sw_jhn_text_ulb/13/16.txt

1 line
366 B
Plaintext

\v 16 Amini, Amini, nawambia, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa ni mkuu kuliko yule aliye mtuma. \v 17 Ikiwa unafahamu mambo haya, umebarikiwa ukiyatenda. \v 18 Sisemi kuhusu ninyi nyote, kwa kuwa nawajua wale ambao nimewachagua - bali nasema haya ili kwamba maandiko yaweze kutimilizwa: 'Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.'