Thu Mar 17 2022 09:27:35 GMT+0200 (South Africa Standard Time)

This commit is contained in:
Tomussone José Machinga 2022-03-17 09:27:37 +02:00
commit 55581e8e81
200 changed files with 266 additions and 0 deletions

1
01/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Paulo, mtumishi wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu. \v 2 Hii ndio ile Injili aliyoiahidi zamani kupitia manabii wake katika maandiko matakatifu. \v 3 Ni kuhusu Mwana wake, aliyezaliwa kutoka ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili.

1
01/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Yeye alitangazwa kwa Mwana wa Mungu kwa nguvu ya Roho ya utakatifu kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu. \v 5 Kupitia yeye tumepokea neema na utume kwa utii wa imani kati ya mataifa yote, kwa ajili ya jina lake. \v 6 Kati ya mataifa haya, ninyi pia mmeitwa kuwa wa Yesu Kristo.

1
01/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Barua hii ni kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watu watakatifu. Neema na iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

1
01/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Kwanza, namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima. \v 9 Kwa maana Mungu ni shahidi wangu, ambaye ninamtumikia kwa roho yangu katika injili ya Mwana wake, jinsi ninavyodumu katika kuwataja. \v 10 Daima naomba katika sala zangu kwamba kwa njia yoyote nipate mwishowe kuwa na mafanikio sasa kwa mapenzi ya Mungu katika kuja kwenu.

1
01/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Maana natamani kuwaona, ili nipate kuwapa ninyi baadhi ya karama za rohoni, nipate kuwaimarisha. \v 12 Yaani, natazamia kutiwa moyo pamoja nanyi, kwa njia ya imani ya kila mmoja wetu, yenu na yangu.

1
01/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Sasa ndugu, sitaki mkose kufahamu kwamba, mara nyingi nimekusudia kuja kwenu, lakini nimezuiliwa mpaka sasa. Nilitaka hivi ili kuwa na matunda kwenu kama ilivyo pia miongoni mwa watu wa mataifa. \v 14 Nadaiwa na Wayunani na wageni pia, werevu na wajinga. \v 15 Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi niko tayari kutangaza injili kwenu pia ninyi mlio huko Roma.

1
01/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Kwa maana siionei haya injili, kwa kuwa ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia. \v 17 Kwa maana haki ya Mungu imedhihirishwa kutoka imani hata imani, kama ilivyo andikwa, "Mwenye haki ataishi kwa imani."

1
01/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa watu, ambao kwa njia ya udhalimu huificha kweli. \v 19 Hii ni kwa sababu, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao. Maana Mungu amewafahamisha.

1
01/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Maana mambo yake yasioonekana vizuri yamekuwa wazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Yanaeleweka kupitia vitu vilivyoumbwa. Mambo haya ni uwezo wake wa milele na asili ya uungu. Matokeo yake, watu hawa hawana udhuru. \v 21 Hii ni kwa sababu, ingawa walijua kuhusu Mungu, hawakumtukuza yeye kama Mungu, wala hawakumpa shukrani. Badala yake, wamekuwa wapumbavu katika mawazo yao, na mioyo yao yenye ujinga ilitiwa giza.

1
01/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Walijiita kuwa ni werevu, lakini wakawa wajinga. \v 23 Waliubadili utukufu wa Mungu asie na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, ya wanyama wenye miguu minne, na ya viumbe vitambaavyo.

1
01/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa za mioyo yao kwa uchafu, kwa miili yao kufedheheshwa baina yao. \v 25 Ni wao walioibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, na ambao waliabudu na kutumikia viumbe badala ya Muumbaji, ambaye anasifiwa milele. Amina.

1
01/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, kwa kuwa wanawake wao walibadilisha matumizi yao ya asili kwa kile kilicho kinyume na asili. \v 27 Hali kadhalika, wanaume pia wakaacha matumizi yao ya asili kwa wanawake na kuwakwa na tamaa dhidi yao wenyewe. Hawa walikuwa wanaume ambao walifanya na wanaume wenzao yasiyo wapasa, na ambao walipokea adhabu iliyostahili upotovu wao.

