\v 24 Hofu ya mwenye uovu humkumba ghafla, bali shauku ya mwenye haki itatimizwa. \v 25 Waovu ni kama dhoruba inayopita, na hawapo tena, bali mwenye haki ni msingi unaodumu milele.