sw_mat_text_ulb/27/11.txt

1 line
364 B
Plaintext

\v 11 Sasa Yesu alisimama mbele ya liwali, na liwali akamwuliza, "Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?" Yesu alimjibu, "Wewe wasema hivyo." \v 12 Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote. \v 13 Kisha Pilato alimwambia, "Hujayasikia mashitaka yote dhidi yako?" \v 14 Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo liwali alijawa na mshangao.