1
01/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Kwa sababu walikataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye mambo yale yasiyofaa.

1
01/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Wamejawa na udhalimu wote, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu, na nia mbaya. \v 30 Wao pia ni wasengenyaji, wasingiziaji, na wenye kumchukia Mungu. Wenye vurugu, kiburi, na majivuno. Wao ni watunga mabaya, na wasiotii wazazi wao. \v 31 Wao hawana ufahamu; wasioaminika, hawana mapenzi ya asili, na wasio na huruma.

1
01/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Wanaelewa kanuni za Mungu, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo wanastahili kifo. Lakini si tu wanafanya mambo hayo, wao pia wanakubaliana na wale wanaofanya mambo hayo.

1
02/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kwa hiyo hauna udhuru, wewe uhukumuye, kwa maana katika yale uhukumuyo mwingine wajitia hatiani mwenyewe. Kwa maana wewe uhukumuye unafanya mambo yale yale. \v 2 Lakini twajua kwamba hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao mambo kama hayo.

1
02/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Lakini wewe tafakari hili, wewe ambaye unahukumu wale wanaotenda mambo hayo ingawa nawe unafanya mambo yayo hayo. Je utaepuka hukumu ya Mungu? \v 4 Au unafikiri kidogo sana juu ya wingi wa wema wake, kuchelewa kwa adhabu yake, na uvumilivu wake? Je, hujui kwamba wema wake unapaswa kukuelekeza katika toba?

1
02/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako na kwa moyo wako usio na toba wajiwekea mwenyewe akiba ya ghadhabu kwa siku ile ya ghadhabu, yaani, siku ile ya ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu. \v 6 Yeye atamlipa kila mtu kipimo sawa na matendo yake: \v 7 kwa wale ambao kwa uthabiti wa matendo mema wametafuta sifa, heshima na kutokuharibika, atawapa uzima wa milele.

1
02/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Lakini kwa wale ambao ni wabinafsi, wasioitii kweli bali hutii dhuluma, ghadhabu na hasira kali itakuja. \v 9 Mungu ataleta dhiki na shida juu ya kila nafsi ya binadamu aliyefanya uovu, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

1
02/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Lakini sifa, heshima na amani itakuja kwa kila mtu atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. \v 11 Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. \v 12 Kwa maana kama vile wengi waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na kama vile wengi waliokosa kulingana na sheria watahukumiwa kwa sheria.

1
02/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Maana si wasikiaji wa sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. \v 14 Kwa maana watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanafanya kwa asili mambo ya sheria, wao, wamekuwa sheria kwa nafsi zao, ingawa wao hawana sheria.

1
02/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Kwa hili wanaonesha kwamba matendo yanayohitajika kwa mujibu wa sheria yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia zinawashuhudia wao, na mawazo yao wenyewe ama huwashitaki au huwalinda wao wenyewe \v 16 na pia kwa Mungu. Haya yatatokea katika siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu wote, sawasawa na injili yangu, kwa njia ya Yesu Kristo.

1
02/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Tuseme kwamba unajiita mwenyewe Myahudi, aliyekaa katika sheria, shangilia kwa kujisifu katika Mungu, \v 18 yajue mapenzi yake, na kupima mambo ambayo yanatofautiana nayo, baada ya kuagizwa na sheria. \v 19 Na tuseme kwamba una ujasiri kwamba wewe mwenyewe ni kiongozi wa kipofu, mwanga kwa wale walio gizani, \v 20 msahihishaji wa wajinga, mwalimu wa watoto, na kwamba unayo katika sheria jinsi ya elimu na kweli.

1
02/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Wewe basi, uhubiriye mwingine, je, hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kutokuiba, je wewe huiba? \v 22 Wewe usemae usizini, je unazini? Wewe uchukiaye sanamu, je unaiba hekaluni?

