sw_mrk_text_ulb/06/01.txt

1 line
465 B
Plaintext

\v 1 Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao, na wanafunzi wake wakamfuata. \v 2 Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikia na wakashangazwa. Wakasema, "Amepata wapi mafundisho haya?" "Ni hekima gani hii aliyopewa?" "Anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?" \v 3 "Je huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si wanaishi papa hapa pamoja nasi?" Na hawakufurahishwa na Yesu.