sw_mat_text_ulb/19/10.txt

1 line
448 B
Plaintext

\v 10 Wanafunzi wakamwambia Yesu, "Kama ndivyo ilivyo kwa mume na mkewe, siyo vizuri kuoa." \v 11 Lakini Yesu akawaambia, "Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya, bali ni kwa wale tu walioruhusiwa kupokea. \v 12 Kwa vile wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama zao. Na vilevile kuna matowashi waliofanywa na watu. Na kuna matowashi waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kupokea mafundisho haya na ayapokee."