\v 32 Na sasa, wanangu, nisikilizeni, maana wale wazishikao njia zangu watakuwa na furaha. \v 33 Sikilizeni fundisho langu na mpate hekima; wala msilipuuze. \v 34 Anisikilizaye atakuwa na furaha- kila siku akitazama katika malango yangu, akinisubiri pembeni mwa milango ya masikani yangu.