sw_act_text_ulb/27/14.txt

1 line
365 B
Plaintext

\v 14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali, ulioitwa Wa kaskazini mashariki, ukaanza kutupiga kutoka ng'ambo ya kisiwa. \v 15 Wakati meli ilipolemewa na kushindwa kuukabili upepo, tukakubaliana na hali hiyo, tukasafirishwa nao. \v 16 Tukakimbia kupitia ule upande uliokuwa unaukinga upepo wa kisiwa kiitwacho Kauda; na kwa taabu sana tulifanikiwa kuuokoa mtumbwi.