sw_num_text_reg/18/30.txt

1 line
499 B
Plaintext

\v 30 Kwa hivyo utawaambia, 'Mnapotoa hayo matoleo mazuri, ndipo itahesabika kwa Walawi kuwa ni mazao yao kutoka kwenye sakafu za kupuria na vinu vyao vya kukamulia. \v 31 Ndipo matakapokula nafaka zote zinazobaki mahali popote, ninyi na familia zenu kwa sababu ndiyo malipo yenu ya kazi kwenye hema ya kukutania. \v 32 Hamtakuwa na hatia yeyote kwa kuvila na kuvinywa, kama mtatoa kwa BWANA matoleo yenu mazuri mliyopokea. Lakini msizinajisi sadaka takatifu za wana wa Israeli, la sivyo mtakufa.,"