sw_num_text_reg/07/42.txt

1 line
454 B
Plaintext

\v 42 Siku ya sita, Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa uzao wa Gadi, alitoa sadaka yake. \v 43 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga. \v 44 Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.