sw_num_text_reg/35/19.txt

1 line
437 B
Plaintext

\v 19 Mwenye kulipa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji. atakapokutana naye, anaweza kumwua. \v 20 Lakini kama yule mtuhumiwa atamshinda mtu yeyote yule anayemchukia au kama atamtupia kitu, wakati akimvizia, kiasi kwamba huyo mtu akafa, \v 21 au kama atampiga ngumi kwa chuki na mtu huyo akafa, ndipo yule mtuhumiwa aliyempiga hakika atauawa. Yeye ni mwuaji. Yule mlipa kisasi cha damu anaweza kumwua muuaji pale atakapokutana naye.