, wewe na watu hawa wote, kuingia katika nchi ambayo ninawapa - watu waisraeli.
\v 3 Nimewapa ninyi kila sehemu ambapo nyayo za miguu yenu itakanyaga. Nimewapa ninyi, kama nilivyomwahidi Musa.
\s5
\v 4 kuanzia jangwani na Lebanoni, hadi mto mkubwa wa Frati, nchi yote ya Wahiti, na hata Bahari kuu, ambako jua huzama, itakuwa nchi yenu.
\v 5 Hakuna mtu awaye yote atakayeweza kusimama kinyume chako siku zote za maisha yako. Nitakuwa pamoja nawe kama nilivyokuwa na Musa. Sitakupungukia wala kukuacha.
\s5
\v 6 Uwe hodari na jasiri. Wewe utawafanya watu hawa wairithi nchi ambayo niliwaahidi baba zao kuwa ningewapa.
\v 7 Uwe hodari na jasiri sana. uwe makini kutii sheria zote ambazo Musa mtumishi wangu alikuagiza. Usikengeuke upande wa kulia au wa kushoto, ili uweze kufanikiwa kila mahali utakapoenda.
\s5
\v 8 Siku zote uuongee juu ya kitabu hiki cha sheria. Utakitafakari mchana na usiku ili kwamba uweze kutii yote yaliyoandikwa humo. Kisha utastawi na kufanikiwa.
\v 9 Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hadori na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko.
\s5
\v 10 Kisha Yoshua akawaagiza viongozi wa watu,
\v 11 "Nendeni katika kambi na waagizeni watu, 'andaeni chakula kwa ajili yenu. Baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani na kuingia ndani na kuimiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi ili kuimiliki.""
\s5
\v 12 Yoshua akawaambia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase,
\v 13 "Kumbukeni maneno ambayo Musa, mtumishi wa Yahweh, aliwaaagiza aliposema, 'Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi pumziko, naye awapeni ninyi nchi hii.'
\s5
\v 14 Wake zenu, na watoto wenu na mifugo yenu itakaa katika nchi ambayo Musa aliwapa ninyi ng'ambo ya Yordani. Lakini watu wenu wa vita wataenda pamoja na ndugu zao na kuwasaidia.
\v 15 Mpaka hapo Yahweh atakapowapa ndugu zenu pumziko kama alivyowapa ninyi. Na wao pia watamiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi. Kisha mtarudi katika nchi yenu na kuimiliki, nchi ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa ninyi ng'ambo ya Yordani, mahali pa mapambazuko ya jua."
\s5
\v 16 Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, " Mambo yote uliyotuagiza tutayafanya, na kila mahali utakapotutuma tutaenda.
\v 17 Tutakutii kama tulivyomtii Musa. Yahweh Mungu wako na awe pamoja nawe tu kama aliyokuwa pamoja na Musa.
\v 18 Yeyote anayeasi maagizo yako na kutotii maneno yako atauawa. Uwe hodari na jasiri tu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha Yoshua mwana wa Nuni aliwatuma watu wawili kwa siri kama wapelelezi kutoka Shitimu. Akisema, "Nendeni mkaiangalie nchi, hasa Yeriko." Walienda na wakafika katika nyumba ya kahaba ambaye jina lake ni Rahabu, na wakalala hapo.
\v 2 Mfalme wa Yeriko aliambiwa, "Tazama watu wa Israeli wamekuja kuipeleleza nchi."
\v 3 Mfalme akatuma neno kwa Rahabu kusema, " Watoe watu waliokuja kwako ambao wameingia nyumbani mwako, kwa kuwa wamekuja kuipeleleza nchi yote."
\s5
\v 4 Lakini mwanamke alikuwa amekwisha kuwachukua wale watu wawili na kuwaficha. Na akasema, "Ndiyo, watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka.
\v 5 Ilipokuwa jioni wakati wa kufungwa kwa lango la mji, waliondoka. Sijui mahali walikoelekea. Mnaweza kuwakamata kama mtawafuata upesi.
\s5
\v 6 Lakini yeye aliwapandisha juu darini na kuwaficha kwa mabua ya kitani ambayo alikuwa ameyalaza darini.
\v 7 Hivyo, watu waliwafuatilia njiani iliyoeleka katika vivuko vya Yordani. Na milango ilifungwa mara tu baada ya wale watu waliofuata kutoka nje.
\s5
\v 8 Wale wanaume walikuwa hajalala usiku, wakati alipowaendea kule darini.
\v 9 Akawaambia, " Ninajua kwamba Yahweh amewapa ninyi nchi na kwamba hofu juu yenu imetuingia. Watu wote wanaoishi katika nchi watayeyuka mbele yenu.
\s5
\v 10 Tumesikia jinsi ambavyo Yahweh alivyokausha maji ya Bahari ya Mianzi kwa ajili yenu wakati mkitoka Misri. Na tumesikia mlichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori walioko upande mwingine wa Yordani - Sihoni na Ogu - ambao mmewaangamiza kabisa.
\v 11 Mara tu tuliposikia, mioyo yetu iliyeyuka na hapakuwa na ujasiri wowote uliosalia kwa mtu yeyote - kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ni Mungu aliye juu mbinguni na chini duniani.
\s5
\v 12 Sasa basi, tafadhali mniapie kwa Yahweh kwamba kama nilivyokuwa mwema kweu, nanyi pia mtaitendea mema nyumba ya baba yangu. Nipeni ishara ya uhakika
\v 13 kwamba mtanihifadhi maisha ya baba, mama, kaka, dada zangu na famiie zao, na kwamba mtatuokoa kutoka katika kifo.
\s5
\v 14 Wanaume wakamjibu, "maisha yetu kwa ajili ya yenu, hata kifo! Kama hamtasema habari zetu, na Yahweh akisha kutupa nchi hii, tutakuwa wenye huruma na waaminifu kwenu."
\s5
\v 15 hivyo aliwashusha chini kwa kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Nyumba ambayo alikuwa anaishi ilijengwa katika ukuta wa mji.
\v 16 Akawaambia, "Nendeni milimani la sivyo watu waliowafuata watawaona. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watu waliowafuata watakaporudi. Kisha nendeni zenu."
\v 17 Wanaume wakamwambia, "Hatutakuwa tumefungwa na ahadi ulizotufanya tuape mbele zako, kama hautalifanya hili.
\s5
\v 18 Tutakapokuja katika nchi, ni lazima uifunge kamba hii nyekundu katika dirisha ulilotushushia chini, na utawakusanya katika nyumba baba yako, mama yako, kaka zako na wote wa nyumba ya baba yako.
\v 19 Na yeyote aendaye mtaani nje ya milango ya nyumba yako,, damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao na hatutakuwa na hatia yoyote. Lakini kama mkono utanyoshwa juu ya mtu yeyote aliye pamoja nawe katika nyumba, damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu.
\s5
\v 20 Na ikiwa utaongea juu ya suala letu, tutakuwa huru dhidi ya kiapo ulichotuapisha.
\v 21 Rahabu akawajibu, " Yote mliyosema nayatimie." Akawatoa mbali na wakaondoka. Kisha akaifunga kamba nyekundu katika dirisha.
\s5
\v 22 Wakaondoka na kwenda juu milimani na walikaa huko kwa siku tatu hadi pale wale waliowafuatilia waliporudi. Wale waliowafuata walitafuta njiani pote bila kuwaona.
\s5
\v 23 Wale watu wawili walirudi na kuvuka mto na wakafika kwa Yoshua mwana wa Nuni, na walimwambia kila kitu kilichotokea kwao.
\v 24 Nao wakasema kwa Joshua, "kwa kweli Yahweh ametupa nchi hii. Wenyeji wote wa nchi wanayeyuka kwasababu yetu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Yoshua aliamka asubuhi na mapema, nao walisafiri kutoka Shitimu. Walifika Yordani, yeye na watu wote wa Israeli, na wakapiga kambi hapo kabla hawajavuka ng'ambo.
\s5
\v 2 Baada ya siku tatu, maafisa walienda katika kambi, wakawaagiza watu,
\v 3 "Mtakapoona sanduku la agano la Yahweh Mungu wenu, na makuhani kutoka miongoni mwa Walawi wamelibeba, ni lazima muondoke sehemu hii na kulifuata.
\v 4 Lazima kuwe na umbali wa dhiraa elfu moja kati yenu na sanduku. Msilisogelee karibu, ili muweze kuiona njia ya kupitia, kwakuwa hamjawahi kupita njia hii kabla.
\s5
\v 5 Yoshua akawaambia watu, "Jitakaseni ninyi wenyewe keso, kwa kuwa Yahweh atafanya maajabu miongoni mwenu."
\v 6 Kisha Yoshua akawaambia makuhani, "Chukueni sanduku la agano, na kulipitisha mbele za watu." Hivyo, wakalichukua sanduku la agano na wakaenda mbele za watu.
\s5
\v 7 Yahweh akamwambia Yoshua, "Siku hii nitakufanya kuwa mtu mkubwa katika macho ya Waisraeli wote. Watajua kuwa kama nilivyokuwa na Musa ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe.
\v 8 Utawaamuru makuhani ambao hulibeba sanduku la agano, 'Mtakapofika katika ukingo wa maji ya Yordani, ni lazima msimame katika Mto Yordani.'"
\s5
\v 9 Kisha Yoshu akawaambia watu wa Israeli, "Njooni hapa na msikilize maneno ya Yahweh Mungu wenu.
\v 10 Kwa hili mtajua kwamba Mungu aliye hai yuko miongoni mwenu na kwamba atawaondosha mbele yenu Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagrigashi, Waamori na Wayebusi.
\v 11 Tazama! Sanduku la agano la Bwana wa nchi yote litavuka mbele yenu katika Yordani.
\s5
\v 12 Sasa chagueni wanaume kumi na wawili kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja katika kila kabila.
\v 13 Wakati nyayo za miguu ya makuhani walichukualo sanduku la Yahweh, Bwana wa nchi yote, zitakapogusa maji ya Yordani, maji ya Yordani yatatindika, na hata maji yatiririkayo kutoka juu yatakoma kutiririka nayo yatasimama kama chuguu.
\s5
\v 14 Hivyo wakati watu walipotoka ili kuvuka Yordani, makuhani waliobeba sanduku la agano waende mbele ya watu.
\v 15 Mara tu wale walichukuao sanduku wakiisha kufika Yordani, na miguu ya watu wale waliobeba sanduku itakapotiwa katika ukingo wa maji (maana sasa Yordani hujaa hadi katika kingo zake zote katika kipindi chote cha mavuno),
\v 16 maji yote yaliyotiririka kutoka juu yalisimama katika chuguu kimoja. Maji yakakoma kutiririka kutoka katika umbali mrefu. Maji yaliacha kutiririka kutoka Adam, mji ulio karibu na Zarethani, hadi bahari ya Negevu, Bahari ya Chumvi. Na watu walivuka ng'ambo karibu na Yeriko.
\s5
\v 17 Makuhani waliolibeba sanduku la agano la Yahweh walisimama katika nchi kavu katikati ya Yordani mpaka watu wote wa Israeli walipokwisha kuvuka katika nchi kavu.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Watu wote walipokwisha kuvuka Yordani, Yahweh akamwambia Yoshua,
\v 2 "Chagueni wenyewe watu waume kumi na wawili, mmoja katika kila kabila.
\v 3 Wape agizo hilo: 'Chukueni mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani mahali wanaposimama makuhani katika nchi kavu, na wayalete na kuyaweka chini katika sehemu ambapo mtalala usiku wa leo.
\s5
\v 4 Kisha Yoshua akawaita wanaume kumi na wawili ambao aliwachagua kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja kutoka kila kabila.
\v 5 Yoshua akawaambia, "Nendeni mbele za sanduku la Yahweh Mungu wenu katikati ya Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe moja mabegani mwake, kulingana na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli.
\s5
\v 6 Hii itakuwa ni ishara miongoni mwenu kwa ajili yenu wakati watoto wenu watakapowauliza katika siku zijazo, 'Nini maana ya mawe haya kwenu?'
\v 7 Ndipo mtakapowaambia, 'Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh. Lililpopitishwa katika Yordani, maji ya Yordani yalisimamishwa. Hivyo, mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.'"
\s5
\v 8 Watu waisraeli walifanya kama Yoshua alivyowaagiza, na walichukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani, kama Yahweh alivyomwambia Yoshua, walipangwa sawa sawa na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli. Waliyachukua mawe mpaka mahali walipolala na wakayaweka chini huko.
\v 9 Kisha Yoshua akayapanga mawe kumi na mbili katikati ya Yordani, katika sehemu ambapo ilisimama miguu ya makuhani waliolichukua sanduku la agano. Na kumbukumbu hiyo ipo hadi leo.
\s5
\v 10 Makuhani waliolichukua sanduku walisimama katikati ya Yordani mpaka pale kila kitu ambacho Yahweh alimwamuru Yoshua kuwaambia watu kilipokamilika, sawa sawa na yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua. Watu walifanya haraka na wakavuka.
\v 11 Wakati watu wote walipokwisha kuvuka, sanduku la Yahweh pamoja na makuhani walivuka mbele za watu.
\s5
\v 12 Kabila la Rubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase walipita kama jeshi mbele ya watu wa Israeli, kama ambavyo Musa alivyowaambia.
\v 13 Yapata watu watu elfu arobaini walioandaliwa kwa vita walipita mbele za Yahweh, kwa ajili ya vita katika uwanda wa Yeriko.
\v 14 Katika siku hiyo Yahweh alimfanya Yoshua kuwa mkuu katika macho ya watu wote wa Israeli. Walimheshimu - kama walivyomheshimu Musa - siku zake zote.
\s5
\v 15 Kisha Yahweh akamwambia Yoshua,
\v 16 "Waamuru makuhani wanaolibeba sanduku la ushuhuda watoke katika Yordani."
\s5
\v 17 Hivyo Yoshua akawaamuru makuhani, '' pandeni mtoke Yordani."
\v 18 Wakati makuhani wenye kulibeba sanduku la agano la Yahweh walitoka katikati ya Yordani, na nyayo za miguu yao ilikuwa imeinuliwa katika nchi kavu, kisha maji ya Yordani yalirudi katika sehemu zake na kujaa hadi katika kingo zake kama ilivyokuwa siku nne zilizopita.
\s5
\v 19 Katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, watu walikwea kutoka Yordani. Wakakaa huko Gilgali, mashariki mwa Yeriko.
\v 20 Mawe kumi na mawili ambayo yalichukuliwa katika Yordani, Yoshuua aliyasimamisha hapo Gilgali.
\v 21 Aliwaambia watu wa Israeli, " wakati watoto wenu watakapowauliza baba zao katika wakai ujao, 'Mawe haya ni ya nini?'
\s5
\v 22 Waambieni watoto wenu, 'Hapa ndipo Waisraeli walivuka Yordani katika nchi kavu.
\v 23 Yahweh Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mpaka hapo Yahweh Mungu wako aliyoyafanya katika bahari ya mianzi, ambayo aliikausha kwa ajili yetu ili tupite juu yakes,
\v 24 ili kwamba watu wote wa nchi wajue kwamba mkono wa Yahweh ni nguvu, na kwamba mtamweshimu Yahweh Mungu wenu milele.''
\s5
\c 5
\p
\v 1 Mara tu waliposikia wafalme wa Waamori walio upande wa magharibi wa Yordani, na wafalme wote wa Wakanaani waliokuwa katika pwani ya Ziwa kuu, waliposikia ya kwamba Yahweh alikuwa ameyakausha maji ya Yordani mpaka pale waisraeli wote walipomaliza kuvuka, mioyo yao ikayeyuka, na hapakuwa na moyo wowote ndani yao kwa sababu ya watu wa Israeli.
\s5
\v 2 Kwa wakati huo Yahweh alimwambia Yoshua, "Tengenezeni visu vya mawe na mara moja mwatahiri wanaume wote wa Israeli."
\v 3 Kisha Yoshua alijifanyia visu vya mawe na akawatahiri wanaume wote wa Gibea Haaraloti.
\s5
\v 4 Na hii ndo sababu ya Yoshua kuwatahiri; wanaume wote waliotoka Misri, pamoja na wanaume wa vita walikuwa wamekwisha kufa njiani katika nyikani, baada ya kukwea kutoka Misri.
\v 5 Ingawa wanaume wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, bado hapakuwa na kijana yeyote aliyekuwa ametahiriwa kati ya vijana wote waliozaliwa nyikani katika njia ya kutoka Misri.
\s5
\v 6 Kwasababu watu wa Israeli walitembea nyikani miaka arobaini, mpaka watu wa vita, yaani wanaume wote waliotoka Misri walikufa, kwasababu hawakuitii sauti ya Yahweh. Yahweh aliwaapia kwamba hawataruhusu kuiona nchi ambayo aliwaapia mababa zao kwamba angetupatia sisi, nchi inayotiririka maziwa na asali.
\v 7 Na badala yao, Yahweh aliwainua watoto wao kuchukua nafasi zao ambao Yoshua aliwatahiri, kwasababu walikuwa bado hajatahiriwa njiani.
\s5
\v 8 Walipokwisha kutahiriwa wote, walibaki mahali walipokuwa katika kambi mpaka walipopona.
\v 9 Na Yahweh akasema na Yoshua, "Siku hii nimeiondoa kwenu aibu ya Misri." Hivyo, mahali pale paliitwa Gilgali hadi leo.
\s5
\v 10 Watu wa Israeli walipiga kambi hapo Gilgali. Waliitunza Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika uwanda wa Yeriko.
\v 11 Na siku iliyofuata baada ya Pasaka, walikula sehemu ya mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka iliyokaangwa katika siku hiyo iyo.
\s5
\v 12 Mana zilikoma siku ile walipokula mazao ya nchi. Hapakuwa tena na mana kwa watu wa Israeli, bali walikula mazao ya nchi ya Kanaani mwaka huo.
\s5
\v 13 Wakati Yoshua alipokaribia Yeriko, aliinua macho na kuangalia, na tazama, mtu alikuwa amesimama mbele yake, alikuwa amechomoa upanga wake na ulikuwa mkononi mwake. Yoshua alimwendea na kumwambia, "Je uko kwa ajili yetu au kwa ajli ya maadui zetu?"
\s5
\v 14 Akajibu, la hasha. Maana mimi ni amiri wa jeshi la Yahweh. Sasa nimekuja. Kisha Yoshua akainamisha uso wake juu ya nchi akaabudu na akamwambia, "Bwana wangu anasema nini kwa mtumwa wake?"
\v 15 Amiri wa jeshi la Yahweh akamwambia Musa, "Vua viatu vyako miguuni mwako, kwasababu sehemu uliyosimama ni takatifu." Na Yoshua akafanya hivyo.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Basi, milango yote ya Yeriko ilikuwa imefungwa kwasababu ya jeshi la Israeli. Hapakuwa na mtu wa kutoka nje au kuingia ndani.
\v 2 Yahweh akamwambia Yoshua, "Tazama, nimeweka Yeriko katika mkono wako, mfalme wake pamoja na wanajeshi wake waliofunzwa.
\s5
\v 3 Ni lazima kutembea kwa kuuzunguka mji, wanaume wote wa vita wauzunguke mji mara moja. Ni lazima mfanye hivi kwa siku sita.
\v 4 Makuhani saba lazima wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele za sanduku. Na katika siku ya saba, ni lazima mtembee kwa kuuzunguka mji mara saba, na makuhani lazima wapulize tarumbeta.
\s5
\v 5 Kisha watapuliza pembe za kondoo waume kwa nguvu kuu, na mtakaposikia sauti za tarumbeta watu wote na wapige kelele kwa mshindo mkuu, na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale. Wanajeshi ni lazime washambulie, kila mmoja eende mbele moja kwa moja.
\s5
\v 6 Ndipo Yoshua mwana wa Nuni, aliwaita makuhani na kuwaambia, "Lichukueni sanduku la agano, na waacheni makuhani saba wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Yahweh."
\v 7 Yoshua aliwaambia watu, "Nendeni na mkatembee kuuzunguka mji, na watu wa vita wataenda mbele ya sanduku la Yahweh."
\s5
\v 8 Makuhani saba walibeba tarumbeta saba za pembe za kondoo mbele ya Yahweh kama Yoshua alivyowaambia watu. Na walivyokuwa akiendelea mbele, walipuliza tarumbeta.
\v 9 Sanduku la Yahweh liliwafuata kwa nyuma yao. Watu wa vita walitembea mbele ya makuhani, na walipuliza tarumbeta zao, lakini walinzi wa nyuma walilifuata sanduku kwa nyuma, na makuhani waliendelea kupuliza tarumbeta zao.
\s5
\v 10 Lakini Yoshua aliwaagiza watu, akisema, "Msipige kelele. Sauti yoyote isitoke vinywani mwenu mpaka siku nitakayowaambia kupiga kelele. Ndipo hapo mtakapopiga kelele."
\v 11 Hivyo, alisababisha sanduku la Yahweh kuuzunguka mji mara moja kwa siku hiyo. Kisha wakaingia katika kambi yao, wakakaa usiku ule katika kambi.
\s5
\v 12 Basi Yoshua aliamka asubuhi na mapema, na makuhani wakalichukua sanduku la Yahweh.
\v 13 Makuhani saba waliobeba tarumbeta saba za pembe za kondoo waume walikuwa mbele ya sanduku la Yahweh, wakitembea kwa ushupavu, huku wakipuliza tarumbeta. Wanajeshi wenye silaha walikuwa wakitembea mbele yao, lakini walinzi wa nyuma walitembea nyuma ya sanduku la Yahweh, huku tarumbeta ziliendelea kupigwa.
\v 14 Walitembea kuuzunguka mji mara moja katika siku ya pili na kisha wakarudi kambini. Walifanya hivi kwa siku sita.
\s5
\v 15 Ilikuwa ni katika siku ya saba ambayo waliamka mapema katika mapambazuko, na walitembea kuuzunguka mji kwa namna ile kama ilivyokuwa kawaida yao, katika siku hii walifanya mara saba.
\v 16 Ilikuwa ni katika siku ya saba ambapo makuhani walipiga tarumbeta, na ya kwamba Yoshua aliwaagiza watu, "Pigeni kelele! Kwa kuwa Yahweh amewapa ninyi mji.
\s5
\v 17 Mji pamoja na vitu vyote ndani yake vitatengwa kwa Yahweh kwa ajili ya uharibifu. Ni Rahabu yule kahaba pekee ataishi - yeye pamoja wote waliokuwa pamoja naye katika nyumba - kwasababu aliwaficha watu tuliowatuma.
\v 18 Lakini kwenu, iweni waangalifu juu ya kuchukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu, ili baada ya kuvitia alama kwa ajili ya kuharibiwa, msichukue hata kimoja wapo. Na kama mtafanya hivi, mtaifanya kambi ya Waisraeli iharibiwe na mtaleta matatizo katika kambi.
\v 19 Fedha zote, dhahabu na vitu vilivyotengenezwa kwa shaba na chuma vilitengwa kwa ajli ya Yahweh."
\s5
\v 20 Hivyo, watu wakapiga kelele, na wakatoa sauti kwa kupuliza tarumbeta. Ilikuwa watu waliposikia sauti za tarumbeta, walipiga kelele kwa sauti kuu, na ukuta ulianguka chini kabisa na kwamba watu waliungia mji, kila mmoja alisonga mbele moja kwa moja. Na waliuteka mji.
\v 21 Waliteketeza kabisa kila kitu kilichokuwa katika mji kwa makali ya upanga - wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa, ng'ombe, kondoo na punda.
\s5
\v 22 Kisha Yoshua akawaambia wale watu wawili walioipeleleza nchi, "Nendeni katika nyumba ya kahaba, mtoeni mwanamke na wote walio pamoja naye, kama mlivyomwapia."
\s5
\v 23 Basi, vijana wale walioipeleleza nchi waliingia ndani na kumtoa Rahabu nje. Walimtoa nje baba yake, mama, kaka, na ndugu wote waliokuwa pamoja naye. waliwaleta katika sehemu ya nje ya kambi ya Waisraeli.
\v 24 Na ndipo waliuteketeza mji na kila kitu ndani yake. Isipokuwa fedha, dhahabu na vyombo vya fedha na chuma viliwekwa kwa hazina ya nyumba ya Yahweh.
\s5
\v 25 Bali Yoshua alimruhusu Rahabu kahaba, nyumba ya baba yake, na wote waliokuwa pamoja naye waishi. Mpaka leo hivi anaishi Israeli kwasababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko.
\s5
\v 26 Kisha katika kipindi hicho, Yoshua aliwaamuru kwa kiapo na kusema, "Alaaniwe machoni pa Yahweh mtu yule anayeujenga mji huu, Yeriko. Ataujenga msingi kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza, na kwa gharama ya mzaliwa wake wa pili atapachika milango yake."
\v 27 Basi Yahweh alikuwa pamoja na Yoshua, na umaarufu wake ulienea katika nchi yote.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Lakini watu wa Israeli hawakutenda katika uaminifu kuhusiana na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu. Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, kutoka katika kabila la Yuda, alivitwaa baadhi ya vitu hivyo vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya uharibifu, na hasira ya Yahweh iliwaka juu yawatu wa Israeli.
\s5
\v 2 Yoshua alituma watu kutoka Yeriko kwenda Ai, mji uliokuwa karibu na Bethi Aveni, mashariki mwa Betheli. Aliwaambia, "Nendeni na mkaipeleleza nchi." Wale watu walikwea na kuipeleleza Ai.
\v 3 Waliporudi kwa Yoshua, walimwambia, "Usitume watu wote kwenda Ai. Tuma tu watu elfu mbili au elfu tatu waende kuiteka Ai. Usiwafanye watu wateseke katika vita, kwani ni watu wachache."
\s5
\v 4 Hivyo ni watu wapatao elfu tatu tu kutoka katika jeshi ndio walioenda, lakini watu hawa waliwakimbia watu wa Ai.
\v 5 Watu wa Ai waliwaua watu wapatao thelathini na sita, waliwafuata katika lango la mji hadi katika machimbo ya mawe, na waliwauwa walipokuwa wakishuka katika kilima. Na mioyo ya watu ilijawa hofu na ujasiri wao ukawatoka.
\s5
\v 6 Basi Yoshua alizirarua nguo zake. Yeye pamoja na wazewe wa Israeli waliweka mavumbi juu ya vichwa vyao na wakainamisha vichwa vyao hadi katika nchi mbele ya sanduku la Yahweh, na walibaki pale mpaka jioni.
\v 7 Kisha Yoshua akasema, "Oo, Yahweh Bwana, kwanini umewavusha watu hawa ng'ambo ya Yordani? Kutuweka katika mikono ya Waamori ili kutuangamiza? ikiwa kama tulifanya maamuzi tofauti na tungekaa katika upande mwingine wa Yordani!
\s5
\v 8 Bwana, niseme nini, baada ya Israeli kuwatega migongo maadui zao?
\v 9 Kwa kuwa Wakaanani na wenyeji wote wa nchi watakaposikia, watatuzunguka na kuwafanya watu wa nchi kulisahau jina letu. Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
\s5
\v 10 Yahweh akamwambia Yoshua, "Inuka! kwanini umelala kifudifudi?
\v 11 Israeli imetenda dhambi. Wamevunja agano langu nililowaagiza. Wameiba baadhi ya vitu vilivyokuwa vimetengwa. Wameiba na kisha pia wakaficha dhambi yao kwa kuweka vitu vile walivyochukua miongoni mwa mali zao wenyewe.
\v 12 Na matokeo yake ni kwamba watu wa Israeli hawataweza kusimama mbele za maadui zao. Walitega migongo yao kwa maadui zao kwasababu wao wenyewe wametengwa kwa ajili ya uharibifu. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka pale mtakapoteketeza vitu vile vilivyotakiwa kuharibiwa, lakini sasa bado viko miongoni mwenu.
\s5
\v 13 Inuka! Waweke watu wakfu kwangu, na uwaambie, 'Jiwekeeni wakfu ninyi wenyewe kesho. Kwa kuwa, Yahweh, Mungu wa Israeli asema hivi, "Kuna vitu vilitengwa ili kuteketezwa ambavyo bado viko miongoni mwenu, Israeli. Hamtaweza kusimama mbele ya maadui zenu mpaka pale mtakapoviondoa miongoni mwenu vitu vyote ambavyo vilitengwa kwa ajili ya kuteketezwa."
\s5
\v 14 Asubuhi, mtajisogeza wenyewe kwa makabila. Kabila lile ambalo Yahweh atalichagua litasogea karibu kwa koo zake. Ukoo ule ambao Yahweh atauchagua lazima usogee karibu kwa nyumba. Nyumba ambayo Yahweh ataichagua lazima isogee karibu kwa mtu mmoja mmoja.
\v 15 Itakuwa hivi mtu yule atakayechaguliwa na aliye navyo vitu hivyo vilivyotengwa kwa ajili ya kuharibiwa, atachomwa moto, yeye na kila kitu alichonacho, kwasababu amelivunja agano la Yahweh na kwasababu amefanya jambo la aibu katika Israeli.'"
\s5
\v 16 Basi, Yoshua aliamka asubuhi na mapema na aliwaleta Israeli karibu, kabila kwa kabila, na kabila la Yuda lilichaguliwa.
\v 17 Yoshua akazisogeza koo za Yuda karibu, na ukoo wa Zera ulichaguliwa. Akausogeza karibu ukoo wa Zera mtu kwa mtu, na Zabdi alichaguliwa.
\v 18 Akaisogeza karibu nyumba ya Zabdi mtu kwa mtu, na Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, kutoka kabila la Yuda, alichaguliwa.
\s5
\v 19 Kisha Yoshua akamwambia Akani, "Mwanangu, niambie ukweli mbele za Yahweh, Mungu wa Israel, na ufanye ukiri wako kwake. Tafadhali niambie kile ulichofanya. Usinifiche."
\v 20 Akani akamjibu Yoshua, " Kwa kweli nimetenda dhambi mbele Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 21 Nilichofanya ni hiki: Nilipoona miongoni mwa nyara mkoti mzuri kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kipande cha dhahabu chenye uzito wa shekeli hamsini, nilivitamani na nikavichukua. Vimefichwa chini ardhini katikati ya hema langu, na fedha iko chini yake."
\s5
\v 22 Yoshua akatuma wajumbe waliokimbia mpaka kwenye hema mahali palipokuwa na vile vitu. Walipoangalia, waliviona vimefichwa katika hema lake, na fedha chini yake.
\v 23 Walivichukua vitu hivyo kutoka katikati ya hema na kuvileta kwa Yoshua na watu wote wa Israeli. Walivimwaga mbele za Yahweh.
\s5
\v 24 Kisha Yoshua na Waisraeli wote pamoja naye, walimchukua Akani mwana wa Zera, na fedha, na koti, na kipande cha dhahabu, wana na binti zake, ng'ombe zake, punda zake, kondoo zake, hema lake, na kila kitu alichokuwa nacho, na wakavileta hata bonde la Akori.
\s5
\v 25 Kisha Yoshua akasema, "Kwanini umetusumbua? Leo Yahweh atakutesa na wewe." Waisraeli wote wakampiga kwa mawe. Na wakawachoma wote kwa moto, na wakawapiga mawe.
\v 26 Kisha wakaweka juu yake kichuguu kikubwa cha mawe ambayo yapo hata leo. Yahweh akaachilia mbali hasira yake. Hivyo basi, jina la mahali hapo likawa Akori hata leo.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Yahweh akamwambia Yoshua, "Usiogope; usivunjike moyo. Chukua pamoja nawe watu wa vita. Pandeni kwenda Ai. Tazama nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai, watu wake, mji wake na nchi yake.
\v 2 Mtafanya hivyo pia huko Ai na mfalme wake kama mlivyofanya kwa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mtachukua nyara na mifugo kwa ajili yenu. Pangeni mashambulizi ya uviziaji nyuma ya mji."
\s5
\v 3 Basi Yoshua aliinuka na akawachukua kwenda Ai watu wote wa vita. Kisha Yoshua akachagua watu elfu thelathini - wenye nguvu na ujasiri - na aliwatuma waende wakati wa usiku.
\v 4 Aliwaamuru, "Tazama, mtalala katika hali ya mashambulizi ya uviziaji dhidi ya mji, kwa nyuma yake. Usiende mbali sana na mji, lakini ninyi nyote muwe tayari.
\s5
\v 5 Mimi pamoja na watu wote walio pamoja nami tutaukaribia mji. Na wakati watakapokuja kutushambulia sisi, tutawakimbia kama tulivyofanya hapo mwanzo.
\v 6 Watatoka nje watukimbize mpaka hapo tutakapokuwa tumewavuta mbali sana na mji, watasema, "Wanatukimbia kama walivyofanya mara ya mwisho.' Hivyo tutawakimbia na kwenda mbali.
\v 7 Kisha mtapanda kutoka sehemu mliyojificha, na mtauteka mji. Yahweh Mungu wenu atawapa mkononi mwenu.
\s5
\v 8 Tazama nimewaamuru, mtakapouteka mji, mtauchoma moto. Mtayafanya haya wakati mtakapotii agizo lililotolewa katika neno la Yahweh."
\v 9 Yoshua akawatuma, na wakaenda sehemu ya uviziajia, na wakajificha kati ya Betheli na Ai sehemu ya magharibi ya Ai. Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku ule.
\s5
\v 10 Yoshua aliamka asubuhi na mapema na akawaandaa tayari wanajeshi wake, Yoshua na wazee wa Israeli walishambuliwa watu wa Ai.
\v 11 Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda na kuukaribia mji. Walisogea karibu na mji na wakapiga kambi sehemu ya kasikazini mwa Ai. Kulikuwa na bonde kati yao na Ai.
\v 12 Alichukua watu wapatao elfu tano hivi na akawaweka katika hali ya kuvizia katika upande wa magharibi mwa mji kati ya Betheli na Ai.
\s5
\v 13 Waliwapanga wanajeshi wote, jeshi kuu katika upande wa kasikazini mwa mji, na walinzi wa nyuma upande wa magharibi mwa mji. Yoshua alilala bondeni usiku ule.
\v 14 Na ilikuwa alipoona hilo mfalme wa Ai, yeye pamoja na jeshi lake, waliamka asubuhi na mapema na walitoka kwa haraka kwenda kuwashambulia Israeli katika eneo linalokabili bonde la Mto Yordani. Hakujua kuwa kulikuwa na shambulizi la kuvizia lilikuwa linasubiria kushambulia kutokea kwa nyuma ya mji.
\s5
\v 15 Yoshua na Waisraeli wote walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu, na wakakimbia kuelekea nyikani.
\v 16 Watu wote waliokuwa kwenye mji waliitwa kwa pamoja waende mbele yao, na walienda mbele ya Yoshua na kwa jinsi hiyo walivutwa mbali na mji.
\v 17 Hapakuwa na mtu mme aliyesalia Ai na Betheli ambaye alikuwa hajaenda nje kuwafuatilia waisraeli. Na walipokuwa wanawafuatilia Waisraeli, Wakatoka na waliuacha mji wazi.
\s5
\v 18 Yahweh akamwambia Yoshua, "Nyosha mkuki huo ulio mkononi mwako kuelekea Ai, kwa kuwa nitaitia Ai mikononi mwako." Yoshua akaunyosha mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea mji.
\v 19 Wanajeshi waliojificha katika hali ya kuvizia walitoka upesi katika eneo lao mara tu alipounyosha mkono wake. Walikimbia mbio na kuuingia mji na kuuteka. Na kwa haraka wakauchoma moto mji.
\s5
\v 20 Watu wa Ai waligeuka na kuangalia nyuma. Waliona moshi kutoka katika mji ukipanda kwenda angani, na hawakuweza kutoroka kwa njia hii au ile. Kwa kuwa wanajeshi wa Israelei waliokuwa wamekimbia katika nyika, sasa walirudi kuwakabili wale waliokuwa wanawafuatilia.
\v 21 Na wakati Yoshua na Israeli wote walipoona kuwa wale watu wa kuvizia wameuteka mji kwa ule moshi uliokuwa ukipanda, waligeuka nyuma na kuwaua watu wa Ai.
\s5
\v 22 Na wanajeshi wengine wa Israeli, wale waliokuwa wameingia ndani ya mji, walitoka nje ili kuwashambulia. Hivyo, watu wa Ai walikamatwa katikati ya majeshi ya Israeli, baadhi katika upande huu na wengine katika upande ule.
\v 23 Lakini walimhifadhi mfalme wa Ai, ambaye walimteka akiwa hai, na kisha wakamleta kwa Yoshua.
\s5
\v 24 Ilikuwa baada ya Israeli walipokuwa wamemaliza kuuwaua wenyeji wote wa Ai katika uwanda kariibu na nyika mahali walipowafuata, na baada ya wao wote, hata yule wa mwisho, walipokuwa wamekwisha kulala kwa ncha ya upanga, Waisraeli wote walirudi Ai. Waliuteka mji kwa ncha ya upanga.
\v 25 Wale wote walikufa siku hiyo walikuwa watu elfu kumi na mbili elfu, wanaume na wanawake, wote ni watu wa Ai.
\v 26 Yoshua hakuukunja mkono wake ambao alikuwa ameunyosha huku akishikilia mkuki wake, mpaka pale alipowateketeza kabisa watu wote wa Ai.
\s5
\v 27 Waisraeli walichukua tu wanyama na nyara kutoka katika mji kwa ajili yao wenyewe, kama Yahweh alivyokuwa amemwagiza Yoshua.
\v 28 Yoshua aliichoma Ai na kuigeuza kuwa kichuguu cha mapango. Ni mahali palipoachwa ukiwa hata leo.
\s5
\v 29 Alimtundika mfalme wa Ai juu ya mti mpaka jioni. Na jua lilipokuwa linaenda kuzama, Yoshua aliwaagiza na wakautoa mwili wa mfalme wakaushusha chini ya mti na kuutupa mbele ya malango ya mji. Huko wakaweka kichuguu kikubwa cha mawe juu yake. Kichuguu hicho kimebaki huko hata leo.
\s5
\v 30 Kisha Yoshua akajenga madhabahu kwa Yahweh, Mungu wa Israeli katika Mlima wa Ebali,
\v 31 kama vile Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza watu wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa: "Madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna mtu yeyote aliyetumia zana ya chuma." Na allimtolea Yahweh sadaka ya kuteketezwa juu yake na wakatoa sadaka ya amani.
\v 32 Na huko aliandika juu ya mawe nakala ya sheria za Musa mbele ya watu wa Israeli.
\s5
\v 33 Waisraeli wote, wazee wao, maafisa, na waamuzi wao walisimama katika sehemu mbili za sanduku mbele ya makuhani na Walawi ambao hulibeba sanduku la Agano la Yahweh - wageni pamoja na wazalia, nusu yao walisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu walisimama mbele ya Mlima Ebali. Waliwabariki watu wa Israeli kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza hapo mwanzo.
\s5
\v 34 Baada ya hayo, Yoshua alisoma maneno yote ya sheria, baraka na laana, kama zilivyoandikwa katika kitabu cha sheria.
\v 35 Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa mbele ya kusanyiko la Waisraeli lilojumuisha wanawake, watoto wadogo na wageni walioishi miongoni mwao.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha wafalme wote walioishi ng'ambo ya mto Yordani katika nchi ya milima, na katika nchi za chini katika pwani za Bahari Kuu mbele ya Lebanoni - Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi -
\v 2 hawa waliungana pamoja chini ya amri moja kuinua vita dhidi ya Yoshua na Israeli.
\s5
\v 3 Waliposikia wenyeji wa Gibeoni juu ya mambo aliyoyafanya Yoshua katika Yeriko na Ai,
\v 4 walipanga mpango wa udanganyifu. Walienda kama wajumbe. Walichukua magunia yaliyochakaa na kuyaweka juu ya punda. Walichukua pia viriba vilivyochakaa na kuchanika chanika na vilivyozibwa zibwa.
\v 5 Walivaa miguuni mwao viatu vilivyozeeka na kutoboka toboka, na walivaa nguo kuukuu, zilichanika chanika. Na mikate yote katika chombo ilikuwa mikavu na yenye uvundo.
\s5
\v 6 Kisha wakamwendea Yoshua katika kambi huko Giligali na wakamwambia yeye pamoja wa watu wa Israeli wakisema, "
\v 7 Tumesafiri kutoka nchi ya mbali, basi fanyeni agano nasi." Watu wa Israeli wakawaamba Wahivi, "Huenda mnaishi karibu nasi. Twawezeje kufanya agano nanyi?"
\v 8 Wakamwambia Yoshua, "Sisi ni watumishi wako."Yoshua akawauliza, "Ninyi ni akina nani? Mnatokea wapi?
\s5
\v 9 Wakamwambia, "Watumishi wako wamekuja hapa kutokea nchi ya mbali, kwasababu ya jina la Yahweh Mungu wako. Tumesikia habari kumhusu na kuhusu kila kitu alichokifanya Misri -
\v 10 na kila kitu alichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori katika upande mwingine wa Yordani - kwa mfalme Sihoni wa Heshiboni, na kwa Ogu wa Bashani aliyekuwa katika Ashitarothi.
\s5
\v 11 Wazee wetu na wenyeji wote wa nchi yetu walituambia," Chukueni chakula mikononi mwenu kwa ajili ya safari. Nendeni mkakutane nao, na kisha muwambie, "Sisi ni watumishi wenu. Fanyeni agano pamoja nasi."
\v 12 Huu ni mkate wetu, ulikuwa wa moto tulipouchukua kutoka katika nyumba zetu katika siku ile tulipotoka kuja kwenu. Lakini sasa, tazama, imekuwa kavu na yenye ukungu.
\v 13 Viriba hivi vilikuwa vipya tulipovijaza, na tazama, sasa vinavuja. Nguo zetu na viatu vyetu vimechakaa na kuwa vikuukuu kwasababu ya safari ndefu."
\s5
\v 14 kwahiyo, Waisraeli wakatwaa sehemu ya vyakula vyao, lakini walifanya hivyo bila ya kumwuliza Yahweh ili awaongoze.
\v 15 Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia.
\s5
\v 16 Siku tatu baada ya Waisraeli kufanya agano pamoja nao, waligundua kuwa walikuwa ni majirani zao na ya kwamba waliishi karibu nao.
\v 17 Kisha watu wa Israeli walisafiri na kufika katika miji yao katika siku ya tatu. Miji yao ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi, na Kiriathi Yearimu.
\s5
\v 18 Watu wa Israeli wahakushambulia kwasababu viongozi wao walikuwa wamewaapia mbele za Yahweh, Mungu wa Israeli. Waisraeli wote walikuwa wananung'unika kinyume na viongozi wao.
\v 19 Lakini viongozi wote waliawaambia watu wote wa Israeli, "Tumeapa kwa Yahweh, Mungu wa Israeli kwa ajili yao, na sasa hatuwezi kuwadhuru.
\s5
\v 20 Hiki ndicho tutakachowafanyia: Tutawaacha waishi ili tuepuke ghadhabu ambayo yaweza kuja juu yetu kwasababu ya kiapo tulichowaapia."
\v 21 Viongozi wakawaambia watu, "Waacheni waishi." Hivyo Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote, kama vile viongozi walivyosema juu yao.
\s5
\v 22 Yoshua aliwaita na kuwaambia, " Kwanini mlitudanya wakati mliposema, "Tuko mbali sana nanyi' wakati mnaishi hapa hapa miongoni mwetu?
\v 23 Na kwasababu hii, mmelaaniwa na baadhi yenu mtakuwa watumwa siku zote, wenye kukata kuni na kuchota maji kwa ajli ya nyumba ya Mungu wangu."
\s5
\v 24 Walimjibu Yoshua na kusema, "Ni kwasababu watumishi wako waliambiwa kwamba Yahweh Mungu wenu alimwagiza Musa mtumishi wake kuwapa ninyi nchi yote, na kuwateteza wenyeji wote wa nchi mbele yenu - hivyo tuliogopa kwasababu yenu kwa ajili ya maisha yetu. Ndio maana tulifanya jambo hili.
\v 25 Tazama sasa, mnatumiliki chini ya utawala wenu. Chochote kilichochema na haki kwenu kutufanyia, fanyeni."
\s5
\v 26 Basi Yoshua aliwafanyia hivi: aliwaondoa katika mamlaka ya watu wa Israeli, na Waisraeli hawakuwaua.
\v 27 Siku hiyo Yoshua aliwafanya Wagibeoni kuwa wakata kuni na wachotaji wa maji kwa jamii, na kwa madhabahu ya Yahweh hadi leo katika sehemu ambayo Yahweh huichagua.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Ikawa Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alisikia kuwa Yoshua ameiteka Ai na ameiteketeza kabisa, kama alivyokwisha kufaya huko Yeriko na mfalme wake. Na alisikia jinsi ambavyo watu wa Gibeoni walivyofanya amani na watu wa Israeli na walikuwa wanaishi miongoni mwao.
\v 2 Watu wa Yerusalemu waliogopa sana kwasababu Gibeoni ulikuwa mji mkubwa, kama mmoja wa miji ya kifalme. Ilikuwa kubwa kuliko Ai, na watu wake wote walikuwa ni mashujaa wenye nguvu.
\s5
\v 3 Hivyo Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alituma ujumbe kwa Hohamu, mfalme wa Hebroni, na kwa Piramu, mfalme wa Yarimuthi, na kwaYafia, mfalme wa Lakishi, na kwa Debiri, mfalme wa Eguloni:
\v 4 "Njooni kwangu na mnisaidie. Tuishambulie Gibeoni kwasababu wamefanya amani na Yoshua pamoja na watu wa Israeli.
\s5
\v 5 Wafalme watano wa Waamori; mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarimuthi, mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Eguloni walikwea, wao pamoja na majeshi yao yote. Walipanga sehemu yao kinyume na Wagibeoni na waliwashambulia.
\s5
\v 6 Watu wa Gibeoni walituma ujumbe kwa Yoshua na kwa jeshi huko Giligali. Walisema, " Upesi! Msiuondoa mkono wenu kutoka kwa watumishi wenu. Kwaeni mje haraka na mtuokoe. Mtusaide, maana wafalme wote wa Waamori wanaoishi katika nchi ya milima wamekusanyika kwa pamoja ili watushambulie.
\v 7 "Yoshua alipanda kutoka Giligali, yeye na watu wote wa vita pamoja naye, na watu wote wapiganaji.
\s5
\v 8 Yahweh akamwambia Yoshua, "Usiwaogope. Nimewatiwa wote katika mkono wako. Hakuna hata mmoja wao atakayeweza kuzuia mashambulizi yako."
\s5
\v 9 Baada ya kutembea usiku kucha kutoka Giligali, ghafla Yoshua aliwafikilia.
\v 10 Na Yahweh alichanganya maadui mbele za Israeli - ambao waliwaua mauaji makubwa mno huko Gibeoni, na wale waliowafuata njiani iendayo Bethi Horoni, nao waliuwaua katika njia iendayo Azeka na Makeda.
\s5
\v 11 Na walipokuwa wakikimbia mbio kutoka kwa Waisraeli, chini ya mlima kutoka Bethi Horoni, Yahweh alitupa mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao wote katika njia iendayo Azeka, nao wakafa. Watu waliouawa kwa mawe walikuwa ni wengi zaidi kuliko wale waliouawa kwa upanga wa watu wa Israeli.
\s5
\v 12 Kisha Yoshua akamwambia Yahweh katika siku ambayo Yahweh aliwapa watu wa Israeli ushindi dhidi ya Waamori. Hiki ndicho Yoshua alichosema kwa Yahweh mbele ya Israeli. " Jua lisimame katika Gibeoni, na mwezi, usimame katika bonde la Aijaloni."
\s5
\v 13 Jua lilisimama, na mwezi ukaacha kwenda mpaka taifa lilipolipiza kisasi dhidi ya maadui zao. Je hili halikuandikwa katika Kitabu cha Yashari? Jua lilikaa katikati ya anga; halilkuzama kwa siku nzima hivi.
\v 14 Haijawahi kutokea siku nyingine kama hiyo kabla au baada yake, wakati Yahweh alipotii sauti ya mtu. Kwa kuwa Yahweh alikuwa akifanya vita badala ya Israeli.
\s5
\v 15 Yoshua na Israeli yote pamoja naye walirudi kambini huko Giligali.
\v 16 Basi wale wafalme watano walikuwa wametoroka na kujificha wao wenyewe katika pango huko Makeda.
\v 17 Taarifa zilimfikia Yoshua kusema, "Wafalme watano wamepatikana wamejificha katika pango huko Makeda!"
\s5
\v 18 Yoshua akasema, "Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.
\v 19 Msibaki na kukaa nyie wenyewe. Bali wafuatilieni maadui zenu na kuwashumbulia kutokea kwa nyuma. Msiwaruhusu kuingia katika miji yao, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu amewatia katika mkono wenu."
\s5
\v 20 Yoshua na wana Waisraeli walikuwa wamemaliza kuwaua kwa mauaji makubwa sana, mpaka pale walipokuwa wameteketezwa kabisa; watu wachache tu walipona waliotoroka walifika miji ya ngome.
\v 21 Kisha jeshi lote lilirudi kwa Yoshua likiwa na amani katika kambi huko Makeda. Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.
\s5
\v 22 Kisha Yoshua akasema, "Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano."
\v 23 Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.
\s5
\v 24 Na walipowaleta wafalme kwa Yoshua, alimwita kila mtu wa Israeli, na aliwaambia maakida wa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani pamoja naye " Kanyageni miguu yenu juu ya shingo zao." Basi walikuja na kukanyaga miguu yao juu ya shingo zao.
\v 25 Kisha akawaambia, 'Msiogope wala kufadhaika. uwe na moyo mkuu na jasiri. Na hiki ndicho Mungu atakachokifanya kwa maadui wenu wote ambao mtapigana nao'.
\s5
\v 26 Kisha Yoshua akawashambulia na kuwaua wafalme. Aliwatundika wote watano juu ya miti. Waliwatundika juu ya miti hata jioni.
\v 27 Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.
\s5
\v 28 Na kwa namna hii, katika siku hiyo Yoshua aliuteka mji wa Makeda na aliwaua watu wote huko kwa upanga, pamoja na mfalme wake. Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia. Alichomfanyia mfalme wa Makeda ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
\s5
\v 29 Yoshua na Israeli wote waliipita Makeda na kufika Libna. Na huko waliingia katika vita dhidi ya Libna.
\v 30 Yahweh pia aliitia katika mkono wa Israeli pamoja na mfalme wake. Yoshua alishambulia kila kiumbe hai ndani yake kwa upanga. Hakuacha hai hata mtu mmoja. Alichomfanyia mfalme ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.
\s5
\v 31 Baadaye Yoshua na Israeli wote pamoja naye walipanda kutoka Libna na kwenda Lakishi. Alipiga kambi karibu yake na wakafanya vita dhidi yake.
\v 32 Yahweh aliitia Lakishi katika mkono wa Israeli. Yoshua aliiteka katika siku ya pili. Alishambulia kwa upanga kilia kiumbe hai kilichokuwa ndani yake, kama vile aliyokuwa amefanya huko Libna.
\s5
\v 33 Kisha Horamu, mfalme wa Gezeri alikwea ili kuisaida Lakishi. Yoshua alimshambulia yeye na jeshi lake mpaka pale ambapo hapakuwa na mtu hata mmoja aliyesalia.
\s5
\v 34 Baada ya hapo, Yoshua na Israeli wote walitoka Lakishi na kwenda Egloni. Walipiga kambi karibu yake na kisha wakafanya vita dhidi yake,
\v 35 na siku hiyo hiyo wakaiteka. Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake kama vile Yoshua alivyofanya huko Lakishi.
\s5
\v 36 Kisha Joshua na Israeli wote wakatoka Egloni na kwenda Hebroni. Wakainua vita dhidi yake.
\v 37 Waliuteka mji na kuwaua kwa upanga watu wote ndani yake pamoja na mfalme wake, kujumuisha na vijiji vyote vilivyoizunguka. Waliteketeza kabisa kila kiumbe hai ndani yake, hawakuacha hata mtu mmoja aliyesalia, ni sawa sawa na vile Yoshua alivyoitenda Egloni. Aliiteketeza kabisa, na kila kiumbe hai ndani yake.
\s5
\v 38 Baada ya hapo, Yoshua alirudi pamoja na jeshi lote la Israeli pamoja naye, wakasafiri kwenda Debiri na kufanya vita dhidi yake.
\v 39 Aliuteka mji na mfalme wake, pamoja na vijiji vyake vya jirani. Waliwaua wote kwa upanga na waliteketeza kila kiumbe hai ndani yake. Joshua hakuacha hata mmoja hai, kama alivyokuwa amefanya kwa Hebroni na mfalme wake, na kama alivyokuwa amefanya kwa Libna na mfalme wake.
\s5
\v 40 Yoshua aliishinda nchi yote, nchi ya milima, Negevu, nchi, nchi ya tambarare na nchi ya miteremko. Hakuna hata mfalme moja aliyebaki hai kati ya wafalme wake wote. Kwa kweli aliteketeza kila kiumbe hai, kama ambavyo Yahweh, Mungu wa Israeli alivyomwaagiza.
\v 41 Yoshua aliwaua kwa upanga kutoka Kadeshi Barnea hadi Gaza, na nchi yote ya Gosheni hata Gibeoni.
\s5
\v 42 Yoshua aliwateka wafalme wote hawa na nchi zao kwa wakati mmoja, kwasababu Yahweh, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli.
\v 43 Baada ya hayo Yoshua na Waisraeli wote pamoja naye, walirudi katika kambi huko Gilgali.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi ikawa aliposikia haya, Yabini, mfalme wa Hazori, alituma ujumbe kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu.
\v 2 Alituma pia ujumbe kwa wafalme walikuwa katika mlima wa kaskazini mwa nchi, katika bonde la Mto Yordani kusini mwa Kinerethi, katika nchi za tambarare, na katika nchi za milima ya Dori kuelekea magharibi.
\v 3 Pia, alituma ujumbe kwa Wakanaani walioko mashariki na magharibi, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wayebusi katika nchi za milima, na Wahivi karibu na Mlima Hermoni katika nchi ya Mizipa.
\s5
\v 4 Maadui zao wote walitoka pamoja nao, wanajeshi wengi sana, hesabu yao ilikuwa kama mchanga wa pwani. Walikuwa na farasi wengi sana na magari.
\v 5 Wafalme wote hawa walikutana katika muda waliokuwa wameupanga, na walipiga kambi katika maji ya Meromu ili kupigana vita na Israeli.
\s5
\v 6 Yahweh akamwambia Yoshua, "Usiogope mbele zao, kwa kuwa muda kama huu kesho ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu. Utaivunja vunja miguu ya farasi zao, na utayachoma moto magari yao."
\v 7 Yoshua na watu wote wa vita walitoka na mara wakafika katika maji ya Meromu, na wakawashambulia maadui.
\s5
\v 8 Yahweh akawatia maadui katika mkono wa Israeli, na waliwapiga kwa upanga na wakawafuata mpaka Sidoni, Misrefothi - Maimu, na katika bonde la Mizipa upande wa mashariki. Waliwaua wote hakuna hata mmoja aliyeachwa hai.
\v 9 Yoshua aliwatendea kama vile Yahweh alivyomwambia. Alivunja miguu ya farasi na magari aliyachoma moto.
\s5
\v 10 Kwa wakati huo, Yoshua alirudi na akauteka mji wa Hazori. Alimwua mfalme wake kwa upanga (Hazori ulikuwa ni kichwa cha falme hizi zote).
\v 11 Waliwapiga kwa upanga kila kiumbe chenye uhai kilichokuwa huko, na alivitenga ili viteketezwe, hivyo hapakuwa na kiumbe hai kilichoachwa hai. Na kisha aliuchoma moto Hazori.
\s5
\v 12 Yoshua aliiteka miji yote ya wafalme hawa. Aliwateka pia wafalme wake wote na akawapiga wote kwa upanga. Aliwateketeza kabisa kwa upanga, kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyoagiza.
\v 13 Waisraeli hawakuchoma moto mji wowote miongoni mwa miji iliyojengwa juu ya vilima vya vifuasi vya udongo, isipokuwa Hazori, ndio mji pekee ambao Yoshua aliuchoma kwa moto.
\s5
\v 14 Jeshi la Israeli lilichukua nyara kutoka katika miji pamoja na mifugo kwa ajili yao wenyewe. Waliua kila mtu kwa upanga hadi pale walipokufa wote. Hakuna kiumbe hai kilichoachwa hai.
\v 15 Kama vile Yahweh alivyomwagiza mtumishi wake Musa, na kwa namna hiyo hiyo, Musa alivyomwagiza Yoshua. Na katika mambo yote ambayo Yahweh alimwamuru Musa kuyafanya, Yoshua hakuacha kufanya hata jambo moja.
\s5
\v 16 Yoshua alitwaa nchi hiyo yote, nchi ya milima, Negevu yote, nchi yote ya Gosheni, nchi ya vilima vidogo, bonde la Mto Yordani, nchi ya milima ya Israeli, na nchi tambarare.
\v 17 Kutoka Mlima Halaki karibu na Edomu, kuelekea kasikazini hadi Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni chini ya Mlima Hermoni, aliwateka wafalme wake wote na kuwaua.
\s5
\v 18 Yoshua alipigana vita na wafalme wote kwa muda mrefu.
\v 19 Hakuna hata mji mmoja uliofanya amani na jeshi la Israeli isipokuwa Wahivi walioishi Gibeoni. Israeli ilitwaa miji yote iliyosalia katika vita.
\v 20 Kwa kuwa alikuwa ni Yahweh ambaye alikuwa ameifanya kuwa migumu mioyo yao ili wapande na kufanya vita dhidi ya Israeli, ili kwamba aweze kuwaangamiza kabisa, na kutowaonesha huruma, kama alivyomwaagiza Musa.
\s5
\v 21 Kisha Yoshua akaja kwa wakati ule na aliiangamiza Anakimu. Aliyafanya haya katika nchi ya milima, huko Hebroni, Debiri, Anabu, na katika nchi yote ya Yuda, na katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua aliwaangamiza kabisa pamoja na miji yao.
\v 22 Hakuna hata mmoja wa watu wa Anakimu aliyeachwa katika nchi ya Israeli, isipokuwa huko Gaza, Gathi na Ashidodi.
\s5
\v 23 Hivyo Yoshua aliiteka nchi yote, kama vile Yahweh alivyomwambia Musa. Yoshua aliwapa Israeli kama urithi, kila kabila lilipewa sehemu yake. Kisha nchi ikapumzika bila vita.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao watu wa Israeli walishindwa. Waisraeli walichukua miliki ya nchi katika upande wa mashariki mwa Yordani sehemu ambako jua huchomoza, kutoka bonde la Mto Arnoni hadi Mlima Hermoni, na nchi yote ya Araba kuelekea kusini.
\v 2 Sihoni, mfalme wa Waamori, aliishi katika Heshiboni. Alitawala kutoka Aroeri, ambayo iko juu ya bonde la Arnoni kutoka katikati ya bonde, na nusu ya Geleadi kushuka mpaka Mto Yaboki katika mpaka wa Waamori.
\s5
\v 3 Sihoni pia alitawala juu ya Araba mpaka Bahari ya Kinerethi, kwenda mashariki, kuelekea Bahari ya Araba (Bahari ya Chumvi) upande wa mashariki, hadi huko Bethi Yeshimothi na upande wa kusini, kuelekea chini ya miteremko wa Mlima Pisiga.
\v 4 Ogu, mfalme wa Bashani, mmoja kati ya mabaki ya Rephaimu, aliyeishi huko Shatarothi na Edrei.
\v 5 Alitawala juu ya Mlima Hermoni, Saleka, na Bahani yote, hadi mpaka wa watu wa Geshuri na Wamakathi, na nusu ya Gleadi, hadi kufika mpaka wa Sihohi, mfalme wa Heshboni.
\s5
\v 6 Musa mtumishi wa Yahweh, na watu wa Israeli walikuwa wamewashinda, na Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa nchi kama mali ya Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.
\s5
\v 7 Hawa ndio wafalme wa nchi ambayo Yoshua na watu wa Israeli waliwashinda katika upande wa magharibi mwa mto Yordani, kutoka Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni hadi Mlima Halaki karibu na Edom. Yoshua aliyapa nchi makabila ya Israeli ili yaimiliki.
\v 8 Aliwapa nchi ya milima, tambarare, Araba, sehemu za milima, nyika na Negevu, nchi ya Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
\s5
\v 9 Wafalme hawa walikuwa ni mfalme wa Yeriko, mfalme wa Ai iliyo karibu na Betheli,
\v 10 mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Enaimu,
\v 11 mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi,
\v 12 mfalme wa Egloni, mfalme wa Gezeri,
\s5
\v 13 mfalme wa Debiri, mfalme wa Gederi,
\v 14 mfalme wa Horima, mfalme wa Aradi,
\v 15 mfalme wa Libna, mfalme wa Adula,
\v 16 mfalme wa Makeda, mfalme wa Betheli,
\s5
\v 17 mfalme wa Tapua, mfalme wa Heferi,
\v 18 mfalme wa Afeki, mfalme wa Lasharoni,
\v 19 mfalme wa Madoni, mfalme wa Hazori,
\v 20 mfalme wa Shimroni - Meroni, mfalme wa Akshafu.
\s5
\v 21 mfalme wa Taanaki, mfalme wa Megido,
\v 22 mfalme wa Kedeshi, mfalme wa Jokineamu katika Karmeli,
\v 23 mfalme wa Dori katika Nafutali Dori, mfalme Goyimu katika Giligali, na
\v 24 mfalme Tiriza. Hesabu ya wafalme ilikuwa ni thelathini na moja kwa ujumla wake.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Sasa Yoshua alikuwa mzee wakati Yahweh alipomwambia, "Umekuwa mzee, lakini bado kuna nchi kubwa ya kuteka.
\s5
\v 2 Nchi iliyosalia ndio hii: mikoa yote ya Wafilisti, na mikoa ile ya Wageshuri,
\v 3 (tangu Shihori, iliyoko mashariki mwa Misri, na upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Ekroni, inayofikiriwa kuwa ni mali ya Wakanaani; wafalme watano wa Wafilisti, wale wafalme wa Gaza, Ashidodi, Ashikeloni, Gathi na Ekroni - miliki ya Waavi.
\s5
\v 4 Katika upande wa kusini, kulisalia nchi yote ya Wakanaani, na Meara ambayo ni miliki ya Wasidoni, hadi Afeki, hata mpaka wa Waamori;
\v 5 nchi ya Wagebali, Lebanoni kuelekea upande wa mapambazuko ya jua, kutoka Baali- Gadi chini ya Mlima Hermoni mpaka Lebo Hamathi.
\s5
\v 6 Pia, wenyeji wote wa nchi ya milima kutoka Lebanoni hadi Misrefothi - Maimu, pamoja na watu wa Sidoni. Nitawafukuza mbele ya jeshi la Israeli. Uwe na uhakika wa kuwapa Waisraeli nchi kama urithi, kama nilivyokuagiza.
\v 7 Igawanye nchi hii kama urithi kwa makabila tisa na kwa nusu ya kabila la Manase.
\s5
\v 8 Pamoja na nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi wamekwisha kupokea urithi wao ambao Musa aliwapa katika upande wa mashariki wa Yordani,
\v 9 kutoka Aroeri, iliyo katika ukingo wa bonde la mto Arnoni (kujumuisha na mji ambao uko katikati ya bonde), kwa nyanda zote za Medeba hadi Diboni;
\s5
\v 10 miji yote ya Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala katika Heshiboni, hata mpaka wa Waamori,
\v 11 Gileadi na mkoa wa Wageshuri na Maakathi, mlima wote wa Hermoni, Bashani yote mpaka Saleka;
\v 12 ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyetawala katika Ashitarothi na Edrei - hawa ni wale waliosalia katika Refaimu - ambao Musa aliwapiga na kuwafukuzia mbali.
\s5
\v 13 Lakini watu wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri wala Wamakathi. Badala yake, Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo.
\s5
\v 14 Kabila la Lawi pekee halikupewa urithi na Musa. Urithi wao ni sadaka za Yahweh, Mungu wa Israeli, zilizotolewa kwa moto, kama Mungu alivyomwagiza Musa.
\s5
\v 15 Musa aliwapa urithi kabila la Rubeni, ukoo kwa ukoo.
\v 16 Miliki yao ilikuwa kutoka Aroeri, juu ya ukingo wa bonde la Mto Arnoni, na mji ulio katikati ya bonde, na nyanda zote za Medeba.
\s5
\v 17 Wareubeni walipata pia Heshiboni, na miji yake yote zilizo katika uwanda, Diboni, na Bamathi Baali, na Bethi Baalimeoni,
\v 18 na Yahazi, na Kedemothi, na Mefaathi,
\v 19 na Kiriathaimu, na Sibuma, na Zerethishahari juu ya kilima cha bonde.
\s5
\v 20 Wareubeni walipata pia Bethi Peori, miteremko ya Pisiga, Bethi Yeshimothi,
\v 21 miji yote ya uwanda, na ufalme wote wa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa ametawala katika Heshiboni, ambaye Musa alikuwa amemshinda pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Zuri, Huri na Reba, wana wa mfalme wa Sihoni, ambao walikuwa wameishi katika nchi.
\s5
\v 22 Pia, watu wa Israeli walimwua kwa upanga Baalam mwana wa Beori, ambaye alifanya mambo ya uaguzi, miongoni mwa wale waliowaua.
\v 23 Mpaka wa kabila la Rubeni ni Mto Yordani; huu ndio mpaka wao. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Rubeni, uliotolewa kwa kila ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.
\s5
\v 24 Hiki ndicho Musa alilipa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:
\v 25 Himaya yao ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Waamoni, hadi Aroeri, iliyo mashariki mwa Raba,
\v 26 kutoka Heshiboni hadi Ramathi - Mizipe na Betonimu, kutoka Mahanaimu mpaka himaya ya Debiri.
\s5
\v 27 Katika bonde, Musa aliwapa Bethi -Haramu, Bethi - Nimra, Sukothi, na Zafoni, ufalme uliobakia wa Sihoni mfalme wa Heshiboni, pamoja na Yordani kama mpaka, katika sehemu za chini za mwisho wa Bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki ng'ambo ya Yordani.
\v 28 Huu ni urithi wa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.
\s5
\v 29 Musa aliwapa urithi nusu ya kabila la Manase. Urithi uligawiwa kwa nusu ya kabila la watu wa Manase kutokana na kabila zao.
\v 30 Miliki yao ilikuwa kutoka Mahanaimu, Bashani yote, ufalme wote wa mfalme Ogu wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;
\v 31 nusu ya Gileadi, na Ashitarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Miji hii iligawanywa kwa ukoo wa Makiri mwana wa Manase -nusu ya watu wa Makiri, walipewa kwa kila familia zao.
\s5
\v 32 Huu ndio urithi ambao Musa aliowagawia katika nyanda za Moabu, ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko.
\v 33 Musa hakulipa urithi kabila la Lawi. kwa kuwa Yahweh, Mungu wa israeli, ni urithi wao, kama vile alivyowaambia.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Maeneo haya ya nchi ambayo watu wa Israeli waliyapokea kama urithi wao katika nchi ya Kanaani. Urith huu uligawanywa kwao na Eliazeri kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya mababu wa familia zao kati ya watu wa Israeli.
\s5
\v 2 Urithi wao ulichaguliwa kwa kupiga kura kwa makabila tisa na nusu, kama vile Yahweh alivyoagiza kwa mkono wa Musa.
\v 3 Kwa kuwa Musa alikuwa amewapa urithi makabila mawili na nusu ng'ambo ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi wowote.
\v 4 Kabila la Yusufu kwa uhalisia yalikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Na hakuna sehemu yoyote ya urithi waliyopewa Walawi katika nchi, lakini walipewa miji ya kuishi ndani yake pamoja na sehemu ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya riziki zao.
\v 5 Watu wa Israeli walifanya hivyo kama vile Yahweh alivyomwagiza Musa, basi waliiganywa nchi.
\s5
\v 6 Kisha kabila la Yuda lilikuja kwa Yoshua huko Giligali. Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, akamwambia,"Unajua kile Yahweh alichomwambia Musa mtu wa Mungu juu yako na mimi huko Barnea.
\v 7 Nilikuwa na umri wa miaka arobani wakati Musa mtumishi wa Yahweh aliponituma kutoka Kadeshi Barnea kuipeleleza nchi. Nilimletea taarifa tena kama nilivyotakiwa kufanya katika moyo wangu.
\s5
\v 8 Lakini ndugu zangu walioenda pamoja nami waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa woga. Lakini mimi nilimfuata Yahweh kabisa.
\v 9 Musa aliapa katika siku hiyo akisema, "Hakika nchi ambayo miguu yako imetembea juu yake itakuwa urithi wako na kwa watoto wako milele, kwasababu umemfuata kabisa Yahweh Mungu wangu.
\s5
\v 10 Tazama! sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano.
\v 11 Bado hata siku hii ya leo nina nguvu kama nilivyokuwa katika siku ile ambayo Musa alinituma. Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile, kwa ajili ya vita na kwa kwenda na kwa kuja.
\s5
\v 12 Sasa basi, nipe nchi hii ya milima, ambayo Yahweh aliniahidi katika siku hiyo. Kwa kuwa ulisikia katika siku hiyo kuwa Wanakimu walikuwa huko katika miji yenye ngome. Itakuwa kwamba Yahweh atakuwa pamoja nami na ya kwamba nitawafukuzia mbali, kama vile Yahweh alivyosema."
\s5
\v 13 Kisha Yoshua alimbariki Kalebu mwana wa Yefune na alimpa Hebroni kama urithi wake.
\v 14 Hivyo Hebroni ikawa urithi wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi hata leo, kwasababu alimfuata kabisa Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 15 Basi, jina la Hebroni hapo mwanzo lilikuwa ni Kiriathi Arba ( Arba ambaye alikuwa ni mtu mkuu miongoni mwa Wanakim). Kisha nchi ikawa na raha bila vita.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.
\v 2 Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.
\s5
\v 3 Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.
\v 4 Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.
\s5
\v 5 Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.
\v 6 Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata JIwe la Bohani mwana wa Rubeni.
\s5
\v 7 Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za Eni Shemeshi na kufika Eni Rogeli.
\v 8 kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi ( ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kasikazini.
\s5
\v 9 Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala ( ambao ndio Kiriathi Yearimu).
\v 10 Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.
\s5
\v 11 Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kasikazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambasamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.
\v 12 Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.
\s5
\v 13 Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).
\v 14 Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.
\v 15 Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).
\s5
\v 16 Kalebu akasema, "Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangau, Akisa, awe mke wake.
\v 17 Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake na Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.
\s5
\v 18 Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, "Unataka nini?"
\s5
\v 19 Akisa akamjibu, "Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negevu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji." Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.
\s5
\v 20 Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na koo zao.
\s5
\v 21 Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,
\v 22 Kina, Dimona, Adada,
\v 23 Kadeshi, Hazor, Ithinani,
\v 24 Zifu, Telemu, Bealothi.
\s5
\v 25 Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),
\v 26 Amamu, shema, Molada,
\v 27 Hazari Gada, Heshimoni, Bethi Peleti,
\v 28 Hazari Shuali, Beerisheba, Biziothia.
\s5
\v 29 Baala, Limu, Ezemu,
\v 30 Eltoladi, Kesili, Horma,
\v 31 Ziklagi, Madimana, Sansana,
\v 32 Lebaothi, Shilihimu, Aini, na Rimoni. Miji hii ilikuwa ishirini na tisa kwa ujumla, kujumlisha na vijiji vyake.
\s5
\v 33 Katika nchi iliyo chini ya mlima upande wa magharibi, kulikuwa na miji ya Eshtaoli, Zora, Ashina,
\v 34 Zanaoa, Eni Ganimu, Tapua, Enamu,
\v 35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
\v 36 Shaaraimu, Adithaimu, na Gedera ( ambayo ndio Gederothaimu). Hesabu ya miji hii ilikuwa ni kumi na nne, pamoja na vijiji vyao.
\s5
\v 37 Zena, Hadasha, Migidagadi,
\v 38 Dileani, Mizipa, Yokitheeli,
\v 39 Lakishi, Bozikathi, Egloni.
\s5
\v 40 Kaboni, Lahmamu, Kitilishi,
\v 41 Gederothi, Bethi Dagoni, Naama, Makeda. Hesabu ya miji hii ilikuwa kumi na sita, kujumlisha na vijiji vyao.
\s5
\v 42 Libna, Etheri, Ashani,
\v 43 Ifuta, Ashina, Nezibu,
\v 44 Keila, Akizibu, na Maresha. Hii ilikuwa ni miji tisa, kujumlisha na vijiji vyao.
\s5
\v 45 Ekroni, pamoja na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka;
\v 46 kutoka Ekroni kuelekea Bahari Kuu, makazi yote ambayo yalikuwa karibu na Ashidodi, pamoja na vijiji vyake.
\v 47 Ashidodi, na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; Gaza na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; hata kufika kijito cha Misri, na kuelekea Bahari Kuu pamoja na ukanda wake wa pwani.
\s5
\v 48 Katika nchi ya milima, kuna miji ya Shamiri, Yatiri, Soko,
\v 49 Dana, Kiriathi Sana (ambayo ndio Debiri),
\v 50 Anabu, Eshitemo, Animu,
\v 51 Gosheni, Holoni, na Gilo. Hii ilikuwa ni miji kumi na moja, kujumuisha na vijiji vyake.
\s5
\v 52 Arabu, Duma, Ehani,
\v 53 Yanimu, Bethi Tapua, Afeka,
\v 54 Humta, Kiriathi Arba (ambayo ndio Hebroni), na Ziori. Hii ilikuwa miji tisa, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
\v 56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
\v 57 Kaini, Gibea, na Timna. Hii ilikuwa ni miji kumi, kujumuisha na vijiji vyake.
\s5
\v 58 Halhuli, Bethi Zuri, Gedori,
\v 59 Maarathi, Bethi Anothi, na Elitekoni. Hii ilikuwa miji sita, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 60 Kiriathi Baali (ambayo ndio Kiriathi Yearimu), na Raba. Hii ilikuwa ni miji miwili, pamoja na vijiji vyake.
\v 61 Katika nyika, kulikuwa na miji ya Bethi Araba, Midini, Sekaka,
\v 62 Nibushani, mji wa chumvi, na Eni Gedi. Hii ilikuwa miji, pamoja na vijiji vyao.
\s5
\v 63 Lakini kwa Wayebusi, wenyeji wa Yerusalemu, kabila la Yuda halikuweza kuwafukuza, na hivyo, Wayebusi wanaishi pamoja na kabila la Yuda hadi leo hii.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Nchi waliyopewa kabila la Yusufu ilianzia katika Yordani huko Yeriko, mashariki mwa chemichemi za Yeriko, kupitia nyikani, kupanda kutoka Yeriko kupitia nchi ya milima ya Betheli.
\v 2 Kisha uliendelea kutoka Betheli hadi Luzi na kupita hata Atarothi, iliyo miliki ya Waarkiti.
\s5
\v 3 Kisha ilishuka chini upande wa magharibi kuelekea himaya ya Wayafuleti, hadi kufika miliki ya Loweri Bethi Horoni, na kisha iliendelea hadi Gezeri; na ilikomea katika bahari.
\v 4 Ilikuwa ni kwa njia hii makabila ya Yusufu, yaani Manase na Efraimu yalipata urithi wao.
\s5
\v 5 Eneo la kabila la Efraimu ambalo lilikuwa limegawanya kwa koo zao lilikuwa kama ifuatavyo: mpaka wa urithi wao katika upande wa mashariki ulikuwa Atarothi Ada uliopanda kuelekea Bethi Horoni ya juu,
\v 6 na kutoka pale uliendelea hadi katika bahari. Kutoka Mikimethathi katika upande wa Kasikazini ulipinda upande wa mashariki kuelkea Taanathi Shilo na kupita ng'ambo yake katika upande wa mashariki kukabili Yanoa.
\v 7 Kisha ulishuka kutoka Yanoa hadi Atarothi na hata Naara, na kisha ukafika Yeriko, na kuishia katika Yordani.
\s5
\v 8 Kutoka Tapua, mpaka uliendelea katika upande wa magharibi hata kijito cha Kana na ulikomea katika bahari. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Efraimu, uliogawanywa katika koo zao,
\v 9 pamoja na miji yao iliyochaguliwa kwa ajili ya kabila la Efraimu iliyokuwa ndani ya urithi wa kabila la Manase - miji yote pamoja na vijiji vyao.
\s5
\v 10 Lakini hawakuwafukuza Wakanaani walioishi katika Gezeri, hivyo basi Wakanaani wanaishi ndani ya Efraimu hadi leo, lakini watu hawa walifanywa kuwa watumwa.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Na huu ndio mgao wa nchi kwa ajili ya kabila la Manase (aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Yusufu), ambayo ilikuwa kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, ambaye alikuwa ni baba wa Gilieadi. Watoto wa Makiri walipewa nchi ya Gileadi na Bashani, kwasababu Makiri alikuwa ni mtu wa vita.
\v 2 Nchi iliyobaki iligawiwa kwa kabila la Manase, walipewa kwa koo zao, ambazo ni Abi Ezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi, na Shemida. Hawa walikuwa ni watoto wa kiume wa Manase mwana wa Yusufu, waliwakilishwa na koo zao.
\s5
\v 3 Basi Zelofehadi mwana wa Heferi mwana wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase hakuwa na watoto wa kiume, bali alikuwa na watoto wa kike tu. Na majina ya binti zake yalikuwa Mahila, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.
\v 4 Walimwendea Eliazeri kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi na wakasema, "Yahweh alimwagiza Musa atupatie urithi wetu pamoja na kaka zetu." Hivyo, kwa kuzingatia agizo la Yahweh, aliwapa wanawake hao urithi miongoni mwa ndugu za baba yao.
\s5
\v 5 Manase alipewa sehemu kumi za nchi katika Gileadi na Bashani, ambayo iko upande mwingine wa Yordani,
\v 6 kwasababu ya binti za Manase walipokea urithi pamona na watoto wake wa kiume. Nchi ya Gileadi iligawanywa kwa kabila la Manase lililosalia.
\s5
\v 7 Eneo la Manase lilianzia Asheri hadi Mikimethathi, ambayo iko mashariki mwa Shekemu. Kisha mpaka ulienda upande wa kusini kwa wale walioishi karibu na chemichemi ya Tapua.
\v 8 ( Nchi ya Tapua ilikuwa ni miliki ya Manase, lakini mji wa Tapua katika mpaka wa Manase ilikuwa ni mali ya kabila la Efraimu.)
\s5
\v 9 Kisha mpaka ulishuka kuelekea kijito cha Kana. Miji hii kusini mwa kijito miongoni mwa miji ya Manase ilikuwa ni mali ya Efraimu. Mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa kijito, na ulikomea katika
\v 10 bahari. Na nchi iliyokuwa upande wa kusini ilikuwa ni ya Efraimu, na nchi iliyo upande wa Kasikazini ilikuwa ni ya Manase; bahari ilikuwa ndoi mpaka. Kwa upande wa kaskazini ulifika hata Asheri, na upande wa mashariki, Isakari.
\s5
\v 11 Pia katika Isakari na katika Asheri, Manase alimiliki Bethi Shani na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, wenyeji wa Dori na vijiji vyake, wenyeji wa Endori na vijiji vyake, wenyeji wa Taanaki na vijiji vyake, na wenyeji wa Megido na vijiji vyake (na mji wa tatu ni Nafethi).
\v 12 Lakini kabila la Manase halikuweza kuimiliki miji hiyo, kwa kuwa Wakanaani waliendelea kuishi katika nchi hii.
\s5
\v 13 Hata wakati watu wa Israeli walipopata nguvu zaidi, hawakuwafukuzia mbali kabisa Wakanaani, bali waliwafanya kuwa watumwa.
\s5
\v 14 Kisha wazawa wa Yusufu wakamwambia Yoshua, wakisema, " Kwanini umetupa mgao mmoja wa nchi na sehemu moja kwa ajili ya urithi, kwa kuwa tuko wengi, na kwa muda wote Yahweh umetubaliriki?
\v 15 Yoshua akawaambia, "Kama ninyi ni watu wengi katika hesabu, pandeni ninyi wenyewe katika msitu na kuisafisha nchi kwa ajili yenu wenyewe katika nchi ya Waperizi na ya Refaimu. Fanyeni hivi kwa kuwa nchi ya milima ya Efraimu ni ndogo kwenu."
\s5
\v 16 Wazawa wa Yusufu wakasema, "Nchi ya milima haitutoshi. Lakini Wakanaani wote wanaoishi katika bonde wana magari ya chuma, wote walio katikaBethi Shani na vijiji vyake, na wale walio katika bonde la Yezreeli."
\v 17 Kisha Yoshua akawaambi nyumba ya Yusufu, ambao ni Efraimu na Manase, " Ninyi ni watu mlio wengi katika hesabu, na mna nguvu kubwa. Hamtakiwi kuwa na sehemu moja ya nchi mliogawiwa.
\v 18 Nchi ya milima itakuwa yenu pia. Ingawa ni msitu, mtaufyeka na kuimiliki hata mipaka yake ya mbali. Mtawafukuzia mbali Wakanaani, ingawa wanayo magari ya chuma na ingawa pia wanazo nguvu."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Kisha kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika pamoja hapo Shilo. Walilijenga hema la kukutania hapo na waliishinda nchi mbele yao.
\v 2 Kulikuwa na makabila saba miongoni mwa watu wa Israeli ambayo yalikuwa bado hayajapewa urithi wao.
\s5
\v 3 Yoshua aliwaambia watu wa Israeli, "Je mtaacha mpaka lini katika kuingia nchi ambayo Yahweh, Mungu wa baba zenu, amewapeni ninyi?
\v 4 Chagueni ninyi wenyewe watu watatu kutoka katika kila kabila, na nitawatuma. Wataenda na kuipeleleza nchi juu na chini. Wataandika maelezo pamoja na maelekezo kuhusu urithi wao, na kisha watarudi kwangu.
\s5
\v 5 Wataigawanya nchi katika sehemu saba. Yuda itasalia katika eneo lao upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu itaendelea katika himaya yao katika upande wa kaskazini.
\v 6 Mtaigawanya nchi katika sehemu saba na kisha mtaniletea maelezo hayo hapa kwangu. Nami nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh Mungu wetu.
\s5
\v 7 Walawi hana sehemu miongoni mwenu, kwa kuwa ukuhani wa Yahweh ni urithi wao. Makabila ya Gadi, Rubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapokea urithi wao ng'ambo ya Yordani. Huu ni urithi ambao Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa wao.
\s5
\v 8 Hivyo, watu waliinuka na wakaenda. Yoshua akawaamuru wale walioenda kuandika maelezo ya nchi, akisema, "Pandeni juu na mshuke chini katika nchi na andikeni maelezo kuhusu nchi na kisha mrejee kwangu. Nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh huko Shilo.
\v 9 Watu walienda na walitembea juu na chini katika nchi na wakaandika maelezo kuihusu nchi hiyo juu ya gombo kwa miji yake katika sehemu saba, kwa kutaja miji, kila mmoja katika sehemu moja. Kisha wakarudi kwa Yoshua katika kambi huko Shilo.
\s5
\v 10 Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za Yahweh. Na hapo Yoshua akaigawa nchi kwa watu wa Israeli, kila kabila lilipewa sehemu ya nchi.
\s5
\v 11 Katika kabila la Benyamini, ugawanaji wa nchi ulifanyika kwa kupewa kwa koo zao. Eneo la nchi waliyopewa lilikuwa kati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu.
\v 12 Katika upande wa kusini, mpaka wao ulianzia katika Yordani. Mpaka ulipanda hata sehemu ya juu kaskazini mwa Yeriko, na kisha ukapita katikati ya nchi ya milima upande wa magharibi. Huko ukafika hadi nyika ya Bethi Aveni.
\s5
\v 13 Kutoka hapo mpaka ulipita upande wa kusini katika mwelekeo wa Luzi (sehemu ile ile inayoitwa Betheli). Kisha mpaka ukashuka chini hata Atarothi Adda, karibu na mlima uliolekea kusini mwa Bethi Horoni.
\v 14 Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali ( ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.
\s5
\v 15 Katika upande wa kusini, mpaka ulianzia nje tu ya Kiriathi Yearimu. Mpaka uliendelea kutoka Efroni hata chemichemi ya maji ya Neftoa.
\v 16 Kisha mpaka ulishuka chini hadi mpaka wa mlima ambao ulikuwa mkabala ya bonde la Beni Hinomu, ambalo lililokuwa katika upande wa kaskazini mwishoni mwa bonde la Refaimu. Kisha ulishuka chini kuelekea bonde la Hinomu, sehemu ya kusini mwa mteremko wa Wayebusi, na uliendelea kushuka chini hadi Eni Rogeli.
\s5
\v 17 Ulizunguka upande wa kaskazini, kuelekea mwelekeo wa Eni Shemeshi, na kutoka hapa ulienda hadi Gelilothi, ambao ulikuwa mkabala na mwinuko wa Adumimu. Kisha ulishuka chini kuelekea Jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.
\v 18 Ulipita kuelekea upande wa kaskazini wa bega la Bethi Araba na chini kuelekea Araba.
\s5
\v 19 Mpaka ulipita hadi upande wa bega la kaskazini la Bethi Hogla. Mpaka ulikome katika ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, katika upande wa kusini mwishoni mwa Yordani. Huu ulikuwa ni mpaka wa upande wa kusini.
\v 20 Yordani ulikuwa mpaka wake katika upande wa mashariki. Na huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini, na walipewa kwa kila ukoo wao, mpaka baada ya mpaka, kwa kuizunguka nchi yote.
\s5
\v 21 Kwa hiyo sasa miji ya kabila la Benyamini kufuatana na koo zao ilikuwa ni Yeriko,
\v 22 Bethi Hogla, Emeki Kezizi, Bethi Araba, Zemaraimu, Betheli,
\v 23 Avimu, Para, Ofra,
\v 24 Kefari Amoni, Ofini, na Geba. Ilikuwa ni miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 25 Kulikuwa pia na miji ya Gibeoni, Rama, Beerothi,
\v 26 Mizpe, Kefira, Moza,
\v 27 Rekemu, Iripeeli, Tarala,
\v 28 Zela, Haelefu, Yebusi (ambao ndio Yerusalemu), Gibea, na Kiriathi. Kulikuwa na miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Huu ulikuwa ni urithi wa Benyamini kufuatana na koo zao.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni na waligawiwa kwa kila ukoo wao. Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.
\s5
\v 2 Urithi waliokuwa nao ni Beerisheba, Sheba, Molada,
\v 3 Hazari Shuali, Bala, Ezemu,
\v 4 Elitoladi, Bethuli na Horma.
\s5
\v 5 Simoni alikuwa pia na Ziklagi, Bethi Markabothi, Hazari Susa,
\v 6 Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile
\v 7 Simoni alimiliki Aini, Rimon, Etheri, na Ashani. Hii ilikuwa ni miji minne pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 8 Miji hii pamoja na vijiji vilivyoizunguka hata kufika Baalathi Beeri (ambao ndio Rama katika Negevu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simoni, waliopewa kwa koo zao.
\v 9 Urithi wa kabila la Simoni ulikuwa sehemu ya himaya ya kabila la Yuda. Hii ni kwasababu nchi waliyopewa kabila la Yuda ilikuwa ni kubwa kwao, na hivyo kabila la Simoni lilipokea urithi wao kutoka katika sehemu yao ya katikati.
\s5
\v 10 Upigaji wa kura ya tatu uliangukia kwa kabila la Zabuloni, na walipewa kwa koo zao. Mpaka wa urithi wao ulianzia huko Saridi.
\v 11 Mpaka wao ulipanda upande wa magharibi kuelekea Marala na ukaigusa Dabeshethi, na kisha ukasonga kuelekea kijito kilichokuwa mkabala na Yokineamu.
\s5
\v 12 Kutoka Saridi mpaka ulizunguka upande wa mashariki kuelekea mashariki na ulienda hadi mpaka wa Kislothi Tabori. Kutoka hapo uliendelea hadi Daberathi na kisha ulipanda hata Yafia.
\v 13 Kutoka hapo ulipita katika upande wa mashariki mwa Gathi Heferi, na kisha ukafika Ethikazini, baadaye ulienda hadi Rimoni na kisha ukageuka kuelekea Nea.
\s5
\v 14 Mpaka ulizunguka kueleka kaskazini ukafika Hanathoni na ulikomea katika bonde la Ifta Eli.
\v 15 Mkoa huu ulijumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala, na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
\v 16 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni, waliopewa kwa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 17 Upigaji kura wa nne uliangukia kwa Isakari, na waligawiwa kufuatana na koo zao.
\v 18 Eneo lao lilijumuisha Jezreelli, Kesuloothi, Shunemu,
\v 19 Hafaraimu, Shioni, na Anaharathi.
\s5
\v 20 Pia ilijumuisha miji ya Rabithi, Kishioni, Ebezi,
\v 21 Remethi, Enganimu, Enihada, na Bethipazezi.
\v 22 Mpaka wao ulifika Tabor, Shahazuma, na Bethi Shemeshi, na ukakomea katika Yordani. Ilikuwa ni miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 23 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari, na walipewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 24 Upigaji wa kura ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri, na walipewa kwa koo zao.
\v 25 Eneo lao lilijumuisha miji ya Helikathi, Hali, Beteni, Akashafu,
\v 26 Alameleki, Amadi, na Mshali. Mpaka wa magharibi ulitanuka hadi Karmeli na Shihori Libnathi.
\s5
\v 27 Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la ifutaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.
\v 28 Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.
\s5
\v 29 Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,
\v 30 Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 31 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 32 Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.
\v 33 Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.
\v 34 Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.
\s5
\v 35 Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinnerethi,
\v 36 Adama, Rama, Hazori,
\v 37 Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.
\s5
\v 38 Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
\v 39 Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.
\s5
\v 40 Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.
\v 41 Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,
\v 42 Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.
\s5
\v 43 Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,
\v 44 Eliteke, Gibethoni, Baalathi,
\v 45 Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,
\v 46 Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.
\s5
\v 47 Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.
\v 48 Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
\s5
\v 49 Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.
\v 50 Kwa amri ya Yahweh walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.
\s5
\v 51 Na huu ndio urithi ambao Eliazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli, waligawa kwa kupiga kura huko Shilo, mbele za Yahweh katika mlango wa hema la kukutania. Na hivyo wakamaliza kuigawa nchi.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Baada ya hayo, Yahweh akamwambia Yoshua,
\v 2 "Waambia watu wa Israeli, na kusema, 'Chagueni miji ya makimbilio ambayo niliwaambia kupitia kwa Musa.
\v 3 Fanyeni hivi ili mtu akiua mtu bila kukusudia aweze kwenda huko. Miji hii itakuwa ni sehemu ya kukimbilia kutoka kwa mtu yeyote yule anayetaka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu aliyeuliwa.
\s5
\v 4 Atakimbilia kwa mji mmoja miongoni mwa miji hiyo na atasimama mlangoni mwa lango la mji, na ataeleza kesi yake kwa wazee wa mji ule. Kisha watamwingiza ndani ya mji na watampatia sehemu yake ya kuishi miongoni mwao.
\s5
\v 5 Na kama mtu akija akataka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu yule ambaye aliuliwa, ndipo watu wa mji hawatatakiwa kumtoa kwa wenye mamlaka mtu huyo aliyeua. Hawaruhusiwi kufanya hivyo kwasababu alimwua jirani bila kukusudia na hakuwa na chuki naye hapo awali.
\v 6 Ni lazima akae katika mji ule mpaka pale atakapokuwa amesimama mbele ya kusanyiko kwa ajili ya kuhukumiwa, hadi pale atakapokufa mtu yule anayetumika katika nafasi ya kuhani mkuu katka siku hizo. Na kisha mtu yule aliyeua bila kukusudia aweza kurudi nyumbani kwake, katika mji ule ulikotoka.
\s5
\v 7 Kwahiyo, Waisraeli wakaichaguia Kedeshi iliyoko Galilaya katika nchi ya milima ya Nafutali, Shekemu katika nchi ya milima ya Efraimu, na Kiriathi Arba (ambayo ndio Herbroni) katika nchi ya milima ya Yuda.
\v 8 Katika ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri huko nyikani katika nyanda za kabila la Rubeni; na Ramothi Gileadi kutoka kabila la Gadi; na Golani katika Bashani, kutoka katika kabila la Manase.
\s5
\v 9 Hii ni miji iliyochaguliwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwao, ili kwamba mtu yeyote amwuaye mtu bila kukusudia aweza kukimbilia huko kwa ajili ya kupata usalama. Mtu huyu hatakufa kwa mkono wa mtu yule anayetake kulipiza kisasi cha damu iliyomwagwa, mpaka hapo kwanza mtuhumiwa atakaposimama mbele ya kusanyiko la watu.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha wakuu wa koo za Walawi walimwendea Eliazari kuhani, na kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli.
\v 2 Waliwaambia, "Yahweh aliwaagizeni ninyi kwa mkono wa Musa kwamba mtupatieni miji ya kuishi yenye maeneo kwa ajili ya kuchungia ya mifugo." waliyasema haya huko Shilo katika nchi ya Kanaani.
\s5
\v 3 Hivyo, kwa agizo la Yahweh, watu wa Israeli waliwapa Walawi kutoka katika urithi wa wao miji ifuatayo pamoja na maeneo yao ya kuchungia.
\s5
\v 4 Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini.
\v 5 Koo zilizobaki za Wakohathi walipokea kwa kupiga kura kwa miji kumi kutoka katika kabila za Efraimu, Dani, na kutoka kwa nusu ya kabila la Manase.
\s5
\v 6 Na watu wazawa wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kwa kupigiwa kura kutoka kwa koo za kabila la Isakari, Asheri, Nafutali, na nusu ya kabila la Manase katika Bashani.
\v 7 Watu waliokuwa wazawa wa Merari walipokea miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Rubeni, Gadi na Zabuloni.
\s5
\v 8 Basi, watu wa Israeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yao ya kuchungia, kwa kupiga kura, kama vile Yahweh alivyokuwa ameagiza kwa mkono wa Musa.
\v 9 Kutoka kwa makabila la Yuda na Simoni, waliwapa nchi katika miji ifuatayo iliyoorodheshwa kwa majina.
\v 10 Miji hii walipewa wazawa wa Haruni, ambao walikuwa miongoni mwa koo za Wakohathi, ambao walitoka katika kabila la Lawi. Kwa kuwa upigaji wa kura ya kwanza uliwaangukiwa wao.
\s5
\v 11 Waisraeli waliwapatia Kiriathi Arba ( Arba alikuwa ni baba wa Anaki), eneo hilo liliitwa pia Hebroni, katika nchi ya milima ya Yuda, pamoja na maeneo ya kulishia mifugo yaliyouzunguka mji.
\v 12 Lakini mashamba ya mji na vijiji vyake vilikuwa tayari ameshapewa Kalebu mwana Yefune, kama mali yake.
\s5
\v 13 Na kwa wana wa Haruni kuhani, waliwapa Hebroni pamoja na eneo lake la kulishia mifugo ambao ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia na Libna pamoja na maeneo ya kulishia mifugo.
\v 14 Na Yatiri pamoaja na maeno yake ya kuchungia, na Eshitemoa pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 15 Lakini pia waliwapa Holoni pamoja na maeneo yake ya malisho, Debiri pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 16 Aini pampoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. Ilikuwa ni miji kumi na tisa ambayo walipewa kutoka katika makabila haya mawilil.
\s5
\v 17 Kutoka katika kabilala Benyamini walipewa Gibea pamoja na maeneo yake ya malisho, na Geba pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 18 na Anathothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na amoni pamoja na vitongoji vyake vinne.
\v 19 Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.
\s5
\v 20 Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.
\v 21 Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 22 na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.
\s5
\v 23 Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na
\v 24 Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.
\s5
\v 25 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 26 Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.
\s5
\v 27 Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.
\s5
\v 28 Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 29 Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Engnimu pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 30 Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali pamoja na maeneo yake ya malisho, Abdoni pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 31 Helikathi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Rehobu pamoja na maeneo yake ya malisho.
\s5
\v 32 Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi katika Galilaya pamoja na maeneo yake ya malisho, ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia; na Hamothidori pamoja na maeneo yake ya malisho, na Kartani pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 33 Kulikuwa na miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumuisha na maeneo yake ya malisho, kwa ajili ya koo za Gershoni.
\s5
\v 34 Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu pamoa na maeneo yake ya marisho, Karta pamoja na maeneo yake ya malisho,
\v 35 Dimna pamoja na maeneo yake ya malisho, na Nahalali pamoja na maeneo yake ya malisho- ilikuwa ni miji minne kwa ujumla.
\s5
\v 36 Kwa mbari za Merari walipewa miji minne kutoka katika kabila la Rubeni: Bezeri pamoja na maeneo yake ya malisho, Yahazi pamoja na maene yake ya malisho,
\v 37 na Kedemothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.
\v 38 Kutoka katika kabila la Gadi walipewa miji ya Ramothi katika Gileadi pamoja na sehemu zake za malisho - huu ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu mwenzake bila kukusudia - na Mahanaimu pamoja na sehemu zake za malisho.
\s5
\v 39 Koo za Merari zilipewa pia Heshiboni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Yazeri pamoja na malisho yake.
\v 40 Hii ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake. Hii yote ilikuwa ni miji ya koo kadhaa za Merari, ambao walitoka katika kabila la Lawi, miji kumi na miwili walipewa wao kwa kupiga kura.
\s5
\v 41 Miji waliyopewa Walawi kutoka katikati ya nchi iliyomilikiwa na watu wa Israeli ilikuwa miji arobaini na nane, kujumuisha na sehemu za malisho yao.
\v 42 Miji hii kila mmoja ulikuwa na maeneo yake ya malisho kwa kuuzunguka mji. Miji hii yote ilikuwa hivyo.
\s5
\v 43 Basi Yahweh aliwapa Israeli nchi yote ambayo aliwaapia baba zao kuwa atawapa. Waisraeli waliimiliki nchi na wakakaa humo.
\v 44 Kisha Yahweh akawapa pumziko kwa kila upande, kama tu alivyowaahidia baba zao. Hakuna hata adui mmoja atakayeweza kuwashinda. Yawhew aliwatia maadui wao wote mikononi mwao.
\v 45 Hakuna hata kitu kimoja miongoni kwa ahadi nzuri ambazo Yahweh alizisema kwa nyumba ya Israeli ambazo hazikutimia. Ahadi zote zilitimia.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kwa wakati huo, Yoshua aliwaita Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase.
\v 2 Aliwaambia, "Mmefanya kila kitu ambacho Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi. Mmeitii sauti yangu katika yote niliyowaagiza.
\v 3 Bado hamjawaacha ndugu zenu hawa kwa siku zote hizi, mpaka siku hii ya leo. Na mmetimiza wajibu unaotakiwa na amri za Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 4 Sasa Yahweh Mungu wenu amewapa pumziko ndugu zenu, kama alivyowaahidi. Hivyo basi, rudini na mwende katika hema zenu katika nchi mnayoimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapeni katika upande mwingine wa Yordani.
\v 5 Lakini zingatieni kuzishika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi, kumpenda Yahweh Mungu wenu, kutembea katika njia zake, kuzitunza amri zake, na kuambatana naye na kumwabudu yeye kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.
\v 6 Basi Yoshua akawabariki na kisha akawaacha waende zao, nao wakarudi katika hema zao.
\s5
\v 7 Na kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa urithi katika Bashani, lakini kwa nusu ya kabila hilo, Yoshua aliwapa urithi karibu na ndugu zao katika nchi magharibi mwa Yordani. Yoshua aliwaaga waende katika hema zao; aliwabarikia,
\v 8 na kisha akawaambia, "Rudini katika hema zenu mkiwa na pesa nyingi, na mkiwa na mifugo mingi, pamoja na na fedha, na dhahabu, na shaba na chuma, na nguo nyingi. Gawaneni na ndugu zenu nyara mlizochukua kutoka kwa maadui zenu.
\s5
\v 9 Hivyo, wazawa wa Rubeni, wazawa wa Gadi na nusu ya kabila la Manase walirudi nyumbani, waliwaacha watu wa Isaeli hapo Shilo, ambayo imo ndani ya nchi ya Kanaani. Waliondoka wakaenda katika mkoa wa Gileadi, katika nchi yao, ambayo wao wenyewe waliimiliki, katika utiifu wa amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.
\s5
\v 10 Nao walipofika hapo Yordani iliyo katika nchi ya Kanaani, Warubeni na Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu karibu na Yordani, madhabahu kubwa na iliyotokeza na mashuhuri.
\v 11 Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseam, "Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli."
\s5
\v 12 Wakati watu wa Israeli waliposikia hivyo, kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande kupigana vita nao.
\s5
\v 13 Kisha watu wa Israeli walituma wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi. Walimtuma pia Finehasi mwana wa Eliezari, kuhani,
\v 14 na viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka katika familia za mababa wa Israeli, na kila mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa ukoo miongoni mwa watu wa Israeli.
\s5
\v 15 Walienda kwa watu wa Rubeni, Gadi, na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakawaambia:
\v 16 "Kusanyiko lote la Yahweh linasema kuwa, ' Ni jambo gani hili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa Israeli, kwa kugeuka badala ya kumfuata Yahweh siku hii na kujijengea wenyewe madhabahu katika uasi kinyume na Yahweh katika siku hii?
\s5
\v 17 Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha? Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo. Kwa ajili ya dhambi ile lilikuja pigo kwa kusanyiko lote la Yahweh.
\v 18 Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh? Kama mtaasi kinyume na Yahweh leo, kesho atakuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.
\s5
\v 19 Na kama nchi ambayo mnaimiliki imetiwa unajisi, basi mwaweza kuvuka katika nchi ambayo Sanduku la Yahweh lasimama na mjichukulie kwa ajili yenu umiliki miongoni mwetu. Hamtakiwi kuasi kinyume na Yahweh tu, wala kuasi kinyume chetu kwa kujenga madhabahu kwa ajili yenu wenyewe badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wa wetu.
\v 20 Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli? Mtu yule hakuangamia peke yake kwa uovu wake.
\s5
\v 21 Kisha makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakawajibu wazee wa koo za Israeli:
\v 22 "Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijue yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo
\v 23 kwa ajili ya kujenga madhabahu ili tugeuka na kuacha kumfuata Yahweh. Kama tumejenga madhabahu hii ili kutoa juu yake sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, au sadaka ya amani, basi Yahweh na atuadhibu.
\s5
\v 24 La hasha, tulifanya hivyo kwa sababu ya hofu kwamba katika siku zijazo watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu, ' Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?
\s5
\v 25 Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote naYahweh.' Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waacha kumwabudu Yahweh.
\s5
\v 26 Basi tukasema, 'Hebu na tujenge sasa madhabahu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa wala si kwa sadaka yoyote ile,
\v 27 ila iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi, na kati ya kizazi chetu baada yetu, kwamba tutafanya ibada ya Yahweh mbele yake, pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa na dhabihu zetu na sadaka zetu za amani, ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, "Hamna sehemu katika Yahweh."'
\s5
\v 28 Hivyo tukasema, 'kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, " Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi."
\v 29 Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh, na kuacha kumfuata yeye kwa kujenga madhabahu kwa ajili sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya nafaka, au kwa dhabihu, badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu ambayo iko mbele ya hema la kukutania.'"
\s5
\v 30 Finehasi kuhani na viongozi wa watu, ambao ni wakuu wa koo za Waisraeli ambao walikuwa pamoja naye, waliposikia maneno amabayo watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, kwamba yalikuwa ni mazuri machoni pao.
\v 31 Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani aliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na Manase, "Leo tumejua kwambaYahweh yuko miongoni mwetu, kwa kuwa hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye. Sasa, mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh."
\s5
\v 32 Kisha Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani, na viongozi walirudi kutoka kwa Warubeni na Wagadi, kutoka katika nchi ya Gileadi, na kurudi katika nchi ya Kanaani, kwa watu wa Israeli, na waliwaletea taarifa.
\v 33 Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu wa Israeli. Watu wa Israeli walimbarikia Mungu na hawakuendelea kusema tena juu ya kuinua vita dhidi ya Warubeni na Wagadi, ili kuiharibu nchi ambayo walikuwa wanaishi.
\s5
\v 34 Warubeni na Wagadi waliita ile madhabahu "Ushahidi," kwa kuwa walisema, "Ni ushahidi miongoni mwetu kuwa Yahweh ni Mungu."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Na baada ya siku nyingi, kipindi ambacho Yahweh alikuwa ameipa Israeli pumziko kutoka maadui zao waliowazunguka,
\v 2 Joshua alikuwa mzee sana. Yoshua aliwaita Waisraeli wote, na wazee wao, na viongozi, na waamuzi, na kwa maafisa, na kisha akawaambia, "Mimi nimezeeka sana.
\v 3 Mmeshaona kila kitu ambacho Yahweh Mungu wenu ameshafanya kwa mataifa haya yote kwa ajili yenu, kwa kuwa ni Yahweh Mungu wenu ambaye amewapigania ninyi.
\s5
\v 4 Tazama! Nimeshawakabidhi kwenu mataifa yaliyosalia ili kuyateka kwa ajili ya kupata urithi ya makabila yenu, sambasamba na mataifa yote ambayo tayari nimeshayaangamiza, tangu Yordani hadi Bahari kuu katika upande wa magharibi.
\v 5 Yahweh Mungu wenu atayaondoa. Atayafukuzia mbali kutoka kwenu. Ataiteka nchi yao, nanyi mtaimiliki nchi yao, kama vile Yahweh Mungu wenu alivyowaahidi ninyi.
\s5
\v 6 Hivyo, iweni jasiri, ili kwamba mtunze na kuyafanya yale yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa, msikengeuke upande wa kulia wala upande wa kushoto,
\v 7 basi msichanganyikane na mataifa haya ambayo yamesalia miongoni mwenu, wala msiyataje majina ya miungu yao, wala msiape kwayo, wala msiiabudu, wala msiipigie magoti.
\v 8 Badala yake, mnatakiwa kumshika sana Yahweh Mungu wenu kama vile mlivyofanya siku hii ya leo.
\s5
\v 9 Kwa kuwa Yahweh ameyafukuzia mbali mbele yenu mataifa makubwa yenye nguvu. Hakuna hata mmoja aliyeweza kusimama mbele yenu hata siku hii ya leo.
\v 10 Mtu yeyote mmoja wa kwenu atawafanya watu elfu wakimbie mbali, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ndiye anayepigania ninyi, kama vile alivyowaahidi.
\v 11 Zingatieni kwa uangalifu ili mmpende Yahweh Mungu wenu.
\s5
\v 12 Lakini kama mkiegeuka na kushikamana na watu walioalia wa mataifa haya waliobaki miongoni mwenu, au kuoana nao, au kama mkishirikiana pamoja nao, na wao pamoja nanyi,
\v 13 jueni kwa hakika kwamba Yahweh Mungu wenu hatayafukuzia mbali mataifa haya yatoke kati yenu. Badala yake, watakuwa kitanzi na mtego kwenu, viboko migongoni mwenu na miiba machoni mwenu, mpaka pale mtakapoangamia katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
\s5
\v 14 Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote, na mnajua kwa moyo na roho zenu zote kwamba hakuna hata neno moja ambalo halijatimia kati ya mambo yote mazuri ambayo Yahweh Mungu wenu aliyaahidi juu yenu. Vitu hivi vyote vimetokea kwa ajili yenu. Hakuna hata moja lililoshindikana.
\v 15 Lakini kama kila neno ambalo Yahweh Mungu wenu alilowaahidi limekwisha kutimia, hivyo Yahweh atawaletea juu yenu mabaya yote mpaka pale atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.
\s5
\v 16 Atafanya hivi kama mtalivunja agano la Yahweh Mungu wenu, ambalo aliwaagizeni kulitunza. Kama mtaenda na kuiabudu miungu mingine na kuiinamia, ndipo hasira ya Yahweh itawaka kinyume nanyi, na ninyi mtaangamia upesi katika nchi nzuri ambayo amekwisha kuwapeni ninyi."
\s5
\c 24
\p
\v 1 Kisha Yoshua aliyakusanya pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu na aliwaita wazee wa Israeli, viongozi, waamuzi na maafisa wao, nao wakajihudhurisha mbele za Mungu.
\v 2 Yoshua akawaambia watu wote, "Hiki ndicho Yahweh, Mungu wa Israeli anachokisema, 'Mababu zenu kwa miaka mingi iliyopita waliishi ng'ambo ya mto Frati - Tera, baba wa Ibrahimu na baba wa Nahori - nao waliabudu miungu mingine.
\s5
\v 3 Lakini nilimchukua baba yenu kutoka ng'ambo ya Frati na nikamwongoza mpaka katika nchi ya Kanaani, na nilimpa watoto wengi kupitia kwa Isaka mwanaye.
\v 4 Na Isaka nikampa Yakobo na Esau. Nilimpa Esau nchi ya milima ya Seiri ili aimiliki, lakini Yakobo na watoto wake walishuka kwenda Misri.
\s5
\v 5 Nilimtuma Musa na Haruni, na niliwapiga Wamisri kwa mapigo. Baada ya hapo, niliwatoa ninyi.
\v 6 Niliwatoa baba zenu nje ya nchi ya Misri, nanyi mkafika hata katika bahari. Wamisri waliwafuata kwa magari na wapanda farasi hata katika bahari ya matete.
\s5
\v 7 Na baba zenu walipomwita Yahweh, aliweka giza kati yenu na Wamisri. Aliileta bahari ije juu yao na kuwafunika. Mliona yale niliyoyakifanya huko Misri. Kisha mliishi jangwaani kwa muda mrefu.
\s5
\v 8 Niliwaleta katika nchi wa Waamori, ambao waliishi katika upande mwingine mwa Yordani. Walipigana nanyi, nami niliwatia katika mkono wenu. Mliimiliki nchi yao, nami niliwaangamiza mbele yenu.
\s5
\v 9 Kisha Balaki mwana wa Zipori, mfalme wa Moabu, aliinuka na kuishambulia Israeli. Alimwita na kumtuma Baalamu mwana wa Beori, ili kuwalaani ninyi.
\v 10 Lakini sikumsikiliza Balaamu. Kwa hakika, aliwabarikia ninyi. Basi, niliwaokoa na mkono wake.
\s5
\v 11 Mlivuka Yordani na mkafika Yeriko. Viongozi wa Yeriko waliinuka wapigane nanyi, pamoja na Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi. Niliwapa ninyi ushindi dhidi yao na niliwaweka chini ya mamlaka yenu.
\v 12 Nilituma manyingu mbele yenu, ambayo yaliwafukuzia mbali na wafalme wawili wa Waamori watoke mbele yenu. Haikutokea kwa sababu ya upanga wenu wala kwa upinde wenu.
\s5
\v 13 Niliwapeni ninyi nchi ambayo hamkuifanyia kazi na miji ambayo hamkuijenga, na sasa mnaishi ndani yake. Mnakula matunda ya mizabibu na na mashamba ya mizeituni ambayo hamkuyapanda'.
\s5
\v 14 Basi sasa mcheni Yahweh na kumwabudu yeye kwa uadilifu na uaminifu wote; jitengeni na miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati na katika Misri, na mkamwabudu Yahweh.
\v 15 Na kama inaonekana kuwa ni vibaya machoni penu kumwabudu Yahweh, chagueni ninyi katika siku hii ya leo ni nani mtakayemtumikia, kama ni miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao ninyi mnakaa ndani ya nchi yao. Lakini kwangu mimi na nyumba yangu, tutumwabudu Yahweh."
\s5
\v 16 Watu walijibu na kusema, "Hatutaweza kumwacha Yahweh na kuitumikia miungu mingine,
\v 17 kwa kuwa ni Yahweh Mungu wetu ambaye alitutoa sisi na baba zetu kutoka katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, na ambaye alifanya hizo ishara kubwa mbele yetu, na ambaye alituhifadhi sisi katika njia zote ambazo sisi tuliziendea, na miongoni mwa mataifa yote ambayo tulipita kati kati yake,
\v 18 Na Yahweh aliwaondoa mbele yetu watu wote, na Waamori walioishi katika nchi hii. Hivyo, tutamwabudu Yahweh pia, kwa kuwa ni Mungu wetu"
\s5
\v 19 Lakini Yoshua akawaambia watu, "Hamwezi kumtumikia Yahweh, kwa kuwa ni Mungu mtakatifu; ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa na dhambi zenu.
\v 20 Kama mtamwacha Yahweh na kuabudu miungu ya kigeni, basi atageuka na kuwaharibu. Atawaangamizeni baada ya kuwa amewatendea mema."
\s5
\v 21 Lakini watu walimwambia Yoshua, "Hapana, tutamwabudu Yahweh."
\v 22 Kisha Yoshua akawaambia watu, "Ninyi ni mashahidi dhidi yenu wenyewe kuwa mmemchagua Yahweh ninyi wenyewe, ili mmwabudu yeye." Watu walijibu, "Sisi ni mashahidi."
\v 23 "Sasa wekeni mbali miungu ya kigeni iliyoko kwenu, na geuzeni moyo wenu umwelekee Yahweh, Mungu wa Israeli."
\s5
\v 24 Watu wakamwambia Yoshua, "Tutamwabudu Yahweh Mungu wetu. Tutaisikiliza sauti yake.
\v 25 Yoshua alifanya agano na watu siku hiyo. Aliziweka maagizo na sheria huko Shekemu.
\v 26 Yoshua aliyaandika maneno haya katika kitabu cha sheria za Mungu. Alichukua jiwe kubwa na kulisimamisha hapo chini ya mti wa mwaloni uliokuwa karibu na mahali pa takatifu pa Yahweh.
\s5
\v 27 Yoshua akawaambia watu, "Tazama, jiwe hili litakuwa ushuhuda dhidi yenu. Limeyasikia maneno yote ambayo Yahweh alitwambia. Hivyo, litakuwa ni shahidi dhidi yenu, hamtakiwi kumkana Mungu wenu."
\v 28 Basi Yoshua aliwaacha watu waende zao, kila mmoja alienda kwenye urithi wake.
\s5
\v 29 Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Yahweh, alikufa akiwa na miaka 110.
\v 30 Walimzika katika mpaka wa urithi wake mwenyewe huko Timnathi Sera, ambayo iko kwenye nchi ya milima ya Efraimu, upande wa Mlima Gaashi.
\s5
\v 31 Israeli ilimwabudu Yahweh siku zote za maisha ya Yoshua, na siku zote za wazee ambao walidumu pamoja na Yoshua, wale ambao waliona kila kitu ambacho Yahweh alikuwa ameifanyia Israeli.
\s5
\v 32 Mifupa ya Yusufu ambayo watu wa Israeli waliileta kutoka Misri, waliizika huko shekemu, katika sehemu ya nchi ambayo Yakobo alikuwa ameinunua kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu. Aliinunua kwa vipande mia moja vya fedha, na ulikuwa urithi kwa wazawa wa Yusufu.
\v 33 Eliazeri mwana wa Haruni alikufa pia. Walimzika huko Gibea, katika mji wa ambao alikuwa amepewa Finehasi mwanaye, na ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu.

1271
07-JDG.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1271 @@
\id JDG
\ide UTF-8
\h Waamuzi
\toc1 Waamuzi
\toc2 Waamuzi
\toc3 jdg
\mt Waamuzi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Baada ya kifo cha Yoshua, wana wa Israeli walimuuliza Yahweh wakisema, "Ni nani atawashambulia kwanza Wakanaani kwa ajili yetu, ili kupigana nao?
\v 2 Yahweh akasema, "Yuda atawashambulia. Tazama, nimewapa kumiliki nchi hii.
\v 3 Watu wa Yuda wakawaambia wana wa Simeoni, ndugu zao, "Njoo pamoja nasi katika eneo letu ambalo tumepewa ili kwa pamoja tupigane na Wakanaani. Na sisi pia tutakwenda nanyi katika eneo mlilopewa." Basi kabila la Simeoni wakaenda pamoja nao.
\s5
\v 4 Watu wa Yuda wakashinda, na Bwana akawapa ushindi juu ya Wakanaani na Waperizi. Wakawaua watu elfu kumi huko Bezeki.
\v 5 Wakamkuta Adoni Bezeki huko Bezeki, nao wakapigana naye na kuwashinda Wakanaani na Waperizi.
\s5
\v 6 Lakini Adoni Bezeki akamkimbilia, wakamfuata na kumshika, nao wakavikata vidole gumba na vidole vyake vikubwa.
\v 7 Adoni Bezek akasema, "Wafalme sabini, ambao na vidole gumba vyako na vidole vikubwa vilivyokatwa, walikusanya chakula chao chini ya meza yangu. Kama nilivyofanya, hata hivyo Mungu amefanya kwangu." Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko.
\s5
\v 8 Watu wa Yuda wakapigana dhidi ya jiji la Yerusalemu na kulichukua. Walishambulia kwa makali ya upanga na wakauwasha mji kwa moto.
\v 9 Baada ya hayo, watu wa Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani waliokaa mlimani, Negebu, na magharibi mwa milima.
\v 10 Yuda akaenda dhidi ya Wakanaani waliokaa Hebroni (jina la Hebroni hapo awali ilikuwa Kiriath-arba), nao wakamshinda Sheshai, Ahimani na Talmai.
\s5
\v 11 Kutoka huko watu wa Yuda walipigana na wenyeji wa Debiri (jina la Debiri hapo awali ilikuwa Kiriath-seferi).
\v 12 Kalebu akasema, Yeyote atakayeivamia Kiriath-seferi na kuichukua, nitampa Aksa, binti yangu, awe mkewe.
\v 13 Otinieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, akaiteka Debiri, naye Kalebu akampa Aksa, binti yake, awe mkewe.
\s5
\v 14 Ndipo Aksa alifika kwa Othnieli, naye akamsihi amuombe baba yake ampe shamba. Alipokuwa akishuka katika punda wake, Kalebu akamwuliza, "Nikufanyie nini?"
\v 15 Akamwambia, Nibariki. Kwa kuwa umenipa nchi ya Negebu, nipe pia chemchemi za maji. Kwa hiyo Kalebu akampa chemchemi za juu na chemchemi za chini.
\s5
\v 16 Kizazi cha Mkeeni shemeji yake na Musa, walikwenda kutoka mji wa Mitende pamoja na watu wa Yuda, mpaka jangwa la Yuda, ambalo liko Negevu, kuishi na watu wa Yuda karibu na Arad.
\v 17 Nao watu wa Yuda wakaenda pamoja na wana wa Simeoni ndugu zao, wakawaangamiza Wakanaani waliokaa Zefathi, wakaiharibu kabisa. Mji uliitwa Horma.
\s5
\v 18 Watu wa Yuda pia waliiteka Gaza na nchi iliyoizunguka, Ashkeloni na nchi iliyoizunguka, na Ekron na nchi iliyoizunguka.
\v 19 Yahweh alikuwa pamoja na watu wa Yuda na wakaimiliki nchi ya milima, lakini hawakuweza kuwatoa wenyeji wa kwenye bonde kwa sababu walikuwa na magari ya chuma.
\s5
\v 20 Hebroni alipewa Kalebu (kama Musa alivyosema), naye akawafukuza kutoka huko wana watatu wa Anaki.
\v 21 Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa Yerusalemu. Basi Wayebusi wakakaa na watu wa Benyamini huko Yerusalemu hata leo.
\s5
\v 22 Nyumba ya Yusufu ilijiandaa kuishambulia Betheli, na Yahweh alikuwa pamoja nao.
\v 23 Walipeleka watu kuipeleleza Betheli (jiji lililoitwa Luzu).
\v 24 Wapelelezi waliona mtu akitoka nje ya jiji, wakamwambia, "Tafadhali tuonyeshe jinsi ya kuingia ndani ya jiji, na tutakutendea mema."
\s5
\v 25 Aliwaonyesha njia ya kuingia kwenye mji. Waliuteka mji kwa makali ya upanga, lakini wakamuacha mtu huyo na ndugu zake wote waondoke.
\v 26 Na mtu huyo akaenda nchi ya Wahiti, akajenga mji, akauita Luzu, ambalo jina lake hata leo.
\s5
\v 27 Watu wa Manase hawakuwafukuza watu waliokuwa katika miji ya Bethsheani na vijiji vyake, au Taanaki na vijiji vyake, au wale waliokaa Dori na vijiji vyake, wala wale waliokaa Ibleamu na vijiji vyake, wala walioshi Megido na vijiji vyake, kwa sababu Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi hiyo.
\v 28 Israeli ipokuwa na nguvu, waliwalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu, lakini hawakuwafukuza kabisa.
\s5
\v 29 Efraimu hakuwafukuza Wakanaani waliokaa Gezeri; kwa hiyo Wakanaani wakakaa kati yao.
\s5
\v 30 Zebuloni hakuwafukuza watu wa Kitroni, wala watu waliokuwa Nahaloli; na Wakanaani wakaendelea kuishi pamoja nao; lakini Zabuloni akawalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu.
\s5
\v 31 Asheri hakuwafukuza watu wanaoishi Aka, au watu wanaoishi Sidoni, au wale wanaoishi Alabu, Akzib, Helba, Afeka, au Rehobu.
\v 32 Kwa hiyo kabila ya Asheri iliishi kati ya Wakanaani (waliokaa katika nchi hiyo), kwa sababu hawakuwafukuza.
\s5
\v 33 Na kabila la Naftali halikuwafukuza watu waliokuwa wakiishi Bethshemeshi, wala waliokuwa wakiishi Bethanathi. Kwa hiyo kabila la Naftali liliishi kati ya Wakanaani (watu waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo). Hata hivyo, wenyeji wa Bethshemeshi na Bethanathi walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwa Naphthali.
\s5
\v 34 Waamori waliwalazimisha kabila la Dani kuishi katika nchi ya kilima, hawakuwaruhusu kuja bondeni.
\v 35 Basi Waamori waliishi katika mlima wa Heresi, huko Aiyaloni, na Shaalbimu, lakini nguvu za kijeshi za nyumba ya Yusufu ziliwashinda, nao wakalazimishwa kuwatumikia kwa kazi ngumu.
\v 36 Mpaka wa Waamori ulikuwa kutoka kilima cha Akrabimu huko Sela hadi nchi ya vilima.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Malaika wa Bwana akatoka Gilgali, akaenda Bokimu, akasema, "Nimekuleta kutoka Misri, na nimekuleta katika nchi niliyoapa kuwapa baba zako.
\v 2 Nikasema, 'Sitakuvunja kamwe agano langu na wewe. Usifanye agano na wale wanaoishi katika nchi hii. Ziangushe madhabahu zao. Lakini hukusikiliza sauti yangu. Je! ni nini hiki ulichokifanya?
\s5
\v 3 Basi sasa nasema, "Sitawafukuza Wakanaani mbele yenu, nao watakuwa miiba kwenu, na miungu yao itakuwa mtego kwa ajili yenu."
\v 4 Malaika wa Bwana alipowaambia maneno hayo kwa watu wote wa Israeli, watu wakapiga kelele na kulia.
\v 5 Waliita mahali hapo Bokimu. Hapo wakatoa dhabihu kwa Bwana.
\s5
\v 6 Yoshua alipowaruhusu watu waende zao, wana wa Israeli kila mmoja akaenda mahali alipopewa, wakiwa na umiliki wa ardhi yao.
\v 7 Watu walimtumikia Bwana wakati wa maisha ya Yoshua na wazee walioendelea baada yake, ni wale waliokuwa wameona matendo yote makuu ya Bwana aliyoyafanya kwa Israeli.
\v 8 Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, alikufa akiwa na umri wa miaka 110.
\s5
\v 9 Wakamzika ndani ya mpaka wa nchi aliyopewa huko Timnath Heresi, katika mlima wa Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaash.
\v 10 Kizazi hicho chote kilikusanyika kwa baba zao. Kizazi kingine kilichofuata baada yao ambao hakikumjua Bwana au kile alichokifanya kwa Israeli.
\s5
\v 11 Watu wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
\v 12 Wakaondoka kwa Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa kutoka Misri. Wakaifuata miungu mingine, miungu ya watu waliokuwa karibu nao, nao wakaisujudia. Wakamkasirisha BWANA kwa sababu
\v 13 waliondoka kwa Bwana na kumwabudu Baal na Maashtoreti.
\s5
\v 14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawapa washambuliaji walioiba mali zao kutoka kwao. Aliwauza kama watumwa waliofanyika kwa nguvu za maadui zao waliowazunguka, hivyo hawakuweza kujikinga dhidi ya adui zao.
\v 15 Israeli walipokwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi yao kuwashinda, kama alivyowaapia. Na walikuwa katika shida kali.
\s5
\v 16 Ndipo Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa katika mikono ya wale waliokuwa wakiba mali zao.
\v 17 Hata hivyo hawakuwasikiliza waamuzi wao. Hawakuwa waaminifu kwa Bwana na wakajitoa wenyewe kama makahaba kwa miungu mingine na kuabudu. Waligeuka upesi na kuiacha njia waliyoishi baba zao-wale waliotii amri za Bwana-lakini wao wenyewe hawakufanya hivyo.
\s5
\v 18 Bwana aliinua waamuzi kwa ajili yao, Bwana akawasaidia waamuzi na kuwakomboa kutoka kwa mikono ya adui zao siku zote muamuzi aliishi. Bwana aliwahurumia walipougua kwa sababu ya wale waliowadhulumu na kuwasumbua.
\v 19 Lakini mwamuzi alipokufa, waligeuka na kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuliko baba zao walivyofanya. Wakaenda kuifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao yote mabaya au njia zao za ukaidi.
\s5
\v 20 Hasira ya Bwana iliwaka juu ya Israeli; akasema, Kwa sababu taifa hili limevunja masharti ya agano langu ambalo nililiweka kwa ajili ya baba zao-kwa sababu hawakuisikiliza sauti yangu.
\v 21 Tangu sasa sitaliondoa mbele yao taifa lolote aliloliacha Yoshua baada ya kufa.
\v 22 Nitafanya hivi ili kuwajaribu Israeli, ikiwa watafuata njia ya Bwana au sivyo, kama vile baba zao walivyoifuata.
\v 23 Ndiyo sababu Bwana aliwaacha mataifa hayo, wala hakuwafukuza haraka na kuwatia mikononi mwa Yoshua.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa Bwana aliyaacha mataifa haya yaijaribu Israeli, yaani kila mtu katika Israeli ambaye hakushiriki vita yoyote huko Kanaani.
\v 2 (Alifanya hivyo ili kuwafundisha vita kizazi kipya cha Waisraeli ambao hawakujua kabla).
\v 3 Haya ndio mataifa: wafalme watano kutoka kwa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni, na Wahivi waliokaa milima ya Lebanoni, kutoka Mlima Baali Hermoni hadi Hamathi.
\s5
\v 4 Mataifa haya yaliachwa kama njia ambayo Bwana angeijaribu Israeli, kuthibitisha kama watazitii amri alizowapa babu zao kupitia Musa.
\v 5 Basi wana wa Israeli wakakaa kati ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Waperizi, na Wahivi, na Wayebusi.
\v 6 Waliwachukua binti zao kuwa wake zao, nao wakawapa wana wao binti zao, nao wakaitumikia miungu yao.
\s5
\v 7 Wana wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wakamsahau Bwana, Mungu wao. Waliabudu Baali na Asherah.
\v 8 Basi, hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawauza mkononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Aram Naharaimu. Watu wa Israeli walitumikia Kushan Rishathaimu kwa miaka nane.
\s5
\v 9 Watu wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamuinua mtu atakayewasaidia wana wa Israeli, na mtu atakayewaokoa: Othnieli mwana wa Kenazi (ndugu mdogo wa Kalebu).
\v 10 Roho wa Bwana akamtia nguvu, naye akahukumu Israeli na akatoka kwenda vitani. Bwana akampa kuishinda Kush-rishataimu mfalme wa Aramu. Mkono wa Othnieli alishinda Kushan Rishathaimu.
\v 11 Nchi ilikuwa na amani kwa miaka arobaini. Ndipo Otinieli mwana wa Kenazi akafa.
\s5
\v 12 Baada ya hayo, Waisraeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; Bwana akampa Egloni mfalme wa Moabu nguvu, kuwashinda Waisraeli.
\v 13 Eglon alijiunga na wana wa Amoni na Waamaleki wakaenda na kuwashinda Israeli, na walichukua mji wa Mitende.
\v 14 Watu wa Israeli walimtumikia Eglon mfalme wa Moabu kwa miaka kumi na nane.
\s5
\v 15 Wana wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamwinua mtu aliyewasaidia, Ehudi mwana wa Gera, Mbenjamini, mtu shoto. Wana wa Israeli wakamtuma kwa Egloni, mfalme wa Moabu, kwa malipo yao ya kodi.
\s5
\v 16 Ehudi akajifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wa dhiraa moja; aliufunga chini ya nguo zake juu ya mguu wake wa kulia.
\v 17 Akampa Egloni Mfalme wa Moabu malipo ya kodi. (Egloni alikuwa mtu mnene sana.)
\v 18 Baada ya Ehudi kulipa malipo ya kodi, aliondoka na wale waliokuwa wameibeba.
\s5
\v 19 Hata hivyo Ehudi mwenyewe, alipofikia mahali ambapo sanamu za kuchonga zilitengenezwa karibu na Gilgali, akageuka na kurudi, akasema, 'Nina ujumbe wa siri kwako, mfalme wangu.' Eglon akasema, 'Nyamazeni kimya!' Kwa hiyo wote waliomtumikia wakatoka kwenye chumba.
\v 20 Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake, peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, 'Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yeko.' Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake.
\s5
\v 21 Ehudi akanyoosha mkono wake wa kushoto na akachukua upanga kutoka mguu wake wa kulia, na akautia ndani ya mwili wa mfalme.
\v 22 Na kipini cha upanga kikaingia ndani yake baada ya upanga, nao ukatokea nyuma yake, na mafuta yakashikamana juu ya upanga, kwa kuwa Ehudi hakuutoa upanga nje ya mwili wake.
\v 23 Kisha Ehudi akatoka kwenye ukumbi na akafunga milango ya chumba cha juu nyuma yake na akawafungia.
\s5
\v 24 Baada ya Ehudi kuondoka, watumishi wa mfalme wakaja; wakaona milango ya chumba cha juu imefungwa, kwa hiyo wakafikiri, 'Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe katika hali ya baridi ya chumba cha juu.'
\v 25 Walizidi kuwa na wasiwasi hata walipoanza kuhisi kuwa walikuwa wakipuuza wajibu wao wakati mfalme bado hakufungua milango ya chumba cha juu. Kwa hiyo walichukua ufunguo wakawafungua, tazama bwana wao, ameanguka chini, amekufa.
\s5
\v 26 Wakati watumishi wakisubiri, wakijiuliza nini wanapaswa kufanya, Ehudi alikimbia na kupita mahali ambako kulikuwa na sanamu za kuchonga, na hivyo akakimbia kwenda Seira.
\v 27 Alipofika, alipiga tarumbeta katika nchi ya mlima wa Efraimu. Kisha wana wa Israeli wakashuka pamoja naye kutoka milimani, naye akawaongoza.
\s5
\v 28 Akawaambia, Nifuate, kwa kuwa Bwana atawashinda adui zenu, Wamoabu. Wakamfuata, wakakamata vivuko vya Bonde la Yordani, toka kwa Wamoabi, wala hawakuruhusu mtu yeyote kuvuka mto.
\v 29 Wakati huo waliwaua watu elfu kumi wa Moabu, na wote walikuwa watu wenye nguvu na wenye uwezo. Hakuna aliyekimbia.
\v 30 Kwa hiyo siku hiyo Moabu ilishindwa na nguvu ya Israeli. Na nchi ilikuwa na amani kwa miaka thelathini.
\s5
\v 31 Baada ya Ehudi, mwamuzi aliyefuata alikuwa Shamgari mwana wa Anathi ambaye aliwaua Wafilisti 600 kwa konzo la ng'ombe. Pia aliwaokoa Israeli kutoka kwenye hatari.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Baada ya Ehudi kufa, watu wa Israeli walifanya tena yaliyo mabaya machoni pa Bwana.
\v 2 Bwana akawatia mkononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyewala huko Hasori. Kamanda wa jeshi lake aitwaye Sisera, naye aliishi Harosheti ya Mataifa.
\v 3 Wana wa Israeli wakamwomba Bwana awasaidie, kwa sababu Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa na akawashinda wana wa Israeli kwa nguvu kwa miaka ishirini.
\s5
\v 4 Basi Debora, nabii wa kike (mke wa Lapidothi), alikuwa mwamuzi anayeongoza katika Israeli wakati huo.
\v 5 Naye aliketi chini ya mtende wa Debora kati ya Rama na Betheli katika nchi ya mlima wa Efraimu, na watu wa Israeli walimwendea ili kutatua migogoro yao.
\s5
\v 6 Akamtuma Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali. Akamwambia, Bwana, Mungu wa Israeli, anakuamuru, Nenda katika mlima wa Tabori, uende pamoja nawe watu elfu kumi kutoka Naftali na Zabuloni.
\v 7 Nitamfukuza Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, akutane nawe karibu na mto Kishoni, pamoja na magari yake na jeshi lake, na nitakupa ushindi juu yake. '
\s5
\v 8 Baraka akamwambia, 'Ikiwa utakwenda nami, nitakwenda, lakini ikiwa huendi pamoja nami, sitaenda.'
\v 9 Alisema, 'Nitakwenda nawe. Hata hivyo, njia unayoienda haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Bwana atamuuza Sisera mkononi mwa mwanamke. Ndipo Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka Kedeshi.
\s5
\v 10 Baraki akawaita wana wa Zebuloni na Naftali kusanyika Kedeshi. Watu elfu kumi walimfuata, na Debora akaenda pamoja naye.
\s5
\v 11 Heberi (Mkeni) alijitenganisha na Wakeni - walikuwa wazao wa Hobabu (mkwe wa Musa) - na akaweka hema yake mwaloni uliopo huko Saanaimu karibu na Kedesh.
\s5
\v 12 Walipomwambia Sisera kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu, alikuwa amekwenda mlima wa Tabori,
\v 13 Sisera akawaita magari yake yote, magari ya farasi mia tisa, na askari wote waliokuwa pamoja naye, kutoka Haroshethi ya Mataifa mpaka Mto Kishoni.
\s5
\v 14 Debora akamwambia Baraka, Nenda! Kwa maana hii ndiyo siku ambayo Bwana amekupa ushindi juu ya Sisera. Je! si Bwana anayekuongoza? Basi Baraka akashuka kutoka mlima wa Tabori na watu kumi elfu wakamfuata.
\s5
\v 15 Bwana alifanya jeshi la Sisera kuchanganyikiwa, magari yake yote, na jeshi lake lote. Watu wa Baraka waliwashinda na Sisera akaanguka kutoka kwenye gari lake na kukimbia kwa miguu.
\v 16 Lakini Baraka akayafuata magari na jeshi mpaka Haroshethi ya Mataifa, na jeshi lote la Sisera likauawa kwa upanga, wala hakuna mtu aliyeokoka.
\s5
\v 17 Lakini Sisera akakimbia kwa miguu mpaka hema ya Yaeli, mkewe Heberi Mkeni; kwa sababu kulikuwa na amani kati ya Yabini mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi Mkeni.
\v 18 Jaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, karibu, bwana wangu; karibu kwangu, wala usiogope. Basi akakaribia kwake, akaingia hemani kwake, naye akamvika bushuti.
\s5
\v 19 Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe, kwa maana nina kiu. Alifungua mfuko wa ngozi ya maziwa akampa anywe, kisha akamfunika tena.
\v 20 Akamwambia, "Simama mlangoni pa hema. Ikiwa mtu atakuja na kukuuliza, 'Je, kuna mtu hapa?', Sema 'Hapana'."
\s5
\v 21 Kisha Jaeli (mke wa Heberi) akachukua kigingi cha hema na nyundo mkononi mwake akamwendea kwa siri, kwa sababu alikuwa amelala usingizi mzito, naye akakitia kigingi cha hema upande wa kichwa chake akamchoma na kikapenya kushuka chini. Hivyo akafa.
\v 22 Baraka alipokuwa akimfuata Sisera, Jaeli alitoka kukutana naye akamwambia, "Njoo, nitakuonyesha mtu unayemtafuta." Basi akaingia pamoja naye, tazama Sisera amekufa, na kigingi cha hema kando ya kichwa chake.
\s5
\v 23 Basi siku hiyo Mungu alimshinda Jabin, mfalme wa Kanaani, mbele ya watu wa Israeli.
\v 24 Uwezo wa watu wa Israeli ulikua na nguvu zaidi dhidi ya Jabin mfalme wa Kanaani, hata walipomwangamiza.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Siku hiyo Debora na Baraka, mwana wa Abinoamu waliimba wimbo huu:
\v 2 'Viongozi wanapoongoza mbele ya Israeli, watu wanapojitolea kupigana vita, tunamsifu Bwana!
\s5
\v 3 Sikiliza, ninyi wafalme! Sikiliza kwa makini, ninyi viongozi! Mimi nitamwimbia Bwana; Nami nitamsifu Bwana, Mungu wa Israeli.
\v 4 Ee Bwana, wakati ulipotoka Seiri, ulipokwenda kutoka Edomu, nchi ilitetemeka, na mbingu pia ilitetemeka; pia mawingu yalitoa maji.
\s5
\v 5 Milima ikatoka mbele ya uso wa Bwana; hata Mlima Sinai ukatetemeka mbele ya uso wa Bwana, Mungu wa Israeli.
\v 6 Katika siku za Shamgari (mwana wa Anathi), katika siku za Jael, barabara kuu ziliachwa, na wale ambao walitembea tu walitumia njia za upepo.
\s5
\v 7 Kulikuwa na mashujaa wachache huko Israeli, mpaka mimi, Debora, nilipochukua amri- mama alichukua amri katika Israeli!
\v 8 Walichagua miungu mpya, kulikuwa na vita katika malango ya jiji lakini bado hapakuwa na ngao au mikuki iliyoonekana kati ya watu elfu arobaini nchini Israeli.
\s5
\v 9 Moyo wangu unawaendea wakuu wa Israeli, pamoja na watu ambao walijitolea -tunambariki Bwana kwa ajili yao!
\v 10 Fikiria juu ya hili- ninyi ambao hupanda punda weupe mmeketi kwenye mazulia, nanyi mnaotembea njiani.
\s5
\v 11 Sikiliza sauti za wale wanaoimba kwenye maeneo ya kutekea maji. Huko wanasema tena juu ya matendo ya haki ya Bwana, na matendo ya haki ya wapiganaji wake katika Israeli. Ndipo watu wa Bwana wakashuka kwenye malango ya mji.
\s5
\v 12 Amka, amka, Debora! Amka, amka, imba wimbo! Simama, Baraka, na uwakamate wafungwa wako, wewe mwana wa Abinoamu.
\v 13 Wale waliokoka wakaja chini kwa watu wenye nguvu; watu wa Bwana walikuja kwangu pamoja na mashujaa.
\s5
\v 14 Walikuja kutoka Efraimu, ambao mizizi yao iko katika Amaleki; watu wa Benyamini walikufuata. Wakuu wa Makiri walitoka, na kutoka Zebuloni wale wanaobeba fimbo ya afisa.
\s5
\v 15 Na wakuu wangu katika Isakari walikuwa pamoja na Debora; na Isakari alikuwa na Baraka waliingia bobdeni kwa kasi chini ya amri yake. Miongoni mwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
\s5
\v 16 Kwa nini uliketi katikati ya moto, ukisikiliza wachungaji wakipiga filimbi yao kwa makundi yao? Na kwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
\s5
\v 17 Gileadi alikaa upande wa pili wa Yordani; na Dani, kwa nini alizunguka juu ya meli? Asheri alibakia pwani na akaishi karibu na bandari zake.
\v 18 Zabuloni lilikuwa kabila ambayo lingeweza kuhatarisha maisha yao mpaka kufikia kifo, Nafthali, pia, katika uwanja wa vita.
\s5
\v 19 Wafalme walikuja, wakapigana; wafalme wa Kanaani wakapigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido. Lakini hawakuondoa fedha kama nyara.
\v 20 Nyota zilipigana kutoka mbinguni, kutoka katika njia zao za mbinguni zilipigana na Sisera
\s5
\v 21 Mto Kishoni uliwaondoa, mto ule wa kale, Mto Kishoni. Endelea mbele nafsi yangu, jipe nguvu!
\v 22 Kisha sauti za hofu za farasi-kupiga mbio, kupigana kwa watu wake wenye nguvu.
\s5
\v 23 'Ilaani Meroz!' asema malaika wa Bwana. 'Hakika walaani wenyeji wake!' Kwa sababu hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana katika vita dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
\s5
\v 24 Yaeli amebarikiawa zaidi kuliko wanawake wengine wote, Yaeli (mke wa Heberi Mkeni), amebarikiwa zaidi kuliko wanawake wote wanaoishi katika hema.
\v 25 Mtu yule aliomba maji, naye akampa maziwa; akamletea siagi katika sahani inayofaa kwa wakuu.
\s5
\v 26 Aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema, na mkono wake wa kuia katika nyundo ya mfanyakazi; kwa nyundo akampiga Sisera, alimpiga kichwani kwake. Aliligawanya fuvu lake vipande vipande wakati alipompiga pembeni ya kichwa chake.
\v 27 Akaanguka katikati ya miguu yake, akaanguka akalala pale. Kati ya miguu yake akaanguka. Mahali alipoanguka ni pale ambapo aliuawa kwa ukatili.
\s5
\v 28 Aliangalia dirishani - mama yake Sisera aliangalia kupitia kamba na akasema kwa huzuni, 'Kwa nini gari lakelimechelewa kuja? Kwa nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake vimechelewa? '
\s5
\v 29 Wafalme wake wenye hekima walijibu, na yeye mwenyewe akajibu jibu lile
\v 30 'Je, hawakupata na kugawanya nyara? Tumbo, matumbo mawili kwa kila mtu; nyara ya kitambaa kilichofunikwa kwa Sisera, nyara ya kitambaa kilichofunikwa, nguo mbili za rangi iliyofunikwa kwa misumari ya wale waliopora?
\s5
\v 31 Naam, adui zako wote wataangamia, Ee Bwana! Lakini marafiki zako watakuwa kama jua wakati linapoongezeka kwa uwezo wake. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Wana wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; naye akawatia mikononi mwa Midiani kwa miaka saba.
\v 2 Uwezo wa Midiani uliwanyanyasa Israeli. Kwa sababu ya Midiani, watu wa Israeli walitengeneza makao wenyewe kutoka kwenye mabwawa katika milima, mapango, na ngome.
\s5
\v 3 Kisha ikawa kwamba wakati wowote Waisraeli walipopanda mazao yao, Wamidiani na Waamaleki na watu kutoka mashariki waliwavamia Waisraeli.
\v 4 Waliweza kutengenezajeshi lao juu ya ardhi na kuharibu mazao, mpaka njia ya Gaza. Hawakuacha chakula huko Israeli, wala kondoo wala ng'ombe wala punda.
\s5
\v 5 Kila wakati wao na mifugo yao na mahema walipokuja, walikuja kama kundi la nzige, na haikuwezekana kuhesabu watu au ngamia zao. Walivamia ardhi ili kuiharibu.
\v 6 Midiani iliwadhoofisha Waisraeli sana mpaka watu wa Israeli wakamwita Bwana.
\s5
\v 7 Watu wa Israeli walipomwomba Bwana kwa sababu ya Midiani,
\v 8 Bwana alimtuma nabii kwa wana wa Israeli. Nabii akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekuleta kutoka Misri; Nilikutoa nje ya nyumba ya utumwa.
\s5
\v 9 Naliwaokoa kutoka kwenye mikono ya Wamisri, na kutoka kwenye mkono wa wote waliokuwa wakikunyanyasa. Niliwafukuza mbele yenu, na nimewapa nchi yao.
\v 10 Niliwaambia, "Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; Nimewaamuru msiabudu miungu ya Waamori, ambao mnaishi katika nchi yao. Lakini hamkuitii sauti yangu."
\s5
\v 11 Basi malaika wa Bwana akaja na kukaa chini ya mwaloni huko Ofra, uliokuwa wa Yoashi (Mwabiyezeri), wakati Gidioni, mwana wa Yoashi, akitenganisha ngano katika sakafu, katika kikapu cha divai-kuificha toka kwa Wamidiani.
\v 12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nanyi, mpiganaji mwenye nguvu!
\s5
\v 13 Gideoni akamwambia, Oo, bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, kwa nini basi yote haya yanatupata? Je, yako wapi matendo yake yote mazuri ambayo baba zetu walituambia, waliposema, 'Je! si Bwana aliyetukomboa kutoka Misri?' Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia mikononi mwa Midiani. '
\s5
\v 14 Bwana akamtazama na kusema, "Nenda katika nguvu uliyo nayo tayari. Uiokoe Israeli kutoka mkononi wa Midiani. Je, sikukutuma?"
\v 15 Gideoni akamwambia, "Tafadhali, Bwana, nawezeje kuwaokoa Israeli? Angalia, familia yangu ni dhaifu zaidi katika Manase, na mimi si muhimu katika nyumba ya baba yangu."
\s5
\v 16 Bwana akamwambia, "Nitakuwa pamoja nawe, nawe utalishinda jeshi lote la Midiani kama mtu mmoja."
\v 17 Gideoni akamwambia, "Ikiwa unapendezwa na mimi, nipe basi ishara kwamba wewe ndio unenena nami.
\v 18 Tafadhali, usiondoke hapa, mpaka nitakapokuja kwako na kuleta zawadi yangu na kuiweka mbele yako." Bwana akasema, "Nitasubiri mpaka utakaporudi."
\s5
\v 19 Gideoni akaenda, akaandaa mwana mbuzi, na efa moja ya unga akafanya mikate isiyotiwa chachu. Akaiweka nyama hiyo katika kikapu, na akaweka mchuzi ndani ya sufuria na kuviletea chini ya mti wa mwaloni, akavitowa.
\v 20 Malaika wa Mungu akamwambia, "Chukua nyama na mikate isiyotiwa chachu, ukaweke juu ya mwamba huu, ukamwage mchuzi juu yake." Gideoni akafanya hivyo.
\s5
\v 21 Kisha malaika wa Bwana akashika ncha ya fimbo mkononi mwake. Kwa hiyo akagusa nyama na mikate isiyotiwa chachu; moto ukatoka nje ya mwamba, ukateketeza nyama na mikate isiyotiwa chachu. Kisha malaika wa Bwana akaenda, na Gideoni hakuweza kumwona tena.
\s5
\v 22 Gideoni alielewa kuwa yule alikuwa malaika wa Bwana. Gideoni akasema, "Ewe Bwana MUNGU! Kwa maana nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!"
\v 23 Bwana akamwambia, "Amani iwe kwako! Usiogope, huwezi kufa."
\v 24 Basi Gideoni akamjengea Bwana madhabahu huko. Aliiita, "Bwana ni Amani." Hadi leo bado iko katika Ofra ya jamaa ya Waabiezeri.
\s5
\v 25 Usiku huo, Bwana akamwambia, "Twaa ng'ombe wa baba yako, na ng'ombe wa pili wa umri wa miaka saba, ukaondoe madhabahu ya Baali, ambayo ni ya baba yako, na kukata Ashera iliyo karibu nayo.
\v 26 Jenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wako juu ya mahali pa kukimbilia, na kuijenga njia sahihi. Toa ng'ombe ya pili kama sadaka ya kuteketezwa, ukitumia kuni kutoka Ashera uliyoikata. '
\s5
\v 27 Gideoni akachukua watumishi wake kumi na kufanya kama Bwana alivyomwambia. Lakini kwa sababu aliogopa sana watu wa nyumba ya baba yake na watu wa mji hakufanya hivyo wakati wa mchana, alifanya hivyo usiku.
\s5
\v 28 Asubuhi wakati watu wa mji walipoamka, madhabahu ya Baali imebomolewa, na Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na ng'ombe wa pili ametolewa sadaka kwenye madhabahu iliyojengwa.
\v 29 Watu wa mji wakaambiana, "Ni nani aliyefanya jambo hili?" Walipokuwa wakiongea na wengine na kutafuta majibu, wakasema, 'Gidioni mwana wa Yoashi amefanya jambo hili."
\s5
\v 30 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi, "Mtoe mtoto wako ili afe, kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali, na kwa sababu ameikata Ashera karibu nayo."
\s5
\v 31 Yoashi akawaambia wote waliompinga, "Je, ninyi mtamsihi Baali? Je, mtamuokoa? Mtu yeyote atakayemtetea, basi atauawa asubuhi hii. Ikiwa Baali ni mungu, basi atajitetea mwenyewe wakati mtu anaibomoa madhabahu yake."
\v 32 Kwa hiyo siku hiyo wakamwita Gideoni "Yerubaali," kwa sababu alisema, "Baali ajijitetee dhidi yake," kwa sababu Gidioni alivunja madhabahu ya Baali.
\s5
\v 33 Basi Wamidiani wote, Waamaleki, na watu wa mashariki walikusanyika pamoja. Wakavuka Yordani na wakapanga katika bonde la Yezreeli.
\s5
\v 34 Lakini Roho wa Bwana akaja juu ya Gideoni. Gideoni akapiga tarumbeta, akawaita jamaa ya Abiezeri, ili wapate kumfuata.
\v 35 Aliwatuma wajumbe wote katika Manase, na wao pia, waliitwa nje kumfuata. Naye akatuma wajumbe kwa Asheri, na Zabuloni, na Naftali; nao wakaenda kumlaki.
\s5
\v 36 Gideoni akamwambia Mungu, "Ikiwa ungependa kunitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema,
\v 37 tazameni, ninaweka ngozi ya samazi kwenye sakafu. Ikiwa kuna umande tu juu ya ngozi, na ni kavu duniani, basi nitajua kwamba utanitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema."
\s5
\v 38 Hivi ndivyo ilivyotokea-Gideoni aliamka mapama asubuhi, akaikamua ngozi hiyo, na akatoa umande kwenye ngozi, wa kutosha kujaza bakuli kwa maji.
\s5
\v 39 Gideoni akamwambia Mungu, 'Usinikasirikie, nitasema tena kwa mara nyingine. Tafadhali niruhusu nijaribu tena kwa kutumia ngozi. Wakati huu uifanye kavu, na iwe na umande juu ya ardhi yote kuzunguka.
\v 40 Mungu alifanya kile alichoomba usiku huo. Ngozi ilikuwa kavu, na kulikuwa na umande katika ardhi yote iliyozunguka.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Ndipo Yerubaali (yaani Gideoni) akainuka mapema, na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaweka kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Midiani ilikuwa kaskazini mwao katika bonde karibu na kilima cha More.
\s5
\v 2 Bwana akamwambia Gideoni, Kuna askari wengi sana kwa mimi kukupa ushindi juu ya Wamidiani, ili Waisraeli wasijisifu juu yangu, wakisema, 'Nguvu zetu zimetuokoa'.
\v 3 Basi, tangaza masikioni mwa watu, ukisema, Yeyote anayeogopa, anayetetemeka, arudi na atoke katika mlima Gileadi. 'Basi, watu elfu ishirini na mbili wakaondoka, na elfu kumi wakabaki.
\s5
\v 4 Bwana akamwambia Gideoni, 'Watu bado ni wengi sana. Wapeleke chini kwenye maji, na nitafanya idadi yao iwe ndogo kwa ajili yako. Kama nikisema, 'Huyu atakwenda pamoja nawe,' atakwenda pamoja nawe; lakini kama nikisema, 'Huyu hawezi kwenda pamoja nawe,' hatakwenda. '
\s5
\v 5 Gideoni akawapeleka watu kwenye maji; Bwana akamwambia, "Ondoa kila mtu atakayelamba maji, kama mbwa alambavyo, kutoka kwa wale wanaopiga magoti na kunywa."
\v 6 Wanaume mia tatu walilamba. Wengine wote walipiga magoti kunywa maji.
\s5
\v 7 Bwana akamwambia Gideoni, "Kwa watu hawa mia tatu waliokwisha kulamba maji, nitakuokoa na kukupa ushindi juu ya Wamidiani. Acha kila mtu arudi mahali pake."
\v 8 Kwa hiyo wale waliochaguliwa walichukua vifaa vyao na tarumbeta zao. Gideoni akawarudisha watu wote wa Israeli, kila mtu kwenda kwenye hema yake, lakini akawaweka watu mia tatu. Basi kambi ya Midiani ilikuwa chini yake katika bonde.
\s5
\v 9 Usiku huo huo Bwana akamwambia, "Simama! Kavamie kambi, kwa maana nitakupa ushindi juu yake.
\v 10 Lakini ikiwa unaogopa kushuka, shka kwenye kambi pamoja na Purh mtumishi wako,
\v 11 na usikilize kile wanachosema, na ujasiri wako utaimarishwa kushambulia kambi." Basi Gidioni akaenda pamoja na Pura mtumishi wake, mpaka chini kwa walinzi wa kambi.
\s5
\v 12 Wamidiani, Waamaleki, na watu wote wa mashariki walikaa karibu na bonde, wengi kama wingu la nzige. Ngamia zao walikuwa zaidi ya mawingu; walikuwa zaidi kuliko idadi ya mchanga katika bahari.
\s5
\v 13 Gideoni alipofika huko, mtu alikuwa akimwambia mwenzake ndoto. Mtu huyo akasema, "Angalia! Niliota ndoto, na nikaona mkate wa shayiri umeanguka ndani ya kambi ya Midiani. Ukaja hemani, na kuipiga kwa nguvu sana hata ikaanguka chini ikapinduka na kulala chini. '
\v 14 Mtu mwingine akasema, 'Hii si kitu kingine isipokuwa upanga wa Gideoni (mwana wa Yoashi), Mwisraeli. Mungu amempa ushindi juu ya Midiani na jeshi lake lote. '
\s5
\v 15 Gideoni aliposikia habari ya ile ndoto na tafsiri yake, akainama chini na kuabudu. Alirudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, "Simameni! Bwana ametupa ushindi juu ya jeshi la Midiani."
\v 16 Akawagawa watu mia tatu katika makundi matatu, na akawapa tarumbeta zote na mitungi tupu, na taa ndani ya kila mtungi.
\s5
\v 17 Akawaambia, 'Niangalieni mimi na kufanya yale ninayoyafanya. Tazama! Ninapofika kwenye mwisho wa kambi, ni lazima mfanye kile ninachofanya.
\v 18 Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote Mlio pamoja nami, basi mtapiga tarumbeta zenu katika kila upande wa kambi nzima na kupiga kelele, "Kwa Bwana na Gideoni!"
\s5
\v 19 Basi Gideoni na watu mia moja waliokuwa pamoja naye walifika mwisho wa kambi, hapo mwanzoni mwa saa ya kati. Wakati Wamidiani walikuwa wakibadilisha walinzi, walipiga tarumbeta na kuvunja mitungi iliyokuwa mikononi mwao.
\s5
\v 20 Vikosi vitatu vilipiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Walikuwa na taa katika mikono yao ya kushoto na tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuwapiga. Walipiga kelele, "Upanga wa Bwana na wa Gideoni."
\v 21 Kila mtu alisimama mahali pake kando ya kambi na jeshi la Midiani likakimbia. Walipiga kelele na kukimbia
\s5
\v 22 Walipopiga tarumbeta mia tatu, Bwana akaweka upanga wa kila mtu wa Midiani dhidi ya wenzake na dhidi ya jeshi lake lote. Jeshi likimbia mpaka Bethshita kuelekea Serera, mpaka mpaka wa Abel Mehola, karibu na Tabathi.
\v 23 Watu wa Israeli kutoka Naftali, Asheri, na Manase wote waliitwa nje, nao wakawafuata Midiani.
\s5
\v 24 Gideoni akatuma wajumbe katika nchi zote za mlima wa Efraimu, akisema, "Nenda chini dhidi ya Midiani na umiliki Mto Yordani mpaka Bethbara, ukawazuie." Basi wanaume wote wa Efraimu walikusanyika pamoja na kuimiliki maji, mpaka Bethbara na Mto Yordani.
\v 25 Wakawatwaa wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamwua Orebu kwenye mwamba wa Orebu, nao wakamwua Zeebu katika shinikizo la divai la Zeebu. Wakawafuata Wamidiani, wakamletea Gideoni vichwa vya Orebu na Zeebu, ng'ambo ya pili ya Yordani.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Watu wa Efraimu wakamwambia Gideoni, "Ni nini hiki umetutenda? Haukuita wakati ulipokwenda kupigana na Midiani." Wakamwambia kwa nguvu.
\s5
\v 2 Akawaambia, "Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi? Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?
\v 3 Mungu amewapa ushindi juu ya wakuu wa Midiani-Orebu na Zeeb! Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?" Hasira yao ikashuka chini aliposema hili.
\s5
\v 4 Gideoni alikuja Yordani na akavuka juu yake, yeye na watu mia tatu waliokuwa pamoja naye. Walikuwa wamechoka, lakini bado waliendelea kufuatilia.
\v 5 Akawaambia watu wa Sukothi, "Tafadhali wape mikate kwa watu wanaonifuata, kwa kuwa wamechoka, nami niwafuatilia Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani.
\s5
\v 6 Na wakuu wakasema, "Je, mikono ya Zeba na Salmuna sasa ipo mikononi mwako? Kwa nini tulipe jeshi lako mikate?"
\v 7 Gideoni akasema, "Bwana akitupa ushindi juu ya Zeba na Salmunna, nitainyunyiza ngozi yenu kwa miiba ya jangwani na michongoma.
\s5
\v 8 Akatoka huko, akaenda Penieli, akawaambia watu maneno hayo hayo; lakini watu wa Penieli wakamjibu kama watu wa Sukothi walivyojibu.
\v 9 Akawaambia pia watu wa Penieli, akasema, "Nitakapokuja kwa amani, nitauangusha mnara huu."
\s5
\v 10 Sasa Zeba na Salmuna walikuwa huko Karkori pamoja na jeshi lao, karibu na watu elfu kumi na tano, wote waliosalia nje ya jeshi lote la watu wa Mashariki, kwa kuwa walianguka watu 120, 000 waliofundishwa kupigana na upanga.
\s5
\v 11 Gideoni akapanda barabara iliyochukuliwa na wakaazi wa hema, Noba na Yogbena. Akalishinda jeshi la adui, kwa sababu hawakuwa wanatarajia shambulio.
\v 12 Zeba na Salmuna walikimbia, na Gideoni alipowafuata, akawatwaa wafalme wawili wa Midiani-Zeba na Salmunna- na kulifanya jeshi lote kuwa na hofu.
\s5
\v 13 Gideoni, mwana wa Yoashi, alirudi kutoka kwenye vita kwenda kupitia Heresi.
\v 14 Akamkimbilia kijana mmoja wa watu wa Sukothi na kutafuta ushauri kutoka kwake. Kijana huyo alimwelezea viongozi wa Sukothi na wazee wake, watu sabini na saba.
\s5
\v 15 Gideoni akaja kwa watu wa Sukothi, akasema, "Tazameni Zeba na Salmuna, ambao mlinidhihaki kwa ajili yao, nikasema, 'Je! mmemshinda Zeba na Salmuna? Hatujui kwamba tunapaswa kulipa jeshi lako mkate."
\v 16 Gideoni akawachukua wazee wa mji, naye akawaadhibu watu wa Sukothi pamoja na miiba ya jangwa na michongoma.
\v 17 Akaangusha mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji huo.
\s5
\v 18 Gideoni akamwambia Zeba na Salmuna, "Ni watu wa aina gani mliwauawa Tabori?" Wakajibu, "Kama wewe ulivyo, ndivyo walivyokuwa. Kila mmoja wao alionekana kama mwana wa mfalme."
\v 19 Gideoni akasema, 'Wao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu. Kama Bwana anaishivyo, kama mngewaacha hai, nisingewauwa."
\s5
\v 20 Akamwambia Yetheri (mzaliwa wake wa kwanza), "Simama uwaue!" Lakini kijana huyo hakutoa upanga wake kwa kuwa aliogopa, kwa sababu alikuwa bado kijana mdogo.
\v 21 Ndipo Zeba na Salmuna wakasema, simama mwenyewe, utuue! Kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Gideoni akasimama na kumwua Zeba na Salmuna. Pia aliondoa mapambo yaliyokuwa juu ya shingo za ngamia zao.
\s5
\v 22 Ndipo wana wa Israeli wakamwambia Gideoni, "Ututawale, wewe, mtoto wako, na mjukuu wako; kwa sababu umetuokoa mikononi mwa Midiani."
\v 23 Gideoni akawaambia, "Mimi sitatawala juu yenu, wala mtoto wangu hatatawala juu yenu. Bwana atatawala juu yenu."
\s5
\v 24 Gideoni akawaambia, "Nina haja yangu niitakayo kwenu kwamba kila mmoja wenu atanipe pete kutoka kwenye nyara zake." (Wamidiani walikuwa na pete za dhahabu kwa sababu walikuwa Waishmaeli.)
\v 25 Wakamjibu, "Tunafurahi kukupa." Wakatandika vazi na kila mtu akatupa pete kutoka kwenye nyara zake.
\s5
\v 26 Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilikuwa shekeli 1, 700 za dhahabu. Nyara hizi zilikuwa ni pamoja na mapambo ya makoja, vidani, nguo ya rangi ya zambarau waliyovaa na wafalme wa Midiani, na zaidi ya minyororo iliyokuwa karibu na shingo za ngamia zao.
\s5
\v 27 Gideoni akafanya efodi kutoka katika pete na kuiweka katika mji wake, huko Ofra, na Israeli wote wakaiandama kwa ukahaba na kuabudu. Ilikuwa mtego kwa Gideoni na kwa wale walio nyumbani kwake.
\v 28 Kwa hiyo Midiani ilishindwa mbele ya watu wa Israeli na hawakuinua vichwa vyao tena. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini siku za Gideoni.
\s5
\v 29 Yerubaali, mwana wa Yoashi, akaenda akakaa nyumbani kwake.
\v 30 Gideoni alikuwa na wana sabini, waliokuwa uzao wake, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.
\v 31 Mwanamke wake, aliyekuwa Shekemu, akamzaa pia mwana, na Gideoni akampa jina lake Abimeleki.
\s5
\v 32 Gideoni, mwana wa Yoashi, akafa katika uzee mzuri, akazikwa huko Ofra katika kaburi la baba yake Joashi, wa jamaa ya Abiyezeri.
\v 33 Ikawa, Gideoni alipokufa, watu wa Israeli wakageuka tena na kujifanyia ukahaba wenyewe kwa kuabudu Mabaali. Wamlifanya Baali Berith kuwa mungu wao.
\s5
\v 34 Watu wa Israeli hawakukumbuka kumtukuza Bwana, Mungu wao, aliyewaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao kila upande.
\v 35 Hawakuweka ahadi zao kwa nyumba ya Yerubaali (yaani Gidioni), kwa ajili ya mema yote aliyoyafanya katika Israeli.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda kwa jamaa za mama yake huko Shekemu, akawaambia, na jamaa yote ya mama yake,
\v 2 Tafadhali sema haya, ili wakuu wote wa Shekemu wasikie, Ni kipi bora kwako Je, wana sabini wote wa Yerubali kutawala juu yenu, au kwamba moja tu atawale juu yenu? Kumbuka kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.
\s5
\v 3 Ndugu za mama yake waliongea kwa niaba yake kwa viongozi wa Shekemu, nao wakakubali kumfuata Abimeleki, wakasema, Yeye ndiye ndugu yetu.
\v 4 Wakampa vipande sabini vya fedha katika nyumba ya Baali Berith; Abimeleki akazitumia kwa kuajiri watu wasio na sheria na wasiokuwa wajinga, waliomfuata.
\s5
\v 5 Abimeleki akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra; na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, wana wa Yerubaali. Yotamu ndiye aliyebaki, mwana mdogo kabisa wa Yerubaali, kwa kuwa alijificha.
\v 6 Wakuu wote wa Shekemu na Beth Milo wakaungana, wakaenda kumfanya Abimeleki mfalme, karibu na mwaloni karibu na nguzo iliyoko Shekemu.
\s5
\v 7 Yotamu alipoambiwa juu ya jambo hilo, akaenda, akasimama juu ya Mlima Gerizimu. Alipiga kelele akawaambia, 'Sikilizeni, enyi viongozi wa Shekemu, ili Mungu awasikilize.
\v 8 Siku moja miti ilikwenda kumtia mafuta mfalme juu yao. Wakauambia mzeituni, tawala juu yetu.
\s5
\v 9 Lakini mti wa mizeituni ukawaambia, Je! Nitaacha mafuta yangu, ambayo hutumiwa kuheshimu miungu na wanadamu, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?
\v 10 Miti hiyo ikamwambia mtini, 'Njoo utawale juu yetu.'
\v 11 Lakini mtini ukawaambia, Je, nitaacha utamu wangu na matunda yangu mazuri, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?
\s5
\v 12 Miti hiyo ikamwambia mzabibu, 'Njoo utawale juu yetu.'
\v 13 Mzabibu ukawaambia, Je, nitaacha divai yangu mpya, ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, na kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?
\v 14 Kisha miti yote ikawaambia mchanga, 'Njoo utawale juu yetu.'
\s5
\v 15 Miti ya miiba ikaiambia miti, 'Ikiwa unataka kunipaka mafuta niwe mfalme juu yako, njoo na upate usalama chini ya kivuli changu. Ikiwa sivyo, basi moto lazima uondoke kwenye mchanga na uiteketeze mierezi ya Lebanoni. '
\v 16 Basi, ikiwa umefanya kweli na uaminifu, ulimfanya Abimeleki mfalme, na ikiwa umefanya vizuri juu ya Yerubaali na nyumba yake, na ikiwa umemuadhibu kama anavyostahili,
\s5
\v 17 - na kufikiri kwamba baba yangu alipigana kwa ajili yenu, akahatarisha maisha yake, na akawaokoa kutoka kwenye mkono wa Midiani -
\v 18 lakini leo umeamka juu ya nyumba ya baba yangu na kuwaua watoto wake, watu sabini, juu ya jiwe moja. Na umemfanya Abimeleki, mwana wa mtumishi wake, awe mfalme juu ya wakuu wa Shekemu, kwa sababu yeye ni ndugu yenu.
\s5
\v 19 Ikiwa mlifanya kwa uaminifu na uelekevu pamoja na Jerubalai na nyumba yake, basi mnapaswa kufurahi katika Abimeleki, naye apate kufurahi ndani yenu.
\v 20 Lakini ikiwa sio, moto utoke kwa Abimeleki, ukawaangamize watu wa Shekemu na Beth Milo. Basi moto utoke kwa watu wa Shekemu na Beth Milo, ili kumteketeza Abimeleki.
\v 21 Yothamu akakimbia, naye akaenda Beeri. Aliishi huko kwa sababu ilikuwa mbali na Abimeleki, kaka yake.
\s5
\v 22 Abimeleki akatawala juu ya Israeli kwa miaka mitatu.
\v 23 Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu. Viongozi wa Shekemu walisaliti uaminifu waliokuwa nao kwa Abimeleki.
\v 24 Mungu alifanya hivyo ili uhalifu uliofanywa kwa wana sabini wa Yerubaali uweze kulipizwa kisasi, na Abimeleki ndugu yao atawajibishwa kwa kuwaua, na watu wa Shekemu watawajibishwa kwa sababu walimsaidia kuua ndugu zake.
\s5
\v 25 Basi wakuu wa Shekemu wakawaweka wanaume wamkisubiri juu ya vilima ili wamwangamize, nao wakawaibia wote waliokuwa wamepita katika barabara hiyo. Hii iliripotiwa kwa Abimeleki.
\s5
\v 26 Gaali mwana wa Ebedi akenda pamoja na ndugu zake, wakavuka Shekemu. Viongozi wa Shekemu walimwamini.
\v 27 Wakaenda shambani wakakusanya zabibu kutoka kwa mizabibu, nao wakazikanyaga. Walifanya sherehe katika nyumba ya mungu wao, walikula na kunywa, kumlaani Abimeleki.
\s5
\v 28 Gaali mwana wa Ebedi, akasema, Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake? Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu! Kwa nini tunapaswa kumtumikia?
\v 29 Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu! Kisha ningemuondoa Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, 'liondoe nje jeshi lako lote.'
\s5
\v 30 Zebul, mkuu wa mji, aliposikia maneno ya Gaali, mwana wa Ebedi, hasira yake ikawaka.
\v 31 Akatuma wajumbe kwa Abimeleki ili wapate kudanganya, akisema, Tazama, Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wanafika Shekemu; nao wanauchochea mji dhidi yako.
\s5
\v 32 Sasa, amka wakati wa usiku, wewe na askari pamoja nawe, na uandae uvamizi katika mashamba.
\v 33 Kisha asubuhi, jua litakapokwisha, inuka mapema na uangamize mji. Na yeye na watu waliokuwa pamoja naye watakapokuja juu yenu, fanyeni chochote mnachoweza.
\s5
\v 34 Basi Abimeleki akainuka usiku, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaandaa uvamizi dhidi ya Shekemu, wakagawanyika vitengo vinne.
\v 35 Gaali mwana wa Ebedi akatoka, akasimama penye mlango wa mji. Abimeleki na watu waliokuwa pamoja naye wakatoka mahali pa kuficha.
\s5
\v 36 Gaali alipowaona hao watu, akamwambia Zebuli, "Tazama, watu wanatoka kwenye vilima!" Zebuli akamwambia, "Wewe unaona vivuli juu ya vilima kama vile watu".
\v 37 Gaali akaongea tena na kusema, "Angalia, watu wanashuka katikati ya nchi, na kitengo kimoja kinakuja kwa njia ya mwaloni wa Maenenimu."
\s5
\v 38 Ndipo Zebuli akamwambia, "Je, maneno yako ya kiburi yako wapi sasa, wewe uliyesema, 'Abimeleki ni nani, ili tumtumikie?' Je, hao sio watu ambao uliwadharau? Toka sasa na pigana nao."
\v 39 Gaali akatoka na alikuwa akiwaongoza watu wa Shekemu, naye alipigana na Abimeleki.
\v 40 Abimeleki akamfukuza, na Gaali akakimbia mbele yake. Na wengi wakaanguka na majeraha ya mauti mbele ya mingilio ya lango la mji.
\s5
\v 41 Abimeleki alikaa Aruma. Zebul akawalazimisha Gaal na ndugu zake watoke Shekemu.
\v 42 Siku ya pili watu wa Shekemu wakatoka shambani, na habari hii ikamfikia Abimeleki.
\v 43 Aliwachukua watu wake, akawagawanywa katika vitengo vitatu, na wakaandaa uvamizi mashambani. Aliangalia na kuona watu wakitoka mjini. Akawakamata na kuwaua.
\s5
\v 44 Abimeleki na vitengo vilivyokuwa pamoja naye vilishambulia na kuzuia maingilio ya lango la mji. Vitengo vingine viwili vilishambulia wote waliokuwa katika shamba na wakawaua.
\v 45 Abimeleki alipigana na huo mji siku nzima. Aliteka mji huo, na kuwaua watu waliokuwa ndani yake. Akabomoa kuta za mji na kueneza chumvi juu yake.
\s5
\v 46 Wakati wakuu wote wa mnara wa Shekemu waliposikia hayo, waliingia katika ngome ya nyumba ya El Berithi.
\v 47 Abimeleki aliambiwa kuwa viongozi wote walikuwa wamekusanyika pamoja kwenye mnara wa Shekemu.
\s5
\v 48 Abimeleki akaenda mpaka mlima wa Salmoni, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. Abimeleki akachukua shoka na kukata matawi. Akaweka juu ya bega lake na kuwaagiza watu waliokuwa pamoja naye, 'Mlichoona nimekifanya fanyeni kama nilivyofanya.'
\v 49 Basi kila mmoja akakata matawi, wakamfuata Abimeleki. Wakayafungia juu ya ukuta wa mnara, nao wakawasha moto, hata watu wote wa mnara wa Shekemu wakafa, wanaume na wanawake elfu.
\s5
\v 50 Abimeleki akaenda Tebezi, naye akapiga kambi dhidi ya Thebezi, akautwaa.
\v 51 Lakini kulikuwa na mnara wenye nguvu katika mji, wanaume na wanawake wote na viongozi wote wa mji walikimbilia na kujifungia wenyewe. Kisha wakaenda juu ya paa la mnara.
\s5
\v 52 Abimeleki alikwenda kwenye mnara na kupigana nao, naye akaenda karibu na mlango wa mnara ili kuuchoma.
\v 53 Lakini mwanamke akatupa jiwe la juu, juu ya kichwa cha Abimeleki likavunja fuvu lake.
\v 54 Kisha akamwita yule kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, akamwambia, "Chukua upanga wako ukaniue, kwa hiyo hakuna mtu atakayesema juu yangu, 'Mwanamke alimwua.'" Basi kijana wake akamchoma naye akafa.
\s5
\v 55 Watu wa Israeli walipoona kwamba Abimeleki amekufa, wakaenda nyumbani.
\v 56 Basi Mungu akalipiza kisasi cha uovu wa Abimeleki alichomfanyia baba yake kwa kuua ndugu zake sabini.
\v 57 Mungu akafanya uovu wote wa watu wa Shekemu ugeuke juu ya vichwa vyao wenyewe, na juu yao ilikuja laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Baada ya Abimeleki, Tola, mwana wa Pua, mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyekaa Shamiri, katika mlima wa Efraimu, akaondoka ili kuwaokoa Israeli.
\v 2 Akawa mwamuzi wa Israeli miaka ishirini na mitatu. Alikufa na kuzikwa Shamiri.
\s5
\v 3 Alifuatiwa na Yairi Mgileadi. Akawa mwamuzi wa Israeli miaka ishirini na miwili.
\v 4 Alikuwa na wana thelathini waliokuwa wakipanda kwenye punda thelathini, na walikuwa na miji thelathini, ambayo inaitwa Hawoth Yairi hata leo, iliyo katika nchi ya Gileadi.
\v 5 Yairi alikufa na kuzikwa Kamoni.
\s5
\v 6 Watu wa Israeli waliendelea kutenda maovu mbele za Bwana, wakaabudu Mabaali, Maashtoreti, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti. Wakamsahau Bwana na hawakamsujudia tena.
\v 7 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawauza mikononi mwa Wafilisti na katika mikono ya wana wa Amoni.
\s5
\v 8 Wakawaangamiza na kuwadhulumu watu wa Israeli mwaka huo, na kwa muda wa miaka kumi na nane waliwafukuza watu wote wa Israeli waliokuwa ng'ambo ya Yordani katika nchi ya Waamori, iliyoko Gileadi.
\v 9 Nao wana wa Amoni wakavuka Yordani, wakapigana na Yuda, na Benyamini, na nyumba ya Efraimu; Israeli akasumbuliwa sana.
\s5
\v 10 Ndipo wana wa Israeli wakamwita Bwana, wakisema, "Tumekukosea, kwa sababu tumemwacha Mungu wetu, tukaabudu Mabaali."
\v 11 Bwana akawaambia wana wa Israeli, "Je, sikuwatoa ninyi kutoka kwa Wamisri, na Waamori, na Waamoni, na Wafilisti,
\v 12 na pia kwa Wasidoni? Waamaleki na Wamaoni walipowakandamiza; mliniita, nami nikawaokoa kutoka katika nguvu zao.
\s5
\v 13 Lakini ninyi mliniacha tena na kuabudu miungu mingine. Kwa hiyo, sitawaokoa tena.
\v 14 Nendeni mkaiite miungu mnayoiabudu. Ili iwaokoe wakati wa shida.
\s5
\v 15 Wana wa Israeli wakamwambia Bwana, Tumefanya dhambi. Tufanyie chochote kinachoonekana kuwa kizuri kwako. Tafadhali, tuokoe leo.
\v 16 Wakaiacha miungu ya kigeni waliyokuwa nayo, nao wakamwabudu Bwana. Naye akawa na subira juu ya taabu ya Israeli.
\s5
\v 17 Ndipo Waamoni wakakusanyika, wakaweka kambi Gileadi. Waisraeli walikutana na kuweka kambi yao huko Mispa.
\v 18 Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana, 'Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Yeye atakuwa kiongozi juu ya wote wanaoishi Gileadi.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Yeftha Mgileadi alikuwa shujaa mwenye nguvu, lakini alikuwa mwana wa kahaba. Gileadi alikuwa baba yake.
\v 2 Mke wa Gileadi pia alizaa wanawe wengine. Wana wa mkewe walipokua, walimlazimisha Yeftha aondoke nyumbani na kumwambia, "Huwezi kurithi chochote kutoka katika familia yetu. Wewe ni mwana wa mwanamke mwingine."
\v 3 Basi Yeftha akaondoka toka kwa ndugu zake, akaishi katika nchi ya Tobu. Watu wasiokuwa na sheria waliungana na Yeftha na wakaja na kwenda pamoja naye.
\s5
\v 4 Siku kadhaa baadaye, wana wa Amoni walipigana na Israeli.
\v 5 Wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumleta Yeftha kutoka nchi ya Tobu.
\v 6 Wakamwambia Yeftha, "Njoo uwe kiongozi wetu ili tupigane na wana wa Amoni."
\s5
\v 7 YEphtha akawaambia viongozi wa Gileadi, "mlinichukia na kunilazimisha kuondoka nyumbani kwa baba yangu. Kwa nini mnakuja kwangu sasa munapokuwa na shida?"
\v 8 Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, "Ndiyo sababu tunakugeukia sasa; njoo pamoja nasi pigana na watu wa Amoni, na wewe utakuwa kiongozi juu ya wote wanaoishi Gileadi.
\s5
\v 9 Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, "Ikiwa mnanirejesha nyumbani tena ili kupigana na wana wa Amoni, na kama Bwana atatupa ushindi juu yao, nitakuwa kiongozi wenu."
\v 10 wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, "Bwana awe shahidi kati yetu ikiwa hatutafanya kama tunavyosema!"
\v 11 Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, nao watu wakamfanya awe msimamizi na mkuu juu yao. Alipokuwa mbele ya Bwana huko Mizpa, Yeftha akarudia ahadi zote alizozifanya.
\s5
\v 12 Ndipo Yeftha akatuma wajumbe kwa mfalme wa wana wa Amoni, akisema, "Ni nini mgogoro huu kati yetu? Kwa nini umekuja kwa nguvu kuchukua ardhi yetu?"
\v 13 Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu wajumbe wa Yeftha, "Kwa sababu Israeli walipopanda kutoka Misri, walichukua nchi yangu toka Arnoni hata Yaboki, mpaka Yordani. Sasa rudisha ardhi hizo kwa amani."
\s5
\v 14 Yefta akatuma tena wajumbe kwa mfalme wa wana wa Amoni,
\v 15 akasema, "Yefita asema hivi, Israeli hawakuchukua nchi ya Moabu na nchi ya wana wa Amoni;
\v 16 lakini walitoka Misri, na Israeli wakaenda kupitia jangwa hadi Bahari ya Shamu na Kadeshi.
\s5
\v 17 Israeli walipomtuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, 'Tafadhali tunaomba ruhusa tupite katika nchi yako,' mfalme wa Edomu hakuwasikiliza. Wakawatuma wajumbe kwa mfalme wa Moabu, lakini akakataa. Basi Israeli wakakaa Kadeshi.
\v 18 Kisha wakapitia jangwani, wakaondoka katika nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu; wakavuka upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga ng'ambo ya Arnoni. Lakini hawakuingia mpaka wa Moabu, maana Arnoni ilikuwa mpaka wa Moabu.
\s5
\v 19 Israeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni; Israeli akamwambia, 'Tafadhali, tunaomba tupite katika nchi yako hata mahali petu.'
\v 20 Lakini Sihoni hakumwamini Israeli apite katika eneo lake. Basi Sihoni akakusanya jeshi lake lote, akalipeleka Yahasa, na huko akapigana na Israeli
\s5
\v 21 Bwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mkononi mwa Israeli, nao wakawashinda. Basi Israeli wakachukua nchi yote ya Waamori waliokaa katika nchi hiyo.
\v 22 Wachukua kila kitu ndani ya wilaya ya Waamori, kutoka Arnoni hadi Yaboki, na kutoka jangwani hadi Yordani.
\s5
\v 23 Basi, Bwana, Mungu wa Israeli, amewafukuza Waamori mbele ya watu wake Israeli, na sasa mnataka kuimiliki nchi yao?
\v 24 Je, huwezi kuchukua nchi ambayo Kemoshi, mungu wako, anakupa? Kwa hiyo nchi yoyote Bwana, Mungu wetu, ametupa, tutachukua.
\v 25 Sasa wewe ni bora zaidi kuliko Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu? Je, alidai kuwa na hoja na Israeli? Je, yeye amewahi kupigana vita dhidi yao?
\s5
\v 26 Wakati Israeli walipoishia miaka mia tatu huko Heshboni na vijiji vyake, na Aroeri na vijiji vyake, na katika miji yote iliyo karibu na Arnoni, kwa nini hamkuwachukua tena wakati huo?
\v 27 Sijawafanyia vibaya, lakini mnanifanyia vibaya kwa kunishambulia. Bwana, mwamuzi, ataamua leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni.
\v 28 Lakini mfalme wa wana wa Amoni akakataa onyo alilotumiwa na Yeftha.
\s5
\v 29 Basi, Roho wa Bwana akamjia Yeftha, akapita Gileadi na Manase, akapitia Mizpa ya Gileadi, na kutoka Mispa ya Gileadi akapita kwa wana wa Amoni.
\v 30 Yeftha akaahidi kwa Bwana, akasema, "Ikiwa utanipa ushindi juu ya wana wa Amoni,
\v 31 chochote kinachotoka mlangoni mwa nyumba yangu kunijia mimi nitakaporudi kwa amani kutoka kwa wana wa Amoni kitakuwa cha Bwana; Nami nitatoa hiyo sadaka ya kuteketezwa."
\s5
\v 32 Basi Yeftha akapita kwa wana wa Amoni ili kupigana nao, naye Bwana akampa ushindi.
\v 33 Akawashinda na kusababisha mauaji makubwa kutoka Aroeri hadi miji ishirini na miwili-na Abeli Keramimu. Basi wana wa Amoni waliwekwa chini ya uangalizi wa watu wa Israeli.
\s5
\v 34 Yeftha alifika nyumbani kwake huko Mizpa, na binti yake akatoka kumlaki na ngoma na kucheza. Alikuwa mtoto wake pekee, na badala yake hakuwa na mwana wa kiume wala binti.
\v 35 Mara tu alipopomwona, alirarua nguo zake akasema, 'Loo! Binti yangu! Umenivunja kwa huzuni, na umekuwa mtu anayenisababishia maumivu yangu! Kwa maana nimeapa kwa Bwana, wala siwezi kurudisha ahadi yangu.
\s5
\v 36 Akamwambia, "Baba yangu, umeweka ahadi kwa Bwana, unifanyie kila kitu ulichoahidi; kwa kuwa Bwana amekulipia kisasi juu ya adui zako, wana wa Amoni."
\v 37 Akamwambia baba yake, "Hebu ahadi hii ihifadhiwe kwa ajili yangu. Niache kwa miezi miwili, nipate kuondoka na kwenda kwenye vilima na kuomboleza juu ya ubikira wangu, mimi na wenzangu."
\s5
\v 38 Akasema, "Nenda." Alimtuma kwa muda wa miezi miwili. Akamwondoa, yeye na wenzake, nao wakauomboleza ubikira wake katika milimani.
\v 39 Mwishoni mwa miezi miwili alirudi kwa baba yake, ambaye alifanya kulingana na ahadi ya aliyoifanya. Sasa alikuwa hajalala na mwanaume, na ikawa desturi katika Israeli
\v 40 kwamba binti za Israeli kila mwaka, kwa siku nne, waweze kurejea hadithi ya binti ya Yeftha Mgileadi.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Watu wa Efraimu walitoka pamoja; nao wakapitia Zafoni, wakamwambia Yeftha, Kwa nini umetangulia kupigana na wana wa Amoni, wala hukutuita twende pamoja nawe? Tutachoma nyumba yako.
\v 2 Yeftha akawaambia, Mimi na watu wangu tulikuwa katika vita kubwa na wana wa Amoni. Nilipokuita, hukuniokoa kutoka kwao.
\s5
\v 3 Nilipoona ya kuwa hamkuniokoa, nikaweka uhai wangu na nguvu yangu mwenyewe, na kupita kipita ili kupigana na wana wa Amoni, na Bwana alinipa ushindi. Kwa nini mmekuja kupigana nami leo?"
\v 4 Yeftha akawakusanya watu wote wa Gileadi na akapigana na Efraimu. Watu wa Gileadi waliwaangamiza wana wa Efraimu kwa sababu walisema, "Ninyi Wagileadi ni wakimbizi katika Efraimu-katika Efraimu na Manase."
\s5
\v 5 Wagileadi waliteketeza ngome za Yordani zinaelekea Efraimu. Ikiwa yeyote kati ya waliopona wa Efraimu akisema, Nipe ruhusa niende juu ya mto; watu wa Gileadi wakamwambia, "Je, wewe ni Mwefraimu?" Ikiwa akasema, "Hapana,"
\v 6 basi watamwambia, Sema Shiboleth. Na kama akisema 'Sibboleth' (kwa maana hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi), Wagileadi watamkamata na kumwua kwenye mabwawa ya Yordani. Waefraimu elfu arobaini waliuawa wakati huo.
\s5
\v 7 Yeftha alikuwa mwamuzi juu ya Israeli kwa miaka sita. Ndipo Yeftha Mgileadi akafa, akazikwa katika moja ya miji ya Gileadi.
\s5
\v 8 Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi juu ya Israeli.
\v 9 Alikuwa na wana thelathini. Aliwapeleka binti thelathini katika ndoa, naye akaleta binti thelathini kutoka nje kwa ajili ya wanawe,. Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka saba.
\s5
\v 10 Ibzani alikufa na kuzikwa huko Bethlehemu.
\v 11 Baada yake, Eloni wa Zabuloni akawa mwamuzi juu ya Israeli. Akawaamua Israeli kwa miaka kumi.
\v 12 Eloni wa Zabuloni akafa, akazikwa huko Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni.
\s5
\v 13 Baada ya huyo, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi juu ya Israeli.
\v 14 Alikuwa na wana arobaini na wajukuu thelathini. Walikuwa wakipanda punda sabini, naye akawaamua Israeli kwa miaka nane.
\v 15 Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, akazikwa huko Pirathoni katika nchi ya Efraimu, katika kilima cha Waamaleki.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Watu wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti kwa miaka arobaini.
\v 2 Kulikuwa na mtu kutoka Sora, wa jamaa ya Wadani, jina lake Manoa. Mke wake hakuweza kupata mimba na hivyo hakuzaa.
\s5
\v 3 Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke akamwambia, Tazame sasa, umeshindwa kupata mimba, wala hujazaa, lakini utakuwa na mimba na utazaa mtoto.
\v 4 Sasa kuwa makini usinywe divai au kileo, wala usile kitu chochote kilicho najisi.
\v 5 Angalia, utakuwa na mjamzito na kuzaliwa mtoto mwanaume. Hakuna wembe itakayotumiwa juu ya kichwa chake, kwa kuwa mtoto atakuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni, naye ataanza kuwaokoa Israeli kutoka mkono wa Wafilisti.
\s5
\v 6 Kisha mwanamke akaenda kumwambia mumewe, "Mtu wa Mungu alikuja kwangu, na kuonekana kwake kulikuwa kama malaika wa Mungu, wa kutisha sana. Sikumwuliza ametokea wapi, na hakuniambia jina lake.
\v 7 Akaniambia, 'Tazama! Utakuwa mjamzito, na utazaa mtoto. Basi usinywe divai au kileo, wala usile chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi, kwa kuwa mtoto huyo atakuwa Mnaziri kwa Mungu tangu akipokuwa tumboni mwako mpaka siku ya kufa kwake."
\s5
\v 8 Ndipo Manoa akamwomba Bwana, akasema, Ee Bwana, tafadhali mruhusu mtu wa Mungu uliyemtuma arudi kwetu ili atufundishe kile tutakachotendea kwa mtoto atakayezaliwa hivi karibuni.
\v 9 Mungu akajibu sala ya Manoa, na malaika wa Mungu akamwendea mwanamke tena akiwa ameketi shambani. Lakini Manoa mumewe hakuwa pamoja naye.
\s5
\v 10 Basi mwanamke akakimbia haraka akamwambia mumewe, "Tazama! Yule mtu ameonekana kwangu-aliyekuja kwangu siku ile!"
\v 11 Manoa akasimama na kumfuata mkewe. Alipofika kwa mtu huyo, akasema, "Je, wewe ndiwe mtu aliyezungumza na mke wangu?'" Mtu huyo akasema, "Ni mimi."
\s5
\v 12 Manoa akasema, Sasa maneno yako yatimike. Je! kuna maagizo gani kwa ajili ya mtoto, na kazi yake itakuwa nini? '
\v 13 Malaika wa Bwana akamwambia Manoa, 'Lazima mkeo afanye kila kitu nilichomwambia.
\v 14 Asile kitu chochote kinachotokana na mizabibu, wala usimruhusu kunywa divai au kileo; usimruhusu ale chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi. Anapaswa kutii kila kitu nilichoamuru afanye.
\s5
\v 15 Manoa akamwambia malaika wa Bwana, Tafadhali keti kwa muda, utupe wakati wa kuandaa mbuzi kwa ajili yako.
\v 16 Malaika wa Bwana akamwambia Manowa, Hata kama nitakaa, sitakula chakula chako. Lakini ukitayarisha sadaka ya kuteketezwa, toa kwa Bwana. ' (Manowa hakujua kwamba alikuwa malaika wa Bwana.)
\s5
\v 17 Manoa akamwambia malaika wa Bwana, Jina lako ni nani, ili tukuheshimu wakati maneno yako yatakapotimia?
\v 18 Malaika wa Bwana akamwambia, Mbona unauliza jina langu? Ni ajabu! '
\s5
\v 19 Manoa akamchukua huyo mbuzi pamoja na sadaka ya nafaka, akatoa sadaka juu ya mwamba kwa Bwana. Alifanya jambo la ajabu wakati Manoah na mke wake walikuwa wakiangalia.
\v 20 Wakati huo moto ukatoka juu ya madhabahu kwenda mbinguni, malaika wa Bwana akapanda katika moto wa madhabahu. Manoah na mkewe waliona jambo hilo wakainamisha vichwa vyao chini.
\s5
\v 21 malaika wa Bwana hakuonekana tena kwa Manoa au mkewe. Manoa akajua kwamba yule ndiye malaika wa Bwana.
\v 22 Manoa akamwambia mkewe, 'Hakika tutakufa, kwa sababu tumemwona Mungu!'
\s5
\v 23 Lakini mkewe akamwambia, Ikiwa Bwana alitaka kutuua, asingepokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka tuliyompa. Asingetuonesha mambo haya yote, wala wakati huu asingeweza kuturuhusu tusikie mambo hayo.
\s5
\v 24 Baadaye mwanamke akamzaa mtoto, akamwita jina lake Samsoni. Mtoto alikua na Bwana akambariki.
\v 25 Roho wa Bwana akaanza kumchochea Mahane Dani, kati ya Sora na Eshtaoli.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Samsoni akashuka kwenda Timna, na huko akaona mwanamke, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Aliporudi, akamwambia baba yake na mama yake,
\v 2 'Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti. Sasa mkanichukulie awe mke wangu.
\s5
\v 3 Baba yake na mama yake wakamwambia, "Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote? Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?" Samsoni akamwambia baba yake, "Nichukulie kwa ajili yangu, kwa maana wakati nilipomwangalia, alinipendeza.'
\v 4 Lakini baba yake na mama yake hawakujua kwamba suala hili lilikuja kutoka kwa Bwana, kwa maana alitaka kutengeneza mgogoro na Wafilisti (kwa wakati huo Wafilisti walikuwa wakitawala Israeli).
\s5
\v 5 Basi Samsoni akaenda Timna pamoja na baba yake na mama yake; nao wakafika kwenye mashamba ya mizabibu ya Timna. Na, tazama, kuna simba mdogo wa alikuja na alikuwa akiunguruma.
\v 6 Roho wa Bwana ghafla akaja juu yake, naye akamrarua simba kwa urahisi kama ambavyo angeweza kumrarua mbuzi mdogo, naye hakuwa na kitu mkononi mwake. Lakini hakuwaambia baba au mama yake kile alichofanya.
\s5
\v 7 Alikwenda na kuzungumza na mwanamke, na alipopomtazama, alimpendeza Samsoni.
\v 8 Siku chache baadaye aliporudi kumwoa, akageuka na kutafuta mzoga wa simba. Na, tazama, kulikuwa na kundi la nyuki na asali katika kile kilichobaki katika mwili wa simba.
\v 9 Akaweka asali mikononi mwake na akaenda, akala huku akienda. Alipokuja kwa baba yake na mama yake, akawapa, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa amechukua asali nje ya kile kilichobaki kwenye mwili wa simba.
\s5
\v 10 Baba yake Samsoni akaenda chini alipokuwa mwanamke, na Samsoni akafanya sikukuu huko, kwa maana hii ilikuwa desturi ya vijana.
\v 11 Mara tu ndugu zake walipomwona, walimletea rafiki zao thelathini kuwa pamoja naye.
\s5
\v 12 Samsoni akawaambia, Hebu nawaambieni kitendawili. Ikiwa mmoja wenu anaweza kuipata na kuniambia jibu wakati wa siku saba za sikukuu, nitatoa nguo za kitani thelathini na seti ya nguo thelathini.
\v 13 Lakini ikiwa hamuwezi kuniambia jibu, basi utanipa nguo za kitani thelathini na seti za nguo thelathini. ' Wakamwambia, Utuambie kitendawili chako, ili tukisikie.
\s5
\v 14 Akawaambia, 'Kati ya mtu aliyekula alikuwa kitu cha kula; nje ya nguvu ilikuwa kitu tamu. Lakini wageni wake hawakuweza kupata jibu katika siku tatu.
\s5
\v 15 Siku ya nne wakamwambia mkewe Samsoni, 'Mdanganye mume wako ili atuambie jibu la kitendawili, au tutakuchoma moto wewe na nyumba ya baba yako. Je, umetualika hapa ili kutufanya maskini? '
\s5
\v 16 Mke wa Samsoni alianza kulia mbele yake; Akasema, 'Yote unayoyafanya ni kunichukia! Hunipendi. Umesema kitendawili kwa baadhi ya watu wangu, lakini hujawaambia jibu. ' Samsoni akamwambia, 'Angalia hapa, kama sijawaambia baba yangu au mama yangu, nikuambie wewe?'
\v 17 Alilia kwa siku saba ambazosikukuu yao iliendelea. Siku ya saba alimwambia jibu kwa sababu alimlazimisha sana. Akawaambia jibu jamaa zake.
\s5
\v 18 Na watu wa mji wakamwambia, siku ya saba kabla ya jua kuzama, 'Ni nini kilicho bora zaidi kuliko asali? Ni kitu gani chenye nguvu kuliko simba? ' Samsoni akawaambia, 'Ikiwa hamkulima na ng'ombe wangu, hamtapata jibu la kitendawili changu.'
\s5
\v 19 Kisha Roho wa Bwana akaja kwa Samsoni kwa nguvu. Samsoni akashuka kwenda Ashkeloni na kuuawa watu thelathini kati ya watu hao. Akachukua mateka yao, na akawapa seti ya nguo kwa wale waliomjibu kitendawili chake. Alikasirika akaenda nyumbani kwa baba yake.
\v 20 Na mke wake akachukuliwa na rafiki yake wa karibu.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Baada ya siku kadhaa, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mbuzi mdogo akaenda kumtembelea mkewe. Akajiambia mwenyewe, "Nitaenda kwenye chumba cha mke wangu." Lakini baba yake hakumruhusu aingie.
\v 2 Baba yake akasema, "Nilidhani umemchukia, hivyo nikampatia rafiki yako. Dada yake mdogo ni mzuri kuliko yeye, Mchukue badala yake."
\s5
\v 3 Samsoni akawaambia, 'Wakati huu sitakuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati nikiwaumiza.'
\v 4 Samsoni akaenda na kukamata mbweha mia tatu akawafunga pamoja kila jozi, mkia hadi mkia. Kisha akachukua taa na kuzifunga katikati ya kila mkia.
\s5
\v 5 Alipokwisha kuviwasha moto vienge, akawaachia mbweha katika nafaka za Wafilisti zilizosimama, nao wakawasha moto nafaka zote zilizopandwa, na nafaka iliyosimama shambani, pamoja na mashamba ya mizabibu na mizeituni.
\v 6 Wafilisti waliuliza, "Ni nani aliyefanya hili?" Wakaambiwa, "Samsoni, mkwe wa Mtimna alifanya hivyo kwa sababu Mtimna alimchukua mke wa Samsoni akampa rafiki yake." Basi Wafilisti wakamwendea wakamchoma kwa moto yeye na baba yake.
\s5
\v 7 Samsoni akawaambia, "Ikiwa ndivyo mnavyofanya, nitalipiza kisasi juu yenu, na baada ya hayo, nitaacha."
\v 8 Kisha akawakata vipande vipande, paja na mguu, kwa kuwauwa sana. Kisha akashuka chini akaishi katika pango katika mwamba wa Etamu.
\s5
\v 9 Ndipo Wafilisti wakaja, wakajitahidi kupigana vita huko Yuda, wakaanzisha jeshi lao huko Lehi.
\v 10 Watu wa Yuda wakasema, "Kwa nini mmekuja kutupiga?" Wakasema, "Tunashambulia ili tuweze kumkamata Samsoni, na tumtendee kama alivyotutendea."
\s5
\v 11 Kisha watu elfu tatu wa Yuda wakashuka hata kwenye pango la Eatamu, wakamwambia Samsoni, "Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! umetutendea nini?" Samsoni akawaambia, "Kwa kadili walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao."
\s5
\v 12 Wakamwambia Samsoni, "Tumeshuka kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti." Samsoni akawaambia, "Niapieni kwamba hamtaniua ninyi wenyewe."
\v 13 Wakamwambia, "La, tutakufunga tu kwa kamba na kukupeleka kwao. Tunakuahidi sisi hatutakuua." Kisha wakamfunga na kamba mbili mpya na kumleta kutoka kwenye mwamba.
\s5
\v 14 Alipofika Lehi, Wafilisti walipiga kelele walipokutana naye. Kisha Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitambaa cha kuteketezwa, na zikaanguka mikononi mwake.
\s5
\v 15 Samsoni alipata mfupa mbichi wa taya ya punda, naye akaichukua na kuua watu elfu kwa mfupa huo.
\v 16 Samsoni akasema, "Kwa taya ya punda, chungu juu ya chungu, na njaa ya punda nimewaua watu elfu."
\s5
\v 17 Samsoni alipomaliza kuzungumza, akatupa taya, na akaita mahali pale Ramath Lehi.
\v 18 Samsoni alikuwa na kiu sana akamwita Bwana na kusema, "Umempa mtumishi wako ushindi mkubwa. Lakini sasa nitakufa kwa kiu na kuanguka mikononi mwa wale wasiootahiriwa?"
\s5
\v 19 Na Mungu akapafungua mahali pa shimo palipo katika Lehi, na maji yakatoka. Alipokunywa, nguvu zake zikarejea na akahuishwa. Kwa hiyo aliita jina la mahali hapo Enhakore, na ni huko Lehi hadi leo.
\v 20 Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli katika siku za Wafilisti kwa miaka ishirini.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Samsoni alikwenda Gaza na akamwona kahaba huko, naye akalala pamoja naye.
\v 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, "Samsoni amekuja hapa." Watu wa Gaza wakazunguka mahali hapo kwa siri, wakamngoja usiku wote katika lango la jiji. Walikaa kimya usiku wote. Wakisema, "Hebu tusubiri mpaka mchana, na kisha tumwuue."
\s5
\v 3 Samsoni akalala kitandani mpaka usiku wa manane. Usiku wa manane akaamka na akashika mlango wa jiji na miimo yake miwili. Akavivuta kutoka nje, komeo na vyote, akaviweka kwenye mabega yake, akavichukua hadi juu ya kilima, mbele ya Hebroni.
\s5
\v 4 Baada ya hayo, Samsoni alimpenda mwanamke aliyeishi katika bonde la Soreki. Jina lake alikuwa Delila.
\v 5 Wale wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, "mdanganye Samsoni ili uone mahali zilipo nguvu zake kuu, na kwa namna gani tunaweza kumshinda, ili tumfunge na kumtesa. Fanya hili, na kila mmoja wetu atakupa vipande 1, 100 vya fedha."
\s5
\v 6 Ndipo Delila akamwambia Samsoni, "Tafadhali, niambie ni kwa jinsi gani wewe ni mwenye nguvu sana, na kwa namna gani mtu anaweza kukufunga, ili aweze kukudhibiti?"
\v 7 Samsoni akamwambia, "Ikiwa watanifunga na kamba saba safi ambazo hazijakauka, nitakuwa dhaifu na kuwa kama mtu mwingine yeyote."
\s5
\v 8 Basi wakuu wa Wafilisti wakamletea Delila kamba saba ambazo hazijakauka, naye akamfunga Samsoni.
\v 9 Sasa alikuwa na watu waliojificha kwa siri, walikaa katika chumba chake cha ndani. Akamwambia, "Wafilisti wako juu yako, Samsoni!" Lakini akazikata kamba kama uzi wakati unapogusa moto. Na hawakujifunza siri ya nguvu zake.
\s5
\v 10 Ndipo Delila akamwambia Samsoni, "Ndivyo ulivyonidanganya mimi na kuniambia uongo. Tafadhali, niambie kwa namna gani unaweza kufungwa."
\v 11 Akamwambia, "Ikiwa watanifunga na kamba mpya ambayo haijawahi kutumika kwa kazi, nitakuwa dhaifu na kama mtu mwingine yeyote."
\v 12 Basi Delila alichukua kamba mpya akamfunga pamoja naye, akamwambia, "Wafilisti wako juu yako Samsoni!" Watu waliokuwa wakisubiri walikuwa ndani ya chumba cha ndani. Lakini Samsoni akaondoa kamba kutoka mikono yake kama kilikuwa kipande cha uzi.
\s5
\v 13 Delila akamwambia Samsoni, "Mpaka sasa umenidanganya na kuniambia uongo. Niambie kwa namna gani unaweza kufungwa." Samsoni akamwambia, 'Ikiwa utavifuma vifungo saba vya nywele zangu na kuvifunga kwenye kitambaa, kisha kufunga kwenye msumari, nitakuwa kama mtu mwingine yeyote."
\v 14 Alipokuwa amelala, Dalila akavifuma vifungo saba vya nywele zake akavifunga ndani ya kitambaa na kuzifunga kwenye msumari, akamwambia, "Wafilisti wako juu yako, Samsoni!" Aliamka kutoka usingizini akang'oa kitambaa na pini zilizokuwa zimefungwa.
\s5
\v 15 Akamwambia, "Wawezaje kusema," Unanipenda, wakati hushiriki siri zako na mimi? Umenidhihaki mara tatu hizi na hukukuambia ni kwa jinsi gani unazo nguvu nyingi."
\v 16 Kila siku alisisitiza kwa bidii na maneno yake, naye akamkemea sana kiasi kwamba alitamani kufa.
\s5
\v 17 Basi Samsoni alimwambia kila kitu, akamwambia, "Wembe haujawahi kukata nywele juu ya kichwa changu, kwa maana nimekuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni mwa mama yangu. Ikiwa kichwa changu kitanyolewa, basi nguvu zangu zitaniacha, nami nitakuwa dhaifu na kuwa kama kila mtu mwingine. '
\s5
\v 18 Delila alipoona kwamba amemwambia ukweli juu ya kila kitu, akawatuma na kuwaita watawala wa Wafilisti, akisema, "Njooni tena, kwa maana ameniambia kila kitu." Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakaleta fedha mkononi mwao.
\v 19 Alimfanya alale katika magoti yake. Alimwita mtu avinyoe vifungo saba vya kichwa chake, naye akaanza kumshinda, kwa maana nguvu zake zilikuwa zimemwacha.
\s5
\v 20 Alisema, "Wafilisti wako juu yako, Samsoni!" Aliamka nje ya usingizi wake akasema, "Nitatoka nje kama nyakati nyingine na kujiweka huru." Lakini hakujua kwamba Bwana amemwacha.
\v 21 Wafilisti walimkamata na kumng'oa macho. Wakampeleka Gaza na kumfunga kwa shaba. Alikuwa akisaga ngano katika gerezani.
\v 22 Lakini nywele juu ya kichwa chake zilianza kukua tena baada ya kunyolewa.
\s5
\v 23 Watawala wa Wafilisti walikusanyika ili kutoa dhabihu kubwa kwa Dagoni mungu wao, na kufurahi. Walisema, "mungu wetu amemshinda Samsoni, adui yetu, na kumtia katika ufahamu wetu."
\v 24 Watu walipomwona, walimsifu mungu wao, kwa sababu walisema, "mungu wetu ameshinda adui yetu na kutupa sisi - mharibifu wa nchi yetu, ambaye aliwaua wengi wetu."
\s5
\v 25 Walipokuwa wakisherehekea, wakasema, 'Mwite Samsoni, aje kutufurahisha.' Walimwita Samsoni nje ya jela na akawafanya wacheke. Walimsimamisha katikati ya nguzo.
\v 26 Samsoni akamwambia yule kijana ambaye alikuwa ameshika mkono wake, 'Niruhusu nishike nguzo zilizoshikilia nyumba hii, ili nipate kuegemea."
\s5
\v 27 Sasa nyumba ilikuwa imejaa wanaume na wanawake. Watawala wote wa Wafilisti walikuwa huko. Juu ya paa kulikuwa na wanaume na wanawake elfu tatu, ambao walikuwa wakiangalia wakati Samsoni alipokuwa akiwafurahisha.
\s5
\v 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, "Bwana MUNGU, nipe nia! Tafadhali niimarishe mara moja tu, Mungu, ili nipate kulipiza kisasi kwa Wafilisti kwa kuchukua macho yangu mawili.
\v 29 Samsoni aliweka nguzo mbili katikati ambzo zinashikilia nyumba hiyo, naye akaegemea juu yake, nguzo moja kwa mkono wake wa kuume, na mwingine kwa kushoto kwake.
\s5
\v 30 Samsoni akasema, "Na nife pamoja na Wafilisti!" Alipanda kwa nguvu zake na jengo likaanguka juu ya watawala na juu ya watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo waliouawa wakati alikufa walikuwa zaidi ya wale waliouawa wakati wa maisha yake.
\v 31 Kisha ndugu zake na nyumba yote ya baba yake wakashuka. Wakamchukua, wakamrudisha na kumzika kati ya Sora na Eshtaoli katika mahali pa kuzikwa Manoa, baba yake. Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Kulikuwa na mtu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na jina lake ni Mika.
\v 2 Akamwambia mama yake, "Shilingi 1, 100 za fedha ambazo zilichukuliwa kutoka kwako, ambazo ulizungumza kwa kiapo, na kuniambia-tazama hapa! Ninazo fedha pamoja nami. Nimeziiba." Mama yake akasema, 'Na Bwana atakubariki, mwanangu!'
\s5
\v 3 Alirejesha vipande 1, 100 vya fedha kwa mama yake na mama yake akasema, "Nimeweka fedha hii kwa Bwana, kwa ajili ya mwanangu kuifanya na kuchonga takwimu za chuma.
\v 4 Kwa hiyo sasa, ninawarejesha." Alipokuwa amrudishia mama yake fedha, mama yake alichukua vipande mia mbili za fedha na akawapa mfanyakazi wa chuma ambaye aliwafanya kuwa sanamu na kuchonga takwimu za chuma, na wakawekwa ndani ya nyumba ya Mika.
\s5
\v 5 Mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya sanamu, naye akafanya efodi na nyumba ya miungu, naye akaajiri mmoja wa wanawe awe mkuhani wake.
\v 6 Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli, na kila mtu alifanya yaliyo sawa machoni pake.
\s5
\v 7 Kisha kulikuwa na kijana mmoja wa Bethlehemu huko Yuda, wa jamaa ya Yuda, ambaye alikuwa Mlawi. Alikaa huko ili kutimiza majukumu yake.
\v 8 Mtu huyo aliondoka Bethlehemu huko Yuda kwenda kutafuta mahali pa kuishi. Alipokuwa akienda, afika nyumbani kwa Mika katika nchi ya mlima wa Efraimu.
\v 9 Mika akamwambia, Unatoka wapi? Huyo mtu akamwambia, Mimi ni Mlawi wa Bethlehemu huko Yuda, ninakwenda kutafuta mahali nipate kuishi.
\s5
\v 10 Mika akamwambia, "kaa pamoja nami, uwe baba yangu na kuhani wangu. Nitawapa vipande kumi vya fedha kwa mwaka, suti ya nguo, na chakula chako." Basi Mlawi akaingia nyumbani mwake.
\v 11 Mlawi alikuwa na furaha ya kuishi na mtu huyo, na huyo kijana kwa Mika akawa kama mmoja wa wanawe.
\s5
\v 12 Mika akamtenga Mlawi kwa ajili ya kazi takatifu, na huyo kijana akawa kuhani wake, naye alikuwa katika nyumba ya Mika.
\v 13 Ndipo Mika akasema, Sasa najua ya kuwa Bwana atanifanyia mema, kwa kuwa Mlawi huyu amekuwa kuhani wangu.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli. Kabila la Wadani lilikuwa linatafuta makazi ya kuishi, kwa maana mpaka siku hiyo hawakupokea urithi wowote kutoka miongoni mwa makabila ya Israeli.
\v 2 Watu wa Dani walituma watu watano kutoka kwa idadi yote ya kabila lao, wanaume wenye ujasiri kutoka Sora na kutoka Eshtaoi, ili kukagua ardhi kwa miguu, na kuiangalia. Wakawaambia, "Nendeni mkaangalie nchi.' Wakafika nchi ya mlima wa Efraimu, kwa nyumba ya Mika wakalala huko.
\s5
\v 3 Walipokuwa karibu na nyumba ya Mika, walitambua maneno ya Mlawi. Basi wakamsimama na kumwuliza, "Nani alikuleta hapa? Unafanya nini hapa? Kwa nini uko hapa?"
\v 4 Akawaambia, "Hivi ndivyo Mika amefanya kwa ajili yangu Yeye aliniajiri mimi kuwa kahani wake."
\s5
\v 5 Wakamwambia, "Tafadhali tafuta ushauri kwa Mungu, ili tuweze kujua kama safari tunayoendea itafanikiwa."
\v 6 Kuhani huyo akawaambia, "Nenda kwa amani. Bwana atakuongoza katika njia unayoiendea."
\s5
\v 7 Kisha wale watu watano wakaondoka na wakafika Laishia, na waliona watu waliokuwa pale waliishi salama- vivyo hivyo Wasidoni waliishi bila kusumbuliwa na kwa usalama. Hapakuwa na mtu aliyewashinda katika nchi hiyo, au aliyewasumbua kwa namna yoyote. Waliishi mbali na Wasidoni, na hawakuwa na ushirikiano na mtu yeyote.
\v 8 Walirudi kwa kabila lao huko Zora na Eshtaol. Ndugu zao waliwauliza, 'Mna habari gani?'
\s5
\v 9 Wakasema, "Njoo! Hebu tuwashambulie! Tumeona ardhi na ni nzuri sana. Je hamfanyi kitu? Msiwe wavivu kushambulia na kuchukua ardhi.
\v 10 Mnapoenda, mtakuta watu wanaofikiri wapo salama, na nchi ni pana! Mungu amewapa ninyi-mahali ambako hapajapungukiwa kitu chochote duniani. '
\s5
\v 11 Watu mia sita wa kabila la Dani, wenye silaha za vita, waliondoka kutoka Sora na Eshtaoli.
\v 12 Wakasafiri, wakapanga Kiriath-yearimu, huko Yuda. Ndio maana watu walipaita mahali pale Mahane Dani hata leo; ni magharibi ya Kiriath yearimu.
\s5
\v 13 Wakaondoka huko na kwenda nchi ya mlima wa Efraimu, wakafika nyumbani kwa Mika.
\v 14 Kisha watu watano waliokuwa wamekwenda kutazama nchi ya Laisha waliwaambia jamaa zao, "Je, mnajua kwamba katika nyumba hizi kuna efodi, miungu ya kaya, sanamu zilizochongwa, na sanamu za chuma? Amua sasa utakachofanya."
\s5
\v 15 Basi wakarudi huko, wakafika nyumbani mwa Mlawi, nyumbani mwa Mika; wakamsalimu.
\v 16 Wana Daniani mia sita, wenye silaha za vita, walisimama kwenye maingilio ya lango.
\s5
\v 17 Wale watu watano waliokuwa wamekwenda kutembelea nchi walikwenda huko na wakachukua sanamu zilizochongwa, efodi, na miungu ya nyumba, na sanamu ya chuma, wakati kuhani alipokuwa amesimama kwenye maingilio ya lango na wanaume mia sita wenye silaha za vita.
\v 18 Walipokuwa wakiingia nyumbani kwa Mika na kuchukua sanamu zilizochongwa, efodi, miungu ya nyumba, na sanamu za chuma, kuhani akasema, "mnafanya nini?"
\s5
\v 19 Wakamwambia, "Tulia! Weka mkono wako kwenye kinywa chako na uje nasi, na uwe kwetu baba na kuhani. Je, ni bora kuwa wewe kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuhani kwa kabila na jamaa katika Israeli?"
\v 20 Moyo wa kuhani ulifurahi. Akachukua efodi, miungu ya nyumba, na sanamu ya kuchongwa, akaenda pamoja na hao watu.
\s5
\v 21 Basi wakageuka wakaenda. Wameweka watoto wadogo mbele yao wenyewe, pamoja na ng'ombe na mali zao.
\v 22 Walipokuwa umbali mzuri kutoka kwa nyumba ya Mika, watu waliokuwa ndani ya nyumba iliyo karibu na nyumba ya Mika waliitwa, nao wakawafikia Wadani.
\v 23 Waliwapigia kelele Wadani, nao wakageuka, wakamwambia Mika, "Kwa nini mmekuja pamoja?
\s5
\v 24 Akasema, "ninyi mmeiba miungu niliyoifanya, mmemchukua kuhani wangu, na mnaondoka. Je, nina nini tena? Unawezaje kuniuliza, 'Ni nini kinachokusumbua?'"
\v 25 'Watu wa Dani wakamwambia," Usiruhusu tusikie chochote unachosema, au baadhi ya watu wenye hasira sana watawapiga, wewe na familia yako mtauawa."
\v 26 Ndipo watu wa Dani wakaenda zao. Mika alipoona kwamba walikuwa na nguvu sana juu yake, akageuka na kurudi nyumbani kwake.
\s5
\v 27 Watu wa Dani walichukua kile alichokifanya Mika, pamoja na kuhani wake, na wakafika Laisha, kwa watu waliokuwa hawasumbuliwi na wenye usalama na salama wakawaua kwa upanga na kuuchoma mji huo.
\v 28 Hapakuwa na mtu wa kuwaokoa kwa sababu palikuwa na umbali mrefu kutoka Sidoni, na hawakuwa na uhusiano na mtu yeyote. Palikuwa katika bonde lililo karibu na Beth Rehobu. Wadani wakaujenga mji na kuishi huko.
\v 29 Wakauita jina lake Dani, jina la baba zao Dani, ambaye alikuwa mmoja wa wana wa Israeli. Lakini jina la mji hapo mwanzo ulikuwa Laisha.
\s5
\v 30 Watu wa Dani walijenga sanamu za kuchonga wenyewe. Naye Yonathani, mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa makuhani wa kabila la Wadani mpaka siku ya uhamisho wa nchi.
\v 31 Basi wakaiabudu sanamu ya kuchonga ya Mika aliyoifanya wakati wa nyumba ya Mungu huko Shilo.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Katika siku hizo, wakati hakuna mfalme katika Israeli, kulikuwa na mtu, Mlawi, aliyekuwa akiishi kwa muda kidogo katika eneo la mbali zaidi ya nchi ya Efraimu. Alijichukulia mwanamke, masuria kutoka Bethlehemu huko Yuda.
\v 2 Lakini mkewe hakuwa mwaminifu kwake; akaondoka na kurudi nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu ya Yuda. Alikaa huko kwa muda wa miezi minne.
\s5
\v 3 Kisha mumewe akaondoka na kumfuata ili kumshawishi arudi. Mtumishi wake alikuwa pamoja naye, na punda wawili. Akamleta nyumbani kwa baba yake. Baba wa msichana alipomwona, alifurahi.
\v 4 Baba mkwe wake, baba wa msichana, alimshawishi kukaa siku tatu. Walikula na kunywa, na walikaa usiku huko.
\s5
\v 5 Siku ya nne waliamka mapema na alijiandaa kuondoka, lakini baba wa msichana akamwambia mkwewe, "Jipe nguvu na mkate kidogo, kisha unaweza kwenda."
\v 6 Basi hao wawili wakaketi kula na kunywa pamoja. Kisha baba ya msichana akasema, "Tafadhali uwe tayari kukaa usiku huu na kuwa na wakati mzuri.'
\s5
\v 7 Mlawi alipoinuka ili aondoke, baba wa mwanamke huyo alimwomba akae, hivyo alibadili mpango wake na akalala usiku tena.
\v 8 Siku ya tano aliamka mapema kuondoka, lakini baba wa msichana akasema, 'Jitie nguvu mwenyewe, na kusubiri mpaka alasiri.' Kwa hiyo hao wawili wakala chakula.
\s5
\v 9 Mlawi na suria wake na mtumishi wake wakainuka ili kuondoka, baba mkwe wake, baba wa msichana akamwambia, "Angalia, sasa mchana unaelekea jioni. Tafadhali kaa usiku mwingine, na uwe na wakati mzuri. Unaweza kuamka kesho mapema na kurudi nyumbani."
\s5
\v 10 Lakini Mlawi hakuwa tayari kukaa usiku. Aliamka na kuondoka. Akaenda kuelekea Yebusi (hiyo ni Yerusalemu). Alikuwa na pande mbili za punda-na masuria wake alikuwa pamoja naye.
\v 11 Walipokuwa karibu na Yebusi, siku hiyo ilikuwa imeenda mno, na mtumishi akamwambia bwana wake, Haya, tupate kwenda kwa mji wa Wayebusi, tukakae ndani yake usiku huu.
\s5
\v 12 Bwana wake akamwambia, "Hatuwezi kwenda katika mji wa wageni ambao si wa wana wa Israeli." Tutakwenda Gibea.
\v 13 Mlawi akamwambia yule kijana, "Njoo, twende sehemu moja wapo, na tukae usiku huko Gibea au Rama."
\s5
\v 14 Basi, wakaenda, na jua likachwea wakiwa karibu na Gibea, katika eneo la Benyamini.
\v 15 Wakageuka huko ili wawezenkukaa usiku huko Gibea. Naye akaingia na kukaa katika njia kuu ya jiji, maana hakuna mtu aliyewaingiza nyumbani kwake usiku.
\s5
\v 16 Lakini mtu mzee alikuwa akija kutoka kazini kwake katika shamba jioni hiyo. Alikuwa kutoka mlima wa Efraimu, naye alikuwa akikaa kwa muda huko Gibea. Lakini watu wanaoishi mahali hapo walikuwa Wabenyamini.
\v 17 Aliinua macho na kumwona msafiri katika njia kuu ya jiji. Huyo mzee akasema, "Unakwenda wapi? Unatoka wapi?"
\s5
\v 18 Mlawi akamwambia, "Tunaenda kutoka Betelehemu ya Yuda mpaka sehemu ya mbali zaidi ya nchi ya kilima ya Efraimu, ambako mimi hutoka. Nilikwenda Bethlehemu huko Yuda, nami nenda nyumbani mwa Bwana; lakini hakuna mtu atakayenichukua nyumbani kwake.
\v 19 Tuna nyasi za kulisha punda zetu, na kuna mkate na divai kwa ajili yangu na mtumishi wako mwanamke hapa, na kwa kijana huyu pamoja na watumishi wako. Hatujapungukiwa chochote. '
\s5
\v 20 Huyo mzee akawasalimu, "Amani iwe na wewe! Nitakupatia mahitaji yako yote. Usikae usiku tu katika njia kuu."
\v 21 Basi huyo mtu akamleta Mlawi nyumbani kwake, akawalisha punda. Wakaosha miguu yao na kula na kunywa.
\s5
\v 22 Walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, watu wengine wa jiji, watu wasiokuwa na maana, walizunguka nyumba, wakipiga mlango. Wakamwambia yule mzee, mwenye nyumba, wakisema, "Mtoe mtu aliyeingia nyumbani kwako, ili tuweze kufanya mapenzi naye."
\v 23 Yule mtu, mwenye nyumba, akawajia, akawaambia, "Hapana, ndugu zangu, tafadhali msifanye jambo baya! Kwa kuwa mtu huyu ni mgeni nyumbani kwangu, musifanye jambo hili baya!"
\s5
\v 24 Angalia, binti yangu bikira na masuria wake hawa hapa. Ngoja niwalete sasa. Wapuuze na kufanya nao chochote mnachopenda. Lakini msifanyie jambo hili mbaya kwa mtu huyu!"
\v 25 Lakini watu hawakumsikiliza, kwa hiyo huyo mwanamume akamshika yule mwanamke, akamleta nje. Walimkamata, wakambaka, na kumtendea uovu usiku mzima, na asubuhi wakamruhusu aende.
\v 26 Asubuhi mwanamke alikuja akaanguka chini ya mlango wa nyumba ya mtu ambapo bwana wake alikuwa, na yeye akalala pale mpaka kulipokucha.
\s5
\v 27 Bwana wake akaondoka asubuhi na kufungua milango ya nyumba, akatoka kwenda njiani. Aliweza kumwona mwanamke wake amelala pale mlangoni, mikono yake ikiwa juu ya kizingiti.
\v 28 Mlawi akamwambia, "Simama twende." Lakini hakujibiwa. Alimuweka juu ya punda, na huyo mtu akaondoka nyumbani.
\s5
\v 29 Mlawi alipofika nyumbani kwake, akachukua kisu, naye akamshika suria wake, akamkataa, mguu kwa mguu, akafanya vipande kumi na viwili, akapeleka vipande kila mahali katika Israeli.
\v 30 Wote waliona hili wakasema, "Kitu hicho hakijawahi kufanyika au kuonekana tangu siku ambayo watu wa Israeli walikuja kutoka nchi ya Misri mpaka leo. Fikiria juu ya hili! Tupe ushauri! Tuambie nini cha kufanya!"
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ndipo watu wote wa Israeli wakatoka kama mtu mmoja, toka Dani mpaka Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi; nao wakakusanyika mbele za Bwana huko Mispa.
\v 2 Viongozi wa watu wote, wa kabila zote za Israeli, wakachukua nafasi zao kwenye kusanyiko la watu wa Mungu-watu 400, 000 waendao kwa miguu, ambao walikuwa tayari kupigana na upanga.
\s5
\v 3 Basi wana wa Benyamini waliposikia kwamba watu wa Israeli walikuwa wamepanda Mispa. Wana wa Israeli wakasema, "Tuambieni ni kwa namna gani huu uovu umefanyika."
\v 4 Mlawi, mume wa mwanamke aliyeuawa, akajibu, Nilikuja Gibea katika nchi ya Benyamini, mimi na suria wangu, ili tulale.
\s5
\v 5 Wakati wa usiku, viongozi wa Gibea walinishambulia, wakizunguka nyumba na wakakusudia kuniua. Walimkamata na kumbaka suria wangu, naye akafa.
\v 6 Nilimchukua suria wangu na kumkata mwili wake vipande vipande, na kuweka katika kila nchi ya urithi wa Israeli, kwa sababu wamefanya uovu huo na upumbavu katika Israeli.
\v 7 Sasa, ninyi Waisraeli wote, toeni maneno na ushauri wenu hapa."
\s5
\v 8 Watu wote wakaondoka pamoja kama mtu mmoja, wakasema, Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda hemani kwake, wala hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake.
\v 9 Lakini sasa hivi ndivyo tutakavyoifanyia Gibea tutaishambulia kama kura inavyotuongoza.
\s5
\v 10 Tutachukua watu kumi katika mia moja katika makabila yote ya Israeli, na mia moja katika elfu, na elfu moja katika elfu kumi, kuwapa chakula kwa ajili ya watu hawa, ili waweze kufika Gibea katika Benyamini, watawaadhibu kwa uovu wao waliofanya katika Israeli.
\v 11 Basi askari wote wa Israeli wakakusanyika juu ya mji, kama mtu mmoja.
\s5
\v 12 Makabila ya Israeli waliwatuma watu kwa kabila lote la Benyamini, wakisema, "Uovu huu uliofanywa kati yenu ni nini?
\v 13 Kwa hiyo, tupeni watu hao waovu wa Gibea, tupate kuwaua, na hivyo tutaondoa kabisa uovu huu kutoka kwa Israeli." Lakini Wabenyamini hawakusikiliza sauti ya ndugu zao, watu wa Israeli,
\v 14 Ndipo wana wa Benyamini wakakusanyika kutoka mijini kwenda Gibea, wakajiandaa kupigana na wana wa Israeli.
\s5
\v 15 Watu wa Benyamini wakakusanya kutoka miji yao ili kupigana siku ile, askari elfu ishirini na sita waliopangwa kupigana na upanga. Walakini, kuna watu mia saba waliochaguliwa kutoka kwa wenyeji wa Gibea.
\v 16 Miongoni mwa askari wote hawa walikuwa watu mia saba waliochaguliwa ambao walikuwa wenye shoto. Kila mmoja wao angeweza kupiga unywele kwa mawe na asikose.
\s5
\v 17 Watu wa Israeli, bila kuhesabu namba kutoka kwa Benyamini, walikuwa na watu 400, 000 waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga. Wote hawa walikuwa watu wa vita.
\v 18 Watu wa Israeli waliondoka, wakaenda Betheli, wakaomba ushauri kutoka kwa Mungu. Wakauliza, "Ni nani kwanza atakayewaangamiza watu wa Benyamini kwa ajili yetu?" Bwana akasema, "Yuda atashambulia kwanza."
\s5
\v 19 Watu wa Israeli waliamka asubuhi na wakahamisha kambi yao karibu na Gibea.
\v 20 Watu wa Israeli walikwenda kupigana na Benyamini. Wakaweka nafasi zao za vita dhidi yao huko Gibea.
\v 21 Watu wa Benyamini wakatoka Gibea, nao wakawaua watu elfu ishirini na mbili wa jeshi la Israeli siku ile.
\s5
\v 22 Wana wa Israeli walijitia nguvu wenyewe, na wakaunda mstari wa vita mahali pale walipokwisha kuchukua nafasi siku ya kwanza.
\v 23 Na wana wa Israeli wakaenda, wakalia mbele za Bwana hata jioni. Walitaka mwongozo kutoka kwa Bwana "Je, tunapaswa kwenda tena kupigana na ndugu zetu, watu wa Benyamini?" Naye Bwana akasema, "Wapigeni!"
\s5
\v 24 Basi watu wa Israeli wakapigana na askari wa Benyamini siku ya pili.
\v 25 Siku ya pili, Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea, nao wakawaua watu wa Israeli elfu kumi na nane. Wote walikuwa watu ambao walijifunza kupigana na upanga.
\s5
\v 26 Basi askari wote wa Israeli na watu wote wakaenda Betheli, wakalia, wakakaa mbele za Bwana; nao wakafunga siku hiyo hata jioni, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
\s5
\v 27 Wana wa Israeli wakamwomba Bwana, - kwa sababu ya sanduku la agano la Mungu lilikuwapo siku hizo;
\v 28 na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, aliyekuwa akihudumia mbele ya sanduku siku hizo. "Je twende vitani tena dhidi ya watu wa Benyamini, ndugu zetu, au tuache?" Bwana akasema, "Wapigeni, kwa maana kesho nitawasaidia kuwashinda.
\s5
\v 29 Basi Israeli akaweka watu mahali pa siri karibu na Gibea.
\v 30 Watu wa Israeli wakapigana na wana wa Benyamini kwa siku ya tatu, nao wakajenga vita vyao juu ya Gibea, kama walivyotangulia.
\s5
\v 31 Watu wa Benyamini wakaenda kupigana na watu, nao wakachukuliwa mbali na mji. Walianza kuua baadhi ya watu. Kulikuwa na watu thelathini wa Israeli ambao walikufa katika mashamba na barabara. Njia moja ilienda Betheli, na nyingine ikaenda Gibea.
\s5
\v 32 Ndipo wana wa Benyamini wakasema, "Wameshindwa na wanatukimbia, kama hapo awali." Lakini askari wa Israeli wakasema, "Hebu tukimbie na kuwavuta mbali na mji hadi barabarani."
\v 33 Watu wote wa Israeli waliondoka kutoka mahali pao na wakajipanga kwa vita huko Baal-Tamari. Basi askari wa Israeli waliokuwa wakijificha mahali pa siri walikimbia kutoka Maare-Geba.
\s5
\v 34 Wakatoka juu ya Gibea watu kumi elfu waliochaguliwa kutoka Israeli yote, na vita vilikuwa kali, lakini Wabenjamini hawakujua kwamba msiba ulikuwa karibu nao.
\v 35 Bwana akamshinda Benyamini mbele ya Israeli. Siku hiyo, askari wa Israeli waliwauawa watu wa Benyamini 25, 100. Wote hawa waliokufa walikuwa wale waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga.
\s5
\v 36 Basi askari wa Benyamini waliona wameshindwa. Wana wa Israeli walikuwa wametoa ardhi kwa Benyamini, kwa kuwa walikuwa wakihesabu watu waliowaweka katika nafasi zilizofichwa nje ya Gibea.
\v 37 Ndipo watu waliokuwa wameficha wakainuka na haraka na wakamkimbia Gibea. Nao wakauawa kila mtu aliyeishi mjini kwa upanga wao.
\v 38 Ishara iliyopangwa kati ya askari wa Israeli na watu waliojificha kwa siri itakuwa wingu kubwa la moshi litatokea nje ya mji.
\s5
\v 39 Ishara ilipokuja askari wa Israeli wakageuka kutoka kwenye vita. Basi Benyamini wakaanza kushambulia na wakawaua watu wa Israeli thelathini, wakasema, "Hakika wanapigwa mbele yetu, kama katika vita vya kwanza."
\s5
\v 40 Lakini wakati nguzo ya moshi ilipoanza kuinuka nje ya mji, Wabenjamini waligeuka na kuona moshi ukitanda mbinguni kutoka mji mzima.
\v 41 Ndipo watu wa Israeli wakawageuka. Wana wa Benyamini waliogopa, kwa sababu waliona kwamba maafa yaliwajia.
\s5
\v 42 Basi wakakimbia kutoka kwa wana wa Israeli, kuelekea njia ya jangwani. Lakini vita viliwapata. Askari wa Israeli walitoka mijini na wakawaua pale waliposimama.
\s5
\v 43 Waliwalzungukia wana wa Benjamini na wakawafuata. Nao wakawakanyaga huko Noha, wakawaua mpaka upande wa mashariki wa Gibea.
\v 44 Kutoka kabila la Benyamini, watu kumi na nane elfu walikufa, wote walikuwa wanaume waliojulikana katika vita.
\s5
\v 45 Wakageuka na kukimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Waisraeli waliuawa zaidi ya elfu tano kati yao barabarani. Waliendelea kuwafuata, wakifuata kwa njia kuu kwenda Gidomu, na huko waliuawa elfu mbili zaidi.
\v 46 Askari wote wa Benyamini walioshuka siku hiyo walikuwa watu ishirini na tano waliokuwa wamejifunza kupigana kwa upanga; wote walikuwa wanajulikana katika vita.
\s5
\v 47 Lakini watu mia sita wakageuka na kukimbilia jangwani, kuelekea mwamba wa Rimoni. Wakakaa katika mwamba wa Rimoni kwa muda wa miezi minne.
\v 48 Askari wa Israeli waliwarudia watu wa Benyamini na wakawashinda na kuwaua-mji mzima, ng'ombe, na kila kitu walichopata. Pia walichoma moto kila mji katika njia yao.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Sasa watu wa Israeli walikuwa wameahidi huko Mispa, "Hakuna hata mmoja wetu atakayempa binti yake kuolewa na Mbenyamini."
\v 2 Ndipo watu wakaenda Betheli, wakakaa huko mbele ya Mungu hata jioni; wakalia kwa sauti kubwa.
\v 3 Walipiga kelele, "Kwa nini, Bwana, Mungu wa Israeli, amefanya jambo hili kwa Waisraeli, kwamba moja ya makabila yetu linapotea leo?"
\s5
\v 4 Siku iliyofuata watu waliamka mapema na wakajenga madhabahu huko na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.
\v 5 Watu wa Israeli wakasema, "Ni nani kati ya kabila zote za Israeli hawakuja katika mkutano wa Bwana?" Kwa kuwa walikuwa wamefanya ahadi muhimu juu ya mtu yeyote ambaye hakuja kwa Bwana huko Mispa. Wakasema, "Hakika yeye atauawa."
\s5
\v 6 Watu wa Israeli walikuwa na huruma kwa ndugu yao Benyamini. Wakasema, "Leo hii kabila moja limekatiliwa mbali kutoka Israeli.
\v 7 Ni nani atakayewapa wale walioachwa wake, kwa kuwa tumeahidi kwa Bwana kwamba hatuwezi kuwaruhusu yeyote kati yao aoe binti zetu?"
\s5
\v 8 Wakasema, "Ni nani kati ya kabila za Israeli hawakuja kwa Bwana huko Mispa? Ilionekana kuwa hakuna mtu aliyekuja kwenye mkusanyiko kutoka Jabeshi-Gileadi.
\v 9 Kwa maana watu walipokuwa wamepangwa kwa utaratibu, tazama, hakuna hata mmoja wa wenyeji wa Yabeshi Gileadi.
\v 10 Mkutano huo uliwatuma watu kumi na wawili wa watu wao wenye ujasiri kwa maagizo ya kwenda Jabeshi-gileadi na kuwaangamiza, na kuwaua, hata wanawake na watoto.
\s5
\v 11 "Fanya hivi unapaswa kuua kila mume na kila mwanamke aliyelala na mwanaume."
\v 12 Watu wale walikuta watu kati ya hao waliokaa Yabeshi-gileadi, wanawake mia nne ambao hawakulala na mwanaume, wakawapeleka kwenye kambi huko Shilo, huko Kanaani.
\s5
\v 13 Mkutano wote ukatuma ujumbe na kuwaambia watu wa Benyamini waliokuwa kwenye mwamba wa Rimoni kwamba walikuwa wanawapa amani.
\v 14 Wabenyamini walirudi wakati huo na walipewa wanawake wa Yabeshi Gileadi, lakini hapakuwa na wanawake wa kutosha kwa wote.
\v 15 Watu waliomboleza kwa kile kilichotokea Benyamini, kwa kuwa Bwana alifanya mgawanyiko kati ya makabila ya Israeli.
\s5
\v 16 Kisha wakuu wa mkutano wakasema, "Tutafanyaje ili Wabenyamini wapate wake, kwa kuwa wanawake wa Benyamini wameuawa?"
\v 17 Wakasema, 'Lazima kuwe na urithi kwa Wabenyamini waliosalia, ili kabila lisiharibiwe kutoka Israeli.
\s5
\v 18 Hatuwezi kuwapa wake kutoka kwa binti zetu, kwa kuwa wana wa Israeli walikuwa wametoa ahadi, 'Na alaaniwe mtu atakayempa Benyamini mke.'"
\v 19 Wakasema, "Mnajua kuwa kuna sikukuu kwa Bwana kila mwaka huko Shilo ( ambayo ni kaskazini ya Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona).
\s5
\v 20 Wakawaagiza wana wa Benyamini, wakisema, "Nendeni, mjifiche kwa siri, na kusubiri katika mashamba ya mizabibu.
\v 21 Tazama wakati ambapo wasichana kutoka Shilo watatoka kucheza, Tokeni nje ya mizabibu na kila mmoja wenu anapaswa kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo, kisha kurudi kwenye nchi ya Benyamini.
\s5
\v 22 Wakati baba zao au ndugu zao watakapokuja kutupinga, tutawaambia, 'Tupeni neema! Waache wabaki kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita. Na ninyi hamna hatia juu ya ahadi, kwa sababu hamkuwapa wao binti zenu.'"
\s5
\v 23 Watu wa Benyamini walifanya hivyo. Walichukua idadi ya wake waliowahitaji kutoka kwa wasichana waliokuwa wakicheza, nao wakawachukua ili wawe wake zao. Wakaenda na kurudi mahali pa urithi wao; wakajenga tena miji, na wakaishi ndani yao.
\v 24 Kisha watu wa Israeli wakatoka mahali hapo na kwenda nyumbani, kila mmoja kwa kabila lake na ukoo, na kila mmoja kwa urithi wake mwenyewe.
\s5
\v 25 Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli. Kila mtu alifanya yaliyo sawa machoni pake mwenyewe.

176
08-RUT.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,176 @@
\id RUT
\ide UTF-8
\h Ruth
\toc1 Ruth
\toc2 Ruth
\toc3 rut
\mt Ruth
\s5
\c 1
\p
\v 1 Ilitokea katika siku za utawala wa majaji kuwa kulikuwa na njaa katika nchi, na mtu mmoja wa Bethelehemu ya Yuda alikwenda katika nchi ya Moabu pamoja na mke wake na watoto wake walili wa kiume.
\v 2 Jina la mtu huyo lilikuwa Elimeleki, na jina la mke wake lilikuwa Naomi. Majina ya watoto wake wawili wa kiume waliitwa Mahiloni na Kileoni, ambao walikuwa Waefraimu wa Betherehemu ya Yuda. Waliwasili katika nchi ya Moabu na kuishi hapo.
\s5
\v 3 Ndipo Elimeleki, mume wa Naomi, alikufa, na Naomi aliachwa na watoto wake wa kiume wawili.
\v 4 Watoto hawa walioa wanawake wa Moabu; jina la mmoja lilikuwa Oripa, na jina la mwingine lilikuwa Ruth. waliishi huko kwa takribani miaka kumi.
\v 5 Kisha wote Mahiloni na Kileoni walikufa, na kumuacha Naomi bila mme wake na bila watoto wake wawili.
\s5
\v 6 Ndipo Naomi aliamua kuondoka Moabu pamoja na wake wa watoto wake na kurudi Yuda kwa sababu alikuwa amesikia katika mkoa wa Moabu kuwa Yahweh amewasaidia watu wake katika uhitaji na amewapa chakula.
\v 7 Hivyo aliondoka sehemu aliyokuwa pamoja na wake wa watoto wake wawili, walitelemka njia kurudi kwenye nchi ya Yuda.
\s5
\v 8 Naomi aliwaambia wake wa watoto wake, "Nendeni, mrudi, kila mmoja wenu, kwenye nyumba ya mama yake. na Mungu aonyeshe wema juu yenu, kama mlivyo onyesha wema kwao waliokufa na kwangu.
\v 9 Mungu awajalie ninyi kupata pumziko, kila mmoja wenu katika nyumba ya mme mwingine." Kisha akawabusu, na wakapaza sauti zao na kulia.
\v 10 Wakamwambia, "Hapana! tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako."
\s5
\v 11 Lakini Naomi alisema, "Rudini, wanangu! Kwa nini mtakwenda na mimi? Kwani bado nina watoto katika tumbo langu kwa ajili yenu, ili kwamba waje wawe waume zenu?
\v 12 Rudini, wanangu, nendeni katika njia zenu wenyewe, kwa kuwa mimi ni mzee sana kuwa na mme. Kama nikisema, 'Natumaini nipate mume usiku huu,' na kisha kuzaa watoto wakiume, kwa hiyo mnaweza kusubiri mpaka wakue?
\v 13 Mtasubiri na msiolewe sasa? Hapana, wanangu! Ina nihuzunisha zaidi, kuliko inavyo wahuzunisha ninyi, kwa sababu mkono wa Yahweh umeenda kinyume na mimi."
\s5
\v 14 Ndipo wake wa watoto wake wakapaza sauti zao na kulia tena. Oripa alimuaga kwa kumbusu, lakini Ruth aliendelea kubaki naye.
\v 15 Naomi alisema, "sikiliza, mwenzako amerudi kwa watu wake na miungu yake. Ruri pamoja naye."
\s5
\v 16 lakini Ruth alisema, "Usiniache niondoke mbali nawe, kwa kuwa uendako, nitakwenda, utakapoishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.
\v 17 Mahali utakapofia, nitafia hapo, na hapo nitazikwa. Yahweh aniwezeshe, na hata zaidi, ikiwa kuna chochote isipokuwa kifo kamwe hakiwezi kututenganisha.
\v 18 Naomi alipoona kuwa Ruth alikuwa ameamua kwenda naye, aliacha kubishana naye.
\s5
\v 19 Hivyo wote wawili walisafiri mpaka walipofika mjini Bethelehemu. Kwa hiyo walipofika Bethlehemu, mji wote uliwafurahia, wanawake walisema, "Huyu ni Naomi?"
\v 20 Lakini aliwaambia, "Msiniite Naomi. Niiteni Mchungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.
\v 21 Nilikwenda nikiwa nimejaa, lakini Yahweh kanirudisha nyumbani nikiwa sina wote. Hivyo kwa nini mnaniita Naomi, wakati mnaona Yahweh amenihukumu, kuwa Mwenyezi Mungu amenitaabisha?"
\s5
\v 22 Kwa hivyo Naomi na Ruth Mmoabu, mke wa mtoto wake, walirudi kutoka nchi ya Moabu. walirudi Bethrehemu mwazo wa mavuno ya shairi.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Basi Elimeleki mme wa Naomi, alikuwa na jamaa aitwaye Boazi, aliye kuwa tajiri, na mtu maarufu.
\v 2 Ruth, Mmoabu, alimwambia Naomi, "Ngoja niende nikakusanye mabaki ya chakula katika shamba. Nitamfuata yeyote ambaye nitapata kibali machoni pake." Hivyo naomi akamwambia, "Nenda, mwanangu."
\s5
\v 3 Ruth alienda kuvuna kwenye shamba akiwafuata kwa nyuma wavunaji. Na kumbe ile sehemu ya shamba ilikuwa ni mali ya Boazi, aliyekuwa na mahusiano na Elimeleki.
\v 4 Tazama, Boazi alikuja kutoka bethelehemu na kuwaambia wavunaji, "Yahweh awe nanyi." Wakamjibu, "Yahweh akubariki."
\s5
\v 5 Ndipo Boazi akamwambia mtumishi wake aliyekuwa akiwasimamia wavunaji, "Vipi bwana huyu msichana ni wa nani?"
\v 6 Mtumishi msimamizi wa wavunaji alijibu na kusema, "Ni msichana Mmoabu aliyerudi na Naomi kutoka nchi ya Moabu.
\v 7 Aliniambia, 'Tafadhali niruhusu kuvuna na kukusanya mabaki ya wavunaji.' Hivyo alikuja na ameendelea kuvuna toka asubuhi mpaka sasa, isipokuwa amepumzika kidogo katika nyumba."
\s5
\v 8 Kisha Boazi akamwambia Ruth, "Unanisikiliza, mwanangu? Usiende kuvuna kwenye shamba lingine; usiondoke shambani kwangu. Badala yake, baki hapa na wasichana wangu wa kazi.
\v 9 Yaelekeze tu macho yako kwenye shamba ambamo wanaume wanavuna na ufuatie nyuma ya wanawake wengine. Je, sikuwaelekeza wanaume wasikuguse? Na upatapo kiu, unaweza kwenda kunywa maji kwenye mtungi ambao wanaume wamejaza."
\s5
\v 10 Ndipo akapiga magoti mbele ya Boazi, na kugusisha kichwa chake chini. Akamwambia, "Kwa nini nimepata kibali machoni pako, hata unijali mimi mgeni?"
\v 11 Boazi akajibu na kumwabia, "Nimekwisha ambiwa, yote uliyo yafanya tangu mme wako afariki. Umewaacha baba yako, mama, na nchi uliyozaliwa kumfuata mama mkwe wako na kuja kwa watu usiowajua.
\v 12 Yahweh akulipe kwa matendo yako. Yahweh akulipe kwa wingi, Mungu wa Israeli, ambaye chini ya mbawa zake umepata kimbilio."
\s5
\v 13 Ruth akasema, "Nipate kibali machoni pako, bwana wangu, kwa kuwa umenifariji, na umeongea wema kwangu, ingawa mimi sio mmoja wa watumishi wako wa kike."
\s5
\v 14 Wakati wa chakula Boazi alimwambia Ruth, "Njoo hapa, ule baadhi ya mikate, na uchovye kipande katika divai." Alikaa kando ya wavunaji, na Boazi akampatia kiasi cha nafaka zilizo kaangwa. Ruth alikula mpaka alipotosheka na kusaza.
\s5
\v 15 Alipoinuka kwenda kuvuna, Boazi aliamuru vijana wake, akisema, "Mwacheni avune hata katika masuke, na msimwambie lolote baya.
\v 16 Na pia muachie baadhi ya masuke katika vifurushi kwa ajili yake, na muaache ili ayavune. Msimkemee."
\s5
\v 17 Kwa hiyo alivuna mpaka jioni. Kisha akatenganisha nafaka na majani ambayo amevuna, nazo nafaka zilikuwa kama efa moja ya shairi.
\v 18 Akazibeba na kwenda katika mji. Ndipo mama mkwe wake aliona kile alichokivuna. Ruth pia alimletea mama mkwe wake nafaka zilizo kaangwa alizobakiza kwenye chakula chake.
\s5
\v 19 Mama mkwe wake akamwambia, "Umevunia wapi uliko vunia leo? Ulienda kufanyia wapi kazi? abarikiwe mtu aliye kusaidia." Ndipo Ruth akamwambia mama mkwe wake kuhusu mtu aliye miliki shamba alilokuwa akifanya kazi. Alimwambia, "Jina la mtu ambaye alimiliki shamba nililokuwa nikifanya kazi ni Boazi."
\v 20 Naomi akamwambia Ruth, "Abarikiwe na Yahweh, ambaye hakuondoa uaminifu wake kwa walio hai na wafu." Naomi akamwambia, "Huyo mtu ni jamaa wa karibu nasi, ni jamaa yetu mkombozi."
\s5
\v 21 Ruth Mmoabu akamwambia, "Ni kweli, aliniambia, 'Ukae karibu na vijana wangu wa kiume mpaka watakapo maliza mavuno yangu yote.'"
\v 22 Naomi akamwambia Ruth mke wa mtoto wake wa kiume, "Ni vizuri, mwanangu, kuwa uende pamoja na wasichana wake wa kazi, ili kwamba usije pata madhara yeyote katika shamba lolote."
\s5
\v 23 Kwa hiyo alikaa karibu na wafanyakazi wa kike ili avune mpaka mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano. Na alikuwa akiishi pamoja na mama mkwe wake.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Naomi, mama mkwe wake, alimwambia, "Mwanangu, hainilazimu kutafuta mahali pa wewe kupumzika, ili kwamba mambo yako yaende vizuri?
\v 2 Naye Boazi, mtu ambaye umekuwa pamoja na wasichana wake wa kazi, yeye si jamaa yetu? Tazama, jioni hii atakuwa akikung'uta shairi katika sakafu ya kupuria.
\s5
\v 3 Kwa hiyo, oga, jipake mafuta, uvae nguo zako nzuri, na ushuke kwenda kwenye sakafu ya kupuria. Lakini usijulikane kwa mtu huyu mpaka atakapo maliza kula na kunywa.
\v 4 Na uhakikishe kuwa, atakapo lala chini, ukumbuke mahali alipo lala ili kwamba baadaye uende kwake, ufunue miguu yake, na ulale hapo. Kisha atakuambia cha kufanya."
\v 5 Ruth alimwambia Naomi, "Nitafanya kila kitu ulicho sema."
\s5
\v 6 Alishuka kwenda kwenye sakafu ya kupuria, na alifuata maelekezo aliyopewa na mama mkwe wake.
\v 7 Boazi alipomaliza kula na kunywa na moyo wake ulikuwa na furaha, alienda kulala chini mwisho wa sehemu ya kuhifadhia nafaka. Kisha Ruth akaenda taratibu, akaaifunua miguu ya Boazi, na kulala hapo chini.
\s5
\v 8 Panapo usiku wa manane Boazi alisituka. Akajigeuza, na hapo mwanamke alikuwa amelala katika miguu yake!
\v 9 Akamwambia, "Wewe ni nani?" Akajibu, "Mimi ni Ruth, mtumishi wako wa kike. Nifunike shuka lako mimi mtumishi wako wa kike, kwa kuwa wewe ni jamaa wa karibu."
\s5
\v 10 Boazi akamwambia, "Mwanangu, Yahweh akubariki. Umeonyesha wema mwishoni kuliko mwazoni, kwa sababu hukwenda kwa wanaume vijana, awe tajiri au masikini.
\v 11 Na sasa, mwanangu, usiogope! Nitakufanyia yote unayosema, kwa sababu mji wa watu wangu wote wanajua kuwa wewe ni mwanamke unayestahili.
\s5
\v 12 Nikweli kuwa mimi ni jamaa wa karibu; hata hivyo, kuna jamaa wa karibu kuliko mimi.
\v 13 Baki hapa usiku huu, na asubuhi, ikiwa atafanya jukumu lake la jamaa wa karibu, vizuri, muache afanye jukumu lake la kindugu. lakini kama hata fanya jukumu la kindugu kwako, ndipo mimi nitafanya, kama Yahweh aishivyo. Lala mpaka asubuhi."
\s5
\v 14 Kwa hiyo Ruth alilala kwenye miguu ya Boazi hadi asubuhi. Lakini aliamka mapema kabla ya yeyote kuweza kumtambua mtu mwingine. Kwa kuwa alikwisha mwambia, "Isijulikane kuwa mwanamke alikuja kwenye sakafu ya kupuria."
\v 15 Kisha Boazi akamwambia, lete mtandio wako na uushikilie." Alipo fanya hivyo, alipima vipimo vikubwa sita vya shairi katika mtandio na kumtwisha Ruth. Kisha Boazi akaenda mjini.
\s5
\v 16 Ruth aliporudi kwa mama mkwe wake, alisema, "Ulifanyaje, mwanangu?" Ndipo Ruth akamwambia mambo yote aliyotendewa na mtu huyo.
\v 17 Alimwambia, "Hivi vipimo sita vya shairi ni vile alivyonipa yeye, kwa kuwa alisema, 'Usiende mikono mitupu kwa mama mkwe wako.'"
\v 18 Kisha Naomi akasema, "Baki hapa, mwanangu, mpaka utakapojua yatakavyo kuwa, kwa kuwa Boazi hata pumzika mpaka atakapolimaliza jambo hili leo."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ndipo Boazi akaenda kwenye lango la Bethelehemu na kukaa chini. Muda mfupi tu akaja ndugu wa karibu ambaye Boazi alimuongelea. Boazi akamwambia, "Rafiki yangu, njoo hapa na uketi. Kisha mtu huyo akaja na kuketi.
\v 2 Ndipo Boazi akakusanya viongozi kumi wa mji na kusema, "Katini hapa." Hivyo wakaketi.
\s5
\v 3 Boazi alimwambia yule jamaa wa karibu, "Naomi aliyerudi kutoka mji wa Moabu, anauza sehemu ya aridhi ambayo ilikuwa ni miliki ya kaka yetu Elimeleki.
\v 4 Nilifikiria kukujulisha na kukwambia, 'Inunue mbele ya hawa waliokaa hapa, na mbele ya viongozi wa watu wangu.' Ikiwa utapenda kuikomboa, ikomboe. Lakini ikiwa hauhitaji kuikomboa, uniambie, ili nijue, kwa kuwa hakuna mwingine wa kuikomboa isipokuwa wewe, na mimi ni mdogo wako." Ndipo huyo mtu mwingine akasema, "Nitalikomboa."
\s5
\v 5 Kisha Boazi akasema, "Ile siku utakayonunua shamba kutoka mkononi mwa Naomi, yakupasa pia kumchukua Ruth Mmoabu, mjane wa mtoto wa Elimeleki, ili kuliinua jina la marehemu kama urithi wake."
\v 6 Ndipo yule jamaa wa karibu akasema, "Mimi siwezi kuikomboa ardhi kwa ajili yangu bila kuleta athari kwenye urithi wangu binafsi. Nakupa wewe haki ya kuikomboa kwa ajili yako mwenyewe, kwa kuwa mimi sitoweza."
\s5
\v 7 Hii ilikuwa ni desturi ya zamani ya Israeli kuhusu ukombozi na kubadilishana mazuri. Kudhibitisha mambo haya yote, mtu huyu alivua kiatu chake na kumpatia jirani yake; hii ilikuwa ni namna ya kufanya makubaliano ya kisheria katika Israeli.
\v 8 Kwa hiyo huyu jamaa wa karibu akamwambia Boazi, "Inunue mwenyewe." Kisha akavua kiatu chake.
\s5
\v 9 Ndipo Boazi akawaambia viongozi na watu wote, "Ninyi ni mashaidi kuwa nimenunua kila kilichokuwa cha Elimeleki na kila kilichokuwa na Kileoni na Mahilon kutoka kwenye mikono ya Naomi.
\v 10 Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo."
\s5
\v 11 Watu wote na viongozi waliokuwa katika lango, walisema, "Tu mashahidi. Yahweh amfanye mwanamke huyu ambaye amekuja nyumbani kwako kama Raheli na Leya, ambao wawili hawa wameijenga nyumba ya Israeli. Na ubarikiwe katika Efrata na kuwa mashuhuri katika Bethelehem.
\v 12 Na nyumba yako kama nyumba ya Peres, ambaye Tamari alimzalia yuda, kupitia uzao ambao Yahweh atakupatia pamoja na msichana huyu."
\s5
\v 13 Hivyo Boazi alimchukua Ruth, na akawa mke wake. Boazi alilala naye, na Yahweh alimruhusu kupata mimba, na alizaa mtoto wa kiume.
\v 14 Wanamke huyu akamwambia Naomi, "Yahweh abarikiwe, ambaye hajakuacha bila ndugu wa karibu, yaani mtoto huyu. Jina lake na liwe maarufu katika Israeli.
\v 15 Na awe kwako mrutubishaji wa maisha na mwenye ruzuku uzeeni mwako, kwa kuwa mtoto wako mkwe, ambaye anakupenda, ambaye ni bora kwako kuliko watoto wa kiume saba, amemzaa.
\s5
\v 16 Kisha naomi akamchukua mtoto, akamlaza kifuani pake, na kumhudumia.
\v 17 Na majirani wa yule mwanamke, wakampa jina, wakisema, "Mtoto amezaliwa kwa Naomi." Wakawita Obedi. Ambaye alikuja kuwa baba yake na Jese, ambaye alikuja kuwa baba yake na Daudi.
\s5
\v 18 Hiki kilikuwa ni kizazi cha Peresi: Peres alimzaa Hezroni,
\v 19 Hezroni akamzaa Ram, Ram akamzaa Aminadabu,
\v 20 Aminadabu akamzaa Nashon, Nashon akamzaa Salmon,
\v 21 Salmon akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obed,
\v 22 Obedi akamzaa Jese, na Jese akamzaa Daudi.

