sw_num_text_reg/14/06.txt

1 line
374 B
Plaintext

\v 6 Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wametumwa kwenda kuipeleleza nchi wakachana mavazi yao. \v 7 Wakawaambia watu wote wa Israeli. Walisema, "Ile nchi tuliyopita katikati yake ni nchi nzuri sana. \v 8 Kama BWANA amependezwa nasi, basi atatuingiza katika nchi hii na kutupatia. Ile nchi inatiririka maziwa na asali.