sw_num_text_reg/07/54.txt

1 line
455 B
Plaintext

\v 54 Siku ya nane, Gamaliel mwana wa Pedazuri, kiongozi wa uzao wa Manase, alitoa sadaka yake. \v 55 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga. \v 56 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.