1
02/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Wewe ujisifuye katika sheria, je haumfedheheshi Mungu katika kuvunja sheria? \v 24 Kwa maana "jina la Mungu linafedheheshwa kati ya watu wa mataifa kwa sababu yenu," kama ilivyoandikwa.

1
02/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Kwa maana Kutahiriwa kweli kwafaa kama ukitii sheria, lakini kama wewe ni mkiukaji wa sheria, kutahiriwa kwako kunakuwa kutokutahiriwa. \v 26 Basi, ikiwa, mtu asiyetahiriwa anaendelea kushika matakwa ya sheria, je kutokutahiriwa kwake hakutachukuliwa kana kwamba ametahiriwa? \v 27 Na yeye asiyetahiriwa kwa asili hatakuhukumu kama akitimiza sheria? Hii ni kwa sababu una maandiko yaliyoandikwa na tohara pia lakini bado u mkiukaji wa sheria!

1
02/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Kwa maana yeye si Myahudi aliye kwa hali ya nje; wala kutahiriwa si kule ambako ni kwa nje tu katika mwili. \v 29 Lakini yeye ni Myahudi aliye kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko. Sifa ya mtu wa namna hiyo haitokani na watu bali yatoka kwa Mungu.

1
03/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kisha ni faida gani aliyo nayo Myahudi? Na faida ya tohara ni nini? \v 2 Ni vyema sana kwa kila njia. Awali ya yote, Wayahudi walikabidhiwa ufunuo kutoka kwa Mungu.

1
03/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Lakini, itakuwaje iwapo baadhi ya Wayahudi hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kuwa batili? \v 4 La hasha. Badala yake, acha Mungu aonekane kuwa kweli, hata kama kila mtu ni mwongo. Kama ilivyokuwa imeandikwa, "Ya kwamba uweze kuonekana kuwa mwenye haki katika maneno yako, na uweze kushinda uingiapo katika hukumu."

1
03/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Lakini ikiwa uovu wetu unaonesha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu si dhalimu atoapo ghadhabu yake, je yupo hivyo? Naongea kutokana na mantiki ya kibinadamu. \v 6 La hasha! Ni jinsi gani basi Mungu atauhukumu ulimwengu?

1
03/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Lakini ikiwa kweli ya Mungu kupitia uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado nahukumiwa kama mwenye dhambi? \v 8 Kwa nini tusiseme, kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyothibitisha kwamba tunasema, "Tufanye uovu, ili mema yaje"? Hukumu juu yao ni ya haki.

1
03/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Ni nini basi? Tunajitetea wenyewe? Hapana kabisa. Kwa kuwa sisi tayari tumewatuhumu Wayahudi na Wayunani wote pamoja, ya kuwa wapo chini ya dhambi. \v 10 Hii ni kama ilivyoandikwa: "Hakuna mwenye haki, hata mmoja.

1
03/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Hakuna mtu ambaye anaelewa. Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu. \v 12 Wote wamegeuka. Wao kwa pamoja wamekuwa hawana maana. Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja.

1
03/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Makoo yao ni kaburi lililo wazi. Ndimi zao zimedanganya. Sumu ya nyoka ipo chini ya midomo yao. \v 14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.

1
03/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu. \v 16 Uharibifu na mateso yapo katika njia zao. \v 17 Watu hawa hawajajua njia ya amani. \v 18 Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao."

1
03/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Sasa tunajua kwamba chochote sheria isemacho, husema na wale walio chini ya sheria. Hii ni ili kwamba kila kinywa kifungwe, na hivyo kwamba ulimwengu wote uweze kuwajibika kwa Mungu. \v 20 Hii ni kwa sababu hakuna mwili utakaohesabiwa haki kwa matendo ya sheria mbele za macho yake. Kwa kuwa kupitia Sheria huja ufahamu wa dhambi.

