sw_num_text_reg/01/01.txt

1 line
533 B
Plaintext

\c 1 \v 1 Mungu alimwambia Musa katika hema ya kukutania walipokuwa katika jangwa la Sinai. Hii ilitokea katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili miaka miwili baadaya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Mungu alisema, \v 2 'fanya sensa ya wanaume wote wa Israel kutoka kila ukoo, katika familia za baba zao. Wahesabu kwa majina, wahesabu kila mume, kila mwanamume \v 3 kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi. Uwahesabu wote wanaoweza kupigana kama askari wa Israel. Wewe na Haroni mtaandika idadi ya wanaume katika makundi ya majeshi yao.