sw_mrk_text_ulb/10/01.txt

1 line
420 B
Plaintext

\v 1 Yesu aliondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Uyahudi na eneo la mbele ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya. \v 2 Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, "Ni halali kwa mwanamume kuachana na mke wake?" \v 3 Yesu akawajibu, "Musa aliwaamuru nini?" \v 4 Wakasema, "Musa aliruhusu kuandika cheti cha kuachana na kisha kumfukuza mwanamke."