sw_mat_text_ulb/21/31.txt

1 line
418 B
Plaintext

\v 31 Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, "Mwana wa kwanza." Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia. \v 32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.