\v 42 Itakuwa hivi vilevile wakati wafu watakapofufuka. Mwili unazikwa katika udongo katika hali ya kuharibika, lakini unapofufuka, unafufuka na hali ya kutoweza kuharibika \v 43 na hali ya utukufu; nao unazikwa katika uzaifu, lakini unafufuka na nguvu. \v 44 Wakati unapozikwa ni mwili wa kimtu, lakini unapofufuka unageuka mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa kimtu, basi kuna mwili wa kiroho vilevile.