sw_mat_text_ulb/17/05.txt

1 line
397 B
Plaintext

\v 5 Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni yeye." \v 6 Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana. \v 7 Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, "Inukeni wala msiogope." \v 8 Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.