2027
09-1SA.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2027 @@
\id 1SA
\ide UTF-8
\h 1Samweli
\toc1 1Samweli
\toc2 1Samweli
\toc3 1sa
\mt 1Samweli
\s5
\c 1
\p 1Samweli 1: 1-2
\v 1 Palikuwa na mtu mmoja wa Rama Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu; jina lake aliitwa Elikana mwana Yerohamu mwana Elihu mwana wa Tohu mwana wa Sufu, Mwefraimu.
\v 2 Mtu huyo alioa wanawake wawili, jina la mke wa kwanza aliitwa Hana, na yule wa pili aliitwa Penina, Penina alizaa watoto, lakini Hana hakuzaa.
1 Samweli 1: 3-4
\s5
\v 3 Kila mwaka, mtu huyu aliondoka mjini kwake kwenda kuabudu na kutoa dhabihu kwa BWANA wa majeshi huko Shilo. Wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwepo huko Shilo.
\v 4 Kila mwaka zamu ya Elikana ya kutoa dhabihu ilipofika, alikuwa daima akimpa sehemu ya nyama Penina mkewe, watoto wake wote wa kiume na wakike
1 Samweli 1: 5-6
\s5
\v 5 Lakini kwa mgawo wa Hana daima alimpa mara mbili zaidi, kwa sababu alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.
\v 6 Hasimu wake alimchokoza sana ili kumkasilisha, kwa sababu BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.
1Samweli 1: 7- 8
\s5
\v 7 Hivyo kila mwaka, alipokuwa akienda katika nyumba ya BWANA pamoja na familia yake, hasimu wake alizidi kumchokoza, Hatimaye alikuwa mtu wa kulia kila wakati na hakula kitu chochote.
\v 8 Elikana mmewe kila wakati alimuuliza, "Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli chakula? Kwa nini una huzuni moyoni mwako? Mimi sibora kwako kuliko wana kumi?
1 Samweli 1: 9-10
\s5
\v 9 Wakati fulani, walipokuwa wamemaliza kula na kunywa huko Shilo, Hana alinyanyuka. Wakati huo Eli, kuhani alikuwa amekaa juu ya kiti chake mlangoni kuelekea nyumba ya BWANA.
\v 10 Hana alijawa na uchungu sana; akamwomba BWANA na akalia mno.
1 Samweli 1: 11
\s5
\v 11 Aliweka nadhili na kusema, "BWANA wa majeshi, kama utalitazama teso la mjakazi wako na kunikumbuka, na usipomsahau mjakazi wako, na kumpatia mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo nitamtoa huyo mtoto kwa BWANA siku zote za maisha yake, na wembe hautapita juu ya kichwa chake kamwe".
\s5
\v 12 1 Samweli 1: 12-14 Hana kiendelea kuomba mbele za BWANA, Eli alikitazama kinywa chake.
\v 13 Hana aliongea moyoni mwake. Midomo yake ilitikisika, lakini sauti yake haikusikika. Hivyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
\v 14 Eli akamwambia, "Utakuwa mlevi mpaka lini? Weka mbali divai yako."
1 Samweli 1: 15-16
\s5
\v 15 Hana akajibu, "Sivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni. Sijanywa divai wala kinywaji chochote cha kulevya, bali nimekuwa nikiimimina nafsi yangu mbele za BWANA."
\v 16 Usimchukulie mjakazi wako kama mwanamke duni; nimekuwa nikiongea kutokana na maumivu na masikitiko yangu."
1 Samweli 1: 17- 18
\s5
\v 17 Kisha Eli alimjibu na kusema, "Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akupatie kile ulichomuomba."
\v 18 Hana akasema, " Na mjakazi wako apate kibali machoni pako." Ndipo huyo mwanamke alienda zake na kula chakula na hakuhuzunika tena.
1 Samweli1: 19- 20
\s5
\v 19 Waliamka asubuhi na mapema wakaenda wakamtukuza BWANA, na baadaye walirudi nyumbani kwao Rama. Elikana alilala na mke wake Hana, na BWANA akamkumbuka.
\v 20 Baada ya muda fulani, Hana alibeba mimba na akazaa mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli, akasema, "Kwa sababu huyu nilimuomba kutoka kwa BWANA."
1 Samweli 1: 21-23
\s5
\v 21 Mara nyingine, Elikana na nyumba yake, walipanda kwenda kumtolea BWANA dhabihu ya Mwaka na kuondoa nadhiri yake.
\v 22 Lakini Hana hakwenda huko; alikuwa amekwisha mwambia mmewe, "Sitaenda huko hadi mtoto aache kunyonya; ndipo nitamleta, ili ahudhurie mbele za BWANA na akae huko daima."
\v 23 Mme wake Hana, Elikana, akamwambia, "Fanya yale yakupendezayo. Ngojea hadi utakapokuwa umemwachisha kunyonya; BWANA aweze peke yake kuthibitisha neno lake." Hivyo yule mwanamke alibaki akimnyonyesha mtoto wake mpaka pale alipomwachisha ziwa.
1 Samweli 1: 24-25
\s5
\v 24 Alipokuwa amemwachisha kunyonya, alimbeba, akimchukua pamoja ng'ombe dume wa miaka mitatu, unga kama kilo thelathini na chupa ya mvinyo, akampeleka katika nyumba ya BWANA huko Shilo. Na mtoto huyo alikuwa bado mdogo.
\v 25 Walimchinja yule ng'ombe, na wakamkabidhi mtoto kwa Eli.
1 Samweli 1: 26-28
\s5
\v 26 Akasema, "Ee bwana wangu! Kama uishivyo, bwana wangu, Mimi ndiye yule mwanamke niliyesimama hapa karibu nawe nikimwomba BWANA.
\v 27 Niliomba kwa ajili ya mtoto huyu na BWANA akawa amenijibu ombi la dua yangu nililomwomba.
\v 28 Nami nimemtoa kwa BWANA; kwa maisha yake yote, nimempa BWANA." Ndipo Elikana na familia yake wakamtukuza BWANA huko Shilo.
\s5
\c 2
\p 1 Samweli 2: 1-1
\v 1 Hana aliomba akasema, "moyo wangu wamtukuza BWANA. Pembe yangu imejulikana katika BWANA. Kinywa changu kinatamba dhidi ya maadui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako.
1 Samweli 2: 2-2
\s5
\v 2 Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA, kwa kuwa hakuna mwingine zaidi yako; hakuna mwamba kama Mungu wetu.
1 Samweli 2: 3-4
\s5
\v 3 Msijivune sana hivyo kwa kiburi; vinywa vyenu visitoke majivuno. Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa; yeye huyapima matendo kwa mizani.
\v 4 Pinde za mashujaa zimevunjika, bali wale wanaojikwaa hujivika nguvu kama mshipi.
1 Samweli 2: 5-5
\s5
\v 5 Wale walio na shibe ya kutosha wamejikodisha ili wapate chakula; wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Hata yule aliye kuwa tasa amezaa watoto saba, bali mwanamke mwenye watoto wengi amenyong'onyea.
1 Samweli 2: 6-7
\s5
\v 6 BWANA huua na huuisha. Hushusha kuzimu na huleta tena juu.
\v 7 BWANA humfanya maskini, na yeye ndiye humtajirisha mtu. Yeye hudhili, lakini pia hukweza
1 Samweli 2: 8
\s5
\v 8 Yeye humwinua juu maskini toka mavumbini: Huwainua wahitaji toka jalalani na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwarithisha kiti cha enzi cha utukufu. Kwa kuwa nguzo za dunia ni za BWANA na ameukalisha ulimwengu juu yake.
1 Samweli 2: 9
\s5
\v 9 Yeye atazilinda nyayo za watu wake waaminifu, bali waovu watanyamazishwa gizani, kwa maana hakuna atayeshinda kwa nguvu zake.
1 Samweli 2: 10-10
\s5
\v 10 Wale wampingao BWANA watavunjwa vipande vipande; atawapiga radi kutokea mbinguni. BWANA atahukumu miisho ya dunia; atampa nguvu mfalme wake na kuinua pembe ya mtiwa mafuta wake."
1 Samweli 2: 11-11
\s5
\v 11 Nndipo Elikana akenda Rama, nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA machoni pa Eli, kuhani.
1 Samweli 2: 12-14
\s5
\v 12 Basi, watoto wa Eli walikuwa wakorofi. Wao hawakumheshimu BWANA.
\v 13 Desturi ya makuhani na watu ilikuwa kwamba endapo mtu yeyote ametoa dhabihu, mtumishi wa kuhani angekuja akiwa na uma wa meno matatu mkononi mwake, nyama ilipokuwa inatokoswa.
\v 14 Naye angeutia uma huo sufuriani, au birikani au chomboni au chunguni; nyama yote ambayo ingeinuliwa na uma huo ingetwaliwa na kuhani mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokwenda huko.
1 Samweli 2: 15-17
\s5
\v 15 Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, mtumishi wa kuhani alikuja, na kumwambia aliyekuwa akitoa dhabihu, " Tenga nyama ya kuchoma kwa ajili ya kuhani; kwa sababu hataikubali ile ya kutokosa kutoka kwako, bali tu ile mbichi."
\v 16 Ikiwa mtu atamwambia, "Wachome mafuta kwanza, na kisha uchukue kiasi utakacho." Ndipo angesema, "Hapana, utanipatia sasa hivi; la sivyo; Nitaichukua kwa lazima."
\v 17 Dhambi ya vijana hawa ilikuwa mbaya sana mbele za BWANA, kwa sababu waliidharau dhabihu ya BWANA.
1 Samweli 2: 18-19
\s5
\v 18 Lakini Samweli alimtumikia BWANA akiwa mdogo akivaa nguo ya naivera ya kitani.
\v 19 Kila mwaka mama yake alimtengenezea kanzu dogo na kumletea, wakati wakija na mmewe kutoa dhabihu ya kila mwaka.
1 Samweli 2: 20-21
\s5
\v 20 Eli aliwabariki Elikana na mke wake na kusema, "BWANA akupatie watoto zaidi kwa mwanamke huyu kwa sababu ya ahadi yake aliyoitoa kwa BWANA." Baadaye walirudi nyumbani kwao.
\v 21 BWANA alimsaidia tena Hana, akawa amebeba mimba nyingine. Akazaa watoto watatu wa kiume na wa kike wawili. Wakati huo huo mtoto Samweli akakua akiwa mbele za BWANA.
1 Samweli 2: 22-24
\s5
\v 22 Basi Eli alikuwa mzee sana, akayasikia yote ambayo watoto wake walikuwa wakiwafanyia Waisraeli wote, na jinsi walivyotembea na mwanamke aliyekuwa akitumika katika lango la hema ya kukutania.
\v 23 Akawaambia, "Kwa nini mnafanya mambo hayo? Kwa maana nasikia matendo yenu maovu kutoka kwa watu hawa wote."
\v 24 Sivyo hivyo, watoto wangu, maana hii ninayoisikia siyo taarifa njema. Mnawakosesha watu wa BWANA.
1 Samweli 2: 25-26
\s5
\v 25 "Kama mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; Lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea mtu huyo?" Lakini hawakuitii sauti ya baba yao, sababu BWANA alinuia kuwaua.
\v 26 Yule mtoto Samweli aliongezeka umri, na kupata kibali kwa BWANA na kwa watu pia.
1 Samweli 2: 27-28
\s5
\v 27 Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli na kumwambia, "BWANA asema, 'Je, sikujifunua mwenyewe kwa nyumba ya baba zako, walipokuwa Misri utumwani nyumbani mwa Farao?
\v 28 Mimi nilimchagua yeye kutoka makabila yote ya Israeli awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu, na kufukiza uvumba, na kuvaa kanzu ya naivera mbele yangu. Niliwapa nyumba ya baba zako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto.
1 Samweli 2: 29-30
\s5
\v 29 Kwanini basi, unaidharau dhabihu yangu na sadaka ambazo ninazitaka mahali ninapoishi? Kwanini unawaheshimu watoto wako kuliko mimi, kwa kujinenepesha ninyi wenyewe kwa uzuri wa kila sadaka ya watu wangu Israeli?'
\v 30 Maana, BWANA, Mungu wa Isareli, asema, niliahidi kwamba nyumba yako, na nyumba ya baba yako, yawapasa kwenda mbele zangu milele,' Lakini sasa BWANA asema. 'Mambo haya yapishe mbali. nami nisifanye hivi, maana nitawaheshimu wanaoniheshimu, bali wanaonidharau mimi hawatakuwa na thamani.
1 Samweli 2: 31-33
\s5
\v 31 Tazama, siku zinakuja nitakapoondoa nguvu zako na nguvu za nyumba za baba yako, ili kwamba pasije kuwepo mtu mzee katika nyumba yako.
\v 32 Nawe utalitazama hangaiko katika makao yangu. Ingawa Israeli watapewa jambo jema, hapatakuwapo tena mtu yeyote mzee katika nyumba yako.
\v 33 Yeyote miongoni mwenu nisiye mwondoa kutoka madhabahuni pangu, Nitasababisha macho yenu yaanguke, na ita nitasababisha huzuni maishani mwenu. Wanaume wote waliozaliwa katika familia yako watakufa.
1Samweli 2: 34-35
\s5
\v 34 Hii ndiyo itakuwa ishara kwako ambayo itawaijia watoto wako wakiume wawili, juu ya Hofni na Finehasi: Wote wawili watakufa siku moja.
\v 35 Nami nitamwinua juu kuhani wangu mwaminifu atakaye fanya kile kilichomo moyoni mwangu na nafisini mwangu. Nami nitamjengea nyumba madhubuti; naye atakwenda mbele ya mfalme wangu mbarikiwa milele.
1 Samweli 2: 36-36
\s5
\v 36 Kila mmoja aliyebakia nyumbani mwako atakuja na kusujudu mbele ya mtu huyo, akiomba kipande cha fedha na mkate mmoja, naye atasema, "Tafadhali uniajiri katika moja ya nafasi za kuhani ili niweze kula kipande cha mkate'"'
\s5
\c 3
\p 1 Samweli 3: 1- 4
\v 1 Yule mtoto Samweli alimtumikia BWANA chini ya uangalizi wa Eli. Neno la BWANA halikupatikana kwa wingi siku hizo; hapakuwa na maono ya mara kwa mara ya kinabii.
\v 2 Wakati huo, nguvu ya macho ya Eli ilikuwa imefifia kiasi cha kutoweza kuona vizuri, na alikuwa amelala kitandani mwake.
\v 3 Ile taa ya BWANA bado ilikuwa bado inawaka, na Samweli alikuwa amelala katika nyumba ya BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu.
\v 4 BWANA akamwita Samweli, naye akaitika, "Niko hapa"
1 Samweli 3: 5-6
\s5
\v 5 Samweli alimwedea Eli na kusema, "Niko hapa, sababu uliniita." Eli akasema, "Sikukuita; kalale tena." Hivyo Samweli akarudi na kulala.
\v 6 BWANA akamwita tena, "Samweli." Saamweli aliamka tena na kwenda kwa Eli na kusema, Niko hapa, sababu umeniita." Eli akajibu, "Sijakuita, mwanangu; kalale tu tena."
1 Samweli 3: 7- 8
\s5
\v 7 Basi Samweli bado hakuwa na uzoefu kuhusu Bwana, wala hakuwahi kupata ujumbe wowote kutoka kwa BWANA ukifunuliwa kwake.
\v 8 BWANA akamwita tena Samweli kwa mara ya tatu. Samweli alinyanyuka tena na kwenda kwa Eli na kusema, "Niko hapa, sababu uliniita," Ndipo Eli alitambua kwamba BWANA alimwita kijana.
1 Samweli 3: 9-9
\s5
\v 9 Kisha Eli aka, mwambia Samweli, "Nenda ukalale tena; ikiwa atakuita tena, sharti useme, 'Sema, BWANA, maana mtumwa wako anasikiliza."' Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake tena.
1 Samweli 3: 10-11
\s5
\v 10 BWANA alikuja na kusimama; akaita vilevile kama vile mwanzoni, "Samweli, Samweli." Ndipo Samweli akasema, "Nena, kwa sababu mtumwa wako anasikiliza."
\v 11 BWANA akasema na Samweli, "Tazama, Niko tayari kufanya jambo katika Israeli ambalo masikio ya kila mmoja akisikia atashtuka.
1 Samweli 3: 12 -14
\s5
\v 12 Siku hiyo nitatimiza kila kitu nilichokisema dhidi ya Eli kuhusu nyumba yake, kutoka mwanzo hadi mwisho.
\v 13 Nimemwambia kwamba niko tayari kuhukumu nyumba yake mara moja kwa ile dhambi aliyoifahamu, kwa sababu watoto wake walijiletea laana juu yao wenyewe na hakuwazuia.
\v 14 Hii ndiyo sababu nimeapa kwa nyumba ya Eli, kwamba dhambi za nyumba yake hazitasahehewa kwa dhabihu au kwa sadaka kamwe."
1 Samweli 3: 13- 16
\s5
\v 15 Samweli akalala hadi asubuhi; baadaye alifungua milango ya nyumba ya BWANA. Lakini Samweli aliogopa kumwambia Eli kuhusu maono hayo.
\v 16 Kisha Eli akamwita Samweli na kusema, "Samweli, mwanangu." Samweli akasema, "Niko hapa."
1 Samweli 3: 17- 18
\s5
\v 17 Akamuuliza, "Ni neno gani alilokusemesha? Tafadhali usinifiche jambo hilo. Mungu akutendee hivyo na kukuzidishia, endapo utanificha kitu chochote kati ya yote ambayo amesema nawe."
\v 18 Samweli akamweleza kila kitu; hakumficha jambo lolote. Eli akasema, "Ni BWANA. Na afanye linaloonekana jema kwake."
1 Samweli 3: 19-21
\s5
\v 19 Samweli akakua, na BWANA alikuwa pamoja naye na hakuacha kutimiza maneno yake ya unabii.
\v 20 Israeli yote tokea Dani hadi Beersheba walijua kwamba Samweli aliteuliwa kuwa nabii wa BWANA.
\v 21 Naye BWANA alionekana tena huko Shilo, maana alijifunua mwenyewe kwa Samweli huko Shilo kwa neno lake.
\s5
\c 4
\p 1Samweli 4: 1-2
\v 1 Neno la Samweli likawafikia Israeli wote. Basi Israeli wakatoka kupigana dhidi ya Wafilisti. Nao wakaweka kambi hapo Ebenezeri, na Wafilisti waliweka kambi yao huko Afeki.
\v 2 Nao Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita dhidi ya Waisraeli. Vita ilipopamba moto, Israeli ilishindwa na Wafilisti, wakauawa watu wapatao elfu nne kwenye uwanja wa vita.
1 Samweli 4: 3-4
\s5
\v 3 Watu walipokuja kambini, wazee wa Israeli walisema, "Kwa nini BWANA ametushinda leo mbele ya Wafilisti? Hebu tulilete hapa sanduku la ushuhuda wa BWANA kutoka Shilo, ili kwamba liwe hapa pamoja nasi, ili litufanye tuwe salama kutokana na nguvu za maadui zetu."
\v 4 Hivyo waliwatuma watu huko Shilo; kutokea huko walilibeba sanduku la ushuhuda wa BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi. Hofni na Finehasi, watoto wawili wa Eli, walikuwapo pamoja na lile sanduku la ushuhuda wa Mungu.
1 Samweli 4: 5-6
\s5
\v 5 Sanduku la ushuhuda wa BWANA lilipofika kambini, watu wote wa Israeli walipiga yowe, na nchi ikavuma.
\v 6 Wafilisti waliposikia kelele za mayowe, wakasema, "sauti hii ya mayowe katika kambi ya Waebrania inamaanisha nini?" Baadaye walitambua kwamba sanduku la BWANA limefika kambini.
1 Samweli 4: 7-9
\s5
\v 7 Wafilisti waliogopa sana, "Mungu ameingia kambini." Wakasema, "Ole wetu! Jambo kama hili halijawahi kutokea huko nyuma!
\v 8 Ole wetu! Ni nani atatulinda dhidi ya nguvu za Mungu mwenye uwezo? Huyu ndiye Mungu aliyewashambulia Wamisri kwa aina tofauti za mapigo mengi jangwani.
\v 9 Enyi Wafilisti, iweni hodari, na fanyeni kiume, vinginevyo mtakuwa watumwa wa Waebrabia, kama walivyokuwa watumwa wenu. Fanyeni kiume, na piganeni nao."
1 Samweli 4: 10-11
\s5
\v 10 Wafilisti walipigana, na Waisraeli wakashindwa. Kila mtu alikimbilia nyumbani kwake, na mauaji yalikuwa makubwa sana; maana askari wa Israeli elfu thelathini waendao kwa miguu vitani, walianguka.
\v 11 Lile sanduku la Mungu lilichukuliwa, na watoto wa Eli, Hofni na Finehasi waliuawa.
1 Samweli 4: 12-13
\s5
\v 12 Mtu mmoja wa Benjamini alikimbia kutoka uwanja wa vita akaja Shilo siku iyo hiyo, aliwasili na mavazi yake yamechanika na matope kichwani pake.
\v 13 Alipofika, Eli alikuwa amekaa kitini pake karibu na barabara akitazama kwa sababu moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kutoa taarifa, mji wote ulilia.
1 Samweli 4: 14-15
\s5
\v 14 Eli aliposikia kelele ya kilio kile, alisema, "Kilio hicho kina maana gani?" Kwa haraka mtu yule alikuja na kumweleza Eli.
\v 15 Basi Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane; macho yake yamepofuka, na hakuweza kuona.
\s5
\v 16 Yule mtu akamwambia Eli, "Mimi ndiye nimechomoka kutoka vitani. Nimetoroka kutoka kwenye mapigano leo." Eli akasema, "Mambo yalienda namna gani, mwanangu?"
\v 17 Yule mtu aliyeleta hizo habari alijibu na kusema, "Israeli wamewakimbia Wafilisti. Pia watu wengi wameuwawa. Watoto wako, Hofni na Finehasi, wamekufa, na sanduku la Mungu limechukuliwa."
1 Samweli 4: 18-18.
\s5
\v 18 Alipotamka sanduku la Mungu, Eli alianguka chali kutoka kwenye kiti chake karibu na mlango. akavunjika shingo lake, na kufariki, kwa sababu alikuwa mzee tena mzito. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka arobaini.
1 Samweli 4: 19-20
\s5
\v 19 Basi mkwewe, mke wa Finihasi, alikuwa mjamzito akikaribia kujifungua. aliposikia habari kwamba sanduku la Mungu limetekwa nyara na kwamba baba mkwe na mme wake wamefariki, alichuchumaa chini akajifungua, lakini utungu wake ulimzidi na ulimtaabisha sana.
\v 20 Alipokaribia kufariki, wanawake waliokuwa wakimhudumia walisema, "Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume." Lakini hakuwajibu lolote au kuzingatia alichoambiwa.
1 Samweli 4: 21-22
\s5
\v 21 Akamwita mtoto Ikabodi, akisema, "Utukufu umetoweka Israeli!" Kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyara, na kwa sababu ya kifo cha baba mkwe na mme wake.
\v 22 Na alisema, "Utukufu umetoweka kutoka Israeli, kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyala."
\s5
\c 5
\p 1 Sammweli 5: 1-3
\v 1 Basi Wafilisti wakawa wamelitwaa sanduku la Mungu, wakalileta kutoka Ebenezeri hadi Ashdodi.
\v 2 Wafilisti walilichukua sanduku la Mungu, wakalileta ndani ya nyumba ya Dagoni, na wakalikalisha pembeni mwa Dagoni.
\v 3 Watu wa Ashdodi walipoamka mapema siku ya pili, tazama, Dagoni ilianguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA. Hivyo waliichukua Dagoni na kuisimamisha tena katika sehemu yake..
1 Samweli 5: 4-5
\s5
\v 4 Lakini walipoamka mapema kesho yake, tazama, Dagoni alikuwa ameanguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA. Kichwa cha Dagoni na vitanga vyake miwili vilikatika na kulala mlangoni. Kiwiliwili cha Dagoni ndicho kilibaki tu.
\v 5 Na hii ndiyo sababu, makuhani wa Dagoni na yeyote aingiae ndani ya nyumba ya Dagoni, hata leo, hawezi kukanyaga mlango wa Dagoni katika Ashdodi.
1 Samweli 5: 6-7
\s5
\v 6 Mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi. Aliwaangamiza akawatesa kwa majipu, Ashdodi na wilaya zake kwa pamoja.
\v 7 Watu wa Ashdodi walipotambua kilichokuwa kinatokea, walisema, "Sanduku la Mungu wa Israeli lisikae kwetu, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya mungu wetu Dagoni."
1 Samweli 5: 8-9
\s5
\v 8 Basi wakawatuma watu wawakusanye pamoja viongozi wote wa Wafilisti; wakawambia, "Tufanye nini na sanduku la Mungu wa Israeli?" Wakawajibu, "Sanduku la Mungu wa Israeli lihamishwe na kupelekwa Gathi." Basi wakalihamisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli hadi huko Gathi.
\v 9 Lakini baada ya kulipeleka huko, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, ukasababisha machafuko makubwa. Akawatesa watu wa mji huo, wakubwa kwa wadogo; na majipu yakaota juu ya miili yao.
1 Samweli 5: 10-10
\s5
\v 10 Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu hadi Ekroni. Lakini mara tu sanduku la Mungu lilipoingia Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele wakisema, "Wametuletea sanduku la Mungu wa Israeli kutuua sisi na watu wetu."
1 Samweli 5: 11-12
\s5
\v 11 Basi wakawatuma watu wawakusanye pamoja viongozi wote wa Wafilisti; wakawambia, "Lipelekeni mbali sanduku la Mungu wa Israeli, na lirudishwe katika makao yake, ili lisije kutuua sisi na watu wetu." Kwa maana kulikuwa na hofu ya kutisha mjini mwote; Mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.
\v 12 Watu ambao hawakufa waliteswa na majipu, na kilio cha mji kilipanda hadi mbinguni.
\s5
\c 6
\p 1 Samweli 6: 1-2
\v 1 Basi sanduku la BWANA lilikaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba.
\v 2 Ndipo Wafilisti wakawaita makuhani na waganga; wakawaambia, "Tulifanyie nini sanduku la BWANA? Twambieni jinsi ambavyo tunapaswa kulirudisha sanduku katika nchi yake."
1 Samweli 6: 3-4
\s5
\v 3 Makuhani na waganga wakasema, "Kama mtalirudisha sanduku la Mungu wa Israeli, msilipeleke bila zawadi; kwa namna yoyote ile mpelekeeni sadakaa ya hatia. Hapo ndipo mtapona, na mtajua ni kwanini mkono wake hadi sasa haujaondoka juu yenu."
\v 4 Ndipo wakawauliza, "Sadaka ya hatia itakuwa nini kwamba tunampelekea?" Wakawajibu, "Majipu matano ya dhahabu na panya watano wa dhahabu, Idadi hiyo ya watano ni sawa na idadi ya viongozi wa Wafilisti. Kwa sababu tauni ya aina moja iliwashambulia ninyi na viongozi wenu.
1 Samweli 6: 5-6
\s5
\v 5 Kwa hiyo, nilazima mtengeneze mifano ya majipu yenu, na mifano ya panya wenu ambayo huiharibu nchi, na mpeni utukufu Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka juu yenu, kutoka juu ya miungu yenu, na kutoka juu ya nchi yenu.
\v 6 Kwanini mfanye mioyo yenu kwa migumu, kama vile Wamisri na Farao walifanya mioyo yao kuwa migumu? Hicho ni kipindi ambacho Mungu wa Israeli aliwashughilikia sana; Je, Wamisri hawakuwaachilia watu, na wakaondoka?
1 Samweli 6: 7-9
\s5
\v 7 Basi sasa, andaeni mkokoteni mpya pamoja na ng'ombe wawili wake wanaonyonyesha, ambao hawajawahi kufungwa nira. Wafungeni ng'ombe hao kwenye mkokoteni, lakini warudisheni wale ndama wao nyumbani.
\v 8 Kisha lichukueni sanduku la BWANA na kuliweka ndani ya mkokoteni. Wekeni ndani ya kasha yale maumbo ya dhahabu mnayompelekea ambyo ni sadaka ya hatia kando yake. Ndipo mlipeleke lipate kuondoka.
\v 9 Kisha muwe makini; kama litapanda kwenda kwa njia hadi nchini mwake hadi Beth Shemeshi, basi mjue kuwa BWANA ndiye aliyetenda pigo hili kubwa. Lakini kama halitakwenda, ndipo tutajua kwamba siyo mkono wake uliotupatia mateso; badala yake tutajua kuwa yaliyotupata ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu.
1 Samweli 6: 10-12
\s5
\v 10 Watu hao wakafanya kama walivyoambiwa, walichukuwa ng'ombe wawili wanaonyonyesha, wakawafunga kwenye mkokoteni, na kuwabakiza ndama wao nyumbani.
\v 11 Wakaliweka sanduku la BWANA juu ya mkokoteni, pamoja na lile kasha lililobeba panya wa dhahabu na yale maumbo ya majipu yao.
\v 12 Hao ng'ombe waliondoka moja kwa moja kuelekea Beth Shemeshi. Walikwenda kwa kuifuata nija moja kuu, wakiteremka walipokuwa wakienda, na hwakugeuka upande wa kushoto au kulia. Viongozi wa Wafilisti walifuata kwa nyuma hadi mpaka wa Beth Shemeshi.
1 Samweli 6: 13-13
\s5
\v 13 Nao watu wa Beth Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao katika bonde. Waliponyanyua macho yao juu na kuliona sanduku, wakafurahi.
\s5
\v 14 Huo mkokoteni ulifikia ndani ya shamba la Yoshua wa Beth Shemeshi na ukasimama hapo. Kulikuapo jiwe kubwa mahali hapo, wakatayarisha kuni kutokana na mkokoteni huo, na wakawatoa ng'ombe hao kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya BWANA.
\v 15 Walawi walilitelemsha sanduku la BWANA chini pamoja na kasha lake lililoyatunza yale maumbo ya dhahabu, wakaweka vitu hivyo juu ya hilo jiwe kubwa. Watu wa Beth Shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa na kutoa dhabihu kwa BWANA siku iyo hiyo.
1 Samweli 6: 16-16
\s5
\v 16 Hao viongozi watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo.
1 Samweli 6: 17-18
\s5
\v 17 Haya ndiyo majipu ya dhahabu ambayo Wafilisti walirudisha kama sadaka ya hatia kwa BWANA: moja kwa ajili ya Ashdodi, moja kwa Gaza, moja kwa Ashkeloni, moja kwa Gathi, na moja kwa Ekroni.
\v 18 Idadi ya wale panya wa dhahabu ilikuwa sawa na ile ya idadi ya miji yote ya Wafilisti inayomilikiwa na viongozi watano, kwa miji iliyojengewa maboma na vijiji vya mashambani. Lile jiwe kubwa, ambalo kando yake waliweka sanduku la BWANA, lipo kama ushuhuda hadi leo katika shamba la Yoshua Mbeth- Shemeshi.
1 Samweli 6: 19-20
\s5
\v 19 BWANA akawashambulia baadhi ya watu wa Bethi Shemeshi kwa sababu walichungulia ndani ya sanduku lake. Aliwaua watu sabini. Watu wakaomboleza, kwa sababu BWANA aliwapa watu pigo kubwa mno.
\v 20 Watu wa Bethi Shemeshi wakasema, "Ni nani mwenye uwezo wa kushindana na BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na atampandia nani akitoka kwetu."" Je, ni nani awezaye kusimama mbele ya BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na ni kwa nani ambako sanduku litaenda likitoka hapa."
1 Samweli 6: 21-21
\s5
\v 21 Wakawatuma wajumbe kwenda kwa wenyeji wa Kiriath Yearimu, wakisema, "Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; teremkeni na mkalipeleke kwenu."
\s5
\c 7
\p 1 Samweli 7: 1-2
\v 1 Watu wa Kiriath Yearimu walikuja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu mlimani iliyokuwa kilimani. Wakamteua Eleazari, mwanawe, kulitunza sanduku la BWANA.
\v 2 Tangu siku ambayo sanduku lilikaa huko Kiiriath Yearimu, ulipita muda mrefu, miaka ishirini. Nyumba yote ya Israeli iliomboleza na ikaazimu kumrudia BWANA.
\s5
\v 3 Samweli akawaambia watu wote wa Israeli, "Kama mtamrudia BWANA kwa moyo wenu wote, mkaiondoa miungu migeni na Ashtorethi kutoka katikati yenu, igeuzeni mioyo yenu kwa BWANA, na mwabuduni yeye peke yake, ndipo atawaokoa kutoka mkono wa Wafilisti."
\v 4 Ndipo watu wa Israeli wakamuondoa Baali na Ashtorethi, na wakamwabudu BWANA peke yake.
1 Samweli 7: 5-6
\s5
\v 5 Ndipo Samweli akasema, "Waleteni Israeli wote hadi Mizpa, nami nitamwomba BWANA kwa ajili yenu."
\v 6 Wakakusanyika Mispa, wakateka maji na kuyamwaga chini mbele za BWANA. Siku hiyo walifunga na kusema, "Tumemfanyia BWANA dhambi." Hapo Mispa ndipo Samweli aliwaamu na kuwaongoza watu wa Iraeli.
1 Samweli 7: -7-8
\s5
\v 7 Basi Wafilisti waliposikiakwamba Waisraeli wamekusanyika hapo Mispa, viongozi wa Wafilisti waliwashambulia Israeli. Waisraeli waliposikia hivyo, waliwaogopa Wafilisti.
\v 8 Ndipo Waisraeli wakamwambia Samweli, "Usiache kumwomba BWANA Mungu wetu kwa ajili yetu, ili atuokoe kutoka mkono wa Wafilisti."
1 Samweli 7: 9-9
\s5
\v 9 Samweli alimchukua kondoo mchanga nakumtoa sadaka ya kuteketezwa kikamilifu kwa BWANA. Ndipo Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli, na BWANA akamjibu.
1 Samweli 7: 10-11
\s5
\v 10 Hata Samweli alipokuwa akitoa sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu kuwashambulia Israeli; lakini BWANA alipiga kwa nguromo ya sauti kubwa siku hiyo dhidi ya Wafilisti na kuwatia kiwewe, na wakashindwa mbele ya Israeli.
\v 11 Waisraeli wakaondoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti na kuwaua hadi kufika chini ya Beth kari.
1 Samweli 7: 12-12
\s5
\v 12 KIsha Samweli akachukua jiwe akalisimamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita hilo jiwe Ebeneza, akisema, "Hata sasa BWANA ametusaidia."
1 Samweli 7: 13-14
\s5
\v 13 Kwa hiyo, Wafilisti walishindwa na hawakuingia katika mipaka ya Israeli. Mkono wa BWANA uliwalemea Wafilisti siku zote za Samweli.
\v 14 Miji ambayo Wafilisti waliitwaa kutoka kwa Israeli ilirudishwa, kutokea Ekroni hadi Gathi; Israeli ikarudisha tena sehemu za nchi zake kutoka kwa Wafilisti. Ndipo ikawa amani kati ya Israeli na Waamori.
1 Samweli 7: 15-17
\s5
\v 15 Samweli akawa mwamuzi wa Israeli siku zote za maisha yake.
\v 16 Kila mwaka alienda Betheli kwa kuzunguka, akienda Gilgali, na huko Mispa.
\v 17 Kisha angerudi Rama, kwa sababu mji wake ulikuwa huko; na huko pia aliwaamua Waisiraeli. Hata huko Rama, pia alimjengea BWANA madhabahu.
\s5
\c 8
\p 1 Samweli 8: 1-3
\v 1 Samweli alipozeeka, aliwaweka watoto wake wawe waamuzi juu ya Israeli.
\v 2 Mtoto wake wa kwanza aliitwa Yoeli, na mtoto wake wa pili aliitwa Abiya. Hawa walikuwa waamuzi katika Bersheba.
\v 3 Watoto wake hawakuenenda katika njia za baba yao, bali walipiga mbio kutafuta mapato ya udhalimu. Walipokea rushwa na na kupotosha hukumu.
1 Samweli 8: 4-5
\s5
\v 4 Ndipo wazee wote wa Israeli walikutana pamoja na kumwendea Samweli huko Rama.
\v 5 Wakamwambia, "Angalia, wewe umekuwa mzee, na watoto wako hawaenendi katika njia zako. Tuchagulie mfalme wakutuamua kama yalivyo mataifa yote."
1 Samweli 8: 6-7
\s5
\v 6 Lakini haikumpendeza Sameli waliposema, "Utupatie mfalme wa kutuamua." Hivyo akamwomba BWANA.
\v 7 Na BWANA akamwambia Samweli, "Sikiliza sauti ya watu kwa kila jambo wanalokwambia; kwa sababu hwajakukataa wewe, bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.
1 Samweli 8: 8-9
\s5
\v 8 Sasa wanafanya kama vile walivyotenda tangu siku ile nilipowatoa huko Misri, kwa kuniacha, na kuwatumikia miungu mingine, na ndivyo hivyo pia wanakufanyia na wewe.
\v 9 Basi sasa uwasikilize; lakini uwaonye sawasawa na uwafahamishe tabia ya mfalme atakaye waongoza.
1Samweli 8: 10-12
\s5
\v 10 Kwa hiyo Samweli akawaambia watu waliokuwa wakiomba mfalme maneno yote ya BWANA.
\v 11 Akasema, "Hivi ndivyo jinsi mfalme atakavyowatawala.
\v 12 Atawachukua watoto wenu wa kiume na kuwaweka juu ya magari ya vita na kuwa wapanda farasi wake, na kukimbia mbele ya magari yake. Atawaweka ma- kapteni wake juu ya maelfu ya askari, na ma-kapteni juu ya askari hamsini. Wengine atawafanya wakulima wamashamba yake, wengine wavunaji wa mazao yake, wengine watatengeneza silaha zake na zana za magari yake.
1Samweli 8: 13-15
\s5
\v 13 Naye atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi, na waoka mikate.
\v 14 Atachukua mashamba yenu mazuri, mashamba ya mizabibu, na yale ya mizeituni na kuwapa watumishi wake.
\v 15 Atachukua moja ya kumi ya nafaka zenu na mizabibu na na kuwapa maofisa na watumishi wake.
1 Samweli 8: 16-18
\s5
\v 16 Atawachukua watumwa wenu na wajakazi wenu na vijana wenu waliowazuri na punda wenu; atawatumikisha wote kwa ajili yake.
\v 17 Atawatoza moja ya kumi ya mifugo yenu, na mtakuwa watumwa wake.
\v 18 Ndipo mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyemchagua kwa ajili yenu; lakini siku ile BWANA hatawajibu
1 Samweli 8: 19-20
\s5
\v 19 Lakini watu walikataa kumsikiliza Samweli; wakasema, "Hapana!" Lazima awepo mfalme juu yetu.
\v 20 Ili tuweze kuwa kama mataifa mengine yote, na hivyo mfalme wetu aweze kutuamua na atoke mbele yetu na atupiganie vita yetu.
1 Samweli 8: 21-22
\s5
\v 21 Naye Samweli aliposikia maneno yote ya watu, akayarudia katika masiko ya BWANA.
\v 22 BWANA akamwambia Samweli, "Sikiliza sauti yao na uwafanyie mfalme." Hivyo Samweli akawaambia watu wa Israeli, "Kila mtu na arudi mjini kwake."
\s5
\c 9
\p Samweli 9: 1-2
\v 1 Basi kulikuwa na mtu mmoja kutoka Benyamini, mtu mashuhuri. Jina lake aliitwa Kishi mwana wa Abieli, mwana wa Zerori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini.
\v 2 Huyu alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Sauli, kijana mzuri wa uso. Hapakuwapo mwanaume mzuri wa uso kuliko huyu miongoni mwa watu wote wa Israeli. Kutoka mabegani kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wengine.
1 Samweli 9: 3-4
\s5
\v 3 Na punda wa Kishi, baba yake na Sauli walipotea. hivyo Kishi akamwambia Sauli mwanawe, "Mchukue mmoja wa watumishi; uamke uende kuwatafuta punda,"
\v 4 Sauli akapita katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu na akaenda akapita katika nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona. Kisha walipita katika nchi ya Shaalimu, lakini hawakuwa huko. Baadaye alipita katika nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwaona wale punda.
1 Samweli 9: 5-6
\s5
\v 5 Na walipofika nchi ya Sufu, Sauli alimwambia mtumishi wake aliyekuwa naye, "Njoo na turudi, pengine baba aweza kuacha kuchunga punda na kuanza kutuhofia sisi."
\v 6 Lakini mtumishi akamwmbia, "Sikiliza, Yupo mtu wa Mungu katika mji huu. Naye ni mtu wa kuheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Hebu twende huko; labda anaweza kutuambia tupitie wapi katika safari yetu."
1 Samweli 9: 7-8
\s5
\v 7 Ndipo Sauli akamwambia mtumish iwake, "Lakini kama tukienda kwake, twaweza kumpelekea nini? Maana hata mkate katika mfuko wetu umekwisha, na hakuna zawadi ya kumpelekea mtumishi wa Mungu. Tuna kitu gani?
\v 8 Huyo mtumishi akamjibu Sauli na kusema, "Hapa, ninayo robo ya shekeli ya fedha ambayo nitampa mtumishi wa Mungu, atuambie ni njia ipi yatupasa tuiendee."
1 Samweli 9: 9-11
\s5
\v 9 (Zamani katika Israeli, mtu alipotaka kujua neno kuhusu mapenzi ya Mungu, alisema, "Njoo, haya twende kwa mwonaji." Kwa maana nabii wa leo, zamani aliitwa Mwonaji).
\v 10 Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, "Umesema vyema. Haya, njoo twende." Basi wakaenda katika mji ambao mtu wa Mungu alikuwamo.
\v 11 Walipopanda mlima kuelekea mjini, walikutana na wasichana wakienda kuteka maji; Sauli na mtumishi wake wakawauliza, "Mwonaji hupo hapa?"
1 Samweli 9: 12-13
\s5
\v 12 Nao wakawajibu, na kusema, "Yupo; tazameni, yuko mbele yenu. Harakisheni, kwa maana anakuja mjini leo, sababu leo watu wanatoa dhabihu zao mahali pa juu.
\v 13 Mara tu mtakapoingia mjini mtamuona, kabla hajapanda mahali pa juu kla chakula. Watu hawatakula hata atakapokuja, kwa sababu ndiye ataibariki dhabihu; na baadaye wale ambao wamealikwa hula. Basi pandeni, mtamuona sasa hivi."
1 Samweli 9: 14-14
\s5
\v 14 Kwa hiyo walikwea kwenda mjini. Walipokuwa wakiingia mjini, walimuona Samweli akija mbele yao, akipanda kwenda mahali pa juu.
1 Samweli 9: 15-16
\s5
\v 15 Siku moja kabla Sauli hajafika, BWANA alikuwa amemfunulia Samweli:
\v 16 "Kesho wakati kama huu nitakutumia mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe utamtia mafuta awe mfalme juu ya watu wangu Israeli. Atawaokoa watu wangu kutoka mkono wa Wafilisti. Kwa kuwa nimewaonea huruma watu wangu na kilio cha kutaka msaada kimenifikia."
1 Samweli 9: 17-19
\s5
\v 17 Samweli alipomuona Sauli, BWANA akamwambia, "Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu."
\v 18 Ndipo Sauli akaja karibu na Samweli katika lango na kusema, "Niambie nyumba ya Mwonaji iko wapi?
\v 19 Samweli akamjibu Sauli akisema, "Mimi ndiye mwonaji. Tangulia mbele hadi mahali pa juu, nami nitakueleza kila kitu kilichomoyoni mwako.
1 Samweli 9: 20-21
\s5
\v 20 Kama punda wenu waliopotea siku tatu zilizopita, msihofu kuhusu hao punda, kwa kuwa wamekwishapatikana. Na yote yaliyotamanika kwa ajili ya Israeli yanamwangukia nani? Siyo kwako na nyumba ya baba yako yote?"
\v 21 Sauli akamjibu na kusema, Siyo mimi Mbenyamini, kutoka kabila lililo dogo sana kwa makabila ya Israeli? Siyo ukoo wangu ulio mdogo sana kwa kabila la Benyamini? Kwa nini basi unaniambia kwa namna hii?"
1 Samweli 9: 22-22
\s5
\v 22 Hivyo Samweli akamchukua Sauli na mtumishi wake, akawaingiza ukumbini, akawakalisha mahali pa heshima pa wale walioalikwa, idadi yao takribani watu thelathini.
1 Samweli 9: 23-24
\s5
\v 23 Samweli akamwambia mpishi, "Lete sehemu niliyokupatia, sehemu ambayo nilikwambia hivi, "Itenge."'
\v 24 Basi mpishi alichukua paja lililokuwa limeinuliwa katika dhabihu na kile kilichokuwa pamoja nalo, akaitenga mbele ya Sauli. Kisha Samweli akasema, "Angalia kile kilichokuwa kimetunzwa kwa ajili yako! Kula, kwa sababu kilitunzwa hadi wakati maalum ufike kwa ajili yako. Na kwa sasa waweza kusema, 'Nimewaalika watu."' Kwa hiyo Sauli alikula pamoja na Samweli siku hiyo.
1 Samweli 9: 25-26
\s5
\v 25 Walipokuwa wamekwisha shuka chini kutoka sehemu ya juu na kuingia mjini, Samweli akazungumza na Sauli darini.
\v 26 Na kulipopambazuka, Samweli alimwita Sauli darini na kusema, "Amka, kusudi nikusindikize uende zako," Hivyo Sauli aliamka, na wote wawili, yeye na Samweli walitoka kwenda mtaani.
1 Samweli 9: 27-27
\s5
\v 27 Walipokuwa wakienda nje ya viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, "Mwambie mtumishi wako atanguliye mbele yetu(na alitangulia mbele), Lakini wewe sharti usubiri kidogo, nipate kukuambia ujumbe wa Mungu."
\s5
\c 10
\p 1 Samweli 10: 1-2
\v 1 Ndipo Samweli akachukua chupa ya mafuta, akayamimina juu ya kichwa cha Sauli, na akambusu. Akasema, "Je, Mungu hajakutia mafuta uwe mtawala juu ya urithi wake?
\v 2 Utakapoondoka kwangu leo, utawaona wanaume wawili na kaburi la Raheli, katika nchi ya Benyamini hapo Selsa. Watu hao watakuambia, 'Wale punda mliokuwa mkiwatafuta wamepatikana. Sasa, Baba yako ameacha kuwatunza punda, na ana hofu juu yenu, anasema, "Nitafanya nini kuhusu mwanangu?"
1 Samweli 10: 3-4
\s5
\v 3 Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na utafika katika mwaloni wa Tabori. Utakutana na watu watatu hapo wakienda kwa Mungu huko Betheli, mmoja akibeba wana-mbuzi watatu, mwingine akibeba mikate mitatu, na mwingine akibeba kiriba cha divai.
\v 4 Watawasalimu na watawapatia mikate miwili, kutoka mikononi mwao.
1 Samweli 10: 5-6
\s5
\v 5 Baada ya hayo, utafika katika mlima wa Mungu, mahali ilipo ngome ya Wafilisti. Utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakiteremka chini kutoka mahali pa juu wakiwa na kinanda, tari, kinubi na filimbi mbele yao; na watakuwa wakitabiri.
\v 6 Roho ya BWANA itakujaza, nawe utatabiri pamoja nao, na utabadilishwa na kuwa mtu tofauti.
1 Samweli 10: 7-8
\s5
\v 7 Basi, ishara hizi zikikufikia, fanya lolote ambalo mikono yako itaona ifanye, kwa sababu Mungu yu pamoja nawe.
\v 8 Nenda ushuke mbele yangu hadi Gilgali. Kisha nitakufuata huko nitoe dhabihu za kuteketezwa na kutoa dhabihu za amani. Nisubiri kwa muda wa siku saba hadi nije kwako na nikuoneshe unachopaswa kufanya."
1 Samweli 10: 9-10
\s5
\v 9 Sauli alipotega mgongo amuache Samweli, Mungu akampa moyo mwingine. Ndipo ishara zote hizi zikatimia siku hiyo.
\v 10 Walipofika mlimani, kundi la manabii lilikutana naye, na Roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu ili atabiri pamoja nao.
\s5
\v 11 Kila mtu aliyemfahamu kabla hajamwona akitabiri pamoja na manabii, watu waliambizana wao kwa wao,:"Kitu gani kimempata mtoto wa Kishi? Hivi Sauli ni mmoja wa manabii siku hizi?"
\v 12 Mtu mmoja kutoka eneo hilo akajibu, "Na ni nani baba yao?" Kwa sababu ya jambo hili, ukawapo msemo, "Hivi Sauli naye ni mmoja wa manabii?"
\v 13 Alipomaliza kutabiri, akafika mahali pa juu.
\s5
\v 14 1 Samweli 10: 14-16 Ndipo baba yake mdogo na akamuuliza Sauli na mtumishi wake, "Mlienda wapi?" Naye akamjibu, "Kuwatafuta punnda; tulipoona kwamba hatuwezi kuwapata, tukaenda kwa Samweli."
\v 15 Baba yake mdogo akasema, "Tafadhali niambie kile alichosema kwako Samweli,"
\v 16 Sauli akamjibu baba yake mdogo, "Alituambia waziwazi kwamba punda wamepatikana." Lakini kuhusu swala la ufalme alilosema Samweli hakumwambia.
1 Samweli 10: 17-19
\s5
\v 17 Basi Samweli aliwaita watu pamoja huko Mispa.
\v 18 Akwaambia watu wa Israeli, "Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli asemavyo: 'Niliwatoa Israeli kutoka Misri, na niliwaokoa kutoka nchi ya Wamisri, na kutoka mkono wa falme zote zilizowaonea.'
\v 19 Lakini leo mmemkataa Mungu wenu, awaokoaye kutoka kwenye majanga na mahangaiko; na mmemwambia, ' Tuwekee mfalme juu yetu,; Sasa jihudhurisheni wenyewe mbele za BWANA kwa kabila na jamaa zenu."
1 Samweli 10: 20-21
\s5
\v 20 Kisha Samweli akawaleta kabila zote za Isareli karibu, na kulichagua kabila la Benyamini.
\v 21 Akawasogeza karibu kabila la Benyamini kwa kufuata jamaa zao; na jamaa ya Wamatri ikachaguliwa; na Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipokwenda kumtafuta, hakuweza kuonekana.
1 Samweli 10: 22-23
\s5
\v 22 Kisha watu walitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, "Bado yupo mtu mwingine ajaye?" BWANA akajibu, " Yeye mwenyewe kajificha kwenye mizigo."
\v 23 Wakaenda mbio na kumleta Sauli kutoka humo. Aliposimama kati yao, alikuwa mrefu kuliko watu wote kuanzia mabega yake kwenda juu.
1 Samweli 10: 24-24
\s5
\v 24 Kisha Samweli akawaambia watu, "Je, mnamuona mtu ambaye BWANA amemchagua? Hakuna mtu kama yeye kati ya watu wote." Watu wote wakapiga Kelele, "Mfalme na aishi"
1 Samweli 10: 25-25
\s5
\v 25 Ndipo Samweli akawaambia watu desturi na sheria za ufalme, akaziandika katika kitabu, na kuziweke mbele za BWANA. Baadaye Samweli akawaruhusu watu waondoke kila mtu aende nyumbani kwake.
1 Samweli 10: 26-27
\s5
\v 26 Sauli pia alienda nyumbani kwake huko Gibea, akiwa na baadhi ya watu wenye nguvu, wenye mioyo iliyoguswa na Mungu.
\v 27 Lakini baadhi ya watu wasiofaa walisema, "Huyu mtu atatuokoaje?" Watu hawa walimdharau Sauli na hawakumletea zawadi zozote. Lakini Sauli alinyamaza kimya.
\s5
\c 11
\p 1 Samweli 11: 1-2
\v 1 Ndipo Nahashi Mwamoni akaenda na kupiga kambi kuzunguka Yabeshi Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, "Fanya mkataba nasi, na tutakutumikia,"
\v 2 Nahashi Mwamoni akawajibu, "Kwa sharti hili nitafanya mkataba na ninyi, kwamba wote niwang'oe macho ya kulia, na kwa kitendo hiki kilete fedheha katika Israeli yote."
1 Samweli 11: 3-3
\s5
\v 3 Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, "Tuache kwa siku saba, ili tuwatume wajumbe katika nchi yote ya Israeli. Ndiposa, kama hakuna mtu wa kutuokoa, tutasalimu amri kwako."
1 Samweli 11: 4-5
\s5
\v 4 Nao wajumbe wakafika Gibea, alipoishi Sauli, na wakawaeleza watu kile kilichotokea. Watu wote wakalia kwa sauti kuu.
\v 5 Na Sauli alikuwa akiwafuata nyuma maksai kutoka shambani. Sauli akauliza, "Watu wamepatwa na nini hadi wanalia?" Ndipo wakamweleza Sauli kile ambacho watu wa Yabeshi walikisema.
1 Samweli 11: 6-8
\s5
\v 6 Sauli aliposikia kile walichosema, Roho ya Mungu ikamjia kwa nguvu, na akakasirika.
\v 7 Akashika nira ya maksai, akawakata hao ng'ombe vipande vipande, na akavituma hivyo vipande katika nchi yote ya Israeli kwa kuwatumia wajumbe, Akasema, "Yeyote asiyejitokeza akimfuata Sauli na Samweli, hivi ndivyo ng'ombe wake watakavyofanywa." Na hofu ya BWANA ikawaingia watu, na wakajitokeza wote kwa pamoja.
\v 8 Alipowahesabu hapo Beseki, watu wa Israeli walikuwa elfu mia tatu, na watu wa Yuda elfu thelathini.
1 Samweli 11: 9-10
\s5
\v 9 Wakawaambia wale wajumbe waliotumwa, "Mtawaambia watu wa Yabeshi Gileadi, 'Kesho, wakati wa jua kali, Mtaokolewa."' Basi wale wajumbe wakaenda na kuwaambia watu wa Yabeshi, na watu wakafurahi.
\v 10 Ndipo watu wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, "Kesho tutasalimu amri kwako, na utaweza kutufanyia chochote unachoona kinakupendeza."
1 Samweli 11: 11-11
\s5
\v 11 Siku iliyofuata Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu. Wakafika katikati ya Kambi wakati wa asubuhi, wakawashambulia na kuwashinda Waamoni ilipofika mchana. Waliosalimika nao walitawanyika, kiasi kwamba hata watu wawili hawakuachwa pamoja.
1 Samweli 11: 12-13
\s5
\v 12 Ndipo watu wakamwambia Samweli, "Wako wapi waliosema, 'Hivi kweli Sauli atatutawala?' Walete watu hao, ili tuwauwe."
\v 13 Lakini Sauli akasema, "Hakuna atakayeuwawa siku ya leo, kwa sababu leo BWANA amemuokoa Isreli."
1 Samweli 11: 14-15
\s5
\v 14 Kisha Samweli akawaambia watu, "Njoni, twendeni Gilgali na tuimarishe ufalme tena huko."
\v 15 Hivyo watu wote wakaenda Gilgali na wakamsimika Sauli kuwa mfalme mbele za BWANA huko Gilgali. Na huko walitoa sadaka za amani mbele za BWANA, na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.
\s5
\c 12
\p 1 Samweli 12: 1-2
\v 1 Samweli aksema na Israeli wote, "Nimesikia kila kitu mlichoniambia, na nimemweka mfalme juu yenu.
\v 2 Basi, yupo hapa mfalme aliyeko mbele yenu, mimi nimezeeka nakujaa mvi; na watoto wangu wako pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu hadi leo.
1 Samweli 12: 3-3
\s5
\v 3 Mimi niko hapa, Nishuhudieni mbele za BWANA na mbele za mtiwa mafuta wake. Nimechukua ng'ombe wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimemdhulumu? Nimemwonea nani? Nimepokea rushwa kutoka mikono ya nani inipofushe macho yangu? Nishuhudieni, nami nitawarudishia
1 Samweli 12: 4-5
\s5
\v 4 Nao wakasema, Haujatudanganya, kutuonea, au kuiba chochote kutoka mkono wa mtu yeyote."
\v 5 Akawaambia, "BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake leo ni shahidi, kwamba hamkuona kitu mkononi mwangu." Na wao wakajibu, "BWANAni shahidi."
1 Samweli 12: 6-7
\s5
\v 6 Samweli akawaambia watu, "BWANA ndiye aliyemteua Musa na Haruni, na ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.
\v 7 Basi sasa, jihudhurisheni, ili niweze kutoa utetezi juu yenu kwa BWANA kuhusu matendo yote ya haki ya BWANA, ambayo aliwafanyia ninyi na baba zenu.
1 Samweli 12: 8-9
\s5
\v 8 Yakobo alipokuwa amefika Misri, na babu zenu walimlilia BWANA. BWANA alimtuma Musa na Haruni, waliowaongoza babu zenu kutoka Misri na wakaja kukaa sehemu hii.
\v 9 Lakini walimsahau BWANA Mungu wao; akawauza katika mkono wa Sisera, jemedari wa majeshi ya Hazori, katika mkono wa Wafilisti, na katika mkono wa mfalme wa Moabu; hawa wote walipigana na babu zenu.
1 Samweli 12: 10-11
\s5
\v 10 Wakamlilia BWANA mkasema, 'Tumefanya dhambi, kwa sababu tumemwacha BWANA na tumewatumikia Mabaali na Mashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya maadui zetu, na tutakutumikia.'
\v 11 Hivyo BWANA akawatuma Yerubu Baali, Bedani, Yefta na Samweli, na akawapa ushindi dhidi ya maadui zenu wote waliowazunguka, na kwamba mliishi kwa amani.
1 Samweli 12: 12-13
\s5
\v 12 Mlipoona kwamba Nahashi mfalme wa watu wa Amoni amekuja dhidi yenu, mkaniambia, 'Hapana! Badala yake, mfalme awepo atawale juu yetu'- ingawa BWANA, Mungu wenu, alikuwa mfalme wenu.
\v 13 Sasa yupo hapa mfalme ambaye mmemchagua, mliyemuomba na ambaye BWANA amemteua awe mfalme juu yenu.
1 Samweli 12: 14-15
\s5
\v 14 Ikiwa mnamhofu BWANA, mtumikieni, muitii sauti yake, msikaidi amri ya BWANA, basi wote wawili ninyi na mfalme anayewatawala mtakuwa wafuasi wa BWANA Mungu wenu.
\v 15 Kama hamtaitii sauti ya BWANA, mkaasi amri za BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya babu zenu.
1 Samweli 12: 16-18
\s5
\v 16 Hata sasa muwepo kabisa na muone jambo kubwa ambalo BWANA atalifanya mbele ya macho yenu.
\v 17 Je, leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, naye ataleta ngurumo na mvua. Ndipo mtajua na kuona kwamba uovu wenu ni mwingi, mlioufanya machoni pa BWANA, kujiombea mfalme wenu ninyi wenyewe."
\v 18 Hivyo Samweli akamwomba BWANA; na siku iyo hiyo BWANA akatuma ngurumo na mvua. Ndipo watu wote wakamwogopa sana BWANA pamoja na Samweli.
1 Samweli 12: 10-21
\s5
\v 19 Kisha watu wote wakamwambia Samweli, "Waombee watumishi wako kwa BWANA Mungu wako, ili tusife. Kwa maana tumeongeza uovu huu juu ya dhambi zetu tulipojiombea mfalme sisi wenyewe."
\v 20 Samweli akawajibu, "Msiogope. Mmefanya uovu wote huu, lakini msigeukie mbali na BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa moyo wenu wote.
\v 21 Wala msigeuke na kufuata mambo matupu yasiyo na faida au kuwaokoa, kwa sababu ni ubatili.
1 Samweli 12: 22-23
\s5
\v 22 Kwa ajili ya jina lake kuu, BWANA hatawakataa watu wake, kwa sababu imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu kwa ajili yake.
\v 23 Kwangu mimi, iwe mbali nami kumtenda BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi. Badala yake, nitawafundisha njia iliyo njema na sahihi.
1 Samweli 12: 24-25
\s5
\v 24 Mcheni BWANA tu na mtumikieni yeye katika kweli kwa moyo wenu wote. Tafakarini mambo makuu aliyowatendeeni.
\v 25 Lakini kama mtadumu kufanya uovu, ninyi wote na mfalme wenu mtaangamizwa."
\s5
\c 13
\p 1 Samweli 13: 1-2
\v 1 Sauli alikwa na umri wa miaka [thelathini] alipoanza kutawala; alipokuwa ametawala Israeli kwa miaka [arobaini],
\v 2 aliwachagua wanaume elfu tatu wa Israeli. Elfu mbili walikuwa pamoja naye huko Mikmashi na katika nchi ya milima ya Betheli, wakati huo wale elfu moja walikuwa pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini. Askari waliobaki aliwarudisha nyumbani, kila mtu hemani kwake.
1 Samweli 13: 3-4
\s5
\v 3 Yonathani akaishinda ngome ya jeshi la Wafilisti iliyokuwa Geba na Wafilisti wakasikia habari hiyo. Baadaye Sauli alipiga tarumbeta katika nchi yote, akisema, "Sikieni enyi Waebrania."
\v 4 Israeli yote imesikia kwamba Sauli ameipiga ngome ya Wafilisti, na pia kwamba Israeli imekuwa uvundo kwa Wafilisti. Ndipo askari wakaitwa kwa pamoja kuungana na Sauli huko Gilgali.
\s5
\v 5 Wafilisti walijikusanya pamoja kupigana dhidi ya Waisraeli: magari elfu tatu, watu elfu sita wakuendesha magari, na majeshi mengi kama mchanga ufukoni mwa bahari. Wakapanda na kupiga kambi huko Mikimashi, mashariki mwa Beth aveni.
1 Samweli 13: 6-7
\s5
\v 6 Watu wa Israeli walipoona kuwa wapo katika matatizo -kwa maana watu walikata tamaa, wakajificha kwenye mapango, kwenye vichaka, kwenye miamba, kwenye visima na katika mashimo.
\v 7 Baadhi ya Waebrania walipanda kwenda Yordani katika nchi ya Gadi na Gileadi. Lakini Sauli alibaki Gilgali, na watu waliomfuata wakitetemeka.
1 Samweli 13: 8-10
\s5
\v 8 Alisubiri kwa siku saba, muda uliopangwa na Samweli. Lakini Samweli hakufika huko Gilgali, na watu wakatawanyika mbali na Sauli.
\v 9 Sauli akasema, "Nileteeni sadaka ya kuteketezwa na sdaka ya amani." Kisha akatoa sadaka ya kuteketezwa.
\v 10 Mara tu alipomaliza kutoa sadaka ya kuteketezwa Samweli akawasili. Sauli akatoka nje wakutane na kumsalimia.
1 Samweli 13: 11-12
\s5
\v 11 Basi Samweli akasema, "Umefanya nini?" Sauli akajibu, "Nilipoona kwamba watu wanaiacha, na kwamba umechelewa hukufika kwa muda uliopangwa, na kwamba Wafilisti wamekwisha jikusanya huko Mikmashi,
\v 12 nikasema, 'Sasa Wafilisti watashuka dhidi yangu huko Gilgali, na sijaomba kibali cha BWANA.' Kwa hiyo nikajilazimisha mwenyewe kutoa sadaka ya kuteketezwa."
1 Samweli 13: 13-14.
\s5
\v 13 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, "Umetenda mambo ya kipumbavu. Hukuheshimu amri ya BWANA Mungu wako aliyokupatia. Kwa maana BWANA angeutengeneza utawala wako juu ya Israeli milele.
\v 14 Lakini sasa utawala wako hautaendelea. BWANA ametafuta mtu anayekubaliwa na moyo wake, kwa sababu wewe hukutii alichokuamuru."
1 Samweli 13: 15-16
\s5
\v 15 Ndipo Samweli akasimama akapanda kutoka Gilgali hadi Gibea ya Benyamini. Basi Sauli akawahesabu watu waliokuwapo pamoja naye, idadi yao ilikuwa kama watu mia sita.
\v 16 Sauli, mtoto wake Yonathani, na watu waliokuwa pamoja nao, wakabaki Geba ya Benyamimni. Lakini Wafilisti wakapiga kambi huko Mikmashi.
1 Samweli 13: 17-18
\s5
\v 17 Wateka nyara makundi matatu wakaja kutoka kambi ya Wafilisti. Kundi moja likapinda kuelekea Ofra, hadi nchi ya Shuali.
\v 18 Kundi jingine likageuka kuelekea Bethholoni, na kundi jingine likaelekea katika mpaka kulikabili bonde la Seboimu kuelekea jangwani.
1 Samweli 13: 19-21
\s5
\v 19 Hakuna hata mhunzi aliyeonekana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walisema, " Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki."
\v 20 Lakini Waisraeli wote huwa wakiteremka kwa Wafilisti, kila mtu kunoa jembe lake, sululu yake, shoka lake na mundu wake.
\v 21 Gharama za kunoa ncha za majembe, sululu, mashoka na kunyoosha michokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.
1 Samweli 13: 22-23
\s5
\v 22 Hivyo siku ya vita, hakukuwa na mapanga au mikuki iliyoonekana katika mikono yoyote ya askali waliokuwa na Sauli na Yonathani; Ni Sauli na mtoto wake tu ndio walikuwa nazo.
\v 23 Vikosi vya Wafilisti wakatokeza katika nija ya Mikmashi.
\s5
\c 14
\p 1 Samweli 14: 1-1
\v 1 Siku moja, Yonathani mwana wa Sauli alimwambia mbeba silaha wake aliye mdogo, "Njoo, hebu twende hadi upande mwingine kwenye ngome ya Wafilisti." Lakini hakumjulisha baba yake.
1 Samweli 14: 2-3
\s5
\v 2 Sauli alikuwa akikaa nje ya mji wa Gibea chini ya mti wa mkomamanga ulio katika Migroni. Takribani watu mia sita walikwa pamoja naye,
\v 3 akiwemo Ahiya mwana wa Ahitubu (nduguye Ikabodi) mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, aliyevaa naivera. Watu hao hawakujua kwamba Yonathani ameondoka.
1 Samweli 14: 4-5
\s5
\v 4 Katikati ya vichochoro, ambavyo Yonathani alinuia kuvipita hadi ngome ya Wafilisti, kulikuwa na mwamba wenye mteremko mkali upande mmoja, na mteremko mkali upande mwingine. Jabali moja liliitwa Bosesi, na jingine liliitwa Sene.
\v 5 Lile jabali lenye mteremko mkali zaidi liliinuka upande wa kaskazini mbele ya Mikmashi, na jingine upande wa kusini mbele ya Geba.
1Samweli 14: 6-7
\s5
\v 6 Yonathani akamwambia kijana mbeba silaha, "Njoo, na tuvuke hadi ngome ya hawa wasiotahiriwa. Pengine BWANA atatenda kwa niaba yetu, kwa maana hakuna kitu kiwezacho kumzuia BWANA asiokoe kwa wengi au kwa watu wachache."
\v 7 Mbeba silaha wake akajibu, "Fanya kila kitu kilicho ndani ya moyo wako. Songa mbele, tazama, niko pamoja nawe, nitatii maagizo yako yote."
1 Samweli 14: 8-10
\s5
\v 8 Ndipo Yonathani akasema, "Tutavuka twende kwa watu hao, na tutajionesha wenyewe kwao.
\v 9 Kama watatuambia, 'Subirini hapo hadi tutakapokuja kwenu' - basi tutabaki katika sehemu yetu na hatutavuka kwenda kwao.
\v 10 Lakini kama watajibu, 'Njoni kwetu,' ndipo tutavuka; kwa sababu BWANA amewaweka mkononi mwetu. Hii ndiyo itakuwa ishara yetu."
1 Samweli 14: 11-12
\s5
\v 11 Kwa hiyo wote wawili wakajifunua mbele ya ngome ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, "Angalia, Webrania wanakuja kutokea kwenye mashimo walimojificha."
\v 12 Ndipo watu wa ile ngome wakamwita Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, "Njoni huku kwetu, tutawaonesha jambo fulani." Na Yonathani akamwambia mbeba silaha wake; "Nifuate nyuma yangu, kwa sababu BWANA amewaweka katika mkono wa Israeli."
1 Samweli 14: 13-14
\s5
\v 13 Yonathani alipanda juu kwa mikono na miguu yake, na mbeba silaha akimfuata nyuma yake. Wafilisti waliuwawa mbele ya Yonathani, na mbeba silaha wake akiwaua baadhi nyuma yake.
\v 14 Hilo shambulio la kwanza walilofanya Yonathani na mbeba silaha wake, waliua watu wapatao ishirini katika urefu wa nusu handaki kwenye eka moja ya ardhi.
1 Samweli 14: 151-15
\s5
\v 15 Kukawa na hofu kubwa katika kambi, uwandani, na katika watu. Hata ngome ya jeshi na watekaji nyara nao wakawa na hofu kubwa
1Samweli 14: 16-17
\s5
\v 16 Ndipo walinzi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona kundi la askari wa Wafilisti likitawanyika, wakienda kule na huku.
\v 17 Kisha Sauli akawaambia watu aliokuwa nao, "Mjihesabu ili muone nani hayupo hapa."Walipokuwa wamehesabu, wakagundua kuwa Yonathani na mbebaji wa silaha zake hawapo.
1 Samweli 14: 18-19
\s5
\v 18 Sauli akamwambia Ahiya, "Lete hapa naivera ya Mungu"- kwa maana siku hiyo Ahiya alivaa naivera akiwa pamoja na askari wa Israeli.
\v 19 Wakati Sauli akiongea na kuhani, kelele na ghasia kubwa iliendelea na kuongezeka katika kambi ya Wafilisti. dipo sauli akamwambia kuhani, "Acha kazi unayofanya."
1 Samweli 14: 20-21
\s5
\v 20 Sauli na watu wote aliokuwa nao wakajipanga na kwenda kwenye mapigano. Upanga wa kila Mfilisti ulikwa juu ya Mfilisti mwenzake, na kulikuwa na ghasia kubwa.
\v 21 Basi Waebrania ambao mwanzoni walijiunga na Wafilisti, na kwenda kwenye kambi yao, wao pia waliungana na Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani.
1 Samweli 14: 22-23
\s5
\v 22 Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika milima karibu na Efraimu waliposikia kwamba Wafilisti wamekimbia, nao pia wakawafuata Wafilisti nakuwafukuza kwenye hiyo vita.
\v 23 Hivyo siku hiyo BWANA aliwaokoa Israeli, na mapigano yalivuka kupitiliza Beth aveni.
1 Samweli 14: 24-26
\s5
\v 24 Siku hiyo watu wa Israeli walifadhaika kwa sababu Sauli aliwaweka watu chini ya kiapo akasema, "Na alaaniwe mtu atakaye kula chakula kabla ya jioni na kabla sijalipiza kisasi kwa maadui zangu." Hivyo hakuna hata mmoja kati ya watu wote aliyeonja chakula.
\v 25 Ndipo watu wote wakaingia msituni na kuona asali ikiwa juu ya ardhi.
\v 26 Watu walipoingia humo msituni, asali ilitiririka, lakini hakuna aliyeweka mkono wake kinywani kwa maana watu waliogopa kiapo.
1 Samweli 14: 27-28
\s5
\v 27 Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kwamba baba yake amewaagiza watu kwa kiapo. Akanyoosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya kwenye sega la asali. Kisha akanyoosha mkono wake hadi kinywani mwake, na macho yake yakaangaziwa.
\v 28 Ndipo mmoja wa watu hao, akamwambia, "Baba yako aliwaagiza watu kwa mkazo na kwa kiapo, kwa kusema, 'Alaaniwe mtu atakaye kula chakula kwa siku ya leo,' ingawa watu wamedhoofika kwa ajili ya njaa."
1 Samweli 14: 29-31
\s5
\v 29 Baadaye Yonathani alisema, "Baba yangu amefanya matatizo katika nchi. Angalia jinsi macho yangu alivyotiwa nuru kwa sababu nilionja asali hii kidogo.
\v 30 Je, siyo vivuri sana kama leo watu wangekula bila kizuizi nyara walizopata kutoka kwa maadui zao? Kwa sababu sasa mauaji hayakuwa makubwa katikati ya Wafilisti."
1 Samweli 14: 31-32
\s5
\v 31 Siku hiyo waliwashambulia Wafilisti kutoka Mikmashi hadi Aiyaloni. Na watu walikuwa wamechoka sana.
\v 32 Hivyo watu wakazivamia nyara na kuchukua kondoo, ng'ombe na ndama na kuwachinja hapo chini. Watu walikula nyama zao pamoja na damu.
1 Samweli 14: 33-34
\s5
\v 33 KIsha wakamwambia Sauli, "Tazama, watu wanamtenda BWANA dhambi kwa kula pamoja na damu." Sauli akasema, "Mmetenda isivyo haki. Sasa, viringisheni jiwe kubwa kwangu." Sauli akasema,
\v 34 "Nendeni kati watu, na muwaambie, 'Kila mtu alete ng'ombe na kondoo wake, wawachinje hapa, na kuwala. Msimtende BWANA dhambi kwa kula na damu."' Kwa hiyo watu wote wakaleta kila mtu na ng'ombe wake usiku huo na kuwachinja mahali hapo.
1 Samweli 14: 35-35
\s5
\v 35 Sauli akamjengea BWANA madhabahu, ambayo ilikuwa ya kwanza kwake kumjengea BWANA.
1 Samweli 14: 36-37
\s5
\v 36 Ndipo Sauli akasema, "Haya tuwafukuze Wafilisti usiku na kuwateka nyara hadi asubuhi; tusimwache hata mtu mmoja akiwa hai." Nao wakamjibu, "Fanya unaloona linakupendeza." Lakini kuhani akasema, "Hebu na tumkaribie Mungu mahali hapa."
\v 37 Sauli alitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, "Je, inanipasa kuwafukuza Wafilisti? Je, utawaweka katika mkono wa Israeli?" Lakini siku hiyo BWANA hakumjibu kitu.
1 Samweli 14: 38-39
\s5
\v 38 Ndipo Sauli akasema, "Njoni hapa, viongozi wote wa watu; mjue na kuona jinsi dhambi hii ilivyotokea leo.
\v 39 Kwa maana, kama BWANA aishivyo, aliyewaokoa Israeli, hata kama angekuwa mwanangu Yonathani, atapaswa kufa." Lakini hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa watu aliye mjibu neno.
1 Samweli 14: 40-42
\s5
\v 40 Basi akawaambia Waisraeli wote, "Simameni upande mmoja, na mimi na Yonathani tutasimama upande mwingine." Kisha watu wakamwambia Sauli, "Fanya lile unaloona jema kwako."
\v 41 Kwa hiyo, Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, "Tuoneshe Thumimu." Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu walinusurika kuchaguliwa.
\v 42 Basi Sauli akasema, "Tupa mawe ya bahati nasibu tuone kati yangu na mwanangu Yonathani." Ndipo Yonathani akatwaliwa.
1 Samweli 14: 43-44
\s5
\v 43 Kisha Sauli akamwambia Yonathani, "Niambie umefanya nini." Yonathani akamwambia baba yake, "Nilionja asali kidogo kwa kutumia ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwangu. Niko hapa; Nitakufa."
\v 44 Sauli akasema, "Mungu afanye hivyo na kuzidi hata kwangu, kama Yonathani hautakufa."
1 Samweli 14: 45-46
\s5
\v 45 Basi watu wakamuuliza Sauli, "Je, inampasa Sauli afe, ni nani aliyetekeleza ushindi huu mkubwa kwa ajili ya Israeli? Mbali na hayo! Kama BWANA aishivyo, hata unywele mmoja wa kichwa chake hautaanguka chini, kwa maana leo amefanya kazi pamoja na Mungu." Hivyo hao watu walimuokoa Yonathani ili asife.
\v 46 Basi Sauli akasita kuwafuatia Wafilisti, nao wakarudi katika makao yao.
1 Samweli 14: 47-48
\s5
\v 47 Sauli alipoanza kutawala juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote kila upande. Alipigana dhidi ya Moabu, dhidi ya watu wa Amoni, Edomu, wafalme wa Zoba, na Wafilisti. Popote alipogeukia aliwapiga kwa adhabu adui zake.
\v 48 Alitenda kwa ushujaa mkubwa na kuwashinda Waamaleki. Aliwaokoa Israeli kutoka mikono ya watu ambao waliwateka nyara.
1 Samweli 14: 49-51
\s5
\v 49 Basi wana wa Sauli walikuwa ni hawa Yonathani, Ishvi, na Malkishua. Na majina ya binti zake wawili yalikuwa ni haya, Merabu mzaliwa wa kwanza, na mdogo aliitwa Mikali.
\v 50 Jina la mke wa Sauli aliitwa Ahinoamu; naye alikuwa binti Ahimaasi. Na jina la Jemedari wa jeshi lake aliitwa Abneri mwana wa Neri, baba mdogo wa Sauli.
\v 51 Kishi alikuwa baba yake Sauli; na Neri alikuwa baba yake na Abneri, wote walikuwa wana wa Abieli.
1 Samweli 14: 52-52
\s5
\v 52 Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti katika siku zote za Sauli. Naye alipomwona mtu yeyote mwenye nguvu, au mtu yeyote jasiri, alimuunganisha kwake.
\s5
\c 15
\p 1 Samweli 15: 1-3
\v 1 Samweli akamwambia Sauli, "BWANA alinituma nikutie mafuta uwe mfalme wa watu wake Israeli. Basi sikiliza maneno ya BWANA.
\v 2 Hivi ndivyo BWANA wa majeshi asemavyo, 'Nilichunguza jinsi Amaleki alivyomfanyia Israeli kwa kuwapinga njiani, walipopanda kutoka Misri.
\v 3 Sasa nenda umshambulie Amaleki na ukaangamize kabisa vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache, ua wote mwanamme na mwanamke, mtoto na mtoto mchanga, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda."'
1 Samweli 15: 4-5
\s5
\v 4 Sauli akwaita watu na kuwahesabu katika mji wa Talemu: watu mia mbili elfu waendao kwa miguu, na watu elfu kumi kutoka Yuda.
\v 5 Kisha Sauli akaja hadi mji wa Amaleki akangoja huko bondeni.
1 Samweli: 15: 6-7
\s5
\v 6 Ndipo Sauli akawaambia Wakeni, "Nendeni, muondoke, mkajitenge na Waamaleki, nisije kuwaangamiza pamoja nao. Kwa maana ulionesha wema kwa watu wote wa Israeli, walipotoka Misri." Kwa hiyo Wakeni wakajitenga na Waamaleki.
\v 7 Kisha sauli akawashambulia Waamaleki, kutoka Havila hadi kufika Shuri, ulio mashariki mwa Misri.
1 Samweli 15: 8-9
\s5
\v 8 Basi akamchukua Agagi mfalme wa Waamaleki akiwa hai; aliwaangamiza kabisa watu wote kwa ncha ya upanga.
\v 9 Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi akiwa hai, pamoja na kondoo wazuri, ng'ombe, ndama wanono, na wanakondoo. Kila kitu kilichokuwa kizuri, hawakukiangamiza. Bali waliangamiza kabisa chochote kilichodharaulika na kisicho na thamani.
1 Samweli 15: 10-11
\s5
\v 10 Baadaye neno la BWANA likamjia Samweli, kusema,
\v 11 "Inanihuzunisha kwamba nimemchagua Samweli awe mfalme, kwa maana aligeuka nyuma asinifuate na hakutekeleza maagizo yangu." Samweli alikasirika; akamlilia BWANA usiku kucha.
1 Samweli 15: 12-13
\s5
\v 12 Samweli aliamka mapema akutane na Sauli wakati wa asubuhi. Samweli aliambiwa, "Sauli alifika Karmeli na amejijengea ukumbusho kwa ajili yake, kisha aligeuka na kuendelea chini hadi Gilgali." Ndipo
\v 13 Samweli akamwendea Sauli, na Sauli akamwambia, "Umebarikiwa na BWANA! Nami nimetekeleza amri ya BWANA."
1 Samweli 15: 14-16
\s5
\v 14 Samweli akasema, "Hicho kilio cha kondoo ni cha nini basi masikioni mwangu, na hiyo milio ya ng'ombe ninayosikia?
\v 15 Sauli akamjibu, "Wao wamewaleta kutoka kwa Waamaleki. Kwa sababu watu waliwaacha hai kondoo wazuri na ng'ombe, kwa ajili ya sadaka kwa BWANA Mungu wako. Zilizobaki tuliziangamiza kabisa."
\v 16 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, "Subiri nitakumbia kile ambacho BWANA amekisema kwangu usiku." Sauli akamwambia, "Sema!"
1 Samweli 15: 17-19
\s5
\v 17 Samweli akasema, "Ingawa wewe ni mdogo machoni pako mwenyewe, je, hukufanywa mkuu wa kabila za Israeli? Na BWANA akakutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli;
\v 18 BWANA alikutuma katika safari yako akisema, 'nenda na uangamize kabisa wenye dhambi, Waamaleki, na upigane dhidi yao hadi wameangamizwa.'
\v 19 Kwa nini basi haukuitii sauti ya BWANA, bali badala yake ulishikilia nyara na ukafanya uovu machoni pa BWANA?"
1 Samweli 15: 20-21
\s5
\v 20 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, "Kweli kabisa niliitii sauti ya BWANA, Na nimeifuata njia ambayo BWANA alinituma. Nimemteka Agagi, mfalme wa Waamaleki, na kuwaangamiza kabisa Waamaleki.
\v 21 Lakini watu walichukua baadhi ya nyara-kondoo na ng'ombe, na vitu vizuri vilivyokusudiwa kuangamizwa, ili wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali."
1 Samweli 15: 22-23
\s5
\v 22 Samweli akajibu, "Je, BWANA hufurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama ilivyo kuitii sauti yake? Utii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia ni bora kuliko mafuta ya beberu.
\v 23 Kwa maana uasi ni sawa na dhambi ya uchawi, na ukaidi ni sawa na uovu na udhalimu. Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, naye pia amekukataa usiwe mfalme."
1 Samweli 15: 24-25
\s5
\v 24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, "Nimetenda dhambi; kwa maana nimevunja amri ya BWANA na maneno yako, kwa sababu niliwaogopa watu na kuitii sauti yao.
\v 25 Sasa, tafadhali nisamehe dhambi yangu, na urudi nami ili nipate kumcha BWANA."
1 Samweli 15: 26-27
\s5
\v 26 Samweli akamwambia Sauli, "Sitarudi pamoja na wewe; kwa sababu umekataa neno la BWANA, naye BWANA amekukataa usiwe mfalme juu ya Israeli."
\v 27 Samweli alipogeuka kuondoka, Sauli akashika pindo la kanzu yake, na likachanika.
1 Samweli 15: 28-29
\s5
\v 28 Samweli akamwambia, "BWANA ameuchana ufalme wa Israeli kutoka kwako leo na amempa ufalme huo jirani yako, aliye bora kuliko wewe.
\v 29 Pia, yeye ni Uwezo wa Israeli hatasema uongo wala kubadili nia yake; kwa sababu si mwanadamu, kwamba abadili nia yake."
1 Samweli 15: 30-31
\s5
\v 30 Kisha Sauli akasema, "Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali nipe heshima wakati huu mbele ya wakuu wa watu wangu na mbele ya Israeli. Urudi tena pamoja nami, kusudi niweze kumcha BWANA, Mungu wako."
\v 31 Hivyo Samweli akamrudia tena Sauli, na Sauli akamcha BWANA.
1 Samweli 15: 32-33
\s5
\v 32 Kisha Samweli akasema, "Mmlete hapa kwangu Agagi mfalme wa Waamaleki." Agagi akafika kwake akiwa amefungwa minyororo na kusema, "Hakika uchungu wa kifo umepita."
\v 33 Naye Samweli akamjibu, "Jinsi upanga wako ulivyofanya wanawake wapoteze watoto, vivyo hivyo mama yako naye hatakuwa na mtoto miongoni mwa wanawake." Kisha Samweli akamkata Agagi vipande vipande mbele za BWANA huko Gilgali.
1 Samweli 15: 34-35
\s5
\v 34 Samweli akaenda Rama, na Sauli akapanda kwenda nyumbani kwake Gibea ya Sauli.
\v 35 Samweli hakumuona tena Sauli hadi siku ya kifo chake, lakini alimwombolezea Sauli. Na BWANA alijuta kwa kumfanya Sauli awe mfalme juu ya Israeli.
\s5
\c 16
\p 1 Samweli 16: 1-1
\v 1 BWANA akamwambia Samweli, "Utamlilia Sauli kwa muda gani, ikiwa nimemkataa asiwe mfalme juu ya Israeli? Ijaze pembe yako mafuta na uende. Nitakutuma kwa Yese akaaye Bethlehemu, maana nimejichagulia mfalme katika wanawe.
1 Samweli 16: 2-3
\s5
\v 2 Samweli akasema, "Jinsi gani nitaenda? Kama Sauli akisikia jambo hili, ataniua." BWANA akasema, "chukua mtamba na useme, 'Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA.'
\v 3 Umwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonesha kile utakachofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakaye kuambia."
1 Samweli 16: 4-5
\s5
\v 4 Samweli akafanya kama BWANA alivyosema na akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji walikuwa wakitetemeka walipokuja kuonana naye na wakasema, "Je, umekuja kwa amani?"
\v 5 Naye akasema, "kwa amani; Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA. Jitoeni wenyewe kwa BWANA kwa ajili ya dhabihu na muandamane nami," Na akamweka wakfu Yese na watoto wake kwa BWANA, na baadaye aliwaita wote kwenye dhabihu.
1 Samweli 16: 6-7
\s5
\v 6 Walipofika, akamwangalia Eliabu na akajisemea mwenyewe kwamba mtiwa mafuta wa BWANA hakika amesimama mbele yake.
\v 7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, "Usimwangalie sura yake ya nje, au kimo cha umbo lake; kwa sababu nimemkataa. Maana BWANA haangalii kama mtu aangaliavyo; mtu hutazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo."
1 Samweli 16: 8-10
\s5
\v 8 Kisha Yese akamwita Abinadabu akamwambia apite mbele ya Samweli. Na Samweli akasema, "Hata huyu BWANA hakumchagua."
\v 9 Kisha Yese akmwambia Shama apite karibu. Na Samweli akasema, "Hata huyu BWANA hakumchagua."
\v 10 Yese akawaleta watoto wake saba wakapita mbele ya Samweli. Na Samweli akamwambia Yese, "Hakuna hata mmoja aliyechaguliwa na BWANA kati ya hawa."
1 Samweli 16: 11-12
\s5
\v 11 Kisha Samweli akamuulia Yese, "Je, watoto wako wote wako hapa?" Naye akajibu, "Yupo mdogo kabisa lakini anachunga kondoo." Samweli akamwambia Yese, "Tuma watu wakamwite; maana hatutakaa chini hadi atakapofika hapa."
\v 12 Yese akawatuma watu wakamleta. Naye kijana huyu alikuwa mwekundu na mwenye macho mazuri na mwenye muonekano mzuri. BWANA akasema, "Amka, umtie mafuta; maana huyu ndiye."
1 Samweli 16: 13-13
\s5
\v 13 Ndipo Samweli akachukua pembe yenye mafuta na kumtia mafuta katikati ya kaka zake. Roho wa BWANA akamwijia Daudi kwa nguvu tangu siku hiyo na kuendelea. Kisha Samweli akanyanyuka na kwenda Rama.
1 Samweli 16: 14-16
\s5
\v 14 Basi Roho wa BWANA akamwacha Sauli, badala yake roho ya ubaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua.
\v 15 Watumishi wa Sauli wakamwambia, "Tazama, roho ya ubaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.
\v 16 Haya bwana wetu hebu sasa amuru watumishi wako walio mbele yako wamtafute mtu mwenye ujuzi wa kupiga kinubi. Basi ikwa roho wa ubaya kutoka kwa Mungu yuko juu yako, atakipiga kinubi nawe utajisikia vizuri."
1 Samweli 16: 17-19
\s5
\v 17 Sauli akawaambia watumishi wake, "Mnitafutie mtu anayeweza kupiga vizuri na mmlete kwangu."
\v 18 Ndipo kijana mmoja kati yao akajibu, na kusema, "Nimemuona mtoto wa Yese Mbethtelehemu, aliye mjuzi katika kupiga, ni mwenye nguvu, mtu jasiri, mtu wa vita, mwenye busara aongeapo, mtu mzuri kwa uso; na BWANA yuko pamoja naye."
\v 19 Hivyo Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, na kusema, "Nitumie mtoto wako Daudi, anayewatunza kondoo."
1 Samweli! 6: 20-21
\s5
\v 20 Yese akamchukua punda aliyebeba mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, na akamtuma kwa Sauli pamoja na vitu hivyo.
\v 21 Ndipo Daudi akafika kwa Sauli na kuanza kazi yake. Sauli alimpenda sana Daudi, na akawa mbeba silaha wake.
1 Samweli 16: 22-23
\s5
\v 22 Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, akisema, "Mruhusu Daudi awe mbele yangu, maana amepata kibali machoni pangu."
\v 23 Wakati wowote roho ya usumbufu kutoka kwa Mungu ikiwapo juu ya Sauli, Daudi alichukuwa kinubi na kukipiga. Hivyo Sauli angeburudishwa na kupona, na huyo roho wa usumbufu angemtoka.
\s5
\c 17
\p 1 Samweli: 17: 1-1
\v 1 Basi Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa ajili ya vita. Walikusanyika huko Soko, iliyoko Yuda. Nao wakapiga kambi kati ya Soko na Aseka katika Efesdamimu.
1 Samweli 17: 2-3
\s5
\v 2 Sauli na watu wa Israeli alijikusanya na kuweka kambi katika bonde la Ela, na wakapanga vita kukutana na Wafilisti.
\v 3 Wafilisti walisimama juu ya mlima upande mmoja, na Iraeli nao walisimama juu ya mlima upande mwingine wakitenganishwa na bonde kati yao.
1 Samweli 17: 4-5
\s5
\v 4 Mtu mmoja mwenye nguvu akatoka katika kambi ya Wafilisti, mtu huyo aliitwa Goliathi wa Gathi, kimo chake mikono sita na shubiri moja.
\v 5 Alikuwa na chepeo ya shaba kichwani mwake, na alivaa dirii ya chuma. Hiyo dirii ilikuwa na uzito wa shekeli elfu hamsini za shaba.
1 Samweli 17: 6-7
\s5
\v 6 Alikuwa na mabampa ya shaba kwenye miguu yake na mkuki wa shaba katikati ya mabega yake.
\v 7 Ule mpini wa mkuki wake ulikuwa mkubwa, wenye kamba iliyo na kitanzi kwa ajili ya kuutupia kama kamba ya sindano ya mfumaji. Kichwa cha mkuki wake kilikuwa na uzito wa shekeli mia sita za chuma. Aliyembebea ngao alitembea mbele yake.
1 Samweli 17: 8-9
\s5
\v 8 Alisimama akayapigia kelele majeshi ya Israeli, "Kwa nini mmekuja na mmejipanga kwa ajili ya vita? Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Chagueni mtu kutoka kwenu ateremke na kuja kwangu.
\v 9 Kama anaweza kupigana nami na kuniua, hapo ndipo tutakuwa watumwa wenu. Lakini kama nitamshinda na kumuua, basi mtakuwa watumwa wetu na kututumikia."
1 Samweli 17: 10-11
\s5
\v 10 Mfilisti huyo akasema tena, "Leo ninayapa changamoto majeshi ya Israeli. Mnipe mtu ili tuweze kupigana naye."
\v 11 Sauli na Israeli wote waliposikia alichosema Mfilisti huyo, walikata tamaa na kuogopa sana.
1 Samweli 17: 12-13
\s5
\v 12 Basi Daudi alikuwa mwana wa Mwefraimu wa Bethtelehemu ya Yuda, aliyeitwa Yese. Naye alikuwa na watoto wanane wa kiume. Yese alikuwa mtu mzee katika siku za Sauli, mwenye umri mkubwa kati ya watu.
\v 13 Watoto watatu wakubwa wa Yese walimfuata Sauli vitani. Majina ya watoto wake watatu waliokwenda vitani yalikwa ni Eliabu mzaliwa wa kwanza, aliyemfuata Abinadabu, na watatu aliitwa Shama.
1 Samweli 17: 14-16
\s5
\v 14 Daudi ndiye aliyekuwa mdogo kabisa. Hao wakubwa watatu walimfuata Sauli.
\v 15 Basi Daudi alikwenda na kurudi akipita kati ya majeshi ya Sauli akiwa na kondoo za baba yake huko Bethtelehemu, ili kuwachunga.
\v 16 Kwa muda wa siku arobaini yule Mfilisti mwenye nguvu alikuwa akijitokeza asubuhi na jioni kwa ajili ya vita.
1 Samweli 17: 17-18
\s5
\v 17 Kisha Yese akamwambia mwanawe Daudi, "Wapelekee kaka zako efa ya bisi na hii mikate kumi, na uzipeleke upesi kule kambini kwa ajili ya kaka zako.
\v 18 Pia peleka hizi jibini kumi kwa jemedari wa kikosi chao cha elfu. Ukawaangalie wako na hali gani kisha uniletee habari kuhusu wanavyoendelea vizuri.
1 Samweli 17: 19-21
\s5
\v 19 Kaka zako wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli katika bonde la Ela, wanapigana na Wafilisti."
\v 20 Daudi aliamka asubuhi na mapema na kuliacha kundi chini ya uangalizi wa mchungaji. Akachukua vile vitu na kuondoka, kama Yese alivyomwamuru. Akafika kambini wakati jeshi linaondoka kwenda uwanja wa vita wakipiga kelele za vita.
\v 21 Nao Israeli na Wafilisti walijipanga kivita, jeshi dhidi ya jeshi.
1 Samweli 17: 22-24
\s5
\v 22 Daudi aliviacha vitu vyake kwa mtunza mahitaji, akalikimbilia jeshi, na kuwasalimia kaka zake.
\v 23 Alipoongea nao, yule mtu mwenye nguvu, Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akajitokeza kutoka majeshi ya Wafilisti, naye akasema maneno yaleyale kama hapo mwanzo. Naye Daudi akayasikia.
\v 24 Watu wote wa Israeli walipomwona Goliathi, walimkimbia na waliogopa sana.
1 Samweli 17: 25-25
\s5
\v 25 Watu wa Israeli walisema, "Umemuona mtu huyu aliyejitokeza? Amekuja kuipa changamoto Israeli. Basi mfalme atampa mali nyingi mtu atakayemua, atamuozesha binti yake, na familia ya baba yake haitalipa kodi katika Israeli."
1 Samweli 17: 26-27
\s5
\v 26 Daudi akawauliza watu waliosimama karibu naye, "Atafanyiwa nini mtu ambaye atamuua Mfilisti huyu na kuiondolea Israeli fedheha? Ni nani Mfilisti huyu asiyetahiriwa ayatukanaye majeshi ya Mungu aliye hai?"
\v 27 Ndipo watu wakarudia kile walichokuwa wamesema na kumwambia, "Ndivyo iitakavyofanyika kwa mtu atakayemuua."
1 Samweli 17: 28-30
\s5
\v 28 Kaka yake mkubwa Eliabu, alisikia wakati akisema na watu. Hasira ya Eliabu ikawaka moto dhidi ya Daudi, naye akamuuliza, "Kwa nini umekuja hapa? Wale kondoo wachache umewaacha na nani huko nyikani? Nakijua kiburi chako, na utundu wa moyo wako; maana umekuja hapa ili uweze kuona mapigano."
\v 29 Naye Daudi akamjibu, "Nimefanya nini sasa? Mimi si nuliuliza swali tu?
\v 30 Akamgeukia mtu mwingine na kumwacha huyo, na kusema vivyo hivyo. Nao watu wakajibu vilevile kama mwanzo.
1 Samweli 17: 31-33
\s5
\v 31 Maneno aliyosema Daudi yaliposikika, askari waliyasema tena kwa Sauli, naye akawatuma kwa Daudi.
\v 32 Kisha Daudi akamwambia Sauli, "Pasiwepo moyo wa mtu atakayezimia kwa sababu ya Mfilisti huyo; Mtumishi wako atakwenda kupigana na Mfilisti huyu."
\v 33 Sauli akamwambia Daudi, "Huwezi kumpinga Mfilisti ama kupigana naye; wewe ni kijana tu, na yeye amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake."
1 Samweli 17: 34-35
\s5
\v 34 Lakini Daudi akamwambia Sauli, "Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake. Mara simba au dubu alikuja akamchukua mwana kondoo kutoka kundini,
\v 35 Nilimfukuza na kumshambulia na kumpokonya kutoka kinywani mwake. Na aliponirukia, nilimshika ndevu zake, nilimpiga, na kumuua.
1 Samweli 17: 36-36
\s5
\v 36 Mtumishi wako amekwisha kmuua simba na dubu. N huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wa wanyama hao, kwa kuwa ameyadharau majeshi ya Mungu aliye hai."
1 Samweli 17: 37-38
\s5
\v 37 Daudi akasema, "BWANA aliyeniokoa kutoka makucha ya simba na makucha ya dubu. Ataniokoa kutoka mkono wa Mfilisti huyu." Kisha Sauli akamwambia Daudi, "Nenda, BWANA awe pamoja nawe."
\v 38 Sauli akamvika Daudi vazi lake la vita. Akamvika chepeo ya shaba kichwani pake, na akamvika koti la chuma.
1 Samweli 17: 39-40
\s5
\v 39 Daudi akaufunga upanga wake juu ya vazi la Sauli. Lakini hakuweza kutembea, kwa sababu hakupata mafunzo kwa mavazi hayo. Ndipo Daudi akamwambia Sauli, "Siwezi kwenda kupigana nikiwa na haya, maana sikupata mafunzo kwa haya." Kwa hiyo Daudi akayavua.
\v 40 Akachukua fimbo mkononi mwake na akachagua mawe matano laini kutoka katika kijito; akayaweka kwenye mfuko wake wa kichungaji. Kombeo lake lilikuwa mkononi akawa anamsogelea yule Mfilisti.
1 Samweli 17: 41-43
\s5
\v 41 Yule Mfilisti akaja na kumsogelea Daudi, mbeba ngao yake akiwa mbele yake.
\v 42 Mfilisti alipotazama kila upande na kumuona Daudi, akamdharau, maana alikuwa kijana tu, mwekundu, na umbo la kupendeza.
\v 43 Ndipo Mfilisti akamuuliza Daudi, "Je, mimi ni mbwa, hata ukanijia na fimbo? Naye Mfilisti kwa miungu yake akamlaani Daudi.
1 Samweli 17: 44-45
\s5
\v 44 Huyo Mfilisti akamwambia Daudi, "Njoo kwangu, na nyama yako nitawatupia ndege wa angani na wanyama wa mwituni."
\v 45 Daudi akamjibu Mfilisti, "Unaniijia kwa upanga, kwa mkuki na mkuki mdogo. Bali mimi nakuijia kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa Majeshi ya Israeli, uliyemdharau.
1 Samweli 17: 46-47
\s5
\v 46 Leo BWANA atanipa ushindi dhidi yako, na nitakuua na kukiondoa kichwa chako kwenye kiwiliwili. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni walioko duniani mizoga ya jeshi la Wafilisti, ili dunia yote ijue kwamba yupo Mungu katika Israeli,
\v 47 na kusanyiko hili lote lijue kwamba BWANA hatoi ushindi kwa upanga wala kwa mkuki. Kwa kuwa vita ni ya BWANA, na atawaweka katika mkono wetu."
1 Samweli 17: 48-49
\s5
\v 48 Mfilisti aliponyanyuka na kukaribia akutane na Daudi, ndipo Daudi akakimbia kwa haraka kuelekea jeshi la adui ili akutane naye.
\v 49 Daudi aliweka mkono wake mfukoni, akachukua jiwe kutoka humo, akalitupa kwa kombeo, na likampiga Mfilisti kwenye paji la uso, akaanguka chini kifudifudi.
1 Samweli 17: 50-51
\s5
\v 50 Daudi alimshinda Mfilisti kwa kombeo na kwa jiwe moja. Alimpiga huyo Mfilisti na kumuua. Mkononi mwa Daudi hakukuwa na upanga.
\v 51 Ndipo Daudi akakimbia akasimama juu ya Mfilisti na kutwaa upanga wake, akauchomoa kutoka alani, akamuua, na kukata kichwa chake kwa upanga huo.
1 Samweli 17: 52-54
\s5
\v 52 Ndipo watu wa Israeli na wale wa Yuda wakaamka kwa kelele, na kuwafukuza Wafilisti kuvuka bonde na malango ya Ekroni. Na maiti za Wafilisti walilala katika njia iendayo Shaaraimu, na njia yote kuelekea Gathi na Ekroni.
\v 53 Watu wa Israeli wakarejea kutoka kuwafukuza Wafilisti, na wakateka nyara kambi yao.
\v 54 Daudi akachukua kichwa cha Mfilisti na kukipeleka Yerusalemu, lakini akaliweka vazi la vita katika hema lake.
1 Samweli 17: 55-56
\s5
\v 55 Sauli alipomuona Daudi akienda kukabiliana na yule Mfilisti, akamwambia Abneri, jemedari wa jeshi, "Abneri, kijana huyu ni mtoto wa nani? Abneri akasema, "Kama uishivyo, mfalme, mimi sijui."
\v 56 Naye mfalme akasema, "Waulize wanaoweza kufahamu, mvulana huyu ni kijana wa nani."
1 Samweli 17: 57-58
\s5
\v 57 Daudi aliporudi kutoka kumuua yule Mfilisti, Abneri alimchukuwa, na kumleta mbele ya Sauli akiwa na kichwa cha Mfilisti mkononi mwake.
\v 58 Sauli akamuuliza, "Kijana, wewe ni mtoto wa nani? Na Daudi akamjibu, "Mimi ni mtoto wa mtumishi wako Yese Mbethlehemu."
\s5
\c 18
\p 1 Samweli 18: 1-2
\v 1 Daudi alipokuwa amemaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ilishikana na roho ya Daudi, na Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
\v 2 Sauli akamweka kazini Daudi siku hiyo, hakumwacha arudi nyumbani kwa baba yake.
1 Samweli 18: 3-4
\s5
\v 3 Kisha Yonathani na Daudi wakafanya makubaliano ya urafiki kwa sababu Yonathani alimenda kama roho yake mwenyewe.
\v 4 Yonathani akavua kanzu aliyokuwa amevaa na kumpa Daudi, akampa na vazi lake la kivita, pamoja na upanga, upinde, na mshipi.
1 Samweli 18: 5-5
\s5
\v 5 Daudi alikwenda popote ambapo Sauli alimtuma, naye alifanikiwa. Sauli akamteua Daudi awe mkuu wa wapiganaji. Jambo hili lilipendeza machoni pa watu na katika macho ya watumishi wa Sauli.
1 Samweli 18: 6-7
\s5
\v 6 Wakati wanarudi nyumbani kutoka kuwapiga Wafilisti, wanawake walitoka miji yote ya Israeli, wakiimba na kucheza, ili kukutana na mfalme Sauli, wakiwa na matowazi, wenye furaha, na wakiwa na ala za muziki.
\v 7 Hao wanawake waliimba kwa kupokezana huku wakicheza; Wakiimba: "Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi ameua makumi elfu yake."
1 Samweli 18: 8-9
\s5
\v 8 Sauli alikasirika sana, na wimbo huu haukumpendeza. Naye akasema, "Wamemsifia Daudi juu ya makumi elfu, lakini wamenisifia melfu tu mimi! Atapata kitu gani zaidi isipokuwa ufalme?
\v 9 Kuanzia siku hiyo na kuendelea, Sauli alimuangalia Daudi kwa mashaka.
\s5
\v 10 Kesho yake yule roho ya ubaya kutoka kwa Mungu ikamwingia Sauli kwa nguvu. Naye akawa anafanya kama mwendawazimu nyumbani mwake. Hivyo Daudi akapiga kifaa chake, kama alivyofanya kila siku. Sauli alikuwa na mkuki wake mkononi.
\v 11 Sauli akatupa mkuki wake, kwani alifikiri, "Nitampigilia ukutani." Lakini Daudi mara mbili aliepa uwepo wa Sauli.
\v 12 Sauli alimwogopa Daudi, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, lakini hakuwa na Sauli tena.
1 Samweli 18: 13-14
\s5
\v 13 Hivyo Sauli alimuondoa Daudi mbele yake na akamteua kuwa kamanda wa kikosi cha askari elfu moja. Kwa namna hii David alitoka na kuingia mbele ya watu.
\v 14 Daudi alikuwa akistawi kwa mambo yake yote, maana BWANA alikuwa pamoja naye.
1 Samweli 18: 15-16
\s5
\v 15 Sauli alipoona kwamba Daudi anastawi, alimwogopa.
\v 16 Lakini Israeli yote na Yuda walimpenda Daudi, maana alitoka na kuingia mbele yao.
1 Samweli 18: 17-18
\s5
\v 17 Kisha Sauli akamwambia Daudi, "Huyu hapa ni binti yangu mkubwa Merabu. Nitakupatia awe mke wako. Ila tu uwe jasiri kwa ajili yangu na upigane vita vya BWANA." Maana Sauli alifikiri, "Usije mkono wangu ukawa juu yake, ila acha mkono wa Wafilisti uwe juu yake."
\v 18 Daudi akamwambia Sauli, "Mimi ni nani, na maisha yangu yana nini, au hata maisha ya familia ya baba yangu katika Israeli, kiasi cha kuwa mkwe wa mfalme?"
1 Samweli 18-19-19
\s5
\v 19 Lakini wakati ambao Merabu, binti Sauli, ilipasa kuwa ameolewa na Daudi, aliozwa kwa Adrieli Mmeholathi.
1 Samweli 18: 20-21
\s5
\v 20 Lakini Mikali, binti Sauli, alimpenda Daudi. Na watu walimwambia Sauli, na jambo hilo likampendeza.
\v 21 Ndipo Sauli akafikiri, "Nitampatia huyu awe mke wake, ili uwe mtego kwake, na hivyo mkono wa Wafilisti pengine uwe juu yake." Kwa hiyo Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, "Wewe utakuwa mkwe wangu."
1 Samweli 18: 22-22
\s5
\v 22 Sauli akawaamuru watumishi wake, "Ongeeni na Daudi kwa njia ya siri, na mseme, 'Tazama, mfalme anakufurahia, na watumishi wake wote wanakupenda. Sasa basi, uwe mkwe wa mfalme.'"
1 Samweli 18: 23-24
\s5
\v 23 Hivyo watumishi wa Sauli wakayasema maneno haya kwa Daudi. Na Daudi akasema, "Kwenu ninyi mnaona ni jambo dogo kuwa mkwe wa mfalme, mimi ni maskini, na heshima yangu ni ndogo."
\v 24 Watumishi wa Sauli wakarudisha kwake taarifa ya maneno ambayo Daudi aliyasema.
1 Samweli 18: 25-26
\s5
\v 25 Na Sauli akasema, "Hivi ndivyo mtakavyo mwambia Daudi, 'Mfalme haitaji mahari yoyote, isipokuwa govi mia moja za Wafilisti, ili ajilipize kisasi kwa adui wa mfalme."' Basi Sauli alifikiri atamwangusha Daudi kwa mkono wa Wafilisti.
\v 26 Watumishi wake walipomwambia maneno haya, yakamvutia Daudi awe mkwe wa mfalme.
1 Samweli 18: 27-29
\s5
\v 27 Kabla siku hizo hazijapita, Daudi aliondoka na watu wake na kuwaua Wafilisti mia mbili. Daudi akazileta govi zao, na kumkadhi mfalme kulingana na idadi yake, ili aweze kufanyika mkwe wa mfalme. Kwa hiyo Sauli akamwoza Mikali, binti yake, awe mkewe.
\v 28 Basi Sauli aliona na kufahamu kwamba BWANA alikuwa pamoja na Daudi. Mikali, binti Sauli, akampenda Daudi.
\v 29 Sauli akazidi kumwogopa Daudi. Sauli akawa adui wa Daudi daima.
1 Samweli 18: 30-30
\s5
\v 30 Ndipo wakuu wa Wafilisti wakajitokeza kwa ajili ya vita, na mara zote walipojitokeza Daudi alifanikiwa zaidi kuliko watumishi wote wa Sauli, hivyo jina lake likapata heshima kubwa.
\s5
\c 19
\p 1 Samweli 19: 1-3
\v 1 Sauli akamwambia Yonathani mwanawe na watumishi wake wote kwamba wanapaswa kumuua Daudi. Lakini Yonathani, mwana wa Sauli, alitamani sana akae na Daudi.
\v 2 Hivyo Yonathani akamwambia Daudi, "Baba yangu Sauli anatafuta kukuua. Kwa hiyo uwe macho wakati wa asubuhi na jifiche mahali pa siri.
\v 3 Nami nitatoka nje na kusimama kando ya baba yangu huko shambani uliko wewe, na nitazungumza na baba yangu kuhusu wewe. Kama nikijua jambo lolote nitakuambia."
1 Samweli 19: 4-5
\s5
\v 4 Yonathani alimsifia Daudi mbele ya Sauli baba yake akisema, "Mfalme asije akafanya dhambi dhidi ya mtumishi wake Daudi. Maana yeye hajakutenda dhambi, mambo aliyofanya yamekusaidia sana.
\v 5 Maana alijitoa maisha yake na kumuua yule Mfilisti, naye BWANA akawaletea Waisraeli wote wokovu mkuu. Tena uliuona na kufurahi. Kwa nini utende dhambi juu damu isiyo na hatia kwa kumuua Daudi bila sababu?"
1 Samweli 19: 6-7
\s5
\v 6 Sauli alimsikiliza Yonathani. Sauli akaapa, "Kama BWANA aishivyo, Yonathani hatauawa."
\v 7 Ndipo Yonathani akamwita Daudi na kumwambia mambo hayo yote. Na Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye Daudi akawa mbele zake kama zamani.
1 Samweli 19: 8-9
\s5
\v 8 Baadaye kukawa na vita tena. Daudi akatoka na kupigana na Wafilisti na kuwashinda kwa mauaji makubwa mno. Nao wakakimbia mbele yake.
\v 9 Yule roho wa ubaya kutoka kwa BWANA ikamjia Sauli alipokuwa ameketi nyumbani mwake na mkuki mkononi mwake, na Daudi akiwa anapiga chombo chake.
1 Samweli 19: 10-11
\s5
\v 10 Sauli alijaribu kumpigilia Daudi ukutani kwa mkuki wake, lakini akaponyoka kutoka machoni pake, na kwamba Sauli akashindilia mkuki ndani ya ukuta. Daudi alikimbia na kutoroka usiku huo.
\v 11 Bado Sauli aliwatuma wajumbe nyumbani kwa Daudi wamvizie kusudi aweze kumuua asubuhi. Mkewe Daudi, Mikali, akamwambia, "Usipoyaokoa maisha yako usiku huu, kesho utauwawa."
1 Samweli 19: 12-13
\s5
\v 12 Hivyo Mikali akamteremsha Daudi kupita dirishani. Naye akaenda, akakimbia na kutoroka.
\v 13 Mikali alichukua kinyago na kukilaza juu ya kitanda. Kisha akaweka mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na akakifunika na nguo.
1 Samweli 19: 14-15
\s5
\v 14 Sauli alipowatuma wajumbe kumchukua Daudi, mkewe akasema, " Daudi ni mgonjwa."
\v 15 Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumtazama; akisema, "Mleteni kwangu akiwa kitandani, ili nimuue."
1 Samweli 19: 16-17
\s5
\v 16 Wale wajumbe walipoingia ndani, tazama, kile kinyago kilikuwa kitandani pamoja na mto wa singa za mbuzi kichwani.
\v 17 Sauli akamuuliza Mikali, "Kwa nini umenidanganya na kumwachilia adui yangu aende, na tena ametoroka?" Mikali akamjibu Sauli, "Aliniambia, 'Acha niende. Kwa nini nikuuwe?"'
1 Samweli 19: 18-20
\s5
\v 18 Basi Daudi akakimbia na kutoroka, na akaenda kwa Samweli huko Rama na kumweleza yote ambayo Sauli amemtendea. Ndipo yeye na Samweli wakaenda na kukaa Nayothi.
\v 19 Naye Sauli akaambiwa kwamba, "Tazama, Daudi yuko huko Nayothi iliyoko Rama."
\v 20 Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumkamata Daudi. Nao walipowaona kundi la manabii wakitabiri, na Samweli akisimama kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akawaingia wale wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.
1 Samweli 19: 21-22
\s5
\v 21 Sauli alipoambiwa hivyo, akawatuma wajumbe wengine, nao pia wakatabiri. Basi Sauli aliwatuma tena wajumbe kwa mara ya tatu, na hao pia wakatabiri.
\v 22 Kisha naye akaenda Rama na kufika katika kisima kirefu kilichoko huko Seku. Akauliza, "Samweli na Daudi wako wapi?" Mtu mmoja akasema, "Angalia, Wako Nayothi huko Rama."
1 Samweli 19: 23-24
\s5
\v 23 Hivyo Sauli akaenda Nayothi huko Rama. Ndipo Roho wa Mungu pia akaja juu yake, naye alipokuwa akienda alitabiri, hadi alipofika Nayothi huko Rama.
\v 24 Na yeye pia, alirarua mavazi yake, naye pia akatabiri mbele ya Samweli siku hiyo akilala uchi mchana kutwa na usiku kucha. Kwa sababu ya jambo hili, watu husema, "Je, Sauli pia ni miongoni mwa manabii?"
\s5
\c 20
\p 1 Samweli 20: 1-2
\v 1 Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akaenda na kumwambia Yonathani, "Nimefanya nini? Uovu wangu ni upi? Dhambi yangu ni ipi kwa baba yako, inayofanya atafute kuutoa uhai wangu."
\v 2 Yonathani akamwambia Daudi, "La hasha; hautakufa. Baba yangu hafanyi jambo kubwa wala dogo bila kunijulisha. Kwa nini inamlazimu baba yangu anifiche jambo hili? La, siyo hivyo?"
1 Samweli 20: 3-3
\s5
\v 3 Bado Daudi aliapa tena na akasema, "Baba yako anajua wazi kwamba nimepata kibali machoni pako. Pengine anasema, 'Asije Yonathani akajua jambo hili, labda atahuzunika.' Lakini kweli kama BWANA aishivyo, kama wewe uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti."
1 Samweli 20: 4-5
\s5
\v 4 Kisha Yonathani akamwambia Daudi, "Lolote utakalosema, nitakufanyia."
\v 5 Daudi akamwambia Yonathani, "Kesho ni siku ya mwezi mpya, na inanibidi kukaa na kula pamoja na mfalme. Lakini acha niende, ili niweze kujificha katika shamba hadi siku ya tatu jioni.
1 Samweli 20: 6-7
\s5
\v 6 Baba yako akinikosa kabisa, ndipo utasema, 'Daudi aliniomba kwa msisitizo ruhusa aondoke kwenda mjini kwake Bethlehemu; kwa sababu huko ni kipindi cha utoaji wa dhabihu ya mwaka kwa familia yao yote.'
\v 7 Kama atasema kuwa ni vyema, 'basi mtumishi wako atakuwa na amani. Lakini kama atakasirika sana, ndipo utajua kwamba ameamua kunitendea uovu.
1 Samweli 20: 8-9
\s5
\v 8 Kwa hiyo, umtendee wema mtumishi wako. Kwa maana umemweka mtumishi katika agano la BWANA pamoja na wewe. Lakini kama kuna dhambi ndani yangu, wewe mwenyewe uniuwe; maana kwa nini basi unipeleke kwa baba yako?"
\v 9 Yonathani akasema, "La hasha! Ikiwa ninajua kwamba baba ameamua baya likupate, siwezi kukuambia?"
1 Samweli 20: 10-11
\s5
\v 10 Ndipo Daudi akamwambia Yonathani, "Ni nani ataniambia ikiwa imetokea, baba yako akakujibu kwa ukali?"
\v 11 Yonathani akamwambia Daudi, "Njoo, hebu twende huko shambani." Ndipo wote wakaondoka kwenda shambani.
1 Samweli 20: 12-13
\s5
\v 12 Yonathani akamwambia Daudi, "Na BWANA, Mungu wa Israeli, awe shahidi. Kesho muda kama huu, nitakuwa nimemuuliza baba yangu, au siku ya tatu, tazama, ikiwa kutakuwa na jambo zuri upande wa Daudi; je, nisikutumie taarifa na kulidhihirisha kwako?
\v 13 Na kama ikimpendeza baba yangu akufanyie madhara, Basi BWANA ayafanye hayo kwa Yonathani na kuzidi ikiwa sitakujulisha jambo na kukupeleka mbali, ili kwamba uende kwa amani. Na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa na baba yangu.
1 Samweli 20: 14-16
\s5
\v 14 Kama bado nikiwa hai, hautanionesha uaminifu wa agano la BWANA, kwamba siwezi kufa?
\v 15 Na usivunje kabisa uaminifu wako wa agano kati yako na nyumba yangu, hata wakati BWANA atakapowaodoa kila mmoja wa adui za Daudi kutoka uso wa dunia."
\v 16 Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi na kusema, "Naye BWANA atawaondoa maadui wa Daudi." (KISWAHILI IDIOM? ==== ULB ENGLISH IDIOM)
1 Samweli 20: 17-19
\s5
\v 17 Yonathani akamtaka Daudi aape tena kwa sababu ya upendo aliokuwa nao juu yake, kwa sababu alimpenda kama alivyopenda roho yake mwenyewe.
\v 18 Kisha Yonathani akamwambia Daudi, "Kesho ni siku ya mwezi mpya. Hautakuwapo, kwa sababu kiti chako kitakuwa wazi.
\v 19 Utakapokuwa umekaa huko siku tatu, uende upesi hadi mahala ulipojificha mara ya kwanza, wakati shughuli ikifanyika, na ukaye karibu jiwe Ezeli.
1 Samweli 20: 20-21
\s5
\v 20 Nitatupa mishale mitatu pembeni mwa jiwe, kama vile ninalenga kitu fulani.
\v 21 Kisha nitamtuma kijana wangu na kumwambia, 'Nenda utafute hiyo mishale.' Kama nitamwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko upande huu wa kwako; kaichukue," ndipo uje; maana hapo kutakuwa na usalama kwako na siyo madhara, kama BWANA aishivyo.
1 Samweli 20: 22-23
\s5
\v 22 "Lakini kama nikimwambia kijana hivi, 'Tazama, mishale iko mbele yako,' ndipo utakapokwenda zako, maana BWANA ametaka uende zako.
\v 23 Kulingana na makubaliano ambayo mimi na wewe tumeongea, angalia, BWANA yupo kati yangu na wewe milele.'"
1 Samweli 20: 24-25
\s5
\v 24 Kwa hiyo Daudi akajificha mle shambani. Pindi mwezi ulipoandama, mfalme aliketi chini ale chakula.
\v 25 Mfalme alikaa juu ya kiti chake, kama kawaida kwenye kiti karibu na ukuta. Yonathani alisimama wima, na Abneri alikaa ubavuni mwa Sauli. Lakini nafasi ya Daudi ilikuwa wazi.
1 Samweli 20: 26-27
\s5
\v 26 Hata hivyo Sauli hakusema kitu siku hiyo, kwa sababu alifikiri, "Kuna jambo limempata Daudi. Hayuko safi; hakika hayuko safi."
\v 27 Lakini siku ya pili, siku moja baada ya mwandamo wa mwezi, bado nafasi ya Daudi ilikuwa tupu. Ndipo Sauli akamuuliza Yonathani mwanaye, "Kwa nini mwana wa Yese hakuja kwenye chakula, jana na hata leo?"
1 Samweli 20: 28-29
\s5
\v 28 Yonathani akamjibu Sauli, "Daudi aliomba kwangu ruhusa kwa dhati ili aende Bethlehemu.
\v 29 Alisema, 'Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.' Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii."
1 Samweli 20: 30-31
\s5
\v 30 Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, "Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua Mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako?
\v 31 Kwa kuwa mwana wa Yese anaishi duniani, siyo wewe wala ufalme wako utakaoimarika. Sasa basi, tuma watu wamlete kwangu, kwa sababu inampasa kufa."
1 Samweli 20: 32-34
\s5
\v 32 Yonathani akamjibu Sauli baba yake, "Kwa sababu gani inampasa kuuwawa? Amefanya nini?"
\v 33 Ndipo Sauli akamtupia mkuki apate kumuua. Kwa hiyo Yonatani akatambua kwamba baba yake alinuia kumuua Daudi.
\v 34 Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
1 Samweli 20: 35-37
\s5
\v 35 Ikawa asubuhi, Yonathani akaenda huko shambani kama walivyoahidiana na Daudi, akiwa pamoja na kijana wake.
\v 36 Akamwambia yule kijana wake, "Kimbia utafute ile mishale niliyoitupa." Na kijana alikimbia, akatupa mshale mwingine mbele yake.
\v 37 Kijana alipofika katika eneo ambapo mshale ulitua, ule alioutuma Yonathani, akamwita tena kijana, na kusema, "Huo mshale hauko mbele yako?"
1 Samweli 20: 38-40
\s5
\v 38 Kisha Yonathani akamwita yule kijana, "Upesi, harakisha, usikawie!" Hivyo kijana wa Yonathani akaikusanya mishale na kurudi kwa bwana wake.
\v 39 Lakini huyo kijana hakujua lolote. Ni Yonathani na Daudi tu ndio walijua habari yenyewe.
\v 40 Yonathani akampa kijana wake silaha na kumwambia, "Nenda, uzipeleke mjini."
1 Samweli 20: 41-42
\s5
\v 41 Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi.
\v 42 Yonathani akamwambia Daudi, "Nenda kwa amani, kwa sababu wote tumeapa kwa jina la BWANA na tulisema, 'BWANA awe kati yangu na wewe, na awe kati ya uzao wangu na uzao wako, milele.'" Kisha Daudi alisimama na akaondoka, na Yonathani akarudi mjini.
\s5
\c 21
\p 1 Samweli 21: 1-2
\v 1 Kisha Daudi akafika Nobu kumuona Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akaja akutane na Daudi huku akitetemeka na kumwambia, "Kwa nini uko peke yako huna mtu wa kuambatana na wewe?"
\v 2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, "Mfalme amenituma kwa jambo maalum na ameniambia hivi, 'Asiwepo hata mtu mmoja anayejua chochote kuhusu shughuli niliyokutuma, na kile nilichokuagiza.' Nimewaelekeza vijana kwenda sehemu fulani.
1 Samweli 21: 3-4
\s5
\v 3 Sasa basi chakula gani kinapatikana hapa? Nipatie mikate mitano, au chochote kilichopo hapa."
\v 4 Huyo Kuhani alimjibu Daudi na kusema, "Hakuna mkate wa kawaida mkononi, lakini ipo mikate takatifu- kama vijana hawajatembea na wanawake."
1 Samweli 21: 5-6
\s5
\v 5 Daudi akamjibu kuhani, "Hakika hatujatembea na wanawake kwa siku hizi tatu. Nilipoanza safari, miili ya vijana iliwekwa wakfu kwa BWANA, ingawa ilikuwa safari ya kawaida. Je, si zaidi sana leo miili yao ikawekwa wakfu kwa BWANA."
\v 6 Hivyo kuhani akampa mikate iliyokuwa imewekwa wakfu kwa BWANA. Maana haikuwepo mikate mingine hapo, isipokuwa tu ile ya wonyesho, ambayo iliondolewa kutoka kwa BWANA, ili sehemu yake iwekwe mikate ya moto, inapokuwa imeondolewa.
1 Samweli 21: 7-7
\s5
\v 7 Basi siku hiyo mmoja wa watumishi wa Sauli alikuwapo mahali hapo, ameshilkiliwa mbele za BWANA. Jina la mtu huyo aliitwa Doegi Mwedomu, mkuu wa wachungaji wa Sauli.
1 Samweli 21: 8-9
\s5
\v 8 Daudi akamwambia Ahimeleki, "Je, hakuna hata mkuki wowote au upanga? Maana mimi sikubeba upanga wangu wala silaha zangu, maana ile shughuli ya mfalme ilikuwa ya muhimu."
\v 9 Kuhani akasema, "Ule upanga wa Mfilisti Goliathi, uliyemuua katika bonde la Ela, uko hapa umefunikwa katika nguo nyuma ya naivera. kama unataka kuuchukua huo, uchukue, maana hakuna silaha nyingine hapa." Daudi akasema, "Hakuna silaha nyingine kama hiyo, nipatie hiyo."
1 Samweli 21: 10-11
\s5
\v 10 Daudi aliamka na kukimbia mbali na Sauli na akaenda kwa Akishi, mfalme wa Gathi.
\v 11 Mtumishi wa Akishi akamwambia, "huyu siye Daudi mfalme wa nchi hii? Je, wanawake hawakupokezana wakiimba na kucheza, 'Sauli ameua maelfu yake, na Daudi makumi elfu yake?"'
1 Samweli 21: 12-13
\s5
\v 12 Daudi akayaweka maneno hayo moyoni mwake na akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi.
\v 13 Daudi akabadili mwenendo wake mbele yao na akajifanya kuwa mwendawazimu machoni pao; akachora-chora alama kwenye vizingiti vya milango huku akitiririsha mate yake chini ya ndevu zake.
1 Samweli 21: 14-15
\s5
\v 14 Ndipo Akishi akawaambia watumishi wake, "Tazameni, mnaona mtu huyu ni mwehu.
\v 15 Kwa nini mmemleta kwangu? Je, mimi nina haja na wehu, kumbe mmemleta mtu huyu ili anifanyie hayo mbele yangu? Hivi kweli huyu ataingia nyumbani mwangu?
\s5
\c 22
\p 1 Samweli 22: 1-2
\v 1 Basi Daudi aliondoka hapo na akatoroka kwenda kwenye pango la Adulamu. Kaka zake na wote wa nyumba ya baba yake waliposikia hayo, wakateremka kumwendea huko.
\v 2 Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao mia nne waliokuwa pamoja naye.
1 Samweli 22: 3-5
\s5
\v 3 Kisha Daudi alitoka huko akaenda Mispa huko Moabu. Akamwambia mfalme wa Moabu, "Tafadhali waruhusu baba na mama yangu wakae kwako hadi hapo nitakapojua kitu gani ambacho Mungu atafanya kwa ajili yangu."
\v 4 Basi akawaacha kwa Mfalme wa Moabu. Baba na mama yake wakakaa na mfalme kwa muda wote ambao Daudi alikuwa kwenye ngome yake.
\v 5 Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, "Usikae tena katika ngome yako. Ondoka na uende katika nchi ya Yuda." Kwa hiyo Daudi akatoka hapo na akaenda katika msitu wa Harethi.
1 Samweli 22: 6-6
\s5
\v 6 Sauli akasikia kwamba Daudi amepatikana, akiwa pamoja na watu aliokuwa nao. Wakati huo Sauli alikuwa akikaa Gibea chini ya mti wa mkwaju huko Rama, akiwa na mkuki wake mkononi mwake, na watumishi wake wote walikuwa wamesimama wamemzunguka.
1 Samweli 22: 7-8
\s5
\v 7 Sauli akawaambia watumishi wake, Sasa sikilizeni, watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya nyote kuwa majemedari wa maelfu na majemedari wa mamia,
\v 8 hata ninyi nyote mnapanga njama dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anafanya agano na mwana wa Yese. Hakuna hata mmoja wenu anayenionea huruma. Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anamchochea mtumishi wangu Daudi awe kinyume changu. Leo mejificha na ananisubiri ili anishambulie."
1 Samweli 22: 9-10
\s5
\v 9 Kisha Doegi Mwedomu, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akajibu, Nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu.
\v 10 Alimwomba BWANA ili apate kumsaidia, na alimpatia mahitaji na upanga wa Goliathi, Mfilisti"
1 Samweli 22: 11-13
\s5
\v 11 Kisha Mfalme akamtuma mtu amwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu na watu wote wa nyumba ya baba yake, makuhani waliokuwa huko Nobu. Wote walifika mbele ya mfalme.
\v 12 Sauli akasema, "Sasa sikiliza, mwana wa Ahitubu," Naye akajibu, "Niko hapa, bwana wangu."
\v 13 Sauli akamwambia, "Kwa nini unapanga njama dhidi yangu, wewe pamoja na mwana wa Yese, kwa kumpatia mikate, na upanga, na umemwomba Mungu kusudi amsaidie Daudi, kusudi aniasi mimi, na kujificha sehemu ya siri, kama alivyofanya leo?"
1 Samweli 22: 14-15
\s5
\v 14 Ndipo Ahimeleki akamjibu mfalme na kusema, "Je, ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliyemwaminifu kama Daudi, ni nani mkwe wa mfalme na yuko juu ya walinzi wako, na mwenye heshima nyumbani mwako?
\v 15 Je, leo ni mara ya kwanza kwangu kumuomba Mungu apate kumsaidia? Hapana! Mfalme usinilaumu mimi mtumishi wako kwa jambo lolote wala jamaa zangu wote. Maana mimi mtumishi wako sijui lolote kuhusu kadhia hii."
1 Samweli 22: 16-17
\s5
\v 16 Mfalme akamjibu, "Hakika utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya nyumba ya baba yako."
\v 17 Mfalme akamwambia mlinzi aliyesimama karibu naye, "Geuka na uwauwe makuhani wa BWANA. Kwa sababu wanamuunga mkono Daudi, na sababu walijua kwamba alikimbia, lakini hawakunijulisha." Lakini watumishi wa mfalme hawakunyoosha mkono wao kuwaua makuhani wa BWANA.
1 Samweli 22: 18-19
\s5
\v 18 Ndipo mfalme akamwambia Doegi, "Geuka na uwauwe makuhani." Hivyo Doegi Mwedomu akageuka na kuwapiga makuhani; akawaua watu themanini na watano waliovaa naivera ya kitani siku hiyo.
\v 19 Kwa ncha ya upanga, aliupiga Nobu, mji wa makuhani, akiwaua wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng'ombe na punda na kondoo. Wote aliwaua kwa ncha ya upanga.
1 Samweli 22: 20-21
\s5
\v 20 Lakini mmoja wa wana wa Ahimeleki mwana wa Ahitubu, aliyeitwa Abiathari, aliponyoka na kukimbilia kwa Daudi.
\v 21 Abiathari akamwambia Daudi kwamba Sauli amewaua manabii wa BWANA.
1 Samweli 22: 22-23
\s5
\v 22 Daudi akamwambia Abiathari, "Nilifahamu kuwa siku hiyo, Doegi Mwedomu alikuwa mahali pale, kwamba hakika angemwambia Sauli. Nina wajibika kwa kifo cha kila mtu katika familia ya baba yako!
\v 23 Kaa pamoja nami na usiogope. Maana mtu anayetafuta roho yako anatafuta pia roho yangu. Utakuwa salama ukiwa pamoja nami."
\s5
\c 23
\p 1 Samweli 23: 1-2
\v 1 Wakamwambia Daudi, "Tazama, Wafilisti wanaupiga Keila na wanapora nafaka inayopurwa."
\v 2 Hivyo Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya msaada, na akamuuliza," Je, niondoke niwapige hawa Wafilisti? BWANA akamwambia Daudi, "Nenda ukawapige Wafilisti na kuokoa Keila."
1 Samweli 23: 3-4
\s5
\v 3 Daudi akaambiwa na watu wake, "Angalia, hapa Yuda tunaogopa. Je, si zaidi sana kama tutaenda Keila kupambana na majeshi ya Wafilisti?"
\v 4 Ndipo Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya msaada, bado tena, BWANA akamjibu, "Amka, uteremke hadi Keila. Maana nitakupatia ushindi dhidi ya Wafilisti."
1 Samweli 23: 5-6
\s5
\v 5 Daudi na watu wake wakaenda Keila na kupigana na Wafilisti. Wakahamisha ng'ombe wao na kuwapiga kwa mauaji makubwa mno. Hivyo Daudi akawaokoa wenyeji wa Keila.
\v 6 Abiathari mwana wa Ahimeleki alipokuwa amekimbilia kwa Daudi huko Keila, alibeba naivera mkononi mwake.
1 Samweli 23: 7-9
\s5
\v 7 Sauli aliambiwa kwamba Daudi amekwenda Keila. Sauli akasema, "Mungu amemweka mkononi mwangu. Bila shaka amefungiwa ndani kwa sababu ameingia katika mji ulio na malango na makomeo."
\v 8 Sauli akayaita majeshi yake yote kwa ajili ya vita, waende hadi Keila, wamteke Daudi na watu wake.
\v 9 Daudi alijua kwamba Sauli alikuwa anapanga njama za kumdhuru yeye. Ndipo akamwambia kuhani Abiathari kuhani, "Ulete hapa naivera."
1 Samweli 23: 10-11
\s5
\v 10 Kisha Daudi akasema, "BWANA, Mungu wa Israeli, mtumishi wako hakika amesikia kwamba Sauli anatafuta namna ya kuja Keila, ili auteketeze mji kwa ajili yangu.
\v 11 Je, watu wa Keila watanisalimisha mkononi mwake? Je, Sauli atashuka hadi huko, kama mtumishi wako alivyosikia? BWANA, Mungu wa Israeli, nakusihi, tafadhali mwambie mtumishi wako. "BWANA akasema, "Atakuja huko."
1 Samweli 23: 12-12
\s5
\v 12 Kisha Daudi akauliza, "Je, watu wa Keila watanisalimisha mimi na watu wangu katika mkono wa Sauli?" BWANA akasema, "Watu hao watawasalimisha kwao."
1 Samweli 23: 13-14
\s5
\v 13 Kisha Daudi na watu wake, waliokuwa kama mia sita, walitoka na kwenda mbali na Keila, na wakazunguka kila sehemu. Kisha Sauli akaambiwa kwamba Daudi ametoroka kutoka Keila, hivyo akasitisha kumfuatia.
\v 14 Daudi alikaa ngomeni katika jangwa, kwenye nchi ya milima katika jangwa la Zifu. Kila siku Sauli alimtafuta, lakini Mungu hakumweka mkononi mwake.
1 Samweli 23: 15-16
\s5
\v 15 Daudi aliona kwamba Sauli amejitokeza kuangamiza maisha yake; basi Daudi alikuwa katika jjangwa la Zifu huko Horeshi.
\v 16 Kisha Yonathani, mwana wa Sauli, akaamuka akaenda kwa Daudi huko Horshi, naye akamtia moyo amtumainie Mungu.
1 Samweli 23: 17-18
\s5
\v 17 Akamwambia, "Usiogope. Kwa maana mkono wa baba yangu Sauli hautakupata. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, na mimi nitakuwa msaidizi wako. Baba yangu Sauli pia anajua hivyo."
\v 18 Basi wote wawili wakafanya agano mbele za BWANA. Kisha Daudi alibaki Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani.
1 Samweli 23: 19-20
\s5
\v 19 Nndipo Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea wakisema, "Je, Daudi hakujificha kati yetu kwenye ngome huko Horeshi, juu ya mlima wa Hakila, ulioko kusini mwa Yeshimoni?
\v 20 Basi uje, mfalme! Kulingana na matakwa yako, uje! Kazi yetu itakuwa kumtia katika mkono wa mfalme."
1 Samweli 23: 21-23
\s5
\v 21 Sauli akasema, "Mbarikiwe na BWANA. Kwa sababu mmenihurumia.
\v 22 Nendeni, mhakikishe sawasawa. Tafuteni na kujua maficho yake yako wapi na ni nani amemwona huko. Nimeambiwa kwamba yeye ni mjanja sana.
\v 23 Kwa hiyo chunguzeni, mjue sehemu zote anakojificha. Baadaye rudini kwangu mkiwa na taarifa kamili, na kisha nitaongozana nanyi. Ikiwa yupo katika nchi, nitamtafuta kutoka miongoni mwa elfu zote za Yuda."
1 Samweli 23: 24-25
\s5
\v 24 Ndipo wakaamka na kwenda hadi Zifu mbele ya Sauli. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa katika jangwa la Maoni, huko Araba upande wa kusini mwa Yeshimoni.
\v 25 Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta Daudi. Na Daudi akaambiwa habari hiyo, hivyo akateremka hadi kwenye mlima wa miamba na akakaa katika jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hivyo, akamfukuza Daudi katika Jangwa la Maoni.
1 Samweli 23: 26-27
\s5
\v 26 Sauli akaenda akawa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa wakienda upande mwingine wa mlima. Daudi kwa haraka akatoweka akae mbali na Sauli. Kwa sababu Sauli na watu wake walikuwa wakimzunguka Daudi na watu wake wawakamate,
\v 27 mjumbe mmoja akaja kwa Sauli na kusema, "Njoo, harakisha maana Wafilisti wamepanga uvamizi juu ya nchi."
1 Samweli 23: 28-29
\s5
\v 28 Kwa hiyo Sauli akarudi asimfuatie Daudi na akaenda kupambana na Wafilisti. Kwa hiyo sehemu ile iliitwa Mwamba wa Maficho.
\v 29 Daudi akapanda kutoka huko na kukaa katika ngome ya Engedi.
\s5
\c 24
\p 1 Samweli 24: 1-2
\v 1 Sauli aliporudi kuwafukuza Wafilisti, akaambiwa kwamba, "Daudi yuko katika jangwa la Engedi."
\v 2 Ndipo Sauli akachukua watu elfu tatu waliochaguliwa kutoka Iraeli yote, wakaenda kumtafuta Daudi na watu wake katika miamba ya Mbuzi Mwitu.
1 Samweli 24: 3-4
\s5
\v 3 Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, mahali palipokuwa na pango. Sauli akaingia ndani yake kujisaidia. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa wamekaa mbali zaidi ndani ya pango lilelile.
\v 4 Watu wake Daudi wakamwambia, "Hii ndiyo siku ambayo BWANA aliisema akikuambia, 'Nitamweka adui wako mkononi mwako, ili umtendee kama unavyotaka."' Kisha Daudi akainuka na kumnyemelea kwa mbele kimya kimya na kulikata pindo la kanzu ya Sauli.
1 Samweli 24: 5-7
\s5
\v 5 Baadaye moyo wa Daudi ukamchoma kwa sababu alilikata pindo la kanzu ya Sauli.
\v 6 Akawaambia watu wake, "BWANA anisamehe, sikupaswa kumtendea jambo hili bwana wangu, Mtiwa mafuta wa BWANA, kwa kunyoosha mkono wangu juu yake, maana yeye ni masihi wa BWANA."
\v 7 Hivyo Daudi akawakemea watu wake kwa maneno haya, na kuwazuia wasimpige Sauli. Sauli akasimama, akatoka pangoni, na kwenda zake.
1 Samweli 24: 8-9
\s5
\v 8 Baadaye tena, Daudi akasimama juu, akatoka pangoni, na kumwita Sauli: "Bwana wangu mfalme." Sauli alipotazama nyuma, Daudi akasujudu hadi chini na kuonyesha heshima.
\v 9 Daudi akamwambia Sauli, "Kwa nini unawasikiliza watu ambao wanasema, "Angalia, Daudi anatafuta kukudhuru?'
1 Samweli 24: 10-11
\s5
\v 10 Leo macho yako yameona jinsi BWANA alivyokuweka mkononi mwangu tulipokuwa ndani ya pango. Wengine waliniambia nikuuwe, lakini nilikuacha hai. Nikasema, 'Sitanyoosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa kuwa ni masihi wa BWANA.'
\v 11 Tazama, baba yangu, angalia pindo la kanzu yako mkononi mwangu. Kwa maana kama nilikata pindo la kanzu yako na sikukuua, basi ujuwe na uone kwamba sina uovu au kosa katika mkono wangu, na sijafanya dhambi juu yako, ingawa unawinda kuutoa uhai wangu.
1 Samweli 24: 12-13
\s5
\v 12 BWANA aamue kati yangu na wewe, na BWANA anilipizie kisasi juu yako, lakini mkono wangu kamwe hautakuwa juu yako.
\v 13 Kama mithali ya wazee isemavyo, 'Katika waovu hutoka uovu.' Lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.
1 Samweli 24: 14-15
\s5
\v 14 Mfalme wa Israeli ametoka kumuandama nani? Unamsaka nani? Unasaka mzoga wa mbwa! Unasaka kiroboto!
\v 15 BWANA na awe mwamuzi na atoe hukumu kati yangu na wewe, na akaione, na akatetee sababu yangu na aniruhusu kuepuka mkono wako."
1 Samweli 24: 16-16
\s5
\v 16 Daudi alipomaliza kuongea maneno haya kwa Sauli, Sauli akasema, "Hii ni sauti yako, mwanangu Daudi?" Sauli alinyanyua sauti yake akalia.
1 Samweli 24: 17-18
\s5
\v 17 Akamwambia Daudi, "Wewe ni mwenye haki kuliko mimi. Kwa sababu umenilipa mazuri, wakati mimi nimekulipa maovu.
\v 18 Leo umetangaza jinsi ulivyonitendea mazuri, kwa sababu hukuniua wakati BWANA aliponiweka katika rehema yako.
1 Samweli 24: 19-20
\s5
\v 19 Kwa kuwa mtu akimpata adui yake, atamwacha aende zake salama? Na BWANA akuzawadie mema kwa kile ulichonifanyia leo.
\v 20 Basi, najua kwa hakika kwamba utakuwa mfalme na kwamba ufalme wa Israeli utaimarika katika mkono wako.
1 Samweli 24: 21-22
\s5
\v 21 Niapie kwa BWANA kwamba baada yangu hautawakatilia mbali uzao wangu, na kwamba hautaliharibu jina langu katika nyumba ya baba yangu."
\v 22 Hivyo Daudi akamwapia Sauli kiapo. Kisha Sauli akaenda nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.
\s5
\c 25
\p 1 Samweli 25: 1-1
\v 1 Basi Samweli akafariki. Waisraeli wote wakakusanyika pamoja na kumwomboleza, na wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akainuka na akashuka hadi jangwa la Parani.
1 Samweli 25: 2-3
\s5
\v 2 Kulikuwa na mtu mmoja huko Maoni, na mali zake zilikuwa huko Karmali. Mtu huyo alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja. Naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.
\v 3 Na mtu huyo aliitwa Nabali, na jina la mke wake aliitwa Abigaili. Mwanamke huyo alikuwa mwenye busara na mzuri kwa sura. Lakini mwanaume alikwa mkaidi na mwovu katika mambo yake. Alikuwa wa uzao wa nyumba ya Kalebu.
1 Samweli 25: 4-6
\s5
\v 4 Daudi akasikia akiwa jangwani kwamba Nabali alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake.
\v 5 Hivyo Daudi aliwatuma kwake vijana kumi. Akawaambia wale vijana, "Pandeni kwanda Karmeli, mwendeeni Nabali, na mkamsalimie kwa jina langu.
\v 6 Mtamwambia, 'Uishi katika baraka, Uwe na amani na nyumba yako iwe na amani, na wote ulionao wawe na amani.
1 Samweli 25: 7-8
\s5
\v 7 Nasikia kwamba unao wakata manyoya. Wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, na hatukuwafanyia ubaya, na muda wote wakiwa Karmeli hawakupotelewa kitu chochote.
\v 8 Waulize vijana wako, nao watakuambia. Basi vijana wangu wapate kibali machoni pako, maana tumefika siku ya sherehe. Tafadhali utoe cho chote ulicho nacho mkononi kwa watumishi wako na kwa Daudi mwanao.'"
1 Samweli 25: 9-11
\s5
\v 9 Vijana wa Daudi walipofika, walimwambia Nabali yote haya kwa niaba ya Daudi na kisha wakasubiri.
\v 10 Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, "Daudi ni nani? Na ni nani mwana wa Yese? Siku hizi wapo watumishi wengi wanaotoroka bwana zao.
\v 11 Je, nichukue mkate wangu na maji yangu na nyama yangu ambayo nimewachinjia wakata manyoya wangu, na niwape watu wanaotoka nisikokujua?"
1 Samweli 25: 12-13
\s5
\v 12 Hivyo vijana wa Daudi waligeuka na kurudi, nakumwambia kila kitu kilichosemwa.
\v 13 Daudi akawaambia watu wake, "Kila mtu ajifunge upanga wake." Kila mtu akajifunga upanga wake. Daudi naye pia akajifunga upanga wake. Yapata kama watu mia nne wakafuatana na Daudi, na wengine mia mbili walibaki kulinda mizigo yao.
1 Samweli 25: 14-15
\s5
\v 14 Lakini kijana mmojawapo alimwambia Abigaili, mke wa Nabali akasema, "Daudi aliwatuma wajumbe kutoka jangwani waje wamsalimu bwana wetu, na yeye akawatukana.
\v 15 Bado watu hawa walitutendea mema. Hatukudhurika na hatukupoteza chochote wakati wote tulipotembea nao tulipokuwa mbugani.
1 Samweli 25: 16-17
\s5
\v 16 Walikuwa ukuta wetu usiku na mchana, wakati wote tulikuwa pamoja nao tukichunga kondoo.
\v 17 Kwa hiyo tambua hili na zingatia utafanya nini, maana ubaya unamvizia bwana wetu, na utakuwa juu ya nyumba yake yote. Yeye ni mtu asiyefaa na hakuna awezaye kushauriana naye."
1 Samweli 25: 18-19
\s5
\v 18 Ndipo Abigaili akaharakisha na akachukuwa mikate mia mbili, chupa mbili za divai, kondoo watano waliokwisha andaliwa, vipimo vitano vya bisi, vishada mia moja vya zabibu, na mikate mia mbili ya tini na akavipakia juu ya punda.
\v 19 Akamwambia kijana wake, "Tangulia mbele yangu, nami nitakuja nyuma yako." Lakini hakumwambia mmewe Nabali.
1 Samweli 25: 20-20
\s5
\v 20 Alipokuwa akienda juu ya punda wake na kutelemka penye kificho cha mlima, Daudi na watu wake walishuka chini wakimwelekea Abigaili, naye akakutana nao.
1 Samweli 25: 21-22
\s5
\v 21 Basi Daudi alikuwa amesema, "Hakika nimelinda bure vyote alivyonavyo mtu huyu huko nyikani, na vyote alivyonavyo hakuna kilichopotea, pamoja na hayo amenilipa mabaya badala ya mema.
\v 22 Mungu na anitendee hivyo mimi, Daudi, pia iwe zaidi, iwapo nitamwacha hata mtu mmoja wa kwake akiwa hai ifikapo kesho asubuhi.
1 Samweli 25: 23-24
\s5
\v 23 Abigaili alipomwona Daudi, aliharakisha na kushuka chini ya punda wake, akalala kifudifudi na kujiinamisha hadi chini.
\v 24 Akamwangukia miguuni pake na kusema, "Juu yangu tu, bwana wangu, na uwe uovu. Tafadhali acha mjakazi wako aseme nawe, tena uyasikilize maneno ya mjakazi wako.
1 Samweli 25: 25-26
\s5
\v 25 Nakusihi bwana wangu usimjali mtu huyu asiyefaa, Nabali, kwa maana kama jina lake lilivyo, ndivyo alivyo. Jina lake ni Nabali, na upumbavu uko pamoja naye. Lakini mimi mjakazi wako sikuwaona vijana wa bwana wangu, uliowatuma.
\v 26 Sasa basi, bwana wangu, kama BWANA aishivyo, na kama unavyoishi, kwa kuwa BWANA amekuondoa kutoka kumwaga damu, na kuacha kulipiza kisasi kwa mkono mwenyewe, basi adui zako, na wale ambao wanatafuta kumfanyia uovu bwana wangu, wawe kama Nabali
1 Samweli 25: 27-28
\s5
\v 27 Na sasa zawadi hii ambayo mjakazi wako ameileta kwa bwana wangu, na wapewe vijana ambao wanamfuata bwana wangu.
\v 28 Tafadhali ulisamehe kosa la mjakazi wako, maana BWANA hakika atamfanyia bwana wangu nyumba imara, kwa sababu bwana wangu anapigana vita vya BWANA; na uovu hautaonekana ndani yako maadamu unaishi.
1 Samweli 25: 29-29
\s5
\v 29 Na ingawa watu wangeinuka na kukuandama ili wakuue, bado uhai wa bwana wangu utafungwa katika furushi la walio hai na BWANA Mungu wako; na atayatupa maisha ya adui zako mbali, kama vile kutoka katika mfuko wa kombeo.
1 Samweli 25: 30-31
\s5
\v 30 Na itakuwa, BWANA atakapokuwa amemtimizia bwana wangu mambo yote mazuri ambayo amekuahidi, na alivyokufanya kiongozi juu ya Israeli,
\v 31 jambo hili halitakuwa huzuni kwako, wala chukizo moyoni kwa bwana wangu, kwa sababu hukumwaga damu bila sababu, na hujajilipizia kisasi. Na BWANA akikuletea mafanikio, umkumbuke mjakazi wako."
1 Samweli 25: 32-33
\s5
\v 32 Ndipo Daudi akamwambia Abigaili, "BWANA, Mungu wa Israeli, abarikiwe, aliyekutuma uonane na mimi leo.
\v 33 Na hekima yako ibarikiwe, nawe umebarikiwa, kwa sababu leo umenizuia nisiwe na hatia ya kumwaga damu, na kutojilipizia kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.
1 Samweli 25: 34-35
\s5
\v 34 Kwa kweli, kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye amenizuia nisikuumize, kama usinge harakisha kuja ukutane nami, kwa hakika kesho asubuhi asinge salia hata mtoto mmoja wa kiume kwa Nabali."
\v 35 Kwa hiyo Daudi akavipokea kutoka mkononi mwake vile alivyokuwa amemletea; akamwambia, "Nenda kwa amani hadi nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako na nimekubali."
1 Samweli 25: 36-36
\s5
\v 36 Abigaili akarudi kwa Nabali; tazama, alikuwa akifanya sherehe katika mji wake, kama sherehe ya mfalme; na moyo wa Nabali ulifurahi ndani yake, kwa sababu alikwa amelewa sana. Kwa hiyo hakumwambia chochote kabisa hadi kulipopambazuka
1 Samweli 25: 37-38
\s5
\v 37 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, basi mkewe akamwambia mambo hayo; moyo wake ukafa ndani yake, na akawa kama jiwe.
\v 38 Ikawa baada ya siku kumi BWANA alimpiga Nabali naye akafa.
1 Samweli 25: 39-40
\s5
\v 39 Naye Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, "BWANA abarikiwe, aliyenichukulia hatua ya shutuma yangu kutoka mkono wa Nabali, na kumzuia mtumishi wake asifanye maovu. Na amemrudishia Nabali tendo la uovu juu ya kichwa chake mwenyewe." Ndipo Daudi akawatuma watu wakaongee na Abigaili, ili amchukue awe mke wake.
\v 40 Watumishi wake Daudi walipofika kwa Abigaili huko Karmeli, wakaongea naye na kusema, "Daudi ametutuma kwako tukuchukue hadi kwake uwe mke wake."
1 Samweli 25: 41-42
\s5
\v 41 Abigaili aliinuka, akainamisha uso chini, na akasema, "Tazama, mjakazi wako ni mtumwa aoshaye miguu ya watumishi wa bwana wangu."
\v 42 Akaharakisha na kuamka, akapanda punda akiwa na vijakazi wake watano waliofuatana naye; akawafuata wajumbe wa Daudi, na akawa mke wake.
1 Samweli 25: 43-44
\s5
\v 43 Daudi pia alimchukua Ahinoamu wa Yezreeli akamwoa; wote wawili wakawa wake zake.
\v 44 Wakati huo Sauli alikuwa amempa Palti, mwana wa Laishi mtu wa Galimu, Mikali, binti yake, aliyekuwa mke wa Daudi.
\s5
\c 26
\p 1 Samweli 26: 1-2
\v 1 Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, "Je, Daudi akujificha katika vilima vya Hakila, ambavyo viko mbele ya jangwa?"
\v 2 Kisha Sauli akaamka na kwenda chini ya jangwa la Zifu, akiwa na watu elfu tatu waliochaguliwa katika Israeli, wamtafute Daudi katika jangwa la Zifu.
1 Samweli 26: 3-4
\s5
\v 3 Sauli akaweka kambi kwenye kilima cha Hakila, kilicho mbele ya jangwa, kando ya barabara. Lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, na akaona kwamba Sauli alikuwa anamfuatia huko jangwani.
\v 4 Hivyo Daudi akawatuma wapelelezi na akafahamu kwamba hakika Sauli alikuwa amekuja.
1 Samweli 26: 5-5
\s5
\v 5 Daudi akaamka na kwenda hadi mahali ambapo Sauli alipiga kambi; akaona mahali alipolala Sauli, na Abneri mwana wa Neri, mkuu wa jeshi lake; Sauli alilala katikati ya kambi, na watu walipiga kambi kumzunguka, na wote wamesinzia.
1 Samweli 26: 6-8
\s5
\v 6 Ndipo Daudi akamwambia Ahimeleki Mhiti, na Abishai mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, "Ni nani atakwenda nami kambini kwa Sauli? Abishai akasema, "Mimi nitashuka pamoja nawe."
\v 7 Hivyo Daudi na Abishai wakaliendea jeshi usiku. Na Sauli alikuwapo akisinzia ndani ya kambi, mkuki wake umechomekwa chini pembeni mwa kichwa chake. Abneri na Askari wake wamelala kwa kumzunguka.
\v 8 Kisha Abishai akamwambia Daudi, "Leo Mungu amemweka adui yako mkononi mwako. Basi tafadhali acha nimchome mkuki nimtoboe hadi chini kwa pigo moja. Sitampiga mara mbili."
1 Samweli 26: 9-10
\s5
\v 9 Daudi akamwambia Abishai, "Usimwangamize; kwa maana nani awezaye kunyoosha mkono wake dhidi ya mtiwa mafuta wa BWANA na asiwe na hatia?"
\v 10 Daudi akasema, "Kama BWANA aishivyo, BWANA atamuua, au siku ya kufa kwake itakuja, au atakwenda katika vita na ataangamia.
1 Samweli 26: 11-12
\s5
\v 11 BWANA apishe mbali nisinyooshe mkono wangu dhidi ya mtiwa mafuta wake; lakini sasa, nakusihi chukua mkuki uliokichwani pake na jagi la maji, tuondoke."
\v 12 Hivyo Daudi akachukua mkuki na jagi la maji kutoka kichwani pa Daudi, wakatoweka. Hakuna mtu aliyewaona au kufahamu habari hii, wala hakuna aliyetoka usingizini, maana wote walisinzia, kwa sababu usingizi mzito kutoka kwa BWANA uliwaangukia.
1 Samweli 26: 13-14
\s5
\v 13 Kisha Daudi akaenda upande mwingine na akasimama juu ya mlima mbali sana; ukiwepo umbali mkubwa katikati yao.
\v 14 Daudi akawapigia kelele watu hao na Abneri mwana Neri; akisema, "Hujibu neno, Abneri?" Ndipo Abneri akajibu na kusema, "Wewe ni nani unayempigia mfalme kelele?"
1 Samweli 26: 15-16
\s5
\v 15 Daudi akamwambia Abneri, "Wewe siye mtu jasiri? Ni nani yuko kama wewe katika Israeli? Kwa nini basi hukukaa macho kumlinda bwana wako mfalme? Kwa maana mtu fulani aliingia kumuua mfalme, bwana wako.
\v 16 Jambo hili ulilolifanya siyo zuri. Kama BWANA aishivyo, unapaswa kufa kwa sababu hukumlinda bwana wako, mtiwa mafuta wa BWANA. Na sasa tazama ulipo mkuki wa mfalme, na jagi la maji lililokuwa kichwani pake."
1 Samweli 26: 17-18
\s5
\v 17 Sauli aliitambua sauti ya Daudi akasema, "Hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?" Daudi akasema, "Ni sauti yangu, mfalme, bwana wangu."
\v 18 Daudi akasema, "Kwa nini bwana wangu anamwandama mtumishi wake? Nimefanya nini? Mkononi mwangu kuna uovu gani?
1 Samweli 26: 19-20
\s5
\v 19 Kwa hiyo sasa, nakusihi, bwana wangu mfalme asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama ni BWANA ndiye amekuchochea dhidi yangu, na aikubali sadaka; lakini kama ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA, maana leo wamenifukuza, nisishikamane na urithi wa BWANA; wameniambia, 'Nenda ukaabudu miungu mingine.'
\v 20 Kwa hiyo, sasa, usiiachilie damu yangu ianguke ardhini mbali na uwepo wa BWANA; kwa kuwa mfalme wa Israeli ametoka nje kutafuta kiroboto, kama vile mtu awindavyo kware milimani."
1 Samweli 26: 21-21
\s5
\v 21 Kisha Sauli akasema, "Nimefanya dhambi. Rudi, Mwanangu, Daudi; maana sitakudhuru tena, kwa sababu leo maisha yangu yalikuwa yenye thamani machoni pako. Tazama, nimetenda upumbavu na nimekosa sana."
1 Samweli 26: 22-23
\s5
\v 22 Daudi akajibu na akasema, "Tazama, mkuki wako uko hapa, mfalme! Mruhusu kijana mmojawapo aje auchukue na aulete kwako.
\v 23 Na BWANA amlipe kila mtu kwa ajili ya uadilifu wake na kwa uaminifu wake; kwa sababu leo BWANA alikuweka mkononi mwangu, lakini nisinge mpiga mtiwa mafuta wake.
1 Samweli 26: 24-25
\s5
\v 24 Na tazama, kama maisha yako leo yalivyokuwa ya thamani machoni pangu, vivyo hivyo maisha yangu yathaminiwe sana machoni pa BWANA, na aweze kuniokoa katika shida zote."
\v 25 Ndipo Sauli akamwambia Daudi, "Na ubarikiwe, mwanangu Daudi, ili uweze kutenda mambo makuu, na hakika uweze kufanikiwa." Ndipo Daudi akaenda zake, na Sauli akarudi kwake.
\s5
\c 27
\p 1 Samweli 27: 1-1
\v 1 Daudi alisema moyoni mwake, "Basi, siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jambo zuri kwangu kuliko kutoroka hadi nchi ya Wafilisti; Sauli atakata tamaa asinitafute tena ndani ya mipaka yote ya Israeli; kwa njia hii nitaponyoka kutoka mkono wake."
1 Samweli 27: 2-4
\s5
\v 2 Daudi akaondoka na kuvuka, akiwa pamoja na watu mia sita hadi kwa Akishi mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.
\v 3 Daudi akaishi na Akishi huko Gathi pamoja na watu wake, na kila mtu na familia yake, na Daudi akiwa na wake zake wawili, Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili Mkarmeli aliyekuwa mke wa Nabali.
\v 4 Sauli akaambiwa kuwa Daudi amekimbilia Gathi, hivyo hakumtafuta tena.
1 Samweli 27: 5-7
\s5
\v 5 Daudi akamwambia Akishi, "Kama nimepata kibali machoni pako, wanipatie mahali katika mojawapo ya miji ya nchi, ili nikae huko: kwa nini mtumishi wako akae pamoja na wewe katika mji wa kifalme?"
\v 6 Hivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi Ziklagi; ndiyo sababu mji wa Ziklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hadi leo.
\v 7 Idadi ya siku ambazo Daudi aliishi katika nchi ya Wafilisti ulikuwa mwaka mmoja na miezi minne.
1 Samweli 27: 8-9
\s5
\v 8 Daudi na watu wake walizipiga sehemu mbalimbali, wakiteka nyara Wageshuri, Wagirizi, na Waamaleki; kwa maana mataifa hayo ndio walikuwa wakaaji wa nchi, kwa uelekeo wa kwenda Shuri hadi kufika nchi ya Misri. Walikuwa wamekaa katika nchi hiyo toka nyakati za zamani.
\v 9 Daudi aliipiga nchi na hakumwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai; akatwaa kondoo, ng'ombe, punda, ngamia, na nguo; kisha alirudi na kufika tena kwa Akishi.
1 Samweli 27: 10-10
\s5
\v 10 Ndipo Akishi humuuliza, "Je, leo umefanya mashambulizi dhidi ya nani?" Daudi humjibu, "Nimefanya dhidi ya kusini mwa Yuda," au dhidi ya kusini mwa Wayerameeli," au "dhidi ya kusini mwa Wakeni."
1 Samweli 27: 11-12
\s5
\v 11 Daudi asingemwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai awalete hadi Gathi, akisema, "ili wasije kututeta, 'Daudi amefanya hivi na vile."' Hivi ndivyo alivyofanya kwa kipindi chote alichokaa katika nchi ya Wafilisti.
\v 12 Akishi alimwamini Daudi, akisema, "Amesababisha watu wake Israeli wamchukie kabisa; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu milele."
\s5
\c 28
\p 1 Samweli 28: 1-2
\v 1 Ikawa katika siku hizo Wafilisti walikusanya majeshi yao pamoja kwa ajili ya vita, wapigane na Israeli. Akishi akamwambia Daudi, "Ujue kwa hakika kwamba utakwenda nami ndani ya jeshi, wewe na watu wako."
\v 2 Naye Daudi akamwambia Akishi, "Sasa utajua kile ambacho mtumishi wako anaweza kufanya." Akishi akamwambia Daudi, "Basi sasa, nitakufanya uwe mlinzi wangu binafsi daima."
1 Samweli 28: 3-4
\s5
\v 3 Samweli alikuwa amefariki; Waisraeli wote walimwomboleza na kumzika huko Rama, katika mji wake mwenyewe. Wakati huo Sauli alikuwa amewafukuza kutoka nchini wote walioongea na wafu au pepo.
\v 4 Wafilisti walijikusanya wao wenyewe wakaja na kuweka kambi huko Shunemu; na Sauli akawakusanya Israeli wote pamoja, na wakaweka kambi yao huko Gilboa.
\s5
\v 5 Sauli alipoona jeshi la Wafilisti, aliogopa na moyo wake ukatetemeka sana.
\v 6 Sauli alipomuomba BWANA kwa ajili ya msaada, BWANA hakumjibu - si kwa ndoto wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
\v 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, "Mnitafutie mwanamke ambaye anaweza kuongea na wafu, ili ni mwendee na kutafuta msaada wake." Watumishi wake wakamwambia, "Tazama, yupo mwanamke huko Endori awezaye kuongea na wafu."
1 Samweli 28: 8-10
\s5
\v 8 Basi Sauli akajigeuza, akavaa nguo nyingine tofauti, akaondoka yeye pamoja na watu wawili; wakamwendea yule mwanamke wakati wa usiku. Akasema, "Nitabirie, nakuomba, kwa kuongea na wafu, na uniinulie yule nitakayekutajia."
\v 9 Yule mwanamke akamwambia, "Tazama, unajua alichofanya Sauli, jinsi alivyowafukuza kutoka katika nchi wanaoongea na wafu au mizimu. Basi kwa nini mnatega mtego kwa ajili ya uhai wangu, ili kuniua?"
\v 10 Sauli akamwapia kwa BWANA na kusema, "Kama BWANA aishivyo, hakuna adhabu utakayopata kutokana na jambo hili."
1 Samweli 28: 11-12
\s5
\v 11 Kisha yule mwanamke akasema, "Je, nikuinulie nani?" Sauli akasema, "Niinulie Samweli."
\v 12 Yule mwanamke alipomwona Samweli, akalia kwa sauti kuu na kusema na Sauli, akisema, "Kwa nini umenidanganya? Maana wewe ni Sauli."
1 Samweli 28: 13-14
\s5
\v 13 Mfalme akamwambia, "Usiogope. Unaona kitu gani?" Yule mwanamke akamwambia Sauli, "Naona mungu akitoka katika nchi." Akamuuliza mwanamke,
\v 14 "Je, anafanana na nani?" Mwanamke akajibu, "Mtu mzee anazuka; naye amevaa kanzu." Sauli akafahamu kuwa huyo ni Samweli, naye Sauli akainamisha uso wake hadi chini akionesha heshima.
1 Samweli 28: 15-15
\s5
\v 15 Samweli akamwambia Sauli, "Kwa nini umenisumbua na kuniinua juu?" Sauli akajibu, "Nimetaabika sana, maana Wafilisti wamepanga vita dhidi yangu, na Mungu ameniacha na hanipi majibu tena, si kwa manabii, wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita, ili unijulishe kile nitakachofanya."
1 Samweli 28: 16-17
\s5
\v 16 Samweli akasema, "Kwa kuwa BWANA amekuacha, basi unaniuliza nini, naye amekuwa adui yako?
\v 17 BWANA amekutendea kile alichosema kuwa angekifanya. BWANA amerarua ufalme kutoka mkononi mwako na amempa ufalme mtu mwingine - amempa Daudi.
1 Samweli 28: 18-19
\s5
\v 18 Kwa sababu hukuitii sauti ya BWANA na hukutekeleza hasira yake kali juu ya Amaleki, kwa hiyo leo naye amefanya hili kwako.
\v 19 Zaidi ya hayo, BWANA atamweka Israeli pamoja na wewe katika mkono wa Wafilisti. Kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. BWANA pia ataliweka jeshi la Israeli katika mkono wa Wafilisti."
1 Samweli 28: 20-21
\s5
\v 20 Ndipo ghafla Sauli alianguka chini kifudifudi na aliogopa kwa sababu ya yale maneno ya Samweli. Aliishiwa nguvu mwilini mwake, kwa kuwa siku hiyo alikuwa hajala chakula, hata kwa usiku huo wote.
\v 21 Ndipo yule mwanamke akaja kwa Sauli na akaona kwamba Sauli amepata shida, naye akamwambia, "Tazama, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako; Nimeyaweka maisha yangu mkononi mwangu na nimeyasikiliza maneno uliyoniambia.
1 Samweli 28: 22-23
\s5
\v 22 Hivyo basi, nakusihi, sikiliza pia sauti ya mjakazi wako, na uniruhusu nilete chakula kidogo mbele yako. Ule ili upate nguvu za kwenda kule uendako."
\v 23 Lakini Sauli alikataa na kusema, "Sitakula." Lakini watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha hatimaye alisikiliza sauti zao. Hivyo aliinuka kutoka chini na kukaa kitandani.
1 Samweli 28: 24-25
\s5
\v 24 Yule mwanamke alikuwa na ndama mnono hapo nyumbani; akafanya haraka na kumchinja; akachua unga, akaukanda, na akatengeneza mikate isiyotiwa chachu kwa unga huo.
\v 25 Akaileta mbele ya Sauli na watumishi wake, nao wakala. Baaadaye waliinuka na kuondoka usiku huo.
\s5
\c 29
\p 1 Samweli 29: 1-2
\v 1 Basi Wafilisti walikusanya pamoja majeshi yao yote huko Afeki; Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli.
\v 2 Nao wakuu wa Wafilisti wakapitwa na mamia kwa maelfu; Daudi na watu wake wakapita wakiwa wa mwisho pamoja na Akishi.
1 Samweli 29: 3-3
\s5
\v 3 Kisha wakuu wa Wafilisti wakasema, "Hawa Waebrania wanafanya nini hapa?" Akishi akawaambia wakuu wengine wa Wafilisti, "Huyu si Daudi, mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amekaa nami kwa siku hizi, au kwa miaka hii, nami nimeona hana kosa tangu aje kwangu hadi leo?"
1 Samweli 29: 4-4
\s5
\v 4 Lakini wale wakuu wa Wafilisti walimkasirikia Akishi; wakamwabia, Mfukuze mtu huyo, aende kwake kule ulikompatia; usimruhusu aende nasi vitani, ili asiwe adui yetu katika vita. Kwa jinsi gani mtu huyu angeweza kufanya amani na bwana wake? Siyo kwa gharama ya vichwa vya watu wetu?
1 Samweli 29: 5-5
\s5
\v 5 Je, huyu siye Daudi ambaye walimuimba kwa kupokezana na kucheza, wakisema: 'Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi makumi elfu yake?"'
1 Samweli 29: 6-7
\s5
\v 6 Ndipo Akishi alimwita Daudi na kumwambia, "Kama BWANA aishivyo, umekuwa mwema, na kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema kama nionavyo mimi; maana sijaona kosa kwako tangu siku unakuja kwangu hadi siku hii ya leo. Hata hivyo, wakuu hawakupendi.
\v 7 Basi sasa rudi na uende kwa amani, ili usiwakwaze wakuu wa Wafilisti."
1 Samweli 29: 8-9
\s5
\v 8 Daudi akamwambia Akishi, "Lakini nimefanya nini? Kitu gani umekiona kwa mtumishi wako kwa muda ambao nimekuwa mbele yako hadi leo, kiasi kwamba nisiende kupigana na adui za bwana wangu mfalme?"
\v 9 Akishi akajibu na kumwambia Daudi, "Najua kwamba hauna lawama mbele zangu kama alivyo malaika wa Mungu; hata hivyo, wale wakuu wa Wafilisti wamesema, Kamwe hatapanda pamoja nasi hadi vitani.'
1 Samweli 29: 10-11
\s5
\v 10 Basi sasa amka asubuhi na mapema na watumishi wa bwana wako waliokuja pamoja nawe; mara tu muamkapo asubuhi na mapema na kupata mwanga, ondokeni."
\v 11 Hivyo Daudi aliamka mapema, yeye pamoja na watu wake, waondoke asubuhi, warudi kule katika nchi ya Wafilisti. Lakini Wafilisti walipanda kwenda Yezreeli.
\s5
\c 30
\p 1 Samweli 30: 1-2
\v 1 Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Ziklagi siku ya tatu, Waamaleki walifanya mashambulizi katika Negevu na Ziklagi. Waliupiga Ziklagi, wakauchoma moto mji,
\v 2 na kuwachukua mateka wanawake na kila mmoja aliyekuwa ndani yake, mkubwa kwa mdogo. Wao hawakuua hata mmoja, lakini waliwachukua watu na kuondoka nao.
1 Samweli 30: 3-4
\s5
\v 3 Daudi na watu wake walipofika kwenye mji, ulikuwa umechomwa moto - na wake zao, watoto wao wakiume na wakike walichukuliwa mateka.
\v 4 Ndipo Daudi na watu aliokuwa nao wakapaza sauti zao na kulia hadi walipokuwa hawana nguvu zaidi za kulia.
1 Samweli 30: 5-6
\s5
\v 5 Wake wawili wa Daudi walichukuliwa mateka, yaani Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili aliyekuwa mke wa Nabali Mkarmeli.
\v 6 Daudi aliguswa sana, maana watu walikuwa wanaongea kuhusu kumpiga mawe, kwa sababu roho za watu wote walihuzunika, kila mtu kwa ajili ya mtoto wake wakiume na wakike, lakini Daudi alijiimarisha katika BWANA, Mungu wake.
1 Samweli 30: 7-8
\s5
\v 7 Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, "Tafadhali, niletee hapa ile naivera."Abiathari akaileta hiyo naivera kwa Daudi.
\v 8 Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya mwongozo, akisema, "Je, kama nikiliandama jeshi hili, nitalipata?" BWANA akamjibu, "Wafuate, maana kweli utawapata, na kwa hakika utarudisha kila kitu."
1 Samweli 30: 9-10
\s5
\v 9 Kwa hiyo Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye; nao wakafika katika kijito cha Bethori, mahali walipokaa wale walioachwa nyuma.
\v 10 Lakini Daudi aliendelea kuwafuata, yeye na watu mia nne; maana wale mia mbili walibaki nyuma, wakiwa wamechoka kiasi cha kutoweza kuvuka kijito cha Besori.
1 Samweli 30: 11-12
\s5
\v 11 Nao walimkuta Mmisri shambani na wakamleta kwa Daudi; wakampatia mkate, na akala; wakampa maji ya kunywa;
\v 12 kisha walimpa kipande cha keki ya tini na vishada viwili vya zabibu. Alipomaliza kula, akapata nguvu tena, kwa kuwa alikuwa hajala mkate wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.
1 Samweli 30: 13-14
\s5
\v 13 Ndipo Daudi akamuuliza, "Wewe ni mtu wa nani? Je, unatoka wapi?" Naye akajibu, "Mimi ni kijana wa Misri, mtumishi wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu siku tatu zilizopita nilikuwa mgonjwa.
\v 14 Tulifanya mashambulizi dhidi ya Negevu ya Wakerethi, na iliyochini ya Yuda, na ile Negevu ya Kalebu, na kuichoma moto Ziklagi."
1 Samweli 30: 15-15
\s5
\v 15 Daudi akamwambia, "Je, utanipeleka hadi kwa jeshi lililofanya mashabulizi?" Huyo Mmisri akasema, "Uniapie kwa Mungu kwamba hautaniua au kunisaliti na kuniweka katika mikono ya bwana wangu, nami nitakupeleka liliko hilo jeshi."
1 Samweli 30: 16-17
\s5
\v 16 Yule Mmisri alipompeleka huko Daudi, hao wateka nyara walikuwa wametawanyika kila sehemu, wakila na kunywa, na wakicheza, kwa sababu ya nyara zote walizokuwa wamezitwaa kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka nchi ya Yuda.
\v 17 Daudi akawashambulia tangu jua lilipozama hadi jioni ya siku ya pili. Hakuna mtu aliyeponyoka isipokuwa vijana mia nne, waliopanda ngamia na kukimbia.
1 Samweli 30: 18-20
\s5
\v 18 Daudi akarudisha vyote ambavyo Waamaleki walikuwa wamevichukua; na Daudi akawaokoa wake zake wawili.
\v 19 Hakuna kilichopotea, si kidogo wala kikubwa, si watoto wa kiume wala wa kike, si mali iliyotekwa, wala chochote ambacho wavamizi alikichukuwa kwa ajili yao. Daudi akawa amerejesha kila kitu.
\v 20 Akachukua makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambayo watu waliyatanguliza mbele ya ng'ombe wengine. Wakisema, "Hizi ni nyara za Daudi."
1 Samweli 30: 21-22
\s5
\v 21 Daudi akafika kwa wale watu mia mbili waliokuwa wamechoka kufuatana naye, wale walioachwa wakae katika kijito cha Besori. Watu hawa wakajitokeza kumlaki na watu waliokuwa naye.
\v 22 Ndipo watu wote waovu na wasiofaa miongoni mwa waliokwenda na Daudi wakasema, "Kwa sababu watu hawa hawakwenda nasi, hatutawapa chochote kutoka katika nyara tulizorudisha. Isipokuwa kila mtu aweza kuchukuwa mke na watoto wake, wawatoe na kwenda zao."
1 Samweli 30: 23-25
\s5
\v 23 Ndipo Daudi akasema, "Ndugu zangu, msifanye hivyo, kwa vitu ambavyo BWANA ametupatia. Ametuhifadhi na kuwaweka mkononi mwetu wavamizi waliotuinukia.
\v 24 Ni nani atawasikiliza kuhusu jambo hili? Kwa maana mgawo ni kwa yeyote aendae vitani, basi pia mgawo ni kwa yeyote aliyelinda mizigo; Nao watapata tena kilicho sawa."
\v 25 Ilikuwa hivyo tangu siku hiyo hadi leo, maana Daudi aliamua iwe sheria na amri kwa Israeli.
1 Samweli 30: 26-28
\s5
\v 26 Daudi alipofika Ziklagi, alituma sehemu ya nyara kwa wazee wa Yuda, kwa rafiki zake, akisema, "Tazama, hii ni zawadi yenu kutokana na nyara za adui wa BWANA."
\v 27 Zawadi zilienda kwa wazee waliokuwa Bethueli, na kwa hao waliokuwa Ramothi iliyoko kusini, na kwa hao waliokuwa Yatiri,
\v 28 na kwa hao waliokuwa Aroeri, na kwa hao waliokuwa Sifmothi, na kwa hao waliokuwa Eshtemoa
1 Samweli 30: 29-31
\s5
\v 29 Pia kwa wazee waliokuwa Rakali, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wayerameeli, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wakeni,
\v 30 na kwa hao waliokuwa Horma, na kwa hao waliokuwa Borashani, na kwa hao waliokuwa Athaki,
\v 31 na kwa hao waliokuwa Hebroni, na kwa sehemu zote ambazo Daudi mwenyewe na watu wake walizoea kwenda.
\s5
\c 31
\p 1 Samweli 31: 1-3
\v 1 Basi Wafilisti wakapigana dhidi ya Waisraeli. Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilisti na wakaanguka chini wakafa katika mlima wa Gilboa.
\v 2 Wafilisti wakamwandama Sauli na wanawe kwa karibu. Wakawaua wanawe Yonathani, Abinadabu, and Malkishua.
\v 3 Vita vikamwelemea Sauli, na wapiga upinde wakampata. Akapata maumivu makali kwa sababu yao.
1 Samweli 31: 4-6
\s5
\v 4 Kisha Sauli akamwambia mbeba silaha wake, "Chomoa upanga wako unichome nao. Vinginevyo, hawa wasiotahiriwa watakuja na kuninyanyasa." Lakini mbeba silaha wake hakukubali, kwa kuwa aliogopa sana. Hivyo Sauli alichukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.
\v 5 Yule mbeba silaha akaona kwamba Sauli amekufa, yeye naye vivyo hivyo akauangukia upanga wake akafa pamoja naye.
\v 6 Kwa hiyo Sauli alikufa, wanawe watatu, na mbeba silaha wake - watu hawa wote walikufa pamoja siku iyo hiyo.
1 Samweli 31: 7-8
\s5
\v 7 Watu wa Israeli waliokuwa upande mwingine wa bonde, na hao waliokuwa ng'ambo ya Yordani, walipoona kwamba Waisraeli wamekimbia, na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliiacha miji yao na kukimbia, nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.
\v 8 IKawa katika siku iliyofuata, Wafilisti wakafika kuchukua nyara za waliokufa, ndipo wakamuona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.
1 Samweli 31: 9-10
\s5
\v 9 Nao wakakata kichwa chake na kuondoa silaha zake, na wakawatuma wajumbe kwenda pande zote katika nchi ya Wafilisti kutangaza habari hizo katika mahekalu yao ya sanamu na kwa watu.
\v 10 Wakaziweka silaha zake katika hekalu la Ashtorethi, nao wakakitundika kiwiliwili chake kwenye ukuta wa mji wa Bethi Shani.
1 Samweli 13: 11-13
\s5
\v 11 Na wenyeji wa Yabeshi Gileadi waliposikia kile Wafilisti walichomfanyia Sauli,
\v 12 wapiganaji wote wakainuka na kwenda usiku wote na wakauondoa mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka ukuta wa Bethi Shani. Nao wakaenda Yabeshi na wakaichoma moto hiyo miili huko.
\v 13 Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.

1364
10-2SA.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1364 @@
\id 2SA
\ide UTF-8
\h 2 Samweli
\toc1 2 Samweli
\toc2 2 Samweli
\toc3 2sa
\mt 2 Samweli
\s5
\c 1
\p
\v 1 Baada ya kifo cha Sauli, Daud alirudi kutoka kuwashambulia Waamaleki na akakaa Siklagi kwa siku mbili.
\v 2 Siku ya tatu, mtu mmoja alikuja kutoka kambi ya Sauli nguo zake zikiwa zimeraruliwa na akiwa na vumbi juu ya kichwa chake. Alipofika kwa Daudi alinamisha uso wake chini akajifanya yeye mwenyewe kuwa si kitu.
\s5
\v 3 Daudi akamuliza, "Unatoka wapi?" Yeye akajibu, "Nimeponyoka kutoka kambi ya Israeli."
\v 4 Daudi akamwambia, "Tafadhari nieleze jinsi mambo yalivyokuwa." Akajibu, "Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wameanguka, na wengi wao wameuawa. Sauli na Yonathani mwanawe pia wameuawa."
\v 5 Daudi akamwuliza kijana, "unajuaje kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wameuawa?"
\s5
\v 6 Yule kijana akajibu, "Kwa bahati nilikuwa juu ya Mlima Gilboa, na pale alikuwepo Sauli ameegemea mkuki wake, na magari ya farasi na waongozaji walikuwa karibu kumkamata.
\v 7 Sauli alipogeuka aliniona na akaniita. Nikajibu, 'Mimi hapa.'
\s5
\v 8 Akaniuliza, 'Wewe ni nani?' Nikamjibu, 'Mimi ni Mwamaleki,'
\v 9 Akaniambia, Tafadhari simama juu yangu uniuwe, kwa kuwa shida kubwa imenipata, lakini uhai ungalimo ndani yangu.'
\v 10 Hivyo nilisimama juu yake nikamuuwa, kwa maana nilijua kwamba asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka. Ndipo nikachukuwa taji iliyokuwa juu ya kichwa chake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, na nimevileta hapa kwako, bwana wangu."
\s5
\v 11 Kisha Daudi akararua mavazi yake, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile.
\v 12 Walilia, wakaomboleza na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli, Yonathani mwanawe, watu wa Yahwe, na kwa ajili ya nyumba ya Israeli kwa maana wameanguka kwa upanga.
\v 13 Daudi akamwambia yule kijana, "Unatokea wapi?" Akajibu, mimi ni kijana wa mgeni Mwamaleki."
\s5
\v 14 Daudi akamwambia, "Kwa nini haukuogopa kumwua mfalme, mtiwa mafuta wa Yahwe kwa mkono wako?"
\v 15 Daudi akamwita mmojawapo wa vijana na akamwambia, "Nenda ukamuue." Hivyo kijana huyo akaenda na kumpiga hata ata chini, Mwamaleki akafa.
\v 16 Ndipo Daudi akamwambia Mwamaleke aliyekufa, "Damu yako iwe juu ya kichwa chako kwa kuwa kinywa chako kimeshuhudia dhidi yako kusema, Nimemuua mfalme mtiwa mafuta wa Yahwe.
\s5
\v 17 Ndipo Daudi akaimba wimbo wa maombolezo juu ya Sauli na Yonathani mwanawe.
\v 18 Akawaamuru watu kuufundisha wimbo wa Bow kwa wana wa Yuda, ambao umeandikwa katika Kitabu cha Yashari.
\v 19 "Utukufu wako, Israel, umeondolewa, umeondolewa juu ya mahali pako pa juu! Jinsi mwenye nguvu alivyoanguka!
\v 20 Msiiseme katika Gathi, msiitangaze katika mitaa ya Ashikeloni, ili binti za wafilisti wasifurahi, ili binti za wasiotailiwa wasisherehekee.
\s5
\v 21 Milima ya Gilboa, kusiwe na umande au mvua juu yenu. wala mashamba yasitoe nafaka kwa ajili ya sadaka, kwa maana hapo ngao ya mwenye nguvu imeharibiwa. Ngao ya Sauli haiwezi tena kutiwa mafuta.
\v 22 Kutoka katika damu ya waliouawa, kutoka katika miili ya wenye nguvu, upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, na upanga wa Sauli haukurudi patupu.
\s5
\v 23 Sauli na Yonathani walikuwa wakipendwa na walikuwa wenye neema maishani, hata wakati wa mauti yao walikuwa pamoja. Walikuwa na kasi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
\v 24 Enyi binti wa Israeli lieni juu ya Sauli, aliyewavika mavazi ya thamani pamoja na vito vya thamani, na aliyetia mapambo ya dhahabu katika mavazi yenu.
\s5
\v 25 Jinsi wenye nguvu walivyoanguka vitani! Yonathani ameuawa juu ya mahali pako pa juu.
\v 26 Nimesikitishwa sana kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu. Ulikuwa mpendwa wangu sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, ukipita upendo wa wanawake.
\v 27 Jinsi wenye nguvu walivyoanguka na silaha za vita zimeteketea!"
\s5
\c 2
\p
\v 1 Ikawa baada ya haya Daudi akamuuliza Yahwe, "Je naweza kuupandia mmojawapo wa miji ya Yuda?" Yahweh akamjibu, "Panda." Daudi akauliza, "Niuendee mji upi? Yahwe akajibu, "Hebroni"
\v 2 Hivyo Daudi akakwea pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, mjane wa Nabali.
\v 3 Daudi akawaleta watu waliokuwa pamoja naye, na kila mmoja akaleta familia yake katika mji wa Hebroni walipoanza kuishi.
\s5
\v 4 Kisha watu wa Yuda wakaja na kumtia Daudi mafuta kuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi, "Watu wa Yabeshi Gileadi wamemzika Sauli."
\v 5 Hivyo Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi Gileadi akawambia, "Mbarikiwe na Yahwe, kwa kuwa mmeonesha utiifu huu kwa bwana wenu Sauli mliyemzika.
\s5
\v 6 Sasa Yahwe awadhihirishie utiifu na uaminifu wa kiagano. Nami pia nitawaonesha wema kwa sababu ya yale mliyoyafanya.
\v 7 Sasa basi, mikono yenu itiwe nguvu; mwe jasiri kwa maana Sauli bwana wenu amekufa, na nyumba yote ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalime wao.
\s5
\v 8 Lakini Abneri mwana wa Neri, mkuu wa jeshi la Sauli, akamchukuwa Ishboshethi mwana wa Sauli akamleta Mahanaimu.
\v 9 Akamfanya Ishboshethi mfalme juu ya Gileadi, Asheri, Yezreeli, Efraimu, Benjamini na juu ya Israeli yote.
\s5
\v 10 Ishiboshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili. Lakini nyumba ya Yuda ikaambatana na Daudi.
\v 11 Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ni miaka saba na miezi sita.
\s5
\v 12 Abneri mwana wa Neri na watumishi wa Ishboshethi mwana wa Sauli walitoka Mahanaimu kwenda Gibeoni.
\v 13 Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wa Daudi wakatoka na kukutana nao katika bwawa la Gibeoni. Wakakaa pale, kundi moja upande huu wa bwawa na kundi lingine upande wa pili.
\s5
\v 14 Abneri akamwambia Yoabu, "haya, vijana na wainuke na kushindana mbele yetu." Yoabu akajibu, "haya na wainuke."
\v 15 Ndipo vijana walipoinuka na kukutana, kumi na wawili kwa ajili ya Banjamini na Ishboshethi mwana wa Sauli, na kumi na wawili kutoka kwa watumishi wa Daudi.
\s5
\v 16 Kila mtu akakamata kichwa cha adui yake na kupiga upanga wake katika ubavu wa adui yake, wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa kwa Kiebrania, "Helkath Hazzurim," yaani "konde la upanga," lililopo Gibeoni.
\v 17 Vita ikawa kali sana siku ile na Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watumishi wa Daudi.
\s5
\v 18 Wana watatu wa Seruya walikuwepo pale: Yoabu, Abishai na Asaheli.
\v 19 Asaheli alikuwa mwepesi miguuni kama paa. Akamfuatilia Abneri kwa karibu bila kugeuka upande wowote.
\s5
\v 20 Abneri akaangalia nyuma yake na kusema, "Ni wewe Asaheli?" Akajibu, "ni mimi."
\v 21 Abneri akamwambia, "Geuka upande wako wa kuria au kushoto umshike mmojawapo wa vijana na kuchukua silaha yake." Lakini Asaheli hakugeuka.
\s5
\v 22 Ndipo Abneri alipomwambia tena Asaheli, "Simama usinifuate. Kwa nini nikupige hata chini? Nitautazamaje uso wa Yoabu ndugu yako?"
\v 23 Lakini Asaheli hakukubari kugeuka. na hivyo Abneri akamchoma kwa nchi ya mkuki wake, hata ukatokea upande wa pili. Asaheli akaanguka chini akafa. Hata ikawa kila mmoja aliyefika mahali pale Asaheli alipoanguka na kufa, alisimama hapo hapo.
\s5
\v 24 Lakini Yoabu na Abishai wakamfuatilia Abneri. Wakati jua linazama walikuwa wamefika mlima wa Amma, uliopo karibu na Gia katika njia ielekeayo nyika ya Gibeoni.
\v 25 Wabenjamini wakajikusanya nyuma ya Abneri na kusimama juu ya kilima.
\s5
\v 26 Kisha Abneri akamwita Yoabu na kusema, "Je ni lazima upanga uendelee kurarua daima? Je haujui kwamba mwisho wake utakuwa mchungu? Hata line ndipo uwaambie watu wako waache kuwafuatia ndugu zao?"
\v 27 Yoabu akajibu, "Kama Mungu aishivyo, usingesema hivyo, askari wangu wangewafuatia ndugu zao hata asubuhi!"
\s5
\v 28 Ndipo Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wake wote wakasimama na hawakuendelea kuwafuata Israeli tena wala hawakupigana tena.
\v 29 Abneri na watu wake wakasafiri usiku wote kupitia Araba. Wakavuka Yordani, wakatembea asubuhi yote iliyofuata, na hata wakafika Mahanaimu.
\s5
\v 30 Yoabu akarudi kutoka katika kumfuatia Abneri. Akawakusanya watu wake wote, ambopo Asahali na askari wengine kumi na tisa wa Daudi walipungua.
\v 31 Lakini watu wa Daudi walikuwa wameua watu 360 wa Benjamini na Abneri.
\v 32 Kisha wakamchukua Asahali na kumzika katika kaburi la baba yake, lililokuwapo Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakasafiri usiku wote, kukacha wakati wanafika Hebroni.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kulikuwa na vita ya mda mrefu kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi. Daudi akaendelea kupata nguvu zaidi, lakini nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika na kuthoofika.
\s5
\v 2 Wana wakazaliwa kwa Daudi huko Hebron. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu wa Yezreeli.
\v 3 Mwanawe wa pili, Kileabu, alizaliwa kwa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. Wa tatu, Absalomu, alikuwa mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri.
\s5
\v 4 Mwana wa nne wa Daudi, Adoniya, alikuwa mwana wa Hagithi. Mwanawe wa tano alikuwa Shefatia mwana wa Abitali,
\v 5 na wa sita, Ithreamu, alikuwa mwana wa Egla mkewe Daudi. Hawa wote walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni.
\s5
\v 6 Ikawa wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi Abneri akajifanya mwenye nguvu katika nyumba ya Sauli.
\v 7 Sauli alikuwa na suria jina lake Rispa, binti Aiya. Ishboshethi akamuuliza Abneri, "Kwa nini umelala na suria wa baba yangu?"
\s5
\v 8 Hata ikawa Abneri akakasirika sana kutokana na maneno ya Ishboshethi naye akasema, "Je mimi ni kichwa cha mbwa wa Yuda? Ninaonesha uaminifu kwa nyumba ya Sauli, baba yako, kwa jamaa yake, na rafiki zake, kwa kutokukuweka katika mkono wa Daudi. Na bado leo unanishutumu kuhusu mwanamke.
\s5
\v 9 Mungu na anifanyie hivyo, Abneri, na kuzidi, ikiwa sitafanya kwa Daudi kama Yahwe alivyomwapia,
\v 10 kuuhamisha ufalme kutoka nyumba ya Sauli na kukisimika kiti cha enzi cha Daudi juu ya Israeli na juu ya Yuda, kutoka Dani hadi Beersheba."
\v 11 Ishboshethi hakuweza kumjibu Abneri neno tena, kwani alimuogopa.
\s5
\v 12 Kisha Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi kusema, "Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, nawe utaona kwamba mkono wangu uko nawe, kuiIeta Israeli yote kwako."
\v 13 Daudi akajibu, "Vema, nitafanya agano nawe. Lakini neno moja ninalolitaka kutoka kwako ni kwamba hautauona uso wangu usipomuleta kwanza Mikali, binti Sauli, unapokuja kuonana nami."
\s5
\v 14 Kisha Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, "Nipe Mikali, mke wangu niliyetoa kwa ajili yake govi mia moja za Wafilisti."
\v 15 Hivyo Ishboshethi akatuma kwa Mikali na kumchukua kutoka kwa mme wake, Paltieli mwana wa Laishi.
\v 16 Mme wake akafuatana naye, huku akilia, akaendelea hadi Bahurimu. Kisha Abneri akamwambia, "basi sasa rudi nyumbani." Hivyo akarudi.
\s5
\v 17 Abneri akaongea na wazee wa Israeli kusema, "Zamani mlitaka Daudi awe mfalme wenu.
\v 18 Basi sasa fanyeni hivyo. Kwa maana Yahwe alisema kuhusu Daudi kusema, "Kwa mkono wa Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka katika mkono wa Wafilisti na kutoka katika mkono wa adui zao wote."
\s5
\v 19 Pia Abneri akasema na watu wa Benjamini ana kwa ana. Kisha Abneri akaenda kuongea na Daudi huko Hebroni akaeleza kila jambo ambalo Israeli na nyumba yote ya Benjamini walitamani kulitimiza.
\v 20 Wakati Abneri na watu ishirini kati ya watu wake walifika Hebroni kumuona Daudi, Daudi akaandaa sherehe kwa ajili yao.
\s5
\v 21 Abneri akamweleza Daudi, "Nitainuka na kukukusanyia Israeli wote, bwana wangu mfalme, ili kwamba wafanye agano nawe, kwamba utawale juu ya yote unayotaka." Hivyo Daudi akamruhusu Abneri kuondoka, Abneri akaondoka kwa amani.
\s5
\v 22 Kisha askari wa Daudi na Yoabu wakarudi kutoka katika kuteka nyara na wakaja na nyara nyingi. Lakini Abneri hakuwepo Hebroni pamoja na Daudi. Daudi alikuwa amemruhusu kuondoka, na alikuwa ameondoka kwa amani.
\v 23 Wakati Yoabu na Jeshi lote walipofika, Yoabu aliambiwa, "Abneri mwana wa Neri alikuja kwa mfalme, na mfalme amemruhusu kuondoka, naye Abneri ameondoka kwa amani."
\s5
\v 24 Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, "Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye amenda?
\v 25 Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?"
\v 26 Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sirah, lakini Daudi hakulijua hili.
\s5
\v 27 Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoka tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.
\s5
\v 28 Daudi alipolisikia jambo hili akasema, "Mimi na ufalme wangu hatuna hatia mbele za Yahwe daima, kuhusiana na damu ya Abneri mwana wa Neri.
\v 29 Hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya Yoabu na nyumba yote ya baba yake. Na asikosekane katika familia ya Yoabu mtu mwenye vidonda, au mwenye ukoma, au kirema atembeaye kwa fimbo au aliyeuawa kwa upanga au mwenye kukosa chakula."
\v 30 Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamwua Abneri, kwa sababu alimwua Asaheli ndugu yao vitani huko Gibeoni.
\s5
\v 31 Daudi akamwambia Yoabu na wote waliokuwa pamoja naye, "Rarueni mavazi yenu, jivikeni nguo za magunia, na muomboleze mbele ya mwili wa Abneri." Na mfalme Daudi akaufuata mwili wa Abneri wakati wa mazishi.
\v 32 Wakamzika Abneri huko Hebroni. Mfalme akalia kwa sauti katika kaburi la Abneri, na watu wote pia wakalia.
\s5
\v 33 Mfalme akamwombolea Abneri naye akaimbo, "Je ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?
\v 34 Mikono yako haikufungwa. Miguu yako hakuwa imefungwa minyororo. Kama mtu aangukavyo mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka." Watu wote wakamlilia zaidi.
\s5
\v 35 Watu wote wakaja kumtaka Daudi ale wakati kungali mchana, lakini Daudi akaapa, "Mungu na anifanyie hivyo, na kuzidi, ikiwa nitaonja mkate au chochote kabla jua halijazama."
\v 36 Watu wote wakaiona huzuni ya Daudi, na ikawapendeza, hivyo kila alichokifanya mfalme kikawapendeza.
\s5
\v 37 Hivyo watu wote na Israeli wote wakatambua siku hiyo kwamba haikuwa nia ya mfalme Abneri mwana wa Neri afe.
\v 38 Mfalme akawaambia watumishi wake, "je hamjui kuwa mtu mkuu ameanguka leo hii katika Israeli?
\v 39 Nami leo nimedhoofika, japokuwa nimetiwa mafuta kuwa mfalme. Watu hawa, wana wa Seruya ni hatari sana kwangu. Yahwe na amrudishie mwovu kwa kumlipa kwa ajili ya uovu wake kama anavyostahili.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ikawa Ishboshethi, mwana wa Sauli, aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, mikono yake ikadhoofika, na Israeli yote ikataabika.
\v 2 Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa wakuu wa vikosi vya askari. Mmoja wao alikuwa Baana na mwingine alikuwa Rekabu, wana wa Rimoni Mbeerothi wa wana wa Benjamini(kwa maana Berothi ilihesabiwa kuwa sehemu ya Benjamini,
\v 3 na Waberothi walikimbilia Gitaimu na wamekuwa wakiishi pale hadi sasa).
\s5
\v 4 Basi Yonathani, mwana wa Sauli, alikuwa na mwana mlemavu wa miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano habari kuhusu Sauli na Yonathani ilipofika Yezreeli. Yaya wake akamchukua ili akimbie. Lakini wakati anakimbia, mwana wa Yonathani alianguka na akawa kirema. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.
\s5
\v 5 Hivyo wana wa Rimoni mbeerothi, Rekabu na Baana, wakasafiri mchana wakati wa jua kali mpaka nyumbani mwa Ishbothethi, yeye alikuwa amepumzika mchana.
\v 6 Mwanamke aliyekuwa akililinda lango alisinzia wakati akipepeta ngano, Rekabu na Baana waliingia ndani polepole na wakampita.
\v 7 Hivyo walipoingia ndani ya nyumba, walimpiga na kumuua wakati amelala chumbani mwake. Kisha wakakata kichwa chake na wakaondoka nacho, wakasafiri njiani usiku kucha mpaka Araba.
\s5
\v 8 Wakaleta kichwa cha Ishboshethi kwa Daudi huko Hebroni, nao wakamwambia mfalme, "Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyekuwa akiutafuta uhai wako. Leo Yahwe amemlipia kisasi bwana wetu mfalme dhidi ya Sauli na uzao wake."
\v 9 Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni mbeerothi, akawambia, "Kama Yahwe aishivyo, aliyeuokoa uhai wangu na kila shida,
\v 10 mtu mmoja aliponiambia, 'Tazama, Sauli amekufa,' akifikiri alileta habari njema, nilimkamata na kumwua huko Siklagi. Huo ndio ujira niliompa kwa habari yake.
\s5
\v 11 Namna gani, mtu mwovu anapomwua mwenye haki kitandi mwake ndani ya nyumba, Je nisiitake damu yake kutoka katika mikono yenu, na kuwaondoa duniani?"
\v 12 Kisha Daudi akawaagiza vijana, nao wakawaua wakakata mikono na miguu yao na kuwatundika kando ya bwawa huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ishboshethi na kukizika katika kaburi la Abneri katika Hebroni.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kisha kabila zote za Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni nao wakasema, "Tazama, sisi ni nyama na mifupa yako.
\v 2 Kipindi kilichopita, Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliyeliongoza jeshi la Waisraeli. Yahwe akakwambia, 'Utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala juu ya Israeli."
\s5
\v 3 Hivyo wazee wote wa Israeli wakaja kwa mfalme huko Hebron na mfalme Daudi akafanya nao agano mbele ya Yahweh. Wakamtawaza Daudi kuwa mfalme wa Israeli.
\v 4 Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini.
\v 5 Alitawala juu ya Yuda miaka saba na miezi sit a huko Hebroni, na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli yote na Yuda.
\s5
\v 6 Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kupigana na wayebusi, waliokuwa wenyeji wa nchi. Wakamwambia Daudi, "Hautaweza kuja hapa kwani hata wipofu na vilema waweza kukudhuia kuingia. Daudi haweze kuja hapa."
\v 7 Lakini, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, ambayo sasa ni mji wa Daudi.
\s5
\v 8 Wakati huo Daudi akasema, "Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie virema na vipofu ambao ni adui wa Daudi." Hii ndiyo maana watu husema, "Vipofu na virema wasingie katika kasri."
\v 9 Hivyo Daudi akaishi ngemeni naye akaiita mji wa Daudi. Akaizungushia ukuta, kuanzia barazani kuelekea ndani.
\v 10 Daudi akawa na nguvu sana kwa maana Yahwe, Mungu wa utukufu, alikuwa pamoja naye.
\s5
\v 11 Kisha Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi seremala na wajenzi. Wakamjengea Daudi nyumba.
\v 12 Daudi akatambua kuwa Yahwe alikuwa amemweka ili awe mfalme juu ya Israeli, na kwamba alikuwa ameutukuza ufalme wake kwa ajili ya Israeli watu wake.
\s5
\v 13 Baada ya Daudi kuondoka Hebroni na kwenda Yerusalemu, akajitwalia wake na masuria wengi huko Yerusalemu, na wana na binti wengi walizaliwa kwake.
\v 14 Haya ndiyo majina ya wanawe waliozaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Selemani,
\v 15 Ibhari, Elishua, Nefegi, Yafia,
\v 16 Elishama, Eliada na Elifeleti.
\s5
\v 17 Basi wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli, wakaenda wote kumtafuta. Daudi aliposikia hilo akashuka ngomeni.
\v 18 Basi Wafilisiti walikuwa wamekuja na kuenea katika bonde la Mrefai.
\s5
\v 19 Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, "Je niwashambulie wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?" Yahwe akamwambia Daudi, "Washambulia, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya wafilisti."
\v 20 Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu.
\v 21 Wafilisiti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.
\s5
\v 22 Kisha wafilisiti wakaja kwa mara nyingine tena na kujieneza zaidi katika bonde la Mrefai.
\v 23 Hivyo Daudi akatafuta msaada tena kutoka kwa Yahweh, naye Yahweh akamwambia, "Usiwashambulie kwa mbele, lakini uwazunguke kwa nyuma na uwaendee kupitia miti ya miforosadi.
\s5
\v 24 Wakati utakaposikia sauti za mwendo katika upepo uvumao juu ya miti ya miforosadi, hapo ushambulie kwa nguvu. Fanya hivi kwa kuwa Yahwe atatangulia mbele yako kulishambulia jeshi la Wafilisiti."
\v 25 Hivyo Daudi akafanya kama Yahwe alivyomwamuru. Akawaua wafilisti njiani mwote toka Geba hadi Gezeri.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Basi kwa mara nyingine Daudi akawakusanya wateuli wa Israeli, elfu thelathini.
\v 2 Daudi akainuka na akaenda na watu wake wote waliokuwa pamoja naye kutoka Baala ulioko Yuda ili alilete sanduku la Mungu, liitwalo kwa jina la Yahwe wa majeshi, akaaye juu ya makerubi.
\s5
\v 3 Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wanawe, wakauongoza mkokoteni.
\v 4 Wakautoa mkokoteni na sanduku la Mungu juu yake nyumbani mwa Abinadabu juu ya kilima. Ahio alikuwa ametangulia mbele ya sanduku.
\v 5 Kisha Daudi na nyumba yote ya Israeli wakaanza kucheza mbele ya Yahwe, wakishangilia kwa vyombo vya mziki, vinubi, vinanda, matari, kayamba na matowazi.
\s5
\v 6 Hata walipofika katika shinikizo la Nasoni, wale ng'ombe wakakwama, Uza akanyosha mkono wake na kulikumbatia sanduku la Mungu, naye akalishikilia.
\v 7 Kisha asira ya Yahweh ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akampiga kwa ajili ya dhambi yake. Uza akafa pale pale kando ya sandaku la Mungu.
\s5
\v 8 Daudi akakasirika kwa kuwa Yahwe alimpiga Uza, naye akapaita mahali pale Peresi Uza. Eneo hilo linaitwa Peres Uza hata leo.
\v 9 Daudi akamwogopa Yahweh siku hiyo. Akasema, "Sanduku la Yahwe lawezaje kuja kwangu?"
\s5
\v 10 Hivyo Daudi hakuwatayari tena kulichukua sanduku la Yahwe katika mji wa Daudi. Badala yake, akaliweka kando katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
\v 11 Sanduku la Yahwe likakaa katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti kwa miezi mitatu. Kwa hiyo Yahwe akambariki yeye na nyumba yake yote.
\s5
\v 12 Kisha mfalme Daudi akaambiwa, "Yahwe ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila kitu alichonacho kwa sababu ya sanduku la Mungu." Hivyo Daudi akaenda na kulipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi kwa furaha.
\v 13 Ikawa waliolibeba sanduku la Yahwe walipochukua hatua sita, akatoa sadaka ng'ombe na ndama aliyenona.
\s5
\v 14 Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee.
\v 15 Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta.
\s5
\v 16 Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamwona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.
\v 17 Wakaliingiza sanduku la Yahwe na kuliweka mahali pake, katikati ya hema ambayo Daudi alikuwa ameliwekea. Kisha Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na matoleo ya amani mbele za Yahwe.
\s5
\v 18 Ikawa Daudi alipomaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi.
\v 19 Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.
\s5
\v 20 Kisha Daudi akarudi ili aibariki familia yake. Mikali, binti Sauli, akatoka ili akutane na Daudi naye akasema, "Jinsi gani mtukufu mfalme wa Israeli alivyokuwa leo, aliyejiacha uchi mbele ya macho ya vijakazi miongoni mwa watumishi wake, kama mmoja wa wapumbavu ambaye bila aibu hujifunua yeye mwenyewe!"
\s5
\v 21 Daudi akamjibu Mikali, "Nilifanya hivyo mbele ya Yahwe, aliyenichagua juu ya baba yako na juu ya familia yake yote, aliyeniweka kuwa kiongozi juu ya watu wa Yahwe, juu ya Israeli. Mbele ya Yahwe nitafurahi!
\v 22 Nitakuwa nisiye na heshima hata zaidi ya hapa, na nitajishusha mbele za macho yangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliowasema, nitaheshimiwa."
\v 23 Hivyo Mikali, binti Sauli, hakuwa na watato hata alipokufa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Ikawa mfalme alipokuwa amekwisha kukaa katika nyumba yake, na baada ya Yahwe kuwa amemstarehesha kutokana na adui zake wate waliomzunguka,
\v 2 mfalme akamwambia nabii Nathani, "Tazama, mimi ninaishi katika nyumba ya mierezi, lakini sanduku la Mungu lipo hemani.
\s5
\v 3 Basi Nathani akamwambia mfalme, "Nenda, fanya lililo moyoni mwako, kwa maana Yahwe yupo nawe."
\v 4 Lakini usiku usiku uleule neno la Yahwe lilimjia Nathani kusema,
\v 5 "Nenda na umwambie mtumishi wangu Daudi, 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Je utanijengea nyumba ya kuishi?"
\s5
\v 6 Kwa maana sijawai kuishi katika nyumba tangu siku ile nilipowaleta wana wa Israeli kutoka Misri hata leo; badala yake nimekuwa nikitembea katika hema, hema la kukutania.
\v 7 Mahali pote ambapo nimekuwa nikihama miongoni mwa wana wote wa Israeli, Je niliwai kusema lolote na viongozi wa Israeli niliowaweka kuwachunga watu wangu Israeli, kusema, "Kwa nini hamjanijengea nyumba ya mierezi?"
\s5
\v 8 Sasa basi, mwambie Daudi, mtumishi wangu, "Hiki ndicho asemacho Yahwe wa majeshi: 'Nilikutwaa kutoka machungani, kutoka katika kuwafuata kondoo, ili uwe mtawala juu ya watu wangu Israeli.
\v 9 Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda na nimewakatilia mbali adui zako wote mbele yako. Na nitakutengenezea jina kubwa, kama jina la mojawapo ya wakuu walio juu ya nchi.
\s5
\v 10 Nitatenga mahali kwa ajili ya watu wangu Israeli nami nitawapanda pale, ili kwamba waweze kuishi mahali pao wenyewe na wasisumbuliwe tena. Waovu hawatawatesa tena, kama walivyofanya mwanzo.
\v 11 Kama walivyofanya tangu siku ile nilipoamuru waamuzi juu ya watu wangu Israeli. Nami nitakustarehesha kutokana na adui zako wote. Zaidi ya hayo, Mimi, Yahwe, nakutamkia kwamba nitakutengenezea nyumba.
\s5
\v 12 Siku zako zitakapokwisha na ukalala pamoja na baba zako, nitainua mzao baada yako, atokaye katika mwili wako mwenyewe, nitauimalisha ufalme wake.
\v 13 Naye atajenga nyumba kwa jina langu, nami nitakiimalisha kiti chake cha enzi daima.
\v 14 Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwanangu. Atakapotenda dhambi, nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu na kwa mapigo ya wana wa watu.
\s5
\v 15 Lakini uaminifu wa agano langu hautamwondokea, kama nilivyouondoa kutoka kwa Sauli, niliyemwondoa mbele yako.
\v 16 Nyumba yako na ufalme wako utathibitiswa mbele yako daima. Kiti chako cha enzi kitakuwa imara daima."
\v 17 Nathani akamwambia Daudi na kumtaarifu maneno haya yote, na akamwambia kuhusu ono lote.
\s5
\v 18 Kisha mfalme Daudi akaingia ndani na kuketi mbele ya Yahwe; akasema, "Mimi ni nani, Yahwe Mungu, na familia yangu ni nini hata umenileta hapa nilipo?
\v 19 Na hili lilikuwa jambo dogo mbele yako, Bwana Yahwe. Hata ukasema kuhusu familia ya mtumishi wako wakati mkuu ujao, nawe umenionesha vizazi vijavyo, Bwana Yahwe!
\v 20 Mimi Daudi, niseme nini zaidi kwako? Umemweshimu mtumishi wako, Bwana Yahwe.
\s5
\v 21 Kwa ajili ya neno lako, na kwa ajili ya kutimiza kusudi lako mwenyewe, umefanya jambo kubwa namna hii na kulidhihirisha kwa mtumishi wako.
\v 22 Kwa hiyo wewe ni mkuu, Bwana Yahwe. Kwa maana hakuna mwingine aliye kama wewe, na hakuna Mungu mwingine badala yako, kama jinsi ambayo tumesikia kwa masikio yetu wenyewe.
\v 23 Kwani kuna taifa lipi lililo kama watu wako Israeli, taifa moja juu ya nchi ambalo wewe, Mungu, ulikwenda na kuwakomboa kwa ajili yako wewe mwenyewe? Ulifanya hivi ili kwamba wawe watu kwa ajili yako mwenyewe, kujifanyia jina kwa ajili yako mwenyewe, na kufanya matendo makuu na ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako. Uliyaondoa mataifa na miungu yao kutoka mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri.
\s5
\v 24 Umeiimarisha Israel kama watu wako daima, na wewe, Yahwe, kuwa Mungu wao.
\v 25 Basi sasa, Yahwe Mungu, ahadi uliyofanya kuhusu mtumishi wako na familia yake iwe imara daima. Ufanye kame uilivyo sema.
\v 26 Na jina lako liwe kuu daima, ili watu waseme, 'Yahwe wa majeshi ni Mungu wa Israeli,' wakati nyumba yangu, Daudi, mtumishi wako itakapokaa imara mbele zako daima.
\s5
\v 27 Kwa maana wewe, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, umedhihirisha kwa mtumishi wako kwamba utamjengea nyumba. Ndiyo maana mimi, mtumishi wako, nimepata ujasiri kuomba kwako.
\v 28 Sasa, Bwana Yahwe, wewe ni Mungu, na maneno yako ni amini, na umefanya ahadi hii njema kwa mtumishi wako.
\v 29 Sasa basi, na ikupendeze kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili iendelee mbele yako daima. Kwa maana wewe, Bwana Yahwe, umeyasema mambo haya, na kwa ahadi yako nyumba ya mtumishi wako itabarikiwa daima.
\s5
\c 8
\p
\v 1 ikawa baada ya haya Daudi aliwashambulia Wafilisti na kuwashinda. Hivyo Daudi akaichukua Gathi na vijiji vyake kutoka katika mamlaka ya wafilisti.
\s5
\v 2 Kisha akaishinda Moabu na akawapima watu wake kwa mstari kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi. Alipima mistari miwili ya kuua, na mstari mmoja kamili kuwahifadhi hai. Hivyo Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakaanza kumlipa kodi.
\s5
\v 3 Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, Hadadezeri aliposafiri kuurudisha ufalme wake katika mto Frati.
\v 4 Daudi aliteka magari 1, 700 ya farasi na askari ishirini elfu waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.
\s5
\v 5 Wakati Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadeziri mfalme wa Soba, Daudi akaua katika Washami watu ishirini na mbili elfu.
\v 6 Daudi akaweka ngome huko Shamu ya Dameski, na Washami wakawa watumishi wake na wakaleta kodi. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alikokwenda.
\s5
\v 7 Daudi akachukua ngao za dhahabu walizokuwa nazo watumishi wa Hadadezeri naye akazileta Yerusalemu.
\v 8 Mfalme Daudi akachukua shaba nyingi kutoka Beta na Berosai, miji ya Hadadezeri.
\s5
\v 9 Wakati Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri,
\v 10 Tou akamtuma Hadoramu mwanawe kwa mfalme Daudi kumpa salamu na kumbariki, kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, maana Hadadezeri alikuwa amepiga vita dhidi ya Tou. Hadoramu akaja pamoja na vitu vya fedha, dhahabu, na shaba.
\s5
\v 11 Mfalme Daudi akaviweka wakfu vitu hivi kwa ajili ya Yahwe, pamoja na fedha na dhahabu kutoka katika mataifa yote aliyokuwa ameyashinda-
\v 12 kutoka Shamu, Moabu, Waamoni, Wafilist, Waamaleki, pamoja na nyara zote alizoziteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.
\s5
\v 13 Jina la Daudi likajulikana sana alipowashinda washami katika bonde la Chumvi, pamoja na watu wao wapatao elfu kumi na nane.
\v 14 Akaweka ngome katika Edomu yote, na Waedomu wote wakawa watumishi wake. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.
\s5
\v 15 Daudi akatawala juu ya Israeli yote, naye akatenda kwa haki na usawa kwa watu wote.
\v 16 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa.
\v 17 Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Seraya alikuwa mwandishi.
\v 18 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Daudi akasema, "Je kuna yeyote aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumwonyesha kwa fadhiri kwa ajili ya Yonathani?
\v 2 Alikuwepo mtumishi katika familia ya Sauli jina lake Siba, akaitwa kwa Daudi. Mfalme akamuuliza, "Je wewe ndiye Siba?" Akajibu, "Mimi ni mtumishi wako, ndiye."
\s5
\v 3 Hivyo mfalme akasema, "Je hakuna aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumuonesha wema wa Mungu?" Siba akamjibu mfalme, "Yonathani ana mwana, ambaye ni mlemavu wa miguu.
\v 4 Mfalme akamwambia, "Yupo wapi?" Siba akamjibu mfalme, "Tazama, yupo katika nyumba ya Makiri mwana wa Amieli huko Lo Debari.
\s5
\v 5 Ndipo mfalme Daudi akatuma watu na kumtoa katika nyumba ya Makiri mwana wa Amieli huko Lo Debari.
\v 6 Hivyo Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, akaja kwa Daudi naye akainama uso wake hadi katika sakafu kwa kumheshimu Daudi. Daudi akasema, "Mefiboshethi." Naye akajibu, "Angalia, mimi ni mtumishi wako!
\s5
\v 7 Daudi akamwambia, "Usiogope, maana hakika nitakufadhiri kwa ajili ya Yonathani baba yako, nami nitakurudishia ardhi yote ya Sauli babu yako, nawe utakula katika meza yangu daima."
\v 8 Mefiboshethi akainama na kusema, "Mtumishi wako ni nani, hata ukamwangalia kwa fadhiri mbwa mfu kama nilivyo?"
\s5
\v 9 Kisha mfalme akamwita Siba, mtumishi wa Sauli, na kumwambia, "Yote yaliyo ya Sauli na familia yake nimempa mjukuu wa bwana wako.
\v 10 Wewe, wanao, na watumishi wako mtalima mashamba kwa ajili yake nanyi mtavuna mazao ili kwamba mjukuu wa bwana wako apate chakula. Kwa maana Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako, atakula katika meza yangu daima." Basi Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumishi ishirini.
\s5
\v 11 Kisha Siba akamwambia mfalme, "Mtumishi wako atafanya yote ambayo bwana wangu mfalme amemwamuru mtumishi wake." Mfalme akaongeza kusema, kwa Mefiboshethi yeye atakula katika meza yangu, kama mmojawapo ya wana wa mfalme."
\v 12 Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo jina lake Mika. Na wote waliokuwa wanaishi katika nyumba ya Siba walikuwa watumishi wa Mefiboshethi.
\v 13 Hivyo Mefiboshethi akaishi Yerusalemu, naye akala chakula cha daima katika meza ya mfalme, japokuwa alikuwa mlemavu wa miguu yote.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Ikawa baadaye mfalme wa watu wa Amoni akafa, na Hanuni mwanaye akawa mfalme mahali pake.
\v 2 Daudi akasema, "Nitaonesha fadhiri Hanuni mwana wa Nahashi, kwa kuwa baba yake alinifadhiri." Hivyo Daudi akatuma watumishi wake kumfariji Hanuni kwa habari ya baba yake. Watumishi wake wakaingia katika nchi ya watu wa Amoni.
\v 3 Lakini viongozi wa watu wa Amoni wakamwambia Hanuni bwana wao, "Je unathani kwa hakika Daudi anamweshimu baba yako hata ametuma watu kukutia moyo? Daudi hajawatuma watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, kuupeleleza, ili kuupindua?
\s5
\v 4 Hivyo Hanuni akawachukuwa watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akachana mavazi yao hadi kwenye matako, naye akawaacha waende zao.
\v 5 Daudi alipoelezwa kuhusu hili, akatuma watu kwenda kuwalaki, kwa kuwa walikuwa wamefedheheshwa sana. Mfalme akawambia, "Kaeni Yeriko mpaka ndevu zenu zitakapoota, ndipo mrudi."
\s5
\v 6 Watu wa Amoni walipoona kwamba wamenuka kwa Daudi, wakatuma wajumbe na kuwaajiri Washami wa Bethi Rehobu na Soba, askari elfu ishirini waendao kwa mguu, na mfalme wa Maaka pamoja na watu elfu, na watu wa Tobu elfu kumi na mbili.
\v 7 Daudi aliposikia, akamtuma Yoabu na jeshi lote la askari.
\v 8 Waamoni wakatoka na wakafanya mistari ya vita katika maingilio ya lango la mji wao, wakati Washami wa Soba na wale wa Rehobu, na watu wa Tobu na Maaka, wakasimama peke yao uwandani.
\s5
\v 9 Yoabu alipoona mistari ya vita ikimkabili pote mbele na nyuma, alichagua baadhi ya waisraeli wajuao kupigana vizuri na akawapanga dhidi ya Washami.
\v 10 Na sehemu iliyosalia ya jeshi, akawaweka chini ya Abishai nduguye, naye akawaweka katika mistari ya vita dhidi ya jeshi la Amoni.
\s5
\v 11 Yoabu akasema, "ikiwa Washami watakuwa na nguvu zaidi juu yangu, kisha wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini ikiwa jeshi la Amoni litakuwa na nguvu zaidi juu yako, nitakuja kukuokoa.
\v 12 Iweni na nguvu, nasi tujioneshe kuwa wenye nguvu kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu, kwa maana Yahwe atatenda yapendezayo kwa ajili ya kusudi lake.
\s5
\v 13 Hivyo Yoabu na askari wa jeshi lake wakasonga mbele katika vita dhidi ya Washami, waliolazimika kukimbia mbele ya jeshi la Israeli.
\v 14 Jeshi la Amoni lilipoona kwamba Washami wamekimbia, nao pia wakakimbia kutoka kwa Abishai wakarudi ndani ya mji. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na akarejea Yerusalemu.
\s5
\v 15 Washami walipoona kwamba wameshindwa na Israeli, walijikusanya pamoja tena.
\v 16 Kisha Hadareza akatuma kuleta vikosi vya Washami ng'ambo ya Mto Frati. Wakaja Helamu pamoja na Shobaki, mkuu wa jeshi la Hadareza juu yao.
\s5
\v 17 Daudi alipoambiwa, aliwakusanya Israeli wote pamoja, akavuka Yordani, na akafika Helamu. Washami wakajipanga katika mistari ya vita dhidi ya Daudi na wakapigana naye.
\v 18 Washami wakakimbia mbele ya Israeli. Daudi akaua askari mia saba wa magari na askari wa farasi elfu arobaini. Shobaki mkuu wa jeshi lao alijeruhiwa na akafa huko.
\v 19 Wafalme wote waliokuwa watumishi wa Hadareza walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Israeli na wakawa watumishi wao. Hivyo washami wakaogopa kuwasaidia watu wa Amoni tena.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ikawa wakati wa majira ya kipupwe, wakati ambapo kwa kawaida wafalme huenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, mtumishi wake, na jeshi lote la Israeli. Wakaliaribu jeshi la Amoni na kuuhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu.
\s5
\v 2 Hivyo ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi akaamka kutoka kitandani na akatembea katika dari la kasri. Akiwa pale akamwona mwanamke aliyekuwa akioga, mwanamke yule alikuwa mzuri sana kwa mwonekano.
\v 3 Hivyo Daudi akatuma na kuuliza watu waliomfahamu yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, "Je huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, naye si mke wa Uria mhiti?
\s5
\v 4 Daudi akatuma wajumbe nao wakamchukua; akaja kwake, na akalala naye(kwani ndo alikuwa amejitakasa kutoka siku zake). Kisha akarudi nyumbani kwake.
\v 5 Mwanamke akawa mjamzito, naye akatuma na kumwambia Daudi; akasema, "mimi ni mjamzito."
\s5
\v 6 Kisha Daudi akatuma watu kwa Yoabu kusema, "Umtume kwangu Uria mhiti." Hivyo Yoabu akamtuma Uria kwa Daudi.
\v 7 Uria alipofika, Daudi akamuuliza hali ya Yoabu. Jinsi jeshi lilivyokuwa likiendelea, na jinsi vita vilivyokuwa vinaendelea.
\v 8 Daudi akamwambia Uria, "Shuka nyumbani kwako, unawe miguu yako. "Hivyo Uria akaondoka katika kasri la mfalme, mfalme akamtumia zawadi kwa Uria.
\s5
\v 9 Lakini Uria akalala pamoja na watumishi wa bwana wake katika lango la kasri, wala hakushuka nyumbani kwake.
\v 10 Daudi alipoambiwa, "Uria hakushuka nyumbani kwake," akamwambia Uria, Je haukutoka safarini? Kwa nini haukushuka nyumbani kwako?"
\v 11 Uria akamjibu Daudi, "Sanduku, na Israeli na Yuda wamo kwenye mahema, na Yoabu na watumishi wa bwana wangu wamepiga hema uwandani. Jinsi gani basi mimi naweza kwenda nyumbani kwangu kula kunywa na kulala na mke wangu? kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo.
\s5
\v 12 Hivyo Daudi akamwambia Uria, "Ukae leo pia, kesho nitakuacha uende." Kwa hiyo uria akakaa Yerusalemu siku hiyo na iliyofuata.
\v 13 Daudi alipomwita, alikula na kunywa pamoja naye, Daudi akamfanya alewe. Wakati wa jioni Uria akaenda kulala kitandani pake pamoja na watumish wa bwana wake; hakushuka nyumbani kwake.
\s5
\v 14 Hivyo asubuhi Daudi akamwandikia Yoabu barua, naye akaituma kwa mkono wa Uria.
\v 15 Ndani ya barua Daudi aliandika hivi, "Mweke Uria mbele ya vita vikali sana, na kisha, mmwache, ili apigwe na afe.
\s5
\v 16 Hivyo Yoabu alipoona mji ukizingirwa, alimweka Uria katika sehemu aliyojua askari adui wenye nguvu wangekuwa wakipigana.
\v 17 Wakati watu wa mji walipotoka na kupigana dhidi ya jeshi la Yoabu, baadhi ya askari wa Daudi wakaanguka, na Uria Mhiti pia akauwawa.
\s5
\v 18 Wakati Yoabu alipotuma neno kwa mfalme kuhusu hali ya vita,
\v 19 alimwagiza mjumbe, kusema, "Utakapomaliza kumwambia mfalme kuhusu hali ya vita,
\v 20 yawezekana mfalme akakasirika, naye akakwambia, 'Kwa nini mlipigana na mji kwa karibu hivyo, hamkujua kwamba wangeweza kushambulia kutokea ukutani?
\s5
\v 21 Ni nani aliyemwua Abimeleki mwana wa Yerubeshethi? Siye mwanamke aliyerusha jiwe la kusagia juu yake kutoka ukutani, hata akafa huko Thebesi? Kwanini basi mliukaribia ukuta jinsi hiyo? Nawe umjibu, 'Uria mtumishi wako amekufa pia."
\s5
\v 22 Hivyo mjumbe akaondoka na kwenda kwa Daudi akamwambia kila jambo ambalo Yoabu alimtuma kusema.
\v 23 Na mjumbe akamwambia Daudi, "Mwanzoni adui walikuwa na nguvu kuliko sisi; walitukabili uwandani, lakini tukawarudisha nyuma kwenye maingilio ya lango.
\s5
\v 24 Na wapiga mishale wao wakawarushia watumishi wako kutoka ukutani, na baadhi ya watumishi wa mfalme wameuawa, na mtumishi wako Uria mhiti pia ameuawa."
\v 25 Kisha Daudi akamwambia mjumbe, "Mwambie hivi Yoabu, 'Usiruhusu jamba hili likuhuzunishe, kwa maana upanga huangamiza huyu kama uangamizavyo na mwingine. Vifanye vita vyako kuwa vyenye nguvu zaidi dhidi ya mji, na uuteke.' Mtie moyo Yoabu."
\s5
\v 26 Hivyo mke Uria aliposikia kwamba mme wake amekufa, akaomboleza sana kwa ajili yake.
\v 27 Huzuni yake ilipoisha, Daudi akatuma na kumchukua kwake katika kasri lake, naye akawa mkewe na akamzalia mwana. Lakini alichokifanya Daudi hakikumpendeza Yahwe.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Kisha Yahwe akamtuma Nathani kwa Daudi. Akaja kwake na kusema, "Kulikuwa na watu wawili katika mji. Mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa masikini.
\v 2 Yule tajiri alikuwa na kundi la ng'ombe na kondoo wengi sana,
\v 3 lakini maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwanakondoo, aliyekuwa amemnunua na kumlisha na kumlea. Akakua pamoja naye na pamoja na watoto wake. Yule mwanakondoo hata alikula naye na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye akalala katika mikono yake na alikuwa kama binti kwake.
\s5
\v 4 Siku moja tajiri akapata mgeni, lakini yeye hakuwa tiyari kuchukua mnyama kutoka katika kundi lake la ng'ombe au kundi la kondoo ili kumwandalia chakula. Badala yake alichukua mwanakondoo wa masikini na akampika kwa ajili ya mgeni wake.
\v 5 Hasira ya Daudi ikawaka dhidi ya tajiri yule, naye akamwambia Nathani kwa hasira, "Kama Yahwe aishivyo, mtu aliyelitenda jambo hili anastahili kufa.
\v 6 Ni lazima alipe mwanakondoo mara nne zaidi kwa ajili ya kile alichokifanya, na kwa sababu hakuwa na huruma kwa mtu maskini.
\s5
\v 7 Ndipo Nathani akamwambia Daudi, "Wewe ndiye yule mtu! Yahweh, Mungu wa Israeli, asema, 'Nilikutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, na nilikuokoa kutoka katika mkono wa Sauli.
\v 8 Nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake zake mikononi mwako. Nilikupa pia nyumba ya Israeli na Yuda. Na ikiwa hayo yalikuwa kidogo zaidi kwako, ningeweza kukuongezea mengine zaidi.
\s5
\v 9 Hivyo basi kwa nini umedharau maagizo ya Yahwe, hata ukafanya yaliyo maovu mbele zake? Umeua Uria Mhiti kwa upanga na umechukua mkewe kuwa mke wako. Uliua kwa upanga wa jeshi la Amoni.
\v 10 Hivyo basi upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria mhiti kuwa mke wako.'
\s5
\v 11 Yahwe asema, 'Tazama, nitaleta maafa dhidi yako kutoka katika nyumba yako mwenyewe. Nitachukua wake zako, mbele ya macho yako na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako wakati wa mchana.
\v 12 Kwa maana wewe ulitenda dhambi hii sirini, lakini mimi nitatenda jambo hili wakati wa mchana mbele za Israeli wote.
\v 13 Ndipo Daudi alipomwambia Nathani, "Nimemtenda dhambi Yahwe." Nathani akamjibu Daudi, "Yahwe naye ameiachilia dhambi yako. Hautakufa.
\s5
\v 14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umemdharau Yahwe, mtoto aliyezaliwa kwako hakika atakufa."
\v 15 Kisha Nathani akaondoka na kwenda kwake. Yahwe akampiga mtoto ambaye mke wa Uria alimzaa kwa Daudi, naye akaugua sana.
\s5
\v 16 Kisha Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya kijana. Daudi akafunga naye akaingia ndani na kulala usiku wote juu ya sakafu.
\v 17 Wazee wa nyumba yake wakainuka na kusimama kando yake, ili wamwinue kutoka sakafuni. Lakini hakuinuka, na hakula pamoja nao.
\v 18 Ikawa siku ya saba mtoto akafa. Watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia kwamba mtoto amekufa, kwa maana walisema, "Tazama, wakati mtoto alipokuwa hai tuliongea naye, lakini hakuisikiliza sauti yetu. Atakuwaje ikiwa tutamwambia kwamba kijana amekufa?!"
\s5
\v 19 Daudi alipoona kwamba watumishi wake walikuwa wakinong'onezana, Akatambua kwamba mtoto amekufa. Akawauliza, "Je mtoto amekufa?" Wakajibu, "Amekufa."
\v 20 Kisha Daudi akainuka kutoka sakafuni naye akaoga, akajipaka mafuta, na kubadili mavazi yake. Akaenda katika hema la kukutania na akaabudu pale, kisha akarudu katika kasri lake. Akataka chakula kiletwe, wakamwandalia, naye akala.
\s5
\v 21 Ndipo watumishi wake walipomwambia, "Kwa nini umefanya jambo hili? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto wakati alipokuwa hai, lakini mtoto alipokufa, ukainuka na kula."
\v 22 Daudi akajibu, "Wakati mtoto alipokuwa hai nilifunga na kulia. Nilisema, Ni nani ajuaye kwamba Yahwe angeweza kunihurumia mtoto akaishi au sivyo?
\v 23 Lakini sasa amekufa, hivyo nifungie nini? Je naweza kumrudisha tena? Nitakwenda kwake, lakini yeye hawezi kunirudia."
\s5
\v 24 Daudi akamfariji Bethsheba mkewe, akaingia kwake, na akalala naye. Baadaye akazaa mtoto wa kiume, naye akaitwa Selemani. Yahwe akampenda
\v 25 naye akatuma neno kupitia nabii Nathani kumwita Yedidia, kwa sababu Yahwe alimpenda.
\s5
\v 26 Basi Yoabu akapigana na Raba, mji wa kifalme wa watu wa Amoni, naye akaiteka ngome yake.
\v 27 Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema, "Nimepigana na Raba, nami nimeshikilia sehemu inayosambaza maji ya mji.
\v 28 Kwa hiyo sasa likusanye jeshi lililosalia uhuzingire mji na kuuteka, kwa maana ikiwa nitauteka, utaitwa kwa jina langu."
\s5
\v 29 Hivyo Daudi akalikusanya jeshi lote na kwenda Raba; akapigana nao na kuuteka.
\v 30 Daudi akachukua taji ya dhahabu kutoka katika kichwa cha mfalme wao iliyokuwa na uzito wa talanta, na ilikuwa na jiwe la thamani ndani yake. Taji ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Kisha akachukua nyara za mji kwa wingi.
\s5
\v 31 Akawatoa watu waliokuwa mjini naye akawalazimisha kufanya kazi kwa misumeno, sululu na shoka; lakini pia akawalazimisha kutengeneza matofali. Daudi akailazimisha miji yote ya watu wa Amoni kufanya kazi hiyo. Kisha Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu
\s5
\c 13
\p
\v 1 Ikawa baada ya hayo kwamba Amnoni mwana wa Daudi, akamtamani sana Tamari dada yake wa kambo aliyekuwa mzuri, alikuwa tumbo moja na Absalome, mwana wingine wa Daudi.
\v 2 Amnoni akasononeka sana kiasi cha kuugua kwa ajili ya Tamari dada yake. Tamari alikuwa bikra, na hivyo ilionekana haiwezekani Amnoni kufanya neno lolote kwake.
\s5
\v 3 Lakini Amnoni alikuwa na rafiki jina lake Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi.
\v 4 Yehonadabu alikuwa mtu mwelevu sana. Akamwambia Amnoni, "Kwa nini, mwana wa mfalme, unadhoofika kila siku? Kwa nini uniambii? Ndipo Amnoni akamjibu, "Nampenda Tamari, dada yake Absalome ndugu yangu."
\s5
\v 5 Ndipo Yehonadabu akamwambia, "Lala kitandani mwako na ujifanye kuwa mgonjwa. Wakati baba yako atakapo kuja kukuona, mwambie, Tafadhari mtume dada yangu Tamari aandaye chakula mbele yangu, ili kwamba nikione na kula kutoka mkononi mwake?"
\v 6 Hivyo Amnoni akalala na kujifanya kuwa mgonjwa. Mfalme alipokuja kumwona, Amnoni akamwambia mfalme, "Tafadhari mtume Tamari dada yangu aandaye chakula kwa ajili ya ugonjwa wangu mbele yangu ili kwamba nikile kutoka mkononi mwake.
\s5
\v 7 Ndipo Daudi katika kasri lake akatuma neno kwa Tamari, kusema, "Nenda katika nyumba ya nduguyo Amnoni na umwandalie chakula. Hivyo
\v 8 Tamari akaenda katika nyumba ya Amnoni nduguye alipokuwa amelala. Akachukua donge na kulifinyanga na kuandaa mkate mbele zake, kisha akauoka.
\v 9 Akachukua kikaangio na kumpa mkate, lakini akakataa kula. Kisha Amnoni akawambia waliokuwepo, "Kila mtu na aondoke." Hivyo kila mmoja akaondoka.
\s5
\v 10 Amnoni akamwambia Tamari, "Lete chakula chumbani kwangu nikile katika mkono wako." Tamari akachukua mkate aliokuwa ameuandaa, na kuuleta katika chumba cha Amnoni kaka yake.
\v 11 Alipoleta chakula kwake, Amnoni akamshikilia na kumwambia, "Njoo, ulale nami, dada yangu."
\v 12 Yeye akamjibu, "Hapana, kaka yangu, usinilazimishe, kwani hakuna jambo kama hili linapaswa kufanyika katika Israeli. Usifanye jambo la aibu kiasi hiki!
\s5
\v 13 Nitakwenda wapi ili nijiepushe na aibu ambayo jambo hili litaileta juu ya maisha yangu? Na tendo hili litakuonesha kuwa mpumbavu usiye na aibu katika Israeli yote. Tafadhari, ninakuomba uongee na mfalme. Yeye atakuruhusu unioe."
\v 14 Lakini Amnoni hakuweza kumsikiliza. Kwa kuwa alikuwa zaidi akamkamata na akalala naye.
\s5
\v 15 Kisha Amnoni akamchukia Tamari kwa chuki kuu. Akamchukia zaidi ya jinsi alivyokuwa amemtamani. Amnoni akamwambia, "Inuka na uondoke."
\v 16 Lakini yeye akamjibu, "Hapana! kwa maana uovu wa kunifanya ni uondoke ni mbaya zaidi ya kile ulichonitenda!" Lakini Amnoni hakumsikiliza.
\v 17 Badala yake, akamwita mtumishi wake na akasema, "Mwondoe mwanamke huyu mbele yangu, na uufunge mlango nyuma yake."
\s5
\v 18 Hivyo mtumishi wake akamtoa na kufunga mlango. Tamari alikuwa amevaa vazi lilinakishiwa kwani ndivyo binti za wafalme waliobikra valivyokuwa wakivaa.
\v 19 Tamari akaweka majivu juu ya kichwa chake na akalirarua vazi lake
\s5
\v 20 Absalome, kaka yake, akamwambia, "Amnoni, kaka yako, amekuwa nawe? Lakini sasa nyamaza, dada yangu. Yeye ni kaka yako. Usiliweke hili moyoni." Hivyo Tamari akakaa peke yake katika nyumba ya Absalomu kaka yake.
\v 21 Mfalme Daudi aliposikia haya yote, alikasirika sana.
\v 22 Absalome hakusema chochote kwa Amnoni, kwa maana Absalome alimchukia kwa kile alichokifanya, kumdhalilisha Tamari, dada yake.
\s5
\v 23 Ikawa baada ya miaka miwili mizima Absalomu akawa na wakatao kondoo manyoya wakifanya kazi huko Baali Hazori, ulioko karibu na Efraim, naye Absalomu akawaarika wana wote wa mfalme kufika huko.
\v 24 Absalomu akamwendea mfalme na kusema, "Tazama sasa, mtumishi wako anao wakatao kondoo manyoya. Tafadhari, naomba mfalme na watumishi wake waende nami, mtumishi wako."
\s5
\v 25 Mfalme akamjibu Absalomu, "hapana mwanangu, tusiende sisi yote kwani tutakuwa mzigo kwako." Absalomu akamhakikishia mfalme, lakini yeye asikubali kwenda, ila alimbariki Absalomu.
\v 26 Kisha Absalomu akasema, "kama sivyo, basi tafadhari mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi." Mfalme akamuliza, "Kwa nini Amnoni aende nanyi?"
\s5
\v 27 Absalomu akamsihi Daudi, hivyo akamruhusu Amnoni na wana wengine wa mfalme kwenda naye.
\v 28 Absalomu akawaamuru watumishi wake kusema, "Sikilizeni kwa makini. Amnoni atakapokuwa amelewa mvinyo, na nitakapowambia, 'Mpigeni Amnoni,' msiogope mwueni. Je siyo mimi niliyewamru? Mwe jasiri na hodari."
\v 29 Hivyo watumishi wa Absalome wakamtendea Amnoni kama walivyoamriwa. Kisha wana wote wa mfalme wakainuka na kila mmoja akapanda nyumbu wake akakimbia.
\s5
\v 30 Hata ikawa wakati wakiwa njiani habari zikafika kwa Daudi kusema, "Absalomu ameua wana wote wa mfalme na hakuna hata mmoja aliyesalia."
\v 31 Kisha mfalme akainuka na kurarua mavazi yake na kujilaza juu ya sakafu; watumishi wake wote wakasimama karibu naye mavazi yao yameraruriwa.
\s5
\v 32 Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi, akajibu na kusema, "Bwana wangu asidhani kuwa vijana wote ambao ni wana wa mfalme wameuawa, kwa maana ni Amnoni pekee ndiye aliyeuawa. Absalomu alilipanga jambo hili tangu siku ile Amnoni alivyomwaribu Tamari, dada yake.
\v 33 Kwa hiyo basi, bwana wangu mfalme asiiweke taarifa hii moyoni, kudhani kwamba wana wote wa mfalme wameuawa, kwani aliyeuawa ni Amnoni peke yake."
\s5
\v 34 Absalomu akakimbia. Mtumishi aliyekuwa akiangalia akainua macho yake na kuona watu wengi wakija njiani kando ya kilima upande wake wa magharibi.
\v 35 Kisha Yehonadabu akamwambia mfalme, "Tazama, wana wa mfalme wanakuja. kama mtumishi wako alivyosema."
\v 36 Ikawa mara alipomaliza kusema wana wa mfalme wakafika, wakainua sauti zao na kulia. Na mfalme pamoja na watumishi wake wote pia wakalia kwa uchungu.
\s5
\v 37 Lakini Absalomu akakimbia na kwenda kwa Talmai mwana wa Amihudi, mfalme wa Geshuri. Mfalme akaomboleza kila siku kwa ajili ya mwanaye.
\v 38 Hivyo Absalomu akakimbia na kwenda Geshuri na akakaa huko kwa miaka mitatu.
\v 39 Moyo wa mfalme Daudi ukatamani kwenda kumwona Absalomu, kwa maana alikuwa amefarijika kwa habari ya kifo cha Amnoni.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Yoabu mwana wa Seruya akatambua kwamba moyo wa mfalme ulitamani kumwona Absalomu.
\v 2 Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwelevu. Akamwambia, "Tafadhari, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa.
\v 3 Kisha ingia kwa mfalme na umwambiye maneno nitakayokueleza." Hivyo Yoabu akamwambia maneno ambayo angeyasema kwa mfalme.
\s5
\v 4 Wakati mwanamke kutoka Tekoa alipoongea na mfalme, aliinamisha uso wake chini na kusema,
\v 5 "Mfalme, anisaidie." Mfalme akamwambia, "Shida yako ni nini?" Akajibu, Ukweli ni kwamba mimi ni mjane, mme wangu alikufa.
\v 6 Mimi, mtumishi wako, nilikuwa na wana wawili, wakagombana shambani, na hakukuwa na wa kuwaachanisha. Mmoja wao akampiga mwenziwe na kumwua.
\s5
\v 7 Na sasa ukoo wote umeinuka juu ya mtumishi wako, wanasema, 'Mtoe aliyempiga nduguye, ili tumwue kulipe uhai wa nduguye aliyeuawa.' Na hivyo watamwangamiza mrithi. Hivyo watalizima kaa liwakalo nililobakiwa, hata kumwondolea mme wangu jina na mzao juu ya uso wa nchi."
\s5
\v 8 Hivyo mfalme akamwambia mwanamke, "Nenda nyumbani kwako, nami nitaagiza jambo la kukufanyia."
\v 9 Mwanamke kutoka Tekoa akamjibu mfalme, "Bwana wangu mfalme, hatia na iwe juu yangu na juu ya familia ya baba yangu. Mfalme na kiti chake cha enzi hawana hatia."
\s5
\v 10 Mfalme akasema, "Yeyote atakayekwambia neno umlete kwangu, naye hatakugusa tena."
\v 11 Kisha mwanamke akasema, "Tafadhari mfalme amkumbuke Yahwe Mungu wake, ili kwamba mlipa kisasi cha damu asiaribu zaidi, ili kwamba wasimwangamize mwanangu." Mfalme akajibu, "Kama Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utaanguka chini."
\s5
\v 12 Kisha mwanamke akasema, "Tafadhari acha mtumishi wako anene neno moja zaidi kwa bwana wangu mfalme." Akasema, "Sema."
\v 13 Hivyo mwanamke akasema, "Kwa nini basi umetenda kwa hila dhidi ya watu Mungu? Maana kwa kusema hivi, mfalme ni kama mtu mwenye hatia, kwa kuwa mfalme hamjamrudisha tena mwanaye aliyeondoka.
\v 14 Kwa maana sisi sote tutakufa, kwa kuwa tu kama maji yamwagwayo juu ya ardhi na kwamba hayawezi kukusanywa tena. Lakini Mungu hatachukua uhai; badala yake, utafuta njia kwa walio mbali kurejeshwa.
\s5
\v 15 Sasa basi, nimesema jambo hili kwa bwana wangu mfalme, kwa sababu watu wamenitisha. Hivyo mtumishi wako akajinenea nafsini mwake, 'Sasa nitaongea na mfalme. Huenda mfalme akampa mtumishi wake haja yake.
\v 16 Kwa maana mfalme atanisikiliza, ili kwamba kumtoa mtumishi wake katika mikono ya mtu ambaye angeniangamiza mimi na mwanangu pamoja, tutoke katika urithi wa Mungu.
\v 17 Kisha mtumishi wako akaomba, 'Yahwe, tafadhari ruhusu neno la bwana wangu mfalme linipe msaada, kwa maana bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu kwa kutofautisha wema na ubaya.' Yahwe, Mungu na awe pamoja nawe."
\s5
\v 18 Ndipo mfalme akajibu na kumwambia yule mwanamke, Tafadhari usinifiche neno lolote nikuulizalo." Mwanamke akajibu, "Basi bwana wangu mfalme na aseme sasa.
\v 19 Mfalme akasema, Je siyo mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu na kusema, "Kama uishivyo bwana wangu mfalme, hakuna awezae kuelekea mkono wa kulia wala wa kushoto kwa yale bwana wangu mfalme aliyosema. Ni mtumishi wako Yoabu aliyeniambia na kuniagiza kusema kile mtumishi wako alichokisema.
\v 20 Mtumishi wako Yoabu amefanya hivi ili kubadilisha hali ya kile kinachotendeka. Bwana wangu ni mwenye akili kama hekima ya malaika wa Mungu, ajuaye yote yatendekayo ndani ya nchi."
\s5
\v 21 Hivyo mfalme akamwambia Yoabu, "Tazama, nitatenda jambo hili. Nenda na umrudishe huyo kijana Absalomu."
\v 22 HivyoYoabu akainamisha uso wake chini juu ya ardhi katika heshima na shukurani kwa mfalme. Yoabu akasema, "Mtumishi wako amejua kwamba amepata neema mbele zako, bwana wangu, mfalme, kwa vile mfalme amempa mtumishi wake haja ya moyo wake.
\s5
\v 23 Hivyo Yoabu akainuka na kwenda Geshuri, akamrejesha Absalomu Yerusalemu tena.
\v 24 Mfalme akasema, "Na arudi nyumbani kwake, lakini hasinione uso wangu." Hivyo Absalomu akarudi katika nyumba yake mwenyewe, na hakuweza kuuona uso wa mfalme.
\s5
\v 25 Hakukuwa na mtu katika Israeli aliyesifiwa kwa uzuri kama Absalomu. Kutoka katika wayo wa mguu wake hadi katika utosi wake hakuwa na waa lolote.
\v 26 Alipokata nywele za kichwa chake mwishoni mwa kila mwaka, kwa sababu zilikuwa nzito juu yake, alipima nywele zake zaidi ya shekeli mia mbili, kwa kiwango cha kipimo cha mfalme.
\v 27 Kwake Absalomu walizaliwa wana watatu na binti mmoja, jina lake Tamari. Alikuwa mwanamke mzuri.
\s5
\v 28 Absalomu akaishi Yerusalem miaka miwili pasipo kuona uso wa mfalme.
\v 29 Kisha Absalome akatuma neno kwa Yoabu ili ampeleke kwa mfalme, lakini Yoabu hakwenda kwake. Hivyo Absalomu akatuma neno mara ya pili, lakini Yoabu hakuja bado.
\s5
\v 30 Hivyo Absalomu akawambia watumishi wake, "Tazameni, shamba la Yoabu lipo karibu na langu, naye ana shayiri kule. Nendeni mkalichome moto" Hivyo watumishi wa Absalome wakalichoma moto lile shamba.
\v 31 Kisha Yoabu akainuka na kwenda nyumbani kwa Absalomu akamwambia, "Kwa nini watumishi wako wamelichoma moto shamba langu?
\s5
\v 32 Absalomu akamjibu Yoabu, "Tazama nilituma neno kwako kusema, 'Njoo ili nikutume kwa mfalme kusema, "Kwa nini nilikuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningesalia huko. Kwa hiyo sasa niache niuone uso wa mfalme na kama nina hatia basi na aniue."
\v 33 Hivyo Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia. Mfalme alipomwita, Absalomu alikuja kwa mfalme na akainama hadi juu ya uso nchi mbele ya mfalme na mfalme akambusu Absalomu.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ikawa baada ya haya Absalomu akaandaa gari la farasi na farasi kwa ajili yake pamoja na watu hamsini wa kwenda mbele zake.
\v 2 Absalomu alikuwa akiamka mapema na kusimama kando ya njia iliyoelekea katika lango la mji. Mtu yeyote aliyekuwa na shauri la kuja kwa mfalme kwa ajili ya hukumu, Absalomu alimwita na kumwuliza, "Unatoka mji upi?" Na mtu yule hujibu, Mtumishi wako anatoka mojawapo ya kabila za Israeli."
\s5
\v 3 Hivyo Absalomu umwambia, "Tazama, shitaka lako ni jema na la haki, lakini hakuna aliyepewa mamlaka na mfalme kusikiliza shitaka lako.
\v 4 Absalomu uongeza, "Natamani kwamba ningefanywa mwamzi ndani ya nchi ili kwamba kila mtu aliye na shitaka angeweza kuja kwangu nami ningempa haki.
\s5
\v 5 Hivyo ikawa kila mtu aliyekuja kumweshimu Absalomu yeye hunyosha mkono na kumshika na kumbusu.
\v 6 Absalomu alifanya hivi kwa Israeli wote waliokuja kwa mfalme kwa ajili ya hukumu. Hivyo Absalomu akaipotosha mioyo ya watu wa Israeli.
\s5
\v 7 Ikawa mwishoni mwa miaka minne Absalomu akamwambia mfalme, "Tafadhari niruhusu niende ili nitimize nadhiri niliyoiweka kwa Yahwe huko Hebroni.
\v 8 Kwa maana mtumishi wako aliweka nadhiri alipokuwako Geshuri katika Shamu akisema, 'Ikiwa Yahwe kweli atanirejesha Yerusalemu, ndipo nitamwabudu yeye."
\s5
\v 9 Hivyo mfalme akamwambia, "Nenda kwa amani". Absalomu akainuka na kwenda Hebroni.
\v 10 Kisha Absalomu akatuma wapelelezi katika jamaa zote za Israeli, kusema, "Mara msikiapo sauti ya tarumbeta semeni, 'Absalomu anatawala katika Hebroni."
\s5
\v 11 Watu mia mbili waliokuwa wamearikwa kutoka Yerusalemu wakaenda na Absalomu. Wakaenda katika ujinga wao bila kujua Absalomu alichokipanga. Wakati
\v 12 Absalomu akitoa dhabihu, alituma watu kwa Ahithofeli katika mji wake huko Gilo. Yeye alikuwa mshauri wa Daudi. Uaini wa Absalomu ukawa na nguvu kwa kuwa watu waliomfuata waliendelea kuongezeka.
\s5
\v 13 Mjumbe akaja kwa Daudi na kusema, "Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu."
\v 14 Hivyo Daudi akawambia watumishi wake waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, "Haya na tuinuke na kukimbia kwani hakuna hata mmoja atakayesalimika kwa Absalomu. Jiandaeni kuondoka mara moja asije akatupata mara hata akasababisha madhara juu yetu na kuushambulia mji kwa makali ya upanga."
\v 15 Watumishi wa mfalme wakamwambia, "Tazama, watumishi wako wapo tiyari kufanya lolote bwana wetu mfalme atakaloamua.
\s5
\v 16 Mfalme akaondoka na familia yake yote pamoja naye, lakini mfalme akawaacha wanawake kumi waliokuwa masuria wa mfalme ili walitunze kasri.
\v 17 Baada ya mfalme kwenda na watu wote pamoja naye, wakasimama katika nyumba ya mwisho.
\v 18 Jeshi lake lote likaenda pamoja naye na mbele yake wakaenda Wakerethi na Wapelethi, na Wagiti mia sita wote waliokuwa wamemfuata kutoka Gathi.
\s5
\v 19 Kisha mfalme akamwambia Itai Mgiti, "Kwa nini wewe pia uende nasi? Rudi na ukae na mfalme Absalomu kwa kuwa wewe ni mgeni tena mfungwa. Rudi mahali pako mwenyewe.
\v 20 Kwani ni jana tu umeondoka, kwa nini nikufanye uzunguke nasi popote? Hata sijui niendako. Hivyo rudi pamoja na wenzako. Utiifu na uaminifu viambatane nawe."
\s5
\v 21 Lakini Itai akamjibu mfalme na kusema, "Kama Yahwe aishivyo na kama bwana wangu mfalme aishivyo, kwa hakika mahali popote bwana wangu mfalme aendako, mtumishi wako pia ndipo atakapokwenda, kwamba ni maisha au kifo."
\v 22 Hivyo Daudi akamwambia Itai, haya tangulia uende pamoja nasi." Hivyo Itai Mgiti akaenda pamoja na mfalme, pamoja na watu wake wote na familia zao zote.
\v 23 Nchi yote ikalia kwa sauti kadili watu walivyokuwa wakivuka Bonde la Kidroni, mfalme naye pia akavuka. Watu wote wakasafiri kuelekea nyikani.
\s5
\v 24 Walikuwepo pia Sadoki pamoja na Walawi wote wamebeba sanduku la Mungu la agano. Wakaliweka sanduku la Mungu chini na kisha Abiathari akaungana nao. Wakasubiri mpaka watu wote walioondoka mjini walipokwisha kupita.
\v 25 Mfalme akamwambia Sadoki, "Ulirudishe sanduku la Mungu mjini. Ikiwa nitaona neema machoni pa Yahwe atanirudisha na kunionesha tena sanduku na mahali likaapo.
\v 26 Lakini ikiwa atasema, sipendezwi nawe,' tazama mimi nipo hapa, na anitendee yaliyo mema machoni pake."
\s5
\v 27 Pia mfalme akamwambia Sadoki kuhani, "Je wewe siyo mwonaji? Rudi mjini kwa amani na wanao wawili, Ahimaazi mwanao na Yonathani mwana wa Abiathari.
\v 28 Tazama nitasubiri katika vivuko vya Araba mpaka nitakapo pata neno kutoka kwenu kunitaarifu."
\v 29 Hivyo Sadoki na Abiathari wakalirudish sanduku la Mungu Yerusalemu nao wakakaa humo.
\s5
\v 30 Lakini Daudi akaenda bila viatu huku akilia hata Mlima wa Mizeituni, naye alikuwa amefunika kichwa chake. Kila mtu miongoni mwao waliokuwa pamoja naye akafunika kichwa chake, nao wakaenda huku wakilia.
\v 31 Mtu mmoja akamwambia Daudi kusema, Ahithofeli ni miongoni mwa waaini walio pamoja na Absalomu." Hivyo Daudi akaomba, "Ee Yahwe, tafadhari badili ushauri wa Ahithofeli kuwa upumbavu."
\s5
\v 32 Ikawa Daudi alipofika juu njiani mahala Mungu alipokuwa akiabudiwa, Hushai Mwarki akaja kumlaki vazi lake limeraruliwa na mavumbi kichwani pake.
\v 33 Daudi akamwambia, "Ikiwa utaenda nami utakuwa mzigo kwangu.
\v 34 Lakini ukirudi mjini na kumwambia Absalomu, 'Nitakuwa mtumishi wa mfalme kama nilivokuwa mtumishi wa baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako,' ndipo utayageuza mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.
\s5
\v 35 Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani? Hivyo chochote ukisikiacho katika kasri, uwaambie Sadoki na Abiathari makuhani.
\v 36 Tazama wanao pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani mwana wa Abiathari. Mniletee habari juu ya kila mnachokisikia."
\v 37 Hivyo Hushai, rafiki wa Daudi, akaja mjini wakati Absalomu anafika na kuingia Yerusalemu.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo.
\v 2 Mfalme akamuliza Siba, "Kwa nini umeleta hivi vitu?" Siba akajibu, "punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili kunywa watakaozimia nyikani."
\s5
\v 3 Mfalme akauliza, "Na mjukuu wa bwana wako yuko wapi?" Siba akamjibu mfalme, "Tazama, yeye amesalia Yerusalemu kwa maana alisema, 'Leo nyumba ya Israeli itanirudishia ufalme wa baba yangu."
\v 4 Kisha mfalme akamwambia Siba, "Tazama, yote yaliyomilikiwa na Mefiboshethi sasa yatakuwa yako." Siba akajibu, "Nainama kwa unyenyekevu kwako bwana wangu mfalme. Na nipate kibari mbele zako."
\s5
\v 5 Mfalme Daudi alipokaribia Bahurimu, akaja mtu kutoka katika ukoo wa Sauli, jina lake Shimei mwana wa Gera. Kadiri alivyokuwa akitembea alikuwa akilaani.
\v 6 Akamrushia Daudi mawe na maofisa wa mfalme, bila kujali jeshi na walinzi wa mfalme waliokuwa kulia na kushoto mwa mfalme.
\s5
\v 7 Shimei akalaani, "Nenda zako, toka hapa, mwovu wewe, mtu wa damu!
\v 8 Yahwe amelipa yote kwa ajili ya damu ya familia ya Sauli, ambaye unatawala badala yake. Yahwe ameweka ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao. Na sasa umeangamia kwa kuwa ni mtu wa damu."
\s5
\v 9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, "Kwa nini mbwa mfu anamlaani bwana wangu mfalme? Tafadhari niache niende nikamwondolee kichwa chake."
\v 10 Lakini mfalme akasema, "Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya? Pengine ananilaani kwa kuwa Yahwe amemwambia, 'Mlaani Daudi.' Nani sasa awezaye kumwambia, 'Kwa nini unamlaani mfalme."
\s5
\v 11 Hivyo Daudi akamwambia Abishai na watumishi wake wote, "Tazameni, mwanangu aliyezaliwa kutoka katika mwili wangu anatafuta uhai wangu. "Si zaidi sana mbenjamini huyu akatamani anguko langu? Mwacheni alaani, kwa maana Yahwe amemwamru kufanya hivyo.
\v 12 Huenda Yahwe akaangalia maangaiko niliyofungiwa, na kunirudishia mema kwa jinsi nilivyolaaniwa leo."
\s5
\v 13 Hivyo Daudi na watu wake wakaendelea njiani wakati Shimei kando yake ubavuni mwa mlima, aliendelea kulaani na kumrushia mavumbi na mawe huku akienda.
\v 14 Kisha mfalme na watu wake wote wakachoka, na akapumzika wakati wa usiku walipopumzika wote.
\s5
\v 15 Absalomu na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye wakaja Yerusalemu na Ahithofeli alikuwa pamoja naye.
\v 16 Ikawa Hushai Mwarki, rafiki yake Daudi, akaja kwa Absalomu, naye akamwambia Absalomu, "Mfalme aishi daima! mfalme aishi daima.
\s5
\v 17 Absalomu akamwambia Hushai, "Je huu ndiyo utiifu wako kwa rafiki yako? Kwa nini haukwenda pamoja naye?"
\v 18 Hushai akamwambia Absalomu, "Hapana! badala yake, yule ambaye Yahwe, watu hawa na watu wote wa Israeli wamemchagua huyo ndiye nitakaye kuwa upande wake na ndiye nitakaye kaa naye.
\s5
\v 19 Kwani ni nani ninayepaswa kumtumikia? Je sipaswi kutumika mbele za mwana? kama nilivyotumika mbele za baba yako ndivyo nitakavyofanya mbele zako"
\s5
\v 20 Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, "Tupe shauri lako kuhusu tunachopaswa kufanya."
\v 21 Ahithofeli akamwambia Absalomu, "Nenda ulale na masuria wa baba yako aliowaacha kutunza kasri, na waisraeli wote watasikia kwamba umekuwa kitu kinachonuka kwa baba yako. Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu."
\s5
\v 22 Hivyo wakatanda hema kwa ajili ya Absalomu juu ya kasri na Absalomu akalala na masuria wa baba yake mbele za Israeli wote.
\v 23 Nyakati hizo ushauri aliokuwa akitoa Ahithofeli ulikuwa ni kama mtu anavyosikia kutoka katika kinywa cha Mungu mwenyewe. Hivyo ndivyo jinsi ushauri wa Ahithofeli ulivyoonekana kwa Daudi na Absalomu
\s5
\c 17
\p
\v 1 Kisha Ahithofeli akamwambia Absalomu, "Niruhusu sasa nichague watu elfu kumi na mbili nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu.
\v 2 Nitampata kwa ghafla wakati amechoka na dhaifu nami nitamstukiza kwa hofu. Watu waliopamoja naye watakimbia nami nitamshambulia mfalme peke yake.
\v 3 Nitawarejesha watu wote kwako kama bibi harusi ajavyo kwa bwana wake, na watu wote watakuwa katika amani chini yako."
\v 4 Alichokisema Ahithofeli kikampendeza mfalme na wazee wote wa Israeli.
\s5
\v 5 Kisha Absalomu akasema, "Sasa mwiteni pia Hushai Mwarki ili tusikie yeye pia anasemavyo."
\v 6 Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamweleza kile ambacho Ahithofeli alikuwa amesema na kisha akamwuliza Hushai, "Je tufanye alivyosema Ahithofeli? Ikiwa hapana, tueleze kile unachoshauri."
\v 7 Hivyo Hushai akamwambia Absalomu, "Ushauri aliotoa Ahithofeli siyo mzuri kwa wakati huu."
\s5
\v 8 Hushai akaongeza, "Unamjua baba yako na kwamba watu wake ni mashujaa na kwa sasa wanauchungu, ni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake mwituni. Baba yako ni mtu wa vita; hatalala na jeshi usiku huu.
\v 9 Tazama, kwa wakati huu pengine amejificha katika shimo fulani au mahali pengine. Itakuwa kwamba baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa mwanzoni mwa shambulio hata kila mtu atakayesikia atasema, mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu.'
\v 10 Kisha hata askari jasiri zaidi ambao moyo wao ni kama moyo wa simba, wataogopa kwa kuwa Israeli yote inajua kwamba baba yako ni mtu mwenye nguvu na kwamba watu alionao ni wenye nguvu sana.
\s5
\v 11 Hivyo ninashauri kwamba Israeli wote wakutanike kwako pamoja kutoka Dani hadi Beersheba, wengi kama mchanga ufuoni mwa bahari na kwamba wewe mwenyewe uende vitani.
\v 12 Kisha tutampata popote atakapokuwa nasi tutamfunika kama umande uangukavyo juu ya nchi. Hatutamwachia hata mmoja aliye hai kati ya watu wake wala yeye mwenyewe.
\s5
\v 13 Ikiwa ataingia ndani ya mji kisha Israeli wote tutaleta kamba juu ya mji huo na kuukokotea mtoni, hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia."
\v 14 Kisha Absalomu na watu wa Israeli wakasema, "Shauri la Hushai Mwarki ni jema kuliko lile la Ahithofeli. Yahwe aliwafanya wakatae shauri jema la Ahithofeli ili kumwangamiza Absalomu.
\s5
\v 15 Kisha Hushai akawambia Sadoki na Abiathari makuhani, "Ahithofeli alimshauri Absalomu na wazee wa Israeli hivi na hivi, lakini mimi nimeshauri vinginevyo.
\v 16 Sasa basi, nendeni haraka na mmtaarifu Daudi kusema, 'Usipige kambi usiku huu katika vivuko vya Araba, lakini kwa namna yoyote vukeni, tofauti na hapo mfalme atamezwa pamoja na watu wote walio pamoja naye."
\s5
\v 17 Yonathani na Ahimaasi walikuwako katika chemichemi za En Rogeli. Hivyo kijakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapasha habari waliyopaswa kuifahamu, ili kwamba wasihatarishe maisha yao kwa kuonwa wakiingia mjini. Ujumbe ulipofika ndipo huenda na kumtaarifu mfalme Daudi.
\v 18 Lakini kijana mmoja akawaoni mara akamwambia Absalomu. Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaenda kwa haraka na wakaingia katika nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu, aliyekuwa na kisima katika ua wake wakaingia humo.
\s5
\v 19 Mke wa mtu huyo akachukua kifuniko na kukikufunika kwenye mlango wa kisima kisha akaanika nafaka juu yake, hivyo hakuna aliyejua kwamba Yonathani na Ahimaasi walikuwa kisimani.
\v 20 Watu wa Absalomu wakaja kwa mwanamke na kumwuliza, "Ahimaasi na Yonathani wako wapi?" Mwanamke akawaambia, "Wamevuka mto." Hivyo baada ya kuwatafuta bila kuwaona kurejea Yerusalemu.
\s5
\v 21 Ikawa baada yao kuondoka Yonathani na Ahimaasi wakatoka ndani ya kisima. Wakaenda kumtaarifu mfalme Daudi; wakamwambia, "Inuka na uvuke maji haraka kwa maana Ahithofeli ametoa mashauri haya na haya juu yako."
\v 22 Kisha Daudi akainuka pamoja na watu wote walikuwa pamoja naye, nao wakauvuka Yordani. Hata ilipofika alfajiri hakuna hata mmoja aliyesalia kwa kutouvuka Yordani.
\s5
\v 23 Ikawa Ahithofeli alipoona kwamba ushauri wake haukufuatwa, akapanda punda wake na kuondoka. Akaenda nyumbani katika mji wake mwenyewe, akaweka mambo yake katika utaratibu na kisha akajinyonga. Kwa hiyo akafa na kuzikwa katika kaburi la baba yake.
\s5
\v 24 Ndipo Daudi akaja Mahanaimu. Lakini Absalomu yeye akavuka Yordani yeye pamoja na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye.
\v 25 Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Naye huyo Amasa alikuwa mwana wa Yetheri Mwishmaeli, aliyekuwa amelala na Abigaili, aliyekuwa binti Nahashi na dada wa Seruya, mamaye Yoabu.
\v 26 Kisha Israeli na Absalomu wakapiga kambi katika nchi ya Gileadi.
\s5
\v 27 Ikawa wakati Daudi alipokuwa amekuja Mahanaimu, huyo Shobi mwana wa Nahashi kutoka Raba ya Waamoni na Makiri mwana wa Amieli wa kutoka Lo Debari, na Berzilai Mgileadi wa Rogelimu,
\v 28 wakaleta magodoro na mabulangeti, mabakuri na vyungu, na ngano, unga wa shayiri, nafaka zilizokaangwa, maharage, dengu,
\v 29 asali, siagi, kondoo na samli, ili kwamba Daudi na watu waliokuwa pamoja naye waweze kula. Kwani walisema, "Watu wana njaa, wamechoka na wana kiu huko nyikani."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Daudi akawahesabu askari waliokuwa pamoja naye na akaweka akida wa elfu na akida wa mia juu yao.
\v 2 Kisha Daudi akalipeleka jeshi, thelusi moja chini ya Yoabu, thelusi nyingine chini ya Abishai mwana wa Seruya, ndugu wa Yoabu, na thelusi nyingine tena chini ya Itai Mgiti. Mfalme akaliambia jeshi, "kwa hakika mimi mwenyewe pia nitakwenda pamoja nanyi.
\s5
\v 3 Lakini watu wakasema, "Wewe usiende vitani, kwani ikiwa tutakimbia hawatatujari sisi, ama nusu yetu wakifa hawatajari. Lakini wewe ni zaidi ya elfu kumi yetu sisi! Kwa hiyo ni afadhari zaidi ukitusaidia ukiwa mjini."
\v 4 Hivyo mfalme akawajibu, "Nitafanya lolote lionekanalo jema machoni penu." Mfalme akasimama kati ya lango la mji wakati jeshi lilipoondoka katika mamia na katika maelfu.
\s5
\v 5 Mfalme akawaagiza Yoabu, Abishai, na Itai kusema, "Mmtendee huyo kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu." Watu wote wakasikia jinsi mfalme alivyowaagiza maakida kuhusu Absalomu.
\s5
\v 6 Hivyo jeshi likaenda nyikani dhidi ya Israeli; vita ikaenea katika msitu wa Efraimu.
\v 7 Jeshi la Israeli likashindwa mbele ya askari wa Daudi; kulikuwa na machinjo makuu kwa watu elfu ishirini siku hiyo.
\v 8 Vita ikaenea katika eneo lote na watu wengi wakaangamizwa na msitu kuliko upanga.
\s5
\v 9 Ikatukia kwamba Absalomu akakutana na askari wa Daudi. Absalomu alikuwa amepanda juu ya nyumbu wake na nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mti wa mwaloni, na kichwa chake kikanaswa katika matawi ya mti. Akaachwa akining'inia kati ya nchi na anga wakati nyumbu alipoendelea mbele.
\v 10 Mtu mmoja akaona lililotukia na akamwambia Yoabu, "Tazama, nilimwona Absalomu akining'inia katika mwaloni!"
\v 11 Yoabu akamwambia aliyemwambia kuhusu Absalomu, "Tazama! Ulimwona! Kwa nini haukumpiga hata chini. Ningekupa shekeli kumi za fedha na mkanda."
\s5
\v 12 Yule mtu akamjibu Yoabu, "Hata kama ningepewa shekeli elfu za fedha hata hivyo nisingeinua mkono wangu juu ya mwana wa mfalme, kwa maana sisi sote tulimsikia mfalme akiwaagiza wewe, Abishai na Itai kusema, mtu asimguse huyo kijana Absalomu.'
\v 13 Ikiwa ningehatarisha maisha yangu kwa uongo(na hakuna jambo linalofichika kwa mfalme), ungejitenga nami."
\s5
\v 14 Ndipo Yoabu aliposema, "sitakusubiri." Kisha akachukua mishale mitatu mkononi mwake na akairusha katika moyo wa Absalomu wakati yu ngali hai na amening'inia katika mwaloni.
\v 15 Kisha vijana kumi waliochukua slaha za Yoabu wakamzunguka Absalomu, wakampiga na kumwua.
\s5
\v 16 Kisha Yoabu akapiga tarumbeta na jeshi likarudi kutoka kuwafuatia Israeli, hivyo Yoabu akalirudisha jeshi.
\v 17 Wakamchukua Absalomu na kumtupa katika shimo kubwa msituni; wakaufukia mwili wake chini ya rundo kubwa la mawe, wakati Israeli wote walipokimbia kila mtu nyumbani kwake.
\s5
\v 18 Wakati Absalomu alipokuwa yu ngali hai alijijengea nguzo kubwa ya jiwe katika Bonde la Mfalme, kwani alisema, "Sina mwana wa kuchukua kumbukumbu ya jina langu." Akaiita nguzo kwa jina lake, hivyo inaitwa Mnara wa Absalomu hata leo.
\s5
\v 19 Kisha Ahimaasi mwana wa Sadoki akasema, "Niruhusu niende kwa mfalme na habari njema, jinsi Yahwe alivyomwokoa kutoka mkono wa adui zake."
\v 20 Yoabu akamjibu, "Wewe hautakuwa mchukua habari leo; utafanya hivyo siku nyingine. Leo hautachukua habari yoyote kwa maana mwana wa mfalme ameuawa."
\s5
\v 21 Ndipo Yoabu akamwambia Mkushi, "Nenda umwambia mfalme ulichokiona." Mkushi akamwinamia Yoabu, na kisha akakimbia.
\v 22 Kisha tena, Ahimaasi mwana wa Sadoki akamwambia Yoabu, "Pamoja na yote yanayoweza kutokea, tafadhari niruhusu nami pia niende nimfuate Mkushi." Yoabu akajibu, "Mwanangu kwa nini unataka kwenda, hautapata thawabu yoyote kwa ajili ya habari hii?"
\v 23 "Vyovyote itakavyokuwa niache niende," Ahimaasi alijibu. Hivyo Yoabu akamjibu, "Nenda." Ndipo Ahimaasi akakimbia kwa njia ya tambarare na akampita Mkushi.
\s5
\v 24 Basi Daudi alikuwa amekaa kati ya lango la ndani na lango la nje. Na mlinzi alikuwa juu ya lango ukutani naye akainua macho yake. Alipokuwa akiangalia, akamwona mtu anakaribia huku akikimbia peke yake.
\v 25 Mlinzi akaita kwa sauti na kumwambia mfalme. Ndipo mfalme akasema, "Ikiwa yupo peke yake ana habari katika kinywa chake." Mkimbiaji akasogea na kuukaribia mji.
\s5
\v 26 Kisha mlinzi akaona mtu mwingine aliyekuwa anakimbia, naye akamwambia bawabu; kusema, "Tazama, kuna mtu mwingine anakimbia peke yake." Mfalme akasema, "Yeye pia analeta habari."
\v 27 Ndipo mlinzi akasema, Nadhani kukimbia kwake mtu aliye mbele ni kama kukimbia kwake Ahimaasi mwana wa Sadoki." Mfalme akasema, "Yeye ni mtu mwema naye anakuja na habari njema."
\s5
\v 28 Ndipo Ahimaasi akaita na kumwambia mfalme, "Yote ni mema." Kisha akainama yeye mwenyewe uso wake chini mbele ya mfalme na kusema, Atukuzwe Yahwe Mungu wako, aliyewatoa watu walioinua mkono wao kinyume cha bwana wangu mfalme."
\v 29 Hivyo mfalme akauliza, "Je huyo kijana Absalomu hajambo?" Ahimaasi akajibu, "Wakati Yoabu ananituma kwako mfalme, mimi mtumishi wa mfalme, niliona fujo kubwa sana lakini sikutambua ilihusu nini."
\v 30 Mfalme akamwambia, "Geuka usimame kando." Hivyo Ahimaasi akageuka na kusimama.
\s5
\v 31 Mara Mkushi akafika na kusema, "Kuna habari njema kwa bwana wangu mfalme kwa kuwa leo Yahwe amekulipia kisasi kwa wale wote walioinuka kinyume chako."
\v 32 Ndipo mfalme akamwuliza, "Je huyo kijana Absalomu ni mzima?" Mkushi akajibu, "Adui wa bwana wangu mfalme na wote wainukao kukudhuru na wawe kama huyo kijana."
\v 33 Ndipo mfalme alipohuzunishwa sana naye akaenda chumbani juu ya lango na kulia. Kadili alivyokwenda aliomboleza, mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! afadhari ningekufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!"
\s5
\c 19
\p
\v 1 Yoabu akaambiwa, "Tazama, mfalme analia na kumwombolea Absalomu."
\v 2 Hivyo siku ile ushindi uligeuzwa kuwa maombolezo kwa jeshi lote, kwa maana jeshi likasikia ikisemwa siku hiyo, "Mfalme anaomboleza kwa ajili ya mwanaye."
\s5
\v 3 Siku ile askari waliingia mjini kwa kunyemelea kimyakimya kama watu waonao haya baada ya kukimbia vitani.
\v 4 Mfalme akafunika uso wake na kulia kwa sauti, "Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwangangu!"
\s5
\v 5 Ndipo Yoabu akaingia ndani kwa mfalme na kumwambia, "Leo umeziaibisha nyuso za askari wako, waliookoa maisha yako leo, maisha ya wanao na binti zako, maisha ya wake zako na maisha ya masuria wako,
\v 6 kwa maana wawapenda wakuchukiao na kuwachukia wakupendao. Kwa kuwa leo umeonesha kwamba maakida na askari si chochote kwako. Natambua sasa kwamba kame Absalomu angesalia na sisi sote tungekufa hilo lingekufurahisha.
\s5
\v 7 Sasa basi, inuka na uende kuongea na askari wako kwa upole, kwani nakuapia kwa Yahwe, ikiwa hutakwenda hakuna mtu hata mmoja atakayesalia nawe usiku huu. Na hii itakuwa vibaya sana kwako kuliko madhara yoyote yaliyowai kukupata tangu ujana wako."
\v 8 Hivyo mfalme akainuka na kuketi kati ya lango la mji, watu wote wakaambiwa, "Tazama, mfalme ameketi kati ya lango." Ndipo watu wote wakaja mbele za mfalme. Walakini, Israeli walikimbia kila mtu nyumbani kwake.
\s5
\v 9 Watu wote wakahojiana wao kwa wao katika jamaa zote za Israeli kusema, "Mfalme alituokoa na mkono wa adui zetu. Alitukomboa na mkono wa Wafilisti lakini sasa ameikimbia nchi mbele ya Absalomu.
\v 10 Na Absalomu tuliyemtia mafuta juu yetu amekufa vitani. Hivyo kwa nini hatuongei juu ya kumrudisha mfalme tena?"
\s5
\v 11 Mfalme Daudi akatuma kwa Sadoki na kwa Abiathari makuhani kusema, "Ongeeni na wazee wa Yuda kusema, Kwa nini ninyi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme kwenye kasri lake tena, kwa vile usemi wa Israeli wote unamtaka mfalme arudi katika kasri lake?
\v 12 Ninyi ni ndugu zangu, mwili na mifupa yangu. Kwa nini basi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme?'
\s5
\v 13 Na mwambieni Amasa, 'Je wewe si mwili na mfupa wangu? Mungu anifanyie hivyo na kuzidi pia ikiwa hautakuwa jamadari wa jeshi langu tangu sasa na baadaye mahali pa Yoabu.
\v 14 Naye akaishinda mioyo ya watu wote wa Yuda kama mtu mmoja, hata wakatuma kwa mfalme kusema, "Rudi sasa na watu wako wote."
\v 15 Hivyo mfalme akarudi naye akaja Yordani. Na watu wa Yuda wakaja Gilgali kwenda kumlaki mfalme ili kumvusha mfalme juu ya Yordani.
\s5
\v 16 Shimei mwana wa Gera, Mbenjamini, kutoka Bahurimu, akaharakisha kushuka pamoja na watu wa Yuda ili kumlaki mfalme Daudi.
\v 17 Kulikuwa na watu elfu moja kutoka Benjamini waliokuwa pamoja naye, na Siba mtumishi wa Sauli na wanawe kumi na watano na watumish wake ishirini walikuwa pamoja naye. Wakavuka Yordani mbele za mfalme.
\v 18 Wakavuka ili kuivusha familia ya mfalme na kumfanyia lolote aliloona jema. Shimei mwana wa Gera akainama chini mbele za mfalme mara alipoanza kuuvuka Yordani.
\s5
\v 19 Shimei akamwambia mfalme, "Bwana wangu asinione mwenye hatia au kuyaweka moyoni ambayo mtumishi wake alifanya kwa ukaidi siku bwana wangu mfalme alipoondoka Yerusalemu. Tafadhari, mfalme na asiyaweke moyoni.
\v 20 Kwa maana mtumishi wako anatambua kwamba amekosa. Tazama, ndiyo maana nimekuja leo wa kwanza katika nyumba ya Yusufu ili kumlaki bwana wangu mfalme."
\s5
\v 21 Lakini Abishai mwana wa Seruya akajibu na kusema, "Je Shimei asife kwa hili kwa vile alivyomlaani mtiwa mafuta wa Yahweh?"
\v 22 Ndipo Daudi akasema, "Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya, hata leo mkawa adui zangu? Je mtu yeyote atauawa leo katika Israeli? Kwani sijui kama leo mimi ni mfalme juu ya Israeli?
\v 23 Hivyo mfalme akamwambia Shimei, "Hautakufa." Mfalme akamwahidi kwa kiapo.
\s5
\v 24 Kisha Mefiboshethi mwana wa Sauli akashuka ili kumlaki mfalme. Hakuwa ameivalisha miguu yake wala kunyoa ndevu zake wala kufua nguo zake tangu siku mfalme alipoondoka hata siku aliporudi kwa amani.
\v 25 Na hivyo alipotoka Yerusalemu ili kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, "Mefiboshethi Kwa nini haukwenda pamoja nami?"
\s5
\v 26 Akajibu, "Bwana wangu mfalme mtumishi wangu alinidanganya, kwani nilisema, nitapanda juu ya punda ili niende na mfalme, kwa kuwa mtumishi wako ni mlemavu.'
\v 27 Mtumishi wangu Siba amenisemea uongo, mtumishi wako, kwa bwana wangu mfalme. Lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu. Kwa hiyo fanya lililojema machoni pako.
\v 28 Kwa maana nyumba yote ya baba yangu walikuwa maiti mbele ya bwana wangu mfalme, lakini ukamweka mtumishi wako miongoni mwao walao mezani pako. Kwa hiyo nililiye haki gani zaidi kwa mfalme?"
\s5
\v 29 "Kisha mfalme akamwambia, "Kwa nini kueleza yote zaidi? Nimekwisha amua kwamba wewe na Siba mtagawana mashamba."
\v 30 Ndipo Mefiboshethi akamjibu mfalme, "Sawa, acha achukue yote kwa vile bwana wangu mfalme amerudi salama nyumbani kwake."
\s5
\v 31 Kisha Berzilai Mgileadi akashuka kutoka Rogelimu ili avuke Yordani pamoja na mfalme, naye akamsaidia mfalme kuuvuka Yordani.
\v 32 Basi Berzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amemsaidia mfalme kwa mahitaji alipokuwako Mahanaimu kwani alikuwa na mali nyingi.
\v 33 Mfalme akamwambia Berzilai, njoo pamoja nami, nami nitaandaa kwa ajili yako huko Yerusalemu."
\s5
\v 34 Berzilai akamjibu mfalme, "Kwani kuna siku ngapi zilizosalia maishani mwangu, hata niende na mfalme huko Yerusalemu?
\v 35 Nina umri wa miaka themanini. Je naweza kutofautisha mema na mabaya? Je mtumishi wako anaweza kuonja ninachokula au kunywa? Je naweza kusikia sauti zaidi za wanaume na wanawake waimbao? Kwa nini basi mtumishi wako awe mzigo kwa bwana wangu mfalme?
\v 36 Mtumishi wako angependa tu kuvuka Yordani pamoja na mfalme. Kwa nini mfalme anilipe kwa thawabu kama hiyo?
\s5
\v 37 Tafadhari mruhusu mtumishi wako arudi nyumbani, ili kwamba nife katika mji wangu katika kaburi la baba na mama yangu. Lakini tazama, huyu hapa mtumishi wako Kimhamu. Haya yeye na avuke na bwana wangu mfalme na umfanyie lolote lipendezalo kwako."
\s5
\v 38 Mfalme akajibu, "Kimhamu atakwenda pamoja nami, nami nitamtendea kila lionekanalo jema kwako, na lolote unalotamani kutoka kwangu nitakutendea."
\v 39 Kisha watu wote wakavuka Yordani, mfalme naye akavuka, kisha mfalme akambusu Berzilai na kumbariki. Kisha Berzilai akarudi nyumbani kwake.
\s5
\v 40 Hivyo mfalme akavuka kuelekea Gilgali, na Kimhamu akavuka pamoja naye. Jeshi la Yuda lote na nusu ya jeshi la Israeli likamleta mfalme.
\v 41 Mara watu wa Israeli wote wakaanza kuja kwa mfalme na kumwambia, "Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda, wamemwiba na kumleta mfalme na familia yake juu ya Yordani na watu wote wa Daudi pamoja naye?
\s5
\v 42 Hivyo watu wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, "Ni kwa kuwa mfalme anahusiana nasi kwa karibu zaidi. Kwa nini basi mkasirike juu ya hili? Je sisi tumekula chochote ambacho mfalme amekitoa? Je ametupa zawadi yoyote?
\v 43 Watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, Sisi tuna kabila kumi zaidi kwa mfalme hivyo tuna sehemu kubwa zaidi kwa Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mlitudharau? Je hatukuwa wa kwanza kupendekeza kumrudisha mfalme wetu? Lakini maneno ya watu wa Yuda hata yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ikatukia pia kuwa katika eneo lilelile kulikuwa mfanya fujo jina lake Sheba mwana wa Bikri Mbenjamini. Akapiga tarumbeta na kusema, "Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya kila mtu na aende nyumbani kwake, Israeli."
\v 2 Hivyo watu wote wa Israeli wakamwacha Daudi na kumfuata Sheba mwana wa Bikri. Lakini watu wa Yuda wakamfuata mfalme wao kwa karibu sana, kutoka Yordani njia yote hadi Yerusalemu.
\s5
\v 3 Daudi alipofika katika kasri lake huko Yerusalemu, akawachukua masuria aliokuwa amewaacha kulitunza kasri, na akawaweka katika nyumba chini ya uangalizi. Aliwaandalia mahitaji yao lakini hakulala nao tena. Hivyo walikuwa wametengwa hadi siku ya kufa kwao, waliishi kama wajane.
\s5
\v 4 Kisha mfalme akamwambia Amasa, "Uwaite watu wa Yuda ndani ya siku hizi tatu; wewe pia uwepo hapa."
\v 5 Hivyo Amasa akaenda kuwaalika watu wote wa Yuda kwa pamoja, lakini akatumia muda mrefu kulika mfalme alivyokuwa amemwamuru.
\s5
\v 6 Hivyo Daudi akamwambia Abishai, "Sasa Sheba mwana wa Bikri atatufanyia madhara zaidi ya Absalomu. Chukua watumishi wa bwana wako, askari wangu, na umfuatie asije akaingia katika mji wenye ngome na kututoroka."
\v 7 Ndipo watu wa Yoabu wakamfuatia, pamoja na Wakerethi na Wapelethi na mashujaa wote. Wakatoka Yerusalemu ili kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.
\s5
\v 8 Walipokuwa katika jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa silaha ya vita aliyokuwa ameivaa, alikuwa pia na upanga uliokuwa umefungwa na mkanda katika kiuno chake. Kadili alivyoendelea mbele upanga ukadondoka.
\s5
\v 9 Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, "Haujambo binamu yangu?" Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu.
\v 10 Amasa hakutambua kwamba kulikuwa na jambia katika mkono wa kushoto wa Yoabu. Yoabu akamchoma Amasa tumboni na matumbo yake yakadondoka chini. Wala Yoabu hakumpiga tena, na Amasa akafa. Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
\s5
\v 11 Kisha mmoja wa watu wa Yoabu akasimama kando ya Amasa naye akasema, "Aliye upande wa Yoabu na aliyeupande wa Daudi na amfuate Yoabu."
\v 12 Amasa akawa anagalagala katika damu yake katikati ya njia. Mtu yule alipoona kwamba watu wote wamesimama, akambeba Amasa na kumweka shambani kando ya njia. Akatupa vazi juu yake kwa maana aliona kila mmoja aliyekuja alisimamaa pale.
\v 13 Baada ya Amasa kuondolewa njiani watu wote wakamfuata Yoabu katika kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.
\s5
\v 14 Sheba akazipita kabila zote za Israeli mpaka Abeli wa Beth Maaka, na katika nchi yote ya Berite ambao pia walijikusanya pamoja pia na kumfuatia Sheba.
\v 15 Walimpata na kumzingira huko Abeli wa Bethi Maaka. Wakajenga buruji ya kuhusuru mji nyuma ya ukuta. Jeshi lote lilokuwa pamoja na Yoabu likaugongagonga ukuta ili uanguke.
\v 16 Ndipo mwanamke mwerevu akapiga kelele kutoka ndani ya mji, "Sikiliza, Yoabu, tafadhari sikiliza! Sogea karibu nami ili niongee nawe."
\s5
\v 17 Hivyo Yoabu akakaribia, mwanamke akamwambia, "Je wewe ni Yoabu? Akajibu, "ni mimi." mwanamke akamwambia, "Sikiliza maneno ya mtumishi wako." Akajibu, "Nasikiliza."
\v 18 Ndipo aliposema,"Hapo zamani ilisemwa, 'Bila shaka tafuteni ushauri huko Abeli,' na kwamba ushauri huo utakata maneno.
\v 19 Sisi ni mji ulio miongoni mwa miji yenye nguvu na aminifu sana katika Israeli. Mnataka kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kuumeza urithi wa Yahwe?"
\s5
\v 20 Ndipo Yoabu alipojibu na kusema, "Iwe mbali, iwe mbali nami, hata nikameze au kuharibu.
\v 21 Hiyo si kweli. Lakini mtu kutoka katika nchi ya milima ya Efraimu, aitwaye Sheba mwana wa Bikri, ameinua mkono wake kinyume cha mfalme, kinyume cha Daudi. Mtoeni yeye nami nitauacha mji." Mwanamke akamwambia Yoabu, "Utarushiwa kichwa chake kutoka juu ya ukuta."
\v 22 Kisha mwanamke akawaendea watu wote wa mji kwa hekima yake. Wakakiondoa kichwa cha Sheba mwana wa Bikri na kumrushia Yoabu. Ndipo alipopiga tarumbeta na watu wa Yoabu wakauacha mji kila mtu nyumbani kwake. Na Yoabu akarejea Yerusalemu kwa mfalme.
\s5
\v 23 Yoabu alikuwa juu ya jeshi lote la Israeli na Benaya mwana wa Yehoiada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi.
\v 24 Adoramu alikuwa juu ya watu waliofanya kazi ya shokoa na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mkumbushaji.
\v 25 Sheva alikuwa mwandishi, na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani.
\v 26 Ira wa Yairi alikuwa mhudumu mkuu wa Daudi.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu katika siku za utawala wa Daudi, na Daudi akautafuta uso wa Yahwe. "Hivyo Yahwe akasema, "njaa hii ni kwa sababu ya mauaji ya Sauli na familia yake, kwa kuwa aliwauwa Wagibeoni."
\s5
\v 2 Basi Wagibeoni hawakuwa uzao wa Israeli; walikuwa ni masalia ya Waamori. Watu wa Israeli walikuwa wameapa kutowauwa, lakini Sauli alitaka kuwaangamiza wote kwa husuda kwa ajili ya watu wa Israeli na Yuda.
\v 3 Ndipo Daudi alipowaita pamoja Wagibeoni na kuwaambia, "Niwafanyie nini kwa ajili ya upatanisho? Ili kwamba mweze kuwabariki watu wa Yahwe wanaorithi wema na ahadi zake?"
\s5
\v 4 Wagibeoni wakamjibu, "Hili siyo jambo la fedha wala dhahabu kati yatu na Sauli au familia yake. Na siyo hitaji letu kumwua mtu yeyote katika Israeli." Daudi akasema, "Chochote mtakacho omba nitawafanyia."
\s5
\v 5 Wakamjibu mfalme, "Mtu aliyetaka kutuuwa aliyepanga kunyume chetu, ili kutuangamiza na kukosa eneo katika mipaka ya Israeli -
\v 6 haya na tupewe watu saba kutoka katika uzao wake, nasi tutawatundika mbele ya Yahwe katika Gibea ya Sauli, palipochaguliwa na Yahwe." Mfalme akasema, "Nitawapeni"
\s5
\v 7 Lakini mfalme akamwifadhi Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Yahwe kati ya Daudi na Yonathani mwana wa Sauli.
\v 8 Mfalme akawachukua wana wawili wa Rispa binti Ayia aliomzalia Sauli, hawa wana wawili waliitwa Armoni na Mefiboshethi; na pia Daudi akawachukua wana watano wa Mikali binti Sauli, aliomzalia Adrieli mwana wa Berzilai Mmeholathi.
\v 9 Akawaweka katika mikono ya Wagibeoni. Nao wakawatundika juu ya mlima mbele za Bwana, na wote saba wakafa pamoja. Waliuawa katika kipindi cha mavuno, katika siku ya kwanza mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
\s5
\v 10 Kisha Rispa, binti Aiya, akachukua nguo ya gunia na akajitanda mwenyewe juu ya mlima kando ya miili ya waliokufa tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati mvua ilipoanza kunyesha. Hakuruhusu ndege wa angani kutua juu ya miili mchana wala ayawani wa mwituni wakati wa usiku.
\v 11 Daudi akaambia alichokifanya Rispa, binti Aiya, suria wa Sauli.
\s5
\v 12 Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumwua Sauli katika Gilboa.
\v 13 Daudi akaiondoa pale mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe, na wakakusanya pia mifupa ya wale watu saba waliotundikwa.
\s5
\v 14 Wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwanawe huko Zela katika nchi ya Benjamini, katika kaburi la Kishi babaye. Wakafanya kila alichoagiza mfalme. Ndipo Mungu akajibu maombi yao kwa ajili ya nchi.
\s5
\v 15 Kisha Wafilisti wakaenda tena katika vita na Israeli. Hivyo Daudi na jeshi lake wakashuka na kupigana na Wafilisti. Akiwa vitani Daudi akachoshwa na vita.
\v 16 Ishbibenobu, wa uzao wa majitu, ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa shekeli mia tatu na alikuwa na upanga mpya, alitaka kumwua Daudi.
\v 17 Lakini Abishai mwana wa Seruya akamwokoa Daudi, akampiga Mfilisti na kumwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, kusema, "Hautakwenda vitani pamoja nasi tena usije ukaizima taa ya Israeli."
\s5
\v 18 Ikawa baadaye kuwa na vita tena kati ya Wafilisti huko Gobu, wakati Sibekai Mhushathi alipomwua Safu, aliyekuwa miongoni mwa uzao wa Warefai.
\v 19 Ikawa tena katika vita na Wafilisti huko Gobu, huyo Elhanani mwana wa Jari Mbethlehemu akamwua Goliathi Mgiti, ambaye fumo la mkuki wake lilikuwa kama mti wa mfumaji.
\s5
\v 20 Ikawa katika vita nyingine huko Gathi kulikuwa na mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Yeye naye alikuwa wa uzao wa Warefai.
\v 21 Alipowatukana Israeli, Yonathani mwana mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua.
\v 22 Hawa walikuwa wa uzao wa Warefai wa Gathi, waliuawa kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa askari wake
\s5
\c 22
\p
\v 1 Daudi akamwimbia Yahwe maneno ya wimbo huu siku ile Yahwe alipomwokoa katika mkono wa adui zake wote na katika mkono wa Sauli.
\v 2 Akaomba hivi, "Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, aliyeniokoa.
\s5
\v 3 Mungu ni mwamba wangu. Yeye ni kimbilio langu. Ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, ngome yangu na kimbilio langu, aniokoaye na mabaya yote.
\v 4 Nitamwita Yahwe, astahiliye kutukuzwa, nami nitaokolewa kutoka kwa adui zangu.
\s5
\v 5 Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maji ya uharibifu yakanishinda.
\v 6 Vifungo vya kuzimu vilinizunguka; kamba za mauti zikaninasa.
\s5
\v 7 Katika shida yangu nalimwita Yahwe; nilimwita Mungu wangu; akaisikia sauti yangu katika hekalu lake, na kilio changu cha msaada kikafika masikioni mwake.
\s5
\v 8 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka. Misingi ya mbingu ikatetemeka na kutikiswa, kwa kuwa Mungu alikasirika.
\v 9 Moshi ukatoka katika pua yake, na miale ya moto ikatoka katika kinywa chake. Makaa yakawashwa nayo.
\s5
\v 10 Alizifungua mbingu akashuka, na giza totoro lilikuwa chini ya miguu yake.
\v 11 Alipanda juu ya kerubi na kuruka. Alionekana katika mawingu ya upepo.
\v 12 Naye akalifanya giza kuwa hema kumzunguka, akakusanya mawingu makubwa ya mvua angani.
\s5
\v 13 Makaa ya moto yalidondoka mbele zake kutoka katika radi.
\v 14 Yahwe alishuka kutoka katika mbingu. Aliyejuu alipiga kelele.
\v 15 Alipiga mishale na kuwatawanya adui zake--miale ya radi na kuwasambaratisha.
\s5
\v 16 Kisha njia za maji zikaonekana; misingi ya dunia ikawa wazi katika kilio cha vita ya Yahweh, katika sauti za pumzi ya pua zake.
\s5
\v 17 Kutoka juu alifika chini; akanishikilia! Aliniondoa katika vilindi vya maji.
\v 18 Aliniokoa kutoka kwa adui zangu wenye nguvu, kwao walionichukia, kwa maana walikuwa na nguvu sana kwangu.
\s5
\v 19 Walikuja kinyume changu siku ya shida yangu, lakini Yahwe alikuwa msaada wangu.
\v 20 Pia aliniweka mahali panapo nafasi. Aliniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
\v 21 Yahwe amenituza kwa kipimo cha haki yangu; amenirejesha kwa kiwango cha usafi wa mikono yangu.
\s5
\v 22 Kwa maana nimezishika njia za Yahwe na sijafanya uovu kwa kugeuka kutoka kwa Mungu.
\v 23 Kwa kuwa maagizo yake yote ya haki yamekuwa mbele yangu; kwa kuwa sheria zake, sikujiepusha nazo.
\s5
\v 24 Nimekuwa bila hatia mbele zake pia, na nimejiepusha na dhambi.
\v 25 Kwa hiyo Yahwe amenirejesha kwa kiasi cha uadilifu wangu, kwa kipimo cha usafi wangu mbele zake.
\s5
\v 26 Kwa mwaminifu, unajionesha kuwa mwaminifu; kwake asiye na hatia; unajionesha kuwa hauna hatia.
\v 27 Kwa usafi unajionesha kuwa msafi, lakini kwa wakaidi unajionesha kuwa mkaidi.
\s5
\v 28 Unaokoa walioteswa, lakini macho yako ni kinyume cha wenye kiburi, unawashusha chini.
\v 29 Kwa maana wewe ni taa yangu, Yahwe. Yahwe huangaza katika giza langu.
\s5
\v 30 Maana kwa ajili yake ninaweza kupita vipingamizi; kwa msaada wa Mungu wangu naweza kuruka juu ya ukuta.
\v 31 Maana njia za Mungu ni kamilifu. Neno la Yahwe ni safi. Yeye ni ngao yao wanaomkimbilia.
\s5
\v 32 Maana ni nani aliye Mungu isipokuwa Yahwe? Na ni nani aliyemwamba isipokuwa Mungu?
\v 33 Mungu ni kimbilio langu, na umwongoza katika njia yake mtu asiye na hatia.
\s5
\v 34 Huifanya myepesi miguu yangu kama kurungu na kuniweka katika vilima virefu.
\v 35 Huifundisha mikono yangu kwa vita, na viganja vyangu kupinda upinde wa shaba.
\s5
\v 36 Umenipa ngao ya wokovu wako, na matakwa yako yamenifanya mkuu.
\v 37 Umeitengenezea miguu yangu nafasi chini yangu, hivyo miguu yangu haikujikwaa.
\s5
\v 38 Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza. Sikurudi nyuma hadi walipoangamizwa.
\v 39 Niliwararua na kuwasambaratisha; hawawezi kuinuka. Wameanguka chini ya miguu yangu.
\s5
\v 40 Unaweka nguvu ndani yangu kama mkanda kwa vita; unawaweka chini yangu wanaoinuka kinyume changu.
\v 41 Ulinipa migongo ya shingo za adui zangu; niliwaangamiza kabisa wale wanaonichukia.
\s5
\v 42 Walilia kwa msaada, lakini hakuna aliyewaokoa; walimlilia Yahwe, lakini hakuwajibu.
\v 43 Niliwaponda katika vipande kama mavumbi juu ya ardhi, niliwakanyaga kama matope mitaani.
\s5
\v 44 Umeniokoa pia kutoka katika mashutumu ya watu wangu. Umeniweka kama kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua wananitumikia.
\v 45 Wageni walishurutishwa kuniinamia. Mara waliposikia kuhusu mimi, walinitii.
\v 46 Wageni walikuja wakitetemeka kutoka katika ngome zao.
\s5
\v 47 Yahwe anaishi! Mwamba wangu atukuzwe. Mungu na ainuliwe, mwamba wa wokovu wangu.
\v 48 Huyu ndiye Mungu anilipiaye kisasi, awawekaye watu chini yangu.
\v 49 Uniweka huru mbali na adui zangu. Hakika, uliniinua juu yao walioinuka kinyume changu. Uliniokoa kutoka kwa watu wenye ghasia.
\s5
\v 50 Kwa hiyo nitakushukuru, Yahwe, kati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.
\v 51 Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na uonesha uaminifu wake wa kiagano kwa mtiwa mafuta wake, kwa Daudi na uzao wake daima."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi-Daudi mwana wa Yese, mtu aliyeheshimiwa sana, aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo, mwandishi mzuri wa zaburi wa Israeli.
\v 2 "Roho ya Yahwe alisema nami, na neno lake lilikuwa ulimini mwangu.
\s5
\v 3 Mungu wa Israeli alinena, Mwamba wa Israeli aliniambia, "Atawalaye kwa haki juu yangu, atawalaye katika hofu ya Mungu.
\v 4 Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua linapochomoza, asubuhi isiyo na mawingu, wakati mche mwororo unapochipua kutoka ardhini kupitia mwangaza wa mng'ao wa jua baada ya mvua.
\s5
\v 5 Hakika, je familia yangu haiko hivi mbele za Mungu? Je hajafanya nami agano la milele, taratibu la uhakika kwa kila njia? Je yeye haongezi wokovu wangu na kutimiza kila hitaji langu?
\s5
\v 6 Lakini yasiyofaa yote yatakuwa kama miiba na kutupwa mbali, kwa maana haiwezekani kukusanywa kwa mikono.
\v 7 Ayagusaye ni lazima atumie chombo cha chuma au au fumo la mkuki. Ni lazima yachomwe mahali yalipo.
\s5
\v 8 Haya ni majina ya askari wa Daudi: Yashobeamu Mhakmoni alikuwa kiongozi wa mashujaa. Aliua watu mia nne wakati mmoja.
\s5
\v 9 Baada yake alikuwa Elieza mwana wa Dodo, mwana wa mwahohi, mmoja wa mashujaa watatu wa Daudi. Alikuwepo walipowashinda Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kwa vita, na wakati watu wa Israeli walipokuwa wamekimbia.
\v 10 Elieza akasimama na kuwapiga Wafilisti mpaka mkono wake ukachoka, mpaka mkono wake ukang'ang'ania mpini wa upanga wake. Siku hiyo Yahwe akatoa ushindi mkuu. Jeshi likarejea kwa ajili ya kuteka tu nyara za waliouawa na Elieza.
\s5
\v 11 Baada yake alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti wakajikusanya pamoja palipokuwa na shamba la dengu, na jeshi likawakimbia.
\v 12 Lakini Shama akasimama katikati ya shamba na kulitetea. Aliwauwa Wafilisti, na Yahwe akaleta ushindi mkuu.
\s5
\v 13 Watatu kati ya askari thelathini walishuka kwa Daudi nyakati za mavuno, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Mrefai.
\v 14 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, wakati Wafilisti walikuwa wanaimilk Bethlehemu.
\s5
\v 15 Daudi alitamani maji na akasema, "Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!"
\v 16 Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe.
\v 17 Kisha akasema, "Iwe mbali nami, Yahwe, kwamba niyanywe haya. Je ninywe damu ya watu waliohatarisha maisha yao?" Hivyo akakataa kuyanywa. Haya ni mambo yaliyofanywa na mashujaa watatu.
\s5
\v 18 Abishai, nduguye Yoabu na mwana wa Seruya, alikuwa akida wa watatu. Alipigana kwa mkuki wake na watu mia tatu na akawauwa wote mara. Mara kwa mara alitajwa kati ya mashujaa watatu.
\v 19 Hakuwa maarufu kuliko wale watatu? Alifanywa akida wao. Lakini, umaarufu wake haukulingana na umaarufu wa wale mashujaa watatu.
\s5
\v 20 Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.
\v 21 Na alimwua Mmisri aliyekuwa mtu mnene sana. Mmisri alikuwa na mkuki mkononi, lakini Benaya alipigana naye kwa fimbo tu. Aliuchukua mkuki mkononi mwa Mmisri na kisha kumwua nao.
\s5
\v 22 Benaya mwana wa Yehoyada alifanya matendo haya, naye alitajwa kati ya mashujaa watatu.
\v 23 Alikuwa na heshima kuliko mashujaa thelathini kwa ujumla wao, lakini hakuwa na heshima kama wale mashujaa watatu. Hata hivyo Daudi alimweka kuwa mlinzi wake.
\s5
\v 24 Wafuatao ni wale watu thelathini: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
\v 25 Shama Mharodi, Elika Mharodi,
\v 26 Helesi Mpeloni, Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi,
\v 27 Abi Ezeri Mwanathothi, Mebunai Mhushathi,
\v 28 Salmoni Mhahoi, Maharai Mnetofathi;
\s5
\v 29 Helebu mwana wa Baana, Mnetofathi, Itai mwana wa Rabai kutoka Gibea ya Wabenjamini,
\v 30 Benaya Mpirathoni, Hidai wa mabonde ya Gaashi.
\v 31 Abieliboni Mwarbathi, Azmawethi Mbarhumi,
\v 32 Eliaba Mshalboni, wana wa Yasheni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;
\s5
\v 33 Ahiamu mwana wa Sharari Mharari,
\v 34 Elifeleti mwana wa Ahasbai Mmaakathi, Eliamu mwana wa Ahithofeli Mgiloni,
\v 35 Hezro Mkarmeli, Parai Mwarbi,
\v 36 Igali mwana wa Nathani kutoka Soba, Bani kutoka kabila la Gadi,
\s5
\v 37 Zeleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,
\v 38 Ira Mwithri, Garebu Mwithri,
\v 39 Uria Mhiti - jumla yao thelathini na wanane.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Kisha hasira ya Yahwe ikawaka dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi kinyume chao kusema, "Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda."
\v 2 Mfalme akamwambia Yoabu, jemedari wa jeshi, aliyekuwa pamoja naye, "Nenda upite katika kabila zote za Israeli, toka Dani mpaka Beersheba, uwahesabu watu wote, ili niweze kujua idadi kamili ya watu wanaofaa kwa vita."
\s5
\v 3 Yoabu akamwambia mfalme, "Yahwe Mungu wako na aizidishe hesabu ya watu mara mia, na macho ya bwana wangu mfalme yaone ikifanyika. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme analitaka jambo hili?
\v 4 Walakini neno la mfalme lilikuwa la mwisho dhidi ya Yoabu na dhidhi ya majemedari wa jeshi. Hivyo Yoabu na majemedari wakatoka mbele ya mfalme kuwahesabu watu wa Israeli.
\s5
\v 5 Wakavuka Yordani na kupiga kambi karibu na Aroeri, kusini mwa mji bondeni. Kisha wakasafiri kupitia Gadi mpaka Yazeri.
\v 6 Wakaja Gileadi na nchi ya Tahtimu Hodshi, kisha Dani, Jaani na karibu kuelekea Sidoni.
\v 7 Wakafika ngome ya Tiro na miji yote ya Wahivi na Wakanaani. Kisha wakaenda Negebu katika Yuda huko Beersheba.
\s5
\v 8 Walipokuwa wamepita katika nchi yote, wakarejea Yerusalemu mwishoni mwa miezi tisa na siku ishirini.
\v 9 Ndipo Yoabu alipotoa taarifa ya hesabu kamili kwa mfalme kuhusu watu wawezao kupigana vita. Katika Israeli kulikuwa na watu 800, 000 jasiri wawezao kutoa upanga, na wale wa Yuda walikuwa watu 500, 000.
\s5
\v 10 Ndipo moyo wa Daudi ukamchoma alipokuwa amewahesabu watu. Hivyo akamwambia Yahwe, "Kwa kufanya hivi nimetenda dhambi sana. Sasa, Yahwe, uiondoe hatia ya mtumishi wako, kwani nimetenda kwa upumbavu."
\s5
\v 11 Daudi alipoinuka asubuhi, neno la Yahwe likamjia nabii Gadi, mwonaji wa Daudi, kusema,
\v 12 Nenda umwambie Daudi; 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: "Ninakupa mambo matatu. Uchague mojawapo."
\s5
\v 13 Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, "Je miaka mitatu ya njaa ije katika nchi yako? au miezi mitatu ukimbie kutoka kwa adui zako huku wakikufuatia? au kuwe na tauni ya siku tatu katika nchi yako? Amua sasa jibu gani nimrudishie aliyenituma."
\v 14 Ndipo Daudi alipomwambia Gadi, "Nipo katika shida kubwa. Haya na tuanguke katika mikono ya Yahwe kuliko kuanguka katika mikono ya mwanadamu, kwani matendo yake ya rehema ni makuu sana."
\s5
\v 15 Hivyo akatuma tauni juu ya Israeli kuanzia asubuhi kwa muda ulioamriwa, na watu sabini na tano elfu kutoka Dani mpaka Beersheba wakafa.
\v 16 Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu, Yahwe akabadili nia yake kuhusu madhara, na akamwambia malaika aliyekuwa tiyari kuwaangamiza watu, "Yatosha! Rudisha mkono wako sasa." Wakati huo malaika wa Yahwe alikuwa amesimama katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.
\s5
\v 17 Daudi alipomwona malaika aliyekuwa amewapiga watu, akamwambia Yahwe kusema, "Nimetenda dhambi, na nimetenda kwa upumbavu. Lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Tafadhari, mkono wako na uniadhibu mimi na familia ya baba yangu!"
\s5
\v 18 Kisha Gadi akaja siku hiyo kwa Daudi na kumwambia, "Kwea na ujenge madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi."
\v 19 Hivyo Daudi akakwea kama Gadi alivyomwelekeza kufanya, kama Yahwe alivyokuwa ameagiza.
\v 20 Arauna akatazama na kumwona mfalme na watumishi wake wakikaribia. Ndipo Arauna akaondoka na kumsujudia mfalme uso wake mpaka juu ya ardhi.
\s5
\v 21 Kisha Arauna akasema, "Kwa nini bwana wangu mfalme amekuja kwangu, mtumishi wake? Daudi akajibu, "Kununua uwanja wako wa kupuria, ili nimjengee Yahwe madhabahu, ili kwamba tauni iondolewe kwa watu."
\v 22 Arauna akamwambia Daudi, "Chukua liwe lako, bwana wangu mfalme. Ulifanyie lolote lolote lililojema machoni pako. Tazama, ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na miganda ya kupuria na nira kwa kuni.
\v 23 Haya yote bwana wangu mfalme, mimi Arauna nakupa." Kisha akamwambia mfalme, "Yahwe Mungu wako na awe nawe."
\s5
\v 24 Mfalme akamwambia Arauna, "Hapana, nahimiza kukinunua kwa thamani yake. Sitatoa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe chochote nisichokigharimia." Hivyo Daudi akakinunua kiwanja cha kupuria na ng'ombe kwa shekeli hamsini za fedha.
\v 25 Daudi akajenga madhabahu kwa Yahwe pale na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Hivyo wakamsihi Yahwe kwa niaba ya nchi, hivyo akaizuia tauni katika katika Israeli yote.

