sw_num_text_reg/05/24.txt

1 line
463 B
Plaintext

\v 24 Naye kuhani atamwelekeza yule mwanamke kunywa yale maji machungu yaletayo laana. Yale maji yaletayo laana yataingia na kuwa machungu. \v 25 Kuhani ataitwaa ile sadaka ya unga ya wivu mikononi mwa yule mwanamke. Atailekeza ile sadaka ya unga mbele ya BWANA na kuileta madhabahuni. \v 26 Kuhani atachukua konzi ya sadaka ya unga mkononi mwake kama sadaka ya kuwakilisha, na kuiteketeza madhabahuni. Ndipo atakapompatia mwanamke yale maji machungu ili ayanywe.