sw_act_text_ulb/20/33.txt

1 line
385 B
Plaintext

\v 33 Sikutamani fedha, dhahabu, au mavazi. \v 34 Mnajua ninyi wenyewe kwamba mikono hii imenipatia mahitaji yangu mwenyewe na mahitaji ya wale waliokuwa pamoja nami. \v 35 Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: "Ni heri kutoa kuliko kupokea."