sw_num_text_reg/18/23.txt

1 line
429 B
Plaintext

\v 23 Walawi wafanya kazi inayohusiana na hema ya kukutania. Watawajibika kwa dhambi inyohusiana na hema. Hii itakuwa sheria ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Na miongoni mwa watu wa Israeli hawa hawatakuwa na urithi. \v 24 Kwa kuwa zaka za wana wa Israeli, wanazotoa kama mchango kwangu -ndivyo hivyo ambavyo nimewapa Walawi kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu ya kuwaambia, Kuwa hawatakuwa na urithi kati ya watu wa Israeli.