1
03/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Lakini sasa pasipo sheria, haki ya Mungu imejulikana. Ilishuhudiwa kwa sheria na Manabii, \v 22 hiyo ni, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Maana hakuna tofauti.

1
03/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. \v 24 Wamehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.

1
03/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Kwa maana Mungu alimtoa Kristo Yesu awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alimtoa Kristo kama ushahidi wa haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizopita \v 26 katika uvumilivu wake. Haya yote yalitokea ili kuonesha haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kujithibitisha mwenyewe kuwa haki, na kuonesha kwamba humhesabia haki mtu yeyote kwa sababu ya imani katika Yesu.

1
03/27.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 27 Kuwapi basi kujisifu? Kumetengwa. Kwa misingi ipi? Misingi ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani. \v 28 Hivyo tunahitimisha kwamba mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.

1
03/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Je yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Ndiyo, wa mataifa pia. \v 30 Ikiwa kwa kweli Mungu ni mmoja, atawahesabia haki walio wa tohara kwa imani, na wasiotahiriwa kwa njia ya imani.

1
03/31.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 31 Je sisi twaibatilisha sheria kwa imani? La hasha! Kinyume cha hayo, sisi twaithibitisha sheria.

1
04/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Tutasema nini tena kwamba Abrahamu, baba yetu kwa jinsi ya mwili, amepatikana? \v 2 Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, angekuwa na sababu ya kujisifu, lakini si mbele za Mungu. \v 3 Kwani maandiko yanasemaje? "Abrahamu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki."

1
04/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Sasa kwa mtu afanyaye kazi, malipo yake hayahesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. \v 5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtaua, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

1
04/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Daudi pia hunena baraka juu ya mtu ambaye Mungu amhesabia haki pasipo matendo. \v 7 Alisema, "Wamebarikiwa wale ambao maovu yao yamesamehewa na ambao dhambi zao zimefunikwa. \v 8 Amebarikiwa mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi."

1
04/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Basi je baraka hizi ni kwa wale waliotahiriwa tu, au pia kwa wale wasiotahiriwa? Kwa maana twasema, "kwa Abrahamu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki." \v 10 Hivyo ilihesabiwaje basi? Wakati Abrahamu alikuwa katika tohara, au kabla hajatahiriwa? Haikuwa katika kutahiriwa, bali katika kutotahiriwa.

1
04/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Abrahamu alipokea alama ya kutahiriwa. Huu ulikuwa muhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo tayari kabla hajatahiriwa. Matokeo ya ishara hii ni kwamba alifanyika kuwa baba wa wote waaminio, hata kama wapo katika kutotahiriwa. Hii ina maana kwamba haki itahesabiwa kwao. \v 12 Hii pia ilimaanisha kuwa Abrahamu alifanyika baba wa tohara si tu kwa wale wanaotokana na tohara, bali pia wale wanaozifuata nyayo za baba yetu Abrahamu. Na hii ndiyo imani aliyokuwa nayo kwa wasiotahiriwa.

1
04/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Kwa maana haikuwa kwa sheria kwamba ahadi ilitolewa kwa Abrahamu na uzao wake, ahadi hii ya kwamba watakuwa warithi wa dunia. isipokuwa, ilikuwa kupitia haki ya imani. \v 14 Kwa maana kama wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika. \v 15 Kwa sababu sheria huleta ghadhabu, lakini pale ambapo hakuna sheria, pia hakuna kutotii.

1
04/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Kwa sababu hii hili hutokea kwa imani, ili iwe kwa neema. Matokeo yake, ahadi ni dhahiri kwa uzao wote. Na wazawa hawa si tu wale wanaojua sheria, bali pia wale ambao ni wa imani ya Abrahamu. Kwa maana yeye ni baba yetu sisi sote, \v 17 kama ilivyoandikwa, "Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi." Abrahamu alikuwa katika uwepo wa yule aliyemwamini, yaani, Mungu ambaye huwapa wafu uzima na kuyaita mambo ambayo hayapo ili yaweze kuwepo.

