sw_rom_text_ulb/09/19.txt

1 line
435 B
Plaintext

\v 19 Kisha utasema kwangu, "Kwa nini bado anaona kosa? Ni yupi ambaye alikwisha kustahimili matakwa yake?" \v 20 Kinyume chake, mwanadamu, wewe ni nani ujibue kinyume na Mungu? Kuna uwezekano wowote wa kilichofinyangwa kusema kwa mfinyanzi, "Kwa nini ulinifanya hivi mimi?" \v 21 Je mfinyazi huwa hana haki juu ya udongo kutengeneza chombo kwa matumizi maalumu kutokana na bonge lile lile, na chombo kingine kwa matumizi ya kila siku?