sw_zec_text_reg/10/11.txt

1 line
292 B
Plaintext

\v 11 Nitapita katika bahari ya mateso yao; nitayapiga mawimbi ya bahari hiyo na nitavikausha vilindi vyote vya Nile. Utukufu wa Ashuru utashushwa chini, na fimbo ya Misri itakwenda mbali kutoka kwa Wamisri. \v 12 Nitawatia nguvu mimi mwenyewe, nao watatembea katika jina langu - asema Yahwe.