sw_jhn_text_ulb/12/34.txt

1 line
476 B
Plaintext

\v 34 Mkutano wakamjibu, "Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, 'Mwana Adamu lazima ainuliwe juu'? Huyu Mwana wa Mtu ni nani?" \v 35 Basi Yesu akawaambia, "Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendaye gizani hajui aendako. \v 36 Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru." Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.