sw_jhn_text_ulb/18/01.txt

1 line
449 B
Plaintext

\v 1 Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea bonde la Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambako yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake. \v 2 Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akienda hili eneo mara kadhaa akiwa na wanafunzi wake. \v 3 Naye Yuda, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.