1
04/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Licha ya hali zote za nje, Abrahamu kwa ujasiri alimuamini Mungu kwa siku zijazo. Hivyo akawa baba wa mataifa mengi, kulingana na kile kilichonenwa,"... Ndivyo utakavyokuwa uzao wako." \v 19 Yeye hakuwa dhaifu katika imani. Abrahamu alikiri kwamba mwili wake mwenyewe ulikwisha kufa - alikuwa na umri wa karibu miaka mia moja. Pia alikubaliana na hali ya kufa ya tumbo la Sara.

1
04/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Lakini kwa sababu ya ahadi ya Mungu, Abrahamu hakusita katika kutokuamini. Bali, alitiwa nguvu katika imani na alimsifu Mungu. \v 21 Alikuwa akijua hakika ya kuwa kile ambacho Mungu ameahidi, alikuwa pia na uwezo wa kukikamilisha. \v 22 Kwa hiyo hii pia ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

1
04/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Sasa haikuandikwa tu kwa faida yake, kwamba ilihesabiwa kwake. \v 24 Iliandikwa kwa ajili yetu pia, kwa waliowekewa kuhesabiwa, sisi ambao tunaamini katika yeye aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka wafu. \v 25 Huyu ni yule ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.

1
05/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa njia ya imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. \v 2 Kupitia yeye sisi pia tuna fursa kwa njia ya imani katika neema hii ambayo ndani yake tunasimama. Tunafurahi katika ujasiri atupao Mungu kwa ajili ya baadaye, ujasiri ambao tutashiriki katika utukufu wa Mungu.

1
05/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu. \v 4 Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye. \v 5 Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu.

1
05/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Kwa tulipokuwa tungali tu dhaifu, kwa wakati muafaka Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. \v 7 Kwa kuwa itakuwa vigumu mmoja kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki. Hii ni kwamba, pengine mtu angethubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.

1
05/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Lakini Mungu amehakikisha upendo wake mwenyewe kwetu, kwa sababu wakati tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. \v 9 Kisha zaidi ya yote, sasa kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa damu yake, tutaokolewa kwa hiyo kutoka katika gadhabu ya Mungu.

1
05/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Kwa kuwa, ikiwa wakati tulipokuwa maadui, tulipatanishwa na Mungu kwa njia ya kifo cha mwanae, zaidi sana, baada ya kuwa tumekwisha patanishwa, tutaokolewa kwa maisha yake. \v 11 Siyo hivi tu, bali pia tunafurahi katika Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo, kupitia yeye ambaye sasa tumepokea upatanisho huu.

1
05/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Kwa hiyo basi, kama kupitia mtu mmoja dhambi iliingia duniani, kwa njia hii kifo kiliingia kwa njia ya dhambi. Na kifo kikasambaa kwa watu wote, kwa sababu wote walifanya dhambi. \v 13 Kwa kuwa hadi sheria, dhambi ilikuwa duniani, lakini dhambi haihesabiki wakati hakuna sheria.

1
05/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Hata hivyo, kifo kilitawala kutoka Adamu hadi Musa, hata juu ya wale ambao hawakufanya dhambi kama kutotii kwa Adamu, ambaye ni mfano wa yeye ambaye angekuja. \v 15 Lakini hata hivyo, zawadi ya bure si kama kosa. Kwa kuwa ikiwa kwa kosa la mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na zawadi kwa neema ya mtu mmoja, Yesu Kristo, imezidi kuongezeka kwa wengi.

1
05/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Kwa kuwa zawadi si kama matokeo ya yule ambaye alifanya dhambi. Kwa kuwa kwa upande mwingine, hukumu ya adhabu ilikuja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Lakini kwa upande mwingine, kipawa cha bure kinachotoka katika kuhesabiwa haki kilikuja baada ya makosa mengi. \v 17 Kwa maana, ikiwa kwa kosa la mmoja, kifo kilitawala kupitia mmoja, zaidi sana wale ambao watapokea neema nyingi pamoja na kipawa cha haki watatawala kupitia maisha ya mmoja, Yesu Kristo.

