sw_mat_text_ulb/04/01.txt

1 line
379 B
Plaintext

\v 1 Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na ibilisi. \v 2 Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa. \v 3 Mjarabu akaja na akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate." \v 4 Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, "Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.'''