1583
11-1KI.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1583 @@
\id 1KI
\ide UTF-8
\h 1Wafalme
\toc1 1Wafalme
\toc2 1Wafalme
\toc3 1ki
\mt 1Wafalme
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mfalme Daudi alipokuwa mzee sana, walimfunika kwa nguo, lakini hakupata joto.
\v 2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, "Na tutafute msichana bikra kwa ajili ya mfalme bwana wetu. Ili amtumikie na kumtunza. Naye atalala kwenye mikono yake ili bwana mfalme wetu apate joto.
\s5
\v 3 Kwa hiyo wakatafuta msichana mrembo katika mipaka yote ya Israeli. Wakampata Abishagi Mshunami wakamlte kwa mfalme.
\v 4 Yule msichana alikuwa mrembo sana. Naye akamtumikia mfalme na kumtunza, Lakini mfalme hakumjua.
\s5
\v 5 Wakati huo, Adoniya mwana wa Hagithi alijiinua akisema, "Nitakuwa mfalme." Kwa hiyo akajiandalia magari na wapanda farasi hamsini ili wapige mbio mbele yake.
\v 6 Baba yake alikuwa hajawahi kumsumbua, kwa kusema, "kwa nini umefanya hili na lile?" Adoniya allikuwa mwanamume mzuri sana aliyezaliwa baada ya Absalomu.
\s5
\v 7 Akashauriana na Yoabu mwana wa Seruya na Abiathari kuhani. Wakamfuata Adoniya wakamsaidia.
\v 8 Lakini Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Nathani, Shimei, Rei, na watu mashujaa wa Daudi hawakumfuata Adoniya.
\s5
\v 9 Adoniya akataoa dhabihu za Kondoo, na ndama walionona kwenye jiwe la Sohelethi, ambalo liko karibu na Eni Rogeli. Akawakaribisha ndugu zake wote, watoto wa mfalme, wanaume wote wa Yuda, na watumishi wa mfalme.
\v 10 Lakini hakumkaribisha nabii Nathan, Benaya, wanaume mashujaa, au ndugu yake Sulemani.
\s5
\v 11 Kisha Nathani akamwambia Bethisheba mama wa Sulemani, akaisema, "Je, haujasikia kuwa Adoniya mwana wa Hagathi amekuwa mfalme, na Daudi bwana wetu halijui hilo?
\v 12 Kwa hiyo sasa nakupa ushauri, ili kwamba uweze kuokoa maisha yako na maisha ya mwanao Suleimani.
\s5
\v 13 Nenda kwa mfalme Daudi; ukamwambie, 'Bwana wangu mfalme, Je, haukumwapia mtumishi wako, ukisema, "Hakika Sulemani mwanao atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?" Kwa nini basi Adoniya anatawala?'
\v 14 Wakati ukiwa pale ukiongea na mfalme, Nitaingia baada yako na kuthibitisha hayo.
\s5
\v 15 Kwa hiyo Bathisheba akaingia chumbani kwa mfalme. Wakati huo mfalme alikuwa mzee sana, na Abishagi Mshunami alikuwa akimtunza mfalme.
\v 16 Bathisheba akaiinama kifudifudi mbele ya mfalme. Na kisha mfalme akasema, "Una haja gani?"
\v 17 Naye akamwambia, "Bwana wangu, ulimwapia mtumishi wako kwa jina la BWANA, Mungu wako, ukisema, 'Hakika Sulemani mwanao atatawala, baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha enzi.'
\s5
\v 18 Sasa, tazama, Adoniya ni mfalme, na bwana wangu mfalme hajui jambo hili.
\v 19 Ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, Abiathari kuhani, na Yoabu jemedari wa jeshi, lakini hajamkaribisha Sulemani mtumishi wako.
\s5
\v 20 Mfalme bwana wangu, macho yote ya Israeli yako kwako, yakisubiri usemi wako juu ya nani atakayeti kwenye kiti cha enzi baada yako, bwana wangu.
\v 21 Vinginevyo itatokea, wakati bwana wangu atakapolala na baba zake, kwamba Mimi na mwanangu Sulemani kuhesabiwa wahaini."
\s5
\v 22 Wakati alipokuwa akiendelea na mfalme, nabii Nathani aliingia.
\v 23 Watumshi wakamwambia mfalme, "Nabii Nathani yuko hapa," Naye alipoingia mbele ya mfalme, akalala kifudifudi mbele ya mfalme na uso wake ukielekea chini.
\s5
\v 24 Nathani akamwambia, "Mfalme bwana wangu, Je, umesema, Adoniya atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?
\v 25 kwani leo ameshuka na ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, jemedari wa jeshi, na Abiatahari kuhani. Nao wanakuka na kunywa mbele zake, na kusema, 'Mfalme Adoniya na aishi milele!'
\s5
\v 26 Lakini mimi, mtumishi wako, Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, na mtumishi wako Suleimani, hajatukaribisha.
\v 27 Je, bwana wangu mfalme amefanya haya pasipo kutuambia sisi, watumishi wako, ni nani atakayeketi kwenye kiti cha enzi baada yake?"
\s5
\v 28 Ndipo mfalme Daudi lipojibu na kusema, "Mwiteni Bathisheba arudi." Naye akaja akasimama mbele ya mfalme.
\v 29 Mfalme akafanya kiapo akasema, "Kama BWANA aishivyo, ambaye ameniokoa toka tabu zote,
\v 30 kama nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikisema, 'Sulemani mwanao atatawala baada yangu, naye ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha enzi, mahali pangu,' Nitafanya hivi leo."
\v 31 Kisha Bathisheba akalala kifudifudi na sura yake ikielekea chini mbele ya mfalme akasema, "Bwana wangu mfalme Daudi n a aishi milele!"
\s5
\v 32 Mflme Daudi akasema, "Niitieni Sadoki kuhani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada." Nao wakaja mbele ya mfalme.
\v 33 Mfalme akawaambia, "Uwachukue watumishi wangu, bwana wako, na umfanye Sulemani mwanangu apande juu ya nyumba yangu mimi na mkamtelemshe mpaka chini Gihoni.
\v 34 Na Sadoki kuhani na nabii Nathani wamtawaze awe mfalme wa Israeli na tarumbeta zipigwe, 'Mfalme Suleimani na uishi milele!'
\s5
\v 35 Kisha njoni mkiwa nyuma yake, naye atakuja na kukaa kwenye kiti changu cha enzi; kwani yeye ndiye atakayekuwa mfalme mahali pangu. Nimemchagua yeye kuwa mtawala wa Israeli na Yuda."
\v 36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, akasema, "Na iwe hivyo! Na BWANA, Mungu wa mfalme bwana wangu, alithibitishe hilo.
\v 37 Kama vile BWANA alivyokuwa na mfalme bwana wangu na awe na Sulemani hivyo hivyo, na kuifanya enzi yake kuwa kubwa kuliko zaidi ya enzi ya bwana wangu Daudi."
\s5
\v 38 Kwa hiyo Sadoki kuhani, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi na Wapelethi wakamfanya Sulemani akapanda juu ya nyumba ya mfalme Daudi; wakamleta Gihoni.
\v 39 Naye Sadoki kuhani akachukua pembe lenye mafuta hemani akamtia mafuta Sulemani kisha wakapiga tarumbeta, na watu wote wakasema, 'Mfalme Sulemani na aishi milele!'
\v 40 Kisha watu wote wakamfuata, na watu wakapiga zomari wakafurahi furaha kubwa mno, kiasi kwamba dunia ikatetemeka kwa sauti zao.
\s5
\v 41 Kisha Adoniya na wageni wake waliokuwa pamoja naye wakasikia hayo walipomaliza kula. Yoabu alipozisikia sauti za panda, akasema, "Kwa nini jiji lilko katika hali ya taharuki?"
\v 42 Wakati alipokuwa akiongea, Yonatahani mwana wa Abiathari kuhani alifika. Adoniya akamwambia, "Karibu, 'kwa kuwa wewe wastahili kutuletea habari."
\s5
\v 43 Naye Yonathani akamjibu Adoniya, "Mfalme bwana wetu Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme.
\v 44 Na mfalme amemtuma pamoja naye Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi pamoja na Wapelethi. Wamempandisha Sulemani juu ya nyumba ya mfalme.
\v 45 Sadoki kuhani na nabii Nathani wamemtawaza kuwa mfalme kule Gihoni, na wametokea huko wakifurahi, ndiyo maana jiji liko katika taharuki. Na hizi ndizo sauti ulizosikia.
\s5
\v 46 Pia, Sulemani ameketi kwenye kiti cha enzi cha ufalme.
\v 47 Zaidi ya yote, watumishi wa mfalme walikuja kumbariki mfalme bwana wetu Daudi, wakisema, 'Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa zuri kuliko jina lako, na kuifanya enzi yako kuwa kubwa kuliko yako.' na mfalme akasujudu mwenyewe kitandani.
\v 48 Mfalme pia alisema, 'Abarikiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amempa mtu kuketi kwenye enzi yangu siku hii ya leo, na kwamba macho yangu yamejionea hilo.'"
\s5
\v 49 Ndipo wageni wote wa Adoniya walipoogopa sana. Wakasimama na kila mtu akaenda njia yake.
\v 50 Pia Adoniya alimwaogopa Sulemani na akasimama, na akaondoka, akachukua pembe la madhabahuni.
\v 51 Kisha Sulemani akaambiwa hilo, wakasema, "Tazama, Adoniya amemwogopa mfalme Sulemani, kwa kuwa ameshikilia pembe la madhabahuni, akisema, 'Mfalme Sulemani na aniapie kwanza kuwa hatamwua mtumishi wake kwa upanga.'"
\s5
\v 52 Sulemani akasema, "Kama atajionyesha kuwa ni mtu wa kweli, hakuna hata unywele mmoja utakaoanguka duniani, bali kama uovu utaonekana kwake, atakufa."
\v 53 Kwa hiyo mfalme Sulemani akatuma watu, waliomleta Adoniya kutoka madhabahuni. Naye akaja akapiga magoti kwa Sulemani, na Sulemani akamwambia, "Nenda nyumbani kwako."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema,
\v 2 "Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amari zake,
\v 3 maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwamngalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa,
\v 4 na BWANA atayatimiza maneno yake aliyosema kuhusu mimi, aliposema, 'kama wanao watajilinda katika tabia zao, wakatembea mbele yangu kwa uaminifu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, hawatakoma kuwa na mtu aliyeketi katika kiti cha enzi cha Israeli.
\s5
\v 5 Wewe pia wajua kile Yoabu mwana wa Seruya alichonifanyia, na kile alichowafnyia majemedari wa majeshi y a Israeli, kwa Abina mwana wa Neri, na kwa Amasa mwana wa Yetheri, ambaye alimwua. Alimwaga damu vitani wakati wa amani na kuiweka ile damu kwenye mshipi uliokuwa kiunoni mwake na kwenye vile viatu miguuni mwake.
\v 6 Mshughulikie Yoabu kwa hekima ambayo umejifunza, lakini usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani.
\s5
\v 7 Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.
\s5
\v 8 Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, 'Sitawaua kwa upanga,'
\v 9 Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu. Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini."
\s5
\v 10 Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.
\v 11 Siku ambazo Daudi alitwala Israeli zilikuwani miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.
\v 12 Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.
\s5
\v 13 Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathisheba mama wa Sulemani., Naye akamwuliza, "Je, unakuja kwa amani?" Naye akajiibu. "kwa amani."
\v 14 Kisha akasema, "Nina jambo la kukuambia." Naye akajibu, "Sema."
\v 15 Adoniya amesema, "Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.
\s5
\v 16 Sasa nina ombi moja kwako. Usinikatalie."Bathisheba akamwambia, "Sema."
\v 17 Naye akamwambia, "Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu."
\v 18 Bathisheba akamwambia, "Vyema sana, nitamwambia mfalme"
\s5
\v 19 Kwa hiyo Bathisheba akaenda kumwambia, mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akaa mkono wa kuume wa mfalme.
\v 20 Ndipo alipomwambia, "Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie." Mfalme, akamjibu, "Mama omba kwa kuwa sitakukatalia."
\v 21 Naya akamwambia, "Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake."
\s5
\v 22 Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, "Kwa nini unamwombea Adoniya huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? - au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?"
\v 23 Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, "Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adoniya hajayasema haya kinyume na maisha yake.
\s5
\v 24 Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo."
\v 25 Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.
\s5
\v 26 Kisha akamwambia Abiathari kuhani, "Nenda kwa Anathothi, kwenye mashamba yako. unastahili kufa, lakini sitakua sasa hivi, kwa sababu ulilbeba sanduku la BWANA mbele ya Daudi baba yangu na kujitabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata tabu."
\v 27 Kwa hiyo Sulemani akamfukuza Abiathari asiwe kuhani wa BWANA, ili kwamba atimilize maneno ya BWANA, aliyokuwa amesema juu ya nyumba ya Eli.
\s5
\v 28 Habari hizo zikamfikia Yoabu, Kwani Yoabu alimuunga mkono Adoniya, ingawa hakumuunga mkono Absalomu. Kwa hiyo Yoabu akakimbilia kwenye hema ya BWANA karibu na madhabahu na akabeba pembe za madhabahu.
\v 29 Sulemani alipoambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema ya BWANA na sasa alikuwa karibu na madhabahu. Ndipo Sulemani alipomtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, "Nenda, ukamwue."
\s5
\v 30 Kwa hiyo Benaya akaenda kwenye hema ya BWANA na kumwambia, "Mfalme anasema utoke hemani." Yoabu akamjibu, "Hapana, Nitafia hapa," Kwa hiyo Benaya akarudi kwa mfalme, akasema, "Yoabu amesema atafia kwenye madhabahu,"
\v 31 Naye mfalme akamwambia, "Kafanye kama alivyosema. Muue na ukamzike, ili kwamba uitoe kwangu na kwenye nyumba ya baba yangu damu ambayo Yoabu alimwaga bila sababu.
\s5
\v 32 BWANA na amrudishie damu yake kichwani kwake, kwa sababu aliwaua wanaume wawili wasio na hatia na wema kuliko yeye na akawaua kwa upanga, Abineri mwana wa Neri, Jemedari wa Jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Jetheri, jemedari wa jeshi la Yuda, bila baba yangu Daudi kujua.
\v 33 Kwa hiyo damu yao na imrudie Yoabu kichwani pake na kwenye vichwa vya uzao wake milele na milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, na nyumba yake, na kwenye kiti chake cha enzi, kuwe na amani ya kudumu kutoka kwa BWANA."
\s5
\v 34 Kisha Benaya mwana wa Yehoyada akaenda akamvamia Yoabu na kumwua. Alizikwa kwenye nyumba yake kule jangwani.
\v 35 Mfalme akamwinua Benaya mwana wa Yehoyada kuwa juu ya jeshi badala yake, na akamweka Sadoki kuhani kwenye nafasi ya Abiatahari.
\s5
\v 36 Kisha Mfalme akatuma watu kumwita Shimei, na akamwambia, "Kajijengee nyumba kwa ajili yako kule Yerusalemu na ushi huko, na usitoke nje ya Huo mji na kwenda mahali pengine.
\v 37 Kwa kuwa siku utakayoenda mahali pengine, na kupita bonde la Kidroni, ujue kwa hakika kuwa utakufa. Damu yako itakuwa juu ya kichwa chako."
\v 38 Kwa hiyo Shimei akamwambia mfalme, "Unachosema ni chema. Kama vike mfalme bwana wangu alivyosema, ndivyo ambavyo mtumishi wako atakavyofanya." Kwa hiyo Shimei akaishi Yerusalemu kwa miaka mingi.
\s5
\v 39 Lakiini mwishoni mwa mwaka wa tatu, watumishi wawili wa Shimei wakakimbilia kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Kwa hiyo wakamwambia Shimei, wakisema, "Tazama, watumishi wako wameenda Gathi,"
\v 40 Kisha Shimei akainuka, akapanda punda wake akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumishi wake. Akaenda na akawaleta watumishi wake toka Gathi.
\s5
\v 41 Sulemani alipoambiwa kuwa Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi na amerudi,
\v 42 mfalme akatuma wito kwa Shimei na kumwambia, "Je, sikukuapisha kwa BWANA na kushuhudia kwako, nikisema, 'Tambua kuwa siku utakayotoka kwenda nje na kwenda mahali popote, hakika utakufa'? Na ukaniambia kuwa unachosema ni chema.'
\s5
\v 43 Kwa nini basi umeshindwa kulinda kiapo chako kwa BWANA na amri niliyokupa?"
\v 44 Pia mfalme akamwambia Shimei, "Unajua katika moyo wako maovu yote uliyofanya kwa baba yangu Daudi. Kwa hiyo BWANA atakurudishia maovu yako kichwani pako.
\s5
\v 45 Lakini Sulemani atabarikiwa na enzi ya Daudi itaimarika mbele ya BWANA milele."
\v 46 Kwa hiyo mfalme akamwamuru Benaya mwana wa Yehoyada kwenda kumwua Shimei. Kwa hiyo ule utawala ulikuwa mwema kwa mkono wa Sulemain.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sulemani akawa na ushirikiano wa kindoa na Farao mfalme wa Misri. Alimwoa binti wa Farao na kumleta katika mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga nyumba yake, nyumba ya BWANA, na ukuta wa Yerusalemu.
\v 2 Watu walikuw wakitoa sadaka kwenye maeneo ya juu, kwa sababu hapakuwa bado na nyumba iliyokuwa imejengwa kwa jina la BWANA.
\v 3 Sulemani alionyesha upendo wake kwa BWANA kwa kutembea katika maagizo ya Daudi baba yake, isipokuwa tu alitoa dhabihu na kuchoma uvumba mahali pa juu.
\s5
\v 4 Mfalme akaenda Gibioni kutoa sadaka kule, kwa kuwa hilo ndilo lilikuwa eneo kuu la juu. Sulemani katoa sadaka maelfu katika madhabu hiyo.
\v 5 BWANA akaonekana kwa Sulemani huko Gibioni katika ndoto ya usiku; akasema, "Omba! uanataka nikupe nini?"
\s5
\v 6 Kwa hiyo Sulemani akasema, "umeonyesha uaminifu wa agano mkuu kwa mtumishi wako, Daudi baba yangu, kwa sababu alitembea mbele yako kwa ukweli na uaminifu, katika haki ya moyo na katika unyofu wa moyo. Umetunza kwa ajili yake hili agano kuu kwa uaminifu na umempa mwana wake kuketi kwenye kiti chake cha enzi leo.
\s5
\v 7 Na sasa, BWANA, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako kuwa mfalme katika nafasi ya Daudi baba yangu, japo mimi ni mtoto mdogo. Sijui namna ya kuiingia na kutoka.
\v 8 Mtumishi wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, kundi kubwa, watu wangi wasiohesabika.
\v 9 Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?"
\s5
\v 10 Ombi hili la Sulemani likampendeza Bwana.
\v 11 Kwa hiyo Mungu akamwambia. "Kwa sababu umeomba jambo hili na haujajiombea maisha marefu au utajiri au uhai wa maadui wako, lakini umeomba ufahamu wa kutambua hukumu ya haki,
\v 12 Tazama sasa nitafanya yote uliyoniomba wakati uliponipa ombi lako. Ninakupa moyo wa hekima na ufahamu, kwa kuwa hapajawahi kuwa na mtu wa kuwa kama wewe kabla yako, na hakuna wa kuwa kama wewe atakayeinuka baada yako.
\s5
\v 13 Pia ninakupa hata ambayo hujaomba, vyote heshima na utajiri, ili kwamba pasije pakawa na mfalme wa kuwa kama wewe katika siku zako zote.
\v 14 Kama utatembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo yangu na maagizo yangu, kama alivyofanya baba yako Daudi, ndipo nitakapoziongeza siku zako."
\s5
\v 15 Kisha Sulemani alipoamka, na tazama, ilikuwa ndoto. Akaja Yerusalemu na akasimama mbele ya sanduku na agano la Bwana. Akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, na akawafanyia sherehe watumishi wake wote.
\s5
\v 16 Kisha wanawake wawili waliokuwa makahaba wakaja mbele ya mfalme wakasimama mbele yake.
\v 17 Mwanamke mmoja akasema, "Aa, bwana wangu, mwanamke huyu na mimi tunaishi katika nyumba moja, Nilizaa mtoto tukiwa pamoj na yeye katika nyumba yetu.
\s5
\v 18 Ikatokea siku ya tatu baada ya kujifungua na yeye akajifungua. Tulikuwa sisi tu. Hapakuwepo na mtu mwingine yeyote katika nyumba yetu, ila sisi tu wawili katika hiyo nyumba.
\v 19 Kisha mtoto wa mwanamke huyu akafa wakati wa usiku, kwa sababu alimlalia.
\v 20 kwa hiyo akamka wakati huo wa usiku wa manane akamchukua mwanangu toka pembeni yangu, wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa usingizini, na akamlaza kwenye kifua chake, na akamlaza mtoto wake aliyekufa juu ya kifua changu.
\s5
\v 21 Asubuhi nilipoamka ili kumhudumia mwanangu, nikaona kuwa alikuwa amekufa. Lakini nilipomwangalia kwa makini wakati huo wa asubuhi, nikagundua kuwa hakuwa yule mwanangu niliyezaa,"
\v 22 Yule mwanamke mwingine akasema, "Hapana, Huyu aliye hai ndiye wangu. Na yule aliyekufa ndiye wako." Yule mwanamke wa kwanza akasema, "Hapana, Yule mtoto aliyekufa ndiye mwanao, na huyu aliye hai ndiye wangu." Hivi ndivyo walivyoongea mbele ya mfalme.
\s5
\v 23 Kisha mfalme akasema, "Mmoja wenu anasema, 'huyu aliye hai ni wangu, na kumbe mwanao ndiye aliye kufa,'na mwingine naye anasema, 'Hapana, mwanao ni yule aliyekufa, na mwanangu ni huyu aliye hai.'"
\v 24 Mfalme akasema, ''Nileteeni upanga." Kwa hiyo wakaleta upanga kwa mfalme.
\v 25 Kisha mfalme akasema, "Mgawe mtoto aliye hai katika vipande viwili, na huyu mwanamke apewe nusu na yule mwingine naye apewe nusu."
\s5
\v 26 Yule mwanamke mwenye mtoto aliyekuwa hai akamwambia mfalme, kwa kuwa moyo wake ulikuwa na huruma sana kwa mwanae, akasema, "Aa, bwana wangu, mpatie huyu mtoto aliye hai, na usimwue kamwe." Lakini yule mwanamke mwingine akasema, "Hatakuwa wangu wala wako. Mgawe."
\v 27 Ndipo mfalme aliposema, "Mpe yule mwanamke wa kwanza mtoto aliye hai, na kamwe usimwue. Yeye ndiye mama wa mtoto huyu."
\v 28 Israeli wote waliposikia hukumu ambayo mafalme ametoa, walimwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake kwa ajili ya kutoa kuhukumu.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Mfalme Sulemani alikuwa mfalme wa Israeli.
\v 2 Hawa ndio waliokuwa wakuu wake: Azaria mwana wa Sadoki alikuwa kuhani.
\v 3 Elihorefu na Ahiya mwana wa Shisha, walikuwa makatibu. Yehoshafati mwana wa Ahilui alikuwa mwandishi.
\v 4 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mkuu wa jeshi. Sadoki na Abiatahari walikuwa makuhani.
\s5
\v 5 Azaria mwana wa Natahani ndiye aliyekuwa juu ya hawa maakida. Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani na rafiki wa mfalme.
\v 6 Ahishari alikuwa mkuu wa nyumba. Adoniramu mwana wa Abda alikuwa mkuu wa watenda kazi.
\s5
\v 7 Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli yote, ambao walitoa chakula kwa mfalme na watu wake wote. Kila mtu alikuwa na zamu ya kuhudumia kwa mwezi mmoja katka mwaka.
\v 8 Majina yao yalikuwa ndiyo haya: Beni Huri, Kutoka milima ya Efraimu;
\v 9 Beni Dekeri wa Makazi, Shaalibimu, Bethi Shemeshi, na Elonbethi Hanaan;
\v 10 Beni Hesed, wa Arubothi (kutoka kwake alipatikana Sokohi na nchi yote ya Hefa);
\s5
\v 11 Ben Abinadabu, wa wilaya yote ya Dori (alikuwa na Tafathi binti wa mfalme ambaye alikuwa mke wake);
\v 12 Baana mwana wa Ahiludi, wa Taanaki na Megido, na Beth Shani iliyo upande mwingine wa Zarethani chini ya Yezreel, Kutoak Bethi Shani mpaka Abeli Mehola iliyo upande mwingine wa Jokimeamu;
\v 13 Ben Geberi, ya Ramothi Gileadi (kutoka kwake tunapata miji ya Yairi mwana wa Manase, ambayo iko Gileadi, na mkoa wa Arigobu ulikuwa wake, ambao uko Bashani, miji sitini yenye maboma na yenye nguzo za malango ya shaba);
\v 14 Ahinadabu mwana wa Ido, wa Mahanaimu;
\s5
\v 15 Ahimaazi, wa Naftali (ambaye pia alimwoa Basimathi binti wa Sulemani kuwa mke wake);
\v 16 Baana mwana wa Hushai, ya Asherina Bealothi;
\v 17 Yehoshafati mwana wa Paruha, kwa Isakari;
\s5
\v 18 Shimei mwana wa Ela, wa Benjamini;
\v 19 na Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, ambayo ni nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na Ogi mfalme wa Bashani, na yeye ndiye akida pekee aliyekuwa katika nchi hiyo.
\s5
\v 20 Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa baharini. Nao walikuwa wakila na kunywa na kufurahi.
\v 21 Suleimani alitawala utawala wote kutoka mtoni hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri. Wote walileta kodi na walimtumikia Sulemani katika siku za maisha yake yote.
\v 22 Mahitaji ya Sulemani kwa siku moja yalikuwa ni Kori thelathini za unga mzuri na kori unga wa ngano,
\v 23 makisai kumi walionona, na fahari ishirini wa malisho, na kondoo mia moja, nje ya ayala, paa, na kulungu na kuku walionona.
\s5
\v 24 Kwa kuwa utawala wake ulikuwa zaidi ya nchi yote upande huu wa mto, kutoka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa mto, naye alikuwa na amani pande zote.
\v 25 Yuda na Israeli waliishi kwa usalama, kila mtu chini y a mzabibu wake na chini ya mtini wake, kutoka Dani mpaka Beerisheba, siku zote za Sulemani.
\s5
\v 26 Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa ajili ya magari yake, na wapanda farasi elfu kumi na mbili.
\v 27 Na maakida walileta chakula kwa Sulemani na kwa wale walioketi kwenye meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake. Walihakikisha hakuna kinachopungua.
\v 28 Na pia walileta kwenye eneo husika shayiri na majani kwa ajili ya wale farasi wa magari na kwa wale farasi wa mbio kila mmoja alileta kadri alivyoweza.
\s5
\v 29 Mungu alimpa Sulemani hekima kubwa, ufahamu, na upana wa uelewa kama mchanga wa baharini.
\v 30 Hekima ya Sulemani ilizidi hekima ya watu wote wa mashariki na hekima yote ya Misri.
\v 31 Alikuwa na hekima kuliko wanaume wote - kuliko Ethani Muezrahi, Hemani, Kaliko, na Darda, wana wa Maholi - na habari zake zikaenea hadi kwenye mataifa yote yaliyomzunguka.
\s5
\v 32 Aliongea mithali elfu tatu na idadi ya nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.
\v 33 Aliifafanua mimea, kuanzia mierezi iliyoko Lebanoni hadi Hisopo imeao ukutani. Aliwafafanua wanyama, ndege, vitu vitambaavyo na samaki. Watu walikuja kutoka mataifa yote kuisikia hekima ya Sulemani.
\v 34 Watu walikuja kutoka falme zote za duniani waliosikia juu ya hekima yake.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Hiramu mfalme wa Tiro aliwatuma watumishi wake kwa Sulemani kwa kuwa alisikia kuwa walikuwa wamemtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwani Hiramu alimpenda Daudi.
\v 2 Sulemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, akisema,
\v 3 "Unajua kuwa Daudi baba yangu hakujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake kwa sababu ya vile vita vilivyomzunguka, kwa kuwa wakati wa uhai wake BWANA alikuwa akiweka maadui wake chini ya nyayo za miguu yake.
\s5
\v 4 Lakini sasa BWANA amenipa mimi pumziko toka pande zote. Hakuna maadui wala majanga.
\v 5 Kwa hiyo ninakusudia kujenga hekalu kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyosema kwa Daudi baba yangu, akisema, 'Mwanao ambaye nitamweka kwenye kiti chako cha enzi mahali pako, ndiye atakayenijengea hekalu kwa jina langu.'
\s5
\v 6 Kwa hiyo sasa amuru wakate mierezi kutoka Lebanoni kwa ajili yangu. Watumishi wangu wataungana na watumishi wako, nami nitakulipa kwa ajili ya watumishi wako ili kwamba upate malipo mazuri kwa kila kitu utakchokubali kukifanya. Kwa kuwa unajua kuwa hakuna mtu mioingoni mwetu anayejua kukata miti kama Wasidoni."
\s5
\v 7 Hiramu aliposikia maneno ya Sulemani, akafurahi sana akasema, "BWANA na abarikiwe leo, ambaye amempa Daudi mwana wa hekiima juu ya kundi hili kubwa."
\v 8 Hiramu akatuma neno kwa Sulemani, akisema, "Nimeupata ujumbe ule ulionitumia. Nitatoa miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo unahitaji.
\s5
\v 9 Watumishi wangu wataileta miti kutoka Lebanoni hadi baharini, nami nitaiendesha baharini mpaka mahali utakaponielekeza. Nitaigawa pale, nawe utaichukua. Utafanya kile ninachohitaji kwa kuwapa chakula watumishi wangu."
\s5
\v 10 Kwa hiyo Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo alihitaji.
\v 11 Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano kwa ajili ya chakula cha watumishi wake na kori ishirii za mafuta safi. Sulemani akavitoa hivi kwa Hiramu mwaka baad ya mwaka.
\v 12 BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyokuwa amemwahidi. Kulikuwa na amani kati ya Hiramu na Sulemani na wote wawili wakafanya agano.
\s5
\v 13 Mfalme Sulemani akaandaa wafanya kazi kutoka Israeli yote. Idadi ya watenda kazi walioandaliwa ilikuwa wanaume elfu thelathini.
\v 14 Aliwatuma kwenda Lebanoni, aliwatuma kwa zamu ya watu elfu kumi kila mwezi. Kwa mwezi mmoja walienda Lebanoni na miezi miwili walikaa nyumbani. Adoniramu ndiye aliyekuwa msimamizi wa watenda kazi.
\s5
\v 15 Sulemani alikuwa na watu elfu sabini waliokuwa wabeba mizigo na watu elfu themanini wa kukata mawe milimani,
\v 16 zaidi ya hao, walikuwepo maakida 3, 300 ambao pia waliokuwa wakiisimamia hiyo kazi.
\s5
\v 17 Kwa amri ya mfalme walileta mawe makubwa ya thamani kwa ajili ya kulaza kwenye msingi wa hekalu.
\v 18 Kwa hiyo wajenzi wa Sulemani na wajenzi wa Hiramu na Wagebaliti walifanya kazi ya kukata na kuandaa mbao kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili.
\v 2 Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13. 5.
\s5
\v 3 Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4. 5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu.
\v 4 Lile hekalu alilitengenezea madirisha ambayo fremu zake kwa nje yalifanya yaonekane membamba kuliko ile sehemu ya ndani.
\s5
\v 5 Na ukuta wa nyumba aliuzungushia vyumba kuzunguka pande zake, kushikamana na vyumba vya nje na vya ndani ya hekalu. Akajenga vyumba katika pande zote.
\v 6 Kile chumba cha chini kilikuwa na upana wa mita 2. 3, kile cha kati kilikuwa na upana wa mita 2. 8. na kile cha tatu kilikuwa na upana wa mita 3. 2. upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane ukutani mwa nyumba.
\s5
\v 7 Hekalu lilijengwa kwa mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni. Hakuna nyundo, wala shoka au chombo chochote cha chuma kilisikika wakati hekalu lilipokuwa likjengwa.
\v 8 Upande wa kusini wa hekalu kulikuwa na lango la chini, ambalo mtu hupanda kwa madaraja mpaka juu kwenye chumba cha kati, na kutoka chumba cha kati hadi chumba cha tatu.
\s5
\v 9 Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi.
\v 10 Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2. 3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.
\s5
\v 11 Neno la BWANA likamjia Sulemani, likisema,
\v 12 "Kuhusu hili hekalu ambalo unajenga, kama utatatembea katika maagizo yangu na kuhukumu kwa haki, na kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo, ndipo ntakapozithibitisha ahadi zangu na wewe ambazo niliziahidi kwa baba yako Daudi.
\v 13 Nitaishi kati ya watu wa Israeli nami sitawatupa."
\s5
\v 14 Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza.
\v 15 Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.
\s5
\v 16 Alijenga mita 9 ndani ya hekalu kwa mbao za miberoshi kutoka sakafuni hadi juu. Hiki ni chumba cha ndani, cha patakatifu sana.
\v 17 Ule ukumbu mkuu, ulikuwa mahali pakatifu amabao ulikuwa mbele ya patakatifu sana, ulikuwa wa mita 18. hapo kulikwa na mbao za mwerezi ndani ya hekalu, zilizokuwa zimechongwa kwa sura ya vibuyu na maua yaliyochanua.
\v 18 Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.
\s5
\v 19 Sulemani alitengeneza kile chumba cha ndani kwa lengo la kuweka sanduku la agano la BWANA.
\v 20 Kile chumba cha ndani kilikuwa na upana wa mita 9, na kimo cha mita 9. Sulemani alizifunika kuta kwa dhabahu na madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi.
\s5
\v 21 Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu.
\v 22 Akalisakafia kwa dhahabu eneo lote la ndani mpaka akamaliza hekalu lote. Pia akalisakafia kwa dhahabu madhahabu yote ya chumba cha ndani.
\s5
\v 23 Sulemani akatengeneza makerubi mawili kwa mbao za mizeituni, kila moja lilikuwa na kimo cha mita 4. 5 kwa ajili ya chumba cha ndani.
\v 24 Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mita 2. 3. Kwa hiyo kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa lingine kulikuwa na umbali wa mita 4. 5. Yule
\v 25 kerubi mwingine naye alikuwa na bawa lenye kipimo cha mita 4. 5 Makerubi hawa walikuwa wanafanana kwa umbo na kwa vipimo.
\v 26 Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mita 4. 5 na yule wa pili alikuwa hivyo hivyo.
\s5
\v 27 Sulemani aliwaweka hao kerubi kwenye chumba cha patakatifu sana. Bawa moja la kerubi lilikuwa limeenea kiasi kwamba bawa moja liligusa ukuta huu na bawa la yule wa pili nalo liligusa ukuta wa upande mwingine. Hayo mabawa yalikuwa yanakutana katikati ya chumba cha patakatifu sana.
\v 28 Sulemani aliwafunika hao kerubi kwa dhahabu.
\s5
\v 29 Akazinakshi kuta zote kwa sura za makerubi, miti ya mitende, na maua yaliyochanua, kwa vyumba vya nje na vya ndani.
\v 30 Sulemani akalisakafia hekalu kwa dhahabu, kwa vyumba vyote vya ndani na vya nje.
\s5
\v 31 Sulemani akatengeneza milango ya mbao za mizeituni kwenye lango la kuingia ndani. Aliweka vizingiti na miimo kwenye pande tano.
\v 32 Kwa hiyo akatengeneza na milango miwili ya mizeituni, na akainakshi kwa makerubi, na mitende, na maua yaliyochanua. Akasakafia kwa dhahabu na akatandaza dhahabu kwenye makerubi na kwenye mitende.
\s5
\v 33 Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo miwili ya mbao za mizeituni yenye pande nne
\v 34 na milango miwili ya mbao za mierezi. Zile mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa zikijikunja na mbao mbili za mlango wa pili nazo zilikuwa zikijikunja pia.
\v 35 Akazinakshi kwa makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na pia akazisakafia kwa dhahabu juu ya zile nakshi.
\s5
\v 36 Akalijengs Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.
\s5
\v 37 Msingi wa hekalu ulijengwa katika mwaka wa nne, wa mwezi wa Ziv.
\v 38 Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake.
\v 2 Aliijenga ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 46, na upanawake ulikuwa mita 23, na kimo chake kilikuwa mita 14. Nayo ilikuwa na safu nne ya nguzo za mierezi na mithili ya mwerezi juu ya nguzo.
\s5
\v 3 Paa la ikulu lilikuwa la mwerezi ambalo lilikaa juu ya mihimili. Mihili hiyo ilikuwa imeshikiliwa na nguzo. Kulikuwa na mihimili arobaini na tano, ambayo ilikuwa katika safu kumi na tano.
\v 4 Nayo mihimili ilikuwa safu tatu, na kila dirisha lilikabili dirisha lingine katika madaraja matatu.
\v 5 Milango yote na miimo ilitengenezwa kwa mraba, na madirisha yalikuwa yakikabiliana katika madaraja matatu
\s5
\v 6 Akatengeneza baraza lenye uerfu wa mita 23 na upana wa mita 14. Mbele yake kulikuwa na ukumbi ulioezekwa.
\s5
\v 7 Sulemani akajenga baraza yenye kiti cha enzi ambacho alitolea hukumu ya haki. Nayo ilikuwa imeezekwa kwa mwerezi kutoka sakafu moja hadi nyingine.
\s5
\v 8 Nyumba ya Sulemani ambayo alikusudia kuishi, katika behewa nyingine ndani ya sehemu ya chini ya ikulu, ilitengenezwa kwa kazi hiyo hiyo. Pia alimjengea binti wa Farao nyumba kama hii, ambaye alikuwa mke wake
\s5
\v 9 Majengo haya yalipmbwa kwa vitu vya thamaini, mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msimeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa pande zote. Mawe ya namna hii ndiyo yale yaliyotumika kuanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza.
\v 10 Msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na ya thamani yenye urefu wa mita 3. 7 na mengine mita 4. 8.
\s5
\v 11 Kwa juu ilipambwa kwa, mawe ya thamani yaliyochongwa sawa sawa kwa msimeno na kwa mihimili ya mierezi.
\v 12 Na behewa kubwa iliyokuwa ikizunguka ikulu ilikuwa na safu tatu za mawe yaliyokatwa na safu moja ya mihimili ya mierezi kama ilivyo kwenye baraza la ndani la hekalu la BWANA na ule ukumbi wa hekalu.
\s5
\v 13 Mfalme Sulemani alituma watu kumleta Huramu kutoka Tiro.
\v 14 Huramu alikuwa mwana wa mjane wa kabila ya Naftali; baba yake alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba. Huramu alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi za kufanya kazi kubwa za shaba. Aliletwa kwa mfalme ili kufanya kazi zilizohusiana na shaba kwa mfalme.
\s5
\v 15 Huramu alizilemba zile nguzo mbili za shaba, kila moja ilikuwa na kimo cha mita 8. 3 na mzingo wa mita 5. 5.
\v 16 Akatengeneza taji mbili za shaba za kuwekwa juu ya zile nguzo. Kimo cha kila taji ilikuwa mita 2. 3.
\v 17 Kulikuwa na nyavu za kuwa kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa ajili ya kuvipamba vile vichwa vya nguzo, nayo yailikuwa saba kwa kila kichwa.
\s5
\v 18 Kwa hiyo Huramu akafanya safu mbili za komamanga kuzunguka vile vichwa vya nguzo ili kuvipamba vile vichwa.
\v 19 Zile taji kwenye vile vichwa vya nguzo za ukumbi zilikuwa zimepambwa kwa maua, yenye vimo vya mita 1. 8.
\s5
\v 20 Hizo taji kwenye hizo nguzo mbili kwenye vichwa vyake, karibu yake kulikuwa na makomamanga mia mbili yote yakiwa kwenye safu.
\v 21 Alisimamisha nguzo kwenye ukumbi wa hekalu. Ile nguzo ya kuume akaipa jina la Yakini, na ile ya kushoto akaipa jina la Boazi.
\v 22 Na juu ya zile nguzo kulikuwa na mapambo kama maua. Hivyo ndivyo zile nguzo zilivyotengenezwa.
\s5
\v 23 Tena akafanya bahari ya kusubu ya, yenye mita 2. 3 kutoka ukingo hadi ukingo, kimo chake kilikuwa mita 4. 6, mziingo wake ulikuwa mita 13. 7.
\v 24 Na chini ya ile bahari kulikuwa na vibuyu vilivyoizunguka, vilikuwa vibuyu kumi na nane katika kila mita, vilivyowekwa katika kila hicho kipande wakati bahari inapokuwa kalibu.
\s5
\v 25 Bahari ikakaa juu ya makisai kumi na mbili, tatu, zilitazama kaskazini, tatu zikitazama magharibi, tatu zikitazama kusini na tatu zikitazama kaskazini. Ile bahari iliwekwa juu yao, na pande zao zote za nyuma zilikuwa ndani.
\v 26 Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwakama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi huingia bathi elfu mbili za maji.
\s5
\v 27 Huramu akatengeneza makalio kumi ya shaba. Kila kalio lilkuwa na urefu wa mita 1. 8, upana wa mita 1. 8, na kimo cha mita 1. 3.
\v 28 Hivi ndivyo kazi za makalio zilivyofanywa. Yalikuwa na papi ambazo zilikaa kati kati ya vipandio,
\v 29 na juu ya papi na vipandio kulikuwa na simba, makisai, na makerubi. Chini na juu simba kulikuwa na masongo ya kazi ya kufuliwa.
\s5
\v 30 Kila kalio lilikuwa na magurudumu ya shaba na vipini, na pande zake nne na miguu yake minne ilikuwa na mataruma chini ya birika. Chini ya birika yalikuweko mataruma ya kusubu yenye masongo katika kila upande.
\v 31 Na kinywa chake kilikuwa cha kuviringana, chenye upana wa sentimita araobaini na sita, na ile taji ilikuwa na sentimita ishirini na tatu. Na kinywa chake kilikuwa na nakshi, na papi zake zilikuwa za mraba, na wala siyo za mvringo.
\s5
\v 32 Yale magurudumu mawili yalikuwa chini ya papi, na mikono ya magurudumu yalikuwa ndani ya makalio. Kimo cha yale magurudumu kilikuwa sentimeta sitini na tisa.
\v 33 Yale magurudumu yalikuwa kama ya gari. Mikono yake, na maduara, matindi yake, na vipande vya ndani vyote vilikuwa vya kusubu.
\s5
\v 34 Kulikuwa na mataruma manne katika pande zake nne za makalio, yaliyokuwa yameshikamanishwa na kalio lenyewe.
\v 35 Juu ya makalio kulikuwa na duara yenye kina cha sentimita ishirini na tatu, na juu ya makalio mashikio yake na papi zake zikiwa zimeshikamanishwa.
\s5
\v 36 Juu ya mabamba na papi zake Huramu akachora makerubi, simba, na mitende ambayo ilifunika nafasi ya juu, nayo ilikuwa imezungukwa na masongo.
\v 37 Alitengeneza makalio kumi kwa jinsi hii. Yote yalikuwa yametengenezwa kwa kufanana, na yalikuwa ya vipimo sawa, na sura inayofanana.
\s5
\v 38 Huramu akatengeneza birika kumi za shaba. Birika moja liliweza kubeba bathi arobaini za maji. Kila birika lilikuwa mita 1. 8 toka birika moja hadi jingine na kulikuwa na birika moja katika kila kalio kati ya yale kumi.
\v 39 Alitengeneza makalio tano upande wa kusini unaoelekea upande wa hekalu. Akatengeneza bahari katika upande wa mashariki, ukielekea upande wa kusini wa hekalu.
\s5
\v 40 Huramu akatengeneza birika na koleo na besini la kunyunyizia. Kisha akamaliza kazi yote aliyofanya kwa mfalme Sulemani katika hekalu la BWANA:
\v 41 Zile nguzo mbili, na lile besini lakawa kama taji ambalo lilikuwa juu ya zile nguzo, na nyavu mbili za mapambo za kufunika zile besini mbili za kuwa kama taji zilizokuwa juu ya nguzo.
\s5
\v 42 Kisha akatengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu mbili za mapambo: safu mbili za makomamamanga kwa kila kazi ya nyavu kwa ajili ya kufunikia zile besini mbili kama taji iliyo juu ya nguzo,
\v 43 yale makalio kumi, na birika kumi kwenye makalio.
\s5
\v 44 Akatengeneza bahari na makisai kumi chini yake;
\v 45 na masufuria, koleo, birika na vyombo vingine vyote. Huramu akivitengeneza kwa shaba iliyosuguliwa, kwa ajili ya mfalme Sulemani, na kawa ajili ya hekalu la BWANA.
\s5
\v 46 Mfalme alivisubu katika uwanda wa Yorodani, katika udongo mfinyanzi kati ya Sukoti na Zarethani.
\v 47 Sulemani hakuvipima vyombo vyote kwa sababu vilikuwa vingi mno kuvipima, na kwa sababu uzito wa shaba ulikuwa hauwezi kupimwa.
\s5
\v 48 Sulemani akatengeneza mapambo yote yaliyokuwa kwenye hekalu la BWANA kwa kutumia dhahabu: Ile madhabahu ya dhahabu na ile meza ambayo iliwekwa mikate ya wonyesho.
\v 49 Vile vinara vya dhahabu, ambavyo vitano vilikuwa upande wa kulia na vitano mkono wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vilikuwa vya dhahabu safi, na maua, na taa na koleo zilikuwa za dhahabu.
\s5
\v 50 Vile vikombe, na makasi, mabakuri, na vijiko, na vyetezo vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi. na bawaba za dhahabu za milango ya ndani, ambazoo ndio mahali patakatifu sana, na milango ya ukumbi mkubwa, vyote vilitengenezwa kwa dhahabu.
\s5
\v 51 Kwa njia hii, kazi yote ambayo mfalme Sulemani alifanya kwa ajili ya hekalu ilimalizika. Kwa Sulemani akaviingiza ndani yake vitu vile vilivyokuwa vimewekwa wakfu na Daudi, baba yake, na fedha na dhahabu, na mapambo, na vile vya ndani ya hazina ya BWANA.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Kisha Sulemani akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wote wa makabila, na viongozi wa familia za wana wa Israeli, mbele yake kuleYerusalemu, ili waliingize ndani lile sanduku la agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.
\v 2 Wanaume wote wa Israeli walikusanyika mbele ya mfalme Sulemani kwenye sherehe, katika mwezi wa Ethanim, ambao ndio mwezi wa saba.
\s5
\v 3 Wazee wote wa Israeli walikuja, na makuhani wakalibeba lile sanduku.
\v 4 Wakalileta lile sanduku la BWANA, lIle hema la kukutania na mapambo yote matakatifu ambayo yalikuwa kwenye hema. Makuhani na Walawi wakavileta vitu hivi.
\v 5 Mfame Sulemani na mkutano wote wa Israeli wakaja pamoja mbele ya sanduku, wakatoa sadaka za kondoo na makisai ambazo hazikuweza kuhasabika.
\s5
\v 6 Makuhani wakalingiza ndani lile sanduku la agano la BWANA na wakaliweka mahali pake, ndani ya chumba cha ndani, patakatifu sana, chini ya yale mabawa ya makerubi.
\v 7 Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao hadi mahali pa sanduku la agano, na walifunika sanduku na miti yake kwani ilitumika kulibeba.
\v 8 Ile miti ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba miishio yake ilionekana tokea kwenye eneo takatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutokea nje. Miti hiyo iko mpaka leo.
\s5
\v 9 Ndani ya sanduku hapakuwemo na kitu chochote isipokuwa vile vidonge vya mawe ambavyo Musa aliviweka alipokuwa mlima Horebu, wakati BWANA alipofanya agano na watu wa Israeli walipotoka kwenye nchi ya Misri.
\v 10 Ilitokea kwamba wakati makuhani walipotoka mahali patakatifu, lile wingu lilifunika hekalu la BWANA.
\v 11 Makuhani hawakuweza kusimama kwa ajili ya kutumika kwa sababu utukufu wa BWANA ulifunika hekalu.
\s5
\v 12 Kisha Sulemani akasema, "BWANA amsema kuwa anaweza kuishi hata kwenye giza nene,
\v 13 Lakinni nimekujengea makao ya kujivunia, mahali pako pa kuishi milele."
\s5
\v 14 Kisha mfalme akageuka na kuwabariki mkusanyiko wa watu wa Israeli, wakati huo mkusanyiko wa Waisraeli walikuwa wamesimama.
\v 15 Akasema, "BWANA, Mungu wa Israeli, asifiwe, ambaye alisema na baba yangu Daudi, na ametimiza kwa mikono yake, akisema,
\v 16 'Tangu siku ile niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji wowote toka kwa makabila yote ya Israeli ambako ningeijenga nyumba, kwa ajili ya jina langu kuwemo humo. Hata hivyo, nilimchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.
\s5
\v 17 Sasa ilikuwa kwenye moyo wa Daudi baba yangu kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.
\v 18 Lakini BWANA alimwambia baba yangu Daudi, 'Ilikuwa ndani ya moyo wako kunijengea nyumba kwa jina langu, ulifanya vyema kwa hilo kuwa ndani ya moyo wako.
\v 19 Ingawa hutanijengea nyumba; badala yake mwanao, mmoja wa wanao atakayezaliwa toka viunoni mwako, atanijengea nyumba kwa jina langu,'
\s5
\v 20 BWANA amelibeba lile neno slilokuwa amesema, kwa kuwa nimeinuka mahali pa baba yangu Daudi, na nimeketi kwenye kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi. Nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.
\v 21 Nimetengeneza mahali kwa ajili ya sanduku ndani yake, ambamo ndani yake kuna agano la BWANA, ambalo alifanya na baba zetu alipowatoa toka nchi ya Misri,"
\s5
\v 22 Sulemani alisimama mbele ya madhabahu ya BWANA, mbela ya mkusanyiko wote wa Waisraeli, naye akanyosha mikono yake kuelekea mbinguni.
\v 23 Akasema, "BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni au chini duniani, ambaye hutunza agano lake kwa uaminifu kwa watumishi wako ambao hutembea mbele yako kwa mioyo yao yote;
\v 24 wewe ambaye umetunza ahadi yako na mtumishi wako Daudi baba yangu ile uliyomwahidi. Naam, ulisema kwa kinywa chako na sasa umeitimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.
\s5
\v 25 Sasa basi, BWANA, Mungu wa Israeli, timiza kile ulichomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu, pale uliposema, 'Hautashindwa kunipa mtu mbele ya macho yangu ambaye ataketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama tu uzao wako watakuwa waangalifu kutembea mbele yangu, kama vile wewe ulivyotembea mbele yangu.'
\v 26 Sasa basi, Mungu wa Israeli, Ninaomba kwamba ile ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, itimie.
\s5
\v 27 Je, ni kweli kwamba Mungu ataishi duniani? Tazama, Ulimwengu wote na mbingu hazikutoshi - sembuse nyumba hii niliyoijenga!
\v 28 Kwa hiyo Mungu naomba uyajali maombi haya ya mtumishi wako na maombi yake, BWANA, Mungu wangu; sikiliza kilio na maombi ambayo mtumishi wako anakuomba leo.
\s5
\v 29 Naomba ulitazame hekalu hili mchana na usiku, mahali ambapo ulisema, 'Jina langu na uwepo wangu utakuwa' - ili niweze kuwa nasikiliza maombi ambayo mtumishi wako ataomba mahali hapa.
\v 30 Kwa hiyo sikia maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli tunapokuwa tunaomba mahali hapa. Ndiyo, sikia kutokea mahali ambapo unaishi, kutoka katika mbingu za mbingu; na unaposikia tafadhali samehe.
\s5
\v 31 Kama mtu atamtendea uovu jirani yake na anapewa sharti la kiapo, na kama atakuja na kuapa mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,
\v 32 basi usikie kutoka mbinguni ukatende na kuwahukumu watumishi wako, ukamhukumu mwovu, ili kuwaletea tabia zake kichwani mwake, na kumtunza mwenye haki kuwa hana hatia, na kumpa thawabu yake ya haki.
\s5
\v 33 Watu wako Israeli watakapopigwa na adui kwa sabau ya kutenda dhambi dhidi yako, na kama watakurudia, na kulikiri jina lako, na kukusihi, na kuomba msamaha kwako katika hekalu hili-
\v 34 tafadhali nakuomba usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi ambayo uliwapa mababu zao.
\s5
\v 35 Kama mbingu zitafungwa na mvua hazinyeshi kwa sababu watu wamekutenda dhambi wewe - na kama wataomba mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kugeuka toka dhambi zao na kama umewapiga -
\v 36 basi sikia tokea mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na za watu wako Israeli, utakapowafundisha njia njema inayowapasa; basi uinyeshee mvua nchi yako, ambayo uliwapa watu wako kuwa urithi.
\s5
\v 37 Na kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna magonjwa, au ukungu, nzige au funza; au kama adui atavamia malango ya mji katika nchi yao, kama kuna tauni au magonjwa yeyote -
\v 38 na kama kuna mtu au wata wa Israeli wataomba - kila mmoja akaijua hiyo tauni katika moyo wake wakati akinyosha mikono yake katika hekalu hili.
\s5
\v 39 Basi usikie kutoka mbinguni, mahali unapoishi, utende na kusamehe, na umpe kila mtu thawabu anayostahili kwa kile anachofanya; wewe unajua moyo wake, kwa sababu ni wewe pekee yako ujuaye mioyo ya watu.
\v 40 Fanya hivi ili kwamba wawe na hofu kwako katika siku zote za maisha yao wanayoishi katika nchi uliyowapa mababu zetu.
\s5
\v 41 Na nyongeza yake, kuhusiana na mgeni ambaye si mtu wako wa Israeli: atakapokuja kutokea nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako -
\v 42 kwa sababu watasikia jina lako lilivyo kuu, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulioinuliwa - atakapokuja na kuomba mahali hapa pa hekalu,
\v 43 tafadhali usikie kutokea katika mbingu, mahali unapoishi, na umfanyie huyo mgeni akuombacho. Fanya hivi ili makundi ya wtu wote duniani wakujue jina lako na kukuhofia, kama wanavyofanya watu Israeli. Fanya hivyo ili wajue kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.
\s5
\v 44 Na kama watu wko wataenda vitani dhidi ya adui, kwa njia yeyote unayoweza kuwatuma, na kama watakuomba wewe, BWANA, kuelekea mji huu uliuchagua, na kuekea nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.
\v 45 Basi sikia tokea mbinguni maombi yao, dua zao, na uwasaidie wanachohitaji.
\s5
\v 46 Na kama watafanya dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna hata mtu mmoja asiyefanya dhambi, na kama una hasira dhidi yao na kuwapeleka kwa maadui, ili kwamba maadui wawachukue mateka katika nchi yao, mbali au karibu.
\v 47 Na kama watatambua kuwa wako katika nchi ya utumwa, na kama watatubu na kuomba neema kwako kutokea katika nchi ya watekaji. Na kama watasema, 'tumetenda kwa ukaidi na tumefanya dhambi. Tumetenda kwa uovu.'
\s5
\v 48 Na kama watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote katika chi ya maadui ambao wanawakamata, na kama watakuomba wewe kuelekea nchi yao, ambayo uliwapa mababu zao, na kuelekea katika mji uliouchagua, nakuelekea kaika nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.
\s5
\v 49 Basi usikie maombi yao, na dua zao tokea mbinguni, mahali unapoishi, na ukaitetee haki yao.
\v 50 Wasamehe watu wako waliotenda dhambi dhidi yako, na dhambi zao zote ambazo kwazo wamekukosea wewe dhidi ya amri zako. Uwahurumie mbele ya maadui zao ambao waliwachukua mateka, ili kwamba maadui zao pia wawahurumie watu wako.
\s5
\v 51 Hawa ni watu wako uliowachagau, ambao uliwaokoa toka nchi ya Misri kama kwamba walikuwa katikati ya tanuru amabamo vyuma huyeyushwa.
\v 52 Naomba kwamba macho yako yatazame dua za mtumishi wako na kwa dua za watu wako Issraeli, ili uwasike kila wanapokulilia.
\v 53 Kwa kuwa uliwatenga toka kwa watu wengine wa duniani ili wawe wako nakupokea ahadi zako, kama vile ulivyomwambia Musa mtumishi wako, wakati ulipowatoa babazetu toka Misri, BWANA."
\s5
\v 54 Kwa hiyo ilitokea wakati Sulemaeni alipomaliza kuomba maombi haya na dua zake kwa BWANA, aliamka toka madhabahu ya BWANA, pale alipokuwa amepiga magoti na mikono yake ikiwa imenyoshwa kuelekea mbinguni.
\v 55 Alisimama na kuubariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu, alisema,
\v 56 "Asifiwe BWANA, aliywapatia pumziko watu hawa Israeli, akitunza ahadi zake zote. Hakuna hata moja ambayo haijatekelezwa katika ahadi njema za BWANA ambazo aliahidi akiwa na Musa mtumishi wake.
\s5
\v 57 BWANA, mungu wetu awe pamoja nasi, kama alivyokuwa pamoja na mababu zetu. Asituache wala kututelekeza,
\v 58 kwamba aunganishe mioyo yetu na yeye, ili tuishi katika njia zake na kuzishika amri zake na taratibu zake na maagizo yake, ambayo aliwaagiza baba zetu.
\s5
\v 59 Na maeneo haya ambayo nimesema, ambayo nimesihi mbele ya BWANA, yawe karibu n a BWANA, Mungu wetu usiku na mchana, ili kwamba awasadie katika haki za mtumishi wake na haki za watu wake Israeli, kama watakavyoomba kila siku;
\v 60 kwamba watu wote duniani wajue kwamba BWANA, ndiye Mungu, na hakuna Mungu mwingine!
\v 61 Kwa hiyo ifanyeni mioyo yenu iwe ya haki mbele ya BWANA. Mungu wetu, ili tutembee katika maagizo na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo.
\s5
\v 62 Kwa hiyo mfalme na watu wote pamoja naye wakatoa sadaka kwa BWANA.
\v 63 Sulemani akatoa sadaka ya amani, ambayo aliifanya kwa BWANA: Nayo ilikuwa makisai elfu ishirini na mbili, na kondoo 120, 000. Kwa hiyo mfalme na watu wa Israeli wakaiweka wakfu nyumba ya BWANA.
\s5
\v 64 Siku hiyo mfalme aliweka wakfu behewa ya katikati mbele ya hekalu la BWANA, kwa kuwa pale ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za unga, na sadaka za mafuta ya amani, kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele ya BWANA ilikuwa ndogo sana kwa sadaka za kuteketezwa, sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani.
\s5
\v 65 Kwa hiyo Sulemani akafanya sherehe wakati huo, Nayo Israeli yote pamoja naye, mkutano mkubwa, kutoka Lebo Hamathi hadi kijito cha Misri, wakaja mbele ya BWANA, Mungu wetu kwa muda wa siku saba na pia kwa siku saba zingine, ambayo jumla yake ni siku kumi na nne.
\v 66 Na ilipofika siku ya nane aliwatawanya watu, nao wakambariki mfalme kisha wakaenda nyumbani kwao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa wema wote ambao BWANA alimwonyesha Daudi, mtumishi wake, na kwa watu wake, Israeli.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Sulemani alipomaliza kulijenga hekalu la BWANA, na ikulu ya mfalme, na baada ya kukamilisha vyote alivyokusudia kufanya,
\v 2 BWANA alionekana kwa Sulemani kwa mara ya pili, kama alivyoonekana kwake kule Gibeoni.
\s5
\v 3 Na BWANA akamwambia, " Nimeyasikia maombi yako na dua zako ambazo umeniomba. Nimeitakasa nyumba hii ambayo umeijenga, kwa ajili yangu, ili niweke jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu yatakuwa humo kwa nyakati zote.
\s5
\v 4 Lakini pia na wewe, kama utatembea mbele zangu kama Daudi baba yako alivyotembea kwa haki na unyofu katika moyo wako, ukitii yote niliyokuamuru na kuyashika maagizo na sheria zangu,
\v 5 ndipo nitakapoimarisha kiti cha enzi kwa Israeli milele, kama nilivyomwahidi baba yako Daudi, nikiseama, 'uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli.
\s5
\v 6 Lakini kama utageuka, wewe au watoto wako, na kutozishika amri zangu na maagizo yangu ambayo nimeyaweka mbele zako, na kama utaenda kuabudu miungu mingine na kuisujidia,
\v 7 basi nitaikatilia mbali Israeli kutoka katika ardhi niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli itakuwa mfano wa kukejeliwa na kitu cha kutusiwa katika mataifa yote.
\s5
\v 8 Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa, kila mtu atakayepita pembeni yake atasituka na kuzoomea. Watajiuliza, 'Kwa nini BWANA amefanya hili katika chi hii na kwa nyumba hii?'
\v 9 Na wengine watajibu, 'Ni kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, ambaye aliwaleta mababu zao toka Misri, na sasa wamegeukia miungu mingine ambayo wameiinamia na kuisujudu. Hiyo ndiyo sababu BWANA amewaletea majanga haya yote."
\s5
\v 10 Ilitokea mwishoni mwa miaka ishirini, Sulemani alikuwa amemaliza kuyajenga majengo yote mawili, hekalu la BWANA na ikulu ya mfalme.
\v 11 Basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mbao za mierezi na miboreshi, pamoa na dhahabu; vitu vyote ambavyo Sulemani alitamani. Kwa hiyo mfalme Sulemani akampatia Hiramu miji ishirini huko Galilaya.
\s5
\v 12 Hiramu akaja kutoka Tiro kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempatia, lakini hakupendezwa nayo.
\v 13 Kwa hiyo Hiramu akasema, "Ndugu yangu, ni miji gani hii uliynipatia? Hiramu akaiita nchi ya Kabuli mpaka leo.
\v 14 Hiramu alikuwa amemtumia mfalme tani nne za dhahabu.
\s5
\v 15 Vifuatavyo ndivyo vigezo ambavyo mfalme Sulemani aliweka: ili kulijenga hekalu la BWANA na ikulu yake, kuijenga Milo na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, Megido, na Gezari.
\v 16 Farao mfalme wa Misri alikuwa ameenda kuitwaa Gezeri, akaichoma moto, na kuwaua Wakanaani katika mji. Kisha Farao akampatia binti yake ule mji, mke wa Sulemani kuwa zawadi ya arusi.
\s5
\v 17 Kwa hiyo Sulemani akaijenga Gezeri na Bethi Horoni ya Loweri,
\v 18 Baalathi na Tamari jangwani katika nchi ya Yuda,
\v 19 na miji yote ya hazina yote iliyokuwa yake, na miji ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na hata kama alipenda kuijenga kwa ajili ya fahari yake kule Yerusalemu, Lebanoni, na katika nchi yote kwenye utawala wake.
\s5
\v 20 Na kwa watu wote waliokuwa wamesalia wa Waamori, Wahiti, Waperezi, Wahivi, na Yebu, ambao hawakuwa Waisraeli,
\v 21 na uzao wao waliokuwa wamesalia baada yao katika nchi, ambao Waisraeli hawakuweza kuwaangamiza kabisa - Sulemani akawafanya kuwa vibarua, ambao wako hata leo.
\s5
\v 22 Hata hivyo, Sulemani hakuwafanya kuwa shokoa watu wa Israeli. Badala yake, walifanyika kuwa wanajeshi wake na watumishi wake, maakida wake, na wakuu wake, na majemedari wake na wapanda farasi wake.
\s5
\v 23 Hawa ndio waliokuwa maakida wakuu waliokuwa wakiwasimamia kazi za Sulemani, watu 550, walikuwa wasimamizi wa watu waliokuwa wakifanya kazi.
\s5
\v 24 Binti wa Farao alihama kutoka mji wa Daudi kwenda kwenye ile nyumba ambayo Sulemani alimjengea. Baadaye, Sulemani akaijenga Milo.
\s5
\v 25 Mara tatu kwa kila mwaka Sulemani alitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani katika madhabahu ambayo alimjengea BWANA, akifukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu ilyokuwa mbele ya BWANA. Kwa hiyo akalimalizia hekalu na sasa alikuwa akilitumia.
\s5
\v 26 Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu.
\v 27 Hiramu alituma watumishi kwenye merikebu ya Sulemani, wanamaji wanaoijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani.
\v 28 Walikwenda kwa Ofri pamoja na watumishi wa Sulemani. Kutoka huko walileta takribani tani 14. 5 za dhahabu kwa Sulemani.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Malkia wa Sheba aliposikia uvumi wa Sulemani kuhusu jina la BWANA, alikuja kumjaribu kwa maswali magumu.
\v 2 Alikuja Yerusalemu na msafara mrefu, pamoja na ngamia waliokuwa wamebeba mizigo ya manukato, dhahabu nyingi, na mawe mengi ya thamani, akamwambia Sulemani yote yaliyokuwa moyoni mwake.
\s5
\v 3 Sulemani akajibu maswali yake yote. Hapakuwepo na swali ambalo aliuliza na mfalme akashindwa kujibu.
\v 4 Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na ikulu aliyokuwa amejenga,
\v 5 chakula cha mezani kwake, kuketi kwa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na kuvaa kwao, pia wanyweshaji wake, na jinsi alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.
\s5
\v 6 Akamwambia mfalme, "Ni kweli, ile taarifa ambayo nimeisikia nchini kwangu juu ya maneno yako na hekima yako.
\v 7 Sikuamini kile nilichosikia hadi nilipofika hapa, na sasa macho yangu yamejionea. Hata nusu ya hekima na utajiri wako! Umezidi uvumi ambao nilikuwa nimesikia.
\s5
\v 8 Tazama jinsi walivyobarikiwa wake zako, na jinsi walivyobarikwa watumishi wako ambao daima husimama mbele yako, kwa sababu wanasikia hekima zako.
\v 9 BWANA, Mungu wako asifiwe, ambaye amependezwa na wewe, ambaye alikuweka kwenye kiti cha enzi cha Israeli. Kwa sababu BWANA aliipenda Israeli milele, na sasa amekufanya wewe kuwa mfalme, ili kwamba utoe hukumu ya kweli na ya haki.
\s5
\v 10 Basi Malikia alimpatia mfalme zaidi ya kilo 4500 za dhahabu na kiasi kikubwa cha mawe ya thamani. Hapakuwahi kutokea kiasi kikubwa cha viungo kama hiki ambacho Malkia wa Sheba alitoa kwa mfalme Sulemani kuwahi kutolewa tena.
\s5
\v 11 Ile merikebu ya Hiramu, ambayo ilileta dhahabu kutoka Ofri, pia ilileta Kutoka Ofri kiasi kikubwa cha miti ya msandali na vito vya thamani.
\v 12 Mfalme alitengeneza nguzo za hekalu kwa ajili ya hekalu la BWANA na kwa nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda kwa hao waimbaji. haijatokea kiasi cha miti ya misandali kama hicho ambacho kimewahi kutokea hadi leo.
\s5
\v 13 Mfame Sulemani alimpatia Malkia wa Sheba kila kitu ambacho alihitaji, na kila kitu alichoomba, na zaidi ya yote Sulemani alimpatia kwa ukarimu wake vitu vya kifalme. Kisha akarudi kwake na watumishi wake.
\s5
\v 14 Kiasi cha dhahabu ambazo zililetwa kwa Sulemani kwa mwaka mmoja kilikuwa takribani kilo elfu ishirini na tatu za dhahabu,
\v 15 zaidi ya dhahabu ambazo wafanya biashara na wachuuzi walileta. Wafame wote wa Uarabuni na maliwali wa nchi pia walileta dhahabu na fedha kwa Sulemani.
\s5
\v 16 Mfalme Sulemani alitengeneza ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa, shekeli mia sita za dhahabu zilichukuliwa pamoja na ngao.
\v 17 Pia alitengeneza ngao mia tatu za dhahabu iliyofuliwa. Mane tatu za dhahabu ziliambatana pamoja na ngao moja moja; mfalme aliviweka katika ikulu ya mwitu ya Lebanoni.
\s5
\v 18 Kisha mfalme akafanya kiti kikubwa cha enzi kwa pembe na akakisakafia kwa dhahabu laini.
\v 19 Hicho kiti kilikuwa na ngazi sita, na kitako chake kilikuwa cha mviringo. Na kilikuwa kimezungushiwa kwa mikono pande zake zote. Na simba wawili walisimama pembeni mwa ile mikono.
\v 20 Kulikuwa na simba kumi na wawili waliokuwa wamesimama kwenye ile ngazi. Moja katika kila upande wa ngazi hizo. Hapakuwepo na kiti kama hicho katika ufalme mwingine.
\s5
\v 21 Vikombe vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu. Na vikombe vyote vya kunywea vya ikulu ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hapakuwepo na kikombe cha fedha, kwa sababu fedha haikuwa na thamani katika siku za Sulemani.
\v 22 Mfalme alikuwa na merikebu za kusafiri pamoja na merikebu za Hiramu. Mara moja kila mwaka merikebu zilileta dhahabu, fedha, na pembe za ndovu, pamoja na nyani na tumbili.
\s5
\v 23 Kwa hiyo mfalme Sulemani aliwazidi wafalme wote ulimwenguni katika utajiri n a hekiima.
\v 24 Dunia yote ilitafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameweka katika moyo wake.
\v 25 Na wote waliomtembelea walilipa Kodi, vyombo vya fedha na vya dhahabu, na nguo na manukato na silaha na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka.
\s5
\v 26 Sulemani alikusanya pamoja magari n a wapanda farasi. Alikuwa na magari 1, 400 na wapanda farasi elfu kumi na mbili ambao alikuwa amewaweka kwenye miji ya magari pamoja naye Yerusalemu.
\v 27 Mfalme alikuwa na fedha kule Yerusalemu, pamoja na mawe ardhini. Alitengeneza miti ya mierezi kuwa mingi kama mikuyu iliyo katika nyanda za chini.
\s5
\v 28 Sulemani alimiliiki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake.
\v 29 Magari yalinunuliwa kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na farasi kwa shekeli 150 kila moja. Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa kwa wafalme wote wa Wahiti na Aramu.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi mfalme Sulemani aliwapenda wanawake wengi wa kigeni: binti wa Farao na wanawake wa Wamoabu, Waamori, Waedomu, Wasidoni, na Wahiti - Haya na
\v 2 mataifa ambayo BWANA alikuwa amewaambia Waisraeli kwamba, "Msiwaoe, wala binti zenu kuolewa nao, kwani kwa hakika wataigeuza mioyo yenu ili mfuate miungu yao." Lakini Sulemani aliwapenda wanawake hao.
\s5
\v 3 Sulemani alikuwa na wanawake halali mia saba na masuria mia tatu. Wake zake waliugeuza moyo wake.
\v 4 Kwa kuwa Sulemani alipozeeka, wake zake waliugeuza moyo wake kwa miungu mingine; hakuutoa moyo wake wote kwa BWANA, Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake.
\s5
\v 5 Kwani Sulemani alimfuata Ashtoreth, mungu mke wa Wasidoni, na alimfuata Milkom, ambayo ni sanamu chukizo ya Waamori.
\v 6 Sulemani akafanya maovu mbele ya BWANA; hakumfuata BWANA kwa moyo wake wote, kama alivyofanya Daudi baba yake.
\s5
\v 7 Kisha Sulemani akajenga mahali pa juu pa Kemoshi, ambayo ni sanamu chukizo ya Wamoabu, mashariki mwa Yerusalemu juu ya kilima, na vivyo hivyo na Moleki, Sanamu chukizo ya Waamoni.
\v 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa sadaka kwa miungu yao.
\s5
\v 9 BWANA alichukizwa na Sulemani, kwa sababu moyo wake ulikuwa umemwacha Mungu wa Israeli, ingawa alikuwa amejionyesha kwake mara mbili
\v 10 na kumwamuru juu ya mambo haya, kwamba asiwaendee miungu wengine. Bali Sulemani hakutii kile ambacho BWANA alikuwa amemwamuru.
\s5
\v 11 Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, "Kwa kuwa umeyafanya haya haukulishika agano langu na maagizo ambayo nilikuamuru, basi nitaugawa ufalme kutoka kwako na kuwapatia watumishi wako.
\v 12 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, sitalifanya hilo wakati wa uhai wako, bali nitaugawa wakati ukiwa chini ya mwanao.
\v 13 Bado sitaugawanya ufalme wote; Nitampa mwanao kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu, ambayo nimeichagua."
\s5
\v 14 Kisha BWANA akamwinulia uadui Sulemani, Hadadi Mwedomu. Alikuwa anatoka kwenye familiia ya mfalme wa Edomu.
\v 15 Daudi alipokuwa Edomu, Yoabu mkuu wa jeshi alikuwa ameenda kuzika mfu, kila mtu aliyekuwa ameuawa kule Edomu.
\v 16 Yoabu na Israeli yote walibaki huko kwa miezi sita mpaka alipokuwa amewaua wanaume wote wa Edomu.
\v 17 Lakini Hadadi alichulukuliwa na Waedomu wengine na watumishi wa baba yake hadi Misri, kuanzia Hadadi alipokuwa mtoto mdogo.
\s5
\v 18 Waliondoka Midiani wakaja Parani, ambapo walichukuliwa na wanaume mpaka Misri, kwa Farao wa Misri, ambaye alimpa nyumba na ardhi yenye chakula.
\v 19 Hadadi alipata neema kubwa machoni pa Farao, kwa hiyoFarao akampatia mke, umbu wa mke wake mwenyewe, umbu la Tapenesi aliyekuwa Malkia.
\s5
\v 20 Naye huyo umbu la Tapenesi alimzalia Hadadi mwana. Wakamwita jina lake Genubathi. Tapenesi akamlea katika ikulu ya Farao. Kwa hiyo Genubathi alikulia kwenye ikulu ya Farao pamoja na watoto wa Farao.
\v 21 Naye alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kuwa Daudi alishalala na mababu zake na kwamba Yoabu mkuu wa majeshi alishakufa, Hadadi akamwambia Farao, "Acha niondoke nirudi nchini kwangu."
\v 22 Lakini Farao alimwambia, "Umepungukiwa nini kwangu, kwamba sasa unatafuta kurudi nchini kwako?" Naye Hadadi akamjibu, "Hapana kitu lakini tafadhali niache niende."
\s5
\v 23 Pia Mungu akamwinulia Sulemani adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyekuwa amemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba.
\v 24 Rezoni alijikusanyia wanaume naye akawa mkuu wa jeshi dogo, Daudi ali[owapiga wanaume wa Soba. Wale wanume Rezoni walienda Dameski kuishi huko, na Rezoni aliitawala Dameski.
\v 25 Yeye akawa adui wa Israeli katika siku zote za mfalme Sulemani, zaidi ya madhara ambayo Hadadi alisababisha. Rezoni akawachukia Israeli na akawa juu ya Shamu
\s5
\v 26 Kisha Yeroboamu mwana wa Nebati, mwefraimu wa Sereda, akida wa Sulemani, ambaye jina la mama yake lilikuwa Serua, mjane, pia akainua mkono wake dhidi ya mfalme.
\v 27 Kisa cha kuinua mkono wake kinyume cha mfalme ilikuwa ni mfalme Sulemani kujenga Milo na kufunga mahali palipobomoka katika mji wa Daudi baba yake.
\s5
\v 28 Yeroboamu alikuwa mtu hodari na shujaa. Sulemani akaona kuwa huyo kijana alikuwa na bidii, kwa hiyo akampa kuwa na mamlaka juu ya wafanyakazi katika nyumba ya Yusufu.
\v 29 Wakati huo, Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya Mshilo akamkuta barabarani. Sasa Ahiya alikuwa amevaa vazi jipya na kwamba hawa wawili walikuwa pekee yao kondeni.
\v 30 Kisha Ahiya akalishika lile vazi jipya ambalo alikuwa nalo na akalichana katika vipande kumi na viwili.
\s5
\v 31 Akamwambia Yeroboamu. "Chukua vipande kumi, kwani BWANA, Mungu wa Israeli, anasema, 'Tazama, Nitaugawa ufalme toka katika mkono wa Sulemani nami nitakupa makabila kumi.
\v 32 (lakini Sulemani atabaki na kabila moja, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na kwa ajili ya mji wangu Yerusalemu - mji ambao nimeuchagua toka kwenye kabila zote za Israeli),
\v 33 kwa kuwa ameniacha na kumwabudu Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, Kemoshi Mungu wa Wamoabu, na Milikomu mungu wa watu wa Amoni. Wameziacha njia zangu, hawakufanya kilicho chema katika macho yangu, wala hawa kuzishika amri na maagizo yangu, kama alivyofanya Daudi baba yake.
\s5
\v 34 Hata hivyo. Stauchukua ufalme wote toka kwenye mkono wa Sulemani. Badala yake, nimemfanya kuwa mtawala katika siku zake zote za uhai wake, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu ambaye nilimchagua, mtu ambaye alizishika amri na maagizo yangu.
\v 35 Bali nitauchukua ufalme ukiwa chini ya mkono wa mwanae na nitakupa wewe, makabila kumi.
\v 36 Nitampa kabila moja mwana wa Sulemani ili kwamba Daudi mtumishi wagu atabaki kuwa nuru mbele yangu huko Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua ili niweke jina langu.
\s5
\v 37 Nami nitakuchukua, nawe utatawala ili kutimiza haja yako, nawe utakuwa mfalme juu ya Israeli.
\v 38 Kama utasikiliza yote ninayokuagaza, na kama utatembea katika njia zangu na kufanya kinachopendeza mbele ya macho yangu, ukayashika maagizo na amri zangu, kama Daudi mtumishi wangu alivyofanya, ndipo nitakapokuwa na wewe na nitakujengea nyumba ya uhakika, kama niliyomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli.
\v 39 Nitawaadhibu uzao wa Daudi, lakini si milele."
\s5
\v 40 Kwa hiyo Sulemani akajaribu kumwua Yeroboamu. Lakini Yeroboamu akaamka na kukimbilia Misri, Kwa Shishaki mfalme wa Misri, naye akabaki Misri mpaka Sulemani alipokufa.
\s5
\v 41 Na kwa mambo mengine yanayomhusu Sulemani, Yote ambayo alifanya na hekima zake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya
\v 42 Sulemani? Sulemani alitawala Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
\v 43 Naye akalala na mababu zake na alizikwa katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu mwanae akawa mfalme mahali pake.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Israeli yote walikuwa wameenda Shekemu kumfanya awe mfalme.
\v 2 Ikatokea kuwa Yeroboamu mwana wa Nebati akayasikia haya (Kwa kuwa alikuwa bado yuko Misri, ambako alikuwa amekimbilia kumkwepa mfalme Sulemani), Kwani Yeroboamu alikuwa anaishi Misri.
\s5
\v 3 Kwa hiyo wakatuma watu kumwita, na Yeroboamu pamoja na mkutano wote wa Israeli wakaja wakamwambia Rehoboamu,
\v 4 Baba yako aliifanya nira yetu kuwa nzito. Sasa ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa nyepesi kuliko nira ngumu ambayo baba yako alituwekea, nasi tutakutumikia."
\v 5 Naye Rehobiamu akawaambia, "Ondokeni kwa siku tatu, kisha nirudieni." Kwa hiyo watu wakaondoka.
\s5
\v 6 Mfalme Rehoboamu akatafuta ushauri kwa wazee waliokuwa wamesimama mbele ya Sulemani baba yake wakati wa uhai wake, naye akasema, "mnanishauri niwajibuje hawa watu?"
\v 7 Nao wakamwambia, "Kama wewe utakuwa mtumishi wa hawa watu na akawatumikia, na akawapa majibu ya maneno mema, ndipo watakapokuwa watumishi wako daima."
\s5
\v 8 Lakini Rehoboamu akapuuzia ushauri aliopewa na wazee na akaenda kuomba ushauri kwa vijana ambao alikua pamoja nao wakasimama mbele yake.
\v 9 Akawaambia, "Mnanipa ushauri gani ili niweze kuwajibu hawa watu waliosema nami kwamba, 'ifanye nyepesi nira ambayo baba yako alituwekea'"
\s5
\v 10 Wale vijana waliokua pamoja na Rehoboamu wakamjibu, wakisema, "Waambie hawa watu kuwa baba yako Sulemani aliifanya nira yenu kuwa nzito lakini ninyi wenyewe mnaweza kuifanya rahisi. Uwaambie hivi, 'Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
\v 11 Kwa hiyo sasa, ingawa baba yangu aliwatwika kongwa zito, Mimi nitaiongeza kongwa lenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, Lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.'"
\s5
\v 12 Kwa hiyo siku ya tatu Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amewaelekeza aliposema, "mrudi kwangu siku ya tatu."
\v 13 Naye mfalme akawaambia wale watu kwa ukali na akapuuzia ushauri wa wale wazee ule waliokuwa wamempatia.
\v 14 Akawaambia akifuata ushauri wa wale vijana; akasema, "Baba yangu aliwatwika kongwa zito, lakini mimi nitaongeze kongwa lenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, mimi nitawaadhibu kwa nge."
\s5
\v 15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza wale watu, kwa kuwa ilikuwa zamu ya tukio lililoletwa na BWANA, ili kwamba aweze kulitimiza neno lake ambalo alikuwa amelisema kupitia Ahiya.
\s5
\v 16 Israeli yote ilipoona kuwa mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu wakimwambia, "Je, tuna sehemu gani kwa Daudi? Hatuna urithi kwa mwana wa Yese! Nenda kwenye hema zako, ewe Israeli. Sasa tazama kwenye nyumba yako, Daudi." Kwa hiyo Israeli akarudi kwenye hema zake.
\v 17 Lakini kwa watu wa Israeli waliokuwa wakiishi kwenye miji ya Yuda, Rehoboamu akawa mfalme juu yao.
\s5
\v 18 Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, lakini Waisraeli wote wakampiga kwa mawe wakamwua kwa mawe. Mflme Rehoboamu akakimbia haraka kwa gari lake kwenda Yerusalemu.
\v 19 Kwa hiyo Israeli wakawa wapinzani dhidi ya nyumba ya Daudi mpaka leo.
\s5
\v 20 Ndipo Israeli yote waliposikia kuwa Yeroboamu alikuwa amerudi, walimwita kwenye kusanyiko lao wakamweka kuwa mfalme wa Israeli. Hapakuwepo na mtu aliyeifuata familia ya Daudi, isipokuwa tu kabila la Yuda.
\s5
\v 21 Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akawakusanya wote wa nyumba ya Yuda na kabila la Benjamini; walichaguliwa wanaume wanajeshi180, 000 ili wapigane na nyumba ya Israeli, kwa lengo la kurudisha ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.
\s5
\v 22 Lakini neno la Mungu likamjia Shemaya, mtu wa Mungu; likisema,
\v 23 "Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na kwa nuymba yote ya Yuda na Benjamini, na kwa watu wote; uwaambie,
\v 24 "BWANA asema hivi, Usipigane wala kuwavamia ndugu zako watu wa Israeli. Kila mtu lazima arudi nyumbani kwake, kwa kuwa jambo hili nimelisababisha mimi." Kwa hiyo wakalisikiliza neno la BWANA na wakrudi nyumbani kwa njia zao na wakalitii neno lake.
\s5
\v 25 Kisha Yeroboamu akaijenga Shekemu katika nchi ya milima ya Efraimu, na akaishi huko. Akatoka huko na kuijenga Penueli.
\v 26 Yeroboamu akafikiri moyoni mwake, "Sasa ufalme utarudi kwenye nyumba ya Daudi.
\v 27 Kama hawa watu wataenda kutoa sadaka kwenye hekalu la BWANA kule Yerusalemu, basi mioyo ya hawa watu itarudi tena kwa bwana wao, kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda. Wataniua na kurudi kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda."
\s5
\v 28 Kwa hiyo mfalme Yeroboamu akatafuta ushauri na akafanya ndama wawili wa dhahabu; akawaambia watu, "Ni vigumu sana kwenu kwenda Yerusalemu. Tazameni, hawa ndiyo miungu yenu, Ee Israeli, iliyowatoa toka nchi ya Misri."
\v 29 Akamweka mmoja Betheli na mwingine Dani.
\v 30 Kwa hiyo jambo hili likawa dhambi. Watu wakaenda kwa huyo na wengine kwa hawa, mpaka huko Dani.
\s5
\v 31 Yeroboamu akajenga nyumba mahali pa juu na kufanya makuhani kutoka kwa watu wote, ambao hawakuwa wana wa Lawi.
\v 32 Yeroboamu akafanya sikukuu katika mwezi wa nane, katika siku ya kumi na tano ya mwezi, kama sikukuu ambayo iko Yuda, na akaenda juu kwenye madhabahu. Akafanya hivyo kule Betheli, akawatolea sadaka wale ndama aliokuwa amewatengeneza, na akaweka kuhani huko Betheli mahali pa juu alipokuwa amepatengeneza.
\s5
\v 33 Yeroboamu akapanda kwenda kwenye madhabahu ambayo aliitengeneza kule Betheli katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, ndio mwezi aliokuwa amefikiri katika akili yake; akafanya sikukuu kwa watu wa Israeli n a akaenda madhabahuni kufukiza uvumba.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Mtu wa Mungu alikuja tokea Yuda kwa neno la BWANA kule Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa amesimama karibu na madhabahu ili kufukiza uvumba.
\v 2 Akalia kinyume na zile madhabahu kwa neno la BWANA: "Ee madhabahu, madhabahu" hivi ndivyo asemavyo BWANA, 'Tazama, mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika familia ya Daudi, na juu yenu atawachinja makuhani ambao sasa wanafukiza uvumba mahali hapa pa juu kwa ajili yako. Juu yako watachoma mifupa ya watu.'"
\v 3 Kisha mtu wa Mungu akatoa ishara siku hiyohiyo, akisema, "Hii ndiyo isharaya kwamba BWANA amesema: 'Tazama, madhabahu zitavuunjika, na majivu yaliyo juu yatamwagika."
\s5
\v 4 Naye mfalme aliposikia kile mtu wa Mungu alichosema, kwamba amelia kinyume cha zile madhabahu kule Betheli, Yeroboamu akanyosha mkono wake kutoka madhabahuni, akisema, "mkamateni." Ndipo ule mkono aliokuwa ameunyosha dhidi ya mtu wa Mungu ukakauka, kiasi kwamba hakuweza kuurudisha mwenyewe.
\v 5 Na ile madhabahu ikavunjika vipande vipande, na yale majivu yakamwagika kutoka madhabahuni, kama ilivyokuwa imefafanuliwa kuwa ndiyo ishara ya kwamba mtu wa Mungu alikuwa amepewa kwa neno la BWANA.
\s5
\v 6 Mfalme Yeroboamu akajibu akimwambia mtu wa Mungu, "Msihi BWANA, Mungu wako akupe neema ili uniombee, ili kwamba mkono wangu urejee kwangu tena." Kwa hiyo mtu wa Mungu akamwomba BWANA, na mkono wa mfalme ukarejea katika hali yake tena, na ukawa kama ulivyokuwa mwanzoni.
\v 7 Yule mfalme akamwambia mtu wa Mungu, "twende nyumbani kwangu upate chakula, nami nitakupa zawadi."
\s5
\v 8 Yule mtu wa Mungu akamwambia mfalme, "Hata kama utanipa nusu ya miliki yako. staende na wewe, wala sitakula au kunywa maji mahali hapa,
\v 9 kwa sababu BWANA ameniamuru kwa neno lake, 'hutakula mkate wala kunywa maji, wala kurudi kwa njia ulioijia.'"
\v 10 Kwa hiyo mtu wa Mungu akaondoka na hakurudi nyumbani kwa njia aliyokuja nayo huko Betheli.
\s5
\v 11 Sasa kulikuwa na nabii mwingine mzee aliyekuwa akiishi Betheli, na mmoja wa wana wake akaja kumwambia mambo yote ambayo mtu wa Mungu amefanya siku hiyo kule Betheli. Wana wake wakamwambia pia maneno ambayo Yule mtu wa Mungu alimwambia mfalme.
\v 12 Baba yao akawaambia, "Alienda kwa njia gani?" Wale wanawe walikuwa wamemwona yule mtu wa Mungu kutoka Yuda njia aliyotumia kurudi.
\v 13 Kwa hiyo akawaambia wanawe, "Nitandikeni punda." Kwa hiyo wakamtandikia punda naye akampanda.
\s5
\v 14 Yule nabii mzee akamfuata yule mtu wa Mungu na akamkuta amekaa chini ya mti wa mwaloni; akamwambia, "Je, wewe ndiye mtu wa Mungu aliyetoka Yuda?" Naye akamjibu, "Mimi ndiye."
\v 15 Kisha yule nabii mzee akamwambia, "twende nyumbani kwangu ukale chakula."
\v 16 Yule mtu wa Mungu akamjibu, "Siwezi kurudi na wewe wala kuingia ndani na wewe, tena sitakula chakula wala kunywa maji pamoja na wewe mahali hapa,
\v 17 kwa sababu niliamuriwa hivyo kwa neno la BWANA, 'Hautakula chakula wala kunywa maji kule, wala kurudi kwa njia utakayokuja nayo.'"
\s5
\v 18 Kwa hiyo yule nabii mzee akamwambia, "Mimi pia ni nabii kama ulivyo, na malaika amesema na mimi neno la BWANA, akisema, 'Mrudishe aje na wewe katika nyumba yako, ili aweze kula chakula na kunywa maji.'" Lakini alikuwa anamdanganya mtu wa Mungu.
\v 19 Kwa hiyo yule mtu wa Mungu akarudi pamoja na yule nabii mzee na akala chakula nyumbani kwake na akanywa maji.
\s5
\v 20 Walipokuwa wamekaa mezani, neno la BWANA likamjia yule nabii aliyemrudisha,
\v 21 naye akalia kwa mtu wa Mungu aliyetoka Yuda, akisema "BWANA anasema, 'Kwa kuwa umeshindwa kutii nenola BWANA na umeshindwa kuishika amri ya BWANA ambayo Mungu wako alikupa,
\v 22 bali umerudi na umekula chakula na kunywa maji mahali ambapo BWANA alikwambia usile chakula wala kunywa maji, basi mwili wako hautazikwa kwenye makaburi ya baba zako.'"
\s5
\v 23 Baada ya kula chakula na kunywa maji, Yule nabii akatandika punda wa mtu wa Mungu, yule mtu aliyerudi naye.
\v 24 Baada ya mtu wa Mungu kuondoka, akakutana na simba njiani na kumwua barabarani, na mwili wake uliachwa barabarani. Na yule punda akasimama pembeni yake, na yule simba naye akasimama pembeni ya ule mwili.
\v 25 Watu walipopita na kuuona ule mwili umeachwa barabarani, na yule simba akisimama karibu na ule mwili, walikuja wakaeleza habari hiyo mjini kule ambako yule nabii mzee aliishi.
\s5
\v 26 Yule nabii aliyemrudisha toka njiani aliposikia, akasema, "Yeye mtu wa Muugu ndiye aliyeshindwa kutii neno la BWANA. Kwa hiyo BWANA alimtoa kwa simba, ambaye amemrarua katika vipande vipande na kumwua, kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limemwonya."
\v 27 Kwa hiyo yule nabii mzee akawaamnbia wanawe, akisema, "Tandikeni punda wangu," nao wakamtandikia.
\v 28 Akaenda akaukuta mwili umeachwa barabarani, punda na simba wamesimama pembeni ya ule mwili. Yule simba hakuula ule mwili, wala hakumshambulia yule punda.
\s5
\v 29 Yule nabii akauchukua ule mwili wa mtu wa Mungu, akaulaza juu ya punda, na akaurudisha. Akaja kwenye mji wake kuomboleza na kuuzika.
\v 30 Akaulaza mwili kwenye kaburi lake, nao wakamwombolezea, wakisema, "Aa! ndugu yangu!"
\s5
\v 31 Kisha baada ya kumzika, yule nabii mzee akawaambia wanawe, akasema, "Nitakapokufa, mtanizika kwenye kaburi ambalo tumemzika mtu wa Mungu. Mtalaza mifupa yangu pembeni mwa mifupa yake.
\v 32 Kwa kuwa ule ujumbe uliosemwa na BWANA, dhidi ya madhabahu kule Betheli na dhidi ya nyumba zote za mahali pa juu katika mji wa Samaria, hakika yatatokea.
\s5
\v 33 Baada ya haya Yeroboamu hakuuacha uovu wake, aliendelea kuchagua makuhani wa kawaida kwa ajili ya mahali pa juu kutoka kwa watu wa kila aina. Yeyote ambaye angeweza kutumika alimtakasa kuwa kuhani.
\v 34 Jambo hili likawa dhambi kwenye familia ya Yeroboamu na kusababisha familia yake kuangamizwa na kuondolewa kabisa katika uso wa dunia.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Wakati huo Abiya mwana wa Yeroboamu akawa mgonjwa sana.
\v 2 Yeroboamu akamwambia mke wake, "amka ujibadilishe, ili wasikutambue kuwa wewe ndiye mke wangu, na uende Shilo, kwa sababu nabii Ahiya yuko huko, yeye ndiye aliyeninea mimi kuwa nitakuwa mfalme juu ya watu hawa.
\v 3 Uchukue mikate kumi, na kaki na mtungi wa asali, na uende kwa Ahiya. Naye atakuambia kitakachotokea kwa mtoto."
\s5
\v 4 Mke wa Yeroboamu akafanya hivyo; akaenda Shilo mpaka kwenye nyumba ya Ahiya. Wakati huo Ahiya alikuwa hawezi kuona, kwa kuwa macho yake yalikuwa yameishiwa nguvu kwa sababu ya umri wake.
\v 5 BWANA akamwambia Ahiya, "Tazama mke wa Ahiya anakuja kutafuta kutaka ushauri toka kwako kuhusiana na mwanae, kwa kuwa ni mgonjwa. Mwambie hivi na hivi, kwa sababu atakapofika atajifanya kuwa ni mwanamke mwingine."
\s5
\v 6 Naye Ahiya aliposikia sauti za miguu yake alipokuwa akiukaribia mlango, akasema, "karibu, mke wa Yeroboamu. Kwa nini unajifanya kuwa mtu mwingine? Nimetumwa kwako nikiwa na habaari mbaya.
\v 7 Nenda ukamwambia Yeroboamu kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, anasema, 'Nilikuinua kutoka kati ya watu na kukufanya uwe kiongozi wa watu wangu Israeli.
\v 8 Niliugawa ufalme kutoka kwa Daudi na kukupa wewe, lakini bado hutaki kuwa kama mtumishi wangu Daudi, ambaye alizishika amri zangu na kunifuata kwa moyo wake wote, na kufanya kilichokuwa sawa mbele ya macho yangu.
\s5
\v 9 Badala yake, umefanya maovu, zaidi ya wote waliokutangulia. Umetengeneza miungu mingine, na umetengeneza sanamu za kuyeyushwa ili kunikasirisha na kunitupa nyuma yako.
\v 10 Kwa hiyo, tazama, Nitaleta majanga kwenye familia yako; Nitawatupilia mbali watoto wako wote wa kiume katika Israeli, kama ni mtumwa au ni huru, na nitaiondoa familia yako, kama mtu anayechoma mavi mpaka yaishe.
\s5
\v 11 Yeyote ambaye ni mwanafamilia yako atakayefia mjini ataliwa na mbwa, na yeyote atakayefia shamabani ataliwa na ndege wa angani, kwa kuwa Mimi BWANA, nimesema;
\v 12 Kwa hiyo inuka wewe mke wa Yeroboamu, na uende nyumbani kwako; na mguu wako utakapokanyaga mjini, yule mtoto wa Abiya atakufa.
\v 13 Na Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Ni yeye pekee katika familia ya Abiya atakayepelekwa makaburini, kwa sababu ni yeye pekee yake kutoka kwenye nyumba ya Abiya, ambaye BWANA, Mungu wa Israeli alimwona kuwa ni mwema.
\s5
\v 14 Pia BWANA atainua mfalme katika Israeli ambaye ataifutilia mbali familia ya Yeroboamu katika siku hiyo. Leo ndiyo siku hiyo, sasa hivi.
\v 15 Kwa kuwa BWANA ataishambulia Israeli kama vile majani yanavyotikiswa majini, na ataing'oa Israeli katika nchi hii njema ambayo aliwpa mababu. Atawatawanya hata ng'ambo ya Mto Frati, kwa sababu wamefanya nguzo za Ashera kumkasirisha BWANA.
\v 16 Ataiacha Israeli kwa sababu ya dhambi ya Yeroboamu, dhambi ambazo ametenda, na kwa hizo ameifanya Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 17 Kwa hiyo mke wa Yeroboamu akainuka na akaondoka na akaenda mpaka Tirza. Naye alipofika kizingitini kwa nyumba yake, yule mtoto akafa.
\v 18 Isareli wote wakamzika na kumwombolezea, kama vile alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA ambalo amelisema kupitia mtumishi wake nabii Ahiya.
\s5
\v 19 Na kwa mambo mengine yanayOmhusu Yeroboamu, jinsi alivyopigana vita na jinsi alivyotawala, tazama yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\v 20 Yeroboamu alitawala kwa miaka ishirini na mbili naye akalala na babu zake, na Nadabu mwanawe akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 21 Sasa Rehoboamu mwana wa Sulemani alikuwa mtawala wa Yuda. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipokuwa mfalme, na akatawala kwa miaka kumi na saba kule Yerusalemu, mji ambao BWANA alikuwa ameuchagua kati ya makabila yote ya Israeli ili aweke jina lake kule. Jina la mama yake alikuwa Naama Mwamori.
\v 22 Yuda ikafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA; wakamtia wivu kwa makosa yao, zaidi ya yote ambayo baba zao walikuwa wamefanya
\s5
\v 23 Kwa kuwa walijijengea wenyewe mahali pa juu, nguzo za mawe, na nguzo za Ashera katika kila mahali pa juu na katika kila mti wenye majani mabichi.
\v 24 Pia kulikuwepo na ukahaba wa kipagani katika nchi. Walifanya machukizo yaleyale kama wa mataifa yale ambayo BWANA alikuwa amewafukuza kutoka kwa watu wa Israeli.
\s5
\v 25 Ilitokea wakati wa mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu wakati Shishaki akiwa mfalme wa Misri, akaja kinyume na Yerusalemu.
\v 26 Akaichukua hazina iliyokuwa kwenye nyumba ya BWANA, na ile hazina iliyokuwa kwenye nyumba ya Mfalme. Akachukua kila kitu; Pia alizichukua zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa ametengeneza.
\s5
\v 27 Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake na akazikabidhi kwa wakuu wa walinzi, ambao walilinda malango ya kuingia kwa mfalme.
\v 28 Na ikawa kila mfalme alipoingia kwenye nyumba ya BWANA, wale walinzi walizibeba na baadaye walizirudisha katika chumba cha walinzi.
\s5
\v 29 Lakini katika mambo mengine kuhusiana na Rehoboamu, na yote yale aliyofanya, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 30 Kulikuwa na mapigano yasiyokoma kati ya nyumba ya Rehoboamu na nyumba ya Yeroboamu.
\v 31 Kwa hiyo Rehoboamu akalala na mababu zake naye akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi Jina la mama yake alikuwa Naama Mwamori. Abiya mwanawe akawa mfalme mahali pake
\s5
\c 15
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na tano wa mfame Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu yaYuda.
\v 2 Alitawala kwa miaka mitata kule Yerusalemu. Jina la mama yake allikuwa Maaka. Alikuwa binti wa Absalomu.
\v 3 Naye alitembea katika dhambi zote ambazo baba yake alizifanya kabla yake; moyo wake haukuwa mkalifu kwa BWANA, Mungu wake kama moyo wa Daudi, babu yake ulivyokuwa.
\s5
\v 4 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake alimpa taa Yerusalemu kwa kumwinua mwanae baada yake ili kuiimarisha Yerusalemu.
\v 5 Mungu alifanya haya kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pake; wakati wote wa uhai wake, hakugeuka wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, isipokuwa tu swala la Uria Mhiti.
\v 6 Sasa kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Jeroboamu katika siku zote za maisha ya Abiya.
\s5
\v 7 Kwa mambo mengine ya Abiya, yote aliyofanya, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Sasa kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
\v 8 Abiya akalala na mababu zake, nao wakamzika katika mji wa Daudi. Asa mwanae akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 9 Katika mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akaanza kutawala Yuda.
\v 10 Alitawala kwa miaka arobaini na moja kule Yerusalemu. Bibi yake alikuwa Maaka, binti wa Absalomu.
\v 11 Asa akafanya yaliyo mema machono mwa BWANA, kama alivyofanya Daudi, babu yake.
\s5
\v 12 Yeye aliwafukuza kutoka katika nchi wale makahaba wa kipagani na akaziondoa sanamu zote ambazo babu zake walikuwa wametengeneza.
\v 13 Pia alimwondoa bibi yake asiwe Malkia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera. Asa aliikata sanamu ya kuchukiza na kuiteketeza katika Bonde la Kidroni.
\s5
\v 14 Lakini pale mahali pa juu hapakuchukuliwa. Hata hivyo. Moyo wa Asa ulikuwa mkamilifu mbele ya BWANA katika siku zake zote.
\v 15 Alivirerjesha katika nyumba ya BWANA vitu vile vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya BWANA, na vile vitu vyake vilivyokuwa vimetengezwa kwa fedha, na dhahabu na vyombo.
\s5
\v 16 Basi kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli, kwa miaka yao yote.
\v 17 Baasha mfalme wa Israeli, akaivamia na kuijenga Rama, kiasi kwamba hakumruhusu yeyote kuondoka au kuingia katika nchi ya Asa mfalme wa Yuda.
\s5
\v 18 Kisha Asa akazichukua zile fedha na dhahabu zilizokuwa zimebaki kwenye hazina kwenye nyumba ya BWANA, na katika hazina ya ikulu ya mfalme. Akaziweka katika mikono ya watumishi wake na kuzituma kwa Beni Hadadi mwana wa Tabrimoni mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu ambaye alikuwa akishi Dameski. Akamwambia,
\v 19 "Naomba tufanye patano kati yangu na wewe, kama ilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, Nimekutumia zawadi ya fedha na dhahabu. Ili uvunje agano lako na Baasha mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache."
\s5
\v 20 Beni Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma wakuu wa majeshi yake, nao wakaishambulia miji ya Israeli. Wakaishambulia Ijoni, Dani, Abeliya Bethi Maaka, na Kinerothi yote, pamoja na nchi yote ya Naftali.
\v 21 Ikawa Baasha aliposikia haya, akaacha kuijenga Rama akarudi Tirza.
\v 22 Kisha mfalme Asa akaitangazia Yuda yote. Hakuna aliyeachwa. Wakayabeba mawe na miti ya Rama ambayo Baasha alikuwa akijengea mji. Kisha mfalme Asa akavitumia hivyo vitu kuijenga Geba ya Benjamini na Mispa.
\s5
\v 23 Mambo mengine yanyohusu utawala wa Asa, uwezo wake wote, yote aliyofanya, na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Lakini wakati wa uzee wake alipata ugonjwa wa miguu.
\v 24 Kisha Asa akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Yehoshafati mwanae akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 25 Nadabu mwana wa Yerobiamu alianza kutawala huko Israeli wakati wa mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda; Aliitawala Israeli kwa miaka miwili.
\v 26 Akafanya yaliyo maovu mbele y a macho ya BWANA naye akatembea katika njia ya baba yake, na katika dhambi yake, aliisababisha Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 27 Baasha mwana wa Ahiya, wa familia ya Isakari, akafanya hila dhidi ya Nadabu; Baasha akamwua huko Gibethoni, ambao ulikuwa mji wa Wafilisti, kwa kuwa Nadabu na Israeli walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.
\v 28 Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha alimwua Nadabu naye akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 29 Mara tu baad ya kuwa mfalme, Baasha aliwaua watu wote wa familia ya Yeroboamu. Hakumwacha hata mmoja wa uzao wa Yeroboamu awe hai; Kwa njia hii akawa ameuharibu ukoo wote wa kifalme, kama vile BWANA alivyokuwa amesema kupitia mtumishi wake Ahiya Mshilo,
\v 30 kwa sababu ya dhambi za Yeroboamu ambazo alifanya na akaisababishia Israeli kufanya dhambi, kwa kuwa alimkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli.
\s5
\v 31 Mambo mengine yanayomhusu Nadabu, na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 32 Kisha kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli katika siku zao zote.
\s5
\v 33 Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kuitawala Israeli yote huko Tirza naye alitawala kwa miaka ishirini na nne.
\v 34 Naye akafanya yaliyo mabaya katika macho ya BWANA na akatembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi yake ambayo kwa hiyo aliifanya Israeli kufanya dhambi.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Neno la BWANA lilimjia Yehu mwana wa Hanani kinyume cha Baasha, likisema,
\v 2 Ingawa Nilikuinua kutoka kwenye mavumbi na kukufanya kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli, Lakini umetembea katika njia za Yeroboamu na umewafanya watu wangu Israeli kufanya dhambi, ili kunikasirisha dhidi ya dhambi zao.
\s5
\v 3 Tazama, Nitamfagia kabisa Baasha na familia yake na nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati.
\v 4 Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani."
\s5
\v 5 Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 6 Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 7 Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.
\s5
\v 8 Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.
\v 9 Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.
\v 10 Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 11 Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.
\v 12 Kwa hiyo Zimri aliingamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,
\v 13 kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi c ha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.
\s5
\v 14 Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\s5
\v 15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.
\v 16 Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika lilksema, "Zimri amepanga njama na amemwua mfalme." Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.
\v 17 Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.
\s5
\v 18 Kwa hiyoZimri alipoona kuwa mji umetekwa, akaingia kwenye ngome na akaivamia ikulu ya mfalme na kulichoma moto jengo lote pamoja na yeye; kwa hiyo akafa kwa moto.
\v 19 Hii ilikuwa ni kwa sababu ya dhambi alizofanya kwa kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, kwa kutembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi ambazo alifanya, kiasi cha kuifanya Israeli wafanye dhambi.
\v 20 Pia kwa mambo mengiine yanayomhusu Zimri, na fitina yake aliyofanya, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\s5
\v 21 Sasa watu wa Israeli walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. Nusu ya watu walimfuata Tibni mwana wa Ginathi, wakamfanya kuwa mfalme, na Nusu walimfufata Omri.
\v 22 Lakini watu waliomfuata Omri walikuwa na nguvu kuliko wale waliomfuata Tibni mwana wa Ginathi. Kwa hiyo Tibni akafa, na Omri akawa mfalme.
\s5
\v 23 Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa mfalme wa Yuda, naye akatawala miaka kumi na miwili. Alitawala akiwa Tirza kwa miaka sita.
\v 24 Akakinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa kilo 68 za fedha. Akajenga mji juu ya mlima na ule mji akauita Samaria, kwa sababu ya jina la Shemeri, mmiliki wa awali wa kile kilima.
\s5
\v 25 Omri akafanya maovu mbele ya BWANA na akafanya yaliyo maovu zaidi kuliko wale waliokuwa kabla yake.
\v 26 Kwa kuwa alitembea katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake ambazo kwa hizo aliwaongoza Waisraeli kufanya dhambi, ili kumkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli, ili kuwa na hasira juu ya sanamu zao za ubatili.
\s5
\v 27 Kwa mambo mengine yanayomhusu Omri ambayo alfanya, na nguvu zake alizoonyesha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 28 Kwa hiyo Omri akalala na mababu zake na akazikwa Samaria na Ahabu mwanae akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 29 Katika mwaka wa thelathiini na nane wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akaanza kutawala juu ya Israeli. Ahabu mwana wa Omri akatawala Israeli kule Samaria kwa miaka ishirini na mbili.
\v 30 Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo maovu mbele ya BWANA, zaidi ya wote waliokuwa kabla yake.
\s5
\v 31 Ikawa kidogo tu Ahabu ayaendee makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa hiyo akamwoa Yezebeli binti wa Ethibaali, mfalme wa Wasidoni; akaenda akamwabudu baali na akamsujudia.
\v 32 Akamjengea madhabahu Baali, ambayo alikuwa ameijenga kule Samaria.
\v 33 Ahabu akatengeneza Ashera. Ahabu akafanya maovu zaidi kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Isareli, akamkasirisha kuliko wafalme wote wa Israeli waliokuwa kabla yake.
\s5
\v 34 Katika siku zake Hieli Mbetheli aliijenga tena Yeriko. Akaijenga misingi ya mji kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, naye akayajenga malango ya mji kwa kufiwa na mwanae mdogo Segebu, na walifanya hivi kwa sababu walitii neno la BWANA, ambalo alikuwa amelinena kwa kinywa cha Joshua mwana wa Nuni.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Eliyas Mtishibi, kutoka Tishibi ya Gileadi, akamwambia Ahabu, "Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninasimama, hakutakuwa na umande wala mvua isiipokuwa kwa neno langu."
\s5
\v 2 Kisha nenola BWANA, likammjia Eliya, likisema,
\v 3 "Ondoka hapa uende mashariki; ukajifiche karibu na kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yorodani.
\v 4 Nawe utakunywa maji ya kijito, na nimewaamuru kunguru kukulisha mahali hapo."
\s5
\v 5 Kwa hiyo Eliya akaenda kama neno la BWANA lilivyomwamuru. Akaenda kuishi karibu na kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yorodani.
\v 6 Nao kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji ya kijito kile.
\v 7 Lakini baada ya muda kile kijito kikakauka kwa sababu hapakuwepo na mvua katika nchi.
\s5
\v 8 Neno la BWANA likamjia, likisema,
\v 9 "Inuka, uende Sarepta, ambao ni mji wa Sidoni, na ukaishi huko. Tazama nimemmwamuru mjane kukulisha."
\v 10 Kwa hiyo akainuka na akaenda Sarepta, na alipofika kwenye lango la mji, kulikuwa na mjane akiokota kuni. Kwa hiyo akamwita na akamwambia, "Tafadhali niletee maji kidogo kwenye jagi ninywe."
\s5
\v 11 Naye alipokuwa akienda kuleta maji alimwita, akamwambia, "tafadhali uniletee na kipande cha mkate mkononi."
\v 12 Naye akamjibu, "Kama BWANA Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, bali konzi moja ya unga katika chombo na mafuta kidogo kwenye chupa. Tazama, ninaokota kuni mbili ili niende kupika kwa ajili yangu na mwanangu, ili tule, na tusubiri kufa."
\v 13 Eliya akamwambia, "Usiogope. Nenda ukafanye kama usemavyo. lakini nitengenezee kwanza mimi na uniletee. Ndipo baadaye ujitenegenezee wewe na mwanao.
\s5
\v 14 Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli anasema 'Lile pipa la unga halitaisha, wala ile chupa ya mafuta kukoma kutoa mafuta, mpaka siku ile BWANA atakapotuma mvua duniani."
\v 15 Kwa hiyo yule mjane akafanya kama Eliya alivyomwelekeza, yeye, na Eliya, na mwanae wakala kwa siku nyingi.
\v 16 Lile pipa la Unga halikuisha, wala ile chupa ya mafuta haikukoma kutoa mafuta, kama vile neno la BWANA lilivyosema, kupitia kinywa cha Eliya.
\s5
\v 17 Baada ya hayo mambo, yule mwana wa yule mwanamke, yule mwanamke mwenye nyumba, aliugua. Ugonjwa wake ukazidi hata akaishiwa pumzi kabisa.
\v 18 Kwa hiyo mama yake akamwambia Eliya, "Je, una nini nami, ewe mtu wa Mungu? Je, umekuja kwangu ili kunikumbusha dhambi zangu na kumwua mwanangu?"
\s5
\v 19 Naye Eliya akamjibu, "Nipe hapa mwanao." Akambeba mtoto mikononi mwake na akampeleka mpaka chumbani alimokuwa akikaa, akamlaza yule mtoto kitanadani pake mwenyewe.
\v 20 Akamlilia BWANA akisema, "BWANA Mungu wangu, kwa nini umeleta majanga kwa mjane ambaye mimi ninakaa, kwa kumwua mwanae?"
\v 21 Kisha Eliya akajinyosha mwenyewe juu ya mtoto mara tatu; akamlilia BWANA akisema, "BWANA Mungu wangu, Ninakuomba, tafadhali uhai wa mtoto huyu umrudie."
\s5
\v 22 BWANA akaisikiliza sauti ya Eliya; uhai wa mtoto ukamrudia, na akawa hai.
\v 23 Eliya akamchukua mtoto na akamtoa toka chumbani kwake akamleta kwenye ile nyumba; akampatia mama yake yule mtoto na akasema, "Tazama, mwanao yuko hai."
\v 24 Yule mwanamke akamwambia Eliya, "Sasa natambua kuwa wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la BWANA kinywani mwako ni la kweli."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Kwa hiyo baada ya siku nyingi neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu wa ukame, likisema, "Nenda ukajionyeshe mwenyewe kwa Ahabu nami nitainyeshea ardhi mvua."
\v 2 Eliya akaenda kujionyesha mwenyewe kwa Ahabu; sasa njaa ilikuwa kali sana kule Samaria.
\s5
\v 3 Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa mkuu wa ikulu. Obadia alimheshimu sana BWANA,
\v 4 kwa kuwa wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alichukua manabii mia akawaficha katika makundi ya hamsini hamsini katika pango na akawalisha kwa mikate na maji.
\s5
\v 5 Ahabu akamwambia Obadia, "Pita katika nchi yote na katika chemichemi zote za maji na vijito. Yamkini tunaweza kupata maji na nyasi ili tuwaokoa hawa farasi na nyumbu, ili tusiwakose wanyama wote."
\v 6 Kwa hiyo wakaigawa nchi kati yao ili wapite kati yake wakitafuta maji. Ahabu akaenda njia yake mwenyewe na Obadia naye akaenda njia yake.
\s5
\v 7 Wakati Obadia akiwa njiani, akakutana na Eliya pasipo kutegemea. Obadia akamtambua na akalala kifudifudi chini. Akamwambia, "Ndiye wewe, bwana wangu Eliya?"
\v 8 Naye Eliya akamjibu, Ni mimi. Nenda umwambie bwana wako, 'Tazama, Eliya yuko hapa.'"
\s5
\v 9 Obadia akamjibu. "Nimekoseaje, kwamba umtoe mtumishi wako katika mkono wa Ahabu ili aniue?
\v 10 Kama BWANA Mungu wako aishivyo, hakuna taifa wala ufalme ambapo bwana wangu hajatuma watu kukutafuta. Kila taifa au ufalme unaposema, "Eliya hayuko hapa,' Ahabu hufanya waape ni kweli hawajakuona.
\v 11 Na sasa wewe unasema, 'Nenda, ukamwambie bwana wako kwamba Eliya yuko hapa.'
\s5
\v 12 Mara tu baada ya kukuacha Roho wa BWANA atakuchukua na kukupeleka mahali ambapo sitapajua. Kisha nikienda na kumwambia Ahabu, na asipokuona, ataniua. Bado, mimi, mtumishi wako, nimekuwa nikimwabudu BWANA kutoka ujana wangu.
\v 13 Je, haujaambiwa, bwana wangu, nilichokifanya wakati Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, jinsi nilivyowaficha wale manabii mia moja wa BWANA katika makundi ya hamsini kwenye pango na kuwalisha kwa mikate na maji?
\s5
\v 14 Na sasa unasema, 'Nenda umwambie bwana wako kwamba Eliya yuko hapa,' kwa hiyo ataniua."
\v 15 Ndipo Eliya alipomjibu, "Kama vile BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye mimi ninasimama, Kwa hakika nitajionyeshakwa Ahabu leo."
\s5
\v 16 Kwa hiyo Obadia akaenda kukutana na Ahabu, nakumwambia kile Eliya alichokuwa amemwambia. Ndipo mfalme alipoenda kukutana na Eliya.
\v 17 Ahabu alipomwona Eliya, akamwambia, "Je, ni wewe? Wewe mtabishaji wa Israeli!"
\s5
\v 18 Eliya akamwambia, "Mimi sijaitabisha Israeli, Lakiini wewe na familia ya baba yako ndio watabishaji kwa kuziacha amri za BWANA na kufuata sanamu za Baali.
\v 19 Kwa hiyo sasa, Tuma neno na unikusanyie Israeli yote katika mlima Kameli, pamoja na manabii 450 wa Baali na wale manabii 400 wa Ashera wanaokula kwenye meza ya Yezebeli."
\s5
\v 20 Kwa hiyo Ahabu akatuma neno kwa watu wote wa Israeli na akawakusanya manabii wote kwenye mlima Kameli.
\v 21 Eliya akaja karibu na watu wote akasema, "Mtaendelea kubadilisha mawazo yenu mpaka lini? Kama BWANA ni Mungu, mfuateni yeye, Lakini kama Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye," Lakini watu hawakumjibu neno.
\s5
\v 22 Kisha Eliya akawaambia wale watu, "Mimi, pekee yangu, ndiye niliyebaki kuwa nabii wa BWANA, lakini manabii wa Baali wako 450.
\v 23 Hebu tutoleeni ng'ombe wawili. Nao wajichagulie ng'ombe mmoja na wamchinje na kumkatakata katika vipnde, na wamweke kwenye kuni, na wasitie moto chini yake. Nami nitamwandaa yule wa pili na kumweke juu ya kuni nami sitatia moto chini yake.
\v 24 Kisha mtaliita jina la mungu wenu, nami nitaliita jina la BWANA, na Mungu atakayejibu kwa moto, huyo ndiye Mungu." Watu wote wakajibu na kusema, "Hilo ni jambo jema."
\s5
\v 25 Kwa Eliya akawaambia manabii wa Baali, "Chagueni ng'ombe mmoja kwa ajili yenu na mwe wa kwanza kumwamdaa, kwa kuwa ninyi ni wengi, Kisha liiteni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto."
\v 26 Nao wakamchukua yule ng'ombe waliokuwa wamepewa na wakamwandaa, na ndipo walipoliita jina la Baali kuanzia asubuhi hadi adhuhuri, wakisema, "Baali, tusikie." Lakini hapakuwepo na Sauti, na wala hakuna aliyejibu. Wakachezacheza kuizunguka madhabahu waliyotengeneza.
\s5
\v 27 Ilipofika adhuhuri Eliya akawakejeli akisema, "Mwiteni kwa nguvu! Huyo ni mungu! labda anawaza kitu, au amepumzika, au yuko safarini, au pengine amelala sharti aamshwe."
\v 28 Kwa hiyo wakamwita kwa nguvu, wakajikatakata kama kawaida yao ilivyokuwa, kwa upanga na nyembe, mpaka damu ikawachuruzika.
\v 29 Ikawa wakati wa adhuhuri ulipopita, na bado walikuwa wakiendelea kutabiri mpaka wakati wa jioni wa kutoa dhabihu, lakini hapakuwepo na sauti wala mtu wa kuwajibu; wala hapakuwepo na yeyote wa kujibu wala wa kuangalia.
\s5
\v 30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, "Nisogeleeni," na watu wote wakamsogelea. Naye akatengeneza ile madhabahu ya BWANA ambayo ilikuwa imeharibika.
\v 31 Eliya akachukua mawe kumi na mawili, kila jiwe moja liliwakilisha kabila moja la wana wa Yakobo - ni kupitia Yakobo kwamba neno la BWANA lilikuja, likisema, "Jina lako litakuwa Israel."
\v 32 Kwa kutumia hayo mawe aliijenga ile madhabahu kwa jina la BWANA na akachimba mfereji kuizunguka ile madhabahu kubwa kiasi cha kubeba lita kumi na tano za maji.
\s5
\v 33 Kisha akaweka kuni kwa ajili ya moto na akamkatakata yule ng'ombe katika vipande vipande na akaweka vile vipande juu ya kuni. Na akasema, "Vijazeni maji hivyo vyombo na yamwageni kwenye hiyo sadaka ya kueketezwa na juu ya hizo kuni."
\v 34 Akasema tena fanyeni hivyo mara ya pili," nao wakafanya kwa mara ya pili. kisha akasema, "Fanyeni mara ya tatu," nao wakafanya kwa mara ya tatu.
\v 35 Maji yakaizunguka ile madhabahu na kuujaza ule mfereji.
\s5
\v 36 Ikawa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea na akasema, "BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako, na kwamba nimeyafanya mambo haya yote kwa jina lako.
\v 37 Nisikie, BWANA, nisike, ili hawa watu wajue kuwa wewe, BWANA, ndiye Mungu, na kwamba umeirudisha mioyo yao kwako tena."
\s5
\v 38 Ndipo moto wa BWANA ukashuka ukairamba ile sadaka, pamoja na zile kuni, mawe na mavumbi, na kuyaramba yale maji yaliyokuwa kwenye ule mfereji.
\v 39 watu wote walipoona haya, wakalala kifudifudi chini wakasema, "BWANA, ndiye Mungu! BWANA ndiye Mungu!
\v 40 Kwa hiyo Eliya akawaambia, "Wakamateni manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja wao atoroke." Kwa hiyo wakawakamata, na Eliya akawaleta manabii wa Baali chini kwenye kijito cha Kishoni na akawaua huko.
\s5
\v 41 Eliya akamwambia Ahabu, "Inuka, ule na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa."
\v 42 Kwa hiyo Ahabu akaenda akala na knywa. Kisha Eliya akaenda juu ya mlima Kameli, akasudu chini na akaweka uso wake katikati ya magoti.
\s5
\v 43 Akamwambia mtumishi wake, "Nenda sasa, utazame upande wa bahari." mtumishi wake akaenda na akasema, "Hakuna kitu," Eliya akamwambia, "Nenda tena, mpaka mara saba."
\v 44 Ile mara ya saba mtumishi wake akasema, "Tazama, kuna wingu linapanda kutoka baharini, ni dogo kama mkono wa mtu." Eliya akamjibu, Nenda ukamwambie Ahabu, 'Andaa gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.'"
\s5
\v 45 Ikatokea baada ya muda mfupi mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, na kulikuwa na mvua kubwa. Ahabu akapanda gari akaenda zake Yezreeli,
\v 46 lakini mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya. Akalikaza vazi lake kwa mshipi wake na akakimbia mbele ya Ahabu kwenye lango la Yezreeli.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ahabu akamwambia Yezebeli mambo yote ambayo Eliya amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.
\v 2 Ndipo Yezebeli alipotuma mjumbe kwa Eliya, akisema, "miungu wanifanye hivyo na mimi, na zaidi yake, kama kesho muda kama huu sitayafanya maisha yako kuwa kama mmoja wa hao manabii waliokufa."
\v 3 Eliya aliposikia hayo, akaiinuka na akakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake akaja mpaka Beerisheba, ambao ni mji wa Yuda, na akamwacha mtumishi wake huko.
\s5
\v 4 Lakini yeye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja huko jangwani, akaja akakaa chini ya mti wa mretemu. Akajiombea mwenyewe kufa, akasema, "Sasa yatosha, BWANA, ichukue roho yangu, kwa kuwa mimi si mzuri kuliko mababu zangu waliokufa."
\v 5 Kwa hiyo akalala chini ya mretemu. Ghafula malaika akamgusa na akamwambia, "Inuka ule."
\v 6 Eliya akatazama, karibu na kichwa chake kulikuwa na mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa na gudulia la maji. Kwa hiyo akala na kunywa na kulala tena.
\s5
\v 7 Malaika wa BWANA akaja tena mara ya pili akamgusa na kumwambia, "Inuka ule, kwa sababu safari bado ndefu kwako."
\v 8 Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
\s5
\v 9 Akaingia kwenye pango akakaa humo. Kisha neno la BWANA likamjia likimwambia, "Unafanya nini hapa, Eliya?"
\v 10 Eliya akajibu, "Nimeona wivu mwingi kwa BWANA, Mungu wa majeshi, kwa kuwa watu wa Israeli wameliacha agano lako, wameziharibu madhabahu zako, na wamewaua manabii wako kwa upanga. Sasa ni mimi, pekee yangu, nimebaki na wanataka kuichukua roho yangu.
\s5
\v 11 BWANA akamwambia, "Nenda nje ukasimame kwenye mlima mbele yangu." Kisha BWANA akapita, na upepo mkali ukaupiga mlima ukavunja miamba katika vipande vipande mbele ya BWANA, lakini BWANA hakuwemo kwenye huo mlima. Kisha baada ya upepo, tetemeko lakaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye hilo tetemeko.
\v 12 Kisha baada ya tetemeko, moto ukaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye moto. Ndipo baada ya moto, sauti ya upole ikaja.
\s5
\v 13 Naye Eliya alipoisikia sauti, akafunika uso wake kwa vazi lake, akatoka nje, akasimama kwenye lango la hilo pango. Na sauti ikaja kwake ikisema, "unafanya nini hapa?,
\v 14 Eliya akajibu, "nimeona wivu sana kwa ajili ya BWANA, Muungu wa majeshi, kwa kuwa watu wa Israeli wameliacha agano lako, wamezihariibu madhabahu zako, na wamewaua manabii kwa upanga. Sasa, ni mimi pekee yangu, nimebaki na wanajaribu kuichukua roho yangu."
\s5
\v 15 Kisha BWANA akamwambia, "Nenda, rudi kwa njia yako kwenye jangwa la Dameski, na utakapofika utamtia mafuta Hazaeli awe Mfalme wa Shamu,
\v 16 na utamtia mafuta Yehu mwana wa Nimshi kuwa mfalme wa Israeli, na utamtia mafuta Elisha mwana wa Shafeti wa Abeli Mehola kuwa nabii mahali pako.
\s5
\v 17 Itakuwa hivi Yehu atamwua kila mmoja atakayejaribu kutoroka upanga wa Hazaeli, na kwamba Elisha atamwua kila atakayejaribu kukwepa upanga wa Yehu.
\v 18 Lakini nitawaacha watu elfu saba katika Israeli kwa ajili yangu, ambao magoti yao hayajawahi kupigwa kwa Baali, na ambao midomo yao haijambusu."
\s5
\v 19 Kwa hiyo Eliya akaondoka mahali pale na akamkuta Elisha mwana wa Shafati, akilima na jozi za makisai kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa akilima na ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akaenda mpaka kwa Elisha akamtupia vazi lake juu yake.
\v 20 Elisha naye akawaacha wale makisai akamkimbilia Eliya; akamwambia, "Tafadhali naomba nikambusu baba yangu na mama yangu kisha nitakufuata." Naye Eliya akamwambia, "Rudi, lakini fikiria juu ya kile nilichokufanyia."
\s5
\v 21 Kwa hiyo Elisha akarudi toka kwa Eliya na akachukua ile jozi ya makisai, akawaua wale wanyama, na akapika ile nyama kwa kuni za ile nira. Kisha akawapa watu wakala. Kisha akaamka, akamfuata Eliya akamtumikia.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Beni Hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote pamoja. Kulikuwa na wafalme thelathini na mbili wasaidizi pamoja naye, na magari na farasi. Akapanda, akaihusuru Samaria na kupigana nayo.
\v 2 Akatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, akamwambia, "Beni Hadadi anasema hivi:
\v 3 Fedha zako na dhahabu zako ni zangu. Pia wake zako na watoto, wale wazuri, sasa ni wangu."
\s5
\v 4 Mfalme wa Israeli akajibu akasema, "Na iwe kama unavyosema, bwana wangu, mfalme. Mimi pamoja na vile nilivyo navyo ni mali yako."
\v 5 Wale wajumbe wakaja tena wakasema, "Beni Hadadi anasema hivi, 'Nilituma neno kwako nikisema kwamba lazima ukabidhi kwangu fedha zako, dhahabu zako, wake zako na watoto wako.
\v 6 Lakini kesho nitatuma watumishi wangu kwako wakati kama huu, nao wataichunguza nyumba yako na nyumba za watumishi wako. Nao watatia mikononi mwao na kukichukua kila wakipendacho machoni mwao.'"
\s5
\v 7 Ndipo mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi pamoja akawaambia, ''Hebu angalieni jinsi huyu mtu anavyotafuta matatizo. Amenitumia ujumbe kwamba anataka kuchukua wake zangu, watoto wangu, fedha na dhahabu zangu, nami sijamkatalia."
\v 8 Wazee wote na watu wote wakamwambia Ahabu, "Usimsikilize wala kukubaliana na matakwa yake."
\s5
\v 9 Ahabu akawaambia wajumbe wa Beni Hadadi, "Mwambieni bwana wangu mfalme kwamba, 'Ninakubaliana na kila kitu ambacho kwanza uliwatuma watumishi wako kufanya kwangu, lakini sikubaliani na matakwa yako haya ya pili.'" Wale watumishi wa Beni Hadadi wakaondoka wakampelekea mrejesho Beni Hadadi.
\v 10 Naye Beni Hadadi akatuma tena majibu yake kwa Ahabu, akaisema, "basi miungu inifanyie hivyo na zaidi, kama hata mavumbi ya Samaria yatawatosheleza watu watu wote wanaonifuata kuchukua kila mmoja angalau konzi mkononi mwake."
\s5
\v 11 Naye mfalme wa Israeli akamjibu akisema, "Mwabieni Beni Hadadi, 'Hakuna abebaye silaha yake, atakayejivuna kama wakati wa kuishusha."'
\v 12 Beni Hadadi aliusikia ujumbe huu wakati alipokuwa akinywa, yeye na wafalme walikuwa pamoja naye waliokuwa kwenye mahema yao. Beni Hadadi akayaamuru majaeshi yake, "Jipangeni katika sehemu zenu kwa ajili ya vita." Kwa hiyo wakajiandaa kivita ili kuuvamia mji.
\s5
\v 13 Tazama, nabii akaja kwa Ahabu mfalme wa Israeli akasema, "BWANA asema, 'Je umeliona hili jeshi kubwa? Tazama, nitaliweka katika mkono wako leo, nawe utatambua kuwa mimi ni BWANA.'"
\v 14 Naye Ahabu akajibu, ''kwa nani? BWANA akamjibu akasema, "kwa kuwatumia viijana wanaotumikia maliwali wa wilaya." kisha Ahabu akasema, "Ni nani atakayepewa hiyo vita?' BWANA akamwambia, "wewe."
\v 15 Ndipo Ahabu alipowataarifu wale vijna wanaowatumikia maliwali wa wilaya. Idadi yao ilikuwa 232. Baada yao aliwahesabu wanajeshi wote, jeshi lote la Israeli; idadi yao ilikuwa elfu saba.
\s5
\v 16 Nao wakatoka wakati wa adhuhuri. Naye Beni Hadadi alikuwa akinywa na kulewa hemani mwake, yeye na wale wafalme wadogo thelathini na mbili waliokuwa wakimsaidia.
\v 17 Wale maakida vijana waliokuwa wakiwasaidia maliwali wa wilaya walitangulia kwanza. Kisha Beni Hadadi alitaarifiwa na wanaskauti aliokuwa amewatuma kwamaba, "kuna watu wanakuja kutoka Samaria."
\s5
\v 18 Beni Hadadi akasema, "wawe wamekuja kwa amani au kwa vita, wakamteni wakiwa hai."
\v 19 Kwa hiyo wale vijvana wanaowatumikia maliwali wa wilaya wakaenda mjini na jeshi likawafuata kwa nyuma.
\s5
\v 20 Kila mmoja akaua adui wake na wale washami wakakimbia. Israeli ikawashinda. Beni Hadadi mfalme wa Shamu akatoroka kwa farasi pamoja na wapanda farasi.
\v 21 Kisha mfalme wa Israeli akaenda akawashambulia farasi na magari, na kuwaua washami kwa mauaji makubwa.
\s5
\v 22 Yule nabii akaja kwa mfalme wa Israeli akamwambia, "Nenda, ukajiimarishe mwenyewe, uelewa na kupanga kile unachofanya, kwa sababu mwakani mfalme wa Shamu atapanda dhidi yako tena."
\v 23 Wale watumishi wa mfalme wa Shamu wakamwambia, "Mungu wao ni mungu wa milimani. Hiyo ndiyo sababu walikuwa na nguvu kuliko tulivyokuwa. Lakini sasa hebu tupigane nao katika nchi tambarare, na kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.
\s5
\v 24 Na ufanye hivi: waondoe wafalme; mwondoe kila mmoja mahali pake ukaweke majemedari mahali pao.
\v 25 Kisha ujihesabie jeshi kama lile jeshi ulilopoteza, farasi kwa farasi na gari kwa gari, nasi tutapigana nao katika nchi tambarare. Kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko walivyo." Kwa hiyo Beni Hadadi akausikiliza ushauri huo naye akafanya kama alivyoshauriwa.
\s5
\v 26 Baada ya mwanzo wa mwaka mpya, Beni Hadadi akawahesabu Washami na akapanda Afeki kupigana na Israeli.
\v 27 Watu wa Israeli walikuwa wamehesabiwa na walikuwa wamejipanga kupigana nao. Watu wa Israeli wakafanya kambi mbele yao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, lakini Washami wakaujaza upande wa nchi.
\s5
\v 28 Ndipo mtu wa Mungu akaja karibu akaongea mfalme wa Israeli akamwambia, "BWANA anasema: 'Kwa kuwa Washami wamesema kuwa BWANA ni mungu wa milima, na wala si mungu wa mabondeni, nitaliweka hili jeshi kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ni BWANA.'"
\s5
\v 29 Kwa hiyo majeshi yakaweka kambi yakikabiliana kwa muda wa siku saba. Kisha siku ya saba vita vikaanza. Watu wa Israeli wakawaua Washami 100, 000 wanajeshi wa ardhini kwa siku moja.
\v 30 Waliobaki wakakimbilia Afeki, mjini, na ule ukuta ukaanguka juu ya watu ishiriinina saba elfu waliobaki. Naye Beni Hadadi akakimbilia mjini. akaingia kwenye chumba cha ndani.
\s5
\v 31 Wale watumishi wa Beni Hadadi wakamwambia, "Tazama sasa, tumesikia kwamba wale wafalme wa nyumba ya Israeli ni wenye rehema. Tafadhali hebu tuvaeni magaunia viunoni mwetu na kamba vichwani mwetu, na twendeni kwa mfalme wa Israeli. Labda atakuokoa roho yako."
\v 32 Kwa hiyo wakavaa magunia viunoni mwao na kujifunga kamba vichwani mwao na kisha wakaenda kwa mfalme wa Israeli wakamwambia, "Mtumishi wako Beni Hadadi, anasema, 'tafadhali niachie uhai wangu." Ahabu akawaambia, "Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu."
\s5
\v 33 Sasa wale watu walikuwa wakisikiliza ishara yeyote kutoka kwa Ahabu, kwa hiyo wakamjibu haraka, "Ndiyo ndugu yako Beni Hadadi bado yuko hai." Ahabu akawaambia, "Nendeni mkamlete." Ndipo Beni Hadadi alipokuja kwake, na Ahabu akamwacha aje kwenye gari lake.
\v 34 Beni Hadadi akamwambia Ahabu, "Nitakurudishia miji yako ambayo baba yangu alichukua toka kwa baba yako, na unaweza kutengeneza masoko kwa ajili yako Dameski, kama baba yangu alivyofanya kule Samaria." Ahabu akajibu, "Nitakuacha uende kwa agano hili." Kwa hiyo Ahabu akafanya agano naye kisha akamwacha aende.
\s5
\v 35 Mtu mmoja, mmoja wana wa wana wa manabii, akamwambia mmoja wa wale manabii wenzake kwa neno la BWANA, "Tafadhali nipige." Lakini yule mtu akakataa kumpiga.
\v 36 Kisha yule nabii akamwambia nabii mwenzake, " Kwa sababu umekataa kutii sauti ya BWANA, mara tu utakaponiacha, simba atakuua." na mara tu baad ya yule mtu kumwacha, simba akamkuta na kumwua.
\s5
\v 37 Kisha yule nabii akamkuta mtu mwingine akamwambia, "Tafadhali nipige."Yule mtu akampiga na kumwumiza.
\v 38 Kisha yule nabii akaondoka akaenda kumsubiri yule mfalme barabarani; naye alikuwa amejibadilisha kwa kilemba machoni pake.
\s5
\v 39 Ikawa mfalme alipokuwa akipita, Yule nabii akamwita mfalme na kumwambia, "Mtumishi wako alienda katikati ya pigano, na askari akasimama akamleta adui kwangu akasema, 'Mwangalie mtu huyu. Na ikiwa kwa vyovyote atatoroka, basi maisha yako yatatolewa kwa ajili ya maisha yake vinginevyo utalipa kilo thelathini za fedha.
\v 40 Lakini kwa kuwa mtumishi wako alikuwa na mambo mengi akienda huku na kule, yule askari adui akatoroka." Basi mfalme wa Israeli akamwambia, Hivyo ndivyo itakavyokuwa hukukmu yako - umejihukumu mwenyewe."
\s5
\v 41 Ndipo yule nabii alipoondoa haraka kile kilemba machoni pake, na mfalme wa Israeli alipotambua kuwa huyo alikuwa mmoja wa manabii.
\v 42 Yule nabii akamwambia mfalme, "BWANA anasema, 'Kwa sababu umemwachia aende mtu yule niliyekuwa nimemhukumu kifo, maisha yako yatachukua nafasi ya maisha yake.'"
\v 43 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akaenda nyumbani kwake akiwa na moyo mzito na mwenye hasira, akafika Samaria.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Basi ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu kule Yezreeli, karibu na ikulu ya Ahabu, mfalme wa Samaria.
\v 2 Ahabu akamwambia Nabothi, akisema, "Nipe shamba lako, ili nilifanye kuwa bustani ya mboga, kwa sababu iko karibu na nyumba yangu. Badala yake nitakupa shamba zuri la mizabibu, au, kama ukipenda nitakulipa thamani yake kwa fedha."
\s5
\v 3 Nabothi akamjibu Ahabu, "BWANA na alizuie hilo nisije nikatoa urithi wa mababu zangu kwako."
\v 4 Ahabu akaingia kwenye ikulu yake akiwa mchovu na mwenye hasira kwa sababu ya jibu ambalo Nabothi Myezreeli alimpa aliposema, "Sitakupa urithi wa mababu zangu." Akalala kitandani kwake, akiwa amegeuza uso wake upande ule, na akagoma kula chakula chochote.
\s5
\v 5 Yezebeli mke wake akaiingia kwake, akamwambia "Kwa nini moyo wako una huzuni, kiasi kwamba hutaki kula?"
\v 6 Naye akamjibu," Niliongea na Nabothi Myezreeli nikamwambia, 'Nipe shamba lako nami nitakupa pesa, au kama inakupendeza, nitakupa shamba jingine ili liwe lako.' Naye akanijibu, 'Sitakupa shamba langu.'"
\v 7 Naye Yezebeli mkewe akamjibu, "Je, wewe si mtawala wa ufalme wa Israeli? Inuka ule; na moyo wako uwe na amani. Nitalichukua hilo shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli kwa ajili yako.
\s5
\v 8 Kwa hiyo Yezebeli akaandika barua kwa jina la Ahabu, akaitia muhuri wake, akazituma kwa wazee na kwa watu tajiri alioketi nao kwenye vikao, na ambao pia waliishi karibu na Nabothi.
\v 9 Katika ile barua aliyoandika, ilisema hivi, "Pigeni mbiu ya kufunga mkamkalishe Nabothi juu mbele ya watu.
\v 10 Pia mwaweke watu wawili wasiokuwa waaminifu pamoja naye na wale watu watoe ushahidi kinyume naye, waseme, 'Ulimlaani Mungu na mfalme."Halafu mchukueni nje mkampige kwa mawe mpaka afe.
\s5
\v 11 Kwa hiyo watu wa mji wake, wazee na watu tajiri waishio kwenye huo mji, wakafanya kama Yezebeli alivyowaeleza, kama ilivyoandikwa kwenye zile baraua ambazo alikuwa amewatumia.
\v 12 Wakapiga mbiu ya kufunga wakamkalisha Nabothi juu mbele ya watu.
\v 13 Na wale watu wawili wasiokuwa waaminifu wakaja wakakaa mbele ya Nabothi; nao wakatoa ushuhuda wao dhidi ya Nabothi kuwa amemlaani Mungu na mfalme." Kisha wakamchukua nje ya mji wakampiga kwa mawe mpaka akafa.
\v 14 Kisha wazee wakatuma neno kwa Yezebeli, wakisema, "Nabothi ameshapigwa mawe na amekufa."
\s5
\v 15 Naye Yezebeli aliposikia kuwa Nabothi ameshapigwa mawe na alikuwa amekufa, akamwabia Ahabu, "Inuka na ukamiliki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ambalo alikataa kukuuzia, kwa sababu Nabothi hayuko hai, bali amekufa."
\v 16 Ahabu aliposikia kuwa Nabothi amekufa, akainuka ili aende kwenye lile shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli na kulimiliki.
\s5
\v 17 Ndipo neno la BWANA likamjia Eliya Mtishibi, likisema,
\v 18 "Inuka uende ukakutane na Ahabu mfalme wa Israeli, ambaye anaishi Samaria. Yumo kwenye shamba la Nabothi, ambako ameenda kuchukua umiliki wa shamba hilo.
\s5
\v 19 Ukaongee naye umwambie kwamba BWANA anasema, 'Je, umeua na kujimilikisha?' na utamwambia kwamba BWANA anasema, 'Mahali pale ambapo mbwa wameramba damu ya Nabothi, ndipo mbwa watakaporamba damu yako, ndiyo, damu yako.'"
\v 20 Ahabu akamwambia Eliya, "Je, umenipatia, adui yangu?" Eliya akamjibu, "Nimekupata wewe kwa sababu, umejiuza mwenyewe kufanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA.
\s5
\v 21 BWANA anakwambia hivi: 'Tazama, Nitaleta janga kwako na litakuangamiza kabisa na kufutilia mbali kila mtoto mume na mtumwa na mtu huru katika Israeli.
\v 22 Nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama familia ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa sababu umenighadhabisha na umewasababisha Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 23 Pia BWANA ameongea kuhusu Yezebeli, amesema, "mbwa watamla Yezebeli pembeni mwa ukuta wa Yezreeli.'
\v 24 Yeyote ambaye ni mtu wa familia ya Ahabu ambaye atafia mjini - mbwa watamla. Na yeyote ambaye atafia shambani - ataliwa na ndege wa angani."
\s5
\v 25 Hapakuwepo na mtu kama Ahabu, ambaye alijiuza mwenyewe kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, ambaye mke wake Yezebeli alimchochea kufanya dhambi.
\v 26 Ahabu alifanya matendo yachukizayo kwa ajili ya sanamu alizofanya, kama vile yale yote ambayo Waamori walifanya, BWANA akawafukuza mbele ya watu wa Israeli.
\s5
\v 27 Ahabu aliposikis maneno haya, Akachana mavazi yake na akavaa magunia kwenye mwili wake na akfaunga, na akalala kwenye magunia na akahuzunika sana.
\v 28 Kisha neno la BWANA likamjia Eliya Mtishibi likisema,
\v 29 "Je, unamwona jinsi Ahabu anavyojinyenyekeza mbele yangu? Kwa sababu anajinyeyenyekeza mwenyewe mbele yangu, Sitaleta lile janga katika siku zake; Ni katika siku za mwanae, nitakpolileta hilo janga katika familia yake."
\s5
\c 22
\p
\v 1 Miaka mitatu ilipita bila kuwepo na vita kati ya Washami na Wisraeli.
\v 2 Ikawa katika mwaka wa tatu, Yehoshafati mfalme wa Israeli akashuka kwa mfalme wa Isreli.
\s5
\v 3 Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia watumishi wake, "Je, mnajua kuwa Ramothi Gileadi ni yetu, ila hatufanyi chochote kuitwaa kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Shamu?"
\v 4 Kwa hiyo akamwambia Yehoshafati, "Je, utakwenda na mimi katika vita huko Ramothi Gileadi?" Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, "Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, na farasi wangu ni kama farasi wako."
\s5
\v 5 Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, "Tafadhali tafuta mwongozo kutoka neno la BWANA juu ya kile unachopaswa kufanya kwanza."
\v 6 Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, walikuwa wanaume elfu nne, akawaambia, "Je, niende Ramothi Gileadi kupigana, au nisiende?" Nao wakamwambia, "Ivamie, kwa kuwa Bwana ataitoa katika mkono wa mfalme."
\s5
\v 7 Lakini Yehoshafati akasema, "Je, hapa hayupo nabii mwingine wa BWANA ambaye tunaweza kupata ushauri?"
\v 8 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, "Bado kuna mtu mmoja ambaye tunaweza kupata ushauri toka kwa BWANA ili kusaidia, Makaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu huwa hanitabirii mazuri yanayonihusu, ila hunitabiria matatizo tu." Lakini Yehoshafat akasema, "mfalme na asiseme hivyo,"
\v 9 Kisha mfalme wa Israeli akmwita akida na akamwamuru, "Kamlete Makaya mwana wa Imla, sasa hivi."
\s5
\v 10 Wakati huo Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi kila mmoja kwenye kiti cha enzi, wamevaa mavazi yao, katika eneo la wazi kwenye lango la kuingilia Samaria, na manabii walikuwa wakiwatabiria.
\v 11 Sedekia mwana wa Kenaana akajitengenezea pembe za chuma akasema, "BWANA asema hivi: 'Kwa hili utawasukuma Washami mpaka watakapoisha.'"
\v 12 Na manabii wengine wote wakasema hivyo, wakisema, "Ishambulie Ramothi Gileadi na ushinde, kwa kuwa BWANA ameiweka kwenye mkono wa mfalme."
\s5
\v 13 Yule mjumbe aliyeenda kumwita Makaya akamwambia, akisema, "Tazama sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja wanatabiri mambo mema kwa mfalme. Tafadhali maneno yako yawe kama yao ukaseme mambo mazuri."
\v 14 Makaya akajibu, "Kama BWANA aishivyo, kile BWANA atakachosema kwangu ndicho nitakachosema.'"
\v 15 Naye alipokuja kwa mfalme, mfalme akamwambia, "Makaya, je twende Ramothi Gileadi kupigana, au tusiende?" Makaya akamjibu, "Ivamie na ushinde. BWANA ataitoa kwenye mkono wa mfalme."
\s5
\v 16 Kisha mfalme akamwambia. "Je, nikutake mara ngapi ili kuniapia ukweli kwa jna la BWANA?"
\v 17 Makaya akasema, "Ninaiona Israeli yote imesambaa kwenye milima, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji, na BWANA amesema, 'Hawa hawana mchungaji. Kila mtu na arudi nyumbani kwake kwa amani.'"
\s5
\v 18 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, "Je sikukwambia kuwa huwa hanitabirii mambo mema yanayonihusu, ila majanga tu?"
\v 19 Kisha Makaya akasema, "Kwa hiyo sikiliza neno la BWANA: Nimemwona BWANA akiwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikuwa yamesimama karibu yake upande wake wa kulia na upande wake wa kushoto.
\v 20 BWANA akasema, 'Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili kwamba apande akafie Ramothi Gileadi? Na mtu mmoja akajibu kwa njia hii, na mwingine akajbu kwa njia ile.
\s5
\v 21 Ndipo pepo moja akajitokeza, akasimama mbele ya BWANA, akasema, 'Mimi nitamdanganya.' BWANA akmwuliza, 'Kwa jinsi gani?'
\v 22 Yule pepo akamjibu, 'Nitakwenda na kuwa roho idanganyayo katika vinywa vya manabii wake,' BWANA akamjibu, 'utaweza kumdanganya, na utafanikiwa. Nenda sasa ukafanye hivyo.'
\v 23 Tazama sasa, BWANA ameweka roho idangayo kwenye vinywa vya hawa manabii wako, na BWANA ametangaza janga kwako."
\s5
\v 24 Kisha Sedekia mwana wa Kenaana, akaja, akamzabua Makaya shavuni, akasema, "Je, yule roho wa Bwana alitokaje kwangu ili asema na wewe?"
\v 25 Makaya akasema, "Tazama, "utatambua hilo katika siku hiyo, utakapokimbilia katika chumba cha ndani kujificha."
\s5
\v 26 Mfalme wa Israeli akamwambia mtumishi wake, "Mkamate Makaya umpeleke kwa Amoni, liwali wa mji, na kwa mwanangu, Yoashi.
\v 27 Mwambie, 'mfalme anasema mweke huyo gerezani na awe anampa mkate kidogo na maji kidogo, mpaka nitakaporudi salama.'"
\v 28 Naye Makaya akasema, "Kama utarudi salama basi BWANA hajasema kupitia kinywa changu." Na akaongeza, "Sikilizeni hili, ninyi watu."
\s5
\v 29 Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati mfalme wa Yuda, wamepanda Ramothi Gileadi.
\v 30 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, "Nitajibadilisha mwenyewe niende vitani, lakini wewe uvae vazi lako la kifalme." Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na akaenda vitani.
\s5
\v 31 Naye mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru majemedari thelathini na mbili wa magari yake, akisema, "Msimwamgamize askari wa muhimu au ambaye si wa muhimu, badala yake mshambulieni mfalme wa Israeli tu."
\v 32 Ikawa wakati majemedari wa magari walipomwona Yehoshafati wakasema, "Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli." Wakageuka ili kumshambulia, kwahiyo Yehoshafati akapiga kelele.
\v 33 Ikawa majemedari wa magari walipoona kuwa yeye hakuwa mfalme wa Israeli, wakamwacha.
\s5
\v 34 Lakini mtu mmoja akavuta upinde wake kwa kubahatisha na akampiga mfalme wa Israeli katikati ya mwunganiko wa mavazi yake ya chuma. Ahabu akamawambia dereva wa gari lake, "geuza unirudishe kutoka vitani, kwa kuwa nimeumizwa sana."
\s5
\v 35 Vita ikawa mbaya sana siku hiyo na mfalme akalazwazwa garini mwake akiwakabili Washami. Akafa jioni hiyo. Damu ilimwagika kutoka kwenye jeraha lake ndani ya gari.
\v 36 Ikawa wakati wa kuzama jua, kilio kikatawala kwa jeshi lote, wakisema, "Kila mtu arudi kwenye mji wake; na kila mtu arudi kwenye mkoa wake!"
\s5
\v 37 Kwa hiyo mfalme Ahabu akafa na akaletwa Samaria, wakamzika huko Samaria.
\v 38 Wakaliosha lile gari kwenye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake (hapa ni mahali ambapo makahaba waliogea), kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limesema.
\s5
\v 39 Kwa mambo mengine yanayohusisana na Ahabu, yote ambayo alifanya, ile nyumba ya pembe aliyojenga, na miji yote aliyojenga, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
\v 40 Kwa hiyo Ahabu akalala pamoja na mababu zake, na Ahaziya mwanae akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 41 Kisha Yehoshafati mwana wa Asa alianza kutawala juu ya Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.
\v 42 Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, na akatawala Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake alikuwa Azuba, binti wa Shilhi.
\s5
\v 43 Akatembea katika njia za Asa, baba yake, hakuziacha; akafanya yaliyokuwa mema mbele ya macho ya BWANA. Lakini bado mahali pa juu palikuwa hapajabomolewa. Watu walikuwa bado wanaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba mahali pa juu.
\v 44 Yehoshafati akafanya amani na mfalme wa Israeli.
\s5
\v 45 Kwa mambo mengine kuhusiana na Yehoshafati, na nguvu zake alizoonyesha, na jinsi alivyopigana vita, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?
\v 46 Aliwaondoa kutoka katka nchi wale makahaba wa kipagani waliokuwa wamebaki katika siku za baba yake Asa.
\v 47 Hapakuwepo mfalme katika Edomu isipokuwa kaimu mtawala.
\s5
\v 48 Yehoshafati alijenga merikebu: ziende Tarshishi na Ofri kuleta dhahabu, lakini hazikusafiri kwa sababu zile merikebu zilivunjika kule Esioni Geberi. Kisha
\v 49 Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, "Naomba watumishi wangu waende pamoja na watumishi wako merikebuni. "Lakini Yehoshafati hakuruhusu hilo.
\v 50 Yehoshafati akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi, babu yake; Yoramu mwanawe akawa mfalme mahali pake.
\s5
\v 51 Ahazia mwana Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli ya Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa mfalme Yehoshafati mfalme wa Yuda, na akatawala kwa mika miwili juu ya Israeli.
\v 52 Naye akafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA akatembea katika njia za baba yake, katika njia za mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwazo aliifanya Israeli kufanya dhambi.
\v 53 Alimtumikia Baali na kumwabudu na kwa hiyo akamghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, katika hasira, kama vile baba yake alivyofanya.

1394
12-2KI.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1394 @@
\id 2KI
\ide UTF-8
\h 2 Wafalme
\toc1 2 Wafalme
\toc2 2 Wafalme
\toc3 2ki
\mt 2 Wafalme
\s5
\c 1
\p
\v 1 Moabu aliasi dhidi ya Israeli baada ya kifo cha Ahabu.
\v 2 Baada hapo Ahazi akaanguka chini ya dirisha lenye waya zinazikinzana kwenye chumba chake juu katika Samaria, na alikuwa amejeruhiwa. Kwa hiyo alituma wajumbe na kuwaambia, "Nendeni, muulizeni Baal Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona hili jeraha."
\s5
\v 3 Lakini malaika wa Yahwe wakamwambia Eliya Mtishbi, " Inuka, nenda ukaonane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, na uwaulize, 'Je ni kwasababu hakuna Mungu katika israeli ambaye mnayekwenda kuuliza pamoja na Zebebu, mungu wa Ekroni?
\v 4 Kwa hiyo Yahwe anasema, "Hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ambacho ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika.""" Baada ya hapo Eliya akaondoka.
\s5
\v 5 wakati wale wajumbe waliporudi kwa Ahazia, akawaambia, "Kwa nini mmerudi?"
\v 6 Wakamwambia, "mtu amekuja kuonana na sisi ambaye ametuambia, 'Turudi kwa mfalme ambaye aliyewatuma, na mkamwambie, Yahwe amesema hivi: 'Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli mpaka mmewatuma watu kwenda kumuuliza kwa Baal Zabubu, mungu wa Ekron? Kwa hiyo hutashuka kutoka kitanda ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika."""
\s5
\v 7 Ahazi akawaambia wajumbe wake, "'Alikuwa mtu wa aina gani, yule ambaye alikuja kuonana na ninyi na akasema haya maneno kwenu?"
\v 8 Wakamjibu, "Alikuwa amevaa kanzu yenye manyaya na alikuwa na mkanda wa ngozi kiunanoni kwake.'" Hivyo mfalme akajibu, '"Yule alikuwa Eliya Mtishbi."
\s5
\v 9 Ndipo mfalme akatuma nahodha wa askari hamsini kwa Elya. Nahodha akaenda mpaka kwa Eliya ambapo alipokuwa amekaa juu ya mlima. Nahodha akamwambia Eliya, " Wewe, mtu wa Mungu, mfalme amesema, 'shuka chini.'"
\v 10 Eliya akajibu na kusema kwa nahodha, "Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke chini kutoka mbinguni na kukula wewe na watu wako hamsini." Kisha moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.
\s5
\v 11 Tena Mfalme Ahazi akamtuma nahodha mwingine pamoja na maaskari wengine hamsini. Huyu nahodha pia akasema kwa Eliya, "Wewe, mtu wa Mungu, mfalme anasema, teremka chini haraka."'
\v 12 Eliya akajibu na kuwaambia, "Kama mimi ni mtu wa Mungu, ngoja moto ushuke kutoka mbinguni na ukule wewe na watu wako hamsini." Moto wa Mungu ukashuka chini tena kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.
\s5
\v 13 Bado tena mfalme alituma kundi la tatu la wapiganaji hamsini. Huyu nahodha akaenda, akaanguka mbele ya miguu ya Eliya, na kumsihi na kumwambia, "Wewe, mtu wa Mungu, Nakuomba, acha uzima wangu na uzima wa hawa watumishi wako hamsini uwe na thamani machoni kwako.
\v 14 Ndipo, moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kuwala wale manahodha wawili wa kwanza pamoja na watu wao, bali sasa acha uzima wangu uwe na thamani machoni kwako."
\s5
\v 15 Malaika wa Yahwe akamwambia Eliya, "'Nenda chini pamoja naye. Usimwogope."' Hivyo Eliya akainuka na kwenda chini pamoja naye kwenda kwa mfalme.
\v 16 Baadye Eliya akamwambia Ahazia, '"Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Umewatuma wajumbe kuzungumza pamoja na Baal-Zebubu, mungu wa Ekron. Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ambaye unayeweza kumuuliza habari? Kwa hiyo sasa, hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ulichokipanda; utakufa hakika.'"
\s5
\v 17 Hivyo Mfalme Ahazia alikufa kulingana na neno la Yahwe ambalo Eliya alilisema. Yoramu alianza kutawala katika eneo lake, katika mwaka wa pili Yoramu mwana wa Yohoshafati mfalme wa Yuda, kwa sababu Ahazia hakuwa na mtoto.
\v 18 Kama mambo mengine yanayomuhusu Ahazia, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\s5
\c 2
\p
\v 1 Hivyo ilipokuja kuhusu, wakati Yahwe alipokuwa akienda kumchukua Eliya kwenda mbinguni kwa uvumi, ambapo Eliya aliondoka pamoja na Elisha kutoka Gigali.
\v 2 Eliya akamwambia Elisha, '"kaa hapa, tafadhali, kwa sababu Yahwe alinituma kwa Betheli.'" Elisha akajibu, "Kama Yahwe aishivyo, na kama uishivyo, sintokuacha.'" Hivyo wakashuka chini kulekea Betheli.
\s5
\v 3 Wana wa manabii ambao walikuwa Betheli walikuja kwa Elisha na kumwambia, je unajua kwamba Yahwe atamwondoa bwana wako kuanzia leo?"' Elisha akajibu, "Ndiyo, nalijua hilo, ila msizungumze kuhusu hilo."'
\v 4 Eliya akamwambia, "Elisha, subiri hapa, tafadhali, kwa kuwa Yahwe amenituma niende Yeriko." Kisha Elisha akajibu, '"Kama Yahwe aishivyo, na kama uishivyo, sintokuacha." Hivyo wakaenda Yeriko.
\s5
\v 5 Kisha wana wa manabii ambao walikuwa Yeriko wakaja kwa Elisha na kumwambia, "'Je unajua kwamba Yahwe atamwondoa bwana wako kutoka kwako leo?" Elisha akajibu, "Ndiyo, nalijua hilo, lakini msilizungumzie hilo."
\v 6 Kisha Eliya akamwambia, '"kaa hapa, tafadhali, kwa kuwa Yahwe amenituma kwenda Yeriko." Elisha akajibu, "Kama Yahwe ishivyo, na kama uishivyo, sintokuacha." Hivyo wawili wakaenda mbele.
\s5
\v 7 Baadaye watu hamsini wa watoto wa wale manabii wakasimama kuwakabili kwa mbali kidogo wale wawili wakasimama karibu na Yordani.
\v 8 Eliya akachukua vazi lake, akaliviringisha, na kuyapiga maji kwa kutumia lile vazi. Ule mto ukagawanyika katika sehemu mbili hivyo basi wawili hao wakatembea hadi nchi kavu.
\s5
\v 9 Ilitokea, walipokwisha kuvuka, kwamba Eliya akamwambia Elisha, "Niambie unachotaka nifanye kwako kabla sijaondolewa kutoka kwako." Elisha akajibu, "Naomba sehemu kubwa ya roho yako ije kwangu.
\v 10 Eliya akajibu, "Umeomba jambo gumu. Hata hivyo, kama ukiniona wakati nitakapoondolewa kutoka kwako, hii itatokea kwako, lakini kama sivyo, haitatokea."
\s5
\v 11 Ikawa walipokuwa bado wakienda mbele na kuzungumza, gari la kukokotwa na farasi lenye moto na farasi wa moto ikatokea, ambapo iliwatenga wale watu wawili kutoka kila mmoja, na Eliya akaenda juu kwa uvumi wa upepo kwenda mbinguni.
\v 12 Elisha akaiona akalia kwa sauti, "Baba yangu, baba yangu, gari la kukokotwa na farasi la Israeli na waendesha farasi!'" Hakumwona Eliya tena, na akashikilia nguo zake mwenyewe na kugawanya kwenye vipande viwili.
\s5
\v 13 Akachukua vazi la Eliya lililokuwa limemwangukia, na kurudi kusimama kwenye ukingo wa Yordani.
\v 14 Akayapiga maji pamoja na lile vazi la Eliya alilokuwa ameliangusha na kusema, "Yahwe yuko wapi, Mungu wa Eliya?'" Wakati alipoyapiga yale maji, yaligawanyika katika pande mbili na Elisha akavuka.
\s5
\v 15 Wakati hao wana wa manabii ambao walitoka Yeriko walipomuona akikatiza kwao, wakasema, "roho ya Eliya imepumzika kwa Elisha!" Hivyo wakaja kuonana naye, na wakasujudu aridhini mbele yake.
\v 16 Wakamwambia, "Ona sasa, miongoni mwa watumishi wako kuna watu hamsini hodari. Tunakuomba Waache waende, na kumtafuta bwana wako, endapo huyo Roho wa Yahwe alipomchukua juu na kumtupa juu ya mlima mmoja au kwenye bonde moja." Elisha akajibu, "Hapana, msiwatume."
\s5
\v 17 Lakini walimsihi Elisha hadi akaona aibu, akasema, "Watume."Ndipo wakawatuma watu hamsini, na wakatafuta kwa mda wa siku tatu, lakini hawakumpata.
\v 18 Wakarudi kwa Elisha, wakati alipokuwa bado yuko Yeriko, na akasema, "Je sikusema, 'msiende'?"
\s5
\v 19 Watu wa mjini wakamwambia Elisha, "Ona, tunakuomba, hali ya mjini hapa ni pazuri, kama bwana wangu awezavyo kuona, lakini maji ni mabaya na hiyo nchi haiwezi kuzaa matunda."
\v 20 Elisha akajibu, "Nileteeni bakuli jipya na muweke chumvi ndani ya hilo bakuli," hivyo wakamletea.
\s5
\v 21 Elisha akaenda hadi kwenye chemichemi za maji na kutupia chumvi ndani; halafu akasema, "Yahwe asema hivi, 'Nimeyaponya haya maji. Kuanzia mda huu, hakutakuwa na kifo au nchi isiyozaa matunda.
\v 22 "Hivyo hayo maji yakaponya hata leo, kwa lile neno ambalo Elisha aliongea.
\s5
\v 23 Ndipo Elisha akapanda kutoka pale mpaka Betheli. Naye alipokuwa akienda hadi kwenye barabara, wakatokea vijana nje ya mji na kumtania, wakamwambia, "Panda juu, wewe mwenye kipara! Panda juu, wewe mwenye kipara!"
\v 24 Elisha alipotazama nyuma yake na kuwaona; alimwambia Yahwe awalaani. Ndipo dubu wa kike wawili wakatokea kichakani na kuwajeruhi vijana arobaini na mbili.
\v 25 Ndipo Elisha alipoondoka pale na kuelekea Mlima Karmeli, na kutoka huko alirudi samaria.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Basi katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshefati mfalme wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ta Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na miwili.
\v 2 Alifanya yaliyo maovo usoni kwa Yahwe, lakini si kama baba yake na mama yake; kwa kuwa aliiondoa ile nguzo ya mungu wa Baali ambayo baba yake aliitengeneza.
\v 3 Hata hivyo alishikilia dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi; wala hakuziacha mbali nao.
\s5
\v 4 Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100, 000 na manyoya ya kondoo dume 100, 000.
\v 5 Ila baada ya Ahabu kufa, yule mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.
\v 6 Hivyo Mfalme Joramu alikaondoka Samaria katika muda huo kuwahamasisha Waisraeli wote kwa ajili ya vita.
\s5
\v 7 Akatuma mjumbe kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akisema, "Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je mtakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?" Yehoshafati akajibu, "Nitaenda. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako."
\v 8 Ndipo akasema, "Tutawashambulia kwa njia gani?" Yehoshafati akajibu, "Kwa njia ya jangwa la Edemu.
\s5
\v 9 Hivyo huyo mfalme wa Israeli, Yuda, na Edomu wakazunguka kwa mda wa siku saba. Hapakuwa na maji kwa ajili ya jeshi lao, wala kwa farasi au wanyama.
\v 10 Basi mfalme wa Israeli akasema, "Hii ni nini? Yahwe amewaita wafalme watatu ili kutekwa mikononi mwa Moabu?"
\s5
\v 11 Lakini Yehoshafati akasema, "je hakuna nabii wa Yahwe, ambaye tunaweza kufanya shauri kuhusu Yahwe kupitia yeye?" Mtumishi mmoja wa wafalme wa Israeli akajibu na kusema, "Elisha mwana wa Shafati yuko hapa, ambaye alikuwa akimimina maji kwenye mikono ya Eliya."
\v 12 Yehoshafati akasema, "Neno la Yahwe liko pamoja nami." Hivyo mfalme wa Israeli, Yehoshaphati, na mfalme wa Edomu wakashuka chini kwenda kwake.
\s5
\v 13 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, "Nifanye nini kwa ajili yako? Nenda kwa manabii wa baba na mama yako." Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia, "Hapana, kwa sababu Yahwe amewaita hawa wafalme watatu pamoja ili kuruhusu jeshi la Moabu liwateke."
\v 14 Elisha akajibu, "Kama Yawhe wa majeshi aishivo, ambaye nimesimama mbele zake, hakika kama nisingemheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yeda, Nisingevuta usikivu kwako, au hata kukutazama.
\s5
\v 15 Lakini sasa niletee mwanamuziki." Ndipo alipokuja mpiga muziki alipocheza, mkono wa Yahwe ukaja juu ya Elisha.
\v 16 Akasema, "'Yahwe asema hivi, 'Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.'
\v 17 Kwa kuwa Yahwe asema hivi, 'Hutaona upepo, wala hamtaona mvua, bali hili bonde la mto litajaa maji, na mtakunywa, ninyi na mifugo yenu na wanyama wenu wote.'
\s5
\v 18 Hiki ni kitu rahisi usoni mwa Yahwe. Pia atawapa ushindi juu ya hao Wamoabu.
\v 19 Mtaiteka kila ngome ya mji na kila mji mzuri, kukata kila mti mzuri, kusimamisha chemichemi zote za maji, na kuharibu kila sehemu nzuri ya nchi na miamba."
\s5
\v 20 Hivyo asubuhi karibia na mda wa kutoa sadaka ya kuteketeza, yakaja maji kutoka uelekeo wa Edomu; nchi ikajaa maji.
\s5
\v 21 Ndipo wakati Wamoabu wote waliposikia kwamba wafalme wamekuja kupigana dhidi yao, walikusanyika pamoja, wote waliotakiwa kubeba silaha, na wakasimama mpakani.
\v 22 Walitembea asubuhi na mapema na jua likang'aa kwenye maji. Wakati Wamoabu walipoyaona yale maji yaliyowaelekea, yanaonekana mekundu kama damu.
\v 23 Wakatamka kwa hasira, "Hii ni damu! Yamkini hao wafalme wameharibiwa, na wameuna wao kwa wao! Sasa basi, Moabu, ngoja tuende tukawateke nyara!"
\s5
\v 24 Wakati walipokuja kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakawashtukiza na kuwashambulia Wamoabi, ambao walikimbia mbele yao. Hilo jeshi la Israeli waliwakimbiza hao Wamoabu hadi kwao wakiwaua.
\v 25 Waliiharibu miji, na kila aina ya amani ya nchi kila mtu alirusha jiwe mpaka ulipojaa. Walizuia kila chemichemi ya maji na kukata chini miti mizuri yote. Kir-haresethi tu ndiyo ilichwa na mawe yake. Lakini hao maaskari wakawashambulia na makombeo wakiwazunguka na kuishambulia.
\s5
\v 26 Ndipo Mfalme Mesha wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa, alichukua watu hodari wa upanga mia saba pamoja naye kwenda kwa mfalme wa Edomu, lakini walishindwa.
\v 27 Ndipo akamchukua mtoto wake wa kwanza, ambaye angetawala baada ya yeye, na akamuudhi kwa kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Hivyo, kulikuwa na hasira kubwa dhidi ya Israeli, na hao Waisraeli, na Jeshi la Israeli likamuacha mfalme Mesha na kurudi kwenye nchi yao.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manbii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, "Mtumishi wako mme wangu amukufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha Yahwe. Basi aliyemuwia amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa."
\v 2 Hivyo Elisha akamwambia, "Nikusaidie nini? Niambie una nini kwenye nyumba yako?" Akamwambia "Mtumishi wako hana kitu kwenye nyumba, isipokuwa chupa ya mafuta."
\s5
\v 3 Kisha Elisha akasema, "Nenda kaazime vyombo kwa majirani zako, vyombo vitupu. Azima vyombo vingi uwezavyo.
\v 4 Kisha lazima uende ndani na kujifungia mlango wewe na watoto wako, na kumiminia mafuta vyombo vyote; vile vilivyojaa ukavitenge."
\s5
\v 5 Basi akamuacha Elisha na kujifungia mlango yeye na watoto wake. Wakavileta vile vyombo kwake, na akivijaza kwa mafuta.
\v 6 Ikawa vyombo vilipojaa, akamwambia mtoto wake, "Niletee chombo kingine." Ila akamwambia, "Hakuna vyombo vingine." Kisha mafuta yakakoma kutoka.
\s5
\v 7 Ndipo akaja na kumwambia mtu wa Mungu. Akasema, "Nenda kauze mafuta; lipa deni lako, na yatakayobaki waachie watoto wako."
\s5
\v 8 Siku moja Elisha alitembea Shunemu ambapo mwanamke muhimu aliishi; alimsihi ale chakula pamoja naye. Ikawa alipopita mara nyingi, angeweza kusimama pale na kula.
\v 9 Huyo mwanamke akamwambia mme wake, "Ona, sasa nadhani kwamba huyu ni mtu mtakatifu wa Mungu ambaye hupita siku zote.
\s5
\v 10 Ngoja tutengeneze chumba kidogo kwenye paa kwa ajili ya Elisha, na tuweke kitanda juu ya hicho chumba, meza, na taa. Kisha atakapokuwa anakuja kwetu, atakuwa anakaa hapo."
\v 11 Ikawa siku moja akaja tena kwamba Elisha akasimama pale, akakaa kwenye hicho chumba na kupumzika hapo.
\s5
\v 12 Elisha akamwambia Gehazi mtumishi wake, "Mwite huyu Mshunami." Wakati alipomuita, alisimama mbele yake.
\v 13 Elisha akamwambia, "Mwambie, 'Umetusumbukia kwa kutujali. Nini kifanyike kwa ajili yako? Tunaweza kukuombea kwa mfalme au amri jeshi?"" Akajibu, "Ninaishi miongoni mwa watu wangu."
\s5
\v 14 Kisha Elisha akajibu, "Tumfanyie nini kwa ajili yake, sasa?" Gehazi akajibu, "Kweli hana mtoto, na mume wake ni
\v 15 mzee." Hivyo Elisha akajibu, "Mwite." Wakati alipomuita, akasimama kwenye mlango.
\v 16 Elisha akasema, "Katika kipindi kama hiki mwakani, katika kipindi cha mwaka mmoja, utakuwa ukimkumbatia mtoto." Akasema "Hapana, bwana wangu na mtu wa Mungu, usidanganye kwa mtumishi wako."
\s5
\v 17 Lakini yule mwanamke akabeba mimba na kujifungua mtoto wakume kipindi hicho hicho katika mwaka uliofuata, kama Elisha alivyokuwa amemwambia.
\v 18 Wakati mtoto alipokuwa mkubwa, akaenda kwa baba yake siku moja, ambaye alikuwa na watu wanaovuna.
\v 19 Akamwambia baba yake, "Kichwa changu, kichwa changu." Baba yake akamwambia mtumishi wake, "Mbebe mpeleke kwa mama yake."
\v 20 Wakati mtumishi alipombeba kumrudisha kwa mama yake, yule mtoto alikaa kwenye magoti yake hadi mchana na baada ya hapo mtoto alikufa.
\s5
\v 21 Hivyo yule mwanamke akambeba na kumlaza kwenye kile kitanda cha mtu wa Mungu, akafunga mlango, na kutoka nje.
\v 22 Akamwita mume wake, na kusema, "Tafadhali nitumie mmoja wa watumishi wako na moja ya punda wako ili niweze kuwahi kwa mtu wa Mungu ili niweze kurudi."
\s5
\v 23 Mume wake akasema, "Kwa nini unataka kwenda kwake leo? Sio mwezi mpya wala Sabato." alijibu, "Itakuwa sawa."
\v 24 Ndipo akatandika kwenye punda na kumwambia mtumishi wake, "Mwendeshe haraka; usinipunguzie mwendo hadi nitakapokwambia ufanye hivyo."
\s5
\v 25 Hivyo alienda na kuja na mtu wa Mungu katika mlima Karmeli. Basi wakati mtu wa Mungu alipomuona kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, "Tazama, mwanamke Mshunami anakuja.
\v 26 Tafadhali mkimbilie na umwambie, 'Hamjambo kwako pamoja na mume wako na mtoto wako?" Akajibu, "Hawajambo."
\s5
\v 27 Baada ya kufika kwa huyo mtu wa Mungu katika mlima, alimkumbatia miguu yake. Gehazi akaja karibu ili kumuondoa lakini mtu wa Mungu akasema, "Muache, kwa kuwa amefadhaika sana. na Yahwe amenificha tatizo kwangu, na hajanambia kitu."
\s5
\v 28 Ndipo aksema, "Nilikuuliza mtoto wako, bwana wangu? Sikusema, 'Usinifiche'?
\v 29 Ndipo Elisha akamwambia Geahazi, "Vaa kwa ajili ya safari na uchukue fimbo yangu mkononi mwako. Nenda kwake. Kama ukimkuta mtu yeyote, usimsalimie, na kama mtu yeyote akikusalimia, usimjibu. Laza fimbo yangu kwenye uso wa mtoto.
\s5
\v 30 Lakini mama yake na huyo mtoto akasema, "Kama Yahwe aishivyo, na kama uishivyo, sintokuacha." Hivyo Elisha akainuka na kumfuata.
\v 31 Gehazi akawatangulia na kulaza ile fimbo kwneye uso wa yule mtoto, lakini yule mtoto hakuongea wala kusikia. Hivyo baada ya hapo Gehazi akarudi kuonana na Elisha na kumwambia akisema, "Mtoto hakuamka."
\s5
\v 32 Ndipo Elisha alipofika kwenye ile nyumba, yule mtoto alikuwa amekufa na alikuwa bado yupo kwenye kitanda.
\v 33 Hivyo Elisha aliingia ndani na kufunga malango yeye mwenyewe na yule mtoto na kuomba kwa Yahwe.
\v 34 Alipanda juu na kulala juu ya yule mtoto; aliweka mdomo wake kwenye mdomo wake, macho yake kweneye macho yake, na mikono yake kwenye mikono yake. Akajinyoosha yeye mwenyewe kwa yule kijna, na mwili wa yule mtoto ukaanza kupata joto.
\s5
\v 35 Baada ya hapo Elisha aliinuka na kuanza kutembea kuzunguka kile chumba na kurudi tena juu na kujinyoosha mwenyewe kwa yule kijana. Yule kijana alipiga chafya mara saba na kisha akafungua macho yake!
\v 36 Hivyo Elisha akamwita Gehazi na kumwambia, "Mwite yule Mshunami!" Hivyo akamwita, na wakati alipofika kwenye kile chumba, Elisha akasema, "Mchukue mtoto wako."
\v 37 Kisha akainamisha uso wake chini kwenye miguu yake na kusujudu, na kisha kumchukua mtoto wake na kuondoka.
\s5
\v 38 Kisha Elisha akarudi tena Gilgali. Kulikuwa na njaa katika nchi, na wana wa manabii walikuwa wamekaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, "Weka sufuria kubwa kwenye moto na pika kwa ajili ya watoto wa manabii."
\v 39 Mmoja wao akaenda kwenye shamba kukusanya mboga mboga. Alikuta matango ya porini na kukusanya ya kutosha hadi alipojaza kwenye nguo yake. Walizikata na kuziweka kwenye sufuria, lakini hakujua zilikuwa za aina gani.
\s5
\v 40 Basi, wakawapakulia na kusambaziwa kwa watu kwa ajili ya kula. Baadae, kadiri walivyokuwa wakiendelea kula, walipiga kelele na kusema, "Mtu wa Mungu, kuna kifo kwenye sufuria!" Hivyo wasingeweza kula tena.
\v 41 Lakini Elisha akasema, "Late unga." Alitupia kwenye sufuria na kusema, "Pakua kwa watu kwa ajili ya kula, kwa hiyo wanaweza kula." Kisha hapakuwa kitu chochote kibaya kwenye ile sufuria.
\s5
\v 42 Akaja mtu kutoka Baal Shalisha kwa mtu wa Mungu na kumletea chakula cha kwanza cha mavuno yake mikate shirirni ya shayiri, na masuke mabichi kwenye gunia. Akasema, "Wape haya watu ili waweze kula."
\v 43 Mtumishi wake akasema, "Je, niandae hii mbele ya watu mia moja?" Lakini Elisha akasema, "Wapeni hawa watu, ili waweze kula, kwa sabau Yahwe anasema, 'Watakula na kingine kitabaki."'
\v 44 Basi mtumishi wake akawaandalia mbele yao; wakala, na kuacha kingine kimebaki, kama neno la Yahwe lilivyokuwa limesema.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Basi Naamani, amri jeshi wa mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa na mtu mwenye kuheshimiwa mbele ya bwana wake, kwa sababu kwa ajili yake Yahwe aliwapa ushindi Washami. Pia alikuwa hodari, mtu shujaa, lakini alikuwa anaukoma.
\v 2 Washami walikuwa wametoka kuongoza kikosi na kumchukua kijana mdogo wa kike kutoka nchi ya Israeli. Akamuhudumia mke wa Naamani.
\s5
\v 3 Yule binti akamwambia bibi yake, "Natamani kwamba bwana wangu angelikuwa na nabii ambaye yupo Samaria! Halafu angelimponya bwana wangu ukoma wake.
\v 4 Hivyo Naamani akaingia na kumwambia mfalme kile ambacho yule binti kutoka nchi ya Israeli alichokuwa amekisechosema.
\s5
\v 5 Kisha mfalme wa Shamu akase, "Nenda sasa, na nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli." Naamani akaondoka na kuchukua talanta zake kumi za fedha, vipande elfu sita vya dhahabu, na nguo kumi za kubadilisha.
\v 6 Pia alichukua barua ya kumpelekea mfalme wa Israeli inayosema, "Sasa wakati hii barua itakapoletwa kwako, utaona kwamba nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, hivyo basi utamponya ukoma wake."
\s5
\v 7 Wakati mfalme wa Israeli alipoisoma ile barua, alichana mavazi yake na kusema, "Je mimi ni Mungu, niue na nirudishe uhai, kwamba huyu mtu anataka nimponye mtu ukoma wake? Inaonekana anatafuta mashindano na mimi."
\s5
\v 8 Ikawa wakati Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alichana nguo zake, akatuma neno kwa mfalme akisema, "Kwa nini umechana nguo zako? Muache aje kwangu sasa, na atajua kwamba kuna nabii katika Israeli."
\v 9 Basi Naamani akaja na farasi wake na mikokoteni yake ya kukokotwa na farasi na kusimama kwenye mlango wa nyumba ya Elisha.
\v 10 Elisha akamtumia mjumbe, akisema, "Nenda na ukazame mwenyewe katika Yordani mara saba, na ngozi ya mwili wako itajirudi; utakuwa msafi."
\s5
\v 11 Lakini Naamani alikasirika na kuondoka na kusema, "Tazama, Nilidhani bila shaka angekuja kwangu na kusimama na kuliita jina la Yahwe Mungu wake, na kupitisha mkono wake kwenye sehemu ya ugonjwa na kuponya ukoma wangu.
\v 12 Je sio Abana na Faepari, mito ya Damaskasi, bora kuliko maji yote ya Israeli?" Je siwezi kuoga ndani yao na kuwa safi?" Hivyo akageuka na kwenda kwa hasira.
\s5
\v 13 Ndipo watumishi wa Naamani wakaja karibbu na kumwambia, "Baba yangu, kama yule nabii alikuamuru kufanya kitu kigumu, singelifanya? Je si zaidi basi, atakapokwambia rahisi, 'Zama mwenyewe na uwe safi?"
\v 14 Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili ya mtoto mdogo, na alikuwa amepona.
\s5
\v 15 Naamani akarudi kwa yule mtu wa Mungu, yeye na watu wake wengine, na kuja na kusimama mbele yake. Akasema, "Tazama, sasa najua kwamba hakuna Mungu katika Dunia nzima isipokuwa katika Israeli. Kwa hiyo basi, chukua zawadi kutoka kwa mtumishi wako tafadhali."
\v 16 Lakini Elisha akajibu, "Kama Yahwe aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sintopokea chochote."Naamani akamsihi Elisha apokee zawadi, lakini alikataa.
\s5
\v 17 Hivyo Naamani akasema, "Kama sivyo, nakuomba ache apewe mtumishi wako pale mzigo wa baghala mbili za aridhi, kwa kuwa kuanzia sasa, mtumishi wako hatotoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa mungu yeyote isipokuwa Yahwe.
\v 18 Katika jambo hili moja Yahwe anaweza kumsamehe mtumishi wako, hii ni, wakati mfalme wangu atakapoenda kwenye nyumba ya Rimoni kuabudu pale, na kujifunza kwenye mikono yangu na kumuinamia mwenyewe kwenye nyumba ya Rimoni, Yahwe aweze kumsamehe mtumishi wako katika hili jambo."
\v 19 Elisha akamwambia, "Nenda kwa amani." Hivyo Naamani akaondoka.
\s5
\v 20 Alikuwa amesafiri lakini umbali mfupi, wakati Gehazi mtumishi wa Elisha mtumishi wa Mungu alisema mwenyewe, "Tazama, bwana wangu amemuandaa huyu Naamani Mshami kwa kuacha kupokea zawadi kutoka kwenye mikono yake ambazo alizileta. Kama Yahwe aishivyo, Nitakimbia nikimfuata na kupokea kitu kutoka kwake.
\v 21 Hivyo Gehazi akamfuata Naamani. Wakati Naamani alipomuona mtu mmoja anakimbia akimfuata, aliruka chini kutoka kwenye gari yake kuonana naye na kusema, "Je kila kitu kiko sawa?"
\v 22 Gehazi akasema, "kila kitu kiko sawa. Bwana wangu amenituma, akisema, 'Tazama, sasa wamekuja kwangu kutoka nchi ya mlima ya Efraimu vijana wawili wa watoto wa manabii. Tafadhali, wapatie talanta ya fedha na nguo mbili za kubadilisha."
\s5
\v 23 Naamani akajibu, "Ninafuraha kubwa kukupatia talanta mbili." Naamani akamsihi Gehazi na kujaribu talanta mbili za fedha kwenye mifuko miwili ya kubebea, pamoja na nguo mbili za kubadilisha, na kutandaza kwa wafanyakazi wake wawili, ambao walikuwa wamebebea ile mifuko miwili ya fedha mbele ya Gehazi.
\v 24 Wakati Gehazi alipokuja kwenye ule mlima, alichukua ile mifuko ya fedha kutoka kwenye mikono yao na kuificha kwenye nyumba; akawatuma wale watu, na wakaondoka.
\v 25 Wakati Gehazi alipoingia na kusimama mbele ya bwana wake, Elisha akamwambia, "Umetokea wapi, Gehazi?" Akajibu, "Mtumishi wako hakwenda mahali."
\s5
\v 26 Elisha akamwambia Gehazi, "Je roho yangu haikuwa na wewe wakati yule mtu alipoyarudisha magari yake ya farasi ili kukutana na wewe? Je uu ni mda wa kupokea pesa na nguo, mashamba ya mzaituni na mizabibu, na kondoo na Ng'ombe, na watumishi wakiume na watumishi wakike?
\v 27 Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima." Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Wana wa manabii wakamwambia Elisha, "Sehemu ambayo tunayoishi na wewe ni ndogo sana kwa ajili ya wote.
\v 2 Tafadhali, tuache tuende Yordani, na umwache kila mtu akate mti hapo ambako tunaweza kuishi." Elisha akajibu, "unaweza kwenda mbele."
\v 3 Mmoja wao akasema, "Nenda na watumishi wako tafadhali." Elisha akajibu, "Nitaenda."
\s5
\v 4 Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti.
\v 5 Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, "la hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!"
\s5
\v 6 Basi mtu wa Mungu akasema, "kiliangukia wapi?" Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. akakata fimbo, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.
\v 7 Elisha akasema, "Kichukue." Basi yule mtu akafikisha mkono wake na kukinyakua.
\s5
\v 8 Basi mfalme wa Shamu alikuwa akipigana vita dhidi ya Israel. Akafanya shauri na watumishi wake, akisema, "kambi yangu itakuwa sehemu flani na flani."
\v 9 Basi huyo mtu wa Mungu akamtuma kwa mfalme wa Israeli, akisema, "Kuwa makini usipite ile sehemu, kwa kuwa ndipo Washamu wanakoshukia hapo."
\s5
\v 10 Mfalme wa Israeli akatuma mjumbe kwenda pale sehemu ambayo mtu wa Mungu alipaongelea na kumtahadharisha. Zaidi ya mara moja au mbili, wakati mfalme alipoenda pale, alikuwa kwenye ulinzi wake.
\v 11 Huyo mfalme wa Shamu alikasirishwa kuhusu haya maonyo, na akawaita watumishi wake na kuwaambia, "Je hamtaniambia ni nani miongoni mwetu aliye upande wa Israeli?"
\s5
\v 12 Hivyo mmoja wa watumishi wake akasema, "Hapana, bwana wangu, mfalme, kwa ajili ya Elisha yule nabii katika Israeli humwambia yule mfalme wa Israeli maneno ambayo uyaongeayo kwenye kitanda chako cha kulala.!"
\v 13 Yule mfalme akajibu, "Nenda na uone Elisha alipo hivyo naweza kutuma watu na kumkamata." Akaambiwa, "Tazama yuko Dothani."
\s5
\v 14 Kwa hiyo yule mfalme akatuma farasi kwenda Donathi, magari ya farasi, na jeshi kubwa. Wakaja usiku na kuzunguka ule mji.
\v 15 Wakati yule mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka mapema na kutoka nje, kumbe, jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yameuzunguka mji. Mtumishi wake akamwabia, "Kumbe, bwana wangu! Tutafanya nini?"
\v 16 Elisha akajibu, "usiogope, wale walio na sisi ni zaidi kuliko wale walio nao."
\s5
\v 17 Elisha akajibu na kusema, "Yahwe, nakuomba kwamba utamfungua macho yake ili kwamba aweze kuona." Ndipo Yahwe alipofungua macho ya mtumishi, na akaona. Kumbe, ule mlima ulikuwa umejaa farasi na magari ya farasi ya moto yamemzunguka Elisha!
\v 18 Wakati hao Washami walipomshukia chini, Elisha aliomba kwa Yahwe na kusema, "Uwapige hawa watu kwa upofu, nakuomba." Hivyo Yahwe akawafanya vipofu, kama Elisha alivyoomba.
\v 19 Kisha Elisha akawaambia Washami, "Hii njia sio, pia mji huu sio. Nifuateni mimi, na nitawaleta kwa yule mtu ambaye mnayemtafuta." Ndipo akawaongoza kweda Samaria.
\s5
\v 20 Hata walipokwisha kufika Samaria, Elisha akasema, "Yahwe, fungua macho ya hawa watu ili waweze kuona." Yahwe akawafungua macho yao na wakaona, na kumbe, walikuwa katikati ya mji wa Samaria.
\v 21 Yule mfalme wa Israeli akamwambia Elisha, wakati alipowaona, "Baba yangu, niwaue? Niwaue?"
\s5
\v 22 Elisha akajibu, "Usiwaue. Ungeweza kuwaua wale ambao uliokuwa umewachukua mateka kwa upanga na upinde wako? Weka mkate na maji mbele yao, ili kwamba waweze kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao."
\v 23 Ndipo mfalme akaandaa chakula kingi kwa ajili yao, na wakati walipokula na kunywa, akawapeleka mbali, na walirudi kwa bwana wao. Lile kundi la jeshi la Wasahami halikurudi kwa mda mrefu katika nchi ya Israeli.
\s5
\v 24 Baadaye baada ya huyu Ben Hadadi mfalme wa Shamu kukusanya majeshi yake yote na kuiteka Samaria na kuizingira.
\v 25 Hivyo kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria. Kumbe, wakauzingira hadi kichwa cha punda kilipouzwa kwa vipande themanini vya fedha, na sehemu ya nne ya sehemu ya kibaba cha kinyesi cha njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
\v 26 Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa akipita karibu na ukuta, mwanamke mmoka akamlilia akisema, "Nisaidie, bwana wangu, mfalme."
\s5
\v 27 Akasema, "Kama Yahwe hawezi kukusaidia, je nitakusaidiaje? je kuna kitu chochote kinakuja kutoka sehemu ya kupuria nafaka au shinikizoni?"
\v 28 Mfalme akaendelea, "Nini kinakusumbua?" Akajibu, "Huyu mwanamke ameniambia, 'Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla leo, na tutamla wakwangu kesho."
\v 29 Hivyo tulimchemsha mtoto wangu na kumla, na siku ya pili yake nikamwambia, "Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla, lakini alikuwa amemficha mtoto wake."
\s5
\v 30 Basi mfalme aliposikia yale maneno ya yule mwanamke, akayachana mavazi yake (sasa alikuwa akitembelea kwenye ukuta), na watu wakatazama na kuona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia chini, dhidi ya ngozi yake.
\v 31 Kisha akasema, "Mungu afanye hivyo kwangu, na zaidi pia, kama kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu yake leo."
\s5
\v 32 Basi Elisha alikuwa ameketi kwenye nyumba yake, na wazee walikuwa wamekaa pamoja naye. Yule mfalme akamtuma mtu wa mbele yake, lakini wakati mjumbe alipokuja kwa Elisha, akawaambia wazee, "Ona jinsi huyu mwana wa muuaji alivytumwa kuchukua kichwa changu? Tazama, wakati yule mjumbe atakapokuja, funga mlango, na uushikilie huo mlango funga dhidi yake asiingie. Je sio sauti ya bwana wake nyuma mguuni pake?"
\v 33 Wakati alipokuwa bado akiongea pamoja nao, kumbe, yule mjumbe alishuka kwake. Mfalme akasema, "Kumbe, masumbuko haya yatoka kwa Yahwe. Kwa nini nimsubiri Yahwe tena?"
\s5
\c 7
\p
\v 1 Elisha akasema, "Sikiliza neno la Yahwe. Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Kesho mda kama huu kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kwenye lango la Samaria.""
\v 2 Basi yule nahodha ambaye alikuwa akitegemea mkono wake amemjibu mtu wa Mungu, na kusema, "Ona, hata kama Yahwe ataweka madirisha mbinguni, je jambo hili linawezekana?" Elisha akajibu, "Ona, utaona ikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hilo."
\s5
\v 3 Basi, kulikuwa na watu wanne wenye ukoma upande wa nje wa lango la mji. Wakaambizana kila mmoja, "Kwa nini tukae hapa hadi hapo tutakapokufa?
\v 4 Kama tukisema kwamba tutaenda kwenye ule mji, maana mjini kuna njaa, na tutakufa hapo. Lakini kama tukiendelea kukaa hapa, bado tutakufa. Sawa, njoni, twendeni kwenye lile jeshi la Washami. Kama wakitupa uhai, tutakuwa hai, na kama wakituua, tutakufa tu."
\s5
\v 5 Hivyo wakaamka asubuhi kabla giza halijaisha kwenda kwenye kambi ya Washami; Wakati walipofika sehemu ya mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu hapo.
\v 6 Kwa kuwa Bwana alikuwa ameunda jeshi la Washami kusikia sauti ya magari ya farasi, na sauti za farasi-sauti za jeshi jingine kubwa, ndipo wakaambizana kila mmoja wao, "Yule mfalme wa Israeli amekodisha wafalme wa Wahiti na Wamisri waje wapigane dhidi yetu."
\s5
\v 7 Hivyo wale maaskari wakaondoka kungali giza; waliacha mahema yao, punda zao, na kambi kama ilivyokuwa, na kukimbia kwa ajili ya maisha yao.
\v 8 Wakati wale watu wenye ukoma walipokuja sehemu ya mwisho wa kambi, wakaenda kwenye hema moja na kula na kunywa, na kubeba fedha na dhahabu na nguo, na kwenda na kuzificha. Wakarudi na kuingia kwenye hema nyingine na kubeba kutoka pale pia, na kwenda kuvificha.
\s5
\v 9 Basi, wakaambizana kila mmoja, "Hatufanyi sahihi. Siku hii ni siku ya habari njema, lakini tunanyamaza kimya kuhusu hili. Kama tukisubiri mpaka kutakapopambazuka, adhabu itakuwa juu yetu. Basi, njoni, twendeni na kuwaambia nyumba ya mfalme."
\v 10 Kwa hiyo wakaenda na kuwaita mabawabu wa mji. Wakawaambia, wakisema, "Tumeenda kambi ya Washami, lakini hapakuwa na mtu pale, hakuna sauti ya mtu yeyote, lakini kulikuwa na farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na zile hema kama zilivyokuwa."
\v 11 Ndipo mabawabu wakatoa habari, ndipo wakaambiwa ndani ya nyumba ya mfalme.
\s5
\v 12 Basi yule mfalme akainuka usiku nakusema kwa watumishi wake, "Nitawaambia sasa kile ambacho Washami walichotufanyia. Wanajua kwamba tunanjaa, hivyo wameondoka kwenye kambi kwenda kujificha kwenye mashamba. Wanasema, 'Wakati watakapotoka mjini, tutawakamata wakiwa hai, na kuingia mjini."
\v 13 Mmoja wa wale watumishi wa mfalme akajibu na kusema, "Nakuomba, ngoja baadhi ya watu wachukue farasi watano wale waliosalia, ambao wamebaki kwenye mji. Wako kama mkutano wote wa Israeli waliobaki-wengi wamekufa; ngoja tuwatume na tuone."
\s5
\v 14 Hivyo wakachukua magari mawili ya farasi pamoja na farasi, na mfalme akawatuma baada ya jeshi la Washami, akisema, "Enendeni mkaone."
\v 15 Wakawafuata kwenda Yordani, na barabara zote zilikuwa zimejaa na vifaa ambavyo Washami walivitupa wapate kukimbia haraka. Kwa hiyo wale wajumbe wakarudi na kumwambia mfalme.
\s5
\v 16 Wale watu wakatoka nje na wakaziteka nyara zile kambi za Washami. Hivyo kipimo cha unga mzuri uliuzwa kwa shekeli moja, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli moja, kama vile ambavyo neno la Yahwe lilivyosema.
\v 17 Naye mfalme alimwagiza yule nahodha ambaye alitegemea mkono wake kuwa mkuu wa lango, na watu wakamkanyaga chini langoni. Alikufa kama mtu wa Mungu alivyosema, ambaye ameongea wakati yule mfalme alipomshukia.
\s5
\v 18 Basi ikatokea kama yule mtu wa Mungu alivyosema kwa mfalme akisema, "Mda kama huu kwenye lango la Samaria, vipimo viwili vya shayiri vitapatikana kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli."
\v 19 Yule nahodha alimjibu yule mtu wa Mungu na kusema, "Tazama, hata kama Yahwe angefanya madirisha mbinguni, je hiki kitu kingeweza kutokea" Elisha akasema, "Tazama, utaona kikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hicho."
\v 20 Hivyo ndivyo haswa kilichompata, kwa kuwa watu wakamkanyaga kwenye lango, na kufa.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Basi, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye alimfufulia mtoto wake. Akamwambia, "Inuka na uenede pamoja na nyumba yako, na uishi popote uwezapo katika nchi nyingine, kwa sababu Yahwe ameiita njaa ambayo itakuja katika hii nchi kwa miaka saba."
\v 2 Basi yule mwanamke akainuka na akatii lile neno la mtumishi wa Mungu. Akaenda na nyumba yake na kuishi kwenye nchi ya Wafilisti miaka saba.
\s5
\v 3 Ikafika kama mwishoni mwa miaka saba yule mwanamke akarudi kutoka kwenye ile nchi ya Wafilisti, na kwenda kwa mfalme kumuomba nyumba yake na kwa ajili ya nchi yake.
\v 4 Basi mfalme alikuwa anaongea na Gehazi yule mtumishi wa Mungu, akisema, "Tafadhali niambie yale mambo makubwa ambayo Elisha ameyafanya."
\s5
\v 5 Basi alipokuwa akimwambia yule mfalme jinsi gani Elisha alivyomfufua yule mtoto aliyekufa, huyo mwanamke ambaye mtoto wake aliyekuwa amefufuliwa akaja kumuomba yule mfalme kwa ajili ya nyumba yake na nchi yake. Gehazi akasema, "Bwana wangu, mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, na huyu ndiye mtoto wake, ambaye Elisha amemfufua."
\v 6 Wakati yule mfalme alipomuuliza yule mwanamke kuhusu mtoto wake, alimwelezea yule mfalme. Ndipo mfalme akamwagizia ofisa makini, akisema, "Mrudishie vyote vilivyokuwa vyake na mavuno yake yote ya kwenye mashamba tangu siku alipoondoka hadi sasa."
\s5
\v 7 Elisha akaja Damaskasi ambako Ben Hadadi yule mfalme wa Shamu alikuwa anaumwa. Yule mfalme aliambiwa, "Yule mtu wa Mungu amekuja hapa."
\v 8 Mfalme akamwambia Hazaeli, "Chukua zawadi kwenye mkono wako na uende ukakutane na mtu wa Mungu, na ukazungumze na Yahwe kupitia yeye, ukisema, "Je nitapona huu ugonjwa wangu?"
\v 9 Basi Hazaeli akaenda kuonana naye na kuchukua zawadi zake za kila kitu kizuri cha Damskasi, akabeba ngamia arobaini. Hivyo Hazaeli akaja na kusimama mbele ya Elisha na kusema, "Mtoto wako Ben Hadadi mfalme wa Shamu amenituma kwako, kusema, "Je nitapona huu ugonjwa?"
\s5
\v 10 Elisha akamwambia, "Nenda, kwa Ben Hadadi, 'Utapona hakika,' lakini Yahwe amenionyesha kwamba atakufa hahkika."
\v 11 Basi Elisha akamtumbulia macho Hazaeli hadi alipojisikia aibu, na yule mtu wa Mungu akalia machozi.
\v 12 Hazaeli akauliza, kwa nini unalia, bwana wangu?" Akajibu, "Kwa sababu najua uovu ambao utakaoufanya kwa watu wa Israeli. Utazichoma moto ngome zao kwa moto, na utawaua vijana wao kwa upanga, kuwaseta vipande vipande watoto wao wachanga, na kuwapasua mimba zao wanawake wenye mimba."
\s5
\v 13 Hazaeli akajibu, Ni nani mtumwa wako, ambaye atafanya jambo hili kubwa? Yeye ni mbwa tu." Elisha akajibu, "Yahwe amenionyesha kwamba utakuwa mfalme juu ya Shamu."
\v 14 Ndipo Hazaeli akamwacha Elisha na kuja kwa bwana wake, ambaye alimwambia, "Je Elisha alikwambiaje?" Akajibu, "Ameniambia kwamba utapona bila shaka."
\v 15 Basi siku ya pili yake Hazaeli akachukua blangeti na kulichovya kwenye maji, na kulitandaza kwenye uso wa Ben Hadadi hivyo akafa. Basi Hazaeli akawa mfalme katika sehemu sehemu yake.
\s5
\v 16 Katika mwaka wa kumi na tano wa Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Yehoramu akaanza kutawala. Alikuwa mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Alianza wakati Yehoshafati alikuwa mfalme wa Yuda.
\v 17 Yoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka minane katika Yerusalemu.
\s5
\v 18 Yoramu akatembea kwenye njia ya huyo mfalme wa Israeli, kama walivyokuwa wakifanya kwenye nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa na binti wa Ahabu kama mke wake, na alifanya uovu usoni kwa Yahwe.
\v 19 Walakini, kwa sababu ya mtumishi wake Daudi, Yahwe hakutaka kuiharibu Yuda, tangu alipomwambia kwamba atampatia wazao.
\s5
\v 20 Katika siku za Yoramu, Edomu akaasi kutoka chini ya mkono wa Yuda, na wakamfanya mfalme juu yao wenyewe.
\v 21 Basi Yehoramu akaenda na maamri jeshi na magari ya farasi yote. Ilitokea kwamba akaamka usiku na kushambulia na kuwazunguka Waedomu, waliokuwa wamemzunguka na wale maamri jeshi wa magari ya farasi. Ndipo wanajeshi wa Yehoramu wakakimbilia wajumbani kwao.
\s5
\v 22 Hivyo Edomu aliasi dhidi ya utawala wa Yuda katika siku hizi. Libna pia aliasi katika kipindi hicho hicho.
\v 23 Kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoramu, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?
\v 24 Yehoramu akafa na kuzikwa pamoja na baba zake, na akalala pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Ndipo Ahazi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\v 25 Katika mwaka wa kumi na mbili wa Yohoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
\v 26 Ahazi alikuwa ana umri wa miaka ishirini na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Athalia; alikuwa mtoto wa Omri, mfalme wa Israeli.
\v 27 Ahazia alitembelea katika nyumba ya Ahabu; alifanya yale yaliyo maovu katika uso wa Yahwe, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa kuwa Ahazia alikuwa mkwe kwenye nyumba ya Aabu.
\s5
\v 28 Ahazia akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Shamu, katika Ramath Geleadi. Washami wakamjeruhi Yoramu.
\v 29 Mfalme Yoramu akarudi ili auguzwe huko Yezreeli kwenye yale majeraha ambayo Washami walimpatia huko Rama. Wakati alipopigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Hivyo Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme Yuda, akashuka kwa Yezreeli kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Nabii Elisha akamwita mmoja wa watoto wa manabii na kumwambia, "Vaa kwa kwa safari, halafu chukua hii chupa ndogo ya mafuta kwenye mikono yako na uende Romoth Geliadi.
\v 2 Wakati utakapofika, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi, na uende ukaingie na kumfanya ainuke kutoka miongoni mwa rafiki zake, na ukampeleke katika chumba cha ndani.
\v 3 Kisha chukua ile chupa ya mafuta na imiminie kwenye kichwa chake na kusema, 'Yahwe anasema hivi: "Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. "Halafu fungua mlango, na kukimbia; usichelewe."
\s5
\v 4 Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Romoth Geliadi.
\v 5 Wakati alipofika, kumbe, wale manahodha wa lile jeshi walikuwa wamekaa. Hivyo yule nabii kijana akasema, "Nimekuja mara moja naneno kwako, nahodha." Yehu akajibu, "kwa yupi katika sisi?" Yule nabii kijana akajibu, "Kwako nahodha."
\v 6 Basi Yehu akainuka na kwenda kwenye nyumba, na yule nabii akammiminia mafuta kwenye kichwa chake na kumwambia Yehu, "Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: 'Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Yahwe, juu ya Isaraeli.
\s5
\v 7 Wewe lazima uiue familia ya Ahabu bwana wako, ili niweze kulipiza kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa Yahwe, ambao waliokuwa wameuawa kwa mkono wa Yezebeli.
\v 8 Kwa kuwa nyumba yote ya Ahabu itaangamia, na nitamkatilia mbali kila mtoto wa kiume wa Ahabu, yeyote awe mtumwa au mtu huru.
\s5
\v 9 Nitaifanya nyumba ya Ahabu kama nyumba ya Yerobohamu mwana wa Nebati na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya.
\v 10 Mbwa watamla Yezebeli katika Yezreeli, na hakutakuwa na mtu wa kumzika." Kisha nabii akafungua mlango na kukimbia.
\s5
\v 11 Kisha Yehu akatoka kwenda kwa watumishi wa bwana wake, na mmoja akamwambia, "Je kila kitu kiko sawa? Kwa nini huyu mwenda wazimu amekuja kwako?" Yehu akawajibu, "Mnamjua huyo mtu na mambo asemayo."
\v 12 Wakasema, "Huo ni uongo. Tuambie." Yehu akajibu, "Alisema hivi na vile juu yangu, na pia akasema, 'hivi ndivyo Yahwe asemavyo: Nimekumiminia mafuta kama mfalme juu ya Israeli.""
\v 13 Kisha kila mmoja wao akachukua vazi haraka na kuweka chini ya Yehu juu ya madaraja. Wakapiga baragumu na kusema, "Yehu ni mfalme."
\s5
\v 14 Katika njia hii Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi akafanya njama juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiilinda Ramothi Gileadi, yeye na Israeli yote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu,
\v 15 lakini mfalme Yoramu alikuwa amesharudi kwa Yezreeli ili kuponywa yale majeraha aliyokuwa ameyapewa na Washami, wakati akiwa anapigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Yehu akawaambia watumishi wa Yoramu, "kama hili ndilo wazo lako, kisha usimwache mtu aondoke na kwenda nje ya mji, ili aende kupeleka habari hii Yezreeli."
\v 16 Basi Yehu akaendesha gari la farasi mpaka Yezreeli; kwa kuwa Yoramu alikuwa amelala huko. Basi Ahazi mfalme wa Yuda alikuwa ameshuka chini kuonana na Yoramu.
\s5
\v 17 Mlinzi alikuwa amesimama juu ya mnara katika Yezreeli, akaliona lile kundi la Yehu alipokuwa akija kwa mbali kidogo; akasema, "Naona kundi la watu wanakuja." Yoramu akasema, "Chukua mwendesha farasi, na umtume akakutane nao; mwambie aseme, "Je mnakuja kwa amani?""
\v 18 Hivyo mwendesha farasi akatoka kumlaki; akasema, "Mfalme asema hivi: Je mnakuja kwa amani?"' Basi Yehu akasema, "Wewe una nini na amani? Geuka na unifuate nyuma." Kisha yule mlinzi akamwambia mfalme, Yule mjumbe ameshaonana nao, lakini anarudi."
\s5
\v 19 Kisha akapeleka mpanda farasi wa pili, ambaye alikuja kwao na kusema, "Mfalme asema hivi: 'Je mnakuja na amani?"' Yehu akajibu, "Wewe una nini na amani? Geuka na kunifuata nyuma.
\v 20 Tena yule mlinzi akatoa taarifa, "Amekwisha kuonana nao, lakini hatorudi. Kwa kuwa hilo gari la farasi limekuwa likiendeshwa ndivyo ambavyo Yehu mwana wa Nimshi aendeshavyo; anaendesha kwa kasi."
\s5
\v 21 Hivyo Yoramu akasema, "Andaa gari langu la farasi liwe tayari." Wakaandaa gari lake la farasi, na Yoramu mfalme wa Israeli na Ahazi mfalme wa Yuda akaendesha, kila mmoja kwenye gari lake la farasi, kumlaki Yehu. Wakamkuta kwenye mali ya Nabothi Myezreeli.
\v 22 Wakati Yoramu alipomuona Yehu, alisema, "Je unakuja katika hali ya amani, Yehu?" Akajibu, "Amani gani hapo, wakati uzinzi wa ukahaba hufanywa na uchawi wa mama yako Yezebeli umejaa tele?"
\s5
\v 23 Basi Yoramu akarudisha magari yake ya farasi na kukimbia na kumwambia Ahazia, "Kuna udanganyifu, Ahazia.
\v 24 Ndipo Yehu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote na kumpiga Yoramu kati ya mabega yake; mshale ukaenda kwenye moyo wake, akaanguka chini kwenye gari lake la farasi.
\s5
\v 25 Ndipo Yehu akamwambia Bidkari nahodha wake, "Mchukue na mtupie kwenye shamba la Nabothi Myezreeni. Fikiria kuhusu vile ambavyo wewe na mimi tulivyoendesha pamoja baada ya Ahabu baba yake, Yahwe aliuweka juu unabii dhidi yake:
\v 26 Jana niliona damu ya Nabothi na damu ya watoto wake - asema Yahwe - na nitahakikisha unalipia hili shamba - asema Yahwe. Sasa basi, mchukue na mtupe kwenye hili shamba, sawa sawa na neno la Yahwe."
\s5
\v 27 Wakati Ahazi yule mfalme wa Yuda alipoliona hili, akakimbia kwa njia ya Bethi Hagani. Lakini Yehu akamfuata, na kusema, "Muulie humo kwenye gari la farasi," na wakampiga mahali pa kupandia Guri, karibu na Ebleamu. Ahazi akakimbilia Megido na kufia pale.
\v 28 Watumishi wake wakaubeba mwili wake kwa magari ya farasi kwenda Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake pamoja na baba zake katika mji wa Daudi.
\s5
\v 29 Basi ilikuwa mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu huyo Ahazia akaanza kutawala juu ya Yuda.
\s5
\v 30 Wakati Yahu alipokuja kwa Yezebeli, Yezebeli akasikia juu ya hilo, akapaka wanja kwenye macho yake, akatengeneza nywele zake vizuri, na kuchungulia kwenye dirisha.
\v 31 Kadiri Yehu alipokuwa akiingia kwenye lango, akamwambia, "Je unakuja kwa amani, wewe Zimri, muuaji wa bwana wako?"
\v 32 Yehu akatazama juu ya dirisha na kusema, "Ni nani yuko upande wangu? Nani?" Matowashi wawili au watatu wakachungulia nje.
\s5
\v 33 Basi Yehu aksema, "Mtupeni chini." Hivyo wakamtupa Yezebeli chini, na damu yake nyingine ikamwagika kwenye ukuta na farasi, na Yehu akamkanyaga kanyaga chini ya miguu.
\v 34 Basi Yehu akaingia hiyo sehemu, akala na kunywa. Kisha akasema, "Mtazamani sasa huyu mwanamke aliyelaaniwa na kumzika, kwa kuwa ni binti wa mfalme."
\s5
\v 35 Wakaenda kumzika, lakini hawakumkuta ila fuvu, miguu, na viganga vya mikono yake.
\v 36 Basi wakarudi na kumwambia Yehu. Akasema, "Hili ndilo neno la Yahwe ambalo ameliongea kupitia Eliya Mtishbi, likisema, 'Katika nchi Yezreeli mbwa ataula mwili wa Yezebeli,
\v 37 na mwili wa Yezebeli utakuwa kama kinyesi juu ya uso wa mashamba katika nchi ya Yezreeli, kwa hiyo basi hakuna atakayeweza kusema, "Huyu ni Yezebeli.""
\s5
\c 10
\p
\v 1 Basi Ahabu alikuwa na watoto sabini katika Samaria. Yehu akaandika barua na kuzituma kwenda Samaria, kwa watawala wa Yezreeli, pamoja na wazee na walinzi wa wana wa Ahabu akisema,
\v 2 "Wana wa bwana wako wako pamoja na wewe, na wewe pia una magari ya farasi na farasi na kuimarisha mji dhidi ya maadui na silaha. Hivyo basi, haraka iwezekanavyo barua hii ikufikiapo,
\v 3 mchagueni aliye bora na anayestahili miongoni mwa mtoto wa bwana wenu na kumuweka kwenye kiti cha kifalme cha baba yake, na kupigania ufalme wa bwana wenu."
\s5
\v 4 Lakini waliogopa na kusema miongoni mwao, "Tazama, wafalme wawili hawatasimama mbele ya Yehu. Hivyo tutasimamaje?"
\v 5 Kisha yule mtu ambaye alikuwa kiongozi kwenye nyumba ya mfalme, na wale waliowalea watoto, wakatuma ujumbe kwa Yehu, kusema, "Sisi ni watumishi wako. Tutafanya chochote utakacho tuamuru. Hatutamfanya mtu yeyote kuwa mfalme. Fanya lile lililojema machoni pako."
\s5
\v 6 Kisha Yehu akaandika barua mara ya pili, akisema, "Kama mko upande wangu, na kama mtasikiliza sauti yangu, mtachukua vichwa vya watu wa wana wa mabwana wenu, na mje kwangu Yezreeli kesho mda kama huu." Ndipo wana wa wafalme, sabini kwa hesabu, waliokuwa watu muhimu huko mjini, ambao walikuwa wakiwaleta.
\v 7 Hivyo barua ilipokuja kwao, waliwachukua wana wa wafalme na kisha kuwaua, watu sabini, wakaweka vichwa vyao kwenye vikapu, na kuivituma kwa Yehu katika Yezreeli.
\s5
\v 8 Mjumbe mmoja akaja kwa Yehu, akisema, "Wamevileta vile vichwa vya watoto wa wafalme." Hivyo akasema, viwekeni kwenye mafungu mawili kwenye lango hadi asubuhi."
\v 9 Asubuhi Yehu akatoka nje na kusimama, na kusema kwa watu wote, "Ninyi hamna hatia. Tazameni, nimefanya fitina dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua hawa wote?
\s5
\v 10 Sasa hakika tafakarini kwamba hakuna sehemu ya neno la Yahwe, lile alilonena Yahwe kuhusu familia ya Ahabu, itaanguka kwenye aridhini, kwa kuwa Yahwe amefanya kile alichokiongea kupitia mtumishi wake Eliya."
\v 11 Basi Yehu akawaua wote waliokuwa wamebakia wa familia ya Ahabu katika Yezreeli, na watu wake muhimu wote, marafiki zake wa karibu, na makuhani wake, hakuna hata mmoja wao alisalia.
\s5
\v 12 Kisha Yehu akainuka na kuondoka; akaenda Samaria. Kadiri alivyokuwa akikaribia Bethi Ekedi ya wachungaji,
\v 13 akamlaki na ndugu wa Ahazia mfalme wa Yuda. Yehu akawaambia, "Ninyi ni akina nani?" Wakajibu, "Sisi ni ndugu zake na Ahazia, na tunashuka chini kuwasalimia watoto wa mfalme na watoto wa Malkia Yezebeli."
\v 14 Yehu akawaambia watu wake mwenyewe, "Wachukue wakiwa hai." Hivyo wakawachukua wakiwa hai na kuwaua kwenye kisima cha Bethi Ekedi, watu wote arobaini na mbili. Hakumwacha hata mmoja wao akiwa hai.
\s5
\v 15 Baada ya Yehu kuondoka huko, akakutana na Yehonadabu mwana wa Rekabu anakuja kukutana naye. Yehu akamsalimia na kisha akamwambia, "Je moyo wako uko na mimi, kama moyo wangu ulivyo pamoja na wako?" Yehonadabu akajibu, Ndio." Yehu akasema, "kama ni ndio, nipatie mkono wako." Kisha Yehonadabu akampatia mkono wake, na Yehu akampandisha Yehonadabu juu kwenye magari ya farasi pamoja naye.
\v 16 Yehu akasema, "Fuatana pamoja nami na uone wivu wangu kwa Yahwe." Hivyo alikuwa na Yehonadabu akiendesha gari la farasi.
\v 17 Wakati alipokuja Samaria, Yehu akawaua wote waliobakia kutoka uzao wa Ahabu katika Samaria, hata akawaangamiza ukoo wa kifalme wa Ahabu, kama walivyokuwa wameambiwa kabla ya neno la Yahwe, ambalo aliloambiwa Eliya.
\s5
\v 18 Kisha Yehu akawakusanya watu wote akwaambia, "Ahabu alimtumikia Baali kidogo, lakini Yehu atamtumikia sana.
\v 19 Basi niitieni manabii wote wa Baali, wote wamwabuduo, na makuhani wake wote. Asikosekane mtu hata mmoja, kwa kuwa nina dhabihu kubwa nataka kutoa kwa Baali. Yeyote atakayeshindwa kuja hataishi." Lakini Yehu alifanya haya kwa udanganyifu, kwa dhamira ya kuwaua wanaomwabudu Baali.
\v 20 Yehu akasema, "Tengeni mda tuwe na mkutano kwa ajili ya Baali." Hivyo wakalitangaza.
\s5
\v 21 Kisha Yehu akatuma Israeli yote na wamwabuduo Baali waje, hivyo basi hakuna mtu hata mmoja ambaye aliacha kuja. Walikuja kwenye hekalu la Baali, na ilijaa kutoka mwanzo hadi mwisho.
\v 22 Yehu akamwambia yule mtu aliyekuwa anatunza kabati la nguo za makuhani, "Uwatolee mavazi wote wamwabuduo Baali." Basi yule mtu akawatolea nguo.
\s5
\v 23 Basi Yehu akaingia pamoja na Yohonadabu mwana wa Rekabu kwenye nyumba ya Baali, na kisha akawaambia wanaomwabudu Baali, "Tafuteni na muhahakishe kwamba hakuna mtu hapa pamoja na ninyi kutoka watumishi wa Yahwe, lakini wamwabuduo Baali peke yao."
\v 24 Kisha wakaenda kutoa dhabihu na sadaka ya kutekeza. Basi Yehu alichagua watu themanini ambao walikuwa wamesimama nje, na aliwaambia, Kama mtu yeyote miongoni mwa hawa watu ambao nimewaleta kwenye mikono yenu atoroke, yeyote atakayemwacha huyo mtu atoroke, maisha yake yatachukuliwa kwa ajili ya yule aliyeokoka."
\s5
\v 25 Hivyo kisha baada ya mda mfupi Yehu alipomaliza kutoa sadaka ya kutekezwa, akamwambia mlinzi na manahodha, "Ingieni na muwaue. Msimwache mtu yeyote atoke." Basi waliwaua kwa makali ya upanga, na mlinzi na manahodha wakawatupa nje na kwenda kwenye chumba cha ndani cha nyumba ya Baali.
\v 26 Wakazitoa nguzo za mawe ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Baali, na kisha kuzichoma.
\v 27 Kisha wakazivunja zile nguzo za Baali, na kuiharibu nyumba ya Baali na kuifanya choo, ambacho kipo hadi leo.
\v 28 Hivi ndivyo ambavyo Yehu alivyomharibu muabudu Baali kutoka Israeli.
\s5
\v 29 Lakini Yehu hakuacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo ilfanya Israeli kutenda dhambi-ambayo ni, kumwabudu ndama wa dhahabu katika Betheli na Dani.
\v 30 Hivyo Yahwe akamwambia Yehu, "Kwa kuwa umefanya vema kwa kufanya yaliyo sahihi kwenye macho yangu, na kumailiza kwenye nyumba ya Ahabu kulingana na yote yaliyokuwa kwenye moyo wangu, uzao wako utakaa kwenye kiti cha Israeli hadi kizazi cha nne."
\v 31 Lakini Yehu hakujali kutembea kwenye sheria ya Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote. Hakugeuka kutoka kwenye dhambi za Yeroboamu, ambayo iliwafanya Israeli kutende dhambi.
\s5
\v 32 Siku zile Yahwe akaanza kupunguza mikoa ya Israeli, na Hazaeli kuwashinda Waisraeli mipakani mwa Israeli,
\v 33 kutoka Yordani upande wa mashariki, nchi yote ya Gileadi, Wagadi, na Wareubeni, na Wamanase, kutoka Aroeri, alipo karibu na bonde la Arnoni, kupita Geleadi hadi Bashani.
\s5
\v 34 Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Yehu, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 35 Yehu akalala na wazee wake, na walimzika katika Samaria. Kisha Yehoahazi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.
\v 36 Mda ambao Yehu alitawala juu ya Israeli katika Samaria ulikuwa miaka ishini na nane.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Basi Athalia, mama yake na Ahazia, alipoona kwamba mtoto wake amekufa, aliinuka na kuwaua watoto wote wa kifalme.
\v 2 Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.
\v 3 Alikuwa pamoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya Yahwe, kwa mda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.
\s5
\v 4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta maamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya Yahwe. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya Yahwe. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.
\v 5 Akawaamuru, akisema, "Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,
\v 6 na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi."
\s5
\v 7 Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya mfalme.
\v 8 Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.
\s5
\v 9 Hivyo mamia ya maamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.
\v 10 Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa maamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 11 Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.
\v 12 Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpatia mikataba ya agano. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, "Mfalme na aishi!"
\s5
\v 13 Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 14 Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na manahodha na wapiga mabaragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, "Uhaini! Uhaini!"
\s5
\v 15 Ndipo Yehoyada yule kuhani akawaagiza maamri jeshi wa mamia ambao waliokuwa juu ya jeshi, akisema, "Mtoeni kwenye safu." Atakayemfuata, muueni kwa upanga." Kwa kuwa kuhani alisema, "Msimwache auawe kwenye nyumba ya Yahwe."
\v 16 Hivyo wakamtwaa kadiri walivyokuwa wakiikaribia hiyo sehemu iliyokuwa na farasi wakaingia chini, na akauawa huko.
\s5
\v 17 Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya Yahwe na mfalme na watu, ambao wangekuwa watu wa Yahwe, na pia kati ya mfalme na watu.
\v 18 Basi watu wote wa nchi wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuingusha chini. Wakaangusha madhabahu ya Baali na sanamu zake wakazivunja vipande vipande, na kumuua Matani, mfalme wa Baali, mbele ya haya madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawachagua walinzi juu ya hekalu la Yahwe.
\s5
\v 19 Yehoyada akawachukua maamiri jeshi wa mamia, Wakari, walinzi, na watu wote wa nchi, na kwa pamoja wakamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe na wakaenda kwenye nyumba ya mfalme, wakaingia kwa njia ya lango la walinzi. Yoashi akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi cha mfalme.
\v 20 Hivyo watu wote wa nchi wakamsifu, na nchi ilikuwa kimya baada ya Athalia kuuawa kwa upanga kwenye nyumba ya mfalme.
\s5
\v 21 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa mda wa miaka arobaini huko Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba.
\v 2 Yoashi akafanya yaliyo mema usoni mwa Yahwe siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alimfundisha.
\v 3 Lakini sehemu ya juu haikuchukuliwa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kuchoma ubani kwenye sehemu za juu.
\s5
\v 4 Yoashi akamwambia kuhani, "Pesa zote zilizokuja kama sadaka takatifu kwenye nyumba ya Yahwe, pesa ya matumizi pesa ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na pesa yote aonayo moyoni mwake kuileta kwenye nyumba ya Yahwe-
\v 5 makuhani watapokea pesa kutoka miongoni mwa mmoja wa watunza pesa na kutengeneza kila sehemu itakayoonekana imeharibika kwenye hekalu."
\s5
\v 6 Lakini kama mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani hawakuwa wameandaa kitu chochote kwenye hekalu.
\v 7 Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na kuhani mwingine; akawaambia, "Kwa nini hamjaandaa kitu chochote kwenye hekalu? Sasa msichukue tena pesa kutoka kwa walipa kodi wenu, lakini chukueni kile kilichokuwa kikikusanywa kwa ajili ya matengenezo ya hekalu na uwapatia wale wanaoweza kufanya matengenezo.
\v 8 Hivyo makuhani wakakubaliana wasichukue pesa tena kutoka kwa watu na wasitengeneze wenyewe.
\s5
\v 9 Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya Yahwe. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 10 Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwadishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 11 Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya Yahwe. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya Yahwe,
\v 12 na waashi na wakata mawe, kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kutengenezea nyumba ya Yahwe, na yote iliyokuwa inahitajika kulipwa kwa ajili ya kuitengeneza.
\s5
\v 13 Lakini ile pesa iliyokuwa imeletwa kwenye nyumba ya Yahwe haikulipwa kwa ajili ya vikombe vya fedha, mabeseni, au dhahabu au fedha yoyote ya vyombo.
\v 14 Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 15 Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu.
\v 16 Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la Yahwe, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.
\s5
\v 17 Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambuliwa na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua.
\v 18 Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye gala la nyumba ya Yahwe na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu.
\s5
\v 19 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 20 Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila.
\v 21 Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoazi mwana wa Yehu alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na saba.
\v 2 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe na kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kuasi; na Yehoazi hakurudi kutoka kwao
\s5
\v 3 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, na akaendelea kuwakabidhi kwenye mikono ya Hazaeli mfalme wa Shamu na kwenye mikono ya Ben Hadadi mwana wa Hazaeli.
\v 4 Hivyo Yehoazi akamsihi Yahwe, na Yahwe akamsikiliza kwa sababu aliona mateso ya Israeli, vile mfalme wa Shamu alivyokuwa akiwatesa.
\v 5 Basi Yahwe akawapa Israeli ulinzi, na wakakimbia kutoka kwenye mikono ya Washami, na watu wa Israeli wakaanza kuishi kwenye nyumba zao kama walivyokuwa kabla.
\s5
\v 6 Hata hivyo, hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambaye alisabisha Israeli kuasi, na wakaendelea katika hayo; na huyo Ashera akabaki hivyo katika Samaria.
\v 7 Washami wakamuacha Yehoazi pamoja na waendesha farasi hamsini tu, magari ya farasi kumi, na watembea kwa miguu elfu kumi, kwa ajili ya mfalme wa Shamu alikuwa ameiharibu na kuwafanya kama makapi yaliyopurwa.
\s5
\v 8 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yehoazi, na yote aliyoyafanya na nguvu zake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 9 Basi Yehoyazi akalala na mababu zake, na wakamzika katika samaria. Yohoashi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\v 10 Katika mwaka wa thelathini na saba wa Yoashi mfalme wa Yuda, utawala wa Yehoashi mwana wa Yehoazi ulianza juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na sita.
\v 11 Akafanya yaliyo maovu kwenye uso wa Yahwe. Hakuacha nyuma dhambi zozote za Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa kuwa aliwafanya Israeli kuasi, lakini alitembea pamoja nao.
\s5
\v 12 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoashi, na yote aliyoyafanya, na shujaa wake ambaye aliyepigana dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 13 Yehoashi akalala na mababu zake, na Yeroboamu akakalia kiti chake cha enzi cha kifalme. Yehoashi akazikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli.
\s5
\v 14 Basi Elisha akaugua ugonjwa ambao baadae ulimuua, hivyo Yehoashi yule mfalme wa Israeli akashuka chini kwake na kumlilia juu yake. Akasema, "Baba yangu, baba yangu, haya magari ya farasi ya Israeli na hawa waendesha farasi wanakuchukua!"
\v 15 Elisha akamwambia, "Chukua upinde na mishale," basi Yoashi akachukua upinde na mishale.
\v 16 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, "Weka mkono wako kwenye upinde," basi akaweka mkono wake kwenye huo. Kisha Elisha akalaza mikono yake kwenye mikono ya mfalme.
\s5
\v 17 Elisha akasema, "Fungua dirisha upande wa mashariki," basi akalifungua. Kisha Elisha akasema, "Funga", na akafunga. Elisha akasema, "Huu ndiyo mshale wa ushindi wa Yahwe, huu mshale wa ushindi juu ya Shamu, kwa kuwa utawapiga Washami katika Afeki hadi utakapowaangamiza."
\v 18 Kisha Elisha aksema, "Chukua mishale," basi Yoashi akaichukua. Akamwambia mfalme wa Israeli, "Piga chini pamoja nao," na akapiga chini mara tatu, kisha akaacha.
\v 19 Lakini mtu wa Mungu alikuwa na hasira naye na akasema, "Ungelipiga chini mara tano au mara sita. Ndipo ungeipiga Shamu hadi kuiangamiza, lakini sasa utaipiga Shamu mara tatu tu."
\s5
\v 20 Kisha Elisha akafa, na wakamzika. Sasa vikundi vya Wamoabi wakaingia kwenye nchi mwanzoni mwa mwaka.
\v 21 Ikawa walipokuwa wakimzika huyo mtu, wakaona kundi la Wamoabi, hivyo wakautupia ule mwili kwenye kaburi la Elisha. Mara yule mtu alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama kwa miguu yake.
\s5
\v 22 Hazaeli mfalme wa Shamu akawatesa Israeli siku zote za Yehoazi.
\v 23 Lakini Yahwe aliwahurumia Israeli, na alikuwa na huruma juu yao na kushuhulika kwa ajili yao, kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Hivyo Yahwe hakuwaangamiza, na bado hakuwatupa kutoka kwenye uwepo wake.
\v 24 Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, na Ben Hadadi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\v 25 Yehoashi mwana wa Yehoazi akairudisha kutoka kwa Ben Hadadi mwana wa Hazaeli miji ambayo aliichukua kutoka Yehoazi baba yake kwa vita. Yehoashi akamshambulia mara tatu, na akaipata miji ya Israeli.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoazi, mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
\v 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tanao wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu.
\v 3 Mama yake alikuwa anaitwa Yehoyadani, wa Yerusalemu. Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa macho ya Yahwe, sio kama baba yake Daudi. Alifanya kila kitu ambacho Yoashi, baba yake, alichukuwa amekifanya.
\s5
\v 4 Lakini sehemu ya juu haikuondolewa. Watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza ubani katika sehemu mahala pa juu.
\v 5 Ikawa mara utawala wake ulipokuwa imara, aliwaua watumishi ambao waliokuwa wamemuua baba yake, mfalme.
\s5
\v 6 Ila hakuwaweka watoto wa wale wauaji kwenye kifo; isipokuwa, alifanya kutokana na kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye sheria, kwenye kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamuru, akisema, "Wababa wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Isipokuwa, kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe."
\v 7 Aliua maaskari elfu kumi wa Edomi kwenye bonde la chumvi; pia alimchukua Sela kwenye vita na kuiita Yoktheeli, ndivyo paitwavyo hadi leo.
\s5
\v 8 Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akisema, "Njoo, tuonane kila mmoja macho kwa macho kwenye mashinadano."
\v 9 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, "Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanuni, kusema, 'Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.
\v 10 Umempiga sana Edomu, na moyo wako umekuinua. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani, kwa nini unataka kujisababishia mataizo na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?"
\s5
\v 11 Lakini Amazia hakutaka kusikia. Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth Shemeshi, ambayo ilikuwa ya Yuda.
\v 12 Yuda walishindwa mbele ya Israeli, na kila mtu akakimbia nyumbani.
\s5
\v 13 Yehoashi mfalme wa Israeli, akamchukua Amazia, mfalme wa Yuda mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, huko Beth Shemeshi. Akaja Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kutoka lango la Efraimu mpaka kwenye pembe ya lango, urefu wa mbali wa dhiraa mia nne.
\v 14 Akachukua dhahabu na fedha zote, na vitu vyote ambavyo vilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na vitu vya thamani kwenye nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia, na kurudi samaria.
\s5
\v 15 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoashi, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Israeli?
\v 16 Kisha Yehoashi akalala na wazee wake na ailizikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, na Yeroboamu, mwanaye, akawa mfalme katika eneo lake.
\s5
\v 17 Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na tano baada ya Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
\v 18 Kama ilivyo kwa mambo mengine yanayomhusu Amazia, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?
\v 19 Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.
\s5
\v 20 Wakamrudisha kwa farasi, na alizikwa pamoja na wazee wake katika mji wa Saudi.
\v 21 Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzaria, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na minne, na walimfanya kuwa mfalme katika nyumba ya kifalme wa baba yake Uzaria.
\v 22 Alikuwa Uzaria ambaye alijenga Elathi na kuirudisha kwa Yuda, baada ya mfalme Uzaria akalala pamoja na mababu zake.
\s5
\v 23 Katika mwaka wa kumi na tano wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka arobaini na moja.
\v 24 Akafanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi zake za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye aliisababisha Israeli kuasi.
\v 25 Akairudisha mipaka ya Israeli kutoka Lebo Hamathi mpaka kwenye Bahari ya Araba, kufuata amri ya neno la Yahwe, Mungu wa Israeli, ambalo aliongea kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, yule nabii, ambaye alitokea Gathi Heferi.
\s5
\v 26 Kwa kuwa Yahwe aliyaona mateso ya Israeli, ambayo yalikuwa makali kwa kila mmoja, wote mtumwa na asyemtumwa, na kwamba hapakuwa na ulinzi kwa ajili ya Israeli.
\v 27 Basi Yahwe akasema kwamba hatoweza kulifuta jina la Israeli chini ya mbingu; badala yake, aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
\s5
\v 28 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yeroboamu, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, jinsi alivyo pigana vita na kuipata tena Damaskasi na Hamathi, ambayo ilikuwa ya Yuda, kwa Israeli, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 29 Yeroboamu akalala na mababu zake, pamoja na mfalme wa Israeli, na Zekaria mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
\v 2 Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu.
\v 3 Alifanya yaliyo mema machoni pa Yahwe, kama baba yake Amazia alivyofanya.
\s5
\v 4 Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu.
\v 5 Yhawe akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.
\s5
\v 6 Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 7 Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake.
\s5
\v 8 Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita.
\v 9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alisababisha Israeli kuasi
\s5
\v 10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.
\v 11 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\v 12 Hili ndilo lililokuwa neno la Yahwe ambalo aliongea na Yehu, kusema, "Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne." Hiyo ikatokea.
\s5
\v 13 Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria.
\v 14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.
\s5
\v 15 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafle wa Israeli.
\v 16 Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwasababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji.
\s5
\v 17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria.
\v 18 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta elfu moja za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake.
\v 20 Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
\s5
\v 21 Kama kwa mabo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya waflme wa Israeli?
\v 22 Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
\s5
\v 23 Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili.
\v 24 Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 25 Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua alipomua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.
\v 26 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\s5
\v 27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini.
\v 28 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru.
\v 30 Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
\v 31 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\s5
\v 32 Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
\v 33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki.
\s5
\v 34 Yotahmu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya.
\v 35 Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitio sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe.
\v 36 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 37 Katika zamani hizo Yahwe akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia.
\v 38 Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akwa mfalme katika mhali pake.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Pemalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda, akaanza kutawala.
\v 2 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Alifanya yasiyo haki usoni mwa Yahwe Mungu wake, kama Daudi babu yake.
\s5
\v 3 Badala yake, akatembea katika njia ya wafalme wa Israeli; hasa, akamuweka mwanaye kwenye moto kama sadaka ya kuteketeza, kufuatana na machukizo ya mataifa, ambayo Yahwe aliwafukuza wana wa Israeli.
\v 4 Akatoa sadaka na kuchoma ubani mahali pa juu, juu ya milima, na chini ya kila mti mbichi.
\s5
\v 5 Kisha Riseni, mfalme wa Shamu na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakaja mpaka Yerusalemu kuteka. Wakamzunguka Ahazi, lakini hawakuweza kumshinda.
\v 6 Katika kipindi hicho, Resini mfalme wa Shamu akamponya Elathi kwa Shamu na kuwapeleka watu wa Yuda nje ya Elathi. Kisha Washami wakaja kwa Elathi ambapo waliishi hadi leo.
\s5
\v 7 Hivyo Ahazi akatuma wajumbe kwenda kwa Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru, akisema, "Mimi ni mtumishi wako na mwanao. Panda juu na uniokoe kutoka kwenye mikononi ya mfalme wa Shamu na kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Israeli, ambao wameniteka."
\v 8 Hivyo Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa imepatikana katika nyumba ya Yahwe na mingoni mwa waweka hazina wa nyumba ya mfalme na kuituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.
\v 9 Kisha mfalme wa Ashuru akamsikiliza, na mfalme wa Ashuru akaenda juu dhidi ya Damaski, akaishinda na kuwabeba watu wake kama wafungwa hadi Kiri. Akamuua Resini pia yule mfalme wa Shamu.
\s5
\v 10 Mfalme Ahazi akaenda Dameski kuonana na Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru. akaiona mdhabahu huko Damski. Akampelekea Uria kuhani mfano wa ile madhabahu na mpangilio wake na mchoro kwa ustadi wote ulikuwa umehitajika.
\v 11 Hivyo Uria yule kuhani akajenga madhabahu kuwa kama mipango ambayo Mfalme Ahazi atakaporudi kutoka Damaski. Akaimaliza kabla mfalme Ahazi hajarudi kutoka Dameski.
\v 12 Kisha mfalme akaja kuto Dameski akaiona ile madhabahu; mfalme akaikaribia ile madhabahu na kutoa sadaka juu yake.
\s5
\v 13 Akatengeneza sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, na kunyunyiza damu ya washirika wake sadaka juu ya madhabahu.
\v 14 Madhabahu ya shaba ambayo ilikuwa mbele ya Yahwe-akaileta kutoka mbele ya hekalu, kutoka kati ya madhabahu yake na hekalu la Yahwe na kuiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
\s5
\v 15 Kisha mfalme Ahazi akamwiamuru Uria kuhani, akisema, "Juu ya madhabahu kubwa teketeza sadaka ya kutekezwa ya asubuhi na sadaka ya kuteketezwa ya nafaka ya jioni, pamoja na sadaka ya watu wote wa nchi, na matoleo ya sadaka ya mazao na sadaka zao za kinywaji. Nyunyiza juu ya hiyo damu yote ya sadaka ya kuteketeza, na damu yote ya kuteketeza. Lakini ile madhabahu ya shaba itakuwa kwa ajili yangu ili niulize ushauri."
\v 16 Uria kuhani akafanya kile ambacho Ahazi aliamuru.
\s5
\v 17 Kisha mfalme Ahazi akaondoa jopo na mabeseni vitako vinavyobebeka; pia akachukua bahari kutoka juu ya ng'ombe wa shaba ambayo ilikuwa chini ya hiyo na kuiweka juu ya sakafu ya mawe.
\v 18 Aliondoa njia iliyokuwa kwa ajili ya kuingia kwenye Sabato ambayo walikuwa wamejenga kwenye hekalu, wote pamoja na mahali pa kuingilia mfalme kwenye hekalu la Yahwe, kwasababu ya mfalme wa Ashuru.
\s5
\v 19 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Ahazi na yale aliyoyafanya, je yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 20 Ahazi alilala pamoja na babu zake na kuzikwa pamoja babu zake katika mji wa Daudi. Hezekia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na moja wa Ahazi mfalme Yuda, utawala wa Hoshea mwana wa Elahi ulianza. Alitawala katika Samaria juu ya Israeli kwa muda wa miaka minane.
\v 2 Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe, ila sio kama waflme wa Israeli ambao ulikuwa kabla yake.
\v 3 Shalmanesa mfalme wa Ashuru akamshambulia, na Hoshea akawa mtumishi na kumletea kodi.
\s5
\v 4 Kisha mfalme wa Ashuru akaona kwamba Hoshea alikuwa na njama dhidi ya yake, kwa kuwa Hoshea aliwatuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri; pia, hakumpatia kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka hadi mwaka.
\v 5 Basi mfalme wa Ashuru akamfunga akamtia kifungoni. Kisha mfalme wa Ashuru akaishambulia nchi yote, akaishambulia Samaria na kuizunguka kwa miaka mitatu.
\v 6 Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaichukua Samaria na akawapeleka Israeli hadi Ashuru. Akawaweka kwenye Hala, kwenye Habori Mto wa Gozani, na katika mji wa Wamedi.
\s5
\v 7 Utekwaji huu ulitokea kwa sababu wana wa Israeli walifanya dhambi dhidi ya Yahwe Mungu wao, ambaye aliwaleta kutoka nchi ya Misri, kutoka chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri. Watu walikuwa wakiabudu miungu mingine
\v 8 na kutembea katika matendo ya wamataifa ambao Yahwe aliwafukuza mbele ya watu wa Israeli, na katika matendo ya wafalme wa Israeli ambayo waliyokuwa wameyafanya.
\s5
\v 9 Wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo mabaya dhidi ya Yahwe Mungu wao. Wakajijengea mahala pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye boma.
\v 10 Pia wakasimamisha nguzo za mawe na Ashera juu ya kila mlima chini ya kila mti mbichi.
\s5
\v 11 Huko wakafukiza ubani katika mahali pa juu pote, kama mataifa walivyokuwa wamefanya, ambao Yahwe aliwafukuza mbele yao. Waisraeli wakafanya mambo maovu ili kuchochea hasira ya Yahwe,
\v 12 wakaabudu sanamu, ambazo Yahwe alizokuwa amewaambia, "Msifanye jambo hili."
\s5
\v 13 Bado Yahwe aliwashuhudia Israeli na Yuda kwa kila nabii na kila muonaji, kusema, "Geukeni kutoka nija zenu mbaya na kuzishika amri zangu na hukumu zangu, na kuwa makini kufuata ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, na ambayo niliwapelekea kwa watumishi wangu manabii."
\s5
\v 14 Lakini hawakuweza kusikia; badala yake walikuwa wakaidi kama baba zao ambao hawakumwamini Yahwe Mungu wao.
\v 15 Walizikataa sheria zake na lile agano ambalo alilifanya pamoja na babu zao, na hilo agano wakakubaliana wapewe. Wakafuata mambo yao yasiyofaa na wakawa hawafai. Wakawafuata mataifa ya kipagani ambao waliwazunguka, ambao Yahwe alikuwa amewaamuru wasiige.
\s5
\v 16 Wakazipuuza amri zote za Yahwe Mungu wao. Wakatengeneza sanamu za kusubu za ndama wawili kuziabudu. Wakatengeza nguzo ya Ashera, na wakaziabudu nyota zote za mbinguni na Baali.
\v 17 Wakawatupia watoto wao wakike kwa wakiume kwenye moto, wakapiga ramli na uchawi, wakajiuza wenyewe kufanya yale ambayo yalikuwa maovu usoni pa Yahwe, na kuichochea hasira yake.
\v 18 Kwa hiyo Yahwe alikuwa na hasira na Israeli na kuwaondoa usoni mwake. Hakubakia mtu hata mmoja isipokuwa kabila la Yuda peke yake.
\s5
\v 19 Hata watu wa Yuda hawakushika amri za Yahwe Mungu wao, lakini badala yake walifuata mambo hayo hayo ya kipagani ambayo Israeli walifuata.
\v 20 Hivyo Yahwe akawakataa vizazi vyote vya Israeli; akawatesa na kuwatia kwenye mkono wa wale wenye kuwateka nyara, hadi atakapokuwa amewatupa usoni mwake.
\s5
\v 21 Akawatoa Israeli kutoka kwenye mstari wa kifalme wa Daudi, na wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nabeti mfalme. Yeroboamu akawapeleka Israeli mbali kutoka kumfuata Yahwe na kuwafanya wafanye dhambi kubwa.
\v 22 Wana wa Israeli wakafuata dhambi zote za Yeroboamu na hawakujiepusha nazo,
\v 23 basi Yahwe akawaondoa Israeli kutoka usoni pake, kama alivyokuwa amesema kupitia watumishi wake wote manabii kwamba angeweza kufanya. Hivyo Israeli walichukuliwa kutoka nchi yao kwenda Ashuru, na iko hivyo hata leo.
\s5
\v 24 Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli na kutoka Kutha, na kutoka Ava, na kutoka Hamathi na Sefarvaimu, na kuwaweka katika mji wa Samaria na kuishi katika huo mji wake.
\v 25 Ikatokea wakati walipoanza kuishi huko hawakumcha Yahwe. Hivyo Yahwe akatuma simba miongoni mwao ambao waliwaua baadhi yao.
\v 26 Basi wakaongea na mfalme wa Ashuru, wakisema, "Wale mataifa uliowaamisha na kuwaweka kwenye miji ya Samaria hawayajui mambo wanayotakiwa kuyafanya kutokana na mungu wa nchi. Hivyo alikuwa amewatuma simba kwenda kwao, na, tazama, wale simba walikuwa wakiwauua watu huko kwa sababu hawakufahamu yale mambo waliyokuwa wanatakiwa kuyafanya kwa mungu wa nchi."
\s5
\v 27 Kisha mfalme wa Ashuru akatoa amri, akisema, "Mchukueni mmoja wa makuhani hapo ambaye mmemleta kutoka huko, na mumwache aende na kuishi huko, na mumwache awafundishe mambo yanayotakiwa kwa mungu wa nchi."
\v 28 Hivyo mmoja wa makuhani ambaye walimchukua kutoka Samaria akaja na kuishi katika Betheli; akawafundisha jinsi wavyotakiwa mcha Yahwe.
\s5
\v 29 Watu wa kila kabila wakajifanyia miungu yao wenyewe, na kuiweka mahala pa juu ambapo Wasamaria walifanya kila kabila katika mji ambako walipoishi.
\v 30 Watu wa Babeli wakatengeneza Sakoth Benithi; watu wa Sakoth wakatengeneza Nergali; watu wa Hamathi wakatengeza Ashima;
\v 31 Waavi wakatengeneza Nibhazi na Tartaki. Nao Wasefarvi wakwachoma watoto wao kwenye moto kwa Adrameleki na Anameleki, wale miungu wa Sefarvaimu.
\s5
\v 32 Pia wakamcha Yahwe, na kuwateua kutoka miongoni mwao makuhani wa mahali pa juu, ambao waliteketeza kwa ajili yao kwenye hekalun mahali pa juu.
\v 33 Wakamcha Yahwe na pia kuabudu miungu yao wenyewe, sawa sawa na tamaduni za mataifa kutoka miongoni mwao waliokuwa wamewachukua.
\s5
\v 34 Hadi siku hii ya leo wameshikilia tamaduni zao za zamani. Wala hawamwogopi Yahwe, wala hawazifuati sheria zake, torati, au amri ambazo Yahwe aliwapa watu wa Yakobo ambaye alemwita jina Israeli
\v 35 pamoja na ambao Yahwe alifanya agano nao na kuwaamuru, "Msiiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuiabudu, wala kuitolea sadaka.
\s5
\v 36 Lakini Yahwe, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri kwa nguvu kubwa na mkono ulionyooshwa, yeye ndiye mnayetakiwa kumwabudu, yeye ndiye manayetakiwa kumsujudia, na yeye ndiye mnayetakiwa kumtolea sadaka.
\v 37 Na sheria na hukumu, na torati na amri ambazo alizoziandika kwa ajili yenu, mtazishika milele. Hivyo msiiche miungu mingine,
\v 38 na agano ambalo nimelifanya pamoja nanyi, hamtalisahau; wala kuicha miungu mingine.
\s5
\v 39 Lakini Yahwe Mungu wenu, ndiye ambaye mtakayemcha. Atawalinda mbali na nguvu ya maadui zenu,"
\v 40 Hawatasikia, kwasababu waliendelea kufanya yale waliyokuwa wameyafanya nyuma.
\v 41 Hivyo haya mataifa wakamcha Yahwe na pia wakaabudu sanamu zao za kuchonga, na watoto wao wakafanya hivyo hivyo na watoto wa watoto wao. Wakaendelea kufanya yale ambayo babu zao waliyoyafanya, hata leo.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
\v 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake alikuwa anaitwa Abija; alikuwa binti wa Zekaria.
\v 3 Alifanya yaliyo mema usoni pa Yahwe, kufuata mfano wa yote ambayo Daudi, babu yake, aliyoyafanya.
\s5
\v 4 Alipaondoa mahali pa juu, akaiharibu nguzo ya jiwe, akaikata hiyo nguzo ya Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ambayo Musa aliyokuwa ameifanya, kwa sababu siku zile wana wa Israeli walikuwa wakichoma ubani katika hiyo; ilikuwa inaitwa "Nehushtani."
\v 5 Hezekia alimwamini Yahwe, Mungu wa Israeli, hivyo basi baada ya yeye hapakuwa kama yeye miongoni mwa wafalme wote wa Yuda, wala miongoni mwa wafalme ambao walikuwa kabla yake.
\s5
\v 6 Aliambatana na Yahwe. Hakuacha kumfuata lakini alizifuata amri zake, ambazo Yahwe alimwamuru Musa.
\v 7 Hivyo Yahwe alikuwa na Hezekia, kila alipokwenda alifanikiwa. Akaasi dhidi ya mfalme wa Ashuru na hakumtumikia.
\v 8 Akawashambulia Wafilisti hadi Gaza na mipaka inayoizunguka, kutoka mnara wa walinzi hadi hadi mji wenye ngome.
\s5
\v 9 Katika mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru akapanda hadi Samaria na kuizunguka.
\v 10 Mwishoni mwa miaka mitatu wakaichukua, katika mwaka wa sita wa Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa Hoshea mfalme wa Israeli; hivi ndivyo Samaria ilivyotekwa.
\s5
\v 11 Basi mfalme wa Ashuru akawachukua Israeli kwenda Ashuru na kuwaweka kwenye Hala, na katika mto Habori katika Gozani, na katika mji wa Wamedi.
\v 12 Alifanya hivi kwasababu hakutii sauti ya Yahwe Mungu wao, lakini walikiuka makubaliano ya agano lake, yote yale ambayo Musa yule mtumishi wa Yahwe aliwaamuru. Walikataa kuyasikiliza au kuyafanya.
\s5
\v 13 Kisha katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senakerebu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote yenye boma na kuwateka mateka.
\v 14 Basi Hezekia mfalme wa Yuda akatuma neno kwenda kwa mfalalme wa Yuda akatuma neno kwa mfalme wa Ashuru, ambaye alikuwa Lachishi, akisema, "Nimekuudhi. Nichukue. Popote utakaponiweka nitavumulia". Mfalme wa Ashuru akamtaka Hezekia mfalme wa Yuda kulipa talanta mia tatu za fedha na talanta thelathini za dhahabu.
\v 15 Hivyo Hezekia akampatia fedha zote ambazo zilikuwa zimepatikana kwenye nyumba ya Yahwe na kawenye hazina nyumba ya mfalme.
\s5
\v 16 Kisha Hezekia akaikata ile dhahabu kutoka kwenye milango ya hekalu la Yahwe na kutoka juu ya nguzo; akampatia dhahabu mfalme wa Ashuru.
\v 17 Lakini mfalme wa Ashuru akalihamasisha jeshi lake kubwa, akawatuma Tartani na Rabsarisi na amiri jeshi mkuu kutoka Lakishi kwenda kwa Hezekia huko Yerusalemu. Wakasafiri hadi kwenye mabarabara na kufika nje ya Yerusalemu. Wakakaribia karibu na mfereji wa birika la juu, kwenye barabara kuu ya shamba la dobi, na kusimama hapo.
\v 18 Wakati walipokuwa wamemwita Mfalme Hezekia, Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme na Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, anayeandika kumbukumbu, wakatoka nje kwenda kuwalaki
\s5
\v 19 Basi yule amiri jeshi mkuu akawaambia wamwambie Hezekia kile alichosema mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, amesema: "Nini chanzo cha ujasiri wako?
\v 20 Unaongea maneno yasiyo na maana, kusema lipo neno na nguvu ya vita. Sasa unamtumainia nani? Nani anakupa ujasiri wa kuasi dhidi yangu?
\v 21 Tazama, unatumainia kutembelea fimbo ya mwanzi huu uliopondeka wa Misri, lakini kama mtu akiutegemea, utamchapa kwenye mkono wake na kuutoboa. Hicho ndicho Farao mfalme wa Misri kwa ymtu yeyote ambaye anayemtumainia.
\s5
\v 22 Lakini kama ukiniambia, 'Tunamwamini Yahwe Mungu watu; je si yeye ambaye mahali pa juu na madhabahu Hezekia amezichukua, na kumwambia Yuda na kwa Yerusalemu, 'Lazima uabudu mbele ya hii madhabahu katika Yerusalemu'?
\v 23 Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi elfu mbili, kama unaweza kuwatafuta kuwaendesha kwa ajili yao.
\s5
\v 24 Wanawezaje kumpinga hata nahodha mmoja wa watumishi walio wadogo? Mmeweka tumaini lenu katika Misri kwa magari ya farasi na waendesha farasi!
\v 25 Je nimesafiri kwenda huko juu bila Yahwe kupapigania hapa mahali na kupaharibu? Yahwe ameniambia, 'Ishambulie hii nchi na uiharibu."'
\s5
\v 26 Kisha Elikana mwana wa Hilkia, na Shebna, na Joa wakamwambia amiri jeshi mkuu, "Tafadhali ongea na watumishi wako katika lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaielewa. Usiongee nasi katika lugha ya Yuda katika masikio ya watu ambao wako ukutani."
\v 27 Lakini yule amiri jeshi mkuu akawaambia, "Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kuwachukua kuongea haya maneno? Je hajanituma kwa hawa watu ambao wameketi kwenye ukuta, ambao watakula kinyesi chao na kunywa mkojo wao wenyewe?"
\s5
\v 28 Kisha yule amiri jeshi mkuu akasimama na akapiga kelele kubwa kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, "Sikilizeni neno la mfalme mkuu, mfale wa Ashuru.
\v 29 Mfalme asema, 'Msimwache Hezekia akawadanganya, kwa kuwa hataweza kuwaokoa kwenye nguvu yangu.
\v 30 Msimwache Hezekia akawatumainisha katika Yahwe, akisema, "Yahwe atatuokoa hakika, na huu mji hautawekwa kwenye mkono wa mfalme wa Ashuru.'"
\s5
\v 31 Msikilize Hezekia, kwa kuwa hivi ndivyo mfalme wa Ashuru asemavyo: 'Fanyeni amani pamoja nami na njooni kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kutoka kwenye mtini wake mwenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji kwenye maji ya birika lake mwenyewe.
\v 32 Mtafanya hivyo hadi nitakapokuja na kuwachukua kwenda kwenye nchi kama nchi yenu, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya miti ya mizaituni na asali, ili muweze kuishi na sio kufa.' Msimsikilize Hezekia wakati atakapojaribu kuwashawishi, akisema, 'Yahwe atatuokoa.'
\s5
\v 33 Je miungu yeyote ya watu inayewaokoa kutoka kwenye nchi ya mfalme wa Ashuru?
\v 34 Iko wapi miungu ya Hamathi na Arpadi? iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena, na Iva? Je imeiokoa Samaria kutoka mkono wangu?
\v 35 Miongoni mwa miungu yote ya nchi, je kuna mungu ambaye ameiokoa nchi yake kutoka kwenye nguvu yangu? Inawezekanaje Yahwe akaiokoa Yerusalemu kutoka kwenye uwezo wangu?"
\s5
\v 36 Lakini watu wakabaki kimya na hawakujibu, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru, "Msimjibu."
\v 37 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa juu ya nyumba ya mfalme; Shebna yule mwandishi; na Joa mwana wa Asafu, mtunza kumbukumbu, akaja kwa Hezekia pamoja na nguo zao zilizoraruliwa, na kumpatia taarifa ya maneno ya yule amiri mkuu.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ikawa kuhusu kwamba wakati Mfalme Hezekia aliposikia taazrifa zao, akararua mavazi yake, akavaa nguo za magunia, na kwenda kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 2 Akamtuma Elkana, ambaye alikua msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna yule mwandishi, na wazee wa makuhani, wote walikuwa wamefunikwa na nguo za magunia, kwenda kwa Isaya mwana wa Amozi, yule nabii.
\s5
\v 3 Wakamwambia, "Hezekia wakisema, 'siku hii ni siku ya mateso, shutuma, na fedheha, kwa kuwa wakati umewadia watoto kuzaliwa, lakini hakuna nguvu ili wazaliwe.
\v 4 Inaweza kuwa Yahwe Mungu wako atasikia maneno yote ya amiri jeshi mkuu, ambaye mfalme wa Ashuru bwana wake amemtuma kumkaidi Mungu aliye hai, naye atayakemea yale maneno ambayo Yahwe Mungu wako aliyasikia. Sasa inua maombi yako juu kwa ajili ya mabaki yaliyo bakia hapo."'
\s5
\v 5 Hivyo watumishi wa mfalme Hezekia wakaja kwa Isaya,
\v 6 na Isaya akawaambia, "Mwambieni bwana wenu: 'Yahwe asema hivi, "Usiyaogope maneno ambayo uliyoyasikia, pamoja na kwamba watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.
\v 7 Tazama, nitaweka roho ndani yake, na yamkini atasikia taarifa na kurudi kwenye nchi yake mwenyewe. Nitamfanya aanguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.""'
\s5
\v 8 Kisha amiri jeshi mkuu akarudi na kumkuta mfalme wa Ashuru akipigana dhidi ya Libna, kwa kuwa alisikia kwamba mfalme alikuwa ameenda kutoka Lakishi.
\v 9 Kisha Senakeribu akasikia kwamba Tirhaka mfalme wa Kushi na Misri alihamasisha kupigana dhidi yake, hivyo akatuma wajumbe tena kwa Hezekia pamoja na ujumbe:
\s5
\v 10 "Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda, 'Asikudanganye Mungu wako unayemwamini, kusema, "Yerusalemu haitawekwa kwenye mikono ya mikono ya mfalme wa Ashuru."
\v 11 Tazama, umesikia kwamba wafalme wa Ashuru wamemaliza nchi zote kwa kuziharibu kabisa. Kwa hiyo je utaokoka?
\s5
\v 12 Je wale miungu wa mataifa wamewaokoa, mataifa ambao baba zangu waliyaharibu: Gozani, Harani, Resefu, na watu wa Edeni katika Telasari?
\v 13 Je yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme Arpadi, mfalme wa miji ya Sefarvaimu, wa Hena, na Iva?"'
\s5
\v 14 Hezekia akapokea hii barua kutoka wale wajumbe na kuisoma. Kisha akapanda hata kwenye nyumba ya Yahwe na kuukunjua mbele yake.
\v 15 Kisha Hezekia akaomba mbele ya Yahwe na kusema, "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya makerubi, wewe ni Mungu wa pekee juu ya tawala zote za dunia. Uliyeziumba mbingu na nchi.
\s5
\v 16 Tega sikio lako, Yahwe, na usikie. Fungua macho yako, Yahwe, na tazama, na sikia maneno ya Senakeribu, ambayo ameyatuma kumdhihaki Mungu aliye hai.
\v 17 Ni kweli, Yahwe, wafalme wa Ashuru ameyaharibu mataifa na nchi zao.
\v 18 Wameiweka miungu yao kwenye moto, kwa kuwa hawakuwa miungu lakini ilikuwa kazi ya mikono ya watu, ilikuwa miti na mawe. Hivyo Waashuru wamewaharibu.
\s5
\v 19 Basi sasa, Yahwe Mungu wetu, tuokoe, nakusihi, kutoka kwenye nguvu zake, ili kwamba mamlaka zote za dunia zipate kujua yakwamba wewe, Yahwe, ndiye Mungu wa pekee."
\s5
\v 20 Kisha Isaya mwana wa Amozi akatuma ujumbe kwa Hezekia, akisema, "Yahwe, Mungu wa Israeli asema, 'Kwasababu umeomba kwangu kuhusiana na Senakeribu mfalme wa Ashuru, nimekusikia.
\v 21 Hili ndilo neno ambalo Yahwe ameliongea kuhusu yeye: "Bikira binti Sayuni amekudharau na kukucheka kwa dharau. Binti wa Yerusalemu akatikisa kichwa juu yako.
\v 22 Je ni nani uliyemchokoza na kumtukana? Dhidi ya nani umeinua sauti yako na kuinua macho yako katika majivuno? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!
\s5
\v 23 Kupitia wajumbe wako wamemdharau Bwana, na kusema, 'Pamoja na wingi wa magari yangu ya farasi nimeenda juu ya vilele ya milima, hata juu ya kilele cha Lebanoni. Nitaikata mierezi mirefu na kuchagua miti ya mivinje huko. Nitaingia sehemu za makazi yake yaliyo mbali, msitu wake uzaao sana.
\v 24 Nimechimba visima na kunywa maji mageni. Nimekausha mito yote ya Misri chini ya soli ya miguu yangu.'
\s5
\v 25 Je hukusikia jinsi nilivyoagiza tangu zamani, na kuyafanya tangu siku za zamani? Sasa ninalileta kupita. Uko hapa kupunguza miji isiyoingilika kwenye rundo la maangamizi.
\v 26 Makazi yao, ya nguvu kidogo, imevunjwa vunjwa na aibu. Wamekuwa mimea katika shamba, majani ya kijani, majani juu kwenye dari au kwenye shamba, lililochomwa kabla halijakua.
\s5
\v 27 Lakini najua kuketi kwako chini, na kutoka kwako, kuingia kwako dhidi yangu.
\v 28 Kwasababu kiburi chako kimeyafikia masikio yangu, Nitaweka kulabu yangu kwenye pua yako, na hatamu yangu kwenye mdomo wako; nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia."
\s5
\v 29 Hii ndiyo itakuwa ishara kwako: Mwaka huu mtakula vitu viotavyo porini, na katika mwaka wa pili vile vikuavyo katika huo. Lakini katika mwaka wa tatu ni lazima mpande na kuvuna, kupanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.
\v 30 Mabaki ya nyumba ya Yuda ambayo yataokoka yatachukua tena mizizi na kuzaa matunda.
\v 31 Kwa kuwa mabaki yatatoka Yerusalemu, kutoka Mlima Sayuni wenye kuokoka utakuja. Wivu wa Yahwe wa majeshi utafanya hivyo.
\s5
\v 32 Kwa hiyo Yahwe asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru: "Hatakuja kwenye huu mji wala kupiga mshale hapa. Wala hatakuja mbele yake na ngao au kujenga boma dhidi yake.
\v 33 Njia ile ile aliyoijia ndiyo njia atakayoondokea; hatoingia mji huu - hivi ndivyo asemavyo Yahwe."
\v 34 Kwa maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa ajili yangu mwenyewe na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu."'
\s5
\v 35 Ikawa kuhusu usiku huo ambao malaika wa Yahwe alitoka na kuvamia kambi ya Waashuru, akawaua maaskari185, 000. Kisha watu wakaamka asubuhi na mapema, miili ya watu waliokuwa wamekufa ilikuwa imelala kila mahali.
\v 36 Hivyo Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka Israeli na kwenda nyumbani na kuishi katika Ninawi.
\v 37 Baadaye, alipokuwa akiabudu kwenye nyumba ya Nisroki mungu wake, watoto wake Adramaleki na Shareza wakamuua kwa upanga. Kisha wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Kisha Esarhodani mwanaye akawa mfalme katika mahali pake.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Katika siku hizo Hezekia aliugua akawa kwenye hatari ya kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, akaja, na kumwambia, "Yahwe asema, 'Weka nyumba yako kwenye mpangilio; kwa kuwa utakufa, na hutapona.'"
\v 2 Kisha Ahazi akageuza uso wake kwenye ukuta na kumuomba Yahwe, akisema,
\v 3 "Tafadhali, Yahwe, ukumbuke jinsi nilivyo mwaminifu kutembea mbele yako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya yaliyo mazuri usoni kwako." Kisha Hezekia akalia kwa sauti.
\s5
\v 4 Kabla ya Isaya hajatoka nje kwenye mji wa kati, neno la Yahwe likamjia, kusema,
\v 5 '"Rudi, na umwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, 'Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yako, asemavyo: "Nimesikia maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Nitakuponya katika siku ya tatu, na utapanda juu kwenye nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 6 Nitakuongeza miaka kumi na tano ya maisha yako, na nitakulinda na huu mji kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu.""'
\v 7 Hivyo Isaya akasema, "Chukueni mkate wa tini." Walifanya hivyo na kuweka kwenye jipu lake, na akapona.
\s5
\v 8 Hezekia akamwambia Isaya, "Je kutakuwa na alama gani ambayo Yahwe ataniponya, na kwamba nitapanda juu hadi kwenye hekalu la Yahwe katika siku ya tatu?"
\v 9 Isaya akajibu, "Hii ndiyo itakuwa ishara kwako kutoka kwa Yahwe, kwamba Yahwe atafanya kitu amacho alichokisema. Je kivuli kitaenda mbele hatua saba, au kurudi nyuma hatua saba?"
\s5
\v 10 Hezekia akajibu, "Ni kitu chepesi kwa kivuli kwenda mbele hatua kumi. Hapana, hicho kivuli kirudi nyuma hatua kumi."
\v 11 Hivyo Isaya nabii akamlilia Yahwe, na akaleta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka pale ambapo zilikuwa zimevuka kwenye ngazi za Ahazi.
\s5
\v 12 Katika kipindi hicho Merodak Baladani mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia, kwa kuwa alisikia kwamba Hezekia alikuwa anaumwa.
\v 13 Hezekia akasikiliza hizo barua, na kisha kuwaonyesha wajumbe sehemu zote na sehemu zake za thamani, fedha, dhahabu, manukato na marhamu na nyumba yenye ghala la silaha zake, na yote yaliyokutwa kwenye ghala za nyumba zake. Hapakuwa na kitu kwenye nyumba, wala kwenye ufalme wake wote, ambao Hezekia hakuwaonyesha.
\s5
\v 14 Kisha Isaya akaja kwa Hezekia na kumuuliza, "Hawa watu walikuwa wanakwambiaje? Wanatokea wapi?" Hezekia aksema, "Wamekuja kutoka nchi ya mbali ya Babeli.
\v 15 Isaya akauliza, "Wameona nini kwenye nyumba yako?" Hezekia akajibu, "Wameona kila kitu kwenye nyumba yangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha."
\s5
\v 16 Basi Isaya akamwambia Hezekia, "Sikiliza neno la Yahwe:
\v 17 'Tazama siku zinakuja wakati kila kitu kwenye kwenye nyumba yako ya kifalme, vitu ambavyo babu zako walivitunza huko hadi leo, vitabebwa kwenda Babeli. Hakuna kitakachobakia, Yahwe asema.
\v 18 Watoto waliozaliwa na wewe, ambao umewazaa wewe mwenyewe-watawachukua mbali, na watakuwa matowashi kwenye nyumba ya kifalme ya mfalme wa Babeli.'"
\s5
\v 19 Hezekia akamwambia Isaya, "neno la Yahwe uliloliongea ni jema." Kwa kuwa alifikiri, Je sivyo ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?"
\v 20 Kama kwa mambo mengine yanamuhusu Hezekia, na ushujaa wake wote, na jinsi alivyotengeza bwawa la maji na mfereji, na kuleta maji kwenye mji-hayakuandikwa kwenye kitabu cha ya matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 21 Hezekia akalala na babu zake, na Manase mwanae akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hefziba.
\v 2 Alifanya maovu usoni kwa Yahwe, kama machukizo ya mataifa ambayo Yahwe aliyafukuza nje mbele ya wana wa Israeli.
\v 3 Kwa kupajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake alipaharibu, na akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali, akafanya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya, akasujudu kwa nyota zote za mbinguni na kuwaabudu wao.
\s5
\v 4 Manase akajenga madhabahu za kipagani kwenye nyumba ya Yahwe, ingawaje Yahwe aliamuru, "Jina langu litakuwa Yerusalemu daima."
\v 5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Yahwe.
\v 6 Akamuweka mtoto wake wa kiume kwenye moto; akatazama bao ushirikina na kujishuhulisha pamoja wale ambao wenye pepo wa utambuzi na wale wachawi. Akafanya maovu mengi usoni kwa Yahwe na kuchochea hasira kwa Mungu.
\s5
\v 7 Sanamu ya kuchongwa ya Ashera ambayo aliitnegeneza, akaiweka kwenye nyumba ya Yahwe. Nyumba hii ndiyo ambayo Yahwe alimwambia Daudi na Sulemani mwanawe; alisema: "Ni nyumba hii na katika Yerusalemu, ambayo nimeichagua kutoka makabila yote ya Isaraeli, ambako nitaliweka jina langu milele.
\v 8 Sintofanya miguu ya Israeli kushindwa tena nje ya nchi ambayo niliwapa babu zao, kama tu watakuwa makini kutii yale yote niliyowaamuru, na kufuata sheria zote ambazo mtumishi wangu Musa aliwaamuru."
\v 9 Lakini watu hawakusikia, na Manase akawaongoza kufanya maovu zaidi kuliko yale ya mataifa ambayo Yahwe aliyaharibu mbele ya watu wa Israeli.
\s5
\v 10 Basi Yahwe akaongea na watumishi wake manabii, akisema,
\v 11 Kwasababu Manase mfalme wa Yuda amefanya haya machukizo, na kutenda maovu zaidi kuliko yote waliyoyatenda Waamori ambao walikuwa mbele yake walikubali, na pia aliwafanya Yuda kuasi kwa sanamu zake,
\v 12 kwa hiyo Yahwe, Mungu wa Israeli, akasema hivi: Tazama, nakaribia kuleta uovu juu ya Yerusalemu na Yuda ambayo kila mtu asikiapo kuhusu hilo, masikio yake yote yatang'aa.
\s5
\v 13 Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kipimo kilichotumika dhidi ya Samaria, na kuangusha msatari utakaotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu; Nitaifuta Yerusalemu safi, kama kufuta sahani, kuifuta na kuifunika juu chini.
\v 14 Nitawatupa masalia ya urithi wangu na kuwaweka mikononi mwa maadui zao. Watakuwa nyara na mateka kwa maadui zao wote,
\v 15 kwa sababu wamefanya yaliyo maovu usoni kwangu, na kunichochea hasira, tangu siku babu zao walipotoka Misri, hadi leo."
\s5
\v 16 Aidha, Manase akazimwaga damu nyingi za wasio na hatia, hadi alipoijaza Yerusalemu kutoka upande huu kwenda mwingine kwa kifo. Hii ilikuwa ni kuongeza kwenye dhambi ambayo aliifanya Yuda kuasi, wakati walipofanya uovu mbele za Yahwe.
\v 17 Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Manase, yote aliyoyafanya, na dhambi ambayo aliyoifanya, je haya hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Yuda?
\v 18 Manase akalala pamoja na babu zake na alizikwa kwenye bustani ya nyumba yake, katika bustani ya Uza. Amoni mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\v 19 Amoni alikuwa na miaka kumi na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Meshlemethi; alikuwa binti wa Haruzi wa Yotba.
\v 20 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama manase baba yake alivyofanya.
\s5
\v 21 Amoni alifuata njia zote ambazo baba yake alizotembelea na kuabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu, na kuzisujudia.
\v 22 Akajitenga na Yahwe, Mungu wa baba zake, na hakutembea katika njia ya Yahwe.
\v 23 Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.
\s5
\v 24 Lakini watu wa nchi wakawaua watu wote waliofanya njama dhidi ya mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia mtoto wake kuwa mfalme katika sehemu yake.
\v 25 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Amoni yale aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 26 Watu wakamzika kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza, na Yosia mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
\v 2 Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa Yahwe. Alitembea kwenye njia zote za Daudi babu yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.
\s5
\v 3 Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya Yahwe, akisema,
\v 4 "Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.
\v 5 Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya Yahwe, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya Yahwe, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.
\s5
\v 6 Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya Yahwe."
\v 7 Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.
\s5
\v 8 Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, "Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe." Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.
\v 9 Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, "Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya Yahwe."
\v 10 Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, "Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu." Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
\s5
\v 11 Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.
\v 12 Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,
\v 13 Nenda na ukaongee pamoja na Yahwe kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya Yahwe ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu babu zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.
\s5
\v 14 Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.
\v 15 Akawaambia, "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, asemavyo: 'Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,
\v 16 "Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: 'Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.
\s5
\v 17 Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya-kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika."'
\v 18 Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya Yahwe, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: "Yahwe, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,
\v 19 kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za Yahwe, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwasaabu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\s5
\v 20 Tazama, nitakukusanya na babu zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu. """ Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Hivyo mfalme akawatuma wajumbe waliokuwa wamemzunguka wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu.
\v 2 Kisha mfalme akapanda hadi kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu pamoja naye, na makuhani, manabii, na watu wote, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Kisha akasoma katika masikioni kwao maneno yote ya kitabu cha agano ambalo lililokuwa limepatikana kwenye nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 3 Mfalme akasimama karibu na nguzo na kufanya agano mbele ya Yahwe, kutembea pamoja na Yahwe na kukumbuka maagizo yake, kanuni zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, kuthibitisha maneno ya hili agano ambalo lililokuwa limeandikwa kwenye hiki kitabu. Hivyo watu wote wakakubaliana kusimama kwenye agano
\s5
\v 4 Mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani mkuu, makuhani chini yake, na walinzi wa lango watoe kwenye hekalu vyombo vilivyokuwa vimetengenezwa kwa ajili ya Baali na Ashera, na kwa ajili ya nyota zote za mbinguni. Akivichoma moto Yerusalimu kwenye mashamba ya bonde la Kidroni na kubeba majivu yake kwenda Betheli.
\v 5 Akawaondoa makuhani waliokuwa wanaabudu miungu ambao wafalme wa Yuda waliwachagua ili kwa ajili ya kufukiza ubani katika mahali pa juu kwenye miji ya Yuda na sehemu zinazoizunguka Yerusalemu-wale waliokuwa wanchoma ubani kwa Baali, kwa juana kwa mwezi, kwa sayari, na kwa nyota zote za mbinguni.
\s5
\v 6 Akaiondoa Ashera kutoka kwenye hekalu la Yahwe, nje ya Yerusalemu hata bonde la Kidroni na kuichoma hapo. Akaipiga kwenye mavumbi na kuiyatupa yale mavumbi kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
\v 7 Akavisafisha vyumba vya makahaba ambao walikuwa kwenye hekalu la Yahwe, ambako wanawake waliposhonea nguo kwa ajili ya Ashera
\s5
\v 8 Yosia akawaleta makuhani wote nje ya miji ya Yuda na kupanajisi mahali pa juu ambako makuhani walipokuwa wakichomea ubani, kutoka Geba hata Bersheba. Akapaharibu mahala pa juu kwenye malango ambayo yaliyokuwa ya kuingilia kwenda kwenye lango la Yoshua (liwali wa mji), upande wa kushoto wa lango la mji.
\v 9 Ingawa makuhani wa mahali pa juu hawakuruhusiwa kuhudumu kwenye madhabahu ya Yahwe katika Yerusalemu, wakala mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.
\s5
\v 10 Yosia akainajisi Tofethi, ambayo ipo kwenye bonde la Ben Hinomu, ili kwamba mtu yeyote asimuweke mtoto wake wa kiume au binti yake kwenye moto kama sadaka kwa Molaki.
\v 11 Akawachukua farasi ambao wafalme wa Yuda waliokuwa wametolewa kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye eneo la lango la uingilia kwenye hekalu la Yahwe, karibu na chumba cha Nathani Meleki, msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. Yosia akayachoma yale magari ya farasi ya jua
\s5
\v 12 Yosia mfalme akayaharibu madhabahu yaliyokuwa kwenye dari ya juu ya chumba cha Ahazi, ambacho wafalme wa Yuda walikitengeneza, na madhabahu ambayo Manase aliyatengeneza kwenye behewa mbili za nyumba ya Yahwe. Yosia akazivunga vipande vipande na kuvitupa kwenye bonde la Kidroni.
\v 13 Mfalme akapaangamiza mahali pa juu magharibi mwa Yerusalemu, kusini mwa mlima wa uharibifu ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alipajenga kwa ajili ya Ashtorithi, chukizo la Wamoabu; sanamu za karaha za Wasidoni; kwa Kemoshi, sanamu za karaha wa Moabu; na kwa Moleki, sanamu wa karaha wa watu wa Amoni.
\v 14 Akazivunja nguzo za jiwe kuwa vipande vipande na kuziangusha chini nguzo za Ashera na kuzijaza zile sehemu kwa mifupa ya watu.
\s5
\v 15 Yosia pia akaiteketeza kabisa madhabahu iliyokuwa Betheli na mahali pa juu ambako Yeroboamu mwana wa Nebati (ambaye aliwafanya Waisraeli kuasi) aliijenga. Pia aliichoma moto ile madhabahu na mahali pa juu na kupapiga hadi pakawa vumbi. Pia akaichoma moto nguzo ya Ashera.
\v 16 Yosia alipotazama kwenye lile eneo, akagundua kwamba yale makaburi yalikuwa juu ya mlima. Akawatuma watu kuichukua mifupa kutoka kwenye yale makaburi; kisha akaichoma kwenye madhabahu, akainajisi. Hii ilitokana na neno la Yahwe ambalo mtu wa Mungu aliliongea, yule mtu aliyekuwa ameongea haya mambo kabla.
\s5
\v 17 Kisha akasema, "Ni ukumbusho wa nani ule ninao uona?" Mtu wa ule mji akamwambia, "Lile ni kaburi la mtu wa Mungu ambaye alikuja kutoka Yuda na kuongea kuhusu haya mambo ambayo ameyafanya dhidi ya madhabahu ya Betheli."
\v 18 Hivyo Yosia akasema, "Mwacheni. Mtu asihamishe mifupa yake." Hivyo wakaacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya nabii ambaye alikuja kutoka Samaria.
\s5
\v 19 Kisha Yosia akahamisha nyumba zote za mahali pa juu ambazo zilikuwa katika mji wa Samaria, ambazo wafalme wa Israeli walizokuwa wamezitengeneza, na ambazo zilizokuwa zimemgadhabisha Yahwe kwa hasira.
\v 20 Aliwafanyia kile ambacho kilikuwa kimefanyika katika Betheli. Aliwachinja makuhani wote wa mahali pa juu ya madhabahu na aliichoma mifupa ya watu juu yao. Kisha akarudi Yerusalemu.
\s5
\v 21 Kisha mfalme akawaamuru watu wote, akisema, "Itunzeni Pasaka ya Yahwe Mungu wenu, kama ilivyoandikwa kwenye hiki kitabu cha agano."
\v 22 Hiyo Pasaka haijawahi kufanyika tangu siku za waamuzi ambao waliiongoza Israeli, wala katika siku zote za wafalme wa Israeli au Yuda.
\v 23 Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yosia hii Pasaka ya Yahwe ilisheherekewa katika Yerusalemu.
\s5
\v 24 Yosia pia akawafukuza wale ambao waliokuwa wameongea na wafu au na roho. Pia aliifukuza miungu ya sananmu, sanamu, na vitu vyote ambavyo ni chukizo vilivyokuwa vinaonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, hivyo kwa kuthibitisha yale maneno ya sheria ambayo iliyokuwa imeandikwa kwenye kitabu cha Hilkia yule kuhani aliyekuwa amepatikana kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 25 Kabla ya Yosia, hapakuwa na mfalme kama yeye, aliyekuwa amemwelekea yahwe kwa moyo wake wote, roho yake yote, na nguvu zake zote, ambaye alifuata sheria zote za Musa. Hapakuwa na mfalme kama Yosia aliyeinuka baada ya yeye.
\s5
\v 26 Walakini, Yahwe hakugeuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, ambayo ilikuwa dhidi ya Yuda kwa waabudu wapagani wote pamoja ambao Manase aliokuwa amemgadhibisha.
\v 27 Hivyo Yahwe akasema, "Pia nitaiondoa Yuda usoni kwangu, kama nilivyoiondoa Israeli, na nitautupilia mbali huu mji ambao nilio uchagua, Yerusalemu, na ile nyumba ambayo niliyokuwa nimesema, 'Jina langu litakuwa humo."'
\s5
\v 28 Kama kwa mambo mengine yanayo muhusu Yosia, kila kitu alichofanya, je vimeandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 29 Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, alienda kupigana dhidi ya mfalme wa Ashuru huko mto Frati. Mfalme Yosia akaenda kuonana na Neco katika mapigano, na Neko akamuua huko Megido.
\v 30 Watumishi wa Yosia wakambeba kwenye gari la farasi akiwa amekufa kutoka Migido, kumleta Yerusalemu, na kumzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, na kumfanya kuwa mfalme katika mahali pake.
\s5
\v 31 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, na alitawala miezi mitatu katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia wa Libana.
\v 32 Yehoahazi alifanya yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama kila kitu ambacho babu zake walichokifanya.
\v 33 Farao Neko akamfunga gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi, hivyo asiweze kutawala katika Yerusalemu. Kisha Neko akaitoza Yuda talanta mia moja za fedha na talanta moja ya dhahabu.
\s5
\v 34 Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia mfalme katika mahali pa Yosia baba yake, na kubadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua mfalme Yehoahazi kwenda Misri, na Yehoahazi akafia huko.
\v 35 Yehoyakimu akalipa fedha na dhahabu kwa Farao. Ili akutane na amri ya Farao, Yehoyakimu akaitoza nchi na kulazimisha kila mtu miongoni mwa watu wa nchi wamlipe fedha na dhahabu kulingana na makadirio yao.
\s5
\v 36 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Zebida; alikuwa binti wa Pedaia wa Ruma.
\v 37 Yehoyakimu akafanya yale yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama waliyoyafanya babu zake.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.
\v 2 Yahwe akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu,, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la Yahwe ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.
\s5
\v 3 Ilikuwa baada ya mda mfupi kwenye kinywa cha Yahwe kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sabau ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,
\v 4 na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. Yahwe hakuwa tayari kusamehe hilo.
\s5
\v 5 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 6 Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\v 7 Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alakuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kitabu cha Misri mpaka Mto wa Frati.
\s5
\v 8 Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.
\v 9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.
\s5
\v 10 Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.
\v 11 Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,
\v 12 na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.
\s5
\v 13 Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya Yahwe, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Suleimani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la Yahwe, kama alivyokuwa amesema ingetokea.
\v 14 Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu maskini katika nchi.
\s5
\v 15 Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.
\v 16 Wapiganaji wote, elfu saba kwa hesabu, na mafundi elfu moja na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga- mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.
\v 17 Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
\s5
\v 18 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.
\v 19 Alifanya yaliyo maovu machoni mwa Yahwe; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.
\v 20 Kupitia hasira ya Yahwe, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Ilitokea kwamba katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedekia, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya huo mwezi, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote kwa ajili ya kupigana dhidi ya Yerusalemu. Akaweka kambi kuelekeana nayo, na wakajenga ukuta kuizunguka.
\v 2 Hivyo mji huo ulizungukwa mpaka miaka kumi na moja ya utawala wa Sedekia.
\v 3 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa huo mwaka, njaa ilikuwa kali sana kwenye huo mji kwamba hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.
\s5
\v 4 Wakati huo ule mji ulikuwa umebomoka ndani, na wapiganaji wote wakakimbia usiku kwa njia ya lango kati ya kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wote wameuzunguka mji. Mfalme akaenda kuelekea upande wa Araba.
\v 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuata mfalme Sedekia na kumchukua katika tambarare ya bonde la Mto Yoradani karibu na Yeriko. Jeshi lake lote lilitawanyika wakamwacha.
\s5
\v 6 Wakamkamata mfalme na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, ambapo walipitisha hukumu juu yake.
\v 7 Kama kwa watoto wa Sedekia, wakawachinja mbele ya macho yake. Kisha akamtoa macho Sedekia, wakamfunga pingu, na kumpeleka hadi Babeli.
\s5
\v 8 Basi katika mwezi wa tano, katika siku ya saba ya mwezi, ambapo ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, mtumishi wa mfalme wa Babeli na amrijeshi wa walinzi wake, wakaja hadi Yerusalemu.
\v 9 Akaichoma moto nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme, na nyumba zote za Yeruselemu; pia kila jengo la muhimu katika mji akayachoma.
\v 10 Kama kwa kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli ambao walikuwa chini ya amrishi wa walinzi wakaziharibu.
\s5
\v 11 Basi watu waliokuwa wamebaki ambao walikuwa wameondoka katika mji, wale waliokuwa wameasi kwa mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu-Nebuzadani, amiri jeshi wa mlinzi, wakachukuliwa kwenda utumwani.
\v 12 Lakini amiri jeshi wa mlinzi aliwaacha baadhi ya maskini wa nchi ili wafanye kazi kwenye shamba la mizabibu na kulima.
\s5
\v 13 Na zile nguzo za shaba ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, na misimamio na bahari ya chuma ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakazivunja vipande vipande na kubeba shaba kuirudisha Babeli.
\v 14 Masufuria, mabeleshi, makasi, vijiko, na vyombo vyote vya shaba ambavyo kuhani alivyokuwa amevitunza kwenye hekalu-Wakaldayo wakavichukua vyote.
\v 15 Masufuria ya kuhamisha majivu na mabakuli ambayo yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu, na yale yaliyotengenezwa kwa fedha-yule nahodha wa mlinzi wa mfalme akavichukua pia.
\s5
\v 16 Zile nguzo mbili, ile bahari, na vile vitako ambavyo Suleimani alivitengeneza kwa ajili ya nyumba ya Yahwe shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
\v 17 Urefu wa ile nguzo ya kwanza ulikuwa ridhaa kumi na nane, na kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Na urefu wa kichwa ulikuwa ridhaa tatu, pamoja na mapambo ya wavu na makomamanga yote yakizunguka kwenye hicho kichwa, vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. Na ile nguzo nyingine ilikuwa vivyo hivyo kama ile ya kwanza pamoja na wavu wake.
\s5
\v 18 Yule amiri jeshi wa mlinzi akamchukua Seraya kuhani mkuu, pamoja za Sefania, yule kuhani wa pili, na walinzi watatu wa kwenye lango.
\v 19 Kutoka mjini akamchukua mlinzi, afisa mmoja ambaye aliyekuwa msimamizi wa maaskari, na watu watano ambao walikuwa wakimshauri mfalme, ambao walikuwa bado katika mji. Pia alimchukua mfungwa wa afisa jeshi la mfalme, kwa ajili ya kuandika watu kwenye jeshi, pamoja na watu sitini muhimu kutoka hiyo nchi ambao walikuwa katika mji.
\s5
\v 20 Kisha Nebuzaradani, amiri wa mlinzi, akawachukua na kuwapeleka kwa mfalme Babeli huko Ribla.
\v 21 Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaiacha nchi yake kwenda utumwani.
\s5
\v 22 Na wale watu waliokuwa wamebakia katika nchi ya Yuda, wale ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwaacha, akamuweka Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, msimamizi wao.
\v 23 Kisha wakati maamiri wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemfanya Gedalia kuwa liwali, wakaenda kwa Gedalia huko Mispa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.
\v 24 Gedalia akafanya kiapo kwa watu wake na kuwaambia, "Msiwaogope Wakaldayo. Muishi katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vema kwenu."
\s5
\v 25 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, kutoka familia ya kifalme, wakaja na watu kumi na kumshambulia Gedalia. Gedalia akafa, pamoja na watu wa Yuda na Wababeli ambao walikuwa pamoja nae huko Mizpa.
\v 26 Kisha wale watu wote, kutoka chini kwenda juu, na maamiri wa jeshi, wakainuka na kwenda Misri, kwasababu walikuwa wanawaogopa Wababeli.
\s5
\v 27 Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala.
\s5
\v 28 Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli.
\v 29 Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,
\v 30 na Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia.

1717
13-1CH.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1717 @@
\id 1CH
\ide UTF-8
\h 1 Mambo ya Nyakati
\toc1 1 Mambo ya Nyakati
\toc2 1 Mambo ya Nyakati
\toc3 1ch
\mt 1 Mambo ya Nyakati
\s5
\c 1
\p
\v 1 Adamu, Sethi, Enoshi,
\v 2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
\v 3 Henoko, Methusela, Lameki.
\v 4 Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.
\s5
\v 5 Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi.
\v 6 Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
\v 7 Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
\s5
\v 8 Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani.
\v 9 Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani.
\v 10 Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia.
\s5
\v 11 Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
\v 12 Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori.
\s5
\v 13 Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi.
\v 14 Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi,
\v 15 Mhivi, Mwarki, Msini,
\v 16 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi.
\s5
\v 17 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
\v 18 Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi.
\v 19 Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani.
\s5
\v 20 Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
\v 21 Hadoramu, Uzali, Dikla,
\v 22 Obali, Abimaeli, Sheba,
\v 23 Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani.
\s5
\v 24 Shemu, Arfaksadi, Sala,
\v 25 Eberi, Pelegi, Reu,
\v 26 Serugi, Nahori, Tera,
\v 27 Abramu, aliye kuwa Ibrahimu.
\s5
\v 28 Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli.
\v 29 Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu,
\v 30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
\v 31 Yeturi, Nafishi, na Kedama. Hawa ndio wana wa Ishamaeli.
\s5
\v 32 Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
\v 33 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura.
\s5
\v 34 Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli.
\v 35 Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora.
\v 36 Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki.
\v 37 Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza.
\s5
\v 38 Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani.
\v 39 Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani.
\v 40 Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana.
\s5
\v 41 Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
\v 42 Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani.
\s5
\v 43 Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba.
\v 44 Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake.
\v 45 Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake.
\s5
\v 46 Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi.
\v 47 Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake.
\v 48 Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake.
\s5
\v 49 Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake.
\v 50 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu.
\s5
\v 51 Hadadi akafa. Wajumbe wa ukoo wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi,
\v 52 Oholibama, Ela, Pinoni,
\v 53 Kenazi, Temani, Mibsari,
\v 54 Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wajumbe wa ukoo wa Edomu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni,
\v 2 Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri.
\s5
\v 3 Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamwua.
\v 4 Tamari, mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano.
\s5
\v 5 Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
\v 6 Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano.
\v 7 Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu.
\v 8 Mwana wa Ethani alikuwa Azaria.
\s5
\v 9 Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu.
\v 10 Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni uzao wa Yuda.
\v 11 Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi.
\v 12 Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese.
\s5
\v 13 Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shama.
\v 14 Nethaneli wa nne, Radai wa tano.
\v 15 Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
\s5
\v 16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu.
\v 17 Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
\s5
\v 18 Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni.
\v 19 Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri.
\v 20 Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli.
\s5
\v 21 Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu.
\v 22 Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
\s5
\v 23 Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi.
\v 24 Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa.
\s5
\v 25 Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya.
\v 26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, Jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu.
\v 27 Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri.
\v 28 Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri.
\s5
\v 29 Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi.
\v 30 Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto.
\v 31 Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai.
\v 32 Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto.
\v 33 Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli.
\s5
\v 34 Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha.
\v 35 Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai.
\s5
\v 36 Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi.
\v 37 Zabadi akawa baba wa Efalali, na Afalali akawa baba wa Obedi.
\v 38 Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria.
\s5
\v 39 Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa.
\v 40 Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu.
\v 41 Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama.
\s5
\v 42 Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni.
\v 43 Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema.
\v 44 Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai.
\s5
\v 45 Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri.
\v 46 Efa, suria wa Kalebu, alimza Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi.
\v 47 Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa.
\s5
\v 48 Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana.
\v 49 Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu.
\v 50 Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu.
\s5
\v 51 Salma baba wa Bethlehemu, na Harefu baba wa Beth-gaderi.
\s5
\v 52 Shobali baba wa kiriath-Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya watu Wamenuthite,
\v 53 na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku.
\s5
\v 54 Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi na Wazori,
\v 55 ukoo wa waandishi walio ishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka katika uzao wa Hamathi, babu wa Warekabu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli;
\v 2 watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi;
\v 3 watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe.
\s5
\v 4 Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu.
\v 5 Hawa wana wa nne, kwa Bathshua binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Nathani, na Sulemani.
\s5
\v 6 Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti,
\v 7 Noga, Nefegi, Yafia,
\v 8 Elishama, na Elifeleti.
\v 9 Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao.
\s5
\v 10 Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati.
\v 11 Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi.
\v 12 Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu.
\s5
\v 13 Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase.
\v 14 Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia.
\s5
\v 15 Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu.
\v 16 Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia.
\s5
\v 17 Wana wa YehoYakini, mateka, walikuwa Shealtieli,
\v 18 Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia.
\s5
\v 19 Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao.
\v 20 Wanae watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi.
\v 21 Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.
\s5
\v 22 Mwana wa Shekania alikuwa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati.
\v 23 Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu.
\v 24 Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Uzao wa Yuda ulikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri, na Shobali.
\v 2 Shobali alikuwa baba wa Reaya. Reaya alikuwa baba wa Yahathi. Yahathi alikuwa baba wa Ahumai na Lahadi. Hawa walikuwa mababu wa koo za Wasorathi.
\s5
\v 3 Hawa walikuwa mababu wa ukoo katika mji wa Etamu: Yezreeli, Ishma, na Idbashi. Babu yao alikuwa Haselelponi.
\v 4 Penueli alikuwa babu wa koo katika mji wa Gedori. Ezeri alikuwa muanzilishi wa koo katika Husha. Hawa walikuwa uzao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi na muanzilishi wa Bethelehemu.
\s5
\v 5 Ashuri baba wa Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
\v 6 Naara alimzalia Ahuzamu, Heferi, Temeni na Ahashtari. Hawa walikua wana wa Naara.
\v 7 Wana wa Hela walikua Serethi, Ishari, Ethnani,
\v 8 na Kozi, alikua baba wa Anubu na Sobeba, na koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu.
\s5
\v 9 Yabesi aliheshimika zaidi ya kaka zake. Mama yake alimuita Yabesi. Alisema, "Kwasababu nimemzaa katika huzuni."
\v 10 Yabesi akamuita Mungu wa Israeli na kusema, "Kama tu utanibariki mimi, ongeza mipaka yangu, na mkono wako ukuwa juu yangu. Ukifanya hivi utaninusuru na mabaya, ili kwamba niwe huru na huzuni!" Kwa hivyo Mungu akamjalia maombi yake.
\s5
\v 11 Kelubu kaka wa Shuha akawa baba wa Mehiri, aliyekuwa baba wa Eshtoni.
\v 12 Eshtoni akawa baba wa Beth-Rafa, Pasea, na Tehina, ambaye alianzisha mji wa Nahashi. Hawa ni wanaume walioishi Reka.
\s5
\v 13 Wana wa Kenazi walikua Othinieli na Seraia. Wana wa Othinieli walikuwa Hathathi na Meonothai.
\v 14 Meonothai akawa baba wa Ofara, na Seraia akawa baba wa Yohabu, mwanzilishi wa Ge Harashimu, ambao watu wake walikua wahunzi.
\v 15 Wana wa Kalebu mwana wa Yefune walikua Iru, Ele na Namu. Wana wa Ela alikua Kenazi.
\v 16 Wana wa Yehaleli walikua Zifi, Zifa, Tiriya, na Azareli.
\s5
\v 17 Wana wa Ezra walikua Yetheri, Meredi, Eferi, na Yaloni.
\v 18 Mke wake Meredi wa Kimisri alimzalia Miriamu, Shamai, na Ishibahi, aliyekua baba wa Eshitemoa. Hawa walikua wana wa Bithia, binti wa Farao, ambaye Meredi alimuoa. Mke wa Kiyahudi wa Meredi alimzalia Yeredi, ambaye alikua baba wa Gedore; Heberi, aliyekua baba wa Soko; na Yekuthieli aliyekua baba wa Zanoa.
\s5
\v 19 Kati ya watoto wawili wa mke wa Hodia, dada wa Nahamu, mmoja wao kawa baba wa Keila Mgarimite. Mwingine alikua Eshitemoa Mmakathite.
\v 20 Wana wa Shimoni walikua Amnoni, Rina, Beni Hanani, na Tilon. Wana wa Ishi walikua Zohethi na Beni Zoheti.
\s5
\v 21 Uzao wa Shela mwana wa Yuda, Ulikua ni Eri baba wa Leka, Laada baba wa Maresha na koo za wafanyakazi wa kushona kule Beth Ashbea,
\v 22 Yoakimu, Wanaume wa Kozeba, na Yoashi na Sarafi, waliokua na mali huko Moabu, lakini walirudi Bethlehemu. ( Maelezo haya yametoka kwenye nakala za zamani.)
\v 23 Baadhi ya watu hawa walikuwa ni wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera na wakawa wafanyakazi wa Mfalme.
\s5
\v 24 Uzao wa Simeoni ulikua Jamini, Jaribu, Zera, na Shauli.
\v 25 Shalumu alikua mwana wa Shauli, Mibisamu mwana wa Shalumu, na Mishima mwana wa Mibisamu.
\v 26 Ukoo wa Mishima ulikua Hamueli mwana wake, Zakuri mjukuu wake, na Shimei kitukuu chake.
\s5
\v 27 Shimei alikua na wana kumi na sita na mabinti sita. Kaka yake hakua na watoto wengi, Hivyo koo zao hazikuongezeka kwa idadi kubwa kama wato wa Yuda walivyoongezeka.
\v 28 Waliishi Beasheba, Molada, na Hazari Shuali.
\s5
\v 29 Pia waliishi Bilha, Ezemu, Toladi,
\v 30 Bethueli, Horma, Zikilagi,
\v 31 Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, na Shaaraimu. Hii ilikua miji yao mpaka utawala wa Daudi.
\s5
\v 32 Vijiji vyao vitano vilikua Etamu, Aini, Tocheni, na Ashani,
\v 33 pamoja na mipaka ya vijiji kwa umbali wa Baali. Haya yalikua makazi yao, na walitunza kumbukumbu za uzao wao.
\s5
\v 34 Viongozi wa ukoo walikua Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia,
\v 35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia mwana wa Asieli,
\v 36 Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia,
\v 37 na Ziza mwana wa Shifi mwana wa Aloni mwana wa Yedaia mwana wa Shimiri mwana wa Shemaia.
\v 38 Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi wa koo zao, na koo zao ziliongezeka sana.
\s5
\v 39 Walienda karibu na Gedori, mashariki mwa bonde, kutafuta malisho ya mifugo yao.
\v 40 Walipata malisho mengi na mazuri. Nchi ilikua tambarare, tulivu na ya amani. Wahamu waliishi hapo awali.
\v 41 Hao walio orodheshwa hapo kwa majina walikuja katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na wakashambulia makazi ya Wahamu na Wameuni, ambao pia walikua hapo. Waliwaangamiza kabisa na kuishi hapo sababu walipata malisho kwa ajili ya mifugo yao.
\s5
\v 42 Wanaume mia tano wa kabila la Simeoni walienda katika mlima Seiri, na viongozi wao Pelatia, Nearia, Refaia, na Uzieli, wana wa Ishi.
\v 43 Waliwashinda wakimbizi wa Waamaleki waliobakia, na wakaishi hapo hadi siku hii.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Wana wa Rubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli - sasa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli kwa sababu Rubeni alinajisi kochi la baba yake. Hivyo hajanakiliwa kama mwana wa kwanza.
\v 2 Yuda alikuwa mwenye nguvu kuliko kaka zake, na kiongozi ata toka kwake. Lakini haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu -
\v 3 wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi.
\s5
\v 4 Uzao wa Yoeli ulikuwa huu: Mwana wa Yoeli alikuwa Shemaia. Mwana wa Shemaia alikuwa Gogi. Mwana wa Gogi alikuwa Shimei.
\v 5 Mwana wa Shimei alikuwa Mika. Mwana wa Mika alikuwa Reaia. Mwana wa Reaia alikuwa Baali.
\v 6 Mwana wa Baali alikuwa Bera, ambaye Tiligathi Pileseri alimpeleka matekani kule Assiria. Bera alikuwa kiongozi katika kabila la Rubeni.
\s5
\v 7 Ndugu wa Bera kwa makabila yao ni hawa wafuatao, wameorodheshwa katika nakala za uzao wao: Yeieli wa kwanza, Zekaria, na
\v 8 Bela mwana wa Azazi mwana wa Shema mwana wa Yoeli. Waliishi Aroeri, kwa umbali wa Nebo na Baali Meoni,
\v 9 na mwanzo wa mashariki mwa jangwa lenye umbali wa hadi Mto Efarati. Hii ni kwa sababu walikuwa na mifugo mingi katika nchi ya Gileadi.
\s5
\v 10 Katika siku za Sauli, kabila la Rubeni lilishambulia Wahagiri na kuwa shinda. Wakaishi ndani ya hema za Wahagiri katika nchi yote mashariki mwa Gileadi.
\s5
\v 11 Kabila la Gadi liliishi karibu nao, katika nchi ya Bashani umbali wa Saleka.
\v 12 Viongozi wao walikuwa Yoeli, aliyekuwa kichwa wa ukoo, na Shafamu alikuwa kichwa wa ukoo mwingine, na Yanai na Shafati walikuwa wa Bashani.
\v 13 Ndugu zao, kwa familia za baba yao, walikuwa Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, na Eberi - jumla saba wote.
\s5
\v 14 Hawa watu walio tajwa hapo juu ni uzao wa Abihaili, na Abihaili alikuwa mwana wa Huri. Huri alikuwa mwana w a Yaroa. Yaroa alikuwa mwana wa Gileadi. Gileadi alikuwa mwana wa Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Yeshishai. Yeshishai alikuwa mwana wa Yado. Yado alikuwa mwana wa Buzi.
\v 15 Ahi mwana wa Abidieli mwana wa Guni, alikuwa kichwa cha familia ya baba yake.
\s5
\v 16 Waliishi Gileadi, Bashani, katika miji, na katika nchi zote za malisho ya Sharoni kwa umbali wa mipaka yake.
\v 17 Hawa wote waliorodheshwa katika nakaka za uzao katika siku za Yothamu mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.
\s5
\v 18 Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase walikuwa na wana jeshi elfu arobaini na nne walio fuzu kwa vita, walio beba ngao na upanga, na pinde na mishale.
\v 19 Waliwashambulia Wahagri, Yeturi, Nafishi, na Nodabu.
\s5
\v 20 Walipokea msaada wa Kimungu dhidi yao. Katika hili Wahagri na wote walio kuwa nao walishindwa. Hii ni kwa sababu Waisraeli walipaza sauti katika vita, na yeye akawajibu, kwa sababu waliweka tumaini lao kwake.
\v 21 Walikamata wanya wao, pamoja na ngamia elfu hamsini, kondoo 250, 000, punda elfu mbili, na wanaume 100, 000.
\v 22 Kwa sababu Mungu aliwapigania, waliua maadui wengi. Waliishi katika nchi yao mpaka mateka.
\s5
\v 23 Baadhi ya watu wa kabila la Manase waliishi katika nchi ya Bashani kwa umbali wa Hermoni na Seniri (hiyo ni, Mlima Hermoni).
\v 24 Hawa walikuwa viongozi wa familia zao: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia, na Yahdieli. Walikuwa wenye nguvu na wanaume wa jasiri, wanaume maharufu, viongozi wa familia zao.
\s5
\v 25 Lakini walikuwa sio wa aminifu kwa Mungu wa babu zao. Badala yake, waliabudu miungu ya watu waio nchi, ambao Mungu aliwaangamiza mbele yao.
\v 26 Mungu wa Israeli alimchochea Puli mfalme wa Assiria ( ambaye pia uitwa Tiligathi Pileseri, mfalme wa Assiria). Aliwa peleka matekani Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase. Aliwaleta kwa Hala, Habori, Hara, na kwenye mto wa Gozani, ambapo wapo adi leo.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Wana wa Levi walikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
\v 2 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
\v 3 Wana wa Amramu walikuwa Aruni, Musa, Miriamu. Wana wa Aruni walikuwa Nadabu, Abihu, Eleazari, na Ithamari.
\s5
\v 4 Eleazari akawa baba wa Finehasi, na Finehasi akawa baba wa Abishua.
\v 5 Abishua akawa baba wa Buki, na Buki akawa baba wa Uzi.
\v 6 Uzi akawa baba wa Zerahia, na Zerahia akawa baba wa Meraioti.
\s5
\v 7 Meraioti akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
\v 8 Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Ahimazi.
\v 9 Ahimazi akawa baba wa Azaria, na Azaria akawa baba wa Yohanani.
\s5
\v 10 Yohanani akawa baba wa Azaria, aliye hudumu katika hekalu alilo lijenga Sulemani ndaniya Yerusalemu.
\v 11 Azaria akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
\v 12 Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Shalumu.
\s5
\v 13 Shalumu akawa baba wa Hilikia, na Hilikia akawa baba wa Azaria.
\v 14 Azaria akawa baba Seraia, na Seraia akawa baba wa Yehozadaki.
\v 15 Yehozadaki akaenda matekani Yahweh alipo wapeleka utumwani Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Nebukadneza.
\s5
\v 16 Wana wa Levi walikuwa Gerishomu, Kohathi, na Merari.
\v 17 Wana wa Gerishomu walikuwa Libini na Shimei.
\v 18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
\s5
\v 19 Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Hawa walikuwa koo za Walawi kwa familia za baba zao.
\v 20 Uzao wa Gerishomu ulianza na mwanae Libini. Mwana wa Libini alikuwa Jahathi. Mwanae alikuwa Zima.
\v 21 Mwanae alikuwa Yoa. Mwanae alikuwa alikuwa Ido. Mwanae alikuwa Zera. Mwanae alikuwa Yeatherai.
\s5
\v 22 Uzao wa Kohathi ulianza na mwanae Aminadabu. Mwanae alikuwa Kora. Mwanae alikuwa Asiri.
\v 23 Mwanae alikuwa Elikana. Mwanae alikuwa Ebiasa. Mwanae alikuwa Asiri.
\v 24 Mwanae alikuwa Tahathi. Mwanae alikuwa Urieli. Mwanae alikuwa uzia. Mwanae alikuwa Shauli.
\s5
\v 25 Wana wa Elikana walikuwa Amasai, Ahimothi, na Elikana.
\v 26 Mwana wa huyu Elikana wa pili alikuwa Zofai. Mwanae alikuwa Nahathi.
\v 27 Mwanae alikuwa Eliabu. Mwanae alikuwa Yehoramu. Mwanae alikuwa Elikana.
\s5
\v 28 Wana wa Samwali walikuwa mzaliwa wa kwanza, Yoeli, na Abija, wa pili.
\v 29 Mwana wa Merari alikuwa Mahili. Mwanae alikuwa Libini.
\v 30 Mwanae alikuwa Shimei. Mwanae alikuwa Uza. Mwanae alikuwa Shimea. Mwanae alikuwa Hagia. Mwana alikuwa Asaia.
\s5
\v 31 Haya ndio majina ya wanaume ambao Daudi waliwaeka kusimamia muziki katika nyumba ya Yahweh, baada ya sanduku kuja hapo.
\v 32 Walitumika kwa kuimba mbele ya hema, hema la kukutania, mpaka Sulemani alipo jenga nyumba ya Yahweh ndani ya Yerusalemu. Walikamilisha wajibu wao kwa kadiri ya maelekezo waliopewa.
\s5
\v 33 Hawa walitumika pamoja na wana wao. Katika makabila ya Wakohathi alitoka Hemani mwana muziki. Babu zake walikuwa hawa, kurudi nyuma ya wakati: Hemani alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Samweli.
\v 34 Samweli alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yerohamu. Yerohamu alikuwa mwana wa Elieli. Elieli alikuwa mwana wa Toa.
\v 35 Toa alikuwa mwana wa Zufi. Zufi alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Mahathi. Mahathi alikuwa mwana wa Amasai. Amasai alikuwa mwana wa Elikana.
\s5
\v 36 Elikana alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Azaria. Azaria alikuwa mwana wa Zefania.
\v 37 Zefania alikuwa mwana wa Tahathi. Tahathi alikuwa mwana wa Asiri. Asiri alikuwa mwana wa Ebiasa. Ebiasa alikuwa mwana wa Kora.
\v 38 Kora alikuwa mwana wa Izhari. Izhari alikuwa mwana wa Kohathi. Kohathi alikuwa mwana wa Levi. Levi alikuwa mwana wa Israeli.
\s5
\v 39 Msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliye simama mkono wake wa kuume. Asafu alikuwa mwana Berekia. Berekia alikuwa mwana wa Shimea.
\v 40 Shimea alikuwa mwana Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Baaseia. Baaseia alikuwa mwana wa Malikiya.
\v 41 Malikiya alikuwa mwana wa Ethini. Ethini alikuwa mwana wa Zera. Zera alikuwa mwana wa Adaia.
\v 42 Adaia alikuwa mwana wa Ethani. Ethani alikuwa mwana wa Zima. Zima alikuwa mwana wa Shimei.
\v 43 Shimei alikuwa mwana wa Yahathi. Yahathi alikuwa mwana wa Gerishomu. Gerishomu alikuwa mwana wa Levi.
\s5
\v 44 Upande wa mkono wa koshoto wa Hemani walikuwa wasaidizi wake wana wa Merari. Alikuwa Ethani mwana wa Kishi. Kishi alikuwa mwana wa Abdi. Abdi alikuwa mwana wa Maluki.
\v 45 Maluki alikuwa mwana wa Hashabia. Hashabia alikuwa mwana wa Amazia. Amazia alikuwa mwana wa Hilikia.
\v 46 Hilikia alikuwa mwana wa Amzi. Amzi alikuwa mwana wa Bani. Bani alikuwa mwana wa Shemeri.
\v 47 Shemeri alikuwa mwana wa Mahili. Mahili alikuwa mwana wa Mushi. Mushi alikuwa mwana wa Merari. Merari alikuwa mwana wa Levi.
\s5
\v 48 Walawi, alipangiwa kufanya kazi zote za hema, nyumba ya Mungu.
\s5
\v 49 Aruni na wana wake walitoa sadaka katika madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketeza; na sadaka katika madhabahu ya uvumba kwa kazi zote katika pa patakatifu. Hizi sadaka zilifanya maombezi kwa ajili ya Waisraeli, kwa kadiri ya yote ambayo Musa mtumishi wa Mungu aliwaamuru.
\s5
\v 50 Uzao wa Aruni una kumbukwa kama ifuatavyo: Mwana wa Aruni alikuwa Eleazari. Mwana Eleazari alikuwa Finehasi. Mwana wa Finehasi alikuwa Abishua.
\v 51 Mwana wa Abishua alikuwa Buki. Mwana wa Buki alikuwa Uzi. Mwana wa Buki alikuwa Zerahia.
\v 52 Mwana wa Zerahia alikuwa Meraiothi. Mwana wa Meraiothi alikuwa Amaria. Mwana wa Amaria alikuwa Ahitubi.
\v 53 Mwana wa Ahitubi alikuwa Zadoki. Mwana wa Zadoki alikuwa Ahimazi.
\s5
\v 54 Hizi ni sehemu ambazo wazao wa Aruni walipangiwa kuishi, wazao wa Aruni ambao walitoka katika koo za Wakohathi (maeneo ya kwanza yalikuwa yao).
\v 55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda na nchi ya malisho,
\v 56 lakini maeneo ya mji na vijiji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
\s5
\v 57 Kwa wazao wa Aruni waliwapa: Hebroni ( mji wa makimblio), na Libina pamoja na nchi ya malisho, Yatiri, Eshitemoa pamoja na nchi ya malisho,
\v 58 Hileni pamoja na nchi ya malisho, na Debiri pamoja na nchi ya malisho.
\s5
\v 59 Waliwapa uzao wa Aruni: Ashani pamoja na nchi ya malisho na Bethi Shemeshi pamoja na nchi ya malisho;
\v 60 na kutoka katika kabila la Benjamini walipewa Geba pamoja na nchi ya malisho, Alemethi pamoja na nchi ya malisho, na Anothothi na nchi ya malisho. Jumla ya miji yao ilikuwa kumi na tatu.
\s5
\v 61 Uzao mwengine wa Kohathi waliwapa kwa sehemu miji kumi kutoka kwa kabila la Manase.
\v 62 Kwa uzao wa Gerishomu kwa koo zao tofauti walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri, Naftali, na nusu ya kabila la Manase huko Bashani.
\s5
\v 63 Kwa uzao wa Merari walipewa miji kumi, kulingana na koo zao, kutoka kwa makabila ya Rubeni, Gadi, na Zebuluni.
\v 64 Hivyo watu wa Israeli walitoa hii miji pamoja na nchi za malisho kwa Walawi.
\v 65 Walitoa kwa sehemu miji iliyo tajwa awali kutoka katika kabila la Yuda, Simeoni, na Benjamini.
\s5
\v 66 Kwa baadhi ya koo za Wakohathi walitoa miji kutoka kwa kabila la Efraimu.
\v 67 Waliwapa: Shekemu ( mji wa makimbilio) pamoja na nchi ya malisho katika milima ya Efraimu, Gezeri na nchi ya malisho,
\v 68 Jokimeamu pamoja na nchi ya malisho, Bethi Horoni pamoja na nchi ya malisho,
\v 69 Aiyaloni pamoja na nchi ya malisho, na Gathi Rimoni pamoja na nchi ya malisho.
\s5
\v 70 Nusu ya kabila la Manase waliwapa Wakohathi: Aneri pamoja na nchi ya malisho na Bileamu pamoja na nchi ya malisho. Hizi zikawa mali za koo za Wakohathi.
\s5
\v 71 Kwa uzao wa Gerishomu kutoka koo za nusu ya kabila la Manase, waliwapa: Golani huko Baashani na nchi ya malisho na Ashitarothi pamoja na nchi ya malisho.
\v 72 Kabila la Isakari liliwapa uzao wa Gerishomu: Kedeshi pamoja na nchi ya malisho, Dabera pamoja na nchi ya malisho,
\v 73 Ramothi pamoja na nchi ya malisho, na Anemu pamoja na nchi ya malisho.
\s5
\v 74 Isakari alipokea kutoka kwa kabila la Asheri: Mashali pamoja na nchi ya malisho, Abdoni pamoja na nchi ya malisho,
\v 75 Hukoki pamoja na nchi ya malisho, na Rehobu pamoja na nchi ya malisho.
\v 76 Walipokea kutoka kabila la Naftali: Kedeshi iliyo Galileya pamoja na nchi ya malisho, Hamoni pamoja na nchi ya malisho, na Kiriathaimu pamoja na nchi ya malisho.
\s5
\v 77 Kwa Walawi wengine, uzao wa Merari, walipewa kutoka kabila la Zebuluni: Rimono pamoja na nchi ya malisho na Tabori pamoja na nchi ya malisho.
\v 78-79 Kwa wao pia walipewa, upande wa pili wa Yordani huko Yeriko, kwa upande wa mashariki mwa mto: Bezeri katika jangwa pamoja na nchi ya malisho, Yahzahi pamoja na nchi ya malisho, Kedemothi pamoka na nchi ya malisho, ma Mefathi pamoja na nchi ya malisho. Hizi zilitolewa kutoka kabila la Rubeni.
\s5
\v 80 Walawi walipokea kutoka kabila la Gadi: Ramothi ya Gileadi pamoja na nchi ya malisho, Mahanaimu pamoja na nchi ya malisho,
\v 81 Heshiboni pamoja na nchi ya malisho, na Yazeri pamoja na nchi ya malisho.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Isiakari alikuwa na wana wanne Tola, Pua, Yashubi, na Shimironi.
\v 2 Wana wa Tola walikuwa Uzi, Refaia, Yerie, Yamai, Ibisami, Shemueli. Walikua vichwa katika nyumba za baba yao, toka uzao wa Tola na waliorodheshwa kama mashujaa hodari miongoni mwa kizazi chao. Katika siku za Daudi walikua na idadi ya 22, 600.
\v 3 Mwana wa Uzi alikua Izrahia. Mwana wake alikua Michaeli, Obadia, Yoeli, na Ishia, wote watano walikua viongozi wa ukoo
\s5
\v 4 Pamoja nao walikua na jeshi la watu elfu thelathini na sita kwa mapambano, Kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao, kwa kuwa walikuwa na wake wengi pamoja na wana.
\v 5 Kaka zao, kabila la Isakari, walikua na wanaume wa vita themanini na saba, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
\s5
\v 6 Wana watatu wa Benjamini walikuwa Bela, Beka, na Yediaeli.
\v 7 Wana watano wa Bela walikuwa Ezibono, Uzi, Uzieli, Yerimoti, na Iri. Walikua ni wanajeshi na waanzilishi wa koo. Watu wao walikuwa na idadi ya wanaume wa vita 22, 034, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
\s5
\v 8 Wana wa Beka walikuwa Zemira, Yoashi, Elieza, Elionai, Omri, Yeremoti, Abiya, Anatoti, na Alemeti. Wote hawa walikuwa wana wake.
\v 9 Orodha ya koo zao ilikua na idadi ya 20, 200 viongozi wa familia na wanaume wa vita.
\v 10 Mwana wa Yediaeli alikuwa Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa Yeushi, Benjamini, Ehudi, Kenaana, Zetani, Tarishishi, na Ahishahari.
\s5
\v 11 Wote hawa waikuwa wana wa Yediaeli. Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17, 200 viongozi na wanaume wa vita imara kwa kazi ya jeshi.
\v 12 (Shupimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri, na Hushimu alikuwa mwana wa Aheri.)
\s5
\v 13 Wana wa Naftali walikuwa Yazieli, Guni, Yezeri, na Shalumu. Hawa walikuwa wajukuu wa Bilhahi.
\s5
\v 14 Manasse alikua na mtoto wa kiume aliitwa Asrieli, Ambaye suria wake wa Kiaramia alimzalia. Pia alimzaa na Makiri, baba wa Gileadi.
\v 15 Makiri alimchukua mke wake kutoka Hupite na Shupite. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwingine wa uzao wa Manasse alikuwa Zalofehadi, ambaye alikuwa na mabinti pekee.
\v 16 Maaka mke wa Makiri, alimzaa mwana na alimuita Pereshi. Kaka yake aliitwa Shereshi, na wana wake walikuwa Ulamu na Rakemu.
\s5
\v 17 Mwana wa Ulami alikuwa Bedani. Hawa walikuwa uzao wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase.
\v 18 Dada wa Gileadi Hamoleketi alimzaa Ishihodi, Abi Ezeri, na Mahila.
\v 19 Wana wa Shemida walikuwa Ahiana, Shekemu, Liki, na Aniamu.
\s5
\v 20 Uzao wa Efraimu ulikuwa kama ifuatavyo: Efraimu mwana wa Shutela. Shutela mwana wa Beredi. Beredi mwana wa Tahati.
\v 21 Tahati mwana wa Eleada. Eleada mwana wa Shutela. (Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi, walipoenda kuiba mifugo yao.
\v 22 Efraimu baba yao aliomboleza kwa siku nyingi, na kaka zake walikuja kumfariji.
\s5
\v 23 Alilala na mkewe. Akapata mimba akamzaa mwana. Efraimu akamuita Beria, kwa sababu maafa yalishakuja nyumbani mwake.
\v 24 Binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga miji juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah.)
\s5
\v 25 Mwana wake alikuwa Rafa. Mwana wa Rafa alikuwa Reshefi. Mwana wa Reshafi alikuwa Tela. Mwana wa Tela alikuwa Tahani.
\v 26 Mwana wa Tahani alikuwa Ladani. Mwana wa Ladani alikuwa Amihudi. Mwana wa Amihudi alikuwa Elishama.
\v 27 Mwana wa Elishama alikuwa Nuni. Mwana wa Nuni alikuwa Joshua.
\s5
\v 28 Mali zao na makazi yao yalikuwa Betheli na yalizungukwa na vijiji. Waliongeza upande wa mashariki hadi Naarani na upande wa magharibi hadi Gezeri na vijiji vyake, na Shekemu na vijiji vyake hadi Aya na vijiji vyake.
\v 29 Katika mipaka pamoja na Manasse kulikuwa na Beti shani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, na Dori na vijiji vyake. Katika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli.
\s5
\v 30 Wana wa Asha walikuwa Imna, Ishiva, Ishivi, na Beria. Sera alikuwa dada yao.
\v 31 Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malchieli, Ambaye alikuwa baba wa Birzaiti.
\v 32 Wana wa Heberi walikuwa Yafeti, Shomer, na Hotamu. dada yao alikuwa Shua.
\s5
\v 33 Wana wa Yafeti walikuwa Pasach, Bimhali, na Ashivati. hawa walikuwa watoto wa yafeti.
\v 34 shoma, kaka wa Yafeti alikuwa na wana hawa: Roga, Yehuba, Aram.
\v 35 Kaka yake Shema, Helemu, alikuwa na wana hawa: Zofa, Imna, Sheleshi na Amali.
\s5
\v 36 Wana wa Zofa walikuwa Sua, Harinefa, Shua, Beri, IMra,
\v 37 Beza, Hodi, Shamma, Shilsha, Ithrani, na Beera.
\v 38 Wana wa Yeta walikuwa Jefune, Pispa, na Ara.
\s5
\v 39 Wana wa Ulla walikwa Ara, Hannieli, na Rizia.
\v 40 Hawa wote walikuwa uzao wa Asha. Walikua mababu wa ukoo, viongozi wa familia, wananume wa kipekee, wanaume wa vita, na machifu kati ya viongozi. Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliokuwa imara kwa kazi ya jeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara,
\v 2 Noha, na Rafa.
\v 3 Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi,
\v 4 Abishau, Naamani, Ahoa,
\v 5 Gera, Shefufani, na Huramu.
\s5
\v 6 Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati:
\v 7 Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi.
\s5
\v 8 Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara.
\v 9 kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu,
\v 10 Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao.
\v 11 Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu.
\s5
\v 12 Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi ( ambao walijenga Ono na Lod pamoja na vijiji vilivyozunguka.)
\v 13 Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya koo walizoishi Aijalon, Ambao waliwaondoa wakazi wa Gati.
\s5
\v 14 Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Jeremothi,
\v 15 Zebadia, Aradi, Eda,
\v 16 Mikaeli, Ishipa, na Joha.
\v 17-18 Elipaa alikuwa na wana hawa: Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba, Ishimerai, Izilia, na Yobabu.
\s5
\v 19 Shimei alikuwa na wana hawa: Yokimu, Zikri, Zabdi,
\v 20 Elienai, Zilletai, Elieli,
\v 21 Adaia, Beraia, na Shimrati.
\s5
\v 22 Shashaki alikuwa na wana hawa: Ishipani, Eba, Elieli,
\v 23 Abdoni, Zikri, Hanani,
\v 24 Hanania, Elamu, Antotoja,
\v 25 Ifdeia, na Penueli.
\s5
\v 26 Yerohamu alikuwa na wana hawa: Shamsherai, Sheharia, Atli,
\v 27 Yaareshia, Elija, na Zikri.
\v 28 Hawa walikuwa vichwa vya koo na viongozi walioishi Yerusalemu.
\s5
\v 29 Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni.
\v 30 Uzao wake wa kwanza alikuwa Abdoni, akafatia Zuri, Kishi, Baali, Nadab,
\v 31 Gedori, Ahio, na Zekari.
\s5
\v 32 Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu.
\v 33 Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
\v 34 Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika.
\s5
\v 35 Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi.
\v 36 Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
\v 37 Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.
\s5
\v 38 Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli.
\v 39 Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu.
\v 40 Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kwa hivyo watu wote wa Israeli walinakiliwa ki uzao. Walinakiliwa katika vitabu vya kifalme vya Israeli. Yuda, walipelekwa matekani Babylon kwasababu ya dhambi zao.
\v 2 Wakwanza kurudi kuishi katika miiji yao walikuwa Waisraeli, Makuhani, Walawi, na Watumishi wa hekalu.
\v 3 Baadhi ya uzao wa Yuda, Benjamin, Efraimu, na Manase waliishi Yerusalemu.
\s5
\v 4 Wahamiaji walijumusha Uthai mwana wa Ammihudi mwana wa Omri mwana wa Bani, moja ya uzao wa Perezi mwana wa Yuda.
\v 5 Kati ya Mashilonite kulikuwa na Asaia mtoto wa kwanza na wana wake.
\v 6 Kati ya uzao wa Zera alikuwa Yeuli. Uzao wao ulikuwa na namba 690.
\s5
\v 7 Katika uzao Benjamini walikuwa Salu mwana wa Meshulamu mwana wa hodavia mwana wa Hssenua.
\v 8 Pia walikuwa Ibneia mwana wa Yerohamu; Ela mwana wa Uzzi mwana wa Mikri; na Meshullam mwana wa Shefatia mwana waReuli mwana wa Ibnija.
\v 9 Ndugu zao waliandika kwenye orodha ya namba 956 ya vizazi vyao. Wanaume wote hawa walikuwa viongozi wa koo za mababu zao.
\s5
\v 10 Makuhani walikuwa Yedaia, Yehoiarib, na Yokini.
\v 11 Walikuwa pia Azaria mwana wa Hilkia mwana wa Meshullamu mwana wa Zadoki mwana wa Meraioti mwana wa Ahitubi, aliyekuwa na mamlaka katika nyumba ya Mungu.
\s5
\v 12 Kulikuwa na Adaia mwana wa Yerohamu mwana wa Pashuri mwana wa Malkija. Pia kulikuwa na Maasai mwanawa Adieli mwana wa Yazera mwana wa Meshulamu mwana wa Meshilemiti mwana wa Imma.
\v 13 Ndugu zao, ambao walikuwa viongozi katika koo za mababu zao, idadi ya 1, 760. Walikuwa ni wanaume wenye uwezo sana wa kufanya kazi katika nyumba ya Mungu.
\s5
\v 14 Kati ya Walawii, kulikuwa na Shemaia mwana wa Hashubu mwana wa Azrikam mwana wa Hashabia, kati ya uzao wa Merari.
\v 15 Walikuwako pia Bakbakari, Hereshi, Galali, na Mattania mwana wa Mika mwana wa Zikri mwana wa Asafu.
\v 16 Walikuwako pia Obadia mwana wa Shemaia mwana wa Galali mwana wa Yedutuni; na Berekia mwana wa Asa mwana wa Elkana, aliyeishikatika vijiji vya Netophathites.
\s5
\v 17 Walinzi wa lango walikuwa Shalumu, Akubi, Talimoni, Ahimani, na uzao wao. Shalumu alikuwa kiongozi wao.
\v 18 Awali walisimama kulinda katika geti la mfalme upande wa mashariki wa kambi ya uzao wa Walawi.
\v 19 Shalumu mwana wa Kore mwana wa Ebiasafu, ambaye kama mwana wa Kora, na ndugu zake kutoka nyumba ya baba yake, Korahite, alikuwa na mamlaka kwa kazi ya huduma, Walilinda mlango wa hema, kama mababu zao walivyolinda kambi ya Yawehi, na pia walilinda lango la kuingilia.
\s5
\v 20 Finehasi mwana wa Eleaza aliwaongoza kipindi cha nyuma, na Yahwehi alikuwa pamoja nae.
\v 21 Zekaria mwana wa Meshelemia alikua mlinzi katika mlango wa kuingilia hekalu, "eneo la kukutania."
\s5
\v 22 Hawa wote walichaguliwa kana walinzi wa mageti ya kuingilia kwa idadi ya 212. Majina yao yaliandikwa kwenye kumbukumbu za watu katika vijiji vyao. Mtabiri aliwaweka Daudi na Samueli katika nafasi ya uaminifu.
\v 23 Kwa hivyo wao na watotot wao walilinda mageti katika nyumba ya Yawehi, hema la kuabudia.
\v 24 Walinzi wa mageti waliwekwa katika pande zote nne, upande wa mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini.
\s5
\v 25 Kaka zao, walioishi kwenye vijiji vyao, walikuja kuwasaidia baada ya mzunguko wa siku saba.
\v 26 Lakini viongozi wanne wa walinzi, ambao walikwa walawi, walipangiwa kulinda vyumba na vyumba vya kuhifadhi katika nyumba ya Mungu.
\v 27 Walitumia usiku wao sehemu walizowekwa kuzunguka nyumba ya Mungu, kwao ilikuwa ni wajibu wao kulinda. Na walifungua geti kila asubuhi.
\s5
\v 28 Baadhi yao waliwajibika katika hekalu la vifaa; walihesabu makala zilizo ingizwa ndani na zilizo tolewa nje.
\v 29 Baadhi yao pia waliwekwa kutunza vitu vitakatifu, vifaa, na vitu, kujuisha unga safi, mvinyo, mafuta, manukato, na uvumba.
\s5
\v 30 Baadhi ya wana wa makuhani walichanganya uvumba.
\v 31 Matithia, mmoja wa walawi, ambaye alikuwa mtoto wa kwanza wa Shalumu wa Wakorahi, alikuwa na wajibu wa kuandaa mikate kwa ajili ya sadaka.
\v 32 Baadhi ya kaka zao, uzao wa kohathite, waliwajibika kwa mikate ya uwepo, kuandaa kila Sabatho.
\s5
\v 33 Waimbaji na viongozi wa familia ya Walawi waliishi ndani ya vyumba katika mahali takatifu walipo kuwa hawafanyi kazi, kwa sababu wapiswa kufanya kazi walio pangiwa usiku na mchana.
\v 34 Hawa walikuwa viongozi wa familia miongoni mwa Walawi, kama ilivyo orodheshwa katika kumbukumbu za uzao wao. Waliishi Yerusalemu.
\s5
\v 35 Baba wa Gibeoni, Yeiel, ambaye mkewe aliitwa Maaka, aliishi Gibeoni.
\v 36 Mtoto wake wa kwanza alikuwa Abdoni, alafu wana wake Zuri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
\v 37 Gedori, Ahio, Zekaria, na Mikloti.
\s5
\v 38 Mikloti alikuwa baba wa Shimeamu. Pia waliishi karibu na kaka yao huko Yerusalemu.
\v 39 Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. sauli alikuwa baba wa Yonathani, malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
\v 40 Mwana wa Jonathani alikuwa Merib baali. Merib baali alikuwa baba wa Mika.
\s5
\v 41 Mwana wa Mika walikuwa pithoni, Meleki, Tahrea, na ahazi.
\v 42 Ahazi alikuwa baba wa Jara. Jara alikuwa baba wa Alemeti, Azmaveti, na zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
\v 43 Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Refaia. Refaia alikuwa baba wa Eleas. eleasa alikuwa baba wa Azeli.
\v 44 Wana sita wa Azeli walikuwa Azrikamu, Bochera, Ishmaeli, shearia, Obdia, na Hanani. hawa walikuwa wana wa Azeli
\s5
\c 10
\p
\v 1 Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Kila mwanaume wa Israeli alikimbia Wafilisti na kuanguka na kufa katika Mlima Giliboa.
\v 2 Wafilisti waliwakimbiza Sauli na mwanae. Waflisti walimuua Yonathani, Abinadabu, na Malichishua, wana wake.
\v 3 Pambano lilikuwa zito kwa Sauli, na wapiga mishale wakamshambulia. Alipatwa na maumivu makali sababu ya wapiga mishale.
\s5
\v 4 Kisha Sauli akasema kwa mbeba ngao wake, "Vuta upanga wako na unichome nao. Lasihivyo, hawa wasio tahiriwa watukuja na kunitesa". Lakini mbeba ngao wake hakutaka, kwa kuwa aliogopa sana. Kwa hiyo Sauli akachukuwa upanga wake na kuuangukia.
\s5
\v 5 Mbeba ngao alivyoona kuwa Sauli amekufa, naye akaangukia upanga wake na kufa.
\v 6 Kwaiyo Sauli akafa, na wana wake watatu, wote wa nyumba yake wakafa pamoja.
\s5
\v 7 Kila mwanaume wa Israeli katika bonde alivyoona kuwa wamekimbia, na Sauli na wana wake wamekufa, walitelekeza miji yao na kukimbia. Kisha Wafilisti wakaja na kuishi humo.
\v 8 Ikawa siku inayofuata, Wafilisti walipo kuja kukagua wafu, walimkuta Sauli na wana wake wameanguka katika Mlima Giliboa.
\s5
\v 9 Wakamvua nguo zote na kuchukuwa kichwa chake na ngao yake. Wakatuma wajumbe wapeleke habari Filistia yote kwa miungu yao na watu wote.
\v 10 Ngao yake wakaeka ndani ya hekalu la miungu yao, na kichwa chake waka kining'iniza katika hekalu la Dagoni.
\s5
\v 11 Yabeshi Gileadi yote ilipo sikia Wafilisti waliyo mtendea Sauli,
\v 12 wanaume wote wa vita wakaenda na kuchukuwa mwili wa Sauli na hiyo ya wanae, na kuirejesha Yabeshi. Walizika mifupa yao chini ya mti huko Yabeshi na wakafunga siku saba.
\s5
\v 13 Kwaiyo Sauli akafa kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.
\v 14 Hakutafuta mwongozo kwa Yahweh, hivyo Yahweh akamua na kupindua ufalme kwa Daudi mwana wa Yese.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Kisha Waisraeli wote walikuja Hebroni kwa Daudi na kusema, "Angalia, sisi ni nyama na mifupa yako.
\v 2 Katika wakati uliopita, Sauli alipoo kuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliye ongoza jeshi la Israeli. Yahweh Mungu wako alisema kwako, 'utawachunga watu wangu wa Isaraeli, na utakuwa mtawala wa watu wangu wa Israeli"'.
\v 3 Kwaiyo wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni, na Daudi akafanya agano nao mbele ya Yahweh. Wakampaka mafuta Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa namna hii, neno la Yahweh lilo nenwa na Samweli likawa kweli.
\s5
\v 4 Daudi na Israeli yote wakaenda Yerusalemu (yani, Yebusi). Sasa Wayebusi, wakazi wa nchi, walikuwa pale.
\v 5 Wakazi wa yebusi wakamwabia Daudi, "Hautakuja humu." Lakini Daudi alichukuwa ngome ya Sayuni, mji wa Daudi.
\v 6 Daudi alisema, "Yeyote atakaye washambulia Wayebusi wa kwanza atakuwa mkuu wa jeshi" kwaiyo Yoabu mwana wa Zeruia akashambulia wa kwanza, hivyo akafanywa mkuu wa jeshi.
\s5
\v 7 Daudi akaanza kuishi katika hiyo ngome. Kwaiyo wakaiita mji wa Daudi.
\v 8 Akaimarisha mji kutoka Milo na hadi mpaka ukuta unao zunguka. Yoabu akaimairisha mji wote uliyo baki.
\v 9 Daudi akawa mkuu na mkuu kwa sababu Yahweh wa Majeshi alikuwa naye.
\s5
\v 10 Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli.
\v 11 Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.
\s5
\v 12 Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari.
\v 13 Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti.
\v 14 Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa.
\s5
\v 15 Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.
\v 16 Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu.
\v 17 Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, "Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!"
\s5
\v 18 Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh.
\v 19 Kisha akasema, "Yahweh, iwe mbali na mimi, kwamba ni yanywe haya maji. Je ninywe damu ya wanaume walio hatarisha maisha yao?" Kwa sababu wameeka maisha ya hatarini, akakataa kunywa. Haya ni mambo wanaume hodari watatu walio fanya.
\s5
\v 20 Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa watatu. Alitumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu.
\v 21 Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao. Japo hakuwa mmoja wa miongoni mwao.
\s5
\v 22 Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa mwanaume mwenye nguvu aliye fanya mambo makuu. Aliua wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ikianguka.
\v 23 Alimua hadi Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu. Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake.
\s5
\v 24 Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu.
\v 25 Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Daudi alimueka kiongozi wa walinzi wake.
\s5
\v 26 Wanaume hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu,
\v 27 Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni,
\v 28 Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abi Eza Manathothi,
\v 29 Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohite,
\s5
\v 30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite,
\v 31 Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni,
\v 32 Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi,
\v 33 Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
\s5
\v 34 Mwana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mhararite,
\v 35 Ahiamu mwana wa Sacari Mhararite, Elifali mwana wa Uri,
\v 36 Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni,
\v 37 Hezro Mcarmeli, Maarai mwana wa Ezibai,
\s5
\v 38 Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri,
\v 39 Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi ( mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia),
\v 40 Ira Mithire, Garebu Mithire,
\v 41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai,
\s5
\v 42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni ( kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja nae,
\v 43 Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini,
\v 44 Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri,
\s5
\v 45 Jediaeli mwana wa Shimri, Joha ( kaka yake Mtize),
\v 46 Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia mwana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi,
\v 47 Elieli, Obedi, na Yaasieli Wamezobai.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Hawa walikuwa wanaume walio kuja kwa Daudi huko Zikilagi, wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa Sauli mwana wa Kishi. Walikuwa miongoni mwa wanajeshi, wasaidizi wake katika mapambano.
\v 2 Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde. Walikuwa Wabenjamini, ndugu wa kabila moja na Sauli.
\s5
\v 3 Kiongozi alikuwa Ahi Eza, halafu Yoashi, Wana wote wa Shemaa Mgibeathi. Kulikuwa na Yezieli na Peleti, wana wa Azimavethi. Kulikuwa pia na Beraka, Yehu Waanathothi,
\v 4 Ishimaia Mgibeoni, mwanajeshi kati ya wale thelathini ( na kiongozi wa wale thelathini); Yeremia, Yahazieli, Yohana, Yozabadi Wagederathi,
\s5
\v 5 Eluzai, Yerimothi, Bealia, Shemaria, Shefatia Waharufi,
\v 6 Wakorahi ni Elkana, Ishia, Azareli, Yoeza, Yashobeamu, na
\v 7 Yoela na Zebadia, wana wa Yeroham wa Gedori.
\s5
\v 8 Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa wanaume wapiganaji, waliofundishwa kwa mapambano, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesi kwenye milima kama swala.
\s5
\v 9 Kulikuwa na Eza kiongozi, Obadia wapili, Eliabu watatu,
\v 10 Mishimana wanne, Yeremia watano,
\v 11 Atai wasita, Elieli wasaba,
\v 12 Yohana wanane, Elizabadi watisa,
\v 13 Yeremia wakumi, Makibanai wakumi na moja.
\s5
\v 14 Wana wa Gadi walikuwa viongozi wa jeshi. Wamwisho aliongoza mia moja, na mkubwa aliongoza elfu moja.
\v 15 Walikatisha Yordani kwa mwezi wa kwanza, wakati vijito vyake vilipofurika, na kuwafukuza wote wanaoishi katika mabonde, pande zote za mashariki na magharibi.
\s5
\v 16 Baadhi ya wanaume wa Benjamini na Yuda walikuja kwenye ngome kwa Daudi.
\v 17 Daudi alienda nje kuwasalimu na kuwahutubia: "kama mmekuja kwa amani kunisaidia, mnaweza kujiunga nami. Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa maadui zangu, Ee Mungu wa mababu zetu awaone na kuwakemea, tangu sijafanya kosa."
\s5
\v 18 Kisha roho ikaja juu ya Amasai, ambaye alikuwa kiongozi wa wale thelathini. Amasai alisema, "Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse. na amani iwe juu ya yeyote atakaye kusaidia. Kuwa Mungu wako anakusaidia." Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakuu wa watu wake.
\s5
\v 19 Baadhi kutoka kwa Manase pia wakamwendea Daudi alipokuja na Wafilisti dhidi ya Sauli katika pambano. Lakini hawakuwasaidia Wafilisti kwasababu mabwana wa Wafilisti walishauriana na wakamfukuza Daudi. Walisema, "Atamwendea Bwana wake Sauli na kuhatarisha maisha yetu."
\v 20 Alipokwenda kwa Zikilagi, wanaume wa Manase walioungana nae walikuwa Adina, Yozabadi, Yediaeli, Yozabadi, Elihu, na Zilethai, viongozi wa maelfu wa Manase.
\s5
\v 21 Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi, maana walikuwa wanaume wa mapambano. Baadae walikuwa wakuu katika jeshi.
\v 22 Siku hadi siku, wanaume walikuja kwa Daudi kumsaidia, mpaka wakawa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
\s5
\v 23 Hii ni kumbukumbu ya wanajeshi wa vita, walio kuja kwa Daudi Hebroni, kuupindua ufalme wa Sauli kwake, ilikutimiza neno la Yahweh.
\v 24 Kutoka Yuda walio beba ngao na mkuki ni 6, 800, tayari kwa vita.
\v 25 Kutoka kwa Wasimeoni walikuwa 7, 100 wanaume wa mapambano.
\s5
\v 26 Kutoka kwa Walawi kulikuwa na wanaume wa mapambano 4, 600.
\v 27 Yehoiada alikuwa kiongozi wa uzao wa Aruni, na kwa yeye walikuwa 3, 700.
\v 28 Kwa Zadoki, kijana, mwenye nguvu, na mjasiri, walikuwa viongozi ishirini na mbili kwa familia ya baba yake.
\s5
\v 29 Kutoka kwa Benjamini, kabila la Sauli, walikuwa elfu tatu. Wengi wao walibaki waaminifu kwa Sauli mpaka muda huu.
\v 30 Kutoka kwa Waefraimu palikuwa na wanume wa mapambano 20, 800, wanaume maharufu kwenye familia za baba zao.
\v 31 Kutoka kabila nusu la Manase palikuwa na wanaume elfu kumi na nane maharufu walio kuja kufanya Daudi mfalme.
\s5
\v 32 Kutoka kwa Isakari, palikuwa na viongozi mia mbili walio kuwa na ufahamu wa nyakati na walijua nini Israeli ya paswa kufanya. Ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
\v 33 Kutoka Zebuloni palikuwa na wanaume elfu hamsini wa mapambano, tayari kwa vita, na silaha zote za vita, na tayari kutoa uwaminifu usio pungua.
\s5
\v 34 Kutoka kwa Naftali palikuwa na askari elfu moja, na pamoja nao wanaume elfu thelathini na saba wenye ngao na mikuki.
\v 35 Kutoka kwa Wadani palikuwa na wanaume 28, 600 wameandaliwa kwa ajili ya pambano.
\s5
\v 36 Kutoka kwa Asheri palikuwa na wanaume elfu arobaini wameandaliwa kwa pambano.
\v 37 Kutoka upande wa pili wa Yordani, kutoka kwa Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase, palikuwa na wanaume 120, 000 wameandaliwa na silaha za kila namna kwa ajili ya pambano.
\s5
\v 38 Wanajeshi hawa wote, waliandaliwa kwa pambano, kuja Hebroni kwa dhumuni maalumu la kumfanya Daudi mfalme wa Israeli yote. Israeli yote ilikubaliana na kumfanya Daudi mfalme.
\v 39 Walikuwa na Daudi siku tatu, kula na kunywa, kwa kuwa ndugu zao waliwapa mahitaji ya kwenda nayo.
\v 40 Kwa kuongezea, wao walio kuwa karibu nao, kwa umbali wa Isakari na Zebuloni na Naftali, walileta mkate kwa punda, ngamia, ng'ombe, na keki, mvinyo, mafuta, ng'ombe, na kondoo, kwa kuwa Israeli walikuwa wana sherehekea
\s5
\c 13
\p
\v 1 Daudi akashuriana na wakuu wa jeshi la maelfu na mamia, na kila kiongozi.
\v 2 Daudi akasema kwa kusanyiko la Isaraeli, "Kama itakuwa vyema, na kama hii inatoka kwa Yahweh Mungu wetu, na tutume wajumbe kila sehemu kwa ndugu zetu walio baki maeneo yote ya Israeli, na kwa makuhani na Walawi walio kwenye miji yao. Waambiwe wajiunge nasi.
\v 3 Na tulete sanduku la Mungu wetu, kwa kuwa hatukutafuta mapenzi yake katika siku za Sauli."
\v 4 Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote.
\s5
\v 5 Kwaiyo Daudi akakusanya Israeli yote, kutoka mto Shihori ulio Misri hadi Lebo Hamathi, kuleta sandaku la Mungu kutoka Kiriathi Yearimu.
\v 6 Daudi na Israeli yote walienda mpaka Baala, ambayo ni, Kiriathi Yearimu, ambao ni ya Yuda, kuleta sanduku la Mungu, ambalo linaitwa kwa jina la Yahweh, Yahweh, ambaye ameketi juu ya makerubi.
\s5
\v 7 Kwaiyo wakaketisha sanduku la Mungu juu ya chombo kipya cha matairi. Wakaleta nje ya nyumba ya Abinadabu. Uza na Ahio walikuwa wakilinda hicho chombo.
\v 8 Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote. Walikuwa wakiimba na vyombo vya uzi, vinubi, upatu, na tarumbeta.
\s5
\v 9 Walipo kuja eneo la kupeta mazao huko Kidoni, Uza alinyoosha mkono wake kuzuia sandaku, sababu ng'ombe aliyekuwa amebeba sanduku aliyumba.
\v 10 Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza, na Yahweh akamua kwasababu Uza alishika na mkono wake sanduku. Akafa pale mbele za Mungu.
\v 11 Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza. Hiyo sehemu inaitwa Perezi Uza hadi leo.
\s5
\v 12 Daudi alimuogopa Mungu hiyo siku. Akasema, "Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?"
\v 13 Kwaiyo Daudi hakuleta sanduku kwenye mji wa Daudi, lakini aliweka pembeni mwa nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
\v 14 Sanduku la Mungu lilibaki nyumbani mwa Obedi Edomu kwa miezi mitatu. Kwaiyo Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Kisha Hiramu mfalme wa Tire alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, maseremala, na wajenzi. Walijenga nyumba kwa ajili yake.
\v 2 Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli, na hivyo ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli
\s5
\v 3 Ndani ya Yerusalemu, Daudi aliongeza wake, na akawa baba wa wana wengi na mabinti.
\v 4 Haya yalikuwa majina ya watoto waliozaliwa nae huko yerusalemu: Shammua, Shobabu, nathani, Solimoni,
\v 5 Ibhari, Elishama, Elpeleti,
\v 6 Noga, Nefegi, Jafia,
\v 7 Elishama, Beliada, na Elifeleti.
\s5
\v 8 Sasa tangu Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo nae akaenda nje kinyume nao.
\v 9 Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.
\s5
\v 10 Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, "Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?" Yahweh akamwambia, " Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako."
\v 11 Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, " Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji." Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.
\v 12 Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.
\s5
\v 13 Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.
\v 14 Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, " Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.
\s5
\v 15 Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti."
\v 16 Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.
\v 17 Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Daudi akajingea nyumba zake katika mji wa Daudi. Akaanda sehemu kwa ajili ya sanduku la Mungu na hema lake.
\v 2 Kisha Daudi akasema, "Walawi pekee ndio watabeba sanduku la Mungu, kwa kuwa walichaguliwa na Yahweh kubeba sanduku la Yahweh, na kumtumikia milele."
\v 3 Kisha Daudi akakusanya Israeli yote Yerusalemu, kuleta sanduku la Yahweh sehemu aliyo iandaa.
\s5
\v 4 Daudi akakusanya uzao wa Aruni na Walawi pamoja.
\v 5 Kutoka uzao wa Kohathi, palikuwa na Urieli kiongozi na ndugu zake, wanaume 120.
\v 6 Kutoka uzao wa Merari, palikuwa na Asaia kiongozi na ndugu zake, wanaume 220.
\s5
\v 7 Kutoka uzao wa Gerishomu, palikuwa na Yoeli kiongozi na ndugu zake, wanaume 130.
\v 8 Kutoka uzao wa Elizafani, palikuwa na Shemaia kiongozi na ndugu zake, wanaume 200.
\v 9 Kutoka uzao wa Hebroni, palikuwa na Elieli kiongozi na ndugu zake, wanaume themanini.
\v 10 Kutoka uzao wa Uzieli, palikuwa na Aminadabu kiongozi na ndugu zake, wanaume 112.
\s5
\v 11 Daudi akaagiza Zadoki kuitwa na Abiathari kuhuani, na Walawi Urieli, Asaia, Yoeli, Shemaia, Elieli, na Aminadabu.
\v 12 Akasema, "Nyinyi ni viongozi wa familia za Kilawi. Jiwekeni wakfu, nyie na ndugu zenu, ilikwamba mlete sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli, kwenye sehemu niliyo iandaa.
\s5
\v 13 Mara ya kwanza hamkubeba. Ndio maana Yahweh Mungu wetu akawa na hasira kwetu, kwa kuwa hatuku mtafuta wala kutii amri yake."
\v 14 Hivyo makuhani na Walawi waka jiweka wakfu iliwaweze kuleta sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 15 Walawi wakabeba sanduku la Mungu katika mabega yao na nguzo, kama Musa alivyo amuru-kwa kufuata sheria zilizo tolewa na Yahweh.
\s5
\v 16 Daudi akazungumza na viongozi wa Walawi kuwapangia ndugu zao kuwa wana muziki wenye vyombo vya muziki, vyombo vya uzi, vinubi na upatu, kwa kupiga kwa sauti na furaha wakipaza sauti zao.
\v 17 Hivyo Walawi wakamchagua Hemani mwana wa Yoeli na mmoja wa kaka zake, Asafu mwana wa Berekia. Pia walimchagua ndugu wa uzao wa Merari na Ethani mwana wa Kushaia.
\v 18 Pamoja nao walikuwa ndugu wa daraja la pili: Zekarai, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaia, Maasaeia, Matithia, Elifelehu, Mikineaia, Obedi Edomu, na Yeieli, mlinzi wa lango.
\s5
\v 19 Wanamuziki Hemani, Asafu, na Ethani walichaguliwa kupiga upatu wa shaba.
\v 20 Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni Eliabu, Maaseia, na Benaia walicheza vyombo vya uzi.
\v 21 Matithia, Elifelehu, Mikineia, Obedi Edomu, Yeieli, na Azazia waliongoza njia na vinubi.
\s5
\v 22 Kenania, kiongozi wa Walawi, aliongoza uimbaji sababu alikuwa mwalimu wa muziki.
\v 23 Berekia na Elikana walikuwa walinzi wa sanduku.
\v 24 Shebania, Yoshafati, Nethanieli, Amasai, Zekaria, Benaia, na Eliezeri, makuhani, walikuwa wa kupuliza matarumbeta mbele ya sanduku la Mungu. Obedi Edomu na Yehia walikuwa walinzi wa sanduku.
\s5
\v 25 Hivyo Daudi, wazee wa Israeli, na wakuu wa maelfu wakaenda kuchukua sanduku la agano la Yahweh kutoka nyumba ya Obedi Edomu kwa shangwe.
\v 26 Wakati Mungu alipo wasaidia Walawi kubeba sanduku la agano la Yahweh, walitoa ng'ombe saba na mbuzi
\s5
\v 27 Daudi alivishwa joho safi la maridadi, pamoja na Walawi walio beba sanduku, waimbaji, na Kenania, kiongozi wa nyimbo na waimbaji. Daudi alivaa juu ya joho lake naivera.
\v 28 Hivyo Israeli yote wakaleta sanduku la agano la Yahweh na kelele za shangwe, na sauti za tarumbeta, ngoma za saani, na vyombo vya uzi na vinubi.
\s5
\v 29 Lakini sanduku la Yahweh lilivyokuja kwa mji wa Daudi, Mikali binti wa Sauli, alitazama nje ya dirisha, Akamuona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea. Kisha akamdharau moyoni mwake.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katika ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.
\v 2 Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.
\v 3 Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.
\s5
\v 4 Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 5 Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze na vyombo vya uzi na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele.
\v 6 Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu.
\s5
\v 7 Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.
\v 8 Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake.
\v 9 Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu.
\s5
\v 10 Jisifuni katika jina lake takatifu; mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie.
\v 11 Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.
\s5
\v 12 Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake,
\v 13 enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake.
\v 14 Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote.
\s5
\v 15 Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja.
\v 16 Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka.
\v 17 Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele.
\v 18 Alisema, "Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako."
\s5
\v 19 Nilisema hili mlipo kuwa wachache kwa idadi, wachache sana, mlipo kuwa wageni katika nchi.
\v 20 Walienda taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
\v 21 Hakuwaruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao.
\v 22 Alisema, " Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu."
\s5
\v 23 Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
\v 24 Kirini utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.
\s5
\v 25 Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.
\v 26 Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliye umba mbingu.
\v 27 Uzuri wa ajabu na utukufu upo uweponi mwake. Uwezo na furaha upo kwake.
\s5
\v 28 Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni sifa Yahweh utukufu na uwezo;
\v 29 Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika utakatifu wa uzuri wake.
\s5
\v 30 Mtetemeke mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika.
\v 31 Mbingu nazo ziwe nafuraha, na dunia ifurahi; na wasema kwa mataifa yote, "Yahweh anatawala."
\s5
\v 32 Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake.
\v 33 Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia.
\s5
\v 34 Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, uaminifu wa agano lake la dumu ata milele.
\v 35 Kisha sema, "Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako."
\s5
\v 36 Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, "Amina" na wakamsifu Yahweh.
\s5
\v 37 Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa.
\v 38 Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango.
\v 39 Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni.
\s5
\v 40 Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria.
\v 41 Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwasababu uaminifu wa agano lake la dumu ata milele
\s5
\v 42 Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango.
\v 43 Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kubariki nyumba yake.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Ikawa baada ya mfalme kuwa katika nyumba yake, akasema kwa Nathani yule nabii, "Angalia, nina ishi katika nyumba iliyo jengwa na mierezi, lakini sanduku la agano la Yahweh lipo kwenye chini ya hema."
\v 2 Kisha Nathani akasema kwa Daudi, Nenda, fanya yalio moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yupo nawe."
\s5
\v 3 Lakini usiku huo neno la Mungu lilimjia Nathani, nakusema,
\v 4 "Nenda umwambie Daudi mtumishi wangu, 'Hivi ndivyo Yahweh asemavyo: Hautanijengea nyumba ya kuishi.
\v 5 Kwa kuwa sijaishi katika nyumba toka ile siku niliyo ileta Israeli hadi leo. Badala yake, nimeishi ndani ya hema, hema la kukusanyikia, sehemu mbali mbali.
\v 6 Katika sehemu zote nilizo enda na Israeli, niliwai kusema lolote kwa viongozi wa Israeli niliyo wachagua kuwa chunga watu wangu, kwa kusema, "Kwa nini haujanijengea mimi nyumba ya mierezi?""
\s5
\v 7 "Kisha sasa, mwambie mtumishi wangu Daudi, 'Hili ndilo Yahweh wa majeshi anasema: Nilikuchugua kutoka malishoni, kufuata kondoo, ilikwamba uwe mtawala wa watu wangu Waisraeli.
\v 8 Nimekuwa nawe pote ulipo enda na nimewakata maadui zako wote, na na nitakufanyia jina, kama jina la wakuu wa dunia.
\s5
\v 9 Nitachagua sehemu ya watu wangu Israeli na nitawapanda hapo, iliwaishi sehemu yao na wasisumbuke tena. Watu wa ovu hawata watesa tena, kama walivyo fanya mwanzo,
\v 10 kama walivyo kuwa wakifanya toka siku zile nilipo waamuru waamuzi kuwa juu ya watu wangu Waisraeli. Kisha nitawatiisha maadui zako wote. Zaidi sana nina kwambia kwamba mimi, Yahweh, nitakujengea nyumba.
\s5
\v 11 Itakuja kuwa hapo siku zako zitapo timia za wewe kwenda kwa baba zako, nitainua uzao wako baada yako, na mmoja wa uzao wako nitaimarisha ufalme wake.
\v 12 Yeye atanijengea nyumba, na nitaimarisha kiti chake cha enzi milele.
\s5
\v 13 Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana wangu. Sitaondoa uwaminifu wa Agano langu kwake, kama nilivyo ondoa kwa Sauli, aliye tawala kabla yako.
\v 14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele."
\v 15 Nathani akanena haya kwa Daudi na kumtaarifu, na akamwambia kuhusu maono yote.
\s5
\v 16 Kisha Daudi mfalme akaenda ndani na kuketi mbele za Yahweh; akasema, "Mimi ni nani, Yahweh Mungu, na familia yangu ni nini, hadi unilete umbali huu?
\v 17 Hili lilikuwa jambo dogo machoni pako, Mungu. Umezungumzia familia ya mtumishi wako kwa muda mrefu ujao, na umenionyesha vizazi vijavyo, Yahweh Mungu.
\v 18 Nini zaidi mimi, Daudi, niseme? Umemheshimu mtumishi wako. Umemtambua kwa kipekee mtumishi wako.
\s5
\v 19 Yahweh, kwa ajili ya mtumishi wako, na kutimiza kusudi lako, umefanya hili ilikudhihirisha matendo yako makuu.
\v 20 Yahweh, hakuna aliye kama wewe, na hakuna Mungu zaidi yako, kama tulivyo sikia mara zote.
\v 21 Ni taifa gani duniani kama watu wako Israeli, ambaye wewe, Mungu, uliwaokoa kutoka Misri iliwawe watu wako, kujifanyia jina lako kwa matendo makuu na yahajabu? Uliondoa mataifa mbele za watu wako, uliye waokoa kutoka Misri.
\s5
\v 22 Ulifanya Israeli watu wako milele, na wewe, Yahweh, ukawa Mungu wao.
\v 23 Hivyo sasa, Yahweh, ile ahadi uliyo iweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake itimizwe milele. Fanya kama ulivyo nena.
\v 24 Jina lako na litukuzwe milele na kuwa kuu, ili watu waseme, 'Yahweh wa majeshi ni Mungu wa Israeli,' na nyumba yangu, mimi Daudi, mtumishi wako ikiwa imeimarishwa mbele zako.
\s5
\v 25 Kwa kuwa wewe, Mungu wangu, umedhihirisha kwa mtumishi wako utamjengea nyumba. Hiyo ndio sababu, mimi mtumishi wako, nimepata ujasiri wa kuomba kwako.
\v 26 Sasa, Yahweh, wewe ni Mungu, na umefanya hii ahadi nzuri kwa mtumishi wako:
\v 27 Sasa imekupendeza kubariki nyumba ya mtumishi wako, iliiendelee milele mbele zako. Wewe, Yahweh, umeibariki, na itabarikiwa milele."
\s5
\c 18
\p
\v 1 Baada ya haya Daudi akawashambulia Wafilisti na kuwashinda. Alichukuwa Gathi na vijiji vyake katika utawala wa Wafilisti.
\v 2 Kisha akamshinda Moabu, na Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakamlipa ushuru maalumu.
\s5
\v 3 Daudi kisha akamshinda Hadadezeri, mfalme wa Zoba huko Hamathi, wakati Hadadezeri alipo kuwa akisafiri kuimarisha utawala wake kwa Mto wa Frati.
\v 4 Daudi akateka magari ya farasi elfu, wanaume wa farasi elfu saba, na wanajeshi wa miguu elfu ishirini. Daudi aliwajeruhi farasi wote wagari, lakini akahifadhi baadhi kwa ajili ya magari ya farasi mia moja.
\s5
\v 5 Waaramia wa Damasko walipo kuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Zoba, Daudi aliua wanaume elfu ishirini na mbili wa Kiaramia.
\v 6 Kisha Daudi akaweka vikosi huko Aramu ya Damasko, na Waaramia wakawa watumishi wake na wakamletea ushuru maalaumu. Yahweh alimpatia Daudi ushindi popote alipoenda.
\s5
\v 7 Daudi alichukua ngao za dhahabu zilizo kuwa kwa watumishi wa Hadadezeri na kuleta Yerusalemu.
\v 8 Kutoka Tibhathi na Kuni, miji ya Hadadezeri, Daudi alichukuwa shaba nyingi sana. Ilikuwa shaba hii ambayo baadae Sulemani alifanya saani ya shaba, nguzo, na vifaa vya shaba.
\s5
\v 9 Wakati Toi, mfalme wa Hamathi, alipo sikia kuwa Daudi ameshinda majeshi yote ya Hadadezeri mfalme wa Zoba,
\v 10 Toi akamtuma Hadoramu mwanae kwa Mfalme Daudi kumsalimia na kumbariki, kwasababu Daudi amepigana na Hadadezeri na kumshinda, na kwasababu Hadadezeri alifanya vita na Toi. Hadoramu alipeleka vifaa vya fedha, dhahabu, na shaba.
\v 11 Mfalme Daudi alivitenga hivi vitu kwa ajili ya Yahweh, pamoja na fedha na dhahabu aliyo ibeba kutoka kwa mataifa yote: Edomu, Moabu, watu wa Amoni, Wafilisti, na Waamaleki.
\s5
\v 12 Abishai mwana wa Zeruia akawaua Waedomi elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.
\v 13 Alieka vikosi huko Edomu, na Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi. Yahweh alimpa Daudi ushindi pote alipoenda.
\s5
\v 14 Daudi alitawala Israeli yote, na alitenda haki na utaua kwa watu wote.
\v 15 Yoabu mwana wa Zeruia walikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mtunza kumbukumbu.
\v 16 Zadoki mwana wa Ahitubi na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Shavisha alikuwa mwandishi.
\v 17 Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa mwangalizi wa Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wakuu wa mfalme.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ikajakuwa baadae kwamba Nahashi, mfalme wa watu wa Amoni, akafa, na mwanae akawa mfalme baada yake.
\v 2 Daudi akasema, "Nitaonyesha ukarimu kwa mwana wa Hanuni wa Nahashi, kwasababu baba yake alionyesha ukarimu kwangu." Hivyo Daudi akatuma wajumbe kumfariji kuhusu baba yake. Watumishi wa Daudi wakaingia nchi ya Waamoni na kumfuata Hanuni, ilikumfariji.
\v 3 Lakini viongozi wakamwambia Hanuni, "Unadhani Daudi anamheshimu baba yako sababu ametuma watu kukufaraji? Je watumishi wake hawajaja kutadhimini nchi iliwaipindue?
\s5
\v 4 Hanuni akawakamata watumishi wa Daudi, akawanyoa, akakata mavazi ya nusu kwenye kiuno kushuka, na kuwarudisha.
\v 5 Walipo eleza haya kwa Daudi, alienda kukutana nao, kwa kuwa walifedheeka sana. Mfalme akasema, "Bakini Yeriko hadi ndevu zenu ziote tena, kisha mrudi."
\s5
\v 6 Waamoni walipoona wamekuwa kikwazo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni walituma talanta elfu moja za fedha kukodisha magari ya farasi kwa Waaremei na wanaume wa farasi kutoka Naharaimu, Maka, na Zoba.
\v 7 Waliwakodishia magari ya farasi elfu thelathini na mbili pamoja na mfalme wa Maka na watu wake, walio kuja na kueka kambi mbele ya Medeba. Waamoni walijikusanya pamoja kutoka miji yao, na wakaja kwa vita.
\s5
\v 8 Daudi alipo sikia, alimtuma Yoabu na wanajeshi wake wote.
\v 9 Watu wa Amoni walikuja na kupanga mstari kwa ajili ya pambano katika lango la mji, wafalme waliokuja walikuwa peke yao katika shamba.
\s5
\v 10 Yoabu alipoona mistari ya pambano imemzunguka mbele na nyuma, alichagua wapambanaji shupavu wa Israeli na kuwa panga dhidi ya Waaremi.
\v 11 Wanajeshi wengine wote, aliwaeka chini ya Abishai kaka yake, akawapanga kwa mstari dhidi ya Amoni.
\s5
\v 12 Yoabu akasema, "Kama Waaremi wananguvu kunizidi, kisha wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini kama jeshi la Waamoni lina nguvu kukuzidi, nitakuja kukuokoa.
\v 13 Kuwa thabiti, natujionyeshe kwa watu wetu kuwa ni wenye nguvu na kwa miji ya Mungu wetu, kwa kuwa Yahweh ata fanya lililo jema kwa kusudi lake."
\s5
\v 14 Hivyo Yoabu na wanajeshi wasogea kwenye pambano dhidi ya Waaremi, walio lazimika kukimbia mbele ya jeshi la Waisraeli.
\v 15 Jeshi la Waamoni walipoona kuwa Waaremi wamekimbia, wao pia wakamkimbia kaka yake Yoabu Abishai na kurudi mjini. Kisha Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na kurudi Yerusalemu.
\s5
\v 16 Waaremi walipoona kuwa wanashindwa na Waisraeli, wakatuma msaada nyuma ya Mto Frati, na Shofaki mkuu wajeshi la Hadadezeri.
\v 17 Daudi alipo ambiwa haya, akakusanya Israeli yote, akuvuka Yordani, na kuja juu yao. Alipanga jeshi kwa ajili ya pambano dhidi ya Waaremi, na wakapigana nao.
\s5
\v 18 Waaremi waliwakimbia Waisraeli, na Daudi akaua waendesha magari ya farasi ya Waaremi elfu saba na wanajeshi wa miguu elfu arobaini. Pia alimuua Shopaki, mkuu wa jeshi.
\v 19 Wafalme wote walio kuwa watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Daudi na kumtumikia. Hivyo watu wa Aramu hawakuwa tayari kuwasaidia Waamoni.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ikaja kuwa wakati wa mvua, kipindi wafalme uenda vitani, Yoabu akaongaza jeshi kwenda kupambana na kusikitisha nchi ya Waamoni. Alienda na kuteka Raba. Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu alishambulia Raba na kuishinda.
\s5
\v 2 Daudi alichukuwa taji la mfalme wao kichwani mwake, na akagundua linauzito wa talanta moja ya dhahabu, na ndani yake kulikuwa na mawe ya thamani. Taji liliwekwa kichwani mwa Daudi, na akaleta mali nyingi za mji.
\v 3 Aliwaleta watu walio kuwa ndani ya mji na kuwalazimisha wafanye kazi kwa msumeno na jembe na shoka. Daudi aliwataka watu wote wa mji kufanya kazi hii. Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu.
\s5
\v 4 Ilikuwa baada ya haya kukawa na pambano huko Gezeri na Wafilisti. Sibekai Mhushathi akamua Sipai, mmoja wa uzao wa Refaimu, na wa Filisti wakazidiwa.
\v 5 Ikawa tena katika pambano na Wafilisti huko Gobu, kwamba Elhanani mwana wa Yari Mbethilehemu akamua Lami kaka wa Goliathi Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa kama gongo la mshonaji.
\s5
\v 6 Ikaja kuwa tena katika pambano lingine huko Gathi kwamba mwanaume mmoja aliye mrefu sana mwenye vidole sita kila mkono na vidole sita mguuni. Naye alikuwa pia wa uzao wa Refaimu.
\v 7 Alipo dhihaki jeshi la Israeli, Yehonadabu mwana wa Shimea, kaka wa Daudi, akamuua.
\v 8 Hawa walikuwa uzao wa Refaimu wa Gathi, na waliuawa na mkono wa Daudi na mkono wa wanajeshi wake.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Adui akainuka dhidi ya Israeli na kumchochea Daudi kuhesabu Israeli.
\v 2 Daudi akamwabia Yoabu na kwa wakuu wa Jeshi, "Nenda, wahesabu watu wa Israeli kutoka Beerisheba mpaka Dani na uniletee taarifa, ilinijue idadi yao."
\v 3 Yoabu akasema, "Yahweh na afanya jeshi lake mara mia zaidi ya lilivyo. Lakini bwana wangu mfalme, kwani wote hawamtumikii bwana wangu? kwa nini bwana wangu anataka hili? Kwa nini ulete hatia kwa Israeli?"
\s5
\v 4 Lakini neno la mfalme halikubadilika kwa Yoabu. Hivyo Yoabu akaondoka na kwenda Israeli yote. Kisha akarudi Yerusalemu.
\v 5 Yoabu akatoa taarifa ya idadi ya jumla ya wanaume wa mapambano kwa Daudi. Kulikuwa ndani ya Israeli wanaume 1, 100, 000 walio beba upanga. Yuda peke yake kulikuwa na wanajeshi 470, 000.
\s5
\v 6 Lakini Levi na Benjamini hawaku hesabiwa miongoni mwao, kwa kuwa amri ya mfalme ilimuudhi Yoabu.
\v 7 Mungu alikwazika na hili tendo, akashambulia Israeli.
\v 8 Daudi akamwambia Mungu, "Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya hili. Sasa chukua hatia ya mtumishi wako, nimetenda kwa ujinga sana."
\s5
\v 9 Yahweh akamwambia Gadi, nabii wa Daudi,
\v 10 "Nenda useme kwa Daudi, "Hili ndilo Yahweh anasema: Ninakupa maamuzi matatu. Chagua moja wapo."
\s5
\v 11 Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kusema, "Yahweh anasema hivi, 'Chagua moja ya haya:
\v 12 kati ya miaka mitatu ya ukame, miezi mitatu unakimbizwa na adui zako na kupatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa Yahweh, yani, pigo katika nchi, malaika wa Yahweh akiharibu nchi yote ya Israeli.' Hivyo sasa, amua jibu gani ni mpelekee yeye aliye nituma."
\s5
\v 13 Kisha Daudi akamwambia Gadi, "Nipo katika shida kubwa sana. Acha nianguke katika mikono ya Yahweh kuliko kuangukia mikono ya mwanadamu, sababu matendo yake ya rehema ni makubwa mno."
\v 14 Hivyo Yahweh akatuma pigo Israeli, na watu elfu sabini wakafa.
\v 15 Mungu akatuma malaika Yerusalemu kuiharibu. Wakati alipo taka kuiharibu, Yahweh akatazama na kubadili nia yake kuhusu shambulio. Akasema kwa malaika wa uharibifu, "Imetosha! Rudisha mkono wako." Wakati huo malaika wa Yahweh alikua amesimama eneo la kupeta la Orinani Myebusi.
\s5
\v 16 Daudi akatazama juu na kuona malaika wa Yahweh amesimama kati ya nchi na mbingu, akiwa na upanga mkonono mwake akiuelekeza Yerusalemu. Kisha Daudi na wazee, wakiwa wamevaa magunia, wakalala chini uso ukiwa kwenye ardhi.
\v 17 Daudi akamwambia Mungu, "Sio mimi niliye amuru jeshi kuhesabiwa? Nimefanya hichi kitu kiovu. Lakini hawa kondoo, wamefanya nini? Yahweh Mungu wangu! Acha mkono wako unipige mimi na familia yangu, lakini usiache pigo iliendelee kubaki kwa watu wako."
\s5
\v 18 Hivyo malaika wa Yahweh akamuamuru Gadi kusema kwa Daudi, kwamba Daudi aende juu na kujenga madhabahu ya Yahweh katika eneo la kupeta la Oranani Myebusi.
\v 19 Daudi akaenda kama Gadi alivyo muelekeza cha kufanya kwa jina la Yahweh.
\v 20 Wakati Orinani akipepeta ngano, aligeuka na kumuona malaika. Yeye na wana wake wanne wakajificha.
\s5
\v 21 Wakati Daudi alipo kuja kwa Orinani, Orinani akatazama na kumuona Daudi. Aliacha eneo la kupeta na akamuinamia Daudi uso wake ukiwa kwenye ardhi.
\v 22 Kisha Daudi akasema kwa Orinani, "Niuzie hili eneo la kupeta, iliniweze kumjenga Yahweh madhabahu. Nitalipa gharama yote, ili pigo liondolewe kwa watu."
\s5
\v 23 Orinani wakwambia Daudi, "Chukuwa kama lako, bwana wangu mfalme. Fanya nalo linalo kupendeza. Tazama, nitakupa ng'ombe kwa sadaka ya kuteketeza, vifaa vya kupeta kwa ajili ya mbao, na ngano kwa sadaka ya mbegu; nitakupa yote wewe."
\v 24 Mfalme Daudi akamwambia Orinani, "Hapana, nina sisitiza kununua kwa bei yote. Sitachukua kilicho chako na kutoa kama sadaka ya kuteketeza kwa Yahweh kama haitanighramu chochote."
\s5
\v 25 Hivyo Daudi akalipa shekeli mia sita ya dhahabu kwa hilo eneo.
\v 26 Daudi akajenga madhabahu ya Yahweh pale na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za ushirika. Akamuita Yahweh, aliye mjibu kwa moto kutoka mbinguni kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.
\v 27 Kisha Yahweh akampa agizo malaika, na malaika akarudisha upanga kwenye mfuko wake.
\s5
\v 28 Daudi alipo ona kuwa Yahweh amemjibu kwenye eneo la kupeta la Orinani Myebusi, alitoa dhabihu pale pale kwa wakati huo.
\v 29 Sasa kwa wakati huo, hema la kuabudia la Yahweh, ambalo Musa alilitengeneza nyikani, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, zilikuwa sehemu ya juu huko Gibeoni.
\v 30 Walakini, Daudi hakuweza kwenda huko kumuliza Mungu muelekeo, kwa kuwa alikuwa anaogopa upanga wa malaika wa Yahweh.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kisha Daudi akasema, "Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli."
\v 2 Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu.
\s5
\v 3 Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo,
\v 4 na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta mboa nyingi za mierezi kwa Daudi azihesabu.)
\v 5 Daudi akasema, "Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine. Hivyo nitaanda ujenzi wake." Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake.
\s5
\v 6 Akaagiza Sulemani mwanae kuitwa na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli.
\v 7 Daudi akasema kwa Sulemani, "Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu.
\v 8 Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, 'Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hauta jenga nyumba kwa jina langu, kwasababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu.
\s5
\v 9 Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake.
\v 10 Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli.
\s5
\v 11 Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga.
\v 12 Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli.
\v 13 Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na mshujaa. Usiogope wala kufadhaika.
\s5
\v 14 Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100, 000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya.
\s5
\v 15 Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, maseremala, wanaume wenye ujuzi mbali mbali,
\v 16 wenye uwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na nishati. Hivyo anza kufanya kazi, na Yahweh awe nawe.
\s5
\v 17 Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema,
\v 18 "Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake.
\v 19 Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Daudi alipo kuwa mzee na kukaribia mwisho wa maisha yake, alimfanya Sulemani mwanae mfalme juu ya Israeli.
\v 2 Aliwakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, na makuhani na Walawi.
\v 3 Walawi walio kuwa miaka thelathini na zaidi walihesabiwa. Idadi ya elfu thelathini na nane.
\s5
\v 4 Kwa hawa, elfu ishirini na nne walikuwa kusimamia kazi ya nyumba ya Yahweh, na elfu sita walikuwa maaskari na waamuzi.
\v 5 Elfu nne walikuwa walinzi wa lango, na elfu nne walikuwa wamsifu Yahweh na vyombo nilivyo vitengeneza vya kusifu." Daudi akasema.
\v 6 Akawatenganisha kwenye vikundi kulingana na wana wa Levi: Gerishoni, Kohathi, na Merari.
\s5
\v 7 Kwa koo za uzao wa Gerishoni, kulilkuwa na Ladani na Shimei.
\v 8 Palikuwa na watatu wa wana wa Ladani: Yehieli kiongozi, Zethami, na Yoeli.
\v 9 Palikuwa na watatu wa wana wa Shimei: Shelomothi, Hazieli, na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa koo ya Ladani.
\s5
\v 10 Palikuwa na wanne wa wana wa Shimei: Yahathi, Ziza, Yeushi, na Beria.
\v 11 Yahathi alikuwa mkubwa, Ziza wapili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi, hivyo walihesabiwa kama ukoo mmoja na kupangiwa kazi sawa.
\s5
\v 12 Palikuwa na wanne wa wana wa Kohathi: Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
\v 13 Hawa walikuwa wana wa Amramu: Aruni na Musa. Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu, yeye na uzao wake watatoa uvumba kwa Yahweh, kumtumikia na kumpa baraka kwa jina lake.
\v 14 Lakini kwa Musa mtu wa Mungu, wana wake walihesabiwa kuwa Walawi.
\s5
\v 15 Wana wa Musa walikuwa Gerishomu na Eliezeri.
\v 16 Uzao wa Gerishomu ulikuwa Shebueli mkubwa.
\v 17 Uzao wa Eliezeri alikuwa Rehabia. Eliezeri hakuwa na wana wengine, lakini Rehabia alikuwa na uzao mkubwa.
\v 18 Mwana wa Izihari alikuwa Shelomithi kiongonzi.
\s5
\v 19 Uzao wa Hebroni ulikuwa Yeria, mkubwa, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
\v 20 Wana wa Uzieli walikuwa Mika mkubwa, na Ishia wapili.
\s5
\v 21 Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Wana wa Mahili walikuwa Eleazari na Kishi.
\v 22 Eleazari alikufa bila mtoto wa kiume. Alikuwa na mabinti tu. Wana wa Kishi waliwaoa.
\v 23 Wana wa Mushi watatu walikuwa Mahili, Ederi, na Yeremothi.
\s5
\v 24 Hawa walikuwa uzao wa Lawi kuligana na koo zao. Walikuwa viongozi, wamehesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, kuanzia koo zilizo fanya kazi katika nyumba ya Yahweh, kutoka miaka ishirini na zaidi.
\v 25 Kwa kuwa Daudi alisema, "Yahweh, Mungu wa Israeli, amewapa pumziko watu wake. Anafanya makao yake Yerusalemu milele.
\v 26 Walawi hawataitaji kubeba hema la kuabuadia na vifaa vyake vinavyo tumika kwenye utumishi wake."
\s5
\v 27 Kwa maneno ya Daudi ya mwisho Walawi walihesabiwa, miaka ishirini na kuendelea.
\v 28 Wajibu wao ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh. Walikuwa washughulikie nyuani, vyumbani, utakasaji wa vitu vyote vya Yahweh, na kazi zingine katika utumishi wa nyumba ya Mungu.
\v 29 Pia walishughulikia mkate wa uwepo, unga safi wa mbegu za sadaka, maandazi ya siotiwa chachu, sadaka za ngano, sadaka ziliochanganywa na mafuta, na vipimo vyote vya idadi n a ukubwa wa vitu.
\s5
\v 30 Pia walisimama kila asubui kumshukuru na kumsifu Yahweh. Pia walifanya hivi jioni
\v 31 na kila wakati sadaka ya kuteketezwa ilipo tolewa kwa Yahweh, siku ya Sabato na sherehe za mwezi mpya na siku za maakuli. Idadi iliyo pangwa, iliyo tolewa kwa amri, ilipaswa kuwa mbele ya Yahweh.
\s5
\v 32 Walikuwa viongozi wa hema la kukutania, patakatifu, na kuwasaidia ndugu zao wa uzao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
\v 2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwahiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani.
\v 3 Daudi pamoja na Zadoki, uzao wa Eleazari, na Ahimeleki, uzao wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi yao ya kazi kama makuhani.
\s5
\v 4 Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao.
\v 5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari.
\s5
\v 6 Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari.
\s5
\v 7 Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia,
\v 8 ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu,
\v 9 ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini,
\v 10 ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija,
\s5
\v 11 ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania,
\v 12 ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu,
\v 13 ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu,
\v 14 ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma,
\s5
\v 15 ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi,
\v 16 ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli,
\v 17 ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli,
\v 18 ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia.
\s5
\v 19 Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza.
\s5
\v 20 Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia.
\v 21 Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi.
\v 22 Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi.
\s5
\v 23 Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
\v 24 Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri.
\v 25 Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria.
\s5
\v 26 Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno.
\v 27 Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri.
\v 28 Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana.
\s5
\v 29 Wana wa Kishi: Yerameli
\v 30 wana wa Mushi: Mahli, Eda, na yerimothi. Walikuwa walawi, walio orodheshwa na familia zao.
\v 31 Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa katika nyumba za baba zao na kila wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Daudi na viongozi wa wafanyakazi wa hema la kuabudia walichaguliwa kwa kazi baadhi walikuwa wana wa Asafu, Hemani, na Yeduthuni. Wanaume hawa walitabiri kwa vinubi, vifaa vya uzi, na upatu. Hii ni orodha ya wanaume walioifanya hii kazi:
\v 2 Kutoka wana wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania, na Asharela, wana wa Asafu, chini ya mwongozo wa Asafu, ambaye alitabiri chini ya uwangalizi wa mfalme.
\v 3 Kutoka wana wa Yeduthuni: Gedalia, Zeri, Yeshaia, Shimei, Hashabia, na Matithia, sita kwa ujumla, chini ya mwongozo wa baba yao Yeduthuni, ambaye alipiga kinubi kwa kutoa shukurani na kumsifu Yahweh.
\s5
\v 4 Kutoka wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na yerimothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti Ezeri, yoshibekasha, Mallothi, Hothiri, na Mahaziothi.
\v 5 Hawa wote walikuwa wana wa Hemani mfalme wa manabii. Mungu alimpa Hemani wana kumi na nne na mabinti watatu kwa ajili ya kumpa heshima.
\s5
\v 6 Hawa wote walikuwa chini ya mwongozo wa baba yao. Walikuwa ni waimbaji katika nyumba ya Yahweh, pamoja na upatu na vifaa vya uzi walivyohudumu katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni, na Hemani walikuwa chini ya uwangalizi wa mfalme.
\v 7 Wao na kaka zao walikuwa na uwelewa na walifundishwa kutengeneza muziki kwa Yahweh walikuwa na idadi ya 288.
\v 8 Walirusha kura kwa majukumu yao, wote sawa, sawa kwa vijana na kwa wazee, kwa walimua na kwa wanafunzi.
\s5
\v 9 Sasa kuhusu wana wa Asafu: kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu; ya pili iliangukia katika familia ya Gedalia, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 10 ya tatu iliangukia kwa Zakuri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 11 ya nne iliangukia kwa Izri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 12 ya tano iliangukia kwa Nethania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\s5
\v 13 ya sita iliangukia kwa Bukia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 14 ya saba iliangukia kwa Yesharela, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 15 ya nane iliangukia kwa Yeshaia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 16 ya tisa iliangukia kwa Matania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\s5
\v 17 ya kumi iliangukia kwa Shimei, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 18 ya kumi na moja iliangukia kwa Azareli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 19 ya kumi na mbili iliangukia kwa Hashabia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 20 ya kumi na tatu iliangukia kwa Shubaeli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\s5
\v 21 ya kumi na nne iliangukia kwa Matithia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 22 ya kumi na tano iliangukia kwa Yeromothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 23 ya kumi na sita iliangukia kwa Hanania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 24 ya kumi na saba iliangukia kwa Yoshibekasha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\s5
\v 25 ya kumi na nane iliangukia kwa Hanani, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 26 ya kumi na tisa iliangukia kwa Malothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 27 ya ishirini iliangukia kwa Eliatha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 28 ya ishirini na moja iliangukia kwa Hothiri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\s5
\v 29 ya ishirini na mbili iliangukia kwa Gidalti, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 30 ya ishirini na tatu iliangukia kwa Mahaziothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
\v 31 ya ishirini na nne iliangukia kwa Romamti Eza, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Huu ulikuwa mgawanyiko wa walinzi wa lango: Kutoka kwa Wakora, Meshelemia mwana wa Kore, wa uzao wa Asafu.
\v 2 Meshelemia alikuwa na wana wa kiume: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wapili, Zebadia watatu, Yathinieli wanne,
\v 3 Elamu watano, Yehohanani wasita, Eliehoenai wasaba.
\s5
\v 4 Obedi alikuwa na wana wa kiume: Shemaia wa kwanza, Yehozabadi wapili, Yoa watatu, na Sakari wanne, na Nethanieli watano,
\v 5 Amieli wasita, Isakari wasaba, Peulethai wanane, kwa kuwa Mungu alimbariki Obedi Edomu.
\v 6 Kwa Shemaia mwanae walizawa wana walio tawala familia zao; walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali.
\s5
\v 7 Wana wa Shemaia walikuwa Othini, Refaeli, Obedi, na Elizabadi. Ndugu zake Elihu na Semakia walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali.
\v 8 Hawa wote walikuwa uzao wa Obedi Edomu. Wao na wanao na ndugu zao walikuwa wanaume wenye uwezo wa kufanya wajibu wao katika huduma ya hema la kuabudia. Palikuwa na sitini na mbili walio kuwa na undugu na Obedi Edomu.
\v 9 Meshelemia alikuwa na wana na ndugu, wanaume wenye uwezo, jumla ya kumi na nane.
\s5
\v 10 Hosa, mzao wa Merari, alikuwa na wana: Shimiri kiongozi (japo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi),
\v 11 Hilikia wapili, Tebalia watatu, Zekaria wanne. Wote wa wana wa Hosa na ndugu walikuwa kumi na tatu kwa idadi.
\s5
\v 12 Huu mgawanyiko wa walinzi wa lango, sambamba na viongozi, ulikuwa na majukumu, kama ndugu zao, kutumika katika nyumba ya Yahweh.
\v 13 Walirusha kura, wadogo kwa wakubwa, kulingana na familia zao, kwa kila lango.
\v 14 Kura ilipo rushwa kwa lango la mashariki, ilimuangukia Shelemia. Kisha wakarusha kura kwa Zekaria mwana wake, mshauri makini, na kura yake ikatokea lango la kaskazini.
\s5
\v 15 Kwa Obedi Edomu kulipangiwa lango la kusini, na wanae walipangiwa nyumba za ghala.
\v 16 Shufimu na Hosa walipangiwa lango la magharibi pamoja na lango la Shalekethi, kwa barabara ya juu. Lindo lilikabiidhiwa kwa kila familia.
\s5
\v 17 Kwa mashariki walikuwa Walawi sita, kaskazini kwa siku moja, kusini kwa siku moja, na nyumba za ghala wawili.
\v 18 Katika ua kuelekea magharibi wanne walipangwa, wanne barabarani, na wawili katika ua.
\v 19 Haya yalikuwa magawanyiko ya walinzi wa lango. Palijazwa na uzao wa Kora na Merari.
\s5
\v 20 Miongoni mwa Walawi, Ahija alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vya Yahweh.
\v 21 Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli na wanae,
\v 22 Zethamu, na Yoeli kaka yake, aliyesimamia ghala za nyumba ya Yahweh.
\s5
\v 23 Kulikuwa na askari walio chukuliwa kwa koo za Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli.
\v 24 Shebueli mwana wa Gerishomu mwana wa Musa, alikuwa msimamizi wa nyumba za ghala.
\v 25 Ndugu zake wa ukoo wa Eliezeri walikuwa Rehabia mwanae, mwana wa Rehabia Yeshaia, mwana wa Yeshaia Yoramu, mwana wa Yoramu Zikiri, na mwana wa Zikiri Shelomothi.
\s5
\v 26 Shelomothi na ndugu zake walikuwa wasimamizi wa nyumba zote za ghala zinazo hifadhi vitu vyote vya Yahweh, ambavyo Daudi mfalme, viongozi wa familia, wakuu wa maelfu na mamia, na wakuu wa jeshi walivyo vitenga.
\v 27 Walitenga vitu walivyo vichukuwa kwenye mapambano kwa ajili ya kutunza nyumba ya Yahweh.
\v 28 Pia walikuwa wahusika wa kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh na Samweli nabii, Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Zeruia. Kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh kilikuwa chini ya ulinzi wa shelomothi na ndugu zake.
\s5
\v 29 Wa uzao wa Izhari, Kenania na wana wake walikuwa wahusika wa mambo ya ndani ya Israeli. Walikuwa maafisa na waamuzi.
\v 30 Wa uzao wa Hebroni, Hashabia na kaka zake, wanaume wenye uwezo 1, 700, walikuwa wahusika wa kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme. Walikuwa upande wa mgharibi mwa Yordani.
\s5
\v 31 Kutoka uzao wa Hebroni, Yeriya alikuwa kiongozi wa uzao wake, walihesabiwa kutoka orodha za familia zao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi walitathimini kumbukumbu na kugundua miongoni mwao wanaume wa uwezo katika Yazeri ya Gileadi.
\v 32 Yerija alikuwa na ndugu 2, 700, walio kuwa viongozi wenye uwezo katika familia. Daudi aliwafanya waangalizi wa makabila ya Rubeni na Gadi, na nusu kabila la Manase, kwa kila jambo linalo muhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Hii ni orodha ya familia za viongozi wa Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, pamoja na maafisa wa jeshi walio mtumikia mfalme kwa namna tofauti. Kila kikosi cha jeshi kilitumika mwenzi hadi mwezi kwa mwaka mzima. Kila kikosi kilikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
\v 2 Kwa mwezi wa kwanza wa kikosi alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
\v 3 Alikuwa miongoni mwa uzao wa Perezi na mhusika wa maafisa wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
\s5
\v 4 Juu ya kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai, wa ukoo wa uliotoka kwa Ahoa. Mikilothi alikuwa wa pili kwa cheo. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 5 Mkuu wa jeshi wa mwezi wa tatu alikuwa Benaia mwana wa Yehoiada, kuhani na kiongozi. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 6 Huyu ni Benaia aliye kuwa kiongozi wa wale thelathini na juu ya wale thelathini. Amizabadi mwanae alikuwa katika kikosi chake.
\s5
\v 7 Mkuu kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli kaka wa Yoabu. Zebadia mwanae akawa mkuu baada yake. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
\v 8 Mkuu kwa mwezi wa tano alikuwa Shamihuthi, mzao wa Izra. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 9 Mkuu kwa mwezi wa sita alikuwa Ira mwana wa Ikeshi, kutoka Tekoa. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\s5
\v 10 Mkuu kwa mwezi wa saba alikuwa Helezi Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 11 Mkuu kwa mwezi wa nane alikuwa Sibekai Mhushathi, kutoka ukoo ulitoka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 12 Mkuu kwa mwezi wa tisa alikuwa Abi Ezeri Manathothi, kutoka kwa kabila la Benjamini. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\s5
\v 13 Mkuu kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai kutoka mji wa Netofa, kutoka ukoo ulio toka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 14 Mkuu kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaia kutoka mji wa Pirathoni, kutoka kabila la Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\v 15 Mkuu kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Helidai kutoka mji wa Netopafa, kutoka ukoo uliotoka kwa Othinieli. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
\s5
\v 16 Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli: Kwa kabila la Rubeni, Eliezeri mwana wa Zikri alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Simeoni, Shefatia mwana wa Maka alikuwa kiongozi.
\v 17 Kwa kabila la Lawi, Hashinia mwana wa Kemueli alikuwa kiongozi, na Zadoki aliongoza uzao wa Aruni.
\v 18 Kwa kabila la Yuda, Elihu, mmoja wa kaka zake Daudi, alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Isakari, Omri mwana wa Mikaeli alikuwa kiongozi.
\s5
\v 19 Kwa kabila la Zebuluni, Ishimaia mwana wa Obadia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Naftali, Yeremothi mwana wa Azirieli alikuwa kiongozi.
\v 20 Kwa kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaia alikuwa kiongozi.
\v 21 Kwa nusu kabila la Manase lililo Gileadi, Ido mwana wa Zekaria alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Benjamini, Yaasieli mwana wa Abneri alikuwa kiongozi.
\v 22 Kwa kabila la Dani, Azareli mwana wa Yerohamu alikuwa kiongozi. Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli.
\s5
\v 23 Daudi hakuwa hesabu wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi, kwasababu Yahweh alihaidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.
\v 24 Yoabu mwana wa Zeruia alianza kuhesabu wanaume, lakini hakumaliza. Gadhabu iliangukia Israeli kwa hili. Hii idadi haikuandikwa kwenye nyakati za mfalme Daudi.
\s5
\v 25 Azimavethi mwana wa Adieli alikuwa mhusika wa hazina za mfalme. Yonathani mwana wa Uzia alikuwa juu ya nyumba za ghala katika mashamba, kwenye miji, na vijijini, na kwenye minara iliyo imarishwa.
\v 26 Ezri mwana wa Kelubi alikuwa juu ya mashamba, hao walio lima ardhi.
\v 27 Shimei kutoka Rama alikuwa juu ya mashamba ya mizabibu, na Zabdi kutoka Shefamu alikuwa juu ya mizabibu na mhifadhi wa mvinyo.
\s5
\v 28 Mwangalizi wa miti mizeituni na miti ya mikuyu iliyo kuwa bondeni alikuwa Baali Hanani kutoka Gederi, na juu ya nyumba za ghala za mafuta alikuwa Yoashi.
\v 29 Juu ya mifugo iliyo kuwa inalishwa huko Sharoni alikuwa Shitrai kutoka Sharoni, na juu ya mifugo iliyo kuwa mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai.
\s5
\v 30 Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri.
\v 31 Hawa wote walikuwa wasimamizi wa mali za Mfalme Daudi.
\s5
\v 32 Yonathani, mjomba wake Daudi alikuwa mshauri, sababu alikuwa na busara na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakimoni aliwajali watoto wa mfalme.
\v 33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme, na Hushai kutoka watu wa Waariki alikuwa mshauri wake wa siri.
\v 34 Nafasi ya Ahithofeli ilichukuliwa na Yehoiada mwana wa Benaia, na Abiathari. Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi la mfalme.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Daudi akakusanya waamuzi wote wa Israeli Yerusalemu: waamuzi wa makabila, maafisa wa vitengo walio mtumikia mfalme katika kazi walizo pangiwa, wakuu wa maelfu na mamia, wasimamizi wa mali zote za mfalme na mwanae, na maafisa na wanaume wa mapambano, ukijumuisha wale wenye ujuzi sana.
\s5
\v 2 Daudi mfalme akainuka kwa miguu yake na kusema, "Sikilizeni mimi, kaka zangu na watu wangu. Ilikuwa dhumuni langu kujenga hekalu kwa ajili ya sanduku la agano la Yahweh; stuli ya miguu kwa ajili ya Mungu wetu, na nimefanya maandalizi kuijenga.
\v 3 Lakini Mungu akaniambia, 'Hautajenga hekalu kwa ajili ya jina la langu, kwasababu wewe ni mwanaume wa vita na umemwaga damu.'
\s5
\v 4 Bado Yahweh, Mungu wa Israeli, alinichagua kutoka katika familia ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Amechagua kabila la Yuda kama kiongozi. Katika kabila la Yuda, na nyumba ya baba yangu, kutoka kwa wana wa baba yangu, amenichagua kuwa mfalme wa Israeli.
\v 5 Kutoka kwa wana wengi ambao Yahweh amenipa, amemchagua Sulemani, mwanangu, kuketi katika kiti cha enzi cha ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli.
\s5
\v 6 Aliniambia, 'Sulemani mwanae atanijengea nyumba yangu na nyuani mwangu, kwa kuwa nimemchagua kuwa mwana wangu, nami nitakuwa baba yake.
\v 7 Nitaimarisha ufalme wake, akidumu kutii sheria na amri zangu, kama ulivyo siku ya leo.'
\s5
\v 8 Kisha sasa, katika macho ya Waisraeli wote, ili kusanyiko la yahweh, na katika uwepo wa Mungu wetu, nyinyi nyote lazima mshike na kufanya amri zote za Yahweh Mungu wenu. Fanyeni hivi ili mmiliki nchi nzuri na kuacha urithi wa watoto wenu baada yenu milele.
\s5
\v 9 Kwako wewe, Sulemani mwanangu, mtii Mungu wa baba yako, mtumikie kwa moyo wako wote na roho ya utayari. Fanya hivi kwasababu yahweh anachunguza mioyo yote na kufahamu amasa ya kila wazo la mtu. Ukimtafuta, ataonekana kwako, lakini ukimtelekeza, atakukataa milele.
\v 10 Elewa kuwa Yahweh amekuchagua kujenga hekalu ili kama sehemu yake takatifu. Kuwa imara na ufanye."
\s5
\v 11 Kisha Daudi akamkabidhi Sulemani mwanae mipango ya baraza la hekalu, jengo la hekalu, vyumba vya hifadhi, vyumba vya juu, vyumba vya ndani, na chumba chenye mfuniko wa maombezi.
\v 12 Alimpatia mipango aliyo chora ya nyuani kwa ajili ya nyumba ya Yahweh, vyumba vyote vilivyo zunguka, vyumba vya hifadhi katika nyumba ya Mungu, na hazina za vitu vya Yahweh.
\s5
\v 13 Alimpatia masharti kwa vitengo vya makuhani na Walawi, kwa majukumu walio pangiwa katika nyumba ya Yahweh, na kwa vyombo vyote vinavyo tumika katika nyumba ya Yahweh.
\v 14 Alimpa uzito wote wa vifaa vya dhahabu kwa kila huduma na vifaa vyote vya fedha, na vitu vyote kwa kila namna ya huduma.
\v 15 Haya maelekezo yalitolewa kwa uzito, ukijumuisha maelekezo yote ya vinara vya taa vya dhahabu na taa za dhahabu, maelekezo kwa uzito kwa kila vinara vya taa, kwa vinara vya taa vya fedha, na maelekezo kwa matumizi sahihi ya vinara vya taa vyote.
\s5
\v 16 Alitoa uzito wa dhahabu kwa meza za mkate wa uwepo, kwa kila meza, na uzito wa fedha kwa meza za fedha.
\v 17 Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa uma za nyama, bakuli, na vikombe. Alitoa uzito kwa kila bakuli ya dhahabu, na uzito kwa kila bakuli ya fedha.
\s5
\v 18 Alitoa uzito wa dhahabu ya kutakasika kwa madhabahu ya uvumba, na kwa dhahabu kwa ajili ya mchoro wa makerubi waliye tanda mabawa yao na kufunika sanduku la agano la Yahweh.
\v 19 Daudi akasema, " Nimeeka haya katika maandishi kama Yahweh alivyo ni elekeza na kunipa kuelewa kuhusu mchoro."
\s5
\v 20 Daudi akasema kwa Sulemani mwanae, "Kuwa hodari na mjasiri. Fanya kazi. Usiogope au kuwa na wasiwasi, kwa kuwa Yahweh Mungu, Mungu wangu, yupo nawe. Hatakuacha wala kukutelekeza mpaka kazi ya huduma ya hekalu la Yahweh imekamilika.
\v 21 Ona, hivi ni vitengo vya makuhani na Walawi kwa huduma katika hekalu la Mungu. Watakuwa nawe, pamoja na wanaume walio tayari na wenye ujuzi, kukusaidia katika kazi na kutenda huduma. Waamuzi na watu wote wako tayari kufuata amri zako."
\s5
\c 29
\p
\v 1 Mfalme Daudi akasema kwa kusanyiko lote, "Sulemani mwanangu, ambaye mwenyewe Mungu amemchagu, bado nimdogo na hana uzoefu, na jukumu ni kubwa. Maana hekalu sio kwa ajili ya watu bali la Mungu.
\v 2 Hivyo nimefanya kwa ubora wangu kutoa kwa ajili ya hekalu la Mungu. Nina toa dhahabu kwa vitu vya kujengwa na dhahabu, fedha kwa vitu vya kujengwa na fedha, shaba kwa vitu vya kujengwa na shaba, nishati kwa vitu vya kujengwa na nishati, na mbao kwa vitu vya kujengwa na mbao. Pia nina toa mawe ya shohamu, mawe ya kupangwa, mawe ya upambaji wandani ya rangi mbali mbali - kila haina ya mawe ya thamani - na marimari kwa wingi.
\s5
\v 3 Sasa, kwasababu ya mapenzi yangu kwa nyumba ya Mungu, Ninatoa hazina yangu binafsi ya dhahabu na fedha. Ninafanya hivi kwa nyongeza kwa yote niliyofanya katika hekalu takatifu:
\v 4 talanta za dhahabu elfu tatu kutoka Ofiri, na talanta elfu saba za fedha zilizotakasika, ili kufunika kuta za majengo.
\v 5 Ninachangia dhahabu kwa vitu vya kujengwa na dhahabu, na fedha kwa vitu vya kujengwa na fedha, na kazi zote zinazotakiwa kufanywa na wajenzi. Nani mwingine anataka kuchangia kwa Yahweh leo na kujitoa kwake?"
\s5
\v 6 Kisha sadaka za hiari zilitolewa na viongozi wa mababu wa familia zao, viongozi wa makabila ya Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, na waamuzi waliojuu ya kazi ya mfalme.
\v 7 Walitoa kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu talanta elfu tano na darkoni elfu kumi za dhahabu, talanta elfu kumi za fedha, talanta elfu nane za fedha, na talanta za chuma 100, 000.
\s5
\v 8 Haao walio na mawe ya thamani waliyatoa katika Hazina ya nyumba Yahweh, chini ya usimamizi wa Yehieli, mzao wa Gerishoni.
\v 9 Watu walifurahi kwa ajili ya hizi sadaka za hiari, kwasababu walitoa kwa moyo wao wote kwa Yahweh. Mfalme Daudi pia alifurahi sana.
\s5
\v 10 Daudi alimbariki Yahweh mbele ya kusanyiko lote. Alisema, "Na uabudiwe, Yahweh, Mungu wa Israeli babu wetu, milele na milele.
\v 11 Kwako, Yahweh, kuna ukuu, nguvu, utukufu, ushindi, na enzi. Kwa kuwa yote yalio mbinguni na duniani ni yako. Kwako ni ufalme, Yahweh, na umetukuzwa kama mtawala juu ya vyote.
\s5
\v 12 Utajiri na heshima utoka kwako, unatawala juu ya watu wote. Mkononi mwako kuna nguvu na uwezo. Unao uweza na nguvu ya kuwafanya watu kuwa mkuu na kumpa uweza yeyote.
\v 13 Kisha sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kusifu jina lako tukufu.
\s5
\v 14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, tustahili kutoa kwa hiari hivi vitu? Kweli, vitu vyote vya toka kwako, na tumerudisha kwako vilivyo vyako.
\v 15 Kwa kuwa sisi ni wageni na wasafiri mbele zako, mababu zetu wote walikuwa. Siku zetu katika dunia ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kubaki duniani.
\s5
\v 16 Yahweh Mungu wetu, utajiri wote tulio kusanya kujenga hekalu kwa kuheshimu jina lako - watoka kwako na ni wako.
\v 17 Ninajua, Mungu wangu, unachunguza moyo na wapendezwa na unyofu. Kwangu mimi, kwa unyofu wa moyo wangu nimetoa kwa hiari vitu vyote, na sasa natazama kwa furaha watu walio hapa wakitoa tunu kwako.
\s5
\v 18 yahweh, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Israeli - mababu zetu - hifadhi hili katika fikra za watu wako. Elekeza mioyo yao kwako.
\v 19 Mjalie Sulemani mwanangu moyo wa shauku wakutii amri zako, shuhuda za agano lako, na maagizo yako, na kutekeleza mipango hii yote ya kujenga nyumba niliyoiandaa."
\s5
\v 20 Daudi akasema kwa kusanyiko lote, "Sasa mbariki Yahweh Mungu wenu." Kusanyiko lote likambariki Yahweh, Munug wa mababu zao, wakainamisha vichwa vyao na kumuabudu Yahweh na kusujudu mbele za mfalme.
\v 21 Kwa siku iliyo fuata, wakatoa dhabiu kwa Yahweh na kumtolea sadaka ya kuteketeza. Walitoa sadaka ya ng'ombe elfu moja, kondoo elfu moja, na wana kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji na dhabihu tele kwa Israeli yote.
\s5
\v 22 Siku ile, walikunywa na kula mbele za Yahweh kwa furaha tele. Walimfanya Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme mara ya pili, na kumpaka mafuta ya mamlaka ya Yahweh kuwa mfalme. Pia walimpaka Zadoki mafuta kuwa mfalme.
\v 23 Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha Yahweh kama mfalme baada ya Daudi baba yake. Alifanikiwa, na Israeli yote ikamtii.
\s5
\v 24 Viongozi wote, wanajeshi, na Mfalme Daudi wanae wakaonyesha utii kwa Mfalme Sulemani.
\v 25 Yahweh alimheshimu sana Sulemani na kumkirimia nguvu kubwa kuliko mfalme yeyote aliyetangulia kabla yake Israeli.
\s5
\v 26 Daudi mwana wa Yese alitawala Israeli yote.
\v 27 Daudi alikuwa mfalme wa Israeli kwa miaka arobaini. Alitawala kwa miaka saba Hebroni na miaka thelathini na tatu Yerusalemu.
\v 28 Alikufa katika umri mzuri mkubwa, baada ya kufurahia maisha marefu, utajiri na heshima. Sulemani mwanae alitawala baada yake.
\s5
\v 29 Mafanikio ya mfalme Daudi yameandikwa katika historia ya Samweli nabii, katika historia ya Nathani nabii, na katika historia ya Gadi nabii.
\v 30 Yalio ekwa kwenye kumbukumbu ni matendo ya utawala wake, mafanikio yake na mambo yalio mdhuru, Israeli, na falme zote za nchi zingine.

