sw_act_text_ulb/27/30.txt

1 line
420 B
Plaintext

\v 30 Wale mabaharia walikuwa wanatafuta namna ya kuitelekeza ile meli na walizishusha majini boti ndogo ndogo za kuokolea maisha, na wakajifanya kwamba wanatupa nanga kutoka sehemu ya mbele ya boti. \v 31 Lakini Paulo akamwambia yule askari wa jeshi la Kiroma na wale askari, "Hamuwezi kuokoka isipokuwa hawa watu wanabaki kwenye meli". \v 32 Kisha wale askari wakakata kamba za ile boti na ikaachwa ichukuliwe na maji.