sw_act_text_ulb/27/27.txt

1 line
481 B
Plaintext

\v 27 Ulipofika usiku wa kumi na nne, tulipokuwa tukiendeshwa huko na huko kwenye bahari ya Adratik, kama usiku wa manane hivi, mabaharia walifikiri kwamba wamekaribia nchi kavu. \v 28 Walitumia milio kupima kina cha maji na wakapata mita thelathini na sita, baada ya muda mfupi wakapima tena wakapata mita ishirini na saba. \v 29 Waliogopa kwanza tunaweza kugonga miamba, hivyo wakashusha nanga nne kutoka katika sehemu ya kuwekea nanga na wakaomba kwamba asubuhi ingekuja mapema.