1615
14-2CH.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,1615 @@
\id 2CH
\ide UTF-8
\h 2 Mambo ya Nyakati
\toc1 2 Mambo ya Nyakati
\toc2 2 Mambo ya Nyakati
\toc3 2ch
\mt 2 Mambo ya Nyakati
\s5
\c 1
\p
\v 1 Selemani mwana wa Daudi, aliimariswa katika utawala wake, na Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye na alimpa nguvu nyingi sana.
\s5
\v 2 Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya.
\v 3 Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani.
\v 4 Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko katika Yerusalemu.
\v 5 Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa. (Maandiko ya zamani yanasema
\s5
\v 6 Selemani akaenda huko kwenye kwenye madhabahu ya shaba mbele za Yahwe, ambayo ilikuwepo mahali pa hema ya kukutamia, na akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
\v 7 Mungu akamtokea Selemani usiku huo na akasema kwake, "Omba! Nikupe nini?"
\s5
\v 8 Selemani akasema kwa Mungu, "Umeonesha agano la uaminifu mkuu kwa Daudi baba yangu, na umenifanya mfalme katika nafasi yaye.
\v 9 Sasa, Yahwe Mungu, ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, maana umenifanya mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya dunia.
\v 10 Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?"
\v 11 Mungu akasema kwa Selemani, "Kwa kuwa hili lilikuwa kwenye moyo wako, na kwa kuwa hujaomba mali, utajiri, au heshima, wala maisha ya wale wanaokuchukia, wala maish marefu kwa jili yako binafsi, lakini umeomba hekima na maarifa kwa ajili yako, ili uwatawale watu wangu, ambao juu yao nimekufanya mfame, na hivi ndivyo nitafanya.
\s5
\v 12 Sasa nitakupa hekima na maarifa, pia nitakupa mali na utajiri, na heshima, kuliko wafalme wote waliokuwepo kabla yako walivyokuwa, na baada yako hakuna yeyote atakayekuwa navyo."
\v 13 Kwa hiyo Selemani akaenda Yerusalemu kutoka sehemu ya juu iliyokuwepo Gibeoni, kutoka mbele ya hema ya kukutania; akatawala juu ya Israeli.
\s5
\v 14 Selemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1, 400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.
\v 15 Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
\v 16 Selemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.
\v 17 Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Sasa Selemani akaamuru kulijengea nyumba jina la Yahwe na nyumamba kwa ajili ya ikulu ya ufalme wake.
\v 2 Selemeni akateua wanaume elfu sabini wabebe mizigo, na wanaume elfu themanini wa kukata mbao katika mlima, na wanaume 3, 600 kwa ajili ya kusimamia.
\v 3 Selemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, ukisema, "Kama ulivyofanya na Daudi baba yangu, ulivyomtumia magogo ya mierezi ili ajenge nyumba ya kuishi, fanya hivyo hivyo na mimi.
\s5
\v 4 Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli.
\v 5 Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
\s5
\v 6 Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbigu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, ispokuwa sadaka kwa ajili ya sadaka za kufukiza mbele zake?
\v 7 Kwa hiyo nileteeni mtu mwenye ujuzi wa kazi katika kazi ya dhahabu, fedha, shaba, na chuma, na ya dhambarau, na nyekundu, na sufu ya samawati, mtu anayejua kutengeza aina zote za mapambo ya mbao. Atakuwa na watu wenye ustadi waliopamoja nami katika Yuda na Yerusalemu, ambao Daudi baba yangu aliwaweka.
\s5
\v 8 Nitumieni pia mierezi, miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni, maana najua ya kuwa watumishi wako wanajua jinsi ya kukata mbao katika Lebanoni. Angalia, watumishi wangu watakuwa na watumishi wako,
\v 9 ili kwamba watayarishe mbao nyingi kwa ajili yangu, maana nyumba ninayotaka kuijenga itakuwa kubwa na ya ajabu.
\v 10 Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta." (Maandishsi ya kale yanasema: "kori ishirini elfu za ngano kama chakula").
\s5
\v 11 Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akajibu kwa maandishi, ambayo alimtumia Selemani: "Kwa kuwa Yahwe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mfalme juu yao."
\v 12 Zaidi ya hayo, Hiramu akasema, "Abarikiwe Yahwe, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia, amempa Daudi mwana mwenye hekima, mwenye karama ya busara na uelewa, ambaye atajenga nyumba kwa aajili ya Yahwe, na nyumba kwa ajili ya ufalme wake.
\s5
\v 13 Sasa nimemtum mtu mwenye ujuzi, mwenye karama ya uelewa, Hiramu, mtaalamu wangu.
\v 14 Ni mwana wa mwanamke wa binti za Dani. Baba yake alikuwa mtu kutoka Tiro. Ana ujuzi katika kazi za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe, na katika mbao, na katika dhambarau, samawati, na sufu yenkundu, na kitani safi. Pia ana ujuzi katika kutengeneza michoro ya aina yoyote na katika kubuni kitu chochote. Apatiwe nafsi miongoni mwa watumishi wako wenye ujuzi, na pamoja na wale wa bwana wangu, Daudi, baba yako.
\s5
\v 15 Sasa, ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, ambayo bwana wangu aliisema, na apeleke sasa vitu hivi kwa watumishi wake.
\v 16 Tutakata mbao kutoka Lebanoni, mbao nyingi kadri unavyohitaji. Tutazileta kwako kama mitumbwi kupitia bahari kwenda Yafa, na utazibeba hadi Yerusalemu."
\v 17 Selemani akawahesabu watu wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli, kwa kutumia njia ya Daudi, baba yake, aliyoitumia kuwahesabu. Walikutwa wako 153, 600.
\v 18 Miongoni mwao aliwateua sabini elfu ili wabebe mizigo, themanini elfu kuwa wakataji wa mbao katika milima, na 3, 600 kuwa wasimamizi wa kuwasimamia watu wafanye kazi.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kisha Selemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.
\v 2 Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake.
\v 3 Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Selemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini.
\s5
\v 4 Urefu wa ukumbi mbele ya nyumba ulikuwa mikono ishirini, ukilingana na upana wa nyumba, urefu wake kwenda juu pia ulikuwa mikono ishirini, na Selemani akaifunika sehemu ya ndani kwa dhahabu halisi.
\v 5 Akailitengeneza paa la ukumbi mkuu kwa miti ya miberoshi, ambayo aliifunika kwa dhahabu halisi, na ambayo aliifunika kwa miti ya mitende na minyororo.
\s5
\v 6 Akaipamba nyumba kwa vito vya thamani; dhahabu ilikuwa dhahabu kutoka Parvaimu.
\v 7 Pia akazifunika boriti zake, vizingiti, kuta, na milango kwa dhahabu; akachonga makerubi juu ya kuta zake.
\s5
\v 8 Akaijenga sehemu ya patakatifu pa patakatifu. Urefu wake ulilingana na upana wa nyumba, mikono ishirini, na upana wake pia ulikuwa mikono ishirini. Aliifunika kwa dhahabu halisi, thamani yake ilikuwa talanta mia sita.
\v 9 Uzito wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Alizifunika sehemu za juu kwa dhahabu.
\s5
\v 10 Akachonga makerubi wawili kwa ajili ya sehemu za patakatifu pa patakatifu, wahunzi wakayafunika kwa dhahabu. (Maandishi ya kale yanasema: makerubi wawili waliochongwa kwenye mbao).
\v 11 Mabawa ya makerubi yalikuwa na urefu wa mikono ishirini yote kwa pamoja; bawa la kerubi mmoja lilikuwa na urefu wa mikono mitano, lilifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa jingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano pia.
\v 12 Bawa la kerubi mwingine lilikuwa mikono mitano, likifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa lake jingine lilikuwa mikono mitano pia, likigusana na bawa la kerubi wa kwanza.
\s5
\v 13 Mabawa ya makerubi hawa yalienea jumla ya mikono mitano. Makerubi yalisimama kwa miguu yake, na nyuso zake zikiuelekea ukumbi mkuu.
\v 14 Akatengeneza pazia la samawati, dhambarau, na sufu nyekundu, na kitani safi, na akachora makerubi juu yake.
\v 15 Selemani pia akatengeneza nguzo mbili, kila moja ikiwa na urefu wa mikono thelathini na tano kwenda juu, kwa maana mbele ya nyumba; taji ambazo zilikuwa juu ya nguzo zilikuwa na urefu wa mikono mitano kwenda juu.
\v 16 Akatengeneza minyororo kwa ajili ya nguzo na akaiweka juu yake, pia akatengeneza maakomamanga mia moja na akayaunganisha kwenye minyororo.
\v 17 Akazisimamisha nguzo mbele ya hekalu, mkono wa kulia, na nyingine mkono wa kushoto; akaiita nguzo ya kulia Yakini, na nguzo ya kushoto akaiita Boazi.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Vivile akatengeneza madhabahu ya shaba; urefu wake ulikuwa mikono ishirini, na upana wake ulikuwa mikono ishirini.
\v 2 Pia akatengeneza bahari ya mduara ya chuma cha kuyeyushwa, mikono kumi kutoka ukingo hadi ukingo. Urefu wake kwenda juu ulikuwa mikono mitano, na bahari ilikuwa na mzunguko wa mikono thelatinini.
\v 3 Chini ya kingo kuzunguka bahari kulikuwapo ng'ombe dume, kumi kila mkono,
\s5
\v 4 Bahari ilisimama juu ya ng'ombe wa kulima kumi na wawili, watatu wakiangalia kaskazini, watatu wakiangalia magharibi, na watatu wakiangalia kusini, na watatu wakiangalia mashariki. Bahari iliwekwa juu yao, na robo ya sehemu zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
\v 5 Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.
\v 6 Pia akatengeneza birika kumi kwa ajili ya kuoshea vitu; tano akaziweka mkono wa kulia, na tano akaziweka kushoto; vifaa vilivyotumika katika kufanayia sadaka za kuteketezwa zilipaswa kuoshwa ndani ya hizo birika. Bahari, vilevile ilikuwa kwa ajili ya makauhani kuoga humo.
\s5
\v 7 Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.
\v 8 Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Akatengeneza birika mia moja za dhahabu.
\s5
\v 9 Zaidi ya hayo akatengeneza mahakama ya makuhani na mahakama kuu, na milangu kwa ajili ya mahakama, akaifunika milango yake kwa shaba.
\v 10 Akaiweka bahari upande wa kulia wa nyumba, masharika, ikielekea upande wa kusini.
\s5
\v 11 Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Selemani katika nyumba ya Mungu:
\v 12 zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo.
\v 13 Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.
\s5
\v 14 Pia akavitengeneza vitako na mabirika juu ya kitako,
\v 15 bahari moja na wale ng'ombe kumi na wawili chini yake,
\v 16 pia masufuria, majembe, nyuma za nyama, na vyombo vingine vyote. Huramu mtaalamu akavifanya kwa ajili ya Mfalme Selemani, kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vya shaba iliyong'arishwa.
\s5
\v 17 Mfalme alikuwa amevisubu katika uwanda wa Yordani, katika udongo wa mfinyanzi kati kati ya Sukothi na Sereda.
\v 18 Hivyo ndivyo Selemani alivyovitengeneza vyombo vyote kwa wingi; kwa kweli, uzito wa shaba haukuweza kujulikana.
\s5
\v 19 Selemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa;
\v 20 vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi;
\v 21 na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi.
\v 22 Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlanago wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Wakati ilipomalizika kazi aliyofanya Selemani kwa ajili ya Yahwe, Selemani akapeleka vitu ndani, ambavyo Daudi, baba yake, aliviweka wakifu kwa kusudi hilo, pamoja na zile fedha, dhahabu, na vyombo vyote akavileta ndani ya hazina ya nyumba ya Mungu.
\s5
\v 2 Kisha Selemanai akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wa makabila yote, na viongozi wa familia za watu wa Israeli, katika Yerusalemu, ili walilete sanduku la agano la Yahwe kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.
\v 3 Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika mbele za mfalme katika sikukuu, ambayo ilikuwa katika mwezi wa saba.
\s5
\v 4 Wazee wote wa Israeli wakaja, na Walawi wakalichukua sanduku.
\v 5 Wakalileta sanduku, hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya hema. Makuhani waliokuwa wa kabila la Lawi wakavileta vtu hivyo.
\v 6 Mfalme Selemanai na kusanyiko lote la Israeli wakaja pamoja, mbele ya sanduku, wakitoa sadaka za kondoo na maksai ambao hawakuweza kuhesabika.
\s5
\v 7 Makuhani wakalileta sanduku la anago la Yahwe ndani mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, kwenye patakatifu pa patakatifu, chini ya mabawa ya makerubi.
\v 8 Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, na walilifunika sanduku na na miti yake ya kulibebea.
\s5
\v 9 Miti ilikuwa mirefu sana kwamba ncha zake zlionekana kutoka ile sehemu takatifu mbele ya chumba cha andani, lakini hazikuweza kuonekana kutoka nje. Zipo hapo hadi leo.
\v 10 Hapakuwa na kitu katika sanaduku isipokuwa zile meza mbili ambazo Musa aliziweka humo huko Horebu, wakati Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka nje ya Misri.
\s5
\v 11 Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhanai wote wliokuwepo wakajiweka wakifu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao.
\v 12 Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakaasimama upande wa mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhuni 120 wakipuliza tarumbeta.
\v 13 Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, "Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele." Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu.
\v 14 Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kisha Selemani akasema, "Yahwe alisema kwamba ataishi katika giza nene,
\v 2 lakini nimekujengea makao makuu, sehemu kwa ajili yako ya kuishi milele."
\v 3 Kisha mfaalme akageuka nyuma na kuwabariki kusanyiko lote la Israeli, wakati kusanyiko lote la Israeli walikuwa wamesimama.
\s5
\v 4 Akasema, "Yahwe, Mungu wa Israeli, usifiwe, uliyesema na Daudi baba yangu, na ametimiza kwa mikono yake mwenyewe, akisema.
\v 5 'Tangu siku nilipowaleta watu wanagu nje ya nchi ya Misiri, sikuchaagua mji wowote nje ya makabaila yote ya Israeli ambamo nyumba ingejengwa, ili jina lanagu liwe humo. Wala sikuchagua mtu yeyote kuwa mfalme juu ya watu wangu Israeli.
\v 6 Aidha, nimechagua Yeruselemu, ili kwamba jina langu liwe humo, na nimemchagua Daudi kuwa juu ya watu wanagu Israeli. '
\s5
\v 7 Sasa ilikuwa ndani ya moyo wa Daudi baba yangu, kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 8 Lakini Yahwe alisema kwa Daudi Baba yanagu. 'Kwmba ilikuwa ndani ya moyo wako kujenga nyumba kwa ajili ya jina langu, ulifanya vizuri kwa hili kuliweka moyono mwako.
\v 9 Aidha, hutaijenga ile nyumba, badala yake, mwanao, mmoja atakayetoka kwenye viuno vyako, ataijenga nyumba kwa ajili ya jina langu.'
\s5
\v 10 Yahwe ameyatimiza maneno aliyokuwa amesema, kwa maana nimeiinua sehemu ya Daudi baba yangu, na ninkaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, kama alivyoahidi Yahwe. Nimeijenga nyumba kwa ajii ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 11 Nimeliweka humo sanduku, amabamo kuna agano la Yahwe, alilofanya na watu wa Israeli."
\s5
\v 12 Selemani akasimama mbele ya madhabahu ya Yahwe mbele za kusanyiko lote la Israeli, na akanyosha mikono yake.
\v 13 Kwa mana alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, lenye urefu wa mikono mitano, upana wa mikono mitano, urefu wake kwenda juu mikono mitatu. Alikuwa ameliweka katika ya uwanja. Akasimama juu yake na kupiga magoti mbele ya kusanyiko la Israeli, kisha akanyosha mikono yake kuzielekea mbingu.
\s5
\v 14 Akasema, "Yahwe, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe katika mbingu, au juu ya dunia, ambaye anatunza agano na upendo imara na watumishi wako ambao hutembea mbele zako kwa moyo wao wote;
\v 15 wewe uliyetimtimizia Daudi baba yanagu, uliyokuwa umemwahidi. Ndiyo, ulisema kwa kinywa chako na umetimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.
\s5
\v 16 Sasa, Yahwe, Mungu wa Israeli, tunza ahadi uliyoahidi kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, uliposema, 'Hautashindwa kupata mtu mbele yangu wa kukaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, ikiwa tu uzao wako ni waangalifu kutembea katika sheria yangu, kama wewe ulivyotembea mbele zangu.
\v 17 Sasa, Mungu wa Israeli, ninaomba kwamba ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi itakuwa kweli.
\s5
\v 18 Lakini kweli Mungu ataishi na wanadamu juu ya dunia? Angalia, dunia yoye na mbugu yenyewe haviwezi kukubeba -sembuse na hekalu hili nililojenga!
\v 19 Nakusihi yaheshimu maombi haya ya mtumishi wako na ombi lake. Yahwe Mungu wangu; sikia kilio na amaombi ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako.
\v 20 Fumbua macho yako kuelekea hekaalu hili usiku na mchana, sehemu aambaayo uliahidi kuliweka jina lako. Nakuomba usikie maombi atakayoomba mtumishi wako kuelekea sehemu hii.
\s5
\v 21 Hivyo sikia maombi ya mtumishi na ya watu wako Israeli tunapoomba kuelekea sehemu hii. Ndiyo, sikia kutoka mahali unapoishi, kutoka mbinguni; na unaposikia, samehe.
\s5
\v 22 Kama mtu atamtenda dhambi jirani yake na ikampasa kuapa kiapo, na ikiwa atakuja na kuapa kiapo mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,
\v 23 basi sikia kutoka mbinguni na kutend na ukawahukumu watumishi wako, ukamlipizie mwovu, ili kuyaleta matendo yake juu ya kichwa chake. Ukamtangaze mwenye haki kuwa hana hatia, ili kumlipa thawabu kwa ajili ya uaminifu wake.
\s5
\v 24 Watu wako watakaposhindwa na adui kwa sababu wamekutenda dhambi, kama watageuka nyuma kwako, wakilikili jina lako, wakisali na kuomba msamaha mbele zako hekaluni—
\v 25 basi tafadhali sikia mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Isaraeli; uwarudishe katika nchi uliyoitoa kwa ajili yao na baba zao.
\s5
\v 26 Wakati mbingu zimefungwa na hakuna mvua kwa sababu watu wamekutenda dhambi—ikiwa wataomba kuelekea sehemu hii, wakilikili jina lako, na kuziacha dhambi zao utakapokuwa umewaadhibu—
\v 27 basi sikia mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na watu wako Israeli, utakapowaelekeza kwenye njia njema iwapasayo kutembea. Tuma mvua juu ya nchi yako, ambayo umewapa watu wako kama urithi.
\s5
\v 28 Kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna ugonjwa, tauni au ukungu, nzige au viwavijeshi, au kama adui wake wameyavamia malango ya mji katika nchi yao, au kwamba kuna pigo lolote au ugonjwa—
\v 29 na ikiwa sala na maombi yamefanywa na mtu au watu wako wote Israel—kila mmoja akilijua pigo na huzuni katika moyo wake akinyosha mikono yake kuelekea hekalu hili.
\v 30 Basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi; samehe, na umlipe kila mtu kwa njia zake zote; uhaujua moyo wake, kwa sababu wewe na ni wewe pekee unaijua mioyo ya wanadamu.
\v 31 Fanya hivyo ili kwamba wakuogope wewe, ili waweze kutembea katika katika njia zako siku zote ambazo wataishi katika nchi uliyowapa baba zetu.
\s5
\v 32 Kwa mgeni ambaye siyo sehemu ya watu wako Israeli, lakini ambaye- kwa sababu ya ukuu wa jina lako, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulionyoshwa- akija na kuomba kuelekea sehemu nyumba hii,
\v 33 basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi, na fanya yote ambayo mgeni atakuomba, ili kwamba watu wote wa dunia walijue jina lako na kukuogopa wewe, kama wafanyavyo watu wako Israeli, na kwamba waweze kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.
\s5
\v 34 Ikiwa kwamba watu wako wakaenda nje kupigana dhidi ya adui zao, kwa njia yoyote amabayo unaweza kuwatuma, na ikiwa kwamba wakaomba kwako kuelekea mji huu ambao umeuchagua, na kuelekea nyumba ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako.
\v 35 Basi sikiliza maombi yao mbinguni, ombi lao, na uwasaidie.
\s5
\v 36 Kama wametenda dhambi dhidi yako—kwa kuwa hakuna asiye tenda dhambi—na ikiwa una hasira nao na kuwakabidhi kwa adui zao, ili kwamba adui wakawabeba na kuwachukua kama mateka kwa ajili ya nchi zao, iwe mbali au karibu.
\v 37 Kisha wakatambua kuwa wako katika nchi ambako wamewekwa utumwani, na ikiwa watatubu na kutafuta msaada kwako katika utumwa wao. ikiwa watasema, 'Tumetenda kinyume na kutenda dhambi. Tumetenda kwa uovu,'
\v 38 ikiwa watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa nia yao yote katika nchi ya utumwa wao, ambako walichuliwa kama mateka, na ikiwa wataomba kukabili nchi yao, uliyowapa babu zao, na kukabili mji ambao uliuchagua na kukabili nyumba ambayo niliijenga kwa ajili ya jina lako.
\v 39 Basi sika kutoka mbinguni, mahali unapoishi, sikia kuomba kwao na maombi na wayaombayo, na uwasaidie shida zao. Wasamehe watu wako, ambao wamekutenda dhambi.
\v 40 Sasa, Mungu wangu, ninakusihi, uyafungue macho yako, na masikio yako yasiskie maombi yatakayofanywa katika sehemu hii.
\v 41 Sasa basi, amka, Yahwe Mungu, kwenye mahali pako pa kupumzikia, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Yahwe Mungu, wavikwe wokovu, na watakatifu wako wafurahi katika wema.
\v 42 Yahwe Mungu, usiugeuze nyuma uso wa masihi wako. Yakumbuke matendo yako katika agano lako la ufalme kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Sasa Selemani alipokuwa amemaliza kuomba, moto ukaja kutoka mbinguni na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, na utukufu wa Yahwe ukaijaza nyumba.
\v 2 Makuhani hawakuweza kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, kwa sababu utukufu wake uliijaza nyumba yake.
\v 3 Watu wote wa Israeli wakaangalia juu moto uliposhuka chini na utukufu wa Yahwe ulikuwa juu ya nyumba. Wakalala kwa nyuso zao juu ya sakafu ya mawe, wakaabudu, na kutoa shukrani kwa Yahwe. Wakasema, "Kwa maana yeye ni mwema, kwa maana agano lake la kifame ladumu milele."
\s5
\v 4 Kwa hiyo mfalme na watu wote wakamtolea Yahwe sadaka Yahwe.
\v 5 Mfalme Selemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu na kondoo 120, 000 na mbuzi. Kwa hiyo mfalme na watu wote wakaiweka wakifu nyumba ya Mungu.
\v 6 Makuhani wakasimama, kila mmoja akasimama mahali pake pa kuhudumu; Walawi pia pamoja na vyombo vya muziki vya Yahwe, ambavyo mfalme Daudi alivitengeza kwa ajili ya kumpa shukrani Yahwe katika nyimbo, "Kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele." Makuhani wote wakapiga matarumbeta mbele yao, na Israeli wote wakasimama.
\s5
\v 7 Selemani akaitakasa sehemu ya katikati ya kiwanja cha mfalme mbele ya nyumba ya Yahwe. Humo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba ambayo alikuwa ametengeza haikuweza kuzibeba sadaka, sadaka za nafaka, na za mafuta.
\s5
\v 8 Kwa hiyo Selemani akaitisha sikukuu wakati huo kwa siku saba, na Israeli wote pamaoja naye, kusanyiko kubwa, kutoka Lebo Hamathi mpaka kijito cha Misiri.
\v 9 Siku ya nane wakaitisha kusanyiko la makini, kwa maana kwa siku saba walishika kuwekwa wakfu kwa ile madhabahu.
\v 10 Katika siku ya ishini na tatu ya mwezi wa saba, Selemani akawatanya watu kwenda kwenye nyumba zao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa sababu ya wema aliokuwa ameuonesha Yahwe kwa Daudi, Selemani, Israeli, na watu wake.
\s5
\v 11 Hivyo Selemani akaimaliza nyumba ya Yahwe na nyumba yake mwenyewe. Kila kitu kilichokuja katika moyo wa Selemani kwa ajili ya kukitengeneza katika nyumba ya mfalme na katika nyumba yake mwenyewe, alikitimiza kwa mafanikio.
\v 12 Yahwe akamtokea Selemani usiku na kusema kwake, "Nimesikia maombi yako, na nimeichagua sehemu hii kwa ajili yangu mwenyewe kama nyumba ya dhabihu.
\s5
\v 13 Kama nitazifunga mbingu ili kwamba kusiwepo mvua, au kama nitaamuru nzige waimeze nchi, au kama nitatuma magonjwa kati kati ya watu wangu,
\v 14 kisha watu wangu, ambao wameitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, kuomba, kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka mbinguni, kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.
\v 15 Sasa macho yangu yatakuwa wazi na masikio yangu yatasikiliza maombi yanayofanywa katika sehemu hii.
\s5
\v 16 Kwa maana sasa nimeichagua na kauitakasa nyumba hii ili kwamba jina langu lipate kuwa humo milele. Masikio yangu na moyo wangu vitakuwako kila siku.
\v 17 Kwako wewe, kama utatembe mbele zangu kama baba yako Daudi alivyotembea, ukitii yote nilyokuamuru na kuzishika sheria zangu na maagizo yangu,
\v 18 basi nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyosema katika agano na Daudi baba yako, niliposema, 'Mzaliwa wako hatashindwa kamwe kuwa mtawala katika Israeli.'
\s5
\v 19 Lakin ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri amabzo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia,
\v 20 basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu amabayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongini mwa watu wote.
\v 21 Ingawa hekalu hili hili zuri sana kwa sasa, kila mtu apitaye karibu yake atashangazwa na ataguna. Watauliza, 'Kwa nini Yahwe ameifanyia hivi nchi hii na nyumba hii',
\v 22 wengine watajibu, 'Kwa sababu walimsahau Yahwe, Mungu wao, ambaye alikuwa amewatoa babu zao nje ya nchi ya Misiri, na wakashikamana na miungu wengine na kuwainamia chini na kuwaabudu. Hii ndiyo maana Yahwe ameleta majanga haya yote juu yao"
\s5
\c 8
\p
\v 1 Ikawa karibu ya mwisho wa miaka ishirini, kipindi ambacho Selemani alikuwa ameijenga nyumba ya Yahwe na ya kwake mwenye,
\v 2 kwamba Selemani akaiajenga miji ambayo Hiramu alikuwa amempa, na ndani yake akawaweka watu wa Israeli.
\s5
\v 3 Selemani akauavamia Hamathzoba, akaushinda.
\v 4 Akaijenga Tadmori katika nyika, na miji yote ya hazina, ambayo aliijenga katika Hamathi.
\s5
\v 5 Pia akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji iliyozungushiwa kwa ukuta, malango, na makomeo.
\v 6 Akaujenga Baalathi na miji yote ya hazina aliyoimiliki, na miji yote kwa ajili ya magari yake na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake, na chochote alichotamani kujenga kwa ajili ya starehe zake katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika nchi zote zilizokuwa chini ya utawala wake.
\s5
\v 7 Kuhusu watu wengine wote ambao walikuwa wamesalia wa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, Wayebusi, ambao hawakuwa wa Israeli,
\v 8 watoto wao ambao waliachwa baada yao katika nchi, ambaoa watu wa Israeli hawakuwaangamiza—Selemani akawafanyisha kazi kwa nguvu, ndivyo walivyo hata leo.
\s5
\v 9 Vile vile, Selemani hakuwafanyisha kazi kwa nguvu watu wa Israeli. Badala yake, wakawa wanajeshsi wake, maakida wake, wakuu wake, na maakida wa magari ya majeshi yake na wapanda farasi wake.
\v 10 Pia hawa walikuwa wakuu wa wakuu wakisimamia wasimamizi waliokuwa wa mfalme Selemani, walikuwa 250, waliowasimamia watu walioifanya kazi.
\s5
\v 11 Selemani akamleta binti Farao nje ya mji wa Daudi kwenye nyumba aaliyokuwa amemjengea, kwa maana alisema, "Mke wangu lazima asiishi kataika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu kila linapokuja sanduku la Yahwe ni takatifu".
\s5
\v 12 Kisha Selemani akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi.
\v 13 Akatoa sadaka kama ilivyohitaka katika ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amari ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda.
\s5
\v 14 Katika kuyatunza maagizo ya baba yake Daudi, Selemani akayapanga makundi ya makuhani kwenye kazi yao, na Walawi kwenye nafasi zao, ili kumsisfu Mungu na kuhudumu mbele za makuhani, kama ilivyotakiwa katika ratiba ya kila siku. Pia akawateua walinda lango kwa zamu zao kwa kila lango, kwa maana Daudi, mtu wa Mungu, alikuwa ameagiza hivyo pia.
\v 15 Watu hawa hawakupotea kutoka kwenye amri ya mfalme kwa makuhani na Walawi kuhusu jambo lolote, au kuhusu vyumba vya hazina.
\s5
\v 16 Kazi yote aliyoagizwa na Selemani ikakamilika, kutoka siku msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika.
\v 17 Kisha Selemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu.
\v 18 Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri na Selemani na watumishi wa Semani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Selemani.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Malikia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Selemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa
\v 2 Selemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Selemani akamjibu maswaali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Selemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.
\s5
\v 3 Malikia wa Sheba alipoiona hekima ya Selemani na ikulu aliyokuwa amejenga,
\v 4 chakula mezani kwake, mahali pa kukaa watumishi wake, kazi ya watumisshi wake na mavazi yao, pia wabebakikombe na mavazi yao, na namna alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe, hapakuwa na roho zaidi ndani yake.
\s5
\v 5 Akasema kwa mfalme, "Ni kweli, taarifa ninioisikia katika nchi yangu kuhusu maneno yako na hekima yako.
\v 6 Sikuamini nilichokisika mpaka nilipokuja hapa, na sasa macho yangu yamekiona. Sikuambiwa nusu kuhusu hekima yako na utajiri wako! Umeuzidi umaarufu niliokuwa nimesikia kuhusu wewe.
\s5
\v 7 Wamebarikiwa watu wako, na watumishi wako ambao husimama mbele yako, kwa sababu wanaisikia hekima yako. (Baadhi ya maandiko yanasema, "Wambarikiwa wake zako", ikidhaniwa kwamba kifungu hicho kinapaswa kusomeka kama ilivyo katika Wafalme 10: 8).
\v 8 Amebarikiwa Yahwe Mungu wako, ambaye amepata raha ndani yako, aliyekuweka juu ya kiti chake cha enzi, ili uwe mfalme kwa ajili ya Yahwe Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako inaipenda Israeli, ili kuwathibisha milele, amekufanya kuwa mfalme juu yao, ili ufanye hukumu na haki.
\s5
\v 9 Akampa mfalme talanta 120 za dhahabu na kiasi kikubwa manukato na vit vya thamani. Selemani hakupewa tena kiasi kikubwa cha manukato kama hiki amabacho alipewa na malakia wa Sheba.
\s5
\v 10 Watumishi wa Hiramau na wa mfalme Selemani, ambaye alileta dhahabu kutoka Ofiri, miti ya msandali,, na vito vya thamani.
\v 11 Kwa miti hiyo ya msandali, mfalme Selemani akatengeneza madari ya nyumba ya Yahwe na nyumba yake, na vinubi na vinanda kwa ajili ya wanamziki. Hapajaonekana tena mbao kama hiyo katika nchi ya Yuda.
\v 12 Mfalme Selemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotaka, chochote alichoomba, zaidi ya vile alivyoleta kwa mfalme Selemani. Kwa hiyo akaondoka na kurudi kwenye nchi yake, yeye na wataumishsi wake.
\s5
\v 13 Sasa uzito wa dhahabu ambayo ililetwa kwa Selemani ndani ya mwaka mmoja ulikuwa talanta 666 za dhahabu,
\v 14 nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Walme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Selemanai dhahabu na fedha.
\s5
\v 15 Mfalme Selemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili za dhahabu iliyofuliwa. Shekeli mia sita za dhahabu zikatumika kwa kila ngao.
\v 16 Pia akatengeneza ngao mia tatu za shahabu iliyopigwa. Minas tatu za dhahabu zikaenda kwa kila ngao; mfalme akaziweka kwenye ikulu ya Msitu wa Lebanoni.
\s5
\v 17 Kisha mfalme atengeneza kiti cha enzi kikubwa cha pembe na kufunika kwa dhahabu safi.
\v 18 Kulikuwa na ngazi sita kwenda kwenye kiti cha enzi, na sehemu ya juu ya kiti cha enzi ilikuwa duara. Kulikuwa na mikono kila upande wa kiti, na simba wawili wamesimama pembeni na hiyo mikono.
\s5
\v 19 Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita.
\v 20 Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Selemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Selemani.
\v 21 Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.
\s5
\v 22 Kwa hiyo Mfalme Selemani aliawazidi utajiri na hekima wafalme wote wa dunia.
\v 23 Dunia yote waliutafuta uwepo wa Selemanai ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.
\v 24 Waliomtembelea walileta kodi, vyombo vya shaba na dhahabu, nguo, silaha, na manukato, na farasi na anyumbu, mwaka baada ya mwaka.
\s5
\v 25 Selemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.
\v 26 Akatawala juu ya wafalme wote kutoka mto Efrati hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misiri.
\s5
\v 27 Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya aridhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini.
\v 28 Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Selemani.
\v 29 Kwa mambo mengine kuhusu Selemani, mwanzo na mwisho, hayajandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati?
\v 30 Selemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
\v 31 Akalala na babu zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa maana Isaraeli wote walikuwa wanakauja Shekemu kwa ajili ya kumfanya yeye mfalme.
\v 2 Ikatokea kwamba Yeroboamu mwana wa Nebati akasikia haya (kwa maana alikuwa katika Misiri, ambako alikuw amekimbilia kutoka kwenye uwepo wa Mfalme Selemanai, lakini Yeroboamu akarudi kutoka Misiri).
\s5
\v 3 Kwa hiyo wakatuma na kumuita yeye, na Yeroboamu na Israeli wote wakaja; wakamwambia Rehoboamu na kusema,
\v 4 "Baba yako aliifanya nira yetu ngumu. Kwa hiyo sasa, ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa rahisi, na ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu, na sisi tutakutumikia wewe."
\v 5 Rehoboamu akawaambia, "Njoni kwangu tena baada ya siku tatu." Kwa hiyo watu wakaondoka.
\s5
\v 6 Mfalme Rehoboamu akaomba ushauri kwa wazee ambao walikuwa wamesimama mbele ya Selemani baba yake wakati alipokuwa hai; akasema, Mnanishauri niwape jibu gani watu hawa?"
\v 7 Wakasema kwake, Ikiwa wewe ni mwema kwa watu hawa na uwapendeze, na sema maneno mazuri kwao, basi siku zote watakuwa watumishi wako."
\s5
\v 8 Lakini Rehoboamu akapuuza ushauri wa wazee ambao walimpa, na akashauriana na wanauame vijana ambao walikuwa wa rika lake, ambao walisimama mbele yake.
\v 9 Akawaamabia, "Mnanipa ushauri gani, ili kwamba niwajibu watu waliozungumza kwangu na kusema, "Ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu'?"
\s5
\v 10 Wanaume vijana mabaoa walikuwa rika la Yeroboamu wakasema kwake, wakisema, "Hivi ndivyo utakavyosema kwa watu waliokuambia kwamba baba yako Selemani aliifanya nira yao nzito, lakini kwamba lazima uifanye nyepesi. Hivi ndivyo utakavyosema kwao, 'Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
\v 11 Kwa hiyo sasa, ingawa babab yangu aliwatwika nira nzito, nitaiongeza nira yenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini nitawaadhibu kwa nge."
\s5
\v 12 Kwa hiyo Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu katika siku ya tatu, kama aliavyosema mfalme, "Rudini kwangu katika siku ya tatu,"
\v 13 Yeroboamu akasema kwa kwao kwa ukatili, akiupuuza aushauri wa wazee.
\v 14 Akasema kwao akiufuata ushauri wa wanaume vijana, akisema, " Baba yangu aliifanya nira yenu nzito, lakini mimi nitaiongeza. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge."
\s5
\v 15 Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa lilikuw tukio lililoletwa na Mungu, kwamba Yahwe aweze kulitimiza neno lake ambalo Ahiya Mshiloni alikuwa amemwambia Yeroboamu mwana wa Nebati.
\s5
\v 16 Israeli wote, walipoona kwamba mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu na kusema, "Tunasehemu gani katika Daudi? Hatuna urith katika wana wa Yese! Kila mmoja wenu anapaswa kwenda katika hema yake, Israeli. Sasa kila mtu aone nyumba yake, Daudi." Kwa hiyo Israeli wote wakarudi kwenye hema zao.
\v 17 Lakini kwa watu wa Yuda walioishi katika miji ya Yuda, Yeroboamu akatawala juu yao.
\v 18 Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, ambaye alikuwa msimamizi wa wafanya kazi, lakini watu wa Israeli walimuua kwa kumpiga mawe. Mfalame Rehoboamu akaingia haraka ndani ya gari lake kwenda Yerusalemu.
\v 19 Kwa hiyo Israeli wakawa waasi dhidi ya nyumba ya Mungu hadi leo.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Rehoroboamu alipofiki Yerusalemu, akawakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, wanaume 180, 000 walaiaochaguliwa amabao wliakuwa wanajeshi, kwa ajili ya kupigana dhiidi ya Israeli, ili kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu.
\s5
\v 2 Lakini neno la Yahwe likamjia Shemaya mtu wa Mungu, likisema,
\v 3 "Sema kwa Rehoboamu mwana wa Selemani, mfalme wa Yuda, na kwa Israeli kataika Yuda na Benyamaini,
\v 4 Yahwe anasema hivi, "Msivamie wala kufanya vita dhidi ya ndugu zako. Kila mmoja lazima arudi kwenye nyumba yake, kwa maana nimesababisha jambo hili kutokea." Kwa hiyo wakayatii maneno ya Yahwe na kuacha kumvamia Yeroboamu.
\s5
\v 5 Yeroboamu akaishi katika Yerusalemu na kujenga miji katika Yuda kwa ajili ya kujilinda.
\v 6 Akaijenga Bethelehemu, EtamuTekoa,
\v 7 Bethsusi, Soko, Adulamu,
\v 8 Gathi, Maresha, Zifu,
\v 9 Adoraimu, Lakishi, Azeka,
\v 10 Sora, Aiyaloni, na Hebroni. Hii ni miji yenye ngome katika Yuda na Benyamini.
\s5
\v 11 Akaziimarisha ngome na kuweka maamri jeshsi ndani yake, pamaoja na hazina ya chakula, mafuta, na divai.
\v 12 Akaweka ngao na mikuki katika miji yote na kuifanya imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benyamini zikawa zake.
\s5
\v 13 Makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote wakaenda kwake kutoka ndani ya mipaka yao.
\v 14 Kwa kuwa Walawi waliacha nchi za malisho yao na mali zao ili kuja Yuda na Yerusalemu, kwa maana
\v 15 Yeroboamu na wanaaye walikuwa wamewafukuza, ili kwamba wasifanye majukumu yao ya kikuhani kwa ajili ya sehemu za juu na mbuzi na sanamu za ndama alizokuwa ametengeneza.
\s5
\v 16 Watu kutoka kabila zote za Israeli wakaja nyuma yao, wale walio wameiilekeza mioyo yao kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli; wakaja Yerusalemu kwa ajili ya kumtolea dhabihu Yahwe. Mungu wa baba zao.
\v 17 Kwa hiyo wakauimarisha ufalame wa Yuda na kumfanya imara Rehoboamu mwana wa Selemani kwa miaka mitatu, na wakatembea kwa miaka mitatu katika njia ya Daudi na Selemani.
\s5
\v 18 Rehoboamu akajitwalia mke: Mahalathi, binti wa Yerimothi, mwana wa Daudi na wa Abihaili, binti wa Eliabu, mwana wa Yese.
\v 19 Akamzalia wana: Yeushi, Shemaraia, na Zahamu.
\s5
\v 20 Baaad ya Mahalathi, Rehoboamu akamchukua Maaka, binti Absalomu; akamzalia Abiya, Atai, Ziza, na Shelomithi.
\v 21 Rehoboamu akampenda Maaka, binti Solomoni, zaidi kuliko wake za wengine wote na masuria (alichukua wake kumi na nane na masuria sitini, na akawa baba wa wana ishirini na nane na mabinti sitini).
\s5
\v 22 Rehoboamu akamteua Abiya mwana wa Maaka kuwa mkuu, kiongozi miongoni mwa ndugu zake alikuwa na wazo la kumfanya mfalme.
\v 23 Rehoboamu akatawala kwa hekima; akawatawanya wanaye katika nchi yote ya Yuda na Benyamini katika kila mji imara. Pia akawapa chakula kwa wingi na akatafuta wake wengi kwa ajili yao.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Ikawa kwamba, Rehoboamu alipokuwa ameimarishwa na mwenye nguvu, kwamba akaikataa sheria ya Yahwe--na Waisraeli wote pamoja naye.
\s5
\v 2 Ilitokea katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu, kwamba, Shishaki, mfalme wa Israeli, akaja kinyume na Yerusalelemu, kwa sababu watu walikuwa wameacha kuwa waaminifu kwa Yahwe.
\v 3 Akaja na magari elfu moja na mia mbili pamoja naye na wapand farasi elfu sitini. Askari wasio hesabika wakaja pamaoja naye kutoka Misri: Walubi, Wasukii, na Waethiopia.
\v 4 Akaiteka miji yenye ngome ya Yuda na akaja Yerusalemu.
\s5
\v 5 Sasa Shemaya nabii akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda ambao walikuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki. Shemaya akasema kwao, "Hivi ndivyo anavyosema Yahwe: Mmenisahau, kwa hiyo pia nimewaweka katika mkono wa Shishaki".
\v 6 Kisha wakuu wa Israeli na mfalme wakajinyenyekeza na kusema, "Yahwe ni mtakatifu."
\s5
\v 7 Yaahwe alipoona kuwa wamejinyenyekeza, neno la Yahwe likamjia Shemaya, likisema, "Wamejinyenyekeza. Stawaadhibu; nitawaokoa kwa hataua fulani, na hasira yangu haitamiminwa juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.
\v 8 Vile vile, watakuwa watumishi wake, ili kwamba wajue nini maana ya kunitumikia mimi na kuwatumikia watawala wa nchi zingine."
\s5
\v 9 Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Selemani. Mfalme
\v 10 Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikoni mwa maamrijeshi wa walinzi, amabao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme.
\s5
\v 11 Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi.
\v 12 Rehoboamu alipojinyenyekeza mwenyewe, ghadhabu ya Yahwe ikampisha mbali, kwa hiyo hakumwangamiza kabisa kabisa; pembeni, bado kulikuwa na baadhi ya wema wa kupatikana katika Yuda.
\s5
\v 13 Hivyo mfalme Rehoboamu akafanya ufalme wake imara katika Yerusalemu, na kwa hiyo akatawala. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka aroabaini na moja alipoanza kutawala, na akatawala kwa muda wa mika kumi na saba katika Yerusalemu, mji ambao Yahwe alikuwa ameuchagua kutoka kwa makabila ya Israeli ili kwamba aliweke jina lake humo. Jina lake aliitwa Naama, Mwamoni.
\v 14 Akafanya yaliyokuwa uovu, kwa sababu hakuuelekeza moyo wake kumtafuta Yahwe.
\v 15 Kwa mambo mengine kuhusu Rehoboamu, mwanzo na mwisho, hayakuandikwa katika maandishi ya Shemaya nabii na ya Ido mwonaji, ambayo pia yana kumbukumbu ya vizazi na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu?
\v 16 Rehoboamu akalala pamoja na babu zake na alizikwa katika mji wa Daudi; Abiya mwanye akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yeroboamu, Abiya akaanza kutawala juu ya Yuda.
\v 2 Akatawala kwa miaka mitatu katika Yerusalemu; jina la mama yake aliitwa Maaka, binti wa Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
\v 3 Abiya akaingia vitani na jeshi la askari, wenye nguvu, hodari, 400, 00 wanaume waliochaguliwa. Yeroboamu akapanga mistari ya vita dhidi yake yenye 800, 00 wanaume askari waliochaguliwa, wenye nguvu, hodari.
\s5
\v 4 Abiya akasimama juu ya mlima Semaraimu, uliopo katika kilima cha nchi ya Efraimu, na akasema, "Nisikilizeni, Yeroboamu na Israeli wote!
\v 5 Hamjui kwamba Yahwe, Mungu wa Israeli, alitoa sheria juu ya Israeli kwa Daudi milele, kwake na kwa wanaye kwa agano rasimi?
\s5
\v 6 Bado Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumishi wa Selemani mwana wa Daudi, akainuka na kuasi dhidi ya bwana wake.
\v 7 Watu wabaya, washirika wa karibu, wakamkusanyikia, wakamjia kinyume Rehoboamu mwana wa Selemani, wakati Rehoboamu alipokuwa mdogo na asiye na uzoefu na hakuweza kuwamudu.
\s5
\v 8 Sasa mnasema kwamba mnaweza kuuzuia utawala wa Yahwe wenye nguvu katika mkono wa uzao wa Daudi. Ninyi ni jeshsi kubwa, na pamoja nanyi kuna ndama wa dhahabu ambao Yeroboamu alitengeneza kama miungu kwa ajili yenu.
\v 9 Hamkuwafukuza nje makuhani wa Yahwe, uzao wa Haruni, na Walawi? Hamkujifanyia makuhani katika namna ya watu wa nchi zingine? Yeyote ajaye kujitakasa mwenyewe na ngo'mbe dume kijana, na madume ya kondoo anaweza kuwa kuhani wa kile ambacho siyo miungu.
\s5
\v 10 Lakini kwetu, Yahwe ni Mungu wetu, na hatujamsahau. Tuna makuhani, uzao wa Haruni, wakimtumikia Yahwe, na Walawi, ambao wako kataika kazi yao.
\v 11 Kila asubuhi na jioni humtolea Yahwe sadaka za kuteketezwa na uvumba mtamu. Pia hupanga mkate wa uwepo juu ya meza takatifu; pia huweka kinara cha dhahabu pamoaja na taa zake, ili watoe sadaka kila jioni. sisi huzishika sheria za Yahwe, Mungu wetu, Lakini ninyi mmemsahau.
\s5
\v 12 Ona, Mungu yuko pamoja nasi katika vichwa vyetu, na makuhani wake wako hapa na tarumbeta kwa ajili ya kutoa sauti dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane na Yahwe, Mungu wa babu zenu, kwa maana hamtafanikiwa."
\s5
\v 13 Lakini Yeroboamu akaandaa mavamizi nyuma yao; jeshi lake lilikuwa mbele ya Yuda, na wavamizi nyuma yao.
\v 14 Yuda walipoanagalia nyuma, tanzama, mapigano yalikuwa pote mbele na nyuma yao. Wakamlilia Yahwe kwa sauti, na makuhani wakayapuliza matarumbeta.
\v 15 Kisha wanaume wa Yuda wakapiga kelele; walipopiga kele, ikawa kwamba Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.
\s5
\v 16 Watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda, na akawatia kwenye mkono wa Yuda.
\v 17 Abiya na jeshi lake wakawaua kwa mauji makuu; 500, 000 watu wanaume waliochaguliwa wa Israeli wakaanguka wamekufa.
\v 18 Katika namna hii hii, watu wa Israeli wakatiishwa chini wakati huo, watu wa Yuda wakashinda kwa sababu walimtegemea Yahwe, Mungu wa babu zao.
\v 19 Abiya akamshawishi Yeroboamu; akachukua miji kutoka kwake; Betheli pamoja na vijiji vyake, Yeshana pamoja na vijiji vyake, na Efroni pamoaaja na vijij vyake.
\v 20 Yeroboamu hakupata naguvu tena katika siku za Abiya; Yahwe akampiga, na akafa.
\v 21 Lakini Abiya akawa na nguvu sana; akachukua wanawake kumi na nne kwa ajili yake na akawa baba wa wana ishirini na mbili na mabinti kumi na sita.
\v 22 Matendo ya Abiya yaliyosalia, tabia yake na maneno yake yameeandikwa katika kamusi ya nabii Ido.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Abiya kalala pamoja na babu zake, na wakamzika kataika maji wa Daudi. Asa, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Katika siku yake nchi ilikuwa na miaka kumi.
\v 2 Asa alifanya yaliyomema na sahihi katika macho ya Yahwe Mungu wake,
\v 3 kwa maana aliziondosha mbali madhabahu za kigeni na sehemu za juu. Akaziangusha chini nguzo za mawe na kuzikata nguzo za Maashera.
\v 4 Akawaamuru Yuda kumtafuta Yahwe, Mungu wa babu zao, na kuzishika sheria na amri.
\s5
\v 5 Pia akaziondosha mbali sehemu za juu na madhabahu za kufukiza kutoka miji yote ya Yuda. Ufalme ulikuwa na pumziko chini yake.
\v 6 Akajenga miji ya ngome katika Yuda, kwa maana nchi ilikuwa tulivu, na hakuwa na vita katika miaka hiyo, kwa sababu Yahwe alikuwa amempa amani.
\s5
\v 7 Kwa maana Asa aliwaambia Yuda, "Tuijenge miji hii na kuizungushia kuta, na minara, mageti, na makomeo; nchi bado yetu kwa sababu tumemtafuta Yahwe Mungu wetu. Tumemtafuta yeye, na ametupa amani katika kila upande." Kwa hiyo walijenga na wakafanikiwa.
\v 8 Asa alikuwa na jeshi ambalo lilibeba ngao na mikuki; kutoka Yuda alikuwa na wanaume 300, 000, na kutoka Benyamini, wanaume 280, 000 waliobeba ngao na kuvuta pinde.
\s5
\v 9 Zera Mwethiopia akaja juu yao na jeshi la wanajeshi milioni moja na magari mia tatu; akaja Maresha.
\v 10 Kisha Asa akatoka nje kukutana naye, na wakapanga mistari ya vita ya mapigano katika bonde la Sefatha huko Maresha.
\v 11 Asa kamlilia Yahwe, Mungu wake,, na akasema, "Yahwe, hakuna aliye kama wewe lakini ni wewe wa kumsaidia mtu asiye na nguvu anapokutana na mengi. Tusaidie, Yahwe, Mungu wetu, kwa maana tunakutegemea wewe, na katika jina lako tumekuja kupambana na idadi hii kubwa ya adui. Yahwe, wewe ni Mungu wetu; usimuache mtu akushinde."
\s5
\v 12 Kwa hiyo Yahwe akawapiga Waethiopia mbele za ASa na Yuda; Waethiopia wakakimbia.
\v 13 Asa pamoja na wanajeshi waliokuwa pamoja naye wakawafukuza hadi Gerari. Kwa hiyo Waethiopia wengi wakajeruhiwa kiasi kwamba hawakuweza kupona, kwa maana waliangamizwa kabisa mbele za Yahwe na jeshi lake. Jeshsi likachukua mateka wengi sana.
\v 14 Jeshi likaviangamiza vijiji vyote jirani na Garari, kwa kuwa hofu ya Yahwe ilikuwa imekuja juu ya wakaaji. Jeshi likateka vijiji vyote, na vilikuwa na hazina nyingi sana ndani yake.
\v 15 Jeshi pia likaipiga hema ya makazi yawachungaji; wakabeba kondoo kwa wingi, ngamia vile vile, na kisha wakarudi Yerusalemu.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Roho ya Mungu ikaja juu ya Azaria mwana wa Odedi.
\v 2 Akaenda nje kukutana na Asa na akamwambia, "Nisikilize, Asa, na Yuda wote na Benyamini: Yahwe yuko pamoja nanyi, pale mnapokuwa naye. Kama mtamtafuta, mtampata; lakini kama mtamsahau, atawasahau ninyi.
\s5
\v 3 Sasa kwa muda mrefu, Israeli hawakuwa na Mungu wa kweli, bila kuhani wa kufundisha, na bila sheria.
\v 4 Lakini katika dhiki yao wakamrudia Yahwe, Mungu wa Israeli, na wakamtafuta, wakamta.
\v 5 Katika nyakati hizo hapakuwa na amani kwake aliyesafiri kwend mbali, wala kwake aliyesafiri kuja hapa; badala yake shsida kubwa zilikuwa juu ya wenyeji wote wa wanchi.
\s5
\v 6 Waligawanyika vikundi vikundi, taifa dhidi ya taifa, na mji dhidi ya mji, kwa maana Mungu aliwapa shsida za kila aina ya kila mateso.
\v 7 Lakini muwe hodari, na msiuache mkono wenu kuwa dhaifu, kwa maana kazi yen itapewa thawabu."
\s5
\v 8 Asa aliposikia maneno haya, unabii wa odedi nabii, akajipa ujasiri na kuviondosha mbali vitu vya kuchukiza kutoka nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji yote aliyokuwa ameiteka kuanzia kilima cha nchi ya Efraimu, na akaijenga tena madhabahu ya Yahwe, ambayo ilikuwa mbele ya ukumbi wa nyumba ya Yahwe.
\v 9 Akawakusanya Yuda wote na Benyamini, na wae waliokaa pamoja nao—watu wa kutoka Efraimu na Manase, na kutoka Simeoni. Kwa maana walikuja kwake katika hesabu kubwa kutoka Israeli, walipoona kwamba Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye.
\s5
\v 10 Kwa hiyo wakakusanyika katika Yerusalemu katika mwezzi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa.
\v 11 Katika siku hiyo walimtolea Yahwe dhabihu baadhi ya nyara ambazo walikuwa wameleta; ng'mbe wa kulima mia saba na kondoo na mbuzi elfu saba.
\s5
\v 12 Wakaingia kataika agano kwa ajili ya kumtafuta Yahwe, Mungu wa babau zao, kwa moyo wao wote na roho yao yote.
\v 13 Wakakubaliana kwamba yeyote atakepuuzia kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli, atapaswa kuuawa, iwe mdogo ama mkubwa, iwe mwanaume ama mwanamke.
\s5
\v 14 Wakaapa kwa Yahwe kwa sauti kubwa, kwa kelele, na kwa sauti za tarumbeta na baragumu.
\v 15 Yuda wote wakakifurahia kile kiaapo. kwa maana walikuwa wameapa kwa moyo wao wote, na walimtafuta Mungu kwa nia yao yote, na walimuona. Yahwe akawapa amani pande zote.
\s5
\v 16 Pia akamwondoa Maaka, asiwe malikia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza ya Maashera. Asa akaivunja vunja sanamu ya kuchukiza, akaiweka kwenye mavumbi akaichoma moto huko kijitoni Kidroni.
\v 17 Lakini sehemu za juu hazikuwa zimeondolewa nje ya Israeli. Vile vile, Moyo wa Asa ulijitoa kikamilifu siku zake zote.
\v 18 Akaleta kwenye nyumba ya Mungu vitu vya baba yake na vitu vyake mwenyewe vilivyokuwa vya Yahwe: vitu vya fedha na dhahabu.
\v 19 Hapakuwa na vita zaidi hadi miaka thelathini na mitano ya utawala wa Asa.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, akatenda kwa ukatili dhidi ya Yuda na akaujenga Rama, ili kwamba asimruhusu mtu yeyote kutoka wala kuingia katika nchi ya Asa, mfalme wa Yuda..
\s5
\v 2 Kisha Asa akaitoa fedha na dhahabu nje ya vyumba vya kuhifadhia katika nyumba ya Yahwe na nje ya nyumba ya mfalme, na akaituma kwa Ben Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye aliishi Dameski. Akasema, pawe na agano kati yako na mimi, kama palivyokuwa na agano kati ya baba yangu na baba yako. Angalia, nimekutumia fedha na dhahabu.
\v 3 Livunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache."
\s5
\v 4 Ben Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma maakida wa majeshsi dhidi ya miji ya Israeli. Wakavamia Iyoni, Dani, Abelimaimu, na miji yoye ya kuhifadhia ya Naftali.
\v 5 Ikawa kwamba Baasha aliposikia hili, akaacha kuujenga Rama, na akaistisha kazi yake.
\v 6 Kisha Asa mfalme akawachukua Yuda wote pamoja naye. Wakayabeba mawe na mbao za Rama ambazo Baasha alikuwa anajengea ule mji. Kisha Mfalme Asa alitumia vifaa hivyo vya ujenzi kwa ajili ya kuijenga Gaba na Mispa.
\s5
\v 7 Wakati huo Hanani mwonaji akaenda kwa Asa, mfalme wa Yuda, na akamwambia, "Kwa sababu umemtegemea mfalme wa Aramu, na hukumtegemea Yahwe Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limetoroka nje ya mikono yako.
\v 8 Waethiopia na Walubi hawakuwa jesi kubwa, wenye magari mengi na wapanda farasi wengi? Na bado, kwa sababau ulimtegemea Yahwe, alikupa ushindi juu yao.
\s5
\v 9 Kwa maana macho ya Yahwe hukimbia kila mahali katika dunia yote, ili kwamba ajioneshe mwenyewe shujaa kwa niaba ya wale amabao mioyo yao ni mikamilifu kumwelekea yeye. Lakini umetenda kipumbavu katika jambo hili. Kwa maana tangu sasa na kuendelea, utakuwa na vita." Kisha Asa akamkasirikia mwonaji, akamuweka gerezani, kwa maana alikuwa na hasira naye juu ya jambao
\v 10 hili. Wakati huo huo, aliwagandamiza baadhi ya watu
\s5
\v 11 Tazma, matendo ya Asa, kutoka mwanzo hadi mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\v 12 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipata ugnjwa kwenye miguu yake; ugonjwa wake ulikuwa mkali sana. Hata hivyo, hakutafuta msaada kutoka kwa Yahwe, lakini kutoka kwa waganga tu.
\s5
\v 13 Asa akalala pamoja na babu zake; alikufa katika mwaka wa arobaiani na moja wa utawala wake. Wakamzika katika kaburi lake, ambalo alilichimba mwenyewe katika mji wa Daudi.
\v 14 Walimlaza juu ya kitanda kilichokuwa kimewekewa manukato na aina mbali mbali ya dawa zilizotayarishwa na wale mafundi wa manukato. KIsha wakatengeneza moto kwa heshima yake.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoshafati akajiimarisha dhidi ya Israeli.
\v 2 Akaweka majeshi katika miji yote Yuda yenye ngome, na akaweka magereza katika nchi ya Yuda na katika miji ya Efraimu, ambayo Asa baba yake alikuwa ameiteka.
\s5
\v 3 Yahwe alikuwa pamoja na Yehoshafati kwa sababu alitembea katika njia za kwanza za baba yake Daudi, na hakuwatafuta Mabaali. (Baadhi ya mandiko ya kale hayana "Daudi", na baadhi ya matoleo ya kisasa yameacha hili jina "Daudi).
\v 4 Badala yake, alimtegemea Mungu wa baba yake, na alitembea katika amri zake, siyo katika tabia ya Israeli.
\s5
\v 5 Kwa hiyo Yahwe akaimarisha sheria katika mkono wake; Yuda wote wakaleta kodi kwa Yehoshafati. Alikuwa na utajiri na heshima kubwa.
\v 6 Moyo wake ulikuwa umejikita katika njia za Yahwe. Pia aliziondoa sehemu za juu na Maashera mbali na Yuda.
\s5
\v 7 Katika mwaka wa tatu wa utawala wake aliwatuma wakuu wake Ben-haili, Obadia, Zekaria, Nethania, na Mikaya, ili wafundishe katika miji ya Yuda.
\v 8 Pamoja nao walikuwepo Walawi: Shemaya, Nethanieli, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, na Tob-adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu.
\v 9 Walifundisha katika Yuda, wakiwa na kitabau cha sheria ya Yahwe. Wakaenda karibu miji yote ya Yuda na kufundisha miongoni mwa watu.
\s5
\v 10 Hofu ya Yahwe ikashuka juu ya falme zote za nchi, zilizouzunguka Yuda, kwa hiyo hazikufanya vita dhidi ya Yehoshafati.
\v 11 Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi, fedha kama kodi. Waarabu pia wakamletea makundi, 7, 700 kondoo waume, na mbuzi 7, 770.
\s5
\v 12 Yehoshafati akawa na nguvu sana.
\v 13 Akajenga ngome na miji ya maghala katika Yuda. Alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda, na wanajeshsi—imara, wanaume hodari—katika Yerusalemu.
\s5
\v 14 Hapa ni rodha yao, wamepangwa kwa majina ya nyumba za baba zo: Kutoka Yuda, maakida wa maelfu; Adna yule jemedari, na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 300, 000;
\v 15 akifuatiwa na Yehonani jemedari, na pamoja naye wanaume 280, 00;
\v 16 akifuatiwa na Amasia mwana wa Zikri, ambaye kwa hiari alijitoa kumtumikia Yahwe; na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 200, 000.
\v 17 Kutoka Benyamini: Eliada mtu jasiri, na pamoja naye watu 200, 000 waliovaa upinde na ngao;
\v 18 akifutiwa na Yehozabadi, na pamoja naye askari 180, 000 waliotayari kwa vita.
\v 19 Hawa walikuwa ni wale ambao walimtumikia mfalme, miongoni mwao wale ambao mfalme aliwaweka katika miji ya ngome katika Yuda yote.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Sasa Yehoshafati alikauwa na utajiri mwingi na heshima kubwa; alifanya undugu na Ahabu mmoja wa watu wa familia yake akamuo binti yake.
\v 2 Baada ya miaka kadhaa, akashsuka chini kwa Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja kondoo na ngo'mbe wengi kwa ajili ya yake na watu waliokuwa pamoja naye. Ahabu pia akamshawishi kuivamia Ramothi-gileadi pamoja naye.
\v 3 Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, "Utakwenda Ramothi-gileadi pamoja nami?" Yehoshafati akamjibu, "Mimi ni kama wewe, na watu wangu ni kama watu wako; tutakuwa pamoja nawe katika vita."
\s5
\v 4 Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Tafadhali litafute neno la Yahwe kwanza kwa ajili ya jibu lako"
\v 5 Kisha mfale wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, wanauame mia nne, na akasema akwao, Tutaenda vitani Ramothi-gileadi, au nisiende?" Wakasema, "Vamia, kwa maana Mungu ataitia mkononi mwa mfalme."
\s5
\v 6 Lakini Yehoshafati akasema, "Hakuna nabii mwingine hapa wa Yahwe ambaye kwake tunapaswa kutafuta ushauri?"
\v 7 Mfale wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Bado kuna mtu mmoja amabaye kwake lazima tuutafute ushauri wa Yahwe, Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu yeye huwa hatabiri mema kamwe kuhusu mimi, bali kila mara maovu," Lakini Yehoshafati akasema, " Mfalme hapaswi kusema hivyo."
\v 8 Kisha mfalme wa Israeli akamwita akida na kusema, Haraka mlete Mikaya mwana wa Imla."
\s5
\v 9 Sasa Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mmoja katika kiti cha enzi, wamevalia kanzu zao, katika sehemu ya uwazi katika maingilia ya lango la Samaria, na manabii wote walikuwa wakitabairi mbele zao.
\v 10 Zedekia mwana wa Kenaani akajitengenezea pembe za chuma na kusema, Yahwe anasema hivi: Kwa kutumia hizi pembe mtawasukuma Waaramu hadi waangamie."
\v 11 Manabii wote wakatabiri kitu kile kile, wakisema, "Vamia Raamothi-gleadi na shinda. kwa maana Yahwe ameutia kwenye mkono wa mfalme."
\s5
\v 12 Mjumbe aliyeenda kumuita Mikaya akasema kwake, akisema, "Sasa angalia, maneno ya manabii yanatangaza mambo mema kwa ajili ya mfalme kwa kinywa kimoja. Tafadhali maneno yako yawe kama maneno ya mmoja wao na sema mambo mema."
\v 13 Mikaya akajibu, "Kama Yahwe aishivyo, mimi nitasema kile mbacho Mungu anasema."
\v 14 Alipokuja kwa mfalme, mfamle akamwambaia, "Mikaya, tutaenda Ramothi -gileadi kwa ajili ya vita, au la?" Mikaya akamjibu, "Vamia na utashinda! kwa maana utakuwa ushinda mkuu."
\s5
\v 15 Kisha mfalme akasema kwake, "Ni mara ngapi ninapaswa kukutaka kuapa kutoniambia kitu chochote sispokuwa kweli katika jina la Yahwe?
\v 16 Kwa hiyo Mikaya akasema, "Niliwaoana Israeli wametawanyika ktika mlima, kama kondoo wasio na mchungaji, na Yahwe akasema, hawa hawana mchungaji. Ebu kila mtu arudi nyumbani kwake kwa amani."
\s5
\v 17 Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, "Sikukuambia kwamba asingeweza kutabiri mema juu yangu, bali majanga tu?
\v 18 Kisha Mikaya akasema, "Kwa hiyo ninyi nyote mnapashwa kulisikia neno la Yahwe: Nilimuon Yahwe amekaa juu ya kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikauwa yamekaa mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto.
\s5
\v 19 Yahwe akasema, Ni nani atakayemrubuni Ahabu, mfalme wa Israeli, ili kwamba aende na kuanguka huko Ramothi-gileadi?' Mmoja alisema hivi na mwingine hivi.
\s5
\v 20 Kisha roho ikaja moja kwa maja na kusimama mbele ya Yahwe na kusema, 'Nitamrubuni.' Yahwe akamwambia, 'Kivipi?'
\v 21 Roho ikajibu, "nitatoka nje na nitakuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.' Yahwe akajibu, 'utamrubuni, na pia utafanikiwa. nenda sasa na fanya hivyo.'
\s5
\v 22 Sasa ona, Yahwe ameweka roho ya uongo katika midomo ya manabii wako hawa, na Yahwe ametangaza majanga kwa ajili yako."
\s5
\v 23 Kisha Zedekia mwana wa Kenaana, akaja, akampiga kofi mika juu ya shavu, na kusema, "Kwa njia gani Roho wa Yahwe alitoka kwangu ili aseme nawe?"
\v 24 Mika akasema, Angalia, utalijua hilo katika siku hiyo, mtakapokimbia katika baadhi ya vyumba vya ndani kwa ajili ya kujificha."
\s5
\v 25 Mfalme wa Israeli akasema kwa baadhi ya watumishi, " Enyi watu mkamateni Mikaya na mmpeleke hadi Amoni, mkuu wa mji na, na kwa Yoashi, mwanangu.
\v 26 Nanyi mtamwambia, 'Mfalme anasema: Mweke gerezanai huyu mtu na umlishe kwa mkate kiogo tu na maji kidogo tu, mpaka nitakaporudi salama."
\v 27 Kisha Mikaya akasema, "Kama utarudi salama, Yahwe hajasema nami."Kisha akaongeza, "Sikiliza haya, enyi watu wote."
\s5
\v 28 Kwa hiyo Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, mfalme wa Yuda, wakaenda juu ya Ramothi-giledi.
\v 29 Mfalme wa Israeli akamwamabia Yehoshafati, "Nitajibadilisha mwenyewe na kwenda vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme." Kwa hiyo mfalame wa Israeli akajibalisha, na wakaenda vitani.
\v 30 Sasa mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msiwavamie wanajeshsi wasio wa muhimu wala wanajeshsi muhimu. Badala yake, mvamieni mfalme wa Israeli pekee,"
\s5
\v 31 Ikawa kwamba maakida wa magari walipomuona Yehoshafati wakasema, "Yule ni mfalme wa Israeli." Wakageka kumzunguka wamvamie, lakini Yehoshafati akalia, na Yahwe akamsaidia. Mungu akawageza nyuma kutoka kwake.
\v 32 Ikawa kwamba maakida wa magari walipoona ya kuwa hakuwa mfalme wa Israeli, wakarudi nyuma wasimfukuze.
\s5
\v 33 Lakini mtu mmoja akauvuta upinde wake kwa kubahatisha na kumpiga mfalme wa Israeli kati kati ya maungio ya mavazi yake. Kisha Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, "Geuza nyuma na nitoe nje ya mapigano, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana."
\v 34 Mapigano yakazidi kuwa makali siku hiyo, na mfalme wa israeli akashikiliwa katika gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Muda jua lilipokaria kwenda chini, akafa.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi salama nyumbani kwake Yerusalemu.
\v 2 Kisha Yehu mwana wa Hanani, mwonaji, akatoka kukutana naye na akasema kwa mfalme Yehoshafati, "Unapaswa kuwa unawasaidia waovu? Unapaswa kuwapenda wanaomchukia Yahwe? Kwa ajili ya tendo hili, ghadhabu toka kwa Yahwe iko juu yako.
\v 3 Aidha, kuna baadhi ya mema ya kuonekana ndani yako, kwamba umeziondosha Maashera nje ya nchi, na umeukaza moyo wako kumtafuta Mungu."
\s5
\v 4 Yehoshafati akaishi katika Yerusalemu; na akaenda nje tena miongoni mwa watu wa Beer- sheba hadi nchi ya kilima ya Efraimu na akawarudisha kwa Yahwe, Mungu wa baba zao.
\v 5 Akaweka waamuzi katika nchi katika miji yote ya Yuda yenye angome, mji kwa mji.
\s5
\v 6 Akawaambia waamuzi, "Zingatieni mnachopaswa kufanya, kwa sababu hamuamui kwa ajili ya mwanadamu, bali kwa ajili ya Yahwe; yuko pamoja nanyi katika kazi ya kuamua,
\v 7 Basi sas iacheni hofu ya Mungu iwe juu yenu. Iweni waangaliafu mnapoamua, kwa maana hakuna uovu wa Yahwe Mungu wetu, wala hakuna upendeleo wala hongo."
\s5
\v 8 Vile vile, katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na baahdhi ya viongozi wa nyumba za mababu wa Israeli, kwa ajili ya kufanya hukumu kwa ajili ya Yahwe, na kwa ajili ya migogoro. Wakaishi katika Yerusalemu.
\v 9 Akawaelekeza, akisema, "Lazima mtumike kwa heshima kwa ajaili ya Yahwe, kwa uaminifu, na na kwa moyo wenu wote.
\s5
\v 10 Kila mgogoro wowote utakapokuja kwenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji yao, iwe inahusu mauji, iwe inhusu torati na amri, lazim muwaonye, ili kwamba wasiwe na hatia mbele za Yahwe, la sivyo ghadhabu itakuja juu yenu na juu ya ndugu zenu. Mnapaswa kufanya hivyo na hamtakuwa na hatia
\s5
\v 11 Ona, Amaria kuhani mkuu yuko juu yenu katika mambo yote ya Yahwe. Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa nyumba ya Yuda, ni kiongozi katika yote katika mambo yote ya mfalme. Pia, Walawi watakuwa wasimamizi wakiwatumikia ninyi. Muwe hodari na tiini maelekezo yenu, na Yahwe awe moja nao walio wema."
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ikawa baada ya hayo, kwamba watu wa Moabu na Amoni, na pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja juu ya Yehoshafati ili kupigana vita. (Mandishi, "baadhi ya Wameuni" yanatoa masahihisho kwa ajili ya maandishi ya Kiebrania, ambayo yanasomeka, "baadhi ya Waamoni". Inadhaniwa kwamba "Wameuni" ndilo neno la asili, na wenye kunukuu walilibadili kuwa "baadhi ya Waamoni". Lakaini jina hili la mwisho halileti maana, kwa sababu Waamoni tayari wamekwisha tajwa katika mstri huu. Vile vile, matoleo tofauti tofauti yanajihusha na tatizo hili katika namna mabli mbali)
\v 2 Kisha baadhi ya watu wakaja wakamwambia Yehoshafati, wakisema, "Umati mkubwa wanakuja juu yako ng'ambo ya Bahari iliyokufa, kutoka Edomu. Ona, wako Hason- tamari", ambayo ndiyo En-gedi. (Badala ya "Edomu" baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasomeka, "Aramu."
\s5
\v 3 Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.
\v 4 Yuda wakakakusanyika pamoja kwa ajili ya kumtafuta Yahwe; wakaja kutoka miji yote ya Yuda kwa ajili ya kumtafauta Yahwe.
\s5
\v 5 Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, kwenye nyumba ya Yahwe, mbele ya kibaraza kipya.
\v 6 Akasema, "Yahwe, Mungu wa babau zetu, hauko mbinguni? Wewe siyo mtawala juu ya falame zote za mataiafa? Nguvu na uweza viko mkononi mwako, kwa hiyao hakuna anayeweza akukupinga wewe.
\v 7 Munagu wetu, Hukuwafuaakuja nje wakaaji wa nchi hii mbe ya watau watau wakop Israeli, na kuitoa milele kwa ajili ya uzaoa wa Abrahamu?
\s5
\v 8 Wakaishi ndani yake na kujenga sehemu takatifu kwa ajili ya jina lako, wakisema,
\v 9 'Ikiwa janga litakuja juu yetu —upanga, hukumu, au ugonjwa, au njaa—tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako (kwa maana jina lako limo ndani ya nyumba hii), na tutakulilia wewe katika mateso yetu, na utatusikia na kutuokoa.' (Badala ya "hukumu" baadhi ya maandiko ya zamani yanasema "mafuriko").
\s5
\v 10 Tazama sasa, hapa kuna watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri ambao hukuwaacha Israeli wawapige waalipotoka nchi ya Misri; badala yake, Israeli waliwageukia mbali na hawakuwaangamiza.
\v 11 Ona jinsi wanavyotuzawadia; wanakuja kutotoa nje ya nchi yako mbayo umetupa kuirithi.
\s5
\v 12 Mungu wetu, hutawahukumu? Kwa maana hatuna nguvu dhidi ya hili jeshi kubwa ambalo linakuja juu yetu. hatujui cha kufanya, lakini macho yetu yako kwako.
\v 13 Yuda wote wakasimama mbele ya Yahwe, pamoja na wadogo wao, wake, na watoto.
\s5
\v 14 Kisha kati kati ya kusanyiko, roho ya Yahwe ikaja juu ya Yahazieli, mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, mwana, Mlawi, mmoja wa wana wa Asafu.
\v 15 Yahazieli akasema, "Sikilizeni, Yuda wote na ninyi wakaaji wa Yerusalemu, na Mfalme Yehoshafati. Hivi ndivyo Yahwe asemavyao kwenu, 'Msiogope: msivunjike moyo kwa sababu ya hili jeshsi kubwa, kwa maana vita siyo yenu, bali ni ya Mungu.
\s5
\v 16 Lazima muende chini juu ya yao kesho, Ona, wanakuja wakipanda kupia njia ya Sisi. Mtawakuta mwishono mwa bondo, mbele ya jangwa la Yerueli.
\v 17 Hamtahitaji kupigana katika vita hii. Simameni katika nafasi zenu, simameni wima, na muone wokovu wa Yahwe pamoja nanyi, Yuda na Yerusalemu. Msiogope wala kukata tamaa. Tokeni nje juu yao kesho, kwa maana yuko pamoja nanyi."
\s5
\v 18 Yehoshafati akainamisha kichwa chake pamaoja na uso wake chini. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakaanguka chini mbele za Yahwe, wakimwabudu yeye.
\v 19 Walawi, wale wa uzao wa Wakohathi na wa uzao wa Wakorahi, wakasimama juu kumsifu Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa sauti kubwa sana.
\s5
\v 20 Asubuhi mapema wakasimama na kwenda nje kwenye bonde la Tekoa. Walipokuwa wakienda nje, Yehoshafati akasimama na kusema, "Nisikilizeni, Yuda, na nnyi wakaaji wa Yerusalemu! Aminini katika Yahwe Mungu wenu, na mtasaidiwa. Aminini katika manabii zake, na mtafanikiwa.
\v 21 Alipokuwa ameshauriana na watu, akawachagaua wale ambao wangemwimbia Yahwe na kumpa sifa kwa ajili ya utukufu wake mtakatifu, walipokuwa wakienda wakilitangulia jeshi, na kusema, "Mshukuruni Yahwe, kwa maana uaminifu wa aganao lake unadumu milele."
\s5
\v 22 Walipoanza kuimba na kusifu, Yahwe akapanga wanaume katika mavamizi juu ya watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri, ambao walikuwa wanakauja dhidi ya Yuda. Walishindwa.
\v 23 Kwa maana watu wa Aamoni na Moabu walisimama kupigana na wakaaji wa Mlima Seiri, ili kuwaua kabisa na kuwangamiza. Waliapokuwa wamemaliza kuwaangamiza wakaaji wa Mlima Seiri, wote wakasaidiana kuangamizana kila mmoja.
\s5
\v 24 Yuda walipokuwa katika sehemu hiyo wakiangalia jangwani, waliangalia nje juu ya jeshi. Tazama, walikuwa wamekufa, wameanguka chini; hakuna aliyekuwa amepona.
\s5
\v 25 Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. (Badala ya "miongoni mwao", baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, "ng'ombe." badala ya "nguo" baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, "miili iliyokufa").
\v 26 Katika siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, Huko wakamsifu Yaahwe, kwa hiyo jina la sehemu hiyo hata leo ni "Bonde la Baraka".
\s5
\v 27 Kisha, wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati katika uongozi wao, kwenda tena Yerusalemu kwa furaha, kwa maana Yahwe alikuwa amewafanya wafurahie juu ya adui zao.
\v 28 Wakaja Yerusalemu na kwenye nyumba ya Yahwe kwa vinanda, vinubi na matarumbeta.
\s5
\v 29 Hofu ya Yahwe ikawa juu ya falme zote za mataifa waliposikia kwamba Yahwe amepigana dhidi ya adui wa Israeli.
\v 30 Kwa hiyo ufaleme wa Yehoshafati ulikuwa mtivu, kwa maana Mungu wake alimpa amani kuzungunga pande zake zote.
\s5
\v 31 Yehoshafati akatawala juu ya Yuda: Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala. Jina la mama yke aliitwa Azubahi, binti wa Shilhi.
\v 32 Akatembea katika njia za Asa, baba yake; hakugeka popote kuziacha; akafanya yaliyo mema katika macaho ya Yahwe.
\v 33 Vile vile, sehemu za juu hazikuwa zimeondoshwa mbali. Watu walikuwa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa babu zao.
\s5
\v 34 Kwa mambo mengine kuhusu Yehoshafati, mwanzo na mwisho, tazama, yameandikwa katika historia ya kitabu cha wafalme wa Israeli.
\s5
\v 35 Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi.
\v 36 Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi.
\v 37 Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, "kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako." Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.
\s5
\c 21
\p
\v 1 Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na akizikwa pamoaja nao katika mji wa Daudi;
\v 2 Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli.
\v 3 Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.
\s5
\v 4 Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongizi wengine mbali mbali wa Israeli.
\v 5 Yehoramu alikuwa na umri wa mika thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu.
\s5
\v 6 Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe.
\v 7 Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake.
\s5
\v 8 Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao.
\v 9 Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake.
\v 10 Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna pia aliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zake.
\s5
\v 11 Zaidi ya hayo, Yehoramu pia alikuwa amezijenga sehemu zake za juu katika milma ya Yuda na akawafanya wakaaji wa Yuda kuishi kama makahaba, na akawaongoza Yuda katika upotevu.
\s5
\v 12 Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda,
\v 13 bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe—
\v 14 ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote.
\v 15 Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa kataika katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku.
\s5
\v 16 Yahwe akaichochea roho ya Wafilisiti dhidi ya Yuda na ya Waarabu waliokuwa karibu na Waethipia.
\v 17 Wakaivamia Yuda, wakavamia katika nyumba ya mfalme. Pia wakawachukua wanaye na wake zake. Hakuna mwana aliyebakizwa kwa ajili yake ispokuwa, Yehoshafati, mwanaye mdogo.
\s5
\v 18 Baada ya haya yote, Yahwe akampiga katika utumbo wake kwa ugonjwa usiopona.
\v 19 Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia babu zake.
\v 20 Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umrai wa miaka thelatahini na mbaili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuaombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Wakaaji wa Yersusalemu wakamfanya Ahazia, mwana mdodgo wa Yehoramu, mfalme katika nafasi yake, kwa maana kundi la watu ambalo lilikuja na Waarabu katika ngome lilikuwa limewauwa wanaye wakubwa wote. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akawa mfalme.
\v 2 Ahazia alikuwa na umri wa mika arobaini na mbili alipoanza kutawala; alitawala kwa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Athalia; alikuwa binti Omri.
\v 3 Pia Ahazia alitembea katika njia za nyumba ya Ahabu kwa maana mama yake alikuwa mshauri katika kufanya mamabo maovu.
\s5
\v 4 Ahazia alifanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama nyumba ya Ahabu walivyokuwa wakifanya, kwa maana walikuwa washauri wake baada ya kifo cha baba yake, hadi kuangamia kwake.
\v 5 Pia aliufuata ushauri wao; akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu, huko Ramothi-gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.
\s5
\v 6 Yoramu akaraudi Yezreeli kwa ajili ya kuponywa majeraha ambayo walipa huko Rama, alipopigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akaenda chini Yezreeli ili kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
\s5
\v 7 Sasa uharibifu wa Ahazia ulikuwa umeletwa na Mungu kupitia kutembelewa na Yoramu. Alipokuwa amewasiri, alienda pamoja na Yeharamu ili kumvamia Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Yahwe alikuwa amemchagua kwa ajili ya kuingamiza nyumba ya Ahabu.
\v 8 Ikawa kwamba, Yehu alikuwa akichukua hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu, kwamba aliwakuta viongozi wa Yuda na wana wa ndugu zake Ahazia wakimtumikia Ahazia. Yehu akawauwa.
\s5
\v 9 Yehu akamtafuta Ahazia; Wakamkamata akiwa amejificha katika Samaraia, wakamleta kwa Yehu, na wakamuuwa. Kisha wakamzika, kwa maana walisema, "Ni mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Yahwe kwa moyo wake wote." Kwa hiyo nyumba ya Ahazia haikuwa na nguvu zaidi kwa ajili ya kuutawala ule ufalme.
\s5
\v 10 Sasa Athalia, mama wa Ahazia, akaoana kwamba mwanaye alikuwa amekufa, akaianuka na kuwauwa watoto wote wa kifalme katika nyumba ya Yehu.
\v 11 Lakini Yehoshaba, binti wa mfalme, akamchukua Yoashi, mwana wa Ahazia, na akamvutia mbali kutoka miongoni mwa wana wa mfalme ambao waliuawa. Akamuweka yeye na mlezi wake katika chumba cha kulala. Kwa hiyo Yehoshaba, binti wa mfalme Yehoramu, mke wa Yehoiada kuhani (kwa maana alikuwa dada yake Ahazia), akamficha asimuone Athalia, kwa hiyo Athalia hakumuuwa.
\v 12 Alikuwa pamoja nao, wakiwa wamejificha katika nyumba ya Mungu kwa miaka sita, Athalia alipotawala juu ya Yuda.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Katika mwaka wa sa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.
\v 2 Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu.
\v 3 Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, "Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.
\s5
\v 4 Hivi ndivyo mtakavyo fanya: theluthi yenu makuhani na Walawi ambao huja kuhudumu siku ya Sabato, mtakuwa walinzi katika milango.
\v 5 Theluthi nyingine mtakuwa katika nyumba ya mfalme, na theluthi nyingine mtakuwa katika Msingi wa Lango. Watu wote watakuwa katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 6 Msimruhusu yeyote kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, isipokuwa makuhani na Walawi wanaoatumika. Wao wanaweza kuingia kwa sababu inawahusu.
\v 7 Lakini watu wengine wote lazima mtii amri ya Yahwe. Walawi lazima wamzunguke mfalme pande zote, kila mtu na silaha zake mkononi mwake. Yeyote atakayeingia katika nyumba, atauawa. Kaeni na mfalme aingiapo ndani na atokapo nje."
\s5
\v 8 Kwa hiyo Walawi na Yuda wote walitumika kwa kila njia kama katika namna ambayo Yehoyada kuhani aliwaamuru. Kila mmoja alichukua watu wake, wale waliotakiwa kuja ndani kuhudumu katika Sabato, na wale watakaoondoka siku ya Sabato, kwa maana
\v 9 Yehoyada, kuhani, hakuwa amezuilia mojawapo ya zamu zao. Kisha Yeliyadaya, kuhani, akaleta kwa maakida mikuki na ngao ndogo na kubwa zilizokuwa za mfalme Daudi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu.
\s5
\v 10 Yehoyada akawaleta wanajeshi wote, kila mtu na mkuki wake katika mkono wake, upande wa kulia wa hekalu hadi upande wa kushoto wa hekalu, pembeni mwa madhabahu na hekalu, wakimzunguka mfalme.
\v 11 Kisha wakamleta nje mwana wa mfalme, wakaiweka taji juu yake, na kumpa agano la sheria. Kisha wakamfanya mfalme, na Yehoyda na wanaye wakampaka mafuta. Kisha wakasema, "Aishi maisha marefu mfalme."
\s5
\v 12 Athalia aliposikia kele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akatoka ili awaone watu katika nyumba ya Yahwe.
\v 13 na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. "Fitina! Fitina!"
\s5
\v 14 Kisha Yehoyada, kuhani, akawaleta nje maakida wa mamia waliokuwa juu ya jeshi na kusema, "Mleteni nje kati ya safu, yeyote atakayemfuata, auwawe kwa upanga." kwa maana kuhani alikwishasema, "Msimuue katika nyumba ya Yahwe."
\v 15 Kwa hiyo wakafanya njia kw ajili yake, na akaenda kwenye nyumba ya mfalme kupita njia ya Lango la Farasi, na huko wakamuuwa.
\s5
\v 16 kisha Yehoyada alifanya agano kati yake mwenyewe, watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa Yahwe.
\v 17 Kwa hiyo watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. wakazivunja vipande vipande madhabahu za Baali na sanamu zake, na wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu hizo.
\s5
\v 18 Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi.
\v 19 Yehoyada akaweka walinzi katika malango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.
\s5
\v 20 Yehoyada akachukua pamoja naye maakida wa mamia, watu wakubwa, watawala wa watu, na watu wote wa nchi. Akamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe; watu wakaja kwenye nyumba ya mfalme kupitia Lango la juu na kumkalisha mfalme juu ya kiti cha enzi cha ufalme. (Baadhi ya maandiko ya ya kisasa yanasema, "wakamshusha chini mfalme")
\v 21 Kwa hiyo watu wote wa nchi wakafurahia, na mji wote ulikuwa kimya. Kuhusu Asa walikuwa wamemuua kwa upanga.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala kwa mika arobaini katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
\v 2 Yoashi alifanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe siku zote za Yehoyada, yule kuhani.
\v 3 Yehoyada akajichukulia wake wawili kwa ajili yake, na akawa baba wa wana na mabinti.
\s5
\v 4 Ikawa baada ya haya, kwamba Yoashi aliamua kuitengeneza nyumba ya Yahwe.
\v 5 Akawakusanya pamoja makuhani na Walawi, na kusema kwao, " Nendeni nje kila mwaka kwenye miji ya Yuda na kukusanya fedha kutoka Israeli yote kwa ajili ya kuikarabati nyumba ya Mungu wenu. Hakikisheni kwamba mnaanza haraka." Walawi hawakufanya kitu kwanza.
\s5
\v 6 Kwa hiyo mfalme akamuita Yehoyada, yule kuhani, na kumwambia, "Kwa nini hukuwaagiza Walawi kuleta kutoka Yud na Yerusalemu kodo iliyoagizwa na Musa mtumishi wa Yahwe na kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya amri za hema ya agano?"
\v 7 Kwa maana wana wa Athalia, yule mwanamke muovu, walikuwa wameivunja nyumba ya Mungu na kuwapa Mabaali vitu vyote vitakatifu vya nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 8 Kwa hiyo mfalme aliamuru, na wakatengeneza kasha na kulileta nje kwenye lango kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 9 Kisha wakafanya tangazo katika Yuda na Yerusalemu, kwa ajili ya watu kuleta kwa Yahwe kodi aliyoiagiza Musa mtumishi wa Mungu juu ya Israeli jangwani.
\v 10 Viongozi wote na watu wote wakafurahia na wakaleta fedha na kuiweka kwenye kasha hadi walipomaliza kulijaza.
\s5
\v 11 Ikatokea kwamba kila lilipoletwa kasha kwa mikono ya Walawi kwa wakuu wa mfalme, na kila walipoona kwamba kulikuwa na fedha nyingi sana ndani yake, waandishi wa mfalme na mkuu wa kuhani mkuu walikuja, kulihamishia fedha kasha, na kulirudisha sehemu yake. Walifanya hivyo siku baada siku, wakikusanya kiasi kikubwa cha fedha.
\v 12 Mfalme na Yehoyada akawapa zile fedha wale waliofanya kazi ya kuhudumu katika nyumba ya Yahwe, Watu hawa waliwaajiri waashi na maseremala ili waijenge nyumba ya Yahwe, na pia wale waliofanya kazi katika chuma na shaba.
\s5
\v 13 Kwa hiyo wafanya kazi wakafanya kazi, na kazi ya kukarabati ikasonga mbele mikononi mwao; waakaisimamisha nyumba ya Mungu katika hali yake halisi na kuiimarisha.
\v 14 Walipomaliza, wakaleta fedha zilizobaki kwa mfalme na Yehoyada. Fedha hizo zilitumika kutengenezea samani kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vyombo vya huduma na kutolea dhabihu—vijiko na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa bila kukomaa katika nyumba ya Yahwe kwa siku zote za Yehoyada.
\s5
\v 15 Yehoyada akazeeka na alaaikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa.
\v 16 Wakamzika katika aamji wa Daudi miongoni mwa wafalme, kwa sababu alikuwa amefanya mema katika Israeli, kwa Mungu, na kwa ajili ya nyumba ya Mungu,
\s5
\v 17 Sasa baada ya kifo cha Yehoyada, kiongozi wa Yuda akaja na kutoa heshima kwa mfalme. Kisha mfalme akawasikiliza.
\v 18 Wakaiacha nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zao, na kuwaabudu miungu na maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababau ya hili kosa lao.
\v 19 Bado akatuma manabii kwao ili kuwaleta tena kwake, Yahwe, manabii wakatangaza juu ya watu, lakini walipuuza kusikiliza.
\s5
\v 20 Roho wa Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada, yule kuhani; Zekaria akasimama juu ya watu na kusema kwao, "Mungu anasema hivi: Kwa nini mnazivunja amri za Yahwe, ili kwamba msifanikiwe? Kwa kuwa mmemsahau Yahwe, pia amewasahau ninyi."
\v 21 Lakini wakapanga njama dhidi yake; kwa amri ya mfalme, wakampiga kwa mawe katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.
\v 22 Katika namna hii hii, Yoashi, yule mfalme, akapuuza ukarimu ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alikuwa amemfanyia.
\s5
\v 23 Ikawa karibu mwisho wa mwaka, kwamba jeshi la Aramu wakaja juu yake Yoashi. Wakaja Yuda na Yerusalemu; wakawaua viongozi wote wa watu na kupeleka nyara zote kutoka kwao kwa mfalme wa Dameski.
\v 24 Jeshsi la Waaramu walikuwa wamekuja na jeshi dogo, lakini Yahwe akawapa ushindi juu ya jeshi kubwa, kwa sababu Yuda alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao. Katika namna hii Waaramu wakaleta hukumu juu ya Yoashi.
\s5
\v 25 Katika muda ambao Waaramu walikuwa wameondoka, Yoashi alikuwa amejeruhiwa vikali. Watumishi wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu ya mauaji ya wana wa Yehoyada, yule kuhani. Wakamuua katika kitanda chake, na akafa; wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya wafalme.
\v 26 Hawa walikuwa watu waliopanaga njama dhidi yake: Zabadi mwana wa Shimeathi, Mwamoni; na Yehozabadi mwana wa Shimrithi, Mwanamke Mmoabu.
\s5
\v 27 Sasa matukio kuhusu wanaye, unabii muhimu uliokuwa umesemwa kumhusu yeye, na kujengwa tena kwa nyumba ya Mungu, ona, yameandikwa katika Kamusi ya kitabu cha wafalme. Amazia mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Amaza alikuwa na umri wa amiaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu.
\v 2 Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu.
\s5
\v 3 Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme.
\v 4 Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyoaandikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamru. "Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe".
\s5
\v 5 Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za babu zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia --wote wa Yuda na wa Benyamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300, 000 wanaume waliochaguliwa, wawezaoa kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao.
\v 6 Pia alikodi wanaume wa kupigana 100, 000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja.
\s5
\v 7 Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, " Mfalme, usiliache jeshi la Istaeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu.
\v 8 Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini".
\s5
\v 9 Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, "Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe anauwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo."
\v 10 Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana zidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasara kali.
\s5
\v 11 Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaueme elfu kumi wa Seiri.
\v 12 Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarushwa chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande.
\s5
\v 13 Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji Yuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana.
\s5
\v 14 Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba.
\v 15 Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka zidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, "Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe zidi ya mkono wako?"
\s5
\v 16 Akiwa kwamaba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, "Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?" Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangaamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikilisa ushauri wangu."
\s5
\v 17 Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. akisema, "Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita".
\s5
\v 18 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amaziahi mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti.
\v 19 Umesema, 'Ona, nimeipiga Edomu,' na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?'
\s5
\v 20 Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu.
\v 21 Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda.
\v 22 Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani.
\s5
\v 23 Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne.
\v 24 Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamanai katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria.
\s5
\v 25 Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
\v 26 Kwa mambo mengingine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli?
\s5
\v 27 Sasa kutoka wakati amabaoa Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njama zidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko.
\v 28 Wakamleta juu ya farasis na wakamzika pamoja na babu zake kataika Mji wa Yuda.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na aumri wa mika kumi na sita, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake Amazia.
\v 2 Ndiye aliuyeijenga tena Elathi na kuurejesha kwa Yuda. Baada ya hapo mfalme akalala pamoja na babu zake.
\v 3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala. Akatawala miaka ishirini na mabili katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yekolia; alikuwa wa Yerusalemu.
\s5
\v 4 Akafanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, katika kila jamabo.
\v 5 Alijitoa kumtafuta Mungu katiaka siku za Zekaria, ambaye alimpa maelekezo kwa ajili ya kumtii Mungu. Kadri alivyomtafuta Yaahwe, Mungu alimfanikisha.
\s5
\v 6 Uzia akaenda na kupigana zidi ya Wafilisti. Akaubomoa ukuta wa mji wa Gathi, Yabne, na Ashdodi; akajenga miji katika nchi ya Ashdodi na miongoni mwa Wafilisti.
\v 7 Mungu aakaamsaidia zidi ya Wafilist, zidi ya Waarabu waliokuwa wakiishi Gur - baali, na zidi ya Wameuni.
\v 8 Waamoni wakalipa kodi kwa Uzia, na umaarufu wake ukaenea, hata kufika maingilio ya Misiri, kwa sababu alikuwa ameanza kuwa maarufu.
\s5
\v 9 Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na pa kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome.
\v 10 Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.
\s5
\v 11 Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi la wanaume wa kupigana vita ambao walienda vitani katika makundi ambayo idadi yake ilikuwa imehesabiwa na Yeieli, mwandishi. na Maaseya, afisa, chini ya mamlaka ya Hanania, mmoja wa maamri jeshi wa mfalme.
\v 12 Jumla ya wakuu wa nyumba za mababu, watu wa kupigana vita, walikuwa 2, 600.
\v 13 Chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la watu 307, 500 ambao walifanya vita kwa nguvu ili kumsaidia mfalme idi ya maadui.
\s5
\v 14 Uzia akaandaa kwa ajili yao—kwa ajili ya jeshi lote — ngao, mikuki, chapeo, deraya za majini, nyuta, na mawe ya kurusha.
\v 15 Katka Yerusalemu alijenga mitambo, iliyobuniwa na watu wenye ujuzi, ili iwe juu ya minara na juu ya buruji, kwa ajili ya kurushia mishale na mawe makaubwa. Umaarufu wake ukaenea hadi nchi za mbali, kwa maana alisaidiwa sana hadi alipokuwa na ngavu sana.
\s5
\v 16 Lakini Uzia alipokuwa amekuwa na nguvu nyingi, moyo wake ulijiinua akatenda kwa uovu; akafanya makosa zidi ya Yahwe, Mungu wake, kwa maana alienda kwenye nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kufukiza uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
\v 17 Azaria, kuhani, akamfuata, na pamoja naye makuhanai themanini wa Yahwe, ambao walikuwa watu wenye ujasiri.
\v 18 Walimzuia Uzia, mfalme, na wakasema kwake, " Siyo jukumu lako, Uzia, kumtolea Yahwe uvumba, bali ni kazi ya makuhani, wana wa Haruni, amabao wametengwa kwa ajili ya kutoa sadaka za uvumba. Toka nje ya sehemu takatifu, kwa maana huna uaminifu na hautaheshimiwa na Yahwe Mungu."
\s5
\v 19 Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba.
\v 20 Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwanagalia, na, tazama, alikuwa amepatwa ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga.
\s5
\v 21 Uzia, mfalme, alikuwa mwenye ukoma hadi siku ya kufa kwake na aliishi katika nyumba ya kutengwa tangu alipokuwa mwenye ukoma, kwa maan alitengwa na nyumba ya Yahwe. Yothamu, mwanaye, alikuwa mkuu wa anyumba ya mfalme na aliwatawala watu wa nchi.
\s5
\v 22 Mambo mengine kuhusu Uzia, mwanzo na mwisho, yako katika kile ambacho Isaya, mwana wa Amozi, nabii, aliandika.
\v 23 Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na babu zake; walimzka pamoja na babu zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, "Ni mwenye ukoma". Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Yothamu alikuwa na umri wa mika ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yerusha; alikuwa binti Sadoki.
\v 2 Akafanya yaliyomema katika macho ya Yawe, akiufuta mfano wa baba yake, Uzia, katika mabo yote. Pia alijiepusha kuingia katika hekalu la Yahwe. Lakini watu bado walikuwa wanaenda katika njia za uovu.
\s5
\v 3 Akalijenga tena lango la juu la nyumba ya Yahwe, na juu ya kilima cha Ofeli akajenga sana.
\v 4 Vilevile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika mistu alijenga ngome na minara.
\s5
\v 5 Pia alipigana na mfalme wa watu wa Amoni na akawashinda. Katika mwaka huo huo, watu wa Amoni walimpa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, kori elfu kumi za shayiri. Watu wa Amoni wakampa hivyo hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
\s5
\v 6 Kwa hiyo Yothamu akawa na nguvu sana kwa sababu alitembea imara mbele za Yahwe Mungu wake.
\v 7 Kwa mambo mengine kuhusu Yothamu, vita vyake vyote, na njia zake zote, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
\s5
\v 8 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi na sita kataika Yerusalemu.
\v 9 Yothamu akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Ahazi, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Hakufanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi babu yake alivyokuwa amefanya.
\v 2 Badala yake, alitembea katika njia za wafalme wa Israeli; pia alitengeneza sanamu za kusubu kwa ajila ya Mabaali.
\s5
\v 3 Zaidi ya hayo, akafukiza uvumba katika bonde la Beni Hinomu na akawaweka watoto wake ndani ya moto, kwa mjibu wa desturi za uzinzi za watu ambao Yahwe aliwafukuza nje ya nchi zao mbele za watu wa Israeli.
\v 4 Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika sehemu za juu na juu ya vilima na chini ya kila mti wenye majani mabichi.
\s5
\v 5 Kwa hiyo Yahwe Mungu wa Ahazi, akamweka katika mikono ya mfalme wa Shamu. Waaramu wakamshinda na kuchukua kutoka kwake kundi kubwa la mateka, wakawapeleka Damesiki. Ahazi pia aliwekwa katika mikono ya mfalme wa Israeli ambaye alimshinda kwa mauji makuu.
\v 6 Kwa maana Peka mwana wa Remalia, aliwaua katika Yuda wanajeshi 120, 00 kwa siku moja, wote walikuwa wanaume hodari, kwa maana walikuwa wamemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao.
\s5
\v 7 Zikri, mtu mwenye nguvu kutoka Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu, mwangalizi mkuu wa ikulu, na Elkana, ambaye alikuwa karibu na mfalme.
\v 8 Jeshsi la Israeli likachukua mateka kutoka kwa ndugu zao 200, 000 wake, wana, na mabinti. Pia wakachukua nyara nyingi, ambazo walipeleka Samaria.
\s5
\v 9 Lakini nabii wa Yahwe alikuwapo huko, jina lake aliitwa Odedi. Alikwenda nje kukutana na jeshi likiingia Samaria. Akawaambia, "Kwa sababu Yahwe, Mungu wa babu zenu, alikuwa na hasiri na Yuda, akawatia katika mikono yenu. Lakini mmewaua katika hasira inayofika juu mbinguni.
\v 10 Sasa ninyi badala ya kuwahifadhi wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu kama watumwa wenu. Lakini je hamko na hatia ya dhambi zenu zidi ya Yahwe Mungu wenu?
\v 11 Sasa basi, nisikilizeni: warudisheni wafubgwa, ambao mmewachukua wa ndugu zenu, kwa maana ghadhabu ya Yahwe iko juu yenu."
\s5
\v 12 Kisha baadhi ya viongozi wa watu wa Efraimu--Azaria mwana wa Yohanani, Berekia mwana wa Meshiremothi, na Yehizikia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai, wakasimama kinyume na wale waliorudi kutoka vitani.
\v 13 Wakasema kwao, "Lazimaa msiwaleta wafungwa hapa, kwa kuwa mlikusudia jambo ambalo litaleta juu yetu dhambi dhidi ya Yahwe, kuongeza dhambi juu yetu na makosa yetu, kwa maana makosa yetu ni makuu, na kuna hasira kali dhidi ya Israeli."
\s5
\v 14 Hivyo watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na mateka mbele ya viongozi wa Israeli na kusanyiko lote
\v 15 Watu ambao walipangwa kwa majina wakanyanyuka na kuwachukua wafungwa, na kuwavika wote waliokuwa uchi miongoni mwa mateka. Wakawavika na kuwapa viatu. Wakawapa chakula wale na kunywa. Wakawahudumia majeraha yao na kuwaweka waliodhaifu juu ya punda. Wakawarudisha kwenye familia zao katika Yeriko, (Ulioitwa mji wa mitende). Kisha wakarudi Samaria.
\s5
\v 16 Wakati huo Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa wafalme wa Ashuru kuwaomba wamsaidie.
\v 17 Kwa maana Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuvamia Yuda, wakachukua wafungwa.
\v 18 Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo.
\s5
\v 19 Kwa kuwa Yahwe aliishusha chini Yuda kwa sababu ya Ahazi, mfalme wa Israeli; kwa maana alikuwa ametenda maovu katika Yuda na alikuwa ametenda dhambi nzito sana dhidi ya Yahwe.
\v 20 Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru, akaja kwake na akampa tabu badala ya kumpa nguvu.
\v 21 Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye.
\s5
\v 22 Mfalme Ahazi huyu huyu akatenda dhambi hata zaidi dhidi ya Yahwe katika muda wa mateso yake.
\v 23 Kwa maana aliwatolea dhabihu mingu wa Dameski, miungu ambao walimshinda. Akasema, "Kwa sababu miungu wa mfalme wa Aramu waliwasaidia, nitawatolea sadaka ili wanisaidie." Lakini walikuwa watesi wake na Israeli yote.
\s5
\v 24 Ahazi akazikusanya pamoja samani za nyumba ya Mungu na kuzikata vipande vipande. Akaifunga milango ya nyumba ya Yahwe na kuzitengeneza madhabahu kwa ajili yake mwenyewe katika kila kona ya Yerusalemu.
\v 25 Katika kila mji wa Yuda akafanya sehemu za juu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu wengine. Akamfanya Yahwe, Mungu wa babu zake, akasirike.
\s5
\v 26 Sasa matendo yake yaliyobaki, na njia zake zote, mwanzo na mwisho, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\v 27 Ahazi akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji, katika Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Hezekia, mwanaye, akawa mfamle katika nafasi yake.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Hezekia alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano; alitawala miaka ishini na nane katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Abiya; alikuwa binti wa Zekaria.
\v 2 Alifanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi baba yake alivyofanya.
\s5
\v 3 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, katika mwezi wa kwanza, Hezekia aliifungua milango ya nyumba ya Yahwe na kuikarabati.
\v 4 Akawaleta ndani makuhani na Walawi, na akawakusanya pamoaja katika uwanda upande wa mashariki.
\v 5 Akawaambia, "Nisikilizeni, ninyi Walawi! Jitakaseni wenyewe, na itakaseni nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zenu, na uondoeni mbali uchafu kutoka kwenye sehemu takatifu.
\s5
\v 6 Kwa kuwa babu zetu walikosea na kufanya kilichokuwa uovu katika macaho ya Yahwe Mungu wetu; walimsahau, wakageuzia mbali nyuso zao kutoka sehemu ambapo Yahwe anaishi, na kuigeuzia migongo yao.
\v 7 Pia waliifunga milango ya ukumbi nakuziweka nje taa; hawakufukiza uvumba au kutoa sadaka za kuteketezwa katika sehemu takatifu kwa Mungu wa Israeli.
\s5
\v 8 Kwa hiyo hasira ya Yahwe ilikuwa imeshuka juu ya Yuda na Yerusalemu, na amewafanya kuwa kitu cha wasiwasi, cha hofu, na cha kudharauriwa, kama mnavyoona kwa macho yenu.
\v 9 Hii ndiyo maana mababu zetu wameanguka kwa upanga, na wana wetu, binti zetu, na wake zetu wako katika utumwa kwa sababu ya hili.
\s5
\v 10 Sasa ni katika moyo wangu kufanya agano na Yahwe, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali iweze kugeukia mbali nasi.
\v 11 Wanangu, msiwe wavivu sas, kwa kuwa Yahwe amewachagua kwa ajili ya kusimama mbe yake, kwa ajili ya kumwabudu yeye, na kwamba muwe watumishi wake na kufukiza uvumba."
\s5
\v 12 Basi Walawi wakainuka; Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa watu wa Kohathi; na wa watu wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wargeshoni, Yoa mwana wa Zimna, na Edeni mwana wa Yoa;
\v 13 wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; wa wana wa Asafu, Zekaria na Matania;
\v 14 wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.
\s5
\v 15 Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa wenyewe, na wakaenda ndani, kama alivyoamru mfalme, wakifuata maneno ya Yahwe, kwa ajili ya kuisafisha nyumba ya Yahwe.
\v 16 Makuhani wakaenda kwenye sehemu za ndani ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kuisafisha; wakaleta nje uchafu wote walioukuta ndani ya hekalu la Yahwe katika uwanja wa nyumba. Walawi wakauchukua kuubeba nje ya hadi kwnye kijito cha Kidroni.
\v 17 Sasa wakaanza utakaso katika siku ya kwanza ya mwezi. Katika siku ya nane ya mwezi wakaufikia ukumbi wa Yahwe. Kisha siku nane zaidi wakaitakasa nyumba ya Yahwe. Katika siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza wakamaliza.
\s5
\v 18 Kisha wakaenda kwa Hezekia, mfalme, ndani ya ikulu na kusema, "Tumeisafisha nyumba yote ya Yahwe, madhabahu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa pamoja na vifaa vyake vyote, na meza ya mkate wa uwepo, pamoja na vifaa vyake vyote.
\v 19 Kwa hiyo tumejiandaa na tumevitakasa vitu vyote ambavyo Mfalme Ahazi aliviondoa wakati alipoenda kwa ukengeufu katika kipindi cha utawala wake, ona, viko mbele ya madhabahu ya Yahwe."
\s5
\v 20 Kisha Hezekia mfalme akaamka mapema asubuhi na kuwakusanya viongozi wa miji; akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 21 Wakaleta ng'ombe waume saba, kondoo waume saba, wanakondoo saba, mbuzi waume saba kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya mfalme, kwa ajili ya patakatifu, kwa ajili ya Yuda. Akawaamuru makuhani, wana wa Haruni, kuwatoa sadaka juu ya madhabahu ya Yahwe.
\s5
\v 22 Kwa hiyo wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu. Wakawachinja kondoo dume, na kunyunyiza damu juu ya madhabahu; Pia wakawachinja wanakondoo na kuinyunyiza damu juu ya madhabahu.
\v 23 Wakawaleta mbuzi kwa ajili ya sadka ya dhambi mbele ya mfalme na kusnyiko; wakaweka mikono yao juu ya hao mbuzi.
\v 24 Makuhani wakawachinja, na wakafanya sadaka ya dhambi kwa damu yao juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa maana mfalme alikuwa ameamuru kuwa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi lazima zifanywe kwa ajili ya Israeli wote.
\s5
\v 25 Hezekia akawaweka Walawi katika nyumba ya Yahwe wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, akiwapanga kwa amri ya Daaudi, Gadi, mwonaji wa mfalme, na Nathani, nabii, kwa maana amri ilitoka kwa Yahwe kupitia manabii wake.
\v 26 Walawi wakasimama na vyombo vya Daudi, na makauhani wakasimama na matarumbeta.
\s5
\v 27 Hezekia akawaamuru kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Sadaka zilipoanza, wimbo wa Yahwe ukaanza pia, kwa matarumbeta, pamoja na vyombo vya Daudi, mfalme wa Israeli.
\v 28 Kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, na wapiga matarumbeta wakapiga; yote hayo yakaendele hadi sadaka za kuteketezwa zilizipokwisha.
\s5
\v 29 Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na watu waliokuwepo pamoja naye wakainama, na kusujudu.
\v 30 Vile vile, Hezekia, mfalme, na viongozi wakawaamuru Walawi kuimba ili kumsifu Yahwe kwa maneno ya Daudi na ya Asafu, mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama chini wakasujudu.
\s5
\v 31 Kisha Hezekia akasema, "Sasa mmejiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe. Njoni hapa na mlete sadaka na dhabihu za shukrani katika nyumba ya Yahwe." Kusanyiko wakaleta sadka na dhabihu za shukrani, na wote waliaokuwa na moyo wa kuhiyalika wakaleta sadka za kuteketezwa.
\s5
\v 32 Hesabu ya sadaka za kuteketezwa ambazo kusanyiko walileta ilikuwa ng'ombe sabini, kondoo waume mia moja, na wanakondo waume mia mbili. Wote hao walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe.
\v 33 Sadaka za kuwekwa wakfu zilikuwa ng'ome mia sita na kondoo elfu tatu.
\s5
\v 34 Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuchuna sadaka zote za kuteketezwa, kwa hiyo ndgugu zao, Walawi, wakawasaidia hadi kazi ilipoisha, na hadi makuhani walipoweza kujitakasa wenyewe, kwa maana Walawi walikuwa makaini sana kujitaksa wenyewe kuliko makuhani.
\s5
\v 35 Zaidi ya hayo, palikuwa na sadaka za kuteketezwa nyingi sana; zilitolewa pamoja na sadaka za mafauta za amani, na kulikuwa na sadaka za vinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo huduma ya nyumba ya Yahwe ikawekwa katika utaratibu.
\v 36 Hezekia akafurahia, na watu pia, kwa sababu ya kile ambacho Mungu alikuwa ameandaa kwa ajili ya watu, kwa maana kazi ilikuwa imekamilika haraka.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Hzekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda, na pia akawaandikia barua Efraimu na Manase, kwamba waje kwenye nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu, kusherekea Pasaka ya Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 2 Kwa maana mfalme, viongozi wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walikuwa wameshauriana pamoja, wakakubaliana kusherekea Pasaka katika mwezi wa pili.
\v 3 Hawakuweza kuisherekea mapema kabla ya hapo, kwa sababu hapakuwa na makuhani wa kutosha waliojitakasa wenyewe, wala watu hawakuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu.
\s5
\v 4 Pendekezo hili likaonekana sahihi katika macho ya mfalme na ya kusanyiko lote.
\v 5 Kwa hiyo wakakubaliana kufanya tangazo katika Israeli yote, kuanzia Beer-sheba hadi Dani, kwamba watu lazima waje kusherehekea Paska ya Yahwe, Mungu wa Israeli, huko Yerusalemu. Kwa maana walikuwa hawakuwa wameisherehekea kwa hesabu kubwa ya watu, kwa mujibu wa jinsi ilivyokuwa imeandikwa.
\s5
\v 6 Hivyo matarishi wakaenda na barua kutoka kwa mfalme na viongozi wake katika Israeli na Yuda yote, kwa agizo la mfalme. wakasema, "Ninyi watu wa Israeli, rudini kwa Yahwe, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili kwamba aweze kuwarudia masalia wenu ninyi mlipona kutoka kwenye mkono wa wafalme wa Ashuru.
\s5
\v 7 Msiwe kama babu zenu au ndugu zenu, ambao walimuasi Yahwe, Mungu wa mababu zao, hivyo akawaweka katika kuangamia, kama mnavyoona.
\v 8 Sasa msiwe wasumbufu, kama babu zenu walivyokuwa; badala yake, jitoeni wenyewe kwa Yahwe na njoeni kwenye sehemu yake takatifu, ambayo ameitakasa milele, na mwabuduni Yahwe Mungu wenu, ili kwamba uso wake wenye hasira uwageukie mbali.
\v 9 Kwa maana ikiwa mtageuka nyuma kwa Yahwe, ndugu zenu na watoto wenu watapata huruma mbele ya hao wanaowaongoza kama wafungwa, na watarudi katika nchi hii. Kwa maana Yahwe Mungu wenu, ni mkarimu na mwenye huruma, na hatawageuzia mbali uso wake, kama mtarudi kwake."
\s5
\v 10 Kwa hiyo matarishi wakapita mji kwa mji katika majimbo ya Efraimu na Manase, njia yote hadi Zabuloni, lakini watu waliwacheka na kuwazomea.
\v 11 Lakini, watu wengine wa Asheri na Manase na Zabuloni walijinyenyekesha wenyewe na wakaja Yerusalemu.
\v 12 Mkono wa Mungu pia ukaja juu ya Yuda, kuwapa moyo mmmoja, ili kulikubali agizo la mfalme na viongozi kwa neno la Yahwe.
\s5
\v 13 Watu wengi, kusanyiko kubwa, likakusanyika Yerusalemu kusherehekea Sikukuu ya Mikate Isiyochacha katika mwezi wa pili.
\v 14 Waliinuka na kuchukua madhabahu zizilizokuwa Yerusalemu, madhabahu zote kwa ajili ya sadaka za kufukiza; wakazirusha katika kijito Kidroni.
\v 15 Kisha wakamuua mwanakondoo wa Paska katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi wakaona aibu, kwa hiyo wakajitakasa wenyewe na kuleta sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 16 Wakasimama katika sehemu zao katika makaundi yao, wakifuata maelekezo yaliyotolewa na sheria ya Musa, mtu wa Mungu. Makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi.
\v 17 Kwa maana walikuwepo wengi katika kusanyikao amaabao hawakuwa wamejitakasa wenyewe. Kwa hiyo Makuhani wakamchinja mwanakondoo wa Pasaka kwa ajili ya kila mmoja ambaye hakuwa amejisafisha na hakuweza kuzitakasa sadaka zake kwa Yahwe.
\s5
\v 18 Kwa kuwa wingi wa watu, wengi wao kutoka Efraimu na Manase, Asakari na Zabuloni, hawakuwa wamejitakasa wenyewe, bado waliula mlo wa Paska, kinyume na maelekezo yaliyoandikwa. Kwa kuwa Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, "Mungu Yahwe amsamehe kila mmoja
\v 19 ambaye anaulekeza moyo wake kumtafuta Mungu, Yahwe, Mungu wa babu zake, hata kama hajasafiswa kwa utakaso wa viwango vya patakatifu."
\v 20 Kwa hiyo Yahwe akamsikiliza Hezekia na akawaponya watu.
\s5
\v 21 Watu wa Israeli waliokuwepo Yerusalemu wakaitunza Sikukuu ya Mikaate Isiyochachwa na furaha kubwa kwa siku saba. Walawi na makuhani wakamsifu Yahwe siku baada ya siku, wakiimwimbia Yahwe kwa vyombo vya sauti kuu.
\v 22 Hezekia akazungumza kwa kuwatia moyo Walawi wote walioilewa ibada ya Yahwe, Kwa hiyo wakala kwa kipindi cha siku saba, wakitoa sadaka za amani, na kufanya toba kwa Yahwe, Mungu wa babu zao.
\s5
\v 23 Kusanyiko lote kisha likaamua kusherehekea kwa siku zingine saba, na wakafanya hivyo kwa furaha.
\v 24 Kwa kuwa Hezekia mfalme wa Yuda aliwapa kusanyiko ng'ombe dume elf moja, na kondoo elfu saba kama sadaka; na viongozi wakawapa kusanyiko ng'ombe dume elfu moja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajitakasa wenyewe.
\s5
\v 25 Kusanyiko lote la Yuda, pamoja na makuhani na Walawi na watu wote walikuja pamoja kutoka nchi ya Israeli na wale walioishi Yuda--wote wakafurahia.
\v 26 Hivyo kulikuwa na furaha kuu katika Yerusalemu, kwa kuwa tangu wakati wa Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hapakuwa na kitu kama hicho katika Yerusalemu.
\v 27 Kisha makuhani, Walawi, wakainuka na kuwabariki watu. Sauti zao zilisikika na maombi yao yakaenda juu mbinguni, sehemu takatifu ambapo Mungu anaishi.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Sasa wakati haya yote yalipokwisha, watu wote wa Israeli waliokuwepo pale wakaenda huko kwenye mji wa Yuda na wakazivunja vipande vipande nguzo za mawe na wakazikata nchi za maashera, na wakazibomoa sehemu za juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, na katika Efraimu na Manase, hadi walipoziharibu zote. Kisha watu wote wa Israeli wakarudi, kila mtu kwenye mali zake na kwenye mji wake.
\s5
\v 2 Hezekia akayapanga makundi ya makuhani na Walawi wakajipanaga kwa makundi yao, kila mtu akapangwa katika kazi yake, wote makuhani na Walawi. Aliwapanga wafanye sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kutoa shukrani, na kusifu katika malango ya hekalu la Yahwe.
\v 3 Pia akawapanga katika sehemu ya mfalme kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kutoka katika mali zake, hiyo ni kwa ajili ya, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya siku za Sabato, mwezi mpya, na sikukuu zisizobadilika, kama ilivyokuwa imeandikwa katika sheria ya Yahwe.
\s5
\v 4 Vilevile, akawaamuru watu walioishi Yerusalemu kutoa fungu kwa ajili ya makuhani na Walawi, ili kwamba wawe makini katika kuitii sheria ya Yahwe.
\v 5 Mapema mara baada ya amri kutolewa, watu wa Israeli kwa ukarimu wakatoa malimbuko ya nafaka, divai mpya, mafuta. asali, na kila kitu kutoka kwenye mavuno ya shamba. Wakaleta ndani fungu la kumi la kila kitu; ambavyo vilikuwa kiasi kikubwa sana.
\s5
\v 6 Watu wa Israeli na Yuda ambao waliishi katika mji wa Yuda pia wakaleta zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vitakatifu amabavyo vilikuwa vimewekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wao, na wakavifunga katika marundo.
\v 7 Ilikuwa mwezi wa tatu wakati walipoanza kufunga michango yao katika marundo, na wakamaliza mwezi wa saba.
\v 8 Hezekia na viongozi walipokuja na kuyaona marundo, wakambariki Yahwe na watu wake Israeli.
\s5
\v 9 Kisha Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu marundo.
\v 10 Azaria, kuhani mkuu, wa nyumba ya Zadoki, akamjibu na akasema, "Tangu watu walipoanza kuleta matoleo katika nyumba ya Yahwe, tumekula na tulikuwa navyo vya kutosha, tulibakiza vingi, kwa maana Yahwe amewabariki watu wake. kilichokuwa kimebaki ni kiasi kikubwa hiki hapa."
\v 11 Kisha Hezekia akaagiza vyumba vya kuhifadhia viandaliwe katika nyumba ya Yahwe, na wakaviandaa.
\v 12 Kisha kwa uaminifu wakayaleta ndani matoleo, zaka, na vitu ambavyo ni vya Yahwe. Konania, Mlawi, alikuwa meneja mkuu wa hivyo vitu, na Shimei, ndu yake, alikuwa wa pili kwake.
\v 13 Yehieli, Azaria, Nahathi, Asaheli, na Yerimothi, Yazabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi, na Benania walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei ndu yake, kwa uteuzi wa Hezekia, mfalme, na Azaria mwanagalizi mkuu wa nyumba ya Mungu.
\s5
\v 14 Kore mwana wa Imna Mlawi, bawabu katika mlango wa mashariki, alikuwa juu ya sadaka za hiari za Mungu, msimamizi wa kugawa sadaka kwa Yahwe na sadaka takatifu kuliko zote.
\v 15 Chini yake walikuwepo Edeni, Miniamini, Yoshua, Shemai, Amaaria, na Shekania, katika miji ya makuhani. Wakazijaza ofisi za uaminifu, ili kutoa sadaka hizi kwa ndugu zao fungu kwa fungu, kwa wote walio muhimu na wasiomuhimu.
\s5
\v 16 Pia wakatoa kwa wale wanaume wenye umri wa miaka mitatu na kuendelea, amabao walikuwa wameandikwa kataika kaitatu cha babu zao walioiingia nyumba ya Yahwe, kwa mujibu wa ratiba ya kila siku, kuifanya kazi katika ofisi zao na zamu zao. (Mandishi ya kale yanasema hivi: "badala ya wanaume wa umri wa miaka mitatu na kuendelea", wanaume wa mika thelathini na kuendelea.").
\s5
\v 17 Waliwaganya makuhani kwa mujibu wa kumbu kumbu za babu zao, na hivyo hivyo kwa Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kwa mujibu wa ofisi zao na zamu zao.
\v 18 Waliwajumuisha watoto wao wadogo wote, wake zao, wana wao, na binti zao, katika jamii yote, kwa maana walikuwa waaminifu katika kujitunza wenye watakatifu.
\v 19 Kwa maana makuhani, uzao wa Haruni, amabao walikuwa katika mashamba ya vijiji wakimilikiwa na miji yao, au katika kila mji, palikuwa na watu walioteuliwa kwa majina kutoa mafungu kwa ajili ya wanaume miongoni mwa makuhani, na kwa wote waliokuwa wameorodheshwa katika kumbukumbu za babu zao kuwa miongoni mwa Walawi.
\s5
\v 20 Hezekia alifanya haya katika Yuda yote. Akakamilisha kilichokuwa chema, haki, na uaminifu mbele za Yahwe Mungu wake.
\v 21 Katika kila jambo ambalo alianzisha katika ibada ya nyumba ya Mungu, sheria, na zile amri, kumtafuta Mungu, alikifanya kwa moyo wake wote, na alifanikiwa.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Baada ya mambo haya na matendo haya ya uaminifu, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja na kuingia Yuda. Alipiga kambi kwa ajili ya kuivamia miji yenye ngome, ambayo alikusudia kuiteka kwa ajili yake.
\s5
\v 2 Sedekia alipoona kwamba Senakeribu amekuja na kwamba amedhamiria kupigana zidi ya Yerusalemu,
\v 3 aliwashirikisha viongozi wake na watu wake wenye nguvu kuyazuia maji ya chemichemi yaliyokuwa nje ya mji; waalimsaidia kufanya hivyo.
\v 4 Kwa hiyo watu wengi wakakusanyika na kuyazuia maji ya chemichemi zote na mikondo yote amabayo ilikuwa inatiririka katikati ya nchi. wakasema, "Kwa nini mfalme wa Ashuru aje na kupata maji mengi?"
\s5
\v 5 Hezekia akijipa ujasiri na kuujeenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Dudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao. (Maanshi ya kale yanasema hivi: " Badala ya, "akajenga minara amirefu", baadhi ya matoleo ya zamani na kisasa yanasema, "akajenga minara mirefu juu yake", Hii ni juu ya ukuta).
\s5
\v 6 Akaweka maamri jeshi juu wa watu. Akawakusanya pamoja kwake katika sehemu pana kwenye lango la mji na akasema kwao kwa ujasiri. Akasema,
\v 7 "Muwe imara na wenye ujasiri mzuri. Msiogope wala kukata tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na jeshi lote ambalo liko naye, kwa maana kuna mtu yuko pamoja nasi ambaye ni mkuu kuliko
\v 8 walio naye mfalme wa Ashuru. walionaye ni jeshi la mwili tu, lakini aliye nasi ni Yahwe, Mungu wetu, kwa ajili ya kutusaidia, na kupiagana vita vyetu." Kisha watu wakajifariji wenyewe kwa maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
\s5
\v 9 Baada ya hayo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliwatuma watumishi wake kwenda Yetusalemu (sasa alikuwa mbe ya Lakishi, na jeshi lake lote lilikuwa pamoja naye), kwa Hezekia, mfaalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walikuwa Yerusalemu. Akasema,
\v 10 "Hivi ndivyo Senakeribu, mfalme wa Ashuru, anasema: Ni kitu gani mnategemea kwa ajili ya kuhimili uvamizi katika Yerusalemu?
\s5
\v 11 Je, Hezekia hawapotoshi ninyi, ili kwamba awatoe kufa kwa njaa na kiu, anapowaambia, "Yahwe Mungu wetu atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru?
\v 12 Je, siyo Hezekia yule yule ambaye amezipeleka juu sehemu zake na madhabahu zake na kuwaamuru Yuda na Yerusalemu, juu ya madhabahu moja lazima muabudu, na juu yake lazima mchome sadaka zenu?
\s5
\v 13 Je, hamjui mimi na babu zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa inchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao zidi ya nguvu zangu?
\v 14 Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo amabayo babu zangu waliwatekeza, je, kulikuwa na muungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi zidi ya nguvu zangu?
\v 15 Sasa msimuruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna muungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa babu zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu?
\s5
\v 16 Watumishi wa Senakeribu hata walinena mabaya zaidi juu ya Yahwe Mungu na juu ya mtumishi wake Hezekia.
\v 17 Senakeribu pia akandika barua ili kumdhihaki Yahwe, Mungu wa Israeli, na kunena kinyume naye. Alisema, "Kama ambavyo miungu ya mataifa haikuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu, hivyo hivyo na Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu."
\s5
\v 18 Wakawalilia kwa lugha ya Wayahudi watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta, ili kuwaogopesha na kuwasumbua, ili kwamba waweze kuuteka mji.
\v 19 Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu kama walivyowanenea miungu wa Dunia, ambao ni kazi ya mikono ya wanadamu tu.
\s5
\v 20 Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni.
\v 21 Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya muungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga.
\s5
\v 22 Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. (Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya "akawapa pumziko juu ya kila pande", baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, "akawaongoza juu ya kila pande").
\v 23 Wengi walikuwa wakileta sadaka kwa Yahwe katika Yarusalemu, na zawadi za thamani kwa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa hiyo aliinuliwa mbele za macho ya mataifa yote toka wakati huo na kuendelea.
\s5
\v 24 Katika siku hizo Hezekia akaugua hadi hatua ya kufa. Akaomba kwa Yahwe, ambaye alisema kwake na kumpa ishara kwamba angeponywa.
\v 25 Lakini Hezekia hakumlipa Yahwe kwa ajili ya msaada uliotolewa kwake, kwa maana moyo wake uliinuliwa juu.
\v 26 Kwa hiyo hasira ikaja juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo, baadaye Hezekia alijinyenyekesha mwenyewe kwa jali ya kiburi cha moyo wake, wote Yeye na wakaaji wa Yerusalemu, hivyo hasira ya Yahwe haikuja juu yao wakati wa siku za Hezekia.
\s5
\v 27 Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima kubwa. Alijipatia mwenyewe vyumba vya kuhifadhia kwa ajili ya fedha, dhahabu, vito vya thamani, na kwa ajili ya manukato, na kwa ajili ya ngao na na vyombo vyote vya thamani pia.
\v 28 Pia alikuwa na nyumba za maghala kwa ajili ya mavuno ya nafaka, divai mpya, na mafuta, na malisho kwa ajili ya aina zote za wanyama.
\v 29 Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alaikuwa amempa afya tele. (Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya "miji" baadji ya matoleo ya kisasa yanasema "punda", na baadhi mengine ya kisasa yanaacaha neno nzima)
\s5
\v 30 Alikuwa ni Hezekia huyu huyu ambaye alisimamisha chemi chemi ya juu ya maji ya Gihoni, na aliye ileta moja kwa moja chini upande wa magharibi mwa mji wa Daudi. Hezekia alifanikiwa katika miradi yake yote.
\v 31 Hata hivyo, katika jambo la mabolozi wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuwauliza waliofahamu, kuhusu ishara za miujiza iliyokuwa imefanywa katika nchi, Mungu alimwachia mwenyewe, ili kumjaribu, na kujua yote yaliyokuwa katika moyo wake.
\s5
\v 32 Kwa mambo mengine kuhusu Hezekia, pamoja na matendo yake ya uaminifu wa agano, unaweza kuona kwamba yameandikwa katika Maono ya Nabii Isaya Mwana wa Amozi, na katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\v 33 Hezekia akalala pamaoja na babu zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu.
\v 2 Akafanya yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe, kama yalivyo mambo ya machukizo ya mataifa ambao Yahwe alikuwa amewafukuza mbele ya watu wa Israeli.
\v 3 Kwa maana alizijenga tena sehemu za juu ambazo baba yake Hezekia alikuwa amezibomoa, na akajenga madhabahu kwa ajili ya mabaali, akatengeneza sanaamu za Maashera, na akaziinamia chini nyota zote za mbinguni na kuziabudu.
\s5
\v 4 Manase akajenga madhbahu za kipagani katika nyumba ya Yahwe, ingawa Yahwe alikuwa amemwamuru, "Ni katika Yerusalemu ambamo jina langu litawekwa milele".
\v 5 Alijenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika vile viwanja viwili vya nyumba ya Yahwe.
\v 6 Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanaye katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akassoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na wale waliozungumza na na roho. Akafanaya maaovu mengi katika mcho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.
\s5
\v 7 Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaipeleka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Selemani mwanaye; alikuwa amesema, "Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchangua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele.
\v 8 Sitawaondoa tena watu wa Israeli katina nchi hii ambayo niliitoa kwa babu zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa."
\v 9 Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.
\s5
\v 10 Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza.
\v 11 Kwa hiyo Yahwe akaleta juu yao maamri jeshsi wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.
\s5
\v 12 Manase alipokuwa katika dhika, alimuomba Yahwe, Mungu wake, na akajinyenyekesha sana mbele za Mungu wa babu zake.
\v 13 Akaomba kwake; na Mungu akamsikiliza, na Mungu akasikia kuomba kwake na akamrudisha Yerusalemu, katika ufalme wake. Kisha Manase akafahamu kwamba Yahwe alikuwa Mungu.
\s5
\v 14 Baada ya hayo, manase akajenga ukuta wa nje ya mji wa Daudi, upande wa magharibi wa Gihoni, katika bonde, hadi kwenye lango la Samaki. Akauzungushia mlima wa Ofeli na akaupandisha ukuta hadi usawa mrefu sana. Akaweka maamri jeshi jasiri katika ngome zote za miji ya Yuda.
\v 15 Akaipeleka mbali miungu yote ya kigeni, akaondoa sanamu zote kwenye nyumba ya Yahwe, na madhabahu zote ambazo alikuwa amejenga juu ya mlima wa nyumba ya Yahwe na katika Yerusalemu, na kuvitupa nje ya mji.
\s5
\v 16 Akaijenga tena madhabahu ya Yahwe na juu yake akatoa sadaka za amani na sadaka za shukrani; akamwamuru Yuda amtumikie Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 17 Hata hivyo watu bado walitoa sadaka mahali pa sehemu za juu, lakini kwa Yahwe, Mungu wao pekee.
\s5
\v 18 Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli.
\v 19 Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maomabi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kambla ya kujinyenyekesha mwenyewe -- na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji. (Maandishi ya kale yanasema hivi, "tarehe ya Hozai," ambayo ni maandishi ya kifungu asili. Lakini matoleo mengi ya kisasa yamesahihisha na kusomeka "tarehe ya waonaj" Pia, matoleo machache ya kisasa yanasema "tarehe ya waonaji".).
\v 20 Kwa hiyo Manase akalala na babu zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\v 21 Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu.
\v 22 Akafanya yaliyokuwa uovu katika macho ya Yaahwe, kama Manase, baba yake, alivyofanya. Amoni alitoa sadaka katika sanamau zote za kuchonga ambazo alitengeneza Manase baba yake, na aliziabudu.
\v 23 Hakujinyenyekesha mbele za Yahwe, kama baba yake Manase alivyokuwa amefanya. Badala yake, Amoni huyu huyu alifanya makosa zaidi na zaidi.
\s5
\v 24 Watumishi wake wakapanga njama wa zidi yake na wakamua katika nyumba yake mwenyewe.
\v 25 Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya njama zidi ya Mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia, mwanaye, mfalme katika nafasi yake.
\s5
\c 34
\p
\v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala miaka thelathini na moja katika Yerusalemu.
\v 2 Alifanya yaliyohaki katika macho ya Yahwe, na alitembea katiaka njia za Daudi babu yake, ha hakugeuka mbali iwe kulia au kushoto.
\v 3 Kwa maana ndani ya miaka minane ya ya utawala wake, alipokuwa bado kijana, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, babu yake. Katika miaka ishirini, alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kutoka sehemu za juu, vituo vya Maashera, na sanamu za kuchonga na sanamu za chuma ya kuyeyushwa.
\s5
\v 4 Watu wakazivunja madhabahu za Baali katika uwepo wake; akazibomoa nguzo za Maashera na na zile sanamu za kuchonga, na sanamu za chuma ya kuyeyushwa katika vipande hadi zikawa mavumbi. Akayasamabaza mavumbi juu ya makaburi ya wale ambao walizitolea sadaka.
\v 5 Akaichoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao. Katika namna hii, akaisafisha Yuda na Yerusalemu.
\s5
\v 6 Alifanya hivyo hivyo katika miji ya Manase, Efraimu, na Simeoni, sehemu zote hadi Neftali, na katika maeneo yaliyoizunguka.
\v 7 Alizivunja madhabahu, akayapiga Maashera, na sanamu za kuchonga kuwa unga, na kuzisambaratisha madhabahu zote za uvumba katika nchi yote ya Israeli; kisha akarudi Yerusalemu.
\s5
\v 8 Sasa katika kipindi cha miaka ishirini ya utawala wake, baada ya Yosia kuisafisha nchi na hekalu, alimtuma Shafani mwana wa Azali, Manaseya, akida wa mji, na Yoa mwana wa Yoahazi katibu, kuikarabati nyumba ya Yahwe Mungu wake.
\v 9 Wakaenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, na wakakabidhi kwake fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumbaa ya Mungu, ambazo Walawi, walinzi wa milingo, walikuwa wamekusanya kutoka Manase na Efraimu, kutoka kwa masalia wote wa Israeli, kutoka Yuda yote na Benyamini, na kutoka kwa wakaaji wa Yerusalemu.
\s5
\v 10 Wakaikabidhi ile fedha kwa watu waliosimamia kazi ya hekalu la Yahwe. Watu wale wakawalipa wafanya kazi walioilikarabati na kulijenga tena hekalu.
\v 11 Wakawalipa maseremala na wajenzi kwa ajili ya kununulia mawe ya kuchonga na mbao kwa ajili ya kuungia, na kutengeneza boriti za nyumba amabazo baadha ya wafalme wa Yuda waliziacha zikachakaa.
\s5
\v 12 Watu waliifanya kazi kwa uaminifu. Wasimamizi wao Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, kutoka kwa wana wa Wakohathi. Walawi wengine, wote kati ya wale waliokuwa wanamziki wazuri sana, kwa ukaribu waliwaelekeza watendakazi.
\v 13 Walawi hawa walikuwa viongoziz wa wale waliobeba vifaa vya ujenzi na watu wengine wote waliofanya kazi kwa namna yoyote ile. Pia palikuwa na Walawi ambao walikuwa makatibu, watawala na walinda lango.
\s5
\v 14 Walipoileta fedha ambayo ilikuwa imeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, Hilkia yule kuhani akakiokota kitabu cha sheri ya Yahwe ambacho kilikuwa kimetolewa kupitia Musa.
\v 15 Hilkia akamwambia Shafani yule mwandishi, "Nimekiokota kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe". Hilikia akakileta kitabu kwa Shefani.
\v 16 Shefani akakipelek kitabu kwa mfalme, na pia akatoa taarifa kwake, akisema, "Watumishi wako wanafanya kila kitu walichokabidhiwa.
\s5
\v 17 Waliitoa feedha yote amabayo ilionekana katika nyumba ya Yahwe, na waliikabidhi katika mikono ya wasimamizi na watendakazi."
\v 18 Shefani mwandishi akamwambia mfalme." Hilkia kuhani amenipa kitabu." Kisha Shefani akamsomea mfalme katika hicho kitabu.
\v 19 Ikawa kwamba mfalme alipokuwa ameyasikia maneno ya sheria, aliyararua mavazi yake.
\s5
\v 20 Mflme akawaamuru Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwaandishi, na Asaya, mtumishi wake, akisema,
\v 21 "Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maani ni kikuu, kwa sababu babu zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake". (Badala ya "ambayo yamemiminwa juu yetu", baadhi ya matoleo yanasema " ambayo yamemulikwa zidi yetu").
\s5
\v 22 Kwa hiyo Hilkia, na wale ambao mfalme alikuwa amewaamuru, wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tohathi mwana wa Hasra, mtunza mavazi (aliishi katika Yerusalemu katika wilaya ya pili), na walizungumza naye katika namna hii.
\s5
\v 23 Akasema kwao, "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema: Mwambie mtu aliyewatuma kwangu,
\v 24 Hivi ndivyo Yahwe anasema: Ona, niko karibu kuleta maafa juu ya sehemu hii na wakaaaji wake, laana zote zilizoandikwa katika kitabu walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda.
\v 25 Kwa sababu wamenisahau na wametoa sadaka za uvumba kwa miungu mingine, ili kwamba waniweke katika hasira kwa matendo yote waliyofanya -- kwa hiyo hasira yangu itamiminwa juu ya hii sehemu, na haitazimishwa. (Badala ya "ambayo yamemiminwa juu yetu", baadhi ya matoleo yana "amabyo yamemlikwa zidi yetu".)
\s5
\v 26 Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumuuliza Yahwe alichopaswa kufanya, hivi ndivyo mtakavyosema kwake, 'Yahwe, Mungu wa Israeli anasema hivi: Kuhusu maneno uliyosika,
\v 27 kwa sababu moyo wako ulipondeka, na ulijinyenyekeza mbele yangu ulipoyasikia maneno yake zidi ya sehemu hii na wakaaji wake, na kwa sababu umejinyenyekeza mwenyewe mbele zangu, pia nimekusikiliza —hili ni azimio la Yahwe—
\v 28 ona, nitakukusanya kwa mababu zako. Utakusanywa katika kaburi lako kwa amani, na macho yako hayataona maafa yoyoye nitakayoleta juu ya sehemu hii na wakaaji wake". Wale watu wakarudisha ujumbe huu kwa mfalme.
\s5
\v 29 Mfalme akatuma wajumbe na kuwakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.
\v 30 Kisha mfalme akaenda kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda wakaaji wa Yerusalemu, na makuhani, Walawi, na watu wote, kuanzia wakubwa hadi wadogo. Kisha akasoma mbele zao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichokuwa kimeokotwa katika nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 31 Mfalme aksimama katika sehemu yake na kufanya aganao mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika agano ambayo yalikuwa yameandikwa katika kitabu hiki.
\v 32 Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
\s5
\v 33 Yosia akapeleka mbali mambo yote ya machukizo kutoka kwenye nchi iliyomilikiw na watu wa Israeli. Akamfanya kila mtu katika Israeli amwabudu Yahwe, Mungu wao. Kwa maisha siku zake zote, hawakugeka mbali kwa kutomfuata Yahwe, Mungu wa mababu zao.
\s5
\c 35
\p
\v 1 Yosia asherehekea Pasaka kwa ajili ya Yahwe katika Yerusalemu, na wakachinja wanakondoo katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
\v 2 Akawaweka makauhuni katika nafasi zao na akawatia moyo katika hudumza za nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 3 Akasema kwa Walawi waliowafundisha Israeli wote na waliokuwa wamewekwa wakifu kwa Yahwe. "Liwekeni sanduka takatifu katika nyumba ambayo Selemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli aliijenga. Msilibebe kuzunguka nalo tena mabegani mwenu. Sasa mwabuduni Yahwe Mungu wenu, na watumikieni watu wake Israeli.
\v 4 Jikusanyeni wenyewe kwa majina ya nyumba za babu zenu na zamu zenu, mkifuata maelekezo ya Daudi, mfalme wa Israeli, na yale ya Selemani, mwaye.
\s5
\v 5 Simeni katika sehemu takatifu, mkichukua nafasi zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa bdugu zenu, uzao wa watu, na mchukue sehemu zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa Walawi.
\v 6 Chinjeni wanakondoo wa Paska, jitakaseni wenyewe, andaeni wankondoo kwa ajili ya ndugu zenu, kufanya sawa sawa na neno la Yahwe ambalo lilitolewa kwa mkono wa Musa".
\s5
\v 7 Yosia akawapa watu wote wanakondoo elfu thelathini na wanambuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote walikuwepo. Pia akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalame.
\v 8 Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilki, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2, 600 na maksai mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Paska.
\v 9 Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi ndama elfu tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.
\s5
\v 10 Kwa hiyo huduma iliandaliwa, na makuhani wakasimama katika sehemu zao, pamoja na Walawi kwa zamu zao, kwa mjibu wa agizo la mfalme.
\v 11 Wakawachinja wanakondoo wa Pasaka, na makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi, na Walawi wakawachuna wanakondoo.
\v 12 Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, ili kuzisambaza katika makundi ya nyumba za mababu wa watu, ili wamtolee Yahwe, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vile vile kwa wale ng'ombe dume.
\s5
\v 13 Wakawaoka kwa moto wanakondoo wa Pasaka wakifuata maelekezo, kuhusu sadaka takatifu, walizichemsha kwenye vyungu, masufuria na makaangoni, na haraka wayapeleka kwa watu.
\v 14 Baadaye waliandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu makuhani, uzao wa Haruni, walikuwa wametingwa katika kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa na za mafuta hadi usiku ulipoingia, kwa hiyo Walawi wakaandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, wana wa Haruni.
\s5
\v 15 Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagiwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuviacha vituo vyao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizi kwa ajili yao.
\s5
\v 16 Kwa hiyo, wakati huo huduma yote ya Yahwe ilifanyika kwa ajili ya kusherekea Pasaka na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Yahwe, Kama alivyoamuru mfalme Yosia.
\v 17 Watu wa Israeli ambao walikuwepo wakaishika Sabato wakati huo, na kisha Sikukuu ya Mikate isiyochachwa kwa siku saba.
\s5
\v 18 Pasika kama hiyo haijafanyika tena katika Israeli tangu siku za nabii Samweli, wala hakuna mfalme yeyote miongoni mwa wafalme wa Israeli ambaye amewahi kusherekea Pasaka kama Yosia alivyofanya, pamoja na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na Israeli waliokuwepo, na wakaaji wote wa Yerusalemu.
\v 19 Pasaka hii ilitunzwa ndani ya miaka kumi na nane ya utawala wa Yosia.
\s5
\v 20 Baada ya haya yote, baada ya Yosia kuliweka hekalu katika utaratibu, Neko, mfalme wa Misiri, akaenda juu kupigana dhidi ya Karkemist karibu na mto Frati, na Yosia akaenda kupigana juu yake.
\v 21 Lakini Niko akatuma wajumbe kwake, akisema, "Nikufanye nini, mfalme wa Yuda? Leo siji kinyume nawe, lakini dhidi ya nyumba ambayo nafanya vita nayo. Mungu ameniamuru kuwahi, hivyo acha kumwingilia Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza."
\s5
\v 22 Hata hivyo, Yosia alipuuzia kurudi nyuma. Akajibadili ili apigane naye. Hakusikiliza maneno ya Neko ambayo yalikuja kutoka kwenye kinywa cha Mungu; hivyo akaenda kupigana kataika bonde la Megido.
\s5
\v 23 Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, na mfalme akawaambia watumishi wake, "Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya."
\v 24 Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alzikwa katika makaburi ya babu zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza.
\s5
\v 25 Yeremia akamwomboleza Yosia; waimbaji wote wa kiume na wa kike wakaomboleza kuhusu Yosia hata leo. Nyimbo hizi zikawa desturi katika Israeli; tazama, zimeandikwa katika nyimbo za maombolezo.
\v 26 Kwa mambao mengine kuhusu Yosia, na matendo yake mema aliyoyafanya katika utii kwa kile kilichoandikwa katika sheria ya Yahwe—
\v 27 na matendo yake, kutoka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
\s5
\c 36
\p
\v 1 Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoazi mwana wa Yosia, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake katika Yerusalemu.
\v 2 Yehoazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na akatawala miezi mitatu katita Yerusalemu.
\s5
\v 3 Mfalme wa Misiri akamwondoa katika Yerusalemu, na akaitoza nchi faini ya talanta za fedha mia moja na talanta moja ya dhahabu.
\v 4 Mfalme wa Misiri akamfanya Eliakimu, ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, na akambadili jina lake kuwa Yehoakimu. Kisha akamchukua ndugu yake Eliakimu - Yeahazi na kumpeleka Misiri.
\s5
\v 5 Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya ambayao yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
\v 6 Kisha Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli.
\v 7 Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.
\s5
\v 8 Kwa mambo mengine kuhusu Yehoyakimu, mambo mabaya aliyofanya, na yaliyopatikana zidi yake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Basi Yehoyakimu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
\s5
\v 9 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miezi mitatu na siku kumi katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe.
\v 10 Katika kipindi cha mwisho wa mwaka, mfalme Nebukadreza akatuma watu na wakampelekea Babeli, vitu vya thamani kutoka katika anyumba ya Yahwe, na kumfanya Sedekia ndugu yake, mfalame juu ya Yuda na Yerusalemu.
\s5
\v 11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka isshirini na moja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliokuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
\v 12 Hakujinyenyekesha mwenyewe mbele za Yeremia nabii, ambaye alisema kutoka kwenye kinywa cha Yahwe.
\s5
\v 13 Sedekia pia akaasi zidi ya Mfalme Nebukadreza, ambaye alikuwa amemfanya aape uaminifu kwake kupitia Mungu. Lakini Sedekia aliishupaza shingo yake na kuufanya moyo wake mgumu usigeuke kwa Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 14 Vilevile, viongozi wote wa makauhanai na wa watu hawakuwa waaminifu, na waliufuata uovu wa mataiafa. Waliigoshi nyumba ya Yahwe ambayo alikuwa ameitakasa katika Yerusalemu.
\s5
\v 15 Yahwe, Mungu wa babu zao, akatuma maneno kwao tena na tena kupitia wajumbe wake, kwa sababu alikuwa na huruma juu ya watu wake na juu ya sehemu anayoishi.
\v 16 Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, wakayadharau maneno yake, na kuwackeka manabii wake, hadi hasira ya Yahwe ilipoinuka zidi ya watu wake, hadi pailipokosekana msaada.
\s5
\v 17 Hivyo Mungu alimpeleka juu yao mfalme wa Wakaldayo, ambaye aliwaua vijana wao kwa upanga ndani ya patakatifu, na hakuwa na huruma juu ya vijana au mabikra, watu wazee au wenye mvi. Mungu akawatoa wote mikononi mwake.
\s5
\v 18 Vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za nyumba ya Yahwe, na hazina za mfalme na watumishi wake—vyote hivi akavipeleka Babeli.
\v 19 Wakaichoma moto nyumba ya Mungu, wakauangusha chini ukuta wa Yerusalemu, wakachoma ikulu zake zote, na wakaharibu vitu vizuri vyote ndani yake.
\s5
\v 20 Mfalme akawapeleka mbali Babeli wale waliokuwa wameoka na upanga. Wakawa watumishi kwa ajili yake na wanawe hadi utawala wa Waajemi.
\v 21 Hili lilitokea ili kulitimiza neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia, hadi nchi itakapokuwa imefurahia mapumziko ya Sabato yake. Iliishika Sabato kwa muda mrefu hadi kukataliwa kwake, ili miaka sabini itimie katika namna hii.
\s5
\v 22 Sasa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa, Yahwe akaipa hamasa roho ya Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba akafanya tangazo katika uflme wake wote, na akaliweka pia katika maandishi. Akasema,
\v 23 "Hivi ndivyo Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia. Ameniagiza nijenge nyumbaa kwa ajili yake katika Yerusalemu, ambao upo Yuda. Yeyote aliyemiongoni mwenu kutoma katika watu wake wote, Yahwe Mungu wenu, awe naye. Aende kwenye ile nchi."

531
15-EZR.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,531 @@
\id EZR
\ide UTF-8
\h Ezra
\toc1 Ezra
\toc2 Ezra
\toc3 ezr
\mt Ezra
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Yahwe akatimiza neno lake ambalo Yeremia alisema, na kuinua roho ya Koreshi. Sauti ya Koreshi ikasambaa na kusikika katika ufalme wake. Hiki ndicho kilichoandikwa na kusemwa:
\v 2 "Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa mimi ufalme wote wa dunia, na ameniteua mimi kumjengea yeye nyumba katika Yerusalem ya Yuda.
\s5
\v 3 Yeyote katika watu wake (Mungu awe pamoja naye) anaweza kwenda Yerusalem na kujenga nyumba kwa ajili ya Yahwe, Mungu wa Israel, Mungu ambaye yuko Yerusalem.
\v 4 Watu wa kila sehemu katika ufalme waliosalia katika nchi na kuishi wanapaswa kuwapa wao fedha na dhahabu, mali na wanyama, pamoja na kutoa kwa hiari kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem."
\s5
\v 5 Ndipo wakuu wa jamii ya Yuda na Benjamini, makuhani na walawi, na kila mmoja ambaye Roho wa Mungu alimwinua kuondoka na kujenga nyumba yake alisimama.
\v 6 Wale waliowazunguka karibu waliwasaidia kwa kuwapa fedha na vitu vya dhahabu, mali, wanyama, vitu vya thamani, na kutoa kwa hiari.
\s5
\v 7 Mfalme Koreshi akarusu vitu ambavyo vilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, ambavyo Nebukadreza alitoa kutoka Yerusalem na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.
\v 8 Koreshi akavikabidhi kwenye mikono ya Mithredathi mtunza fedha, ambaye akavitoa na kuhesabu kwa Sheshbaza, kiongozi wa Yuda
\s5
\v 9 Hii ilikuwa idadi yake: beseni thelathini za dhahabu, beseni elfu moja za fedha, beseni zingine ishirini na tisa,
\v 10 mabakuli thelathini ya dhahabu, mabakuli madogo ya fedha 410, na vitu elfu moja vya kuongezea.
\v 11 Kulikuwa na vitu 5, 400 vya fedha na dhahabu. Sheshbaza akavileta vyote wakati wa uhamisho kutoka Babeli kwenda Yerusalem.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Hawa ndio watu katika jimbo waliochukuliwa mateka na kwenda na mfalme Nebukadneza, yeye aliwachukua utumwani Babeli, watu wakarudi katika miji yao ya Yerusalem na Yuda.
\v 2 Walikuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari., Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndio idadi ya wanaume ya watu wa Israeli.
\s5
\v 3 Waporoshi: 2, 172
\v 4 Wana wa Shefatia: 372
\v 5 Wana wa Ara: 775.
\v 6 Wana wa Path-Moabu, kupitia Yeshua na Yoabu: 2, 812.
\s5
\v 7 Wana wa Eliamu: 1, 254.
\v 8 Wana wa Zatu: 945.
\v 9 Wana wa Zakai: 760.
\v 10 Wana wa Binui: 642.
\s5
\v 11 Wana wa Bebai: 623.
\v 12 Wana wa Azgadi: 1, 222.
\v 13 Wana wa Adonikamu: 666.
\v 14 Wana wa Bigwai: 2, 056.
\s5
\v 15 Wana wa Adini: 454.
\v 16 Wana wa Ateri kupitia Hezekiah: tisini na nane.
\v 17 Wana wa Besai: 323.
\v 18 Wana wa Harifu: 112.
\s5
\v 19 Wanaume wa Hashimu: 223.
\v 20 Wanaume wa Gibeoni: Tisini na tano.
\v 21 Wanaume wa Bethlehemu: 123.
\v 22 Wanaume wa Netofa: Hamsini na sita.
\s5
\v 23 Wanaume wa Anathothi: 128.
\v 24 Wanaume wa Beth-Azmawethi: Arobaini na mbili.
\v 25 Wanaume wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi: Mia saba arobaini na tatu.
\v 26 Wanaume wa Rama na Geba: 621.
\s5
\v 27 Wanaume wa Mikmashi: 122.
\v 28 Wanaume wa Betheli, na Ai: 223.
\v 29 Wanaume wa Nebo: Hamsini na mbili.
\v 30 Wanaume wa Magbishi: 156.
\s5
\v 31 Wanaume wengine wa Elamu: 1, 254.
\v 32 nne. Wanaume wa Harimu: 320.
\v 33 Wanaume wa Lodi, na Hadidi, na Ono: 725.
\s5
\v 34 Wanaume wa Yeriko: 345.
\v 35 Wanaume wa Senaa: 3, 630.
\s5
\v 36 Wana wa Yedaya kuhani wa nyumba ya Yoshua: 973.
\v 37 Wana wa Imeri: 1, 052.
\v 38 Wana wa Pashuri: 1, 247.
\v 39 Wana wa Harimu: 1, 017.
\s5
\v 40 Walawi: Wana wa Yeshua, na Kadmieli, wana wa Hodavia: Sabini na
\v 41 nne. Waimbaji hekaluni wana wa Asafu: 128.
\v 42 Walinzi: wana wa Shalumu, Ateri na, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai: 139 jumla.
\s5
\v 43 Wale walichaguliwa kuhudumu ndani ya Hekalu: wana wa Siha, Hasufa, Tabaothi:
\v 44 Keros, Siaha, Padoni.
\v 45 Lebana, Hagaba, Akubu,
\v 46 Hagabu, Salmai, Hanani
\s5
\v 47 Wana wa Gideli, Gahari, Reaya,
\v 48 Resini, Nekoda, Gazamu,
\v 49 Uza, Pasea, Besai,
\v 50 Asna, Meunimu, Nefusimu:
\s5
\v 51 Wana wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri:
\v 52 Basluthi, Mehida, Barsha:
\v 53 Barkosi, Sisera, Tema:
\v 54 Nesia, Tefa
\s5
\v 55 Wana wa watumishi wa Selemani: Wana wa Sotai, Soferethi, Peruda,
\v 56 Yaala, Darkoni, Gideli,
\v 57 Shefatia, Hatili, Pokereth-Sebaimu, Amoni,
\v 58 Walikuwa jumla ya watumishi mia tatu tisini na mbili waliochaguliwa kutumika katika Hekalu pamoja na wana wa watumishi wa Selemani.
\s5
\v 59 Wale ambao walitoka Tel-mela, Tel-harsha, Kerubu, Adani, na Imeri, Lakini hawakuweza kuthibitisha kizazi chao kilitoka Israeli-
\v 60 pamoja na mia sita hamsini na mbili wana wa Delaya, Tobia na Nekoda.
\s5
\v 61 Vilevile, kutoka kwa wana wa kuhani: Wana wa Habaya, Hakosi, Barzilai {ambaye alipata mke kutoka kwa binti ya Barzilai, Mgileadi na akaitwa kwa jina lao}
\v 62 Walitafuta kumbukumbu ya kizazi chao, lakini haikupatikana, hivyo wakaondolewa kwenye ukuhani kama wasiosafi.
\v 63 Hivyo kiongozi akawakataza wasile kitu chochote kitakatifu kilichotakaswa mpaka kuhani mwenye Urimu na Thumimu athibitishe.
\s5
\v 64 Jumla ya kundi 42, 360,
\v 65 ukiondoa watumishi na wasaidizi (wao walikuwa 7, 337) waimbaji Hekaluni wanaume na wanawake (mia mbili)
\s5
\v 66 Farasi wao: 736, Nyumbu wao: 245.
\v 67 Ngamia wao: 435. Punda wao: 6, 720.
\s5
\v 68 Walipokwenda kwenye nyumba ya Yahwe Yerusalem, wakuu wa mababa walijitoa kwa hiari kujenga nyumba.
\v 69 Walitoa kadiri ya uwezo wao katika kufadhili kazi: Dhahabu za darkoni sitini na moja elfu, mane za fedha elfi tano na mavazi mia moja ya makuhani.
\s5
\v 70 Basi makuhani na walawi, watu, waimbaji hekaluni, na walinzi wa getini, na wale waliochaguliwa kutumika katika Hekalu walikaa katika miji yao. Watu wote katika Israel walikuwa katika miji yao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ilikuwa miezi saba baaada ya watu wa Israeli kurudi kwenye miji yao, ndipo walipojikusanya pamoja kama mtu mmoja katika Yerusalem.
\v 2 Yeshua mwana wa Yosadaki na kaka yake kuhani, na Zerubabeli mwana wa Sheatieli na kaka yake wakainuka na kujenga madhabahu ya Mungu wa Israeli na kutoa sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoagizwa katika sheria ya Musa, Mtu wa Mungu.
\s5
\v 3 Ndipo wakaanzisha madhabahu juu ya msingi, kwa hofu waliokuwa nayo kwa sababu ya watu wa nchi/ Wakatoa sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe asubuhi na jioni.
\v 4 Pia vilevile wakaichunguza sikukuu ya vibanda kama ilivyoandikwa na wakatoa sadaka ya kuteketezwa siku kwa siku kama ilivyoagizwa, kila siku kwa siku yake.
\v 5 Kulikuwa na sadaka ya kila siku ya kuteketezwa na mwezi mara moja na sadaka za siku ya Yahwe za kudumu, pamoja na sadaka zote za hiari.
\s5
\v 6 Walianza kutoa sadaka za kuteketezwa za Yahwe siku ya kwanza ya mwezi wa saba, ingawa hekalu lilikuwa halijaanza kujengwa.
\v 7 Hivyo wakatoa fedha kwa wahunzi na fundi wa mkono, na wakawapa chakula, vinywaji na mafuta kwa watu wa Sidoni na Tiro, ili kwamba walete miti ya mierezi kupitia baharini kutoka Lebanoni mpaka Yafa, na kama walivyo ruhusiwa na mfalme Koreshi wa Uajemi.
\s5
\v 8 Ndipo mwezi wa pili katika mwaka wa pili baadae wakaja kwenye nyumba ya Mungu Yerusalem, Zerubabeli, Yoshua mwana wa Yosadaki, na baadhi ya makuhani na walawi na wale walikuja kutoka uhamishoni kurudi Yerusalem wakaanza kazi. Wakawachagua walawi walikuwa na miaka ishirini na zaidi kusimamia kazi ya nyumba ya Yahwe,
\v 9 Yoshua akamsimamisha kijana wake na kaka yake, Kadmiel na watoto wake, na kizazi cha yuda kusimamia kufanya kazi katika nyumba ya Mungu. Pamoja na wao kulikuwa na wana wa Henadadi, na uzao wao, na pia jamaa zao walawi.
\s5
\v 10 Wajenzi wakasimamisha msingi wa Hekalu la Yahwe, Na hii ikawawezesha makuhani kusimama na mavazi yao wakiwa na tarumbeta, na walawi wana wa Asafu, kumtukuza Yahwe kwa matoazi, kama mkono wa mfalme Daudi wa Israel alivyoagiza.
\v 11 Waliimba kwa kumsifu na kumshukuru Yahwe. "Yeye ni mwema! Agano lake ni kweli kwa Israel ladumu milele."Watu wote wakapiga kelele kwa sauti kuu za shangwe wakimsifu Yahwe kwa sababu misingi ya Hekalu ilikuwa imekamilika.
\s5
\v 12 Lakini wengi wa Makuhani, walawi, wakuu wa kale, na wazeee wa zamani walioiona nyumba ya kwanza, wakati misingi ilipowekwa wakaishuhudia kwa macho yao, walilia kwa sauti. Lakiniwengi walipiga kelele kwa sauti za shangwe na furaha na sauti za kushangaza.
\v 13 Na matokeo yake, watu hawakuweza kutofautisha sauti za furaha na sauti za shangwe na sauti za watu waliokuwa wanalia, kwa kuwa watu walikuwa wanalia kwa sauti kuu ya shangwe na sauti ilisikika kutoka mbali.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ndipo maadui wa Yuda na Benjamini waliposikia kwamba watu waliokuwa uhamishoni walikuwa wanajenga Hekalu la Yahwe, Mungu wa Israel.
\v 2 Hivyo wakamkaribia Zerubabeli na wakuu wa jamii yao. Wakawaambia,: Mturuhusu tujenge pamoja nanyi, kama ninyi, tunamtafuta mungu wenu, na tumejitoa kwake tangu siku ambapo, Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru alipotuleta mahali hapa."
\s5
\v 3 Lakini Zerubabeli, Yoshua na wakuu wa kale wa jamii wakasema, "sio wewe, lakini sisi ndio tunaowajibika kujenga nyumba ya Mungu wetu, Sisi ndio tutakaomjengea Yawe, Mungu wa Israel, kama vile mfalme koreshi mfalme wa Ashuru alivyoagiza."
\s5
\v 4 Hivyo watu wa nchi wakadhoofisha mikono ya wayahudi, wakawafanya wayahudi waogope kujenga nyumba.
\v 5 Pia wakawahonga washauri ili kuwachanganya katika mipango yao. Walitenda haya kipindi chote cha Koreshi na kipindi cha utawala wa Dario mfalme wa Uajemi.
\v 6 Tena katika kuanza kutawala kwake Ahasuero wakaandika mashitaka dhidi ya wenyeji wa Yuda na Yerusalem
\s5
\v 7 Ilikuwa siku za Ahasuero ambazo Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na wenzake wakamwandikia Ahasuero. Barua iliandikwa Kiaramu na kutafsiliwa.
\v 8 Rehumu jemedari na Shimshai mwandishi wakaandika hivi kwa Artashasta kuhusu Yerusalem.
\s5
\v 9 Tena Rehumu, Shimshai na wenzao ambao ni waamuzi na maofisa wengine wa Serikali, kutoka Waarkewi, Wababeli na washushami katika Waelami,
\v 10 nao wakaandika barua na waliungana na watu wakuu na mheshimiwa Asur - bani - pali aliwalazimisha kukaa Samalia pamoja na waliobaki katika mji ngambo ya mto.
\s5
\v 11 Hii ni nakala waliotuma kwa Artashasta: "Watumishi wako, watu wa mji ngambo ya mto, waandika hivi:
\v 12 Mfalme atambue kwamba Wayahudi waliotoka kwako wamefanya kinyume chetu hapa Yerusalem wamejenga mji wa uasi. Wamekamilisha ukuta na marekebisho ya misingi.
\s5
\v 13 Sasa mfalme atambue kwamba endapo mji utajengwa na kuta zake kukamilika, hawatatoa ushuru na kodi, lakini watawadhuru wafalme.
\s5
\v 14 Hakika kwa kuwa tumekula chumvi ya Ikulu, haitopendeza sisi kuona heshima ya mfalme inavunjwa, kwa sababu hiyo tunamtaarifu mfalme
\v 15 kufanya uchunguzi wa kumbukumbu ya baba yake, na kujiridhisha kuwa mji huu ulikuwa wa uharibifu ambao utawadhuru wafalme na miji. Ulisababisha matatizo mengi kwa wafalme na miji. Ilikuwa ni kitovu cha uhalibifu tokea siku nyingi. Ni kwa sababu hiyo mji uliteketezwa.
\v 16 Tunamtaarifu mfalme kuwa endapo mji na ukuta ukijengwa, Hakuna kitakachobakia kwa ajili yako katika mji ngambo ya mto."
\s5
\v 17 Ndipo mfalme akarudisha majibu kwa Rehumu na Shimshai na wenzao katika Samalia na waliobaki katika mji ngambo ya mto. "Amani iwe pamoja nanyi.
\v 18 Barua mliyonitumia imetafsiliwa na kusomwa kwangu.
\v 19 Hivyo niliagiza uchunguzi ufanywe na ikabainika kwamba zamani uliasi na kuwafitinisha wafalme.
\s5
\v 20 Wafalme wakuu walitawala Yerusalem yote na kuongoza kila sehemu ya mji ngambo ya mto. Ada na kodi walilipwa.
\v 21 Sasa, wekeni agizo kwa watu hawa wasiendelee na kujenga mji mpaka nitakapotoa amri.
\v 22 Muwe waangalifu msipuuze hili. Kwa nini kuruhusu tishio hili kuongezeka na kusababisha hasara kwa matakwa ya ufalme?
\s5
\v 23 Baada ya amri ya mfalme Artashasta kusomwa mbele ya Rehumu, Shimshai na wenzao, wakaondoka haraka kwenda Yerusalem, na wakawalazimisha Wayahudi kuacha kujenga.
\v 24 Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu Yerusalem ikasitishwa mpaka kutawala mara ya pili kwa mfalme Dario wa Uajemi.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ndipo Hagai nabii na Zakaria mtoto wa Ido nabii wakatabiri kwa jina la Mungu wa Israel kwa wayahudi wa Yuda na Yerusalem.
\v 2 Zerubabeli mtoto wa Shealtieli na Yoshua mtoto wa Yosadaki wakainuka na kuanza kujenga nyumba ya Mungu Yerusalem pamoja na manabii ambao waliwahamasisha wao.
\s5
\v 3 Ndipo Tatenai Mkuu wa mji ngambo ya mto, Shethar - Bozenai, na mshirika wao, wakaja na kusema kwao, "Nani aliyewapa agizo la kujenga nyumba hii na kukamilisha ukuta?"
\v 4 Vilevile walisema, "Ni majina ya watu gani wanaoshughulika na ujenzi huu?"
\v 5 Lakini jicho la Mungu lilikuwa pamoja na viongozi wa Wayahudi na maadui wao hawakuweza kuwazuia. Walikuwa wakisubiri barua kutumwa kwa mfalme na amri kurudi kwao kwa ajili ya suala hili.
\s5
\v 6 Hii ni nakala ya barua kwa Tatenai, mkuu wa mji ngambo ya mto, na Shethar - Bozenai na wenzao katika mji ngambo ya Mto, ambao waliwatuma kwa mfalme Dario.
\v 7 Wakatuma ujumbe, wakiandika kwa mfalme Dario, "Amani tele iwe kwako"
\s5
\v 8 Mfalme atambue kwamba tulikwenda Yuda kwenye nyumba ya Mungu Mkuu. Imeshajengwa kwa mawe makubwa na mbao zimewekwa katika kuta. Hii kazi inafanyika kwa utaratibu na inaendelea vizuri kwa mikono yao.
\v 9 Tukawauliza wazee, ni nani aliyewapa agizo la kujenga nyumba na ukuta?'
\v 10 Pia tuliwauliza majina yao ili kwamba ujue majina ya kila mtu ambaye aliwaongoza.
\s5
\v 11 Nao wakatujibu na kusema, "Sisi tu watumishi wa Mungu wa mbingu na nchi na sisi tunaijenga nyumba hii ambayo ilijengwa miaka mingi iliyopita wakati mfalme mkuu wa Israel alijenga na kuikamisha.
\s5
\v 12 Ingawa, watangulizi wetu walipomchukiza Mungu wa mbinguni, Mungu akawatia katika mikono ya mfalme wa Babeli Nebukadineza, ambaye alivunja nyumba na kuwachukua watu mateka Babeli.
\v 13 Pia, katika mwaka wa kwanza wa kutawala Koreshi mfalme wa Babeli, Koreshi aliamuru nyumba ya Mungu kujengwa.
\s5
\v 14 Mfalme Koreshi pia alirudisha vitu vya dhahabu na fedha vya nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kwenye hekalu Yerusalem na kuvipeleka kwenye hekalu Babeli. Naye akavitunza kwa Sheshbaza, ambaye alimchagua kuwa kiongozi.
\v 15 Naye akamwambia, "Chukua hivi vitu. Uondoke na kuviweka kwenye Hekalu Yerusalem. Na nyumba ya Mungu ijengwe kule."
\s5
\v 16 Ndipo huyu Sheshbaza akaja na kuweka msingi kwa nyumba ya Mungu katika Yerusalem: na ikaendelea kujengwa, lakini bado haijakamilika
\s5
\v 17 Sasa ikiwa itampendeza mfalme, na uchunguzi ufanyike kwenye nyumba ya ukumbusho Babeli Ikiwapo hukumu ya mfalme wa Koreshi ya kujenga nyumba ya Mungu Yerusalem. Na mfalme anaweza kutuma uamuzi wake kwetu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Na mfalme dario akaamuru uchunguzi ufanyike katika nyumba ya kumbukumbu Babeli.
\v 2 Na katika mji wa Akmetha huko media chuo kilionekana: Kumbukumbu yake ilisema:
\s5
\v 3 "Katika mwaka wa kwanza mfalme Koresh, Koreshi alitoa amri kuhusu nyumba ya Mungu Yerusalem:'Na nyumba ijengwe iwe sehemu ya kutoa dhabihu, misingi yake iwekwe, urefu wake uwe sitini,
\v 4 na upana wake uwe sitini, sehemu tatu za mawe makubwa na sehemu moja ya mbao mpya, na gharama hizo zitalipwa kutoka nyumba ya mfalme.
\v 5 Sasa vilirudishwe tena vitu vya dhahabu na fedha vilivyokuwa kwenye nyumba ya Mungu ambavyo Nebukadineza alivichukua kuvipeleka Babeli kutoka kwenye Hekalu Yerusalem. Na avirudishe tena Yerusalem Hekaluni. Na utaviweka tena kwenye nyumba ya Mungu.
\s5
\v 6 Sasa Tetanai, mkuu wa jimbo ngambo ya mto, Shethar - Bozenai na wenzao walio katika mji ngambo ya mto, wakajitenga,
\v 7 wakaacha kazi ya nyumba ya Mungu pekee. Viongozi na wazee wa kiyahudi watajenga nyumba ya Mungu mahali pake.
\s5
\v 8 Ninatoa agizo kwamba lazima lifanyike kwa wazee wa kiyahudi wanaojenga nyumba ya Mungu: Mchango kutoka kwa mfalme ushuru ngambo ya mto, utatumika katika kuwalipa watu hawa ili kwamba kazi yao isiweze kusimama.
\v 9 Chochote kitakachohitajika, ngombe wachanga, kondoo au kondoo wa sadaka ya kutekezwa kwa ajili ya Mungu wa mbinguni, ngano, chumvi, divai na mafuta kadri ya maagizo ya makuhani wa Yerusalem - wapatie vitu hivi kila siku bila kikomo.
\v 10 fanya hivyo ili kwamba wataleta sadaka kwa Mungu wa mbinguni na wataomba kwa ajili yangu mfalme na watoto wangu.
\s5
\v 11 Mimi nina agiza kwamba yeyote atakayevunja amri hii, Chuma kitolewe katika nyumba yake. Na awekwe juu yake. Na nyumba yake itabadilishwa kuwa takataka kwa sababu hii.
\v 12 Mungu huyu aliyesababisha jina lake kuwepo atamwondoa mfalme au mtu atakayebadili agizo hili au kuondosha nyumba ya Mungu katika Yerusalem. Mimi Dario nimeagiza hili, lifanyike kwa makini.
\s5
\v 13 Na kwa sababu ya amri iliyotumwa na mfalme Dario, Tatenai kiongozi mji ngambo ya mto na Sheshthar -Bozenai na wenzao. wakafanya kila kitu kama Mfalme Dario alivyoagiza.
\v 14 Hivyo wazee wa kiyahudi wakajenga kama Hagai na Zakaria walivyoelekeza kwa kutabiri. Wakajenga kama amri ilivyotolewa na Mungu wa Israel na Koreshi, Dario na Artashasta mfalme wa Uajemi.
\v 15 Nyumba ikakamilika siku ya tatu ya mwezi wa adari, katika mwaka wa sita wa kutawala mfalme Dario.
\s5
\v 16 watu wa Israel, makuhani, walawi na watu waliobaki wa uhamisho wakasheherekea kuweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.
\v 17 Wakatoa ngombe mia moja, kondoo mia moja na kondoo wengine mia nne kwa ajili ya kuweka wakfu nyumba ya Mungu. Mbuzi wa kiume kumi na wawili walitolewa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya waisrael wote kila kabila katika Israel.
\v 18 Pia wakawapa wajibu makuhani na walawi kufanya mgawanyo wa kazi ya Mungu katika Yerusalem. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa.
\s5
\v 19 Hivyo wale waliokuwa utumwani wakasherehekea pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
\v 20 Makuhani na walawi wakajitakasa wenyewe na wakachinja pasaka ya sadaka kwa ajili ya waliokuwa mateka wakiwemo na wao wenyewe.
\s5
\v 21 watu wa Israel ambao walikula nyama ya Pasaka ni wale waliorudi kutoka uhamishoni na walikuwa wamejitenga wenyewe kutoka kwa watu wasio safi wa nchi ile na kumchagua Yahwe, Mungu wa Israel.
\v 22 Walifurahi na kushangilia siku kuu ya mikate isiyochacha kwa siku saba, kwa sababu Yahwe amewarejeshea furaha na ameugeuza moyo wa mfalme wa Ashuru, na kuwatia nguvu kwa kazi ya nyumba, nyumba ya Mungu wa Israel.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Sasa baada ya hili, kipindi cha kutawala Artashasta mfalme wa Uajemi, Ezra akaja kutoka Babeli. Watangulizi wa Ezra walikuwa: Seraya, Azaria, Hilkia,
\v 2 Shalumu, Sadoki, Ahitubu,
\v 3 Amaria, Azaria, Merayothi,
\v 4 Zerahia, Uzi, Buki,
\v 5 Abishaua, Fineasi, Eliazari ambaye ni mtoto wa Haruni kuhani mkuu.
\s5
\v 6 Ezra akaja kutoka Babeli na alikuwa mtalaam mwandishi wa sheria ya Musa, ambayo Yahwe, Mungu wa Israel aliwapa. Mfalme akampatia kila kitu alichooomba kwa kuwa mkono wa Yahwe ulikuwa pamoja naye.
\v 7 Baadhi ya wazao wa Israel, na makuhani, walawi, waimbaji, walinzi, na wale waliochaguliwa kuhudumu katika Hekalu pia wakaenda Yerusalem katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.
\s5
\v 8 Naye akafika Yerusalem mwezi wa tano kama mwaka huo.
\v 9 Naye akaondoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. Ilikuwa siku ya kwanza ya mwezi wa tano ambapo alifika Yerusalem, kwa kuwa mkono mzuri wa Mungu ulikuwa pamoja naye.
\v 10 Ezra alikuwa ametoa moyo wake kusoma, kutenda, na kufundisha maagizo na sheria za Yahwe.
\s5
\v 11 Hii ndio amri ambayo mfalme Artashasta alimpa Ezra kuhani na mwandishi wa sheria za Yahwe na maagizo kwa Israeli.
\v 12 Mfalme wa wafalme Artashasta, kwa kuhani Ezra, mwandishi wa sheria za Mungu wa mbinguni.
\v 13 Ninatoa amri kwamba mtu yeyote Israel katika ufalme wangu pamoja na makuhani na walawi ambao wanatamani kwenda Yerusalem, wanaweza kwenda pamoja na wewe.
\s5
\v 14 Mimi mfalme na washauri wangu saba, tunawatuma wote kwenda kufahamu kuhusu Yuda na Yerusalem kuhusiana na sheria ya Mungu, ambayo iko mkononi mwako.
\v 15 Itakupasa kuleta Dhahabu na fedha ambazo walitoa kwa ajili ya Mungu wa Israel, ambaye makazi yake ni Yerusalem.
\v 16 Fedha iliyotolewa kwa hiari na Dhahabu yote iliyotolewa Babeli pamoja na matoleo ya hiari waliotoa watu na makuhani kwa ajili ya nyumba ya Mungu katika Yerusalem.
\s5
\v 17 Basi ununue vyote sadaka ya kondoo, beberu, kondoo, unga na kinywaji, uvitoe kwenye madhabahu ambayo ni nyumba ya Mungu wako katika Yerusalem.
\v 18 Fanya hivyo pamoja na sehemu ya fedha na dhahabu, vyovyote utakavyoona inakupendeza wewe na ndugu zako, kumpendeza Mungu.
\s5
\v 19 Viweke vitu vilivyotolewa kwa hiari mbele yako kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu Yerusalem.
\v 20 Kitu chochote kingine ambacho kinahitajika kwenye nyumba ya Mungu wako ambacho unahitaji, Gharama yake itatoka kwenye hazina yangu.
\s5
\v 21 Mimi mfalme Artashasta, natoa amri kwa wotunza hazina wote mjini ngambo ya mto, chochote Ezra atakachoomba kwenu anapaswa kupewa chote,
\v 22 hata zaidi ya talanta mia moja za fedha, vipimo mia vya ngano, bathi mia za divai na bathi mia za mafuta, pia na chumvi isiyo na kikomo.
\v 23 Chochote ambacho kimeamriwa kutoka kwa Mungu wa mbinguni, kifanye hicho kwa utukufu wa nyumba yake. Kwa nini hasira yake ije kwenye ufalme wangu na watoto wangu?
\s5
\v 24 Tutawapa taarifa wao kuhusu ninyi kwamba wasiwatoze ushuru wowote au kodi kwa kuhani, mlawi, mwimbaji, mlinzi au kwa mtu aliyechaguliwa kwenye huduma ya Hekalu na mtumishi katika nyumba ya Mungu.
\s5
\v 25 Ezra, kwa hekima aliyokupa Mungu, inakulazimu kuteua waamuzi na mtu muelewa kuwahudumia watu katika mji ngambo ya mto na kusaidia yeyote anayejua sheria za Mungu wako. Pia inakubidi ufundishe wale ambao hawajui sheria.
\v 26 Toa adhabu kwa yeyote asiyetii sheria ya Mungu au sheria ya mfalme, ikiwezekana kwa kifo, kuhamishwa, kuchukuliwa mali zake au kufungwa.
\s5
\v 27 Atukuzwe, Yahwe, Mungu wa watangulizi wetu, ambaye aliweka ndani ya moyo wa mfalme ili kutuza Nyumba ya Yahwe Yerusalem,
\v 28 ambaye akaendeleza agano kwangu kwa uaminifu mbele ya mfalme, na washauri wake na wakuu wake wenye mamlaka, nilitiwa nguvu na mikono ya Yahwe, Mungu wangu, nami nikawakusanya viongozi kutoka Israel kwenda pamoja nami.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Hawa ni viongozi wa watangulizi familia ambazo zilitoka babeli pamoja nami kipindi cha utawala wa mfalme Artashasta.
\v 2 Mwana wa Finehasi, Gershoni. Mwana wa Ithamari, Daniel. Mwana wa Daudi, Hatushi ambaye ni mwana Shekania,
\v 3 ambaye pia ni mwana wa Paroshi na Zekaria na pamoja na yeye kulikuwa na wanaume mia moja na hamsini walitajwa kwenye idadi ya ukoo wake.
\s5
\v 4 Wana wa Pahath- Moabu, Eliehoenai mwana wa Zerahia na pamoja naye wanaume mia mbili. Wana wa
\v 5 Shekaniah, Yahazieli na pamoja naye wanaume mia tatu. Wana wa
\v 6 adini, Ebedi mwana wa Yonathani na pamoja naye waliorodheshwa wanaume hamsini.
\v 7 Wana wa Elamu, Yeshaya mwana wa Athalia na pamoja naye waliorodheshwa wanaume sabini.
\s5
\v 8 Wana wa Shefatia, Zebadia, mwana wa Mikaeli na pamoja naye waliorodheshwa wanaume themanini.
\v 9 Wana wa Yoabu, Obadia mwana wa Yehieli pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia mbili kumi na wanane. Wana wa Binui,
\v 10 Sheromithi, mwana wa Yosifia na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na sitini.
\v 11 Wana wa Bebai, zekaria mwana wa Bebai na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume ishirini na wanane.
\s5
\v 12 Wana wa Azgadi, Yohana mwana wa Hakatani na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume mia moja na kumi.
\v 13 Wale wana wa Adonikamu wakaja baadaye. Na haya ndio majina yao: Elifereti, Yeueli na Shemaya na pamoja na wao wakaja wanaume sitini.
\v 14 Wana wa Bigwai, Uthai, mwana wa zabudi na pamoja na yeye waliorodheshwa wanaume sabini
\s5
\v 15 Nikawakusanya wasafiri bandari iliyokuwa inaelekea Ahava. Tukaweka kambi muda wa siku tatu, nikawachunguza watu na makuhani, lakini sikuwaona wana wa Levi miongoni.
\v 16 Hivyo nikatuma kwa Eliezeri, arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu na Elnathani na Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na kwa Yoyaribu na Elnathani ambao walikuwa ni walimu.
\s5
\v 17 Tena nikawatuma kwa Ido, kiongozi wa Kasifia. Nikawaaambia kile watachomweleza Ido. na jamaa zake, watumishi wa Hekalu waliishi Kasifia, kwa hiyo, kutuma kwetu watumishi kwa ajili ya nyumba ya Mungu.
\s5
\v 18 Hivyo wakatutuma sisi kwa Mungu na mkono mzuri wa mtu aliyeitwa Ishekeli. Alikuwa mwana wa mali Mwana wa Levi mwana wa Israel. Akaja na wana kumi na wanane na ndugu,
\v 19 pamoja naye Hashabia, pamoja na Yeshaya wa wana wa Merari na ndugu zake na wana wake jumla watu ishirini wote. Miongoni
\v 20 mwao walichaguliwa kutumika katika Hekalu, ambapo Daudi na wakuu waliwapa kuwahudumia walawi: mia mbili ishirini kila mmoja wao aliagizwa kwa majina.
\s5
\v 21 Tena nikatangaza kufunga mto Ahava ili kujinyenyekeza mbele za Mungu, kutafuta njia iliyoonyoka kutoka kwake kwa ajili yetu, watoto wetu na mali zetu,
\v 22 Niliona aibu kumwomba mfalme kwa ajili ya jeshi au mpandafarasi kwa ajili ya kutulinda tunapokuwa njiani, tangu tumemwambia mfalme "mkono wa Mungu uko pamoja na wote wanaomtafuta kwa mazuri. lakini uweza wake na ghazabu yake ni juu ya wale wote wanaomwasi yeye.
\v 23 Hivyo tulifunga na kumsihi Mungu kwa jambo hilo.
\s5
\v 24 Tena nikachagua watu kumi na wawili kutoka kwa kuhani: Sherebia na Hashabia na ndugu zao wengine kumi.
\v 25 Nikapima kwa ajili yao fedha, dhahabu na vyombo na sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu kwa wafalme, washauri, na wakuu na Israel wote walitoa kwa hiari.
\s5
\v 26 Hivyo nikawapimia kwenye mikono yao talanta za fedha mia sita na hamsini, talanta mia moja ya vyombo vya fedha, talanta mia moja za dhahabu.
\v 27 vifaa ishirini vya dhahabu kwa pamoja vilikuwa na thamani ya elfu moja darkoni na vitu viwili vya sanamu vivyonakshiwa kama dhahabu ya kupendeza.
\s5
\v 28 Kisha nikawaambia, mmewekwa wakfu kwa Bwana, na hivi vyombo pia na fedha na dhahabu, vimetolewa kwa hiari kwa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu.
\v 29 mviangalie na kuvitunza hadi mtakapovipima mbele ya makuhani, walawi, na viongozi wa wataangulizi wa jamii ya Israel katika Yerusalem katika nyumba ya Mungu.
\v 30 Makuhani na walawi walikubali vipimo vya fedha na dhahabu na vyombo kwa ajili ya kuvichukua na kuvipeleka Yerusalem, kwenye nyumba ya Mungu wetu.
\s5
\v 31 Tukatoka kwenda mto Ahava siku ya kumi na mbili katika mwezi wa kwanza kwenda Yerusalem, Mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, ulitulinda na mikono ya adui na wale waliotaka kutufanyia fujo njiani.
\v 32 Hivyo tukaingia Yerusalem na kukaa humo kwa siku tatu.
\s5
\v 33 Tena siku ya nne fedha na dhahabu na vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa mikono ya Meremothi mwana wa Uria kuhani, na pamoja nao alikuwepo Eleazari mwana wa Finehasi, Yozabadi mwana wa Yeshua, na Noadia mwana wa Binui, Walawi.
\v 34 Idadi na uzito wa kila kitu uliweza kujulikana. Uzito wote uliweza kuandikwa katika kipindi hicho
\s5
\v 35 Na wale waliokuja kutoka matekani, watu wa uhamisho, wakatoa sadaka ya kutekezwa kwa Mungu wa Israel, kondoo tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi wa kiume kumi na wawili kama sadaka ya dhambi. Zote zilikuwa sadaka za kutekezwa kwa ajili ya Yahwe.
\v 36 Tena wakawapa amri za mfalme kwa wakuu wa wafalme na wakuu katika mji ngambo ya mto, na wakawasaidia watu na nyumba ya Mungu.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kipindi mambo hayo yanatendeka, wakuu wakaja kwangu na kuniambia,"Watu wa Israel, Makuhani na walawi hawakuweza kujitenga wenyewe kutoka kwa watu wa nchi zingine na maovu yao: Wakanaani, Wahiti, Waperuzi, wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori.
\v 2 Kwa kuwa wamewachukua baadhi ya binti na watoto wa kiume, wamejichanganya watu watakatifu na watu wa nchi nyingine na wakuu na viongozi wamekuwa wa kwanza katika imani hii potofu.
\s5
\v 3 Niliposikia haya, nikachana nguo zangu na kanzu na kunyoa nywele kichwani na ndevu na nikakaa chini kutafakari.
\v 4 Na wale wote waliotetemeka kwa neno la Mungu wa Israel kuhusu imani potofu walikusanyika kwangu wakati nimakaa chini nikiwa na aibu hadi kufikia kipindi cha sadaka za jioni.
\s5
\v 5 Lakini katika sadaka ya jioni nikasimama kwenye nafasi yangu nikiwa mnyenyekevu na nguo ilichanika na kanzu, na nikapiga magoti na kunyoosha mikono yangu kwa Yahwe Mungu wangu. Nikasema
\v 6 "Mungu wangu, nina aibu na sistahili kuinua uso wangu kwako, makosa yetu yamekuwa hadi kuvuka kichwani na maovu yetu yameongezeka kufika mbinguni.
\s5
\v 7 Kuanzia siku ya watangulizi wetu mpaka sasa tumekuwa katika maovu makuu. Makosa yetu, viongozi, makuhani, walikuwa katika mikono ya mfalme wa dunia hii, katika upanga, matekani na kunyanyaswa na tuna aibu ya uso hata leo.
\s5
\v 8 sasa kwa kipindi kifupi, neema kutoka kwa Yahwe Mungu wetu imekuja kutuacha mabaki wachache na kutupa kuhimmili sehemu takatifu. Hii ilikuwa ni kwa ajili ya Mungu wetu kututia nuru macho yetu na kutupa unafuuu sisi tulio watumwa.
\v 9 Kwa kuwa sisi tu watumwa, lakini Mungu bado hajatusahau lakini ameongeza agano la uaminifu kwetu, ameyatenda haya mbele ya macho ya mfalme wa Uajemi ili kwamba haweze kutupatia nguvu mpya. Ili kwamba tuweze kujenga nyumba ya Mungu na tuweze kuondoa majuto. Alitenda hayo ili kwamba aweze kutupatia msingi wa usalama katika Yuda na Yerusalem.
\s5
\v 10 Lakini sasa Mungu wetu, tuseme nini baaada ya haya? Tumesahau amri zako.
\v 11 amri ambazo uliwapa manabii watumishi wako, pale uliposema, "Nchi hii mnayoingia kuimiliki ni nchi chafu. Imechanganyikana na watu wasio na utaratibu. ameenea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa uchafu wao.
\v 12 Hivyo sasa, msiwape binti zenu kwa watoto wao, msichukue binti zao kwa ajili ya watoto wenu, msitafute amani kwao na fadhili, ili kwamba muweze kuwa imara na kula vizuri vya nchi, hivyo utasababisha watoto wenu kumiliki kwa wakati wote."
\s5
\v 13 Baada ya yote kutokea kwetu kwa sababu ya uovu wetu na makosa yetu makuu, tokea hapo, Mungu wetu, hukutazama makosa yetu na kutuadhibu tulivyostahili na ukatuacha kama mabaki.
\v 14 Tunaweza kuvunja tena amri zako na kuingiliana katika ndoa, na hawa watu wasiofuata utaratibu? Je hautachukia na kututowesha sote hakuna wa kubaki, hakuna wa kutoroka?
\s5
\v 15 Yahwe, Mungu wa Israel, wewe ni mwenye haki, kwa kuwa tumebaki wachache mabaki hadi siku ya leo. Tazama, tuko mbele yako na makosa yetu, kwa kuwa hakuna hata mmoja anayeweza kusimama mbele kwa sababu ya hili.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Wakati Ezra akiomba na kutubu, akalia na kujirusha chini mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa la wanaume Israel, wanawake na watoto wakakusanyika kwake, kwa kuwa watu walikuwa wakilia sana.
\v 2 Shekania mtoto wa Yehieli, mwana wa Elamu akamwambia Ezra, "Tumekuwa sio waaminifu kwa Mungu na tumeoa wanawake wa kigeni kutoka nchi nyingine. Lakini pamoja na hilo, bado kuna tumaini kwa Israel.
\s5
\v 3 sasa natuweke agano pamoja na Mungu wetu kuwaondoa wanawake wote na watoto wao kulingana na maelekezo ya Bwana, na maelekezo ya wale wanaotetemeka kutokana na amri za Mungu wetu. na hii ifanyike kutokana na sheria.
\v 4 Simama, jambo hili linakuhusu wewe, na sisis tuko pamoja na wewe, Uwe imara na kufanya hili.
\s5
\v 5 Hivyo Ezra akasimama na kufanya makuhani na walawi na waisrael wote wakaahidi kufanya kwa njia hiyo. Hivyo wote wakatoa kiapo.
\v 6 Ndipo Ezra akainuka kutoka mbele ya nyumba ya Mungu na kwenda kwenye chumba ya Yehohanani mtoto wa Eliashibu, Yeye hakula mkate au kunywa maji. Tangu alipokuwa akiomboleza kuhusiana na wale wenye imani haba waliokuwa uhamishoni.
\s5
\v 7 Hivyo wakatuma neno katika Yuda na Yerusalem kwa watu wote waliorudi kutoka utumwani kukusanyika Yerusalem.
\v 8 Yeyote ambaye hakuja katika siku tatu kutokana na maelekezo kutoka kwa wakuu na viongozi atachukuliwa mali zote na atatengwa na kusanyiko kuu la watu ambao walikuja kutoka uhamisho.
\s5
\v 9 Hivyo watu wote wa Yuda na Benjamini wakakusanyika Yerusalem kwa siku tatu. Ilikuwa ni mwezi wa tisa na siku ya ishirini ya mwezi. watu wote wakasimama mbele ya nyumba ya Mungu na wakatetemeka kwa sababu ya neno na mvua.
\v 10 Ezra kuhani akasimama na kusema, "Ninyi wenyewe mmefanya uasi, ninyi mmeishi na wanawake wa kigeni na kuongeza makosa ya Israel.
\s5
\v 11 Lakini sasa mpeni sifa Yahwe, Mungu wa watangulizi wenu, na mfanye mapenzi yake, mjitenge na watu wa nchi na wanawake wa kigeni.
\s5
\v 12 Kusanyiko lote likajibu kwa sauti. "Tutatenda kama ulivyosema,
\v 13 haijalishi, kuna watu wengi na ni kipindi cha mvua. Hatuna nguvu ya kusimama nje na hii si siku moja au mbili za kufanya kazi, kwa kuwa tumekosea katika jambo hili.
\s5
\v 14 Hivyo wakuu wetu wawakilishe kusanyiko lote, iwe kwamba wote walioruhusu wanawake wa kigeni kuishi katika miji yetu waje katika muda uliopangwa na viongozi wa mji na waamuzi wa mji hadi hapo hasira ya Mungu itakapoondoka kutoka kwetu.
\v 15 Yonathan mtoto Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa wakapinga hili, Meshulamu na Shabethai mlawi wakawaunga mkono wao.
\s5
\v 16 Hivyo watu waliotoka uhamishoni wakafanya hivi, Ezra kuhani akachagua wanaume, viongozi watamgulizi wa ukoo na nyumba, wao wote kwa majina na wakaliangalia suala hili siku ya kwanza ya mwezi wa kumi.
\v 17 Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kuchunguza wale wanaume walioishi na wanawake wa kigeni.
\s5
\v 18 Miongoni mwa wana wa kikuhani kuna wale walioishi na wanawake wa kigeni. Miongoni mwa wana wa Yoshua mtoto wa Yosadaki na kaka zake ambao walikuwa Maasela, Eliazeri, na Yaribu na Gedalia.
\v 19 Hivyo wakaamua kuwaondoa wake zao. kwa kuwa walikuwa na makosa, wakatoa sadaka ya kondoo kwenye mifugo kwa ajili ya makosa yao.
\s5
\v 20 Miongoni mwa wana wa Imeri, Hanani, na Zebadia.
\v 21 Miongoni mwa wana wa Harimu, Maaseya, na Eliya na Shemaya, na Yehieli na Uzia.
\v 22 Miongoni mwa wana wa Pashuri, Elasa
\s5
\v 23 Miongoni mwa walawi: Yozabadi na Shimei na Kelaya (ndiye Kelita) na Pethaia, na Yuda na Eliezeri. Miongoni mwa waimbaji Eliashibu na. Miongoni mwa walinzi Shalumu, Telemu na Uri.
\v 24 Miongoni mwa Israel waliobaki -
\v 25 Miongoni mwa wana wa Paroshi, Ramia na Izia na Malkiya na Miyamini na Eliazari na Malkiya na Benaya
\s5
\v 26 Miongoni mwa wana wa Elamu Mataniana Zekaria, na yeehieli, na Abdi na Yeremothi na Eliya.
\v 27 Miongoni mwa wana wa Zatu: Elionai, na Eliashibu, na Matania na Yeremothi na Zabadi na Aziza.
\v 28 Miongoni mwa wana wa Bebai Yehohanani, na Hanania na Zakai na Athlai.
\v 29 Miongoni mwa wana wa bani: Meshulami na Maluki, na Adaya na Yashubu na Sheali na Yeremothi.
\s5
\v 30 Miongoni mwa wana wa Pahath-Moabu, Adna, na kelali, na Benaya na Maaseya, na Matania, na Besaleli na Binti na Manase.
\v 31 Na miongoni mwa wana wa Harimu: Eliezeri na Ishiya, na Malkiya na Shemaya na Shimeoni, na
\v 32 Benyamini na Maluki na Shemaria
\s5
\v 33 Miongoni mwa wana Hashumu: Matenai, na Matatana Zabadi, na Elifereti na Yeremai, na Manase, na Shimei.
\v 34 Miongoni mwa wana wa Bani: Maadai, na Amramu na Aueli, na
\v 35 Benaya, na Bedeya na Keluhi, na
\v 36 wania, na Meremothi, Eliashibu,
\s5
\v 37 Matania, na Matenai. na
\v 38 Yaasi. Miongoni mwa wana wa Binui: Shimei,
\v 39 Sheremia, na Nathani, na Adaya, na
\v 40 Maknadebai, na Shashai, na Sharai
\s5
\v 41 Azareri, na Sheremia, na Shemaria, na
\v 42 Shalumu, na Amaria, na Yusufu.
\v 43 Miongoni wa wana wa Nebo: Yeieli, na Mathiana zabadi, na Zebina, na Ido, na Yoeli na Benaya.
\v 44 Hawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni na walikuwa wamezaa watoto baadhi yao.

767
16-NEH.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,767 @@
\id NEH
\ide UTF-8
\h Nehemia
\toc1 Nehemia
\toc2 Nehemia
\toc3 neh
\mt Nehemia
\s5
\c 1
\p
\v 1 Maneno ya Nehemia mwana wa Hakalia Ikawa, katika mwezi wa Kisleu, katika mwaka wa ishirini, nilikuwa katika mji mkuu wa Sushani,
\v 2 mmoja wa ndugu zangu, Hanani, alikuja pamoja na watu wengine kutoka Yuda, nami nikawauliza kuhusu Wayahudi waliopona, Wayahudi waliosalia waliokuwa huko, na kuhusu Yerusalemu.
\s5
\v 3 Wakaniambia, "Wale waliokuwa katika mkoa ule waliookoka katika kifungo wapo katika shida kubwa na aibu kwa sababu ukuta wa Yerusalemu umebomolewa na milango yake imeteketezwa kwa moto."
\s5
\v 4 Na mara tu niliposikia maneno haya, nikakaa na kulia, na kwa siku niliendelea kuomboleza na kufunga na kuomba mbele ya Mungu wa mbinguni.
\v 5 Ndipo nikasema, "Wewe ndiwe Bwana, Mungu wa mbinguni, Mungu uliye mkuu na kushangaza, unayetimiza agano na upendo wa kudumu pamoja na wale wanaokupenda na kushika amri zake.
\s5
\v 6 Sikiliza maombi yangu na fungua macho yako, ili uisikie sala ya mtumishi wako kwamba sasa nasali mbele yako mchana na usiku kwa ajili ya watu wa Israeli watumishi wako. Mimi ninakiri dhambi za watu wa Israeli, ambazo tumefanya dhidi yako. Wote mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.
\v 7 Tumefanya uovu sana juu yako, na hatukuzingatia amri, sheria, na hukumu ambazo ulimwamuru mtumishi wako Musa.
\s5
\v 8 Tafadhali kumbuka neno ulilomuamuru mtumishi wako Musa, 'mkitenda pasipo uaminifu, nitawatawanya kati ya mataifa,
\v 9 lakini mkirudi kwangu na kufuata amri zangu na kuzifanya, ingawa watu wako walienea chini ya mbingu za mbali, Nami nitawakusanya kutoka huko na kuwaleta mahali pale nilipopachagua ili kulifanya jina langu.'
\s5
\v 10 Sasa wao ni watumishi wako na watu wako, ambao uliwaokoa kwa nguvu yako kubwa na kwa mkono wako wenye nguvu.
\v 11 Bwana, naomba, sikiliza sasa maombi ya watumishi wako na sala ya watumishi wako ambao hufurahia kuheshimu jina lako. Sasa unifanikishe mimi mtumishi wako leo, na unijalie rehema mbele ya mtu huyu." Nilikuwa mnyweshaji wa mfalme.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Katika mwezi wa Nisani, katika mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, alichagua divai, na nikachukua divai na kumpa mfalme. Sasa sikuwahi kusikitikaa mbele yake.
\v 2 Lakini mfalme akaniambia, "Kwa nini uso wako una huzuni? Hauonekani kuwa mgonjwa. Hii lazima iwe huzuni ya moyo." Kisha nikaogopa sana.
\s5
\v 3 Nikamwambia mfalme, "Mfalme aishi milele! Kwa nini uso wangu usiwe na huzuni? ikiwa mji, mahali pa makaburi ya baba yangu, uko katika magofu, na malango yake yameharibiwa kwa moto."
\s5
\v 4 Ndipo mfalme akaniambia, "Unataka nini nifanye?" Kwa hiyo nikamwomba Mungu wa mbinguni.
\v 5 Nikamwambia mfalme, "Mfalme akiona vema, na ikiwa mtumishi wako amefanya vizuri machoni pako, unaweza kunituma Yuda, mji wa kaburi za baba zangu, ili nipate kuujenga tena."
\v 6 Mfalme akanijibu (na malkia pia alikuwa amekaa karibu naye), "Utakaa kawa muda gani mpaka urudi?" Mfalme akaona vema kunipeleka nami nikampka muda.
\s5
\v 7 Ndipo nikamwambia mfalme, "Ikiwa itampendeza mfalme, nipe barua kwa ajili ya wakuu ng'ambo ya Mto, ili wapate kuniruhusu nipite katika maeneo yao njiani kwenda Yuda.
\v 8 Pia iwepo barua kwa Asafu, mlinzi wa msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kufanya mihimili ya malango ya ngome karibu na hekalu, na kwa ukuta wa mji, na kwa nyumba ambayo Nitaishi." Kwa hiyo kwa sababu mkono mzuri wa Mungu ulikuwa juu yangu, mfalme alinipa hitaji langu.
\s5
\v 9 Nilifika kwa wakuu ng'ambo ya Mto, na kuwapa barua za mfalme. Basi mfalme alikuwa amepeleka maofisa wa jeshi na wapanda farasi pamoja nami.
\v 10 Sanbalati Mhoroni na Tobbia mtumishi wa Amoni waliposikia jambo hili, walipendezwa sana kwa kuwa mtu alikuja ambaye alikuwa akijaribu kuwasaidia watu wa Israeli.
\s5
\v 11 Basi, nikarudi Yerusalemu, na nilikuwa huko siku tatu.
\v 12 Niliamka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami. Sikumwambia mtu yeyote kile Mungu wangu alichoweka ndani ya moyo wangu kufanya Yerusalemu. Hakukuwa na mnyama pamoja nami, isipokuwa yule niliyekuwa nimempanda.
\s5
\v 13 Niliondoka usiku kwa njia ya lango la bondeni, kuelekea kisima cha joka na kwenye mlango wa jaa, na kukagua kuta za Yerusalemu, ambazo zimebomolewa, na milango ya mbao iliharibiwa na moto.
\v 14 Kisha nikaenda kwenye lango na Chemchemi ya Mfalme. Nafasi ilikuwa nyembamba sana kwa mnyama niliyekuwa nimempanda kupita.
\s5
\v 15 Kwa hiyo nilikwenda usiku huo kando ya bonde na kuchunguza ukuta, nikarudi nyuma na kuingia kwa lango la bondeni, na hivyo nikarudi.
\v 16 Watawala hawakujua nilipokwenda au kile nilichofanya, na sikuwaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala watawala, wala wengine waliofanya kazi hiyo.
\s5
\v 17 Nikawaambia, "Unaona shida tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu iko katika magofu na milango yake imeharibiwa kwa moto. Njoni, tujenge upya ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe na aibu tena."
\v 18 Niliwaambia kuwa mkono mzuri wa Mungu wangu ulikuwa juu yangu na pia kuhusu maneno ya mfalme ambayo aliniambia. Wakasema, "Hebu tuondoke na kujenga." Kwa hiyo wakaimarisha mikono yao kwa ajili ya kazi nzuri.
\s5
\v 19 Lakini Sanbalati Mhoroni, na Tobia mtumishi wake Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, waliposikia habari hiyo, wakatucheka na kututukana; wakasema, "Unafanya nini? Je, unamgombana na mfalme?"
\v 20 Ndipo nikawajibu, "Mungu wa mbinguni atatupa ufanisi. Sisi ni watumishi wake na tutaondoka na kujenga. Lakini huna sehemu, hakuna haki, na hakuna dai la kihistoria huko Yerusalemu."
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kisha Eliashibu, kuhani mkuu, akasimama pamoja na ndugu zake makuhani, wakajenga lango la kondoo. Walitakasa na kuweka milango yake. Waliweka wakfu hadi mnara wa Hamea na hadi mnara wa Hananeli.
\v 2 Baada yao watu wa Yeriko walijenga, na baada yao Zakuri mwana wa Imri alijenga.
\s5
\v 3 Wana wa Senaa wakajenga lango la samaki. Wanaweka mihimili yake na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake.
\v 4 Meremoth aliandaa sehemu inayofuata. Yeye ni mwana wa Uria mwana wa Hakosi. Na baada yao Meshulamu akatengeneza. Yeye ni mwana wa Berekia mwana wa Meshezabeli. Karibu nao Sadoki akatengeneza. Yeye ni mwana wa Baana.
\v 5 Baada yao Watekoi wakatengeneza, lakini viongozi wao walikataa kufanya kazi iliyoagizwa na wakuu wao.
\s5
\v 6 Yoyada mwana wa Pasea, na Meshulamu mwana wa Besodeya, walitengeneza lango la Kale. Wanaweka mihimili, na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake.
\v 7 Nao, Melatia Mgibeoni, na Yadoni Meronothi, watu wa Gibeoni na Mispa, walifanyia matengenezo juu ya sehemu ambapo mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto aliishi.
\s5
\v 8 Na baada yake Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa wafua dhahabu, akatengeneza; na baada yake Hanania, mtengenezaji wa manukato. Wakajenga tena Yerusalemu mpaka Ukuta mpana.
\v 9 Na baada yao Refaya mwana wa Huri akajenga. Alikuwa mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu.
\v 10 Na baada yao Yedaya mwana wa Harumafu akajenga karibu na nyumba yake. Na baada yake Hatushi mwana wa Hashabneya akajenga.
\s5
\v 11 Malkiya mwana wa Harimu na Hashubu mwana wa Pahat Moabu, wajenga sehemu nyingine pamoja na mnara wa tanuu.
\v 12 Baada yao Shalumu mwana wa Haloheshi, mkuu wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, akajenga, pamoja na binti zake.
\s5
\v 13 Hanuni na wenyeji wa Zanoa walijenga lango la bondeni. Walijenga tena na kuweka milango yake, na vyuma vyake na makomeo yake. Walijenga dhiraa elfu hadi lango la jaa.
\s5
\v 14 Malkiya, mwana wa Rekabu, mkuu wa wilaya ya Beth-Hakeremu, akajenga lango la jaa. Alijenga na kuweka milango yake, na vyuma vyake na makomeo yake.
\v 15 Shalumu mwana wa Kolhoze, mkuu wa wilaya ya Mispa, akajenga lango la Chemchemi. Alijenga, na kuweka kifuniko juu yake na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake. Alijenga upya ukuta wa Pwani wa Silowamu kwa bustani ya mfalme, hadi ngazi ya kuongoza kutoka mji wa Daudi.
\s5
\v 16 Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-suri, akajenga mahali hapo, toka maburini ya Daudi, mpaka birika lililojengwa na watu, na nyumba ya watu wenye nguvu.
\v 17 Baada yake, Walawi walijenga, pamoja na Rehumi mwana wa Bani na baada yake, Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila, kwa wilaya yake.
\s5
\v 18 Baada yake watu wa nchi zao walijenga, ikiwa ni pamoja na Binui mwana wa Henadadi, mkuu wa nusu ya wilaya ya Keila.
\v 19 Baada yake alijenga Ezeri, mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alijenga sehemu nyingine kuelekea ghala ya silaha, kwenye kona ya ukuta.
\s5
\v 20 Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akajenga kwa hiari sehemu nyingine, toka kona ya ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu.
\v 21 Baada yake Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, akajenga sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.
\s5
\v 22 Kisha baada yake makuhani, watu wa eneo hilo karibu na Yerusalemu, walijenga.
\v 23 Baada yao Benyamini na Hashubu walijenga kuielekea nyumba yao. Baada yao Azaria mwana wa Maaseya, mwana wa Anania, alijenga karibu na nyumba yake.
\v 24 Baada yake Binui mwana wa Henadadi akajenga sehemu nyingine, kutoka nyumba ya Azaria hadi kona ya ukuta.
\s5
\v 25 Palali, mwana wa Uzai, akajenga juu ya kona ya ukuta na mnara unaoenea juu kutoka nyumba ya juu ya mfalme katika uwanda wa walinzi. Baada yake Pedaya mwana wa Paroshi akajenga.
\v 26 Sasa watumishi wa hekalu waliokaa Ofeli walijenga mpaka upande wa Hifadhi ya Maji upande wa mashariki wa mnara unaojitokeza.
\v 27 Baada yake, Watekoi walijenga sehemu nyingine, kuelekea mnara mkubwa ulio nje, mpaka ukuta wa Ofeli.
\s5
\v 28 Makuhani wakajenga juu ya lango la farasi, kila mmoja kuelekea nyumba yake.
\v 29 Baada yao Sadoki, mwana wa Imeri, alijenga sehemu hiyo kuelekea nyumba yake. Na baada yake Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa lango la mashariki, akajenga.
\v 30 Baada yake Hanania, mwana wa Shelemia, na Hanuni, mwana wa sita wa Salafu, wakajenga sehemu nyingine. Meshulamu mwana wa Berekia akajenga kuelekea kwenye vyumba vyake.
\s5
\v 31 Baada yake Malkiya, mmoja wa wafua dhahabu, akajenga mpaka nyumba ya watumishi wa hekalu na wafanyabiashara waliokuwa wakielekea lango la gereza na mpaka chumba cha juu cha pembeni.
\v 32 Wafanyabiashara wa dhahabu na wafanyabiashara walijenga kati ya chumba cha juu cha kona na Lango la Kondoo.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Sanbalati alipoposikia tulikuwa tukijenga ukuta, akaghadhabika ndani yake, naye akakasirika sana, akawacheka Wayahudi.
\v 2 Mbele ya ndugu zake na jeshi la Samaria, akasema, "Wayahudi dhaifu hawa wanafanya nini? Je, watajifanyia mji wenyewe? Je, watatoa dhabihu? Je, wataimaliza kazi siku moja? Je! Watawaletea mawe kutoka kwenye kifusi baada ya kuchomwa moto?
\v 3 Tobia Mwamoni alikuwa pamoja naye, naye akasema, 'Ikiwa tu mbweha angepanda juu ya hichi wanachokijenga, angeubomoa ukuta huo wa mawe."
\s5
\v 4 Tusikilize, Mungu wetu, kwa maana sisi tunatukanwa. Rudisha malalamiko yao juu ya vichwa vyao wenyewe na kuwapa wapate kutekwa katika nchi ambapo wao ni wafungwa.
\v 5 Usiufunike uovu wao, wala usiondoe dhambi zao mbele yako; kwa sababu wamewachukiza wanaojenga.
\v 6 Kwa hiyo tulijenga ukuta na ukuta wote uliunganishwa kwa nusu ya urefu wake, kwa kuwa watu walikuwa na hamu ya kufanya kazi
\s5
\v 7 Lakini Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni, na Waashdodi waliposikia kwamba kazi ya ukarabati wa kuta za Yerusalemu ilikuwa ikiendelea, na kwamba sehemu zilizovunjika katika ukuta zilikuwa zimefungwa, ghadhabu kubwa ikawaka ndani yao.
\v 8 Wote walifanya shauri pamoja, na walikuja kupigana dhidi ya Yerusalemu na kusababisha machafuko ndani yake.
\v 9 Lakini tuliomba kwa Mungu wetu na kuweka walinzi kama ulinzi dhidi yao mchana na usiku kwa sababu ya tishio lao.
\s5
\v 10 Kisha watu wa Yuda wakasema, "Nguvu ya wale wanaobeba mizigo inashindwa. Kuna kifusi kikubwa, na hatuwezi kujenga ukuta."
\v 11 Na adui zetu wakasema," Wala hawatajua au kuona mpaka tutakapokuja kati yao na kuwaua, na kuisimamisha kazi."
\s5
\v 12 Wakati huo Wayahudi waliokuwa wakiishi karibu nao walitoka pande zote na kuzungumza nasi mara kumi, wakituonya juu ya mipango waliyofanya dhidi yetu.
\v 13 Kwa hiyo nikaweka watu katika sehemu za chini za ukuta katika sehemu zilizo wazi. Niliweka kila familia wenye upanga, mikuki, na upinde.
\v 14 Nikatazama, nikasimama, nikawaambia wakuu, na watawala, na watu wengine, "Msiogope. mkumbukeni Bwana, ambaye ni mkuu na wa kushangaza. Wapiganie ndugu zenu, wana zenu, binti zenu, wake zenu na nyumba zenu.
\s5
\v 15 Ilipokuwa wakati adui zetu waliposikia kwamba mipango yao ilikuwa inayojulikana kwetu, na Mungu alikuwa amebatilisha mipango yao, sote tulirudi ukutani, kila mmoja kwa kazi yake.
\v 16 Kwa hiyo tangu wakati huo nusu ya watumishi wangu walifanya kazi tu juu ya kujenga ukuta, na nusu yao wakaishika mikuki, ngao, pinde, na kuvaa silaha, wakati viongozi walisimama nyuma ya watu wote wa Yuda.
\s5
\v 17 Na hivyo wafanyakazi haohao ambao walikuwa wakijenga ukuta na kubeba mizigo walikuwa pia wakilinda nafasi zao. Kila mtu alifanya kazi kwa mkono mmoja, na kwa mkono mwingine alikuwa na silaha yake.
\v 18 Kila mjenzi alivaa upanga wake ubavuni mwake na ndivyo alivyojenga. Yule aliyepiga tarumbeta akakaa karibu nami.
\s5
\v 19 Niliwaambia wakuu na viongozi na watu wengine, "Kazi ni nzuri na ya kina, na tumejitenga kwenye ukuta, mbali na mtu mwingine.
\v 20 Lazima mkimbilie mahali ambapo mtasikia sauti ya tarumbeta na kusanyika huko. Mungu wetu atatupigania."
\s5
\v 21 Kwa hiyo tulifanya kazi hiyo. Nusu yao walikuwa wakichukua mikuki kutoka kupambazuka asubuhi hadi kutokea kwa nyota.
\v 22 Nikawaambia watu wakati huo, "Kila mtu na mtumishi wake waende usiku katikati ya Yerusalemu, ili wawe walinzi wakati wa usiku na mfanyakazi wakati huo."
\v 23 Basi si mimi, wala ndugu zangu, wala watumishi wangu, wala watu wa walinzi waliokuwa wananifuata, hakuna hata mmoja wetu aliyebadili nguo zake, na kila mmoja wetu alichukua silaha yake, hata kama angeenda kwa ajili ya kuteka maji.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kisha wale wanaume na wake zao wakalia kwa nguvu dhidi ya Wayahudi wenzao.
\v 2 Kwa maana kulikuwa na baadhi ya watu ambao walisema, "Sisi na wana wetu na binti zetu tupo wengi. Basi hebu tupate nafaka tuweze kula na tukae tuishi."
\v 3 Pia kulikuwa na baadhi ya watu ambao walisema, "Tunaweka rehani mashamba yetu, mizabibu yetu, na nyumba zetu ili tupate nafaka wakati wa njaa."
\s5
\v 4 Wengine pia walisema, "Tumekopesha pesa kulipa kodi ya mfalme kwenye mashamba yetu na mashamba yetu ya mizabibu.
\v 5 Hata hivyo sasa miili yetu na damu ni sawa na ndugu zetu, na watoto wetu ni sawa na watoto wao. Tunalazimishwa kuuza wana wetu na binti zetu kuwa watumwa. Baadhi ya binti zetu tayari wamekuwa watumwa. Lakini hatuna nguvu za kusaidia kwa sababu watu wengine sasa wana mashamba yetu na mizabibu yetu."
\s5
\v 6 Nilikasirika sana niliposikia kilio chao na maneno haya.
\v 7 Kisha nikafikiri juu ya hili, na kuleta mashtaka dhidi ya wakuu na viongozi. Nikawaambia, "Ninyi mnatafuta riba, kila mmoja kutoka kwa ndugu yake mwenyewe." Nikakutanisha kusanyiko kubwa juu yao
\v 8 na kuwaambia, "Sisi, kwa kadiri tulivyoweza, tumewakomboa toka utumwani ndugu zetu wa Kiyahudi ambao walikuwa wameuzwa kwa mataifa, lakini hata mnawauza ndugu na dada zenu ili wauzwe tena kwetu!" Walikuwa kimya na hawakupata neno la kusema.
\s5
\v 9 Pia nikasema, 'Mnachokifanya sio kizuri. Je, hampaswi kutembea katika hofu ya Mungu wetu ili kuzuia malalamiko ya mataifa ambayo ni adui zetu?
\v 10 Mimi na ndugu zangu na watumishi wangu tunawapa fedha na nafaka. Lakini lazima tuache kutoza riba juu ya mikopo hii.
\v 11 Warudishieni leo leo mashamba yao, mizabibu yao, mashamba yao ya mizeituni, na nyumba zao na asilimia ya fedha, nafaka, divai mpya, na mafuta mliyowatoza."
\s5
\v 12 Wakasema, "Tutarudisha kile tulichochukua kutoka kwao, wala hatutahitaji kitu kutoka kwao. Tutafanya kama unavyosema." Ndipo nikawaita makuhani, na kuwaapisha kuwafanya kama walivyoahidi.
\v 13 Nikakung'uta vazi langu, nikasema, "Basi Mungu aondoe nyumba na mali ya kila mtu asiyetimiza ahadi yake. Kwa hiyo akung'utwe na kuwa hana kitu. Kusanyiko lote likasema "Amina," na wakamsifu Bwana. Na watu wakafanya kama walivyoahidi.
\s5
\v 14 Kwa hiyo tangu wakati niliowekwa kuwa mkuu wao katika nchi ya Yuda, tangu mwaka wa ishirini mpaka mwaka wa thelathini na pili wa mfalme Artashasta, miaka kumi na miwili, mimi na ndugu zangu hatukula chakula kilichotolewa kwa gavana.
\v 15 Lakini wakuu wa zamani waliokuwa kabla yangu waliwaweka watu mizigo mizito, na wakachukua kwao shekeli arobaini za fedha kwa ajili ya chakula na divai yao ya kila siku. Hata watumishi wao waliwadhulumu watu. Lakini sikufanya hivyo kwa sababu ya hofu ya Mungu.
\s5
\v 16 Niliendelea kufanya kazi kwenye ukuta, na hatukununua ardhi. Na watumishi wangu wote walikusanyika huko kwa ajili ya kazi hiyo.
\v 17 Katika meza yangu walikuwa Wayahudi na maafisa, watu 150, isipokuwa wale waliokuja kwetu kutoka kwa mataifa waliokuwa wakituzunguka.
\s5
\v 18 Kila kitu kilichoandaliwa kila siku kilikuwa ng'ombe moja, kondoo sita waliochaguliwa, na ndege, na kila siku kumi aina zote za divai nyingi. Na hata kwa haya yote sikuhitaji mahitaji ya chakula cha gavana, kwa sababu madai yalikuwa mazito sana juu ya watu.
\v 19 Nikumbuke, Ee Mungu wangu, kwa wema, kwa sababu ya yote niliyoyafanya kwa watu hawa.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Wakati Sanbalati, Tobia, Geshemu Mwarabu na adui zetu wengine waliposikia kwamba nilijenga upya ukuta na kwamba hakuna sehemu yoyote iliyoachwa ya wazi, ingawa sijawaweka milango katika malango,
\v 2 Sanbalati na Geshemu akatuma wajumbe akasema, "Njoni, tukutane pamoja mahali fulani katika tambarare ya Ono." Lakini walitaka kunidhuru.
\s5
\v 3 Niliwatuma wajumbe kwao, nikasema, "Ninafanya kazi kubwa na siwezi kushuka. Kwa nini kazi isimame wakati nitakapoondoka na kuja kwako?"
\v 4 Walituma ujumbe huo huo mara nne, na mimi niliwajibu vile vile kila wakati.
\s5
\v 5 Sanbalati alimtuma mtumishi wake kwangu kwa njia ile ile mara ya tano, na barua iliyo wazi mkononi mwake.
\v 6 Imeandikwa, "Inaripotiwa kati ya mataifa, na Geshemu pia anasema, kwamba wewe na Wayahudi mna mpango wa kuasi, kwa sababu hiyo ndio mnajenga ukuta. Kutokana na taarifa hizi, unakaribia kuwa mfalme wao.
\s5
\v 7 Nawe umewachagua manabii kutangaza habari zako juu ya Yerusalemu, wakisema, "Kuna mfalme huko Yuda!" Unaweza kuwa na hakika mfalme atasikia ripoti hizi. Basi, hebu njoo tuzungumze.
\s5
\v 8 Kisha nikamtuma neno nikisema, "mambo kama hayo hayajafanyika kama unavyosema, kwa maana ndani ya moyo wako umeyabuni."
\v 9 Kwa maana wote walitaka kututisha, wakifikiri, "Wataacha mikono yao kufanya kazi hiyo, na haitafanyika." Lakini sasa, Mungu, tafadhali imarisha mikono yangu.
\s5
\v 10 Nikaenda nyumbani kwa Shemaya mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyefungwa nyumbani mwake. Akasema, "Hebu tukutane pamoja katika nyumba ya Mungu, ndani ya hekalu, na tufunge milango ya hekalu, kwa maana wanakuja kukuua. Usiku wanakuja kukuua."
\v 11 Nikajibu, "Je! Mtu kama mimi ninaweza kukimbia? Na mtu kama mimi ninaweza kuingia hekaluni ili nipate kuishi? Sitaingia."
\s5
\v 12 Niligundua kwamba sio Mungu aliyemtuma, lakini alikuwa amefanya unabii dhidi yangu. Tobia na Sanbalati walimwajiri.
\v 13 Walimpa kazi kunifanya niwe na hofu, ili nifanye kile alichosema na kutenda dhambi, hivyo wangeweza kunipa jina baya ili kuniaibisha.
\v 14 Mungu wangu, wakumbuke Tobia na Sanbalati, na yote waliyofanya. Pia mkumbuke nabii Noadia na manabii wengine ambao walijaribu kunifanya niogope.
\s5
\v 15 Kwa hiyo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, baada ya siku hamsini na mbili.
\v 16 Adui zetu wote waliposikia hayo, mataifa yote yaliyotuzunguka, waliogopa na wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe. Kwa maana walijua kazi hiyo ilifanyika kwa msaada wa Mungu wetu.
\s5
\v 17 Wakati huu wakuu wa Yuda walituma barua nyingi kwa Tobia, na barua za Tobia zikawajia.
\v 18 Kwa maana walikuwa wengi huko Yuda waliofungwa kwa kiapo chake, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara. Mwanawe Yehohanani alikuwa amekuwa mkewe Meshulamu mwana wa Berekia.
\v 19 Pia walizungumza nami kuhusu matendo yake mema na kumwambia maneno yangu. Barua zililetwa kwangu kutoka kwa Tobia kunitisha.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Wakati ukuta ulipomalizika na milango nimekwisha kuisimamisha, na walinzi wa malango na waimbaji na Walawi walikuwa wamechaguliwa,
\v 2 nikampa ndugu yangu Hanani kuwa na amri juu ya Yerusalemu, pamoja na Hanania ambaye alikuwa msimamizi wa kijiji, kwa kuwa alikuwa mwaminifu na alimuogopa Mungu zaidi kuliko wengi.
\s5
\v 3 Nami nikawaambia, Msifungue malango ya Yerusalemu mpaka jua litakapokuwa kali. Wakati walinzi wa mlango wanalinda, unaweza kufunga milango na kuikaza. Chagua walinzi kutoka kwa wale wanaoishi Yerusalemu, wengine mahali pa kituo chao cha ulinzi, na wengine mbele ya nyumba zao wenyewe.
\v 4 Sasa jiji lilikuwa pana na kubwa, lakini kulikuwa na watu wachache ndani yake, na hakuna nyumba zilizojengwa tena.
\s5
\v 5 Mungu wangu aliweka moyoni mwangu, kuwakusanya pamoja wakuu, maafisa, na watu kuwaandikisha katika familia zao. Nilipata Kitabu cha kizazi cha wale ambao walirudi kwanza na nikaona kwamba imeandikwa humo.
\s5
\v 6 Hawa ndio watu wa jimbo ambao walikwenda kutoka kwenye uhamisho wa wale waliohamishwa ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwachukua mateka. Wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenda kwenye mji wake.
\v 7 Walikuja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana. Idadi ya wana wa Israeli ilikuwa.
\s5
\v 8 Wana wa Paroshi, 2, 172.
\v 9 Wana wa Shefatia, 372.
\v 10 Wana wa Ara, 652.
\s5
\v 11 Wana wa Pahath Moabu,
\v 12 kwa wana wa Yeshua na Yoabu, 2, 818.
\v 13 Wana wa Elamu, 1, 254.
\v 14 Wana wa Zatu, 845. Wana wa Zakai, 760.
\s5
\v 15 Wana wa Binnui, 648.
\v 16 Wana wa Bebai, 628.
\v 17 Wana wa Azgadi, 2, 322.
\v 18 Wana wa Adonikamu, 667.
\s5
\v 19 Wana wa Bigwai, 2, 067.
\v 20 Wana wa Adini, 655.
\v 21 Wana wa Ateri, wa Hezekia, 98.
\v 22 Wana wa Hashumu, 328.
\s5
\v 23 Wana wa Besai, 324.
\v 24 Wana wa Harifu, 112.
\v 25 Wana wa Gibeoni, 95.
\v 26 Watu kutoka Bethlehemu na Netofa, 188.
\s5
\v 27 Watu wa Anathothi, 128.
\v 28 Watu wa Beth Azmaweth, 42.
\v 29 Watu wa Kiriath Yearimu, Kefira, na Beerothi, 743.
\v 30 Watu wa Rama na Geba, 621.
\s5
\v 31 Watu wa Mikmasi, 122.
\v 32 Watu wa Betheli na Ai, 123.
\v 33 Watu wa Nebo, 52.
\v 34 Watu wa Elamu wa pili, 1, 254.
\s5
\v 35 Watu wa Harimu, 320.
\v 36 Watu wa Yeriko, 345.
\v 37 Watu wa Lodi, Hadidi, na Ono, 721.
\v 38 Watu wa Senaa, 3, 930.
\s5
\v 39 makuhani Wana wa Yedaya (wa nyumba ya Yeshua), 973.
\v 40 Wana wa Imeri, 1, 052.
\v 41 Wana wa Pashuri, 1, 247.
\v 42 Wana wa Harimu, 1, 017.
\s5
\v 43 Walawi, wana wa Yeshua, wa Kadmieli, wa Binui, wa Hodavia, 74.
\v 44 Waimbaji wana wa Asafu; 148.
\v 45 Waliofungua mlango wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni; wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, 138.
\s5
\v 46 Watumishi wa Hekalu wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi,
\v 47 wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni,
\v 48 wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai,
\v 49 wana wa wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari.
\s5
\v 50 Wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda,
\v 51 wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea,
\v 52 wana wa Besai, wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu.
\s5
\v 53 Wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri,
\v 54 wana wa Baslith, wana wa Mehida, wana wa Harsha,
\v 55 wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema,
\v 56 wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
\s5
\v 57 Wana wa Sulemani, wana wa Sotai, wana wa Sofeereth, wana wa Peruda,
\v 58 wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli,
\v 59 wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokerethi Sebaimu, wana wa Amoni.
\v 60 Watumishi wote wa hekalu, na wana wa watumishi wa Sulemani, walikuwa 392.
\s5
\v 61 Hawa ndio watu waliokwenda kutoka Tel Mela, Tel harsha, Kerub, Addon, na Imeri. Lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba wao au jamaa za baba zao walikuwa wana wa Israeli,
\v 62 wana wa Delaya, wana wa Tobia, na wana wa Nekoda, 642.
\v 63 Na kutoka kwa makuhani Wana wa Habaya, Hakosi, na Barzilai ( akamchukua mkewe kutoka kwa binti za Barzilai wa Gileadi na akaitwa kwa jina lao).
\s5
\v 64 Hawa walitafuta rekodi zao kati ya waliojiunga na kizazi chao, lakini hawakuweza kupatikana, kwa hivyo waliondolewa katika ukuhani kama walio najisi.
\v 65 Naye mkuu wa gavana akawaambia wasiruhusiwe kula chakula cha makuhani kutoka kwenye dhabihu mpaka atakapoinuka kuhani mwenye Urimu na Thumimu.
\s5
\v 66 Kusanyiko lote lilikuwa 42, 360,
\v 67 isipokuwa watumishi wao wa kiume na watumishi wao wa kike, ambao walikuwa 7, 337. Walikuwa na wanaume na wanawake wa kuimba 245.
\s5
\v 68 Farasi zao zilikuwa 736 kwa idadi, nyumbu zao, 245,
\v 69 ngamia zao, 435, na punda zao, 6, 720.
\s5
\v 70 Baadhi ya wakuu wa familia za baba zao walitoa zawadi kwa ajili ya kazi. Gavana alitoa sadaka ya darkoni elfu ya dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 ya makuhani.
\v 71 Baadhi ya wakuu wa familia za baba zao waliwapa katika hazina kwa kazi darkroni elfu ishirini za dhahabu na mane 2, 200 za fedha.
\v 72 Watu wengine waliwapa darkoni za dhahabu ishirini elfu, na dhahabu elfu mbili za fedha, na mavazi sitini na saba kwa makuhani.
\s5
\v 73 Basi makuhani, Walawi, walinzi wa malango, waimbaji, watu wengine, watumishi wa hekalu, na Israeli wote waliishi katika miji yao. Hata mwezi wa saba watu wa Israeli walikuwa wakiishi katika miji yao."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Watu wote walikusanyika kama mtu mmoja katika eneo la wazi mbele ya lango la maji. Wakamwomba Ezra mwandishi akilete Kitabu cha Sheria ya Musa, ambacho Bwana aliwaamuru Israeli.
\v 2 Siku ya kwanza ya mwezi wa saba, Ezra, kuhani, akaleta sheria mbele ya mkutano, wanaume na wanawake, na wote waliokuwa na uwezo wa kusikia na kuelewa.
\v 3 Akatizama eneo lililo wazi mbele ya lango la Maji, na akasoma toka asubuhi hadi adhuhuri, mbele ya wanaume na wanawake, na yeyote ambaye angeweza kuelewa. Na wote wakasikiliza kwa makini kitabu cha Sheria.
\s5
\v 4 Na Ezra, mwandishi, alisimama juu ya jukwaa la mbao ambalo watu walikuwa wametengeneza kwa kusudi hilo. Pembeni yake walisimama Matithia, Shema, Anaya, Uria, Hilkia na Maaseya, upande wake wa kuume; na Pedaya, Misbaeli, Malkiya, Hashumu, Hashbadani, Zekaria na Meshulamu walikuwa wamesimama upande wake wa kushoto.
\v 5 Ezra alifungua kitabu mbele ya watu wote, kwa kuwa alikuwa amesimama juu ya watu, na alipoufungua watu wote wakasimama.
\s5
\v 6 Ezra akamshukuru Bwana, Mungu mkuu; na watu wote wakainua mikono yao, wakajibu, "Amina! Amina!" Wakainamisha vichwa vyao, wakamwabudu Bwana kwa nyuso zao zikiwa chini.
\v 7 Yeshua, Bani, Sherebia, Yamini, Akubu, Shabethai, Hodai, Maaseya, Kelita, Azaria, Yozabidi, Hanania, Pelaya nao ni Walawi, waliwasaidia watu kuelewa sheria, watu wakakaa mahali pao.
\v 8 Wao walisoma katika kitabu, Sheria ya Mungu, wakaeleza wazi kwa tafsiri na kutoa maana ili watu waelewe yaliyosomwa.
\s5
\v 9 Nehemia, gavana, na Ezra kuhani, na mwandishi, na Walawi waliokuwa wakitafsiri kwa watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa Bwana, Mungu wenu. Msiomboleze au kulia. Kwa kuwa watu wote walilia wakati waliposikia maneno ya sheria.
\v 10 Nehemia akawaambia, 'Nendeni, mle kilichonona, mkate na maji ya kunywa, na mpelekeni mtu asiye na kitu, kwa maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu. Msiwe na huzuni, kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.
\s5
\v 11 Basi Walawi wakawafanya watu kuwa na utulivu, wakisema, "Nyamazeni! kwa maana siku hii ni takatifu. Msiwe na huzuni."
\v 12 Watu wote wakaenda kula na kunywa na kugawana chakula na kusherehekea kwa furaha kubwa kwa sababu walielewa maneno waliyohubiriwa.
\s5
\v 13 Siku ya pili viongozi wa nyumba za mababu kutoka kwa watu wote, makuhani na Walawi, wakakusanyika kwa Ezra, mwandishi ili kupata ufahamu kutoka kwenye maneno ya sheria.
\v 14 Wakaona imeandikwa katika sheria namna Bwana alivyomuamuru Musa kwamba wana wa Israeli waishi katika hema wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba.
\v 15 Wanapaswa kutoa tamko katika miji yao yote, na huko Yerusalemu, wakisema, 'Nendeni nje kwenye nchi ya vilima, na mkalete matawi kutoka kwenye mzeituni mwitu, na matawi ya mihadsi, na matawi ya mitende na matawi ya miti minene ili kufanya vibanda vya muda kama ilivyoandikwa."
\s5
\v 16 Basi watu wakatoka na kuleta matawi, wakajifanyia mahema, kila mmoja juu ya paa zao, katika ua zao, katika mahakama za nyumba ya Mungu, mahali pa wazi pa lango la Maji, na katika mraba wa lango la Efraimu.
\v 17 Kisha kusanyiko lote la wale waliorudi kutoka kifungoni wakafanya mahema na kukaa ndani yake. Kwa kuwa tangu siku za Yoshua, mwana wa Nuni hata siku hiyo, watu wa Israeli hawakuadhimisha sikukuu hii. Na furaha ilikuwa kubwa sana.
\s5
\v 18 Pia siku kwa siku, tangu siku ya kwanza hadi mwisho, Ezra alisoma kutoka Kitabu cha Sheria ya Mungu. Walifanya sikukuu kwa siku saba na siku ya nane kilikuwa na kusanyiko zuri, kwa utiifu wa amri.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo huo watu wa Israeli walikusanyika, nao walikuwa wamefunga, nao walikuwa wamevaa magunia, nao wakaweka vumbi juu ya vichwa vyao.
\v 2 Wazao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Walisimama na kukiri dhambi zao wenyewe na matendo maovu ya baba zao.
\s5
\v 3 Walisimama mahali pao, na robo ya siku walisoma kutoka Kitabu cha Sheria ya Bwana Mungu wao. Na robo nyingine ya siku walikiri na kuinama mbele ya Bwana Mungu wao.
\v 4 Walawi, Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebaniya, Buni, Sherebia, Bani na Kenani, walisimama juu ya ngazi, wakamwita Bwana, Mungu wao kwa sauti kubwa.
\s5
\v 5 Ndipo Walawi, na Yeshua, na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethalia, wakasema, "Simameni, mkamsifu Bwana, Mungu wenu, milele na milele." "Libarikiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.
\v 6 Wewe ni Bwana. Wewe peke yako. Wewe umefanya mbinguni, mbingu za juu, na malaika wote wa vita vita, na dunia na kila kitu kilicho juu yake, na bahari na vyote vilivyomo. Unawapa wote uzima, na majeshi ya malaika wanakusujudia.
\s5
\v 7 Wewe ndiwe Bwana, Mungu aliyemchagua Abramu, akamtoa kutoka Uri wa Wakaldayo, akamwita Ibrahimu.
\v 8 Uliona moyo wake ulikuwa mkamilifu mbele yako, nawe ukafanya pamoja naye agano la kuwapa wazao wake nchi ya Wakanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Perizi, na Myebusi, na Wagirgashi. Umeweka ahadi yako kwa sababu wewe ni mwenye haki.
\s5
\v 9 Uliona shida ya baba zetu Misri na ukasikia kilio chao kando ya bahari ya shamu.
\v 10 Wewe ulifanya ishara na maajabu juu ya Farao, na watumishi wake wote, na watu wote wa nchi yake, kwa maana ulijua kwamba Wamisri walifanya kwa kujivunia. Lakini ulijifanyia jina ambalo linasimama hadi siku leo.
\s5
\v 11 Ukagawanya bahari mbele yao, wakavuka katikati ya bahari juu ya nchi kavu; na ukawatupa wale waliowa ndani ya kina, kama jiwe ndani ya maji ya kina.
\s5
\v 12 Wewe uliwaongoza kwa nguzo ya wingu wakati wa mchana, na kwa nguzo ya moto wakati wa usiku, ili kuwamulikia njiani waweze kutembea katika nuru yake.
\v 13 Ulishuka juu ya Mlima Sinai ukazungumza nao kutoka mbinguni ukawapa amri za haki na sheria za kweli, amri nzuri na maagizo.
\s5
\v 14 Uliwajulisha sabato yako takatifu, ukawapa amri, maagizo, na sheria kupitia Musa mtumishi wako.
\v 15 Uliwapa chakula kutoka mbinguni kwa ajili ya njaa yao, na maji kutoka mwamba kwa kiu yao, ukawaambia waende kuimiliki nchi uliyowaapa kwa kiapo kuwapa.
\s5
\v 16 Lakini wao na baba zetu walifanya uasi, nao walikuwa wakaidi, wala hawakuzitii amri zako.
\v 17 Walikataa kusikiliza, na hawakufikiri juu ya maajabu uliyofanya kati yao, lakini wakawa wakaidi, na katika uasi wao waliweka kiongozi ili wairudie hali ya utumwa. Lakini wewe ni Mungu ambaye amejaa msamaha, mwenye rehema na huruma, si mwepesi wa hasira, na wingi katika upendo thabiti. Wewe haukuwaacha.
\s5
\v 18 Wala hukuwaacha hata walipokwisha kutoa ndama katika chuma kilichochomwa na kusema, "Huyu ndio Mungu wenu aliyekuleta kutoka Misri," wakati walipopotoka sana.
\v 19 Wewe, kwa huruma yako, hukuwaacha katika jangwa. Nguzo ya wingu iliyowangoza njiani haikuwaacha wakati wa mchana, wala nguzo ya moto usiku iliwaangazia barabara ambayo walipaswa kutembea.
\s5
\v 20 Uliwapa Roho wako mzuri kuwafundisha, na mana yako haukuwanyima kinywani mwao, na ukawapa maji kwa kiu yao.
\v 21 Kwa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, na hawakukosa chochote. Nguo zao hazikuchakaa na miguu yao haikuvimba.
\s5
\v 22 Uliwapa falme na watu, na ukawapa ardhi katika kila kona ya mbali. Basi wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.
\s5
\v 23 Uliwafanya watoto wao kuwa wengi kama nyota za mbinguni, na ukawaingiza katika nchi. Uliwaambia baba zao waingie na kumiliki.
\v 24 Basi watu wakaingia, wakaimiliki nchi, ukawashinda wenyeji wa nchi hiyo, Wakanaani. Ukawatia mikononi mwao, pamoja na wafalme wao na watu wa nchi, ili Israeli afanye nao kama walivyotaka.
\s5
\v 25 Wao waliteka miji yenye nguvu na nchi yenye ustawi, nao wakachukua nyumba zenye vitu vyote vyema, birika zilizochimbwa, mizabibu na miti ya mizeituni, na miti ya matunda mengi. Kwa hiyo walikula na wakashiba na wakatosheka, na wakafurahi kwa wema wako.
\s5
\v 26 Basi hawakukutii na wakawaasi. Walitupa sheria yako nyuma ya migongo yao. Waliwaua manabii wako waliowaonya wakurudie wewe, nao wakafanya ukatili mkubwa.
\v 27 Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa adui zao, aliyewatesa. Na wakati wa mateso yao, walikulilia na wewe uliwasikia kutoka mbinguni na mara nyingi ukawaokoa katika mikono ya adui zao, kwa sababu ya huruma zako nyingi.
\s5
\v 28 Lakini baada ya kupumzika, wakafanya mabaya tena mbele yako, nawe ukawaacha mikononi mwa adui zao, kwa hiyo adui zao wakatawala juu yao. Hata walipokurudia na kukulilia, ukasikia kutoka mbinguni, mara nyingi ukawaokoa kwa sababu ya huruma yako.
\v 29 Uliwaonya ili wapate kurudi kwenye sheria yako. Hata hivyo walifanya kiburi na hawakusikiliza amri zako. Walifanya dhambi dhidi ya amri zako ambazo humpa uzima mtu yeyote anayezitii. Hawakuzitii, hawakuzitenda na walikataa kuzisikiliza.
\s5
\v 30 Kwa miaka mingi ukachukiliana nao na kuwaonya kwa Roho wako kwa njia ya manabii wako. Hata hivyo hawakusikiliza. Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa watu wa jirani.
\v 31 Lakini kwa huruma zako kubwa hukuwakomesha kabisa, au kuwaacha, kwa maana wewe ni Mungu mwenye rehema na mwenye huruma.
\s5
\v 32 Basi, Mungu wetu, Mungu wetu mkuu, mwenye nguvu na mwenye kutisha, unayeweka agano lako na upendo wako, shida zote zilizotupata sisi, wafalme wetu, wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote tangu siku za wafalme wa Ashuru mpaka leo usizihesabu kuwa ni kidogo.
\v 33 Wewe ni mwenye haki katika yote yaliyotupata, kwa kuwa umetenda kwa uaminifu, na tumefanya uovu.
\v 34 Wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, na baba zetu hawakuishika sheria yako, wala hawakuzingatia amri zako au shuhuda zako ulizowashuhudia.
\s5
\v 35 Hata katika ufalme wao wenyewe, wakati walifurahia wema wako kwao, katika nchi kubwa na yenye mazao uliyoweka mbele yao, hawakukutumikia au kuacha njia zao mbaya.
\s5
\v 36 Sasa sisi ni watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu kufurahia matunda yake na zawadi zake nzuri, na tazama, sisi ni watumwa!
\v 37 Mavuno mazuri kutoka nchi yetu huenda kwa wafalme uliowaweka juu yetu kwa sababu ya dhambi zetu. Watawala juu ya miili yetu na juu ya mifugo kama wanavyopenda. Tuna shida kubwa.
\s5
\v 38 Kwa sababu ya yote haya, tunafanya agano thabiti kwa kuandika. Kwenye hati iliyofungwa ni majina ya wakuu wetu, Walawi, na makuhani."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Wale ambao waliweka majina yao kwenye nyaraka zilizofunikwa walikuwa Nehemia mwana wa Hakalia gavana, na makuhani waliowekwa walikuwa Sedekia,
\v 2 Seraya, Azaria, Yeremia,
\v 3 Pashuri, Amaria, Malkiya,
\s5
\v 4 Hamshi, Shekania, Maluki,
\v 5 Harimu, Meremothi, Obadia,
\v 6 Danieli, Ginethoni, Baruki,
\v 7 Meshulamu, Abiya, Miyamini,
\v 8 Maazia, Bilgai na Shemaya. Hawa walikuwa makuhani.
\s5
\v 9 Walawi walikuwa Yeshua mwana wa Azania, Binui wa jamaa ya Henadadi, Kadmieli,
\v 10 na Walawi wenzake, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,
\v 11 Mika, Rehobu, Hashabia,
\v 12 Zakuri, Sherebia, Shebania,
\v 13 Hodiya, Bani na Beninu.
\v 14 Viongozi wa watu walikuwa Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,
\s5
\v 15 Buni, Azgadi, Bebai,
\v 16 Adoniya, Bigwai, Adini,
\v 17 Ateri, Hezekia, Azuri,
\v 18 Hodia, Hashumu, Besai,
\v 19 Harifu, Anathothi, Nobai,
\v 20 Magpiashi, Meshulamu, Heziri,
\v 21 Meshezabeli, Sadoki, Yadua,
\s5
\v 22 Pelatia, Hanani, AnaYA,
\v 23 Hoshea, Hanania, Hashubu,
\v 24 Haloheshi, Pilha, Shobeki,
\v 25 Rehumu, Hashabna, Maaseya,
\v 26 Ahia, Hanani, Anani,
\v 27 Maluki, Harimu na Baana.
\s5
\v 28 Na watu wengine waliokuwa makuhani, na Walawi, na walinzi wa malango, na waimbaji, na watumishi wa hekalu, na wote waliokuwa wamejitenga wenyewe na watu wa nchi za jirani, kwa sheria ya Mungu, na wanawake zao, na wana wao, na Binti zao, wote walio na ujuzi na ufahamu,
\v 29 walijiunga na ndugu zao, wakuu wao, na kujifunga katika laana na kiapo cha kutembea katika sheria ya Mungu, iliyotolewa na Musa mtumishi wa Mungu, na kuzingatia na kutii amri zote za Bwana Mungu wetu na hukumu zake na sheria zake.
\s5
\v 30 Tuliahidi kuwa hatuwezi kuwapa binti zetu watu wa nchi au kuchukua binti zao kwa wana wetu.
\v 31 Pia tuliahidi kwamba ikiwa watu wa nchi wataleta bidhaa au nafaka yoyote ya kuuza siku ya Sabato, hatuwezi kununua kutoka kwao siku ya Sabato au siku yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba tutaacha mashamba yetu kupumzika, na tutafuta madeni yote yaliyotokana na Wayahudi wengine.
\s5
\v 32 Tulikubali amri za kutoa shilingi ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu wetu,
\v 33 kutoa mkate wa uwepo, na sadaka ya nafaka ya kawaida, sadaka za kuteketezwa siku za Sabato, sikukuu mpya za mwezi na sikukuu za kuteketezwa, na sadaka takatifu, na sadaka za dhambi za kufanya upatanisho kwa Israeli, pamoja na kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.
\s5
\v 34 Na makuhani, Walawi, na watu wakapiga kura kwa ajili ya sadaka ya kuni. Kura ilichagua ni nani wa familia zetu ataleta kuni ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati zilizowekwa kila mwaka. Kuni hizo zilichomwa juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika sheria.
\v 35 Tuliahidi kuleta nyumbani kwa Bwana matunda ya kwanza yaliyotokana na udongo wetu, na matunda ya kwanza ya mti kila mwaka.
\v 36 Na kama ilivyoandikwa katika sheria, tuliahidi kuleta nyumbani kwa Mungu na kwa makuhani watumikao hapo wazaliwa wa kwanza wa wana wetu ma wanyama wetu.
\s5
\v 37 Tutaleta unga wa kwanza na sadaka zetu za nafaka, na matunda ya kila mti, na divai mpya na mafuta tutaleta kwa makuhani, kwenye vyumba vya kuhifadhi vya nyumba ya Mungu wetu. Tutawaletea Walawi sehemu ya kumi kutoka kwenye udongo wetu kwa sababu Walawi hukusanya zaka katika miji yote tunayofanya kazi.
\v 38 Kuhani, mzao wa Haruni, lazima awe na Walawi wakati wanapopokea zaka. Walawi wanapaswa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu kwenye vyumba vya kuhifadhi hazima.
\s5
\v 39 Kwa maana wana wa Israeli na wana wa Lawi, wataleta sadaka za nafaka, divai mpya, na mafuta katika vyumba vya kuhifadhi ambapo vitu vya patakatifu vinasimamishwa, na mahali pa makuhani watumishi, na walinzi wa mlango, na waimbaji. Hatuwezi kuacha nyumba ya Mungu wetu.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Viongozi wa watu waliishi Yerusalemu, na watu wengine walipiga kura ili kuleta mmoja kati ya watu kumi kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, na wengine tisa walibakia katika miji mingine.
\v 2 Na watu wakawabariki wote waliojitoa kwa hiari kuishi Yerusalemu.
\s5
\v 3 Hawa ndio viongozi wa mkoa ambao waliishi Yerusalemu. Hata hivyo, katika miji ya Yuda kila mtu aliishi katika nchi yake mwenyewe, ikiwa ni pamoja na Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa hekalu, na wazao wa watumishi wa Sulemani.
\v 4 Katika Yerusalemu waliishi baadhi ya wana wa Yuda na baadhi ya wana wa Benyamini. Watu wa Yuda walikuwa pamoja na Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli, mwana wa Peresi.
\s5
\v 5 Na Maaseya, mwana wa Baruki, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zakaria, mwana wa Mshelani, alikuwa mwana wa Baruki.
\v 6 Wana wote wa Peresi waliokaa Yerusalemu walikuwa 468. Walikuwa masujaa.
\s5
\v 7 Hao ndio wana wa Benyamini, Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseva, mwana wa Ithieli, mwana wa Yehaya.
\v 8 Na baada yake, Gabai na Salai, watu 928.
\v 9 Yoeli mwana wa Zikri alikuwa mwangalizi wao; na Yuda mwana wa Hasenua alikuwa mkuu wa pili juu ya mji.
\s5
\v 10 Kutoka kwa makuhani Yedaya, mwana wa Yoyaribu, Yakini,
\v 11 Seraya mwana wa Hilikia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayoti, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu,
\v 12 na wenzake waliofanya kazi ya ukoo, watu 822. na Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pelalia, mwana wa Amzi, mwana wa Zekaria, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya.
\s5
\v 13 Nao walikuwa washirika wake waliokuwa wakuu wa jamaa, wanaume 242, na Maasai mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri;
\v 14 na ndugu zao, 128 wapiganaji wenye ujasiri, wenye ujasiri; Waziri wao aliyeongoza alikuwa Zabdieli, mwana wa Hageoli.
\s5
\v 15 Na Walawi Shemaya mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, mwana wa Buni,
\v 16 na Shabethai, na Yozabadi, ambao walikuwa ni viongozi wa Walawi, waliosimamia kazi za nje ya nyumba ya Mungu.
\s5
\v 17 Alikuwepo Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zakri, mwana wa Asafu, aliyekuwa mkurugenzi aliyeanza shukrani kwa sala, na Bakbukia, wa pili miongoni mwa ndugu zake, na Abda mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
\v 18 Katika mji wote mtakatifu walikuwa Walawi 284.
\s5
\v 19 Walinzi wa malango Akubu, Talmoni, na washirika wao, ambao waliolinda milango, wanaume 172.
\v 20 Na wale waliosalia wa Israeli, na makuhani, na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda. Kila mtu aliishi katika milki yake mwenyewe.
\v 21 Wafanyakazi wa hekalu waliishi Ofeli, na Siha na Gishpa walikuwa wakiwaongoza.
\s5
\v 22 Mtawala mkuu juu ya Walawi waliokuwa wakitumikia Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika, wa wana wa Asafu, ambao walikuwa waimbaji wa kazi katika nyumba ya Mungu.
\v 23 Walikuwa chini ya maagizo kutoka kwa mfalme na maagizo imara yalitolewa kwa waimbaji kila siku inavyohitajika.
\v 24 Pethahia mwana wa Meshezabeli, mwana wa Zera, mwana wa Yuda, alikuwa upande wa mfalme kwa habari zote za watu.
\s5
\v 25 Kuhusu vijiji na mashamba yao, baadhi ya watu wa Yuda wakakaa Kiriath-arba, na vijiji vyake, na Diboni, na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake.
\v 26 Wakaishi katika Yeshua, Molada, Beth-Peleti,
\v 27 Hazar-Shuali, Beersheba na vijiji vyake.
\s5
\v 28 Nao wakakaa Siklagi, na Mekona, na vijiji vyake,
\v 29 Enrimoni, Sora, Yarmuthi,
\v 30 Zanoa, Adulamu, na vijiji vyake, na Lakishi, na mashamba yake, na Azeka, na vijiji vyake. Basi wakakaa kutoka Beer-sheba mpaka bonde la Hinomu.
\v 31 Watu wa Benyamini pia walikuwa wakiishi kutoka Geba, kwenda Mikmashi na Aiya, na Beth-eli na vijiji vyake.
\v 32 Waliishi Anathothi, Nobu, Anania,
\v 33 Hazori, Rama, Gitaimu,
\v 34 Hadidi, Seboimu, Nebalati,
\v 35 Lodi, na Ono, bonde la wafundi.
\v 36 Walawi wengine waliishi Yuda wengine Benyamini.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Hawa ndio makuhani na Walawi waliokuja pamoja na Zerubabeli mwana wa Shealueli, pamoja na Yoshua Seraya, Yeremia, Ezra,
\v 2 Amaria, Maluki, Hatushi,
\v 3 Shekania, Harimu na Meremothi.
\s5
\v 4 Kulikuwa na Iddo, Ginethoni, Abiya,
\v 5 Miyamini, Maazia, Bilgai,
\v 6 Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,
\v 7 Salu, Amoki, Hilkia, na Yedaya. Hawa walikuwa wakuu wa makuhani na washirika wao katika siku za Yoshua.
\s5
\v 8 Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa akiongoza nyimbo za shukrani, pamoja na washirika wake.
\v 9 Bakbukia na Uno, washirika wao, walisimama pembeni yao wakati wa huduma.
\s5
\v 10 Yoshua alikuwa babaye Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa babaye Yoyada,
\v 11 Yoyada alimzaa Yonathani, Yonathani akamzaa Yadua.
\s5
\v 12 Katika siku za Yoyakimu hawa walikuwa makuhani, wakuu wa jamaa; Meraya alikuwa mkuu wa Seraya, Hanania alikuwa kiongozi wa Yeremia,
\v 13 Meshulam alikuwa kiongozi wa Ezra, Yehohanani alikuwa kiongozi wa Amaria,
\v 14 Yonathani alikuwa kiongozi wa Maluki, na Yusufu alikuwa kiongozi wa Shekania.
\s5
\v 15 Ili kuendelea, Adna alikuwa kiongozi wa Harimu, Helkai kiongozi wa Meremothi,
\v 16 Zekaria alikuwa kiongozi wa Ido, Meshulamu alikuwa kiongozi wa Ginethoni, na
\v 17 Zikri alikuwa kiongozi wa Abia wa Miyaamini. Piltai alikuwa kiongozi wa Maazia.
\v 18 Shamua alikuwa kiongozi wa Bilgai, Yehonathani alikuwa kiongozi wa Shemaya,
\v 19 Matenai alikuwa kiongozi wa Yoyaribu, Uzi alikuwa kiongozi wa Yedaya,
\v 20 Kalai alikuwa kiongozi wa Salu, Eberi alikuwa kiongozi wa Amok,
\v 21 Hashabia alikuwa kiongozi wa Hilkia, na Nethanel alikuwa kiongozi wa Yedaya.
\s5
\v 22 Katika siku za Eliashibu, Walawi Eliashibu, Yoyada, Yohana, na Yadua waliandikwa kama vichwa vya familia, na makuhani waliandikwa wakati wa utawala wa Dariyo wa Persia.
\v 23 Wana wa Lawi na viongozi wao wa familia waliandikwa katika Kitabu cha tarehe hadi siku za Yohana mwana wa Eliashibu.
\s5
\v 24 Wakuu wa Walawi walikuwa Hashabia, Sherebia, na Yeshua mwana wa Kadmieli, pamoja na washirika wao, waliokuwa wamesimama mbele yao kumtukuza na kumshukuru, akijibu sehemu kwa sehemu, kwa kutii amri ya Daudi, mtu wa Mungu.
\v 25 Matania, Bakbukia, Obadiya, Meshulamu, Talmoni na Akubu walikuwa walinzi wa malango waliokuwa wakiwa wamesimama katika vyumba vya hazina penye malango.
\v 26 Walitumika katika siku za Yoyakimu, mwana wa Yoshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za Nehemiya, gavana na Ezra kuhani na mwandishi.
\s5
\v 27 Katika kujitolea kwa ukuta wa Yerusalemu, watu walitafuta Walawi popote walipokuwa wakiishi, wakawaleta Yerusalemu ili kusherehekea kujitolea kwa furaha, pamoja na shukrani na kuimba kwa ngoma, vinanda na vinubi.
\v 28 Ushirika wa waimbaji walikusanyika pamoja kutoka wilaya iliyozunguka Yerusalemu na kutoka vijiji vya Wanetofathi.
\s5
\v 29 Walikuja kutoka Beth-gilgali na kutoka katika mashamba ya Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji karibu na Yerusalemu.
\v 30 Makuhani na Walawi wakajitakasa, kisha wakawatakasa watu, milango na ukuta.
\s5
\v 31 Kisha nilikuwa na viongozi wa Yuda kwenda juu ya ukuta, na mimi kuteua mikutano miwili mikubwa ya hao walioshukuru. Mmoja alienda upande wa kulia juu ya ukuta kuelekea lango la jaa.
\s5
\v 32 Hoshaya na nusu ya viongozi wa Yuda walimfuata,
\v 33 na baada yake akaenda Azaria, Ezra na Meshulamu,
\v 34 Yuda, Benyamini, Shemaya, Yeremia
\v 35 na wana wa makuhani waliokuwa na tarumbeta, na Zekaria mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Mataniya, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu.
\s5
\v 36 Na pia jamaa za Zekaria, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda, Hanani, pamoja na vyombo vya muziki vya Daudi mtu wa Mungu. Ezra mwandishi alikuwa mbele yao.
\v 37 Na kwa Lango la Chemchemi walikwenda moja kwa moja na madaraja ya mji wa Daudi juu ya kupanda kwa ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, kwenye lango la Maji upande wa mashariki.
\s5
\v 38 Na waimbaji wengine ambao walishukuru wakaenda upande mwingine. Niliwafuata juu ya ukuta pamoja na nusu ya watu, juu ya mnara wa vinyago, hadi kuta kubwa,
\v 39 na juu ya lango la Efraimu, na mlango wa kale, na kwa lango la samaki na mnara wa Hananeli na mnara wa Hamea, kwa lango la Kondoo, na wakasimama kwenye mlango wa walinzi.
\s5
\v 40 Kwa hiyo, mikutano miwili ya wale waliomshukuru walipata nafasi yao katika nyumba ya Mungu, na mimi pia nikachukua nafasi yangu na nusu ya viongozi pamoja nami.
\v 41 Na makuhani wakachukua nafasi zao Eliakimu, Maaseya, Miyamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria, na Hanania wenye tarumbeta,
\v 42 Maaseya, na Shemaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu, Ezeri. Waimbaji waliimba na Yezrahia kama wasimamizi.
\s5
\v 43 Walitoa dhabihu kubwa siku ile, wakafurahi, kwa sababu Mungu alikuwa amewafurahisha kwa furaha kubwa. Pia wanawake na watoto walifurahi. Hivyo furaha ya Yerusalemu ikasikiwa toka mbali.
\s5
\v 44 Siku hiyo watu waliteuliwa juu ya nyumba ya hazina kwa ajili ya michango, matunda ya kwanza, na zaka, ili kuzikusanya ndani yao sehemu zinazohitajika katika sheria za makuhani na Walawi. Kila mmoja aliteuliwa kufanya kazi mashambani karibu na miji. Kwa maana Yuda alifurahi juu ya makuhani na Walawi waliokuwa wamesimama mbele yao.
\v 45 Walifanya utumishi wa Mungu wao, na huduma ya utakaso, kwa mujibu wa amri ya Daudi na ya mwanawe Sulemani, na hivyo
\s5
\v 46 Zamani za kale, katika siku za Daudi na Asafu, kulikuwa na wasimamizi wa waimbaji, na kulikuwa na nyimbo za sifa na shukrani kwa Mungu.
\v 47 Katika siku za Zerubabeli na katika siku za Nehemia, Israeli wote walitoa sehemu za kila siku kwa waimbaji na walinzi wa mlango. Wakaweka pembeni sehemu ya Walawi, na Walawi waliweka sehemu ya wana wa Haruni.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Siku hiyo walisoma Kitabu cha Musa katika masikio ya watu. Ilionekana imeandikwa ndani yake kwamba hakuna Mwamoni au Mmoabu anapaswa kuja katika kusanyiko la Mungu, milele.
\v 2 Hii ilikuwa kwa sababu hawakuja kwa watu wa Israeli na mkate na maji, bali walikuwa wamemwajiri Balaamu kulaani Israeli. Hata hivyo, Mungu wetu aligeuza laana kuwa baraka.
\v 3 Mara tu waliposikia sheria, waliwatenga Israeli toka kwa kila mgeni.
\s5
\v 4 Sasa kabla ya hapo Eliashibu kuhani akawekwa juu ya vyumba vya nyumba ya Mungu wetu. Alikuwa na uhusiano na Tobia.
\v 5 Eliashibu alimuandalia Tobia chumba kikubwa, ambako hapo awali waliweka sadaka ya nafaka, uvumba, makala, na sehemu ya kumi ya nafaka, divai, na mafuta, ambazo ziliwekwa kwa ajili ya Walawi, waimbaji, walinzi wa mlango, na michango kwa makuhani.
\s5
\v 6 Lakini wakati huu wote sikuwepo Yerusalemu. Kwa mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme wa Babeli, nilikwenda kwa mfalme. Baada ya muda nikamwomba mfalme ruhusa ya kuondoka,
\v 7 na nikarudi Yerusalemu. Nikafahamu mabaya ambayo Eliashibu alikuwa amefanya kwa kumpa Tobia chumba cha kuhifadhi katika mahakama ya nyumba ya Mungu.
\s5
\v 8 Nilikuwa na hasira sana na nikatupa vitabu vya nyumba ya Tobia nje ya chumba cha kuhifadhi.
\v 9 Niliamuru kwamba watakase vituo vya kuhifadhi, nami nikarudisha ndani yao makala ya nyumba ya Mungu, sadaka ya nafaka, na uvumba.
\s5
\v 10 Niligundua kwamba sehemu zilizotolewa kwa ajili ya kuwapa Walawi hazikutolewa kwao, ili waweze kuondoka haraka hekaluni, kila mmoja kwenda shambani kwake, kama waimbaji waliofanya walivyoondoka.
\v 11 Kwa hiyo nikawasiliana na maafisa na kusema, 'Kwa nini nyumba ya Mungu imeachwa?' Niliwakusanya pamoja na kuwaweka kwenye nafasi zao.
\s5
\v 12 Kisha Yuda wote wakaleta zaka ya nafaka, divai mpya, na mafuta kwenye vituo vya kuhifadhi.
\v 13 Nikawaweka kama watunza hazina juu ya hazina, Shelemia kuhani, na Sadoki mwandishi, na Walawi, Pedaya. Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania, alikuwa na wafuasi wao, kwa sababu walihesabiwa kuwa waaminifu. Kazi yao ilikuwa kusambaza vifaa kwa washirika wao.
\v 14 Nikumbuke, Ee Mungu wangu, juu ya hili, wala usiondoe matendo mema niliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu na huduma zake.
\s5
\v 15 Siku hizo nikaona watu wa Yuda waliokanyaga mvinyo siku ya Sabato, na kuleta makundi ya nafaka, na kuwapakia punda, na divai, na zabibu, na tini, na kila aina ya mizigo nzito, waliyoleta Yerusalemu siku ya Sabato. Nikashuhudia kuwa walikuwa wakiuza chakula siku hiyo.
\s5
\v 16 Watu kutoka Tiro waliokaa Yerusalemu walileta samaki na kila aina ya bidhaa, na wakawauza siku ya Sabato kwa watu wa Yuda na katika mji!
\v 17 Kisha nikawaambia viongozi wa Yuda, "Je! ni ubaya gani huu mnafanya, kuinajisi siku ya Sabato?
\v 18 Je! Baba zenu hawakufanya hivyo? Je, Mungu wetu hakuleta mabaya haya juu yetu na juu ya mji huu? Sasa unaleta ghadhabu zaidi juu ya Israeli kwa kudharau Sabato."
\s5
\v 19 Mara ilipokuwa giza kwenye milango ya Yerusalemu kabla ya Sabato, niliamuru milango ifungwe na kwamba haifai kufunguliwa hadi baada ya Sabato. Niliwaweka baadhi ya watumishi wangu kwenye malango ili mzigo wowote usiweze kuletwa siku ya Sabato.
\v 20 Wafanyabiashara na wauzaji wa kila aina ya bidhaa walikimbia nje ya Yerusalemu mara moja au mbili.
\s5
\v 21 Lakini niliwaonya, "Mbona mnakaa nje ya ukuta? Ikiwa mtafanya hivyo tena, nitakuweka mikononi!" Kutoka wakati huo hawakuja siku ya sabato.
\v 22 Nikawaamuru Walawi kujitakasa, na kuja kulinda milango, ili kutakasa siku ya Sabato. Nikumbuke kwa hili pia, Mungu wangu, na kunipatia huruma kwa sababu ya uaminifu wa agano ulilonalo kwangu.
\s5
\v 23 Katika siku hizo niliona Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, Amoni na Moabu.
\v 24 Nusu ya watoto wao walizungumza lugha ya Ashdodi, lakini hawakuweza kuzungumza lugha ya Yuda, lakini lugha ya mmoja wa watu wengine.
\s5
\v 25 Nami nikawasiliana nao, na mimi niliwaadhibu, na nikawapiga baadhi yao na kuvuta nywele zao. Naliwaapisha kwa Mungu, nikisema, Msiwape wana wao binti zenu, wala msiwachukue binti zao kwa ajili ya wana wenu, wala ninyi wenyewe.
\v 26 Je, Sulemani mfalme wa Israeli hakufanya dhambi kwa sababu ya wanawake hawa? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwa na mfalme kama yeye, na alipendwa na Mungu wake. Mungu akamfanya awe mfalme juu ya Israeli wote. Hata hivyo, wake zake wa kigeni walimfanya atende dhambi.
\v 27 Je, tunapaswa kukusikiliza na kufanya uovu huu hata kumhalifu Mungu wetu na kuwaoa wanawake wageni?
\s5
\v 28 Mmoja wa wana wa Yoyada, mwana wa Eliashibu, kuhani mkuu, alikuwa mkwewe na Sanbalati Mhoroni. Kwa hiyo nilimondoa kutoka mbele yangu.
\v 29 Wakukumbushe, Mungu wangu, kwa sababu wameunajisi ukuhani, na agano la ukuhani na Walawi.
\s5
\v 30 Kwa hiyo nimewatakasa kutoka kila kitu kigeni, na kuimarisha kazi za makuhani na Walawi, kila mmoja kwa kazi yake mwenyewe.
\v 31 Nilitoa sadaka za kuni wakati uliowekwa na matunda ya kwanza. Nikumbuke, Mungu wangu, kwa mema.

344
17-EST.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,344 @@
\id EST
\ide UTF-8
\h Esta
\toc1 Esta
\toc2 Esta
\toc3 est
\mt Esta
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika siku za utawala wa Ahasuero (huyu ni Ahasuero aliyetawala toka India hadi Ethiopa, zaidi ya majimbo 127),
\v 2 katika siku hizo Mfalme Ahasuero aliketi katika kiti chake cha utawala katika ngome ya Shushani.
\s5
\v 3 mwaka wa tatu wa utawala wake aliwaandalia sherehe viongozi na watumwa wake wote. Waliohudhuria katika sherehe hiyo walikuwa wakuu wa jeshi la Uajemi na Umedi, watu wenye vyeo, na viongozi wa majimbo.
\v 4 Mfalme akaweka wazi utajiri na utukufu wa ufalme wake na heshima ya ukufu wa ukuu alio upata kwa siku nyingi, kwa siku180.
\s5
\v 5 Siku hizi zilipotimia, Mfalme aliaandaa karamu iliyodumu kwa siku saba. Karamu hii ilikuwa kwa watu wote walioishi katika ikulu ya Shushani, tangu mkubwa hadi mdogo. Behewa la bustani ya ikulu ya mfalme ndiyo karamu ilipofanyikia.
\v 6 Behewa la bustani lilipambwa kwa mapazia meupe ya pamba na urujuani, yalifungwa kwa kamba za kitani safi na zambarau, yakiwa yametundikwa kwa pete za fedha na nguzo za marimari. Kulikuwa na makochi ya dhahabu na fedha juu ya sakafu ya marimari, mawe mekundu na meupe, na ya manjano na meusi.
\s5
\v 7 Vinywaji viliandaliwa katika vikombe vya dhahabu. Na kila kikombe kilikuwa ni cha kipekee na kwa sababu ya ukarimu wa mfalme kulikuwa mvinyo mwingi.
\v 8 Mfalme aliwambia wahudumu watu wagawiwe vinywaji kwa kila mtu kulingana na matakwa yake. Maana tayari mfalme alikuwa ametoa agizo kwa watumishi wa ikulu kuwafanyia wageni kulingana na matakwa ya kila mgeni.
\s5
\v 9 Wanawake nao walikuwa wamealikwa katika karamu na Malkia Vashiti katika ikulu ya Mfalme Ahusuero.
\v 10 katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipokuwa na furaha kwa sababu ya mvinyo, aliwaagiza Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkas (hawa saba ndio waliohudumu mbele ya mfalme)
\v 11 kumleta Malkia Vashiti akiwa katika mavazi yake ya kimalkia. Akiwa na lengo la kuwaonyesha watu na maakida urembo wake, maana alikuwa mrembo.
\s5
\v 12 Pamoja na maagizo ya Mfalme, Malkia Vashiti alikataa kwenda kama alivyokuwa amewaagiza viongozi wake. Hivyo mfalme akakasirika sana; ghadhabu yake ikawaka ndani yake
\s5
\v 13 Mfalme akawandea wenye hekima, waliofahamu nyakati (kwa kuwa huu ndio uliokuwa utaratibu wa mfalme kuhusu wale waliokuwa watalaamu wa sheria na hukumu.
\v 14 Carshena, Shethar, Admatha, Tarshish, Meres, Marsena, na Memucan, majimbo saba ya Uajemi na Umedi walikuwa karibu na mfalme na walikuwa na vyeo vikubwa katika ufalme.
\v 15 Katika kutafsiri nini kifanyike kwa mjibu wa sheria kutoka na mgomo wa Malkia Vashiti dhidi ya agizo la mfalme Ahusiero kwa Malkia Vashiti.
\s5
\v 16 Mmoja wao aliyejulikana kwa jina la Memukani alisema mbele ya Mfalme na mbele ya viongozi, Malkia Vashiti hajamkosea tu mfame na wakuu na watu wote walio katika majimbo ya mfale Ahusiero.
\v 17 kwa kuwa jambo la malkia litafahamika kwa wanawake wote. watawatendea waume zao vibaya. Watasema, 'Mfalme Ahusiero Malkia Vashiti hakumtii mme wake, Mfalme Ahusiero alipotaka ahudhurie mbele yake.'
\v 18 Kabla ya siku hii wanawake wa wakuu wa Uajemi na Umedi walipata taarifa ya mgomo wa malkia Vashiti watawatendea waume zao, viongozi wa mfalme. kutakuwa na ghasia na nyingi hasira.
\s5
\v 19 kama ni jambo jema kwa mfalme, ruhusu tangazo litolewe, na iwe katika sheria ya Waajemi na Wamedi, ambao haiwezi kutanguliwa, kwamba Vashiti hatakuja tena mbele za mfalme kama malkia. Nafasi ya Vashiti apewe mwingine ambaye ni bora zaidi ya Vashiti.
\v 20 Tangazo la mfalme litakapotolewa katika ufalme wote, wanawake wote watawaheshimu waume zao, tangu mwenye cheo hadi asiye na cheo."
\s5
\v 21 Ushauri huu ulikuwa mzuri kwa mfalme na wakuu wengine, mfalme akafamya kama Memkani alivyopendekeza.
\v 22 Akatuma barua katika majimbo yote ya mfalme, kwa kilajambo na andiko lake, na watu kwa makabila yao. Aliamuru kwamba kila mme awe msimamizi katika nyumba yake mwenyewe. Tangazo hili lilitolewa katika lungha ya kila mtu katika ufalme.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Baada ya mambo haya na baada ya hasira ya mfalme Ahusiero kutulia, alifikiri kuhusu Malkia Vashiti na alichokuwa amekifanya na tangazo alilokuwa ameamuru litolewe ya Vashiti kupoteza sifa za kuwa malkia.
\v 2 Kisha vijana waliomtumikia mfalme wakasema, mfalme atafutiwemabikira warembo.
\s5
\v 3 Mfalme na achague wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wawakusanye mabikira warembo wote harem katika ikulu ya Susa. Mabikira hawa wawe chini ya usimamizi wa Hegai, msimamizi, ambaye ni mkuu wa wanawake, na wapewe vipodozi vyao vyote.
\v 4 Na binti yule atakaye mfurahisha mfalme ndiye atakaye kuwa Malkia badala ya Vashiti." Mfalme alupenda ushauri na akafanya kama alivoshauriwa,
\s5
\v 5 Katika mji wa Shushani alikuwepo Myahudi aliyeitwa Modekai mwana wa Jaira mwana wa Shimei mwana wa Kishi, aliye kuwa wa kabila la Benjamini.
\v 6 Yeye ni miongoni mwa Wayahudi waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda kutoka Yerusalemu na kupelekwa uhamishoni na mfalme Nebukadreza.
\s5
\v 7 Modekai alikuwa akimlea, Hadasa, yaani Esta, binti wa mjomba wake kwa sababu hakuwa na wazaai wake wote wawili. Modekai alimchukuwa kama binti yake. Esta alikuwa na umbo zuri na uso wa kupendeza.
\s5
\v 8 Wasichana wengi waliletwa ikulu Shushani, baada ya tangazo na amri ya mfalme kutolewa. Waliwekwa chini ya usimamizi wa Hegai. Esta naye alikuwa ni miongoni mwa wasichana walioletwa na kuwekwa chini ya usimamizi wa Hegai, mwangalizi wa wanawake.
\v 9 Esta alimfurahisha, na akapata kibali mbele ya Hegai. Akampa vipodozi na sehemu ya chakula. Akampa wahudumu wa kike saba kutoka katika ikulu ya mfalme, na akampeleka na wahudumu wa kike katika sehemu bora katika nyumba ya wanawake.
\s5
\v 10 Esta hakuwa amemweleza mtu yeyote kuhusu jamaa zake kwa sababu Modekai alikuwa amemzuia.
\v 11 kila siku Modekai alienda na kurudi mbele nje ya ua wa nyumba ya wanawake, ili kwamba asikie kuhusu mambo ya Esta na atakachofanyiwa.
\s5
\v 12 Zamu ilipofika ya kila msichana kwenda kwa mfalme Ahusero kwa kufuata maelekezo kwa wanawake, kila msichana alitakiwa kumaliza miezi kumi na miwili ya urembo, miezi sita ya mafuta ya manemane na miezi sita ya vipodozi.
\v 13 wakati msichana alipoenda kwa mfalme, alipewa chochote alichotamani kutoka katika nyumba ya wanawake ili aende nacho katika nyuma ya mfalme.
\s5
\v 14 Msichana alipaswa kwenda wakati wa usiku na kurudi katika nyumba ya wanawake, na kwa msimamizi Shaashigazi, msimamizi wa mfalme, ambaye alikuwa mwenye kuwalinda masulia. Msichana hakuruhusiwa kwenda tena kwa mfalme isipokuwa amemfurahiha mfalme na mfalme akaamuru arudi tena.
\s5
\v 15 Zamu ya Esta ilipotimia( mwana wa Abihaili, mjomba wa Modekai alikuw amemchukua kama kama binti yake) kwenda mbele ya mfalme, hakutaka kitu chochote isipokuwa vile ambavyo Hegai, msimamizi wa wanawake alimtaka avichukue.
\v 16 Esta akapata kibali mbele ya kila aliyemwona. Esta akapelekwa kwa Mfalme Ahusiero katika makazi ya kifalme mwezi wa kumi, ambao ni mwezi wa Tabeti, katika mwaka wa saba wa utawala wake.
\s5
\v 17 Mfalme alimpenda Esta zaidi kuliko wanawake wengine, na alipata kibali kuliko na wema mbele zake zaidi kuliko mabikira wengine na hivyo mfalme akamvika taji ya kimalkia badala ya Vashiti.
\v 18 mfalme akawafanyia karamu kubwa wasimamizi na wahudumu wake wote, karamu ya Esta na akawapa unafuu wa kodi katika majimbo. Pia akawapa zawadi kwa ukarimu.
\s5
\v 19 Modekai alikuwa ameketi katika lango la mfalme wakati mabikira walipokuwa wamekusanyika kwa mara ya pili.
\v 20 Esta alifuata ushauri Modekai ya kutomwambia mtu yeyote kuhusu jamaa zake. aliendelea kufuata ushauri wa Modekai kama alivyofanya alipokuwa mdogo.
\v 21 katika siku hizo ambazo Modekai alikuwa ameketi getini kwa mfalme, Bighani na Tereshi, wasimamizi wa mfalme walio linda lando, walikasirika na wakatafuta kumuua mfalme Ahusiero.
\s5
\v 22 Jambo lilipowekwa wazi kwa Modekai, alimtaarifu Malkia Esta na Esta akamweleza kile achoelezwa na Modekai.
\v 23 Habari hii ilipepelelezwa na kuonekana kuwa kweli na wanaume wawili walinyongwa juu ya mti. Na habari hii ikaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Baada ya mambo haya, Mfalme Ahusiero alimpandisha cheo Hamani mwana wa Hammedatha mwagagi, na akaweka kiti chake cha ukuu juu ya wakuu wote waliokuwa pamoja naye.
\v 2 Na watumishi wote wa mfalme waliokuwa katika lango la mfalme walipaswa kupiga magoti na kusujudia Hamani, kama mfalme alivyoagiza. Lakini Modekai hakupiga magoti wala kusujudu mbele ya Hamani.
\s5
\v 3 Kisha watumishi wa mfalme waliokuwa langoni mwa mfalme walimwambia Modekai, kwa nini hautii amri ya mfalme?
\v 4 Walisema naye siku kwa siku, lakini alikataa kufuata matakwa yao. Hivyo wakaongea na Hamani kuona kama swala la Modekai lingebaki hivyo alikuwa amewataarifu kuwa Modekai alikuwa Muyahudi.
\s5
\v 5 Hamani alipoona kuwa Modekai hapigi magoti wala kumsujudia, alipatwa na hasira.
\v 6 Alikuwa na wazo la kumuua Modekai, watumishi wa mfalme walikuwa wamemueleza kuwa Modekai na jamaa zake walikuwa Wayahudi. Hamani akaazimu kuwaangamiza Wayahudi wote, watu wa Modekai, ambao walikuwa katika ufalme wa Ahusiero.
\s5
\v 7 Katika mwezi wa kwanza, (ambao ni mwezi wa Nisani) ndani ya mwaka wa kumi na mbili wa Mfalme Ahusiero, walipiga kura mbele ya Hamani kura kila siku na mwezi, kuchagua siku na mwezi hadi walipochagua mwezi wa kumi na mbili, (mwezi wa Adari.
\s5
\v 8 Kisha Hamani akamwambia mfalme Ahusiro, "kuna watu fulani katika majimbo yote ya ufalme wako wasiofuata sheria zako. Na kwa tabia yao ya kutofuata sheria zako hawapasi kuendelea kuwa hai.
\v 9 Kama ikimpendeza mfalme, toa amri watu hawa wote wakatiliwe mbali, nami nitapima talanta elfu kumi za fedha katika mikono ya wale ambao ni wasimamizi wa maswala ya mfalme, ili kwamba waweke katika hazina ya mfalme."
\s5
\v 10 Ndipo mfamle akavua pete yake ya muhuri na kumpa Hamani, adui wa Wayahudi.
\v 11 Mfalme akamwambia Hamani, "Nitahakikisha kwamba fedha inarudi kwako na kwa watu wako. Ili muitumie kama mpendavyo."
\s5
\v 12 Kisha waandishi wa mfalme walikusanyika katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza, na mbiu iliyokuwa na matakwa ya Hamani yalikuwa yameandikwa na kupelekwa kwa wasimamizi wa majimbo, na wale wote waliokuwa juu ya wasimamizi wa majimbo yote, na wasimamizi wa watu, na kwa kila jimbo kwa andiko lao, na kila watu na lugha yao. Mbiu hii ilikuwa imeandikwa kwa jina la mfalme Ahusiero na kupigwa muhuri wa pete yake.
\v 13 Barua hizi za kutaka kuwakatilia mbali Wayahudi wote zilizambazwa katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kuangamiza, kuua na kuwaharibu Wayahudi wote, tangu mdogo hadi mkubwa, watoto na wanawake, ndani ya siku moja katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili (ambao ni mwezi wa Adari) na kuteka mali zo.
\s5
\v 14 Nakala ya ilifanywa kuwa sheria na kupelekwa kila jimbo. Taarifa juu ya maangamizi ya Wayahudi ilienea katika kila jimbo kwamba watu wote wajiandae katika siku hiyo.
\v 15 Wasambazajia walisambaza agizo la mfalme. Tangazo hili pioa lilitolewa na kusambazwa katika mji wa Shushani. Mfalme alikuwa na Hamani walikaa na kunywa, lakini mji wa Shushani, lakini mjiwa Shushani ulikuwa katika uangamivu.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Modeka aliposikia kilichokuwa kimepangwa dhidi yao, alirarua mavazi yake na kuvaa maguni na majivu. Akaenda katikati mwa mji na kulia kwa sauti na uchungu mwingi.
\v 2 Akaenda hadi langoni mwa mfalme; kwa sababu hakuna aliye ruhusiwa kuingia akiwa amevaa magunia.
\v 3 Amri hii ilipofika katika kila jimbo, kulikuwa na kilio kikubwa kwa Wayahudi, na kufunga, kulia na maombolezo. Wengi wao walilala katika magunia na majivu.
\s5
\v 4 Malkia Esta alipopata habari kutoka kwa wahudumu wake, alipatwa na majonzi. Akatuma watu wampelekee nguo Modekai ili avue magunia na kuvaa nguo nzuri, lakini Modekai hakukubali.
\v 5 kisha Esta akamwita Hathaki, mmoja wa wasimamizi wa mfalme, ambaye alikuwa amepewa wajibu wa kumuhudumia. Akamwagiza kwenda kwa Modekai ili afahamu kwa nini Modekai ameamua kufanya hivyo.
\s5
\v 6 Hivyo Hathaki akaenda kwa Modekai katika mji mbele ya lango la mfalme.
\v 7 Modekai akamweleza Hathaki mambo yote kuhusu maangamizi ya Wayahudi yaliyo pangwa na kiasi cha fedha ambacho Hamani ameahidi kuwapa wahazini wa mfalme, ili kuwaua Wayahudi.
\v 8 Na kisha akampa nakala ya mbiu ambayo ilitolewa Shushani kwa uangamivu wa Wayahudi. Alifanya hiivyo ili kwamba Hathaki amwambie Esta achukue jukumu la kwenda na kumuomba mfalme na kumsihi kwa niaba ya Wayahudi.
\s5
\v 9 Hivyo, Hathaki akaenda na kumweleza Esta kile alicho ambiwa na Modekai.
\v 10 Esta akaongea na Hathaki na akamwambia arudi kwa Modekai.
\v 11 Esta akamwambia Hathaki, "Watumishi wote wa mfalme na watu wote katika majimbo yote wanafahamu kuwa mtu yeyote aingiae kwa mfalme bila kibali anapaswa kufa isipokuwa yule ambaye mfalme atamunyoshea fimbo yake ya dhahabu. Ni siku thelathini sasa sijaenda mbele ya mfalme.
\v 12 Hathaki akamwambia Modekai maneno aliyoambiwa na Esta.
\s5
\v 13 Modekai akarudisha ujumbe: "usifikiri kwamba wewe utasalimika kuliko Wayahudi wote.
\v 14 Kama ukikaa kimya kwa wakati huu, Mungu ataleta wokovu kwa njia nyingine, lakini wewe na nyumba ya baba yako mtaangamia. Ni nani ajuaye umekuja katika nafasi hii kwa wakati muafaka kama huu.
\s5
\v 15 Kisha Esta akatuma ujumbe kwa Modekai,
\v 16 "Nenda, uwakusanyea Wayahudi wote wanaoishi katika mji wa Shushani, na wafunge kwa ajili yangu. Wasile wala kunywa kwa muda wa siku tatu. Mimi na watumishi watumishi wangu wa kike tutafunga kwa siku hizo. Na kisha nitaenda mbele ya mfalme kinyume cha sheria. Na kama nitakufa na nife.
\v 17 Modekai akaenda na akafanya yote ambayo Esta aliyo mwagiza kufanya.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Baada ya siku tatu, Esta akajivika mavazi yake ya kimalkia na akasimama sehemu ya ndani ya ua wa ikulu ya mfalme, mbele ya nyumba ya mfalme. mfalme alikuwa ameketi katika kiti chake cha enzi na akitazama mlango wa kuingilia.
\v 2 Mfalme alipomwona malkia Esta alipata kibali kwa mfalme. Alimpa fimbo ya dhahabu mikononi mwa Esta. Hivyo Esta akamsogelea mfalme na kuishika fimbo ya utawala.
\s5
\v 3 Kisha mfalme akamwambia Malkia Esta, "Unahitaji upewe nini? Ombi lako ni lipi? Hata nusu ya ufalme wangu utapewa."
\v 4 Malkia Esta akamwambia mfalme, kama nimepata kibali machoni pako, naomba wewe na Hamani muhudhurie leo katika karamu niliyoiandaa kwa ajili yake."
\s5
\v 5 Mfalme akasema, "Mleteni haraka Hamani sawa sawa na matakwa ya Malkia Esta." Mfalme pamoja na Hamani wakahuduria katika karamu aliyoandaa malkia Esta.
\v 6 Mvinyo ulipohudumiwa katika karamu, mfalme akamuuliza Malkia Esta hitaji lako ni nini? Na ombi lako ni lipi? Utapewa hata nusu ya ufalme."
\s5
\v 7 Esta akajibu mfalme, "Hitaji na ombi langu ni hili,
\v 8 kama ikikupendeza mfalme, kwa kunipa haja yangu na kuheshimu ombi langu, wewe na Hamani muhudhurie tena katika karamu nitakayoiandaa kesho na hapo ndipo nitakapo kuambia haja yangu.
\s5
\v 9 Hamani akaenda nyumbani kwakwe huku akiwa amejawa na furaha moyoni mwake. Lakini alipomwona Modekai katika lango la mfalme, modekai hasimami wala kutetemeka mbele zake, alijawa na ghadhabu kwa ajili ya Modekai.
\v 10 Lakini akajizuia na akaenda nyumbani kwake. Akawaarika marafiki zake wakakusanyika pamoja na Zereshi, mkewe.
\v 11 Hamani akawaeleza juu ya utukufu wa mali na idadi ya watoto aliokuwa nao, na vile alivyo juu kuliko wasimamizi na watumishi wote wa mfalme.
\s5
\v 12 Hamani akawambia, "Hata jana Malkia Esta aliandaa karamu kwa ajili ya mfalme na ni mimi tu na mfalme tulio hudhuria katika karamu aliyoiandaa Malkia Esta. Na hata kesho tuna mwaliko mwingine pamoja na mfalme.
\v 13 Lakini haya yote sio kitu kama Modekai ataendelea kukaa katika lango la mfalme.
\s5
\v 14 Kisha Zereshi, mkewe Hamani akamwambia Mmewe na rafiki zake wote, "Andaeni mti wenye urefu wa futi hamsini. Na wakati wa ahsubuhi ongea na mfalme ili Modekai atundikwe katika mti huo. Kisha nenda kwa furaha na mfalme katika karamu aliyoiandaa Malkia.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi. Akaagiza vitabu vya kumbukumbu vya matukio ya ufalme wake viletwe na visomwe mbele zake. Vitabu visomwa kwa sauti mbele ya mfalme.
\v 2 Ikakutwa kuwa Modekai alikuwa ametoa taarifa kuhusu Bighana na Tereshi, walinzi walio linda lango, waliokuwa wamepanga kumuangamiza Mfalme Ahusiero.
\v 3 Kisha mfalme akauliza, Modekai alifanyiwa nini cha heshima kwa kwa taarifa aliyoitoa? Ndipo watumishi wa mfalme wakamwambia, "Hakufanyiwa kitu chochote."
\s5
\v 4 Kisha mfalme akauliza, "Ni nani aliye ndani ya ua." Na Hamani alikuwa ameingia katika ua wa mfalme ili amwombe mfalme atoe kibali ili Modekai atundikwe kwenye mti aliouandaa.
\v 5 Watumishi wakamjibu, "Hamani amesimama katika ua ya mfalme." Mfalme akasema, "Mwambieni aingie ndani."
\v 6 Mara tu Hamani alipoingia, mfalme akamuuliza, afanyiewe nini mtu yule ambaye mfalme anampenda na kumheshimu?" Hamani akafikiri moyoni mwake, "Ni nani ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu zaidi yangu?
\s5
\v 7 Hamani amjibu mfame, Kwa mtu yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu,
\v 8 avikwe nguo za kifalme, mavazi ambayo mfalme amekwisha yavaa na farasi ambaye ametumiwa na mfalme na ambaye ana taji ya kifalme kichwani mwake.
\v 9 Nguo hizo na farasi apewe msimamizi bora kuliko wote. Na wamvike yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu, na wampandishe juu ya farasi na kumpitisha katika mitaa yote ya mji. Na watangaze mbele yake, "Hivi ndivyo alivyofanyiwa mtu yule ambaye mfalme ampenda na kumuheshimu!"
\s5
\v 10 Kisha mfalme akamwambia, Hamani "fanya hima, mvike Modekai nguo na umpandishe kwenye farasi, na lisipungue hata jambo moja katika hayo uliyo yasema."
\v 11 Kisha Hamani akachukua mavazi na farasi. Akamvika Modekai na akampandisha kwenye farasi na kumpitisha katika mitaa yote ya mji. Akatangaza mbele zake, "Hii imefanyika kwa mtu ambaye mfalme anampenda na kumuheshimu!"
\s5
\v 12 Baada ya hayo Modekai alirudi kwenye lango la mfalme. Huku Hamani akarudi kwa haraka nyumbani kwake, huku akiomboleza, na akiwa ameinamisha kichwa chake.
\v 13 Akawaeleza rafiki zake pamoja na Zereshi mkewe. Kisha rafiki zake wenye hekima pamoja na Zereshi mkewe. Kama Modekai, ambaye umeanza kuanguka mbele zake ni wa uzao wa Wayahudi, hautamshinda, bali utandelea kuanguka mbele zake."
\v 14 Walipokuwa wakiendelea na maongezi, wasimamizi wa mfalme wakamjia Hamani ili aende kwenye karamu aliyoiandaa Esta.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Kwa hiyo mfalme na Hamani wakaenda kausherekea na malkia Esta.
\v 2 Katika siku ya pili, baada ya kuletwa mvinyo, mfalme akamwambia Esta, "Ni nini haja ya moyo wako? Na nini ombi lako? Hata nusu ya ufalme wangu utapewa."
\s5
\v 3 Kisha Malkia amwambia mfalme, kama nimepata kibali machoni pako, na kama ikikupendeza, nipewe maisha yangu, na hili ndio haja ya moyo wangu, na hili pia ni ombi kwa watu wangu pia.
\v 4 Kwa kuwa mimi na watu wangu tumeuzwa, ili tuharibiwe, tuuwawe, na tungamizwe. Kama tungeuzwa utumwani, kama wanaume na wanawake, ningenyamaza kimya, na nisingeweza kumsumbua mfame."
\v 5 Kisha Mfalme Ahusiero akamwambia malkia Esta, "Ni nani huyo? Ni nani aliyekusudia moyoni mwake kutenda jambo hili?
\s5
\v 6 Esta akasema, "Ni huyu mwovu Hamani, adui!" Hamani akashikwa na Hofu mbele za mfalme na malkia.
\v 7 Na kwa ghadhabu mfalme akatoka karamuni katika sehemu ya mvinyo na akaenda katika bustani ya ikulu, Lakini Hamani alibaki akimsihi Malkia Esta ili aokoe maisha yake. Kwa sababu aliona mfalme amemkusudia ubaya.
\s5
\v 8 Mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ikulu, na kuingia katika chumba ambamo kulikuwamo mvinyo. Hamani alikuwa ameanguka chini ya kochi alilokuwa ameketi Esta. Mfalme akakasirika na kusema, "atamdharirisha malkia mbele zangu katika nyumba yangu?" Mara tu maneno haya yalipotoka kinywani mwa mfalme, watumizhi wakafunika uso wa Hamani.
\s5
\v 9 Kisha Habona, mmoja wa watumishi aliye mtumikia mfalme akamwambia mfalme, "Mti wenye urefu wa futi hamsini uko nyumbani kwa Hamani. Ulikuwa umeandaliwa kwa ajili ya Modekai, aliye toa taarifa kuhusu mpango wa kuangamizwa kwako." Mfalme akesema,"Mtundikeni Hamani juu yake."
\v 10 Kwa hiyo wakamtundika Hamani kwenye mti aliuandaa kwa ajili ya Modekai. Na hasira ya mfalme ikatulia.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Siku hiyo Mfalme Ahusiero akampa Malkia Esta mali yote ya Hamani, adui wa Wayahudi. Na kisha akampandisha cheo Modekai ili atumike mbele zake, kwa sababu Malkia Esta alikuwa amemueleza Mfalme uhusiano wake na Modekai.
\v 2 Kisha Mfalme akampa pete yake aliyokuwa amempa Hamani. Malkia Esta akampandisha Modekai ili awe mkuu katika shamba la Hamani.
\s5
\v 3 Kisha Esta akaongea tena na mfalme. Akaanguka chini na kulia mbele za mfalme akimsihi Mfalme abatilishe njama ya kuwaua Wayahudi wote iliyokuwa imetangazwa na Hamani Muagagi
\v 4 kisha mfalme akamnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu, akainuka na kusimama mbele ya mfalme.
\s5
\v 5 Esta akasema, "Kama ikikupendeza na kama nimepata kibali mbele zako, agiza mbiu ipigwe ili kubatilisha barua zilizoandikwa na Hamani mwana wa Hammedatha muagagi, barua alizoziandika ili kuwa angamiza Wayahudi wote walikuwa katika majimbo yote ya mfalme.
\v 6 Ninawezaje kuona ubaya ukiwapa watu wangu? Ninawezaje kutazama uharibifu wa jamaa zangu?"
\s5
\v 7 Mfalme Ahusiero akamwambia Esta na Modekai, Muyahudi, tazama nimempa Esta nyumba yote ya Hamani na wamemtundika Hamani katika mti kwa sababu alikuwa amekusudia kuwaangamiza Wayahudi wote.
\v 8 Hivyo andika mbiu nyingine kwa ajili ya Wayahudi kwa jina la mfalme na uipige muhuri kwa pete ya mfalme. Kwa sababu mbiu imekwisha andikwa kwa jina la mfalme na kugongwa muhuri kwa pete ya mfamle na haiwezi kubatilishwa."
\s5
\v 9 Kisha waandishi wa mfalme wakakusanyika kwa wakati huo huo katika mwezi wa tatu, ambao ni mwezi wa Sivani, siku ya ishirini ya mwezi wa tatu. Mbiu iliandikwa yote ambayo Modekai aliyaamuru kwa Wayahudi watendewe na wenyeji wa kila jimbo. Mbiu iliandikwa kwa maakida magavana na wakuu wa majimbo yote yaliyokuwa toka India hadi Ethiopia, majimbo 127 kila jimbo iliandikwa kuwa maandishi yake, na kila watu kwa lugha yao, na kwa Wayahudi kwa maandishi na lugha yao.
\s5
\v 10 Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme.
\v 11 Mfalme akawapa Wayahudi wote katika majimbo ya utawala wake kibali cha kukusanyika na kujilinda na ruhusa ya kuangamiza, kuua na kuharibu mtu yeyote aliyekuwa na kusudi la kuwaua Wayahudi wote na kupora mali zao.
\v 12 Jambo hili lilipaswa litekelezwe katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, siku ya ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ambao ni mwezi wa Adari.
\s5
\v 13 Nakala ya mbiu ilipaswa kutolewa kama sheria na kutangazwa kwa watu wote. Wayahudi walikuwa tayari kwa siku hiyo kulipa kisasi kwa adui zao.
\v 14 Hivyo matarishi wakaendesha farasi waliokuwa wakitumiwa katika huduma za kifalme. Walienda kwa haraka sana. Mbiu hii pia ilikuwa imetolewa katika mji wa Shushani pia.
\s5
\v 15 Kisha Mosekai akaondoka mbele za mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme, nguo buluu na nyeupe na taji kubwa ya dhahabu na joho la zambarau. Mji wa Shushani ukafurahia.
\v 16 Wayahudi walikuwa na nuru, na furaha na heshima. Mji wowote ambao mbiu hii ilipigwa, Wayahudi walifurahia na walifanya karamu na pumziko.
\v 17 Watu wengi wakatamani kuwa Wayahudi sababu ya hofu ya Wayahudi iliyokuwa juu yao.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Sasa katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya kumi na tatu ambayo ni siku ya Adari, siku ambayo adui wa Wayahudi walitarajia kutekeleza sheria ya mfalme na kupata nguvu dhidi ya Wayahudi. Badala yake Wayahudi wakapata nguvu dhidi ya adui zao.
\v 2 Wayahudi wote wakakusanyika katika miji yao katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kutia mikono juu ya wale waliokusudia ubaya. Hakuna aliye kuwa tayari kusimama zao kwa sababu hofu yao ilikuwa imewaangukia watu wote.
\s5
\v 3 Wakuu wote wa majimbo, maakida na magavana, na watawala wa mfalme, waliwasaidia Wayahudi kwa kuwa hofu ya Modekai ilikuwa imewaangukia.
\v 4 Kwa kuwa Modekai alikuwa mkuu katika nyumba ya mfalme, na umaarufu wake ukasambaa katika majimbo yote, kwa kuwa Modekai alikuwa akifanyika mkuu.
\v 5 Wayahudi wakawavamia maadi zao kwa upanga, wakiwatenda vibaya kama walivyokuwa wamekusudiwa mabaya dhidi yao Wakawatenda kama walivyo ona vyema machoni pao.
\s5
\v 6 Katika ngome ya mji wa Shushani pekee jumla ya maadui waliouawa na na kuharibiwa na Wayahudi ni wanaume mia tano.
\v 7 Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na Parishandatha, Dalphoni, Aspatha,
\v 8 Poratha, Adalia, Aridatha,
\v 9 Parimashita, Arisai, Aridai, Vaizatha,
\v 10 na wana kumi wa Hamani, mwana wa Hammedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchua mateka yoyote.
\s5
\v 11 Idadi ya wale waliouawa siku hiyo katika mji wa Shushani, ilifikishwa kwa Mfalme Ahusiero.
\v 12 Mfalme akamwambia malkia Esta. Mfalme akamwambia Malkia Esta, "Wayahudi wameua wanaume mia tano katika mji wa Shushani, wakiwemo wana kumi wa Hamani adui wa Wayahudi. Je wamefanya nini katika majimbo mengine? Na sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini?"
\s5
\v 13 Esta akamjibu, "Mfalme kama ikikupendeza, ruhusu Wayuadi walio katika mji wa Shushani wapige mbiu hii na kesho, na miili ya watoto wa Hamani itundikwe juu ya miti."
\v 14 Mfalme akaamuru ombi la Esta litekelezwe. Mbiu ilipigwa katika mji wa Shushani, na wana kumi wa Hamani wakatundikwa juu ya miti.
\s5
\v 15 Wayahudi katika mji wa Shushani walisanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na kuwaua maadui zao mia tatu katika mji wa Shushani, lakini hawakugusa nyara zao.
\v 16 Na Wayahudi katika majimbo mengine wakakusanyika ili kujilinda na wakapata faraja kutoka kwa maadui na wakawaua maadui zao elfu sabini na tano, lakini hawakugusa mikono yao kwa vitu vya thamani wale waliouwawa.
\s5
\v 17 Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari, Wayahudi wakapumzika katika siku ya kumi na nne, wakapumzika siku hiyo ya karamu na furaha.
\v 18 Lakini Wayahudi walioishi katika mji wa Shushani wakaja pamoja siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne. Na siku ya kumi na tano wakapumzika na wafanya karamu na kufurahia.
\v 19 Hii ndiyo sababu Wayahudi wa vijijini, wanaishi maeneo ya vijijini, huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu na siku ambayo hutumiana zawadi kwa kila mmoja.
\s5
\v 20 Modekai akaweka mambo haya na akatuma nyaraka kwa Wayahudi wote waliokuwa katika utawala wa Mfalme Ahusiero,
\v 21 akiwataka kuazimisha siku ya kumi na nne na kumi na tano ya mwezi wa Adari kila mwaka.
\v 22 Hizi zilikuwa ndizo siku ambazo Wahudi walipata faraja kutoka kwa maadui zao na wakati huu ndio wakati ambao huzuni ya Wayahudi iligeuzwa kuwa furaha, na kutoka kwa maombolezo hadi kwenye pumziko. Walipaswa kuzifanya siku za karamu na furaha, na kutumiana zawadi ya chakula, na zawadi kwa masikini.
\s5
\v 23 Wayahudi wakaendelea na maadhimisho wakifanya kile ambacho Modekai alikuwa amewaandikia.
\v 24 Na wakati huo Modekai mwana wa Hammedatha mwagagi, adui wa Wayahudi aliyekuwa amepanga njama ya kuwaangamiza Wayahudi, na kwa kupiga Puri (yaani akapiga kura) ili kuwaangamiza kabisa.
\v 25 Lakini Mfalme Ahusiero alipopata taarifa ya mpango mbaya huu alioupanga Modekai dhidi ya Wayahudi, aliagiza kwa nyaraka afanyiwe Modekai mwenyewe, na kwamba yeye na wana wake wanyongwe juu ya miti.
\s5
\v 26 Hivyo Wayahudi wakaziita siku hizi Purimu, kutokana na jina Puri. Kwa sababu ya mambo yote yaliyo kuwa yameandika katika barua, na mambo yote ambayo walikuwa wameyaona kwa macho yao, na yale yalikuwa yamewapata,
\v 27 Wayahudi wakapokea jukumu na desturi mpya. Desturi hii iwe kwa ajili yao, watoto wao, na kila ambaye aliyeungana nao. Na itakuwa kwamba maadhimisho haya watayafanya kwa kila mwaka. Wataadhimisha kwa namna fulani na nyakati hizo hizo kila mwaka.
\v 28 Siku hizi zilipaswa kuadhimishwa katika kila kizazi, kila familia, kila jimbo na kwa kila mji. Wayahudi hawa na watoto wao hawakuacha kuadhimisha siku hizi za Purimu, ili kwamba wasizisahau.
\s5
\v 29 Malkia Esta na Modekai wakaandika kwa mamlaka yote na kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
\s5
\v 30 Barua zilipelekwa katika majimbo 127 ya mfalme Ahusiero, zikiwatakia Wayahudi wote amani na kweli.
\v 31 Na kuthibitisha siku za Purimu sawa sawa na maelekezo ya Modekai na Esta yaliyowataka Wayahudi waadhimishe. Wayahudi wakatii maagizo kwa ajili yao na uzao wao, kama walivyotii siku za kufunga na kuomboleza.
\v 32 Agizo la Esta likahakikisha sheria hizi kuhusu Purimu, na ikaandikwa katika kitabu.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kisha Mfalme Ahusiero akaweka kodi juu ya nchi na maeneo ya bahari.
\v 2 Mafanikio yote na nguvu na ukuu wake, pamoja na wa Modekai ambao mfalme alimwinua, yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu ya wafalme wa Wamedi na Waajemi.
\s5
\v 3 Modekai Muyahudi alikuwa wa pili kutoka kwa Mfalme Ahusiero. Alikuwa mkuu na maarufu miongoni mwa ndugu zake Wayahudi, kwa sababu alitetea mahitaji ya watu wake na haki za watu na akatetea amani kwa watu wote.

