\v 1 Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka plae kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao, \v 2 na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake, \v 3 na wakamuuliza, "Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?"