sw_num_text_reg/04/01.txt

1 line
428 B
Plaintext

\c 4 \v 1 BWANA akanena na Musa na Haroni. Akasema, \v 2 Fanya sensa ya uzao wa waume wa Kohathi kutoka kwa Walawi, kwa kufuata jamaa na familia za ukoo. \v 3 Uwahesabu wanaume ambao wana umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Hawa wataungana na kundi linalotumika kutoa huduma kwenye hema ya kukutania. \v 4 Uzao wa Kohathi watalinda vile vitu vitakatifu zaidi vilivyohifadhiwa kwa ajili yangu katika hema ya kukutania.