sw_zec_text_reg/10/04.txt

1 line
339 B
Plaintext

\v 4 Kutoka kwao litatoka jiwe kuu la pembeni; kutoka kwao kitatoka kigingi cha hema; kutoka kwao utatoka upinde wa vita; kutoka kwao watakuja viongozi wote kwa pamoja. \v 5 Watakuwa kama mashujaa wawakanyagao adui zao katika matope ya mitaani vitani; watafanya vita, kwa maana Yahwe yu pamoja nao, nao watawaabisha wapanda farasi wa vita.