sw_mrk_text_ulb/06/04.txt

1 line
311 B
Plaintext

\v 4 Yesu akawaambia, "Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika mji wake na miongoni mwa ndugu zake na nyumbani mwake." \v 5 Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya. \v 6 Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.