sw_num_text_reg/29/14.txt

1 line
407 B
Plaintext

\v 14 Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembaba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa kila fahari katika hao kumi na tatu, sehemu mbili za kumi kwa kila hao kondoo dume wawili, \v 15 na sehemu ya kumi ya efa ya hao wanakondoo kumi na nne. \v 16 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa, sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka za vinywaji.