sw_zec_text_reg/11/01.txt

1 line
392 B
Plaintext

\v 1 Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mielezi yako! \v 2 Omboleza, enyi miti ya misonobari, kwani mierezi imeanguka! Kilichokuwa cha fahari kimeteketezwa! Ombolezeni, enyi mialoni ya Bashani, kwani msitu wenye nguvu umeshushwa. \v 3 Wachungaji wanapiga yowe, kwa kuwa utukufu wao umeharibiwa! Sauti ya mungurumo wa wana simba, kwa kuwa kiburi cha Mto Yordani kimeharibiwa!