sw_mat_text_ulb/09/03.txt

1 line
427 B
Plaintext

\v 3 Tazama, Baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, "Huyu mtu anakufuru" \v 4 Yesu akatambua mawazo yao na kusema, "Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu? \v 5 Kipi kilicho rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema, 'Simama na utembee?' \v 6 Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi..." aliyasema haya kwa yule aliyepooza, "Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako"