sw_mat_text_ulb/11/20.txt

1 line
377 B
Plaintext

\v 20 Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu, \v 21 Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yangetendeka Tiro na Sidoni yale yaliyotendeka hapa, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. \v 22 Lakini itakuwa uvumilivu kwa Tiro na Sidoni siku ya hukumu kuliko kwako.