1
05/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Hivyo basi, kama kupitia kosa moja watu wote walikuja kwenye hukumu, ingawa kupitia tendo moja la haki kulikuja kuhesabiwa haki ya maisha kwa watu wote. \v 19 Kwa kuwa kama kupitia kutotii kwa mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, hivyo kupitia utii wa mmoja wengi watafanywa wenye haki.

1
05/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Lakini sheria iliingia pamoja, ili kwamba kosa liweze kuenea. Lakini mahali ambapo dhambi ilizidi kuwa nyingi, neema iliongezeka hata zaidi. \v 21 Hii ilitokea ili kwamba, kama dhambi ilivyotawala katika kifo, ndivyo hata neema inaweza kutawala kupitia haki kwa ajili ya maisha ya milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.

1
06/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Tuseme nini basi? Tuendelee katika dhambi ili neema iongezeke? \v 2 La hasha. Sisi tuliokufa katika dhambi, tunawezaje tena kuishi katika hiyo? \v 3 Je hamjui ya kuwa wale waliobatizwa katika Kristo walibatizwa katika mauti yake?

1
06/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Tulikuwa tumezikwa pamoja naye kupitia ubatizo katika kifo. Hii ilifanyika ili kwamba kama vile Kristo alivyoinuliwa kutoka mauti kupitia utukufu wa Baba, ili kwamba nasi tuweze kutembea katika upya wa maisha. \v 5 Maana ikiwa tumeunganishwa pamoja naye katika mfano wa kifo chake, pia tutaunganishwa katika ufufuo wake.

1
06/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Sisi tunajua hivi, utu wetu wa zamani ulisulubiwa pamoja naye, ili kwamba mwili wa dhambi uharibiwe. Hii ilitokea ili kwamba tusiendelee kuwa watumwa wa dhambi. \v 7 Yeye aliyekufa amefanywa mwenye haki kulingana na dhambi.

1
06/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Lakini kama tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi pamoja naye pia. \v 9 Tunajua kwamba Kristo amefufuliwa kutoka katika wafu, na kwamba si mfu tena. Kifo hakimtawali tena.

1
06/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Maana kwa habari ya kifo alichokufa kwa dhambi, alikufa mara moja kwa ajili ya wote. Hata hivyo, maisha anayoishi, anaishi kwa ajili ya Mungu. \v 11 Kwa njia iyo hiyo, nanyi pia mnapaswa kujihesabu kuwa wafu katika dhambi, bali hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

1
06/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Kwa sababu hiyo usiruhusu dhambi itawale mwili wako ili kusudi uweze kuzitii tamaa zake. \v 13 Usitoe sehemu za mwili wako katika dhambi kama vyombo visivyo na haki, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu, kama walio hai kutoka mautini. Na zitoeni sehemu za miili yenu kama vyombo vya haki kwa Mungu. \v 14 Msiiruhusu dhambi iwatawale. Kwa kuwa hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.

1
06/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Nini basi? Tutende dhambi kwa kuwa hatupo chini ya sheria, bali chini ya neema? La hasha. \v 16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa wenyewe kama watumishi ndiye ambaye ninyi mnakuwa watumishi wake, yeye mnayepaswa kumtii? Hii ni kweli hata kama ninyi ni watumwa katika dhambi ambayo inapelekea mauti, au watumwa wa utii unaopelekea haki.

1
06/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Lakini ashukuriwe Mungu! Kwa kuwa mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mmetii kutoka moyoni ile namna ya fundisho mliopewa. \v 18 Mmefanywa huru kutoka kwenye dhambi, na mmefanywa watumwa wa haki.

