sw_num_text_reg/18/03.txt

1 line
446 B
Plaintext

\v 3 Watakutumikia wewe na hema yote. Hata hivyo, wasisonge karibu na chochote ndani ya mahali pa patakatifu au kwa kitu chochote kilichounganishwa na madhabahu,la sivyo, wewe na wao mtakufa. \v 4 Wataungana na wewe na kuitunza hema ya kukutania, kwa kazi zote zinazohusiana na hema. Mtu mgeni hasikukaribie. \v 5 Wewe utawajibika kwa ajili ya mahali papatakatifu na kwa ajili ya madhabahu ili kwamba hasira yangu isiwajilie watu wa Israeli tena.