Wed Mar 16 2022 16:34:26 GMT+0300 (East Africa Time)

This commit is contained in:
nicholuskombo 2022-03-16 16:34:26 +03:00
commit c9f11a4e16
25 changed files with 49 additions and 1 deletions

1
01/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo ambao Mungu alimpa ili kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee karibuni. Aliyafanya yajulikane kwa kumtuma malaika wake kwa mtumishi wake Yohana. \v 2 Yohana alitoa ushuhuda wa kila kitu alichoona kuhusiana na neno la Mungu na kwa ushuhuda uliotolewa kuhusu Yesu Kristo. \v 3 Amebarikiwa yeye asomaye kwa sauti na wale wote wanaoyasikia maneno ya unabii huu na kutii kilichoandikwa humo, kwa sababu muda umekaribia.

1
01/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo, na atakayekuja, na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi, \v 5 na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mtawala wa wafalme wa dunia hii. Kwake yeye atupendaye na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake, \v 6 ametufanya kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba yake - kwake kuwa utukufu na nguvu milele daima. Amina.

1
01/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Tazama, anakuja na mawingu; kila jicho litamwona, pamoja na wote waliomchoma. Na kabila zote za dunia wataomboleza kwake. Ndiyo, Amina. \v 8 "Mimi ni Alfa na Omega," asema Bwana Mungu, "Yeye aliyepo, na aliyekuwepo, na ambaye anakuja, Mwenye nguvu."

1
01/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Mimi, Yohana - ndugu yenu na mmoja anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu; nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patimo kwa sababu ya neno la Mungu na ushuhuda kuhusu Yesu. \v 10 Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana. Nilisikia nyuma yangu sauti ya juu kama ya tarumbeta, \v 11 ikisema, "andika katika kitabu unayo yaona, na uyatume kwa makanisa saba, kwenda Efeso, kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia."

1
01/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Nikageuka kuona ni sauti ya nani aliyekuwa akiongea nami, na nilipogeuka niliona kinara cha dhahabu cha taa saba. \v 13 Katikati ya kinara cha taa alikuwemo mmoja kama Mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu iliyofika chini ya miguu yake, na mkanda wa dhababu kuzunguka kifua chake.

1
01/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji, na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. \v 15 Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi. \v 16 Alikuwa ameshikilia nyota saba katika mkono wake wa kuume, na kutoka kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa uking'aa kama mwanga mkali wa jua.

1
01/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Nilipomwona, nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, "Usiogope! Mimi ni wa kwanza na wa Mwisho, \v 18 na ambaye ninaishi. Nalikuwa nimekufa, lakini tazama, ninaishi milele! Na ninazo funguo za mauti na kuzimu.

1
01/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Kwa hiyo, yaandike uliyoyaona, yaliyopo sasa, na yale yatakayotokea baada ya haya. \v 20 Kwa maana iliyojificha kuhusu nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na kile kinara cha dhahabu cha taa saba: nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na kinara cha taa saba ni yale makanisa saba."

1
01/title.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
Mlango 1

1
02/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 "Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: 'Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi, " \v 2 '"Najua ambacho umetenda na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, na umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo.

1
02/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado. \v 4 Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza. \v 5 Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.

1
02/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Lakini wewe una hili, unachukia yale ambayo Wanikolai wameyatenda, ambayo hata mimi nayachukia. \v 7 Kama una sikio, sikiliza yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Na kwa yeye ashindaye nitampa kibali cha kula kutoka katika mti wa uzima ulio katika paradiso ya Mungu.'

1
02/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 "Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika: 'Haya ni maneno ya yule ambaye ni mwanzo na mwisho ambaye alikufa na kuwa hai tena: \v 9 '"Nayajua mateso yako na umasikini wako (lakini wewe ni tajiri), na uongo wa wale wanaojiita ni wayahudi (lakini siyo - wao ni sinagogi la Shetani).

1
02/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Tazama! Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani ili mpate kujaribiwa, na mtateseka kwa siku kumi. Iweni waaminifu hadi kufa, na nitawapa taji ya uzima. \v 11 Kama una sikio, sikiliza Roho anavyoyaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapata madhara ya mauti ya pili.'

1
02/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 "Kwa malaika wa kanisa la Pergamo andika: 'Haya ndiyo anenayo yeye aliye nao huo upanga mkali, wenye makali kuwili. \v 13 '"Najua mahali unapoishi -mahali kilipo kiti cha enzi cha shetani. Hata hivyo wewe walishika sana jina langu, na hukuikana imani yako iliyo kwangu, hata siku zile za Antipasi shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa miongoni mwenu, hapo ndipo Shetani anaishi.

1
02/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israel, ili wale vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu na kuzini. \v 15 Katika hali iyo hiyo, hata wewe unao baadhi yao wanaoshika mafundisho ya Wanikolai.

1
02/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Basi tubu! Na usipofanya hivyo, naja upesi, na nitafanya vita dhidi yao kwa upanga utokao katika kinywa changu. \v 17 Kama una sikio, sikiliza Roho anachowaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, pia nitampa jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu ya jiwe, jina ambalo hakuna alijuaye isipokuwa yeye alipokeaye.'

1
02/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 "Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika: "Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na nyayo kama shaba iliyosuguliwa sana: \v 19 '"Najua ambacho umefanya - upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti, na kwamba kile ulichofanya hivi karibuni ni zaidi ya kile ulichofanya mwanzo.

1
02/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Lakini ninalo hili dhidi yako: unamvumilia mwanamke Yezebeli anayejiita mwenyewe nabii mke. Kwa mafundisho yake, anawapotosha watumishi wangu kuzini na kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu. \v 21 Nilimpa muda wa kutubu, lakini hayuko tayari kuutubia uovu wake.

1
02/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Angalia! Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi, na wale watendao uasherati naye kwenye mateso makali, vinginevyo watubu kwa alichofanya. \v 23 Nitawapiga wanawe wafe na makanisa yote watajua kwamba mimi ndiye niyachunguzaye mawazo na tamaa. Nitampa kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.

1
02/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Lakini kwa baadhi yenu mliosalia katika Thiatira, kwa wale wote msioshika fundisho hili, na msiojua kile ambacho baadhi huita mafumbo ya Shetani, nasema kwenu, 'sitaweka juu yenu mzigo wowote.' \v 25 Kwa jambo lolote, lazima muwe imara mpaka nitakapokuja.

1
02/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Yeyote ashindaye na kufanya kile nilichofanya hadi mwisho, kwake yeye nitampa mamlaka juu ya mataifa. \v 27 'Atawatawala kwa fimbo ya chuma, kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande.' \v 28 Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu, nitampa pia nyota ya asubuhi. \v 29 Ukiwa na sikio, sikiliza kile ambacho Roho anayaambia makanisa.'

1
02/title.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
Mlango 2 nicholus

1
front/title.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
Ufunuo martin

View File

@ -46,6 +46,30 @@
"03-14",
"03-17",
"03-19",
"03-21"
"03-21",
"02-title",
"02-01",
"02-03",
"02-06",
"02-08",
"02-10",
"02-12",
"02-14",
"02-16",
"02-18",
"02-20",
"02-22",
"02-24",
"02-26",
"front-title",
"01-title",
"01-01",
"01-04",
"01-07",
"01-09",
"01-12",
"01-14",
"01-17",
"01-19"
]
}