sw_num_text_reg/34/13.txt

1 line
507 B
Plaintext

\v 13 Kisha Musa akawaamuru watu wa Israeli akasema, "Hii ndiyo nchi ambayo mtaipokes kwa kura, ambayo BWANA ameamuru kuwapa wale makabila tisa na nusu. \v 14 Kabila ya uzao wa Reubeni, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na uzao wa kabila la Gadi, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na nusu ya Manase wamepata ardhi yao. \v 15 Wale makabila mawili na nusu wameshapata mgao wao ng'ambo ya mto Yorodani upande wa mashariki, kuelekea kule linakotokea jua."