1
06/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Ninazungumza kama mtu kwa sababu ya madhaifu ya miili yenu. Kwa maana kama vile mlivyotoa viungo vya miili yenu kuwa watumwa kwa uchafu na uovu, kwa jinsi iyo hiyo, sasa toeni viungo vya miili yenu kuwa watumwa wa haki kwa utakaso. \v 20 Kwa kuwa mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. \v 21 Kwa wakati huo, mlikuwa na tunda lipi kwa mambo ambayo kwa sasa mnaona aibu kwayo? Kwa kuwa matokeo ya mambo hayo ni kifo.

1
06/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Lakini kwa kuwa sasa mmefanywa huru mbali na dhambi na mmefanyika watumwa kwa Mungu, mna tunda kwa ajili ya utakaso. Tokeo ni uzima wa milele. \v 23 Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, bali zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

1
07/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Au hamjui, ndugu zangu (kwa kuwa naongea na watu wanaoijua sheria), kwamba sheria humtawala mtu anapokuwa hai?

1
07/02.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 2 Kwa maana mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria kwa yule mme wake anapokuwa hai, lakini ikiwa mme wake atakufa, atakuwa amewekwa huru kutoka sheria ya ndoa. \v 3 Hivyo basi, wakati mme wake angali akiishi, ikiwa anaishi na mwanamme mwingine, ataitwa mzinzi. Lakini ikiwa mme wake akifa, yuko huru dhidi ya sheria, hivyo hatakuwa mzinzi ikiwa anaishi na mwanamme mwingine.

1
07/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Kwa hiyo, ndugu zangu, ninyi pia mlifanywa wafu kwa sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Imekuwa hivi ili mpate kuunganishwa na mwingine, kwake yeye ambaye alifufuliwa kutoka wafu ili tuweze kumzalia Mungu matunda. \v 5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi ziliamshwa katika viungo vyetu kwa njia ya sheria na kuizalia mauti matunda.

1
07/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Lakini sasa tumefunguliwa kutoka katika sheria. Tumeifia ile hali iliyotupinga. Ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya Roho, na si katika hali ya zamani ya andiko.

1
07/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Tusemeje basi? Sheria ni dhambi? La hasha. Hata hivyo, nisingelitambua dhambi, isingelikuwa kwa njia ya sheria. Kwa kuwa nisingelijua kutamani kama sheria isingelisema, "Usitamani." \v 8 Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri na ikaleta ndani yangu kila aina ya kutamani. Kwa maana dhambi pasipo sheria imekufa.

1
07/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria, lakini ilipokuja ile amri, dhambi ilipata uhai, nami nikafa. \v 10 Ile amri na ambayo ingelileta uzima iligeuka kuwa mauti kwangu.

1
07/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Kwa maana dhambi ilipata nafasi kwa ile amri na ikanidanganya. Kupitia ile amri, iliniua. \v 12 Hivyo sheria ni takatifu, na ile amri ni takatifu, ya yaki, na njema.

1
07/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Hivyo basi ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Isiwe hivyo kamwe. Lakini dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa kupitia ile njema, ilileta mauti ndani yangu. Hii ilikuwa ili kwamba kupitia ile amri, dhambi izidi kuwa mbaya mno. \v 14 Kwa maana twajua ya kuwa sheria asili yake ni ya rohoni, lakini mimi ni mtu wa mwilini. Nimeuzwa chini ya utumwa wa dhambi.

1
07/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Maana nifanyalo, silielewi dhahiri. Kwa kuwa lile nilipendalo kutenda, silitendi, na lile nilichukialo, ndilo ninalolitenda. \v 16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, nakubaliana na sheria ya kuwa sheria ni njema.

1
07/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Lakini sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. \v 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai jambo jema. Kwa kuwa tamaa ya lililo jema imo ndani yangu, lakini silitendi.

1
07/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi, bali lile ovu nisilolipenda ndilo nilitendalo. \v 20 Sasa kama natenda lile nisilolipenda, si mimi binafsi nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. \v 21 Nimefahama, tena, imo kanuni ndani yangu ya kutaka kutenda lililo jema, lakini uovu hakika umo ndani yangu.