2027
18-JOB.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2027 @@
\id JOB
\ide UTF-8
\h Ayubu
\toc1 Ayubu
\toc2 Ayubu
\toc3 job
\mt Ayubu
\s5
\c 1
\p
\v 1 Kulikuwa na mtu katika nchi ya Usi jina lake Ayubu; na Ayubu alikuwa mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na
\v 2 uovu. Wakazaliwa kwake watoto saba wa kiume na mabinti watatu.
\v 3 Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu mkuu wa watu wote wa mashariki.
\s5
\v 4 Kwa siku yake kila mtoto wa kiume, hufanya karamu katika nyumba yake. Wakatuma na kuwaita dada zao watatu waje kula na kunywa pamoja nao.
\v 5 Baada ya siku za karamu zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao na kuwatakasa. Aliamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa kila mtoto wake, kwa kusema, "Yawezekana kwamba wanangu wamefanya dhambi na kumkufuru Mungu mioyoni mwao." Siku zote Ayubu alifanya hivi.
\s5
\v 6 Kisha ilikuwa siku ambayo watoto wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Shetani pia akaenda pamoja nao.
\v 7 BWANA akamuuliza Shetani, "Umetoka wapi wewe?" Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo."
\v 8 BWANA akamuuliza Shetani, "Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu."
\s5
\v 9 Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Je Ayubu amcha Mungu bila sababu?
\v 10 Wewe hukumwekea kinga pande zote, kuzunguka nyumba yake, na kuzunguka vitu vyote alivyo navyo kutoka kila upande? Wewe umebariki kazi za mikono yake, na mifugo yake imeongezeka katika nchi.
\v 11 Lakini sasa nyosha mkono wako na uguse yote hayo aliyonayo, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako."
\v 12 BWANA akamwambia Shetani, "Tazama, hayo yote aliyonayo yamo mkononi mwako. Isipokuwa juu yake yeye mwenyewe usinyoshe mkono wako." Kisha Shetani akatoka mbele za BWANA.
\s5
\v 13 Ilitokea siku moja, wana wake wa kiume na binti zake walipokuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa.
\v 14 Mjumbe akamfikia Ayubu na kusema, "Hao maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakichunga karibu nao.
\v 15 Waseba wakawaangukia na kutoweka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."
\s5
\v 16 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, "Moto wa Mungu umeanguka toka mbinguni na kuwateketeza kondoo na watumishi. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."
\v 17 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, "Wakaldayo walifanya vikundi vitatu, wakawashambulia ngamia, na kuondoka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari."
\s5
\v 18 Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, "Wana wako wa kiume na binti zako walikuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa.
\v 19 Upepo wenye nguvu ulitokea jangwani na ukapiga pembe nne za nyumba. Ikawaangukia vijana hao, na wakafa wote. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.
\s5
\v 20 Kisha Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, akanyoa kichwa chake, akaanguka chini kifudifudi na kumwabudu Mungu.
\v 21 Akasema, "Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu ni uchi, nami nitakuwa uchi wakati nitakaporudi huko. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa. Jina la BWANA libarikiwe."
\v 22 Katika mambo hayo yote, Ayubu hakutenda dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa uovu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha kulikuwa na siku wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Shetani pia alikwenda kati yao kujihudhulisha mbele za BWANA.
\v 2 BWANA akamuuliza Shetani, "umetoka wapi wewe?" Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo."
\s5
\v 3 BWANA akamuuliza Shetani, "Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliye mcha Mungu na kuepukana na uovu. Hata sasa anashikamana na utimilifu wake, japokuwa ulinichochea juu yake, nimwangamize pasipo sababu."
\s5
\v 4 Shetani akamjibu BWANA na kusema, "Ngozi kwa ngozi, kweli; mtu atatoa vyote alivyo navyo kwaajili ya uhai wake.
\v 5 Lakini nyosha mkono wako sasa na uguse mifupa yake na nyama yake, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako."
\v 6 BWANA akamwambia Shetani, "Tazama, yumo mkononi mwako; ni uhai wake tu ambao lazima uutunze."
\s5
\v 7 Kisha Shetani akatoka mbele ya uso wa BWANA. Akampiga Ayubu na majipu mabaya toka wayo wa mguu hadi kichwani.
\v 8 Ayubu akachukua kipande cha kigae kujikunia, na akaketi chini majivuni.
\s5
\v 9 Kisha mkewe akamuuliza, "Je hata sasa wewe unashikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu na ufe.
\v 10 Lakini yeye akamwambia, "Wewe unaongea kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu waongeavyo. Je sisi tupate mema toka kwa Mungu na tusipate mabaya?" Katika mambo hayo yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake.
\s5
\v 11 Sasa wakati rafiki zake watatu wa Ayubu walipopata habari ya mabaya yaliyompata, kila mmoja wao akaja kutoka mahali pake: Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi. Wakatenga muda ili waende kuomboleza naye na kumfariji.
\s5
\v 12 Walipoinua macho yao wakiwa mbali, hawakuweza kumtambua. Wakapaza sauti zao na kulia; kila mmoja wao akararua joho lake na kurusha majivu hewani na juu ya kichwa chake.
\v 13 Kisha wakaketi chini pamoja naye kwa muda wa siku saba-mchana na usiku. Hakuna hata mmoja aliyesema naye neno, kwa kuwa waliona kuwa huzuni yake ilikuwa kuu mno.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Baada ya hayo, Ayubu akafunua kinywa chake na kuilani siku aliyozaliwa.
\v 2 Akasema,
\v 3 "Na ipotelee mbali siku niliyozaliwa mimi, usiku uliosema, 'Mimba ya mtoto wa kiume imetungwa.'
\s5
\v 4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu toka juu asiifikilie, wala mwanga usiiangazie.
\v 5 Ishikwe na giza na giza la mauti liwe lake. Wingu na likae juu yake; kila kitu kiifanyacho siku kuwa giza kweli na kiitishe.
\s5
\v 6 Usiku huo, na ukamatwe na giza tororo. Usihesabiwe miongoni mwa siku za mwaka; na usiwekwe katika hesabu ya miezi.
\v 7 Tazama, usiku huo na uwe tasa; na sauti ya shangwe isiwe ndani yake.
\s5
\v 8 Na wailani siku hiyo, hao wafahamuo namna ya kumuamsha lewiathani.
\v 9 Nyota za mapambazuko yake zitiwe giza. Siku hiyo iutafute mwanga, lakini isiupate; wala makope ya mapambazuko isiyaone,
\v 10 kwasababu haikuifunga milango ya tumbo la mama yangu, na kwasababu haikunifichia taabu machoni pangu.
\s5
\v 11 Kwanini si-kufa wakati lipotokeza katika tumbo la uzazi? Kwanini sikuitoa roho yangu hapo mama aliponizaa?
\v 12 kwanini magoti yake yalinipokea? Kwanini maziwa yake yanipokee hata ninyonye?
\s5
\v 13 Kwa sasa ningelikuwa nimelala chini kimya kimya. Ningelala usingizi na kupata pumziko
\v 14 pamoja na wafalme na washauri wa dunia, ambao walijijengea makaburi ambayo sasa ni magofu.
\s5
\v 15 Au Ningelikuwa nimelala pamoja na wakuu wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao fedha.
\v 16 Au pengine ningekuwa sijazaliwa, kama watoto wachanga wasio uona mwanga kabisa.
\s5
\v 17 Huko waovu huacha kusumbua; huko waliochoka hupumzika.
\v 18 Huko wafungwa kwa pamoja hupata amani; hawaisikii sauti ya msimamizi wa watumwa.
\v 19 Wote wadogo na watu maarufu wako huko; mtumishi yuko huru kwa bwana wake huko.
\s5
\v 20 Kwa nini yeye aliye mashakani kupewa mwanga? Kwa nini hao wenye uchungu moyoni kupewa uhai,
\v 21 ambao hutamani mauti lakini hawapati; ambao huyachimbulia mauti zaidi ya kutafuta hazina iliyofichika?
\v 22 Kwa nini kupewa mwanga ambao hushangilia mno na kufurahi walionapo kaburi?
\s5
\v 23 Kwanini kupewa mwanga mtu ambaye njia zake zimefichika, mtu ambaye Mungu amemzungushia uwa?
\v 24 Kwa kuwa kushusha kwangu pumzi kwatokea badala ya kula; kuugua kwangu kumemiminika kama maji.
\s5
\v 25 Maana jambo lile niliogopalo limenipata; nalo linitialo hofu limenijilia.
\v 26 Mimi sioni raha, sipati utulivu, na sipati pumziko; badala yake huja taabu."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
\v 2 Kama mtu yeyote akijaribu kuzungumza na wewe, je utakosa ustahimilivu? Lakini ni nani anaweza kujizuia asizungumze?
\v 3 Tazama, wewe umewafunza wengi; wewe imeipa nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.
\s5
\v 4 Maneno yako yamemsaidia yeye mwanamme aliyekuwa anaanguka; wewe umeyaimarisha magoti dhaifu.
\v 5 Lakini sasa matatizo yamekuja kwako, na wewe umechoka; yanakugusa wewe, na wewe umetatizika.
\v 6 Je si hofu yako imani yako, na ukamilifu wa njia zako tumaini lako?
\s5
\v 7 Tafakari juu ya hili, tafadhari: ni nani aliyeangamia akiwa hana kosa? Au ni lini watu wakamilifu walikatiliwa mbali?
\v 8 Kutokana na vile nilivyoona, wale walimao uovu na kupanda taabu huvuna hayo.
\v 9 Kwa pumzi ya Mungu huangamia; kwa mlipuko wa hasira zake huteketea.
\s5
\v 10 Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika.
\v 11 Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali.
\s5
\v 12 Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri, na sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo.
\v 13 Kisha yakaja mawazo kupitia ndoto wakati wa usiku, wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu..
\s5
\v 14 Ilikuwa usiku wakati nilipopatwa hofu na kutetemeka, na mifupa yangu yote ikatikisika.
\v 15 Kisha nafsi ikapita mbele ya uso wangu, na nywele zangu za mwili zilisimama.
\s5
\v 16 Nafsi ilisimama kimya, lakini sikuweza kupambanua sura yake. Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu; kulikuwa kimya, nami nikasikia sauti ikisema,
\v 17 "Je binadamu anaweza kuwa mwenye haki zaidi kuliko Mungu? Je mtu anaweza kuwa msafi zaidi kuliko muumba wake?
\s5
\v 18 Tazama, kama Mungu hawaamini watumishi wake; kama hulaumu upumbavu wa malaika zake,
\v 19 je si zaidi sana ukweli huu kwa wale waishio katika nyumba za udongo, ambao misingi yao ipo katika vumbi, wale waliopondwa mbele ya nondo?
\s5
\v 20 Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa; wameangamia milele wala bila yeyote kuwatambua.
\v 21 Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao? Wanakufa; wanakufa bila hekima.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Ita sasa; je kuna yeyote ambaye atakujibu? Utamrudia yupi katika watakatifu hao?
\v 2 Kwa kuwa hasira huua mtu mpumbavu; wivu huua mjinga.
\v 3 Nimemuona mtu mpumbavu akishika mzizi, lakini ghafla niliyalaani makazi yake.
\s5
\v 4 Watoto wake wako mbali na uzima; wameangamia langoni mwa mji. Hakuna yeyote atakaye waponya.
\v 5 Mwenye njaa hula mavuno yao; hata huyachukua katikati ya miiba. Wenye kiu huzihemea mali zao.
\s5
\v 6 Kwa kuwa magumu hayatoki udongoni; wala taabu haichipuki katika nchi.
\v 7 Badala yake, wanadamu huzaliwa kwaajili ya taabu, kama tu cheche za moto zirukavyo juu.
\s5
\v 8 Lakini kwa mimi, ningemrudia Mungu mwenyewe; kwake ningeaminisha kusudi langu -
\v 9 yeye afanyae makuu na mambo yasiyochunguzika, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu.
\v 10 Hutoa mvua juu ya nchi, na huyapeleka maji mashambani.
\s5
\v 11 Hufanya haya kwaajili ya kuwainua juu hao walio chini; huwapandisha sehemu salama hao waombolezao.
\v 12 Yeye huharibu mipango ya watu wenye hila, ili mikono yao isipate mafanikio.
\v 13 Yeye huwanasa watu wenye hekima katika matendo ya hila zao wenyewe; mipango ya watu waliogeuzwa huharibika haraka.
\s5
\v 14 Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, na hupapasa mchana kama vile ni usiku.
\v 15 Lakini yeye huokoa maskini kwa upanga wa vinywa vyao na mhitaji kwa mkono wa mtu mwenye nguvu.
\v 16 Hivyo mtu maskini ana matumaini, na udhalimu hufumba kinywa chake mwenyewe.
\s5
\v 17 Tazama, amebarikiwa mtu ambaye hutiwa adabu na Mungu; kwa sababu hiyo, usidharau uongozi wa Mwenyezi.
\v 18 Kwa kuwa yeye hujeruhi na kisha huuguza; yeye hutia jeraha na kisha mikono yake huponya.
\v 19 Yeye atakuokoa na mateso sita; kweli, katika mateso saba, hakuna uovu utakao kugusa.
\s5
\v 20 Wakati wa njaa atakukomboa na kifo, na kwa uwezo wa upanga wakati wa vita.
\v 21 Wewe utafichwa na mateso ya ulimi; na usitishike na uharibifu utakapokuja.
\v 22 Wewe utaufurahia uharibifu na njaa, na hutatishika na wanyama wakali wa nchi.
\s5
\v 23 Kwa kuwa wewe utakuwa na mapatano na mawe ya shambani mwako, na wanyama wa mwituni watakuwa na amani na wewe.
\v 24 Wewe utajua kwamba hema lako lina usalama; utatembelea zizi la kondoo wako na hutakosa kitu chochote.
\v 25 Pia utafahamu kwamba uzao wako utakuwa mwingi, na vizazi vyako vitakuwa kama nyasi ardhini.
\s5
\v 26 Wewe utafika kaburini kwako mwenye umri kamili, kama vile rundo la mashuke ya nafaka liendavyo juu wakati wake.
\v 27 Tazama, tumelipeleleza jambo hili; ndivyo lilivyo; lisikie, na ulifahamu kwa ajili yako mwenyewe."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Oo, laiti maumivu yangu makubwa yangepimwa; laiti misiba yangu yote mikubwa ingewekwa kwenye mizani!
\v 3 Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa baharini. Kwa sababu hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
\s5
\v 4 Kwa kuwa mishale ya Mwenyezi ipo ndani yangu, moyo wangu umelewa sumu; Vitisho vya Mungu vimejipanga vyenyewe dhidi yangu.
\v 5 Je punda mwitu hulia akiwa na malisho? Au ng'ombe huwa dhaifu wakati wa njaa ambapo anachakula?
\v 6 Je inawezekana kitu kisicho na ladha kulika bila chumvi? Au kuna radha yoyote katika ute mweupe wa yai?
\s5
\v 7 Nakataa kuvigusa; kwangu mimi vinafanana na chakula kichukizacho.
\v 8 Oo, kama nigeweza kupata haja yangu; oo, kama Mungu angeridhia jambo nilitamanilo sana:
\v 9 kama Mungu ingempendeza kuniangamiza mara moja, kwamba angeulegeza mkono wake na kuyakatilia mbali maisha yangu!
\s5
\v 10 Hii ingeweza kuwa faraja yangu hata sasa - hata kama nafurahia sana maumivu yasiyopungua: kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.
\v 11 Nguvu yangu ni ipi, hata nijaribu kusubiri? Mwisho wangu ni upi, utakao refusha maisha yangu?
\s5
\v 12 Je nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu umeumbwa kwa shaba nyeusi?
\v 13 Je si kweli kwamba sina msaada ndani yangu, na kwamba hekima imeondolewa mbali nami?
\s5
\v 14 Kwa mtu ambaye yu karibu kuzirai, inapasa uaminifu uonyeshwe na rafiki zake; hata kwake yeye aachaye kumcha Mwenyezi.
\v 15 Lakini ndugu zangu wamekuwa waaminifu kwangu kama mkondo wa maji jangwani, mfano wa mifereji ya maji ipitayo mpaka pasipo kitu,
\v 16 ambayo imekuwa mieusi kwa sababu ya barafu juu yake, na kwa sababu ya theluji ambayo hujificha yenyewe ndani yake.
\v 17 Wakati zikiyeyuka, hutoweka; kukiwa na joto, hutoweka mahali hapo.
\s5
\v 18 Misafara ambayo husafiri kwa njia yao hugeuka na maji; huzurura jangwani na kisha hupotea.
\v 19 Misafara kutoka Tema huitazama, wakati majeshi ya Sheba huitarajia.
\v 20 Wamevunjika moyo kwa sababu walitumaini kupata maji. Wakaenda huko, lakini walidanganywa.
\s5
\v 21 Kwa sasa ninyi rafiki si kitu kwangu; mmeona hali yangu ya kutisha nanyi mwaogopa.
\v 22 Je nilisema kwenu, 'Nipeni kitu furani?' Au, 'nitoleeni zawadi katika mali zenu?'
\v 23 Au, 'Niokoeni toka mkononi mwa mtesi wangu?' Au, 'Nitoleeni fidia kwa watesi wangu?'
\s5
\v 24 Nifundishe, nami nitaishika amani yangu; nifanye nifahamu wapi nilipokosea.
\v 25 Jinsi gani maneno ya kweli yanavyo umiza! Lakini hoja zenu, jee hasa zimenionya nini mimi?
\s5
\v 26 Je mnapanga kuyakemea maneno yangu, mnayachukulia maneno ya mtu mwenye kukata tamaa sawa na upepo?
\v 27 Hasa, mna piga kura kwa ajili ya yatima, na kupatana bei juu ya rafiki yenu kama bidhaa.
\s5
\v 28 Sasa, kwa sababu hiyo, tafadhari nitazame, kwa hakika sitasema uongo usoni penu.
\v 29 Rudini, nawasihi; lisiwepo neno la uonevu na nyinyi; Hasa, rudini, sababu zangu ni za haki.
\v 30 Je mna uovu ulimini mwangu? Je kinywa changu hakiwezi kungundua madhara?
\s5
\c 7
\p
\v 1 Je mtu hana kazi ngumu juu ya nchi? Je siku zake si kama siku za mwajiriwa?
\v 2 Kama mtumwa atamaniye sana kivuli cha jioni, kama mwajiriwa atafutaye ujira wake -
\v 3 hivyo nami nimeumbwa kuvumilia miezi ya taabu; Nami nimepewa taabu - zimeujaza usiku.
\s5
\v 4 Hapo nilalapo chini, najiuliza mwenyewe, 'Lini nitatoka kitandani na lini usiku utatoweka?' Nimejawa na kujitupa huku na huko hadi mwanzo wa siku.
\v 5 Mwili wangu umevikwa minyoo na madonda yenye vumbi; maumivu katika ngozi yangu yamekuwa magumu na kisha hutoweka na huendelea tena.
\s5
\v 6 Siku zangu zinakimbia kuliko chombo cha kufumia; zinapita bila tumaini.
\v 7 Mungu, anakumbuka kwamba maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona mema tena.
\s5
\v 8 Jicho lake Mungu, huyo anionaye mimi, halitaniangalia tena; Macho ya Mungu yatanitazama, lakini sitakuwako.
\v 9 kama vile wingu liishavyo na kutoweka, hivyo wale waendao sheoli hawatarudi tena kabisa.
\v 10 Yeye hatarudi tena nyumbani kwake, wala mahali pake hapatamtambua tena.
\s5
\v 11 Kwa sababu hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitasema juu ya maumivu makubwa ya roho yangu; Nitanung'unika juu ya uchungu wa nafsi yangu.
\v 12 Je mimi ni bahari au kiumbe cha kutisha baharini hata ukaweka mlinzi juu yangu?
\s5
\v 13 Hapo nisemapo, 'kitanda changu kitanifariji, na malazi yangu yatatuliza manung'uniko yangu,'
\v 14 halafu unitishapo kwa ndoto na kunitisha kwa maono,
\v 15 ili nichague kunyongwa na kufa kuliko kulinda mifupa yangu hii.
\s5
\v 16 Ninayachukia kabisa maisha yangu; sitamani siku zote kuwa hai; usinisumbue maana siku zangu hazifai.
\v 17 Je mtu ni nini hata ukatia bidii kwake, na ukaweka akili yako kwake,
\v 18 na kumwangalia kila asubuhi, na kumjaribu kila mara?
\s5
\v 19 Je itachukuwa muda gani kabla hujaacha kuniangalia, wala kunisumbua muda wa kutosha kwaajili ya kumeza mate yangu?
\v 20 Hata kama nimefanya dhambi, itakusaidia nini, wewe ulindaye wanadamu? Kwa nini umenifanya shabaha yako, kiasi kwamba nimekuwa mzigo kwako?
\s5
\v 21 Kwa nini hunisamehi makosa yangu na kuniondolea uovu wangu? kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; na wewe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwako."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Kisha Bildadi huyo Mshuhi akajibu na kusema,
\v 2 "hata lini wewe utasema mambo haya? Kwa muda gani maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo wenye nguvu?
\v 3 Je Mungu hupotosha hukumu? Je Mwenyezi hupotosha haki?
\s5
\v 4 Watoto wako wametenda dhambi dhidi yake; tunalifahamu hili, kwa kuwa amewatia mkononi kwa makosa yao.
\v 5 Lakini wewe unaonaje ukimtafuta Mungu kwa bidii na kufikisha haja yako kwa huyo Mwenyezi.
\s5
\v 6 Ukiwa wewe ni msafi na mkamilifu, hakika angeamka mwenyewe kwa niaba yako na kukurudisha kwenye makazi ya haki yako.
\v 7 Japokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, hata hivyo hali yako ya mwisho itaongezeka sana.
\s5
\v 8 Tafadhari uwaulize vizazi vya zamani, na utie bidii katika hayo mababu zetu waliyojifunza.
\v 9 (Sisi ni wa jana tu na hatujui chochote kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli).
\v 10 Je hawatakufunza wao na kukuambia? Je hawatatamka maneno yatokayo mioyoni mwao?
\s5
\v 11 Je hayo mafunjo yaota pasipo matope? Je mafunjo yaota pasipo maji?
\v 12 Wakati yakiwa bado ya kijani na hayajakatwa, hunyauka kabla ya mmea mwingine.
\s5
\v 13 Hivyo pia njia ya wote wamsahauo Mungu, na matumaini ya asiyeamini Mungu yatatoweka.
\v 14 Ujasiri wake utavunjika, na matumaini yake ni dhaifu kama utando wa buibui.
\v 15 Ataitegemea nyumba yake, lakini haitamsaidia; atashikamana nayo, lakini isidumu.
\s5
\v 16 Yeye huwa mti mbichi chini ya jua, na machipukizi yake huenea katika bustani yake yote.
\v 17 Mizizi yake hujifunga funga kwenye rundo la mawe; huangalia mahali pazuri katikati ya mawe;
\v 18 Lakini mtu huyu aking'olewa mahali pake, kisha mahali pale patamkana, na kusema, 'mimi sikukuona.'
\s5
\v 19 Tazama, hii ni "furaha" ya mtu mwenye tabia hiyo; mimea mingine itachipuka toka katika udongo ule ule mahali pake.
\v 20 Tazama, Mungu hatamtupa mtu asiye na kosa; wala hatawathibitisha watendao uovu.
\s5
\v 21 Yeye atakijaza kinywa chako na kicheko, midomo yako na shangwe.
\v 22 Wale ambao wanakuchukia wewe watavishwa aibu; nayo hema yake mwovu haitakuwepo tena.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "kweli najua kwamba ndivyo hivyo. Lakini ni kwa namna gani mtu anakuwa na haki kwa Mungu?
\v 3 Kama akitaka kujibishana na Mungu, hatamjibu yeye mara moja katika elfu zaidi.
\s5
\v 4 Mungu ni mwenye hekima moyoni na ukuu katika nguvu; ni nani daima aliyejifanya mwenyewe kuwa mgumu dhidi yake na akafanikiwa? -
\v 5 ambaye huiondoa milima bila kumtahadharisha yeyote wakati akiipindua katika hasira zake -
\v 6 ambaye huitikisa nchi itoke mahali pake na mihimili yake hutikisika.
\s5
\v 7 Ni Mungu yule yule ambaye huliamuru jua lisichomoze, nalo halichomozi, na ambaye huzihifadhi nyota,
\v 8 ambaye peke yake ni mwenye kupanua mbingu na kuyatuliza mawimbi ya bahari,
\v 9 ambaye huumba Dubu, Orioni, kilima, na makundi ya nyota ya kusini.
\s5
\v 10 Ni Mungu yule yule atendaye mambo makuu, mambo yasiyofahamika - hasa, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
\v 11 Tazama, huenda karibu nami, na siwezi kumuona yeye; pia hupita kwenda mbele, lakini ni simtambue.
\v 12 Kama akichukua kitu chochote, nani atamzuia? Nani awezaye kumuuliza, 'unafanya nini?'
\s5
\v 13 Mungu hataondoa hasira yake; wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
\v 14 Je ni upungufu kiasi gani mimi nitamjibu, je nichague maneno kuhojiana naye?
\v 15 Hata kama ni mwenye haki, nisingelimjibu; ningeomba msamaha tu kwa hukumu yangu.
\s5
\v 16 Hata kama ningelimwita na yeye akanitikia, nisingeamini kuwa ameisikia sauti yangu.
\v 17 kwa kuwa yeye anidhoofishaye kwa dhoruba na kuyaongeza majeraha yangu pasipo sababu.
\v 18 Yeye hataki hata kuniruhusu nipate kuvuta pumzi; badala yake, hunijaza uchungu.
\s5
\v 19 Kama ni habari ya nguvu, tazama! yeye ni mwenye uwezo! Kama ni habari ya haki, ni nani atakaye mhukumu?
\v 20 Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu; na ingawa ni mtakatifu, maneno yangu yatashuhudia kuwa ni mwenye kosa.
\s5
\v 21 Mimi ni mtakatifu, lakini siijali zaidi nafsi yangu; Naudharau uhai wangu mwenyewe.
\v 22 Haileti tofauti yoyote, kwa sababu hiyo nasema kwamba yeye huangamiza watu wasio na makosa na waovu pia.
\v 23 Kama hilo pigo likiua ghafla, yeye atafurahi mateso yake mtu asiye na kosa.
\v 24 Dunia imetiwa mkononi mwa watu waovu; Mungu hufunika nyuso za waamuzi wake. kama si yeye hufanya, ni nani basi?
\s5
\v 25 Siku zangu zinapita haraka kuliko tarishi akimbiae; siku zangu zinakimbia mbali; wala hazioni mema mahali popote.
\v 26 Zinapita kama mashua zilizoundwa kwa mafunjo ziendazo kwa kasi, na zinakasi kama tai ashukaye upesi katika mawindo yake.
\s5
\v 27 Kama ni kisema kwamba mimi nitasahau kuhusu manung'uniko yangu, kwamba nitaacha kuonyesha sura ya huzuni na kuwa na furaha,
\v 28 Mimi nitaziogopa huzuni zangu zote kwa sababu nafahamu kuwa hutanihesabu kuwa sina hatia.
\v 29 Nitahukumiwa; kwa nini, basi, nitaabike bure?
\s5
\v 30 Kama najiosha mwenyewe kwa maji ya theluji na kuitakasa mikono yangu na kuwa safi zaidi,
\v 31 Mungu atanitumbukiza shimoni, na nguo zangu mwenyewe zitanichukia.
\s5
\v 32 Kwa kuwa Mungu si mtu, kama mimi, kwamba naweza kumjibu, hata tukaribiane katika hukumu.
\v 33 Hakuna hakimu baina yetu awezaye kuweka mkono wake juu yetu sote.
\s5
\v 34 Hakuna hakimu mwingine ambaye anaweza kuniondolea fimbo ya Mungu, awezaye kuzuia kitisho chake kisinitie hofu. kisha ningesema na nisimuogope.
\v 35 Lakini kama mambo yalivyo sasa, sitaweza kufanya hivyo.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Nimechoka na maisha yangu; Nitanena wazi manung'uniko yangu; nitasema kwa uchungu wa roho yangu.
\v 2 Nitamwambia Mungu, 'Usinihukumie makosa; nionyeshe sababu za wewe kunilaumu mimi. Je
\v 3 ni vizuri kwako wewe kunionea mimi, kudharau kazi ya mikono yako wakati unafurahia juu ya mipango ya waovu?
\s5
\v 4 Je wewe una macho ya kimwili? Je wewe unaona kama mtu aonavyo?
\v 5 Je siku zako ni kama siku za wanadamu au miaka yako ni kama miaka ya watu,
\v 6 hata ukauliza habari za uovu wangu na kuitafuta dhambi yangu,
\v 7 ingawa wewe wafahamu mimi sina kosa na hapana mwingine awezaye kuniokoa mimi na mkono wako?
\s5
\v 8 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga kwa wakati mmoja nawe kunizunguka, hata hivyo unaniangamiza.
\v 9 Kumbuka, nakuomba, ulivyonifinyanga kama vile udongo; je utanirudisha mavumbini tena?
\s5
\v 10 Je wewe hukunimimina kama maziwa na kunigandisha mfano wa jibini?
\v 11 Umenivika ngozi na nyama na kuniunganisha pamoja kwa mifupa na misuli..
\s5
\v 12 Wewe umenizawadia mimi uhai na ahadi ya upendeleo na usaidizi wako umeilinda roho yangu.
\v 13 Hata hivyo mambo haya uliyaficha moyoni mwako - nafahamu kwamba hivi ndivyo ufikirivyo:
\v 14 kuwa kama nimefanya dhambi, wewe utaizingatia; hutaniachilia na uovu wangu.
\s5
\v 15 Kama mimi ni muovu, ole wangu; hata kama ni mwenye haki, sitaweza kuinua kichwa changu, kwa kuwa nimejaa aibu na kuyaangalia mateso yangu.
\v 16 Kama kichwa changu kikijiinua chenyewe, waniwinda kama simba; tena wajionyesha mwenyewe kuwa ni mwenye nguvu kwangu.
\s5
\v 17 Wewe unaleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira zako dhidi yangu; wanishambulia na majeshi mapya.
\s5
\v 18 Kwa nini, basi, ulinitoa tumboni? Natamani ningekata roho na ili jicho lolote lisinione.
\v 19 Ningelikuwa kama asiyekuwepo; ningelichukuliwa kutoka tumboni mpaka kaburini.
\s5
\v 20 Je si siku zangu pekee ni chache? Acha basi, usinisumbue, ili kwamba nipate kupumzika kidogo
\v 21 kabla sijaenda huko ambako sitarudi, kwenye nchi ya giza na kivuli cha mauti,
\v 22 ni nchi ya giza kama usiku wa manane, nchi ya kivuli cha mauti, isiyokuwa na mpangilio, ambayo nuru yake ni kama usiku wa manane.'"
\s5
\c 11
\p
\v 1 Ndipo Sofari Mnaamathi alijibu na kusema,
\v 2 " Huo wingi wa maneno haupaswi kujibiwa? Mtu huyu, aliyejaa maneno mengi awe wa kuaminiwa?
\v 3 Kujivuna kwako kunapaswa kuwafanya wengine wabaki wamenyamaza? Wakati unapoyadhihaki mafundisho yetu, hakuna awaye yote atakayekufanya wewe ujisikie mwenye aibu?
\s5
\v 4 Kwa kuwa wewe unasema kwa Mungu, 'Imani yangu ni safi, Mimi sina waa lolote machoni pako.'
\v 5 Lakini, laiti, Mungu huyo angesema na kufungua midomo yake dhidi yako;
\v 6 hivyo angekuonyesha wewe siri za hekima! Kwa kuwa yeye ni mkuu katika ufahamu. Tena tambua huyo Mungu anataka kutoka kwako kidogo kuliko uovu wako unavyostahili.
\s5
\v 7 Je, wewe unaweza kumfahamu Mungu kwa kumtafuta yeye? Unaweza kumtambua aliye mkuu kwa ukamilifu?
\v 8 Upeo uko juu kama mbingu; unaweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kirefu kuliko kuzimu; waweza kufahamu nini wewe?
\v 9 Vipimo vyake ni virefu kuliko nchi, na vipana kuliko bahari.
\s5
\v 10 kama yeye akipita kati na kumyamazisha mtu yeyote, kama yeye akimwita mtu yeyote hukumuni, tena ni nani anayeweza kumzuia yeye?
\v 11 Kwa maana anawajua watu waongo; wakati anapoona uovu, hawezi yeye kuukumbuka?
\v 12 Lakini watu wapumbavu hawana ufahamu; wataupata wakati punda mwitu atakapozaa mtu.
\s5
\v 13 Lakini ikiwa umeuelekeza moyo wako kwa haki na umeunyosha mkono wako karibu na Mungu;
\v 14 ikiwa huo uovu ulikuwa katika mikono yako, lakini hivyo tena unauweka mbali nawe, na haukuruhusu kutokuwa mwenye haki kukaa hemani mwako.
\s5
\v 15 Ndipo kwa hakika ungeinua juu uso wako bila ishara ya aibu; Ni dhahiri, ungethibitika na usingeogopa.
\v 16 Wewe ungesahau mateso yako; ungeyakumbuka hayo tu kama maji ambayo yametiririka mbali.
\v 17 Maisha yako yangekuwa angavu kuliko adhuhuri; japokuwa kulikuwa na giza, litakuwa kama asubuhi.
\s5
\v 18 Ungekuwa salama kwa sababu kuna tumaini; ni dhahiri, wewe utapata usalama juu yako na utachukua pumziko lako katika usalama.
\v 19 Pia ungelala chini katika pumziko, na hakuna ambaye angekufanya wewe uogope; hakika wengi wangetafuta upendeleo wako.
\s5
\v 20 Lakini macho ya watu waovu yatashindwa; hawatakuwa na njia ya kukimbia; tumaini lao la pekee litakuwa pumzi yao ya mwisho ya uhai.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Hakuna shaka ninyi wanadamu; Hekima mtakufa nayo.
\v 3 Lakini nina ufahamu kama vile ninyi; Mimi siyo duni kwenu. Ni dhhiri, ni nani asiyefahamu vitu hivyo kama hivi?
\s5
\v 4 Mimi ni kitu cha kuchekwa na jirani-Mimi, ni mmoja aliyemwita Mungu na ambaye alijibiwa na yeye! Mimi, ni mwenye haki na mtu asiyekuwa na hatia-Mimi sasa nimekuwa kitu cha kuchekwa.
\v 5 Katika mawazo yake mtu fulani aliye katika kufurahi, kuna kudharau kwa mashaka; hufikiri katika njia ambayo huleta mambo mabaya zaidi kwa wale ambao miguu yao inateleza.
\v 6 Hema za wezi hufanikiwa, na wale ambao humkasirisha Mungu huhisi salama; mikono yao wenyewe ni miungu wao.
\s5
\v 7 Lakini sasa waulize hao wanyama wa mwituni, na watakufundisha wewe; waulize ndege wa angani, na watakuambia wewe.
\v 8 Au iambie ardhi, na itakufundisha wewe; samaki wa baharini watakutangazia wewe.
\s5
\v 9 Ni myama yupi miongoni mwa hawa asiyefahamu kuwa mkono wa Yahwe umetenda haya?
\v 10 Katika mkono wake mna uzima wa kila kiumbe hai na pumzi ya wanadamu wote.
\s5
\v 11 Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile kaakaa lionjavyo chakula chake?
\v 12 Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu.
\s5
\v 13 Pamoja na Mungu mna hekima na ukuu; yeye anayo mashauri na ufahamu.
\v 14 Tazama, yeye huangusha chini, na haiwezekani kujengwa tena; kama yeye akimtia gerezani mtu yeyote, hakutakuwa tena kufunguliwa.
\v 15 Tazama, kama yeye akiyazuia maji, yanakauka; na kama akiyaachilia nje yanaitaabisha ardhi.
\s5
\v 16 Pamoja na yeye mna nguvu na hekima; watu ambao wamedanganywa na mdanganyi wote pamoja wako katika nguvu zake.
\v 17 Yeye huwaongoza washauri mbali bila kuvaa viatu katika huzuni; huwarudisha hakimu katika upumbavu.
\v 18 Yeye Huondoa minyororo ya mamlaka kutoka kwa wafalme; yeye hufunika viuno vyao kwa nguo.
\s5
\v 19 Yeye huwaongoza makuhani mbali bila kuvaa viatu na kuwapindua watu wakuu.
\v 20 Yeye huondoa hotuba ya wale waliokuwa wameaminiwa na huondoa mbali ufahamu wa wazee.
\v 21 Yeye humwaga aibu juu ya binti za wafalme na hufungua mishipi ya watu wenye nguvu.
\s5
\v 22 Yeye huweka wazi vitu vya kina kutoka katika giza na kuvileta nje kumuika vivuli mahali ambapa watu waliokufa wapo.
\v 23 Yeye huyafanya mataifa kuwa na nguvu, na pia huyaharibu; Yeye pia huyakuza mataifa, na pia yeye huyaongoza mbali kama wafungwa.
\s5
\v 24 Yeye huondoa mbali ufahamu kutoka kwa viongozi wa watu wa nchi; huwafanya wao kutangatanga msituni mahali pasipo na njia.
\v 25 Wao wanapapasa katika giza bila kuwa na mwanga; yeye huwafanya wao kuweweseka kama mtu mlevi.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Tazama, jicho langu limeyaona haya yote; sikio langu limeyasikia na kuyaelewa hayo.
\v 2 Kile mnachokifahamu, ndicho hicho mimi pia ninachokifahamu; Mimi siyo duni kwenu ninyi.
\s5
\v 3 Hata hivyo, Mimi ningeweza kuzungumza na mwenye nguvu; Mimi natamani kusemezana na Mungu.
\v 4 Lakini ninyi mnauficha ukweli kwa uongo; ninyi nyote ni tabibu msiokuwa na thamani.
\v 5 Laiti, kwamba kwa pamoja mngeshikilia amani yenu! Hilo lingekuwa hekima yenu ninyi.
\s5
\v 6 Sikia sasa kuhoji kwangu; Sikiliza kusihi kwa midomo yangu mwenyewe.
\v 7 Ninyi mtazungumza visivyo haki kwa ajili ya Mungu, na ninyi mtazungumza udanganyifu kwa yeye? Ni kweli ninyi mngeonyesha ukarimu kwa yeye?
\v 8 Ni kweli ninyi mngetetea katika mahakama kama mawakili wa Mungu?
\s5
\v 9 Je, kweli ingekuwa vizuri kwenu wakati yeye akiwatafuta ninyi? Mngeweza ninyi kumdanganya yeye kama mlivyoweza kuwadanganya watu?
\v 10 Yeye kwa hakika angewathibitisha upya ninyi ikiwa katika siri ninyi mmeonyesha kutokukamilika.
\s5
\v 11 Je, ukuu wake usingewafanya ninyi muogope? Je, utisho wake usingeshuka juu yenu?
\v 12 Hadithi zenu za misemo ya kukariri, ni mithali zimetengenezwa kwa majivu; utetezi wenu ni utetezi uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi.
\s5
\v 13 Shikilieni amani yenu, mniache peke yangu, ili ya kwamba nipate kusema, acheni yaje yale yanayoweza kuja kwangu.
\v 14 Nitaichukua nyama yangu mwenywewe katika meno yangu; Nitayachukua maisha yangu katika mikono yangu.
\v 15 Tazama, ikiwa ataniua mimi, sitakuwa na tumaini lililobakia; hata hivyo, nitazitetea njia zangu mbele zake yeye.
\s5
\v 16 Hiki kitakuwa sababu ya kutohesabiwa hatia, kwamba mimi sikuja mbele zake kama mtu asiyemcha Mungu.
\v 17 Mungu, sikiliza kwa makini kuzungumza kwangu; ruhusu kutangaza kwangu kuje kwenye masikio yako.
\s5
\v 18 Tazama sasa, Nimeuweka utetezi wangu katika mpangilio, Mimi ninafahamu kwamba mimi sina hatia.
\v 19 Ni nani anayeweza kushindana na mimi katika mahakama? Ikiwa mlikuja kufanya hivyo, na kama mimi nilithibitishwa kukosea, ndipo ningekuwa kimya na kuyatoa maisha yangu.
\s5
\v 20 Mungu, fanya mambo mawili kwa ajili yangu, na tena Mimi sitajificha kutoka katika uso wako.
\v 21 Ondoa kutoka kwangu mkono wako unaotesa, na usiache utisho wako unifanye mimi kuogopa.
\v 22 Ndipo niite mimi, na mimi nitakujibu; au uniache mimi niseme na wewe na wewe unijibu mimi.
\s5
\v 23 Je, maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
\v 24 Kwa nini unaficha uso wako kutoka kwangu mimi na kunitendea mimi kama adui yako?
\v 25 Je, wewe utalitesa jani linalopeperushwa? Je, utaendelea kulifuatilia bua kavu?
\s5
\v 26 Kwa maana wew unaandika chini vitu vichungu dhidi yangu mimi; wewe unanifanya mimi kurithi uovu wa ujana wangu.
\v 27 Wewe pia unaiweka miguu yangu katika nguo nyembamba; wewe waangalia njia zangu zote; wewe wachunguza chini mahali ambapo nyayo za miguu yangu zimekanyaga.
\v 28 japokuwa mimi ni kama kitu kilichooza ambacho hutupwa mbali, kama vazi lile ambalo nondo wamelila.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Mwanadamu, ambaye amezaliwa na mwanamke, huishi siku chache tu na amejaa mahangaiko.
\v 2 Yeye huchanua kutoka katika ardhi kama ua na kukatwa chini; yeye hukimbia kama kivuli na hawezi kudumu.
\v 3 Je, wewe unatazama chochote katika hivi? Mnanileta mimi hukumuni pamoja nanyi?
\s5
\v 4 Ni nani anayeweza kukileta kitu safi kutoka katika kitu kichafu? Hakuna awaye yote.
\v 5 Siku za mwanadamu zimeamriwa. Idadi ya miezi yake unayo wewe; umekiweka kikomo chake ambacho hawezi kukivuka.
\v 6 Tazama mbali kutoka kwake kwamba yeye aweze kupumzika, ili kwamba aweze kufurahia siku yake kama mtu aliyekodishwa kama yeye anaweza kufanya hivyo.
\s5
\v 7 Kunaweza kuwa na tumaini kwa mti; kama ukikatwa chini, unaweza kuchipua tena, hivyo chipukizi lake halitapotea.
\v 8 Japokuwa mizizi yake inakua na kuzeeka katika ardhi, na shina lake kufa katika udongo,
\v 9 hata kama bado lina harufu ya maji pekee, litachipua tena na kutoa nje matawi kama mche.
\s5
\v 10 Lakini mwanadamu hufa; yeye huwa dhaifu; haswaa, mwanadamu hukoma kupumua, na tena yuko wapi yeye?
\v 11 Kama maji yanavyopotea kutoka ziwani, na kama vile mto upotezavyo maji na kukauka,
\v 12 vivyo hivyo watu hulala chini na hawaamki tena. Mpaka pale mbingu zitakapokuwa hazipo tena, hawataamka wala kuamshwa kutoka katika kulala kwao.
\s5
\v 13 Laiti, kwamba ungenificha mimi mbali katika kuzimu mbali kutoka katika mahangaiko, na kwamba ungenitunza mimi katika siri hadi hasira yake imalizike, kwamba ungeniwekea mimi muda maalumu wa kukaa huko na kisha kuniita mimi katika fahamu!
\v 14 Ikiwa mwanadamu akifa, yeye ataishi tena? Ikiwa hivyo, ningependa kusubiri kule muda wangu wote wa kuharibika mpaka kufunguliwa kwangu kutakapokuja.
\s5
\v 15 Wewe ungeita, na mimi ningekujibu wewe. Wewe ungekuwa na shauku ya kazi ya mikono yako.
\v 16 Wewe ungehesabu na kutunza nyayo zangu; Wewe usingejali kumbukumbu ya dhambi yangu.
\v 17 Uovu wangu ungetiwa muhuri katika mkoba; wewe ungeufunga uovu wangu.
\s5
\v 18 Lakini hata milima huanguka na kuwa si chochote; hata miamba huhamishwa kutoka mahali pake;
\v 19 maji yaliyokuwa chini ya mawe; kufurika kwake huondoa mbali mavumbi ya nchi. Kama hivi, ninyi mnavyoharibu matumaini ya mwanadamu.
\s5
\v 20 Ninyi daima humshinda yeye, na yeye hupita mbali; Ninyi mnabadilisha uso wake na kumtuma yeye mbali kufa.
\v 21 Kama watoto wake wa kiume ni wa kuheshimiwa, yeye, hatambui hicho; na kama wakishushwa chini, yeye haoni hicho.
\v 22 Yeye hujisikia tu maumivu ya mwili wake mwenyewe, na hujiombolezea yeye mwenyewe.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Ndipo Elifazi Mtemani alijibu na kusema,
\v 2 Mtu mwenye hekima anapaswa kujibu kwa maarifa yasiyofaa na kujijaza mwenyewe na upepo wa mashariki?
\v 3 Anapaswa kuhojiana na mazungumzo yasiyo na faida au na hotuba ambazo kwa hizo yeye hawezi kufanya mema?
\s5
\v 4 Dhahiri, wewe wafifisha heshima ya Mungu; Wewe wazuia heshima kwa yeye,
\v 5 kwa maana uovu wako hufundisha midomo yako; Wewe wachagua kuwa na ulimi wa mtu mwenye hila.
\v 6 Mdomo wako mwenyewe hukukukumu wewe, siyo wangu; hakika, midomo yako mwenyewe hushuhudia dhidi yako wewe.
\s5
\v 7 Je, wewe ni mwanadamu wa kwanza ambaye aliyezaliwa? Wewe ulikuwepo kabla ya vilima kuwepo?
\v 8 Wewe Umewahi kusikia maarifa ya siri ya Mungu? Je, wewe wajihesabia mwenye hekima wewe mwenyewe?
\v 9 Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho sisi hatukijui? Ni kitu gani unachokifahamu wewe ambacho hakiko katika sisi?
\s5
\v 10 Pamoja nasi wapo pia wenye mvi na watu wazee sana ambao ni wazee zaidi kuliko baba yako.
\v 11 Je, faraja ya Mungu ni ndogo sana kwako, maneno ambayo ni ya upole dhidi yako wewe?
\s5
\v 12 Kwa nini moyo wako wewe unakupeleka mbali? Kwa nini macho yako yananga'ra,
\v 13 ili ya kwamba kuirejesha roho yako kwa Mungu na kuyatoa maneno hayo kutoka katika mdomo wako?
\v 14 Je, mwanadamu yeye ni nini kwamba yeye anapaswa kuwa safi? Yeye mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ni nini kwamba yeye anapaswa awe mwenye haki?
\s5
\v 15 Tazama, Mungu haweki tumaini lake hata kwa mmoja wake aliye mtakatifu; Hakika, mbingu haziko safi machoni pake yeye;
\v 16 jinsi gani asivyo safi ni mmoja aliye mbaya na mla rushwa, mtu ambaye hunywa uovu kama maji!
\s5
\v 17 Mimi nitakuonyesha wewe; Nisikilize mimi; Mimi nitakutangazia wewe vitu ambavyo nimeviona,
\v 18 vitu ambavyo watu wenye hekima wamepita chini yake kutoka kwa baba zao, vile vitu ambavyo mababu zao hawakuvificha.
\s5
\v 19 Hawa walikuwa mababu zao, ambao kwao pekee nchi walipewa, na miongoni mwao hakuna mgeni aliyepita.
\v 20 Mtu mwovu hupitia katika maumivu siku zake zote, idadi ya miaka iliyowekwa juu kwa mtesaji kuteseka.
\v 21 Sauti ya vitisho katika masikio yake; pindi yeye yuko katika kufanikiwa, mharibu atakuja juu yake yeye.
\s5
\v 22 Yeye hafikiri kwamba yeye atarudi kutoka katika giza; Upanga humngojea yeye.
\v 23 Yeye huenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya mkate, akisema, 'Kiko wapi? ' Yeye anatambua kuwa siku ya giza iko mkononi.
\v 24 Dhiki na mateso makali humfanya aogope; wao hushinda dhidi yake yeye, kama mfalme tayari kwa vita.
\s5
\v 25 Kwa sababu yeye ameunyosha mkono wake dhidi ya Mungu na ameishi kwa kiburi dhidi ya aliye mkuu,
\v 26 huyu mtu mwovu hukimbia kwa Mungu na shingo ngumu, kwa vifundo vikubwa vya ngao.
\s5
\v 27 Hii ni kweli, hata ingawa yeye amefunika uso wake kwa mafuta yake na amekusanya mafuta juu ya viuno vyake,
\v 28 na ameishi katika miji yenye ukiwa; katika nyumba ambazo hakuna mwanadamu anayeishi humo sasa na ambazo zilikuwa tayari kuwa magofu.
\s5
\v 29 Yeye hatakuwa tajiri; utajiri wake yeye hautadumu; hata kivuli chake hakitadumu katika nchi.
\v 30 Yeye hatatoka nje ya giza; mwali wa moto utakausha matawi yake; katika pumzi ya kinywa cha Mungu yeye ataenda zake.
\s5
\v 31 Mwacheni yeye asitumaini katika vitu visivyofanya kazi, akijidanganya yeye mwenyewe; maana upuuzi utakuwa mshahara wake yeye.
\v 32 Itatokea kabla ya wakati wake yeye atapaswa kufa; tawi lake halitakuwa kijani.
\v 33 Yeye atazipukutisha zabibu zake zisizovunwa kama mzabibu; yeye atayaondoa maua yake kama mti wa mzeituni.
\s5
\v 34 Kwa maana msaada wa watu wasiomcha Mungu utakuwa tasa; moto utateketeza hema za rushwa.
\v 35 Wao wanabeba mimba yenye ubaya na kuzaa uovu; tumbo lao hutunga mimba ya udanganifu.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Mimi nimevisikia vitu hivyo vingi; ninyi nyote ni wafariji wenye kuhuzunisha.
\v 3 Maneno yenye upuuzi daima yanaweza kuwa na mwisho? Nini kimeharibika kwenu kwamba mnajibu kama hivi?
\s5
\v 4 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi mnavyofanya, kama ninyi mngekuwa katika nafasi yangu; Mimi ningekusanya na kuunganisha maneno pamoja dhidi yenu na kutikisa kichwa changu kwenu ninyi katika dhihaka.
\v 5 Laiti, jinsi gani Mimi ningewatia moyo na midomo yangu! Jinsi gani faraja kutoka midomo yangu ingenga'risha huzuni yenu!
\s5
\v 6 Ikiwa Mimi ninazungumza, kuomboleza kwangu hakujasikilizwa; Ikiwa nikiendelea katika kuzungumza, jinsi gani mimi ninaidiwa?
\v 7 Lakini sasa, Mungu,
\v 8 wewe umenifanya mimi kuchoka; wewe umeifanya familia yangu yote kuwa ukiwa. Wewe umenifanya mimi kukauka, ambayo yenyewe ni ushuhuda dhidi yangu mimi; kukonda kwa mwili wangu huinuka dhidi yangu, na kunashuhudia dhidi ya macho yangu.
\s5
\v 9 Mungu amenirarua mimi katika ghadhabu yake na amenitesa mimi; Yeye amenisaga mimi kwa meno yake; Adui yangu amenikazia macho yake juu yangu kama yeye anavyonirarua mimi vipande.
\v 10 Watu wameachama na midomo iliyowazi juu yangu; wamenipiga mimi katika shavu kwa kunitukana; wamekusanyika pamoja kinyume changu mimi.
\s5
\v 11 Mungu amenikabidhi mimi juu ya watu wasio mcha Mungu, na kunitupa mimi ndani ya mikono ya watu waovu.
\v 12 Mimi nilikuwa katika wepesi, na yeye amenivunjavunja mimi vipande. Hakika, amenichukua mimi kwa shingo na ameniponda mimi vipande vipande; yeye pia ameniweka mimi juu kama shabaha yake.
\s5
\v 13 Wapiga upinde wake wote wamenizunguka mimi; Mungu huzikata vipande vipande figo zangu, na haniokoi mimi; yeye humwaga nje nyongo yangu juu ya ardhi.
\v 14 yeye hukanyaga kanyaga kupitia ukuta wangu tena na tena; yeye hukimbia juu yangu mimi kama shujaa.
\s5
\v 15 nguo ya magunia juu ya ngozi yangu; Mimi nimeisukuma kwa nguvu pembe yangu ndani ya ardhi.
\v 16 Uso wangu ni mwekundu na kuomboleza; juu ya ngozi inayofunika macho kuna kivuli cha mauti
\v 17 ingawa hakuna dhuluma katika mikono yangu, na kuomba kwangu ni safi.
\s5
\v 18 Nchi, haifuniki juu damu yangu mimi; acha kulia kwangu kuwe hakuna mahali pa kupumzika.
\v 19 Hata sasa, tazama, ushuhuda wangu uko mbinguni; yeye ambaye ashuhudiaye kwa ajili yangu mimi yuko juu.
\s5
\v 20 Rafiki zangu wananicheka kwa dharau, lakini jicho langu linamwaga machozi kwa Mungu.
\v 21 Mimi ninaomba ule ushuhuda ulioko mbinguni kumtetea mtu huyu na Mungu kama mwanadamu afanyavyo na jirani yake.
\v 22 Kwa maana wakati miaka michache itakapokuwa imepita, Mimi nitakwenda mahali ambapo mimi sitaweza kurudi.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Roho yangu imemezwa, na siku zangu zimekwisha; kaburi lipo tayari kwa ajili yangu mimi.
\v 2 Hakika kuna wenye mzaha pamoja nami; ni lazima daima jicho langu litazame kukasirisha kwao.
\v 3 Nipe sasa ahadi, uwe uthibitisho kwangu mimi pamoja na wewe mwenyewe; nani mwingine yuko pale ambaye atanisaidia mimi?
\s5
\v 4 Kwa kuwa wewe Mungu umemeitunza mioyo yao kutoka katika ufahamu; kwa hiyo, wewe hautawaheshimisha wao juu yangu mimi.
\v 5 Yeye ambaye huwapinga rafiki zake hadharani, kwa ajili ya tuzo, macho ya watoto wake yatashindwa kuona.
\s5
\v 6 Lakini amenifanya mimi kuwa neno la kuzungumziwa na watu; wao wananitemea mate katika uso wangu mimi.
\v 7 Jicho langu pia halioni vizuri kwa sababu ya huzuni; sehemu zangu zote za mwili ni nyembamba kama vivuli.
\v 8 Watu wanyoofu watapendezwa na hiki; mtu asiye na hatia atajitia yeye mwenyewe juu ya kushindana dhidi ya watu wasiomcha Mungu.
\s5
\v 9 Mtu mwenye haki ataendelea katika njia yake; yeye ambaye ana mikono iliyo safi ataendelea kuwa mwenye nguvu zaidi na zaidi.
\v 10 Lakini kama ilivyo kwenu ninyi nyote, njooni sasa; Mimi sitampata mtu mwenye hekima miongoni mwenu ninyi.
\s5
\v 11 Siku zangu zimepita; mipango yangu imenyamazishwa na hivyo ni matumaini ya moyo wangu.
\v 12 Watu hawa, wenye kukejeli, badili usiku kuwa mchana; mchana uko karibu kuwa giza.
\s5
\v 13 Tangu mimi nitazame katika Kuzimu kama nyumbani kwangu; tangu Mimi nimetandaza kiti changu katika giza;
\v 14 tangu Mimi nimesema na shimo 'Wewe ni baba yangu,' na kwa funza, 'Wewe ni mama yangu au dada yangu;
\v 15 liko wapi tena tumaini langu? Kama kwa tumaini langu, nani awezaye kuona chochote?
\v 16 Tumaini litakwenda pamoja na mimi katika milango ya Kuzimu wakati sisi tutakapokwenda katika mavumbi?
\s5
\c 18
\p
\v 1 Ndipo Bildadi Mshuhi alijibu na kusema, "
\v 2 Je, lini utaacha kusema kwako? Fikiri, na baadaye tutazungumza.
\s5
\v 3 Kwa nini sisi tumehesabiwa kama wanyama mwitu; kwa nini tumekuwa wapumbavu machoni pako?
\v 4 Wewe ambaye wajirarua mwenyewe katika hasira yako, nchi haipaswi kuachwa kwa ajili yako au miamba inapaswa kuondolewa kutoka mahali pake?
\s5
\v 5 Ni dhahiri, nuru ya watu waovu itawekwa nje; cheche ya moto wake haitanga'ra.
\v 6 Nuru itakuwa giza katika hema yake; taa yake juu yake yeye itawekwa nje.
\s5
\v 7 Hatua za nguvu zake yeye zitafanywa kuwa fupi; mipango yake yeye mwenyewe itamwangusha yeye chini.
\v 8 Kwa maana yeye atatupwa katika mtego kwa miguu yake mwenyewe; yeye atatembea katika mahangaiko.
\s5
\v 9 Tanzi litamchukua yeye kwa kisigino; mtego utabaki kushikilia juu yake.
\v 10 Tanzi limefichwa kwa ajili yake chini ya ardhi; na mtego kwa ajili yake katika njia.
\v 11 Watishao watamfanya yeye aogope juu ya sehemu zote; wao watamkimbiza yeye kwenye visigino vyake.
\s5
\v 12 Utajiri wake utageuka kuwa njaa, na majanga yatakuwa tayari upande wake.
\v 13 Sehemu za mwili wake zitakuwa zimemezwa; Hakika, mzaliwa wa kwanza wa kifo atazila sehemu zake yeye.
\s5
\v 14 Yeye ameraruliwa kutoka kwenye usalama wa hema yake na hakuweza kutembea kwenda kwa mfalme mwenye utisho.
\v 15 Watu ambao siyo wa kwake wataishi kwenye hema yake baada ya kuona ule moto mesambaa ndani ya nyumba yake yeye.
\s5
\v 16 Mizizi yake itanyauka chini yake; juu tawi lake yeye litakatwa.
\v 17 Kumbukumbu lake yeye litapotea kutoka katika nchi; yeye hatakuwa na jina katika mtaa.
\s5
\v 18 Yeye atafukuzwa kutoka katika nuru mpaka kwenye giza na kuwa amefukuzwa nje na ulimwengu huu.
\v 19 Hatakuwa na mtoto wa kiume wala mjukuu miongonni mwa watu wake, wala kizazi chochote kitakachobakia mahali alipokuwa amekaa.
\v 20 Wale wanaoishi upande wa magharibi watakuwa wametiwa hofu kwa kile kitakachotokea kwake siku moja; wale wanaoishi upande wa mashariki watakuwa wameogopeshwa kwa hicho.
\s5
\v 21 Hakika hizo ni nyumba za watu wasio haki, ni sehemu ya wale wasiomjua Mungu."
\s5
\c 19
\p
\v 1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 lini mtanifanya mimi kuteseka na kunivunja vunja mimi vipande vipnde kwa maneno?
\s5
\v 3 Mara kumi hivi mmenishutumu mimi; ninyi hamuoni aibu kwamba mmenitendea mimi kwa ukatili.
\v 4 Kama ni dhahiri kweli mimi nimekosa, makosa yangu hubaki kuwa wajibu wangu.
\s5
\v 5 Kama ni dhahiri ninyi mtajiinua juu yangu mimi na kuutumia uvumilivu wangu kunipinga mimi,
\v 6 kisha ninyi mnapaswa kutambua kwamba Mungu amefanya mabaya kwangu mimi na amenikamata mimi katika mtego wake yeye.
\s5
\v 7 Tazama, Mimi ninalia kwa sauti, "dhuluma!" lakini sipati jibu. Mimi ninaita kwa ajili ya msaada, lakini hakuna haki.
\v 8 Yeye ameiwekea ukuta njia yangu, ili kwamba mimi nisiweze kupita, na yeye ameweka giza katika njia yangu.
\v 9 Yeye ameniondoa Mimi kutoka katika utukufu wangu, na ameichukua taji kutoka kwenye kichwa changu mimi.
\s5
\v 10 Yeye amenivunjavunja mimi chini kwa kila upande, na Mimi nimetoweka; yeye amelikokota juu tumaini langu kama mti.
\v 11 Yeye pia ameiongeza ghadhabu yake dhidi yangu mimi; yeye ananihesabu mimi kama mmoja wa adui zake.
\v 12 Majeshi yake huja juu pamoja; wao wananikosesha tumaini kwa kuniteka nyara kwa kundi kubwa kupigana na mimi wakizunguka hema yangu.
\s5
\v 13 Yeye amewaweka ndugu zangu mbali kutoka kwangu mimi; watu wangu wa karibu wote wamejitenga kutoka kwangu mimi.
\v 14 Vizazi vyangu vimeniangusha mimi; rafiki zangu wa karibu wamenisahamu mimi.
\s5
\v 15 Wale ambao mwanzoni walikaa kama wageni ndani ya nyumba yangu na watumishi wangu wa kike, hunihesabu mimi kama mgeni. Mimi nimekuwa mgeni katika macho yao.
\v 16 Mimi ninamwita mtumishi wangu, lakini yeye hanipi jibu japokuwa Mimi nimemsihi yeye kwa midomo yangu.
\s5
\v 17 Pumzi yangu mimi ni chukizo kwa mke wangu; Hata mimi ninachukiwa na wale ambao walizaliwa kutoka katika tumbo la mama yangu mimi.
\v 18 Hata watoto wachanga wananichukia mimi; ikiwa Mimi nitainuka kuzungumza, wao huzungumza dhidi yangu mimi.
\v 19 Rafiki zangu wote ninaowazoea wananichukia sana mimi; wale ambao Mimi ninawapenda wamegeuka kinyume na mimi.
\s5
\v 20 Mifupa yangu inashikamana kwenye ngozi yangu na kwenye mwili wangu; Mimi ninaishi tu kwa ngozi ya meno yangu.
\v 21 Iweni na huruma juu yangu mimi, muwe na huruma juu yangu mimi, rafiki zangu, kwa maana mkono wa Mungu umenigusa mimi.
\v 22 Kwa nini mnanitesa mimi kama ninyi mlikuwa Mungu? kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu?
\s5
\v 23 Laiti, hayo maneno yangu yangekuwa yameandikwa chini! Laiti, hayo yangekuwa yameandikwa katika kitabu!
\v 24 Laiti, kwa kalamu ya chuma na risasi hayo yangekuwa yamechorwa katika mwamba siku zote!
\s5
\v 25 Lakini kama ilivyo kwangu mimi, Mimi ninafahamu kwamba mkombozi wangu anaishi, na kwamba hata mwisho atasimama katika nchi;
\v 26 baada ya ngozi yangu, hivyo ndivyo, mwili huu, unaharibiwa, ndipo katika mwili wangu mimi Nitamwona Mungu.
\v 27 Mimi nitamwona yeye kwa macho yangu mwenyewe-Mimi, na siyo mtu mwingine. Moyo wangu hushindwa ndani yangu mimi.
\s5
\v 28 Kama mnatasema, 'Kwa jinsi gani tutamtesa yeye? Mzizi wa mahangaiko yake unakaa katika yeye;
\v 29 ndipo uwe umeogopeshwa kwa ule upanga, kwa sababu ghadhabu huleta hukumu ya upanga, hivyo kwamba wewe uweze kutambua kuna hukumu."
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ndipo Sofari, Mnaamathi alijibu na kusema,
\v 2 "Mawazo yangu yananifanya mimi nijibu kwa haraka kwa sababu ya mashaka yaliyomo ndani yangu mimi.
\v 3 Mimi ninasikia kukemewa ambako kunaniondolea heshima mimi, lakini roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.
\s5
\v 4 Je, unafahamu kwamba ukweli huu kutoka enzi za kale, wakati Mungu alipomweka mwanadamu juu ya nchi:
\v 5 ushindi wa mtu mwovu ni mfupi, na furaha ya mtu asiyemcha Mungu hudumu kwa kitambo tu?
\s5
\v 6 Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu, na kichwa chake yeye kufikia kwenye mawingu,
\v 7 bado mtu huyo atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe; wale waliokuwa wamemuona yeye watasema, 'Yuko wapi yeye'?
\s5
\v 8 Yeye atapaa mbali kama ndoto na hataonekana; ndivyo ilivyo, yeye atakuwa amefukuzwa mbali kama ono la
\v 9 usiku. Jicho ambalo lilimuona yeye halitamuona yeye tena; mahali pake hapatamuona yeye tena.
\s5
\v 10 Watoto wake wataomba msamaha kwa watu maskini, mikono yake itaweza kurudisha utajiri wake.
\v 11 Mifupa yake imejaa nguvu za ujanani, lakini zitalala naye chini katika mavumbi.
\s5
\v 12 Japokuwa uovu ni mtamu katika mdomo wake yeye, japokuwa yeye anauficha chini ya ulimi wake yeye,
\v 13 japokuwa anaushikilia pale na hauruhusu kwenda lakini bado huushikilia katika mdomo wake yeye -
\v 14 chakula katika koromeo lake yeye hugeuka kuwa uchungu; hugeuka kuwa sumu ya majoka ndani yake yeye.
\s5
\v 15 Yeye humeza chini utajiri, lakini yeye atautapika tena; Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake yeye.
\v 16 Yeye atamumunya sumu ya majoka; ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.
\s5
\v 17 Yeye hatafurahia vijito vya maji, wingi wa asali na siagi.
\v 18 Yeye atayarudisha matunda ya kazi yake na hataweza kuyala; yeye hatafurahia utajiri alioupata kwa biashara zake yeye.
\v 19 Kwa kuwa yeye amewakandamiza na kuwasahau watu maskini; yeye kwa uonevu, amezichukua mbali nyumba ambazo hakuzijenga yeye.
\s5
\v 20 Kwa sababu yeye mwenyewe hakujua utoshelevu wowote, yeye hataweza kuokoa kitu chochote katika kile ambacho alijifurahisha.
\v 21 Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza; kwa hiyo mafanikio yake yeye hayatakuwa ya kudumu.
\v 22 katika wingi wa utajiri wake yeye ataanguka katika mahangaiko; mkono wa kila mmoja ambaye yuko katika umaskini utakuja kinyume chake yeye.
\s5
\v 23 Wakati akiwa katika kulijaza tumbo lake, Mungu atatupa hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye; Mungu ataunyeshea chini juu yake yeye wakati yeye anakula.
\v 24 Ingawa mtu huyo atakimbia kutoka katika silaha ya chuma, upinde wa shaba utampiga yeye.
\v 25 Mshale utatoboa kupitia mgongoni mwake na utatokezea; ni dhahiri, ncha inayong'ra itatokezea nje kupitia ini lake yeye; watesi huja tena juu yake.
\s5
\v 26 Giza lliilo kamilika limetunzwa kwa akiba zake; moto usiopulizwa utamla yeye kwa haraka; utameza kile kilichoachwa katika hema yake.
\v 27 Mbingu zitauweka wazi uovu wake, na nchi itainuka juu dhidi yake yeye kama shahidi.
\s5
\v 28 Utajiri wa nyumba yake utatoweka; bidhaa zake zitamwagika mbali siku ya ghadhabu ya Mungu.
\v 29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kutoka kwa Mungu, urithi uliotunzwa akiba na Mungu kwa ajili yake yeye."
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Sikilizeni hotuba yangu kwa makini, hii na iwe faraja yenu.
\v 3 Nimeteswa, lakini pia nitasema; nikisha kusema, endeleeni kudhihaki.
\s5
\v 4 Lakini kwangu mimi, malalamikio yangu ni kwa mtu? Kwa nini nisiwe mwenye subira?
\v 5 Nitazameni na mshangae, nanyi wekeni mkono wenu midomoni mwenu.
\v 6 Ninapoyafikiria mateso yangu, ninaumizwa, mwili wangu unaogopa.
\s5
\v 7 Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wanazeeka, na kuwa na uwezo katika madaraka?
\v 8 Wazao wao wanathibitishwa mbele zao, na uzao wao unaimarika machoni pao.
\v 9 Nyumba zao ziko salama mbali na hofu; wala fimbo ya Mungu haiko juu yao.
\s5
\v 10 Dume lao la ng'ombe linazalisha; halishindwi kufanya hivyo; ng'ombe wao anazaa na hafishi ndama wake akiwa mchanga.
\v 11 Wanawapeleka wadogo wao kama kundi la kondoo, na watoto wao hucheza.
\v 12 Wanaimba kwa tari na vinubi na hufurahi kwa muziki na zomari.
\s5
\v 13 Wanatumia siku zao katika mafanikio, na wanashuka kuzimu kwa utulivu.
\v 14 Wanamwambia Mungu, 'Ondoka kwetu kwani hatutaki ufahamu wowote juu ya njia zako.
\v 15 Mwenye enzi ni nani, hata tumwabudu? Tutafaidika na nini tukimwabudu? Tutapata faida gani ikiwa tutamwomba?
\s5
\v 16 Tazama, je mafanikio yao hayamo katika mikono yao wenyewe? Sina cha kufanya na ushauri wa waovu.
\v 17 Mara ngapi taa za waovu huzimwa, au kwamba majanga huja juu yao? Mara ngapi inatokea kwamba Mungu husambaza huzuni kwao kwa hasira?
\v 18 Ni mara ngapi inatokea kwamba wanakuwa kama mabua mbele ya upepo au kama makapi yanayopeperushwa na dhoruba?
\s5
\v 19 Mnasema, 'Mungu huweka hatia ya mtu kwa watoto wake kuilipa.' Na alipe yeye mwenyewe, ili kwamba aweze kujua hatia yake mwenyewe.
\v 20 Acha macho yake yaone uangamivu wake mwenyewe, na acha anywe gadhabu ya Mwenyezi.
\v 21 Kwani anaangaliaje familia yake mbele yake idadi ya miezi yake inapokwisha.
\s5
\v 22 Je kuna mtu anaweza kumfundisha Mungu maarifa kwa kuwa yeye huwaukumu hata walio juu?
\v 23 Mtu mmoja ufa katika nguvu zake kamili, akiwa na utulivu kabisa na kwa amani.
\v 24 Mwili wake hauna uhitaji, na kiini cha mifupa yake ina unyevu na afya njema.
\s5
\v 25 Mtu mwingine ufa kwa uchungu wa nafsi, bila kujifurahisha kwa jambo lolote jema.
\v 26 Wanazikwa kaburini wote kwa pamoja, funza wanawafunika wote.
\s5
\v 27 Tazama, nayajua mawazo yenu, na jinsi mnavyotaka kunikosesha.
\v 28 Kwa kuwa mwasema, 'Iko wapi sasa nyumba ya mwana wa mfalme? Liko wapi kao alipokaa mwovu?'
\s5
\v 29 Je hamjawauliza wasafiri? Hamfahamu wanavyoweza kusema,
\v 30 kwamba mwovu anaepushwa na siku ya shida, na kwamba anawekwa mbali na siku ya gadhabu?
\s5
\v 31 Ni nani atakaye ituhumu siku ya mwovu mbele yake? Ni nani atakayemwadhibu kwa alichokifanya?
\v 32 Hata hivyo atapelekwa kaburini; watu wataliona kaburi lake.
\v 33 Udongo wa bondeni utakuwa mtamu kwake; watu wote watamfuata, hata kuwe na watu wengi mbele yake.
\s5
\v 34 Ni jinsi gani basi mtanifariji bila kufikiri, kwa kuwa majibu yenu hayana lolote ila uongo?"
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kisha Elifazi Mtemani akajibu na kusema,
\v 2 Je mtu anaweza kumfaa Mungu "Je mwenye hekima anaweza kufaa kwake.
\v 3 Je inafurahisha kwa Mwenyezi ikiwa u mwenye haki? Je ni faida yake ukiyafanya safi maisha yako?
\s5
\v 4 Je ni kwa sababu ya uchaji wako kwake hata akukemee na kukuadhibu?
\v 5 Je si kwa sababu ya wingi wa uovu wako? Je hakuna mwisho wa makosa yako?
\s5
\v 6 Kwa maana umechukua dhamana kutoka kwa ndugu yako bila sababu; umechukua mavazi ya mtu na kumwacha uchi.
\v 7 Haukuwapa wenye kiu maji ya kunywea; umewanyima chakula wenye njaa
\v 8 japokuwa wewe, mwenye uwezo, uliimiliki nchi, japokuwa wewe, mwenye kuheshimiwa, uliishi ndani yake.
\s5
\v 9 Umewaacha wajane waondoke bila kitu; umewatesa yatima.
\v 10 Kwa hiyo, mabaya yanakuzunguka, na hofu za ghafla zinakusumbua.
\v 11 Kuna giza, hata usione; gharika inakufunika.
\s5
\v 12 Je Mungu hayupo juu mbinguni? Anaangalia juu ya nyota, jinsi zilivyo juu!
\v 13 Unasema, 'Mungu anajua nini? Je anaweza kuamua kupitia giza totoro?
\v 14 Mawingu ni kifuniko chake, hata asituone; anatembea anga la mbinguni.'
\s5
\v 15 Je utayaishi maisha ya zamani walioishi waovu -
\v 16 walioondolewa kabla ya siku zao, ambao misingi yao imeondolewa kama mto,
\v 17 waliomwambia Mungu, 'Ondoka kwetu'; waliosema, 'Mwenyezi anaweza kututenda nini?
\s5
\v 18 Hata hivyo bado alizijaza nyumba zao kwa mema; mipango ya waovu iko mbali nami.
\v 19 Wenye haki wanayaona yawapatayo waovu na kufurahi; wasio na hatia wanawacheka kwa dhihaka.
\v 20 Wanasema, 'Bila shaka walioinuka kinyume chetu wameondolewa; moto umeteketeza mali zao.'
\s5
\v 21 Basi patana na Mungu na uwe na amani naye; kwa njia hiyo, mema yatakujia.
\v 22 Nakusihi, pokea, maelekezo yake; uyatii maneno yake.
\s5
\v 23 Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa, ukiacha kutenda uovu makaoni mwako.
\v 24 Weka hazina zako mavumbini, dhahabu ya Ofiri kati ya mawe ya vijito,
\v 25 na Mwenyezi atakuwa hazina zako, fedha ya thamani kwako.
\s5
\v 26 Nawe utajifurahisha katika Mwenyezi; utamwangalia Mungu.
\v 27 Utamwomba, naye atakusikiliza; utamtolea nadhiri.
\v 28 Lakini pia utatamka lolote, nawe utapewa; nuru itaangaza maishani mwako.
\s5
\v 29 Mungu humshusha mwenye kiburi, naye humwinua mnyenyekevu.
\v 30 Atamwokoa asiye na hatia; utaokolewa kupitia usafi wa mikono yako."
\s5
\c 23
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Hata leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu.
\s5
\v 3 Ee, ningejua niwezapokumwona! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo!
\v 4 Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja.
\v 5 Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu.
\s5
\v 6 Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza.
\v 7 Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu.
\s5
\v 8 Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona.
\v 9 Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone.
\s5
\v 10 Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu.
\v 11 Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka.
\v 12 Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
\s5
\v 13 Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda.
\v 14 Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo.
\s5
\v 15 Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa.
\v 16 Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha.
\v 17 Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Kwa nini nyakati za kuwahukumu waovu hazikuwekwa na Mwenyezi? Kwa nini siyo wale waliowaaminifu kwa Mungu huziona siku za hukumu zikija?
\s5
\v 2 Kuna waovu waondoao alama za mipaka; kuna waovu walichukua kundi kwa nguvu na kulifanya lao.
\v 3 Wanawadhurumu wanyonge punda wao; wanachukua ng'ombe wa mjane kuwa dhamana.
\v 4 Wanawaondoa wahitaji katika njia zao kwa lazima; masikini wa dunia yote wanajificha kutoka kwao.
\s5
\v 5 Tazama, masikini hawa huenda kufanya kazi kama punda-mwitu mwituni, akitafuta chakula kwa uangalifu; pengine Araba itawapatia chakula kwa ajili ya watoto wao.
\v 6 Masikini huvuna katika mashamba ya wengine usiku; wanakusanya zabibu kidogo kutokana na mapato ya waovu.
\v 7 Wana lala bila kujifunika wakati wa usiku; hawana cha kujifunika wakati wa baridi.
\s5
\v 8 Wanalowanishwa na mvua ya milimani; wanalala pembeni mwa miamba mikubwa kwani hawana makao.
\v 9 Kuna waovu wanaowapokonya yatima katika kifua cha mama zao, na waovu wawachukuao watoto kama dhamana kutoka kwa masikini.
\v 10 Lakini masikini wanatembea uchi; wajapokaa na njaa, wanabebea wengine chakula.
\s5
\v 11 Masikini wanazalisha vinono ndani ya nyumba za waovu; wanakanyaga mashinikizo ya waovu, lakini wanakiu.
\v 12 Watu wananung'unika mjini; waliojeruhiwa wanaomboleza, lakini Mungu hasikilizi maombi yao.
\s5
\v 13 Baadhi ya waovu hawa wanaiasi nuru; hawafahamu njia zake, wala kukaa katika njia zake.
\v 14 Muaji huinuka na nuru; huuwa masikini na waitaji; ni kama mwizi wakati wa usiku.
\s5
\v 15 Pia, mzinifu hungoja wakati wa usiku; husema, 'Hakuna anionaye.' Hujibadilisha.
\v 16 Waovu huingia katika nyumba gizani, lakini hujifungia wakati wa mchana; hawajari nuru.
\v 17 Kwa kuwa asubuhi kwao wote ni kama giza totoro; wanaamani na vitisho vya giza totoro.
\s5
\v 18 Wanapotea polepole, lakini, kama povu juu ya maji; shamba lao limelaaniwa; hakuna anayekwenda kufanya kazi katika mashamba yao ya mizabibu.
\v 19 Kiangazi na joto huondoa barafu; ndivyo kuzimu pia kunavyowaaribu waliotenda dhambi.
\s5
\v 20 Mama yake atamsahau; polepole funza watamuuma; hatakumbukwa tena; kwa hiyo, waovu watavunjika kama mti.
\v 21 Mwovu anamrarua mgumba; hawatendi jema lolote kwa mjane.
\s5
\v 22 Bado Mungu huwaondoa wenye nguvu kwa nguvu zake; huinuka na kuwadhoofisha.
\v 23 Mungu huwaacha wajione wako salama, na wanalifurahia hilo, lakini anayaangalia maisha yao.
\s5
\v 24 Watu hawa wanatukuzwa; bado, kitambo tu, watapotea; hakika, watashushwa; watakusanywa kama wengine wote; wataondolewa kama sehemu ya juu ya masikio ya nafaka.
\v 25 Ikiwa sivyo, nani atanithibitisha kuwa mwongo; atakaye fanya maneno yangu kuwa si kitu?"
\s5
\c 25
\p
\v 1 Kisha Bilidadi Mshuhi akajibu na kusema,
\v 2 "Utawala na hofu vipo naye; anaagiza mahali pa juu pake mbinguni.
\v 3 Je kuna idadi ya majeshi yake? Ni wapi pasipo na nuru yake?
\s5
\v 4 Jinsi gani basi mtu awe mwenye haki kama Mungu? Jinsi gani aliyezaliwa na mwanamke awe safi, amekubaliwa naye?
\v 5 Tazama, hata mwezi kwake haungazii; nyota hazikosafi mbele zake.
\v 6 Ni vipi mtu, aliyemdudu - mwana wa mtu, aliye mdudu!"
\s5
\c 26
\p
\v 1 Kisha Ayubu akajibu na kusema,
\v 2 "Mmemsaidiaje aliyedhaifu!
\v 3 Jinsi gani mmemshauri asiye na hekima na kutamka maneno yenye maarifa kwake!
\v 4 Kwa msaada wa nani mmesema maneno haya? Ni roho ya nani iliyotoka ndani yenu?
\s5
\v 5 Maiti inatetemeka chini ya maji, na vyote wilivyomo ndani yake.
\v 6 Kuzimu kuko wazi mbele ya Mungu; uharibifu hauna kizuizi dhidi yake.
\s5
\v 7 Huitandaza kaskazi juu ya nafasi wazi na kuining'iniza dunia hewani.
\v 8 Huyafunga maji katika mawingu yake mazito, lakini hayagawanyiki chini yake.
\s5
\v 9 Huufunika uso wa mwezi na kueneza mawingu yake juu yake.
\v 10 Amechora ukingo wa duara juu ya maji kama mpaka kati ya nuru na giza.
\s5
\v 11 Nguzo za mbinguni zinatikisika na zimestushwa na kukemea kwake.
\v 12 Aliituliza bahari kwa uwezo wake; kwa ufahamu wake alimwaribu Rahab
\s5
\v 13 Kwa pumzi yake, aliziondoa mbingu kwa dhorubu; mbingu ziliondolewa kwa dhorubu; mkono wake ulimchoma nyoka anayekimbia.
\v 14 Tazama, hizi si zaidi ya madogo ya njia zake; Jinsi gani tunasikia akitunong'oneza! Ni nani awezaye kufahamu uwezo wake.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Ayubu akaendelea kuoengea na kusema,
\v 2 "Kama aishivyo Mungu, ameniondolea haki yangu, Mwenyezi, aliyeyafanya machungu maisha yangu,
\v 3 kadili uhai ungalimo ndani yangu uzima wa Mungu upo puani mwangu.
\s5
\v 4 Hakika midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu kunena uongo.
\v 5 Sitakiri kwamba mko sahihi; hata nifapo sitakana uadilifu wangu.
\s5
\v 6 Naishikilia haki yangu na sitaiacha; nafsi yangu haitanisuta kadili ninavyoishi.
\v 7 Adui yangu na awe kama mwovu; anayeinuka kunyume changu na awe kama asiye haki.
\s5
\v 8 Kwani tumaini la mwovu ni nini Mungu anapomwondoa, Mungu anapochukua uhai wake?
\v 9 Je Mungu atasikiliza kilio chake tabu zinapompat?
\v 10 Je atajifurahisha katika Mwenyezi na kumwita Mungu nyakati zote
\s5
\v 11 Nitawafundisha kuhusu uwezo wa Mungu; sitabatilisha mawazo ya Mwenyezi.
\v 12 Tazama, ninyi nyote mmeona; kwa nini basi mmeongea yasiyo na maana.
\s5
\v 13 Hii ndiyo hatima ya waovu mbele za Mungu, urithi wa mtesaji aupokeao kutoka kwa Mwenyezi.
\v 14 Ikiwa watoto wake wataongezeka, ni kwa upanga; uzao wake utakuwa na njaa.
\s5
\v 15 Wanaomsalia watauawa kwa tauni, na wajane wao hawatawaombolezea.
\v 16 Japokuwa waovu hurundika mali kama mavumbi,
\v 17 na kukusanya mavazi kama udongo, atakusanya mavazi, lakini mwenye haki atavaa, na wasio na hatia watagawana mali.
\s5
\v 18 Hujenga nyumba yake kama buibui, kama kibanda cha muda afanyacho mlinzi.
\v 19 Hulala kitandani akiwa tajiri, lakini hataendelea hivyo; na afumbuapo macho, hana kitu.
\s5
\v 20 Vitisho humpata kama maji, dhoruba humwondoa usiku.
\v 21 Upepo wa mashariki umwondoa, naye huondoka; humwondoa mahali pake.
\s5
\v 22 Humpiga bila kukoma; hujaribu kumnasua katika uwezo wake.
\v 23 Unampigia makofi kwa kejeli; humwondoa mahali pake.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Hakika kuna machimbo ya fedha, wanaposafisha dhahabu.
\v 2 Chuma uchimbwa; shaba uyeyushwa kutoka katika jiwe.
\s5
\v 3 Mtu anaondoa giza na kutafuta, katika mpaka wa mbali, mawe hayaonekani na giza totoro.
\v 4 Huchimba shimo mbali na makazi ya watu, mahali pasipopitwa na mtu. Huning'inia mbali na watu; uharakisha kwenda na kurudi.
\s5
\v 5 Kwa nchi, kizalishwapo chakula, inapinduliwa kama kwa moto.
\v 6 Mawe yake yana johari, na vumbi lake lina dhahabu.
\s5
\v 7 Hata ndege mwindaji hapajui, wala jicho la kipanga halijapaona.
\v 8 Ndege mwenye majivuna hajawai kuiona njia hiyo, wala simba mkali kupita pale.
\s5
\v 9 Mtu huchimba mwamba mgumu; hupindua milima katika vyanzo vyake.
\v 10 Huweka njia katika miamba; macho yake pale kila kilicho cha thamani.
\v 11 Hufunga vyanzo hata wasiondoke; kilichofichika pale hukifunua.
\s5
\v 12 Hekima itakuwa wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
\v 13 Mtu hafahamu thamani yake; wala haipatikani katika nchi ya walio hai.
\v 14 Vilindi vya maji chini ya nchi husema, 'Haiko kwangu'; bahari husema, 'Haipo pamoja nami.'
\s5
\v 15 Hainunuliwi kwa dhahabu; wala hailinganishwi na fedha.
\v 16 Haiwezi kuthamanishwa na dhahabu ya Ofiri, kwa jiwe jeusi la thamani au johari.
\v 17 Dhahabu na fuwele hailingani nayo kwa thamani; wala haiwezi kubadilishwa kwa vito vya dhahabu safi.
\s5
\v 18 Hailinganishwi na marijani wala yaspi; hakika, thamani ya hekima inapita madini ya rubi.
\v 19 Topazi ya Ethiopia hailinganishwi nayo; wala kuthamanishwa kwa dhahabu safi.
\s5
\v 20 Je hekima inatoka wapi? Mahali pa ufahamu ni wapi?
\v 21 Hekima imejificha mbali na macho ya viumbe wote na ndege wa angani.
\v 22 Mauti na uharibifu husema, 'Tumesikia tu tetesi kwa masikio yetu.'
\s5
\v 23 Mungu hufahamu njia ya kuipata; anapafahamu ilipo.
\v 24 Kwani uona miisho yote ya dunia na huona chini ya mbingu zote.
\v 25 Hapo kale, alifanya nguvu za upepo na kuyagawanya maji kwa kipimo.
\s5
\v 26 Aliiwekea mvua tamko na njia ya radi na munguromo.
\v 27 Kisha akaiona hekima na kuitangaza; aliianzisha, bila shaka, na kuipima.
\v 28 Aliwambia watu, 'Tazameni, kumcha Bwana - ni hekima; kuacha uovu ni ufahamu."
\s5
\c 29
\p
\v 1 Ayubu akaendelea na kusema,
\v 2 Ee, ningekuwa kama nilivyokuwa miezi iliyopita wakati Mungu aliponiagalia,
\v 3 taa yake ilipowaka kichwani pangu, na pale nilipotembea gizani kwa nuru yake.
\s5
\v 4 Ee, kwamba ningekuwa kama nilivyokuwa katika siku za ujana wangu uhusiano wangu na Mungu ulivyokuwa mzuri,
\v 5 wakati Mwenyezi alipokuwa pamoja nami, na wanangu walipokuwa karibu nami,
\v 6 wakati maisha yangu yalipokuwa yamejawa na utele, na mwamba uliponichuruzishia chemichemi za mafuta.
\s5
\v 7 Nilipokwenda langoni mwa mji, nilipokaa katika eneo la mji,
\v 8 vijana waliniona na walikaa mbali kwa kuniheshimu, na wazee waliinuka na kusimama kwa ajili yangu.
\s5
\v 9 Wana wa mfalme waliacha kuongea nilipofika; wangeweka mkono wao katika vinywa vyao.
\v 10 Sauti za waheshimiwa zililazimishwa, na ndimi zao hazikuweza kuongea vinywani mwao.
\s5
\v 11 Kwani baada ya kunisikia, wangenibariki; waliponiona, wangeniona na kuniheshimu
\v 12 kwa maana nilikuwa nikiwasaidia masikini waliokuwa wakiteseka, na yatima, asiye na msaada.
\v 13 Baraka zao waliokuwa karibu kuangamia zilinipata; niliufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
\s5
\v 14 Nilijivika utakatifu, nao ulinifunika; haki yangu ilikuwa kama kanzu na kilemba.
\v 15 Niliwasaidia vipofu; niliwasaidia walemavu.
\v 16 Niliwasaidia wahitaji; niliwasaidia hata wasionijua.
\s5
\v 17 Nilimnyamazisha mwovu; nilimpokonya manusura kutoka katika meno yake.
\v 18 Kisha nilisema nitakufa mahali salama; nitazizidisha siku zangu kama mchanga.
\v 19 Mizizi yangu imeenea majini, na umande kukaa usiku wote katika matawi yangu.
\s5
\v 20 Heshima yangu ni mpya daima, na nguvu za upinde wangu zipo katika mkono wangu kila wakati.
\v 21 Watu walinisikiliza; walinisubiri; walisikiliza ushauri wangu.
\v 22 Nilipo maliza kuongea hawakunena tena, maneno yangu yaliwatia nguvu kama mvua.
\s5
\v 23 Waliningoja kama kungoja mvua; waliyathamini maneno yangu, kama walivyotamani mvua iliyokawia.
\v 24 Niliwafurahia bila wao kutarajia; hawakukataa uzuri wa uso wangu.
\s5
\v 25 Nilikuwa kama mfalme wao na kuwachagulia cha kufanya; nilikuwa kama mfalme katika jeshi lake, kama awafarijiye waombolezaji mazishini.
\s5
\c 30
\p
\v 1 Sasa vijana wananidhihaki - vijana ambao baba zao wasingeweza hata kuwahudumia mbwa wa kundi langu.
\v 2 Kwa kweli, nguvu za mikono ya baba zao, zingenisaidia nini - watu ambao hawakuwa na nguvu wakati wa kukua kwao?
\v 3 Walidhoofishwa na umasikini na njaa; walisaga nchi kavu mafichoni.
\s5
\v 4 Walichuma mche chumvi na majani ya vichaka; mizizi ya mti wa ufagio ilikuwa ndiyo chakula chao.
\v 5 Waliondolewa miongoni mwa watu waliopiga kelele nyuma yao kama ambavyo mtu angempigia kelele mwizi.
\v 6 Hivyo walipaswa kuishi katika mabonde ya mto, katika mashimo ya ardhi na miamba.
\s5
\v 7 Walilia kwa uchungu porini kama punda; chini ya vichaka walikutana.
\v 8 Walikuwa uzao wa wapumbavu, hakika, wa watu wasiofaa; waliondolewa duniani kama waarifu.
\s5
\v 9 Lakini sasa, nimekua sababu ya wimbo wa dhihaka kwa wana wao; hakika, nimekuwa mzaa kwao.
\v 10 Wananichukia na kusimama mbali nami; hawaachi kunitemea usoni.
\v 11 Kwa maana Mungu ameondoa kamba katika upinde wangu na amenipiga, na hivyo watu hawa wanashindwa kujizuia mbele yangu.
\s5
\v 12 Kundi la vijana wabaya wanashambulia nguvu zangu; wananiondolea mbali na kukusanya kinyume changu rundo la kuhusuru.
\v 13 Wanaharibu maisha yangu; wanapeleka mbele maangamizi yangu, watu wasio na wakuwazuia.
\s5
\v 14 Wanakuja kinyume changu kama jeshi katika tundu pana katika ukuta wa mji; katikati ya maangamizi wanajizungusha juu yangu.
\v 15 Hofu zimeniandama; heshima yangu imeondolewa mbali nami kama kwa upepo; mafanikio yangu yameondolewa kama wingu.
\s5
\v 16 Sasa uhai wangu umeondolewa ndani yangu; siku nyingi za maumivu zimenipita.
\v 17 Mifupa inauma ndani yangu wakati wa usiku; maumivu yanayonisaga hayaishi.
\s5
\v 18 Nguvu kuu ya Mungu imeshika mavazi yangu; yananizunguka kama kala ya vazi langu.
\v 19 Amenitupa matopeni; nimekuwa kama vumbi na majivu.
\s5
\v 20 Nakulilia wewe, Mungu, lakini haunijibu; ninasimama, nawe unaniangalia tu.
\v 21 Umegeuka na kuwa mkali kwangu; kwa nguvu za mkono wako umenitesa.
\s5
\v 22 Unaniinua katika upepo na kuufanya unikokote; unanirusha huku na kule katika dhoruba.
\v 23 Kwa maana najua ya kwamba utanipeleka mautini, nyumba ya hatima kwa viumbe vyote.
\s5
\v 24 Lakini, je hakuna ainuaye mkono wake kuomba msaada aangukapo? Je hakuna aombaye msaada akiwa tabuni?
\v 25 Je sikulia kwa ajili yake aliyekuwa tabuni? Je sijahuzunika kwa ajili ya mwitaji?
\v 26 Nilipotazamia mema, ndipo yalipokuja mabaya; niliposubiri nuru, giza lilikuja badala yake.
\s5
\v 27 Moyo wangu umetaabika na hautulii; siku za mateso zimenipata.
\v 28 Nimekuwa na ngozi nyeusi lakini si kwa sababu ya jua; nasimama katika kusanyiko na kulilia msaada.
\v 29 Nimekuwa ndugu kwa mbwea, mshirika wa mbuni.
\s5
\v 30 Ngozi yangu imekuwa nyeusi na inapukutika; mifupa yangu imeunguzwa na joto.
\v 31 Kwa hiyo kinubi changu kimefunguliwa kwa nyimbo za maombolezo, zomari yangu kwa kuimba kwao waombolezao.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Nimefanya patano na macho yangu; ni kwa namna gani tena napaswa kumtazama mwanamwali kwa tamaa?
\v 2 Ni sehemu gani kutoka kwa Mungu juu, na urithi gani kutoka kwake mwenye nguvu aliye juu?
\s5
\v 3 Nilikuwa nafikiri kwamba majanga ni kwa watu wasio na haki, na misiba ni kwa ajili ya watu watendao mabaya.
\v 4 Je Mungu hazioni njia zangu na kuzihesabu hatua zangu zote?
\s5
\v 5 Kama nimetembea katika udanganyifu, kama mguu wangu umeharakisha katika uongo,
\v 6 na nipimwe katika vipimo vilivyo sawa ili kwamba Mungu aujue uadilifu wangu.
\s5
\v 7 Kama hatua zangu zimegeuka kutoka katika njia sahihi, kama moyo wangu umetembea kwa kufuata macho yangu, na kama doa lolote la uchafu limeng'ang'ania katika mikono yangu,
\v 8 na kisha mimi nipande na mtu mwingine na ale; mavuno na yang'olewe katika shamba langu.
\s5
\v 9 Na kama moyo wangu umevutiwa na mwanamke mwingine, ikiwa nimelala na mke wa jirani yangu katika hali ya kusubiria katika mlango wake,
\v 10 na ndipo mke wangu na asage nafaka kwa mwanaume mwingine, na wanaume wengine na walale naye.
\s5
\v 11 Na kwa hilo litakuwa ni kosa kubwa; kwa kweli, utakuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi.
\v 12 Kwa kuwa ni moto ambao unateketeza kila kitu kwa uharibifu, na kwamba utaunguza mavuno yangu yote.
\s5
\v 13 Ikiwa nilikataa ombi la haki kutoka kwa watumishi wangu wa kiume na wa kike wakati walipohojiana nami,
\v 14 kisha nini basi ningefanya wakati Mungu anapoinuka ili kunishitaki mimi? Atakapokuja kunihukumu, nitamjibuje?
\v 15 Je yeye aliyenifanya mimi tumboni hakuwafanya wao pia? Je yeye si yeye yule aliyetuumba sisi wote katika tumbo?
\s5
\v 16 kama nimewanyima watu masikini matakwa yao, au kama nimesababisha macho ya wajane yafifie kwa kulia,
\v 17 au ikiwa kama nimekula kipande changu na sijawaruhusu wale wasio na baba kukila pia -
\v 18 kwasababu tangu ujana wangu yatima walikua pamoja nami kama kuwa na baba, nami nimemwongoza mama yake, mjane, tangu katika tumbo la mama yangu mwenyewe.
\s5
\v 19 ikiwa nimemwona yeyote akiangamia kwa kwa kukosa mavazi, au kama nimemwona mtu mhitaji akiwa hana nguo;
\v 20 ikiwa moyo wake haujanibariki kwasababu amekuwa hajatiwa joto na sufu ya kondoo zangu,
\v 21 ikiwa nimeinua juu mkono wangu kinyume na watu wasio na baba kwa kuwa niliona msaada wangu katika lango la mji, na kisha kuleta mashitaka dhidi yangu.
\s5
\v 22 Ndipo bega langu na lianguake kutoka katika sehemu yake, na mkono wangu uvunjike katika kiungo chake.
\v 23 Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu; kwasababu ya mawazo ya ukuu wake, nisingeweza kufanya mambo hayo.
\s5
\v 24 Kama ningeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, na kama ningesema kwa dhahabu safi, 'wewe unanifanya kuwa na tumaini';
\v 25 na kama nimefurahi kwasababu ya utajiri wangu ulikuwa mkubwa, kwa kuwa mkono wangu umepata mali nyingi, na kisha kuleta mashitaka dhidi yangu!
\s5
\v 26 Ikiwa nimeliona jua lilipowaka, au mwezi ukitembea katika mng'ao wake,
\v 27 na kama moyo wangu umevutwa kwa siri, ili kwamba mdomo wangu umeubusu mkono wangu katika ibada yao -
\v 28 hili nalo pia lingekuwa ni ubaya wa kuadhibiwa na waamuzi, kwa kuwa ningekuwa nimemkana Mungu aliyejuu.
\s5
\v 29 Ikiwa nimefurahia uharibifu wa yeyote ambaye ananichukia mimi, au kuwapa hongera wakati majanga yanapowapata, ndipo ulete mashitaka dhidi yangu!
\v 30 Kwa kweli sijauruhusu hata mdomo wangu kutenda dhambi kwa kuuomba uhai wake kwa laana.
\s5
\v 31 Ikiwa watu wa hema yangu hawajasema,' Nani aweza kumpata mtu ambaye hayashibishwa na chakula cha Ayubu?
\v 32 (hata mgeni hajawahi kukaa katika pembe ya mji, kwa kuwa siku zote nimefungua milango yangu kwa ajili ya wasafiri), na kama haiko hivyo, ndipo mlete mashitaka kinyume nami!
\s5
\v 33 Ikiwa, kama binadamu nimezificha dhambi zangu kwa kuficha hatia ndani ya kanzu yangu -
\v 34 kwa kuwa niliogopa kusanyiko kubwa, kwasababu ya matwezo ya familia yaliniogopesha, hivyo basi nilinyamaza kimya na sikuweza kwenda nje, basi nileteni mashitaka dhidi yangu!
\s5
\v 35 Ee, kama nilikuwa na mtu wa kunisikiliza! Ona, hii ni saini yangu; na Mwenye nguvu na anijibu! Ikiwa nilikuwa na shitaka rasmi ambalo adui yangu ameliandika!
\v 36 Hakika ningelibeba hadharani juu ya bega langu; ningeliweka juu kama taji.
\v 37 Ningemweleza hesabu ya hatua zangu; na kama mwana wa mfalme mwenye kujiamini ningepanda kwenda kwake.
\s5
\v 38 Kama nchi yangu ingelia dhidi yangu, na matuta yake yaomboleza pamoja,
\v 39 ikiwa nimekula mavuno yake bila kulipia au kama nimesababisha wamiliki wake kupoteza maisha yao,
\v 40 ndipo miiba na iote badala ya ngano na magugu badala ya shayiri." Maneno ya Ayubu yamemalizika.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Hivyo hawa watu watatu walikoma kumjibu Ayubu kwasababu alikuwa ni mwenye haki katika macho yake mwenyewe.
\v 2 Ndipo iliwaka hasira ya Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi, wa familia ya Ramu, iliwaka dhidi ya Ayubu kwa kuwa alijihesabia haki mwenyewe kuliko Mungu.
\s5
\v 3 Hasira ya Elihu iliwaka pia kinyume cha marafiki zake watatu kwasababu hawakupata jibu kwa ajili ya Ayubu, na bado walimhukumu Ayubu.
\v 4 Sasa Elihu alikuwa amemsubiri Ayubu ili aweze kuzungumza naye kwa kuwa watu wengine walikuwa wakubwa kuliko yeye.
\v 5 Hata hivyo, wakati Elihu alipoona ya kuwa hapakuwa na jibu katika midomo ya watu hawa watatu, hasira yake iliwaka.
\s5
\v 6 Ndipo Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi alinena na kusema, "Mimi ni mdogo, na ninyi ni wazee. Hii ndio sababu nilijizuia na sikuthubutu kuzungumza mawazo yangu mwenyewe.
\v 7 Nilisema, "Urefu wa siku utazungumza; na wingi wa miaka utatufundisha hekima.
\s5
\v 8 Lakini kuna roho ndani ya mtu; pumzi ya Mwenye nguvu humpa yeye ufahamu.
\v 9 Si tu watu wakubwa ndio wenye hekima, wala watu wazee pekee ambao hufahamu haki.
\v 10 Hivyo basi nakwambia wewe, "Nisikilizeni mimi; Nitakwambia pia uelewa wangu.'
\s5
\v 11 Tazama, niliyasubiria maneno yenu; nilisikiliza hoja zenu wakati mlipokuwa mnafikiri juu ya kile cha kusema.
\v 12 Hakika, niliwajali sana ninyi, lakini, tazama, hakuna hata mmoja wenu aliyeweza kumshawishi Ayubu wala ambaye aliweza kumjibu maneno yake.
\s5
\v 13 Iweni waangalifu msije mkasema, 'Tumepata hekima!' Mungu atakuwa amemshinda Ayubu; mtu wa kawaida hawezi akafanya hivyo.
\v 14 Kwa kuwa Ayubu hajasema mojamoja maneno yake juu yangu, basi sitamjibu kwa maneno yenu.
\s5
\v 15 Hawa watu watatu wamep igwa bumbuwazi; hawawezi kuendelea kumjibu Ayubu; hawana neno zaidi la kusema.
\v 16 Je ninapaswa kusubiria kwasababu hawazungumzi, kwa kuwa wamesimama pale kimya na wala hawajibu zaidi?
\s5
\v 17 La, nitajibu pia upande wangu; Nitawaambia pia ufahamu wangu.
\v 18 Kwa kuwa nimejawa na maneno mengi, roho ndani yangu inanisukuma.
\v 19 Tazama, kifua changu ni kama divai yenye chachu ambayo haina tundu; kama viriba vipya, kiko tayari kupasuka.
\s5
\v 20 Nitazungumza ili kwamba niweze kuburudishwa; nitafungua kimya changu na kusema.
\v 21 Sitaonesha upendeleo; wala sitatoa sifa za majina kwa mtu yeyote.
\v 22 Kwa kuwa sijui namna ya kutoa sifa; kama nitafanya hivyo, Muumba wangu atanikatilia mimi mbali.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Kwahiyo sasa, nakuomba wewe, Ayubu, usikilize hotuba yangu; sikiliza maneno yangu yote.
\v 2 Tazama sasa, nimeufumbua mdomo wangu; ulimi wangu umesema maneno ndani ya mdomo wangu.
\v 3 Maneno yangu yatasema uadilifu wa moyo wangu; yatasema kwa unyofu yale ambayo mdomo wangu unayajua.
\s5
\v 4 Roho ya Mungu imeniumba; pumzi ya Mwenye nguvu imenipatia uhai.
\v 5 Kama unaweza, nijibu; weka maneno yako katika mpangilio mbele yangu na kisha usimame.
\s5
\v 6 Tazama, niko kama wewe ulivyo mbele za Mungu; nimeumbwa pia kutoka katika udongo.
\v 7 Ona, tishio langu halitakufanya wewe uogope; wala mzigo wangu hautakuwa mzito kwako.
\s5
\v 8 Umesema kwa hakika katika masikio yangu; nimeisikia sauti ya maneno yakeo yakisema,
\v 9 'Mimi ni safi na bila hila; sina hatia, na hakuna dhambi ndani yangu.
\s5
\v 10 Tazama, Mungu huona nafasi za kunishambulia mimi; huniangalia mimi kama adui yake.
\v 11 Huweka miguu yangu akiba; naye huangalia njia zangu zote.'
\v 12 Tazama, katika hili hauko sawa, nitakujibu, kwa kuwa Mungu ni mkuu kuliko mtu.
\s5
\v 13 Kwanini unashindana naye? Huwa hahesabu matendo yake yoyote.
\v 14 Kwa kuwa Mungu huzungumza mara moja, naam, mara mbili, ingawa mwanadamu hawezi kutambua.
\v 15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito unapowapata watu, katika usingizi kitandani -
\s5
\v 16 basi Mungu hufungua masikio ya watu, na kuwatisha kwa vitisho,
\v 17 kwa kusudi la kumvuta mtu atoke katika makusudio yake maovu, na kuyaweka majivuno mbali naye.
\v 18 Mungu huyaokoa maisha ya mwanadamu kutoka katika shimo, na uhai wake dhidi ya kifo.
\s5
\v 19 Mtu huadhidibiwa pia na maumivu kitandani mwake, na maumivu makali yanayodumu katika mifupa yake,
\v 20 ili kwamba maisha yake yachukie chakula, na roho yake ichukie vyakula vizuri.
\s5
\v 21 Nyama yake imeharibiwa ili kwamba usionekane; mifupa yake, mara moja isionekane, sasa basi ng'ang'ania.
\v 22 Hakika, roho yake inasogea shimoni, na uhai wake unasogea kwa wale wanaotaka kuuharibu.
\s5
\v 23 Lakini kama kuna malaika anayeweza kuwa mpatanishi kwa ajili yake, mpatanishi mmoja miongoni mwa maelfu ya malaika, kumwonesha kile kilicho cha haki ili atende haki,
\v 24 na kama malaika ni mpole kwake na kumwambia Mungu, 'Mwokoe mtu huyu ili asishuke chini shimoni; nimepata fidia kwa ajili yake,'
\s5
\v 25 kisha mwili wake utakuwa mororo kuliko mwili wa mtoto, atazirudia siku za nguvu za ujana wake.
\v 26 Atamwomba Mungu, na Mungu atakuwa mwema kwake, ili kwamba auone uso wa Mungu akiwa mwenye furaha. Mungu atampa mtu ushindi wake.
\s5
\v 27 Ndipo mtu huyo ataimba mbele ya watu wengine na kusema, 'Nilitenda dhambi na kuasi kile kilichokuwa cha haki, lakini dhambi yangu haikuadhibiwa.
\v 28 Mungu ameiokoa roho yangu isiende chini shimoni; maisha yangu yataendelea kuuona mwanga.'
\s5
\v 29 Tazama, Mungu hufanya mambo haya yote pamoja na mwanadamu, mara mbili, naam, hata mara tatu,
\v 30 kuirudisha roho yake kutoka shimoni, ili kwamba aweze kumlikwa na mwanga wa maisha.
\s5
\v 31 Ayubu, zingatia na unisikilize mimi; nyamaza nami nitasema.
\v 32 Ikiwa una kitu cha kusema, na unijibu; sema, maana nataka kuhakikisha kwamba wewe uko katika haki.
\v 33 Kama sivyo, basi nisikilize, ubaki kimya, nami nitakufundisha wewe hekima."
\s5
\c 34
\p
\v 1 Zaidi ya hayo, Elihu aliendelea kusema:
\v 2 "Sikilizeni maneno yangu, ninyi watu wenye hekima; nisikieni, ninyi mlio na maarifa.
\v 3 Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama ambavyo kaakaa huonja chakula.
\s5
\v 4 Na tujichagulie sisi wenyewe yale yenye adili: na tujigundulie miongoni mwetu yale yaliyo mazuri.
\v 5 Kwa kuwa Ayubu amesema, 'mimi ni mwenye haki, lakini Mungu ameondoa haki zangu.
\v 6 Pamoja na haki zangu, ninaangaliwa kama mwongo. Kidonda changu hakiponyeki, ingawa mimi sina dhambi.'
\s5
\v 7 Ni mtu gani aliye kama Ayubu ambaye hunywa dharau kama maji,
\v 8 ambaye huzunguka katika ushirika wa watu ambao ni waovu, na ambaye hutembea pamoja na watu waovu?
\v 9 Kwa kuwa anasema, ' Hakuna faida kwa mtu kujifurahisha kwa kufanya mambo ambayo Mungu anayataka.'
\s5
\v 10 Basi nisikilizeni mimi, enyi watu wenye ufahamu: na iwe mbali na Mungu kwamba atatenda uovu;
\v 11 na iwe mbali na Mwenye enzi kwamba atatenda dhambi. Kwa kuwa humlipa mtu kutokana na kazi yake; na humfanya mtu apate thawabu za njia zake mwenyewe.
\v 12 Kwa hakika, Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaIpotosha haki.
\s5
\v 13 Ni nani aliyemweka kuwa mtawala wa dunia? Ni nani aliyeiweka dunia yote chini yake?
\v 14 Ikiwa aliweka makusudio yake juu yake mwenyewe, na kama amejikusanyia mwenyewe nafsi yake na pumzi yake,
\v 15 basi miili yote itateketea pamoja; mwanadamu angerudi mavumbini tena.
\s5
\v 16 Kama sasa mna ufahamu, sikilizeni haya; sikilizeni sauti ya maneno yangu.
\v 17 Je yeye anayeichukia haki aweza kutawala? Je mtamhukumu Mungu kuwa ni mwenye makosa, ambaye ni mwenye haki na mwenye nguvu?
\s5
\v 18 Mungu ambaye humwambia mfalme, ' Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?
\v 19 Mungu ambaye haoneshi upendeleo kwa viongozi na ambaye hawakubali zaidi watu matajiri kuliko masikini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake.
\v 20 Watakufa kwa muda mfupi; wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita; watu wenye nguvu watatwaliwa mbali, lakini si kwa mikono ya wanadamu.
\s5
\v 21 Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote.
\v 22 Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe.
\v 23 Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.
\s5
\v 24 Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi; huwaweka watu wengine katika nafasi zao.
\v 25 Kwa namna hii ana maarifa juu ya matendo yao; huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.
\s5
\v 26 Huwaua kwa matendo yao mabaya kama wakosaji dhahiri mbele za watu wengine
\v 27 kwasababu wamegeuka na kuacha kumfuata yeye na wamekataa kuzisadiki njia zake zozote.
\v 28 Na kwa namna hii, wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie; amekisikia kilio cha watu walioteswa.
\s5
\v 29 Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,
\v 30 ili kwamba watu wasiomjua Mungu wasije wakatawala, ili kwamba asiwepo mtu wa kuwanasa watu.
\s5
\v 31 Fikiria mtu akimwambia Mungu, ' Mimi ni mwenye hatia kabisa, lakini sitatenda dhambi tena;
\v 32 nifunze kile ambacho siwezi kukiona; nimetenda dhambi, lakini sitafanya tena.'
\v 33 Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda? Ni lazima uchague, siyo mimi. Basi sema yale ambayo unayajua.
\s5
\v 34 Watu wenye ufahamu wataniambia, kwa kweli, kila mtu mwenye hekima ambaye hunisikia atasema,
\v 35 Ayubu anazungumza bila maarifa; maneno yake hayana hekima.'
\s5
\v 36 Kama Ayubu alijaribiwa kwa kitu kidogo kabisa katika kesi yake kwasababu ya kuongea kwake kama watu waovu.
\v 37 Kwa kuwa anaongeza uasi juu ya dhambi yake; anapiga makofi ya dharau kati yetu; anaweka maneno kinyume na Mungu."
\s5
\c 35
\p
\v 1 Aidha, Elihu aliendelea kusema,
\v 2 "Je unadhani hii ni sawa unaposema, 'Haki yangu mbele ya Mungu?
\v 3 Kwa kuwa unauliza, 'Inafaa nini kwangu' na 'Ingekuwa nzuri kwangu kama ningekuwa nimetenda dhambi?'
\s5
\v 4 Nitakujibu, wewe pamoja na marafiki zako.
\v 5 Tazama juu angani, na ulione; angalia anga, ambalo liko juu sana kuliko wewe.
\s5
\v 6 Kama umetenda dhambi, ni madhara gani huwa unayafanya kwa Mungu? Ikiwa makosa yako yameongezeka zaidi, je huwa unafanya nini kwake?
\v 7 Kama wewe ni mwenye haki, unaweza kumpa nini? Je atapokea nini mkononi mwako?
\v 8 Uovu wako waweza kuwaumiza mtu, kama ulivyo wewe ni mtu, na haki yako yaweza kumnufaisha mwana mwingine wa mtu.
\s5
\v 9 Watu wanalia kwasababu ya matendo mengi ya unyanyasaji; wanaomba msaada katika mikono ya watu wenye nguvu.
\v 10 Lakini hakuna hata mmoja asemaye, ' Mungu Muumba wangu yuko wapi, ambaye hutoa nyimbo wakati wa usiku,
\v 11 ambaye hutufundisha sisi zaidi anavyowafundisha wanyama wa dunia, na ambaye hutufanya sisi kuwa wenye hekima kuliko ndege wa angani?
\s5
\v 12 Huko wanalia, lakini Mungu hawajibu kwasababu ya kibriu ya watu waovu.
\v 13 Kwa hakika Mungu hatasikia kilio cha kipumbavu; Mwenye nguvu wala hatajali.
\v 14 Ni kwa namna gani atakujibu ikiwa unasema haumwoni, na ya kwamba hoja yako iko mbele yake, na ya kuwa unamngojea yeye!
\s5
\v 15 Ni kwa jinsi gani atakujibu kama unasema kwamba hamwadhibu yeyote kwa hasira, na ya kwamba hajishughulishi na kiburi cha watu.
\v 16 Basi Ayubu hufumbua kinywa chake tu ili kusema upumbavu; huongeza maneno bila maarifa."
\s5
\c 36
\p
\v 1 Elihu aliendelea na kusema,
\v 2 "Niruhusu niseme kidogo zaidi, nami nitakuonesha baadhi ya mambo kwasababu nina maneno machache ya kusema kwa ajili ya Mungu.
\v 3 Nitapata maarifa yangu kutoka mbali; nitatambua kwamba haki ni ya Muumba wangu.
\s5
\v 4 Kwa kweli, maneno yangu hayatakuwa ya uongo; mtu fulani aliyekomaa katika maarifa yu pamoja nawe.
\v 5 Angalia, Mungu ni mwenye nguvu, na hamdharau mtu yeyote; yeye ni mwenye nguvu katika uweza wa ufahamu.
\s5
\v 6 Yeye huwa hayahifadhi maisha ya watu waovu bali badala yake hufanya yaliyo ya haki kwa wale wanaoteseka.
\v 7 Haondoi macho yake kwa wenye haki bali badala yake huwaweka juu ya viti vya enzi kama wafalme milele, nao wameinuliwa juu.
\s5
\v 8 Ikiwa wamefungwa minyororo na kunaswa katika kamba za mateso,
\v 9 kisha huwafunulia kile walichokifanya, na maovu yao na kiburi chao.
\s5
\v 10 Hufungua pia masikio yao kwa ajili ya agizo lake, na huwaamuru wageuke kutoka katika uovu.
\v 11 Ikiwa watamsikiliza na kumwabudu yeye, wataishi katika mafanikio katika siku zao, na miaka yao katika hali ya kuridhika.
\v 12 Hata hivyo, kama hawatasikiliza, wataangamia kwa upanga; watakufa kwasababu hawana maarifa.
\s5
\v 13 Na wale wasiomjua Mungu hutunza hasiria zao katika mioyo; hawaombi msaada hata wakati ambapo Mungu huwafunga.
\v 14 Hawa hufa katika ujana wao; na maisha yao hukoma kati ya makahaba.
\s5
\v 15 Mungu huwainua watu walioonewa kwa njia ya mateso yao; hufungua masikio yao kwa njia ya uonevu wao.
\v 16 Kwa hakika, yeye angependa kuwatoa ninyi katika mateso na kuwaweka katika sehemu pana ambapo hakuna masumbufu na mahali ambapo meza yenu ingewekwa ikiwa na chakula kilichojaa mafuta.
\s5
\v 17 Lakini wewe umejaa hukumu juu ya watu waovu; hukumu na haki umeziachilia.
\v 18 Usiuache utajiri ukuvute katika udanganyifu; na sehemu kubwa ya rushwa isikugeuze upande kutoka katika haki.
\s5
\v 19 Je utajiri wako waweza kukunufaisha, ili kwamba usiwe katika taabu, au nguvu zako zote za uwezo zaweza kukusaidia?
\v 20 Usiutamani usiku ili utende dhambi dhidi ya wengine wakati ambapo mataifa hukatiliwa mbali katika nafasi zao.
\v 21 Uwe mwangalifu ili kwamba usigeukie dhambi kwasababu unajaribiwa kwa mateso ili kwamba ukae mbali na dhambi.
\s5
\v 22 Angalia, Mungu ameinuliwa katika nguvu zake; ni nani aliye mwalimu kama yeye?
\v 23 Ni nani alishamwalekeza njia yake? Nani anayeweza kumwambia, 'Wewe umetenda mambo yasiyo ya haki?'
\v 24 Kumbuka kuyasifu matendo yake, ambayo watu wameyaimba.
\s5
\v 25 Watu wote wameshayatazama hayo matendo, lakini wanayaona tu matendo hayo kwa mbali sana.
\v 26 Tazama, Mungu ni mkuu, lakini sisi hatumfahamu yeye vizuri; hesabu ya miaka yake haihesabiki.
\s5
\v 27 Kwa kuwa yeye huvuta matone ya maji ili kuyachuja kama mvua katka mvuke wake,
\v 28 ambayo mawingu yake huyamwaga chini na kuyandondosha kwa wingi kwa mwanadamu.
\v 29 Hakika, kuna hata mmoja awezaye kuelewa kwa undani kusambaa kwa mawingu na radi kutoka katika nyumba yake?
\s5
\v 30 Angalia, hueneza mwanga wake kumzunguka na kufunika mizizi ya bahari.
\v 31 Kwa namna hii huyahukumu mataifa na kuwapa chakula kwa wingi.
\s5
\v 32 Yeye huuijaza mikono yake kwa mwanga mpaka pale anapouamuru kupiga shabaha yake.
\v 33 Na muungurumo wake huonya kwa dhoruba, wanyama wanaweza kusikia kuja kwake.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Hakika, moyo wangu hutetemeka kwa hili; umeondolewa kutoka katika sehemu yake.
\v 2 Sikia, Ee, Sikia kelele za sauti yake, sauti inayotoka katika mdomo wake.
\v 3 Huiagiza sauti chini ya mbingu yote, na huutuma mwanga wake katika mipaka ya dunia.
\s5
\v 4 Sauti huunguruma baada yake; yeye huunguruma kwa sauti ya ukuu wake; hauzuii mshindo wa mwanga wakati sauti yake inaposikika.
\v 5 Mungu huunguruma kwa sauti yake kwa namna ya ajabu; yeye hufanya mambo makubwa ambayo sisi hatuwezi kuyafahamu.
\v 6 Kwa kuwa huiambia theluji, 'Angukeni juu ya dunia'; hali kadhalika kwa manyunyu ya mvua, 'Iweni manyunyu makubwa ya mvua.'
\s5
\v 7 Huuzuia mkono wa kila mtu usifanye kazi, ili kwamba watu wote aliowaumba wataona matendo yake.
\v 8 Kisha hayawani huenda na kujificha na kukaa katika mapango yake.
\v 9 Dhoruba hutoka katika chumba chake upande wa kusini na baridi kutoka katika pepo zilizotawanyika katika upande wa Kaskazini.
\s5
\v 10 Barafu imetolewa kwa pumzi ya Mungu; upana wa maji umeganda kama chuma.
\v 11 Hakika, huyapima mawingu manene yenye unyevu; yeye huusambaza mwanga wake katika mawingu.
\s5
\v 12 Yeye huyazungusha mawingu kwa uongozi wake, ili yafanye chochote anayoyaagiza juu ya uso wote wa ulimwengu.
\v 13 Huyafanya haya yote yatokee; wakati mwingine hutokea kwa ajili ya kusahihisha, wakati mwingine kwa ajili ya nchi yake, na wakati mwingine ni kwa matendo ya agano la uaminifu.
\s5
\v 14 Yasikilize haya, Ayubu; acha na ufikiri juu matendo ya ajabu ya Mungu.
\v 15 Je unajua ni kwa namna gani Mungu hushurutisha mawingu na kuufanya mwanga wa radi ung'ae ndani yake?
\s5
\v 16 Je unafahamu kuelea kwa mawingu, matendo ya ajabu ya Mungu, Je ni nani aliyemkamilifu katika maarifa?
\v 17 Je unafahamu ni kwa jinsi gani mavazi yako huwa ya moto wakati nchi ikiwa imetulia kwasababu ya upepo unaotoka upande wa kusini?
\s5
\v 18 Je unaweza kulitandaza anga kama anavyofanya - anga ambalo lina nguvu kama kioo cha chuma kigumu?
\v 19 Tufundishe sisi kile tunachopaswa kumwambia yeye, kwa kuwa hatuwezi kutoa hoja zetu katika mpangilio kwasababu ya kiza katika akili zetu.
\v 20 Je anapaswa kuambiwa kwamba ninapenda kuongea naye? Je mtu angependa kumezwa?
\s5
\v 21 Sasa, watu hawawezi kulitazama jua wakati linang'aa katika anga baada ya upepo kupita katikati yake na umelisafisha kwa mawingu yake.
\v 22 Kutoka upande wa kaskazini hutokea fahari ya dhahabu - juu ya Mungu kuna ukuu wa kutisha.
\s5
\v 23 Na kuhusu Mwenye nguvu, hatuwezi kumpata; yeye ni mkuu katika nguvu na haki. Yeye hatesi watu.
\v 24 Hivyo basi, watu humwogopa. Yeye huwa hawajali wale ambao ni wenye hekima katika akili zao wenyewe."
\s5
\c 38
\p
\v 1 Ndipo Yahweh alimwita Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kumwambia,
\v 2 "Huyu ni nani aletaye giza katika mipango kwa njia ya maneno bila maarifa?
\v 3 Basi sasa jifunge kiunoni mwako kama mwanaume kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
\s5
\v 4 Wewe ulikuwa wapi wakati nilipoitandaza misingi ya dunia? Niambie, kama unao ufahamu zaidi.
\v 5 Je ni nani aliyeamuru vipimo vyake? Niambie, kama unajua, ni nani alivinyosha vipimo juu yake?
\s5
\v 6 Misingi yake ilitandazwa juu ya nini? Ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni
\v 7 wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
\s5
\v 8 Ni nani huifunga bahari kwa milango wakati inapofurika, kana kwamba inatoka katika tumbo,
\v 9 wakati nilipoyafanya mawingu kuwa ni mavazi yake, na giza nene kuwa mkanda wake wa kujifungia?
\s5
\v 10 Hapo ilikuwa wakati nilipoweka bahari mpaka wangu, na nilipoweka makomeo yake na milango,
\v 11 na wakati nilipoiambia, 'Unaweza kuja hapa kutoka mbali, lakini si zaidi; na hapa ndipo nitauweka mpaka kwa fahari ya mawimbi yako.'
\s5
\v 12 Je tangu mwanzo wa siku zako, ulishawahi kuigiza asubuhi ianze, na kuyafanya mapambazuko yajue sehemu yake katika mpangilio wa vitu,
\v 13 ili kwamba ishikilie sehemu za dunia ili watu waovu watikiswe mbali nayo.
\s5
\v 14 Dunia imebadilishwa katika mwonekano kama udongo unavyobadilika chini ya muhuri; vitu vyote husimama juu yake dhahiri kama cha kibindo cha nguo.
\v 15 'Mwanga' wao umeondolewa kutoka kwa watu waovu; na mkono wao ulioinuliwa umevunjwa.
\s5
\v 16 Je umeshaenda kwenye vyanzo vya maji ya bahari? Je umeshatembea sehemu za chini kabisa za kilindi?
\v 17 Je malango ya mauti yamefunuliwa kwako? Je umeshaona malango ya uvuli wa mauti?
\v 18 Je umeifahamu dunia katika upana wake? Niambie kama unayajua yote hayo.
\s5
\v 19 Je iko wapi njia ya sehemu ya kupumzikia kwa mwanga, na kama ilivyo kwa giza, iko wapi sehemu yake?
\v 20 Je unaweza kuuongoza mwanga na giza katika sehemu zake za kazi? Waweza kuitambua njia ya kurudi katika nyumba zao?
\v 21 Bila shaka unajua, kwa kuwa ulizaliwa wakati huo; hesabu ya siku zako ni kubwa sana!
\s5
\v 22 Je ulishaingia katika ghala ya barafu, au umeshaiona ghala ya mawe ya mvua,
\v 23 vitu hivi nimeviweka kwa ajili ya siku za mateso, kwa siku za mapigano na vita?
\v 24 Je iko wapi njia ya mshindo wa mwanga hutokea au je upepo husambazwa kutoka mashariki juu ya dunia?
\s5
\v 25 Ni nani aliyezitengeneza mifereji ya gharika ya mvua, au ni nani aliyezifanya njia za milipuko ya radi,
\v 26 na kuifanya mvua inyeshe juu ya nchi ambazo hakuna mtu aishiye ndani yake, na juu ya jangwa, ambayo ndani yake hakuna mtu yeyote,
\v 27 kwa kusudi la kutimiza mahitaji ya mikoa iliyo kame na yenye ukiwa, na kuyastawisha majani mororo?
\s5
\v 28 Je kuna baba wa mvua? Ni nani aliyeyafanya matone ya umande?
\v 29 Je barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na ni nani aliyeizaa theluji nyeupe katika anga?
\v 30 Maji hujificha menyewe na kuwa kama jiwe; sehemu za juu za vilindi huwa kama barafu.
\s5
\v 31 Je unaweza kuzifunga minyororo ya Kilimia, au kuvifungua vifundo vya Orioni?
\v 32 Je unaweza kuziongoza nyota kutokea katika nyakati zake? Je waweza kuongoza dubu pamoja na watoto wake?
\v 33 Je unazijua sheria za anga? Wewe uliweza kuanzisha sheria za anga juu ya dunia?
\s5
\v 34 Je waweza kupaza sauti yako hadi mawinguni, ili kwamba maji mengi ya mvua yakufunike?
\v 35 Je waweza kuagiza miali ya mwanga ili itokee, na kukwambia, 'Sisi tupo hapa'?
\s5
\v 36 Ni nani ameweka hekima katika mawingu au ni nani ameweka ufahamu kwa ukungu?
\v 37 Nani anaweza kuyahesabu mawingu kwa maarifa yake? Na ni nani awezaye kuvimwaga viriba vya anga
\v 38 wakati mavumbi yanapoungana kuwa kitu kigumu na mabonge ya dunia yanaposhikama kwa pamoja?
\s5
\v 39 Je waweza kuwinda mawindo kwa ajili ya simba jike au kutosheleza hamu ya watoto wadogo wa simba
\v 40 wakati wanapokwaruza kwaruza katika pango lao na kukaa katika kificho ili kulala katika hali ya kuvizia?
\s5
\v 41 Ni nani aletaye mawindo kwa ajili ya kunguru wakati ambapo watoto wao wanapomlilia Mungu na kutangatanga kwa kukosa chakula?
\s5
\c 39
\p
\v 1 Je unajua ni wakati gani mbuzi mwitu huzaa watoto wao katika miamba? Je waweza kuwangalia paa wakati wanapozaa watoto wao?
\v 2 Waweza kuhesabu miezi ya kuchukua mimba? Je unaujua muda ambao huzaa watoto wao?
\s5
\v 3 Wanainama chini na kuzaa watoto wao, na kisha maumivu yao ya uzazi yanaishi.
\v 4 Watoto wao huwa na nguvu na kukua katika uwanda wa wazi; hutoka nje na hawarudi tena.
\s5
\v 5 Ni nani huwaacha punda mwitu waende huru? Je nani amevilegeza vifungo vya punda wepesi,
\v 6 ni nyumba ya nani nimeifanya katika Araba, au nyumba yake katika nchi ya chumvi?
\s5
\v 7 Hucheka kwa dharau katika kelele katika mji; hasikilizi kelele za mwongozaji.
\v 8 Hutembeatembea juu ya milima kama malisho yake; huko hutafuta kila mmea ulio wa kijani kwa ajili ya kula.
\s5
\v 9 Je nyati atakuwa na furaha kukutumikia? Je atakubali kukaa katika zizi lako?
\v 10 Waweza kumwongoza nyati kulima mtaro kwa kamba? Je atachimba bonde kwa ajili yako?
\s5
\v 11 Je waweza kumtumaini kwasababu ya nguvu zake nyingi? Je waweza kumwachia kazi yako ili aifanye?
\v 12 Je waweza kumtegemea akuletee nyumbani nafaka, au kukusanya nafaka katika uwanda wako wa kupuria?
\s5
\v 13 Mabawa ya mbuni hupunga kwa majivuno, bali je mabawa na manyoya yana upendo?
\v 14 Kwa maana huuacha mayai yake katika nchi, na huyaacha yapate joto katika mavumbi;
\v 15 husahau kuwa mguu waweza kuyaharibu au kwamba mnyama mwitu aweza kuyakanyaga.
\s5
\v 16 Huyatendea vibaya makinda yake kana kwamba si yake; haogopi kwamba kazi yake yaweza kupotea bure,
\v 17 kwasababu Mungu amemnyima hekima na hajampa ufahamu wowote.
\v 18 Na wakati anapokimbia kwa haraka, huwacheka kwa dharau farasi na mpanda farasi wake.
\s5
\v 19 Je umempa farasi nguvu zake? Je umeivika shingo yake kwa manyoya?
\v 20 Je umemfanya aruke kama panzi? Enzi ya mlio wake ni wa kutisha.
\s5
\v 21 Hurarua kwa nguvu na kufurahia katika nguvu zake; hukimbia upesi kukutana na silaha.
\v 22 Huidharau hofu na hashangazwi; huwa harudi nyuma kutoka katika upanga.
\v 23 Podo hugongagonga ubavuni mwake, pamoja na mkuki unaong'aa na fumo.
\s5
\v 24 Huimeza nchi kwa hasira na ghadhabu; katika sauti ya tarumbeta, hawezi kusimama sehemu moja.
\v 25 Wakati wowote tarumbeta inapolia, husema, 'Ooh! Huisikia harufu ya vita kutoka mbali - vishindo vya radi za makamanda na makelele.
\s5
\v 26 Je ni kwa hekima yako kwamba mwewe hupaa juu, na ya kuwa huyanyosha mabawa yake kwa upande wa kusini?
\s5
\v 27 Je ni kwa agizo lako kwamba tai huruka juu na kufanya kiota chake katika sehemu za juu?
\v 28 Huishi katika majabali na hufanya makao yake katika vilele vya majabali, na ngomeni.
\s5
\v 29 Kutoka huko hutafuta mawindo; macho yake huyaona mawindo kutoka mbali.
\v 30 Makinda yake hunywa damu pia; na pale walipo watu wafu, ndipo na yeye alipo.
\s5
\c 40
\p
\v 1 Yahweh aliendelea kuongea na Ayubu na kusema,
\v 2 "Je mtu yeyote anayetaka kukosoa na ajaribu kumsahihisha Mwenye enzi? Na yeye anayehojiana na Mungu, na ajibu yeye."
\s5
\v 3 Ndipo Ayubu akamjibu Yahweh na kusema, "
\v 4 Tazama, mimi si mtu muhimu; je nawezaje kukujibu? Ninauweka mkono wangu juu ya mdomo wangu.
\v 5 Ninazungumza mara moja, na sitakujibu; hakika, mara mbili, lakini sitaendelea zaidi."
\s5
\v 6 Kisha Yahweh akamjibu Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kusema,
\v 7 "Jifunge sasa mkanda kiunoni mwako kama mwanaume, kwa kuwa nitakuuliza maswali, nawe lazima unijibu.
\s5
\v 8 Je waweza kusema kwa hakika kwamba mimi si mwenye haki? Je utanihukumu mimi ili useme wewe ni mwenye haki?
\v 9 Je una mkono kama wa Mungu? Je waweza kutoa kishindo kwa sauti kama yeye?
\s5
\v 10 Jivike sasa katika utukufu na katika utu; jivalie mwenyewe heshima na enzi.
\v 11 Sambaza ziada ya hasira yako; mtazame kila mmoja mwenye kiburi na umshushe chini.
\s5
\v 12 Mwangalie kila mmoja mwenye kiburi na umweke chini; wakanyage chini watu waovu mahali wanaposimama.
\v 13 Wazike ardhini pamoja; zifunge nyuso zao katika sehemu zilizositirika.
\v 14 Ndipo pia nitakapokubali ya kwamba mkono wako wa kulia waweza kukuokoa.
\s5
\v 15 Mwangalie sasa kiboko, ambaye niliwafanya kama nilivyokufanya wewe; anakula nyasi kama ng'ombe.
\v 16 Ona sasa, nguvu zake ziko katika viuno vyake; nguvu zake zi katika mishipa ya tumbo lake.
\s5
\v 17 Yeye huuondoa mkia wake kama mti wa mwerezi; mishipa ya paja lake imeunganishwa pamoja.
\v 18 Mifupa yake ni kama ya mirija ya shaba; na miguu yake ni kama kipande cha chuma.
\s5
\v 19 Yeye ni mkuu wa viumbe vya Mungu. Ni Mungu pekee, ambaye alimwumba, anaweza kumshinda.
\v 20 Kwa kuwa milima humpatia chakula; hayawani wa mashambani hucheza karibu.
\v 21 Hujilaza chini ya mimiea ya kivuli katika makao ya mianzi, na katika bwawa la matope.
\s5
\v 22 Miti yenye vivuli humfunika katika vivuli vyake; mierebi ya kijito inamzunguka pande zote.
\v 23 Tazama, kama mto utazigharikisha kingo zake, hatikisiki; yeye anajiamini, hata kama Mto wa Yordani unajaa hadi katika pua yake.
\v 24 Je mtu yeyote aweza kumnasa kwa ndoano, au kuichoma pua yake kwa mtego?
\s5
\c 41
\p
\v 1 Je waweza kumvua mamba kwa ndoano ya samaki? Au kumfunga taya zake kwa kamba?
\v 2 Je waweza kuweka kamba katika pua zake, au kumtoboa taya yake kwa ndoano?
\v 3 Je atafanya maombi mengi kwako? Je atazungumza na wewe kwa maneno laini?
\s5
\v 4 Je atafanya agano na wewe, ili kwamba umchukue kwa ajili ya mtumishi milele?
\v 5 Je utacheza pamoja naye kama ambavyo ungecheza na ndege? Je utamfunga kwa ajili ya mtumishi wako wa kike?
\v 6 Je makundi ya wavuvi waweza kumfanyia biashara? Je watamgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara?
\s5
\v 7 Je waweza kuijaza ngozi yake kwa vyusa au kichwa chake kwa mikuki ya kuvulia?
\v 8 Weka mkono wako juu yake mara moja, nawe utaikumbuka vita na hautaendelea kufanya hivyo tena.
\v 9 Tazama, matumaini ya kila mtu ambaye hufanya hivyo ni uongo; je si kila mmoja atatupwa chini katika nchi mbele yake?
\s5
\v 10 Hakuna aliye mkali ambaye aweza kuthubutu kumtikisa mamba; Ni nani basi awezaye kusimama mbele yake?
\v 11 Ni nani kwanza aliyenipa kitu chochote ili kwamba niweze kumlipa? Chochote kilicho chini ya anga ni changu.
\v 12 Sitanyamaza kimya kuhusu miguu ya mamba, wala kuhusu jambo linalohusu nguvu zake, wala kuhusu umbo lake zuri.
\s5
\v 13 Nani awezaye kuiondoa ngozi yake? Nani anaweza kumchoma kwa silaha mara mbili?
\v 14 Nani awezaye kuifungua milango ya uso wake, imezungukwa na meno yake ambayo yanaogofya?
\v 15 Mgongo wake umefanywa kwa magamba yenye mistari, yamefungwa kwa pamoja kama chapa.
\s5
\v 16 Moja li karibu na jingine na ya kuwa hakuna hewa inaweza kupita katikati yake.
\v 17 Yameunganishwa moja kwa jingine; yamegandamana kwa pamoja, ili kwamba hayawezi kutenganishwa.
\v 18 Mwanga hung'ara kutoka katika kupumua kwake; macho yake ni kama kope za mapambazuko ya asubuhi.
\s5
\v 19 Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje.
\v 20 Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana.
\v 21 Pumzi yake huwasha mkaa na kuwa mwali; moto hutoka katika mdomo wake.
\s5
\v 22 Katika shingo yake kuna nguvu, na kitisho hucheza mbele yake.
\v 23 Nofu za mwili wake zimeunganishwa pamoja; ziko imara katika yeye; wala haziwezi kuondolewa.
\v 24 Moyo wake ni mgumu kama jiwe - hakika, ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia.
\s5
\v 25 Na anaposimama mwenyewe, hata miungu huogopa; hurudi nyuma kwasababu ya hofu.
\v 26 Na ikiwa atapigwa kwa upanga, hauwezi kumfanya kitu chochote, wala mkuki, wala mshale, wala aina yoyote ya silaha iliyochongoka.
\v 27 Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu na hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza.
\s5
\v 28 Mshale hauwezi akamfanya akimbie; kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.
\v 29 Marungu huyaangalia kama majani makavu; yeye hucheka juu ya mkuki unaovuma.
\v 30 Sehemu zake za chini zi kama vipande vilivyochongoka vya vyungu; huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.
\s5
\v 31 Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto; huifanya bahari kama chungu cha lihamu.
\v 32 Yeye huifanya njia ing'are nyuma yake; mtu mmoja angedhani kilindi kuwa cheupe.
\s5
\v 33 Hakuna cha kumlinganisha juu ya dunia, ambaye yeye alikuwa ameumbwa kuishi pasipo hofu.
\v 34 Hukiona kila kitu chenye kiburi; yeye ni mfalme juu ya wana wote wa kiburi."
\s5
\c 42
\p
\v 1 Kisha Ayubu akamjibu Yahweh na kusema,
\v 2 "Ninajua kwamba unaweza kufanya mambo yote, ya kuwa hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa.
\v 3 Ni nani huyo ambaye pasipo maarifa huificha mipango? Kwa kweli nilisema mambo ambayo sikuyaelewa, mambo magumu kwangu kuyafahamu, ambayo juu yake sikujua chochote.
\s5
\v 4 Uliniambia, 'Sikiliza sasa, nami nitasema; nitakuuliza mambo, nawe utaniambia.'
\v 5 Nimekuwa nikikusikia kwa usikivu wa sikio langu, lakini sasa jicho langu linakuona wewe.
\v 6 Basi ninajidharau mwenyewe; ninatubu kwa mavumbi na majivu."
\s5
\v 7 Ilitokea baada ya kuwa amekwisha kusema maneno hata kwa Ayubu, Yahweh alimwambia Elifazi Mtemani, " Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na dhidi ya marafiki zako wawili kwa kuwa hamkusema maneno ya haki juu yangu kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.
\v 8 Sasa basi, jitwalieni mafahari saba na mabeberu saba, kisha mmwendee mtumishi wangu Ayubu na mtoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Ndipo Mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi, nami nitayapokea maombi yake, ili kwamba nisiwashughulikie sawasawa na upumbavu wenu. Maana hamkusema mambo ya haki juu yangu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu."
\v 9 Basi Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi na Zofari Mnaamathi walienda na kufanya kama vile Yahweh alivyowaamuru, na Mungu alimtakabali Ayubu.
\s5
\v 10 Na wakati Ayubu alimpowaombea rafiki zake, Yahweh alirejeza bahati yake. Yahweh alimjalia mara mbili ya kile alichokimiliki hapo awali.
\v 11 Ndipo ndugu zake na Ayubu, na wale jamaa zake wote walikuwa wanajuana naye hapo mwanzo, walikuja hapo kwake na kula chakula pamoja naye katika nyumba yake. Waliomboleza pamoja naye na walimfariji kwa ajili majanga yote ambayo Yahweh alikuwa ameyaleta juu yake. Kila mtu alimpa Ayubu kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
\s5
\v 12 Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja.
\v 13 Pia alikuwa na wana saba na mabinti watatu.
\v 14 Binti wa kwanza alimwita Yemima, na wa pili Kezia, na wa tatu Kerenihapuki.
\s5
\v 15 Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao.
\v 16 Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne.
\v 17 Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.

5039
19-PSA.usfm Normal file

File diff suppressed because it is too large Load Diff

481
21-ECC.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,481 @@
\id ECC
\ide UTF-8
\h Mhubiri
\toc1 Mhubiri
\toc2 Mhubiri
\toc3 ecc
\mt Mhubiri
\s5
\c 1
\p
\v 1 Haya ni maneno ya Mwalimu, mwana wa Daudi na mfalme katika Yerusalemu.
\v 2 Mwalimu asema hivi, "Kama mvuke wa ukungu, kama upepo mwanana katika upepo, kila kitu hutoweka na kuacha maswali mengi.
\v 3 Ni faida gani wanadamu huipata kutoka katika kazi zote wazifanyazo chini ya jua?
\s5
\v 4 Kizazi kimoja huenda, na kizazi kingine huja, lakini nchi yabaki milele.
\v 5 Jua huchomoza na jua huzama na kwenda kwa kasi, na kurudi mahali linapochomozea tena.
\v 6 Upepo huvuma kusini na huzunguka kasikazi, na mara zote ukizunguka katika njia yake na kurudi tena.
\s5
\v 7 Mito yote hutiririka katika bahari, lakini bahari haijai. Mahali mito inakoenda, ndiko inakoenda tena.
\v 8 Kila kitu huwa uchovu, na hakuna yeyote awezae kukielezea. Jicho halishibina kile linachokiona, wala sikio halishibi na kile linachosikia.
\s5
\v 9 Chochote kilichopo ndicho kitakachokuwepo, kila kilichofanyika ndicho kitakachofanyika. Hakuna jipya chini ya jua.
\v 10 Je kuna jambo lolote ambalo watu wanaweza kusema, 'Tazama, hili ni jipya'? Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo muda mwingi, wakati uliokuwepo kabla yetu.
\v 11 Hakuna anayeonekana kukumbuka kilichotokea nyakati za zamani. Na mambo yaliyo tokea siku zilizo pita na yale yatakayo tokea siku za mbele nayo hayatakumbukwa."
\s5
\v 12 Mimi ni mwalimu, na nimekuwa mfalme juu ya Isareli katika Yerusalemu.
\v 13 Nilitia akili yangu katika kusoma na kutafuta kwa hekima kila kitu kinachofanywa chini ya mbingu. Hili nalo ni jukumu zito ambalo Mungu amewapa wana wa watu kujishughulisha nalo.
\v 14 Nimeona matendo yote ambayo yanafanyika chini ya jua, na tazama yote ni mvuke ni kujaribu kuuchunga upepo.
\v 15 Palipopinda hapawezi kunyoshwa! Kisicho kuwepo hakiwezi kuhesabiwa!
\s5
\v 16 Nimeuambia moyo wangu nikisema, "Tazama, nimepata hekima kubwa kuliko walioishi Yerusalemu kabla yangu. Akili yangu imeona hekima kubwa na ufahamu."
\v 17 nimetia moyo wangu kujua hekima na upumbuvu na ujinga. Nikagundua kuwa hili nalo pia lilikuwa ni kujaribu kuuchunga upepo.
\v 18 Kwa kuwa katika wingi wa hekima kuna masumbufu mengi, naye aongezae ujuzi, aongeza masikitiko.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Nikasema moyoni, "Njoo, na nitakujaribu kwa kwa furaha. Kwa hiyo furahia." Lakini tazama, huu nao ulikuwa ni upepo wa muda.
\v 2 Nikasema juu ya kicheko, "Ni wazimu," na kuhusu furaha, "Yafaa nini?"
\s5
\v 3 Nikajipeleleza moyoni mwangu katika jinsi ya kutimiza hamu yangu kwa mvinyo. Nikaruhusu akili yangu iongozwe na hekima ingawa bado nilikuwa nikishikilia ujinga. Nilitaka kutafuta jambo lililo jema kwa wanadamu kufanya chini ya mbingu wakati wa siku za maisha yao.
\s5
\v 4 Nilitimiza mambo makubwa. Nilijenga nyumba kwa ajili yangu na kupanda miti ya mizabibu.
\v 5 Nilitengeneza bustani na viwanja; nikapanda aina zote za matunda ndani yake.
\v 6 Nikatengeneza mabwawa ya maji ili kumwagilia msitu mahali miti ilikuwa imepandwa.
\s5
\v 7 Nilinunua watumwa wa kiume na wa kiume; nilikuwa na watumwa waliozaliwa katika ikulu yangu. Pia nikawa na makundi makubwa na wanyama wa kufugwa, zaidi ya mfalme yeyote aliyetawala kabla yangu katika Yerusalemu.
\v 8 Pia nilijikusanyia fedha na dhahabu, hazina ya wafalme na majimbo. Nikapata waimbaji wanaume na wanawake kwa ajili yangu, na kufurahia kutoka kwa wana wa wanadamu, masulia na wanawake.
\s5
\v 9 Hivyo nikawa mkuu na tajiri kuliko wote waliokuwa Yerusalemu kabla yangu, na hekima yangu ilikuwa ndani yangu.
\v 10 Lolote ambalo macho yangu yalikitamani sikuyazuia. Sikuuzuia moyo wangu katika furaha yeyote, kwa sababu moyo wangu ulifurahi katika katka kazi yangu zote na furaha ilikuwa ni tunu kwa kazi zangu zote.
\s5
\v 11 Kisha nikatazama matendo yote ambayo mikono yangu iliyokwisha kuyatimiliza na juu ya kazi niliyokuwa nimeifanya, lakini tena, kila kitu kilikuwa ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo. Hakukuwa na faida chini ya jua.
\v 12 Kisha nikageuka kuipambanua hekima, na upumbavu na ujinga. Kwa maana ni kitu gani mfalme anayekuja baada yangu afanye, ambacho hakijafanyika?
\s5
\v 13 Kisha nikaanza kuelewa kwamba hekima ina faida kuliko upumbavu, kama nuru ilivyo bora kuliko giza.
\v 14 Mwenye hekima hutumia macho yake katika kichwa chake kuona mahali anakoenda, lakini mpumbavu hutembea katika giza, ingawa ninafahamu kuwa mwisho wa aina moja umetunzwa kwa kila mmoja.
\s5
\v 15 Kisha nikasema moyoni mwangu, "Kinachotokea kwa mpumbavu, ndicho kitachotokea na kwangu. Hivyo kuna utofauti gani kama mimi ni mwenye hekima sana?" Nikahitimisha moyoni mwangu, "Huu pia ni mvuke tu."
\v 16 Kwa kuwa mwenye hekima, kama mpumbavu, hakumbukwi kwa muda mrefu. Katika siku zijazo, kila kitu kitakuwa kimesahauliwa. Mwenye hekima hufa kama navyokufa mpumbavu.
\s5
\v 17 Hivyo nikauchukia uhai kwa sababu kazi zote zilizofanyika chini ya jua zilikuwa mbaya kwangu. Hii ni kwa sababu kila kitu ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
\v 18 Nikachukia yote niliyoyatimiza, ambayo nilikuwa nimekwisha yafanya chini ya jua kwa sababu ni lazima niyaache kwa mtu anaye kuja baada yangu.
\s5
\v 19 Na ni nani ajuaye kama atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Ila atakuwa msimamizi juu ya kila kitu chini ya jua ambayo kazi yangu na hekima yangu imeyajenga. Huu pia ni mvuke.
\v 20 Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi zote nilizozifanya chini ya jua.
\s5
\v 21 Kwa kuwa kunaweza kuwa na mtu anayefanya kazi kwa hekima, ufahamu, na umahili, lakini ataacha kila kitu alichonacho kwa mtu ambaye hajafanya chochote. Huu nao ni mvuke na hatari kubwa.
\v 22 Kwa maana ni faida gani mtu hupata ambaye hufanya kazi kwa juhudi na kujaribu moyoni mwake kutimiza kazi zake chini ya jua?
\v 23 Kila siku kazi yake ni maumivu na masikitiko, hivyo wakati wa usiku roho yake haipumziki. Huu pia ni mvuke.
\s5
\v 24 Hakuna jambo jema kwa mtu yeyote zaidi ya kula na kunywa na kuridhika na kile kilichochema katika kazi yake. Nikaona kwamba ukweli huu unatoka kutoka mkononi mwa Mungu.
\v 25 Kwa kuwa ni nani anaweza kula au anaweza kupata furaha yoyote tofauti na Mungu?
\s5
\v 26 Kwa kuwa kwa kila anayemfurahisha yeye, Mungu humpa hekimana ufahamu ba furaha. Ingawa, kwa mwenye dhambi humpa kazi ya kukusanya na kutunza ili kwamba ampe mtu anayempendeza Mungu. Huu pia ni sawa na mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kwa kuwa kila kitu na wakati wake, na majira kwa kila kusudi chini ya mbingu.
\v 2 Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa,
\v 3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya, wakati wa kubomo na wakati wa kujenga.
\s5
\v 4 Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati kucheza,
\v 5 wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe, wakati wa kukumbatia watu wengine wakati wa kutokumbatia.
\s5
\v 6 Kuna wakati wa kutafuta vitu na wakati wa kutotafuta, wakati wa kutunza vitu na wakati wa kuvitupa,
\v 7 wakati kuchana mavazi na wakati wa kuyashona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza.
\s5
\v 8 Kuna wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.
\v 9 Ni faida gani mfanyakazi aipatayo katika kazi yake?
\v 10 Nimeona kazi ambayo Mungu amewapa wanadamu kuitimiza.
\s5
\v 11 Mungu amefanya kila kitu kufaa kwa wakati wake. Pia ameweka umilele ndani ya mioyo yao. Lakini mwanadamu hawezi kuelewa matendo ambayo Mungu ameyafanya, tangu mwanzo wao hadi mwisho.
\s5
\v 12 Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi-
\v 13 na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
\s5
\v 14 Ninajua kwamba chochote afanyacho Mungu kinadumu milele. Hakuna kinaweza kuongezwa au kuondolea, kwa sababu Mungu ndiye aliyekifanya, ili kwamba watu wamsogelee kwa heshima.
\v 15 Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo; chochote kitakachokuwepo kimekwisha kuwepo. Mungu huwafanya wanadamu kutafuka vitu vilivyjificha.
\s5
\v 16 Na nimeona kwamba chini ya jua ubaya upo mahali palipopaswa kuwa na haki, na sehemu ya haki mara nyingi ina ubaya.
\v 17 Nikasema moyoni mwangu, "Mungu atahukumu mwenye haki na mbaya kwa wakati muafaka kwa kila jambo na kila tendo.
\s5
\v 18 Nikasema moyoni mwangu, "Mungu huwajaribu wanadamu kuwaonyesha kwamba wao ni kama wanyama."
\s5
\v 19 Kwa kuwa mwisho watoto wa wanadamu na mwisho wa wanyama ni sawa. Kifo cha mmoja ni sawa na kifo cha mwingine. Wote wana pumzi sawa. Hakuna faida kwa mwanadamu zaidi ya wanyama. Kwa kuwa hakuna kila kitu isipokuwa pumzi?
\v 20 Kila kitu kinaenda sehemu moja. Kila kitu kinatoka mavumbini, na kila kitu kinarudi katika mavumbini.
\s5
\v 21 Ni nani ajuaye kama roho ya mwanadamu inaenda juu na roho ya wanyama inaenda chini ya nchi?
\v 22 kwa hiyo tena nikatambua kwamba hakuna lililo jema kwa yeyote zaidi ya kufurahia kazi yake, kwa kuwa hilo ndilo jukumu lake. Ni nani awezaye kumleta tena kuona kinachotokea baada yake?
\s5
\c 4
\p
\v 1 Kisha tena nikafikiri kuhusu mateso yote yaliyo chini ya jua. Tazama machozi ya watu walioteswa. Hakuna anaye mfariji kwa ajili yao. Nguvu iko katika mikononi mwa watesaji, lakini wateswaji hawana mfariji.
\s5
\v 2 Hivyo nikawapongeza watu walio kufa, wale ambao tayari wamekufa, sio wanaoishi, wale ambao wako hai.
\v 3 Ingawa, bahati zaidi kuliko wote wawili ni yule ambaye hajaishi, yeye ambaye hajaona matendo yoyote mabaya ambayo yanafanyika chini ya jua.
\s5
\v 4 Kisha nikaona kwamba kila tendo la kazi na kila kazi ya utashi ikawa wivu wa jirani ya mtu. Huu pia ni mvuke na kujaribu kuchunga upepo.
\s5
\v 5 Mpumbavu hukunja mikono yake na hafanyi kazi, hivyo chakula chake in mwili wake.
\v 6 Lakini afadhari konzi ya faida pamoja na kazi ya haraka kuliko konzi mbili pamoja na kazi ambayo hujaribu kuuchunga upepo.
\s5
\v 7 Kisha nikafikiri tena zaidi kuhusu ubatili, mvuke upoteao zaidi chini ya jua.
\v 8 Kuna aina ya mtu ambaye yuko peke yake. Hana mtu, hana mwana, wala ndugu. Hakuna mwisho wa kazi zake zote, na macho yake hayatosheki kwa kupata utajiri. Anashangaa, "Ninajishumbua na kuharibu furaha yangu kwa ajili ya nani?" Huu pia ni mvuke, hali mbaya.
\s5
\v 9 Watu wawili wanafanya vizuri zaidi ya mmoja; kwa pamoja wanaweza kupata malipo mazuri kwa ajili ya kazi yao.
\v 10 Kwa kuwa kama mmoja akianguka, mwingine anaweza kumwinua rafiki yake. Ingawa, huzuni humfuata yeye aliye peke yake anapoanguka kama hakuna mtu wa kumwinua.
\v 11 Na kama wawili wakilala pamoja, wanaweza kupata joto, lakini mtu mmoja anawezaje kupata joto akiwa mwenyewe?
\s5
\v 12 Mtu akiwa peke yake anaweza kushindwa nguvu, lakini wawili wanaweza kusimama katika shambulio, na kama ya nyuzi tatu haikatika upesi.
\s5
\v 13 Ni bora kuwa kijana masikini kuliko kuwa mfalme mzee na mpumbavu ambaye hajui jinsi ya kusikiliza maonyo.
\v 14 Hii ni kweli hata kama mtu mdogo anapokuwa mfalme kutoka gerezani, au hata kama alizaliwa masikini katika ufalme wake.
\s5
\v 15 Ingawa, niliona kila mmoja aliye kuwa hai na kuzunguka chini ya jua wakijitia chini kwa kijana mdogo aliyeinuka kama mfalme.
\v 16 Hakuna mwisho kwa watu wote wanaotaka kumtii mfalme mpya, lakini wengi wao hawatamsifu yeye. Hakika hali hii ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Linda mwenendo wako unapoenda kwenye nyumba ya Mungu. Nenda kule usikilize. Kusikiliza ni bora kuliko wapumbavu wanapotoa dhabihu wakati hawajuikuwa wanachofanya katika maisha ni kibaya.
\s5
\v 2 Usiwe mwepesi wa kuongea kwa mdomo wako, na usiufanye moyo wako kuleta jambo lolote kwa haraka mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni, lakini uko chini, kwa hiyo maneno yako yawe machache.
\v 3 Kama una mambo mengi ya kufanya na kuhangaika, pengine utapata ndoto mbaya. Na pengine utaongea maneno mengi ya upumbavu.
\s5
\v 4 Ukiweka nadhili kwa Mungu, usichelewe kuifanya, kwa kuwa Mungu hafurahii upumbavu. Fanya kile ulichoapa utakifanya.
\v 5 Ni bora kutokuweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri ambayo usiyoiondoa.
\s5
\v 6 Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi. Usiseme kwa mtumwa wa kuhani, "Kile kiapo kilikuwa kwa makosa." Kwani nini kumfanya Mungu akasirike kwa kuapa kwa uongo, kumchochea Mungu aharibu kazi ya mikono yako?
\v 7 Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna mvuke ubatili. Hivyo mwogope Mungu.
\s5
\v 8 Unapomwona masikini akiteswa na kunyang'anywa haki na kutendewa vibaya katika jimbo lako, usishangae kama kwamba hakuna anaye fahamu, kwa sababu kuna watu katika mamlaka ambao hutazama, kuna hata walio juu yao.
\v 9 Kwa nyongeza uzalishaji wa ardhi ni kwa kila mmoja, na mfalme mwenyewe huchukua uzalishaji kutoka mashambani.
\s5
\v 10 Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.
\v 11 Kadri mafanikio yanapoongezeka, ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia. Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?
\s5
\v 12 Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu, kama anakula kidogo au sana, lakini utajiri wa mtu tajiri haumuruhusu yeye kulala vizuri.
\s5
\v 13 Kuna jambo baya zaidi ambalo nimeliona chini ya jua: mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo, inamsababishia taabu mwenyewe.
\v 14 Wakati tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, ambaye amemzaa, habakiziwi chochote mikononi mwake.
\s5
\v 15 Kama mtu azaliwavyo uchi kutoka tumboni mwa mamaye, vivyo hivyo ataondoka katika maisha haya akiwa uchi. Hachukui chochote kutoka katika kazi yake.
\v 16 Jambo jingine baya kabisa, kama mtu alivyo kuja ni lazima aende vivyo hivyo. Hivyo ni faida gani mtu yeyote aipatayo katika kufanya kwa ajili ya upepo?
\v 17 Wakati wa siku zake anakula gizani na anafedheheshwa sana na magonjwa na hasira.
\s5
\v 18 Tazama, kile nilichokiona kuwa kizuri kufaaa ni kula na knywa na kufurahia faida kutoka katika kazi zetu zote, tuzifanyazo chini ya jua wakati wa siku za maisha haya ambayo Mungu ametupa. Kwa kuwa huu ni wajibu wa mtu.
\s5
\v 19 Yeyote ambaye Mungu amempa mali na utajiri na uwezo wa kupokea sehemu yake na kufurahi katika kazi yake hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
\v 20 Kwa kuwa mara kadhaa hakumbuki siku za maisha yake, kwa sababu Mungu anamfanya kuhangaika na mambo ambayo anafurahia kuyafanya.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kuna ubaya ambao nimeuona chini ya jua, na ni mbaya kwa watu.
\v 2 Mungu anaweza kumpa mtu mali na utajiri na heshima kwa kiasi kwamba hakosi chochote anachokitamani mwenyewe, lakini kisha hampi uwezo wa kukifurahia. Badala yake mtu mwingine hutumia vitu vyake. Huu ni mvuke, teso baya.
\s5
\v 3 Kama mtu akizaa watoto mia moja na kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi, lakini kama moyo wake hautosheki kwa mema na hazikwi kwa heshima, kisha ninasema kwamba, mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa ni bora kuliko alivyo.
\v 4 Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida na anapita katika giza, na jina lake linabaki limefichika.
\s5
\v 5 Ingawa mtoto huyu haoni jua au kujua kitu chochote, ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika.
\v 6 Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufuraia vitu vizuri, aenda sehemu moja kama mtu yeyote yule.
\s5
\v 7 Ingawa kazi yote ya mtu ni kujaza mdomo wake, ila hamu yake haishibi.
\v 8 Hakika ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu? Ni faida gani aliyo nayo masikini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?
\s5
\v 9 Ni bora kuridhika na kile ambacho macho hukiona kuliko kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani, ambayo pia ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.
\v 10 Chochote ambacho kimekuwepo, tayari kimekwisha kupewa jina lake, na vile mtu alivyo ni kama tayari amekwisha fahamika. Hivyo imekuwa haifai kugombana na yule ambaye ni muhukumu mkuu wa wote.
\v 11 Maneno mengi ambayo yanaongelewa, ndivyo yasiyo na maana yanaongezeka, kwa hiyo ni faida gani iliyopo kwa mwanadamu?
\v 12 Kwa kuwa ni nani ajuaye nini kilicho kizuri kwa mtu katika maisha yake wakati wa ubatili wake, siku zilizo hesabika ambazo kwa hizo anapita kama kivuri? Ni nina anayeweza kumwambia mtu kile kitakacho kuja chini ya jua baada ya kupita?
\s5
\c 7
\p
\v 1 Jina zuri ni bora kuliko manukato ya gharama, na siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.
\v 2 Ni bora kwenda kwenye nyumba ya maombolezo kuliko nyumba ya karamu, kwa kuwa maombolezo huja kwa watu wote wakati wa mwisho wa uhai, kwa hiyo watu wanaoishi ni lazima waweke hili moyoni.
\s5
\v 3 Huzuni ni bora kuliko kicheko, kwa kuwa baada ya uso wa huzuni huja furaha ya moyo.
\v 4 Moyo wa mwenye hekima uko katika nyumba ya maombolezo, lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya karamu.
\s5
\v 5 Ni bora kusikiliza maonyo ya mtu mwenye hekima kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
\v 6 Kwa kuwa kama mlio wa miiba chini ya chungu, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Huu pia ni mvuke.
\s5
\v 7 kweli jeuri humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, na rusha huharibu moyo.
\s5
\v 8 Ni heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo; na watu wenye uvumilivu ni bora kuliko wenye majivuno rohoni.
\v 9 Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
\s5
\v 10 Usiseme, "Kwa nini siku za zamani zilikuwa bora kuliko siku hizi?" Kwa kuwa sio kwa sababu ya hekima kwamba unauliza swali hili.
\s5
\v 11 Hekima ni njema kama vitu vya thamani tunavyorithi kutoka kwa wazazi wetu. Inatoa faida kwa wale wanaoliona jua.
\v 12 Kwa kuwa hekima hutoa ulinzi kama vile fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai kwa yeyote aliye nayo.
\s5
\v 13 Tafakaria matendo ya Mungu: Ni nani awezaye kuimarisha chochote alichokipindisha?
\s5
\v 14 Wakati nyakati vinakuwa njema, ishi kwa furaha katika hali hiyo, lakini wakati unapokuwa mbaya, tafakari hili: Mungu ameruhusu hali zote ziwepo, Kwa sababu hii, hakuna mwanadamu yeyote atakaye fahamu chochote kinacho kuja baada yake.
\s5
\v 15 Nimeona mambo mengi katika siku zangu za ubatili. Kuna watu wenye haki ambao wanaangamia licha ya kwamba wana haki, na kuna watu waovu wanaoishi maisha marefu licha ya kwamba ni waovu.
\v 16 Usiwe mwenye haki katika macho yako mwenyewe. Kwa nini kujiharibu mwenyewe?
\s5
\v 17 Usiwe mwovu sana au mpumbavu. Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?
\v 18 Ni vyema kwamba ushike hekima hii, na kwamba usiache haki iende zake. Kwa kuwa mtu amchae Mungu atatimiza ahadi zake zote.
\s5
\v 19 Hekima ina nguvu ndani ya mwenye hekima, zaidi ya watawala kumi katika mji.
\v 20 Hakuna mtu mwenye haki juu ya nchi anayefanya mema na hatendi dhambi.
\s5
\v 21 Usisikilize kila neno linaongelewa, kwa sababu unaweza kusikia mtumishi wako anakulaani.
\v 22 Vivyo hivyo unafahamu mwenyewe ndani ya moyo wako umewalaani wengine mara kadhaa.
\s5
\v 23 Haya yote nimeyathibitisha kwa hekima. Nikasema, "nitakuwa mwenye hekima," lakini zaidi ambavyo ningekuwa.
\v 24 Hekima i mbali na kina sana. Ni nani awezaye kuipata?
\v 25 Nikageuza moyo wangu kujifunza kuchunguza na kutafuta hekima na ufafanuzi wa ukweli, na kufahamu kwamba ubaya ni ujinga na kwamba upumbavu ni wazimu.
\s5
\v 26 Nikapata kufahamu kwamba uchungu kuliko kifo, ndivo alivyo mwanamke yeyote ambaye moyo wake umejaa mitego, na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo. Yeyote ampendezaye Mungu ataponyoka kutoka kwake, lakini mwenye dhambi atachukuliwa naye.
\s5
\v 27 "Tafakari kile nilichovumbua," asema Mwalimu. "Nimekuwa nikiongeza uvumbuzi mmoja hadi mwingine ili kwamba nipate ufafanuzi wa ukweli.
\v 28 Hii ndiyo bado natafuta, lakini bado sijapata. Sikupata mwanamme mmoja mwenye haki miongoni mwa elfu, lakini sikupata mwanamke miongoni mwa wale wote.
\s5
\v 29 Nimegundua hili: kwamba Mungu alimuumba binadamu akiwa mnyoofu, lakini wametoka katika hali ya unyofu wakitafuta magumu mengi.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Ni mtu gani mwenye hekima? Ambaye anafahamu matukio yana maana gani katika maisha? Hekima ndani ya mtu husababisha uso wake kung'ara, na ugumu wa uso wake hubadilika.
\s5
\v 2 Ninakushauri kuitii amri ya mfalme kwa sababu ya kiapo cha Mungu cha kumlinda yeye.
\v 3 Usiharakishe kuondoka mbele ya uwepo wake, na usisimame kuunga mkono jambo lisilofaa, kwa kuwa mfalme anafanya chochote anacho tamani.
\v 4 Neno la mfalme hutawala, kwa hiyo ni nani atakaye mwambia, 'Unafanya nini?
\s5
\v 5 Yeyote ashikaye amri za mfalme hukwepa madhara. Moyo wa mwenye hekima hutambua mwelekeo muafaka na muda wa kuenda.
\v 6 Kwa kuwa kila jambo lina jibu sahihi, na wakati wa kujibu, kwa sababu taabu ya mtu ni kubwa.
\v 7 Hakuna anaye fahamu kinacho fuata. Ni nani awezaye kumwambia nini kinacho kuja?
\s5
\v 8 Hakuna aliye mtawala wa pumzi yake hata kuisimamisha pumzi.
\v 9
\s5
\v 10 Hivyo niliwaona wabaya wakizikwa hadharani. Waliondolewa mahali patakatifu na kuzikwa mahali waliposifiwa na watu katika mji walipokuwa wamefanya matendo maovu. Hii nayo haifai.
\v 11 Wakati hukumu dhidi ya tendo ovu haihukumiwi haraka, hushawishi mioyo ya wanadamu kutenda ubaya.
\s5
\v 12 Hata kama mwenye dhambi afanye uovu mara mia moja na bado aishi kwa muda mrefu, bado ninafahamu itakuwa vyema kwa wale wanao muheshimu Mungu, wanaouheshimu uwepo wake walio nao.
\v 13 Lakini haitakuwa vyema kwa mtu mwovu; mkewe hatacheleweshwa. Siku zake kama kizuri kitowekacho upesi, kwa sababu hamuheshimu Mungu.
\s5
\v 14 Kuna mvuke mwingine usio faa, jambo jingine linaofanyika juu ya dunia. Mambo hutokea kwa watu wenye haki kama yatokeavyo kwa watu waovu, na mambo hutokea kwa wenye haki kama yatokeavyo kwa waovu. Ninasema hili pia ni mvuke usiofaa.
\v 15 Kwa hiyo nikapendekeza furaha, kwa sababu mtu hana jambo bora chini ya jua zaidi ya kula na kunywa na kuwa na furaha. furaha ndiyo itamfuata katika kazi zake kwa siku zote za maisha yake ambayo Mungu amempa chini ya jua.
\s5
\v 16 Nikauweka moyo wangu kufamu hekima na kufahamu kazi inayofanyika juu ya nchi, kazi ambayo inafanyika mara nyingi pasipo kufumba macho usiku au mchana.
\v 17 Kisha nika tafakari matendo yote ya Mungu, na kwamba mtu hawezi kuelewa kazi inayofanyika chini ya jua. Bila kujali mtu anafanya kupata majibu, hatayapata. Ingawa mwenye hekima anaweza kuamini anajua, kitu kweli hajui.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kwa kuwa nilifikiri haya yote katika akili zangu kufahamu kuhusu watu wenye haki na wenye hekima na matendo yao. Wote wako katika mikono ya Mungu. Hakuna anayefahamu kama upendo au chuki itakuja kwa mtu.
\s5
\v 2 kila mmoja ana mwisho sawa. Mwisho sawa una subiria watu wenye haki na waovu, wema, walio safi na wasio safi, yeye atoaye dhabibu na yule asiye dhabihu. Kama vile watu wema watakufa wenye dhambi nao watakufa vivyo hivyo. kama vile yule anayeapa atakavyo kufa, vivyo hivyo mtu yule aogopaye kuweka kiapo naye atakufa.
\s5
\v 3 Kuna mwisho mwovu kwa kila kitu kinachofanyika chini ya jua, na mwisho kwa kila mtu. Moyo wa mwanadamu umejaa uovu, na wazimu uko katika mioyo yao wakati wanaishi. Hivyo baada ya hilo wanaenda kwa wafu.
\s5
\v 4 Kwa kuwa yeyote anayeungana na wote walio hai kuna tumaini, kama vile mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliye kufa.
\v 5 Kwa kuwa watu walio hai, lakini walio kufa hawajui chochote. Hawana tena tuzo yeyote kwa sababu kumbukumbu yao imesahaulika.
\s5
\v 6 Upendo wao, chuki na wivu vimekatiliwa mbali muda mwingi. Hawatapata sehemu katika kitu chochote kinachofanyika chini ya jua.
\v 7 Nenda zako, kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha, kwa kuwa Mungu huruhusu kusherehekea kazi njema.
\v 8 Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta.
\s5
\v 9 Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye siku zako zote za maisha yako ya ubatili, siku ambazo Mungu amekupatia chini ya jua wakati wa siku zako za ubatili. Hiyo ni thawabu kwa ajili ya kazi yako chini ya jua.
\v 10 Chochote mkono wako unakifanya, kifanye kwa nguvu zako kwa sababu hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima katika Sheol, unapoenda.
\s5
\v 11 Nimeona baadhi ya vitu vyakuvutia chini ya jua: Mashindano hayatokani na watu wenye mbio. Vita havitokani na watu imara. Mkate hautokani na watu wenye busara. Mali hazitokani na watu wenye ufahamu. Kibali hakitokani na watu wenye ujuzi. Badala yake muda na bahati huwaathiri wao wote.
\v 12 Kwa kuwa hakuna anaye fahamu wakati wake wa kufa, kama vile samaki wanaswavyo katika nyavu ya kifo, au kama vile ndege akamatwavyo katika mtego. Kama wanyama wanadamu wamefungwa katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia.
\s5
\v 13 Pia nimeona hekima chini ya jua kwa namna ambayo kwangu ilionekana kubwa.
\v 14 Kulikuwa na mji mdogo na watu wachache ndani yake, na mfalme mkuu akaja kinyume na mji huo na akauzingira na akajenga mahandaki kwa ajili ya kuushambulia.
\v 15 Na katika mji kulikuwa na masikini, mtu mwenye hekima, ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji. Ila baadaye aliye mkumbuka yule masikini.
\s5
\v 16 Hivyo, nikasema, "Hekima ni bora kuliko nguvu, lakini hekima ya mtu masikini hudharauliwa, na maneno yake hayasikilizwi."
\s5
\v 17 Maneno ya watu wenye hekima yaliongewa polepole yanasikiwa vizuri kuliko makelele ya mtawala yeyote miongoni mwa wapumbavu.
\v 18 Hekima ni bora kuliko silaha za vita, lakini mwenye dhambi mmoja anaweza kuharibu mazuri mengi.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Kama nzi walio kufa husababisha manukato kutoa harufu ya uozo, hivyo hivyo upumbavu kidogo hushinda hekima na heshima.
\v 2 Moyo wa mtu mwenye hekima huelekea kulia, lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.
\v 3 Wakati mpumbavu anapotembea barabarani, fikira zake zina upungufu, ikithibitisha kwa kila mtu kwamba ni mpumbavu.
\s5
\v 4 Kama jaziba za mtawala zikiinuka kinyume na wewe, usiache kazi yako. Utulivu unaweza kutuliza ukatili mkubwa.
\s5
\v 5 Kuna uovu niliouona chini ya jua, aina ya kosa ambalo huja kutoka kwa mtawala:
\v 6 Wapumbavu wanapewa nafasi za uongozi, wakati watu walio faulu wanapewa nafasi za chini.
\v 7 Nimewaona watumwa wakipanda farasi, na watu walio faulu wakitembea kama watumwa juu ya ardhi.
\s5
\v 8 Yeyote anayechimba shimo anaweza kutumbukia yake, na popote mtu anayevunja ukuja, nyoka anaweza kumuuma.
\v 9 Yeyote achongaye mwawe, anaweza kuumizwa nayo. Na mtu achongaye mbao, anaweza kujihatarisha kwa hiyo.
\s5
\v 10 Kama chuma bapa kisicho na makali, na mtu hainoi, kisha ni lazima atumie nguvu nyingi, lakini hekima hutoa faida kwa ufaulu.
\v 11 Kama nyoka akiuma kabla hajafurahi, hivyo hakuna faida kwa mfurahishaji.
\s5
\v 12 Maneno ya kinywa cha mtu mwenye hekima yana huruma. Lakini midomo ya mpumbavu humumeza mwenyewe.
\s5
\v 13 Kama maneno yanavyo anza kutiririka mdomoni mwa mpumbavu, ujinga hutoka, na mwisho mdomo wake hutiririka wazimu mbaya.
\v 14 Mpumbavu huongeza maneno, lakini hakuna ajuaye kinachokuja. Ni nani ajuaye baada yake?
\s5
\v 15 Jasho la wapumbavu huwavaa wao, hivyo hawajui hata barabara ya kwenda mjini.
\s5
\v 16 Ole wako ardhi kama mfalme wako ni kijana mdogo, na kama viongozi wako huanza karamu ahsubuhi!
\v 17 Lakini umebarikiwa ardhi kama mfalme wako ni mwana wa waungwana, na kama vingozi wako hula wakati muafaka, kwa nguvu, na sio kwa ulevi.
\s5
\v 18 Kwa sababu ya uvivu paa huanguka. Na kwa sababu isiyo fanya kazi nyumba hupata ufa.
\v 19 Watu huandaa chakula kwa kicheko, divai huleta furaha maishani, na fedha hutimiza hitaji kwa kila kitu.
\s5
\v 20 Usimlaani mfalme, hata katika akili, na usiwalaani wenye mali katika chumba chako cha kulala. Kwa kuwa ndege wa angani inaweza kuchukua maneno yako. Chochote kilicho na mabawa kinaweza kusambaza jambo.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Peleka mkate wako juu ya maji, kwa kuwa utaupata tena baada ya siku nyingi.
\v 2 Shiriki mkate na watu saba, hata wanane kwa kuwa haujui ni majanga gani yanayo kuja juu ya nchi.
\v 3 Kama mawingu yamejaa mvua, yanajivua yenyewe chini ya nchi. Na kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, popote mti unapoangukia papo hapo utabakia.
\s5
\v 4 Yeyote autazamaye upepo yawezekana asipande, na yeyote atazamaye mawingu yawezekana asivune.
\v 5 Kama usivyo jua njia ya upepo, wala vile ambavyo mtoto akuavyo tumboni, vivyo hivyo huwezi kuielewa kazi ya Mungu, aliye umba kila kitu.
\s5
\v 6 Asubuhi panda mbegu yako; hadi jioni, fanya kazi kwa mikono yako kama inavyo hitajika kwa kuwa haujui ni ipi itafanikiwa, jioni au asubuhi, au hii au ile au zote zitakuwa nzuri.
\v 7 Kweli nuru ni tamu, na ni kitu cha kufurahisha kwa ajili ya macho kuona jua.
\v 8 Kama mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote, lakina na afikiri juu ya siku zijazo za giza, kwa kuwa zitakuwa nyingi. Kila kitu kijacho ni mvuke unaoteketea.
\s5
\v 9 Furahia kijana, katika ujana wako, na moyo wako ufurahie siku za ujana wako. fuatilia yale mema ya moyo wako, chochote kilicho mbele ya macho yako. Ingawa, fahamu kwamba MUngu atakuleta hukumuni kwa ajili ya vitu hivi vyote.
\v 10 Ondoa hasira kutoka moyoni mwako, na usijali maumivu yoyote katika mwili wako, kwa sababu ujana na nguvu zake ni mvuke.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Pia mkumbuke Muumba wako katika siku za za ujana, kabla ya siku za ugumu hazijaja, na kabla ya miaka haijafika utakapo sema, "Mimi sina furaha katika hizo,"
\v 2 fanya hivi kabla ya nuru ya jua na mwezi na nyota havijawa giza, na mawingu kurudi baada ya mvua.
\s5
\v 3 Huo utakuwa wakati ambapo mlinzi wa ikulu atatetemeka, na wanaume imara wameinama, na wanawake wanao saga kukoma, kwa sababu ni wachache, na wale wanao chungulia dirishani hawaoni vizuri tena.
\s5
\v 4 Huo utakuwa wakati ambao milango imefungwa katika mtaa, na mlio wa kusanga kukoma, wakati wanaume watasitushwa kwa mlio wa ndege, na wimbo wa sauti ya wasichana kukoma.
\s5
\v 5 Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji watelemka mitaani.
\s5
\v 6 Mkumbuke Muumba wako kabla ya kamba ya fedha kukatwa, au bakuli ya dhahabu kupasuka, au gudulia kuvunjwa kwenye chemuchemi, au torori la maji kuvunjika kisimani,
\v 7 kabla mavumbi kurudia mahali yalipotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
\s5
\v 8 Kama ukungu wa mvuke," asema mwalimu, kila kitu ni mvuke upoteao.
\v 9 Mwalimu alikuwa na hekima na aliwafundisha watu maarifa. Alisoma na kuazimu na kutunga mithali nyingi katika mpangilio.
\s5
\v 10 Mwalimu alitafuta kuandika kwa kutumia vithibitisho dhahiri, maneno ya kweli yaliyo wima.
\v 11 Maneno ya watu wenye hekima ni kama mchokoo. Kama misumari ilivyogongomewa kwa undani, ndivyo yalivyo maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao, ambayo yamefundishwa na mchungaji mmoja.
\s5
\v 12 Mwanangu kuwa makini na kitu zaidi, utengezaji wa vitabu vingi, ambacho hakina mwisho, na kusoma kwingi huleta uchovu mwilini.
\s5
\v 13 Mwisho wa jambo baada ya kila kitu umesikika, ni kwamba ni lazima umche Mungu na kushika amri zake, kwa kuwa huu ndilo jukumu lote la mwanadamu.
\v 14 Kwa kuwa Mungu ataleta kila tendo hukumuni, pamoja na kila kitu kilichofichika, kizuri au kibaya.

296
22-SNG.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,296 @@
\id SNG
\ide UTF-8
\h Wimbo wa Sulemani
\toc1 Wimbo wa Sulemani
\toc2 Wimbo wa Sulemani
\toc3 sng
\mt Wimbo wa Sulemani
\s5
\c 1
\p
\v 1 Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Wanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake
\v 2 O, laiti ungenibusu na mabasu ya mdomo wako, kwa kuwa upendo wako ni bora kuliko mvinyo.
\v 3 Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda.
\v 4 Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake nina furuha; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
\s5
\v 5 Mimi ni mweusi lakini mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, muzuri kama mapazia ya Sulemani.
\v 6 Usinishangae kwasababu ni mweusi, kwasababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzi wa mashamba ya mizabibu, lakini mshamba langu la mizabibu sijatunza. Wanamke akizungumza na mpenzi wake.
\s5
\v 7 Niambie, wewe ninaye kupenda, wapi unalisha mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
\s5
\v 8 Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
\s5
\v 9 Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
\v 10 Mashavu yako ni mazuri na mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
\v 11 Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
\s5
\v 12 Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza arufu.
\v 13 Mpenzi wangu ni kwangu kama mkebe wa marashi unao lala usiku katika ya maziwa yangu.
\v 14 Mpenzi wangu ni kwangu kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye
\s5
\v 15 Ona, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
\s5
\v 16 Ona, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi mtanashati.
\v 17 Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Mimi ni ua katika tambarare, nyinyoro katika bonde. Mwanaume akizungumza naye
\v 2 Kama nyinyoro miongoni mwa mimba, ndivyo wewe, mpenzi wangu, miongoni mwa mabinti wengine wote. Mwanamke akizungumza mwenyewe
\s5
\v 3 Kama mti wa mpera ulivyo miongoni mwa miti ya misituni, ndivyo mpenzi wangu alivyo miongoni mwa wanaume. Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana, na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu.
\v 4 Amenileta kwenye ukumbi wa maakuli, na bendera yake juu yangu ilikuwa upendo. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
\s5
\v 5 Ni uishe kwa keki za mizabibu na kuniuisha na mapera, kwa kuwa nimedhohofika na mapenzi. Mwanamke akizungumza mwenyewe
\v 6 Mkono wake wakushuto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
\s5
\v 7 Ninataka muhaidi, mabinti wa Yerusalemu, kwa swala na paa wa porini, kwamba hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke akizungumza mwenyewe.
\s5
\v 8 Sauti ya mpenzi wangu hiyo! O, huyu yuwaja, akiruka ruka juu milima, akiruka vilimani.
\v 9 Mpenzi wangu ni kama swala au mtoto mdogo wa paa; angalia, amesimama nyuma ya ukuta wetu, akishangaa kupitia dirishani, akichungulia wavuni.
\s5
\v 10 Mpenzi wangu alizungumza na mimi na kusema, "Amka, mpenzi wangu; mzuri wangu, twende pamoja nami.
\v 11 Angalia, baridi imepita; mvua imeisha na kwenda.
\s5
\v 12 Maua yametokeza juu ya nchi; wakati wa kupunguza matawi na kuimba kwa ndege umekuja, na sauti za hua zimesikika nchini kwetu.
\v 13 Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imestawi; yatoa marashi yake. Inuka, mpenzi wangu, mzuri wangu, na uje nami.
\s5
\v 14 Hua wangu, katika miamba ya mawe, katika miamba ya siri ya mipasuko ya milima, acha nione uso wako. Acha nisikie sauti yako, kwa kuwa sauti ni tamu, na uso wako ni mzuri." Mwanamke akiongea mwenyewe
\s5
\v 15 Wakamate mbweha kwa ajili yetu, mbweha wadogo wanao haribu shamba za mizabibu, kwa kuwa shamba la mizabibu limestawi.
\s5
\v 16 Mpenzi wangu ni wangu, na mimi ni wake; anakula penye nyinyoro kwa raha. Mwanamke anaongea na mpenzi wake
\v 17 Enenda zako, mpenzi wangu, kabla pepo za jioni hazija vuma na vivuli kutoweka. Nenda zako; kuwa kama ayala au mtoto mdogo wa paa katika milima mawe mengi.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Usiku katika kitanda changu nilikuwa na shauku ya yeye ni mpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.
\v 2 Nilisema binafsi, "Nitainuka na kwenda kupitia mji, kupitia mitaa na sokoni; nitamtafuta." Nilimtafuta, lakini sikumpata.
\s5
\v 3 Walinzi walinipata walipo kuwa doria katika mji. Nikawauliza, "Mmemuona mpenzi wangu?"
\v 4 Ni baada ya mda mfupi kupita nilipo wapita nikampata ninaye mpenda. Nilimshika na sikumuacha hadi nilipo mleta nyumbani mwa mama yangu, katika chumba cha yeye aliyenichukua mimba. Mwanamke akiongea na wanawake wengine.
\s5
\v 5 Ninataka muape, mabinti wa wanaume waYerusalemu, kwa ayala na paa wa porini, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\s5
\v 6 Nini hiyo inayo toka nyikani kama nguzo za moshi, umefukizwa manemane na ubani, pamoja na unga wote wa manukato unao uzwa na wafanya biashara?
\v 7 Angalia, nikitanda cha Sulemani; mashujaa sitini wamekizunguka, wanajeshi elfu sitini wa Israeli
\s5
\v 8 Wao ni wazoefu wa upanga na wanaujuzi wa vita. Kila mwanaume ana upanga wake pembeni yake, akijizatiti na maasi ya usiku.
\v 9 Mfalme Sulemani akajijengea kiti cha kifalme cha kubebwa na mbao za Lebanoni.
\s5
\v 10 Nguzo zake zilijengwa kwa fedha; nyuma kuliekwa dhahabu, na kiti kitambaa cha zambarau. Ndani mwake kulipambwa na upendo na mabinti wa wanaume wa Yerusalemu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa Yerusalemu
\v 11 Nenda nje, mabinti wa wanaume wa Sayuni, na mtazame mfalme Sulemani, akivikwa taji ambalo mamaye alimvika siku ya arusi yake, katika siku ya furaha ya maisha yake.
\s5
\c 4
\p
\v 1 O, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; wewe ni mzuri. Macho yako ni ya hua nyuma kitamba chako cha uso. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likienda chini kutoka Mlima Gileadi.
\s5
\v 2 Meno yako ni kama kondoo walio nyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna ata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
\s5
\v 3 Mdomo wako ni kama uzi mwekendu; mdo wako wapendeza. Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso.
\s5
\v 4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake, ngao zote za wanajeshi.
\v 5 Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.
\s5
\v 6 Hadi jioni ifike na vivuli viondoke, nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.
\v 7 Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
\s5
\v 8 Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya Amana, kutoka juu ya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, kutoka mashimo ya milima ya chuwi.
\s5
\v 9 Umeuiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeuiba moyo wangu, kwa mtazamo mmoja tu wako kwangu, kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
\s5
\v 10 Jinisi gani upendo wako ulivyo mzuri, dada yangu, bibi arusi wangu! Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo, na arufu ya marashi yako kuliko manukato yeyote.
\v 11 Midomo yako, bibi arusi wangu, yatiririka asali; asali na maziwa vichini ya ulimi wako; arufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni.
\s5
\v 12 Dada yangu, bibi arusi wangu ni bustani ilio fungwa, bustani ilio fungwa, chemchemi iliyo fungwa kwa muhuri.
\v 13 Matawi yako ni kichaka cha miti ya komamanga yenye matunda tofauti, na ya mimea ya hina na nardo,
\v 14 Nardo na Zafarani, mchai na mdalasini pamoja na aina zote za uvumba, manemane na udi na aina tofauti za manukato.
\s5
\v 15 Wewe ni bustani ya chemchemi, kisima cha maji safi, mifereji inayo shuka kutoka Lebanoni. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
\v 16 Amka, upepo wa kaskazini; njoo, upepo wa kusini; vuma katika bustani yangu ili manukato yake yatoe marashi. Mpenzi wangu na aje katika bustani yake na kula matunda ya chaguo lake.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Nimekuja katika bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; Nimekusanya udi wangu na manukato yangu. Nimekula mziga wangu wa asali na asali yangu; Nimekunywa mvinyo wangu pamoja na maziwa yangu. Marafiki wanazungumza na wapenzi Kuleni, marafiki; kunyweni na mlewe na mapenzi. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\s5
\v 2 Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu ulikuwa umeamka katika ndoto. Sauti ya mpenzi wangu yabisha na kusema, "Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, wangu usiye na doa, kwa kuwa kichwa changu kimelowa na matone, nywele zangu na unyevu wa usiku."
\s5
\v 3 "Nimevua joho langu; lazima nilivae tena? Nimeosha miguu yangu; lazima ni ichafue?"
\v 4 Mpenzi wangu anaeka mkono wake kwenye kitasa, na moyo wangu ukawaka kwa ajili yake.
\s5
\v 5 Nimeamka kumfungulia mlango mpenzi wangu; mikono yangu ikawa yamiminika na udi, vidole vyangu na unyevu wa udi, katika komeo la mlango.
\s5
\v 6 Nimemfungulia mlango mpenzi wangu, lakini mpenzi wangu aligeuka na kwenda. Moyo wangu ukadidimia; nikakosa tumaini. Nikamtafuta, lakini sikumpata; nikamuita, lakini hakunijibu.
\s5
\v 7 Walinzi waliokuwa wakizunguka mjini walinipata mimi; walinipiga chini na kunijeruhi; askari katika ukuta walichukua nguo yangu ya juu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji
\s5
\v 8 Ninataka uhaidi, mabinti wa Yerusalemu, kwamba mkimuona mpenzi wangu, mwambie ninaumwa sababu ya upendo wangu kwake. Wanawake wa mji wakizungumza na mwanamke mdogo
\s5
\v 9 Mpenzi wako ana ubora gani kuliko mwanaume mwengine, wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwanini mpenzi wako bora kuliko mpenzi mwengine, hadi utuulize tuweke nadhiri kama hii? Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji
\s5
\v 10 Mpenzi wangu amenawiri na ana ng'aa, kati ya wanaume elfu kumi.
\v 11 Kichwa chake ni dhahabu safi; nywele zake ni laini na nyeusi kama kunguru.
\s5
\v 12 Macho yake ni kama ya hua pembezoni ya vijito vya maji, yameoshwa na maziwa, yameundwa kama mikufu.
\s5
\v 13 Mashavu yake ni kama vitanda vya manukato, vinavyotoa arufu ya marashi. Midomo yake nni nyinyoro, inayo tiririka udi.
\s5
\v 14 Mikono yake ni ya mianzi ya dhahabu iliyo zungushiwa mikufu; tumbo lake ni pembe lililo funikwa yakuti samawi.
\s5
\v 15 Miguu yake ni nguzo za marimari, iliyo ekwa juu ya dhahabu safi; muonekano wake ni kama Lebanoni, mizuri kama mierezi.
\s5
\v 16 Mdomo wake ni mtamu; ni mzuri sana. Huyu ni mpenzi wangu, na huyu ni rafiki yangu, mabinti wa Yerusalemu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Mpenzi wako ameenda wapi, ulio mzuri miongoni mwa wanawake? Kwa njia gani mpenzi wako ameenda? ilitumtafute nawe? Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\s5
\v 2 Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.
\v 3 Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; na kula katika nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
\s5
\v 4 Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele.
\s5
\v 5 Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yana nizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi.
\s5
\v 6 Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja aliyefiwa.
\v 7 Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake
\s5
\v 8 Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wadogo bila idadi.
\v 9 Hua wangu, asiye na doa wangu, ni yeye pekee; ni binti muhimu wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wamalikia na masuria walimuona pia, na wakamsifu: Kile walicho sema wamalikia na masuria
\s5
\v 10 "Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, ana ng'aa kama jua, uamasisha kama bendera ya jeshi?" Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe
\s5
\v 11 Nimeenda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu imechipua, na kama mikomamanga imestawi.
\v 12 Nilikuwa nina furaha nikahisi kama nimepakia gari ya farasi la mtoto wa mfalme. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
\s5
\v 13 Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mkamilifu; geuka nyuma, geuka nyuma iliniweze kukushangaa. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katika ya mistari miwili ya wachezaji?
\s5
\c 7
\p
\v 1 Jinsi gani miguu yako ilivyo yaonekana mizuri kwenye viatu, binti wa mfalme! Mapaja yako ni kama mikufu, kama kazi ya mjenzi.
\s5
\v 2 Kitovu chako ni kama duara la bakuli; kamwe kisikose mchanganyiko wa mvinyo. Tumbo lako ni kama ngano iliyo umuka na kuzungushiwa nyinyoro.
\s5
\v 3 Maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala.
\v 4 Shingo yako ni kama mnara wa pembe; macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni kwenye lango la Bathi Rabimu. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ambao watazama Damasko.
\s5
\v 5 Kichwa chako ni kama Karmeli; nywele kichwani mwako ni za zambarau nyeusi. Mfalme amestaajabishwa na vifundo vyake vya nywele.
\v 6 Jinsi gani ulivyo mzuri na wakupendeza, mpenzi, na mazuri yako.
\s5
\v 7 Urefu wako ni wa kama mti wa mtende, na maziwa yako kama vifungu vya matunda.
\v 8 Niliwaza, "Ninataka kuupanda huo mti wa mtende; nitashika matawi yake." Maziwa yako nayawe kama vifungu vya mizabibu, na harufu ya pua yako yawe kama mapera.
\s5
\v 9 Mdomo wako na uwe kama mvinyo bora, ukishuka taratibu kwa mpenzi wangu, ukiteleza kwenye midomo yetu na meno. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\s5
\v 10 Mimi ni wa mpenzi wangu, na ananitamani.
\v 11 Njoo, mpenzi wangu, twende nje ya mji; tu lala usiku kwenye vijiji.
\s5
\v 12 Tuamke mapema twende kwenye mashamba ya mizabibu; tuone kama mizabibu imemea, kama imechipua, na kama mikomamanga imetoa mau. Pale nitakupa penzi langu.
\s5
\v 13 Mitunguja ya toa harufu yake; katika mlango wa tunapoishi kuna kila aina ya matunda, mpya na ya kale, niliyo kuhifadhia, mpenzi wangu.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliye nyonya ziwa la mama yangu. Ili kwamba kila ningekuona nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.
\s5
\v 2 Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, na utanifundisha. Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\v 3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine
\s5
\v 4 Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza
\s5
\v 5 Ni nani huyu anaye kuja kutoka nyikani, amemuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe.
\s5
\v 6 Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.
\s5
\v 7 Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe
\s5
\v 8 Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Nini tutamfanyia dada yetu siku hatakayo ahidiwa kuolewa?
\s5
\v 9 Kama ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
\s5
\v 10 Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
\s5
\v 11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao watalitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake.
\v 12 Shamba langu ka mzabibu ni langu, shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanao tunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.
\s5
\v 13 Wewe unaye ishi katika bustani, marafiki zangu wanasikiliza sauti yako; acha na mimi niweanaye isikia pia. Mwanamke mdogo akiongea na mpenzi wake
\s5
\v 14 Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.

