sw_num_text_reg/11/18.txt

1 line
551 B
Plaintext

\v 18 Waambie watu, 'Jitakaseni ninyi wenyewe, kwa kuwa kesho mtakula nyama, kwa kuwa mmelia na BWANA amesikia, "Mlipokuwa mkisema kuwa nani atakayetupa nyama tule? Kule Misri tulikula chakula kizuri!" Kwa hiyo BWANA atawapeni nyama, nanyi mtakula nyama. \v 19 Hamtakula nyama kwa siku moja tu, au siku mbili, au siku tano, au siku kumi, au siku ishirini, \v 20 Lakini mtakula nyama kwa mwezi mmoja mpaka zitakapowatokea puani. Mpaka mutazikinai kwa sababu mmemkataa BWANA ambaye yuko kati yenu. Mmelia mbele yake. mmesema, "Kwa nini tulitoka Misri?""