sw_num_text_reg/21/01.txt

1 line
471 B
Plaintext

\v 1 Aradi mfalme wa Wakanaani, aliyekuwa akiishi Negebu, aliposikia kuwa Israeli alikuwa akisafiri kwa kupitia barabara kuelekea Atharimu, akapigana dhidi ya Israeli na kujitwalia baadhi ya mateka. \v 2 Israeli akaapa mbele ya BWANA akasema, "Kama utatupa ushindi dhidi ya hawa watu, ndipo tutakapoingamiza kabisa miji yao," \v 3 BWANA akaisikia sautiya Israeli na kuwapa ushindi dhidi ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. Mahali pale paliitwa Horima.