sw_mat_text_ulb/12/38.txt

1 line
475 B
Plaintext

\v 38 Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema" Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako." \v 39 Lakini Yesu alijibu na kuwaambia, "Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii. \v 40 Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.