sw_act_text_ulb/08/14.txt

1 line
390 B
Plaintext

\v 14 Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria imepokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana. \v 15 Wakati walipokuwa wakishuka wakawaombea; kwamba wampokee Roho Mtakatifu. \v 16 Mpaka muda huo, Roho Mtakatifu alikuwa hajawashukia hata mmoja wao; walikuwa tu wamebatizwa kwa jina la Bwana Yesu. \v 17 Ndipo Petro na Yohana wakawawekea mikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu.