sw_jhn_text_ulb/04/43.txt

1 line
352 B
Plaintext

\v 43 Baada ya siku hizo mbili, akaondoka na kuelekea Galilaya. \v 44 Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ametangaza kuwa nabii hana heshima katika nchi yake mwenyewe. \v 45 Alipokuja kutoka Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha. Walikuwa wameona mambo yote aliyoyafanya Yerusalemu kwenye sikukuu, kwa sababu na wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye sikukuu.