sw_mat_text_ulb/25/34.txt

1 line
368 B
Plaintext

\v 34 Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, 'Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu. \v 35 Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha; \v 36 Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.'