sw_mat_text_ulb/09/07.txt

1 line
355 B
Plaintext

\v 7 Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake. \v 8 Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu. \v 9 Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, "Nifuate mimi" Naye akasimama na kumfuata.