sw_jhn_text_ulb/10/14.txt

1 line
328 B
Plaintext

\v 14 Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi. \v 15 Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. \v 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.