1
07/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani. \v 23 Lakini naona kanuni iliyo tofauti katika viungo vya mwili wangu. Inapiga vita dhidi ya kanuni mpya katika akili zangu. Inanifanya mimi mateka kwa kanuni ya dhambi iliyo katika viungo vya mwili wangu.

1
07/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Mimi ni mtu wa huzuni! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? \v 25 Lakini shukrani kwa Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi. Mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu. Bali, kwa mwili naitumikia kanuni ya dhambi.

1
08/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. \v 2 Kwa kuwa kanuni ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imenifanya mimi kuwa huru mbali na kanuni ya dhambi na mauti.

1
08/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya. Alimtuma Mwana wake wa pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi awe sadaka ya dhambi, na akaihukumu dhambi katika mwili. \v 4 Alifanya hivi ili maagizo ya sheria yatimilizwe ndani yetu, sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali kwa kufuata mambo ya Roho. \v 5 Wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, lakini wale waifuatao Roho huyafikiri mambo ya Roho.

1
08/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya Roho ni uzima na amani. \v 7 Hii ni kwa sababu ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. \v 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

1
08/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Hata hivyo, hampo katika mwili bali katika Roho, kama ni kweli kwamba Roho wa Mungu huishi ndani yenu. Lakini kama mtu hana Roho wa Kristo, yeye si wake. \v 10 Kama Kristo yumo ndani yenu, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, bali roho ni hai kwa mambo ya haki.

1
08/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka wafu huishi ndani yenu, yeye yule aliyemfufua Kristo kutoka katika wafu ataipa pia miili yenu ya mauti uhai kwa njia ya Roho wake, aishie ndani yenu.

1
08/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Hivyo basi, ndugu zangu, sisi tu wadeni, lakini si kwa mwili kwamba tuishi kwa jinsi ya mwili. \v 13 Maana ikiwa mnaishi kwa jinsi ya mwili, mpo karibu kufa, lakini ikiwa kwa Roho mnayafisha matendo ya mwili, nanyi mtaishi.

1
08/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu, hawa ni wana wa Mungu. \v 15 Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, "Abba, Baba!"

1
08/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa tu watoto wa Mungu. \v 17 Ikiwa tu watoto, basi tu warithi pia, warithi wa Mungu. Na sisi tu warithi pamoja na Kristo, ikiwa kwa kweli tunateseka na yeye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.

1
08/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu. \v 19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.

1
08/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Kwa maana uumbaji pia ulitiishwa chini ya ubatili, si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha. Ni katika tumaini \v 21 kwamba uumbaji wenyewe nao utawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, na kuingizwa katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. \v 22 Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa.

1
08/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Si hivyo tu, ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho - sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukisubiri kufanywa wana, yaani ukombozi wa miili yetu. \v 24 Kwa maana ni kwa taraja hili tuliokolewa. Lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena, kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? \v 25 Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.

1
08/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Kwa jinsi iyo hiyo, Roho naye hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. \v 27 Na yeye aichunguzaye mioyo huijua akili ya Roho, kwa sababu huomba kwa niaba yao walioamini kulingana na mapenzi ya Mungu.

1
08/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Nasi twajua ya kuwa kwa wote wampendao Mungu, yeye hufanya mambo yote pamoja kwa wema, kwa wale wote walioitwa kwa kusudi lake. \v 29 Kwa sababu wale wote aliowajua tangu asili, pia aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miogoni mwa ndugu wengi. \v 30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao aliwaita pia. Na wale aliowaita, hao aliwahesabia haki. Na wale aliowahesabia haki, hao pia akawatukuza.

1
08/31.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 31 Tuseme nini basi juu ya mambo haya? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu? \v 32 Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

1
08/33.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. \v 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa kwa ajili yetu, na zaidi ya hayo, yeye pia alifufuliwa. Naye anatawala pamoja na Mungu mahali pa heshima, na tena ndiye anayetuombea sisi.

Some files were not shown because too many files have changed in this diff Show More