2811
23-ISA.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2811 @@
\id ISA
\ide UTF-8
\h Isaya
\toc1 Isaya
\toc2 Isaya
\toc3 isa
\mt Isaya
\s5
\c 1
\p
\v 1 Maono ya Isaya mtoto wa Amozi ambayo aliyaona kuhusu Yuda na Yerusalemu katika vipindi vya utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda.
\s5
\v 2 Sikia enyi mbingu, tega sikio ewe nchi; kwa kuwa Yahwe amesema: ''Nimewatunza na kuwalea watoto, lakini wamenigeuka.
\v 3 Ng'ombe anamjua anayemmiliki na punda anajua sehemu anapowekewa chakula, lakini Israeli hawajui, wala hawafahamu.''
\s5
\v 4 Ole! Taifa, wenye zambi, mtu muovu, watoto wa wenye zambi, watoto wanaoenda kinyume, Wamemtelekeza Yahwe, wamedharau aliye Mtakatifu wa Israeli, wamejitenga wenyew kutoka kwake.
\s5
\v 5 Kwa nini ulikuwa unaendelea kupigwa? Kwa nini unazidi kuasi zaudi na zaidi? Kichwa chote kinauma, moyo wote ni dhaifu.
\v 6 Kutoka kwenye unyayo wa mguu mpaka kichwani kila sehemu ina maumivu; ni madonda na majeraha mabichi yaliyoachwa wazi, ambayo hayajafungwa, kuasifishwa, kuwafunga vidonda vyao, wala kuwaponya kwa mafuta.
\s5
\v 7 Nchi yenu imeharibiwa; miji yenu imechomwa moto; mashamba yenu--- mbele, wageni wamehiaribu; wamepatelekeza katika uharibifu, ulioangushwa na wageni
\v 8 Binti Sayuni ameacha kama kibanda katika shamba la mzabu, kama kivuli kitika shamba la matango, kama mji unaomba.
\s5
\v 9 Kama Yahwe wa majeshi hakutuasha kwa mda mfupi tungekuwa kama Sodoma, tungekuwa kama Gomora.
\s5
\v 10 Sikiliza neno la Yahwe, enyi viongozi wa Sodomu; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora:
\v 11 ''Sadaka zenu ni nyingi kiasi gani kwangu?'' asema Yahwe. ''Nimesikia vya kutosha kuhusu sadaka yenu ya mwana kondoo, na mnyama alionona; na damu ya ng'ombe, ndama, au mbuzi si vifurahii.
\s5
\v 12 Ulipokuja kuonekaa mbele yangu, Ni nani aliyehitaji hili juu yako, kukanyaga katika mahama yangu
\v 13 Msilete tena sadaka zisizo na maana; maana zinaniongezea uchafu mmekusanyika katika siku yenu mpya ya mwenzi na sabato--Mimi siwezi vumlia mikusanyio hii ya waovu.
\s5
\v 14 Ninaichukia sherehe yenu mpya ya mwenzi na sherehe zilizoteuliwa; ni mzigo kwangu; nimechoka kuubeba.
\v 15 Hivyo basi mnapotawanya mikono yenu kitkika maombi, sitawangalia hata kama mkiomba sana, sitawasikiliza; mikono yenu imejaa damu.
\s5
\v 16 Jiosheni, jitakaseni wenyewe; ondoeni matendo maovu mbele ya macho yangu; acheni kutenda dhambi;
\v 17 jifunze kutenda mema; tafuta ukweli; msiwanyanyase, wapeni haki yatima, walindeni wajane.''
\s5
\v 18 Njooni sasa, njooni tusemezane, asema Yahwe, japokuwa dhambi zenu ni nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama theluji; japokuwa ni myekundu kama damu zitakuwa kama sufi.
\s5
\v 19 Kama utakubali na kutii, utakula mema ya nchi,
\v 20 lakini ukikataa na kugeuka, upanga utakuangamiza, maama Yahwe amesema.
\s5
\v 21 Ni kwa jinsi gani mji ulioaminika umekuwa kahaba! ulikuwa ni mij wenye usawa na haki, lakini sasa mji umejaa mauwaji.
\v 22 Fedha zenu zimechafuka, na mvinyo wenu umechanganjwa na maji.
\s5
\v 23 Viongozi wenu wamemgeuka Mungu wamekuwa marafiki wa wezi; yeyote anayopenda rushwa na kuikimbilia. Hawawajali yatima, wala wajane wanaokuja kuwanyenyekea mbele yao.
\s5
\v 24 Hivyo basi hili ndilo tamko la Bwana, Yahwe wa majeshi, Shujaa wa Israeli: Ole wao! nitachukua hatua kwa wale walio kinyume na mimi na niwaadhibu wale wanaonipinga;
\v 25 Nitaugeuza mkono wangu juu yako, nitatakasa chuma kilicho chakaa na kuondoa kutu yote.
\s5
\v 26 Nitailinda hukumu yako kama ilivyokuwa mwanzo, na washauri wako kama ilivyokuwa hapo mwanzo; baada ya hapo mtaitwa mji wa haki, mji wa imani.''
\s5
\v 27 Sayuni itakombolewa kwa haki, na wanaotubu kwa haki.
\v 28 Waasi na wenye dhambi wataangamizwa pamoja, na wale wataenda kinyume na Yahwe watauliwa.
\s5
\v 29 Kwakukuwa utaona aibu juu ya miti ya mialoni uliyoitamani, na utakuwa na hofu juu ya bustani uliyoichagua.
\v 30 Kwa kukuwa utakuwa kama mualoni ambao majani yake yamenyauka, na kama bustani isiyokuwa na maji.
\s5
\v 31 Mtu mwenye nguvu atakuwa kama kitu kikavu, na kazi yake itakuwa kama cheche; zitawaka moto kwa pamoja, na hakuna hata mmoja ataweza kuuzima''.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu.
\v 2 Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale.
\s5
\v 3 Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu.
\s5
\v 4 Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena.
\s5
\v 5 Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe.
\v 6 Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni.
\s5
\v 7 Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari.
\v 8 Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza.
\s5
\v 9 Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu.
\v 10 Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake.
\v 11 Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
\s5
\v 12 Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini-
\v 13 na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani.
\s5
\v 14 Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu,
\v 15 na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukutaunaojitokeza,
\v 16 na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli.
\s5
\v 17 Kiburi cha mwanaume kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
\v 18 Sanamu zote zitaondolewa.
\v 19 Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi.
\s5
\v 20 Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo.
\v 21 Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake,
\v 22 usimwaminia mtu, ambae pumzi yake inatokea katika pua yake, ni kwa kiasi gan?
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ona, Bwana, Yahwe wa majeshi, anakaribia kuwachukua kutoka Yerusalema na Yudawasaidizi na wafanyakazi: wasambazaji wote wa mikate, wasambazaji wote wa maji;
\v 2 mtu mwenye nguvu, shuja, hakimu, nabii, dalili za msomaji, na mzee;
\v 3 naodha wa hamsini, raia husika, mshauri, fundi mtarajiwa, na mchawi stadi.
\s5
\v 4 Nitamuweka kijana tu kama kiongozi wenu, kijana atawaongoza wao.
\v 5 Watu watanyanyasika, kila mmoja mmoja na kila mmoja na jirani yake; watoto watawatusi wazee, na mivutano itawapa changamoto waheshimiwa.
\s5
\v 6 Mwanaume atamshikilia ndugu yake katika nyumba ya baba yake na kusema, 'Unayo kanzu; uwe kiongozi wetu, na uharibifu huu uwe mikononi mwako.
\v 7 'Siku hiyo atapaza sauti na kusema, 'hautakuwa mganga; sina mkate wala mavazi. Hatanifanya kuwa kiongozi wa watu.
\s5
\v 8 Kwa maana Yerusalemu kuna mashaka, na Yuda imeanguka, kwa sababu mazungumzo yao na matendo yao yako kinyume na Yahwe, wanayapinga macho ya utukufu wake.
\v 9 Angalia nyuso zao zinashudia kinyume nao; na watasema dhambi zao kama Sodoma; hawatazificha, Ole wao! Maana wanakamilisha janga lao wenyewe.
\s5
\v 10 Mwambie mtu mwenye haki kwamba itakuwa vizuri, maana watakula matunda ya matendo yao.
\v 11 Ole kwa wakosaji! itakuwa vibaya kwa yeye, maana malipo ya mikono yake yatafanyika kwake pia.
\v 12 Watu wangu-watoto wangu wanawakandamiza, na wanawake wanawaongoza wao. Watu wangu, wale wanaowaongoza wanawaongoza vibaya na kuchanganya muelekeo wa nja yenu.
\s5
\v 13 Yahwe simama juu ya mashitaka; yeye amesimama kuwashaki watu.
\v 14 Yahwe atakuja na hukumu juu ya wazee na watu wao na viongozi wao: ''Umeharibu shamba; nyara kutoka kwa masikni ziko kwenye nyumba zako.
\v 15 Kwa nini unaponda watu wangu na kusaga nyuso za masikini?'' Hili ni tamko Bwana, Yahwe wa majeshi.
\s5
\v 16 Yahwe anasema hivyo kwa sababu mabinti wa Sayuni wanajigamba, wanatembea pekee yao vichwa vyao vikiwa juu, na kutaniana kwa macho yao, na kutakata kokote waendako na kuamua upatu kwa miguu yao,
\v 17 Kwa hiyo Bwana atafanya magonjwa ya mapele kwenye kishwa cha mabinti wa Sayuni, na Yahwe atawafanya upaa.
\s5
\v 18 Siku hiyo Bwana ataondoa mapambo mazuri yaliyoko kwenye kifundo cha miguu, bendi za kichwa chao, kaya zao; bangili za masikio,
\v 19 bangili za miguu na taji zao;
\v 20 kitambaa cha kichwa, chaini za miguu, mafurungu na maboksi ya marashi na na haiba ya bahati.
\s5
\v 21 Atatoa bangili na kipini kwenye pua;
\v 22 sherehe za mavazi, mapazia na mabegi ya mkononi;
\v 23 vioo vya mkononi, sanda nzuri, vilemba vya kichwa na taji.
\s5
\v 24 Badala ya manukato mazuri kutakuwa na arufu mbaya; na badala ya ukunda, kamba, kufunika kwa vazi la gunia; kitia alama mwilini kwa moto badala ya uzuri. wanaume wao wataanguka kwa upanga,
\v 25 na wanaume wenye nguvu wataanguka kwenye vita.
\v 26 Lango la Yerusalemu litaomboleza na kuomboleza; na atakuwa peke yake amekaa chini ya ardhi.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Siku hiyo wanawake saba watamchukua mwanaume mmoja na kusema, ''Tutakula chakula chetu wenyewe, tutavaa nguo zetu wenyewe. lakini tunahitaji kuchukua jina lako ili tuondoe haibu zetu.''
\v 2 Na siku hiyo tawi zuri la Yahwe na utukufu, na matunda yatakuwa na ladha nzuri na kupendeza kwa wale wanaoishi Israeli.
\s5
\v 3 Itatokea kwa yule aliyeachwa Sayuni na wale waliobakia Yerusalemu wataitwa watakatifu, yeyeto aliyeandikwa chini anaishi Yerusalemu.
\v 4 Hii itatokea pale ambapo Bwana atasafisha uchafu wa mabinti wa Sayuni, na atasafisha madoa ya damu kutoka kati ya Yerusalemu, kwa namna ya roho ya hukumu na roho ya kuungua na moto.
\s5
\v 5 Tena juu ya mlima wote wa Sayuni na mahali pakuksanyikia, Yahwe atafanya wingu na moshi kwa wakati wa mchana na moto unaong'a wakati wa usiku; na itakuwa dari juu ya utukufu wote.
\v 6 kutakuwa na kivuli kwenye makazi wakati mchana kuzuia jua, na kimbilio na mfuniko kutoka kwenye mawimbi na mvua.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Acha niimbe kwa mpendwa wangu mzuri, wimbo wa mpendwa wangu kuhusu shamba la mzabibu. Mpendwa wangu ana shamba kwenye mlima wenye rutuba.
\v 2 Analilima, anaondoa mawe, na anaotesha aina ya mizabibu iliyo bora. Na hujenga mnara katikati ya shamba akichimba shinkizo ndani yake. Anasubiria mzabibu uzae matunda lakini unazaa zabibu mwitu.
\s5
\v 3 Kwa hiyo sasa, wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda, toa hukumu kati yangu na shamba la mzabibu.
\v 4 Je ni kitu gani cha ziada unaweza ukakifanya kwenye shamba langu la mizabibu, ambacho sijakifanya? ninapotamzamia izae matunda, kwa nini inazaa matunda mwitu?
\s5
\v 5 Sasa nitawambia kitu nitakacho kifanya kwenye shamba langu la mzabibu: nitaondoa uzio, nitaligeuza kuwa malisho, Nitavunja ukuta wake chini. Na itakanyagwa chini.
\v 6 Nami nitaliharibu wala halitapaliliwa wala kuilmwa, bali litatoa mbigiri na miba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshee mvua juu yake.
\s5
\v 7 Maana shamba la mzabibu la Yahwe Bwana wa majeshi ni nyumba ya Israeli, na mtu wa Yuda ndio mazao yake ya kupendeza; anaisubiria haki lakini badala ya yaki kuna mauwaji; maana haki, lakini badala yake ni kelele zikihitaji msaada.
\s5
\v 8 Ole wao wanaoungana nyumba kwa nyumba, shamba kwa shamba, mpaka wanamaliza, na umebaki mwenyewe kwenye shamba!
\v 9 Yahwe wa majeshi ameniambia mimi, nyumba nyingi zitakuwa wazi, hata kubwa na zinazovutia, hakuna mwenyeji yeyote.
\v 10 Maana mashamba ya mizabibu la nira kumi lilitoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu.
\s5
\v 11 Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema kutafuta pombe kali, wale wanaokaa usiku wa manane mpaka pombe inawaka moto.
\v 12 Wanasherekea kwa kinubi, kinanda, kigoma, filimbi, na mvinyo, lakini hawazitambui kazi za Yahwe, wala hawaziangalii kazi za mikono yake.
\s5
\v 13 Kwa hiyo watu wangu wameenda kifungoni kwa kukosa uelewa; viongozi wao wakuheshimiwa wanashinda na njaa, na watu wao hana kitu cha kunjwa.
\v 14 Hivyo basi kuzimu kumeongeza ladha yake na imefungua kinywa chake kwa kiasi kikubwa; wasomi wao, viongozi wao, manabii na wenye furaha miongoni mwao, watashuka kuzimu.
\s5
\v 15 Mtu atalazimishwa kuinama chini, na watu watakuwa wayenyekevu; na macho yao ya kujivuna yatatupwa chini,
\v 16 Yahwe wa majeshi atainuliwa katika haki yake, na Mungu mtakatifu atajidhirisha kuwa mtakatifu kwa haki yake.
\v 17 Ndipo kondoo watalishwa kama wako kwenye malisho yao wenyewe, na katika uharibifu, kondoo watachungwa kama wageni.
\s5
\v 18 Ole wao wanaovuta pamoja na waovu kwa kamba isiyo na maana na wanaovuta pamoja na dhambi kwa kamba za gari.
\v 19 Ole kwa wale wasemao, '' Basi na Mungu afanye haraka, basi afanya upesi, ili tuweze kuona kinachotokea; na tuache mipango ya Mtakatifu wa Israeli ije, ili tuifahamu.''
\s5
\v 20 Ole wao waitao uovu wema, na wema ni uovu; inayowakilisha giza kama mwanga, na mwanga kama giza; inayowakilisha kitu kichungu kama kitamu, na kitamu kama kichungu!
\v 21 Ole kwa wale wenye busara machoni mwao, na buasra kwa uelewa wao!
\s5
\v 22 Ole wao ambao ni washindi kwa kunjwa mvinyo, na wazoefu wa kuchanganya pombe kali;
\v 23 ambao wako huru kumpa haki mtenda maovu, na kuwanyima haki wenye haki!
\s5
\v 24 Hivyo basi kama ndimi za moto zinazokula mabua, kama majani makavu yanavyochomwa na moto, hivyo basi mizizi yake itaoza na maua yake yataperuka kama mavumbi. Hii itatokea kwa sababu wameikataa sheria ya Yahwe wa majeshi, na kwa sababu wamedharau neno la Mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 25 Hivyo basi hasira ya Yahwe imewaka juu ya watu wake. Ameunyoosh mkono wake juu yao na kuwaadhibu wao. Milima inatikisika, na maiti ni kama takata mitaani. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake, ameonyoosha mkono wake nje.
\s5
\v 26 Atapandisha bendera ya ishara mabali na mataifa na atapuliza filimbi kwa wale walio mwisho wa nchi. Tazama watakuja wakikimbia mara moja.
\s5
\v 27 Hakuna tairi wala mashaka miongoni mwao; hakuna asinzae wala kulala usingizi. Au kama mkanda uliolegea, wala kamba za viatu kukatika.
\v 28 Mishale yao ni mikali na upinde wao umejikunja; kwato za farasi wao' ni kama jiwe, na gari lao magurudumu yake ni kama miba.
\s5
\v 29 Mngurumo wao utakuwa kama wa simba, wataunguruma kama mtoto wa simba. Watanguruma na kukamata mawindo na kuvuta mbali, na hakuna hatakayeokolewa.
\v 30 Siku hiyo ataunguruma juu ya mawindo kama vile bahari kwa kishindo. Yeyote atakayeangalia nchi, ataona giza na mateso; hata mwanga hutafanjwa kuwa mweusi kwa mawingu.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Nyakati zile za kifo cha mfalme Uzzia, nilimuona Bwana akiketi katika kiti cha cha enzi; alikuw juu na mahali palipo inuka, na pindo la vazi lake limejaa hekaluni.
\v 2 Juu yake kuna maserafi; kila moja lina mabwa sita; mawili yamefunika uso wake, na mawili yamefunika miguu yake, na mawili ya kurukia.
\s5
\v 3 Kila mmoja anaitana na mwenzake nakusema, ''Mtakakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. ni Yahwe wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.''
\s5
\v 4 Misingi ya vizingiti imeshtuka kwa sauti ya mtu aliye nje, na njumba imejaa moshi.
\v 5 Ndipo nikasema,'' Ole wangu'' ninastahili adhabu maan mimi ni mtu mwenye midomo michafu, na ninaishi na watu wenye midomo michafu, maana macho yangu yamemuona Mfalme, Yahwe, Yahwe wa majeshi.''
\s5
\v 6 Ndipo mmoja wa maserafi akaruka juu yangu; mkononi mwake akiwa amebeba makaa ya mawe yanayong'aa, ameyachukuwa kwa koleo mathebauni.
\v 7 Akaugusa mdomo wangu kwa makaa ya mawe na akasema, ''Ona, makaa ya mawe yameshika midomo yako; maovu yako yameondolewa, na dhambi zako zimelipiwa kwa hili.''
\s5
\v 8 Nilisikia sauti ya Bwana ikisema, Nimtume nani; nani ataenda kwa niaba yetu?'' Ndipo nikasema, Niko hapa; nitume mimi.''
\v 9 Akasema nenda na uwambie watu, ' mnasikiliza lakini hamelewi; anaona lakini hamuangalii. '
\s5
\v 10 Nenda ufanye mioyo ya watu hawa kuwa migumu, na masikio yao kuwa mazito, na macho yao kuwa vipofu. Hivyo basi wanaweza kuona kwa macho yao, kusikia kwa masikioa yao, na kuelewa kwa mioyo yao wakajeuka na kuponjwa.
\s5
\v 11 Ndipo nikasema, ''Bwana, mda gani?'' Akanijibu, mpaka mji itakapopata ajali na kuharibiwa na pasipo wakazi, na nyumba hazina watu, na nchi imeanguka katika ukiwa mtupu,
\v 12 na mpaka pale Yahwe atakapo wapeleka watu mbali, na upweke wa nchi ni mkubwa.
\s5
\v 13 Hata kama makumi ya watu watabaki kwenye nchi, itaharibiwa kwa mara nyingine kama mwaloni uliokatwa chini na shina lake likabaki, mbegu takatifu kwenye kisiki chake.''
\s5
\c 7
\p
\v 1 Siku zile wakati Ahazi mtoto wa Yothani mtoto wa Uzia, mfalme wa Yuda, Rezeni mfalme wa Amramu, na Peka mtoto wa Remaelia, mfalme wa Israeli, walienda Yerusalemu kupigana vita nao, lakini hawakuweza kushinda vita.
\v 2 Ilitaarifiwa kwa nyumba ya Daudi kwamba Amramu amejiunga na Efraimu. Moyo wake na moyo watu wake ukatetemeka, kama vile miti ya misitu inavyopepea kwa upepo.
\s5
\v 3 Ndipo Yahwe akamwambia Isaya, ''Nenda nje na kijana wako, Sheari Jashubu ukaonane na Ahazi mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja Dobi.
\v 4 Mwambie, 'awe makini, awe mtulivu, asiogope au vitisho kwa sababu ya mikia hii miwili ya vingi hivi vitokavyo moshi, kwa sababu ya hasira kubwa ya Resini na Amramu, na mtoto wa Remalia.
\s5
\v 5 Amramu, Ephraimu, na mtoto wa Remaeli wamepanga mabaya juu yako; wamesema, '' njooni tuwavamie Yuda na kuwaogopesha,
\v 6 njooni tujipange na tumueweke mfalme wetu ndani ya Yuda, mtoto wa Tabaeli.''
\s5
\v 7 Bwana Yahwe asema, ''haitatokea; haitaonekana,
\v 8 maana kichwa cha Amramu ni Damaskasi, na kishwa cha Damaskasi ni Rezini. Ndani ya miaka sitini na tano, ndoto za Ephraimu zitasambaratishwa na hapatakuwa na watu.
\v 9 Efraimu ni kichwa Samaria, na kishwa cha Samaria ni mtoto wa Remaria. Na kama hamtasimama imara katika imani yenu, hakika hamtakuwa salama''.
\s5
\v 10 Bwana akaongea tena na Ahazi,
\v 11 ''Omba ishara ya Yahwe Mungu wako; omba juu ya hilo kwa kina au kwa kiwango cha juu.''
\v 12 Lakini Ahazi anasema, sintomba wala kumjaribu Yahwe.''
\s5
\v 13 Hivyo Isaya akajibu, ''sikilizen, nyumba ya Daudi. Je haijatosha kwa watu kuujaribu uvumilivu wa watu? Je ni lazima kuujaribu uvumilivu wa Mungu?
\v 14 Hivyo basi Mungu mwenyewe atawapa yeye mwenywe ishara: ona, mwanamke bikira atapata mimba na kumzaa mtoto, na atamwita Emanueli.
\v 15 Atakula siagi na asali na wakati anapojua kuyakataa maovu na kuchagua mema.
\s5
\v 16 Maana kabla mtoto ajajua kuyakataa maovu na kuchagua mema, nchi ambayo wewe unawachukia wafalme itakuwa ukiwa.
\v 17 Yahwe ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako siku hazijatimmia tangu Efraimu alipompokea Yuda- atamleta mfalme wa Asiria.''
\s5
\v 18 Mda huo Yahwe atapuliza filimbikwa ajili ya kupaa kutoka mkondo wa umbali wa Misri, na maana nyuki kutoka nchi ya Asiria.
\v 19 Zitakuja na kukaa chini ya korongo, ndani ya mapango ya miamba, kwenye vichaka vya miba, na kwenye malisho.
\s5
\v 20 Katika mda huo Bwana atamnyoa kichwani kichwani na nywele za miguuni kwa wembe ulioazimwa mto Efrarate-- mfalme wa Asiria - na vilevile utasafisha ndevu zote.
\v 21 Siku hiyo, mtu atahifadhi ndama na na kondoo wawili,
\v 22 na kwasababu ya maziwa yatakayo patikana ni mengi, atakula siagi, maana kila atakaye bakia kwnye nchi atakula siagi na asali.
\s5
\v 23 Mda huo, kutakuwa na maelfu ya mizabibu na thamani elfu za shekeli, hakutakuwa na kitu zaidi ya kuzalisha mbigiri na miiba.
\v 24 Watu watenda pale kuwinda kwa upinde, kwa sababu nchi yote itazalisha mbigiri na miiba.
\v 25 Watakaa mbali na vilima vitalimwa kwa jembe, kwa sababu ya hofu ya mbigiri na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kuchungia ngo'mbe na kondoo
\s5
\c 8
\p
\v 1 Yahwe ameniambia mimi, '' chukua meza kubwa na uandike juu yake, 'Maheri Shalal Hash Baz.'
\v 2 Nitachagua mashahidi waaminifu wanishuhudie mimi, kuhani Uria, Zakaria mototo wa Yeberekia.''
\s5
\v 3 Nilienda kwa huyo nabii mwanamke alipata mimba na kumzaa mtoto. Halafu Yahwe akaniambia, ''Muite jina lake Shalal Hash Baz;
\v 4 Maana kabla mtoto ajajua kulia, 'Baba yangu, 'Mama yangu; utajiri wa Damaskasi, na mateka wa Samaria watachuliwa na mfalme wa Asiria.
\s5
\v 5 Yahwe aliongea na mimi tena,
\v 6 Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa na ni furaha kwa Rezeni na mtoto wa Remalia,
\v 7 Hivyo basi Bwana anakairbia kuwaletea maji maji ya mto, yenye nguvu na mengi, mfalme Asiria na utukufu wake utakuja juu na kupita juu ya mifereji yake atafurika juu ya kingo zote.
\s5
\v 8 Mto utafurika kuelekea Yuda, utafurika mpaka kufika kwenye shingo yako. Mabawa yake yaliyonyooshwa utajaza upana wa nchi, Emanueli.''
\s5
\v 9 Nyie watu mtavunjika vipande vipande, Sikilizeni, nyote muishio nchi zilizo mbali; jiandaeni wenyewe na mtavunyika vipande vipande.
\v 10 utatengeneza mpango, lakini haufanyiwa kazi; maana Mungu yuko pamoja nasi.
\s5
\v 11 Yahwe ameiniambia mimi, kwa mkono wake imara juu yangu, na amenikataza nisitembee katika njia za watu hawa. Nisiseme,
\v 12 Ni fitina habari ya mambo ambayo watu hawatasema, ni fitina msihofu wala msiogope.
\v 13 Yahwe wa majeshi ambaye mtakaye muheshimu kama mtakatifu; yeye ndie mtakayemuogopa na yeye ndiye mtakayemuhofia.
\s5
\v 14 mtakatifu; lakinia takuwa kama jiwe la kikwazo na mwamba wa kujikwaza kwa nyumba zote za Israeli. Na atakuwa mtego na mtego kwa watu wake Yerusalemu.
\v 15 Wengi watajikwaa juu yao na kuanguka na kuvunjika, na kutekwa na kukamata mateka.
\s5
\v 16 Ufunge huo ushuhuda, tia muhuri, na uwape wafuasi wangu,
\v 17 Nitamsubiri Yahwe, afichaye uso wake kutoka nyumba ya Yakobo; Nitamsubiri yeye.
\v 18 Ona, Mimi na watoto ambaye Yahwe amenipa mimi ni ishara na maajabu tu katika Israeli kutoka kwa Yahwe wa Majeshi yeye aishiye mlima wa Sayuni.
\s5
\v 19 Watakuambia wewe, ''tafuta habari kwa watu wenye pepo na wachawi'', walio kama ndege na kunong'ona dua. Lakini hawataacha kutafuta habari kwa Mungu wao? Je waenende kwa watu waliokufa badala ya walio hai?
\v 20 Kwa sheria na kwa ushuhuda! kama hawatayasema mambo hayo ni kwa sababu hakuna mwanga wa alfajiri.
\s5
\v 21 Nawatapita katikati ya nchi kwa shida kubwa na njaa. Walipokuwa na njaa, walipatwa na hasira na kumlaani mfalme wao na Mungu wao, na wakajeuza macho yao juu.
\v 22 Wataiangalia nchi na kuona dhiki, giza, na ukandamizaji wa viza. Watapelekwa kwenye nchi ya giza.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Viza itaondolewa kwa yeyote ambaye yuko kwenye dhiki. Katika kipindi cha awali aliifedhehesha nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali, lakini kipindi cha baadae ataifanya itukuke, njia ya kuelekea baharini, mbele ya Yordani na mataifa ya Galilaya.
\v 2 Watu wanotembeakatika giza wameona wameona mwanga mkubwa; wale waishio katika nchi ya uvuli wa mauti, mwanga umewaka juu yao.
\s5
\v 3 Umeliongeza taifa; umeongeza furaha yao. Wamefurahia mbele yako kama furaha ya kipindi cha mavuno, kama watu wanavyofurahi kugawanya nyara.
\s5
\v 4 Maana nira ya mzigo wake, boriti katika mabega yake, fimbo ya mkandamizaji, umesambaratisha ndoto kama siku ya Midiamu.
\v 5 Kila buti likanyagalo gasia na vazi limekwisha kwenye damu itachomwa, mafuta kwa moto.
\s5
\v 6 Kwetu mtoto amezaliwa, kwetu mtoto ametoka; na mtawala atakuwa kwenye mabega yake; na jina lake ataitwa mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani.
\v 7 Enzi yake na amani yake haitakuwa na mwisho, maana anatawala katika kiti cha enzi cha Daudi, na juu ya ufalme wake, ataanzisha hukumu ya haki, tangu sasa na hata milele. Bidii ya Yahwenwa majeshi itafanya haya.
\s5
\v 8 Bwana alituma neno juu ya Yakobo, na ikaanguka juu ya Israeli,
\v 9 Watu wote watajua, Hata Samaria na wakazi wote wa Samaria, wanaongea kwa kiburi na moyo wenye kiburi,
\v 10 Matofali yameanguka, lakini tutajenga tena kwa jiwe la patasi; mkuyu umekatwa chini, lakini tutaotesha mierezi katika eneo lao.
\s5
\v 11 Hivyo basi Yahwe atamwinua juu yao Rezini, adui zake, atawakoroga adui zake,
\v 12 Waaramea upande wa mashariki, na wafilisti upande wa magharibi. Nao watamla Israeli kwa mdomo uliowazi. katika mambo yote haya hasira yake haijapungua; badala yake ameunyosha mkono wake nje.
\s5
\v 13 Lakini hawatageuka kwa yule anayewapiga wao, wala kumtafuta Yahwe wa majeshi.
\v 14 Hivyo basi yao atakata kichwa nakiwiwili cha Israeli, kuti na nyasi, katika siku moja.
\v 15 Viongozi na watu wenye vyeo na manabii wanaofundisha kuwa uongo ni mkia.
\s5
\v 16 Wale wanaowaongoza watu hawa wanawaongoza vibaya, na wale wanaongozwa wameangamia.
\v 17 Hivyo basi Bwana atafurahia juu ya vijana wadogo wala hatakuwa na huruma kwa yatima na wajane, maana kila mmoja hana Mungu na ni watenda dhambi, na kila mdomo unazungumza matendo mabaya. Mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake umenyooka hata sasa.
\s5
\v 18 Matendo mabaya yataungua kama moto, moto hulao mbigili na miiba; itachoma hata vichaka vya mwitu, na safu ya moshi mkubwa upaa.
\v 19 Japo hasira ya Yahwe wa majeshi imeunguza, na watu ni kama mafuta kwenye moto. Hakuna mtu aliyemuacha ndugu yake.
\s5
\v 20 Watanyakuwa chakula katika mkono kulia lakini bado watasikia njaa; watakula chakula kwa mkono wa kushoto lakini hawataridhika. Kila mmoja atakula nyama ya mkono wake mwenyewe.
\v 21 Manase; kwa pamoja watavamia Yuda. Mambo yote haya, hasira yake haitapungua; badala yake, amenyoosha mkono wake hata sasa.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Ole wao watimizao sheria zisizo za haki na waandikao sheria zisizo na haki.
\v 2 Wanawanyima wahitaji haki yao, wanawaibia watu wangu walio masikini haki zao, wajane mateka wao, na kuwafanya waliofiwa na baba zao mawindo yao!
\s5
\v 3 Hutafanya nini siku ya hukumu pale siku ya uaribifu itakapokuja kutoka mbali, utakimbilia msaada kwa nani? na utauacha utajiri wako wapi?
\v 4 Hakuna kitakachobaki, utaota miongoni mwa wafungwa au kuanguka miongoni mwa wauwaji. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake ameunjoosha hata sasa.
\s5
\v 5 Ole kwa watu wa Asiria klabu ya asira yangu, fimbo ya asira yangu!
\v 6 Nimemtuma juu ya taifa lenye kiburi na juu ya watu waliobeba uwingi wa hasira. Ninaamuru chukua nyara, chukua mawindo, na kuwakanyaga wao kama matope mitaani.
\s5
\v 7 Lakini hichi sicho alichomaanisha, wala sivyo afikiriavyo. Maana katika moyo wake ni kuharibu na kuondoa mataifa.
\v 8 Maana amesema, '' wakuu wote sio wafalme?
\v 9 Je? kalno si kama Karkemish? Je Hamathi si kama Arpadi? Je Samaria si kama Demeski?
\s5
\v 10 Kama mikono yangu imeshinda falme za ibada ya sanamu, ikiwa sanamu zao za kuchonga ni bora kuliko sanamu za Yerusalemu
\v 11 na Kama nilivyofanya kule Samaria na sanamu zake zisizo na maana, je sitaweza kufanya hivyo Yerusalemu na sanamu zake?''
\s5
\v 12 Pindi ambapo Bwana alipoimaliza kazi kwenye mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu maneno ya moyo wenye kiburi ya mfalme wa Asiria na majivuno yake.
\v 13 Kwa maana amesema, ''Kwa nguvu zangu na kwa hekima yangu niliyoifanya. na Nimeelewa, na nimeondoa mipaka ya watu. nimewaibia akiba yao, ni kama nilioileta chini kwa wenyeji wake.
\s5
\v 14 Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama vile mtu ayakusanyavyo mayai, kama nilivyokusanya dunia yote. Hakuna atakayeperusha mabawa yake au kufungua midomo yake au kulia.''
\s5
\v 15 Je shoka lijisifu lenyewe juu ya mtu anayelitumia? Je litajisifia lenyewe zaidi ya yule anaelitumia kukatia? Au fimbo imuinuae yeye ambaye si mti.
\v 16 Hivyo basi Yahwe wa majeshi atatuma wadhaifu miongoni mwa wasomi wa kijeshi; na chini ya utukufu na kuteketea kama kuteketea kwa moto.
\s5
\v 17 Mwanga wa Isreli utakuwa moto, na Mtakatifu wake atakuwa ni moto unaoteketeza na kula mbigiri siku moja.
\v 18 Yahwe atauteketeza utukufu wa msitu wake na shamba lake linalostawi, vyote nafsi na mwili; itakuwa kama vile mgonjwa apotezae maisha yake.
\v 19 Mabaka ya miti ya misitu itakuwa michache sana, ambayo mtoto anaweza kuyahesabu.
\s5
\v 20 Siku hiyo, mabaki ya Israeli, familia ya Yakobo ambayo imekimbia, hawatategemea kushindwa, lakini watamtegemea Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
\v 21 Mabaki ya Yakobo yatarudi kwa Mungu mwenye nguvu.
\s5
\v 22 Kwa kupitia watu wako, Israeli ni kama mchanga kama pwani ya bahari, Mabaki yao tu ndio yatakayorudi. Uaribifu wa amri, na mahitaji ya wingi wa haki.
\v 23 Maana Bwana wa majeshi, anakaribia kuleta uharibifu utachukua nafasi kubwa kitika nchi.
\s5
\v 24 Hivyo basi Bwana Yahwe wa majeshi anasema, ''watu wangu mhishio Sayuni, msiwaogope watu wa Asiria. Atawangamiza nyie kwa fimbo na atawanyua wafanyakazi juu yenu, kama ilivyotokea kwa Wamisri.
\v 25 Msimuogope, kwa mda mfupi hasira yangu itakwisha juu yenu, na hasira yangu italeta uharibifu.''
\s5
\v 26 Hivyo Yahwe wa majeshi atapiga mjeledi juu yenu kama vile alivyoishinda Midiani karibu na mwamba Orebu. Na atanyanyua fimbo yake juu ya bahari kama alivyofanya kule Misri.
\v 27 Siku hiyo mzigo wake utanyanyuliwa kwenye mabeba yako na nira katika shingo yako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya unene.
\s5
\v 28 Adui amekuja Aiathi na amepitia Migroni; katika Michmashi ameyahifadhi mahitaji yake.
\v 29 Wamevuka juu ya njia na wamepunzika huko Geba. Rama inatetemeka na Gibea ya Sauli imekimbia.
\s5
\v 30 Lia kwa sauti, ewe binti wa Galimu! sikiliza, Laishashi! Maskini Anathothi!
\v 31 Madmena ni mkimbizi na mkazi wa Gebuni wamejikusanya wanakimbia kutafuta msada.
\v 32 Siku hizi za leo atasimulia huko Nobi na atatingisha mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.
\s5
\v 33 Tazama, Bwana Yahwe wa majeshi atapunguza matawi kwa nguvu za kutisha; miti mirefu itakatwa chini, wanaojivuna wataangushwa.
\v 34 Atang'oa vichaka vya msitu kwa shoka, Lebanoni na utukufu wake utaanguka.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Miti itachipukia katika mizizi ya Yese, na matawi yanayotokana na mizizi yatazaa matunda.
\v 2 Na roho wa Bwana atashuka juu yake, roho wa hekima na maelewano, roho ya maelekezo na ukuu, roho ya maarifa na hofu ya Yahwe.
\s5
\v 3 Furaha yake itakuwa hofu ya Bwana; hatatoa hukumu kwa kile anachokiona, wala atatoa maamuzi kwa kile anachokisikia.
\v 4 Badala yake atawahukumu masikini kwa haki na atafanya maamuzi kwa usawa na unyenyekevu. Ataamurisha mgomo wa dunia kwa fimbo ya mdomo wake, na punzi ya midomo yake, atawauwa waovu.
\v 5 Haki itakuwa mkanda wa viuno kiuno chake kuzunguka mapaja yake.
\s5
\v 6 Mbwa mwitu atakaa pamoja na kondoo, na chui watalala chini pamoja na mtoto wa mbuzi, ndama, mtoto wa simba na ndama pamoja na ndama aliyenona. Mtoto mdogo atawaongoza wao.
\v 7 Ng'ombe na dubu watachungwa pamoja. Na watoto wao watalala pamoja. Simba atakula majani kama ng'ombe.
\s5
\v 8 Mtoto atacheza juu ya chimo la nyoka, na mtoto aliyeachwa ataweka mkono wake katika pango la nyoka.
\v 9 Hawataumizwa wala kuharibiwa kwenye mlima mtakatifu; kwa maana dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe, kama maji yajaavyo kwenye bahari.
\s5
\v 10 Siku hiyo mzizi wa Yese utasimama kama bendera ya watu. Taifa litamtafuta yeye nje, na mahali pake pakupumzikia patatukuka.
\v 11 Siku hiyo, Bwana ataunyoosha mkono wake tena kuokoa mabaki ya watu wake yaliyosalia huko Asiria, Misri, Pathrosi, Kushi, Shinari, Hamathi, na kisiwa cha bahari.
\s5
\v 12 Ataweka bendera kwa kwa mataifa na atakusanya Waisrel waliotupwa na watu wa Juuda waliotawanyika kitika pembe nne za dunia.
\v 13 Ataujeuza wivu wa Efraimu, na ukatili wa Yuda utakomeshwa. Efraimu atamuonea wivu Yuda, Yuda hatakuwa adui wa Efraimu tena.
\s5
\v 14 Badala yake, watashuka chini kwenye mlima wa Wafilisti upande wa magharibi, na pamoja watateka watu mashariki. Watavamia Edomu na Moabu, na watu wa Amoni watawatii wao.
\v 15 Yahwe atauharibu kabisa ghuba ya bahari ya Misri. Kwa mawimbi makali ambayo yanavuma juu ya mtoto Efurate na itagawanyika katika mifereji saba, hivyo unaweza ukapita juu kwa viatu.
\s5
\v 16 Kutakuwa na njia kuu kwa ajili ya mabaki ya watu kurudi kutoka Asiria, maana kuna Waisraeli wanaokuja kutoka nchi ya Misri.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Siku hiyo utasema, ''Nitakushukuru wewe, Yahwe. Japo ulikuwa na hasira na mimi, laana yako imeondoka mbali, na umenifariji mimi,
\v 2 Ona Bwana ni wokovu wangu; nitamwamini na sitakuwa na hofu, kwa Yahwe, ndio, Yahwe ni nguvu yangu na wimbo wangu. Amekuwa wokovu wangu.''
\s5
\v 3 Kwa furaha utachota maji kwenye kisima cha wokovu.
\v 4 Siku hiyo utasema, ''Mshukuru Yahwe na ita jina lake; tangaza matendo yake miongoni mwa watu, tangaza jina lake limeinuliwa.
\s5
\v 5 Mwiimbie Yahwe, maana ametenda matendo yaliotukuka; acha hili lijulikane dunia nzima.
\v 6 Lia kwa nguvu na piga kelele kwa furaha, enyi wakazi wa Sayuni, maana katikati yenu ni mtakatifu wa Israeli.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Tamko kuhusu Babeli, ambalo Isaya mtoto wa Amozi alipokea:
\v 2 Kwenye mlima wa wazi imewekwa bendera ya ishara, lia kwa sauti kwao, wapungie mikono waende kwenye lango la wenye vyeo.
\v 3 Nimewamuru watakatifu wangu, ndio, nimewaita watu wangu wenye nguvu kutekeleza asira yangu, na hata watu wangu wanojigmba na kujiinua wenyewe.
\s5
\v 4 Kelele za umati wa watu kwenye milima, za watu wengi! Kelele za ghasiaza ufalme kama mataifa mengi yamekusanyika pamoja! Yahwe wa majeshi anapanga jeshi kwa vita.
\v 5 Wametoka katika nchi ya mbali, kutoka juu ya upeo wa macho. Ni Yahwe na silaha zake za hukumu, kuhiharibu nchi yetu.
\s5
\v 6 Omboleza maana siku ya Yahwe imekaribia; itakuja na uharibifu kutoka kwa Mwenyenzi.
\v 7 Hivyo basi mikono ining'inizwe kama kiwete, na kila moyo ulioyeyuka.
\v 8 Itawatisha; maumivu na uchungu atawapa wao, kama mwanamke ambaye anajifungua. Watangalia kwa kushangaa kwa kila mmoja mmoja; nyuso zao zitakuwa kama moto.
\s5
\v 9 Tazama, siku za Yahwe zinakuja na laana kali wingi wa hasira, kuifanya nchi yenye ukiwa na kuharibu wenye dhambi katika nchi.
\v 10 Nyota ya mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake. Jua litakuwa giza na hata mwenzi hautaangaza.
\s5
\v 11 Nitaihadhibu nchi kwa maovu yake na makosa ya uovu wao. Nitamaliza kiburi cha majivuno na nitawashusha wenye kiburi wasiwe makali.
\v 12 Nitawafanya watu kuwa nadra zaidi ya dhahabu nzuri na watu kuwa vigumu kupatikana zaidi ya dhahabu safi ya Ofiri.
\s5
\v 13 Hivyo basi nitazifanya mbingu kutingishika, na dunia itayumba kutoka sehemu iliyoko, Kwa hasira ya Yahwe wa majeshi, na siku ya hasira yake.
\v 14 Kama Paa anayewindwa au kama kondoo wasio na mchungaji, kila mtu atageukia watu wake na kukimbia kwenye nchi yake.
\s5
\v 15 Kwa yeyote atakayeonekana atauliwa, na yeyote atakayekamatwa atauliwa kwa upanga.
\v 16 Watoto wao watakatwa vipandevipande mbele ya macho yao. Nyumba zao zitavamiwa na wake zao watabakwa.
\s5
\v 17 Tazama, ninakaribia kuwakoroga Wamede ili wawavamie wao, ambao hawaoni maana ya fedha wala furaha ya dhahabu.
\v 18 Mishale yao itawachoma vijana wadogo. Hakutakuwa na shimo kwa watoto wao na hawatawacha watoto wao.
\s5
\v 19 Na Babali ufalme unaovutia zaidi, fahari ya mapambo ya wakaldyo, itaangamizwa na Mungu kama Sodoma na Gomora.
\v 20 Hapatakuwa na wenyeji wala wakazi kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Mwarabu atapiga hema lake uko wala wachungaji hawatalaza mifugo yao pale.
\s5
\v 21 Lakini wanyama pori wa jangwani watalala pale. Nyumba zao zitajaa bundi; na mbuni watakaa huko na mbuzi pori wataruka pale.
\v 22 Fisi watalia kwenye ngome yao, na mbeha katika maeneo yao mazuri. Mda wao umekaribia, na siku zao hazitachelewa.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Yahwe atakuwa na huruma juu ya Yakobo; atamchagua tena Israeli na kumrudisha tena kwenye nchi yake. Wageni wataungana nao na wataambatana wenyewe na nyumba ya Yakobo.
\v 2 Mataifa yataletwa katika maeneo yao wenyewe. Ndipo nyumba ya Israeli itawachukwa katika nchi ya Yahwe kwa watumishi wa kiume na wakike. Watachukuwa wafungwa wale waliokamatwa, na watawaongoza wale waliokuwa wanawanyanyasa.
\s5
\v 3 Siku hiyo Yahwe atatoa pumziko kutoka kwenye mateso na maumivu, na kutoka kwenye kazi ngumu ambayo waliitajika kuzifanya,
\v 4 mtaimba hii kauli wimbo juu ya mfalme wa Babeli, ''Ni kwa jinsi gani wayanyasaji wamefika mwisho, kiburi cha hasira kimekwisha!
\s5
\v 5 Yahwe amevunja wafanyakazi waovu, fimbo ya hao viongozi,
\v 6 inayowapeleka watu kwenye laana na mapigo yasiyopimika, wanoongoza taifa kwa hasira,.
\s5
\v 7 yote iko katika punziko na utulivu; wmeanza kusherekea kwa kiimba.
\v 8 Hata mti wa mseprasi inafuhaia pamoja mierezi ya Lebanoni; inasema, Tangu ulipoweka chini, hakuna mkata kuni aliyekuja kutungusha sisi,
\v 9 Kuzimu haina hamu kwa ajili yako unaye enda pale. Watafufuka waliokufa kwa ajili yako, wafalme wote wa dunia, wafanje watoke katika viti vyao vya enzi, wafalme wote wa mataifa.
\s5
\v 10 Watazungumza na kukuambia wewe, 'umekuwa dhaifu kama sisi.
\v 11 Kiburi chako kimeshushwa kuzimu na sauti kifaa cha kamba yako. Buu wameongezeka chini yako na vijidudu vinakufunika wewe.'
\s5
\v 12 Kwa jinsi gani ulivyoanguka kutoka mbinguni, nyota ya siku, jua la asubuhi! ni kwa jinsi gani mlivyoshushwa chini, umeyashinda mataifa!
\v 13 Unasema katika moyo wako, ' Nitapaa kutoka juu mbinguni, nitanyanyua enzi yangu juu ya nyota za Mungu, na nitakaa kwenye mlima wa kukusanyikia, kwa mbali kufika kaskazini.
\v 14 Nitapaa juu umbali wa mawingu; Nitalifanya mimi mwenyewe kama Mungu aliye juu zaidi.'
\s5
\v 15 Lakini kwa sasa umeshushwa chini kuzimu, kwenye kina cha shimo.
\v 16 Wale wanaokuona watakuangalia wewe, watakuangalia sana. Watasema, Je ni huyu mtu aliyefanya dunia itetemeke, nani aliyetingisha falme,
\v 17 ni nani aliyefanya dunia kama jangwa, ni nani aliyeharibu miji yake, na hataki kuwachia wafungwa waende nyumbani?'
\s5
\v 18 Wafalme wote wamataifa, wote kwa pamoja wamelala chini kwa heshima, kila mtu kwa kaburi lake.
\v 19 Lakini umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lilivyotupwa mbali. Maiti imekufunika kama vazi, na wale wanaochomwa kwa upanga, nani wale washukao mpaka misingi ya shimo.
\v 20 Hautaunganishwa pamoja katika mazishi, kwa sababu umeiharibu nchi yako na kuuwa watu wako. Watoto wa watenda maovu hawatatajwa tena.''
\s5
\v 21 Anda machinjio kwa ajili ya watoto wake, kwa sababu ya uovu wa mababu zao, hivyo basi hawatanyanyuka juu na na kuimiliki aridhi ya nchi iliyojaa miji ya dunia yote.''
\v 22 Nitapanda juu yao''- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi. Nitang'oa jina katika Babeli, uzao, na ukoo''- hili ndilo tamko la Yahwe.
\v 23 Tena nitaifanya nchi hiyo kuwa makao ya bundi, dimbwi la maji, nanitawafagia kwa mfagio wa uharibifu''- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi.
\s5
\v 24 Yahwe wa majeshi ameapa, ''Hakika, kama nilivyodhamiria, itakuwa kama ilivyo; na kama nilivyo kusudia itakuwa:
\v 25 Nitawavunja Waasiria kwa mikono yangu, na kukanyaga milima kwa miguu yangu mwenyewe. Hivyo nira yake itanyanyuliwa juu yao na mzigo juu ya mabega yao.''
\s5
\v 26 Huu ni mpango uliokusudiwa katika nchi yote, na huu ndio mkono ulionyanyuliwa juu ya mataifa.
\v 27 Kwa maana Yahwe wa majeshi amepanga hivi; ni nani atakayemzia yeye? Mkono wake umenyanyuliwa juu, ni nani atakajemrudisha nyuma?
\s5
\v 28 Katika miaka ambayo mfalme Ahazi alipokufa, hili ndio tamko lilokuja:
\v 29 Msishangilie, enyi wafilisti wote, kwamba fimbo ya kukupigia wewe imevunjika. Maana katika njia ya nyoka atatoka fira, na watoto wake watakuwa moto nyoka wanaopaa.
\v 30 Na mtoto wa kwanza wa maskini watachunga kondoo wao kwenye malisho yangu, na wahitaji watalala chini salama. Nitaiuwa mizizi yenu kwa njaa ambayo atawauwa wakazi wenu wote.
\s5
\v 31 Omboleza, ewe lang, lia, ewe mji; ninyi nyote mtayeyukia mbali, Ufilisti. Maana kutoka kaskazini limetoka wingu la moshi, na hakuna hata mmoja atakaye odoka kwenye nafasi yake.
\v 32 Ni kivipi mtu mmoja atamjibu mjumbe wa taifa? Kwamba Yahwe ameipata Sayuni, na ndani yake walionewa watatafuta kimbilio.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Tamko kuhusu Moabu, Kweli, kwa usiku mmoja Ari ya Moabu imeharibiwa kabisa na kuangamizwa; kweli, kwa usiku mmoja Kira ya Moabu itaharibiwa na kuangamizwa.
\v 2 Wamenda juu hekaluni, watu wa Diboni wamenda juu kuomboleza; Moabu wanaomboleza juu ya Nebo na juu ya madeba. Vichwa vyao vimenyolewa viko wazi na na ndevu zao zimenyolewa.
\s5
\v 3 Wamevaa nguo za magunia katka mitaa yao; juu ya dari zao na kila kona ya mitaa yao, kuyeyuka kwa kumwaga machozi.
\v 4 Hishiboni na Elealehi wanalia wakihitaji msaada; Sauti zao zinasikika mpaka Jahazi. Hivyo basi vijana wa vita wa Moabu wanalia wakihitaji msaada; wanatetemeka wao wenyewe.
\s5
\v 5 Moyo wangu unalia juu ya Moabu; watuhumiwa wamekimbilia Zoari na Elgathi Shelishiyahi. Wanapaa juu ya Luhithi wakilia; katika barabara ya kwenda Horonaimu wanapiga kelele ole juu ya uharibifu.
\v 6 Maji ya Nimrimu yamekauka; majani yamepooza na majani yanyochikia yanakufa; hakuna ukijani hata kidogo.
\v 7 Hivyo basi vitu vingi vimekuwa na hifadhi wameipeleka juu ya kijito maarufu.
\s5
\v 8 Kilio kimezunguka katika himaya ya Moabu; malalamiko yamefika hata Eglaimu na Beer-Elimu.
\v 9 Maana maji ya Dimoni imejaa damu; Simba atawavamia wale waliokimbia kutoka Moabu pia na walbakia katika nchi.
\s5
\c 16
\p
\v 1 Mpeleke mwana kondoo kuongoza nchi kutoka Sela huko jangwani, kwenye mlima wa binti Sayuni.
\v 2 Kama ndege wazururao, viota vimetapakaa, hivyo basi wanawake wa Moabu watavuka kwenye mto Arnoni.
\s5
\v 3 Toa maelekezo, tekeleza haki; toa kivuli kama usiku wakati wa mchana; wahifadhi watuhumiwa; msiwahini watuhumiwa.
\v 4 Waache waishi miongoni mwenu, wakimbizi kutoka Moabu; muwe mahali pakujifichia wao wasiangamizwe.'' maana mateso yatakwisha, na uharibifu utapungua utakuwa na kikomo, wale wanotetemeka watapotea katika nchi.
\s5
\v 5 Kiti cha enzi kitaanzishwa katika agano la uaminifu; na mmoja katika hema la Daudi atakaa pale kwa uaminifu. Atahukumu kwa kufuata haki na atatenda haki.
\s5
\v 6 Tumesikia kiburi cha Moabu, kiburi chake, majivuno yake, na hasira yake. Lakini majivuno yake ni maneno tu.
\v 7 Hivyo basi Moabu atalia juu ya Moabu-wote watalia! wataomboleza, nyie mlioharibiwa kabisa, mikate ya Kira Haresethi.
\s5
\v 8 Shamba la Heshboni limekauka kabisa pamoja na mizabibu ya Sibma. Kiongozi wa mataifa amekanyaga mizabibu iliyochaguliwa na kuelekea Jazeri na kuelekea jangwani. Mizizi yake nje ya nchi; imenda juu ya bahari.
\s5
\v 9 Kweli nitalia pamoja Jazeri kwasababu ya shamba la mizabibu la Sibma. Nitakuloanisha kwa machozi yangu, Heshboni, na Eleale. Maana katika mashamba yenu kipindi cha majira ya joto matunda na mazao nitaishia kwa kupiga kelele za furaha.
\v 10 Furaha na shangwe zimezimwa na matunda ya miti ya shambani; na hakuna nyimbo wala kelele katika mashamba ya mizabibu, maana nimeweka mwisho wa kupiga kelele kwa yeyote anayetembea.
\s5
\v 11 Hivyo, moyo wangu unalia kama kinubi, na ndani yangu maana kwa ajili ya Kiri Hareseth.
\v 12 Pindi ambapo Moabu wamejivika mahali pa juu, na kuingia katika hekalu kuomba, maombi yake hayatatimiza chochote.
\s5
\v 13 Haya ndio maneno aliyoyazungumza Yahwe kuhusu Moabu iliyopita.
\v 14 Tena Yahwe amesema, ''Ndani ya miaka mitatu utukufuwa Moabu utatoweka; japo watu wake wengi, watakao bakia ni wachache, na wasionafaida.
\s5
\c 17
\p
\v 1 Tamko kuhusu Damaskasi.
\v 2 Miji ya Aroera itaharibiwa. Patakuwa na nafasi kwa ajili ya kutunzia mifugo, na hakuna hatakayeizuia.
\v 3 Miji ilioachwa itatoweka kutoka Efraimu, ufalme katuka Damskasi, na walobaki Aramu-watakuwa kama utukufu wa watu wa Israeli-Hili ni tamko la Yahwe wa majeshi.
\s5
\v 4 Itakuwa siku hiyo utukufu wa Yakobo utapungua, utakuwa mwembamba na kunona kwa mwili wake utapungua.
\v 5 Itakuwa kama mvuna ikusanyavyo mavuno, na mkono wake huvuna maganda ya mazao. Itakuwa kama mtu atoae maganda ya mavuno katika bonde la Refaimu.
\s5
\v 6 Masalia yataachwa, hata hivyo, mti wa mzabibu utatingishwa: Mizeituni miwili au mitatu iliyo juu sana matawi yake yako juu, manne au matano katka tawi la juu katika mti unaozaa-hili ni tamko la Yahwe, Mungu wa Israeli.
\v 7 Siku hiyo watu watawangalia Muumba wake, na macho yatamuangalia Mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 8 Hawatangalia madhabahu, kazi za mikono yao, wala hataangalia kile kinachofanywa na vidole vyao, nguzo za Ashera na picha ya jua.
\v 9 Siku hiyo miji yenye nguvu itakuwa kama msitu uliotelekezwa na juu ya kilele cha mlima, na palipo achwa kwa sababu ya wana wa Israeli patakuwa ukiwa.
\s5
\v 10 Maana mmemsahau Mungu wa wakovu wenu, na umeudharau mwamba wa nguvu zako. Hivyo basi umeotesha miti mizuri, na mizabibu mizuri iliyotoka ugenini,
\v 11 Siku hiyo uliootesha na fensi na kulima. Mbegu zako zitaota mapema na kukua, lakini mavuno yatashindikana siku hiyo itakuwa huzuni na kukata tamaa.
\s5
\v 12 Ole! Watu wenye ghasia, Kishindo chake ni kama mngurumo wa bahari, na kasi ya mataifa, wananguruma kama ngurumo ya maji mengi!
\v 13 Mataifa yataunguruma kama maji mengi yaendao kasi, lakini Mungu atawakemea.
\v 14 Watakimbia mbali sana na watafukuzwa kama pumba kwenye mlima mbele ya upepo, kama mavumbi yazungukayo kwenye dhoruba. Wakati wa usiku, ona, hofu! Na kabla ya alfajiri watakwenda; hili ndilo eneo la wale waliotupora, na wale wanaotunyang'anya mali zetu.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Ole kwa nchi ya wezi wa mabawa, iliyoko mbali kupitia mito ya Ethiopia;
\v 2 wanowatuma mabalozi wao kwa kupitia bahari, na vyombo vya majani juu ya maji. Nendeni enyi wajumbe wepesi, kwa watu warefu na laini waishio kwenye nchi, kwa watu wanogopa mbali na karibu, taifa lenye nguvu, wakanyagao watu, ambao mito imegawanya nchi yao.
\s5
\v 3 Watu wote wakaao duniani nao wakaao katika nchi, pale ishara itakaponyanyuliwa juu ya milima, angalia; na sikilizeni mbiu itakapopulizwa.
\s5
\v 4 Yahwe asema hivi, ''nitachunguza kimyakimya kutoka nyumbani kwangu, kama kupika joto kwenye jua, na kama ukungu kwenye joto la mavuno.
\v 5 Kabla ya mavuno, pale kipindi cha maua kinapoisha, na maua yako tayari kuwa zabibu. Atakata matawi kwa kupogoa ndoano, na atakatiwa chini na kuchukua matawi yaliyotawanyika.
\s5
\v 6 Wataachwa kwa pamoja maana ndege wa milimani na wanyama wa duniani. Ndege watatua kwao majira ya joto, na wanyama wote watakuwa kwao kipindi cha baridi.''
\v 7 Kwa mda huo kodi italetwa kwa Yahwe wa majeshi kwa watu warefu na laini, kwa watu wanohofia umbali na ukaribu, taifa imara na kukanyagwa chini, ambayo nchi yao imegawanjwa na mito, Kwa sehemu ya jina la Yahwe wa majeshi, mpaka mlima Sayuni.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Tamko kuhusu Misri. Ona, Yahwe atasafiri katika mawimbi mepesi na anakuja Misri; Sanamu za Misri zitatemeka mbele yake, na mioyo ya Wamisri itayeyuka ndani yao wenyewe.
\v 2 Nitawachanganya Wamisri juu dhidi ya Wamisiri: Mtu atapigana dhidi ya ndugu yake, mji dhidi ya miji, na ufalme dhidi ya ufalme.
\s5
\v 3 Roho ya Misri itadhohofishwa kutoka ndani. Nitauharibu ushauri wake, japo wanafikiria ushauri wa sanamu, roho za watu waliokufa, na mizimu, na
\v 4 Nitawacha Wamisiri kwenye mikono ya viongozi wakatili, kiongozi imara atawaongoza wao- Hili ni tamko la Yahwe Bwana wa majehi.''
\s5
\v 5 Maji ya bahari yatakauka juu, na mto uakauka na kuwa mtupu.
\v 6 Mito itakuwa michafu; mikondo ya Misri itakuwa dhii na kukauka; mwanzi na bendera zake zitapeperushwa mbali.
\s5
\v 7 Mianzi ya Nile, kwa mdomo wa mto Nile, na mbegu zote zitakazo katika mashamba ya Nilezitakauka zote, zitageuka kuwa mavumbi, na kupeperukia mbali.
\v 8 Wavuvi watalia na kuomboleza, na wale watakao shusha neti kwenye maji watauzunika.
\s5
\v 9 Wafanyakazi ya kuchana kitani watafaidika na hao washonao nguo nyeupe watajeuka kuwa mchonaji.
\v 10 Washona nguo wa Misri wataangamizwa; na wote waloajiriwa watahuzunika nafsini mwao.
\s5
\v 11 Wakuu wa Zoana ni wajinga kabisa. Washauri wenye busara wa Farao ni wapumbavu. Unawezaje kumwambia Farao, ''Mimi ni mtoto wa watu wenye busara,
\v 12 ''Wako wapi hao watu wenye busara? mtoto wa mfalme wa zamani? Waache wakuambie? na ijulikane kitu ambacho Yahwe wa majeshi amekipanga kuhusiana na Misri.
\s5
\v 13 Wakuu wa Zoani wamekuwa wajinga, wakuu wa Memphisi wamegawanyika; wameifanya Misri iende kinyume, na mawe ya pembeni ya makabila yao.
\v 14 Yahwe amechanganya roho wa kuvurugwa katika yao, na wamefanya Wamisri kwenda kinyume kwa yote wanoyafanya, kama mlevi anavyoyumbayumba uku akitapika.
\v 15 Hakuna kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukifanya kwa ajili ya Misri, kama kichwa au mkia, tawi au mwanzi.
\s5
\v 16 Siku hiyo, Wamisri watakuwa kama wanawake. watatemeka na kuogopa mkono wa Yahwe wa majeshi ulioinuliwa juu yao.
\v 17 Nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri. Yeyote atakao wakumbusha wao kuhusu yeye, wataogopa sana, kwa sababu ya mpango wa Yahwe, anaoukusudia juu yao.
\s5
\v 18 Siku hiyo kutakuwa na miji mitano katika nchi ya Misri wanaozungumza lugha ya Kanaani na kuapa kimtii Yahwe wa majeshi. Moja kati ya miji hii itaitwa mji wa ulioharibiwa.
\s5
\v 19 Siku hiyo kutakuwa madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika ya nchi ya Misri, na jiwe la chumvi karibu na Yahwe.
\v 20 Itakuwa kama ishara na ushahidi kwa Yahwe wa majeshi katika nchi ya Misri. Atawatumia mkombozi na mlinzi, na atawokoa wao.
\s5
\v 21 Yahwe atajulikana Misri, na Wamisri watamkubali Yahwe siku hiyo. Watamuabudu kwa sadaka na matoleo, na wataweka agano na kulitimiza.
\v 22 Yahwe ataipga Misri, ataipiga na kuiponya. Halafu watamrudia Yahwe; atasikiliza maombi yao na kuwaponya.
\s5
\v 23 Siku hiyo kutakuwa na njia kuu kutoka Misri kwenda Asiria, na Waasira watakuja Misri, na Wamisri watakwenda Asira; na Wamisri wataabudu pamoja na Waasiria.
\s5
\v 24 Siku hiyo, Israeli itakuwa ya tatu pamoja na Misri na Asiria, baraka katikati ya nchi;
\v 25 Yahwe wa majeshi atawabariki na kusema, '' wabarikiwe Wamisri, watu wangu; Wasiria, kazi ya mikono yangu; na Israeli urithi wangu.
\s5
\c 20
\p
\v 1 Katika mwaka ambao Tartani alipofika kwa Ashdodi, alipotumwa na Sarjoni mfalme wa Asiria, nae akapigana na Ashdodd na akachukua.
\v 2 Mda huo Yahwe alizungumza na Isaya mwana wa Amozi, ''Nenda ukaondoe nguo za magunia katika kiuno chako, na ondoeni viatu vyenu kwenye miguu.'' Alifanya hivyo, tembeeni uchi na miguu wazi.
\s5
\v 3 Yahwe asema, ''Kama ilivyokuwa kwa mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na pasipo kuvaa viatu kwa miaka mitatu, ni ishara na dalili kuhusu Misri na kuhusu Ethiopia---
\v 4 katika njia hii mfalme wa Asiria atawaongoza mateka wa Misri, na walioko uhamishoni Ethiopia, watoto kwa wazee, waliouchi na wasio na viatu, na ambao hawajajisitiri kuiweka Misri katika aibu.
\s5
\v 5 Watafadhaika na kuona aibu, kwa sababu ya Ethiopia ni matumaini yao na Misri ni utukufu wao.
\v 6 Wenyeji wa pwani hiiwatasema siku hiyo, 'Kweli, hichi ndicho chanzo chetu cha matumaini, tulipokimbilia kuhitaji msaada kutoka kwa mfalme wa Asiria, je ni kwa jisi gani tunaweza kupona?''
\s5
\c 21
\p
\v 1 Tamko kuhusu jangwa pembezoni mwa bahari. Kama dhuruba yenye upepo inayotokea kupita Negevi kuelekea jangwani, kutoka kwenye aridhi ya kutisha.
\v 2 Nimepewa maono ya kusikitisha: Wasaliti wamepanga hila, na waharibifu kuharibu. Nenda juu na uvamie, Elamu; zingira Media; Mimi nitasimamisha maumivu yao yote.
\s5
\v 3 Hivyo basi simba wangu wamejawa na maumivu; ni kama mwanamke anayejifungua kwa uchungu yamenipata mimi; Nimeina chini kwa kile nilichokisikia; nimesumbuliwa kwa kile nilichokiona.
\v 4 Moyo wangu unajinga, nimetitishika kwa hofu. Mapema jioni, mda wangu mzuri kwa siku, imeniletea hofu.
\s5
\v 5 Wameandaa meza, wametawanya vitambaa, na wanakula na kunjwa; tokea, mkuu, pakeni ngao yenu kwa mafuta.
\s5
\v 6 Hiili ndilo Bwana aliloniambia, ''Nenda, baada ya mlinzi; lazima atoe taarifa kwa kile atakacho kiona.
\v 7 Kama ataona gari, jozi ya farasi, farasi juu ya punda na farasi juu ya ngamia, hivyo basi anatakiwa kuwa makini na kuwa macho.''
\s5
\v 8 Mlinzi analia nje, ''Bwana, ninasimama juu ya mnara siku zote, kila siku, na kwa nguzo yangu nitasimama usiku wote.''
\v 9 Tazama gari linakuja na wakiwa wawili wawili. anaita, ''Babeli umeanguka, umeanguka, na sanamu za kuchonga za miungu yao zimevunjika chini.''
\s5
\v 10 Watu wangu niliwapururu na kuwapepeta, watoto niliyewatoa kwenye sakafu yangu mwenyeweNilichokisikia kutoka kwa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, Nimekutangazia wewe.
\s5
\v 11 Tamko kuhusu Duma. Mtu mmoja amenita mimi kutoka Seiri, ''Mlinzi, ni kitu gani kilichobakizwa usiku?
\v 12 Mlinzi akasema, ''Asubuhi itafika na vilevile usiku. Ikiwa unataka kuuliza basi uliza; na urudi tena.''
\s5
\v 13 Tamko kuhusu Arabia. Katika jangwa la Arabia mmeutumia usiku, enyi misafara ya Dedanite.
\v 14 Leteni maji kwa wenye kiu; wenyeji wa nchi ya Tema, waoneni watuhumiwa kwa mikate.
\v 15 Maana wameukimbia upanga, kutoka upanga unaotolewa, kutoka kwenye upinde ulopinda, na kutokana na uzito wa vita.
\s5
\v 16 Maana hili ndilo Bwana alichosema na mimi, ''Ndani ya mwaka mmoja, kama mtu aliyeajiriwa kwa mwaka ataona, utukufu wa Kedari utakwisha.
\v 17 Ni baadhi ya ya wavuta upinde, mashujaa wa Kader watabakia,'' maana Bwana, Mungu wa Israeli, amesema.
\s5
\c 22
\p
\v 1 Tamko kuhusu bonde la maono:
\v 2 Mji wenye kelele, mji umejaa maovu; wafu hawajauwawa kwa upanga, na hawakuuwawa kwenye vita.
\s5
\v 3 Viongozi wenu wamekimbia pamoja, lakini wamekamatwa pasipo na upinde, wote kwa pamoja wamekamatwa na wamekamatwa pamoja; walikimbia kutoka mbali.
\v 4 Hivyo basi, Msiniangalie mimi, nitalia kwa uchungu; msijaribu kunifariji kuhusiana na kuharibika kwa binti ya watu wangu.
\s5
\v 5 Maana kuna siku za ghasia, akanyagaye chini, na fujo za Bwana, Yahwe wa majeshi, katika bonge la maono, kuanguka chini kwa ukuta, na watu wanalia juu ya milima.
\v 6 Elamu chukua podo juu, na gari la watu na farasi, na kirghizameweka ngao wazi.
\v 7 Siku hiyo ambapo mabonde ulioyachagua yatajaa magari, na farasi watachukua nafasi zao katika lango.
\s5
\v 8 Atauodoa mbali ulinzi wa Yuda; na utaona siku hiyo utaona silaha katika jumba la msitu.
\v 9 Umeona matawi ya mji wa Daudi, jinsi mlivyowengi, na kukusanya maji katika birika la chini.
\s5
\v 10 Umehesabu nyumba za Yerusalemu, na umerarua nyumba chini kuuimarish ukuta.
\v 11 Na umefanya hifadhi katika ya kuta mbili maana maji ya birika la zamani. Maana haukuwahusisha walioujenga mji, walioupanga mji kutoka zamani.
\s5
\v 12 Bwana, Yahwe wa majeshi amewaita siku hiyo watu waje kuomboleza na kulia, wanyoe vichwa vyao na kuvaa nguo za magunia.
\v 13 Lakini angalia, badala yake sherehe na furaha, kuuwa ng'ombe na kuchinga kondoo, njooni tule na kunjwa mvinjo maana kesho tutakufa.
\v 14 Hili limebanika kwenye masikio yangu na Yahwe wa majeshi: Hakika maovu haya hayatasamehewa, hata utakapokufa, ''Amesema Bwana wa majeshi.
\s5
\v 15 Bwana, Yahwe wa majeshi, asema hivi, ''Nenda kwa huyu kiongozi, kwa Shebana, aliye juu ya nyumba, na umwambie,
\v 16 Ni nina aliyekuruhusu kuchimba kaburi lako mwenyewe, kukata juu ya kaburi na juu ya urefu katika mahali pa kupunzikia ndani mwamba?''
\s5
\v 17 Yahwe anakaribia kukutupa chini; mtu mwenye nguvu, anakaribia kukutupa chini; atakuzongazonga.
\v 18 Atahakikisha anatuzungusha zungusha, na kutupa msukosuko kama mpira kwenye nchi kubwa. Pale utakapokufa, na pale gari lako tukufu litakapo kuwa; utakuwa aibu ya nyumba ya bwana wako!
\v 19 ''Nami nitakuondoa katika ofisi yako na katika kituo chako. Na utavutwa chini.
\s5
\v 20 Na itakuwa hivi kuhusu siku hiyo nitamchukua Eliakimu mtoto wa Hilkia mtumishi wangu.
\v 21 Nitamvisha yeye kwa kanzu yenu na kumvika mkanda wenu, na nitahamisha mamlaka yenu kwenye mikono yake. Atakuwa baba wa wenyeji wa Yerusalemu na katika nyumba ya Yuda.
\v 22 Nitaziweka funguo za nyumba ya Daudi kwenye mabega yake; Atafungua, na hakuna atakayefunga; na atafunga na hakuna atakayefungua.
\s5
\v 23 Nami nitamuimarisha yeye, kigingi katika mahali salama, na atakuwa kiti cha utukufu katika nyumba ya baba yake.
\v 24 Nao wataangukia juu yake utukufu wote wa baba nyumba ya baba yake, watoto wake na uzao wake na kila chombo kidogo kutoka vikombe mpaka majagi yote.
\s5
\v 25 Siku hiyo- hili ndilo tamko la Yahwe wa majeshi- kigingi kilichowekwa katika mazingira imara kitatoa njia, utavunjika, na kuanguka, na uzito ulionao utaondoleawa- maana Yahwe amesema.
\s5
\c 23
\p
\v 1 Tamko kuhusu Tiro, Ombolezeni, enyi kondoo wa Tarishishi;
\v 2 maana hakuna nyumba wala bandari; kutoka katika nchi ya Kyprusi wamefunuliwa hilo.
\v 3 Na juu ya maji mengi ni nafaka za shiho, mazao ya Nile, na uzalishaji wao; mlikuwa wafanya biashara wa kimataifa.
\s5
\v 4 Kuwa na aibu, Sidoni; maana bahari imenena, mkuu wa bahari. Amesema, ''Sijafanya kazi wala kuzaa wala kukuza vijana wadogo wala kuwalea mabinti.
\v 5 ''Pale taarifa ilipofika Misri, watauzunika kuhusu Tire.
\s5
\v 6 Katiza juu ya Tarshishi; Ole wenu, enyi wakazi wa pwani.
\v 7 Je hili limeshawahi kuwatokea, mji wenye furaha, ambao kwa asili yake umetoka katika kipindi cha kale. Ambapo miguu yake imempeleka mbali kuishi kwenye maeneo ya ugenini?
\s5
\v 8 Ni nani aliyepanga haya dhidi ya Tire, mtoa mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wakuu, ambao wafanyabiashara ni watu wa kuheshimika duniani?
\v 9 Yahwe wa majeshi amepanga kuharibu kiburi chake na utukufu wake, na kuwahaibisha waheshimiwa wote wa dunia.
\s5
\v 10 Lima katika shamba lako, kama mtu alimavyo Nile, ewe binti Tarishishi. Maana hakuna tena eneo la soko huko Tite.
\v 11 Yahwe amenyoosha mkono wake juu ya bahari, na ametingisha falme; na amepewa amri juu ya Fonensia, kuziharibu ngome.
\v 12 Amesema, ''Hamtofurahia tena, binti bikira wa Sidoni uliyenyanyasika; nyanyuka, pitia Kyprusi; lakini wala hapatakuwa na punziko.''
\s5
\v 13 Tazama nchi ya Wakaldayo. Hawa watu wamesitisha kuishi pale; Waasiria wamelifanya jangwa la wanyama pori. Wameizingira minara; wameliharibu eneo lao; wamelifanya kuwa chungu cha uharibifu.
\v 14 Omboleza ewe kondoo wa Tarishishi; maana kimbilio lako limeharibiwa.
\s5
\v 15 Katika siku hiyo, Tire itasaulika kwa miaka sabini, kama siku za mfalme. Baada ya miaka sabini kuisha huko Tire kutatokea kitu kama wimbo wa malaya.
\v 16 Chukua kinubi, nenda zunguka mji, mmewasahau malaya; cheza kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili uweze kukumbuka.
\s5
\v 17 Itatokea baada ya miaka sabini, Yahwe ataisaidia Tire, na wataanza kututafuta pesa tena kwa kufanya kazi ya umalaya, na atafanya utumishi wake katika falme za dunia.
\v 18 Faida yake na mapato yake yatatengwa kwa ajili ya Yahwe. Hayatahifadhiwa wala hayatakuwa na hazina, maana faida yao watapewa wale wanoishi mdhebauni mwa Yahwe na yatatumika kuwasambazia chakula cha kutosha na kupata mavazi yenye viwango bora.
\s5
\c 24
\p
\v 1 Angalia Yahwe anakaribia kuifanya dunia kuwa utupu, kuhiharibu, kuharibu uso wake, na kuwatawanya wenyeji wake.
\v 2 Itakuwa kama ilivyo kwa watu itakuwa hivyo hivyo kwa kuhani; na kwa watumishi na kwa bwana wake, na kwa mfanyakazi wa ndani itakuwa hivyo na kwa tajiri yake, ndivyo itakavyokuwa kwa anayeuza na anayenunua; ndivyo itakavyokwa kwa wenye kupata faida na wenye madeni, na wale wennye kupokea faida itakuwa hivyo hivyo kwa wale wenye kutoa faida.
\s5
\v 3 Dunia itaharibiwa kabisa na kufanjwa ukiwa; maana Yahwe amenena maneno hayo. Dunia imekauka kabisa na kunyauka,
\v 4 Dunia inazimia n kudhohofika. Watu maarufu wa duniani watapotezwa.
\v 5 Dunia inavutwa na watu wakao ndani yake kwa sababu wamepindisha sheria, wameibadili amri na wamevunja agano la milele.
\s5
\v 6 Hivyo basi laana inaitafuna nchi, na wenyeji wake wamekutwa na makosa. Wakaao duniani wanateketea, na watu wachache wameachwa.
\v 7 Divai mpya imekauka, mizabibu imenyauka, na mioyo yote iliyochangamka inaugua.
\s5
\v 8 Sauti ya furha ya kigoma inasimama, na kelele za wenye furaha zimekwisha, na furaha ya kinubi imesitishwa.
\v 9 Hawatakunjwa mvinyo tena na kuimba, bia chungu kwa wale wanokunywa.
\s5
\v 10 Mji uliochafuka umeangushwa chini; kila nyumba imefungwa na hakuna kitu.
\v 11 Kuna kilio mtaani kwa sababu ya mvinyo; furaha yote imetiwa giza, furaha ya nchi imetoweka.
\s5
\v 12 Ndani ya mji kumebaki ukiwa, na lango limebolewa kwa uharibifu.
\v 13 Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa dunia yote mwiongoni mwa mataifa, pale mti wa mzabibu utakapopigwa, na waokotapo zabibu baada mavuno yake kuwa tayari.
\s5
\v 14 Watanyanyua saut zao na kupiga keleleYahwe mwenye enzi, na utapaza sauti kutoka kwenye bahari.
\v 15 Hivyo basi mashariki mtukuze Yahwe, na katika kisiwa cha bahari tukuzeni jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
\s5
\v 16 Kutoka umbali wa sehemu ya dunia tumesika nyimbo, ''Utukufu kwa watu wenye haki! Lakini nikasema, ''Nimepita mbali, Ole juu wangu! Wasaliti walshulika na wenye hila; ndio, wasaliti walishuhulika na wenye hila.''
\s5
\v 17 Hofu, shimo, na mtego yako juu yako, wenyeji wa dunia.
\v 18 Amekimbia maana sauti ya hofu itaanguka kwenye shimo, na anayekuja juu katikati ya shimo atanaswa na mtego. Madirisha ya mbinguni yatafunguliwa, na misingi ya dunia itatikisika.
\s5
\v 19 Dunia itangamizwa kabisa, dunia itapasukia mbali; dunia itatatikisika vikali.
\v 20 Dunia itajikongoja kama mlevi na itachezacheza kurudi nyuma na mbele kama kibanda. Dhambi zao zitakuwa nzito juu yao na zitaanguka na hazitasimama tena.
\s5
\v 21 Itakuwa siku hiyo ambayo Yahwe ataliadhibu jeshi la aliye juu mahali pa juu, na falme za dunia katika dunia.
\v 22 Watakusanyika pamoja, wafungwa katika shimo, na watafungw gerezani; na baada ya siku nying watadhibiwa.
\v 23 Halafu Mwenzi utatiwa aibu na jua pia litatwa aibu, maana Yahwe wa majeshi atatawala katika mlima Sayuni na Yerusalemu, kabla ya wazee wake katika utukufu.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Yahwe wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe, nitalisifu jina lako; maana umetenda matendo ya ajabu, mambo uliyoyapanga toka zamaini, kwa uaminifu na ukamilifu.
\v 2 Maana umeufanya mji kuwa chungu, ngome ya mji, uharibifu na ngome ya wageni kuwa si mji.
\v 3 Hivyo basi watu wenye nguvu watakutukuza wewe; na mji waishio watu wasio na ukatili watakuogopa wewe.
\s5
\v 4 Maana umekuwa katika eneo salama kwa aliye masikni, makazi kwa mhitaji ambaye yuko kwenye dhiki- makazi kwa aliyeko kwenye dhoruba na kivuli kwa aliyeko kwenye jua. Pale punzi ya watu wakatili imekuwa kama dhoruba dhidi ya ukuta,
\v 5 na jua kwenye aridhi kavu, na watazuia kelele za wageni, kama vile jua linavyozuiliwa na kivuli cha mawingu, hivyo basi nyimbo wasio na makosa zimejibiwa.
\s5
\v 6 Katika mlima huu Yahwe wa majeshi atafanya kwa watu sikukuu ya ya vitu vilivyonona, na mvinyo uliochaguliwa, zabuni ya nyama na sikuku juu ya sira.
\v 7 Na katika mlima huu atauharibu mfuniko uliowekwa juu watu wote, na mtandao wa kusuka juu ya mataifa.
\v 8 Atameza kifo daima, na Bwana Yahwe atayafuta machozi katika nyuso zetu; na aibu ya watu wake itatupwa mbali kutoka duniani kote, maana Yahwe amesema hivyo.
\s5
\v 9 Yatazungumzwa katika siku hiyo, ''Huyu ni Mungu wetu; na tunayemngoja, na atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tuliyemngoja, tutafurahia na kushangilia wokovu wake.''
\v 10 Maana katika mlima huu mkono wa Bwana utashuka; na Moabu itakanyagwakangwa chini kwenye eneo lake, na hata majani yatakanyagwakanyagwa chini katika shimo lililojaa mbolea.
\s5
\v 11 Wataitawnya mikono yao katikati yao, kama vile mpiga mbizi atawanyavyo mikono yake wakati akipiga mbizi. Lakini Bwana atashusha kiburi chao chini japo kuwa na ujuzi katika mikono yao.
\v 12 Na ataiangusha chini kwenye aridhi kuta za ngome, kwenye mavumbi.
\s5
\c 26
\p
\v 1 Siku hiyo wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji imara; Mungu amefanya wokovu katika kuta na ngome zake.
\v 2 Fungua lango, ili mataifa yenye haki yaweze na yenye kutunza imani yaweze kuingia ndani.
\s5
\v 3 Akili mlionayo, mtamuhifadhi yeye katika amani kamili, maana anawamini ninyi.
\v 4 Mwamini Yahwe daima; maana Yaha, Yahwe, ni mwamba wa milele.
\s5
\v 5 Maana atawashusha wale wote wenye kiburi; mji ulio juu atushusha chini, ataushusha chini kwenye aridhi; na ataulinganisha na mavumbi.
\v 6 Utakanyagwakanyagwa chini na miguu ya walio masikini na wahitaji.
\s5
\v 7 Mapito ya mwenye haki yamenyooka, Wenye haki; mapito ya wenye haki umeyanyoosha.
\v 8 Ndio, kaika mapito ya hukumu yako, Yahwe, tunakusubiri wewe; jina lako na sifa zako ni matamanio yetu.
\v 9 Nimekutamani wewe wakati wa usiku; ndio, roho iliyo ndani yangu ina kutafuta kwa bidii. Pindi hukumu yako itakapokuja duniani, wenyeji wa duniani watajua kuhusu haki.
\s5
\v 10 Na tuonyeshe upendeleo kwa waovu, lakini hawatajifunza haki. katika nchi ya wanyofu anatenda maovu na haoni ukuu wa Yahwe.
\s5
\v 11 Yahwe, mkono wako umenyanyuliwa juu, lakini hawapati hizo taarifa. Lakini wataona bidii kwa watu na wataona aibu, kwa sababu idadi ya maadui watawatafuna.
\v 12 Yahwe, utaleta amani kwetu, maana kweli, umekamilisha kazi zetu zote.
\s5
\v 13 Yahwe Mungu wetu, viongozi wengine badala yako wametutawala sisi; Lakini tunalitukuza jina lako.
\v 14 Wamekufa, hawataishi tena; ni maremu hao, hawatafufuka tena. Kweli, umekuja kuwahukumu na kuwaharibu wao, na umefanya kila kumbukumbu kutoweka.
\s5
\v 15 Umeliongeza taifa, Yahwe, umeliongeza taifa; umeheshimiwa; umeinuliwa katika mipaka yote ya nchi.
\s5
\v 16 Yahwe, katika mateso yao walikuangalia wewe; walipatwa na wasiwasi katika maombi yao maana adhabu yako ilikuwa juu yao.
\v 17 Kama mwanamke mjamzito anayekaribia kujifungua, hupatwa na uchungu na hulia kwa uchungu, hivyo ndivyo tulivyokuwa kabla, Bwana.
\s5
\v 18 Tulikuwa wajawazito, tumekuwa katika mateso, lakini ni kama tumeshajifungua katika akili zetu. Hatujauleta wokovu duniani, na wakazi wa duniani hawakuanguka.
\s5
\v 19 Wafu wenu wataishi; watu wenu walio kufa watafufuka. Amka na uimbe kwa furaha, njie muishio mavumbini; maana umande wenu ni umande wa mwanga, na dunia itawaleta mbele wafu wake.
\s5
\v 20 Enendeni, watu wangu, ingieni katika vyumba vyenu na mfunge mlango nyuma yenu; jificheni kwa mda mfupi, mpaka hasira itakapopita.
\v 21 Maana, angalia, Yahwe anakaribia kutoka katika eneo lake kuwahadhibu watu waishio duniani kwa ajili ya makosa yao; dunia itaachia umwagaji wa damu, na hawatawaficha tena waliokufa.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Katika siku hiyo Yahwe kwa upanga wake ulio mgumu, mkubwa na mkali, atamadhibu Leviathani na nyoka yule anayetambaa kwa kupenya, na atamuua mnyama anayeishi baharini.
\v 2 Siku hiyo: Shamba la zabibu, litawaimbia.
\v 3 ''Mimi Yahwe ni mlinzi wake; Ninalimwagia maji kila wakati; hivyo hakuna anayelimiza, Ninalilinda usiku na mchana.
\s5
\v 4 Sina hasira, Oh, kama mbigiri na miiba! Katika vita nitatembea dhidi yao; Nitawachoma wote kwa pamoja;
\v 5 labda wafahamu ulinzi wangu na wafanye amani na mimi, waache wafanye amani na mimi.
\s5
\v 6 Kwa siku inayokuja, Yakobo atachukua mzizi; Israeli itatoa maua na kuchipua; na itaijaza aridhi yote kwa matunda.''
\s5
\v 7 Je Yahwe alimshambulia Yakobo na Israeli na hayo mataifa yaliyomshambulia? Je Yakobo na Israeli waliuliwa na wao kama mliowachinja katika mataifa mliowauwa wao?
\v 8 Kitika kipimo halisi cha kuridhisha, watume Yakobo na Israeli mbali; aliwaondosha mbali kwa upepo mkali, katika siku ya upepo wa mashariki.
\s5
\v 9 Hivyo kwa njia hii, maovu ya Yakobo yatalipiwa, maana hii itakuwa matunda yote yakuomdolewa dhambi zake: pale atakapofanya mathebau ya mawe kama chokaa na kuviangamiza katika vipande vipande, na hakuna nguzo za Ashera au madhebau itakayoachwa imesimama.
\s5
\v 10 Maana mji imara umeharibiwa, makao yake na faragha yake yameachwa kama jangwa. Kuna ndama wanachungwa, na huko ndiko atakapo lala na kuyala matawi yake.
\v 11 Matawi yake yatakaponyauka yatanguka. Wanawake watakuja na kuyatumia kutengeneza moto, maana hawa sio watu waelewa. Hivyo basi Muumba wao hatakuwa na huruma juu yao, na yeye aliyewaumba atakuwa na huruma juu yao.
\s5
\v 12 Na siku hiyo itakuwa kwamba Yahwe atapururua kutoka mto Efrate mpaka Wadi ya Misri na njie, watu wa Israeli, tutakusanyika mahali pamoja mmoja mmoja.
\v 13 Siku hiyo tarumbeta kubwa litapulizwa; na watu waliopotea katika nchi ya Asiria watakuja, na waliotupwa katika nchi ya Misri, watamuabudu Yahwe katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
\s5
\c 28
\p
\v 1 Ole kwa taji la kiburi ambalo huvaliwa na kila mlevi wa Efraimu, na ua linalofifia la utukufu wa uzuri wake, ua lililowekwa kichwani mwa bonde linalostawi na hao wanoshindwa na nvinyo!
\v 2 Tazama Bwana anamtuma aliye hodari na nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo mkali unaoharibu, na atatupa kila taji la ua chini kwenye aridhi.
\s5
\v 3 Taji ya kiburi ya walevi wa Efraimu lililoko chini ya paa.
\v 4 Ua lililofifia la utukufu wa uzuri wake, juu ya kichwa cha bonde la utajiri, itakuwa kama tunda lililoiva mtini kabla ya maji yake, kwamba, wakati mtu anapoliona tunda, wakati likiwa bado mikononi mwake, analigugumia chini.
\s5
\v 5 Katika siku hiyo Yahwe wa majeshi atakuwa taji nzuri na taji ya uzuri kwa watu wake waliobakia,
\v 6 roho ya haki kwa yeye aliyekaa katika hukumu, nguvu kwa wale waliobadilisha adui zao katika malango yao.
\s5
\v 7 Lakini wale wanaoyumbayumba kwa ajili ya mvinyo, na wanojikongoja kwa ajili ya pombe kali. Kuhani na nabii watayumbayuma kwa ajili ya pombe kali, na watamezwa na mvinjo. Watajikongoja kwa ajili ya pombe kali, Kujikongoja katika maono na kuyumbayuma katika maamuzi.
\v 8 Hakika, meza zote zimejaa matapishi. Hivyo basi hakuna sehemu iliyosafi.
\s5
\v 9 Ni nani atakaye tufundisha maarifa, na nani atayetuelezea ujumbe? Kwa walioachishwa maziwa au kwa wanonyonya?
\v 10 Maana ni amri juu ya amri, utawala juu ya utawala; na hapa kidogo na pale kidogo.
\s5
\v 11 Kweli, kwa mdomo wa dharau na lugha za kigeni atazungumza na watu wake.
\v 12 Wakati uliopita aliwambia, '''Hawa ni wengine, wape punziko walio choka; maana huku ni kujifurahisha,'' lakini hawakusikiliza.
\s5
\v 13 Hivyo basi neno la Yahwe litakuwa kwao amri juu ya amri, amri juu ya amri, utawala juu ya utawala; na kidogo hapa na kidogo pale, ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, kutegwa, na kukamatwa.
\s5
\v 14 Hivyo basi sikiliza neno la Yahwe, yeyote afaanyae maskhara, wewe unaowaongoza watu hawa ambao wako Yerusalemu.
\v 15 Hii itatokea kwa sababu umesema, '' Tumefannya magano na kifo; maana kuzimu wameyafikia makubaliano. Hivyo basi hukumu itakapopitishwa kwa wingi, haitatufika sisi, maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, na uongo kuwa makazi yetu.
\s5
\v 16 Hivyo basi Bwana Yahwe asema hivi, ''Ona: Nitaiwekea Sayuni msingi wa mawe, jiwe la kujaribu, jiwe la pembeni lenye samani, msingi wa uhakika. Na yeyote atayeuamini ataaibika kamwe.
\s5
\v 17 Nitafanya haki kuwa fimbo ya usawa, na kuwa haki pima maji. Atasafishia mbali kimbilio la waongo, na mafuriko yatajaa balaa katika mahali pa siri.
\s5
\v 18 Agano lako na kifo litafutwa, na makubaliano yako na kuzimu hayatasimama. Pindi mafuriko makali yatapta, yatawazomba njie.
\v 19 Maana pindi yatakopita, yatawazomba nyie yatapita asubuhi na asubuhi, na yatapita tena mchana na usiku utafika. Pale ujumbe utakapofika utasababisha hofu.
\s5
\v 20 Maana kitanda ni kifupi kwa mtu kunyoosha mkono wake nje, na blangeti ni jembamba kwa yeye kujizungushia ndani''
\v 21 Yahwe atanyanyuka kama mlima Perazimu; Atawahimiza yeye mwenye kufanya kazi yake katika bonde la Gibeoni, kazi ya ajabu, na kufanya matendo ya ajabu.
\s5
\v 22 Hivyo sasa msifanye maskhara, dhamana yako itakazwa, Nimesikia kutoka kwa Bwana, Yahwe wa majeshi, amri ya kuiharibu nchi.
\s5
\v 23 Kuwa tayari na sikiliza saut yangu; kuwa makini na sikiliza maneno yangu.
\v 24 Je mkulima anayelima siku zote kwa ajili ya kupanda, analima tu kwenye aridhi? Je anaendelea kulima shamba lake pasipo kupanda?
\s5
\v 25 Pindi anapolindaa shamba lake, Je hatawanji jira ya mbegu, anapanda jira, anaweka ngano katika mstari, shairi katika mahali pake, na yameandikw sehemu mbili?
\v 26 Mungu wake amemuelekeza; anamfuundisha yeye kwa busara.
\s5
\v 27 Zaidi ya hayo, jira zile hazipuruliwi kwa chombo kikali; wala gurudumu la kukatia linalozunguka juu ya jira; lakini jira linapigwa kwa fimbo, na jira kwa fimbo.
\v 28 Nafaka ni mwanzo mkate lakini ni laini sana, japo gurudumu la gari lake na farasi wamezitawanya, na farasi wake hawajaiponda ponda.
\s5
\v 29 Haya yanatoka kwa Yahwe wa majeshi, yeye aliye mshauri wa ajabu na na mwenye ubara wa hekima.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Ole kwa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi ameweka kambi! mwaka hadi mwaka unaongezeka; basi tamasha linakaribia kuja.
\v 2 Lakini nitauzingira Arieli, na watalia na kuomboleza; na watakuwa kwangu kama Arieli.
\s5
\v 3 Nitaweka kambi dhidi yako katika mzunguko, nitakuzingira kwa kuweka uzio dhidi yako.
\v 4 Utaletwa chini na utazungumza kutoka chini kwenye aridhi; maongezi yako yatashushwa kutoka mavumbini. Sauti yako itakuwa kama ya pepo kwenye ardhi, na maneno yako yatakuwa dhaifu kutoka mavumbini.
\s5
\v 5 Jeshi la maadui wako watakuwa kama vumbi dogo, na wingi wa wasiotisha utakuwa kama makapi yanayopita. Itatokea mara moja, papo hapo.
\v 6 Yahwe wa majeshi atakuja kwenu kwa radi, tetemeko la aridhi, sauti kubwa, na upepo mkali na dhoruba kali, na mwali wa moto uteketezao.
\s5
\v 7 Itakuwa kama ndoto, maono ya usiku: Jeshi la mataifa yote yatapigana dhidi ya Arieli na ngome zake. Watawavamia yeye na ngome zinazowanyanyasa wao.
\v 8 Itakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula, lakini pindi anapoamka tumbo halina kitu. Itakuwa kama mtu mwenye kiu anayeota anakunywa maji, lakini anapoamka, anazirai, kwa sababu ya kiu na sio kuizima. Ndio, itakavyokuwa idadi kubwa ya wapiganaji dhidi ya Mlima Sayuni.
\s5
\v 9 Shangaeni wenyewe na mjishangae; jifanye kipofu na uwe kipofu! uwe mlevi lakini sio wa mvinyo; yumbayumba lakini sio kwa bia.
\v 10 Maana Yahwe ameachila roho wake katika usingizi wa kina, Ameyafunga macho yako, manabii, na amefunika kichwa chako, waonaji.
\s5
\v 11 Ufunuo wote umekuja kwako kama maneno ya kitabu kilichotiwa muhuri, ambacho watu wanaweza kumpa mtu anayejifunza, na kusema hivi, ''Soma hiki.'' na atasema, ''Siwezi maana imetiwa muhuri.''
\v 12 Kama kitabu kitapewa kwa mtu asiyeweza kusoma, na kumwambia, '''Soma hiki,'' na anasema, ''Siwezi kusoma.''
\s5
\v 13 Bwana asema, ''Watu hawa wananikaribia mimi na kunishimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbalii na mimi. Heshima yao kwangu ni kwa sababu tu ya amri waliofundishwa.
\v 14 Hivyo basi, tazama, Nitaendelea kufanya mambo ya ajabu mwiongoni mwa watu hawa, maajabu baada ya maajabu. Hekima ya wenye busara itatoweka, na uelewa wa watu wenye busara utatokomea.''
\s5
\v 15 Ole wao wale wanaoficha mipango yao kwa Yahwe, na wale ambao matendo yao ni ya giza. Wanasema, ''Nani anayetuona sisi, na ni nani anayetutambua sisi?
\s5
\v 16 Nyie mnaebadilisha vitu juu chini! Je mfinyanzi anaweza kufikiriwa kama udongo, hivyo basi vitu vinavyotengeneza vitasema kuhusu aliyevitengeneza, ''Hajanitengeneza mimi, ''au vitu vinavyotngenezwa viseme kuhusu aliyevitengeneza, Hajaelewa''?
\s5
\v 17 Katika mda mdogo uliobakia, Lebanoni itajeuzwa kuwa shamba, na shamba litakuwa msitu.
\v 18 Siku hiyo viziwi watasikia maneno ya kitabu, na macho ya vipofu yataona katika giza nene.
\v 19 Waliodhulumiwa watafuurahia pamoja na Yahwe, na masikini miongoni mwa watu watafurahia kwa Mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 20 Maana watu wasio katili watakwisha, na wenye dharau watatoweka. Wale wote wanopendakuteda maovu wataondolewa,
\v 21 nani na kwa neno linamfanya mtu kuwa mkosaji. Watamuekea mtego kwa yeye anayeitafuta haki katika geti na kuweka haki chini kwa uongo usio na kitu.
\s5
\v 22 Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu nyumba ya Yakobo- Yahwe aliyemkomboa Ibrahimu, ''Yakobo hataaibika tena, wala uso wake hautabadilika rangi yake.
\v 23 Lakini anapowaona watoto wake, kazi ya mikono yangu, watalitakasa jina langu, Watalitakasa jina langu Mtakatifu wa Yakobo, na wtasimama katika hofu ya Mungu wa Israeli.
\v 24 Wale watakaopotea kiroho watapata uelewa na walalamikaji watajifunza maarifa.''
\s5
\c 30
\p
\v 1 Ole wa watoto waasi, ''Hili ni tamko la Yahwe. ''Wataweka mipango, lakini haitatoka kwangu; wataungana na mataifa mengine, lakini hawakuongozwa na Roho wangu, hivyo wanongeza dhambi baada ya dhambi.
\v 2 Wanapanga kushuka chini Misri, lakini hawajaniomba niwaelekeze. Wanatafuta ulinzi kutoka kwa Farao kuchukua kimbilio katika kivuli cha Misri.
\s5
\v 3 Hivyo basi ulinzi wa Farao utakuwa aibu yenu, na kimbilio lenu katika kivuli cha Misri, kitakuwa udhalilishaji wenu,
\v 4 japo wakuu wako Sayuni, na wajumbe wao wamekuja Hanesi.
\v 5 Watahaibika kwa sababu ya watu ambao hawawezi kuwasaidia, wala kuwa na faida, lakini ni aibu, na fedheha.
\s5
\v 6 Tamko kuhusu mnyama wa Negevi: kupitia kwenye mlango wa mateso na hatari, wa simba jike na simba dume, nyoka na nyoka wa moto aneyepaa, wamebeba utajiri wao kwenye mgongo wa punda, na hazina yao katika mabega ya ngamia, kwa watu ambao hawana msaada kwao.
\v 7 Maana msaada Misri hauna maana; hivyo basi nimemwita Rahabu, aliyekaa bado.
\s5
\v 8 Sasa nenda, andika hili mbele yao juu ya meza, na uyaandike katika kitabu, iliyaifadhiwe kwa mda mrefu kama ushuhuda.
\v 9 Maana ni watu waasi, watoto waongo, watoto ambao hawaskilizi maelekezo ya Yahwe.
\s5
\v 10 Wanawambia waonaji, ''msiangalie; na kwa manabii, ''msitabiri yaliyoyakweli kwetu; zungumza maneno ya kujipendeza kwetu, tabiri udanganyifu. Geukeni katika njia,
\v 11 ondokeni kwenye njia; maana Mtakatifu wa Israeli amesitisha kuongea mbele ya uso wetu.
\s5
\v 12 Hivyo basi mtakatifu wa Israeli asema, ''Kwa sababu umekataa maneno haya na kujifunza ukandamizaji na udanganyifu,
\v 13 hivyo dhambi hii itakuwa kwenu kama kitu kilichovunjika tayari kwa kuanguka, kama kitu katika ukuta mrefu ambao anguko lake linakaribia, papo kwa hapo.''
\s5
\v 14 Atavunja kama chombo cha mfinyanyanzi kivunjavyo, hivyo basi hakitabaki kitu, hivyo hakuna vipande vyovyote vya kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, kuchota maji kisimani.
\s5
\v 15 Maana Bwana Yahwe, Mtakatifu wa Israeli asema hivi, ''Kwa kurudi na kwa kupumzika mtaokolewa; katika utulivu na imani itakuwa ni nguvu zako, Lakini hamkuwa tayari.
\v 16 Amesema, 'Hapana, maana kukimbia kwa farasi; hivyo tutakimbia; tutakimbia kwa kutumia farasi mwepesi; hivyo basi watakaojingiza watakuwa wepesi.
\s5
\v 17 Watu eflu moja watakimbia kwa kumuhofia mtu mmoja; kwa vitisho vya watu watano mtakimbia mpaka mtakuwa kama nguzu ya bendera iliyoko juu ya mlima, au kama bendera kwenye kilima.''
\s5
\v 18 Lakini Bwana anawasubiri ili awape neema yake, Hivyo basi yuko tayari kuwaonyesha huruma. Maana Yahwe na Mungu wa haki; Huwabarikiwe wale wanaomsubiri yeye.
\v 19 Maana watu wataishi Sayuni, na Yerusalemu na hawatalia tena. Hakika atakuwa neema kwenu kwa sauti ya kilio chenu. Atakaposikia tu, atawajibu ninyi.
\s5
\v 20 Kupitia Yahwe tunapata mkate wa shida na maji ya mateso, hata sasa, mwalimu wako hatajifisha mwenyewe tena, lakini utamuona mwalimu wako kwa macho yako mwenyewe.
\v 21 Masikio yako yatasikia maneno yanayosemwa nyuma, Hii ndio njia, pitia hii, ''utakapogeuka upande wa kulia au utakageuka upande wa kushoto.
\s5
\v 22 Mtakinajisi kifuniko chenu mlichokiweka juu ya pesa na dhahabu na kukitupa. Mtakitupa mbali kama hedhi kali, '''utawambia wao, ''Ondokeni hapa.''
\s5
\v 23 Naye atatoa mvua kwanye mbegu zenu mtakapopanda kwenye aridhi, na mkate utakuwa kwa wingi kutoka kwenye aridhi na mazao yatazaa kwa wingi. Katika siku hizo ng'ombe zako zitachungwa katika eneo kubwa.
\v 24 Ng'ombe na punda, wanaolima kwenye aridhi, watakula chakula cha majira kilicho tawnywa kwa koleo na uma.
\s5
\v 25 Juu ya mlima mrefu na juu ya kilima kirefu, kutapitasha vijito na mifereji ya maji, katika siku siku ya machinjio makuu pale minara yote itakapoanguka.
\v 26 Mwanga wa mwenzi utakuwa kama mwanga wa jua, na mwanga wa jua utang'aa mara saba, kama mwanga wa siku saba. Yahwe atakapofunga kuvujwa kwa watu wake na kuyaponya majeraha waliyoyapata.
\s5
\v 27 jina la Yahwe limekuja kutoka sehemu ya mbali, Linawaka kwa hasira yake na katika moshi mnene. Midomo yake imejaa hasira, na lugha yake nia kama moto unaoangamiza.
\v 28 Punzi yake ni kama maji yaliyojaa yanayofika mpaka katikati ya shingo, kwa ajili kuchuja mataifa kwa kuhamasisha uharibifu. Pumzi yake ni mzabuni katika taya za watu wanowasababisha kutangatanga mbali.
\s5
\v 29 Utakuwa na wimbo kama usiku pale sherehe takatifu itakapofanyika, na moyo wenye furaha, pindi mmoja atakopo kwenda na katika mlima wa Yahwe, katika mwamba wa Israeli.
\s5
\v 30 Yahwe atafanya mapambo ya sauti yake inayosikika na atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo na dhouba ya hasira yake na moto uwakao, pamoja na upepo mkubwa, mvua kubwa, na mvua ya mawe.
\s5
\v 31 Maana kwa sauti ya Yahwe, Asiria itanyamazishwa; atahiaribu kwa fimbo.
\v 32 Na kila adhabu iliyochaguliwa amechagua fimbo ambayo Yahwe ataiweka juu yao na wakisidikizwa na mziki wa kigoma na kinubi kama wataanzisha vita na kupgana nao.
\s5
\v 33 Maana sehemu ya kuchoma iliandaliwa toka zamani. kweli, imeandaliwa kwa mfalme, na Mungu amelifanya kuwa na kina na upana. Rundo liko tayari kwa moto na kuni za kutosha. Punzi ya Yahwe, ni kama mkondo kiberiti, na utawsha moto.
\s5
\c 31
\p
\v 1 Ole wao washukao Misri kuomba msaada na kutegemea farasi, kuweka imani katika magari (maana wako wengi) na ( maana faras haziesabiki). Lakini hawausiani na Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Yahwe!
\v 2 Lakini ni mwenye busara, na ataleta maafa na atakanusha maneno yake. Na atakuja juu ya nyumba zitendazo maovu, na dhidi ya wale wanaowasaidia kuteda dhambi.
\s5
\v 3 Misri ni mtu na sio Mungu, ni farasi wa mwili na sio wa roho. Yahwe atakapota nje kwa mkono wake, wote waliowasaidia watakuwa na mashaka, na yeyote atakayesidia atanguka; wote kwa pamoja watatoweka.
\s5
\v 4 Hivi ndivyo Yahwe alivyosema na mimi, '' kama simba, na hata mtoto wa simba, hunguruma juu ya mawindo yake, pale makundi ya wachungaji yanapoita dhidi yake, lakini hatatemeka kwa sauti zao, wala hatakwenda kwa sababu ya kelele zao, hivyo Yahwe wa majeshi atashuka kupigana kwenye mlima Sayuni, katika kilima hicho.
\s5
\v 5 Kama ndege apaavyo, hivyo Yahwe wa majeshi atailinda Yerusalemu; atailinda na kuiokoa kama apitavyo juu na kuilinda.
\v 6 Mrudieni yeye kutoka huyo mliyemgeukia, watu wa Israeli.
\v 7 Maana katika siku hiyo kila mmoja ataondoa miungu ya fedha na miungu ya dhahabu iliyotegenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.
\v 8 Asiria atangamizwa kwa upanga; na upanga usioshikiwa na mtu utumaliza yeye. Ataukimbia upanga, na vijana wake wadogo watafanyishwa kazi ngumu.
\v 9 Na watashindwa kujiani kwa sababu ya hofu, na mkuu wao ataogopa mbele ya bendera ya jeshi la Yahwe.''- Hili ni tamko la Yahwe, ambao moto uko Sayuni na ambayo sufuria ya moto iko Yerusalemu.
\s5
\c 32
\p
\v 1 Tazama, mfalme atatawala kwa haki, wakuu wataongoza kwa haki.
\v 2 Kila mmoja atakuwa kama makazi kutoka kwenye upepo na kimbilio kutoka kwenye dhoruba, kama mifereji kwenye sehemu kavu, kama kivuli kwenye mwamba mkubwa katika nchi iliyochoka.
\v 3 Halafu macho ya waie wanaoona hayataona giza, na masikio ya wale wanosikia yatasikia vizuri.
\s5
\v 4 Wenye upele watafikiria kwa makini kwa uelewa wao, na wenye kigugumizi watazungumza dhahiri na kwa urahisi.
\v 5 Mjinga hataitwa tena muheshimiwa, wala muongo hataitwa mkuu.
\v 6 Maana mjinga anazungumza ujinga, na moyo wake unapanga maovu na matendo ya wasiomcha Mungu, na anaongea mambo mabaya kuhusu Yahwe. Na anawafanya wenye njaa kuwa tupu na wenye kiu kukosa maji
\s5
\v 7 Njia ya muongo ni maovu. Anajua kubuni mipango mibaya ya kuwalagai masikini kwa uongo, na hata kama masikini atazungumza ukweli.
\v 8 Lakini watu wa heshima wanapanga mipango ya kuheshimika; na kwa sabaubau ya matendo ya wenye heshima tuatasimama.
\s5
\v 9 Nyanyukeni juu, enyi wanawake mlio wepesi, na sikilizeni sauti yangu; enyi mabinti msiowangalifu, nisikilizeni mimi.
\v 10 Maana kwa mda mfupi zaidi ya mwaka ujasiri wenu utavunjika, nyie wanawake msiojali, maana mavuno ya zabibu yatakwama, mavuno hayatakuwepo.
\s5
\v 11 Tetemekeni, enyi wanawake, mliowadhaifu; taabikeni enyi msikuwa wangalifu; ondoeni nguo zenu nzuri mbaki wazi;
\v 12 Vaeni nguo za magunia katika viuno vyenu. Ole watakaojichukulia mashamba mazuri, kwa mzabibu ulio zaa sana.
\v 13 Kwenye aridhi ya watu wangu kutamea miiba na mbigiri, hata juu ya nyumba za furaha na mji ulio na shangwe.
\s5
\v 14 Maana jumba litaachwa, mji uliosongamana utakuwa faragha; kilima na mnara vitakuwa mapango daima, furaha ya punda, malisho ya mifugo;
\v 15 mpaka roho itushukie sisi kutoka juu, na jangwa litakuwa shamba linalozaa, na shamba linalozaa litachukuliwa kama msitu.
\s5
\v 16 Wenye haki wataishi jangwani; na wenye haki wataishi katika shamba linalozaa matunda.
\v 17 Kazi ya mwenye haki itakuwa ni ya amani; na matokeo ya wenye haki, ni utulivu na kujiamini daima.
\v 18 Watu wangu wataishi katika makao ya amani, na katika nyumba salama na mahali tulivu pa kupumzikia.
\s5
\v 19 Lakini hata kama ni mvua ya mawe na msitu umeharibiwa, na mji umeteketezwa,
\v 20 yule ambae anaye panda pembezoni mwa mifereji atabarikiwa, na yule atakaye wapeleka ng'ombe na punda kuchunga.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Ole wenu, waharibifu ambao hamjaharibiwa! Ole wao wasaliti ambao hamjaslitiwa! Pindi mtakapoacha uaribifu, nanyi mtaharibiwa. Pindi mtakapoacha usaliti, nayi mtasalitiwa.
\s5
\v 2 Yahwe, tuurumie sisi; tumekusubiri wewe; umekuwa mkono wetu kila asubuhi, na wokovu wetu katika kipindi cha mateso.
\s5
\v 3 Watu wamekimbia kwa kusikia sauti kubwa; uliponyanyuka, mataifa yametawanyika,
\v 4 Mateka wako wamejikusanya kama mkasanyiko wa nzige; kama nzige warukavyo, watu wataruka juu yake.
\s5
\v 5 Yahwe ameinuliwa. Anaishi mahali pa juu. Ataijaza Sayuni kwa haki na usawa.
\v 6 Atakuwa imara katika kipidi chenu, wingi wa wokovu, busara, na maarifa; hofu ya Yahwe iko katika hazina yake.
\s5
\v 7 Tazama, wujumbe wanalia mtaani; wanadiplomasia wanamatumaini ya amani kwa kulia kwa uchungu.
\v 8 Barabara kuu imeachwa faragha; hakuna wasafiri tena. Maagano yamevujika, mashahidi wanadharaulika, na utu wa mtu hauheshimiki.
\s5
\v 9 Nchi imeomboleza na kunyaukia mbali; Lebanoni inaibisha na kunyaukia mbali; Sharoni imekuwa kama jangwa wazi; Bashani na Kermeli zimepuputisha majani yake.
\s5
\v 10 ''Sasa nitanyanyuka, ''asema Yahwe; '' sasa nitanyanyuliwa juu; sasa nitainuliwa.
\v 11 Utashika mimba ya makapi na utazaa mabua; na punzi yako ni moto ambao utakuunguza wewe.
\v 12 Watu watachomwa na kuwa kama chokaa, kama miiba ya porini inavyokatwa na kuchomwa.
\s5
\v 13 Enyi mlio mbali sana, sikiliza nilicho kifanya; na enyi mlio karibu, kirini ukuu wangu.''
\v 14 Watenda zambi wa Sayuni wanogopa; tetemeko limewakuta wasio na Mungu. Ni nani miongoni mwetu anayeweza kukaa kwenye moto mkali? Na ni nani miongoni mwetu anayeweza kukaa kwenye moto wa milele?
\s5
\v 15 Nyie mnaotembe katika haki na kuongea kw uaminifu; yeye anayedharau mapato ya ukandamizaji, yeye anayekataa kuchuka rushwa, ambaye hausiki kwenye kupanga vurugu za kihalifu, na ambaye haangali maovu-
\v 16 Ataiweka nyumba yake juu; sehemu yake ya ulinzi itakuwa ni ngome ya mwamba; chakula na maji yake hayataisha.
\s5
\v 17 Macho yako yatamuona mfalme katika uzuri wake; watatazama nchi kubwa.
\v 18 Moyo wako utakumbuka hofu; yuko wapi mwandishi, yuko wapi yule aliayepima pesa? na yuko wapi yeye aesabue minara?
\v 19 Hautawaona watu wanaopinga, watu weye lugha ya ajabu ambayo hautaweza kuielewa.
\s5
\v 20 Itazame Sayuni, mji wa sikukuu yetu; macho yako yataiona Yerusalemu kama makao tulivu, hema ambalo halitatolewa, vigingi vyake havitatolewa wala kamba zake hazitakatika.
\v 21 Badala yake Yahwe katika ukuu wake atakuwa pamoja na sisi, katika eneo la maji mengi na mifereji mingi. Hakuna manuari na mpiga makasia watakayepita hapo, na hakuna mashua itakayopita uko.
\s5
\v 22 Maana Yahwe ni hakimu wetu, Yahwe ni mwanasheria wet, Yahwe ni mfalme wetu; atatukomboa sisi.
\s5
\v 23 Kamba zako zimelegea; haziwezi kushika mlingoti katika eneo lake; haziwezi kuzunguka meli; pindi mateka wanavyogawanyika, hata vilema watawatoa nje kama mateka.
\v 24 Na wenyeji watasema, ''Ninaumwa;'' watu wanaoishi pale watasamehewa maovu yao.
\s5
\c 34
\p
\v 1 Njooni karibu enyi mataifa, sikilizeni na muwe makini, enyi watu! Dunia na vyote vijazavyo vinatakiwa kusikiliza, dunia na vyote vitokavyo,
\v 2 Maana Yahwe ana hasira na mataifa yote, ana hasira dhidi ya majeshi yao; amewaangamiza wao kabisa, ameawakabidhi kwa wachinjaji.
\s5
\v 3 Miili ya watu wao waliokufa itatupwa nje. Harufu ya miili iliyokffa itakuwa kila mahali; na mlilima italowekwa kwa damu yao.
\v 4 Nyota zote angani zitafifia, na anga litakunjwa kama kitabu; na nyota zake zitafifia mbali, kama tawi linavyonyauka kwenye mzabibu, kama tunda lilokomaa kwenye mti.
\s5
\v 5 Maana pale upanga wangu utakapokunywa na kushiba mbinguni; tazama, maana sasa utakuja chini huko Edomu, kwa watu ambao nimewaweka mbali na adhabu.
\v 6 Upanga wa Yahwe unadondosha matone ya damu na kufunikwa kwa mafuta, matone ya damu ya kondoo na mbuzi, yamefunikwa kwa figo za kondoo. Maana Yahwe ametoa sadaka katika Bozra na mauwaji katika nchi ya Edomu.
\s5
\v 7 Ng'ombe wa porini watachinjwa pamoja na wao, fahali wakubwa na fahali wadogo. Nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatafanjwa kuwa mafuta na mafuta yaliyonona.
\s5
\v 8 Maana itakuwa ni siku ya kisasi kwa Yahwe na mwaka ambao anawalipa kwa sababu ya Sayuni.
\v 9 Mifereji ya Edomu itageuka kuwa lami, na mavumbi yake yatakuwa kiberiti na nchi itakuwa kama lami inayoungua.
\v 10 Itaungua usiku na mchana; moshi wake utatoka daima; na patakuwa nyika kizazi hata kizazi; na hakuna hata mmoja atakayepita hapo milele na milele.
\s5
\v 11 Lakini ndege na wanyama porini wataishi pale; bundi na kunguru watatengeneza viota vyao pale. Atanjoosha juu yake futi kamba ya uharibifu na pima maji ya uharibifu.
\v 12 Wenye vyeo hawatakuwa na kitu kilichobakia kuita ufalme, na wakuu wote watakuwa si kitu.
\s5
\v 13 Miiba itaota katika maeneo yao, viwavi na mbigiri vitakuwa katika ngome zao. Yatakuwa makao ya mbweha, makazi ya mbuni.
\v 14 Wanyama wa porini na fisi watakusanyika pale, na mbuzi wa porini watalia wao kwa wao. Nyakati za usiku wanyama watakaa pale na watajitafutia wenywe mahali pa kupumzikia.
\v 15 Bundi watatengeneza viota vyao, na kutotolea mayai yao, kila mmoja na mwenzake.
\s5
\v 16 Kutafuta kupitia kitabu cha Yahwe; hakuna hata kimoja ambacho hakitakuwepo. Hakuna kitakacho kosa mwenzake; maana mdoma wake umeamuru hivyo, roho yake imewakusanya wao.
\v 17 Atapiga kura katika eneo lao, na mkono wake umewapima kwa kamba. Wataimiliki daima; kutoka kizazi hata kizazi wataishi pale.
\s5
\c 35
\p
\v 1 Jangwa na Arabu watafurahia; na jangwa litafurahia na kuchanua. Kama waridi,
\v 2 Yatachanua kwa wingi na yatashangilia kwa furaha na nyimbo; litapewa utukufu wa Lebanoni, mapambo ya Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Yahwe, mapambo ya Mungu wetu.
\s5
\v 3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, na badala ya magoti yanayotingishika.
\v 4 Waambie wenye moyo wa uwoga, ''Wawe imara, wasiogope! Tazama, Mungu wako anakuja na kisasi, kwa ajili ya malipo ya Mungu. Atakuja na kutuokoa.''
\s5
\v 5 Halafu macho ya vipofu yataona, na masikio ya viziwi yatasikia.
\v 6 Halafu kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wa bubu utaimba, maana maji yatabubujika Araba, na mifereji jangwani.
\v 7 Mchanga ulioungua utakuwa kisima, na aridhi iliyo na kiu itakua chemchem; katika makazi mbweha, pale waliopokuwa wanaishi, kutakuwa na nyasi pamoja na mianzi.
\s5
\v 8 Barabara kuu itaitwa Njia takatifu. Wasio safi hawatasifiri kwa kutumia njia hiyo. Lakini itakuwa kwa ajili ya mtu yeyote anayetembea juu yake. Hakuna mjinga atakayeipitia.
\v 9 Hakuna simba pale, wala mnyama mkali katika barabara hiyo; hawatakuwepo kabisa pale, lakini waliokombolewa watapita pale.
\s5
\v 10 Fidia ya Yahwe itarudi na itakuja kwa wimbo wa Sayuni, na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao; furaha na shangwe vitawazidi wao; huzuni na magonjwa yataondoshwa mbali.
\s5
\c 36
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senacherebi, mfalme wa Asiria, alivamia miji yote ya Yuda na kuwakamata.
\v 2 Halafu mfalme wa Asiria akamtuma kamanda mkuu na jeshi kubwa kutoka Lachishi mpaka Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Alipofika kwenye mfereji katika kisima cha juu, katika njia kuu na katika shamba la dobi na akasimama pale.
\v 3 Maofisa wa Israeli waliotumwa kuzungumza nao walikuwa ni Eliakimu mtoto wa Hilkia, kiongozi wa jumba, Shebna katibu wa mfalme, na Joa mtoto wa Asapha, anayeandika makubaliano ya serekali.
\s5
\v 4 Kamanda mkuu wa jeshi akawaambia wao, ''Mwambieni Hezekia kwamba mfalme mkuu, mfalme Asiria, asema, 'Nini chanzo cha ujasiri wako?
\v 5 Unaongea maneno yasiyo na maana tu, nasema kama kuna shauri na nguvu za vita. Sasa ni nani unayemuamini? na ni nani aliyekupa ujasiri wa kuniasi mimi.
\s5
\v 6 Tazama, umeweka imani yako Misri, maana banzi la mwanzi unalolitumia kama fimbo ya kutembelea, ikiwa mtu ataiegemea na kuishika kwenye mkono wake itamchoma. Hivyo ndovyo jinsi Farao mfalme wa Misri alivyo kwa yeyote anayemuamini.
\v 7 Lakini ikiwa utasema nami, ''Tunamwamini Yahwe Mungu wetu,''Je sio yeye ambaye Hezekia ameondosha mahali palipoinuka na madhebau, asema kwa Yuda na Yerusalemu, ''Lazima tuabudu mbele ya madhebau hii katika Yerusalemu''?
\s5
\v 8 Hivyo sasa, nataka kukufanya wewe kuwa zawadi nzuri kwa Bwana mfalme Asiria. Nitakupa farasi elfu mbili, kama utaweza kuwatafutia dereva.
\s5
\v 9 Ni kwa jinsi gani unaweza kumpinga moja kati ya nahodha aliye mdogo katika watumishi wa Bwana wangu? Mmeweka imani yenu Misri katika gari na farasi!
\v 10 Halafu sasa, Je nimewezaje kusafiri mpaka hapa pasipo Yahwe kupigana dhidi ya nchi hii na kuhiaribu? Yahwe asema nami, Vamia nchi hii na uhiharibu.
\s5
\v 11 Halafu Eliakimu mtoto wa Hilkia, na Shebna na Joa asema kwa kamanda mkuu, Tafadhali zungumza na watu wako kwa lugha ya kiashuru, maana kiashuru tunakielewa. Usiongee na sisi kwa lugha kiyahudi katika masikio ya watu ambao wako ukutani.''
\v 12 Lakini kamanda mkuu akasema, ''Je bwana wenu ametuma kwa bwana wako na kuzungumza haya maneno? Je hajanituma kwa watu walio kaa kwenye ukuta, ili wale kinyesi chaao mwenyewe na kunywa mkojo waomwenyewe?
\s5
\v 13 Halafu kamanda mkuu akasimama na kupiga kelele kwa sauti kubwa kwa lugha ya kiyahudi, na akisema,
\v 14 ''Mfalme asema, ' Msimruhusu Hezekia awadanganye ninyi, maana hataweza kuwaokoa ninyi.
\v 15 Msimruhusu Hezekia awafanye muumuamini Yahwe, Nawambieni Hakika Yahwe atatukomboa sisi; mjii huu hautachukuliwa na mfalme wa Asiria.''
\s5
\v 16 Msimsikilize Hezekia, maana hivi ndivyo mfalme wa Asiria anavyosema: 'Fanyeni amani na mimi na mje kwangu. Halafu kila mmoja wenu atakula kwenye mzabibu wake mwenyewe na tunda la mti wake mwenyewe, na kunjwa maji ya kisima chake mwenyewe.
\v 17 Mtafanya hivi mpaka nije kuwachukua na kuwapeleka kwenye nchi kama ya kwenu. nchi ya mavuno na mvinyo mpya, nchi ya mkate na shamba.
\s5
\v 18 Msimruhusu Hezekia awapotoshe nyie, akisema, Yahwe atatuokoa nyie; Je kuna miungu ya aina yeyote ya watu iliyowakomboa kutoka mikononi mwa mfalme wa Asiria?
\v 19 Wako wapi miungu wa Hamathi na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je wameikomboa Samaria kutoka kwenye nguvu zangu?
\v 20 Miongoni mwa miungu yote ya nchi hii, Je kuna miungu ya aina yeyote iliyoikomboa nchi yao kutoka kwenye nguvu yangu, ni kama Yahwe anaweza kuawokoa Yerusalemu kutoka kwenye nguvu yangu?''
\s5
\v 21 Lakini watu wanabaki kimya na hawataki kujibu, maana amri ya mfalme ilikuwa, ''Msimjibu''.
\v 22 Halafu Eliakimu mtoto wa Hilkia, yeye aliye juu ya kaya, Shebna mwandishi, na Joa mtoto wa Asafu, na mtunza kumbukumbu, walikuja kwa Hezekia na nguo zilizotoboka na wakapeleka maneno ya kamanda mkuu.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Ikawa siku hiyo mfalme Hezekia aliposika taarifa zao, alichana mavazi yake, na kujifunika nguo za magunia, na akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 2 Na alimtuma Eliakimu, ambae ni kiongozi wa kaya na Shebna mwandishi, na wazee wa makuhani, wote walijifunika nguo za magunia, kwa Isaya mtoto wa Amozi, nabii.
\s5
\v 3 Wakamwambia yeye, Hezekia akasema hivi, 'Siku hii ni siku ya dhiki, kukemewa, na aibu, ni kama mtoto aliye tayari kuzaliwa lakini mama yake hana nguvu za kumsukuma mtoto.
\v 4 Itakuwa Yahwe Mungu wenu atasikia maneno ya kamanda mkuu, ambao mfalme wa Asira Bwana wake alimtuma kumpinga Mungu anayeishi, na atakemea maneno ambayo Yahwe Mungu wenu ameyasikia. Sasa inueni maombi yenu juu mabaki yaliyoobakia hapa.''
\s5
\v 5 Sasa watumishi wa mfalme Hezekia walikuja kwa Isaya,
\v 6 na Isaya akawambia, ''Mwambieni Bwana wenu: 'Yahwe amesma, ''Msiogope kwa maneno mliyoyasikia, maneno ambayo mfalme wa Asiria amenitusi mimi.
\v 7 Tazama nitaiweka roho yangu ndani yake na atasikiliiza taarifa fulani na atarudi kwenye nchi yake mwenyewe. Na nitamfanya anguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.''
\s5
\v 8 Basi kamanda mkuu alirudi na kumkuta mfalme wa Asira anapigana dhidi ya Libna, Maana aliskia kwamba mfalme amekwenda mbali kutoka Lachishi.
\v 9 Halafu Sennacheribi alisikia kwamba Tirkhaka mfalme wa Ethiopia na Misri wamehamasishana kupigna dhidi yake. Hivyo akamtuma mjumbe mara nyingine kwa Hezekia apeleke ujumbe:
\v 10 ''Mwambie Hezekia, mfalme wa Yuda, 'Usimruhusu Mungu unayemwamini akudanganye, ''Yerusalemu haitatiwa mikononi mwa mfalme wa Asiria.''
\s5
\v 11 umesikia kitu ambacho mfalme wa Asiria alichokifanya kwa nchi yote kwa kuiangamiza kabisa. Je utawaokoa?
\v 12 Je miungu ya mataifa imewakomboa? taifa ambalo baba yangu aliliangamiza: Gozani, Harani, Rezefi na watu wa Edeni katika Telassari?
\v 13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa miji ya Sefarvaaimi, wa Hema na Ivva?''
\s5
\v 14 Hezekia alipokea barua hii kutoka mikononi mwa mjumbe na kisoma. Halafu akaenda juu kwenye nyumba ya Yahwe na kuusoma mbele yake.
\v 15 Hezekia alimuomba Mungu:
\v 16 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, wewe ambae uko juu ya makerubi, wewe ni Mungu mwenywe juu falme zote za dunia. umezifanya mbingu na nchi.
\s5
\v 17 Jeuza masikio yako, Yahwe, na sikiliza. Fungua macho yako, Ee Yahwe na uone, na usikilize maneno ya Sanacheribi, ambayo ameyatuma kumfanyia mzadha Mungu anayeishi.
\v 18 Ni kweli Yahwe, mfalme wa Asiria ameangamiza mataifa yote na aridhi yao.
\s5
\v 19 Wameiweka miungu yao katika moto, maana haikuwa miungu lakini kazi ya mikono ya wanadamu, ni kuni na jiwe tu.
\v 20 Hivyo Waasira wameawaangamiza wao. hivyo saa Yahwe Mungu wetu, tuokoe kwa nguvu zako, ili falme zote za duniani zijue kwamba wewe ni Yahwe peke yako.''
\s5
\v 21 Basi Isaya mtoto wa Amozi alituma ujumbe kwa Hezekia, na kusema, Yahwe Mungu wa Israeli amesema, Kwa sababu umeomba kwangu kuhusu Sannacheribi mfalme wa Asiria,
\v 22 Haya ndiyo maneno ambayo Yahwe amezungumza kuhusu yeye, ''Binti bikira wa Sayuni wanakudharau na kukucheka kwa dharau; mabinti wa Yerusalemu wanatingisha vichwa vyao kwa ajili yako.
\v 23 Ni nani unayempinga na kumtusi? na dhidi ya nani unayenyanyua sauti yako na kunyanyua macho yako kwa kiburi? dhidi ya mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 24 Kwa kupitia watumishi wako umempinga Bwana na amesema, 'Kwa wingi wa gari nimepanda juu kwenye kilele cha milima, katika kilele cha mwuinuko wa Lebanoni. Nitaikata mierezi yake na kuchagua miti ya miseprasi pale, ni msitu uzao sana.
\v 25 Nimechimba kisima na kunywa maji; nimechimba mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yangu.'
\s5
\v 26 Je haujasikia jinsi nilivyoamua toka siku nyingi na nimelifanyia kazi toka kipindi cha kale? ninayaleta sasa ili yaweze kutimia. Mko hapa kuhiaribu miji imara na yenye ulinzi wa kutosha na kuwa chungu cha uharibifu.
\v 27 Wakazi wake, waliowadhaifu, waliokata tamaa na wenye aibu. Wanaotesha shambani, majani mabichi, majani juu paa au kwenye shamba kabla ya upepo wa mashariki.
\s5
\v 28 Lakini najua kukaa kwenu chini, kutoka kwenu nje, mnapoingia ndani, na mnapokuwa wakali dhidi yangu.
\v 29 Kwa sababu mnakuwa wakali dhidi yangu, maana kiburi chenu kimeyafikia masikio yangu, Nitaweka ndoano katika pua zenu, na sauti katika midomo yenu; Nitawageuza nyuma kwenye njia mliyokuja nayo.
\s5
\v 30 Hii itakuwa wimbo kwenu: mwaka huu mtakula kinachoota porini na mwaka pili mtakula kinachoota hapo hapo. Lakini mwaka wa tatu lazima mpande na mvune, pandeni mizabibu na mle matunda yake.
\s5
\v 31 Mabaki ya nyumba ya Yuda ambao wanaishi watachukua mzizi tena na kuzalisha matunda.
\v 32 Maana katika Yerusalemu waliobaki watatoka; Kutoka kwenye mlima Sayuni waliobaki watakuja. Bidii ya Yahwe wa majeshi itafanikisha hili.''
\s5
\v 33 Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu Asiria: ''Atakuja katika miji, wala kurusha mkuki hapa. Wala atakuja hapa mbele kwa ngao au kujenga uzio njia panda dhidi yao.
\v 34 Njia atakayojia itakuwa njia hiyo hiyo atakayorudia; ataingia katika mji huu. Hili ni Tamko ya Yahwe.
\s5
\v 35 Maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba Daudi mtumishi wangu.''
\s5
\v 36 Halafu malaika wa Yahwe alienda nje na kuvamia kambi ya Waasiria, na kuwauwa askari 185, 000. Watu walipoamka asubuhi na mapema, miili iliyokufa imelala kila mahali.
\v 37 Hivyo Sennacheribi mfalme wa Asiria aliiacha Israeli na kwenda nyumbani na akakaa Ninewi.
\s5
\v 38 Baadaye, na alipokuwa anabudu katika nyumba ya Nisrochi mungu wake, mtoto wake Adramaleki na Shareza alimuua kwa upanga. Halafu wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Halafu Esarhadoni mtoto wake akatawala katika sehemu ya baba yake.
\s5
\c 38
\p
\v 1 Siku zile Hezekia alikuwa anaumwa karibia na kufa. Hivyo Isaya mtoto wa Amozi, nabii alikuja kwake na kumwambia, ''Yahwe amesema, 'panga mambo yako maana utakufa, hautaishi.'
\v 2 'Halafu Hezekia akaugeukia ukuta na akamuomba Yahwe.
\v 3 Na akasema, ''samahani Yahwe, kumbuka jinsi nilivyoenenda kwa uaminifu mbele zako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya matendo mema katika macho yako.'' Na Hezekia akalia kwa sauti.
\s5
\v 4 Basi neno la Yawe likamjia Isaya, na kusema,
\v 5 ''Nenda ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ''Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yenu, amesema: Nimeyasikiliza maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Ona ninakaribia kuongeza miaka kumi na tano katika maisha yako.
\v 6 Na nitakukomboa wewe pamoja mji huu kutoka kwenye mkono wamfalme wa Asiria, na nitaulinda huu mji.
\s5
\v 7 Na hii itakuwa alama kwako kutoka kwangu, Yahwe, kwamba nitafanya nilichokisema:
\v 8 Angalia, nitasababisha kimvuli katika nyumba ya Ahazi kwenda nyuma hautua kumi.'' hivvyo basi kivuli kilirudi nyuma hatua kumi juu ya nyumba iliyopanda juu.
\s5
\v 9 Haya ndiyo maandishi ya maombi ya Hezekia mfalme wa Yuda, alipokuwa anaumwa halafu akapona:
\v 10 ''Nimesema kwamba nusu ya maisha yangu nitapita katika mlango wa kuzimu; Nilitumwa pale miaka yangu yote.
\v 11 Nikasema sitamuona tena Yahwe, Yahwe kaika nchi ninayoishi; sitaangalia watu tena au wenyeji wa dunia hii.
\s5
\v 12 Maisha yangu yameondolea na kupelekwa mbali na mimi kama hema la mchungaji; Niliyakunja maisha yangu juu kama mfumaji; ameniondoa katika kifungo; kati ya mchana na usiku ameyakomesha maisha yangu.
\v 13 Nililia mpaka asubuhi; kama simba anaivunja mifupa yangu. Kati ya usiku na mchana ameyakomesha maisha yangu.
\s5
\v 14 Kama mbayuwayu ndivyo nilivyolia; nililia kama njiwa; macho yangu yalichoka kuangalia juu. Bwana ninateseka; nisaidie mimi.
\v 15 Niseme nini? wote wameongea na mimi na amefanya hivyo; Nitatembea taratibu miaka yangu yote maana ninayashinda kwa huzuni.
\s5
\v 16 Bwana, mateso uliyoyatuma ni mazuri kwangu; ikiwezekana nirudishiwe tena maisha yangu; umeyahifadhi maisha maisha yangu na afya yangu.
\v 17 Ni kwa faida yangu kwamba nimwpitia huzuni kama hii. Umenikomboa kutoka kwenye shimo la uharibifu; maana umetupa dhambi zangu nyuma yako.
\s5
\v 18 Maana kuzimu hapata kushukuru wewe; kifo hakikusifu wewe; wale wote waendao ndani ya shimo hawana matumaini ya uaminifu wako.
\v 19 Mtu anayeishi, mtu anayeishi, ndiye anayekushukuru wewe, kama ninavyofanya leo; baba atawjulisha watoto uaminifu wako.
\s5
\v 20 Yahwe anakarbia kunikomboa mimi, na tutasherekea kwa mziki siku zote za maisha yetu katika nyumba ya Yahwe.''
\s5
\v 21 Sasa Isaya alisema, ''Waacheni wachukue donge mitini na kuliweka kweye jipu naye atapona.
\v 22 ''Hezekia pia alisema, ''Je ni ishara gan ya kwamba nitaiende juu katika nyumba ya Yahwe?''
\s5
\c 39
\p
\v 1 Katika mda ule Merodaki mtoto wa Baladani, mfalme wa Babeli, alituma zawadi na barua kwa Hezekia; maana alisikia Hezekia alikuwa anaumwa na amepona.
\v 2 Hezekia alifurahishwa na hivi vitu; alimuonyesha mjumbe nyumba ya ghala la vitu vya thamani- vitu kama fedha, dhahabu, viungo, na mafuta ya thamani, ghala la kuwekea silaha zake, na vitu vyote vilivyopatikana kwenye stoo yake. Hapakuwa na kitu katika nyumba yake, wala ufalme wake wote, Hezekia hakuwaonyesha wao.
\s5
\v 3 Basi Isaya nabii alikuja kwa mfalme Hezekia na kumuuliza, ''Je watu hawa wamekuambia nini? wametoka wapi?, ''Wamekuja kwangu kutoka mbali nchi ya Babeli.''
\v 4 Isaya akamuuliza je ni vitu gani walivyoviona katika nyumba yako? Hezekia akajibu, ''Wameona kila kitu katika nyumba nyangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.''
\s5
\v 5 Basi Isaya akamwambia Hezekia, ''Sikiliza neno la Yahwe wa majeshi:
\v 6 'Tazama siku inakaribia kuja pale kila kitu katika nyumba yako, vitu ambavyo mababu zako wamevihifadhi mbali mpaka mda huu wa sasa Vitapelekwa Babeli. Hakuna kitakachobakizwa, asema Yahwe.
\s5
\v 7 Na watoto watazaliwa kutoka kwako, ambao wewe mwenyewe utawazaa- watachukuliwa mbali, na watakuwa matoashi katika jumba la mfalme wa Babeli.''
\v 8 Basi Hezekia akamwambia Isaya, ''Neno la Yahwe alilolizunumza ni zuri.'' Maana alifikiria, ''Patakuwa na amani na utulivu katika siku zangu.''
\s5
\c 40
\p
\v 1 ''Faraja, faraja watu wangu,'' amesema Mungu.
\v 2 ''Ongea kwa upole kwa Yerusalemu; na tangaza vita vimeisha, maana maovu yao yamesamehewa, maana alipokea mara mbili kutoka kwa mkono wa Yahwe kwa dhambi zao.''
\s5
\v 3 Sauti inalia nje, ''Katika jangwa tengeneza njia ya Yahwe; njoosha njia ya Araba katika njia kuu ya Mungu.''
\v 4 Kila bonde litanyanyuliwa juu, kila mlima na kilima kitasawazishwa; na aridhi ya mwinuko itasawazishwa, mahali palipokwaruzwa patakuwa na usawa;
\v 5 na utukufu wa Mungu utafunuliwa, na watu wote wataona kwa pamoja; maana mdomo wa Yahwe umezungumza.
\s5
\v 6 Sauti inasema, ''Lia.'' Jibu lingine, ''Kwa nini nilie?'' ''Mwili wote ni nyasi na maagano yaliyoaminika ni kama ua kwenye shamba.
\v 7 Nyasi zinanyauka na maua yanaperuka pale Yehwe atakapo puliza punzi yake juu yake; hakika ubinadamu ni nyasi.
\v 8 Nyasi hunyauka, maua hupepea, lakini neno la Yahwe litasimama daima.''
\s5
\v 9 Nenda juu ya mlima mrefu, Sayuni, mbeba taarifa njema. waambie miji ya Yuda, ''Hapa ni Mungu wako!''
\v 10 Angalia, Bwana Yahwe anakuja kama mpiganaji shujaa na jeshi imara linatawa juu yake. Ona, zawadi yako iko kwake, na wale walikombolewa wataenda mbele yake.
\s5
\v 11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya kondoo katika jeshi lake, na kulichukua karibu na moyo wake, kwa upole atawongoza wake kuwauuguza watoto wao.
\s5
\v 12 Ni nani aliyepima maji ya mashimo kwa mkono wake, anayepima anga kwa urefu wa mkono wake, na kuweka vumbi za nchi katika kikapu, kupima milima kwa mizani, au vilima kwa usawa?
\s5
\v 13 Ni nani aliyeelewa akili za Yahwe, au kumuelekeza yeye kama mshauri?
\v 14 Ni kutka kwa nani alipokea maelekezo milele? Nani alikufundisha njia sahihi ya kufanya vitu, kumfundisha yeye maarifa, au kumuonyesha njia ya ufahamu?
\s5
\v 15 Tazama, Mataifa ni kama tone katika ndoo, na kama mavumbi kwenye mizani; ona, na alipima kisiwa kama tundu.
\v 16 Lebanoni sio mafuta ya kutosha, wala wanyama pori wake hawatoshi kwa dhabihu ya kuteketezwa.
\v 17 Mataifa yote hayatochelezi mbele yake; wanachukuliwa na yeye kama hakuna kitu.
\s5
\v 18 Ni nanibasi utayemlingalisha na Mungu? Ni kwa sanamu ipi utakayomfananisha nayo?
\v 19 Sanamu! ambayo fundi ameitupa: Mfua dhahabu ameka pamoja na mikufu bandi ya fedha.
\v 20 Kuafanya sadaka hii mtu atachagua kuni ambayo haiozi; anamtafuta fundi mwenye ujuzi wa kutengeneza sanamu ambayo haitaanguka.
\s5
\v 21 Je hamkujua? Je hamjasikia? Je hamkuambiwa tokea mwanzo? Je hamkuelewa toka misingi ya nchi?
\v 22 Yeye ndiye aketie juu ya upeo wa macho ya nchi? na wenyeji wake ni kama panzi mbele yake. Akijinyoosha nje ya mbingu ni kama pazia na kutawnya nje kama hema la kuishi.
\s5
\v 23 Anawapunguza viongozi kuwa si kitu na amewafanya viongozi wa nchi kwa sio wenye umuhimu.
\v 24 Tazama wamekuwa wagumu kuotesha; tazama wamekuwa wagumu kupanda; imekuwa ni vigumu kuchukua mzizi katika nchi, kabla ajapuliza juu yao, na wakanyauka, na upepo unawaondosha mbali kama majani.
\s5
\v 25 Ni nani tena utakayemfananisha na mimi, ni nani ninayefanan nae?'' amesema mtakatifu.
\v 26 Tazama juu kwenye anga! Nani aliyeziumba nyota hizi zote? Analileta nje jeshi na anawaita kwa majina yote. Kwa ukuu wa nguvu zake na kwa uimara wa nguvu zake, hakuna hata mmoja atakayekosa.
\s5
\v 27 Kwa nini unasema, Yakobo, na kutangaza, Israeli, ''Njia yangu imefichwa Yahwe asione, na Mungu wangu hakuwekwa wazi kuhusiana na uthibitisho wangu''?
\v 28 Je hakufahamu? Mungu wa milele, Yahwe, Muumbaji wa miisho ya nchi, apatwi na uchovu wala hachoki; hakuna mipaka katika ufahamu wake.
\s5
\v 29 Anawapa nguvu waliochoka; na atawapa nguvu mpya waliowadhaifu.
\v 30 Hata vijana wadogo watapatwa na uchovu na kuchoka, vijana wadogo watapata mashaka na kuanguka:
\v 31 Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mbawa kama malaika; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.
\s5
\c 41
\p
\v 1 ''Sikilizeni mbele yangu kwa ukimya, enyi mkao pwani; wacha mataifa yapate nguvu kwa upya; waache waje karibu na kuzungumza; na tusogee karibu tujadili mgogoro.
\v 2 Nani aliyechochea juu mmoja kutoka mashariki, anamuita katika haki yake kwenye huduma yake? Amemkabidhi mataifa juu yake ili amsaidie yeye kuwaangamiza wafalme. Aliwajeuza kuwa mavumbi kwa neno lake, kama upepo unaovuma kwenye mabua kwa upinde wake.
\s5
\v 3 Aliwachukuwa wao na kuwapitisha salama, katika njia nyepesi ambayo miguu yake imegusa shida.
\v 4 Ni nani aliyeyafanya na kukamilisha matendo haya? Ni nanialiyechagua kizazi kutoka mwanzo? Mimi, Yahwe ni mwanzo na mwisho, mimi ndiye.
\s5
\v 5 Visiwa vimeona na kuogopa; miisho ya dunia yatetemeka; walikaribia n kuja.
\v 6 Kila mmoja amsaidie jirani yake, na kila mmoja asemezane na mwenzake, 'Kuwa mfariji;
\v 7 Hivyo basi seremala anamfariji mfua dhahabu, na yule anayefanya kazi kwa kutumia nyundo anamfariji anayefanya kazi kwa chuma, akisema kwa msemo wa kurehemu, ''Ni mizuri; Naye ataupigilia kwa makini misumari ili isipinduke.
\s5
\v 8 Lakini wewe, Israeli mtumishi wangu, Yakobo niliyekuchagua, mtoto wa Ibrahimu rafiki yangu,
\v 9 wewe ambaye ninakurudisha kutoka miisho ya nchi, na ambaye niliyekuita kutoka sehemu ya mbali, na kwako niliyekuambia, 'Wewe ni mtumishi wangu,; 'Nimekuchagua wewe na sijakukataa.
\s5
\v 10 Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.
\s5
\v 11 Tazama, watakuwa na aibu na hawataheshimiwa, wale wote waliokuwa na hasira na wewe; watakuwa si kitu na watatokomea, wale watakao kupinga wewe.
\s5
\v 12 Utawatafuta na wala hautawapata wale wanaopingana na wewe; wale wafanyao vita dhidi yako watakuwa kama si kitu, si kitu kabisa.
\v 13 Maana mimi Yahwe Mungu wako, nitawashika mkono wako wa kiume, nikikuambia wewe, 'Usiogope; Nitakusaidia wewe.
\s5
\v 14 Usiogope, Yakobo wewe mdudu, na enyi watu wa Israeli; Nitawasaidia''- hili ni tamko la Yahwe, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli.
\v 15 Tazama, ninakufanya wewe kuwa chombo kikali cha kuparulia chenye makali pande mbili; utaparua milima na kuiponda; utafanya vilima kama makapi.
\s5
\v 16 Utawatawanya wao, na upepo utawabeba na kuwapeka mbali; upepo utawatanya wao. Utashanglia katika Yahwe, utashangiliakatika mtakatifu wa Israeli
\s5
\v 17 Waliodhulumiwa na masikini wanatafuta maji, lakini hakuna kitu, ndimi zao zimekauka kwa kiu; Mimi Yahwe, nitajibu maombi yao; Mimi Mungu wa Israeli, sitawacha wao.
\v 18 Nitatengeneza mikondo ya maji kushusha chini, na chemichem katikati ya mabonde; nitalifanya jangwa kuwa kisima cha maji, na aridhi kavu kuwa chemichem ya maji.
\s5
\v 19 Katika jangwa nitapanda mierezi, mshita, mhadisi, na mti wa mizeituni. Nitaotesha mberoshi katika uwazi wa jangwa, pamoja na mbono nitapanda mberoshi kitika jangwa lililowazi.
\v 20 Nitayafanya haya ili waweze kuona, kutambua na kuelewa kwa pamoja, kwamba mkono wa Yahwe umetenda haya, kama Mtakatifu wa Israeli aliyeliumba.
\s5
\v 21 Wakilisha keshi yako, '' asema Yahwe; ''wakilisha hoja zenu nzuri kwa sanamu yenu,'' asema Mfalme wa Yakobo.
\v 22 Waache walete hoja zao wenyewe; waache waje mbele na watutangazie sisi nini kitakachotokea, ili tuweze kuelewa haya mambo vizuri. Tuawaache watupe tamko mapema, ili tuweze kulitafakari na tuweze kujua n kwa jinsi gani litatimia.
\s5
\v 23 Wajulishe kitu kuhusu baadaye, ili tujue kuwa ninyi ni miungu; fanya kitu kizuri au kibaya, ambacho kitatutisha na kutushangaza.
\v 24 Tazama sanamu zenu si kitu na matendo yenu si kitu; aliyewachagua ni machukizo.
\s5
\v 25 Nimemnyanyua mmoja kutoka kaskazini, naye amekuja kutoka mawio ya jua nimemchagua yeye alitajae jina langu, na atawakanyaga viongozi kama matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo.
\v 26 Ni nani aliyetangaza hili tangu mwanzo, ili tuweze kujua? na kabla ya mda, ili tuseme, ''Yuko sawasawa''? Kweli hakuna hata mmoja aliyekiri hili, ndio hakuna hata mmoja aliyekusikia ukisema chochote.
\s5
\v 27 Kwanza nilizungumza na Sayuni, ''Tazama hapo walipo;'' Nimemtuma mhubiri Yerusalemu.
\v 28 Nilipoangalia, hakuna hata mmoja, hakuna hata miongoni mwao ambaye anaweza kutoa ushauri mzuri, nani, lini nimulize, awezaye kunijibu neno.
\v 29 Tazama, matendo yao si kitu; sanamu zao za chuma zilizotupwa ni upepo na utupu.
\s5
\c 42
\p
\v 1 Tazama, mtumishi wangu, niliyekushika; niliyekuchagua, kwake ninapata furaha. Nimeiweka roho yangu juu yake; ataleta haki kwa mataifa.
\v 2 Hatalia wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika mitaani.
\s5
\v 3 Mwanzi ulioangamizwa hatauvunja, na wala utambi unaowaka na kutoa mwanga hautaungua: atatekeleza haki kwa uaminifu.
\v 4 wala hatazimia wala kukata tamaa mpaka atakapoanzisha haki katika nchi; na pwani inasubiria sheria yake.
\s5
\v 5 Mungu Yahwe asema hivi--yeye aliyeziumba mbingu na yeye zinyoosha nje, yeye aliyeiumba nchi na vitu vyote izalishavyo, yeye aliyewapa punzi watu na wale waishio juu:
\v 6 Mimi Yahwe nimekuita kwa haki yangu na nitakushika kwa mkono wangu. Nitakutunza wewe, na nitakuweka wewe kama agano kwa watu wangu, kama mwanga wa wayunani
\s5
\v 7 Kuyafungua macho ya vipofu, kuwatoa waliofungwa gerezani, kuwatoa wale walio gizani kutoka kwenye nyumba iliyofungiwa.
\s5
\v 8 Mimi ni Yahwe, Hilo ndilo jina langu; na utukufu wangu sitashiriana na mtu mwingine wala sifa zangu sitashirkiana na sanamu ya kuchonga.
\v 9 Tazama, mambo ya nyuma yamekuja na kupita, sasa ninakaribia kutangaza mambo mapya. Kabla hayajaanza kutokea nitawambia kuhusu wao.''
\s5
\v 10 Mwimbieni Yahwe wimbo mpya, na sifa zake kutoka mwisho wa nchi; wewe ushukae chini kwenye bahari, na vyote vilivyomo ndani yake, waishio pwani na wale wanaoishi huko.
\v 11 Wacha jangwa na miji ilie, vijiji anavyoishi na Kaderi, lia kwa furaha! waache wenyeji wa Sela waimbe; waache wapige kelele juu ya kilele cha mlima.
\s5
\v 12 waache wamtukuze Yahwe na kutangaza sifa zake katika aridhi ya pwani.
\v 13 Yahwe atatoka nje kama shujaa; kama mtu wa vita ataichochea bidii yake. Atapiga kelele, ndio, atalia kw kishindo katika vita yake; atawaonyesha adui zake nguvu zake.
\s5
\v 14 Nimenyamaza kimyi kwa mda mrefu; bado nimendelea kujizuia mimi mwenyewe; Nitalia kama mwanamke anayetaka kuzaa; nitatweta na kuugua.
\v 15 Nitaiharibu milima na vilima na kukausha uoto wake wa asili; nitajeuza mito kuwa visiwa na nitakausha matindiga.
\s5
\v 16 Nitawaleta vipofu kwa njia wasioijua; katika njia wasiyoijua Nitawapitisha wao. Nitaligeuza giza kuwa mwanga mbele yao, na kupanyoosha mahali palipopotoka. Mambo yote haya nitayafanya, na sitaachana na wao.
\s5
\v 17 Watageuka nyuma, wataabishwa sana, wale wote wanaoiamini sanamu ya kuchonga, wanaosema na kuziambia sanamu za chuma, ''Nyinyi ni miungu wetu.''
\s5
\v 18 Sikilizeni ewe kiziwi; tazama, ewe kipofu, ili uweze kuona.
\v 19 aliye kipofu ila mtumishi wangu? au kiziwi ni kama mjumbe niliyemtuma? Ni nani aliye kipofu kama mpenzi wangu wa agano, au kipofu kama mtumishi wa Yahwe?
\s5
\v 20 Mmeona mambo mengi, lakini hamuelewi; masikio yamefunguka, lakini hakuna anayesikia.
\v 21 Itampendeza Yahwe kuisifu haki yake na kuitukuza sheria yake.
\s5
\v 22 Lakini watu hawa ni wale waliokamtw na kutekwa; wote wamenaswa kwenye mashimo; wafungwa wote wamewekwa gerezani; wamekuwa mateka na hakuna hata mmoja wa kuwaokoa wao, hakuna asemaye, warudisheni.''
\s5
\v 23 Ni nani miongoni mwenu atalisikiliza hili? nani atayasikia na ni nani atasikia wakati ujao?
\v 24 Ni nani aliyemtoa Yakobo kwa majambazi, na Israeli kwa wanyang'anyi? Je hakuwa Yahwe, dhidi ya wale waliotenda dhambi, waliokataa kutembea katika njia zako na wale waliokataa kusheshimu sheria yako.
\s5
\v 25 Hivyo basi humwaga asira yake kali nje dhidi yao, kwa uharibifu wa vita. Iliwaka kuwazunguka wao, hata hawakujua hilo, lakini hawakuyachukulia hayo moyoni mwao.
\s5
\c 43
\p
\v 1 Lakini sasa haya ndio Yahwe asemayo, yeye aliyekuumba ewe, Yakobo, na yeye aliyekuumba ewe, Israeli: ''Usiogope, kwa maana nimekukomboa wewe; nmeikuita kwa jina lako, wewe ni wangu.
\s5
\v 2 Utakapopita katika maji, Nitakuwa pamoja na wewe; na katika mito, hayatakuzuru wewe. Utakapotembea katika moto hautaungua, na moto hautakuharibu wewe.
\v 3 Maana mimi Yahwe Mungu wako, Mtakatifu wa Israeli Mkombozi wenu. Nimewapa Misri kama fidia yenu, Ethiopia na Seba watabadilishana kwako.
\s5
\v 4 Kwa maana ulikuwa wa thamani na maalumu katika macho yangu, Ninakupenda; kwa sababu hiyo Nitatoa watu kwa ajili yako, na watu wengine kwa ajili ya maisha yako.
\v 5 Usiogope, maana Mimi niko pamoja na wewe; Nitawarudisha watoto wako kutoka mashariki, na kuwakusanya nyie kutoka magharibi.
\s5
\v 6 Nitasema na kaskazini, 'Wakabidhini wao; na kwa kusini, Usiangalie ya nyuma; Leteni vijana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka vijiji vya mikoani katika nchi,
\v 7 yeyote aitwe kw jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu mwenyewe, Niliyemuumba, ndio, Mimi niliyemfanya.
\s5
\v 8 Waleteni nje watu ambao ni vipofu, hata kama wana macho, na viziwi, hata kama wana masikio.
\v 9 Mataifa yote yatakusanyika kwa pamoja na watu watakusanyika. Ni nani miongoni mwenu atakaye tamka na kutangaza kutumia mambo ya mwanzo? Waache walete mashahidi kuwashuhudia wao kama wako sahihi, waache wasikilize na kuthibitisha, 'kama ni kweli'.
\s5
\v 10 Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, ''na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu.
\v 11 Mimi, Mimi Yahwe, na hakuna Mkombozi zaidi yangu.
\s5
\v 12 Nimetangaza, nimeokoa, na kutangaza, na hakuna Mungu mwingine miongoni mwenu, Ninyi ni mashahidi wangu asema Yahwe, ''Mimi ni Mungu.
\v 13 Kuanzia leo na kuendelea mimi ndiye, na hakuna hata mmoja atakayewakomboa kwenye mkono wangu. Nitafanya, na nani awezae kunizuia?''
\s5
\v 14 Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, yeye Mtakatifu wa Israeli: ''Kwa niaba yenu nimemtuma mjumbe kwenda Babeli na kuwaongoza wao wote chini kama watuhumiwa, kubadilisha kelele za furaha za watu wa Babeli' kuwa wimbo wa maombolezo.
\v 15 Mimi ni Yahwe, niliye Mtakatifu, Muumbaji wa Israeli, Mfalme wenu.
\s5
\v 16 Yahwe asema hivi, Ni nani aliyefungua njia katika bahari, na njia katika maji yenye nguvu,
\v 17 ni nani anayeongoza gari na farasi, majeshi na jeshi kuu. Walianguka chini kwa pamoja; hawakunyanyuka tena; wamezimwa, kama utambi unaoungua.
\s5
\v 18 Msifikirie hayo mambo yaliyopita, wala kuyafikiria mambo ya zamani.
\v 19 Tazama ninakaribia kufanya mambo mapya; sasa yanakaribia kutokea; Je humyajui haya? Nitafanya njia jangani na na mikondo ya maji katika jangwa
\s5
\v 20 Wanyama pori wa shambani wataniheshimu mimi, Mbweha na mbuni, kwa sababu ninatoa maji jangwani, na mito jangwani, ili watu wangu niliowachuga wapate kunjwa,
\v 21 Watu hawa niliowaumba mwenyewe, kwamba wahesabu tena sifa zangu.
\s5
\v 22 Lakini hamjanita mimi, Yakobo; umechoka na mimi, Israeli.
\v 23 Haujaniletea hata kondoo wako kama sadaka ya kuteketeza; na wala haujaniheshimu mimi kwa sadaka yako Sijakutumisha wewe kwa sadaka ya mazao, wala sijawachosha kwa sadaka yenu ya ubani.
\s5
\v 24 Hamkuninunulia mimi manukato mazuri kwa fedha, hakumwagia mimi mafuta ya sadaka zenu; Lakini mnanichosha mimi na dhambi zenu na mnanichosha mimi kwa matendo yenu mabaya.
\s5
\v 25 Mimi, ndio, Mimi, ndiye niliyafaye maovu yenu kwa niaba yangu mmi mwenyewe; na Sitawaita na kuwakumbusha dhambi zenu tena.
\v 26 Nikumbusheni mimi kilichotokea. Njooni tusemezane pamoja; leta hoja zako, ili kusudi uthibitishe kuwa hauna hatia.
\s5
\v 27 Baba yako wa kwanza alitenda dhambi, na viongozi wenu walitenda dhambi dhidi yangu.
\v 28 Hivyo basi Nitawatia unajisi viongozi watakatifu; Nitamkabidhi Yakobo kuwaharibu kabisa, na Israeli kulaani udhalilishaji.
\s5
\c 44
\p
\v 1 Sasa, sikiliza, Yakobo mtumishi wangu, na Isreli, Niliyekuchagua:
\v 2 Yahwe asema hivi, yeye aliyekufanya na kukuumba wewe katika tumbo na yeye aliye kusadia wewe: Usiogope, Yakobo mtumishi wangu; na wewe Yeshuruni, niliyekuchagua.
\s5
\v 3 Maana nitashusha mvua kwenye aridhi yenye kiu, na mikondo ya maji kwenye ardhi kavu; Nitashusha roho yangu kwa watoto wako, na baraka zangu kwa watoto wako.
\v 4 Watakuwa miongoni mwa nyasi, kama mti pembeni ya mkondo wa maji.
\s5
\v 5 Mmoja atasema, 'Mimi ni wa Yahwe; na mwingine ataita jina la Yakobo, na mwingine ataandika kwenye mkono wake 'Mimi ni wa Yahwe, na kujiita mwenyewe kwa jina la Israeli.''
\s5
\v 6 Yahwe asema hivi--Mfalme wa Israeli na Mkombozi wake, Yahwe wa majeshi: ''Mimi ni mwanzo na ni mwisho; na hakuna mungu ila mimi.
\s5
\v 7 Ni nani aliye kama mimi? Na atangaze na anielezee matukio yaliyotokea tangu nilipoanzisha watu wangu wa kale, na waache watangaze matukio yajayo.
\s5
\v 8 Usiogope wala usifadhaike. Je si mimi niliyekutangazia toka zamani, na nikatangaza? ninyi ni mashaidi wangu: Je kuna Mungu mwingine zaidi yangu? Hakuna Mwamba mwingine zaidi yangu; Ninajua hakuna.''
\s5
\v 9 Mitindo yote ya sanamu si kitu; vitu wanavyo vifurahia ndani havina maana; mashahidi wake hawawezi kuona au kujua chochote, na watapatwa katika aibu.
\v 10 Ni nani atengenezae miungu au sanamu zisizo na maana?
\s5
\v 11 Tazama, washirika wote watapatwa na aibu; mafundi ni watu tu. waache washikilie msimamao wao kwa pamoja; wataogopa na kuhaibishwa.
\s5
\v 12 Mhunzi anafanya kazi kwa vyombo vyake, kutengeneza, kufanya kazi kwenye makaa ya mawe. Hurekebisha kwa kutumia nyundo na hufanya kazi kwa mkono wake wenye nguvu. Hupata njaa, na nguvu zake humuishia; Hajanywa maji na huzimia.
\s5
\v 13 Seremala hupima mbao kwa kamba na kuiweka alama kwa kitu kikali. Huichonga kwa vyombo vyake na kuweka alama kwa kutumia dira. Huichonga baada ya sanamu ya mtu, kama mtu anyevutia, ili iweze kukaa ndani ya nyumba.
\s5
\v 14 Huikata chini mierezi, huchagua miti ya miseprasi au miti ya mialoni. Huchukua mti yeye mwenyewe katika msitu. huotesha mvinje na mvua huifanya ikue.
\s5
\v 15 Basi mtu hutumia kwa moto na kujipatia joto. Ndio, huwasha moto kuwooka mkate. Halafu hutengeneza miungu ili ausujudie;
\v 16 Huchoma sehemu ya kuni kwa moto, na huchoma nyama yake juu yake. hula na kushiba. huota moto na kusema, ''Ah, Nimepata joto, nimeouna moto.''
\s5
\v 17 Kwa kutumia mbao hutengeneza miungu, sanamu yake; huisujudu na kuhieshimu, huipa sifa na kusema, ''Niokoe mimi, maana wewe ni mungu wangu.''
\s5
\v 18 Hawajui, wala hawaelewi, maana macho yao yamepofuka na hawaoni, na mioyo yao haiwezi kufahamu.
\s5
\v 19 Hakuna anayefikiria, wala kuelewa na kusema, ''Nimechoma sehemu ya mbao kwenye moto; na pia nimewooka mkate kwa kutumia makaa yake. Nimechoma nyama kwa makaa yake nikala. Sasa Je ninaweza kutengeneza kitu kinachochukiza kwa ajili ya kuabudia kwa sehemu ya mbao iliyobakia? Je ninaweza kusujudia sanamu ya mbao?''
\s5
\v 20 Ni kama anayejilisha majivu; moyo wke mdanganyifu unampoteza yeye. Huwezi kujiokoa mwenyewe, wala hawezi kusema, ''Hiki kitu katika mkono wangu wa kulia sio mungu wa kweli.''
\s5
\v 21 Fikiria kuhusu vitu hivi, Yakobo na Israeli, maana wewe ni mtumishi wangu: Nimekuumba wewe; wewe ni mtumishi wangu:
\v 22 Nimeyafuta makosa yako, kama wingu zito, matendo yako mabaya, na wingu, ni kama dhambi zako; maana nimekukomboa wewe.
\s5
\v 23 Imba, enyi mbingu, maana Yahwe ameyafanya haya; piga kelele enyi mkaao katika nchi. Pazeni sauti enyi mlima milima, enyi misitu yenye miti ndani yake, ewe mlima, ewe msitu wenye kila aina ya mti ndani yak,; Maana Yahwe amemkomboa Yakobo, na nitakuonyesha utukufu wake katika Israeli.
\s5
\v 24 Yahwe asema hivi, Mkombozi wako, yeye aliyekuumba wewe kutoka tumboni: ''Mimi ni Yahwe, niliyefanya kila kitu, mimi mwenyewe nizinyooshae mbigu, mimi peke niitngenezae nchi.
\v 25 Mimi niliyezikata dalili za waongo na kuwaabisha wanaosoma dalili zake; Mimi niliyezigeuza busara za wenye hekima na kujeuza ushauri wao kuwa ujinga.
\s5
\v 26 Mimi, Yahwe, niliyethibitisha maneno ya mtumishi wake na kuutimiza utabiri wa mjumbe wake. Aliyezungumza kuhusu Yerusalemu, 'Atakuwa mwenyeji; na katika mji wa Yuda, 'Watatengeneza tena, na nitapatengeneza palipoharibika;
\v 27 awezae kusema kwa bahari kubwa, 'Kauka,' na yanakauka mda huo.'
\s5
\v 28 Yahwe ndiye amwambiye Koreshi, 'Ni mchungaji wangu, atafanya kila nilitakalo; atatoa amri kuhusu Yerusalemu, 'Utajengwa kwa upya, 'na kuhusu Hekalu, 'Basi na msingi wake uanzwe kuwekwa.''
\s5
\c 45
\p
\v 1 Yahwe asema hivi kwa mapakwa mafuta, kwa Koreshi, niliyemshika kwa mkono wa kuume, illi niweze kuangamiza mataifa mbele yake, kuwalinda wafalme, kufunguo milango mbele yao, ili lango liwe wazi:
\s5
\v 2 ''Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja vipandevivande milango ya shaba na kukuta vipandevipande nguzo za chuma,
\v 3 Nitakupa hazina iliyo gizani na utajiri uliofichwa mbali, ili ujue kwamba ni mimi Yahwe, niliyekuita kwa jina lako, Mimi, Mungu wa Israeli.
\s5
\v 4 Kwa niaba ya Jakobo mtumishi wangu, na Israeli chaguo langu, Nimekuita wewe kwa jina lako: nimekupa heshima iliyotukuka, jabo hakunijua mimi.
\v 5 Mimi ni Yahwe na hapana mwingine; hakuna Mungu ila mimi. Nitakuimarisha katika vita, japo hamkunifamu mimi;
\v 6 kwamba watu wajue kutoka mapambazuko ya jua, na kutoka magharibi, kwamba hakuna mungu mwngine ila mimi: Mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
\s5
\v 7 Nimefanya mwanga na nimeumba giza; Ninanateta amani na ninaumba majanga; Mimi Yahwe, nifanyae haya yote.
\v 8 Enyi mbingu, nyesha kutoka juu! Acha anga lishushe chini haki, na acha nchi inyonje haki, ili wokovu uweze kuchipukia juu, na haki kutawanyika kwa pamoja. Mimi Yahwe nimewumba wote kwa pamoja.
\s5
\v 9 Ole kwa yeyote anayesema kwa yule aliyemfanya yeye, kwake yeye ni kama chungu cha udongo miongoni mwa vyingu vya udongo katika aridhi! Je udongo umwambia mfinyanzi, 'Unatengeneza nini? au ' Kazi yako haina kitu cha kushika?
\s5
\v 10 Ole wake asemae kwa baba, 'Unanizaa nini? au kwa mwanamke, 'unanizaa mimi nin?'
\s5
\v 11 Yahwe asema hivi, yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, muumbaji wake: 'Kwa nini unauliza swali kuhusu nini nitakacho kifanya kwa watoto wangu? Je unaweza kuniambia kuuhusiana na kazi ya mikono yangu?
\s5
\v 12 Nimeifanya nchi na kuumba mtu juu yake. Ni mkono yangu mimi nilioinyoosha ju ya mbingu, na nikazimuru nyota zote kutokea.
\s5
\v 13 Nimemuinua Keroshi juu katika haki yangu, na nitalainisha njia zake zote. Ataujenga mji wangu kwa upya; atawachia walioko uhamishoni kurudi nyumbani kwao, na so kwa pesa wala kwa rushwa,'' asema Yahwe wa majeshi.
\s5
\v 14 Yahwe asema hivi, mapato ya Misri na bidhaa ya Ethiopia pamoja na Waseba jamii ya watu werefu, tatawaleta kwenu. Watakuwa wa kwenu. Watafuata baada yenu, watakuja na minyororo. Watakuinamia chini na kukuomba huku wakisema, 'Hakika Mungu yuko pamoja na wewe na hakuna mwingine ila yeye.''
\v 15 Hakika mna Mungu aliyejifisha ndani yenu, Mungu wa Israeli, Mkombozi.
\s5
\v 16 Wote wataabishwa na kuzaraliwa kwa pamoja; wale wachongao sanamu watatembea katika udhalilishaji.
\v 17 Lakini Israeli itakombolewa na Yahwe kawa wokovu wa milele; na wala hautaabika tena au kudhalilishwa.
\s5
\v 18 Yahwe asem hivi, nani aliyeziumba mbingu, Mungu wa kweli ndiye aliyeiumbwa nchi na kuifaya, ndiye aliyeianzisha nchi. Aliiumba yeye, sio kama taka, aliimba ili pawe na wenyeji: ''mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
\s5
\v 19 Sijaongea katika siri, katika maeneo ya siri; Sijauambia ukoo wa Daudi, 'Nitafute bure! Mimi ni Yahwe ninayezungumza ukweli; Ninatangaza vitu vilivyo vya kweli.
\s5
\v 20 Jikusanjeni wenyewe na mje! kusanyikeni kwa pamoja, enyi wakimbizi kutoka miongoni mwa mataifa! Hawana maarifa, wale wanaobeba sanamu ya kuchonga na kuiomba miungu asiyewasidia.
\s5
\v 21 Sogeeni karibu na mnitangazie mimi, leteni ushahidi! waache walete mashauri kwa pamoja. Ni nani aliyewaonyesha haya kutoka zamani? Ni nani aliyetangaza? Je sikuwa mimi, Yahwe? na hakuna Mungu mwingine ila mimi, Mungu mwenye haki; na mkombozi; hakuna mwingine zaidi yake.
\s5
\v 22 Nijeukieni mimi, na mkaokolewe, miisho yote ya nchi; Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine. Mimi mwenyewe ninaapa, ninaongea katika haki yangu, na sitarudi nyuma:
\v 23 'kwangu kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri.
\s5
\v 24 Wataniambia mimi, Ni katika Yahwe peke yake kuna wokovu na nguvu.'' wataaibika wale wote wenye hasira na Mungu.
\v 25 Katika Yahwe makabila yote ya Israeli yataalalishwa; watachukua kiburi katika yeye.
\s5
\c 46
\p
\v 1 Beli huaguka chini, Nebo husujudu; miungu yao imebebwa na wanyama na mzigo wa mnyama. Sanamu hizi mlizobeba ni mzigo mzito kwa wanyama kuchoka.
\v 2 Kwa pamoja wanashuka chini; hawawezi kuziokoa sanamu zao, na wao wenyewe wameenda uhamishoni.
\s5
\v 3 Nisikilizeni mimi, nyumba ya Yakobo, wote mliobaki kwenye nyumba ya Israeli mliochukuliwa na mimi kutoka kabla amjazaliwa, mlichukuliwa mkiwa tumboni.
\v 4 Hata kwa njie wazee Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitwachukua nyie na nitawakomboa nyie.
\s5
\v 5 Je utanifananisha mimi na nani? na mimi nimefanana na nani, ili utulinganishe?
\v 6 Watu humwaga dhahabu kutoka kwenye mabegi yao na uzito wa fedha kwenye uzani. Humuajiri mfua dhahabu, na hutengeneza kuwa dhahabu; na huinama chini na kuzisuju.
\s5
\v 7 Wanazinyanyua juu ya mabega yao na kuzibeba; wanaziweka katika sehemu yake, na itasimama katika eneo lake na alitasogea kutoka pale, hulilia, lakini haiwezi kujibu wala kumuokoa yeyote kwenye matatizo.
\s5
\v 8 Tafakari kuhusu hivi vitu; katu usivipuuzie, enyi waasi!
\v 9 Tafakari kuhusu vitu vya awali, nyakati zile zilizopita, Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine, Mimi ni Mungu na hakuna kama mimi.
\s5
\v 10 Mimi ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya kitu ambacho hakijatokea; Ninasema, ''Mpango wangu utatokea na nitafanya kama ninavyotamani.''
\v 11 Nitamuita ndege wa mawindo kutoka mashariki, Mtu ambaye ni chaguo langu kutoka nchi ya mbali; Ndio nimesema; na pia nitayatimiza haya, nimekusudia, na pia nitafanya hivyo.
\s5
\v 12 Nisikilize mimi, enyi watu makaidi, ambao mko mbali na kutenda mema.
\v 13 Ninaileta haki yangu karibu; na wala sio mbali, na wokovu wangu hausubiri; na nitatoa wokovu wangu kwa Sayuni na uzuri wangu kwa Israeli.
\s5
\c 47
\p
\v 1 Njoo chini na ukae kwenye mavumbi, binti bikira wa Babeli; kaa juu ya aridhi pasipo enzi, ewe binti wa Wakaldayo. Hautaitwa tena mpenda anasa na maisha ya anasa.
\v 2 Chukua jiwe la kusagia na usage unga; ondoa pazia lako, ondoa mavazi yako, ondoa viatu miguuni, na vuka mkondo wa maji.
\s5
\v 3 Uchi wako utafunuliwa, ndio, na aibu yako itaonekana; Nitachukua kizazi na sitamuacha mtu,
\v 4 Mkombozi, Yahwe wa majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.
\v 5 Kaa kimya na nenda katika giza, ewe binti wa Wakaldoyo; maana hautaitwa tena malikia wa falme.
\s5
\v 6 Nilikuwa na hasira na watu wangu; Nimeunajisi urithi wangu na kuwakabidhi nyie katika mkono wenu, lakini hamkuomyesha huruma; umeweka nira kubwa kwa wazee.
\v 7 Umesema, ''Nitaongoza daima kama malikia huru.'' Haukuvichukua vitu hivi katika moyo, wala hakutafakari jinsi hivi vitu vitakavyojeuka.
\s5
\v 8 Hivyo sasa sikiliza hili, Ewe upendae anasa na kukaa salama; ewe usemae katika moyo wako, 'Ninaishi, na hakuna mwingine kama mimi; Sitakaa kama mjane wala sitazoea kufiwa na watoto.
\v 9 ''Lakini vitu hivi vitakuja kwako siku moja katika kipindi cha siku moja; kwa nguvu za kutosha yatakuja kwako, japo uchawi wako na dua zako na hirizi.
\s5
\v 10 Umeweka imani katika mapungufu yako; na kusema, ''Hakuna anayeniona mimi''; hekima na maarifa yako yanakupoteza, lakini unasema katika moyo wako, ''Nipo na hakuna hata mmoja kama mimi.''
\v 11 Maafa yatakuzidi wewe; hautaweza kuyaondoa kwa dua zako mwenyewe. Uharibifu utakuwa juu yako; hautaweza kuukata. Maafa yatakuangamiza ghafla, kabla haujajua kitu.
\s5
\v 12 Endeleni kutoa uganga wako na wachawi wengi ambao mlioaminishwa kusoma toka utotoni mwao; labda utafanikiwa, labda utayashinda maafa.
\v 13 Umejaribu sana kwa kushauriwa sana; waache hao watu wasimame na kukuokoa wewe- wale wanaoangalia mbingu na wanoangalia nyota, wale wanotangaza mwenzi mpya- waache wawaokoe nyie kutoka kwenye yaliyowapata.
\s5
\v 14 Tazama, watakuwa kama mabua. Moto utayachoma juu. Hayataweza kujisaidia yenyewe kutoka kwenye mkono wa moto. Hakuna makaa kuwapa joto wao na hakuna moto uliowekwa pembeni kwa ajili yao!
\v 15 Hivi ndio wamekuwa kwako, wale unaofanya nao kazi, na unauza na kununua na wao toka ulipo kuwa mdogo, na wale wanaendelea kufanya mambo yao ya kijinga; na unapolia kuhitaji msaada, hakuna hata mmjoa ambaye atakukomboa wewe.''
\s5
\c 48
\p
\v 1 Sikiliza hili, nyumba ya Jakobo, mlioitwa kwa jina la Israeli, na mmetoka katika mbegu ya Yuda; yeye akirie kwa jina la Yahwe na kumuhusisha Mungu wa Israeli, lakini sio kweli wala kwa namna ya haki.
\v 2 Maana wanajiita wenyewewatu wa mji mtakatifu na kumuamini Mungu wa Israeli; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
\s5
\v 3 ''Nimetangaza vitu kutoka siku nyingi; Wamekuja nje kutoka mdomoni mwangu, na nimewafanya wajulikane; halafu gafla nimewafanyia, na yakatimia.
\v 4 Kwa sababu nilijua kwamba wewe ni mkaiidi, misuli ya shingo yako ni kama ya chuma, na paji la uso ni kama shaba,
\v 5 Hivyo basi nilitangaza vitu hivi kabla havijatokeo hivyo, nilikujulisha wewe, 'Sanamu yangu imefanya haya au sanamu yangu ya kuchonga na sanamu yangu ya kuyeyusha, yamekwishisha vitu.
\s5
\v 6 Umesikia kuhusu mambo haya; angalia ushahidi wote; na wewe, Je hautakubali kwamba ninacho kisema ni cha kweli? Kuanzia sasa na kuendelea Nitawaonyesha vitu vipya, mambo yaliyofichika ambayo hamkuyajua.
\v 7 Sasa, na sio yaliyopita, yamekuwa sasa, na kabla ya leo hamkusikia kuhusu wao, hivyo hautaweza kusema, 'Ndio, nilijua kuhusu wao.'
\s5
\v 8 Haukusikia; haukuelewa; haya mambo hayakufuniliwa katika masikio kabla ya. Maana nilijua kwamba umekuwa mdanganyifu, na kwamba umekuwa muasi kutoka kuzaliwa.
\s5
\v 9 Kwa niaba ya jina langu nitahairisha asira yangu, na kwa heshima yangu nitajizuia kutokumuharibu yeye.
\v 10 Tazama, Mimi niliwaandaa ninyi, lakini sio kama fedha; Nimekusafisha wewe katika tanuru la mateso.
\v 11 Kwa niaba yangu, kwa niaba yangu nitafanya; maana ni kwa jinsi gani niruhusu jina langu lisiheshimike? Sitampa utukufu wangu mtu yeyote.
\s5
\v 12 Nisikilize mimi, Yakobo, na Israeli niliyekuita: Mimi ndiye; Mimi ni wa kwanza, na pia wa mwisho.
\v 13 Ndio, mkono wangu umeweka msingi wa nchi, na mkono wangu wa kuume ulizitawanya mbingu, zimesimama juu kwa pamoja.
\s5
\v 14 Jikusanyeni wenyewe, nyinyi nyote, na sikilizeni; ni nani miongoni mwenu atangazaye mambo haya? Yahwe atakamilisha lengo lake dhidi ya Babeli. Atachukua mapenzi ya Yahwe dhidi ya wa Wakaldayo.
\v 15 Mimi, nimezungumza, ndio, nimemchagua yeye, nimemleta yeye, na yeye atafanikiwa.
\s5
\v 16 Sogea karibu na mimi, sikiliza hili; kutoka mwanzo sikuzungumza katika siri; lakini ilipotokea, Mimi niko hapa; na sasa Bwana Mungu amenituma mimi, na Roho wake.''
\s5
\v 17 Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli anasema, ''Mimi ni Yahwe Mungu wenu, ninayewafundisha juu ya kufanikiwa, ninayewaonyesha njia mtakayoiptia.
\v 18 Ikiwa kama mtaheshimu amri zangu! Hivyo amani na maendeleo yatatiririka kama mto, na wokovu wenu ni kama mawimbi kwenye bahari.
\s5
\v 19 Watoto wako watakuwa wengi kama mchanga, na watoto kutoka kwenye tombo zenu watakuwa wengi kama nafaka kwenye mchanga; majina yao hayataondolewa wala kufutwa mbele yangu.
\s5
\v 20 Tokeni nje ya Babeli! wakimbieni Wakaldayo! kwa sauti ya kupiga kelele tangaza kwamba! hakikisha hili linajulikana, hakikisha hili linafika mpaka miisho ya nchi! sema 'Yahwe amemkomboa Yakobo mtumishi wake.
\s5
\v 21 Hawakupatwa na kiu alipowaongoza katika jangwa, alifanya maji kutokea kwenye mwamba kwa ajili yao; aliugawa na kufungua mwamba, na maji yakatoka nje.
\v 22 Hakuna amani kwa watenda makosa- amesema Yahwe.''
\s5
\c 49
\p
\v 1 Nisikilize mimi, enyi mkao pwani! na kuwa makini, enyi watu mkao mbali. Yahwe amenita mimi kutoka kuzaliwa kwa jina, mama yangu aliponileta duniani.
\v 2 Amefanya mdomo wangu kuwa kama upanga mkali; amenificha mimi katika kivuli cha mkono wake; amenifanya mimi kuwa mshale unaong'aa; katika podo yake amenificha mimi.
\s5
\v 3 Amesema na mimi, ''Wewe ni mtumishi wangu, Israeli, kupitia yeye nitaonyesha utukufu wangu.''
\v 4 Lakini nilimjibu, ''Japo nilifikiria nilifanya kazi bure, nimetumia nguvu zangu bure, ikiwa haki yangu iko pamoja na Yahwe, na zawadi yangu iko kwa Mungu wangu.
\s5
\v 5 Na sasa Yahwe asema hivi, yeye aliyeniumba mimi toka kuzaliwa na kuwa mtumishi wake, kumrejesha Yakobo tena kwake mwenyewe, na Israeli wakusanyike kwake. Mimi ninaheshimika katika macho ya Yahwe, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu.
\v 6 Asema hivi, ''Ni kitu kidogo sana kwa wewe kuwa mtumishi wangu ili kuanzisha ukoo wa Yakobo, na kuwarejesha wanaoishi Israeli. Nitakufanya wewe kuwa mwanga kwa Wayunani, ili uwe wokovu wangu katika mipaka ya nchi.
\s5
\v 7 Yahwe asema hivi, Mkombozi wa Israeli, Mtatakatifu wao, kwa yeye ambae maisha yake yamedharauliwa, kuchukiwa na mataifa, na mtumwa wa viongozi, ''Mfalme atakuona wewe na nyanyuka, na wakuu watakuona wewe na inama chini, kwa sababu ya Yahwe ambae ni mwaminifu, hata mtakatifu wa Israeli, aliyewachagua ninyi.''
\s5
\v 8 Yahwe asema hivi, ''Kwa mda huu nimeamua kuwaonyesha neema yangu na nitawajibu ninyi, na siku ya wokovu nitawasaidi ninyi; Nitakulinda wewe; na nitawapa kama agano kwa watu, kuitengeneza tena nchi, kuwarihtisha urithi uliokuwa na ukiwa.
\s5
\v 9 Utasema kwa wafungwa, 'Tokeni nje; kwa wale mlio katika giza gerezani, 'Jionyeshe mwenyewe. 'Watachunga pembeni ya barabara, na juu ya miteremko ya wazi yatakuwa malisho yake.
\s5
\v 10 Hawatasikia njaa wala kiu; wala joto au jua halitawaunguza, kwa yeye mwenye huruma juu yao atawaongoza wao; atawaongoza wao kwenye mikondo ya maji.
\v 11 Na nitafanya milima yote kuwa barabara, na kufanya njia za juu kuwa sawa''
\s5
\v 12 Tazama, haya yatatoka kutoka mbali, baadhi kutoka kaskazini na magharibi; na wengine kutoka nchi ya Sinimi.
\v 13 Imba, ewe mbingu, na uwe na furaha, ewe nchi pazeni sauti ya kuimmba enyi milima! maana Yahwe anawafariji watu wake, na watakuwa na huruma kwa wale wanoteseka.
\s5
\v 14 Lakin Sayuni asema, Yahwe ameniacha mimi, na Bwana amenisahau mimi.''
\v 15 ''Je mwanamke anaweza kumsahau mtoto wake, aliyemnyonyesha, hivyo hana huruma na mtoto aliye mzaa? ndio, hawakusahau, lakini siwezi kukusahau wewe.
\s5
\v 16 Tazama, nimeliandika jina lako kwenye kiganja cha mkono wangu; Kuta zako zinaendelea kuwa mbele yangu.
\v 17 Watoto wangu wamerudi haraka, wakati wale wanowaangaimiza nyie wameenda mbali.
\v 18 Tazama karibu na uone, wote wamekusanyika na wanakuja kwako. Nitahakikisha kama ninaishi- hili ni tamko la Yahwe- hakika mtavivaaa kama kama kijiti; utajifungia kama bibi harusi.
\s5
\v 19 Japo umeharibiwa na kuwa na ukiwa, nchi iliyoharibiwa, sasa itakuwa ndogo sana kwa wenyeji, na wale wanao waliokumeza watakuwa mbali,
\v 20 Watoto watakaozaliwa katika kipindi cha msiba watasema mkiwa mnawasikiliza, 'Sehemu hii ni duni kwetu, tengeneza chumba kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi hapa.
\s5
\v 21 Halafu utajiuliza mwenyewe, ni nani aliyewazaa watu hawa kwangu? Mimi nilifiwa na ni tasa, niliyefungwa na kupewa talaka. Ni nani aliyewalea hawa watoto? Tazama, niliachiwa yote mimi mwenyewe; Je haya yametoka wapi?''
\s5
\v 22 Yahwe asema hivi, ''Tazama, nitanyanyua mkono wangu juu ya mataifa; Nitanyanyua bendera yangu ya ishara kwa watu. Watawaleta watoto wako kwenye mikono yao na watawabeba binti zako juu ya mabega yao.
\s5
\v 23 Wafalme watakuwa baba zako wa kambo, na malikia watakuwa wafanyakazi wa ndani; watakuinamia chini wewe kw uso wao kwa nchi na kukung'uta mavumbi ya miguu yenu; wale wanonisubiri mimi hawataabika.''
\s5
\v 24 Je mateka wanaweza kuchukuliwa kwa shujaa, au wafungwa kukombolewa kutoka kwa mkali?
\v 25 Lakini Yahwe asema hivi, ''Wafungwa watachukuliwa kutoka kwa shujaa, na maeteka watakombolewa; maana utampinga adui yako na kuwakomboa watoto wako.
\s5
\v 26 Na nitawalisha wanowaonea kwa mwili wao wenyewe; na watalewa kwa damu zao wenyewe, kama iliyo mvinyo; na watu wote watajua kwamba Mimi Yahwe, ni Mokozi wenu na Mkombozi wenu, yeye aliyemkuu wa Isareli.
\s5
\c 50
\p
\v 1 Yahwe asema hivi, ''Kiko wapi cheti cha talaka ambacho nimempa tataka mama yako? na kwa nani niliowauza mimi? Tazama, umewauza kwa sababu ya dhambi zako, na kwa sababu ya uasi wako, na mama yako amepelekwa mbali.
\s5
\v 2 Kwa nini nimekuja maana hakuna mtu pale? Kwa nini nimeita lakini hakuna aliyejibu? Je mkono wangu ni mfupi kukufidia wewe? Je hakuna nguvu katika ukombozi wngu kwako? Tazama, maonyo yangu, nimeikausha bahari; nimeufanya mto kuwa jangwa; samaki wake wamekufa na kuoza kwa kukosa maji.
\v 3 Nimelivisha giza; na ku kwa ngfunika nguo za magunia.''
\s5
\v 4 Bwana Yahwe amenipa mimi lugha kama wale wanayofundishwa, ili kwamba nizungumze maneno ya kudumisha kwa yeye aliyechoka; huniamsha mimi asubuhi kwa asubuhi; huyaamsha masikio yangu kama wale wanofundisha.
\s5
\v 5 Bwana Yahwe amefungua sikio langu, na sikuaasi, wala kurudi nyuma.
\v 6 Niliwapa mgongo wangu wale wanaonipiga mimi, na shavu langu kwa wale wanaopokonya nje ndevu zangu; Sitouficha uso wangu kutokana na matendo ya aibu na kutema mate.
\s5
\v 7 Maana Bwana Yahwe atanisaidia mimi; hivyo basi sitapatwa na aibu; hivyo nimeufanya uso wangu kama jiwe, maana ninajua kwamba sitaabishwa.
\s5
\v 8 Yeye aliye nitakasa mimi yu karibu. Ni nani atakayenipinga mimi? Basi na tusimame tufarijiane mmoja mmoja. Nani aliye mshitaki? Muache aje karibu na mimi.
\v 9 Tazama, Bwana Yahwe atanisaidia mimi. Nani atakayetangaza kuwa mimi ni mwenye hatia? Tazama, watavaa nje kama vazi; mdomo utawala wao juu.
\s5
\v 10 Ni nani miongoni mwenu anayemuogopa Yahwe? Ni nani anayehieshimu sauti ya Yahwe? Ni nani atakayetembea kwenye giza nene pasipo mwanga?
\s5
\v 11 Tazama, ninyi nyote mnaowasha, ni nani aliyewapa wenyewe kwa tochi: tembeni katika mwanga wa moto wenu na katika moto mliouwasha. Hili ndilo mlilopokea kutoka kwangu: utalala chini katika mahali pachungu.
\s5
\c 51
\p
\v 1 Nisikilizeni mimi, enyi mtendao haki, enyi mtafutaye Yahwe: Tazama katika mwamba uliouchonga nakuchimba kutoka pale ulipopakata.
\s5
\v 2 Mtazameni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa ninyi; maan alipokuwa na upweke yeye mwenyewe, Nilimuita yeye. Nikambariki yeye na kumfanya yeye kuwa wengi.
\s5
\v 3 Ndio, Yahwe ataifariji Sayuni; Ataifariji miji yake yote iliyo na ukiwa; jangwa lake atalifanya kama Edeni, na jangwa lililo wazi pembeni ya bonde la mto Yordani kama bustani ya Yahwe; Furaha na shangwe vitakuwa kwake, shukrani, na sauti ya kuimba.
\s5
\v 4 ''Kuwa makini kwangu, watu wangu; na nisikilizeni mimi, watu wangu! Maana nitatoa amri, na nitaifanya haki yangu kuwa sheria ya mataifa.
\v 5 Haki yangu ipo karibu; wokovu wangu utaenda nje, na mikono yangu itahihukumu mataifa; Pwani itanisubiri mimi; maana wanashauku ya kuhusubiria mkono wangu.
\s5
\v 6 Nyanyueni macho yanu juu angani, na tazama nchi chini, maana mbingu zitatoweka mbali kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, na wenyeji wake watakufa kama inzi. Lakini wokovu wangu utaendelea daima, na haki yangu haitaacha kutenda kazi.
\s5
\v 7 Nisikizeni mimi, enyi mnaotambua ukweli, enyi watu wangu mliobeba sheria yangu katika mioyo yenu: Msiogope matusi ya watu, wala kukatishwa tamaa na unyanyasaji wao.
\v 8 Maana Nonda watawala wao kama vazi, na minyoo itawala wao kama sufu; lakini haki yangu itakwa daima, na wokovu wangu katika vizazi vyote.''
\s5
\v 9 Amka, amka, jivishe wewe mwenyewe kwa nguvu, mkono wa Yahwe. Amka kama siku za zamani, kizazi cha nyaktii za kale, Je sio wewe uliyeangamiza mnyama wa baharini, na uliyemchoma joka?
\v 10 Je haukukausha bahari, maji ya kina kirefu, na kufanya kina cha bahari kuwa nija ya ukombozi kupita?
\s5
\v 11 Fidia ya Yahwe itarudi na kwenda Sayuni kwa kilio cha furaha na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao, na huzuni na kuomboleza vitatoweka mbali.
\s5
\v 12 ''Mimi, mimi ndiye niwapae faraja. Kwa nini uwaogope watu, ambao wanakufa, watatoto wa wanadamu, waliofanywa kama majani?
\s5
\v 13 Kwa nini umemsahau Yahwe Muumba, yeye azinyooshayembingu na kuweka misingi ya nchi? Nyie ambao mna hofu za mara kwa mara kila siku kwa sababu ya hasira ya moto ya wanyanyasaji anapo fanya maamuzi ya kuangamiza. Iko wapi hasira ya wanyanyasaji?
\s5
\v 14 Yeye aliyeinama chini, Yahwe atafanya haraka kumuachia; hatakufa wala kwenda chini katika shimo, wala hatakosa mkate.
\v 15 Maana Yahwe Mungu wenu, anaye ifanya bahari itembee, hivyo mawimbi yake yavume kwa kishindo- Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
\s5
\v 16 Niweka maneno yangu mdomoni mwako, na nimekufunika wewe kwa kivuli cha mkono wangu, ili niweze kupanda mbingu, kuweka misingi ya nchi, na kutamkia Sayuni, 'ninyi ni watu wangu.''
\s5
\v 17 Amka, amka, simama juu, Yerusalemu, ewe unyweae katika kikombe cha hasira ya Yahwe kutoka mkononi mwako; umekunjwa katika kikombe, kikombe cha mateso, na umekunjwa na kumaliza.
\v 18 Hakuna hata mmoja miongoni mwa watoto aliyewazaa wa kumuongoza yeye; hakuna hata mmoja miongoni mwa wote aliyewalea wa kumshika mkono wake.
\s5
\v 19 Shida hizi mbili ziliwatokea ninyi- ni nani atahuzunika pamja nanyi? - ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga. Ni nani atakayekufariji wewe?
\v 20 Watoto wako walizimia; walilala kila kona ya mtaa, kama swala kwenye mtego; Wamejawa na hasira ya Yahwe, Laana ya Mungu wako.
\s5
\v 21 Lakini sasa sikiliza hili, ewe uliodhulumiwa na kulewa, lakini sio kwa mvinyo:
\v 22 Bwana wenu Yahwe Mungu, anayewasihi watu wake, asema hivi, ''Tazama, Nimechukua kikombe cha ukubwa mkononi mwako- ukubwa wa kikombe cha hasira yangu - ili usiweze kunjwa tena.
\s5
\v 23 Nitakuweka kwenye mikono ya watesaji, wale waliokuambia wewe, Lala chini, ili tutembee juu yako'; wameufanya mgongo wako kama uwanjwa na kama wao wa.''
\s5
\c 52
\p
\v 1 Amka, amka, vaa nguvu zako, Sayuni; vaa vazi lako zuri, mji mtakatifu; maana hakuna tena kutotahiriwa wala wasio safi kuingia kwako.
\s5
\v 2 Jikung'ute mwenyewe kutoka mavumbini; nyanyuka na ukae, ewe Yerusalemu; ondoa shanga katika shingo yako, wafungwa, binti ya Sayuni.
\v 3 Maana Yahwe asema hivi, umeuzwa bure, na utakombolewa pasipo pesa.''
\s5
\v 4 Maana Bwana Yahwe asema hivi, ''Hapo mwanzo watu wangu walishuka chini Misri kuishi kwa muda mfupi; Waasiria waliwanyanyasa wao hivi karibuni.
\s5
\v 5 Sasa ni kitu gani nilicho nacho hapa- Hili ni tamko Yahwe- aonae kwamba watu wake wanachukuliwa bure tu? Wale wanowaongoza wao wanafanya mzaha-Hili ni tamko la Yahwe- jina langu linakashifiwa mchan kutwa.
\v 6 Hivyo basi watu wangu watalijua jina langu; watajua kwamba siku hiyo kwamba mimi ndiye ninayesema ''Ndiyo, Ni Mimi!''
\s5
\v 7 Ni kwa uzuri gani juu miliima ni miguu ya mjumbe aliyeleta habari njema, atangazae amani, aliyebeba uzuri wa ukuu, aliyetangaza wokovu, anayesema kwa Sayuni, ''Mungu wako anatawala!''
\v 8 Sikiliza enyi walinzi nyanyueni sauti zenu, kwa pamoja pigeni kelele kwa furaha, maana mtamuona, kwa kila jicho lenu, kurejea kwa Yahwe Sayuni.
\s5
\v 9 Pazeni sauti kwa kuimba kwa furaha, enyi mateka wa Yerusalemu; maana Yahwe amefariji watu wake; ameikomboa Yerusalemu.
\v 10 Yahwe amewaonyesha kwamba mkono wake mtakatifu katika macho ya mataifa yote; nchi yote itauona wokovu wa Mungu wetu.
\s5
\v 11 Ondokeni, ondokeni, enendeni mbali na hapa; msiguse kitu chochote ambacho ni najisi; au kuishi katikati yake; jitakase mwenyewe, enyi mliobeba vyombo vya Yahwe.
\v 12 Maana hautakwenda nje kwa kukimbia, wala hautaondoka kwa hofu; Maana Yahwe atakuwa mbele yako; na Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi wako nyuma.
\s5
\v 13 Tazameni, mtumishi wangu atafanya hekima; atakuwa juu na atanyanyuliwa juu, na atapandishwa juu.
\v 14 Na wengi watamstajabia yeye- muonekano wake umekunjamana nje ya muonekano wa mwanadamu, hivyo basi upande wake ulikuwa mbali na kitu chochote ambacho ni binadamu-
\s5
\v 15 Na hivyo, mtumishi wangu atanyunyizia mataifa mengi na wafme watafunga midomo yao kwa sababu yake. Kana kwamba hawajawahi kuambiwa, wataona, kana kwamba hawakusikia, wataelewa.
\s5
\c 53
\p
\v 1 Ni nani angeweza kuamini tuliyasikia? Na mkono wa Yahwe, kwake uliojidhihirisha?
\v 2 Maana amekuwa mbele za Yahwe kama sampuli, na kama chipukizikatika aridhi kavu; hakuna maajabu yalionekana au mapambo; tulipo muona yeye, hapakuwa na uzuri kutuvutia sisi.
\s5
\v 3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni, na mwenye maumivu. Kama mmoja aliyetoka kwa watu wafichao nyuso zao, alidharauliwa; na kujfikiria kuwa asiye na faida.
\s5
\v 4 Lakini hakika amezaliwa ugonjwa wetu na kubeba huzuni yetu; tulidhani aliadhibiwa na Mungu, amepigwa na Mungu, na kutaabishwa.
\s5
\v 5 Lakini alichomwa kwa sababu ya uaasi wa matendo yetu; aliangamizwa kwa sababu ya dhambi zetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
\s5
\v 6 Sisi ni kama kondoo tumepotoka; kila mmoja amejeuka katika njia yake, na Yahwe amemueka juu yake maovu kwetu sisi sote.
\s5
\v 7 Aliteswa; lakini alinyenyekea mwenyewe, hakufungua mdomo wake; kama kondooendae kuchinjwa, na kama kondoo mbele ya mtu anayemkata mnyoa yake taratibu, hivyo hakufungua mdomo wake.
\s5
\v 8 Kwa kutumia nguvu na hukumu yeye aliyelaaniwa; ni katika kizazi hicho atafikiria zaidi kuhusu yeye? Lakini aliondolewa katika aridhi ya walio hai; kwa sababu ya makosa ya watu wangu na adhabu ilikuwa juu yake.
\v 9 Wameliweka kaburi lake pamoja nawahalifu, kwa utajiri wa mtu katika kifo chake ingawa hakuwa na vurugu wala udanganyifu wowote katika mdomo wake.
\s5
\v 10 Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Yahwe kumponda yeye na kumfanya yeye apone. Alipoyafanya maisha yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi, ataona watoto wake, ataongeza siku zao, na mapenzi ya Yahwe yatatimizwa kupitia yeye.
\v 11 Baada ya mateso ya maisha yake, ataona mwanga na ataridhika kwa maarifa yake.
\s5
\v 12 Hivyo basi Je ninaweza kumpa yeye sehemu yake miongoni mwa wengi, naye atatawnya mateka kwa wengi, kwa sabubu amejionyesha yeye mwenye kwenye kifo na amehesabiwa na wahalifu. Amezaa dhambi za wengi na kufanya maombolezo kwa wahalifu.
\s5
\c 54
\p
\v 1 ''Imba, ewe mwanamke tasa, ewe ambaye haujazaa; imba wimbo kwa furaha na lia kwa nguvu ewe ambaye hujapata uchungu wa kuzaa. Maana watoto walio katika ukiwa ni wengi kuliko watoto wa wanawake waliolewa,'' asema Yahwe.
\s5
\v 2 Fanya hema lako kuwa kubwa na tawanya mapazia mbali, sio kidogo; nyoosha kamba zako na imarisha vigingi vyako.
\v 3 Maana utawanjwa katika mkono wa kulia na wa kushoto, na ukoo wako utashinda mataifa na kuwapatia miji iliyo na ukiwa.
\s5
\v 4 Usiogope maana hautahaibika, wala kukatishwa tamaa maana hautapatwa na aibu; hutasahau aibu ya ujana wako na aibu ya kutelekezwa.
\s5
\v 5 Maana Muumba ni mume wako; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. Mtakatifu wa Israeli yeye ni mkombozi wenu; anaitwa Mungu wa nchi yote.
\v 6 Yahwe anakuita wew urudi kama mwanamke aliyetelekezwa na mwenye roho ya huzuni, kama mwanamke mdogo aliyeolewa na kukataliwa, asema Mungu.
\s5
\v 7 ''Kwa kipindi kifupi nimewatelekeza ninyi, lakini kwa huruma kubwa nitawakusanya ninyi.
\v 8 Katika gharikia ya hasira nimeuficha uso wangu kwa muda. lakini kwa agano la milele la kuaminika nitakuwa na huruma na ninyi- amesema Yahwe, aliyewakomboa ninyi.
\s5
\v 9 Maana haya ni kama Nuhu kwangu: kama nilivyoapa maji ya Nuhu hayuatapita tena katika nchi, Hivyo nimeapa kwama sitapatwa na hasira na ninyi wala kuwakemea ninji.
\v 10 Japo milima yaweza kuanguka na vilima vyaweza kutikiswa, japo uimara wa pendo langu hautageuka nyuma kutoka kwenu, wala agano langu la amani kutikiswa- asema Yahwe, Yeye mwenye huruma juu yenu.
\s5
\v 11 Wanaotaabika, wanaopitia dhoruba na wasio na faraja, tazama, nitaweka lami kwa rangi nzuri, na kuweka misingi kwa yakuti.
\v 12 Nitaufanya mnara wa akiki na lango yake ya almasi na kuta zake za nje ni za mawe mazuri.
\s5
\v 13 Na watoto wako wote watafundishwa na Yahwe; na amani ya watoto wako itakuwakubwa.
\v 14 Katika haki nitakuanzisha tena. Hautaona dhiki tena, maana hautaogopa, na hakuna kitu cha kutisha kitakachokuja karibu yako.
\s5
\v 15 Tazama, ikiwa yeyote atakaye koroga matatizo, hayatako kwangu; yeyote atakaye changanya matatizo pamaoja na wewe ataanguka kwa kishindo.
\v 16 Tazama, nimemumba fundi, anayepuliza makaa yanayoungua na na kuanda a silsha kama kazi yake, na nimemumba mharibifu ili awaharibu.
\s5
\v 17 Hakuna silaha iliyotengenezwa dhidi yako ikafanikiwa; na utamlaani kila mmjoa anayekutusi wewe. Huu ndio urithi wa watumishi wa Yahwe, na uthibitisho wake kutoka kwangu- Hili ndilo tamko la Yahwe.''
\s5
\c 55
\p
\v 1 ''Njooni, kila aliye na kiu, njooni kwenye maji! na ewe usio na pesa, njoo, ununua na ule! Njoo, nunua mvinyo na maziwa pasipo pesa na pasipo gharama.
\s5
\v 2 Kwa nini tunapima fedha kwa kitu ambacho sio mkate? na kufanya kazi isiyoridhisha? Nisikilizeni mimi kwa makini na ule kilicho kizuri, na kujifurahisha mwenyewe kwa unono.
\s5
\v 3 Jeuzeni masikio yenu, na mje kwangu! Sikiliza, iliuweze kuishi! Nitafanya agano ya milele na ninyi; pendo langu la kuaminika nililomuhaidi Daudi.
\v 4 Tazama, nimwemuweka yeye kama shahidi kwa mataifa, kama kiiongozi na kamanda wa watu.
\s5
\v 5 Tazama, utaliita taifa ambalo haulijui; na taifa ambalo halikujui wewe litakukimbilia wewe kwa sababu wewe ni Yahwe Mungu wao, Mtakatifu wa Israeli, yeye aliyekutukuza wewe.
\s5
\v 6 Mtafuteni Yahwe maana anapatikana; muiteni yeye maana yu karibu.
\v 7 Tuwaache waovu waziache njia zao, na mtu mwenye dhambi mawazo yake. Muache yeye arudi kwa Yahwe, na atamuhurumia yeye, na kwa Mungu wetu, yeye ambaye atamsamehe huyo kwa wingi.
\s5
\v 8 Maana mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zangu sio njia zenu- Hili ni tamko la Yahwe-
\v 9 maana kama vile mbingu zilivyo juu kuliko nchi, hivyo ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
\s5
\v 10 Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji,
\v 11 hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lilie nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma.
\s5
\v 12 Maana utakwenda nje katika furaha na utaongozwa kwa amani; Milima na vilima vitapaza sauti kwa furaha mbele yako, na miti yote shambani itapiga makofi.
\v 13 Badala ya miiba ya porini, misonobari itakuwa; na badala ya mbigiri, mihadasi inaota, na itakuwa kwa Yahwe, maana jina lake, ni kama alama ya milele ambayo haiwezi kuondolewa.''
\s5
\c 56
\p
\v 1 Yahwe asema hivi, ''Fanyeni yaliyo sahihi, fanyeni yaliyo ya haki; maana wakovu wangu u karibu, na haki yangu inakaribia kujidhihirisha.
\v 2 Abarikiwe mtu yule ataendae haya, anayeyashika sana. Anaifuata sabato, na haitii unajisi, azuiaye mkono wake usitende maovu.''
\s5
\v 3 Usimuache mgeni yeyote aliyekuwa mfuasi wa Yahwe aseme, ''Yahwe atahakikisha ananiondoa kwa watu wake.'' Toashi ataweza kusema, ''tazama, mimi ni mti mkavu.''
\s5
\v 4 Yahwe asema hivi, kwa matoashi wanaoitimiza sabato yangu huchagua mambo yanayonipendeza mimi, na hushika kwanza agano langu,
\v 5 kwao nitaiweka nyumba yangu na ndani ya kuta zangu kumbukumbu ambayo ni kubwa kuliko kuwa na vijana na mabinti. Nitawapa kumbumbu ya milele ambalo halitaondolewa.
\s5
\v 6 Pia wageni ambao wataungana wenyewe kwa Yahwe- kwa ajili ya kumtumikia yeye, na yeye alipendae jina la Yahwe, kumuabudu yeye, na kila anayeheshimu sabato na wale wanoitunza isitiwe najisi, na wale walishikao agano langu
\v 7 nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu na kuwafaya muwe na furaha katika nyumba yangu ya maombi; matoleo na sadaka zenu zitakubalika katika mathebau yangu. Maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi kwa mataifa yote.
\s5
\v 8 Hili ni tamko la Yahwe, anayewakusanya watu wenye ukiwa katika Israeli- nitaendelea kuwakusanya wenginwe ili kuwaongeza wao.''
\s5
\v 9 Enyi nyote wanyama pori mlioko porini, njooni na mle, enyi wanyama mlioko msituni, Walinzi wao wote ni vipofu, hawaelewi.
\v 10 Wote ni mbwa wapole ambao hawawezi kubweka. Wanaota, na wanalala chini maana wanapenda kulala.
\s5
\v 11 Mbwa wanahamu kubwa; hawajawahi kuridhika; wachungaji wao hawawatambui; wamejeuka katika njia zao wenyewe, kila mmoja ana tamaa kupata faida isiyo yaa haki.
\v 12 ''Njooni, ''Tunywe mvinyo na pombe. Kesho itakuwa kama leo, siku kubwa zaidi ya kipimo.''
\s5
\c 57
\p
\v 1 Wenye waki watatoweka, lakini hakuna mtu atakayelitia maanani, na watu wa agano la kuaminika wamekusanyika mbali, lakini hakuna mtu anayefahamu kuwa wenye haki wamekusanyika mbali na maovu,.
\v 2 Wameingia katika amani; wamepumzika katika vitanda vyao, wale wanotembea katika haki.
\s5
\v 3 Lakini njooni hapa, enyi watoto wa wachawi, watoto wa wazinifu na mwanamke anayefanya ukahaba.
\v 4 Ni nani mnayemfanyia mzaha? dhidi ya wale wanofungua midomo yao na kutoa nje ndimi zao? Je ninyi sio watoto wa uaasi, watoto wa uongo?
\s5
\v 5 Enyi unaowasha wenywe kwa kulala pamoja chini ya mualoni, kila chini ya mti mbichi, ewe unaeua watoto wako katika mabonde yaliyokauka, chini ya miamba inayoning'inia.
\s5
\v 6 Miongoni mwa vitu vilaini katika bonde la mto ni mambo uliyopewa uyafanyie kazi. Ni vitu vya ibada yako. Umemwaga nje kinywaji chako kwao na kutoa sadaka ya mazao. Katika haya mambo Je ninaweza kuwa radhi na mambo haya?
\s5
\v 7 Umeandaa kitanda chako juu ya mlima mrefu; pia umeeda pale juu kutoa sadaka.
\v 8 Nyuma ya mlango na mihimili ya milango umeweka ishara zako; umeniweka mimi furagha, umejifunua wewe mwenywe, na kwenda juu; umekifanya kitanda changu kuwa kikubwa. Umefanya agano na wao; ulipenda vitanda vyao; uliona sehemu zao za siri.
\s5
\v 9 Ulienda kwa Moleki pamoja na mafuta; umeongeza marashi. Ulimtuma balozi wako mbali sana; Alikwenda chini kuzimu.
\v 10 Ulichoka kwa safari yako ndefu, lakini haukusema, ''Haina matumaini.'' Umeyatafuta maisha katika mkono wako; Hivyo basi haukudhoofika.
\s5
\v 11 Ni uliyemuogopa? Ni nani uliye muhofia zaidi ambaye aliyekufanya wewe kutenda udanganyifu, kwa wingi namna hiyo ambapo hauwezi kunikumbuka mimi au kufikiria kuhusu mimi? Maana nilikuwa kimya kwa mda mrefu, hauniogopi mimi tena.
\v 12 Nitatangaza matendo haki yako na nitawaambia kila kitu ulichokifanya, lakini hawatakusaidia.
\s5
\v 13 Utakapolia nje, wacha sanamu ulizozikusnya zikusaidie wewe. Badala yake upepo utavipeperusha vyote, punzi itavipeperusha mbali. Lakini yeye anayenikimbilia mimi atairithi aridhi na atachukua umiliki katika mlima wangu mtakatifu.
\s5
\v 14 Atasema, 'Jenga, jenga! safisha njia! ondoeni vizuizi vyote katika njia ya watu wangu!''
\v 15 Maana yeye allye juu palipoinuka, anayeishi katika uzima wa milele, ambaye jina lake ni mtakatifu, asema hivi, ''Ninaishi mahali pa juu na mahali patakatifu pamoja na yeye pia aliyemnyenyekevu na moyo uliopondeka, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu na kufufua mioyo ya wanaojutia.
\s5
\v 16 Maana sitawahukumu milele, wala sitakuwa na hasira milele, Kisha roho ya mtu itazimia mbele yangu, maisha niliyowafanyia.
\v 17 Kwa sababu ya dhambi ya mapato ya vurugu zake, Nilipatwa na hasira, na nikamuadhibu yeye; niliuficha uso wangu, nilikuwa na hasira, lakini alirudi nyuma katika njia za moyo wake mwenyewe.
\s5
\v 18 Nimeziona njia zake, lakini nitamoponya yeye. Nitamuongoza yeye na kumfariji na kuwashauri wale wanomliliia yeye,
\v 19 na natengeneza tunda la midomo. Amani, amani, kwa wale walio mbali sana na wale walio karibu-asema Yahwe nitawaponya ninyi.
\s5
\v 20 Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka, haiwezi kutulia, na maji yake yametanda juu ya matope.
\v 21 Hakuna amani kwa wakosaji asema Mungu.''
\s5
\c 58
\p
\v 1 ''Lia kwa sauti; usinyamaze. Paza sauti yako juu kama mbiu. Kabiliana na watu wangu wenye uasi, na nyumba ya Yakobo na dhambi zao.
\v 2 Bali wananitafuta mimi kila siku na kufurahia katika maarifa ya njia zangu, kama taifa linalotenda haki na hawakuiacha sheria ya Mungu wao. Wananiuliza mimi kuhusu hukumu ya haki; wamepata furaha katika mawazo yao ya kwa kumkaribia Mungu
\s5
\v 3 Kwa niini tulifunga; walisema, 'Lakini hamkuona hilo? Kwa nini tulijinyenyekeza wenywe, lakini hakutambua?' Tazama, siku ya kufunda kwanu utatafuta furaha yanu mwenyewe na kuwanyanyasa wafanyakazi wenu wote.
\s5
\v 4 Tazama, ninyi mnafunga ili muwe wepesi wa kugombana na kupigana, na kupiga kwa ngumi ya uovu wako; haujafunga leo kuifanya sauti yako isikike juu.
\v 5 Kwa uhalisi aina ya mfungo huu ndio ambao ninauhitaji: Siku ambayo kila mtu hunyenyekea mwenyewe, huinamisha kichwa chake chini kama mwanzi, na hutawanya mavazi ya magunia na majivu chini yake? Je kweli unauita huu ni mfungo, siku ya kumfurahisha Yahwe.?
\s5
\v 6 Hii sio mfungo ambao niliuchagua mimi: kufungua vifungo vya waovu, kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioangamizwa, na kuharibu kila nira?
\v 7 Sio kwamba kula mkate na wenye njaa na kuwaleta masikini na kuwaleta wasio na makazi katika nyuma yako?'' Unapomuana mtu yuko uchi, unatakiwa vumvishe mavazi; na usijifiche mwenyewe na ndugu zako.
\s5
\v 8 Halafu mwanga wako utafunguliwa kama jua, na uponyaji wako utachipukia juu kwa haraka; haki yako itaenda mbele zake, na na utukufu wa Yahwe utakuwa nyuma kukulinda.
\s5
\v 9 Halafu utamuita, na Yahwe atakuitikia; utalia ukihitaji msaada, na atasema, ''Nipo hapa.'' Ikiwa utaitoa nira isiwepo miongoni mwako, kidole kinachoshataki, maongezi ya waovu,
\v 10 Ikiwa wewe mwenyewe utawapa wenye njaa na kuwaridhisha wahitaji katika shida, na giza lako litakuwa kama mchana.
\s5
\v 11 Halafu Yahwe ataendelea kuwaongoza ninyi na kuwa ridhisha ninyi katika mikoa ambayo hakuna maji, Ataimarisha mifupa yenu. Mtakuwa kama bustani iliyonyeshewa maji, na kama mkondo wa maji, ambaopo maji yake hayapungui.
\s5
\v 12 Baadhi yenu mtajenga tena sehumu za kale zilizoharibiwa; mtatengeneza sehemu zilizoharibiwana vizazi vingi; na mtaitwa ''Mrekebishaji wa ukuta,'' kuwarejesha katika mtaa ya kuishi.''
\s5
\v 13 Tuseme kwamba ukigeuza nyuma miguu yenu kutoka safarini katika siku ya sabato, kufanya anasa siku yangu takatifu, Tuseme kwamba umeiita sabato siku ya furaha, na umeiita siku ya Bwana Yahwe mtakatifu na yenye kuheshimiwa. Tuseme kwamba unahieshimu sabato kwa kuacha biashara zako, na hautafuti anasa zako mwenyewe na uzungumzi maneno yako mwenyewe.
\s5
\v 14 ''Halafu utapata furaha kwa Yahwe; na nitaifanya safari yako juu ya urefu wa nchi; Nitakulisha wewe kwenye urithi wa Yakobo baba yenu- maana mdomo wa Yahwe umezungumza.''
\s5
\c 59
\p
\v 1 Tazama, mkono wa Yahwe sio mfupi ambao hautweza kukuokoa wewe; wala sikio lake sio zito, ambalo haliwezi kusikia.
\v 2 Matendo yako ya dhambi, hata hivyo, zimekutenga wewe na Mungu, na dhambi zenu zimemfanya aufiche uso wake msimuone wala kumsikia yeye.
\s5
\v 3 Maana mikono yenu ina madoa ya damu na vidole vyenu vimejaa dhambi. Midomo yenu inazungumza uongo na ulimi wenu unazungumza kwa nia mbaya.
\v 4 Hakuna hata mmoja aitae haki, na hakuna anayewasihi kesi yake katika haki. Wanayamini maneno yasiyo ya haki, maneno ya uongo; wanashika matatizo na kuzaa dhambi.
\s5
\v 5 Wanetotoa mayai ya nyoka wenye sumu na hufuma mtandao wa buibui. Yeyote alaye mayai yake atakufa, na ikiwa yai litavunjika, litatotoa nyoka mwenye sumu.
\v 6 Mitando yao haitatumika kama mavazi, wala hawawezi kujifukia wenyewe kwa kazi yao. Kazi zao ni kazi za dhambi, na matendo ya vurugu yako mikononi mwao.
\s5
\v 7 Miguu yao inakimbilia uovu, na wanakimbilia kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yao ni mawazo ya dhambi; vurugu na uharibifu ndio njia yao.
\v 8 Njia ya amani hawaijuyui, na hakuna haki katika njia zao. Wametengeneza njia njia zlizopotoka; yeyote atakaye safiri kupitia njia hizi njia hizi hazijui amani.
\s5
\v 9 Hivyo basi haki iko mbali a sisi, wala haki haijatufikia sisi. Tunasubiri mwanga tunaona giza; tunatafuta mwangaza, lakini tunatembea gizani. Tunapapasa kwenywe ukuta kama kipofu, kama wale wasiona,
\v 10 Tuna mashaka mchana kweupe kama kwenye mwanga unaofifia; miongoni mwa wenye nguvu tuko kama watu waliokufa.
\s5
\v 11 Sisi tunaunguruma kama dubu na kuomboleza kama njiwa; tunasubiria haki, lakini hakuna kitu; kwa ukombozi, lakini uko mbali na sisi.
\s5
\v 12 Maana makosa yetu mengi yako mbele zako, na dhambi zetu zinatushuhudia sisi; maana makosa yako pamoja na sisi.
\v 13 Tumeaasi, kumkana Yahwe na kuacha kumfuata Mungu. Tulizungumzia ulafi kujeuka nyuma, na kuanza kulalamika kutoka moyoni na maneno ya uongo.
\s5
\v 14 Haki imerudishwa nyuma, wenye haki wamesimama mbali sana; maana ukweli uko mashakani katika mraba wa umma, haki haiwezi kuja.
\v 15 Waaminifu wamenda zao, na yeyote anayegeuka mbali na maovu anajiathiri mwenyewe. Yahwe aliliona hilo na hakupendezwa maana hakuna haki.
\s5
\v 16 Aliona kwamba hakuna mtu, na akastaajabu kwamba hakuna mtu wa kuoma. Hivyo basi mkono wake uliletao wakovu kwake, na haki yake unamtosheleza yeye.
\s5
\v 17 Huivaa haki kama ngao kifuani na kofia ya chuma ya wokovu kichwani mwake. Anajivika mwenyewe kwa mavazi ya kisasi na kuvaa vazi la bidii.
\v 18 Analipa tena kwa kilichotokea, hukumu ya hasira kwa adui zake na kwa adui atairidisha adhabu ya kisiwa kama zawadi yao.
\s5
\v 19 Hivyo wataliogopa jina la Yahwe kutoka magharibi na utukufu wake kutoka mashariki; maana atakuja kama mkondo wa mto, inaendeshwa na pumzi ya Yahwe.
\v 20 Mkombozi atakuja Sayuni na wale watkaojeuka kutoka matendo yao ya uasi katika nyumba ya Yakobo- Hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 21 Na kama mimi, hili ni agano langu pamoja nao- asema Yahwe- Roho yangu iliyo juu yenu, na maneno yangu niliyoyaweka kinywani mwenu, hayataondoka midomo mwenu au kuodoka mbali na midomo wajukuu wenu, au kwenda mbali asema Yahwe- kuanziia sasa na hata milele.''
\s5
\c 60
\p
\v 1 Nyanyuka, uangaze; maana mwanga wako umekuja, na utukufu wa Yahwe umekuja kwako.
\s5
\v 2 Japokuwa giza litatanda katika nchi, na giza nene katika mataifa; Lakini Yahwe atakuja juu yenu, na utukufu wake utaonekana kwenu.
\v 3 Mataifa yatakuja kwenye mwanga wako, na wafalme katika mwanga wako mkali uliokuja
\s5
\v 4 Tazama na angalia pande zote. Wamekusanyika wao wenyewe kwa pamoja na wanakuja kwako. Watoto wako watatoka mbali, na binti zao watabebwa katika mikono yenu.
\v 5 Halafu wataangalia na kuwa furaha, na moyo wako utafurahia na kufurika, maana wingi wa maji utamwagwa juu yenu, utajiri wa mataifa utakuja kwenu.
\s5
\v 6 Msafara wa ngamia utawafunika ninyi, na ngamia wa Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Sheba; wataleta dhahabu na ubani, wataimba sifa kwa Yahwe.
\v 7 Makundi yote ya Kedari yatakusanika kwa pamoja kwako, kondoo wa Nebaioti watabeba mahitaji yako; watakubalika kutolewa sadaka katika madhebau yangu; na nitaitukuza nyumba yangu takatifu.
\s5
\v 8 Ni nani hawa wanopaa wenyewe kama mawingu, na kama njiwa kwenye makazi yao?
\v 9 Pwani itanitafuta mimi, na meli ya Tarshishi huwaongoza, huwaleta watoto wenu kutoka mbali, pamoja na fedha zao na dhahabu zao, maana jina la Yahwe Mungu wenu, na Mtakatifu wa Israeli, maana amekuheshimu wewe.
\s5
\v 10 Watoto wa wageni watajenga tena kuta zenu, n awafalme wao watawatumikia ninyi; japo katika laana yangu nimewaadhibu ninyi, lakini kwa neema yangu nitawahurumia ninyi.
\v 11 Milango yenu itaendelea kuwa wazi; haitafungwa mchana au usiku, hivyo utajiri wa mataifa ili uweze kuletwa, pamoja na viongozi wanowaongoza.
\s5
\v 12 Kweli, mataifa na falme ambayo hayatakutumikia wewe yatatoweka; mataifa hayo yataangamizwa kabisa.
\v 13 Utukufu wa Lebanoni utakuja kwako, mti wa msonobari, mtidhari, pamoja na msonobari ili kupamba madhebau yangu; na Nitalitukuza eneo la miguu yangu.
\s5
\v 14 Watakuja kwako kukusujudia wewe, watoto wa wale wanaokunyenyekea wewe; wataisujudia miguu yako; watakuita wewe mji wa Yahwe, sayani ya Mtakatifu wa Israeli.
\s5
\v 15 Badala yake uwepo wenu umetelekezwa na kuchukiwa, kwa kuwa hakuna hata mmoja anayepita ndani yenu, nitawafanya kuwa kitu cha kiburi milele, furaha kutoka kizazi hata kizazi.
\v 16 Pia utakunywa maziwa ya mataifa, utatunzwa katika kifua cha wafalme; utajua kwamba Mimi Yahwe, Mimi ni mwokozi na mkombozi wenu, aliye Mkuu wa Israeli.
\s5
\v 17 Badala ya shaba Nitaleta dhahabu, badaia ya chuma nitaleta fedha; badala ya mbao, shabana badala ya jiwe, chuma. Nitachagua amani kwa kiongozi wenu, na haki kiongozi wenu.
\v 18 Vurugu hazitasikika katika aridhi yenu, uharibifu wala uvunjaji katika mipaka yenu; lakini mtaita kuta zenu wokovu, na malngo yenu mtayaita sifa.
\s5
\v 19 Jua halitakuwa mwanga wenu wakati wa mchana, wala mwanga wa mwenzi wakati wa usiku hautawawakia ninyi; Lakini Yahwe atakuwa mwanga wenu wa milele, na Mungu wenu na utukufu wenu.
\v 20 Jua lenu halitakuewepo wala mweni utaondoshwa na kutoweka; maana Yahwe atakuwa mwanga wenu daima, na siku za maombolezo zitakwisha.
\s5
\v 21 Watu wako wote watakuwa wenye haki; watachukuwa urithi wa nchi kwa mda wote, tawi la mazao yangu, kazi ya mikono yangu, ili niweze kuitukuza.
\v 22 Mtoto atakuwa maelfu, na mdogo atakuwa taifa la wenye nguvu; Mimi Yahwe Nitayatimiza hayo mda utakapowadia.
\s5
\c 61
\p
\v 1 Roho ya Bwana Yahwe i juu yangu, maana Yahwe amenipaka mafuta mimi kuhiubiri habari njema kwa wenye taabu. Amenituma mimi kuwaponywa waliopondeka mioyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kufungua gereza ili waliofungwa waweze kutoka.
\s5
\v 2 Amenituma mimi kuutangaza mwaka wa Yahwe uliokubalika, siku ya kisasi cha Mungu wetu, na kuwafariji wale wote wanaomboleza.
\s5
\v 3 Amenituma mimi - kuwapa wale waoombolezao katika Sayuni -kuwapa wao kilemba cha majivu, mafuta ya furaha badala ya kuomboleza, vazi la kusifu katika eneo la roho ya ubutu, kuwaita mialoni ya haki, iliyooteshwa na Yahwe, ili aweze kutukuzwa.
\s5
\v 4 Wataijenga tena mahali pa kale palipohaibiwa; wataparejesha mahali palipokuwa na ukiwa. Watairejesha miji iliyoharibiwa, Mahali penye ukiwa kutoka vizazi vingi vilivyopita.
\v 5 Wageni watasimama na kulisha makumdi yako, na watoto wa wageni watafanya kazi kwenye mashamba yako na mizabu.
\s5
\v 6 Mtaitwa makuhani wa Yahwe; watawaita watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, na utajivuinia katika utajiri wake.
\v 7 Badala yake aibu yenu itaongezeka; na badala ya fedhea walifurahia juu ya sehemu yao. Hivyo basi sehemu yao itaongezeka mara mbili katika nchi na furaha ya milele itakuwa yao.
\s5
\v 8 Maana Mimi, Yahwe, ninapenda haki, na ninachukia wizi na vurugu zisizo za haki. Nitawalipa wao kataka haki na Nitafanya agano la milele na wao.
\v 9 Uzao wao utajulikana miongoni mwa mataifa, na watoto wao miongoni mwa watu. Wote watakaowaona watawakubali wao, kwamba ni watu wangu ambao Yahwe amewabariki.
\s5
\v 10 Nitafurahia sana katika Yahwe; Katika Mungu nitafurahia. Maana amenivika mimi kwa vazi la wokovu; amenivika mimi kwa vazi la haki, kama bwana harusi aliyejipamba mwenywe kwa kilemba, na kama bibi harusi aliyejipamba kwa vito.
\v 11 Maana kama nchi inavyozalisha miti inayochipukia na kama bustani inavyofanya miti yake ikuie, hivyo Bwana atasasbabisha haki na sifa kuchipukia mbele ya mataifa yote.
\s5
\c 62
\p
\v 1 Kwa niaba ya Sayuni sitatulia, na kwa naiba ya Yerusalemu sitanyamaza kimya, mpaka haki yake itakapotokea, na wokovu wake kama tochi.
\v 2 Mataifa yataona haki yako, na wafalme wote wataona utukufu wako. Utaitwa kwa jina jipya ambalo Yahwe atalichagua.
\s5
\v 3 Pia utakuwa taji zuri katika mkono wa Yahwe, na kilemba cha ufalme katika mkono wa Mungu wako.
\v 4 Hautaambiwa tena, ''Umetelekezwa''; wala kwa nchi yako hautasema tena, ''Ukiwa.'' kweli, itaitwa ''Neema yangu iko kwake'', na nchi yao ''ndoa'' mana furaha ya Yahwe ndani yenu, na nchi yenu itaolewa.
\s5
\v 5 Hakika, kama kijana mdogo akimuoa mwanamke mdogo, hivyo watoto wako watawaoa ninyi, na kama bwana harusi anavyofurahia juu ya bibi harusi, Mungu wenu atafuhai juu yenu.
\s5
\v 6 Nimemuweka mlinzi katika kuta zenu, Yerusalemu; hawatatulia mchana wala usiku. Utabaki kuwa Yahwe, usitulie.
\v 7 Usimuache apumzike mpaka ainzishe tena Yerusalemu na kmfanya asifiwe duniani.
\s5
\v 8 Yahwe ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wa nguvu zake, ''Hakika sitawapa tena nafaka kama chakula cha maadui zenu. Wageni hawatakunjwa mvinyo wenu uliompya maana mlifanya kazi.
\v 9 Kwale watakao vuna nafaka watazila na kumsifu Yahwe, na wale wanaochuma zabibu watakunjwa mvinyo katika mahakama ya madhebau yangu takatifu.''
\s5
\v 10 Njooni pitieni, pitieni katika lango! Tenegenezeni mapito ya watu! Itengenezeni, Tengeneza njia kuu! kusanyeni mawe! Nyanyueni juu ishara ya bendera kwa mataifa!
\s5
\v 11 Tazama, Yahwe ametangaza mwisho wa nchi, ''Waambie binti Sayuni: Tazama, Mkombozi wenu anakuja! Angalia, amebeba zawadi zake, na malipo yake yapo mbele yake.''
\v 12 Watakuita wewe, ''Mtu mtakatifu; Mkombozi wa Yahwe,'' nawe utaitwa ''Ulioacha kabla; mji usiotelekezwa.''
\s5
\c 63
\p
\v 1 Ni nani ajaye kutoka Edomu, aliyevaa mavazi rangi nyekundu kutoka Bozra? Ni nani aliye katika mavazi ya kifahari, anayetembea kwa kujiamini kwa sababu ya ukuu wa nguvu zake? Ndiye mimi, nizungumzae haki na uwezo mkubwa wa kuokoa.
\v 2 Kwa nini umevaa mavazi ya rangi nyekundu, na kwan nini wanaonekana kama akanyagae mizabibu katika vyombo vyake.
\s5
\v 3 Nimekanyaga zabibu lililoko katika vyombo vyenyewe, na hakuna hata mmoja kutoka mataifa aliyeungana na mimi. Niliwakanyaga kwa hasira yangu na niliwakanyaga wao kwa hasira yangu. Damu zao zimeruka katika nguo zangu na kuweka madoa nguo zangu zote.
\v 4 Maana niliangalia mbele katika siku ya kisasi, na mwaka wa ukombozi ulikwishawadia.
\s5
\v 5 Mimi nilitazama, na hapo hapakuwa na mtu mmoja hata wa kutoa msaada, lakini mkono wangu mwenywe uliniletea ushindi mimi, na hasira yangu kubwa iliniongoza mimi.
\v 6 Niliwakanyaga watu wangu chini kwa hasira yangu na kuwafanya wao wanywe laana yangu, na nilimwaga damu zao juu ya nchi.
\s5
\v 7 Nitakusimulia matendo ya agano la Yahwe lenye kuaminika, matendo ya kusifu ya Yahwe. Nitawasimulia yote ambayo Yahwe ametutendea sisi, na ukuu wa uzuri wake katika nyumba ya Israeli. Huruma hii aliyetuonyesha sisi kwa sababu ya rehema zake na matendo ya agano lake la kuaminika.
\v 8 Maana alisema, ''Baadhi yao ni watu wangu, watoto ambao sio waaminifu.'' Amekuwa mwokozi wao.
\s5
\v 9 Kupitia mateso yao yote, aliteseka pia, na malaika kutoka mbele yake aliwaokoa wao. Katika upendo wake na rehema aliwakomboa wao, na aliwanyanyua juu na aliwabeba wote katika kipindi chote cha kale.
\s5
\v 10 Lakini walimuasi na kumuuzunisha roho mtakatifu. Hivyo basi akkawa adui wao na kupigana dhidi yao.
\s5
\v 11 Watu wake walifikiri kuhushu nyakati za kale za Musa. Walisema, ''Yuko wapi Mungu, aliyewaleta juu nje ya bahari pamoja na mchungaji wa kundi lake? Yuko wapi Mungu, ambaye aliyeweka roho mtakatifu mwiongoni mwenu?
\s5
\v 12 Yuko wapi Mungu, aliyeufanya wingi wa utukufu wake kwenda katika mkono wa kuume wa Musa, na ukaganya maji mbele yao, kulifanya jina lake milele yeye mwenyewe?
\v 13 Yuko wapi Mungu, aliyewaongoza katika maji mengi? Kama farasi anayekimbia kwenye aridhi ambayo ni tambarare, hawakua na mashaka.
\s5
\v 14 Kama ng'ombe anayeshuka chini kwenye bonde, Roho ya Yahwe imewapa punziko. Hivyo umewaongoza watu wako, kufanya wewe mwenyewe jina la kusifu.
\s5
\v 15 Tazama chini kutoka mbinguni na pata taarifa kutoka kwenye makao ya utukufu wako. Iko wapi bidii yenu na matendo makuu? Uruatendo yako ya uruma yamezuiliwaa kutoka kwetu.
\v 16 Maana wewe n baba yetu, Japokuwa Ibrahimu hatujui sisi, na Israeli haitutambui sisi, wewe, Yahwe, wewe ni baba yetu. Mkombozi wetu limekuwa jina lako kutoka nyakati za kale.
\s5
\v 17 Yahwe, kwa nini unatufanya tangetange na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, hivyo hatukukuheshimu wewe? Rudi kwa niaba ya watumishi wako, kabila la urithi wako.
\s5
\v 18 Watu wako walirithi mahali patakatifu kwa mda mfupi, halafu maadui zetu waliwakanyaga.
\v 19 Tumekuwa kama juu ya wale ambao hawajawai kuongoza, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.
\s5
\c 64
\p
\v 1 ''Oh, ikiwa umeigawa kwa kuifungua mbingu na kushuka chini! Milima inetikisika mbele yako,
\v 2 ni kama vile moto uunguzao vichaka, moto uchemshao maji. Oh, jina lako lingejulikana kwa maadui wako, na ya kwamba mataifa yangetetemeka mbele yako!
\s5
\v 3 Awali, ulipofanya mambo ya ajabu ambayo hatukuyategemea, ulishuka chini, milima ikatetemeka mbele zako.
\v 4 Tangu nyakati za kale hakuna hata mmoja aliyesikia au kujua, wala jicho kuona Mungu yeyote karibu yake, ni nani afanyae mambo haya kwake anayemsubiri yeye.
\s5
\v 5 Umekuja kuwasidia wale wanaofurahia kutenda yaliyo ya haki, wale wanaowaita kuwakumbusha njia zake na kumheshimu yeye. Ulipatwa na hasira tulipotenda dhambi. Katika njia zako daima tutakombolewa.
\s5
\v 6 Maana sote tumekuwa kama mmoja aliye na unajisi, na matendo yetu ya haki yamekuwa kama hedhi kali. Sote tumenyauka kama majani; maovu yetu, ni kama upepo, unaotupeperusha sisi mbali.
\v 7 Hakuna hata mmoja anayeita jina lako, hakuna anayefanya jitihada za kukushika wewe; maana umeuficha uso wako mbali na sisi na kutufanya sisi kuwa takataka katika mkono wa maovu yetu.
\s5
\v 8 Na lakini, Yahwe, wewe ni baba yetu; sisi ni udongo. Wewe ni mfinyanzi wetu; sisi ni kazi ya mkono wako.
\v 9 Usiwe na hasira kubwa, Yahwe, wala daima usikumbuke maovu dhidi yetu, tafadhali sisi sote, watu wako.
\s5
\v 10 Miji yenu mitakatifu imekuwa jangwa; Sayuni imekuwa jangwa, Yerusalemu imekuwa ukiwa.
\v 11 Hekalu letu takatifu na zuri. mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, limeangamizwa kwa moto, na kila kilichokuwa karibu kiliharibiwa.
\v 12 Je unawezaje kuendelea kumshika, Yahwe? Unawezaje kutulia kimya na kuendelea kutufedhehesha sisi?''
\s5
\c 65
\p
\v 1 Nilikuwa tayari kuchaguliwa na wale ambao hawakuniomba; Nilikuwa tayari kupatikana kwa wale ambao hawakunitafuta. Nilisema, ''Niko hapa!' kwa taifa ambalo halikuita jina langu.
\v 2 Nimetawanya mikono yangu siku zote kuwasumbua watu wangu, wanao tembea katika njia isiyopasa, wanaotembea kwa kufuata mawazo yao wenyewe na mipango yao.
\s5
\v 3 Kuna watu wanoendelea kunipinga mimi, wanatoa sadaka zao katika bustani, na kuchoma ubani juu ya matofali.
\v 4 Wamekaa miongoni mwa makaburi na kuangalia usiku kucha, na hula nyama ya nguruwe na mchuzi mchafu wa nyama katika vyombo vyao.
\s5
\v 5 Wanasema, 'Simama mbali, usisogee karibu na mimi, maana mimi ni mtakatifu zaidi yako.' Vitu hivi ni moshi katika pua zangu, moto uwakao mchana kutwa.
\s5
\v 6 Tazama, imeandikwa mbele yangu: Sitanyamaza, Maana nitawalipa wao tena; nitafanya malipo yao katika miguu yao,
\v 7 kwa sababu ya dhambi zao na dhambi za baba zao kwa pamoja.'' asema Yahwe. ''Nitawajibu wao kwa kuchoma ubani juu ya milima na kunifanyia mimi juu ya vilima. Hivyo basi nitapima juu ya matendo yao ya kale katika miguu yao.''
\s5
\v 8 Yahwe asema hivi, ''Ikiwa kama juisi itapatikana katika nguzo ya zabibu, wakati mmoja ataposema, 'Usihiaribu hiyo, maa kuna uzuri ndani yake; hichi ndicho nitakachokifanya kwa niaba ya watumishi wangu: Sitawaribu wao wote.
\s5
\v 9 Nitazileta koo kutoka kwa Yakobo, na kutoka Yuda wao ambao watairithi milima yangu. Niliowachagua watairithi aridhi, na watumishi wangu wataishi pale.
\v 10 Sharoni itakuwa malisho ya makundi, na bonde la Akori itakuwa sehemu ya kupumzikia ya makundi yangu, kwa watu wangu wanaonitafuta mimi.
\s5
\v 11 Lakini yeye aliyeachana na Yehwe, anayeusahau mlima wangu mtakatifu, anayeandaa meza kwa bahati ya mungu, na kujaza kikombe cha mvinyo uliochanganywa na miungu inayoitwa Hatama.
\s5
\v 12 Nitaufikisha mwisho wenu kwa upanga, na wato mtainama chini kwa kuchinjwa, Kwa sababu nilipokuita wewe, haukuitikia; nilipozungumza haukunisikliza. lakini mlifanya yaliyo mabaya katika macho yangu na kuchagua kufanya yasiyo nipendeza mimi.''
\s5
\v 13 Bwana Yahwe asema hivi, ''Tazama, mtumishi atakula, lakini atashikwa na njaa; tazama mtumishi wangu atakunywa lakini atakuwa na kiu; tazama mtumishi wangu atashangilia, lakini atatiwa katika aibu.
\v 14 Tazama, mtumishi wangu atapiga kelele za furaha kwa sababu ya furaha ya moyo, lakini utalia kwa sababu ya maumivu ya moyo, na mtapiga kelele kwa sababu ya kusagwa kwa roho zenu.
\s5
\v 15 Nanyi mtaliacha jina lenu nyuma kama laana kwa watu niliowachagua wazungumze; Mimi Bwana Yahwe, Nitakuwa wewe; Nitawaita watumishi wangu kwa jina lingine.
\v 16 Yeyote atakaye tamka baraka juu ya nchi atabarikiwa na mimi, Mungu wa kweli. Yeyote achukuae kiapo juu ya nchi anaapa na mimi, Mungu wa kweli, kwa sababu matatizo ya nyuma yatasaulika, maana yatafichwa machoni pangu.
\s5
\v 17 Maana tazama, Ninakaribia kuumba mbingu mpya na nchi mpya; na mambo ya kale hayatakumbukwa tena wala kufikiriwa katika akili.
\v 18 Lakini mtakuwa na furaha na kushangilia daima kwa nitakachokiumba. Tazama, Ninakaribia kuumba Yerusalemu mpya kama furaha na watu wake wenye furaha.
\v 19 Nitafurahia juu ya Yerusalemu watu wangu; kuomboleza na kilio cha dhiki akitasikika tena ndani yake.
\s5
\v 20 Hakuna tena mtoto atakayeishi pale japo kwa siku chache; wala mzee kufa kabla ya mda wake. Yule atakayekufa katika umri wa miaka mia moja atachukuliwa kama mtu mdogo. Yeyote ambaye atashindwa kufikia umri wa miaka mia moja atachukuliwa kama laana.
\v 21 Watazijenga nyumba na kukaa huko, na watapanda mizabibu na kula matunda yake.
\s5
\v 22 Hawatajenga nyumba na wengine waishi humo; hawatapanda, na wengine wale; maana kama siku za miti zitakuwa siku za watu wangu. Watu wangu wataishi kikamilifu kwa kazi ya mikono yao.
\v 23 Hawatafanya kazi bure, wala kuzaa kwa kusikitishwa. Maana ni watoto wa waliobarikiwa na Yahwe, pamoj na koo zao.
\s5
\v 24 Kabla hawajaita, nitaitika; na wakati wanaendele kuzungumza, ntisikia. Mbwa mwitu na kondoo watachungwa pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; lakini udongo utakuwa chakula cha nyoka.
\v 25 Hawataumiza tena wala kuharibujuu ya mlima wangu mtakatifu,'' asema Yahwe.
\s5
\c 66
\p
\v 1 Yahwe asema hivi, ''Mbinguni ni makao yangu, na nchi ni miguu yangu. Iko wapi nyumba uliyonitengenezea mimi? iko wapi sehemu amabayo ninaweza kupumzika?
\s5
\v 2 Mkono wangu umeyafanya haya yote; hivi ndovyo jinsi ambavyo vitu vitatokeavyo---hili ndilo tamko la Yahwe. Mtu niliyempitisha, mwenye roho iliyopondeka na mwenye kujutia roho, na atetemekaye kwa ajili ya neno langu.
\s5
\v 3 Yeyote achinjae ng'ombe humuua mtu pia; yeye anayetoa sadaka ya kondoo huvunja shingo ya mbwa pia; yeye anayetoa sadaka ya mavuno anatoa sadaka ya damu yangurue; yeye anayetoa kumbukumbuvumba huwabariki wakosaji pia. Wamechagua njia zao wenyewe wanachukua radhi kwa uchafu wao wenyewe.
\s5
\v 4 Katika njia hiyo hiyo nitachagua adhabu yao wenyewe; Nitaleta juu yao kitu wanachokiogopa, maana niilpowaita, hakuna aliyeitika; nilipozungumza aliyenisikiliza mimi. Walifanya yaliyo maovu mbele yangu, na kuchagua yasiyo nipenindeza mimi.''
\s5
\v 5 Sikiliza neno la Yahwe, ewe utemekae kwa neno lake, ''Kaka zako wanaonichukia na kukutenga wewe kwa ajili ya jina langu walisema, 'Na atukuzwe Yahwe, halafu tutaiona furaha yenu; lakini mtatiwa katika aibu.
\s5
\v 6 Sauti ya vita vya ghasi vinakuja katika mji, sauti kutoka hekaluni, sauti ya Yahwe anawarudia maadui zake.
\s5
\v 7 Kabla ajaenda katika chumba, hujifungua; kabla ya uchungu kumtoka hujifungua mtoto wa kiume.
\v 8 Ni nani asikiaye mambo haya? Ni nani aonae mambo haya? Je taifa linaweza kuanzishwa kwa wakati mmoja? lakini kwa haraka Sayuni inapokwenda katika chumba, hujifungua watoto wake.
\s5
\v 9 Ninawezaje kumleta mtoto azaliwe na nisimruhusu mtoto azaliwe? Yahwe auliza? -- au Je ninamleta mtoto wakati tu wa kujifungua na halafu nimshikilie tena - anauliza Yahwe.''
\s5
\v 10 Furahia na Yerusalemu na fuhahia kwa ajili yake, ninyi nyote mnaopenda yeye; furahia pamoja na yeye, ninyi mnaomboleza juu yake!
\v 11 Maana utamuuguza na ataridhika, katika maziwa yake atakufariji; utakunywa mpaka ushibe na kufurahia kwa wingi wa utukufu wake.
\s5
\v 12 Yahwe asema hivi, ''Ni nanakaribia kutawanya mafanikio juu katika mto, na utajiri wa mataifa kama wingi wa mkondo wa maji. Utamuuguza kwa upande wake, na kubebwa katika mikono yake, mtabebwa juu ya magoti yake.
\v 13 Kama vile mama anavyomfariji mtoto wake, hivyo basi nami nitawafariji ninyi, na mtapata faraja katika Yerusalemu.''
\s5
\v 14 Utayaona haya, na moyo wako utafurahia, na mifupa yako itachipukia kama zabuni ya nyasi. Aridhi ya Yahweitajulikana kwa watumishi wake, lakini atawaonyesha hasira yake dhidi ya maadui zake.
\s5
\v 15 Kwa kutazama, Yahwe anakuja kwa moto, na gari lake linakuja kama upepo wa dhoruba kuleta joto katika hasira yake na kukemea kwake ni kama moto uwakao.
\v 16 Maana Yahwe ametekeleza hukumu juu ya watu kwa moto na kwa upanga wake. Wale watakaouliwa na Yahwe watakuwa wengi.
\s5
\v 17 Watajiweka wakfu wenyewe na kujisafisha wenywe, ili waweze kuingia katika bustani, kumfuata aliyeko katikati ya wale walao nyama ya nguruwe na vitu haramu kama panya. ''Watafika mwisho - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 18 Maana ninayajua matendo yao na mawazo yao. Wakatiutafika nitakapoyakusanya mataifa yote na lugha zote. Watakuja na kuona utukufu wangu.
\v 19 Nitaweka ishara ya ukuu wangu miongoni mwao. Halafu nitawatuma wakazi kutoka miongoni mwao kwa mataifa. Kwa Tarshishi, Puti, na Ludi, upinde wale wanaochukua upinde wao, kwa Tubali, Javani, na umbali kuelekea katika pwani kule ambapo hawajasikia chochote kuhusu mimi wala kuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.
\s5
\v 20 Watawaleta kaka zako wote nje ya mataifa yote, kama sadaka kwa Yahwe. Watakuja kwa farasi na kwa gari, na kwa gari, juu ya nyumbu na juu ya ngamia, kuelekea mlima wangu mtakatifu Yerusalemu - asema Yahwe. Maana watu wangu wa Israeli wataleta sadaka ya mavuno kwenye vyombo visafi katika nyumba ya Yahwe.
\v 21 Baadhi ya vitu hivi nitavichagua kama makuhani na walawi -- asema Yahwe.
\s5
\v 22 Maana itakuwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo nitakayoifanya ibaki mbele zangu-- Hili ndilo tamko la Yahwe-- Hivyo ndivyo ukoo wenu utakavyobakia, na jina lenu litabaki.
\v 23 Kutoka mwenzi mmoja mpaka mwingine, na kutoka sabato moja mpaka nyingine, watu wote watakuja kukuinamia chini--- asema Yahwe.
\s5
\v 24 Watakwenda nje na kuona miili ya wafu ya watu walioniasi mimi, maana wadudu wawalao wao hatakufa, na moto huwaunguzao hautazimika; na itakuwa ni chuki kwa wale wote wenye mwili.''

2615
24-JER.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2615 @@
\id JER
\ide UTF-8
\h Yeremia
\toc1 Yeremia
\toc2 Yeremia
\toc3 jer
\mt Yeremia
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hili ndilo neno la Yeremia mwana wa Hilikia; yeye alikuwa mmoja wa makuhani kule Anatothi katika nchi ya Benjamini.
\v 2 Neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wake.
\v 3 Lakini pia lilimjia katika wakati wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa Zedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipochukuliwa kuwa watumwa.
\s5
\v 4 Neno la BWANA lilinijia, likisema,
\v 5 "kabla sijakuumba tumboni, Nilikuchagua; kabla hujazailiwa toka tumboni Nilikutenga; Nilikufanya kuwa nabii kwa mataifa."
\v 6 "Ahaa, BWANA!" Nilisema, "mimi sijui kusema, kwa kuwa mimi ni mtoto."
\s5
\v 7 Lakini BWANA akaniambia, "Usiseme, 'mimi ni mtoto.' Utaenda kila mahali ninapokutuma, na utasema kila kitu ninachokuamuru!
\v 8 Usiwaogpe hao, kwa kuwa Mimi niko pamoja na wewe kukuokoa- asema BWANA."
\s5
\v 9 Kisha BWANA akanyosh mkono wake, akagusa kinywa changu, na akaniambia, "Nimeweka maneno yangu kinywani mwako.
\v 10 Nimekuchagua leo juu ya mataifa na juu ya mataifa, ili kung'oa na kuvunja, kuharibu na kutupa, kujenga na kupanda."
\s5
\v 11 Neno la BWANA lilinijia, likisema, "Yeremia, unaona nini?" Nikasema, "Ninaona tawi la mlozi."
\v 12 BWANA akaniambia, "umeona vyema, kwa kuwa ninaliangalia neno langu ili nilitimize."
\s5
\v 13 Neno la BWANA likaniji mara ya pili likisema, "Unaona nini? "Nikasema, "Ninaona chungu kikichemuka, ambacho mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini,"
\v 14 BWANA akaniambia, "Janga litatokea kaskazini juu ya wote wanaoishi katika nchi hii.
\s5
\v 15 Kwa kuwa ninayaita makabila yote ya falme za kaskazini, asema BWANA. Yatakuja, na kila mmoja atasimika enzi yake katika malango ya Yerusalemu, dhidi ya kuta zote zinazoizunguka, na dhidi ya miji ya Yuda.
\v 16 Nitatamka hukumu dhidi yao juu ya uovu wao wa kuniacha, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kwa kuabudu kile walichotengeneza kwa mikono yao.
\s5
\v 17 Jiandae! Simama ukawaambie kila kitu ninachokuamuru. Usifdhaike mbele zao nisije nikakufadhaisha wewe mbele zao!
\v 18 Tazama! Leo nimekufanya kuwa mji ulio na ngome, kuwa ngome ya chuma, na ukata wa shaba dhidi ya nchi yote - dhidi ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wote wa nchi.
\v 19 Watapigana na wewe, lakinai hawatakushinda, kwa kuwa nitakuwa pamoja na wewe ili kukuokoa- asema BWANA."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Neno la BWANA lilinijia likisema,
\v 2 "Nenda ukanene katika masikio ya Yerusalemu. Useme; BWANA asema hivi: Ninakumbuka agano la uaminifu la ujana wako, upendo wako wakati tulipokuwa tumechumbiana, ulipokuwa ukinihitaji kule jangwani, katika ile nchi iliyokuwa haijapandwa.
\v 3 Israeli alikuwa ametengwa kwa BWANA, malimbuko yake ya mavuno yake! Wote waliokula malimbuko yake walikuwa na hatia! majanga yaliwajia--asema BWANA.'"
\s5
\v 4 Sikilizeni neno la BWANA, enyi nyumba ya Yakobo na kila familia katika nyumba ya Israeli.
\v 5 BWANA anasema hivi, "Ni makosa gani ambayo baba zenu waliyaona kwangu, hata wakatae kunifuata mimi? hata wazifuate sanamu ambazo hazina chochote na wao kuwa si kitu?
\v 6 Wala hawakusema, BWANA yuko wapi, ambaye alitutoa katika nchi ya Misri? BWANA yuko wapi, ambaye alituongoza katika jangwa, katika nchi ya Araba na mashimo, katika nchi ya ukame na giza nene, katika nchi ambayo hakuna mtu apitaye wala hakuna mtu anayeishi humo?
\s5
\v 7 Lakini nilwaleta katika nchi ya Kameli, ili mle matunda yake na vitu vingine vyema! Lakini mlipokuja, mliitia unajisi nchi yangu, mliufany urithi wangu kuwa chukizo!
\v 8 Hata makuhani hawakusema, 'BWANA yuko wapi?' na watalamu wa sheria hawakunijali mimi! wachungaji wametenda dhambi dhidi yangu. Manabii wamemtolea Baali unabii na kuvitafuta vitu ambvyo havina faida.
\s5
\v 9 Kwa hiyo nitaendelea kuwashitaki - hili ni neno la BWANA - na nitawashitiki watoto wa watoto wenu.
\v 10 Kwa kuvuka kwenda hadi pwani ya Kitimu na kutazama. Tuma wajumbe kwenda Kedari na tafuta uone kama kama iliwahi kutokea hapo awali vitu kama hivi.
\v 11 Je, taifa limebadilisha miungu, hata kama haikuwa miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia.
\s5
\v 12 Sitajabuni, enyi mbingu kwa sababu ya hili! Tetemekeni na kuogopa -asema BWANA.
\v 13 Kwa kuwa watu wangu wametenda maovu mawili dhidi yangu: Wameziacha chemichemi za maji ya uhai kwa kuchimba mabarika kwa ajili yao, mabarika yanayovuja yasiyoweza kutunza maji!
\s5
\v 14 Je, Israeli ni mtumwa? Kwani hakuzaliwa nyumbani? Kwa nini sasa amekuwa nyara?
\v 15 Wanasimba wameunguruma dhidi yake. Wamepiga kelele sana na kuifanya kuwa ukiwa. Miji yake imeharibiwa na kubaki bila watu.
\v 16 Pia watu wa Nufu na Tahapanesi watakinyoa kichwa chako.
\v 17 Je, hamkufanya haya kwa ajili yenu mlipomwacha BWANA, wakati Mungu wenu, alipokuwa akiwaongoza njiani?
\s5
\v 18 Kwa hiyo, kwa nini kutafuta msaada Misri na kunywa maji ya Shihori? Kwa nini kutafuta msaada Ashuru na kunywa maji ya Mto Frati?
\v 19 Uovu wako unakukemea, na maasi yako yatakuadhibu. Kwa hiyo yafikiri hayo; tambua kuwa ni uovu na uchungu kwenu ninyi kuniacha mimi, BWANA Mungu wako, na kutokuwa na hofu yangu - asema BWANA wa majeshi.
\s5
\v 20 Kwa kuwa niliivunja nira yenu mliyokuwa nayo wakati wa kale; Nilivichana vifungo vyako kutoka kwako. Lakini bado ulisema, 'Sitamtumikia!' tangu ulipopiga magoti katika kila kilima kuusogelea kila mti wenye majani mabichhi, enyi makahaba.
\v 21 Lakini mimi mwenyewe niliwapanda kama mzabibu niliouchagua, mbegu iliyokamilika. Lakini tazama jinsi ulivyobadilika mbele yangu, na kuwa mzabibu usiofaa na mzabibu pori!
\v 22 Kwa kuwa hata kama utajisafisha mwenyewe mtoni na kuoga kwa sabuni kali, bado dhambi yako ni madoa mbele yangu - asema BWANA Mungu.
\s5
\v 23 Wawezaje kusema, 'Mimi sijanajisika! Mimi sjaenda kwa Mabaal?' Tazama tabia zako zilivyokuwa bondeni! Tambua kile ulichofanya, wewe ngamia mwepesi! akimbiaye katika njia yake!
\v 24 Wewe ni punda wa mwitu, aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo usiofaa katika tamaa ya kuishi! Ni nani awezaye kumgeuza anapotafuta dume la kumpanda? Na punda dume amtafutaye hajichoshi mwenyewe. Huenda kwake wakati wa mwezi wa kupandwa.
\v 25 Lazima uizuie miguu yako isikose kiatu na koo lako kuwa na kiu! Lakini umesema, 'Hakuna matumaini! Hapana! Nawapenda wageni nami huwatafuta!'
\s5
\v 26 Kama aibu ya mwizi ilivyo anapokuwa amekamatwa, ndivyo aibu ya Israeli itakavyokuwa - wao, wafalme wao, malikia wao, makuhani na manabii wao!
\v 27 Hawa ndio wale waiambiayo miti, 'Ninyi ndio baba zangu,' na mawe, 'Ninyi ndio mlinizaa.' Kwa kuwa migongo yao hunitazama na siyo nyuso zao. Hata hivyo, wakati wa shida husema, 'Amka utuokoe!'
\v 28 Lakini iko wapi ile miungu mliyojitengenezea? Acha hao wainuke kama wanaweza kuwaokoa wakati wa shida, kwa kuwa hizo sanamu zenu zina idadi sawa na miji yenu, katika Yuda.
\s5
\v 29 Kwa hiyo kwa nini kunituhumu kwa kufanya makosa? Ninyi nyote mmeniasi - asema BWANA wa majeshi.
\v 30 Nimewadhibu watu wenu bure. Wala hawakutaka kurudiwa. Upanga wako umewaangamiza manabii wenu kama kama simba aangamizaye!
\v 31 Enyi watu wa kizazi hiki! Sikilizeni neno langu, neno la BWANA! Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza nene? Kwa nini watu wangu husema, 'Acha tuzungukezunguke, hatutakuja kwako tena'?
\s5
\v 32 Je, mwanamwali anaweza kusahau mapambo yake, na bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wngu wamenisahau mimi kwa siku nyingi!
\v 33 Jinsi mlivyotengeneza njia zenu vizuri ili kutafuta mapenzi. Hata mmewafundisha njia zenu wanawake waovu.
\v 34 Damu ambayo ilikuwa ndio uhai wa watu wasio na hatia, imeonekana katika mavazi yenu. Hawa watu hawajawahi kuonekana katika matendo maovu.
\s5
\v 35 Pamoja na mambo haya yote, wewe unaeendelea kusema kuwa hauna hatia. Kwa hakika hasira ya BWANA itageuka kutoka kwangu. 'Lakini tazama! Utahukumiwa kwa sababu, 'Sikutenda dhambi.'
\v 36 Kwa nini mnatangatanga kwa urahisi katika njia zenu? Pia Misri itawahuzunisha sana, kama ilivyokuwa kwa Ashuru.
\v 37 Mtaondoka hapo mkiwa mmehuzunika sana, mkiwa mmeweka mikono vichwani mwenu, kwa kuwa BWANA amemkutaa yule mliyemtumainia, kwa hiyo hamtapata msaada toka kwao,"
\s5
\c 3
\p
\v 1 Wanaema, 'Mwanamume akimfukuza mke wake, naye akaondoka kwake na kuwa mke wa mwanamume mwingine. Je, anaweza kumrudia tena? Je huyo si najisi kabisa?' Huyo mwanamke ndiyo hii nchi! Mmetenda kama kama Kahaba aliye na wapenzi wengi, na sasa mnapenda kurudi kwangu tena? - asema BWANA wa majeshi.
\v 2 Inua macho yako uvitazame vielele tasa! Je kuna mahali ambapo hukufanya ukahaba? Pembeni mwa barabara ulikaa ukisubiri wapenzi wako, kama vile Mwarabu jangwani. Uneiharibu nchi kwa ukahaba na uovu wako.
\s5
\v 3 Kwa hiyo chemichemi za mvua zilizuiliwa na mvua za vuli hazikunyesha. Lakini uso wako una kiburi, kama uso wa mwanamke kahaba. Unakataa kuona aibu.
\v 4 Na sasa hutaniita mimi: 'Baba yangu, hata marafiki zangu wa tangu ujanani! Je, atakuwa na hasira dhidi yangu milele?
\v 5 Je, utaendelea kuwa na hasira zako?' Tazama! Umesema kuwa utatenda maovu, na kweli umetenda hivyo. kwa hiyo endelea kufanya hivyo!"
\s5
\v 6 Kisha BWANA akanena nami katika siku za mfalme Yosia, "Je, unaona jinsi Israeli alivyoniasi? Yeye anaenda kwenye kila kilima na katika kila mti wenye majani mabichi, na kule anafanya kama mwanamke kahaba.
\v 7 Nikisema, 'Baada ya kuwa amefanya mambo haya yote, atanirudia,' lakini hakurudi. Kisha dada yake Yuda ambaye ni mwasi pia aliona alichokifanya.
\s5
\v 8 Kwa hiyo nami nikaona kuwa kwa sababu amefanya uzinzi huu wote. Huyo Israeli aliyeasi! Nilimfukuza na kumpatia talaka ya ndoa. Lakini dada yake Yuda mwenye hiana hakuwa na hofu, na yeye akaenda kuafanya kama mwanamke kahaba!
\v 9 Hukusikitika kuwa ameinajisi nchi, kwa hiyo wakatengeneza sanamu za mti na za jiwe.
\v 10 Kisha baada ya haya yote, wala Yuda dada yake muasi hakurudi kwangu na moyo wake wote, bali alikuja na uongo! -asema BWANA wa majeshi,"
\s5
\v 11 Kisha BWANA akanena na mimi, "Israeli muasi amekuwa mwenye haki zaidi kuliko Yuda muasi!
\v 12 Nenda ukaseme maneno haya huko kaskazini. Uwaambie, 'Rudi wewe Israeli uliyeasi! - asema BWANA - sitakuwa na hasira dhidi yako. Kwa kuwa mimi ni mwaminifu - asema BWANA - sitakuwa na hasira milele.
\s5
\v 13 Kiri uovu wako, kwa kuwa umefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wako; umemshirikisha njia zako mgeni chini ya kila mti wenye majani mabichi! wala hukuisikiliza sauti yangu! - asema BWANA.
\v 14 Rudini, enyi watu waasi! - asema BWANA - kwa kuwa mimi nimekuoa wewe! Nitakurudisha wewe mmoja katika mji, wawili katika ukoo mmoja, na nitawarudisha Sayuni!
\v 15 Nitawapa wachungaji niwapendao, na watawachunga kwa maarifa na ufahamu.
\s5
\v 16 Ndipo itakapotokea kuwa utaongezeka na kuzaa matunda katika nchi hiyo siku hizo-asema BWANA. Hawataweza kusema kuwa, "Sanduku la agano la BWANA! Jambo hili hawatalikumbuka tena katika mioyo yao, kwa kuwa hawataliwaza tena wala kulijali tena. Usemi huu hawatausema tena.'
\s5
\v 17 Katiak wakati huo watasema juu ya Yerusalemu, 'Hii ndiyo enzi ya BWANA,' na mataifa mengine yote yatakusanyika Yerusalemu katika jna la BWANA. Hawataishi katika taabu ya uovu wa mioyo yao.
\v 18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaishi na nyumba ya Israeli. Watarudi pamoja kutoka katika nchi ya kaskazini katika nchi niliyowapa mababu wao kuwa urithi.
\s5
\v 19 Lakini mimi, Nilisema, 'Jinsi nipendavyo kukuheshimu kama mwanangu na kukupa nchi ipendezayo, kuwa urithi mzuri kuliko ulio katika taifa lolote!' Nami nikasema, ''mtaniita baba yangu''.'Nami nitasema kwamba hamtageuka na kuacha kunifuata.
\v 20 Lakini kama mwanamke aliyemwasi mume wake, mmenisaliti, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA."
\s5
\v 21 Sauti ilisikika juu ya nyanda, kilio na kusihi kwa watu wa Israeli! kwa kuwa wamezibadili njia; wamemsahau BWANA, Mungu wao.
\v 22 "Rudini enyi watu mlioasi! Nami nitawaponya na uasi wenu!" "Tazama! tutakuja kwako, kwa kuwa wewe ni BWANA, Mungu wetu!
\s5
\v 23 Uongo hutoka kwenye vilima, kutoka kwenye milima mingi. Kwa hakika wokovu wa Israeli unapatikana kwa BWANA, Mungu wetu.
\v 24 Lakini miungu ya aibu imeramba kazi ambayo mababu zetu waliifanya - makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao!
\v 25 Na tulale chini kwa aibu. Aibu yetu na itufunike, kwa kuwa tumefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wetu! Sisi wenyewe na mababu zetu, kutoka wakati wa ujana wetu hadi leo, hatujaisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wetu!"
\s5
\c 4
\p
\v 1 "Kama utarudi, Israeli- asema BWANA - ikawa kwangu kwamba umerudi. Kama utaondoa hayo mambo yachukizayo mbele yangu na ukaacha kunikimbia mimi tena,
\v 2 na ukaapa hivi, 'kama BWANA aishivyo katika kweli, na haki, na katika hukumu.' mataifa yataniomba baraka, na yatanisifu mimi.
\v 3 Kwa kuwa BWANA asema hivi kwa kila mmoja katika Yuda na Yerusalemu; 'Limeni shamba zenu na msipande katika miiba.
\s5
\v 4 Mtahiriwe kwa BWANA na kuondoa govi za mioyo yenu, ninyi wanaume wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, vinginevyo hasira yangu itawaka kama moto na kuteketeteza, na hakutakuwa na mtu wa kuizima. Hii itatokea kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
\v 5 Waambie Yuda na Yerusalemu isikie. Waambie, "pigeni baragumu katika nchi." Tangazeni, "Kusanyeni pamoja. Twendeni kwenye miji ya Maboma."
\v 6 Inueni ishara za bendera na zielekezeni Sayuni, na kimbilieni usalama! Msibaki, kwa kuwa ninaleta majanga kutokea kaskazini na anguko kubwa.
\s5
\v 7 Simba anakuja kutokea kwenye kichaka chake na yeye atakayeyaharaibu mataifa ameanza kuja. Anaondoka kwenye eneo lake ili aache hofu katika nchi yenu, kuibadili miji yenu kuwa uharibifu, ambapo hakuna hata mmoja atakayeishi. Kwa sababu hii vaeni magunia, lieni na kuomboleza.
\v 8 Kwa kuwa nguvu ya hasira ya BWANA haijaondoka kwetu.
\s5
\v 9 Ndipo itakapotokea katika siku hiyo - asema BWANA - mioyo ya mfalme na wakuu itakufa. Makuhani watasitaajabu na manabii watashangaa.'"
\v 10 Kwa hiyo nikasema, "Ahaa! BWANA. Kwa hakika umewadanganya watu hawa na Yerusalemu kwa kuwaambia, 'Kutakuwa na amani kwenu.'Wakati upanga unawaangukia dhidi ya maisha yao."
\s5
\v 11 Wakati huo itasemwa juu ya mji huu na Yerusalemu kuwa, "Upepo uwakao kutoka katika nyanda za jangwani utachukua njia yake kuelekea kwa binti ya watu wangu. Hautapepetwa wala kuwatakasa.
\v 12 Upepo ulio na nguvu sana utakaokuja kwa amri yangu, na sasa nitapitisha hukumu dhidi yao.
\s5
\v 13 Tazama anavamia kama wingu, na magari yake ni kama dhoruba. Farasi wake wana mbio kuliko tai. Ole wetu kwa kuwa tutaharibiwa!
\v 14 Itakaseni mioyo yenu kutoka uovu wenu, Yerusalemu, ili kwamba muokolewe. Mawazo yako mabaya yatafikiri juu ya kutenda dhambi mpaka lini?
\v 15 Kwa kuwa kuna sauti iletayo habari kutoka Dani, na janga lijalo linasikika kutoka vilele vya milima ya Efraimu.
\s5
\v 16 Yafanyeni mataifa kulifikiria hili: Tazama, na uwatangazie Yerusalemu kuwa wale watekaji wanakuja kutoka katika nchi ya mbali ili kupiga kelel za vita juu ya miji ya Yuda.
\v 17 Watakuwa kama walinzi wa shamba liliolimwa dhidi yake pande zote, kwa kuwa amekuwa mpinzani wangu - asema BWANA -
\v 18 tabia na matendo yako yamesababisha haya yatokee kwako. Hii itakuwa adhabu yako. Jinsi itakavyokuwa vibaya kwako! itakupiga moyo wako.
\s5
\v 19 Moyo wangu! Moyo wangu! Niko katika maumivu ya moyo. Moyo wangu umefadhaika ndani yangu. Siwezi kunyamaza kwa kuwa nasikia sauti za pembe, sauti za vita.
\v 20 Anguko baada ya anguko limetangazwa, kwa nchi yote imeharibika mara. Wanaharibu masikani yangu na hema yangu ghafula.
\s5
\v 21 Vita hivi vitaendelea mpaka lini? Ni mpaka lini nitasikiliza sauti za pembe?
\v 22 Kwa kuwa upumbavu wa watu wangu - hawanijui mimi. Ni watu wajinga wasio na ufahamu. Wanaufahamu wa mambo maovu, tena hawajui kutenda mema.
\s5
\v 23 Niliiona nchi, na kuiona! ilikuwa ukiwa na utupu. Kwa kuwa hapakuwa na taa za mbinguni.
\v 24 Nilitazama katka miliima. Tazama, ilikuwa inatetemeka, na vilima vyote vilikuwa vinatikisika.
\v 25 Nilitazama. Tazama, hapakuwa na mtu, na ndege wote wa angani walikuwa wamekimbia.
\v 26 Nikaangalia. Tazama, mashamba yalikuwa jangwa na miji imeangushwa mbele za BWANA, mbele ya hasira yake."
\s5
\v 27 Hiki ndicho BWANA asemacho, "Nchi yote itakuwa uharibifu, lakini sitawaharibu wote kabisa.
\v 28 Kwa sababu hii nchi itaomboleza, na mbingu juu zitatiwa giza. Kwa kuwa nimesema haya na kuyakusudia; sitarudi nyuma; Sitaacha kuyatekeleza.
\v 29 Kila mji utakimbia kutoka katka kelele za wapandafarasi na wenye pinde; Watakimbilia msituni, Kila mji utapanda hadi mahali pa miamba. Miji itatelekezwa, kwa kuwa hakutakuwa na mtu wa kuishi katika miji hiyo.
\s5
\v 30 Sasa umeharibiwa, utafanya nini? Japokuwa unavaa mavazi mekundu, unajipamba na mapambo ya dhahabu, na kuyafanya macho yako yaonekane makubwa na kupakwa wanja, wale wanaume waliokutamani sasa wanakukataa. Badala yake wanajaribu kukuua.
\v 31 Kwa hiyo nasikia sauti ya maumivu, yenye utungu kama ya mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti wa Sayuni. Atwetaye kupata pumzi. Ananyosha mikono yake na kusema, 'Ole wangu mimi! ninazimia kwa sababu ya wauaji hawa.'"
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kimbieni mkapite katika mitaa ya Yerusalemu, Tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja anayetenda kwa haki na kufanya kwa uaminifu, basi nitaisamehe Yerusalemu.
\v 2 Hata kama wanasema, 'Kama BWANA aishivyo,' wanaapa uongo."
\v 3 BWANA, macho yako hayatazami uaminifu? Unawapiga watu, lakini hawasikii maumivu. Umewaangsmiza kabisa, lakini bado wanakataa kuwa waadilifu. Wanafanya nyuso zao kuwa ngumu kama mwamba. kwa kuwa wanakataa kutubu.
\s5
\v 4 Kwa hiyo nilisema, "Hakika hawa ni watu masikini, Ni wapumbavu, Kwa kuwa hawazijui njia za BWANA, wala maagizo ya Mungu wao.
\v 5 Nitaenda kwa watu wa muhimu na kutangaza ujumbe wa Mungu kwao, kwa kuwa angalau wanazijua njia za BWANA, maagizo ya Mungu wao. Lakini wote wanavunja nira yao pamoja; wote wanaivunja ile minyororo inayowafunga kwa ajili ya Mungu.
\v 6 Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawavamia. Mbweha kutoka Arabaha atawaangamiza. Chui ataivunja miji yao. Mtu yeyota anayeenda nje ya mji wake atavunjwavunjwa. Kwa kuwa maovu yao yameongezeka. Matendo yao ya uasi hayana ukomo.
\s5
\v 7 Kwa nini niwasamehe hawa watu? Wana wenu wameniacha na wamefanya viapo na wale ambao si miungu. Niliwalisha vya kutosha, lakini wamefanya uasherati na kuchukua alama za nyumba ya uzinzi.
\v 8 Walikuwa farasi wanaotafuta kupandwa. Walitembea huku na huku wakitafutwa kupandwa. Kila mwanamume alimkaribia mke wa jirani yake.
\v 9 Kwa hiyo kwa nini nisiwaadhibu - asema BWANA - na kwa nini nisijilipizie kisasi juu ya taifa kama hili?
\s5
\v 10 Nenda hadi kwenye kuta za shamba lake la mizabibu na zihariibuni. Lakini wao msiwaharibu kabisa. Ondoeni matawi kwa sababu hayatoki kwa BWANA.
\v 11 Kwa sababu nyumba ya Yuda na Israeli wamenisaliti kabisa - asema BWANA -
\v 12 na wamenikataa. Wanasema, ''Yeye si halisi. Maovu hayawezi kutupata, wala hatutaona upanga wala njaa.
\v 13 Kwa kuwa manabii wamekuwa si kitu kama upepo na hakuna mtu mwiingine wa kunena ujumbe wa BWANA kwetu. Vitisho vyao na viwjie wao wenyewe."'
\s5
\v 14 Kwa hiyo BWANA, Mungu wa majeshi asema hivi, tazama nataka kuweka maneno yangu katika kinywa chako. Yatakuwa kama moto na watu hawa watakuwa kama kuni! Kwa kuwa utawaramba.
\v 15 Tazama nataka kuleta taifa dhidi yenu kutoka mbali, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA - ni taifa linalodumu, taifa la kale! Ni taifa ambalo lugha yake hamuijui, wala hamtaelewa wasemacho.
\s5
\v 16 Podo lao ni kaburi wazi. Wote ni wanajeshi.
\v 17 Kwa hiyo mavuno yako yataliwa, wana wako na binti zako pia, na chakula chako. Watakula kondoo wako na ng'ombe wako, watakula matunda ya zabibu zako na ya mitiini. Wataiangusha chini miji yenu na boma zake ambazo mnazitumainia.
\s5
\v 18 Lakini hata katika siku hizo - asema BWANA - sikusudii kuwaharibu kabisa.
\v 19 Itatokea kwenu, ninyi Yuda na Israeli, mkisema, 'Kwa nini BWANA, Mungu wetu ametufanyia haya yote?' kwamba wewe Yeremia, utawaambia, 'Kama vile mlivyomwacha BWANA na kuabudu miungu mingine katika nchi yenu, vivyo hivyo mtawatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.'
\s5
\v 20 Waambia haya watu wa nyumba ya Yakobo na yasikike katika Yuda. Waambie,
\v 21 'Sikilizeni hili, eny watu wapumbavu! Sanamu hazina matakwa; zina masikio lakini haziwawezi kusikia.
\v 22 Je, hamnihofu mimi - asema BWANA - au kutetemeka mbele ya uso wangu? Nimeweka mpaka wa mchanga kwenye bahari, ambao ni agizo la kudumu ambalo halibomoki - hata kama bahari ina kupwa na kujaa, bado hauwenzi kubomoka. Hata kama mawimbi yake yanaunguruma, hayawezi kuvuka.
\s5
\v 23 Lakini hawa watu wana mioyo ya usumbufu. Hugeuka kuwa wapinzani na kuondoka.
\v 24 Kwa kuwa hawasemi mioyoni mwao, "basi na tumche BWANA, Mungu wetu, yeye aletaye mvua za awali na mvua za vuli - kwa wakati wake, ambaye hutuzna majuma ya mavuno kwa ajili yetu."
\v 25 uovu wako umezuia haya yasitokee. Dhambi zako zimeyazuia mambo mema yasitokee.
\s5
\v 26 Kwa watu waovu wamo kati ya watu wangu. Wanatazama kama mtu anayenyatia ili kukamata ndege; wanaweka mitego na kukamata watu;
\v 27 Kama tundu la mtego lijaavyo ndege, nyumba zao zimejaa uongo. Kwa hiyo wanakua na kutajirika.
\v 28 Wamenenepa; wanang'aa na kupendeza. Wamepitiliza hata mipika ya maovu. Wala hawajali sababu ya kuwepo kwa watu na wala uwepo wa yatima. Wanafanikiwa hata kama hawatoi hukumu ya haki kwa yatima.
\v 29 Kwa nini nisiwadhibu kwa sababu ya haya - asema BWANA - sitajilipizia kisasi juu ya taifa la namna hii?
\s5
\v 30 Jambo la ajabu na la kuchukiza limetokea katika nchi hii.
\v 31 Mananbii wanatabiri kwa uongo, na makuhani wanatwala kwa msaada wa wa hao. Watu wangu wanapenda mambo ya hivyo, lakini mwisho kitatokea nini?
\s5
\c 6
\p
\v 1 Tafuteni mahali salama, enyi watu wa Benjamini, kwa kuondoka Yerusalemu. Pigeni tarumbeta zaTekoa. Simamisheni ishara juu ya Beth- Hakeremu, kwa uovu unaonekana ukitokea kaskazinni; pigo kubwa linakuja.
\v 2 Binti za Sayuni, warembo na mwororo, wataangamizwa.
\v 3 Wachungaji na kondoo wao watawaendea; wataweka hema zao zikiwazunguka pande zote; kila mtu atachunga kwa mkono wake.
\s5
\v 4 Jitakaseni wenyewe kwa miungu kwa ajili ya vita. Twendeni tukamvamie wakati wa adhuhuri. Ni vibaya sana kwamba mchana unatoweka na vivuli vya jioni vinakuja.
\v 5 Lakini tumvamieni usiku na na tuharibu ngome zake.
\s5
\v 6 Kwa kuwa BWANA wa majeshi asema hivi: Kateni miti yake, na tengenezeni vifusi vya kuitekea Yerualemu. Huu ndio mji sahihi kuuteka, Kwa sababu umejaa ukandamizaji.
\v 7 Kama vile kisima kitoavyo maji, vivyo hivyo mji huu uzaavyo uovu. Uaribifu na jeuri vimesikika kwake. Mateso na tauni viko mbele yangu daima.
\v 8 Uadhibiswhe, ee Yerusalemu, vingenevyo nitaondoka kwako na kukufanya ukiwa, na nchi isiyokaliwa na watu.
\s5
\v 9 BWANA wa majeshi asema hivi, "Hakika wataokota mabaki ya Isreli waliobaki kama zabibu. Nyosha mkono wako ili uchume zabibu.
\v 10 Nitamwambia nani na kumwonya nani ili wasikilize? Tazama! Masikio yao hayakutahariwa; hayawezi kutilia manani! Tazama! Neno la BWANA limekuja kuwarudi, lakini hawalitaki."
\s5
\v 11 Lakini nimejazwa na hasira za BWANA. Nimechoka kuizuia. Aliniambia, "Imwage mbele ya watoto mitaani na katika makundi ya vijana. Kwa kuwa kila mume atachukuliwa pamoja na mke wake; na kila mzee mwenye miaka mingi.
\v 12 Nyumba zao watapewa watu wengine, kwa kuwa nitawavamia wakazi wa nchi kwa mkono wangu - asema BWANA wa majeshi.
\s5
\v 13 BWANA amesema hayo kutoka kwa mdogo hadi kwa mkubwa, kila mmoja anatamani mapato ya udanganyifu. Kuanzia kuhani hadi nabii, Kila mmoja anafanya hila.
\v 14 Lakini wameponya vidonda vya watu wangu kwa juu juu tu. Wanasema, 'Amani! Amani! na kumbe amani haipo.
\v 15 Je, waliona aibu walipofanya machukizo? Hasha, hawakuona aibu! Hawakuwa na aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoj na wale watakaoanguka wakati nitakpowaadhibu. Wataangushwa chini," asema BWANA.
\s5
\v 16 BWANA asema hivi, `Simama kwenye njia panda utazame; uliza nzile njia za zamani, 'Je, hii tabia njema iko wapi?' Kisha endelea nayo na tafuta mahali pa kupumzika. Lakini watu wanasema, 'Hatutaenda.'
\v 17 Niliweka walinzi juu yenu ili wasikilize tarumbeta. Lakini walisema, 'Hatutasikiliza.'
\v 18 Kwa hiyo, sikilizeni, enyi mataifa! Tazameni, enyi mashahidi, muone kile kitakachowapata.
\v 19 Sikia, wewe dunia! Tazama, niko tayari kuleta janga kwa watu hawa - matunda ya fikra zao. Hawakusikiliza neno langu wala sheria zangu, badala yake walizikataa.
\s5
\v 20 Huu ubani kutoka sheba unaopanda una maana gani kwangu? Au huu uudi kutoka nchi ya mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliki kwangu wala dhabihu zenu.
\v 21 Kwa hiyo BWANA asema hivi, 'Tazama, 'Niko tayari kuweka kikwazo dhidi ya watu hawa. Watajikwaa juu yake - baba na watoto wao kwa pamoja watajikwaa. Wakazi na jirani zao pia watapotea.'
\v 22 BWANA asema hivi, 'Tazama watu wanakuja toka nchi ya kaskazini. Kwa kuwa taifa kubwa limechochewa kutoka nchi ya mbali.
\s5
\v 23 Watachukua pinde na mishale yao. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama muungurumo wa bahari, na wapanda farasi katika mfumo wa wanaume wa vita, enyi binti wa Sayuni,"'
\v 24 Tumesikia habai zao. Mikono yetu inalegea kwa dhiki. Na maumivu yametukamata kama utungu wa mwanamke anayezaa.
\s5
\v 25 Usiende nje mashambani, na usitembee barabarani, kwa kuwa upanga wa adui na hofu vimekaribia.
\v 26 Binti za watu wangu, jivikeni magunia na kugaagaa kwenye majivu ya maombolezo ya mwana pekee. Ombolezeni kwa huzuni kuu, kwa kuwa anayewaangamiza anakuja kwetu ghafula juu yetu.
\s5
\v 27 "Nimekufanya wewe, Yeremia, kuwajaribu watu wangu kama mtu anayepima fedha, kwa hiyo utachunguza na kupima njia zao.
\v 28 Wao ni watu wasumbufu miongoni mwa watu, wanaoenda huko na kule wakisingizia wengine. Wote ni shaba na chuma, wakitenda kwa dhuluma.
\v 29 Mifuo inafukuta kwa moto unaoziunguza; risasi inaunguzwa na moto. Risasi tu ndiyo inayotoka kati yake, lakini haifai kitu kwa sababu uovu haujaondolewa.
\v 30 Wataitwa taka za fedha, kwa sababu BWANA amewakataa.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Yermia,
\v 2 Simama katika lango la nyumba ya BWANA na utangaze ujumbe huu! Sikiilizeni neno la BWANA, ninyi nyote watu wa Yuda, ninyi mnaoingia katika malango haya kumwabudu BWANA.
\s5
\v 3 BWANA wsa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Tengenezeni njia zenu na kufanya mema, nami nitawaacha muishi hapa.
\v 4 Msitumainie maneno ya uongo mkisema, "Hekalu la BWANA!, Hekalu la BWANA! Hekalu la BWANA!"
\s5
\v 5 Bali kama mtazitengeneza njia zenu na kufanya mema, kama mtatoa hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake
\v 6 -kama hamtanyonya anayekaa katika nchi, yatima, mjane, na kama hamtamwaga damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa, na kama hataenda kwa miungu mingine kwa ajili ya maumivu yenu
\v 7 -ndipo nitakapowaacha mkae mahali hapa, katika nchi ambayo niliwapia mababu zenu toka zamani na hata milele.
\s5
\v 8 Tazama! Mnatumainia maneno ya uongo ambayo hayawasaidii.
\v 9 Je, mnaiba. mnaua, manafanya uzinzi? na mnaapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kwenda kwa miungu mingine ambao hamkuwajua?
\v 10 Je, mnakuja na kusimama mbele yangu katika nyumba hii ambapo jina langu linatangazwa na kusema, "Tumeokoka." hivyo mnaweza kufanya machukizo yote haya?
\v 11 Je, hii ndiyo nyumba inayobeba jina langu, pango la wanyang'anyi mbele ya macho yenu? Lakini tazama, Nimeiona - BWANA asema.'
\s5
\v 12 Kwa hiyo uende mahali pangu kule Shiloh, Kule ambako mwanzoni niliruhusu jina langu kukaa, na tazama kile nilichofanya pale kwa sababu ya maovu ya watu wangu Israeli.
\v 13 Kwa hiyo sasa, kwa sababu ya matendo yako haya yote - asema BWANA - Nilikuambia mara kadhaa, lakini hukusikiliza. Nilikuita, lakini hukuitika.
\v 14 Kwa hiyo kile nilichofanya Shilo, ndicho ambacho pia nitakachofanya kwa nyumba yangu hii inayoitwa kwa jina langu, nyumba amabyo ninyi mmeitumainia, mahali hapa ambapo niliwapa ninyi na mababu zenu.
\v 15 Kwa kuwa nitawafukuza mtoke kwangu kama vile nilivyowafukuza ndugu zenu wote, uzao wote wa Efraimu.'
\s5
\v 16 Na wewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa, na usiinue maombolezo ya kilio au kuomba sala kwa niaba yao, na usinishi, kwa kuwa sitakusikiliza.
\v 17 Kwani huoni kile wanachofanya katika miji ya Yuda na katika mitaa ya Yerusalemu?
\v 18 Watoto wanakusanya kuni na baba zao huwasha moto! Wanawake hukanda unga ili kuoka mikate kwa ajili ya malikia wa mbinguni na kumimina sadaka ya vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha mimi.
\s5
\v 19 Ni kweli wananikasirisha mimi? - asema BWANA - Je, si wao wanaojikasirisha, ili kwamba aibu iwe juu yao?
\v 20 Kwa hiyo BWANA, Mungu asema hivi, 'Tazama, hasira na ghahdabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, kwa watu wote na wanyama, juu ya miti katika mashamba na mazao ya ardhi, Itawaka nayo haitazimishwa.
\s5
\v 21 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Jiongezeeni sadaka za kuteketezwa katika dhabihu zenu na nyama zake.
\v 22 Kwani wakati nilipowatoa mababu zenu kutoka nchi ya Misri, Sikuhitaji chochote kutoka kwao. Sikuwapa amri juu ya maswala ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu.
\v 23 Niliwapa amri hii tu, "Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Kwa hiyo muishi katika njia ambazo ninawaamuru, ili mambo yenu yawe mazuri."
\s5
\v 24 Lakini hawkunisikiliza wala kuzingatia. Walishi kwa kufuata mipango yao ya uasi ya mioyo ya maovu, kwa hiyo walirudi nyuma badala ya kuendelea mbele.
\v 25 Tangu siku ambayo mababu zenu walitoka katika nchi ya Misri mpaka leo, Nimetuma watumishi wangu, manabii wangu, kwenu. Niliendelea kuwatuma.
\v 26 Lakini hawakuwasikiliza. Hawakuzingatia. Badala yake walishupaza shingo zao. Walikuwa waovu zaidi ya mababu zao.
\s5
\v 27 Kwa hiyo yatangaze maneno haya yote kwao, japo hawatakusikiliza. Yatangaze mambo haya kwao, lakini hawatakujibu.
\v 28 Waambie kuwa hili ni taifa ambalo haliisikilizi sauti ya BWANA, Mungu wake na lisilopokea mafundisho. Ukweli uneharibiwa na kukatwa kutoka kwenye vinywa vyao.
\s5
\v 29 Zikate nywele zako na kujinyoa, na kuzitupa. Imba wimbo wa maombolezo katika maeneo yaliyo wazi. Kwa kuwa BWANA amekikataa na kukitupa kizazi hiki cha hasira yake.
\v 30 Kwa kuwa wana wa Yuda wamefanya maovu mbele ya macho yangu - asema BWANA - wameweka machukizo yao katika nyumba ambayo jina langu hunenwa, ili kulinajisi.
\s5
\v 31 Kisha wamejenga mahali palipoinuka pa Tofethi ambapo pako kwenye bonde la Ben Hinomu. Walifanya hivi ili kuwachoma wana na binti zao kwenye moto - kitu ambacho mimi sikuamuru, wala kuweka jambo hilo katika akili zangu.
\v 32 Kwa hiyo, tazama siku zinakuja - asema BWANA - ambapo hapataitwa tena Tofethi au bonde la Ben Hinomu. Litakuwa bonde la machinjio; watazika maiti hapo Tofethi mpaka eneo lote lienee.
\s5
\v 33 Mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa duniani, na hakutakuwa na mtu wa kuwafukuza.
\v 34 Nitazikomesha katika miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalaemu sauti za kuiniuliwa na vicheko, Sauti ya bwana arusi na ya bibi arusi; kwa kuwa nchi hiyo itakuwa ukiwa."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Wakati huo - BWANA asema - wataleta kutoka makaburini mifupa ya wafalme wa Yuda na wakuu wake, mifupa ya makuhani na ya manabii na mifupa ya wakazi wa Yerusalemu.
\v 2 Kisha wataitandaza nje mchana kweupe na mbalamwezi na nyota zote za angani; hivi vitu katika anga vimenifuata na kunitumikia, na kwamba vimetembea na kutafuta, na kwamba vimeniabudu. Mifupa haitakusanywa na kuzikwa tena. Itakuwa kama mavi juu ya uso wa dunia.
\v 3 Na katika kila eneo lililobaki ambalo nimewafukuza, Watachagua mauti badala ya uzima kwa ajili yao, wote ambao watasalia kutokana na taifa hili ovu - asema BWANA wa majeshi.
\s5
\v 4 Kwa hiyo uwaambie, 'BWANA asema hivi: Je, kuna mtu anyeanguka na hasimami? Je, kuna mtu anayepotea na hawezi kujaribu kurudi?
\v 5 Kwa nini hawa watu, Yerusalemu, wamegeukia uasi daima? Wanashikilia uongo na wanakataa kutubu.
\s5
\v 6 Nilikaa kwa uangalifu na nikasikiliza, lakini hawakuongea kilicho sahihi; hakuna aliyetubia uovu wake, hakuna asemaye, "Nimefanya nini?" Kila mmoja wao huenda kule anakotaka, kama farasi aendaye kasi vitani.
\v 7 Hata koikoi angani hujua wakati sahihi; na njiwa, na mbayuayu, n a korongo. Huhama kwa wakati sahihi, lakini watu wangu hawayajui maagizo ya BWANA.
\s5
\v 8 Kwa nini mnasema, "Sisi tuna hekima! na sheria ya BWANA tunayoi?" Hakika, Tazama! Kalamu yenye uongo ya mwandishi imefanya uongo.
\v 9 Wenye hekima wataaibishwa. Wameyeyuka na na kunaswa. Tazama! wanakataa neno la BWANA, kwa hiyo hekima yao ni kwa ajili ya matumizi gani?
\v 10 Kwa wake zao nitawapa wengine, na mashamba yao kwa wale watakaowamiliki, kwa kuwa kuanzia kijana hadi mkuu, kwa pamoja ni wachoyo! Kuanzia nabii hadi kuhani, wote wanasema uongo.
\s5
\v 11 Kwa kuwa wametibu jeraha ya binti za watu wangu kwa juu juu. Walijisemea, "Amani, Amani," na kumbe hapakuwa na amani.
\v 12 Je, waliona aibu walipofanya machukizo? Hawakuaibika. Hawakuwa na utu. Kwa hiyo wataanguka wakati wa adhabu, pamoja na wale walioanguka. Watatupwa chini, asema BWANA.
\v 13 Nitawaondoa kabisa - asema BWANA - hapatakuwa na zabibu kwenye mizabibu yao, wala tini katika mitini yao. kwa kuwa jani litanyauka, na kile nilichowapatia kitaisha.
\s5
\v 14 Kwa nini tunakaa hapa? Njoni pamoja; twendeni kwenye hiyo miji yenye maboma, na tutakaa kimya kule katika kifo. Kwa kuwa BWANA, Mungu wetu atatunyamazisha. Atatufanya tunywe sumu, kwa kuwa tumemtenda dhambi.
\v 15 Tunatumainia amani, lakini hakutakuwa na jema. Tunatumainia wakati wa uponyaji, lakini tazama kutakuwa na hofu.
\s5
\v 16 Mkoromo wa farasi wake umesikika kutoka Dani. Dunia nzima inatikisika kwa sababu ya sauti ya kukaribia kwa farasi wake wenye nguvu. Kwa kuwa watakuja kuiangamiza nchi na utajiri wake, mji na wote wakaao nadani yake.
\v 17 Hebu tazama, ninawatuma nyoka kati yenu, fira ambao hawawezi kuzuiliwa kwa uganga. Watawauma - asema BWANA,."
\s5
\v 18 Huzuni yangu haina ukomo, na moyo wangu unaugua.
\v 19 Tazama! sauti ya maumivu ya binti wa watu wangu kutoka mbali! Je, BWANA hayumo Sayuni? Je, mfalme wake hayumo ndani yake? Kwa nini sasa wananichukiza kwa vitu vya kuchongwa na sanamu za kigeni zilizo batili?
\s5
\v 20 Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha. Lakini sisi hatujaokoka.
\v 21 Nimeumia kwa sababu ya maumivu ya binti wa watu wangu. Ninaomboleza kwa sababu ya mambo ya kushangaza ambayo yametokea kwake; Nimeyeyuka.
\v 22 Je, kule Gileadi hakuan dawa? Je, huko hayuko mponyaji? Kwa nini uponyaji wa binti wa watu wangu hautokei?
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kama kichwa changu kingetoa maji, na macho yangu kuwa chemichemi ya machozi! kwa kuwa natamani kulia usiku na mchana kwa ajili yao waliokuwa binti za watu wangu ambao wameuawa.
\v 2 Kama mtu anganipatia mahali pa wasafiri nyikani ili nikae, mahali ambapo ningeenda kuwatelekeza watu wangu. Kama ningewaacha, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la wenye hiana!
\v 3 asema BWANA, "Huupinda ulimi wao kana kwamba ni upinde ili wapate kuongea uongo, lakini si kwa uamiinifu wao kwamba wanapata nguvu duniani. Wanatoka uovu mmoja hadi mwiingine. Hawanijui mimi."
\s5
\v 4 Kila mmoja wenu, awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote. kwa kuwa kila ndugu ni mwongo,
\v 5 kila jirani anatembea akilaghai. Kila mwanamume anakejeli jirani yake na haongei ukweli. Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo. Hujidhofisha ili kusema uongo.
\v 6 Makazi yenu yako kati ya udanganyifu; kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi. Asema BWANA."
\s5
\v 7 Kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, "Tazama, Niko tayari kuwajaribu. Nitawajaribu nione. Jinsi gani niwezavyo kufanya kwa binti za watu wangu?
\v 8 Ndimi zao ni mishale iliyochongoka; huongea vitu vya uasi. Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao, lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubri.
\v 9 Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya - asema BWANA na kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili?
\s5
\v 10 Nitaimba wimbo wa kuomboleza na kulia kwa ajili ya milima, na wimbo wa mazishi utaimbwa nyikani. Kwa kuwa wameteketezwa kwa hiyo hakuna anAyeweza kupita kati kati yao. Hawatasikia sauti ya ng'ombe yeyote. Ndege wa angani na wanyama wote wamekimbia.
\v 11 Kwa hiyo nitaigeuza Yerusalemu kuwa vifusi vya ukiwa, maficho ya mbweha. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa miji iliyoharibiwa isiyokaliwa na watu.
\v 12 Ni nani mwenye hekima anayeyaelewa haya? Je, kinywa cha BWANA kinatangaza nini kwake ili aweze kuyasema? Kwa nini nchi imepotea? Imeharibiwa kama jangwa, ambapo hakuna apitaye kati kati yake.
\s5
\v 13 BWANA asema, "Ni kwa sababu wameziacha sheria zake ambazo niliwatengenezea, kwa sababu hawaisikilizi sauti yangu au kuishi kwa kuifuta.
\v 14 Ni kwa sababu wameishi kwa ushupavu wa mioyo yao na wamewafuata Mabaali kama baba zao walivyowafundisha kufanya.
\s5
\v 15 Kwa hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, Ninataka kuwafanya hawa watu wale pakanga na kunywa maji ya sumu.
\v 16 Ndipo nitakapowasambaza kati ya mataifa ambayo hawajayajua, wao wala mababu zao. Nitatuma upanga kwa ajili yao mpaka nimewaangamiza wote kabisa.'"
\s5
\v 17 BWANA wa majeshi asema hivi, "Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje.
\v 18 Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.
\s5
\v 19 Kwa kuwa sauti ya kilio imesikika Sayuni, 'Jinsi tulivyoharibiwa. Tumeaibishwa sana, kwa kuwa tumeitelekeza nchi tangu walIpoangusha nyumba zetu.'
\v 20 Kwa hiyo ninyi wanawake, sikieni neno la BWANA; zingatieni ujumbe unaokuja toka kinywani mwake. Kisha wafundisheni binti zenu wimbo wa maombolezo, na kila mwanamke wa jirani wimbo wa kilio.
\s5
\v 21 Kwa kuwa vifo vimekuja kupitia dirishani; vinaelekea mahali petu. Vinawaharibu watoto kutoka nje na vijana kwenye viwanja vya miji.
\v 22 Uyatangaze haya, 'Asema BWANA - mizoga ya wanaume itaanguka kama mavi kwenye mashamba na kama mabua baada ya mvunaji, na hapatakuwa na mtu wa kuyakusanya.'"
\s5
\v 23 BWANA asema hivi, "Usimwache mtu mwenye busara ajivune kwa ajili ya hekima yake, au shujaa kwa sababu ya uwezo wake. Usimwache mtu tajiri ajivunie utajiri wake.
\v 24 Kwa kuwa kama mtu atajivunia chochote kile, acha iwe hivi, yeye awe na busra na kunijua mimi. Kwa kuwa mimi ni BWANA, atendaye katika agano la wema, haki, na hukumu duniani. Ni katika hili kwamba ninafurahia- asema BWANA.
\s5
\v 25 Tazama, siku zaja - asema BWANA wakati nitakapowaadhibu wote ambao hawajatahiriwa ambao wako hivyo hivyo katika miili yao.
\v 26 Nitaiadhibu Misri na Yuda, Edomu, watu wa Amoni, Moabu, na watu wote wanaonyoa denge. Kwani mataifa yote haya hayajatahiriwa, na nyumba yote ya Israeli ina moyo ambao haujatahiriwa."
\s5
\c 10
\p
\v 1 "Sikilizeni neno ambalo BWANA anawaambieni, enyi nyumba ya Israeli.
\v 2 BWANA asema hivi, 'msijifunze njia za mataifa, na msishangazwe na ishara za mbinguni, kwa kuwa mataifa hushangazwa na haya.
\s5
\v 3 Kwa kuwa desturi za watu ni ubatili. Kwa kuwa mtu mmoja hukata mti msituni; kazi ya mikono ya mtu na shoka.
\v 4 Kisha huzipamba kwa fedha na dhahabu. Huikaza kwa misumari na nyundo ili isitikisike.
\v 5 Sanamu hizi ni mfano wa sanamu za kutishia ndege katika shamba la matango, kwa kuwa haziwezi kusema chochote. Hubebwa, kwa kuwa haziwezi hata kusogea hatua moja. Usiwaogope, Kwani hawawezi kutenda maovu wala mema."
\s5
\v 6 Hakuna aliye kama wewe, BWANA. Wewe ni mkuu, na jina lako lina nguvu.
\v 7 Ni nani asiyekuwa na hofu juu yako, wafalme wa mataifa? Kwa kuwa hiki ndicho unachostahili, kwa kuwa hakuna wa kuwa kama wewe kati ya wote wenye hekima katika mataifa yote au katika hali yao ya enzi.
\s5
\v 8 Wote wako sawa, ni kama wanyama na wapumbavu, wanafunzi wa samamu ambazo si chochote isipokuwa miti tu.
\v 9 Wanaleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi iliyotengenezwa na sonara, ni kazi ya ustadi. Mavazi yao ni ya rangi ya samawi na urujuani. Watu wao stadi waliyafanya haya yote.
\v 10 Lakini BWANA ni Mungu wa kweli. Yeye ni Mungu aliye hai na mfalme wa milele. Matetemeko yako katika hasira yake, na mataifa hayawezi kuvumilia hasira yake.
\s5
\v 11 Utawaambia hivi, "Miungu ambayo haikuumba mbingu na nchi itaangamia katika dunia hii na chini ya mbingu."
\v 12 Aliyeiumba dunia kwa nguvu zake aliumba nchi kavu kwa hekima zake na kuzitandaza mbingu kwa fahamu zake.
\v 13 Sauti yake ndiyo itengenezayo muungurumo wa maji mbinguni, naye huzileta mbingu katika mwisho wa dunia. Hutengeneza radi kwa ajili ya mvua na kutuma upepo kutoka katika hazina yake.
\s5
\v 14 Kila mtu amekuwa mjinga, hawana maarifa. Kila mfua chuma ameaibishwa kwa sanamu zake. Maana sanamu yake ya kuyeyushwa ni uongo; hakuna pumzi ndani yake.
\v 15 Ni ubatili tu, ni kazi ya udanganyifu; zitapotea wakati wa hukumu.
\v 16 Lakini Mungu ni fungu la Yakobo, si kama hawa, kwa kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; BWANA wa majeshi ndiye jina lake.
\s5
\v 17 Kusanya vitu vyako na uiache nchi, wewe ambaye umekuwa ukiishi katika mazingiwa haya.
\v 18 Kwa kuwa BWANA asema hivi, "Tazama, Ni tayari kuwatupa wakazi wa nchi nje wakati huu. Nitawasababishia huzuni, na itakuwa hivyo."
\s5
\v 19 Ole wangu! Kwa sababu ya mifupa yangu iliyovunjika, Jeraha zangu zimeumia. Kwa hiyo nilisema. "Hakika haya ni maumivu, lakini lazima nivumilie."
\v 20 Hema yangu imeharibiwa, na kamba za hema yangu zote zimekatwa. Wamewachukua watoto wangu wote, Kwa hiyo hawaishi tena. Hakuna tena mtu wa kuitandaza hema yangu au wa kuziinua pazia za hema yangu.
\s5
\v 21 Kwa kuwa wachungaji wamekuwa wapumbavu. Hawamtafuti BWANA. Kwa hiyo hawana mafanikio; Kondoo wao wote wamesambaa.
\v 22 Taarifa imewadia, "Tazama! inakuja, tetemeko kubwa linakuja kutoka katika nchi ya kaskazini kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, na maficho ya mbweha.
\s5
\v 23 Ninajua, BWANA, kwamba njia ya mtu haiji kutoka kwake. Wala hakuna mtu atembeaye anayeongoza hatua zake mwenyewe.
\v 24 Ee BWANA, unirudi, kwa hukumu za haki, si kwa hasira zako vinginevyo utaniangamiza.
\v 25 Mwaga hasira zako kwa mataifa ambao hawakujui na katika familia ambazo hawakuiti kwa jina lako. Kwa kuwa wamemla Yakobo na kumwangamiza kabisa na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Hili ndilo neno lililojia Yeremia kutoka kwa Bwana, akasema,
\v 2 "Sikiliza maneno ya agano hili, uwaambie kila mtu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
\s5
\v 3 Uwaambie, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: na alaaniwe yeyote asiyesikiliza maneno ya agano hili.
\v 4 Hili ndilo agano nililowaamuru baba zenu walishike siku nilipowatoa kutoka katika nchi ya Misri, kutoka tanuru ya chuma. Nikawaambia, "Sikilizeni sauti yangu na mfanye mambo yote kama nilivyowaamuru, kwa kuwa mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu."
\v 5 Nisikilizeni ili nipate kukitimiza kiapo nilichoapa kwa baba zenu, kiapo kwamba nitawapa nchi iliyojaa maziwa na asali kama ilivyo leo.'" Kisha mimi Yeremia nikajibu na kusema, "Ndio, Bwana!"
\s5
\v 6 Bwana akaniambia, "Hubiri habari hizi yote katika miji ya Yuda, na katika njia za Yerusalemu. Sema, "Sikilizeni maneno ya agano hili na mkayafanye.
\v 7 Kwa maana nimewaagiza wazee wenu tangu siku ile niliyowaleta kutoka nchi ya Misri hadi wakati huu wa sasa, nimewaonya mara kwa mara na kusema, "Sikilizeni sauti yangu.'"
\v 8 Lakini hawakusikiliza au wala kutega masikio yao. Kila mtu amekuwa akitembea katika ukaidi wa moyo wake mbaya. Kwa hiyo nilileta laana zote katika agano hili nililoamuru kuja juu yao. Lakini watu bado hawakuitii."
\s5
\v 9 Kisha Bwana akaniambia, "Njama imeonekana kati ya watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
\v 10 Wameugeukia uovu wa mababu zao wa mwanzo, ambao walikataa kusikiliza neno langu, ambao badala yake walifuata miungu mingine ili kuabudu. Waisraeli na nyumba ya Yuda walivunja agano langu nililoweka na baba zao.
\s5
\v 11 Kwa hiyo Bwana asema hivi, 'Tazameni, nitawaletea majanga juu yao, majanga ambayo hawataweza kuyaepuka. Ndipo wataniita, lakini sitawasikiliza.
\v 12 Miji ya Yuda na wenyeji wa Yerusalemu watakwenda na kuiita miungu ambayo walitoa sadaka, lakini hakika hawatawaokoa wakati wa majanga yao.
\v 13 Kwa kuwa idadi ya miungu yako ewe Yuda imeongezeka sawa na idadi ya miji yako. Na umefanya idadi ya madhabahu ya aibu huko Yerusalemu, madhabahu ya kufukiza uvumba kwa Baali, sawa na idadi ya njia zake.
\s5
\v 14 Kwa hiyo wewe mwenyewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa. Lazima usiomboleze au kuomba kwa niaba yao. Kwa maana siwezi kusikiliza wakati wananiita katika majanga yao.
\v 15 Mpendwa wangu anafanya nini nyumbani kwangu, ikiwa amekuwa na nia mbaya? Nyama za sadaka yako hazitakusaidia. Unafurahi kwa sababu ya matendo yako mabaya.
\v 16 Katika siku za nyuma Bwana alikuita mti wa mzeituni wenye majani, mzuri wenye matunda mazuri. Lakini atawasha moto juu yake ambayo itaonekana kama sauti ya dhoruba; matawi yake yatavunjika.
\s5
\v 17 Kwa maana Bwana wa majeshi, aliyekua amekusudia maafa juu yako, kwa sababu ya matendo mabaya ambayo nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamefanya-wamenikasirisha kwa kumtolea Baali sadaka.'"
\s5
\v 18 Bwana alinijulisha mambo haya, kwa hiyo nakayajua. Wewe, Bwana, umenifanya nione matendo yao.
\v 19 Nilikuwa kama kondoo mpole unayeongozwa na mchinjaji. Sikujua kwamba walikuwa wameunda mipango dhidi yangu, "Hebu tuangamize mti na matunda yake! Hebu tumkatilie mbali na nchi ya walio hai ili jina lake lisikumbukwe tena.
\v 20 Lakini Bwana wa majeshi ndiye mwamuzi mwenye haki ambaye huchunguza moyo na akili. Mimi nitashuhudia kisasi chako dhidi yao, kwa kuwa nimekuletea kesi yangu kwako.
\s5
\v 21 Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya watu wa Anathothi, wanaotafuta uhai wako, "wanasema, 'Usifanye unabii kwa jina la Bwana, usije utakufa kwa mkono wetu.'
\v 22 Kwa hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, 'Tazameni, nitawaadhibu. Vijana wao wenye nguvu watakufa kwa upanga. Wana wao na binti zao watakufa kwa njaa.
\v 23 Hakuna hata mmoja atakayeachwa, kwa maana nitaleta maafa dhidi ya watu wa Anathothi, mwaka wa adhabu yao.'"
\s5
\c 12
\p
\v 1 Wewe ni mwenye haki, Bwana, wakati wowote ninapoleta mashitaka kwako. Lazima nikuambie sababu yangu ya kulalamika: Kwa nini njia za waovu hufanikiwa? Watu wote wasiokuwa na imani wanafanikiwa.
\v 2 Wewe uliwapanda nao wakawa na mizizi. Wanaendelea kuzaa matunda. Wewe upo karibu nao katika vinywa vyao, lakini mbali na mioyo yao.
\s5
\v 3 Lakini wewe mwenyewe unanijua, Bwana. Umeona mimi na kuchunguza moyo wangu. Waondoe kama kondoo wa kuchinjwa. Ukakaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
\v 4 Je! Nchi itakauka kwa muda gani, na mimea katika kila shamba itaota kwa sababu ya uovu wa wenyeji wake? Wanyama na ndege wameondolewa. Hakika, watu wanasema, "Mungu hajui nini kitatokea kwetu."
\s5
\v 5 Bwana akasema, "Kweli, wewe, Yeremia, umetembea na askari wa miguu na wamechoka, unawezaje kushindana dhidi ya farasi? Ikiwa unashuka chini ya nchi iliyo salama, utafanyaje katika misitu karibu na Yordani?
\v 6 Kwa maana hata ndugu zako na familia ya baba yako wamekudharau na kukukemea kwa sauti kubwa. Usiwaamini, hata kama wanasema mambo mazuri kwako.
\s5
\v 7 Nimeiacha nyumba yangu; Nimeacha urithi wangu. Nimewatia watu wangu wapendwa mikononi mwa adui zake.
\v 8 Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba katika tundu; yeye hujiweka juu yangu kwa sauti yake mwenyewe, hivyo nimemchukia.
\v 9 Malipo yangu ya thamani ni fisi, na ndege wenye madoadoa karibu na kichwa chake. Nenda, ukakusanye viumbe vyote vilivyomo katika mashamba, na uwalete ili wale.
\s5
\v 10 Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu. Wameipoteza sehemu yangu yote ya ardhi; Waligeuza sehemu yangu nzuri kuwa jangwa, ukiwa.
\v 11 Wamemfanya kuwa ukiwa. Ninaomboleza kwa ajili yake; yeye ni ukiwa. Nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa maana hakuna mtu aliyeweka haya moyoni mwake.
\s5
\v 12 Waangamizi wamekuja juu ya maeneo yote yaliyo wazi jangwani, kwa maana upanga wa Bwana unakula kutoka upande mmoja wa nchi hadi mwingine. Hakuna usalama katika nchi kwa kiumbe chochote kilicho hai.
\v 13 Walipanda ngano lakini mavuno ya miiba. Wao wamechoka kutokana na kazi lakini hawajapata chochote. Basi muaibike kwa faida yenu kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana."
\s5
\v 14 Bwana asema hivi dhidi ya majirani zangu wote, waovu wanaopiga milki niliyowarithisha watu wangu Israeli, "Tazama, mimi ndimi ambaye nitawafukuza kutoka nchi yao wenyewe, nami nitaifuta nyumba ya Yuda kutoka kati yao.
\v 15 Ndipo baada ya kuangamiza mataifa hayo, itatokea kwamba nitakuwa na huruma juu yao na kuwaleta tena; Nitawarudi-kila mtu kwa urithi wake na nchi yake.
\s5
\v 16 Kisha itakuwa ikiwa mataifa hayo yatajifunza kwa makini njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu 'Kama Bwana anaishivyo!' vile vile kama walivyowafundishwa watu wangu kuapa kwa Baali, basi watajengwa katikati ya watu wangu.
\v 17 Lakini kama hakuna yeyote anayesikiliza, basi nitaling'oa taifa hilo. Kwa hakika litang'olewa na kuharibiwa-hili ndilo tamko la Bwana."
\s5
\c 13
\p
\v 1 Bwana aliniambia hivi, "Nenda ukape nguo ya kitani na kuiweka karibu na kiuno chako, lakini usiiweke kwenye maji kwanza."
\v 2 Kwa hiyo nilinunua vazi kama vile Bwana alivyoagiza, na nikafunga karibu na kiuno changu.
\v 3 Ndipo neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema,
\v 4 "Twaa vazi lako ulilolinunua lililo karibu na kiuno chako, uinuke, ukasafiri mpaka Frati. Ukaifiche huko katika mwamba wa jabali.
\s5
\v 5 Basi nikaenda na kuificha katika Frati kama vile Bwana alivyoniamuru.
\v 6 Baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia, "Simama, urudi Frati. Ukaichukue nguo ambayo nilikuambia ufiche."
\v 7 Kwa hiyo nikarudi Frati na kuchimba na kuchukua nguo mahali pale nilipoificha. Lakini tazama! Nguo hiyo ilikuwa imeharibika; haikuwa nzuri kabisa.
\s5
\v 8 Ndipo neno la Bwana likanijia tena, kusema,
\v 9 "Bwana asema hivi, Nitakiangamiza kiburi cha Yuda na Yerusalemu.
\v 10 Watu hawa waovu wanaokataa kusikia neno langu, ambao huenda katika ugumu wa mioyo yao, ambao hufuata miungu mingine ili kuabudu na kuinama-watakuwa kama hii nguo isiyofaa kwa lolote.
\v 11 Kwa maana kama vile vazi lililofungwa kwenye viuno vya mtu, ndivyo nimefainya nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda zimefungwa kwangu- hili ndilo tamko la Bwana-wawe watu wangu, ili kunifanya jina, sifa, na heshima. Lakini hawakunisikiliza.
\s5
\v 12 Basi uwaambie neno hili, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi Kila chupa itajazwa divai.' Watakuambia, 'Je, hatujui kwamba kila chupa itajazwa divai?'
\v 13 Basi uwaambie,' Bwana asema hivi: Tazama, nitawajaza kila mkaaji wa nchi hii ulevi, na wafalme wanaokaa kiti cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.
\v 14 Ndipo nitawagonganisha kila mtu na mwenzake baba na watoto wao pamoja; hili ndilo tamko la Bwana-sitawahurumia au kuwa na huruma, wala sitawarehemu kutoka kwenye uharibifu.
\s5
\v 15 Sikilizeni na makini. Msiwe na kiburi, kwa kuwa Bwana amesema.
\v 16 Mtukuze Bwana, Mungu wako, kabla ya hajaleta giza, na kabla ya kuifanya miguu yako kuwa na mashaka juu ya milima wakati wa jioni. Kwa maana unatarajia mwanga, lakini ataugeuza kuwa mahali pa giza, na kuwa giza nene.
\v 17 Kwa hiyo ikiwa husikilizi, nitaomboleza peke yangu kwa sababu ya kiburi chako. Hakika macho yangu yatalia na kutoa machozi, kwa sababu kundi la Bwana limechukuliwa mateka.
\s5
\v 18 "Mwambieni mfalme na mama wa malkia, 'Jinyenyekezeni, na kukaa chini, kwa maana taji juu ya kichwa chako, kiburi chako na utukufu wako, umeanguka.'
\v 19 Miji ya Negebu itafungwa, bila mtu wa kufungua. Yuda watachukuliwa mateka, wote uhamishoni.
\s5
\v 20 Inua macho yako na angalia wale wanaokuja kutoka kaskazini. Je, ni kundi gani alilokupa, kundi ambalo lilikuwa zuri sana kwako?
\v 21 Je, unasema nini wakati Mungu anawaweka wale ambao uliwafundisha kuwa marafiki? Je, huu si mwanzo wa maumivu ya utungu ambayo yatakuchukua kama mwanamke aliye katika kuzaa?
\s5
\v 22 Kisha unaweza kusema moyoni mwako, 'Kwa nini mambo haya yanatokea kwangu?' Itakuwa kwa uovu wa maovu yako ambapo marinda yako yamefunuliwa na umeumizwa.
\v 23 Je, watu wa Kushi hubadilisha rangi yao ya ngozi, au chui hubadilisha madoa yake? Ikiwa ndivyo, basi wewe mwenyewe, ingawa unazoea uovu, utaweza kufanya mema.
\v 24 Kwa hiyo nitawaangamiza kama makapi ambayo yanaangamia katika upepo wa jangwa.
\s5
\v 25 Hii ndiyo niliyokupa, sehemu ambayo nimekuagiza kwako-hili ndilo tamko la Bwana - kwa sababu umenisahau na kuamini katika udanganyifu.
\v 26 Kwa hiyo mimi mwenyewe nitaondoa nguo zako, na sehemu zako za siri zitaonekana.
\v 27 Uzinzi na ubembe wako, aibu ya tabia yako ya uasherati kwenye milima na katika mashamba! Nitayafanya yaonekane, mambo haya ya machukizo! Ole wako, Yerusalemu! Hutaki kuwa safi. Je! Hili litaendelea kwa muda gani?"
\s5
\c 14
\p
\v 1 Neno la Bwana lilimjia Yeremia kuhusu ukame,
\v 2 "Wayahudi waomboleze; basi milango yake ianguke. Wao wanaomboleza kwa ajili ya ardhi; Kilio chao kwa Yerusalemu kimepaa juu.
\v 3 Wenye nguvu huwatuma watumishi wao kwa ajili ya maji. Wanapoingia kwenye visima, hawawezi kupata maji. Wote wanarudi hawajafanikiwa; Wao hufunika vichwa vyao na aibu.
\s5
\v 4 Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao.
\v 5 Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
\v 6 Punda mwitu husimama kwenye mabonde yaliyo wazi na hupiga upepo kama mbweha. Macho yao yanashindwa kufanya kazi, kwa maana hakuna mimea.
\s5
\v 7 Hata ingawa maovu yetu yanatushuhudia, Bwana, tenda kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu matendo yetu yasiyo na imani yamezidi; tumekutenda dhambi.
\v 8 Matumaini ya Israeli, yule anayemwokoa wakati wa dhiki, kwa nini utakuwa kama mgeni katika nchi, kama mtu akaaye nchi ya kigeni ambaye hujinyoosha na kutumia hutumia usiku mmoja tu?
\v 9 Kwa nini utakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kama shujaa ambaye hawezi kuokoa mtu yeyote? Kwa maana wewe u katikati yetu, Bwana! Jina lako limetangazwa juu yetu. Usiondoke
\s5
\v 10 Bwana awaambia hivi watu hawa "Kwa kuwa wanapenda kutanga tanga, hawakuzuia miguu yao kufanya hivyo." Bwana hafurahi nao. Sasa anawakumbusha uovu wao na ameadhibu dhambi zao.
\v 11 Bwana akaniambia, Usiombe kwa ajili ya watu hawa.
\v 12 Maana ikiwa wanafunga, sitasikiliza kulia kwao; na wanapotoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za unga, sitawafurahia. Kwa maana nitawaangamiza kwa upanga, njaa, na tauni.
\s5
\v 13 Ndipo nikasema, "Ee Bwana, Bwana! Angalia! mabii wanawaambia watu, 'Huwezi kuona upanga; hakutakuwa na njaa kwako, kwa kuwa nitakupa usalama wa kweli mahali hapa.'"
\v 14 Bwana akaniambia, 'manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwafukuza, wala sikuwapa amri au kusema nao. Lakini maono ya udanganyifu na ya maana, uchawi wa udanganyifu unaotokana na akili zao ndicho wanachowahubiria."
\s5
\v 15 Kwa hiyo Bwana asema hivi, "Kwa habari ya manabii wakihubiri kwa jina langu, ambao mimi siwakutuma; wale wanaosema kuwa hakutakuwa na upanga wala njaa katika nchi hii mabii hawa wataangamia kwa upanga na njaa.
\v 16 Na watu waliopewa utabiri watafukuzwa nje ya barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga; kwa kuwa hakuna mtu wa kuwazikas-wao, na wake zao, na wana wao, wala binti zao; kwa maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.
\s5
\v 17 Sema neno hili kwao 'Acha macho yangu yatokwe machozi, usiku na mchana. wala yasikome, kwa kuwa kutakuwa na kuanguka kwa bikira, binti ya watu wangu - jeraha kubwa lisilotibika.
\v 18 Ikiwa nitatoka kwenye shamba basi angalia! kuna wale waliouawa kwa upanga. Na kama nitakuja mjini, basi, tazama! kuna wale walio na ugonjwa wa njaa. Hata nabii na kuhani wote wanatembea juu ya nchi bila maarifa.'"
\s5
\v 19 Je! Umemkataa kabisa Yuda? Je, unaichukia Sayuni? Kwa nini umetupiga wakati hakuna uponyaji kwetu? Tulitumaini amani, lakini hapakuwa na kitu kizuri-na kwa wakati wa uponyaji, lakini tazama, kuna hofu tu.
\v 20 Tunakubali, Bwana, makosa yetu, uovu wa babu zetu, kwa kuwa tumekukosea.
\s5
\v 21 Usitukatae! Kwa ajili ya jina lako, usikifedheheshe kiti chako cha enzi cha utukufu. Kumbuka na usivunje agano lako na sisi.
\v 22 Je, kuna miongoni mwa sanamu za mataifa yeyote zinazoweza kuifanya mbingu kutoa mvua? Je, si wewe, Bwana Mungu wetu, ambaye hufanya jambo hili? Tunatumaini kwako, kwa kuwa umefanya mambo haya yote.
\s5
\c 15
\p
\v 1 Kisha Bwana akaniambia, "Hata kama Musa au Samweli walisimama mbele yangu, bado sitawafikiria watu hawa. Watoe mbele yangu, ili waweze kuondoka.
\v 2 Ikiwa watakuambia, 'Tunapaswa kwenda wapi?' Kisha uwaambie, 'Bwana asema hivi Wale wanaotakiwa kufa wanapaswa kufa; wale waliotayarishwa kwa upanga wanapaswa kwenda kwa upanga. Wale waliopelekwa kwa njaa wanapaswa kwenda kwa njaa; na wale waliopelekwa uhamisho wanapaswa kuhamishwa.'
\s5
\v 3 Kwa kuwa nitawapa kwa makundi manne-hili ndilo tamko la Bwana-upanga wa kuua wengine, mbwa wararue, ndege wa angani na mnyama mkali wale na kuangamiza.
\v 4 Nitawafanyia jambo lenye kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu Manase mwana wa Hezekia, mfalme wa Yuda, alifanya huko Yerusalemu.
\s5
\v 5 Kwa maana ni nani atakayewahurumia, Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? Nani atakayegeuka kuuliza kuhusu ustawi wako?
\v 6 Umeniacha-hili ndilo tamko la Bwana-umerudi nyuma. Kwa hiyo nitawapiga kwa mkono wangu na kukuangamiza. Nimechoka kuwahurumia.
\v 7 Kwa hiyo nitawapepea kwa kipepeo katika milango ya nchi. Nitawafukuza. Nitawaangamiza watu wangu kwani hawakurudi na kuziacha njia zao.
\s5
\v 8 Nitawafanya wajane wao kuwa zaidi ya mchanga wa bahari. Dhidi ya mama wa vijana nitamtuma mwangamizi mchana. Nitafanya mshtuko na hofu ghafla kuanguka juu yao.
\v 9 Mama aliyezaa watoto saba ataharibika. Atashuka. Jua lake limekuchwa wakati bado ni siku. Yeye atakuwa na aibu na kufedheheka, kwa kuwa nitawatoa wale waliosalia kwa upanga mbele ya maadui zao-hili ndilo tamko la Bwana."
\s5
\v 10 Ole wangu, mama yangu! Kwa maana umenizaa, mimi ambaye ni mtu wa kushindana na hoja katika nchi yote. Sijakopesha, wala hakuna mtu aliyenikopesha, lakini wote wananilaani.
\v 11 Bwana akasema "Je sitakuokoa kwa manufaa? Kwa hakika nitawafanya maadui wako waombe msaada wakati wa msiba na dhiki.
\v 12 Je, mtu anaweza kusaga chuma? Hasa chuma kutoka kaskazini iliyochanganywa na shaba?
\s5
\v 13 Nitawapa adui zako utajiri wako na hazina yako kama nyara za bure. Nitafanya hili kwa sababu ya dhambi zako zote zilizofanywa ndani ya mipaka yako yote.
\v 14 Ndipo nitakufanya utumikie adui zako katika nchi ambayo huijui, maana moto utawaka, ukawaka katika ghadhabu yangu juu yako."
\s5
\v 15 Wewe mwenyewe wajua, Bwana! Unikumbuke na kunisaidia. Ukanilipie kisasi kwa ajili ya wanaonifuata. Katika uvumilivu wako usiniondoe. Utambue kwamba nimekuwa na aibu kwa ajili yako. Maneno yako yamepatikana, na nikayala.
\v 16 Maneno yako yalikuwa furaha kwangu, furaha yangu kwa moyo wangu; kwa maana jina lako linatangazwa juu yangu, Bwana, Mungu wa majeshi.
\s5
\v 17 Sikuketi katika mkutano wa wale waliosherehekea au waliofurahi. Nimeketi kwa faragha kwa sababu ya mkono wako wenye nguvu, kwa maana umenijaza na hasira.
\v 18 Kwa nini maumivu yangu yanaendelea na jeraha langu halitibiki, linakataa kuponywa? Je, utakuwa kama maji ya udanganyifu kwangu, maji yanayokauka?
\s5
\v 19 Kwa hiyo Bwana asema hivi, "Yeremia, Ikiwa utatubu, nitakurejesha, nawe utasimama mbele yangu na kunitumikia. Kwa maana ukitenganisha mambo ya kipumbavu kwa vitu vya thamani, utakuwa kama kinywa changu. Watu watakuja kwako, lakini wewe mwenyewe usirudi kwao.
\v 20 Nitakufanya kama ukuta wa shaba usioweza kuingilika kwa watu hawa, nao watapigana vita dhidi yako. Lakini hawatakushinda, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe ili kuokoa na kukuponya-hili ndilo tamko la Bwana-
\v 21 kwa maana nitakuokoa mikononi mwa waovu na kukukomboa katika mkono wa mshindani."
\s5
\c 16
\p
\v 1 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
\v 2 "Usiwe na mke, wala usiwe na wana au binti hapa.
\v 3 Kwa kuwa Bwana asema hivi kwa wana na binti ambao wamezaliwa hapa, kwa mama waliowabeba, na kwa baba waliowafanya wazaliwe katika nchi hii,
\v 4 'Watakufa vifo vya magonjwa. Hawataliliwa wala kuzikwa. Watakuwa kama samadi juu ya nchi. Kwa maana wataangamizwa kwa upanga na njaa, na miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.'
\s5
\v 5 Maana Bwana asema hivi, 'Usiingie nyumba yoyote yenye kuomboleza. Usiende kuwaombolezea, wala usihuzunike kwa ajili ya watu hawa. Kwa maana nimeondoa amani yangu, uaminifu wa agano, na huruma, kutoka kwa watu hawa! Ndivyo asemavyo Bwana;
\v 6 kwa hiyo wakuu na wadogo watakufa katika nchi hii. Wala hawatazikwa, wala hakuna yeyote atakayeomboleza kwa ajili yao. Hakuna mtu atakayejikata-kata au kunyoa vichwa vyao kwa ajili yao.
\s5
\v 7 Hakuna mtu anayepaswa kugawa chakula chochote wakati wa kuomboleza ili kuwafariji kwa sababu ya vifo, na hawatawapa kikombe cha faraja kwa baba yake au mama yake ili kuwafariji.
\v 8 Usiende kwenye nyumba ya karamu ili ukae pamoja nao ili kula au kunywa.
\v 9 Kwa maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, mbele yako, siku zako na mahali hapa, nitakomesha sauti ya furaha na sherehe, sauti ya bwana na bibi arusi. '
\s5
\v 10 Kisha itatokea kwamba utawaambia watu hawa maneno haya yote, na watakuambia, 'Mbona Bwana amesema maafa yote haya juu yetu? Uovu wetu ni uovu gani na dhambi yetu tuliyomtendea Bwana, Mungu wetu?'
\v 11 Basi uwaambie, 'hii ndiyo ahadi ya Bwana; Kwa sababu baba zenu waliniacha, nao wakafuata miungu mingine, wakaiabudu na kuisujudia. Waliniacha na hawakuishika sheria yangu.
\s5
\v 12 Lakini ninyi wenyewe mmeleta uovu zaidi kuliko baba zenu, kwa maana, kila mtu anaenda kwa ukaidi wa moyo wake mbaya; hakuna mtu anayenisikiliza.
\v 13 Kwa hiyo nitawafukuza kutoka nchi hii mpaka nchi msiyoijua, wewe wala baba zako, nanyi mtaiabudu miungu mingine huko mchana na usiku, kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu.'
\s5
\v 14 Kwa hiyo tazama! Siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo hawatasema tena, 'Kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.'
\v 15 Kwa maana, kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi aliyowaangamiza, nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.
\s5
\v 16 Angalia! hili ni tamko la Bwana-Nitatuma wavuvi wengi-kwa hiyo watawavua watu. Baada ya hayo nitatuma wawindaji wengi ili waweze kuwinda kati ya milima na vilima vyote, na katika miamba ya mwamba.
\v 17 Kwa kuwa macho yangu yapo juu ya njia zao zote; hawawezi kujificha mbele yangu. Uovu wao hauwezi kufichika mbele ya macho yangu.
\v 18 Nami kwanza nitawalipa mara mbili uovu na dhambi zao kwa kuwa wameichafua nchi yangu sanamu za machukizo, na kwa kujaza urithi wangu na sanamu zao za machukizo.
\s5
\v 19 Ee Bwana, wewe ndiwe ngome yangu, na kimbilio langu, na mahali pa usalama wangu siku ya shida. Mataifa yatakujia kwako kutoka mwisho wa dunia na kusema, 'Hakika baba zetu walirithi udanganyifu. Ubatili mtupu; hakuna faida ndani yao. Je!
\v 20 Watu hufanya miungu kwa ajili yao wenyewe? Lakini wao sio miungu.
\v 21 Kwa hiyo tazama! Nitawafanya wajue wakati huu, nitawafanya watambue mkono wangu na nguvu zangu, kwa hiyo watajua kwamba Yahweh ni jina langu."
\s5
\c 17
\p
\v 1 "Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma yenye ncha ya almasi. Imechongwa kwenye kibao cha mioyo yao na kwenye pembe za madhabahu zako.
\v 2 Watoto wao wanakumbuka madhabahu zao na miti yao ya Ashera kwa miti ya majani kwenye milima mirefu.
\s5
\v 3 Mlima wangu katika nchi ya wazi na mali yako yote pamoja na hazina zako zote, nitakupa kama nyara kwa wengine. Hiyo ndiyo thamani ya maeneo yako ya juu na dhambi iliyo katika maeneo yako yote.
\v 4 Utapoteza urithi niliokupa. Nitakutumikisha kwa adui zako katika nchi ambayo hujui, kwa maana umewasha moto katika ghadhabu yangu, ambao utakawaka milele."
\s5
\v 5 Bwana asema, "Mtu anayemtegemea mwanadamu amelaaniwa; amfanyaye mwanadamu kuwa nguvu yake na kugeuza moyo wake mbali na Bwana.
\v 6 Kwa maana atakuwa kama msitu mdogo katika Araba na hawezi kuona kitu kizuri kikija. Atakaa katika maeneo ya mawe jangwani, nchi isiyokuwa na wakazi.
\s5
\v 7 Lakini mtu anayemtegemea Bwana amebarikiwa, kwa kuwa Bwana ndiye tumaini lake.
\v 8 Kwa maana atakuwa kama mmea karibu na maji kando ya mto; mizizi yake itaenea. Hawezi kuona joto likija, kwa kuwa majani yake yatakuwa mabichi. Kisha mwaka wa ukame hawezi kuwa na wasiwasi, wala hataacha kuzalisha matunda.
\s5
\v 9 Moyo ni mdanganyifu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Una mgonjwa; ni nani anayeweza kuelewa?
\v 10 Mimi ni Bwana, ninayechunguza akili, ambaye hujaribu viuno. Ninampa kila mtu kulingana na njia zake, kulingana na matunda ya matendo yake.
\v 11 kama Kware akusanyaye mayai asiyotaga. Mtu anaweza kuwa tajiri kwa udhalimu, lakini wakati nusu ya siku zake ukipita, utajiri huo utamuacha, na mwishowe atakuwa mpumbavu."
\s5
\v 12 "Mahali pa hekalu letu ni kiti cha enzi cha utukufu, kilichoinuliwa tangu mwanzo.
\v 13 Bwana ni tumaini la Israeli. Wote ambao wanakuacha watakuwa na aibu. Wale walio katika nchi ambao wanageuka kutoka kwako watauliwa. Kwa maana wamwacha Bwana, chemchemi ya maji yaliyo hai.
\v 14 Niponye, Bwana, na mimi nitaponywa! Niokoe mimi, nami nitaokolewa. Kwa maana wewe ndio wimbo wangu wa sifa.
\s5
\v 15 Tazama, wananiambia, 'Neno la Bwana liko wapi? Hebu lije!'
\v 16 Mimi sikuwahi kuacha kuwa mchungaji nyuma yako. Sikuitamani siku ya maafa. Unajua yaliyotoka mdomoni mwangu. Yalifanyika mbele ya uwepo wako.
\s5
\v 17 Usiwe sababu ya hofu kwangu. Wewe ni kimbilio langu siku ya msiba.
\v 18 Waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi. Wataogopa, lakini usiache nifadhaike. Tuma siku ya maafa dhidi yao na kuwaangamiza maradufu."
\s5
\v 19 Bwana akaniambia hivi,: "Nenda ukasimame katika lango la watu ambako wafalme wa Yuda wanaingia na kutoka, basi katika malango mengine yote ya Yerusalemu.
\v 20 Uwaambie, 'Sikieni neno la Bwana, wafalme wa Yuda, na ninyi watu wote wa Yuda, na kila mtu wa Yerusalemu atakayeingia kwa njia ya malango haya.
\s5
\v 21 Bwana asema hivi: "Jihadharini kwa ajili ya maisha yenu na msichukue mzigo siku ya sabato ili muilete katika malango ya Yerusalemu.
\v 22 Wala msilete mzigo nje ya nyumba zenu siku ya sabato. Msifanye kazi yoyote, lakini muitenge siku ya Sabato, kama nilivyowaagiza wazee wako kufanya.'"
\v 23 Hawakusikiliza wala kutaega masikio yao, lakini walifanya shingo zao kuwa ngumu ili wasinisikilize wala kukubali maonyo.
\s5
\v 24 Itatokea kwamba ikiwa mtanisikiliza kweli-hili ndilo tamko la Bwana-na msilete mzigo kwenye malango ya jiji hili siku ya sabato lakini badala yake mkatenga siku ya sabato kwa Bwana na msifanye kazi yoyote juu yake -
\v 25 basi wafalme, wakuu, na wale wanaokaa kiti cha Daudi wataingia malango ya mji huu kwa magari na farasi, wao na viongozi wao, watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu. Na mji huu utakaa milele.
\s5
\v 26 Watakuja kutoka miji ya Yuda na kutoka pande zote za Yerusalemu, kutoka nchi ya Benyamini na visiwa vya chini, kutoka milimani na kutoka kaskazini, wakileta sadaka za kuteketezwa, dhabihu, sadaka za nafaka na ubani, sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Bwana.
\v 27 Lakini ikiwa hamtasikiliza-kutakasa siku ya Sabato, kutochukua mizigo nzito, wala msiingie milango ya Yerusalemu siku ya sabato, nitawasha moto katika malango yake, nao utaangamiza majumba kuteketeza ngome za Yerusalemu, na hauwezi kuzimika.
\s5
\c 18
\p
\v 1 Neno la Bwana lilimjia Yeremia, kusema,
\v 2 "Simama, uende kwa nyumba ya mfinyanzi; kwa maana nitakusikilizisha neno langu huko.
\v 3 Basi, nikaenda nyumbani kwa mfinyanzi, na tazama! Mfinyanzi alikuwa akifanya kazi kwenye gurudumu la mfinyanzi.
\v 4 Lakini chombo cha udongo ambacho alikuwa akikifinyanga kiliharibika mkononi mwake, kwa hiyo alibadili mawazo yake na akafanya kitu kingine ambacho kilionekana kuwa kizuri machoni pake.
\s5
\v 5 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
\v 6 "Je, siwezi kuwa kama huyu mfinyanzi kwenu, nyumba ya Israeli? Angalia! Kama udongo katika mkono wa mfinyanzi-ndivyo ulivyo mkononi mwangu, nyumba ya Israeli.
\v 7 Kwa wakati mmoja, ninaweza kutangaza jambo fulani juu ya taifa au ufalme, kwamba nitaufukuza, kuuvunja, au kuuharibu.
\v 8 Lakini kama taifa ambalo nimefanya tamko hilo linageuka na kuacha maovu yake, basi nitaghairi nisitende maafa niliyokuwa nimepanga.
\s5
\v 9 Wakati mwingine, ninaweza kutangaza jambo fulani kuhusu taifa au ufalme, kwamba nitaujenga au kuupanda.
\v 10 Lakini ikiwa watafanya mabaya machoni pangu kwa kutosikiliza sauti yangu, basi nitaghairi mema ambayo nilikuwa nimewaambia nitawafanyia.
\s5
\v 11 Basi sasa, waambie watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, ukisema, 'Bwana asema hivi: Tazameni, nitawaangamiza. Mimi ni karibu kufinyanga mabaya dhidi yenu. Tubuni, kila mtu kutoka njia yake mbaya, hivyo njia zako na matendo yako yatakuletea mema.'
\v 12 Lakini watasema, 'Hili halina maana. Tutafanya kulingana na mipango yetu wenyewe. Kila mmoja wetu atafanya mabaya kwa kuufuata uchupavu wa moyo wake.'
\s5
\v 13 Kwa hiyo Bwana asema hivi, 'Uliza watu wa mataifa, ambao wamewahi kusikia habari kama hii? Bikira wa Israeli amefanya kitendo cha kutisha.
\v 14 Je, theluji ya Lebanoni imetoka milima yenye miamba juu ya pande zake? Je, mito ya mlima inayotoka mbali iliharibiwa, mito hiyo ya baridi?
\s5
\v 15 Hata hivyo watu wangu wamesahau. Wamefanya sadaka kwa sanamu zisizo na maana na wamefanya mashaka katika njia zao; wameacha njia za kale za kutembea katika njia ndogo.
\v 16 Nchi yao itakuwa ya hofu, kitu cha kuzomewa milele. Kila mtu atakayepita karibu naye atashuhudia na kutingisha kichwa chake.
\v 17 Nitawaangamiza mbele ya adui zao kama upepo wa mashariki. Nitawageuzia kisogo, wala sio uso wangu, siku ya msiba wao.'"
\s5
\v 18 Basi watu wakasema, "Njoni, tufanye njama dhidi ya Yeremia, maana sheria haitapotea kabisa kwa makuhani, wala ushauri kutoka kwa wenye hekima, au maneno ya manabii. Njoo, mshambulie kwa maneno yetu na tusisikilize tena chochote anachosema."
\v 19 Sikiliza, Ee Bwana! Na kusikiliza sauti ya adui yangu.
\v 20 Je, maafa kutoka kwao itakuwa malipo yangu kwa kuwa mema kwao? Kwa maana wamenichimbia shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele yako ili niseme mema kwa ajili yao na kugeuza ghadhabu yako isiwapate.
\s5
\v 21 Basi uwape watoto wao njaa, na uwatie mikononi mwa wale wanaotumia upanga. Basi, waache wanawake wao wafiwe na kuwa wajane, na watu wao watauawa, na vijana wao wauawe kwa upanga wa vita.
\v 22 Kelele ya kusikitisha isikiwe kutoka katika nyumba zao, kama utakapoleta washambuliaji ghafla juu yao. Kwa kuwa wamechimba shimo kunikamata na wameficha mitego katika miguu yangu.
\v 23 Lakini wewe, Bwana, unajua mipango yao yote dhidi yangu ya kuniua. Usisamehe uovu na dhambi zao. Usiondoe dhambi zao mbali nawe. Badala yake, waache waangamizwe mbele yako. Tenda juu yao wakati wa ghadhabu yako.
\s5
\c 19
\p
\v 1 Bwana akasema hivi, "Nenda ukanunue chupa ya udongo wakati ukiwa na wazee wa watu na makuhani.
\v 2 Kisha uende mpaka bonde la Ben Hinomu wakati wa kuingia kwenye mlango uliovunjika wa mfinyanzi, na huko utangaza maneno nitakayokuambia.
\v 3 Ukisema, 'Sikilizeni neno la Bwana, wafalme wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu! Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Tazameni, na nitaletea msiba juu ya mahali hapa, na masikio ya kila mtu anayesikia yatawaka.
\s5
\v 4 Nitafanya hivyo kwa sababu wameniacha na kudharau mahali hapa. Katika mahali hapa wanatoa sadaka kwa miungu mingine ambayo hawakuijua. Wao, baba zao, na wafalme wa Yuda pia wamejaza mahali damu isiyo na hatia.
\v 5 Walimjengea Baali mahali pa juu na kuwachoma watoto wao kwa moto kama sadaka za kuteketezwa kwake-kitu ambacho sijawaamuru au kutaja, wala hakuingia ndani ya akili yangu.
\s5
\v 6 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, bonde la Ben Hinomu, kwa kuwa litakuwa bonde la machinjo.
\v 7 Katika mahali hapa nitatamgua mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya wapate kuuawa kwa upanga mbele ya adui zao na kwa mkono wa wale wanaotafuta maisha yao. Ndipo nitawapa miili yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.
\v 8 Ndipo nitaifanya mji huu kuwa uharibifu na kitu cha kuzomewa, kila mtu anayepita atashangaa na kuzomea kwa sababu mateso yake yote.
\v 9 Nitawafanya wale nyama ya wana wao na binti zao; kila mtu atakula mwili wa jirani yake katika dhiki na katika uchungu ambao umeletwa kwao na maadui zao na wale wanaotaka maisha yao.'"
\s5
\v 10 Kisha utavunja chupa ya udongo mbele ya watu ambao walikwenda pamoja nawe.
\v 11 Uwaambie,'Bwana wa majeshi asema hivi: nitafanya jambo hili kwa watu hawa na mji huu- hii ndiyo ahadi ya Bwana, kama vile Yeremia alivyovunja chupa ya udongo ili isiweze kutengenezwa tena. Watu watazika wafu huko Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.
\s5
\v 12 Hivyo ndivyo nitakavyopafanya mahali hapa na wenyeji wake nitakapofanya jiji hili kama Tofethi, hili ndio tamko la Bwana;
\v 13 kwa hiyo nyumba za Yerusalemu na wafalme wa Yuda watakuwa kama Tofethi, nyumba zote zilizo juu ya watu waovu wanaoabudu nyota zote za mbinguni na kumwaga sadaka za kinywaji kwa miungu mingine.'"
\s5
\v 14 Ndipo Yeremia akatoka Tofethi, ambako Bwana amemtuma ahubiri. Akasimama katika ua wa nyumba ya Bwana, akawaambia watu wote,
\v 15 "Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazameni, nitawaletea mji huu na miji yake yote maafa yote niliyonena dhidi yake, kwa kuwa walifanya shingo zao kuwa ngumu na kukataa kusikiliza maneno yangu.'"
\s5
\c 20
\p
\v 1 Pashuri, mwana wa Imeri, kuhani, alikuwa msimamizi mkuu, akamsikia Yeremia akihubiri maneno haya mbele ya nyumba ya Bwana.
\v 2 Basi Pashuri akampiga nabii Yeremia, akamtia katika masanduku yaliyokuwa kwenye lango la juu la Benyamini ndani ya nyumba ya Bwana.
\s5
\v 3 Ikawa siku ya pili Pashuri akamtoa Yeremia nje ya makabati. Yeremia akamwambia, "Bwana hakukuita Pashuri, lakini wewe ni Magor-Misabibu.
\v 4 Kwa maana Bwana asema hivi, 'Tazama, nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wewe na wapendwa wako wote; kwa maana wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona. Nitawatia Yuda mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atawafanya kuwa mateka huko Babeli au kuwaangamiza kwa upanga.
\s5
\v 5 Nitampa mali zote za jiji hili na utajiri wake wote, vitu vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Nitaweka vitu hivi mikononi mwa adui zako, nao watawakamata. Nao watawachukua na kuwaleta Babeli.
\v 6 Lakini wewe Pashuri, na wenyeji wote wa nyumba yako watakwenda mateka. Utakwenda Babeli na kufa huko. Wewe na wapendwa wako wote ambao uliwatabiria maneno ya uongo mtazikwa huko.'"
\s5
\v 7 "Umenidanganya, Bwana. Kwa hakika nimedanganyika. Wewe ulinikamata na kunishinda. Nimekuwa kitu cha kuchekesha. Watu wananidharau kila siku, siku zote.
\v 8 Kwa maana wakati wowote nimenena, nimeita na kutangaza, 'Vurugu na uharibifu.' Na neno la Bwana limefanywa shutumu na dhihaka kwangu kila siku.
\v 9 Nami nikisema, 'Sitafikiria juu ya Bwana tena. Sitatangaza tena jina lake.' Ni kama moto moyoni mwangu, uliofanyika ndani ya mifupa yangu. Kwa hiyo ninajitahidi kustahimili lakini siwezi.
\s5
\v 10 Nimesikia habari za ugaidi kutoka kwa watu wengi pande zote. 'Mshitaki! Lazima tumshitaki' Wale walio karibu nami kuangalia kama nitaanguka. 'Labda anaweza kudanganywa. Ikiwa ndivyo, tunaweza kumshinda na kujilipiza kisasi kwake.'
\v 11 Lakini Bwana yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu, hivyo wale wanaonifuata watajikwaa. Hawatanishinda. Watakuwa na aibu sana, kwa sababu hawatafanikiwa. Watakuwa na aibu ya kudumu, haitasahauliwa kamwe.
\s5
\v 12 Lakini wewe, Bwana wa majeshi, wewe unayemtazama wenye haki na ambaye huona akili na moyo. Hebu nipate kuona kisasi chako juu yao kwa maana nimekuletea shitaka langu kwako.
\v 13 Mwimbieni Bwana! Msifuni Bwana! Kwa kuwa ameokoa maisha ya wale waliokandamizwa kutoka kwenye mikono ya waovu.
\s5
\v 14 Na ilaaniwe siku niliyozaliwa. Usiruhusu siku ambayo mama yangu alinizaa ibarikiwe.
\v 15 Na alaaniwe mtu aliyemwambia baba yangu akisema, 'Amezaliwa mtoto wa kiume,' na kusababisha furaha kubwa.
\s5
\v 16 Mtu huyo atakuwa kama miji ambayo Bwana aliiangamiza bila huruma. Na asikie wito wa msaada asubuhi na sauti ya vita wakati wa mchana.
\v 17 Hiyo itatokea, kwa kuwa Bwana hakuniua tumboni au kumfanya mama yangu kaburi langu, tumbo la ujauzito milele.
\v 18 Kwa nini nilitoka tumboni ili kuona matatizo na uchungu, ili siku zangu zijazwe na aibu?"
\s5
\c 21
\p
\v 1 Hili ndilo neno lililotoka kwa Bwana kwa Yeremia wakati mfalme Sedekia alimtuma Pashuri mwana wa Malkiya na Sefania mwana wa Maaseya, kuhani. Wakamwambia,
\v 2 "Pata ushauri kutoka kwa Bwana kwa ajili yetu, kwa kuwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita. Labda Bwana atafanya miujiza kwetu, kama ilivyokuwa zamani, na kumfanya aondoke kwetu."
\s5
\v 3 Basi Yeremia akawaambia, "Hivi ndivyo mtakavyomwambia Sedekia
\v 4 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, niageuza nyuma vyombo vya vita vilivyo mkononi mwenu, ambavyo mnapigana dhidi ya mfalme wa Babeli na Wakaldayo wanaokufunga kutoka nje ya kuta! Kwa maana nitawakusanya katikati ya jiji hili.
\v 5 Nami nitapigana nanyi kwa mkono ulioinuka na mkono wenye nguvu, na ukali, ghadhabu, na hasira kubwa.
\s5
\v 6 Kwa maana nitawaangamiza wenyeji wa mji huu, wanadamu na wanyama, watakufa kwa tauni kali.
\v 7 Baada ya hayo- hii ndiyo ahadi ya Bwana-Sedekia mfalme wa Yuda, watumishi wake, watu, na kila mtu aishiye katika mji huu baada ya tauni, upanga na njaa, nitawatia wote mkononi mwa Nebukadreza mfalme wa Babeli, na mikononi mwa adui zao, na katika mkono wa wale wanaotaka uhai wao. Ndipo atawaua kwa makali ya upanga. Hatawahurumia, hatawaokoa, au kuwa na rehema.'
\s5
\v 8 Basi uwaambie watu hawa, 'Bwana asema hivi Angalia, nitaweka mbele yako njia ya uzima na njia ya mauti.
\v 9 Mtu yeyote anayeishi katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa, na tauni; lakini mtu yeyote atakayetoka na kuanguka kwa magoti mbele ya Wakaldayo ambao wamefungwa dhidi yako ataishi. Yeye ataokoka na maisha yake.
\v 10 Kwa maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu ili kuleta maafa na sio kuleta mema-hili ndilo tamko la Bwana. Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza.'
\s5
\v 11 Kuhusu nyumba ya mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Bwana.
\v 12 Nyumba ya Daudi, Bwana asema, "Hukumuni kwa haki asubuhi. Umuokoe yule aliyeibiwa kwa mkono wa mwenye kuonea, au ghadhabu yangu itatoka kama moto na kuchoma, na hakuna mtu anayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yako mabaya.
\s5
\v 13 Angalia, mwenyeji wa bonde na mwamba wa nchi ya wazi! Mimi niko juu yako, - hii ndiyo ahadi ya Bwana- Mimi ni juu ya mtu yeyote anayesema, 'Ni nani atashuka kutupiga?' au 'Ni nani atakayeingia kwenye nyumba zetu?'
\v 14 Nitawaadhibu kutokana na matunda ya matendo yako-hili ndilo tamko la Bwana- na nitawasha moto katika misitu, na utateketeza kila kitu.'"
\s5
\c 22
\p
\v 1 Bwana asema hivi, "Nenda kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda, utangaze neno hili huko.
\v 2 Ukaseme, 'Ewe Mfalme wa Yuda, wewe aliyeketi kiti cha Daudi, usikilize neno la Bwana. Nisikilizeni, enyi watumishi wake, na ninyi, watu wake mnaokuja kwa malango haya.
\v 3 Bwana asema hivi, "Fanya haki na uadilifu, na mtu yeyote ambaye ameibiwa-muokoeni kutoka mkononi mwa mshindani. Usimtendee mabaya mgeni yeyote katika nchi yako, au yatima au mjane. Usifanye vurugu au kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa.
\s5
\v 4 Kwa kuwa mkifanya mambo hayo, basi wafalme wanaoketi kiti cha Daudi wataingia milango ya nyumba hii wakiendesha gari na farasi, yeye, watumishi wake, na watu wake!
\v 5 Lakini ikiwa hamsikilizi maneno haya kutoka kwangu ambayo nimeyasema-hili ndilo tamko la Bwana-basi nyumba hii ya kifalme itaharibiwa.'"
\s5
\v 6 Kwa maana Bwana asema hivi juu ya nyumba ya mfalme wa Yuda, "Wewe uko kama Gileadi, au kama kilele cha Lebanoni kwangu. Hata hivyo nitakugeuza kuwa jangwa, katika miji isiyo na wenyeji.
\v 7 Kwa kuwa nimewaagiza waharibifu kuja juu yenu! Watu wenye silaha zao watakata mierezi yako iliyo bora na kuiacha kuanguka kwenye moto.
\s5
\v 8 Kisha mataifa mengi yatapita kwenye mji huu. Kila mtu atamwambia yule anayefuata, "Mbona Bwana amefanya hivi kwa jiji hili kuu?"
\v 9 Na mwingine atajibu, "Kwa sababu waliiacha agano la Bwana, Mungu wao, wakainama kwa miungu mingine, wakaiabudu."
\s5
\v 10 Usilie kwa ajili ya aliyekufa. Usiomboleze kwa ajili yake. Lakini mlilie mtu yeyote anayeingia kifungoni, kwa maana hatarudi tena kuiona nchi aliyozaliwa.'
\s5
\v 11 Maana Bwana asema hivi juu ya Yehoahazi, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyekuwa mfalme badala ya Yosia babaye, 'ametoka mahali hapa, wala hatarudi.
\v 12 Atakufa huko mahali ambapo walimchukua mateka, na hataiona tena nchi hii.'
\s5
\v 13 Ole mtu yeyote anayejenga nyumba yake kwa uovu na vyumba vyake vya juu katika udhalimu; ambao wengine hufanya kazi, lakini hawalipwi.
\v 14 Ole mtu yeyote atakayesema, 'Nitajenga nyumba ndefu na vyumba vya juu vipana, na hujenga madirisha mapana, na kuta zenye mwerezi, na huipaka rangi nyekundu.'
\s5
\v 15 Je, hii ndiyo inakufanya uwe mfalme mzuri, kwamba unataka kuwa na mbao za mwerezi? Je baba yako hakula na kunywa, lakini lakini alifanya hukumu na haki? Kisha mambo yakawa mazuri kwa ajili yake.
\v 16 Alihukumu maneno ya masikini na mhitaji. Ilikuwa vizuri. Je, huku siko kunijua mimi? - hili ni tamko la Bwana.
\s5
\v 17 Lakini hakuna kitu machoni na moyoni mwako isipokuwa wasiwasi kwa faida yako isiyo ya haki na kwa kumwaga damu isiyo na hatia, kwa ukandamizaji kuwatendea jeuri wengine.
\v 18 Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Hawatamwomboleza wakisema 'ole, ndugu yangu! au 'Ole, dada yangu!' Hawataomboleza kwa kusema 'Ole, bwana! ' au 'ole, utukufu!'
\v 19 Atazikwa maziko ya punda, ataburuzwa mbali na kutupwa nje ya milango ya Yerusalemu.
\s5
\v 20 Panda milima ya Lebanoni piga kelele. Paza sauti yako Bashani. Piga kelele kutoka kwenye milima ya Abarimu, kwa maana marafiki zako wote wataharibiwa.
\v 21 Nilinena nawe wakati ulioko salama, lakini ukasema, 'Sitasikia.' Hii ilikuwa desturi yako tangu ujana wako, kwani hukusikiliza sauti yangu.
\s5
\v 22 Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na marafiki zako watakwenda kufungwa. Hakika wewe utakuwa na aibu na kufadhaika kwa matendo yako yote mabaya.
\v 23 Wewe mfalme, wewe ambaye huishi katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni, wewe aliyefanya kiota kati ya mierezi, utakuwa na hali ya kuhurumiwa utakapopata utungu kama wakati wa kuzaa."
\s5
\v 24 "Kama mimi niishivyo-hili ndilo tamko la Bwana-hata kama wewe, Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ulikuwa alama ya mkono wangu wa kulia, ningekuangusha.
\v 25 Kwa kuwa nimewatia mikono ya wale wanaotaka uhai wenu na kwenye mkono wa wale ambao mnawaogopa, hata mkononi mwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Wakaldayo.
\v 26 Nitawatupa wewe na mama yako aliyekuzaa katika nchi nyingine, nchi ambayo hujazaliwa, na huko utakufa.
\s5
\v 27 Na kuhusu eneo hili ambalo watataka kurudi, hawatarudi hapa.
\v 28 Je! Hiki ni chombo kilichodharauliwa na kilichopasuka? Je, Konia ni chombo kilichodharauliwa? Kwa nini wamemtupa yeye na wazao wake, kumpeleka katika nchi wasiyoijua?
\s5
\v 29 Ee Ardhi, Ardhi, Ardhi! Sikieni neno la Bwana!
\v 30 Bwana asema hivi, 'Andika juu ya mtu huyu Konia Yeye hatakuwa na mtoto. Hatafanikiwa wakati wa siku zake, wala hakuna hata mmoja kati ya uzao wake atakayefanikiwa au kuketi tena kwenye kiti cha Daudi na kutawala juu ya Yuda.'"
\s5
\c 23
\p
\v 1 "Ole wao wachungaji ambao huangamiza na kuwatawanya kondoo wa malisho yangu-hii ndiyo ahadi ya Bwana."
\v 2 Kwa hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi juu ya wachungaji ambao wanawachunga watu wake, "Ninyi mnawatawanya kundi langu na kuwafukuza. Hamuwajali hata kidogo. Tambueni hili! Mimi nitawalipiza uovu wa matendo yenu-hili ni tamko la Bwana.
\s5
\v 3 Mimi mwenyewe nitakusanya mabaki ya kondoo wangu kutoka nchi zote nilizowafukuza, nami nitawarejesha kwenye eneo la malisho, ambako watazaa na kuongezeka.
\v 4 Ndipo nitawainua wachungaji juu yao ambao watawachunga hivyo hawataogopa tena au kupotezwa. Hakuna hata mmoja atakayepotea-hili ni tamko la Bwana.
\s5
\v 5 Angalia, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-nitakapomuinulia Daudi tawi la haki. Atatawala kama mfalme; atatenda kwa busara na kusababisha hukumu na haki katika nchi.
\v 6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli wataishi kwa usalama. Na jina lake atakayeitwa Bwana ni haki yetu.
\s5
\v 7 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-hawatasema tena, 'Kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.'
\v 8 Badala yake watasema, 'Kama Bwana aishivyo, ambaye aliwaleta na ambaye aliwaongoza wana wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote walizofukuzwa.' Nao watakaa katika nchi yao wenyewe."
\s5
\v 9 Kuhusu manabii, moyo wangu umevunjika ndani yangu, na mifupa yangu yote imetetemeka. Nimekuwa kama mlevi, kama mtu ambaye ameshindwa na divai, kwa sababu ya Bwana na maneno yake matakatifu.
\v 10 Kwa maana nchi imejaa wazinzi. Kwa sababu ya hayo nchi imeuka. Milima katika jangwa imekauka. Njia hizi za manabii ni mbaya; nguvu zao hazitumiwi kwa namna sahihi.
\s5
\v 11 Kwa maana manabii na makuhani wote wamekufuru. Nimeona uovu wao ndani ya nyumba yangu! - hili ndilo tamko la Bwana;
\v 12 kwa hiyo njia yao itakuwa kama mahali pa kupumzika katika giza. Watasukumwa chini. Wao wataanguka ndani yake. Kwa maana nitawatuma mabaya juu yao katika mwaka wa adhabu yao; hili ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 13 kwa maana nimeona uchungu kati ya manabii huko Samaria. Walitabiri kwa Baali na wakawaongoza watu wangu Israeli kwenye njia sahihi.
\v 14 Na miongoni mwa manabii huko Yerusalemu nimeona mambo ya kutisha: wanafanya uzinzi na huenda kwa udanganyifu. Wanaimarisha mikono ya waovu; hakuna mtu anarejea na kuacha uovu wake. Wote wamekuwa kama Sodoma kwangu na wenyeji wake kama Gomora!"
\v 15 Kwa hiyo, Bwana wa majeshi asema hivi juu ya manabii, "Tazameni, nitawafanya wale magugu na kunywa maji yenye sumu, kwa maana kufuru imetoka kwa manabii wa Yerusalemu na kuingia katika nchi yote."
\s5
\v 16 Bwana wa majeshi asema hivi, "Usisikilize maneno ya manabii wanaokuhubiri. Wamekudanganya! Wanatangaza maono kutoka kwenye mawazo yao wenyewe, si kwa kinywa cha Bwana.
\v 17 Wanasema daima kwa wale wanaonidharau mimi, 'Bwana asema kutakuwa na amani kwako.' Na kila mtu anayetembea katika ukaidi wa moyo wake anasema, 'mabaya hayatakuja kwenu.'
\v 18 Lakini nani amesimama katika mkutano wa baraza la Bwana? Ni nani anayeona na kusikia neno lake? Ni nani anayezingatia maneno yake na kusikiliza?
\s5
\v 19 Tazama, kuna dhoruba inayotoka kwa Bwana! Hasira yake inatoka, na dhoruba inazunguka. Inazunguka vichwa vya waovu.
\v 20 Hasira za Bwana hazitarejea mpaka zitakapotimiza nia ya moyo wake. Katika siku za mwisho, utaelewa.
\s5
\v 21 Sikuwatuma manabii hawa. Wao tu walionekana. Sikuwahubiri jambo lolote kwao, lakini bado wanatabiri.
\v 22 Kwa kuwa kama walisimama katika mkutano wangu wa baraza, wangeweza kuwasababisha watu wangu kusikia neno langu; wangewafanya wapate kuacha maneno yao mabaya na mazoea mabaya.
\s5
\v 23 Mimi ni Mungu aliye karibu-hili ni tamko la Bwana-mimi sio Mungu aliye mbali?
\v 24 Je, kuna mtu yeyote anayejificha mahali penye siri ili nisiweze kumwona? -Hili ndilo tamko la Bwana-Je mbingu na nchi hazikujawa nami? -hili Ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 25 Nimesikia yale waliyosema manabii, wale waliokuwa wanatabiri uongo kwa jina langu. Wakisema, 'Nilikuwa na ndoto!
\v 26 Nilikuwa na ndoto!' Je, hii itaendelea mpaka lini, manabii wanaotabiri uongo kutoka kwa akili zao, na wanasema nini kutokana na udanganyifu mioyoni mwao?
\v 27 Wana mpango wa kuwafanya watu wangu kusahau jina langu kwa ndoto ambazo wanazoripoti, kila mmoja kwa jirani yake, kama vile babu zao walivyosahau jina langu kwa ajili ya jina la Baali.
\s5
\v 28 Nabii aliye na ndoto, aseme ndoto hiyo. Lakini yule ambaye nimemwambia kitu fulani, basi aseme neno langu kwa kweli. Je, majani yanahusiana na nafaka? - hili ni tamko la Bwana-
\v 29 Na neno langu si kama moto? -Hili ni tamko la Bwana-na kama mwamba wenye kupiga nyundo?
\v 30 Tazameni, ninapingana na nabii-hii ndiyo ahadi ya Bwana-yeyote anayeiba maneno kutoka kwa mtu mwingine na anasema yanatoka kwangu.
\s5
\v 31 Tazama, ninapingana na manabii-hili ndilo tamko la Bwana-ambao hutumia lugha zao kutabiri maneno.
\v 32 Tazameni, ninapingana na manabii wanaoota ndoto-hii ndiyo ahadi ya Bwana-na kisha kuwahubiri na kwa njia hii kuwadanganya watu wangu kwa udanganyifu wao na kujivunia. Mimi ni juu yao, kwa kuwa sikuwatuma wala kuwapa amri. Kwa hivyo hawatawasaidia watu hawa - hili ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 33 Watu hawa au nabii au kuhani wakakuuliza, 'Je, ni nini tamko la Bwana?' basi lazima uwaambie, 'Ni tamko gani? Kwa maana nimekuacha wewe-hili ndilo tamko la Bwana.
\v 34 Kwa habari ya manabii, makuhani, na watu wanaosema, 'Hili ndilo tamko la Bwana,' nitamuadhibu mtu huyo na nyumba yake.
\s5
\v 35 Endelea kusema, kila mtu kwa jirani yake na kila mtu kwa ndugu yake, 'Bwana alijibu nini?' na 'Bwana alitangaza nini?'
\v 36 Lakini usizungumze tena juu ya tamko la Bwana, kwa kuwa kila tamko kutoka kwa kila mtu limekuwa ujumbe wake mwenyewe, na umepotosha maneno ya Mungu aliye hai, Bwana wa majeshi, Mungu wetu.
\s5
\v 37 Utamuuliza nabii hivi, 'Bwana alikujibu nini? Je, Bwana alisema nini? Kisha unasema tamko kutoka kwa Bwana;
\v 38 lakini Bwana asema hivi, Sema hivi, "Hili ni tamko la Bwana" ingawa nimekuagiza na kusema, "Usiseme: Hili ni tamko kutoka kwa Bwana."
\v 39 Kwa hiyo, angalia, nitawachukua na kukutupa mbali na mimi, pamoja na jiji ambalo nilikupa wewe na baba zako.
\v 40 Ndipo nitaweka aibu ya milele na fedheha juu yenu ambayo haitasahauliwa.'"
\s5
\c 24
\p
\v 1 Bwana alinionyeshea kitu. Tazama, vikapu viwili vya tini viliwekwa mbele ya hekalu la Bwana. (Maono haya yalitokea baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, maofisa wa Yuda, mafundi na wafua vyuma kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babeli.)
\v 2 Kikapu kimoja cha tini kilikuwa nzuri sana, kama tini za kwanza zilizoiva, lakini kikapu kingine cha tini zilizokuwa mbaya sana zisizoweza kuliwa.
\v 3 Bwana akaniambia, "Unaona nini Yeremia?" Nikasema, "Tini. Tini ambazo ni nzuri sana na tini ambazo ni mbaya sana haziwezi kuliwa."
\s5
\v 4 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
\v 5 "Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: nitawaangalia mateka wa Yuda kwa manufaa yao, kama vile tini hizi nzuri, nilipowatoa mateka kutoka hapa mpaka nchi ya Wakaldayo.
\v 6 Nitaweka macho yangu kwao wapate mema na kuwarejeshea nchi hii. Nitawajenga, wala sitawaangamiza.
\v 7 Nitawapanda, wala sitawang'oa. Ndipo nitawapa moyo wa kunijua; kwa kuwa mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu na mimi nitakuwa Mungu wao, hivyo watanirudia kwa moyo wao yote.
\s5
\v 8 Lakini kama vile tini mbaya ambazo ni hazifai kuliwa - asema Bwana - nitatenda hivi kwa Sedekia, mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wake, na pamoja na wengine wa Yerusalemu ambao wanabaki katika nchi hii au kwenda kukaa katika nchi ya Misri.
\v 9 Nitawafanya kuwa kitu cha kutisha, wapate maafa, mbele ya falme zote duniani, aibu na somo kwa mithali, matusi, na laana mahali pote nitakapowafukuza.
\v 10 Nitatuma upanga, njaa, na tauni dhidi yao watapotelea mbali kutoka kwenye nchi niliyowapa wao na baba zao."
\s5
\c 25
\p
\v 1 Hili ndilo neno ambalo lilimjia Yeremia juu ya watu wote wa Yuda. Ikawa mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Huo ndio mwaka wa kwanza wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli.
\v 2 Yeremia nabii aliwahubiria watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu.
\s5
\v 3 Akasema, "Kwa miaka ishirini na mitatu, tangu mwaka wa kumi na tatu wa Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda mpaka leo, maneno ya Bwana yamekuja kwangu. Nimewahubiria ninyi. Nilikuwa na nia ya kutangaza, lakini hamkunisikiliza.
\v 4 Bwana akawapeleka watumishi wake wote manabii kwako. Walikuwa na nia ya kwenda, lakini hukusikiliza wala kutega masikio.
\s5
\v 5 Manabaii hawa walisema, 'Kila mtu auache uovu wake na udhalimu wa matendo yake na kurudi kwenye nchi ambayo Yahwe aliitoa wakati wa zamanai kwa ajili ya babu zenu na ninyi, kama zawadi ya kudumu.
\v 6 Kwa hiyo msiifuate miungu mingine ili kuiabudu au kuiinamia chini, na msimkasirishe kwa kazi ya mikono yenu ili kwamba awaumize.
\s5
\v 7 Lakini hamkunisikiliza-hili ndilo tamko la Bwana-kwa hiyo umenikasirisha kwa kazi ya mikono yako ili kujidhuru nafsi zemu.
\v 8 Basi, Bwana wa majeshi asema hivi, 'Kwa kuwa hukusikiliza maneno yangu,
\v 9 tazama, nitaagiza amri ya kukusanya watu wote wa kaskazini- asema Bwana- na Nebukadreza, mtumishi wangu, mfalme wa Babeli, na kuwaleta juu ya nchi hii na wenyeji wake, na juu ya mataifa yote yaliyo karibu nawe. Kwa maana nitawaangamiza. Nitawageuza kuwa na hofu, kuwa kitu cha kuzomewa na ukiwa wa daima.
\s5
\v 10 Sauti ya furaha na sherehe-sauti ya bwana arusi na bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia na mwanga wa taa-nitafanya mambo yote haya kutoweka kutoka kwa mataifa haya.
\v 11 Ndipo nchi hii yote itakuwa ukiwa na hofu, na mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.
\s5
\v 12 Kisha miaka sabini itakapokamilika, nitamuadhibu mfalme wa Babeli na taifa hilo, nchi ya Wakaldayo-hili ndilo tamko la Bwana-kwa uovu wao na kuifanya kuwa ukiwa milele.
\v 13 Nami nitaleta juu ya nchi hiyo maneno yote niliyosema, na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hiki ambacho Yeremia ametabiri juu ya mataifa yote.
\v 14 Kwa maana pia mataifa mengi na wafalme wakuu watapata watumwa kutoka mataifa haya. Nitawalipa kwa matendo yao na kazi za mikono yao.'"
\s5
\v 15 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Chukua kikombe hiki cha divai ya ghadhabu kutoka mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote niliyokutuma.
\v 16 Kwa maana watakunywa na kisha watalewa na kufanya wazimu mbele ya upanga ambao nitaupeleka kati yao."
\s5
\v 17 Basi, nikakichukua kikombe mkononi mwa Bwana, nikawanywesha mataifa yote ambayo Bwana alinituma:
\v 18 Yerusalemu, miji ya Yuda, na wafalme wake, na wakuu wake, na kuwafanya kuwa ukiwa na kitu cha kutisha, na kuwa kitu cha kuzomewa na laana, kama ilivyo hata leo..
\s5
\v 19 Mataifa mengine pia walipaswa kunywa: Farao mfalme wa Misri na watumishi wake; maafisa wake na watu wake wote;
\v 20 watu wote wa urithi wa mchanganyiko na wafalme wote wa nchi ya Uzi; na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;
\v 21 Edomu na Moabu na wana wa Amoni.
\s5
\v 22 Wafalme wa Tiro na Sidoni, wafalme wa pwani ng'ambo ya pili ya bahari,
\v 23 Dedani, Tema, na Busi pamoja na wale wanyoao nywele zao upande wa pili wa vichwa vyao, pia walipaswa kukinywa.
\s5
\v 24 Watu hawa pia walitakiwa kukinywa; wafalme wote wa Uarabuni na wafalme wote wa watu wa asili mchanganyiko wanaoishi nyikani;
\v 25 wafalme wote wa Zimri, wafalme wote wa Elamu, na wafalme wote wa Wamedi;
\v 26 wafalme wote wa kaskazini, wale wa karibu na wale wa mbali—kila mmoja na ndugu zake na falme zote za ulimwengu ambazo ziko chini ya uso wa dunia. Hatimaye mfalme wa Babeli atakunywa baada yao wote.
\s5
\v 27 Bwana akaniambia, "Basi, uwaambie, 'Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi kunywa na kulewa, kisha tapika, uanguke, wala usisimame mbele ya upanga nitakaoutuma kati yenu.'
\v 28 Kisha itatokea kwamba ikiwa wanakataa kuchukua kikombe mkononi mwako ili kunywa, utawaambia, 'Bwana wa majeshi asema hii lazima mnywe.
\v 29 Kwa maana, tazama, nitaleta janga juu ya mji ulioitwa kwa jina langu, je ninyi mtaachiliwa msiadhibiwe? Hutakuwa huru, kwa maana nitaita upanga juu ya wenyeji wote wa nchi! - ndilo tamko la Bwana wa majeshi.'
\s5
\v 30 Basi wewe mwenyewe, Yeremia, tabiri kwao maneno haya yote. Uwaambie, 'Bwana atanguruma kutoka juu, naye atapaza sauti yake toka makao yake matakatifu, na radi kutoka mahali pake patakatifu; naye atapiga kelele kama wale wakanyagao zabibu dhidi ya wote wanaoishi duniani.
\v 31 Kelele huja mpaka mwisho wa nchi, kwa sababu mgogoro kutoka kwa Bwana utaleta mashtaka dhidi ya mataifa. Ataleta haki kwa wote wenye mwili. Yeye atawatia waovu katika upanga-hili ndi'o tamko la Bwana.'
\s5
\v 32 Bwana wa majeshi asema hivi, 'Tazameni, taabu itatokea toka kwa taifa hadi taifa, na dhoruba kubwa itatokea toka pande za mwisho za dunia.
\v 33 Kisha wale waliouawa na Bwana watakuja kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine; hawataomboleza, kukusanyika, au kuzikwa. Watakuwa kama samadi chini.
\s5
\v 34 Pigeni Yowe, wachungaji, na pigeni kelele ya kuomba msaada! Gaagaa katika ardhi, enyi mlio hodari katika kundi. Kwa kuwa siku yako ya kuuawa na kutawanywa imekuja. Utaanguka kama kondoo waliochaguliwa.
\v 35 Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia. Hakuna kutoroka kwa watu walio hodari katika kundi.
\v 36 Kuna mlio wa wasiwasi wa wachungaji na milio ya kulalama kwa watu walio hodari katika kundi, kwa kuwa Yahweh anayaharibu malisho yao.
\s5
\v 37 Kwa hiyo, malisho ya amani yataharibiwa kwa sababu ya hasira ya Bwana.
\v 38 Kama simba, ameacha shimo lake, kwa kuwa ardhi yao itakuwa kitu cha kushangaza kwa sababu ya hasira ya muonevu, kwa sababu ya ghadhabu yake kali'"
\s5
\c 26
\p
\v 1 Mwanzoni mwa utawala wake Yehoyakimu mwana wa Yosia, neno likaja kutoka kwa Yeremia, likisema,
\v 2 "Yahwe anasema hivi: Simama katika uwanja wa nyumba yangu na sema kuhusu miji yote ya Yuda ambao huja kuabudu katika nyumba yangu. Tangaza maneno yote niliyokuamuru kuyasema kwao. Usipunguze neno lolote!
\v 3 Labda watasikiliza, kwamba kila mtu ataziacha njia zake mbaya, ili nighairi majanga ninayokusudia kuyaleta juu yao kwa sababu ya uovu wa matendo yao.
\s5
\v 4 Kwa hiyo lazima useme kwao, 'Yahwe anasema hivi: Kama hamtanisikiliza ili mtembee katika sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu—
\v 5 kama hamsikilizi maneno ya watumishi wangu manabii ambao naendelea kuwatuma kwenu—lakini hamjasikiliza! —
\v 6 kisha nitaifanya nyumba hii kuwa kama Shilo; nitaifanya nyumba hii kuwa laana katika macho ya mataifa yote juu ya dunia.
\s5
\v 7 Makuhani, manabii, na watu wote wakamsikia Yeremia akitangaza maneno haya katika nyumba ya Yahwe.
\v 8 Kwa hiyo ikatokea kwamba Yeremia alipomaliza kutangaza aliyokuwa Yahwe alimwwamuru kuyasema kwa watu wote, makuhani, manabii, na watu wote wakamsimamisha na kusema, "Hakika utakufa!
\v 9 Kwa nini umetabiri katika jina la Yahwe na kusema kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa, pasipo wakaaji?" Kwa maana watu wote wameunda kundi dhidi ya nyumba ya Yeremia.
\s5
\v 10 Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahwe. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahwe.
\v 11 Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, "Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!"
\v 12 Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, "Yeremia amenituma kutabiri juu ya nyumb hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia.
\s5
\v 13 Kwa hiyo sasa, imarisheni njia zenu na matendo yenu, na sikilizeni sauti ya Yahwe Mungu wenu kwamba ataghairi kuhusu janga ambalo ametangaza dhidi yenu.
\v 14 Mimi mwenyewe—niangalieni! —niko mikononi mwenu. Nitendeeni yaliyo mema na sahihi katika macho yenu.
\v 15 Lakini kwa hakika lazima mjue kwamba kama mtaniua mimi, basi mnaiweka damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wakaaji wake, kwa maana Yahwe amenituma kweli kwenu ili nitangaze maneno yote kwa ajili ya masikio yenu."
\s5
\v 16 Kisha wakuu na watu wote wakasema kwa makuhani na manabii, "Si vyema kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametangaza mambo haya kwetu katika jina la Yahwe Mungu wetu."
\v 17 Kisha watu kutoka wazee wa nchi wakasimama na kusema kwa kusanyiko lote la watu.
\s5
\v 18 Wakasema, "Mikaya Mmorashi alikuwa akitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Alinena kwa watu wote wa Yuda na kusema, 'Yahwe wa majeshi anasema hivi: Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la magofu, na mlima wa hekalu utakuwa kilima kilichoota vichaka.' Hezekia mfalme wa Yuda na Yunda wote walimuua?
\v 19 Hakumwogopa Yahwe na kuutaka radhi uso wa Yahwe ili kwamba Yahwe angeghairi kuhusu janga ambalo alilitangaza kwao? Kwa hiyo tutafanya maovu makubwa zaidi juu ya maisha yetu sisi wenyewe?"
\s5
\v 20 Wakati huo huo palikuwa na mtu mwingine ambaye alitabiri katika jina la Yahwe—Uria mwan wa Shemaya kutoka Kiriath Yearimu—pia alitabiri juu ya mji na nchi hii, akikubaliana na maneno yote ya Yeremia.
\v 21 Lakini Mfalme Yohoyakimu na wanajeshi wake wote na watumishi wake wote waliposikia maneno yake, kisha mfalme alijaribu kumuua, lakini Uria alisikia na kuogopa, kwa hiyo alikimbia na akaenda Misiri
\s5
\v 22 Kisha mfalme Yehoyakimu alituma watu kwenda Misiri—Elnathani mwana wa Achbori na watu kwenda Misiri kumfuata Uria.
\v 23 Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
\v 24 Lakini mkno wa Ahikamu mwana wa Shapni alikuwa pamoja na Yeremia, hivyo hakutiwa mikonono mwa watu ili auawe.
\s5
\c 27
\p
\v 1 Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hil lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahwe. (Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema "Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema "Sedekia", kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake).
\v 2 Hiki ndicho Yahwe alisema kwangu, "Tengeneza vifungo na nira kwa ajili yako mwenyewe. Ziweke shingoni mwako.
\v 3 Kisha akawatuma kwenda kw mfalme wa Edomu, mfalme wa Moabu, mfalme wa watu wa amoni, mfalme wa Tiro, na kwa mfalme wa Sidoni. Watume kwa mkono wa wajumbe hao wa wafalme ambao walikuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.
\v 4 Toa amri kwao kwa ajili ya mabwana zao na sema, ' Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hivyo ndivyo utakavyosema kwa mabwana zenu,
\s5
\v 5 Mimi mwenyewe niliiumba dunia kwa nguvu zangu kuu na mkono wangu ulioinuka. Pia niliwaumba watu na wanyama juu ya dunia, na nikawatoa kwa yeyote aliyesahihi katika macho yangu.
\v 6 Kwa hiyo sasa, Mimi mwenyewe naziweka nchi hizi zote kwenye mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu. Pia, ninavikabidhi kwake viumbe hai vyote katika mashamba ili vimtumikie.
\v 7 Kwa maana mataifa yote watamtumikia yeye, wanaye, na wajukuu zake hadi muda wa nchi yake ufike. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamtiisha.
\s5
\v 8 Kwa hiyo taifa na ufalme ambo haumtumikii Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na ule usioweka shingo yake chini ya nira ya Nebukadreza mfalme wa Babeli—nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa, na pigo—hili ni tangazo la Yahwe—hadi nitakapokuwa nimewateketeza kwa mkono wake.
\s5
\v 9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, wabashiri wenu, waonaji wenu, ndoto zenu, watambuzi wenu, ambao wamekuw wakisema kwenu na kusema, ' Msimtumikie mfalme wa Babeli.'
\v 10 Kwa maana wanatabiri uongo kwenu ili kuwapeleka mbali na nchi zenu, kwa maana nitawapeleka mbali, na mtakufa.
\v 11 Lakini taifa ambalo wataweka shingo zao chini ya nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitawaruhusu kupumzika katika nchi yao—hili ni tangazo la Yahwe—na watailima na kufanya nyumba zao humo.""
\s5
\v 12 Kwa hiyo nilisema kwa Sedekia mfalme wa Yuda na kumpa ujumbe huu, "Ziwekeni shingo zenu chini ya nira ya mfalme wa Babeli na mtumikieni yeye na watu wake, na mtaishi.
\v 13 Kwa nini mfe—wewe na watu wako—kwa upanga, njaa, na pigo, kama vile nilivyotangaza kuhusu taifa ambalo watapuuza kumtumikia mfalme wa Babeli?
\s5
\v 14 Msisikilize maneno ya manabii wanaozungumza kwenu na kusema, 'Msimtumikie mfalme wa Babeli', kwa maana wanatabiri uongo kwenu.
\v 15 'Kwa maana mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana wanatabiri uongo katika jina langu ili kwamba niwafukeze inje na muangamie, ninyi nyote na manabii wanaotabiri kwenu."'
\s5
\v 16 Nilitangaza hili kwa makuhani na watu wote na kusema, "Yahwe anasema hivi: Msisikilize maneno ya manabii wanaotabiri kwenu na kusema, 'Angalia! Vyombo vya nyumba ya Yahwe vinarudishwa kutoka Babeli sasa hivi!' Wanatabiri uongo kwenu.
\v 17 Msiwasikilize. Mtamtumikia mfalme wa Babeli na mtaishi. Kwa nini mji huu uangamizwe?
\v 18 Kama ni manabii, na kama neno la Mungu limekuja kwao kweli, basi wamwombe Yahwe wa majeshi asivipeleke Babeli vyombo vilivyosalia katika nyumba, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu.
\s5
\v 19 Yahwe wa majeshi anasema hivi kuhusu zile nguzo, bahari, na kitako, na vyombo vyote vilivyosalia katika mji huu—
\v 20 vyombo ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika utumwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.
\s5
\v 21 Yahwe wa majeshsi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu vyombo vilivyosalia katika nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu,
\v 22 'Vitaletwa Babeli, na vitabaki huko hadi siku niyovipangia kutimia—hili ni tangazo la Yahwe—kisha nitavileta na kuvirudisha kataika sehemu hii."
\s5
\c 28
\p
\v 1 Ilitokea katika mwaka ule, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne na mwezi wa tano, Hanania mwana wa Azuri nabii, alikuwa wa Gibeoni, alisema kwangu katika nyumba ya Yahwe mbele za makuhani na watu wote. Alisema,
\v 2 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeivunja nira iliyowekwa na mfalme wa Babeli.
\s5
\v 3 Ndani ya miaka miwili nitavirudisha katika sehemu hii vyombo vyote vya nyumba ya Yahwe ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli livichukua kutoka sehemu hii na kuvisafirisha hadi Babeli.
\v 4 Kisha nitawarudisha katika sehemu hii Yekonia mwana wa Yehotakimu, mfalme wa Yuda, na mateka wote wa Yuda ambao walipelekwa Babeli—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli."
\s5
\v 5 Kwa hiyo Yeremia nabii akasema kwa Hanania nabii mbele ya makuhani na kwa watu wote waliosimama katika nyumba ya Yahwe.
\v 6 Yeremia nabii akasema, "Yahwe afanye hivi! Yahwe ayathibitishe maneno ambayao ulitabiri na kuvirudisha katika sehemsu hii vyombo vya nyumb a ya Yahwe, na mateka wote kutoka Babeli.
\v 7 Vile vile, sikilizeni neno ambaloo ninalitangaza katika masikio yenu na katika masikio ya watu wote.
\s5
\v 8 Manabii ambao walikuwepo mbele yangu na na mbele yenu muda mrefu uliopita pia walitabiri kuhusu mataifa mengi na juu ya falme kuu, kuhusu vita, njaa, na mapigo.
\v 9 Kwa hiyo nabii anayetabiri kwamba kutakuwa na amani—kama neno lake litatimia, basi itajulikana kwamba yeye ni nabii kweli aliyetumwa na Yahwe."
\s5
\v 10 Lakini Hanania nabii akaichukua nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia na kuivunja.
\v 11 Kisha Hanania akanena mbele ya watu wote na kusema, "Yahwe anasema hivi: Kama hivi tu, ndani ya miaka miwili nitaivunja nira iliyowekwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo ya kila taifa." Kisha Yeremia nabii akaenda njia yake.
\s5
\v 12 Baada ya Hanania nabii kuivunja nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia nabii, neno la Yahwe likamjia Yeremia. likisema,
\v 13 Nenda na ukaseme kwa Hanania na useme, Yahwe anasema hivi: Uliivunja nira ya mbao, lakini badala yake nitafanya nira ya chuma.'
\v 14 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeweka nira ya chuma shingoni mwa mataifa haya yote ili wamtumikea Nebukadreza mfalme wa Babeli, na watamtumikia. Pia nimempa wanyama wa mashambani awatawale."
\s5
\v 15 Kisha nabii Yeremia akamwambia Hanania nabii, "Sikiliza Hanania! Yahwe hajakutuma, bali wewe mwenyewe umewasababisha watu hawa kuamini katika uongo.
\v 16 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kukutuma nje ya dunia. Mwaka huu utakufa."
\v 17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, Hanania nabii akafa.
\s5
\c 29
\p
\v 1 Haya ni maneno katika waraka ambao Yeremia nabii alituma kutoka Yerusalemu kwa wazee waliosalia miongoni mwa mateka na makuhuni, manabii, na watu wote ambao Nebukadreza aliwapeleka utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli.
\v 2 Hii ilikuwa baada ya Yekonia mfalme, mama yake mfalme, na watumishi wakuu, viongozi wa Yuda na Yerusalemu, na wahunzi walikuwa wamepelekwa mbali na Yerusalemu.
\v 3 Aliutuma waraka huu kwa mkono wa Elasa mwana wa Shafani, Gemaria, mwana wa Hilkia, ambaye Sedekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amemtuma kwa Nebukadreza mfalme wa Babeli
\s5
\v 4 Waraka ulisema, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kwa mateka ambao niliwasababisha kuwa mateka kutoka Yerusalemu hadi Babeli,
\v 5 'Jengeni nyumba na muishi ndani yake. Pandeni bustani na mle matunda yake.
\s5
\v 6 Chukueni wake na mzae wana na mabinti. Kisha Kisha chukueni wake kwa ajili ya wana wenu, na wapatieni waume binti zenu. Wazae wana na mabinti na waongezeke ili msiwe wachache sana.
\v 7 Itafuteni amani ya mji ambako nimewafanya kuwa watumwa, na mkauombee kwangu kwa niaba yake kwa kuwa kutakuwa na amani kwenu kama mji uko katika amani.'
\s5
\v 8 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Msiwaache manabii ambao wako katikati yenu na wabashiri wenu kuwadanganya, na msizisikilize ndoto ambazo ninyi wenyewe mnaota.
\v 9 Kwa maana wanatabiri uongo kwenu katika jina langu. Mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe.'
\s5
\v 10 Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Babeli atakapokuwa amewatawala kwa muda wa mika sabini, nitawasaidia ninyi na kulitimiza neno langu jema kwa ajili yenu ili kuwarudisha ninyi katika sehemu hii.
\v 11 Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipangao niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahwe—mipango kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini na siku zenu za mwisho.
\s5
\v 12 Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza.
\v 13 Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.
\v 14 Kisha nitapatikana kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawarudisha watu wenu waliofungwa; nitawakusanya kutoka mataifa yote na sehehemu zote ambako nimewatawanya—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawarudisha kutoka sehemu ambako niliwasababisha kuwa mateka.
\s5
\v 15 Tangu mliposema kwamba Yahwe ameinua manabii kwa ajili yetu katika Babeli,
\v 16 Yahwe anasema hivi kwa mfalme aliyeketi katika kiti cha enzi cha Daudi na watu wote wakaao katika mji huo, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi utumwani—
\v 17 Yahwe wa majeshi anasema hivi, ''Ona, niko karibu kutuma upanga, njaa, na ugonjwa juu yao. Kwa maana nitawafanya kuwa kama tini mbovu ambazo ni mbaya sana hazifai kuliwa.
\s5
\v 18 Kisha nitawafuata kwa upanga, njaa, na tauni na kuwafanya kuwa kitu cha kushangaza kwa falme zote juu ya dunia—kitu cha kuogofya, kitu cha kulaaniwa na kuzomewa, na kitu cha aibu miongoni mwa mataifa yote ambako nilimtawanya.
\v 19 Hii ni kwa sababu hawakulisikiliza neno langu—hili ni tangazo la Yahwe—ambalo nililituma kwao kupitia watumishi wangu manabii. Niliwatuma tena na tena, lakini hamkusikiliza—hili ni tangazo la Yahwe. '
\s5
\v 20 Kwa hiyo ninyi wenyewe sikilizeni neno la Yahwe, ninyi mateka wote ambao amewatuma kutoka Yerusalemu hadi Babeli,
\v 21 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya na Sedekia mwana wa Maaseya, watabirio uongo kwenu katika jina langu: Ona, niko karibu kuwaweka katika mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli. Atawaua mbele ya macho yenu.
\s5
\v 22 Kisha laana itatamkwa na wafungwa wote wa Yuda katika Babeli kuhusu watu hawa. Laana itasema: Yahwe awafanye kuwa kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka kwenye moto.
\v 23 Hili litatokea kwa sababu ya mambo ya aibu waliyofanya katika Israeli walipofanya uzinzi na wake za majarani zao na kutangaza maneno ya uongo katika jina langu, mambo ambayo sikuwaamuru wayaseme. Kwa maana mimi ndiye nijuaye; mimi ni shahidi—hili ni tangazo la Yahwe."'
\s5
\v 24 Kuhusu Shemaya Mnehelami, sema hivi:
\v 25 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kwa sababu ulituma barua kwa jina lako kwa watu wote katika Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa Maaseya kuhani, na kwa makuhani wote, na ulisema,
\v 26 "Yahwe aliwafanya ninyi kuwa makuhani badala ya Yehoyada kuhani, ili muwe wasimamizi wa nyumba ya Yahwe. Ninyi ni viongozi wa watu wote wajitiao wazimu na kujifanya wenyewe manabii. Mtawaweka katika mkatale na minyororo.
\s5
\v 27 Kwa hiyo sasa, kwa nini hamkumkemea Yeremia wa Anathothi, ambaye hujifanya mwenyewe nabii juu yenu?
\v 28 Kwa maana ametutumia sisi katika Babeli, 'Itakuwa muda mrefu. Jengeni nyumba na muishi ndani yake, na pandeni busitani na mule matunda yake.""
\v 29 Sefania kuhani akaisoma barua hii mbele ya Yeremia nabii.
\s5
\v 30 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 31 "tuma neno kwa mateka wote na sema, 'Yahwe anasema hivi kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi wakati mimi sikumtuma, na amewaongoza kuamini uongo,
\v 32 kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kumwadhibu Shemaya Mnehelami na uzao wake. Hapatakuwa na mtu wa kukaa miongoni mwa watu hawa kwa ajili yake. Hataona mema nitakayofanya kwa ajili ya watu wangu—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana ametangaza uasi dhidi ya Yahwe.""
\s5
\c 30
\p
\v 1 Neno lilokuja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe likisema,
\v 2 "Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema, 'Jiandikie mwenyewe katika baraua maneno yote niliyotangaza kwako katika barua.
\v 3 Maana ona, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapowarudisha mateka wa watu wangu Israeli na Yuda. Mimi, Yahwe, nimesema hili. Kwa maana nitawarudisha kwenye nchi ambayo niliwapa babu zao, na wataimiliki."'
\s5
\v 4 Haya ni maneno ambayo Yahwe anatangaza kuhusu Israeli na Yuda,
\v 5 "Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Tumesikia sauti ya kutetemesha ya hofu na wala siyo ya amani.
\s5
\v 6 Ulizeni na muone kama mwanaume anamwogopa mtoto. Mbona ninamwona kila mwanaume kijana ameshika mikono yake juu ya kiuno chake kama mwanamke anayejifungua mtoto? Kwa nini nyuso zao wote zimegeuka rangi?
\v 7 Ole! Kwa maana siku hiyo itakuwa kuu, isiyofanana na yoyote. Utakuwa wakati wa huzuni kwa Yakobo, lakini ataokolewa.
\s5
\v 8 Kwa maana itakuwa katika siku hiyo—hili ni tangazo la Yahwe wa majeshi—kwamba nitaivunja nira ya shingo zenu, na nitaisambaza minyororo yenu, kwa hiyo wageni hawatawafanya watumwa tena.
\v 9 Bali watamwabudu Yahwe Mungu wao na kumtumikia Daudi mfalme wao, ambaye nitamfanya mfalme juu yao.
\s5
\v 10 Kwa hiyo wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope—hili ni tangazo la Yahwe—na usikate tamaa, Israeli. Maana ona, niko karibu kukurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya utumwa,. Yakobo atarudi na kuwa katika amani; ataokolewa, na hapatakuwa na hofu zaidi.
\v 11 Kwa maana niko pamoja nawe—hili ni tangazo la Yahwe—ili kukuokoa. Kisha nitaleta mwisho kamili kwa mataifa yote ambako nimewatawanya. Bali sitaweka mwisho kwako, ingawa ninakuadhibu kwa haki na kwa hakika sitakuacha bila kukuadhibu.'
\s5
\v 12 Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Jeraha lako si la kupona; kidonda chako kimeenea.
\v 13 Hakuna mtu wa kukutetea kesi yako; hakuna utetezi kwa ajili ya kidonda chako ili upone.
\s5
\v 14 Wapenzi wako wote wamekusahau. Hawatakuangalia, kwa maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui na nidhimu ya bwana mkatili kwa sababu ya uovu wako mwingi na dhambi zako zisizohesabika.
\v 15 Kwa nini unaita msaada kwa ajili ya jeraha lako? Maumivu yako hayaponyeki. kwa sambabu ya uovu wako mwingi, dhambi zako zisizohesabika, nimefanya mambo haya kwako.
\s5
\v 16 Kila mtu akulaye ataliwa, na adui zako wote wataenda utumwani. Kwa maana kila aliyekuteka nyara atatekwa, na nitawafanya wote wanaokuwinda kuwa mawindo.
\v 17 Kwa maana nitaleta uponyaji juu yako; nitakuponya majeraha yako—hili ni tangazo la Yahwe—nitafanya hivyo kwa sababu walikuita: Mwenyekutupwa. Hakuna anayeujali Sayuni."
\s5
\v 18 Yahwe anasema hivi, "Ona, niko karibu kuwarudisha mateka wa hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu, na jumba litakuwepo tena kama ilivyokuwa kawaida.
\v 19 Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya ya shangwe itasikika kutoka kwao, kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza; nitawaheshimu ili kwamba wasifanywe wanyonge.
\s5
\v 20 Kisha watu watakuwa kama ilivyokuwa mwanzo, na kusanyiko lao litaanzishwa mbele yangu wakati nitakapowaadhibu wote wanaowatesa kwa sasa.
\v 21 Kiongozi wao atatoka miongoni mwao. Atatokeza kutoka kati yao nitakapomleta karibu na atakapanikaribia mimi. kama sitafanya hivyo, ni nani atakayethubutu kunisogelea? —hili ni tangazo la Yahwe.
\v 22 Kisha mtakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu.
\s5
\v 23 Ona, tufani ya Yahwe, ghadhabu yake, imekwenda nje. Ni tufani isiyokoma. Itazunguka juu ya vichwa vya watu waovu.
\v 24 Hasira ya Yahwe haitarudi mpaka itoke na kutimiza makusudi ya moyo wake. Katika siku za mwisho mtalielewa hili."
\s5
\c 31
\p
\v 1 "Katika wakati huo—hili ni tangazo la Yahwe—Nitakuwa Mungu wa familia zote za Israel, na watakuwa watu wangu."
\v 2 Yahwe anasema hivi, "Watu ambao wamenusurika na upanga wamepata kibali katika nyika; nitatoka nje kuwapa pumziko Israeli."
\v 3 Yahwe alionitokea zamani na kusema, "Nimekupenda wewe, Israeli, kwa upendo wa milele. Kwa hiyo nimekuvuta kwang kwa agano la uaminifu.
\s5
\v 4 Nitakujenga tena kwa hiyo utakuwa umejengwa, bikra wa Israeli..... na kwenda nje michezo ya furaha.
\v 5 Utapanda mizabibu tena juu ya milima Samaria; wakulima watatapanda na kuweka matunda kwa ajili ya matumizi mazuri.
\v 6 Kwa maana siku itakuja wakati walizi watakapotangaza katika milima ya Efraimu, 'Inuka, twndeni juu kwenye mlimaa wa Yahwe Mungu wetu.'
\s5
\v 7 Kwa maana Yahwe anasema hivi, Piga kelele za shangwe juu ya Yakobo! Pigeni za furaha kwa ajili ya watu wakuu wa mataifa! Sifa zisikike. Sema, ''Yahwe amewaokoa watu wake, masalia wa Israeli.'
\s5
\v 8 Ona, niko karibu kuwaletaa kutoka nchi za kusini. Nitawakusanya kutoka sehemu zaa mbali za dunia. Vipofu na wenye ulemavu watakuwa kati kati yao; wanawake wajawazito na wale waliokaribu kujifungua wataakuwa pamoja nao. Kusanyiko kubwa litarudi hapa.
\v 9 Watakuja kwa kuomboleza; nitawaongoza huku wakifanya maoambi yao. Nitawafanya wasafiri kataika mikondo ya maji katika bara bara ilinyoka. Hawatajikwaa juu yake, kwa maana nitakuwa baba kwa Israeli, na Afraimu atakuwa mzaliwa wanagau wwa kwanza
\s5
\v 10 Sikia neno la Yahwe, mataifa. Litangazeni pembezoni mwa visiwa mbali. Enyi mataifa lazima museme, 'Yule aliyemtawanya Israeli anamkusanya tena na kuwalinda kama mchungaji alindavyo kondoo.'
\v 11 Kwa maana Yahwe amemfidia Yakobo na kumkomboa kutoka mkono ambao ulikuwa na nguvu sana kwake.
\s5
\v 12 Kisha watakuja na kufurahia katika vilele vya Sayuni. Nyuso zao zitamelemeta kwa sababu ya wema wa Yahwe, juu ya nafaka na divai mpya, juu ya mafuta na malimbuko ya kwanza ya makundi na ng'ombe. Kwa maana maisha yao yatakuwa kama busitani iliyomwagiliwa, na hatatajisikia huzuni tena.
\s5
\v 13 Kisha wanawali watafurahia kwa kucheza, na vijana na wanaume wazee watakuwa pamaoja. Kwa maana nitayageuza maombolezo yao kuwa sherehe. Nitakuwa na huruma juu yao na kuwafanya kufurahi badala ya kuhuzunika.
\v 14 Kisha nitayaloanaisha sana maisha ya makuhani. Watu wangu watajijaza wenyewe kwa wema—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 15 Yahwe anasema hivi: "Sauti imesikika katika Rama, kilio na maombolezo mengi. Ni Raheli akiomboleza kwa ajili watoto wake. Hataki kufarijiwa tena juu yao, kwa maana hawako hai tena."
\s5
\v 16 Yahwe anasema hivi, Zuia sauti yako usilie na macho yako yasitoe machizi; kwa maana kuna fidia kwa ajili ya mateso yako—hili ni tangazo la Yahwe—watoto wako watarudi kutoka nchi ya adui.
\v 17 Kuna matumaini kwa ajili ya siku zenu za baadaye—hili ni tangazo la Yahwe—uzao wako watarudi ndani ya mipaka yao."
\s5
\v 18 Kwa hakika nimemsikia Efraimu akilia, 'Uliniadhibu, nami nieadhibika kama ndama assiye na mafunzo. Nirudisha na nitarudishwa, kwa maana wewe ni Yahwe Mungu wangu.
\v 19 Kwa maana baada ya kurudi kwako, nilikuwa na huzuni; baada ya kufundiswa, nilijipiga kofi sshavu langu. Niliaibika ana dharirika, kwa maana nilizaliwa na hataia ya ujana wangu.'
\v 20 Efraimu siyo mtoto wangu wa thamani? Yeye si mpendwa wangu, mwanangu anipendezaye? Kwa maana kila ninaponena juu yake, bado nina mwita kipenzi cha akili yangu. Kwa namna hii moyo wangu unamtamani. Kwa hakika nitaakuwa na huruma ajuu yake—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 21 Jiwekee alama za bara bara kwa ajili yako mwenyewe. Weka matangaazo ya maelekezo kwa ajili yako mwenyewe. Iweke akili yako juu ya njia sahihi, njia unayopaswa kufuata. Rudii, bikra Israeli! Rudi kwenye hii miji yako.
\v 22 Utatanga tanga hadi lini, binti usiye mwaminifu? Kwa maana Yahwe ameumba kitu fulani kipya juu ya dunia—mwanamke anamzunguka mwanaume.
\s5
\v 23 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, '"Nitakapowarudisha watu katika nchi yao, watasema hivi katika anchi ya Yuda na miji yake, "Yahwe akubariki, wewe sehemu takatifu ambapo anaishi, ewe mlima mtakatifu.'
\v 24 Kwa maana Yuda na miji yake yote wataishi pamoja humo, kama vile watakavyoishi wakulima na wachungaji pamaoja na makundi yao.
\v 25 Kwa maana nitawapa majai ya kunywa waliochoaka, na nitamjaza kila anayeteseka na kiu."
\v 26 Baada ya haya niliamka, na nikagundua kwamba usingizi wangu ulikuwa unaburudisha.
\s5
\v 27 Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yaahwe—nitakapoipanda nyumba ua Israeli na Yuda pamoja na wazawa wa wanadamaau na wanyama.
\v 28 Zamani, niliwaweka katika uangalizi ili kuwang'oa na kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu, na kuwaletea madhara. Lakini katika siku zijazo, nitawaangalia, ili niwajenge na kuwapanda—hili ji tangazo la Yahwe.
\s5
\v 29 Katika siku hizo hakuna atakayesema tena, "Baba za watu wamekula zabibu kali, bali meno ya watoto ni butu.'
\v 30 Kwa maana kila mtu atakuwa katika uovu wake mwenyewe; kila alaye zabibu kalai, meno yake yataakuwa butu.
\s5
\v 31 Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—nitakapoanzisha aganao jipya pamaoja na nyumba aya Israeli na nyumba ya Yuda.
\v 32 Halitakuwa kama agano ambalo nilianzisha na baba zao nilipowatoa kwa mkono wao nje ya nchi ya Missiri. Hizo zzilikuwa siku ambapo walilivunja aaganao lanaahu, ingawa nilikuwa mme kwao—hili ni tangazo la Yahwe.
\s5
\v 33 Lakaini hili ni agano nitakaloanzisha na nyumba ya Israeli baada ya siku hizi—hili ni tangazo la Yahwe: Nitaiweka sheria yangu ndani yao na nitaiandika juu ya mioyo yao, kwa maana nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watau wangu.
\v 34 Kisha kila mtu hatamfundisha jiranai yake, wala mtu hatamfundisha ngugu yake akisema, 'Mjue Yahwe!' Kwa maana wao wote, kuanzia mdogo wao hata mkubwa, watanijua—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawasamehe uovu wao na sitazikumbuka tena dhambi zao."'
\s5
\v 35 Yahwe anasema hivi—Yahwe, yeye afanyaye jua kuangaza mchana na kuzipanga mwezi na nyota kuangaza usiku. Yeye ndiye aiwekaye bahari katika mwendo ili mawimbi yake yaungurume. Yahwe wa majeshi katika ajina lake.
\v 36 Anasema hivi, ikiwa tu mambo haya ya akudumu yakitoweka machoni panaagu—hili ni agizo la Yahwe—uzao wa Israeli hawatasimama mbaalai nami wasiwe taiafa."
\s5
\v 37 Yahwe anasema hivi, "Kama tu urefu wa mbingu unaweza kupimwa, na kama tu misingi ya dunia chini inaweza kugunduliwa, nitawakataa uzao wote wa Israeli kwa sababu ya yote waliyofanya—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 38 "Angalia, siku zinakuja—hili ni tanagazo la Yahwe—ambapo mji utajengwa tena kwa ajili yanagu, kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye Lango la Pembeni.
\v 39 Kisha mistari ya kupimia itaenda nje hadi mbali, hadi kwenye kilima cha Garebu na kuzunguka Goa.
\v 40 Bonde lote la miili iliyokufa na majivu, na shamaba lenye matuta linalofika hadi Bonde la Kidroni mbali hadi kwenye kona ya Lango la Farasi upande wa mashariki, litateuliwa kwa ajili ya Yahwe. Mji hautang'olewa wala kupinduliwa tena, milele."
\s5
\c 32
\p
\v 1 Neno likaja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe katika mwaka wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza.
\v 2 Katika wakati huo, jeshsi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka Yerusalemu, na Nehemia nabii alikuwwa amefungwa katika uwanja wa walinzi katika nyumba ya mfalme wa Yuda.
\s5
\v 3 Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga na kusema, "Kwa nini unatabiri na kusema, 'Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kuweka mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, na atauteka.
\v 4 Sedekia mfalme wa Yuda hatapona kutoka kwenye mikono ya Wakaldayo, kwa maana hakika atatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli. Mdomo wake utazumzia kwenye mdomo wa mfalme, na macho yake yatayaona macho ya mfalme.
\v 5 Atampeleka Sedekia Babeli, na atabaki huko hadi nimuadhibu—hili ni tangazo la Yahwe. Ingawa unapigana dhidi ya Wakaldayo, hautafanikiwa."
\s5
\v 6 Yeremia akasema, "Neno la Yahwe likaja kwangu, likisema, Angalia, Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako anakuja kwako na atasema,
\v 7 "Linunue shamba langu ambalo liko katika Anathothi kwa ajili yako, kwa maana haki ya kununua ni yako.""
\s5
\v 8 Kisha, kama Yahwe alivyotangaza, Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akaja kwangu katika uwanja wa walinzi, na akasema kwangu, 'Linunue shamba langu kwa ajili yako ambalo liko Anathothi katika nchi ya Benyamini, kwa maana haki ya urithi ni ya kwako, na haki ya kulinunua ni yako. Linunue kwa ajili yako.' Kisha nilijua kuwa hili lilikuwa neno la Yahwe.
\v 9 Kwa hiyo nililinua shamba katika Anathothi kutoka kwa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na nilipima fedha kwa ajili yake, shekeli kumi na saba katika uzito.
\s5
\v 10 Kisha niliandika katika barua na kuitia muhuri, na kulikuwa na mashadi wakaishuhudia. Kisha nikampa fedha katika mizani.
\v 11 Kisha nikaichukua hati ya manunuzi ambayo ilikuwa imepigwa muhuri, kwa kuifuata amri na taratibu, na kama ilivyo ada.
\v 12 Ile barua nikampa Baruku mwana wa Neria wa Maaseya mbele ya Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mashahidi waliotia sahihi kwenye barua iliyopigwa muhuri, na mbele ya Wayahudi wote waliokaa katika uwanja wa walinzi.
\s5
\v 13 Kwa hiyo nikampa amri Baruku mbele yao. Nilisema,
\v 14 Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Chukua nyaraka hizi, vyote hati hii ya manunuzi iliyopigwa muhuri na nakala zisizopigwa muhuri za manunuzi, na uziweke katika chungu cha udongo ili vidumu kwa muda mrefu.
\v 15 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nyumba, mashamba, na mashamba ya mizabibu vitanunuliwa tena katika nchi hii.
\s5
\v 16 Baada ya kumpa Baruki mwana wa Neria ile hati ya manunuzi, nikaomba kwa Yahwe nikasema,
\v 17 Ole, Bwana Yahwe! Angalia! Wewe peke yako umezitengeneza mbingu na dunia kwa nguvu zako kuu na kwa mkono wako ulioinuka. Hakuna kitu ambacho ukisema kwako ni kigumu sana kukifanya.
\v 18 Wewe huonesha agano la uaminifu kwa maelfu na kumimina makosa ya wanadamu katika mapaja ya watoto wao baada yao. Wewe ni Mungu mkuu na mwenye nguvu.
\s5
\v 19 Wewe ni mkuu katika hekima na una nguvu katika matendo, kwa maana macho yako yanaona njia zote za watu, ili kumlipa kila mtu stahiki ya matendo yake.
\v 20 Ulifanya ishara na maajabu katika nchi ya Misiri. Hata leo hapa Israeli na kati ya wanadamu wengine wote, umelifanya jina lako kuwa maarufu.
\v 21 Kwa maana uliwanunua watu wako Israeli kwa ishira na maajabu, kwa mkono hodari, kwa mkono ulioinuka, na kwa hofu kuu.
\s5
\v 22 Kisha uliwapa nchi hii—ambayo uliapa kwa babu zao kwamba utawapa—nchi itiririkayo maziwa na asali.
\v 23 Hivyo walingia na kuimiliki. Lakini hawakuitii sauti yako wala kuishi kwa kuitii sheria yako. Hawakufanya chochote ulichowaamuru kufanya, kwa hiyo umeleta juu yao majanga haya yote.
\s5
\v 24 Angalia! Urefu wa maboma haya umefika hadi kwenye mji ili kuuteka. Kwa sababu ya upanga, njaa, na tauni, mji umetiwa kwenye mikono ya Wakaldayo wanaopigana dhidi yake. Kwa maana ulichosema kitatokea sasa kinatokea, na ona, unatazama.
\v 25 Kisha wewe mwenyewe uliniambia, "Nunua shamba kwa fedha kwa ajili yako na mashahidi wameshuhudia, ingawa mji huu unatiwa mikononi mwa Wakaldayo.""
\s5
\v 26 Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 27 "Angalia! Mimi ni Yahwe, Mungu wa wanadamu wote. Kuna kitu cho chote kigumu sana kwangu kukifanya?
\v 28 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi, 'Ona, niko karibu kuutia mji huu kwenye mikono ya Wakaldayo na Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Atauteka.
\s5
\v 29 Wakaldayo wanaopigana dhidi ya mji huu watakuja na kuwasha moto kwenye mji huu na kuunguza, pamoja na nyumba juu ya paa la watu waliomwabudu Baali na kumimina dhabihu kwa miungu wengine ili kunikasirisha.
\v 30 Kwa maana watu wa Israeli na Yuda hakika wamekuwa watu wanaofanya maovu mbele ya macho yangu tangu ujana wao. Watu wa Israeli hakika wameniudhi kwa matendo ya mikono yao—hili ni tangazo la Yahwe.
\s5
\v 31 Yahwe anatangaza kwamba mji huu umekuwa sababu ya hasira yangu na ghadhabu yangu tangu siku walipoujenga. Umekuwa hivyo hata leo. Kwa hiyo nitaundoa mbele ya uso wangu
\v 32 kwa sababu ya uovu wote wa watu wa Israeli na Yuda, mambo waliyofanya ili kunichukiza—wao, wafalme wao, wana wa wafalme, makuhani, manabii, na kila mtu katika Yuda na wakaaji wa Yerusalemu.
\s5
\v 33 Wamenigeuzia migongo yao badala ya nyuso zao, ingawa niliwafundisha kwa furaha. Nilijitahidi kuwafundisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyenisikiliza ili kupokea marekebisho.
\v 34 Walisimamisha sanamu zao za ajabu katika nyumba inayoitwa kwa jina langu, ili kunitia unajisi.
\v 35 Wakazijenga sehemu za juu katika Bonde la Beni Hinomu ili kuwatia katika moto wana wao na binti zao kwa ajili ya Moleki. Mimi sikuwaagiza. Sikuweka akilini mwangu kamwe kwamba watafanya mambo maovu na kwa hiyo kuwasabisha Yuda watende dhambi.
\s5
\v 36 Kwa hiyo sasa, Mimi, Yahwe, Mungu wa Israeli, kuhusu mji huu ninasema hivi, 'mji ambao mnasema, 'Umetiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli kwa upanga, njaa, na pigo.'
\v 37 Ona, niko karibu kuwakusanya kutoka kila nchi nilikowapeleka katika hasira yangu, ghadhabu, hasira kuu. Niko karibu kuwarudisha kwenye sehemu hii na kuwawezesha kuishi katika usalama.
\s5
\v 38 Kisha watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
\v 39 Nitawapa moyo mmjoa na na njia moja ya kuniheshimu kila siku ili kwamba yawepo mema kwa ajili yao na uzao wao baada yao.
\v 40 Kisha nitafanya pamoja nao agano la milele, ili nisiache kufanya mema kwa ajili yao. nitajiwekea heshima katika mioyo yao, ili kwamba wasiniache.
\s5
\v 41 Kisha nitajifurahisha katika kufanya mema kwao. Kwa uaminifu nitawapanda katika anchi hii kwa moyo wangu wote na maisha yangu yoye.
\v 42 Kwa amaana Yahwe anasema hivi, 'Kama tu nilivyoyaleta majanga haya makubwa yote juu ya watu hawa, hivyo hivyo nitaleta juu yao mambo mema niliyosema kwamba nitafanya kwa ajili yao.
\s5
\v 43 Basi mashamba yatanunuliwa katika nchi hii, ambayo mnaisema, "Hii ni nchi iliyoharibiwa, isiyo na mwanadamu wala mnyama. Imetiwa mikononi mwa Wakaldayo"
\v 44 Watanunua mashamba kwa fedha na kuandika katika barua zilizopigwa muhuri. Watawakusanya mashahidi katika nchi ya Benyamini, wote kuzunguka Yerusalemu na miji ya Yuda katika miji ya nchi yenye vilima, na katika nchi tambarare, na katika miji ya Negebu. Kwa maana nitawarejesha wafungwa wao—hili ni tangazo la Yahwe."'
\s5
\c 33
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia mara ya pili, alipokuwa bado amefungwa ndani ya uwanja wa walinzi, likisema,
\v 2 Yahwe muumbaji, anasema hivi—Yahwe, aumbaye ili athibitishishe—Yahwe ndilo jina lake,
\v 3 'Niite, na nitakuitika, nitakuelezea mambo makuu, siri ambazo huzielewi.'
\s5
\v 4 Kwa maana Yahwe, Mungu wa Israel, anasema hivi kuhusu nyumba zilizo katika mji huu na nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa kwa sababu ya maboma na upanga,
\v 5 Wakaldayao wanakuja kupigana na kuzijaza nyumba kwa hizi kwa majeshi ya watu ambao wataua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, nitakapouficha mji huu uso wangu kwa sababu ya uovu wao wote.
\s5
\v 6 Lakini ona, niko karibu kuleta uponyaji na tiba, kwa maana nitawaponya na nitawapa wingi wa, amani na uamainifu.
\v 7 Kwa maana nitawarudhisha wafungwa wao wa Yuda na Israeli; nitawajenga tena kama ilivyokuw mwanzo.
\v 8 Kisha nitawatakasa uovu wote walioufanya dhidi yangu. Nitasamehe makosa yote waliyonitenda, na na njia zote walizo asi dhidi yangu.
\v 9 Kwa maana mji huu kwa ajili yangu utakuwa chombo cha furaha, nyimbo, sifa na heshima kwa mataiafa yote ya dunia ambao watasikia mambo yote mema ninayokwenda kufanya kwa ajili ya huu mji. Kisha wataogopa na kutetemeka kwa sababu ya mambo yote mema na amani nitayoupa mji huu.'
\s5
\v 10 Yahwe anasema hivi, 'Katika sehemu hii ambayo sasa mnaisema, "Imetengwa, sehemu isiyo na mwanadamu wala mnyama," katika mji huu wa Yuda, na katika mitaa ya Yerusalemu ambayo imetengwa bila mwanadamu wala mnyama, zitasikika tena
\v 11 sauti za furaha na sauti za shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti za wale wasemao, wanapoleta shukrani katika nyumba ya Yahwe, "Mshukuruni Yahwe wa majeshi, kwa maana Yahwe ni mwema, na upendo wake usioshindwa wadumu milele!" Kwa maana nitawafanaya tena wafungwa wa nchi kuwa walivyokuwa mwanzo,' asema Yahwe.
\s5
\v 12 Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika sehemu hii ya ukiwa, ambamo sasa hakuna mwanadamu wala mnyama—katika miji yake yote kutakuwepo tena malisho ambapo wachungaji wataweza kupumzisha makundi yao.
\v 13 Katika miji hii katika nchi ya vilima, nchi tambarare, na Negevu katika nchi ya Benyamini na kuzunguka Yerusalemu yote, na katika miji ya Yuda, makundi yatapata njia chini ya mkono wa yule anayewahesabu,' asema Yahwe.
\s5
\v 14 Angalia! Siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—ambapo nitafanya niliyoahidi kwa nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
\v 15 Katika siku hizo na katika wakati huo nitachipua shina la haki kwa ajili ya Daudi, na litafanaya hukumu na haki katika nchi.
\v 16 Katika siku hizo Yuda wataokolewa, na Yurusalemu utaishi katika usalama, kwa maana hivi ndivyo atakavyoitwa, "Yahwe ni haki ni haki yetu."
\s5
\v 17 Kwa maana Yahwe anasema hivi: 'Mwana kutoka ukoo wa Daudi hatakosa kuketi katika kiti cha nyumba ya Israeli,
\v 18 wala mtu kutoka ukuhani wa Kilawi hatakosa kutoa sadaka za kuteketezwa mbele zangu, kutoa sadaka za chakula, na kutoa sadaka za nafaka wakati wote."'
\s5
\v 19 Neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 20 "Yahwe anasema hivi: 'Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana na usiku ili kwamba siku isikawie wala usiku usikawie kuja kwa wakati wake,
\v 21 basi mtaweza u kulivunja agano langu na Daudi mtumishi wangu, ili kwamba aspate mwana wa kuketi juu ya kiti chake cha enzi, na gano langu na makuhuni wa Kilawi, watumishsi wangu.
\v 22 Kama vile majeshsi ya mbinguni yasivyoweza kuhesabika, na kama vile mchanga wa ufukwe wa bahari usivyoweza kupimwa, ndivyo nitakavyouongeza uzao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi watumikao mbele zangu."
\s5
\v 23 Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 24 Hamkuzingatia walichotangaza watu hawa waliposema, 'Zile Familia mbili ambazo Yahwe alizichagua, sasa amezikataa'? Kwa jinsi hii hii waliwapuuza watu wangu, wakisema kwamba si taifa tena katika macho yao.
\s5
\v 25 Mimi, Yahwe, nasema hivi, 'Kama sijalithibitisha agano la mchana na usiku, na kama sijaziweka sheria za mbingu na dunia,
\v 26 basi nitawakataa uzao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na nisilete mtu kutoka kati yao wa kutawala juu ya uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha wafubgwa wao na kuonesha huruma kwao."'
\s5
\c 34
\p
\v 1 Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yahwe, wakati Nebukadreza mfalme wa Babeli, majeshi yake yote, pamoja na falme zote za dunia, maeneo yote yaliyo chini ya mamlaka yake, na watu wake wote walikuwa wanapigana vita dhidi ya Yerusalemu na miji yake yote, kusema:
\v 2 'Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nenda na uzungumze kwa Sedekia mfalme wa Yuda na useme kwake, 'Yahwe asema hivi: Angalia, niko karibu kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atauchoma moto.
\v 3 Hautapona kutoka mkono wake, kwa maana kwa hakika utakamatwa na kutiwa mkononi mwake. Macho yako yatayaangalia macho ya mfalme wa Babeli; atazungumza kwako moja kwa moja ukiwa unaenda Babeli.'
\s5
\v 4 Sedekia mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Yahwe! Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, 'Hautakufa kwa upanga.
\v 5 Utakufa katika amani. Kama kwenye mafukizo ya babu zako, wafalme waliokuwepo kabla yako, watauchoma mwili wako. Watasema, 'Ole, bwana!" Watakuomboleza. Sasa nimesema—hili ni tangazo la Yahwe."
\s5
\v 6 Kwa hiyo Yeremia nabii akatangaza kwa Sedekia mfalme wa Yuda maneno haya yote katika Yerusalemu.
\v 7 Jeshi la mfalme wa Babeli likafanya dhidi ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda iliyobaki: Lakishi, na Azeka. Miji hii ya yuda ilisalia kama miji yenye maboma.
\s5
\v 8 Neno lilomjia Yeremia kutoka kwa Yahwe baada ya mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote katika Yurusalemu, ili kuwatanagazia uhuru
\v 9 ya kwamba kila mtu lazima amwachie huru mtumwa wake wa Kiebrania, wote wa kiume na wa kike, kwa hiyo mtu alipaswa kutomtumikisha Myahudi, ambaye alikuwa ndugu yake.
\s5
\v 10 Kwa hiyo watu wote na viongozi wakaingia katika agano kwamba kila mtu amwachie huru mtumwa wake wa kiume na waikke ili asiwe mtumwa tena. Walitii na kuwaweka huru.
\v 11 Lakini baada ya hapo walibadili akili zao. Wakawarudisha watumwa ambao walikuwa wamewaachia huru. Wakawalazimisha kuwa wataumwa tena.
\s5
\v 12 Kwa hiyo neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 13 "Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Mimi mwenyewe nilifanya agano na babu zenu katika siku ambayo niliwatoa nje ya nchi ya Misiri, nje ya nyumba ya utumwa. Hapo ndipo niliposema,
\v 14 Katika mwisho wa mwaka wa saba, kila mtu lazima amwachie ndugu yake, Mwebrania mwenzake aliyejiuza mwenyewe kwako ili kukutumikia kwa miaka sita. Mwagize aende kwa uhuru." Lakini babu zenu hawakunisikiliza wala kutega masikio yao kwangu.
\s5
\v 15 Sasa ninyi wenyewe mlitubu na kuanza yaliyomema katika macho yangu. Mlitangaza uhuru, kila mtu kwa jirani yake, na mlifanya agano mbele zangu kwenye nyumba iitwayo kwa jina langu.
\v 16 Lakini tena mmegeuka na kulichafua jina langu; mmemsababisha kila mtu kumleta tena mtumwa wake wa kiume na wa kike, wale mliowachie kwenda walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa tena.'
\s5
\v 17 Kwa hiyo Yahwe asema hivi, 'Ninyi wenyewe hamkunisikiliza. Mlipaswa kuwa mmetangaza uhuru, kila mmoja wenu, kwa ndugu zenu na Waisraeli wenzenu. Kwa hiyo angalia! Niko karibu kutangaza uhuru kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—uhuru wa upanga, tauni, na njaa, kwa maana naenda kuwafanya kitu cha ajabu katika macho aya kila ufalme juu ya dunia.
\v 18 Kisha nitashughulika na watu waliolivuja agano langu, ambao hawakuyashika maneno ya agano ambalo walilithibitisha mbele zangu walipomkata ng'ombe dume katika vipande viwili na kutembea katika vipande vyake,
\v 19 na kisha viongozi wa Yuda na Yerusalemu, matowashi na makuhani, na watu wote wa nchi wakatembea katika vipande vya yule ng'ombe dume.
\s5
\v 20 Nitawatia katika mikono ya adui zao na katika mikono ya hao wanaoutafuta uhai wao. Miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama juu ya dunia.
\v 21 Kwa hiyo nitawatia Sedekia mfalme wa Yuda na viongozi wake kwenye mikono ya adui zao na kwenye miko ya wale wanaoutafuta uhai wao na katika mikono ya majeshi ya mfalme wa Babeli ambayo yameinuka dhidi yenu.
\v 22 Angalia, niko karibu kutoa amari—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawaleta tena kwenye mji huu ili wapigane dhidi yake, na kuunguza kwa moto. Kwa maana nitaigeuza miji ya Yuda kuwa sehemu za ukiwa ambamo hapatakuwa na wakaaji."
\s5
\c 35
\p
\v 1 Neno kutoka kwa Yahwe likamjia Yeremia katika siku za Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, kusema,
\v 2 "Nenda kwenye familia ya Warekabi na zungumza nao. Kisha uwalete kwenye nyumba yangu, mle ndani ya moyawapo ya vyumba, na uwape divai wanywe."
\s5
\v 3 Hivyo nilimchukua Yaazania mwana wa Yeremia mwana wa Habasinia na ndugu zake, wanawe wote, na familia yote ya Warekabi.
\v 4 Nikawapeleka wote kwenye nyumba ya Yahwe, katika vyumba vya wana wa Hanani mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu. Vyumba hivi vilikuwa karibu na chumba cha viongozi, ambacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya mwana wa Shalumu, mtunza lango.
\s5
\v 5 Kisha nikaleta mabakuli na vikombe vilivyojaa divai mbele ya Warekabi na kusema kwao, 'Kunyeni divai."
\v 6 Lakini walisema, "hatutakunywa divai yoyote, kwa maana babu yetu, Yonadabu mwana wa Rekabu, alituamuru, Msinywe divai yoyote, ninyi wala uzao wenu, milele.
\v 7 Pia, msijenge nyumba yoyote, kupanda mbegu zozote, wala kupanda shamba lolote la mizabibu; hivi siyo kwa ajili yenu. Kwa maana lazima muishi katika hema maisha yenu yote, ili kwamba muweze kuishsi siku nyingi katika nchi mnayoishi kama wageni.'
\s5
\v 8 Tumeitii sauti ya Yonadabu mwana wa Rekabu, babu yetu, katika yote aliyotuamuru, kutokunywa divai maisha yetu yote, sisi, wake zetu, wana wetu, na binti zetu.
\v 9 Hatutajenga nyumba kwa ajili ya kuishi ndani, na hatutakuwa na shamba la mizabu, konde, wala mbegu ya kumiliki sisi.
\v 10 Tumeishi katika hema na tumetii na kufanya yote aliyotuamuru Yonadabu babu yetu.
\v 11 Lakini Nebukadreza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi, tulisema, 'Njoo, lazima twende Yerusalemu ili tupone na mkono wa Wakaldayo na majeshi ya Waaramu. 'Kwa hiyo tunaishi Yerusalemu."
\s5
\v 12 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
\v 13 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Nenda na useme kwa wanaume wa Yuda na wakaaji wa Yeruslemu, 'Hamtapokea maelekezo na kulisikiliza neno langu? —hili ni tangazo la Yahwe.
\v 14 Maneno ya Yonadabu mwana wa Rekabu aliyowapa wanawe kama amri. wasinywe divai yoyote, yameheshimiwa hadi leo. Wameitii amri ya babu yao. Lakini mimi, nimekuwa nikifanya matangazo kwenu bila kukoma, lakini hamnisikilizi.
\s5
\v 15 Niliwatuma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nilikuwa nawatuma bila kukom ili waseme, 'Kila mtu auache uovu wake na kutenda matendo mema; asiwepo mtu wa kuifuata miungu mingine tena na kuiabudu. Bdala yake, rudini kwenye nchi niliyowapa ninyi na babu zenu,' bado hamtanisikiliza wala kutega maskio yenu kwangu.
\v 16 Kwa maana uzao wa Yonadabu mwana wa Rekabu wamezishika amri za babu yao alizowapa, lakini watu hawa hupuuza kunisikiliza."
\s5
\v 17 Kwa hiyo Yahwe, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Angalia, Ninaleta juu ya Yuda na juu ya kila mtu anayeishi Yerusalemu, majanga yote niyotamka dhidi yao kwa sababu niliwaambia, lakini hawakusikiliza; niliwaita, lakini hawakuitika."
\s5
\v 18 Yeremia akasema kwa familia ya Warekabi, "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: mmezisikiliza amri za Yonadabu babu yenu na kuzishika zote—mmeyatii yote aliyowaamuru kufanya—
\v 19 kwa hiyo Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Siku zote kutakuwa na mtu kutoka uzao wa Yonadabu mwana wa Rekabu kwa ajili ya kunitumikia."'
\s5
\c 36
\p
\v 1 Ilikuja tokea katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosiah mfalme wa Yuda, kwamba neno hili lilikuja kwa Yeremiah kutoka kwa Yahwe, na alisema,
\v 2 "Chukua kitabu kwa ajili yako na uandike juu yake maneno yote ambayo nimekwisha kukuambia kuhusiana na Israel na Yuda, na kila taifa. Fanya hivi kwa kila kitu nilichokuambia tokea siku za Yosia mpaka siku ile.
\v 3 Huenda watu wa Yuda watasikiliza majanga yote ambayo ninakusudia kuleta juu yao. Huenda kila mmoja ataacha njia zake mbaya, ili kwamba niweze kuwasamehe maovu yao na dhambi zao."
\s5
\v 4 Kisha Yeremia alimwita Baruku mwana wa Neria, na Baruku aliandika kwenye kitabu, kwa imla ya Yeremia, maneno yote ya Yahwe yalizunguzwa kwake.
\v 5 Kisha Yeremia alitoa amri kwa Baruku. Alisema, "Niko gerezani na siwezi kwenda kwenye nyumba ya Yahwe.
\v 6 Kwa hiyo unapaswa uende na kusoma kutoka kwenye kitabu ulichoandika kwa imla yangu. Kwa siku ya kufunga, unapaswa usome maneno ya Yahwe kwenye masikio ya watu katika nyumba yake, na pia kwenye masikio ya Yuda yote waliokuja kutoka katika miji yao. Tangaza maneno haya kwao.
\s5
\v 7 Huenda maombi yao ya rehema yatakuja mbele ya Yahwe. Huenda kila mtu ataacha njia mbaya, kwani gathabu na hasira ya Yahwe imetangazwa dhidi ya watu kwa ukali."
\v 8 Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alifanya kila kitu ambacho Yeremia nabii alimwamuru yeye kufanya. Alisoma kwa sauti maneno ya Yahwe ndani mwa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 9 Ilikuja tokea katika mwaka wa tano na mwezi wa tisa kwa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kwamba watu wote Yerusalemu na watu waliotoka Yerusalemu toka miji ya Yuda walitangaza kufunga kwa kumheshimu Yahwe.
\v 10 Baruku alisoma kwa sauti maneno ya Yeremia katika nyumba ya Yahwe, kutoka kwenye chumba cha Gamaria mwana wa Shafani mwandishi, katika ua wa juu, kwa mlango wa kuingilia wa nyumba ya Yahwe. Alifanya hivi kwa masikio ya watu wote.
\s5
\v 11 Basi Mikaya mwana wa Gemaria alisikia maneno yote ya Yahwe kwenye kitabu.
\v 12 Alienda chini kwenye nyumba ya mfalme, kwenye chumba cha katibu. Tazama, maafisa wote walikuwa wamekaa hapo: Elishama mwandishi, Delaiah mwana wa Shemaiah, Elnathan mwana wa Achbor, Gemaria mwana wa Shefani, na Sedekia mwana wa Hananiah, na maafisa wote.
\s5
\v 13 Kisha Mikaya alitoa taarifa ya maneno yote kwao ambayo alikuwa amesikia ambayo Baruku alisoma kwa sauti kwenye masikio ya watu.
\v 14 Kwa hiyo maafisa wote walimtuma Jehudi mwana wa Nethania mwana wa Shelemiah mwana wa Kushi, kwa Baruku. Jehudi alisema kwa Baruku, "Chukua kitabu katika mkono wako, kitabu ambacho ulikuwa unakisoma kwa masikio ya watu and kuja." Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alichukua kitabu katika mkono wake na alienda kwa maafisa.
\v 15 Kisha walisema naye,"Kaa chini na usome haya katika masikio yetu." Kwa hiyo Baruku akasoma kitabu.
\s5
\v 16 Ilitokea wakati waliposikia haya maneno yote, kila mtu alipatwa na hofu kwa mtu aliye karibu naye na kusema kwa Baruku, "Kwa hakika tunapaswa kutoa taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme."
\v 17 Kisha walimuuliza Baruku, "Tuambie, ulipataje kuandika maneno yote haya kwa imla ya Yeremia?"
\v 18 Baruku aliwaambia, "Alitoa imla ya maneno haya yote kwangu, na nikayaandika kwa wino kwenye kitabu hiki."
\v 19 Kisha maafisa walisema kwa Baruku, "Nenda, jifiche mwenyewe, na Yeremiah, pia. Usipatikane mtu yeyote kujua uko wapi."
\s5
\v 20 Kisha walienda kwa uwanja wa mfalme na wakatoa taarifa ya maneno haya kwake. Lakini kwanza walikihifadhi kitabu kwenye chumba cha katibu Elishama.
\v 21 Basi mfalme alimtuma Yehudi kuchukua kitabu. Yehudi alikichukua toka chumba cha Elishama katibu. Kisha alikisoma kwa sauti kwa mfalme na wote maafisa walikuwa wamesimama karibu naye.
\v 22 Sasa mfalme alikuwa amesimama kwenye nyumba ya majira ya baridi katika mwezi wa tisa, na mkaa ulikuwa unawaka mbele yake.
\s5
\v 23 Ilitokea wakati Yehudi aliposoma kurusa tatu au nne, mfalme angeweza kuikata kwa kisu na kuitupa kwenye moto katika mkaa mpaka kitabu chote kiliteketea.
\v 24 Lakini wala mfalme wala yeyote wa mjakazi wake aliyesikia haya maneno yote aliogopa, wala hawakuchana nguo zao.
\s5
\v 25 Elnathani, Delaya, na Gemaria walikuwa wamemuomba mfalme asikichome kitabu, lakini hakuwasikiliza.
\v 26 Basi mfalme alimwamuru Yerameeli, ndugu, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kumfunga Baruku mwandishi na Yeremia nabii, lakini Yahwe alikuwa amewaficha.
\s5
\v 27 Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia baada ya mfalme kuwa amechoma kitabu na maneno ya Baruku yaliyokuwa yameandikwa kwa imla ya Yeremia, na alisema,
\v 28 "Rudi, chukua kitabu kingine kwa ajili yako, na uandike maneno haya yote ambayo yalikuwa kwenye kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikichoma.
\v 29 Kisha unapaswa kusema hivi kwa mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda: 'Ulichoma hicho kitabu! Na ulisema: Kwanini umeandika juu yake, " Mfalme wa Babeli hakika atakuja na kuharibu nchi hii, kwa kuwa atawaangamiza wanaume wote na wanyama ndani yake?"
\s5
\v 30 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, Yehoyakimu mfalme wa Yuda: "Hakuna mzao wako atawahi kukaa kwenye kiti cha Daudi. Kama wewe, maiti yako itatupwa kwenye siku ya joto na usiku wa baridi.
\v 31 Kwa kuwa nitakuadhibu, wazao wako, na wajakazi wako kwa maovu yenu yote. Nitaleta kwenu, kwa wakazi wote wa Yerusalemu, na kwa kila mtu Yuda majanga ambayo nimewatishia ninyi, lakini kwa hamkuwa makini."
\s5
\v 32 Kwa hiyo Yeremia alichukua kitabu kingine na akampa Baruku mwana wa Neria mwandishi. Baruku aliandika juu yake kwa imla ya Yeremia maneno yote ambayo yalikuwa katika kitabu kilichochomwa moto na mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda. Zaidi, maneno mengi ya kufanana yaliongezwa kwenye kitabu hiki.
\s5
\c 37
\p
\v 1 Sasa Sedekia mwana wa Yosia alitawala kama mfalme badala ya Yehoyachin mwana wa Yehoyakimu. Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa amemfanya Sedekia mfalme juu ya nchi ya Yuda.
\v 2 Lakini Sedekia, wajakazi wake, na watu wa nchi hawakusikiliza maneno ya Yahwe ambayo alitangaza kwa mkono wa Yeremia nabii.
\s5
\v 3 Kwa hiyo Mfalme Sedekia, Yehukali mwana wa Shelemia, na Zefania mwana wa Maaseia kuhani alituma ujumbe kwa Yeremia nabii. Walisema, "Omba kwa niaba kwa Yahwe Mungu wetu."
\v 4 Sasa Yeremia alikuwa anakuja na kwenda miongoni mwa watu, kwa kuwa alikuwa bado hajawekwa ndani ya gereza.
\v 5 Jeshi la Farao lilitoka Misri, na Wakaldayo waliozingira Yerusalem walisikia habari kuhusu wao na kuondoka Yerusalem.
\s5
\v 6 Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia nabii na kusema,
\v 7 "Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi: Hiki ndivyo utakavyosema kwa mfalme wa Yuda, kwa sababu amekutuma wewe kutafuta ushauri toka kwangu, 'Ona, jeshi la Farao, ambalo lilikuja kukusaidia, liko tayari kurudi Misri, kwenye nchi yao.
\v 8 Wakaldayo watarudi. Watapigana dhidi ya mji huu, kuuteka, na kuuchoma.'
\s5
\v 9 Yahwe asema hivi: Msidaganyane kwa kusema, "Hakika Wakaldayo wanatuacha sisi,' kwa kuwa hawatatuacha.
\v 10 Hata kama mmelishinda jeshi la Wakaldayo lote ambalo linapigana nanyi ili kwamba wanaume waliojeruhiwa walibakizwa katika mahema yao, wangeweza kunyanyuka na kuchoma mji huu."
\s5
\v 11 Basi ilikuwa wakati jeshi la Wakaldayo lilipoondoka Yerusalem wakati jeshi la Farao lilikuwa linakuja,
\v 12 kisha Yeremia alienda toka Yerusalem kwenda nchi ya Benjamini. Alitaka kumiliki njia ya nchi huko miongoni mwa watu wake.
\v 13 Kama alivyokuwa katika mlango wa Benjamini, mlinzi mkuu aliyekuwa hapo. Jina lake lilikuwa Yeria mwana wa Shelemia mwana wa Hanania. Alimshika kwa kumnyakua Yeremia nabii na kusema, " Mnatoka jangwani kwa Wakaldayo."
\s5
\v 14 Lakini Yeremia alisema, "Hiyo si kweli. Siendi jangwani kwa Wakaldayo." Lakini Yeria hakumsikiliza. Alimchukua Yeremia na kumleta kwa maafisa.
\v 15 Maafisa walikuwa wamemkasirikia Yeremia. Walimpiga na kumweka gerezani, ambayo ilikuwa nyumba ya Yonathani mwandishi, kwa kuwa waligeuza kuwa gereza.
\s5
\v 16 Kwa hiyo Yeremia alikuwa amewekwa kwenye kifungo cha chini, ambako alikuwa huko kwa siku nyingi.
\v 17 Kisha mfalme Sedekia alimtuma mtu mmoja aliyemleta kwenye ikulu. Kwenye nyumba yake, mfalme alimuuliza binafsi, "Kuna neno: Utatiwa kwenye mkono wa mfalme wa Babeli."
\s5
\v 18 Kisha Yeremia alisema kwa mfalme Sedekia, "Kwa namna gani nimekutenda dhambi, mjakazi wako, au watu hawa kwamba umeniweke mimi kwenye gereza?
\v 19 Wako wapi nabii wako, wale waliotabiri kwa ajili yako na kusema mfalme wa Babeli hatakuja dhidi yako au dhidi ya nchi hii?
\v 20 Lakini sasa sikiliza, bwana wangu mfalme! Acha ombi langu liwe mbele yako. Usinirudie mimi kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, au nitakufa huko."
\s5
\v 21 Kwa hiyo mfalme Sedekia alitoa amri. Wajakazi wake walimwekea mipaka Yeremia katika uwanja wa walinzi. Alipewa mkate kila siku kutoka mtaa wa waokaji mkate, mpaka mkate wote mjini uliisha. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja walinzi.
\s5
\c 38
\p
\v 1 Shefatia mwana wa Matani, Gedalia mwana wa Pashuri, na Pashuri mwana wa Malkiya alisikia maneno ambayo Yeremia alikuwa akitanganza kwa wato wote. Alikuwa akisema,
\v 2 "Yahwe asema hivi: Yeyote anayeishi kwenye mji huu atauwawa kwa upanga, njaa, na pigo. Lakini yeyote ambaye aendae kwa Wakaldayo ataishi. Atatoroka pamoja na maisha yake mwenyewe, na kuishi.
\v 3 Yahwe asema hivi: Huu mji huu utapewa kwa mkono wa jeshi la mfalme wa Babeli, na ataukamata."
\s5
\v 4 Kwa hiyo maafisa walisema kwa mfalme, "Acha mtu huu afe, kwa kuwa kwa njia hii anadhofisha mikono ya wanaume wapiganaji waliobaki kwenye mji huu, na mikono ya watu wote. Anatanganza maneno haya, kwa kuwa huyu mtu hafanyi kwa usalama wa watu hawa, lakini kwa majanga."
\v 5 Basi mfalme Sedekia alisema, "Tazama, yuko mkononi mwako kwa kuwa hakuna mfalme awezae kumpinga."
\s5
\v 6 Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.
\s5
\v 7 Sasa Ebed Meleki Mkushi alikuwa mmoja wa watowashi katika nyumba ya mfalme. Alisikia kwamba walikuwa wamemuweka Yeremia kwenye kisima. Sasa mfalme alikuwa ameketi kwa mlango wa Benjamini.
\v 8 Basi Ebed Meleki alienda toka nyumba ya mfalme na kuzungumza na mfalme.
\v 9 Alisema, "Bwana wangu mfalme, hawa wanaume wamefanya uovu kwa namna walivyomtendea Yeremia nabii. Walimtupa kwenye kisima kwa ajili ya kufa kutokana na njaa, tangu hakuna chakula zaidi katika mji."
\s5
\v 10 Kisha mfalme alitoa amri kwa Ebed Meleki Mkushi. Alisema, "Chukua amri ya watu thelasini kutoka hapa na mtoe Yeremia nabii nje ya kisima kabla hajafa."
\v 11 Basi Ebed Meleki alichukua amri ya watu hao na akaenda nyumba ya mfalme, kwenye ghala la nguo chini ya nyumba. Toka hapo alichukua vitambaa na nguo zilizochanika na kuyashusha chini kwa kamba kwa Yeremia ndani ya kisima.
\s5
\v 12 Ebed Meleki Mkushi alisema kwa Yeremia, "Weka matambara na nguo zilizoraruka chini ya mikono yako na juu ya kamba." Basi Yeremia alifanya hivyo.
\v 13 Kisha walimvuta Yeremia kwa kamba. Kwa njia hii walimtoa kutoka kisimani. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi.
\s5
\v 14 Kisha Mfalme Sedekia alituma neno na kumleta Yeremia nabii kwake, kwenye lango la tatu la nyumba ya Yahwe. Mfalme alisema kwa Yeremia, "Nataka nikuulize kitu. Usinizuilie jibu mimi."
\v 15 Yeremia alisema kwa Sedekia, "Kama nakujibu, hautaniuawa kwa hakika? Na kama nakupa ushauri, hautanisikiliza mimi."
\v 16 Lakini Mfalme Sedekia aliapa kwa Yeremia kwa siri na kusema, "Kama Yahwe aishivyo, yeye aliyetufanya sisi, Sitakuuwa au kukuweka kwenye mkono wa watu wale wanaotafuta maisha yako."
\s5
\v 17 Kwa hiyo Yeremia alisema kwa Sedekia, "Yahwe, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama kwa kweli utatoka kwenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli basi utaishi, and mji huu hautachomwa. Wewe na familia yako mtaishi.
\v 18 Lakini kama hautaenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, basi mji huu utachukuliwa kwa mkono wa Wakaldayo. Watauchoma, na hautakwepa kutoka mkono wao."
\s5
\v 19 Mfalme Sedekia alisema kwa Yeremia, "Lakini ninaogopa watu wa Yuda waliotoka jangwani kwenda kwa Wakaldayo, kwa sababu nitapewa katika mkono wao, kwa kunifanyia vibaya."
\s5
\v 20 Yeremia alisema, "Hawatakutoa kwao. Tii ujumbe toka kwa Yahwe ambao ninakuambia, ili kusudi mambo yataenda vizuri kwako, na ili kusudi utaishi.
\v 21 Lakini kama unakataa kutoka, hivi ndivyo Yahwe amenionesha mimi.
\s5
\v 22 Tazama! Wanawake wote walioachwa kwenye nyumba yako, mfalme wa Yuda, ataletwa kwa maafisa wa mfalme wa Babeli. Hawa wanawake watasema kwako, "Umedaganywa na rafiki zako; wamekuharibu. Miguu yako sasa imezama kwenye matope, na rafiki zako watakimbia.'
\v 23 Kwa kuwa wake zenu wote na watoto wataletwa kwa Wakaldayo, na wewe mwenyewe hautatoroka nchi yao. Utashikwa na mkono wa mfalme wa Babeli, na mji huu utachomwa."
\s5
\v 24 Kisha Sedekia alisema kwa Yeremia, "Usimjulishe yeyote kuhusu maneno haya, ili kwamba usije kufa.
\v 25 Kama maafisa wanasikia kwamba nimeongea na wewe- kama wanakuja na kusema kwako, 'Tuambia umezungumza nini pamoja na mfalme. Usitufiche, au tutakuuwa. Na tuambie nini mfalme amesema kwako'-
\v 26 kisha unapaswa kusema nao, "Nilishawishiana pamoja na mfalme asirudi kwangu kwa nyumba ya Yonathan nitakufa humo."
\s5
\v 27 Kisha maafisa wote walikuja kwa Yeremia na kumuuliza, basi aliwajibu kama mfalme alivyomuelekeza. Basi waliacha kuongea pamoja naye, kwa sababu hawakusikia mazungumzo kati ya Yeremia na mfalme.
\v 28 Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi mpaka siku ile Yerusalem ilipotekwa.
\s5
\c 39
\p
\v 1 Katika mwaka wa tisa na mwezi wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem na kuizingira.
\v 2 Katika mwaka wa kumi na moja na mwezi wa nne wa Sekeia, siku ya tisa ya mwezi, mji uliharibiwa.
\v 3 Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli walikuja na kukaa kwenye lango la katikati: Nergali Sharezeri, Samgari Nebo, na Sarsechimu, afisa muhimu. Nerga Sharezeri alikuwa afisa mkuu na wote waliobaki maafisa wa mfalme wa Babeli.
\s5
\v 4 Ilitokea kwamba wakati Sedekia, mfalme wa Yuda, na wanaume wapiganaji wake wote walipowaona, walikimbia. Walitoka nje usiku toka kwenye mji kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango la kati la kuta mbili. Mfalme alitoka nje katika mwelekeo wa Arabah.
\v 5 Lakini jeshi la Wakaldayo walimfatilia na kumpata Sedekia kwenye tambarare za mto Yordani karibu na Yeriko. Kisha walimshika na kumleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Riblah kwenye nchi ya Hamath, ambapo Nebukadreza alipitisha sentensi juu yake.
\s5
\v 6 Mfalme wa Babeli alimchinja binti wa Sedekia mbele ya macho yake huko Ribla. Pia aliwachinja wanaume wote wa heshima wa Yuda.
\v 7 Kisha alingoa macho ya Sedekia na kumfunga mnyororo wa shaba ili kusudi kumpeleka Babeli.
\s5
\v 8 Kisha Wakaldayo walichoma nyumba ya mfalme na nyumba za watu. Pia walivunja kuta za Yerusalem.
\v 9 Nebukadreza, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliwachukua katika mateka watu wengine waliobaki katika mji. Hii ilijumuisha watu waliotoka jangwa kwenda Wakaldayo na watu wengine walioachwa katika mji.
\v 10 Lakini Nebukadreza nahodha wa walinzi wa mfalme aliwaruhusu watu maskini ambayo hawakuwa na chochote wao kubaki katika chi ya Yuda. Aliwapa mashamba ya mizabibu na maeneo katika siku ile.
\s5
\v 11 Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa amri kuhusu Yeremia kwa Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme. Alikuwa amesema,
\v 12 "Mchukue na umjali. Usimdhuru. Fanya kwa ajili yake chochote anachokuambia."
\v 13 Basi Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme, Nebushazbani mkuu wa matoashi, Nergali Sharezeri afisa mkuu, na wote maafisa wa muhimu wa mfalme wa Babeli walituma watu nje.
\v 14 Watu wao walimchukua Yeremia kutoka uwanja wa mlinzi na kumkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikami mwana wa Shafani, kumchua nyumbani, basi Yeremia alibaki miongoni mwa watu.
\s5
\v 15 Sasa neno la Yahwe lilikuwa limekuja kwa Yeremia wakati alipokuwa chini ya kifungo kwenye uwanja wa mlinzi, na alisema,
\v 16 "Zungumza kwa Ebedi Meleki Mkushi na sema, 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Ona, Nimekaribia kubeba maneno yangu dhidi ya mji huu kwa ajili ya janga na si kwa uzuri. Kwa kuwa yatakuwa kweli mbele yako katika siku hiyo.
\s5
\v 17 Lakini nitakuokoa katika siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe - na hautatiwa katika mkono wa wanaume ambayo unawaogopa.
\v 18 Kwa kuwa nitakuokoa hakika. Hautaanguka kwa upanga. Utatoroka pamoja na maisha yako, kwani unanitumaini - hili lilikuwa tamko la Yahwe."
\s5
\c 40
\p
\v 1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia toka kwa Yahwe baada ya Nebuzaradni, amri wa walinzi wa mfalme, amemtuma mbali kutoka Ramah. Huko ndiko Yeremia alikuwa amechukuliwa, na huko alikuwa amefungwa kwa minyororo. Alikuwa miongoni mwa mateka wote ya Yerusalem na Yuda ambayo walipaswa kuwa matekani Babeli.
\v 2 Mlinzi mkuu alimchukua Yeremia na kusema kwake, "Yahwe Mungu wako aliamrisha maafa haya dhidi ya eneo hili.
\s5
\v 3 Basi Yahwe alileta. Alifanya kama alivyoamrisha, kwani ninyi watu mmefanya dhambi dhidi yake na hamkutii sauti yake. Hii ni sababu ya jambo hili limetokea kwenu. Lakini sasa tazama!
\v 4 Nimekuacha huru leo toka kwenye minyororo iliyokuwa kwenye mikono yako. Kama ni vizuri katika macho yako kuja nami Babeli, njoo, na nitakujali. Lakini kama si vizuri katika macho yako kuja pamoja nami, basi usifanye hivyo. Tazama nchi yote mbele yako. Nenda ambapo ni pazuri na sawa katika macho yako kwenda."
\s5
\v 5 Wakati Yeremia hakujibu, Nebuzaradani alisema, "Nenda kwa Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka msimamizi wa miji ya Yuda. Baki pamoja naye miongoni mwa watu au nenda popote ni pazuri katika macho yako kwenda." Amri wa walinzi wa mfalme alimpa chakula na zawadi, na kisha akamtuma mbali.
\v 6 Basi Yeremia alienda kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpah. Alibaki pamoja naye miongoni mwa watu ambao walibaki nyuma katika nchi.
\s5
\v 7 Sasa baadhi ya amri wa wanawajeshi wa Yuda ambao walikuwa bado katika uwanja- wao na watu wao - walisikia kuwa mfalme wa Babeli alimfanya Gedalia mwana wa Ahikam, liwali juu ya nchi. Pia walisikia kuwa amemweka kusimamia wanaume, wanawake, na watoto ambao walikuwa watu maskini katika nchi, wale ambao hawakuwa wamechukuliwa mateka Babeli.
\v 8 Basi walienda kwa Gedalia huko Mizpa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana Nethania; Yonathan na Yonathani, wana wa Kareaa; Seraya mwana wa Tanhumethi; wana wa Efai Netophathite; na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.
\s5
\v 9 Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, alichukua kiapo kwao na kwa watu wao, na kusema kwao, "Usiogope kuwatumikia maafisa wa Wakaldayo. Ishi katika nchi na kumtumkia mfalme wa Babeli, na itakuwa vizuri kwenu.
\v 10 Na tazama, Ninaishi Mizpa kukutana pamoja na Wakaldayo waliokuja kwetu. Basi vuna mvinyo, matunda ya kiangazi, na mafuta na viweke kwenye vyombo vyako. Uishi katika miji ambayo umechukua."
\s5
\v 11 Kisha Wayahudi wote katika Moabu, miongoni mwa watu wa Ammoni, na katika Edomu, na katika kila nchi ilisikiwa kwamba mfalme wa Babalei ameruhusu mabaki ya Yuda kubaki, kwamba alimteua Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani juu yao.
\v 12 Basi Wayahudi wote walirudi toka kila eneo ambako walikuwa wametawanyika. Walirudi kwenye nchi ya Yuda, kwa Gedalia huko Mizpa. Walivuna mvinyo na matunda ya kiangazi kwa wingi.
\s5
\v 13 Yonathan mwana wa Karea na amri wote wa jeshi katika uwanja walikuja kwa Gedalia huko Mizpa.
\v 14 Walisema kwake, "Haujui kuwa Baalis mfalme wa watu wa Ammoni amemtuma Ishmael mwana wa Nethania kukuua?" Lakini Gedalia mwana wa Ahikim hakuwaamini.
\s5
\v 15 Basi Yonathan mwana wa Karea alizungumza kwa siri kwa Gedalia huko Mizpa na kusema, "Niruhusu niende kumuua Ishmael mwana wa Nethania. Hakuna atakaye nituhumu. Kwanini asikuue wewe? Kwanini kuruhusu Yuda yote ambayo imekusanywa kwako kutawanyishwa na mabaki ya Yuda kuharibiwa?"
\v 16 Lakini Gedalia mwana wa Ahikam alisema kwa Yonathan mwana wa Karea, "Usifanye jambo hili, kwa kuwa unasema uongo kuhusu Ishmael."
\s5
\c 41
\p
\v 1 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmael mwana wa Nethania mwana wa Elishama, toka familia ya kifalme, na maafisa baadhi wa mfalme, walikuja - wanaume kumi walikuwa pamoja naye - kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpa. Walikula chakula pamoja hukp Mizpa.
\v 2 Lakini Ishmael mwana wa Nethania, na wanaume kumi ambao walikuwa pamoja naye waliinuka na kumvamia Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, kwa upanga. Ishmael alimuua Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alimweka kuwa msimamizi wa nchi.
\v 3 Kisha Ishmael aliwauwa Wayahudi wote ambao walikuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na Wakaldayo wanaume wa kupigana kukutwa huko.
\s5
\v 4 Kisha ilikuwa siku ya pili baada ya kumuua Gedila, lakini hakuna moja aliyejua.
\v 5 Wanaume baadhi walikuja toka Shechem, toka Shiloh, na toka Samaria-wanaume semanini ambayo walikuwa wamenyoa ndevu zao, walirarua nguo zao, na kujikata wenyewe- pamoja na chakula cha sadaka na ubani katika mikono yao kwenda kwa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 6 Basi Ishmael mwana wa Nethania alienda toka Mizpa kukutana nao kama walivyoenda, wakitembea na kulia. Kisha ilitokea kwamba kama alivyokutana nao, alisema nao, "Njoo kwa Gedalia mwana wa Ahikam!"
\v 7 Ilikuja kuwa kwamba wakati walipokuja katika mji, Ishmaeil mwana wa Nethania aliwauwa na kuwatupa kwenye shimo, yeye na wanaume ambao walikuwa pamoja naye.
\s5
\v 8 Lakini palikuwa na wanaume kumi miongoni mwao ambao walisema kwa Ishmael, " Usituue, kwa kuwa kuna riziki zetu kwenye shamba: ngano na shayiri, mafuta na asili" Kwa hiyo hakuwauwa pamoja na rafiki zao wengine.
\v 9 Kisima ambacho Ishmael alitupa miili yote ya waliokufa ambaye yeye na Gedalia waliwapiga, kilikuwa ni kilekile ambacho mfalme Asa alichimba wakati alipokuwa akivamiwa na mfalme Baasha wa Israel. Ishmael mwana wa Nethania alilijaza wale ambao walikuwa wameuawa.
\s5
\v 10 Badae Ishmael aliwashika watu wengine wote ambao walikuwa huko Mizpa, mabinti wa mfalme na watu wote ambao walikuwa wameachwa huko Mizpa ambayo Nebuzaradani mlinzi mkuu alikuwa amewakabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikam. Basi Ishmael mwana wa Nethania aliwashika na kuvuka kwa watu wa Ammon.
\s5
\v 11 Lakini Yonathani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi pamoja naye walisikia madhara yote ambayo Ishmael mwana wa Nethania alikuwa amefanya.
\v 12 Basi waliwachukua wanaume wao na kwenda kupigana dhidi ya Ishmanel mwana wa Nethania. Walipigana naye huko kwenye kisima kuu cha Gibeoni.
\s5
\v 13 Kisha ilitokea kwamba wakati watu wote ambao walikuwa na Ishmael kuona Yonathani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi ambao walikuwa pamoja naye, walikuwa na furaha.
\v 14 Basi watu wote ambao Ishmael alikuwa amewashika huko Mizpa waligeuka na kwenda kwa Yonathani mwana wa Karea.
\s5
\v 15 Lakini Ishmael mwana wa Nethania alitoroka na wanaume wanane toka kwa Yonathani. Alienda kwa watu wa Ammon.
\v 16 Yonathani mwana wa Karea na amri jeshi pamoja naye walichukua toka Mizpa watu wote ambao walikuwa wameokolewa kutoka kwa Ishmael mwana wa Nethania. Hii ilikuwa baada ya Ishmael kuwa amemuuwa Gedalia mwana wa Ahikam. Yonathan na rafiki zake walichukua wanaume shujaa, wanaume wapiganaji, wanawake na watoto, na mtoashi ambaye alikuwa ameokolewa huko Gibeoni.
\s5
\v 17 Kisha walienda na kubaki kwa muda huko Geruthi Chimham, ambayo iko karibu Bethelemu. Walikuwa wakienda Misri
\v 18 kwa sababu ya Wakaldayo. Walikuwa wakiwaogopa kwani Ishmael mwana wa Nethania alikuwa amemua Gedalia mwana wa Ahikam, ambaye mfamle wa Babeli amewekwa kwenye usimamizi wa nchi.
\s5
\c 42
\p
\v 1 Kisha amri wote wa jeshi na Yonathan mwana wa Karea, Jezania mwana wa Hoshaia, na watu wote kutoka mdogo kwa mkubwa walimkaribia Yeremia nabii.
\v 2 Walisema naye, "Acha maombi yetu yaje mbele yako. Omba kwa ajili yetu kwa Yahwe Mungu wako kwa ajili ya watu hawa ambao wanabaki kwani tuko wachache katika idadi, kama unavyoona.
\v 3 Muulize Yahwe Mungu wako atuambia sisi njia yakuendea na nini tufanye."
\s5
\v 4 Basi Yeremia nabii alisema nao, "Nimewasikia, Tazama, Nitaomba kwa Yahwe Mungu wenu kama mlivyoomba. Vyovyote Yahwe ananijibu, Nitawambia. Sitawaficha chochote ninyi."
\v 5 Walisema na Yeremia, "Na Yawhe awe shahidi mkweli na mwaminifu dhidi yenu, kama hatutafanya kila kitu ambacho Yahwe Mungu wenu anatuambia kufanya.
\v 6 Hata kama ni vizuri au vibaya, tutatii sauti ya Yahwe Mungu wetu, ambaye tunawatuma ninyi, ili kwamba iwe vizuri pamoja nasi wakati tunatii sauti ya Yahwe Mungu wetu."
\s5
\v 7 Basi ilitokea kwamba baada ya siku kumi, neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia.
\v 8 Kwa hiyo Yeremia alimwita Yonathan mwana wa Karea na amri wote jeshi pamoja naye, na watu wote kutoka mdogo kwa mkubwa.
\v 9 Na alisema nao, "Yahwe, Mungu wa Israel, ambaye umenituma mimi ili niweze kuweka maombi yako mbele zake. Yahwe asema hivi,
\v 10 Kama mtarudi na kuishi katika nchi hii, basi nitawajenga na sitawararua chini; Nitapanda na sitawangoa, kwa kuwa nitageuza maafa ambayo nimeleta juu yako.
\s5
\v 11 Msimugope mfalme wa Babeli, ambaye mnamuogopa. Msimuogope-hili ni tamko la Yahwe kwani niko pamoja nanyi kuwahifadhi na kuwaokoa toka mkono wake.
\v 12 Kwa kuwa nitawapa rehema. Nitakuwa na huruma juu yenu, na nitawarudisha kwenye nchi yenu.
\s5
\v 13 Lakini tudhani kusema kwamba, "Hatutakaa katika nchi hii"- kama hamtasikiliza sauti yangu, sauti ya Yahwe Mungu wenu.
\v 14 Tudhani kwamba mnasema, "Hapana! Tutaenda kwenye nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita yoyote, ambayo hatutasikia sauti ya tarumbeta, na hatutaona njaa ya chakula. Tutaishi huko."
\s5
\v 15 Sasa sikiliza neno hili la Yahwe, wewe mabaki ya Yuda. Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Kama kweli mtatoka kwenda Misri, kwenda na kuishi huko,
\v 16 basi upanga ambao mnauogopa utawapita huko kwenye nchi ya Misri. Njaa ambayo mnawasiwasi nayo itawafatilia huko Misri. Na mtakufa huko.
\v 17 Basi itatokea kwamba wanaume wote waliondoka kwenda Misri kuishi huko watakufa kwa upanga, njaa, au pigo. Hapatakuwa na mwathirika wao, hakuna atakayetoroka maafa ambayo nitaleta juu yao.
\s5
\v 18 Kwa kuwa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama gadhabu yangu na hasira yangu imemwanga juu ya wakazi wa Yerusalem, kwa njia hiyo hasira yangu itamwangwa juu yenu kama mtaenda Misri. Mtakuwa sababu ya hasira na hofu, sababu la kuzungumza laana, na kitu kisichokuwa na heshima. Na hamtaona eneo hili tena."
\v 19 Basi Yeremia alisema, "Yahwe amezungumza kuhusu ninyi - mabaki ya Yuda. Msiende Misri! Unajua kwa hakika kwamba nimekuwa shahidi dhidi yenu leo.
\s5
\v 20 Kwa kuwa mmejidanganya vibaya wenyewe wakati mliponituma mimi kwenda kwa Yahwe Mungu wenu na kusema, 'Omba kwa Yahwe Mungu wetu kwa ajili yetu. Kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema, tuambie, na tutaibeba.'
\v 21 Kwa kuwa nimekwisha toa taarifa kwako leo, lakini hajusikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu au kwa chochote kuhusu ambacho alinituma mimi kwako.
\v 22 Basi sasa, utajua kwa hakika kwamba utakufa kwa upanga, njaa, na pigo katika eneo ambalo ulitamani kwenda kuishi."
\s5
\c 43
\p
\v 1 Ilitokea kwamba Yeremia alimaliza kuhubiri kwa watu wote maneno yote ya Yahwe Mungu wao kwamba Yahwe Mungu wao alimwambia kusema.
\v 2 Azaria mwana wa Hoshaia, Yonathani mwana wa Karea, na watu wenye kiburi walisema kwa Yeremia, "Unasema uongo. Yahwe Mungu wetu hajakutuma wewe kusema, 'Usiende Misri kuishi huko.'
\v 3 Kwa kuwa Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu kututoa sisi kwenye mkono wa Wakaldayo, kwa kuwa wewe umesababisha kifo chetu na kutufanya sisi mateka huko Babeli."
\s5
\v 4 Basi Yonathani mwana wa Karea, wakuu wa jeshi, na watu wote walikataa kusikiliza sauti ya Yahwe kuishi kwenye nchi ya Yuda.
\v 5 Yonathani mwana wa Karea na amri jeshi wote waliwachukua mabaki wa Yuda ambao walikuwa wamerudi kutoka mataifa yote ambapo walikuwa wametawanyika kuishi katika nchi ya Yuda.
\v 6 Waliwachukua wanaume na wanawake, watoto na mabinti wa mfalme, na kila mtu ambaye Nebuzaradani, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliruhusu kubaki pamoja na Gedali mwana wa Ahikam mwana wa Shafan. Pia walimchukua Yeremia nabii na Baruku mwana wa Neria.
\v 7 Walienda nchi ya Misri, kwa Tahpanhesi, kwa sababu hawakusikiliza sauti ya Yahwe.
\s5
\v 8 Basi neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia huko Tahpanhesi na kusema,
\v 9 "Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwenye macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi.
\v 10 Kisha wakasema nao, "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, 'Ona, nimekaribia kutuma wajumbe kumchukua Nebukadreza mfalme wa Babeli kama mtumwa wangu. Nitaweka kiti cha enzi juu ya mawe haya ambayo wewe, Yeremia, umeyazika. Nebukadreza ataweka banda lake juu yao.
\s5
\v 11 Kwa kuwa atakuja na kuvamia nchi ya Misri. Yeyote aliyeandikiwa kufa atakufa. Yeyote aliyeandikiwa mateka atachukuliwa mateka. Na yeyote aliyeandikiwa kwa upanga atakufa kwa upanga.
\v 12 Kisha nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri. Nebukadreza atawachoma na kuwashika. Atasafisha nchi ya Misri kama wachungaji wanavyosafisha wanyama waharibio nguo zao. Ataenda nje kutoka eneo hilo kwa ushindi.
\v 13 Atavunja nguzo za mawe huko Heliopolisi kwenye nchi ya Misri. Atachoma mahekalu ya miungu ya Misri."
\s5
\c 44
\p
\v 1 Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi katika nchi ya Misri, wale wanaoishi Migdoli, Tahpanhesi, Memphis, na katika nchi ya Patrosi.
\v 2 "Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Wewe mwenyewe umeyaona maafa yote niliyoleta juu ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Ona, ni ukiwa leo. Hakuna yeyote anaishi mwao.
\v 3 Hii ni kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya kunikosea mimi kwa kwenda kuchoma ubani na kuabudu miungu mengine. Hawa walikuwa miungu ambao wala wao wenyewe, wala ninyi, wala mababu zenu walijua.
\s5
\v 4 Basi nirudie kuwatuma watumwa wangu wote manabii kwao. Niliwatuma wao kusema, 'Acha kufanya vitu hivi machukizo ambayo nachukia.
\v 5 Lakini hawakunisikiliza. Walikataa kuwa makini au kuyaacha maovu kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine.
\v 6 Basi hasira yangu na gadhabu yangu zilimwanga na kuwasha moto kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Basi waliharibiwa na kuteketezwa, kama katika siku ya leo."
\s5
\v 7 Basi sasa Yahwe, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israel, asema hivi, "Kwanini unafanya maovu makubwa dhidi yenu? Kwanini mnasababisha ninyi wenyewe kujitenga kutoka miongoni mwa Yuda - wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao? Hakuna mabaki yenu yatabaki.
\v 8 Kwa maovu yenu mmenikosea pamoja na matendo ya mikono yenu, kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine kwenye nchi ya Misri, ambapo mmekwenda kuishi. Mmeenda huko ili kwamba mtaangamizwa, ili kwamba mtalaaniwa na mashutumu miongoni mwa mataifa yote ya duniani.
\s5
\v 9 Mmesahau maovu yaliyofanywa na mababu zenu na maouvu yaliyofanywa na wafalme wa Yuda na wake zao? Mmesahau uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu?
\v 10 Kwa siku hii, hawajanyenyekea bado. Hawashimu sheria yangu au maagizo niliyoweka mbele yao na mababu zao, wala hawatembei nazo."
\s5
\v 11 Kwa hiyo sasa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, "Ona, Nimekaribia kuweka uso wangu dhidi yenu kuleta maafa kwenu na kuiharibu Yuda yote.
\v 12 Kwa kuwa nitachukua mabaki wa Yuda ambaye ameanza safari kwenda nchi ya Misri kuishi huko. Nitafanya hivi ili kwamba wataangamia wote katika nchi ya Misri. Wataanguka kwa upanga na njaa. Kutoka wadogo kwa wakubwa wataangamia kwa upanga na njaa. Watakufa na watakuwa sababu ya kuaapa, kulaani, mashutumu, na kitu kibaya.
\s5
\v 13 Kwa kuwa nitawaadhibu watu wakazi wa nchi ya Misri kama nilivyoadhibu Yerusalem kwa upanga, njaa, na pigo.
\v 14 Hakuna mkimbizi au mwathirika wa mabaki ya Yuda ambaye wataenda kuishi huko kwenye nchi ya Misri watarudi kwenye nchi ya Yuda, hata kama wanataka kurudi na kuishi huko. Hakuna kati yao atarudi, ijapokuwa wachache ambayo watatoroka kutoka huko."
\s5
\v 15 Kisha watu wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakichoma ubani kwa miungu mingine, na wanawake wote waliokuwa katika kusanyiko kuu, na watu wote ambao walikuwa wakiishi kwenye nchi ya Misri katika Pathrosi walimjibu Yeremia.
\v 16 Walisema, "Kuhusu neno ambalo mmetuambia sisi kwa jina la Yahwe: Hatutakusikiliza.
\v 17 Kwa hakika tutafanya mambo yote ambayo tulisema tungefanya: kuchoma ubani kwa malkia wa Mbingu na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake kama sisi, mababu zetu, wafalme wetu, na viongozi wetu walivyofanya kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Kisha tutajazwa pamoja na chakula na tutafanikiwa, pasipo kupata maafa yoyote.
\s5
\v 18 Wakati tunajiepusha kutofanya mambo haya, si kutoa sadaka ya ubani kwa Malkia wa Mbinguni na si kumwanga kinywaji cha sadaka kwake, tulikuwa wote tunaumwa umaskini na tulikuwa tunakufa kwa upanga na njaa."
\v 19 Wanawake walisema, "Wakati tulipokuwa tunatengeneza ubani wa sadaka mbele ya Malkia wa Mbinguni na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake, tulifanya hivi vitu pasipo waume wetu kujua."
\s5
\v 20 Kisha Yeremia alisema kwa watu wote - kwa wanaume na wanawake, na watu wote waliomjibu yeye - alihubiri na kusema,
\v 21 "Je Yahwe hakukumbuka ubani ambao mliuchoma kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalem - wewe na mababu zenu, wafalme wenu na viongozi, na watu wa nchi? Kwa kuwa Yahwe anakumbuka hili kwenye akili; inakuja kwenye mawazo yake.
\s5
\v 22 Basi hawakuweza tena kuvumilia kwa sababu ya matendo yenu maovu, kwa sababu machukizo ambayo mlifanya. Basi nchi yenu imekuwa ukiwa, kutisha, na laana basi hapakuwa na mkazi tena kwa siku hii.
\v 23 Kwa sababu mlichoma ubani na kufanya dhambi dhidi ya Yahwe, na kwa sababu msingesikiliza sauti yake, sheria yake, amri zake, au maagizo ya agano lake, maafa haya dhidi yenu yemetokea kama kwa siku hii. "
\s5
\v 24 Kisha Yeremia alisema kwa watu wote na wanawake wote, " Sikia neno la Yahwe, Yuda yote ambao wamo katika nchi ya Misri.
\v 25 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, Wewe na wake zako wote mmesema kwa vinywa vyenu na kubeba kwa mikono yenu kile mlichosema, " Hakika tutabeba viapo ambavyo tulifanya kumwabudu Malkia wa Mbinguni, kwanga kinywaji cha sadaka kwake." Sasa timiza viapo vyenu, vibebe."
\s5
\v 26 Basi, sikiliza neno la Yahwe, Yuda yote ambao mnaishi katika nchi ya Misri, 'Ona, Nimeapa kwa jina langu kuu-asema Yahwe. Jina langu halitaitwa kwa vinywa vya wanaume wowote wa Yuda kwenye nchi ya Misri, wewe ambaye sasa unasema, "Kama Bwana Yahwe aishivyo."
\v 27 Ona, Ninakutazama juu yako kwa ajili ya maafa na si kwa uzuri. Kila mtu wa Yuda katika nchi ya Misri ataangamia kwa upanga na njaa mpaka wote wameishia.
\v 28 Kisha waathirika wa upanga watarudi kutoka nchi ya Misri kwa nchi ya Yuda, peke idadi ndogo yao. Basi mabaki yote ya Yuda walioenda kwenye nchi ya Misri kuishi huko watajua ambao neno litakuwa kweli: yangu au yao.
\s5
\v 29 Hii itakuwa ishara kwa ajili yako - hili ni tamko la Yahwe - kwamba ninaweka dhidi yenu katika eneo hili, ili kwamba mtajua kwamba maneno yangu hakika yatawavamia pamoja na maafa.
\v 30 Yahwe asema hivi, 'Tazama, ninakaribia kumtoa Farao Hofra mfalme wa Misri kwenye mkono wa adui zake na kwenye mkono wa wale wanaotafuta kumuua. Itakuwa sawa kama wakati nilimpa Sedekia mfalme wa Yuda kwenye mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, adui wake aliyetafuta maisha yake.
\s5
\c 45
\p
\v 1 Hili ni neno ambalo Yeremia nabii alimwambia Baruku mwana wa Neria. Hii ilitokea wakati alipoandika kwenye kitabu maneno haya kwa imla ya Yeremia - hii ilikuwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, na alisema,
\v 2 "Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi kwako, Baruku:
\v 3 Umesema, Ole mimi, kwa kuwa Yahwe ameongeza uchungu wa maumivu. Kuugua kwangu kumenichosha; sipati pumziko.'
\s5
\v 4 Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: "Yahwe asema hivi: Ona, nilichojenga, sasa ninararua chini. Nilichopanda, sasa ninangoa. Hii ni kweli juu ya dunia.
\v 5 Lakini unategema mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja kwa binadamu wote - hii ni tamko la Yahwe - lakini ninakupa maisha yangu kama nyara popote utakakoenda."
\s5
\c 46
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe lililomjia Yeremia nabii juu ya mataifa.
\v 2 Juu ya Misri; "Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
\v 3 Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge vitani.
\v 4 Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
\s5
\v 5 Ninaona nini hapa? Wana woga na wanakimbia, maana askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa usalama na hawaangalii nyuma. Kitisho kipo mahali pote - hili ni tamko la Yahwe -
\v 6 wepesi hawawezi kukimbia, na askari hawezi kukwepa. Wana jikwaa kaskazini na kuanguaka kando ya mto Frati.
\s5
\v 7 Ni nani hawa wainukao kama Nile, ambao maji yao yanaruka juu na chini kama mito?
\v 8 Misri huinuka kama mto Nile, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Anasema, 'nitapanda juu; nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wake.
\v 9 Inukeni, farasi. Mwe na hasira, ninyi vibandawazi. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.
\s5
\v 10 Siku hiyo itakuwa siku ya kisasi kwa Bwana Yahwe wa majeshi, naye atajilipizia kisasa juu ya adui zake. Upanga utararua na kujirishisha. Utakula na kujishibisha kwa damu yao. Kwa maana kutakuwa na sadaka kwa Bwana Yahwe wa majeshi katika nchi ya kaskazini kando ya mto Frati.
\s5
\v 11 Panda Gileadi ujipatie dawa, binti wa Misri uliyebikra. Haifai kwamba unaweka dawa nyingi juu yako. Hakuna uponyaji kwako.
\v 12 Mataifa wamesikia kuaibika kwako. Nchi imejawa na maombolezo yako, maana askari anajikwaa juu ya askari; na wote wawili uanguka pamoja."
\s5
\v 13 Hili ndilo neno Yahwe alilomwambia nabii Yeremia wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokuja na kushambulia nchi ya Misri:
\v 14 Toa taarifa kwa Misri na isikiwe katika Migdoli na Memfisi. Wamesema katika Tapenesi, wekeni kituo na mwe imara, kwa maana upanga unakula wote kati yenu.
\s5
\v 15 Kwa nini Apisi mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahwe amemwangusha chini.
\v 16 Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anaanguka kinyume cha anayefuata. Wanasema, "Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuuache upanga huu unaotuuwa."
\v 17 Walitangaza pale, "Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, ameuacha wasaa wake mbali."
\s5
\v 18 Kama niishivyo - hili ni tamko la mfalme - Yahwe wa majeshi kwa jina, kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
\v 19 Wekeni masanduku yenu kuyachukua uhamishoni, binti mwishio Misri. Kwani Memfisi haitafaa, magofu. Hakuna atakayeishi huko.
\s5
\v 20 Misri ni mtamba mzuri sana, lakini mdudu aumaye anakuja kutoka kaskazini. Anakuja.
\v 21 Askari wake wakukodiwa ni kama dume la ng'ombe lililonona kati yake. lakini wao pia watageuka na kukimbia. Hawatasimama pamoja, kwani siku yao ya madhara inakuja kunyume chao, wakatik wa kuadhibiwa kwao.
\v 22 Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa. maana adui yake anajiandaa kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.
\s5
\v 23 Wataangusha misitu - japokuwa ni mingi sana - hili ni tamko la Yahwe. Kwa maana adui watakuwa wengi kuliko nzige, wasiohesabika.
\v 24 Binti Misri ataaibishwa. Atawekwa mkononi mwa watu kutoka kaskazini."
\s5
\v 25 Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema, "Tazama, niko karibu kumwadhibu Amoni wa Thebesi, Farao, Misri na miungu yake, Farao mfalme wake, na wote wanaomtumaini.
\v 26 Nitawaweka katika mkono wa wanaoyaona maisha yao, na katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli na watumishi wake. Kisha baada ya haya Misri itakaliwa kama mwanzo - asema Yahwe."
\s5
\v 27 Lakini, wewe Yakobo mtumishi wangu, usihofu. Usifadhaike, Israeli, maana tazama, nitakurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya mateka. Kisha Yakobo atarudi, tafuta amani, na kuwa salama, na hapatakuwa na wa kumwogofya.
\v 28 Wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope - asema Yahwe - kwa maana nipo nawe, hivyo nitaleta maangamizi makamilifu dhidi ya mataifa yote nilikokupeleka. Lakini sitakuharibu kabisa. Hata hivyo nitakuadhibu kwa haki na hakika sitakuacha bila adhabu."
\s5
\c 47
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabi juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza.
\v 2 "Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mtu atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.
\s5
\v 3 Kwa sauti ya kukanyaga kwa kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa mwungurumo wa vibandawazi vyao na kelele za magurudumu yao, wazazi hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wao.
\v 4 Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahwe anawaangamiza Wafilisiti, waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.
\s5
\v 5 Maombolezo yatakuja juu ya Gaza. Hata kwa Ashikeloni, watu waliosalia bondeni watakuwa kimya. Ni kwa muda gani mtajiondoa katika maombolezo?
\v 6 Ole, upanga wa Yahwe! itachukua muda gani hata unyamaze? Rudini alani mwenu! Acha na unyamaze.
\v 7 Wawezaje kuwa kimya, maana Yahwe amekuagiza. Amekuamuru kumpiga Ashikeloni na dhidi ya nchi ya pwani ya bahari.
\s5
\c 48
\p
\v 1 Juu ya Moabu, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, "Ole kwa Nebo, kwani umekuwa ukiwa. Kiriathaimu umetekwa na kuaibishwa. Ngome zake zimeangushwa na kuaibishwa.
\v 2 Heshima ya Moabu haipo tena. Adui zake katika Heshboni walipanga njama za kumwangamiza. Walisema, 'Njoni tumwangamize kama taifa. Madmena pia itaangamizwa - upanga utakutangulia.'
\s5
\v 3 Sikilizeni! Sauti ya mvumo inakuja kutoka Horonaimu.
\v 4 Moabu ameangamizwa. Vilio vya watoto wake vinasikika.
\v 5 Wanapanda kilima cha Luhithi wakilia, njia yote kuelekea Horonaimu, vilio vinasikika kutokana na maangamizi.
\s5
\v 6 Kimbieni! okeeni maisha yenu kama kichaka cha mreteni katika nyika.
\v 7 Maana kwa sababu ya tumaini lenu katika matendo na utajiri wenu, ninyi pia mtatekwa. Kisha Kemoshi atachukuliwa matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
\s5
\v 8 Maana mwaribu atafika kila mji; hakuna mji utakaookoka. Hivyo bonde litaangamia na tambarare itateketezwa, kama alivyosema Yahwe.
\v 9 Mpeni Moabu mabawa, maana ni lazima aruke mbali bila shaka. Miji yake itakuwa magofu, pasipo na mtu wa kuishi humo.
\v 10 Na alaaniwe kila aliye mvivu katika kufanya kazi ya Yahwe! Na alaaniwe kila auzuiaye upanga wake usimwage damu!
\s5
\v 11 Moabu amekuwa akijisikia salama tangu alipokuwa kijana. Yeye ni kama mvinyo wake ambao haujamiminwa kutoka mtungi kwenda mtungi mwingine. Hajaenda matekani. Hivyo radha yake ni njema kama mwanzo; radha yake haibadiliki.
\v 12 Hivyo tazama, siku zinakuja - asema Yahwe - nitakapompelekea watakao mchovya na kumwaga mitungi yake yote na kupasua mitungi yake.
\s5
\v 13 Kisha Moabu atamwaibikia Kemoshi kama ambavyo nyumba ya Israeli ilivyoiabikia Betheli, tumaini lao.
\v 14 Utawezaje kusema, 'Tu askari, wapiganaji wenye nguvu'?
\s5
\v 15 Moabu itaangamizwa na miji yake kushambuliwa. Kwa maana vijana wake wazuri wameshuka katika eneo la machinjo. Hili ni tamko la mfalme! Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
\v 16 Maangazizo ya Moabu yanakaribia; maafa yanaharakisha.
\v 17 Ninyi nyote mlio karibu na Moabu, ombolezeni. Nanyi mjuao fahari yake, pigeni kelele hivi, 'Ole, fimbo yenye nguvu, fimbo yenye heshima, imevunjwa.'
\s5
\v 18 Shukeni kutoka mahali penu pa heshima na kuketi katika nchi kavu, ewe binti uishie Diboni. Maana aiangamizaye Moabu anakushambulia, atakayeziharibu ngome zako.
\v 19 Simameni njiani na kuangalia, enyi mwishio katika Aroeri. Waulizeni wanaokimbia na kutoroka. Sema, 'Nini kimetokea?'
\v 20 Moabu ameaibika, maana amevujwa. Lieni kwa sauti na uchungu; pigeni yowe kuomba msaada. Wambieni watu waliokando ya Mto Arinoni kwamba Moabu ameangamizwa.
\s5
\v 21 Basi maangamizi yamefika katika nchi ya kilima, huko Holoni, Yakza, na Mefathi,
\v 22 huko Diboni, Nebo, na Bethi Diblathaimu,
\v 23 huko Kiriatahaimu, Beth Gamul, na Bethi Meoni,
\v 24 huko Keriothi na Bozra, na katika miji yote iliyomo katika nchi ya Moabu - miji iliyoko mbali na karibu.
\v 25 Nguvu za Moabu zimekwisha; mkono wake umevunjwa - asema Yahwe.
\s5
\v 26 Mnywesheni, maana alitenda kwa kiburi kinyume changu, Yahwe. Basi Moabu anapiga makofi kwa machukizo kwa matapiko yake mwenyewe, hivyo amekuwa pia kitu cha kuchekesha.
\v 27 Maana Israeli hakuwa kitu cha kuchekesha kwako? Alionekana miongoni mwa wezi, kwamba ulitikisa kichwa chako kwake mara ulipoongea juu yake?
\s5
\v 28 Jitengeni na miji na kuweka kambi katika minuko, enyi watu wa Moabu. Kuwa kama njiwa anayeatamia juu ya mlango wa tundu katika miamba.
\v 29 Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu - majivuno yake, maringo, kiburi, utukufu binafsi na kujiinua moyoni.
\s5
\v 30 Hili ni tamko la Yahwe - mimi mwenyewe najua maneno yake ya ukaidi, yasiyosaidia chochote, kama matendo yake.
\v 31 Hivyo nitavumisha maombolezo kwa ajili ya Moabu, na nitapiga kelele katika uzuni kwa ajili ya Moabu. Nitaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir Hereshi.
\v 32 Nitalia zaidi kwa ajili yenu kuliko nilivyofanya kwa Yazeri, mzabibu wa Sibma! Matawi yako yalipita katika Bahari ya Chumvi na kufika hata Yazeri. Mwaribu ameshambulia matunda yenu ya kiangazi na mzabibu wenu.
\s5
\v 33 Hivyo sherehe na furaha vimeondolewa kutoka miti ya matunda na nchi ya Moabu. Nimekomesha mvinyo kutoka mashinikizo yao. Hawatakanyaga kwa kelele za furaha. Kelele yoyote haitakuwa kelele ya furaha.
\s5
\v 34 Kutoka kelele huko Heshiboni hata kufika Eleale, sauti yao inasikika hata Yahazi, kutoka Soari hata Horonaimu na Eglathi Shelishiya, hata maji ya Nimrimu yamekauka.
\v 35 Maana nitamkomesha kila mtu katika Moabu atoaye sadaka mahali pa juu na kuteketeza uvumba kwa miungu yake - asema Yahwe.
\s5
\v 36 Hivyo moyo wangu unamwombolezea Moabu kama zomari. Moyo wangu unaomboleza kama zomari kwa ajili ya watu wa Kir Heresi. Utajiri walioupata umekwisha.
\v 37 Maana kila kichwa kina upaa na kila kidevu kimenyolewa. Chale zipo katika kila mkono, na nguo za magunia katika viuno vyao.
\s5
\v 38 Maombolezo yapo kila mahali, juu ya kila paa la nyumba ya Moabu na katika masoko ya Moabu. Kwa maana nimeivunja Moabu kama chungu kisichotakiwa tena - asema Yahwe.
\v 39 Jinsi gani imeharibiwa! Jinsi wanavyopiga kelele katika maombolezo yao! Moabu ameigeuza kwa aibu! Hivyo Moabu atakuwa kitu cha kuchekwa na kitisho kwa wote wanaomzunguka."
\s5
\v 40 Maana Yahwe asema hivi, "Tazama, adui atakuja akiruka kama tai, akieneza mabawa yake juu ya Moabu.
\v 41 Keriothi umetekwa, na ngome zake zimekamatwa. Maana siku hiyo myoyo ya askari wa Moabu itakuwa kama mioyo ya wanawake katika uchungu wa kujifungua.
\s5
\v 42 Hivyo Moabu utaharibiwa kama watu, kwa kuwa walijivuna kinyume changu, Yahwe.
\v 43 Hofu na shimo, na mtego vinakujia, watu wa Moabu - asema Yahwe.
\v 44 Kila akimbiaye kwa sababu ya hofu ataanguka shimoni, na kila atokaye shimoni atanaswa na mtego, maana nitayaleta haya juu yao katika mwaka wa kisasi changu dhidi yao - asema Yahwe.
\s5
\v 45 Wakimbiao watasimama katika kivuli cha Heshboni bila nguvu, maana moto utatoka Heshboni, miale kutoka katikati ya Sihoni. Utateketeza paji la uso wa Moabu na juu ya vichwa vya watu wenye majivuno.
\s5
\v 46 Ole wako, Moabu! watu wa Kemoshi wameangamizwa, Kwa maana wana wako wamechukuliwa kama mateka na binti zako matekani.
\v 47 Lakini nitazirejesha siku njema za Moabu katika siku zijazo - asema Yahwe." Hukumu ya Moabu inaishia hapa.
\s5
\c 49
\p
\v 1 Juu ya watu wa Amoni, Yahwe asema hivi, "Je Israeli hana watoto? Je hakuna mtu wa kurithi chochote katika Israeli? Kwa nini Moleki aikalie Gadi, na watu wake kukaa katika miji yake?
\v 2 Hivyo angalia, siku zinakuja - asema Yahwe - nitakapo sikizisha ishara ya vita juu ya Raba miongoni mwa watu wa Amoni, hivyo itakuwa rundo lililoachwa na binti zake watawasha moto. Maana Israeli atawamiliki wanaommiliki," asema Yahwe.
\s5
\v 3 Piga kelele kwa maombolezo, Heshboni, maana Ai utaangamizwa! Piga kelele, Binti za Raba! Vaeni nguo za magunia. Ombolezeni na kukimbia kwa kuchanganyikiwa, maana Moleki anakwenda matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
\v 4 Kwa nini mnajivunia nguvu zenu? Nguvu zenu zitakwisha, binti wasioamini, ninyi mnaotumaini utajiri wenu. Mwasema, "Nani atakayekuja kinyume changu?'
\s5
\v 5 Tazama, nitaleta kitisho juu yenu - hili ni tamko la Yahwe, Bwana wa majeshi - kitisho hiki kitatoka kwao wote wanaowazunguka. Kila mmoja wenu atatawanyika mbele yake. Hakutakuwa na wa kuwakusanya wanaotawanyika.
\v 6 Lakini baada ya haya nitarejesha mema ya watu wa Amoni - hili ni tamko la Yahwe."
\s5
\v 7 Juu ya Edomu, Yahwe wa majeshi asema hivi, Je hakuna tena hekima katika Temani? Je ushauri mwema umepotea kutoka kwa wenye ufahamu? Je hekima yao imeharibika?
\v 8 Kimbieni! Rudini nyuma! Bakini katika mashimo katika ardhi, wenyeji wa Dedani. Maana naleta maafa ya Esau juu yake wakati ninaomwadhibu.
\s5
\v 9 Ikiwa wavunaji wa zabibu walikuja kwako, je wasinge acha kidogo? Ikiwa wezi walikuja usiku, je wasingeiba kiasi walichotaka?
\v 10 Lakini nimempiga Esau kwa ukiwa. Nimefunua maficho yao. Hivyo hataweza kujificha mwenyewe. Watoto wake, ndugu zake, na jirani zake wameharibiwa, wamepotea.
\v 11 Acha nyuma yatima wako. Nitachukua uhai wao, na wajane wako wanaweza kuniamini."
\s5
\v 12 Maana Yahwe asema hivi, "Tazama, wasiostahili ni lazima wanywe sehemu ya kikombe. Je mnadhani mtaachwa bila kuhadhibiwa? Hapana, maana hakika mtakunywa.
\v 13 Maana nimekwisha apa kwangu mimi mwenyewe - asema Yahwe - Hiyo Bozra itakuwa hofu, aibu, magofu, na kitu cha laana. Miji yake yote itakuwa magofu daima.
\s5
\v 14 Nimesikia habari kutoka kwa Yahwe, na mjumbe ametumwa katika mataifa, 'Kusanyikeni na kumpiga. Jiandaeni kwa vita.'
\v 15 "Maana tazama, nimekufanya kuwa mdogo kulinganisha na mataifa mengine, yenye kudharauliwa na watu.
\s5
\v 16 Na kwa hofu yenu, kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wakaaji wa maeneo ya mwinuko, ninyi mliomiliki vilele vya vilima ili mfanye viota vyenu kama tai. Nitawashusha kutoka huko - asema Yahwe.
\s5
\v 17 Edomu atakuwa kitisho kwa kila aipitaye. Kila mtu atatetemeka na kutoa sauti kwa sababu ya maafa yake.
\v 18 Kama maangamizi ya Sodoma na Gomora na jirani zake," asema Yahwe, "hakuna atakayeishi pale; hakuna mtu atakayekaa huko.
\s5
\v 19 Tazama, nitapanda kama simba kutoka katika misitu ya Yordani hata eneo la malisho mabichi. Maana nitaharakisha kumfanya Edomu kumkimbia, nami nitamweka mwingine atakayekuwa amechaguliwa kwa usimamizi huo. Maana ni nani aliyekama mimi, ni nani atakayeniagiza kuja? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
\s5
\v 20 Hivyo sikiliza mipango ambayo Yahwe ameamua dhidi ya Edom, mipango aliyoifanya kinyume cha wakaao Temani. Bila shaka wataondolewa, hata kundi dogo kuliko yote. Nchi yao yenye malisho yao mabichi itageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
\s5
\v 21 Kwa kishindo cha kuanguka kwao nchi hutikisika. Sauti ya milio ya kukata tamaa inasikika katika Bahari ya Shamu.
\v 22 Tazama, mtu fulani atapiga kama tai, na kushuka chini kwa kasi na kueneza mabawa yake juu ya Bozra. Kisha katika siku hiyo, mioyo ya askari wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika kuzaa."
\s5
\v 23 Juu ya Dameski: "Hamathi na Arpadi zitaaibika, maana wamesikia habari ya madhara. Wanayeyuka! Wamesumbuka kama bahari, isiyotulia.
\v 24 Dameski umekuwa dhaifu sana. Unageuka kukimbia; hofu imeushika, Maangaiko na maumivu yameupata, kama uchungu wa mwanamke ajifunguaye.
\v 25 Watu wake wanasema, "Umekuwaje mji maarufu, mji ambao nimeufurahia, kabla haujaachwa?
\s5
\v 26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika mitaa yake na askari wake wote watateketea siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi."
\v 27 "Maana nitawasha moto katika kuta za Dameski, nami nitazivunja ngome za Beni Hadadi."
\s5
\v 28 Juu ya Kedari na falme za Hazori, Yahwe amwambia hivi Nebukadneza (Basi Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa akienda kuyashambulia maeneo haya): "Inuka na uipige Kedari na kuwaharibu wale watu wa mashariki.
\v 29 Jeshi lake litachukua hema zao na makundi yao, nguzo za hema yao, na vitu vyao vyote. Watachukua ngamia wao kutoka kwa watu wa Kedari na kuwambia, 'Hofu ipo pande zote!"
\s5
\v 30 Kimbia, Tangatanga mbali! Kaa katika maandaki ardhini, mkaao Hazori - asema Yahwe - maana Nebukadneza mfalme wa Babeli amepanga mpango kinyume chenu. Kimbieni! Geukeni!
\v 31 Simama! lishambulie taifa lililokatika amani, waishio salama," asema Yahwe. Hawana malango wala nguzo ndani yao, na watu wake wanakaa wenyewe.
\s5
\v 32 Maana farasi wao watakuwa mateka, na wingi wa mali zao utakuwa mateka wa vita. Kisha nitawatawanya katika kila upepo wanaonyoa pembe za nywele zao, nami nitaleta madhara juu yao kutoka kila upande - hili ni tamko ya Yahwe.
\v 33 Hazori utakuwa makao ya mbwea, nchi isiyofaa daima. Hakuna atakayeishi huko; hakuna mwanadamu atakayekaa huko."
\s5
\v 34 Hili ni neno la Yahwe lililomwijia Yeremia nabii kuhusu Elamu. Ilikuwa wakati wa mwanzo wa kutawala kwake Sedekia mfalme wa Yuda, naye akasema,
\v 35 "Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, ninakaribia kumvunja mpiga upinde wa Elamu, sehemu kuu ya nguvu zao.
\v 36 Maana nitaleta pepo nne kutoka katika pande nne za mbingu, nami nitawatawanya watu wa Elamu katika pepo hizo zote. Hakuta kuwa na taifa ambalo kwalo waliotawanywa kutoka Elamu hawatakwenda.
\s5
\v 37 Hivyo nitawavunjavunja Elamu mbele ya adui zao na mbele ya watafutao uhai wao. Maana nitaleta maangamizo dhidi yao, hasira ya gadhabu yangu - hili ni tamko la Yahwe - nami nitapeleka upanga nyuma yao hata nitakapowafuta wote.
\v 38 Kisha nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu na kumwangamiza mfalme na viongozi wao kutoka huko - asema Yahwe -
\v 39 na itakuwa siku zijazo kwamba nitarejesha mema ya Elamu - asema Yahwe."
\s5
\c 50
\p
\v 1 Hili ni neno alilolisema Yahwe juu ya Babeli, nchi ya Wakalidayo, kwa mkono wa Yeremia nabii,
\v 2 "Wajulishe mataifa ili wasikie. Toa ishara ili wasikie. Usiiache. Sema, 'Babeli imetwaliwa. Beli ameaibika. Merodaki amefadhaika. Sanamu zake zimeaibishwa; vinyago vyake vimefadhaika
\s5
\v 3 Taifa kutoka kaskazini litainuka kinyume chake, ili kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja, awe mtu au mnyama, atakayeishi ndani yake. Wataondoka.
\v 4 Katika siku hizo na wakati huo - hili ni tamko ya Yahwe - watu wa Israeli na watu wa Yuda watakusanyika ili kwenda kwa kulia na kumtafuta Yahwe Mungu wao.
\v 5 Watauliza njia ya kwenda Sayuni nao watakwenda huko, wakisema, tutakwenda wenyewe ili kuungana na Yahwe katika agano la milele lisilosahaulikal
\s5
\v 6 Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea. Wachungaji wao wamewapoteza milimani; wamewageuza kutoka mlima hata mlima. Walikwenda, wakasahau mahali walipokuwa wanaishi.
\v 7 Kila awaendeaye anawararua. Washitaki wao walisema, 'Hatuna hatia, kwa sababu walimtenda dhambi Yahwe, nyumbani kwao halisi - Yahwe, tumaini la mababu zao.'
\s5
\v 8 Tokeni kati ya Babeli; tokeni katika nchi ya Wakalidayo; iweni kama wafanyavyo mabeberu mbele ya kundi lote.
\v 9 Maana tazama, ninaelekea kupeleka na kuinua kinyume cha Babeli kundi la mataifa makubwa kutoka kaskazini. Yatajipanga yenyewe kinyume chake. Kutoka hapo Babeli utatekwa. Mishale yao ni kama shujaa mzoefu asiyerudi mikono tupu.
\v 10 Ukaldayo itakuwa mateka. Wate waitekao wataridhika - asema Yahwe.
\s5
\v 11 Mnafurahi, mnasherehekea kuteka urithi wangu; mnarukaruka kama ndama anayekanyaga katika malisho yake; mnalia kama farasi mwenye nguvu.
\v 12 Hivyo mama yenu ataaibika sana; aliyewazaa atafadhaika. Tazama, atakuwa wa mwisho katika mataifa, nyika, nchi kame, na jangwa.
\v 13 Kwa sababu ya hasira ya Yahwe, Babeli haitakaliwa, lakini itakuwa ukiwa mtupu. Kila apitaye kando ataogopa kwa sababu ya Babeli na atatoa sauti kwa sababu ya majeraha yake.
\s5
\v 14 Jipangeni wenyewe kumzunguka Babeli kinyume chake. Kila apindaye upinde na ampige. Msizuie mshale wenu wowote, maana amemtenda dhambi Yahwe.
\v 15 Pigeni kelele za ushindi kinyume chake ninyi nyote mmzungukao. Amesalimu mamlaka yake; minara yake imeanguka. Kuta zake zimebomolewa, maana hiki ni kisasi cha Yahwe. Jilipizeni kisasi juu yake! Mtendeeni kama alivyoyatenda mataifa mengine.
\s5
\v 16 Waaribuni wote mkulima apandaye mbegu naye atumiaye mundu wakati wa mavuno katika Babeli. Haya kila mtu na arudi kwa watu wake kutoka upanga wa mtesaji; na wakimbilie katika nchi yao wenyewe.
\s5
\v 17 Israeli ni kondoo aliyetawanywa na kupelekwa na simba mbali. Kwanza mfalme wa Ashuru alimrarua; kisha baadaye, Nebukadneza mfalme wa Babeli akavunja mifupa yake.
\v 18 Kwa hiyo Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
\s5
\v 19 Nitamrudisha Israeli katika nchi yake; atajilisha katika Karmeli na Bashani. Kisha atajishibisha katika nchi ya kilima ya Efraimu na Gileadi.
\v 20 Siku hizo na wakati huo, asema Yahwe, uovu utatafutwa katika Israeli, lakini hautaonekana. Nitauliza kuhusu dhambi za Yuda, lakini hazitaonekana, maana nitawasamehe mabaki niliowaacha."
\s5
\v 21 Inuka dhidi ya nchi ya Merathaimu, kinyume chake nao waishio Pekodi. Wapigeni kwa makali ya upanga na mwatenge kwa ajili ya maangamizo - asema Yahwe - fanyeni kila ninachowaamru.
\v 22 Sauti ya vita na maangamizi ya kustaajabisha yamo katika nchi.
\s5
\v 23 Jinsi gani nyundo ya mataifa yote imekatiliwa mbali na kuharibiwa. Jinsi Babeli amekuwa kitu cha kushangaza kati ya mataifa.
\v 24 Nimetega mtego dhidi yako. Umenaswa, Babeli, nawe haukutambua! Ulionekana na kukamatwa, tangu uliponidhihaki, Yahwe.
\s5
\v 25 Yahwe amefungua ghala lake la silaha na anachukua silaha kwa ajili ya kutekekeleza hasira yake. Kuna kazi kwa ajili ya Yahwe wa majeshi katika nchi ya Wakaldayo.
\v 26 Mshambulie kutokea mbali. Fungua maghala yake ya chakula na kumrundika kama marundo ya nafaka. Mtenge mbali na maangamizi. Usimbakizie masalia.
\s5
\v 27 Ua madume wake wote wa ng'ombe. Washushe sehemu ya machinjio. Ole wao, maana siku yao imefika - wakati wa kuadhibiwa kwao.
\v 28 Kuna sauti ya wale wanaokimbia, walionusurika, katika nchi ya Babeli. Hawa watatoa taarifa ya kisasi cha Yahwe Mungu wetu kwa Sayuni, kisasi kwa hekalu lake."
\s5
\v 29 Ita wapiga pinde dhidi ya Babeli - wale wote wapindao pinde zao. Piga kambi kinyume chake, na msimwache yeyote kutoroka. Mlipeni kwa kile alichofanya. Mfanyieni kwa kipimo alichotumia. Maana amemdharau Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
\v 30 Hivyo vijana wake wataanguka katika viwanja vya mji, na wapiganaji wake wote wataangamizwa siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe."
\s5
\v 31 Tazama, mimi ni kunyume chako, mwenye majivuno - hili ni tamko la Bwana Yahwe wa majeshi - maana siku yako imefika, mwenye kiburi, wakati nitakapokuadhibu.
\v 32 Hivyo wenye kiburi watajikwaa na kuanguka. Hakuna atakaye wainua. Nitawasha moto katika miji yao; utateketeza kila kitu kati yake.
\s5
\v 33 Yahwe wa majeshi asema hivi: watu wa Israeli wamenyanyaswa, pamoja na watu wa Yuda. Wate waliowateka bado wanawashikilia; wanakataa kuwaacha waondoke.
\v 34 Yeye awaokoaye ni mwenye nguvu. Yahwe wa majeshi ni jina lake. Kwa hakika atalitetea shitaka lao, ili kuleta pumziko katika nchi, na kuwapiga wakaao Babeli.
\s5
\v 35 Upanga u juu ya Wakalidayo - asema Yahwe - na juu ya wakaao Babeli, viongozi wake, na wenye hekima wake.
\v 36 Upanga unakuja juu ya waganga, ili wajione kuwa wajinga. Upanga utakuwa juu ya askari wake, hivyo watajaa hofu.
\v 37 Upanga utakuwa juu ya farasi wake, vibandawazi vyao na na watu wote waliomo Babeli, hivyo watakuwa kama wanawake. Upanga utakuwa juu ya ghala zake, nazo zitatekwa.
\s5
\v 38 Ukame unakuja juu ya maji yake, hivyo yatakauka. Maana ni nchi ya miungu wasiofaa, na wanafanya kama watu waliofanywa punguani kwa miungu yao isiyosaidia.
\v 39 Hivyo wanyama wa jangwani wakaishi na mbwea wataishi huko, na watoto wa mbuni wataishi ndani yake. Kwa muda wote, hatakaliwa tena. Kutoka kizazi hata kizazi, hatakaliwa tena na watu.
\v 40 Kama vile Mungu alivyoziangamiza Sodoma na Gomora na majirani zake - asema Yahwe - hakuna atakayeishi huko; hakuna mtu atakayekaa ndani yake."
\s5
\v 41 "Tazama, watu wanakuja kutoka kaskazini, maana taifa kubwa na wafalme wengi wamemtikisa kutokea mbali.
\v 42 Watachukua pinde na mishale. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama mngurumo wa bahari, na wamepanda farasi katika mpangilio kama watu wapiganao, dhidi yako, bindi Babeli.
\v 43 Mfalme wa Babeli amesikia habari yao na mikono yake imelegea kwa huzuni. Mashaka yamemshika kama mwanamke katika utungu.
\s5
\v 44 Tazama! Anakwenda juu kama simba atokaye katika miinuko ya Yordani kuelekea katika eneo la malisho ya uvumilivu. Maana kwa haraka nitawafanya wakimbie kutoka humo, nami nitamweka mtu aliyechaguliwa kwa uangalizi wake. Maana ni nani aliye kama mimi, na ni nani atakayeniagiza? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
\s5
\v 45 Sikilizeni mipango ambayo Yahwe ameamua juu ya Babeli, mipango aliyonayo dhidi ya nchi ya Wakaldayo. Kwa hakika wataondolewa, hata kundi dogo zaidi. Eneo lao la malisho litageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
\v 46 Kwa sauti ya kuangushwa kwa Babeli nchi inatikisika, na sauti ya mateso yao inasikiwa kati ya mataifa."
\s5
\c 51
\p
\v 1 Yahwe asema hivi: Tazama, ninakwenda kuleta upepo wa maangamizi dhidi ya Babeli na dhidi yao waishio ndani ya Leb Kamei.
\v 2 Nitawatuma Babeli wageni. Watamtawanya na wataifanya ukiwa nchi yake, maana watakuja kinyume chake kutoka pote siku ya madhara.
\s5
\v 3 Msiwaache wapiga mishale wakapinda pinde zao; msiwache wakavaa silaha zao. Msiwahifadhi vijana wake wa kiume; litengeni jeshi lake lote kwa maangamizi.
\v 4 Maana watu waliojeruhiwa wataanguka katika nchi ya Wakaldayo; waliouawa wataanguka katika mitaa yake.
\s5
\v 5 Maana Israeli na Yuda hawajaachwa na Mungu wao, na Yahwe wa majeshi, japokuwa nchi yao imejaa na maasi yaliyotendwa kinyume cha Mmoja aliye Mtakatifu wa Israeli.
\v 6 Kimbieni kutoka Babeli; kila mtu na ajiokoe mwenyewe. Msiangamie katika maasi yake. Maana ni wakati wa kisasi cha Yahwe. Atamlipa kwa yote.
\s5
\v 7 Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Yahwe kilichoinywesha nchi yote; mataifa walikunywa mvinyo wake wakawa wendawazimu.
\v 8 Babeli utaanguka ghafla na kuangamizwa. Mwombolezeeni! mpeni dawa kwa maumivu yake; pengine aweza kupona.
\s5
\v 9 Tulinuia kumponya Babeli, lakini hajaponywa, haya na tumwache twende, katika nchi yetu. Maana hatia yake imefika juu mbinguni; imerundikwa kufika mawinguni.
\v 10 Yahwe ametamka kwamba sisi hatuna hatia. Njooni, teseme katika Sayuni matendo ya Yahwe Mungu wetu.'
\s5
\v 11 Noweni mishale na kuchukua ngao. Yahwe anaiimiza roho ya mfalme wa Umedi katika mpango wa kuiangamiza Babeli. Hii ni kwa kisasi cha Yahwe, kisasi kwa maangamizi ya hekalu lake.
\v 12 Inueni bendela juu ya kuta za Babeli; wekeni walinzi. Wekeni waangalizi; wekeni askari waviziao ili kumkamata kila akimbiliaye mjini, maana Yahwe atafanya kile alichokipanga. Atafanya alichokisema juu ya wakaao Babeli.
\s5
\v 13 Enyi mwishio kati ya chemchemi nyingi za maji, ninyi mlio na wingi wa hazina, mwisho wenu umefika. upindo wa maisha yenu umepunguzwa.
\v 14 Yahwe wa majeshi ameapa kwa maisha yake, 'nitakujaza na adui zako, kama pigo la nzige; watainua kelele za vita juu yako.'
\s5
\v 15 Ameifanya dunia kwa nguvu zake; akaiweka dunia mahali kwa hekima yake. Kwa ufahamu wake alizitanda mbingu.
\v 16 Anapovuma, kunakuwa na mvumo wa maji mbinguni, maana huleta umande kutoka miisho ya dunia. Hufanya radi kwa ajili ya mvua na kuituma na kuutuma upepo kutoka katika maghala ya nyumba zake.
\s5
\v 17 Kila mtu anakuwa kama mnyama asiye na akili; kila mfua chuma ameaibishwa na sanamu zake. Maana mwonekano wake unadanganya; maana hakuna uzima ndani yake.
\v 18 Hazifai, kazi ya wafanya mzaa; wataangamizwa wakati wa kuadhibiwa kwao.
\v 19 Lakini Mungu, urithi wa Yakobo, siyo kama hawa, maana yeye ndiye afanyaye vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; Yahwe wa majeshi ni jina lake.
\s5
\v 20 Wewe ni nyundo ya vita yao, silaha ya vita yangu. Kwa wewe nitawaponda mataifa na kuharibu falme.
\v 21 Kwa wewe nitaponda farasi na wawapandao; kwa wewe nitaponda vibandawazi na madereva wake.
\s5
\v 22 Kwa wewe nitawafutilia mbali mme na mke; kwa wewe nitafutilia mbali mzee na kijana. Kwa wewe nitafutilia mbali kijana wa kiume na wasichana bikra.
\v 23 Kwa wewe nitafutilia mbali wachungaji na makundi yao; kwa wewe nitawafutilia mbali wakulima na jozi zao za kulimia. kwa wewe nitawafutilia mbali watawala na maafsa.
\s5
\v 24 Maana mbele yako nitamlipa Babeli na wote wakaao Ukaldayo kwa maovu yote waliyoyafanya huko Sayuni - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 25 Tazama, mimi ni kinyume chako, ewe mlima, wewe unayewaharibu watu wengine - hili ni tamko la Yahwe - kuiharibu dunia yote. Nitakupiga na mikono yangu na kuvingirisha chini kutoka ukingo wa kilima. Kisha nitakufanya mlima ulioteketezwa kabisa kwa moto.
\v 26 Hivyo hawatachukua kwako jiwe lolote ili kujengea pembe ya nyumba au msingi; kwani utakuwa ukiwa wa milele - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 27 Inua bendela ya vita juu ya nchi. Piga tarumbeta katika mataifa. Yaite mataifa yamshambuliye: Ararati, Mini na Ashkenazi. Teua majemedari wa kumshambulia; leta farasi kama nzige warukao.
\v 28 Waandae mataifa kumshambulia: wafalme wa Umedi na magavana wao, maafsa wake wote na nchi yake yete.
\s5
\v 29 Maana nchi itatikisika na kudhoofika, kwa kuwa mipango ya Yahwe inaendelea juu ya Babeli, kuifanya nchi ya Babeli kuwa nchi isiyofaa mahali pasipo na mtu.
\s5
\v 30 Maaskari wameacha kupigana huko Babeli; wamekaa katika ngome zao. Nguvu zao zimeshindwa; wamekuwa wanawake - nyumba zake zipo motoni, makomeo ya malango yake yamevunjika.
\v 31 Mjumbe hukimbia ili amwambie mjumbe mwingine, na mtoa habari humwambia mtoa habari mwingine ili amwambie mfalme wa Babeli kwamba mji wake umetwaliwa kutoka mwisho hata mwisho.
\v 32 Hivyo vivuko katika mito vimekamatwa; adui anaunguza mafunjo ya bwawa, na wapiganaji wa Babeli wamechanganyikiwa.
\s5
\v 33 Maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria. Ni muda wa kumkanyaga. Ni kitambo kidogo wakati wa mavuno utakuja juu yake.
\s5
\v 34 Yerusalemu husema, 'Nebukadneza mfalme wa Babeli amenirarua. Amenikausha na amenifanya kuwa mtungi mtupu. Amenimeza kama joka. Alijishibisha kwa chakula changu chema. Amenitupa mbali.'
\v 35 Wenyeji wa Sayuni watasema, 'Gasia nilizofanyiwa na mwili wangu na ziwe kwa Babeli.' Yerusalem atasema, Damu yangu na iwe juu ya wakaao Ukaldayo.'
\s5
\v 36 Kwa hiyo Yahwe asema hivi: Tazama, nikotayari kulitetea shitaka lako na kuleta kisasi kwa ajili yako. Maana nitayakausha maji ya Babeli na kufanya vyanzo vyake kukauka.
\v 37 Babeli utakuwa rundo la magofu, pango la mbwea, sehemu itishayo, kitu cha kutoa sauti ya nyoka, pasipo na watu.
\s5
\v 38 Wababeli wataunguruma kwa pamoja kama wanasimba. Watanguruma kama watoto wa simba.
\v 39 wanapopashwa moto kwa hasira, nitawafanyia sherehe; nitawalewesha hata wafurahi, na kisha kulala usingizi usio na mwisho hata wasiamke - hili ni tamko la Yahwe -
\v 40 nitawapeleka chini kama wanakondoo kwa mchinjaji, kama kondoo dume pamoja na mbuzi majike.
\s5
\v 41 Jinsi Babeli ulivyotekwa! Hivyo fahari ya dunia yote imekamatwa. Jinsi Babeli ulivyofanyika sehemu yenye magofu kati ya mataifa.
\v 42 Bahari imekuja juu ya Babeli! Amefunikwa na mawimbi yavumayo.
\s5
\v 43 Miji yake imekuwa ukiwa, sehemu kame na nyika, nchi isiyo na watu, na hakuna mtu apitaye hapo.
\v 44 Hivyo nitamwadhibu Beli huko Babeli; nitakitoa kinywani mwake alichokimeza, na mataifa hawatamminikia tena pamoja na wazao wao. Kuta za Babeli zitaanguka.
\s5
\v 45 Tokeni kati yake, enyi watu wangu. Kila mmoja wenu aokowe maisha yake kutoka katika hasira ya gadhabu yangu.
\v 46 Msiache mioyo yenu ikaogopa au kuhofu habari iliyosikiwa nchini, maana habari itakuja siku moja. Baada yake mwaka unaofuata kutakuwa na habari, na ghasia zitakuwa nchini. Mtawala atakuwa kinyume cha mtawala.
\s5
\v 47 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja nitakapoadhibu sanamu za Babeli. Nchi yake yote itaaibika, na wote waliochinjwa wataanguka ndani yake.
\v 48 Kisha mbingu na nchi, na vyote vilivyomo ndani yake vitafurahi juu ya Babeli. Maana mwalibifu atamwijia kutoka kaskazini - hili ni tamko la Yahwe.
\v 49 "Kama Babeli alivyowafanya waliouawa wa Israeli kuanguka, hivyo waliouawa katika nchi yake wataanguka katika Babeli.
\s5
\v 50 Ondokeni!, manusura wa vita, Msikawiye. Mkumbukeni Yahwe tokea mbali; Yerusalemu na ikumbukwe.
\v 51 Tumeaibika, maana tumesikia matusi; dhihaka imefunika nyuso zetu, maana wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya Yahwe.
\s5
\v 52 Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja - hivi ndivyo asemavyo Yahwe - nitakapoziadhibu sanamu zake, na waliojeruhiwa watanung'unika kwa maumivu katika nchi yake yote.
\v 53 Maana hata kama Babeli angepanda mbinguni au kujenga ngome zake ndefu, aharibuye kutoka kwangu angemwendea - hili ni tamko la Yahwe.
\s5
\v 54 Kelele ya maangamizi ilitoka Babeli, anguko kubwa kutoka nchi ya Wakaldayo.
\v 55 Maana Yahwe anaiharibu Babeli. Anaifanya kelele ya sauti yake kuisha. Adui zake wanaunguruma kama mawimbi ya maji mengi; kelele yao imekuwa na nguvu.
\v 56 Maana aharibuye amekuja kinyume chake - kinyume cha Babeli! - na shujaa wake wametekwa. Pinde zao zimevunjwa, maana Yahwe ni Mungu wa kisasi; atatekeleza kisasi hiki.
\s5
\v 57 Maana nitawafanya wana wafalme wake, wenye hekima wake, maofsa wake, na maaskari wake kulewa, nao watalala usingizi kwa usingizi usioisha na bila kuamka - hili ni tamko la mfalme: Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
\v 58 Yahwe wa majeshi asema hivi: Ukuta mnene wa Babeli utaangushwa kabisa, na malango marefu yataunguzwa. Kisha watu wanaokuja kumsaidia watafanya kazi isiyofaa; kila mataifa wanachojaribu kikifanya kwa ajili yake kitateketezwa kwa moto."
\s5
\v 59 Hili ndilo neno Yeremia nabii alilomwamru Seraya mwana wa Neria mwana wa Makseya alipokwenda na Sedekia mfalme wa Yuda huko Babeli katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. Basi Seraya alikuwa afsa mwandamizi.
\v 60 Maana Yeremia alikuwa ameandika katika gombo kuhusu madhara yote yeliyokuwa yakienda kutendeka juu ya Babeli - maneno haya yote yaliyokuwa yameandikwa juu ya Babeli
\s5
\v 61 Yeremia akamwambia Seraya, "Unapokwenda Babeli, hakikisha unayasoma maneno haya yote.
\v 62 Nawe utasema, 'Yahwe, wewe! - wewe mwenyewe umesema kwamba utapaharibu mahali hapa. Hapatakuwa na wa kukaa, kwamba ni watu au wanyama. Patakuwa nchi isiyofaa daima.'
\s5
\v 63 Kisha mtakapomaliza kusoma gombo hili, funga jiwe kubwa juu yake na ulitupe katikati ya Frati.
\v 64 Sema, 'Babeli utazama kama hivi. Hautainuka kwa sababu ya mabaya ninayoyapeleka juu yake, nao wataanguka." Maneno ya Yeremia yanaishia hapa.
\s5
\c 52
\p
\v 1 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Jina la mamaye lilikuwa Hamutali; alikuwa binti Yeremia wa Libna.
\v 2 Akafanya maovu machoni pa Yahwe; akafanya kila alichokifanya Yehoyakimu.
\v 3 Kwa hasira ya Yahwe, matukio haya yote yalitukia Yerusalemu na Yuda, hata alipowatoa mbele yake mwenyewe. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
\s5
\v 4 Ikawa katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedeki, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alikuja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem. Wakapiga kambi kuukabili, nao wakajenga ukuta wa kuusuria kuuzunguka.
\v 5 Hivyo mji ukausuriwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa mfalme Sedekia.
\s5
\v 6 Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwaka huo, njaa ikawa kali sana mjini hata hakukuwa na chakula kwa watu wa nchi.
\v 7 Kisha mji ukatobolewa, na wapiganaji wote wakakimbia nje ya mji wakati wa usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili, kwa bustani ya mfalme, japokuwa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Hivyo wakaenda kwa njia ya Araba.
\v 8 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata Sedekia katika tambarare za bonde la Mto Yordani karibu na Yeriko. Jeshi lote lilikuwa limetawanyika mbali naye.
\s5
\v 9 Wakamkamata mfalme na kumleta hadi kwa mfalme wa Babeli huko Ribla katika nchi ya Hamathi, alipotoa hukumu juu yake.
\v 10 Mfalme wa Babeli akawachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na huko Ribla akawachinja viongozi wote wa Yuda.
\v 11 Kisha akayaondoa macho ya Sedekia, akamfunga katika vifungo vya shaba, na kumleta Babeli. Mfalme wa Babeli akamweka kifungoni hata siku ya kufa kwake.
\s5
\v 12 Basi mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani akaja Yerusalemu. Alikuwa jemedari wa walinzi wa mfalme na mtumishi wa mfalme wa Babeli.
\v 13 Akaiteketeza nyumba ya Yahwe, kasiri, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo mhimu mjini alilichoma.
\v 14 Kama kwa kuta za kuuzunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli lililokuwa pamoja na jemedari wa mlinzi wakaviaribu.
\s5
\v 15 Kama kwa watu maskini sana, watu waliosalia walioachwa katika mji, waliokuwa wamemwendea mfalme wa Babeli, na baadhi ya watu wenye ujuzi - Nebuzaradan, jemedari wa askari walinzi, akawachukua baadhi yao uhamishoni.
\v 16 Lakini Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawaacha baadhi ya maskini sana wa nchi kuitunza mizabibu na mashamba.
\s5
\v 17 Lakini kwa nguzo za shaba lilizokuwa katika nyumba ya Yahwe, mishikio na bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakaivunja vipande wakaondoka navyo kurudi Babeli.
\v 18 Vyungu, makoleo, kinara cha taa, mabakuri, na vitu vyote vya shaba ambavyo makuhani walikuwa wakivitumia hekaluni - Wakaldayo wakavichukua vyote.
\v 19 Makalai na chetezo cha uvumba, mabakuri, vyungu, kinara cha taa, vikaango, makalai zilizotengenezwa kwa dhahabu, na zilizotengenezwa kwa dhahabu - kapteni wa mlinzi wa mfalme akazichukua pia.
\s5
\v 20 Nguzo mbili, bahari, na ng'ombe kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, vitu Selemani alivyokuwa amevifanya kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vikiwa na shaba nyingi sana isiyoweza kupimwa.
\v 21 Nguzo zilikuwa na urefu wa dhiraha kumi na nane kila moja, na mstari kuzunguka kila moja wenye urefu wa dhiraha kumi na mbili. Kila moja ilikuwa na unene wa vidole vinne na tundu.
\s5
\v 22 Kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Kichwa kilikuwa dhiraha tano urefu wake, kazi ya waya zinazokingamana na makomamanga kukizunguka. Chote kilitengenezwa kwa shaba. Na nguzo nyingine ilikuwa na makomamanga yake vilikuwa kama ya kwanza.
\v 23 Hivyo kulikuwa na makomamanga tisini na sita ubavuni mwa kila kichwa, na makomamanga mia moja juu ya nyaya zilizokingamana kukizunguka.
\s5
\v 24 Jemedari wa mlinzi akamchukua Seraya mfungwa, kuhani mkuu, pamoja na Sefania, kuhani wa pili, na wale mabawaba watatu.
\v 25 Kutoka mjini akamchukua mfungwa afsa aliyekuwa juu ya askari, na watu saba wa wale waliomshauri mfalme, waliokuwa wamesalia mjini. Akamchukua mfungwa afsa wa jeshi la mfalme aliyekuwa na wajibu wa kuwaingiza watu katika jeshi, pamoja na watu mashuhuri sitini kutoka katika nchi waliokuwamo mjini.
\s5
\v 26 Kisha Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawachukuwa na kuwaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.
\v 27 Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaondoka katika nchi yake na kwenda uhamishoni.
\s5
\v 28 Hawa walikuwa watu Nebukadneza aliwaamisha: katika mwaka wa saba, Wayudea 3, 023.
\v 29 Katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadneza alichukuwa 832 kutoka Yerusalemu.
\v 30 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, jemedari wa walinzi wa mfalme, aliwahamisha Wayudea 745. Jumla ya watu walioamishwa walikuwa 4, 600.
\s5
\v 31 Ikawa baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa kufungwa kwake Yohoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evili Merodaki, mfalme wa Babeli akamfungua Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka kifungoni. Ilikuwa mwaka ambao Evili Merodaki alianza kutawala.
\s5
\v 32 Akaongea naye kwa upole na akampa kiti cha heshima kuliko cha wafalme wengine aliokuwa pamoja nao huko Babeli.
\v 33 Evili Merodaki akaondoa mavazi ya gerezani ya Yehoyakini, na Yehoyakini akala chakula cha daima katika meza ya mfalme siku zote zilizosalia za maisha yake.
\v 34 Na alipewa posho ya chakula cha kila siku kwa maisha yake yote yaliyosalia mpaka siku ya kufa kwake.

