sw_act_text_ulb/08/09.txt

1 line
386 B
Plaintext

\v 9 Lakini palikuwa na mtu mmoja katika mji ule jina lake Simon, ambaye alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu. \v 10 Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa, wakamsikiliza; wakasema;"mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu." \v 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mrefu kwa uchawi wake.