305
25-LAM.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,305 @@
\id LAM
\ide UTF-8
\h Maombolezo
\toc1 Maombolezo
\toc2 Maombolezo
\toc3 lam
\mt Maombolezo
\s5
\c 1
\p
\v 1 Mji ambao mwanzo ulikuwa na watu wengi sasa umekaa peke yake. Amekuwa kama mjane, japo alikuwa taifa kubwa. Alikuwa mtoto wa mfalme miongoni mwa mataifa, lakini sasa amelazimishwa utumwani.
\v 2 Analia na kuomboleza usiku, na machozi yake yanafunika mashavu yake. Hamna ata mpenzi wake anaye mliwaza. Marafiki wake wote wamemsaliti. wamekuwa maadui wake.
\s5
\v 3 Baada ya umaskini na mateso, Yuda ameenda matekani. Anaishi miongoni mwa mataifa na hapati pumziko lolote. Wanao wakimbiza wamewapata katika upweke wake.
\s5
\v 4 Barabara za Sayuni zinaomboleza kwasababu hakuna anaye kuja kwenye sherehe iliyo andaliwa. Malango yake yote ni ukiwa. Makuhani wake wote wana sononeka. Mabikra wake wana uzuni na yeye mwenyewe yupo katika ugumu.
\v 5 Maadui wake wamekuwa bwana zake; maadui wake wana fanikiwa. Yahweh amemuadhibu kwa dhambi zake nyingi. Watoto wake wadogo wanaenda matekani kwa maadui zake.
\s5
\v 6 Uzuri umemwacha binti wa Sayuni. Watoto wa mfalme wamekuwa kama ayala ambaye haoni malisho, na wanaenda bila uwezo kwa wanao wakimbiza.
\s5
\v 7 Katika siku za mateso yake na kutokuwa na nyumba, Yerusalemu itakumbuka hazina zake za dhamani alizo kuwa nazo awali. Wakati watu wake walipo angukia mikononi mwa adui, hakuna aliye msaidia. Maadui waliwaona na kucheka maangamizo yake.
\s5
\v 8 Yerusalemu ili tenda dhambi sana, hivyo basi, amedhalillika kama kitu kichafu. Wote walio mheshimu sasa wana mdharau kwa kuwa wameona uchi wake. Anasononeka na kujaribu kugeuka pembeni.
\v 9 Amekuwa mchafu chini ya sketi yake. Hakuwaza hatima yake. Anguko lake lilikuwa baya. Hakukuwa na wakumliwaza. Alilia, "Angalia mateso yangu, Yahweh, kwa kuwa adui amekuwa mkuu sana."
\s5
\v 10 Adui ameeka mkono wake kwenye hazina zetu za dhamani. Ameona mataifa yakiingia sehemu yake takatifu, japo uliamuru wasiingie katika sehemu yako ya kukusanyikia.
\s5
\v 11 Watu wote wana sononeka wanapo tafuta mkate. Wametoa hazina zao za dhamani kwa ajili ya chakula cha kurejesha uhai wao. Tazama, Yahweh, ni kumbuke mimi, kwa kuwa nimekuwa sina faida.
\v 12 Sio kitu kwako, wote mnao pita? Angalia na uone kama kuna mtu mwenye uzuni kama uzuni ninao teswa nao, tangu Yahweh amenitesa mimi katika siku ya hasira yake kali.
\s5
\v 13 Ni kutoka juu ndipo alipo tuma moto kwenye mifupa yangu na umenishinda. Ametanda nyavu kwa miguu yangu na kunigeuza. Amenifanya ukiwa na dhahifu.
\v 14 Nira ya makosa yangu imefungwa na mikono yake. Zimesokotwa na kuekwa shingoni mwangu. Amefanya uweza wangu kushindwa. Bwana amenikabidhi mikononi mwa, na siwezi kusimama.
\s5
\v 15 Bwana ametupa pembeni wanaume wangu hodari walio niokoa. Ameitisha kusanyiko dhidi yangu kuponda wanaume wangu imara. Bwana amewakanyaga binti bikra wa Yuda kwenye chombo cha kusagia mvinyo.
\s5
\v 16 Kwa vitu hivi ninalia. Macho yangu, maji yanashuka chini ya macho yangu tangu mfariji aliye paswa kurejesha maisha yangu yuko mbali na mimi. Watoto wangu wamekuwa ukiwa kwasababu adui yangu ameshinda.
\v 17 Sayuni ametandaza mikono yake; hakuna wakuwa mliwaza. Yahweh ameamuru hao karibu na Yakobo wawemaadui wake. Yerusalemu ni kitu kichafu kwao.
\s5
\v 18 Yahweh ni mwenye haki, kwa kuwa nimeasi dhidi ya amri zake. Sikia, ninyi watu, na muone uzuni wangu. Mabikra wangu na wanaume imara wameenda matekani.
\v 19 Niliita marafiki zangu, lakini walikuwa na hila kwangu. Makuhani wangu na wazee waliangamia kwenye mji, walipo kuwa wanatafuta chakula cha kurejesha uhai wao.
\s5
\v 20 Tazama, Yahweh, kwa kuwa nipo kwenye ugumu; tumbo langu lina nguruma, moyo wangu umetibuka ndani yangu, kwa kuwa nimekuwa muasi sana. Nje, upanga umemliza mama, ndani ya nyumba kuna mauti tu.
\s5
\v 21 Wamesikia sononeko langu, lakini hakuna wakuni liwaza. Maadui zangu wote wamesikia shida zangu na wamefurahi umenifanyia hivi. Umeleta siku uliyo ahidi; sasa acha wawe kama mimi.
\v 22 Acha uovu wote uje mbele zako. Shughulika nao kama ulivyo shughulika na mimi kwasababu ya makosa yangu yote. Masononeko yangu ni mengi na moyo umezimia.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Bwana amemfunika binti wa Sayuni chini ya wingu la hasira yake. Ametupa utukufu wa Israeli chini kutoka mbinguni hadi duniani. Hajakumba stuli yake ya miguu siku ya hasira yake.
\v 2 Bwana amemeza na hajawa na huruma kwa miji yote ya Yakobo. Siku za hasira zake ameangusha miji imara ya binti wa Yuda; kwa aibu ameshusha chini ufalme na watala wake.
\s5
\v 3 Kwa hasira kali amekata kila pembe ya Israeli. Ameurudisha mkono wake kutoka kwa adui. Amechoma Yakobo kama moto mkali unao teketeza kila kitu karibu yake.
\v 4 Kama adui amepindisha upinde wake kuelekea kwetu, na wakulia wake yupo tayari kushambulia. Amewachinja wote walio kuwa wanampendeza katika hema la binti wa Sayuni; Amemwaga gadhabu yake kama moto
\s5
\v 5 Bwana amekuwa kama adui. Amemeza Israeli. Amemeza majumba yake yote. Ameharibu ngome zake. Ameongeza kilio na maombolezo kati ya mabinti wa Yuda.
\v 6 Ameshambulia hema lake la kukutania kama kajumba cha bustani. Ameharibu sehemu ya kukusanyikia. Yahweh amesababisha kukusanyika na Sabato kusahaulika Sayuni, kwa kuwa amemdharau mfalme na kuhani katika ukali wa hasira yake.
\s5
\v 7 Bwana amekataa madhabahu yake na kukana sehemu yake takatifu. Ametoa kuta za majumba mikononi mwa adui. Wamepaza sauti nyumbani mwa Yahweh, kama siku ya sherehe.
\s5
\v 8 Yahweh aliamua kuharibu ukuta wa mji wa binti wa Sayuni. Amenyoosha kamba ya kipimo na hajauzuia mkono wake kutoharibu ukuta. Amefanya minara na ukuta kuomboleza; pamoja vilipotea.
\v 9 Malango yake yameanguka chini, ameharibu na kuvunja chuma za ukuta. Mfalme wake na watoto wa mfalme wapo miongoni mwa mataifa, sheria haipo tena na manabii wake hawapati maono kutoka kwa Yahweh.
\s5
\v 10 Wazee wa binti wa Sayuni wameketi chini na ukimya. Wamerusha vumbi kichwani mwao na kuvaa magunia. Mabikra wa Yerusalemu wameinamisha vichwa vyao chini.
\s5
\v 11 Macho yangu yamekaukiwa machozi yake; tumbo langu la nguruma; sehemu zangu za ndani zimemwagika chini kwasababu ya uharibifu wa binti wa watu wangu, watoto na wachanga wamezimia mitaani mwa mji.
\v 12 Wanasema kwa mama zao, "Mbegu ziko wapi na mvinyo?" kama wanavyo zimia kama mtu aliye jeruhiwa mitaani mwa mji, maisha yao yamemwaga kwenye kifua cha mama zao.
\s5
\v 13 Nini naeza kusema kwako, binti wa Yerusalemu? Naweza kufananisha na nini, ili ni kufariji, binti bikra wa Sayuni? Jera lako ni kubwa kama bahari. Nani anaweza kukuponya?
\v 14 Manabii wako wameona uongo na maono batili kwa ajili yako. Hawaja weka wazi dhambi zako kurejesha mali zako, lakini kwako wametoa matamko ya uongo na ya kupotosha.
\s5
\v 15 Wote wanao pita pembeni mwa barabara wana piga makofi kwako. Wanaguna na kutikisa vichwa vyao dhidi ya binti wa Yerusalemu na kusema, "Huu ndio mji walio uita 'Ukamilifu wa uzuri,' 'Furaha ya Dunia Yote'?"
\v 16 Maadui zako wote walifungua vinywa vyao na kukudhihaki. Walizomea na kusaga meno na kusema, "Tumemmeza yeye! Hii ni siku tulio subiri! Tumeishi kuweza kuiona!"
\s5
\v 17 Yahweh amefanya alivyo panga kufanya. Ametimiza neno lake. Amekupindua bila huruma, kwa kuwa amemruhusu adui kukusherehekea; amenyanyua pembe za maadui zako.
\s5
\v 18 Mioyo yao ikamlilia Bwana, kuta za binti wa Sayuni! Fanya machozi yako kutiririka chini kama mto usiku na mchana. Usijipatie hauweni, macho yako bila hauweni.
\v 19 Nyanyuka, lia usiku, mwanzo usiku wa manane! Mwaga moyo wako kama maji mbele za uso wa Bwana. Nyoosha juu mikono yako kwa ajili ya uzima wa watoto wako wanao zimia kwa njaa kwenye njia ya kila mtaa.
\s5
\v 20 Ona, Yahweh, na ukumbuke hao ulio watende haya. Wanawake wale tunda la uzazi wao, watoto walio wajali? Makuhani na manabii wa chinjwe sehemu takatifu ya Bwana?
\s5
\v 21 Wote wadogo kwa wakubwa wana keti kwenye udongo wa mitaa. Wanawake wangu wadogo na wanaume wangu wadogo wameanguaka kwa upanga; umewachinja pasipo kuwa hurumia.
\v 22 Umeitisha, kama ungewaita watu katika siku ya maakuli, hofu yangu kila sehemu, katika siku ya hasira ya Yahweh hakuna aliye toroka; hao niliyo wajali na kuwakuza, adui wangu amewaharibu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Mimi ni mwanaume nilyeona maangaiko chini ya gongo la hasira ya Yahweh.
\v 2 Amenifukuza na kunisababisha kutembea kwenye giza kuliko kwenye nuru.
\v 3 Hakika amenigeuzia mkono wake dhidi yangu tena na tena, siku yote.
\v 4 Amefanya mwili wangu na ngozi yangu kufifia; amevunja mifupa yangu.
\s5
\v 5 Amejenga vifusi vya udogo dhidi yangu, na kunizingira na uchungu na ugumu.
\v 6 Amefanya ni ishi sehemu za giza, kama hao walio kufa zamani.
\v 7 Amejenga ukuta kunizunguka na siwezi kutoroka. Amefanya minyororo yangu mizito
\v 8 na japo nina ita na kulilia msaada, anazima maombi yangu.
\s5
\v 9 Ameziba njia yangu kwa ukuta wa mawe ya kuchonga; amefanya njia yangu mbaya.
\v 10 Yeye ni kama dubu anasubiri kunishambulia, simba katika maficho;
\v 11 amegeuza pembeni njia zangu, amenifanya ukiwa.
\s5
\v 12 Amepindisha upinde wake na kunifanya mimi kama lengo la mshale wake.
\v 13 Ametoboa maini yangu kwa mishale ya mfuko wake.
\v 14 Nilikuwa kichekesho kwa watu wangu wote, kielelezo cha dhihaka yao siku nzima.
\v 15 Amenijaza kwa uchungu na kunilazimisha kunywa maji machungu.
\s5
\v 16 Alivunja meno yangu na kokoto; amenisukuma chini kwenye fumbi.
\v 17 Nafsi yangu imenyimwa amani; nimesahau furaha ni nini.
\v 18 Hivyo na sema, "Ustahimilivu wangu umeangamia na pia tumaini langu kwa Yahweh."
\s5
\v 19 Kumbuka mateso yangu na kuangaika kwangu, maji machungu na uchungu.
\v 20 Ninaendelea kukumbuka na nimeinama ndani yangu.
\v 21 Lakini ni vuta hili akilini mwangu na hivyo nina matumaini:
\s5
\v 22 Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi,
\v 23 ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa.
\v 24 "Yahweh ni urithi wangu," Nilisema, hivyo nitamtumainia.
\s5
\v 25 Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta.
\v 26 Ni vizuri kusubiri taratibu kwa uwokovu wa Yahweh.
\v 27 Ni vizuri kwa mtu kubeba nira katika ujana.
\v 28 Acha aketi peke yake katika utulivu, inapo kuwa imewekwa juu yake.
\v 29 Acha aeke mdomo wake kwenye vumbi - kunaweza bado kuwa na matumaini.
\s5
\v 30 Acha atoa shavu lake kwa yeye anaye mpiga, na ajazwe tele kwa aibu.
\v 31 Kwa kuwa Bwana hatatukataa milele,
\v 32 lakini japo anatia uzuni, ata kuwa na huruma kwa kadiri ya mwingi wa upendo wake dhabiti.
\v 33 Kwa kuwa haadhibu kutoka moyoni mwake au kutesa watoto wa mwanadamu.
\s5
\v 34 Kukanyaga chini ya mguu wafungwa wote wa dunia,
\v 35 kumnyima haki mtu mbele ya uwepo wa Aliye Juu,
\v 36 mkunyima haki mtu - Bwana hataidhinisha vitu kama hivyo!
\s5
\v 37 Ni nani aliye zungumza na ikatimia, kama sio Bwana kutamka?
\v 38 Sio kutoka mdomoni mwa Aliye Juu majanga na mazuri yanakuja?
\v 39 Mtu aliye hai anawezaje kulalamika? Mtu anawezaje kulalamika kwa adhabu ya dhambi zake?
\s5
\v 40 Natujichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Yahweh.
\v 41 Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu kwa Yahweh mbinguni:
\v 42 "Tumekosea na kuasi, na haujasamehe.
\v 43 Umejifunika na hasira na kutukimbiza, umeua na haujanusuru.
\s5
\v 44 Umejifunika na wingu ili kwamba kusiwe na ombi linaloweza kupita.
\v 45 Umetufanya kama uchafu na taka miongoni mwa mataifa.
\v 46 Maadui wetu wote wametulaani,
\v 47 wasiwasi na shimo limetujia, maafa na uharibifu.
\s5
\v 48 Macho yangu yanatiririka na miferiji ya machozi kwasababu ya watu wangu.
\v 49 Macho yangu yatatoa machozi pasipo kikomo; pasipo hauweni,
\v 50 mpaka atakapo tazama chini na Yahweh ataona kutoka mbinguni.
\s5
\v 51 Macho yangu yana ni sababishia uzuni kwasababu ya mabinti wa mji wangu.
\v 52 Nimewindwa kama ndege hao walio kuwa maadui zangu; wameniwinda pasipo sababu.
\v 53 Wamenitupa kwenye shimo na wakanitupia jiwe,
\v 54 na maji yaka mwagika juu ya kichwa changu. Nilisema, "Nimekatwa mbali!"
\s5
\v 55 Nililiita jna lako, Yahweh, kutoka kina cha shimo.
\v 56 Ulisikia sauti yangu. Ulisikia sauti yangu nilipo sema, "Usifunge sikio lako kwa kilio changu cha msaada."
\v 57 Ulikuja karibu siku niliyo kuiita; ulisema, "Usiogope"
\s5
\v 58 Bwana, ulitetea kesi yangu, uliokoa maisha yangu!
\v 59 Yahweh, umeona mabaya waliyo ni fanyia, hukumu kesi yangu.
\v 60 Umeona matusi yao, mipango yao yote dhidi yangu -
\v 61 Umesikia dhihaka yao, Yahweh, na mipango yao kunihusu.
\s5
\v 62 Midomo ya hao wanao inuka kinyume changu, na mashtaka yao, inakuja dhidi yangu siku nzima.
\v 63 Ngalia jinsi wanavyo keti na kuinuka; wana nidhihaki na nyimbo zao.
\s5
\v 64 Walipize, Yahweh, kwa kadiri ya waliyo fanya.
\v 65 Utaacha mioyo yao bila lawama! Hukumu yako iwe juu yao!
\v 66 Una wakimbiza kwa hasira na kuwaharibu nchini ya mbingu, Yahweh!
\s5
\c 4
\p
\v 1 Dhahabu imechakaa; jinsi gani dhahabu safi imebadilika! Mawe matakatifu yamezagaa katika kila njia ya mtaa.
\v 2 Wana wa dhamani wa Sayuni walikuwa na dhamani ya uzito wa dhahabu safi, lakini sasa hawana dhamani zaidi ya majagi ya udogo, kazi ya mikono ya mfinyazi!
\s5
\v 3 Ata mbwa wa mitaani wanatoa maziwa yao kuwanyonyesha watoto wao, lakini binti wa watu wangu amekuwa katili, kama mbuni katika jangwa.
\s5
\v 4 Ulimi wa mtoto mchanga anaye nyonya unagota juu mdomo wake kwa kiu; watoto wanaomba chakula, lakini hakuna kwa ajili yao.
\v 5 Wao walizoea kula chakula cha gharama sasa wana shinda njaa mitaani; wao walio lelewa kwa kuvaa nguo za zambarau, sasa wamelala katika majalala.
\s5
\v 6 Hukumu ya binti wa watu wangu ni kubwa kuliko hiyo ya Sodoma, na ilipinduliwa kwa dakika na hakuna aliye yanyua mkono kumsaidia.
\s5
\v 7 Viongozi wake walikuwa wasafi kuliko theluji, weupe kuliko maziwa; miili yao ilikuwa imara kuliko jiwe, mwili wao ulikuwa kama yakuti samawi.
\v 8 Muonekano wao umekuwa mweusi kama giza; hawatambuliki mitaani. Ngozi zao zimesinya kwenye mifupa yao; imekuwa kavu kama kuni.
\s5
\v 9 Hao walio uawa kwa upanga walikuwa na furaha zaidi kuliko hao walio kufa kwa njaa, walio potea, wakatobolewa kwa ukosefu wa mavuno shambani.
\v 10 Mikono ya wanawake wenye huruma imewachemsha watoto wao; wamekuwa chakula chao wakati ambapo binti wa watu wangu alipo kuwa akiharibiwa.
\s5
\v 11 Yahweh alionyesha gadhabu yake yote; alimwaga hasira yake kali. Aliwasha moto Sayuni uliteketeza misingi yake.
\s5
\v 12 Wafalme wa dunia hawaku amini, wala wakazi wa dunia, kwamba maadui au wapinzani waliweza kuingia malangoni ya Yerusalemu.
\v 13 Haya yalitokea kwasababu ya dhambi za manabii na na maasi ya makuhani walio mwaga damu ya wenye haki mbele zake.
\s5
\v 14 Walitanga, kwa upofu, mitaani. Walikuwa wamejitia unajisi kwa damu hiyo ambapo hakuna aliye ruhusiwa kushika nguo zao.
\v 15 "Kaa mbali! Wewe mnajisi!" Watu waliwapazia sauti. "Kaa mbali! Kaa mbali! Usiguse!" Hivyo wakatanga; watu walisema miongoni mwa mataifa, "Hawawezi kukaa hapa tena."
\s5
\v 16 Yahweh mwenyewe akawatawanyisha; hawatazami tena. Hawa waheshimu makuhani, na hawaonyeshi upendeleo kwa wazee.
\s5
\v 17 Macho yetu yalikwama, yakitazama bure kwa msaada; kutoka minara yetu ya ulinzi tulitazama taifa lisilo weza tuokoa.
\v 18 Walifuata hatua zetu, hatukuweza kutembea mitaani mwetu. Mwisho wetu ulikuwa karibu na siku zetu zilihesabiwa, mwisho wetu ulifika.
\s5
\v 19 Walio tukimbiza walikuwa wepesi kuliko tai wa aangani. Walitukimbiza kwenye milima na kutuwinda nyikani.
\v 20 Pumzi katika pua zetu - mpakwa mafuta wa Yahweh - ndiye aliye kamatwa katika shimo; ambaye ndiye aliye semewa, "Chini ya kivuli chake tutaishi miongoni mwa mataifa."
\s5
\v 21 Shangilia na ufurahi, binti wa Edomu, wewe unaye ishi nchi ya Uzi. Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa; utalewa na kuvua nguo.
\v 22 Binti wa Sayuni, hukumu yako itafika mwisho, hataongeza mateka yako lakini binti wa Edomu, ata muhadhibu; ata funua dhambi zako.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kumbuka, Yahweh, yaliyo tutokea na uone aibu yetu.
\v 2 Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni; nyumba zetu kwa wageni.
\v 3 Tumekuwa yatima, bila baba, na mama zetu ni kama wajane.
\v 4 Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa, na tulipe fedha kupata mbao zetu.
\s5
\v 5 Hao wanakuja kwetu wamekaribia nyuma yetu; tumechoka na hatuwezi pata mapumziko.
\v 6 Tumejitoa kwa Misri na kwa Assiria tupate chakula cha kutosha.
\v 7 Baba zetu walifanya dhambi, na hawapo tena, na tumebeba dhambi zao.
\s5
\v 8 Watumwa walitutawala, na hakuna wa kutuokoa na mikono yao.
\v 9 Tunapata mkate wetu pale tunapo hatarisha maisha, kwasababu ya upanga wa nyikani.
\v 10 Ngozi zetu zimekuwa na moto kama jiko kwasababu ya joto la njaa.
\s5
\v 11 Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda.
\v 12 Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee.
\s5
\v 13 Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.
\v 14 Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki.
\s5
\v 15 Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio.
\v 16 Taji limeanguka kichwani mwetu; ole wetu, kwa kuwa tumetenda dhambi!
\s5
\v 17 Kwa kuwa moyo wetu umekuwa unaumwa, na machozi yetu ya fifia, kwa vitu hivi macho yetu yanafifia
\v 18 maana Mlima Sayuni umelala ukiwa, mbwa wa mitaani wacheza juu yake.
\s5
\v 19 Lakini wewe, Yahweh, unatawala milele, na utaketi katika kiti chako cha enzi vizazi na vizazi. Kwanini unatusahau milele?
\v 20 Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi?
\v 21 Turejeshe kwako, Yahweh, na sisi tutarejea. Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani -
\v 22 vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi.

2474
26-EZK.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,2474 @@
\id EZK
\ide UTF-8
\h Ezekieli
\toc1 Ezekieli
\toc2 Ezekieli
\toc3 ezk
\mt Ezekieli
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, na siku ya tano ya mwezi, ikawa kuhusu kwamba nilikuwa nikiishi miongoni mwa wafungwa karibu na Kebari Kanali. Mbingu zilifunguka, na kuona maono ya Mungu.
\v 2 Katika siku ya tano katika mwezi huo-ilikuwa mwaka wa tano wa utumwani wa Mfalme Yehoyakini-
\v 3 Neno la Yahwe likamjia Ezekieli mwana wa Buzi kuhani, katika nchi ya Wakaldayo karibu na Keberi Kanali, na mkono wa Yahwe ulikuwa juu yake hapo.
\s5
\v 4 Kisha nikaona, kulikuwa na upepo wa dhoruba unakuja kutoka kaskazini; wingu kubwa pamoja na moto wa nuru ndani yake na kung'aa ukizunguka ndani yake, na moto ulikuwa na rangi ya kaharabu ndani ya hilo wingu.
\v 5 Katikati kulikuwa na viumbe vinne vinavyofanana. Mwonekano wao ulikuwa hivi: walikuwa wanamfanano wa mtu,
\v 6 lakini walikuwa na sura nne kila mmoja, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne.
\s5
\v 7 Miguu yao ilikuwa imenyooka, lakini nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za ndama zilizokuwa zinang'aa kama shaba iliyosuguliwa.
\v 8 Bado walikuwa na mikono ya binadamu chini ya mabawa yao chini kwenye pande zote nne. Kwa wote wanne, nyuso zao na mabawa vilikuwa hivi:
\v 9 mabawa yao yalikuwa yameungana na kiumbe kingine, na hawakurudi walipokuwa wameenda; badala yake, kila mmoja alienda mbele.
\s5
\v 10 Mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama uso wa mwanadamu. Wanne hao walikuwa na uso wa simba kwa upande wa kuume. Hao wanne pia walikuwa na uso wa tai.
\v 11 Nyuso zao zilikuwa hivyo, na mabawa yao yalikuwa yametawanyika juu, hivyo basi kila kiumbe kilikuwa na jozi ya za mabawa yaliyokuwa yameshikamana na bawa la kiumbe kingine, na pia jozi za mabawa yaliyokuwa yamefunika miili yao.
\v 12 Kila mmoja alienda mbele, hivyo basi popote Roho alipowaelekeza kwanda, walienda bila kurudi.
\s5
\v 13 Kama kwa mfanano wa hao viumbe hai, mwonekano wao ulikuwa ni kama kuchoma kaa la moto, kama mwonekano wa nuru; mng'ao wa moto pia ulihama karibu na miongoni mwa viumbe, na kulikuwa na nuru za radi.
\v 14 Hao viumbe hai vilikuwa vikihama mbio mbele na nyuma, na walikuwa na mwonekano wa radi!
\s5
\v 15 Kisha nikawatazama wale viumbe hai; kulikuwa na gurudumu moja juu ya aridhi kando ya vile viumbe hai.
\v 16 Huu ndio ulikuwa mwonekano na umbo wa hizo gurudumu: kila gurudumu lilikuwa kama zabarajadi, na manne hayo yalikuwa na mfano mmoja; mwonekano wao na umbo vilikuwa kama gurudumu lililoungana na jingine.
\s5
\v 17 Wakati yale magurudumu yalipokuwa yakitembea, yalienda bila kurudi kwenye mwelekeo wowote viumbe vilipokuwa vimeelekea.
\v 18 Kama kwa upande kingo, walikuwa warefu na wakutisha, kwa upande kingo kulikuwa na macho yamezunguka kote.
\s5
\v 19 Popote vile viumbe hai vilipokuwa vikielekea, yale magurudumu yalielekea karibu nao. Wakati vile viumbe hai vilipoinuka kutoka kwenye nchi, na yale magurudumu yaliinuka pia.
\v 20 Popote Roho alipokwenda, walikwenda, na yale magurudumu yaliinuka karibu nao, roho wa kiumbe hai ilikuwa magurudumu.
\v 21 Popote vile viumbe vilipoelekea, magurudumu pia yalielekea huko; na wakati wale viumbe viliposimama hata hivyo, magurudumu yalisimama bado; wakati viumbe viliposimama kutoka kwenye nchi, magurudumu yalisimama karibu nao, kwa sababu yule roho wa wale viumbe alikuwa kwenye magurudumu.
\s5
\v 22 Juu ya vichwa vya wale viumbe hai kulikuwa na mfanano wa anga la kutanuka; ilikuwa inang'aa kama mfano wa barafu juu ya vichwa vyao.
\v 23 Chini ya anga, kila mabawa ya kiumbe kimoja yalinyooshwa mbele na kugusana kila mabawa na kiumbe kimoja. Pia kila kiumbe hai kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika vyenyewe; kila kimoja kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika mwili wake mwenyewe.
\s5
\v 24 Kisha nikasikia sauti ya mabawa yao. Kama mlio wa maji mengi. Kama sauti ya mwenye enzi popote walipoelekea. Kama sauti ya jeshi. Popote pale waliposimama, walishusha mabawa yao.
\v 25 Sauti ikaja kutoka juu ya anga juu ya vichwa vyao popote waliposimama na kushusha mabawa yao.
\s5
\v 26 Juu ya anga juu ya vichwa vyao kulikuwa na mfanao wa kiti cha enzi ambacho kilikuwa na mwonekano wa jiwe la samawati, na juu mfano wa kiti cha enzi kilifanana kama mwonekano wa mwanadamu.
\s5
\v 27 Nikaona umbo lenye mwonekano wa chuma chenye kung'aa pamoja na moto ndani yake kutoka kwenye mwonekano wa juu ya nyonga zake juu; Nikaona kutoka kwenye mwonekano wa nyonga zake upande wa chini mwonekano wa moto na mng'ao umezunguka kote.
\v 28 Kama mwonekano wa upinde wa mvua kwenye mawingu katika siku ya mvua ulikuwa na mwonekano wa taa iliyowaka imeizunguka. ulikuwa na mwonekano unaofanana na utukufu wa Yahwe. Wakati nilipouona, nilihisi kwenye uso wangu, na nikasikia sauti ikiongea.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Akanambia, "Mwana wa adamu, simama kwa miguu yako; kisha nitaongea na wewe."
\v 2 Kisha, alipokuwa akiongea na mimi, Roho akaingia ndani yangu na ikaniweka kwenye miguu yangu, na nikamsikia akiongea na mimi.
\v 3 Akanambia, "Mwana wa adamu, nakutuma kwa watu wa Israeli, kwa mataifa yanayoasi ambayo yameasi dhidi yangu-wote wao na babu zao wameasi juu yangu hata hivi leo!
\s5
\v 4 Vizazi vyao vina sura za kikaidi na mioyo migumu. Nakutuma wewe kwenda kwao, na utawaambia, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
\v 5 Labda watasikia au hawatasikia. Ni nyumba za uasi, lakini angalau watajua kwamba nabii alikuwa miongoni mwao.
\s5
\v 6 Wewe, mwanadamu, usiwaogope au maneno yao. Usiogope, ingawa utakuwa pamoja na mitemba na miiba na ijapokuwa unaishi na nge. Usiogope maneno yao au kuvunjika moyo kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba zenye kuasi..
\s5
\v 7 Lakini utawaambia maneno yangu, labda watasikia au hapana, kwa sababu ni waasi mno.
\v 8 Lakini wewe, mwanadamu, silikiliza kile nisemacho kwako. Usiwe muasi kama nyumba za uasi. Fungua mdomo wako na ule kile ninachotaka kukupa!"
\s5
\v 9 Kisha nikaona, na mkono ulikuwa umenyooshwa kwangu; ndani yake kulikuwa na hati ya kukunja.
\v 10 Akaikinjua mbele yangu; ilikuwa imeandikwa pande zote mbele na nyuma, na yalikuwa yameandikwa maombolezo kwenye hiyo hati ya kukunja, na huzuni, na ole.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Akanambia, "Mwanadamu, kile ulichokikuta, kula. Kula hili gombo, kisha nenda kaongee na nyumba ya Israeli."
\v 2 Basi nikafungua kinywa changu, na akanilisha hilo gombo.
\v 3 Akanambia, "Mwana wa adamu, lisha tumbo lako na jaza tumbo lako kwa hili gombo ambalo nimekupa!" Basi nikalila, na lilikuwa tamu kama asali kwenye mdomo wangu.
\s5
\v 4 Kisha akanambia, "Mwana wa adamu, nenda kwenye nyumba ya Israeli na ongea maneno yangu kwao.
\v 5 Kwa kuwa hujatumwa kwa watu wenye maneno ya kushangaza au lugha ngumu, lakini kwa nyumba ya Israeli-
\v 6 sio kwa taifa lenye nguvu ya maneno ya ajabu au lugha ngumu ambao maneno yao hutaweza kuyaelewa! Kama nikikutuma kwao, watakusikiliza.
\v 7 Lakini nyumba ya Israeli haitakuwa tayari kukusikiliza, kwa kuwa hawako tayari kunisikiliza mimi. Hivyo nyumba yote ya Israeli ni paji gumu na moyo mgumu.
\s5
\v 8 Kumbe nimeufanya uso wako kama kaidi kama nyuso zao na paji lako kuwa gumu kama mapaji yao.
\v 9 Nimekufanya paji lako kama almasi, gumu kuliko jiwe la kiberiti! Usiwaogope wala kufadhaika kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba ya uasi."
\s5
\v 10 Kisha akanambia, "Mwana wa adamu, maneno yote niliyokutangazia-yachukue kwenye moyo wako na wasikize kwa sikio lako!
\v 11 Kisha nenda kwa watumwa, kwa watu wako, na uzungumze nao. Waambie, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo; iwapo watasikia au hapana."
\s5
\v 12 Kisha Roho akaniinua juu, na nikasikia nyuma yangu sauti yenye tetemeko la aridhi: "Ubarikiwe utukufu wa Yahwe kutoka mahali pake!"
\v 13 Ilikuwa sauti ya mabawa ya viumbe hai vilipokuwa vikigusana kila kimoja, na sauti ya magurudumu ambayo yalikuwa pamoja na hivyo viumbe, na sauti ya tetemeko kubwa arithi.
\s5
\v 14 Roho akaniinua juu na kunichukua, Nikaenda kwa uchungu katika hasira kali rohoni mwangu, kwa kuwa mkono wa Yahwe ulikuwa na nguvu ukigandamiza juu yangu!
\v 15 Hivyo nikaenda kwa watumwa huko Tel Abibu waliokuwa wakiishi karibu na Kebari Kanali, na niliishi miongoni mwao huko kwa mda wa miaka saba, kushinda kabisa katika mshangao.
\s5
\v 16 Kisha ikatokea baada ya siku saba kwamba neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 17 "Mwana wa adamu, nimekufanya uwe mwangalizi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, hivyo sikiliza neno kutoka kinywani mwangu, na uwapatie onyo langu.
\v 18 Nitakaposema kwa waovu, 'Utakufa hakika' na usimuonye au kuzungumza onyo kwa waovu kuhusu matendo yao maovu hivyo anaweza kuishi-yule muovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.
\v 19 Lakini kama ukimuonya muovo, na asiuache uovu wake au kutoka matendo yake maovu, kisha atakufa kwa dhambi yake, lakini utaokoa maisha yako mwenyewe.
\s5
\v 20 Kama mwenye haki ataicha haki yake na kutenda yasiyohaki, na nikaweka kizuizi mbele yake, atakufa. Kwasababu hukumuonya, atakufa katika dhambi yake, na sintokumbuka matendo ya haki aliyoyafanya, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.
\v 21 Lakini kama ukimuonya mwenye mtu mwenye haki kuacha kufanya dhambi halafu akaacha kutenda dhambi, ataishi hakika tangu alipo unywa; na utakuwa umeokoa maisha yako mwenyewe."
\s5
\v 22 Hivyo mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu huko, akanambia, "Inuka! nenda uwandani, na nitaongea na wewe huko!"
\v 23 Nikainuka na kwenda uwandani, na huko utukufu wa Yahwe ulisimama, kama utukufu ambao niliokuwa nimeuona karibu na Kebari Kanali; hivyo nikaanguka kifudifudi.
\s5
\v 24 Roho akaja kwangu na kusimama juu ya miguu yangu; akaongea na mimi, na kunambia, "Nenda na jifungie mwenyewe kwenye nyumba yako,
\v 25 kwa sasa, mwana wa adamu, wataweka kamba juu yako na kukufunga ili usiweze kutoka nje miongoni mwao.
\s5
\v 26 Nitaufanya ulimi wako ugandamane na paa ya mdomo wako, ili kwamba uwe kimya, na hutaweza kuwakemea, kwa kuwa ni nyumba ya waasi.
\v 27 Lakini nitakapozungumza na wewe, nitafungua mdomo wako hivyo utawaambia, 'Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.' Yeye asikiaye na asikie; yeye asiyesikia na asisikie, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi!"
\s5
\c 4
\p
\v 1 "Lakini wewe, mwana wa adamu, chukua tofali wewe mwenyewe na uliweke mbele yako. Kisha chonga mji wa Yerusalemu juu yake.
\v 2 Kisha laza kuizunguka, ngome juu yake. Anza kushambulia juu yake na weka makambi kuizunguka. Weka shambulio la ghasia kuizunguka.
\v 3 Kisha chukua kwa ajili yako mwenyewe sufuria ya chuma na itumie kama ukuta wa chuma kati yako mwenyewe na mji na weka uso wako dhidi yake. Kwa kuwa utazingirwa, na utaweka ukombozi juu yake. Hii itakuwa alama kwa nyumba ya Israeli.
\s5
\v 4 Kisha, lala juu upande wako wa kushoto na weka dhambi ya nyumba ya Israeli juu yake; utazibeba dhambi zao kwa hesabu za siku ambazo ulizolala juu ya nyumba ya Israeli.
\v 5 Mimi mwenyewe nakuagiza kwako siku moja kuwakilisha kila mwaka wa adhabu yao: siku 390! Katika njia hii, utachukua dhambi ya nyumba ya Israeli.
\s5
\v 6 Wakati utakapomaliza hizi siku, kisha lala chini kwa mara ya pili kwa upande wako wa kulia, kwa kuwa utabeba dhambi ya nyumba ya Yuda kwa siku arobaini. Nakuteua wewe siku moja kwa kila mwaka.
\v 7 Weka uso wako chini kuelekea Yerusalemu ambayo ni chini ya ngome, na kwa mkono wako funua unabii dhidi
\v 8 yake. Tazama! naweka vifungo juu yako hivyo hutarudi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine hadi utakapoliza siku zako za kuzingirwa kwako.
\s5
\v 9 Chukua ngano kwa ajili yako, shayiri, dengu, mtama, kusemethi; viweke kwenye chombo kimoja na tengeneza mkate kwa ajili yako kulingana na hesabu ya siku ambazo utakazo lala katika ya upande wako. Kwa siku 390 utaula.
\v 10 Chakula utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku, na utakila kwa mda uliopangwa kila siku.
\v 11 Kisha utakunywa maji, kwa kuyapima sehemu ya sita ya hini, na utayanywa kwa mda uliopangwa.
\s5
\v 12 Utakila kama keki za shayiri, lakini utaioka kwenye kinyesi kikavu cha mwanadamu mbele ya macho yao!"
\v 13 Kwa kuwa Yahwe asema, "Hii inamaana kwamba ule mkate ambao watu wa Israeli watakula kitakuwa kinajisi, huko miongoni mwa mataifa ambapo nitakaowafukuza."
\s5
\v 14 Lakini nikasema, "Ee, Bwana Yahwe! Sijawahi kuwa najisi! sijawahi kula kitu chochote ambacho kimekufa au kitu chochote kilichouawa na wanyama, kutoka mdomoni mwangu hadi sasa, wala nyama ya kunuka haijawahi kuingia kinywani mwangu!"
\v 15 Ndivyo alivvyo niambia, "Tazama! Nimekupa mbolea ya ng'ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu ili uweze kuandaa mkate wako juu ya hayo."
\s5
\v 16 Pia akanambia, "Mwana wa adamu! Tazama! Nalivunja gongo la mkate katika Yerusalemu, na watakula mkate ukiwa umepimwa katika wasiwasi na kunywa maji kwa kuyapima katika hofu.
\v 17 Kwa sabau watapungukiwa na mkate na maji, kila mtu atafadhaishwa na ndugu yake na kumpoteza kwa sababu ya udhalimu wao."
\s5
\c 5
\p
\v 1 "Kisha wewe mwana wa adamu, chukua upanga mkali kama wembe wa kinyozi kwa ajili yako mwenyewe, na pitisha hayo makali juu ya kichwa chako na ndevu zako, kisha chukua mizani za kupimia uzito na uzigawanye nywele zako.
\v 2 Choma theluthi ya tatu ya hiyo kwa moto katikati ya mji wakati siku za kuzingirwa zitakapokamilika, na chukua theluthi ya nywele na uipige kwa panga na kuuzunguka mji. Kisha tawanya theluthi yake kwenye upepo, na nitasogeza panga karibu ili kufukuza watu.
\s5
\v 3 Lakini chukua kiasi kidogo cha nywele na zifunge kwenye pindo za nguo yako.
\v 4 Kisha chukua tena zile nyewele na zitupe katikati ya moto; na zichome kwenye moto; kutoka hapo utatoka nje kwenda nyumba zote za Israeli."
\s5
\v 5 Bwana Yahwe asema hivi, "Hii ndio Yerusalemu katikati ya mataifa, nilipomuweka, na ambapo nilipomzunguka kwa nchi zingine.
\v 6 Lakini anaudhaifu wa kukataa amri zangu zaidi kuliko mataifa yalivyo, na sheria yangu zaidi kuliko mataifa ambayo yanayomzunguka. Watu wamezikataa humuku zangu na kuacha kutembea katika sheria zangu."
\s5
\v 7 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, "Kwa sababu mmekuwa kikwazo kuliko mataifa ambayo yanayowazunguka na kuacha kutembea kwenye amri zangu wala kutenda kulingana na amri zangu, wala hata kutenda kulingana na amri za mataifa yanayowazunguka,"
\v 8 kwa hiyo Bwana asema hivi, "Tazama! Mimi mwenyewe nitatenda juu yenu. Nitato hukumu kati yenu ili mataifa waone.
\s5
\v 9 Nitawafanyia yale ambayo sijawahi kuyafanya na kile ambacho sintokifanya tena, kwa sababu ya matendo yenu ya kuchukiza.
\v 10 Kwa hiyo baba watawala watoto kati yenu, na watoto watawala baba zao, kwa kuwa nitafanya hukumu juu yenu na kuwatawanya kila mahali wote ninyi mliobaki.
\s5
\v 11 Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hii ilikuwa kwa sababu umapanajisi patakatifu pangu kwa mambo ya machukizo yako yote na kwa matendo yako yote niyachukiayo, kwamba mimi mwenyewe nitakupunguza katika hesabu; jicho langu halitakuhurumia, na sintoacha kukuharibu.
\v 12 Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na wataliwa na njaa katikati yenu. Theluthi wataanguka kwa upanga likiwazunguka. Kisha nitawatawanya theluthi katika mahali pote, na nitafuatisha upanga kuwafukuza pia.
\s5
\v 13 Hivi ndivyo ghadhabu yangu itavyokamilika, na nitasababisha ghadhabu yangu juu yao hata kulala. Nitajiridhisha, na watajua kwamba, mimi Yahwe, nimenena kwa ghadhabu yangu wakati nitakapo kamilisha ghadhabu yangu dhidi yao.
\v 14 Nitakufanya mkiwa kwa mataifa yanayokuzunguka kwenye uso wa kila mtu apitaye karibu.
\s5
\v 15 Hivyo Yerusalemu itakuwa jambo kwa watu wengine kushutumu na kufanya mzaha, na chukizo kwa mataifa ambayo yanayowazunguka. Nitafanya hukumu dhidi yenu kwa ghadhabu na hasira, na kwa kukemea kwa hasira-Mimi, Yahwe nimesema hivi!
\v 16 Nitatuma mishale mikali ya njaa juu yenu ambayo itakuwa na maana ya kwamba nitawaharibu. Kwa kuwa nitaongeza njaa juu yenu na kuvunja tegemeo lenu la mkate.
\v 17 Nitaleta njaa na majanga dhidi yenu hivyo mtakuwa wagumba. Tauni na damu zitapita kati yako, na nitaleta upanga dhidi yenu-Mimi Yahwe, nimesema hivi."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 2 "Mwana wa adamu, weka uso wako dhidi ya milima ya Israeli na uwatabirie.
\v 3 Sema, 'Milima ya Israeli, silikilizeni neno la Bwana Yahwe! Bwana Yahwe asema hivi kwenye milima kwenye vilele, kwenye vijito na kwenye mabonde: Tazama! Naleta upanga dhidi yenu, na nitapaharibu pahali penu pa juu.
\s5
\v 4 Kisha madhabahu zenu zitakuwa ukiwa na nguzo zenu zitaharibiwa, na nitatupa chini wafu wenu mbele ya sanamu zao.
\v 5 Nitalaza miili iliyokufa kwa watu wa Israeli mbele ya sanamu zao, na kuitawanya mifupa yenu kuzizunguka madhabahu zenu.
\s5
\v 6 Kila mahali utaishi, miji itaharibiwa na mahali pa juu kuangamia, hivyo basi madhabahu zenu zitaharibiwa na kufanywa ukiwa. Kisha zitavunjwa na kupotea, nguzo zenu zitaangushwa chini na kazi zenu zitafutwa mbali.
\v 7 Waliokufa wataanguka chini kati yenu nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 8 Lakini nitahifadhi mabaki kwenu, na kutakuwa na wale watakao toroka upanga miongoni mwa mataifa,
\v 9 Kisha wale watakao toroka watanikumbuka miongoni mwa mataifa amabapo watakapochukuliwa mateka, ndivyo nitakavoyowaponda mioyo yao ya kikahaba ambayo imeniacha, na kwa macho yao ya kikahaba kufuata sanamu zao. Kisha wataonyesha chuki kwenye nyuso zao kwa udhaifu walioufanya kwa machukizo yao yote.
\v 10 Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe. Kulikuwa na sababu kwamba nimesema nitaleta huu uovu kwao.
\s5
\v 11 Bwana Yahwe asema hivi: Piga makofi na kanyaga kwa mguu wako! Sema! 'Ole!' kwa sababu ya uovu wote wa chukizo wa nyumba ya Israeli! Wataanguka kwa upanga, njaa, na tauni.
\v 12 Yule aliye mbali sana atakufa kwa tauni, na yule aliyekaribu ataanguka kwa upanga. Wale watakaobaki na kuishi watakufa kwa upanga. Kwa njia hii ndivyo nitakavyo kamilisha madhabahu yangu dhidi yao.
\s5
\v 13 Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati waliokufa watakapolala kati ya sanamu zao, kuzizunguka madhabahu, kwa kila mlima mrefu-juu ya vilele vya mlima, na chini ya mti wenye majani mabichi na mwalo mnene-sehemu wanapochomea ubani kwa sanamu zao zote.
\v 14 Nitapiga kwa mkono wangu na kuifanya nchi ukiwa na isiyofaa, kutoka jangwa hata Dibla, kupita sehemu zote wanapoishi. Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe."
\s5
\c 7
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 2 Wewe, mwanadamu-Bwana Yahwe asema hivi kwa nchi ya Israeli." 'Mwisho! Mwisho umekuja kwenye mipaka minne ya nchi.
\s5
\v 3 Sasa mwisho uko juu yako, kwa kuwa natuma ghadhabu yangu juu yako, nitakuhukumu kulingana na njia zako; nitaleta machukizo yako yote juu yako.
\v 4 Kwa kuwa macho yangu hayatakuhurumia, na sitakuharibu. Badala yake, nitaleta njia zako zote juu yako, na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako, hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 5 Bwana Yahwe asema hivi: Msiba! Msiba wa pekee! Tazama, unakuja.
\v 6 Mwisho unakuja hakika. Mwisho umeamsha dhidi yenu. Tazama! unakuja!
\v 7 Kifo chako kinakuja kwako ukaaye kwenye nchi. Mda umefika; siku ya uharibifu iko karibu, na milima haitakuwa na shangwe tena.
\s5
\v 8 Sasa baada ya mda mfupi nitamwaga dhahabu yangu juu yako na kujaza hasira yangu juu yako wakati nitakapokuhukumu kulingana na njia zako na kuleta machukizo yako yote juu yako.
\v 9 Kwa kuwa jicho langu halitaona kwa huruma, sitakuharibu, kama ulivyofanya, nitafanya kwako; na machukizo yako yatakuwa katikati yako hivyo utajua kwamba ni mimi Yahwe, anayekuadhibu.
\s5
\v 10 Tazama, siku! Tazama, inakuja! Kifo kimetoka! fimbo ya kuadhibia imechanua, kiburi kimechipua!
\v 11 Udhalimu umekua kwenye fimbo ya udhaifu-hakuna kati yao, na hakuna katika ya kundi lao, hakuna katika utajiri wao, na hakuna wa muhimu wao atakaye baki!
\s5
\v 12 Muda unakuja; siku imekaribia. Usimuache anayenunua shangwe, wala asihuzunike auzaye, kwa kuwa hasira yangu iko juu ya kikundi kizima!
\v 13 Kwa kuwa muuzaji hatarudia kile kilichouzwa, kadiri wanapoendelea kuishi, kwa kuwa maono yako juu yako kikundi kizima. Hawatarudi, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi kwenye dhambi atakayejitia nguvu!
\s5
\v 14 Wamepiga tarumbeta na kufanya kila kitu tayari, lakini hakuna mtu anayeenda kupigana; kwa kuwa hasira yangu iko juu ya kundi zima.
\v 15 Upanga uko nje, na tauni na njaa viko nje kwenye jengo. Wale walioko shambani watakufa kwa upanga, wakati njaa na tauni zitakapowala wale waliopo kwenye mji.
\v 16 Lakini watakao salia watatoroka kutoka miongoni mwao, na watakwenda kwenye milima. Kama hua wa mabondeni, wote watalia-kila mtu kwa ajili ya uovu wake.
\s5
\v 17 Kila mkono utasita na kila goti litakuwa dhaifu kama maji, na watavaa nguo za magunia, na hofu kuu itawafunika,
\v 18 na aibu itakuwa juu ya kila uso, na upara juu ya vichwa vyao vyote.
\v 19 Watatupa fedha yao kwenye mitaa na dhahabu yao itakuwa kama jalala. Fedha yao na dhahabu yao haitaweza kuwaokoa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe. Maisha yao hayataokolewa, na njaa yao haitashiba, kwa sababu uovu wao umekuwa kizuizi.
\s5
\v 20 Kwenye fahari yao walichukua kito yake nzuri za mapambo, pamoja nao wakatengeza sanamu zao za vinyago, na vitu vyao vichukizavyo. Kwa hiyo, nayabadilisha haya kuwa kitu najisi kwao.
\v 21 Kisha nitawapatia hivyo vitu kwenye mikono ya wageni kama mateka na kwa waovu wa dunia kama mateka, na watapanajisi.
\v 22 Kisha nitaugeuza uso wangu mbali kutoka kwao watakapo najisi mahali pangu pa siri; maharamia wataingia humo na kupanajisi.
\s5
\v 23 Tengeneza mnyororo, kwa sababu nchi imejaa hukumu ya damu, na mji umejaa udhalimu.
\v 24 Hivyo nitaleta waovu wengi wa mataifa, na watamilki nyumba zao, na nitaleta mwisho kwenye fahari ya uweza, kwenda mahali pao patakatifu patanajisiwa!
\v 25 Hofu itakuja! Wataitafuta amani, lakini haitakuwepo.
\s5
\v 26 Majanga juu ya majanga yatakuja juu yangu, na kutakuwa na tetesi juu ya tetesi. Kisha watatafuta ono moja kutoka kwa nabii, lakini sheria itawaangamiza kutoka kwa kuhani na shauri kutoka kwa wazee.
\v 27 Mfalme ataomboleza na mwana wa mfalme atakata tamaa, wakati mikono ya watu wa nchi itatetemeka kwa hofu. Kulingana na njia zao wenyewe nitafanya hivi kwao! Nitawahukumu sawa sawa na wanavyostahili hadi watakapojua yakwamba mimi ni Yahwe.'"
\s5
\c 8
\p
\v 1 Hivyo ikawa kuhusu katika mwaka wa sita na mwezi wa sita, katika siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa nimeketi kwenye nyumba yangu na wazee wa Yuda waliketi mbele yangu, kwamba mkono wa Bwana Yahwe ukanijaza juu yangu huko.
\v 2 Hivyo nikaona, na tazama, kulikuwa na mfano kama mwonekano wa mwanadamu. Kutoka kwenye mwonekano wake wa nyonga kwenda chini kulikuwa na moto. Na kutoka kwenye nyonga kwenda juu kulikuwa na mwonekano wa kitu kinachong'aa, kama mng'ao wa chuma.
\s5
\v 3 Kisha akanyoosha kutoka kwenye mkono na kunichukua kwa nywele za kichwa changu; Roho akaniacha juu kati ya dunia na mbingu, na katika maono kutoka kwa Mungu, akaniletea hata Yerusalemu, kwenye mlango wa kuingia ndani ya lango la kaskazini, ambako sanamu ile iletayo wivu mkubwa ilipokuwa imesiamama.
\v 4 Kisha tazama, utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa huko, kulingana na ono nililokuwa nimeliona kwenye uwanda.
\s5
\v 5 Kisha akanambia, "Mwanadamu, inua juu macho yako kwenda upande wa kaskazini." Hivyo nikainua macho yangu kuelekea kaskazini, na kwenye lango la kaskazini kulekea kwenye madhabahu, huko kwenye lango la kuingilia, kulikuwa na sanamu ya wivu.
\v 6 Hivyo akanambia, "Mwanadamu, unaona wanayoyafanya? Haya ni machukizo makubwa ambayo nyumba ya Israeli wanayoyafanya hapa kunifanya niende mbali kutoka patakatifu pangu. Lakini utageuka na kuona machukizo makubwa zaidi."
\s5
\v 7 Kisha akanileta hata kwenye mlango wa uzio, na nikatazama, kulikuwa na shimo kwenye ukuta."
\v 8 Akanambia, "Mwanadamu, chimba kwenye huu ukuta." Basi nikachimba kwenye huo ukuta, na kulikuwa na mlango.
\v 9 Kisha akanambia, "Nenda na ukaone machukizo ya uovu ambayo wanayoyafanya hapa."
\s5
\v 10 Basi nilipokuwa nikienda ndani na nikaona, na tazama! Kulikuwa na kila umbo la vitu vikitembea polepole na mnyama achukizaye sana! Kila sanamu wa nyumba ya Israeli ilikuwa imechongwa kwenye ukuta pande zote.
\v 11 Wazee sabini wa wa nyumba ya Israeli walikuwa huko, na Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama katikati yao. Walikuwa wamesimama mbele ya picha, na kila mtu alikuwa na chetezo kwenye mkono wake ili kwamba harufu ya ubani ingeweza kupanda juu.
\s5
\v 12 Akanambia, "mwanadamu, unaona kile ambacho wazee wa nyumba ya Israeli wanachokifanya kwenye giza? Kila mmoja hufanya hivi kwenye chumba cha sanamu yake, kwa kuwa husema, 'Yahwe hatuone! Yahwe ameitelekeza hii nchi."'
\v 13 Kisha akanambia, "Geuka tena na tazama machukizo makubwa ambayo wanayoyafanya."
\s5
\v 14 Tena akanileta kwenye lango la kuingia la nyumba ya Yahwe lililokuwa upande waa kaskazini, na tazama! Wanawake walikuwa wameketi huko wakimlilia Tamuzi.
\v 15 Hivyo akanambia, "Umeiona hii, mwanadamu? Geuka tena na uone machukizo makubwana zaidi kuliko hayo."
\s5
\v 16 Akanileta hata kwenye uzio wa ndani wa nyumba ya Yahwe, na tazama! huko kwenye lango la kuingia kwenye madhabahu, kulikuwa na takribani watu ishirini na tano waliokuwa wamelipa mgongo hekalu la Yahwe na nyuso zao kuelekea mashariki, na walikuwa wakiabudu jua.
\s5
\v 17 Akanambia, "Unaona hii, mwanadamu? Je ni kitu kidigo kwa ajili ya nyumba ya Yuda kufanya haya machukizo wanayoyafanya? Kwa kuwa wameijaza nchi kwa uovu na wamerudi tena ili kuniletea hasira, kuweka tawi kwenye pua zao.
\v 18 Hivyo nitatenda miongoni mwao pia; jicho langu halitakuwa na huruma, sitaacha kuwaharibu. hata watalia kwenye masikio yangu kwa sauti kubwa, sitawasikia."
\s5
\c 9
\p
\v 1 Kisha akalia kwa sauti kubwa nikasikia kwenye masikio yangu, huku akisema, "Waache walinzi waje kwenye mji, kila mmoja na silaha yake ya uharibifu kwenye mkono wake."
\v 2 Kisha tazama! watu wanne watakuja kutokea njia ya lango la juu linaloelekea kaskazini, kila mmoja na silaha yake ya kuchinjia kwenye mkono wake. Kulikuwa na mtu mmoja miongoni mwao alikuwa amevaa nguo ya kitani pamoja na kifaa cha uandishi ubavuni mwake. Hivyo waliingia na kusimama karibu na madhabahu ya shaba.
\s5
\v 3 Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli ukapanda juu kutoka kwa kerubi ambapo ilikuwa kwenye kisingiti cha nyumba. Akamwita yule mtu aliyekuwa amevaa nguo ya kitani na kifaa cha uandishi ubavuni mwake.
\v 4 Yahwe akamwambia, "Pita kati ya mji-kati ya Yerusalemu-na weka alama katika vipaji vya uso vya wale waliolemewa na kuona kuhusu machukizo yote yanafanyika kati ya mji."
\s5
\v 5 Kisha akaongea na wengine kupitia kusikia kwangu, "Pita kwenye mji baada ya yeye na kuua. Msiache macho yenu yawe na huruma, na msiogope kuharibu
\v 6 iwe mzee, kijana, msichana, mtoto mdogo au wanawake. Waueni watu wote! Lakini msimkaribie mtu yeyote ambaye mwenye alama kwenye kichwa chake. Anzeni katika patakatifu pangu!" Hivyo wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
\s5
\v 7 Akawaambia, "Najisi nyumba, na kujaza zio zake kwa waliokufa. Endeleeni!" Hivyo wakaenda na kuushambulia mji.
\v 8 Walipokuwa wakiushambulia, nikajikuta mwenyewe na nikaangukia kwenye uso wangu na kulia kwa sauti na kusema, "Ee, Bwana Yahwe, utayaharibu mabaki yote ya Israeli wakati wa kumwaga ghadhabu yao juu ya Yerusalemu?"
\s5
\v 9 Akanambia, "Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda unaongezeka sana. Nchi imejaa damu na mji umejaa upotovu, tangu waliposema, 'Yahwe ameisahau nchi; na Yahwe haoni!'
\v 10 Hivyo kisha, macho yangu hataangalia kwa huruma, na sintoacha kuwaharibu. Badala yake nitaileta juu ya vichwa vyao."
\v 11 Tazama! yule mtu aliyekuwa amevaa nguo ya kitani aliyekuwa na kifaa cha uandishi kwa uapende wa ubavuni mwake. Alitoa taarifa na kusema, "Nimemaliza yale yote uliyoniamuru."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Nilipokuwa nikingalia mbele ya anga ambalo liliyokuwa juu ya vichwa vya kerubi; kitu kikawatokea juu yao kama rangi ya samawati mwonekano wake ulikuwa kama kiti cha enzi.
\v 2 Kisha Yahwe akaongea na yule mtu alikuwa maevaa nguo za kitani na kusema, "Nenda kati ya magurudumu chini ya kerubi, na jaza mikono yako yote na watawanye juu ya mji." Kisha yule mtu akaenda ndani nikiwa natazama.
\s5
\v 3 Kerubi likasimama juu ya upande wa kulia wa nyumba wakati yule mtu alipoingia, na wingu likaja a ndani ya uzio.
\v 4 Utukufu wa Yahwe ukainuka kutoka kwenye kerubi na kusimama kwenye kizingiti cha nyumba. Ukaijaza nyumaba kwa wingu, na uzio ulikuwa umejaa nuru ya utukufu wa Yahwe.
\v 5 Sauti ya mabawa ya kerubi ikasikika kwa mbali nje ya uzio, kama sauti ya Mungu mwenyezi wakati akiwa anaongea.
\s5
\v 6 Ikawa kuhusu, Mungu alipoamwamuru yule mtu aliyekuwa amevaa nguo za kitani na kusema, "Chukua moto kutoka kwenye ya kerubi," yule mtu akaenda na kusimama karibu na gurudumu.
\v 7 Kerubi akaunyoosha mkono wake kwenye kerubi kwenye moto uliokuwa miongoni mwa kerubi, na kuiacha juu na kuiweka kwenye mikono ya yule mtu aliyekuwa amevaa vazi la kitani. Yule mtu akaichukua na kurudi.
\v 8 Nikaona juu ya kerubi kitu kama mkono wa mtu juu ya mabawa yao.
\s5
\v 9 Hivyo nikaona, na tazama! Magurudumu manne yalikuwa karibu na kerubi-gurudumu moja karibu na kila kerubi-na mwonekano wa hayo magurudumu ulikuwa kama jiwe la zabarajadi.
\v 10 Mwonekano wake ulikuwa unaofanana kama wa wote wanne, kama gurudumu lililokuwa kwenye gurudumu lingine.
\v 11 wakati walipokuwa wakitembea, walienda katika pande zote nne bila kugeuka katika kwenye njia nyingine. Badala yake, popote kichwa kilipoelekea, walilifuata. Hawakugeuka kwenye njia yeyote nyingine walipokuwa wakienda.
\s5
\v 12 Mwili wao wote-pamoja na migongo yao, mikono yao, na mabawa yao-vilikuwa vimefunikwa kwa macho, na macho kufunika magurudumu manne kuzunguka pote pia.
\v 13 Nilikuwa nasikia, magurudumu yalikuwa yakiita, "Kuzunguka."
\v 14 Walikuwa na nyuso nne kila moja; uso wa kwanza ulikuwa uso wa kerubi, uso wa pili ulikuwa uso wa mtu, uso wa tatu ulikuwa uso wa simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa malaika.
\s5
\v 15 Kisha makerubi-hawa walikuwa viumbe hai nilivyokuwa nimeviona karibu na Keberi Kanali-wakainuka juu.
\v 16 Popote makerubi walipoenda, magurudumu yalienda karibu nao, na popote makerubi walipoinua juu mabawa yao kupaa juu kutoka kwenye nchi, magurudumu hayakugeuka. Yaliendelea kuwa karibu nao.
\v 17 Wakati makerubi waliposimama, magurudumu yalisimama pia, na wakati walipoinuka juu, magurudumu yaliinuka juu pamoja nao, kwa kuwa roho wa vile viumbe hai walikuwa kwenye magurudumu.
\s5
\v 18 Kisha utukufu wa Yahwe ukaja kutoka juu ya kizingiti cha nyumba na kusimama juu ya kerubi.
\v 19 Lile kerubi likaacha juu mabawa na kuinuka kutoka kwenye jicho langu wakati walipotoka nje, na yale magurudumu yakafanya vivyo hivyo karibu yao. Wakasimama upande wa mashariki kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, na utukufu wa Mungu wa Israeili ukaja juu yao kutoka juu.
\s5
\v 20 Hawa walikuwa viumbe hai ambao niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na Kebari Kanali, hivyo nilijua kwamba walikuwa makerubi!
\v 21 Walikuwa na macho manne kila mmoja na mabawa manne, na mfanano wa nyuso zao zilikuwa na mfanano wa mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao,
\v 22 na mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama nyuso nilizokuwa nimeziona kwa maono huko Keberi Kanali, na kila mmoja wao alienda mbele.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Kisha Roho akaniacha juu na kunileta kwenye lango la mashariki la nyumba ya Yahwe, kuelekea mashariki, na tazama, kwenye njia ya mlango wa lango kulikuwa na watu ishirini na tano. Nikamwona Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu, miongoni mwao.
\s5
\v 2 Mungu akanambia, "Mwana wa adamu, hawa ndio wale watu walioshauri udhalimu, na kuamua mipango miovu kwenye huu mji.
\v 3 Wakisema, 'Mda wa kujenga nyumba sio sasa; huu mji ni sufuria, na sisi ni nyama.'
\v 4 Kwa hiyo tabiri juu yao. Tabiri, mwana wa adamu."'
\s5
\v 5 Kisha Roho wa Yahwe akanijaza na akaniambia, "akisema: Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: kama usemavyo, nyumba ya Israeli; kwa kuwa najua kinachoendelea kwenye fikra zenu.
\v 6 Mmewazidisha watu mliowaua kwenye huu mji na kuijaza mitaa kwa hao.
\v 7 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Wale watu milowaua, ambao mmeilaza miili yao kati ya Yerusalemu, ni nyama, na huu mji ni sufuria. Lakini mnaenda kutolewa nje kutoka kati ya huu mji.
\s5
\v 8 Mmeuogopa upanga, kwa hiyo nauleta huo upanga juu yenu-huu ndio usemi wa Bwana Yahwe.
\v 9 Nitawatoa nje kutoka kati ya mji, na kuwaweka kwenye mikono ya wageni, kwa kuwa nitaleta hukumu dhidi yenu.
\v 10 Mtaanguka kwa upanga. Nitawahukumu kati ya mipaka ya Israeli hivyo mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 11 Huu mji hautakua sufuria yenu ya kupikia, wala hamtakuwa nyama ndani yake. Nitawahukumu kati ya mipaka ya Israeli.
\v 12 Kisha mtajua yakwamba mimi ni Yahwe, yule ambaye hamuishe kwenye amri zake na ambaye hamkuzishika sheria zake. Badala yake, mmebeba hukumu za mataifa wanayowazunguka."
\s5
\v 13 Ikawa kwamba nilipokuwa natabiri, Pelatia mwana wa Benaya, akafa. Hivyo nikaanguka kwenye uso wangu na kulia kwa sauti na kusema, "Ee, Bwana Yahwe, Je utayaharibu kabisa mabaki ya Israeli?"
\s5
\v 14 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 15 "Mwana wa adamu, ndugu zako! Ndugu zako! Watu wa ukoo wako na nyumba yote ya Israeli! Wote hao ndio hao ambao inasemekana wale wanaoishi Yerusalemu, 'Wako mbali sana kutoka kwa Yahwe! Hii nchi tulipewa sisi kama milki yetu.'
\s5
\v 16 Kwa hiyo sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: kote nimewapitisha mbali kati ya mataifa, na kote nimewasambaza kati ya nchi, bado nimekuwa patakatifu kwa ajili yao kwa mda kidogo kwenye nchi ambazo walizoenda.'
\v 17 Kwa hiyo sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Nitawakusanya kutoka kwa watu, na kuwakutanisha kutoka kwenye nchi mlizokuwa mmetawanyika, na nitawapatia nchi ya Israeli.'
\v 18 Kisha wataenda huko na kuondoa kila kitu chenye karaha na kila chukizo kutoka hiyo sehemu.
\s5
\v 19 Nitawapatia moyo mmoja, na nitaweka roho mpya kati yao. Nitaondoa moyo wa jiwe kutoka kwenye miili wao na kuwapatia moyo wa nyama,
\v 20 ili kwamba waweze kutembea kwenye amri zangu, watayachukua maagizo yangu na kuyatenda. Kisha watakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wao.
\v 21 Lakini kwa wale watembeao kwa kujifanya kuendeleza mambo yao ya karaha na machukizo yao, nitaleta tabia yao kwenye vichwa vyao-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\v 22 Makerubi wakainua mabawa yao na magurudumu yaliyokuwa karibu nao, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.
\v 23 Kisha utukufu wa Yahwe ukaenda juu kutoka katikati ya mji na kusimama kwenye mlima hata mashariki mwa mji.
\s5
\v 24 Roho akanichukua juu na kunileta hata Ukaldayo, hata uhamishoni, katika maono kutoka kwa Roho wa Mungu, na maono niliyokuwa nimeyaona yakaenda juu yakaniacha.
\v 25 Kisha nikawaambia wale watumwa mambo yote ya Yahwe niliyokuwa nimeyaona.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwana wa adamu, unaishi kwenye nyumba ya uasi, wana macho ya kuona lakini hawaoni; na wana masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa sababu wao ni nyumba iliyoasi.
\s5
\v 3 Kwa hiyo wewe mwanadamu, andaa mambo yako kwa ajili ya uhamisho, na anza kuondoka mchana usoni kwao, kwa kuwa nitakuhamisha kwenye uso wao kutoka sehemu yao kwenda sehemu nyingine. Labda wataanza kuona, kuwa wao ni nyumba ya uasi.
\s5
\v 4 Utatoa vitu vyako kwa ajili ya kuhamisha mchana katika macho yao; toka jioni kwenye macho yao kama ambavyo uendavyo kwenye uhamisho.
\v 5 Chimba shimo ukutani kwenye uso wa macho yao, na ingia ndani yake.
\v 6 Kwenye macho yao, chukua vitu vyako kwenye mabega yako, na uwalete kwenye giza. Funika uso wako kama ishara kwenye nyumba ya Israeli."
\s5
\v 7 Hivyo nikafanya hivyo, kama nilivyokuwa nimeamriwa. Nikatoa vitu vya uhamisho wakati wa mchana, na katika jioni nikachimba shimo hata kwenye ukuta kwa mkono. Nikachukua vitu vyangu kwenye giza, na kuviweka juu kwenye bega langu katika macho yao.
\s5
\v 8 Kisha neno la Yahwe likanijia asubuhi, likisema,
\v 9 Mwanadamu, je nyumba ya Israeli, ile ni nyumba ya uasi, hawakukwambia, 'Unafanya nini?'
\v 10 Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: hili tendo la kinabii linamhuusu mwana wa mfalme wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.'
\s5
\v 11 Sema, 'Mimi ni ishara kwenu. Kama nilivyofanya, itafanyika kwao; watakwenda uhamishoni na kuwa wafungwa.
\v 12 Yule mwana wa mfalme aliye miongoni mwao atavibeba vitu vyake kwenye bega lake katika giza, na ataenda zake kupitia kwenye ukuta. Watachimba kwenye ukuta na kutoa vitu vyao nje. Atafunika uso wake, hivyo hataona nchi kwa macho yake.
\v 13 Nitausambaza wavu wangu juu yake naye atanaswa kwenye mtego wangu; kisha nitamleta Babeli, ncha ya Wakaldayo, lakini hataiona. Atafia huko.
\s5
\v 14 Pia nitatawatawanya katika kila mwelekeo wale wote waliomzunguka wanaomsaidia na jeshi lake lote, na nitaufuata upanga nyuma yao.
\v 15 Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakapo watawanya kwenye nchi zote.
\v 16 Lakini nitaacha kuwaangamiza watu wachache kutoka miongoni mwao kutoka kwenye upanga, njaa, na tauni, hivyo wanaweza kukumbuka maovu yao yote katika nchi zao nilipowachukulia, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\v 17 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 18 "Mwanadamu, kula mkate wako kwa kutetemeka, na kunywa maji yako kwa mtetemo na hofu.
\s5
\v 19 Kisha waambie watu wa nchi, 'Bwana Yahwe asema hivi kuhusiana na wale wakaao Yerusalemu, na nchi ya Israeli: Watakula mikate yao kwa kutetemeka na kunywa maji yao wakiwa wanatetemeka, kwa kuwa nchi itaporwa vitu vyote viijazavyo kwa sababu ya kuwa kinyume na waishio huko.
\v 20 Hivyo ile miji iliyokuwa wenyeji itachukuliwa, na nchi itakuwa ukiwa; hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\v 21 Tena neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 22 "Mwanadamu, je ni mithali gani hii mlio nayo katika nchi ya Israeli mliyoisema, 'Siku zimerefushwa, na kila ono linaanguka'?
\v 23 Kwa hiyo, waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Nitaweka mwisho wa hii mithali, na watu wa Israeli hawataitumia tena.' Waambie, 'Siku zi karibu wakati kila ono litatimizwa.
\s5
\v 24 Kwa kuwa hakutakuwa na maono ya uongo yoyote wala upendeleo wa mgawanyiko kati ya nyumba ya Israeli.
\v 25 Kwa kuwa mimi Yahwe! Nimesema, na nitayatiza yale maneno nilyoyasema. Hakuna kitu kitakacho chelewesha. Kwa kuwa nitaongea hili neno katika siku zenu, nyumba ya uasi, na nitalitimiza! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.""
\s5
\v 26 Tena neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 27 "Mwanadamu! Tazama, nyumba ya Israeli imesema, 'Lile ono alionalo ni kwa siku nyingi kutoka sasa, na ametabiri kipindi kilicho mbali sana.'
\v 28 Kwa hiyo waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Neno langu halitacheleweshwa sana, lakini lile neno nililoliongea litatimizwa-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.'"
\s5
\c 13
\p
\v 1 Tena, neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wanaotabiri katika Israeli, na uwaambie wale wanotabiri nje ya fikra zao wenyewe, 'Lisikilizeni neno la Yahwe.
\v 3 Bwana Yahwe asema hivi: Ole wao manbii wajinga ambao wafwatao roho zao wenyewe, lakini wale wasioona kitu!
\v 4 Israeli, manabii zako wamekuwa kama mbeha kwenye aridhi iliyoharibiwa na vita.
\s5
\v 5 Hamkwenda kwenye nyufa katika ukuta uliozunguka nyumba ya Israeli kwa ajili ya kuukarabati, ili kupigana katika vita katika siku ya Yahwe.
\v 6 Watu wameona uongo na kufanya utabiri wa uongo, wale wasemao, "Hivi na hivi ndvyo Yahwe asemavyo." Yahwe hajawatuma, lakini hata hivyo wamewafanya watu kutumaini kwamba ujumbe wao utakuwa kweli.
\v 7 Je hamkusikia maono ya uongo na kufanya utabiri wa uongo, ninyi msemao, "Hivi na hivi ndivyo Yahwe asemavyo" Wakati mimi mwenyewe sikuongea?'
\s5
\v 8 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu mmesikia maono ya uongo na kuwaambia uongo-kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo dhidi yenu:
\v 9 Mkono wangu utakuwa juu yenu ninyi manabii mliodanganya maono na wale waliofanya unabii wa uongo. Hawatakuwepo kwenye kusanyiko la watu wangu, au kuandikishwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli; hawataenda kwenye nchi ya Israeli. Kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Bwana Yahwe!
\s5
\v 10 Kwa sababu hiyo, na kwa sababu wamewaongoza watu wangu kuwapotosha na kusema, "Amani!" wakati hakuna amani, wanajenga ukuta ambao wataupaka rangi ya chokaa.'
\v 11 Waambie wale wanaopaka chokaa ukuta, 'Utaanguka chini; kutakuwa na mvua ya kufurika, na nitaleta mvua ya mawe kuufanya uanguke chini, na upepo wa dhoruba kupuliza hata kuuvunja chini.
\v 12 Tazama, ukuta utaanguka chini. Je wengine hawakuwaambia, "Iko wapi chokaa mliyoipaka juu yake?"
\s5
\v 13 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitaleta upepo wa dhoruba katika ghadhabu yangu, na kutakuwa na mafuriko ya mvua kwenye ghadhabu yangu! Mvua ya mawe katika ghadhabu yangu itauharibu kabisa.
\v 14 Kwa kuwa nitaurarua chini ukuta ambao mlioufunika kwa chokaa, na nitaubomoa hata kwenye nchi na kuifunua misingi yake. Hivyo utaanguka, nanyi nyote mtaangamizwa katikati ya huo.
\s5
\v 15 Ndivyo nitakavouangamiza kwa ghadhabu yangu ukuta na wale walioupaka chokaa. Nitawaambia, "Ukuta hautaonekana tena, wala watu wanaoupaka chokaa-
\v 16 manabii wa Israeli wale waliotabiri kuhusu Yerusalemu na wale waliokuwa wameona amani kwa ajili yake. Lakini hakuna amani! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\v 17 Hivyo wewe, mwanadamu, weka uso wako dhidi ya binti za watu wako wale wanaotabiri kwa akili zao wenyewe, na kutabiri dhidi yao.
\v 18 Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa wanawake washonao hiziri kwenye kila sehemu ya mkono wao na kutengeza vitambaa vya shela kwa ajili ya vichwa vyao kwa kila kipimo, ili kuwinda watu. Je mtawawinda watu wangu ila kuokoa maisha yenu wenyewe?
\s5
\v 19 Ninyi mmenikufuru mbele ya watu wangu kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, kuwaua watu ambao hawakutakiwa kufa, na kuyalinda maisha ya wale ambao hawatakiwi kuendelea kuishi, kwa sababu ya uongo wenu kwa watu wangu walio wasikiliza.
\s5
\v 20 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Niko kinyume dhidi ya hirizi ambazo mlizozitumia kuyakamata kwa hila maisha ya watu kana kwamba wamekuwa ndege. Naam, nitazichana kutoka kwenye mikono yenu; na wale watu mlio watega kama ndege-nitawaacha waende huru.
\v 21 Nitavichana mbali vitambaa vya shela na kuwaokoa watu wangu kutoka kwenye mikono yangu, kwa hiyo hawatategwa tena kwenye mikono yenu. Mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 22 Kwa sababu mmeuvunja moyo wa mtu mwenye haki kwa uongo, ingawa hata mimi sikutamani kuvunjwa kwake moyo, na kwa sababu mmemtia moyo badala yake matendo ya mtu mwovu ili kwamba asitaweze kurudi kutoka kwenye njia yake kuokoa maisha yake-
\v 23 kwa hiyo hamtayaona tena maono ya uongo au kuendelea kufanya utabiri, kwa kuwa nitawaokoa watu wangu kutoka kwenye mkono wako. Nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.'"
\s5
\c 14
\p
\v 1 Baadhi ya viongozi wa Israeli wakaja kwangu na kuketi mbele yangu.
\v 2 Ndipo neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 3 "Mwanadamu, hawa watu wamchukua sanamu zao kwenye mioyo yao na kuweka pingamizi la uovu wao mbele ya nyuso zao wenyewe. Je naweza kuulizwa yote na wao?
\s5
\v 4 Kwa hiyo watangazie hivi na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kila mtu wa nyumba ya Israeli achukuaye sanamu moyoni mwake, au awekeye pingamizi la uovu mbele ya uso wake, na kisha yule ajaye kwa nabii-Mimi, Yahwe, nitamjibu kulingana na sanamu zake.
\v 5 Nitafanya hivi ili kwamba niweze kuirudisha nyumba ya Israeli katika mioyo yao ambayo ilikuwa mbali nami kwa ajili ya sanamu zao.'
\s5
\v 6 Kwa hiyo sema kwa nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tubuni na rudini kutoka kwenye sanamu zenu! Rudisheni nyuma nyuso zenu kutoka kwenye kachukizo yenu yote.
\s5
\v 7 Kwa kuwa kila mmoja kutoka kwenye nyumba ya Israeli na kila mmoja wa wageni wanaoishi katika Israeli ajitengaye nami, achukuaye sanamu zake kwenye moyo wake na kuweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake mwenyewe, na kisha yule ajaye kwa nabii kunitafuta-mimi, Yahwe, nitamjibu mimi mwenyewe.
\v 8 Hivyo nitauweka uso wangu juu ya huyo mtu na kumfanya ishara na mithali, kwa kuwa nitamkata kutoka kati ya watu wangu, na mtajua kuwa mimi ni Yahwe.
\s5
\v 9 Kama nabii atadanganywa na kuongea ujumbe, kisha Mimi Yahwe, nitamdanganya huyo nabii; Nitanyoosha mkono wangu na kumwangamizaku toka kati watu wangu Israeli.
\v 10 Watabeba uovu wao wenyewe; uwovu wa nabii utakua uleule kama uovu wa yule aulizaye kutoka kwake.
\v 11 Kwa sababu hiyo basi, nyumba ya Israeli haitaenda mbali kutoka kunifuata mimi wala kujinajisi wenyewe kupitia dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao-hivi ndivyo Yahwe asemavyo."'
\s5
\v 12 Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 13 "Mwanadamu, wakati nchi itakapo asi dhidi yangu kwa kufanya dhambi ili kwamba ninyooshe mkono wangu dhidi yake na kuvunja tegemea la mkate wake, na kuleta njaa juu yake na kukata mnyama kutoka kwenye nchi;
\v 14 kisha hata kama hawa watu watatu-Nuhu, Danieli, na Ayubu-walikuwa katikati ya nchi, wangeweza kuokoa maisha yao wenyewe kwa haki-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 15 Kama nikileta wanyama waovu kwenye nchi na kuwafanya wasizae hivyo basi itakuwa hakuna mtu asiweze kupita kwa sababu ya hao wanyama,
\v 16 kisha hata kama watu hawa hawa watatu ndani yake-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa hata watoto wao wala binti; isipokuwa maisha yao yataokoka, lakini nchi itakuwa ukiwa.
\s5
\v 17 Au nikileta upanga juu ya hiyo nchi na kusema, 'Upanga, nenda kwenye nchi na wakate wote mtu na mnyama kutoka huo',
\v 18 kisha hata kama hawa watu watatu watakuwa katikatai ya nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa japo watoto wao wala binti; ila tu maisha yao wenyewe yangeokolewa.
\s5
\v 19 Au kama nikipeleka tauni juu ya nchi na kumwaga dhahabu yangu juu yake kwa damu, ili kuwakata mtu na mnyama,
\v 20 kisha hata kama Nuhu, Danieli, na Ayubu wangekuwa kwenye hiyo nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuokoa hata watoto wao au binti; maisha yao pekee yangeokoka kwa haki.
\s5
\v 21 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: hakika nitafanya mambo makali sana kwa kuleta adhabu zangu nne-njaa, upanga, wanyama wa porini, na tauni-juu ya Yerusalemu kuwakata wote mtu na mnyama kutoka kwake.
\s5
\v 22 Kisha, tazama! mabaki yatasalia kwake, watakaokoka wataenda pamoja na wana na binti. Tazama! Watawatokea, na mtaona njia zao na matendo yao yakiwafariji kuhusu adhabu niliyoipeleka Yerusalemu, na kuhusu kila kitu kingine ambacho nilichopeleka juu ya nchi.
\v 23 Waliokoka watawafariji ninyi mtakapoona njia zao na matendo yao, hivyo mtayajua haya mambo niliyoyafanya juu yake, kwamba sijayafanya bure! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\c 15
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, liksema,
\v 2 "Mwanadamu, je ni jisni gani mzabibu ulivo bora kuliko mti na matawi yaliyomo kwenye miti katika msitu?
\v 3 Je watu huwa wanachukua mbao kutoka kwenye mzabbibu kufanyia chochote? au huwa wanatengenezea vitu kutokana na huo kuning'iniza chochote juu ya huo?
\v 4 Tazama! Kama umetupwa kwenye moto kama kuni, na kama moto umezichoma ncha zake zote na katikati pia, je unafaa kwa chochote?
\s5
\v 5 Tazama! Wakati ulipokuwa umekamilika, haukuweza kufanya chochote; kisha hakika, wakati moto ulipouchoma, lakini bado haukuweza kutengeneza kitu chochote kwa ajili ya matumizi yoyote.
\v 6 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: haufanani na miti katika misitu, niliyoitoa mzabibu kama kuni kwa moto; nitatenda vivyo hivyo mbele ya wakaao Yerusalemu.
\s5
\v 7 Kwa kuwa nitauweka uso wangu juu yao. Ingawa watatoka kutoka kwenye moto, bado moto utawala; hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakapoona uso wangu juu yenu.
\v 8 Kisha nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamefanya dhambi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\c 16
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, mwambie Yerusalemu kuhusu machukizo yake,
\v 3 na useme, 'Bwana Yahwe asema hivi kwa Yerusalemu: Mwanzo wako na kuzaliwa kwako kulichukua nafasi katika nchi ya Kanaani; baba yako alikuwa Mwamori, na mama yako alikuwa Mhiti.
\s5
\v 4 Katika siku ya kuzaliwa kwako, mama yako hakukata kitovu chako, wala hakukuosha kwenye maji usafishwe au kukuchua kwa chumvi, wala kukusitiri nguo.
\v 5 Hakuna jicho lililokuhurumia kufanya haya mambo kwa ajili yako, kukuhurumia wewe. Katika siku uliyozaliwa, kwa kuchukiwa uhai wako, ulitupwa nje uwandani.
\s5
\v 6 Lakini nilipita karibu nawe, nalikuona ukijinyonga kwa damu yako mwenyewe, "kubaki hai!"
\v 7 Nimekufanya ukue kama mmea katika shamba. Umeongezeka na kuwa mkubwa, na umekuwa mzuri wa wazuri. Maziwa yako yakawa thabiti, na nywele zako zikawa nyingi, ingawa ulikuwa uchi huna nguo.
\s5
\v 8 Nilipita karibu nawe tena, na nalikuona. Tazama! wakati wa upendo umefika kwako, hivyo nikatandika joho langu juu yako na kufunika uchi wako. Kisha nikaapa kwako na kukuleta kwenye agano-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na ukawa wangu.
\s5
\v 9 Basi nilikuosha kwa maji na kukufuta damu yako, na kukupaka mafuta.
\v 10 Nilikuvalisha nguo ya taraza na kukuwekea makuzi ya ngozi kwenye miguu yako. Nilikufungia kwa kitani kizuri na kukufunika kwa hariri.
\v 11 Kisha nalikupamba kwa vito, na kukuvalisha vikuku kwenye mikono yako, na mkufu kwenye shingo yako.
\v 12 Nalitia hazama katika pua yako na hereni katika masikio yako, na taji nzuri juu ya kichwa chako.
\s5
\v 13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, na ulivaa kitani safi, hariri, na ngu za taraza; ulikula unga mzuri, asali, na mafuta, na ulikuwa mzuri sana, na ukawa malkia.
\v 14 Umaarufu wako ukaenda miongoni mwa mataifa kwa sababu ya uzuri wako, kwa kuwa ulikuwa mkamili katika ukuu niliokuwa nimekupa-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 15 Lakini ulitumaini uzuri wako, na ukafanya kama kahaba kwa sababu ya umaarufu wako; umeyamwaga matendo yako ya kikahaba kwa kila aliyepita karibu, ili kwamba uzuri wako uwe wake.
\v 16 Kisha ulichukua nguo zako na pamoja nao umepatengeneza mahali pa juu kwa ajili yako palipambwa kwa rangi tofauti tofauti, na hapo ulifanya kama kahaba. Hii haitatokea. Wala haitatokea.
\s5
\v 17 Umevichukua vito vizuri vya dhahabu na fedha nilizowapatia, na umejitengenezea sanamu za wanaume, na umefanya pamoja nao ukahaba afanyao.
\v 18 Ulichukua nguo zako za tarizi na kuwafunika, na kuwawekea mafuta yangu na manukato mbele yao.
\v 19 Mkate wangu niliokupatia-ulitengenezwa kwa unga mzuri, mafuta, na asali-umeviweka mbele yao kwa ajili ya kunukia harufu nzuri, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyotokea-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 20 Kisha uliwachukua watoto wako ulionizalia, na kuwatoa sadaka kwa picha ili waliwe kama chakula. Je! matendo yako ya kikahaba ni kitu kidogo?
\v 21 Umewachinja watoto wangu na kuwatupia kwenye moto.
\v 22 Katika machukizo yako yote na matendo yako ya kikahaba hukutafakari kuhusu siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi na bila nguo kama kama umepigwa katika damu.
\s5
\v 23 Ole! Ole wako! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwahiyo, zaidi ya hapo kwa haya maovu yote,
\v 24 umejijengea chumba cha chini kwa chini katika kila sehemu ya watu wengi.
\s5
\v 25 Umepajenga mahali pako palipoinuka kwenye kichwa cha kila njia na kuunajisi uzuri wako, kwa kuwa umeutoa mwili wako kwa kila mtu apitaye karibu na umefanya matendo mengi zaidi ya ukahaba.
\v 26 Umetenda kama kahaba pamoja na Wamisri, tamaa ya jirani zako, na umetenda matendo mengi zaidi ya kikahaba, ili kuchochea hasira yangu.
\s5
\v 27 Tazama! Nitakunyooshea mkono wangu na kupunguza chakula chako. Nitauchukua uhai wako juu ya adui zako, binti za Wafilisti, ambao walikuwa na haya ya tabia yako ya uchafu.
\v 28 Umetenda kama kahaba pamoja na Waashuru kwa sababu hukuweza kuridhika. Umetenda kama kahaba na bado hukuridhika.
\v 29 Umefanya matendo mengi zaidi ya kikahaba katika nchi ya jamii ya wana maji wa Ukaldayo, na wala hukuridhika kwa hayo.
\s5
\v 30 Jinsi moyo wako ulivyo dhaifu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwamba utaweza kuyafanya haya mambo yote, matendo ya aibu ya kikahaba?
\v 31 Mmepajenga mahali penu pa juu kwenye kichwa cha kila mtaa na kufanya chumba cha chini kwa chini katika kila sehemu ya watu wengi. Bado hukuwa kama kahaba kwa sababu ulikataa kulipwa ujira.
\s5
\v 32 Wewe mwanamke mzinifu, wewe upokeaye wageni badala ya mume wako.
\v 33 Watu hulipa kwa kila kahaba, lakini wewe huwapa mshara wako wapenzi wako wote na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote kwa matendo yako ya kikahaba.
\v 34 Hivyo kuna tofauti kati yako na hao wanawake wengine, kwa kuwa hakuna hata mmoja ajaye kwako kukuuliza kulala pamoja nao. Badala yake, unawalipa. Hakuna akulipaye.
\s5
\v 35 Kwa hiyo, wewe kahaba, lisikilize neno la Yahwe.
\v 36 Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umemwaga tamaa yako na kuonyesha sehemu zako za siri kupitia matendo yako ya ukahaba pamoja na wapenzi wako wote pamoja na sanamu zako za chukizo, na kwa sababu ya damu ya watoto wako uliyowapatia sanamu zako,
\v 37 kwa hiyo, tazama! Nitawakusanya wapenzi wako wote uliokutana nao, wote ambao uliowapenda na wote uliowachukia, na nitawakusanya juu yako kila upande. Nitawaonyesha wazi sehemu zako za siri hivyo wanaweza kuona uchi wako wote.
\s5
\v 38 Kwa kuwa nitakuadhibu kwa uasherati na kumwaga damu, na nitaleta juu yako damu ya hasira yangu na hasira kali.
\v 39 Nitakutia kwenye mikono yao hivyo watakutupa chini kwenye chumba cha chini kwa chini na kupavunja mahali pako pa juu na watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vyote. watakuacha uchi bila nguo.
\s5
\v 40 Kisha wataleta kundi la watu juu yako na kukupiga kwa mawe, na kukukata kwa panga zao.
\v 41 Watachoma nyumba zako na kufanya matendo mengi ya adhabu juu yako kwenye uso wa wanawake wengi, kwa kuwa nitakusimamisha ukahaba wako, na hutawalipa tena wapenzi wako.
\v 42 Kisha nitatuliza ghadhabu yangu juu yako; hasira yangu itakuacha, kwa kuwa nitaridhika, na sitakuwa na hasira tena.
\s5
\v 43 Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako na kunifanya nitetemeke kwa hasira kwa sababu ya haya mambo yote, kwa hiyo, tazama! Mimi mwenyewe nitashusha kwa kichwa chako mwenyewe adhabu kwa kile ulichokifanya-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Hutaongeza ukahaba kwa matendo yako yote ya machukizo?
\s5
\v 44 Tazama! Kila mtu azungumzaye Mithali kuhusu wewe atasema, "Kama alivyo, hivyo pia ni binti yake."
\v 45 Wewe ni binti wa mama yako, amchukiaye mume wake na mtoto wake, na wewe ni dada wa dada zako aliyewachukia waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako alikuwa Mwamori.
\s5
\v 46 Dada yako mkubwa alikuwa Samaria na binti zake walikuwa wale waliokuwa wakiishi kaskazini, wakati dada yako mdogo alikuwa ni yule aliyekuwa akiishi kusini mwako, ambaye ni, Sodoma na binti zake.
\s5
\v 47 Hukuenenda katika njia zao na kuchukua tabia zao na matendo yao, lakini katika njia zako zote ulikuwa mbaya zaidi kuliko walivyokuwa wao.
\v 48 Kama niishivyo- hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-dada yako Sodoma na binti zake, hawajafanya uovu mwingi kama wewe ulivyofanya na binti zako walivyofanya.
\s5
\v 49 Tazama! Hii ilikuwa dhambi ya dada yako Sodoma: Alikuwa na kiburi katika mafanikio yake, uzembe na kutojali kuhusu chochote. Hakuitia nguvu mikono ya maskini na watu wahitaji.
\v 50 Alikuwa na kiburi na kufanya machukizo mbele yangu, hivyo niliwatoa kama nilivyoona.
\s5
\v 51 Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi zako; badala yake, umefanya machukizo mengi kuliko walivyofanya, na umewonyesha hayo dada zako walikuwa bora kuliko wewe kwa sababu ya machukizo yako uyafanyayo!
\v 52 Hasa wewe, umeonyesha aibu yako mwenyewe; kwa njia hii umewaonyesha dada zako walikuwa bora kuliko wewe, kwa sababu ya dhambi ulizozifanya katika hayo machukizo yako yote. Dada zako sasa wanaonekana bora kuliko wewe. Hasa wewe, umeonyesha aibu yako mwenyewe, kwa njia hii umewaonyesha kwamba dada zako walikuwa bora kuliko wewe.
\s5
\v 53 Kwa kuwa nitarudisha masalia wao-masalia ya Sodoma na binti zake, na masalia ya Samaria na binti zake; lakini masalia yako yatakuwa miongoni mwao.
\v 54 Kwa kufikiria haya mambo utaonyesha aibu yako; utakuwa mnyenyekevu kwa sababu ya kila kitu ulichokifanya, na kwa njia hii utakuwa faraja kwao.
\v 55 Hivyo dada yako Sodoma na binti zake watarudishwa kwenye hali yao ya zamani, na Samaria na binti zake watarudishwa kwenye mashamba yao ya zamani. Kisha wewe na binti zako watarudishwa kwenye hali yako ya kawaida.
\s5
\v 56 Sodoma dada yako hakutajwa hata kwa kinywa chako katika siku ulipojiinua,
\v 57 kabla uovu wako haujafunuliwa. Lakini sasa wewe ni kitu cha dharau kwa binti za Edomu na binti wote wa Wafilisti waliomzunguka. Watu wote wanakudharau wewe.
\v 58 Utaonyesha aibu yako na matendo yako ya machukizo! -hivi ndivyo Yahwe asemavyo!
\s5
\v 59 Bwana Yahwe asema hivi: Nitashughulika na wewe kama unavyostahili, wewe uliyedharau kiapo chako kwa kulivunja agano.
\s5
\v 60 Lakini mimi mwenyewe nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe katika siku za ujana wako, nitaliimarisha agano la milele pamoja na wewe.
\v 61 Kisha utazikumbuka njia zako na kuona aibu utakapo wapokea dada zako wakubwa na dada zako wadogo. Nitakupatia wao kama binti zako, lakini kwa sababu ya agano lako.
\s5
\v 62 Mimi nitaweka imara agano lango pamoja nawe, nawe utajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\v 63 Kwa sababu ya haya mambo, utakumbuka kila kitu na kuona aibu, hutafungua mdomo wako tena kuongea kwa sababu ya aibu yako, wakati nitakapokusamehe kwa yale yote uliyoyafanya-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\c 17
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, tega kitendawili na sema fumbo kwa nyumba ya Israeli.
\v 3 Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tai mkubwa pamoja na mabawa makubwa na vipapatio virefu, mwenye kujaa manyoya, na aliyekuwa na rangi nyingi alienda Lebanoni na kuchukua kilele cha mti wa mkangazi.
\v 4 Akakata ncha za matawi na kuzichukua hata nchi ya Kanaani; akaipanda katika mji wa manahodha.
\s5
\v 5 Pia akachukua mbegu ya nchi na kuipanda katika udongo wenye rutuba. Akaiweka kando ya maji mengi kama mti umeao karibu na maji.
\v 6 Kisha ukachipusha na mzabibu wenye kusambaa chini kwenye aridhi. Matawi yake yakamwelekea yeye, na mizizi yake ikakua chini yake. Hivyo ukawa mzabibu na kuzaa matawi na kutoa matawi.
\s5
\v 7 Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa wenye mabawa makubwa na manyoya mengi. Tazama! Huu mzabibu ukabadilisha mizizi yake kumwelekea tai, na ukasamabaza matawi yake kumwelekea tai kutoka mahali ulipokuwa umepandwa basi upate kumwagiliwa.
\v 8 Ulikuwa umepandwa kwenye udongo mzuri kando ya maji mengi hivyo ungezaa matawi na kuanza kutoa matunda, ili kuwa mzabibu mzuri kabisa.'
\s5
\v 9 Waambie watu, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! huo utafanikiwa? Je! Haitaing'oa mizizi yake na kuyakata matunda yake ili kwamba unyauke, na majani yake yote mabichi yanyauke? Hakuna jeshi imara au watu wengi watahitajika kuivuta kwa mizizi yake.
\v 10 Basi tazama! Baada ya kuwa umepandwa, je utakuwa? Je hautanyauka wakati upepo wa mashariki utakapoupiga? Utanyauka kabisa katika kiwanja chake."'
\s5
\v 11 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 12 "Waambie nyumba ya uasi, 'Je! hamjui haya mambo yana gana gani? Tazama! Mfalme wa Babeli amekuja Yerusalemu na kumchukua mfalme wake na wakuu wake na kuwaleta kwake mpaka Babebli.
\s5
\v 13 Kisha akauchukua ukoo wa kifalme, akafanya agano pamoja naye, na kumleta chini ya kiapo. Akawachukua watu wa nchi wenye nguvu,
\v 14 basi ufalme uwe duni na usijiinue wenyewe. Kwa kulitunza agano lake nchi itaokoka.
\s5
\v 15 Lakini mfalme wa Yerusalemu ameasi juu yake kwa kupeleka mabalozi kwenda Misri ili kujipatia farasi na jeshi. Je! Atafanikiwa? Je! yeye anayeyafanya haya mambo ataokoka?
\v 16 Kama niishivyo! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-atakufa hakika katika nchi ya mfalme aliyemfanya mfalme, yule mfalme ambaye aliyekidharau kiapo chake, na ambaye aliyevunja agano lake. atakufa kati ya Babeli.
\s5
\v 17 Farao na jeshi lake lenye nguvu na kusanyiko la watu wengi kwa ajili ya vita hawatamlinda katika vita, wakati jeshi la Wababeli watakapojenga tuta la ngome na kuta za ngome ili kuyaharibu maisha ya wengi.
\v 18 Kwa kuwa mfalme amedharau kiapo chake kwa kulivunja agano. Tazama, ameunyoosha kwa mkono wake ili kufanya ahadi na bado ameyafanya haya mambo yote. Hataokoka.
\s5
\v 19 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, Je! hiki hakikuwa kiapo changu kwamba alidharau agano langu alilo livunja? Basi nitaleta nitamwadhibu juu ya kichwa chake!
\v 20 Nitausambaza wavu wangu juu yake, na atanaswa katika wavu wangu wa kutegea. Kisha nitamleta hata Babeli na kuzitekeleza hukumu juu yake huko kwa ajili ya uhaini wake alioufanya amenisaliti!
\v 21 Wakimbizi wake wote katika majeshi yake yataanguka kwa upanga, na wale watakaobakia watatawanyika kila mahali. Kisha utajua yakwamba mimi ni Yahwe; nimesema hili litatokea."
\s5
\v 22 Bwana Yahwe asema hivi, 'Basi mimi mwenyewe nitaichukua sehemu ya juu ya mti wa mkangazi, na nitaupanda mbali na matawi yake laini. Nitaukata, na mimi mwenyewe nitaupanda juu ya mlima mrefu.
\v 23 Nitaupanda juu ya milima ya Israeli hivyo utazaa matawi na kuzaa matunda, na utakuwa mkangazi wa fahari ili kwamba kila ndege arukaye ataishi chini ya huo. Watajenga viota chini ya kivuli cha matawi yake.
\s5
\v 24 Kisha miti yote ya shambani itajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeishusha miti mirefu na nimeiinua juu miti mifupi. Naunyausha mti mbichi na kuufanya mti mkavu kuchanua. Mimi Yahwe, nimesema hivyo hii itatokea; nami nimelifanya hili.'"
\s5
\c 18
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,
\v 2 "Je mnamaana gani, ninyi mliotumia hii mithali kuhusiana na nchi ya Israeli na kusema, 'Wababa wamekula zabibu mbichi, na meno ya watoto imetiwa ganzi'?
\s5
\v 3 Kama nishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hakutakuwa na fursa yoyote tena kwa ajili yenu kuitumia hii mithali katika Israeli.
\v 4 Tazama! Kila uhai ni mali yangu-uhai wa baba na uhai wa mwana pia, ni mali yangu! roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa!
\s5
\v 5 Itasemwaje kuhusu mtu mwenye haki na achukuaye yaliyo halali na haki-
\v 6 kama asipokula juu ya milima au kuinua macho yake kwa sananmu za nyumba ya Israeli, na hakumnajisi mke wa jirani yake, wala kumsemesha mwanamke katika kipindi chake cha mwezi, je! Yu mwenye haki?
\s5
\v 7 Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakumkandamiza yeyote, na kumrudisha mdeni wake kwa kile kilichokuwa kimewekwa kwa ajili ya rehani, na hakuiba lakini kuwapatia chakula wenye njaa na kuwafunika uchi kwa nguo, je yu mwenye haki?
\v 8 Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakuchukua faida kubwa kwa ile pesa aliyokopa, na hakuchukua faida kubwa kwa kile alichokiuza?
\v 9 Amesemwa kwamba amechukua yaliyo halali na kuimarisha uaminifu kati ya watu. Kama huyo mtu akitembea katika sheria zangu na kuzishika hukumu zangu kufanya kwa uaminifu, kisha ahadi kwa ajili ya mtu mwenye haki ni hii: Ataishi hakika! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 10 Lakini akizaa mwana mnyang'anyi mmwaga damu na kufanya mengi katika haya mambo kama yalivyotajwa hapa,
\v 11 hata kama baba yake hakufanya mojawapo katika haya mambo, lakini akala juu ya milima na akamnajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
\s5
\v 12 Huyu mtu huwakandamiza maskini na wahitaji, na huwakamata na kuwanyang'anya, na hawarudishii dhamana, na huyanua macho yake kwa sanamu na kufanya matendo maovu,
\v 13 na hukopesha pesa kwa faida ya juu sana na kufanya faida kubwa juu ya anachokiuza, Je! huyo mtu ataishi? Hakika hataishi! Atakufa hakika na damu yake itakuwa juu yake kwa sababu amefanya haya mambo ya chuki.
\s5
\v 14 Lakini Tazama! tuseme kuna mtu aliyezaa mwana, na mwana wake huona dhambi zote za baba yake alizozifanya, na kupitia kuziona, hakuyafanya hayo mambo.
\v 15 Huyo mwana hakula juu ya milima, na hakuinua macho yake kwa sanamu za nyumba ya Israeli, na hakumtia unajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
\s5
\v 16 Yule mwana hakumkandamiza yeyote, au kutwaa dhamana, au kupoteza vitu, lakini badala yake kutoa chakula chake kwa wenye njaa na kuwafunika wenye uchi kwa nguo.
\v 17 Huyo mwana hakumkandamiza yeyote au au kuchukua faida ambayo ni ya juu sana au kufanya manufaa kwa ajili ya mkopo, lakini ameyashika maagizo yangu na kuenenda sawa sawa na sheria zangu; huyo mwana hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake: Ataishi hakika!
\s5
\v 18 Baba yake, kwa kuwa aliwakandamiza wengine kwa nguvu nyingi na kumnyang'anya ndugu yake, na kufanya yasiyo mema miongoni mwa watu wake-tazama, atakufa katika uovu wake.
\s5
\v 19 Lakini ninyi husema, 'Kwa nini mwana asibebe uovu wa baba yake?' Kwa sababu mwana hubeba yaliyo halali na haki na kuzitunza amri zangu; huzifanya. Ataishi hakika!
\v 20 Yule atendaye dhambi, ndiye ambaye atakufa. Mwana hatabeba uovu wa baba yake, na baba hatabeba uovu wa mwana wake. Haki ya yule atendaye haki itakuwa juu yakwe mwenyewe, na uovu wa mwenye uovu utakuwa juu yake mwenyewe.
\s5
\v 21 Lakini kama mwovu ageukapo kutoka dhambi zake zote alizofanya, na kuzitunza sheria zangu zote na kufanya yaliyo halali na haki, kisha hakika ataishi na hatakufa.
\v 22 Makosa yote aliyoyafanya hayatakumbukwa juu yake. Ataishi kwa hiyo haki aliyoitenda.
\s5
\v 23 Je! Nitafurahia juu ya kifo cha mwovu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na sio katika kugeuka kwake kutoka njia yake ili kwamba aweze kuishi?
\s5
\v 24 Lakini kama mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki yake na kufanya maovu na kutenda machukizo kama machukizo yote ambayo mtu mwovu afanyayo, basi ataishi? Haki yake yote aliyoifanya haitakumbukwa wakati atakaponisaliti katika uhaini wake. Hivyo atakufa katika dhambi alizofanya.
\s5
\v 25 Lakini ninyi husema, 'Njia ya Bwana si sawa!' sikilizeni, nyumba ya Israeli! Je njia zangu haziko sawa? Je si njia ambazo haziko sawa?
\v 26 Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye makosa yake, na kufanya maovu na kufa kwa sababu ya hayo, kisha atakufa katika uovu ambao alioufanya.
\s5
\v 27 Lakini wakati mtu mwovu ageukapo kutoka uovu wake alioufanya na kufanya yaliyo halali na haki, kisha ataulinda uhai wake.
\v 28 Kwa kuwa ameona na kugeuka kutokana na makosa yake yote ambayo aliyoyafanya. Hakika ataishi, na hatakufa.
\s5
\v 29 Lakini nyumba ya Israeli husema, 'Njia ya Bwana haiko sawa!' Ni namna gani njia zangu si sawa, nyumba ya Israeli? Ni njia zenu ndizo si sawa.
\v 30 Kwa hiyo nitamuhukumu kila mtu miongoni mwenu kulingana na njia zake, nyumba ya Israeli! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Tubuni na rudini kutoka kwenye makosa yenu yote ili kwamba wasiwe kikwazo cha uovu dhidi yenu.
\s5
\v 31 Tupilia mbali makosa yenu yote mliyoyafanya; jifanyieni moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, nyumba ya Israeli?
\v 32 Kwa kuwa sifurahii kifo cha yule afaye-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo tubuni na muishi!"
\s5
\c 19
\p
\v 1 "Tena wewe, chukua maombolezo juu ya viongozi wa Israeli
\v 2 na sema, 'Mama yako alikuwa nani? Simba jike mmoja, aliishi na mtoto wa simba dume; katikati ya simba wadogo, aliwalisha watoto wake.
\v 3 Alimlea mmoja wa wale watoto kurarua wanyama wengine, na kisha alijifunza jinsi ya kuwinda watu na kuwala.
\v 4 Kisha mataifa wakasikia kuhusu yeye. Akakamatwa kwenye mtego wao, na wakamleta kwa kulabu hata nchi ya Misri.
\s5
\v 5 Kisha alipoona kwamba ingawa alikuwa akimsubiri arudi, matumaini yake sasa yalienda, hivyo alimchukua mtoto wake wengine katika watoto wake na kumlea hata kuwa mwana simba.
\v 6 Huyu mwana simba alitembea huku na huku katikati ya simba. Akawa mwana simba na kujifunza kuwinda mawindo; akala watu.
\v 7 Akawakamata wajane na kuiharibu miji. Nchi na viijazavyo vilitelekezwa kwa sababu ya sauti ya kunguruma kwake.
\s5
\v 8 Lakini mataifa yakaja juu yake kutoka mikoa yote; wakatengeneza nyavu juu yake. Akakamatwa kwenye mtego wao.
\v 9 Kwa kulabu wakamuweka kwenye tundu na kisha wakamleta hata kwa mfalme wa Babeli. Wakamleta hata kwenye ngome imara ili kwamba sauti yake isiweze kusikika juu ya milima ya Israeli.
\s5
\v 10 Mama yako alikuwa kama mzabibu uliopandwa kwenye damu yako karibu na maji. ulizaa matunda na kujaa matawi kwa sababu ya wingi wa maji.
\v 11 Ulikuwa na matawi imara yaliyokuwa yakitumika kwa ajili ya fimbo ya utawala, na kipimo chake kiliinuka juu ya matawi, na kina wake ulionekana kwa ukubwa wa majani yake.
\s5
\v 12 Lakini mzabibu uling'olewa kwa ghadhabu na kutupwa chini hata aridhini, na upepo wa mashariki uliuvunja na kunyauka na moto ukavila.
\v 13 Hivyo sasa, umepandwa jangwani, kwenye nchi ya ukame na kavu.
\s5
\v 14 Kwa kuwa moto ulitoka kwenye matawi makubwa na kuyala matunda yake. Hakuna tawi imara juu yake, hakuna fimbo ya kifalme kutawala.' Haya ni maombolezo na yataimbwa kama maombolezo."
\s5
\c 20
\p
\v 1 Ikawa ikaja katika mwaka wa saba, siku ya kumi ya mwezi wa tano, wazee wa Israeli wakaja kumuuliza Yahwe na kuketi mbele yangu.
\s5
\v 2 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 3 "mwanadamu, tangaza kwa wazee wa Israeli na uwaambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! Mmekuja kuniuliza swali? Kama niishivyo, sitaulizwa swali na ninyi! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
\s5
\v 4 Je! Utawahukumu? Utamuhukumu, mwanadamu? Wajulishe kuhusu machukizo ya baba zao.
\v 5 Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyoichagua Israeli na kuinua mkono wangu kuapa kiapo kwa uzao wa nyumba ya Yakobo, na kufanya kujulikana mimi mwenyewe kwao katika nchi ya Misri, wakati nilipoinua mkono wangu kuapa kiapo kwao. Nalisema, "Mimi ni Yahwe Mungu wenu"-
\v 6 siku hiyo niliinua mkono wangu kuapa kiapo kwa ajili yao kwamba nitawatoa kutoka nchi ya Misri kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimeichagua kwa umakini kwa ajili yao. Ilikuwa ikitiririka maziwa na asali; ilikuwa nzuri sana utukufu miongoni mwa nchi mbali mbali.
\s5
\v 7 Nikawaambia, "Kila mtu atupilie mabli mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake na sanamu za Misri. Msijitie unajisi; mimi ni Yahwe Mungu wenu."
\s5
\v 8 Lakini wameasi juu yangu hawakuwa tayari kunisikiliza. Kila mtu hakutupilia mbali mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake wala kwa ajili ya sanamu za Misri, hivyo nikaona nimwage ghadhabu yangu juu yao kukamilisha hasira yangu miongoni mwao katikati ya nchi ya Misri.
\v 9 Nilifanya kwa ajili ya jina langu ili lisinajisiwe katika macho ya mataifa ambao walikaa pamoja nao. Nilijifanya mwenyewe kujulikana kwao, katika macho yao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
\s5
\v 10 Basi nikawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta kwenye jangwa.
\v 11 Kisha nikawapa amri zangu na kufanya maagizo yangu kujulikana kwao, kwa kila mwanadamu atakayezishika ataishi.
\v 12 Pia nikawapatia Sabato zangu kama ishara kati yangu na wao, ili wajue kwamba mimi ni Yahwe niwafanyao wawe watakatifu.
\s5
\v 13 Lakini nyumba ya Israeli imeasi dhidi yangu jangwani. Hawakuenenda katika amri zangu; badala yake, wameyakataa maagizo yangu, ambayo mwanadamu ataishi kama akiyatii. Wamezinajisi Sabato zangu sana, basi nikasema nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani ili kuwamalliza.
\v 14 Lakini nilifanya kwa ajili ya jina langu hivyo lisinajisiwe katika macho ya mataifa, ambao niliwatoa mbele ya macho yao kutoka Misri.
\s5
\v 15 Basi mimi mwenyewe pia nimeinua mkono wangu kuapa kiapo kwao jangwani sitawarudisha kwenye nchi ile niliyokuwa naenda kuwapatia, nchi inayotiririkayo maziwa na asali, ambayo ilikuwa nzuri sana ambayo ni nzuri kati ya nchi zote.
\v 16 Nimeapa hivi kwa sababu walikataa maagizo yangu na kutotembea katika amri zangu, na wazikufuru Sabato zangu.
\v 17 Lakini jicho langu likawahurumia kutokana na uharibifu na sikuwaangamiza jangwani.
\s5
\v 18 Nikawaambia watoto wao jangwani, "Msitembee kutokana na amri za wazazi wenu; msiweke maagizo yao au kujinajisi wenyewe kwa sanamu.
\v 19 Mimi ni Yahwe Mungu wenu, tembeeni katika amri zangu; tunzeni maagizo yangu na kuyatii.
\v 20 Zitunzeni Sabato zangu takatifu ili kwamba zitakuwa ishara kati yangu na ninyi, hivyo basi mtajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wenu."
\s5
\v 21 Lakini watoto wao waliniasi. Hawakutembea kwenye sheria zangu au kushika maagizo yangu, ambazo mwanadamu ataishi kama akizitii. Wamezinajisi Sabato zangu, hivyo nimeamua kumwaga ghadhabu yangu juu yao kutimiza ghadhabu yangu dhidi yao katika jangwa.
\v 22 Lakini niliurudisha mkono wangu na kutenda kwa ajili ya jina langu, hivyo lisitiwe unajisi katika macho ya mataifa ambao mbele ya macho yao niliwatoa Waisraeli.
\s5
\v 23 Mimi mwenyewe pia nimeuinua mkono wangu kuapa juu yao jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya maifa na kuwatawanya miongoni mwa nchi mabali mbali.
\v 24 Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa hawakuzitii amri zangu, na tangu walipo zikataa sheria zangu na kuzinajisi Sabato zangu. Macho yao yalizitamani sanamu za baba zao.
\s5
\v 25 Kisha niliwapa amri ambazo hazikuwa nzuri, na maagizo ambayo hawakuweza kuishi kwayo.
\v 26 Nikawafanya unajisi kwa zawadi zao wakati walipofanya dhabihu za kila limbuko la tumbo la uzazi na kutupa kwenye moto. Nalifanya hivi ili kuwaogofya hivyo wangeweza kujua kwamba mimi ni Yahwe!'
\s5
\v 27 Kwa hiyo, mwanadamu, waambie nyumba ya Israeli na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika hili pia baba zenu walinikufuru wakati walipokuwa sio waaminifu kwangu.
\v 28 Wakati nilipowaleta kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimewaapia kuwapatia, na kisha popote walipoona jiwe lolote refu na mti wenye majani, walitoa sadaka zao, walinikasirisha kwa sadaka zao, na huko pia walichoma ubani wao wa kunukia na kumwaga sadaka zao za kinywaji.
\v 29 Kisha nikawaambia, "Nini maana ya mahali palipoinuka ambapo mmeleta sadaka huko?" Hivyo jina lake linaitwa Bana hata leo.'
\s5
\v 30 Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! Kwa nini unajinajisi mwenyewe kwa njia za baba zako? Kwahiyo kwa nini unatenda kama makahaba, kutafuta kwa ajili ya mambo ya machukizo?
\v 31 Kwa kuwa wakati mtoapo zawadi zenu na kuwaweka watoto wenu kwenye moto, siku hii mnajitia unajisi pamoja na sanamu zenu zote. Kwa hiyo kwa nini niwaache mniulize mimi, nyumba ya Israeli? Kama niishivyo-Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Sitawaacha mniulize swali.
\v 32 Mawazo yanayoumbika kwenye moyo wako hayatatokea kamwe. Mmesema, "Ngoja tuwe kama mataifa mengine, kama koo za nchi nyingine waabuduo mti na jiwe."
\s5
\v 33 Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Nitatawala hakika juu yenu kwa mkono wenye nguvu, mkono ulionyooshwa, na ghadhabu itakayomwagwa juu yenu.
\v 34 Nitawatoa kutoka kwa watu wengine na kuwakusanya kutoka kwenye nchi mlizotawanyika ndani mwao. Nitafanya hivi kwa mkono hodari na kwa ghadhabu iliyomwagika.
\v 35 Kisha nitawaleta kwenye jangwa la watu, na huko nitawahukumu uso kwa uso.
\s5
\v 36 Kama nilivyo wahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, hivyo pia nitawahukumu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 37 Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, na nitawafanya kutii maagizo yangu ya agano.
\v 38 Nitawasafisha kutoka miongoni mwenu maasi na wale ambao walionichukiza. Nitawatoa kutoka nchi ambayo wanayoishi kama wageni, lakini hawataingia kwenye nchi ya Israeli. Kisha mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 39 Basi kwenu, nyumba ya Israeli, Bwana Yahwe asema hivi: Kila mmoja wenu ataenda kwa sanamu zake mwenyewe. Muwaabudu kama mtakataa kunisikiliza, lakini hamtalikufuru tena jina langu takatifu kwa zawadi zenu na sanamu zenu.
\s5
\v 40 Kwa kuwa juu ya mlima wangu mtakatifu, juu ya kilele cha mlima wa Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-wote wa nyumba ya Israeli mtaniabudu huko katika nchi. Nitabarikiwa kwa kutaka sadaka zenu huko, na pia malimbuko yenu ya shukrani pamoja na vitu vyenu vyote vitakatifu.
\v 41 Nitawapokea kama harufu nzuri ya ubani wakati nitakapowatoa kutoka wale watu na kuwakusanya toka nchi ambazo mlizotawanyika. Nitajifunua mimi mwenyewe kama mtakatifu ndani yenu kwa ajili ya mataifa waone.
\s5
\v 42 Kisha, wakati nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, kwenye nchi ambayo niliuinulia mkono wangu kuapa kuwapatia baba zenu, mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\v 43 Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya huko, na matendo yenu yote machafu mliyoyafanya wenyewe, na mtajichukia wenyewe katika macho yenu kwa matendo yenu yote maovu mliyoyafanya.
\v 44 Hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe nifanyapo haya kwenu kwa ajili ya jina langu, sio kwa njia zenu mbaya au matendo yenu mabovu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\v 45 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 46 "Mwanadamu, weka uso wako kuelekea nchi za kusini, na kuongea juu ya kusini; tabiri juu ya msitu wa Negebu.
\v 47 Uuambie msitu wa Negebu, 'Hivi ndivyo Yahwe asemavyo-Bwana Yahwe asema hivi: Tazama, nitaweka moto ndani yako. Utakula kila mti mbichi na kila mti mkavu ndani yako. Miali ya moto haitazimika; na kila uso utokao kusini hata kaskazini utateketezwa kwa moto.
\s5
\v 48 Kisha watu wote wenye mwili watajua yakwamba mimi ni Yahwe nimeuwasha moto, na hautazimika."'
\v 49 Kisha nimesema, Ee! Bwana Yahwe, Wananisema mimi, 'Je! yeye sio mwenye kusema mafumbo?"'
\s5
\c 21
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, weka uso wako kuelekea Yerusalemu, na neno juu ya patakatifu; tabiri juu ya nchi ya Israeli.
\v 3 Sema juu ya nchi ya Israeli, 'Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako! Nitautoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake na kuwakatilia mbali wote yaani mtu mwenye haki na mtu mwovu kutoka kwako!
\s5
\v 4 Ili niwakatilie mbali wote, mwenye haki na mwovu kutoka kwako, upanga wangu utatoka kwenye ala yake juu ya wote wenye mwili kutoka kusini hata kaskazini.
\v 5 Kisha wote wenye mwili watajua yakwamba mimi, Yahwe, nimeutoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake. Hautarudi tena!'
\s5
\v 6 Kwa hiyo, mwanadamu, gumia kama kuvunjika kwa viuno vyako! Katika uchungu gumia mbele ya macho yao!
\v 7 Kisha itatokea kwamba watakuuliza, 'Kwa sababu gani unalia?' Kisha utasema, 'Kwa sababu ya habari inayokuja, kwa kuwa kila moyo utakuwa dhaifu, na kila mkono utasita! Kila roho itazimia, na kila goti litatiririrka kama maji. Tazama! Inakuja na itakuwa kama hivi! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\v 8 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 9 "Mwanadamu, tabiri na sema, 'Bwana asema hivi: sema: Upanga! Upanga! Utachongwa na kusuguliwa!
\s5
\v 10 Utanolewa ili kushiriki katika machinjio makubwa! Utasuguliwa ili uwe kama mng'ao wa radi! Je! Tufanye furaha katika fimbo ya mwana wa mfalme? Upanga ujao huchukia kila hiyo fimbo!
\v 11 Hivyo upanga utatolewa kwa ajili ya kusuguliwa, na kisha kushikika kwa mkono! Upanga umechongwa na umesuguliwa na utatolewa kwenye mkono wa yule auaye!'
\s5
\v 12 Ita msaada na omboleza, mwanadamu! Kwa kuwa upanga umekuja juu ya watu wangu! Uko juu ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa dhidi ya upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo, piga paja lako!
\v 13 Kwa kuwa kuna kujaribiwa, lakini itakuwaje kama fimbo ya kifalme haitakuwepo tena? -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 14 Basi wewe, mwanadamu, tabiri, na piga makofi, kwa kuwa upanga utakushambulia hata mara tatu! Upanga kwa wale watakaochinjwa! Utakuwa upanga kwa ajili ya kuchinjia, ukiwatoboa pande zote!
\s5
\v 15 Ili kuyeyusha mioyo yao na kuongeza kuanguka kwao, nimeweka machinjio ya upanga juu ya malango! Ole! Umeundwa kama mng'ao wa radi, umetengwa kwa ajili ya kuua!
\v 16 Wewe, upanga! Nyooka upande wa kuume! Nyooka upande wa kushoto! Nenda popote ulipoelekeza uso wako.
\v 17 Kwa kuwa pia nitapiga mikono yangu miwili kwa pamoja (makofi), na kisha nitaleta ghadhabu yangu kwa waliobakia! Mimi, Yahwe, nimesema hivi!"
\s5
\v 18 Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,
\v 19 "Sasa wewe, mwanadamu, teua njia mbili kwa ajili ya upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja. Njia hizo mbili zitaanza katika nchi moja, na kibao cha barabarani kitamwonyesha mmoja wao kama kuuelekea mji.
\v 20 Onyesha njia moja kwa ajili ya jeshi la Wababeli kuja Raba, mji wa Waamoni. Onyesha nyingine kuelekea jeshi la Yuda na mji wa Yerusalemu, ambayo imeimarishwa.
\s5
\v 21 Kwa kuwa mfalme wa Babeli atasimama kwenye makutano ya barabara, kwenye njia panda, ili kufanya uganga. Alitingisha mishale na kuuliza mwelekeo kutoka kwa sanamu na atalichunguza ini.
\v 22 Katika mkono wake wa kuume kutakuwa na dalili kuhusu Yerusalemu, kuweka mitambo ya kubomolea juu ya hiyo, kufungua kinywa chake kupanga kuchinja, kutoa sauti ya vita, kuweka mitambo ya kubomolea juu ya malango, kujenga ngazi, na kusimamisha wima minara ya boma.
\v 23 Itaonekana kuwa ishara isiyofaa katika macho ya wale walio katika Yerusalemu, wale walioapa kiapo kwa Wababeli! Lakini mfalme atawashtaki kwa kuvunja sheria ya mkataba ili kuwabariki!
\s5
\v 24 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umeuleta uovu wako kwenye kumbukumbu zangu, makosa yenu yatafunuliwa! Dhambi zenu zitaonekana katika matendo yenu yote! Kwa sababu hii utamkumbusha kila mtu mtakamatwa kwa mkono wa adui yenu!
\s5
\v 25 Kama wewe, mchafu na mtawala mwovu wa Israeli, ambaye siku ya hukumu imekuja, na ambaye mda wa kufanya uovu umekoma,
\v 26 Bwana Yahwe asema hivi kwako: Toa kilemba na vua taji! Mambo hayatakuwa tena kama yalivyokuwa! Kiinue kilicho chini na kiinue kilichoinuka!
\v 27 Uharibifu! Uharibifu! Nitaiharibu! Haitakuwa tena hadi atakapokuja yeye ambaye ameteuliwa kutekeleza hukumu.
\s5
\v 28 Basi wewe, mwanadamu, tabiri na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi hawa ni watu wa Amoni kuhusiana na ujio wa aibu yao: Upanga, upanga umechirwa! Umenolewa kwa ajili ya kuchinja, hivyo utakuwa kama kimuli muli cha radi!
\v 29 Wakati manabii wameona maono ya uongo juu yako, wakati watakapofanya matambiko kuuijia kwa uongo juu yako, huu upanga utaanguka chini juu ya shingo za mwovu ambao wako karibu kuuawa, ambao siku ya ghadhabu imekuja na ambao mda wa uovu unakaribia kuisha.
\s5
\v 30 Rudisha upanga kwenye gala yake. Katika mahali ulipoumbwa, katika nchi ya chimbuko lako, nitakuhukumu!
\v 31 Nitamwaga hasira yangu juu yako! Nitapuliza upepo wa moto wa ghadhabu juu yako na kukuweka kwenye mkono wa watu wakatili, watu wajuao kuangamiza!
\s5
\v 32 Utakuwa kuni kwa ajili ya moto! Damu yako itakuwa kati ya nchi. Hutakumbukwa tena, kwa kuwa mimi, Yahwe nimesema hivi!"'
\s5
\c 22
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Sasa wewe, mwanadamu, Je! Utanihukumu? Utauhukumu mji kwa damu? Mfanye ajue machukizo yake yote.
\v 3 Utasema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Huu ndiyo mji umbao umwagao damu kati yake ili kwamba mda wake ufike; mji ufanyao sanamu ili ujitie unajisi.
\s5
\v 4 Umekuwa na hatia kwa damu uliyoimwaga, na kufanya unajisi kwa sanamu ulizozitengeneza. Kwa kuwa umezileta karibu siku zako na kuzikaribia siku zako za mwisho. Kwa hiyo nitakufanya lawama kwa mataifa na kejeli katika uso wa kila nchi.
\v 5 Wote walio karibu na wale walio mbali nawe watakudhihaki, wewe mji mchafu, ujulikanao kila mahali kwa sifa mbaya kama kujaa machafuko.
\s5
\v 6 Tazama! Wakuu wa Israeli, kila mmoja kwa nguvu yake, wamekuja kwako kumwaga damu.
\v 7 Wamefanya udanganyifu kwa baba na mama ndani yako, na wametenda yaliyo kinyume juu ya wageni kati yako. Wamewatenda vibaya yatima na wajane ndani mwako.
\v 8 Umevidharau vitu vyangu vitakatifu na kuinajisi Sabato yangu.
\v 9 Watu wasingiziaji wamekuja kati yako ili kumwaga damu, na hula juu ya milima. Hufanya uovu kati yako.
\s5
\v 10 Uchi wa baba umefunuliwa ndani yako. Wamemtukana mwanamke mchafu ndani yako wakati wa uchafu wake.
\v 11 Watu waliofanya machukizo pamoja na wake za majirani zao, na watu wafanyao uchafu wa aibu kwa mke wa mwanao mwenyewe; watu wawatukanao dada zao wenyewe-binti za baba zao wenyewe-haya yote yapo miongoni mwanu.
\v 12 Hawa watu huchukua rushwa kati yenu ili kumwaga damu. Umechukua faida na kuongeza riba nyingi sana, na umenisahau-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 13 Tazama! Kwa mkono wangu nimeipiga faida ambayo uliyoitengeneza kwa njia isiyo halali, na damu iliyo kati yako.
\v 14 Je! Moyo wako utasimama, mikono yako itakuwa hodari katika siku wakati mimi mwenyewe nitakapo kushughulikia? Mimi, Yahwe, nasema hivi, na nitalifanya.
\v 15 Hivyo nitakutawanya kati ya mataifa na kukutawanya kati ya nchi mbali mbali. Katika njia hii, nitausafisha uchafu kutoka kwako.
\v 16 Hivyo utakuwa mchafu machoni mwa mataifa. Kisha utajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\v 17 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 18 "Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa takataka kwangu. Wote wamekuwa masazo ya shaba na bati, na chuma na risasi kati yenu. Watakuwa kama takataka ya fedha katika tanuu.
\v 19 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu mmekuwa kama takataka, kwa hiyo, tazama! Nataka kuwakusanya katikakati ya mji wa Yerusalemu.
\s5
\v 20 Kama kukusanya fedha na shaba, chuma, risasi na chuma kati ya tanuu ili kuvifukutia moto na kuviyeyusha juu yake, nitawayeyusha. Hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu. Nitawaweka hapo na kufukutisha moto juu yake ili kuiyeyusha; hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu, na nitawaweka hapo na kuwayeyusha.
\v 21 Basi nitawakusanya na kuwafukutia kwa moto wa hasira yangu juu yenu hivyo basi mtamwagwa kati yake.
\v 22 Kama kuyeyusha fedha kati ya tanuu, mtayeyushwa chini kati yake, na mtajua yakwamba mimi, Yahwe, nimemwaga ghdhabu yangu juu yenu!"'
\s5
\v 23 Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 24 "Mwanadamu, mwambie, 'Wewe ni nchi ambayo haijasafishwa. Hakuna mvua siku ya hasira!
\v 25 Kuna njama ya manabii wake kati yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo. Wamekula uhai na kuchukua utajiri wa thamani; wamewafanya wajane wengi ndani yake!
\s5
\v 26 Makuhani wake hufanya kinyume na sheria yangu, na wamevinajisi vitu vyangu vitakatifu. Hawawezi kutofautisha kati ya vitu vitakatifu na vitu vya najisi. Wanaficha macho yao kutoka Sabato zangu hivyo basi nimetiwa unajisi kati yao.
\v 27 Wakuu wake ndani mwake wamekuwa kama mbwa mwitu wakirarua mawindo yao. Wamemwaga damu na kuharibu maisha, ili kupata faida kwa njia ya udanganyifu.
\v 28 Manabii wake wamepakwa chokaa; wanaona maono ya uongo na kutabiri uongo kwao. Wanasema "Bwana Yahwe asema hivi"' wakati Yahwe hajanena.
\s5
\v 29 Watu wa nchi wamewakandamiza kwa kutaka kwa nguvu na kuwanyang'anya kwa nguvu, na wamewatesa maskini na wahitaji, na kuwakandamiza wageni bila haki.
\s5
\v 30 Hivyo nimetafuta mtu kutoka kwao ambaye ataweza kujenga ukuta na ambaye atakayeweza kusimama mbele yangu katika uvunjaji wake kwa ajili ya nchi basi sitaweza kuiharibu, lakini sikuona mtu.
\v 31 Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao. Nitawamaliza kwa moto wa ghadhabu yangu na kuweka njia yao juu ya vichwa vyao wenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\c 23
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, Kulikuwa na wanawake wawili, binti za mama mmoja.
\v 3 Walifanya ukahaba katika Misri katika kipindi cha ujana wao. Walitenda kama makahaba huko. Maziwa yao yalikuwa yamebana na ubikira wa chuchu zao zilipapaswa huko.
\v 4 Majina yao yalikuwa Ohola-dada mkubwa-na Oholiba-dada yake mdogo. Kisha wakawa wangu na kuzaa wana na binti. Majina yao yalikuwa yakimaanasha hivi: Ohola maana yake Samaria, na Oholiba maana yake Yerusalemu.
\s5
\v 5 Lakini Ohola alifanya kama kahaba hata alipokuwa wangu; aliwatamani wapenzi wake, kwa kuwa Waashuri na nguvu,
\v 6 liwali aliyekuwa amevaa urijuana, na kwa ajili ya maafisa wake, waliokuwa hodari na wanaume wa kuvutia, wote walikuwa waendesha farasi.
\v 7 Hivyo akajitoa yeye mwenyewe kama kahaba kwao, kwa watu bora wa Ashuru, na alijitia mwenyewe uchafu pamoja na kila mmoja aliyekuwa amemtamani-pamoja na sanamu zake zote.
\s5
\v 8 Kwa kuwa hakuacha tabia zake za kihaba nyuma katika Misri, wakati walipolala naye wakati alipokuwa msichana mdogo, wakati walipoanza kwanza kupapasa ubikira wa maziwa yake, wakati walipoanza kummwagia tabia ya uzinzi wao juu yake.
\v 9 Kwa hiyo nilimtia kwenye mkono wa wapenzi wake, kwenye mkono wa Waashuru kwa kuwa aliwatamani.
\v 10 Wakamfunua uchi wake. Wakawachukua wana wake na binti, na wakamuua kwa upanga, na akawa aibu kwa wanawake wengine, hivyo wakapitisha hukumu juu yake.
\s5
\v 11 Dada yake Oholiba akaliona hili, lakini aliyatamani zaidi na kufanya kama kahaba hata zaidi kuliko dada yake.
\v 12 Aliwatamanai Waashuru, mabosi na watawala waliokuwa wamevaa ngua za ushawishi, walikuwa watu waendesha farasi. Wote walikuwa hodari, wote vijana wa kuvutia.
\v 13 Nikaona kwamba alikuwa amefanya uchafu mwenyewe. Ilikuwa kama kwa wadada wote.
\s5
\v 14 Kisha akaongeza ukahaba wake tena zaidi. Aliona watu waume waliokuwa wamechorwa juu ya kuta, michoro ya Wakaldayo iliyochorwa kwa rangi nyekundu,
\v 15 waliovaa mikanda kuzunguka viuno vyao, na vilemba virefu juu ya vichwa vyao. Wote walikuwa na mwonekano wa maafisa wa jeshi la waendesha farasi, mfano wa wana wa Wababeli, ambao asili ya nchi ni Ukaldayo.
\s5
\v 16 Na mara macho yake yalipowaona, aliwatamani, hivyo akawatuma wajumbe wake kwao katika Ukaldayo.
\v 17 Kisha Wababeli wakaja katika kitanda chake cha tamaa, na walimfanya unajisi kwa uzinzi wao. Kwa kile alichokuwa amekifanya alifanya unajisi, basi akageuka mwenyewe kutoka kwao katika karaha.
\s5
\v 18 Alionyesha matendo yake ya ukahaba na alionyesha uchi wake, hivyo roho yangu ikagauka kutoka kwake, kama roho yangu ilivyogeuka kutoka kwa dada yake.
\v 19 Kisha alifanya matendo mengi zaidi ya ukahaba, akakumbuka na kutafakari siku za ujana wake, wakati alipotenda kama kahaba katika nchi ya Misri.
\s5
\v 20 Basi akawatamani wapenzi wake, ambao sehemu zao za siri zilikuwa kama zile za punda, na kile kizaliwacho hutoka kilikuwa kama wale farasi.
\v 21 Hivi ndivyo ulivyofanya matendo ya aibu ya ujana wako, wakati Wamisri walipopapasa chuchu zako kuyaminya maziwa ya ujana wako.
\s5
\v 22 Kwa hiyo, Oholiba, Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama! Nitawarudisha wapenzi wako dhidi yako. Wale ambao uliowarudisha, nitawaleta juu yako kutoka kila upande.
\v 23 Wababeli na Wakaldayo wote, Pekodi, Shoa, na Koa, na Waashuru wote pamoja nao, hodari, vijana wa kutamanika, magavana na maamiri jeshi, wote ni maafisa na watu wote wenye sifa, wote wenye kuendesha farasi.
\s5
\v 24 Watakuja juu yako kwa silaha, na kwa magari ya farasi na mikokoteni, na kundi kubwa la watu. Watapanga ngao kubwa, ngao ndogo, na kofia za chuma juu yako pande zote. Nitawapatia nafasi kukuadhibu, na watakuadhibu kwa matendo yao.
\v 25 Kwa kuwa nitaweka hasira yangu ya wivu juu yako, na watashughulika na wewe kwa hasira. Watakukatilia mbali pua zako na masikio yako, na masalia yako wataanguka kwa upanga. Watawachukua wana wako na binti zako, na masalia yako watateketea kwa moto.
\s5
\v 26 Watakuvua nguo zako na kuchukua mapambo yako ya vito.
\v 27 Hivyo nitaiondoa tabia yako ya aibu kutoka kwako na matendo yako ya kikahaba kutoka nchi ya Misri. Hutainua macho yako kuwaelekea kwa sahauku, na hutaikumbuka Misri tena.'
\s5
\v 28 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama! Nitakutia katika mkono wa wale uwachukiao, kukurudisha kwenye mkono wa wale ambao uliokuwa umewarudisha.
\v 29 Watashughulika pamoja nawe kwa chuki; watachukua milki zako zote na kukutelekeza uchi na kukuweka wazi. Uchi wa aibu ya ukahaba wako utafunuliwa, tabia yako ya aibu na uzinzi wako.
\s5
\v 30 Haya mambo yatafanyika kwako kwa kuwa umetenda kama kahaba, tamaa za mataifa kwazo umetiwa unajisi kwa sanamu zao.
\v 31 Umetembea katika njia za dada yako, hivyo nitaweka kikombe chake cha adhabu kwenye mkono wako.'
\s5
\v 32 Bwana Yahwe asema hivi, 'Utakinywea kikombe cha dada yako ambacho ni kirefu na kikubwa. Utakuwa dhihaka na kutawaliwa na dharau-hiki kikombe kimejaa kiasi kikubwa.
\s5
\v 33 Utajazwa kwa ulevi na huzuni, kikombe cha ushangao na uharibifu; kikombe cha dada yako Samaria.
\v 34 Utakinywea na kubakia kitupu; kisha utakivunja vunja na kuyararua maziwa yako kuwa vipande vipande. Kwa kuwa nimesema hivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
\s5
\v 35 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu umenisahau na kunitupa mbali nyumba ya mgongo wako, basi pia utachukua matokeo ya tabia zako za aibu na matendo ya uasherati."'
\s5
\v 36 Yahwe akanambia, "Mwanadamu, Je! utamhukumu Ohola na Oholiba? Basi waambie matendo yao ya machukizo,
\v 37 kwa kuwa wamefanya uzinzi, na kwa kuwa kuna damu juu ya vichwa vyao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, na wamewaweka hata wana wao kwenye moto, kama chakula cha sanamu zao.
\s5
\v 38 Kisha waliendelea kufanya hivi kwa ajili yangu: Wamepafanya patakatifu pangu unajisi, na katika siku hiyo hiyo wakainajisi Sabato zangu.
\v 39 Kwa kuwa walipokuwa wamewachinjia watoto wao kwa ajili ya sanamu zao, kisha wakaja hata patakatifu pangu siku hiyo hiyo kupanajisi! Hivyo tazama! Hivi ndivyo walivyofanya kati ya nyumba yangu.
\s5
\v 40 Mmewatuma watu kutoka mbali, ambao wajumbe waliwatuma-sasa tazama. Wakaja kweli, ambao uliojiosha kwa ajili yao, uliweka rangi macho yako, na kujipamba kwa mapambo ya vito.
\v 41 Huko ulikaa kwenye kitanda kizuri na kwenye meza iliyokuwa imepangwa mbele yake ulikuwa umeweka ubani na mafuta yangu.
\s5
\v 42 Hivyo sauti za watu zilikuwa zimemzunguka; pamoja na watu wa kila aina, hata walevi waliletwa kutoka jangwani, na wakawavalisha vikuku mikononi mwao na mataji mazuri juu ya vichwa vyao.
\s5
\v 43 Kisha nikasema juu yake aliyekuwa ameonywa kwa uzinzi, 'Sasa watazini pamoja naye, na yeye pamoja nao.'
\v 44 Wakamwingilia na kulala naye kama watu wamwingiliavyo kahaba. Katika njia hii walilala Ohola na Oholiba, waliokuwa wanawake wazinzi.
\v 45 Lakini watu wenye haki watapitisha hukumu na kuwaadhibu kama wazinzi, na watawaadhibu kwa hukumu kwa wale wamwagao damu, kwa sababu wao ni wazinzi na damu iko mikononi mwao.
\s5
\v 46 Hivyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitainua kundi la watu juu yao na kuwatoa kuwa kitisho na kuteka nyara.
\v 47 Kisha hilo kundi la watu litawapiga kwa mawe na kuwakatilia chini kwa panga zao. Watawaua wana wao na binti na kuzichoma nyumba zao.
\s5
\v 48 Kwa kuwa nitaondoa tabia ya aibu kutoka kwenye nchi na nidhamu wanawake wote hivyo hawatatenda kama makahaba.
\v 49 Hivyo wataweka tabia yenu ya aibu juu yenu. Mtachukua hatia ya dhambi zenu pamoja na sanamu zenu, na kwa njia hii mtajua yakuwa mimi ni Bwana Yahwe."
\s5
\c 24
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia katika mwaka wa nane mwezi wa kumi na siku ya kumi ya mwezi, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, andika kwa ajili yako jina la hii siku, siku hii sahihi mfalme wa Babeli ameizingira Yerusalimu.
\s5
\v 3 Basi nena mithali juu ya hii nyumba ya kuasi, fumbo moja. Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: weka sufuria ya kupikia. Iweke na weka maji kwenye hiyo.
\v 4 Vikusanye vipande vya chakula ndani yake, kila kipande kizuri-paja na bega-na ijaze kwa mifupa bora.
\v 5 Chukua kundi bora na jaza mifupa chini yake. Ilete kuchemsha na ipike mifupa ndani yake.
\s5
\v 6 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa mji wa damu. Nitakiongeza chungu cha mbao. Weka kuni nyingi na washa moto. Pika nyama vizuri na changanya katika viungo na iacha mifupa iteketee.
\s5
\v 7 Kwa kuwa damu iko kati yake. Ameiweka juu ya jiwe laini; hakuimwaga juu ya nchi kuifunika kwa mavumbi,
\v 8 hivyo inaleta hasira ya kulipa kisasi. Nimeweka damu yake juu ya jiwe laini ili isifunikwe.
\s5
\v 9 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa mji wa damu. Nitakiongeza chungu cha mbao.
\v 10 Weka kuni nyingi na washa moto. Pika nyama vizuri na changanya katika viungo na acha mifupa iteketee.
\s5
\v 11 Kisha weka chungu kitupu juu ya mkaa, ili kuchemsha na kuchoma shaba yake, hivyo uchafu wake ndani yake itayeyushwa, kutu yake imekula.'
\v 12 Amechoka kwa sababu ya kazi ya taabu, lakini kutu yake haitoki kweke kwa moto.
\s5
\v 13 Tabia yako ya aibu iko ndani ya uchafu wako, kwa sababu nimekusafisha, lakini bado hutaweza kuwa msafi. Bado hutakuwa huru kutoka uchafu wako hadi hasira yako itakapotulia kutoka kwako.
\s5
\v 14 Mimi, Yahwe, nimesema hili, na nitalifanya. Sintotulia wala kupumzika kwa ajili ya hili. Kama njia zako zilivyokuwa, na kama matendo yako, yatakuhukumu! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\v 15 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 16 "mwanadamu! Tazama, ninachukua tamaa ya macho yako kutoka kwako pamoja na tauni, lakini hutaomboleza wala kulia, na machozi yako hayatatoka.
\v 17 Utagugumia bila kusikika. Usiendeshe mazishi kwa ajili ya aliyekufa. Funga kilemba chako juu yako na vaa makubazi miguuni pako, lakini usivalishe shela nywele zako au kula mkate wa watu waombolezao kwa ajili ya kuwapoteza wake zao."
\s5
\v 18 Hivyo nimeongea na watu asubuhi, na mke wangu amekufa asubuhi. Asubuhi nimefanya kile nilichokuwa nimeambiwa kukifanya.
\s5
\v 19 Watu wameniuliza, "Ji! hautatuambia haya mambo yanamaana gani, mambo ambayo unayoyafanya?"
\v 20 Hivyo nimewaambia, "Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 21 'Waambie nyumba ya Israeli, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nitapanajisi patakatifu pangu-fahari ya nguvu yenu, mahali panapopendeza macho yenu, na panapotamaniwa na roho zenu, na wana wenu na binti zenu ambao mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.
\s5
\v 22 Kisha mtafanya hasa kama nilivyofanya: hutafunika nywele za sehemu ya chini za uso, wala kula mkate wa watu wanaoomboleza!
\v 23 Badala yake, vilemba vyenu vitakuwa juu ya vichwa, na makubadhi yenu miguuni mwenu; hutaomboleza wala kulia, kwa kuwa mtayeyuka katika maovu yenu, na kila mtu atagugumia kwa ya ajili ya ndugu yake.
\v 24 Hivyo Ezekieli atakuwa ishara kwenu, kama kila kitu ambacho alichokifanya mtafanya wakati hili litakapokuja. Kisha mtajua yakwamba mimi ni Bwana Yahwe!"'
\s5
\v 25 "Lakini wewe, mwanadamu, siku ambayo nitachukua hekalu lao, ambalo ni furaha yao, kiburi chao, na kile waonacho na kutamani-na wakati nikiwachukua wana wao na binti-
\v 26 siku hiyo, mgeni atakuja kwako kukupatia habari!
\v 27 Siku hiyo kinywa chako kitafunguliwa kwa huyo mgeni na utaongea-hutakuwa bubu tena. Utakuwa ishara kwao hivyo basi watajua kwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\c 25
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, weka uso wako juu ya watu wa Amoni na tabiri juu yao.
\s5
\v 3 Waambie watu wa Amoni, 'Sikiliza neno la Bwana Yahwe. Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Kwa sababu umesema, "Aha!" juu ya patakatifu pangu wakati palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli wakati ilipokuwa ukiwa, na juu ya nyumba ya Yuda wakati walipoenda utumwani,
\v 4 kwa hiyo, tazama, nitakupatia kwa watu katika mashariki kama milki yao. Watafanya kambi juu yako na kuweka mahema miongoni mwako. Watakula matunda yako na watakunywa maziwa yako.
\v 5 Nitamfanya Raba malisho ya ngamia na watu wa Amoni shamba la mifugo. Kisha utajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 6 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Umepigia makofi mikono yako na kupiga chapa miguu yako, na kufurahi pamoja na dharau ndani yako dhidi ya nchi ya Israeli.
\v 7 Kwa hiyo, tazama! Nitanyoosha mkono wangu na kukupatia kama mateka kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka watu na kukuangamiza kutoka miongoni mwa nchi! Nitakuharibu, na utajua yakwamba mimi ni Yahwe.'
\s5
\v 8 Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu Moabu na Seiri husema "Tazama! Nyumba ya Yuda ni kama kila taifa jingine."
\v 9 Kwa hiyo, tazama! ntafungua miteremko ya Moabu, kuanzia kwenye miji yake juu ya mpaka-uzuri wa Beth Yeshimothi, Baal Meoni, na Kiriathaimu-
\v 10 kwa watu wa mashariki waliokuwa juu ya watu wa Amoni. Nitawapatia kama milki ili kwamba watu wa Amoni hawatakumbukwa miongoni mwa mataifa.
\v 11 Hivyo nitafanya hukumu juu ya Moabu, na watajua yakwamba mimi ni Yahwe.'
\s5
\v 12 Bwana Yahwe asema hivi, Edomu amelipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda na amefanya makosa katika kufanya hivyo.
\v 13 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Nitaunyoosha mkono wangu juu ya Edomu na kumharibu kila mtu na wanyama huko. Nitawaharibu, sehemu ya ukiwa, kutoka Temani hata Dedani. Wataanguka kwa upanga.
\s5
\v 14 Nitaweka kisasi changu juu ya Edomu kwa mkono wa watu wangu Israeli, na watafanya kwa Edomu kulingana na hasira yangu na ghadhabu yangu, na wakitajua kisasi changu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
\s5
\v 15 Bwana Yahwe asema hivi, 'Wafilisti wamelipiza kisasi pamoja na uovu na kutoka ndani yao wamejaribu kuiharibu Yuda tena na tena.
\v 16 Basi hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Tazam! Nitanyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, na nitakalia mbali Wakerethi na kuwaharibu mabaki yaliyobaki karibu na pwani.
\v 17 Kwa kuwa nitalipiza kisasi kikubwa dhidi yao pamoja na matendo ya ghadhabu kubwa ya adhabu, hivyo watajua yakwamba mimi ni Yahwe, nitakapolipiza kisasi juu yao."'
\s5
\c 26
\p
\v 1 Hivyo ilikuwa katika mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema juu ya Yerusalemuu, 'Aha! Malango ya watu waliovunjika! Amenigeukia; Nitajazwa kwa sababu ameharibika.'
\s5
\v 3 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama! Niko juu yako, Tiro, na nitayainua mataifa mengi juu yako kama bahari iiunuavyo mawimbi yake.
\v 4 Wataziharibu kuta za Tiro na kuiangusha chini minara yao. Nitafagia mavumbi yake mbali na kumfanya kama jiwe tupu.
\s5
\v 5 Atakuwa sehemu ya kuwekea nyavu kati ya bahari, kwa kuwa nimesema hilo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na atakuwa mateka kwa ajili ya mataifa.
\v 6 Binti zake walioko mashambani watachinjwa kwa panga, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.'
\s5
\v 7 Kwa kuwa hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Tazama, kutoka kaskazini namleta Nebukadreza mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, dhidi ya Tiro, pamoja na farasi na magari ya farasi, na pamoja na waendesha farasi na watu wengi.
\v 8 Atawaua binti zako katika shamba. Ataweka kazi ya boma na kujenga ulaghai dhidi ya kuta zako na kuziinua ngao dhidi yao.
\s5
\v 9 Ataweka vyombo vya kubomolea dhidi ya kuta zako, na vyombo vyake vitaanguka chini ya minara yako.
\v 10 Farasi zake zitakuwa nyingi kwamba mavumbi yao yatawafunika. Kuta zako zitatikisika kwa mlio wa waendesha farasi, magurudumu, na magari ya farasi. Wakati atakapoingia malango yako, ataingia kama watu waingiavyo kwenye mji ambao kuta zimebomolewa.
\v 11 Kwato za farasi zake zitaikanyaga mitaa yako yote. Atawaua watu wako kwa upanga na nguzo za uweza wako zitaanguka chini.
\s5
\v 12 Watauteka nyara utajiri wako na bidhaa iliyoporwa. Watabomoa kuta zako na kuziharibu nyumba zako za kifahari. Mawe yako, mbao zako, na kokoto watazitupa kwenye maji.
\v 13 Nitaikomesha sauti ya nyimbo zako. Sauti ya vinubi haitasikika tena.
\v 14 Nitakufanya jiwe tupu, utakuwa mahali ambapo nyavu zitasambazwa kuzikausha. Hutajengwa tena, kwa kuwa mimi, Bwana Yahwe nimesema-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 15 Bwana Yahwe amwambia hivi Tiro, 'Je visiwa havitatetemeka kwa mlio wa kuanguka kwako, na pamoja na watakaogumia kwa jeraha wakati machinjio mabaya yatakapokuwa kati yako?
\v 16 Kisha wakuu wote wa bahari watakaposhuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuvua mavazi yao rasmi na kutupa mavazi yaliyonakshiwa. Watavaa wenyewe kwa kutetemeka, wataketi chini na kutetemeka kila wakati, na wataogopa kwa sababu yako.
\s5
\v 17 Watainua maombolezo juu yako na kukwambia, umekuwaje, uliyekuwa umekaliwa na manahodha wa meli, umeharibika. Mji mashuhuri ulikuwa imara sana-sasa umetoka kwenye bahari. Wale wanaoishi ndani yake wanaotia hofu kuhusu wenyewe juu ya kila mmoja aliyeishi karibu nao.
\v 18 Sasa fukwe zitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako. Visiwa katika bahari vimeogofya, kwa sababu umekufa.'
\s5
\v 19 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: wakati nitakapokufanya wewe mji kuwa ukiwa, kama miji mingine ambayo haikaliwi, wakati nitakapoviinua vilindi dhidi yako, na wakati maji makuu yatakapokufunika,
\v 20 kisha nitakushusha chini kwenda kwa watu wa nyakati za zamani, kama wengingine walioenda chini kwenye shimo; kwa kuwa nitakufanya uishi katika falme za chini za dunia kama uharibifu wa nyakati za zamani. Kwa sababu hii hutarudi na kusimama katika nchi ya walio hai.
\v 21 Nitaweka janga juu yako, na hutakuwepo tena milele. Kisha utatafutwa, lakini hutapatikana milele tena-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\c 27
\p
\v 1 Tena neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Sasa wewe, mwanadamu, anza kuomboleza kuhusiana na Tiro,
\v 3 na mwambie Tiro, aishiye kwenye malango ya bahari, manahodha wa watu hata visiwa vingi, Bwana Yahwe asema hivi kwako: Tiro, umesema, mimi ni ukamilifu katika uzuri.'
\s5
\v 4 Mipaka yako iko kwenye moyo wa bahari; majengo yako yamekamilisha uzuri wako.
\v 5 Wametengeneza mbao nene na pana kwa mvinje kutoka Mlima Hermoni; wamechukua mkangazi kutoka Lebanoni kuufanya mlingoti.
\s5
\v 6 Wametengeneza makasia yako kutoka kwenye mialo ya Bashani; wametengeza sitaha zako kwa mbao za mvinje kutoka Kitimu, na wametengeneza kwa pembe.
\v 7 Tanga zako zilikuwa za rangi za kitani kutoka Misri ambazo zilikuwa kama beramu!
\s5
\v 8 Wale waliokuwa wakiishi Sidoni na Arvadi walikuwa wavuta makasia wako; wenye busara wa Tire walikuwa ndani yenu; walikuwa marubani wako.
\v 9 Mafundistadi wenye uzoefu wa hali ya juu kutoka Gabeli walijaza mishono; meli zote za bahari na mabaharia wao miongoni mwenu walikuwa wakiwabeba manahodha kwaajili ya biashara.
\s5
\v 10 Uajemi, Ludi, na Putu walikuwa katika jeshi lako, watu wako wa vita. Walining'iniza ngao na chapeo ndani yako; walionyesha uzuri wako.
\v 11 Watu wa Arvadi na Heleki katika jeshi lako walikuwa juu ya kuta zako wamekuzunguka, na watu wa Gamadi walikuwa kwenye minara yako. Walinin'giniza juu ngao zao juu ya kuta zako zote zilizokuzunguka! Wakaukamilisha uzuri wako.
\s5
\v 12 Tarshishi alikuwa mdau wa biashara pamoja nawe kwa sababu ya wingi wa utajiri wako wa kuuza mizigo: fedha, chuma, bati, na risasi. Walinunua na kuuza bidhaa za biashara!
\v 13 Yavani, Tubali, na Mesheki-waliwauza watumwa na katika vitu kutengeneza shaba. Walibeba bidhaa zako.
\s5
\v 14 Beth Togarma waliandaa farasi, farasi dume, na nyumbu kama kama bidhaa zako.
\v 15 Watu wa Dedani walikuwa wafanya biashara wako kwenye pwani nyingi. Bidhaa zilikuwa mkononi mwako; walikutumia pembe, pembe za ndovu, na mpingo kama ushuru!
\s5
\v 16 Shamu alikuwa mchuuzi katika bidhaa zako nyingi; waliandaa zumaridi, zambarau, nguo zenye rangi mbali mbali, kitambaa kizuri, lulu, na kito chekundu cha thamani kama bidhaa zako.
\v 17 Yuda na nchi ya Israeli walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe. Waliandaa ngano kutoka Minithi, keki, asali, mafuta, na lihamu kama bidhaa zako.
\v 18 Dameski alikuwa mfanya biashara wa bidhaa zako zote, za utajiri mkubwa mno, na ya divai ya Helboni na sufu ya Zahari.
\s5
\v 19 Dani na Yavani kutoka Uzali walikwandalia bidhaa ya chuma kilichofuliwa, na mdalasini, na mchai. Hivi vikawa bidhaa yako.
\v 20 Dedani alikuwa mchuuzi katika nguo nzuri za kutandika.
\v 21 Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe; walikuandalia wanakondoo, kondoo dume na mbuzi.
\s5
\v 22 Wafanya biashara wa Sheba na Raama walikuja kukuuzia kila aina ya viungo vizuri katika vito vyote vya thamani; waliuza dhahabu kwa ajili ya bidhaa.
\v 23 Harani, Kane, na Adina walikuwa wafanya biashara pamoja nawe, karibu na Sheba, Ashuru, na Kilmadi.
\s5
\v 24 Hawa walikuwa wachuuzi wako mapambo ya joho ya nguo za urujuani pamoja na rangi zilibuniwa, na nguo zilizo sanifiwa vizuri katika sehemu zako za soko.
\v 25 Merikebu za Tarshishi zilikuwa misafara ya bidhaa yako! Hivyo ulijaa, shehena nzito katika moyo wa bahari!
\s5
\v 26 Wapiga makasia wako walikuleta kwenye bahari kuu mno; upepo wa mashariki umekuvunja kati yao.
\v 27 Utajiri wako, bidhaa, na mizigo ya biashara; wapiga makasia wako na marubani, na waunzi wa meli; wafanya biashara wako wa bidhaa na watu wote wa vita walio ndani yako, na jeshi lako-watazama kwenye kina cha bahari siku ya kuangamia kwako.
\s5
\v 28 Miji iliyopo kwenye bahari sauti itatetemeka kulia kwa rubani zako;
\v 29 Wote wavutao kasia watashuka chini kutoka meli katika zao; wanamaji na marubani wote juu ya bahari watasimama juu ya nchi.
\v 30 Kisha watakufanya kusikiliza sauti yao na kulia kwa uchungu; watarusha vumbi juu ya vichwa vyao. Watabingirika katika majivu.
\s5
\v 31 Watanyo vichwa vyao upara kwa ajili yako na kujifunga wenyewe kwa nguo za magunia, na watalia kwa sauti.
\v 32 Watakuinulia maombolezo ya kuomboleza kwa ajili yako na kuimba nyimbo za maombolezo juu yako, ni nani aliye kama Tiro, ambaye sasa ameletwa kunyamazishwa kati ya bahari?
\v 33 Wakati bidhaa yako ilipoenda ufukweni kutoka kwenye bahari, imewarithisha watu wengi; uliwatajirisha wafalme wa dunia kwa wingi wa utajiri wako mkubwa na bidhaa!
\s5
\v 34 Lakini wakati ulipo vunjwavunjwa kwa bahari, kwa vilindi vya maji, bidhaa yako na wafanya kazi wako wote kuzama!
\v 35 Wote wakaao pwani walikuogopa, na wafalme wao kuvunjwa vunjwa katika kitisho! Nyuso zao zimetetemeka!
\v 36 Wafanya biashara wa meli wa watu wakuzomea; umekuwa tishio, na hutakuwepo tena milele."
\s5
\c 28
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, waambie watawala wa Tiro, 'Bwana Yahwe asema hivi: Moyo wako unakiburi! Umesema, "mimi ni mungu! Nitakaa kwenye kiti cha miungu katika moyo wa bahari!" Ingawa wewe ni mtu na sio mungu, unaufanya moyo wako kama moyo wa mungu,
\v 3 unafikiri kwamba unahekima kuliko Danieli, na kwamba hakuna siri ikushangazayo!
\s5
\v 4 Umejitajirisha mwenyewe pamoja na hekima na ujuzi, na kujipatia dhahabu na fedha katika hazina yako!
\v 5 Kwa hekima kubwa na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, hivyo moyo wako una kiburi kwa sababu ya utajiri yako.
\s5
\v 6 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umetengeza moyo wako kama moyo wa mungu,
\v 7 kwa hiyo nitaleta wageni juu yako, watu wa kuogofya kutoka mataifa mengine. Wataleta panga zao juu hekima ya uzuri wako, na watauchafua uzuri wako.
\s5
\v 8 Watakupeleka chini hata kwenye shimo, na utakufa kifo cha waliokufa katika Bahari.
\v 9 Je! kweli utasema, "Mimi ni mungu" mbele ya uso wa yule akuuaye? Wewe ni mwanadamu na sio Mungu, na utakuwa kwenye mkono wa yule akujeruaye.
\v 10 Utakufa kifo cha asiyetahiriwa kwa mkono wa wageni kwa kuwa nimesema hili-asema Bwana Yahwe.
\s5
\v 11 Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 12 "Mwanadamu, inua maombolezo kwa ajili ya mfalme wa Tiro na umwambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Uliumbwa mkamilifu, umejaa hekima na ukamilifu wa hekima.
\v 13 Ulikuwa katika Edeni, bustani ya Mungu. Kila jiwe la thamani lilikufunika: akiki, yakuti manjano, almasi, zabarajadi, shohamu, yaspi, yakuti samawi, zumaridi, baharamani, na dhahabu. Ilikuwa siku uliyokuwa umeiumba ambayo walikuwa wameiandaa.
\s5
\v 14 Nimekuweka juu ya mlima mtakatifu wa Mungu kama kerubi nimekutia mafuta kwa ajili ya kumlinda mwanadamu. Ulikuwa kati ya mawe ya moto ulipozunguka.
\v 15 Ulikuwa mwadilifu kwenye njia zako kutoka siku ulipoumbwa hadi uovu ulipoonekana ndani yako.
\s5
\v 16 Kupitia biashara yako kubwa uliyokuwa umeijaza kwa udhalimu, hivyo umetenda dhambi. Hivyo nimekutupilia mbali ya mlima wa Mungu, kama mmoja wao wa aliyekuwa ameninajisi, na nimekuharibu, kerubi mlinzi, na kukutoa miongono mwa mawe ya moto.
\v 17 Moyo wako ulikuwa na kiburi kwa uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako. Nimekupeleka chini kwenye dunia. Nimekuweka mbele ya wafalme ili waweze kukuona.
\s5
\v 18 Kwa sababu ya wingi wa dhambi zako na biashara za udanganyifu, umepanajisi mahali pako patakatifu. Basi nimetengeneza moto kutoka ndani yako; utakula wewe. Nitakugeuza kwenye majivu juu ya dunia katika macho ya wote wakutazamao.
\v 19 Wale wote waliokujua miongoni mwa watu watakao kutetemekewa; watakuwa watu wa kutisha, na hutakuwepo tena milele."'
\s5
\v 20 Kisha neno la Bwana Yahwe likanijia, kusema,
\v 21 "Mwanadamu, elekeza uso wako Sidoni na toa utabiri juu yake.
\v 22 Sema, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu yako, Sidoni! Kwa kuwa nitatukuzwa kati yako hivyo watu wako watajua kwamba mimi ni Yahwe wakati nitakapokuwa nimezitekeleza hukumu ndani yako. Nitaonyesha utakatifu ndani yako.
\s5
\v 23 Nitapeleka tauni juu yako na tazama mitaa yako, na walioua wataanguka kati yako. Wakati upanga utakapokuja juu yao kutoka pande zote, kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
\v 24 Kisha hakutakuwa na mtemba uchomao na maumivu ya miba kwa ajili ya nyumba ya Israeli kutoka wale wote waliomzunguka wanaowadharau watu wake, hivyo watajua kwamba mimi ni Bwana Yahwe!'
\s5
\v 25 Bwana Yahwe asema hivi, Nitakapowakusanya nyumba ya Israeli kutoka miongni mwa watu waliokuwa wamekusanyika, na wakati nilipokuwa nimewatenga miongoni mwao, hivyo mataifa aanaweza kuona, kisha watafanya nyumba zao katika nchi nitakayo mpatia mtumishi wangu Yakobo.
\v 26 Kisha wataishi salama ndani yake na kujenga nyumba, kulima mizabibu, na kuishi salama wakati nitakapo zitekeleza hukumu juu ya wote wale ambao sasa wanawadharau kutoka sehemu zote; basi watajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wao!"'
\s5
\c 29
\p
\v 1 Katika siku ya kumi, katika mwezi wa kumi siku ya kumi na moja ya mwezi, neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, weka uso wako juu ya Farao, mfalme wa Misri; toa unabii juu yake na juu ya Israeli yote.
\v 3 Nena na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Farao, mfalme wa Misri. Wewe joka kubwa ambaye ujifichaye kati ya mto, husema, "Mto wangu ni wangu mwenyewe. Nimeufanya kwa ajili yangu mwenyewe."
\s5
\v 4 Kwa kuwa nitaweka kalabu katika taya zako, nasamaki za mto wako zitashikamana na magamba yako; nitakuinua juu kutoka kati ya mto wako karibu na samaki zote za mto walioshikamana na maganda yako.
\v 5 Nitakutupa chini kwenye jangwa, wewe pamoja na samaki wako wote kutoka kwenye mto wako. Utaanguka kwenye shamba la wazi; hutakusanya wala kuinua. Nitakupatia kama chakula kwa viumbe hai vya dunia na kwenye ndege wa angani.
\s5
\v 6 Kisha wote wakaao Misri watajua kwamba mimi Yahwe, kwa sababu wamekuwa mwanzi wa kutegemewa hata kwenye nyumba ya Israeli.
\v 7 Wakati watakapokushika kwa mkono wao, ulivunjika na kurarua wazi mabega yao; na watakapojifunza juu yako, ulivunjika, na kusababisha miguu yao kutokuwa imara.
\s5
\v 8 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! nitaleta upanga juu yako. Nitawakatilia mbali wote mwanadamu na mnyama mbali nawe.
\v 9 Hivyo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa. Ndipo watakapojua kwamba mimi ni Yahwe, kwa sababu jitu la kutisha liliseama, "Huu mto ni wangu, kwa kuwa nimeufanya mimi."
\v 10 Kwa hiyo, tazama! Ni juu yako na juu ya mto wako, hivyo nitaitoa nchi ya Misri juu ya ukiwa na jangwa, na utakuwa nchi yenye jangwa kutoka Migdoli hata Sewene na mipaka ya Kushi.
\s5
\v 11 Hakutakuwa na mguu wa mtu kupitia, na hakuna mguu wa wanyama pori watakao upitia. Haitakuwa makao kwa miaka arobaini.
\v 12 Kwa kuwa nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa kati ya nchi zilizoharibiwa, na miji yake kati ya miji isiyotumika itakuwa ukiwa kwa miaka arobaini; kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa, nitawatapanya kati ya nchi mbali mbali.
\s5
\v 13 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Mwisho wa miaka arobaini nitaikusanya Misri kutoka kwa watu miongoni mwao wale waliokuwa wametawanyika.
\v 14 Nitawarudisha wageni wa Misri na kuwarudisha hata mkoa wa Pathrosi, hata kwenye nchi ya asili yao. Kisha huko watakuwa ufalme wa chini.
\s5
\v 15 Utakuwa chini ya falme, na hautajiinua tena juu ya mataifa. Nitawapunguza hivyo hawatatawala tena juu ya mataifa.
\v 16 Wamisri hawatakuwa sababu kwa ajili ya imani kwa ajili ya nyumba ya Israeli. Badala yake, watakuwa kumbusho la uovu ambao Israeli umeufanya walipogeukia Misri kwa ajili ya msaada. Kisha watajua kwamba mimi ni Bwana Yahwe."'
\s5
\v 17 Kisha ikawa katika mwaka wa ishirini na saba siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 18 "Mwanadamu, Nebukadreza mfalme wa Babeli amelinda jeshi lake kufanya kazi ngumu juu ya Tiro. Kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega lilifanywa mali ghafi. Kisha yeye na jeshi lake hawakupokea malipo kutoka Tiro kwa kazi ngumu aliyokuwa ameimaliza dhidi yake.
\s5
\v 19 Kwa hiyo Bwana Mungu asema hivi, 'Tazama! ninawapatia Nebukadreza nchi ya Misri mfalme wa Babeli, na atachukua utajiri wake, kuziteka nyara milki zake, na kuchukua yote atakayoyakuta huko; nayo yatakuwa mshahara wa jeshi lake.
\v 20 Nimempatia nchi ya Misri kama mshahara kwa ajili ya kazi waliyonifanyia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 21 siku hiyo nitachipusha pembe kwa ajili ya nyumba ya Israeli, na nitakufanya uzungumze kati yao, ili kwamba wajue yakwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\c 30
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, toa unabii na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Maombolezo. "Ole unakuja siku hiyo."
\v 3 siku ikaribu. Siku ikaribu kwa ajili ya Yahwe. Itakuwa siku ya mawingu, mda wa hukumu kwa ajili ya mataifa.
\s5
\v 4 Kisha upanga utakuja dhidi ya Misri, na huko kutakuwa na maumivu makali katika Kushi wakati wauaji wa watu watakapoanguka katika Misri-wakati watakapochukua utajiri, na wakati misingi yake itakapoharibiwa.
\v 5 Kushi, Putu, na Ludi, na wageni wote, pamoja na watu wa nyumba ya agano-wote wataanguka chini kwa upanga.
\s5
\v 6 Yahwe asema hivi: Basi wale wanaoisaidia Misri wataanguka, na kiburi cha uweza wake kitashuka chini. Kutoka Migdoli hata Sewene maaskari wao wataanguka kwa upanga-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 7 Wataogofya kati ya nchi zilizotupwa, na miji yao itakuwa miongoni mwa miji yote iliharibika.
\s5
\v 8 Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapouweka moto katika Misri, na wakati wasaidizi wake wote watakapoharibiwa.
\v 9 Katika siku hiyo wajumbe watatoka mbele yangu katika meli ili kuitia hofu Kushi iliyo salama, na kutakuwa na maumivu makali miongoni mwao katika siku ya kuangamizwa Misri. Kwa kuwa tazama! inakuja.
\s5
\v 10 Bwana Yahwe asema hivi: Nitaufanya mwisho wa watu wa Misri kwa mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli.
\v 11 Yeye na jeshi lake pamoja naye, hofu ya mataifa, italetwa kuiharibu nchi; watafuta panga zao juu ya Misri na kuijaza nchi pamoja na watu waliokufa.
\s5
\v 12 Nitaifanya mito kuwa nchi kavu, na nitaiuza nchi kwenye mkono wa watu waovu. Nitaifanya nchi na viijazavyo ukiwa kwa mkono wa wageni-mimi, Yahwe, nimesema.
\s5
\v 13 Bwana Yahwe asema hivi: Nitaziharibu sanamu, na nitaleta mwisho wa sanamu za ubatili za Nofu. Hakutakuwa na mkuu katika Misri, na nitaweka hofu katika nchi ya Misri.
\v 14 Kisha nitaifanya Pathrosi ukiwa na kuweka moto katika Soani, nitatekeleza matendo ya hukumu katika No.
\s5
\v 15 Kwa kuwa nitamwaga ghadhabu yangu juu Sini, ngome ya Misri, na kuwakatilia mbali watu wa mataifa.
\v 16 Kisha nitaweka moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, No itavunjika, na Nofu itakabiliana na maadui kila siku.
\s5
\v 17 Vijana katika Oni na Pi-besethi wataanguka kwa upanga, na miji yao itaenda utumwani.
\v 18 Huko Tapanesi, siku itabadilika kuwa usiku nitakapo ivunja nira ya Misri huko, na kiburi cha uwezo wake kitaisha. Kutakuwa na wingu likimfunika, na binti zake wataenda utumwani.
\v 19 Nitatekeleza matendo ya hukumu katika Misri, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\v 20 Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa kwanza, katika siku ya saba ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 21 "Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Tazama! Haukufungwa, au kufungwa kwa kitambaa cha bendeji ili upone, hivyo basi uweze kuwa imara kushika upanga.
\s5
\v 22 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama, mimi niko juu ya Farao, mfalme wa Misri. Kwa kuwa nitauvunja mkono wake, wote yule aliye hodari na yule aliyevunjika, nitaufanya upanga wangu kuanguka kutoka kwenye mkono wake.
\v 23 Kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbali mbali.
\v 24 Nitaunyoosha mikono kwa mfalme wa Babeli na kuweka upanga wangu katika mkono wake ili kwamba niweze kuiharibu mikono ya Farao. Atagugumia mbele ya mfalme wa Babeli kwa mgumio wa mtu anayekufa.
\s5
\v 25 Kwa kuwa nitainyoosha mikono ya mfalme wa Babeli, wakati mkono wa Farao utakapoanguka. Kisha watajua yakwamba mimi ni Yahwe, nitakapoweka upanga wangu kwenye mkono wa mfalme wa Babeli; kwa kuwa ataishambulia nchi ya Misri kwa huo.
\v 26 Hivyo nitaitawanya miongoni mwa mataifa na kuyatawanya kwenye nchi tofauti tofauti. Kisha watajua yakwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\c 31
\p
\v 1 Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, mwambie Farao, mfalme wa Misri, na watu wake wanaomzunguka, 'Katika ukuu wako, je! wewe ni kama nani?
\s5
\v 3 Tazama! Ashuru ilikuwa mwerezi katika Lebanoni pamoja na matawi mazuri, yakitoa kivuli kwenye msitu, na mirefu katika kimo, na matawi yalitengeneza kilele cha mti wake.
\v 4 Maji mengi yaliufanya kuwa mrefu; maji ya chini yaliufanya kuwa mkuba. Mito ilitiririka sehemu zake zote, kwa kuwa mifereji yake ilitoa kuelekea kwenye miti yote katika shamba.
\s5
\v 5 Kimo chake kikubwa kilikuwa zaidi kuliko miti mingine yote katika shamba, na matawi yake yakawa mengi; matawi yake yalikuwa marefu kwa sababu ya maji mengi yalipokuwa yakikua.
\v 6 Kila ndege wa mbinguni alitengeza kiota kwenye matawi yake, wakati kila kiumbe hai cha shamba kilizaa mtoto chini ya tawi. Mataifa mengi yote yaliishi chini ya kivuli chake.
\v 7 Kwa kuwa ulikuwa uzuri katika ukuu wake na kimo cha matawi yake, kwa kuwa mizizi yake ilikuwa katika maji mengi.
\s5
\v 8 Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kuwa sawa nayo. Hakuna miongoni mwa miti ya mivinje iliyofanana matawi yake, na miti ya miamori haikuweza kuwa sawa na majani yake. Hapakuwa na mti mwingine katika bustani ya Mungu ulikuwa kama huo katika uzuri wake.
\v 9 Nimeufanya kuwa mzuri pamoja na matawi yake mengi na miti yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu ilimwonea wivu.
\s5
\v 10 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ilikuwa mirefu kwa kina, na imekiweka kilele chake kati ya matawi yake, moyo wake umeinua kwa sababu ya urefu wake.
\v 11 Nimeuweka kwenye mikono ya yeye mwenye uweza wa mataifa, kuishughulikia kulingana na yale maovu anayostahili. Nimeufukuza.
\s5
\v 12 Wageni waliokuwa wakiogofya wa mataifa yote wameikatilia mbali kuiacha ife. Matawi yake yameanguka kwenye milima na mabonde yote, na matawi yake yameanguka katika mito yote ya nchi. Kisha mataifa yote juu ya nchi wakatoka nje kutoka chini ya kivuli na kwenda zao wakamwacha.
\s5
\v 13 Ndege wa agani watapumzika kwenye shina la mti ulioanguka, na kila mnyama wa shambani atakuja kwenye matawi yake.
\v 14 Hii litokea ili kwamba pasiwe na miti mingine itakayopandwa karibu na maji yatang'oa majani yake hata kwenye kina cha miti mirefu, na kwamba hakuna miti mingine itakayomea karibu na maji itakayofikia kwenye hicho kina. Wote wametolewa kufa, chini ya nchi, miongoni mwa watoto wa binadamu, pamoja na wale washukao chini.
\s5
\v 15 Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku wakati mkangazi uliposhuka chini nilileta maombolezo kwenye dunia. Niliyafunika maji ya chini juu yake, nikayarudisha maji ya bahari. Nilizuia maji makuu, nikaleta maombolezo hata Lebanoni kwa ajili yake. Hivyo miti yote ya shambani ikaomboleza kwa sababu yake.
\s5
\v 16 Nimeleta tetemeko kwa mataifa wa sauti ya kuanguka kwake, wakati nitakapomtupa chini mpaka kuzimu pamoja na wale walioenda chini kwenye shimo. Hivyo niliitia moyo miti ya Edeni yote katika pande zote za nchi. Hii ilikuwa imechaguliwa na miti iliyokuwa bora ya Lenanoni; miti iliyokunywa maji.
\s5
\v 17 Kwa kuwa walikwenda chini pia pamoja nayo hata kuzimu, kwa wale waliokuwa wameuawa kwa upanga. Kulikuwa na jeshi lake imara, yale mataifa yalikuwa yakiishi kati kivuli chake.
\v 18 Umefanana na nani hivi katika utukufu na ukuu kati ya mti wa Edeni? Kwa kuwa utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni hata pande zote nne za dunia miongoni mwa wasiotahiriwa; utaishi pamoja na watu wake wote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavy."
\s5
\c 32
\p
\v 1 Kisha ikawa katika mwezi wa kumi na mbili wa mwaka wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, inua maombolezo kuhusu Farao mfalme wa Misri; mwambie, 'Wewe ni kama simba mdogo juu ya mataifa, lakini kama jitu la kutisha, unatoka kwenye maji, unayachafua maji kwa miguu yako na kuyachafua maji yao.
\s5
\v 3 Bwana Yahwe asema hivi: Basi nitautandaza wavu wangu juu yako katika kusanyiko la watu wengi, na watawainua juu katika wavu wangu.
\v 4 Nitakuacha katika nchi. Nitakutupa kwenye shamba na kufanya ndege wote wa angani watue juu yako; njaa ya wanyama wote waishio juu ya nchi watashibishwa na wewe.
\s5
\v 5 Kwa kuwa nitaiweka nyama yako juu ya milima, na nitayajaza mabonde kwa funza wako waliokufa.
\v 6 Kisha nitamwaga damu yako juu ya milima, na vitanda vya kijito vitajazwa kwa damu yako.
\s5
\v 7 Kisha wakati nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu na kuzitia giza nyota zake; nitalifunika jua kwa mawingu, na mwezi hautatoa nuru yake usiku.
\v 8 Mianga ya mbinguni nitaiweka giza juu yako, na nitaweka giza juu ya nchi-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
\s5
\v 9 Hivyo nitaitisha mioyo ya watu wengi katika nchi ambao huwajui, wakati nitakapoleta kuhusu uvunjifu miongoni mwa mataifa, miongoni mwa nchi ambazo hukuzijua.
\v 10 Nitawashangaza watu wengi kuhusiana na wewe; wafalme wao watatetemeka kwa hofu kuhusiana na wewe nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao. Kila wakati kila mmoja atatetemeka kwa sababu yako, katika siku ya kuanguka kwako.
\s5
\v 11 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja juu yako.
\v 12 Nitawafanya watu wako kuanguka kwa panga za mashujaa-kila shujaa ni tishio la mataifa. Hawa mashujaa watateketeza kiburi cha Misri na kuangamiza watu wake wote.
\s5
\v 13 Kwa kuwa nitaiharibu mifugo yote kutoka karibu na maji mengi; na mguu wa mtu hautayatibua tena, wala kwato za wanyama hazitayatibua.
\v 14 Kisha nitayafanya maji yao kuwa matulivu na kufanya mito yao kukimbia kama mafuta-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
\s5
\v 15 Wakati nitakapoifanya nchi ya Misri sehemu iliyojitenga, wakati nchi iliyopungukiwa na vitu viijazavyo, wakati nitakapo washambulia wakaao ndani yake, watajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\v 16 Kutakuwa na maombolezo; binti za mataifa wataomboleza juu yake; wataomboleza juu ya Misri, juu ya watu wake wote wataomboleza-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\v 17 Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya kumi na tano ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 18 "Mwanadamu, omboleza kwa ajili watu wa misri na walete chini-yeye na binti za mataifa mashuhuri-hata chini ya dunia pamoja na wale walioshuka chini kwenye shimo.
\s5
\v 19 'Je! wewe ni mzuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote? Nenda chini na lala chini pamoja na wasiotahiriwa.'
\v 20 Wataanguka miongoni mwao waliokuwa wameuawa kwa upanga. Upanga ulikuwa umewekwa! Alikuwa amepatiwa upanga; watamkamata na watu wake.
\v 21 Hodari wa wapiganaji katika Sheoli atasema kuhusu Misri na rafiki zake, 'Wameshuka chini hapa! Watalala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale waliokuwa wameuawa kwa upanga.'
\s5
\v 22 Ashuru yupo huko pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yamemzunguka; wote waliuawa kwa upanga.
\v 23 Wale ambao makaburi yao yamewekwa katika maficho ya mashimo yaliyo huko, pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yakiwazunguka wote waliokuwa wameuawa, walioanguka kwa upanga, wale walioleta hofu juu ya nchi ya walio hai.
\s5
\v 24 Elamu yupo huko pamoja na watu wake wote. Makaburi yake yamemzunguka; wote walikuwa wameuawa. Wale walioawa kwa upanga, walioshuka chini wasiotahiriwa hata sehemu ya chini kabisa ya dunia, waliowatia hofu juu ya nchi ya walio hai na wale waliobeba aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao chini kwenye shimo.
\v 25 Wamemuwekea kitanda kwa ajili ya Elamu na watu wake wote kati ya wachinjaji; kaburi lake limemzunguka. Wote hawajatahiriwa, kukatwa vipande kwa upanga, kwa sababu waliwaleta mashujaa wao juu ya nchi ya walio hai. Hivyo wamechukua aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao kwenye shimo miongoni mwa wote waliouawa, wale washukao kwenda shimoni. Elamu yu miongoni mwa wale waliokuwa wameuawa.
\s5
\v 26 Mesheki, Tubali, na watu wake wote wako huko! Makaburi yao yamewazunguka. Wote hawajatahiriwa, wameuawa kwa upanga, kwa sababu walileta utiisho wao juu ya nchi ya walio hai.
\v 27 Wasilale pamoja mashujaa walioanguka wa wasiotahiriwa walioshuka chini kwa Sheoli pamoja na silaha zao zote za vita, na pamoja na panga zao zote walizoziweka chini ya vichwa vyao na maovu yao juu ya mifupa yao. Kwa kuwa walikuwa tishio kwa mashujaa katika nchi ya walio hai.
\s5
\v 28 Basi wewe, Misri, utavunjika kati yao wasiotahiriwa! Utalala karibu nao waliokuwa wamekatwa vipande vipande kwa upanga.
\v 29 Edomu yuko huko na wafalme na viongozi wake wote. Walikuwa wamehifadhiwa katika uwezo wao pamoja na wale walioawa kwa upanga. Pamoja na wasiotahiriwa wamelala, pamoja na wale walioshuka kwenye shimo.
\s5
\v 30 Wakuu wa kaskazini wako huko-wote na Wasidoni wote walioshuka chini pamoja na hao waliokuwa wamekatwa vipande vipande. Walikuwa na nguvu na kuwafanya wengine kuogopa, lakini sasa wako huko kwa aibu, wasiotahiriwa pamoja na wale waliokatwa vipande vipande kwa upanga. Wamebeba aibu yao wenyewe, pamoja nao waendao kwenye shimo.
\s5
\v 31 Farao ataona na kupata faraja kuhusu kundi lake waliokatwa vipande vipande kwa upanga -Farao na jeshi lake lote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 32 Natamuweka kama utiisho wangu katika nchi ya walio hai, lakini atakuwa amelazwa chini katikati yao wasiotahiriwa, miongoni mwa wale walio katwa vipande kwa upanga, Farao na makundi yake yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\c 33
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, sema hivi kwa watu wako; waambie, 'Nitakapoleta upanga juu ya nchi, kisha watu wa hiyo nchi wakamchukua mtu mmoja kutoka mingoni mwao na kumfanya awe mlinzi wao.
\v 3 Atazamapo kwa upanga kama unakuja juu ya nchi, na apige tarumbeta kuwaonya watu!
\v 4 Kama watu wakisikia sauti ya tarumbeta lakini bila kusikia, na kama upanga ukija na kuwaua, kisha damu ya kila mmoja iko juu ya kichwa chake mwenyewe.
\s5
\v 5 Kama mtu akisikia sauti ya tarumbeta na hakusikiliza, damu yake iko juu yake; lakini kama akisikia, ataokoa maisha yake mwenyewe.
\v 6 Bali, kama mlinzi akiona upanga unakuja, lakini kama asipopiga tarumbeta, pamoja na matokeo kwamba watu hawajaonywa, na kama upanga ukija na kuchukua uhai wa mtu yeyote, kisha yule mtu akafa kwenye dhambi yake mwenyewe, lakini nitaitaka damu yake kutoka mlinzi.'
\s5
\v 7 Sasa wewe mwenyewe, mwanadamu! Nimekufanya kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli; utasikia maneno kutoka kinywani mwangu na uwaonye badala yangu.
\v 8 Kama nikimwambia mtu mwovu, 'Mwovu, hakika utakufa!' lakini kama hutangazi hivi ili kwa ajili ya kumuonya mtu mwovu kuhusu hii njia, kisha huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako!
\v 9 Lakini wewe, kama ukimwonya mwovu kuhusu hii njia, hivyo basi anaweza kurudi kutoka hiyo, na kama kama asipogeuka kutoka njia yake, kisha atakufa katika dhambi yake, lakini wewe mwenyewe utakuwa umeokoa maisha yako.
\s5
\v 10 Basi wewe, mwanadamu, sema kwa nyumba ya Israeli, 'Mnasema hivi, Makosa yetu na dhambi zetu zi juu yetu, na tunadhoofika kwa ajili yao! Je! tutaishije?"'
\v 11 Waambie, 'Kama niishivyo-asema Bwana Yahwe-sifurahii kifo cha mwovu, kwa kuwa kama mwovu akitubu kutoka njia yake, kisha ataishi! Tubu! Tubu kutoka njia zako mbaya! Kwa nini mnataka kufa, nyumba ya Israeli?'
\s5
\v 12 Hivyo basi wewe, mwanadamu, waambe watu wako, 'Haki ya mwenye haki haitamwokoa kama akikosa! Uovu wa mtu mwovu hautamfanya kuangamia kama akitubu dhambi zake! Kwa kuwa mtu mwenye haki hataweza kuishi kwa sababu ya haki yake kama akikosa.
\v 13 Kama nikisema kwa mwenye haki, "Hakika ataisha!" na kama akiamini katika haki yake na kisha akafanya udhalimu, sitokumbuka haki yake yoyote. Atakufa kwa ajili ya uovu alioufanya.
\s5
\v 14 Hivyo kama nikisema kwa mwovu, "Utakufa hakika," lakini kama akitubu kutoka kwenye dhambi zake na kufanya yaliyo halali na haki-
\v 15 kama akirudisha dhamana ambayo aliyomnyang'anya, au kama akirudisha alichokipoteza, na kama akitembea katika amri zitoazo uhai na bila kufanya dhambi-kisha ataishi hakika. Hatakufa.
\v 16 Dhambi alizozifanya hazitakumbukwa kwa ajili yake. Ametenda halali na haki, na hivyo, ataishi hakika!
\s5
\v 17 Lakini watu wako husema, "Njia ya Bwana haiko sawa!" lakini ni njia zako ndizo haziko sawa!
\v 18 Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki na kufanya dhambi, kisha atakufa katika hiyo!
\v 19 Wakati mtu mbaya ageukapo kutoka kwenye ubaya wake na kufanya iliyo halali na haki, ataishi kwa sababu ya hayo mambo!
\v 20 Lakini ninyi watu husema, "Njia ya Bwana haiko sawa!" Nitawahukumu kila mmoja wenu kulingana na njia yake, nyumba ya Israeli!"'
\s5
\v 21 Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya tano ya mwezi wa kumi ya uhamisho wetu, mtu mmoja akatoroka kutoka Yerusalemuna kusema, "Mji umetekwa!"
\v 22 Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu jioni kabla yule mtoro hajaja, na mdomo wangu ulikuwa wazi mda huo alikuja kwangu wakati wa mapambazuko. Hivyo mdomo wangu ulikuwa wazi; sikuwa bubu tena!
\s5
\v 23 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 24 "Mwanadamu, wale waishio mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli huongea na kusema, 'Ibrahimu alikuwa mtu pekee, na alirithi nchi, lakini sisi tukowengi! Tumepewa nchi kama wamiliki."
\s5
\v 25 Kwa hiyo waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Mnakula damu, na mmeziinulia macho yenu sanamu, kisha mnazimwagia damu za watu. Je! mna uhakika wa kuimiliki hii nchi?
\v 26 Mnategemea upanga wenu na mmetenda mambo maovu; kila mtu amemnajisi mke wa jirani yake. Je! kweli mtaimiliki nchi?'
\s5
\v 27 Utawaambia hivi, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, hakika wale walio katika uharibifu wataanguka kwa upanga, na nitawapatia wale walio katika mashamba viumbe hai kama chakula, na wale walio katika ngome na mapango watakufa kwa tauni.
\v 28 Kisha nitairudisha nchi kwenye ukiwa na tishio, na kiburi cha uwezo wake kitakoma, kwa kuwa milima ya Israeli itakuwa jangwa, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayewapitia.'
\v 29 Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapoifanya nchi ukiwa na tishio kwa sababu ya machukizo yote waliyoyafanya.
\s5
\v 30 Hivyo basi wewe, mwanadamu-watu wako wanasema mambo yako karibu na kuta na malango ya nyumba, na kila mmoja anaambizana na mwenzake-kila mtu na ndugu yake, 'Twende na tukasikilize neno la nabii lililotoka kwa Yahwe!
\v 31 Hivyo watu wangu watakuja kwako, kama wafanyavyo mara nyingi, na nitaketi mbele yako na kusikiliza maneno yako, lakini mioyo yao inafuata udhalimu kwa faida yao.
\s5
\v 32 Kwa kuwa umekuwa kama wimbo mzuri kwao, sauti nzuri awezaye kucheza kinanda vizuri, hivyo watasikia maneno yako, lakini hakuna atakaye yatii.
\v 33 Hivyo wakati haya yote yatakapotokea-tazama! itatokea! -watajua yakwamba nabii alikuwa miongoni mwao."
\s5
\c 34
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, tabiri dhidi ya wachungaji wa Israeli. Toa unabii na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi kwa wachungaji: Ole kwa wachungaji wa Israeli wanaojilisha wenyewe. Je! wachungaji hawapaswi kulilinda kundi?
\v 3 Mnakula mafungu yaliyonona na mnavaa sufu. Mnawachinja walionona. Hamkuwalisha siku zote.
\s5
\v 4 Hamkuwatia nguvu wagonjwa, wala hamkuwaponya wenye maradhi. Hamkuwafungua wale waliovunjika, hamkuwarudisha waliofukuzwa au kuwatafuta waliopotea. Badala yake, mmetawala juu yao kwa nguvu na vurugu.
\v 5 Kisha walikuwa wametawanyika bila mchungaji, na wakawa chakula kwa wanyama wote waishio katika mashamba, walipokuwa wametawanyika.
\v 6 Kundi langu limetawanyika juu ya milima yote na juu ya kilima kirefu, na limetawanyika juu ya uso wote wa dunia. Wala hakuna anayewatafua.
\s5
\v 7 Kwa hiyo, wachungaji, sikilizeni neno la Yahwe:
\v 8 Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwa sababu kundi langu limekuwa mateka na chakula kwa ajili ya wanyama katika mashamba, kwa sababu hapakuwa na mchungaji yeyote, lakini wachungaji walijilisha wenyewe na hawakulisha kundi langu.
\s5
\v 9 Kwa hiyo, wachungaji, lisikilizeni neno la Yahwe:
\v 10 Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu ya wachungaji, na nitalitaka kundi langu kutoka mkononi mwake. Kisha nitawaachisha kutoka kulichunga kundi; wala wachungaji hawatajilisha wenyewe tena kwa kuwa nitaliondoa kundi langu kutoka midomoni mwao, ili kwamba kundi langu lisiwe chakula kwa ajili yao tena.
\s5
\v 11 Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! mimi mwenyewe nitawatafuta kondoo wangu na kuwaulizia,
\v 12 kama mchungaji atafutaye kundi lake juu ya siku hiyo yupo ndani ya kundi lake lililotawanyika. Hivyo nitalitafuta kundi langu, na nitalichunga kutoka sehemu lilipokuwa limetawanyika siku ya mawingu na giza.
\v 13 Kisha nitalileta kutoka miongoni mwa watu; nitalikusanya kutoka nchi mbali mbali na kulileta kwenye nchi yao. Nitaliweka kwenye malisho juu ya pande za milima ya Israeli, karibu na vijito, na katika kila makazi katika nchi.
\s5
\v 14 Nitawaweka kwenye malisho mema; juu ya milima ya Israeli itakuwa sehemu za malisho yao. Watalala chini huko katika sehemu nzuri kwa ajili ya malisho, katika malisho mengi, na watalisha juu ya milima ya Israeli.
\v 15 Mimi mwenyewe nitachunga kondoo wangu, na mimi mwenyewe nitawalaza chini-hivi ndivyo Bwana Yahwe
\v 16 asemavyo-Nitawatafuta waliopotea nitawarudisha waliofukuzwa. Nitawafunga waliovunjika na kuwaponya kondoo waliougua lakini wanene na wenye nguvu nitawaharibu. Nitawalisha kwa haki.
\s5
\v 17 Hivyo sasa ninyi, kundi langu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-tazama, nitakuwa hakimu kati ya kondoo na kondoo na kati ya kondoo dume na mbuzi dume.
\v 18 Je! haitoshi kulisha juu ya malisho mazuri, ambayo mtayakanyaga chini kwa miguu yenu kile kilichobakia kwenye malisho; na kunywa kutoka maji masafi, ambayo hakuna budi kuikanyaga mito kwa miguu yenu?
\v 19 Kondoo zangu zitakula kile mlichokanyagwa kwa miguu yenu, na kunywa maji yale mliyoyakanyaga kwa miguu yenu?
\s5
\v 20 Kwa hiyo Bwana Yahwe anawaambia hivi; Tazama! Mimi mwenyewe nitahukumu kati ya wanene na waliokonda,
\v 21 Kwa kuwa mmewasukuma kwa ubavu wenu na mabega, na kuwapiga kwa pembe wadhaifu wote kwa pembe zenu hadi mtakapowatawanya mbali kutoka kwenye nchi.
\s5
\v 22 Nitaliokoa kundi langu na hawatakuwa mateka tena, na nitahukumu kati ya kondoo mmoja na mwingine!
\v 23 Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi. Atawachunga, atawalisha, na atakuwa mchungaji wao.
\v 24 Kwa kuwa mimi, Yahwe, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu kati yao-mimi, Yahwe, nimesema hivi.
\s5
\v 25 Kisha nitafanya agano la amani pamoja nao na kuwaondoa wanyama waovu kutoka kwenye nchi, ili kwamba waishi salama katika jangwa na walale salama katika misitu.
\v 26 Pia nitaleta baraka juu yao na juu ya maeneo yazungukao kilima changu, kwa kuwa nitaleta manyunyu kwa wakati wake. Haya yatakuwa manyunyu ya baraka.
\v 27 Kisha miti ya shambani itazaa matunda yake, na dunia itashindwa kuzaa matunda yake. Kondoo wangu watakuwa salama katika nchi yao; kisha watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakazipovunja fito za kongwa zao, na wakati nitakapowalinda kutoka kwenye mkono wa wale walio watumikisha.
\s5
\v 28 Hawatakuwa mateka tena kwa mataifa, na wanyama pori juu ya dunia hawatawameza tena. Kwa kuwa wataishi salama na wala hakuna mtu atakayewatia hofu.
\v 29 Kwa kuwa nitatengeneza sehemu ya kulimia nzuri kwa ajili yao hivyo hawataangamia kwa njaa katika nchi, na mataifa hayataleta matukano juu ya yao.
\s5
\v 30 Kisha watajua kwamba mimi, Yahwe Mungu wao, niko pamoja nao. Ni watu wangu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.
\v 31 Kwa kuwa ninyi ni kondoo wangu, kundi la malisho yangu, na watu wangu, na mimi ni Mungu wenu-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo."
\s5
\c 35
\p
\v 1 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 2 "Mwanadamu, weka uso wako juu ya Mlima Seiri na tabiri dhidi yake.
\v 3 Uiambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! ni juu yako, Mlima Seiri, nitakupiga kwa mkono wangu na kukufanya ukiwa na tishio.
\s5
\v 4 Nitaiharibu miji yenu, na wewe mwenyewe utakuwa ukiwa; kisha utajua kuwa mimi ni Yahwe.
\v 5 Kwa sababu umekuwa adui kwa watu wangu Israeli siku zote, na kwa sababu umewatoa kwenye mikono ya upanga wakati wa mateso yao, wakati adhabu yao itakapokuwa katika ukubwa wake.
\v 6 Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-nitaandaa kwa ajili ya damu, na damu na kukufutilia! Kwa kuwa hukuchukia damu, damu itakufuatilia.
\s5
\v 7 Nitaufanya Mlima Seiri mkamilifu na ukiwa wakati nitakapoukatilia mbali kutoka huo yeyote apitaye na arudiye tena.
\v 8 Kisha nitaijaza milima kwa watu wao waliokufa. Milima yako na mabonde na mifereji-wale walioawa kwa upanga wataanguka kati yao.
\v 9 Nitakufanya mkiwa daima. Miji yako haitakaliwa na watu, lakini mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 10 Umesema, "Haya mataifa mawili na hizi nchi mbili zitakuwa zangu, na tutazimiliki," hata wakati Yahwe alipokuwa pamoja nao.
\v 11 Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo nitafanya kulingana na hasira yako na kulingana na wivu wako ambao uliousikia katika chuki yako ya Israeli, na nitajidhihirisha kwao nitakapokuhukumu.
\s5
\v 12 Hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeyasikia matukano yako yote uliyasema dhidi ya milima ya Israeli, uliposema, "Wameharibiwa; wametolewa kwetu tuwale.
\v 13 "Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa kile mlichokisema, na mmeongeza maneno juu yangu; na kuyasikia yote.
\s5
\v 14 Bwana Yahwe asema hivi: Nitakufanya ukiwa, wakati dunia nzima itakapofurahi.
\v 15 Kama vile unavyofurahi juu ya urithi wa watu wa Israeli kwa sababu ukiwa ya wake, ndivyo nitakavyokutenda wewe. Utakuwa ukiwa, Mlima Seiri, na Edomu yote! Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\c 36
\p
\v 1 "Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, 'Milima ya Israeli, lisikilizeni neno la Yahwe.
\v 2 Bwana Yahwe asema hivi: Adui amesema kuhusu ninyi, "Aha!" na "Mahala pa juu pa zamani pamekuwa milki yetu."'
\v 3 Kwa hiyo tabiri na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ya ukiwa wenu na kwa sababu mashambulizi yaliyokuja juu yenu kutoka pande zote, mmekuwa milki ya mataifa mengine; mmeambiwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu.
\s5
\v 4 Kwa hiyo, milima ya Israeli, sikilizeni neno la Bwana Yahwe: Bwana Yahwe asema hivi kwa milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, mahali palipoharibika kuwa ukiwa na miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kutokuwa huru kwa kutaniwa na mataifa yaliyowazunguka-
\v 5 kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Hakika nimeongea katika moto wa hasira yangu juu ya mataifa meningine, juu ya Edemu na wote waliochukua nchi yangu kwa ajili yao wenyewe kama milki, dhidi ya wale walikuwa na furaha yote katika mioyo yao na dharau katika roho zao, kama walivyoitwaa nchi yangu kwamba wangeweza kudai nchi za malisho kwa ajili yao.
\v 6 Kwa hiyo, tabiri kwa nchi ya Israeli na sema kwa milima na vilima, hata kwenye mifereji na mabonde, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Katika ghadhabu yangu na hasira yangu nasema hivi kwa sababu mmechukua fedheha za mataifa.
\s5
\v 7 Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Mimi mwenyewe nitainua mkono wangu kuapa kwamba mataifa yanayowazunguka yamkini yatawabebea aibu yao wenyewe.
\s5
\v 8 Lakini ninyi, milima ya Israeli, mtachipuza matawi na kuzaa matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa kuwa watarudi kwenu.
\v 9 Maana tazama, nipo kwa ajili yenu, na kuwachukulia kwa fadhili; mtalimwa na kupandwa mbegu.
\s5
\v 10 Hivyo nitawaongeza juu ya milima yenu watu katika nyumba ya Israeli, yote. Miji itakaa na palipoharibiwa kujengwa.
\v 11 Nitaongeza mtu na wanyama juu yenu milima ili kwamba itaongezeka na kuzaa. Kisha nitawafanya kuishi kama mlivyokuwa, na nitawafanya kustawi zaidi kuliko mlivyokuwa zamani, kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\v 12 Nitawaleta watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watakumiliki, na utakuwa urithi wao, na hutasababisha tena watoto wao kufa.
\s5
\v 13 Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu wanakwambia, "Wewe unakula watu, na watoto wa nchi yako wamekufa,"
\v 14 kwa hiyo hautawala watu wangu tena, na hutalifanya tena taifa lako kuomboleza vifo vyao. Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 15 Wala sintokuruhusu kusikiliza fedhiha za mataifa tena; hautachukua tena aibu ya watu au kufanya taifa lako kuanguka-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\v 16 Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
\v 17 "Mwanadamu, wakati nyumba ya Israeli walipoikalia nchi yao, waliinajisi kwa njia zao na matendo yao. Njia zao zilikuwa kama uchafu wa hedhi ya mwanamke mbele yangu.
\v 18 Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa ajili ya damu ambayo waliyoimwaga juu ya nchi na kwa ajili ya uchafu wa hiyo kwa sanamu zao.
\s5
\v 19 Nimewatawanya miongoni mwa mataifa; walitawanyika katika nchi nyingi. Nimewahukumu kulingana na njia zao na matendo yao.
\v 20 Kisha wakaenda kati ya mataifa, na popote walipoenda, walilitukana jina langu takatifu wakati watu waliwasema, 'Je! hawa kweli ni watu wa Yahwe? Kwa kuwa wamefukuzwa nje ya nchi yake.
\v 21 Lakini nilikuwa na huruma kwa ajili ya jina langu takatifu ambalo nyumba ya Israeli walilinajisi miongoni mwa mataifa, walipoenda huko.
\s5
\v 22 Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Sifanyi haya kwa ajili yenu, nyumba ya Israeli, lakini jina langu, mlilolitukana miongoni mwa mataifa kila sehemu mlipoenda.
\v 23 Kwa kuwa nitalifanya jina langu kuu kuwa takatifu, mlilolitukana miongoni mwa mataifa-katikati ya mataifa, mmelitukana. Kisha mataifa watajua kwamba mimi ni Yahwe-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe-asemavyo-wakati mtakapoona kwamba mimi ni mtakatifu.
\s5
\v 24 Nitawachukua kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka kila nchi, na nitawaleta hata nchi yenu.
\v 25 Kisha nitanyunyiza maji masafi juu yenu ili muwe wasafi kutoka kwenye uchafu wote, na nitawasafisha kutoka sanamu zenu zenu.
\s5
\v 26 Nitawapatia moyo mpya na roho mpya sehemu zenu za ndani, na nitautoa moyo wa jiwe kutoka kwenye nyama zenu. Kwa kuwa nitawapatia moyo wa nyama.
\v 27 Nitaiweka Roho yangu ndani yenu na kuwawezesha kutembea katika sheria zangu na kuziweka hukumu zangu, hivyo mtazitenda.
\v 28 Kisha mtakaa katika nchi niliyowapa babu zenu; mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.
\s5
\v 29 Kwa kuwa nitawaokoa kutokana na uchafu wenu wote. Nitaita ngano kuiongeza. Sitaweka tena njaa juu yenu.
\v 30 Nitaongeza tunda la mti na kuzalisha kwenye mashamba ili kwamba msichukue tena aibu ya njaa juu ya mataifa.
\v 31 Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya na matendo yenu ambayo hayakuwa mazuri, na mtaonyesha chuki kwenye nyuso zenu kwa sababu ya dhambi zenu na matendo yenu maovu.
\s5
\v 32 Sifanyi hili kwa ajili yenu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ijulikane kwenu. Hivyo tahayarikeni na kufadhaika kwa sababu ya njia zenu, nyumba ya Israeli.
\v 33 Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyowatakasa kutoka kwenye uovu wenu wote, nitawafanya miji ikaliwe na kuzijenga sehemu zilizoharibiwa.
\v 34 Kwa kuwa mtailima nchi iliyoharibiwa hadi itakapoonekana haijaaharibika mbele za macho ya wote wapitao karibu.
\s5
\v 35 Kisha watasema, "Hii nchi ilikuwa ukiwa, lakini imekuwa kama bustani ya Edeni; miji ya ukiwa na isiyo na wakaaji iliyo magofu ambayo ilibomolewa sasa inakaliwa.
\v 36 Kisha mataifa mengine waliowazunguka watajua yakwamba mimi ni Yahwe, kwamba nimejenga palipokuwa pameharibiwa na kuipanda mbegu sehemu iliyokuwa ukiwa.
\s5
\v 37 Bwana Yahwe asema hivi: Tena nitaulizwa na nyumba ya Israeli kufanya hivi kwa ajili yao, kuwaongeza kama kundi la watu.
\v 38 Kama kundi lililotengwa kwa ajili ya sadaka, kama kundi katika Yerusalimu katika sikukuu yake iliyoteuliwa, hivyo miji itaharibiwa kwa kujazwa na makundi ya watu na watajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\c 37
\p
\v 1 Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu, na akanitoa kwa Roho wa Bwana Yahwe na kuniweka chini katikati ya bonde; lilikuwa limejaa mifupa.
\v 2 Kisha akanifanya kupita kati yao kuizunguka pande zote. Tazama! Mingi yao mikubwa ilikuwa katika bonde! Ilikuwa mikavu sana.
\v 3 Akanambia, "Mwanadamu, Je! Hii mifupa inaweza kuishi kinyume?" Hivyo nikasema, "Bwana Yahwe, wajua wewe pekee."
\s5
\v 4 Kisha akanambia, "Tabiri juu ya hii mifupa na iambie, 'Mifupa mikavu. Lisikilizeni neno la Yahwe.
\v 5 Bwana Yahwe asema hivi kwenye hii mifupa: Tazama! nakaribia kuweka pumzi juu yenu, nanyi mtaishi.
\v 6 Nitaweka mishipa juu yenu na kuleta nyama juu yenu. Nitawafunika kwa ngozi na kuweka pumzi ndani yenu hivyo mtaishi. Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe."'
\s5
\v 7 Hivyo nimetoa unabii kama nilivyokuwa nimeamriwa: nimetabiri, tazama, sauti ikaja, iliyokuwa ya mtetememo. Kisha mifupa ikasogeleana pamoja-mfupa juu ya mfupa.
\v 8 Nikatazama na, kumbe, mishipa ilikuwa juu sasa, na nyama ikatoka juu na ngozi ikazifunika. Lakini hapakuwa na pumzi juu yao.
\s5
\v 9 Kisha Yahwe akanambia, "Itabirie pumzi, tabiri, mwanadamu, na iambie pumzi, 'Bwana Yahwe asema hivi: Pumzi, hutoka pepo nne, na pumzi juu ya hawa walioawa, hivyo wanaweza kuishi."'
\v 10 Hivyo nimetabiri kama nilivyokuwa nimeamriwa; pumzi ikawajilia na wakaishi. Kisha wakasimama kwa miguu yao, jeshi moja kubwa sana.
\s5
\v 11 Kisha Yahwe akanambia, "Mwanadamu, mifupa hii yote ni ya nyumba ya Israeli. Tazama! Wanasema, 'Mifupa yetu imekauka, na tumaini letu limepotea. Tumekatwa.'
\v 12 Kwa hiyo tabiri na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nitayafunua makabiri yenu na kuwapandisha kutoka kwayo, watu wangu. Nitakurudisha hata katika nchi ya Israeli.
\s5
\v 13 Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapo yafunua makaburi yenu na kuwatoa kutoka kwao, watu wangu.
\v 14 Nitaweka Roho wangu ndani yenu hivyo mtaishi, na nitawafanya kupumzika katika nchi yenu mtakapojua yakwamba mimi ni Yahwe. Nasema na nitayafanya hayo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."'
\s5
\v 15 Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 16 "Sasa wewe, mwanadamu, chukua fimbo moja kwa ajili yako na andika juu yake, 'Kwa ajili Yuda na kwa ajili ya watu wa Israeli, wenzake,' Kisha fimbo nyingine andika juu yake, 'Kwa kuwa Yusufu, tawi la Efraimu, na kwa ajili ya watu wa Israeli, wenzake.
\v 17 Walete wote pamoja kwenye fimbo moja, ili wawe kitu kimoja katika mkono wako.
\s5
\v 18 Wakati watu wako watakapokwambia na kusema, 'Je! hutatuambia haya mambo yako yana maana gani?'
\v 19 kisha waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nalichukua tawi la Yusufu ambalo lipo kwenye mkono wa Efraimu na kabila za Israeli wenzake na kuungana nalo hata kwenye tawi la Yuda, ili kwamba wawe tawi moja, na watakuwa kitu kimoja katika mikono yangu.'
\v 20 Shika kwenye mkono wako na matawi uliyoandika mbele ya macho yao.
\s5
\v 21 Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! nakaribia kuwachukua watu wa Israeli kutoka miongoni mwa mataifa walipoenda. Nitawakusanya kutoka nchi zilizozunguka na nitawaleta kwenye nchi yao.
\v 22 Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, juu ya milima ya Israeli, na kutakuwa na mfalme mmoja kama mfalme juu yao wote, na hawatakuwa mataifa mawili tena. Hawatagawanyika kwenye falme mbili tena.
\v 23 Kisha hawatajitia unajisi tena kwa sanamu zao, mambo yao yachukizao, au dhambi zao nyingine. Kwa kuwa nitawaokoa kutoka matendo yao ya uongo ambayo wamefanya dhambi, na nitawatakasa, hivyo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.
\s5
\v 24 Daudi mtumishi wangu atakuwa mfalme juu yao. Hivyo kutakuwa na mchungaji mmoja juu yao wote, na wataishi kulingana na sheria zangu na watazitunza amri zangu na kuzitii.
\v 25 Wataishi katika nchi niliwapatia watumishi wangu Yakobo, ambapo baba zenu walipoishi. Wataishi humo milele-wao, watoto wao, na wajukuu zao, kwa Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele.
\s5
\v 26 Nitaweka agano la amani pamoja nao. Litakuwa agano la milele pamoja nao. Nitawaweka na kuwazidisha na kupaweka mahali patakatifu pangu katikati yao milele.
\v 27 Maskani yangu yatakuwa pamoja nao; Nitakuwa Mungu wao, na watakuwa watu wangu.
\v 28 Kisha mataifa watajua yakwamba mimi ni Yahwe niliyewatenga Israeli, wakati mahali pangu patakatifu patakapokuwa katikati yao milele."
\s5
\c 38
\p
\v 1 Neno la Yahwe likanijia, likisema,
\v 2 "Mwanadamu, weka uso wako kumwelekea Gogu, nchi ya Magogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali; na kutabiri dhidi yake.
\v 3 Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Gogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali.
\s5
\v 4 Hivyo nitakugeuza na kuweka kulabu kwenye taya yako; nitakupeleka nje pamoja na jeshi lako lote, farasi, na waendesha farasi, wote wakiwa wamevaa silaha, kusanyiko kubwa pamoja na ngao ndogo na ngao kubwa, wote wakishikilia panga!
\v 5 Persia, Kushi, Uajemi wapo pamoja nao, wote pamoja na ngao na chapeo!
\v 6 Gomeri na jeshi lake lote, na Beth-Togarma, kutoka sehemu za mbali ya kaskazini, na jeshi lake lote! Watu wengi wako pamoja nawe!
\s5
\v 7 Kuwa tayari! Ndio, jiandae na jeshi lako waliokusanyika pamoja na wewe, na amiri wao mkuu.
\v 8 Utaitwa baada ya siku nyingi, na baada ya miaka michache utaenda kwenye nchi iliyofunikwa kutoka upanga na ambayo iliyokusanywa kutoka watu wengi, iliyowkusanya kuwarudisha milima ya Israeli ambayo imeendelea kuangamizwa. Lakini watu wa nchi watatolewa na kabila za watu, na wataishi salama, wote!
\v 9 Hivyo utapanda juu kama tufani iendavyo; utakuwa kama wingu lililofunika nchi, wewe na jeshi lako lote, maaskari wako wote pamoja na wewe.
\s5
\v 10 Bwana Yahwe asema hivi: Itakuwa siku hiyo hayo mawazo yataingia moyoni mwako, na utatunga njama mbaya.'
\v 11 Kisha utasema, 'nitapanda hata nchi iliyowazi; nitaenda hata kwa watu wapole waishio salama, wote wakiishi mahali ambapo hakuna kuta wala makomeo, na mahali ambapo hakuna malango ya mji.
\v 12 Nitanyakua mateka na kuiba mateka, ili nilete mkono wangu juu kuwaangamiza wale wakazi wapya, na juu ya watu waliokusanyika kutoka mataifa, watu wale waongezao wanyama na mali, na wale waishio katikatika ya dunia.'
\s5
\v 13 Sheba na Denani, na wafanya biashara wa Tarshishi pamoja na mahodari wake wote watakwambia, 'Je, umekuja kuteka nyara? Je, umewakusanya majeshi yako kuchukua mateka, kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua mifugo yao na mali na kuwakokota mateka wengi sana?'
\s5
\v 14 Kwa hiyo tabiri, mwanadamu, na mwambie Gogu, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku hiyo, wakati watu wangu Israeli watakapoishi salama, je, hutajifunza kuhusu wao?
\v 15 Utakuja kutoka mahali pangu mbali katika kaskazini pamoja na jeshi kubwa, wote wakiendesha farasi, kusanyiko kubwa, jeshi kubwa.
\v 16 Utawashambulia watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Katika siku za baadaye nitakuleta juu ya nchi yangu, ili mataifa wanijue nitakapojifunua mwenyewe kupitia wewe, Gogu, kuwa mtakatifu mbele ya macho yao.
\s5
\v 17 Bwana Yahwe asema hivi: Je, wewe siye yule ambaye niliyeongea naye katika siku za zamani kwa mkono wa watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri katika mda wao wenyewe kwa miaka niliyowaleta juu yao?
\v 18 Basi itakuwa katika siku hiyo wakati Gogu atakapo ishambulia nchi ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ghadhabu yangu itapanda katika hasira yangu.
\s5
\v 19 Katika wivu wangu katika hasira ya moto wangu, ninasema kwamba katika siku hiyo kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi katika nchi ya Israeli.
\v 20 Watatetemeka mbele yangu-samaki wa baharini na ndege wa angani, wanyama wa mashambani, na viumbe watambaao juu ya nchi, na kila mtu aliyeko juu ya uso wa nchi. Milima itaangushwa chini majabali yataanguka, hadi kila ukuta utaanguka kwenye nchi.
\s5
\v 21 Nitaita upanga dhidi yake juu ya milima yangu yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-upanga wa kila mtu utakuwa kinyume na ndugu yake.
\v 22 Kisha nitamuhukumu kwa tauni na damu; nakufurika mvua na mvua ya mawe na kuchoma asidi nitainyeshea chini juu yake na jeshi lake na mataifa mengi yaliyo pamoja naye.
\v 23 Kwa kuwa nitaonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu na nitafanya kujulikana mimi mwenyewe katiaka macho ya mataifa mengi, na watajua kwamba mimi ni Yahwe."
\s5
\c 39
\p
\v 1 "Kisha wewe, mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! ni kinyume nawe, Gogu, mkuu wa Mesheki na Tubali.
\v 2 Nitakugeuza na kukuongoza; nitakupandisha juu kutoka mbali kaskazini na kukuleta hata milima ya Israeli.
\v 3 Kisha nitaufunga upinde wako utoke katika mkono wako wa kushoto na kuifanya mishale kuanguka kutoka kwenye mkono wako wa kuume.
\s5
\v 4 Utaanguka juu ya milima ya Israeli-wewe na jeshi lako late na maaskari walio pamoja nawe. Nitawapatia ndege mbua na wanyama pori wa mashambani kwa ajili ya chakula.
\v 5 Utaanguka juu ya uso wa shamba, kwa kuwa mimi mwenyewe nimesema hivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 6 Kisha nitapeleka moto juu ya Magogu na kwa wale waishio salama juu ya pwani, na watajua yakwamba mimi ni Yahwe.
\s5
\v 7 Kwa kuwa nitalifanya jina langu takatifu lijulikane kati ya watu wangu Israeli, na sitaruhusu tena jina langu takatifu litukanwe; mataifa watajua kwamba mimi ni Yahwe, Mtakatifu katika Israeli.
\v 8 Tazama! Siku inakuja, na itachukua nafasi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 9 Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka nje na watatumia silaha kuwasha moto na kutengeneza moto na kuwachoma-ngao ndogo, ngao kubwa, pinde, mishale, rungu, na mikuki; watatengeneza mioto pamoja nao kwa muda wa siku saba.
\v 10 Hawatakusanya kuni kutoka mashambani wala kukata miti kutoka kwenye misitu, kwa kuwa watazichoma hizo silaha; watawateka nyara wale watakaotaka kuwateka nyara-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\v 11 Kisha itakuwa katika hiyo siku ambayo nitaifanya sehemu huko kwa ajili ya Gogu-kaburi la Israeli, bonde kwa ajili ya wale wanaosafiri hata mashariki ya bahari. Litawazuia wale wanaotegemea kupita. Huko watamzika Gogu pamoja na kundi lake lote. Watapaita bonde la Hamon-Gogu.
\s5
\v 12 Kwa muda wa siku saba nyumba ya Israeli itawazika ili kuitakasa nchi.
\v 13 Kwa kuwa watu wa nchi watawazika; itakuwa siku ya kukumbukwa kwao wakati nitakapotukuzwa-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 14 Kisha watawateua watu kuendelea kwenda kwenye nchi, kuwatafuta wale waliokuwa wakisafiri, lakini waliokufa na miili yao kubaki juu ya uso wa nchi, ili kwamba waweze kuwazika, kwa ajili ya kusafisha nchi. Katika siku ya mwisho ya mwezi wa saba wataanza kutafuta.
\v 15 Kama hawa watu wapitao kwenye nchi, watakapoona mfupa wowote wa binadamu, wataweka alama kwa huo, hadi wachimba kaburi watakapokuja na kuizika katika bonde la Hamoni Gogu.
\v 16 Kutakuwa na mji huko unaitwa Hamona. Wataitakasa nchi kwa njia hii.
\s5
\v 17 Kwako wewe, mwanadamu, Bwana Yahwe asema hivi: Waambie ndege wote wenye mabawa na wanyama wote wa porini katika mashamba, 'Kusanyikeni pamoja na mje. Kusanyikeni kutoka pande zote kwenda kwenye dhabihu yote ambayo mimi mwenyewe ninayoifanya kwa ajili yako, dhabihu kubwa juu ya milima ya Israeli, ili kwamba mle nyama na kunywa damu.
\v 18 Mtakula nyama ya walio hodari na kunywa damu ya wakuu wa dunia; watakuwa kondoo waume, wana kondoo, mbuzi, na ng'ombe, wote walikuwa wanene katika Basheni.
\s5
\v 19 Kisha mtakula mafuta hata kuridhika kwenu; mtakunywa damu hadi kulewa; hii itakuwa dhabihu nitakayoichinja kwa ajili yenu.
\v 20 Mtatosheka kwenye meza yangu pamoja na farasi, magari ya farasi, shujaa, na kila mtu wa vita-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
\s5
\v 21 Nitauweka utukufu wangu kati ya mataifa, na mataifa yote yataona hukumu yangu ninayoionyesha na mkono wangu nimeuweka juu yao.
\v 22 Nyumba ya Israeli itajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wao kutoka hiyo siku na kuendelea.
\s5
\v 23 Mataifa yatajua kwamba nyumba ya Israeli wameenda uhamishoni kwa sababu ya udhalimu wao kwa kunisaliti, hivyo naficha uso wangu kwao na kuwaweka kwenye mkono wa maadui zao ili kwamba wote waanguke kwa upanga.
\v 24 Nimewafanyia kutokana na uchafu wao na dhambi zao, nitakapokuwa nimeuficha uso wangu kwao.
\s5
\v 25 Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Sasa nitawarudisha watu wa Yakobo, na kuwa na huruma juu ya nyumba yote ya Israeli, wakati nitakapoona wivu kwa ajili ya jina langu.
\v 26 Kisha watabeba aibu yao na uhaini mkubwa walio nihaini. Watayasahau haya yote watakapopumzika katika nchi yao katika usalama, wala hakuna mtu atakaye waogofya.
\v 27 Wakati nitakapokuwa nimewarudisha kutoka kwa watu na kuwakusanya kutoka kwenye nchi za maadui zao, nitajionyesha mimi mwenyewe kuwa mtakatifu kwenye uso wa mataifa mengi.
\s5
\v 28 Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe Mungu wao, kwa kuwa nimewapeleka utumwani kati ya mataifa, lakini kisha nitawakusanya kuwarudisha hata nchi yao. Sitamuacha hata mmoja wao kati ya mataifa.
\v 29 Sitawaficha uso wangu kwao wakati nitakapomwaga Roho wangu katika nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\c 40
\p
\v 1 Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu mwanzoni mwa mwaka siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya mji kuchukuliwa-katika siku hiyo hiyo, mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu na alinichukua huko.
\v 2 Katika maono ya Mungu akanileta hata nchi ya Israeli. Akanileta kupumzika juu ya kila mlima mrefu sana; upande wa kusini kulikuwa na monekano kana kwamba majengo ya mji.
\s5
\v 3 Kisha akanileta huko. Tazama, kulikuwa na mtu! Mwonekano wake ulikuwa kama mwonekano wa shaba. Alikuwa na uzi wa kitani na mwanzi wa kupimia mkononi mwake, na alisimama katika lango la mji.
\v 4 Huyo mtu akanambia, "Mwanadamu, tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako, na elekeza moyo wako juu ya yote ninayokufunulia, kwa kuwa ulinileta hapa ili niweze kukufunulia haya wewe. Toa taarifa ya kila kitu utakachokiona kwa nyumba ya Israeli.
\s5
\v 5 Kulikuwa ukuta uliokuwa umezunguka eneo la hekalu. Urefu wa kipimo cha mwanzi katika mkono wa mtu ulikuwa dhiraa sita urefu, kila urefu wa dhiraa ulikuwa dhiraa moja na kipimo cha kiganja cha mkono urefu. Aliupima ukuta; ulikuwa kipimo cha mwanzi mmoja na ufito mmoja urefu.
\v 6 Kisha akaenda hata kwenye lango la hekalu lililokuwa limeelekea mashariki. Akapanda ngazi na kuipima kizingiti cha lango-mwanzi mmoja upana.
\v 7 Vyumba vya ulinzi vilikuwa kila mwanzi mmoja urefu na mwanzi mmoja upana; kulikuwa na dhiraa tano katika kila vyumba viwili, na kizingiti cha lango la hekalu karibu na tawa la hekalu kilikuwa mwanzi mmoja urefu.
\s5
\v 8 Akapima tawa la lango; ulikuwa mwanzi mmoja urefu.
\v 9 Akapima tawa la lango. Ilikuwa mwanzi mmoja kwenda chini. Mihimili ilikuwa dhiraa mbili upana. Hili lilikuwa tawa la lango kuelekea hekalu.
\v 10 Kulikuwa na vyumba vitatu vya ulinzi pande zote za lango la mashariki, na yote yalikuwa na kipimo kile kile, na kuta zilizokuwa zimezigawanya zilikuwa na kipimo kile kile.
\s5
\v 11 Kisha yule mtu akapima upana wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi; na akapima urefu wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi na tatu.
\v 12 Akaupima ukuta uliokuwa mpaka mbele ya vyumba-dhiraa moja urefu. Vyumba vilipimwa dhiraa sita kila upande.
\v 13 Kisha akapima lango la njia kutoka kwenye paa ya chumba kimoja kuelekea chumba kingine-dhiraa ishirini na tano, kutoka lango la kuingia chumba cha kwanza kuelekea kile cha pili.
\s5
\v 14 Kisha akapima ukuta uliokuwa umeenda kati ya vyumba vya ulinzi-dhiraa sitini urefu; alipima kwa mbali na tawa la lango.
\v 15 Lango la kuingia kutoka lango la mbele kuelekea lango jingine la tawa la mwisho lilikuwa dhiraa hamsini.
\v 16 Kulikuwa na madirisha yaliyokuwa yamefungwa kuelekea vyumba na kuelekea nguzo zake kati ya malango kuzunguka kote; na vivyo hivyo kwa mabaraza. Kulikuwa na madirisha pande zote za ndani, na kila mhimili ulikuwa umepambwa kwa mitende.
\s5
\v 17 Kisha huyo mtu akanileta hata ua wa nje mwa hekalu. Tazama, kulikuwa na vyumba, na kulikuwa na kibamba katika ua, pamoja na vyumba thelathini baada ya kibamba.
\v 18 Kibamba kilienda juu hata upande wa malango, na upana wake ulikuwa sawsawa na urefu wa malango. Hiki kilikuwa kibamba cha chini.
\v 19 Kisha huyo mtu akapima umbali kutoka mebele ya lango la chini hata mbele ya lango la ndani; ilikuwa dhiraa mia moja upande wa mashariki, na sawasawa na upande wa kaskazini.
\s5
\v 20 Kisha akapima urefu na upana wa lango lililokuwa upande wa kaskazini mwa ua wa nje.
\v 21 Kulikuwa na vyumba vitatu pande zote za lango, na lango na matawa yake yalipimwa sawa na lango kubwa-dhiraa hamsini upana wote na dhiraa ishirini na tano upana.
\s5
\v 22 Madirisha yake, tawa, vyumba, na mitende yake vilikabiliana na lango ambalo linaloelekea mashariki. Ngazi saba kuupandia juu hata kwenye tawa lake.
\v 23 Kulikuwa na lango kwenye ua wa ndani mbele kuelekea mashariki; huyo mtu alipima kutoka lango moja hadi lango jingine-dhiraa mia moja umbali.
\s5
\v 24 Kisha huyo mtu akanileta hata kwenye lango la kuingia la kusini, na kuta zake na tawa vilipimwa sawa kama malango mengine ya nje.
\v 25 Kulikuwa na madirisha yaliyofungwa katika lango la njia na tawa lake kama lile lango. Lango la kusini na tawa lake vilipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
\s5
\v 26 Kulikuwa na ngazi saba hadi kwenye lango na matawa yake, na kulikuwa na mitende iliyochongoka juu ya kuta pande zote.
\v 27 Kulikuwa na lango la ua wa ndani upande wa kusini, na yule mtu akapima kutoka hilo lango hata lango la kuingia upande wa kusini-dhiraa mia moja umbali.
\s5
\v 28 Kishi huyo mtu akanileta hata ua wa ndani karibu na lango lake la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo vile vile kama malango mengine.
\v 29 Vyumba vyake, kuta, na matao vilipimwa sawa kama malango mengine; kulikuwa na madirisha kuzunguka matao yote. Lango la ndani na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
\v 30 Pia kulikuwa na matao pande zote za kuta za ndani; haya yalikuwa dhiraa ishirini na tano urefu na dhiraa tano upana.
\v 31 Hili tawa lilielekea ua wa nje pamoja na mitende iliyochongwa juu ya kuta zake na ngazi nane kuupandia.
\s5
\v 32 Kisha yule mtu akanileta hata kwenye ua wa ndani karibu na njia ya kaskazini na kulipima lango, ambalo lilikuwa na vipimo sawa kama malango mengine.
\v 33 Vyumba vyake, kuta, na matawa yalikuwa na kipima sawa kama cha malango, na kulikuwa na madirisha pande zote. Laango la ndani na matawa yake yalikuwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
\v 34 Matawa yake yalielekea nje ya ua; ilikuwa na mitende pande zote za hiyo na ngazi nane za kuupandia.
\s5
\v 35 Kisha huyo mtu akanileta hata lango la kaskazini na kulipima; likapimwa vivyo hivyo kama malango mengine.
\v 36 Vyumba vyake, kuta, na ukumbi vilipimwa sawa na malango mengine, na kulikuwa na madirisha pande zote. Njia ya lango na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na upana dhiraa ishirini na tano.
\v 37 Tatawa lake lilielekea ua wa nje; ilikuwa na mitende pande zote za huo na ngazi nane kuupandia.
\s5
\v 38 Kulikuwa na chumba pamoja na mlango karibu na kila lango la ndani. Hapa ndipo ambako walipooshea sadaka za kutekezwa.
\v 39 Kulikuwa na meza mbili kila upande wa kila ukumbi, ambako sadaka ya kuteketezwa ilipochinjiwa, na pia sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
\s5
\v 40 Karibu na ukuta wa ua, kuelekea juu kwenye lango kuelekea kaskazini, kulikuwa na meza mbili. Pia kwa upande mwingine kulikuwa na meza mbili kwenye lango la ukumbi.
\v 41 Kulikuwa na meza nne pande zote karibu na lango; wakachinja wanyama juu ya meza nane.
\s5
\v 42 Kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, dhiraa moja na nusu urefu, dhiraa moja na nusu upana, na kimo dhiraa moja. Juu yake waliweka vyombo pamoja ambavyo walivichinjia sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya sadaka.
\v 43 Kulabu mbili ujazo wa kiganja urefu uliokuwa umeunganishwa katika ua pande zote, na nyama ya matoleo ilikuwa imewekwa juu ya meza.
\s5
\v 44 Karibu na lango la ndani, katika ua wa ndani, kulikuwa na vyumba vya waimbaji. Moja ya hivi vyumba kilikuwa upande wa kaskazini, na kingine kusini.
\v 45 Kisha yule mtu akanambia, "Hiki chumba kinachoelekea kusini ni kwa ajili ya makuhani walio zamu katika hekalu.
\s5
\v 46 Chumba kilichoelekea kaskazini kilikuwa kwa ajili ya makuhani waliokuwa zamu kwenye madhabahu. Hawa ni wana wa Sadoki ambaye huja humkaribia Yahwe kumtumikia; ambao ni miongoni mwa wana wa Lawi."
\v 47 Kisha akaupima ule ua-dhiraa mia moja urefu na dhiraa mia moja upana mraba, pamoja na madhabahu mbele ya nyumba.
\s5
\v 48 Kisha yule mtu akanileta hata kwenye varanda ya nyumba na kupima mwimo wa milango yake-ilikuwa dhiraa tano unene upande huu. Njia ya kuingilia yenyewe ilikuwa dhiraa kumi na nne, na kuta pande zote za huo zilikuwa dhraa tatu upana.
\v 49 Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa kumi na moja. Kulikuwa na ngazi zilizokuwa zimepanda juu na nguzo zilizokuwa zimesimama pande zote za huo.
\s5
\c 41
\p
\v 1 Kisha yule mtu akanileta mahali patakatifu pa hekalu na mihimili-dhiraa sita upana pande zote.
\v 2 Upana wa maingilio ulikuwa dhiraa kumi; ukuta kila upande dhiraa tano urefu kila upande. Kisha yule mtu akapima ukubwa wa mahali patakatifu-dhiraa arobaini upana urefu na dhiraa ishirini upana.
\s5
\v 3 Kisha yule mtu akaenda hata mahali patakatifu sana na kuipima miimili ya matokeo-dhiraa mbili-kuta pande zote zilikuwa dhiraa saba upana.
\v 4 Kisha akapima urefu wa vyumba-dhiraa ishirini. Upana wake-dhiraa ishirini hata mbele kwenye ukumbi wa hekalu. Kisha akanambia, "Hapa ndipo mahali patakatifu sana."
\s5
\v 5 Kisha yule akapima kuta za nyumba-zilikuwa dhiraa sita unene. Upana wa kila upande wa chumba kuzunguka nyumba dhiraa nne upana.
\v 6 Kulikuwa na pande tatu za vyumba, chumba kimoja juu ya kingine, vyumba thelathini, kulikuwa na kibao kitokezacho ukutani kuzunguka ukuta wa nyumba, kusaidia pande zote za vyumba, kwa kuwa hapakuwa na msaada uliokuwa umewekwa kwenye ukuta wa nyumba.
\v 7 Hivyo mbavu za nyumba zilipanuka na kuzunguka kwenda juu, kwa kuwa nyumba ilizunguka kwenda juu, na ngazi kuelekea juu hata sehemu ya juu, kupitia sehemu ya katikati.
\s5
\v 8 Kisha nikaona sehemu iliyoinuka kuzunguka nyumba, msingi kwa ajili ya pande za vyumba; ikapimwa fimbo nzima urefu-dhiraa sita.
\v 9 Upana wa ukuta wa vyumba vya pembeni kwa upande wa nje ulikuwa dhiraa tano. Kulikuwa na sehemu ya wazi kwa upande wa nje wa hivi vyumba katika patakatifu.
\s5
\v 10 Kwa upande mwingine wa hii sehemu ya wazi kulikuwa na vyumba vya makuhani upande wa nje; hii sehemu ilikuwa na dhiraa ishirini upana kupazunguka patakatifu.
\v 11 Kulikuwa na milango kwenye vyumba vya pembeni kutoka sehemu ya wazi nyingine-njia ya mlango moja uliokuwa upande wa kaskazini, na mwingine upande wa kusini. Upana wa hili eneo la wazi ulikuwa na dhiraa tano kupazunguka.
\s5
\v 12 Lile jengo lililokuwa limeelekea kwenye ua upande wa magaribi dhiraa sabini upana. Ukuta wake ulipimwa dhiraa tano pande zote, na ilikuwa dhiraa tisini urefu.
\v 13 Kisha yule mtu akapapima patakatifu-dhiraa mia moja urefu. jengo lililokuwa limetengeka, kuta zake, na kwenye ua pia palipimwa dhiraa mia moja urefu.
\v 14 Upana wa mbele kwenye ua mbele ya patakatifu pia kulikuwa dhiraa mia moja.
\s5
\v 15 Kisha yule mtu akapima urefu wa jengo karibu na patakatifu, kwa upande wake wa magharibi, na juu ya baraza pande zote-dhiraa mia moja. Mahali patakatifu na varanda,
\v 16 kuta za ndani na madirisha, pamoja na madirisha madogo, na baraza za pande zote kwenye pande tatu, zilikuwa zimefungwa kwa mbao.
\v 17 Juu ya lango la kuingilia hata patakatifu pa ndani na kuwekwa karibu na kuta kulikuwa na pazia lililokuwa limepimwa.
\s5
\v 18 Palikuwa pamepambwa na makerubi mitende; pamoja na mitende kati ya kerubi na kerubi, na kila kerubi lilikuwa na nyuso mbili:
\v 19 uso wa mtu aliyekuwa ameelekea mtende mmoja, na uso wa mwana simba ulitazama kuelekea mtende kwa upande mwingine. Vilifunikwa kuzunguka malango ya kuingia yote ya nyumba.
\v 20 Kutoka chini hata juu kwenye njia ya mlango, makerubi na mtende vilifunikwa na ukuta wa nje ya nyumba.
\s5
\v 21 Mihimili ya lango la mahali patakatifu lilikuwa mraba. Umbo lao lilikuwa kama umbo la
\v 22 kwanza madhabahu ya mbao mbele ya mahali patakatifu, ambapo kulikuwa na dhiraa tatu kwenda juu na dhiraa urefu kwa kila upande. Pembe zake mihimili, kitako, na kiunzi kilitengenezwa kwa mbao. Kisha yule mtu akanambia, "Hii ni meza ambayo itakuwa kwa ajili ya Yahwe."
\v 23 Kulikuwa na milango miwili kwa ajili ya mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.
\v 24 Hii milango ilikuwa na bawaba mbili kila mlango paneli, paneli mbili kwa ajili ya mlango mmoja na paneli mbili kwa ajili ya mwingine.
\s5
\v 25 Ilifunikwa-juu ya milango ya mahali patakatifu ambapo makerubi na mti wa mtende kama kuta ilipambwa, kulikuwa na paa ya mbao juu ya varanda kwa mbele.
\v 26 Kulikuwa na madidsha madogo miti ya mitende kwenye varanda pande zote. Hivyo vilikuwa vyumba vya pembeni ya nyumba, na pia ilizielekea dari.
\s5
\c 42
\p
\v 1 Kisha yule mtu akanituma kwenda ua wa nje upande wa kaskazini, akanileta kwenye vyumba mbele ya ua wa nje na ukuta wa nje kaskazini.
\v 2 Hivyo vyumba vilikuwa dhiraa mia moja karibu na mbele yake na dhiraa hamsini upana.
\v 3 Baadhi ya hivyo vyumba vilielekea ua wa ndani na vilikuwa na dhiraa ishirini kutoka patakatifu. Kulikuwa na vyumba vitatu vinavyolingana, na kingine juu kilichokuwa kimetazama chini kuelekea kingine vilikuwa vimefunguliwa, vilikuwa na pakutokea. Baadhi ya vyumba vilielekea nje kwenye ua wa nje.
\s5
\v 4 Njia dhiraa kumi upana dhiraa mia moja urefu kueleikea mbele ya vyumba. Milango ya vyumba ilikuwa mbele kaskazini.
\v 5 Lakini kumbi za juu zilikuwa ndogo, kwa ajili ya njia za kutembea zilichukua kutoka kwazo sehemu kubwa kulikuwa walivyofanya kwenye vyumba vya chini na katikati usawa wa jengo.
\v 6 Kwa kuwa orofa tatu hapakuwa na mihimili, kama zile nyua, ambazo zilikuwa na mihimili. Hivyo usawa wa vyumba vya juu vilikuwa sawa sawa katika kipimo cha kulinganisha na vyumba vya chini na usawa wa katikakati.
\s5
\v 7 Ukuta wa nje karibu na vyumba mbele ya ua wa nje, ua uliokuwa mbele ya vyumba. Huo ukuta ulikuwa dhiraa hamsini urefu.
\v 8 Urefu wa vyumba vya ua wa nje ulikuwa dhiraa hamsini, na vyumba vilivyokuwa vimeelekea patakatifu vilikuwa dhiraa mia moja urefu.
\v 9 Kulikuwa na mahali pa kuingilia kwenye vyumba vidogo zaidi kutoka upande mashariki, kuingia kutoka ua wa nje.
\s5
\v 10 Karibu na ukuta wa ua wa nje juu ya upande wa mgaribi pa ua wa ndani, mbele ya patakatifu pa ua wa nje, pia kulikuwa na vyumba na njia ya mbele yao.
\v 11 zilikuwa kama umbo la vyumba kwa upande wa kaskazini. Zilikuwa urefu ule ule na upana na matokeo yale yale na mipangilio na madirisha.
\v 12 Kwa upande wa kusini kulikuwa na madirisha kwenye vyumba ambavyo vilikuwa kama yale yaliyokuwa upande wa kaskazini. Aya iliyokuwa ndani ilikuwa na mlango kwenye kichwa chake, na njia ilifunguliwa kwenye vyumba tafauti. Upande mashariki kulikuwa na malango wa njia kwenye njia mwishoni.
\s5
\v 13 Kisha yule mtu akanambia, "Vyumba vya kaskazini na vyumba vya kusini vilivyokuwa mbele ya ua wa nje ni vyumba vitakatifu amabapo makuhani wafanyao kazi karibu sana na Yahwe waweze kula chakula kitakatifu sana. Wataweka vitu vitakatifu sana-sadaka ya chakula, sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia-kwa kuwa hapa ni mahali patakatifu.
\v 14 Wakati makuhani watakapoingia hapo, wasitoke nje ya mahali patakatifu kwa ua wa nje, bila kuweka mavazi karibu mahali wahudumupo, kwa kuwa hapa ni patakatifu. Hivyo watavalia mahali pengine nguo kabla ya kwenda karibu na watu."
\s5
\v 15 Yule mtu akamaliza kupima ndani ya nyumba na kisha akanichukua nje ya lango lililokuwa limeelekea magharibi na kuzipima sehemu zote zilizokuwa zimepazunguka hapo.
\s5
\v 16 Akaupima upande wa mashariki na fimbo ya kupimia-dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia.
\v 17 akaupima upande wa kaskazini-dhiraa mia tano na fimbo ya kupimia.
\v 18 Pia akaupima upande wa kusini dhraa mia tano na fimbo ya kupimia.
\v 19 Pia akageuka na kuupima upande wa magharibi dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia,
\s5
\v 20 Akaipima pande nne. Ilikuwa na ukuta umeizunguka ilikuwa dhiraa mia tano urefu, na dhiraa mia tano upana, kulitenganisha umbo takatifu kutoka ambapo ni pa kawada.
\s5
\c 43
\p
\v 1 Yule mtu kisha akanileta hata kwenye lango lililokuwa linaelekea mashariki.
\v 2 Tazama! Utukufu wa Mungu wa Israeli ukaja kutoka mashariki; sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi, na nchi iling'aa kwa utukufu wake.
\s5
\v 3 Yalikuwa yanalingana na sura ya ono nililolona, kulingana na ono nililokuwa nimeliona wakati alipokuja kuuteketeza mji, na maono yalikuwa kama maono ambayo niliyokuwa nimeyaona Keberi Kanali nikaanguka kifudi fudi.
\v 4 Hivyo utukufu wa Yahwe ukaja kwenye nyumba ya karibu na njia ya lango lililokuwa wazi kwa upande wa magharibi.
\v 5 Kisha Roho akanichukua na kunileta kwenye ua wa ndanni. Tazama! Utukufu wa Yahwe ulikuwa umeijaza nyumba.
\s5
\v 6 Mtu alisimama karibu na mimi, na nikamsikia mtu mwingine akizungumza na mimi kutoka kwenye nyumba.
\v 7 Akanambia, "Mwanadamu, hapa ndipo mahali pangu pa enzi na mahali kwa ajili ya ya miguu yangu, ambapo nitaishi kati ya watu wa Israeli milele. Nyumba ya Israeli haitalikufuru tena jina langu takatifu-wao au wafalme wao katika mahali patakatifu pao.
\v 8 Hawatalikufuru tena jina langu takatifu kwa kuweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu, na nguzo yao ya lango karibu na nguzo yangu ya lango, bila kitu lakini ukuta kati yangu na wao. Wamelikufuru jina langu kwa matendo yao machafu, hivyo nimewala kwa hasira yangu.
\s5
\v 9 Sasa waache waondoe udanganyifu wao na maiti za wafalme wao kutoka kwangu, na nitaishi katikati yao milele.
\s5
\v 10 Mwanadamu, wewe mwenyewe utaiambia nyumba ya Israeli kuhusu nyumba hii hivyo watajiskia aibu ya uovu wao. Wanaweza kutafakari kuhusu haya maelezo.
\v 11 Kwa kuwa wameaibika kwa yote waliyoyafanya, kisha waonyeshe mchoro wa nyumba, maelezo yake, matokeo yake, maingio yake, na mchoro wake, sheria zake zote na kanuni. Kisha andika hivi chini mbele ya macho yao ili waweze kutunza michoro yote na kanuni zake zote, hivyo kama wazitiivo.
\s5
\v 12 Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba: Kutoka kwenye kilele cha mlima hata mpaka wote unaoizunguka, patakuwa patakatifu sana. Tazama! Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba.
\s5
\v 13 Hivi vitakuwa vipimo vya madhabahu katika dhiraa-hiyo dhiraa kuwa dhiraa ya kawaida na urefu wa kiganja. Hivyo mfereji ulio uzunguka madhabahu utakuwa dhiraa moja chini, na upana wake pia utakuwa dhiraa moja. Mpaka wa karibu uizungukayo machinjio shubiri moja. Hii itakuwa kitako cha madhabahu.
\v 14 Usawa wa kutoka kwenye mferji hadi kwenye machinijo ya chini ya madhabahu itakuwa dhiraa mbili, na hiyo machinjio yenyewe itakuwa dhiraa moja upana. Kisha kutoka machinjio madogo hadi kwenye machinjio makubwa ya madhabahu, itakuwa dhiraa nne, na machinjio makubwa yatakuwa dhraa moja upana.
\s5
\v 15 Meko juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ni dhiraa nne juu, na kuna pembe nne zilizoelekea juu kwenye meku.
\v 16 Meku ina dhiraa kumi na moja urefu na dhiraa kumi na mbili upana, za mraba.
\v 17 Mpaka wake ni dhiraa kumi na nne urefu na dhiraa kumi na nne upana pande zake zote nne, na ukingo wake ni nusu dhiraa upana. Mfereji ni dhiraa moja upana kuzuka kote pamoja na ngazi zielekeazo mashariki."
\s5
\v 18 Kisha akanambia, "Mwanadamu, Bwana Yahwe asema hivi: Hizi ndizo sheria kwa ajili ya madhabahu katika siku watakayoitengeza, kwa ajili kutoa sadaka ya kuteketezwa kwenye hiyo, na kwa jili ya kunyunyiza damu juu yake.
\v 19 Utatoa ng'ombe kutoka kwenye kundi kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya Walawi makuhani ambao ni uzao wa Zadoki, wale wajao karibu nami kunitumikia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 20 Kisha utachukua baadhi ya damu yake na kuiweka juu pembe nne za madhabahu na pande nne za machinjio na kuuzunguka ukingo; utaitakasa na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
\v 21 Kisha chukua ng'ombe kama sadaka ya dhambi na iteketezwe katika eneneo lililotengwa la nje ya patakatifu.
\s5
\v 22 Kisha katika siku ya pili utatoa mbuzi dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini kama sadaka ya dhambi; makuhani wataisafisha madhabahu kama walivyoisafisha kwa ng'ombe.
\v 23 Utakapomaliza kusafisha, toa ng'ombe asiyekuwa na dosari kutoka kwenye mifugo na kondoo dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini.
\v 24 Watoe mbele ya Yahwe; makuhani watanyunyiza chumvi juu yao na kuwainua juu kama sadaka ya kutekezwa kwa Yahwe.
\s5
\v 25 Utaandaa mbuzi dume kama sadaka ya dhambi kila siku kwa mda wa siku saba, na makuhani pia wataandaa ng'ombe asiye na dosari kutoka kwenye kundi na kondoo dume kutoka kwenye kundi.
\v 26 Wataipatanisha madhabahu kwa siku saba na kuitakasa, wataitakasa kwa njia hii.
\v 27 Watamaliza hizi siku saba, na katika siku ya nane na kuendelea itakuwa kwamba makuhani wataandaa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani kwenye madhabahu, ndipo nitakapowakubali-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\c 44
\p
\v 1 Kisha yule mtu akanirudisha hata lango la nje la patakatifu linaloelekea mashariki; lilikuwa limefungwa kwa kukazwa.
\v 2 Yahwe akanambia, "Hili lango litakuwa limefungwa; halitafunguliwa. Hakuna mtu atakaye pitia hapo, kwa kuwa Yahwe, Mungu wa Israeli ameingia kwa hilo, hivyo lilikuwa limefungwa kwa kukazwa.
\v 3 Mtawala wa Israeli atakaa katika hilo kula chakula mbele ya Yahwe. Ataingia kwa njia ya varanda na kutoka kwa njia hiyo hiyo."
\s5
\v 4 Kisha akaniletea kwa njia ya lango la kaskazini linaloelekea kwenye nyumba. Hivyo nikaona na kutazama, utukufu wa Yahwe umejaa kwenye nyumba ya Yahwe, nikaanguka kifudifudi.
\v 5 Kisha Yahwe akanambia, "Mwanadamu, andaa moyo wako na tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako kwa yote yale nikuambiayo, kwa amri zote za nyumba ya Yahwe na maagizo yote. Fikiri kuhusu malango ya nyumba na na matokeo ya malango.
\s5
\v 6 Kisha waambie wale walioasi, nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Acheni matendo yenu maovu kwenu, nyumba ya Israeli-
\v 7 ambayo mmewaleta wageni pamoja na wasiotahiriwa mioyo na wasiotahiriwa mwili kuwa katika patakatifu pangu, kuikufuru nyumba yangu, wakati mlipokuwa mnanitolea chakula, mafuta na damu-mmevunja agano langu kwa matendo yenu maovu.
\s5
\v 8 Hamkumaliza kazi zenu zinazohusiana na vitu vitakatifu, lakini mmewateua wengine kuchukua kazi zenu, na mmewatuma kupaangalia mahali patakatifu pangu.
\v 9 Bwana Yahe asema hivi: hakuna mgeni, ambaye hajatahiriwa kwenye moyo wake na mwili, kutoka yeyote wa hao waishio miongoni mwa watu wa Israeli, awezaye kuingia patakatifu pangu.
\s5
\v 10 Kisha Walawi wakaenda mbali nami-wakapotea mbali nami, kwenda kwenye sanamu zao-lakini watalipa kwa ajili ya dhambi yao.
\v 11 Wao ni watumishi katika patakatifu pangu, waangalizi wa malango ya nyumba na kutumika kwenye nyumba na kuchinja sadaka za kuteketezwa na dhabihu za watu, na watasimama mbele za watu na kuwatumikia.
\v 12 Lakini kwa sababu wamefanya dhabihu mbele ya sanamu zao, wamekuwa kikwazo kwa dhambi ya nyumba ya Israeli. Kwa hiyo nitainua mkono wangu kuapa kiapo dhidi yao-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-watabeba adhabu yao.
\s5
\v 13 Hawatakuja karibu nami kufanya kama makuhani au kukaribiakila vitu vyangu vitakatifu, vitu vitakatifu sana. Badala yake, watabeba lawama zao na hatia zao kwa ajili ya matendo yao ya karaha waliyoyafanya.
\v 14 Lakini nitawaweka kama watunzaji wa kazi katika nyumba, kwa kazi zote na kila kitu kitakachofanyika ndani yake.
\s5
\v 15 Kisha makuhani walawi, hao wana wa Zadoki ambao waliokamilisha kazi ya patakatifu pangu wakati wana wa Israeli walipotea mbali nami-watakuja karibu nami kuniambudu. Watasimama mbele yangu kunitolea mafuta na damu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 16 Watakuja hata patakatifu pangu; wataikaribia meza yangu kuniabudu na kukamilisha kazi zao kwangu.
\s5
\v 17 Hivyo itakuwa kwamba watakapokuja kwenye malango ya ua wa ndani, watatakiwa kuvaa mavazi ya kitani, kwa kuwa hawatakuja na sufu ndani ya lango la ua wa ndani na nyumba yake.
\v 18 Kutakuwa na vilemba juu ya vichwa vyao na kitani ndani ya viuno vyao. Ndani wasivae nguo ambayo itawafanya watoke jasho.
\s5
\v 19 Wakati watakapotoka nje ya ua wa nje, hata kwenye ua wa ndani ili kwenda kwa watu, watavua nguo zao walizokuwa wamezivaa kisha wakatumika; watazivua na kuziweka chini katika chumba kitakatifu, hivyo wasiwafanye wengine watakatifu kwa kugusana na nguo zao maalumu.
\s5
\v 20 Hawatanyoa vichwa vyao wala kuruhusu nywele zao kuwa ndefu, watapunguza nywele za vichwa vyao.
\v 21 Hakuna kuhani atakaye ruhusiwa kunywa mvinyo wakati atakapoingia kwenye uwa wa ndani,
\v 22 hakuna kuchukua mjane au mwanamke aliyetalikiwa kama mke kwa ajili yake, lakini mwali kutoka safu ya nyumba ya Israeli au mjane aliyekuwa ameolewa na kuhani aliyepita.
\s5
\v 23 Kwa kuwa watawafundisha watu wangu tofauti kati ya utakatifu na kukufuru; watawafanya kujua uchafu kutoka usafi.
\v 24 Katika kubishana watasimama kwenye hukumu pamoja na amri yangu; watakuwa waadilifu. Watashika sheria yangu na amri zangu katika sikukuu, na watasherekea siku yangu ya Sabato.
\s5
\v 25 Hawataenda kwa mtu aliyekufa ili wasiwe najisi, vinginevyo awe ni baba au mama yao, mwana wa kiume au binti, kaka au dada ambaye hajawahi kulala na mtu; vinginevyo, watakuwa najisi.
\v 26 Baada ya kuhani kuwa najisi, watahesabu mda wa siku saba kwa ajili yake.
\v 27 Katika siku atakayoingia mahali patakatifu, ndani kwenye uzio kutumika katika mahali patakatifu, ataleta sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 28 Hapa patakuwa urithi wao: Mimi ndiyo urithi wao, na usiwapatie mali katika Israeli; nitakuwa mali yao!
\v 29 Watakula chakula cha sadaka, sadaka za dhambi, sadaka za hatia, na kila kitakachotolewa kwa ajili ya Yahwe katika Israeli, vitakuwa vyao.
\s5
\v 30 Malimbuko ya kwanza ya vitu na kila sadaka, kila kitu kitokanacho na sadaka zenu vitakuwa mali ya makuhani, mtatoa sadaka ya chakula kizuri kwa makuhani ili kwamba baraka iweze kukaa katika nyumba zenu.
\v 31 Makuhani hawatakula mzoga au mnyama aliyeraruliwa, iwe ni ndege au mnyama.
\s5
\c 45
\p
\v 1 Wakati mtakapogawanya nchi kama urithi, mtafanya sadakwa kwa Yahwe; sadaka hiyo itakuwa sehemu takatifu ya nchi, dhiraa elfu ishirini na tano urefu, na dhiraa elfu kumi upana. Patakuwa patakatifu, ndani ya mipaka yake yote.
\v 2 Kutoka hapa kutakuwa na dhiraa mia tano kwa dhiraa mia tano za mraba kuzunguka mahali patakatifu, kwa kuuzunguka mpaka dhiraa hamsini upana.
\s5
\v 3 Kutoka hili eneo utapima fungu ambalo ni dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana; patakuwa patakatifu; mahali patakatifu palipo tukuka.
\v 4 Patakuwa patakatifu katika nchi kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Yahwe, ajaye kwa Yahwe kumtumikia. Patakuwa mahali kwa ajili ya nyumba na eneo takatifu kwa ajili mahali patakatifu.
\v 5 Hivyo itakuwa dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana, patakuwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaotumika kwenye nyumba.
\s5
\v 6 Mtadhihirisha eneo moja kwa ajili ya mji, dhiraa elfu tano na urefu ishirini na tano, hapo patakuwa kando kando ya eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu; huu mji utakuwa wa mali ya nyumba yote ya Israeli.
\v 7 Nchi ya mwana mfalme itakuwa kwa pande zote za eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu na mji. Patakuwa kwa upande wao wa magaharibi na upande wa mashariki. Urefu utalingana na urefu wa moja ya hayo mafungu, kutoka magaribi hata mashariki.
\s5
\v 8 Hii nchi itakuwa mali ya mwana mfalme katika Isaraeli. Wana wafalme hawatawakandamiza watu wangu; badala yake, watawapatia nchi kwa nyumba ya Israeli, kwa ajili ya makabila yao.
\s5
\v 9 Bwana Yahwe asema hivi: Inatosha kwa ajili yenu, mwana mfalme wa Israeli! Ondoa dhuluma na mgogoro; fanya hukumu na haki! Usiwafukuze wapangaji wa watu wangu! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\v 10 Mtakuwa na mzani sahihi, efa sahihi, na bathi sahihi!
\v 11 Efa na bathi zitakuwa kiasi kile kile, ili kwamba bathi iwe zaka ya homeri; efa itakuwa zaka ya hamori moja. Vipimo vyao vitakuwa vinafanana na homeri.
\v 12 Shekeli zitakuwa gera ishirini, shekeli sita zitakuwa mane yenu.
\s5
\v 13 Hili ndilo toleo mtakalotoa: efa sita kwa kila homeri ya ngano, na mtatoa efa sita kwa kila homeri ya shayiri.
\v 14 Sadaka ya kawaida ya mafuta itakuwa zaka ya bathi kwa kila kori (ambazo ni bathi), au kwa kila hamori, kwa kuwa hamori moja ni bathi kumi pia.
\v 15 Kondoo mmoja au mbuzi kutoka mifugo kwa kila wanyama mia mbili kutoka malisho ya maji ya mikoa ya Israeli yatatumika kwa sadaka ya kuteketezwa yoyote au sadaka ya amani kufanya upatanisho kwa ajili ya watu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 16 Watu wote wa nchi watatoa hii sadaka kwa mwana mfalme wa Israeli.
\v 17 Utakuwa wajibu wa mwana mfalme kutoa wanyama kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka ya unga, sadaka ya kinywaji, katika siku za sikukuu na sherehe za mwezi mpya, na katika siku za Sabato-sikukuu zote za kudumu za nyumba ya Israeli. Ataandaa kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za unga, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani kwa ajili ya upatanisho badala ya nyumba ya Israeli.
\s5
\v 18 Bwana Yahwe asema hivi: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utachukua ng'ombe mmoja asiyekuwa na dosari kutoka kwenye kundi na kufanya sadaka ya dhambi kwa ajili ya patakatifu.
\v 19 Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi na kuiweka juu ya miimo ya mlango na kwenye pembe nne za mpaka wa madhabahu, na miimo ya lango la uzio wa ndani.
\v 20 Utafanya hivyo siku ya saba ya mwezi kwa dhambi ya kila mtu kwa ajali au ujinga; katika njia hii mtaipatanisha hekalu.
\s5
\v 21 Katika siku ya mwezi siku ya kumi na nne ya mwezi, mtakuwa na sikukuu, sikukuu ya siku saba. Matakula makate usiotiwa chachu.
\v 22 Siku hiyo, mwana mfalme ataandaa ng'ombe kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wote wa nchi kama sadaka ya dhambi.
\s5
\v 23 Kwa siku saba za sikukuu, mwana wa mfalme ataandaa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Yahwe: ng'ombe saba na kondoo dume saba zisizokuwa na dosari kila siku kwa mda wa siku saba, na mbuzi dume kila siku kama sadaka ya dhambi.
\v 24 Kisha mwana mfalme atatengeneza sadaka ya chakula ya efa moja kwa kila ng'ombe na efa moja kwa kila kondoo dume pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
\s5
\v 25 Katika siku ya saba ya mwezi siku ya kumi na tano ya mwezi, katika sikukuu, mwana wa mfalme atafanya matoleo katika siku hizi saba: sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za chakula, na sadaka za mafuta.
\s5
\c 46
\p
\v 1 Bwana Yahwe asema hivi: Lango la uzio wa ndani, linaloelekea mashariki, litafungwa kwa mda wa siku sita za kazi, lakini katika siku za Sabato litakuwa wazi, na katika siku ya mwezi mpya litafunguliwa.
\v 2 Mwana wa mfalme ataingia kwa kutumia lango la njia ya nyuma ya varanda upande wa nje, na atasimama mbele ya muhimili wa mwimo wa lango la ndani wakati makuhani wakiwa wakitengeza sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani. Kisha ataabudu kwenye kizingiti cha lango la ndani na kutoka nje, lakini lango halitakuwa linafungwa hadi jioni.
\s5
\v 3 Watu wa nchi pia wataabudu mbele ya Yahwe kwenye hili lango la kuingilia katika siku ya Sabato na siku mpya za mwezi.
\v 4 Sadaka ya kuteketezwa ambayo mwana wa mfalme aitoayo kwa Yahwe katika siku ya Sabato itakuwa wanakondoo sita wasiokuwa na dosari na kondoo dume asiyekuwa na dosari.
\v 5 Sadaka ya unga pamoja na kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya unga pamoja na wanakondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta pamoja na kila efa ya unga.
\s5
\v 6 Katika siku ya mwezi mpya atatoa ng'ombe mchanga asiyekuwa na dosari kutoka kuchungwa, wanakondoo sita, na kondoo asyekuwa na dosari.
\v 7 Atatengeneza sadaka ya unga ya efa moja kwa ajili ya ng'ombe na efa moja kwa ajili ya kondoo, na kwa kiasi awezacho kukitoa kwa ajili ya wanakondoo, na hini ya mafuta kwa kila efa ya unga.
\v 8 Wakati mwana wa mfalme atakapokuwa anaingia kwa njia ya lango lenye varanda, ataondoka kwa njia hiyo hiyo.
\s5
\v 9 Lakini wakati watu wa nchi watakakuja kwa Yahwe katika sikukuu zilizoteuliwa, kila mmoja kuingia kupitia kwenye lango la kaskazini kuabudu ataondoka kupitia lango la kusini; na kila atakayeingillia kupitia lango la kusini atatoka kupitia lango la kaskazini. Hakuna atakayerudia kwa lile lango aliloingilia, kwa kuwa atatoka nje moja kwa moja.
\v 10 Mwana wa mfalme atakuwa kati yao; watakapoingia, ataingia ndani, na watakapoondoka, atatoka nao.
\s5
\v 11 Kwenye sikukuu hizo, sadaka ya unga itakuwa efa moja ya unga kwa ng'ombe mmoja na efa moja kwa kondoo dume, na chochote atakacho kitoa pamoja na wanakondoo, na hini moja ya mafuta kwa kila efa.
\v 12 Wakati mwana wa mfalme atakapotoa sadaka atakayojisikia kutoa, labda sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani kwa Yahwe, lango la kuelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka ya amani kama afanyavyo siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, na baada ya kutoka lango litafungwa.
\s5
\v 13 Kwa kuongeza, utatoa mwanakondoo asiyekuwa na dosari mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe kila siku; utafanya hivi kila asubuhi.
\v 14 Utatoa sadaka ya unga pamoja nayo kila asubuhi, efa sita na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta kuchanganya na sadaka ya unga kwa ajili ya Yahwe, kulingana na sheria ilivyo.
\v 15 Watandaa mwanakondoo, sadaka ya kuteketezwa, na mafuta kila asubuhi, sadaka ya kuteketezwa ya kudumu.
\s5
\v 16 Bwana Yahwe asema hivi: Kama mwana wa mfalme akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wake, imekuwa urithi wake. Itakuwa mali ya mtoto wake, imekuwa urithi.
\v 17 Lakini kama akimpatia zawadi kutoka urithi wake kwa mmoja wa watumishi wake, kisha itakuwa ya huyo mtumishi mpaka mwaka wa uhuru, na kisha itarudi kwa mwana wa mfalme. Urithi wake yamkini ukawa kwa ajili ya watoto wake.
\v 18 Mwana wa mfalme hatawaondolea urithi wa watu kutoka kwenye mali zao wenyewe; ataandaa kwa ajili ya watoto wake mali ili kwamba watu wangu wasitawanyike, kila mtu kutoka mali kwenye yake mwenyewe."
\s5
\v 19 Kisha yule mtu akaniletea kwenye lango la kutokea hata kwenye vyumba vitakatifu kwa ajili ya makuhani, vilivyokuwa vimeelekea kaskazini na tazama! Kulikuwa na sehemu mbele magharibi.
\v 20 Akanambia, "Hii ndio sehemu ambayo makuhani watakapo chemshia sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na walipookea sadaka ya unga. Wasilete sadaka nje ya uzio, kwa kuwa watu watatakaswa."
\s5
\v 21 Kisha akanileta kwenye uzio wa nje akaniongoza kuzunguka pembe nne za uzio, nikaona kwamba katika kila pembe ya uzio kulikuwa na uwanja.
\v 22 Katika hizo pembe nne za nje ya uzio kulikuwa na nzio nne ndogo, dhiraa arobaini urefu na thelathini upana. Ukubwa ule ule kwa nzio zote nne.
\v 23 Kulikuwa na safu zilizokuwa zimetengenezwa kwa mawe kuzizunguka zote nne, na meko ya kupikia ilikuwa chini ya safu ya jiwe.
\v 24 Yule mtu akanambia, "Hizi ndizo sehemu ambazo watumishi watachemshia dhabihu za watu."
\s5
\c 47
\p
\v 1 Kisha yule mtu akanirudisha nyuma kwenye lango la kuingia la hekalu, na kulikuwa na maji yakitiririka nje kutoka chini ya hekalu kizingiti cha nyumba kuelekea masharikii-kwa mbele ya hekalu kulekea mashariki-na maji yalikuwa yakitiririka chini upande wa kusini mwa hekalu, kuelekea upande wa kuume wa madhabahu.
\v 2 Hivyo akanileta kwenye lango la kaskazini na kuniongoza kuzunguka lango kuelekea mashariki, na hapo maji yalikuwa yakitiririka kutoka lango hili kwa upande wa kusini yake.
\s5
\v 3 Yule mtu alipokuwa akienda mashariki, kulikuwa na kamba ya kupimia kwenye mkono wake; akapima dhiraa elfu moja akanivusha kwenye maji hata maji yakafika kwenye magoti.
\v 4 Kisha akapima dhiraa elfu moja ten akanivusha kwenye yale maji yaliyofika kwenye magoti; akapima dhiraa elfu kumi nyingine na kunivusha maji yakafika hata kwenye nyonga.
\v 5 Tena akapima dhiraa elfu moja nyingine, lakini ulikuwa mto ambao sikuweza kuuvuka kwa sababu maji yalizidi na yalijaa maji ya kuogelea ndani-yalikuwa mto usiovukika
\s5
\v 6 Yule mtu akanambia, "Mwanadamu, unaona hii?" akanipeleka na kunirudisha karibu na ukingo wa mto.
\v 7 Nilipokuwa nikirudi, hapo kwenye ukingo wa mto kulikuwa na miti mingi katika huu upande na upande mwingine pia.
\v 8 Yule mtu akanambia, "Haya maji yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki na chini hata Araba; haya maji hutiririka kwenye Bahari ya Chumvi itaifanya kuwa mpya.
\s5
\v 9 Itakuwa kwamba kila kiumbe hai kisongamanacho kitaishi mahali maji yanapoelekea; kutakuwa na samaki wengi, kwenye hayo maji yatiririkayo huko. Itafanya maji ya chumvi kuwa mapya. Kila kitu kitaishi popote mto utakapoelekea.
\v 10 Kisha itatokea kwamba wavuvi wa En Gedi watasimama karibu na maji, na kutakuwa na sehemu ya kutandazia nyavu za samaki karibu na En Eglaimu. Kutakuwa na samaki nyingi za aina tofauti tofauti katika Bahari ya Chumvi, kama samaki kwenye Bahari Kuu kwa wingi wao.
\s5
\v 11 Lakini Bahari ya Chumvi ikajaa maji na matope hayataachwa mapya; yataachwa yawe kwa ajili ya kutengeneza chumvi.
\v 12 Karibu na huo mto juu ya ukingo wake, pande zote, aina zote za miti utazaa chakula. Majani yake hayatanyauka na matunda yake hayataacha kukua. Kila mwezi miti itazaa matunda, kwa sababu maji kutoka patakatifu yatatirirka kwenda kwenye hiyo miti. Matunda yake yatakuwa kwa ajili ya chakula, na majani yake yatakuwa kwa ajili ya dawa.
\s5
\v 13 Bwana Yahwe asema hivi: Hii itakuwa njia ambayo mtaigawanya nchi kwa ajili ya kabila kumi na mbili za Israeli: Yusufu atakuwa na mafungu mawili.
\v 14 Mtaigawa kila mtu sawa sawa ambayo niliinua mkono wangu na kuapa kuwapa baba zenu. Hii nchi itakuja kuwa urithi kwenu.
\s5
\v 15 Huu utakuwa mpaka wa nchi upande wa kaskazini kutoka Bahari Kubwa kwa njia ya Hethloni, na kisha kuelekea Zedada.
\v 16 Kisha mpaka utaenda hata Berotha, hadi Sibraimu, iliyopo kati ya Damaskasi na Hamathi, na kisha hata Hazer-hatikoni, iliyopo karibu na mpaka wa Haurani.
\v 17 Hivyo mpaka utaenda kutoka kwenye bahari hadi Hazar-enoni kwenye mpaka wa Damaskasi na Hamathi hata kaskazini. Huu utakuwa upande wa kaskazini.
\s5
\v 18 Kwa upande wa mashariki, kati ya Haurani na Damaskasi na kati ya Geliadi na nchi ya Israeli kutakuwa na mto Yordani. Mtapima kutoka kwenye mpaka hata kwenye bahari ya mashariki; huo wote utakuwa mpaka wa mashariki.
\v 19 Kisha upande wa kusini: kusini mwa Tamari hadi kwenye maji ya Meriba Kadeshi, kijito cha Misri hata Bahari Kuu, na upande wa kusini kuelekea kusini.
\v 20 Kisha mpaka wa magharibi utakuwa Bahari Kuu utaelekea hata nyuma ya Hamathi. Huu utakuwa upande wa mgharibi.
\s5
\v 21 Kwa njia hii mtaigawanya hii nchi kwa ajili yenu wenyewe, kwa kabila za Israeli.
\v 22 Hivyo mtagawana urithi kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya wageni walio kati yenu, wale watakaozaa watoto kati yenu na waliokuwa, kati yenu, kama wazaliwa wa watu wa Israeli. Mtapewa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli.
\v 23 Kisha itatokea kwamba wageni watakuwa pamoja na kabila miongoni mwa yule anayeishi. Mtapatia urithi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo."
\s5
\c 48
\p
\v 1 Haya ndiyo majina ya makabila. Kabila la Dani litapokea sehemu moja ya nchi; mipaka yake itakuwa karibu na upande wa mashariki mpaka wa Israeli karibu na njia ya Hethloni na Lebo Hamathi. Mpaka wake utaenda hata karibu na Hazari Enani na karibu na mpaka wa Damaskasi hata upande wa kaskazini na kisha karibu na Hamathi. Mpaka wa Dani utaenda kutoka mashariki moja kwa moja hata Bahari Kubwa.
\v 2 Kupakana na mpaka wa Dani, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, Asheri itakuwa na fungu moja.
\v 3 Kupakana na mpaka wa Asheri kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Naftali atakuwa na fungu moja.
\s5
\v 4 Kupakana na mpaka wa Naftali kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Manase atakuwa na fungu moja.
\v 5 Kupakana na mpaka wa Manase kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Efraimu atakuwa na fungu moja.
\v 6 Kupakana na mapaka wa Efraimu kutoka mashariki hata magharibi, Rubeni atakuwa na fungu moja.
\v 7 Kupakana na mpaka wa Rubeni kutoka mashariki hata magharibi, Yuda atakuwa na fungu moja.
\s5
\v 8 Sadaka ya nchi ambayo mtaifanya itakuwa karibu na mpaka wa Yuda na hapohapo kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano upana. Urefu unakaribiana na fungu la kabila moja kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, na hekalu litakuwa katikati yake.
\v 9 Huu mji mtakao utoa sadaka kwa ajili ya Yahwe utakuwa na ridhaa elfu ishirini na tano urefu wake na ridhaa elfu kumi upana.
\s5
\v 10 Haya yatakuwa matoleo ya hili fungu takatifu la nchi: makuhani watakuwa na nchi watakayopewa kipimo chake ridhaa elfu ishirini na tano urefu kwa upande kaskazini; ridhaa elfu kumi upana upande wa magharibi; urefu wa ridhaa elfu kumi upande wa magharibi; na urefu rithaa elfu ishirini na tano upande wa kusini, pamoja na mahali patakatifu pa Yahwe katikati yake.
\v 11 Hii itakuwa wakfu na makuhani wa safu ya Zadoki, aliyenitumikia kwa uaminifu na ambaye hakwenda nje ya mstari wakati watu wa Israeli walipoeenda nje ya mstari, kama Walawi walivyofanya.
\v 12 Sadaka yao itakuwa fungu la hiyo nchi takatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi.
\s5
\v 13 Nchi ya Walawi karibu na mpaka wa nchi ya makuhani itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano urefu na ridhaa elfu kumi upana. Urefu wote wa eneo la nchi utakuwa ridhaa elfu ishirini na tano urefu na ridhaa elfu ishirini upana.
\v 14 Hawataiuza au kuibadilisha; hakuna malimbuko ya hiyo nchi ya Israeli itakayogawanywa kutoka haya maeneo, kwa kuwa yote ni matakatifu kwa ajili ya Yahwe.
\s5
\v 15 Nchi iliyobaki, ridhaa elfu kumi na tano upana na ridhaa elfu ishirini na tano urefu, itakuwa kwa wote wanayoitumia hiyo nchi, nyumba, na sehemu ya malisho; huo mji utakuwa katikati yake.
\v 16 Hivi ndivyo vitakuwa vipimo vya mji: upande wa kaskazini utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; upande wa kusini utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; upande wa magharibi utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; na magharibi itakuwa ridhaa 4, 500 urefu.
\s5
\v 17 Kutakuwa na malisho ya mji kuelekea kaskazini, ridhaa 250 kwenda chini; hata kusini, ridhaa 250 kwenda chini; kuelekea mashariki, ridhaa 250 kwenda chini, na kuelekea magharibi ridhaa 250 kwenda chini.
\v 18 Eneo lililobaki la matoleo matakatifu litanyooshwa ridhaa elfu kumi hata mashariki na ridhaa elfu kumi kuelekea magharibi. Litanyooshwa karibu na mpaka wa matoleo matakatifu, na mazao yake yatakuwa chakula kwa ajili ya wale wanaofanya kazi katika nchi.
\s5
\v 19 Wale wafanyao kazi katika mji, watu wote wa kabila za Israeli, watailima hiyo nchi.
\v 20 Matoleo yote ya nchi yatapimwa ridhaa elfu ishirini na moja kwa ridhaa elfu ishirini na tano. Kwa njia hii mtatengeneza matoleo matakatifu ya nchi, pamoja na nchi kwa ajili mji.
\s5
\v 21 Mabaki ya nchi mojawapo upande wa matoleo matakatifu na eneo la mji litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme. Eneo la nchi ya mwana wa mfalme kuelekea mashariki litanyooshwa kwa ridhaa elfu ishirini na tano kutoka kwenye mpaka wa matoleo matakatifu hata mpaka wa mashariki-na eneo lake kuelekea mpaka wa magharibi. Katikati kutakuwa matolea matakatifu, na mahali patakatifu pa hekalu patakuwa katikati yake.
\v 22 Nchi imenyooka kutoka mali ya Walawi na eneo la mji katikati yake litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme; itakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benjamini-hiyo nchi itakuwa kwa ajili ya mwana wa mfame.
\s5
\v 23 Kwa kabila zitakazobaki, mafungu yao yataunganishwa kutoka upande wa mashariki. Benjamini atapokea fungu moja.
\v 24 Kupakana na mpaka wa Benjamini kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Simioni atakuwa na fungu moja.
\v 25 Kupakana na mpaka wa Isakari kutakuwa na fungu moja.
\v 26 Kupakana na mpaka wa Isakari kutoka mashariki hata magharibi, Zebuloni atakuwa na fungu moja.
\s5
\v 27 Hata kusini mwa mpaka wa Zebuloni, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magahribi, kutakuwa na nchi ya Gadi-fungu moja.
\v 28 Mpaka wa kusini mwa Gadi kutanyooshwa kutoka Tamari hata kwenye maji ya Meriba Kadeshi, mbele hadi kijito cha Misri, na kisha hata Bahari kuu.
\v 29 Hii ndiyo nchi ambayo mtakazo gawana; kutakuwa na urithi wa makabila ya Israeli. Haya yatakuwa mafungu yao. Hivi ndivy Bwana Yahwe asemavyo.
\s5
\v 30 Hawa ndio watakaoishi kutoka kwenye nchi: upande wa kaskazini, ambapo patapimwa ridhaa 4, 500 kwa urefu,
\v 31 kutakuwa na malango matatu, yaitwayo kwa ajili ya Israeli: lango moja kwa ajili ya Rubeni, lango moja kwa ajili ya Yuda, na lango moja kwa ajili ya Walawi.
\v 32 Kwa upande wa mashariki, ambapo patapimwa ridhaa 4, 500 kwa urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Yusufu, lango moja kwa ajili ya Benjamini, na lango moja kwa ajili ya Dani.
\s5
\v 33 Kwa upande wa mashariki, kutakuwa na kipimo cha ridhaa 4, 500 urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Simioni, lango moja kwa ajili ya Isakari, na moja kwa ajili ya Zebuloni.
\v 34 Kwa upande wa magharibi, ambao kipimo chake kitakuwa ridhaa 4, 500, kutakuwa ba malango matatu: lango moja kwa ajili ya Gadi, lango moja kwa ajili ya Asheri, na lango moja kwa ajili ya Naftali.
\v 35 Umbali kuuzunguka mji utakuwa ridhaa elfu kumi na nane; kutoka hiyo siku, jina la huo mji litakuwa "Yahwe yupo hapo."

738
27-DAN.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,738 @@
\id DAN
\ide UTF-8
\h Danieli
\toc1 Danieli
\toc2 Danieli
\toc3 dan
\mt Danieli
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja Yerusalemu na kuuzunguka mji ili kuzuia mahitaji yake yote.
\v 2 Bwana alimpa Nebukadneza ushindi dhidi ya Yehoyakimu mfalme wa Yuda, na alimpatia vitu vitakatifu kutoka nyumba ya Mungu. Alivipeleka vitu hivyo mpaka katika nchi ya Babeli, kwa nyumba ya mungu wake, na aliviweka vitu vitakatifu katika hazina ya mungu wake.
\s5
\v 3 Mfalme akamwambia Ashipenazi, afisa wake mkuu, awalete baadhi ya watu wa Israeli, wa familia ya kifalme na za kiungwana -
\v 4 vijana wasio na hila, wenye mwonekano wa kuvutia, wenye ujuzi katika hekima yote, wenye kujawa na ufahamu na weledi, na wenye sifa za kutumika katika ikulu ya mfalme. Alitakiwa kuwafundisha maandiko na lugha ya Babeli.
\v 5 Mfalme aliwatengea kwa ajili yao fungu kutoka katika chakula chake kizuri kwa kila siku na katika divai aliyokunywa. Vijana hawa walitakiwa kufunzwa kwa miaka mitatu, na baada ya hapo, wangeweza kumtumikia mfalme.
\s5
\v 6 Miongoni mwao walikuwa ni Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria, baadhi ya watu wa Yuda.
\v 7 Afisa mkuu aliwapa majina: Danieli alimwita Belteshaza, Hanania alimwita Shadraka, Mishaeli alimwita Meshaki, na Azaria alimwita Abedinego.
\s5
\v 8 Lakini Danieli alinuia katika akili yake kuwa asingejitia ujanisi mwenyewe kwa chakula kizuri cha mfalme wala kwa divai ambayo alikunywa.
\v 9 Basi, aliomba ruhusa kutoka kwa afisa mkuu ili kwamba asije akajitia uchafu yeye mwenyewe. Hivyo, Mungu alimpa Danieli kibali na huruma kupitia katika heshima ambayo afisa mkuu alikuwa nayo kwake.
\v 10 Afisa mkuu alimwambia Danieli, "Ninamwogopa bwana wangu mfalme. Ameagiza aina ya chakula na vinywaji mnavyotakiwa kutumia. Kwa nini awaone ninyi mkiwa mnaonekana vibaya kuliko vijana wengine wa umri wenu? Mfalme aweza kukitwaa kichwa changu kwa sababu yenu.
\s5
\v 11 Kisha Daniel akamwambia msimamizi ambaye afisa mkuu alikuwa amemweka juu ya Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria.
\v 12 Alisema, "Tafadhari tujaribuni, sisi watumishi wako kwa siku kumi. Tupatieni tu mboga mboga za kula na maji ya kunywa.
\v 13 Kisha ulinganishe mwonekano wetu na mwonekano wa vijana wanaokula vyakula vya mfalme, na mtutendee, sisi watu wako kulingana na kile unachokiona." '
\s5
\v 14 Hivyo msimamizi alikubaliana naye kufanya hivi, na aliwajaribu kwa siku kumi.
\v 15 Katika mwisho wa siku kumi mwonekano wao ulikuwa ni wenye afya nzuri kuliko wa wale vijana waliokula vyakula vya kifalme.
\v 16 Basi, msimamizi aliliondoa fungu lao la chakula na vivywaji vyao na walipewa mboga mboga tu.
\s5
\v 17 Na kuhusu vijana hawa nne Mungu aliwapa uelewa na ufahamu katika maandiko yote na hekima, na Danieli aliweza kupambanua aina zote za maono na ndoto.
\v 18 Katika mwisho wa muda uliokuwa umepangwa na mfalme kuwaleta ndani, afisa mkuu aliwaleta mbele ya Nebukadneza.
\s5
\v 19 Mfalme aliongea nao, na miongoni mwa kundi lote hapo hapakuwa na wa kuwalinganisha na akina Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria. Walisimama mbele ya mfalme, wakiwa tayari kumtumikia.
\v 20 Katika kila swali la hekima na ufahamu ambalo mfalme aliwauliza, aliwakuta wakiwa na uwezo mara kumi kuliko waganga wote na wale waliojidai kusema na wafu, waliokuwa katika ufalme wake wote.
\v 21 Danieli alikuwa hapo mpaka mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadneza, alikuwa na ndoto. Akili yake ilisumbuka, na hakuweza kulala.
\v 2 Ndipo mfalme alipowaita waganga na wale wenye kuongea na wafu. Lakini pia aliwaita wachawi na watu wenye hekima. Aliwataka wamwambie juu ya ndoto zake. Basi walikuja na kusimama mbele za mfalme.
\s5
\v 3 Mfalme akawambia, "Nilikuwa na ndoto, na akili yangu ina mashaka nataka kujua ndoto hiyo nini maana yake."
\v 4 Kisha watu wenye hekima wakamwambia mfalme katika Kiaramaiki, " Mfalme, aishi milele! Twambie sisi ndoto, watumishi wako, nasi tutaifunua maana yake."
\s5
\v 5 Mfalme akawajibu watu wenye hekima, " Jambo hili limeshamalizika. Kama hamtaweza kuiweka wazi ndoto kwangu na kuitafsiri, miili yenu itakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vichuguu vya uchafu.
\v 6 Lakini kama mtaniambia ndoto na maana yake, mtapokea zawadi kutoka kwangu, thawabu, na heshima kubwa. Basi niambie ndoto na maana yake."
\s5
\v 7 Wakamjibu tena na kusema, "Mfalme na atuambie, watumishi wake, ndoto nasi tukwambia maana yake."
\v 8 Mfalme akawajibu, " Ninajua kwa hakika mnahitaji muda zaidi kwasababu mmeona maamuzi yangu ni magumu kuhusu jambo hili.
\v 9 Lakini kama hamtaweza kuniambia ndoto, kuna sentensi moja tu kwa ajili yenu. Mmeamua kuandaa uongo na maneno ya kudanganya ambayo mmekubaliana kwa pamoja kuniambia mpaka pale nitakapobadili akili zangu. Basi, niambieni ndoto, na kisha nitajua kuwa mnaweza kuitafsiri kwa ajili yangu."
\s5
\v 10 Watu wenye hekima wakamjibu mfalme, " Hakuna mtu katika dunia anayeweza kutimiza matakwa ya mfalme. Hakuna mfalme yoyote mkuu na mwenye nguvu ambaye alishataka jambo kama hilo kutoka kwa wachawi, wala wenye kuongea na wafu, wala mwenye hekima.
\v 11 Kile anachokitaka mfalme ni kigumu, na hakuna yeyote awezaye kumwambia mfalme isipokuwa miungu, ambayo haishi miongoni mwa watu."
\s5
\v 12 Jambo hili lilimfanya mfalme akasirike na kughadhabika sana, na alitoa amri kuwaangamiza wale wote waliojulikana kuwa ni wenye hekima zao katika Babeli.
\v 13 Hivyo, amri ilitoka kwamba wale wote waliojulikana kwa hekima yao ni lazima wauawe. Na kwa sababu ya amri hii, walimtafuta Daniel na rafiki zake ili kwamba wauawe.
\s5
\v 14 Ndipo Daniel alipomjibu kwa busara na umakini, Arioki, kamanda wa walinzi wa mfalme, ambaye alikuwa amekuja kuwaua wale wote waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.
\v 15 Danieli alimwuliza kamanda wa mfalme, " Kwanini amri ya mfalme ni ya haraka hivyo?" Hivyo, Arioki akamwambia Danieli kile kilichotokea.
\v 16 Ndipo Danieli aliingia ndani na akaomba ahadi ya muda wa kuonana na mfalme ili kwamba aweze kuwasilisha tafsiri kwa mfalme.
\s5
\v 17 Kisha Danieli aliingia ndani ya nyumba na aliwaelezea Hanania, Mishaeli, na Azaria, kile kilichotokea.
\v 18 Aliwasihi kutafuta rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusiana na siri hii ili kwamba yeye na wao wasije wakauawa pamoja na watu wengine waliosalia waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.
\s5
\v 19 Usiku ule siri ilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Kisha Danieli akamtukuza Mungu wa mbinguni
\v 20 na kusema, "Litukuzwa jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na nguvu ni zake.
\s5
\v 21 Anabadili wakati na majira; anaondoa wafalme na kuweka wafalme katika viti vyao vya enzi. Anawapa hekima wenye hekima na ufahamu kwa wenye weledi.
\v 22 Hufunua vitu vya chini na vilifichika kwa sababu anajua kile kilicho gizani, naye anaishi pamoja na mwanga.
\s5
\v 23 Mungu wa baba zetu, ninakushukuru na kukutukuza wewe kwa ajili ya hekima na nguvu uliyonipa. Sasa umeyafanya yawe wazi kwetu yale tuliyokuomba; umetujulisha mambo yamhusuyo mfalme."
\s5
\v 24 Ndipo Danieli alienda kumwona Arioki ( yule ambaye mfalme alimchagua kuua kila mtu aliyekuwa na hekima katika Babeli). Alimwendea na kumwambia, "Usiwauwe watu wenye hekima katika Babeli. Nipeleke kwa mfalme na nitamwonesha mfalme tafsiri ya ndoto yake."
\s5
\v 25 Kisha Arioki kwa haraka alimleta Danieli mbele za mfalme na kusema, " Nimempata miongoni wa watu wa mateka wa Yuda mtu ambaye atafunua maana ya ndoto ya mfalme."
\v 26 Mfalme akamwambia Danieli (ambaye alikuwa akiitwa Beliteshaza), "Je unaweza kunimbia ndoto niliyoiona na maana yake?"
\s5
\v 27 Danieli alimjibu mfalme na kusema, "Siri ambayo mfalme ameiomba haiwezi kufunuliwa na watu wenye hekima, wala wale wenye kuongea na wafu, wala wachawi, na wala wataalamu wa nyota.
\v 28 Isipokuwa kuna Mungu ambaye anaishi mbinguni, ambaye hufunua siri, na amekwisha kukujulisha wewe, mfalme Nebukadneza, kile kitakachotokea katika siku zijazo. Hizi ndizo Ndoto na maono ya akili zako uliyoyaona wakati ulipokuwa umelala kitandani mwako.
\s5
\v 29 Na kwako Wewe, mfalme, mawazo yako kitandani mwako yalikuwa ni juu ya mambo yajayo, na yule afichuaye siri ameifanya ijulikane kwako kuhusu kile kilicho karibu kutokea.
\v 30 Na kuhusu mimi, siri hii haikufunuliwa kwangu kwa sababu ya hekima yoyote niliyo nayo zaidi ya mtu yoyote anayeishi. Siri hii imefunliwa kwangu ili kwamba wewe, mfalme, uweze kufahamu maana, na ili kwamba ujuwe mawazo yaliyo ndani mwako.
\s5
\v 31 Mfalme, uliangalia juu na ukaona sanamu kubwa. Sanamu hii ambayo ilikuwa yenye nguvu na yenye kung'aa, ilisimama mbele yako. Mng'ao wake ulikuwa unatisha.
\v 32 Kichwa cha sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi. Matiti yake na mikono ilikuwa ya fedha. Sehemu ya katikati na mapaja yake yalikuwa yametengenezwa kwa shaba,
\v 33 na miguu yake ilikuwa imetengenezwa kwa chuma. Miguu yake ilikuwa ilitengenezwa kwa sehemu chuma na sehemu kwa udongo.
\s5
\v 34 Ulitazama juu, na jiwe lilikuwa limechongwa, ingawa si kwa mikono ya wanadamu, na liliipiga sanamu katika miguu yake ya chuma na udongo, na ponda ponda.
\v 35 Kisha chuma, udongo, fedha, na dhahabu zilivunjwa katika vipande vipande kwa wakati mmoja na yakawa kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi. Upepo huyapeperushia mbali na hakuna alama inayoachwa. Lakini jiwe lililoipiga sanammu likawa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.
\s5
\v 36 Hii ndiyo ilikuwa ndotoyako. Na sasa tutamwambia mfalme maana yake.
\v 37 Wewe, mfalme, ni mfalme wa wafalme kwa wale ambao Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, nguvu, uweza na heshima.
\v 38 Amevitia mkononi mwako sehemu ambazo binadamu huishi. Amekupa wanyama wa mwituni na ndege wa angani katika mkono wako, na amekufanya wewe utawale juu yao wote. Wewe u kichwa cha dhahabu cha sanamu.
\s5
\v 39 Baada yako, ufalme mwingine utainuka ambao ni mdogo kwako, na hata ufalme wa tatu wa shaba utatawala juu ya dunia yote.
\s5
\v 40 Kutakuwa na ufalme wa tatu, wenye nguvu kama chuma, kwa kuwa chuma huvunja vipande vipande vitu vingine na kuponda ponda kila kitu. Itaviharibu vitu hivi vyote na kuvisaga.
\s5
\v 41 Kama vile ulivyoona, miguu na vidole vilikuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo na kwa sehemu vimefanywa kwa chuma, hivyo utakuwa ni ufalme uliogawanyika; baadhi ya nguvu za chuma zitakuwa ndani yake, kama tu ulivyoona kuwa chuma kimechanganyikana na udongo laini.
\v 42 Kama vile vidole vya miguuni vilivyokuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa chuma na kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo, ndivyo ufalme utakuwa kwa sehemu una nguvu na kwa sehemu utakuwa dhaifu.
\v 43 Kama ulivyoona chuma kimechanganywa na udongo laini, na hivyo na watu watakuwa wamechanganyikana; hawakaa kwa pamoja, kama vile chuma kisivyoweza kushikamana na udongo
\s5
\v 44 Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao hautaweza kuangushwa, wala kushindwa na watu wengine. Utazivunja falme zingine vipande vipande na kuzikomesha zote, nao utadumu milele.
\v 45 Kama tu ulivyoona, jiwe lilichongwa kutoka katika mlima, lakini si kwa mikono ya wanadamu. Lilivunja vunja chuma, shaba, udongo, fedha, na dhahabu katika vipande vipande. Mungu mkuu amekujulisha wewe, mfalme, kile kitakachotokea baada ya haya. Ndoto ni ya kweli na tafsiri yake ni ya kuaminika.
\s5
\v 46 Mfalme Nebukadneza alianguka kifudifudi mbele ya Daniel na alimweshimu; aliamuru kwamba sadaka zitolewe na manukato yatolewe kwake.
\v 47 Mfalme alimwambia Danieli, " Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, Bwana wa wafalme, na ambaye hufunua mafumbo, kwa kuwa umekuwa ukiweza kufumbua mafumbo haya."
\s5
\v 48 Ndipo mfalme alimfanya Danieli kuwa wa kuheshiwa sana na alimpa zawadi nyingi nzuri. Alimfanya kuwa mtawala juu ya jimbo lote la Babeli. Danieli akawa liwali mkuu juu watu wenye hekima wa Babeli.
\v 49 Danieli alipeleka ombi kwa mfalme, na mfalme aliwateua Shadraka, Meshaki na Abedinego kuwa watawala juu ya jimbo la Babeli. Lakini Danieli alisalia katika ikulu ya mfalme.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu ambayo ilikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa sita. Aliiweka katika uwanda wa Dura katika jimbo la Babeli.
\v 2 Kisha Nebukadneza alituma ujumbe wa kuwaita pamoja magavana wote wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na na washauiri, wahazini, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wakuu wa majimbo ili waje kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu aliyokuwa ameiweka.
\s5
\v 3 Ndipo magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na washauri, wahasibu, waamuzi, mahakimu, na maafisa wa juu wa majimbo walikusanyika kwa pamoja katika uzinduzi wa sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka. Walisimama mbele yake.
\v 4 Kisha mtangazaji alipiga kelele, "Enyi watu, mataifa, na lugha mmeamriwa
\v 5 kwamba mtakaposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, ni sharti kuanguka na kuisujudia ninyi wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameiweka.
\s5
\v 6 Na yeyote asiyeanguka na kuiabuda, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto."
\v 7 Basi watu walilposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, watu wote, mataifa na lugha walianguka na kuisujudia wao wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.
\s5
\v 8 Wakati huu baadhi ya Walkadayo walikuja na kuleta mashitaka kinyume na Wayahudi.
\v 9 Walimwambia mfalme Nebukadneza, "mfalme aishi milele!
\v 10 Ewe mfalme, umeweka amri kwamba kila mtu aisikiye sauti ya pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari, na aina zote za muziki, lazima kuanguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu.
\s5
\v 11 Mtu yeyote asiyeanguka na kuiabudu sharti atupwe katika tanuru linalowaka moto.
\v 12 Sasa kuna baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu masuala ya jimbo la Babeli; majina yao ni Shadraka, Meshaki, na Abednego. Mfalme, hawa watu hawakutii wewe. Hawataiabudu, kuitumikia wala kuisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka."
\s5
\v 13 Ndipo Nebukadneza alijawa na hasira na ghadhabu, aliagiza kwamba Shadraka, Meshaki na Abednego waletwe kwake. Hivyo, waliwalete hawa watu mbele ya mfalme.
\v 14 Nebukadneza aliwaambia, "Je mmejipanga katika akili zenu, enyi Shadraka, Meshaki na Abedinego, kwamba hamtaiabudu miungu yangu wala kuisujudia wenyewe sanamu ile ya dhahabu ambayo nimeiweka?
\s5
\v 15 Basi sasa kama mko tayari - mtakaposikia sauti pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinumbi na zumari, aina zote za muziki - kuanguka chini na kuisujudia wenyewe sanamu ile ambayo nimeitengeneza, mambo yote yatakuwa mazuri. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa mara katika tanuru la moto. Ni mungu gani atakayeweza kuwaokoa katika mikono yangu?"
\s5
\v 16 Shadraka, Meshaki, na Abednego wakamjibu mfalme, "Nebukadneza, hatuhitaji kukujibu wewe katika jambo hili.
\v 17 Kama kuna jibu, ni kwamba Mungu wetu ambaye tunamtumikia anaweza kutuhifadhi sisi salama katika katika tanuru la moto, na atatuokoa sisi katika mkono wako, mfalme.
\v 18 Kama sivyo, na ijulikane kwako, wewe mfalme, kwamba hatutaiabudu miungu yako, na wala hatutaisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu uliyoiweka.
\s5
\v 19 Ndipo Nebukadneza alijawa na ghadhabu; mwonekano wa uso wake ulibadilika kinyume na Shadraka, Meshaki na Abedinego. Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida.
\v 20 Kisha aliwaamuru baadhi ya watu wenye nguvu katika jeshi lake kuwafunga Shadraka, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika tanuru liwakalo moto.
\s5
\v 21 Walifungwa akali wakiwa wamevaa nguo zao, kanzu, kilemba, na mavazi mengine, na walitupa katika tanuru liwakalo moto.
\v 22 Kwasababu ya agizo la mfalme lilifuatwa na tanuru lilikuwa na joto sana, miali ya moto iliwaua watu waliowatupa Shadraka, Meshaki, na Abedinego.
\v 23 Hawa wanaume watatu, Shadraka, Meshaki, na Abednego, waliangukia katika tanuru liwakalo moto wakali wamefungwa.
\s5
\v 24 Kisha Nebukadneza mfalme alishangazwa na alisimam haraka. Aliwauliza washauri wake, "Je hatukutupa watu watatu wakiwa wamefungwa katika moto?" Nao walimjibu mfalme, "Hakika mfalme."
\v 25 Alisema, "Lakini ninaona watu wanne ambao hawajafungwa wakizunguka katika moto, na hawajaumizwa. Mng'ao wa mtu wa nne ni kama mwana wa miungu."
\s5
\v 26 Ndipo Nebukadneza aliposogea karibu na mlango wa tanuru liwakalo moto na akaaita, "Shadraka, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni nje! Njooni hapa! Ndipo Shadraka, Meshaki na Abednego walitoka nje ya moto.
\v 27 Magavana wa majimbo, magavana wengine, na washauri wa mfalme waliokuwa wamekusanyika kwa pamoja waliwaona watu hawa. Moto haukuunguza miili yao; nywele katika vichwa vyao hazikuungua; mavazi yao yalikuwa hayajaharibiwa; na hawakuwa na harufu ya moto.
\s5
\v 28 Nebukadneza alisema, "Na tumsifu Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego, ambaye amemtuma mjumbe wake na amewapa ujumbe watumishi wake. Walimtumaini yeye wakati walipoikana amri yangu, na waliitoa miili yao badala ya kuabudu au kusujudia mungu mwingine isipokuwa Mungu wao.
\s5
\v 29 Hivyo basi ninaagiza kwamba watu wote, taifa au lugha ambayo itazungumza kitu chochote kinyume na Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego lazima wakatwe vipande, na ya kwamba nyumba zao lazima zifanywe kuwa vichuguu vya uchafu kwasababu hakuna mungu mwingine anayeweza kuokoa kama hivi."
\v 30 Ndipo mfalme aliwapandisha cheo Shadraka, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Mfalme Nebukadneza aliituma amri hii kwa watu wote, mataifa, na lugha walioishi katika nchi: "Na amani yenu na iongezeke.
\v 2 Imeonekana vizuri kwangu kuwaambia juu ya ishara na maajabu ambayo Mungu Mkuu Aliye juu amenifanyia.
\v 3 Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake yana nguvu! Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizazi."
\s5
\v 4 Mimi, Nebukadneza, nilikuwa ninaishi kwa furaha katika nyumba yangu, na nilikuwa nikifurahia mafanikio katika ikulu yangu.
\v 5 Lakini ndoto niliyoiota ilifanya niogope. Nilipokuwa nimejilaza pale, taswira niliyoiona na maono katika akili yangu yalinitaabisha.
\v 6 Basi nilitoa agizo la kuwaleta mbele yangu watu wote wa Babeli waliokuwa na hekima ili kwamba waweze kunitafsiria ndoto.
\s5
\v 7 Kisha walikuja wachawi, wale ambao hudai kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wasoma nyota. Niliwaambia juu ya ndoto, lakini hawakuweza kunitafsiria.
\v 8 Bali mwishoni Danieli aliingia ndani - yeye ambaye huitwa Belteshaza jina la mungu wangu, na ambaye ndani yake kuna roho ya miungu mitakatifu - na nilimwambia juu ya ndoto.
\v 9 "Belteshaza, mkuu wa wachawi, ninajua kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako na ya kwamba hakuna siri iliyo ngumu kwako. Niambie kile nilichokiona katika ndoto yangu na nini maana yake.
\s5
\v 10 Haya ndiyo niliyoyaona katika akili zangu nilipokuwa nimejilaza katika kitanda changu: Nilitazama, na kulikuwa na mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana.
\v 11 Mti ulikua na ukawa wenye nguvu. Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote.
\v 12 Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliisha katika matawi yake. Viumbe vyote hai vililishwa katika mti huo.
\s5
\v 13 Nilipokuwa nimelala kitandani kwangu, niliona katika akili zangu, mjumbe mtakatifu alishuka kutoka mbinguni.
\v 14 Alipiga kelele na kusema, 'Ukateni mti na yafyekeni matawi yake, yapukutisheni majani yake, na kuyasambaza matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wapae mbali kutoka katika matawi yake.
\s5
\v 15 Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na fungu la chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini.
\v 16 Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.
\s5
\v 17 Uamuzi huu ni kutokana na amri iliyotolewa na mjumbe. Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu ili kwamba hao walio hai wajue kwamba Mungu aliye juu sana anatawala juu ya falme za watu na huwapa kwa kila mmoja apendaye kumweka juu yao, hata kwa watu wale wanyenyekevu sana.'
\v 18 Mimi, Mfalme Nebukadneza nilipata ndoto hii. Sasa, wewe Belteshaza, niambie tafsiri yake, kwasababu hakuna mtu mwenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunitafsiria. Lakini wewe unaweza kufanya hivyo, kwa kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako."
\s5
\v 19 Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza, alihuzunishwa kwa muda, na mawazo yake yalimshitua. Mfalme akasema, " Belteshaza, usifadhaishwe na ndoto au tafsiri yake." Belteshaza akajibu, " Bwana wangu, ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako.
\s5
\v 20 Mti ule uliouona - uliokua na ukawa na wenye nguvu, na ambao sehemu yake ya juu ilifika hata mbinguni, na ambao waweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote -
\v 21 ambao majani yake ni mazuri, na matunda yake yalikuwa ni mengi, ili kwamba ndani yake kulikuwa na chakula cha wote, na chini yake wanyama wa mwituni walipata kivuli, na ndani yake ndege wa angani waliishi -
\v 22 huu mti ni wewe, mfalme, wewe uliyekua na kuwa na nguvu. Ukuu wako umeongezeka na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika hata miisho ya dunia.
\s5
\v 23 Ewe mfalme, ulimwona mjumbe akishuka kutoka mbinguni na akisema, "Ukateni mti na uteketezeni, lakni kiacheni kisiki cha mizizi yake katika nchi, kifungeni kwa ukanda wa chuma na shaba, katikati ya mche mororo katika shamba. Na kilowanishwe na umande kutoka mbinguni. Kiache kiishi katika wanyama wa mwituni katika mashamba mpaka ipite miaka saba.'
\s5
\v 24 Mfalme, hii ni tafsiri yake. Ni agizo la Yeye Aliye Juu ambalo limekufikia, bwana wangu mfalme.
\v 25 Utafukuzwa utoke miongoni mwa watu, na utaishi pamoja na wanyama wa mwituni huko mashambani. Utafanywa uwe unakula majani kama ng'ombe, na utalowanishwa na umande wa kutoka mbinguni, miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme zote za watu na ya kwamba yeye humpa falme hizo mtu yeyote amtakaye.
\s5
\v 26 Kama ilivyoamriwa kwamba kukiacha kisiki cha mizizi ya mti, kwa njia hii ufalme wako utarudishiwa katika kipindi ambacho utajifunza kwamba mbingu inatawala.
\v 27 Hivyo basi, mfalme, ushauri wangu na ukubalike kwako. Acha kutenda dhambi na utende haki. Geuka uache uovu wako wa kuonesha huruma kwa walionewa, na itakuwa kwamba mafanikio yako yataongezwa."
\s5
\v 28 Vitu hivi vyote vilitokea kwa mfalme Nebukadneza.
\v 29 Baada ya miezi wa kumi na miwili alipokuwa akitembea juu ya dari la ikulu ya kifalme katika Babeli,
\v 30 na alisema, " Je hii si Babeli kuu, ambayo nimeijenga kwa ajili ya makao yangu ya kifalme, kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?"
\s5
\v 31 Wakati maneno yakali katika midomo ya mfalme, sauti ilisikika kutoka mbinguni: "Mfalme Nebukadneza, imetangazwa kwako kwamba ufalme huu umeondolewa kutoka kwako.
\v 32 Utafukuziwa mbali kutoka miongoni mwa watu, na makao yao yatakuwa pamoja na wanyama wa mwitu katika mashamba. Utafanywa kulamajani kama ng'ombe. Miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na humpa falme mtu yeyote amtakaye."
\s5
\v 33 Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.
\s5
\v 34 Na katika mwisho wa siku, mimi, Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, utimamu wa akili nilirudishiwa. "Nilimsifu Mungu Aliye Juu sana, na nilimheshimu na kumtukuza yeye aishiye milele. Kwa kuwa utawala wake ni wa milele, na ufalme wake unadumu katoka katika vizazi vyote hadi vizazi vyote.
\s5
\v 35 Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure; hufanya lolote limpendezalo miongoni mwa jeshi la mbinguni na wakazi wa dunia. Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia au kumpa changamoto. Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, "Mbona umefanya hivi?"
\s5
\v 36 Kwa wakati ule ule utimamu wa akili zangu uliponirudia, utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na watu wenye heshima walitafuta msaada wangu. Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi.
\v 37 Sasa basi, mimi Nebukadneza, ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake yote ni ya haki, na njia zake ni za adili. Anaweza kuwashusha wale wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Mfalme Belshaza alifanya sherehe kubwa kwa kwa ajili ya wakuu wake wa kuheshimiwa wapatao elfu moja, na alikunywa divai mbele yao wote watu elfu moja.
\v 2 Wakati Belshaza alipokuwa akionja divai, alitoa agizo la kuleta vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu au kwa fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka katika hekalu huko Yerusalemu, ambavyo yeye, na wakuu wake, na wake zake, na masuria waliweza kuvinywea.
\s5
\v 3 Watumishi walivileta vyombo ya dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu, nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Mfalme na wakuu wake, na wake zake na masuria walivinywea.
\v 4 Walikunywa divai na kuzisifu sanamu zao zilizotengenezwa kwa dhahabu na fedha, shaba, chuma, mbao na mawe.
\s5
\v 5 Kwa wakati huo huo vidole vya mkono wa mtu vilionekana mbele ya kinara cha taa na kuandika katika ukuta uliopigwa lipu katika ikulu ya mfalme. Mfalme aliweza kuona sehemu ya mkono ulipokuwa unaandika.
\v 6 Ndipo uso wa mfalme ulibadilika na mawazo yake yalimwogopesha; miguu yake haikuweza kumfanya asimame, na magoti yake yalikuwa yakigongana kwa pamoja.
\s5
\v 7 Mfalme alitoa agizo kwa kupiga kelele, waletwe ndani wale ambao hudai wanaweza kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wataalamu wa nyota. Mfalme akawaambia wale waliojulikana kwa hekima katika Babeli, "Yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naye atakuwa mtawala wa tatu wa juu kwa mamlaka katika ufalme."
\s5
\v 8 Ndipo watu wote wa mfalme walikuwa wakijulikana kwa hekima yao waliingia ndani, lakini hawakuweza kuyasoma maandishi wala kueleza maana yake kwa mfalme.
\v 9 Kisha mfalme Belshaza alishitushwa sana na mwonekano wa uso wake ulibadilika. Wakuu wake nao walishangazwa sana.
\s5
\v 10 Ndipo sasa malkia alikuja katika nyumba ya sherehe kwasababu ya kile ambacho mfalme na wakuu wake walikuwa wamekisema. Malkia akasema, "Mfalme na aishi milele! Usiache mawazo yako yakakusumbua. Usiruhusu mwonekano wa uso wako ubadilike.
\s5
\v 11 Kuna mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu watakatifu dani yake. Katika siku za baba yako, mwanga na weledi na hekima ya miungu ilipatikana ndani yake. Mfalme Nebukadneza, baba yako mfalme, alimfanya kuwa mkuu wa waganga, pamoja na mkuu wa wale wanazungumza na wafu, na wa wenye hekima, na wa wataalamu wa nyota.
\v 12 Roho bora, ufahamu, weledi, kutafsiri ndoto, kufafanua mafumbo na kutatua matatizo - hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Sasa mwiteni Danieli naye atawaambia maana ya kile kilichoandikwa."
\s5
\v 13 Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamwambia, "Wewe ni yule Danieli, mmoja kati ya watu wa mateka wa Yuda, ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda.
\v 14 Nimesikia habari kukuhusu wewe, kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako.
\s5
\v 15 Na sasa watu wanaojulikana kwa hekima na wale wanaozungumza na wafu, wamekwisha kuletwa mbele yangu, ili kusoma maandishi haya na kunijulisha maana ya tafsiri yake, lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri yake.
\v 16 Nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo. Sasa kama utaweza kusoma maandishi na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na kuwa na kuvalishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako, na utakuwa mtawala wa tatu mwenye mamlaka katika ufalme."
\s5
\v 17 Kisha Danieli akajibu mbele ya mfalme, "Zawadi yako na iwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu yako na umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwaambia maana.
\v 18 Na juu yako, Ewe mfalme, Mungu Aliye juu sana alimpa Nebukadneza baba yako ufalme, ukuu, heshima na enzi.
\v 19 Na kwasababu ya ukuu huo, Mungu alimpa watu wote, mataifa, na lugha walimtetemekea na kumwogopa. Aliwauwa wale aliotaka wafe na aliwaacha hai wale aliotaka waishi. Aliwainua wale aliowataka, na aliwashusha wale aliowataka.
\s5
\v 20 Lakini wakati moyo ulipokuwa na kiburi na roho yake ilifanywa kuwa mgumu na kwasababu hiyo alitenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake.
\v 21 Aliondolewa katika ubinadamu, alikuwa na akili za mnyama, na aliishi na punda wa mwituni. Alikula majani kama ng'ombe. Mwili wake ulilowanishwa kwa umande wa kutoka mbinguni mpaka pale alipojifunza kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na ya kwamba humweka mtu yeyote amtakaye juu yake.
\s5
\v 22 Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa aliyajua haya yote.
\v 23 Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni. Katika nyumba yake walikuletea vyombo ambavyo wewe, wakuu wako, wake zako na masuria wako walivinywea, na kisha ukaisifia sana sanamu zilitengenezwa kwa fedha na dhahabu, shaba, chuma, mbao, na mawe - sanamu ambazo haziwezi kuona, kusikia wa kujua kitu chochote. Haujamheshimu Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake na ambaye anazijua njia zako zote.
\v 24 Ndipo Mungu aliutuma mkono kutoka katika makao yake na maandishi haya yaliandikwa.
\s5
\v 25 Haya ndiyo maandishi ambayo yaliandikwa: 'Mene, Mene, Tekeli na Peresin.'
\v 26 Maana yake ni: 'Mene,' 'Mungu ameuhesabu ufalme wako na ameukomesha.'
\v 27 'Tekeli' 'umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.'
\v 28 'Peresi' 'ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.'"
\s5
\v 29 Ndipo Belshaza alitoa agizo, na walimvalisha Danieli mavazi ya zambarau. Mkufu wa dhahabu walimvisha shingoni, na mfalme alitoa tamko juu ya Danieli kuwa atakuwa mtawala mwenye mamlaka ya nafasi ya tatu katika ufalme.
\v 30 Usiku ule Belshaza, mfalme wa Babeli aliuawa,
\v 31 na Dario Mwajemi aliuchukua ufalme alipokuwa na miaka ipatayo sitini na miwili.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Ilimpendeza Dario kuchagua juu ya ufalme magavana wa majimbo 120 ambao wangetawala juu ya ufalme wote.
\v 2 Juu yao kulikuwa na watawala wakuu watatu, na Daniel alikuwa mmoja wao. Hawa watawala waliwekwa ili waweze kuwasimamia magavana wa majimbo, ili kwamba mfalme asipate hasara.
\v 3 Danieli alipambanuliwa juu ya watawala wakuu na juu ya magavana wa majimbo kwasababu alikuwa na roho isiyo ya kawaida. Mfalme alikuwa akipanga kumweka juu ya ufalme wote.
\s5
\v 4 Basi watawala wakuu wengine na magavana wa majimbo walitafuta makosa katika kazi ambazo Danieli alizifanya kwa ufalme, lakini hawakuweza kuona ufisadi au kushindwa katika majukumu yake kwasababu alikuwa mwaminifu. Hakuna kosa au uzembe uliopatikana ndani yake.
\v 5 Kisha watu hawa wakasema, "Hatukuweza kupata sababu yoyote ya kumshitaki huyu Danieli isipokuwa tukitafuta kitu fulani dhidi yake kuhusiana na sheria za Mungu wake.'"
\s5
\v 6 Ndipo watawala hawa na magavana walileta mpango mbele ya mfalme. Walimwambia, "Mfalme Dario, uishi milele!
\v 7 Watawala wote wakuu wa ufalme, magavana wa mikoa, na magavana wa majimbo, washauri, na magavana wameshauriana kwa pamoja na kuamua kuwa wewe, mfalme, unapaswa kupitisha amri na kuitekeleza, ili kwamba mtu yeyote anayefanya dua kwa mungu yeyote au mtu kwa siku thelathini, isipokuwa wewe mfalme, mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba.
\s5
\v 8 Sasa mfalme, litoe agizo na utie saini nyaraka ili kwamba isije ikabadilika, kama ilivyoelekezwa katika sheria za Wamedi na Waajemi, hivyo haiweze ikabatilishwa.
\v 9 Basi, mfalme Dario alitia saini nyaraka kwa kuifanya amri kuwa sheria.
\s5
\v 10 Danieli alipojua kuwa nyaraka imekwisha kusainiwa kuwa sheria, alienda ndani ya nyumba yake (madirisha yake katika chumba cha juu yalikuwa wazi kuelekea Yerusalemu), na alipiga magoti yake, kama alivyokuwa akifanya mara tatu kwa siku, na aliomba na kushukuru mbele ya Mungu wake, kama alivyofanya hapo kabla.
\v 11 Kisha watu hawa walikuwa wameunda hila kwa pamoja walimwona Danieli akiomba na kutafuta msaada kutoka kwa Mungu.
\s5
\v 12 Ndipo walipomwendea mfalme na kuongea naye kuhusiana na amri yake: "Je haukuweka amri kwamba mtu yeyote akayefanya maombi kwa mungu mwingine au kwa binadamu ndani ya siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, mfalme, lazima mtu huyo atupwe katika tundu la simba? Mfalme akajibu, "Jambo hili ni la hakika, kama ilivyoelekezwa katika sheria za Wamedi na Waajemi; ambazo haziwezi zikabatilishwa."
\s5
\v 13 Kisha wakamjibu mfalme, " Mtu yule Daniel, ambaye ni mmoja wa watu wa mateka kutoka Yuda, hakutii wewe, mfalme wala maagizo yako uliyoyasaini. Yeye humwomba Mungu wake mara tatu kwa siku."
\v 14 Mfalme aliposikia haya, alisikitishwa sana, alitumia akili jinsi ya kumwokoa kutoka katika utawala huu. Alisumbuka sana mpaka wakati wa kuzama kwa jua akijaribu kumwokoa Danieli.
\s5
\v 15 Kisha watu hawa waliokuwa wamepanga njama walikusanyika kwa pamoja na mfalme, na wakamwambia, "Ujue mfalme kwamba ni sheria ya Wamedi na Waajemi kwamba hakuna amri au sanamu ambayo mfalme anaipitisha yaweza kubadilishwa."
\s5
\v 16 Ndipo mfalme alitoa agizo, na walimleta ndani Danieli, na kisha wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, "Mungu wako, ambaye unamtumikia daima, na akuokoe.''
\s5
\v 17 Jiwe lililetwa katika mlango wa tundu, na mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake ili kwamba chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli.
\v 18 Basi mfalme alienda kwenye ikulu yake na usiku ule alikuwa na mfungo. Hakuna starehe yoyote iliyoletwa mbele yake, nao usingizi ulimkimbia.
\s5
\v 19 Kisha katika mapambazuko mfalme aliamka na kwa haraka alienda kwenye tundu la simba.
\v 20 Na alipokaribia kwenye tundu, alimwita Danieli kwa sauti ya huzuni, akimwambia Danieli, "Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je Mungu wako ambaye anamtumkia daima ameweza kukuokoa kutoka katika simba?
\s5
\v 21 Ndipo Danieli akamwambia mfalme, "Mfalme, uishi milele!
\v 22 Mungu wangu amemtuma mjumbe na amevifunga vinywa vya simba, na hazijaweza kunidhuru. Kwa kuwa sikuwa na hatia yoyote mbele yake na pia mbele yako, ewe mfalme, na sijakufanyia jambo lolote la kukudhuru."
\s5
\v 23 Basi mfalme alikuwa na furaha sana. Alitoa agizo kwamba wanatakiwa wamtoe Danieli nje ya tundu. Hivyo Danieli aliondolewa kutoka katika tundu. Hakuna dhara lolote lililoonekana kwake, kwa kuwa alikuwa amemtumainia Mungu wake.
\s5
\v 24 Mfalme alitoa agizo, waletwe wale watu waliomshitaki Danieli na kisha akawatupa wao katika tundu la simba - wao, na watoto wao, na wake zao. Kabla hawajafika sakafuni, simba waliwararua na kuvunjavunja mifupa yao vipande vipande.
\v 25 Kisha mfalme Dario aliandika ujumbe kwa watu wote, mataifa na lugha ambazo ziliishi katika dunia yote: "Amani na iongezeke kwenu.
\s5
\v 26 Ninaagiza kwamba katika utawala wote wa ufalme wangu watu watetemeka na kumcha mbele ya Mungu wa Danieli, kwa kuwa ni Mungu aliye hai na huishi milele, na ufalme wake hauwezi kuharibiwa; utawala wake utakuwepo hadi mwisho.
\v 27 Yeye anatuhifadhi salama na kutuokoa, na anafanya ishara na maajabu mbinguni na duniani; amemhifadhi Danieli salama dhidi ya uwezo wa simba."
\s5
\v 28 Na hivyo basi, Danieli alifanikiwa katika utawala wa Dario na katika utawala wa Koreshi Mwajemi.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babelli, Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake. Kisha akayaandika yale aliyoyaona katika ndoto. Aliandika matukio ya muhimu sana:
\v 2 Danieli alieleza, "Usiku katika ndoto zangu niliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu.
\v 3 Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari.
\s5
\v 4 Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, lakini alikuwa na mabawa ya tai. Nilipokuwa natazama, mabawa yake yalikuwa yamepasuka na alikuwa ameinuliwa katika ardhi na alikuwa amesimama kwa miguu miwili kama mtu. Na alipewa akili za kibinadamu.
\v 5 Na kulikuwa na mnyama wa pili, alikuwa kama dubu, na alikuwa ameinama, alikuwa na mbavu tatu katikati ya meno yake katika mdomo wake. Aliambiwa, 'Inuka na umeze watu wangi.'
\s5
\v 6 Baada ya hili, niliangalia tena. Kulikuwa na mnyama mwingine ambaye alionekana kama chui. Mgongoni mwake alikuwa na mabawa manne kama mabawa ya ndege, na alikuwa na vichwa vinne. Alipewa mamlaka ya kutawala.
\v 7 Baada haya, niliona usiku katika ndoto yangu mnyama wa nne, mwenye kuogofya, na kutisha na mwenye nguvu. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; aliteketeza, na kuvunja vunja katika vipande, na kusaga saga katika miguuni pake kile kilichosalia. Alikuwa ni wa tofauti na wanyama wengine, na alikuwa na pembe kumi.
\s5
\v 8 Na wakati nilipokuwa natafakari juu ya pembe, nilitazama na niliona pembe nyingine ndogo ilichipuka katikati ya pembe zingine. Mizizi ya pembe tatu kati ya pembe za mwanzo iling'olewa. Niliona katika pembe hii macho kama macho ya mtu na mdomo ambao ulikuwa ukijivuna kwa mambo makubwa.
\s5
\v 9 Na nilipotazama, viti vya enzi vilikuwa vimewekwa, na Mtu wa siku za kale alikaa sehemu yake. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto.
\s5
\v 10 Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na mamilioni ya watu walimtumikia, na wengine mia moja milioni walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa.
\s5
\v 11 Niliendelea kuangalia kwasababu ya maneno ya kiburi yaliyosemwa na pembe. Nilitazama wakati mnyama anauliwa, na mwili wake uliharibiwa, na ulitolewa kwa ajili ya kuchomwa moto.
\v 12 Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezea kwa kipindi fulani cha muda.
\s5
\v 13 Katika maono yangu usiku ule, nilimwona mtu mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake.
\v 14 Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa.
\s5
\v 15 Na kwangu mimi, Danieli, roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu, na maono niliyoyaona katika akili zangu yalinisumbua.
\v 16 Nilimsogelea mmoja wa hawa walikuwa wamesimama hapo na nikamwomba anioneshe maana ya mambo haya.
\s5
\v 17 Hawa wanyama nne wakubwa ni wafalme wanne ambao watatoa katika nchi.
\v 18 Lakini watu watakatifu wa Mungu aliyejuu wataupokea ufalme na wataumiliki milele na milele.'
\s5
\v 19 Ndipo nilipotaka kujua zaidi juu ya mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti sana na wengine na alikuwa wa kutisha pamoja na meno yake ya chuma na makucha ya shaba; alimeza, na alivunja vipande vipande, na alisaga saga kwa miguu yake kile kilichokuwa kimesalia.
\v 20 Nilitaka kujua juu ya pembe kumi katika kichwa chake, na kuhusu pembe nyingine iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini. Nilitaka kujua kuhusu pembe yenye macho na kuhusu mdomo uliokuwa unajisifu kwa mambo makubwa na ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko zingine.
\s5
\v 21 Na nilipotazama, pembe hii iliinua vita dhidi ya watu watakatifu na ilikuwa inawawashinda mpaka pale
\v 22 Mzee wa Siku alipokuja, na watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu Sana. Ndipo wakati ulipowadia ambapo watu watakatifu waliupokea ufalme.
\s5
\v 23 Hiki ndicho mtu yule alichokisema, 'Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunja vunja vipande vipande.
\v 24 Na kuhusu pembe kumi, kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka, na mwingine atainuka baada yao. Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia, na atawashinda wale wafalme watatu.
\s5
\v 25 Atazungumza maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu sana na atawatesa watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu. Atajaribu kuzibadili sikukuu na sheria. Mambo haya atapewa mikononi mwake kwa mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka.
\v 26 Lakini kikao cha mahakama kitaitishwa, na watazichukua nguvu zake za kifalme ili mwisho aweza kuharibiwa na kuteketezwa.
\s5
\v 27 Ufalme na utawala, ukubwa wa falme chini ya mbingu yote, watapewa watu walio wa watu watakatifu wa Yeye Aliye juu Sana. Ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zingine zote zitamtumikia na kumtii yeye.'
\v 28 Na huu ndio mwisho wa mambo. Na kuhusu mimi, Danieli, mawazo yangu yanihuzunisha sana mimi na mwonekano wa uso wangu ulibadilika. Lakini mambo haya niliyahifadhi mimi mwenyewe."
\s5
\c 8
\p
\v 1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza, mimi Danieli niliona maono (baada ya maono ya awali yaliyonipata).
\v 2 Nilipokuwa nikiangalia katika ndoto, niliona kwamba nilikuwa katika mji wa Shushani wenye ngome katika jimbo la Elamu. Niliona katika ndoto kuwa nilikuwa karibu na mfereji wa Ulai.
\s5
\v 3 Nilitazama juu na nikaona mbele yangu kondoo dume lenye mapembe mawili, limesimama pembeni mwa mfereji. Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine.
\v 4 Niliona kondoo mme akiishambulia magharibi, kisha kaskazini, na baadaye kusini; hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana.
\s5
\v 5 Na nilipokuwa natafakari juu ya haya, niliona beberu akitoka magharibi, na kuvuka katika uso wa dunia yote, akikimbia kwa kasi kana kwamba hakuonekana kama aligusa ardhini. Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake.
\v 6 Alienda mpaka kwa kondoo aliyekuwa na pembe mbili, nilikuwa nimemwona kondoo dume amesimama katika ukingo wa mfereji na mbuzi alikimbia kumwelekea kondoo dume kwa hasira kali.
\s5
\v 7 Niliiona mbuzi ikija karibu na kondoo. Mbuzi alikuwa na hasira na kondoo, alimpiga kondoo na alizivunja pembe zake mbili. Kondoo hakuwa na nguvu za kusimama mbele zake. Mbuzi alimgonga kondoo akaanguka chini na akamkanyaga. Hapakuwa na yeyote wa kumwokoa kutoka katika nguvu zake.
\v 8 Ndipo mbuzi alikua akawa mkubwa, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.
\s5
\v 9 Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri.
\v 10 Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni. Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani, na zilikanyagwa.
\s5
\v 11 Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi.
\v 12 Kwasababu ya uasi, pembe ya mbuzi ilipewa jeshi, na sadaka za kuteketezwa zitasitishwa. Pembe itautupa ukweli chini ardhini, na itafanikiwa katika kila jambo ilifanyalo.
\s5
\v 13 Kisha nilimsikia mtakatifu mmoja akiongea na mtakatifu mwingine akamjibu, " Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, ukabidhiajia wa sehemu takatifu, na jeshi la mbinguni kukanyagwa?
\v 14 Aliniambia, " Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2, 300. Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa."
\s5
\v 15 Wakati mimi Danieli, nilipoona maono, nilijaribu kuyaelewa. na hapo mbele yangu alisimama yule aliyeoneakana kama mtu.
\v 16 Niliisikia sauti ya mtu ikiita katikati ya kingo za mfereji wa Ulai. Alisema, "Gabrieli, msaidie mtu huyu kuelewa maono."
\v 17 Basi alikuja karibu na mahali niliposimama. Na alipokuja, niliogopa na nilisujudia hadi chini. Aliniambia,"Fahamu, mwana wa mtu, kwamba maono ni kwa ajili ya wakati wa mwisho."
\s5
\v 18 Alipokuwa anaongea na mimi, nilipata usiingizi mzito nikiwa nimelala kifudifudi. Kisha alinishika na kunisimamisha.
\v 19 Akaniambia, "Tazama, nitakuonyesha kile kitachotokea baadaye katika kipindi cha ghadhabu, kwasababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho uliopangwa.
\s5
\v 20 Na kuhusu kondoo mme uliyemwona, yule mwenye pembe mbili - ni wafalme wawili wa Umedi na Uajemi.
\v 21 Mbuzi dume ni mfalme wa Ugiriki. Pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
\s5
\v 22 Na kuhusu pembe iliyovunjika, ambayo katika nafasi yake pembe zingine nne zilichipuka - hizi ni falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake, lakini hazitakuwa na nguvu kubwa.
\v 23 Katika siku zijazo za falme hizo, wakati ambapo wahalifu watakuwa wamefikia kikomo chao, mfalme mwenye uso katili, na yeye mwenye akili sana, atainuka.
\s5
\v 24 Nguvu zake zitakuwa kubwa, lakini si kwa nguvu zake mwenyewe. Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu.
\v 25 Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwasababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme, na atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu.
\s5
\v 26 Maono kuhusu jioni na asubuhi ulizoambiwa ni ya kweli. Lakini uyafunge maono haya, kwa kuwa yanahusu siku nyingi za wakati ujao.
\s5
\v 27 Ndipo mimi, Danieli nilichoka sana na nikalala nikiwa dhaifu kwa siku kadhaa. Kisha nikainuka na nikaenda kufanya kazi za mfalme. Lakini nilikuwa nimetishwa sana na maono, na hapakuwa na mtu yeyote aliyeweza kuyaelewa.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Dario mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi. Alikuwa na Ahasuero ambaye alifanywa mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.
\v 2 Sasa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario, mimi Danieli, nilikuwa najisomea vitabu vilivyo na neno la Yahweh, neno ambalo lilikuwa limemjia Yeremia nabii. Niligundua kwamba kungekuwa na miaka sabini hadi mwisho wa kuachwa kwa Yerusalemu ungefika.
\s5
\v 3 Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.
\v 4 Nilimwomba Yahweh Mungu wangu, na niliungama dhambi zetu. Nilisema, "Tafadhali, Bwana, wewe ni Mungu mkuu na mwenye kuheshimiwa, wewe hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda wewe na kuzishika amri zako.
\s5
\v 5 Tumetenda dhambi na tumefanya yaliyo mabaya. Tumeenenda kwa uovu na tumeasi, tumegeuka upande kinyume na amri na maagizo yako.
\v 6 Hatujawasikiliza watumishi wako manabii walizungumza na wafalme wetu, viongozi wetu, baba zetu, na kwa watu wote wa nchi kwa jina lako.
\s5
\v 7 Kwako Bwana, kuna uadilifu. Hata hivyo, kwetu kuna aibu katika nyuso zetu, kwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalem, na kwa Israeli yote. Hii ni pamoja na wale walio karibu na wale walio mbali katika nchi zote ambazo kwazo uliwatawanya. Hii ni kwasababu ya udanganyifu mkubwa tulioufanya kinyume chako.
\v 8 Kwetu sisi, Yahweh, kuna fedheha katika nyuso, na kwa wafalme wetu, na kwa viongozi wetu, na kwa baba zetu, kwasababu tumekutenda dhambi wewe.
\s5
\v 9 Kwa Bwana Mungu wetu kuna huruma na msamaha, kwa kuwa tumemwasi yeye.
\v 10 Hatujaitii sauti ya Yahweh Mungu wetu kwa kutembea katika sheria zake alizotupatia kupitia watumishi wake manabii.
\v 11 Israeli wote wameiasi sheria yako na kugeukia upande, kwa kukataa kuitii sauti yako. Laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu, zimemwagwa juu yetu kwa kuwa tummetenda dhambi.
\s5
\v 12 Yahweh ameyathibitisha maneno ambayo aliyasema kinyume na sisi na kinyume na viongozi wetu juu yetu, kwa kuleta juu yetu janga kubwa. Kwa kuwa chini ya mbingu yote haijawahi kufanyika kitu chochote ambacho kinaweza kulinganishwa na kile kilichofanyika huko Yerusalemu.
\v 13 Kama ilivyoandikwa kwenye sheria ya Musa, baa hili lote limetupata, ingawa bado hatujaomba rehema kutoka kwa Yahweh Mungu wetu kwa kugeuka na kuacha maovu yetu na kuufuata ukweli wako.
\v 14 Hivyo basi, Yahweh ameyaweka tayari maafa na ameyaleta juu yetu, kwa kuwa Yahweh Mungu wetu ni mwenye haki katika matendo yote anayoyafanya, ingawa bado hatujaitii sauti yake.
\s5
\v 15 Basi sasa, Bwana Mungu wetu, uliwatoa watu wako katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu, na umejifanyia jina maarufu kwa ajli yako mwenyewe, hata siku hii ya leo. Lakini bado tumekutenda dhambi; tumefanya mambo ya hila. Kwasababu ya matendo yako yote ya haki,
\v 16 Bwana, iache hasira na ghadhabu yako iwe mbali na mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Hii ni kwasababu ya dhambi zetu, na kwasababu ya uovu wa baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamekuwa kitu cha kudharauliwa na wote wanaotuzunguka.
\s5
\v 17 Basi sasa, Mungu wetu, sikiliza sala za mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema; kwa ajili yako, Bwana ufanye uso wako ung'ae katika sehemu yako takatifu iliyoachwa ukiwa.
\v 18 Mungu wangu, fungua masikio yako na usikie; fumbua macho yako na uone. Tumeharibiwa; utazame mji unaoitwa kwa jina lako. Hatukuombi msaada wako kwasababu ya haki yetu, ila kwasababu ya rehema zako kuu.
\v 19 Bwana, sikiliza! Bwana, samehe! Bwana, tuangalie na ufanye jambo! Kwa ajili yako mwenyewe, usichelewe, Mungu wangu, kwa kuwa mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako."
\s5
\v 20 Nilipokuwa ninaongea kwa kuomba na kuungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuwasilisha maombi yangu mbele ya Yahweh Mungu wangu kwa niaba ya mlima mtakatifu wa Mungu.
\v 21 Nilipokuwa ninaomba, mtu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika ndoto hapo awali, alipaa kwa kasi kushuka kuja nilipo, ilikuwa ni wakati wa sadaka ya jioni.
\s5
\v 22 Alinipa ufahamu na aliniambia, "Danieli, nimekuja sasa ili nikupe utambuzi na ufahamu.
\v 23 Ulipoanza kuomba rehema, amri ilitolewa na nimekuja kukueleza jibu, kwa kuwa unapendwa sana. Hivyo basi, tafakari neno hili na uufahamu ufunuo.
\s5
\v 24 Miaka sabini na saba zimeamriwa kwa ajili ya watu wako na mji wako mtakatifu kukomesha hatia na kumaliza dhambi, na kuleta haki ya milele, na kutimiza maono na unabii, na kupaweka wakfu mahali patakatifu sana.
\v 25 Ujue na kufahamu kuwa tangu kupitishwa kwa amri ya kurudi na kuijenga upya Yerusalemu mpaka ujio wa mpakwa mafuta (atakayekuwa kiongozi), kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili. Yerusalemu itajengwa pamoja na mitaa yake na handaki, licha ya kuwepo kwa nyakati za shida
\s5
\v 26 Baada ya miaka ya majuma sitini na mbili, mtiwa mafuta ataharibiwa na atakuwa hana kitu chochote. Jeshi la kiongozi ajaye litauangamiza mji na mahali patakatifu. Mwisho wake utatatokea kwa gharika, na kutakuwa na vita hata mwisho. Uharibifu umekwisha amriwa.
\s5
\v 27 Atalithibitisha agano pamoja na watu wengi kwa miaka saba. Katikati ya miaka saba atakomesha dhabihu na sadaka. Baada ya chukizo la uharibifu atatokea mtu atakayeleta ukiwa. Mwisho kamili na uharibifu umeamriwa kutokea kwa yeye aliyesababisha ukiwa."
\s5
\c 10
\p
\v 1 Katika mwaka wa tatu wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ujumbe ulifunuliwa kwa Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza. Ujumbe huu ulikuwa ni wa kwelil. Ulihusu vita kuu. Danieli aliufahamu ujumbe alipopata ufumbuzi kutoka katika maono.
\s5
\v 2 Katika siku hizo, mimi Danieli, nilikuwa katika maombolezo kwa wiki tatu.
\v 3 Sikula chakula kizuri, sikula nyama, sikunywa divai, na sikujipaka mafuta mwenyewe mpaka ukamilifu wa wiki tatu nzima.
\s5
\v 4 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa niko karibu na mto mkubwa (ambao ni Tigrisi),
\v 5 Nilitazama juu na nikamwona mtu aliyevaa kitani, akiwa na mkanda kiunoni mwake uliotengenezwa kwa dhahabu safi kutoka Ufazi.
\v 6 Mwili wake ulikuwa kama kito, na sura yake ilikuwa kama radi. Macho yake yalikuwa kama miali ya tochi, na mikono yake na miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosafishwa. Sauti ya maneno yake ilikuwa kama sauti ya umati mkubwa wa watu.
\s5
\v 7 Mimi, Danieli peke yangu niliyaona maono, na watu niliokuwa na pamoja hawakuyaona maono. Lakini, jambo kuu la kuogofya liliwaijia juu yao, na walikimbia na kujificha wao wenyewe.
\v 8 Hivyo niliachwa peke yangu na niliyaona maono haya ajabu. Hakuna nguvu iliyobakia ndani yangu; mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu, na hazikubakia nguvu ndani yangu.
\v 9 Kisha nikasikia maneno yake, na nilipoyasikia, nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito.
\s5
\v 10 Mkono ulinigusa, na ilinifanya nitetemeke katika magoti yangu na viganja vya mikono yangu.
\v 11 Malaika aliniambia, "Danieli, mtu aliyetunzwa sana, yafahamu maneno ninayokwambia wewe. Simama wima, kwa kuwa nimeshakutuma." Na alipomaliza kuniambia ujumbe huu, nilisimama nikiwa natetemeka.
\s5
\v 12 Kisha aliniambia, "Usiogope, Danieli. Tangu siku ya kwanza ulipoiweka akili yako kutaka kufahamu na kujinyenyekeza mwenyewe mbele ya Mungu, maneno yako yalisikiwa, na nimekuja kwasababu ya maneno yako.
\v 13 Mwana wa mfalme wa ufalme wa Uajemi alinizuia, na niliwekwa huko na mfalme wa Uajemi kwa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja kati ya wakuu alikuja kunisaidia.
\s5
\v 14 Sasa nimekuja kukusaidia ili ufahamu kile kitakachotokea kwa watu wako katika siku za mwisho. Kwa kuwa maono ni kwa ajili siku ambazo hazijatokea bado.
\v 15 Na alipokuwa akali akiniambia maneno haya, niligeuza uso wangu na kuuelekeza chini na sikuwa na uwezo wa kuzungumza.
\s5
\v 16 Yeye aliyekuwa kama wana wa mtu alinigusa mdomo wangu na nifumbua kinywa changu na nilimwambia huyo aliyekuwa amesimam mbele yangu: "Bwana wangu, niko katika masumbuko makali kwasababu ya maono; sina nguvu ndani yangu iliyosalia.
\v 17 Mimi ni mtumishi wako. Je ninawezaje kuongea na Bwana wangu? Kwa kuwa sasa sina nguvu, na hakuna pumzi iliyosalia ndani yangu."
\s5
\v 18 Tena yule mwenye mwonekano wa mtu alinigusa na kunitia nguvu.
\v 19 Alisema, "Usiogope, mtu ulithaminiwa sana. Amani na iwe kwako! Uwe mwenye nguvu, uwe na nguvu!" Na alipokuwa anaongea na mimi, nilipata nguvu. Nilimwambia, "Bwana wangu na aseme, kwa kuwa umenitia nguvu."
\s5
\v 20 Aliniambia, "Je unajua ni kwanini nimekuja kwako? Nitarudi hivi karibuni kupigana na mkuu wa Uajemi. Na nitakapoenda, mkuu wa Ugiriki atakuja.
\v 21 Lakini nitakwambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Ukweli. Hakuna yeyote anayejionesha kuwa na nguvu pamoja nami dhidi yao, isipokuwa Mikaeli mkuu wenu."
\s5
\c 11
\p
\v 1 Katika mwaka wa kwanza wa Dario Mmedi, mimi mwenyewe nilikuja kumwezesha na kumlinda Mikaeli.
\v 2 Na sasa nitakufunulia ukweli. Wafalme watatu watainuka katika Uajemi, na mfalme wa nne atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Na wakati atakapopata nguvu kupitia utajiri wake, atamwamsha kila mtu kinyume na ufalme wa Ugiriki.
\s5
\v 3 Mfalme wenye nguvu atainuka ambaye atatawala ufalme mkubwa, na ataenenda kufuatana na matakwa yake mwenyewe.
\v 4 Na atakapokuwa ameinuka, ufalme wake utavunjika na utagawanyika katika pepo nne za mbinguni, lakini hawatakuwa wazao wake mwenyewe, na si kwa nguvu zake kwa wakati alipokuwa akitawala. Kwa kuwa ufalme wake utang'olewa kwa ajili ya wengine tofauti na wazawa wake.
\s5
\v 5 Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja kati ya maamiri jeshi wake atakuwa mwenye nguvu kuliko yeye na atautawala ufalme wake kwa nguvu kubwa.
\v 6 Baada ya miaka michache, wakati muda utakapokuwa sawa, watafanya mwungano. Binti wa mfalme wa Kusini atakuja kwa mfalme wa Kaskazini kuyathibitisha makubaliano yao. Lakini hataweza kuzitunza nguvu za mkono wake, wala mfalme hatasimama wala mkono wake. Ataachwa na wale waliomleta, na baba yake, na yeye aliyemwunga mkono katika nyakati hizo.
\s5
\v 7 Lakini tawi kutoka katika mizizi yake litachipuka katika nafasi yake. Atalishambulia jeshi na kuingia ngome ya mfalme wa Kaskazini. Atapigana nao, na atawashinda.
\v 8 Ataichukua miungu yao mpaka Misri pamoa na sanamu zao za chuma na vyombo vyao vya fedha na vya dhahabu vyenye thamani. Kwa miaka mingi atakaa mbali na mfalme wa Kaskazini.
\v 9 Kisha mfalme wa Kaskazini atauvamia ufalme wa mfalme wa Kusini, lakini atajitoa na kwenda katika nchi yake mwenyewe.
\s5
\v 10 Wana wake watajiweka tayari na kuunganisha jeshi kubwa. Litaendelea kukua na litagharikisha kila kitu, litapita katikati hadi kwenye ngome yake.
\s5
\v 11 Ndipo mfalme wa Kusini atakasirika, na ataenda na kupigana naye, mfalme wa Kaskazini. Mfalme wa Kaskazini atainua jeshi kubwa, bali jeshi litatiwa katika mkono wake.
\v 12 Jeshi litachukuliwa, na moyo wa mfalme wa Kusini utainuliwa juu, na atawafanya makumi maelfu kuanguka, lakini hataweza kuwa mshindi.
\s5
\v 13 Kisha mfalme wa Kaskazini atainua jeshi jingine, kubwa kuliko la kwanza. Baada ya miaka kadhaa, mfalme wa Kaskazini atakuja na jeshi kubwa likiwa na vifaa vingi.
\s5
\v 14 Katika siku hizo wengi watainuka kinyume na mfalmea wa Kusini. Wana wa vurugu miongoni mwa watu wake watasimama wao wenyewe ili kuyatimiliza maono, lakini watajikwaa.
\s5
\v 15 Mfalme wa Kaskazini atakuja, kuizingira nchi kwa kuweka vilima, na kuuteka mji wenye ngome. Majeshi ya Kusini hayataweza kusimama, hata wanajeshi wake bora. Hawatakuwa na nguvu za kusimama.
\v 16 Badala yake, yeye ajaye ataenenda kwa kufuata tamaa zake kinyume chake; hakuna yeyote atakayesimama katika njia yake. Atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi wake.
\s5
\v 17 Mfalme wa Kaskazini atauelekeza uso wake ili kuja kwa nguvu za ufalme wake wote, na kutakuwa na makubaliano atakayoyafanya na mfalme wa Kusini. Atampatia katika ndoa binti wa wanawake ili kuuharibu ufalme wa Kusini. Lakini mpango huo hautafanikiwa wala kumsaidia.
\v 18 Baada ya hayo, mfalme atafuatilia nchi za pwani na ataziteka nchi nyingi. Lakini amiri jeshi atakikomesha kiburi chake na atakisababisha kiburi chake kiishe.
\v 19 Kisha atafuatilia miji yenye ngome katika nchi yake mwenyewe, lakini atajikwaa na kuanguka; na hatapatikana tena.
\s5
\v 20 Kisha mtu mwingine atainuka katika nafasi ambaye atamfanya mtoza ushuru apite kwa ajili ya ufahari wa ufalme. Lakini katika siku zijazo atakatiliwa mbali, lakini si kwa hasira wala si katika vita.
\v 21 Katika nafasi atainuka mtu wa kudharauliwa ambaye watu hawatampa heshima ya nguvu ya kifalme; atakuja bila kukusudiwa na atautwaa ufalme kwa ulaghai.
\v 22 Mbele yake, kila jeshi litafutiliwa mbali kama gharika. Jeshi na kiongozi wa agano wataangamizwa wote kwa pamoja.
\s5
\v 23 Tangu katika kipindi kile ambacho makubaliano yalifanywa pamoja naye, ataenenda kwa kwa hila; atakuwa mwenye nguvu akiwa na watu wachache tu.
\v 24 Kwa ghafla ataingia katika sehemu tajiri sana za jimbo, na atafanya kile ambacho si baba yake wala baba wa baba yake alishakifanya. Atagawanya mateka, nyara, na mali zake miongoni mwa wafuasi wake. Atapanga mpango wa kuiangusha ngome, lakini ni kwa muda tu.
\s5
\v 25 Ataamsha nguvu zake na moyo wake kinyume na mfalme wa Kusini kwa jeshi kubwa. Mfalme wa Kusini atapigana vita akiwa na jeshi kubwa lenye nguvu, lakini hataweza kusimama kwa kuwa wengine watafanya njama dhidi yake.
\v 26 Hata wale wanaokula chakula chake kizuri watajaribu kumwangamiza. Jeshi lake litakatiliwa mbali kama gharika, na wengi wao watauawa.
\v 27 Wafalme wote hawa wawili, wakiwa na mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake, watakaa katika meza moja na kudanganyana, lakini haitakuwa na maana yoyote. Kwa kuwa mwisho utatokea katika kipindi ambacho kimeshapangwa.
\s5
\v 28 Kisha mfalme wa Kaskazini atarudi katika nchi yake akiwa na utajiri mkubwa, na moyo wake ukipinga vikali agano takatifu. Atatenda na kisha atarudi katika nchi yake mwenyewe.
\s5
\v 29 Katika muda uloamriwa atarudi na kuushambulia ufalme wa Kusini. Lakini katika kipindi hiki hakitakuwa kama awali.
\v 30 Kwa kuwa meli kutoka Kitimu zitamshambulia, naye ataogopa na kurudi nyuma. Atakuwa mwenye hasira dhidi ya agano takatifu, na atawaonyesha mema wale watakaoliacha agano takatifu.
\s5
\v 31 Majeshi yake yatainuka na kukufuru sehemu takatifu katika ngome. Wataziondoa sadaka za kawaida za kuteketezwa, na watasimamisha chukizo la uharibifu litakalosababisha ukiwa.
\v 32 Na kwa wale walioenenda kwa ouvu kinyume na agano, atawadanganya na kuwatia uovu. Bali watu wale wanaomjua Mungu wao watakuwa jasiri na watachukua hatua.
\s5
\v 33 Watu wenye hekima miongobi mwa watu watawafanya watu waelewe. Lakini watajikwaa kwa upanga na kwa miali ya moto; watatiwa mateka na kunyang'anywa kwa siku.
\v 34 Katika siku za kujikwaa kwao, watasaidiwa kwa msaada kidogo. Watu wengi watajiunga nao wenyewe katika unafiki.
\v 35 Baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa ili kujisafisha kutokee kwao, na kujiosha, na kujitakasa, mpaka wakati wa mwisho. Kwa kuwa wakati ulioamriwa haujaja bado.
\s5
\v 36 Mfalme atafanya kutokana na matakwa yake. Atajiinua mwenyewe na kujifanya mkubwa kuliko kila mungu. Kinyume cha Mungu wa miungu, atasema vitu vibaya, kwa kuwa atafanikiwa mpaka pale ghadhabu itakapokuwa imekamilika. Kwa ajili kile kilichoamriwa kitakapokuwa kimefanyika.
\v 37 Hatazijali miungu ya baba zake wala mungu anayependwa na wanawake. Wala hatamjali mungu mwingine yeyote. Kwa kuwa zaidi ya mtu yeyote atajifanya mwenyewe kuwa mkuu.
\s5
\v 38 Atamheshimu mungu wa ngome badala ya haya. Ni mungu ambaye baba zake hawakumkubali ambaye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa mawe ya thamani na zawadi zenye kuthaminiwa.
\v 39 Atazishambulia ngome imara sana kwa msaada wa mungu mgeni. Atampa heshima kubwa yeyote anayemkubali. Atawafanya kuwa watawala juu ya watu wengi, na ataigawanya nchi kama thawabu.
\s5
\v 40 Kwa wakati wa mwisho mfalme wa Kusini atamshambulia. Mfalme wa Kaskazini atamvamia kwa ukali wa magari na wapanda farasi, na meli nyingi. Naye ataenda kinyume cha nchi, kuwagharikisha, na kupita katikati.
\v 41 Naye ataingia katika nchi ya uzuri, makumi elfu ya Waisraeli wataanguka. Lakini watu hawa watatoroka kutoka katika mkono wake: Waedomu, Wamoabu, na mabaki ya watu wa Amoni.
\s5
\v 42 Naye ataunyosha mkono katika nchi; nchi ya Misri haitaokolewa.
\v 43 Atakuwa na mamlaka juu ya hazina za dhahabu na za fedha, na juu ya utajiri wote wa Misri; watu wa Libya na Ethiopia watakuwa chini katika nyayo za miguu yake.
\s5
\v 44 Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamwogopesha, naye atatoka akiwa mwenye hasira nyingi kuwa ili kuwaharibu kabisa na kuwahifadhi kwa ajli ya uharibifu.
\v 45 Naye ataisimamisha hema ya makao yake ya kifalme kati ya bahari na milima ya uzuri wa utakatifu. Ataufikia mwisho wake, na hapatakuwa na msaidizi wa kumsadia.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Katika kipindi hicho, Mikaeli, jemedari mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwa na wakati wa mateso ambao haujawahi kutokea tangu mwanzo wa taifa lolote mpaka kipindi hicho. Katika muda huo watu wako wataokolewa, yeyote ambaye jina lake litapatikana katika kitabu.
\v 2 Na wengi wa wale waliolala katika mavumbi ya dunia watainuka. baadhi kwa uzima wa milele na baadhi kwa ajili ya fedheha na matwezo ya milele.
\s5
\v 3 Wale wenye hekima watang'ara kama mng'ao wa anga la juu, na wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki, watakuwa kama nyota milele na milele.
\v 4 Lakini wewe, Danieli, yafunge maneno haya; kihifadhi kitabu kikiwa kimetiwa chapa mpaka nyakati za mwisho. Watu wengi watakimbia huku na kule, na maarifa yataongezeka.
\s5
\v 5 Kisha mimi, Danieli, nilitazama, na kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama. Mmoja alisimama katika upande huu wa ukingo wa mto, na mwingine alisimama katika ukingo wa upande mwingine wa mto.
\v 6 Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani, yeye aliyekuwa juu ya mkondo wa mto, "Je itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza?"
\s5
\v 7 Nilimsikia mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu katika mkondo wa mto, aliinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni na kuapa kwa yeye aishiye milele kwamba itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati. Na wakati nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimeshaharibiwa, mambo haya yote yatakuwa yamemalizika.
\s5
\v 8 Nilisikia, lakini sikufahamu. Basi nikamwuliza, "Bwana wangu, mambo haya yote yatakuwa na matokeo gani?"
\v 9 Alisema, "Nenda zako Danieli, kwa kuwa maneno yamefungwa na kutiwa chapa mpaka wakati wa mwisho.
\s5
\v 10 Watu wengi watakuwa wametakaswa, wameoshwa, na kusafishwa, lakini waovu wataenenda katika uovu.
\v 11 Katika muda ule ambapo sadaka ya kawaida ya kuteketezwa itakapokuwa imeondolewa na chukizo la uharibifu liliosababisha ukiwa limesimamishwa, kutakuwa na siku zipatazo 1, 290.
\s5
\v 12 Ana heri mtu yule anayengojea mpaka mwisho wa siku 1, 335.
\v 13 Unapaswa uondoke uende njia yako hata mwisho, na kisha utapumzika. Utainuka katika sehemu uliyopewa, mwishoni mwa siku."

434
28-HOS.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,434 @@
\id HOS
\ide UTF-8
\h Hosea
\toc1 Hosea
\toc2 Hosea
\toc3 hos
\mt Hosea
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hili ni neno la Bwana lililofika kwa Hosea mwana wa Beeri siku za Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na katika siku za Yeroboamu mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli.
\v 2 Wakati Bwana alipozungumza kwanza kupitia Hosea, akamwambia, "Nenda ukajitwalie mke ambaye ni kahaba. Atakuwa na watoto ambao ni matokeo ya ukahaba wake. Kwa maana nchi inafanya uzinzi mkubwa kwa kumwacha Bwana."
\s5
\v 3 Basi Hosea akaenda akamwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba, akazaa mtoti mwanamume.
\v 4 Bwana akamwambia Hosea, Mwite jina lake Yezreeli. Kwa maana kwa muda mfupi nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa sababu ya kumwaga damu huko Yezreeli; nami nitamaliza ufalme wa nyumba ya Israeli.
\v 5 Itatokea siku ile nitakapovunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli.
\s5
\v 6 Gomeri akachukua mimba tena akamzaa binti. Ndipo Bwana akamwambia Hosea, "Mwite jina lake Lo Ruhama; kwa maana sitawahurumia tena nyumba ya Israeli, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.
\v 7 Hata hivyo nitawahurumia nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa mwenyewe, Bwana, Mungu wao. Sitawaokoa kwa upinde, upanga, vita, farasi, au wapanda farasi. '
\s5
\v 8 Baada ya Gomeri kumwachisha Lo Ruhama, alipata mimba na kuzaa mtoto mwingine mwanamume.
\v 9 Ndipo Bwana akasema, "Mwite jina la Lo Ami; kwa kuwa ninyi si watu wangu, wala mimi si Mungu wenu."
\s5
\v 10 Hata hivyo idadi ya watu wa Israeli itakuwa kama mchanga wa bahari, ambayo haiwezi kupimwa au kuhesabiwa. Itakuwa pale ambapo waliambiwa, "Ninyi si watu wangu," wataambiwa, "Ninyi ni watu wa Mungu aliye hai."
\v 11 Watu wa Yuda na watu wa Israeli watakusanyika pamoja. Wao wataweka kiongozi mmoja wao wenyewe, na watatoka kutoka nchi, kwa maana itakuwa siku ya Yezreeli kuu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Waambie ndugu zenu wanaume, 'Watu wangu!' na kwa dada zako, 'umeonyeshwa huruma.'"
\s5
\v 2 Leteni mashtaka dhidi ya mama yenu, leteni mashtaka, kwa kuwa yeye si mke wangu, wala mimi si mumewe. Na auondoe uzinzi wake mbele yake, na matendo yake ya uzinzi kati ya matiti yake.
\v 3 Ikiwa sio, nitamvua nguo na kumuonyesha uchi wake kama siku aliyozaliwa. Nami nitamfanya kama jangwa, kama nchi iliyoharibika, nami nitamfanya afe kutokana na kiu.
\s5
\v 4 Sitakuwa na rehema kwa watoto wake, kwa maana wao ni watoto wa ukahaba.
\v 5 Maana mama yao amekuwa kahaba, na yeye aliye mimba amefanya mambo ya aibu. Alisema, "Nitawafuata wapenzi wangu, kwa maana wananipa mkate wangu na maji, sufu yangu na kitani, mafuta yangu na kinyweji."
\s5
\v 6 Kwa hiyo nitajenga ua wa kuzuia njia yake kwa miiba. Nitajenga ukuta dhidi yake ili asiweze kupata njia. Yeye atawafuatilia wapenzi wake, lakini yeye hatawafikia.
\v 7 Yeye atawatafuta, lakini hatawapata. Kisha atasema, "Nitarejea kwa mume wangu wa kwanza, kwa maana ilikuwa ni bora kwangu zamani kuliko sasa."
\s5
\v 8 Kwa maana hakujua kwamba mimi ndimi niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta, na ambaye nilimwongezea fedha na dhahabu, ambazo walizitumia kwa Baali.
\v 9 Kwa hiyo nitachukua nafaka yake wakati wa mavuno, na divai yangu mpya katika msimu wake. Nitachukua sufu yangu na kitambaa kilichotumiwa kufunika uchi wake.
\s5
\v 10 Ndipo nitamvua nguo machoni pa wapenzi wake, wala hakuna mtu atakayemwokoa mkononi mwangu.
\v 11 Nitasitisha furaha yake yote- sikukuu zake, mwandamo wa mwezi, sabato zake na sikukuu zake zote zilizowekwa.
\s5
\v 12 Nitaharibu mizabibu yake na mtini wake, ambayo alisema, 'Hii ni mishahara ambayo wapenzi wangu walinipa.' Nitawafanya kuwa msitu, na wanyama wa shambani watakula.
\v 13 Nami nitamuadhibu kwa ajili ya Sikukuu ya Baali, alipowafukizia uvumba, akijipamba kwa pete zake na mavazi yake, naye akafuata wapenzi wake, akanisahau." Hili ndilo tamko la Bwana.
\s5
\v 14 Kwa hiyo nitaenda kumshawishi. Nitamleta jangwani na kumwambia kwa huruma.
\v 15 Nami nitamrudishia mizabibu yake, na bonde la Akori kama mlango wa tumaini. Yeye atanijibu huko kama alivyofanya katika siku za ujana wake, kama katika siku ambazo alitoka katika nchi ya Misri.
\s5
\v 16 "Itakuwa katika siku hiyo"-hili ndilo tamko la Bwana-"kwamba utaniita, 'Mume wangu,' na hutaniita tena mimi, 'Baal wangu.'
\v 17 Kwa maana nitaondoa majina ya Baali kinywani mwake; majina yao hayatakumbukwa tena."
\s5
\v 18 "Siku hiyo nitafanya agano pamoja na wanyama katika mashamba kwa ajili yao, na ndege wa angani, na vitu vya kutambaa chini. Nitaondoa upinde, upanga, na vita katika nchi, nami nitakufanya ulale kwa usalama.
\s5
\v 19 Nitakuwa mume wako milele. Nitakuwa mume wako katika haki, hukumu, uaminifu wa agano, na huruma.
\v 20 Nitakuwa mume wako kwa uaminifu. Nawe utanijua mimi, Bwana.
\s5
\v 21 Na siku ile, nitajibu"-hili ndilo tamko la Bwana. "Nitazijibu mbingu, nao watajibu dunia.
\v 22 Dunia itashughulikia nafaka, divai mpya na mafuta, na watajibu Yezreeli.
\s5
\v 23 Nitatampanda mwenyewe katika nchi kwa ajili yangu, na nitamhurumia Lo Ruhama. Nami nitamwambia Lo Ami, 'Wewe ni Ami Ata,' nao wataniambia, 'Wewe ni Mungu wangu.'"
\s5
\c 3
\p
\v 1 Bwana akaniambia, "Nenda tena, mpendeni mwanamke, aliyependwa na mumewe; lakini ni mzinzi. Mpende kama mimi, Bwana, ninavyowapenda watu wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine na kupenda mikate ya zabibu."
\v 2 Kwa hiyo nimemnunulia mwenyewe kwa vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri.
\v 3 Nilimwambia, "Lazima uishi pamoja nami siku nyingi. Huwezi kuwa kahaba au kuwa na mtu mwingine yeyote. Kwa njia hiyo hiyo, nitakuwa pamoja nanyi."
\s5
\v 4 Kwa maana wana wa Israeli wataishi kwa siku nyingi bila mfalme, mtu mkuu, dhabihu, nguzo ya mawe, efodi au sanamu za nyumbani.
\v 5 Baadaye watu wa Israeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Na katika siku za mwisho, watakuja wakitetemeka mbele za Bwana na wema wake.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Sikilizeni neno la Bwana, enyi watu wa Israeli. Bwana ana mashtaka dhidi ya wenyeji wa nchi, kwa sababu hakuna ukweli au uaminifu wa agano, hakuna ujuzi wa Mungu katika nchi.
\v 2 Kuna laana, uongo, mauaji, wizi na uzinzi. Watu wamevunja mipaka yote, na damu inakuja baada ya damu.
\s5
\v 3 Kwa hiyo nchi inakauka, na kila mtu aliyeishi ndani yake anaangamia; wanyama katika mashamba na ndege angani, hata samaki katika bahari, wanaondolewa.
\s5
\v 4 Lakini usiruhusu mtu yeyote kuleta mashtaka; msiruhusu mtu yeyote ahukumu mtu mwingine. Kwa maana ninyi ndio makuhani, ninaowashtaki.
\v 5 Ninyi makuhani mtajikwaa wakati wa mchana; manabii pia watajikwaa pamoja nanyi usiku, nami nitamwangamiza mama yako.
\s5
\v 6 Watu wangu wanaharibiwa kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Kwa sababu makuhani wamekataa maarifa, nami nitawakataa msiwe makuhani kwangu. Kwa sababu umesahau sheria yangu, ingawa mimi ni Mungu wako, nami pia nitasahau watoto wako.
\v 7 Makuhani wengi waliongezeka, zaidi walifanya dhambi dhidi yangu. Walibadilisha heshima zao kwa aibu.
\s5
\v 8 Wanajilisha dhambi ya watu wangu; wao ni wenye tamaa zaidi ya uovu wao.
\v 9 Itakuwa sawa kwa watu kama kwa makuhani: nitawaadhibu wote kwa matendo yao; Nitawalipa kwa matendo yao.
\s5
\v 10 Watakula lakini hawatashiba; watafanya uzinzi lakini hawataongezeka, kwa sababu wamekwenda mbali na Bwana.
\s5
\v 11 Wanapenda uasherati, divai, na divai mpya, ambayo imechukua uelewa wao.
\v 12 Watu wangu hutaka shauri kwa sanamu zao za mbao, na fimbo zao za kutembelea huwapa unabii. Kwa maana mawazo ya uasherati yamewadanganya, na wamefanya kama makahaba badala ya kuwa mwaminifu kwa Mungu wao.
\s5
\v 13 Wanatoa sadaka juu ya milima na kuteketeza uvumba kwenye milima, chini ya mialoni, milibua na miela, kwa sababu kivuli ni nzuri. Basi binti zenu hufanya uasherati, na binti zenu wanazini.
\v 14 Mimi siwaadhibu binti zako wakati wanachagua kutenda uasherati, wala binti zako wakati wazini. Kwa maana wanaume pia wanajitoa kwa makahaba, na hutoa dhabihu ili waweze kufanya vitendo vya uasherati na makahaba. Hivyo watu wasiofahamu wataangamizwa.
\s5
\v 15 Ingawa wewe, Israeli, umefanya uzinzi, lakini Yuda asiwe na hatia. Ninyi msiende Gilgali; msiende hadi Beth Aven. Wala msiape, "Aishivyo Bwana."
\v 16 Kwa maana Israeli amefanya ukaidi, kama ndama mkaidi. Je! Bwana anaweza kuwaleta kwenye malisho kama kondoo mahali penye nafasi?
\s5
\v 17 Efraimu alijiunga na sanamu; mwache peke yake.
\v 18 Hata wakati kileo chao kimeondoka wakaendelea kufanya uzinzi; watawala wake hupenda sana aibu yao.
\v 19 Upepo utamfunga kwa mabawa yake; nao wataona aibu kwa sababu ya dhabihu zao.
\s5
\c 5
\p
\v 1 Sikilizeni haya, makuhani! kuweni makini, nyumba ya Israeli! Sikilizeni, nyumba ya mfalme! Kwa maana hukumu itakuja juu yenu nyote. Mmekuwa mtego huko Mizpa na wavu uliosambazwa juu ya Tabori.
\v 2 Waasi husimama sana katika mauaji, lakini nitawaadhibu wote.
\s5
\v 3 Najua Efraimu, na Israeli hajajificha kwangu. Efraimu, sasa umekuwa kama kahaba; Israeli ni unajisi.
\v 4 Matendo yao hayawataruhusu kumgeukia Mungu, maana mawazo ya uzinzi yako ndani yao, na hawatamjua Bwana.
\s5
\v 5 Kiburi cha Israeli kinawashuhudia; Kwa hiyo Israeli na Efraimu watajikwaa kwa hatia zao; na Yuda pia wataanguka pamoja nao.
\v 6 Watakwenda pamoja na kondoo zao na ng'ombe zao kumtafuta Bwana, lakini hawatamuona, kwa kuwa amejiondoa kutoka kwao.
\v 7 Walikuwa wasio waaminifu kwa Bwana, kwa kuwa wamezaa watoto haramu. Sasa sherehe mpya za mwezi zitawaangamiza na mashamba yao.
\s5
\v 8 Piga tarumbeta huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Sauti ya kilio cha vita huko Beth Aveni 'Tutakufuata, Benyamini!'
\v 9 Efraimu itakuwa ukiwa siku ya adhabu. Miongoni mwa makabila ya Israeli nimetangaza habari itakayotokea.
\s5
\v 10 Viongozi wa Yuda ni kama wale wanaondoao jiwe la mipaka. Nami nitamwaga ghadhabu yangu juu yao kama maji.
\v 11 Efraimu ameangamizwa; ameangamizwa kwa hukumu, kwa sababu ametembea kwa hiari kufuata sanamu.
\s5
\v 12 Kwa hiyo nitakuwa kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa nyumba ya Yuda.
\v 13 Efraimu alipoona ugonjwa wake, Yuda akaona jeraha lake; Efraimu akaenda Ashuru; Yuda akatuma wajumbe kwa mfalme mkuu. Lakini hakuweza kuwaponya watu au kuponya jeraha lako.
\s5
\v 14 Kwa hiyo nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama simba kwa nyumba ya Yuda. Mimi, naam mimi, nitapotea na kwenda mbali; Nitawachukua, na hakutakuwa na mtu wa kuwaokoa.
\v 15 Nitakwenda na kurudi mahali pangu, mpaka watambue hatia yao na kutafuta uso wangu, hata wakanitafute kwa bidii katika dhiki yao.
\s5
\c 6
\p
\v 1 "Njoo, turudi kwa Bwana. Kwa maana ametuvunja vipande vipande, lakini atatuponya; ametujeruhi, lakini atatufunga majeraha yetu.
\v 2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, na tutaishi mbele yake.
\v 3 Nasi tumjue Bwana; tukaendelee kumjua Bwana. Kuja kwake ni hakika kama asubuhi; atakuja kwetu kama mvua, kama mvua ya vuli ambayo huinyeshea ardhi."
\s5
\v 4 Efuraimu, nikufanyie nini? Yuda, nikufanyie nini? Uaminifu wako ni kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
\v 5 Kwa hiyo nimewavunja vipande vipande kwa vinywa vya manabii, nimewaua kwa maneno ya kinywa changu. Maagizo yako ni kama nuru inayoangaza.
\s5
\v 6 Kwa maana natamani uaminifu wala si dhabihu, na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
\v 7 Kama Adamu wamevunja agano; hawakuwa waaminifu kwangu.
\s5
\v 8 Gileadi ni jiji la wahalifu wenye miguu ya damu.
\v 9 Kama makundi ya wanyang'anyi wanaomngojea mtu, hivyo makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu; wamefanya uhalifu wa aibu.
\s5
\v 10 Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo baya; Uzinzi wa Efraimu ukopale, na Israeli ametiwa unajisi.
\v 11 Kwa maana wewe, Yuda, mavuno yameteuliwa, nitakaporudisha urithi wa watu wangu.
\s5
\c 7
\p
\v 1 Wakati wowote ninapotaka kuponya Israeli, dhambi ya Efraimu inafunuliwa, pamoja na matendo maovu ya Samaria, kwa sababu wanafanya udanganyifu; mwizi huingia, na kundi la wanyang'anyi hushambulia mitaani.
\v 2 Hawatambui mioyoni mwao kwamba ninakumbuka matendo yao mabaya. Sasa matendo yao huwazunguka; yapo mbele ya uso wangu.
\s5
\v 3 Kwa sababu ya uovu wao wamemfanya mfalme awe na furaha, na maofisa wao kwa uongo wao.
\v 4 Wote ni wazinzi, kama tanuru iliyochomwa na mwokaji, ambaye huacha kuuchochea moto tangu kukanda unga mpaka kuwa chachu.
\v 5 Siku ya mfalme wetu, viongozi walijifanya wagonjwa na ukali wa divai. Alinyoosha mkono wake kwa wale waliokuwa wakidhihaki.
\s5
\v 6 kwa mioyo kama tanuri, wao hupanga mipango yao ya udanganyifu. Hasira zao hulala usiku wote; asubuhi huwaka juu kama moto.
\v 7 Wote wamepata moto kama tanuru, na huwaangamiza wale wanaowatawala. Wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao ananiita.
\s5
\v 8 Efraimu anajichanganya mwenyewe kati ya watu. Efraimu ni mkate ambayo haujawahi kugeuzwa.
\v 9 Wageni wamekula nguvu zake, lakini hajui. Nywele za mvi hunyunyiza juu yake, lakini hajui.
\s5
\v 10 Kiburi cha Israeli kinawashuhudia; hata hivyo, hawajarudi kwa Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta licha ya hayo yote.
\v 11 Efraimu ni kama njiwa, baradhuli na asiye na busara, humwita kwenda Misri, kisha huruka kwenda Ashuru.
\s5
\v 12 Wakienda, nitasambaza wavu wangu juu yao, nami nitawaangusha kama ndege wa angani. Nitawaadhibu katika kusonga kwao pamoja.
\v 13 Ole wao! Kwa maana wamepotea kutoka kwangu. Uharibifu unawajia! Wao wameasi dhidi yangu! Napenda kuwaokoa, lakini waliongea uongo dhidi yangu.
\s5
\v 14 Wala hawakunililia kwa moyo wao wote, lakini wanaomboleza kwenye vitanda vyao. Wanakusanyika kwa ajili ya nafaka na divai mpya, nao wananiasi mimi.
\v 15 Ingawa niliwafundisha na kuimarisha mikono yao, sasa wanapanga mabaya dhidi yangu.
\s5
\v 16 Wanarudi, lakini harudi kwangu, Niliye Juu. Wao ni kama upinde usiotumainika. Maofisa wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya udhalimu wa vinywa. Hii itakuwa ni aibu yao katika nchi ya Misri.
\s5
\c 8
\p
\v 1 "Weka tarumbeta katika midomo yako! Tai anakuja juu ya nyumba ya Bwana kwa sababu watu wamevunja agano langu na waliasi dhidi ya sheria yangu.
\v 2 Wananililia,'Mungu wangu, sisi katika Israeli tunakujua.'
\v 3 Lakini Israeli amekataa mema, na adui atamfuata.
\s5
\v 4 Wameweka wafalme, lakini sio kwa shauri langu. Wamewafanya wakuu, lakini sikuwa na habari. Kwa fedha zao na dhahabu wamejifanyia sanamu wenyewe, ili wakatiliwe mbali."
\v 5 "Ndama yako imekataliwa, Samaria. Hasira yangu inawaka juu ya watu hawa. Kwa muda gani watakuwa na hatia?
\s5
\v 6 Kwa maana sanamu hii ilitoka Israeli; fundi aliifanya; si Mungu! Ndama ya Samaria itavunjwa vipande vipande.
\v 7 Kwa maana watu hupanda upepo na kuvuna kimbunga. Mbegu zilizosimama hazina vichwa; haitoi unga. Ikiwa itakomaa, wageni watakula.
\s5
\v 8 Israeli imemezwa; sasa wanalala kati ya mataifa kama kitu kisicho na maana.
\v 9 Kwa maana walikwenda Ashuru kama punda wa mwitu pekee. Efraimu ameajiri wapenzi kwa ajili yake mwenyewe.
\v 10 Hata ingawa wameajiri wapenzi kati ya mataifa, sasa nitawakusanya pamoja. Wao wataanza kupotea kwa sababu ya unyanyasaji wa mfalme wa wakuu.
\s5
\v 11 Kwa maana Efraimu imeongeza madhabahu kwa sadaka za dhambi, lakini zimekuwa madhabahu kwa kufanya dhambi.
\v 12 Niliweza kuandika sheria yangu kwao mara elfu kumi, lakini wangeiona kama kitu cha ajabu kwao.
\s5
\v 13 Kwa ajili ya dhabihu za sadaka zangu, hutoa nyama na kuila, lakini mimi, Bwana, siwakubali. Sasa nitafikiri juu ya uovu wao na kuadhibu dhambi zao. Watarudi Misri.
\v 14 Israeli amenisahau mimi, Muumba wake, na amejenga majumba. Yuda ameimarisha miji mingi, lakini nitatuma moto juu ya miji yake; itaharibu ngome zake.
\s5
\c 9
\p
\v 1 Usifurahi, Israeli, kwa furaha kama watu wengine. Kwa maana haukuwa mwaminifu, umemuacha Mungu wako. Unapenda kulipa mshahara kwa kahaba kwenye sakafu zote za nafaka.
\v 2 Lakini sakafu na divai hazitawalisha; divai mpya itampungukia.
\s5
\v 3 Hawawezi kuendelea kuishi katika nchi ya Bwana; badala yake, Efraimu atarudi Misri, na siku moja watakula chakula kichafu katika Ashuru.
\v 4 Hawatamtolea Bwana sadaka za divai, wala hawatamfurahisha. Dhabihu zao zitakuwa kwao kama chakula cha matanga wote wanaolila watakuwa wamejisikia. Maana chakula chao kitakuwa chao pekee; hautakuingia nyumbani mwa Bwana.
\s5
\v 5 Utafanya nini siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi, siku ya sikukuu ya Yahweh?
\v 6 Kwa maana, angalia, wamekimbia uharibifu, Misri itawakusanya, na Nofu itawazika. Maana hazina zao za pesa za fedha zitakuwa nao, na miiba itajaza hema zao.
\s5
\v 7 Siku za adhabu zinakuja; siku za kulipiza kisasi zinakuja. Waisraeli wote wajue mambo haya. Nabii ni mpumbavu, na mtu aliyevuviwa ni mwendawazimu, kwa sababu ya uovu wako mkubwa na uadui mkubwa.
\s5
\v 8 Nabii ndiye mlinzi wa Mungu wangu juu ya Efraimu. Lakini mtego wa ndege ni juu ya njia zake zote, na uadui umo katika nyumba ya Mungu wake.
\v 9 Wamejiharibu wenyewe kama siku za Gibea. Mungu atawakumbusha uovu wao, naye atawaadhibu dhambi zao.
\s5
\v 10 Bwana asema, "Nilipoikuta Israeli, ilikuwa kama kutafuta zabibu jangwani. Kama matunda ya kwanza ya msimu kwenye mtini, nimewaona baba zenu. Lakini wakaenda Baal Peori, nao wakajitoa kwenye sanamu ya aibu. Walikuwa chukizo kama sanamu waliyoipenda.
\s5
\v 11 Na kwa ajili ya Efraimu, utukufu wao utatoka kama ndege. Hakutakuwa na kuzaa, hakuna mimba, wala achukuaye mimba.
\v 12 Ingawa wameleta watoto, nitawachukua ili asibaki hata mmoja. Ole wao nikiwaacha!
\s5
\v 13 Nimeiona Efraimu, kama vile Tiro, alipandwa katika mlima, lakini Efraimu atatoa watoto wake kwa mtu atakayewaua.
\v 14 Wape, Bwana-utawapa nini? Wape tumbo lenye kuharibu mimba na matiti ambayo haitoi maziwa.
\s5
\v 15 'Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali, ndivyo nilipowachukia. Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi, nitawafukuza nje ya nyumba yangu. Sitawapenda tena; maofisa wao wote ni waasi.
\s5
\v 16 Efraimu ni mgonjwa, na mizizi yao imekauka; hawazai matunda. Hata ikiwa wana watoto, nitawaua watoto wao wapendwa.
\v 17 Mungu wangu atawakataa kwa sababu hawakumtii. Watakuwa watu wa kutangatanga kati ya mataifa.
\s5
\c 10
\p
\v 1 Israeli ni mzabibu mzuri ambao huzaa matunda yake. kwa kadiri matunda yake yanavyoongezeka vivyo hivyo anajenga madhabahu nyingi. Kwa kuwa nchi yake ilizalishwa zaidi, aliboresha nguzo zake.
\v 2 Moyo wao ni udanganyifu; sasa wanapaswa kubeba hatia yao. Bwana ataharibu madhabahu zao; ataharibu nguzo zao.
\s5
\v 3 Kwa maana watasema, "Hatuna mfalme, kwa maana hatukumcha Bwana. Na mfalme-angeweza kutufanyia nini?"
\v 4 Wanasema maneno tupu na kufanya maagano kwa kuapa uongo. Kwa hivyo haki inakuja kama magugu yenye sumu katika mito ya shamba.
\s5
\v 5 Wakazi wa Samaria wataogopa kwa sababu ya ndama za Beth Aveni. Watu wake waliomboleza juu yao, kama walivyofanya wale makuhani wa sanamu ambao walikuwa wamefurahi juu yao na utukufu wao, lakini hawako tena.
\v 6 Wao watachukuliwa kwenda Ashuru kama sadaka kwa mfalme mkuu. Efraimu atakuwa na aibu, na Israeli atakuwa na aibu kwa sanamu yake.
\s5
\v 7 Mfalme wa Samaria ataangamizwa, kama chipu cha kuni juu ya uso wa maji.
\v 8 Sehemu za juu za uovu zitaharibiwa. Hii ndiyo dhambi ya Israeli! Miti na vichaka vitakua juu ya madhabahu zao. Watu wataiambia milima, "Tufunike sisi!" na kwa vilima, "Tuangukieni!"
\s5
\v 9 Ee Israeli, umetenda dhambi tangu siku za Gibea; huko umebaki. Je, vita vitawapata wana wa uovu huko Gibea?
\s5
\v 10 Nitakapotaka, nitawaadhibu. Mataifa wataungana pamoja nao na kuwaweka katika vifungo kwa uovu wao mara mbili.
\v 11 Efraimu ni ndama mwenye mafunzo ambayo anapenda kupura nafaka, hivyo nitaweka jozi juu ya shingo yake nzuri. Efraimu nitauweka jozi; Yuda ataimea; Yakobo atauvuta pigo kwa nafsi yake.
\s5
\v 12 Jifanyieni haki, vuneni matunda ya uaminifu wa agano. Chimbueni ardhi yenu isiyopandwa, kwa maana ni wakati wa kumtafuta Bwana, mpaka atakapokuja na kuinua haki juu yenu.
\v 13 Mmelima uovu; mmevuna udhalimu. Mmekula matunda ya udanganyifu kwa sababu uliamini katika mipango yako na katika askari wako wengi.
\s5
\v 14 Kwa hiyo mlipuko wa vita utafufuka kati ya watu wako, na miji yako yote yenye ngome itaharibiwa. Itakuwa kama Shalmani aliharibu Beth Arbeli siku ya vita, wakati mama alivunjika vipande vipande na watoto wake.
\v 15 Kwa hiyo itakuwa kwako, Betheli, kwa sababu ya uovu wako mkubwa. Wakati wa mchana mfalme wa Israeli atakatwa kabisa.
\s5
\c 11
\p
\v 1 "Wakati Israeli alikuwa kijana nilimpenda, na nikamwita mtoto wangu kutoka Misri.
\v 2 Kwa kadiri waliyoitwa, ndivyo walivyoondoka kwangu. Wakawafanyia dhabihu Baali, wakatafuta uvumba kwa sanamu.
\s5
\v 3 Lakini mimi ndio niliyemfundisha Efraimu kutembea. Ndiye niliyewainua kwa silaha zao, lakini hawakujua kwamba niliwajali.
\v 4 Niliwaongoza kwa kamba za ubinadamu, na mafungo ya upendo. Mimi nilikuwa kama mtu aliyepunguza jozi juu ya taya zao, na nikainama na kuwalisha.
\s5
\v 5 Je, hawatarudi nchi ya Misri? Je, Ashuru haitatawala juu yao kwa sababu wanakataa kurudi kwangu?
\v 6 Upanga utaanguka juu ya miji yao na kuharibu makomeo ya milango yao; itawaangamiza kwa sababu ya mipango yao wenyewe.
\v 7 Watu wangu wameamua kuniacha. Ingawa wanaita kwa Aliye Juu, hakuna mtu atawasaidia.
\s5
\v 8 Ninawezaje kukuacha, Efraimu? Ninawezaje kukupeleka, Israeli? Ninawezaje kukufanya kama Adma? Ninawezaje kukufanya kama Seboimu? Moyo wangu umebadilika ndani yangu; huruma zangu zote zimeongezeka.
\v 9 Sitafanya hasira yangu kali; Mimi sitawaangamiza Efraimu tena. Kwa maana mimi ni Mungu, wala si mtu; Mimi ni Mtakatifu kati yenu, nami sitakuja katika ghadhabu.
\s5
\v 10 Watanifuata, Bwana. Nitanguruma kama simba. Nami nitaomboleza, na watu watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
\v 11 Watakuja wakitetemeka kama ndege kutoka Misri, kama njiwa kutoka nchi ya Ashuru. Nitawafanya wapate kuishi katika nyumba zao." Hii ndiyo tamko la Bwana.
\s5
\v 12 Efraimu ananizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu. Lakini Yuda bado anaendelea nami, Mungu, na ni mwaminifu kwangu, Mtakatifu.
\s5
\c 12
\p
\v 1 Efraimu hujilisha upepo na kufuata upepo wa mashariki. Yeye daima huzidisha uongo na unyanyasaji. Wanafanya agano na Ashuru na huchukua mafuta ya Misri.
\v 2 Bwana pia ana mashtaka dhidi ya Yuda na ataadhibu Yakobo kwa yale aliyoyatenda; atamlipa kwa matendo yake.
\s5
\v 3 Katika tumbo Yakobo akamshika ndugu yake kisigino, na katika ubinadamu wake alijitahidi kwa Mungu.
\v 4 Alishindana na malaika akashinda. Alilia na kuomba kwa neema yake. Alikutana na Mungu huko Betheli; huko Mungu aliongea naye.
\s5
\v 5 Huyu ndiye Bwana, Mungu wa majeshi; "Yahweh" ndilo jina lake.
\v 6 Basi tembea kwa Mungu wako. Shika uaminifu na uhuru wa agano, na umsubiri Mungu wako daima.
\s5
\v 7 Wafanyabiashara wana mizani ya uongo mikononi mwao; wanapenda kudanganya.
\v 8 Efraimu akasema, "Kwa hakika mimi ni tajiri sana; Nimepata utajiri kwa nafsi yangu. Katika kazi yangu yote hawataona uovu wowote ndani yangu, chochote ambacho kitakuwa dhambi."
\s5
\v 9 Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, tangu ulipotoka nchi ya Misri. Nitakufanya uishi tena katika hema, kama siku za karamu iliyowekwa.
\v 10 Niliwaambia manabii, na nimewapa maono mengi kwa ajili yenu. Kwa mkono wa manabii nilitoa mifano.
\s5
\v 11 Ikiwa kuna uovu huko Gileadi, hakika watu hawafai. Gilgali wanachinja ng'ombe; madhabahu zao zitakuwa kama miundo ya jiwe katika miamba ya mashamba.
\v 12 Yakobo akakimbia mpaka nchi ya Aramu; Israeli alifanya kazi ili kupata mke; naye akachunga kundi la kondoo ili kupata mke.
\s5
\v 13 Bwana akawaleta Israeli kutoka Misri kwa kutumia nabii, naye akawatunza kwa nabii.
\v 14 Efraimu amemkasirisha sana Bwana. Basi Bwana wake ataachia damu yake, naye atamrudishia aibu yake.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Efraimu alipozungumza, kulikuwa na tetemeko. Alijikuza katika Israeli, lakini akawa na hatia kwa sababu ya ibada ya Baali, naye akafa.
\v 2 Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi. Wanatengeneza sanamu za chuma kutoka kwenye fedha zao, sanamu kwa kadiri ya ufanisi wao, zote ni kazi ya mafundi. Watu wanasema juu yao, 'Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama.'
\s5
\v 3 Kwa hiyo watakuwa kama mawingu ya asubuhi, kama umande unaoondoka mapema, kama makapi yanayotokana na upepo kutoka kwenye sakafu, na kama moshi utokao kwenye bomba.
\s5
\v 4 Lakini mimi ndimi Bwana, Mungu weko, tangu nchi ya Misri. Hutamjua Mungu mwingine bali mimi; wala zaidi yangu, hakuna mkombozi mwingine.
\v 5 Nilikujua jangwani, katika nchi yenye kame.
\v 6 Wakati ulipokuwa na malisho, ulishiba; na wakati uliposhiba, moyo wako ukainuliwa. Kwa sababu hiyo umenisahau.
\s5
\v 7 Nitakuwa kama simba; kama chui nitaangalia kando ya njia.
\v 8 Nitawaangamiza kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nami nitararua vifua vyao, na huko nitawaangamiza kama simba, kama vile mnyama wa mwitu atakayerarua vipande vipande.
\s5
\v 9 Nitawaangamiza, Israeli; nani atakayekusaidia?
\v 10 Mfalme wako yuko wapi, ili akuokoe katika miji yako yote? Wako wapi wakuu, ambao kwao umeniambia hivi, 'Nipe mfalme na wakuu'?
\v 11 Nimekupa mfalme kwa hasira yangu, nikamchukua kwa ghadhabu yangu.
\s5
\v 12 Uovu wa Efraimu umehifadhiwa; hatia yake imehifadhiwa.
\v 13 Atakuwa na uchungu wa kujifungua, lakini ni mwana mjinga, kwa maana wakati wa kuzaliwa, hatatoka tumboni.
\s5
\v 14 Je, nitawaokoa na mkono wa kaburi? Je, nitawaokoa na kifo? Ewe Mauti yako wapi mapigo yako? Ewe kaburi kuko wapi kuharibu kwako? Huruma itafichwa na macho yangu.
\s5
\v 15 Ingawa Efraimu anafanikiwa kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja; upepo wa Bwana utapiga kutoka jangwani. Kijito cha maji cha Efraimu kitauka, na kisima chake hakitakuwa na maji. Adui yake atapora ghala lake la kila kitu cha thamani.
\s5
\v 16 Samaria itakuwa na hatia, kwa sababu amemuasi dhidi ya Mungu wake. Wataanguka kwa upanga; watoto wao wadogo watavunjwa, na wanawake wao wajawazito watatambuliwa wazi.
\s5
\c 14
\p
\v 1 Israeli, rudi kwa Bwana, Mungu wako, kwa kuwa umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
\v 2 Chukueni maneno pamoja nanyi na mrudieni Yahweh. Mwambieni, "Ondoa uovu wetu wote, uyakubali mema, ili tuweze kukupa matunda ya midomo yetu.
\s5
\v 3 Ashuru haitatuokoa; hatutapanda farasi kwenda vitani. Hatuwezi tena kuiambia kazi ya mikono yetu, 'ninyi ni miungu yetu,' kwa maana kwako mtu asiye na baba hupata huruma."
\s5
\v 4 'Nitawaponya kugeuka kwao; Nami nitawapenda kwa moyo, kwa maana hasira yangu itaondoka kwake.
\v 5 Nitakuwa kama umande kwa Israeli; atachanua kama maua na kuchukua mizizi kama mwerezi nchini Lebanoni.
\v 6 Matawi yake yataenea; Uzuri wake utakuwa kama mizeituni, na harufu yake kama mierezi ya Lebanoni.
\s5
\v 7 Watu wanaoishi katika kivuli chake watarejea; watafufuliwa kama nafaka na maua kama mizabibu. Utukufu wake utakuwa kama divai ya Lebanoni.
\v 8 Efraimu, nifanye nini tena na sanamu? Mimi nitamjibu na kumtunza. Mimi ni kama mberoshi majani yake ni ya kijani daima; kutoka kwangu huja matunda yako."
\s5
\v 9 Nani mwenye busara ili aelewe mambo haya? Nani anaelewa mambo haya ili awatambue? Kwa kuwa njia za Bwana ni sawa, na wenye haki watatembea ndani yao, lakini waasi wataanguka ndani yake.

158
29-JOL.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,158 @@
\id JOL
\ide UTF-8
\h Joeli
\toc1 Joeli
\toc2 Joeli
\toc3 jol
\mt Joeli
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hili ni neno la Bwana lililomjia Yoeli mwana wa Pethueli.
\v 2 Sikieni haya, ninyi wazee, na sikieni, ninyi wenyeji wa nchi. Je! Hii imewahi kuwa kabla ya siku zenu au katika siku za baba zenu?
\v 3 Waambie watoto wako kuhusu hilo, na waache watoto wako kuwaambie watoto wao, na watoto wao kizazi kijacho.
\s5
\v 4 Yale yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige wakubwa; yale yaliyosazwa na nzige panzi wameyala; na yaliyosazwa na panzi yameliwa na madumadu
\s5
\v 5 Amkeni, enyi walevi, lieni! Omboleza, ninyi nyote mnywao divai, kwa sababu divai nzuri imekatwa kutoka kwenu.
\v 6 Kwa maana taifa limekuja juu ya nchi yangu, imara na bila idadi. Meno yake ni meno ya simba, neye ana meno ya simba.
\v 7 Amelifanya shamba langu la mizabibu kuwa mahali pa kutisha, amechukua mtini wangu. Amechukua gome lake na kulitupa mbali; matawi yake yamekuwa meupe.
\s5
\v 8 Omboleza kama bikira aliyevaa magunia kwa kifo cha mumewe mdogo.
\v 9 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana. Makuhani, watumishi wa Bwana, huomboleza.
\v 10 Mashamba yameharibiwa, na nchi imekuwa dhaifu. Kwa maana nafaka imeharibiwa, divai mpya imekauka, na mafuta yameharibiwa.
\s5
\v 11 Oneni aibu, enyi wakulima, lieni, wakulima wa mzabibu, kwa ngano na shayiri. Kwa mavuno ya mashamba yameharibika.
\v 12 Mizabibu imeharibika na miti ya mtini imekauka, miti ya mkomamanga, pia mitende, na miti ya epo - miti yote ya shambani imeharibika. Kwa furaha imeharibika kutoka kwa wana wa wanadamu.
\s5
\v 13 Panda magunia na omboleza, enyi makuhani! Mwalia, enyi watumishi wa madhabahu. Njoo, ulala usiku wote kwenye magunia, enyi watumishi wa Mungu wangu. Maana sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimezuiliwa nyumbani mwa Mungu wenu.
\v 14 Iteni kwa funga takatifu, na iteni kusanyiko takatifu. Mkusanyieni wazee na wenyeji wote wa nchi wafike nyumbani kwa Bwana Mungu wenu, na kumlilia Bwana.
\s5
\v 15 Ole kwa siku! Kwa maana siku ya Bwana imekaribia. Nayo itakuja uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
\v 16 Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu, na furaha na kicheko kutoka nyumbani mwa Mungu wetu?
\v 17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake, ghala zimekuwa ukiwa, na mabanda yamevunjika, kwa maana nafaka imeharibika.
\s5
\v 18 Jinsi wanyama hulia! Ng'ombe wa ngome wanateseka kwa sababu hawana malisho. Pia, makundi ya kondoo yanateseka.
\v 19 Bwana, nakulilia wewe. Kwa maana moto umekula malisho ya jangwani, na moto umeteketeza miti yote ya mashamba.
\v 20 Hata wanyama wa mashambani wanapanda kwa ajili yako, kwa maana mito ya maji imekauka, na moto umekula malisho ya jangwani.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Piga tarumbeta katika Sayuni, na piga kelele juu ya mlima wangu mtakatifu! Wakazi wote wa nchi watetemeke kwa hofu; maana siku ya Bwana inakuja; Hakika iko karibu.
\v 2 Ni siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza nene. Kama asubuhi inayoenea kwenye milima, jeshi kubwa na la nguvu linakaribia. Hakujawahi kuwako jeshi kama hilo, na hakutakuwa tena, hata baada ya vizazi vingi.
\s5
\v 3 Moto unatumia kila kitu mbele yake, na nyuma yake moto unawaka. Nchi hiyo ni kama bustani ya Edeni mbele yake, lakini nyuma yake kuna jangwa lililoharibika. Hakika hakuna chochote kitakayotoroka.
\s5
\v 4 Muonekano wa jeshi ni kama farasi, na wanakimbia kama wapanda farasi.
\v 5 Wanaruka kwa kelele kama ile ya magari juu ya vilele vya milima, kama kelele za muale wa moto ambao huangamiza majani, kama jeshi la nguvu lililo tayari kwa vita.
\s5
\v 6 Mbele yao watu wako katika maumivu na nyuso zao zote zinakuwa za rangi.
\v 7 Wanakimbia kama wapiganaji wenye nguvu; wanapanda kuta kama askari; wanasonga, kila mmoja kwa hatua, na hawavunji safu zao.
\s5
\v 8 Wala hakuna mmoja anayemsukuma mwingine kando; wanasonga, kila mmoja katika njia yake; wao huvunja kwa njia ya ulinzi na si kuanguka nje ya mstari.
\v 9 Wanakimbilia jiji, wanakimbia kwenye ukuta, wanapanda ndani ya nyumba, na hupita kupitia madirisha kama wezi.
\s5
\v 10 Nchi hutikisika mbele yao, mbingu hutetemeka, jua na mwezi ni giza, na nyota zinaacha kuangaza.
\v 11 Bwana huinua sauti yake mbele ya jeshi lake; maana wapiganaji wake ni wengi sana; kwa maana wao ni wenye nguvu, wale wanaofanya amri zake. Kwa maana siku ya Bwana ni kubwa na ya kutisha sana. Nani anayeweza kuishi?
\s5
\v 12 "Lakini hata sasa," asema Bwana, "Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote. Haraka, lia na omboleza."
\v 13 Rarueni miyoyo yenu, si mavazi yenu tu, na kurudi kwa Bwana Mungu wenu. Kwa maana ni mwenye neema na mwenye huruma, si mwepesi wa hasira na wingi katika uaminifu wa agano, na angependa kugeuka kutokana na adhabu.
\s5
\v 14 Nani anajua? Labda angegeuka na kuwa na huruma, na kuacha baraka nyuma yake, sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji kwa Bwana, Mungu wenu?
\s5
\v 15 Piga tarumbeta huko Sayuni, itisha kwa ajili ya funga takatifu, na itisheni kusanyiko takatifu.
\v 16 Kusanyeni watu, wito kwa kusanyiko takatifu. Kusanya wazee, kukusanya watoto na watoto wachanga. Bwana arusi waweze kutoka nje ya vyumba vyao, na bibi arusi kutoka kwenye vyumba vyao.
\s5
\v 17 Basi makuhani, watumishi wa Bwana, waliao kati ya patakatifu na madhabahu. Wawaambie, Waitie watu wako, Ee Bwana, wala usitoe urithi wako kwa aibu, ili mataifa watawawale juu yao. Kwa nini wanapaswa kusema kati ya mataifa, "Yuko wapi Mungu wao?"
\s5
\v 18 Ndipo Bwana alikuwa mwenye bidii kwa nchi yake na kuwahurumia watu wake.
\v 19 Bwana akawajibu watu wake, Tazama, nitawaletea nafaka, divai mpya, na mafuta. Utaridhishwa nao, wala sitawafanya kuwa aibu kati ya mataifa.
\s5
\v 20 Nitawaondoa washambuliaji wa kaskazini mbali nanyi, na nitawapitisha katika nchi kavu na iliyoachwa. Sehemu ya mbele ya jeshi lao itaingia bahari ya mashariki, na sehemuya nyuma itaingia bahari ya magharibi. Uvundo wake utainuka juu, na harufu yake mbaya itainuka juu. Hakika, amefanya mambo makuu.
\s5
\v 21 Msiogope, nchi, shangilieni na kufurahi, kwa kuwa Bwana atafanya mambo makuu.
\v 22 Usiogope, wanyama wa kondeni, kwa kuwa malisho ya jangwa yatakua, miti itazaa matunda yake, na miti ya mizabibu na mizabibu itazaa mavuno yao yote.
\v 23 Furahini, enyi watu wa Sayuni, na kufurahi katika Bwana, Mungu wenu. Kwa maana atakupa mvua ya vuli kwa kiasi na kuleta mvua kwa ajili yenu, mvua ya vuli na mvua ya masika kama hapo awali.
\s5
\v 24 Sakafu ya kupepetea zitajaa ngano, na vyombo vitafurika kwa divai mpya na mafuta.
\v 25 "Nitawawezesha miaka ya mazao ambayo nzige walikula, Palale, nzige, na nzige wakuteketeza - jeshi langu lenye nguvu ambalo nimelituma kati yenu.
\s5
\v 26 Mutakula chakula tele na kushiba, na kulitukuza jina la Bwana, Mungu wenu, aliyefanya miujiza kati yenu, wala sitawaletea tena watu wangu.
\v 27 Utajua ya kwamba mimi niko kati ya Israeli, na kwamba mimi ni Bwana, Mungu wako, wala hakuna mwingine, wala sitawaletea aibu watu wangu.
\s5
\v 28 Itakuwa baada ya hayo nitamimina Roho yangu juu ya wenye mwili yote, na wana wenu na binti zenu watatabiri. Wazee wenu wataota ndoto, vijana wenu wataona maono.
\v 29 Pia juu ya watumishi na watumishi wa kike, siku hizo nitaimimina Roho wangu.
\s5
\v 30 Nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, moto na nguzo za moshi.
\v 31 Jua litakuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla ya siku kuu na ya kutisha ya Bwana itakapokuja.
\s5
\v 32 Itakuwa kwamba kila mtu anayeita jina la Yahweh ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na Yerusalemu watakuwa na wale waliokoka, kama Bwana alivyosema, na kati ya wale walisalia, wale ambao Bwana anawaita.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Tazama, katika siku hizo na wakati huo, nitakaporudi mateka wa Yuda na Yerusalemu,
\v 2 Nami nitakusanya mataifa yote, na kuwaleta mpaka bonde la Yehoshafati. Nitawahukumu huko, kwa sababu ya watu wangu na warithi wangu Israeli, ambao waliwatawanya kati ya mataifa, na kwa sababu waligawanya nchi yangu.
\v 3 Wamepiga kura kwa ajili ya watu wangu, walinunua kijana kwa ajili ya kahaba, kuuza msichana kwa divai ili waweze kunywa.
\s5
\v 4 Sasa, kwa nini unanikasirikia, Tiro, Sidoni na mikoa yote ya Wafilisti? Je! mutanirudishia malipo? Hata kama mutanilipa, mara moja nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
\v 5 Kwa maana mumechukua fedha zangu na dhahabu zangu, nanyi mukachukua hazina zangu za thamani na kuzileta katika hekalu zenu.
\v 6 Mumewauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kuwaondoa mbali na maeneo yao.
\s5
\v 7 Tazama, nitawaamsha, watoke mahali ambako muliwauza, na nitawarudishia malipo juu ya vichwa vyenu wenyewe.
\v 8 Nitawauza wana wako na binti zako, kwa mkono wa watu wa Yuda. Wao watawauza Sheba, kwa taifa mbali. Kwa maana Bwana amesema.
\s5
\v 9 Tangaza hii kati ya mataifa, 'Jitayarisheni wenyewe kwa ajili ya vita, waamsheni mashujaa, waacheni wakaribie, mashujaa wote wa vita wapande juu.
\v 10 Yafueni majembe yenu kuwa panga na visu vyenu vya kuchongea kuwa mikuki. Basi wadhaifu waseme, 'Nina nguvu.'
\s5
\v 11 Haraka na mje, mataifa yote ya karibu, jikusanyeni pamoja huko. Ee Bwana, washushe mashujaa wako.
\s5
\v 12 Naam, mataifa yajihimize yenyewe kuja hadi bonde la Yehoshafati. Kwa maana nitakaa huko kuhukumu mataifa yote ya jirani.
\v 13 Wekeni katiki mundu, kwa maana mavuno yameiva. Njoo, muponde zabibu, kwa ajiri pipa la divai limejaa. Vipuri vilivyofurika, kwa sababu uovu wao ni mkubwa sana.
\s5
\v 14 Kuna mshtuko, mshtuko katika bonde la Hukumu. Kwa maana siku ya Bwana i karibu katika bonde la hukumu.
\v 15 Jua na mwezi vinakuwa giza, nyota zimeacha kuangaza.
\s5
\v 16 Bwana ataunguruma kutoka Sayuni, na kuinua sauti yake kutoka Yerusalemu. Mbingu na nchi zitatikisika, lakini Bwana atakuwa makao kwa ajili ya watu wake, na ngome kwa wana wa Israeli.
\v 17 Kwa hiyo mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, anayeishi Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Kisha Yerusalemu itakuwa takatifu, na hakuna jeshi litaklozunguka tena.
\s5
\v 18 Katika siku hiyo, milima itatayarisha divai nzuri, milima itatiririsha maziwa, miito yote ya Yuda itapita katikati ya maji, na chemchemi zitakuja kutoka nyumba ya Bwana na maji ya bonde la Shitimu.
\v 19 Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya vurugu iliyofanyika kwa watu wa Yuda, kwa sababu walimwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.
\s5
\v 20 Lakini Yuda utakua mwenyeji milele, na Yerusalemu itakuwa kizazi hata kizazi.
\v 21 Nitawalipizia damu yao, ambayo sijajilipizia kisasi, kwa maana Bwana anaishi Sayuni.

325
30-AMO.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,325 @@
\id AMO
\ide UTF-8
\h Amosi
\toc1 Amosi
\toc2 Amosi
\toc3 amo
\mt Amosi
\s5
\c 1
\p
\v 1 Haya ni mambo yanayoihusu Israeli ambayo Amosi, mmoja wa wachungaji katika Tekoa, aliyapokea katika ufunuo. Alipokea haya mambo katika siku za Uzia mfalme wa Yuda, na pia katika siku za Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la aridhi.
\v 2 Alisema, "Yahwe atanguruma kutoka Sayuni; atainua sauti yake kutoka Yerusalemu. Malisho ya wachungaji yatanyamaza kimya; kilele cha Karmeli kitanyauka."
\s5
\v 3 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Kwa dhambi tatu za Damaskasi, hata kwa nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya chuma.
\v 4 Nitapeleka moto kwenye nyumba ya Hazaeli, na utaiteketeza ngome za Ben Hadadi.
\s5
\v 5 Nitazivunja komeo za Damaskasi na kumkatilia mbali mtu ambaye aishiye katika Biqati Aveni, na pia yule mtu ashikaye fimbo ya kifalme katika Beth Edeni. Na watu wa shamu watakwenda utumwani hata Kiri," asema Yahwe.
\s5
\v 6 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Kwa dhambi tatu za Gaza, hata nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu waliwachukua mateka watu wote, kuwaweka juu ya mkono wa Edomu.
\v 7 Nitatuma moto kwenye kuta za Gaza, na kuziteketeza ngome zake.
\s5
\v 8 Nitamkatilia mbali yule mtu aishiye katika Ashdodi na mtu ashikaye fimbo ya kifalme kutoka Ashkeloni. Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, na mabaki ya Wafilisti wataangamia," asema Bwana Yahwe.
\s5
\v 9 Hivi ndivyo Yhawe asemavyo: "Kwa dhambi tatu za Tiro, hata kwa nne, sintobadili adhabu, kwa sababu waliwapelekea watu wote wa Edomu, na wamevunja agano lao la undugu.
\v 10 Nitapeleka moto kwenye kuta za Tiro, nao utaziteketeza ngome zake."
\s5
\v 11 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, "Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu alimfuatilia ndugu yake kwa upanga na kutupilia mbali huruma zote. Hasira yake ikaendelea kuwa kali, na ghadhabu yake ikabaki milele.
\v 12 Nitapeleka moto juu ya Temani, na utaziteketeza nyumb a za kifalme za Bozra."
\s5
\v 13 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, "Kwa dhambi tatu za watu wa Amoni, hata kwa nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili waweze kupanua mipaka yao.
\s5
\v 14 Nitawasha moto katika kuta za Raba, nao utaziteketeza nyumba za kifalme, pamoja na kupiga kelele katika siku ya vita, pamoja na dhoruba katika siku ya kimbunga.
\v 15 Mfalme wao ataenda utumwani, yeye na maafisa wake pamoja," asema Yahwe.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Kwa dhambi tatu za Moabu, hata kwa nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu amechoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hadi kuwa chokaa.
\s5
\v 2 Nitatuma moto juu ya Moabu, na utaangamiza ngome za Keriothi. Moabu atakufa katika gasia, pamoja na kelele na sauti ya tarumbeta.
\v 3 Nitamuharibu mwamuzi kati yake, na nitawaua wana wa mfalme pamoja na yeye," asema Yahwe.
\s5
\v 4 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu wameikataa sheria ya Yahwe na hawakuzishika amri zake. Uongo wao umesababisha kupotea, ambao baba zao pia waliufuata.
\v 5 Nitatuma moto juu ya Yuda, na utaimeza ngome ya Yerusalemu."
\s5
\v 6 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Kwa dhambi tatu za Israeli, hata kwa nne, sintobadilisha adhabu, kwa sababu wamewauza wasio na hatia kwa fedha na maskini kwa jozi moja ya makubadhi.
\s5
\v 7 Nao hukanyaga juu ya vichwa vya maskini kama kukanyaga kwenye mavumbi juu ya aridhi; wanasukuma kukandamiza. Mtu mmoja na baba yake walilala na msichana mmoja na hivyo kukufuru jina langu takatifu.
\v 8 Nao hulala chini karibu na kila madhabahu kwenye nguo zilizowekwa dhamana, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya wale ambao walitozwa faini.
\s5
\v 9 Bado nimemwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi; alikuwa na nguvu kama mialoni. Kisha nikaharibu matunda yake juu na mizizi yake chini.
\v 10 Pia, niliwapandisha kutoka nchi ya Misri na kuwaongoza miaka arobaini nyikani ili mmiliki nchi ya Wamori.
\s5
\v 11 Nimewainua manabii kutoka miongoni mwa watoto wanu wawe Wanadhiri kutoka vijana wenu. Je sio hivyo, watu wa Israeli? -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\v 12 Lakini mmewashawishi Wanadhiri kunywa mvinyo na kuwaamuru manabii wasifanye unabii.
\s5
\v 13 Tazama, nitawakanyaga kama mkokoteni uliojaa miganda inayoweza kumkanyaga mtu.
\v 14 Mtu akimbiaye hatapata kimbilio; mwenye nguvu hatoongeza nguvu zake mwenyewe; wala shujaa kujiokoa mwenyewe.
\s5
\v 15 Apindaye upinde hatasimama; mkimbiaji sana hatakimbia; mwendesha farasi hatajiokoa mwenyewe.
\v 16 Hata wapiganaji shujaa watakimbia uchi katika siku hiyo -hivi ndivyo Yahwe asemavy."
\s5
\c 3
\p
\v 1 Sikieni neno la Yahwe aliloongea juu yenu, watu wa Israeli, juu ya familia nzima ambayo niliwatoa kutoka nchi ya Misri,
\v 2 "Nimewachagua ninyi tu kutoka familia zote za dunia. Kwa hiyo nitawaadhibu kwa dhambi zenu zote."
\s5
\v 3 Je wawili wanaweza kutembea pamoja isipokuwa wamekubaliana?
\v 4 Je simba huunguruma msituni wakati hakuna mawindo? Je mwana simba ataunguruma kutoka pangoni mwake kama hajakamata kitu?
\s5
\v 5 Je ndege ataanguka kwenye mtego aridhini wakati hakuna chambo kimewekwa kwa ajili yake? Je mtego utafyatuka juu aridhini wakati hakuna kitu cha kukamata?
\v 6 Je tarumbeta itapigwa mjini na watu wasitetemeke? Je janga laweza kuja mjini lisiyoletwa na Yahwe?
\s5
\v 7 Hakika Bwna Yahwe hatafanya kitu vinginevyo amewafunulia mpango watumishi wake manabii.
\v 8 Simba ameshaunguruma; nani hatoogopa? Bwana Yahwe amekwisha ongea; nani hatotabiri?
\s5
\v 9 Tangaza hii katika ngome huko Ashdodi, na katika ngome za nchi ya Misri; sema, "Kusanyikeni kwenye milima ya Samaria na oneni vile mchafuko ulivyomkubwa kwake, na ukandamizaji uliopo katika yeye.
\v 10 Kwa kuwa hawajui jinsi ya kufanya haki -hivi ndivyo Yahwe asemavyo- hao watunzao nguvu na uharibifu katika ngome zao."
\s5
\v 11 Kwa hiyo, hivi ndivyo Yahwe asemavyo, "Adui ataizunguka nchi. Atazivuta chini nguvu zako na ngome zenu zitatekwa nyara."
\v 12 Hivi ndivyo Yahwe asemavyo," Kama mchungaji aokoavyo miguu miwili tu kwenye mdomo wa simba, au kipande cha sikio, ndivyo wana wa Israeli watakavyookolewa wale waishio katika Samaria, pamoja na pembe ya kulalia, au pembe ya kitanda."
\s5
\v 13 Sikieni na kushudia juu ya nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi,
\v 14 "Kwa kuwa katika siku ambayo nimeadhibu dhambi za Israeli, pia nitaziadhibu madhabahu za Betheli. Pembe za madhabahu zitakatwa na kuanguka chini.
\s5
\v 15 Nitaiharibu nyumba ya baridi pamoja na nyumba ya hari. Nyumba za pembe zitaangamia, na nyumba kubwa zitatoweka, -hivi ndivyo Yahwe asemavyo."
\s5
\c 4
\p
\v 1 Lisikilizeni neno hili, ninyi ng'ombe wa Bashani, ninyi mliomo katika mlima wa Samaria, ninyi mnaowakandamiza maskini, ninyi mnaowaponda wahitaji, ninyi muwaambiao waume zenu, "Tuleteeni vinywaji."
\v 2 Bwana Yahwe ameapa kwa utukufu wake, "Tazama, siku zitakuja kwenu wakati watakapowaondoa kwa ndoana, wa mwisho wenu na ndoana za kuvulia samaki.
\s5
\v 3 Mtatoka kupitia mahali palipo bomolewa kwenye kuta za mji, kila mmoja wenu kwenda moja kwa moja kupitia hapo, na mtajitupa mbele ya Harmoni -hivi ndivyo asemavyo Yahwe."
\s5
\v 4 "Nendeni Betheli na uovu, hata Gilgali mkaongeza dhambi, leteni dhabihu zenu kila asubuhi, zaka zenu kila baada ya siku tatu.
\v 5 Toeni dhabihu za shukurani pamoja na mkate; tangazeni sadaka za hiari; watangazieni, kwa kuwa hii ndiyo iwapendezayo, ninyi watu wa Israeli -hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
\s5
\v 6 Nawapatia usafi wa meno katika miji yenu na na kupungukiwa na mkate katika sehemu zenu zote. Bado hamkurudi kwangu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\v 7 Pia nimeizuia mvua kutoka kwenu wakati bado kulikuwa na miezi mitatu kwa mavuno. Nikaifanya inyeshe juu ya mji, na kuifanya isinyeshe katika mji mwingine. Kipande kimoja cha nchi ilinyesha, lakini kipande kingine cha nchi ambapo haikunyesha palikuwa pakavu.
\s5
\v 8 Walizunguka miji miwili au mitatu kwenda mji mwingine kunywa maji, lakini hawakutosheka. Bado hawakunirudia mimi -asema Yahwe.
\v 9 Nimewapiga kwa maradhi yanayosababisha kuvu. Wingi wa bustani, mashamba yenu ya zabibu, mitini yenu, na mizaituni-kuteketeza yote. Bado hamkunirudia hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\s5
\v 10 Nimetuma tauni kwenu kama ya Misri. Nimewaua watoto wenu kwa upanga, kubeba farasi zenu, na kuufanya uvundo wa kambi zenu na kuingiza kwenye pua zenu. Bado hamkunirudia mimi -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
\v 11 Nimeiangamiza miji miongoni mwenu, kama wakati Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora. Mlikuwa kama kijinga kilichonyakuliwa kutoka kwenye moto. Bado hamkunirudia - asema Yahwe.
\s5
\v 12 Kwa hiyo nitafanya jambo baya kwako, Israeli; na kwa sababu nitafanya jambo baya kwako, jiandae kukutana na Mungu, Israeli!
\v 13 Kwa kuwa, tazama, yeye atangenezaye milima pia ndiye aumbaye upepo, humfunulia mawazo yake mwanadamu, hufanya asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahala pa juu ya dunia. Yahwe, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake."
\s5
\c 5
\p
\v 1 Sikilizeni hili neno ambalo nisemalo kama maombelezo juu yenu, nyumba ya Israeli.
\v 2 Bikira wa Israeli ameanguka; hatoinuka tena; ametoroka kwenye nchi yake, hakuna mtu wa kumwinua.
\s5
\v 3 Kwa kuwa hivi ndivyo Yahwe asemavyo: "Mji ambao umetoka nje kwa elfu watabaki mia, na walioenda nje mia watabaki kumi wa mali ya nyumba ya Israeli."
\s5
\v 4 Kwa kuwa hivi ndivyo Yahwe asemavyo kwa nyumba ya Israeli: "Nitafuteni na mtaishi!
\v 5 Msimtafute Betheli; wala kuingia Gilgali; msisafiri kwenda Bersheba. Kwa kuwa Gilgali watakwenda utumwani hakika, na Betheli haitakuwa kitu.
\s5
\v 6 Mtafuteni Yahwe mtaishi, au atawaka kama moto kwenye nyumba ya Yusufu. Utateketeza, na hakutakuwa na mtu hata mmoja kuuzima katika Betheli.
\v 7 Wale watu wageuzao haki kuwa jambo chungu na kuiangusha haki chini!"
\s5
\v 8 Mungu aliiumba Pleidezi na Orioni; amebadilisha giza kuwa asubuhu; hufanya siku kuwa giza na usiku na kuita maji ya bahari; yeye huyamwaga juu ya uso wa dunia. Yahwe ndilo jina lake!
\v 9 Yeye huleta uharibifu wa ghafla juu ya waliohodari ili kwamba uharibifu uje juu ya ngome.
\s5
\v 10 Wanamchukia kila awasahihishaye katika lango la mji, nao humchukia sana yeyote asemaye ukweli.
\v 11 Kwa sababu mnamkanyaga chini maskini na kuchukua sehemu ya ngano kutoka kwake- ingawa mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, hamtaishi kwenye nyumba hizo. Mmependezwa na mashamba ya mizabibu, lakini hamtakunywa mvinyo wake.
\s5
\v 12 Kwa kuwa najua ni jinsi gani mlivyo na makosa mengi na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa- ninyi mnaowaonea wenye haki, chukueni rushwa, na kuwageuza wahitaji kwenye lango la mji.
\v 13 Kwa hiyo kila mtu mwenye busara atanyamaza kimya kwenye wakati kama huo, kwa kuwa ni wakati wa uovu.
\s5
\v 14 Tafuteni mazuri na sio mabaya, ili kwamba mpate kuishi. Hivyo Yahwe, Mungu wa majeshi, atakuwa na ninyi tayari, kama msemavyo yeye ndiye.
\v 15 Chukieni uovu, imarisheni haki katika lango la mji. Huenda Yahwe, Mungu wa majeshi, atawafadhili mabaki ya Yusufu.
\s5
\v 16 Kwa hiyo, hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, Bwana, "Kutakuwa na maombolezo kwenye miraba yote, na watasema kwenye mitaa yote, 'Ole! Ole!' Watawaita wakulima kuomboleza na walio hodari wa kulia na kuomboleza.
\v 17 Katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwa na kilio, kwa kuwa nitapita katikati yako," asema Yahwe.
\s5
\v 18 Ole wenu ninyi mnaoitamani siku ya Yahwe! Kwa nini mnaitamani? Itakuwa giza na sio nuru,
\v 19 kama wakati mtu anamkimbia simba na kukutana na dubu, au aliingia katika nyumba na kuweka mkono wake kwenye ukuta na kung'atwa na nyoka.
\v 20 Je siku ya Yahwe itakuwa giza na sio nuru? Huzuni na sio furaha?
\s5
\v 21 "Nachukia, nazidharau sikukuu zenu, naichukia mikutano yenu ya dini.
\v 22 Hata kama mnanitolea sadaka ya kuteketeza na sadaka za unga, sintozipokea, wala kuzitazama kwenye sadaka za ushirika wa wanyama walionona.
\s5
\v 23 Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; sintosikiliza sauti za vinubi vyenu.
\v 24 Badala yake, acheni haki itiririke kama maji, na haki kama mkondo utiririkao siku zote.
\s5
\v 25 Je mmeniletea dhambihu na sadaka za kuteketeza jangwani kwa mda wa miaka arobaini?
\v 26 Mtamwinua Sikuthi kama mfalme wenu, na Kiuni, nyota yenu ya miungu-ambayo mmeifanya kwa ajili yenu wenyewe.
\s5
\v 27 Kwa hiyo nitawahamisha upande wa pili wa Damaskasi," asema Yahwe, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.
\s5
\c 6
\p
\v 1 Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na kwa wale ambao wameokoka katika nchi ya mlima wa Samaria, watu mashuhuri bora wa mataifa, ambao nyumba ya Israeli huja kwa ajili ya msaada!
\v 2 Viongozi wenu husema, "Pita kwenda Kalne na mkatazame; kutoka huko nendeni hadi Hamathi, mji mkubwa; kisha nendeni chini hata Gathi ya Wapelestina. Je ni wabora kuliko falme zenu mbili? Je kuna mpaka mkubwa kuliko mpaka wenu?"
\s5
\v 3 Ole wao wale waiwekao siku ya majanga na kufanya ufalme kuwa kinyume kusogea karibu.
\v 4 Wamelala juu ya vitanda vya pembe na kupumzika juu ya viti vyao. Wakala wana kondoo kutoka kwenye kundi na ndama kutoka kwenye zizi.
\s5
\v 5 Wanaimba nyimbo za kijinga kwenye muziki wa kinubi; wanatunga kwenye vyombo kama vya Daudi.
\v 6 Wanakunywa mvinyo kutoka kwenye bakuli na kujipaka mafuta wenyewe kwa mafuta ya marahamu, lakini hawahuzuniki juu ya mateso ya Yusufu.
\s5
\v 7 Hivyo sasa watakwenda utumwani pamoja na watumwa wakwanza, na kelele za hao waliojinyoosha zitapita.
\v 8 "Mimi Bwana Yahwe, nimeapa kwa nafsi yangu -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, naizira fahari ya Yakobo; nachukia boma zake. Kwa hiyo nitautoa huo mji pamoja vyote vilivyomo humo."
\s5
\v 9 Itakuja kuhusu kwamba kama kuna wanaume kumi waliobakia kwenye nyumba moja, watakufa.
\v 10 Wakati ndugu wa mtu huyo atakapokuja kuchukua miili yao-yule ambaye awachomaye baada ya kuleta maiti katika nyumba-kama akisema kwa mtu katika nyumba, "Je kuna mtu yuko pamoja nawe?" Vipi kama yule akisema, "Hapana." Kisha atasema, "Kaa kimya, kwa kuwa hatulitaja jina la Yahwe."
\s5
\v 11 Tazama, Yahwe atatoa amri, na nyumba kubwa itapigwa kuwa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa na nyufa.
\s5
\v 12 Je farasi watakimbia juu ya mteremko wa miamba? Je mtu atalima huko na ng'ome? Bado mmegeuza haki kuwa sumu na tunda la haki kuwa uchungu.
\v 13 Ninyi mnaofurahia juu ya Lo Debari, msemao, "Je hatukuchukua Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?"
\s5
\v 14 Lakini tazama, nitainua juu yenu taifa, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe, Mungu wa majeshi. Watawatesa ninyi kutoka Lebo Hamathi hata kijito cha Araba."
\s5
\c 7
\p
\v 1 Hivi ndivyo ambavyo Bwana Yahwe alivyonionyesha. Tazama, aliumba kundi kubwa la nzige wakati wa kuchipuka kwa mmea, na, tazama, ulikuwa ni mmea wa mwisho baada ya mavuno ya mfalme.
\v 2 Wakati walipomaliza kula mbogamboga za nchi, kisha nikasema, "Bwana Yahwe, tafadhali nisamehe; Je Yakobo ataishije? kwa kuwa yeye ni mdogo sana."
\v 3 Yahwe akapunguza hasira kuhusu hili. "Haitatokea," akasema.
\s5
\v 4 Hivi ndivyo ambavyo Bwana Yahwe alivyonionyesha: Tazama, Bwana Yahwe aliita juu ya moto kuhukumu. Nao ukakausha sana, kilindi chini ya dunia na kutaka kuitekeza nchi, pia.
\v 5 Lakini nikasema, "Bwana Yahwe, acha tafadhali; Yakobo ataishije? Kwa kuwa yeye ni mdigo sana."
\v 6 Yahwe akagairi kuhusiana na hili, "Hili halitajitokeza pia," asema Bwana Yahwe.
\s5
\v 7 Hivi ndivyo ambavyo Yahwe alivyo nionyesha: Tazama, Bwana amesimama karibu na ukuta, pamoja na uzi wa timiza kwenye mkono wake.
\v 8 Yahwe akanambia, "Amosi, unaona nini?" nikasema, "Uzi wa timazi." Kisha Bwana akasema, "Tazama, nitaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli. Sintowaharibu tena.
\s5
\v 9 Mahala pa juu pa Isaka pataharibiwa, patakatifu pa Israeli pataangamia, na nitainuka juu ya nyumba ya Yeroboamu kwa upanga."
\s5
\v 10 Kisha Amazia, yule kuhani wa Betheli, akatuma ujumbe kwa Yeroboamu, mfalme wa Israeli: "amosi amefanya njama dhidi yako katikati ya nyumba ya Israeli. Nchi haiwezi kubeba maneno yote haya.
\v 11 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Amosi, 'Yeroboamu atakufa kwa upanga, na hakika Israeli itakwenda utumwani kutoka nchi yake."'
\s5
\v 12 Amazia akamwambia Amosi, "Mwonaji, nenda, kimbia irudie nchi ya Yuda, na hapo ule mkate na kutabiri.
\v 13 Lakini usitabiri tena hapa katika Betheli, kwa kuwa ni patakatifu pa mfalme na nyumba ya kifalme."
\s5
\v 14 Kisha Amosi akamwambia Amazia, "Mimi sio nabii wala mwana wa nabii. Mimi ni mchungaji wa mifugo, na mtunza mikuyu.
\v 15 Lakini Yahwe akanichukua kutoka kuchunga mifugo na kunambia, 'Nenda, katabiri kwa watu wangu Israeli.'
\s5
\v 16 Sasa sikia neno la Yahwe. Wewe usemaye, 'Usitabiri juu ya Israeli, na usiongee juu ya nyumba ya Isaka.
\v 17 Kwa hiyo hivi ndivyo Yahwe asemavyo, 'Mke wako atakuwa kahaba katika mji; wana wako waume na binti zako wataanguka kwa upanga; nchi yako itapimwa na kugawanywa; utakufa katika nchi najisi, na Israeli hakika itakwenda utumwani kutoka nchi yake."'
\s5
\c 8
\p
\v 1 Hiki ndicho ambacho bwana Yahwe amenionyesha. Tazama, kikapu cha matunda ya hari!
\v 2 Akasema, "Unaona nini, Amosi?" Nikasema, "Kikapu cha matunda ya hari." Kisha Yahwe akanambia, "Mwisho umefika kwa watu wangu Israeli; sintowaumiza tena.
\v 3 Nyimbo za kwenye hekalu zitakuwa vilio. Katika siku hiyo-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe. Mizoga itakuwa mingi, katika kila sehemu wataitupa katika ukimya!"
\s5
\v 4 Lisikilizeni hili, ninyi mkanyagao maskini na kumuondoa fukara wa nchi.
\v 5 wakisema, "Wakati mwezi mpya utakapoisha, hivyo tunaweza kuuza mazao tena? Wakati siku ya Sabato itakapoisha, ili kwamba tuuze ngano? Tutafanya kipimo kidogo na kuongeza bei, tukidanganya kwa mizani za udanganyifu.
\v 6 Hivi ndivyo ambavyo tunaweza kuuza ngano mbaya, kununua fukara kwa fedha, na masikini kwa jozi moja ya kubadhi."
\s5
\v 7 Yahwe ameapa kwa fahari ya Yakobo, "Hakika sintoweza kusahau kazi zao hata moja."
\v 8 Je nchi haitatetemeka kwa hili, na kila mmoja aishiye kuombolezea? Yote hayo yatainuka kama Mto Naili, nayo itataabika juu na kupwa tena, kama mto wa Misri.
\s5
\v 9 "Itakuja siku ambayo -huu ndio usemi wa Bwana Yahwe- kwamba nitafanya jua litue wakati wa mchana, na nitaiweka giza dunia wakati wa mchana.
\v 10 Nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo na nyimbo zenu zote kuwa masikitiko. Nitawafanya wote kuvaa nguo za magunia na kipara juu ya kila kichwa. Nitayafanya haya kama maombolezo kwa mwana pekee, na siku ya uchungu mwisho wake.
\s5
\v 11 Tazama, siku zinakuja -asema Bwana Yahwe- wakati nitakapoleta njaa katika nchi, sio njaa ya mkate, wala kiu ya maji, ila kusikia maneno ya Yahwe.
\v 12 watatangatanga kutoka bahari hata bahari; watakimbia kutoka kaskazini kwenda magharibi kutafuta neno la Yahwe, lakini hawatalipata.
\s5
\v 13 Katika siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kutokana na njaa.
\v 14 Wale waapao kwa dhambi ya Samaria wataanguka na hawatainuka tena."
\s5
\c 9
\p
\v 1 Nilimwona Bwana amesimama karibu na madhabahu, na akasema, "Vipige vichwa vya nguzo ili kwamba misingi itikisike. Vivunje vipande vipande juu ya vichwa vyao vyote, nami nitamwua kwa upanga wa mwisho wao. Hakuna hata mmoja wao atakaye kimbia, hakuna hata mmoja wao atakayekimbia. Hata kama watachimba kwenye Sheoli, kuna mkono wangu utawachukua.
\v 2 Hata kama watapanda juu kwenda mbingunu, huko nitawaleta chini.
\s5
\v 3 Hata kama watajificha juu ya Karmeli, nitawatafuta huko na kuwachukua. Hata kama watajificha kwenye vilindi vya bahari nisiwaone, nimwagiza joka, na atawang'ata.
\v 4 Hata kama wataenda kwenye utumwa, watabanwa na maadui zao mbele yao, nitauagiza upanga huko, na utawau. Nitaelekeza macho yangu juu yao kwa ubaya sio kwa uzuri."
\s5
\v 5 Bwana Mungu wa majeshi ndiye agusaye nchi na ikayeyuka; wote waishio humo wataomboleza; yote yatainuka kama Mto, na itadidimia tena kama mto wa Misri.
\v 6 Ni yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuanzisha kuba yake juu ya dunia. Yeye huita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa dunia, Yahwe ndiye jina lake.
\s5
\v 7 "Je ninyi sio kama watu wa Kushi kwangu, wana wa Israeli? -hivi ndivyo Yahwe asemavyo. Je sikuwapandisha Israeli kutoka nchi ya misri, Wafilisti kutoka Krete, na Washami kutoka Kiri?
\v 8 Tazama, macho ya Bwana Yahwe yako juu ya ufalme wenye dhambi, na nitauharibu kutoka kwenye uso wa dunia, isipokuwa kwamba sintoiharibu kabisa nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
\s5
\v 9 Tazama, nitaamuru, na nitaipepeta nyumba ya Israeli miongoni mwa mataifa yote, kama mtu apepetaye ngano kwenye ungo, hivyo basi hakuna hata chembe ya jiwe itakayoanguka kwenye aridhi.
\v 10 Watenda dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, wale wasemao, 'Majanga hayatatupita au kukutana nasi.'
\s5
\v 11 Katika siku hiyo nitainua hema ya Daudi iliyokuwa imeanguka, na kuyafunga matawi yake. Nitayainua magofu yake, na kuijenga tena kama katika siku za zamani,
\v 12 Kwamba wamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote ambayo yameitwa kwa jina langu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo-afanyayo haya.
\s5
\v 13 Tazama, siku zitakuja-hivi ndivyo Yahwe asemavyo-wakati mlimaji atampita mvunaji, na akanyagaye zabibu atampita yeye apandaye mbegu. Milima itadondosha divai tamu, na milima yote itabubujika kwa nayo.
\s5
\v 14 Nitawarudisha kutoka utumwani watu wangu Israeli. Watajenga magofu ya miji na kuishi humo, watapanda bustani za mizabibu na kunywa divai, na watafanya bustani na kula matunda yao.
\v 15 Nitaipanda hadi kwenye nchi yao, na hawataing'oa tena kutoka kwenye nchi ambayo niliyowapatia," asema Yahwe Mungu wako.

50
31-OBA.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,50 @@
\id OBA
\ide UTF-8
\h Obadia
\toc1 Obadia
\toc2 Obadia
\toc3 oba
\mt Obadia
\s5
\c 1
\p
\v 1 Maono ya Obadia. Bwana MUNGU asema hivi juu ya Edomu Tumesikia habari kutoka kwa Bwana, na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, akisema, Inukeni! Tuinuke dhidi yake kwa vita!"
\v 2 Tazama, nitawafanya wadogo kati ya mataifa, mutadharauliwa sana.
\s5
\v 3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya wewe, wewe ambaye unishi katika makaburi ya miamba, katika nyumba yako ya juu; asemaye moyoni mwako, 'Ni nani atakayenishusha mimi chini?'
\v 4 Ingawa unasimama juu kama tai na ingawa kiota chako huwekwa kati ya nyota, nitakushusha chini kutoka huko, asema Yahweh.
\s5
\v 5 Kama wezi walikuja kwako, ikiwa wanyang'anyi wangekujilia usiku (jinsi ungekatilwa mbali!), Wasingeweza kuiba vya kuwatosha? Ikiwa wakusanya zabibu wangekujilia, wasingeacha mavuno?
\v 6 Jinsi Esau amekwisha kupigwa, na hazina zake zilizofichwa zimewekwa nje!
\s5
\v 7 Watu wote wa ushirikiano wako watakupeleka katika njiani ya hadi mpakani. Watu waliokuwa na amani pamoja nawe wamekudanganya, na kukushinda. Wale wanaokula mkate wako wameweka mtego chini yako. Hakuna uelewa ndani yake.
\v 8 Je! Sikuweza siku hiyo, asema Bwana, kuwaangamiza watu wenye hekima kutoka Edomu na kuelewa kutoka mlima wa Esau?
\v 9 Mashujaa wako watafadhaika, Temani, ili kila mtu akatiliwe mbali kutoka mlima wa Esau kwa kuuawa.
\s5
\v 10 Kwa sababu ya ukatili uliofanywa kwa ndugu yako Yakobo, utafunikwa na aibu, nawe utakatiliwa mbali milele.
\v 11 Siku ile ulikuwa umesimama, siku wageni walichukua mali zake, na waliokuwa wageni katika malango yake, na kupiga kura kwa Yerusalemu, wewe ulikuwa kama mmoja wao.
\s5
\v 12 Lakini usifurahi siku ya ndugu yako, siku ya msiba wake, wala usifurahi juu ya watu wa Yuda siku ya uharibifu wao; msijisifu siku ya dhiki yao.
\v 13 Usiingie mlango wa watu wangu siku ya msiba wao; usifurahi juu ya taabu yao siku ya msiba wao, wala msipotee utajiri wao siku ya uharibifu wao.
\v 14 Usisimama kwenye njia panda, ili kuwakatilia mbali wakimbizi wake na usiwatoe waathirika wake katika siku ya dhiki.
\s5
\v 15 Kwa maana siku ya Bwana iko karibu na mataifa yote. Kama ulivyofanya, itafanyika kwako; matendo yako yatarudi juu ya kichwa chako mwenyewe.
\v 16 Kwa vile mlivyokunywa katika mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote yatakavyo kunywa daima. Watakunywa na kumeza na itakuwa kana kwamba hawakuwepo kabisa.
\s5
\v 17 Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwa na wale waliookoka na watakuwa watakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki miliki zao.
\v 18 Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu ni mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaunguza, na kuwateketeza. Hakutakuwa na waathirika kwa nyumba ya Esau, kwa kuwa Bwana amesema.
\s5
\v 19 Wote kutoka Negebu watamiliki mlima wa Esau na wale wa Shepela watamiliki nchi ya Wafilisti. Wao wataimiliki nchi ya Efraimu na nchi ya Samaria; na Benyamini atamiliki Gileadi.
\s5
\v 20 Wahamiaji wa jeshi hili la watu wa Israeli watamiliki ardhi ya Kanaani mpaka Sarepta. Wahamiaji wa Yerusalemu, waliopo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu.
\v 21 Waokoaji watakwenda hadi juu ya Mlima Sayuni kutawala nchi ya vilima ya Esau, na ufalme utakuwa wa Bwana.

107
32-JON.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,107 @@
\id JON
\ide UTF-8
\h Yona
\toc1 Yona
\toc2 Yona
\toc3 jon
\mt Yona
\s5
\c 1
\p
\v 1 Ndipo neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amittai, kusema,
\v 2 "Simama uende Ninawi, mji kuu, na ukapaze sauti dhidi yake, kwa sababu uovu wao umeinuka mbele yangu."
\v 3 Lakini Yona akaondoka kukimbia kutoka mbele ya Bwana na kwenda Tarshishi. Akatelemka mpaka Yafa na akaona melikebu inayokwenda Tarshishi. Kwa hiyo alilipa nauli na akapanda melikebu kwenda nayo Tarishishi, mbali na uwepo wa Yahweh.
\s5
\v 4 Lakini Bwana akatuma upepo mkubwa juu ya bahari, ikawa tufani juu ya bahari. Hivi karibuni ikaonekana kwamba meli ilikuwa inataka kuvunjika.
\v 5 Wale baharia waliogopa sana na kila mtu alilia kwa mungu wake mwenyewe. Wakatupa mizigo bahari iliyokuwa merikebuni ili kuifungua. Yona alikuwa ameshuka hapa pande za ndani ya melikebu, naye alikuwa amelala huko usingizi.
\s5
\v 6 Basi nahoza akamwendea akamwambia, "kwa nini unalala? Amka! ukamwombe mungu wako! Labda mungu wako atatutambua na hatutapotea."
\v 7 Wote wakaambiana, 'Njoni, tupige kura, ili tujue ni nani ndiye sababu ya mabaya haya yanayotupata.' Basi wakapiga kura, na kura ikaangukia kwa Yona.
\s5
\v 8 Kisha wakamwambia Yona, "Tafadhali tuambie ni nani ndiye sababu ya mabaya haya yanayotupata. Unafanya kazi gani, na umetoka wapi? Nchi yako ni ipi, na kutoka kwa watu wa kabila gani?"
\v 9 Yona akawaambia, Mimi ni Mhebrania; Nami namuogopa Bwana, Mungu wa mbinguni, aliyeifanya bahari na nchi kavu.
\v 10 Ndipo watu hao waliogopa zaidi, wakamwambia Yona, Ni jambo gani hili ulilolifanya? Kwa maana hao watu walijua kwamba alikuwa akikimbia mbele ya Bwana, kwa sababu alikuwa amewaambia.
\s5
\v 11 Ndipo wakamwambia Yona, Tukufanyie nini ili bahari iweze kutulia? Kwa maana bahari ilikuwa imechafuka zaidi na zaidi.
\v 12 Yona akawaambia, "Nikamateni na nitupeni baharini. Kisha bahari itatulia kwa ajili yenu, kwa maana najua kwamba ni kwa sababu yangu kwamba tufani hii kubwa iwapate."
\v 13 Hata hivyo, watu hao wavuta makasia kwa bidii ili kurudi nchi kavu, lakini hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu bahari ilikuwa imechafuka zaidi dhidi yao.
\s5
\v 14 Basi wakamwomba Bwana, wakasema, Tunakuomba, Bwana, tunakuomba, usiache tuangamize kwa sababu ya maisha ya mtu huyu; wala usituwekee hatia ya kufa kwake, kwa kuwa wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.
\v 15 Basi wakamchukua Yona wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.
\v 16 Ndipo watu wale wakamuogopa Bwana sana. Wakamtolea dhabihu Bwana na kuweka nadhiri.
\s5
\v 17 Bwana alikuwa ameandaa samaki mkubwa kummeza Yona, na Yona alikuwa ndani ya tumbo lasamaki siku tatu na usiku wa tatu.
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha Yona akamwomba Bwana Mungu wake kutoka katika tumbo la samaki.
\v 2 Akasema, Nimemwita Bwana juu ya shida yangu naye akanijibu; kutoka tumbo la Kuzimu nililia kwa msaada! Uliisikia sauti yangu.
\s5
\v 3 Ulikuwa umenitupa ndani ya kina, ndani ya moyo wa bahari, na maji yaliyonizunguka; mawimbi yako yote na gharika yalipita juu yangu.
\v 4 Nikasema, 'Nimefukuzwa mbele ya macho yako; lakini nitaangalia tena juu ya hekalu lako takatifu. '
\s5
\v 5 Maji yalifunika kunizunguka karibu na shingo yangu; kina kilinizunguka; mwani ukakizinga kichwa changu.
\v 6 Nilikwenda chini ya milima; nchi na baa zake zimefungwa juu yangu milele. Lakini wewe umeinua uhai wangu shimoni, Bwana, Mungu wangu!
\s5
\v 7 Wakati nafsi yangu ilipozimia ndani yangu, nikamwita Bwana; basi sala yangu ilikujia, katika hekalu lako takatifu.
\v 8 Wote ambao huzingatia miungu isiyofaa hukataa uaminifu wako wao wenyewe.
\s5
\v 9 Lakini mimi, nitakuchinjia kwa sauti ya shukrani; Nitayatimiza yale niliyoapa. Wokovu hutoka kwa Bwana!
\v 10 Kisha Bwana akanena na samaki, akamtapika Yona juu ya nchi kavu.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, akisema,
\v 2 "Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, na uhubiri ujumbe ule ambao nitakuagiza."
\v 3 Basi Yona akaondoka akaenda Niniawi kwa kutii neno la Bwana. Sasa Ninawi ilikuwa mji mkubwa sana, ilikuwa safari ya siku tatu.
\s5
\v 4 Yona akaanza kuingia ndani ya mji, na baada ya safari ya siku, akapaza sauti, akasema, "Katika siku arobaini Ninawi itaangamizwa."
\v 5 Watu wa Ninawi walimwamini Mungu na wakatangaza kufunga. Wote hwakavaa nguo za magunia, kutoka aliyemkubwa hata mdogo.
\s5
\v 6 Mapema habari zilimfikia mfalme wa Ninawi. Akasimama kutoka kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika magunia, akaketi katika majivu.
\v 7 Alitoa tangazo ambalo lilsemalo, "katika mji wa Ninawi, kwa mamlaka ya mfalme na wakuu wake, msiruhusu mtu wala mnyama, ng'ombe wala kundi, asionje kitu chochote. Wao wasile wala kunywe maji.
\s5
\v 8 Lakini watu na wanyama wawe wamefunikwa kwa magunia na walie kwa sauti kubwa kwa Mungu. Kila mtu ageuke na kuacha njia yake mbaya na kutoka katika udhalimu uliyopo mikononi mwake.
\v 9 Nani anajua? Mungu anaweza kurejea na kubadili mawazo yake na kuacha ghadhabu yake kali ili tusiangamie."
\s5
\v 10 Mungu akaona yale waliyoyafanya, wakaziacha njia zao mbaya. Kwa hiyo Mungu alibadili mawazo yake juu ya adhabu aliyowaambia angewafanyia, nae hakufanya hivyo.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Lakini hili lilimchukiza Yona naye akakasirika.
\v 2 Basi Yona akamwomba Bwana akasema, "Ee, Bwana, hiya sio yale niliyosema wakati niliporudi katika nchi yangu? Ndiyo maana nilifanya haraka na kujaribu kukimbia Tarshishi-kwa sababu nilijua kuwa wewe ni Mungu mwenye neema, mwenye huruma, si meingi wa hasira, mwingi kwa uaminifu, na hughairi maafa.
\v 3 Kwa hiyo sasa, Bwana, nakuomba, uniondoe uhai wangu, kwa maana ni bora kwangu kufa kuliko kuishi."
\s5
\v 4 Bwana akasema, Je, ni vema kwamba umekasirika?"
\v 5 Kisha Yona akaondoka mjini akaketi upande wa mashariki wa jiji. Huko alifanya makao na akaketi chini yake katika kivuli ili aweze kuona mji utakuwaje.
\s5
\v 6 Bwana Mungu aliandaa mmea na kuukuza juu ya Yona ili uwe kivuli juu ya kichwa chake ili kupunguza dhiki yake. Yona alikuwa na furaha kubwa kwa sababu ya mmea.
\v 7 Lakini Mungu aliandaa mdudu kulipopambazuka asubuhi iliyofuata. Alishambulia mmea na mmea ukapooza.
\s5
\v 8 Ikawa wakati jua lilipochomoza asubuhi, Mungu aliandaa upepo mkali wa mashariki. Pia, jua lilipiga kichwa cha Yona na akaanguka. Kisha Yona alitamani kufa. Akajiambia, "Ni bora kwangu kufa kuliko kuishi."
\v 9 Kisha Mungu akamwambia Yona, "Je, ni vema wewe kuwa na hasira juu ya mmea?" Yona akasema, Ni vyema kuwa nimekasirika hata kufa.
\s5
\v 10 Bwana akasema, Umeuhurumia mmea, ambao haukuufanyia kazi wala haukukua. Uliomea katika usiku na kufa usiku.
\v 11 Kwa hiyo mimi, haikunipassa kuuhurumia Ninawi, mji mkuu, ambalo kuna watu zaidi ya mia na ishirini elfu ambao hawajui tofauti kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto, na pia ng'ombe wengi?

228
33-MIC.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,228 @@
\id MIC
\ide UTF-8
\h Mika
\toc1 Mika
\toc2 Mika
\toc3 mic
\mt Mika
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Mika Mmorashti katika siku za Yotahamu, Ahazi, na Hezekeia, mfalme wa Yuda, lile neno aliloliona kuhusiana na Samaria na Yerusalemu.
\s5
\v 2 Sikilizeni, ninyi watu wote. Sikilizeni, dunia, na vyote vilivyomo kwenye dunia. Acheni Yahwe ashuhudiwe dhidi yenu, Bwana kutoka kwenye hekalu lake takatifu.
\v 3 Tazama, Yahwe anakuja kutoka mahali pake; atashuka chini na kupakanyaga mahali pa juu katika dunia.
\v 4 Milima itayeyuka chini yake; mabonde yatapasuka vipande vipande kama mshumaa mbele ya moto, kama maji ambayo yamemwagika chini ya mteremko mkali.
\s5
\v 5 Haya yote ni kwasababu ya uasi wa Yakobo, na kwasababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Je sababu ilikuwa nini kwa uasi wa Yakobo? Je ilikuwa Samaria? Je sababu ilikuwa nini kwa mahali pa juu pa Yuda? Je haiukuwa Yerusalemu?
\s5
\v 6 "Nitaifanya Samaria rundo la uharibifu katika shamba, kama eneo la kupandia mizabibu. Nitayavuta mawe ya jengo lake kwenda kwenye bonde; Nitaifunua misingi yake.
\v 7 Sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa vipande vipande; na zawadi zake zote zitachomwa moto. Kwa kuwa zawadi zake za ukahaba amezikusanya, na kama malipo ya ukahaba yatarudi."
\s5
\v 8 Kwa sababu hii nitalia na kuomboleza; nitaenda peku peku na uchi; Nitaomboleza kama mbeha na kuomboleza kama bundi.
\v 9 Kwa kuwa jeraha lake haliponi, kwa kuwa imefika kwa Yuda. Imefikia lango la watu wangu, hadi Yerusalemu.
\v 10 Msiache kuwambia kuhusu katika Gathi; msilie tena. Katika Bethi Leafra nabiringisha mwenyewe kwenye mavumbi.
\s5
\v 11 Piteni karibu na, makao ya Shafiri, katika uchi na aibu. Makazi ya Zaanani hayatatoka nje. Maombolezo ya Beth Ezeli, kwa ajili ya ulinzi yamechukuliwa.
\v 12 Kwa kuwa wakaaji wa Marothi hungoja habari njema, kwa sababu hofu, kwa sababu msiba umetoka kwa Yahwe hadi kwenye malango ya Yerusalemu.
\s5
\v 13 Wfuungeni lijamu farasi wakokote gari la farasi, makazi ya Lakishi. Wewe Lakishi, ulikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalionekana kwako.
\v 14 Hivyo utaipa zawadi ya kuagia Moreshethi Gathi; mji wa Akzibu utawavunja moyo wafalme wa Israeli.
\s5
\v 15 Tena nitaleta ushindi kwako, makazi ya Maresha; uzuri wa Israeli utakuja Adulamu.
\v 16 Kata kipara chako na kata nywele zako kwa ajili ya watoto ambao unaowafurahisha. Fanya kipara chako mwenyewe kama tai, kwa ajili ya watoto wako watakao kwenda utumwani kutoka kwako
\s5
\c 2
\p
\v 1 Ole wao wale wanao wanaokusudia mabaya, kwa wale wanaokusudia kwenye vitanda vyao kufanya maovu. Katika asubuhi wanayafanya kwa sababu wana nguvu.
\v 2 Wanatamani mashamba na kuyapunguza; wanazitamani nyumba na kuzichukua. Wanadhulumu mtu na nyumba yake, mtu na urithi wake.
\s5
\v 3 Kwa hiyo Yahwe asema hivi, "Tazama, nakaribia kuleta janga dhidi ya huu ukoo, ambalo hamtazitoa shingo zenu. Hamtatembea kwa kiburi, kwa kuwa itakuwa wakati wa uovu.
\v 4 Katika siku hiyo maadui zako wataimba wimbo kuhusu wewe, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni. Wataimba, 'Sisi Waisraeli tumeangamizwa kabisa; Yahwe hubadilisha eneo la watu wangu. Je ataliondoaje kutoka kwangu? Huwagawia mshamba yetu kusaliti."'
\v 5 Kwa hiyo, ninyi watu matajiri hamtakuwa uzao kugawanya eneo kwa kupiga kura katika mkutano wa Yahwe.
\s5
\v 6 "Msitabiri," wanasema. "Hawatayatabiri haya mambo; lawama hazitakuja."
\v 7 Je litasemwa kweli, nyumba ya Yakobo, "je Roho ya Yahwe? Je haya ni matendo yake kweli?" Maneno yangu hayafai kwa kila mmoja atembeaye kwa unyoofu?
\v 8 Hivi karibuni watu wangu wameinuka kama adui. Mmelivua joho, nguo, kutoka wale wapitao wasioshutumiwa, kama maaskari kurudi kutoka kwenye vita kwa kile wakifikiriacho ni salama.
\s5
\v 9 Mnawaendesha wanawake wangu kwa watu wangu kutoka kwenye nyumba nzuri; mnachukua baraka kutoka kwa watoto wao wadogo daima.
\v 10 Inukeni na muondoke, kwa kuwa hii sio sehemu ambayo mnaweza kuishi, kwa sababu ya unajisi wake; imeangamizwa kwa maangamizo kabisa.
\v 11 Kama mtu akija kwenu katika roho ya uongo na kudanganya na kusema, "Nitatabiri kwenu kuhusu mvinyo na kilevi kikali," angeweza kufikiriwa kuwa nabii kwa ajili ya hawa watu.
\s5
\v 12 Nitawaleta pamoja wote hakika, Yakobo. Hakika nitawakusanya mabaki ya Israeli. Nitawaleta pamoja kama kondoo katika zizi, kama kundi la wanyama katika malisho. Kutakuwa na kelele kwasababu ya wingi wa watu.
\v 13 Mtu avunjaye hufungua njia zao kwa ajili yao kwenda mbele yao. Wamebomoa kupitia lango na kutoka nje; mfalme wao atapita mbele yao. Yahwe atakuwa mbele yao.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Nimesema' "Sasa sikilizeni, ninyi viongozi wa Yakobo na kutawala nyumba ya Israeli: Je siyo sahihi kwenu kuielewa haki?
\v 2 Ninyi manaochukia mazuri na kupenda uovu, ninyi mnaoambua ngozi yao, miili yao kutoka kwenye mifupa yao-
\v 3 ninyi mnaokula pia miili ya watu wangu, na kuambua ngozi yao, kuvunja mifupa yao, na kuwakatakata katika vipande vipande, kama nyama kwenye chungu, kama nyama kwenye sufuria kubwa.
\s5
\v 4 Kisha ninyi watawala mtalia kwa Yahwe, lakini hatawajibu. Atauficha uso wake kutoka kwenu kipindi hicho, kwasababu mmefanya matendo maovu."
\s5
\v 5 Yahwe asema hivi kuhusu manabii ambao wawafanyao watu wangu kushindwa, "Kwa wale wawalishao wanatangaza, 'Kutakuwa na ustawi.' Lakini kwa wale wasioweka kitu kwenye vinywa vyao, wanaanzisha vita dhidi yake.
\v 6 Kwa hiyo, itakuwa usiku kwenu usiokuwa na maono juu yenu; itakuwa giza ili kwamba msiweze kubashiri. Jua litakwenda chini juu ya manabii, na siku itakuwa giza juu yao.
\v 7 Waonaji watawekwa kwenye aibu, waaguzi wa watachanganyikiwa. Wote watafunga midomo yao, kwa kuwa hakuna jibu kutoka kwangu."
\s5
\v 8 Lakini kwangu, nimejazwa nguvu kutoka kwa Roho wa Yahwe, na nimejaa haki na uweza, kumwambia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
\s5
\v 9 Sasa sikieni hii, ninyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, na watawala wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao mnaochukia haki, na kupotosha kila haki.
\v 10 Mnaijenga Sayuni kwa damu na Yerusalemu kwa uovu.
\v 11 Viongozi wenu huhukumu kwa rushwa, makuhani wenu hufundisha kwa hijara, na manabii wenu hufanya utabiri kwa ajili ya pesa. Hata hivyo bado mtamtegemea Yahwe na kusema, "Je hayupo Yahwe pamoja nasi? Hakuna uovu utakaokuja juu yetu."
\s5
\v 12 Kwa hiyo, kwasababu yenu, Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa rundo la kifusi, na mwinuko wa hekalu utakuwa kama mwinuko wa msituni.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Lakini katika siku za mwisho itakuja kuhusu kwamba mlima wa nyumba ya Yahwe utawekwa imare juu ya milima mingine. Utainuliwa juu ya milima, na watu watautakabisha.
\s5
\v 2 Mataifa mengi yataenda na kusema, "Njoni, twendeni juu kwenye mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, na tutembea katika njia zake." Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu.
\v 3 Atahukumu miongoni mwa watu na kuamua kuhusiana na mataifa mengi ya mbali. Watapoga mapanga yao kuwa plau na mikuki yao kuwa miuundu ya kupogolea. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa, wala kutawala kwa vita tena.
\s5
\v 4 Badala yake, wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake. Hakuna mtu atakayewafanya waogope, kwa kuwa mdomo wa Yahwe wa majeshi umesema.
\v 5 Kwa kuwa watu wote wataenenda, kila mmoja, katika jina la mungu wake. Lakini sisi tutaenenda katika jina la Yahwe Mungu wetu milele na milele.
\s5
\v 6 "Katika siku hiyo," aseme Yahwe, "Nitamkusanya achechemeaye na kumkusanya aliyefukuzwa, wale ambao nimewatesa.
\v 7 Nitamrudisha aliyechechemea kwenye mabaki, na yeye aliyetupwa kwenye taifa imara, na mimi, Yahwe, nitatawala juu yao katika Milima Sayuni, sasa na milele.
\v 8 Kama kwako, mnara wa saa kwa ajili ya kundi, mlima wa binti wa Sayuni-utakuja kwenu, utawala wenu wa zamani utarudishwa, ufalme ambao unaomilikiwa na binti wa Yerusalemu.
\s5
\v 9 Sasa, kwa nini unapiga kelele kwa sauti kuu? Je hakuna mfalme miongoni mwenu? Je mshauri wako amekufa? Kwa nini uchungu umekushika kama yule mwanamke akiwa anazaa?
\v 10 Kuwa katika uchungu wa kuzaa ili uzae, binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu. Kwa sasa utatoka nje ya mji, kuishi kwenye shamba, na kwenda Babeli. Huko utaokolewa. Huko Yahwe atakuokoa kutoka kwenye mikono ya maadui.
\s5
\v 11 Sasa mataifa mengi yamekusanyika juu yako; wakisema; 'Atiwe unajisi; macho yenu yaangalie Sayuni."'
\v 12 Nabii asema, "Hawayajui mawazo ya Yahwe, wala hawaelewi mpango wake, kwa kuwa wamewakusanaya kama miganda kupura sakafuni."
\s5
\v 13 Yahwe asema, "siamama na upure, binti Sayuni, kwa kuwa nitaifanya pembe yako kuwa chuma, na nitazifanya kwato zako kuwa shaba. Utaponda watu wengi. Nitaweka wakfu udhalimu wao kwangu mwenyewe, Yahwe, miliki zao kwangu, Bwana wa dunia nzima."
\s5
\c 5
\p
\v 1 Sasa njoni pamoja katika safu ya kupigana, binti wa maaskari; maaskari wameuzingira mji, kwa ufito watampiga mwamuzi wa Israeli kwenye shavu.
\s5
\v 2 Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, hata kama uko mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kweko mmoja atakuja kwangu kutawala Israeli, ambaye mwanzo wake ni kutoka nyakati za kale, toka milele.
\v 3 Kwa hiyo Mungu atawapa, hata mda wa yeye aliye katika uchungu kuzaa mtoto, na mabaki ya ndugu zake yatawarudia wana wa Israeli.
\s5
\v 4 Atasimama na kuchunga kundi lake kwa nguvu za Yahwe, kwa ukuu wa enzi ya jina la Yahwe Mungu wake. Watabaki, kwa kuwa atakuwa mashuhuri hata mwisho wa dunia.
\v 5 Atakuwa amani yetu. Wakati Waashuru watakapokuja kwenye nchi yetu, wakati wakitembea dhidi ya boma yetu, kisha kisha tutainuka juu yao wachungaji saba na viongozi nane juu ya watu.
\s5
\v 6 Watachunga nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake. Atatuokoa kutoka kwa Waashuru, watakapokuja kwenye nchi yetu, watakapoingia kwenye mipaka yetu.
\v 7 Mabaki ya Yakobo yatakuwa katika kabila za watu wengi, kama umande utokao kwa Yahwe, kama manyunyu kwenye majani, ambayo hayamsubiri mtu, na hayawasubiri watoto wa mwanadamu.
\s5
\v 8 Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, miongoni mwa watu wengi, kama simba katikati ya kundi la kondoo. wakati akipita katikati yao, atawakanyaga juu yao na kuwachachana kuwa vipande vipande, na hakutakuwa na mtu wa kuwaokoa.
\v 9 Mkono wako utainuliwa dhidi ya maadui zako, na utawaharibu.
\s5
\v 10 "Itatokea siku hiyo," asema Yahwe, "kwamba nitawaharibu farasi wako kutoka miongoni mwenu na nitayavunja magari yako ya farasi.
\v 11 Nitaiharibu miji katika nchi yako na kuzingusha ngome zako zote.
\s5
\v 12 Nitauharibu uchawi kwenye mkono wako, na hakutakuwa na waaguzi tena.
\v 13 Nitaziaharibu sanamu zako za pango na nguzo za mawe kutoka miongoni mwako. Hautaabudu tena ustadi wa mikono yako.
\v 14 Nitazin'goa nguzo zako za Ashera kutoka miongoni mwenu, na nitaiharibu miji yenu.
\v 15 Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu juu ya mataifa ambayo hayakusikiliza."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Sasa sikilizeni kile ambacho Yahwe asemacho, "Inuka na ueleze kesi yako mbele ya milima; acha milima isikie sauti yako.
\v 2 Sikilizeni madai ya Yahwe, enyi milima, na ninyi misingi mivumilivu ya dunia. Kwa kuwa Yahwe anavumilia pamoja na watu wake, na atapigana katika mahakama juu ya Israeli."
\s5
\v 3 Watu wangu, nimefanya nini kwenu? nimewachosha mara ngapi? shuhudieni dhidi yangu!
\v 4 Kwa kuwa niliwaleta kutoka nchi ya Msiri na kuwaokoa kutoka kwenye nyumba ya utumwa. Nawatuma Musa, Aruni, na Mariamu kwako.
\v 5 Watu wangu, kumbukeni ambavyo Balaki mfalme wa Moabu alivyotunga, na vile ambavyo Balamu mwana wa Beori alivyomjibu kama ulipokuwa ukienda kutoka kwa Gilgali, hivyo mnaweza kujua matendo ya haki ya Yahwe."
\s5
\v 6 Je nilete nini kwa Yahwe, ninapoenda kumwinamia Mungu aliye juu? Je ninaweza kuja kwake na sadaka za kuteketeza, pamoja na ndama wenye mwaka mmoja?
\v 7 Je Yahwe atapendezwa na maelfu ya kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, tunda la mwili wangu kwa ajili ya dhambi yangu mwenyewe?
\v 8 Amekwambia, mtu, kile kilicho bora, na kile ambacho Yahwe atakacho kutoka kwako: Kutenda haki, kupenda ukarimu, na kutembea kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wako.
\s5
\v 9 Sauti ya Yahwe inatangaza kwenye mji-hata sasa hekima hukukiri jina lako: "Kaa tayari kwa ajili ya fimbo, na kwa yule aliyeiweka.
\v 10 Kuna utajiri katika nyumba za waovu, na kipimo cha uongo hilo ni chukizo mno.
\s5
\v 11 Ningeweza kumfikira mtu kuwa hana hatia kama anatumia kipimo cha ulaghai, pamoja na mfuko wa kipimo wa udanganyifu?
\v 12 Matajiri wamejaa uharibifu, makazi yao yamesema uongo, na ulimi wao katika midomo yao unaudanganyifu.
\s5
\v 13 Kwa hiyo nimekupiga kwa pigo linaloumiza, nimekufanya gofu kwa sababu ya dhambi zako.
\v 14 Utakula lakini hutatosheka; utupu wako utabakia ndani yako. Utatunza mizigo mbali lakini hutahifadhi, na kile unachokihifadhi nitakitoa kwa upanga.
\v 15 Utapanda lakini huatavuna; utazikusanya zaituni lakini hutajipaka mafuta; utasindika zabibu lakini hutakunywa divai.
\s5
\v 16 Kanuni zilizotengenezwa na Omri zimetunzwa, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu. Mnatembea kwa ushauri wao. Hivyo nitakufanya wewe, mji, gofu, na makazi yako jambo la zomeo, na matabeba dharau kama watu wangu."
\s5
\c 7
\p
\v 1 Ole wangu! Kwangu mimi ni kama msimu wa mavuno ulipokwisha, na pia makombo ya mavuno ya zabibu kwenye shamba la mizabibu: Hakuna tena kishamba cha matunda kinachoonekana, hakuna matini ya malimbuka ambayo ninayoyatamani.
\v 2 Watu waaminifu wamepotelea kutoka kwenye nchi, hakuna mtu mwadilifu katika wanadamu wote. Wote hudanganya katika kusubiri kumwaga damu; kila mtu humuwinda ndugu yake mwenyewe kwa wavu.
\s5
\v 3 Mikono yao ni mizuri mno kwa kufanya madhara. watawala huuliza pesa, hakimu yuko tayari kwa rushwa, na mtu mwenye nguvu anawaambia wengine kile anachokitaka kujipatia. Hivyo ndivyo waundavyo kwa pamoja.
\v 4 Mtu bora kwao ni kama mitemba, mwadilifu sana ni kama mche wa miba. Imefika siku iliyosemwa nyuma na walinzi wako, siku ya hukumu. Sasa ni mda wa machafuko.
\s5
\v 5 Msimwamini kila jirani; msimuweke kiongozi katika rafiki yeyote. Kuweni makini kuhusiana na kile msemacho hata kwa mwanamke ambaye adanganyaye kwenye mikono yenu.
\v 6 Kwa kuwa mwana humfedhehesha baba yake, binti huinuka kushindana na mama yake, na mke wa mwana wa kiume hushindana na mama mkwe wake. Adui wa watu ni watu wa nyumba yake mwenyewe.
\s5
\v 7 Lakini kama kwangu mimi, nitamtazama Yahwe. Nitamsubiri Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu ataniskia.
\v 8 Usifurahi juu yangu, adui yangu. Niangukapo, nitainuka. Wakati nitakapokuwa nimekaa katika giza, Yahwe atakuwa mwanga kwangu.
\s5
\v 9 Kwasababu nimetenda dhambi dhidi ya Yahwe, nitachukua ghadhabu yake hata aniteteapo kosa langu, na kutekeleza hukumu kwa ajili yangu. Atanileta kwenye nuru, na nitamwona akiniokoa kwenye haki yake.
\s5
\v 10 Kisha adui yangu atakapoliona hilo, na aibu itamfunika yule aliyeniambia, "Yahwe Mungu wako yuko wapi?" macho yangu yatamtazama; atakanyagwa chini kama tope kwenye mitaa.
\s5
\v 11 Siku ya ya kujenga kuta zako zitafika; siku hiyo mipaka itasogezwa mbali sana.
\v 12 Siku hiyo watu watakuja kwako, kutoka Ashuru na miji katika Misri, kutoka Misri hata mto mkubwa, kutoka bahari kwenda bahari, na kutoka mlima kwenda mlima.
\v 13 Hizo nchi zitakuwa zimejitenga kwasababu ya watu ambao wanaishi huko sasa, kwasababu ya tunda la matendo yao.
\s5
\v 14 Chunga watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako. Wanaishi wenyewe kwenye msitu, katikati ya msitu. Wachunge katika Bashani na Gileadi kama siku za zamani.
\v 15 Kama katika siku wakati mlipotoka nje ya nchi ya Misri, nitawaonyesha maajabu.
\s5
\v 16 Mataifa yataona na kuwa na aibu ya nguvu zao zote. Wataweka mikono yao kwenye midomo yao; masikio yao yatakuwa kiziwi.
\v 17 Watalamba vumbi kama nyoka, kama viumbe vitaambavyo juu ya nchi. Watatoka nje kwenye maficho kwa hofu; watakuja kwako kwa hofu, Yahwe Mungu wetu, na wataogopa kwa sababu yako.
\s5
\v 18 Ni nani aliye Mungu kama wewe, wewe uchukuaye dhambi, wewe upitaye juu ya kosa la mabaki ya mrithi wako? Hutunzi hasira yako milele, kwa sababu unapenda kutuonyesha agano lako la aminifu.
\s5
\v 19 Tena utakuwa na huruma juu yetu; utayakanyaga maovu chini ya miguu yako. Utazitupa dhambi zetu zote kwenye vilindi vya bahari.
\v 20 Utampatia ukweli Yakobo na agano aminifu kwa Abrahamu, ulipoapa kwa babu zetu katika siku za kale.

127
35-HAB.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,127 @@
\id HAB
\ide UTF-8
\h Habakuki
\toc1 Habakuki
\toc2 Habakuki
\toc3 hab
\mt Habakuki
\s5
\c 1
\p
\v 1 Ujumbe ambao habakuki nabii alipokea,
\v 2 Yahwe, kwa muda gani nitalilia msaada, na hutasikia? Nimekulilia wewe katika kitisho, 'vurugu' lakini hutaniokoa.
\s5
\v 3 Kwanini unanifanya nione mabaya na kuangalia matendo mabaya. Uharibifu na vurugu uko mbele yangu; kuna mapambano, na ushindani unainuka.
\v 4 Walakini sheria ni dhaifu, na haki haiishi kwa wakati wowote. Sababu uovu umezunguka haki; walakini haki ya uongo inatoweka. "Yahwe" anamjibu habakuki
\s5
\v 5 "Angalia mataifa na uwajaribu; stajaabishwa na shangazwa! Sababu nina uhakika kuhusu kufanya kitu katika siku zako kwamba hutaamini itakapotaarifiwa kwenu.
\v 6 Sababu angalia! nakaribia kuwainua Wakaldayo - taifa katili na lenye kishindo - wanatembea kupitia upana wa nchi kuteka nyumba zisizo za kwao.
\v 7 Wanahofu na kuogopa; hukumu yao na uzuri kutoka kwao unaendelea.
\s5
\v 8 Farasi wao pia wanambio sana kuliko chui, wepesi sana kuliko mbwa mwitu wa jioni. Farasi wao huwaseta, na wapanda farasi wao wanakuja kutoka mbali - wanapaa kama tai anayewahi kula.
\v 9 Wote wanakuja kwa vurugu; makundi yao yanakwenda kama upepo wa jangwani, na wanakusanya mateka kama mchanga.
\s5
\v 10 Wanawadhihaki wafalme, na viongozi ni dhihaka kwaajili yao. Huicheka kila ngome, maana hurundika mavumbi na kuyaondoa.
\v 11 Ndipo upepo utapita; itaendelea kupita - watu wenye hatia, ambao uwezo wao ni katika mungu." Habakuki anamuuliza Yahwe swali lingine
\s5
\v 12 "Wewe si wa tangu nyakati za zamani, Yahwe Mungu wangu, uliye Mtakatifu? Sisi hatutakufa. Yahwe aliwatenga kwaajili ya hukumu, na ninyi, Mwamba, mmeimarisha kwaajili ya kusahihisha.
\s5
\v 13 Macho yenu ni safi kuangaza juu ya uovu, lakini hamuwezi kuangalia matendo mabaya kwa fadhila; kwa nini mnaangalia kwa upendeleo hivyo juu ambao wanasaliti? Kwanini kunyamaza wakati uovu unameza sana wenye haki zaidi yao?
\v 14 unawafanya watu kama samaki baharini, kama vitu vitambaavyo bila kiongozi juu yao.
\s5
\v 15 Wao wanawaleta wote kwa ndoano; wanawakokota watu kutoka kwenye nyavu za samaki na kuwakusanya kwenye wavu wao. Hii ndiyo sababu wanafurahi na kupiga kelele kwa uchangamfu sana.
\v 16 Walakini wanatoa sadaka kwenye nyavu zao za kuvulia na kuchoma ubani kwenye nyavu zao, sababu wanyama wanene ni sehemu yao, na nyama iliyonona ni chakula chao.
\v 17 Kwa sababu hiyo watamaliza nyavu zao za kuvulia na kuendelea kuchicha mataifa, bila kuhisi huruma"?
\s5
\c 2
\p
\v 1 Nitasimama kwenye nguzo yangu ya ulinzi na kujiweka mwenyewe juu ya mnara wa mlinzi, na nitatazama kwa makini kuona yeye atasema nini kwangu na namna gani nitageuka kutoka kwenye lawama yangu.
\s5
\v 2 Yahwe alinijibu na alisema, "Rekodi maono haya, na uandike dhahiri juu ya kibao ili kwamba anayesoma anaweza kukimbia.
\v 3 Sababu maono haya bado ni kwa wakati ujao na hatimaye atazungumza bila kuanguka. Ingawa inachelewa, isubiri. Sababu kwa hakika itatakuja na haitachelewa.
\s5
\v 4 Tazama! yule ambae hamu yake siyo sawa ndani yake anapumua kwa nguvu. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani.
\v 5 Sababu mvinyo ni msaliti wa kijana mwenye kiburi ili kwamba asistahimili, lakini hukuza tamaa yake kama kaburi na, kama kifo, haitaweza kuridhishwa. Yeye anajikusanyia kila taifa na anakusanya kwaajili yake watu wote.
\s5
\v 6 Haya yote hayatatengeneza usemi kumdhihaki na wimbo wa dhihaka unaomhusu, 'ole wake yule aongezaye visivyo vya kwake! kwa muda gani utaongeza uzito wa dhamana uliyochukua?'
\v 7 Wale wanao ngojea kwako hawatainuka ghafla? na wale wanaokutetemesha kuamka? Utakuwa mwathirika kwaajili yao.
\v 8 Kwasababu umeteka nyara watu wengi, mabaki yote ya watu, yatakuteka nyara wewe. Sababu umemwaga damu nyingi za watu na umetenda kwa uasi kinyume cha nchi, miji, na wote wanaokaa ndani yake.
\s5
\v 9 Ole kwa yule anayechonga mapato maovu kwaajili ya nyumba yake, hivyo anaweza kutengeneza kiota chake juu kumweka yeye salama mbali na mikono ya uovu.
\v 10 Umebuni aibu kwa nyumba yako kwa kuwakata watu wengi, na umefanya dhambi dhidi yako mwenyewe.
\v 11 Sababu jiwe litapaza sauti kutoka ukutani, na pao la mbao litawajibu,
\s5
\v 12 'Ole wake yule ajengaye mji kwa damu, na anayeimarisha mji kwa katika uovu.
\v 13 Hii haitoki kwa Yahwe wa majeshi kwamba watu wafanye kazi kwa moto na mataifa yote mengine yanachakaa menyewe bila kitu?
\v 14 Bado nchi itajaa maarifa ya utukufu wa Yahwe kama maji yanavyojaza bahari.
\s5
\v 15 'Ole wake yule anayemfanya jirani yake alewe, wewe ambaye unaye ongeza sumu uwafanye walewe ili uweze kutazama uchi wao.
\v 16 Utavimbiwa na aibu zaidi kuliko utukufu. Kunywa hiyo vilevile, na funua uchi wako mwenyewe. Kikombe cha mkono wa kuume wa Yahwe utakuja katika kukugeukia wewe, na aibu itafunika heshima yako.
\s5
\v 17 Vurugu iliyofanywa kwa Lebanoni itakufunika na uharibifu wa wanyama utakuogopesha. Sababu umemwaga damu za watu na umetenda kwa uasi dhidi ya ile nchi, miji, na wote wanaokaa humo.
\s5
\v 18 Sanamu iliyochongwa inakufaidia nini? Sababu yule aliyeichonga hiyo, au ambaye kaisubu kwa kuiyeyusha metali, ni mwalimu wa uongo; Sababu anaiamini kazi ya mikono yake anapotengeneza miungu hii isiyoongea.
\v 19 'Ole kwa yule anayeuambia ubao, Amka! Au kwa jiwe lisiloongea, Inuka!' Vitu hivi vinafundisha? Angalia, hiki juu kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, lakini ndani yake hakipumui kabisa.
\v 20 Lakini Yahwe yumo katika hekalu lake takatifu! Nchi yote iwe kimya mbele zake.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Maombi ya Habakuki nabii:
\v 2 Yahwe, nimesikia taarifa zako, na mimi naogopa. Yahwe, fufua kazi yako katikati wakati; katikati ya muda huu; fanya hiyo ijulikane; kumbuka kuwa na rehema katika ghadhabu yako.
\s5
\v 3 Mungu alikuja kutoka Temani, na yule Mtakatifu kutoka Parani. Sela. Utukufu wake umezifunika mbingu, na dunia ilikuwa imejaa utukufu wake.
\s5
\v 4 Miali miwili ya mikono yake ilikuwa iking'aa kama mwanga, ambapo uweza wake ulifichwa.
\v 5 Ugonjwa wa kuua ulitangulia mbele yake, na adha iliifuta miguu yake.
\s5
\v 6 Yeye alisimama na akaipima nchi; aliangalia na aliyatikisa mataifa. Hata milima ya milele iliharibiwa kabisa, na vilima vya milele vilianguka chini. Njia yake ni ya milele.
\s5
\v 7 Niliona mahema ya Wakushi katika mateso, na vitambaa vya mahema katika Midiani vinatetema.
\v 8 Yahwe alikuwa na hasira pale mtoni? Ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya mito, au hasira yako dhidi ya bahari, unapopanda juu ya farasi wenye mikokoteni na wa ushindi wako?
\s5
\v 9 Umeleta upinde wako bila mfuniko; unaweka mishale kwenye upinde wako! Sela. uliigawa nchi na mito.
\v 10 Milima ilikuona wewe na kugeuka kwa huzuni. Maji yaliyomwagwa chini yalipita juu yao; kina cha bahari kilipaza sauti. Mawimbi yake yakainuka juu.
\s5
\v 11 Jua na mwezi vilisimama imara juu mahali pake katika mwanga wa mishale yako na ilipaa, pale katika uangavu wa mwanga wa mikuki yako.
\v 12 Umetembea juu ya nchi kwa uchungu. Katika ghadhabu umepukuchua mataifa.
\s5
\v 13 Ulikwenda nje kwaajili ya wokovu wa watu wako, Kwaajili ya wokovu wa mteule wako. Wewe pondaponda kichwa cha nyumba ya mwovu kuweka wazi msingi wa shingo. Sela.
\s5
\v 14 Umekichoma kichwa cha wapiganaji wake kwa mshale wake mwenyewe sababu walikuja kama upepo kututawanya sisi, wivu wao ulikuwa kama mtu ambaye anamteketeza masikini katika mahali pamaficho.
\v 15 Umesafiri juu ya bahari kwa farasi wako, na kuyapita maji makuu.
\s5
\v 16 Nilisikia, na ndani yangu nilitetemeka! midomo yangu ilitetemesha sauti. Uozo unakuja katika mifupa yangu, na chini yangu mwenyewe nilitetemeka kama nasubiri kwaajili ya siku ya kuhuzunisha ifike juu ya watu waliotushambulia sisi.
\s5
\v 17 Ingawa mtini hauchipui na hauzai kutokana na mzababibu; na ingawa kuzaa kwa mti wa mzaituni hakuridhishi na mashamba hayatoi chakula; na ingawa kundi mifugo limetoweka na hakuna ng'ombe katika zizi, hiki ndicho nitakacho kifanya.
\s5
\v 18 Bado, nitafurahia katika Yahwe. Nitakuwa nafuraha kwa sababu ya Mungu wa wokovu wangu.
\v 19 Bwana Yahwe ni nguvu yangu na anaifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya mimi niende mbele mahali pangu pa juu. - kufuata maelekezo ya muziki, katika vyombo vyangu vya nyuzi.

114
36-ZEP.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,114 @@
\id ZEP
\ide UTF-8
\h Sefania
\toc1 Sefania
\toc2 Sefania
\toc3 zep
\mt Sefania
\s5
\c 1
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Sefania mwana wa Kushi mwana wa Gedalia mwana wa Amaria mwana Hezekia, katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda. "
\v 2 Nitaangamiza kabisa kila kitu kutoka usoni mwa dunia - hili ni tamko la Bwana mwenyewe.
\v 3 Nitamwangamiza mtu na mnyama; Nitawaangamiza ndege wa mbinguni na samaki wa baharini, uharibifu pamoja na waovu. Hivyo nitamfutilia mbali mtu kutoka uso wa dunia - hili ni tamko la Bwana mwenyewe.
\s5
\v 4 Nitafika kwa mkono wangu juu ya Yuda na wote wenyeji wa Yerusalemu. Nitafutilia mbali kila mabaki ya Baali kutoka sehemu hii na majina ya watu waabuduo sanamu miongoni mwa makuhani,
\v 5 watu ambao juu ya nyumba huabudu miili ya mbinguni, na watu ambao huabudu na kuapa kwa Yahwe bali ambao pia huapa kwa mfalme wao.
\v 6 Nitawafutilia mbali pia wale ambao wamegeuka nyuma kutoka kumfuata Yahwe, wale ambao pia humtafuta Yahwe pasipo kuuliza ulinzi wake.
\s5
\v 7 Uwe kimya mbele ya Bwana Yahwe! Kwa kuwa siku ya Yahwe ni karibu, Yahwe ameandaa dhabihu na amewatenga wageni wake.
\v 8 "Itakuja katika siku ya dhabihu ya Bwana, hivyo nitawapiga wakuu na wana wa mfalme, na kila mmoja aliyevikwa mavazi ya kigeni.
\v 9 Katika siku hiyo nitawapiga wote wale ambao huruka juu ya kizingiti, wale ambao hujaza nyumba ya bwana wao kwa vurugu na udanganyifu.
\s5
\v 10 Itakuwa katika siku ile - hili ni tangazo la Yahwe - kwamba kilio cha huzuni kitakuja kutoka kwenye mlango wa samaki, ikipiga yowe kutoka Wilaya ya Pili, na sauti ya kishindo kikuu kutoka vilimani.
\v 11 Pigeni yowe, wenyeji wa Soko la Wilaya, kwa wote wafanyabiashara watakuwa wameharibiwa, wote wale ambao hupima fedha watakuwa wamefutiliwa mbali.
\s5
\v 12 Itakuwa katika siku ile nitaitafuta Yerusalemu kwa taa na kuwapiga wanaume ambao watakuwa wamekaa kwenye mvinyo wao na kusema mioyoni mwao, 'Yahwe hatafanya chochote, ama kizuri au kiovu.'.
\v 13 Mali zao zitakuja kuporwa, na nyumba zao zitakuwa zimetelekezwa kwa maangamizi!. Watajenga nyumba lakini hawataishi humo, na kupanda mizabibu lakini hawatakunywa mvinyo wake.
\s5
\v 14 Siku kubwa ya Yahwe ni karibu, karibu na inaharakisha upesi! Sauti ya siku ya Yahwe itakuwa ya kilio cha uchungu wa kishujaa!
\v 15 Siku hiyo itakuwa siku ya ghadabu, siku ya huzuni na uchungu, siku ya dhoruba na maangamizi, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza nene.
\v 16 Itakuwa siku ya parapanda na kengele dhidi ya ngome mijini na buruji ndefu.
\s5
\v 17 Hivyo nitaleta dhiki juu ya wanadamu, kwa hiyo watatembea karibu kama wanaume vipofu tangu walipofanya dhambi dhidi ya Yahwe. Damu yao itamwagwa kama vumbi, na sehemu zao za ndani kama kinyesi.
\v 18 Wala fedha zao wala dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa juu ya ghadhabu ya Yahwe. Ndani ya moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, hivyo ataleta ukamilifu, miwisho wa kutisha kwa wote wakaao duniani."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kusanyikeni pamoja ninyi wenyewe mkutano wa hadhara na kusanyikeni, taifa lisilokuwa na aibu -
\v 2 kabla amri kuchukua madhara na siku hiyo kupita kama makapi, kabla hasira kali ya ghadhabu ya Yahwe kuja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya Bwana kuja juu yenu.
\v 3 Mtafuteni Yahwe, ninyi watu wote wanyenyekevu duniani mnaozitii amri zake! Tafuteni haki yake. Tafuteni unyenyekevu, na labda mtalindwa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe.
\s5
\v 4 hivyo Gaza utatelekezwa, na Ashkeloni utageuka kuwa uharibifu. Watauondoshea mbali Ashdodi wakati wa mchana, na wataung'oa Ekroni!.
\v 5 Ole kwa wanaokaa kando ya bahari, taifa la Wakerethi! Yahwe amesema dhidi yenu, Kanaani, nchi ya Wafilisiti. Nitawaangamiza hakuna mkazi atakayebakia.
\s5
\v 6 Hiyo nchi ya kando ya bahari itakuwa malisho kwa wachungaji na kwa mazizi ya kondoo.
\v 7 Nchi ya kando ya bahari itakuwa mali ya mabaki ya watu wa nyumba ya Yuda, watakaochungia makundi yao huko. Watu wao watalala jioni katika nyumba ya Ashikeloni, kwa kuwa Yahwe Mungu wao atawatunza na kurejesha wafungwa wao.
\s5
\v 8 Nilizisikia dhihaka za Moabu na wakiwatukana watu wa Amoni wakati walipowadhihaki watu wangu na kujitukuza mipakani mwao.
\v 9 Kwa hiyo, kama ninavyoishi - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, - Moabu itakuja kuwa kama Sodoma, na watu wa Amoni kama Gomora; mahali pa viwavi na shimo la chumvi, jangwa la daima. Lakini watu wangu waliosalia watawateka mateka, na watu wa taifa langu waliobaki watachukua umiliki wao.'
\s5
\v 10 Hili litatokea kwa Moabu na Amoni kwa sababu ya kiburi chao, tangu walipowadhihaki na kuwatukana watu wa Yahwe wa majeshi.
\v 11 Ndipo watamwogopa Yahwe, kwa kuwa ataidhihaki miungu yote ya dunia. Kila mmoja atamwabudu yeye, kila mmoja kutoka mahali pake, kutoka kila upande wa pwani.
\s5
\v 12 Ninyi Wakushi pia mtakufa kwa upanga wangu,
\v 13 na mkono wa Mungu utaishambulia kaskazini na kuiangamiza Ashuru, Kwa hiyo Ninawi utatelekezwa kwa kuteketezwa, kuwa pakavu kama jangwa.
\v 14 Ndipo makundi ya wanyama yatalala pale, kila mnyama wa mataifa, wote kirukanjia na nungunungu watapumzika juu ya safu zao. Sauti itasikika kutoka madirishani; kifusi kitakuwa milangoni; nakshi za mwerezi wao mihimili itakuwa imeifunua.
\s5
\v 15 huu ni mji wa kushangiliwa ambao umekaa pasipo hofu, ambaye husema moyoni mwake, "Mimi niko, na hakuna mwingine wa kufanana na Mimi". Kwa namna ulivyokuwa wa kutisha, mahali pa kulala wanyama ndani yake. Kila mmoja ambaye hupitia kwake huuhisia na kutingisha ngumi kwake.
\s5
\c 3
\p
\v 1 Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa.
\v 2 Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake.
\s5
\v 3 Wafalme wao ni simba wanaounguruma miongoni mwao. Waamuzi wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza kitu ambacho kitakuwa kimemung'unywa asubuhi yake.
\v 4 Manabii wake wanakiburi na wanaume wasaliti. Makuhani wake wamepanajisi mahali patakatifu na wameifanyia vurugu sheria.
\s5
\v 5 Yahwe ni mwenye haki miongoni mwao. Hawezi kufanya makosa. Kila asubuhi husimamia haki yake! Haitafichika nuruni, hata hivyo watu wasio wenye haki hawajui kuona aibu.
\s5
\v 6 Nimeyaharibu mataifa; ngome zao zimeharibiwa. Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna hata mmoja anayepitia kwake. Miji yao imeharibiwa kwa hiyo hakuna mtu anayeikaa.
\v 7 Nikasema, 'Hakika mtaniogopa mimi. Pokeeni masahihisho na msikatiliwe mbali kutoka kwenye miji yenu kwa yote yale niliyokuwa nimeyapanga kuyafanya kwenu.' Lakini walikuwa na shauku kuanza kila siku kwa kuharibu matendo yao yote.
\s5
\v 8 Kwa hiyo ningojeni - hili ni tamko la Yahwe - mpaka siku ambayo nitainuka kwa ajili ya waathirika. Uaamuzi wangu nikuwakusanya mataifa, kuzikusanya falme, na kumwaga juu yao hasira yangu, uchungu wangu wote mkali, hivyo nchi yote itamezwa kwa moto wa hasira yangu.
\s5
\v 9 Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega.
\v 10 Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu.
\v 11 Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu.
\s5
\v 12 Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe.
\v 13 Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa."
\s5
\v 14 Imba, binti Sayuni! Piga kelele, Israeli. Ufurahi na kushangilia kwa moyo wako wote, binti wa Yerusalemu.
\v 15 Yahwe ameiondoa hukumu yako; amewafukuzia mbali adui zako! Yahwe ni mfalme wa Israeli miongoni mwenu. Kamwe hamtamwogopa tena mwovu!.
\v 16 Katika siku hizo watasema kwa Yerusalemi, "Usiogope, Sayuni. Usiiache mikono yako ilegee.
\s5
\v 17 Yahwe Mungu wako yuko katikati yenu, mwenye nguvu wa kuwaokoa. Atasherehekea juu yenu na kwa furaha atakuwa kimya juu yenu kwa upendo wake. Atakuwa na furaha juu yenu na atashangilia kwa furaha,
\v 18 katika siku maalumu ya sherehe. Nitaondoa maafa kutoka kwenu; si muda mrefu hamtabeba aibu kwa ajili yake.
\s5
\v 19 Tazama, Niko tayari kuwashughulikia watesi wenu wote. Katika wakati ule, Nitawaokoa waliolemaa na kuwakusanya waliotupiliwa mbali. Nitawafanya kuwa sifa, na nitaibadilisha aibu yao iwe sifa katika dunia yote.
\v 20 Katika wakati ule nitawaongoza; katika wakati ule nitawakusanya pamoja. Nitawafanya mataifa yote ya dunia kuwaheshimu na kuwasifu, wakati mtakapoona hivyo, Nitakuwa nimewarudisha", asema Yahwe.

434
38-ZEC.usfm Normal file
View File

@ -0,0 +1,434 @@
\id ZEC
\ide UTF-8
\h Zekaria
\toc1 Zekaria
\toc2 Zekaria
\toc3 zec
\mt Zekaria
\s5
\c 1
\p
\v 1 Katika mwezi wa nane mwaka wa pili wa kutawala kwake Dario, neno la Yahwe lilimjia nabii Zekaria, mwana wa Berekia mwana wa Ido, kusema,
\v 2 "Yawhe alikuwa na hasira sana juu ya baba zenu!
\v 3 Wambie, 'Yahwe wa majeshi asema hivi: Nirudieni! - nami nitawarudia ninyi, asema Yahwe wa majeshi.
\s5
\v 4 Msiwe kama baba zenu ambao hapo zamani manabii waliwambia, wakisema, "Yahwe wa majeshi asema hivi: Geukeni kutoka katika njia zenu za mbaya na matendo yenu mabaya!" Lakini hawakuweza kusikia wala kunijari - asema Yahwe.'
\v 5 Wako wapi baba zenu? Na manabii, je wapo hapa daima?
\v 6 Lakini maneno yangu na maagizo niliyowaamru watumishi wangu manabii, je hayakuwapata baba zenu? Hivyo walitubu na kusema, 'Kama vile Yahwe wa majeshi alivyokusudia kututenda kwa kadili zinavyostahili njia na matendo yetu, ndivyo alivyotutenda."
\s5
\v 7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, ndiyo mwezi wa Shebati, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Yahwe lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido, akasema,
\v 8 "niliona wakati wa usiku, na tazama! mtu alikuwa amepanda farasi mwekundu, naye alikuwa kati ya miti ya mihadasi iliyoko bondeni; na nyuma yake kulikuwa na farasi mwekundu, farasi wa kijivu, na farasi mweupe."
\v 9 Nikauliza, " Bwana, hivi ni vitu gani?" Malaika aliyesema nami akaniambia, "Nitakueleza vitu hivi ni nini."
\s5
\v 10 Kisha mtu aliyesimama kati ya miti ya mihadasi akajibu na kusema, "Hawa ndiyo Yahwe aliowatuma kuzunguka katika dunia yote."
\v 11 Wakamjibu malaika wa Yahwe aliyekuwa amesimama kati ya miti ya mihadasi na kumwambia, "Tumekuwa tukizunguka duniani pote; tazama, dunia yote imekaa na kutulia."
\s5
\v 12 Ndipo malaika wa Yahwe alipojibu na kusema, "Yahwe wa majeshi, hata lini usiuhurumie Yerusalemu na miji ya Yuda ambayo imeteswa na kudhurumiwa miaka hii sabini?"
\v 13 Yahwe akamjibu malaika aliyekuwa amesema nami, kwa maneno mazuri, maneno ya faraja.
\s5
\v 14 Hivyo malaika aliyekuwa anaongea nami akaniambia, "Ita kwa sauti na useme 'Yahwe wa majeshi asema: Nina wivu kwa ajili ya Yerusalemu yaani Sayuni kwa uchungu mkubwa!
\v 15 Nami nina hasira juu ya mataifa yaliyo na utulivu. Kwa maana nilikasirika kidogo tu, lakini wao wakasababisha madhara mabaya.
\s5
\v 16 Kwa hiyo Yahwe wa majeshi asema hivi: Nimeirudia Yerusalema kwa huruma. Hivyo nyumba yangu itajengwa ndani yake - asema Yahwe wa majeshi. Kipimo kitanyoshwa juu ya Yerusalemu!
\v 17 Ita tena, ukisema, 'Yahwe wa majeshi asema hivi: Miji yangu kwa mara nyingine itajawa na uzuri, na Yahwe ataifariji tena Sayuni, na kuichagua Yerusalemu kwa mara nyingine tena."
\s5
\v 18 Kisha nikainua macho na kuona pembe nne!
\v 19 Nikaongea na malaika aliyesema nami, "Hivi ni vitu gani? Akanijibu "hizi ni pembe zilisosababisha kutawanyika kwa Yuda, Israeli, na Yerusalemu."
\s5
\v 20 Kisha Yahwe akanionesha mafundi stadi wanne.
\v 21 Nikasema, "Watu hawa wanakuja kufanya nini?" Akajibu na kusema, "Hizi ni pembe zililoitawanya Yuda na hakuna mtu angeweza kuinua kichwa chake. Lakini watu hawa wanakuja kuziondoa, kutupa chini pembe za mataifa yaliyoinua nguvu zao kinyume cha nchi ya Yuda na kuisambaza."
\s5
\c 2
\p
\v 1 Kisha nikainua macho yangu na kuona mtu akiwa na timazi mkononi mwake.
\v 2 Nikamwuliza, "Unakwenda wapi?" Akaniambia, "Ninakwenda kuupima Yerusalemu ili kujua upana na urefu wake."
\s5
\v 3 Ndipo malaika aliyekuwa anaongea nami akaondoka na malaika mwingine akaenda kukutana naye.
\v 4 Malaika wa pili akamwambia, "Nenda uongee na yule kijana umwambie, 'Yerusalemu utakuwa bila kuta kwa sababu ya wingi wa watu na wanyama ndani yake.
\v 5 Kwa maana Yahwe asema, Nitakuwa ulinzi wake, na nitakuwa utukufu katikati yake.
\s5
\v 6 Kimbieni! kimbieni! kimbieni kutoka nchi ya kaskazini - asema Yahwe - kwa maana nimewatawanya kama pepo nne za anga! - Asema Yahwe.
\v 7 Kimbilieni Sayuni haraka! ninyi mnaokaa na binti Babeli!" Asema Yahwe.
\s5
\v 8 Kwa maana baada ya Yahwe wa majeshi kuniheshimu aliniweka kinyume na mataifa yaliyowateka - kwani awagusaye, agusa mboni ya jicho la Mungu! - baada ya Yahwe kutenda hivi, alisema,
\v 9 "Mimi mwenyewe nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka kwa watumwa wao." Ndipo mtakapojua kwamba Yahwe wa majeshi amenituma.
\s5
\v 10 "Imba kwa furaha, binti Sayuni, kwa maana mimi mwenyewe nitakaa nawe! - asema Yahwe
\v 11 Mataifa makubwa yataungana na Yahwe siku hiyo. "Nanyi mtakuwa watu wangu; kwa kuwa nitakaa kati yenu," nanyi mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.
\s5
\v 12 Kwa maana Yahwe ataimilki Yuda kama milki yake halali katika nchi takatifu na kwa mara nyingine tena atauchagua Yerusalema kwa ajili yake mwenyewe.
\v 13 Nyamazeni, mbele za Yahwe, ninyi wote wenye mwili, maana ameinuka kutoka mahali patakatifu pake!
\s5
\c 3
\p
\v 1 Kisha Yahwe akanionesha Yoshua kuhani mkuu amesimama mbele za malaika wa Yahwe na Shetani amesimama mkono wake wa kushoto kumshitaki kwa ajili ya dhambi.
\v 2 Malaika wa Yahwe akamwambia Shetani, "Yahwe na akukemee, Yahwe, aliyeuchagua Yerusalemu, akukemee! Je hiki si kinga kilichotolewa motoni"
\v 3 Yoshua alikuwa na mavazi machafu aliposimama mbele ya malaika.
\s5
\v 4 Malaika akawaambia waliosimama mbele yake, "Mvulisheni hayo mavazi machafu." Kisha akamwambia Yoshua, "Tazama! nimeuondoa uovu wako na nitakuvika mavazi safi."
\v 5 Haya wamvike kilemba safi kichwani!" Hivyo wakaweka kilemba safi kichwani pa Yoshua na wakamvika mavazi safi wakati malaika wa Yahwe amesimama kando.
\s5
\v 6 Kisha malaika wa Yahwe akamwagiza Yoshua na kusema,
\v 7 Yahwe wa majeshi asema hivi: "Ikiwa utatembea katika njia zangu, na kutunza amri zangu, ndipo utakapoisimamia nyumba yangu na kulinda nyua zangu, kwa maana nitakuruhusu kwenda na kutoka kati ya wasimamao mbele zangu.
\s5
\v 8 WeweYoshua kuhani mkuu na wenzako wanaoishi nawe! Sikilizeni. Watu hawa ni ishara, kwa kuwa mimi mwenyewe nitamwinua mtumishi wangu aitwaye Tawi.
\v 9 Tazameni jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua. Kuna macho saba juu ya jiwe hili moja, nami nitaandika maneno juu yake - asema Yahwe wa majeshi - nami nitaondoa dhambi katika nchi hii kwa siku moja.
\s5
\v 10 Katika siku hiyo kila mtu atamwalika jirani yake kukaa chini ya mzabibu na mtini wake." asema Yahwe wa majeshi.
\s5
\c 4
\p
\v 1 Ndipo malaika aliyekuwa akiongea nami akageuka na kuniamsha kama mtu aamshwavyo usingizini.
\v 2 Akaniuliza, "Unaona nini?" Nikasema, "Ninaona kinara cha taa kimetengenezwa kwa dhahabu tupu, na bakuli juu yake. Kina taa saba juu yake na mirija mmoja kwa kila taa.
\v 3 Kando yake kuna mizeituni miwili, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto."
\s5
\v 4 Kisha nikamwiliza tena na malaika aliyeongea nami. "Mambo haya yanamaana gani, bwana wangu?"
\v 5 Naye akanijibu na kusema, Haujui mambo haya yanamaanisha nini?" Nikasema, "ndiyo sijui bwana wangu."
\s5
\v 6 Hivyo akaniambia, "Hili ni neno la Yahwe kwa Zerubabeli: lisemalo siyo kwa uwezo wala kwa nguvu, lakini ni kwa Roho wangu, asema Yahwe wa majeshi.
\v 7 U nini wewe, mlima mrefu? Mbele ya Zerubabeli utakuwa tambarare, naye ataondoa jiwe la juu kwa kelele ya 'Neema! Neema kwake!"
\s5
\v 8 Neno la Yahwe likanijia kusema,
\v 9 "Mikono ya Zerubabeli imeweka misingi ya nyumba hii nayo itaimaliza. Ndipo mtakapojua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.
\v 10 Ni nani aliyedharau siku ya mambo madogo? Watu hawa wataona jiwe la kupimia mkononi mwa Zerubabeli, nao watafurahi. (Taa saba ni macho ya Yahwe yanayozunguka duniani mwote.)"
\v 11 Ndipo nilipomwuliza malaika, Mizeituni hii miwili isimamayo upande wa kushoto na kulia wa kinara cha taa ni nini?"
\s5
\v 12 Nikauliza kwa mara nyingine tena, "Haya matawi mawili ya mizeituni kando ya mirija miwili ya dhahabu iliyo na mafuta ya dhahabu yanatiririka kutoka ndani yake?
\v 13 Naye akaniambia, " Hauvijui vitu hivi ni nini?" Nami nikasema, "Hapana, bwana wangu."
\s5
\v 14 Akasema, "Hawa ni wana wa mafuta mabichi ya mizeituni wasimamao mbele ya Bwana wa dunia yote."
\s5
\c 5
\p
\v 1 Kisha nikageuka na kuinua macho yangu, nami nikaona, tazama, gombo lirukalo!
\v 2 Malaika akaniuliza, "Unaona nini?" Nikajibu, "Ninaona gombo lirukalo, urefu wake dhiraa ishirini na upana wake dhiraa kumi."
\s5
\v 3 Ndipo aliponiambia, "Hii ni laana iendayo juu ya uso wa nchi yote, kwani tangu sasa kila mwivi ataondolewa kulingana na lisemavyo upande mmoja, wakati kila aapaye kiapo cha uongo ataondolewa kulingana na lisemavyo upande mwingine, kwa kadili ya maneno yake.
\v 4 "Nitalituma - asema Yahwe wa majeshi - hivyo litaingia nyumbani mwa mwivi na nyumbani mwa aapaye kwa uongo kwa jina langu. Litasalia nyumbani mwake na kuteketeza mbao na mawe yake."
\s5
\v 5 Ndipo malaika aliyekuwa akisema nami alipoenda nje na kuniambia, "Inua macho yako uone kinachokuja!"
\v 6 Nikasema, "Ni nini hiki?" Akasema, "Hiki ni kikapu kilicho na efa ijayo. Huu ni uovu wao katika nchi yote."
\v 7 Kisha mfuniko wa risasi ukainuliwa kutoka ndani ya kikapu na kulikuwa na mwanamke chini yake amekaa ndani yake!
\s5
\v 8 Malaika akasema, "Huu ni uovu!" na akamtupa tena kikapuni, na kurusha mfuniko wa risasi mlango pake.
\v 9 Nilipoinua macho nikaona wanawake wawili wakija kwangu, na upepo ulikuwa ndani ya mabawa yao - walikuwa na mabawa kama mabawa ya korongo. Wakainua kikapu kati ya mbingu na nchi.
\s5
\v 10 Hivyo nikamwuliza malaika aliyesema nami, "Wanapeleka wapi kikapu?"
\v 11 Akaniambia, "Wanakwenda kujengea hekalu katika nchi ya Shinari kwa ajili yake, hekalu litakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa kwenye msingi ulioandaliwa kwa ajili yake."
\s5
\c 6
\p
\v 1 Kisha nikageuka na kuinua macho na nikaona vibandawazi vinne vya farasi vikija kutoka kati ya milima miwili; na milima hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa shaba.
\v 2 Kibandawazi cha kwanza kilikuwa na farasi wekundu, kibandawazi cha pili kilikuwa na farasi weusi,
\v 3 kibandawazi cha tatu kilikuwa na farasi weupe, na kibandawazi cha nne kilikuwa na farasi wa kijivu.
\v 4 Hivyo nikamwuliza malaika aliyesema nami, "Ni vitu gani hivi bwana wangu?"
\s5
\v 5 Malaika akajibu na kuniambia, "Hizi ni pepo nne za mbinguni zisimamazo mbele ya Bwana wa dunia yote.
\v 6 Lenye farasi weusi linakwenda nchi ya kaskazini; farasi weupe wanakwenda nchi ya magharibi; na farasi wa kijivu wanakwenda nchi ya kusini."
\s5
\v 7 Farasi hawa wenye nguvu walitoka na wanatafuta kwenda na kuzunguka juu ya nchi, hivyo malaika akasema, "Nendeni na mzunguke juu ya nchi!" nao wakaenda juu ya dunia yote.
\v 8 Kisha akaniita na kuniambia, "Tazama wale wanaokwenda nchi ya kaskazini, wataituliza roho yangu juu nchi hiyo."
\s5
\v 9 Hivyo neno la Yahwe likanijia kusema,
\v 10 "Chukua sadaka kutoka kwa waliohamishwa - kutoka kwa Helidai, Tobiya na Yedaya - leo hii uende na kuipeleka katika nyumba ya Yosia mwana wa Zefania, aliyetoka Babeli.
\v 11 Kisha uchukue fedha na dhahabu, ufanye taji na uivike katika kichwa cha Yoshua mwana wa Yehosadaki kuhani mkuu.
\s5
\v 12 Ongea naye na useme, Yahwe wa majeshi asema hivi: Mtu huyu, jina lake Tawi! Naye atakuwa alipo na kisha atajenga hekalu la Yahwe!
\v 13 Ndiye atakayejenga hekalu la Yahwe naye atauinua utukufu wake; kisha ataketi na kutawala katika kiti chake cha enzi. Atakuwa kuhani juu ya kiti cha enzi na ufahamu wa amani utakuwa kati ya vyote viwili.
\s5
\v 14 Taji itawekwa hekaluni mwa Yahwe kwa heshima ya Heldai, Tobiya na Yedaya na kama kumbukumbu ya ukarimu wa mwana wa Zefania.
\v 15 Ndipo waliombali watakapokuja na kulijenga hekalu la Yahwe, hivyo mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu; kwani ikiwa kweli mnaisikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu hili litatendeka!"
\s5
\c 7
\p
\v 1 Mwaka wa minne wa utawala mfalme Dario, siku ya nne ya mwezi wa Kisleu(ambao ni mwezi wa tisa), neno la Yahwe lilimjia Zekaria kusema.
\v 2 Watu wa Betheli wamemtuma Shareza, Regemu Meleki na watu wao kuomba mbele ya uso wa Yahwe.
\v 3 Wakaongea na makuhani waliokuwa katika nyumba ya Yahwe wa majeshi na kwa manabii; wakasema, "Je niomboleze katika mwezi wa tano kwa njia ya kufunga, kama nilivyofanya miaka mingi hii?"
\s5
\v 4 Ndipo neno la Yahwe wa majeshi liliponijia kusema,
\v 5 "Ongea na watu wote wa nchi na makuhani uwaambie, "Mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba katika hii miaka sabini, je kweli mlifunga kwa ajili yangu?
\v 6 Na mlipokula na kunywa, hamkula na kunywa kwa ajili yenu wenyewe?
\v 7 Je hayo siyo maneno aliyosema Yahwe kwa vinywa vya manabii wa zamani, mlipokuwa bado mnaishi Yerusalemu na miji ya kandokando yenye mafanikio na iliyokaa Negebu, na upande wa magharibi chini ya vilima?"
\s5
\v 8 Neno la Yahwe likamjia Zekaria kusema,
\v 9 "Yahwe wa majeshi asema hivi, 'Hukumuni kwa haki, uaminifu wa agano, na rehema. Kila mtu na amtendee hivi ndugu yake.
\v 10 Juu ya mjane na yatima, mgeni, na masikini - usiwanyanyase, na asiwepo miongoni mwenu anayepanga madhara yoyote dhidi ya mwingine mioyoni mwenu.
\s5
\v 11 Lakini waliyashupaza mabega yao na hawakujari. Waliziba masikio yao ili wasisikie.
\v 12 Waliifanya mioyo yao kuwa migumu kama mwamba ili wasiisikie sheria au neno la Yahwe wa majeshi. Alipeleka ujumbe kwa watu nyakati za zamani kwa Roho wake, kwa vinywa vya manabii. Lakini watu hawakusikia, hivyo Yahwe wa majeshi aliwakasirikia sana.
\s5
\v 13 Hata ikawa alipoita hawakusikia. Vilevile," asema Yahwe wa majeshi, "wataniita, lakini sitasikiliza.
\v 14 Kwa maana nitawatawanya kwa upepo wa kisurisuri katika mataifa yote ambayo hawajawai kuyaona, na baada yao nchi itakuwa wazi. Kwa kuwa hakuna hata mmoja atakayepita au kukaa katika hiyo nchi kwa kuwa wameigeuza nchi yao yenye kupendeza kuwa isiyofaa.
\s5
\c 8
\p
\v 1 Neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema,
\v 2 "Yahwe wa majeshi asema hivi: Nina huzuni kwa ajili ya Sayuni kwa wivu mkuu na ninamaumivu kwa hasira nyingi!
\v 3 Yahwe wa majeshi asema hivi: Nitairudia Sayuni nami nitakaa kati ya Yerusalemu, kwa kuwa Yerusalemu itaitwa mji wa kweli na mlima wa Yahwe wa majeshi utaitwa Mlima Mtakatifu!
\s5
\v 4 Yahwe wa majeshi asema hivi: Kwa mara nyingine tena kutakuwa na vikongwe katika mitaa ya Yerusalemu, na kila mtu ataitaji mkongojo mkononi mwake kwa vile alivyo mzee.
\v 5 Pia mitaa ya mji itajazwa na vijana wa kiume na kike wachezao.
\s5
\v 6 Yahwe wa majeshi asema hivi: ikiwa jambo laonekana haliwezekani katika macho ya masalia ya watu hawa katika siku hizo, je haliwezekani pia machoni pangu? - asema Yahwe.
\v 7 Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, nipo tayari kuwaokoa watu wangu kutoka nchi ya mawio na ya machweo ya jua!
\v 8 Kwa maana nitawarudisha tena, nao wataishi ndani ya Yerusalemu, hivyo watakuwa watu wangu tena, nami nitakuwa Mungu wao katika kweli na utakatifu!
\s5
\v 9 Yahwe wa majeshi asema hivi: Ninyi mnaoendelea kusikia maneno yaleyale yaliyotoka katika vinywa vya manabii msingi wa nyumba yangu ulipowekwa - hii nyumba yangu, Yahwe wa majeshi: Itieni nguvu mikono yenu ili hekalu lijengwe.
\v 10 Kwani kabla ya siku hizo hakuna mazao yaliyokusanywa na yeyote ndani yake, hakukuwa na faida siyo kwa mtu hata mnyama, na hakukuwa na amani kutoka kwa adui kwa kila aliyekwenda au kuja. Nilimfanya kila mtu kuwa kinyume cha mwenzake.
\s5
\v 11 Lakini sasa haitakuwa kama mwanzo, nitakuwa pamoja na masalia ya watu hawa - asema Yahwe wa majeshi.
\v 12 Kwani mbegu za amani zitapandwa; mzabibu unaokua utatoa matunda yake na nchi itatoa mazao yake; anga zitatoa umande, kwa maana nitawapa masalia ya watu hawa kumilki haya yote.
\s5
\v 13 Ulikuwa mfano wa laana kwa mataifa mengine, enyi nyumba ya Yuda na nyumba ya Israeli. Hivyo nitawaokoa nanyi mtakuwa baraka. Msiogope; haya mikono yenu itiwe nguvu!
\v 14 Kwa maana Yahwe wa majeshi asema hivi: Kama nilivyopanga kuwatenda mabaya babu zenu walipochokoza hasira yangu - asema Yahwe wa majeshi - na wala sikujuta,
\v 15 ndivyo nitakavyoazimia kuutenda mema tena Yerusalemu na nyumba ya Yuda katika siku hizi! Msiogope!
\s5
\v 16 Haya ndiyo mambo mnayopaswa kufanya: Kasemeni kweli, kila mtu na jirani yake. Hukumuni kwa haki, usawa na amani katika malango yenu.
\v 17 Na asiwepo miongoni mwenu anayeazimu uovu moyoni mwake dhidi ya jirani yake, wala kuvutwa na viapo vya uongo; kwani haya yote ndiyo mambo ninayoyachukia! - asema Yahwe."
\s5
\v 18 Kisha neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema,
\v 19 "Yahwe wa majeshi asema hivi: Mifungo ya mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa saba na mwezi wa kumi itakuwa nyakati za furaha ya kila aina, kwa nyumba ya Yuda! Kwa hiyo pendeni kweli na amani!
\s5
\v 20 Yahwe wa majeshi asema hivi: Watu watakuja tena, hata wanaoishi miji mingine.
\v 21 Watu wa mji mmoja watakwenda mji mwingine na kusema, "Haya twendeni haraka mbele ya Yahwe tukaombe na kumtafuta Yahwe wa majeshi! Sisi wenyewe tunakwenda pia.
\v 22 Watu wengi na mataifa yenye nguvu yatakuja kumtafuta Yahwe wa majeshi huko Yerusalemu na kuomba upendeleo kwa Yahwe!
\s5
\v 23 Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika siku hizo watu kumi kutoka katika kila lugha na taifa watashika upindo wa kanzu zenu na kusema, "Haya sisi nasi tutakwenda pamoja nanyi, kwani tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nayi!"
\s5
\c 9
\p
\v 1 Hili ni tamko la neno la Yahwe kuhusu nchi ya Hadraki na Damesiki. Kwa maana jicho la Yahwe liko juu ya wanadamu wote, na juu ya kabila zote za Israeli pia.
\v 2 Azimio hili pia linaihusu Hamathi, inayopakana na Damesiki, na linahusu Tiro na Sidoni, japokuwa ni werevu sana.
\s5
\v 3 Tiro amejijengea ngome na kurundika fedha kama mavumbi na dhahabu safi kama matope mitaani.
\v 4 Tazama! Bwana atamnyang'anya na kuharibu nguvu zake juu ya bahari, kwa hiyo atateketezwa kwa moto.
\s5
\v 5 Ashikeloni ataona na kuogopa! Gaza pia atatemeka sana! Ekroni, tumanini lake litatikiswa! Mfalme ataangamizwa kuanzia Gaza, na Ashikeloni haitakuwa na watu tena!
\v 6 Wageni watafanya makao yao katika Ashidodi, nami nitakiondoa kiburi cha Wafilisiti.
\v 7 Kwani nitaondoa damu yao katika vinywa vyao na machukizo yao kutoka kati ya meno yao. Ndipo watakapokuwa masalia kwa Mungu wetu kama ukoo katika Yuda, na Ekironi atakuwa kama Wayebusi.
\s5
\v 8 Nitaweka kambi kuzunguka nchi yangu kinyume cha majeshi ya adui hata hakuna atakayeweza kupita ndani yake tena, kwani hakuna mtesaji atakayeipita tena. Kwa kuwa sasa nitaangalia nchi yangu kwa macho yangu mwenyewe!
\s5
\v 9 Piga kelele kwa furaha, ewe binti Sayuni! Piga kelele kwa shangwe, ewe binti Yerusalem! Tazama! Mfalme wako anakuja kwako pamoja na uadilifu na anakuokoa. Ni mnyenyekevu, amepanda punda, mwanapunda.
\v 10 Ndipo nitakapoondoa kibandawazi kutoka Efraimu na farasi kutoka Yerusalemu, na upinde utaondolewa katika vita; kwani atasema amani kwa mataifa, na utawala wake utakuwa kutoka bahari hata bahari, na kutoka katika mto hadi miisho ya dunia!
\s5
\v 11 Lakini kwenu, kwa sababu ya damu ya agano langu nanyi, nitawaweka wafungwa wenu huru kutoka shimoni pasipo na maji.
\v 12 Rudini ngomeni, wafungwa wa matumaini! Hata leo natamka kwamba nitawarudishia mara mbili, kwani nimempinda Yuda kama upinde wangu.
\v 13 Hata nimelijaza podo langu pamoja na Efraimu. Nimewainua wana wenu, Sayuni, kinyume cha wana wenu, Ugiriki, na amekufanya wewe, Sayuni, kama upanga wa shujaa!
\s5
\v 14 Yahwe atawatokea, na mishale yake itapiga kama radi! Kwa maana Yahwe Bwana wangu atapiga tarumbeta naye ataendelea pamoja na dhoruba kutoka Temani.
\v 15 Yahwe wa majeshi atawatetea, nao watawararua na kuyashinda mawe ya kombeo. Ndipo watakapo kunywa na kupiga kelele kama mtu aliyelewa kwa mvunyo, nao watajazwa na mvinyo kama mabakuri, kama pembe za madhabahu.
\s5
\v 16 Hivyo Yahwe Mungu wao atawaokoa siku hiyo; watakuwa kama kundi la kondoo lililo na watu wake, kwani watakuwa mapambo ya taji, yaliyoinuliwa juu ya nchi yake.
\v 17 Jinsi gani watakavyokuwa wazuri na warembo! vijana watastawi juu ya nafaka na bikra juu ya divai tamu!
\s5
\c 10
\p
\v 1 Mwombeni Yahwe mvua nyakati za kipupwe - Yahwe afanyaye mvua ya radi - naye hufanya mvua inyeshe kwa kila mmoja na uoto kondeni.
\v 2 Kwani sanamu za wenye nyumba husema uongo; waganga hunena uongo; wanasema ndoto za udanganyifu na hutoa faraja tupu, hivyo wapotea kama kondoo na wanaumia kwa sababu hakuna mchungaji.
\s5
\v 3 Gadhabu yangu inawaka dhidi ya wachungaji; ni mabeberu - viongozi - nitakao waadhibu. Yahwe wa majeshi atalihudumia pia kundi la kondoo wake, nyumba ya Yuda, na kuwafanya kama farasi wake wa vita!
\s5
\v 4 Kutoka kwao litatoka jiwe kuu la pembeni; kutoka kwao kitatoka kigingi cha hema; kutoka kwao utatoka upinde wa vita; kutoka kwao watakuja viongozi wote kwa pamoja.
\v 5 Watakuwa kama mashujaa wawakanyagao adui zao katika matope ya mitaani vitani; watafanya vita, kwa maana Yahwe yu pamoja nao, nao watawaabisha wapanda farasi wa vita.
\s5
\v 6 Nitaitia nguvu nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yusufu; kwani nitawarejesha na kuwahurumia. Watakuwa kama nilikuwa sijawaondoa, kwani mimi ni Yahwe Mungu wao, nami nitawaitikia.
\v 7 Ndipo Efraimu atakapokuwa kama shujaa, na mioyo yao itafurahi kama kwa mvinyo; wana wao wataona na kufurahi. Mioyo yao itanifurahia!
\s5
\v 8 Nitawanong'oneza na kuwakusanya, kwani nitawaokoa, nao watakuwa wakuu kama walivyokuwa mwanzo!
\v 9 Niliwapanda kati ya watu, lakini watanikumbuka katika nchi ya mbali, hivyo wao na wana wao wataishi na kurejea.
\v 10 Kwa maana nitawarejesha kutoka nchi ya Misri na kuwakusanya kutoka Ashuru. Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni mpaka kutakapokuwa hakuna nafasi tena kwa ajili yao.
\s5
\v 11 Nitapita katika bahari ya mateso yao; nitayapiga mawimbi ya bahari hiyo na nitavikausha vilindi vyote vya Nile. Utukufu wa Ashuru utashushwa chini, na fimbo ya Misri itakwenda mbali kutoka kwa Wamisri.
\v 12 Nitawatia nguvu katika mimi mwenyewe, nao watatembea katika jina langu - asema Yahwe.
\s5
\c 11
\p
\v 1 Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mielezi yako!
\v 2 Omboleza, enyi miti ya misonobari, kwani mierezi imeanguka! Kilichokuwa cha fahari kimeteketezwa! Ombolezeni, enyi mialoni ya Bashani, kwani msitu wenye nguvu umeshushwa.
\v 3 Wachungaji wanapiga yowe, kwa kuwa utukufu wao umeharibiwa! Sauti ya mungurumo wa wana simba, kwa kuwa kiburi cha Mto Yordani kimeharibiwa!
\s5
\v 4 Hivi ndivyo asemavyo Yahwe Mungu wangu, "Lichungeni kundi la kondoo lililotiyari kuchinjwa!
\v 5 (Wanaowanunua wanawachinja bila kuhadhibiwa, nao wawauzao husema, 'Atukuzwe Yahwe! Nimetajirika! Kwa maana wachungaji wafanyao kazi kwa wenye kondoo hawawahurumii.)
\v 6 Kwa maana hiyo sitawahurumia tena wenyeji wa nchi! - hivi ndivyo asemavyo Yahwe. Tazama! Mimi mwenyewe nipo tiyari kumwelekeza kila mtu katika mkono wa jirani yake na katika mkono wa mfalme wake, nao wataiharibu nchi na hakuna hata mmoja wao nitakayemwokoa kutoka katika mkono wao."
\s5
\v 7 Hivyo nikawa mchungaji wa kondoo walioamriwa kuchinjwa, kwa wanaowashughulikia kondoo. Nilichukua fimbo mbili; fimbo moja nikaiita "Neema" na nyingine nikaiita "Umoja." Kwa njia hii niliwachunga kondoo.
\v 8 Ndani ya mwezi mmoja niliwaangamiza wachungaji watatu, kwa maana sikuwavumilia tena, wao pia walinichukia.
\v 9 Ndipo nilipowaambia wamiliki, "Sitafanya kazi kama mchungaji wenu tena. Wakondoo wafao - na wafe; kondoo wanaoangamizwa - na waangamizwe. Na kondoo wasaliao kila mmoja ale nyama ya jirani yake."
\s5
\v 10 Hivyo nikaichukua fimbo yangu "Neema" na nikaivunja kuvunja agano nililokuwa nimelifanya na kabila zangu zote.
\v 11 Katika siku hiyo agano lilivunjwa, na wale wanaoshughulika na kondoo na waliokuwa wakiniangalia walifahamu kwamba Yahwe amesema.
\v 12 Nikawaambia, "Ikiwa itawapendeza, nilipeni ujira wangu. Kama sivyo, msifanye hivyo." Hivyo wakapima ujira wangu - vipande thelathini vya fedha.
\s5
\v 13 Kisha Yahwe akaniambia, "Weka fedha katika hazina, thamani nzuri zaidi ambayo walikupa!" Hivyo nikachukua vipande thelathini vya fedha na kuviweka katika hazina ndani ya nyumbani Yahwe.
\v 14 Kisha nikavunja fimbo yangu ya pili, "Umoja," kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli.
\s5
\v 15 Yahwe akaniambia, "Tena, chukua chombo cha mchungaji mpumbavu kwa ajili yako mwenyewe,
\v 16 kwa maana tazama, niko tiyari kumweka mahali mchungaji katika nchi. Hataangalia kondoo wanaoangamia. Hatatafuta kondoo wapoteao, wala kuwaponya kondoo wachechemeao. Hatawalisha kondoo wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo walionona naye atapasua kwato zao.
\s5
\v 17 Ole kwa wachungaji wasiofaa wanaoliacha kundi la kondoo! Upanga na uje dhidi ya mkono wake na jicho lake la kulia! Mkono wake na ukauke na jicho lake la kulia lipofuke!
\s5
\c 12
\p
\v 1 Hili ni tamko la neno la Yahwe kwa Israeli - Bwana asema, azitandaye mbingu na kuweka msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mtu ndani yake,
\v 2 "Tazama, nitaifanya Yerusalemu kuwa kikombe kiwafadhaishacho watu wote wamzungukao. Itakuwa hivyo hivyo pia kwa Yuda wakati wa kuhusuriwa kwa Yerusalemu.
\v 3 Katika siku hiyo, nitaifanya Yerusalemu kuwa jiwe zito kwa watu wa jamaa zote. Kila atakayejaribu kuliinua jiwe hilo atajihumiza sana, na mataifa yote ya dunia yatakusanyika kinyume cha mji huo.
\s5
\v 4 Katika siku hiyo asema Yahwe - nitampiga kila farasi kwa ushangao na kila mpanda farasi kwa wendawazimu. Nitaiangalia nyumba ya Yuda kwa upendeleo na nami nitawapiga kwa upofu farasi wa majeshi.
\v 5 Ndipo watawala wa Yuda watakapojisemea mioyoni mwao, 'Wakaao Yerusalemu ndio nguvu yetu kwa sababu ya Yahwe wa majeshi, Mungu wao.'
\s5
\v 6 Katika siku hiyo nitawafanya watawala wa Yuda kuwa kama mitungi ya moto katika miti na kama miali ya moto kati ya nafaka isimamayo, kwani utateketeza watu wote walio karibu upande wao wa kulia na kushoto. Yerusalemu atakaa mahali pake tena.
\s5
\v 7 Yahwe ataziokoa hema za Yuda kwanza, ili kwamba utukufu ya nyumba ya Daudi na utukufu wa wale waishio Yerusalemu hautazidi sehemu iliyosalia ya Yuda.
\v 8 Katika siku hiyo Yahwe atakuwa mtetezi wa wakao Yerusalemu, na siku hiyo waliodhaifu miongoni mwao watakuwa kama Daudi, wakati nyumba ya Daudi watakuwa kama Mungu, kama malaika wa Yahwe mbele yao.
\v 9 "Itakuwa kwamba katika siku hiyo nitaanza kuyaharibu mataifa yote yajayo kinyume cha Yerusalemu.
\s5
\v 10 Lakini nitamwaga roho ya huruma na kuiombea nyumba ya Daudi na wakao Yerusalemu, hivyo wataniangalia mimi, waliomchoma kwa mkuki. Wataniombolezea, kama amwombolezeaye mwana wa pekee; watamwombolezea kwa uchungu sana kama aombolezaye kifo cha mzaliwa wa kwanza.
\v 11 Katika siku hiyo maombolezo huko Yerusalemu yatakuwa kama maombolezo ya Hadadi Rimoni katika tambarare za Megido.
\s5
\v 12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi utakuwa peke yake na wake zao watakuwa peke yao mbali na wanaume. Ukoo wa nyumba ya Nathani utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume.
\v 13 Ukoo wa nyumba ya Lawi utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume. Ukoo wa Washimei utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume.
\v 14 Kila ukoo uliosalia - kila mmoja utakuwa peke yake na wake watakuwa pekee mbali na waume.
\s5
\c 13
\p
\v 1 Katika siku hiyo kijito kitafunguliwa kwa ajili ya nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, kwa ajili ya dhambi na uchafu wao.
\v 2 Katika siku hiyo - asema Yahwe wa majeshi - kwamba nitaondoa majina ya sanamu katika nchi ili kwamba yasikumbukwe tena. Nitawaondoa pia katika nchi manabii wa uongo na roho wao mchafu
\s5
\v 3 Ikiwa mtu yeyote ataendelea kutoa unabii, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, 'Hautaishi, kwa kuwa umenena uongo kwa jina la Yahwe! Ndipo baba na mama waliomzaa watakapomchoma wakati akitabiri.
\s5
\v 4 Katika siku hiyo kila nabii ataonea aibu maono yake aelekeapo kutoa unabii. Manabii hawa hawatavaa tena vazi la singa, ili kuwadanganya watu.
\v 5 Kwa maana kila mmoja atasema, 'Mimi siyo nabii! mimi ni mkulima, kwa maana ardhi ndiyo kazi yangu tangu ujana wangu!
\v 6 Lakini mtu mwingine atamwambia, 'Majeraha haya kati ya mikono yako ni ya nini?' naye atajibu, nilijeruhiwa na waliokuwa katika nyumba ya rafiki zangu."
\s5
\v 7 Upanga! inuka mwenyewe dhidi ya mchungaji wangu, mtu asimamaye karibu nami - hivi ndivyo asemavyo Yahwe wa majeshi. Mpige mchungaji, na kondoo watatawanyika! Kwa maana nitageuza mkono wangu dhidi ya wadogo.
\s5
\v 8 Kisha itakuwa kwamba katika nchi yote - hivi ndivyo asemavyo Yahwe - kwamba theluthi mbili yake itaondolewa! Watu hao wataangamia; theluthi moja tu ndiyo itakayosalia.
\v 9 Nitaipitisha hiyo ya tatu motoni na kuwasafisha kama fedha isafishwavyo; nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo. Wataliitia jina langu nami nitawajibu na kusema, 'Hawa ni watu wangu!' nao watasema, Yahwe ndiye Mungu wangu!"
\s5
\c 14
\p
\v 1 Tazama! Siku ya Yahwe inakuja wakati mateka wenu watakapogawanywa katikati yenu.
\v 2 Kwa maana nitayakusanya mataifa yote kinyume cha Yerusalemu kwa vita na mji utatekwa. Nyumba zitatekwa na wanawake watabakwa. Nusu ya mji itapelekwa matekani, lakini kumbukumbu ya watu haitaondolewa mjini.
\s5
\v 3 Lakini Yahwe ataondoka na kufanya vita dhidi ya mataifa kama apigavyo vita katika siku ya vita.
\v 4 Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, uliopo kando ya Yerusalemu upande wa mashariki. Mlima wa Mizeituni utagawanyika katikati kati ya mashariki na magharibi kwa bonde kubwa sana na nusu ya mlima itarudi nyuma kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.
\s5
\v 5 Ndipo mtakapokimbia katika bonde kati ya milima ya Yahwe, kwa kuwa bonde kati ya hiyo milima litafika hata Azali. Mtakimbia kama siku mliyokimbia tetemeko la nchi siku za Uzia, mfalme wa Yuda. Ndipo Yahwe Mungu wangu atakapokuja na watakatifu wake wote.
\s5
\v 6 Hakutakuwa na nuru katika siku hiyo, lakini hakuna baridi wala barafu.
\v 7 Siku hiyo, siku aijuaye Yahwe peke yake, hakutakuwa tena na mchana wala usiku, kwani jioni itakuwa wakati wa nuru.
\v 8 Siku hiyo maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu. Nusu yake yatatiririka kuelekea bahari ya mashariki na nusu bahari ya magharibi, wakati wa masika na wakati wa kiangazi.
\s5
\v 9 Yahwe atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo kutakuwa na Yahwe, Mungu mmoja, na jina lake pekee.
\v 10 Nchi yote itakuwa kama Araba, kuanzia Geba hadi Rimoni kusini mwa Yerusalemu. Na Yerusalemu itaendelea kuwa juu. Ataishi mahali pake mwenyewe, kutoka lango la Benjamini hata mahali lilipokuwa lango la kwanza, hata Lango la Pembeni, na kutoka Mnara wa Hananeli hata shinikizo la mfalme.
\v 11 Watu watakaa Yerusalemu na hakutakuwa na maangamizi kamili tena kutoka kwa Mungu dhidi yao. Yerusalemu itakuwa salama.
\s5
\v 12 Hii itakuwa tauni ambayo kwayo Yahwe atawapiga jamaa zote za watu wapigao vita juu ya Yerusalemu: miili yao itaoza hata wakiwa wamesimama kwa miguu yao. Macho yao yataoza katika matundu yake na ndimi zao zitaoza katika vinywa vyao.
\v 13 Siku hiyo ile hofu kuu kutoka kwa Yahwe itakuwa miongoni mwao. Kila mmoja ataushika mkono wa mwingine, na mkono wa mwingine utainuliwa kinyume cha mkono wa mwenzake.
\s5
\v 14 Yuda pia atapigana na Yerusalemu. Watakusanya utajiri wa mataifa yote yanayowazunguka - dhahabu, fedha, na wingi wa nguo safi.
\v 15 Tauni itakuwa pia juu ya farasi na nyumbu, ngamia na punda, na kila mnyama katika kambi hizo atapigwa kwa hilo pigo.
\s5
\v 16 Kisha itakuwa wote watakaosalia katika mataifa yaliyo kinyume na Yerusalemu watakwenda mwaka kwa mwaka kumwabudu mfalme, Yahwe wa majeshi, na kutunza Sikukuu ya Vibanda.
\v 17 Na itakuwa kwamba ikiwa mtu yeyote kutoka katika mataifa yote ya dunia haendi Yerusalemu kumwabudu mfalme, Yahwe wa majeshi, ndipo Yahwe hataleta mvua juu yao.
\v 18 Na ikiwa nchi ya Misri hawatakwenda, ndipo hawatapata mvua. Tauni kutoka kwa Yahwe itayashambulia mataifa yote yasiyokwea kutunza Sikukuu ya Vibanda.
\s5
\v 19 Hii itakuwa ni adhabu kwa Misri na adhabu kwa kila taifa lisilopanda kutunza Sikukuu ya Vibanda.
\s5
\v 20 Lakini katika siku hiyo, kengele za farasi zitasema, "Jitengeni kwa ajili ya Yahwe," na makalai katika nyumba ya Yahwe yatakuwa kama mabakuri mbele ya madhabahu.
\v 21 Kwa kuwa kila chungu katika Yerusalemu na Yuda kitatengwa kwa ajili ya Yahwe wa majeshi na kila mmoja aletaye sadaka atakula ndani yake na kuyachemshia. Hakutakuwa na wafanyabiashara tena katika nyumba ya Yahwe wa majeshi siku hiyo.

View File

@ -1,36 +1,41 @@
---
dublin_core:
dublin_core:
conformsto: 'rc0.2'
contributor:
- "Alfred Danjuma"
- "Bariki Malisa"
- "Christina Abraham Kileo"
- "Cloud Roman"
- "Compiler"
- "Daniel Marura Chacha"
- "Danjuma_alfred_h"
- "Dina Mast"
- "Dina Roman"
- "Donald Shadarck Dutuyi"
- "Emmanuel Masanja Mbaaga"
- "Emmanuel Nyamalya"
- "Erasmus Peter Malelo"
- "Ev. Lazaro Chalomhola"
- "Ezekiel Manala"
- "Fred"
- "Gabriel Gidale"
- "Gabriel Gidale Merus"
- "Gabriel Lwitakubi Mazige"
- "James Makula"
- "James Semnkai"
- "Jeremiah Masasi"
- "Jesse Katabi Masolwa"
- "John Ojasi"
- "Joyce Gilbert Masasi"
- "Karen Riecks"
- "Kazwanomo"
- "Kennedy"
- "Ker"
- "Lameck Yakobo Tobotobo"
- "Ev. Lazaro Chalomhola"
- "Laurent Petro Malelo"
- "Lazarus David Chalomhola"
- "Majama, Musa Isaya"
- "Makene Mafwele"
- "Marco Luma Mahushi"
- "Mathew Nkusa"
- "Mathias William"
- "Mr. James Semnkai .It."
- "Musa Isaya Majama"
- "Musa Luzali"
- "Pastor John Kerim"
- "Pastor Jordan"
@ -42,21 +47,24 @@ dublin_core:
- "Sadiki Kulwa"
- "Samson Nungwana"
- "Thobias Kazwanomo"
- "Yohana Dutuyi"
- "Yohana Magera"
- "Zelote Loilang'akaki Lukumay"
creator: 'Door43 World Missions Community'
description: 'An unrestricted literal Bible'
format: 'text/usfm'
identifier: 'ulb'
issued: '2017-11-14'
issued: '2018-09-27'
language:
direction: 'ltr'
identifier: 'sw'
title: 'Swahili'
modified: '2017-11-14'
modified: '2018-09-27'
publisher: 'Door43'
relation:
- 'sw/tn'
- 'sw/tq'
- 'sw/tw'
- 'sw/udb'
rights: 'CC BY-SA 4.0'
source:
@ -67,7 +75,7 @@ dublin_core:
subject: 'Bible'
title: 'Swahili Unlocked Literal Bible'
type: 'bundle'
version: '7.1'
version: '7.2'
checking:
checking_entity:
@ -91,10 +99,247 @@ checking:
- "Rev. Yekonia M. Koko"
- "Rev. Elisande Mhanga"
- "Ev. James A. Makula"
checking_level: '3'
projects:
-
title: '1 Mambo ya Nyakati '
versification: ufw
identifier: '1ch'
sort: 13
path: ./13-1CH.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: '1Wafalme '
versification: ufw
identifier: '1ki'
sort: 11
path: ./11-1KI.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: '1Samweli '
versification: ufw
identifier: '1sa'
sort: 9
path: ./09-1SA.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: '2 Mambo ya Nyakati '
versification: ufw
identifier: '2ch'
sort: 14
path: ./14-2CH.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: '2 Wafalme '
versification: ufw
identifier: '2ki'
sort: 12
path: ./12-2KI.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: '2 Samweli '
versification: ufw
identifier: '2sa'
sort: 10
path: ./10-2SA.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Amosi '
versification: ufw
identifier: 'amo'
sort: 30
path: ./30-AMO.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Danieli '
versification: ufw
identifier: 'dan'
sort: 27
path: ./27-DAN.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Mhubiri '
versification: ufw
identifier: 'ecc'
sort: 21
path: ./21-ECC.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Esta '
versification: ufw
identifier: 'est'
sort: 17
path: ./17-EST.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Kutoka '
versification: ufw
identifier: 'exo'
sort: 2
path: ./02-EXO.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Ezekieli '
versification: ufw
identifier: 'ezk'
sort: 26
path: ./26-EZK.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Ezra '
versification: ufw
identifier: 'ezr'
sort: 15
path: ./15-EZR.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Mwanzo '
versification: ufw
identifier: 'gen'
sort: 1
path: ./01-GEN.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Habakuki '
versification: ufw
identifier: 'hab'
sort: 35
path: ./35-HAB.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Hosea '
versification: ufw
identifier: 'hos'
sort: 28
path: ./28-HOS.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Isaya '
versification: ufw
identifier: 'isa'
sort: 23
path: ./23-ISA.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Waamuzi '
versification: ufw
identifier: 'jdg'
sort: 7
path: ./07-JDG.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Yeremia '
versification: ufw
identifier: 'jer'
sort: 24
path: ./24-JER.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Ayubu '
versification: ufw
identifier: 'job'
sort: 18
path: ./18-JOB.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Joeli '
versification: ufw
identifier: 'jol'
sort: 29
path: ./29-JOL.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Yona '
versification: ufw
identifier: 'jon'
sort: 32
path: ./32-JON.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Yoshua '
versification: ufw
identifier: 'jos'
sort: 6
path: ./06-JOS.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Maombolezo '
versification: ufw
identifier: 'lam'
sort: 25
path: ./25-LAM.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Mambo ya Walawi '
versification: ufw
identifier: 'lev'
sort: 3
path: ./03-LEV.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Mika '
versification: ufw
identifier: 'mic'
sort: 33
path: ./33-MIC.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Nehemia '
versification: ufw
identifier: 'neh'
sort: 16
path: ./16-NEH.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Hesabu '
versification: ufw
identifier: 'num'
sort: 4
path: ./04-NUM.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Obadia '
versification: ufw
identifier: 'oba'
sort: 31
path: ./31-OBA.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Zaburi '
versification: ufw
identifier: 'psa'
sort: 19
path: ./19-PSA.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Ruth '
versification: ufw
identifier: 'rut'
sort: 8
path: ./08-RUT.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Wimbo wa Sulemani '
versification: ufw
identifier: 'sng'
sort: 22
path: ./22-SNG.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Zekaria '
versification: ufw
identifier: 'zec'
sort: 38
path: ./38-ZEC.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Sefania '
versification: ufw
identifier: 'zep'
sort: 36
path: ./36-ZEP.usfm
categories: [ 'bible-ot' ]
-
title: 'Mathayo '
versification: 'ufw'